annur toleo la ijumaa

16
ISSN 0856 - 3861 Na. 1053 SAFAR 1434, IJUMAA JANUARI 11 - 17, 2013 BEI TShs 500/=, Kshs 50/= Sauti ya Waislamu www.annuurpapers.co.tz Uk. 16 QUR’AN katika SuraAl Buruji (85) aya ya 10 inasema kuwa: “Hakika wale waliowaadhibu Waislamu wanaume na Mwisho, mwanzo mbaya kwa Masheikh Wako wapi miamba, watesaji waliotamba? Waliowatesa Waislamu kisha hawakutubia Wapo makaburini hawafurukuti, wanapata jaza yao Imekuwa ya Watende wao kina mwafulani Ajabu... Kitenda wenzao, kutwa midomoni’ Padre Ambrose Vs Sheikh Soraga Waislamu wanawake, kisha wasitubie, basi watapata adhabu ya Jahannamu na Inaendelea Uk. 3 SMZ inaendelea kukamata Uamsho Uk. 4 Isisahau kumuenzi ‘nabii’ wa Mkuranga Mtwara, Lindi watendewe haki katika gesi-Lipumba Kama ‘nchi’ haina Dini ni huko Bara si Zanzibar Uk. 3 WANACHOTAKA wananchi wa mikoa ya Kusini, ni kutendewa haki na uadilifu katika neema ya gesi iliyopatikana. Hayo yamesemwa na Profesa Ibrahimu Lipumba akiongea na waumini wa dini ya Kiislamu mara baada ya ibada ya swala ya Ijumaa, wiki iliyopita katika Msikiti wa Mwinyimkuu, Magomeni Jijini Dar es Salaam. Uk. 16 Asema Pro. Sharif na kusisitiza kuwa… Wazanzibari ni Waislamu toka zama RAIS Kikwete RAIS Shein SHEIKH Ponda IGP Said Mwema Kamishna Mussa Sheikh Farid Sheikh Msellem Sheikh Azzan

Upload: annurtanzania

Post on 28-Apr-2015

1.219 views

Category:

Documents


1 download

DESCRIPTION

Soma Annur kila Ijumaa

TRANSCRIPT

Page 1: Annur toleo la Ijumaa

ISSN 0856 - 3861 Na. 1053 SAFAR 1434, IJUMAA JANUARI 11 - 17, 2013 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Sauti ya Waislamuwww.annuurpapers.co.tz

Uk. 16

QUR’AN katika Sura Al Buruji (85) aya ya 10 inasema kuwa: “Hakika wale waliowaadhibu Wais lamu wanaume na

Mwisho, mwanzo mbaya kwa MasheikhWako wapi miamba, watesaji waliotamba?Waliowatesa Waislamu kisha hawakutubiaWapo makaburini hawafurukuti, wanapata jaza yao

Imekuwa ya Watende wao kina mwafulani Ajabu... Kitenda wenzao, kutwa midomoni’

Padre Ambrose Vs

Sheikh Soraga

Waislamu wanawake, kisha wasitubie, basi watapata adhabu ya Jahannamu na

Inaendelea Uk. 3

SMZ inaendelea kukamata Uamsho

Uk. 4

Isisahau kumuenzi ‘nabii’ wa Mkuranga

Mtwara, Lindi watendewe haki katika gesi-Lipumba

Kama ‘nchi’ haina Dini ni huko Bara si Zanzibar

Uk. 3

W A N A C H O T A K A wananchi wa mikoa ya Kusini, ni kutendewa haki na uadilifu katika neema ya gesi iliyopatikana.

Hayo yamesemwa na Profesa Ibrahimu Lipumba

akiongea na waumini wa dini ya Kiislamu mara baada ya ibada ya swala ya Ijumaa, wiki iliyopita katika Msikiti wa Mwinyimkuu, Magomeni Jijini Dar es Salaam. Uk. 16

Asema Pro. Sharif na kusisitiza kuwa…Wazanzibari ni Waislamu toka zama

RAIS Kikwete RAIS Shein SHEIKH Ponda

IGP Said Mwema Kamishna Mussa

Sheikh Farid Sheikh MsellemSheikh Azzan

Page 2: Annur toleo la Ijumaa

2 AN-NUURSAFAR 1434, IJUMAA JANUARI 4 - 10, 2013

AN-NUUR S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786

Cel: 0784 370 208, 0755 260 087 , DSM. www.annuurpapers.co.tz E-mail: [email protected]

Ofisi zetu zipo: Manzese Tip TopUsangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

MAONI YETU

Tahariri/Habari

JAMII ya walio wengi w a n a a m i n i k u w a Maaskofu ni watu wa dini. Bila shaka jamii pia inawafahamu kuwa ni watu wanaotekeleza wajibu wa kufunza watu wengine waishi kwa mujibu wa matakwa ya Mungu.

Dini inatizamwa kama mfumo wa kimaisha ya mwanadamu, unaomtaka binadamu kuishi kistaarabu na kiadilifu. Watu wanaamini kuwa Dini ni mfumo wa maisha ambao upo mbali na matendo maovu, dhuluma, ghiliba, chuki, ubinafsi na mambo machafu mengine m e n g i y a n a y o d h u r u wanadamu na kumchukiza Mungu.

Viongozi wa dini kwa jinsi wanavyoaminiwa na kuheshimiwa na jamii, si rahisi kudhaniwa kwamba wanaweza waka fanya mambo ambayo hayana i t h i b a t i , a u m a m b o wasiyokuwa na uhakika nayo au wakapotosha ukweli kwa ajili ya maslahi yake.

Hii ni kwa sababu ni aibu na ni dhambi kubwa kwa kiongozi wa dini, kwa makusudi akasema urongo hadharani, huku nafsi yake ikijua fika kuwa anachokisema au kukitetea ni urongo na upotoshaji ulio mkubwa.

K a t i k a s i k u k u u y a Christmas, viongozi wa Umoja wa Makanisa walikuja na tamko lao. Pamoja na mambo mengine, lakini sehemu kubwa ya tamko lao liliwalenga Waislamu na taasisi zao.

Wa k i i t a k a s e r i k a l i kuchukua kali dhidi ya walioitwa watu wachache w a n a o t u m i a m w a n y a wa dini kuvuruga amani nchini. Moja ya hatua hizo ni kuzifuta taasisi za dini ambazo wamedai kuwa ndio chanzo cha upotevu huo wa amani kwa kutumia mgongo wa dini.

Bila shaka kauli hizi z i n a s h a d i d i w a z a i d i na kuwepo matukio ya k u c h o m w a m a k a n i s a kadhaa nchini siku za hivi karibuni.

Amani haitakuwepo kwakuendeleza Mfumokristo

Lakini pia Maaskofu wamekuwa wakikerwa na kilio cha Waislamu kwamba, kuna mfumo kristo ndani ya mamlaka za serikali na ndio sababu kubwa ya kuwepo dhuluma na unyanyaswaji kwa jamii ya Waislamu nchini.

“Labda niwakumbushe, viongozi wote waandamizi wa ngazi za juu nchini, asilimia 90 ni Waislamu. Itakuwaje nchi iendeshwe kwa mfumo wa kristo?” Alikaririwa akihoji Askofu Martin Shao, kutoka Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini, katika mkutano wao wa Umoja wa Makanisa nchini.

Walitajwa Rais, Makamu wa Rais, Mkuu wa Usalama wa Taifa, IGP, Jaji Mkuu. Na kudaiwa kwamba hawa ni asilimia 90 ya viongozi waandamizi wa ngazi za juu na kwamba ni Waislamu.

Zanzibar ilielezwa kuwa asilimia mia moja ya viongozi wote ni Waislamu na kwamba si kweli kwamba Zanzibar hakuna Wakristo wenye sifa ya kuongoza.

Uwakilishi katika Tume ya Kukusanya na kuratibu Maoni ya Katiba Mpya, ilielezwa kuwa theluthi mbili ya wajumbe wake ni Waislamu.

Hoja hizi, zimechukuliwa k w a m b a z i n a k i d h i kuthibitisha na kuhalalisha kutokuwepo mfumo kristo nchini, unaopigiwa kelele na Waislamu.

Ili kutetea hoja yao kwamba hakuna mfumo Kris to , Maaskofu kwa kusukumwa na imani ya kidini ambayo tunaamini husimamia zaidi ukweli na haki, wana wajibu wa kuja na kauli zilizothibiti ukweli ili kuondoa hili ombwe lililopo la kuwepo ubaguzi na upendeleo wa kiimani katika mamlaka ya nchi.

Waache kauli za mwamba ngoma, ambazo haziwezi kutanzua hitilafu zilizopo, zaidi ya kuendeleza mivutano ya kutetea maslahi ya watu wa imani fulani dhidi ya watu wa imani nyingine badala ya kutetea haki.

Bila hiyana, Maaskofu walitakiwa kueleza bayana

uwiano kati ya Waislamu na Wakristo, katika ngazi zote za kiutendaji au kitumishi serikalini, ili kujiridhisha na hoja yao kwamba mfumo Kristo unaopigiwa kelele haupo katika maeneo hayo, badala ya kutizama nyadhifa mbili tatu za juu, na kuishia hapo.

Wasituhadae kwa kutaka kutuhalalishia hoja zao kwa kutoa mifano michache ya ghiliba, kama walivyoitaja Rais, Makamu wa Rais, Jaji, IGP na Mkuu wa Usalama, Tume ya Katiba. Hawa ni tone katika bahari ya wasimamizi, watumishi na watendaji wa serikali kwa ujumla.

Kama utaanzia juu, basi tutaanza na Rais na idara mbalimbali katika Ofisi yake.

Kuna Mahakama, Wizara za serikali, Mashirika na taasisi za umma za serikali, Mawakala wa serikali, Tume za serikali, kuna balozi, nk.

Kote huko kuna watendaji na watumishi wake. Wapo Majaji, wakuu wa majeshi, M a w a z i r i , M a n a i b u Mawaziri, Makatibu Wakuu wa Mawizara, Manaibu wao, Wakurugenzi wa Wizara,

Makamishna, Wakuu wa Idara na watumishi wake kwa ujumla.

Wapo Wakuu wa mikoa, Makatibu Wakuu wa mikoa, Wakurugenzi wa Halmashauri, Manispaa na Miji na maofisa au watumishi wengine kwa ngazi hiyo.

Kuna Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya, maofisa wa idara mbalimbali na watumishi wa kada mbalimbali ngazi ya wilaya.

Wapo Makatibu Tarafa, Watendaji Kata hadi wa serikali za mitaa.

L a k i n i h u k o k o t e hawakutaka kugusa kwa kuwa wanatambua huko wapo wa namna gani na wana maslahi gani kwao.

Pia ni vyema ikaeleweka k u w a , W a i s l a m u walishabainisha kuwa tatizo la mfumno kristo halikuanzia awamu hii ya madaraka.

Wamebainisha, tena kwa mifano ya wazi kwamba tatizo lilianza toka kuja kwa wakoloni wa Kijerumani na ndio maana Waislamu walikuwa mstari wambele katioka kupitgania uhuru. Bahati mbaya Tanzania huru imerithi na kuendeleza

mfumo ule ule ulioachwa na wakoloni wa kuwabagua na kuwakandamiza Waislamu.

Kuhusu suala la kuchomwa makanisa , so te tunajua kwamba kwa mafundisho ya dini, iwe ni Uislamu au Ukristo, wafuasi wake wanafahamu kitendo hicho sio cha kibinadamu.

Wa l i c h o k i d h i h i r i s h a Maaskofu n i chuk i ya makusudi na kuwatukana Waislamu na taasisi zao.

Lakini kwa kuwa tayari kuna kes i z inaende lea mahakani juu ya kuchomwa makanisa, basi Maaskofu wangefanya uungwana kwa kutoa au kuleta ushahidi katika vyombo husika ili kuisaidia serikali kuthibitisha wahalifu, ili uchugunguzi ufanyike na wahusika wabainike na sheria ichukue mkondo wake. Sio kutusi Waislamu na Taasisi zao, na kuwachongea serikalini.

A m a n i w a n a y o d a i k u i p i g a n i a n a k u i l i l i a maaskofu haiwezi kuwepo na kudumu kwa kuleta kauli za ghilba za kuendeleza mfumo kandamizi na wa kibaguzi-mfumokristo.

INNA Lillaahi wa inaa Ilayhi Raaji’oon. Hakika kila mwanadamu atarejea k w a m u u m b a w a k e . M w a k a h u u j a m i i y a wasanii imempoteza msanii mwenziwao, almarhum Juma Kilowako, almaruufu Sajuki. Nimeamua kuandika makala haya leo si kwa sababu nyengine isipokuwa n i k u e l e z a m t a z a m o wangu katika utetezi wa mafundisho ya dini yetu tukufu ya Kiislamu.

Awali ya yote nataka kumpa pole mjane wa marehemu Juma, Bi. Wastara Juma. Huyu ni mwanamke ambaye ameonesha upendo wa dhati kwa mumewe wakati wa uhai wake. Kubwa zaidi ambalo limenisukuma ni namna Bi. Wastara alivyosimama imara kulinda, kuenzi na kuheshimu mila, silka na utamaduni wa Kiislamu unaosimamiwa chini ya Quran tukufu.

A k i w a m w a n a m k e wa Kiislamu, Bi. Wastara amejiheshimu, hakutaka kuivunjia heshima dini yake

Ya kujifunza kutokana na msiba wa Sajuki

Na Juma Mohammed, China

na aila yake. Nimekuwa nikifuatilia habari za kifo cha Juma na moja nililobaini ni umakini wa Wastara namna alivovaa vazi lenye heshima kwa mwanamke wa Kiislamu hususan kizuka. Hakubabaika, hakuwa na khofu kuwa ataambiwa Mujahidina maana siku hizi ukivaa vazi la heshima lenye kumstiri mwanamke na ikiwa mwanamke mwenyewe ni Muislamu ataambiwa ana imani kali ya kidini.

H a k u t a k a k u f u a t a mila na desturi zisizo za Kiislamu, mnaweza kujiuliza nimemuonaje ilhali nami sikuwepo nyumbani kwa K i z u k a ? K w a k u p i t i a mitandao mbalimbali ya kijamii nimeona picha ambazo amepigwa kizuka alipokuwa akipewa mkono wa pole ama na viongozi au na wananchi wengine. Wastara amejisitiri na Inshaallah Mwenzi Mungu atamsitiri.

Tunaambiwa na Maulamaa kwamba ku j i s i t i r i kwa m w a n a m k e k u n a k u w a muhimu zaidi katika sehemu za makundi, kama msibani, maeneo ya sherehe, hospitali, na mashule, hata kama

ku takuwepo wanawake tu, kwa sababu baadhi ya wanaume ambao si Mahram na hata vijana wanaweza kuwaona au kuwachukua picha hali ya kuwa hawana stara zao kamili, na hiyo itakuwa ni sababu ya fitnah kwa wale wanaowaona.

Bi. Wastara alichukuliwa picha ya mnato akiwa katika vazi linalotakiwa katika Uislamu. Ni mfano bora wa kuigwa na wanawake wengine hususan wale maarufu ambao wanadhani kuwa umaarufu wao utawasaidia kitu mbele ya Allah, kumbe hakuna kitakachowafaa zaidi ya matendo mema. Tunawaona wanasiasa wanawake wakiiga mila na desturi zisozokuwa za Kiislamu na wanaume pia tunawaona misibani wanavyoiga mambo ambayo ni kinyume kabisa na Uislamu.

M t u m e M u h a m m a d S .A .W anasema “Aina mbili za watu wa motoni siwaoni... Wanawake ambao wamevaa lakini wako uchi, wanawashawishi wanaume wawatongoze, na wanaelekea kwao (kwa kuwa warahisi).

Inaendelea Uk. 7

Page 3: Annur toleo la Ijumaa

3 AN-NUURSAFAR 1434, IJUMAA JANUARI 4 - 10, 2013Habari

Mwisho, mwanzo mbaya kwa MasheikhInatoka Uk. 1

watapata adhabu ya kuungua (barabara).”

Kabla ya aya hiyo katika sura hiyo hiyo tunasoma kuwa kwa hakika hao waliowatesa Waislamu, wale waliowaadhibu Waislamu, “hawajaona baya lolote kwao (Waislamu) ila kumuamini Mwenyezi Mungu mwenye kushinda (na) mwenye kusifiwa.” (85:8)

Tunapoandika maoni haya Sheikh Issa Ponda Issa bado yupo ndani akiwa kanyimwa haki ya kupata dhamana katika kesi inayomkabili. Kama ipo haki, kama ipo sheria kwa mujibu wa katiba ya nchi hii na kwa mujibu wa sheria na haki za binadamu za kimataifa, inayomnyima Ponda haki ya kupata dhamana kwa mujibu wa kesi inayomkabili, wanaomzuilia wanajua. Na kama wanafanya hivyo kwa msukumo wa kisiasa, kwa chuki binafsi na kwa kutaka kumkomoa kwa sababu yoyote ile, wanajua pia. Nafsi zao zinawashuhudia na Mungu wao anashuhudia na anajua vyema pia kama wana sababu za msingi au ni katika kutumia mamlaka yao vibaya.

Hal i n i h iyo h iyo kwa wanaowashikilia Sheikh Farid, Msellem, Azzan na Masheikh weng ine wa Jumuiya ya Uamsho.

Hawa ni Masheikh ambao umekuwa mwisho mbaya wa mwaka 2012 na mwanzo m b a y a w a m w a k a 2 0 1 3 . Wamemaliza mwaka wakiwa rumande na wameanza mwaka wakiwa rumande. Kama ilivyo kwa Sheikh Ponda, kama ipo sheria kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar na ya Jamhuri ya Muungano, na kwa mujibu wa sheria za Zanzibar/Tanzania, inayoelekeza kuwa Masheikh hao wanyimwe haki yao ya dhamana kutokana na kesi inayowakabili; viongozi wa Zanzibar na wakuu wa Mahakama na vyombo vya dola wanajua.

La kama wanafanya hivyo kwa sababu za kisiasa, kwa matashi yao tu, kwa chuki na kutaka kuwakomoa Masheikh hao kwa sababu yoyote ile, nafsi zao zinajua na Mola wao Muumba Hakimu wa Mahakimu na Mfalme wa Siku ya Malipo, anawashuhudia wala hawawezi kumdanganya kuwa walikuwa wakisimamia sheria za nchi.

A m b a l o t u n g e p e n d a kuwakumbusha ni kuwa kila mchunga ataulizwa. Na kila unapokuwa na mamlaka , madaraka na cheo kikubwa, ndio masuuliya yako yanakuwa makubwa zaidi.

Ifike mahali mtu ajiulize, atamjibu nini Mwenyezi Mungu kama kuna mtu alidhulumiwa kat ika utawala wake kwa kuwekwa rumande bila ya kosa?

Wanasema wasemaji kuwa madaraka hulevya. Lakini madaraka yana mwisho. Hata kama hakuna wa kukung’oa, lakini kifo huwezi kukiepuka. Walikuwepo miamba lakini

leo kimyaa! Wapo makaburini hawafurukuti.

Wa p o w e n g i n e b a d o wanapumua ila ukomandoo wao umekwisha. Wale aliowalundika jela akitoa kauli za kejeli kuwa sio mapapai kuwa yataoza,

wanatembea na afya zao. Lakini komandoo ni wa kushikwa mkono kuonyeshwa njia. Mwenye macho yake kaleta Qadari yake.

“Enyi watu (Enyi wanasiasa, Enyi wenye madaraka katika Mahakama na vyombo vya

Dola)! Mcheni Mola wenu, hakika mtetemeko wa Kiama ni jambo kubwa (kabisa).”

Siku mtakapokiona (hicho K i a m a ) - k i l a m w a n a m k e anyonyeshaye a t amsahau amnyonyeshaye, na kila mwenye

mimba ataizaa mimba yake (kabla ya wakati kufika). Na utawaona watu wamelewa; kumbe hawakulewa, lakini ni adhabu ya Mwenyezi Mungu iliyo kali.” (22:1-2)

SMZ inaendelea kukamata UamshoMwandishi Wetu

ZIPO habari kuwa kuna mama mmoja amejitokeza na kujitangaza au kusema kuwa yeye ni ‘Nabii’.

M a m a h u y o k u t o k a Mkuranga, Mkoa wa Pwani anazunguka katika mitaa ya Zanzibar akitafuta wafuasi.

Taarifa zaidi zinafahamisha kuwa miongoni mwa madai yake ni kuwa ameshawahi kufika Uwingu wa Saba pamoja na madai mengi ya kufru.

Habari kutoka ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar na baadhi ya Ulamaa zinafahamisha

kuwa washakutana na mama huyu na kusikia madaia yake.

Hata hivyo hadi sasa hakuna matamko ya dhati wala harakati madhubuti za kuhakikisha kuwa Mama huyo haendelei na kufru zake.

Ufupi wa maneno na ubaya wa suala lenyewe, hawa wote pamoja na elimu zao, wameshindwa kuchukua hatua dhidi ya kufru hii.

Hata hivyo, ofisi ya Mufti inasemekana kutoa kauli kuwa mama huyu aache kwenda misikitini na kuhubiri.

Pili inasemekana pia kuwa kumetolewa fat’wa kuwa

ahamishwe na kurejeshwa kwao Tanganyika.

Hata hivyo, suala hilo limepingwa na Idara ya Uhamiaji (Immigration) w a k i d a i k u w a m a m a huyo ni Mtanzania hivyo hawezi kuondoshwa kutoka Zanzibar.

Baadhi ya watu wanahoji, mbona Sheikh Kurwa Shauri alihamishwa kutoka Zanzibar na kupelekwa Tabora na mpaka hivi sasa anaishi Tabora?

Huyu mama anayedai kuwa ni Nabii, Uhamiaji wanasema kuwa hawezi kuhamishwa kutoka sehemu moja ya Tanziania hadi nyengine.

Lakini mbona Mapalala aliwahi kuhamishwa? Kwa upande mwingine Abdullah R a s h i d a l i p o k u w a R C Kaskazini Unguja, alizuia watu wa upande mmoja wa kisiwa cha Unguja kwenda kwengine.

Kwa sheria za Kiislamu, huyu mama ni murtad – lakini Kaimu Katibu wa Mufti anaitwa Jongo anadaiwa kumtetea au ksuhindwa kuchukua hatua madhubuti.

Wanachohoji Waislamu ni je , mbona hadi sasa hazijasikika sauti na kauli za kukemea kama inavyosikika katika masuala mengine?

Kama ‘nchi’ haina Dini ni huko Bara si ZanzibarSERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetahadharishwa isilete hoja ya nchi kutokuwa na dini katika Katiba ya nchi kwani Wazanzibari hawatakubali kupokonywa haki zao za kidini kama Mahkama ya Kadhi.

Ushauri huo umetolewa na Mwenyekiti wa Baraza la Katiba Zanzibar, Professa Abdul Sherif muda mfupi baada ya kutoka kwenye meza ya utoaji wa maoni mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba yaliofanyika juzi katika ukumbi wa Eacrotanal Mjini Unguja ambapo aliwasilisha maoni ya Baraza la Katiba Zanzibar.

Professa Sherif amesema mabadiliko ya katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yanayofanyika yazingatie suala la dini kwani katiba ya Tanzania inazungumzia serikali haina dini lakini katiba ya Zanzibar haina kifungu hicho na hivyo suala la dini waachiwe watu wenyewe badala ya kuingizwa katika katiba.

Alisema, huenda kuingizwa kifungu hicho kunaweza kuleta matatizo hasa kwa kuzingatia Zanzibar ina asilimia 99 ya Waislamu na hivyo hawawezi kukubali kufutwa Mahakama yao ya Kadhi ambayo wameikuta tokea miaka kadhaa ya wazazi wao.

“Kuwepo kwa kifungu cha katiba kuhusu dini kunaweza kuchochea sua l a ha t a l a Mahakama ya Kadhi nadhani Wazanzibari hawatakubali kuambiwa Mahakama ya Kadhi

Na Alghaithiyyah, Zanzibar ifutwe, sasa sisi tunashauri suala hili lisiingizwe katika katiba katiba”. Alishauri.

Professa Sherif ambaye ni bingwa wa his tor ia na ameshawahi kupokea tunzo mbali mbali duniani kutokana na mchango wake mkubwa katika kuandika vitabu kadhaa vya historia amesema Wazanzibari wana haki ya kuwa na Mahakama ya Kadhi kutokana na kuwa idadi yao ni kubwa na hivyo wana haki ya kujiamulia mfumo wa wanaoutaka katika kuendesha nchi yao.

Aidha alisema miaka kadhaa Wazanzibari wameishi bila ya kutokea ugomvi wa aina yoyote kuhusiana na dini na ndio maana hata wakati wa utawala wa Uingereza kuna makanisa makubwa yalijengwa Zanzibar ambapo wakati huo Wakristo walikuwa wachache mno lakini kutokana na kuheshimu dini nyengine utawala wa Sultan ambaye ni Muislamu alithubutu kutoa kibali cha kujengwa makanisa.

“Miaka yote Wazanzibari hawajawahi kugombana kwa habari ya dini, wanagombana kwa mambo mengine lakini sio dini, wamekuwa na uvumilivu mkubwa na kushirikiana na ndio maana kuna mahekalu, misikini na makanisa, lakini watu wake hawagombani”, alisema Professa Sherif.

Akizungumzia masuala mengine kwa ujumla alisema bunge la Tanzania halikuwa na haki wala mamlaka ya kupunguza au kuongeza mambo ya muungano ambao yalikubaliwa katika hati ya Muungano kati ya Tanganyika

na Zanzibar zilipoungana ambapo awali yalikuwa mambo 11 tu.

P ro fe s sa Abdu l She r i f amesema mambo yaliongezwa yamefanyika kinyume cha sheria na hivyo yalioongezwa yote yamekuwa batili kwa mujibu wa sheria kwa kuwa bunge halikuwa na madaraka hayo.

Wakati huo huo, CHAMA Cha Wanasheria Zanzibar (ZLS) kimependekeza katika katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwepo kwa mfumo wa serikali TATU pamoja na kuwepo kwa fursa ya mgombea binafsi kuwania uongozi wa nchi badala ya mfumo uliopo sasa.

Akiwasilisha maoni yake mbele ya tume ya mabadiliko ya katiba jana, Katibu wa chama hicho, Mussa Kombo alisema mfumo wa kuwepo kwa serikali tatu ndio utakaofaa kwa sasa pamoja na kupendekeza kuwepo kwa mgombea binafsi katika kuwania nafasi za urais nchini.

“Sisi kama ZLS tunaona mfumo wa serikali tatu ndio unaofaa kwa sasa kuingizwa katika katiba mpya kuwepo na serikali ya Zanzibar na kuwepo na serikali nyengine jina lolote litakaloitwa na pia kuwepo na serikali ya muungano ambayo hiyo itakuwa ni ndogo itashughulikia masuala ya muungano tu”, alisema Mussa nje ya mkutano wa utoaji wa maoni yaliofanyika ukumbi wa Eacrotanal Mjini Unguja.

Kombo alisema katiba mpya iainishe waziwazi hizo serikali tatu na mamlaka zake ili kusiwepo na utata kwani mfumo uliopo sasa haujaelezwa kikamilifu katika katiba na hivyo kumekuwepo na

malalamiko mengi kutoka pande mbili zilizoungana.

Aidha alisema ZLS imeona kuwepo na mgombea binafsi atakayewania nafasi ya urais kwani imani yao ni kwamba anaweza kupatikana kiongozi mzuri atakayetokana nje ya chama cha siasa.

Kombo al isema mambo ambayo sio ya muungano yanapaswa kuamuliwa kwa pamoja na kwa r idhaa ya pande mbili zilizoungana huku kila serikali iwe na chombo chake cha maamuzi ambapo walipendekeza kuwepo na bunge la Zanzibar, bunge la bara au vyovyotelitakavyotwa na kuwepo na bunge la pamoja.

Alisema tabia ya serikali ya upande mmoja kujiamulia na serikali ya pili kushindwa kutoa maamuzi haipendezi na hivyo wameshauri jambo lolote liamuliwe kwa pande mbili tena kwa makubaliano.

Akizungumzia suala la haki za binaadamu kuingizwa katika katiba Professa Chris Peter Maina wa Kituo Cha Huduma za Sheria Zanzibar, alisema haki zote za binaadamu ziwekwe katika katiba ikiwa pamoja na haki ya kupata elimu na afya iwe ni ya lazima pamoja na ile haki ya msingi ya kuishi.

Professa Maina alisema katiba mpya ianishe haki ya kuandamana na uhuru wa vyombo vya habari badala ya katiba ya sasa inavyosema uhuru wa kupata habari peke yake.

Mambo mengine aliyotaka yawemo katika katiba ni uhuru wa fikra na maoni iwe ni pake yake na uhuru wa dini na imani huku akipendekeza haki ya kupiga kura kwa watu waliofungwa au waliopo rumande na kulindwa kwa mali iliyopatikana kihalali.

Page 4: Annur toleo la Ijumaa

4 AN-NUURSAFAR 1434, IJUMAA JANUARI 4 - 10, 2013Habari

ENZI zile Zanzibar kuna Taarab, kikundi kimoja kiliwahi kuimba wimbo uitwao ‘Watende wao’. Katika wimbo huo mwimbaji anasema, ‘Watende wao kina mwafulani. Kitendo wenzao, kutwa midomoni’. Kisha mwimbaji anaendelea kwa kusema, ‘ajabu ya watu hao, ajabu yakini, ajabu yakini, ajabu ya hao, yao hawaoni’. Mwisho wa kunukuu.

Nalaz imika kunukuu vipande hivi vya wimbo, baada ya tukio la kupigwa risasi na kujeruhiwa vibaya, Padre Ambrose Mkenda jioni ya siku ya Krismasi, huko nyumbani kwake Tomondo. Nanukuu si kwa maana ya kuhalalisha kitendo alichofanyiwa Padre, kwani si kitendo cha kiungwana wala cha kibinadamu. Na kwa hili naungana na watu wote kulaani kitendo hicho cha kinyama dhidi ya Padri Mkenda.

Kama kuna msomaj i anafuatilia makala zetu nyingi hapa katika mzalendo, ataona kuwa mara nyingi tunapigania usawa na haki ya Mzanzibari katika Muungano.Ya kwamba, Muungano uwepo au usiwepo, kwa nguvu moja tunasema haumtendei haki Mzanzibar, na hasa akiwa Muislamu. Kwamba kosa lolote lenye udogo mithili ya mdudu chungu, ilhali amelifanya M z a n z i b a r - M u i s l a m u , hilo huwa ‘mwao’. Huwa m’boga, ukatambaa, usifike mwisho. Dogo hukuzwa, na kusemwa na wakubwa na wanene wa nchi. Likawa jambo likatuojea.

Ni kweli kabisa, kitendo cha kujeruhiwa vibaya kwa Padre Mkenda, si cha kiungwana. Na bila shaka kinastahiki uchunguzi haraka wa Polisi. Na kwa sasa polisi ya Zanzibar, imeshafunguwa upelelezi kabambe juu ya tukio hilo. Naamini kwa jinsi tukio lilivyotokea, polisi Zanzibar inatosha kufuatilia na kuweza kutambua ukweli na undani wa tukio hilo. Hii ni kwa sababu tunaliamini jeshi la polisi juu ya upelelezi, na ufanisi wa kesi kama hizi.

Tumeona jinsi sayansi na teknolijia ilivyotumika kuwatia nguvuni wahusika wa vurugu za Bububu zi l izopelekea kuuwawa kwa askari polisi. Polisi, ilifanya upelelezi wake, na tuliyaona waliyoyagundua. Na kwa hili pia hatuna shaka wanaliweza.

Cha ajabu, licha ya kuwa tukio lenyewe ni kubwa sana,

Padre Ambrose Vs Sheikh SoragaImekuwa ya Watende wao kina mwafulani Ajabu... Kitenda wenzao, kutwa midomoni’

sioni haja ya kuletwa tena makachero ‘waliobobea’ kutoka bora , kwa k i le kinachoi twa ‘kuongeza nguvu’ juu ya tukio hili. Suali la kuletwa makachero wa bara, wakati hapa kwetu tuna kitengo maalum, chenye ujuzi na uzoefu wa upelelezi, kunanipa shaka nyingi sana kuliko imani ya utendaji w e n y e w e u n a o l e n g w a kuongeza ‘nguvu’ na ufanisi unaodaiwa.

Hofu yangu ya kwanza ni kwamba kwanini kitengo cha polisi cha upelelezi cha Zanzibar kiongezewe nguvu kutoka bara? Kwani kiliomba kusaidiwa, baada ya kuzidiwa na hali? Na upande wa pili ni pale ukijadili dhana ya kuongeza nguvu inapohitajika. Kiuozoefu tunaongezea nguvu pahala palipoonesha kuzidiwa na hali iliyopo. Jee hili lishajitokeza kuwa Jeshi la polisi limeshazidiwa na ufuatiliaji wa upelelezi wa kesi hii? Nahisi bado mapema kuomba msaada wa aina hii bado.

U p a n d e m w e n g i n e , unaposema unaliongezea nguvu jeshi, tena kwa kuleta makachero ‘waliobobea’ kutoka bara, unamaanisha kuwa makachero waliopo

hapa Zanzibar ni ‘vibwengo, v i chamba umande , au vimasantula’ tu, visivyo n a u z o e f u ? H u k u n i kuwadhalilisha askari hawa ambao Wazanzibari wana imani nao. Na kama hivi ndivyo, nalazimika kuleta tena shaka nyengine ya kwanini nguvu hii iongezwe kwa kujeruhiwa Padre Mkenda tu?

Alitoweka Sheikh Farid, lakini kwa bahati mbaya si jeshi la polisi Zanzibar wala bara lilianza upelelezi wowote. Suali la Farid liliachwa kama alietekwa ni paka au mbuzi tu, na hata baada ya kuonekana aliishia kutiwa hatiani na kufungiwa rumande badala ya kuwatafuta waliomteka na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria. Je, mtu akidai kuwa kisa, ni kwa sababu ni Mzanzibari na Muislamu, atakuwa amekosea?

Karibuni hivi alimwagiwa tindikali Sheikh Fadhili Soraga. Kwa sadfa ya tukio hili utaona Sheikh Soraga ni ‘mwenzao’. Kwa ufupi na lilipotokea la Soraga, kila kiongozi alipania kumuona kumjulia hali Sheikh. Kwa upande wa jeshi la polisi Zanzibar, waliapa kuanzisha

upelelezi mkali dhidi ya kadhia hii . Kwa bahati mbaya tena, hatukuwasikia makachero wowote kutoka b a r a w a l i o l e t w a k u j a kupeleleza kadhia ya Soraga, na mpaka hii leo hatujui kesi hii ilipokomea. Au hili halikuhitaji kuongezewa nguvu?

Sambamba na haya , kuna matokeo chekea ya uhalifu nchini hapa ambayo yalipuuzwa kufuatiliwa na wala hayakuchukuliwa hatua zozote za kufaa. Cha ajabu, akijeruhiwa mtu wa kanisa hata kama alikuwa na ugomvi na watu wengine, kwa bahati mbaya au kwa maswali yao ya mipango binafsi basi

hilo hufanywa kubwa. Na kuanzia hapo tunaanza kulipa ukubwa na kulizidisha mada na shadda, tukianzia na ni sisi Wazanzibari wenyewe.

Kwa mfano, mara tu baada ya tukio, taarifa ya awali ya polisi ilihusisha tukio hilo la ujambazi na uwezekano wa padre huyo kuwa na pesa alizozipata katika michango ya waumini siku hiyo ya Krismasi. Kauli hii aliekimbilia kuitoa, inaonekana haikuwaridhisha wakubwa wa Bara na Jamhuri k w a n i h a i k u t e g e m e w a isukwe hivyo. Taarifa kama hii ilikuwa isukwe, kwa kuhusishwa Waislamu na jumuiya ya Uamsho. Hapo wenzetu na viongozi wetu wangeridhika, japo kuwa sio kweli.

Pia Balozi Sei f Idd, alikuwa kiongozi wa kwanza wa Zanzibar kulikozesha tukio hili. Na ni kwa sababu ya kauli yake yeye ndie makachero ‘waliobobea’ wakaletwa. Na kwa wale wajuzi wa lugha wajue kuwa hii ‘kubobea’ hapa ni kuwa na ujuzi uliopindukia wa kuchonga, kuumba-umba na kuzua mambo yaliyokuwa ndiyo na yasiyokuayo. Ya kweli na ya uongo. Huo ndio ubobevu wenyewe.

Hofu yangu, kwanini iwe hivi, tena kwa matukio yawahusuyo watu fulani tu kuwa yaonekane ndio wenye haki zaidi mbele ya sheria na akina fulani wawe si chochote si lolote? Nakumbusha tena kuwa silioni dogo tukio la Padri Mkenda, lakini kwanini iwe kwa akina hawa tu? Nionavyo, kuna kijambo kinatafutwa hapa. Sio bure maana kama ni la upelelezi tu, hakukuwa na haja ya kulikozesha na kulitia madda na shadda kiasi hiki. Tutende haki, tukiamini watu wote wana haki sawa mbele ya sheria.

Natoa hoja.( M a o n i h a y a

y a m e a n d i k w a n a mwanamtandao 28/12/2012 na kuwekwa katika mtandao wa Mzalendo)

1.2259 sqm - 8 Milion2.1470 sqm - 4.5Milion3.1341 sqm - 4 Milion4.1566 sqm - 5Milion5. 1115 sqm - 3.5Milion6. 1136 sqm - 3.6Milion

Vipo Barabara ya Kongowe-SogaKilomita moja toka barabara ya Morogoro.

Simu No.0755 090 754/0715 090 754.

Viwanja vilivyopimwa vinauzwaKongowe Kibaha

Padre Ambrose Mkenda

Page 5: Annur toleo la Ijumaa

5 AN-NUURSAFAR 1434, IJUMAA JANUARI 4 - 10, 2013Habari za Kimataifa

SERIKALI ya Mapinduzi y a Z a n z i b a r i m e f i k a njia panda kutokana na matukio mabaya na ya ghafla yanayotokea hapa Zanzibar, hasa yanayobeba sura ya ‘hit and run attacks’ ambayo pia yanaingia katika sura ya visasi — kuanzia lile la Sheikh Soraga hadi la huyu Padri.

Kuna nadharia nyingi hapa zinazohusu uhalifu (theories on criminology) — au hata conspiracy theory. Nadharia 1: Hujuma inafanyika lakini hakuna hata alama ya namna uhalifu ulivyofanyika — hapa inakuwa taabu kwa wapelelezi kugundua namna ya uhalifu huo ulivyofanyika, au vipi umefanyika, na hata kuanzia pa kufanya upelelezi.

Nadharia ya 2: Uhalifu umefanyika, aliyefanyiwa uhalifu yuko hai, na kauli thabiti anaweza kusema. Hapa inakuwa rahisi sana

PARISVitendo vya chuki na kukanyagwa haki za Wa i s l a m u v i m e k u w a vikiongezeka kila siku nchini Ufaransa.

Propaganda na uchochezi wa kidini unaofanywa na vyombo vya habari vya nchi hiyo, pia umeongeza vitendo vya mabavu na uadui dhidi ya Waislamu pamoja na taasisi zao nchini humo.

Katika kitendo cha hivi karibuni kinachodhihirisha kuwepo chuki dhidi ya Uislamu, wabaguzi wa rangi nchini Ufaransa waliandika matusi kwenye kuta za msikiti wa Tuba, ulioko katika jimbo la Kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Msikiti huo ambao una uwezo wa kuchukua watu 200 na uliofunguliwa rasmi mwezi Ramadhani uliopita, umeshambuliwa na watu hao mara nne tokea mwezi Julai hadi Desemba mwaka jana.

Ni wazi kuwa mashambulio ya kiuadui dhidi ya Waislamu nchini Ufaransa hayatimii kwa njia hii tu, bali jamii ya Waislamu wa Ufaransa imekuwa ikihujumiwa pia kupitia vyombo vya habari vya nchi hiyo.

Vitendo vya kibaguzi dhidi ya misikiti nchini Ufaransa

Mfano mzuri wa jambo hilo ni namna vikatuni vya kukashifu na kumkosea heshima Mtume Mtukufu (saw) vilivyochapishwa na jarida la nchi hiyo la Charlie Hebdo, jambo lililokabiliwa n a w i m b i k u b w a l a malalamiko ya Waislamu.

Jarida hilo hata kabla ya kuchapisha katuni hizo, lilitoa taarifa na mapema juu ya mpango wake huo wa kutoa vikatuni vya kumchafua Mtume Muhammad (saw), lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa na mamlaka husika nchini humo.

Hii ni katika hali ambayo hivi karibuni Baraza la Waislamu wa Ufaransa lililalamikia vikali vitendo vya chuki dhidi ya Waislamu na matukufu yao vinavyoenezwa nchini humo na wafuasi wa mrengo wa kulia.

Kuhusiana na suala hilo, Muhammad Musa, Mkuu wa baraza hilo amebainisha wazi wasiwasi wake mkubwa kuhusiana na kuongezeka kwa vitendo vya mabavu na chuki dhidi ya jamii ya Waislamu wa Ufaransa.

Musa ameashiria kitendo cha kutekwa msikiti wa

Poitiers, mwezi Oktoba uliopita na kundi la watu 70 wafuasi wa mrengo wa kihafidhina uliopindukia mipaka, linalojiita Generation Identitaire na kuongeza kuwa, jambo kama hilo lilikuwa halijawahi kutokea katika historia ya nchi hiyo.

Kundi hilo linahubiri chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu na kudai kwamba, kuenea Uislamu nchini Ufaransa ni hatari kubwa kwa usalama wa nchi hiyo. Linataka kura ya maoni ifanyike nchini humo kuhusiana na suala la wahajiri wa Kiislamu na ujenzi wa taasisi za Kiislamu katika ardhi ya Ufaransa.

Jamii ya Waislamu huko Ufaransa ndiyo jamii kubwa zaidi ya kidini katika nchi zote za Ulaya. Licha ya kuwa na idadi hiyo kubwa inayochangia maenedeleo ya Ufaransa, lakini jamii hiyo ya Kiislamu inabanwa kwa kila njia na kunyimwa haki zake za kiraia, kisiasa na kijamii.

Waislamu wamekuwa wakiteswa na kubanwa kwa njia tofauti, zikiwemo za kueneza propaganda chafu dhidi yao na kubaguliwa katika idara za serikali.

KANO W a t u w a t a t u wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa, baada ya kundi la watu waliokuwa na silaha nchini Nigeria k u w a s h a m b u l i a waumini wa dini ya Kiislamu waliokuwa wakitekeleza ibada ya swala.

S h a m b u l i o h i l o lilifanyika Jumatatu wiki hii dhidi ya watu waliokuwa wakiswali s w a l a y a A l a s i r i katika mji wa Kano, ulioko kaskazini mwa Nigeria.

V i o n g o z i w a Nigeria wamesema kuwa, shambulio hilo lilifanywa na watu waliokuwa wamepanda pikipiki.

Waislamu washambuliwa msikitini Nigeria

R WA N D A i m e p i n g a kutumiwa ndege za ujasusi zisizo na rubani huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kama ilivyopendekezwa na Umoja wa Mataifa.

Msimamo huo wa Rwanda umetolewa Jumanne ya wiki hii, ambapo imetaka kwanza iwepo tathmini kamili ya kutumiwa ndege hizo na kusisitiza kwamba, haitaki kuona Afrika inakuwa bara la vyombo vya kijasusi vya nchi za kigeni.

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Herve Ladsous, anayehusika na vikosi vya kulinda amani a m e l i a m b i a B a r a z a l a Usalama la umoja huo kwenye kikao cha faragha kwamba, ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko Kongo DRC una mpango wa kutuma ndege tatu zisizo na rubani katika mikoa iliyokumbwa na vita ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Itakumbukwa kuwa Umoja wa Mataifa ulitaka kutumwa ndege hizo za ujasusi huko mashariki mwa Kongo tangu mwaka 2008.

Rwanda yapinga matumizi ya ndege zisizo na rubani DRC

KITENDAWILI CHA KUJERUHIWA KWA PADRI ZANZIBARsana kwa makachero kujua na kuanza upelelezi wa kina. Kesi zote mbili zilizotokea Zanzibar (Sheikh Fadhili Soraga na Padri zinaingia hapa).

Wote wazima na wote wana kauli thabiti. Padri ameweza kuzungumza na kuweza kuidhalilisha POLISI kama taasisi pale alipotoa kauli yake kumpinga RPC Aziz.

Kauli ya Padri dhidi ya jeshi la polisi inaonyesha dhahiri kuwa kanisa linataka watendewe vile wanavyotaka wao; na sio hali halisi ilivyo. Ingawa hakusema wazi wazi, lakini kwa maana isiyo wazi, ana maana ya kusema kuwa ‘polisi ni waongo’. Hii ni idhalali kubwa kwa jeshi la polisi. Kwa uhakika ni kuwa Padri huyu alikuwa anashika pesa, ama awe mhasibu kwa utaalamu au ka. Kwa uhakika 100% padri huyu ndiye

muidhinisha malipo.Bila yeye haitoki pesa. Je,

na hili atalipinga? Naomba hao makachero wa kutajika kutoka Dar es Salaam, waanzie hapa kama ndio ‘lead’ yao. Tumelewana? Muanzie hapa. Je, haiwi kuwa mpango wa ndani? (‘internal job’). Angalia mlingano wa kihalifu katika matukio ya kihalifu yalizofanyika Tanzania Bara karibuni:

i. Afisa wa kuzuia rushwa apigwa na kuul iwa na mwenzake Dar es Salaam

ii. RPC Mwanza apigwa risasi na kuuliwa Mwanza.

iii. Pesa nyingi zimeibiwa duka la Dar es Salaam (150m) — kitendawili mpaka leo???? Au kwa sababu hili limetokea Zanzibar? Acheni kuwa bias!

iv. Kuna mauwaji mengi yametokea Dar es Salaam wakat i wa Sikukuu ya Krisimasi. Mzungu mmoja amenyongwa hotelini, na wengine kuuwawa kikatili

…kimya! kimya!Nadharia 3: Nadhani

kanisa, CCM TZ na serikali zote zitafurahi sana kama ripoti ya makachero hayo zitasema kuwa UAMSHO ndio waliofanya kosa hilo. Mimi naomba kuwasaidia kitu. Mpaka sasa, ukweli ni kuwa, Waislamu wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla, hawajafikia kiwango hicho cha kutumia silaha au kuhujumu. Hili linajulikana na liko wazi. Kisocholojia, bora hata siasa Zanzibar zinaweza kuwa ni ‘tatizo’ kuliko dini. Mimi naomba serikali ya JK, Shein na IGP Said Mwema muwe waangalifu sana na mwelekeo huu unaozidi kushamiri. Mjaribu sana kuwa wakweli – vinginevyo, mnaimaliza nchi hivi mnajiona.

Hapa nazungumzia ile hali inayotaka kujengwa na kulazimishwa ionekane kuwa Waislamu ni watu waovu na maharamia na zaidi wale wa Zanzibar (Uamsho?).

N a o m b a n i w a u l i z e

wanasiasa na viongozi wa SMZ walipigana vikumbo k w e n d a k u m u o n a n a kumjulia hali Padiri, mbona hawajaenda kumuona Fadhil Soraga mpaka leo?

N a o m b a t e n a h a o m a k a c h e r o w a l i o k u j a Zanzibar pengine waanzie B e n k i a n a p o k w e n d a kuchukua ‘hela’ padri huyu! Inawezekana zikaonekana t r an sac t i on a l i zokuwa anazifanya padri huyo, na zikasaidia uchunguzi. Hii yaweza kuwa pamoja na kujua iwapo hali ya makusanyo na matumizi ya kanisa yanaridhia financial regulations za Tanzania, Zanzibar na Bank of Tanzania. Check …kama kuna any kind of money laundering hapo? Kwa ufupi matukio haya bado yamebaki kuwa kitendawili (unresolved mystery).

(Makala hii imeandikwa 29/12/2012 na kupatikana k a t i k a m t a n d a o w a Mzalendo)

Page 6: Annur toleo la Ijumaa

6 AN-NUURSAFAR 1434, IJUMAA JANUARI 4 - 10, 2013Makala/Tangazo

KINACHOENDELEA sasa nchini petu ni mfano wa maajabu na dhihaka. Kila kiongozi wa ngazi ya juu ameharakia ubavuni mwa kitanda alikolala Padre Ambrose Mkenda katika kitengo cha mifupa (MOI) cha Hospital i ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

Padre Mkenda wa Kanisa Katoliki (RC) anayeongoza Parokia ya Mpendae, mjini Zanzibar, amelazwa hapo akiuguza majeraha aliyopata baada ya kupigwa risasi na wahalifu wasiofahamika. Ni katika tukio la majira ya saa 3 usiku wa Desemba 2 5 , a k i w a a n a s u b i r i kufunguliwa geti ili kuingia kwenye nyumba anayoishi eneo la Tomondo. Alikuwa anaingiza gari kwenye geti wakati aliposhtukia anavuja damu sehemu ya chini ya kidevu.

Wa l i a n z a v i o n g o z i wachache wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar asubuhi ya siku ya pili alipokuwa anafanyiwa mipango ya kusafirishwa jijini Dar es Salaam baada ya madaktari wa Hospi ta l i Kuu ya Mnazimmoja kusalimu amri kuwa hawangeweza kutoa risasi zilizomganda mwilini.

Inasemekana Padre huyo alipigwa risasi kadhaa na watu wawili waliokimbia kwa kutumia pikipiki. Awal i , Padre Mkenda alipelekwa hospitali binafsi ya Al Rahma ambako baada ya kumpatia huduma ya kwanza, madaktari waliagiza apelekwe hospital i ya serikali kwa kuwa hawana ujuzi wa kumsaidia zaidi kwani alikuwa na risasi mwilini.

A l i p o f i k i s h w a t u Muhimbili, viongozi wakuu wa dola katika Jamhuri ya Muungano wakaanza hamkani kupigana vikumbo kumjulia hali. Akaanza Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Akafika kumjulia hali. Akafuata Msaidizi wake Namba Moja, Dk. Mohamed Gharib Bilal ambaye ni Makamu wa Rais. Akaruka kwa ndege Msaidizi Mkuu wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idi, ambaye mara

Mfano wa ajabu na dhihaka wa Padre aliyepigwa risasiJabir Idrissa, kwa mara yupo angani kwa

kuruka kati ya Zanzibar, Dar es Salaam na Dodoma wakati wa vikao vya Bunge na vile vya ngazi ya juu vya CCM, chama kilichompa ul’wa akianzia na ubunge jimboni Kitope, Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Mvumo wa viongozi wakuu wa nchi kuharakia kumkagua Padre Mkenda u l i s h a a n z a m a p e m a . Jeshi la Polisi lilishatoa msimamo wa kuhakikisha litawatia nguvuni wahalifu waliohusika kutaka kumtoa roho Padre Mkenda.

Jeshi h i l i l imetuma wapelelezi maalum kutoka Makao Makuu Dar es Salaam kusaidiana na waliopo Zanzibar ili kusaka wabaya wa kiongozi huyu wa dini inayostahiwa sana na dola ya Tanzania.

Shaka ya kwanza: Iweje mara tu baada ya Padre Mkato l ik i ku jeruhiwa kwa risasi, Polisi itume makachero mahsusi kusaka wahalifu wakati haifanyi hivyo kwenye matukio m e n g i y a n a y o w a s i b u wananchi?

Mpaka sasa chombo hichi cha ulinzi na usalama wa raia hakijakamata mtu hata mmoja kuhusiana na tukio la kujeruhiwa kwa tindikali (acid) Sheikh Fadhil Soraga, Katibu wa Mufti wa Zanzibar. Sheikh Soraga, kijana mbichi, alimwagiwa acid akiwa anakakamua mwili (jogging) kwa kupita pembeni mwa barabara ya Kiembesamaki/Mwanakwerekwe-Amani/Mtoni, mapema mwezi Novemba uliopita eneo la Nyerere.

I n g a w a a m e r u d i matibabuni nchini India kiasi cha siku kumi hivi zilizopita, walio karibu naye wanaieleza hali yake kama isiyoridhisha kutokana na majeraha ya usoni na kifuani kuendelea kumsumbua.

H a k u n a m a k a c h e r o maalum waliotumwa kusaka mhalifu wake na wendaji wa viongozi wakuu wa Zanzibar na wale wa dola ya Tanzania kumkagua haufanani na unaoonekana kwa Padre Mkenda. Mwezi kabla, askari polisi wa FFU, Koplo Said Abdulrahman Juma aliyekuwa akitoka kazini alipigwa na kuuliwa eneo la Bububu katika tukio lililohusisha makumi ya vijana waliokuwa na hasira baada ya kupotea kwa kiongozi wa Jumuia ya Uamsho, Sheikh Farid Hadi

Ahmed siku mbili kabla.H a k u n a v i o n g o z i

waliochakarika na kuagiza upelelezi maalum ufanywe kukamata wahusika. Badala yake, kilichofanywa ni dola kutuma askari wa vikosi v i s ivyo n idhamu vya Zanzibar na kuamuru kupiga na kudhalilisha wananchi usiku na mchana majumbani na mitaani.

Taarifa za karibuni kabisa za Polisi zimethibitisha kuwa hakuna mtu aliyefikishwa mahakamani ingawa mamia ya watu walikamatwa katika ile hali ya kukurupuka baada ya tukio. Inatoa matamko yanayoashiria kutuhumu makundi ya wanaharakati wa Uamsho kuhusika nayo. Hawa sasa ndio taulo la dola kila kunapotokea uhalifu.

Hali kama hii maisha haitaleta tija katika kazi ya vyombo hivi vya kutunza usalama wa wananchi.

Badala yake, vitakuwa vinachochea chuki dhidi ya askari wenyewe na dola kwa ujumla wake. Hapatakalika.

Kama polisi wamekosa watuhumiwa wa matukio mawili ya awali kwa kuwa h a w a k u j i s h u g h u l i s h a ki taalamu kuwatafuta, inakua je watoe ahadi na kutunisha misuli leo kufuatia kujeruhiwa kwa Padre Mkenda?

Mtu atakuwa na kosa gani akisema anaona mienendo ya kibaguzi, kidini na kiasili ya mtu atokako, katika utendaji kazi wa vyombo hivi vya ulinzi na usalama nchini? Hana kosa lolote. Matarajio ya wananchi ni kuona matukio ya uhalifu yanachukuliwa kwa uzito unaowiana hata kama mazingira yake yaweza kutofautiana. Uhalifu ni uhalifu tu; hakuna uhalifu

mkubwa na uhalifu mdogo hasa pa le unapokuwa umehusisha kuhatarisha maisha ya mtu.

Nilidhani Polisi wajisikie a i b u k w a k u s h i n d w a kumkamata mtu katika matukio mawili ya awali na wa j iu l i ze kwanin i wameshindwa kubaini mbinu za wahalifu husika? Sijui kama wanajiuliza. Basi niseme kuwa umefika wakati sasa Polisi warudi kwenye mstari ulionyooka kwa kutenda kazi yao ngumu ya kulinda raia kwa kuzingatia misingi ya weledi na mbinu za kisasa za kipelelezi. Wasikurupuke.

Vi n g i n e v y o t a a s i s i hii itaendelea kugeuzwa chombo cha mzaha mtupu kinachotenda kazi kwa kufuata amri za wanasiasa watawala. Na kwa hapa Ta n z a n i a w a n a s i a s a hawa wamebanwa na mfumokristo.

Kituo cha mafunzo na stadi za kazi Dar es Salaam kinawatangazia OFA MAALUM ya nafasi za masomo katika kozi zifuatazo:-

Uwalimu wa Chekechea (miezi tisa ada 450,000 tu),

Matumizi na ufundi wa kompyuta (Miezi Mitano ada 100,000) [Utasoma Introduction to Computer, MS Office (Word, Execel, Powerpoint), Networking and Internet, Web Designing, Database, PC Maintenance na Open Office],

Usafi wa maofisini (Mwezi Mmoja na Nusu Ada 100,000), Ushonaji na kudarizi (miezi sita ada 100,000).

Ni muhimu kuwa: wote watakaosoma ualimu wa chekechea na usafi wa maofisini watasomeshwa kiingereza bure,

Wanafunzi watapata masomo kwa vitendo chini ya usimamizi wa kituo, Wanafunzi watakaofaulu vizuri watasaidiwa kutafuta ajira mara watakapomaliza.

Kituo kipo Tabata Nyuma ya Alfaruk Sekondari School (Africa Muslim Agency) palipokuwa na chuo cha uwalimu SAFINA.

Kwa upande wa ushonaji na kudarizi kituo kipo Temeke Masjid Tungi.

Kozi zitaanza tarehe 14 Januari 2013

Kujiunga fika ofisi za TAM PRO Magomeni, Kituo cha TABATA ama MASJID TUNGI kuchukua fomu au piga simu 0714 151 532, 0767 151 532 au 0718 807 228, 0778 776 226 kwa maelezo zaidi.

Dar es Salaam SDC tunakuongoza katika maisha yako.WAHl SASA NAFASI NI CHACHE.

DAR ES SALAAM SKILLS DEVELOPMENT CENTRE (SDC)

Page 7: Annur toleo la Ijumaa

7 AN-NUURSAFAR 1434, IJUMAA JANUARI 4 - 10, 2013Makala

MKUU wa Takwimu katika Wizara ya Wafungwa katika Mamlaka ya Taifa la Palestina Abdul Nasser Farawana, ambae pia ni mjumbe wa kamati ya muda inayoshughulikia mambo ya wizara hiyo mjini Gaza, amebaini kutekwa kwa Wapalestina wapatao 3,848 mwaka huu wa 2012, wakiwemo watoto 881, wanawake 67 na wawakilishi au wabunge 11.

Aidha walikuwepo pia wahar i r i 9 wa “Wafau Ahrar”, akiwemo Hanau Shalabiy, vilevile wasomi kadhaa, waandishi wa habari, walimu, viongozi wa kisiasa, kitaaluma na kijamii. Huku akiweka wazi kuwa, utekwaji huo kwa mwaka huu wa 2012 umefikia wastani wa watu 321 kwa mwezi, sawa na watu 11 kwa siku.

Farawana ameongeza kusema kuwa, kutekwa au kutiwa mbaroni huku dhidi ya Wapalestina kumeathiri makundi yote ya jamii bila kubagua, huku kukijumuisha pia majeruhi, wagonjwa na wazee, jambo linaloonekana kuwa ni la kila siku na lenye kuleta kero kubwa.

I d a d i k u b w a y a waliotekwa ilikuwa ni kwa lengo la kulipiza kisasi kwa Wapalestina na viongozi wao, wala haina uhusiano na suala la ulinzi kama unavyodai utawala wa kivamizi wa Israeli, kwani hatua hiyo hata katika kanuni zao za kidhalimu haipo isipokuwa

Wapalestina 3,848 wawekwa kizuizini mwaka 2012, wakiwemo watoto 881

kwa uchache sana.Vi l e v i l e F a r a w a n a

ameongeza kuwa, hatua hiyo ya utekwaji imefanyika k inyume na she r i a za kimataifa pia misingi ya haki za binaadamu, kufuatia namna yake na hata mazingira ya kuwekwa kiziwizini. Kwani kila aliyetekwa alikumbana na mateso ya aina mbalimbali, tena mbele ya familia yake.

Waliotiwa mbaroni zaidi ya 3,759 ambao ni sawa na asilimia 97.7, wanatokea Ukingo wa Magharibi na

i d a d i y a v i o n g o z i waliokamatwa na kurundikwa katika magereza ya wavamizi wa Israeli , imeonekana kupungua kufuatia migomo binafsi dhidi ya uonevu huo ujulikanao kama “Utekaji wa viongozi”.

Kwani walifikia viongozi 320 na kupungua hadi kufikia 160 mwanzoni mwa mwezi wa Novemba uliopita. Baadae takwimu zikaonyesha ongezeko hadi kuf ik ia viongozi 190 mwishoni mwa mwaka 2012, zikiwa vilevile ni takwimu za hatari mno.

Akikamilisha ripoti yake, Farawana amebainisha tena kuwa, idadi ya wafungwa wakongwe waliopo gerezani tokea kabla ya mapatano ya Oslo na kuasisiwa kwa Utawala wa Kitaifa wa Palestina, mnamo 4/5/1994, imepungua hadi kufikia 109, mwishoni mwa mwaka 2012.

Upungufu huo umetokana na kuachwa huru baadhi yao, baada ya kumaliza adhabu zao. Huku wale waitwao “Wakuu wa wafungwa”, kwa mujibu wa msamiati wa Kipalestina kwa wafungwa wenye miaka 20 na zaidi, idadi yao ikizidi hadi kufikia 70.

Aidha idadi ya “Majenerali wa subira”, nao ni wale walio tumikia kifungo cha zaidi ya miaka 25 mfululizo kwa mujibu wa msamiati wa kipalestina, ikiongezeka na kufikia wafungwa 23.

Jerusalem. Ambapo kiasi cha watu 89 tu ndio wanaotokea Ukanda wa Gaza, huku wengi wao wakiwa ni wavuvi wal iokamatwa wakiwa baharini.

Farawana pia ameweka wazi kuwa, takwimu za kukamatwa watu hao ndani ya mwaka 2012, zinaonyesha kama ifuatavyo: Januari watu 298, Februari 327, Machi 362, Aprili 298, Mei 295, Juni 261, Julai 272, Agosti 236, Septemba 254, Oktoba 315, Novemba 535

na Desemba ni 455.A m e o n g e z a k u s e m a

kuwa, rekodi zinaonyesha idadi ya utekwaji imepungua tokea mwaka 2007, huku ikiongezaka mnamo mwaka 2012 kwa asilimia 16.2, ukilinganisha na mwaka 2011.

Hii ni hatua mbaya sana na ya hatari, huku Wapalestina hao wakizidi kunyimwa haki zao, pia za ndugu zao waliopo katika magereza ya Israeli.

Kwa upande mwingine,

BAADHI ya waandishi wa habari toka sehemu mbalimbali duniani walipotembelea Palestine mwishoni mwa mwaka jana.

Ya kujifunza kutokana na msiba wa SajukiInatoka Uk. 2

Vichwa vyao kama nundu za ngamia zinazoyumba (aina ya msuko wa nywele wanaosuka wanawake). Hawataingia Peponi wala hawatasikia harufu yake ingawa harufu yake inaweza kunuswa kutoka masafa kadhaa na kadhaa

Suala la mavazi kwa mwanamke wa Kiislamu ni maagizo ya Quran ambapo mavaz i hayo k ims ing i yanamtofautisha yeye na kama ndugu zake wanaume. Katika Suratul -Ahzaab aya ya 59 inasema “Ee Mtume waambie wake zako, na binti zako, na wanawake wa Kiislamu wajiteremshie uzuri nguo zao. Kufanya hivyo kutapelekea upesi wajulikane wasiudhiwe. Kwa vazi alilovaa Bi. Wastara hakuna m u u n g w a n a a n a e w e z a

kumbughudhi labda awe amefurutu ada kwa uhuni na ushenzi.

Nikiwa Muumin makini wa Kiislamu sitaweza kuwa bakhili wa kutumia taalum yangu katika kutoa mchango wa ukarimu kwa Kizuka Bi. Wastara ambaye ni mfano wa kuingwa na wasanii wengine na wanaweke wa kiislam kwa ujumla hasa mnapopatwa na faradhi. Imam Hassan Bin Ali Bin Abi Talib amesema kwamba “Atakae kuwa mkarimu atapata utukufu, na atakae kuwa bakhili atadharauliwa na kwa hakika aliye mkarimu mno kwa watu ni yule anaetoa na kumpa asiyetarajia kitu kwake na hakika mkombozimkubwa kwa watu ni yule anayekomboa kutokana na kudra”

S u a l a l a k u p a t w a na matatizo, misiba na

misukosuko mbali mbali ni jambo la kawaida katika maisha ya hapa duniani. Hatuna budi kufahamu kuwa ulimwengu huu haukusudiwa na Allah uwe pepo. Bali umekusudiwa uwe mtihani kwa mwanaadamu. Hivyo viumbe vyote vilivyomzingira pamoja na matukio na miondoko yote ya maisha viko pale kama ni mtihani kwetu.

Katika msiba ule kuna vituko ambavyo vilijitokeza vinavyokwenda kinyume kabisa na mila, desturi na mafundisho ya Kiislamu. Mosi kuna kitendo kimefanyika ambacho si katika jambo lenye kufurahisha, vijana wa kiume ambao ni watangazaji wa kituo kimoja cha Radio wakajumuika na vijana wa kike eti kusaidia kazi msibani. Hili halikuwa kosa,

isipokuwa lilipokihirisha na kunichefua pengine sio mimi tu nilieona kwenye picha bali hata wale wenye kuheshimu Uislamu walikirihishwa.

Watu mbali mbali walifika nyumbani kwa marehemu, wapo viongozi wa kisiasa, wafanyabiashara, wasanii wa filamu, muziki, waandishi wa habari na watangazaji. J a m b o m o j a a m b a l o nimekuwa nikiliona hasa miaka ya hivi karibuni ni kuwa katika pahala ambapo kuna msiba ukimuhusisha mtu maarufu, basi taratibu za Kiislamu mara nyingi zinakuwa hazizingatiwi, ama kwa makusudi au kwa kutokujuwa.

Wa l e w a n a o k w e n d a kuomboleza kwa mfano wanawake kwa siku za nyuma hata wakiwa si Waislamu wanatafuta kivazi ambacho

kinaendana na wanawake wa Kiislamu watakaowakuta msibani , wanaume nao hufanya hivyo hivyo, ilikuwa nadra kumuona mwanamke ambae si Muislamu akifika kwenye msiba wa Muislamu akiwa na kivazi kisichofanana na waliopo pale.

V i j a n a w a k i u m e waliheshimu, walisubiri maelekezo ya wakubwa, katafuteni kuni, kanunue hichi au kile, tandika jamvi, kat ika maeneo ambayo yanashida ya maji, vijana wa k iume wana tumwa kuchota maji, kuwakaribisha wageni na kuzungumza nao. Mambo leo ni tofauti kabisa, wanaume wanakwenda msibani wakiwa makwapa wazi, suruali kipande huku wanawake wakivaa majinzi

Page 8: Annur toleo la Ijumaa

8 AN-NUURSAFAR 1434, IJUMAA JANUARI 4 - 10, 2013

Makala

IBADA ya Hijja, ambayo Waislamu huisafiria kwenda kuitekeleza kule Makka, Saudi Arabia, kila mwaka, ni moja ya ibada kongwe kabisa kuletewa wanadamu na muumba wao Allah hapa duniani.

Ibada hii, hasa iliasisiwa na Nabii Ibrahim (A.S.W), miaka takriban 4000 BC (kabla ya kuzaliwa Yessu Kristo), pale alipoamriwa na Mola wake ahame kutoka kwao maeneo ya Iraq kwenda nchi ya Hijaz (Saudia Arabia siku hizi) na huko ajenge Kaaba tukufu kwa ajili ya kuabudiwa Allah.

Wengi wa watu — wakiwamo waumini wa dini ya Kiislamu pia — wanaichukulia visivyo (false assumption) au kimazoea, kwamba Hijja iliasisiwa na Mtume Muhammad (S.A.W) – la hasha! Mitume wote waliokuja baada ya Ibrahim na kabla ya Muhammad — Nuhu, Ismail, Ishaaq, Mussa, Daud na

HIJJA: Ibada kongwe kwa wanadamu wote

Na Alhaj Abdallah Tambaza

wengineo — walifundisha juu ya Ibada hii adhimu yenye malipo mengi sana pengine kuliko ibada yeyote ile ikiwamo funga na sala. Ukimaliza kuhiji Allah huwa amekufutia madhambi yako yote ukabaki bila dhambi kama ulivyozaliwa!

Mtume (SAW) anasema, “...malipo kwa ajili ya Hijja iliyofanywa vizuri na kukubaliwa hakuna ila ni kutiwa peponi tu…”

Anasema pia Mtume wa Mwenyezi Mungu; Sala moja katika Masjid l’haram pale Makka ni sawa na sala laki moja katika misikiti mingine kama vile ya kwetu huku; na msikiti wa Mtume kule Madina ni sawa na sala elfu moja za Tanzania. Haya utayapataje kama hukwenda kuhiji?

Habari zinasema, Kaaba Tukufu ilianza kujengwa kwa mara ya kwanza na Nabii Adam mwenyewe, lakini baadaye ikavunjika, ndipo Ibrahim

alipoamriwa kuja kuijenga upya mahala pale pale na katika msingi uleule wa awali.

Ibada ya Hijja ina nguzo kuu nne tu; ya kwanza ni mtu kuwa katika vazi la Ihram, yaani zile shuka mbili nyeupe moja juu na nyengine chini; nguzo ya pili kusimama Arafat; ya tatu ni Kutufu katika Kaaba na ya mwisho ni Sai, yaani kutembea baina ya vilima viwili Safaa na Marwa.

Mambo mengine ambayo ni ya wajib na lazima ndani ya ibada ya hijja ni kusali sehemu inayojulikana kama Makamu Ibrahim iliyo pembezoni mwa Kaaba; kunywa maji ya Zamzam pale Hijri Ismail; kuchinja mnyama pamoja na kupiga shetani mawe kule Jamaraat.

Cha ajabu leo hii ni kuona kwamba watu wa dini nyingine, hususan ya Kikristo, na vyombo vya habari (mainstream media) kushindwa kuripoti sawasawa juu ya historia ya Hijja, wakati

wakiwa wanawafahamu mitume waliopita Ibrahim, Mussa, Ismail, Ishaaq, Yaakub na wengineo ambao nao pia walihiji kama hivi tufanyavyo sisi.

Isitoshe vitabu vya Taurati, Zaburi na Injili vyote pia v inazungumza habar i za Ibrahim na kisa cha kuamrishwa kumchinja Ismail; habari za Sarah na mbio zake za Saffa na Marwa na miujiza ya yale maji ya Zamzam yaliyo pembezoni mwa kaaba yalivyopatikana kutokana na mtoto mchanga kupigapiga miguu yake na chemchem ikatokeza.

Mambo haya yote yalitendeka karne nyingi nyuma, si tu kabla Muhammad kuja, lakini pia Issa na Mussa hawakuwapo. Sasa iweje leo Waislamu peke yao ndio wafanye ibada hiyo?

Moja ya nguzo muhimu katika Hijja ni kile kitendo cha kusimama pale kwenye uwanda wa Arafat. Umuhimu mkubwa wa mahala hapa ni kwamba ndipo mahala ambapo baba yetu Adam na mama yetu Hawa walipokutanishwa tena baada ya kuondolewa na Allah kule peponi wakatupwa ardhini kila mmoja akiangukia sehemu yake.

Ilikuwa ni katika uwanda wa Arafat ambapo walianza maisha yao na hatimaye kuzaliwa sisi wanadamu wengine mpaka kujaza dunia hii. Hakuna kitu cha Mtume Muhammad hapo Arafat, ila pana mazingatio kwamba sote binadamu (human species) – tuwe Wahindi, Mayahudi, Waafrika, Wazungu, Waarabu na watu wa dini mbalimbali — kuwa ndio chimbuko letu.

Arafat pia, ndio mahala ambapo Malaika Jibril (Gabriel) a l i p o m f u n d i s h a I b r a h i m (A.S.W.) baba wa mitume yote, namna ya kutekeleza ibada ya Hijja ili akawafundishe watu wengine. Ibrahim huyu ni yule yule anayetajwa kwenye vitabu vingine.

Nguzo nyingine ya Hijja ni ile ya kuzunguka Kaaba (circumbulating) mara saba na kunywa maji ya Zamzam kutoka Kisima cha Ismail; kusali rakaa mbili sehemu takatifu ambayo inajulikana kama Makamu Ibrahim. Kingine ni kufanya Sai (kutembea) baina ya vilima vya Safa na Marwa.

Sasa , sua l a l a ms ing i linalonisumbua mimi ni pale ninapoona kwamba Ibada hii, ambayo ndiyo kongwe kabisa kuletewa binadamu na pia ikaunganishwa na kisimamo cha Arafat pale mahala ambapo ni nyumbani kwa Baba yetu Adam na Hawa, iwe ni ibada ya Waislamu peke yao na siyo kizazi chote cha Adam (humanity)? Hawa watu wa dini nyingine chimbuko lao ni wapi? Hata Adam na Eve basi hawamjui?

Nini inaweza kuwa sababu ya utengano huu? Je! Ni kwa sababu Uislamu umeiweka

ibada ya Hijja kama nguzo ya tano ya Uislamu na hivyo kuwafanya wasio Waislamu kudhani kwamba Kaaba ni ya Waislamu? Au kule kuelekea kwetu Kaaba kila tunaposali inaonekana kwamba hiyo Kaaba ni ya dini ya Muhammad ambaye hawamwamini?

Ni nini hasa kilichofanya h a l i k u w a h i v i w a k a t i wanakubali sisi wote ni wana wa Adam; na Adam ndiyo huyo tunayekwenda kusimama mahala alipokutanishwa na Hawa na kuanzisha umma wote huu wa kibinadamu? Sipati picha hata kidogo — nonsensical!

Sasa hebu tuiangalie Qurani inatufundisha nini kuhusu hili la dini ya wanadamu kuwa na chimbuko moja kutoka kwa Ibrahim. Ndani ya Surat Bakarah, Surat l’Haaj, Surat Ibrahim na Al-Imran mna aya nyingi sana zilizofafanua jambo hili:

“ … n a i p i g a n i e n i d i n i ya Mwenyezi Mungu kama inavyos tah ik i… na wa la hakuweka mambo mazito katika Dini. (Nayo ni Dini hii) ni mila ya baba yenu IBRAHIM. Yeye Mwenyezi Mungu alikwiteni Waislamu tangu (katika VITABU VYA ZAMANI) huko; na katika Qurani hii pia (mumeitwa jina hilo), ili Mtume awe shahidi na nyinyi muwe mashahidi kwa watu wote. (Qurani Surat Haaj 22:78)

Katika Suratil Al- Imran 3.96 Allah anasema, “Kwa yakini nyumba ya kwanza iliyowekwa kwa ajili ya watu kufanya ibada ni ile iliyoko Makka, yenye baraka na uongozi kwa ajili ya WALIMWENGU wote. Humo mna ishara zilizowazi za kuonyesha utukufu wake na ukongwe wake…miongoni mwa hizo ni mahala alipokuwa a k i s i m a m a I b r a h i m … n a anayeingia nchi hiyo anakuwa katika salama…Mwenyezi Mungu amewawajibisha watu wafanye Hijja katika nyumba hiyo na … yule atakayekanusha Mwenyezi Mungu si muhitaji kuwahitajia walimwengu…”

Na katika aya nyingine, (Surat Bakarah 2:136) Allah (SWT) anafafanua zaidi kuhusu dini miongoni mwa wanadamu kuwa ni moja na ni ile ile waliofundishwa mitume wote waliotangulia kupitia Malaika Jibril (Gabriel):

Semeni nyinyi (Waislamu waambien i Mayahudi na M a n a s a r a ; w a a m b i e n i ) : “Tumemwamini Mwenyezi Mungu na

yale tuliyoteremshiwa, na yale yaliyoteremshwa kwa Ibrahim na Ismail na Is-haqa na Yaaqubu na (kizazi chake Yaaqubu) na waliyopewa Mussa na Issa pia yale waliopewa manabii wengine kutoka kwa Mola wao…wote tunawaamini”

Uislamu hauna tatizo katika kuwakubali mitume waliopita. Kwetu sisi msikiti wa tatu kwa

Inaendelea Uk. 9

Page 9: Annur toleo la Ijumaa

9 AN-NUURSAFAR 1434, IJUMAA JANUARI 4 - 10, 2013Makala

KISA cha watu wa pangoni, yaani kwa lugha ya Kiarabu, ‘Ashaabul-kahfi’, ni miongoni mwa visa vikongwe katika historia ya dini na maisha y a m w a n a d a m u . K i s a hiki ambacho ni moja ya visa vingi vinavyoonesha utukufu na uwezo mkubwa wa Mola wetu Muumba, Allah Subhaanahu Wataala, si maarufu katika Uislamu tu, bali hata katika dini na jamii nyengine duniani.

Kwa muhtasar i , k isa h ik i k inawahusu wa tu wasiopungua saba, na mbwa wao, waliokimbia mateso ya utawala kandamizi katika nchi yao. Katika kimbia kimbia yao hiyo, walifika pahala wakaingia kwenye pango kujipumzisha. Hapo Mola mtukufu aliwalaza usingizi mrefu zaidi kuliko usingizi wowote aliowahi kulazwa mwanadamu na Mola wake, ukitoa maiti waliokwishatangulia mbele ya haki. Watu hawa waliamka baada ya kulala kwa miaka inayosadikiwa kutimu 300 na ushei. Ambapo, walipoamka walikuwa wageni katika ardhi yao waliyozaliwa na kukulia humo. Allah Akbar!

N i m e l a z i m i k a kukikumbuka kisa hiki kikongwe kwa kukinasibisha na maisha halisi wanayoishi Wazanzibari wakiwa chini ya himaya ya Muungano. Himaya, kwa maana wakiwa chini ya uangalizi na udhibiti wa Muungano huo ambao kwa kughafilika na kulala kwao kwingi, wamejikutia au watajikutia wakiamka mbali na zama za siku walizolala. Pia wameamka au wataamka wakiwa wageni katika nchi yao kama walivyokuwa ‘As-haabul-kahfi’.

Ikiwa imepita miaka 48 sasa ya Muungano, huku Zanzibar ikizidi kupoteza himaya yake na kila kitu chake, kuna kila dalili kwamba sehemu kubwa ya wahusika wa kuitetea nchi hii kuwa bado hawajaamka. Wamelala pangoni bi la kujitambuwa.

Wazanzibari tumelala usingizi mnene, mzito, uliojaa mkoromo, korozo, na ndoto za mwasande (mwanamke a n a e m j i a m w a n a m m e ndotoni kimapenzi), tena katika bustani za Adeni. Wakati sisi tukistarehe na mwasande, wenzetu hawalali, wanakusanya kila kilicho chetu. Na yule mbwa wetu tuliemchukuwa kule pangoni, ka tup iwa fupa ambalo

Wazanzibari na usingizi wa ‘As-Habul-Kahafi’Na Mwandishi Maalum hugunya, akichoka nae hulala.

Hata habweki, maskini.Na kwa usingizi huu,

tumepoteza utambulisho wetu, utaifa, mila na desturi zetu, na kila kitu. Kwa kulala kwetu huko kusikokwisha, tukipumbazwa na ndoto za mwasande, huku tukiamini mbwa wetu yupo kutulinda, b i la kutanabahi hasara inayotukabili. Kumbe vile tunarudi nyuma kimaendeleo h u k u w a s h i r i k a w e t u wakikimbia kwa kasi ya ajabu. Kasi ambayo hata siku tukiamka, tutalala tena kwa kukata tamaa kwa walivyotuacha duni na umbali walioko wao.

Kwa sababu ya usingizi wetu mzito, Wazanzibari ambao kiasili ni magwiji, wazawa na wamiliki halisi wa lugha ya KISWAHILI duniani, leo wanasomeshwa Kiswahili na watu wa Bara. Pamoja na kasumba zinazoenezwa na wenzetu wa Kenya na Tanganyika kuwaambia w a g e n i n a k u a n d i k a vitabuni kuwa Kiswahili hakina wenyewe, ukweli unabaki kuwa wenyewe hasa ni Wazanzibari ambao hawazaliwi na lugha nyengine yoyote ukiacha Kiswahili, seuze wao wanaozungumza Kiswahili kama lugha yao ya tatu au ya nne.

Hata hivyo, sishangai sana kuwasikia wenzetu wa Bara na Kenya wakisema Kiswahili hakina wenyewe. Ni kweli kiasi fulani maana kama wapo kweli Waswahili, wangesema, wangejibu, au hata kujitetea kwa njia moja au nyengine. Lakini tupo, tumelala, watu wanajivunia Kiswahili chetu na kujipatia utajiri mkubwa na shahada za juu za Elimu huku sisi tukizidi kutokwa na ‘dovuo’ (madenda) kwa usingizi mzito uliotuvaa.

Ni jambo la aibu na fedheha kuona Wizara ya Elimu Zanzibar, ikiwapiga chenga wataalamu wa Kiswahili waliopo taasisi ya Kiswahili na Lugha za Kigeni (SUZA), na kukimbilia waandishi wa Bara kuwatungia vitabu vya kufundishia Kiswahili Zanzibar. Iweje wenzetu wa bara, japo wana shahada kubwa za Kiswahili, lakini ukweli wao sio Waswahili, wawe ndio mabingwa wa kutuandikia sisi vitabu vya Kiswahili? Haya sio yale ya ‘kuku kupanda basikeli na bata kuvaa raizoni’?

Ukwel i tunahesh imu sana taaluma ya wenzetu na kila mtu, lakini ikumbukwe

kwamba zamani vi tabu vyetu vya Kiswahili ndivyo vilivyovikitumika Afrika Mashariki nzima na duniani kufundishia Kiswahili. Na vilikuwa vizuri na vyenye kufunza Kiswahi l i cha kikweli. Lakini ukiviangalia v i t a b u v y a K i s w a h i l i tunavyoandikiwa Bara na Kamusi, ni ‘korogo-vyogo’ tu!

Sambamba na haya , kuna ombwe la vilio juu ya Kiswahili kinavyoharibiwa na wenzetu wa Kenya na Bara. Tena kwa bahat i mbaya, kinaharibiwa na wale wanaoitangazia dunia kuwa wao ndio wajuzi wa Kiswahili. Ama kweli, penye vipofu, chongo huwa mfalme. Wakati sisi tumelala, wao wanajichumia na kututungia maneno yasiyokuwa na nyuma wala mbele.

Isitoshe mengi ya hayo maneno , kwa mi l a na desturi zetu ni matusi ya laana, lakini kwa vile hii si lugha yao hawalijui hilo. Je, tunategemea nini iwapo wao hawatajuwa mipaka, miko na itikadi ya lugha hii ambayo wenyewe wameisahau chini ya vitanda vyao walivyolalia usingizi mzito wa watu wa pangoni?

Kuna wenzetu wa Bara na Kenya wametajirika kwa kufundisha Kiswahili nje ya nchi na kuandika vitabu vya Kiswahili. Japo vingi ya vitabu vyao hivyo na hasa kamusi, ni vyenye kiwango duni, lakini madamu hakuna chengine, wao ndio watatambulika. Sisi

Wazanzibari tupo, hatuandiki, hatuziombi kazi hizo hata zikitangazwa kiasi gani. Letu dharau nyingi tu, tukitajiwa ku fund i sha Ki swah i l i . Utasikia ‘ah! Kiswahili kitu gani? Tunawaachia wenzetu wakifaidika bure!

Leo hii kumkuta Mzanzibari anayefundisha Kiswahili nje ya nchi ni nadra. Na sijui hata kama yupo. Na kama wapo, ni mmoja kwa mia. Kiswahili kina Wakenya na Wabara tu kule Marekani, Uingereza, na kila pahala ni Mkenya, Mbara tu. Zanzibar tumelala, huku tukisondogewa na dume la ng’ombe lililokata kamba liitwalo Muungano bila huruma na wala hatufanyi jitihada ya kujitetea.

Pamoja na yote haya, suali hi l i l inachangiwa na viongozi, taasisi zetu za elimu, na wasomi wa Kizanzibari waliopo. Ambao, wao ni nguvu kazi kubwa na wanaopaswa kusimama na kukikingia kifua Kiswahili, kukitetea na kukirejeashea hadhi yake.

Bahati mbaya hakuna msomi anaeandika tena hapa petu. Ukitoa wale wachache waliowakiandika hadithi na mashairi siku hizo, hakuna mwengine. Na bahati mbaya hawa pia vitabu vyao haviingizwi katika silabasi ya Bara kwa madai Kiswahili chao ni kigumu, hakimo katika kamusi zao. Lakini yote haya ni kwa sababu hapana Kiongozi anaelipa kipaumbele suali hili. Ndio maana ukaona hata

ile TAKILUKI pale SUZA, imedorora. Haichapishi, haiandiki kitu, inasubiri tuandikiwe kamusi na vitabu kutoka bara. Kamusi zenye maneno ya kikabila, mengi yakiwa ya matusi, yasiyoingia akilini, tuwafundishe watoto wetu. Kule Baraza la Kiswahili Zanzibar (BAKIZA), japo wametoa kamusi lakini ni la lugha moja tu, halikidhi haja. Pia wanaonekana kufunikwa sana na wenzao wa kule Bara.

Kwa kweli, ipo haja kwa Serikali, viongozi, wasomi, na taasisi husika Zanzibar kulivalia njuga suali hili. Kwan i Zanz iba r kama Zanzibar, tumeshapoteza vingi katika Muungano, na ni vigumu kuvirudisha tena. Basi na hili la Kiswahili kuna dalili ya kukipoteza. Kiswahili, lugha ya mama na baba zetu. Lugha ya wahenga wetu, utu wetu, na utambulisho wetu? Hatuoni hata kimeme, tunakiacha kikifaidisha watu wengine. Bado tumelala tu.

Tuamkeni Wazanzibari, tujiandikie vitabu vyetu, k a m u s i z e t u . K a m u s i zinazosawiri muktadha wa mazingira na tamaduni zetu. Vitabu, vyenye kuandika Kiswahili chetu na sio chao. Hili tunaweza na halihitaji, tume ya Warioba kamwe.

Hivi hatuoni aibu, hata Kiswahili tufundishwe na Bara? Tuamke.

Inatosha, kwani ‘Mwana m t a m b u w a s h i b a e , hashibiwi’.

MAKAMU wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Idd Seif

Page 10: Annur toleo la Ijumaa

10 AN-NUURSAFAR 1434, IJUMAA JANUARI 4 - 10, 2013Makala

HIJJA: Ibada kongwe kwa wanadamu woteInatoka Uk. 8

utukufu ni ule wa Bait l’Maqdis u l iopo Je rusa lem ambao ulijengwa na Mtume Yaakub bin Ishaaq bin Ibrahim. Ingawa uko Jerusalem, lakini mahala hapo kwetu ni muhimu sana kwani ndipo Jibril alipomkutanisha Mtume Muhammad na mitume iliyomtangulia ‘Uli l’azmi’ (Issa, Mussa, Ibrahim, Nuhu n.k) wakaswali pamoja kabla ya yeye kwenda safari yake ya Miiraj (juu mbinguni). Sala hiyo iliongozwa na Muhammad pale mihrabuni, Je, waliswali swala ya Mungu yupi?

Katika makala yake ya kitafiti aliyoipa jina Biblical Abraham (Ibrahim ndani ya Biblia), iliyochapishwa May, 2004, Myahudi mmoja Abe Weisman, ameelezea kwa kirefu kuhusu Ibrahim na umuhimu wake katika dini ya Juda, Ukristo na Uislamu. Pamoja na mambo mengine Weisman anakubali; na hapa nanukuu:

“For the past couple of months I have been researching the Biblical Abraham. Abraham is an extremely complex figure and plays an important role in not only Judaism, but also Chr is t iani ty and Is lam… Abraham’s obedience to God forms a critical component f o r J e w s , M u s l i m s a n d Christians…”

(Angalia:www.ilperez.org/graduates/abe_weisman).

Tafsiri isiyo rasmi ya maneno ya Weisman ni:

“Kat ika miez i ya h iv i karibuni nimekuwa nikifanya utafiti kuhusu Abraham ndani ya Biblia na nimegundua kwamba Abraham ni mtu aliyefanya mengi si tu katika dini ya Juda, lakini pia ndani ya UISLAMU na UKRISTO… Unyenyekevu wake kwa Mungu ni kiungo (mazingatio) muhimu sana kwa Wayahudi, Waislamu na Wakristo!”

Kwa kweli ingependeza sana kuona siku moja Binadamu wote tukiacha tofauti zetu hizi za kibaguzi na kujiona bora kuliko watu wengine baina ya mataifa, makabila, nchi n.k. ili sote tuwe tunamwabudu Mwenyezi Mungu mmoja aliyetuumba sote kupitia Baba yetu Adam na mama yetu Hawa. Ni Jambo la kuhuzunisha leo hii tunaabudu miungu tofauti wakati hao mitume wote, pamoja na Baba yetu Adam, mwalimu wao alikuwa ni malaika Jibril (Gabriel)?

Haiingi akilini hata kidogo kwa watu wenye akili timamu, kwamba Jibril awe amefundisha habari za miungu tofauti kwa mitume tofauti! Hivyo basi ni wakati muafaka (kwa fikra zangu) tufanye ‘interfaith dialogue’ baina ya dini mbalimbali, hasa zile zinazotokana na kizazi cha Ibrahim, kuitafakari na kuifanya Ibada ya Hijja iwe kielelezo muhimu kwamba sote sisi ni watu wa Mungu mmoja anayepaswa kuabudiwa kwa haki.

Ni jukumu la viongozi wa dini duniani kuondosha upotovu huu usio na maana ili Mungu wa kweli aabudiwe kwa haki. Mambo mazito kama haya yanayomhusu Mungu hayapaswi kufanyiwa mchezo na kufananishwa kama vile siasa za CCM na Chadema au Simba na Yanga, ambazo kauli mbiu zake huwa ni ‘kubisha mpaka ufe’ hata ukiuona ukweli uukatae.

Ni jambo la kushangaza sana, wakati kuna tukio la Hijja ambalo watu wasiopungua milioni 6 kutoka kila kona duniani wanakusanyika pamoja kwa ibada moja kila mwaka na vyombo vya habari vikiwa havizungumzi chochote kuhusu tukio la namna hiyo na kulifanya kama vile ni kongamano au warsha tu ya Waislamu isiyo na muhimu wowote.

Mahala ambapo hata marais, wafalme na mawaziri huwapo kwa ibada hiyo, iweje paonekane kama ni tukio dogo tu? Kwa hapa kwetu hata viongozi wakuu wakienda kule basi jambo hilo huwa haliandikwi wala kutangazwa katika taarifa za habari. Utakuja kusikia tu mtu anaitwa Alhaji lakini kenda lini haikuripotiwa.

Matukio ya kutafuta mrembo wa Umiss, au Bongo Star Search, Kombe la Dunia na Mashindano ya mbio za Olympic ambayo ushiriki wake haufikii idadi ya watu wanaokusanyika kwa Hijja utaona yanajaza kurasa na kurasa za magazeti kila kukicha.

Alhaji Ali Hassan Mwinyi, ni Rais Mstaafu wa Tanzania, a l i k u w a m i o n g o n i m w a mahujaji pale Makka mwaka huu. Tulimshitukia tu pale Minna, lakini hakuna chombo kilichoripoti habari hiyo, ila anapohudhuria kwenye hafla za kutangaza mambo ya Ukimwi na mambo mengine ya namna hiyo, basi hiyo huwa ni habari kubwa sana.

Dk. Shein, Dk. Salmin, Dk. Karume na wengineo wengi tu, leo hii ni maalhaji; walikwenda na kurudi lini hakuna anayejua! Ndio maana wakati mmoja m w a n a s i a s a m m o j a n a mgombea kiti cha urais nchini, kat ika kuonyesha dharau yake alitutangazia kwamba atafuta safari za Hijja kama atachaguliwa kuwa kiongozi wa nchi! Inna Lillah.

Masheikh wetu nao hapa nyumbani pia wanachangia katika kuifanya ibada hii kuwa kama kitu kidogo tu kinachofanyika kule Makka na kwamba mtu aende au asiende ni sawa tu. Kwa kushabikia ushabiki wao wa Kibakwata na Kianswar Sunna, masheikh wakubwa kabisa wamekuwa wakikataa kabisa kufuata tarehe za Saudia huku wakijua Hijja ina miezi na siku maalumu na mahala maalumu.

Miaka nenda miaka rudi wamekuwa wakiwafungisha watu siku tofauti na kisimamo cha Arafat kwa kisingizio cha mwezi

kuwa haujaonekana Tanzania. Lakini cha kushangaza ni kwamba, wakati wakiwafundisha watu upotovu huo, wao wote huwa wameshakuwapo kule M a k k a ( m a s h e k h e w o t e waandamizi huwa Makka kila mwaka kuongoza Ibada ya Hijja) wakifanya Ibada iliyo sawa na sahihi.

“…kila mtu Arafat yake ni pale kwao unapomuandamia mwezi!” Hivyo haiwezekani na hakuna haja Waislamu duniani kuwa na siku moja ya Arafat na siku moja ya kusali Iddi…”

Sisi hapa Tanzania mara nyingi tunasali siku ya pili wakati hakuna tena fadhila za sala hiyo ikiwa umefanya makusudi kutosali jana wakati habari unazo!

Kwa wale Waislamu wenzangu ambao bado hawajapata bahati ya kwenda kuhiji, napenda kuchukua fursa hii kuwasisitizia kwamba ni vizuri wakamwomba Mungu awawezeshe kwenda Makka na Madina kufanya ibada hii muhimu. Mambo watakayokutana nayo huko hayatokuwa ya hasara kwao hata kidogo.

Nenda ukaone ms ik i t i mkubwa kabisa duniani ambao, kwa mwaka huu nimeshuhudia sala ya Ijumaa pale Makka watu wanaokisiwa milioni sita wakisali nyuma ya Imam mmoja. Idadi hiyo ni kama mara mbili ya watu wote wa Dar es Salaam na vitongoji vyake.

Nenda ukaone Hijri Ismail, penye kisima cha Zamzam kilichochimbwa kimiujiza na mtoto mchanga ambapo maji yake hunywewa kwa kunuia. Ukinua yakate kiu basi yatafanya kazi hiyo; ukinuia yawe tiba kwa maradhi yoyote mwilini yatanya kazi hiyo; na ukinuia yawe chakula yatakushibisha bila kula chochote!

Hijri Ismail hutoa lita 29,600 za maji kila baada ya saa moja. Maji yake ni meupe kuliko maelezo na hayajapata kuwa yamekatika na kuwa hayatoki kama vile tunavyoambiwa sijui Ruvu Juu au Ruvu Chini imekauka! Na siku ya kuondoka nyie wageni (milioni sita) chukueni tani yenu hakuna kiwango na mtayaacha yanakutizameni.

Nenda ukasali ‘Makamu Ibrahim’ mahala ambapo nyayo za Nabii Ibrahim zimehifadhiwa — mpaka leo zinaonekana — alipokuwa kasimama hapo kuijenga Kaaba tukufu!

M s o m a j i m a c h o z i yatakulengalenga utakapofika ‘Jabal Hirra’ ambapo ndipo kwenye mlima mkubwa wenye msitu, mahala ambapo ndipo Jibril alipomfuata Muhammad na kumsomesha aya ya mwanzo ya Qurani Iqraa bismirabika…

Nenda ukaone maha la panapoi twa Jabal Rahma ambapo Mtume Muhammad alitoa khutba yake ya kuaga ulimwengu yenye maneno ya mazingatio kwelikweli. Mtume alifariki siku 80 baada ya kutoa hiyo ‘khutbat lwadaa’.

Utauona pia mlima mwingine mrefu unaoitwa Ghar Thour ambapo Nabii Muhammad (ASW) na Sayidna Abubakar walijificha kuwakimbia makafiri wa Makka waliokusudia kuwaua kabla hawajakimbilia Madinna.

Mimi kabla sijaenda Hijja, dhana yangu ya Jabal Thour ni kijabali kidogo tu ambamo Mtume na Abubakar walijibanza. Sivyo. Ni mahala panapotisha kwelikweli ukizingatia Mtume alikuwa katika woga kiasi mkubwa kabla wale buibui hawajatanda pale nje ya jabali hilo ‘kupoteza maboya’.

Msomaji, utajisikiaje pale kiongozi wa msafara atakapofika mahala na kusema:

“…Sasa hapa tulipo ndio iliposhuka Alamtara… hapa ndipo iliposhuka Idhajaa…na huu Msikiti unaitwa Masjid Ljinni ambamo ndani yake walisilimu majini kadhaa baada ya kuisikia Qurani ya ajabu ikisomwa na kuiamini!” Sijui wewe utakuwaje; lakini mimi nilipata fadhaa kubwa sana.

Tu k i w a p a l e k w e n y e Uwanda wa Arrafat tunasubiri kuondoka kwenda Minna kupitia Muzdallifah, Sheikh wetu Twaha Suleiman Banne alitusimulia habari za mahala panapoitwa Wadi L’Mukhassir:

“…chungeni sana mkifika eneo hili kwani ni mahala palipolaaniwa na Allah kwani ndipo Majeshi ya Abraha aliyetajwa katika Surat lfil (alamtara) alipoangamizwa na jeshi lake la Tembo wakati akiwa njiani …kwenda kuibomoa Kaaba tukufu.

“Allah alituma ndege wadogo kutoka mbinguni wakiwa na vijiwe vya moto na kila kijiwe kikiwa kina jina la mtu maalum (precision bombing) pale chini na wote wakaangamia akabaki askari mmoja aliyerudi kutoa habari kwao.

“…alipomaliza kusimulia mkasa uliowapata wenzake ghafla akamwona ndege juu na… kusema; ‘tena ndege mwenyewe ni kama yule,’ hapo ndipo kijiwe kilipoangushwa kwake mbele ya jamaa zake kikammaliza kwani aliachiwa arudi awe shahidi tu,” alisema Sheikh Banne

Pale Jamarat, utapata fursa ya kupiga mawe shetani; tukio ambalo bila shaka yeyote litakujenga na kuboresha imani yako katika Dini. Tukio la Ibrahim kutakiwa kumchinja mwanawe na wao wakawa tayari kutekeleza amri hiyo lina mazingatio makubwa sana.

Isingewezekana kwa watu wenye imani ndogo kama zetu hizi kukubali kumtoa roho mwanawe kwa ndoto ya usiku tu.

Hebu f ik i r i , mwenzetu kaambiwa amchinje mwanawe kakubali; sisi tumeambiwa tuchinje mnyama, hatufanyi hivyo kwa kisingizio cha eti tu masikini tusiona uwezo. Hivi ni kweli hatuwezi kununua mbuzi; kwani mbuzi anauzwa shilingi ngapi mpaka iwe ghali

kwetu? Mpaka lini tutaendelea kumdanganya Mungu kwa kuchinja jogoo siku ya Iddi waka t i amr i n i kuch in ja mnyama?

U k i f i k a M a d i n n a t utashangazwa na Msikiti wa Mtume wenye historia kemkem. Ndani ya msikiti kuna sehemu takatifu inaitwa ‘Raudhwa’ iliyotajwa ndani ya Qurani. Ukisali hapo ni kama umesali peponi.

R a u d h a n d i p o m a h a l a alipokuwa anaishi Mtume na ndipo alipozikwa; na wewe mwenzangu mimi utakwenda kumwombea dua pale alipolala kaburini kwake. Wapi tena utaipata nafasi kama hiyo. Kuyaona makaburi ya Mtume, Sayidna Abubakar na Omar kutakupa fazaa kubwa sana isiyomithilika.

U t a p a o n a p i a m a h a l a ilipokuwa nyumba yake Mtume na pia utaiona membar yake aliyokuwa akipanda kutoa khutba za Ijumaa. Ipo pale mpaka leo ingawa haitumiki tena. Utapita mlango unaoitwa Babu Jibril ukiwa unatoka nje ya Rawdha, mlango ambao Jibril alikuwa akiutumia kuja nyumbani kwa mtume kumletea wahyi. Wewe pia utapita hapo alipokanyaga Jibril na watu wengine watukufu katika dini.

I l i m r a d i , m a m b o y a kushuhudia Madina ni mengi sana yakiwamo ya maajabu ya tende za Madina. Tende za Madina ni za kipekee na ziko za aina nyingi ambazo huku kwetu huwa haziji. Hata huko pia haziuzwi rahisi. Moja ya tende hizo ni ile inayojulikana kama Ajwan! Tende hizi za Ajwan, pamoja ya kuwa ni chakula, lakini pia ni dawa (detoxifer).

Ukiwa Madina utapata pia fursa ya kutembelea vilima vya Uhud ambapo ilipiganwa vita na Waislamu 70 wakapoteza maisha yao katika vita hiyo ya kupigania Uislamu. Makaburi yote 70 yapo pale na la Sayidna Hamza likiwa mbele.

Mambo hayo ukishayaona, shilingi zako milioni 6 ulizotumia utaona kama ni kidogo kwani thamani ya safari ile kwako itakuwa kubwa kuliko hizo pesa.

Mwisho, napenda kutoa shukrani nyingi sana kwa Masheikh wale wa Taasisi ya Tawheed Development Network, wakiongozwa na Amiri wa msafara wetu Alhaj Mussa Kundecha (Mzee wa falsafa ya Makundi), Sheikh Muharram Juma Doga, Sheikh Twaha Suleiman Banne, Sheikh Abdallah Ndauga na Alhaj Macherenga ambao wamefanya kazi nzuri sana ya kutuongoza na kutuelimisha katika kila hatua ya safari yetu ya Hijja na hatimaye kufanya Hijja yetu kuwa Mabrura! Mungu awajaze kheir InshaAllah.

( S i m u : 0715808864/0784808864

[email protected])

Page 11: Annur toleo la Ijumaa

11 AN-NUURSAFAR 1434, IJUMAA JANUARI 4 - 10, 2013Makala

K U M K O M B O A mwanamke kiuchumi, s i l a z i m a k u m f a n y e awe muovu ilimradi tu apate pesa na amuasi m w a n a u m e , a m b a y e anatangazwa kuwa ndiye adui wake mkubwa wa kumyima uhuru kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Lugha ya kumkomboa mwanamke, imesababisha k u a n z i s h w a v y a m a vya kitaifa na kimataifa vinavyojishughulisha na harakati za kumkomboa m w a n a m k e s e h e m u mbalimbali duniani, lakini zaidi katika nchi za Afrika.

K i l a k u k i c h a , wanaharakati wamekuwa wakibuni kampeni za k u w a t o a w a n a w a k e majumbani mwao , za kudai haki za wanawake na kupinga kudhalilishwa.

J i t i h a d a h i z o z a wanaharakati, kwa kiasi f u l a n i z i m e w a f a n y a wanawake walio wengi, ku j i t umbuk iza ka t ika harakati za vyama hivyo wakiamini kuwa ndiyo mkombozi wao, na kuacha mafundisho ya Dini zao juu ya haki za wanawake na ni namna gani wanapaswa kujikwamua kimaisha wao na familia zao. Badala yake, wamekuwa mstari wa mbele kutangaza vita na Allah (s.w).

U h u r u u l i o k u w a ukipiganiwa, umewafanya wengi kutumbukia katika mienendo miovu, zaidi katika zinaa, ili kukidhi haja zao za kimaslahi (wenyewe wanaita ATM au Vidumu).

B a a d h i y a a k i n a dada uhuru walioupata wamejikuta wakiingia katika uchangudoa.

Kwa ujumla ndio kusema kwamba wanawake wengi wamekuwa wakijali zaidi j i n s i y a k u j i k w a m u a kimaisha au kiuchumi, bila kujali kazi wanazofanya kama zinaendana na staha na utu kwa kuzingatia maumbile yao.

Wale walioolewa, waume zao hawana nafasi ya kuhoji, na wale wanao bahatika kuhoj i hawas ik i l izwi , matokeo yake ni kufikia hatma mbaya ya kuvunjika kwa ndoa.

Kazi kwa mwanamke si lazima adhalilikeWala si lazima ahalifu wajibu katika familiaNa Pendo Masasa

Wanaofanya biashara ya miili yao wakiulizwa wanajibu wapo kazini. We n g i n e w a n a t a f u t a wanaamua kushindana mashindano ya urembo, kunadi uzuri wa sura na maumbile yao mbele ya kadamnasi bila kutizama lengo la waandaaji ya mashindano hayo ni nini. Wanachojali wao ni kupata pesa.

Baadhi wapo radhi sura na maumbile yao kuwa kivutio cha matangazo ya biashara katika televisheni na mabango barabarani, tena bila stara ili kuvutia k i m a h a b a i l i m r a d i wanachojali ni pesa.

Wengine wanafanya kazi katika ofisi na makampuni, waajiri wao wanawapa sheria ya kutovaa mavazi ya stara, ilimradi tu kukidhi haja ya mwajiri katika kuvutia wateja kwa matamanio ya zinaa na jimai, ambayo mara nyingi huzaa uhalifu wa ndoa, maradhi na uzembe kazini.

Mambo haya na mengine kama hayo, yamechangia kwa kiasi kikubwa baadhi ya wanawake kukosa stara na haya tangu kazini hadi majumbani kwao. Haya ambayo ni msingi wa imani na ngao ya kumkinga mtu

na maovu.Mtume (s.a.w) amesema,

“kila dini ina maadili yake na maadili ya Uislamu ni haya”.

Sote tunaelewa kwamba kufanya kazi au biashara kwa mwanamke, si jambo baya kwani hata Bi. Khadija, mke wa Mtume (s.a.w) alikuwa mfanyabiashara mkubwa na alitoa mali yake kwa ajili ya kuendeleza Uislamu.

Kinachotakiwa hapa ni kufahamu kazi gani inayofaa kwa mwanamke kufanya bila kuhalifu utu na heshima yake. Na mwanamke mwenye kuujua uanamke wake, huyo atakuwa anajuwa majukumu yake ya msingi ya ulezi wa familia yanayomkabili. Siku hizi majukumu hayo wameachiwa mayaya.

Kutokana na majukumu ya ulezi kuachiwa mayaya badala ya wazazi, ndio maana watoto wengi wa siku hizi wamekosa malezi bora na maadili. Nafasi ya wazazi katika kuwalea watoto imechukuliwa na wasiokuwa na uchungu na familia, kwani haziwahusu chochote zaidi ya kuwa kazini tu.

Wanawake wengi ambao ndio nguzo ya malezi ya familia, hawana muda wa kupata mafundisho ya dini

yao juu ya malezi ya familia zao, na namna ya kujipatia riziki zao.

Bi. Zaituni Chande, mkazi wa Segerea, ni mjasiria mali ambaye anatumia muda wake kutafuta riziki na kulea familia yake. Yeye ni fundi nguo na alianza kazi ya kushona mwaka 1988. Siku za nyuma alikuwa akifanya kazi ya kuuza mkaa, lakini kutokana na ugumu wa kufuatilia na kuipata bidhaa h iyo ambapo a l ikuwa akitumia muda mwingi kukaa nje ya familia, aliamua kubadili kazi hiyo na kuwa fundi nguo. Alifanya hivyo baada ya kujiunga na Chuo cha Ufundi cha Muslim kilichopo Tabata Bima na kuhitimu.

Kipindi fulani mume wake anayeitwa Hamisi Mitumba, alipata mtihani wa maradhi ya TB yaliyomweka ndani bila kufanya kazi ya aina yoyote kwa muda wa miezi nane.

Kwa kuwa mkewe Bi. Zaituni alishakuwa fundi mzuri wa kushona nguo, alifungua ofisi nyumbani kwake. Wateja walifika ofisini kwake na ikawa ni rahisi kuhumia familia n a m u m e w a k e h a d i alivyopona.

Kushona nguo kuliweza kumuongezea kipato na

mwaka 1991 yeye na mumewe waliweza kununua kiwanja Tabata Segerea.

Kipato chake kilisaidia kwa kiwango kikubwa kujenga nyumba na kumudu kulipa karo za watoto. Mbele ya nyumba yao Bi. Zeituni alijenga fremu ya kushonea na kununua vyerehani saba. Hapo anawafundisha pia wanafunzi wengine kushona.

I l i kuweza kutimiza malengo yake na kufanya kazi yake kwa ufanisi zaidi, kujihakikishia soko la uhakika, Bi. Zeitun alijiunga na mafunzo ya ujasiriamali ambayo yanatolewa na Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislam (T).

Mkurugenzi Mtendaji wa TAMPRO SACCOS, Sadiki Suleimani Gogo, ambaye katika taasisi yao kuna chuo cha kuendeleza ujuzi na ufundi stadi, kilichopo jijini Dar es Salaam, alisema kwa kujua umuhimu wa mwanamke kufanya kazi zinazoendana na maumbile yao, wanafunzi wa kike wanaomaliza elimu ya kidato cha nne, wanajiunga na chuo chao kilichoanzishwa m a h u s i k w a a j i l i y a kuwawezesha wanawake kujifunza ujasiriamali na kujiajiri.

Bi. Zaitun amehitimu mafunzo hayo wiki iliyopita na kusema kuwa yamejengea uwezo wa kufanya vizuri zaidi katika biashara yake.

J a m b o l a k w a n z a tunalotakiwa kujifunza wanawake kupitia somo hili, ni mwanamke kujiamini. Bi. Zaituni alijiamini.

Pia mwanamke anastahili kuwa na mapenzi na familia yake. Bi. Zeituni hakutaka k u a c h a w a t o t o w a k e walelewe na yaya. Mapenzi kwa mumewe hususan katika kipindi cha shida.

Kwa kujali utu na maadili, m w a n a m k e a n a w e z a kufanya kazi bila taabu na akaendelea kuheshimika.

Leo Bi. Zeitun kwa juhudi zake, pia kaweza kuwapatia ajira watu saba pamoja na kuwapatia mafunzo ya ushonaji.

Pia amedhihirisha kuwa mwanamke anaweza kufanya kazi bila kuwa na tamaa au kuingia katika vishahwishi vinavyoweza kumdhalilisha yeye na familia yake.

Page 12: Annur toleo la Ijumaa

12 AN-NUURSAFAR 1434, IJUMAA JANUARI 11 - 17, 2013Makala

U P O U s e m i u n a o s e m a “mnyonge myongeni haki yake mpeni.”

Wananchi wa Mtwara na Mikoa ya Kusini kwa ujumla wamekuwa wakilalamikia hatua ya Serikali kusafirisha Gesi Asili, iliyogundulika Mkoani Mtwara kwenda Jijini Dar es Salaam.

Ho ja kuu ya Se r ika l i ni kwamba inafanya hivyo kutokana na kwamba Dar es Salaam, ni kitovu cha uchumi wa Tanzania, na kwamba kuna takriban viwanda 34, vinatumia Gesi Asili.

Pamoja na hoja hiyo ya Serikali, wakazi wa Mtwara wao wanasema wanataka kuona Gesi hiyo Asili, inaleta manufaa kwao kwanza, kutokana na kuachwa nyuma kimaendeleo s ab a b u k u b w a i k i w a n i kutokuwapo kwa vichocheo vya kimaendeleo.

Sasa kupatikana kwa Gesi hiyo, wanaona ni neema kwa Mikoa ya Kusini kuwa na chanzo cha kukuza uchumi wao na Taifa kwa ujumla, ikiwa Gesi hiyo itaanza kufanyiwa kazi Mkoani humo kabla ya kusafirishwa kwingine kama inavyokusudiwa.

K u j e n g w a k w a k i t u o cha kufulia Gesi Asili, hiyo Mkoani Mtwara, badala ya Kinyerezi Jijini Dar es Salaam, ni fursa kubwa ya kushawishi wawekezaji ambao wataweza kujenga viwanda vitakavyotumia malighafi ya Gesi Asili.

Moja ya kauli mbiu ya Rais Jakaya Kikwete na CCM yake ni ‘Maisha bora kwa kila Mtanzania’, kwa nini Serikali isione kuna haja ya kuikomalia Gesi Asili hiyo kuboresha maisha ya wananchi hao kwanza, ambao kwa asilimia kubwa wapo hoi kiuchumi kulinganisha na mikoa mingine nchini.

Serikali inaposema, Dar es Salaam kuna viwanda vingi ndio sababu ya Gesi hiyo isafirishwe, hiyo ni kutokana na kuwa Jiji limewezeshwa. Ilikuwa ni wakati muafaka kwa Serikali kutanua wigo mikoani ili viwanda hivyo sasa vihamie katika mikoa mingine, kuliko kujazana Dar es Salaam, ili mwisho wa siku Mikoa yote Tanzania isheheni viwanda.

Kama sababu ni vyanzo vya kuendesha mitambo, ilikuwa ni wakati wa kushukuru kwamba Mtwara, imepatikana Gesi Asili, kazi kubwa ya Serikali ibaki kusimamia na kuelekeza wawekezaji kuelekea Mikoa ya Kusini, kwenda kufungua viwanda.

K w a n i n i r a s i l i m a l i zihamishwe kutoka mikoani kwenda Dar es Salaam, kama hoja ni mji wa kibiashara vipi mji wa Mtwara na mingine isiwezeshwe nayo ije kuwa ni miji ya kibiashara wakati rasilimali zipo.

Nani asiyejua hali ya Jiji la Dar es Salaam hivi sasa lilivyokuwa kero, kwa msongamano wa watu magari na viwanda, hali ambayo kiukweli inachelewesha ufanisi

Wananchi wa Mikoa ya Kusini wasipuuzweNi wahanga wa dhulma kwa muda mrefu

Na Bakari Mwakangwale

na utendaji wa ujenzi wa Taifa, huku kila kukicha wananchi wakimiminika Jijini kutoka Mikoani hususani mikoa ya Kusini, wakija kusaka ajira.

Kuna faida gani ikiwa wazawa wanakula mabaki ya samaki (Mapanki) wanaovuliwa katika maliasili ya maziwa yao, kisha Wazungu wanaondoka na minofu ya samaki wao!

U k i u l i z a u n a a m b i w a wanalipa kodi, kodi ambayo eti, ndiyo inalipa watumishi wa Serikali, kama madaktari, walimu na watumishai wengine, lakini hao hao hawaishi kugoma wakidai maslahi duni, na kuwaacha wananchi wanatabika.

Ni vigumu kwa wananchi kuendelea kukubaliana na mwenendo huo kuwa Mali Asili ya sehemu husika ni mali ya Taifa, huku wakazi wa eneo hilo wakiwa hoi taabani kiuchumi.

Hii ni hatari, kwani huko mbele huenda hujuma zikawa nyingi badala ya faida, sasa ikawa hasara, ni dhahir i wananchi wa sasa si wale wa enzi ya Baba wa Taifa! Ambao walikuwa hawaruhusiwi kuhoji chochote!

Unapozungumzia nch i masikini Duniani, Tanzania imo, pamoja na kusheheni maliasili kibao na zingine ndio hizo zinaendelea kuibuka! Na unapozungumzia umasikini ndani ya Tanzania , bas i wananchi wa Mikoa ya Kusini ni masikini zaidi, kisha tunasema maliasili ni mali ya Taifa, kwa Watanzania wote, wakati usawa na uwiano haupo.

Huwezi kumlinganisha mwananchi wa Mikoa ya Kaskazini na mwananchi wa Mikoa ya Kusini, inaonekana kabisa kuwa Watanzania wa Kaskazini wananufaika zaidi na rasilimali za mikoa yao kwa sababu rasilimali za mikoa hiyo

imo humo na imesaidia kuiweka juu mikoa hiyo.

Imefika wakati sasa Serikali kuipa kipaumbele Mikoa ambayo ipo nyuma kimaendeleo, kwani sababu za kusogezea maendeleo zinaanza kujitokeza, japo pia hakuna sababu ya msingi ya kuwa nyuma kimaendeleo, sasa huu ujanjaujanja unaotaka kufanywa na Serikali hakuna lugha nyinginye itakayoweza kutumika bali ni ‘dhulma’ dhidi ya wananchi wa Kusini.

Madai ya wananchi wa Mikoa ya Kusini, kutaka Gesi hiyo kuanza kuwanufaisha wao kwanza yana lojiki, na hayapaswi kupuuzwa wala hawapaswi kubezwa.

Madai ya wananchi wa Mtwara , p ia yanaungwa mkono na Umoja wa Mataifa, kwani suala hilo limewekewa muongozo na umoja huo, kuhusiana na kupambana na umasiki.

Katika moja ya mikakati yake (UN) juu ya namna ya kupunguza umasikini duniani kupitia Maliasili (rasilimali), i n a t ak a w an u f a ik a j i w a mwanzo wawe ni wanakijiji (wakazi) ambapo mali hiyo inapopatikana.

Lakini, Serikali ifahamu kwamba siku zote, ‘mjinga akierevuka mjanja huwa matatani’, ndiyo hayo sasa wananchi wa Mtwara, wameanza kuandamana wakipinga Gesi kuondoshwa jumla kwenda Dar es salaam.

Historia inaonyesha kwamba wananchi wa Kusini wamekuwa wahanga wa dhulma ndani ya Taifa lao kabla na baada ya Uhuru, mpaka sasa!

Mwaka 1972, walikuja Wakuweit (Waislamu) nchini, ambao walipita katika barabara ya Dar es Salaam, Lindi, Mtwara hadi Songea. Watu wa Kuweiti wakagundua Mikoa ya Kusini ni

Mikoa tajiri, wakati huo Kusini ikiitwa South Part of Tanzania. Baada ya kugundua utajiri huo walisema, watu wa kusini wana usafiri wa maji tu, wakasema wao watajenga barabara ya lami itakayoanzia Dar es Salaam kupitia Lindi, Mtwara mpaka Songea. Pesa zile zikapokelewa na Serikali ya Rais wa awamu ya kwanza, Julius Kambarage Nyerere. Barabara haikujengwa na yapo madai kuwa fedha zile zilitiwa katika mfuko wa kujenga hospitali moja ya rufaa ya Kanisa Katoliki nchini.

Kama haitoshi, baada ya utawala wa Julius Nyerere, alipoingia Rais Ally Hassan Mwinyi, akajitosa kuomba msaada nchini Kuweit wa kujengewa daraja lililokuwa kero kwenda Mikoa ya Kusini. Pesa hiyo imekuja na kujenga daraja hilo ambalo leo limepewa jina la daraja la Mkapa (Mkapa Bridge) , inadaiwa fungu lilikuwa kubwa, lakini kwa kuwa suala lenyewe ni kuhusu watu wa Kusini, ndio hivyo tena!

Kupitia dhulma hiyo, mpaka leo barabara iendayo Mikoa ya Kusini, ni kitendawili. Miaka 51 ya Uhuru wananchi wa Kusini mvua ikinyesha ni tatizo kuingia ama kutoka.

Lakini, pia kabla ya Uhuru, yupo Mholanzi mmoja alifika maeneo ya Kusini, akafanya utafiti wake akiuita ‘Colonial Pol icy and Educat ion in Equality’. Kisha kupitia utafiti huo, akaandika kitabu chake ‘The Colonial rule and Political development in Tanzania’.

Mholanzi huyo ameandika kwamba, Waislamu wa Kusini walipeleka malalamiko yao dhidi ya Serikali ya Uingereza, wakidai Serikali ya Kiingereza inawapendelea sana Wakristo, kwa mfano Wamakonde

walilalamika kwamba, kwa sababu walipa kodi wakubwa wa Kusini mwa Tanzania ni Waislamu, ni matumaini yao kuwa Serikali ya Kiingereza ingewajali na wao katika kuwapa elimu.

Kinyume chake Serikali hiyo imekuwa ikiwapendelea Wakristo kwa kuwapa kodi hiyo ili Shule zao za Kikristo ziweze kujiendesha, dhulma!

Hivyo unaweza ukapata picha halisi kwa haya yanayoendelea sasa, kwamba kinadharia tunaambiwa kuwa maliasili ni mali ya Taifa kwa Watanzania wote. Lakini ni mika 51 tokea uhuru sasa, Mikoa ya Kusini ambayo ina Waislamu wengi ipo nyuma k imaende leo ukilinganisha na ile mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Iringa na Mbeya, yenye Wakristo wengi.

Unaweza ukajiuliza, kwani Tanzania hii ilipata Uhuru vipande vipande? Kama jibu hapana ni kwa nini basi mikoa mingine iwe mbele kimaendeleo na mingine iwe nyuma? Ikiwa maliasili ya maeneo husika ni mali ya Watanzania wote!

Wananchi wa Mtwara , wamekuwa waki la lamika wak ida i , wameng’o lewa mashine yao ya maji Kitangali Newala, ikiwa ni msaada kutoka nchini Finland, ikapelekwa Dodoma, wamevumilia!

Wanadai wamepindishiwa mipango ya kujengewa kiwanda cha Samaki Mtwara, mpango huo umepelekwa Dar es Salaam, wamevumilia!

Kama haitoshi, ‘Wameng’oa taa za mwanga mkali za uwanja wa ndege wa Mtwara wakapeleka A r u s h a . Wa k a p i n d i s h a mkataba wa kutumika kwa Bandari ya Mtwara kibiashara, wakapeleka Bagamoyo, bado tumewavumilia!

“Na leo gesi, wanataka kuipeleka Dar es Salaam, ili tuendelee kubaki masikini, wakati wenzetu wakipiga hatua kiuchumi, uvumilivu umetushinda, kwa hili tusikubali wazelendo wa Mtwara!”

Hayo ni baadhi ya maoni, au machungu ya wasomaji wetu waliyoyatuma kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu (sms) kutoka Mkoani Mtwara, wakilalamikia jinsi Serikali yao inavyowanyonga kila wanapopata neema, katika Mikoa yao, na sasa Gesi Asili, kutoka Mtwara kwenda Jijini Dar es Salaam.

Ukitafakari, hayo unaweza kupata jibu kwamba hii ni mipango maalum, kwa kuangalia ni mikoa gani ithaminiwe na mikoa gani ipuuzwe.

Kama mada i hayo ya wasomaji ni kweli, wanastahiki kusema wamechoka, ni jukumu la Serikali kutumia busara kulimaliza sakata hili.

Wa n a n c h i w a K u s i n i hawasemi Taifa lisinufaike na Gesi hiyo, lakini wanataka mikoa ya Kusini ipewe kipaumbe, kwani wapo nyuma kwa muda mrefu, kwa nini uchumi huo unaoanzia kwao wanyang’awe, kwa maana uanze kuwanufaisha wengine kabla ya [email protected] 111669

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda (kushoto) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Joseph Simbakalia.

Page 13: Annur toleo la Ijumaa

13 AN-NUURSAFAR 1434, IJUMAA JANUARI 11 - 17, 2013Makala

NENO “Ujamaa” lilivuma sana miaka ya sitini na sabini hapa nyumbani Tanzania; Dunia wakati huo ilikuwa imegawanyika kwenye makundi mawili; kundi la kwanza ni lile linalofuata siasa za Kibepari na la pili ni lile linalofuata siasa za Kijamaa. Ilikuwa ni vita ya vuta nikuvute (Cold War), kila upande unapigia debe upande wake ili upate nchi wanachama wengi. Fidel Castro wa Cuba aliwahi kudiriki kusema kwamba aidha “Ujamaa au Kifo” akiwa na maana kwamba ni heri Wacuba wote wafe kuliko kutokufuata siasa za Ki jamaa; Nyerere a l i d h u b u t u k u s e m a “Watanzania wameamua kufuata siasa ya Ujamaa na kujitegemea”. Sasa sijui kama Watanzania w a l i u l i z w a a u waliwakilishwa kuamua h ivyo! Kusema kwe l i Ujamaa ul ivuma sana hasa hapa nchini kwetu Tanzania.

Moja kati ya silaha ambazo hutumiwa sana na nchi zinazofuata au zilizokuwa zinafuata siasa za Kikomunist (Kijamaa) kama vile Urusi ya zamani, North Korea, Ethiopia, A n g o l a , M o z a m b i q u e , Nicaragua, Cuba, Poland, Romania , Tanzan ia na nyingine nyingi, ni vyombo vya habari ambavyo asilimia mia moja (100%) hudhibitiwa na serikali na vyombo hivyo hutumika kueneza Propaganda za kuwapumbaza watu na kuwaelekeza kule ambapo serikali inapotaka hata kama huko inapowaelekeza hakuna maslahi kwa wananchi hao. Vyombo vya habari vyote vinadhibitiwa na serikali kuu na wote wanaofanya kazi katika vyombo hivi lazima wawe ni watu wanaotoka katika kitengo cha Usalama wa Taifa wa nchi husika au kwa maneno mepesi wawe ni watu wa System. Wajamaa ni wataalamu wazuri sana wa kujenga “Mitandao” hivyo kitengo cha Usalama wa Taifa ndicho hasa kinachosimamia na kuratibu shughuli zote za serikali hasa katika kujenga mitandao mbali mbali ya kuimarisha shughuli za serikali. Wengi mtakumbuka enzi za kitengo cha usalama wa taifa cha Kirusi “KGB” kilivuma ndani na nje ya Urusi. KGB (Komitet Gosudarstvennoy Bezopasnosti) ilikuwa na wigo (network) mkubwa wa

Je, Nyerere ni kikwazo cha Katiba ya umma?Na Dr. Noordin Jella kutisha, kwa wale waliowahi

kuishi Urusi enzi hizo wanakumbuka muziki wa KGB ulikuwa mzito!

Katika nchi za Kijamaa serikali inakuwa haijiamini mbele ya raia wake, wakati wote wana wasi wasi na yale yote inayoyafanya. Hivyo askari wa Usalama wa Taifa wanakuwa wengi kupita kiasi, kila nyumba lazima kuwe na mwakilishi na hata wakati mwingine unakuta kila mtu ndani ya nyumba ni Usalama wa Taifa na kila mmoja anamchunguza mwenzie bila wao wenyewe kujuana! Ukikuta watu wawili wapo chini ya mti, au kijiweni au kwa Shoe shiner, au wauza magazeti utashangaa wote ni Usalama wa Taifa na hawajuani, na kila mmoja anajitahidi kupata habari toka kwa mwenzie! Kila idara iliyopo kwenye nchi ya Kijamaa iwe ya serikali au iwe ya mtu binafsi lazima Usalama wa Taifa wahakikishe kwamba kuna mwakilishi wao, hata kwa Mama Ntilie utakuta aidha Mama Ntilie mwenyewe ni mwakilishi au anayemsaidia k u p a k u a U b w a b w a n i mwakilishi. Wanataka hata unapomchukua mwanamke kwenda kustarehe naye Guest House pia wawe na mwakilishi wao atakayeweza kudaka yale yote mliyokuwa mnaongea wakati wa starehe zenu na hata akiweza awachukue picha za video bila ya nyie wenyewe kujua! Wanafanya hivi makusudi kwa vile hawana imani na mtu yeyote. Ujamaa ni ugandamizaji, w a n a a m i n i s i k u m o j a unaweza kuwa mjeuri kupita kiasi, basi picha hizo za video zaweza kutumika kukutuliza na hata wakati mwingine kukudhalilisha kabisa mbele ya jamii husika.

Kwenye nchi yoyote ile ya Kijamaa asilimia tisini na tano (95%) ya vichaa wanaozurura mitaani na kuokota makopo au wanaokusanya chupa kama vile za “Uhai na Sayona” siyo vichaa wa kweli bali jioni wanapeleka taarifa kwa bwana mkubwa kwamba amesikia nini na ameona nini au amemuona nani akiwa na nani au na nini!? Utashangaa mtu ni kichaa anaokota makopo lakini watoto wake watano wote wanasoma shule za Academy ambazo karo zake kwa mwaka siyo chini ya Dollar za Kimarekani Elfu moja (US $ 1000)! Hawa vichaa usiwadharau, mchana wanakula Msosi wa nguvu uliotoka Sheraton

Hotel na wanapoozea na maji ya Kilimanjaro ya lita moja na nusu. Vichaa wa namna hii ni wengi sana na wakati mwingine huvamia mtu na kumuumiza, na wakati mwingine hata hupasua viyoo vya gari n.k., haya yote huwa hayatokei kwa bahati mbaya bali yamepangwa; watawala wanatoa onyo na vitisho kwamba ukiendelea na tabia yako maisha yako yapo hatarini. Watawala wa nchi za Kijamaa wana vitisho na silaha nyingi za kila aina, kwenye kitengo cha Usalama wa Taifa wa nchi zote za Kikomunist kuna vitengo vingine vingi tu kama vile: Kitengo cha Vibaka na Majambazi ; Kitengo cha “Chemical and Biological weapons”; Kitengo cha Wanawake Malaya “Machangudoa” , hawa wamegawanyika sehemu mbili: kundi la kwanza ni li le la Machangudoa wazima yaani wenye afya, siyo wagonjwa, na kundi la pili ni Machangudoa wale wagonjwa wa maradhi mbali mbali ya kutisha; Kitengo cha mateso, uzalilishaji na mauaji (kitengo hiki hutumia kuwaadhibu wale wote wanaoipinga serikali au wanaotaka kuonyesha udhaifu wa serikali: Waweza kuvamiwa na kundi la watu ambao magari yao yapo tinted na wamevalia miwani inayoziba vyuso zao), na kukuchukua kwa nguvu kukupeleka uwanja wa mateso na vitendo vya kinyama, magari yao pia huwa na namba za uwongo ili iwe vigumu kuwatafuta na ukose ushahidi, mara nyingi tukio la utekaji nyara likitokea lazima ujue kwamba wale watu wote uliokuwa nao wakati unatekwa huwa ni watu wa usalama wa taifa ambao wewe huwajui, na hasa ndiyo

wanafanikisha zoezi zima la utekaji. Watekaji nyara hawawezi kumteka mtu akiwa na watu wasiowafahamu, haiwezekani kabisa, ili zoezi lao lifanikiwe vizuri ni lazima watu wao wawe na yule wanayemuhitaji. Kitengo cha Propaganda, kitengo hiki hujumuisha media kwa ujumla (magazeti, radio, TV, na Internet), zaidi ya asilimia tisini na tano (95%) ya watu wanaofanya kazi kwenye media ni watu wa usalama wa taifa, hawa hutumia kuisafisha serikali au kiongozi wa serikali pale wanapokuwa wamebanwa na Wananchi. Pia kitengo hiki hutumiwa kuwachafua maadui wa serikali mbele ya jamii na pia kwa upande mwingine kuwasafisha wale waliokuwa wamechafuka au kuwajengea umaarufu wale wanaotakiwa wawe viongozi wa jamii hata kama hawana sifa n.k.

Kitengo cha nguvu za giza “Ushirikina” , kitengo hiki kina uchawi wa kila kona ya dunia, na kazi yake ni kuwashughulikia wale wote wanaoonekana maadui wa serikali. Kitengo cha Umbea na Unafiki (hawa hukaa sana sehemu mbali mbali za vijiweni kujifanya wanaikosoa serikali lakini mwisho wa maongezi hugeuza maneno na kuanza kuisifia serikali). Kitengo cha Kupanga ajali za Barabarani, (Ajali ikitokea tu wao ndiyo wa kwanza kufika kwenye eneo la ajali, badala ya kukupa msaada wa kwanza wao ndiyo wa kwanza kukupiga kabari au kukupiga nyundo, au chuma cha kichwani ili ukate roho haraka haraka ili wao wakirudi ofisini waonekane kwa bwana mkubwa kwamba wanafanya kazi vizuri) nakadhalika. Vitengo vyote hivi hutumiwa na watawala kama silaha m b a d a l a “ I n f o r m a l Treatment” kuwadhibiti wale wote wanaoonekana ni Tishio kwa serikali zao zenye mfumo wa Kijamaa. Watawala wengi wa Kijamaa hupendelea kuwadhibiti maadui zao kwa kuanzia na silaha ya “Nguvu za Giza”, ikishindikana, h u t u m i a k i t e n g o c h a M a c h a n g u d o a k a m a wewe ni Kilafi usiyepitwa na Skirt, basi utanasa tu. Ukiwakacha Machangudoa, basi chemical na biological weapons zinasambazwa kila wanapojua kuwa waweza kula au kunywa. Ukijifungia nyumbani kwako, bas i Mkurugenzi wa kitengo cha Vibaka na Majambazi

anaachiwa jukumu la kutuma vijana wakushughulikie.

Wafanyikazi wote kwenye Hotel, Migahawa na sehemu mbali mbali za kuuza vyakula lazima wawe watu wa System ili wakitaka kukudhibiti chakula chako kibatizwe au mashuka utakayolalia huko hotelini yapakwe poda ili ulale fofofo uachane na taabu za dunia hii. Kwa wale jamaa zangu wanaosoma chuoni wakij ifanya wanakosoa sana serikali na kushabikia mageuzi, basi jiandae kudisco na kama wakikuhurumia sana waweza maliza chuo ukapata digrii lakini kazi hupati ng’o. Utatembea kila ofisi mpaka miguu itaingia tumboni, kwa vile kila ofisi utakayoenda wanafiki unaanza kukutana nao getini hadi kwa meneja mkuu wote wanatoka ofisi kuu. Pia uombe mungu usije ukaugua na kwenda hospitalini kwani asilimia tisini na tano (95%) ya Madaktari na Wauguzi mbali mbali ni Watiifu na wanachama namba moja wa System. Hivyo ukafika huko waweza usirudi salama, waweza ongezewa ugonjwa mwingine au waweza rudi kilema au waweza usirudi bali urudishwe ukapumzike kwenye nyumba yako ya m i l e l e . Wa t a w a l a w a mfumo wa Kijamaa huwa wanalindana sana na ni wataalamu wazuri sana wa kutengeneza “Mitandao ya Uhalifu” au kwa jina la kigeni “Mob of Organized Crimes (Mafia)”. ukimkorifisha Fidel Castro wa Cuba ukakimbilia Nor th Korea u s idhan i umepona, Kim Ul Sung atakushughulikia kikamilifu; Ukimuudhi Agustino Neto wa Angola ukakimbilia Ethiopia bado hupo salama kwa vile Mengitsu Haille Mariam atakuangamiza. Watawala wote wa nchi za Kijamaa ndivyo walivyo, wanajua fika kwamba hawawatendei raia wao ipasavyo lakini pia hawataki wakosolewe na wala hawataki wajadiliwe, na kama ikabidi kufanya hivyo, basi ifanyike ndani ya vikao vya wao kwa wao ili kila kitu kibakie na kiiendelee kuwa siri, siri kwa wale wanaowagandamiza. Ndiyo maana katika tawala za Kijamaa ukishaingia kwenye System hata ufanye Ufisadi wa kupindukia, huwezi kujiuzulu wala kufukuzwa kazi, ukiwa na bahati mbaya sana utatolewa Uwaziri lakini utapelekwa kuwa Balozi

Inaendelea Uk. 14

MWALIMU Nyerere

Page 14: Annur toleo la Ijumaa

14 AN-NUURSAFAR 1434, IJUMAA JANUARI 4 - 10, 2013Makala

IJUMAA ya Desemba 28 mwaka 2012, binti wa miaka 23, ambaye ni mwanafunzi wa udaktari alifanyiwa ukatili wa kutisha, baada ya kubakwa na genge la wanaume sita kwenye basi mjini New Delhi, India. Siku chache baadaye binti yule alipoteza maisha kutokana na majeraha aliyopata.

Sua l a l a b in t i huyu likasababisha maandamano makubwa nchini India dhidi ya Polisi na Serikali ya nchi hiyo, kama tulivyoshuhudia kupitia vyombo vya habari. Wananchi wa India walikuwa wakipaza sauti zao dhidi ya uzembe wa serikali , katika kuwalinda wanawake kutokana na ukati l i wa ngono.

Ubakaji ni tatizo sugu nchini India na kiukweli ndiyo uhalifu unaokuwa kwa kasi zaidi nchini humo. India inatajwa kuwa ni demokrasia kubwa zaidi duniani . Mashambul iz i mengi ya ubakaji nchini India hayaripotiwi kwa sababu wanawake wengi nchini humo wamepoteza imani na mifumo iliyowekwa kulinda heshima yao.

Hali hii imechangia zaidi ukubwa wa tatizo, hasa ukizingatia utamaduni wa kutojali unaofanywa na Polisi kwa watendaji wa makosa hayo, ik iwemo adhabu

Ubakaji nchini IndiaSaid Rajab

ndogo wanazopewa baada ya kesi kuchukua muda mrefu mahakamani. Kwa mujibu wa Al -Jazeera, mwanamke mmoja anabakwa nchini India kila dakika ishirini zinazopita, na zaidi ya matukio 24,000 ya ubakaji yameripotiwa mwaka jana peke yake.

Al - Jazeera pia imeripoti kwamba zaidi ya asilimia themanini ya wanawake mjini Delhi wamefanyiwa unyanyasaji wa kingono, waka t i gaze t i l a ‘The Times of India’ limeripoti kwamba ubakaji nchini India umeongezeka kwa asilimia 792 katika kipindi cha miaka 40 iliyopita.

Wa k a t i m a t a i f a y a Maghar ib i yakiendelea kuuza ‘Demokrasia’ kwenye nchi za Waislamu, kama mfumo bora kabisa unaolinda hadhi, heshima na haki za wanawake, nchi iliyokomaa kidemokrasia duniani kama India, imeshindwa kabisa kulinda wanawake wake.

Kiwango kikubwa cha uhalifu wa ngono dhidi ya wanawake nchini humo, tabia ya Polisi kuwalinda wabakaji, na hali ya kutojali ya Serikali katika kuwalinda wanawake, ni matokeo ya utaratibu uliopangwa wa k u w a s h u s h a t h a m a n i

wanawake, kupitia utamaduni wa kiliberali uliokumbatiwa na dola na kupigiwa chapuo na Bollywood (Tasnia ya Filamu India).

U t a m a d u n i h u u w a Bol lywood, pamoja na burudani nyingine, ikiwemo matangazo ya biashara na fi lamu za ngono, kama ilivyoidhinishwa na Serikali ya Kidemokrasia ya India, ambayo inafuata misingi ya Kisekula na Kiliberali, imemfanya mwanamke aonekane kama kifaa cha kutul iza matamanio ya wanaume.

Mfumo huo umeunda jamii ya ‘kingono-ngono’ nchini India, ambapo watu wamekuwa wabinafsi mno na wakati wote wanafikiria jinsi ya kutuliza matamanio ya kimwili, kwa sababu mfumo umehamasisha sana mahusiano ya nje ya ndoa, ikiwa ni pamoja na kupalilia utamaduni wa kimalaya, hivyo kudunisha kabisa mahusiano ya staha kati ya mwanamke na mwanaume.

Hali hii imeondoa kabisa hofu katika fikra za wanaume wengi nchini India, ambayo ilipaswa kuwepo kabla ya kufanya kitendo chochote cha kuvunja heshima ya mwanamke. Kwa hiyo si

ajabu India sasa inakaribiana sana na mataifa mengine ya Kiliberali kama Marekani na Uingereza, ambayo ndiyo yanayoongoza duniani kwa ukatili dhidi ya wanawake.

Mfumo wa Kisekula na Demokrasia ya Kiliberali, ambao nusu ya raia huishi kwa hofu na mashaka ndani ya nchi yao, kusema ukweli si mfano wa kuigwa na mataifa ya Waislamu. Ni Uislamu pekee ndiyo wenye sheria na taratibu bora zaidi za kulinda hadhi na heshima ya mwanamke.

Kwanza Uislamu unakataa uhuru usio na mipaka na pia unahamasisha zaidi taqwa (hofu ya Mwenyezi Mungu) ndani ya jamii, hatua ambayo inapalilia moyo wa uwajibikaji katika namna ya kuwaangalia na kuwatendea wanawake.

U i s l a m u u n a k a t a z a kuifanya jamii i f ik i r ie ngono wakati wote, ikiwa ni pamoja na kutumia miili ya wanawake kama vifaa au vivutio vya biashara, hatua ambayo hufanya mahusiano ya kijinsia kati ya wanawake na wanaume yawe na hadhi inayostahili.

Dini ya Kiislamu ina mfumo madhubuti wa kijamii

ambao unaratibu vyema mahusiano kati ya wanaume na wanawake, kwa mfano uvaaji wa mavazi ya staha, kutenganisha wanawake na wanaume na kupiga marufuku mahusiano ya nje ya ndoa. Hayo yote yanaelekeza kwamba matamanio ya kimwili yanatakiwa kutulizwa ndani ya mahusiano ya ndoa peke yake, hatua ambayo huwalinda wanawake na jamii kwa ujumla.

Dini ya Kiislamu pia ina mfumo madhubuti wenye ufanisi mkubwa katika utoaji na usimamizi wa haki. Uislamu una taratibu nzuri sana za kupambana na uhalifu wa kijinga kama ubakaji kwa kutoa adhabu nzito kweli kweli, kama vile kucharazwa bakora kwa kuwadhalilisha wanawake, au hata adhabu ya kifo kwa kuvunja heshima ya mwanamke.

Kuvunja heshima ya mwanamke hata moja kupitia kuangalia, maneno machafu au kitendo cha udhalilishaji, i nachukul iwa kuwa n i uhalifu mkubwa katika mazingira ya Kiislamu ambao hauwezi kuvumilika. Hali hii inawajengea wanawake jamii salama kwa kujisomea, kufanyakazi, kusafiri na kuishi. Uislamu una misingi, sera, kanuni na sheria bora kabisa za kuwalinda wanawake, tofauti na inavyopotoshwa na maadui.

Je, Nyerere ni kikwazo cha Katiba ya umma?Inatoka Uk. 13

huko nchi za nje, au utapewa Ukuu wa Mkoa au ukurugenzi wa shirika lolote la Umma. Huwezi kuachwa hivi hivi uzurure mitaani kwa vile ukichanganyika na wavuja jasho unaweza kuropoka siri za wazee na matokeo yake ukawaweka katika hali mbaya.

Nchi zinazofuata mfumo wa Kijamaa zinaonekana ni nchi safi kwa wale walioko nje ya mfumo wa utawala yaani wananchi wa kawaida ambao hasa ndiyo wanaotumikishwa kama punda na wachache walioko madarakani, lakini ukiingia ndani ya mfumo w a u t a w a l a w e n y e w e utakuta kuna uozo na vituko visivyosimulika. lakini kwa vile hao hao watawala ndiyo wanaodhibiti vyombo vya habari, ni vigumu kwa raia wa kawaida kuuona uozo huo, na kama ikatokea bahati mbaya mvuja jasho akauona uozo huo, basi ili asiwaeleze wengine atavutwa shati na kupewa kitengo kulingana na

shule yake, na kama ikatokea bahat i mbaya akakataa kujiunga na mtandao wa kula, basi maisha yake yapo hatarini; ingawa watu jasiri kama hao wapo wachache sana dunia ya leo. Na hii ndiyo sababu kubwa ambayo imeifanya dunia kushindwa kabisa kuuangamiza ufisadi, kwa vile ukigundua ufisadi na wewe unaingizwa kwenye ufisadi kwa kukatiwa kile kilichofisadiwa au uingizwe kwenye kitengo ambacho mafisadi wanaamini siku za usoni hata kama si leo au kesho lakini siku moja na wewe utafanikiwa kuwa fisadi waliolala usingizi kama ulivyokuwa wewe.

Kwenye nchi za Kijamaa wananchi wa kawaida siku zote hawapo huru kwa lolote lile kwani hata hupangiwa waishi vipi; wawe marafiki wa nani; wawe maadui wa nani; wavae nini; wale nini; waende wapi na wapi wasiende. Hata uhuru wa

kufikiri na kutoa maoni yako kulingana na uelewa wako huna, bali hupangiwa ufikiri vipi na useme nini; na huu unakuwa ni mkakati wa serikali kuu kuhakikisha wanaeneza Propaganda nchi nzima ili wananchi wafikiri kama watawala wanavyotaka na hata kama mwelekeo huo hauna maslahi kwa raia hao potelea mbali. Jambo muhimu ni kwamba watawala w a l i o k o m a d a r a k a n i watawale kiurahisi bila bughudha zozote, na vyombo vinavyotumika kuwalainisha raia ni vyombo vya habari na kitengo cha usalama wa taifa cha nchi husika. Kwenye nchi za Kijamaa Kiongozi yeyote akifanya Ufisadi ukajulikana kwa watawaliwa, basi badala ya kufikishwa mbele ya haki (Mahakama) ili ajibu shutuma zake, wao huunda tume ya kumchunguza lakini kiukweli tume hii si ya kumchunguza bali wanatafuta njia mbadala ya kumsafisha kwa vile

t u m e i n a y o c h a g u l i w a kumchunguza ni watu wale wale wa system ambao kabla ya tume hiyo kuanza kazi wanaitwa na kuelekezwa walete uchunguzi gani au walete ripoti ya namna gani, ili mwenzao asije akaadhirika. Hivyo tume hizi hutumia pesa nyingi sana za wananchi walipa kodi kukaa vikao ambavyo tayari matokeo ya tume hiyo yanajulikana (Danganya toto).

Kwenye nchi za Kijamaa ukiwa mfanyibiashara lazima uwe mwanachama wa chama cha Kikomunist na uwe unakichangia chama, kinyume na hivyo biashara zako zitafungwa na utafilisiwa. Kwenye nchi za Kijamaa kama ni msomi lazima uwe mwanachama wa chama cha Kikomunist kinyume na hivyo huwezi kupata kazi hata kama utaalam wako unahitajika kwa jamii. Kwenye nchi za Kijamaa Mahakama zote zipo chini ya kitengo cha Usalama wa Taifa. Wao

ndiyo wanaopanga hukumu, wao nd iyo waendesha mashitaka chini kwa chini, wao ndiyo mashahidi na wakati mwingine wao ndiyo walalamikaj i ! Ikatokea kwamba Jaji au Hakimu akataka afuate sheria badala ya kuwasikiliza usalama taifa, basi ajue kwamba maisha yake yapo hatarini kwani aweza kuuwawa au kubambikwa kesi ya kupokea rushwa, na atatafutwa hakimu mwingine mtiifu wa mtandao amfunge miaka mingi jela. Itaendelea.

(Makala hii imeandikwa na Dr. Noordin Jella (Ph.D . i n E c o n o m i c s ) Former Lecturer of Mzumbe, Open & KIU – D a r, U n i v e r s i t i e s . Currently: Freelance Journalist & Seasonal Political Analyst Email: [email protected] Mobile: +255 782 000 131)

Page 15: Annur toleo la Ijumaa

15 AN-NUURSAFAR 1434, IJUMAA JANUARI 4 - 10, 2013Makala/Habari

NATANGULIZA kusema kuwa katika kuandika maoni haya, sikusudii k u i n g i l i a u h u r u w a Mahakama. La hasha. Ila nalazimika kusema kwa sababu nahisi kuna watu wananyimwa haki zao za kibinadamu na kisheria kwa mujibu wa Katiba ya Nchi, pia kinyume na haki/ Sheria za Kimataifa, kwa kizingizio cha ‘Sheria’. Na hii si haki.

Ikiwa ni takribani miezi mitatu sasa tangu viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiisalmu Zanzibar watiwe ndani, hali na mwenendo wa tukio zima la ukamatwaji wenyewe na mashitaka yanayowakabili wahusika hao inazidi kuzua utata mkubwa.

K w a k u j i k u m b u s h a tu, viongozi wa jumuiya y a U a m s h o Z a n z i b a r walikamatwa mwishoni mwa mwezi Oktaoba, mwaka jana. Kesi yao ilianzia kwa kufanyiwa na mahojiano na po l i s i na ha t imae , walikamatwa na kufikishwa mahakamani rasmi mnamo tarehe 22/10/2012, kujibu mashitaka ya kuhatarisha usalama wa nchi.

Tukio la kukamatwa kwa viongozi hao nane wa Uamsho, lilikuja mara baada ya kuzuka ghasia zilizotokana na kupotea katika mazingira ya kutatanisha kwa kiongozi wa jumuiya hio Ustadh Farid Hadi Ahmed katikati ya mwezi Oktoba mwaka jana.

Tukio la kupotea kwa s h e i k h F a r i d , a m b a l o lilibainika kuwa ni jaribio la kutekwa nyara na watu ‘wasiojulikana’, lilizua fujo na ghasia ambazo bila shaka zilipelekea watekaji hao, kumuachia huru kiongozi huyo wa Uamsho, ama kwa shinikizo hilo la umma au kwa kutimia lengo lilokusudiwa.

Mwenye macho haambiwi tazama. Ukichunguza kwa undani mwenendo mzima wa vi tuko na v i tewej i vi l ivyofanyika kuanzia kutekwa kwa Sheikh Farid, na kubambikizwa viporo vya kesi, vilivyosokolowa miezi ya nyuma, tena siku moja tu baada ya kunusurika ku toweka na wa teka j i ‘wasiojulikana’, ndio hasa suali lenye kutia mashaka.

Na kwa mazingira ya u ta tan i sh i kama haya , tunanusa kuwepo kwa usanii mkubwa wa dola katika uendeshaji wa kesi na tuhuma zinazowakabili viongozi wa jumuiya ya Uamsho hapa Zanzibar.

Tukianzia na hili la msingi, la kutekwa kwa Sheikh Farid. Kitendo hichi cha kumteka Sheikh Farid linajidhihirisha kuwa ni sehemu ya mpango

Uamsho na usanii wa DolaFitna ni mbaya kuliko kuuwa

maalumu uliotegemewa kuzaa matunda ambayo mengine ni haya tunayoyaona sasa. Kwa vile hakuna mwenye ushahidi kati yetu kama watekaji walilenga kumuuwa au kumpoteza ustadh Farid, bila shaka dhamira na lengo jengine farike ya hili litakuwa na ukweli fulani.

K w a m i n t a r a f u h i i , tutabaki kuiamini hoja kuwa watekaji hao ‘wasiojulikana’ walimteka kiongozi huyo mashuhuri, ili watu wafanye fujo, na wao wapate kibali cha kuwakamata viongozi hao wa Uamsho. Kama ni hili, basi lilifanikiwa. Na bila shaka hakuna asiyejua kama huo ulikuwa ni usanii, uliokosa ufundi na umalenga wa hali ya juu. Umekosa ufundi kwani hakuna aliekuwa hajui kuwa utekaji ule ulikuwa na mkono mrefu ndani yake. Hili halijifichi, liko kweupe, kuzimu hakuna nyota.

Kama hi lo hal i toshi , u k i a n g a l i a m a s h i t a k a w a l i y o s h i t a k i w a Viongozi hao na tarehe waliyoyafanya makosa hayo wanayotuhumiwa, utaona wazi kuwa kuna sanaa ndani ya utunzi wa kesi hii. Kwani washitakiwa wamesomewa shitaka la kufanya uchochezi unaohatarisha usalama wa nchi, mnamo tarehe 7 Agosti, 2010, huko Magogoni , Zanzibar.

Sasa uk i tazama kwa undani, kutoka siku hiyo waliyofanya kosa mpaka siku waliyokamatwa yaani tarehe 20/10/2012, Serikali i l ikuwa wapi? Naul iza ilikuwa wapi kwa sababu nina uhakika viongozi wote wa Uamsho walikuwepo na wala hawakuwa na habari yoyote kwamba walitenda kosa.

Na kwa vile hawakuwa na was i was i , hakuna aliyekimbia, kwani hapakuwa na haja ya kufanya hivyo. Na lait i wangekuwa na hofu ya kutenda makosa, wangeshakimbia, kwani miezi miwili ingetosha kwao kutoweka nchini.

C h a k u s h a n g a z a n i kuwa kosa la viongozi hao liliibuliwa mara tu baada ya mpango wa ‘kumficha’ Ustaadh Farid kwenye tumbo la chewa wa Nabii Yunus, kushindwa. Na ingekuwa hakukuwa na zogo lile, watu wakanyamaza, basi Uamsho wasingekuwa hapo walipo leo. Huu ni usanii wa mbala mwezi wa dola dhidi ya

viongozi wa Uamsho.Kioja chengine kinakuja

mara baada ya watu wale kupandishwa mahakamani. Hapa kuna masuala mawili ya ajabu mno, tena ya kushangaza nyoyoni. La kwanza, ni pale kesi hii ilipopangiwa Jaji aliyekuwa hana mamlaka ya kutoa maamuzi. Na kwa maana hiyo pale mahakamani washitakiwa hao walikuwa wakipelekwa ili ionekane tu kama tayari wamefikishwa katika vyombo vya sheria.

Nyuma ya pazia, lengo ni kuwasogezea muda wa kuwaweka rumande, i l i wapate kuwadhihaki na kuwadhalilisha huku kesi yao ikiendeshwa mbio za kobe, mpaka wakome kwa adabu. Hii si haki na imetendeka dhidi ya watuhumiwa.

La pili, ni vile kuihamishia kesi hii mahakama ya Vuga bila kuwapa taarifa mawakili wa washitakiwa, kuhusu maamuzi hayo. Hiki ni kioja kikubwa kilichofanyika bila kuona haya wala kinaya. Sasa kama huu si usanii tuite kitu gani?

Kama hayo hayatoshi, kesi hii inafisidiwa kwa nguvu ya kisheria na Idara ya Mkurugenzi wa Mashtaka. Katika hali isiyotegemewa, idara hii imezuia viongozi hao kupatiwa dhamana, tena hata baada ya mahakama kuweka mashariti magumu ya dhamana , Ida ra ya Mkurugenzi wa Mashitaka i m e s h i k i l i a k u t o w a p a dhamana washitakiwa hao kinyume na haki, kwani vigezo wanavyotoa havina mashiko kimantiki.

Uzoefu wa kesi hii na Idara ya Mkurugenzi wa Mashitaka, inapotakiwa kuchukuwa hatua na maamuzi ya haraka juu ya hali walizonazo watuhumiwa, huchukuwa muda mrefu, ili kuchelewesha juhudi za kuwapunguzi shida na mateso watuhumiwa. Hii pia nayo ni hujuma ambayo hufanywa kisanii zaidi chini ya mwavuli wa sheria na dhamana ya idara husika.

Kwa mtiririko huu, utaona kuwa kuna mtandao mpana wa dola unaopika na kusuka vituko, visa, na mikasa

ya ‘kisanii’ kwa kutumia nguvu za kile wanachokiita ‘sheria’, ili watimize malengo wanayoyajua wenyewe dhidi ya viongozi wa Uamsho.

Uk ianga l i a m tandao huu, utaona kuwa kuna mashirikiano na mawasiliano ya karibu kati ya Mahakama, Idara ya Mkurugenzi wa Mashitaka na vyombo ya ulinzi na usalama. Na mfungamano mkubwa wa vyombo hivi, pamoja na viroja na ‘usanii’ wanaoutenda dhidi ya kesi hii, uwezekano wa kutendeka haki katika hali kama hii unapotea kimaumbile.

Na kwa v i le hakuna shinikizo lolote lile kutoka kwa wananchi, Serikali na hata taasisi za kisheria na Jumuiya za Kimataifa zinazosimamia haki za binadamu, hali hii itazidi kuwa ngumu. Tumeona hivi majuzi tu, viongozi wengine wawili wa Uamsho wameshikiliwa na sasa wako pamoja na wenzao kule rumande.

Hii inaifanya idadi ya washitakiwa wa Jumuiya hii ya Uamsho kutimia kumi. Na kwa hali ilivyo, tutegemee makubwa za id i , kwani ‘usanii’ huu ni fitina, Na fitina ni mbaya kuliko kuuwa.

Allah a’lam!Mwananchi Mpenda

Haki na Uadilifu

Mtwara, Lindi watendewe haki katika gesiInatoka Uk. 12

kitajengwa kituo cha kufuata umeme Mtwara, lakini kwa mikakati iliyopo inaonekana kuwa mpango huo unayeyuka.

Lakini pia alisema, kupitia ges i h iyo kuna kampuni imehitaji kujenga kiwanda cha kutengeneza mbolea huko huko inapoanzia gesi, jambo ambalo lingesaidia wananchi wa Kusini kupata ajira na kufungua milango kwa wawekezaji katika Mikoa hiyo nayo iwe yenye hadhi kama ile ya Arusha, Moshi au Iringa.

“Sasa Serikali badala ya kujibu hoja za msingi, wanabaki kuwabeza na kuwalaumu, eti wanataka kuigawa nchi, hawahitaji kufanya hivyo bali wanahitaji nao wawe raia wa daraja la kwanza na mikoa yao nayo iwe na hadhi kama ilivyo mikoa mingine inayonufaika kwa rasilimali zilizopo katika mikoa hiyo”. Alisema Prof. Lipumba.

Alisema, ameona atumie fursa hiyo kueleza kwamba wananchi wa Mtwara hawana nia mbaya ya kuzuia gesi bali wanahitaji usawa, haki na kutendewa uadilifu kama Sheikh (Khatibu) alivyonasihi.

Prof. Lipumba alisema kwa

sababu za kiuchumi zimeonyesha kwamba ikiwa gesi hiyo itaanza kutumika sehemu husika kisha kiwanda kujengwa pale itakuwa na manufaa zaidi, kisha ndipo isambazwe sehemu nyingine.

Alisema, taarifa zinaeleza k w a m b a k i w a n d a h i c h o kingeweza kupata faida zaidi ikiwa kitajegwa kiwanda cha kutengeneza mbolea Mtwara, ili waweze kutumia gesi hiyo kama malighafi.

Alisema, kiwanda hicho kingekuwa ni kikubwa Afrika Mashariki , na kingeweza kuuza mbolea ndani na nchi za nje, lakini sasa ile kampuni imeambiwa kwamba ile gesi linaunganishwa bomba iweze kuja Dar es Salaam.

Aidha, Profesa Lipumba, alisema Jambo muhimu katika maisha ya mwanaadamu ni kumuogopa Mwenyezi Mungu, katika shughuli zote za kila siku huku akijua kwamba hapa duniani ni pa kupita tu, na kwamba ipo siku ataulizwa na muumba wake.

“Tumefahamishwa kama Waislamu kwamba jambo kubwa ni kumuogopa Mwenyezi Mungu katika shughuli zetu zote tukizingatia kwamba sisi hapa duniani ni wa kupita tu na tujiandae siku moja kutoa majibu

kwa yale ambayo tumeyatenda na kuyasimamia hapa duniani.” Aliasa Prof. Lipumba.

Akizungumzia ha l i ya Waislamu nchini, aliwataka kuungana na kuwa kitu kimoja ili waweze kuwa na sauti moja kwamba wakisimama na kusema ijulikane Waislamu wamesema.

Alisema, historia ya Waislamu inaonyesha kwamba wazee wa Kiislamu huko nyuma walikuwa kitu kimoja na sauti moja jambo ambalo lilisaidi kwa umoja wao kumng’oa mkoloni, wakiwa na matumaini na malengo mengi.

“Sasa tuna miaka 51, wazee wa Kiislamu walijitolea kupigania Uhuru ili na wao waweze kuwa raia wa daraja la kwanza katika nchi yao.”

“Sasa la kujiuliza ndani ya miaka hiyo 51 nini haswa hatima ya wajukuu na watoto wa wazee waliopigania uhuru?” Al isema Prof . Lipumba na kuhoji.

Hivi karibuni wananchi wa Mkoani Mtwara, waliandamana wakidai kutaka pawepo na mikakati ya kunufaika na gesi iliyogundulika mkoani humo, badala ya uwamuzi wa Serikali wa kutaka kuisafirisha kwenda Jijini Dar es Salaam.

Page 16: Annur toleo la Ijumaa

16 AN-NUURSAFAR 1434, IJUMAA JANUARI 4 - 10, 2013

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.

AN-NUUR16 SAFAR 1434, IJUMAA JANUARI 11 - 17, 2013

Usikose nakala yako ya AN-NUUR kila

Ijumaa

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, amesema serikali inaweka mkazo katika kuziendeleza sekta kuu za kiuchumi zikiwemo Utalii, Kilimo na Uvuvi, ikiwa ni jitihada za kukuza uchumi wa Taifa.

Amesema kuwa sekta hizo zina mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa taifa na kwamba, zitaendelea kupewa kipaumbele ili kuhakikisha kuwa uchumi wa Zanzibar unakua hadi kufikia asilimia tisa kwa mwaka.

Akizungumza na ujumbe wa wanafunzi wa Chuo Cha Ulinzi Cha Taifa kilichoko Dar es Salaam, waliofika ofisini kwake Migombani na kuonana naye, Maalim Seif amesema licha ya matatizo ya kiuchumi ya mara kwa mara yanayoikabili dunia, hali ya uchumi wa Zanzibar inaendelea vizuri ukiwa ni kati ya asilimia sita hadi saba kwa mwaka.

Amesema athari za kiuchumi zinazotokea duniani zimekuwa z i k i s a m b a a k a t i k a n c h i mbalimbali ikiwemo Zanzibar, lakini athari hizo zimekuwa zikidhibitiwa na serikali kwa kuweka mipango imara ya kudhibiti uchumi wake.

Ameitaja mipango hiyo kuwa ni pamoja kudhibiti mfumko wa thamani ya dola dhidi ya shilingi ya Tanzania na kuimarisha sekta za kiuchumi zinazokwenda na wakati kulingana na mabadiliko ya kiuchumi duniani.

Ameielezea sekta ya utalii kama kiongozi kwa uchumi wa Zanzibar baada ya kuporomoka kwa zao la karafuu.

Hata hivyo alisema jitihada zaidi zinafanywa kuiendeleza dhana ya utalii kwa wote, ili kila mwananchi aweze kunufaika moja kwa moja na sekta hiyo.

Maalim Seif amefahamisha kuwa katika kutimiza malengo yake ya kukuza uchumi, serikali inaendelea kuwahamasisha wawekezaji wa sekta ya utalii kuja kuwekeza, hasa katika ujenzi wa hoteli za hadhi ya nyota tano.

Aidha amesema serikali inakusudia kuimarisha ulinzi katika maeneo ya utalii, ili kuhakikisha kuwa watalii wanaokuja wanaishi kwa furaha na amani na kutangaza utalii wa Zanzibar duniani.

“Sekta ya utalii “is very sensitive”, watalii wanaposikia v u r u g u k i d o g o t u , h a o wanakwenda zao.

Zanzibar kuendeleza sekta kuu za uchumiNa Mwandishi Wetu Awali baadhi ya mapapasi

walikuwa wakiwanyanyasa na wengine kutishia usalama wa watalii, lakini sasa serikali inajipanga kuhakikisha kuwa watalii wanaishi kwa usalama na kufurahia ziara zao nchini mwetu”, alifafanua Maalim Seif.

Alisema iwapo mikakati hiyo itafaulu, serikali inalenga kupokea watalii wapatao laki tano ifikapo mwaka 2015, ambao itakuwa ni ongezeko la asilimia mia moja ya watalii wanaoingia Zanzibar kwa sasa.

Akizungumzia kuhusu k i l i m o , M a k a m u w a Kwanza wa Rais amesema serikali inaendelea vyema na mpango wake wa kilimo cha umwagiliaji.

Al isema washir ika wa maendeleo wanatoa ushirikiano wao ikiwemo Korea ya Kusini, ambayo imekubali kusaidia uimarishaji wa miuondombinu ya umwagiliaji.

Amesema wakulima wengi wa Zanzibar wameshakuwa tayari kuendeleza kilimo, baada ya serikali kuamua kupunguza gharama za kilimo ikiwa ni pamoja na gharama za kulimia pamoja pembejeo.

Kuhusu Uvuvi, imeelezwa kuwa sekta hiyo pia inapaswa kuende l ezwa kwa kuwa inawagusa wananchi wengi wa visiwa vya Unguja na Pemba, na kuwa miongoni mwa sekta zinazoweza kuwakomboa wananchi kiuchumi.

Amesema kwa sasa wavuvi wanapaswa kujiandaa kwa uvuvi wa bahari kuu, ambao mafanikio y a k e y a t a w a h a m a s i s h a wawekezaji wa mazao ya baharini kuja kuwekeza katika sekta hiyo na kuongeza pato la Taifa.

Naye kiongozi wa ujumbe wa wanafunzi hao wanaojifunza masuala ya kiuchumi, Brigedia General R. S. Laswai, ameelezea matumaini yake ya kuendeleza kozi hiyo kwa mafanikio kufutia maelekezo na mashirikiano wanayoyapata kutoka kwa viongozi wa serikali.

H i y o n i k o z i y a p i l i kuendeshwa na chuo hicho tangu kuanzishwa rasmi mwezi Septemba mwaka jana, ambapo kozi ya mwanzo ilihusu mafunzo ya kijamii “Social studies” na zimekuwa zikiwashirikisha watendaji wa taasisi tofauti zikiwemo vikosi vya ulinzi Bara na Zanzibar pamoja na taasisi za kijamii.

WANACHOTAKA wananchi wa mikoa ya Kusini, ni kutendewa haki na uadilifu k a t i k a n e e m a y a g e s i iliyopatikana.

H a y o y a m e s e m w a n a Profesa Ibrahimu Lipumba akiongea na waumini wa dini ya Kiislamu mara baada ya ibada ya swala ya Ijumaa, wiki iliyopita katika Msikiti wa Mwinyimkuu, Magomeni Jijini Dar es Salaam.

L i p u m b a a l i k u w a a k i s h e r e h e s h a h o t u b a iliyotolewa Msikitini hapo ikihimiza kufanyiana uadilifu.

Profesa Lipumba ambaye ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Wananchi (CUF), alisema utaratibu unaoanza kujitokeza hivi sasa wa kuwabeza wananchi wa Mikoa ya Kusini, sio ishara nzuri ya matumizi mazuri ya rasilimali za nchi kuanzia katika eneo husika.

“Inatubindi katika masuala ya kutenda haki na uadilifu, na kwa mujibu wa hotuba iliyotolewa

Mtwara, Lindi watendewe haki katika gesi-Lipumba

Na Bakari Mwakangwale leo , kwamba tu ish i kwa kumuogopa Mwenyezi Mungu, basi pia viongozi wawasikilize wananchi wa Mtwara kwamba gesi iliyogundulika huko ianze kutumika na kuwanufaisha wao kwanza.” Alisema Prof. Lipumba.

Alisema, ni lazima mipango madhubut i ipangwe kwa uadilifu wa hali ya juu huku wasimamizi wakizingatia kuwa juu yao yupo Mwenyezi Mungu, ili rasilimali zinazo wazunguuka Watanzania zisije kutumiwa na wajanja wachache na kuwaacha wananchi wakiwa katika dimbwi la umasikini, kama walivyo watu wa Mikoa ya Kusini hivi sasa.

Alisema, ni jambo la busara kwamba pangekuwa na Serikali wenye watendaji sikivu, makini na waadilifu ingeweza kuiona hoja ya wananchi wa Kusini na kuifanyia kazi badala ya kuwabeza jambo ambalo linatia shaka katika kuwatendea haki kutokana na mapato ya gesi.

Alisema, suala la rasilimali katika nchi nyingi badala ya

kuwa linaleta neema, huwa zinaleta balaa, akitolea mfano wa nchini Nigeria.

“Sisi tunasema kwamba ni lazima tujipange tuweze kuona kwamba hii rasilimali, mali ya asili ya nchi yetu inatumika kwa uadilifu na kwa manufaa ya wananchi wote na haswa ikianza kulenga wakazi wa eneo husika na si vinginevyo.” Alisema.

Al isema, wananchi wa Mtwara sio kwamba hawataki gesi hiyo isitumike katika maeneo mengine, bali wanachosema ni kwamba wametelekezwa kwa muda mrefu, hivyo kwa kuwa neema imeanza kutokea ndani ya mikoa yao, basi wasiendelee kupokwa neema hiyo.

Al isema, wananchi wa Mikoa ya Kusini ni haki yao kulalamikia mpango huo wa Serikali kusafirisha gesi hiyo, kwani tayari wana mfano wa gesi ya Songosongo, ambayo kwa kiasi kikubwa mpaka sasa hawanufaiki nayo ipasavyo.

Alisema, awali mipango ya Serikali ilionyesha kwamba

Inaendelea Uk. 15

MAKAMU wa kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad (mwenye suti nyeusi) akiwa na baadhi ya watendaji wa serikali yake katika moja ya ziara zake za kikazi kisiwani humo hivi karibuni.