annuur 1144

16
ISSN 0856 - 3861 Na. 1144 DHULQAAD, IJUMAA , SEPTEMBA 26-OKTOBA 2, 2014 BEI TShs 500/=, Kshs 50/= Sauti ya Waislamu www.annuurpapers.co.tz Uk. 16 MUUNGANO wa kweli ni wa kuheshimiana, wa kufuata haki na usawa kwa kila upande. SMZ itavuruga amani Zanzibar Inarudia yale ya Wareno, Mapinduzi Makkah walikimbilia kwa mfalme Najash Masheikh Zanzibar nao wakimbilie wapi? ‘Mujahidina feki’ Kifaa cha maadui wa Uislamu Watumika kuangamiza Waarabu RAIS wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein. SHEIKH Mohamed Idd Mohamed. Watanzania tujifunze kutoka UK, Scotland Kura ya maoni ya wananchi muhimu Tusidharauliane kwa ukubwa, udogo Wala kwa kejeli za wauza vitunguu Tunapojadili faida za muungano, tujikite katika uzito wa hoja si kelele za mchele wa Mbeya na tashtiti za dharau kwa wengine. Khofu ya jeshi kuchukuwa nchi na tashtiti za kutuita wauza vitunguu, haitasaidia kurejesha umoja tunaoutamani. (Soma uk. 3) WAPIGANAJI ISIS katika nchi za Iraq na Syria. NIMEHUZUNISHWA sana kwa maneno ya “uongo” kutoka mdomoni mwa kiongozi wa kidini mwenye cheo cha Upadre. Kama Padre anaweza Askofu anapokuwa muongo waumini wake watakuwaje! Padri Mapunda unampima vipi Kikwete, Mkapa Mwache Mzee Mwinyi, waulize Kingunge, Slaa Ila asante kwa kutuzindua Waislamu usingizini kusema uongo ili kufanikisha matakwa yake, je, waumini wafanye nini? Hivi kumbe mgogoro wa Somalia wanagombea Ukadhi? (Soma Uk. 6, 7) Nafasi ya mwanamke ni kubwa katika jamii ya Kiislamu

Upload: zanzibariyetu

Post on 26-Dec-2015

899 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: ANNUUR 1144

ISSN 0856 - 3861 Na. 1144 DHULQAAD, IJUMAA , SEPTEMBA 26-OKTOBA 2, 2014 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Sauti ya Waislamuwww.annuurpapers.co.tz

Uk. 16

M U U N G A N O wa kweli ni wa kuheshimiana, wa kufuata haki na usawa kwa ki la upande.

SMZ itavuruga amani Zanzibar

Inarudia yale ya Wareno, MapinduziMakkah walikimbilia kwa mfalme NajashMasheikh Zanzibar nao wakimbilie wapi?

‘Mujahidina feki’Kifaa cha maadui wa UislamuWatumika kuangamiza Waarabu

RAIS wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein.

SHEIKH Mohamed Idd Mohamed.

Watanzania tujifunze kutoka UK, Scotland

Kura ya maoni ya wananchi muhimuTusidharauliane kwa ukubwa, udogoWala kwa kejeli za wauza vitunguu

T u n a p o j a d i l i faida za muungano, tujikite katika uzito wa hoja si kelele za mchele wa Mbeya na tashtiti za dharau kwa wengine.

Khofu ya j esh i kuchukuwa nchi na tashtiti za kutuita wauza vitunguu, haitasaidia kurejesha umoja tunaoutamani. (Soma uk. 3)

WAPIGANAJI ISIS katika nchi za Iraq na Syria.

NIMEHUZUNISHWA sana kwa maneno ya “uongo” kutoka mdomoni mwa kiongozi wa kidini mwenye cheo cha Upadre.

Kama Padre anaweza

Askofu anapokuwa muongowaumini wake watakuwaje!

Padri Mapunda unampima vipi Kikwete, MkapaMwache Mzee Mwinyi, waulize Kingunge, SlaaIla asante kwa kutuzindua Waislamu usingizini

k u s e m a u o n g o i l i kufanikisha matakwa yake, je, waumini wafanye nini?

Hivi kumbe mgogoro wa Somalia wanagombea Ukadhi? (Soma Uk. 6, 7)

Nafasi ya mwanamke ni kubwa katika jamii ya Kiislamu

Page 2: ANNUUR 1144

2 AN-NUURDHULQAAD 1435, IJUMAA SEPTEMBA 26-OKTOBA 2, 2014

AN-NUUR S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786

Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM. www.annuurpapers.co.tz E-mail: [email protected]

Ofisi zetu zipo: Manzese Tip TopUsangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

Tahariri/Tangazo

P.O.BOX 55105 , TEL: NO 2450069, Mob: No 0712974428 & 0786457719 Dar Es Salaam.

UBUNGO ISLAMIC HIGH SCHOOL

PRE– FORM ONE PROGRAM 22/09/2014 - 28/11/2014

Program hii itaendeshwa hapa UBUNGO ISLAMIC HIGH SCHOOL kwa wanafunzi wa Kiislamu wanaojiandaa kujiunga na kidato cha kwanza Januari, 2015.Masomo yafuatayo yatafundishwa:Elimu ya Dini ya Kiislamu, Mathematics, Arabic language na English language ADA: 80,000/= kwa program yote.Jumatatu - Ijumaa kuanzia saa 2:00 asubuhi—8:30 mchana.Jumamosi kuanzia saa 2:00 Asubuhi—6:30 mchana Masomo yataanza rasmi tarehe 22/09/2014Jiandikishe kuanzia 18/09/2014 ofisi ya Mkuu wa Shule Ubungo Islamic High School kuanzia saa 1:30 asubuhi hadi saa 8:30 mchana .

Wahi mapema nafasi hii adhimu Wabillah tawfiiqMKUU WA SHULE

“ H I J A H n i m i e z i m a a l u m . N a anayekusudia kufanya Hijah katika (miezi) hiyo , basi as iseme m a n e n o m a c h a f u wala asifanye vitendo vichafu wala asibishane katika hiyo Hijjah. N a k h e r i y o y o t e mnayoifanya, Allah huijua. Na chukueni masurufu (ya kutumia njiani, msiombe). Na hakika masurufu bora ni yale yanayomfanya mtu as iombe (kwa kuwa yanamtosha) . N a n i c h e n i M i m i , enyi wenye akili.” (Al Baqarah: 197)

“Hakika nyumba ya kwanza waliyowekewa watu kwa ibada ni ile iliyoko Bakka (Makka), i l i y o b a r i k i w a n a yenye uwongofu kwa walimwengu wote.” (TMQ 3:96)

Hija hutukumbusha Waislamu kuj izat i t i vilivyo na majukumu ya Uislamu. Hija ni mafunzo makubwa ya ucha Mungu. Kujifunga vilivyo na kipimo cha halali na haramu katika matendo yetu, kumpinga na kupambana na shetani na kila taratibu na mfumo wake, ili hatimaye kuishi chini ya bendera moja ya Uislamu ili kuhifadhi umoja na udugu.

Hivi sasa Mahujaji k u t o k a s e h e m u mbalimbali duniani, wanamiminika nchini Saudi Arabia kuitikia mwito wa Mola wao kwa ajili ya ibada ya Hija.

Kat ika kuamrisha ibada hii, Mwenyezi Mungu anatue leza : N a ( K u m b u k e n i ) tulipoifanya nyumba ya (Al-Ka’ba) iwe mahali pa kuendewa na watu, na mahala pa amani. Na mahali alipokuwa

Kila la kheri Mahujaji wetuMuhimu zingatieni lengo

akis imama Ibrahim pafanyeni pawe pa kusalia. (2:125).

U k i a c h a m w e z i Mtukufu wa Ramadhani na siku za Eid, kipindi cha Hija kinashuhudiwa d u n i a n i k o t e n a kudhihirisha nuru ya Umma wa Kiislamu. Hivi sasa ni harakati kubwa za mahujaji kwenda Makka kutimiza nguzo ya tano katika Uislamu.

H a r a k a t i h i z i huchochea hisia za imani na ari ya kushikamana na maamrisho ya Mwenyezi Mungu. Hata hivyo, tunaona kwamba kwa vile Ibada hii kwa wengi ni ya mara moja katika uhai wao, ni vyema Mahujaji wakaelewa na wakawa na yakini katika mioyo yao kuwa nini wanachokwenda kukifanya huko na kwa malengo gani.

Halitakuwa jambo zuri mtu akapoteza muda muhimu kwa kutokuelewa nini cha kufanya. Tunafahamu kuwa taasaisi zetu za kusafirisha Mahujaji huwa zinatoa semina ya makusudio na namna ya kutekeleza ibada hiyo kabla ya mahujaji kuondoka nchini. Lakini kuzingatia maelekezo na kuujaza moyo kwa nia ni jambo jingine.

T u n a c h o p e n d a k u s i s i t i z a h a p a n i kwamba, halitakuwa jambo jema, au kielelezo cha mafanikio ya Hija k wa H u j a j i , i wa p o atakamilisha Hija na asiweze kupata athari ya Hija yenyewe, na akabakia kuwa kama hakuwahi kuhiji.

Lengo la Hi ja s io kujipatia anwani ya Alhaj au Hajat fulani. Hija kama zilivyo ibada nyingine ina lengo lake maalum na lisipofikiwa

inakuwa zoezi zima limeishia kuwa utalii. Hija humuandaa mja afikie kilele cha Ucha Mungu, ili awe mfano kwa wengine kwa kuwa tayari kwa moyo, kujitoa, kutoa kwa mali na nafsi, kuihuisha, kuisimamisha na kuilinda dini ya Allah (sw). Mtu anapokuwa katika hija, ni sawa na mtu aliye ndani ya kambi ya mazoezi ya kijeshi ya kuandaa kuwa tayari kuihuisha na kuipigania

dini ya Allah na kwamba akitoka hapo ataishi maisha yake yote kwa uchamungu wa hali ya juu na kuwa tayari kujitoa kwa kila alicho n a c h o k u u p i g a n i a mfumo wa maisha wa Kiislamu.

N i i m a n i y e t u kwamba mahujaji wetu wakifunga safari huku wakizingatia lengo ibada yenyewe, watarejea na kuwa kiigizo chema kwa umma na jamii

kwa ujumla na Uislamu utasonga mbele.

Tunamuomba Allah ( s w ) a w a w e z e s h e Mahujaji wetu kutekeleza salama na kwa usahihi ibada hii na kufikia daraja ya kutakabaliwa/h a j j - m a b r o o r , p i a tunamuomba Muumba kuwawezesha Waislamu wengine kupata fursa adhimu ya kutekeleza i b a d a h i i k a b l a ya k u o n do k a du n i a n i . Ameen

Page 3: ANNUUR 1144

3 AN-NUURDHULQAAD 1435, IJUMAA SEPTEMBA 26-OKTOBA 2, 2014Habari

K U R A z a h a p a n a zilizoshinda leo hazijaja kwa urahisi maana ahadi za kurejesha mamlaka m a k u b w a S c o t l a n d yataifanya nchi hii kuwa na mfumo mpya wa muungano wao. Bwana Alex Salmond namuona ni mwenye kipaji kikubwa na mwenye kujiamini, anajuwa anachokifanya na nina hakika hii ilikuwa ni vita ya mtu mmoja dhidi ya vyama vyote vikuu. Hata wakubwa waliostaafu na kubezwa katika siasa za nchi kama Gordon Brown naye pia alijitumbukiza kuhakikisha hawajitengi na umoja wao. Dunia nzima ilihamia Scotland kuhakikisha no vote inapatikana. Nakumbuka hata Bill Clinton nae aliwasihi kutojitenga kwa vile madhara yake ni makubwa zaidi kwa ‘alliance’ wa Marekani wanaemtegemea.

Kura za asilimia 45 ni nyingi ukitazama namna gani alivyoshinda dhidi ya mfumo wa miaka 300 ya umoja wao. Lakini naamini hakufanya tu bila ya mpango maalum wa kuhakikisha madai ya Scotland yanasikika vizuri upande wa pili na pia mabadilko makubwa zaidi ya matarajio ya wengi ya k imamlaka kwao yanapewa nguvu hasa pale wataposhindwa kujitenga. Kwa Waskotish leo, ni ushindi juu yao kwa vile miezi minane inayokuja tutaona namna gani mamlaka makubwa yakielekea Kaskazini kuanzia masula ya fedha, kodi , na hata uwezo wa kupanga sera zao za fedha. Chancelor wa fedha anaporwa mamlaka makubwa ya maamuzi kuelekea ‘devolution’ ya bunge la scotland huku hata mgao wa fedha kwa Scotland ukiongezeka maradufu kuliko kwa Waingereza wenyewe. Hio ndio gharama ya umoja wao.

Mustakabli wa Waskochi

M i r a d i m i k u b w a kubwa kama ya ustawi wa jamii na hata pensioni z i tawanufa isha za id i Waskotish kutokana na mamlaka waliokubaliwa kupewa. Lakini kuna uwezekano mkubwa kwa England nayo kupewa ‘devolution’ ya bunge lake. Hili halina mjadala, ninaamini katika miezi minane ijayo kilio cha Wa i n g e r e z a k i t a z i d i kukuwa hasa baada ya UKIP kulival ia n juga suala zima la mamlaka makubwa kwa Scotland wakiwa si wapingaji bali wakidai nao usawa kwa bunge lao mahsusi kwa yale yaliokuwa hayamo katika umoja wao. Kwa sasa mamlaka waliopewa Waskotish yatazidisha kelele za ‘devolution’ kwa England ili kuepusha wabunge Waskot land kuchangia masuala yasio wahusu ambayo kwa sasa yatazidi kuwa makubwa zaidi.

W a n a o m d h a r a u Alex Salmond hawajui mikakati yake na ya SNP waliyoipanga: kwanza w a t a e n d e l e a k u w a madarakani kwa muda mrefu zaidi, kwa vile asilimia kubwa ya kura walizopata zinaonyesha wataweza kuunda serikali hasa kutokana na ukweli wa kutoiva kwa Labour na Tory katika uundaji wa serikali ya pamoja.

P i l i w a t a e n d e l e a

k u y a t u m i a m a m l a k a watakayoongozewa kwa faida ya watu wao na zaidi kwamba wameweza kukidhi ahadi walioitoa ya kuleta kura ya maoni baada ya kuchaguliwa. Hil i kwa upande wa Uingereza chini ya uongozi wa Cameron linawaumiza kichwa kwa vile ahadi yao ya kura ya maoni kwa EU wameshindwa kuitekeleza kwa woga wa kushindwa na hata Labour pia anafahamu changamoto zinazowakabili mbele yao.

N i l i o y a s o m a k w a wenzetu:-Kwanza ustaarabu walioutumia kuhakisha kampeni zao zinakwenda kisheria na kuheshimiana.

Pili, uhuru wa maoni ya kila mmoja bila ya kufukuzana, kupandikiziana kesi na kutishana kwa uingiaji wa msituni kupinga ukuwaji wa maoni ya wananchi.

Ta t u , h a k u k u wa n a matusi yal ioelekezwa kwa aliekuja na kura ya maoni kwa sababu uhuru wa kusikiliza maoni ya wananchi unaheshimiwa na demokrasia ni nguzo ya utawala wenye nguvu.

Nne, umoja umelindwa k w a k u s i k i l i z w a m a l a l a m i k o y a o n a kuhakikisha unalindwa kwa kuwapa mamlaka yao Waskotish wanayoyadai.

Tano, kwa lolote lenye mashaka, njia bora ni kurejea kwa wananchi na kuweza kupata kauli moja kubwa ya kuondosha utata.

Sita, wingi wa wabunge wa SNP katika Scotland haukuwafanya kupindisha

taratibu au kupandikiza maoni yao kwa jambo lenye nguvu ya wananchi, walikubali kulirejesha moja kwa moja kwa wananchi kusikiliza maoni yao.

Saba, umoja wa kweli ni wa kuheshimiana, wa kufuata haki na usawa kwa kila upande.

N a n e , h a t a k a t i k a miungano mikubwa yenye faida kwa pande zote ikiwa hakuna haki, usawa, heshima na kusikilizwa kwa maoni ya wananchi hakuna guarantee ya kudumu kwa miungano hio.

Tisa, tunapojadili faida za miungano tujikite katika uzito wa hoja si kelele za mchele wa Mbeya na tashtiti za dharau kwa wengine. Khofu ya jeshi kuchukuwa nchi na tashtiti za kutuita wauza vitunguu haitasaidia kurejesha umoja tunaoutamani.

Kumi, tunapopima faida za kuwepo kwa muungano, tusidharau mchango wa sehemu nyengine kwa sababu ya udogo wake na udogo wa IDADI yake ya watu. Uingereza ina idadi ya watu milioni sitini, Scotland milioni sita, Uwiano wa 6:1. Na kwetu pia milioni arobaini kwa milioni moja haiwapi haki walio, wengi na kuzima kwa wachache.

Nimalizie kwa waliofurahia referendum ya No vote kwa Scotland, wafahamu kwanza faida ya referendum ambayo kwa upande wetu imekuwa ikichezewa chezewa kisiasa.

Pili, ikiwa referndum ya no vote ya 55% ni ya kupigiwa makofi na kupongezana, wakumbuke pia mabadiliko ya Zanzibar ya katiba ya 2010 yalikuja na ushindi wa asilimia 66. Fikiria kama No vote wangelipata ukubwa wa wingi wa asilimia 66.

Wito wangu ni kwa wenye mamlaka kutuuliza nasi wananchi wa nchi h iz i mfumo gani wa serikali tunaoutaka katika muungano na mabadiliko tunayoyatarajia. Tunahitaji kura ya maoni kutuuliza kwa uwazi muelekeo wetu sio vyama kubeba hatamu na matashi ya wananchi.

(Kwa hisani ya Farrell Foum)

Page 4: ANNUUR 1144

4 AN-NUURDHULQAAD 1435, IJUMAA SEPTEMBA 26-OKTOBA 2, 2014Habari

IMEELEZWA kuwa kwa hali ilivyo hivi sasa Zanzibar, serikali ndiyo itavunja amani na wala sio raia.

Hayo yameelezwa kufuatia hatua ya kukamatwa watu wanaotuhumiwa kwa ugaidi na kutolewa madai kuwa w a n a f a n y i w a m a t e n d o machafu huku serikali ikikaa kimya kana kwamba inaridhia mambo hayo.

Hayo yamezungumzwa na Mzee Amiri Bin Amir Soud, wa Kijiji cha Bwejuu, Mkoa wa Kusini Zanzibar, akiwa Jijini Dar es Salaam, akitoa maoni yake juu ya kukamatwa kwa Maamir (Masheikh) wa Kiislamu wa Zanzibar.

Mzee Soud, aliyedai kwamba amezama katika historia ya Zanzibar, alisema matendo m a c h a f u y a n a y o d a i w a kufanyiwa watuhumiwa hao kutoka Zanzibar, ni kuita laana katika nchi.

Alisema, kwa ujumla hivi sasa Zanzibar kwa Waislamu si salama na hai jul ikani watakimbilia wapi.

M z e e S o u d , a l i s e m a kiuhalisia Wazanzibar wapo katika hali mbaya na wengi wao hawana pa kukimbilia akiilinganisha hali hiyo na kipindi cha Hijra wakati wa Mtume (s a w).

Alisema, katika kipindi hicho cha Makka, baada ya mateso kukithiri kwa Waislamu, wengine kuuwawa na wengine kutekwa miongoni mwao walienda Ethiopia na wengine Madina, hata hivyo si wote walioondoka bali walibaki.

“Kule Zanzibar, kuna watu hawana uwezo hata wa kufika pale Tumbatu si kwambii kwingine zaidi ya hapo, sasa kulingana na hali hiyo ukirejea na kipindi cha Waislamu Makka, bila shaka hapa kuna Tawhid”. Alisema Mzee Soud.

Mzee Suod, alisema kwa sasa Visiwani Zanzibar, baadhi ya Msheikh wenye il imu wanatamani wakimbie nchi kama walivyokimbi katika miaka ya 1964, akadai na ikitokea hivyo katika kipindi hiki itakuwa ni pigo kubwa kwa Zanzibar.

Alisema, wakati Mwenyezi Mungu anawataja waja wake

SMZ itavuruga amani ZanzibarInarudia yale ya Wareno, MapinduziMakkah walikimbilia kwa mfalme NajashMasheikh Zanzibar nao wakimbilie wapi?

Na Bakari Mwakangwale

wema pia aliwataja watu wenye ilimu, lakini sasa Zanzibar, watu kama hao wapo ndani wanafanyiwa mambo machafu, na wengine wameingia hofu kubwa akadai huo ni mtikisiko mkubwa.

M z e e S o u d , a l i s e m a Mwenyezi Mungu amewapa Wazanzibar mtihani mkubwa kutokana na hayo yanayojiri hivi sasa, na kwamba mtihani huo haujakomea Zanzibar tu bali unawagusa hata Tanzania Bara, wakiangal iwa nini utakuwa msimamo wao kwa ujumla kama Waislamu.

A l i s e m a , Wa t u we n g i wa n a f i k i r i k u wa a m a n i inavurugwa na raia tu, jambo ambalo si sahihi kwani hata watawala wanaweza kuvuruga amani kulingana na kutokana na kuwatendea ndivyo sivyo raia wake.

Alisema, mtihani huo kwa Masheikh wao kufanyiwa mambo machafu ni wa tatu kutokana na kumbu kumbu zake za matukio Visiwani humo toka Visiwa hivyo vianze kukaliwa.

Aliutaja mtihani wa mwanzo kuikumba Zanzibar ulikuwa ni mwaka 1792, wakati huo ikitawaliwa na Mreno, baada ya Msikiti Mkuu kuvunjwa, na mtihani wa pili ulitokea mwaka 1994, ambapo alidai hakuna asiye ujua.

Al i sema , kutokana na

m a m b o h a y o a m b a y o yanaashiria mwisho mbaya

kama hayatatafutiwa ufumbuzi a l i l azmika kukutana na Kamishna wa Jeshi la Polisi Z a z i b a r , n a k u m we l e z a masuala hayo na hatma ya wanakokwenda.

“ N a n i k a m t h i b i t i s h i a kwamba tokea Mapinduzi ya Zanzibar, yeye ni Kamishna wa nane lakini nilimweleza mtihani huu tokea yeye kuwa Kamishna, ni mtihani mkubwa mno”. Alisema Mzee Soud.

M z e e S o u d , a l i z i t a k a mamlaka husika kuwachukulia hatua za kinidhamu wale wote watakaobanika kuwatendea uchafu Masheikh na Waislamu hao kwani kulifumbia macho ni kama vile Serikali ya Jamhuri ya Muungano inaunga mkono ufedhuli huo wa watendaji wake.

Mzee Amiri Bin Amir Soud.

Page 5: ANNUUR 1144

5 AN-NUURDHULQAAD 1435, IJUMAA SEPTEMBA 26-OKTOBA 2, 2014Habari za Kimataifa

KABLA ya kuanza makala hii, ningependa kuwatahadharisha ndugu zangu Waislamu, kuhusu watu wanaoingiza mawazo yao binafsi kwenye masuala ya Dini. Kwa sababu watu wa namna hii ni maadui wa Sunna. Wameshindwa kulinda na kuhifadhi miongozo halisi ya Kiislamu, sasa wanazungumza kwa kutumia fikra na maono yao binafsi. Watu hawa hakika wamepotoka na wanawapotosha wengine.

Mwenyezi Mungu Mtukufu ameyaumba maisha haya na kuyawekea mfumo maalumu ambao hayawezi kuukiuka. Anasema ndani ya Qur'an: "Hii ni kawaida ya Mwenyezi Mungu ilivyokuwa kwa wale waliopita zamani; wala hutapata mabadiliko katika kawaida ya Mwenyezi Mungu"Qur(33:62).

Na katika Aya nyingine, Mwenyezi Mungu anasema: "Ndiyo desturi ya wale tuliowatuma (tuliowapa Utume) kabla yako katika Mitume wetu. Wala hutapata mabadiliko katika desturi yetu"Qur(17:77).

Sehemu ya mfumo huu wa Mwenyezi Mungu ni msuguano wa kudumu baina ya Haki na Batili. Yaani mgongano uliopo kati ya ukweli na upotofu. Hata siku moja Haki haitavumilia Batili, wala Batili kuikubali Haki. Msuguano huo ni wa milele, na unaweza kuchukua sura mbalimbali, kuanzia kitaaluma, kiuchumi, kijamii, kisiasa na hata kimapigano.

Mapitio ya haraka katika Sira ya Mtume Muhammad (saw) yanaonyesha kwamba alifanya harakati za kupambana na Batili. Pale Makkah wakati ule, Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuwa akionyesha upotofu wa Imani za Maqurayshi, mifumo yao ya maadili na utamaduni, bila ya woga wala kulegeza msimamo (compromise), ili kuleta maelewano.

Kiukweli, Mitume na Manabii wote wa Mwenyezi Mungu, walibeba kasumba hii na kufuata mwendo huo, na matokeo yake, kila Mtume na Nabii, alipingwa vikali na Ukafiri uliokuwepo wakati wake. Mjini Madina, wakati Muhammad (saw) alipoasisi Dola ya Kiislamu, dola hii ilitumika kama jukwaa la kueneza Uislamu kwenye mataifa mengine, ikiwa ni pamoja na kuipa changamoto mifumo ya maisha ya Kikafiri kwa kutumia mfumo wa Kiislamu.

Mtume wa Mwenyezi Mungu, mara kwa mara, alikuwa akihusiana na watu wa mataifa mengine, kwa lengo la kuifanya Haki kuwa juu ya mifumo yote ya maisha wakati ule. Mapambano haya ya Haki na Batili yameendelea hata baada ya kifo chake.

Umma wa Kiislamu ulipambana na mataifa mengine, yawe ya washirikina, Wafursi, Watatari, Wa m o g h u l , M a k r u s e d a , a u Wakomunisti.

Hata leo, Umma wa Kiislamu bado uko katika mapambano dhidi ya mataifa ya Kibeberu ya Kisekula. Kwa hiyo, msuguano kati ya Umma wa Kiislamu na mataifa mengine ni jambo la kimaumbile, kutokana na ukweli kwamba jukumu la msingi la Umma wa Kiislamu ni kueneza Uislamu kama Itikadi, ambayo ndani yake kuna mfumo kamili wa maisha.

Sasa mazingira ya kazi hiyo, yanaupa jukumu Umma wa Kiislamu duniani la kuzipa changamoto fikra za Kikafiri, ili kufichua upotofu wake, lengo likiwa kuufanya mfumo wa Mwenyezi Mungu na Itikadi yake, kuwa juu ya mifumo yote, kwa ajili ya binadamu wote. Hiyo ndiyo sababu ndugu zangu, ya msuguano huu usiokwisha, baina ya Uislamu na Ukafiri na baina ya Haki na Batili.

Ingawa msuguano huu ni uhalisia wa uumbaji wa Mwenyezi Mungu,

Said Rajab

lakini nyenzo, mbinu, sura na methodolojia za mapambano yake hubadilika. Kwa mfano, Ulimwengu wa Magharibi ulitaka kuwaritadisha Waislamu moja kwa moja, kwa kutumia Wamissionari. Walitaka Waislamu waukumbatie Ukristo na Usekula, lakini walishindwa vibaya! Waislamu walikataa kabisa kuacha Dini yao Tukufu na kushika mawazo ya Kikafiri ya Ukristo na Usekula.

Baada ya kushindwa, Ulimwengu wa Magharibi ukabadili mbinu na kuja na nyingine iliyo bora zaidi, ambayo imewaletea mafanikio makubwa. Mbinu hiyo ni kutambulisha fikra za Kimagharibi katika mafundisho ya Uislamu na kuonyesha kuwa fikra hizo zinalingana na Uislamu.

Kwa hiyo, badala ya kuwategemea Wamissionari na 'Orientalists ' kusambaza fikra hizo potofu, sasa wanawategemea wanafiki katika Uislamu, au makundi ya Waislamu yaliyotayarishwa kufanya kazi hiyo. Watu hawa ndiyo vifaa vyao muhimu vya kusambaza upotofu katika jamii za Waislamu.

Imefikia mahali , baadhi ya Waislamu, bila hata hofu ya Mwenyezi Mungu, wanajaribu kuwachuza Waislamu wenzao, waikumbatie Serikali ambayo imeonyesha wazi uadui wake dhidi yao. Kwa kuwa wao wamekubali kuwa watumishi wa mfumo wa maadui dhidi ya Waislamu wenzao, sasa wanataka kuhalalisha uovu wao huo kwa kupotosha visa vya Manabii!

Yusuph (as) hakuwahi kushiriki kwenye uongozi wa ser ika l i ya Kikafiri. Kitendo kama hicho hakiwezi kufanywa na Nabii wa Mwenyezi Mungu, kwa sababu ni kinyume kabisa na dhana nzima ya Unabii, kama Aya zinavyobainisha hapo juu.

Watu hawa wanaoingiza fikra potofu za Kimagharibi kwenye Dini ya Mwenyezi Mungu, wanatumikia maslahi ya maadui, na hivyo wanakuwa ni wasaliti wa Mwenyezi Mungu, Mtume wake na Umma wa Kiislamu. Bila ya kuzingatia nia zao, athari ya kile wanachokifanya ni ile ile. Wanapanda mizizi ya Kufru kwenye shamba la Kiitikadi la Umma, hatua ambayo inawaweka mbali zaidi Waislamu na methodolojia sahihi ya kuhuisha dini yao.

Kama vile uhalisia wa kimaumbile unavyotaka, mgongano na msuguano huu baina ya Haki na Batili lazima uendelee, basi na uenezaji wa fikra potofu za Kikafiri katika Umma wa Kiislamu nao utaendelea tu. Hasa ikizingatiwa kwamba Waislamu hawana mfumo wa kinga ya kuzuia hilo.

Nimejaribu kuangalia fikra kadhaa kubwa, ambazo zinaletwa kwa Waislamu kama fikra za Kiislamu, wakati uhalisia wake ni fikra za Kikafiri ambazo hazina uhusiano wowote na Uislamu:

Fikra ya kwanza: Kutenganisha Dini na Dola - Dhana ya kutenganisha dini kutoka kwenye maisha ya kawaida au uendeshaji wa Dola ndiyo chimbuko la ustaarabu wa Kimagharibi na msingi wa mtazamo wake kuhusu maisha. Dini katika msamiati wa Kimagharibi, ni mpangilio wa taratibu za kiibada zinazomuhusu mtu binafsi na haihusiani kabisa na jamii.

Katika ulimwengu wa Magharibi, d in i inashughul ik ia masuala maalumu kama ndoa, talaka, ibada, vifo na baadhi ya maadili, lakini haihusiki kabisa na uchumi, utawala, mfumo wa elimu, sera ya nje au masuala ya kisiasa. Dhana hii potofu inaletwa kwa Waislamu, siyo tu na masekula peke yao, bali na hata wale

wanaoitwa wanaharakati, Masheikh na makundi ya Kiislamu.

Uenezaji wa Usekula miongoni mwa Waislamun unafanyika kupitia njia mbili ambazo zote zinatumia nyenzo ile ile:

Wa n a z u o n i w a K i i s l a m u waliopigwa msasa. Ya kwanza ni pale Waislamu wanapoamrishwa kuacha kuingilia masuala yanayohusu uendeshaji wa jamii zao. Kauli kama, "Jihusisheni na mambo yenu tu", "Achana na siasa na jenga Imani yako" au "Acheni mambo hayo na mjipinde katika Ibada na kutafuta elimu".

Wanazuoni hawa pia wanatoa fatwa za kidini zinazowalazimisha Wais lamu kuwa wat i i fu kwa watawala, hata kama watawala hawa wanawadhulumu. Wanawakataza Waislamu kuwapinga watawala hawa, kwa hoja kwamba hatua hiyo itasababisha fitna.Wanasema Uislamu lazima ufuatwe kwa awamu. Awamu ya kwanza ni kushughulikia nafsi yako.

Kwa miongo kadhaa Umma wa Kiislamu umekuwa na kazi ya kushughulikia na kutathmini nafsi tu, na haujawa tayari kuanza kazi ya Kiislamu ya kushughulikia matatizo ya kijamii katika Umma! Njia nyingine inayotumiwa na wanazuoni hawa imekuwa ni kuweka mkazo katika ufundishaji wa kanuni binafsi za Kiislamu.

Wanaushughulisha Umma wa Kiislamu na taratibu za Swala, Zaka, Hija na Funga kwa mtazamo wa kibinafsi zaidi kuliko inavyopaswa kuwa. Methodolojia inayofuatwa katika ufundishaji wa Ibada hizo siyo sahihi. Hazifundishwi kama sehemu ya mfumo kamili wa maisha unaotoka ndani ya Aqida ya Kiislamu.

B a d a l a y a k e , I b a d a h i z i zinafundishwa katika namna ambayo zinatenganishwa na maisha ya kila siku ya watu. Wanazuoni hawa wanapuuza kabisa kufundisha kanuni zinazohusiana na Huduud (penal code), Jihad, Jizya, Bay'ah na uhalisia kama nchi wanayoishi Waislamu ni Dar ul -Islam au Dar ul - Kufr, na vipi Waislamu wajipange katika mazingira hayo mawili tofauti! Mada nyingi tu muhimu kuhusu Uislamu hazifundishwi kabisa.

Mafanikio ya njia hii ni makubwa sana kwa maadui wa dini ya Mwenyezi Mungu. Uislamu umebaki kuwa ni vitendo vya Ibada tu 'rituals' katika fikra za Umma wa Kiislamu. Muislamu leo anaweza kumfokea kwa hasira mwenzake anayeingia msikitini kwa kutanguliza mguu wa kushoto, na asione tatizo sheria za Kikafiri kuongoza jamii yao, badala ya sheria za Mwenyezi Mungu.

Waislamu wanaweza kugombana na mwenzao ambaye hakuzingatia M a n d o u b ( v i t e n d o a m b a v y o vikifanywa, Muislamu anapata thawabu, lakini visipofanywa haadhibiwi), lakini wakawa kimya kabisa dhidi ya Kufru inayotekelezwa juu yao, ambayo si tu ni haramu, bali inapingana kabisa na msingi wa uwepo wao.

Wamefundishwa kwamba ya kwanza ndiyo kupinga Uislamu, bila ya kupewa ufahamu wa dhana ya pili. Hata wale wanaoona kuongozwa Kikafiri ni tatizo, hawaoni hilo katika namna ambayo Uislamu unaona. Uislamu unaliangalia hilo kama jambo la kufa na kupona.

Tunajifunza katika historia, wakati Washirikina wa Makkah walipomfuata Abu Talib, baba yake mdogo Mtume, ili amwambie Mtume aache kushambulia imani zao, Abu Talib alifikisha ujumbe huo kwa Mtume. Majibu ya Mtume wa Mwenyezi Mungu yalikuwa haya:

"O baba yangu mdogo, hata wakiweka jua kwenye mkono wangu wa kuume na mwezi kwenye mkono wangu wa kushoto, sitoacha hili mpaka Sheria ya Mwenyezi Mungu isimame au nife"

Tofauti kabisa na Mtume wa Mwenyezi Mungu, Waislamu leo wanaona kusimamisha mfumo wa Sheria za Mwenyezi Mungu kwenye jamii zao ni jambo la mbali, ambalo hatimaye litashuka tu kutoka mbinguni kwenye kisahani, ambapo sasa mazingatio yote yawekwe kwenye maadili, "kuhesabu nafsi zetu" na taratibu binafsi za Ibada. Njia hiyo si lolote zaidi ya kuitenga dini ya Mwenyezi Mungu kutoka kwenye maisha ya kila siku ya jamii.

Fikra ya Pili: Kigezo cha Faida - Kigezo cha kutenda mambo katika ulimwengu wa Magharibi ni faida au manufaa. Kigezo hiki ni matokeo ya kutenganisha dini na maisha. Ulimwengu wa Magharibi umetafsiri furaha kama kufikia anasa kubwa zaidi. Kwa hiyo wanaamua jambo gani wafanye, kulingana na faida yake, kama mawazo yao yanavyofahamu faida hiyo.

Fikra hiyo potofu inaingizwa kwenye Umma wa Kiislamu, siyo tu na mwanaharakati mmoja mmoja, bali hata makundi ya Kiislamu. Nao wamegeuza faida kama kigezo chao cha kuendea mambo, baada ya kuivisha ladha ya Kiislamu. Kwa hiyo kinachotokea ni kuwaondoa Waislamu kutoka kwenye 'Ahkam Shariah', ambayo ndiyo kigezo chao cha kutenda mambo. Matokeo ya hilo, Sheria za Kiislamu, hata zile

Uchakachuaji wa Aqida ya Kiislamu

Inaendelea Uk. 12

Page 6: ANNUUR 1144

6 AN-NUURDHULQAAD 1435, IJUMAA SEPTEMBA 26-OKTOBA 2, 2014Makala

SIKU ya Jumatano tarehe 17/09/2014 nimebahatika kusoma makala ya kaka yangu Padre Baptiste Mapunda yenye kichwa cha habari “CCM na kitanzi chake cha Mahakama ya Kadhi”.

Nilipoisoma mara ya kwanza n i l i s taa jabu “ho ja dhai fu” alizozitoa Mheshimiwa Padre Mapunda, lakini nilipoipitia kwa mara ya pili nilijiridhisha kwamba kwa misingi ya kutetea “imani” yake aliwajibika kuandika aliyoyaandika.

Pamoja na kustaajabu hayo, kuna “maeneo” ya makala yake yamenihuzunisha na baadhi ya maeneo yamenifurahisha sana.

Katika makala yangu hi i niliyokusudia kumuelimisha Padre Mapunda na Mtanzania mwengine yeyote, nimeigawa katika maeneo makuu matatu:

(1) Maeneo yaliyonistaajabisha katika maneno ya Mheshimiwa Mapunda.

(2) Maeneo yaliyonihuzunisha katika maneno ya Mheshimiwa Mapunda.

(3) Na maeneo yaliyonifurahisha.Kabla sijaanza uchambuzi

huo, nichukue fursa hii kutoa ufafanuzi ufuatao juu ya kadhia ya Mahakama ya Kadhi hapa kwetu Tanzania:

M a h a k a m a ya K a d h i n i mahakama maalum inayohusika na kesi za ndoa, talaka, miirathi, waqfu, wasia na malezi ya watoto kwa mujibu wa sheria ya Dini ya Kiislamu. Hakimu wa Mahakama hiyo ambaye anaitwa Kadhi, ni Muislamu anayejua vyema ufumbuzi wa kadhia hizo. Kesi zote za jinai hata kama iwe kati ya Muislamu na Muislamu zitabakia katika mfumo wa kawaida wa Mahakama wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

HUU NDIO UKWELI KUHUSU UKADHI:Padre Mapunda amepinda, tumuelimishe aelimike

Na Sheikh Mohamed Iddi Mohamed

Hitajio la Waislamu katika Ukadhi:K u k o s e k a n a k wa K a d h i

kunawanyima Waislamu haki ya kutekeleza Ibada ya Ndoa kwa ukamilifu wake, kwani kwa mujibu wa sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwenye mamlaka ya kutoa talaka ni Mahakama tu, wakati Uislamu unafundisha mtoaji talaka ni yule yule aliyeoa. Na pindi Muislamu akitoa talaka, serikali haiikubali talaka hiyo muda wa kuwa haijathibitishwa na Mahakama. Na pindi Mahakama ikitoa talaka, Uislamu hauikubali talaka hiyo kwa kuwa ndoa iliyofungwa kwa sheria za Kiislamu haivunjiki kwa sheria nyengine. Hii ni adha kwa Waislamu na mtatuzi wake ni Mahakama ya Kadhi.

Waislamu wanaamini kuwa zipo baadhi ya ndoa haziwezi kuendelea kwa mujibu wa mafundisho ya dini yao. Kwa mfano; ndoa ya mume aliyefungwa gerezani muda mrefu na hana mapato yatakayomkimu mkewe mpaka amalize kifungo, au ndoa ya Muislamu aliyekwenda nje ya Tanzania akazamia huko kwa muda mrefu kutafuta maisha na mkewe amemtelekeza, au Muislamu yupo hapa hapa nchini lakini ni mjeuri, anamtesa mkewe na anasema anajua kuoa hajui kuacha, kiasi kwamba mkewe huyu anataabika sana.

Kuzivunja ndoa za aina hiyo kunahitajia nguvu mbili: kwanza, nguvu ya Kidini ili imani na sheria ya Kiislamu iliyotumika kuwafungisha ndoa ifanye kazi yake kwani ndoa iliyofungwa kiimani inavunjwa kiimani pia. Pili, nguvu ya kiserikali ili mume kama hatoridhika asiweze kuleta madhara baada ya ndoa yake kuvunjwa, na serikali pia ikubali kuwa ndoa imevunjika ili isimtambue mwanamume huyo kuwa ni mume wa mwanamke huyo kwa mujibu wa sheria za nchi.

Katika muda huu ambao hakuna Mahakama ya Kadhi, ndoa zote zinazovunjwa na Mahakama za kawaida bila ya wale waume zao kutoa talaka, pindi watalaka wao (wanawake) wakiolewa tena na waume wengine, hizo ni ndoa ndani ya ndoa. Na ndoa hii ya pili haiswihi (haikubaliki) kwa mujibu wa sheria ya Dini ya Kiislamu na ni batili.

Tatizo hili haliwezi kuondoka kama hakuna Mahakama ya Kadhi, na mwanamke huyu Muislamu analazimishwa imma azini (endapo atafuata hukumu

hiyo ya Mahakama ya kawaida na yeye kukubali kuolewa tena na mume mwengine) au afe mjane (kwa kukubali talaka hiyo ya Mahakama ya kawaida na kukataa kuolewa tena).

Waislamu wa Tanzania kwa k u z i n g a t i a u m u h i m u h u o waliiomba serikali yao “huduma” hiyo katika awamu zote za utawala wa nchi hii kuanzia awamu ya kwanza hadi hii awamu ya nne, lakini bado hawajafanikiwa katika hilo na bado Waislamu wanaendelea kuomba.

Sasa nirudi kwenye makala ya kaka yangu Mheshimiwa Mapunda katika maeneo matatu niliyoigawanya:

(1) Maeneo niliyostaajibishwa katika maneno ya Mheshimiwa Mapunda:

N i m e s t a a j a b i s h wa s a n a na kauli yake yenye lengo la “kumsaliti” Mzee Ali Hassan Mwinyi ili aonekane katika jamii kwamba ndiye anayewachochea Waislamu kudai Mahakama ya Kadhi. Namnukuu Mheshimimwa Mapunda aliposema:

“Raisi wa Awamu ya Pili, Alhajj Ali Hassan Mwinyi siku si nyingi alisikika akitetea Mahakama hizo za Kadhi, Je, alikuwa wapi kuanzisha alipokuwa madarakani? (mwisho wa kunukuu).

Katika hoja hiyo naomba nimkumbushe kaka Mapunda kuwa Raisi Mstaafu, Mzee Ali Hassan Mwinyi hana kosa kufanya hivyo kwa sababu yeye alikuwa Raisi wa Zanzibar kabla ya kuwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kule Zanzibar Mahakama ya Kadhi ipo na Wakristo wapo tena ni wachache na wala haina madhara yoyote .

K u h u s u s u a l a k wa m b a , kwanini hakusema wakati yuko madarakani? Huenda alisema lakini “mfumo” ambao wewe kaka yangu Mapunda unaujua “ulimdhibit i” na hakufikia mafanikio katika hilo.

N a o m b a n i m k u m b u s h e tena Mheshimiwa Mapunda ili aelimike kwamba katika uongozi wa Awamu ya Tatu chini ya Mheshimiwa Raisi Mstaafu Benjamin Wil l iam Mkapa, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania liliunda Tume ya kufuatilia Mahakama ya Kadhi chini ya uenyekiti wa Mheshimiwa Athumani Janguo (Mbunge mstaafu wa Kisarawe) na Tume hiyo ilitumia fedha za walipa kodi hawa hawa. Miongoni mwa wajumbe wa Tume hiyo ni:

(a) Marehemu Mheshimiwa Mzee Abdallah Saidi Fundikira.

(b) Mheshimiwa Rosemary Nyerere.

(c ) Mheshimiwa Nimrod Mkono.

(d) Mheshimiwa Wilbroad Slaa.(e) Mheshimiwa Kingunge

Ngombale Mwiru.(f) Mheshimiwa Mbunge wa

Masasi wa wakati huo.(g) Mheshimiwa Shoka kutoka

Zanzibar.Kama kitendo cha Mheshimiwa

Mzee Ali Hassan Mwinyi kulitaja tu suala la Ukadhi, unamuuliza alikuwa wapi kufanya hivyo al ipokuwa madarakani . Je , Mheshimiwa Benjamin Mkapa ambaye Tume iliundwa katika wakati wake na mpaka leo majibu ya Tume hiyo “yamekaliwa” na hayakutolewa unampa tafsiri gani? Kwamba kumbe mtu akiwa madarakani ndivyo anavyotakiwa

Inaendelea Uk. 7

Page 7: ANNUUR 1144

7 AN-NUURDHULQAAD 1435, IJUMAA SEPTEMBA 26-OKTOBA 2, 2014Makala

Padre Mapunda amepinda, tumuelimishe aelimikeInatoka Uk. 6kuwa? Endapo fedha zikitumika na “mfumo” ukazuia ripoti isitoke, kumbe ni halali? Je, zile fedha zilizotumika kwenye ile kamati ambayo imejumuisha mpaka wajumbe Wakristo kwenda kufuatilia suala lenye masilahi ya Dini ya Kiislamu tu zilikuwa halali?

Inastaajabisha zaidi pale Mheshimiwa Padre Mapunda “anapolikoleza” suala la Ukadhi kwa kulihusisha na CCM ili Waislamu wajenge “hasira” na CCM, hiyo ni mbinu ya kitoto kwa sababu CCM wameliweka suala la Ukadhi kwenye ilani yake katika Uchaguzi wa mwaka 2010 na Tume ya Mheshimiwa Arcardo Ntagazwa ambaye baada ya kuteuliwa kuwa waziri i l iongozwa na Mheshimiwa Athumani Janguo juu ya suala la Ukadhi ilikuwepo kabla ya mwaka 2010. Je, kuihusisha CCM kwa sababu tu Waislamu waamini kwamba “mbaya” wao ni CCM ili waigomee kuipa kura hauoni kuwa ni usaliti kwa CCM ambayo Mwenyekiti wake kwa sasa ni Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete? Mbona CCM ilipokuwa chini ya uenyekiti wa Mheshimiwa Benjamin William Mkapa, yeye hakubebeshwa shutuma hizo ijapokuwa hiyo ilani inayoelezea ahadi ya Mahakama ya Kadhi imetayarishwa chini ya uenyekiti wake? Kwanini utayarishaji wa ilani hiyo uliofanywa chini ya uenyekiti wa Mheshimiwa Mkapa lawama zake abebeshwe Mheshimiwa Jakaya Kikwete? Je, kweli huo ni uadilifu kaka yangu Padre Mapunda?

(2) Maeneo niliyohuzunishwa katika maneno ya Mheshimiwa Mapunda:

Nimehuzunishwa sana na maneno ya Mheshimiwa Padre Mapunda aliposema (namnukuu):

“Viongozi wa dini ya Kikrsito kwa upendo wote waliposema Mahakama ya Kadhi haitakiwi kujadiliwa bungeni wali jua wal i chokuwa wakik i sema. Wanajua ubaya wa Mahakama hizo na wanajua kwa mifano kwa nchi nyengine kama Sudan, Somalia, na sasa Nigeria jinsi ambavyo kumezuka mizozo.” (mwisho wa kunukuu).

Nimehuzunishwa sana kwa maneno hayo ya “uongo” kutoka mdomoni mwa kiongozi wa kidini mwenye cheo cha Upadre. Kama Padre anaweza kusema uongo ili kufanikisha matakwa yake, Je waumini wafanye nini? Hivi mgogoro wa Sudan kumbe wanagombea Ukadhi? Hivi mgogoro wa Somalia nao wanagombea Ukadhi? Na hata Nigeria kumbe Boko Haram nao wanataka Ukadhi?

Inahuzunisha sana kuusema uongo huo i l i Watanzania

RAIS Mstaafu Benjamin William Mkapa.

waogope na wasitamani tena k u s i k i a c h o c h o t e k u h u s u Mahakama ya Kadhi. Kama kaka yangu Padre Mapunda alikusudia kusema ukweli kwanini hakuitaja Zanzibar ambayo ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ina Mahakama ya Kadhi? Kwanini hakuitaja Kenya (ambayo Waislamu ni chini ya asilimia ishirini) lakini Mahakama ya Kadhi ipo? Mahakama za Kadhi zipo Kenya na Zanzibar na hakujaripotiwa mauaji au migogoro kama ya huko Sudan, Somalia na Nigeria? Ni v ip i k iongoz i wa d in i anakuwa mwongo? Na kwa nini amelazimika kuwa mwongo?

Hiv i pa le Mahakamani pakiandaliwa chumba maalum kisha akawepo Sheikh ambaye z i k i j a M a h a k a m a n i k e s i zinazohusu ndoa, talaka, miirathi, waqfu, wasia na malezi ya watoto; yule Sheikh awe anazitolea maamuzi, Je, huyo mtu mwengine anauliwa kwa kosa lipi?

Kwa kitendo cha ndugu yangu Padre Mapunda kufananisha maombi ya Waislamu juu ya Mahakama ya Kadhi na kuuliwa kwa watu Sudan, Somalia na Nigeria, amefanya uchochezi, kejeli na dharau dhidi ya Uislamu na Waislamu.

(3) Maeneo niliyofurahishwa katika maneno ya Mheshimiwa Mapunda:

Nimefurahishwa sana na

mambo matatu kutoka kwa kaka yangu Padre Mapunda: Jambo la kwanza: Nimefurahishwa sana na kitendo chake cha kutushauri Waislamu kwamba tuanzishe hizo Mahakama za Kadhi sisi wenyewe. Katika hili yako maswali kadhaa ambayo tunamuomba Mheshimiwa Padre Mapunda atutafutie majibu:

(i) Je, baada ya Waislamu kuanzisha Mahakama zetu za Kadhi kisha ikatokea Muislamu mmoja akatenda jinai ya wizi au kupiga au chochote akahukumiwa na Mahakama ya kisekula kwenda jela miaka mingi, na mke wa mfungwa huyu akaenda kwa Kadhi ili aombe talaka kwa mumewe huyo na Kadhi akaandika barua kwa Mkuu wa Gereza ili mfungwa huyo aletwe kwa Kadhi kwa ajili ya shauri hili jipya la mkewe, Je, Mkuu wa Gereza atatoa gari na askari ili mfungwa huyu aletwe na wamlinde katika Mahakama ya Kadhi mpaka kesi iishe? Je, Bwana Jela anawajibika kutii agizo la Taasisi binafsi isiyohusika na serikali?

(ii) Tutakapounda Mahakama yetu wenyewe kisha Kadhi akaivunja ndoa ya Muislamu fulani, ikatokea kwamba yule Muislamu hakuridhika akaenda Mahakama ya kisekula kumshitaki Kadhi kwa kuwa amemvunjia ndoa yake, Je ni upi ulinzi wa kisheria kwa Kadhi huyo?

(iii) Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haitambui talaka ya Muislamu. Kwa mfano, Muislamu akiamua kumpa mkewe talaka, na mke huyo akakaa eda (na ikaisha eda hiyo), baada ya eda kuisha ikatokea mume kafariki na yule mke aliyeachwa akaja kudai na yeye miirathi, na kesi ikafikishwa kwa Kadhi na talaka ya mume yule ikaletwa kama ushahidi kwamba mke huyo aliachika na mke akadai hiyo ni dhamira tu kwani mvunjaji wa ndoa ni Mahakama ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kadhi akahukumu kwamba huyu mke aliyeachwa harithi kwa kuwa aliachika kwa mujibu wa mafundisho ya Dini ya Kiislamu, halafu mke huyu akaenda kwenye Mahakama ya kisekula kumshitaki Kadhi kwa kumnyima kurithi mali ya anayemuita kuwa ni mumewe na Hakimu wa Mahakama ya kisekula akahukumu kuwa mke huyu ni mrithi kwa mujibu wa sheria za nchi. Je, ni upi umuhimu wa Kadhi huyo kama hukumu zake za kidini zinaweza kuvunjwa na Mahakama isiyo ya kidini?

Jambo la pili: Nimefurahishwa sana pale kaka yangu Padre Mapunda alipotoa “ushuhuda” kwa kusema kwamba: “Viongozi wa Dini wa Madhehebu ya Kikristo walishatoa maelezo ya kutosha kwa serikali na misimamo yao ipo wazi kabisa”.

Katika hili ni vizuri ndugu yangu Mheshimiwa Mapunda akaendelea kubainisha ni vipi Mahakama ya Kadhi iliyoombwa serikalini na Waislamu kwa sababu zao halafu viongozi wa Medhehebu ya Kikristo waingilie kati? Je, wanahusikaje mpaka kufikia kutoa hizo sababu zilizotosha? Na Je, ni ipi tafsiri au maana ya sababu zilizotosha? Ni kuwa zina msingi sana sababu hizo? Au ni kuwa serikali imezikubali sababu hizo na sasa inawanyima Waislamu Mahakama ya Kadhi kwa kutumia sababu za viongozi wa Madhehebu ya Kikristo?

Ninavyoona mimi Madhehebu ya Kikristo hayana sababu hata moja ya msingi ya kuiambia serikali iwanyime Waislamu Mahakama ya Kadhi, na kama ipo ninakuomba kaka yangu Padre Mapunda uitaje ili sisi Waislamu tujiridhishe kwani tunapenda kuishi pamoja nanyi kwa amani. Na sababu hiyo kama ipo basi wangeitoa pia Wakristo wa Kenya ili kuzuia Mahakama ya Kadhi kutambulika katika Katiba ya nchi yao.

Amma maneno yako kwamba (nanukuu): “Wakisto hawaikatai Mahakama hiyo iwepo kama zilivyo Mahakama nyengine mfano wa Mahakama za Kanisa Katoliki ambazo zipo nje ya Katiba

Inaendelea Uk. 11

Page 8: ANNUUR 1144

8 AN-NUURDHULQAAD 1435, IJUMAA SEPTEMBA 26-OKTOBA 2, 2014Makala

Inaendelea Uk. 9

KUKATWA kichwa kulikotia k inyaa duniani kote kwa mfanyakazi wa asasi ya kusambaza misaada wa Uingereza na kundi la kigaidi la ISIS nchini Syria hivi karibuni, kulisababisha onyo kali kutoka kwa Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron ambaye aliapa "kuwatafuta wauaji" kwa "kitendo chao cha uovu uliopindukia."

Mhanga huyo wa Uingereza alikuwa akiitwa David Haines, mfanyakazi wa asasi ya kutoa misaada mwenye umri wa miaka 44, ambaye alikuwa ametekwa nyara nchini Syria kwa miezi mingi. Video ya kina iliyotolewa na wauaji wake ilimwonyesha Haines akiwa amepiga magoti akiwa amevaa vazi la njano linalopwaya huku muuaji aliyefunikwa uso kininja akimkata shingo yake kwa kisu. Mwili mfu wa mtu huyo unapigwa picha ya video ukiwa hauna kichwa, na kichwa kilichojaa damu kimewekwa juu ya mwili huo.

B a a d h i ya wa c h a m b u z i wamehoji usahihi wa video hiyo, wakisema ni ya kubuni. Lakini hali aliyokuwa nayo Haines na maneno yake ya mwisho yaliyosemwa mbele ya kamera yanaelekea

ISIS inachinja watu kwa maelekezokutoka Washington DC na London?

Na Finian Cunningham

Septemba 16, 2014 'Mtandao wa Kupeleka Habari' na SCF

Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron.

RAIS Barack Obama wa Marekani.

kudhihirisha kuwa video hiyo ni ya kweli.

Serikali ya Uingereza pia i m e s e m a k u w a i n a a m i n i

kilichoonyeshwa ni sahihi.Haines alikuwa mtu wa tatu

kutoka nchi za Magharibi kuuawa na wapiganaji wa ISIS katika kipindi cha wiki nne katika mazingira hayo hayo ya kutisha. Mapema mwezi Septemba, video ilimwonyesha mwandishi wa habari wa Marekani Steven Sotloff pia akikatwa kichwa kwa njia hiyo. Wiki mbili kabla, mtekwa nyara mwingine wa Marekani, James Foley, aliyekuwa pia mwandishi wa habari, alifikia hatima hiyo nzito mikononi mwa watekaji wake.

Mtu wa nne, mwanahabari mwingine wa Uingereza aitwaye Alan Hemming, anahofiwa kuwa mhanga anayefuata wa ISIS, huku taarifa zilizokuwa hazijathibitishwa za kukatwa kichwa kwake zikiwa zimewekwa katika mtandao mwisho wa wiki ya pili ya Septemba.

Mandhari hayo ya kushtua ya ukatili yamezua hasira kubwa miongoni mwa watu nchini Marekani na kwingineko duniani. Rais Obama alilihutunia taifa katika muda wa jioni ambako kuna watazamaji wengi ambako alitangaza kuwa vikosi cha Marekani vitawafuatil ia na kuwateketeza magaidi hao wa ISIS. Kundi hilo pia linajulikana kwa majina yake ya IS au ISIL, yanayoonyesha nia ya kuunda himaya ya Kiislamu ambayo inajumuisha Irak na Syria. Wakati

MTANDAO wa gazeti la Mail 4 November 2013 ulitokeza na habari, chini ya muandishi wake James Nye akisema: Madaktari wa Kijeshi wa Marekani wamekula kiapo cha kubuni mbinu mpya za utesaji zitakazo tumika katika gereza la Guantanamo Bay.

Wakati Marekani wanaandaa mbinu na njia hizo mpya za kutesa binaadamu. Watetezi wa haki za binaadamu mwaka 2009, waliorodhesha aina 11 za mateso ambayo wanateswa watuhumiwa wa Ugaidi katika magereza ya Abu Ghraib, Kandahar na Bagram, kabla ya kupelekwa Guantanamo Bay, kisha wanaedelezewa mateso hayo huko Bay.

Torture Techniques used in Guantanamo zilizoandikwa katika ripoti ya shirika la The Justice Campaign: Manyanyaso ya kijinsia , Kunyimwa usingizi, Kunyimwa hisia , Kuwaweka mtu pekee , Kuwadhihaki , Kuwalaz imisha mat ibabu , Kutumia mbwa kuwatisha,

Tunaanza Bay, Abuja hadi TanzaniaNi mateso na unyama wa kutishaNa Rashid Abdallah

Kuwaweka katika joto la kupita kiasi, Kuwekea sauti kali kupita kiasi, Kuangalia wengine wakati wanateswa, Mbinu za kuwaathiri kisaikokolijia. Manyanayaso ya kijinsia ni pamoja na kuwekwa uchi mbele ya askari wa kike wa Kimarekani, kuwaingiza mafagio na bunduki katika sehemu za nyuma, kuwachezea sehemu zao za siri, kuwalazimisha waangalie picha na video za ngono wakiwa uchi, kuwabaka au kuwatishia kuwabaka, kisha ripoti ikasema, Sexual violence is a war crime.

Kunyima usingizi husababisha maumivu ya kichwa, shinikizo la damu, magonjwa ya moyo, stress, wasiwasi na huzuni pia kupoteza kumbukumbu na matat izo mengine mengi.

P i a wa n a wa p a m a d a wa ambayo yanaaathiri mishipa yao ya ufahamu na kusababisha kuwa na mawazo mabaya yakiwemo ya kujiuwa. (Angalia katika ripoti ya Amnesty International Australi iliyopewa jina la Human Experimentation in Guantanamo

Bay, 28 th September 2009)Katika Gazeti la New York

Times, October 17th 2004;‘Torture and Democracy’ ilitaja aina hii ya mateso ambayo inafanywa kule Bay. Katika jambo la sauti kupita kiasa, huwasikilizisha miziki kwa lazima nakuwawekea heardphone masikioni na kuwafungulia miziki hadi sauti ya mwisho ama huwawekea masabufa chini ya masikio yao, huku wakiwa wamewafunga wasipate kujiziba masikio. Nyimbo kama za Eminem na wasanii wengine huchezwa kwa sauti ya mwisho.

Uchambuzi wa mateso haya unaweza kuyapata pia katika mtandao wa shirika la New Sexurity Action lenye makao makuu yake Marekani, chini ya anuani Torture At Guantanamo, ya mwaka 2009.

Hayo ndio yanayofanyika Guntanamo Bay. Gereza lenye siri kubwa na idhlal kubwa dhidi ya watuhumiwa wa ugaidi. Mateso na manyanyaso bado yanaendelea na mbinu mpya kila

mwaka hubuniwa. Si dhani kama anayetoka Bay anakuwa mzima tena kwa mateso hayo.

Chini ya anuani "Remember #Bring Back Our Girls? This Is What Has Happened In The 5 Months Since", mwandishi C h a r l o t t e A l f r e d wa T h e World Post, September 2014 anasema kuwa Jeshi la Negeria linatuhumiwa kutesa, kuteka na kuuwa raia wasiohesabika kwa kuwatuhumu kuwa ni wafuasi wa kundi la Boko Haram.

Alhamisi ya wiki iliyopita shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty Internationala lenye makao makuu yake mjini London nchini Uingereza l imetoa ripoti mpya iliyoipa jina la "KARIBU KWENYE MOTO WA JEHANNAM" iliyokusanywa kutoka kwa mamia ya wahanga ndani ya kipindi cha zaidi ya miaka 10 iliyopita.

Netsanet Belay ambaye ni mtafiti na mwanasheria mkuu katika shirika hilo anasema katika taarifa yake aliyoitoa kando ya ripoti hiyo kwamba uchunguzi

Inaendelea Uk. 9

Page 9: ANNUUR 1144

9 AN-NUURDHULQAAD 1435, IJUMAA SEPTEMBA 26-OKTOBA 2, 2014Makala

Inatoka Uk. 8 ISIS inachinja watu kwa maelekezokutoka Washington DC na London?

huo huo Obama akihutubia taifa, Waziri wa Mambo ya Nje John Kerry alikuwa Mashariki ya Kati akitafuta kuungwa mkono kwa uundwaji wa mkusanyiko wa majeshi kimataifa ukiongozwa na Marekani kuanza mashambulizi dhidi ya ISIS, ambao ngome zake kuu ziko kaskazini ya Irak, eneo linalopakana na mashariki ya Syria.

ISIS imekuwa na nguvu zaidi kati ya makundi kadhaa ya wapiganaji ambayo yamekuwa yakiendesha vita dhidi ya serikali ya Syria tangu Machi 2011. Kuna ushahidi wa kuridhisha kuwa serikali za nchi za Magharibi zimekuwa zikiiunga mkono ISIS kwa kificho na makundi mengine yenye siasa kali chini ya kivuli cha kusaidia 'waasi wa siasa za wastani' kwa nia ya jumla ya kuivuruga serikali ya Assad nchini Syria na kufikia mabadiliko ya utawala. Assad ni rafiki mkubwa wa Russia na Iran, na hivyo ni mmoja kati ya wale ambao nchi za Magharibi zingetaka serikali kama hiyo iondolewe.

Lakini hivi karibuni ISIS imekuwa na sifa mbaya ya kuteka na kuua wananchi wa nchi za Magharibi. Ushirika mpya wa kijeshi unaoundwa dhidi ya ISIS unajumuisha nchi 10 za Kiarabu, zikiwemo Misri, Lebanon, Irak na Jordan, pamoja na himaya za Ghuba kama Saudia, Bahrain,

Kuwait, Qatar, Falme za Kiarabu na Oman. Cha kushangaza ni kuwa inaelekea Saudi Arabia na Qatar

zimeshambuliwa kuwa zilikuwa zinapeleka fedha kwa makundi ya waasi yanayopigana nchini Syria, ikiwa ni pamoja na ISIS.

Lakini uhusiano huu haushangazi sana pale unapoangalia nafasi iliyotengenezwa na nchi za Magharibi kwa kundi hilo la kigaidi, kama tutakavyoona.

Marekani pia, na hii haishangazi, imefaulu kuzivuta Uingereza, Ufaransa, Ujerumani. Canada na Australia kuiunga mkono katika mkusanyiko huo dhidi ya ISIS.

Mkutano uliofanyika jijini Paris katikati ya mwezi ulipewa jukumu la kuweka bayana mbinu za kijeshi, jinsi Marekani na washirika wake wangeanza mashambulio. Hadi sasa, Marekani imesema haitaweka majeshi ardhini kama ilivyofanya katika vita vilivyopita nchini Irak (2003 hadi 2012) na katika kampeni dhidi ya Taliban inayoendelea nchini Afghanistan. Obama alisema mfumo wa kupambana na ISIS utakuwa kama 'operesheni za kupambana na ugaidi nchini Yemen na Somalia' ambako uwezo wa kutumia ndege wa Marekani unasaidia na 'washirika ardhini.'

Serikali dhaifu ya Waziri Mkuu Haider al Abadi imekaribisha mashambul iz i ya anga ya Marekani. Tangu mwezi Agosti, ndege za Marekani zimefanya mashambulio karibu 150 dhidi ya maeneo yanayoshukiwa ni vituo vya ISIS kaskazini ya Irak. Katikati ya Septemba, mashambulizi hayo yalienea kufikia maeneo ya magharibi ya

Tunaanza Bay, Abuja hadi TanzaniaInatoka Uk. 9

huo unakwenda mbali zaidi ya mateso na mauaji yaliyofanywa dhidi ya washukiwa wa kundi la Boko Haram.

Nigeria umefanyika unyama na ukatili wa hadi kubaka dhidi ya wanawake, wanaume na hata watoto, wahusika wakiwa ni maafisa wa serikali wanaotakiwa kimsingi kuwalinda wananchi.

Kwa mujibu wa shirika hilo la Amnesty International kuna aina 12 za mateso yanayofanyika nchini humo ikiwa ni pamoja na watu kupigwa na kufyetuliwa risasi, kung'olewa kucha na meno, kuwanyima chakula wanaozuiliwa, kuwakalisha kwenye sehemu zenye vitu vyenye ncha miongoni mwa mengine.

Wanawaweka katika sehemu zenye incha kali, huenda ni juu ya vyuma, mawe yenye ncha kali wakiwa uchi n.k. Wamewafungia lakini p ia wanawakosesha chakula. Na vipigo vya kutisha na kuumiza, haya ni machache kati ya mengi ya kuumiza. Pia usisahau kuwa wanang'olewa

kucha na meno bila ya ganzi. Huumii ukiyasikia haya?

Gazeti moja la kila siku la hapa nchini, ndani ya wiki iliyopita limeandika habari kuhusu kesi ya washukiwa wa ugaidi kule Arusha. Mshukiwa Abdallah Maginga akiwa mahakamani amenukuliwa akisema “Mheshimiwa Hakimu naomba mahakama yako inipe ruhusa ya kutohudhuria siku ya kesi, sababu ninapopanda gari napata maumivu makali sana sehemu za siri kunauma, kwa sababu polisi walinitesa kwa kuniingizia mti kwenye njia ya haja kubwa na kuminya sehemu zangu za siri,”

Najaribu kushusha pumzi ili niendelee kwani sitaki nishindwe kuyasema. Lakini hayo ndio wafanyiwayo watuhumiwa wa ugaidi kutoka Guantanao Bay, Nigeria na sasa tupo Bongo lakini hali si shuari ni hamkani tupu.

Alidai kuwa mbali na maumivu ya sehemu za siri pia mguu wake uliokatwa hospitalini bado una maumivu makali , al i iomba Mahakama iagize Magereza

wamruhusu akatibiwe hospitalini, kwani alitakiwa kwenda kupata matibabu Septemba 5 mwaka huu lakini amezuiwa hadi sasa.

Nikukumbushe kuwa, huo mguu uliokatwa haukukatwa kwa sababu alinguka mnazi au kupata ajali, lakini ulioza baada ya kupata kipigo wakati wa kukamatwa, na wakati wa kuhojiwa.

Ta a r i f a z i n a s e m a k u wa watuhumiwa hao huteswa hadi wakapoteza fahamu na kuhojiwa wakiwa uchi na wengine ndio wanatiwa majiti na kuingiliwa kinyume na maumbile. Hakuna tofauti na yale tul iyosema yanatendeka Guantanamo Bay.

Hili la Arusha ni mabali na lile la mtuhumiwa wa Ugaidi kutoka Zanzibar, yeye alilalamika kama ifuatavyo: Mheshimiwa tunalazimishwa kutoa maelezo wanayoyataka wao, wanatuingilia k i n y u m e c h a m a u m b i l e , wanaingiza maj i t i , chupa , wengine wanavuja nyuma, kama unaweza hakimu twende faragha nikakuonyeshe”

“Askari ameniingilia kisha

akaniingiza jiti mpaka likakatika, k u n g e k u w a n a s e h e m u ningekuonyesha, Jeshi la Polisi la kwanza kuvunja sheria , waliofanya madhila haya wa nawatukanisha Watanganyika na kufanya waonekane wabaya” Hayo yalisemwa na Bwana Salim Ali Salim na kunukuliwa na vyombo vingi vya habari.

Ni safari ya kuangalia haki za watuhumiwa wa Ugaidi katika mataifa matatu tu ulimwenguni. Marekani inayomiliki Gereza la Mateso la Guantanamo Bay lililopo Cuba. Nigeri katika mji mkuu wake Abuja na miji mengine kama Lagos, Kanu n.k. Tukahitimisha na Tanzania katika Mikoa ya Arusha na Dar es Salaam.

Hali hairidhishi hata sehemu moja kati ya hizo, ni mbaya kupita maelezo. Wenye kuweza kutatua tatizo hili ni watesaji wenyewe, wawe wanafikiria kuwa wanayafanya haya si kwa mawe ila ni binaadamu wenye hisia na kuumia kupita kiasi. Watambue kuwa watesa na wateswaji wote wataondoka.

Inaendelea Uk. 11

Page 10: ANNUUR 1144

10 AN-NUURDHULQAAD 1435, IJUMAA SEPTEMBA 26-OKTOBA 2, 2014TAMKO

JUMATATU wiki hii Bunge Maalum la Katiba ambalo limesusiwa na baadhi ya wajumbe wake, lilikaa kikao ili kujadili na kubadili kanuni ili kumruhusu mjumbe ambaye hatokuwepo siku ya kupiga kura yakupitisha rasimu ya katiba mpya, apate hiyo inayoitwa haki yake popote alipo.

Jambo hilo lilifanikiwa hivyo, popote pale mjumbe atakapokuwepo atapiga kura yake. I la wakati mjadala huo ukiwa unaendelea, nilimsikia Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta, akimwambia mjumbe mmoja kwamba asiwe na wasiwasi, yeye aende tu Hija kwani atapiga kura katika mji wa Jeddah nchini Saudi Arabia na “kila kitu kimeshapangwa”, halafu akacheka kwa namna ya kujishtukia kama mtu aliyeongea jambo la siri, sijui alikuwa anaamanisha nini, mimi sijui.

Kuna maswali mengi ya kujadili juu ya uamuzi huo wa kubadili kanuni na kumruhusu hata aliyeamua zake kulala nyumbani, aipigie kura rasimu hiyo ambayo wengi wanaitazama kama ni ya upande mmoja, yaani ya vigogo wachache wa serikali kutokana na vipengele muhimu vilivyopendekezwa na iliyokuwa Tume ya Jaj i Joseph Warioba, kunyofolewa kama vile vya tunu, maadili, muundo wa serikali tatu n.k , ambavyo ni afya kwa taifa.

Naomba hayo niyaache, nijikite zaidi katika suala la Hija kuonekana muhimu kwa wajumbe wa Bunge Maalum wanaokwenda Hija, ambalo lina umuhimu mkubwa kwa waumini wa dini ya Kiislam, ikiwa ni moja ya nguzo ya Kiislamu inayotakiwa kutekelezwa kama inavyoamriwa na Allah (S.W.T) na Mtume wake Muhammad (S.A.W), kwani jambo hilo linalompendeza Allah nani ibada.

Akiwa anasimamia mjadala wa kubadili kanuni, Bw. Sitta alionekana kuipenda sana hoja ya wajumbe wanaokwenda Hija kama zana muhimu ya kujengea hoja ya kuwashawishi wajumbe waridhie mabadiliko ya kanuni hizo. Kwamba wajumbe waendao Hija waweze kupiga kura wakiwa nje ya Bunge hilo (huko Saudia).

Utamu ulimkolea zaidi pale palipozuka mvutano baina ya wajumbe waliokuwa wakibishana kipi kinaruhusiwa na kipi hapana wakati wa Hija, katika kutizama kama inawezekana kupiga kura huko Makka. Aliibuka mjumbe mmoja na kusema kuwa yeye anajua kanuni za huko Makka, kwani yeye alishawahi kwenda Hija na kwamba hata kupiga kura huko inawezekana.

Mjumbe huyo alimwagiwa sifa kemkem na Mhe. Sitta, kwamba yeye ni Muislam safi, sio Muislam jina kama yule aliyetetea na kusema kuna baadhi ya mambo hayaruhusiwi huko Hija. Mhe. Sitta alijenga hoja yake kwa kusema amesoma tu maandiko, bila kujua Waislamu kwa Waislamu wamefitinishwa.

H a p o n i k a j u a n i S i t t a t u , ndiye ataipigia debe zaidi hoja hiyo, mara nikaona Waislamu

Hija sawa, Mahakama ya Kadhi hamtakiNa Yusufu Ahmadi

wenzetu wakiongea kwa sauti ya juu wakisaidiwa na wale wa dini nyingine kwamba kuhiji ni haki yao ya msingi na ni jambo ambalo ni muhimu mno katika dini yao, hivyo wakawanasihi wajumbe wabadili kanuni ili waruhusiwe kupiga kura wakiwa huko.

Mhe. Sitta naye akakazia hapo hapo, lazima wapewe haki yao ya kupiga kura, kwamba Hija ni muhimu katika dini ya Kiislamu, waachwe waende huko, akawahakikishia ushindi mkubwa Mahujaji wetu na wale wanaoenda kwa mara ya kwanza.

Nilimshangaa Sitta, Wajumbe Mahujaji na wajumbe wengine, kwanini wameona tu suala la Hija yao ndio muhimu hapo bungeni, lakini hoja ya Mahakama ya Kadhi bungeni hapo sio! Au kwa sababu suala hilo la Hija linatumika kupitisha rasimu hiyo inayonung’unikiwa na umma mkubwa wa Tanzania, ambayo wengi wanaitazama kuwa ni ya kuendelea kuwafanya waliopo madarakani waendeleze mduara wao.

Ndani ya Bunge hilo hilo la katiba, hivi karibuni mjumbe wake Bw. Mtutura Abdallah Mtutura, akichangia sura za nane na kumi za rasimu ya Katiba, alitoa hoja mbalimbali za kuonesha kuwa Mahakama ya Kadhi ni haki ya Waislamu na inapaswa kuwemo kwenye katiba ikizingatiwa unyeti wa shughuli za chombo hicho.

Bwana Mtutura alibainisha kuwa, Waislamu ambao nao inakadiriwa kuwa ni nusu ya raia wa nchi hii, wanapaswa kupewa Mahakama ya Kadhi kama yalivyopewa makundi ya wengine ambayo ni ya wachache.

Alishangazwa pia na tabia za watu ambao jambo haliwahusu hata haligusi imani zao, lakini wanaliingilia na kulipinga.

“Haya mambo ni ibada kwetu, ndiyo maana tunasema wewe mama Katiba tunaomba utambue mambo haya, lakini anatokea kaka ambaye hata jambo hili halimhusu, anasema usimpe, tunawashangaa,” alisema Mtutura.

Alishangazwa pia na madai ya

wale wanaosema kuwa Mahakama hiyo itasababisha vurugu nchini endapo tu itaruhusiwa.

“Hivi tunataka kujenga ‘society’ ya namna gani, narudia kusema Uganda inayo Mahakama ya Kadhi, Kenya wanayo Mahakama ya Kadhi, Zanzibar wanayo Mahakama ya Kadhi na kote huko hatujawahi kusikia zimetokea vurugu kwa sababu ya Mahakama ya Kadhi,” alifafanua Bw. Mtutura.

Bw. Mtutura alikwenda mbali zaidi na kusema kuwa, wapo wanaotoa hoja kwamba serikali haina fedha za kuhudumia mahakama hiyo. Yeye akasema.

“Mlisema hatuwezi kuwapa Mahakama ya Kadhi kwa sababu hatuna fedha, Waislamu tukasema tupeni tutaiendesha wenyewe, lakini bado mnatusumbua, hivi mnachotaka Waislamu wafanye nini?” alihoji.

H o j a h i z o a m b a z o b a a d a e ziliungwa mkono katika tamko lililotolewa na Taasisi ya Masheikh na Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania hapo Septemba 14 mwaka huu, katika kufafanua zaidi baada ya mvutano kutokea ndani ya Bunge la Katiba na kuonesha mahakama hiyo kweli ni haki yao na inapaswa kutambuliwa kikatiba.

Awali Mjumbe mwingine, Alhaji Mohamed Misanga, naye katika kuchangia vifungu vya muswada huo wa katiba mpya, alizungunmzia kwa mapana kidogo suala la mahakama ya Kadhi na kulitaka Bunge hilo kulitambua katika rasimu hiyo.

Zaidi ya huyo, Bw. Mtutura hakupata usaidiz i wa maana kumsaidia kutetea suala hilo ndani ya Bunge hilo, hakuna aliyejitokeza kwa dhati na kusema “mimi nimesoma elimu ya dini ya Kiislamu, jambo hili ni kadha wa kadha, ni haki yetu” badala yake walimuacha abebe msalaba peke yake, ‘Mahujaji wetu’ bungeni hapo hawakuiona haki hii? Zaidi ya kukomalia ya Hija tu.

B w . M t u t u r a a l i o n e k a n a mchochezi, anayetaka kuleta chuki kwa jamii akaambiwa aombe radhi kwamba amezunguza maneno ya uchochezi (hate speech) kisa kasema

ataitisha viongozi wa dini ya Kiislamu waitishe maandamano kupinga jambo hilo, masikini yeye akasema aliongea kwa jazba kwani si hulka yake, akatii amri (?).

Kuonesha kuwa jambo hilo ni haki ya Waislamu na ilipaswa kuwemo kwenye katiba, Ibara ya 19 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 iliyofanyiwa mabadiliko (amendment) mwaka 2005, inabainisha uhuru wa kidini katika kuabudu kwa dini zote”.

Katika Uislamu, neno ibada ni kila jambo lililoamriwa na Allah na linampendeza yeye, hivyo Mahakama ya Kadhi kwa kuwa ni amri zake, nako ni kuabudu.

Huko nyuma iliwahi kujengwa hoja kwamba Mahakama ya Kadhi sio ibada, kwamba ibada ni zile nguzo tano tu za Uislamu, hivyo ikatolewa hoja Waislam wasidai Mahakama hiyo kwa kisingizio cha kusema ni ibada.

Kuna watu wanasema kama ni haki, basi ibaki kwenye sheria za kawaida tu na si kwenye Katiba, tamko la Waislamu na ndio miongoni mwa hoja kuu ni kuwa mahakama hiyo kutambuliwa kikatiba ni kuipa nguvu sawa na mahakama nyingine na hivyo kufanya hukumu zitolewazo zisikose nguvu za kisheria mbele ya Mahakama hizo ambazo zitakuwa juu kwani zipo kikatiba.

P i a k u e p u s h a w a t u k u j a kuichezeachezea kwa malengo wanayoyajua wenyewe na kutaka kuondolewa kirahisi na hata kwa mlango wa nyuma pasi na umma kufahamu.

Kuna hoja kuwa mahakama hiyo itakuwa ni mzigo, hicho ni kioja kwani Waislamu katika nchi hii ni wengi na wanalipa kodi, hata tamko la Waislamu halijazungumzia ufadhili wa serikali, bali hukumu zake ziwe na nguvu za kikatiba, shida hii inakuja kutokana na kupuuziwa mbali kwa kile kipengele cha dini katika kuhesabu sensa.

Hoja kuwa italeta vurugu, nani athibitishe kwa mifano toka kwenye nchi zenye mahakama hiyo. Kuna gazeti moja la kila siku limechapisha makala ambayo mwandishi wake anasema vurugu za Uganda, Kenya na Congo DRC zinasababishwa na Mahakama ya Kadhi . Hil i nitalijadili wakati mwingine. Bahati mbaya ameshindwa kuonesha jinsi zinavyosababisha vurugu, pia hata vyanzo vya vurugu katika nchi hizo hana ufahamu navyo.

Mwandishi huyo ameongeza kuwa kuingiza kipengele cha dini ni sawa na kutamka Tanzania ni nchi ya Kiislamu, kiufupi hilo si kweli lakini hili nitalijadili kiundani wakati mwingine. Kwenye rasimu yetu kuna ibara ya wasanii, je, tuseme nchi hii ni ya wasanii sasa?

Waislamu wamesema wazi kuwa mahakama hiyo itashughulika na mambo ya Kiislamu na itawahusu Waislamu tu na si mtu wa imani nyingine, hoja zikaja kwamba wana hofu itagusa na imani zingine, hofu na ujenzi wa hoja nyepesi.

Sidhani kama Mhe. Sitta na Mahujaji wetu na wajumbe wengine wameelewa hoja hizo na kuona

Inaendelea Uk. 13

JAJI Joseph Sinde Warioba (kushoto), Dkt. Salim Ahmed Salim (kulia)

Page 11: ANNUUR 1144

11 AN-NUURDHULQAAD 1435, IJUMAA SEPTEMBA 26-OKTOBA 2, 2014Makala

Inaendelea Uk. 12

na zinajiendesha zenyewe”.Ninachotaka kukifahamu hapo

kaka yangu Padre Mapunda, ni wapi iliko hiyo Mahakama ya Kanisa Katoliki? Hakimu wake ni nani? Na Je amevunja ndoa ngapi za Wakatoliki? Na kwa ambaye hakuridhika na hukumu za Mahakama hiyo ya Kanisa Katoliki, anafuata utaratibu gani?

Kwa nijuavyo mimi, ndoa ya Kikatoliki haina talaka wala haivunjwi, Je huyo Hakimu wa Mahakama ya Kanisa Katoliki ni msuluhishi tu endapo mume na mke wamegombana au ni Hakimu mwenye mamlaka kamili? Na Je anatumia kitabu gani katika kuhukumu?

A i d h a , k u h u s u m a n e n o “Zijiendeshe Zenyewe”, hapana shaka kwamba tatizo lako ni juu ya mishahara ya Makadhi kwa kuwa Ukadhi ni jambo la kidini. Katika hilo naomba majibu ya maswali haya:

(a) Hivi sasa hizo kesi za ndoa, talaka na miirathi zipo katika Mahakama za kawaida (kisekula) na zinatolewa hukumu, isipokuwa zinakosewa kutokana na Mahakimu wengi kutojua vyema mafundisho ya Dini ya Kiislamu pamoja na sheria zake. Huyu anayewalipa hao wanaokosea hukumu za kesi hizo ni serikali kwa kutumia

Padre Mapunda amepinda, tumuelimishe aelimikeInatoka Uk. 7

fedha hizi hizi za Walipa kodi, ni vipi akipatikana Kadhi (ambaye anajua vyema mafundisho ya Dini ya Kiislamu na sheria zake) upate wasiwasi wa kuwa atalipwa na nani? Kwani serikali inapenda Waislamu wadhulumike na walalamike ili ilipe fedha hizo lakini wakipumzika na wakitulia haitalipa, Je kuna kitendawili gani hapo?

K a m a t a b u n i k o d i z a Watanzania wote wenye dini na wasio na dini kutumika kuendeshea Mahakama ya Kadhi, tafakari hili lifuatalo: Hivi Mheshimiwa Raisi anapokwenda kwenye sherehe za “kumsimika” Askofu, ule msafara wake wa magari na mafuta yake pamoja na ulinzi ni kodi za Watanzania wote, Je hawa Watanzania wengine wanaponyamaza kuhusu hilo ni woga au ustaarabu tuliojizoesha? Hivi kusimikwa kwa Askofu Waislamu wanafaidika nini mpaka kodi zao zitumike? Na ni vipi huyu Raisi ambaye anaongoza nchi isiyo na dini kikatiba anapokwenda kwenye sherehe za kumsimika Askofu? Je huo si udini au kuiingiza serikali kwenye mambo ya kidini? Kwanini “usimikaji” wa Maaskofu usiishie kwa Wakristo wenyewe kama ambavyo mtakavyo Ukadhi uishie kwa Waislamu wenyewe?

Ahsante sana kaka yangu Mheshimiwa Mapunda kwa kutuzindua usingizini.

ISIS inachinja watu kwa maelekezokutoka Washington DC na London?

Inatoka Uk. 9Irak karibu na Haditha. Kutokana na kuungwa mkono na serikali ya Irak, Marekani na washirika wake wana uwezo wa kisheria wa kufanya operesheni nchini Irak. Lakini hali si hiyo nchini Syria. Serikali ya Bashir al Assad wa Syria haijatoa kibali kwa mipango hiyo ya Marekani, na haikuulizwa pia. Marekani inasema kuwa Assad hana ridhaa ya wananchi ya kutawala au kutumia haki ya kitaifa ya nchi hiyo kwa sababu inadai kuwa utawala wake umekuwa ukiwakandamiza raia - madai ambayo wachambuzi wanasema yanapingwa na kuchaguliwa tena kwa Assad kama rais kwa asilimia 88.7 ya kura, katika mandari ya asilimia 73.4 ya walio na sifa ya kupiga kura kujitokeza.

Syria imesema kuwa shughuli yoyote ile ya kijeshi katika ardhi yake - hata kama itakuwa dhidi ya maadui wa mtandao wa ISIS

- itakuwa ni uchokozi dhidi ya serikali ya Syria.

Mwelekeo sahihi wa kisheria uliainishwa pia na serikali ya Russia wakati huo huo. Wakuu wa serikali Moscow walisema kuwa bila kibali cha Syria au azimio mahsusi la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, mashambulio yoyote ya ndege ndani ya Syria yatakuwa ni 'ukiukwaji mkubwa wa sheria za kimataifa.'

Hata hivyo, Obama amesema bila kigugumizi kuwa ushirika h u o wa k i j e s h i u t a f a n ya mashamhulio dhidi ya ISIS nchini Syria. Hatma ya ushirika huo

kisheria, hata hivyo, inaelekea kuwasumbua washirika muhimu wa NATO - Uingereza, Ufaransa na Ujerumani.

Mjini Berlin katikati ya mwezi wa Septemba, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier na mwenzake wa Uingereza Philip Hammond walitoa taarifa zinazosema wazi kuwa nchi zao hazitashiriki kufanya mashambulio nchini Syria.

Hammond, kama Steinmeier, al iunga mkono kwa nguvu mashambulio ya Marekani dhidi ya ISIS nchini I rak , lakini akaliambia shirika la habari la Reuters: 'Nataka hili lieleweke; Uingereza haitashiriki mashambulizi ya ndege nchini Syria. Tayari tumekuwa na mjadala huo bungeni mwaka jana na hatutaanza kuhoji msimamo huo.' Mwanadiplomasia mkuu wa Uingereza aliongeza kuwa k u k u b a l i wa k i s h e r i a k wa mashambulizi nchini Irak na Syria kulikuwa tofauti kabisa.

H a m m o n d a l i k u w a akizungumzia kupiga kura katika Bunge la Uingereza mwaka jana ambako wabunge walipinga kwa wingi wao Uingereza kujiunga na uingiliaji wa Marekani nchini Syria, kufuatia mashambulizi mabaya ya kutumia silaha za kemikali karibu na Damascus mnamo Agosti 21. Marekani ilikuwa inajiandaa kwa mashambulio ya anga dhidi ya Syria kwa madai ya kulipa kisasi kwa mauaji ya mamia ya wananchi kutokana na gesi ya sumu. Tukio hilo lililaumiwa kwa majeshi ya serikali ya Assad lakini ikaonyeshwa baadaye kuwa ilikuwa ni kazi ya chinichini ya makundi ya wapinzani wa serikali, ikiwa na nia ya kuinua bendera feki ya udhalimu ili kuvuta uingiliaji kijeshi wa nchi za Magharibi.

Bunge la Uingereza kwa njia hiyo lilidhihirishwa kuwa sahihi katika kupiga kura dhidi ya uingiliaji kijeshi nchini Syria, na upigaji kura huo ukakwamisha mpango wa Marekani kwa wakati huo. Ilikuwa ni tukio la aina yake katika 'uhusiano maalum' kati ya Marekani na Uingereza, ambako kwa kawaida Uingereza ni mshirika mtiifu hafifu kwa mikikimikiki ya ki jeshi ya Marekani maeneo tofauti duniani. Wakati wa kupiga kura bungeni

Uingereza mwisho wa Agosti 2013, kiongozi wa Uingereza David Cameron alihuzunishwa na kukataliwa kwa pendekezo l a k u i n g i l i a n c h i n i S y r i a . Ikikumbukwa kuwa serikali ya Uingereza ni mshirika muhimu wa njama zinazoongozwa na Marekani za kubadili utawala nchini Syria, masikitiko ya Cameron yalikuwa yanaeleweka.

Baada ya waziri Hammond kutangaza jijini Berlin kutoingilia n c h i n i S y r i a , a l i o n e k a n a kukataliwa na bosi wake, mtaa wa Downing kitalu namba 10, jinini London. David Cameron alimkanusha waziri wake wa mambo ya nje kwa kuviambia vyombo vya habari kuwa 'hakuna kilichowekwa pembeni' kuhusu ushiriki wa Uingereza katika mkusanyiko wa washirika wa Marekani dhidi ya ISIS. Cameron alikuwa akionyesha dhahiri kuwa ndege za kivita za Uingereza z i n a we z a k a b i s a k u f a n ya mashambulio nchini Syria. Hatua hiyo ingepindua matokeo ya kura bungeni ya kukataza kisheria uingiliaji kijeshi nchini Syria. Pia ingepuuzia hisia za watu walio wengi miongoni mwa wananchi wa Uingereza, ambazo zimekuwa zikipinga kwa nguvu serikali kuingilia kijeshi nchini Syria.

Hata hivyo, maonyesho ya picha za video za wauaji wa siasa kali wakimchinja mfanyakazi wa asasi ya kutoa misaada ya Uingereza inaweza kubadili kila kitu. Ni vigumu kufikiria tendo baya zaidi la kikatili na unyama uliokithiri kugeuza hisia za watu kutoka katika upinzani wake wa awali kuhusu vita na kutoa rukhsa kwa azma hiyo, kama Cameron alivyosema, 'kuupatiliza uovu huu habithi.'

Ikimbukwe pia kuwa katika wiki kadhaa zilizotangulia serikali za nchi za Magharibi na vyombo vyao vya habari zimekuwa zikieleza wasiwasi wa usalama kutokana na mujahidina wanaotoka nchi za Magharibi ambao wangerudi katika nchi zao kufanya vitendo vya kigaidi. Serikali ya Australia ya waziri mkuu Tony Abbott ni ya hivi karibuni zaidi kuiweka nchi katika hali ya 'tahadhari ya hali ya juu.' Abbott aliviambia vyombo vya habari kuwa serikali yake ilikuwa inapeleka kikosi cha askari 600 Mashariki ya Kati kujiunga na mkusanyiko wa kijeshi unaoongozwa na Marekani, akielezea uchinjwaji wa kishenzi wa raia wa Uingereza kama sehemu ya sababu za kupeleka kikosi cha Australia.

M a u a j i y a k u t i s h a yaliyoonyeshwa kwenye video pia yamepindua hisia ya kupinga vita nchini Marekani. Wakati Obama

Page 12: ANNUUR 1144

12 AN-NUURDHULQAAD 1435, IJUMAA SEPTEMBA 26-OKTOBA 2, 201412 Barua/Mashairi

ISIS inachinja watu kwa maelekezokutoka Washington DC na London?

Inatoka Uk. 11akiwa anapanga kufanya mashambulizi ya anga nchini Syria mwaka jana kufuatia tukio la matumizi ya silaha za kemikali, kura za maoni zilionyesha k u w a w a t u w e n g i zaidi - takriban asilimia 70 - nchini Marekani walikuwa wanapinga hatua zozote za kuingilia kati . Upinzani huo, pamoja na kukataliwa kwa pendekezo hilo kwa kura bungeni Uingereza, ilikuwa ni sababu muhimu ya Obama kurudi nyuma katika azma yake ya mashambulizi mwezi Septemba 2013.

Lakini baada ya video ya hivi karibuni ikionyesha waandishi wa habari wawil i wa Marekani wakiuawa kikatili, maoni ya watu nchini Marekani, kwa mujibu wa kura za hivi karibuni, yanaunga m k o n o k w a n g u v u mpango wa Obama wa kuipiga mabomu ISIS, n a s i y o t u k u f a n ya operesheni hizo nchini Irak lakini zaidi, watu wa Marekani wanataka mkusanyiko huo wa kijeshi uwafuate ISIS ndani ya Syria vile vile. Hivyo, wakati ambapo dhahma ya matumizi ya silaha za kemikali mwaka jana ilishindwa kuwafanya wananchi wa Marekani waunge mkono mashambilizi ya anga nchini Syria, kukata vichwa watekwa nyara wa Marekani kumefaulu kuyakinisha azma hiyo.

K w a u t a w a l a w a Washington na swahiba wake wa London, maoni ya raia wa Uingereza ni kiungo muhimu cha kuvutwa upande wao. Inakuwa ni zaidi ya tukio la kubahatisha kuwa ISIS imetekeleza mauaji hayo ya kusononesha dhidi ya raia wa Uingereza kama ilivyofanya kwa wa-Marekani wawili. Rais Obama alisema baada ya video inayoonyesha k u ch i n jwa k wa r a i a wa Uingereza David Haines kuwa Marekani 'inasimama bega kwa bega' na watu wa Uingereza.

Swali ni hil i hapa: mauaji haya ya kutisha,

pamoja na utengenezaji wa video kuyaonyesha, yanatumiwa kubadilisha hisia ili kukubaliwa kwa uingiliaj i wa nchi za Magharibi kijeshi nchini Syria? Kama ni hivyo, ISIS haifanyi hivyo kutokana tu na kuwa nje ya hisia ya sheria, ikiwageuka wakubwa zao wa kijasusi wa nchi za Magharibi, lakini inatekeleza amri kama kawaida, kama sehemu ya mpango wa kutisha wa kuwezesha uingiliaji kijeshi wa nchi za Magharibi.

Kwa mara nyingine, tunachokiona ni mojawapo ya visingizio vya 'misaada ya kibinadamu' kuweka njia ya ajenda iliyojificha na kubwa zaidi ya mpango wa nchi za Magharibi wa k u b a d i l i t a wa l a katika nchi za nje. Njia hiyo ilitumiwa awali na majeshi ya NATO katika iliyokuwa Yugoslavia mwishoni mwa miaka ya 1990 na hivi karibuni zaidi nchini Libya mwaka 2011. Imeshaelezwa kwa kina kuwa ISIS, IS au ISIL, ni mtandao wa kigaidi ulioundwa na mashirika ya ujasusi wa kijeshi ya Marekani, Uingereza na Saudia kuanzia wakati wa miaka ya awali ya vita ya Irak kuanzia mwaka 2003, wakat i kundi hilo lilipochukua nafasi muhimu kuchochea uhasama wa kidini nchini Irak kwa faida ya majeshi ya uvamizi ya nchi za Magharibi. Mtandao huo una vianzio katika ushirika wa nchi za Magharibi na mamluki wa Kiislamu nchini Afghanistan katika miaka ya 1980 dhidi ya iliyokuwa Urusi, ambayo ilifikia kuanzishwa kwa Al Qaeda, na pia huko Chechnya katikati ya miaka ya 1990.

K i o n g o z i wa I S I S Abu Bakr al Baghdadi anafahamika kuwa ni chombo cha kijasusi cha Marekani, kwa mujibu wa Nabil Naim, mshirika mwandamizi wa zamani wa Al Qaeda, miongoni mwa vianzio vingine. Maofisa wa zamani w CIA wamefichua pia kwamba ISIS, kama Al Qaeda,

iliundwa kufanikisha malengo ya kimkakati ya Marekani na washirika wake huko Mashariki ya Kati. Malengo haya ni pamoja na kubadili tawala katika nchi zinazolengwa, kwa mfano Syria, na k u e n d e l e z a m a s l a h i ya ushirika wa wenye viwanda na jeshi nchini Marekani wenye faida kubwa kwa kutengeneza hatar i za k iusa lama zisizoisha. Kwa maelezo rasmi , mtandao huo unaweza kuwa ni kundi marufuku la kigaidi na 'adui wa taifa.' Lakini k a t i k a m a n d h a r i ya kijasusi ya operesheni za kificho, ISIS ni chombo cha siri cha serikali ya Marekani na maslahi ya makampuni hodhi.

Kutokana na umuhimu wa lengo la Marekani la kubadili utawala nchini Syria - na hasa umuhimu wa kuungwa mkono na wananchi kuingilia k i jeshi nchini humo - siyo suala linalovuka mpaka wa uwezekano kuwa mtandao wa ISIS unawakata vichwa raia wa nchi za Magharibi kwa amri ya wasimamizi wao katika Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) na Idara ya Ujasusi wa Kijeshi ya Uingereza (M16) . Inawezekana hata uongozi wa k i m a s o m a s o wa kisiasa mjini Washington na London, wa Obama na Cameron, hawana habari ya njama za kifedhuli z i n a z o e n d e l e a , h a l i ambayo inafanya hisia zao za kuchukizwa na vitendo hivyo ziwe na mandhari ya uhalisi na ukweli.

Ni wazi kuwa matokeo ya kisiasa ya kuuawa hivi karibuni zaidi kwa David Haines, raia wa Uingereza pamoja na Jim Foley na Steven Sotloff raia wa Marekani yanaonyesha kwa nguvu njama za kisaikolojia za nchi za Magharibi. Hiyo inafanya watawala wa Washington na London kuwa na hatia ya kuwaua raia wao wenyewe kwa mikakati ya ki jeshi kimataifa . Wahanga hawa ni kondoo wa kafara katika maana iliyo mbaya zaidi.

Uchakachuaji wa Aqida ya KiislamuInatoka Uk. 5

ambazo ziko wazi kabisa zinakiukwa.

Fikra ya Tatu: Matumizi ya Aki l i - Ul imwengu wa Magharibi unafikiri kwamba dini na akili ni vitu visivyohusiana. Kwao wao, dini inaangal iwa kihisia zaidi kuliko kiakili. Kwa mujibu wa fikra za Kimagharibi, dini na akili ziko katika mgongano wa kudumu baina yao.

M g o n g a n o h u o unawasilishwa na mgogoro wa karne nyingi kati ya wasomi na kanisa, ambao ulisababisha kuyaweka masuala yote ya kidini mikononi mwa kanisa na kuiacha akili ishughulike na masuala ya dunia na sayansi.

Baadhi ya Waislamu ambao hawajaelewa vizuri Dini yao, wanaingiza dhana hii ya Kimagharibi ya dini kwenye Umma wa Kiislamu. Wanalenga kuwafundisha Waislamu Uislamu kama urithi ambao umepokelewa k u t o k a k w a w e m a waliotangulia (Salaf) bila ya tathmini yoyote ya kiakili. Wais lamu wanatakiwa kusalimu amri bila hata ya kuhoji. Hata Aqida, ambayo ndiyo msingi wa Uislamu, inabadilishwa na kuwa katika misingi ya 'Aqida ya Salaf'.

W a i s l a m u h a w a wanamshambulia yeyote anayesema kwamba Aqida lazima izingatie akili na kwamba matumizi ya akili ndiyo yanayothibitisha usahihi wa Uislamu na upotofu wa imani zingine.

Kutokana na ukwel i k wa m b a h a wa f a h a m u methodolojia ya kuikubali Aqida na nafasi ya akili katika Uislamu, ndugu zetu hawa wanachangia sana kueneza dhana potofu za Kimagharibi kuhusu dini kuwa ni theoloj ia isiyohitaji matumizi ya akili. Vilevile wanafanyakazi ya kupandikiza mgogoro kati ya akili na dini, ikiwa ni pamoja na kuufanya Uislamu kuwa miliki ya watu maalumu, kama ilivyo kwenye ulimwengu wa Magharibi.

Fikra ya Nne: Kufunika Ukweli kwamba Watawala wa nchi za Waislamu ni Mawakala - Ni ukweli u n a o f a h a m i k a v y e m a kwamba historia haijawahi kushuhudia hali ambayo watawala wa nchi wanakuwa mawakala wa nchi zingine. Zamani, watawala walikuwa wakati wote upande wa raia wao dhidi ya maadui. Hata wakishindwa mapigano, watawala wangeshirikiana na watu wao dhidi ya maadui.

Lakini hali ya sasa ni tofauti sana kwa sababu watawala wanashughulika na kuelekeza rasilimali za kisiasa, kiuchumi na kijeshi za watu wao kwa maslahi ya nchi nyingine. Na pia watawala hawa wanakuwa ndiyo macho na masikio ya mabeberu dhidi ya watu wao wenyewe.

Hal i h i i n i mo ja ya m a j a n g a m a k u b w a ya l i y o u k u m b a U m m a wa Kiislamu duniani leo. Wakati mataifa ya kikoloni yalipozikalia kimabavu ardhi za Waislamu, yalichukua tahadhari kubwa ya kuuficha Umma usitambue kwamba watawala wao ni vibaraka

wa wakoloni. Wamewekwa tu kul inda maslahi ya mabeberu.

M a b e b e r u h a w a wanawapa silaha vibaraka wao na baadhi ya mamluki ndani ya Umma, lengo likiwa kulinda na kudumisha maslahi ya nchi za mabeberu kwa damu ya Waislamu. W a n a w a g o m b a n i s h a Waislamu il i wapigane wenyewe kwa wenyewe.

M a wa k a l a h a wa wa Mabeberu wanapambana na wanaharakati halisi wa Kiislamu katika nchi zao. Hao ndiyo tishio pekee la ushawishi wa Kimagharibi katika nchi za Waislamu. H a r a k a t i n y i n g i n e hazikuonyesha uadui kwa Mabeberu, bali zilitumika tu kuwadanganya Waislamu kwa kipindi kifupi.

Jambo la msingi hapa n i k wa m b a Wa i s l a m u wasidanganyike na njama za hawa vibaraka, hata maneno yao yakionekana mazuri kiasi gani, hata wakijifanya wema kiasi gani! Hawa ni watu waovu. Waislamu wa n a o f a h a m u m a m b o haya ni vizuri wakaendelea kuwafichua vibaraka hawa waliopandikizwa kwenye U m m a w a K i i s l a m u . Tufichue uwepo wao na vitendo vyao. Tuwageuze kuwa mada ya kudumu katika majadiliano yetu. Hawa ni wasaliti wa Uislamu na wale wanaowatawala.

Fikra ya tano: Kuficha Uhalisia wa Mapambano kati ya Uislamu na Ukafiri - Ni ukweli unaofahamika vyema kwamba iwapo fikra na dhana zitafichwa vitabuni bila ya kuwekwa wazi kwenye jamii , i l i kuanzisha harakati, basi Itikadi inayotetewa na dhana na fikra hizo, haitakuwa na maana yoyote zaidi ya kuwa taarifa tu ya kale.

Tawala nyingi za Kisekula zinaeneza fikra na dhana potofu zinazolenga kuzimua mgongano uliopo kati ya Uislamu na Ukafiri, lengo likiwa kuzidi kuwabakisha Waislamu kwenye ujinga kuhusu uhalisia kwamba Uislamu na Ukafiri haviwezi kukaa pamoja.

Mifano ya fikra kama hizo ni pamoja na 'Interfaith Dialogue' (kwa lengo la kuunganisha Uis lamu, Ukristo na Uyahudi kama dini moja ya Kiabrahamu), na Mitaala ya Dini Mseto.

Usambazaj i wa f ikra kama hizo utaondoa hisia za Kiislamu katika nyoyo za Waislamu na kuwafanya waache jukumu lao la msingi la kuufanya Uislamu kuwa juu ya Itikadi zote. Uislamu unazipa changamoto dini nyingine zote:

"Yeye ndiye aliyemleta Mtume wake kwa uongofu na dini ya haki ili aijaalie kushinda dini zote; japokuwa watachukia hao makafiri" Qur(9:33)

I w a p o W a i s l a m u wa t a k u b a l i f i k r a h i z i zilizojengwa kwa misingi ya uongo na mitazamo potofu, bila shaka wataacha Uislamu wao. Baadhi ya Waislamu duniani leo, wameegemeza harakati zao kwa kuzingatia fikra hizo. Uwepo wa fikra hizo kwenye jamii, imekuwa ni kikwazo katika uhuishaji wa harakat i sahihi za Kiislamu.

Page 13: ANNUUR 1144

13 AN-NUURDHULQAAD 1435, IJUMAA SEPTEMBA 26-OKTOBA 2, 2014MAKALA

Hija sawa, Mahakama ya Kadhi hamtakiInatoka Uk. 11haswa kwamba, kumbe n a M a h a k a m a y a Kadhi nayo ni haki ya Waislamu na inafaa k u w e m o k w e n y e katiba. Sio Hija tu, h u e n d a w e n z e t u wanaona Hija sio suala la dini na si muhimu kwao, au kwa sababu safari hii sera ya chama cha jembe na nyundo haijasema na haijaona maslahi kwenye hili katika kuitumia kuingia kwenye ‘ulaji’.

I n a t o l e w a h o j a k wa m b a k u i n g i z a kipengele hicho ni sawa na kuchanganya dini na siasa, kiongozi mzalendo wa nchini I n d i a , M a h a t m a Gandhi alisema, ”Hao wanaopiga kelele juu ya k ut eng anish wa dini na siasa yumkini hawavijui vyote hivyo.”

Naye Professa Tariq R a m a d a n , k u t o k a Islamic Contemporary S t u d i e s , O x f o r d n c h i n i M a r e k a n i al ipoulizwa kat ika kipindi cha ‘Head to Head’ kinachorushwa n a t e l e v i s h e n i ya Aljazeera kama dini (Uislam) na siasa ni vitu viwili tofauti, alisema kwamba, “ I would say we should never ever

distinguish or separate or divorce politics from ethics and ethics has to do with religion,” kuwa huwezi kuvitenganisha vitu hivyo kwani Siasa ni maadili na maadili ni dini.

Maana yake bila dini hakuna maadili na bila maadili hakuna siasa, je siasa gani zitaendeshwa p a s i n a m a a d i l i , ambayo kwa k ias i kikubwa yanapatikana kwenye dini, itakuwa n i v u r u g u t u p u . Huenda wanasiasa wetu nawapiga debe wao kanuni na sheria wanazozitumia bila kujua kuwa msingi wake ni dini. Hata akina Socrate, ambao misingi yao tunaitumia leo katika siasa zetu w a l i a m i n i k a t i k a kuyaendesha mambo katika maadili (dini). R e j e a k i t a b u , T h e apology of Socrate k i l ichoandikwa na Plato.

Wa n a s i a s a we t u wasione umuhimu w a d i n i p a l e wanapoomba kura za kuingia madarakani, kupitisha mambo yao kama hayo ya katiba ambapo ‘Mahuja j i ’ wetu wamependwa au

wananchi wanapoamka k u d a i h a k i z a o utawaona wanapanda m a j u k wa a n i , h a d i nyumba za ibada na kunadi ‘ombeeni amani’, wale v izur i . Wana wa Allah wakiomba w a o , w a t a s i k i k a “msichanganye dini na siasa”.

Nihitimishe kwa kusema kuwa Mhe. S i t ta , wa jumbe na wengineo wakiwemo wajumbe Mahujaji wetu, wanapaswa kutambua kuwa Mahakama ya Kadhi nayo ni haki ya Waislamu, sio Hija tu, hivyo wana wajibu wa kutambua hisia za wengine ambao ni raia halali wa nchi hii.

Rejea kitabu cha Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes, k i l i choandikwa na Sheikh Mohamed Said.

P i a k u w a n y i m a Waislamu Mahakama yao ya Kadhi ni sawa na kuwatakia moto wa JAHANAM huko ahera, kwani mambo yao ya mirathi, ndoa, talaka n.k yataendelea kuendeshwa kinyume n a u t a r a t i b u w a mafundisho sahihi ya dini hiyo.

Tutakiane heri.

P.O. BOX 80059, TEL: 022-2860694, 0754/ 0655-462777, 0754-377897 DAR ES SALAAM (TZ)

QUR’AN, TAALUMA , MAADILI.

PRE-FORM-ONE 2015.MASOMO YATAANZA TAREHE 14/10/2014 (SIKU YA INTERVIEW)

HADI 14/12/2014.

MASOMO YATAKAYOFUNDISHWA NI QUR’AN, MATHEMATICS, MAARIFA YA UISLAM NA KIINGEREZA.

WANAFUNZI WATAKAA BWENI (BOADING).

MAHITAJI: MAVAZI YA KIISLAM, MADAFTARI (HARD COVER), MAS-HAF AU JUZUU NA MAHITAJI YA KUMUWEZESHA KUKAA BWENI.

ADA KWA MUDA WOTE HUO NI T.SHS 200,000/= TU.

KWA WANAFUNZI WALIOMALIZA DARASA LA SABA (7) DAARUL-ARQAM SCHOOLS WATASOMA BURE.

USAILI (INTERVIEW) 2015.USAILI KWA WANAFUNZI WA SHULE YA AWALI, MSINGI NA

SEKONDARI (2015) ITAFANYIKA SHULENI DAARUL ARQAM KIGAMBONI DSM JUMANNE TAREHE 14/10/2014 (NYERERE DAY) SAA 2 ASUBUHI. FORM NI TSHS 10,000/= TU.

SIMU 0717 190 242 AU 0658 190 079.

DAARUL ARQAM SCHOOLS

NDUGU Mhariri, k w a n z a k a b i s a nakupa hongera sana kwa kutufungua m a c h o Wa i s l a m wa Tanganyika na Zanzibar na kote u l i m w e n g u n i wanaosoma An-nuur.

N i m e k u w a nikilisoma gazeti hili tangu mwaka 2006 hadi sasa 2014.

N i t o e t u ushuhuda kidogo, mimi ni mwalimu wa shule ya msingi T a b o r a m j i n i . Niliweza kufanya mtihani wangu wa historia kidato cha sita (form six) mwaka 2010 bila kusoma historia sawasawa, l a k i n i u l i p o k u j a m t i h a n i w a k e , nilifaulu kutokana

Hongera Mhariri An-nuur kutufungua macho Waislamna kusoma makala za An-nuur. Watu walishangaa sana kuona nimefaulu h u k u n i k i w a nimesoma kat ika moja ya shule za mchepuo wa ufundi (technical school), ambazo ni sayansi.

K u m b e m i m i ni l isoma histor ia ya Nigeria kwenye gazeti la An-nnur n a k we n ye i m l a (essay), nikachagua swali la 'Civil war in Nigeria' kwa kuwa wewe ulituelimisha juu ya hi lo , kwa kweli hongera sana, Allah azidi kukupa mwanga zaidi na kesho akukir imu pepo yake Inshaalah.

Mwalimu Amiri Omary

MABINTI walioripotiwa kutekwa na kundi la Boko Harram nchini Nigeria.

Page 14: ANNUUR 1144

14 AN-NUURDHULQAAD 1435, IJUMAA SEPTEMBA 26-OKTOBA 2, 2014Habari/Makala/Tangazo

SHUKURANI zote anastahiki Mwenyezi Mungu mola mlezi wa ulimwengu na rehema na amani zimfikie mbora wa mitume nabii muhammad na jamaa zake na sahaba zake wote. Ama baada ya utangulizi huu mfupi;-

Uislamu umetiia umuhimu juu ya malezi na ukaweka namna mbalimbali za malezi ya watoto wa kike na wa kiume. Malezi ya watoto wa kike ni bora sana katika Uislamu kwa umuhimu wa mwanamke katika maisha ya jamii na mchango wake mkubwa katika jamii. Malezi ya mtoto wa kike katika Uislamu yana utukufu mkubwa, tena yanazidi usawa kati ya mwanamume na mwanamke katika Uislamu.

Imefafanuliwa ukubwa wa mapenzi na uadilifu katika Uislamu kati ya watoto wa kike na wa kiume. Na kati ya yale yaliyoandikwa katika makala hii ni kutokana na muongozo wa Mtume [saw] unaotubainisha ubora wa malezi ya watoto wa kike na kupanga ubora wa ki-dunia na ki-akhera.

Imefafanua mwanzo wake na kanuni zake ambazo anatakiwa kusimamia juu ya malezi katika mzunguko wa familia na jamii, nao si mwingine isipokuwa ni majukumu. Amesema mwenyezi Mungu mtukufu (enyi mlioamini, jiokoeni nafsi zenu na watu wenu na moto ambao kuni zake ni watu na mawe na wanausimamia ni malaika wakali, wenye nguvu hawamuasi mwenyezi Mungu kwa amri zake na wanatenda wanayoamrishwa yote) Surat at-Tahrim aya ya (6).

Anasema mwalimu wa umma huu Mtume [saw] kwamba,

Umuhimu wa kulea watoto wa kike katika Uislamu

Na Sheikh Salah Sayed Husen Miftah

(hakika mwenyezi Mungu atamuuliza kila mchungaji kwa kile alichokichunga, amekihifadhi au amekitupa, atamuuliza hadi mwanamume juu ya watu wa nyumbani mwake). Muulizaji ni mwenyezi Mungu mtukufu, atakayeulizwa ni kila mchungaji, wale wote walio chini ya mikono yake na wale anaowaongoza, ataulizwa mwanamume juu ya familia yake. Ameichunga au ameitupa tu?

Hao wategemee malipo yake kuwa ni thawabu au adhabu. Hapo inakuja mipaka ya sura kamil i maalumu baada ya kuulizwa mwanamume, ambaye yeye ni mchungaji mkuu wa nyumba na watu wake, ikiwa ni mke wake, watoto wake wa kiume na wa kike amewafanyia nini? Na amewatengenezea nini kwa ajili yao na je, amewalea kwa mujibu wa mwenyezi Mungu na ametekeleza wajibu wake?

Usimamizi wa mwanamume katika malezi sio wa hiyari, ni wa lazima katika nafasi yake ya kawaida katika maisha na nafasi ya kijamii na ikalazimisha kila jambo kwa njia zake na kuweka mpango wake kwa watu wake.

M w e n y e z i M u n g u ameshapanga hilo na suala l a k u u l i z wa h a l i k we p e k i . Yamegawanywa majukumu ya malezi kati ya mume na mke kwa watoto wao (mwanamume ni mchunga na ataulizwa juu ya kile alichokichunga na mwanamke ni mchunga katika nyumba ya mume wake, naye ataulizwa juu ya kile alichokichunga. Hivyo basi mwanamke (mke) anabeba fungu la jukumu lake la kuchunga nyumba hiyo, ndiyo nafasi yake na ndio wadhifa wa kawaida.

Nafasi hii na wadhifa huu una sehemu zake nyingi na yaliyo muhimu ni malezi ya watoto wa kike na wa kiume na hakuna makosa kwa maelekezo haya. Majukumu haya ni miongoni mwa mambo makubwa kwa binadamu katika harakati zake na wala asidhanie mtu kuwa au kwamba kuna mahusiano yoyote ya ki-maana kati ya kauli yake mwenyezi Mungu mtukufu, (na pale anapobashiriwa mmoja wenu amepata mtoto wa kike, hugeuka uso wake mweusi akiwa na hasira, ima awe naye kwa udhalili au amfukie mchangani).

Na kati ya kauli ya Mtume [saw] amesema, (atakayethaniwa na watoto wa kike kwa kitu chochote…) kwa kuegemea neno “kuthaniwa” hii ni muhimu kwani maana ya mtihani hapa ni majaribio, kitu ambacho

hudhaniwa ni sehemu ya malezi ya mtoto wa kike kutokana na taabu na matatizo, kwani yeye ni mwenye umuhimu na thamani ya juu.

Je hujaona neno la Mtume [saw] (... ukiwalea vizuri watoto wa kike inakua ni stara ya mtoto)? Sitara maana yake ni kuhifadhika na moto wa jehanamu.

Pale utakapomlea vizuri na kwa ufanisi na kwa njia ya upole, utapata njia ya mwenyezi Mungu na radhi zake Allah. Na kujikinga na joto la moto na katika amri ya malezi ya watoto wa kike, amesema Sheikh bin Abasi [ra], amesema Mtume [saw] (yule mwenye watoto watatu akavumilia juu yao, akawapa vinywaji, akawavesha, watakuwa ni kinga ya moto).

Je, itakuwa kinga ya moto kwa baba tu au hadi mama ambaye ni mshirika wa malezi? Na mimi ninao, namshukuru mwenyezi Mungu mabinti watatu.

Jibu: Shukurani zote anastahiki mwenyezi Mungu kuwa hadithi hii ni ya wote wawili yaani baba na mama. Kwa kauli yake Mtume [saw] (yeyote atakayekuwa na watoto wawili wa kike na akawalea vizuri watakuwa ni kinga ya moto). Na hivyo ndivyo vivyo hivyo akiwa na wadada au mama wadogo au shangazi au mfano wa hao, sisi tunataraji kuipata pepo kwani anapowalea vizuri anapata malipo makubwa na humkinga na moto na humkinga kati yake na moto kwa matendo yake mema. Hii ni maalumu kwa Waislamu tu.

Muislamu atakavyofanya hivi kwa nia nzuri na kwa ajili ya mwenyezi Mungu, humsababishia kufaulu na kuokoka na moto na kuingia peponi inasababu nyingi. Inatakikana muumini kufanya

kwa wingi matendo hayo na Uislamu wenyewe ndio shina pekee, nao ndio sababu ya msingi ya kuingia peponi na kuokoka na moto.

Pia kuna matendo mengine anapoyafanya anaingia peponi na ataokoka na moto. Kama vile Muislamu akiwa na watoto wa kike au madda na akawalea vizuri, watakuwa ni kinga ya moto na vile vile atakayefiwa na watoto watatu, ambao hawajafika balehe watakuwa ni kinga ya moto.

Wakasema, ewe Mtume; na wawili, akasema “na wawili”, na wala hawakuuliza mmoja. Na imesihi kwa Mtume [saw] amesema kwamba: Amesema mwenyezi Mungu mtukufu (hana mja wangu muumini kwake malipo atakapochukuliwa mtoto wake katika watu wa dunia na akataraji malipo mema isipokuwa ni pepo tu).

A k a b a i n i s h a m w e n y e z i Mungu kwamba hana mja muumini , mwenye mal ipo atakayochukualiwa mtoto wake katika watu wa dunia na akasubiri na akatarajia malipo mema isipokuwa pepo, mmoja miongoni mwetu anaingia katika hadithi hii pale anapomchukua mtoto wake kwa kifo na akasubiri baba yake au mama yake au wote wawili na wakatarajia malipo mema, hao wote wawili wana pepo.

Na hizi ni fadhila za mwenyezi Mungu, basi huyu ni mume na mke na ndugu wa karibu na marafiki pale wanaposubiri na wakatarajia malipo mema, wataingia katika hadithi hii pamoja na kuchunga usalama wao juu ya yale yatakayowazuilia malipo hayo kutokana na kufa katika madhambi yaliyo makubwa.

Tu n a m u o m b a m we n ye z i Mungu amani.

Page 15: ANNUUR 1144

15 AN-NUURDHULQAAD 1435, IJUMAA SEPTEMBA 26-OKTOBA 2, 2014Tangazo

Bismillahir Rahmanir Rahiim

ISLAMIC PROPAGATION CENTRENAFASI ZA KIDATO CHA KWANZA – 2015

Waislamu kote nchini mnatangaziwa nafasi za kidato cha Kwanza kwa shule zifuatazo:• Mkuzo Islamic High School - Bweni tu - SONGEA• Kirinjiko Islamic Sec. School - Bweni tu – SAME - KILIMANJARO• Nyasaka Islamic Sec.School - Bweni tu - MWANZA• Ubungo Islamic High School - Kutwa tu – DAR ES SALAAM

1. Shule hizi ni za Kiislamu, zenye lengo la kuwapa watoto elimu bora na kuwalea kwa malezi mazuri ya Kiislamu.

2. Masomo yanayofundishwa ni haya yafuatayo:Elimu ya Dini ya Kiislamu, Usomaji Qur’an na mafunzo yake, Hadithi za Mtume(s.a.w), Lugha ya Kiarabu, Kiswahili, English, Basic Mathematics,

Physics, Chemistry, Biology, Geography, History, Civics, Book – keeping na Commerce.

3. Patakuwa na mtihani tarehe 29/11/2014 saa 2:00 asubuhi katika vituo mbali mbali kote nchini. Muombaji anaweza kufanyia mtihani katika kituo chochote.

4. Mwisho wa kuchukua fomu ni tarehe 28/11/2014.

5. Fomu za Maombi zinapatikana kwa gharama ya shilingi 10,000/= katika vituo vilivyoorodheshwa hapa chini.

6. Pia, fomu zinapatikana kwenye Tovuti: www.ipctz.org. Ikumbukwe kuwa atakayepata fomu kupitia tovuti (download) atatakiwa kulipia wakati wa kurejesha siku ya mtihani.

• Arusha -OfisiyaIslamicEducationPanel,JamboPlastic,Ghorofaya2mkabalana msikiti Mkuu Bondeni : 0763 282 371/ 0783552414.

• Kilimanjaro - Moshi: Msikiti wa Riadha : 0654 723 418. - Same Juhudi Studio mkabala na Bank ya NMB Same: 0757 013344.

- Same: Kirinjiko Islamic Secondry School: 0784 296424/0655 697 075 - Usangi- Falhum Kibakaya : 0787 142054. - Ugweno – Kifula Shopping Centre- Yusuph Shanga : 078458776.

• Tanga - Twalut Islamc Centre – Mabovu Darajani : 0715 894111/0789 410914.- Uongofu Bookshop: 0784 982525

- Korogwe: SHEMEA SHOP : 0754 690007. - Mandia Shop - Lushoto: 0782257533.

• Mwanza - Nyasaka Islamic Secondary School : 0717 417685/0786 417685.-OfisiyaIslamicEducationPanel–MtaawaRufijimkabalanaMsikitiAl-Amin0785086770.

• Musoma -OfisiyaIslamicEdPanel-MtaawaKarume,NyumbaNa.05:0784721015/0765024623• Kagera -Bukoba:AlhudaCaféKwamzeeKinobekaribunaofisizaTRA.:0684701175.• Shinyanga - Msikiti wa Majengo karibu na Manispaa ya Shinyanga Mjini :0752180426-KahamaofisiyaAN–NUURKaribunamsikitiwaIbadhi:0753993930.

• Dar es Salaam - Ubungo Islamic High School : 0712974428/0712033556.-OfisiyaIslamicEd.Panel–Temeke-MsikitiwaNurulYakin:0655144474.

• Morogoro - Wasiliana na Ramadhani Chale : 0715704380.

• Dodoma - Hijra Islamic Primary School : 0716 544757/0712 325086.

• Singida -OfisiyaIslamicEducation.Panel–karibunaNurusnackHotel:0786425838/0784928039.

• Manyara -OfisiyaIslamicEd.Panel–MasjidRahma:0764469870/0789174902.

• Kigoma - Msikiti wa Mugera – Mwandiga: 0714 717727. - Kibondo – Islamic Nursery School: 0784 442860. - Kasulu: Murubona Isl.SS: 0714710802.

• Lindi - Wapemba Store: 0784 974041/0783 488444/0653 705627.

• Mtwara - Amana Islamic S.S: 0715 465158/0787 231007.• Songea - Kwa Kawanga Karibu na Msikiti wa NURU : 0713249264/0683670772.

- Mkuzo Islamic High School : 0717348375.• Mbeya -OfisizaIslamicEducationPanelUhindini–0785425319.• - Rexona Video mkabala na Mbeya RETICO: 0713 200209/0785425319.

.Rukwa - Sumbawanga: Masjid TAQWA: 0717082 073.

• Tabora - Kituo cha Kiislamu Isevya: 0784 944566.

• Iringa - Madrastun – Najah: 0714 522 122.• Pemba -Wete: Wete Islamic School : 0777 432331/0712772326.• Unguja - Madrasatul – Fallah: 0777125074. • Mafia -OfisiyaUst.YusufuAllyjiraninamsikitimkuu:0773580703.

USIKOSE NAFASI HII ADHIMU – WAHI KUCHUKUA FOMU SASA!

MKRUGENZIWABILLAH TAWFIIQ

1

Page 16: ANNUUR 1144

16 AN-NUURDHULQAAD 1435, IJUMAA SEPTEMBA 26-OKTOBA 2, 201416 MAKALA

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na POA Printing Works Limited, S.L.P. 4605 Dar es Salaam.

AN-NUUR16 DHULQAAD 1435, IJUMAA SEPTEMBA 26-OKTOBA 2, 2014

Soma gazeti la

AN-NUUR kila Ijumaa

IMEELEZWA kuwa nafasi ya mwanamke katika malezi na kuboresha jamii ya Kiislamu ni ya kipekee na inastahili kulindwa na kuheshimiwa barabara.

H a y o ya m e e l e z wa k a t i k a k o n g a m a n o lililokuwa likihusu nafasi ya mwanamke katika jamii ndani ya Uislamu lililoandaliwa na Kituo cha Kiislamu cha Kimisri Chang’ombe na kufanyika katika ukumbi wa chuo hicho jijini Da es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.

K o n g a m a n o h i l o liliongozwa na Sheikh Muhammadi Obaidi llah Mohammedi Ally, ambaye ni mwalimu wa al Azhar Sharifu tawi la Tanzania, ambapo Masheikh na Ukht mbalimbali waliwasilisha mada zao.

Akianza kuzungumzia nafasi ya mwanamke katika jamii ya Kiislamu, Mkurugenzi wa Markaz, Sheikh Ahmad Rajabu al-Shishtawi, alisema Mtume (saw) al ikuwa akitoa kauli mbalimbali juu ya wanawake na kwamba, kutokana na nafasi hiyo, alieleza kuwa wanawake ni ndugu wa wanaume.

Alieleza jinsi wanawake walivyokuwa msaada m k u b wa wa k a t i wa kuhama na wakati wa vita na akamtolea mfano mama Ummu Salama katika sulhu Hudaybia.

Baadae aliwasilisha mada yake Bi. Halima binti Abubakar, ambaye alisema mwanamke ni k i o n g o z i m i o n g o n i viongozi wanaoinyanyua jamii.

Alitoa somo namna mwanamke katika jamii anavyotumia nafasi yake kufanya kazi ambazo zinaendana na tabia zake.

Pia al igusia juu ya h a k i ya m wa n a m k e katika kuishi na kuacha kumfanyia uadui wa aina yoyote katika haki hiyo.

Nafasi ya mwanamke ni kubwa katika jamii ya KiislamuNa Azza Ally Ahmed Alisema kuwa zamani

kabla ya kuja Uislamu, watoto wa kike walikuwa wakifukiwa hai , bi la kufanya kosa lo lo te kwa kuwa walikuwa hawatakiwi katika jamii.

Aidha alizungumzia muongozo wa Mtume katika kubadilisha majina mabaya.

Alitoa mfano kutoka k w a M t u m e ( s a w ) kwamba alikuwepo kwa Omary binti aliyekuwa anai twa Aswia , kwa maana mfanya makosa, na Mtume aliposikia jina hilo, akambadilisha.

Pia aliwataka wazazi kutowatukuza watoto wa kiume kuliko wa kike na badala yake wanatakiwa kuwatendea usawa kati yao.

Naye Dkt. Abdallah Daruwesh, ambaye ni mwalimu wa al-Azhari Sharifu tawi la Tanzania, a l i wa s i l i s h a m a d a yenye anwani ‘nafasi ya mwanamke katika kulea watoto’.

Kat ika mada hiyo, a l i f a f a n u a j u u y a majukumu ya mwanamke katika kulea watoto.

Alisema mwanamke ndiye nusu ya kulea jamii na malezi ni nusu ya maisha.

Al iongeza kusema kuwa mwanamke n i mchunga katika nyumba y a m u m e w e , n a y e ataulizwa juu ya kile alichokichunga.

Aidha alizungumzia juu ya umuhimu wa mtoto kumuiga mama yake, kwani wakati mwingi huwa anakuwa naye kuliko baba.

Alisema hata vitendo v i n g i v y a m t o t o humtazama zaidi mama yake.

“ M t o t o h u m u i g a mama yake kwa chochote anachokifanya, kama mama ataongopa, basi na mtoto ataongopa na mama kupuuza malezi ya mtoto wake ni jambo la hatari sana kwani huharibu jamii. Amesema mshairi…uyatima siyo kufiwa na wazazi bali wanaweza wakawa hai na ukadhalil ika, bali uyatima ni pale mama a n a p o k u t e l e k e z a n a

baba anapokosa muda wa kukulea kwa wingi s h u n g h u l i z a k e . ” . A l i b a i n i s h a D k t . Daruwesh.

K wa u p a n de wa k e Sheikh Ally Mbwera, Katibu Mkuu wa Shule za Awali za Kiislamu Tanzania na Imamu wa Msikiti wa Ibadirahmani Ilala, alizungumzia somo juu ya haki ya mwanamke katika kushiriki kazi za kijamii na kisiasa.

Alisema mwanamke ana haki ya kushiriki katika kazi za kijamii na za kheri, pia haki yake ya kuongoza katika cheo chochote serikalini.

Naye Sheikhe Dkt . Oukil Mohamed Oukil, ambaye pia ni mwalimu wa al-Azhar Sharifu tawi la Tanzania, aliwasilisha mada iliyokuwa na anwani ya mwanamke kati ya ujahili na Uislam.

Yeye alifafanua juu ya vipaji vya kila binadamu, a m b a p o a l i s e m a mwanamke ana kipaji na ni kiumbe mtukufu a m b a y e m w e n y e z i M u n g u a m e m u u m b a na akamuweka sawa n a k u m t u k u z a n a amemboresha kul iko

viumbe vingine, hasa pale aliposema mwenyezi M u n g u k u w a a m b i a watu kwa kuwaamrisha kumuabudia yeye aliye wataja kwa asili yao kuwa ni viumbe wanaotokana na nafsi moja na nafsi hiyo ameiumbia mke wake.

Amesema mwenyezi M u n g u m t u k u f u katika Surat Nisai Aya ya (1-2) , “Enyi watu muogopeni Mola wenu ambaye amekuumbeni kutokana na nafsi moja na akamuumba kutoka katika nafsi hiyo mke wake na akawatoa kutokana na wao wawili wanamume wengi na wanawake. Na muogopeni mwenyezi M u n g u a m b a y e atawaulizeni juu kuunga u d u g u , k wa h a k i k a mwenyezi Mungu ni mwenye kukusubirini”.

Mwanamke wakati wa ujahili na zama za kiza, wakitazamwa Waarabu kabla ya Uislamu, wao walikuwa wakidhalilisha wanawake sana hadi kufikia kuwafukia wakiwa hai, pale tu anapozaliwa mtoto wa kike hutupwa s h i m o n i h a d i p a l e u l i p o o k u j a U i s l a m u na kukataza vitendo

hivyo vibaya. Alisema mwenyezi Mungu katika Surat Takwir, aya ya (8)(3), “Wakati huo watakapo ulizwa wale watoto wa kike.

Al i sema nafas i ya m w a n a m k e k a t i k a Uislamu ni muhimu kama ilivyo kwa mama dada au mke. Alisema hapa unaonekana Uislamu haukusahau nafasi ya mwanamke hata kidogo, bali umezitaja nafasi hizo katika mambo mengi na utukufu wa thamani yake hiyo.

B i . F a u z i a b i n t i Hashimu Halfani, ambaye ni Naibu Mkurugenzi wa Madrasat Abuhuraira, katika mada yenye anwani nafasi ya mwanamke katika kuijenga familia, al izungumzia juu ya nafasi ya mwanamke katika kulea watoto katika tabia nzuri na bora.

K o n g a m a n o h i l o l i l i h i t i m i s h w a k w a maswali na majibu na Mkurugenzi wa Markazi, S h e k h e A h m e d i a l -Sheshtawi kutoa neno la shukrani kwa walioshiriki.

MASHEIKH wa Kituo cha Kiislamu cha Kimisri Chang’ombe wakiendesha kongamano juu ya nafasi ya mwanamke katika malezi lililofanyika katika ukumbi wa chuo hicho jijini Da es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.