12.vizuizi vya imani (1)...2018/08/12  · 12.vizuizi vya imani (1) • shetani anashambulia imani...

9
12.VIZUIZI VYA IMANI (1) Shetani anashambulia imani kila wakati. Imani inathibitisha ukweli wa neno la Mungu na inawavuta watu kwake. Lazima shetani ashambulie imani. Wakati mwingine tunahitaji kuondoa yale yanayofanya imani izuiliwe katika maisha yetu, yale yanayofanya imani ishindwe kukua na kukomaa. Kwa hiyo tunahitaji kujua ni vitu gani vinavyozuia imani.

Upload: others

Post on 04-Feb-2021

30 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

  • 12.VIZUIZI VYA IMANI (1)

    • Shetani anashambulia imani kila wakati. Imani inathibitisha ukweli wa neno la Mungu na inawavuta watu kwake. Lazima shetani ashambulie imani.

    • Wakati mwingine tunahitaji kuondoa yale yanayofanya imani izuiliwe katika maisha yetu, yale yanayofanya imani ishindwe kukua na kukomaa. Kwa hiyo tunahitaji kujua ni vitu gani vinavyozuia imani.

  • 12.VIZUIZI VYA IMANI (2)

    • KIZUIZI CHA KWANZA; KUTOKUFAHAMU KWAMBA NINAMILIKI IMANI.

    • Yoh 14:12 12Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba. 


    • Rum 12:3 3 Kwa maana kwa neema niliyopewa namwambia kila mtu aliyeko kwenu asinie makuu kupita ilivyompasa kunia; bali awe na nia ya kiasi, kama Mungu alivyomgawia kila mtu kiasi cha imani.

    • 1The 1:3 3Wala hatuachi kuikumbuka kazi yenu ya imani, na taabu yenu ya upendo, na saburi yenu ya tumaini lililo katika Bwana wetu Yesu Kristo,

    mbele za Mungu Baba yetu

  • 12.VIZUIZI VYA IMANI (3)

    • KIZUIZI CHA PILI; KUTOKUFAHAMU MAPENZI YA MUNGU • Imani inafanya kazi pale ambapo mapenzi ya Mungu yanafahamika.

    • Katika eneo ambapo unafahamu mapenzi ya Mungu, imani yako itafanya kazi vizuri

    • Kama kuna eneo fulani amapo hujafahamu vizuri mapenzi ya Mungu, mashaka inaingia na unashindwa kuamini.

    • Tunaweza kulinganisha maisha yetu kama eneo la mashamba madogo madogo, kila shamba ndogo ni mfano wa eneo moja katika maisha yetu. Pale ambapo tunapanda tunavuna, na pale ambapo hatupandi mavuno yanakosekana.

    • Kutafuta kujua mapenzi ya Mungu katika kile eneo ya maisha yetu ni muhimu sana kama tutaweza kuvuna kote kote

    • Efe 1:17-19

  • 12.VIZUIZI VYA IMANI (4)

    • KIZUIZI CHA TATU; KUTOKUPENDA KUTII. • Rum 1:5 5ambaye katika yeye tulipokea neema na utume ili mataifa yote

    wapate kujitiisha kwa imani Imani haisikilizi tu bai inatenda kufuatana na neno.

    • Hoja na mazoea mara nyingi yanapenda kuleta ubishi kwa kwa ahadi za Mungu. Tunahitaji kujiweka chini ya neno la Mungu kusudi tupate kushiriki ahadi hizo.

  • 12.VIZUIZI VYA IMANI (5)

    • KIZUIZI CHA NNE: UPUNGUFU WA ”KUKIRI IMANI VJEMA/ ukiri wa kweli / ukiri bora / maungamo mazuri (the good confession) 


    • Kama unafahamu mapenzi ya Mungu lakini unatamka maneno (imani) kinyume na mapenzi yake itafanya kazi katika upinzani na mapenzi ya Mungu.

    • Tunatakiwa kunena kwa imani si kinyume chake.

    • Mdomo wako na moyo wako yanahitaji kwenda sambamba na mapenzi ya Mungu, na kukiri sawa na mapenzi yake.

  • 12.VIZUIZI VYA IMANI (6)

    • KIZUIZI YA TANO; UPUNGUFU WA UTENDAJI. • Yak 2:26

    • Yoh 14:21

    • Yoh 2:5

    • Tunapotenda nguvu inafanya kazi.

    • Wakati Joshua alipoanza kuzunguka mji wa Yeriko makuta ya mji yakabomoka.

    • Abrahamu alipata kuona nchi ya ahadi kwa sababu alisafiri kufuatana na muongozo wa Mungu.

    • Wakati Musa aliponyosha fimbo lake ndipo bahari liligawanyika.

    • Wakati Naamani alipooga mara saba ndipo alipopona

    • Wakati wale wakoma kumi walipokwenda kwa makuhani ndipo walipona.

    • Wakati yule bwana mwenye mkono uliyopooza alipo nyosha mkono wake ukapona.

    • Wakati yule mama aliye kuwa akitoka damu kwa miaka 12 alipomgusa Yesu akapona.

    • Wakati watumishi walipojaza mitungi na maji ikabadilika ikawa divsai

    • Imani ni utendaji!

  • 12.VIZUIZI VYA IMANI (7)

    • KIZUIZI CHA SITA: UPUNGUFU WA KUVUMILIA. • Mbinguni muda haupo, lakini sisi tunaishi katika au ndani ya mipaka ya

    muda. Mara kwa mara tunachoka tunaposubiri muujiza. Yesu anatupa ahadi ya kiushikilia wakati tunaposubiri Mk 11:24

    • Mara nyingi tunafuata mtindo wa Abrahamu, tunajaribu kumsaidia Mungu kkujibu.

    • Ni hekima kumwachia Mungu kuhusika na VIPI na Lini tukishikili KUA litafanyika.

    • Kuishi maisha ya imani katika utendaji ni zoezi ya maisha, siyo jambo linayokuja kama barua. Tunapofanyia zoezi hili kazi tutakutana na mapingamizi kutoka kwa shetani, maana yeye hapendi tuishi maisha ya jinsi hiyo. Lakini Mungu anatupa nguvu, ndani yetu Mungu amesha weka hiyo imani, ni zawadi yake kwetu, tulipewa wakati wa kuingia katika agano naye. Na nguvu hiyo inatubeba ahdi tunaona yele yasiyoonekana hadi yasiyooneka yanaanza kuonekana.

  • 12.VIZUIZI VYA IMANI (8)

    • KIZUIZI YA SABA; UPUNGUFU WA UPENDO. • Yak 3:8-12 Hatuwezi kusimama imara katika imani tukimbariki Mungu wakati

    tunapowasema watu vibaya. Ukikosa majibu ya maombi yako ebu cheki maisha yako yalivyo…

    • Mara kwa mara tukijichunguza vizuri tunagundua matatizo yanayozuia kazi ya Mungu kufanyika ndani yamaisha yetu na kuitia maisha yetu. Tusipo ishi maisha ya upendoo hiyo ni kizuizi kwa kazi ya Mungu.

    • Ukimwomba Mungu atume uamsho huko ukiwasema watu vibaya, Mungu hatakujibu!

    • Labda unamahitaji yako ya kibinafsi, lakini kila wakati unawasema watu vibaya, hushi katika upendo na majibu ya maombi yako yanazuiliwa na maisha yako.

    • Mk 11:25-26 Sharti moja ya kujibiwa ombi ni kusamehe, maana yeke ni kwamba ukikataa kumsamehe mtu kitu chochote inakuwa kizuizi

    • Haijalishi watu wamekutendea kitu gani, unadaiwa kuwasamehe, na unaweza kuwasamehe kwa sababu Rum 5:5 Mungu amekupatia uwezo wa kusamehe.

    • Ku samehe ni kusahau Ebr 10:17 1

    • Uchungu (bitterness) ni ugonjwa wa hatari sana wa kiroho. Uchungu unasema vibaya, unatafuta udhaifu kwa watu. Biblia inatutahadhalisha kukaa pamoja na wenye mizaha Zab 1:1

  • 12.VIZUIZI VYA IMANI (9)

    • Badala yake katika 2Tim 2:22b tunambiwa Tushirikiane na watu wazuri watakuambukiza uzuri wao, ukishirikana na wabaya nao pia watakuambukiza ubaya wao.

    • Kusamehe ni kazi ya upande mmoja, huwezi kumdai mtu akusamehe, lakini unaweza kusamehe mwenyewe wanaokukosea. Wewe mwenyewe unaamua kama unapenda kuwa mwepesi wa kuomba na kutoa msamaha.

    • Kama mkristo wewe ni kiungo ndani ya mwili wa Kristo ushirikiano huo tunaiita koinonia, huwezi ukawa pote na pia huwezi kuelewa vyote. Lakini unaweza kuwapenda wote na kuwabariki wote ndani ya hiyo familia. Huo ni ufunguo unaofungua mlango mpana sana.

    • Wapo wengine ndani ya hiyo familia ambao wanaonekana kua tofauti sana na wewe, lakini kumbuka mnashiriki mengi sana, jitahidi kufurahia yale unayoweza kufurahia na umshukuru Mungu kwa ajili yao.

    • Mungu anafanya kazi nyingi sana pote duniani, na anapenda sana kufanya mambo mengi na makuu kupitia maisha ya kila anayemuamini. Imani inafungua nguvu za Munug, chukua changamoto ya kozi hii, anza maisha mapya leo. Chukua hatua nyingine mpya ya imani na utaona kwamba Mungu ataanza kutenda mambo makuu sana ndani ya maisha yako na katika mazingira yako.