annuur 1034

16
ISSN 0856 - 3861 Na. 1034 SHAWWAL 1434, IJUMAA SEPTEMBA 14 - 20, 2012 BEI TShs 500/=, Kshs 50/= Sauti ya Waislamu Uandikishaji unaendelea. Gharama za Hijja ni kama Hijja iliyopita mwaka jana, USD 3850. Tarehe za safari ni 19 Oktoba, 2012 na kurudi tarehe 11 Novemba, 2012. Wahi kujiandikisha sasa. Kumhijia mtu ni $900. Semina zitaanza Oktoba 7-16, 2012 Kwa mawasiliano: +255 22 2181577, +25 22 2182370, 0754 498888, 0786383820, 0754 261910 E-mail: [email protected], [email protected] Website: wwwhajjtrusttz.org Safari ya Hijja Hijiria 1433 Mufti kuokolewa na Maaskofu Wao, Mrema ndio walioipa Bakwata uhai 1993 NECTA haitizami mtoto wa Ponda wala wa Alhad Walioandamana wadai hawajahesabiwa Sensa Baada ya Sensa: Hatari yanukia kwa Masheikh Waanza kuandamwa na polisi Waislamu, Bakwata katu hawatauwana Walishaiambia Serikali mwaka 1992 Akisema Pengo, Serikali ni kusikia, kutii Je, akisema Mufti wa Bakwata Simba…! ISLAMIC EDUCATION PANEL imetangaza matokeo Elimu ya Dini ya Kiislamu Darasa la Saba: Wete, Muleba zaongoza Mtihani Darasa la Saba Na Mwandishi Wetu ya mtihani wa kuhitimu Elimu ya Msingi wa Elimu ya Dini ya Kiislamu uliofanyika Julai 25, 2012. Inaendelea Uk. 3 RAIS Jakaya Kikwete (kulia) akisalimiana na Muft wa Bakwata, Issa Shaaban Simba Polycarp Kardinali Pengo, Askofu Jimbo Kuu la Dar KATIBU Mtendaji NECTA Dkt. Joyce Ndalichako

Upload: annurtanzania

Post on 19-Feb-2015

676 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: ANNUUR 1034

ISSN 0856 - 3861 Na. 1034 SHAWWAL 1434, IJUMAA SEPTEMBA 14 - 20, 2012 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Sauti ya WaislamuUandikishaji unaendelea. Gharama za Hijja ni kama Hijja iliyopita mwaka jana, USD 3850. Tarehe za safari ni 19 Oktoba, 2012 na kurudi tarehe 11 Novemba, 2012. Wahi kujiandikisha sasa.Kumhijia mtu ni $900. Semina zitaanza Oktoba 7-16, 2012Kwa mawasiliano:+255 22 2181577, +25 22 2182370, 0754 498888, 0786383820, 0754 261910E-mail: [email protected], [email protected] Website: wwwhajjtrusttz.org

Safari ya Hijja Hijiria 1433

Mufti kuokolewa na Maaskofu Wao, Mrema ndio walioipa Bakwata uhai 1993NECTA haitizami mtoto wa Ponda wala wa AlhadWalioandamana wadai hawajahesabiwa Sensa

Baada ya Sensa:

Hatari yanukia kwa Masheikh Waanza kuandamwa na polisi

Waislamu, Bakwata katu hawatauwana

Walishaiambia Serikali mwaka 1992Akisema Pengo, Serikali ni kusikia, kutiiJe, akisema Mufti wa Bakwata Simba…!

ISLAMIC EDUCATION PANEL imetangaza matokeo

Elimu ya Dini ya Kiislamu Darasa la Saba:

Wete, Muleba zaongoza Mtihani Darasa la Saba

Na Mwandishi Wetu ya mtihani wa kuhitimu Elimu ya Msingi wa Elimu ya Dini ya Kiislamu uliofanyika Julai 25, 2012.

Inaendelea Uk. 3

RAIS Jakaya Kikwete (kulia) akisalimiana na Muft wa Bakwata, Issa Shaaban Simba

Polycarp Kardinali Pengo, Askofu Jimbo Kuu la Dar

KATIBU Mtendaji NECTA Dkt. Joyce Ndalichako

Page 2: ANNUUR 1034

2 AN-NUURSHAWWAL 1433, IJUMAA SEPTEMBA 14 - 20, 2012

AN-NUUR S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786

Cel: 0784 370 208, 0755 260 087 0713 110148, DSM. www.ipctz.org E-mail: [email protected]

Ofisi zetu zipo: Manzese Tip TopUsangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

MAONI YETU

Tahariri/Tangazo

P.O. Box 55105, Tel: 2450069, 0754 260241 Fax: 2450822 Dar es Salaam

E-mail: [email protected]

UBUNGO ISLAMIC HIGH SCHOOL

Maandalizi ya Kidato cha Kwanza 2013

Shule ya Kiislamu ya Ubungo (Ubungo Islamic High School) inatangaza PROGRAMU maalum ya maandalizi ya kujiandaa na Kidato cha Kwanza 2013 kwa wanafunzi Waislamu.Programu hii itaanza tarehe 15/09/2012 hadi tarehe 10/12/2012 Jumatatu hadi Jumamosi saa 3:00 asubuhi hadi saa 8:30 mchana.Masomo yatakayofundishwa katika programu hii ni:1. Elimu ya Dini ya Kiislamu2. English Language3. Arabic Language4. Mathematics6. Introduction to ComputerNi programu maalumu ya miezi mitatu (15/09/20212 hadi 10/12/2012)Ada ya masomo kwa programu yote ni Tshs 50,000/= inalipwa yote mwanzoni mwa programu.

Fomu za kujiunga zinapatikana Shuleni - BURE

Kwa mawasiliano zaidi: 0714 888557, 0659 204013, 0717 295107

MLETE MWANAO APATE ELIMU BORA NA MALEZI MEMA YA KIISLAMU

Wabillah TawfiiqMKUU WA SHULE

Bismillahir Rahmaanir Rahiim

Hatari yanukia kwa Masheikh BAADHI ya Maimam na Masheikh jijini Dar es Sa laam wameanza kuandamwa na jeshi la Polisi nchini, na ipo hatari ya kuanza kukamatwa w a k i d a i w a k u w a n i wachochezi.

Taar i fa z inaba in isha kwamba tayari baadhi ya Masheikh na Maimamu wameshatumiwa barua za kutakiwa kujisalimisha kituo cha polisi Oysterbay kujibu tuhuma za kutoa kauli za uchochezi na vitisho kwa viongozi wa nchi katika misikiti.

“Tayari amri ya kuitwa polisi Masheikh hao imetolewa wakitakiwa kuripoti kituo cha polisi Oysterbay, hivyo Masheikh jijini Dar es Salaam tunakutana na kujadili amri hiyo kabla ya kuchukua hatua zaidi”, alisema mmoja wa Masheikh hao alipozungumza na An-nuur juzi Jumatano.

H a t a h i v y o t a a r i f a zinaeleza kwamba kufuatia barua hiyo ya polisi, tayari Masheikh jijini Dar es Salaam wamekutana kuijadili barua hiyo kwanza kabla ya kukata shauri juu ya sakata hilo.

Imedaiwa kuwa kuna hatari ya kuanza kamatakamata ya Masheikh kipindi hiki, kufuatia msimamo uliotolewa na Jumuia na Taasisi za Kiislamu nchini, kufanya maandamano makubwa ya kupinga kuendelea kuwepo uongozi wa Baraza la Mitihani Tanzania NACTE.

Pia wasiwasi mkubwa umeonekana kuwa ni kuwepo mipango ya kuandamana hadi makao makuu ya BAKWATA na kumuondoa madarakani Mufti ya taasisi hiyo Issa Shaaban Simba, akidaiwa kushindwa kusimamia na kutetea maslahi ya Jamii ya Waislamu nchini.

Tayari agenda hizo zimezua hofu ambapo Mufti Simba

Na Shaban Rajab ametangaza kulinda uongozi wake kwa gharama yoyote na kuiomba serikali kutumia vyombo vyake vya dola kusaidia kuzima mapinduzi.

Naye Sheikh Mkuu wa BAKWATA mkoa wa Dar es Salaam Alhad Musa amezungumza na vyombo vya habari akionya wale wanaokusudia kuondoa uongozi uliopo kuchukua kuacha mara moja nia yao hiyo ambayo aliita kuwa ni kinyume na Uislamu.

Al i sema uongoz i wa BAKWATA umesimikwa madarakani kisheria na unatambulika kisheria na kwamba hata kama kuna

watu wanaona hautekelezi majukumu yake vizuri au unadhulumu mali za Waislamu, basi kuna njia nyingine stahiki za kuchukua kisheria.

Hivi sasa vyombo kadhaa vya habari na uongozi wa juu wa Bakwata umekuwa katika kampeni nzito dhidi ya Katibu wa Jumuia na Taasisi za Kiislamu Sheikh Ponda Issa Ponda, kuwa sio raia halali wa Tanzania.

Baadhi ya Wachunguzi wa mambo ya kidini wanaona kuwa kampeni hizo ni mbinu za kujaribu kuzima fukuto la Waislamu la kutekeleza a g e n d a z a o , h u s u s a n kufanyiwa marekebisho Baraza la Mitihani nchini.

PACIFIOUS Cleophace Simon, askari wa jeshi la Polisi mwenye namba G 2573, anayetuhumiwa kwa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa Channel Ten mkoani Iringa Daudi Mwangosi, juzi alipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza, kat ika mahakama ya hakimu mkazi mkoani Iringa.

Hiyo ni hatua sahihi kuchukuliwa na serikali dhidi ya watuhumiwa wa mauaji ambao ni watumishi katika vyombo vya dola.

Tunalazimika kusema hatua hiyo ni sahihi kwa kuwa mara nyingi kesi za mauaji ya raia zinazowakabili askari wa majeshi, huishia katika ngazi ya vituo vya polisi au katika vyombo vya kushughulikia kesi za makosa za kijeshi.

Kuna taarifa kwamba Bw. Pacifious tayari amevuliwa upolis i wake. Nayo ni hatua nzuri ya kumkabili mtuhumiwa kwa kosa la mauaji.

Hata hivyo tunaona tatizo bado lipo kwenye mfumo wa kuendesha kesi za jinai kama hii ya mauaji pale zinapowakabili watumishi wa vyombo vya dola. Mfumo wa upelelezi wa kesi za jinai bado upo mikononi mwa polisi, uendeshaji wa mashi taka nao pia bado baadhi ya mahakama unaendeshwa na polisi, aidha wakati mwingine polisi hao hao husimama kama mashahidi. Hii inaashiria kuwa bado uendeshaji wa kesi zinazowahusu askari si huru sana na haki kama inavyotakikana.

Ni katika mazingira hayo, bado wasiwasi ungalipo iwapo uendeshwaji wa kesi dhidi ya mtuhumiwa utakidhi viwango vya uwazi na haki.

Katika baadhi ya nchi, kuna vyombo huru maalum vinavyohusika na masuala ya upelelezi na uendeshaji wa kesi z inazowahusu watumishi wa dola. Kwa mfano polisi wa New York Police Department -NYPD Marekani akituhumiwa kuua, basi chombo kama FBI kinaweza kuchukua hatamu

Tunatarajia haki itatendeka za kufanya uchunguzi na upelelezi dhidi ya mtuhumiwa. Na akifikishwa mahakamani, basi kunakuwa na Idara za uendeshaji mashitaka ambazo hufanya kazi hiyo wala si FBI tena. Huu ndio utaratibu ambao si rahisi mtuhumiwa kuwa mwendesha mashitaka, mpelelezi, mchunguzi na shahidi mahakamani.

Tunaona kwamba ili na sisi Watanzania kujiridhisha na uendeshaji wa kesi wa haki na ulio huru, basi kuna haja ya serikali kwa makusudi kuanzisha utaratibu huu ili kuondoa kitendawili hiki ambacho kimekuwa uchochoro mkubwa wa askari na watumishi wengine wa vyombo vya dola kukwepa mkono wa sher ia pa le wanapofanya makosa ya jinai dhidi ya raia.

Tu n a a m i n i k w a m b a iwapo chombo cha namna hii kingekuwepo, hatudhani kwamba ak ina Afande C h a g o n j a n a w e n z a k e wangekuwa wepesi wa kutoa amri hatarishi dhidi ya raia, hata pale ambapo hapastahili. Kwani wangethubutu kufanya hivyo wangekwishafikiwa na mkono huru wa sheria.

Kama serikali ingekuwa na ada ya kuwashughulikia kikamilifu polisi wanaoua raia katika matukio yaliyowahi kutokea siku za nyuma, hatudhani kwamba mchezo huu wa polisi kuua kiholela ungeendelea hadi leo.

Hata hivyo pamoja na hatua nzuri zilizochukuliwa na serikali, bado hatuamini kama marehemu Mwangosi aliuliwa na askari mmoja. Hata wale waliompiga na kumpora vitendea kazi vyake nao wana kesi ya kujibu kwa kuwa wameshiriki kwa namna moja au nyingine kumsulubu marehemu. Nao wakamatwe na kuunganishwa na mwenzao Pacifious kwani nao wana kesi ya kujibu. Tena wanakabiliwa na kesi nyingine ya uporaji.

Japokuwa hatujawa na FBI yetu ya kukabiliana na kesi za namna hii kiasi kwamba bado tunalazimika kuwategemea hao hao polisi, kwa dalili ambazo zimeshaonyeshwa na serikali kukabiliana na wanaotuhumiwa kumuua M w a n g o s i , t u n a d h a n i

kwamba kesi itaendeshwa kwa uwazi ili haki na kweli ijulikane. Aidha hatutarajii kesi hii kuchukua muda mrefu kiasi cha kufikia hatua ya watuhumiwa kusahaulika na hatimaye kupata mwanya wa ‘kuokoka’.

Hata hivyo tunalazimika kutoa angalizo moja. Kwamba vyombo vya habari vina mchango mkubwa katika

kupaza kelele dhidi ya dhulma. Mitaani wananchi wameshangaa kuona vyombo vya habari kwa pamoja v i k i s h u p a l i a b a r a b a r a mauaji ya Mwangosi na kutoa changamoto kali kwa serikali.

Lakini wanadai ni vyombo hivyo hivyo vya habari vinapiga kimya au kuripoti kwa uchache matukio ya

polisi kuua baadhi ya raia ambao sio waandishi. Hivyo wanabainisha kwamba kama waandishi walivyoguswa na mauaji ya Mwangosi, basi hata raia wengine wakiuliwa na polisi wapaze sauti kwa kiwango hicho hicho kwani yote ni mauji yanayofanywa na vyombo vya dola dhidi ya raia wasiokuwa na hatia.

Page 3: ANNUUR 1034

3 AN-NUURSHAWWAL 1433, IJUMAA SEPTEMBA 14 - 20, 2012Habari

Labda Maaskofu wakamuondoe Mufti KAMA ni kung’o lewa Bakwata Mufti na Sheikh Mkuu wa Baraza hilo, labda ang’olewe na Maaskofu ambao ndio pia waliochukua jukumu la kuipa uhai Bakwata pale ilipotakiwa kufutwa mwaka 1993.

Mwaka huo ilikuwa serikali iifute Bakwata baada ya kuonekana kuwa imeshindwa kutekeleza wajibu wa kisheria kulingana na Katiba yake ndio maaskofu wakihamasishwa na kuongozwa na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Augustino Lyatonga Mrema wakachangishana fedha kufanikisha Mkutano Mkuu wa Bakwata uliofanyika Dodoma.

“Hivi kama Waislamu wanai thamini Bakwata , wanashindwa kuchanga pesa za kuendesha mkutano wake mkuu? Sasa kama hawakujali ilipokuwa inataka kufutwa, kipi cha kuwafanya waione ya maana hivi leo mpaka waache shughuli zao wakapige kambi Kinondoni kumlinda Mufti? Hao hao Maaskofu na Mrema wao ndio wanajua wanavyofaidika na Bakwata ndio maana waliingia tabu kuipa uhai na wao ndio wa kujua kama viongozi walipo hivi sasa bado wanawafaa au la”.

Alisema muumini mmoja baada ya kusikia ile kauli iliyotolewa na Sheikh wa Bakwata Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa akitoa wito kwa Waislamu kutoka ‘ J ihad’ kwenda kumhami Mufti Simba.

“ K a m a n i k i b a n o , mfumokristo hauchagui mtoto wa Alhad, Sheikh wa Bakwata au wa Shura ya Maimamu, wote wanabamizwa, kama ni hujuma NECTA, yumo mtoto wa Ponda na wa ‘Mufti’ au japo mjukuu wake, kama ni kunyimwa ajira na vyeo kazini, mfumo hautofautishi a l iyehesabiwa sensa au aliyekataa.”

Alisema muumini huyo aliyejitambulisha kwa jina la Kombo Hassan na kuongeza kuwa “kama ni kufanikiwa, Waislamu watafanikiwa kwa kuunganisha nguvu zao katika kupambana na mfumokristo a m b a p o i t a b i d i p i a wawaelimishe Bakwata nao wajitambue na washirikiane na Waislamu wenzao katika ‘Jihad hii’ ya ukombozi wa Waislamu.

“Wanachoshindwa kuelewa Masheikh wetu wa Bakwata ni kuwa ‘mfumo’ hauangalii kuwa ni mtoto wa mjomba wake Alhad au Sheikh Mataka, ikija kama ni kuhujumiwa katika elimu, ajira, kupata vyeo na kupuuza masuala ya Kiislamu, mawakala wa ‘mfumo’ wanachotizama ni Uislamu na Muislamu, sio

Na Bakari Mwakangwale Ubakwata wala u-Baraza Kuu.” Alisema Kombo.

Wakati huo huo, maelfu ya Waislamu Jijini Dar es Salaam, waliojitokeza katika maandamano Ijumaa iliyopita, wamedai hawajajiandikisha katika Sensa ya Watu na Makazi.

Hayo yamebainishwa na Waislamu hao waliokuwa wakiandamana kuelekea Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupinga wenzao kukamatwa baada ya kugoma kuhesabiwa wakati wa Sensa ya Watu na Makazi.

Wa a n d a m a n a j i h a o waliipasha An nuur, kwamba wanaandamana kupinga wenzao kukamatwa kwa kugoma kuhesabiwa kama walivyogoma wao katika sehemu mbalimbali za Jijini Dar es Salaam.

Walidai, Mkurugenzi wa Sensa, Bi. Amina Mrisho, anaupo to sha umma na kuifariji Serikali kuwa Sensa yao imefanikiwa kwa asilimia tisini hadi tisini na tano.

Waislamu hao wake kwa waume, walikuwa wamebeba mabango baadhi yakiandikwa ‘Wislamu hatujahesabiwa’, ‘Tusinge andamana kama tungehesabiwa’, ‘NECTA ifumuliwe’ ‘Sensa 2012, changa la macho’ ‘Mataifa ya Ulaya mmeliwa’.

Abdul razak Mustafa , amesema zoezi la Sensa limekuwa na dosari kubwa, “lau kama kungekuwa na sheria ya wasimamizi kutoka nje ya nchi, basi nadhani wasingeipitisha sensa hii.”

Sheikh Awadhi Mukadam, aliye Imam wa Masjid Tawfiq, Mbagala Kuu, amesema walichofanya Serikali ni kuyadanganya mataiafa ya Nje, lakini alidai Watanzania na hata wenyewe wanajua Sensa imefeli.

Alisema, kimsingi Sensa ya mwaka huu imekuwa ni ya watu kushurutishwa, jambo ambalo si utaratibu wa sensa, na walioweza kuwalazimisha na kukubali kuhesabiwa ni wachache kuliko wale waliogoma kabisa.

“Angalia, umati wote huu unadhani watakuwa wamejiandikisha kweli, na kama ndiyo hapa wamefuata nini. Serikali inajidanganya yenyewe hakuna Sensa mwaka huu.” Alisema Sheikh Mukadam.

Baadhi ya wanawake wa Kiislamu katika maandamano hayo walitoboa siri wakisema kwamba, waliamua kuweka tiki katika milango ya nyumba zoa.

B i . A i s h a S h o m a r i , akifafanua zaidi alisema, baada ya kuona kamatakamata imehamia kwao, baada ya wakuu wa Kaya (Wanaume) kutopatikana majumbani mwao, waliamua kufanya hivyo.

“Kulikuwa na utaratibu wa makarani, kuweka tiki kila nyumba walimopita, ikabidi kutia tiki katika milango yetu na tulipigiana simu Waislamu w e n g i , j a m b o a m b a l o liliwachanganya makarani.” Alisema.

K w a u p a n d e w a k e Ustadhi Ally Jumaa, alisema anashangaa kuona Serikali na Jeshi la Polisi, wakiwakamata Waislamu kwa madai kuwa wanavuruga Sensa.

Alisema, kama Serikali ingekuwa ni adilifu, basi wa kuwakamata ni watendaji wa Televisheni ya Taifa, TBC1, pamoja na asasi zote zilizotoa Takwimu zisizo rasmi.

“Waislamu kugomea Sensa ni matokeo ya takwimu zile, hao ndio walipaswa kuwajibishwa na ndio chanzo cha sisi kugomea, tena baada ya kuitahadharisha sana Serikali, lakini wakatupuuza kwa kuwa wamejiaminisha kuwa sisi ni jamii ya kupuuzwa tu humu nchini.” Alisema ustadh Jumaa.

Alisema, kwa msimamo waliouonyesha katika hili la Sensa, Serikali imepata majibu, na kudhihirisha kwamba Bakwata si Taasisi ya Waislamu nchini, bali itabaki kuwa ni kipaza sauti chao (serikali) na wao (Waislamu) wataipuuza daima.

M a a n d a m a n o h a y o yaliyoratibiwa na Jumiya na Taasisi za Kiislamu nchini, ambayo yalikuwa ya aina yake, Waislamu walitoka katika Misikiti mbalimbali Jijini, na kuelekea katikati ya Jiji, yalipo Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani

ya Nchi.Askari Polisi waliokuwa

katika kona mbalimbali, za barabara Kuu za Jiji, walibaki kuwaangalia tu, Waislamu hao waliokuwa katika vikundi vidogovidogo, wakikatisha mitaa.

Waislamu wengi waliswali katika Misikiti ya Kariakoo, ikiwemo Idrisa, Mtoro, Manyema, Lindi, Rawdhwa, pamoja na baadhi ya Miskiti hiyo kutothibitisha au kusema kuna maandamano, Waislamu walitoka na kwa Takbir, wakielekea Wizarani.

Waislamu wengine walitoka makundi kwa makundi katika Misikiti ya Kichangani (TIC), Rahma Magomeni Kagera, M t a m b a n i , K i n o n d o n i ambapo Waislamu wengine walioswalia mbali waliingia kwa daladala Kariakoo na kuzamia mitaa ya Posta,

Ghafla, maelfu ya Waislamu walianza kuonekana kwa wingi jirani kabisa na Wizara hiyo, na kufunga barabara za Ohio na Ghana zinazozunguka Wizara hiyo na kusababisha shughuli katikati ya Jiji kusimama, kwa muda wa masaa matano, na kusababisha foleni ya magari na msongamano mkubwa.

Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, akiwa na maofisa wengine wa Polisi, nje ya Wizara hiyo na Makao Makuu ya Jeshi hilo, walikuwa na wakati mgumu kuwatuliza Waislamu hao, ambao muda mwingi walikuwa wakitamka, ‘Takbir’ na wengine wakiitikia ‘Allah Akbar’.

Waislamu hao, walitulia baada ya Katibu wa Masjidi

Mtambani, kusimama na kuwatuliza na kuwaeleza kuwa viongozi wao wataingia ndani kuongea na Katibu Mkuu, Wizara wa Mambo ya Ndani ya Nchi ili kufikisha kilio chao.

Baada ya mazungumzo yaliyochukua zaidi ya masaa mawili, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Mbaraka A b d u l w a k i l , a l i t o k a sambamba na viongozi wa Waislamu, ambapo alipokea risala ya Waislamu, baada ya kusomewa.

Katika risala yao, Waislamu walilaani Jeshi la Polisi kuwakamata, kuwanyanyasa na kuwadhalilisha Waislamu kwa kukataa kuhesabiwa katika Sensa ya Watu na Makazi nchini, na kutaka vitendo hivyo vilaaniwe na kukomeshwa.

“Jeshi la Polisi limekuwa likiwakamata wanawake wa Kiislamu na kuwavua nguo (Hijabu) na wakati mwingine watuhumiwa kuwanyima haki ya dhamana kinyume cha sheria.” Amesema Ustadhi Mukkadam Swaleh, akisoma risala hiyo.

A i d h a r i s a l a h i y o ikalalamikia kitendo cha Polisi kuvunja nyumba za Waislamu usiku kwa kushirikiana na maofisa wa Sensa, kisha wakiwalazimisha kuhesabiwa chini ya mtutu wa bunduki.

Kufuat ia mandamano hayo na kupokea risala ya Waislamu, Katibu Mkuu, Abdulwakil, alisema, anatoa agizo kwa Makamanda wate nchini kuwaachia watuhumiwa wote waliokamatwa kwa dhamana.

Wete, Muleba zaongoza Mtihani Darasa la Saba

Inatoka Uk. 1Akitangaza matokeo hayo

mbele ya waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari, Maelezo, Afisa Mwandamizi wa Islamic Education Panel, Suleiman Daudi amezitaja shule za Wete (Pemba) na Kamachumu (Muleba), kuongoza katika mitihani hiyo.

Akawataja wanafunzi walioibuka kidedea kwa kuongoza kwa alama za juu kuwa ni Hijra Khamisi Omar (Wete ) , Rehema Karungi Yunusu (Muleba) na Mohammed Athumani Rajab wa Ilala, jijini Dar es Salaam.

Wengine walio katika kumi bora ni Muhammad Ayub Kijuu (Moshi), Nasibu Abdallah Idd (Moshi), Tajuddin Idrisa Mwijage (Ilemela), Hadija Ally Amiri (Ilala), Feisal Suleiman (Kinondoni), Ismail Abdallah Kibakaya (Same) na Abdallah Nuhu Abdallah (Ilemela).

Jumla ya shule 1,746 katika mikoa 24 na wilaya 81 zilifanya mtihani huo ikilinganishwa na shule 519 zilizofanya mwaka jana 2011.

Ongezeko hilo la shule zilizoshiriki, limeongeza pia idadi ya watoto waliofanya

mtihani ambapo kulikuwa na jumla ya watahiniwa 55,557.

Mwaka jana watahiniwa waliofanya mtihani huu walikuwa 24,892.

Hii ina maana kuwa idadi ya watahiniwa imeongezeka kwa kiasi cha watahiniwa 30,665 sawa na asilimia 123.2 (123.2/%.).

S a b a b u k u b w a y a kuongezeka idadi h iyo imeelezwa kuwa ni kutokana na kuimarika kwa ufundishaji na upatikanaji wa vitabu katika maeneo mengi nchini.

Pia wanafunzi wengi wamehamasishwa na matokeo ya mtihani ya mwaka jana.

Page 4: ANNUUR 1034

4 AN-NUURSHAWWAL 1433, IJUMAA SEPTEMBA 14 - 20, 2012Habari

Januari 11, 1992 kilifanyika kikao Ikulu cha pande mbili kati ya wawakilishi wa Waislamu waliokuwa w a m e v a m i a o f i s i z a Bakwata na kuwatimua viongozi wake pamoja na uongozi wa Bakwata ukiongozwa na Mufti wake Sheikh Hemed Bin Juma Bin Hemed. Lengo la kikao hicho ilikuwa kuleta sulhu na kutizama namna ya kulirekebisha Bakwata liwe chombo cha Waislamu na kikubalike kwa Waislamu. Uvamizi wa ofisi za Bakwata na kutekwa ofisi zake za mkoa wa Dar es Salaam na Shule ya Alharamaini, ulifanywa kufuatia kikao cha Waislamu nchi nzima a m b a c h o k i l i f a n y i k a ukumbi wa mikutano wa Nkrumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam 15 Septemba, 1991.

Mkutano huo ambao ulifunguliwa na Waziri katika Ofisi ya Rais anayeshughulikia Ulinzi na Jeshi la Kujenga T a i f a , M h e s h i m i w a Abdurahman Kinana pamoja na mambo mengine, uliamua kuwaondosha madarakani Kaimu Mwenyekit i wa Bakwata Bwana Suleiman Hegga na Kaimu Katibu Mkuu Bwana Rajab Kundya. Na kisha kuteuwa kamati ya muda ambayo itasimamia shughuli za kila siku za Bakwata Makao Makuu na kuandaa Rasimu ya marekebisho ya Katiba ya Bakwata (Rasimu ambayo baadae imekuwa ndio Katiba ya Baraza Kuu).

Ilikuwa ni katika harakati hizo za kulisafisha Bakwata, Mufti wake Hemed Bin Juma alisema kuwa Rais Alli Hassan Mwinyi haijui Bakwata , anayei jua n i Nyerere. Bakwata wakakataa ushauri wa Mheshimiwa Alli Hassan Mwinyi wa kuunda Kamati ya pamoja ya kulisafisha Bakwata.

“Nendeni mkauwane, tutaleta vyombo vya dola.” Alisema Mzee Mwinyi baada ya kuona kuwa kikao hakina muafaka.

“ T u n a k u h a k i k i s h i a Waislamu hawatauwana.” Alisema Mzee Salum Khamis ambaye alikuwa mwenyekiti wa wawakilishi Waislamu ambao wakati huo walikuwa wamekusanyika Magomeni Kichangani kusubiri matokeo mazungumzo ya Ikulu.

Na kwel i , Wais lamu hawakuuwana. Walimuacha Mufti Hemed Bin Jumaa na Bakwata yake, wakaanzisha Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu ambalo lilisajiliwa mwaka 1 9 9 2 . ( S o m a m a k a l a i l i y o a m b a t a n i s h w a y a kuundwa Baraza Kuu).

Waislamu, Bakwata katu hawatauwanaWalishaiambia Serikali mwaka 1992Akisema Pengo, Serikali ni kusikia, kutiiJe, akisema Mufti wa Bakwata Simba…!

Na Omar Msangi

Baada ya u tangu l iz i huo, niseme kuwa katika jumla ya mambo ambayo yamewaunganisha Waislamu katika madai yao serikalini, ni suala la OIC na Mahakama ya Kadhi. Katika masuala haya, kauli ya Waislamu imekuwa moja, kutoka Mufti wa Bakwata, Baraza Kuu, Shura ya Maimamu, Ansaar Sunnah na taasisi mbalimbali za Kiislamu nchini.

Kwa upande wa Serikali, baada ya kufanya uchunguzi, utafiti na kupata uzoefu kutoka nchi mbalimbali za Kiafrika ambazo tayari ni wanachama wa OIC, ilisema kuwa imejiridhisha kuwa kujiunga na OIC ni jambo jema lenye manufaa na nchi

na hivyo ipo katika hatua za kujiunga. Msimamo huo wa serikali ulielezwa rasmi na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa Bernad Membe Bungeni hivi karibuni.

Hata hivyo, kwa bahati mbaya msimamo huo wa serikali ulikuwa kinyume n a u l e w a M a a s k o f u . Kilichotokea ni kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu, Kanisa Katoliki Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kadinali Pengo, wala hakutaka kujipa tabu kufunga safari kwenda ofisini kwa Mheshimiwa Membe; alimwita tu naye akaenda mbio kusikiliza Baba Askofu anasema nini.

Sasa ukitaka kujua kile alichoambiwa Membe na Baba Askofu Pengo, muulize Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mizengo Pinda; Tanzania itajiunga lini na OIC?

Kwa upande mwingine, hivi karibuni tumeshuhudia ile kashfa ya Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) kuhujumu watoto wa Kiislamu hata ilipozomewa ikalazimika kubadili matokeo.

Katika kashfa hi i ya NECTA, Mufti wa Bakwata na She ikh Mkuu, I s sa Shaaban Simba aliungana na Waislamu wote nchini kulani hujuma hiyo na akatoa tamko kali. Katika Tamko hilo la Mufti Simba, ilielezwa

kuwa NECTA imekosa sifa ya kuwa chombo cha kitaifa kwa sababu toka imeanzishwa imekuwa ikiongozwa na viongozi wa Kikristo watupu katika vitengo vyote muhimu. Mufti akasema kuwa umefika wakati Baraza hilo lifumuliwe na kuundwa upya ili kulipa sura ya kitaifa.

A l i s e m a p i a k u w a k u t o k a n a n a N E C TA kudhibitiwa na Wakristo watupu, kuna uwezekano kuwa watoto wa Kiislamu wamekuwa wakihujumiwa katika mitihani ya kitaifa kwa miaka mingi. Kwa hiyo kauli ya Mufti ikataka iundwe Tume huru ya uchunguzi na Baraza hilo lichunguzwe kwa uchache kwa miaka 10 iliyopita. Lakini pia akataka kuwa wale wote ambao wamehusika katika kashfa hii ya kuchakachua matokeo ya watoto wa Kiislamu wachukuliwe hatua haraka.

Sasa labda tuulizane, toka Mufti wa Bakwata Simba ametoa kauli hiyo, serikali imefanya nini juu ya kashfa ya NECTA?

Je, kuna ishara yoyote kuwa huko serikalini kuna mtu anajali kuwa Mufti Simba kasema kitu?

S a n a s a n a n i y a l e maandamano ya Waislamu yaliyopelekea serikali japo kupokea rasmi malalamiko ya Waislamu na kuunda Tume ambayo hata hivyo haijulikani ilichofanya nini kwa sababu ilikuwa kama namna ya kuwazubaisha Waislamu joto lipoe NECTA iendelee na hujuma zake dhidi ya watoto wa Kiislamu.

Lakini rudi sasa serikali inapokuwa na lake na inataka ‘Masheikh’ wasaidie, hapo ndio Mufti, akina Alhad na Sheikh Mataka wataonekana wa maana. Watapelekeshwa mbio kama tulivyowaona wakipewa fursa kat ika v y o m b o v y a h a b a r i kuhamasisha Waislamu washiriki sensa ya watu na makazi, utadhani kulikuwa na Muislamu asiyejua maana na umuhimu wa sensa.

Katika hali kama hii, nafasi na hadhi ya Mufti Simba, Sheikh Alhad na Ponda Issa Ponda ni moja katika nchi hii. Wote wanatafunwa na ‘mfumo’ ndio maana hata katika lile Baraza la Idd pale Dodoma, Masheikh wa Bakwata badala ya kupewa kauli ya unyenyekevu na ahadi njema kama inavyokuwa kwa Maskofu, walijikuta wakishushuliwa na Rais baada ya kumsomea risala ya madai ya Waislamu.

Katika kipindi chote cha uongozi wa Mwalimu Nyerere na hasa baada ya kuvunjwa kwa E.A.M.W.S na jumuiya nyingine za Waislamu, h a i k u r u h u s i w a kusajiliwa Jumuiya au Taasisi yoyote ya Kiislamu ila sharti ipate kibali cha BAKWATA, n a i w e c h i n i y a BAKWATA. Kwa hiyo, BAKWATA, iliyofanya kazi ya kuuhujumu Uislamu zaidi kuliko kuuendeleza, ilikuwa ndiyo Jumuiya pekee ya Wais lamu kwa kipindi cha miaka kumi na sita (16) kuanzia 1 5 D e s e m b a , 1 9 6 8 i l i p o a n z i s h w a B A K WA T A h a d i 1985 alipong’atuka Mwalimu Nyerere.

R a i s M w i n y i alipoingia madarakani mwishoni mwa mwaka 1 9 8 5 , i l i g u n d u l i k a kwa Waislamu kuwa hapakuwa na sheria yoyote ya nchi iliyoipa BAKWATA ukiritimba bali ilikuwa ni sera binafsi ya Nyerere na kanisa lake. Baada ya Waislamu kugundua hili, kwa hamasa na hamu kubwa walianzisha utitiri

Kuanzishwa BARAZA KUU 1992 wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu kwa kiasi kwamba hata misikiti ilisajiliwa kama taasisi ili kujitoa kwenye makucha ya BAKWATA.

BAKWATA iliyolewa ukiritimba uliodumu kwa miongo miwili haikuwa radhi kuona ule mfumuko wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu zilizosajiliwa kihalali na Serikali bila ya kibali chake. Katika Baraza la Iddi el-Haji mwaka 1991 ambalo mgeni rasmi alikuwa Mheshimiwa Rais Ali Hassan Mwinyi; Bwana Suleiman Hegga a l i y e k u w a K a i m u Makamu Mwenyekiti w a B A K W A T A aliilaumu Serikali kwa nini imeruhusu kuwepo kwa vikundi vingi vya Kiislamu. Aidha aliitaka Serikali ividhibiti vikundi hivyo. Wakati Bwana Hega analilia kubakishwa kwa uki r i t imba wa B A K WATA , t a y a r i Serikali ilikwishaingia kwenye sera ya vyama vingi vya siasa.

Mheshimiwa Rais wakati wa kujibu risala hiyo, alikataa suala la kudhibitiwa Taasisi na Jumuiya za Waislamu,

kwani mchango wake katika kuleta maendeleo ya Waislamu ulikuwa mkubwa kul iko ule wa BAKWATA. Rais aliinasihi BAKWATA ikutanishe vikundi vyote vya Waislamu ili tofauti ziilizopo zijadiliwe ili hat imaye upat ikane umoja na Mshikamano wa Waislamu unaohitajika na ulioamrishwa katika Qur-an (3:103).

B A K W A T A hawakutekeleza nasaha hizo. Lakini walitokea wanaharakti wa Kiislamu waliotumia fursa ile na kuandaa mkutano ambapo walialikwa wawakilishi toka Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini kote. Aidha v iongozi wa BAKWATA toka ngazi za wilaya hadi makao makuu wa l i a l ikwa . Lengo la mkutano huo liIikuwa kujadili namna ya kuifanya BAKWATA ifanye kazi kwa maslahi ya Uislamu na Waislamu wa nchi hii.

L a k i n i w a k a t i maandalizi ya mkutano h u o y a n a e n d e l e a BAKWATA i l ikuwa ikiendesha kampeni k u j a r i b u k u w a z u i a

Inaendelea Uk. 7

Page 5: ANNUUR 1034

5 AN-NUURSHAWWAL 1433, IJUMAA SEPTEMBA 14 - 20, 2012Habari za Kimataifa

J e s h i l a K e n y a limetangaza kuwa askari wake 22 wamepoteza maisha tangu liingie Somalia mwezi Oktoba mwaka jana.

Msemaji wa Jeshi hilo Cyrus Oguna, amesema kuwa wanajeshi wengine kadhaa pia walijeruhiwa kwenye mapambano hayo.

Oguna ametangaza k w a m b a O k t o b a 1 4 ki la mwaka i takuwa siku ya kuwakumbuka

K A S I S I m w e n y e misimamo mikali ya chuki kupindukia wa madhehebu ya Kiprotestan nchini Marekani, Terry Jones, ameendeleza harakati zake za kupiga vita Uislamu baada ya kutangaza nia yake, eti ya kumfungulia m a s h i t a k a M t u m e Muhammad (saw)!

Tovuti ya Russia Today, imeripoti kuwa Kasisi Terry Jones, ameanzisha harakati h iyo ya k i jeur i ak ida i kuwa mafundisho ya Nabii Muhammad (saw) yalikuwa na athari katika mashambulio ya Septemba 11 mwaka 2001 dhidi ya majengo mapacha mjini New York.

Hivyo kwa msingi huo amesema atamhukumu Mtume Muhammad (saw) tarehe 11 Septemba sambamba na kumbukumbuku za tukio hilo!

Mhubir i wa Kikr is to mwenye asili ya Misri, Usama Daqduq, naye atafuatana na Kasisi Jones na filamu ya tukio hilo la kifedhuli litarushwa hewani na televisheni moja huko Marekani.

Kasis i Jones al iwahi kuchoma moto nakala za

Waislamu Uingereza wapinga upotoshaji historia ya Uislamu LONDONKipindi kilichoonyeshwa na Channel 4 ya televisheni ya Uingereza kuhusu historia ya Uislamu, kimezua tafrani na malalamiko kutoka kwa watazamaji na wanahistoria Waislamu wa nchi hiyo.

K a t i k a k i p i n d i c h a “Uislamu, kisa ambacho h a k i j a s i m u l i w a ” kilichorushwa hewani na channel h iyo ambacho k i l i e n d e s h w a n a mwanahistoria wa Chuo Kikuu cha Cambridge, akiutaja Uislamu kuwa ni dini iliyobuniwa na wanadamu.

Uchambuzi wake huo umezusha wimbi kubwa la malalamiko dhidi msomi huyo, akidaiwa kuwa ni mpotoshaji mkubwa.

Ripoti zinasema kuwa mwanahistoria huyo wa Chuo Kikuu cha Cambridge, amedai kuwa jina la mji wa

Makka halikutajwa katika Qur’ani kuwa ndio kituo kikuu cha Uislamu!

Baada ya kumalizika kipindi hicho, Waislamu na

wanahistoria waliwasilisha mashitaka yao dhidi ya mwanahistoria huyo kwa s h i r i k a l i n a l o s i m a m i a vyombo vya habari nchini

Uingereza, wakilitaka shirika hilo kuchunguza matamshi ya mwendeshaji wa kipindi hicho yanayopotosha historia ya Uislamu.

Kasisi Jones aendeleza wendawazimu wakeSasa anataka kumhukumu Mtume (saw)

Qur ’ani Tukufu kat ika jitihada zake za kuupiga vita Uislamu.

Kundi moja vijana wa Kiislamu limelaani vitendo vya kasisi huyo na kutangaza kuwa misimamo dhaifu ya Waislamu ya kutokabiliana vi l ivyo na kasis i huyo wakat i akichoma moto nakala za Qur’ani, kumezidi

kumtia kiburi na kuendelea kuwatukana Waislamu na sasa anapanga kumvunjia heshima Mtume Muhammad (saw).

Kwa muda mrefu kasisi Jones amekuwa akiendeleza mahubiri yake ya chuki za kidini dhidi ya Waislamu na Uislamu hasa baada ya tukio la Septemba 11, lakini serikali

ya Marekani imeendelea kupiga kimya dhidi ya kasisi huyo licha ya kuonyesha hatari ya kulipuka vurugu kutokana na mahubiri yake.

Hata hivyo wachunguzi wanasema iwapo jamii ya Waislamu itajaribu kuchukua hatua dhidi yake, hapo serikali inaweza kuchukua hatua mara moja kuwashughulikia.

Kenya yapoteza wanajeshi 22 Somalia w a l i o p o t e z a m a i s h a pamoja na kuwapongeza wanajeshi wanaoendelea na oparesheni ya kupambana n a A l - s h a b a b h u k o Somalia.

T a y a r i K e n y a imewaondoa wanajeshi wasiopungua 400 kutoka Somalia, ambao siku ya Jumamosi walipokelewa m j i n i N a i r o b i k w a mapokezi ya kishujaa.

Hata hivyo Wanajeshi waliobaki wanatarajiwa kushiriki oparesheni kali ya

kuukomboa mji wa bandari wa Kismayu huko Somalia ambao unadaiwa kuwa unatumiwa na Al-shabab kama kitega uchumi.

U k i a c h a k u p o t e z a wanajeshi na wengine k u j e r u h i w a k a t i k a operesheni inayoendelea, nchini Kenya nako hali ya amani imekuwa ni tete kufuatia kuwepo matukio ya mashambulizi ambayo yamegharinu maisha ya watu tangu jeshi la nchi hiyo lilipoingia somalia.

CHICAGOMaelfu ya walimu katika jimbo la Chicago, Marekani wamegoma wakilalamikia hali duni ya maisha jimboni humo.

Mgomo huo umeanza kufua t ia kush ind ikana kupatikana mwafaka kati ya chama cha walimu na viongozi wa jimbo hilo.

Huo ni mgomo mkubwa zaidi kuwahi kufanywa na walimu tangu miaka 25 iliyopita jimboni Chicago.

Ch icago n i eneo l a tatu kubwa la kielimu na ufundishaji nchini Marekani amba lo l ina jumla ya wanafunzi laki nne, hivyo mgomo huo umeonekana kuwa pigo kubwa kwa Rahm Emanuel, Meya wa mji huo.

Rahm Emanuel aliyekuwa mkuu wa ofisi ya Rais Barack Obama wa Marekani, ni miongoni mwa waungaji m k o n o w a k u b w a k w a utawala dhalimu wa Israel.

Maelfu ya walimu wagoma Marekani

Kwa mara nyingine tena Marekani imepinga suala la Palestina kupewa uanachama kamili katika Umoja wa Mataifa, UN.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Victoria Nuland, amesema Washington inapinga juhud i z inazo fanywa na Mamlaka ya Ndani ya Palestina za kutambuliwa rasmi kama nchi huru.

Siku chache zil izopita, Kiongozi wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina Mahmoud Abbas, alitangaza kuwa Septemba 27 mwaka huu Palestina itawasilisha tena ombi la kupewa uanachama kamili katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Mpango wa Palestina kupewa unachama kamili katika Umoja wa Mataifa na kuwa nchi huru na mji wake mkuu ukiwa Baitul Muqaddas, unaungwa mkono na nchi 140 wanachama wa umoja huo na kupingwa vikali na Marekani na swahiba wake Israel.

Wakati Marekani ikiwa kinara wa kupinga taifa huru la Palestina UN, Taifa hilo hilo ndilo inayojinasibu kuwa msuluhishi mkubwa wa mzozo wa Israel kuikalia Palestina kupitia mipango yake ya ghiliba na kilaghai ya ‘roadmap!’.

Marekani yapinga Palestina kupewa uanachama wa UN

Page 6: ANNUUR 1034

6 AN-NUURSHAWWAL 1433, IJUMAA SEPTEMBA 14 - 20, 2012Habari/Matangazo

Inawatangazia Mahujaji wake wote kuwa Safari ya kuondoka ni tarehe 09/ 10/2012 na 11/10/2012Kurudi ni tarehe 03/ 11/2012 na 05/11/2012Mahujaji wote wamalize kuchanja haraka iwezekanavyoPaspoti zipelekwe ofisini kwa ajili ya Viza na SafariSemina Dar es salaam siku ya Jumapili tarehe 30/ 09/ 2012 Madrasatul Jabalhira Magomeni karibu na ofisiniZanzibar ni Suni Madrasa Mkunazini tarehe 08/09/2012.Wamalize malipo na taratibu zote za safari.Nafasi bado zipo bei zetu ni USD 3,375 tu kwa huduma zote pamoja na mahema maalumu ( VIP). Kwa mawasiliano zaidi piga simu.FOMU ZINAPA TIKANA A. Ofisi ya Ahlul Daawa Dar es salaam Mtaa wa Dosi na Mkadini Nyumba Namba 26 Mkabala na Showroom ya Magari Tel- 0713 730444 au 0773 804 101 AU 0785 930 444 AU 0773 930444.B. Ofisi ya Ahlul Daawa Zanzibar Raha leo Tel- 0777 484 982 0777 413987C. Abubakari Maulana wa Markaz wa Kiwalani Dar es salaam Tel- 0784 453 838D. Abdallah Salehe Mazrui (Hoko) Dar es Salaam Tel-0715724444E. Salim Is-Haq Dar es Salaam Tel-0754 286010 au 0774 786101F. Dukani kwa Abdalla Hafidh Mazrui Wete-Pemba Tel-0777482665G. Dukani kwa Mohammed Hafidh Mazrui Mkoani Pemba Tel-0777456911H. Sheikh Daud Hamis Sheha Tel-0777 679692I. Maalim Seif Humoud Hamed Kijichi Zanzibar Tel-0777 417736

Wahi kulipiaUsisahau kikundi cha Ahlul Daawa ni cha bei nafuu kuliko vingine na huduma bora kuliko wengi

Wabillah Tawfiq

AHLUDAAWA HAJJ AND TRAVEL AGENCY

MHADHIRI wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mchambuzi maarufu wa siasa nchini Dkt. Exavery Lwaitama, amebainisha kwamba kukithiri kwa m a u a j i y a n a y o d a i w a kufanywa na polisi dhidi ya raia ni matokeo ya polisi kubebeshwa kazi zinazostahili kufanywa na wanasiasa, ili kulinda maslahi ya wanasiasa hao.

Dkt. Lwaitama aliyasema hayo wakati akihutubia katika

Wanasiasa chanzo cha mauaji Polisi wanatumiwa tu. Nao wanapigika pia

Na Shaban Rajab mkusanyiko wa maandamano ya kimya kimya yaliyofanywa na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Jumanne wiki hii.

“Wandishi ni walimu wakuu kutokana na jukumu lao la kufanya kazi kubwa ya kuuelimisha umma. Wao ndio wanaofanya kazi ya kuwafahamisha watu mambo mbalimbali yanayotokea katika nchi yao, akiuliwa mwandishi kauliwa mwalimu mkuu” . Al i sema Dkt . Lwaitama.

Mantiki ya kauli hiyo ya Dkt. Lwaitama ni kwamba

anapoul iwa mwandishi wa habari ambaye ndiye m p a s h a h a b a r i w a wananchi juu ya mambo mbalimbali yanayofanyika katika nchi, anayeathirika zaidi ni mwananchi huyo anayemtegemea mwalimu wake kupata taarifa na u f a h a m u w a m a m b o yanayohusu nchi yake.

Dkt. Lwaitama aliongeza kwamba t a t i zo kubwa linalosababisha kukithiri k w a w i m b i l a m a u a j i yanayofanywa na polisi dhidi ya raia ni mazoea yaliyopo kwamba wanasiasa (watawala) wamekuwa wakiwatumia vibaya polisi kufanya kazi wanazostahili kufanya wao.

“Hawa polisi mishahara yao midogo sana, wanaacha kazi ya kufukuza wezi wanashurutishwa kufuata maelekezo ya wanasiasa w a n a o w a t u m i a v i b a y a kulinda maslahi yao, tatizo hapa ni wanasiasa, wahariri wasaidieni polisi hawa, wanapigika kama ninyi”.

Alifafanua zaidi kwamba kutokana na kukithiri tabia ya wanasiasa kushurutisha polisi kutekeleza majukumu ya kisiasa, polisi wataendelea kuua bi la ushahidi , na kwakuwa waandishi nao wanauliwa, maana yake ni kwamba utakosekana ushahidi wa kihabari na yatabakia maelezo na taarifa za akina Chagonja pekee.

H i v y o a l i w a t a k a waandishi wa habari na wahariri kupambana kwanza na wanasiasa ambao ndio wanaowatuma polisi kufanya kazi za kiasiasa ambazo si zao badala ya kupewa majukumu yao ya kipolisi ambayo ni kulinda raia na mali zao.

Mtazamo huo wa Lwaitama unakuja ikizingatiwa kwamba mauaji mengi yanayofanywa na polisi yanafanywa katika matukio ya kisiasa kuliko ya kihalifu, jambo ambalo linatafsiriwa kwamba ni katika harakati za watawala kuzima changamoto za wanasiasa wanademokrasia, ambao ni tishio kwao kwa kuwa wanakosoa mamlaka zilizo madarakani.

Naye Katibu wa Jukwaa la Wahariri nchini Nevile

Meena, amesema harakati za waandishi wa habari h a z i t a k o m a h a d i p a l e waliohusika na mauaji wa marehemu Daudi Mwangosi wanakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.

A i d h a B w. M e e n a amesema wanaitaka serikali kuwahakikishia waandishi wa habari usalama wao kazini na sehemu hatarishi, na kuondoa sheria kandamizi za habari zilizopo hivi sasa katika katiba kwa kuruhusu sheria mpya zilizopendekezwa na wadau wa habari na wale wa sheria nchini.

P a m o j a n a k w a m b a tayari wadau wa habari walishawasilisha rasimu yao ya sheria ya habari serikalini miaka kadhaa iliyopita, hadi leo serikali imepiga kimya juu ya rasimu hiyo na kuendelea kukumbatia sheria ya habari kandamizi.

Naye mhariri mkongwe Masoud Sanan, akizungumza katika maandamano hayo, ameitaka polisi kurejesha komputa pakato (laptop) na kamera ya marehemu Daudi Mwangosi kwani sio mali yao.JUMLA ya yatima na wajane

131 wa Jijini Dar es Salaam w a m e b a h a t i k a k u p a t a misaada mbalimbali kama sehemu ya jamii inayohitaji kusaidiwa kutoka kwa ndugu zao Waislamu.

Misaada hiyo imetolewa Jumapili ya wiki iliyopita chini ya Taasisi ya Munira Madrasa and Propaga t ion Cen t re , iliyopo Magomeni Jijini Dar es Salaam.

“Leo tupo katika hafla hii tukiwa tunatekeleza kivitendo lengo la kuisaidia jamii. Kwa awamu hi i tumewatafut ia misaada mbalimbali wajane na yatima ambao kwa kiasi kikubwa wanahitaji huruma na msaada.” Alisema Ustadhi. Ally Salum Jongo

Akiongea kwa niaba ya Katibu wa Taasisi hiyo, (Ust. Juma Rashid) Ust. Jongo, alisema wahitaji hao wamegawanyika katika makundi mawili, ambapo kundi la kwanza ni la yatima wapatao 101.

Alisema, katika kundi hilo miongoni mwao ni yatima ambao wanasoma katika shule za Sekondari, ambao wao wamelipiwa ada.

“Miongoni mwao ni yatima wanaosoma shule za msingi, hawa tumewatafutia sare za shule na wengine ni watoto wenye hali ngumu hawa tumewapatia vyandarua.” Alisema Ustadh Jongo.

Akaongeza kuwa, kundi la pili ni la wajane wapatao

Madrasa Munira wasaidia yatima, wajane jijini DarNa Bakari Mwakangwale 30, ambao baadhi wamepata

pesa tasilim na wengine wamepata majokofu (friji) kama mitaji kwa ajili ya biashara ndogo ndogo.

Akasema, misaada hiyo ni midogo kulingana na mahitaji ya uendeshaji maisha pamoja na kwamba lengo la misaada hiyo ni kuwakwamua katika umasikini.

Ustadh Jongo alifafanua kuwa Munira Madrasa, inas imamia suala h i lo ikitambua wajibu wa jamii katika kuangalia yatima na wajane huku wakitaraji radhi za Mwenyezi Mungu.

Aidha, Usth . Jongo, aliitaka jamii kutokuwa mbali na makundi hayo katika jamii, kwa kuwapatia misaada kwa kiasi chochote, kwani alidai mbele ya Allah, wema na uovu hata wenye uzito wa mdudu chungu hulipwa.

“Tukiwa na nia ya dhati tukawa na mipango mikakati, basi yatima aliye jirani nawe hutoshindwa vazi la sikuku au hata mjane kumkidhi haja yake ya kimahitaji japo kanga kulingana na hali yako. Naomba tujipange vizuri katika kuiendea ibada hii.” Alisema Jongo.

Ta a s i s i y a M u n i r a Madrasa, ilianzishwa mwaka 1990, ambapo mbali ya malengo mengine, inasaidia jamii inayowazunguka katika masuala ya kijamii.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa ni Sheikh Yusuph Kidago, ambaye pia ni mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Munira Madrasa.

Page 7: ANNUUR 1034

7 AN-NUURSHAWWAL 1433, IJUMAA SEPTEMBA 14 - 20, 2012Makala

1

KINGDOM OF SAUDI ARABIA

COMMITTEE OF DA-AWAH IN AFRICA

MAJINA YA WASHINDI WA MASHINDANO YA FAMILIA YA MTUME (S.A.W.) NA SWAHABA 1433H/2012.

Yafuatayo ni majina ya washindi wa mashindano ya Familia ya Mtume na Swaha yaliyofanyika kati ya mwezi wa saba na wa nane 2012:

ZAWADI ALIYOPATA NAMBA YA SIMU JINA LA MSHINDI Na.

SAFARI YA HIJA 717710811 255+ SAID MOHAMED MOHAMED 1

SAFARI YA HIJA 71527054 255+ MBARAKA BAKARI SAID 2

SAFARI YA HIJA 777450642 255+ SAID MOHAMED IBRAHIM 3

KOMPYUTA (LAPTOP) 653459922 255+ AISHA KHALFAN 4

KOMPYUTA (LAPTOP) 776657806 255+ AISHA SULEIMAN NASORO 5

KIFAA CHA KUFUNDISHIA QUR'ANI

712734431 255+ ASIA MBELWA 6

KIFAA CHA KUFUNDISHIA QUR'ANI

773480284 255+ AZIZA MOHAMED NASORO 7

KIFAA CHA KUFUNDISHIA QUR'ANI

718480540 255+ SHIFAA OMARI 8

SIMU YA MKONONI 788162316 255+ SOFIA IBRAHIM HAJI 9

SIMU YA MKONONI 754740725 255+ KHALIL HASAN SOKA 10

WASHINDI WATAFAHAMISHWA KUPITIA NAMBA ZAO ZA SIMU NAMNA WATAKAVYO KABIDHIWA ZAWADI ZAO

Kuanzishwa BARAZA KUU 1992 Inatoka Uk. 4Waislamu wasihudhurie mkutano huo. Hata hivyo juhudi zao hizo hazikuzaa matunda kwani maelfu ya Waislamu walikutana Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika Ukumbi wa Nkurumah s iku ya Jumapili tarehe 15 Septemba, 1991.

M k u t a n o h u o ambao ulifunguliwa na aliyekuwa Waziri katika Ofisi ya Rais anayeshughulikia Ulinzi na Jeshi la Kujenga Tai fa , Mheshimiwa Abdurahman Kinana p a m o j a n a m a m b o meng ine u l ip i t i sha maazimio yafuatayo:

( 1 ) K u w a o n d o a mada rakan i Ka imu Makamu Mwenyekiti wa Bakwata Bwana Suleiman Hegga na Kaimu Katibu Mkuu Bwana Rajab Kundya.

(2) Kuteua kamati ya muda ambayo itasimamia shughuli za kila siku za Bakwata Makao Makuu na kuandaa Rasimu ya marekebisho ya Katiba ya Bakwata.

Kiutekelezaji azimio la kuwaondoa Bwana H e g g a n a K u n d y a

lilikwama. Aidha, kwa v i l e m a b w a n a h a o hawakukubali kuachia ofisi, kamati ya muda iliyoundwa kusimamia shughuli za kila siku za Baraza Makao Makuu ha ikuweza kufanya kazi.

Hata hivyo kamati i l i ende lea kuandaa rasimu ya marekebisho ya katiba ya Bakwata. Zoezi hilo lilipokamilika uliitishwa mkutano mkuu ambao ulifanyika katika ukumbi wa Diamond

Jubilee jijini Dar es Salaam.

Pamoja na kupitishwa kwa rasimu ya katiba Waislamu waliamua kulitwaa Bakwata kwa nguvu ambapo ofisi za Bakwata Makao Makuu, ofisi ya mkoa Dar es Salaam na shule ya Alharamain ilizingirwa na kuzuia watendaji wa ofisi hizo kuingia.

Ofisi hizo zilizingirwa kwa muda wa wiki moja hadi Rais Ali Hassan Mwinyi alipoingilia kati

na kuzikutanisha pande mbili, 11 Januari,1992. Viongozi wa Bakwata na viongozi wa kamati teule iliyowekwa na mkutano wa 15 Septemba,1991, walikubaliana mbele ya Rais Mwinyi kuwa zichaguliwe kamati za kusimamia uchaguzi toka ngazi ya chini hadi Taifa ambapo BAKWATA watatoa watu watano na “kamati teule” watu watano. Lengo lilikuwa k w a m b a e n d a p o uchaguzi utasimamiwa vyema watapatikana v iongoz i waad i l i fu wanaokubalika watakao simamia maendeleo ya Uislamu na Waislamu. BAKWATA walivunja makubaliano yale kwa madai kuwa, kwa kauli ya aliyekuwa Sheikh Mkuu wa BAKWATA Hemed bin Juma bin Hemed katika Baraza la Idd kule Shinyanga, kuwa Rais Mwinyi ameingilia kati kitu asichokijua asili yake na madhumuni yake. Akaeleza Sheikh M k u u h u y o k u w a BAKWATA iliundwa na Serikali iIi kudhibiti na kuzuia uanzishwaji wa vikundi mbalimbali vya Kiislamu vitakavyoweza kufanya harakati za kuleta maendeleo ya Uislamu na Waislamu. Katika Baraza hilo, Sheikh Mkuu a l imsik i t ik ia ndugu yake, Sheikh Mohamed Ali, kuwa aliponzwa na vijana wa “Warsha” aliowaingiza ndani ya BAKWATA ambao walikuwa na azma ya kusimamisha Dola ya Kiislamu hapa nchini, ikabidi alazimishwe k u j i u z u l u u k a t i b u Mkuu wa BAKWATA. Rais Mwinyi baada ya kugundua kuwa BAKWATA ni zimwi la watu, alizira na kujitoa katika usimamizi wa suluhu ile.

Kufikia hapo wale w a l i o k u w a k a t i k a harakati za kuirekebisha BAKWATA wakaona waiache BAKWATA kama ilivyo na waanzishe Baraza litakalo kuwa mbadala, Baraza Kuu la Jumulya na Taasisi za Kiislamu, kwa ufupi BARAZA KUU. Baraza Kuu lilisajiliwa rasmi mwaka huo wa 1992.

Page 8: ANNUUR 1034

8 AN-NUURSHAWWAL 1433, IJUMAA SEPTEMBA 14 - 20, 2012Makala

KUHARIBIWA kwa Syria sasa kuaendelea moto mmoja, Kilichoanza kama wimbi la kupinga serikali miezi 17 iliyopita sasa ni vita kamili ya wenyewe kwa wenyewe ikisukumwa na tawala za ukanda wa Ghuba na za kimataifa a m b a y o i n a h a t a r i y a kuenea katika eneo lote la Mashariki ya Kati. Jinsi m ap igan o k u zu n gu k a mji wa miaka mingi wa Aleppo yanavyoendelea kusugua na mauaji ya raia yanayofanywa na pande zote mbili yanaongezeka, hatari ya vita hivyo kuenea nje ya mipaka ya Syria inaongezeka.

Kubadilisha kambi kwa Waziri Mkuu wa Syria ndiyo hatua ya kusisimua zaidi katika mpango unaofadhiliwa kwa fedha nyingi, licha ya kuwa haielekei kuwa hatua hiyo inafikisha uwezekano wa kuanguka kwa utawala wa Syria hivi karibuni. Ila kukamatwa kwa mahujaji 48 wa Iran - au wapiganaji waliojificha kulingana na nani unayemwamini - pamoja na hatari inayoongezeka ya Uturuki kushambulia maeneo ya Wakurdi nchini Syria na kuingia kwa wapiganaji jihad kunatoa ladha ya kile kinachohofiwa kutokea.

Uingiliaji sasa unaielekeza Syria kutumbukia katika gizaNchi za Magharibi na Ghuba kuunga mkono wapiganaji waasi siyo kuleta uhuru kwa watu wa Syria ila kupanua ugomvi wa kidini na vita

Na Seamus Milne Kinachosukuma mgogoro huo ni uingiliaji wa nchi za magharibi na za ukanda huo. Hii siyo Irak, bila shaka, ikiwa na mamia ya maelfu ya askari (wa nje) kwenye ardhi yake, au Libya, ikiteketezwa na mvua ya mabomu kutoka angani.

Lakini kuongezeka kwa kasi kwa uingizaji wa silaha, kupeleka fedha na misaada ya kiufundi ya Marekani, Saudia, Qatar, Uturuki na nchi nyingine katika miezi ya karibuni, kumeongeza kwa kiasi kikubwa uwezo wa waasi, pamoja na wingi wa vifo.

B a r a c k O b a m a h a d i sasa amekataa miito ya wakereketwa wa kambi yake (ya kisiasa) wanaopenda vita na wahafidhina wanaotaka kuingilia kijeshi moja kwa moja. Badala yake ameruhusu kutumiwa mbinu za jadi za ushiriki wa CIA kutoa misaada ya kijeshi, kama nchini Nicaragua, kwa waasi wa Syria.

Marekani, ambayo ilifadhili mapinduzi ya kwanza ya CIA nchini Syria mwaka 1949, imekuwa kwa miaka mingi inafadhili vikundi vya upinzani. Lakini mapema mwaka huu Obama alitoa amri ya siri kuruhusu utoaji wa misaada kwa uwazi kwa vikundi vya upinzani, pamoja na kuwapa fedha na kuwaunga mkono kidiplomasia kwa siri. Hii ni pamoja na kuwekwa

kwa wanamgambo wa CIA katika uwanja wa vita, kuwekwa vituo vya kutolea amri na kusimamia mapigano, na misaada ya mawadiliano, pamoja na kufanikisha upelekaji wa silaha kutoka nchi za Ghuba kwenda kwa vikundi vya upinzani kupitia mpaka wa Uturuki.

Baada ya Russia na China kuzuia jaribio lake la mwisho la kupata baraka za Umoja wa Mataifa kubadilisha serikali nchini humo mwezi uliopita, Marekani ilieleza nia yake ya kuongeza misaada kwa wapiganaji wa upinzani na kuratibu mipango ya ‘serikali mpya’ kwa Syria kupitia Israeli na Uturuki.

“Utakuwa umeona katika miez i miwi l i i l iyop i ta upinzani umeimarika,”ofisa mmoja wa juu wa Marekani aliliambia gazeti la New York Times hivi karibuni. “Sasa tuko tayari kuharakisha hilo.” Ili asipitwe, William Hague (Waziri wa Mambo ya Nje) alitamba kuwa Uingereza nayo pia inaongeza ‘misaada isiyo ya maangamizi’ kwa waasi.

Tawala za kiimla za Saudia na Qatar zinatoa fedha na silaha, kama Baraza la Kitaifa la Syria linaloungwa mkono na Marekani lilivyokiri hivi karibuni, wakati mwanachama wa NATO, Uturuki, ameunda kambi ya kupeleka vifaa na kufundishia askari wa Jeshi Huru la Syria karibu

na au ndani ya kambi ya jeshi la anga la Marekani ya Incirlik.

Kwa wa tu wa Syr i a wanaotaka heshima na demokrasia katika nchi huru, utegemezi unaoongezeka kwa mataifa ya nje ni balaa - zaidi ya hata ilivyokuwa kwa Libya. Kwa mfano, inafahamika wazi kuwa maofisa wa utawala wa kidikteta na wa kundi moja la kidini wa Saudia ndiyo wanaoamua ni nani au kundi gani lenye silaha linapata fedha, siyo Wasyria wenyewe. Na ni maofisa wa kijasusi kutoka Marekani ambao wanasimamia kukamatwa kwa maeneo ya Syria na Israeli pamoja na tawala la kidikteta katika ukanda wote, ambao wanaamua ni makundi gani ya waasi yanapata silaha.

Waharakati wa upinzani wanasisitza kuwa watalinda uhuru wao wa kuamua ambao unatokana na kuungwa mkono na wananchi wengi nchini Syria. Ila mkondo wa misaada kutoka n je inaonyesha hatari ya wazi ya kugeuza makundi yanayotegemea wafadhili hao kuwa nyenzo zao, badala ya watu ambao wanataka kuwawakilisha. Utoaji wa fedha kutoka Ghuba tayari umefanya migawanyiko ya kidini kuwa mikali zaidi katika makundi ya waasi, wakati habari za watu wengi kutowaamini waasi huko Aleppo hivi ka r ibun i inadh ih i r i sha hatari za makundi ya waasi yanayotegemea watu wa nje na siyo jumuia zao wenyewe.

Utawala wa Syria ni wazi unaungwa mkono na Iran na Russia, kama ambavyo imekuwa kwa miongo kadhaa. Ila mfano unaofaa zaidi kwa ushiriki wa nchi za magharibi na za Ghuba katika uasi nchini Syria ingekuwa ni Iran na Russia kufadhili uasi wa kijeshi, tuseme nchini Saudia.

Kwa vyombo vya habari vya magharibi, ambavyo vimekuwa vikiripoti kuhusu Syria kama vile ni mkondo tu wa kupigania uhuru, ushahidi us iopingika wa utesaj i unaofanywa na waasi pamoja na kuuawa kwa mateka - pamoja na utekaji nyara unaofanywa na makundi ya aina ya Al Qaeda ambao kwa mara nyingine wanajikuta wakiwa katika upande mmoja na Marekani imekuja kama mshtuko kidogo.

Katika hali halisi hata hivyo, mzozo wa Syria miaka yote umekuwa na mapana na marefu yanayopenya katika nyufa za hatari zaidi za ukanda huo wote. Mzozo huo kuanzia mwanzo ulikuwa mkondo halisi wa kupinga utawala wa kiimla. Lakini umebadi l ika j ins i s iku

zinavyokwenda kuwa mzozo wa kijumuia ambako kundi la Walawi wanaoendesha serikali ya Assad limeweza kujitambulisha kama mlinzi wa makundi ya wachache nchini humo - Walawi, Wakristo na Wakurdi - dhidi ya mkondo wa upinzani wa mwelekeo wa ki-Sunni.

Kuingilia kati kwa Saudia na tawala nyingine za kiimla za Ghuba, ambazo zimejaribu kujilinda dhidi ya wimbi la jumla la kupinga uimla katika nchi za Kiarabu kwa kucheza kadi ya kupinga u-Shia kutaka madaraka, kuna madhumuni ya ushindi wa jumuia ya kidini, siyo matokeo ya kidemokrasia. Lakini ni upande wa tatu - wa Syria kuwa upande mmoja na Tehran (Iran) na kundi la kipiganaji la ki-Shia nchini Lebanon, yaani Hezbollah - ambayo imefanya mzozo wa Syria kuwa vita ya kuazima dhidi ya Iran na ugomvi mpana wa kimataifa.

Wengi katika upinzani nchini Syria watasisitiza kuwa hawana njia isipokuwa kukubali misaada kutoka nje ili waweze kujilinda dhidi ya ukatili wa utawala uliopo. Lakini kama mpinzani wa kujitegemea Haytham Manna anavyosema, kugeuza wimbi la upinzani kuwa harakati ya kivita kumedhoofisha msingi wake kiraia na kidemokrasia - na pia kuongeza kwa nguvu idadi ya waliokufa.

K u n a k i l a a i n a y a uwezekano kuwa vita hiyo itaenea nje ya Syria. Uturuki, ambayo ina idadi kubwa ya Walawi na wa-Kurdi ambao kwa miaka mingi wamekuwa wakikandamizwa, iliainisha haki yake ya kuingilia dhidi ya waasi wa ki-Kurdi nchini Syria, baada ya askari wa serikali (ya Syria) kuondoka katika miji ya wa-Kurdi. Mapigano yanayochochewa na mzozo wa Syria yamezidi nchini Lebanon, Ikiwa Syria i t agawanyika v ipande , mfumo mzima wa kuunda nchi baada ya kuanguka kwa himaya ya Kituruki utakuwa umeingia mashakani hali hiyo ikiwepo.

Hiyo inaweza kutokea bila kujali Assad na utawala wake wanadumu kwa muda gani. Lakini kuingilia Syria kunarefusha mgogoro, siyo kutoa pigo la mwisho la uhakika. Ni msukumo tu wa muafaka kutokana na majadiliano, ambayo nchi za magharibi na marafiki zao wamezuia kwa nguvu zote, ambayo yanaweza kuwapa watu wa Syria nafasi ya kuamua hali yao ya baadaye - na kuzuia nchi hiyo kutumbukia gizani.

(Agosti 08, 2012 ‘The Guardian’ (Uingereza) – Mfasiri kwa Kiswahili Anil Kija)

RAIS wa Syria, Dk. Assad al-Bashar akimjulia hali majeruhi wa machafuko ya Syria

Page 9: ANNUUR 1034

9 AN-NUURSHAWWAL 1433, IJUMAA SEPTEMBA 14 - 20, 2012Makala

“HAKIKA Firauni alitakabari katika ardhi, na akawafanya watu wa huko makundi mbalimbali. Akalidhohofisha kundi moja miongoni mwao, akiwachinja watoto wao wanaume na kuwaacha hai watoto wao wanawake. Hakika yeye alikuwa miongoni mwa waharibifu kabisa” Qur(28:2).

Katika Aya hizo za Qur’an, Mwenyezi Mungu Mtukufu anawapasha habari Waislamu kuhusu mtawala muovu na dhalimu aliyepata kutokea katika Misri ya kale, ambaye alikuwa akiwabagua wananchi wake; akilipendelea kundi moja na lingine akilikandamiza. Mtawala huyu, maarufu kama Firauni, kwa sababu ya uovu wake, Mwenyezi Mungu amehifadhi historia yake mpaka leo, ili iwe fundisho la kudumu kwa binadamu watakaokuja baada yake.

Kisa cha Bani Israili na Firauni ndani ya Qur’an Tukufu kinasisimua sana na kina mafunzo mengi mno. Tuangalie kidogo Aya hizo za Mwenyezi Mungu kuhusu Firauni na kadhia ya Waislamu wa Tanzania kugomea Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012. Kwa mtu mwenye uwezo duni wa kufikiri, anaweza kudhani Waislamu ni wakorofi tu, na walikuwa na lengo la kuhujumu zoezi la sensa kwa maendeleo ya taifa.

Jambo la msingi ambalo halizingatiwi katika kadhia hii ni kwamba Waislamu wanafahamu sana hatari ya kupunguzwa idadi yao. Qur’an imeshawapa elimu ya kutosha kuhusu mbinu za watawala madhalimu. Kwa mujibu wa Aya tulizotanguliza kutoka Surat Qasas, Firauni alikuwa akiwachinja watoto wa kiume wa Bani Israili, ili kudhibiti idadi ya watu wa jamii hiyo. Alikuwa anaogopa siku moja utawala wake wa kidhalimu ungeangushwa na wale aliokuwa akiwabagua na kuwakandamiza.

Hapa kwetu, kama ilivyokuwa wakati wa Firauni kule Misri, t u m e w e k e w a m f u m o w a kibaguzi kwa misingi ya dini, ambapo kundi moja la wananchi (Wakristo) linapendelewa na Utawala na kundi l ingine (Waislamu) linakandamizwa. Mfumo huo wa k ibaguzi umeasisiwa na wakoloni na kuendelezwa na baba wa taifa, hata baada ya uhuru. Tofauti yake na mfumo wa Firauni ni mbinu tu za kufikia malengo yale yale!

Wakati Firauni alikuwa akiwachinja kabisa (physically) watoto wa Bani Israili, hapa kwetu wanaotawala nchi wanawach in j a Wa i s l amu Kisaikolojia. Wanataka Waislamu wajihisi wanyonge na dhaifu kwa kuwa idadi yao ni ndogo mno ikilinganishwa na wenzao Wakristo. Lengo ni kuhalalisha

Sensa Tanzania, kisa cha Firauni na Bani IsrailiNa Said Rajab

ASKARI Polisi wakiwa na mitutu yao wakimlazimisha mmoja wa Waislamu kujiandikisha sensa kwa nguvu jijini Arusha.hujuma wanazowafanyia au wanazopanga kuwafanyia Waislamu. Kupunguza idadi ya watu wa kundi moja katika nchi moja, iwe ‘physically’ au ‘psychologically’, nia yake hasa siyo njema. Hiyo ni sehemu tu ya mpango mpana zaidi wa kuhujumu kundi hilo.

Wakati wa uongozi wa Nyerere (1961- mpaka sasa), Wakristo wamekuwa na uhuru mkubwa wa dini yao, ambao umelindwa vizuri na Katiba ya nchi. Uhuru wao ni pamoja na kuwabatiza Waislamu na kuwahubiria Injili. Lakini Waislamu, walio wahanga wa kubatizwa, hawakuwa na ruhusa wala uhuru wa kupanga na kuendesha mambo yao wenyewe, bila ya kuingiliwa na mamlaka kuu ya nchi.

Masuala yote yanayowahusu Wa i s l a m u w a Ta n z a n i a , yakawekwa mikononi mwa Bakwata, baraza lililoundwa kwa minajili ya kuwahujumu Waislamu wa Tanzania, baada ya Nyerere kuvunja chombo kilichoundwa na Waislamu wenyewe , kwa l engo l a kusimamia maendeleo yao eneo zima la Afrika Mashariki. Bakwata linafanyakazi chini ya ulinzi na maelekezo ya serikali inayoendeshwa kwa misingi ya mfumo wa kuwapendelea Wakristo.

Serikali inaweza kusema takwimu zilizotolewa na baadhi ya taasisi na kuonyeha Waislamu Tanzania ni wachache siyo rasmi na hazitoki ofisi ya taifa ya takwimu, lakini Waislamu walianza kulalamika mapema sana kuhusu takwimu hizo,

na serikali kama kawaida yake ikapuuza malalamiko ya Waislamu. Mpaka pale Waislamu walipoamua kugomea sensa ya mwaka 2012, ndipo serikali ilipogutuka na kuanza kutoa vitisho na kauli za hadaa.

Waislamu walikuwa na haki ya kugomea zoezi la Sensa kwa sababu madai yao ya msingi yamepuuzwa. Wale wanaotamani Waislamu waonekane wachache, ndani na nje ya nchi, wakati wanajua kwamba ni wengi kuliko wao, wana malengo ya Kifirauni dhidi ya Waislamu. Msimamo madhubut i wa Waislamu katika sensa ya mwaka huu umewaumbua! Wanagwaya kukabiliana na hoja za Waislamu kutokana na uzito, mantiki na ukweli wake. Wao wamezoea uongo, hila, ghushi na kupendelewa.

Wanadai Serikali haipangi mipango ya maendeleo ya wananchi kwa kuzingatia dini. Kama hiyo ingekuwa kweli, basi miji yote ya Waislamu kama Kilwa, Pangani, Kigoma, Bagamoyo, Mafia, Rufiji, ambayo ilishakuwa miji mikubwa tangu zamani isingeachwa idumae. Kilwa ilikuwa kitovu cha biashara kabla ya kushambuliwa na Wareno (Wakristo) mwaka 1505. Sasa imebaki magofu tu ya kihistoria. Bagamoyo pia ulikuwa mji na bandari maarufu, lakini ukaachwa ufe kwa sababu mipango ya Serikali haitaki dini ya wananchi wa Bagamoyo!

Jambo l a ku t i a f a r a j a katika sensa ya mwaka huu ni mwamko mkubwa wa Waislamu kuigomea. Inafurahisha sana kuona Waislamu wanamjua

v izur i adui yao , ambaye amejificha kwenye kivuli cha Serikali, na wanaunganisha nguvu zao kumkabili kwa vitendo. Hiyo ni hatua kubwa sana. Waislamu wanamfahamu anayekwamisha OIC, wanamjua anayefelisha watoto wao Baraza la Mitihani, na pia wanamtambua anayevuruga mchakato wa Mahakama ya Kadhi. Kupitia sensa ya mwaka huu, Waislamu wametoa indhari kwamba wako tayari kukabiliana na yeyote anayepanga kuwahujumu. Uislamu kwanza, Utanzania baadaye!

Kupitia makala hii fupi, ningependa kutoa pongezi zangu za dhati kwa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, ambazo zilikuwa pamoja na Waislamu mpaka dakika ya mwisho katika ajenda hii ya kugomea sensa. Vyombo vya habari vya Waislamu, hususan Radio Imaan, Radio Kheri, Radio Nnuur, Radio Qiblatein na gazeti la An-nuur, kwa kweli vimefanya kazi nzuri inayostahili kupigiwa mfano. Vyombo hivi kusema kweli, ndivyo vilivyowaunganisha Waislamu kwenye ajenda hii ngumu lakini muhimu. Vimekuwa na ‘Istiqama’ ya kweli na kamwe havikuwasaliti Waislamu, licha ya kuwepo vitisho, hadaa na vishawishi vingi.

Tumeshuhudia vyombo vingine, vinavyoitwa vya ‘Waislamu’ vikifanya juhudi za makusudi kuwagawa Waislamu katika ajenda hii muhimu! Wakati wa zoezi la sensa, vimehujumu umoja wa Waislamu; siku mbili baada ya zoezi hilo, vinasisitiza

umoja, udugu na mshikamano wa Waislamu! Akili za Waislamu siyo fupi kiasi hicho. Wana maarifa ya kutosha kumtambua ndugu wa kujenga naye umoja na adui wa kumuepuka, ingawa wote wanaweza kuonekana ndugu kwa su ra ya n je . Mwenyezi Mungu anawachukia sana wale wanaosema mambo wasiyoyatenda:

“Enyi Mlioamini! Mbona mnasema ms iyoya tenda? Ni chukizo kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu kusema msiyoyatenda. Kwa yakini Mwenyezi Mungu anawapenda wale wanaopigana katika njia yake safusafu; kama kwamba wao ni jengo lililokamatana barabara” Qur(61:2-4)

Tumeona pia masheikh maslahi wakiwashambulia Waislamu waliogomea sensa, huku wakipotosha kwa makusudi sababu hasa zilizowafanya Waislamu wagome kuhesabiwa. Masheikh hawa, vigeu vigeu, mara zote wamekuwa silaha kali ya maadui dhidi ya Waislamu wenzao. Wanapigana vita upande wa maadui, huku wakidhani Waislamu ni wajinga sana hawatajua. Hawa ni wanafiki! Kama huwafahamu, unaweza kudhani ni watu wa maana sana. Kwa sababu ni fasaha wa lugha, wanavaa vizuri, wananukia udi, wanatembea na tasbihi kubwa mkononi, lakini ni maboya tu! Mwenyezi Mungu mwenyewe anawaeleza vizuri ndani ya Qur’an:

“Na unapowaona miili yao inakupendeza, na kama wakisema unasikiliza usemi wao (kwa vile unavyopendeza); lakini wao ni kama boriti zilizoegemezwa, wanadhani k i la k i sh indo (kinachozuka) ni juu yao (ni cha kuwatafuta wao). Hao ni maadui, jihadhari nao. Mwenyezi Mungu awaangamizilie mbali! Vipi wanapotoka na haki!”Qur (63:4).

Kwa mujibu wa Aya hizo za Qur’an, wanafiki hawatambuliki kwa muonekano wao wa nje au kwa namna wanavyojieleza. Huwa wana j i t ah id i s ana kuonekana Waislamu safi kwa kujiweka nadhifu wakati wote. Ni vigumu kidogo kuwatofautisha na Waislamu wengine waadilifu. Hata hivyo, ukituliza akili kidogo tu utawajua, kwa sababu wanaugua maradhi ya uchafu wa roho, ambayo yameingia katika kila kipengele cha maisha yao. Katika Aya...”Basi wapuuzieni mbali. Bila shaka wao ni najisi na makazi yao ni Jahanamu” (9:95), Mwenyezi Mungu anatupasha habari za ndani kabisa kuhusu wanafiki na anataka tuwaepuke.

Nuru ya imani kamwe haionekani kwenye nyuso za wanafiki, kwa sababu mawazo yao wakati wote yanafikiria kupanga uovu, kula njama, kufanya hadaa, kulipiza kisasi, kupika majungu, kusambaza

Inaendelea Uk. 10

Page 10: ANNUUR 1034

10 AN-NUURSHAWWAL 1433, IJUMAA SEPTEMBA 14 - 20, 2012Makala

Na Khalid S Mtwangi

Sensa Tanzania, kisa cha Firauni na Bani IsrailiInatoka Uk. 9chuki, fitna, uongo, propaganda na kuona gere. Wamekalia hayo tu na wala hawana mpango wowote wa kuinusuru jamii ya Waislamu.

Mashe ikh zangu , Al ly Bassaleh, Salim Barahiyan, Ponda Issa Ponda, Mohammed Issa, Farid Hadi, Mussa Kundecha, Kondo Bungo na wengine kama hao, Mwenyezi Mungu awalipe malipo mema kwa kusimamia kikamilifu ajenda za Waislamu bila woga wala kutanguliza maslahi binafsi. Msimamo wenu madhubuti kama viongozi wa dini ya Kiislamu umetujengea heshima wote.

Kupigania haki za Waislamu kwa dhati kabisa ni jambo la

hatari katika nchi kama zetu. Ni kujitoa muhanga! Si wote wanaoitwa Waislamu wanaweza, isipokuwa wale tu waliofunga ahadi na Mwenyezi Mungu na kutarajia malipo kutoka kwake. Mmekuwa na msimamo usioyumba mara zote maslahi ya Waislamu yanapohatarishwa. Mwenyez i Mungu nd iye anayewajua zaidi waja wake wa namna hii:

“Wapo watu miongoni mwa walioamini waliotimiza ahadi wal iyoahid iana na Mwenyezi Mungu: Baadhi yao wamekwishamaliza umri wao (wamekwisha kufa), na baadhi yao wanangoja (siku yao kufika), wala hawakubadilisha (ahadi yao) hata kidogo” Qur(33:23)

ZOGO la sensa limeleta m a f u n z o m e n g i k w a Waislamu na wasio kuwa Waislamu. Lililojitokeza kwa wazi zaidi, ingawa limekuwa likijulikana kila siku, ni ile dharau waliyonayo wasio Waislamu na wakiionyesha wazi wazi juu ya Uislamu na Waislamu. Kwa kukumbusha tu hebu tafakari aliyoyasema Askofu Mkuu wa Anglikana Muhasham Mokiwa. Kweli m t u m i s h i w a M u n g u anathubutu kutumia lugha ya namna hiyo anapohusisha Uislamu! Waislamu tafadhali amkeni; hawa jamaa wanajua kabisa mmelala fofofo ndio maana wanapata kibri cha kiasi hicho.

Hakika mantiki ingemtuma mtu yeyote mwenye busara na mpenda haki anaweza kumkumbusha Baba Askofu M k u u k u w a Wa i s l a m u wamepinga sensa kutokana na zile dhulma wanazo twishwa na wafuasi wake walio madarakani katika Serekali. Basi ni wao Waislamu ndio wangestahili na wangekuwa na haki ya kusema kuwa “uvumilivu sasa basi”. Wao ndio wamekuwa wakionewa na kunyimwa haki zao kila siku hasa tangu nchi hii ipate uhuru. Watakacho wao watapata kwa njia za haki salama ama za nguvu.

Jambo la pili ambalo ni lakusikitisha zaidi ni kutanabahi kuwa kumbe kusoma sana sio kuelimika. Ufinyu wa mawazo na kutotambua mengi zaidi ya yale aliyofundishwa seminari vimedhihirika wazi sana sasa kuliko wakati wowote ule. Labda rai hii inaweza kuonekana kuwa kama ni upuuzi kwa vile viongozi wengi wa makanisa ni watu waliosoma sana wakiwemo wengi wenye shahada mpaka tatu na wakiitwa Rev. Daktari huyu ama Rev. Dak ta r i Askofu yule. Lakini kama ilivyodokezwa, mtu anaweza kusoma bila kuelimika, hivyo anapatikana mhandisi ambaye kila daraja analolisanifu na kulijenga linaporomoka. Hivyo hivyo padri ama Askofu ambaye kila anapojaribu kutafsiri ama kufasiri mafundisho ya dini yake yeye anatibua tu.

Ni bahati mbaya kabisa kuwa upotoshaji huu ndio unarithishwa kwa wafuasi wanaofurika makanisani siku za Jumapili. Hawana jingine wanalolifahamu, na mfano mzuri

Shangwe kwa Mapadri na Wachungaji Tanzaniani kama yule mwandishi wa habari aliyeapa kuwa atapigana vita (silaha ikiwa kalamu ama zana zingine) kuhakikisha kuwa Tanzania haitajiunga na OIC wala kurudisha Mahakama ya Kadhi. Hakika huo ni ufinyu wa mawazo ambao unaweza kustaajabisha kuwa anao mwandishi wa habari. Wanataaluma hawa hutegemewa kuwa na upeo mpana wa mawazo kwa vile kazi zao zinawataka wasome sana vitabu vya kila fani, majarida na magazeti mengi pia. Sio kuyasoma tu bali waelewe fika wanayoyasoma.

Ni bahati mbaya kuwa wengi wa waandishi wa Tanzania hakika inaelekea si wasomi wa v i tabu ama magazet i zaidi ya yale wanayohariri ama wanayoyafanyia kazi. Mjadala uliozuka kuhusu sensa umedhihirisha hayo. Waandishi wengi waliridhika na kunukuu maono potofu ya upande mmoja tu; wale waliokuwa wakipinga hawakupewa nafasi ya kueleza yao ili wananchi wapate nafasi ya kuwaelewa. Linganisha hali hii na wale waandisi katika magazeti ya Kenya kwa mfano wakati huu wa rabsha zilizotokea Mombasa hivi juzi. Hawa wanapoandika makala ama habari zozote kuhusu Uislamu na Waislamu, wao mara nyingi hawasumbuliwi na Ukristo wao ama kuwa na dharau. Huwa “objective” kiasi kwamba huwashambulia kwa hoja nzito nzito viongozi wa makanisa wanaoonekana wanapotosha ukweli. Mwandishi huyu kwa mfano ameweza kuwanukuu Professor Phillip Ochieng mara nyingi.

Haijatokea hata siku moja mwandishi katika magazeti ya Tanzania aliyekuwa na mawazo ya wazi kama hayo. Lazima wafuate ule ukali na mawazo mgando yaliyopandikizwa na baba askofu ama nabii au mtume anayehakikisha kuwa anajitokeza akiwa katika suti ya thamani kabisa ili kuwatisha na kuwakoga waumini.

Hawa waandishi na Wakristo wengine wa nchi hii pia inaelekea wameachwa nyuma na wenzi wao wa Ulaya. Kuna baadhi ya waandishi hawa na Wakristo wengine wengi tu wanaoona kuwa Ukristo na utamaduni w a k i M a g h a r i b i n i k i t u kimoja. Huko Ulaya hivi sasa wanaoitwa Wakristo wameamka k ias i kuwa inasemekana idadi ya wale wanaohudhuria kanisani imepungua sana. Hakika wanajiuliza maswali mengi kuhusu Ukristo kama unavyohubiriwa hivi leo.

Bila shaka kuna wasomaji wengi wanaomfahamu au wamemsikia Professor Hans Kung wa Ujeremani. Huyu alikuwa akifundisha Ecumenical Theology huko Chuo Kikuu Tubingen, akiwa pamoja na Joseph Cardinal Retzinger ambaye leo hii ni Papa Benedict XVI. Lakini urafiki wao ulizorota sana wakati Joseph Cardinal Retzinger alipohamia Vatican

na kuwa kiongozi wa kitengo ambacho zamani kilisimamia “inquisition”. Huyu Professor Hans Kung alikuwa na mpaka leo hakubaliani na mafundisho mengi ya kanisa na maandishi yake yamekuwa ni mwiba ukilichoma Kanisa kiasi kwamba alipigwa marufuku kuingia Vatican na kusimamishwa kazi ya Ualimu.

B i l a s h a k a b a a d h i y a wasomaji watakumbuka huyu Prof. Hans Kung alitembelea Tanzania katika miaka ya themanini. Ilikuwa aendeshe mihadhaa siku mbili mfululizo pale Goethe Institute. Waislamu wengi walihudhuria siku ile ya kwanza wakiongozwa na Al Marhum Sheikh Abubakar Juma Mwilima. Maswali aliyoulizwa na hoja zilizotolewa na Waislamu hao zilikuwa nzito kiasi kwamba ule muhadhara wa siku ya pili ulifutwa bila maelezo yeyote.

Professor Kung aliandika makala ambayo ilichapishwa kwanza na The New York Times na kunukuliwa na THE DAILY NATION ya Kenya ya tarehe April 17, 2006. Kuna paragraph moja inasomeka hivi:-

“Given all the DEFECTS OF CHRISTIANITY AND THE POSITIVE POINTS OF OTHER FAITHS, will this Pope be able to combine his conviction of the truth of his own faith with respect for the truth of other faiths?”

Tafsiri “Kutokana na YALE MAPUNGUFU YALIYOMO KATIKA UKRISTO NA NUKTA ZA UHAKIKA ZILIZOMO KATIKA IMANI ZINGINE, jee Papa huyu ataweza kuunganisha anayoamini kuwa ni ukweli katika imani yake pamoja na kuyapa heshima ukweli na uliomo katika imani zingine?”

Msisitizo ulioko katika nukuu hii ni wa mwandishi wa makala haya.

Inasikitisha kuwa mwalimu huyu wa mafunzo ya dini ya

Kikristo anaelewa kuwa kuna ukweli katika dini zingine lakini wengi wa wasomi Tanzania hawaelewi hayo. Huvalia tu vibwebwe vita vya kuwadhulumu Waislamu wa nchi hii haki zao. Labda huu unaweza kuwa wimbo ambao wengi watasema wamechoka nao; lakini ni muhimu kuwakumbusha kila mtu hali ilivyokuwa na ilivyo hivi sasa. Lakini wanaweza kubadilika?

Wa s o m a j i w a t a k u w a wamemsikia Mtakatifu Ignitius wa Loyola ambaye alikuwa akijulikana kama DON INIGO LOPEZ DE RECALDO wa LOYOLA ambaye nd iye aliyeanzisha utawa wa Jesuits. A l i k u w a n a m a d h u m u n i mawili:-

“Ignatius de Loyola created the Jesuits to secretly accomplish two major goals for the Roman Catholic Church: (1) Universal political power and (2) a universal church.” Yaani madhumuni ya

utawa huwo ni kushika utawala wa kisiasa wa dunia nzima na kulifanya Kanisa Katoliki ndilo lenyewe tu duniani.

Haya yameandikwa na Dr Alberto Rivera katika kitabu The Secret History of the Jesuits ambaye yeye alikuwa ni Jesuit Priest. Huyu Mtakatifu Inigo de Loyola ana historia yake ambayo mambo yake mengi hayakuwa matakatifu.

Ushahidi uliopo ni kuwa wengi wa waandishi wa habari, Tanzania na wafuasi wa dini ya Kikristo kwa jumla, wawe Anglican ama Pentecoste hawayafahamu haya. Mapadre, paroko, manabii na mitume wapiga masuti wanafanya kazi nzuri kabisa kuwafundisha waumini wao kuwa na akili mgando. Wasilofundishwa na hawa, basi halipo duniani.

Subhana wa Taala awanusuru Waislamu na mawazo finyu kiasi hicho na mazingira ya aina hiyo.

WAISLAMU wakiswali nje ya Wizara ya Mambo ya Ndani kutaka wenzao waliokamatwa nchini kote kufuatia sakata la sensa kuachiwa mara moja.

Page 11: ANNUUR 1034

11 AN-NUURSHAWWAL 1433, IJUMAA SEPTEMBA 14 - 20, 2012Makala

KATIKA siku tulizonazo a m b a p o u l i m w e n g u umegawanyika vipande vipande kwa kutokua na uaminifu pamoja na siasa za kinafiki katika ngazi ya taifa pamoja na ya kimataifa, ni muhimu sana kuhakikisha umuhimu wa ahadi katika jamii ya Kiislamu iwekwe wazi, kwa sababu katika kipindi cha kisasa ambacho kinaitwa ‘’Kimaendeleo” a h a d i p a m o j a n a makubaliano zimekuwa hazina thamani zaidi ya kuwa kwenye makaratasi yaliyochapishwa tu. Allah amesema: “Je, anayejua ya kwamba yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Mola wako ni haki (akayafuata, basi) ni kama aliye kipofu? Wenye akili ndio wanaozingatia; (Nao ni hawa) Ambao wao hutimiza ahadi ya Allah wala hawavunji ahadi (za wanaadamu wenzao); Na ambao huyaunga aliyoamuru Allah yaungwe, na humuogopa Mola wao, na huiogopa hisabu mbaya (itakayowapata wabaya huko Akhera, kwa hivyo wakajitahidi kujiepusha n a v i t e n d o v y a o h a o wabaya); Na ambao husubiri (wakastahmilia wenziwao) kwa kutaka radhi za Mola wao, na wakasimamisha Sala na wakatoa katika vile Tulivyowapa, (wakavitoa) kwa siri na dhahiri , na wakayaondoa maovu kwa mema. Hao ndio watakaopata malipo (mema) ya nyumba (ya Akhera); Mabustani ya milele watayaingia wao (pamoja) na waliofanya wema miongoni mwa wazee wao na wake wao na kizazi chao. Na Malaika wanawaingilia katika kila milango; (Wanawaambia): ‘Iwe amani juu yenu, kwa sababu mlisubiri (mlistahmili k a t i k a k u f a n y a m e m a na kuacha mabaya na mkastahmiliana mkakaa vizuri na wenzenu).’ Basi ni mema yaliyoje matokeo ya nyumba (ya Akhera kwa wanaomcha Allah); Na wale wanaovunja ahadi ya Allah (na za wanaadamu wenzao) baada ya kuzifunga, na wanakata aliyoamuru Allah yaungwe, na wanafanya uharibifu katika ardhi; hao ndio watakaopata laana, na watapata nyumba mbaya.” (Surah ar-Ra’d, 13: 19-25).

Allah ni mkweli katika ahadi Zake na msimamo thab i t i ka t ika maneno Yake . Kwa h iyo wa le wanaojitangaza kuwa ni watumwa Wake nao pia ni lazima wawe imara katika ahadi zao na wawe wakweli kwa yale waliyokubaliana. Ni

Umuhimu wa kutekeleza ahadiNa Munir Ahmad Mughal, B.A., LL.B., D. Pharm.

WAISLAMU Jijini Dar es Salaam wakiwa katika maandamano ya kupinga dhulma zinazofanywa na NECTA kwa wanafunzi Waislamu shule za Sekondari nchini.

moja kati ya sifa za Muislamu wa kweli kwamba chochote wanachoahidi hut imiza na k i la wanachotamka hutekeleza. Na ni heshima kwa Muislamu wa kweli kutokwenda kinyume katika jukumu lolote alilochukua kulitekeleza. Hata kama itabidi kuondoa milima au kukausha bahari Muislamu wa kweli atakamilisha ahadi yake.

Kwa kawaida neno ahadi linamaanisha ‘Makubaliano’. K i s h e r i a m a a n a y a k e ni makubaliano baina ya pande mbili zinazoshindana, juu ya jambo la kisheria kwa hiari zao, kwa malipo yanayokubalika kisheria pamoja na muamala wa kisheria ndani ya vifungu vya ahadi. Kwa hiyo neno hili dogo limejumuisha tabia za mwanaadamu kiakili, kisheria, kimaadili na kidini.

Q u r - a n t u k u f u imeigawanya ahadi katika mafungu matatu. Ahadi ya kwanza ni ile ambayo mwanadamu anaingia pamoja na Muumba wake na hii inaitwa ‘Ahadi ya Asili’. Hii ni ahadi, ambayo utekelezaji wa ahadi hii yalifanywa siku ya kwanza ya uumbwaji na utekelezaji wake, ni wajibu kwa kila mmoja wetu.

Ahadi ya pili ni ile iliyoingiwa kwa jina la Allah katika umbo la ahadi. Ahadi ya tatu ni ile ambayo kwa kawaida inafanywa kati ya pande mbili katika shughuli zao za kila siku. Inajumuisha zile ahadi ambazo zinatokea

ghafula na kuhamisha na kusababisha kukabidhi ahadi hiyo kwa mtu mwengine. A l l a h ( A l i y e t u k u k a ) ametuma amri zilizo wazi ili zitekelezwe na kila mmoja katika makundi matatu haya ya ahadi.

Allah amesema: “..Na mnaposema (katika shahada na penginepo) semeni kwa uadilifu hata kama ni jamaa wako wa karibu (usimpendelee kwa ajili ya ujamaa uliyo baina yenu). Na tekelezeni ahadi ya Allah. Amekuusieni haya ili mpate kukumbuka.” (Surah al-An’am, 6: 152).

Allah pia anasema: “Na timizeni ahadi mnazozitoa kwa Jina la Allah mnapoahidi; wala msivunje hizo ahadi baada ya kuzithubutisha, hali mumekwisha mfanya Allah kuwa shahidi wenu. Hakika Allah anayajua (yote) mnayoyafanya.” (Surah al-Nahl, 16: 91).

Allah pia amesema: “Na wala msiyakaribie (msiyaguse) mali ya yatima, isipokuwa kwa njia iliyo bora (kwa hao mayatima) mpaka afike baleghe yake (huyo yatima akabidhiwe mwenyewe). Na timizeni ahadi. Kwa hakika ahadi itaulizwa (Siku ya Kiyama). N a t i m i z e n i k i p i m o mnapopima; na pimeni kwa mizani zilizo sawa. Hayo ni wema kwenu na bora mwishoni (kwake).” (Surah Bani Israil, 17: 34-35).

Vile vile Allah amesema: “Na ambao amana zao na ahadi zao wanaziangalia

(wanazitekeleza).”(Surah al-Mu’minun, 23: 8).

Na pia Allah amesema : “ N a w a l e w e n y e kutekeleza ahadi zao pindi wanapoahidi.”(Surah al-Baqarah, 2: 177).

Katika muktadha ‘Al’na aina zote za ahadi kadhalika na mikataba inajumuisha pia miongoni mwa maana zake ni haki za kurithi kwa binadamu na haki za Allah.

Katika nukuu zilizotajwa katika kitabu kitukufu aina zote za ahadi pamoja na mikataba zimetajwa. Katika historia ya Uislamu kuna mifano mbalimbali juu ya kutimiza ahadi na hii inawapa mwangaza Waislamu juu ya utekelezaji wa kazi pamoja na ukweli.

Vi le v i le mkataba ulifungwa huko Hudaibiyya na wasiokuwa Waislamu. Mashari t i yal iyowekwa katika mkataba huu yalikuwa kinyume na matakwa ya Wa i s l a m u k a d h a l i k a wanasiasa. Lakini baaada ya makubaliano haya matakatifu w a s i o a m i n i w a l i a n z a kushindwa na Waislamu wakashinda. Katika hali hii haikuwa vigumu kwa Waisilamu kuvunja mkataba huo bali ilikuwa ni wakati muafaka ambapo imani ya Waislamu iliweza kujaribiwa ili kuthitisha ni kwa kiasi gani watu hawa walioamini wataweza kuwa na msimamo katika maneno yao. Hivyo ndio maana Allah aliwaonya ku tunza ahad i zao na akawaamrisha kutovunja

m k a t a b a h u o . I n g a w a waliruhusiwa kupigana dhidi ya washirikina waliovunja mkataba, na ingawa walivamia Makkah, makubaliano ya miezi minne yaliwekwa kwa washirikina hao.

Allah anasema: “(Hili ni) tangazo la kujitoa katika dhima (ahadi), litokalo kwa Allah na Mtume Wake, kwa wale mlioahidiana nao miongoni washirikina. (Waambieni): ‘Basi tembeeni katika nchi miezi minne (kwa salama, kisha vitakuwa vita baina yenu na sisi); na jueni kwamba nyinyi hamuwezi kumshinda Allah, na kwamba A l l a h n d i y e M w e n y e kuwadhalilisha makafiri.’” (Surah at-Tawba, 9: 1-2).

Pale Uislamu unapoagiza kukamilishwa kwa ahadi na Waislamu, hivyo hivyo wanataraji hayo hayo kutoka kwa wengine. Uislamu unaheshimu wale wanaofanya hivyo , wakiwa katika dini yoyote.

Allah anazungumzia wenye kuabudu masanamu walioheshimu mkataba wa hudaibiyya,

A l l a h a n a s e m a : “ I s i p o k u w a w a l e mlioahidiana nao miongoni mwa hao wash i r ik ina , kisha hawakukupunguzieni c h o c h o t e w a l a hawakumsaid ia yoyote juu yenu, basi watimizieni ahadi yao mpaka muda wao. Hakika Allah anawapenda wanaomuogopa.” (Surah at-Tawba, 9: 4).

Allah kwa mara nyingine a n a w a o n y a Wa i s l a m u kutohal i fu mkataba na makafiri, Allah anasema: “Itakuwaje kuwapo ahadi na washirikina mbele ya Allah na mbele na Mtume Wake i s i pokuwa wa l e mlioahidiana nao mbele ya Msikiti mtukufu (al-Ka’ba, na wakatekeleza ahadi zao)? basi maadamu wanakunyookeeni k w a u z u r i , n a n y i p i a wanyokeeni kwa uzuri , Hakika Allah anawapenda wanaomuogopa.” (Surah at-Tawba, 9: 7).

Katika aya hii ‘kuchunga majukumu yao’ inamaanisha ‘kuchunga makubaliano’.

Wale wote wanaochunga maneno yao wanazingatiwa kuwa ni wacha Mungu. Katika lugha ya Qur’an Muttaqi ni neno la kumtukuza mja. Muttaqi ni wale ambao watapata furaha ya Allah pamoja na mapenzi yake.

Katika kitabu kitukufu neno ‘Aqd’ (umoja) au ‘uqud’(wingi) hutumika kumaanisha ‘Ahd’. ‘Ahd’ ina maana ya ‘kufunga fundo’ na inaonyesha umuhimu wa kukamilisha makubaliano ambayo mtu huingia katika

Inaendelea Uk. 13

Page 12: ANNUUR 1034

12 AN-NUURBarua/Shairi SHAWWAL 1433, IJUMAA SEPTEMBA 14 - 20, 2012

Ndugu Mhariri,Assalaam alaikumNaomba niwafahamishe wananchi wa Kilwa kuwa kitendo kilichofanywa na Mbunge wao kwenda kuwaona wapiga kura wake waliokamatwa kwa dhulma kwa madai kuwa wamegoma kuhesabiwa, kiwe mfano kwa wabunge

Hongera Mbunge Kilwawengine.

Tunawaomba watu wa Kilwa wawaunge mkono wabunge kama hawa. Pia nitoe changamoto

kwa Waislamu kuwalinda wabunge kama hawa kwani historia inaonyesha kuwatisha na kuwashughulikia vibaya w a b u n g e w a n a o j i t o a kupigania haki za wanyonge.

Mfano yuko wapi leo mbunge Msambia?

Huyu alitetea haki za wanyonge Waislamu kwa kusema tu pale bungeni, lakini MFUMO uliahidi hatorudi bungeni na kweli hakurudi uchaguzi uliofuata.

Salum Hamisi na Mazo Matata

Temeke, Dar es Salaam

Salamu alaikum, kwanza nakusalimuniNinyi nyote Isilamu, mlio Bara na PwaniNimeishika kalamu, lengo kukukumbusheniMbuyu kuwa mnene, chanzoche kama mchicha Hakika shule za kata, zilizojaa nchiniUkiamua kupita, mengi utayabainiMazuri utayapata, mabaya nayo kundiniMbuyu kuwa mnene, chanzoche kama mchicha Kwa dhati ninatamka, hali huko sio shwariWatoto wanasumbuka, wanayakosa mazuriWaweza kusikitika, uwaonapo vizuriMbuyu kuwa mnene, chanzoche kama mchicha Ukifanya uchunguzi, wa idadi mashuleniWengi wa wanafunzi, ni Waislamu yaqiniWametupwa kama mbuzi, waso na kamba shingoniMbuyu kuwa mnene, chanzoche kama mchicha Jaribu fanya tafiti, ya idadi ya walimuWengi wao kwa dhati, ni manaswara fahamuRatiba hawazifati, wapiga domo kwa ghammuMbuyu kuwa mnene, chanzoche kama mchicha Mtoto akija feli, alaumiwa hasomiHili mimi sikubali, nikiwa kama msomiWalimu si wakubali, kufundisha darasaniMbuyu kuwa mnene, chanzoche kama mchicha Hapo sasa mmeona, chanzo cha hilo tatizoVizuri ni kushikana, kuliondoa tatizoKwa dhati kushikamana, kuuondoa uozoMbuyu kuwa mnene, chanzoche kama mchicha Lengole KATA PROGRAMU, ni msaada kuutoaWanafunzi Waisilamu, elimu kuwapatiaUjira kwake Rahimu, wewe dini piganiaMbuyu kuwa mnene, chanzoche kama mchicha Walimu twawatafuta, mlojaa mashuleniHata kidato cha sita, watokapo masomoniWadogo zetu wasota, jamani hamuwaoni?Mbuyu kuwa mnene, chanzoche kama mchicha

Nionapo matokeo, huwa ninasikitikaYa shule hizi za leo, waziitazo za KATAKwa hakika ni kilio, kwa ziro wanazopataMbuyu kuwa mnene, chanzoche kama mchicha Sasa muda mewadia, wa kuleta ukomboziTusaidie kwa nia, hawa wetu wanafunziShida zilowafikia, kwetu iwe njema ngaziMbuyu kuwa mnene, chanzoche kama mchicha Waratibu mikoani, hili lipromotiniWambieni waumini, watoe yao hisaniVituo vifungueni, ianzisheni TWISHENIUjira wa hii kazi, upo kwake Rhamani Kwa kuwa nina huzuni, naomba niseme basiHali ni mbaya nchini, wanafunzi hawapasiNamuomba Rahmani, atuinue kwa kasiKila mjuzi jueni, anadhima Qiyamani

Mwalimu Mohammed MakimuUITC-Dar es [email protected]+255 715465158

KATA PROGRAMU

Amnesty International: Nyenzo ya propaganda ya kivita?

Na Felicity Arbutnot

August 08, 20-12 ‘Global Research” –

AMNESTY International imetoa picha za satellite za ‘mashimo makubwa’ nchini Syria, ikieleza kuwa yanatokana na kutumiwa kwa wingi kwa silaha nzito, hata karibu na maeneo ya makazi. BBC ilitangaza, ikiinukuu Amnesty: Picha kutoka Anadan zilionyesha zaidi ya mashimo 600 ambayo inawezekana yanatokana na mapigano makubwa kati ya majeshi ya Syria na wapinzani wenye silaha.”

Zaidi: “Kugeuza mji wenye watu wengi zaidi nchini Syria kuwa eneo la mapigano kutakuwa na madhara mengi kwa raia. Maafa Syria tayari yanayongezeka,” alionya Christipher Koettl, meneja wa shughuli za dharura katika Amnesty International nchini Marekani, bila kutaja kuwa mauaji ya raia yanafanywa na majeshi ya Free Syrian Army yanayoungwa mkono na Marekani na NATO, na siyo na serikali.

Digital Globe kupitia Amnesty In ternat ional i k a s e m a “ z a i d i y a mash imo 600 ambayo inaelekea yamesababishwa na makombora mazi to yalionekana Anadan, karibu na Aleppo, kulingana na Amnesty International.”

“Majeshi ya Syria na wapiganaji wa upinzani lazima wote wazingatie sheria ya kimataifa kuhusu kulinda uhai wa binadamu, ambayo inakataza kabisa kutumia

mbinu na silaha ambazo zinashindwa kutofautisha lengwa za kijeshi na kiraia,” aliongeza.

Rekod i ya Amnes ty kuhusu kutokupendelea upande wowote katika vita iliharibika wakati iliposema mapema Januari 1991 pale iliposema kuwa askari wa Irak waliwatoa watoto wachanga kutoka hifadhi maalum ya joto na kuwaacha wafe katika sakafu ya kitengo cha uzazi cha hospitali Kuwait. Taarifa hiyo ilikamilisha mahitaji ya Marekani kuvamia Irak kuhusiana na kutwaliwa kwa Kuwait mwezi Agosti m w a k a 1 9 9 0 . H a b a r i hiyo ambayo serikali ya Kuwait iliizawadia dola za Marekani nusu milioni kwa kukubali kutangaza uwongo huo, bado haijaondoka, na kiasi ninavyofahamu, bado haijakanushwa (kuwa Amnesty ilipewa fedha hizo).

Amnesty walijiumiza kwa goli lingine la kujifunga kwa kuandaa maandamano mwaka jana nje ya ubalozi wa Syria mjini London pamoja na CAABU (asasi ya uelewano kati ya Uingereza na nchi za Kiarabu) yakitaka serikali ya nchi huru ya Syria iondolewe madarakani, mpango ulioainishwa na ubalozi wa Marekani mjini Damascus mwezi Desemba mwaka 2005. Hatua hiyo bila ubishi inaendana na tafsiri ya kuchochea ugaidi, kama ilivyoainishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hapo Mei 4, 2012.

Serikali ya Syria inafanya

kile ambacho nchi yoyote i le ingefanya kujil inda inaposhambuliwa na magaidi, wengi wao kutoka nje na pia wengi wakiwa na lafudhi ya Kiingereza, kufuatana na waandishi wa habari wa Uingereza na Uholanzi waliokuwa wametekwa nyara na kutoroka hivi karibuni..

Lak in i t u rud ie ya l e mashimo 600. Wapiganaji wa upinzani wanaelekea wana silaha za kurusha maguruneti na wamewahi kutamba kuwa wamekamata vifaru vyenye silaha nzito. Hata kuwe na mashimo machache kiasi gani, watakuwa wanahusika na mengi ka t i yao na hawatakuwa na mikono iliyo safi. Isitoshe, sikumbuki k u w a s i k i a A m n e s t y wakiwashutumu Waingereza na Wamarekani kwa kuua, k u b a k a , k u a n g a m i z a familia nzima za Wairak na Waafghani, ambao pia walivamiwa kinyume cha sheria, ambao walitaka tu kurudisha nchi zao, au walikuwa waathirika wa vita wasio na hatia.

Hakuna shaka kila kitu sasa kinasimamiwa na mkuu wa Amnesty nchini Marekani, ambaye h iv i ka r ibun i alikuwa msaidizi wa karibu wa Waziri wa Mambo ya Nje Bi. Hillary Clinton ambaye anaelekea kutowapenda wasio wa Magharibi, na hasa wa Mashariki ya Kati au walio zaidi na utamaduni wa Kiislamu.

Amnesty imekwenda mba l i ku toka kwenye malengo yenye hisia njema ya kuanzishwa kwake.

Page 13: ANNUUR 1034

13 AN-NUURSHAWWAL 1433, IJUMAA SEPTEMBA 14 - 20, 2012Makala/Tangazo

Umuhimu wa kutekeleza ahadiInatoka Uk. 11shughuli za biashara kila siku. Makubaliano ya ndoa, makubaliano ya maneno na mambo yote yanayoingia katika maana aya ‘Ahd’.

Allah anasema: “Enyi mlioamini! Tekelezeni wajibu (wenu).”(Surah al-Maidah, 5: 1).

Imam razi katika tafsiri yake (al-kabir) ameielezea aya hii kama ifuatavyo:

‘Kutimiza ahadi zenu’ kuna kamilisha msemo wa Allah ‘Tekelezeni wajibu wenu’.

Na msemo huu wa Allah unakusanya aina zote za makubaliano kama vile majukumu ya kibiashara, ubia, Aqd-i-Yamin, na mikataba ya ndoa. Kwa kifupi aya hizi zinamtaka mja kutimiza ahadi na malengo yake kutokana na masharti yaliyotajwa. (Tafseer al-kabir, part 5, p.585).

Ieleweke kuwa ‘Aqd’ inahusiana na makubaliano tu, na ‘Ahadi’ ina maana pana zaidi ya ‘Aqd’.

S w a h a b a A n a s ( r. a ) anahusisha na kila khutba ya Mtume (s.a.w) alipokuwa akisema: “Asiyechunga ahadi basi huyo hachungi Dini.” (Imepokewa na Ahmad).

Kwa lugha nyingine, dini imekusanya zile ahadi ambazo ni kati ya mtu na mtu na zile ambao ni kati mtu na Allah. Mtu ambae hatatekeleza atakua amevunja Imani ya Dini.

Ka t ika ma i sha ya uchamungu ya Mtume wa mwisho Muhammad (s.a.w) mifano mingi inaweza kuchukuliwa ili kuelezea tabia yake njema, ukarimu na uaminifu katika kila sura ya maisha yake.

Mama Aisha ( r. a ) anasimulia hakupata wivu na mwanamke yoyote zaidi ya Mama Khadija. “Kifo chake kimetokea miaka mitatu kabla ya harusi yangu. Lakini Mtume (s.a.w) alikuwa akimkumbuka yeye, na anapotoa sadaka ya mbuzi alikuwa akituma nyama kwa jamaa zake.

Siku moja mwanamke mtu mzima alikuja kwa Mtume (s.a.w). Alionyesha kumjali sana na akamuuliza juu ya maisha yake. Wakati alipoondoka Mama Aisha (r.a) akamuuliza Mtume (s.a.w) kwa nini alimjali sana yule mwanamke. Mtume (s.a.w) akasema, ‘Aisha, huyu alikuwa akija wakati wa Khadija na kutendea wageni kwa usawa ni dalili ya Imani ya mtu’.

Kuhitimisha, utekelezaji wa ahadi ni sifa ya maisha ya mwanadamu inamfanya mtu aaminiwe na kuwa maarufu mbele ya Muumba (Allah)

WAISLAMU wakiandamana jijini Dar es Salaam kushinikiza wenzao waliokamatwa katika zoezi la sensa na polisi waachiwe huru.

pamoja na wale anaoishi nao. Binadamu anajisikia kuwajibika kwa mtu ambae ni muaminfu na anatekeleza ahadi zake. Maneno yake yanakuwa na uzito katika jamii yake. Hii ni baraka ambayo mtu amekirimiwa mpaka mauti yatakapo mfika. Na matunda ya tabia hii, ambayo ameipata kutoka kwa Allah yamezungumziwa katika sehemu tofauti katika Qur’an. Kama amri kutoka kwa Allah na kama moja ya baraka Zake aya hizo zinatosha, Allah anasema:

“Kwa hakika Allah anaamrisha uadilifu, na kufanya ihsani.” (Surah al-Nahl, 16: 90).

“...na ufanye wema kama Allah alivyokufanyia, wala usitafute kufanya ufisadi katika nchi; bila shaka Allah hawapendi mafisadi.” (Surah al-Qasas, 28: 77).

Mtume (s.a.w) amesema: “Katika Siku ya Hukumu watu bora mbele ya Allah ni wale wenye kutekeleza ahadi zao kwa mioyo mikunjufu.” (Imepokewa na Aisha (r.a)).

Swahaba Ali (r.a) alipokea, Mtume (s.a.w) amesema: “Ahadi ya Muislamu ni kama deni, na inaweza ikawa zaidi ya deni.”

Kwa kifupi katika tabia njema zote iliyokuwa bora zaidi ni utekelezaji wa ahadi. Ahadi inaweza kujumuisha makubaliano ya maneno au vitendo, katika mambo ya kawaida au ya kibiashara, katika hali zote utekelezaji wake utaitwa wema (Ihsan).

Sifa yenye kupendeza zaidi kwa wale wanaoongoza watu wengine ni lazima daima wawe wenye kufanikiwa

na kutawala. Utawala huu unaweza kupatikana kwa wepesi kwa kutokwenda kinyume na wanayoahidi.

Kama serekali zinatekeleza ahadi zake basi zinaweza kupata uaminifu kwa haraka kutoka kwa jamii (umma). Na endapo wahusika wakiweza k u t e k e l e z a a h a d i z a o watajikuta wanapata baraka na ridhaa.

Hivyo kama tunajiangalia wenyewe tutajikuta tuko mbali na mafundiso haya ya Qur’an na Sunnah. Sisi ni Waisilamu na Imani yetu ya msingi ni kushuhudia ya kwamba hakuna mwenye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah na kwamba Muhammad (s.a.w) ni Mtume wa Allah. Hii inaashiria ya kwamba hatupaswi kutii maamrisho ya yeyote isipokuwa ya Allah na Mtume wake katika hatua zote za maisha. Hivyo katika muamala wetu wa kila siku, makubaliano ya kijamii au binafsi, makubaliano ya kisiasa na mikataba ya kiuchumi ni lazima tuwe madhubuti na haipaswi kugeuka hata kidogo katika yale tuliyoahidi kufanya. Hili ni jukumu letu na tutaulizwa juu ya hilo siku ya Qiyama. Hebu, tujaribu sisi, wenyewe kuamua kutekeleza maneno yetu si kwa sababu wengine watusifu, bali ni kwa sababu ni amri ya Allah na Mtume (s.a.w). Tabia hii bila shaka itapelekea kuimarika kwa hali zetu za kimaisha pamoja na kiimani.

Jumuiya ya Wataalamu wa Kiislam Tanzania (TAMPRO) kupitia Kituo chake cha mafunzo na Ajira inawatangazia Semina ya Mafunzo ya Ufugaji Kuku wa Kienyeji na Ujasirimali kwa kutumia wataalamu wenye uzoefu wanaoshughulikia masuala hayo kwa muda mrefu. Semina itakuwa kama ifuatavyo:-

Walengwa: Wafugaji, wanaotaka kuanza kufuga, wajasiriamali wadogo wadogo na watakaopenda .

Siku: Kuanzia Jumamosi, JumapiIi na jumatatu terehe 15 -17 Septemba 2012

Muda: Saa 2:00 asubuhi - 10:00 jioni

Mahala: Ofisi Kuu ya T AMPRO Magomeni Usalama, Dar es Salaam

Mada: Njia za ufugaji wa kuku, Uchaguzi wa kuku kwa ajili ya kufuga, Kuandaa chakula bora, magojwa ya kuku na tiba yake, Utunzaji wa vifaranga na mayai nk. Vile vile mafunzo ya kutafuta soko la bidhaa zinazotokana na kuku, kutunza mahesabu na kumbukumbu za fedha pamoja jinsi ya kukuza mtaji yatatolewa.

Kujisajili: Shilingi 50,000/= kwa mtu mmoja. (Kwa ajili ya cheti cha ushiriki, Kitabu cha muongozo,na chakula kwa siku zote tatu)

Muhimu: Washiriki watapatiwa vyeti na kitabu cha muongozo wa ufugaji kuku kilichoandikwa kwa lugha ya Kiswahili ili kukidhi haja.

Kujisajili: IIi kujisajili piga 0714 151 532, 0767 151 532,0716 574 266 au fika TAMPRO Makao Makuu, Magomeni Usalama, jirani na Halmshauri ya Manispaa ya Kinondoni.

Wahi kuijiandikisha kwani nafasi ni chache

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia 0714 151 532,0767 151 532,0716 574 266 au info(@)tampro.org

MRATIBU MAFUNZOTAMPRO MAKAO MAKUU

SEMINA YA UFUGAJI BORA WA KUKU WA KIENYEJIKITUO CHA MAFUNZO NA AJIRA CHA TAMPRO

Page 14: ANNUUR 1034

14 AN-NUURSHAWWAL 1433, IJUMAA SEPTEMBA 14 - 20, 2012Makala

KAMA kuipa msukumo au kuondoa dukuduku na woga kuwa jamii iliyo elimika imetoa waathirika, mara nyingi wameonekana kuchagua ueneaj i wa maradhi ya mi l ipuko ya madawa ya kulevya. Haishangazi kuwa takwimu za mwenendo wa kusikitisha zinachukua nafasi ya juu. Kuanzia kuzongwa na kukata tamaa, sababu za kulaumika kwa matumizi mabaya ya madawa yana sababisha hatari kubwa kwa watumiaji wake.

Matumizi mabaya ya m a d a w a n i m a t u m i z i e n d e l e v u y a s i y o w e z a kudhibitika yanayo badili akili kutokana na matatizo ya kibanafsi, kijamii, na/au ya kimwili yanayo sababishwa na matumizi ya madawa ya kulevya. Matumizi hayo yana sababisha utegemezi ambapo kiasi kikubwa cha madawa kina hitajika ili kupata athari tarajiwa au kiwango cha kilevi, na mgonjwa ametawaliwa na ulevi.

Kutawaliwa na ulevi ni hali ya ubongo ambapo mtu huwa hajitambui kijamii, kimwili, na/au kisheria kutokana na kujiingiza kwenye ulevi wa kukithiri na kuwa na madawa ya kulevya na kuyatumia na kuwa lengo lake kuu. Baada ya muda kipimo/kiwango kile kile cha madawa ya kulevya kita sababisha hisia kidogo kuliko kilicho tarajiwa, na uvumilivu unatoweka. Ili

Madawa ya kulevya na madhara ya matumizi yake

andelee kuhisi athari ya madawa ya kulevya, atatakiwa kuongeza kipimo cha madawa (dozi) kila mara.

Karibu madawa yote yanayo levya yana changamsha mno mfumo wa ubongo, ina ujaza na madawa ya kulevya yanayo ambukiza ugonjwa wa akili (Neurotransmitter Dopamine) ambao unasababisha furaha tele. Furaha iliyo zidi ina shurutisha ubongo kuhitaji hisia zile tena na tena.

Madawa ya ku levya yanayo tumiwa sana na watu wa kawaida: Pombe/Mvinyo, Kokeini, Opioids (Morphine, Heroin), Benzodiazepines (Valium) na Sedatives/Tranquilizers (Barbiturates). Mengine ni St imulants (Amphetamines, Ecstasy), Cannabinoids (Marijuana, Hashish), Hallucinogens (Angel Dust) na Inhalants (Anesthesia gaves, paint, thinner, glue)

U k u b w a w a Ta t i z o : Matumizi ya madawa ya kulevya haya chagui kabila, taifa, utamaduni, elimu na hadhi ya kijamii na kiuchumi. Hapana kundi lisiloguswa na madhara yake yanayo tisha, kukiwa na takribani watu milioni 200 wanao tumia madawa ya kulevya kila siku duniani. Nchini Marekani peke yake kwa mujibu wa utafiti uliofanywa 2005 na ‘National Survey on Drug Use and Health’, kiasi cha Wamerikani milioni 110 wenye umri wa miaka 12 na

watu wazima (46%) walitumia angalau aina moja ya dawa za kulevya maishani mwao, ambapo takriba watu milioni 19 wanatumia madawa ya kulevya leo.

Hali kadhalika nchini Pakistan hali inahuzunisha sana. Utafiti uliofanyika mashuleni na vyuoni katika vitongoji vya Clifton na Defence, Pakistan, mwaka 2005, imebainisha kuwa 34% wanatumia madawa ya kulevya (wanaume 21% na wanawake 13%) 52% ili ripotiwa wanavuta sigara, kati yao 33% walikuwa wanaume na 19% wanawake, ambapo wanafunzi walitumia madawa yanayo fahamika, Pombe, Ectacy na Hashish, ambayo ni 37.9% kwa jumla.

K WA N I N I WAT U WANATUMIA MADAWA YA KULEVYA? Ni mambo gani yanayo wafanya watu kuhilikisha maisha yao namna hiyo.! Baadhi ya sababu hatarishi zimetambuliwa zikiwa na uhusiano tata lakini inakubalika kwa ujumla kuwa Vijana wako hatarini zaidi.

Sababu hizo zinaweza k u o r o d h e s h w a k a m a ifuatavyo: Mazingira ya nyumbani yenye mtafaruku, M v i n y o w a m a w a z o , Magonjwa ya akili kama m s o n g o w a m a w a z o (depression) na Historia ya Familia kutumia uraibu.

Katika utafiti uliofanywa Karachi (uliotajwa hapo juu), 17% ya wazazi wa mateja

walitalakiana au kutengana 31% ya wote waliosailiwa maraf ik i zao wakubwa walikuwa wanatumia madawa ya kulevya kati yao 22% walikuwa nao ni watumiaji (mateja). Jumla ya 35% ya wanafunzi walioarifu kuwa wazazi wao walibobea katika unjwaji wa pombe/matumizi ya madawa ya kulevya.

Kwa sababu hiyo uhusiano u l io wazi upo ka t i ya matumizi ya madawa ya kulevya, mbinu za kiishilizo, kujizuia, mahusiano ya rika na mahusiano na mzazi. Hili likasababisha athari ambapo mazingira duni ya nyumba/malezi na makundi mabaya yanazalisha mateja ambao watakuwa wazazi wa vizazi vya waathirika na madawa ya kulevya.

ATHARI HASI ZA MADAWA YA KULEVYA

Kwa ujumla, athari za kimwili ni pamoja na kwenda/kutembea taratibu, njozi na ‘psychosis’ kutegemea dawa aliyotumia (kihamasishi, kichosha akili, kisababishi cha njozi). Baadhi ya athari hasi zinategemea aina ya utumiaji kama vile kunusa cocain kwa pua kuna weza kusababisha kutokwa na damu puani, uvimbe puani, na hata kumomonyoka kwa ‘nasal septum’ (umbile linalo tenganisha tundu mbili za pua). Vivyo hivyo uchomaji wa sindano kupitia kwenye mishipa ya damu wa madawa ya kulevya ni njia kuu ya kuambukiza HIV (ukimwi), Homa ya manjano B & C.

Kuzidisha kipimo cha dawa ni tatizo linalo sababishwa na matumizi mabaya ya dawa. Kuzidisha kipimo cha dawa kunaweza kufanywa kwa kudhamiria (kwa lengo la kujiua), au kusababishwa na uzembe. Aidha inaweza kusababishwa na kuzidisha kwa kipimo ambacho mtu ana lazimika kukitumia ambacho a n a k i m u d u , k u z i d i s h a kipimo cha dawa kunaweza kuhatarisha maisha, kukiwa na dalili mahususi kutegemea aina ya dawa iliyotumiwa.

Endapo u tumia j i wa madawa ukiachwa ghafla, mwili wa binadamu kwa k u k o s e k a n a m a d a w a , utendaji utapungua kutokana na matumizi ya madawa, u t a o n g e z e k a g h a f l a , ambapo hapo awali utendaji uliochochewa utapungua. Matokeo haya yana athari mbaya, yanayo julikana kama dalili za kujiondoa.

Kwa upande mwingine,

athari za kijamii za madawa ya kulevya ni pamoja na kuacha shule au kupoteza kazi mfululizo, kupigana, na uhusiano wa kigomvi, na matatizo ya kisheria kuanzia kuendesha gari akiwa mlevi mpaka kufanya makosa ya jinai yanayo dhamiria kupata fedha zinazo hitajika kusaidia tabia ya kutumia madawa ghali.

Matumizi ya madawa ya kulevya yana sambaratisha jamii, kutokana na gharama kubwa za kisiasa, kijamii, kiuchumi na kiafya. Haya ni matokeo ya kupungua kwa kazi za uongezaji tija, uhudhuriaji , uongezeko wa huduma za afya, na kuongezeka kwa vitendo vya uvunjaji sheria kwa kutumia nguvu. Madawa halali na haramu peke yake yana igharimu Marekani (U.S.A) kiasi cha dola nusu trilioni kwa mwaka, ikilinganishwa na kisukari, saratani ambayo yanagharimu kiasi cha $ bilioni 132 na $ bilioni 219, sawia.

A M R I YA K I S H E R I A YA K I I S L A M U I N AY O K ATA Z A MATUMIZI YA VITU VINAVYO LEVYA.

Uislamu ni ujumbe wa mwisho, Mjumbe wa Allah (SAW) aliharamisha aina zote za vitu vinavyo levya kwa muda wote kwa kusema; Kila kinacholevya ni pombe (mvinyo) na kila pombe ni haramu.

Kutokana na Hadith ya hapo juu na kutokana na ithibati iliyopo ni kuwa maonyo na makatazo mbalimbali ndani ya Qur’an Tukufu na Hadith kuhusiana na mvinyo na pombe unahusu madawa yote ya kulevya.

Allah anasema: “Enyi ml ioamini ! Bi la shaka ulevi, kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya Shetani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa. Hakika Shetani anataka kutia kati yenu uadui na chuki kwa ulevi na kamari, na akuzuieni kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kusali. Basi je, mmeacha? (Al-Maidah 5:90-91)

Vivyo hivyo, kwa kuelewa kuenea kwa athari za sumu ya vilevi kwenye jamii kwa ujumla, Mtume Mtukufu (SAW) alisema’ “Jiepusheni na mvinyo’ ni mama wa machukizo” (An-Nasai).

Ni dhambi kubwa mbele ya Allah (Swt) kiasi cha Mtume (SAW) kwenda mbali kwa

MKURUGENZI wa Upelelezi wa Mkosa ya Jinai nchini, Robert Manumba.

Inaendelea Uk. 14

Page 15: ANNUUR 1034

15 AN-NUURSHAWWAL 1433, IJUMAA SEPTEMBA 14 - 20, 2012Habari

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar M a a l i m S e i f S h a r i f Hamad, amewahakikishia Wazanzibari wanaoishi nchi za nje kuwa Serikali imeanzisha Idara maalum kwa ajili ya kushughulikia masuala ya Diaspora ili kuwa karibu zaidi na Wazanzibari walioko nje ya nchi.

Amesema, hatua hiyo i m e l e n g a k u r a h i s i s h a mawasiliano kati ya serikali na Wazanzibari hao, ikiwa ni hatua muhimu katika kusogeza mbele maendeleo ya nchi na Wazanzibari hao.

Maalim Seif ametoa changamoto h iyo h iv i k a r i b u n i a l i p o k u w a akizungumza na viongozi wa Jumuiya ya Wazanzibari wanaoishi nchini Marekani ZADIA, katika ukumbi wa hoteli ya Marriott mjini Washington.

A m e w a p o n g e z a Wazanzibari hao kutokana na hatua yao ya kuanzisha

Nasaha za Maalim kwa Wazanzibari Marekani

jumuiya h iyo , ambayo itasaidia kuunganisha nguvu zao na kuwa na sauti ya pamoja katika kushughulikia masuala mbali mbali yanayohusu maendeleo yao na taifa kwa ujumla.

Amewataka wana-diaspora hao kuangalia uwezekano wa kusaidia harakati za maendeleo Zanzibar, na kuwaasa kutojisahau wakati wanapokuwa nje ya nchi, ili kujiwekea mazingira bora ya maisha yao ya baadae.

Maalim Seif ameelezea umuhimu wa Wazanzibari hao kuendelea kutafuta takwimu za Wazanzibari wanaoishi nchini Marekani, ili kurahisisha mipango yao na serikali.

K w a u p a n d e w a k e mwenyekiti wa jumuiya hiyo Bw. Omar Ali, amemueleza M a a l i m S e i f k u w a Wazanzibar wanaoishi nje ya nchi wanahitaji kupatiwa nyenzo na mashirikiano ya karibu kutoka serikalini, ili kurahisisha harakati za maendeleo.

Amesema, Jumuiya ya ZADIA ina wataalamu wengi wenye ujuzi wa fani mbali mbali zikiwemo elimu, utafiti na ufundi ambao iwapo

watatumiwa vizuri wanaweza kuisaidia Zanzibar katika harakati zake za kujitafutia maendeleo.

Mapema Wana-diaspora hao walimkabidhi Maalim

Seif nakala ya hati ya usajili ya jumuiya yao ili ziwekwe katika kumbukumbu za Idara ya Diaspora Zanzibar.

(Habari na Mwandishi maalum, USA)

Madawa ya kulevya na madhara ya matumizi yakeInatoka Uk. 14

kusema, “Allah atawanyima watu watatu kuingia peponi; mlevi, mtu asiye waheshima wazazi wake na kuwadi (kijumbe) anaye ridhia familia yake kufanya yaliyokatazwa” (Ahmad).

KUUENDEA UFUMBUZI.Duniani kote kumekuwa

na juhudi mbalimbali za kuwawezesha mateja kurejea kwenye maisha ya kawaida kupitia vituo vya kurekebisha tabia na vikundi saidizi, lakini kutokana na viwango vya juu kurudia rudia matumizi ya madawa kufuatia msongo wa jamii ulioenea, inakubalika na wengi kuwa kinga ndio ufunguo wa mafanikio.

M i k a k a t i y a k i n g a inawalenga zaidi vijana, ambao wako kwenye hatari zaidi ya kufanyiwa majaribio ya madawa ya kulevya. Elimu kuhusu hatari na madhara ya matumizi ya madawa ya kulevya, vile vile kuwafunza kujizuia na shinikizo la ushawishi. Yote hayo ni muhimu kwa programu

ya kinga (kuzuia), lakini programu hizo hazijaonyesha mafanikio katika nchi za Magharibi.

Ni dhahiri kuwa kiini cha uovu huu kipo kwenye mazingira ya nyumbani yaliyotapanyika, shinikizo kubwa na ugumu wa kuhimili sh in ik izo unaope lekea magonjwa ya akili kama vile mfadhaiko na dukuduku. Mpaka hapo visababishi vikuu vitakapo shughulikiwa hapana matumaini yoyote. Kumwamini Allah (Swt) na kushikamana na misingi ya Uislamu ndio saluhisho (jawabu).

Shinikizo la vishawishi ni kazi yenye nguvu sana ambayo Mtume Mtukufu (SAW) ameielezea kuwa “Mtu yuko kwenye Dini ya rafiki yake, hivyo angalia unayefanya naye urafiki” (Abu Dawood na Tiimidhi). Kwa sababu hiyo marafiki na makundi lazima yachaguliwe kwa uangalifu mkubwa. Msingi ya Qur’an lazima wakati wote izingatiwe,

“Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na kuweni pamoja na wakweli”. (At-Tawbah 9:119)

Mwisho lakini si kwa umuhimu ni kukuza uwezo wa nafsi (moyo) kukabiliana na matatizo ya maisha na kutafuta amani na utulivu hata hali yenye majaribu (mitihani) Allah (Swt) anasema:

“Hakika kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu ndio nyoyo hutua! (ArRa’d 13:28)

Ni vipi kumkumbuka Allah (Swt) kunaleta utulivu ndani ya nyoyo zetu? Ni kwa kutumia muda na watu wanaopendwa na Allah.

Tunaomba Allah (Swt) amlinde kila mmoja wetu na uovu huu ambao hatimaye unamfanya kuwa na maisha ya kusikitisha na hivyo kuwa na masikitiko siku ya kiama.

(Maelezo ya madhara ya kuogofya ya kuenea kwa matumizi ya madawa ya kulevya. Mwandishi, D k t . A k b a r Z u b a i r. Mfasiri, Hassan A. Mnjeja (0715633166). Mtayarishaji, Hashim Garana

MAKAMU wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad (katikati) akiwa ziara ya kikazi nchini Uingereza hivi karibuni.

MHADHIRI mashuhuri nchini, SHEIKH SAID RICCO ni mgonjwa wa macho. Jicho lake la kushoto linavuja damu kwa ndani. Ametibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, KCMC Moshi, CCBRT Dar es Salaam bila mafanikio.

Hatimaye alipelekwa Hospitali ya NM India. Baada ya uchunguzi ilionekana unahitajika upasuaji mkubwa na kwa gharama za dola 5500 sawa na 8,800,000 za Kitanzania.

Alirejea nyumbani na mpaka sasa amefanikiwa kupata dola 4,000 bado Dola 1,750 ili aweze kurejea India kwa ajili ya matibabu. Tayari tiketi ya ndege anayo ya Emerate Airlines Flight No. EK 726 na anatakiwa kuondoka tarehe 30 Septemba mwaka huu.

Hivyo anahitaji anahitaji msaada wa haraka wa kiasi kilichosalia.

Mchango wako upeleke AKAUNTI Na. 048201001220 NBC tawi lolote au TIGOPESA 0715 979779 AU M-PESA 0753 979779.

Anawashukuru sana Waislamu wa Arusha, Tanga, Mwanza na Morogoro kwa kumsaidia kupata Dola 4000 na tiketi ya ndege.

WABILLAH TAWFIIQ

Sheikh SAID RICCO anahitaji msaada wa haraka

Page 16: ANNUUR 1034

16 AN-NUURSHAWWAL 1433, IJUMAA SEPTEMBA 14 - 20, 2012

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.

AN-NUUR16 SHAWWAL 1433, IJUMAA SEPT. 7-13 , 2012

www.tawheedtz.orgUnakuhimiza ufanye Ibada ya Hijja 2012Fanyeni Haraka Kuhiji. Maana Hajui Mmoja Wenu Kitakachomtokea – Ibn AbbasMkabala na Msikiti wa Makonde, Kariakoo, Dar es Salaam022 2182068; 0776 070770; 0719 689528

Mtandao wa Tawheed

TRIPOLILE Vita ya Msalaba (Crusade) inayopiganwa kupitia vyombo vya habari, filamu na kwa silaha za moto, imepelekea kuuwawa kwa Balozi wa Marekani nchini Libya.

Balozi huyo Chriss Stevens na wafanyakazi wengine wa ubalozi huo wameuawa kutokana na mashambulizi ya roket i ka t ika mj i wa Benghazi yanayohusishwa na maandamano ya Waislamu kupinga filamu inayomkashifu Mtume wao.

Afisa mmoja wa serikali ya Libya amethibitisha kwamba Balozi Stevens na wafanyakazi wengine watatu wa ubalozi huo waliuawa kwa roketi lililorushwa kwenye gari la ubalozi.

Hata hivyo, haikufahamika mara moja kama balozi huyo a l ikuwamo kwenye ga r i iliyoshambuliwa, au alikufa usiku wa kuamkia Jumatano, baada ya waandamanaji wenye silaha kuvamia ubalozi huo mjini Benghazi.

W a a n d a m a n a j i h a o wamefanya tukio hilo baada ya kukasirishwa na filamu moja ya Hollywood, ambayo inamkashifu kiongozi wa Waislamu, Mtume Muhammad (s.a.w).

Maandamano kama hayo pia yalifanyika mjini Cairo, Misri, ambako maelfu ya waandamanaji waliuvamia ubalozi wa Marekani, lakini bila kuwapo mashambulizi.

Hollywood na makampuni mbalimbali ya filamu Marekani na Ulaya, yamekuwa yakitumiwa na maadui wa Uislamu katika kutoa picha chafu za kukashifu Uislamu.

Makampuni haya ya filamu pamoja na vyombo vya habari, ndio yaliyomstari wa mbele ka t ika kurused i ambayo inaanza kwa kuwapachika Wa i s l a m u u o v u k a b l a wanajeshi hawajashika silaha kuwashambulia.

Filamu hiyo ambayo ndicho kitovu cha machafuko na maandamano hayo imeandaliwa na raia wa Marekani mwenye asili ya Israel, ambaye anauelezea Uislamu kama kidonda ndugu

Vita ya Msalaba:

Balozi Marekani Libya auawan a k u m u o n e s h a M t u m e Muhammad (s.a.w) akilala na wanawake, kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa na gazeti la Wall Street Journal la Marekani.

Awali, mjni Tripoli, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Libya, Wanish al Sharif, aliliambia shirika la habari la Ufaransa (AFP), kuwa ofisa mmoja wa Marekani aliuawa na mwengine kujeruhiwa wakiwa mikononi mwa waandamanaji huku wafanyakazi wengine wakiokolewa na wapo salama.

Sharif alisema waandamanaji waliuvamia ubalozi huo wa Marekani na kuanza kurusha risasi hewani kabla ya kuingia ndani na kuanza kuwashambulia wafanyakazi.

Wakristo wa madhehebu ya Koptik Misri nao wamekusudia kufanya maandamano kupinga filamu hiyo, wakisema kuwa ni matusi kwa imani za watu wote.

Kufuatia shambulizi hilo, mgombea Urais Marekani kupitia chama cha Republican, Mitt Romney, amelitumia tukio hilo kuushambulia utawala wa Rais Obama akidai kuwa kiongozi huyo wa Republican amekuwa pamoja na waandamanaji wa Kiislamu wenye siasa kali na sio pamoja na Wamarekani.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilitoa tamko la kulaani vikali mashambulizi hayo huku Waziri wa Mambo ya Nje, Hillary Clinton, akisema amezungumza na Rais Mohammed al-Magariaf wa Libya juu ya mashambulizi hayo na kukubaliana kuchukua hatua za haraka.

Msemaji wa wizara hiyo, Abde lmonoem a l -Hor r , alisema guruneti lililorushwa kwenye ubalozi huo liliripuka kwenye bustani iliyoko karibu na ubalozi huo.

Watu walioshuhudia tukio hilo wamesema wavamizi waliiteremsha bendera ya Marekani iliyokuwepo kwenye ubalozi huo na kisha kuanza kuuchoma moto ubalozi huo.

Raia mwengine aliyeshuhudia tukio hilo alisema waandamanaji waliokuwa na silaha walifunga barabara za mitaa inayoelekea

kweye ubalozi huo.Hata hivyo, maandamano

hayo yamepingwa na Baraza Kuu la Uongozi la Libya, ambalo katika taarifa yake limekiita kitendo hicho ni kiovu na kisichotarajiwa kutokea kwa ubalozi wa Marekani mjini Benghazi.

Tukio la maandamano nchini Libya l inafuatia tukio kama hilo lililofanywa na waandamanaji mjini Cairo Jumanne ambapo waandamanaj i wapatao 3,000, walipoandamana katika ubalozi wa Marekani nchini humo kupinga filamu hiyo inayomkashifu Mtume Muhammad (S.A.W)

Mamia ya watu waliuzingira ubalozi wa Marekani na kisha kuiteremsha bendera ya Marekani na kupandisha bendera ya rangi nyeusi i l iyokuwa na alama ya Kiislamu, na kisha kusema M u n g u n i m m o j a n a Muhammad ni Mtume wa Mungu. Balozi wa Marekani nchini Libya, Chriss Stevens

Shule ya Kiis lam y a s e k o n d a r i y a Daarul-arqam iliyopo kitongoji cha Amani-Gomvu (Kigamboni) Manispaa ya Temeke j i j i n i D ’ s a l a a m i m e p a t a u s a j i l i kamili.

Katika barua yenye kumbukumbu namba JA/287/1976/0l /27 kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ya tarehe 09/08/2012 iliyotiwa sahihi na Kaimu Kamishna wa Elimu aliyomuandikia M k u r u g e n z i w a shule hiyo Shawwal Abdu laz i z Msami (ambayo nakala tunayo) imeeleza kuwa shule

DAARUL-ARQAM SEKONDARI YAPATA USAJILI KAMILI

hiyo imesajiliwa kuanzia t a r e h e 0 7 / 0 9 / 2 0 1 2 kwa namba S.4628 na kwamba jina rasmi la shule hiyo ni DAARUL-ARQAM SEMINARI.

K u s a j i l i w a k w a Shule ya Kiislam ya Daarul-Arqam Seminari kunaongeza idada ya shule za sekondari za Kiislam hapa nchini na hivyo kuzidisha fursa kwa vijana wa Kiislam wenye sifa ya kuanza kidato cha kwanza kupata mafunzo ya elimu ya Kiislam, mazingira na malezi ya Kiislam.

Shu l e ya Daa ru l A r q a m S e m i n a r i inasimamiwa na Taasisi

ya Kiislam ya Daarul-Arqam Islamic Centre (DAlC) iliyosajiliwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ambayo pia inasimamia shule za Daarul-Arqam - Msingi na Chekechea zilizoko Amani-Gomvu na Ilala jijini D’salaam.

Akizungumza na An nuur kufuatia usajili h u o , M k u r u g e n z i mwendeshaji wa Shule z a D a a r u l - A r q a m ame toa w i to kwa Serikali kuchukua hatua za dhati kulirekebisha Baraza la Mitihani ili kurudisha imani kwa Waislam.