annex 1. muongozo wa mafunzo ya ukusanyaji wa taarifa kuzuia

14
0 ANNEX 1. MUONGOZO WA MAFUNZO YA UKUSANYAJI WA TAARIFA KUZUIA MLUNDIKANO WA VIUATILIFU KATIKA NGAZI YA JAMII BONDE LA ZIWA EYASI, WILAYA YA KARATU MUONGOZO WA MAFUNZO JUU YA UKUSANYAJI WA TAARIFA ZA ATHARI KWA AFYA NA MAZINGIRA KUTOKANA NA MATUMIZI YA VIUATILIFU KATIKA JAMII Imetayarishwa na

Upload: doanhuong

Post on 28-Jan-2017

428 views

Category:

Documents


9 download

TRANSCRIPT

0

ANNEX 1. MUONGOZO WA MAFUNZO YA UKUSANYAJI WA TAARIFA

KUZUIA MLUNDIKANO WA VIUATILIFU KATIKA NGAZI YA JAMII BONDE LA ZIWA EYASI, WILAYA YA KARATU

MUONGOZO WA MAFUNZO JUU YA UKUSANYAJI WA TAARIFA ZA ATHARI KWA AFYA NA MAZINGIRA KUTOKANA NA MATUMIZI YA VIUATILIFU KATIKA JAMII

Imetayarishwa na

1

TAPOHE LTD S.L.P. 15482

Dar-es-Salaam

April 19 - 28, 2010

2

MFUMO WA MKULIMA KUJICHUNGUZA BINAFSI KUATHIRIKA NA VIUATILIFU

Jina: M/mume/M/mke (Mjamzito?)

Anuani: Tukio la Upuliziaji la #:

Tarehe/Mwezi:

Zao lililopuliziwa:

Jaza fomu kila baada ya tukio la upuliziaji. Weka alama kwenye ishara na dalili kama

imetokea wakati au ndani ya masaa 24 baada ya kupulizia.

Kope za macho kucheza (2)

Kuona maruerue (2)

Pua kuchomachoma (1)

Kukosa usingizi (1)

Machozi kupita kiasi (1) Macho kuchomachoma/kuwasha (1)

Jicho jekundu (1)

Mafua (1)

Mate mengi kupita kiasi (1)

Kizungu zungu (1) Kifafa (3)

Kikohozi (1)

Koo kuuma (1)

Uchovu (1)

Kupoteza fahamu (3)

Kifua kuuma (kubana/kuchomachoma (2)

Kutapika (2)

Kichefuchefu (2)

Tumbo kukakamaa (2) Ganzi (1) Kuharisha (2) Kuwashwa ngozi (1) Jasho jingi kupita kiasi (1) Mwendo wa kuyumba (2)

Vipele vya ngozi (1) - wekundu - vipele vyeupe - kuchanika/magamba - malengelenge - kukauka

Misuli kukakamaa (2) Mtetemo (2) Misuli kukosa nguvu (1)

Kichwa kuuma (1)

Kuishiwa pumzi (1)

Viuatilifu vilivyotumika: Idadi (#) ya tangi/drum zilizotumika= Muda uliotumika kupulizia: Ishara/dalili nyingine: Idadi ya:

(1) Kidogo

(2) Wastani

(3) Kali

Kundi la maradhi ya tukio la upuliziaji:

(0) Hakuna ishara/dalili

(1) Kidogo (zilizo wakewa (1) tu))

(2) Wastani (angalau moja iliwekwa (3))

(3) Kali (angalau moja iliyowekewa (3))

3

LENGO KUU Kushirikisha jamii katika kutambua na kunukuu athari za viuatilifu kwa afya na mazingira. Malengo mahususi Kufikia mwisho wa somo hili, utakuwa na uwezo wa kufanya yafuatayo:

Ø Kuongeza ufahamu wa wakulima kuhusu maradhi yanayosababishwa na matumizi holela ya viuatilifu Ø Kuhimiza mkulima kupunguza wingi wa upuliziaji viuatilifu Ø Kuhimiza wakulima kupunguza matumizi ya chemikali zilizo kwenye makundi yenye sumu kali kupita kiasi, kali sana na za wastani

(zilizoainisha na WHO kundi 1a, 1b, na II ) kwa kudhibiti visumbufu Ø Kuhimiza utafutaji wa mbinu mbadala za kudhibiti visumbufu. Ø Kutoa taarifa za athari ndogo na za wastani zitokanazo na sumu za viuatilifu ambazo sio lazima ziwe zimeonwa ndani ya au

kufikishwa kwenye mfumo wa huduma za afya za jamii. Mbinu

Kusanya Kikundi cha Uongozi

Kikundi cha uongozi kinatakiwa kiendeshe huu mradi wa uchunguzi binafsi. Majukumu yao ni

• Kuchagua wakulima binafsi watoa taarifa • Kufundisha wakulima binafsi watoa taarifa • Kukusanya fomu za taarifa binafsi kila wiki • Kuchambua taarifa hizo kila mwezi • Kufanya mikutano ya upokeaji (feedback) wa taarifa pamoja na washiriki wakulima binafsi waliotoa taarifa.

Kikundi cha uongozi ni budi kiwe na wajumbe wanaoishi karibu na wakulima binafsi watoa taarifa. Kila mjumbe wa kikundi ni budi awajibike na wakulima binafsi watoa taarifa 5-10. Wana kikundi wanaweza kuwa

• Mkulima aliyepitia mafunzo ya IPM • Waalimu ndani ya jamii wasio kwenye elimu rasmi • Wafanyakazi wa NGO kwenye jamii • Wanafunzi wa shule (umri miaka 12-13 wanaojua kutafuta asilimia (%) • Asasi ya wanawake • Wafanyakazi wa kujitolea afya ya jamii.

4

Kuchagua sampuli ya wakulima

• Sampuli ya wakulima ni budi iwe na wakulima 30-50 wanaotumia viuatilifu kwa kijiji • Lazima wakubali kuwa watoa taarifa binafsi kwa kipindi chote cha miezi minne hadi sita • Toa namba kwa kila kaya ndani ya jamii inayochunguzwa • Bila kupanga chagua kaya 30-50 • Tembelea kaya na omba mkulima kushiriki. Kama mkulima akikataa chagua kaya nyingine yenye namba (weka orodha ya sababu za

kukataa) • Wakaribishe kwa mafunzo wakulima binafsi watoa taarifa na wenza wao na mwanafunzi mmoja (atakayewasaidia) • Baada ya kumalizika kwa kipindi cha kutoa taarifa (miezi minne hadi sita) kila mkulima aliyeshiriki apewe njia mbadala ya kudhibiti

visumbufu kama vile IPM or kilimo hai. Utoaji binafsi wa taarifa Kila mkulima anatakiwa kujaza fomu kila anapopulizia kiuatilifu. Taarifa itakayonukuliwa inajumuisha

• Jina • Jinsia (kama mwanamke eleza kama ni mjamzito) • Anuani • Tarehe • Namba ya Tukio la upuliziaji • Mazao yaliyopuliziwa • Orodha ya viuatilifu vilivyotumika • Idadi ya matangi/drum yaliyotumika • Muda uliotumika kupulizia

Ishara au dalili zozote zilizotokea wakati au ndani ya masaa 24 baada ya kupulizia lazima zizungushiwe duara kwenye ramani ya mwili inayoonesha ishara na dalili 31 zinazoweza kutokea kwa kusababishwa na kuathirika na viuatilifu. (Athari nyingine yoyote isiyokuwa kwenye ramani ya mwili inaweza kuandikwa ndani). Hizi ishara na dalili zimepangwa kama Kidogo (1), Wastani (2) au Kali (3) kama inavyofafanuliwa hapa chini.

1. Kidogo: haina uhakika, haijafafanuliwa vizuri, au matokeo ya athari za muwasho utokanao na viuatilifu 2. Wastani: uwezekano wa athari ya mishipa ya fahamu iliyofafanuliwa kwa ufasaha (vimengenya vya kolinesteresi*) 3. Kali: athari kali ya mishipa ya fahamu (kupoteza fahamu, kifafa)

*Japo kutokwa na jasho, mate, machozi kwa wingi kunaweza kutokana na kutindikiwa kwa asetailkolinesteresi kutokana na kuchangamshwa kwa kupita kiasi kwa sehemu hizo, dalili hizi kwa kawaida huwa zinachanganywa na hali ya mazingira au kuwashwa kutokanako na viuatilifu (joto, kiu and kuwashwa macho). Kwa hiyo zinawekwa kwenye kundi la athari kidogo. Mwisho wa kila wiki, wanakikundi wa jamii waliofundishwa watakusanya fomu kutoka kwenye kaya na kuchambua na kufupisha matokeo. Mkutano wa jamii utafanyika kila mwezi pamoja na wakulima binafsi watoa taarifa and daktari wa kijiji/kata kujadili na kugrafu/kuchora taarifa.

5

Mafunzo kwa Wakulima na wanafunzi wa shule za sekondari Inabidi mbinu hiyo hiyo ya kufundisha itumike kwa wakulima na vikundi cha uongozi vya jamii. Tofauti pekee ni kuhusu viuatilifu. Kwa sababu vikundi cha uongozi vya jamii lazima vitapanga viuatilifu kwa daraja za hatari za WHO na familia za kemikali taarifa za ziada watapewa wao. Baadae wakati wa mikutano ya marejeo taarifa hizo wanaweza kupewa wakulima washiriki. Hatua za ufundishaji zinaainishwa kama ifuatavyo:- Dhumuni la Ufundishaji 1. Kueleza dhumuni la ufuatiliaji wa athari za viuatilifu na utaratibu ulivyo 2. Kuelezea ramani ya mwili 3 Tofauti kati ya ishara na dalili 4. Mchezo wa ishara na dalili 5. Kutambua aina za viuatilifu (Kikundi cha jamii cha uongozi tu) 6 Kuelezea jinsi fomu inavyotakiwa kujazwa 7 Kufanya mazoezi kutumia fomu na kuziweka takwimu kwa ufupi 8. Kuchambua takwimu Ufafanuzi wa madhumuni

1. Kueleza dhumuni la ufuatiliaji wa athari za viuatilifu na utaratibu ulivyo Kwamba ushahidi wa athari za viuatilifu unaweza kuisaidia Serikali kuboresha sheria za viuatilifu nchini na kuunda taratibu na sera za kimataifa za kudhibiti viuatilifu Ukusanyaji wa taarifa wa jamii ni utaratibu wa wakulima kuandika athari za viuatilifu sehemu wanakoishi Katika utaratibu wa kuandika mgusano na madhara yatokanayo na viuatilifu, jamii hufahamu hatari zake, ambayo ni hatua ya kwanza katika kukubali shughuli za kilimo kinachojali mazingira na kilicho endelevu na kupunguza kutegemea viuatilifu vya kemikali

2. Kuelezea ramani ya mwili • washiriki wapangwe katika vikundi vitano • Mmoja kati yao alale juu ya karatasi iliyounganishwa kwa gundi • Ramani ya mwili wake ichorwe • Vipande vidogo 31 vya karatasi nyingine vikatwe • Kila kikundi kijadili ishara na dalili za kuathirika na sumu kulikoshawahi kuwapata au walizoona kwa wakulima wengine • Waandike ishara na dalili katika kipande cha karatasi na kukipachika katika ramani ya mwili waliouchora. [picha hii ya awali

itampa mwezeshaji uelewa wa kiwango cha athari kinachotokea katika jamii] • Sambaza fomu ya ramani ya mwili inayoonesha ishara na dalili zote

6

• Chukua kadi moja moja ya ishara na dalili walizofikiria kuwa ni athari za viuatilifu na kujadili na kuelezea kwa nini hazionekani kwenye fomu ulizowasambazia (huenda zikawa athari zisizojulikana au zinazotokana na matatizo mengine yanayohusiana na kazi kama vile kuumwa mgongo na viungo)

3. Tofauti kati ya ishara na dalili

• Bandika karatasi 2 moja ikiwa imeandikwa ISHARA na nyingine DALILI • Uliza darasa kama wanajua tofauti • Eleza maana ya ISHARA: athari ya afya INAYOONEKANA (kama vile kutapika, mtetemo, mwendo wa kuyumba nk) • Eleza maana ya DALILI: athari ya afya ambayo haionekani lakini mtu anakuwa na hisia nayo (kama kichefuchefu, kichwa kuuma,

kizunguzungu nk)

4. Mchezo wa ishara na dalili • Panga darasa katika mviringo • Kila mshiriki, mmoja mmoja, achague kadi moja ya ishara na dalili toka kwenye kofia • Kila amshiriki ama aigize ishara na dalili aliyookota au aelezee bila kutumia maneno kikundi kubuni • Andika hilo neno kwenye karatasi ya ishara au dalili (muigizaji na darasa kuamua) • Mwezeshaji kuonesha jinsi ya kuchunguza ishara zifuatazo: mtetemo, mwedo wa kuyumba, jicho kucheza, kutokuona vizuri, jicho

jekundu • Baada ya neno, darasa liorodheshe maradhi yote au hali ambazo hazitokani na viuatilifu lakini zinaweza kuwa na ishara na dalili

kama hiyo Kwa mfano mwendo wa kuyumba ukiwa mlevi [Zoezi hili litahakikisha kila mmoja anaelewa maana na kwamba ishara na dalili zinaweza kusababishwa na vitu vingine)

5. Kutambua aina za viuatilifu (Kikundi cha jamii cha uongozi tu)

• Chukua chupa ya kiuatilifu na ukisoma kibandiko onesha lipi ni jina la biashara na lipi jina la kawaida • Sambaza viuatilifu vilivyoletwa kwenye mkutano nje kwenye vituo vilivyoandikwa namba • Sambaza kila kikundi kwenye kituo kimojawapo • Waagize washiriki kuandika majina ya biashara na kawaida kwa kila kiuatilifu • Baada ya dakika 1-2 piga filimbi kwa kila kikundi kusogea kwenye namba nyingine • Endelea hivyo hadi wawe wametembelea na kuandika majina yaliyoko katika vituo vyote • Katika karatasi tengeneza tebo yenye mshazari wa kuandika jina la kibiashara na mwingine jina la kawaida • Kwa vikundi wape jukumu watu 3-5 kwa kila kikundi (mf kituo 1–5, 6-10) • Agiza kila kikundi kutengeneza tebo yenye mishazari kama ifuatayo

• Kila kikundi Kituo # Jina la Biashara Jina kawaida Aina Daraja la hatari la WHO Familia ya kemikali

7

kijaze kwenye tebo jina la biashara na jina la kawaida • Kutoka kwenye orodha itakayotolewa kila kikundi kitafute jina la kawaida na kujaza Daraja la hatari la WHO na familia ya

kemikali • Mkufunzi aeleze maana ya Daraja la hatari kwa binadamu la WHO (Shirika la Afya Duniani). • Kama kikundi darasa liainishe orodha ya viuatilifu kwa Daraja la hatari kwa afya la WHO (mf. Watengeneze bango kwa kila

daraja 1a, 1b, II, III, IV, likiwa na jina la biashara na jina la kawaida). • Mkufunzi aelezee familia za kemikali. • Kama kikundi darasa liainishe orodha ya viuatilifu kwa familia ya kemikali (mf Watengeneze bango kwa kila familia: OP –

organofosfati, C-kabameti, OC- Oganoklorini, PY – pairethroidi) • Mkufunzi aelezee familia za kemikali na madhara yake kiafya, akirejea ramani ya mwili. • Kwa kikundi kilichofika mbali mkufunzi anaweza kuelezea jinsi oganofosfati na kabameti zinavyoingilia mfumo wa neva.

6. Kuelezea jinsi fomu inavyotakiwa kujazwa

• Jaza baada ya KILA upuliziaji (hasa kama HAKUNA dalili ambapo kila mmoja atajaza kila kitu isipokuwa picha) • Weka alama ishara na dalili zinazotokea wakati au saa 24 baada ya kupulizia/kunyunyizia (isipokua kwa vipele vya ngozi) • Anza kujaza siku ambapo mhusika amepumzika kwa angalau siku tatu bila kupulizia/kunyunyizia kiuatilifu. • Kutokwa jasho ijazwe tu kama mtu ameshatoka kwenye jua na kupata muda wa kutulia na kupoa. • Tumia fomu moja kwa kila anayenyunyizia kama ni zaidi ya mtu mmoja kwa nyumba • Kama mnyunyiziaji ni mwanamke eleza kama ni mja mzito au hapana (elezea kuwa hii ni muhimu kuweza kuelezea kichefuchefu

na kutapika). Mwanamke yeyote anayejijua ni mja mzito ASISHIRIKISHWE kwenye huu utoaji wa taarifa na atahadharishwe kuwa unyunyiziaji unaweza kuhatarisha afya ya mtoto wake.

• Elezea kila kisanduku cha kujazwa: jina, anuani nk • Orodhesha kila kiuatilifu kwa jina la kibiashara (sio tu kiuagugu, kiuadudu au kiuakuvu) • Familia inaweza kuongeza jumla kwenye fomu (# ishara na dalili nyepesi, wastani, kali) • Familia inaweza kutengeneza jumla ya kila mwezi kwenye form ya ziada ya tukio la kupulizia

§ Idadi ya kichwa kuuma, kizunguzungu nk § Orodha ya viuatilifu vilivyotumika katika mwezi § Orodha ya ishara na dalili nyingine zilizotokea § Jumla ya dalili ndogo, za wastani na kali § Idadi ya vipindi vya unyunyiziaji alivyonavyo mtu

• HAKUNA ishara au dalili • Ishara au dalili ndogo (1) TU • Ishara au dalili za wastani (angalau 2) • Ishara au dalili za wastani (angalau 3)

8

7. Kufanya mazoezi kutumia fomu na kuziweka takwimu kwa ufupi • Sambaza fomu za kujichunguza binafsi kwa kila mshiriki • Kila mshiriki ajaze fomu kama vile yeye ni mkulima anayetoa taarifa kwenye tukio la unyunyiziaji/upuliziaji au kwenye tukio la

unyunyiziaji wake wa mwisho • Changana jumla ya ishara na dalili ndogo, wastani na kali zilizoandikwa • Jaza kundi la maradhi katika tukio la upuliziaji: Hakuna maradhi, kidogo, wastani au kali • Kuchambua matokeo, swali kwa swali weka alama ya jumla kwa kuchanganya matokea ya darasa zima kwenye karatasi moja

kubwa. • Chambua na kufupisha kama ifuatavyo

Taarifa Uchambuzi wa Takwimu M/me/M/ke Idadi na Asilimia Mazao yaliyopuliziwa Orodhesha aina pamoja na idadi na asilimia Ishara na dalili Kwenye ramani ya mwili iliyokuzwa andika kwa kila ishara na dalili idadi ya matukio ya upuliziaji (forms)

yaliyoripoti kila ishara au dalili/ idadi ya jumla ya matukio ya upuliziaji. Mfano kichwa kuuma fomu 6/10

Viuatilifu Orodhesha kila kiuatilifu kwa jina la kibiasha na la kawaida. Halafu kila baada ya jina ongeza daraja la hatari la WHO na familia ya kemikali. Chambua # na % ya viuatilifu vilivyotumika vilivyo kwenye daraja Ia, Ib, II, III, na IV na vilivyo Op, C, OC, Py.

Matangi au drum yaliyotumika

Orodhesha idadi ya madrum au tangi yaliyotumika katika kila tukio la upuliziaji. Changanua uwingi (# ya matangi/drum ya chini kuliko zote – ya juu kuliko zote) na wastani wa idadi ya matangi/drum kwa kila tukio .

Masaa yaliyotumika kupulizia

Orodhesha muda wa masaa uliotumika kukamilisha kila tukio la kupulizia/kumwagilia. Changanua uwingi (# ya masaa yaliyotumika ya chini kuliko zote – ya juu kuliko zote) na wastani wa idadi ya masaa yaliyotumika kupulizia/kunyunyizia .

Idadi ya ishara na dalili ndogo

Orodhesha idadi ya ishara na dalili ndogo kutoka kila tukio la upuliziaji/umwagiliaji (fomu). Changanua uwingi (# ya chini kuliko zote – ya juu kuliko zote ya ishara na dalili ndogo) na wastani

Idadi ya ishara na dalili za wastani

Orodhesha idadi ya ishara na dalili za wastani kutoka kila tukio la upuliziaji/umwagiliaji (fomu). Changanua uwingi (# ya chini kuliko zote – ya juu kuliko zote ya ishara na dalili za wastani) na wastani

9

Idadi ya ishara na dalili kali

Orodhesha idadi ya ishara na dalili kali kutoka kila tukio la upuliziaji/umwagiliaji (fomu). Changanua uwingi (# ya chini kuliko zote – ya juu kuliko zote ya ishara na dalili kali) na wastani

Kundi la maradhi ya tukio la upuliziajiaji

Uliza darasa kuona ni matukio (fomu) mangapi zilikuwa na �hakuna ishara au dalili zilizowekwa � Ishara na dalili za wastani tu (1) zimewekwa

� Ishara au dalili za wastani angalau moja (2) � Ishara au dalili za wastani angalau moja (3)

Changanua idadi na % ya matukio ya upuliziaji

4. Ishara: Jinsi ya kuchunguza ishara ISHARA JINSI YA KUCHUNGUZA

∗ Mtetemo

Mikono na vidole kutikisika wakati wa kushika kitu kama karatasi

∗ Kope za macho kucheza

Mwambie mkulima afunge macho na kujifanya amelala. Angalia kucheza kwa kope pembe hadi pembe

∗ Kutoka jasho jingi kupita kiasi

Angalia kwenye paji la uso na midomo ya juu kuona matone ya jasho

∗ Wekundu wa macho Sehemu nyeupe ya macho kuonekana nyekundu

∗ Mafua/kutokwa na makamasi Angalia kuona kama mkulima anafuta pua sana . He ni tofauti na mafua ya kawaida. Makamasi yanatakiwa kuwa meupe tofauti na mafua yanatoka ya njano au kijani.

∗ Kikohozi

Sikiliza kusikia kama anakohoa sana (inawezekana kikasababishwa na uvutaji sigara kwa hiyo muulize kama

10

kinazidi akipulizia viuatilifu).

∗ Kupumua kwa shida

Mtu anatoa sauti kama kupiga filimbi wakati wa kupumua

∗ Mwendo wa kuyumba

Mtake mkulima atembee kwenye mstari ulionyooka kisigino kwa dole gumba mikono ikiwa imenyooshwa pembeni. Akishindwa kutembea kwa kunyooka huko ndiko kuyumba. Anaonekana kama kalewa.

∗ Kuharisha Haja kubwa mara nyingi ikiwa maji maji

∗ Wekundu wa ngozi

Muulize kama ameona vipele vyovyote na angalia viganja, mikono, miguu.

∗ Viraka vyeupe kwenye ngozi Uliza kama kuna vipele vyovyote na angalia viganja, mikono, miguu

∗ Ngozi kubanduka magamba

Uliza kama kuna vipele vyovyote na angalia viganja, mikono, miguu (kama magamba ya samaki)

∗ Kupoteza fahamu/coma Mkulima kuzimia, kuanguka chini na huwezi kumuamsha.

∗ Kifafa/degedege Degedege, misuli yote inajikunja kama watoto wadogo wanavyokuwa wakishikwa na homa kali. Macho yanageuka na huuma meno, mwili mzima unakakamaa.

∗ Kutapika

Kila kitu tumboni kinatoka nje.

Hali nyingine zinaweza kutokea kabla na baada ya kupulizia kwa sababu zinaweza zikawa sugu kutokana na matumizi ya viuatilifu kwa muda mrefu. Hali zifuatazo zinaweza kuwa sugu:-

• Mwendo wa kuyumba • Kope za macho kucheza • Mitetemo

11

• Mapele ya ngozi, wekundu, mabaka meupe, kubanduka nk. 5. Dalili: Jinsi ya kudodosa dalili DALILI HISIA ZAKE

∗ Koo Kukauka

Unahisi kama unavyoamka asubuhi ikiwa ulilala mdomo wazi

∗ Uchovu

Unahisi kama umepanda mlima siku nzima

∗ Kukosa usingizi au usingizi wa mang’amung’amu

Ndoto mbaya, unashindwa kulala usiku kucha

∗ Kifua kuuma/kuhisi kuchoma choma

Kama unavyohisi ukipumua kwenye baridi kali au moshi

∗ Ganzi

Unahisi kama vile unapokalia mguu wako kwa muda mrefu … kama vile kuna sisimizi au pini na sindano kwenye ngozi

∗ Macho kuchomachoma/kuuma Unahisi kama moshi au sabuni machoni

∗ Macho kuwasha Unahisi kama vile pollen kwenye macho

∗ Kutokuona vizuri

Hii ni kama ukiangalia sinema au picha isiyo toka vizuri (out of focus) au kuona maruerue.

∗ Kuishiwa pumzi

Angalia kama mkulima anapumua haraka haraka kama vile hapati hewa ya kutosha

∗ Kizunguzungu

Unahisi kama vile umejizungusha mahali pamoja mara nyingi.

∗ Kichefuchefu Hisia inayopatikana kabla ya kutapika

∗ Kutokwa mate mengi kupita kiasi

Ona kama mkulima anatema mate sana na muulize kama anahisi kuwa na mate mengi, kama vile amekula

12

limao.

∗ Koo kuuma Linauma ukimeza

∗ Pua kuchomachoma

Hisia kama ukiwa jikoni mtu akawa anakaanga pilipili

∗ Misuli kukakamaa

Hisia kama ukicheza mpira siku nzima na misuli ya miguu kukamata na kukakamaa na kuuma

∗ Kichwa kuuma

Maumivu makali au ya kubana kichwani.

∗ Tumbo kukakamaa/kuuma

Maumivu kama unayopata kabla tu ya kuharisha

∗ Ngozi kuwasha

Kama umeumwa na mbu wengi

13

VIUATILIFU NI HATARI KWA MAISHA NA MAZINGIRA YAKO

USIKUBALI KUATHIRIKA NA VIUATILIFU

Mgusano hutokea

wakati wa kujishughu

-lisha na viuatilifu

Utupaji ovyo wa viwekeo vitupu vya viuatilifu unahatarisha maisha

ATHARI  ZA  VIUATILIFU  KWA  AFYA  

Ulemavu wa viungo

Ulemavu wa ngozi

Ugonjwa wa ngozi

Kichwa maji

Kucha kung’ooka