1 / in the bank (part 1) - hatua kwa hatuakiingerezahatuakwahatua.com/books/kiingereza - hatua kwa...

24

Upload: others

Post on 31-Oct-2020

12 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: 1 / In the bank (part 1) - Hatua kwa Hatuakiingerezahatuakwahatua.com/books/Kiingereza - Hatua kwa Hatua 3… · behind (nyuma ya) in front of (mbele ya) bihaind frānt av next to
Page 2: 1 / In the bank (part 1) - Hatua kwa Hatuakiingerezahatuakwahatua.com/books/Kiingereza - Hatua kwa Hatua 3… · behind (nyuma ya) in front of (mbele ya) bihaind frānt av next to

1

1 ► In the bank (part 1) /in dha bank1/ /waaka/

A (bank worker): Good morning. /gud mooning/

B (Nicholas): Good morning. Sorry I'm late. My name is Mister Phillips. I'm here to open an account. (1) (2) (3) gud

mooning sori aim leit mai neim iz mista filips aim hia tuu oupan an akount/

A: That's no problem. I have the forms here, Mister Phillips. I need a little information. First, what is your full name? (4) /dhats nou problam ai hav dha foomz hia mista filips ai niid a litl infameishan

faast wot iz yoo ful neim/

B: It's Nicholas Matthew Phillips. /its nikalas mathyuu filips/

A: What's the spelling of your surname please? (5) /wots dha speling av yoo saaneim pliiz/

B: It's P-H-I-L-L-I-P-S. /its pii eich ai el el ai pii es/

A: Thank you...and what's your job? /thank yuu and wots yoo job/

B: I'm a shop manager. /aim a shop manija/

(1) Sorry I'm late. I'm on time. (Nimefika kwa muda ulipangwa.) I'm early. (Nimewahi.) /on taim aali/

(2) I'm... I'm = I am He's = He is /aim ai am hiiz hii iz She's = She is It's = It is shiiz shii iz its it iz They're = They are You're = You are dhea dhei aa yoo yuu aa/

(3) open an account close a bank account (funga akaunti ya benki) open a door (fungua mlango) close a door (funga mlango) /klouz doo/

2 ► In the bank (part 2)

A: Are you married? (1) /aa yuu marid/

B: No. I'm not. (2) /nou aim not/

A: Single...what's your address2? /singl wots yoor adres/

B: It's 2 North Street, Cardiff. /its tuu nooth striit kaadif/

A: Could I have your home telephone number, please? (3) /kud ai hav yoo houm telifoun nāmba pliiz/

1 Maandishi haya huonyesha matamshi ya maneno. Maelekezo ya namna ya

kuyasoma vizuri yanapatikana ukurasa wa 19. 2 Barua hupelekwa moja kwa moja mpaka nyumbani Uingereza. PO Box ni neno la

Kiingereza badala ya SLP /pii ou boks/.

Page 3: 1 / In the bank (part 1) - Hatua kwa Hatuakiingerezahatuakwahatua.com/books/Kiingereza - Hatua kwa Hatua 3… · behind (nyuma ya) in front of (mbele ya) bihaind frānt av next to

2

Ndani ya benki (sehemu ya 1)

A (mfanyakazi wa benki): Habari za asubuhi? bank-benki worker-mfanyakazi (good--zuri morning-asubuhi)

B (Nicholas): Nzuri. Samahani, nimechelewa. Jina langu ni Bwana Phillips. Niko hapa kufungua akaunti. my-angu sorry-samahani I'm late-nimechelewa name-jina open-fungua account-akaunti

A: Hilo si tatizo. Nina fomu hapa, Bwana Phillips. Nahitaji taarifa kidogo. Kwanza, jina lako kamili ni nani? problem-tatizo form-fomu Mister-Bwana need-hitaji a little-kidogo information-taarifa (what-nini) first-kwanza full name-jina kamili

B: Ni Nicholas Matthew Phillips. it's-(hili) ni

A: Nitajie herufi za jina lako la mwisho tafadhali? spelling-herufi surname-jina la mwisho, ukoo

B: Ni P-H-I-L-L-I-P-S.

A: Asante... na unafanya kazi gani? job-kazi

B: Mimi ni meneja wa duka manager-meneja, mkurugenzi shop-duka (4) full name Waingereza wengi wana majina matatu; jina la kwanza 'first name' au 'forename', (pia huitwa jina la kikristu 'Christian name' kama ni wakristu), jina la kati 'middle name' na jina la mwisho au la ukoo 'surname' au 'family name' – Jina la kati huwa halihitajiki kwa matumizi rasmi. /faast fooneim kristian midl saaneim famali/

(5) What's = What is the spelling3 ni mfumo wa herufi na mpangilio wake katika neno.

Ndani ya benki (sehemu ya pili)

A: Umeoa? married- -oa, -olewa

B: Hapana. Sijaoa no-hapana

A: Hajaoa... Anuani yako ni ipi? single-hajaoa, hajaolewa (bila mke au mume), address-anuani

B: Ni 2 North Street, Cardiff (north-kusini street-mtaa) Cardiff-jina la mji

A: Naweza kupata nambari yako ya simu ya nyumbani tafadhali? home-nyumbani telephone-simu number-nambari

3 Tunaweza pia kusema ‘How do you spell your name?’ (Unaandikaje jina lako?)

/hau duu yuu spel yoo neim/

Page 4: 1 / In the bank (part 1) - Hatua kwa Hatuakiingerezahatuakwahatua.com/books/Kiingereza - Hatua kwa Hatua 3… · behind (nyuma ya) in front of (mbele ya) bihaind frānt av next to

3

B: It's 130519 /its wān thrii ou faiv wān nain/

A: ...and your office number? /and yoor ofis nāmba/

B: 13211414. /its wān thrii tuu wān wān foo wān foo/

A: Thank you, and how old are you? /thank yuu and hau ould aa yuu/

B: I'm thirty-six. (4) /aim thaati siks/

A: Thank you. /thank yuu/

(1) Are you married? He is a doctor. (Yeye ni daktari.) Is he a doctor? ((Je), yeye ni daktari?) /dokta

They are doctors. (Wao ni madaktari.) doktaz/ Are they doctors? (Wao ni madaktari?)

I am late. (Nimechelewa.) Am I late? Nimechelewa?)

They are here. (Wapo.) Are they here? (Wapo?)

His name is John. (Jina lake ni John.) What is his name? (Jina lake ni nani?)

He is outside (Yeye yupo nje.) /autsaid Where is he? (Yeye yupo wapi?) wear iz hii

You are from Cardiff. (Unatokea Cardiff.) from Where are you from? (Unatokea wapi?) wear aa/

The meeting is tomorrow. (Mkutano upo/ni kesho.) miiting tamorou

When is the meeting? (Mkutano upo/ni lini?) wen/

(2) No, I'm not. Kwenye baadhi ya mazungumzo, kusema tu ndio 'yes' au hapana 'no' huonekana kuwa ni lugha ya mkato sana. Pale mtu anapouliza swali kwa kutumia is/am/are, maneno haya hutumika pia kwenye majibu. Baadhi ya mifano ni kama ifuatavyo:

3 ► Yes, I am. No, I'm not. Yes, he is. No, he isn't. Yes, she is. No, she isn't. Yes, it is. No, it isn't. Yes, we are. No, we aren't. Yes, they are. No, they aren't. Yes, you are. No, you aren't.

Zingatia kuwa katika kiingereza 'you' hutumika kuzungumzia zaidi ya mtu mmoja.

(3) Could I have your...Ilivyotumika hapa , 'Could I have...?' ni namna nyingine ya kusema 'Can I have...?'. Namna zote mbili hutumika

Page 5: 1 / In the bank (part 1) - Hatua kwa Hatuakiingerezahatuakwahatua.com/books/Kiingereza - Hatua kwa Hatua 3… · behind (nyuma ya) in front of (mbele ya) bihaind frānt av next to

4

B: Ni 130519

A: ... na nambari ya ofisini? office-ofisi

B: 13211414.

A: Asante, na una umri gani? old- -zee, (umri)

B: Nina miaka thelathini na sita thirty-thelathini six-sita

A: Asante.

kuomba kitu. /kan ai hav/

(4) I'm thirty-six Zingatia kuwa, kuzungumzia umri wa mtu au kitu kwa Kiingereza tunatumia am/is/are sio 'have'; kwa 'How old are you?', tunaweza kujibu 'I am thirty-six years old.' au 'I am thirty-six'. Hatusemi 'I have thirty-six years'. /yaaz ould/

Jaza nafasi zilizoachwa wazi (1): 1) Where i _ he? He'_ outside. 2) W _ _ _ is his name? I_'_ John. 3) A _ _ you married? No. I'_ not. I'm s_ _ _ _ _. 4) How o_ _ are your children? John i_ twelve and Mary i_ s_ _. 5) A _ I late? No, y _ _' r _ not. You are on time.

Mazoezi ya kuongea4 4 ► What's your name? address What's your address? his What's his address? your What's your address? job What's your job? telephone number What's your telephone number?

5 ► Are you a manager? she Is she a manager? teacher Is she a teacher? they Are they teachers? doctors Are they doctors? late Are they late? I Am I late? he Is he late? married Is he married? single Is he single?

4 Kama huna uhakika wa juinsi ya kufanya zoezi hili, tazama ukurasa wa 23.

Page 6: 1 / In the bank (part 1) - Hatua kwa Hatuakiingerezahatuakwahatua.com/books/Kiingereza - Hatua kwa Hatua 3… · behind (nyuma ya) in front of (mbele ya) bihaind frānt av next to

5

6 ► The way to the museum (part 1)

A (tourist): Excuse me. What’s the way to the museum please? (1) (2) /ikskuuz mii wots dha wei ta dha myuuziam pliiz/ /tuarist/

B (local person): The museum? Go straight on for a hundred metres, until the traffic lights. (3) (4) /loukal paasan/ /dha myuuziam gou streit on far a hāndrad miitaz āntil dha trafik laits/

A: Yes. /yes/

B: Then turn left... /dhen taan left/

A: Okay. Thank you... /oukei thank yuu/

B: ...then you go down the hill, take the second turning on the right and walk over the bridge... /dhen yuu gou daun dha hil teik dha sekand taaning on dha rait and wook ouva

dha brij/

A: ...over the bridge, yes...

B: ...then go along the road, go past the football stadium... /gou along dha roud gou paast dha futbool steidiam/

A: ...er...okay...(5) /aa oukei/

(1) the way to the museum the way to the shop (njia ya kwenda dukani) the way to my house (njia ya kwenda nyumbani kwangu) Tell me the way to the hospital (niambie njia ya kwenda hospitali) /dha shop mai haus tel mii dha hospital/

(2) the museum (3) the traffic lights Zingatia kuwa 'the'5 hutumika kwenye kiingereza wakati 1) Kuna idadi kitu kimoja tu kinachongelewa (mf. Kuna jumba moja tu la makumbusho katika mji huu) au 2) wote wawili, mzungumzajia na sikilizaji wanakifahamu kitu gani au vitu gani wanavyovionglea (Hapa, ni wazi kwa msikilizaji ni taa gani za trafiki mzungumzaji anaziongelea).

(4) go straight on We can also say ‘go straight ahead’ Note: straight road (barabara iliyonyooka) /ahed roud/

(5) er... Hii haina maana. Ni sauti inayotumika wakati mzungumzaji

anafikiria. Sio neno linalotumika katika Kiingereza cha maandishi. (Tazama ukarasa 20)

5 ‘the’ inaweza kutamkwa kama /dha/ na /dhii/

Page 7: 1 / In the bank (part 1) - Hatua kwa Hatuakiingerezahatuakwahatua.com/books/Kiingereza - Hatua kwa Hatua 3… · behind (nyuma ya) in front of (mbele ya) bihaind frānt av next to

6

Njia ya kwenda makumbusho (sehemu ya 1)

A (mtalii): Samahani. Njia ya kwenda makumbusho ni ipi tafadhali? excuse me-samahani museum-makumbusho please-tafadhali

B (mwenyeji): Makumbusho? Nenda moja kwa moja kwa mita mia moja, mpaka taa za trafiki. (person-mtu) go-enda go straight-nenda moja kwa moja hundred-mia moja metre-mita until-mpaka traffic-trafiki light-taa

A: Ndio

B: Halafu kata kushoto... then-halafu turn-geuka, kata left-kushoto

A: Sawa. Asante...

B: ...halafu unashuka kilima, katiza njia ya pili upande wa kulia na uvuke kwenye daraja down-chini hill-kilima go down-shuka take the second turning-katiza kona ya pili second-ya pili right-kulia (walk-tembea) bridge-daraja

A: ...juu ya daraja, ndio... over-juu ya

B: ...halafu fuatana na barabara, nenda mpaka baada ya uwanja wa mpira wa miguu.. go along the road- -fuatana barabara road-barabara go past-enda mpaka baada ya, pita football-mpira wa miguu stadium-uwanja

A: ...er... sawa...

7 ► turn left (geuka kushoto) turn right (geuka kulia) /taan left rait

on the right (ipo upande wa kulia) on the left (ipo upande wa kushoto) on on the other side (ipo upande wa pili) ādha said

behind (nyuma ya) in front of (mbele ya) bihaind frānt av

next to (pembeni ya) by (pembeni ya) nekst ta bai

take the first turning (katiza kona ya kwanza) teik dha faast taaning

take the second turning (katiza kona ya pili) sekand

go straight on (nenda moja kwa moja) gou streit on

go past the church (nenda mpaka baada ya kanisa) paast dha chaach

go up the hill (panda kilima) āp dha hil

keep going (endelea kwenda) kiip gouing/

Page 8: 1 / In the bank (part 1) - Hatua kwa Hatuakiingerezahatuakwahatua.com/books/Kiingereza - Hatua kwa Hatua 3… · behind (nyuma ya) in front of (mbele ya) bihaind frānt av next to

7

8 ► The way to the museum (part 2)

B: ...then keep going until you see a big car park. The museum is behind the car park. It has flags outside. /dhen kiip gouing āntil yuu sii a big kaa paak dha myuuziam iz bihaind dha kaa

paak it haz flagz autsaid/

A: Thanks. So I go left after the lights, then take the first...no, the second road on the right...it's near the football stadium. /thanks sou ai gou left aafta dha laits dhen teik dha faast nou dha sekand roud

on dha rait its nia dha futbool steidiam/

B: Yes, on the other side of the river. /yes on dhii ādha said av dha riva/

A: Hmm...how far is it? (1) (2) /hmm hau faar iz it/

B: Two or three miles6 - it is about forty minutes if you walk. (3) /tuu oo thrii mailz it iz abaut footi minits if yuu wook/

A: Can I get a taxi around here? (4) /kan ai get a taksi araund hia/

B: Yes, but they are expensive. You can take a bus there. They go every fifteen minutes. (5) /yes bāt dhei aar ikspensiv yuu kan teik a bās dhea dhei gou evri fiftiin minits/

A: Thanks very much. /thanks veri māch/

B: You're welcome. (6) /yoo welkam/

(1) hmm... Hii haina maana. Ni sauti inayotumika wakati mzungumzaji anafikiria. Sio neno linalotumika katika Kiingereza cha maandishi.

(2) How far is it? how inaweza kutumika pamoja na maneno mengine kuuliza maswali: 9 ► How old are you? (How+old) (Una umri gani?) How far is it? (Ni mbali kiasi gani?) How big is your house? (Nyumba yako ina ukubwa gani?) How good is that job? (Kazi hiyo ni nzuri kiasi gani?) How new is his car? (Gari lake ni jipya kiasi gani) How tall is he? (Yeye ni mrefu kiasi gani?) How fast is that car? (Gari hilo lina kasi kiasi gani?)

6 Uingereza au Marekani, ni kawaida zaidi kutumia miles (maili), ila watu

wanafahamu pia kilometa. maili 1= kilomita 1.609

Page 9: 1 / In the bank (part 1) - Hatua kwa Hatuakiingerezahatuakwahatua.com/books/Kiingereza - Hatua kwa Hatua 3… · behind (nyuma ya) in front of (mbele ya) bihaind frānt av next to

8

Njia ya kwenda makumbusho (sehemu ya pili)

B: ...halafu endelea kwenda mpaka utakapoona uwanja mkubwa wa kupaki magari. Makumbusho yapo nyuma ya uwanja wa kupaki magari. Kuna bendera nje. keep going-endelea kwenda big-kubwa car park-uwanja wa kupaki magari flag-bendera outside-nje

A: Asante. Kwa hiyo naenda kushoto baada ya taa, halfu naenda njia ya kwanza...hapana, ya pili upande wa kulia...Ni karibu na uwanja wa mpira wa miguu. near-karibu ya...

B: Ndio, upande wa pili wa mto. (other-mwingine) side-upande river-mto

A: Hmm... Ni mbali kiasi gani? far-mbali

B: Maili mbili au tatu - ni kama dakika arobaini kama ukitembea. mile-maili about-kama minute-dakika if-kama

A: Naweza kupata teksi maeneo haya? get-pata taxi-teksi around-karibu na here-hapa

B: Ndio, lakini ni ghali. Unaweza kupata basi pale. Yanakwenda kila dakika 15. but-lakini expensive-ghali (take-chukua,) there-pale go-enda every-kila minute-dakika

A: Asante sana

B: Karibu

10 ► How old are you? tall How tall are you? he How fast is it? they How tall is he? big How fast are they? old How big is he? it How old are they? good How big is it? fast How good are they?

(3) about 40 minutes Tunaweza pia kusema around 40 minutes

11 ► /araund/ second (sekunde) minute (dakika) hour (saa) /sekand minit aua

day (siku) week (wiki) month (mwezi) year (mwaka) dei wiik mānth yia/

(4) around here around there (maeneo yale) /dhea/

(5) They go every 15 minutes. They go every hour. (Wanakwenda kila saa.) I work every day. (Ninafanya kazi kila siku.)

(6) welcome welcome guests (karibisa wageni) Welcome to London! (Karibu London!) /lāndan/

Page 10: 1 / In the bank (part 1) - Hatua kwa Hatuakiingerezahatuakwahatua.com/books/Kiingereza - Hatua kwa Hatua 3… · behind (nyuma ya) in front of (mbele ya) bihaind frānt av next to

9

Jaza nafasi zilizoachwa wazi (2): 1) How f _ _ is it? About a mile. 2) Keep going until the traffic lights and then t _ _ _ left. 3) Go o _ _ _

12 ► Dinner guests (part 1) /dina gests/

A (Anne): Where is the big knife? /wear iz dha big naif/ /an/

B (Trevor): I don't know. Look on the table. (2) (3) /treva/

/ai dount nou luk on dha teibl/

A: It isn't on there. /it iznt on dhea/

B: Try on the fridge. (4) /trai on dha frij/

A: No, it isn't here - ah, I see it. It is under the newspaper. (5) /nou it iznt hia a ai sii it it iz ānda dha nyuuspeipa/

B: Can you bring the plates, too? (6) /kan yuu bring dha pleits tuu/

A: Yes. Is the meat still in the fridge? (7) /yes iz dha miit stil in dha frij/

B: No. I have it. /nou ai hav it/

(1) guests Kiingereza pia kina maneno 'foreigner' (mtu atokaye nje ya nchi) na 'stranger' (mtu usiyemfahamu). 'Guest' ni neno linalotumika kwa ajili ya mtu anayekutembelea au anakuja kuishi na wewe. /forana streinja/

(2) I don't know. ('k' kwenye 'know' haitamkwi). Tunatengeneza Negative ya 'I know' kama hivi kwa sababu 'know' ni verb (aina ya neno linaloonyesha kitendo kinachotendeka au kilichotendeka). Ili kutengeneza Negative ya 'I know', tunahitaji kuongeza maneno 'do' na 'not': Positive: I know (Najua) Negative: I don't (do not) know. (Sijui) ('do not' ni sawa, lakini kwa kawaida kwa Kiingereza cha mazungumzo tunatumia 'don't'.) I have (Nina) I don’t have (Sina) I walk (Natembea.) I don’t walk (Sitembei). Kumbuka pia: to be (am/is/are)7 + Noun (Maneno yanayoonesha jina la kitu) farmer (mkulima) taxi (teksi)

I am a farmer. (Mimi ni mkulima) I'm not a farmer. (Mimi si mkulima.) It is a taxi. (Hii ni teksi.) It isn't a taxi. (Hii si teksi.)

13 ►

Dinner guests (part 2)

A: Do we have enough food? (1) /duu wii hav ināf fuud/

7 to be = kuwa /bii/

Page 11: 1 / In the bank (part 1) - Hatua kwa Hatuakiingerezahatuakwahatua.com/books/Kiingereza - Hatua kwa Hatua 3… · behind (nyuma ya) in front of (mbele ya) bihaind frānt av next to

10

the bridge. 4) Take the second turning on the r _ _ _ _. 5) Go s _ _ _ _ _ _ on for about a hundred metres.

Wageni wa chakula cha jioni (sehemu ya kwanza)

A (Anne): Kisu kikubwa kipo wapi? where-wapi big-kubwa knife-kisu

B (Trevor): Sijui. Angalia juu ya meza. know-jua look-angalia on the table-juu ya meza, mezani

A: Hakipo pale.

B: Jaribu juu ya jokofu. try-jaribu fridge-friji, jokofu

A: Hapana, hakipo hapa- ah, nakiona. Kipo chini ya gazeti. here-hapa under-chini ya see-ona newspaper-gazeti

B: Unaweza kuleta na sahani, pia? can-weza bring-leta plate-sahani

A: Ndio. Nyama bado ipo ndani ya jokofu? too-pia meat-nyama still in-bado ndani ya

B: Hapana. Ninayo

to be (am/is/are) + Adjective (maneno yanayotoa maelezo kuhusu noun): big (-kubwa) fast (kasi) I am big. (Mimi ni mkubwa.) I'm not big. (Mimi si mkubwa.) It is fast. (Kitu kina kasi.) It isn't fast. (Kitu hakina kasi.)

Aina hizi tatu za maneno (verbs, nouns na adjectives) hutumika kwa namna tofauti. Hii itaelezewa zaidi baadae katika kozi.

(3) Look on the table Look under the table. (Angalia chini ya meza.) Look behind the table. (Angalia nyuma ya meza.) /ānda bihaind/

(4) fridge Neno hili linatokana na neno 'refrigerator'. Maneno yote mawili yana maana sawa. /rifrijareita/

(5) ah sauti inayotumika na wazungumzaji wa Kiingereza - haina maana yoyote (angalia ‘Maongezi’ uk.20)

(6) too (pia) John is here, and Michael too. (John yupo hapa, na Michael pia.) Get water, and orange juice too. (Chukua maji, na maji ya machungwa pia.)

(7) still in the fridge The meat is in the fridge.(Nyama ipo ndani ya jokofu) The meat is still in the fridge. (Nyama bado ipo ndani ya jokofu.)

Wageni wa chakula cha jioni (Sehemu ya pili)

A: Tuna chakula cha kutosha? we-sisi enough-kutosha food-chakula

Page 12: 1 / In the bank (part 1) - Hatua kwa Hatuakiingerezahatuakwahatua.com/books/Kiingereza - Hatua kwa Hatua 3… · behind (nyuma ya) in front of (mbele ya) bihaind frānt av next to

11

B: I'm not sure. How many guests do we have? (2) /aim not shoo hau meni gests duu wii hav/

A: George and Mary and their children. That's four...plus Michael and Tina. That's six altogether. /jooj and meari and dhea

childran dhats foo plās maikal and tiina dhats siks ooltagedha/

B: Okay. Together with four of us, that makes ten. /oukei tagedha widh foo av ās dhat meiks ten/

A: We have enough meat and enough vegetables. (3) /wii hav ināf miit and ināf vejtablz/

B: Do we have enough rice? /duu wii hav ināf rais/

A: Yes. We have plenty of rice - oh, where is the salt? (4) (5) /wii hav plenti av rais ou wear iz dha soolt/

B: It is finished. I can walk to the shop. (6) /it iz finisht ai kan wook tuu dha shop/

A: Okay. Get orange juice too. /oukei get orinj juus tuu/

B: Okay. /oukei/

(1) Do we have...? Tunaongeza 'do' kutengeneza maswali katika sentensi zifuatazo: (question-swali) /kweschan/

We have enough food. (Positive) (Tuna chakula cha kutosha.) Do we have enough food? (Question) ((Je) Tuna chakula cha kutosha?) They have children. ((Wao) Wana watoto.) Do they have children? (Wana watoto?) They go to school. ((Wao) Wanakwenda shule.) /skuul

Do they go to school? (Wanakwenda shule?) You live in Manchester. ((Wewe) Unaishi Manchester.) manchista

Do you live in Manchester. (Unaishi Manchester?) Where do you live? (Unaishi wapi?) wea

(2) How many guests do we have? Tunatumia 'How many?' kuuliza idadi ya kitu kinachohesabika: How many lemons do you have? (Una malimao mangapi?) How many cups do we need? (Tunahitaji vikombe vingapi) Kwa kisa cha vitu visivyohesabika, tunatumia 'How much'? kāps lemanz hau māch/

14 ►

Dinner guests (part 3)

A: Now where is the small frying pan? /nau wear iz dha smool fraiing pan/

Page 13: 1 / In the bank (part 1) - Hatua kwa Hatuakiingerezahatuakwahatua.com/books/Kiingereza - Hatua kwa Hatua 3… · behind (nyuma ya) in front of (mbele ya) bihaind frānt av next to

12

B: Sina uhakika. Tuna wageni wangapi? sure- -na uhakika guests-wageni how many-wangapi

A: George na Mary na watoto wao. Hao ni wanne... Pamoja na Michael na Tina. Hao ni sita kwa pamoja. Their-- wao children-watoto four-nne plus-pamoja na six-sita altogether-kwa pamoja

B: Sawa. Pamoja na sisi wanne, tunakuwa kumi. make-fanya/kuwa ten-kumi

A: Tuna nyama ya kutosha na mbogamboga za kutosha vegetable-mbogamboga

B: Tuna mchele wa kutosha? rice-mchele, wali

A: Ndio. Tuna mchele mwingi - oh, chumvi ipo wapi? salt-chumvi

B: Imeisha. Naweza kutembea kwenda dukani. finish-isha walk-- tembea shop-- duka

A: Sawa. Lete maji ya machungwa pia. orange-chungwa juice-maji ya matunda B: Sawa

How much water do you have? (Una maji kiasi gani?) How much rice do we need? (Tunahitaji mchele kiasi gani?) Zingatia kuwa tunatumia 'much' pia kuuliza bei ya kitu: 'How much is it?' (Ni bei gani?)

(3) enough meat enough vegetables Katika Kiingereza, nyama haiwezi kuhesabika, ila mbogamboga zinaweza, kwa hiyo tunatumia wingi (Plural) (vegetables) pamoja na 'enough': enough water (maji ya kutosha) enough lemons (malimau ya kutosha)

(4) plenty Zaidi ya kutosha.

(5) oh - sauti inayotumika na wazungumzaji wa Kiingereza (angalia uk. 20)

(6) It is finished: Tunaweza pia kusema 'It is all gone'. /ool gon/

Jaza nafasi zilizoachwa wazi (3): 1) Where is the big knife? I d _ _ ‘_ know. 2) Do we have enough rice? Yes. We have p _ _ _ _ _. 3) Is the meat in the fridge? No, it i _ _ ' _. It is _ _ the table. 4) Buy juice - and milk t _ _.

Wageni wa chakula cha jioni (sehemu ya 3)

A: Sasa, kikaango kikubwa kipo wapi? now-sasa where-wapi small-ndogo frying pan-kikaango

Page 14: 1 / In the bank (part 1) - Hatua kwa Hatuakiingerezahatuakwahatua.com/books/Kiingereza - Hatua kwa Hatua 3… · behind (nyuma ya) in front of (mbele ya) bihaind frānt av next to

13

B: I think it is in the cupboard. Pass me the salt. (1) /ai think it iz in dha kābad paas mii dha solt/

A: Here you are. Can you check the rice? (2) /hia yuu aa kan yuu chek dha rais/

B: It's fine and the meat is cooked. (3) /its fain and dha miit iz kukt/

A: We should take the potatoes out of the oven now. They are ready. (4) /wii shud teik dha pateitouz aut av dhii āvan nau dhei aa redi/

B: OK. It's time to lay the table. (5) (6) /its taim ta lei dha teibl/

A: We need to boil more water for the other vegetables. Do we have another big pot? (7) /wii niid ta boil moo woota foo dhii ādha vejtablz duu wii hav anādha big pot/

B: Give me the oil. We can fry them. /giv mii dhii oil wii kan frai dham/

A: Okay. How many glasses do we need? /oukei hau meni glaasiz duu wii niid/

B: Er...nine. Tina can't come now. (8) /aa nain tiina kaant kām nau/

A: Okay. /oukei/

B: Uh oh! They're already here! (9) /ā ou dhear oolredi hia/

(1) Pass me Namna nyingine ya kusema give me (nipatie) Ni namna ya heshima kutumia pass me kuomba kitu tunachoweza kukiona juu ya meza ya chakula (mf. chumvi). /giv mii/

(2) check Humaanisha kuhakikisha kama kitu kipo sahihi.

(3) cooked cooked meat (nyama iliyopikwa) uncooked/raw meat (Nyama isiyopikwa/ mbichi) /ānkukt roo/

(4) We should...Hapa, 'should' inaonesha ni wazo zuri kufanya kitu: We should go. (Tunapaswa kwenda) You should take a bus. (Unapaswa kuchukua basi)

(5) It's time to... It's time to go home. (Ni muda wa kwenda nyumbani.) /gou houm/ (6) lay the table Msemo huu humaanisha kuweka sahani, vikombe, visu na uma n.k kwenye meza tayari kwa mlo.

(7) another big pot Hapa, 'another' humaanisa 'ya nyongeza'.

(8) Tina can't come Negative ya can ni can’t (cannot). Kwa kawaida tunatumia kifupisho: You can't go. (Huwezi kuenda) /kanot kaant/

Kutengeneza swali, tunaweka can kwanza: Can you go? (Unaweza kwenda?)

Page 15: 1 / In the bank (part 1) - Hatua kwa Hatuakiingerezahatuakwahatua.com/books/Kiingereza - Hatua kwa Hatua 3… · behind (nyuma ya) in front of (mbele ya) bihaind frānt av next to

14

B: Nadhani kipo ndani ya kabati. Nipasie chumvi. think-fikiri cupboard-kabati pass-pasia salt-chumvi

A: Hii hapa. Unaweza kuangalia wali? check-angalia, tazama rice-wali, mchele

B: Upo sawa na nyama imeiva. fine-sawa, nzuri cooked-iliyoiva

A: Tutoe viazi kutoka kwenye tanuri sasa. Vipo tayari. potatoes-viazi oven-tanuri, jiko la kuokea ready-tayari

B: Sawa. Ni muda wa kuandaa meza. time-muda lay-andaa table-meza

A: Tunahitaji kuchemsha maji zaidi kwa ajili ya zile mbogamboga nyingine. Je tuna sufuria nyingine kubwa? need- -hitaji boil- -chemsha water-maji other- -ingine another-nyingine big-kubwa pot-sufuria

B: Nipatie mafuta. Tutazikaanga. oil-mafuta fry-kaanga

A: Sawa. Tunahitaji gilasi ngapi? glass-gilasi, bilauri

B: Er... Tisa. Tina hawezi kuja sasa. nine-tisa can-weza come-kuja

A: Sawa

B: Uh oh! Tayari wamefika! they-wao already-tayari (here-hapa)

Kama tulivyoona, tunaweza pia kutumia can kuuliza kufanya kitu au kuomba watu wengine wafanye kitu kwa ajili yetu na 'Can I have...' kama namna ya kuomba kitu: Can you bring the water (please)? (Unaweza kuleta hayo maji (tafadhali)?) Can I have the meat (please)? (Naweza kupata nyama (tafadhali)?) please kwa kawaida hutumika kwenye mazungumzo rasmi. Tunatumia 'can' pia kwa kitu tunachoweza kufanya au tunachijua namna ya kufanya: I can cook.(Naweza kupika) I can drive.(Naweza kuendesha) /draiv/

9) Uh oh! Hii haina maana maalumu- ni sauti inayotumika na wazungumzaji wa kiingereza wanapogundua kuna tatizo 'There's a problem!' (kuna tatizo). Haitumiki katika KIingereza rasmi cha maandishi. Jaza nafasi zilizoachwa wazi (4): 1) Where is the small frying pan? It is i _ the cupboard. 2) a) P _ _ _ me the salt. b) Here you are. 3) How many glasses d _ we need? Four. 4) Uh oh! - They are a _ _ _ _ _ _ here.

15 ► Misamiati: in the kitchen (jikoni) /in dha kichin

pot (chungu/sufuria) pot

saucepan sufuria (of medium size) soospan

Page 16: 1 / In the bank (part 1) - Hatua kwa Hatuakiingerezahatuakwahatua.com/books/Kiingereza - Hatua kwa Hatua 3… · behind (nyuma ya) in front of (mbele ya) bihaind frānt av next to

15

frying pan (kikaango) fraiing pan

cook (pika) boil (chemsha) kuk boil bake (oka) grill (banika) beik gril

Mazoezi ya kuongea 16 ► We need more pots. plates We need more plates. cups We need more cups. [Question] Do we need more cups? rice Do we need more rice? water Do we need more water. [Positive] We need more water. food We need more food.

17 ► We have enough rice. [Negative] We don't have enough rice. water We don't have enough water. [Positive] We have enough water. meat We have enough meat. [Negative] We don't have enough meat. ...for the guests We don't have enough meat for the guests.

18 ► I can come. We We can come. He He can come. cook He can cook. She She can cook. [Negative] She can't cook. You You can't cook. go You can't go. [Positive] You can go. [Question] Can you go? cook Can you cook?

Herufi na matamshi8 1) Kuna maneno mengi katika kiingereza ambayo hutumia herufi ambazo hazitamkwi. Zingatia matamshi ya maneno yafuatayo:

8 Unaweza kuangalia maana ya maneno haya mwisho wa kitabu hiki kwenye sehemu

ya kamusi.

Page 17: 1 / In the bank (part 1) - Hatua kwa Hatuakiingerezahatuakwahatua.com/books/Kiingereza - Hatua kwa Hatua 3… · behind (nyuma ya) in front of (mbele ya) bihaind frānt av next to

16

19 ► when who where /wen huu wea

knife know half naif nou haaf

every vegetable omelette evri vejtabl omlat/

2) Sikiliza jinsi maneno haya yanavyotamkwa, halafu uyatamke kwa sauti. Kama huwezi kusikiliza rekodi, maandishi ya matamshi yapo ukurasa wa 21. 20 ► or before morning order for forty north fork (uma) short

21 ► bad bag bank man add name bake day

22 ► big it in think hill side rice nine fine

Mazoezi: A) Jaza nafasi zilizoachwa wazi kwa kutumia 'a', 'an' au 'the': It is far. We need a taxi. Pass me the salt. 1) Excuse me, where is ____ hospital please? ___ old hospital or ___ new hospital? 2) Where is the big knife? It is there - on ___ table. 3) What is your job? I am __ doctor. 4) Where is ___ car? It is in the car park. 5) Can I help you? ___ orange and ___ bottle of water, please.

B) Jaza nafasi zilizoachwa wazi kwa kutumia 'have' or 'has': I have the meat. He has a glass. 1) It ____ flags outside. 2) We ____ enough rice. 3) He ____ enough water. 4) They don't _____ a car. 5) She ____ a shop. 6) Do we ____ another big pot?

C) fridge meat orange pan table boil glasses Where is the meat? It is in the fridge. 1) Pass me the small frying _____. 2) This _____ is not cooked. It is raw. 3) How much is the ______ juice? Two pounds. 4) We need a pot to _____ the water. 5) We have six _______. 6) The big knife is on the _______.

D) past bridge turning side going until behind up Go past the football stadium. 1) Take the second ________ on the left. 2) Walk _____ the hill. 3) Go over the ______.4) It is on the other ______ of the street. 5) Keep _____ ______ you see the station. 6) It is ________ the museum.

E) She is not tall = She's not tall. = She isn't tall. They do not have a pot = They don't have a pot. 1) We do not need a frying pan. = We ______ need a frying pan. 2) They are not teachers. = ______ ____ teachers = ______ _____ teachers. 3) We do not know him. = We ______ know him.

Page 18: 1 / In the bank (part 1) - Hatua kwa Hatuakiingerezahatuakwahatua.com/books/Kiingereza - Hatua kwa Hatua 3… · behind (nyuma ya) in front of (mbele ya) bihaind frānt av next to

17

4) It is not big. = ______ _____ big. = _____ _______ big. 5) Do not turn right. = ________ turn right.

F) They are doctors. Are they doctors? They can come. Can they come? You need a glass. Do you need a glass? 1) It is big. ____ ____ big? 2) He is a farmer. _____ _____ a farmer? 3) We have enough water. ______ we have enough water? 4) You think that is enough. ______ you think that is enough? 5) They are here. ______ _____ here? 6) It is far. ______ _____ far? G) on over and in on with to to to The shop is on the left. 1) Go ____ the bridge. 2) It is time ___ cook the meat. 3) The salt is ____ the table. 4) Six guests, together ____ four of us, is ten. 5) Check ___ see if they're already here. 6) Go ___ the shop. 7) We have enough meat ___ enough vegetables.

Misamiati ya ziada (1) 23 ► drive (endesha) go on foot (enda kwa mguu) draiv gou on fut

junction (makutano) roundabout (mzunguko) raundabaut jānkshan

opposite (mkabala) stop (simama, acha) opasit stop

turn around (geuka (kurudi nyuma)) follow (fuata) taan araund folou overtake (pita kwa mwendo kasi zaidi) ouvateik

kilometre (kilomita) kilamiita

Misamiati ya ziada (2): 24 ► spoon (kijiko) ladle (upawa) kettle (birika) /spuun leidl ketl filter (chujio) tap (bomba) sink (sinki) filta tap sink fire (moto) charcoal (mkaa) firewood9 (kuni) faia chaakoul faiawud

stove (jiko) kerosene stove (jiko la mafuta) stouv kerasiin stouv freezer (friza) chopping board (kibao cha kukatia) friiza choping bood

hot (-enye joto) cold (-baridi) opener (opena) hot kould oupana

bowl (bakuli) bin (pipa la uchafu) boul bin/

Maneno magumu Maneno haya ni magumu kuyatamka kutokana na jinsi yanavyoandikwa. Yaangalie tena. Kama huna , maandishi ya matamshi yanapatikana ukurasa wa 18.

25 ► answer could foreigner right straight

Majibu: Jaza nafasi zilizoachwa wazi (1) 1) is He's 2) What It's 3) Are I'm single 4) old is is six 5) Am you're (2) 1) far 2) turn 3) over 4) right 5) straight (3) 1) don't 2) plenty 3) isn't on 4) too (4) 1) in 2) Pass 3) do 4) already Mazoezi: (A) 1) the The the 2) the 3) a 4) the 5) An a (B)

9 wood (mbao) /wud/

Page 19: 1 / In the bank (part 1) - Hatua kwa Hatuakiingerezahatuakwahatua.com/books/Kiingereza - Hatua kwa Hatua 3… · behind (nyuma ya) in front of (mbele ya) bihaind frānt av next to

18

1) has 2) have 3) has 4) have 5) has 6) have (C) 1) pan 2) meat 3) orange 4) boil 5) glasess 6) table (D) 1) turning 2) up 3) bridge 4) side 5) going until 6) behind (E) 1) don't 2) They're not They aren't 3) We don't 4) It's not It isn't 5) Don't (F) 1) Is it 2) Is he 3) Do 4) Do 5) Are they 6) Is it (G) 1) over 2) to 3) on 4) with 5) to 6) to

Maandishi ya matamshi ya 20: oo bifoo mooning ooda foo footi

nooth fook shoot

Maandishi ya matamshi kwa ajili ya REKODI 21: bad bag bank man ad

neim beik kreit dei

Maandishi ya matamshi kwa ajili ya REKODI 22: big it in think hil

said rais nain fain

Maandishi ya matamshi kwa ajili ya REKODI 25: aansa kud forana rait streit

Tumia Kiingereza ulichojifunza: Kama una ndugu au rafiki anayejifunza Kiingereza pia, au anayejua Kiingereza, jaribu kufanya naye mazungumzo haya: 1) Ulizia na toa taarifa, kama vile jina lako kamili na anuani kwa ajili ya matumii rasmi. 2) Ulizia na to maelekezo kwenda mahali mjini au kijijini kwenu. 3) Igiza kama mnaandaa chakula kwa ajili ya wageni kwa pamoja.

Maneno ya kiingereza yaliyotumika kitabu hiki:

1) Vowel (irabu) /vaual/

Vowel ni sauti inayotamkwa wakati mdomo wa juu haugusi mdomo wa chini. Katika Kiingereza kwa kawaida huandikwa kama inavyoandikwa katika Kiswahili kwa herufi a,e,i,o na u. (Hata hivyo mara nyingine katika Kiingereza inawezekana kwamba sauti ya vowel inatokana na herufi nyingine tofauti).

2) Short form (short-fupi) /shoot foom/ Kuna njia ndefu na fupi ambazo mara nyingi hutumika katika Kiingereza. Kiingereza kina namna zote mbili: mfano: I am = I'm

I'm ni short form ya I am. Wazungumzaji wa Kiingereza hutumia namna zote mbili lakini hupendelea zaidi njia fupi wanapozungumza haraka. Short form haitumiki katika barua za kiofisi.

3) Weak form (weak-dhaifu) /wiik foom/ Baadhi ya maneno katika Kiingereza yana namna zaidi ya moja yanavyotamkwa hasa maneno mafupi ambayo hutumika mara nyingi. Kwa mfano the inaweza kutamkwa kama /dhii/ na pia kama /dha/ na neno and (na) linaweza kutamkwa kama /and/ au /and/. (/and/ ni weak form ya /and/ na /dha/ ni weak form ya /dhii/). Njia zote ni sahihi lakini wazumgaji wa Kiingereza wanapendelea zaidi weak form (ambayo ni ya haraka) wanapozungumza haraka.

Page 20: 1 / In the bank (part 1) - Hatua kwa Hatuakiingerezahatuakwahatua.com/books/Kiingereza - Hatua kwa Hatua 3… · behind (nyuma ya) in front of (mbele ya) bihaind frānt av next to

19

4.) Positive, negative na question /pozativ negativ kweschan/

Katika Kiingereza, kuna aina tatu za sentensi. Sentensi inayotumika huathiri maneno yanayotumika na orodha ya maandishi yake: Positive (chanya): He is in London. (Yeye yupo London.) They are teachers. (Wao ni walimu.) They go to school. (Wanakwenda shule.) Negative (hasi): He is not in London. (Yeye hayupo London.) They are not teachers. (Wao sio walimu.) They don't go to school. (Hawaendi shule.) Question (swali): Is he in London? (Je) yeye yupo London?) Are they teachers? (Wao ni walimu?) Do they go to school? (Wanakwenda shule?)

Maandishi ya Matamshi: 1) Utangulizi: Tofauti na Kiswahili, Kiingereza cha kuandika mara nyingi hakitumii herufi zilezile kuwakilisha matamshi yaleyale katika Kiingereza cha kuongea. Namna nzuri ya kujifunza matamshi ya Kiingereza ni kusikiliza rekodi za maneno zilizoambatanishwa kwenye kozi. Lakini njia hii ikishindikana, tumia maandishi ya matamshi. teacher (mwalimu) /tiicha/ office (ofisi) /ofis/

Maandishi ya matamshi yameandikwa katikati ya mistari miwili na ni madogo zaidi kuhakikisha hayachanganywi na maneno halisi ya Kiingereza yaliyoandikwa.

2) Mistari: Herufi ambazo zina tofauti kubwa kati ya lugha mbili zinaoneshwa kwa mstari (aidha juu au chini): a ā i u mf. bus (basi) /bās/ linapozungumzwa na mzungumzaji, sauti ya katikati ya neno hili si sawa na sauti ya neno la Kiswahili 'basi'. Herufi bila mstari huashiria kuwa matamshi ni sawa au yanakaribiana na Kiswahili.

3) Italic: Baadhi ya herufi zinaandikwa katika italic(italiki): aa ii uu ai ea oo /italik/

/e f g h i j k l m n/ (herufi i, j na k zimeandikwa katika staili ya italic)

Hii ni kuwakumbusha wasomaji kuwa katika Kiingereza sauti zinazotokana na herufi hizi mbili pamoja zinazungumzwa kama silabi moja na siyo silabi mbili. Kwa maana hiyo sauti ii katika neno la Kiingereza teacher (/tiicha/) ni tofauti na sauti ii katika neno la Kiswahili 'mtalii'.

4) Bold (mkazo): Mara nyingi sehemu ya neno inaandikwa katika staili ya bold: /bould/

/a b c d e f g h i j/ (herufi f,g na h zimeandikwa staili ya bold)

Hii inaonesha kuwa sehemu ya neno lililoandikwa kwa staili ya bold linatamkwa kwa mkazo zaidi kuliko sehemu isiyoandikwa kwa aina ya bold. mf: teacher (/tiicha/) Sehemu ya kwanza; tea- inatajwa kwa nguvu zaidi kuliko ya pili -cher. Katika neno behind (nyuma -a) /bihaind/, ni sehemu ya pili inayotamkwa kwa nguvu zaidi.

Page 21: 1 / In the bank (part 1) - Hatua kwa Hatuakiingerezahatuakwahatua.com/books/Kiingereza - Hatua kwa Hatua 3… · behind (nyuma ya) in front of (mbele ya) bihaind frānt av next to

20

5) r Herufi r haijatokea katika maandishi ya baadhi ya maneno. mf. farm (shamba) /faam/ teacher /tiicha/ Hii ni kwa sababu wazungumzaji wengi wa Kiingereza hawatamki herufi hii (katika maneno haya) Kama neno linaishia na irabu na r, herufi r hutamkwa iwapo tu neno linalofuatia linaanza na sauti ya irabu pia. car (gari) /kaa/ His car is blue. (gari lake ni la buluu) /hiz kaar iz bluu/ Wazungumzaji wengi wa kimarekani na baadhi ya waingereza hutamka herufi r katika maneno haya na si kosa kufanya hivyo. Maandishi ya matamshi yanawakilisha matamshi ya wazungumzaji wa Kiingereza (cha Uingereza) kama kwenye rekodi.

Maongezi: Maongezi yaliyotumika katika kitabu hiki yanaonyesha mazungumzo ya kila siku ya kiingereza hivyo yameambatana na alama zinazoashiria kusita katika mazungumzo (wakati mzungumzaji anapoacha kuzungumza ili kufikiri. Zingatia kwamba vitu hivi kwa kawaida havipo katika lugha ya maandishi. Doti tatu (...) hutumika kuonesha pale mzungumzaji anapoacha au kuendelea kwa maongezi. Pia, baadhi ya sauti zinazotumika katika maongezi ya Kiingereza kama 'oh' na 'um' (ambazo uonesha mshangao na kusita katika maongezi) huwepo lakini hayawezi kutumika katika maandishi rasmi, kama barua ya kikazi. Maneno haya yamebanishwa kila yanapotokea. Tafsiri ya maandishi inawakilisha maana ya jumla na si ya neno kwa neno. Kwa kuwa mtiririko wa maneno ya Kiingereza na Kiswahili ni tofauti, maneno ya Kiingereza yametafsiriwa katikati ya maandishi, Pia, pale ambapo maneno yaliyotumika ni tofauti sana na Kiswahili, tafsiri ya neno kwa neno imetumika pamoja na tafsiri ya jumla.

Jinsi ya kufanya Mazoezi ya Kuongea: Mazoezi haya yanakupa nafasi ya kutumiamaneno uliyojifunza katika sentensi ambazo zina sarufi sahihi.

1.) Kubadilisha neno: Msikilize mzungumzaji anavyobadilisha neno katika sentensi kwa kutumia neno jingine kuunda sentensi mpya na ufanye kama alivyofanya. a) Mzumgumzaji atasoma sentensi na atakapomaliza neno jipya litatokea: Where is the hospital? school b) Mzungumzaji anatengeneza sentensi mpya kwa kutumia neno jipya na kuondoa neno liliokuwepo: Where is the school? Hivi ndivyo zoezi litaonekana katika Kiswahili: Hospitali iko wapi? shule Shule iko wapi? 2.) Kufanya mabadiliko mengine: Unapobadilisha neno moja katika sentensi mara nyingi utatakiwa kubadilisha neno jingine au maneno mengine ili sentensi mpya kwa sahihi mf.: Duka liko wapi? Yeye Yeye yuko wapi?

Page 22: 1 / In the bank (part 1) - Hatua kwa Hatuakiingerezahatuakwahatua.com/books/Kiingereza - Hatua kwa Hatua 3… · behind (nyuma ya) in front of (mbele ya) bihaind frānt av next to

21

Katika Kiswahili si sahihi kusema 'Yeye liko wapi? Huu ni mfano wa Kiingereza: I am a manager She She is a manager. Katika Kiingereza si sahihi kusema 'She am'. Kwa hiyo ni lazima tubadilishe 'am' kwenda 'is' wakati tunapobadilisha 'I' kwenda 'she'. Kwenye sauti zilizorekodiwa kuna muda wa kutosha wa kusema sentensi wewe mwenyewe halafu uangalie kama huko sahihi wakati mzungumzaji atakaposoma sentensi inayofuata. Jaribu kufanya mazoezi bila kuangalia kitabuni.

Orodha ya maneno yaliyotumika katika sehemu ya pili, yameorodheshwa kwa orodha ya alphabetiki. (Maneno mengi ya Kiingereza yana maana zaidi ya moja- tafsiri iliyotolewa hapa ni ile tu kama ilivyotumika katika kitabu hiki.)

a /ei, a*/

about (2 km) kama (2km) /abaut/ account akaunti /akaunt/ add ongeza /ad/ address anuani /adres/ after baada ya /aafta/

ah uk. 9,10 /a/ all -ote /ool/ all gone yote imeisha /ool

gon/ already tayari /oolredi/

altogether kwa pamoja /ooltagedha/ am kuwa, ni uk 1,3,9,10 /am, am*/ an uk.1 /an, an*/ and na /and, and*/

Anne Jina la mtu /an/ another nyingine /anādha/ answer jibu, jawabu /aansa/ are kuwa, ni uk.1,3,4,7 /aa, a*/

around (2km) kama (2km) /araund/ around (here) karibu (na hapa) /araund/

bad -baya /bad/ bag begi /bag/ bake oka /beik/

bank benki /bank/ before kabla ya /bifoo/

behind nyuma ya /bihaind/ big kubwa /big/

bin pipa la uchafu /bin/

blue buluu /bluu/ board kibao /bood/ boil chemsha /boil/ bottle chupa /botl/ bowl bakuli /boul/ box boksi /boks/ bridge daraja /brij/ bring leta /bring/ bus basi /bās/ but lakini /bāt/ buy nunua /bai/ by pembeni ya /bai/ can weza /kan, kan*/ car gari /kaa/

car park uwanja ya kupaki magari /kaa paak/

Cardiff Jina la mji /kaadif/ check cheki, /chek/

children watoto /childran/ chop kata vipande vidogo /chop/

chopping board kibao cha kukatia /choping bood/

Christian name jina la kikristu /kristian neim/

church kanisa /chaach/ cold -baridi /kould/

come kuja, njoo /kām/ cook pika /kuk/ cooked iliyoiva /kukt/ could weza (uk.) /kud/ cup kikombe /kāp/ cupboard kabati /kābad/

day siku /dei/

dinner chakula cha jioni /dina/ do fanya /duu/

do kutengenza maswali uk.9,11,12 /duu, da*/

doctor daktari /dokta/ down chini /daun/ drive endesha /draiv/ early mapema /aali/ enough -a kutosha /ināf/ er uk.9 /aa/ every kila /evri/ excuse me samahani /ikskuuz mii/ expensive iliyo ghali /ikspensiv/

family familia /famli, famali/ far mbali /faa/ farmer mkulima /faama/ fast enye kasi /faast/ filter chujio /filta/

fine nzuri, zima /fain/

finished kwiisha/ malizika /finisht/ first -a kwanza /faast/

first name jina la kwanza /faast neim/

flag bendera /flag/ food chakula /fuud/ foot mguu /fut/

football mpira wa miguu /futbool/ for kwa ajili ya /foo, fa*/ for uk. 5 /foo, fa*/ foreigner mgeni /forana/

Page 23: 1 / In the bank (part 1) - Hatua kwa Hatuakiingerezahatuakwahatua.com/books/Kiingereza - Hatua kwa Hatua 3… · behind (nyuma ya) in front of (mbele ya) bihaind frānt av next to

22

forename jina la kwanza /fooneim/

fork uma /fook/ form fomu /foom/ forty arobaini /footi/ four nne /foo/ freezer friza /friiza/ fridge jokofu,friji /frij/ from kutoka kwa /from,

fram*/ front mbele /frānt/ fry kaanga /frai/

frying pan kikaango /fraiing pan/ full (name) (jina) kamili /ful neim/ George jina la mtu /jooj/ get pata /get/ give toa, pa /giv/

glass gilasi, bilauri /glaas/ go enda /gou/

go along (the road) fuatana na (barabara) go past pita, enda mpaka baada ya /gou paast/ good iliyo nzuri /gud/ grill banika /gril/ guest mgeni /gest/ half nusu /haaf/ have kuwa na uk.1 /hav/ he yeye (mume) /hii/ help msaada /help/ here hapa /hia/ hill kilima /hil/ him yeye (mume) /him/ his -ake (mume) /hiz/ hmm /hmm/ home nyumbani /houm/

hospital hospitali /hospital/ hot -enya joto /hot/ hour saa /aua/ house nyumba /haus/ how vipi /hau/

how many? ngapi? /hau

meni/

how much? ngapi? /hau

māch/

hundred mia moja /hāndrad/

I mimi /ai/ if kama /if/ in ndani ya, katika /in/

information taarifa /infameishan/ is kuwa, ni uk.1,2,3,7,10

/iz/ it hii, hiki n.k. /it/ job kazi, ajira /job/ John Jina la mtu /jon/

juice maji ya matunda /juus/ junction makutano /jānkshan/ keep going endelea kwenda /kiip gouing/ kettle birika /ketl/

kilometre kilomita /kilomita, kilamiita/

kitchen jiko (chumba) /kichin/ knife kisu /naif/ know jua/fahamu /nou/ ladle upawa /leidl/ late iliyo chelewa /leit/

lay (the table) andaa (meza) /lei/ left ya kushoto /left/ lemon limao /leman/ little -dogo /litl/ (a) little kidogo /a litl/ live ishi /liv/

local ya karibu/iliyo mwenyeji /loukal/

local person mwenyeji /loukal paasan/

look angalia, tazama /luk/ make tengeneza, /meik/

make (hesabu) uk. 11,12 man mwanaume /man/

manager meneja, mkurugenzi /manija/

Manchester jina la mji /manchista/ many nyingi /meni/

married aliyeoa/olewa /marid/ Mary jina la mtu /meari/

Matthew jina la mtu /mathyuu/

me mimi /mii/ meat nyama /miit/

meeting mkutano /miiting/ metre mita /miita/

Michael Jina la mtu /maikal/ middle ya kati /midl/

mile maili (km 1.609) /mail/ milk maziwa /milk/

minute dakika /minit/ month mwezi /mānth/ more zaidi /moo/ morning asubuhi /mooning/ Mister Bwana /mista/ much nyingi /māch/

museum nyumba ya makumbusho /myuuziam/

my -angu /mai/ name jina /neim/ near ya karibu /nia/ need hitaji /niid/ new -pya /nyuu/

newspaper gazeti /nyuuspeipa/ next inayofuata /nekst/ next to pembeni ya /nekst

ta, nekst tuu/

Nicholas jina la mtu /nikalas/ nine tisa /nain/

no hapana, si, hamna n.k. /nou/ north kusini /nooth/ now sasa /nau/ number namba /nāmba/

of -a uk.1, 7, 11 /ov, av*/

office ofisi /ofis/ oh uk.11,12,20 /ou/ oil mafuta /oil/ okay sawa /oukei/

old iliyozeeka/chakavu /ould/ omelette yai omlet /omlat/ on juu ya /on/

on uk. 5,9 /on/ open fungua /oupan/

opener opena /oupana/ opposite mkabala /opasit/

or au /oo/

orange chungwa /orinj/ order oda /ooda/ other nyingine /ādha/ out nje /aut/ outside nje /autsaid,

autsaid/ oven tanuri /āvan/ over juu ya /ouva/

overtake pita kwa mwendo

kasi zaidi /ouvateik/ P.O.Box S.L.P /pii ou boks/ pan sufuria /pan/ pass pita /paas/

pass pasia /paas/

person mtu /paasan/

Page 24: 1 / In the bank (part 1) - Hatua kwa Hatuakiingerezahatuakwahatua.com/books/Kiingereza - Hatua kwa Hatua 3… · behind (nyuma ya) in front of (mbele ya) bihaind frānt av next to

23

Phillips jina la mtu /filips/ plate sahani /pleit/ please tafadhali /pliiz/ plenty nyingi /plenti/

plus jumlisha, ongeza, na /plās/ pot chungu, sufuria /pot/ potato kiazi /pateitou/

pound paundi /paund/ problem tatizo /problam/ raw mbichi /roo/ ready tayari /redi/

refrigerator jokofu, friji /rifrijareita/

rice mchele, wali /rais/

Trevor jina la mtu /treva/ right ya kulia /rait/ river mto (wa maji) mto /riva/ road barabara /roud/

roundabout mzunguko (barabarani) /raundabaut/ salt chumvi /solt/

saucepan sufuria /soospan/

school shule second sekunde /sekand/ see ona /sii/ she yeye (mke) /shii/ shop duka /shop/ short -fupi /shoot/ should uk. 13 /shud/

side upande /said/ single asiyeoa/olewa /singl/ sink sinki /sink/ six sita /siks/ small -dogo /smool/ so kwa hiyo /sou/ sorry samahani /sori/ spelling herufi /speling/ spoon kijiko /spuun/

stadium uwanja /steidiam/ station stesheni /steishan/ still bado /stil/

stop acha, simama /stop/

straight iliyonyooka /streit/

(go) straight ahead (enda) moja kwa moja /streit ahed/

(go) straight on (enda) moja kwa moja /streit on/ stranger mgeni /streinja/ street mtaa /striit/ sure sawa, uhakika /shoo/

surname jina la ukoo /saaneim/

table meza /teibl/ take chukua /teik/ tall iliyo refu /tool/ tap bomba (la maji) /tap/ taxi teksi /taksi/ teacher mwalimu /tiicha/ telephone simu /telifoun/ tell ambia /tel/ ten kumi /ten/ thank you asante /thank

yuu/ thanks asante /thanks/ that ile, kile n.k. /dhat/ the uk. 1,2,3.5 n.k. /dhii,

dha*/

their yao /dhea/ them wao /dhem/ then halafu /dhen/ there pale /dhea/ they wao /dhei/

think waza, dhani /think/

thirty-six thelathini na sita /thaati siks/ this hii, hiki n.k. /dhis/ time muda /taim/

tin bati /tin/ Tina Jina la mtu /tiina/ to uk.1, 5, 9, 11 /tuu, ta*/

together pamoja /tagedha/

tomorrow kesho /tamorou/ too pia /tuu/

traffic trafiki /trafik/

traffic lights taa za trafiki /trafik laits/

train treni /trein/ try jaribu /trai/ turn geuka, pinda /taan/

turn around geuka (kurudi nyuma) turning mgeuko /taaning/ twelve kumi na mbili /twelv/

twenty-one ishirina na moja /twenti wān/ two mbili /tuu/ uh oh! uk. 13, 14 /ā ou/ uncooked mbichi /ānkukd/ under chini ya /ānda/ until mpaka /āntil, antil/ up juu /āp/ us sisi /ās/

vegetable mbogamboga /vejtabl/

very zaidi /veri/ walk tembea /wook/ water maji /woota/

(the) way (to) njia (ya kwenda) /wei/ we sisi /wii/ week wiki /wiik/ welcome karibu /welkam/ what nini /wot/ when saa ngapi, lini /wen/ where wapi /wea/

who nani /huu/ with pamoja na /widh/

work kazi, fanya kazi /waak/ year mwaka /yaa/ yes ndio /yes/ you wewe /yuu/

you're welcome karibu, unakaribishwa /yoo welkam/

*Weak Form (angalia ukurasa 18)

© copyright James Munn 2016