darasa v kazi ya nyumbani kiswahili jina la ......jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya raisi...

13
EPUKA COVID-19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA MEI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAISI TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA DARASA V KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA LA MWANAFUNZI: _____________________ MAELEKEZO 1. Kumbuka kuandika majina yako matatu kwa usahihi. 2. Jibu maswali yote kulingana na maelekezo. 3. Soma maswali kwa ufasaha kabla SHULE YA MSINGI MARTIN LUTHER S. L. P 1786 Dodoma. Simu. +255 26 2395029, +255 784 449098 Fax +255 26 2395030 (www.martinlutherschooldodoma.com) “Quality Education for the New Generation”

Upload: others

Post on 19-Jun-2020

136 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

EPUKA COVID-19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA MEI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAISI

TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

DARASA V – KAZI YA NYUMBANI

KISWAHILI

JINA LA MWANAFUNZI: _____________________

MAELEKEZO

1. Kumbuka kuandika majina yako matatu kwa usahihi.

2. Jibu maswali yote kulingana na maelekezo.

3. Soma maswali kwa ufasaha kabla

SHULE YA MSINGI MARTIN LUTHER S. L. P 1786 Dodoma. Simu. +255 26 2395029, +255 784 449098

Fax +255 26 2395030 (www.martinlutherschooldodoma.com)

“Quality Education for the New Generation”

EPUKA COVID-19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA MEI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,

OFISI YA RAISI TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

SHULE YA MSINGI MARTIN LUTHER KISWAHILI, KAZI WAKATI WA LIKIZO MAY, 2020

JINA____________________________________ DARASA LA V ________ MUDA: SAA 1

1. Wakitaka wavune mazao mengi……………..kulima kwa bidii. A. hawana budi B. hatuna budi C. huna budi D. sina budi [ ]

2. Wingi wa sentensi “kuku anakimbia” ni upi? A. makuku yanakimbia B. kuku wanakimbia C. kuku inakimbia D. kuku zinakimbia [ ]

3. Ameshindwa kujibu swali vizuri. Sentensi hii ipo katika nafsi gani?................ A. ya kwanza umoja B. ya tatu umoja C. ya pili umoja D. ya tatu wingi [ ]

4. Ungali chelewa kufika………..na basi. A. ungeachwa B. ungeliachwa C. ungaachwa D. ungaliachwa [ ]

5. Wanafunzi hawataimba wimbo wa shule. Katika sentensi hii neno lipi linaonesha ukanushi?.......... A. wanafunzi B. wimbo C. hawataimba D. shule [ ]

6. Aliwaeleza kuwa watunze mazingira yawe safi. Hii ni aina gani ya kauli?............... A. mkwaju B. halisi C. mapatano D. taarifa [ ]

7. Walipanda mbegu shambani. Katika sentensi hii silabi ipi inaonesha wakati? A. wa B. li C. ngu D. sha [ ]

8. Juma anaimba. Ukanushi wa sentensi hii ni upi?

A. Juma kaimbe B. Juma ataimba C. Juma haimbi D. Juma kamwimbie [ ] 9. “Niletee maji ya kunywa”. Hii ni aina gani ya kauli?............

A. halisi B. taarifa C. ya kule D. nipe maji [ ]

10. Raisi wa Tanzania alichaguliwa na wananchi wote kwa kumpigia…………………za ndiyo. A. kula B. kulia C. kulilia D. kura [ ]

11. Mwaga maji………….ni machafu. A. hiki B. wawa C. haya D. hilo [ ]

12. Mkulima………..nalinda mazao shambani. A. cha B. a C. wa D. za [ ]

13. Andika sentensi hii “Nimeandika maneno yote” katika wakati ujao. A. Niliandika maneno yote B. Ninaandika maneno yote C. Nitaandika maneno yote D. huandika maneno yote [ ]

14. Kuku ana miguu mingapi? A. mmoja B. mitatu C. kumi D. miwili [ ]

15. Mtu anayefanya kazi ya kuhudumia wagonjwa hospitalini huitwa………………… A. muuguzi B. cheupe C. mganga D. mtaalamu [ ]

16. Wasafiri wataingia ndani ya……….kuanza safari A. gari moshi B. moto C. moshi D. majivu [ ]

EPUKA COVID-19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA MEI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

17. Ukitaka kusafiri kupita baharini utatumia chombo kama……….

A. baiskeli B. meli C. gari D. ndege [ ]

18. Neno lipi liko tofauti na mengine kati ya haya……..…. A. Juma B. Ana C. Kuku D. Rehema [ ]

19. Kinyume cha sentensi hii “Vuta dawati” ni………………… A. sukuma dawati B. leta dawati C. peleka dawati D. vunja dawati [ ]

20. Methali yenye maana sawa na Baada ya dhiki faraja ni ipi?......... A. sikio la kufa halisikii dawa B. haraka haraka haina Baraka C. mchumia juani hulia kivulini D. mganga hajigangi [ ]

21. Kamilisha methali hii chombo cha kuzama hakina…….. A. rangi B. picha C. mkanda D. usukani [ ]

22. Tegua kitendawili. Hesabu yake haina faida……….. A. kucha B. kunguru C. nywele D. mlima [ ]

23. Jeni amekuwa popo maana yake ni…… A. kama mnyama B. mtundu C. anarukaruka D. kigeugeu [ ]

24. Methali inayopingana na hii “Jifya moja haliinjiki chungu” ni..................…..

A. Damu nzito kuliko maji B. Manahodha wengi chombo huenda mrama C. Haraka haraka haina Baraka D. kawia ufike [ ]

25. Tukifanya kazi tuliyopewa……tutaimaliza sasa hivi A. kwa bega B. kwa bega bega C. bega bega D. bega kwa bega [ ]

26. Kamilisha methali ifuatayo. Asiyeuliza……. A. ni mpole B. hajaelewa C. hana ajifunzalo D. anaogopa [ ]

27. Maana ya methali isemayo kutoa ni moyo si utajiri ni ipi?........................ A. kutoa kunataka kukaza moyo ili mali isipungue B. kutoa ni utajiri moyo hausaidii chochote C. kutoa si lazima kuwa na vitu vingi hata kidogo inafaa D. kutoa kunategemea utajiri [ ]

28. Nikimpiga mwanangu watu hucheza. Tegua kitendawili…… A. kinyonga B. ngoma C. ubuyu D. mchezo [ ]

29. Nini maana ya nahau “Vimba kichwa”……….

A. kuwa mlevi B. kuwa na kiburi C. mchoyo D. oa [ ]

SEHEMU C: USHAIRI Soma shairi lifuatalo kwa makini kisha jibu swali la 31 – 36 kwa kuchagua herufi ya jibu sahihi.

Mazingira ni muhimu, kwetu sisi binadamu

Usije kuyahujumu, viumbe utadhulumu,

Ni letu sote jukumu, Mazingira kuhudumu,

Tuyatunze mazingira, ili nayo yatutunze,

Chakula nayo makazi, mazingira tupatia,

Hewa safi kama kazi, yote tunajivunia,

Hata kama kiangazi, maji tunajipatia,

EPUKA COVID-19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA MEI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

Tuyatunze mazingira, ili nayo yatutunze.

30. Shairi hili linatoa ujumbe gani kwetu?............... A. Kulima bustani B. kupanda maharage C. kuyatunza mazingira yetu D. kukata miti ovyo. [ ]

31. Mshairi ana maana gani anaposema “Usije yahujumu?”……….. A .Usile mazingira B. usikae kwenye mazingira C. kiumbe duniani D. Usije ukayaharibu mazingira. [ ]

32. Je, ni jukumu la nani kuyatunza mazingira?.........A. Askari B. Polisi C. Kila mtu D. Mwalimu [ ]

33. Ni nini maana ya neno mazingira?.......... A. Nguo zilizokwisha valiwa B. upashanaji wa habari C .Mti wenye matunda tu. D. mambo yote yanayomzunguka binadamu. [ ]

34. Vina vya kati na vya mwisho katika ubeti wa pili ni vipi?....

A. mu, tu B. zi, a C. Ha, ka D. ju, te. [ ]

35. Katika ubeti wa pili mwandishi wa shairi anasema mazingira hupatia chakula, makazi, maji na ……… A. nyuki B .Hewa C. Mbingu D. mayai. [ ]

UTUNGAJI Umepewa sentensi nne zilizochanganywa. Zipange sentensi hizo katika mtiririko unaofaa ili zilete maana sahihi ya habari kwa kautumai herufi A, B, C, D.

36. Baada ya kusubiri kwa nusu saa, basi liliwasili na nikapanda basi hilo kwenda Bunda. [ ]

37. Abiria wote walishuka kutoka kwenye gari moshi, Nami nilishuka na kwenda moja kwa moja hadi kwenye kituo cha mabasi. [ ]

38. Lilipowasili mjini Mwanza, gari moshi lilisimama taratibu na kutangaza kuwa hapo ndipo ulikuwa mwisho wa safari yake. [ ] 39. Mimi na abiria wenzangu tulisafiri kwa amani na kufika Bunda salama jioni. [ ]

40. Mwaka ...............nitasoma kwa bidii zaidi ili niwe wa kwanza Darasani. A. hiki B. huu C. haya D. hawa [ ]

41. Kikombe………..kina rangi nyekundu. A. kangu B. vyao C. changu D. vyetu [ ] 42. Jana baba hakununua kitabu……… A. chochote B. lolote C. yeyote D. wowote [ ] 43. Mashamba……….ni ya wenye mali. A. hili B. haya C. hiki D. hicho [ ] 44. Unakwenda……….? Neno lipi linakamilisha sentensi hiyo. A. nini B. gani C. wapi D. ipi [ ] 45. Kaka……….dada wanacheza mpira. A. na B. ila C. wa D. cha [ ] 46. Nini kirefu cha neno UKIMWI? A. Ukimpiga mwalimu utakamatwa B. Upungufu wa kinga mwilini

C. Ukiruka utakamatwa na polisi D. ni kwa ajili yetu [ ] 47. Asingalifanya uzembe………shindwa mtihani wake. A. asinge B. asingeli C. asingali D. ange [ ]

EPUKA COVID-19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA MEI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

48. Wingi wa sentensi “Ukuta huu una ufa” ni upi? A. Nyukuta hizi zina nyufa B. Kuta hizi zina maufa

C. Maukuta haya yana ufa D. Kuta hizi zina nyufa [ ] 49. Kiranja mkuu alipokea zawadi……ya wanafunzi wote. A. kwa bahati B. kwa niaba C. kwa D. kwa kelele [ ]

50. Neno mng’ang’anizi lina silabi ngapi?......... A. moja B. nne C. sita D. tano [ ]

51. Ili tufanye vizuri mithani………kusoma kwa bidii. A. ni budi B. sina budi C. hatuna budi D. bila budi [ ] 52. “Msisahau kukusanya madaftari yenu” Mwalimu alisema hii ni kauli………………..

A. shuruti B. halisi C. taarifa D. ombi [ ]

53. Mwanafunzi mkorofi atachapwa na mwalimu. Sentensi hii ipo katika wakati gani?..................... A. ujao B. uliopo C. uliopita D. mtimilifu [ ]

54. “Kichwa kinaniuma” kauli taarifa ya sentensi hii ni……………… A. Kichwa kinaniumiza B. Alisema kichwa hasa kichwa C. Alisema kwamba kichwa kinamuuma D. Kichwa wee acha tu [ ]

55. ……………………za ugonjwa wa homa ya bonde la ufa zinatishia usalama wetu. A. Athali B. Adhali C. Asali D. Athari [ ]

56. Kwa sasa………..yake siyo nzuri. A. sia B. siha C. Thiaha D. Ziha [ ]

57. Mzigo ulioibwa una……….ya milioni sita. A. Dhamani B. Thamani C. Samani D. Zamani [ ]

58. Kitu kitolewacho kwa ajili ya kuwafariji wafiwa huitwa…………………….. A. maombolezo B. matanga C. sadaka D. rambirambi [ ]

59. John ni mahiri wa kughani mashairi na tenzi. Neno “mahiri” lina maana ya……………….. A. sahihi B. nadhifu C. bingwa D. mjinga [ ]

60. Nahau ipi inabeba ujumbe wa mtu kufanya mipango ya siri yenye hila. A. kula kiapo B. kula yamini C. kula ugali D. kula njama [ ]

61. Kuku wangu hutagia miibani. Neno lipi linaonesha hali ya mazoea katika kitendawili hicho?………. A. kuku B. hutagia C. wangu D. miibani [ ]

62. Watoto wa tajiri wa nguo hulala na kutembea uchi. Tegua kitendawili………………….. A. Jongoo B. nyota C. maboga D. mwezi [ ]

63. Kwa kawaida mtu humthamini ndugu yake zaidi kuliko mtu mwingine. Methali ipi inaweza kutumika katika maelezo hayo?....................... A. Baniani mbaya kiatu chake dawa B. Cha mlevi huliwa na mgema C. Baada ya dhiki faraja D. Damu nzito kuliko maji [ ]

64. Kamilisha methali hii. Chanda chema………………………. A. si ujinga B. huvikwa pete C. uliwa na wageni D. huisha bila habari [ ]

65. Chungu cha mwitu hakiwapiki wapishi wake wakaiva. Jibu la kitendawili hiki ni……………………… A. yai na kuku B. ulimi na meno C. mzinga wa nyuki D. katani [ ]

66. “Kaa chonjo”. Nahau hii ina maana gani?........ A. Jihadhari B. kaa vizuri C. kazana D. jitahidi [ ]

EPUKA COVID-19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA MEI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

67. Mwakilima ameniunga mkono katika suala hili. Maana yake ni…………………. A. amenipiga B. amenikwepa C. amekubaliana na mimi D. amenichangamkia [ ]

68. Methali ukiona vyaelea vimeundwa. Ina maana gani?............. A. vilivyotengenezwa havithaminiwi B. kila kizuri hugharamiwa C. unda vyombo vielee D. vinavyozama havijaundwa [ ]

69. “Nina kamba yangu ndefu lakini haifungi kuni”. Jibu la kitendawili hiki ni………………… A. mkanda B. kanga C. mkufu D. njia [ ]

70. Fundi …….. likuwa anajenga nyumba ya babu. A. seremala B. mwashi C. cherehani D. mitindo [ ]

71. Ugali wa mtama unahitaji ……… kizuri. A. maandalizi B. maji na kuni C. kitoweo D. sufuria [ ]

72. Ng’ombe alimkanyaga kwa ukwato wake akapata ….. makali.

A. maumivu B. furaha C. hasira D. kicheko [ ]

73. Hatuezi kupata …….. wa tatizo hili mpaka tujue chanzo chake.

A. finyanga B. uongo C. ndoto D. ufumbuzi [ ]

74. Neno lenye maana sawa na hela ni …… A. pesa B. bakora C. fimbo D. mapato [ ]

75. Mbwa wetu akimwona adui …….. na kumfukuza. A. hulia B. humlea C. hubweka D. husema njoo [ ]

76. ……… maji ya kunywa ili yawe salama. A. Koroga B. Twanga C. Pooza D. Chemsha [ ]

77. Mtoto mwenye adabu …….. A. hulia ovyo

B. hupendwa na watu wengi C. hupigwa na walimu D. hukimbiza mbwa [ ]

78. Mbuzi …….. ni wa kisasa. A. hivi B. vyao C. hizi D. hawa [ ]

79. Mzee Adolph …….. shamba lake jana. A. anapalilia B. atapalilia C. alipalilia D. amepalilia [ ]

80. Unaposafiri kwa gari fedha unazolipa huitwa …….. A. posho B. safari C. mwendo D. nauli [ ]

81. Siku ya pili baada ya siku ya leo ni …….. A. kesho kutwa B. leo leo C. kesho D. jumamosi [ ]

82. Mtu anayetengeza vyombo vya udongo kama vile vyungu huitwa …………

A. mfumaji B. mhunzi C. mfinyazi D. mkorogaji [ ]

83. Mti mnene mrefu utumiwao kujengea dari za nyumba huitwa ……..

A. fimbo B. mgange C. boriti D. mgando [ ]

84. Neno lenye maana sawa na mtoto ni …….. A. mwanadamu B. mwana C. kitoto D. kichanga [ ]

85. Paka kwa jina jingine anaitwa ……… A. chui B. mapaka C. kipaka D. nyau [ ]

86. Sentensi hii ikiandikwa katika wingi itakuwaje?......”Amepanda miti”

A. tulipanda miti B. tutapanda miti C. wamepanda miti D. mmepanda miti [ ]

87. Ukitembea ….. utaachwa nyuma. A. polepole B. mbuga C. gari C. pikipiki [ ]

EPUKA COVID-19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA MEI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

88. Leo moto unawaka, kwesho moto ………. A. uliwaka B. umewaka C. huaka D. utawaka [ ]

89. Reli ni njia ya …………... A. malori B. meli C. treni D. ndege [ ]

90. Wanafunzi wa darasa la tano ni ……… A. msafi B. visafi C. Wasafi D. masafi [ ]

91. Ng’ombe …………….… mkubwa kuliko. A. na B. ni C. ka D. la [ ]

92. Nyumba ……..ziliezuliwa na upepo. A. mengi B. kingi C. vingi D. nyingi [ ]

93. Kiatu cha Anna ………. A. vimechafuka B. imechafuka C. kimechafuka D. zimechafuka [ ]

94. Kibuyu ………. kimejaa maji. A. hii B. hicho C. huyo D. haya [ ]

95. Paa ni sehemu gani ya nyumba? ……………… A. chini B. juu C. ndani D. nyuma [ ]

96. “Mchuma janga hula na wakwao” maana ya methali nii ni …………………..

A. haifai mtu kuwa mchoyo B. mali ya mjinga huliwa na mwerevu

C. si vizuri kula mikahawani hali una kwenu D. jikisoe mwenyewe kwanza kabla hujakosoa wengine [ ]

97. Kamilisha sentensi ifuatayo; kufa ...... A. ni kufariki B. kwaja C. ni kubaya D. kufaana E. ni lazima [ ]

98. Asha hujikwatua kila siku “ kujikwatua” maana yake ni nini?

A. kujiremaba B. kujisugua C. kujipiga D. kujipenda E. kujitakasa [ ]

99. Mambo yote yametibuka maana yake ni kwamba ………

A. yamepotoka B. yametoka C. yamefumuka D. yameharibika [ ]

100. ……… ni kuona mengi. A. Kuishi kwingi B. Kufumbua macho C. Kunapokucha D. kuangalia [ ]

101. Kila shetani ………… kamilsha methali hiyo.

A. kumpongeza B. mchimbaji C. anawanga usiku D. na mbuyu wake [ ]

102. Mama ………….. Kwa kosa nililofanya.

A. ninaomba razi B. ninaomba rathi C. ninaomba radhi D. ninaomba unikumbuke [ ]

103. Hakuna masika yasiyo na …………. A. mende B. mbu C. ncha D. viazi [ ]

104. Tegua kitendawili hiki.Mjomba hataki tuonane. A. kucha B. ulimi C. kisogo D. kiungo cha pilau [ ]

105. Nini maana ya nahau “Kumpa heko”……………….

A. kumletea B. kupiga makofi C. kumpongeza D. kumlilia [ ]

SEHEMU C: USHAIRI.

Soma shairi lifuatalo kwa makini kisha jibu swali la 46 – 50 kwa kuchagua herufi ya jibu sahihi.

Alijaliwa watoto, wakawa wadogo zangu,

Mimi ndiye dada Doto, Wakanipenda wenzangu,

Kama samaki na mto, au mvua na mawingu,

Mama wa kambo ni mama, mimi naye twapendana

EPUKA COVID-19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA MEI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

MASWALI.

106. Silabi za kati na za mwisho katika ubeti wa shairi huitwa…… A. mshororo B. mizani C. vina D. kituo [ ]

107. Mstari wa mwisho wa ubeti unaitwaje?.......... A. kituo B. mstari wa pembeni C. kina D. pengo [ ]

108. Ubeti mmoja wa shairi una jumla ya mishororo mingapi?..... A.miwili B. mitatu C. mitano D. minne [ ]

109. Mstari wa pili katika shairi hilo una mizani mingapi?.......... A. 10 B. 16 C. 8 D. 64 [ ]

110. Shairi hilo linabeti ngapi?................ A. ubeti mmoja B. beti tatu C. beti mamoja D. ubeti sita [ ]

111. Katika shairi hilo mstari wa tatu mwandishi anasema kama samaki na mto au mvua na ………. A. dalili B. giza C. mawingu D. dagaa [ ]

112. Wingi wa sentensi “hakuishi na mtoto mwizi” ni upi?.................. A. hawakuishi na mitoto mijizi B. hawakuishi na watoto wezi C. hakuishi na mitoto mizi D. hawakuishi na vitoto vizi [ ]

113. Bibi………..nyumba nzuri na babu. A. amejengeka B. amejengwa C. amejengana D. amejengewa [ ]

114. Tumefaulu vizuri mitihani yetu yote. Sentensi hii ipo katika wakati gani?.................... A. mtimilifu B. ujao C. uliopita D. uliopo [ ]

115. Ungewahi kuondoka……..mapema nyumbani. A. ungalifika B. ungefika C. ungelifika D. ungafika [ ]

116. MNASUKA. Neno hili lipo katika nafsi ipi?...... A. III – umoja B. III – wingi C. I – umoja D. II – wingi [ ]

117. Huyu……….mtoto aliyekuwa amepotea. A. ndio B. ndiyo C. ndiye D. ndivyo [ ]

118. Ili nipike chakula kitamu………..….kuongeza viungo. A. ni budi B. kuna budi C. sina budi D. hatuna budi [ ]

119. Mbwa………..ameonekana. Neno lipi ni sahihi kukamilisha sentensi hiyo?................. A. aliyepotea B. amepotea C. iliyopotea D. anayepotea [ ]

120. Wingi wa sentensi hii “kijana amefaulu mtihani wake ni……………. A. vijana wamefaulu mitihani yao B. vijana amefaulu mitihani yake C. vijana hufaulu mtihani wake D. vijana anafaulu mtihani wake [ ]

121. Watu wa Mwanza walilalamika……….wezi waliwaibia mali zao. A. ili B. kabla C. kuwa D. kwa [ ]

122. ....................ni mojawapo ya athari za uharibifu wa mazingira. A. masika B. jangwa C. kiangazi D. mvua na mazao [ ]

123. Neno ndugu yake likiandikwa kwa kifupi litakuwa….....................… A. nduguye B. nduguche C. nduguze D. nduguyo [ ]

124. Jeni………..mdogo wake kwa mjomba wao. A. walimfuata B. alimfuata C. alifuata D. alifuta [ ]

125. Mwalimu alifika………….kutuona tulipokuwa hospitalini A. yeye mwenyewe B. sisi wenyewe C. yeye wenyewe D. wao yenyewe [ ]

EPUKA COVID-19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA MEI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

126. Sote tutakuwepo kwenye………….…lile ili tumsikilize kiongozi.

A. mkutano B. uwanja C. kusanyiko D. maandamano [ ]

127. Kukiri maana yake ni………. A. kukanusha B. kukataa C. kukubali D. kusahau [ ]

128. Mjumbe wa nyumba kumi anaitwa……………. A. balozi B. mwenyekiti C. katibu D. mhazini [ ]

129. Tendo la watu kurudi kutoka mahali fulani linaitwa…. A. kulegea B. kuerekea C. kutoka D. kurejea [ ]

130. Umoja wa neno mbao ni upi?............. A. vibao B. mbarao C. ubao D. mbao [ ]

131. Andika neno la Kiswahili kutokana na herufi hizi NIHUUZ……. A. huuni B. uhuni C. ziinu D. huzuni [ ]

132. Nini maana ya nahau “Teka nyara”………………………….… A. kula nyanya B. tendo la kuchukua kwa nguvu C. pigana D. nenda manyara [ ]

133. Kamilisha methali ifuatayo:- “Ng’ombe haelemewi na…….” A. nunduye B. mguu C. kichwa D. tumbo [ ]

134. Bibi na babu wana watoto sitini. Tegua kitendawili kwa usahihi….. A. mhindi B. ng’ombe C. saa D. taa [ ]

135. Kamilisha methali; Milima haikutani………… A. vichaka hukutana B. mawe hukutana C. kiatu chake dawa D. binadamu hukutana [ ]

136. Nahau “Pandwa na hasira” ina maana gani?...........

A. kasirika B. furahia C. cheka D. piga makofi [ ]

137. …………..aeleke jiwe. Mwanzo wa methali hii ni upi?

A. asiye na kwao B. asiye na huruma C. asiye na mwana D. asiye na woga [ ]

138. Mla ni mla leo…………kamilisha methali hiyo.

A. mla jana kala nini B. leo mpe mihogo C. usipende kula D. kula na wewe [ ]

139. Mgema akisifiwa…................... A. wote tunapiga makofi B. tembo hulitia maji C. wote tunacheka D. hajitibu mwenyewe [ ]

140. Ukumbuu wa babu ni mrefu. Jibu la kitendawiili hiki ni…… A. mkanda B. mkufu C. njia D. kinyonga [ ]

141. Nahau “Changanya miguu” ina maana gani? A. kushoto na kulia B. mbele kwa nyuma C. mrefu na mfupi D. tembea upesi upesi [ ]

142. “Chukua mbao zako zote”. Hii ni aina gani ya kauli? A. taarifa B. wingi C. moja D. halisi [ ]

143. Shangazi aliimba wimbo wa Taifa. Sentensi hii ipo katika wakati gani? A. uliop B. uliopita C. ujao D. mtimilifu [ ]

144. Wingi wa sentensi “Mwalimu ananawa mkono wake” ni upi? A. walimu wananawa mikono yao B. walimu ananawa mkono wao C. mwalimu ananawa mikono yao D. mwalimu wananawa mkono wao [ ]

145. Kanusha sentensi ifuatayo “Barua imepokelewa” .............. A. barua haikupokelewa B. barua hitapokelewa C. barua haijapokelewa D. barua haitapokelewa [ ]

EPUKA COVID-19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA MEI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

146. Muda ..........tunatakiwa kuwa darasani. A. hii B. hichi C. hiki D. huu [ ]

147. Kuku hawa .................sana. Neno lili linakamilisha sentensi hii? A. wanakimbia B. zinakimbia C. yanakimbia D. kinakimbia [ ]

148. Umoja wa sentensi hii ni upi? “Watoto wamevunja vioo vya madirisha” A. kitoto kimevunja kioo cha dirisha B. mitoto imevunja vioo vya dirisha C. mtoto amevunja kioo cha dirisha D. katoto kamevunja kaoo ka madirisha [ ]

149. Neno mjomba lina silabi ngapi? A. kumi B. sita C. moja D. tatu [ ]

150. Angewahi ...............A. angelimkuta B. angalimkuta C. angemkuta D. angamkuta [ ]

151. Alisema kuwa atakuchorea picha nzuri. Hii ni aina gani ya kauli? A. taarifa B. mbanano C. halisi D. nyepesi [ ]

152. Ili waweze kufaulu mtihani ......................”kusoma kwa bidii”.

A. sina budi B. hawana budi C. hatuna budi D. ni budi [ ]

153. Unaweza kuamua kusuka ..............kunyoa. A. kwa B. wa C. au D. cha [ ]

154. Hapa ............anapoishi chifu Mkwawa. A. ndimo B. ndiko C. ndio D. ndipo [ ]

155. Sentensi ifuatayo ikiwa katika wakati mtimilifu itakuwajawe? “Waziri mkuu ataitisha mkutano” .......... A. Waziri mkuu aliitisha mkutano B. Waziri mkuu ameitisha mkutano C. Waziri mkuu mkutano huo D. Waziri mkuu huitisha mkutano [ ] 156. Jina lako unaitwa nani alama gani inaweza kutumiwa katika sentensi hiyo?.................... A. ! B. , C. ? D. . [ ] 157. Babu yangu amekuwa ..........ana miaka mia moja sasa. Neno lipi linakamilisha sentensi hiyo? ....... A. mgane B. shaibu C. ajuza D. kizika [ ]

158. ....................ni mbolea inayotokana na kinyesi cha wanyama. A. samli B. mtindi C. ngozi D. samadi [ ]

159. Kisawe cha neno “Tochi” ni kipi? A. kibatari B. umeme C. kurunzi D. nishati [ ]

160. Kuwasili ni sawa na neno lipi kati aya haya yafuatayo: A. chelewa B. kufika C. kuwasiliana D. wajibu [ ]

161. Neno “mziwanda: ni sawa na ........................ A. mtoto wa shangazi B. kifungua mimba C. kitinda mimba D. mtoto wa bibi [ ] 162. Nina mtoto wangu nikimpa chakula analia, nikimyima halii. Jibu la kitendawili hiki ni lipi? .......... A. redio B. nyoka C. kobe D. kinyonga [ ]

163. Kamilisha methali ifuatayo ........................ni kama usiku wa giza. A. mwenda pole B. jambo usilolijua C. mchuma janga D. mtoto umleanvyo [ ]

164. ....... alipomwambia kwamba jina lake aliliona kwenye orodha ya mafisadi. Nahau ipi inafaa kukamilisha sentensi hiyo? A. alimkata maini B. alimkata shauri C. alikata pua D. alimpa magoti [ ]

EPUKA COVID-19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA MEI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

165. Tegua kitendawili hiki : “ maskini huyu hata umchangie namna gani haliziki” A. kalamu B. macho C. tumbo D. andazi [ ]

166. Usiache mbachao .....................kamilisha methali hiyo. A. kwa msala upitao B. ukaenda kula ugali C. ukala wali D. kichwa wazi [ ]

167. Nini maana ya nahau “njia ya mkato” ...................... A. kichochoro B. njia ndefu C. njia nyembamba D. njia fupi [ ]

168. Mdharau biu, hubiuka yeye. Methali hii inafanana na ipi kati ya hizi zifuatazo: A. mkataa pema pabaya panamuita B.mchuma janga hula na wakwao C. mtapata maji haachi kufa D. mdharau mwiba mguu huota tende [ ]

169. Kaka yangu amepata jiko. Maana yake ni ......................... A. amepata sehemu ya kupikia B. anishi jikoni C. ameoa D. amejenga jiko [ ]

170. Kuzaliwa na kufa kwa binadamu, hutoa maana ya kitendawili kipi kati ya hivi vifuatavyo? ........... A. huchagui wala hushauriwi B. tajiri wa rangi C. kulia kwake ni kicheko kwetu D. prrrrr mpaka maka [ ]

171. Kamilisha methali ifuatayo: Njia ya mwongo ni ........................ A. ndefu B. arobaini C. fupi D. nene [ ]

USHAIRI Soma shairi lifuatalo kwa makini kisha jibu swali la 31 – 36 kwa kuchagua herufi ya jibu sahihi. Soma uwe mashuhuri, pia uwe maridhia, Soma ondoa kiburi, na mema kujiombea, Mwerevu ni jemadari, vitani akiingia, Elimu ninakwambia, hazina isiyokwisha.

Sisome kuwa jahili, bali ujue sheria, Ili uweze jadili, na mambo kufafanua, Mambo yakikukabili, uweze kuyatatua, Elimu ninakwambia, hazina isiyokwisha.

Mwenye elimu tajiri, fumbo gumu kufumbua, Tena huweza tabiri, mambo yanayomjia, Akayajua ya shari, na wapi pa kutupia, Elimu ninakwambia, hazina isiyokwisha. MASWALI. 172. Neno jahili kama lilivyotumiwa na mwandishi katika ubeti wa pili lina maana gani?.............. A. Jalali B. Mjinga C. jaivu D .tabia. [ ]

173. Mwandishi anasema mtu mwerevu ni ……. A. Jemadari B .V itani C. ondoa D. kibaka. [ ]

174. Katika ubeti wa kwanza mstari wa pili una jumla ya mizani mingapi?.... A. 8 B. 12 C. 10 D. 16. [ ]

175. Vina vya kati na vya mwisho katika ubeti wa tatu ni ………. A. ka, li B. si, ta C. ri, a D. vi, ma [ ]

EPUKA COVID-19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA MEI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

176. Mstari wa mwisho kwa kila ubeti huitwa ……… A. Kituo B . kitambo C. kitanda D. kitabu. [ ]

177. Shairi hili lina jumla ya mistari mingapi? A. kumi na sita B. kumi na mbili C. kumi na tano D. saba. [ ]

UTUNGAJI Umepewa sentensi nne zilizochanganywa. Zipange sentensi hizo katika mtiririko unaofaa ili zilete maana sahihi ya habari kwa kautumai herufi A, B, C, D.

178. Hatimaye alipelekwa mahakamani na kuhukumiwa kifungo cha maisha. [ ]

179. Siku moja Chausiku alitumwa sokoni. [ ]

180. Alilia na kupiga kelele mwizi! Mwizi! Mwizi alifukuzwa na kukamatwa na wananchi [ ]

181. Njiani alikutana na mwizi akamnyang’anya fedha na kikapu. [ ]

SEHEMU C: USHAIRI. Soma shairi lifuatalo kwa makini kisha jibu maswali yote kwa kuchagua herufi ya jibu sahihi.

Uwanjani naingia, kuleta zangu nasaha,

Watoto wote sikia, msije leta mzaha

Elimu kushikilia, ili msije kuhaha

Ongezeni jitihada, kwani Elimu bahari

Walimu wanafundisha, ili muweze elewa

Leo ninawakumbusha, jitihada yatakiwa

Huna budi jikumbusha, uweze kufanikwa

Ongezeni jitihada, kwani Elimu bahari

Maswali.

182. Mtunzi wa shairi anaposema “Mzaha” ana maana gani?................ A. majigambo B. utani C. shida D. ukweli [ ]

183. Msemo “Elimu ni bahari” una maana kwamba Elimu……..........…… A. ni maji B. si ufunguo C. ni bwawa D. haina mwisho [ ]

184. Mwandishi anaposema kuwa “huna budi” ana maana kwamba……………… A. ni lazima B. si muhimu C. hutakiwi D. si lazima [ ]

185. Shairi lina mishororo mingapi kwa kila ubeti………. A. kumi B. minne C. mitano D. nane [ ]

186. Vina vya kati katika ubeti wa pili ni……… A. sha B. wa C. a D. ha [ ]

187. Kituo cha shairi hili ni kipi?........... A. Uweze kufanikiwa B. Leo ninawakumbusha

C. Ongezeni jitihada kwani Elimu bahari D. ili muweze elewa. [ ]

SEHEMU D: UTUNGAJI. Umepewa sentensi nne zilizochanganywa. Zipange kwa kuzipa herufi A, B, C, D. ili zilete maana sahihi ya habari.

188. Lakini walipiga moyo konde. [ ]

189. Safari haikuwa mbaya wala nzuri, kwani walikutana na wanyama wakali. [ ]

190. Wakaendelea na safari yao. [ ]

191. Na hata watu wenye sura za kutisha. [ ]

EPUKA COVID-19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA MEI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

SEHEMU E. UFAHAMU.

Soma habari ifuatayo kwa usahihi kisha jibu swali la 41 – 45 kwa kujaza nafasi zilizoachwa wazi.

Katika kijiji chetu kulikuwa na mzee mmoja aliyejulikana kwa jina la Komba. Mzee Komba alikuwa mtu wa ajabu. Alipenda

kufuga ndege wa aina mbalimbali. Nyumba yake ilikuwa imezungukwa na vibanda vya ndege hao. Wakati nyumba nyingine

pale kijijini zikiwa na kelele za ng’ombe, mbuzi na kondoo hali ilikuwa tofauti kwa mzee Komba, kwani nyumba yake ilitawaliwa

na kelele za ndege. Mzee Komba alikuwa na tabia ya kudamka asubuhi na kuhudumia ndege wake.

Siku moja Mzee Komba alitembelewa na mgeni kutoka kijiji cha jirani. Mgeni huyo alikuwa anaitwa Soga. Mzee Soga

alivutiwa na mandhari ya mahali pale. Baada ya kusalimiana na Mzee Komba alimtembeza mgeni wake sehemu zote za

nyumba yake na kumweleza juu ya kila aina ya ndege aliyekuwepo hapo. Kibanda cha kwanza alichompeleka kilikuwa na

ndege wawili aina ya mbuni. Mgeni alishangaa kuwaona ndege wakubwa namna ile. Alimuuliza mwenyeji wake, Je, hawa

ndege walivyo wakubwa hivi wanaweza kuruka? Mzee ngalomba alitabasamu kidogo kisha akajibu “La hasha, hawa ni ndege

wa ajabu kidogo. Hawewezi kuruka kwa sababu ya ukubwa wao. Hata hivyo wao wana uwezo wa kukimbia mwendo mrefu

bila kuchoka. Kinachowafanya walingane na ndege wengine ni kwamba wana umbo la ndege, wana miguu miwili, mabawa na

manyoya. Pia wanataga mayai kama ndege wengine.”

Maswali: Jibu maswali haya kwa ufasaha

192. Je kijiji alichoishi mzee Komba kinaitwaje?……………….................................................................………….……

193. Kibanda cha kwanza kilikuwa na ndege wawili aina ya ……………………………………………….......……..…….

194. Mgeni aliyemtembelea mzee Komba aliitwa nani? …………………………………………………………...……….....

195. Kwa nini mbuni hawezi kuruka? ………………………………………………………...…………………...…….……..

196. Pendekeza kichwa cha habari uliyosoma.................................................................................................................

......................................................................................................................................................................................

SEHEMU D: UTUNGAJI Umepewa sentensi nne zilizoandikwa bila kufuata mpangilio wenye mantiki. Zipange sentensi hizo kwa mapangilio

mzuri ili zilete maana kamili kwa kutumia herufi A, B, C, D.

197. Wanyama wadogo ni swala, digidigi, mbuzi mwitu,sungura poli na paa. [ ]

198. Katika hifadhi hii kuna wanyama wengi wakubwa na wadogo. [ ]

199. Kijiji cha Makuti kinapakana na hifadhi ya wanyamapori inayoitwa Mikumi. [ ]

200. Kuna tembo, twiga, Simba, chui na nyati. [ ]