Transcript
Page 1: Imaan Newspaper issue 33

www.islamicftz.org6 muharram 1437, jumatatu oktoba 19 - 25, 2015

huwatoa watu gizani

Head office, Lumumba Street, Opp: Viwanja vya Mnazi Mmoja, P. O Box 779 Dar es Salaam, TanzaniaTell: 255 22 2182482/ 255 222184419, Fax: 255 22 2181424, E-mail: [email protected]

TIF yaTumIa mIl. 700 kuchImba vIsIma bagamoyo -uk 5

Sheikh Alhad akosoa malumbano ajali ya Makka- uk 5

aref Nahdi

Sheikh Chembea

Sheikh Ibrahim

ayatollah ali khamenei

Viongozi TiF wawaasa waTanzania:

Marekani na Boko Haram

Busara itumike kulinda amani

ISSN 5618 - N0. 033 bEI: Sh800/- kSh80/- uSh1,200/-

Sheikh Ponda asubiriwa kwa hamu

Uk 7Uk 6

Page 2: Imaan Newspaper issue 33

Uboreshaji wa matangazo ya tV imaan

Kuanzia tarehe 10, Agost, 2015 kwa watumiaji wa receiver, TV Imaan itahama kutoka MPEG2 na kuwa MPEG4 (HD)Masafa ya satEllitE

Satellite: IntelSat 906 Frequency: 4066.25 Symbol rate: 1613.475 FEC: 2/3 DVBS2 Vile vile unaweza kuangalia TV Imaan kwa njia ya mtandao (online) kupitia

http:// www.ustream.tv/channel/radio-imaan-fm-2

HaBari / Tangazo2 Na. mjI aLFajr Dhuhur aSr maGharIb ISha 9 KIGOMA 11:28 6:45 09:57 12:52 1:59 10 MWANZA 11:18 6:34 09:48 12:39 1:45 11 KAGERA 11:25 6:43 09:55 12:49 1:56 12 TABORA 11:16 6:34 09:45 12:41 1:48 13 SHINYANGA 11:17 6:33 09:46 12:39 1:46 14 SINGIDA 11:09 6:27 09:38 12:35 1:41 15 IRINGA 11:04 6:25 09:32 12:35 1:43

Na. mjI aLFajr Dhuhur aSr maGharIb ISha 1 DAR ES SALAAM 10:49 6:08 09:18 12:17 1:23 2 ZANZIBAR 10:49 6:08 09:19 12:16 1:23 3 TANGA 10:55 6:12 09:24 12:19 1:26 4 MOROGORO 10:57 6:17 09:25 12:27 1:34 5 MTWARA 10:46 6:09 09:13 12:21 1:28 6 ARUSHA 11:05 6:21 09:35 12:27 1:33 7 DODOMA 11:03 6:21 09:32 12:29 1:36 8 MBEYA 11:13 6:33 09:40 12:43 1:50 oktoba 19 -25, 2015

Na Kassim Lyimomorogoro

TAASISI ya The Islamic Foundation (TIF) im-eziunganisha Shule ya Sekondari ya Imaan na

Shule ya Sekondari ya Forest Hill ili kukuza viwango vya taaluma katika shule hizo.

Taarifa hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa TIF, Aref Nahdi wakati akizungumza na wazazi wa wanafunzi wa Shule ya Imaan katika ukumbi wa Shule ya Forest Hill.

Nahdi alisema kuwa uamuzi huo umefikiwa baada ya Bodi ya Shule ya Forest Hill kuomba uon-gozi wa taasisi ya TIF kuingani-sha shule hiyo na Shule ya Imaan, ambazo zote zinamilikiwa na taa-sisi hiyo.

“Ni muda mrefu tumepokea maombi kutoka kwa Bodi ya Shule ya Forest Hill ya kuungani-sha shule hiyo na Shule ya Imaan, sasa leo tumewaita wazazi ili tu-waambie jambo hili ili nanyi mtoe maoni yenu”, alisema Nah-di.

Nahdi alisema kuwa watawa-punguzia wazazi wa Shule ya Im-aan gharama za vitu mbalimbali, ikiwemo ada pamoja na kutoa usafiri bure kwa wanafunzi wa bweni.

“Pia, tunampango wa kuten-geneza mabweni katika shule hii ya Forest kwani tuna eneo kubwa

ambalo litasaidia kujengwa kwa mabweni hayo,” Al isema Mwenyekiti huyo. Nae, Gavana wa Shule ya Imaan, Khamis Al-Jabr, amewataka wazazi kushiri-

kiana na walimu katika kusima mia maadili, kutokana na mu-ungano wa shule hizo, ili kuima-risha maadili ya Kiislamu katika shule hizo Hali kadhalika, wazazi

wa Shule ya Imaan wameponge-za hatua hiyo na kuongeza kuwa itasaidia kuboresha viwango vya ufaulu kwa wanafunzi wa shule hizo.

shule za sekondari Forest Hill, imaan kuungana

seLemaNi magaLi

Taasisi ya The Islamic Founda-tion (TIF) imempeleka mwa-nafunzi Juma Kapilimbi kati-ka chuo cha kuhifadhisha

Qur’an kiitwacho Tarteel Qur’an kili-chopo katika mji wa Azadvil mjini Jo-hansburg ikiwa ni jitihada za kumu-wezesha kijana huyo kuhifadhi kitabu kitukufu cha Allah. Akizungumza na gazeti Imaan, Katibu Mkuu wa taasisi hiyo, Sheikh Ally Ajirani alisema kijana huyo ni mwanafunzi ambaye alikuwa akilelewa katika kituo cha yatima kina-chofahamika kwa jina la Darul Imaan kilichopo Kola hili Mjini Morogoro .

Sheikh Ajirani ameongeza kuwa ki-jana huyo atakuwa masomoni katika kipindi cha miaka miwili ambapo baada ya hapo anatarajiwa kurudi nchini ili kuendelea na masomo yake ya elimu ya mazingira katika shule ya Forest Hill ambayo pia inamilikiwa na TIF.

Katika hatua nyingine, Sheikh Ajira-ni amebainisha kuwa licha ya kituo cha Darul Imaan, pia taasisi ya The Islamic Foundation inamiliki vituo vingine vi-wili ambavyo vimejikita katika kuwalea watoto yatima hapa nchini.

TiF yafadhili yatima masomo afrika ya Kusini

Shule za sekondari za Forest (pichani juu) na Imaan zilizopo mjini morogoro.

Page 3: Imaan Newspaper issue 33

www.islamicftz.org

6 MuHarraM 1437, juMaTaTu oKToBa 19 - 25, 2015

3MaKala

mussa imaNi sheha , ZaNZibar

Kila binadamu ana mchango katika jamii na hakuna awezae kuishi bila ya msaada

wa wengine. Tajiri humuhitaji maskini, mkulima humuhitaji mchuuzi, mfanya biashara nae huhitaji mazao ya mkulima. Abiria anahitaji chombo cha der-eva, na dereva hana kazi bila abiria. Mgonjwa na daktari, mwanafunzi na mwalimu; wote hawa hutegemeana.

Yaani mshonano huu wa aja-bu unaonesha kila mtu ni mtu-mishi wa mwingine na watu hutegemeana ndio maisha yakawa. Quran inasema: “Ni wake yeye (Allah) ufalme wa mbingu na ardhi na wala hakuji-fanyia mtoto na wala hana mshirika katika ufalme wake na ameumba kila kitu na kukiwekea vipimo vizuri” (25:2)

Kwa hivyo, ni vyema kwa kila mtu kumheshimu, kumjali na kumtumia mwingine kwa nafasi yake. Uislamu unasisitiza kum-tunza na kumtumia kila mtu ka-tika jamii kwa vile alivyo na kwa nafasi yake ili atoe mchango wake (nguvu, elimu, ufundi, fikra, ushauri, mali n.k.) alimradi maisha yarahisike na yawezekane ili kutimiza lengo la kuumbwa mwanadamu.

Maustaadh katika jamiiMingoni mwa watu muhimu

katika jamii ni wale tunaowaita ‘ma – ustaadh’. Ingawa maana halisi ya neno ustaadh kwa lugha ya kiarabu ni mhadhiri wa Chuo Kikuu chochote kile kiwe cha Ki-islamu au cha maarifa ya dunia, hapa Tanzania neno ustaadh lina maana nyingi, pana na zinazoto-fautiana. Katika jamii ya kitan-zania, ustaadh ni yule afundishae dini, Qur’an, kiarabu na masomo mengine katika madrasa, msikitini au shule za Kiislamu, Mwalimu wa shule za kawaida ni nadra kuitwa ustaadh. Pia, mha-dhiri wa dini ya Kiislamu iwe kwa sura ya mijadala au nyingin-ezo nae huitwa ustaadh.

Wakati mwingine Watanza-nia wametanua zaidi maana ya neno hilo kwa kumuita ustaadh hata mvaa kofia au kilemba, anayefuga ndevu au anayevaa kanzu fupi. Pia neno ustaadh limenasibishwa na mtu mstaara-bu, mkarimu, maridadi, mpole, apendae kusamehe anapoko-sewa, mwenye kuijali dini yake kwa kujitahidi kuyatekeleza kivi-tendo maagizo ya Mola wake na ambaye hujiepusha na makatazo yake.

Mchango waoMaustaadh wakiwa ni sehe-

mu ya jamii, wana umuhimu na mchango mkubwa katika mai-sha ya kila siku hasa katika jamii ambazo zina idadi kubwa ya Waislamu. Maustaadh ni tegem-eo kubwa la jamii katika kusima-

mia dini na imani. Hufundisha watu, wakubwa na wadogo, wake kwa waume, katika muda wote usiku na mchana katika misikiti, vyuo na viwanja vya mi-hadhara ili jamii ijue, ijali na ishikamane na mafunzo ya dini yao. Kwa maana nyingine, hu-fundisha jinsi ya kujenga uhu-siano na Muumba wao ili wajue na kufikia lengo la kuumbwa kwao.

Watu wengi katika jamii zetu, ikiwemo wakubwa, hawajui cho-chote juu ya dini. Baadhi hawajui sio tu namna ya utekelezaji wa majukumu yao bali hata maju-kumu yenyewe. Mama mmoja alipolinganiwa kuhusu swala al-isema: “Kwani mwanamke nae anapaswa kuswali? Mimi nilid-hani swala ni kwa ajili ya wa-naume tu!”

Wengine wamefanya mengi kumkasirisha Allah Taala katika maisha yao kiasi hata hawawezi kuyataja mbele za watu. Wana-tafuta njia ya kutubu wao lakini hawajui waanzie wapi. Na hapo huwatafuta maustaadh ambao huwapokea, huwaongoza jinsi ya kutubia na kuwafundisha ibada mpaka wanakuwa sawa sawa.

Maustaadh wamekuwa waki-wasaidia vijana wanaotaka ku-fanya mitihani ya taifa ya kidato pili, nne na cha sita katika somo la dini na kiarabu na vijana hao wamekuwa wakifaulu vizuri na kupata daraja zilizowawezesha kujiunga na masomo ya juu! Maustaadh wamekuwa wakiwa-saidia watahiniwa hao bila ku-choka na kwa moyo mkunjufu kwa njia zote za mawasiliano ikiwemo simu ili wafikie lengo.

Kiuzoefu na kiutamaduni, wazee wengi Waislamu huwape-leka watoto wao madrasa waki-

wa bado wadogo kupata mafunzo ya awali muhimu kwa ajili ya kuyakabili maisha yao hapa duniani na maustaadh hupokea watoto na vijana hao wa Kiis-lamu katika madrasa zao. Baadhi ya wa-toto hao huwa hawajaweza hata kutun-za usafi wa miili na nguo zao. Maus-taadh katika asasi zao hizo huwafundis-ha vijana Qur’an ambayo ni muongozo wa maisha kwa kuanza kuwatamkisha herufi kwa herufi, neno kwa neno mpa-ka wanaweza kusoma Qur’an.

Maustaadh pia hufundisha vijana misingi ya uhusiano na mola wao kama vile swala, swaumu, dua na nyiradi, pamoja na jinsi ya kuamiliana na vi-umbe wenzao kwa huruma,upendo, ukweli, uaminifu, moyo wa kujitolea, kuwaheshimu wakubwa, kuwafanyia wema wazazi, ushujaa kupitia maisha (sira) ya Mtume wao. Athari ya mafunzo hayo huendelea hadi ukubwani.

Kwa ujumla, madrasa ni vituo muhimu vya kuwafinyanga vijana, wak-iwa wadogo ili wawe wanajamii bora. Katika madrasa, utawaona watoto wa familia masikini na hata za waheshimi-wa viongozi na matajiri wakiamini kwamba watoto wao wasipopitia ma-drasa wakanyooshwa na maustaadh, watawasumbua sana hapo baadae. Wa-toto wengine wanakuwa wameshindika-na huko majumbani.

Hebu niambie msomaji, kwa maju-kumu kama haya unamzingatia us-taadh kama nani katika jamii?

Vile vile maustaadh hutatua mi-gogoro na ugomvi baina ya wanajamii, hasa wanandoa, baada ya kuombwa na wahusika au wazazi na mara nyingi Al-lah husaidia lengo kufikiwa. Jamii hu-wabebesha maustaadh jukumu hili zito kwa kuamini wana busara na wenye heshima kubwa mbele ya macho na nyoyo za wanajamii.

Katika mkasa uliomkumba ustaadh wangu Abuu Hussein, akiwa amelala nyumbani kwake majira ya saa saba na nusu, alishtuliwa na hodi mlangoni

kwake. Alipofungua, watu wawili, mke na mume aliowajua kama jirani zake walimkabili na kumuomba awapatan-ishe. Sheikh kwa busara na hekima, alit-uliza joto lao na kuwaomba warudi ny-umbani usiku ule wakapumzike na kes-ho yake atakwenda nyumbani kwao wakayazungumze.

Maustaadh hawapatanishi mi-gogoro ya wanandoa tu, bali hata ya wa-naushirika, majirani wenye ugomvi wa viwanja, wazazi dhidi ya watoto, masokoni na kwingineko. Utakuta watu jasho linawatoka, matusi na ngumi mkononi! Kisha ustaadh huitwa kusu-luhisha naye huitikia mwito wa Allah ulio katika kauli yake: “Hakuna kheri katika mengi ya mazungumzo yao ya siri ila kwa yule aamrishae kutoa sadaka au wema au kuwapatanisha watu” (4:114)

Maustaadh pia ni hitajio muhimu wakati wa kufungisha ndoa (akdi) ha-rusini. Licha ya maasi yanayofanywa katika harusi nyingi za Waislamu, bado jamii itamuita sheikh au ustaadh atoe khutba, aisimamie ndoa na kutoa mion-gozo ya kisharia. Ndio utaona ustaadh hupewa nafasi yake katika ufanikishaji wa mipango ya harusi. Utasikia wa-naulizana: “Lakini sheikh hatujampata jamani”, “Ustaadh Rama tunaye mbo-na?” Akichelewa kidogo, wanaume hu-washa prado zao kumfuata.

Umuhimu wa maustaadhi pia huonekana wakati wa kuwasindikiza wagonjwa saa ya kufa na katika taratibu (hududi) za mazishi. Kifo kinatisha. Jamaa wa mgonjwa huanza ku-muogopa jamaa yao wakati wa kuaga dunia. Utasikia wakisema: “Nendeni kamuiteni ustaadhi hapo jirani.” Na baada kufa ndio kabisa.

Maustaadhi hukunja kanzu zao ku-kabiliana na hali hiyo ngumu itakayom-kumba kila mtu na kuosha, kukafini, kusalia na hadi kuzika. Jamaa wa mare-hemu huwashukuru maustaadh kisha huwasahau mpaka litokezee tena. Shu-ghuli hizi ni nadra sana kuziona zikifan-ywa na wasomi wa fani za kisekula, vi-gogo au waheshimiwa. Wote hao huwa-tegea masheikh na maustaadh ambao hufanya bila khiana wakielewa kuwa huo ni wajibu wa kidini na kijamii.

Mazingatio muhimu Basi ona ndugu msomaji mchango

wa maustaadhi katika jamii kisha fikiria wasingekuwapo maisha yangalikuwaje! Hapa ndio tunapata ukweli wa maneno ya Taabii (mwanafunzi wa Maswahaba) Bwana Hassan Albaswry aliposema: “Lau si kuwepo wanazuoni (maus-taadh) watu wangaliishi kama wanya-ma”

Kwa kumalizia, ikiwa huu ndio mchango, nafasi na kazi za maustaadh, masheikh na walimu wa madrasa katika jamii zetu, hatuoni mantiki ya serikali wao kutolipwa mishahara. Ni kawaida kukuta maustaadh wakizifanya kazi hizi ngumu kwa mtindo wa kujitolea bila ya kutaraji kuunyoosha mkono mwisho wa mwezi. Maisha yao ni ya kupapatua tu. Lakini baya zaidi ni mamlaka na jamii kuwachukulia maustaadh kuwa wakorofi wanaohatarisha amani katika jamii na kuwatia misukosuko na ku-wadhulumu. Inafaa tujiulize kulikoni jamii inadharau maustaadh Maustaadh kiasi hiki! Kweli shukrani ya punda ni mateke.

KatiKa jamii ya

Kitanzania, ustaadh

ni yule afundishae dini, Qur’an,

Kiarabu na masomo

mengine KatiKa

madrasa, msiKitini au

shule za Kiislamu

Kwa nini jamii imewasahau maustaadh?

Page 4: Imaan Newspaper issue 33

www.islamicftz.org

6 MuHarraM 1437, juMaTaTu oKToBa 19 - 25, 2015

4

Hatua hii ilifuatia mapamba-no ya miaka mingi kati ya majeshi ya watawala wa Andalusia enzi hizo na yale ya Waislamu kutoka Magharibi na Kaskazini mwa Af-rika. Waislamu walivuka bahari kuiteka Andalusia ili kuzuia ma-shambulizi mapya dhidi yao.

Tariq bin Ziyad alikuwa ame-faulu kutia nanga mahali penye milima paitwapo Jabal Tariq (Mlima wa Twaariq) hivi leo kwa kumbukumbu ya jina lake. Ku-ficha historia hii iliyotukuka ya Waislamu, wazungu wakapaita Gilbrater. Huo ulikuwa mwaka 711 Miladia sawa na mwaka wa 92 Hijriya, enzi za utawala wa bani Umayya uliotawala dola kubwa ya Kiislamu kutokea Da-mascus (Dameshqi) nchini Syria. Kilikuwa ni kipindi cha dola ya Kiislamu kupanuka hadi China na India.

Mara tu baada ya majahazi yaliyowabeba Waislamu kutia nanga, walijikuta wakikabiliwa na jeshi kubwa la maadui zao. Tariq bin Ziyad akaona dalili za hofu toka kwa wapiganaji wake. Hapo ndipo Tariq bin Ziyad al-ipofikia maamuzi yake ya kucho-ma moto majahazi waliyotumia kuvuka bahari na kila kilichomo ndani yake.

Baada ya hapo, Tariq bin Ziyad akatoa hutba kali yenye mguso wa aina yake kwa kusema: “Ndu-gu zangu katika imani, tuko hapa kulieneza neno la Allah. Maadui wako mbele yenu na bahari nyu-ma yenu. Na hamna chakula wala maji ila kile mtakachokiteka kutoka kwa maadui zenu kwa panga zenu. Kwa hiyo hapa ni aidha ushindi au kufa shahidi”.

Allahu akbar! Hiki kilikuwa kilele cha kumtegemea Allah na azma ya kupigana kwa ajili yake kilichooneshwa na Tariq bin Ziy-ad. Kwa wapiganaji katika jeshi lake, kuitii amri ya kamanda wao kuyachoma moto majahazi yenye kila kitu chao kilikuwa kilele cha utii.

Tariq bin Ziyad alikuwa mtu wa kabila la Ulhasa katika waber-iberi (Berbers) aliyeingia katika Uislamu kutoka nchini Algeria. Awali alikuwa mtumwa na alipo-silimu akaachwa huru na bwana wake. Huyu ndiye mtu aliyeiteka Andalusia (Hispania) na kuupe-leka Uislamu Ulaya.

Watu kama Tariq bin Ziyad, waliokuwa watu duni kabla ya Uislamu lakini wakapata hadhi

kubwa baada ya kusilimu ni wen-gi. Miongoni mwao ni Salman Al -Farsi, Bilal bin Rabbah na Zayd bin Al-Haaritha (Allah awe radhi nao wote).

Jemadari wa majeshi ya Wais-lamu, Kaskazini mwa Afrika alikuwa Musa bin Nusair, mmoja wa majemadari mahiri wa Kiis-lamu. Tariq bin Ziyad alivuka ba-hari akiwa na wanajeshi 300 waarabu na waberiberi 10,000 waliosilimu.

Mfalme Roderic wa Andalu-sia aliwakabili akiwa na askari 100,000 dhidi ya Waislamu 10,300. Ni wazi lazima wal-iokuwa katika jeshi la Waislamu wawe na hofu ya kuteketezwa na jeshi kubwa lakini imani yao kwa Allah iliwapa utulivu.

Tariq bin Ziyad akamuomba Jemadari Musa bin Nusair nyongeza ya wapiganaji na akam-tumia wapiganaji 7,000 chini ya kamanda Taarif bin Maalik Na-qiy ambaye mji wa Tarifa nchini Hispania leo unabeba jina lake.

Kabla Taarif na jeshi lake hajafikia Waislamu, vita vikaanza na Waislamu wakawakabili maa-dui kishujaa. Majeshi mawili, lile la Waislamu na lile la makafiri yakakabiliana katika vita vya Guadalete ambapo Mfalme Ro-deric alishindwa na kuuawa mwezi 28 Ramadhan mwaka 92 Hijriya.

Jeshi la Wahispania li-liloshindwa likarejea nyuma kuelekea makao makuu ya dola mjini Toledo. Tariq bin Ziyad aka-ligawa jeshi lake vikosi vinne. Kikosi kimoja kikalekea mji wa Cordoba (Qurtuubah) na kuute-ka.

Kikosi cha pili kikaelekea mji wa Murcia na kuuteka na cha tatu kilielekea mji wa Zaragoza. Ka-manda Tariq bin Ziyad mwenyewe alielekea Toledo, wakazi wake wakajisalimisha pasina kupigana ikawa mwisho wa Mfalme Roderic.

Baada ya kupata habari za ushindi wa Waislamu, Jemadari Musa bin Nusair akafanya hara-ka kwenda kuongeza nguvu ili

maadui wasije kujikusanya akiwa na wapiganaji 18,000. Majeshi ya Waislamu kwa muda mfupi yakateka theluthi mbili ya ghuba ya Iberia.

Miji ya Zaragoza, Barcelona na sehemu ya Ureno ikaangukia mikononi mwa Waislamu. Mwa-ka uliofuata Waislamu wakavuka mto Pyrenees na kuingia mji wa Lyons nchini Ufaransa.

Huo ukawa mwanzo wa dola ya Bani Umayya ya Magharibi chini ya Khalifa Walid bin , dola iliyotawala Hispania (Andalusia) kwa miaka 750 tangu mwaka 711 hadi 1492 Waislamu walipotim-uliwa Hispania katika vita ya msalaba iliyoitwa, ‘November Crusade’.

Kasi ya majeshi ya Waislamu chini ya Tariq bin Ziyad kuteka ardhi ya Andalusia na Waislamu kufanikiwa kuikalia kwa miaka 750 inaingia katika historia ya vita duniani zama za kati.

Athari ya utawala wa kiislamu Hispania

Kabla ya Waislamu kuingia Hispania, watawala wake wa-likuwa watu kutoka nchi za Skandnavia waitwao Visigoths. Mnamo karne ya tano Miladiya, hawa Visigoths waliiteka His-pania na kuweka utawala wao mji mkuu ukiwa Toledo.

Kwa kuwa hawakuwa wastaarabu wajuzi wa kutawala, walikaribisha Kanisa la Roma mwaka 565 kuendesha mambo ya utawala. Kanisa likapata kibali cha kueneza Ukristo na kukusan-ya kodi.

Watu wakawa katika tabu kubwa, wakilipa kodi mara mbili moja kwa watawala na nyingine kwa kanisa. Kulikuwa na Waya-hudi wengi Hispania, kipindi cha watawala Waislamu Wayahudi waklipata mateso makubwa sana. Kwanza walinyimwa haki ya kumiliki ardhi na pili walika-tazwa kuabudu kwa dini yao ya kiyahudi. Walipojaribu kupinga hali hiyo, kanisa likawapa mateso zaidi.

Mwaka 707 Mfalme Vietza al-

ipoonesha kuwahurumia Waya-hudi, viongozi wa kanisa wal-impindua na kumweka madar-akani Mfalme Rodriguez. Waya-hudi wanaume wakatiwa utumwani na wanawake wao ku-fanywa masuaria majumbani.

Utawala wa haki wa Waislamu

Mara baada ya Waislamu kuiteka Andalusia (Hispania), haki ikatawala. Hakuna mali ya wenyeji iliyotaifishwa. Waislamu waliwatendea watu wote kwa haki, wakiwemo Wayahudi, isipokuwa waliweka mfumo wa kodi wenye uadilifu ambapo wal-iolipa ni wenye uwezo tu.

Wakiongozwa na Qur’an na Sunna ya Mtume (Rehma na amani iwe juu yake), Waislamu waliingiza ustaarabu wa Kiisla-mu Ulaya na popote majeshi ya Waislamu yalipokwenda yal-ipokelewa kwa mikono miwili na wakazi wa maeneo hayo.

Utawala wa Waislamu uka-fanya Hispania kuwa nchi ya kistaarabu iliyojaa haki, uadilifu na elimu. Mtumwa yeyote aliye-ingia katika Uislamu aliachwa huru mara moja. Idadi kubwa ya wahispani awakaingia katika dini ya Uislamu. Watu wa dini mbali mbali wakiwemo Waislamu na Wayahudi waliruhusiwa uhuru wa kuabudu kwa mujibu wa dini zao. Siyo hivyo tu kila mwenye elimu, ujuzi na maarifa aliruhusi-wa kupata ajira katika kuhudu-mia jamii.

Vituo na vyuo vya elimu vikafunguliwa huko Toledo na Cordoba na yeyote aliruhusiwa kuchukua elimu bure. Magwiji wa elimu za hisabati, jiografia, kemia, baiolojia na unajimu wakazalishwa kutoka vyuo vikuu huko Toledo na Cordoba.

Chini ya Waislamu, Hispania ikawa alama ya sayansi, utama-duni na ustaarabu katikati ya Ulaya iliyokuwa katika zama zi-julikanazo kama zama za giza. Mirefeji ya maji ilichimbwa, ma-zao mapya yakaingizwa na kuin-ua uchumi wa Hispania.

Miji ikakuwa na idadi ya wakazi kuongezeka. Mji wa Cor-doba ukawa kitovu cha elimu Ulaya nzima na hadi kufikia karne ya 10 Miladiya, mji huo ulikuwa na wakazi wapatao Mil-ioni moja yaani Manispaa.

Mwanahistoria mmoja Mkristo anaandika: “Waislamu walianzisha ufalme ule wa Cor-doba uliokuwa fahari ya enzi za zama za kati, zama ambazo wakati Ulaya nzima ilikuwa ime-zama katika ujinga na vurugu, mji huo ulikuwa nuru ya elimu na ustaarabu ikiuangazia ulimwen-gu wa magharibi”.

Khalifa Walid bin bin Mar-waan aliwaalika Jemadari Musa bin Nusair na Tariq bin Ziyad mjini Damascus. Lakini walipofi-ka walimkuta akiwa mahututi. Aliwashukuru na kuwapa sehe-mu ya mali waliyoileta kutoka ka-tika mapato waliyokusanya.

Khalifa Walid alipofariki, Suleiman bin Abdulmalik akam-fuatia katika utawala. Tariq bin Ziyad alifariki mwaka 720 Mi-ladia. Historia ya Uislamu na ul-imwengu haiwezi kamwe kum-sahau Tariq bin Ziyad.

KuToKa MisiKiTini

Na mwaNdishi wetu

Mlinganiaji maarufu nchini am-baye pia ni imamu wa msikiti wa Vetenary uliopo Temeke jijini Dar es salaam Sheikh

Nurdin Kishki amewaasa wag-ombea wa nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi

mkuu wa mwaka huu kutam-bua dhima waliyonao endapo

watachaguliwa kuwaongoza watu.

Sheikh Kishki ameyase-ma hayo wakati wa khutba ya ibada ya swala ya ijumaa iliyoswaliwa katika msikiti huo wiki iliyopita

na kuongeza kuwa watu wengi hupenda uon-gozi huku wakijifa-harisha kwa vyeo na

kusahau kuwa uongozi ni dhima inayoweza ku-

pelekea majuto ya hali ya juu mbele ya Allah Ta’ala siku ya kiyama.

“Kama tungelijua dhima ya mtu kiongozi ni ngumu kiasi gani siku ya kiyama sote tungekimbia uongozi na madaraka kama vile Punda anavyomkimbia

Simba”alidokeza Sheikh Kishki huku akiwataka waislamu wazidi kumuomba Allah kuipitisha sala-ma siku ya uchaguzi na kuepusha shari zinazoweza kujitokeza.

Kuhusiana na zoezi la uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa juma hili Sheikh Kishki amesema hivi sasa watan-zania wapo katika kipindi kigumu kutokana na mawazo,fikra na hamasa zao kuzielekeza katika uchaguzi jambo linalopelekea watu kusahau hata kutekeleza ibada muhimu za dini.

Na hassaN NiNga

Waislamu nchini wametakiwa kua-dhimisha mwaka mpya wa kiislamu kwa kuamrisha familia zao kutekeleza mambo ya kheri ikiwemo swala tano kama sehe-mu ya jitihada ya dini wakati wanapoingia katika mwaka mpya wa 1437 Hijriya.

Nasaha hizo zimetolewa na Sheikh Issa Othman Issa wakati wa ibada ya swala ya ijumaa iliyoswaliwa katika msikiti wa Ma’amuur uliopo Upanga jijini Dar es salaam na kuwataka waislamu kujenga mahusiano mema na familia na kwamba kufanya hivyo ndio kutekeleza mafunzo ya mtume rehema na amani ya Allah ziwe juu yake.

Sheikh Othman alinukuliwa akisema:“Tunapoingia kwenye mwaka mpya wa kiislamu,lazima tufahamu mahu-siano yetu na watoto wetu yakoje na je, mwaka uliopita tulipata nafasi ya kukaa nao na kuwahimiza kufanya ibada au tulikaa nao na kuwahimiza kufanya bidii kwenye masomo tu”.

Aidha Sheikh Othman aliwataka wazazi kutambua kuwa,ni jukumu lao kuwahimi-za watoto na familia kwa ujumla kutekele-za ibada mbalimbali na kwamba kama waliteleza katika kuyaamrisha hayo basi mwaka mpya wa kiislamu uwe ni fursa ya kubadilisha mwenendo wa familia zao.

Uongozi ni majuto siku ya kiyama - Sheikh kishki

Waislamu wahimizwa kuamrisha familia zao kufanya ibada

Chini ya Waislamu, hispania iKaWa alama ya sayansi, utamaduni

na ustaarabu KatiKati ya ulaya iliyoKuWa KatiKa zama

zijuliKanazo Kama zama za giza.

Tariq bin ziyad“Choma moto majahazi”. Ilikuwa ni amri kwa Waislamu kuto-ka kwa kamanda wa majeshi yaliyovuka bahari ya Meditera-nia kwa lengo la kuiteka Hispania au Andalusia kama inavyo-

julikana katika historia ya Uislamu.

sheiKh mohammad issa

TujiKuMBusHe

Page 5: Imaan Newspaper issue 33

www.islamicftz.org

6 MuHarraM 1437, juMaTaTu oKToBa 19 - 25, 2015

5MaKala / Tangazo

“Afya”is natural source of sweet drinking water from under-

ground stream which is blended

with essential minerals to sup-port and aid per-fect metabolism.

WATERCOM LIMITEDP.o. Box 20409, Plot N.4005, Kisarawe11 area

Temeke,Daresalaam, Tanzaniawww.watercomtz.com, E-mail:[email protected]

Na athumaNi sho-mari, bagamoyo

Taasisi ya The Is-lamic Foundation (TIF) ya mjini Mo-rogoro ambayo pia

ni wamiliki wa redio, TV na gazeti Imaan, imetumia zai-di ya milioni 700 kuchimba visima wilayani Bagamoyo.

Hayo yalibainishwa hivi karibuni mjini Bagamoyo na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Sheikh Ibrahim Twaha wakati alipokuwa kwenye ziara ya kutembelea miradi inayoendeshwa na taasisi hiyo wilayani humo.

Sheikh Ibrahim alisema kuwa katika kipindi cha mi-aka minane taasisi hiyo ime-fanikiwa kuchimba visima zaidi ya 170 wilayani Baga-moyo vyenye thamani ya za-idi ya milioni 700.

Aidha, alisema kuwa, uchimbaji wa visima hivyo katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Bagamoyo ume-saidia kwa kiasi kikubwa kuondoa tatizo la maji wilay-ani humo.

Alizitaja baadhi ya sehe-mu zilizochimbwa visima katika wilaya hiyo kuwa ni pamoja na Dunda, Mago-meni, Kingani, Kiromo, Zinga Mlingotini na Kerege. Aliongeza kuwa huduma hiyo ya maji imelenga katika maeneo yenye mchangan-yiko wa watu ambayo yana shida ya maji ambapo kwa kuzingatia hilo visima hivyo

vimechimbwa katika mae-neo ya soko, shuleni, kwenye zahanati, misikitini na mae-neo ya wazi ili kila mwa-nanchi aweze kufaidika na huduma hiyo.

Hata hivyo, Mkurugenzi huyo wa TIF alisema kuwa bado kuna maombi mengi kutoka kwa jamii ya kuch-imbiwa visima yaliyowasil-ishwa na wananchi wa Bag-amoyo, na kwamba uchim-baji huo wa visima unaende-lea wilayani humo ili kuwafi-kia wananchi wote wenye shida ya maji katika maeneo yao.

Akizungumzia umuhimu wa maji katika jamii, Sheikh Twaha alisema Mwenyezi

Mungu ndani ya Qur ani tukufu amesema amejaalia katika kila kitu uhai kutoka-na na maji. Hivyo basi, TIF kama taasisi ya kiislamu ina-zingatia kauli hiyo ya Allah na kutoa umuhimu wa pe-kee katika huduma hiyo ya maji. Kwa upande wao, baa-dhi ya wananchi wa wilaya Bagamoyo waliofaidika na msaada wa TIF wamesema kuwa wanaishukuru taasisi ya TIF kwa kuwachimbia vi-sima katika mitaa mbali mbali ya Bagamoyo na ku-waondolea adha ya ukosefu au uhaba wa maji.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Majid Hemed Mwanga, ameipongeza Is-lamic Foundation kwa uch-imbaji wa visima wilayani humo na kuongeza kuwa serikali inathamini mchango wa taasisi hiyo katika kutoa huduma za kijamii kama hiyo ya visima. Hemed al-

iongeza kuwa serikali inath-amini mchango huo na wa-nanchi pia wanapaswa

kuthamini mchango huo mkubwa uliotolewa na TIF na kuongeza kuwa jukumu la ku-

vitunza visima hivyo ni la wa-nanchi ili huduma hiyo iwe endelevu.

uChimbaji Wa visima

hivyo KatiKa

maeneo mbalimbali

ya Wilaya ya bagamoyo umesaidia KWa Kiasi KiKubWa Kuondoa

tatizo la maji

Wilayani humo

TiF yatumia Mil. 700 kuchimba visima Bagamoyo

seLemaNi magaLi

Imeelezwa kuwa hakuna muda wa kuendeleza malumbano juu ya vifo vya mahujaji, badala

yake Waislamu wanapaswa kujikita katika maombi ili Mwenyezi Mungu awalipe pepo mahujaji wote waliofa-riki katika tukio la mkanya-gano huko Jamaarat.

Wito huo umetolewa na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Musa Salum ambapo alisema waliofariki katika ardhi ya Makka waki-wa katika Ibada, Allah huwa-hesabu ni waja wa peponi kutokana na ardhi hiyo ku-barikiwa kwa kuzikwa man-

abii na mitume.Bila shaka wito wa Alhad

unawalenga Mashia ambao tangu ajali ilipotokea wame-kuwa wakiuandama Utawa-la wa Kisunni wa Ufalme wa Saudia kwa tuhuma mbalim-bali ambazo hazina msigi na zimejaa uongo. “Kufa Makka na Madina si sawa na kufa Manzese na Tandale, watu wanapaswa kuomba kufa katika ardhi ile kwa sababu ni ardhi tukufu iliyobeba watu maarufu hususan man-abii na maswahaba,” Alhad alisema.

Aidha, akizungumzia ma-hujaji ambao hawajulikani walipo, Sheikh Alhad alise-ma ana wasiwasi kuwa huen-

da baadhi yao ni katika wal-iozikwa mapema kabla ha-wajatambuliwa.

“Ni wakati mgumu kwa wanandugu, lakini ni-waombe Waislamu ku-waombea ndugu zetu wawe ni watu waliokufa mashahidi na Allah awawezeshe kuwa watu wa peponi” Alisema Sheikh Alhad.

Aidha kuhusu suala la vi-ongozi wa dini moja kutoa lugha za kejeli na matusi dhi-di ya viongozi wa dini ny-ingine kutokana na tofauti ya mitazamo ya kisiasa amese-ma suala hilo linapaswa kukemewa kwa dhati kwani litasababisha uvunjifu wa amani.

sheikh alhad akosoa malumbano ajali ya Makka

Mkuu wa wilaya aipongeza

mkurugenzi mtendaji wa tIF sheikh Ibrahim twaha akionja maji kutoka katika kisima kilichochimbwa kwenye makazi ya polisi bagamoyo.

Page 6: Imaan Newspaper issue 33

Jumatano iliyopita ilikuwa ni siku muhimu kwa Watanzania kwa kuwa ni siku ambayo taifa lilikum-buka kifo cha muasisi wa taifa hili,

hayati Mwalimu Julius Kambarage Ny-erere, ambaye pia baadhi ya watu hupenda kumuita baba wa taifa.

Wengi wameazimisha siku hiyo kwa ku-kumbuka harakati ambazo Nyerere aliz-ifanya, akishirikiana na wenzake na am-bazo zilileta ukombozi kutoka katika makucha ya wakoloni. Na pia anakum-bukwa kwa misingi aliyoijenga ambayo im-elihakikishia taifa la Tanzania amani ya muda mrefu.

Ni kupitia jitihada zake, Tanzania imet-ambulika duniani kote kama ni kisiwa cha amani, utulivu na upendo. Na watu wake wanasifika mpaka leo kwa kuwa wakarimu jambo ambalo hakika tunajivunia kwa sifa hizo mbele ya nchi za kimataifa.

Hata hivyo, kumbukumbu ya Nyerere pia inakumbusha jamii ya Waislamu kuhu-su changamoto ilizopitia tangu kupatikana kwa uhuru mwaka 1961. Sehemu kubwa ya changamoto, ambazo zimeleta udhalili kwa jamii yetu, zinahusu mahusiano yetu na Serikali ambapo Serikali imekuwa ikidhibi-ti maendeleo ya Waislamu kwa kuwaundia taasisi na kuwateulia viongozi wa kuwaon-goza.

Jumatano hiyo hiyo, ilikuwa ni siku muhimu kwa Waislamu ambao nao wal-isherehekea mwaka mpya wa Kiislamu wa 1437, Hijria yaani tangu Mtume Muham-mad (Rehma na amani ziwe juu yake) al-ipohama kutoka Makka kwenda Madina.

Lilikuwa ni wazo la Swahaba Umar, Khalifa wa Pili wa Uislamu (Mungu amu-wie radhi) kuanza kuhesabu miaka hii ya Kiislamu hususan baada ya kuona kuwa kwa mara ya kwanza wanahamia katika mji wa Madina ambao wataanza kutumia shar-ia ya Kiislamu. Kwa maana nyingine, ni wakati ambao dola ya Kiislamu ilianza kusimama na waumini wake walipata uhu-ru wa kujitegemea na hivyo kuanza kufanya ibada zao kwa mujibu wa kitabu kitukufu cha Uislamu.

Kuingia kwa mwaka huo mpya wa Kiis-lamu, kuna mambo mengi sana ya mazin-gatio ambayo waumini wanapaswa kuyapi-ma na kuchukua hatua ili kuendelea kufan-ya vema katika kuimarisha dini ya Kiislamu na pia kujiwekea mazingira mazuri ya kuwa na mwisho mwema mara tutakapoiacha

dunia. Nilipata bahati ya kuzungumza na Maalim Kassim Abdalah wa Al-Madrasat Nuur ya Kigogo Luhanga kuhusu mafun-zo, mazingatio na nini kifanyike ili Waisla-mu kuendelea kufanya mema katika kipin-d i h i k i a m b a c h o wamepewa fursa ny-ingine na mola wao muumba

Maalim Abdallah al-isema kuna changamo-to nyingi ambazo Wais-lamu tunapaswa kuzi-fanyia kazi, moja ikiwa ni tatizo la maradhi ya roho. Kutokana na tati-zo hili, Waislamu kwa Waislamu wamefikia hatua ya kutoleana maneno yasiyofaa kisa ni kupishana kwa mita-zamo.

Maalim Abdallah anatoa mfano wa wal-inganiaji wa dini ambao mara nyingi wamekuwa wakiacha kazi yao na badala yake kuzama ka-tika kutangaza misi-mamo yao ya kimadh-habi, jambo ambalo ni lina taathira mbaya kwa mustakabali wa Uisla-mu. Maalim Abdallah alisema kwa miaka mingi masheikh, wanazuoni na viongozi wengine wa dini ambao wamekuwa na msimamo tofauti wa kimadhahabi wame-kuwa vitovu vya kuzalisha uhasama mion-

goni mwa Waislamu bila ya sababu za msingi.

Katika hatua nyingine, Maalim Abdal-lah amezielezea mbinu ambazo Mtume Muhammad (Rehma na amani ziwe juu

yake) amekuwa akiz-itumia katika kulin-gania watu kuwa si za kawaida na zimejaa hekima na uvumilivu jambo lilomfanya ku-fanikiwa kwa kiwan-go cha hali ya juu ku-usambaza Uislamu duniani kote.

Aidha, Maalim Abdallah alishauri jamii ya Kiislamu kuanza kuingiza mtaala wa ulinganiaji kat ika madrasa , markazi na vyuo v inavyofundisha elimu ya dini ili wal-inganiaji wa leo waweze kufanya kazi zao kwa weledi. “Kulingania kuna hatua zake, ni somo maalum kabisa hu-wezi leo hii ukamlin-gania mtu ambaye hajui kabisa hata Tawhid akawa sawa na yule anayejua japo

kidogo hiyo Tawhid,” alisema Abdallah.Naye kwa upande wake, Msemaji wa Ju-

muiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Raja-bu Katimba aliwataka Waislamu kutumia

siku hizi za mwanzo za mwanzo wa mwaka kwa kujitafakari katika miezi 12 iliyopita walifanya nini, wamekosea wapi na wafan-ye nini sasa wakati wakiuanza mwaka huo mpya.

“Ni wakati muafaka kwa Waislamu ku-jiuliza kwa nini wameweza kupata fursa ya kuanza mwaka mpya wa Kiislamu huku wengine wakishindwa, wamefanya yapi ya-nayompendeza Mungu na kujipanga kwa kufanya mema zaidi kwa faida yao, ”alisema Katimba

Aidha Katimba alitumia fusa hiyo ku-waonya vijana ambao wanapandikizwa itikadi ambayo sio sahihi watumie muda wao kusoma vizuri Qur’an na sunna ili ku-weza kubaini ukweli. Pia, alikariri mwito wa Maalim Abdallah wa kuzingatia na ku-jiuliza mbinu sahihi ambazo zimetumika kusambaza dini kwani hivi sasa kumezuka njia potofu za kufikisha ujumbe kwa watu.

Aliongeza kusema walinganiaji wengi wa leo wana mapungufu mengi ikiwemo kutokuwa na uvumilivu pamoja na kukosa maneno ya hekima katika kufikisha ma-waidha kwa watu wanaowalingania.

Katimba alisema alisema lazima kuwe na mabadiliko kuanzia ngazi ya walingani-aji, masheikh na wanazuoni ili utaratibu wa awali wa kulingania ambao ulikuwa ukitu-miwa na Mtume uweze kutamalaki.

Niungane na masheikh kuwatakia Wais-lamu wote tafakuli iliyo njema juu ya mam-bo ambayo tumeyafanya mwaka uliopita na tujikite sasa kuendeleza mema kwa ku-fanya ibada na kusaidia jamii kwa ujumla ikiwemo wajane, yatima, na wagonjwa ili Allah awe mwenye kutuhurumia wakati tu-takaporejea kwake.

Tofauti ya madhehebu zisiwe kikwazo cha ulinganiaji

HuTolewa na KucHapisHwaThe islamic Foundation, p.o. Box 6011 Morogoro, Tanzania, e-mail: [email protected]

MHariri MTendaji: 0715 559 944, MHariri: 0786 779 669, aFisa MasoKo: 0785 500 502ToVuTi: www.islamicftz.org

6 MuHarraM 1437, juMaTaTu oKToBa 19 - 25, 2015

TaHariri / nasaHa6

Hijra ya Mtume itufunze uvumilivu na subra katika dini

seleMani Magali

nasaHa za wiKi

Tumeingia mwaka wa 1437 tangu tukio la Mtume (Rehma na amani ya Al-lah ziwe juu yake) pamoja

na maswahaba (Allah awe radhi nae) kuhama kutoka mji wa Makka na kuhamia Madina kwa sababu za madhila waliokuwa wakifanyiwa na watu wa kabila la Maqureysh.

Msingi mkuu wa tukio la ‘Hijra’ ni Waislamu kunyimwa fursa ya uhuru wa kuabudu hali ambayo kwa uhakika wake bado haijafutika kabisa katika uso wa dunia. Hata hivyo, yapo mambo ya msingi ya kujifunza kupitia tukio la Hijra. Miongoni mwa hayo ni Waislamu kujipamba na sifa ya ‘subra’ na ‘uvu-milivu’.

Tunasema hayo kwa sababu kabla ya Hijra (Maisha ya Mtume alipokuwa Makka), Mtume (Reh-

ma na amani ya Allah ziwe juu yake) aliweza kuwa na subira ndani ya nafsi yake licha ya madhila aliy-okuwa akifanyiwa kabla ya kupewa amri ya kuhama na Mola wake hivyo. Katika hili, kuna mazingatio makubwa ndani yake.

Ili kujenga mustakbali mwema wa maendeleo ya Uislamu na Wais-lamu, dhana ya umoja ambayo ndio msingi mkuu wa mafanikio ya kila jambo haiwezi kuepukika kwani hata ukiona jamii fulani imesam-baratika, sababu kubwa huwa ni watu wake kukosa subira na uvu-milivu.

Ukosefu wa subira na uvumilivu hudhoofisha juhudi za maendeleo ya dini na pia huchochea chuki na uadui hivyo tutumie mafundisho ya Hijra kujenga tabia ya kuvumiliana na kusubiri kwani hiyo ndio sababu

ya kupata radhi na baraka za Allah Taala.

Hii ni kwa sababu nafasi ya subi-ra katika kufikia utukufu ni kubwa na kwamba, pasina mtu kujipamba kwa sifa hii muhimu na yenye tha-mani ni vigumu mtu huyo kujiku-rubisha kwa Mwenyezi Mungu kama inavyobainisha Qur’an Tuku-fu: “Lakini hawapewi wema huu ila wanao subiri, wala hawapewi ila wenye bahati kubwa (ya imani na uchamungu) ”(41:35).

Tukio la Hijra ya Mtume ni na-fasi muhimu katika kutayarisha mazingira ya uvumilivu na kusubiri hatimae kuziunganisha nyoyo za Waislamu katika wakati mmoja na kuelekea kwenye lengo moja kama Allah Taala anavyobainisha ndani ya Qur’an: “Na shikamaneni kwa kamba ya Mwenyezi Mungu nyote

pamoja, wala msifarikiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu: vile mlivyo kuwa nyinyi kwa nyinyi maadui naye akaziunganisha nyoyo zenu; kwa neema yake mkawa ndugu..” (3:103).

Moja ya masharti manne ya kusimamisha Uislamu ni kuhusi-ana kufanya subira. Allah anasema katika Qur’an: “Naapa kwa Zama! Hakika binaadamu bila ya shaka yumo katika hasara, Ila wale walio-amini, na wakatenda mema, na wakausiana kwa haki, na wakahu-siana kusubiri” (103:1-3).

Tofauti za kimtazamo ni jambo la asili, lakini suluhu yake ni watu kujipamba na sifa ya subra na uvu-milivu na hili litapelekea hata pindi zitakapojitokeza tofauti basi wa-takaa chini na kunasihiana kama

inavyobainishwa hadithi iliy-opokewa na Swahaba Tamim bin Aus Addaariy (Allah awe radhi nae).

Mtume (Rehma na amani ya Al-lah ziwe juu yake) amesema: “Dini ni nasiha. Tukauliza: Kwa nani? Akasema kwa Allah, Kitabu chake, na Mtume wake, na kwa viongozi wa Waislamu na watu wa kawaida” (Muslim).

Wakati tukiadhimisha mwaka mpya wa Kiislamu wa 1437, ni wakati pia wa Waislamu kuamka kutoka usingizini na kutumia fursa hii kama mwanzo mpya wa kujie-pusha na chuki na uadui na kuji-pamaba na sifa ya subira na uvu-milivu na hayo ndio maadhimisho yaliyo bora ya Hijra ya Mtume (Re-hma na amani ya Allah ziwe juu yake).

ni Kupitia jitihada zaKe,

tanzania imetambuliKa duniani Kote

Kama ni KisiWa Cha amani, utulivu na upendo. na Watu WaKe WanasifiKa

mpaKa leo KWa KuWa WaKarimu

jambo ambalo haKiKa

tunajivunia KWa sifa hizo

mbele ya nChi za Kimataifa

Page 7: Imaan Newspaper issue 33

www.islamicftz.org

6 MuHarraM 1437, juMaTaTu oKToBa 19 - 25, 2015

7HaBari

Na Kassim Lyimo

Wakati wiki moja tu iki-wa imebakia kabla Watanzania hawa-j a c h a g u a r a i s ,

wabunge na madiwani, wawakili-shi na masheka, viongozi wa taasisi ya The Islamic Foundation (TIF) wamewanasihi wadau wote katika uchaguzi huu kutumia busara kwa ajili ya kudumisha amani iliyopo hapa nchini.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Aref Nahdi wakati akizungumza katika kipindi maalumu kuhusu amani kilichorushwa hewani na Radio na Tv Imaan, siku ya Alhamisi.

Nahdi alisema kuwa baadhi ya viongozi na watendaji wa serikali, viongozi wa vyama vya siasa na hata wa dini wamekuwa wakitoa kauli zinazoweza kusababisha au kuchangia uvunjifu wa amani.

“Watanzania tunalilia amani, bila amani watoto hawawezi kwen-da shule, kuna baadhi ya nchi wato-to wanahangaika hawasomi, ki-namama wananyanyasika, kutoka-na na nchi zao kutokuwa na amani”, alisema Nahdi.

“Hivi sasa katika nchi yetu kuna viashiria vimeanza kuibuka vya uvunjifu wa amani, visipozun-gumzwa basi baada ya muda mfupi hali ya amani itakuwa ni mbaya na hatutampata mtu hata mmoja wa kumlaumu”, alisema Mwenyekiti huyo wa TIF.

Katika hatua nyingine, Nahdi amewataka wanasiasa kuangalia maeneo wanayoyazungumza kati-ka majukwaa yao ya kisiasa, na kuacha maneno ya kuchafua na kudharauliana miongoni mwao, kwani hali ikichwa itachangia ama-ni kupotea.

Kadhalika, alisema kuwa Wais-lamu wanajukumu kubwa la kulin-da amani, kwa sababu mafundisho ya dini ya Kiislamu yamehimiza amani kwa wafuasi wake na watu wote duniani.

“Waislamu na wasiokuwa Wais-

lamu tuishi kwa amani, viashiria vya uvunjifu wa amani vimeanza kuonekana, sisi wote ni Watanzania haina haja ya kufikia wakati tu-kaanza kugombana kutokana na sababu ndogo ndogo ambazo zinaweza kutatuliwa,” alisema Nah-di.

Akizungumzia uchaguzi, Arif Nahdi aliwataka Waislam wote ku-shiriki uchaguzi mkuu na kwa am-

ani kwa kwenda kupiga kura kisha kurudi majumbani kwani hawawa-jibiki kulinda kura bali hiyo ni kazi ya mawakala wa vyama vya siasa.

Nahdi alisema kukaa vituoni kunaweza kusababisha uvunjifu wa amani hali ya kuwa Uislam unawa-taka Waislam kuwa walinzi wa am-ani badala ya kuleta visababishi vya uvunjifu wa amani.

Kwa upande wake, Mkurugenzi

Mtendaji wa Taasisi ya The Islamic Foundation, Sheikh Ibrahim Twa-ha ambaye aliambatana na Mwenyekiti Nahdi katika kipindi hicho maalum, aliwataka Viongozi wa Serikali kutekeleza ahadi zao kwa wananchi, kwani kutoa ahadi ambazo huwezi kuzitekeleza hu-sababisha maneno miongoni mwa jamii.

Aidha, Sheikh Twaha alisema

kuwa ahadi hizo, ambazo haz-itekelezeki huchangia uvunjifu wa amani, na pia aliwataka Waislamu kuwa mbele katika kusimamia am-ani

“Uislamu ni amani ili watu waabudu Allahni vizuri suala la amani lizingatiwe katika jamii”, Sheikh Twaha alisema. Alisema ni kwa kutambua umuhimu wa ama-ni ndio maana taasisi ya TIF ina malengo ya kuwajenga watu kiro-ho.

“Kwa hivyo, kuzungumza amani ni jambo la lazima kwetu kwa saba-bu Watanzania wengi wanaiamni Taasisi kwa kuwapa mazuri ya Waislamu”, alisema Sheikh Twaha.

“Ni kheri tufe katika kufanya mambo ya heri wala tusipoteze maisha yetu katika vurugu za kisia-sa kwani lengo la kuletwa duniani ni kumuabudu Allah Taala,” alise-ma Mkurugenzi huyo wa Taasisi ya TIF.

Hali kadhalika, Sheikh Twaha alisema kuwa ni aibu kubwa kwa Muislamu kuhusika katika uvunji-fu wa amani kwani dini ya Kiislamu ni dini ya amani na wala sio dini ya vuruga na kusababisha machafuko katika jamii.

Viongozi TiF wawaasa watanzaniamwenyekiti wa the Islamic Foundation, aref Nahdi.

KatiKa hatua nyingine, nahdi

ameWataKa Wanasiasa Kuangalia

maeneo Wanayo yazungumza

KatiKa majuKWaa yao ya Kisiasa, na KuaCha maneno ya KuChafua na Kudharauliana

miongoni mWao, KWani hali iKiChWa

itaChangia amani Kupotea.

seLemaNi magaLi

Mamia ya wakazi wa mji wa Morogoro wa-nategemewa kufurika katika mahakama ya

Hakimu Mkazi mkoani humo kusikiliza hukumu ya kesi inayom-kabili Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Issa Ponda inayotarajiwa kutolewa leo.

Kwa mujibu wa Wakili wa Sheikh Ponda Juma Nassor, huku-mu ya kesi hiyo inatolewa kufuatia mashahidi wa pande zote mbili ku-maliza kutoa ushahidi wao na pia upande wa mashitaka kuwasilisha hoja zao za majumuisho ya kesi hiyo kwa maandishi.

Wakili Nassor alisema umefika wakati mahakama kutimiza wajibu wake katika kutenda haki na kwamba ana matumaini makubwa kuwa mteja wake ataachiwa kwani hata muda wa miaka miwili am-

bayo mteja wake ameutumikia aki-wa mahabusu inatosha kuwa hu-kumu.

Katika kesi hiyo, Sheikh Ponda anakabiliwa na mashtaka mawili, kutoa matamko ya kuumiza hisia za kidini na lile la kukusanyika kinyume cha sheria katika eneo la msikiti wa ‘Dini Moja, Mungu Mmoja’ ulioko eneo la Uwanja wa Ndege, Morogoro.

Awali, Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Morogoro ilipanga Septemba 4 mwaka huu kuwa siku ya hukumu ya kesi hiyo, lakini ili-pofika tarehe hiyo hakimu alilaz-imika kuiahirisha kufuatia mawak-ili wa serikali kushindwa kuwasili-sha hoja za majumuisho, kama ma-hakama ilivyoagiza, jambo ambalo

Wakili Nassoro alililalamikia. Wakili Nassoro alisema: “Agosti

7 mwaka huu mimi na mwenzangu Iddi Mselem tulimaliza kutoa usha-hidi kisha mahakama iliagiza pande zote mbili kuwasilisha majumuisho ya kesi na mwisho ifikapo Agosti 28. Sisi tuliwasilisha ila upande wa mashitaka haukufanya hivyo na badala yake walileta majumuisho yao nje ya muda Septemba 17, mwa-ka huu kinyume na amri ya ma-hakama.”

“Tulitarajia kesi hii ingefika tamati yake Septemba 4 mwaka huu lakini zoezi hilo halikuwezeka-na baada ya mawakili wa upande wa mashtaka kudai hawakujua kama walipaswa kuwasilisha hoja hizo pamoja na ukweli kuwa walisi-

kia maagizo ya mahakama,” alisema Wakili Nassoro.

Siku hiyo ya Septemba 4, mabis-hano ya kisheria yaliibuka mahaka-mani huku mawakili wa mshtakiwa wakijaribu kupinga ombi la upande wa mawakili wa upande wa Serikali la kutaka kuongezewa muda. Hata hivyo, mahakama iliahirisha kesi hiyo kufuatia ombi hilo la mawakili mpaka Septemba 18, 2015 ili kuan-galia uwezekano wa kuwaongezea muda mawakili hao kujiandaa ku-wasilisha hoja zao au la!

Wakili Nassoro, amesema wao (upande wa utetezi) walipinga ki-tendo cha upande wa mashtaka kuchelewa kuleta majumuisho hata hivyo hakimu aliahidi kutolea ua-muzi suala hilo siku hiyo ya huku-

mu. Safari ya Sheikh Ponda ya ku-kaa gerezani ilianza Agosti 10, 2013 alipokamatwa baada ya kupigwa risasi na polisi mjini Morogoro dakika chache tu baada ya kumaliza kuhutubia Waislamu siku ya Idi ka-tika msikiti wa ‘Dini Moja, Mungu Mmoja’ ulioko eneo la Uwanja wa Ndege.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi mkoa-ni Morogoro lilikanusha kumpiga risasi Sheikh Ponda Issa Ponda. Ka-manda wa Polisi mkoani Morogoro ACP Faustine Shilogile alisema polisi walikwenda kumkamata la-kini kwa kusaidiwa na wafuasi wake, Sheikh Ponda aliwatoroka.

Baada ya kujeruhiwa, Sheikh Ponda alikwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kupatiwa matibabu yatokanayo na kupigwa risasi lakini polisi wakamtia nguvu-ni na kumfungulia mashitaka kati-ka Mahakama ya Hakimu mkazi mjini Morogoro.

sheikh ponda asubiriwa kwa hamu

Page 8: Imaan Newspaper issue 33

www.islamicftz.org

6 MuHarraM 1437, juMaTaTu oKToBa 19 - 25, 2015

8

Miongoni mwa makosa ya-nayopelekea mtu kuhukumi-wa adhabu ya kifo katika Uis-lamu ni kuua kwa makusudi. Tena, ili adhabu hii itekelezwe ni lazima ithibitike pasina sha-ka yoyote kuwa kweli mtuhu-miwa kaua kwa makusudi.

Anasema Allah aliyetukuka katika Quran Tukufu: “Na Tu-mewaandikia (Sharia) humo kwamba uhai kwa uhai, na ji-cho kwa jicho, na pua kwa pua, na sikio kwa sikio, jino kwa jino; na majeraha (kulipizana) kisasi. Lakini atakayetolea sadaka (haki yake akasemehe) kwayo, basi itakuwa ni kafara kwake. Na yeyote asiyehuku-mu kwa yale aliyoyateremsha Allah, basi hao ndio mad-

halimu. (5 : 45). Hii ni simulizi ya Qur’an juu

ya Sharia ya Taurati kuwa miongoni mwa hukumu zili-zokuwamo katika kitabu hicho kilichoshushwa kwa Nabii Musa ni adhabu ya kifo. Kama adhabu hiyo haiko hivi leo ndani ya kinachodaiwa kuwa Kumbukumbu la Taurati, basi watu wameiondoa, na kwa

hakika mengi yameon-dolewa.

Allah anasema ndani ya Qur’an: “Na tumekuterem-shia (ee Muhammad) Kitabu kwa haki kinachosadikisha yale (yaliyokuja katika) vita-bu vilivyokuwa kabla yake na chenye kudhibiti, kushuhu-dia na kuhukumu (muhay-minan) juu yake (hivyo Vita-bu). Basi, hukumu baina yao kwa yale aliyoyateremsha Al-lah; na wala usifuate hawaa zao kwa kuacha haki iliyoku-jia. Kwa kila (umma) katika nyinyi tumeujaalia sharia na njia (Shariy’ah na manhaj). Na kama angetaka, Allah an-gelikufanyeni umma mmoja; lakini (Allah amekufanyeni hivyo) ili akujaribuni katika yale aliyokupeni. Basi shin-daneni katika mambo ya kheri. Kwa Allah pekee ndio marejeo yenu nyote; kisha atakujulisheni yale (yote) mliyokuwa mkikhitilafiana” (5: 48).

Adhabu hii ya kifo ime-thibitishwa na Qur’an, Allah aliyetukuka anasema katika Qur’an: “Enyi mlioamini! mmeandikiwa (Shariy’ah ya kulipiza) kisasi waliouawa. Muungwana kwa muung-wana, na mtumwa kwa mtumwa, na mwanamke kwa mwanamke, na anaye-samehewa na nduguye kwa lolote basi kufuatilizwa kwake kuwe kwa wema na kumlipa kwake iwe kwa ih-saan. Hiyo ni tahafifu kutoka kwa Mola wenu na rahma. Na atakayeruka mipaka baa-da ya hapo basi atapata ad-habu iumizayo. Na mtapata katika (kulipiza) kisasi (kuokoa) uhai enyi wenye akili mpate kuwa na taqwa” (2: 178-179).

Wakati Wakristo wengi, kama si wote hivi leo wanao-na kuwa kwa mujibu wa ma-fundisho ya Biblia (ambayo ndani yake kuna Kumbuku-mbu la Torati) haifai kumhu-

kumu mtu adhabu ya kifo na pia haifai kulipa kisasi; ma-funzo ni akupigaye shavu la kushoto, mgeuzie na la kulia.

Mmoja wa wanathiolojia wakubwa wa Kikristo aliwa-hi kusema: “If anyone at-tempted to rule the world by the Gospel and to abolish all temporal law and sword on the plea that all are baptized and Christian, and that, ac-cording to the Gospel, there shall be among them no law or sword, tell me friend, what would he be doing?”

Mwanathiolojia huyo anaendelea: “He would be loosing the ropes and chains of the savage wild beasts and letting them bite and mangle everyone, meanwhile insist-ing that they were harmless, tame, and gentle creatures; but I would have the proof in my wounds. Just so would the wicked under the name of Christian abuse evangeli-cal freedom, carry on their rascality, and insist that they were Christians subject nei-ther to law nor sword, as some are already raving and ranting”.

Maana ya maneno hayo ya mwanathiolojia huyo ni: “Kama mtu yoyote yule an-gelijaribu kutawala ulim-wengu kwa kutumia Injili na akaondoa sheria na adhabu zote kwa madai kuwa watu wote ni Wakristo na wame-batizwa, na kuwa kwa muji-bu wa Biblia pasiwe na sheria au adhabu; niambie rafiki yangu angekuwa anafanya nini kwa kitendo chake hi-cho?”

Mwanathioljia anajibu swali lake hilo: “Bila shaka atakachokuwa akifanya ni kuwafungulia kamba na minyororo wanyama wakali n a h i v y o k u w a a c h i a wamng’ate na kumtafuna kila mtu huku yeye akiende-lea kusisitiza kuwa hawana madhara, wanafugwa au ni

wapole; lakini mimi niliyeng’atwa ningekuwa na ushahidi dhidi yao katika majeraha yangu. Ni kwa namna hiyo waovu kwa jina la Ukristo watautumia uhuru huo vibaya, na hivyo kutenda maovu huku wakisistiza kuwa wao ni Wakristo kwa hiyo hawako chini ya sheria au adhabu kama baadhi wal-ivyoanza kufanya”

Wanaopinga kuendelea kwa adhabu ya kifo sio kuwa hawaoni umuhimu na ud-harura wa kuwepo na kuen-delea kwa adhabu hiyo, bali ni kuwa wakati mwingine wanaostahili kuhukumu au kutekeleza hukumu hizo wao wenyewe ni wauaji. Sasa uk-weli huu unawasuta. Wana-kosa uhalali wa kiroho au (moral authority). Vipi jaji atamhukumu adhabu ya kifo muuaji wakati jaji mwenyewe anajijua wazi kuwa amewahi kuua tena pengine si mtu mmoja, wawili au watatu bali watu kadhaa?

Katika badhi ya nchi, ma-jaji wanaweza kuhukumu adhabu za kifo lakini maraisi wa nchi hizo wakasuasua au wakakataa kusaini adhabu hizo zisitekelezwe. Ndiyo yale ya: “All cats love fish, but fear to wet their paws.” Yaani, “Paka wote wanapenda sa-maki lakini huchelea kulow-anisha viganja vyao”.

Katika makala hii na ijayo sikusudii kuzungumza na kutoa hoja za kwa nini adha-bu ya kifo iendelee kwani nimeshawahi kufanya hivyo katika moja ya vipindi vya ‘Mada Nyeti’ vya TV na redio Imaan, wala sitozungumza udhaifu wa hoja za wanaop-inga adhabu ya kifo isien-delee. Hata hivyo nashangaa sana wapingaji wa adhabu hiyo wanaocheza wimbo huu huku mishipa ya uso ikiwa imewatoka wanatunzwa na kuchaguliwa wimbo na nani safari hii, maana Wamerika-ni wanayo adhabu hii na ha-wataki kabisa kuitokomeza.

Pamoja na wanaojiita wa-naharakati wa haki za binad-amu kukomalia adhabu ya kifo iondolewe ni dhahiri kuwa wanachoimba na ku-kataa ni watu kunyongwa kwa utaratibu wa kisheria ila pale wanapovamiwa na ma-jambazi bila shaka hujitoa na kukabiliana nao kwa marun-gu na mapanga, na ‘ama zan-gu ama zako’ huku wakiwa-hukumu kifo majambazi waliowavamia. Huwezi ku-vamiwa na jambazi kisha ukamuelekeza kwa lugha ya haki za binadamu eti ukiniua utapelekwa mahakamani na huko hutohukumiwa kifo kwa sababu ni kinyume na haki za binadamu! Haya yat-akuwa yale ya Waswahili ukistaajabu ya Musa…

Itaendelea ([email protected])

Morogoro -TIF Media makao makuu yaThe Islamic Foundation, Msamvu

Dar es salaam - katika ofisi ya The Islamic Foundation iliyopo Kariakoo mtaa wa Mafia na Sikukuu jijini

Dar es Salaam.

kwa mawasiliano piga simunamba 0713 596 223.

CD za Anaashid zinazorushwa kupitia redio Imaan zinapatikana katika sehemu zifuatazo

sHeiKH TawaKKal juMa

KuToKa KaTiKa Qur’an’ na sunnaH

Mpenzi msomaji, katika makala kadhaa zilizotangulia tulizungumzia ubaya wa kuua kwa mujibu wa Uislamu. Tuligusia pia kuwa katika Uislamu mtu huuwawa kwa kufanya makosa maalumu na adhabu hiyo ya kifo hufanyika kwa utaratibu maalumu wa kisheria.

adhabu ya kifo huliwaza wafiwa, hulinda uhai na kuleta amani

Page 9: Imaan Newspaper issue 33

www.islamicftz.org

6 MuHarraM 1437, juMaTaTu oKToBa 19 - 25, 2015

9

Vita dhidi ya kundi la Boko Haram nchini Ni-geria, Cameroon, Niger na Chad imeingia katika

hatua nyingine kufuatia taarifa kwamba Marekani inapelekea wa-najeshi 300 na ndegevita sizizo na rubani nchini Cameroon.

Rais Muhamadu Bukhari wa Nigeria aliyeingia madarakani miezi saba iliyopita, amekuwa aki-fanya kila awezalo kutimiza ahadi ya kuwafyekea mbali Boko Haram aliyoitoa katika kampeni za ucha-guzi.

Badala ya mashambulizi ya Boko Haram kupungua, ndiyo kwanza yameongezeka hususan matukio ya ugaidi wa kujilipua ka-tika maeneo yenye watu wengi na kusababisha vifo vya maelfu ya watu wasio na hatia.

Marekani yakataa kuiuzia silaha Nigeria

Mwezi Julai mwaka huu, rais Muhamadu Bukhari aliomba mataifa ya kimagharibi, hususan Marekani, yaiuzie Nigeria silaha za kisasa ili kuliwezesha jeshi la Ni-geria kupambana vilivyo na Boko Haram lakini alikataliwa.

Kwa mujibu wa rais Bukhari, Marekani ilikataa kuiuzia silaha nchi yake kwa madai kuwa kufanya hivyo ni kwenda kinyume cha she-ria iitwayo, “Leahy law” ambayo in-aizuia serikali ya Marekani kuiuzia silaha nchi yenye rekodi mbaya ya haki za binadamu.

Ripoti ya Shirika la Kimataifa la Kupigania Haki za Binadamu (Amnesty International), jeshi la Nigeria linatuhumiwa kuvunja haki za binadamu katika mapamb-ano yake dhidi ya Boko Haram.

Njama za MarekaniRipoti mbali mbali za wachun-

guzi wa mambo zinadai kuwa Marekani inahusika katika kuan-zishwa Boko Haram kwa lengo la kuivuruga Nigeria ili kufaidika na hazina ya mafuta yaliyogunduliwa nchini Chad na Cameroon.

Marekani imekuwa ikiahidi kui-saidia Nigeria kukabiliana na kit-isho cha Boko Haram lakini wac-hunguzi wa mambo wanashangaa kama kweli Marekani ina nia nje-ma, kwa nini basi ikatae kuiuzia si-laha Nigeria?

Kana kwamba hilo halitoshi, pamoja na uwepo wa maafisa wa kijasusi wa Marekani na wale wa Israeli nchini Nigeria, masham-bulizi ya Boko Haram ndio kwanza yanaongezeka kila uchao. Hapo kuna nini?

Ni vita ya mafutaKatika kitabu, ‘Petroleum and

its Impact on Three Wars in Africa: Angola, Nigeria and Sudan’,

mwandishi Adrian Gonzalez anaandika: “Oil and gas supplies are becoming scarcer and more ex-pensive. The hunt for the world’s remaining resources is creating new alliances and the danger of fresh conflicts”.

Tafsiri: Upatikanaji wa mafuta na gesi unazidi kuadimika na kuwa ghali zaidi. Utafutaji rasilimali chache za ulimwengu zilizobaki unasababisha ushirika mpya na hatari ya migogoro mipya”.

Mgogoro wa Nigeria unaosaba-bishwa na Boko Haram na ule wa Sudan Kusini kati ya majeshi ya serikali ya rais Salva Kiir na waasi wanaoongozwa na Riek Machar ni miongoni mwa migogoro mipya inayotokana na mataifa tajiri, Marekani kwa upande mmoja na China kwa upande mwingine kugombania mafuta.

“China is moving aggressively to satiate its growing appetite for en-ergy, potentially setting up conflict with the United States over the dwindling resources of the Middle East and Africa”

Tafsiri: “China inavamia kwa kasi kukidhi kiu yake ya nishati inayoongezeka, kwa kufanya hivyo inasababisha mgongano na Marekani kuhusu rasilimali zinaz-opungua za Mashariki ya Kati na Afrika”.

Boko Haram na Ajenda ya Mafuta

Ripoti za wachunguzi wa masu-ala ya migogoro ya kimataifa wa-nafichua kwamba kundi la Boko Haram lilianzisha mashambulizi ili kuinyima Nigeria fursa ya kuchim-ba hazina yake mpya ya mafuta ka-tika majimbo ya bonde la Chad.

Hazina ya mafuta katika bonde

la Chad inapanuka hadi katika nchi za Niger, Cameroon na Nigeria. Miaka ya karibuni, Chad imekuwa mchimbaji na msafirishaji wa ma-futa kupitia bomba la kusafirisha mafuta lenye urefu wa kilometa 1070 kupitia Cameroon.

Inasadikiwa kwamba hazina kubwa ya mafuta hayo iko katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa Nigeria kwenye majimbo ya Yobe, Borno na Adamawa, majimbo am-bayo mashambulizi ya Boko Har-am yameshamiri.

Lengo ni kuizuia Nigeria kuendesha shughuli za uchimbaji wa mafuta katika eneo hilo kutoka-na na mashambulizi ya Boko Har-am huku Chad, Cameroon na Ni-ger zikiendelea na uchimbaji huo.

Wataalamu wa uchunguzi na uchimbaji mafuta walilazimika kusimamisha shughuli zao kwa hofu ya kutekwa au kuuawa na wa-piganaji wa Boko Haram huku

wataalamu wa miamba (geologists) wa Shirika la Mafuta la Nigeria (NNPC) wakishindwa kufanya kazi.

Kwa mujibu wa E&P Mag, ma-tumaini ya kuongeza uzalishaji wa mafuta Nigeria ili kuinua pato la taifa katika upande wa bonde la Chad Kaskazini mwa Nigeria yametoweka kutokana na vitendo vya kikatili vya Boko Haram.

“Uchunguzi wa mafuta ulikuwa unakwenda vizuri na uchimbaji kibiashara ulikuwa unatazamiwa kuanza mwishoni mwa 2013 au mwanzoni mwa 2014”, alisema Na-madi Sambo, aliyekuwa Makamu wa Rais wa Nigeria katika serikali ya rais Goodluck Jonathan.

Marekani na wizi wa mafutaMashambulizi ya Boko Haram

yamewezesha Chad chini ya serikali ya rais Idris Derby kuiba mafuta ya Nigeria kwa kutumia kiitwacho, ‘3D oil drilling’.

Mafuta hupatikana katikati ya miamba na yanaweza kusambaa chini ya ardhi kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine. Kisima cha mafuta kinapochimbwa, mafuta kutoka chini ya ardhi hutiririka kwenda pale palipochimbwa.

Matokeo yake ni kwamba, kama mwamba ulioenea nchi mbili haukuchimbwa upande wa nchi moja, mafuta yaliyo chini ya ardhi ya nchi ambayo haichimbi yana-vutwa kwenda kule yanakochim-bwa kitendo kitwacho, ‘capturing’.

Kutokana na mashambulizi ya Boko Haram, nchi za Chad, Cam-eroon na Niger hivi sasa zinachim-ba mafuta kwa ushirikiano na ma-shirika ya mafuta ya Ufaransa, Uingereza na Marekani na hivyo kusababisha mafuta ya Nigeria

kutiririka kwenda katika nchi hizo.Kwa mujibu wa kile kiitwacho,

‘Rule of Capture’, uchimbaji huo wa mafuta ya nchi unaruhusiwa alim-radi uchimbaji ufanyike ndani ya mipaka ya nchi inayochimba. Ma-futa, gesi asilia na maji yanaweza kuchimbwa kwa jinsi hii hata kama yatatiririka kutoka nchi nyingine.

Kulikuwa na mzozo wa eneo lenye hazina ya mafuta kati ya Ni-geria na Cameroon liitwalo Bakassi Peninsula. Kesi iliyofunguliwa ka-tika mahakama huko The Hegue Uholanzi iliipa ushindi Cameroon .

Cameroon hivi sasa inafaidika na uchimbaji wa mafuta yanayotir-irika kutoka ghuba ya Guinea nchi-ni Nigeria. Uchimbaji huu unainu-faisha Cameroon na mashirika ya wawekezaji kutoka Ufaransa.

Njama dhidi ya NigeriaKutokana na mashambulizi ya

Boko Haram, wawekezaji wa uch-imbaji wa mafuta wa kimataifa wa-meikimbia Nigeria kwa sababu za kiusalama na mabilioni ya dola yamewekezwa Chad, Cameroon na Niger.

Hivi sasa Chad imeongeza uzal-ishaji wa mafuta katika ziwa Chad na kuhifadhiwa katika meli maa-lum ziitwazo ‘Floating, Production, Storage and Offloading vessels’ zenye uwezo wa kutunza kiasi cha mapipa milioni mbili.

Mafuta haya husafirishwa kuto-ka Chad kwenda bandari ya Le Ha-vre nchini Ufaransa. Kwa hiyo, maana yake ni kuwa Ufaransa ina-faidika sana na mashambulizi ya Boko Haram kaskazini mwa Ni-geria, mashambulizi ambayo ya-naizuia Nigeria kuchimba mafuta yake. Mtandao wa kufichua siri wa Wikileaks uliwahi kuweka hadha-rani kwamba mtu ajulikanaye kama Abu Mahjin kutoka Chad ali-yepewa mafunzo katika kambi ya Marekani nchini humo, ndie hasa muasisi wa mashambulizi ya Boko Haram.

Lengo la uwepo wa Boko Har-am ni kuinyima utulivu Nigeria ili isichimbe mafuta eneo la Kaskazini Mashariki na hivyo kutoa fursa kwa mataifa ya magharibi kuiibia rasili-mali yake kupitia Chad, Cameroon na Nigeria.

Hivyo haishangazi hata kidogo kwamba mashambulizi ya Boko Haram yanazidi kila uchao, Marekani inakataa kuiuzia Nigeria silaha za kupambana na Boko Har-am na Marekani hiyo hiyo inapele-ka majeshi yake nchini Cameroon.

Kuongezeka kwa mashambulizi na kuikatalia Nigeria kununua sila-ha yana lengo la kuendelea kuizuia Nigeria isichimbe mafuta upande wake hivyo kuruhusu mafuta yake kuibiwa kupitia nchi jirani yake.

Majeshi ya Marekani kuwekwa nchini Cameroon kama yalivyo nchini Chad ni kwa ajili ya kulinda wizi huo wa mafuta ya Nigeria, kuikomoa nchi hiyo kiuchumi na kuidhoofisha ili isiwe tishio kwa Marekani ukanda huo.

ncHa ya KalaMu

Marekani na karata ya Boko Haram

mareKani imeKuWa iKiahidi

Kuisaidia nigeria

KuKabiliana na Kitisho Cha boKo

haram laKini WaChunguzi

Wa mambo Wanashangaa

Kama KWeli mareKani ina

nia njema, KWa nini basi iKatae Kuiuzia silaha

nigeria?

sHeiKH MuHaMMad issa

Yainyima silaha Nigeria Yapeleka wanajeshi Cameroon Lengo ni mafuta, ugaidi ni daraja tu

Page 10: Imaan Newspaper issue 33

www.islamicftz.org

6 muharram 1437, jumatatu oktoba 19 - 25, 2015

10 www.islamicftz.org

6 muharram 1437, jumatatu oktoba 19 - 25, 2015

11makala

Sheikh MohaMMad iSSa

Hakika idadi ya miezi mbele ya Allah ni kumi na miwili, tan-gu siku aliyoziumba mbingu na ardhi. Hiyo ndiyo dini ya

haki kwa hiyo msizidhulumu nafsi zenu katika miezi hiyo” (Qur’an 9:36).

Katika hadithi iliyopokewa na Abu Bakira (siyo Khalifa Abubakr) Allah awe radhi nao wawili hao, Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) amesema: “Mwaka una miezi kumi na miwili na minne kati ya hiyo ni mitakatifu; mitatu imefuatana Dhul Qa’dah, Dhul Hijja na Muharram na Rajab Mudhar unaokuja kati ya Jumaadal Akhir na Shaaban” (Bukhari)

Naam, tungali katika miezi mitakatifu mitatu iliyofuatana na huu mwezi wa Muharram ukiwa ndio wa mwisho kati-ka mfululizo huo, ikiwa leo ni tarehe 6 Muharram. Allah Taala atujaalie uwe kwetu mwezi wa kheri na baraka kwa ajili ya dunia na akhera yetu.

Mambo ya kufanya katika Muhar-ram

Miongoni mwa mambo ya kufanywa na Muislamu katika mwezi huu wa Mu-harram ni pamoja na kukithirisha mam-bo ya heri sadaka, dhikr na swaumu na kujizuia na kutenda maasi.

Swahaba Abu Huraira (Allah awe ra-dhi nae) amesema, Mtume wa Allah amesema: “Funga bora baada ya (mwezi wa) Ramadhan ni funga ya mwezi wa Al-lah wa Muharram” (Muslim).

Kule kusemwa, ‘mwezi wa Allah wa Muharram’ ni ushahidi wa msisitizo wa umuhimu wa mwezi huu. Pamoja na hayo haikuthibitika Mtume wa Allah (Rehma na amani ziwe juu yake) kufun-ga mwezi wa Muharram wote.

Historia ya siku ya AshuraJina ‘Ashura linatokana na siku ya

kumi (‘Asharah) ya mwezi wa Muhar-ram. Swahaba Abdallah bin Abbas (Al-lah awe radhi nae) anasimulia: “Mtume wa Allah alipofika Madina aliwakuta Mayahudi wakisherehekea siku ya Ashu-ra.

Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) akawauliza: “Ni siku gani hii?” Wa-kasema: “Hii ni sikukuu, siku Allah alip-owaokoa wana wa Israili dhidi ya maadui zao, kwa hiyo (Nabii) Musa alifunga swaumu siku hii”.

Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) akasema: “Sisi (Waislamu) tunayo haki zaidi juu ya Musa kuliko ninyi kwa hiyo akafunga siku hiyo na akaifanya

sunna” (Bukhari).Katika upokezi wa Imam Ahmad (Al-

lah amrahamu): “Hii ni siku ambayo Safina (ya Nuh) ilisimama juu ya mlima Juudiy, kwa hiyo Nuuh akafunga kumshukuru Allah” (Ahmad).

Mayahudi walikuwa wameifanya siku hii kuwa sikukuu ya kusherehekewa na wanawake wao wakivaa mapambo mbali mbali. Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) akawaamrisha maswahaba wa-jitofautishe na Mayahudi kwa kufunga swaumu siku hii ya Ashura.

Siku ya Ashura, Mayahudi walikuwa waliisherehekea kama sikukuu. Mtume wa Allah (Rehma na amani ziwe juu yake) akatufundisha kufunga swaumu ili tujitofautishe na Mayahudi kuhusu siku hii ya kihistoria ya ukombozi kwa watu wa Nabii Musa na Nuh (Amani ya Allah iwe juu yao).

Swaumu ya Ashura ilitangulia swaumu ya Ramadhan

Kufunga siku ya Ashura kulikuja kab-la ya kufaradhishwa swaumu ya Ramad-hani mwaka wa pili baada ya Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) kuha-mia Madina. Hii ni hIkma ya Allah ku-wazoesha watu kitu kabla ya kukiamri-sha. Mtume wa Allah alipofika Madina, aliwaagiza Waislamu kufunga siku tatu kila mwezi (masiku meupe) na siku ya Ashura. Kisha Allah akaifanya swaumu faradh (lazima) kwa Waislamu alipose-ma “Enyi mlioamini imefaradhishwa swaumu kwenu…” (2:183).

Fadhila ya funga ya AshuraImepokewa kutoka kwa Bin Abbas

(Allah awe radhi naye): “Sikupata ku-muona Mtume wa Allah akiwa na shauku ya kufunga siku yoyote kwa umuhimu mkubwa kuliko siku hii, siku ya Ashura, na mwezi huu” (Bukhari).

Shauku na umuhimu huu ni kutokana na fadhila au faida za kufunga swaumu ya Ashura kwani Mtume wa Allah (Reh-ma na amani ziwe juu yake) amesema: “Kwa kufunga siku ya Ashura, nataraji Allah ataikubali iwe kafara ya madhambi ya mwaka uliokwisha” (Muslim).

Tazama fadhila kubwa ya Allah Taala juu yetu kwamba kwa kufunga swaumu ya siku moja tu, unafutiwa madhambi ya mwaka mzima uliopita. Kweli Allah ni mwenye fadhila kubwa kabisa. Ni heri il-iyoje kwa wenye kukimbilia msamaha wa Allah?

Ashura ni siku gani?Imam Nawawi (Allah amrehemu)

anasema siku ya kumi ya Muharram

(‘Ashuurah) na ya tisa (Taasu’ah), ni maji-na mawili yanayotamkwa kwa kuvutwa (madd) katika lugha ya kiarabu. Mwana-wazuoni Bin Qudamah Al-Maqdasiy (Al-lah amrehemu) anasema: “Ashura ni siku ya kumi ya Muharram” na vivyo hivyo bin Abbas anasema: “Mtume wa Allah alitu-amrisha tufunge siku ya kumi ya Muhar-ram: (Tirmidhi).

Kilicho SunnahKilicho sunna ni Muislamu kufunga

siku zote mbili yaani yaani tarehe tisa Muharram (Taasu’ah) na kumi (‘Ashuu-rah). Bin Abbas (Allah awe radhi nae) anasema: “Mtume alipofunga swaumu siku ya Ashura na akawaamrisha Waisla-mu, wakasema, ‘ee Mtume wa Allah, hii ni siku inayotukuzwa na Mayahudi na Wakristo’. Mtume wa Allah akasema: “Kama nitajaaliwa kufika mwaka ujao, nitafunga na siku ya tisa vile vile. Lakini ikatokea Mtume akafariki kabla ya mwa-ka uliofuata” (Muslim).

Kwa hiyo sababu ya kufunga na siku ya tisa (Taasu’ah) ni kuwatofautisha Waisla-

mu kutokamana na Mayahudi ambao kwao siku ya kumi (‘Ashuurah) ni sikukuu. Faid anyingine ni kwamba kwa kufunga siku ya tisa, mtu ataepuka kuikosa siku ya Ashura iwapo atakuwa hakujaaliwa kuuo-na mwezi wa Muharram.

Funga hata kama ni Ijumaa, Juma-mosi au Jumapili.

Imam At-Wahawiy (Allah amrehemu) anasema: “Mtume wa Allah (Rehma na amani ziwe juu yake) alitufundisha kufun-ga siku ya Ashura. Hakutuambia kama ikiangukia Jumamosi tusifunge” (Tazama Mushkil al-Athar, Mjalada wa 2, Bab Sawm Yawm as-Sabt).

Kwa hiyo hukumu ni hiyo hiyo kama siku ya Ashura itaangukia Ijumaa au Ju-mapili kwani iwapo swaumu aliyozoea mtu kuifunga itaangukia katika siku hizi –Ijumaa, Jumamosi na Jumapili, ataifun-ga pasina ubaya wowote.

Siku ya Ashura kwa MashiaWaislamu Ahlu Sunnah tujihadhari

sana kwa sababu siku hizi sikukuu za

mashia zimeanza kuenezwa katika miji na vijiji vyetu. Wengi katika Waislamu kwa kukosa elimu hawajui asili wala maana za sikukuu hizi za kishia.

Mashia huomboleza siku aliyouawa mjukuu wa Mtume Hussein bin Ali (Allah awe radhi nae na baba yake pia) siku ya Ashura, wanazo pia sikukuu za kushere-hekea kuuawa kwa Umar ibn Khattwaab na kufa kwa Aisha (Allah awe radhi nao) na kadhalika.

Sheikh bin Taymiyyah (Allah amrehe-mu) anasema kuelezea mashia kuifanya siku ya Ashura siku ya maombolezo: “Kundi la wajinga na waovu na wapotofu walijifanya kumtii Hussein na watu wa ny-umba ya Mtume (Ahlul Bayt)”.

Alipouawa Hussein bin Ali, mashia wakaifanya siku ya Ashura kuwa siku ya kuomboleza na kulia ambapo hudhihiri-sha desturi za enzi za kijahiliya kama vile kujipiga mashavu, kuchana nguo zao na kuomboleza kijahili…

Shetani amewapambia na wameifanya siku ya Ashura kuwa siku ya kujiadhibu, kulia, kuomboleza, kusoma tenzi na

mashairi yaliyojaa uongo mwingi. Hadithi na simulizi zao hazina lengo zaidi ya kua-msha upya hisia zao na kuchochea chuki baina ya Waislamu.

Chuki hizo huzifanya kwa kuwalaani wale waliowatangulia (katika maswahaba wa Mtume). Baadhi ya wajinga, kama vile Naasibiyyuuna, wanaowapinga mashia na wenye chuki dhidi ya Hussein bin Ali, wameifanya siku hii kuwa sherehe.

Makundi yote hayo mawili (wanaoom-boleza yaani mashia na wanaosherehekea yaani Naasibiyuuna) ni wapotofu. Yote ya-fanywayo si katika sunna ya Mtume wala makhalifa waongofu. Hayo hayakukuku-baliwa na imam yeyote si Maalik, Sufyaan At-thawriy, Al-laythiy, Abu Hanifah, Al-Awza’iy, As-shaafiy, Ahmad bin Hambal au Ishaaq Ar-rahwayh wala mwanachuo-ni yeyote wa Waislamu (Al-Fataawa al-Kubra). Kwa hiyo Waislamu wa madhhe-bu za Ahlu Sunnah wal Jamaa-Shaafi’iyyah, Hanaabilah, Haanafiyyah na Maalikiyyah tujiepushe na kuifanya siku ya Ashura sherehe kama Mayahudi au maombolezo kama mashia.

Miongoni Mwa MaMbo ya kufanywa na MuislaMu katika Mwezi huu wa MuharraM ni paMoja na kukithirisha MaMbo ya heri

sadaka, dhikr na swauMu na kujizuia na kutenda Maasi.

Siku ya aShura:

Yatakiwayo na yasiyotakiwa

Said Rajab

Ni ukweli unao-fahamika vye-m a k w a m b a M t u m e w a

Mwenyezi Mungu, Mu-hammad (Rehma na ama-ni ya Allah iiwe juu yake) ndie kiongozi aliyefaniki-wa zaidi katika kipindi chote cha historia ya mwa-nadamu. Lakini Mtume huyu hakuwa tu ni shujaa, kama mwandishi wa kim-agharibi, Thomas Carlyle alivyomwita. Kwa mujibu wa Qur’an Tukufu, yeye ni mfano bora wa wanadamu wote na ametuonyesha njia ya kufikia mafanikio makubwa hapa duniani.

Kwa kusoma maisha ya Mtume Muhammad (Re-hma na amani ya Allah iiwe juu yake) tunaweza kuchota ile misingi mikuu ambayo Mtume aliifuata katika kufanya mambo. Kwa hakika Muhammad (Rehma na amani ya Allah iiwe juu yake ) alikuwa ni ‘positive thinker’ kwa maana halisi ya neno hilo. Shughuli zake zote zililen-ga kuleta matokeo mazuri. Alikwepa kabisa kuchukua hatua ambazo zingeweza kuleta madhara au kuk-wamisha mambo.

Ni vyema tukawaletea wasomaji, japo kwa ufupi, baadhi ya misingi ambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu aliitumia katika kufanikisha shughuli zake.

Msingi wa kwanza - Kuanza kufanya jambo pale l inapowezekana. Msingi huu unafafanuliwa vyema na msemo wa mama Aishah, mke wa Mtume, pale aliposema: “Kila Mtume alipolazimi-ka kuchagua kati ya mam-bo mawili, mara kwa mara alichagua chaguo rahisi zaidi” (Bukhari). Kucha-gua chaguo rahisi, maana yake ni kuanza jambo pale panapowezekana, na mtu anayefanya hivyo bila sha-ka atafikia lengo lake.

Msingi wa pili - Kuona fursa katika changamoto. Waislamu wa awali pale Makka, walikabiliwa na matatizo na changamoto nyingi sana. Katika kipin-di kile kigumu, Aya ya ku-waongoza Waislamu nda-ni ya Qur’an ilishuka: “Basi kwa hakika pamoja na uzito kuna wepesi. Hakika pamoja na uzito kuna wepesi” (94:5-6).

Hii ina maana kwamba kama kuna changamoto,

basi na fursa pia zipo hapo hapo. Kwa hiyo, njia ya kupata mafanikio ni kup-uuza changamoto na ku-fanyia kazi zaidi fursa.

Mfano, tunapolalamika kwamba Waislamu wana-baguliwa kielimu hapa nchini, ingawa kweli hiyo ni changamoto nzito kwetu, lakini pia Waisla-mu wanayo fursa ya ku-jenga na kuendesha shule zao. Sasa ni vyema, kwa mafundisho ya Mtume, tukashikilia zaidi fursa zi-lizopo kuliko kuendelea kuishi kwenye changamo-to tu.

Msingi wa tatu - Ku-badili eneo la harakati. Msingi huu unatokana na Hijra. Hijra haikuwa tu ni tukio la kuhama kutoka Makka kwenda Madina. I l ik uwa n i hat ua y a kutafuta eneo bora zaidi la kufanya harakati za Kiis-lamu, kama baadaye his-toria ilivyokuja kuthibiti-sha.

H a p a M t u m e w a Mwenyezi Mungu ametu-fundisha kubadili mbinu na maeneo ya kufanyia harakati, ili mradi hatua hizo hazipingani na Aqida y a K i i s l a m u . Tusing’ang’anie kufanya harakati katika eneo moja tu. Makka ilipokuwa ngu-mu zaidi kwa Waislamu wa awali, basi walihamia Ma d i n a n a h a r a k a t i zikaendelea kama kawa-ida na hatimaye wakarudi kuikomboa Makka.

Msingi wa nne - Kum-geuza adui kuwa rafiki. Mtume wa Mwenyezi Mungu mara kwa mara alikabiliwa na vitendo vya uchokozi kutoka kwa makafir i . Wakati ule

Q u r ’a n i l i m u e l e k e z a Mtume kulipa wema kwa ubaya aliotendewa:

“Mambo mazuri na ma-baya hayawi sawa. Ondo-sha (ubaya unaofanyiwa kwa wema; tahamaki yule ambaye baina yako na bai-n a y a ke k u n a u a d u i atakuwa kama jamaa (yako) mwenye kukufia uchungu”(41:34).

Hii ina maana kwamba jambo jema linalotendwa kama malipo ya ubaya ul-iofanywa, lina athari ya mapigo kwa wale walio-fanya ubaya. Na maisha ya Mtume wa Mwenyezi Mungu ni ushahidi wa ki-historia kuhusu msingi huu.

Msingi wa tano - Ku-badilisha hasi kuwa chan-ya. Baada ya vita vya Badr, zaidi ya makafiri 70 wa-likamatwa kama mateka wa vita. Walikuwa ni watu walioelimika. Mtume wa Mwenyezi Mungu alitan-gaza, iwapo kila mmoja wao atawafundisha Wais-lamu kumi kusoma na kuandika ataachiwa huru.

Hii ilikuwa ni shule ya kwanza katika historia ya Uislamu, ambapo wa-nafunzi wote walikuwa Waislamu, na walimu wote wakiwa maadui wa Waislamu. Hapa napenda kumnukuu mwandishi mmoja wa Uingereza, am-baye amemueleza Mtume wa Mwenyezi Mungu, kama mtu aliyeweza kuo-na mafanikio kutokana na hali ya kushindwa - “He was determined to write success out of failure”

Msingi wa sita - Nguvu ya amani ni imara zaidi kuliko nguvu ya vurugu. Wakati Makka ilipokom-bolewa, wapinzani na maadui wote wa Mtume wa Mwenyezi Mungu wal-iletwa mbele yake. Wa-likuwa ni wahalifu wa kivita, kwa maana zote za neno hilo. Lakini Mtume hakuagiza wauawe. Bada-la yake alisema: “Nendeni, mko huru”. Matokeo ya ki-tendo kile cha wema ya-likuwa makubwa sana. Wengi wao walisilimu siku ile.

Msingi wa saba - Kuto-kuwa na fikra mgando.Tusifikiri kwa kutumia vipimo viwili tu, kwamba kama jambo haliko hivi, basi lazima liwe vile. Kuna jicho la tatu pia. Katika vita maarufu vya Mu’tah, Khalid bin Waliyd (Allah awe radhi naye), kamanda w a

Misingi ya ufanisi wa uongozi wa Mtume

Msingi wa nne - kuMgeuza adui kuwa

rafiki. MtuMe wa Mwenyezi Mungu Mara

kwa Mara alikabiliwa na vitendo

vya uchokozi kutoka kwa

Makafiri. wakati

ule Qur’an iliMuelekeza

MtuMe kulipa weMa

kwa ubaya aliotendewa inaendelea Uk 12

Page 11: Imaan Newspaper issue 33

www.islamicftz.org

6 muharram 1437, jumatatu oktoba 19 - 25, 2015

12

majeshi ya Wais-lamu aliamua kuondoa vikosi vyake kwenye uwanja wa mapam-bano, baada ya kugundua kwamba idadi ya wapiganaji wake ilikuwa ndogo mno, ikilin-ganishwa na makafiri.

Walipofika Madina, baadhi ya Waislamu waliwapokea kwa ke-jeli wakiwazomea “Waoga hao! (Furrar!). Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema: “Hapana, siyo waoga! (Hao ni Kurrar) wenye kuona mbali.Watu wale wa Madi-na walikuwa na akili mgando - ama kupigana au kusalimu amri, lakini siyo kukataa kabisa kupi-gana, kama alivyofanya Khalid bin Waliyd.

Mtume ameonyesha kwamba mara zote kuna ‘option’ ya tatu, ambayo ni kuepuka vita na kutafuta muda wa kujipanga vi-zuri zaidi. Historia inatuonyesha kwamba baada ya miaka mitatu ya matayarisho, Waislamu walielekea kwenye mpaka wa Warumi, wakapambana vikali na kupata ushindi mkubwa.

Msingi wa nane - Kupeleka vita kwenye uwanja tunaouweza. Msingi huu unatokana na vita vya Hudaybiyyah. Katika kipindi kile, makafiri walidhamiria kuwaingi-za vitani Waislamu, kwa sababu walikuwa katika mazingira maz-uri ya kushinda.

Lakini Mtume wa Mwenyezi Mungu, kwa uangalifu mkubwa, alikubali masharti ya makafiri na kuingia nao mkataba. Ulikuwa ni mkataba wa amani wa miaka kumi. Kabla ya mkataba huo, ma-hali pa kukutana kati ya Waisla-mu na makafiri, ilikuwa ni kwenye uwanja wa vita tu.

Baada ya mkataba maarufu wa Hudaybiyyah kusainiwa, eneo la mapigano likabadilika, na sasa uwanja mpya wa mapambano ukawa mdahalo wa kiitikadi. Ndani ya kipindi cha miaka mi-wili tu, Uislamu ukashinda kwa kishindo, kutokana na ubora wa Itikadi yake.

Msingi wa Tisa - Kuwa yakini-fu kwenye masuala yenye utata. Wakati wa kuandika mkataba wa H u d a y b i y y a h , M t u m e w a Mwenyez i Mungu a l i sema yaandikwe maneno haya: “Hii ni kutoka kwa Muhammad, Mtume wa Mwenyezi Mungu”. Mjumbe wa Maqurayshi akapinga vikali maneno hayo kuandikwa kwenye hati ya mkataba.

Haraka sana Mtume alipoona jambo lile lingeleta mzozo usio wa lazima, na kukwamisha ajen-da ya msingi ya Waislamu kwenye mkataba ule , akabadil isha maneno yale na kuagiza iandikwe tu: “Muhammad, mtoto wa Ab-dullah”, na mambo yakaenda kama yalivyopangwa.

Hii ni baadhi tu ya misingi am-bayo Mtume wa Mwenyezi Mun-gu, aliitumia na kupata mafaniko makubwa katika harakati zake za kusimamisha Uislamu, mafani-kio ambayo wanahistoria wote maarufu duniani wameyatam-bua.

Katika mambo yanay-oweza kuonekana ni ya kizamani na mwiko kwa wakati wa sasa ni

kula pamoja kama familia. Uki-wa kama mkuu wa familia, jiulize mara ya mwisho ilikuwa lini familia yako yote ilikutana na kula pamoja mlo wa asubuhi, mchana au usiku.

Kutokana na kubanwa na kazi, mazowea mabaya au kwen-da na wakati, kula pamoja kama familia inayoishi nyumba moja ni jambo gumu sana kwa watu wengi wa zama hizi.

Hata hivyo, katika dini ya Ki-islamu, kula pamoja ni jambo li-liloruhusiwa na kuhimizwa kama tunavyoliona katika Qur’an na Sunna. Katika Qur’an Mwenyezi Mungu anasema: “Si vibaya kwa kipofu, wala si vibaya kwa kiguru, wala si vibaya kwa mgonjwa, wala kwenu nyinyi, mkila katika nyumba zenu, au nyumba za baba zenu, au nyum-ba za mama zenu, au nyumba za kaka zenu, au nyumba za dada zenu, au nyumba za ami zenu, au nyumba za shangazi zenu, au ny-umba za wajomba zenu, au ny-umba za dada wa mama zenu, au za mlio washikia funguo zao, au rafiki yenu”.

Aya inaendelea: “Si vibaya kwenu mkila pamoja au mbali mbali. Na mkiingia katika ny-umba, toleaneni salamu, kuwa ni maamkio yanayotoka kwa Mwenyezi Mungu, yenye baraka n a m e m a . Hi v y o n d i v y o Mwenyezi Mungu anavyo ku-bainishieni aya zake mpate kuelewa” (24: 61).

Katika Sunna, Mtume Mu-hammad, (Rehema na amani za Allah zimshukie), amehimiza kula pamoja kwa ksema: “Ku-sanyikeni kwenye chakula chenu ili kibarikiwe” (Imepokewa na Abu Dawud na Tirmidh).

Tafiti za sasa za kisayansi zi-naonyesha kuwa kuna umuhimu mkubwa sana wa kula pamoja kama familia. Tafiti hizo zinap-endekeza kuwa familia iwe in-akula pamoja angalau mara tano mpaka sita kwa wiki kwa mlo wa asubuhi, mchana au usiku.

Familia inayokula pamoja mara nyingi huwa na umoja kwa sababu kula pamoja kunaipa fa-milia fursa ya kukutana ana kwa ana na kuzungumzia kero ndani ya familia, kuwaunganisha wa-nafamilia, kupanga na kujifunza kutoka kwa kila mwanafamilia.

Katika kula pamoja, ndipo tu-napopata wasaa wa kuhakikisha watoto wetu wanakula kwa mila za dini na zile zitazowafanya wa-heshimike katika jamii yetu. Humo pia, ndipo tunapopata nafasi ya kudumisha utamaduni wetu kwani bila ya utamaduni tutakuwa hatuna utambulisho (identity).

Kula ni sehemu ya furaha ya kimaisha. Watu wanaposhiriki-ana katika furaha basi mara ny-

ingi matokeo yake huwa ni kushikamana kwa mapenzi bai-na yao. Hapo hupatikana mshikamano kutoka moyoni (emotional attachment) ambayo ni uti wa mgongo wa maisha ya familia.

Kula pamoja pia, kunasaidia kubadilishana taarifa za siku ile. Kadhalika, wazazi au walezi kupata muda wa kuwaangalia kwa karibu watoto na vijana wao. Mlo wa pamoja wa familia unaongeza mapenzi, huruma, usalama na kila mtu kujisikia kuwa ni mwana familia hata kama baba au mama ni rais wa nchi au waziri au profesa wa chuo kikuu.

Vilevile, kula pamoja kama

familia ni shamba darasa. Ndio kusema, wakati wa kula kama familia ni fursa ya pekee kwa wa-zazi au walezi kuwapa elimu, ujuzi, miiko na kurekebisha tabia mbaya za watoto na vijana wao juu ya ulaji.

Wazazi au walezi wawe rafiki kwa watoto na vijana wao, na wawe walimu kwa matendo yao badala ya maneno makali na ya vitisho. La sivyo, watoto wa-takimbia kula na wazazi hao.

Zaidi ya hayo, kula pamoja kunasaidia kupanua wigo wa

ufahamu kuhusu aina bora ya vyakula. Baadhi ya watoto ha-wapendi kabisa baadhi ya vyaku-la kama vile ugali wa dona, mboga za majani, maziwa ya mtindi, kande, n.k. Kula pamoja kama familia ni fursa nyingine ya kujenga tabia za watoto na vi-jana ili wapende vyakula bora zaidi kiafya kuliko kupenda chipsi mayai, kuku kila siku.

Watoto na vijana wajaribish-

we na kuonyeshwa vyakula hata kutoka makabila mengine ilim-radi, vyakula hivyo viwe bora kwa afya zao kama vile mlo wa ndizi na samaki. Mlo huu un-aimarisha ubongo na akili ya mtoto.

Wazazi wakumbuke kuwa mtoto anachukumua muda mre-fu kukikubali chakula asichoki-jua au asichokipenda, kwahiyo uvumilifu unahitajika sana.

Mlo wa familia mara nyingi huandaliwa nyumbani kwa hiyo huwa na matunda na mboga za majani za kutosha, maziwa au mtindi. Vyakula hivyo ni chanzo kikubwa cha nyuzi lishe, madini kama ya calcium na vitamini kama A, C, na folate (vitamini B9), virutubisho ambavyo kwa watoto huwa wanavikosa kuto-kana na wazazi kupenda fast food.

Kwa wanaojali afya za watoto wao, mlo wa nyumbani huwa sio wenye vyakula vya kukaanga kila siku, havina chumvi na sukari nyingi, na matumizi ya vinywaji vyenye sukari nyingi kama vile soda na juisi za viwandani huwa ni kiwango kidogo.

Familia inayokula pamoja mara nyingi huwa na umoja kwa

sababu kula pamoja kunaipa Familia Fursa ya kukutana ana kwa ana na kuzungumzia kero

ndani ya Familia

Misingi ya uongozi wa Mtume

Pazi MwinyiMvuaafya yako

umuhimu wa kula pamoja kama familia

inatoka Uk 1

Page 12: Imaan Newspaper issue 33

www.islamicftz.org

6 muharram 1437, jumatatu oktoba 19 - 25, 2015

13

Shukrani njema ni zake Muumba wa mbingu na ardhi. Rehma na amani zimfikie Mu-

hammad aliye mkweli mua-minifu na mwisho wa mitume. Kisha salamu kwa wenye kufua-ta muongozo.

Bima inakubalika katika Uis-lamu pale tu inapofanywa kati-ka utaratibu wa kudhaminiana (takaful) au kushirikiana (ta’awun) kwa pamoja katika kubeba hasara kwa pamoja hasara atakayoipata mmoja wapom katika kundi.

Hivyo, bima katika Uislamu sio mkataba wa kuuza na ku-nunua ambapo upande mmoja unatoa na unauza ulinzi (pro-tection) na mwingine unakubali na kununua huduma kwa ghar-ama au bei fulani.

Bali katika Uislamu, bima ni utaratibu wa kundi la watu wenye maslahi ya pamoja kud-haminiana au kujilinda kwa pamoja kutokana na majanga fulani kwa kuunda mfuko maa-lumu unaochangiwa kutoka ka-tika rasilimali zao, mfuko huu utatumika kulipa fidia na kugharamia shughuli zote za kibima.

Katika makala haya, tutadu-rusu juu ya tofauti kati ya bima ya Kiislamu (takaful) na bima ya kawaida.

Moja, msukumo mkubwa katika bima ya kawaida ni kupa-ta faida na kukuza faida kwa wanahisa. Biashara ya bima ina-milikiwa na wanahisa wa kam-puni ya bima.

Kwa upande mwingine bima ya Kiislamu imejikita katika us-tawi wa jamii na uhifadhi wa jamii dhidi ya majanga. Hudu-ma ya bima yenyewe si biashara ya kupatia faida. Huduma ya takaful inaendeshwa na kam-puni ambayo huitwa mwende-shaj i wa takaful ambayo hupokea malipo kama ada au gawio kutoka katika uwekezaji. Hivyo basi, biashara ya bima humilikiwa na washiriki wa

bima huku kampuni ya bima in-akuwa kama wakala wa kusima-mia shughuli hiyo.

Pili, katika bima ya kawaida faida hujumuisha ziada (under writing surplus) ambayo ni to-fauti kati ya jumla ya mishango (premium) iliyokusanywa kuto-ka kwa wateja na jumla ya madai, fidia iliyolipwa.

Hivyo, faida hujumuisha zia-da katika bima na faida kutoka katika uwekezaji. Pia ugawaji wa faida au ziada unategemea uamuzi wa uongozi wa kampuni ya bima. Kwa upande mwingine katika takaful faida haijumuishi ziada inayopatikana baada ya kutoa malipo ya fidia katika mishango (premium). Pia mkataba wa takaful ndio un-aobainisha wakati na namna ya

ugawaji wa faida na sio uongozi wa kampuni ya bima.

Tatu, katika bima ya kawaida chanzo cha sheria na taratibu za kuongoza mfumo wa bima ni watu. Katika takaful chanzo cha sharia na taratibu ni ufunuo kutoka kwa Allah.

Nne, katika bima ya kawaida uwekezaji wa michango (premi-um) unategemea maamuzi ya kampuni ya bima pekee bila ku-wahusisha wateja (policy hold-er). Na mara nyingi uwekezaji huo unahusisha mambo yaliy-okatazwa kama uwekezaji kati-ka riba, maisir na maeneo men-gine ya haramu. Katika bima ya Kiislamu mkataba wa Takaful unabainisha wapi na namna ambayo michango itawekezwa. Na kwa ujumla uwekezaji huo

hautahusisha maeneo yaliyoka-tazwa kisharia.

Tano, iwapo kampuni ya bima ya kawaida itavunjwa, ak-iba (reserves) na ziada (surplus) zinamilikiwa na wanahisa wa kampuni hiyo. Lakini katika bima ya kiislamu akiba na ziada endapo kampuni ya bima ita-vunjwa hurudishwa kwa wa-shiriki wa Takaful (policy hold-ers) au hutolewa kama sadaka. Wanazuoni wengi wanapendlea zaidi kutoa kama sadaka.

Sita, kampuni ya bima ya Ki-islamu ina jukumu la ziada la kulipa zakat kila mwaka, tofauti za kampuni za kawaida ambazo hazilazimiki kulipa zaka.

[email protected] +255713 996 031

bima kwa mtizamo wa kiislamu - (2)uchumi na biashara

JaMaL iSSa

Dr. Maurice Bucaille

How could a man, from being illiterate, become the most important author, in terms of literary merits, in the whole of Arabic literature?

How could he then pronounce truths of a scientific nature that no other human being could possibly have developed at that time?

Tafsiri: “inawezekanaje mwanadamu kutoka hali ya kutokujua kusoma na kuandika awe mwandi-shi muhimu kuliko wote kwa mujibu wa sifa za kitaaluma katika fasihi yote ya kiarabu? inawezeka-naje wakati huo kutamka hakika za kisayansi ambazo hakuna mwanadamu mwingine angeweza kuzivumbua zama hizo?. (the Bible, the Qur’an and Science, 1978, p 125)

Watu maarufu WasiokuWa Waislamu waseMavyo kuhusu uislaMu

bima ni utaratibu wa kundi la watu

wenye maslahi ya pamoja

kudhaminiana au kujilinda kwa pamoja

kutokana na majanga Fulani kwa

kuunda mFuko maalumu

unaochangiwa kutoka katika rasilimali zao

Page 13: Imaan Newspaper issue 33

www.islamicftz.org

6 muharram 1437, jumatatu oktoba 19 - 25, 2015

14 makala

Hatua hii ilifuatia mapambano ya miaka mingi kati ya majeshi ya watawala wa Andalusia enzi hizo na yale ya Waislamu kutoka Ma-gharibi na Kaskazini mwa Afrika. Waislamu walivuka bahari kuite-ka Andalusia ili kuzuia masham-bulizi mapya dhidi yao.

Tariq bin Ziyad alikuwa ame-faulu kutia nanga mahali penye milima paitwapo Jabal Tariq (Mlima wa Twaariq) hivi leo kwa kumbukumbu ya jina lake. Ku-ficha historia hii iliyotukuka ya Waislamu, wazungu wakapaita Gilbrater.

Huo ulikuwa mwaka 711 Mi-ladia sawa na mwaka wa 92 Hijri-ya, enzi za utawala wa bani Umayya uliotawala dola kubwa ya Kiislamu kutokea Damascus (Dameshqi) nchini Syria. Ki-likuwa ni kipindi cha dola ya Kiis-lamu kupanuka hadi China na In-dia.

Mara tu baada ya majahazi yal-iyowabeba Waislamu kutia nanga, walijikuta wakikabiliwa na jeshi kubwa la maadui zao. Tariq bin Ziyad akaona dalili za hofu toka kwa wapiganaji wake. Hapo ndipo Tariq bin Ziyad alipofikia maa-muzi yake ya kuchoma moto ma-jahazi waliyotumia kuvuka bahari na kila kilichomo ndani yake.

Baada ya hapo, Tariq bin Ziyad akatoa hutba kali yenye mguso wa aina yake kwa kusema: “Ndugu zangu katika imani, tuko hapa kulieneza neno la Allah. Maadui wako mbele yenu na bahari nyu-ma yenu. Na hamna chakula wala maji ila kile mtakachokiteka kuto-ka kwa maadui zenu kwa panga zenu. Kwa hiyo hapa ni aidha ush-indi au kufa shahidi”.

Allahu akbar! Hiki kilikuwa kilele cha kumtegemea Allah na azma ya kupigana kwa ajili yake kilichooneshwa na Tariq bin Ziy-ad. Kwa wapiganaji katika jeshi lake, kuitii amri ya kamanda wao kuyachoma moto majahazi yenye kila kitu chao kilikuwa kilele cha utii.

Tariq bin Ziyad alikuwa mtu wa kabila la Ulhasa katika waber-iberi (Berbers) aliyeingia katika Uislamu kutoka nchini Algeria.

Awali alikuwa mtumwa na alipo-silimu akaachwa huru na bwana wake. Huyu ndiye mtu aliyeiteka Andalusia (Hispania) na kuupele-ka Uislamu Ulaya.

Watu kama Tariq bin Ziyad, waliokuwa watu duni kabla ya Uislamu lakini wakapata hadhi kubwa baada ya kusilimu ni wen-gi. Miongoni mwao ni Salman Al -Farsi, Bilal bin Rabbah na Zayd bin Al-Haaritha (Allah awe radhi nao wote).

Jemadari wa majeshi ya Wais-lamu, Kaskazini mwa Afrika alikuwa Musa bin Nusair, mmoja wa majemadari mahiri wa Kiisla-mu. Tariq bin Ziyad alivuka bahari akiwa na wanajeshi 300 waarabu na waberiberi 10,000 waliosil-imu.

Mfalme Roderic wa Andalusia aliwakabili akiwa na askari 100,000 dhidi ya Waislamu 10,300. Ni wazi lazima waliokuwa katika jeshi la Waislamu wawe na hofu ya kuteketezwa na jeshi kubwa lakini imani yao kwa Allah

iliwapa utulivu.Tariq bin Ziyad akamuomba

Jemadari Musa bin Nusair nyongeza ya wapiganaji na akam-tumia wapiganaji 7,000 chini ya kamanda Taarif bin Maalik Naqiy ambaye mji wa Tarifa nchini His-pania leo unabeba jina lake.

Kabla Taarif na jeshi lake hajafikia Waislamu, vita vikaanza na Waislamu wakawakabili maa-dui kishujaa. Majeshi mawili, lile la Waislamu na lile la makafiri yakakabiliana katika vita vya Guadalete ambapo Mfalme Ro-deric alishindwa na kuuawa mwe-

zi 28 Ramadhan mwaka 92 Hijri-ya.

Jeshi la Wahispania l i -liloshindwa likarejea nyuma kuelekea makao makuu ya dola mjini Toledo. Tariq bin Ziyad aka-ligawa jeshi lake vikosi vinne. Kikosi kimoja kikalekea mji wa Cordoba (Qurtuubah) na kuute-ka.

Kikosi cha pili kikaelekea mji wa Murcia na kuuteka na cha tatu kilielekea mji wa Zaragoza. Ka-manda Tariq bin Ziyad mwenyewe alielekea Toledo, wakazi wake wakajisalimisha pasina kupigana

ikawa mwisho wa Mfalme Roder-ic.

Baada ya kupata habari za ush-indi wa Waislamu, Jemadari Musa bin Nusair akafanya haraka kwenda kuongeza nguvu ili maa-dui wasije kujikusanya akiwa na wapiganaji 18,000. Majeshi ya Waislamu kwa muda mfupi yakateka theluthi mbili ya ghuba ya Iberia.

Miji ya Zaragoza, Barcelona na sehemu ya Ureno ikaangukia mikononi mwa Waislamu. Mwa-ka uliofuata Waislamu wakavuka mto Pyrenees na kuingia mji wa Lyons nchini Ufaransa.

Huo ukawa mwanzo wa dola ya Bani Umayya ya Magharibi chini ya Khalifa Walid bin , dola iliyota-wala Hispania (Andalusia) kwa miaka 750 tangu mwaka 711 hadi 1492 Waislamu walipotimuliwa Hispania katika vita ya msalaba iliyoitwa, ‘November Crusade’.

Kasi ya majeshi ya Waislamu chini ya Tariq bin Ziyad kuteka ar-dhi ya Andalusia na Waislamu ku-

Vituo na Vyuo Vya elimu VikaFunguliwa huko toledo na

cordoba na yeyote aliruhusiwa kuchukua elimu bure. magwiji

wa elimu za hisabati, jiograFia, kemia, baiolojia na unajimu

wakazalishwa kutoka Vyuo Vikuu huko toledo na cordoba

“Choma moto majahazi”. Ilikuwa ni amri kwa Waislamu kutoka kwa kamanda wa majeshi yaliyovuka bahari ya Mediterania kwa lengo la kuiteka Hispania au Andalusia kama inavyojulikana katika historia ya Uislamu.

Mlima aliotia nanga chini yake tariq bin Ziyad.

tariq bin ziyad:

Shujaa wa kiislamu aliyeitekaSheikh MohaMMad iSSa

Page 14: Imaan Newspaper issue 33

www.islamicftz.org

6 muharram 1437, jumatatu oktoba 19 - 25, 2015

15

Oktoba 25, itakuwa ni siku muhimu kwetu kama Watanzania. Ukihesabu kuanzia siku ya kutoka toleo hili Oktoba 19, zimebaki siku 6, kabla ya siku ya uchaguzi. Moja ya mambo ynayojadili-wa sana ni namna wanan-achi tunavyotakiwa kushiriki siku hiyo.

Katika mambo yanayo-husu ushiriki wetu ni lile la je watu wabaki vituoni mara baada ya kupiga kura au la. Mpaka naandika makala haya, msimamo wa Tume ya Uchaguzi (NEC) ni kuwa kila mwanachi arejee nyumbani kwake mara tu baada ya ku-piga kura, akisubiri taarifa za matokeo.

Hata hivyo, sheria kwa upande mwingine inasema mtu atatakiwa kuwa umbali wa takriban mita mia mbili (kiufupi ni kwamba asiwepo jirani na eneo/kituo cha ku-pigia kura).

Ukitazama kwa makini, jambo moja utakaloligundua ni kuwa sisi wanajamii, kuto-kana na matukio yanayoji-tokeza na namna tunavyoi-shi, kuaminiana hakuko miongoni mwetu. Pia, jambo la pili utakaloligundua ni kuwa kumekuwa na kutawa-la kwa khiyana miongoni mwetu.

Jamii yoyote ikifika hapo, ikakosa kuaminiana, jua

kuwa inaelekea kuangamia kuliko kubaya sana. Bahati mbaya inayotukabili ni kuwa si jambo rahisi kujenga kua-miniana ndani ya kipindi hiki kifupi kabla ya uchaguzi kwa sababu tabia hizi mbili zinafunzwa, zinajengwa na zinalindwa zisiharibike miongoni mwa wanajamii.

Kwa bahati mbaya, katika jamii zetu hatuna mlezi wa kudumu wa kuzifunza na kuzisimamia tabia hizi. Kutokana na kukosekana kwa mlezi katika jamii yetu, haya yanayotokea hay-ashangazi.

Mazao yoyote tunayoyao-na ikiwemo hii hali ya kukosa mlezi wa kujenga na ku-fundisha uaminifu, ni sisi wanajamii na viongozi wetu ndio tulioyapanda. Kama tu-navyokariri mara kwa mara, maradhi haya ya nafsi huwa hayaishii kummaliza mtu mmoja bali huwa yanaua ki-zazi na kizazi.

Kimsingi, hisia ya kua-

miniana ni msingi wa jamii iliyo nzima na iliyo imara jamii. Jamii inaweza kuwa na furaha pindi tu mizizi ya ua-minifu inapoimarishwa barabara miongoni mwa wa-najamii. Lakini watu wana-pokiuka misingi hiyo na wakaipa khiyana kipaumbele basi jamii hiyo huingia katika migogoro isiyo na msingi.

Kuna kanuni zinazo rati-bu vipengele vyote vya mai-sha ya wanadamu. Na kila umuonaye anao mchango katika kanuni hizo kwa ku-wajibika kwake kiakili, ki-maumbile, kiimani, kidini, kikabila na kinamna yeyote ile. Kimaumbile, binadamu hana budi ila kuishi na wana-jamii wenzake na kwa kuwa huwa pana wajibu na haki ya kutekelezeana baina ya wa-najamii, binadamu hulaz-imika kufuata utaratibu wa sheria ili kuhifadhi mfumo wa jamii kutokana na mach-afuko na matatizo.

Kuishi huko kwa ushiriki-

ano baina ya wanajamii ku-narahisisha kupatikana kwa njia ya ufumbuzi wa matatizo yao. Mwanadamu anapenda kupata ufanisi na mafanikio bila ya kutaabika kwa kuwa ni sifa yake ya kiasili, lakini ni lazima tufahamu kwamba raha haipatikani ila kwa kutekeleza wajibu kama wal-ivyosema wahenga: “Raha ni malipo ya kutekeleza waji-bu”.

Katika kuyaendea maisha kwa namna iliyo nzuri, hatu-wezi kuishi bila kuwa na vi-ongozi wanaosimamia mambo yetu. Viongozi hao watakuwa daraja baina yetu na tusioweza kuwafikia pasi na kusahau kuwa wao ndio tutawateua kusimamia rasili-mali zetu kwa uadilifu.

Kwa bahati mbaya, baa-dhi ya wasimamizi wetu huwa wanatuthamini sisi tu-naowapa dhamana kipindi cha uchaguzi. Mara tu baada ya kuwachagua, wao hawawi daraja tena la kutuunganisha bali wao ndio huwa wapitaji na sisi raia tunabaki ku-washangaa tukisubiri kipindi kingine cha kubembelezwa.

hata hiVyo, sheria kwa upande mwingine inasema

mtu atatakiwa kuwa umbali wa takriban mita mia mbili

(kiuFupi ni kwamba asiwepo jirani na eneo/kituo cha

kupigia kura)

kuelekeauchaguzi

2015na iddi Jengo

kuaminiana na kuepuka khiana

kuelekea uchaguzi mkuu na tatizo la maradhi ya nafSi - (5)

fanikiwa kuikalia kwa miaka 750 inaingia katika histo-ria ya vita duniani zama za kati.

athari ya utawala wa kiislamu hispaniaKabla ya Waislamu kuingia Hispania, watawala

wake walikuwa watu kutoka nchi za Skandnavia wait-wao Visigoths. Mnamo karne ya tano Miladiya, hawa Visigoths waliiteka Hispania na kuweka utawala wao mji mkuu ukiwa Toledo.

Kwa kuwa hawakuwa wastaarabu wajuzi wa kuta-wala, walikaribisha Kanisa la Roma mwaka 565 kuendesha mambo ya utawala. Kanisa likapata kibali cha kueneza Ukristo na kukusanya kodi.

Watu wakawa katika tabu kubwa, wakilipa kodi mara mbili moja kwa watawala na nyingine kwa kanisa. Kulikuwa na Wayahudi wengi Hispania, kipindi cha watawala Waislamu Wayahudi waklipata mateso makubwa sana.

Kwanza walinyimwa haki ya kumiliki ardhi na pili walikatazwa kuabudu kwa dini yao ya kiyahudi. Wal-ipojaribu kupinga hali hiyo, kanisa likawapa mateso za-idi.

Mwaka 707 Mfalme Vietza alipoonesha kuwahuru-mia Wayahudi, viongozi wa kanisa walimpindua na kumweka madarakani Mfalme Rodriguez. Wayahudi wanaume wakatiwa utumwani na wanawake wao ku-fanywa masuaria majumbani.

utawala wa haki wa waislamuMara baada ya Waislamu kuiteka Andalusia (His-

pania), haki ikatawala. Hakuna mali ya wenyeji iliyo-taifishwa. Waislamu waliwatendea watu wote kwa haki, wakiwemo Wayahudi, isipokuwa waliweka mfumo wa kodi wenye uadilifu ambapo waliolipa ni wenye uwezo tu.

Wakiongozwa na Qur’an na Sunna ya Mtume (Reh-ma na amani iwe juu yake), Waislamu waliingiza us-taarabu wa Kiislamu Ulaya na popote majeshi ya Wais-lamu yalipokwenda yalipokelewa kwa mikono miwili na wakazi wa maeneo hayo.

Utawala wa Waislamu ukafanya Hispania kuwa nchi ya kistaarabu iliyojaa haki, uadilifu na elimu. Mtumwa yeyote aliyeingia katika Uislamu aliachwa huru mara moja. Idadi kubwa ya wahispani awakaingia katika dini ya Uislamu. Watu wa dini mbali mbali wakiwemo Wais-lamu na Wayahudi waliruhusiwa uhuru wa kuabudu kwa mujibu wa dini zao. Siyo hivyo tu kila mwenye elimu, ujuzi na maarifa aliruhusiwa kupata ajira katika kuhudumia jamii.

Vituo na vyuo vya elimu vikafunguliwa huko Toledo na Cordoba na yeyote aliruhusiwa kuchukua elimu bure. Magwiji wa elimu za hisabati, jiografia, kemia, baiolojia na unajimu wakazalishwa kutoka vyuo vikuu huko Toledo na Cordoba.

Chini ya Waislamu, Hispania ikawa alama ya sayan-si, utamaduni na ustaarabu katikati ya Ulaya iliyokuwa katika zama zijulikanazo kama zama za giza. Mirefeji ya maji ilichimbwa, mazao mapya yakaingizwa na kuinua uchumi wa Hispania.

Miji ikakuwa na idadi ya wakazi kuongezeka. Mji wa Cordoba ukawa kitovu cha elimu Ulaya nzima na hadi kufikia karne ya 10 Miladiya, mji huo ulikuwa na wakazi wapatao Milioni moja yaani Manispaa.

Mwanahistoria mmoja Mkristo anaandika: “Waisla-mu walianzisha ufalme ule wa Cordoba uliokuwa fahari ya enzi za zama za kati, zama ambazo wakati Ulaya nzi-ma ilikuwa imezama katika ujinga na vurugu, mji huo ulikuwa nuru ya elimu na ustaarabu ikiuangazia ulim-wengu wa magharibi”.

Khalifa Walid bin bin Marwaan aliwaalika Jemadari Musa bin Nusair na Tariq bin Ziyad mjini Damascus. Lakini walipofika walimkuta akiwa mahututi. Ali-washukuru na kuwapa sehemu ya mali waliyoileta kutoka katika mapato waliyokusanya.

Khalifa Walid alipofariki, Suleiman bin Abdulmalik akamfuatia katika utawala. Tariq bin Ziyad alifariki mwaka 720 Miladia. Historia ya Uislamu na ulimwen-gu haiwezi kamwe kumsahau Tariq bin Ziyad.

hispania

Page 15: Imaan Newspaper issue 33

www.islamicftz.org

6 muharram 1437, jumatatu oktoba 19 - 25, 2015

16 makala

na yuSuPh aMin

Lugha ya vitendo ina nguvu zaidi ku-liko maneno. Maana yake ni kwamba vitendo vina nguvu zaidi ya maneno. Na hii ni njia bora zaidi ya ulinganiaji

dini kwani Mtume Muhammad (Rehma na amani ya Allah ziwe juu yake alikuwa mbora wa tabia (Husnul Khuluuq).

Tabia njema ni kati ya sifa muhimu zaidi ambazo hupelekea kuibuka mahaba katika mahusiano ya kijamii.Tabia njema pia ndio silaha aliyoitumia Mtume (Rehma na amani ya Allah ziwe juu yake) katika kulingania jambo lililopekea hata wasiokuwa Waislamu kuvutiwa na mwenendo wake na hatimae kusilimu.

Kulithibisha hilo ni pale Allah Taala ana-posema: “Basi ni kwa sababu ya rehema itokayo kwa Mwenyezi Mungu ndio ume-kuwa laini kwao. Na lau ungelikuwa mkali, mwenye moyo mgumu, bila ya shaka wange-likukimbia” (3:159).

Hata hivyo jambo linalosikikitisha katika zama tulizonazo ni kushuhudia baadhi ya Waislamu kutosheka kwa kuwa na majina mazuri ya Kiislamu na kudhani majina yao yatawapa mafanikio pasipo kutendea kazi mambo yaliyoamrishwa na dini na mbaya zaidi ni kujenga matumaini ya kupata malipo mema akhera bila kufanya kheri yeyote hapa duniani.

Kimsingi, mafanikio na ubora wa mwan-adamu hutokana na maadili na tabia njema na kinyume chake ni kwamba, jamii ambayo huwa haina maadili na kuwa mbali na ma-fundisho ya dini huwa katika mkondo wa kuangamia kimaadili.

Tafiti mbalimbali zinaonesha kupo-romoka na kuangamia kwa mataifa mengi duniani hakutokani tu na migogoro ya kijeshi, kisiasa au kiuchumi bali hutokana na kutoweka kwa maadili bora. Kwa maana ny-ingine naweza kusema misukosuko katika misingi ya kimaadili ni mambo ambayo huangamiza jamii kuliko uharibifu unaosab-abishwa na majanga ya asili kama vile mate-temeko ya ardhi.

Samuel Smiles, mwandishi maarufu wa Uingereza aliwahi kuandika: “Ustawi na up-ungufu wowote katika maisha unatokana na nguvu za dhati na uwezo wa kifikra au ki-maumbile wa mwanaadamu. Ukweli ni kuwa mafanikio na ufanisi wa mtu kwa kiasi kikubwa hutegemea maadili bora na ukar-imu wao kwa wengine”.

Kutokana na Uislamu kutofautiana na dini nyingine katika kipengele cha maadili na tabia njema, taarifa za miaka ya hivi karibuni zinaonesha idadi isiyowahi kutokea ya Waingereza, takribani wote wakiwa ni wa-nawake, wanaingia kwa wingi katika Uisla-mu katika kipindi ambacho kuna migawan-yiko mikubwa kabisa ndani ya makanisa ya Anglikana na Katoliki.

Tathmini ya mabadiliko haya imesababi-sha kutabiriwa kuwa Uislamu utakuwa kwa haraka sana na kuja kuwa dini kubwa yenye nguvu katika nchi hii ya Uingereza.

“Katika kipindi cha miaka 20 ijayo, idadi ya Waingereza watakaosilimu italingana au itashinda idadi ya jamii ya wahamiaji wa Ki-islamu walioleta dini hii hapa nchini”, alise-ma Rose Kendrick, ambaye ni mwalimu wa mafunzo ya dini katika shule maalum ya Hull na mtunzi wa kitabu cha kiada cha muongo-zo wa Qur’an.

Anasema: “Uislamu ni dini kubwa dun-iani kama ilivyo kwa kanisa la Katoliki. Haku-na mtu anayeweza kudai kuwa dini husika ni mali yake”. Uislam pia unaenea kwa kasi kubwa katika bara hili na Amerika kwa ujumla”.

Katika makala hii nitaangazia jinsi Uisla-mu unavyomtaka Muislamu kujikita na tabia njema ambayo ni nguzo muhimu katika kuendeleza Uislamu kwani Qur’an inatueleza jinsi tabia ya mtume rehema na amani ya Al-

lah ziwe juu yake ilivyosaidia kueneza na kuz-ivuta nyoyo za watu katika kuukubali Uisla-mu.

Kabla ya kusonga mbele zaidi tunapaswa kufahamu kuwa tabia njema na upole ni za-wadi toka kwa Allah Taala kwani hizo ni kati-ka sifa zake hivyo tunapaswa kushikamana nazo hivyo wale wenye mioyo migumu ni vema wakadhibiti nafsi zao kwa kuwa wak-iendelea kufanya hivyo hawawezi kuwavuta watu katika jambo lolote la mashauriano juu ya mambo muhimu.

Ukipitia historia ya maisha ya Mtume (Reh-ma na amani ya Allah ziwe juu yake), tunaweza kupata mifano bora ya kuigwa katika maana nz-ima ya tabia njema na maadili kwa mujibu wa Uislamu.

Mtume Muhammad (Rehma na amani ya Al-lah ziwe juu yake) pamoja na kuwa alikuwa aki-himiza tabia njema pia binafsi alikuwa mstari wa mbele kutekeleza kwa vi-tendo mambo yote aliy-okuwa akiwafahamisha watu na kutaka wayaige kutoka kwake.

Hakika Mtume (Rehma na amani ya Al-lah ziwe juu yake) katika kila nyanja ya mai-sha yake amejawa na tabia njema kama ana-vyosifiwa katika Qur’an pale Allah Taala ana-posema: “Na kwa hakika wewe (Muham-mad) una tabia njema” (68:4).

Pia swahaba Anas Bin Malik ambaye

alikuwa mtumishi wa Mtume wa Mwenyezi Mungu na mara zote alikuwa akizungumza kuhusu tabia njema ya Mtume.

Katika kipindi cha miaka 10 ya utumishi nyumbani kwa Mtume Muhammad (Rehma na amani ya Allah ziwe juu yake) alipata fa-hari kubwa ya kumhudumia Mtume na kati-ka kipindi hicho kamwe hakuona uso wake ukiwa umekunjika na hata wakati alipo-

tendewa vitendo vya kid-halimu hakuwahi kuvuta nyusi zake wala kutumia nguvu.

Dini ya Kiislamu, dai-ma imekuwa ikiwataka wafuasi wake waishi kwa upole, ukarimu na kujen-ga mahusiano mema na watu wa jamii au dini ny-ingine. Tabia ya Mtume (Rehma na amani ya Al-lah ziwe juu yake) ni muhimu katika kuende-lea kwa Uislamu kutoka-na na kukubaliana na maumbile ya mwanada-mu na ndio maana Mtume kwa kiasi kikubwa alijipamba na mazun-gumzo ya bashasha na hakuwaponda maadui zake na aliwaheshimu.

Katika historia ya Uis-lamu tumeweza kush-

uhudia visa mbali mbali vya tabia njema ya Mtume (Rehma na amani ya Allah ziwe juu yake). Mfano, ukiaangalia mitume na mana-bii wote wa Allah walitumwa duniani kwa ajili ya kuwaita watu na kuwafundisha nam-na ya kutimiza jukumu waliloumbwa kwalo nalo ni kumuabudu Allah wakifanya kazi

hiyo kwa upole na lugha ya laini. Shughuli ny-ingi za kilinganiaji hazina budi kufungamana na tabia njema kwa walinganiaji wake na ndio maana nasema vitendo vina nguvu zaidi kuliko maneno. Bahati mbaya wengi tume-kosa hili. Kusema usichokitenda ni katika hatari iliyo kubwa mbele ya Allah Taala ana-posema: “Enyi mlio amini! Kwa nini mnase-ma msiyo yatenda?” (61:2).

Licha ya kuwa ni dini iliyosheheni desturi zinazokubaliana na akili na kumpa mtu uon-gofu unaoupa nuru moyo, Uislamu pia ni dini inayobeba maendeleo yanayofaa kwa hali, mahala na zama zote na kwamba sheria yake (sharia) inakidhi hali na mahitaji yote ya jamii katika nyanja zote za maisha lakini haya yote yamekosa mashiko kuokana na wengi wetu kuwa wazungumzaji bila kuonesha matendo ya kile tunachokizungumza.

Ukweli ni kwamba, maadili yetu na sheria vimepoteza chanzo pekee cha nguvu yake, yaani dini. Hii imetokana na jamii ya Kiisla-mu kuthamini na kutukuza tamaduni za nchi za kimagharibi jambo linalopelekea watu wa baadhi ya jamii ya Kiislamu hususan vijana wa kike na kiume kuathirika zaidi na wimbi hili la umagharibi.

Nimalizie kwa kusema Waislamu makini wanafahamu kuwa propaganda dhidi ya sharia za Kiislamu kama mauaji yanayo-tekelezwa na makundi ya kigaidi kama ‘IS’ na Boko Haraam si chochote bali ni udanganyi-fu wa nchi za Magharibi. Hivyo, katika ku-uthibitisha ulimwengu kuwa Uislamu ni dini ya maadili na tabia njema hatuna budi kuiga mazuri yaliyofundishwa na Uislamu na si vinginevyo.

Kwa mtazamo wa watu wenye busara kuz-idisha vitendo vinavyoashiria tabia njema za Uislamu ni bora zaidi kuliko hata mazun-gumzo ya muda mrefu yahusuyo dini kwani ukiangalia riwaya mbalimbali utagundua kuwa Mtume (Rehma na amani ya Allah ziwe juu yake) alitenda wema kwa ubaya hata kwa wasio Waislamu walipomkosea jambo lililopekea wengi wao kuukubali Uislamu.

Jambo la muhimu ni kushikamana na matendo mema yaliyoamrishwa na dini kwani tukifanya hivyo hata wale wanao-pandikiza mbegu za chuki juu ya Uislamu watakosa hila na mbinu chafu katika kuupiga vita Uislamu na Waislamu hivyo kudidimiza azma yao.

kutokana na uislamu

kutoFautiana na dini nyingine

katika kipengele cha maadili na

tabia njema, taariFa za miaka ya hiVi karibuni

zinaonesha idadi isiyowahi

kutokea ya waingereza,

takribani wote wakiwa ni wanawake,

wanaingia kwa wingi katika

uislamu

ulinganiaji bora ni matendo yetu mema

Page 16: Imaan Newspaper issue 33

www.islamicftz.org

6 muharram 1437, jumatatu oktoba 19 - 25, 2015

17makala

iddi Jengo

Katika muendelezo wa makala zetu, leo tunaanza kuutafiti Uislamu katika sura

yake halisi na namna wenyewe unavyojieleza. Kwanza, ninuk-uu maneno ya msomi wa kim-agharibi ambaye sasa ni Muis-lamu safi, bwana Hofman Murad aliyejaribu kuuelezea Uislamu.

Murad alisema: “Nilianza kuuona Uislamu kupitia ma-cho yake yenyewe (Uislamu) imani iliyokuwa haijapo-toshwa, imani nzuri ya kua-mini mungu mmoja na atakaye baki kuwa mmoja, ambaye Yeye ni wa pekee, am-baye ndiye Mkusudiwa, am-baye hakuzaa wala hakuzali-wa, wala hana anayefanana naye hata mmoja ukilingani-sha na miungu ya kikabila, kimila na utatu”.

Murad anaendelea: “Qur’an imenionesha mwono ambao uliokuwa rahisi kuonekana na kueleweka. Taarifa za kiasili za Qur’an, mafundisho yake yenye maadili zilinivutia sana na kuwa ndio kitu kizuri na bora kama dhahabu. Hivyo hakukuwa na nafasi ya kun-ishawishi nisiamini ukweli wa utume wa Muhammad. Wale wanaouelewa uasili wa mwa-n a a d a m u h a w a w e z i kushindwa kuamini hekima isiyo na mwisho aliyopatiwa b inadamu kutoka kwa Mwenyezi Mungu katika njia ya Qur’an.”

Huo ni ushuhuda wa Mu-rad, msomi mkubwa na mwa-nadiplomasia aliyeshika nafasi nyingi. Kimsingi Uislamu ni dini sahihi pekee inayostahiki kuwa chaguo la kila mwanad-amu mwenye akili timamu kwa sababu zilizo wazi.

Kwanza, Uislamu ni dini ya Mwenyezi Mungu, aliyemu-umba mwanadamu kwa lengo maalumu. Ni muumba pekee anayejua mahitajio halisi ya mwanadamu na ni yeye pekee anayejua njia sahihi ya kum-fikisha mwanadamu kwenye lengo lake la maisha kwa usha-hidi wa Qur’an.

Allah Taala anasema: “Bila ya shaka dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu. Na wal io pe wa k i tabu hawakukhitalifiana ila baada ya kuwajia ujuzi, kwa sababu ya uhasidi ulio kuwa baina yao. Na anayezikataa Ishara za Mwenyezi Mungu basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu. Na pindi wakikuhoji, basi sema: Mimi nimeusalimisha uso wangu kumwelekea Mwenyezi Mun-gu, na kadhaalika walio nifua-ta. Na waambie walio pewa Kitabu na wasio na kisomo: Je! Mmesilimu? Wakisilimu b a s i w a m e o n g o k a . Na wakikengeuka basi juu yako ni kufikisha ujumbe tu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaona waja wake” (3:19-

20).Allah Taala anaendelea kutia msisitizo katika kitabu chake kitukufu: “Hakika ni juu yetu kuonyesha uwongofu (njia sahihi). Na hakika ni yetu Sisi Akhera na dunia. Basi na-kuonyeni na Moto unao waka!” (92:12-14)

Pili, Uislamu ndio dini pe-kee inayotosheleza kwa uka-milifu vipengele vyote vya sifa za dini sahihi. Hii ni kwa saba-bu Uislamu unaeleza ukweli juu ya Muumba na nafasi ya mwanadamu hapa ulimwen-guni.

Uislamu unatufahamisha kuwa ulimwengu huu na vote vilivyomo umeumbwa na Al-lah taala kwa lengo maalum, na kwa lengo hilo ndo huku-mu itapitishwa juu yake, juu ya kulipwa kheri ama shari juu ya yale yote aliyoyafanya.

Katika Qur’an tuanaelezwa k w a m b a m w a n a d a m u ameumbwa kwa lengo la kum-tumikia Allah Taala : “Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi. Na sitaki kwao riziki, wala sitaki wanil-ishe. Hakika Mwenyezi Mun-gu ndiye Mwenye kuruzuku, Mwenye nguvu, Madhubuti” (51:56-58).

Na msistizo mwingine juu ya lengo la kuumbwa adamu kama ndio amri kuu li-naelezwa katika Qur’an 98:5 isemayo: “Nao hawakuam-

rishwa kitu ila wamuabudu Mwenye-zi Mungu kwa kumtakasia dini, wawe waongofu, na washike Sala, na watoe Zaka. Na hiyo ndiyo dini mad-hubuti.

Si lengo la kuumbwa mwanada-mu pekee ndio limeelezwa ndani ya Qur’an bali lengo la kuumbwa ulim-wengu na vote vilivyomo pia limeelezwa kwa ukamilifu wake ka-tika Sura 2:29: “Yeye ndiye aliyeku-umbieni vyote vilivyomo katika ar-dhi. Tena akazielekea mbingu, na akazifanya mbingu saba. Naye ndiye Mjuzi wa kila kitu.

Uislamu ni dini ya kusimamia haki, usawa na uadilifu katika jamii. Miongoni mwa mambo yanayovu-ruga amani ulimwenguni ni kuwepo kwa dhulma katika jamii na dhulma haiondoki mpaka haki iwepo katika jamii.

Dini zote zilizoundwa na watu ziko pale kustawisha dhulma katika jamii matajiri na wenye hadhi huwakandamiza raia masikini na wanyonge. Uislamu ndio dini pekee inayoweza kumkomboa mwanada-mu kutokana na dhulma zote. Moja ya masharti manne ya kusimamisha Uislamu ni kusimamia haki.

Allah anasema katika Qur’an: “Naapa kwa Zama! Hakika binaad-amu bila ya shaka yumo katika khasara, Ila wale walio amini, na wakatenda mema, na wakausiana kwa haki, na wakausiana kusubiri” (103:1-3).

Aya hizo kwa ufupi zinatufahami-sha kuwa Uislamu utasimama kwa

mtu binafsi na kwa jamii kwa ujumla iwapo mambo manne yatatekelezwa kwa pamoja na kwa ukamilifu ikiwemo , kuamini, kutenda mema, kuusiana kusimamisha haki na kuu-siana kufanya subira.

Uislamu ni dini ya walimwengu wote wa nyakati zote, ndio dini pe-kee inayofuatwa na walimwengu wote wa sehemu zote na wa nyakati zote na ndio dini inayokua kwa kasi ulimwenguni.

Msomi mmoja, Jeremy Rifkin al-isema: “….Uislamu ndio dini ikuayo kwa kasi zaidi duniani. Wanatak-wimu wanatabiri kwamba katika kila watu wanne, mmoja atakuwa Muislamu miaka 24 ijayo. Kama takwimu ni nguvu basi tujue dunia inaegemea kwenye karne ya Wais-lam”.

Kuhusu hilo, Allah anatukumbu-sha: “Amekuamrisheni dini ile ile al-iyomuusia Nuhu na tulio kufunulia wewe, na tuliyowausia Ibrahim na Musa na Isa, kwamba shikeni nini wala msifarikiane kwayo. Ni magu-mu kwa washirikina hayo unayow-aitia. Mwenyezi Mungu humteua kwake amtakaye, na humwongoa kwake aelekeaye”.

Katika aya inayofuatia hiyo: “Na hawakufarikiana ila baada ya kuwa-jia ilimu kwa sababu ya husuda iliyo kuwa baina yao. Na lau kuwa haik-wisha tangulia kauli kutoka kwa Mola wako Mlezi ya kuakhirisha mpaka muda maalumu, basi bila ya shaka palingeli hukumiwa baina yao. Na hakika walio rithishwa Kitabu baada yao wanakitilia shaka inayo wahangaisha” (42:13-14).

Uislamu ni utaratibu wa maisha uliokamilika. Ni mfumo unamuele-keza binadamu namna ya kuendesha kila kipengele cha maisha yake ya ki-binafsi na ya kijamii. Ni mfumo ulio na utaratibu unaozingatia watu kama walivyo. Kwa kutambua kuwa mtu anakamilika kwa kuwa na mwili na roho, Uislamu umeweka utarati-bu wa kuustawisha mwili na roho.

Uislamu ni mfumo uliotuwekea kanuni na sheria zinazotuwezesha kujenga afya zetu na kukuza utu (uchamungu) wetu. Pia, kwa kutam-bua kuwa watu ni viumbe wanaotak-iwa waishi kijamii (social beings) na kutegemeana, Uislamu unatoa muongozo na kuweka kanuni na sheria ambazo humuwezesha kila mtu binafsi na jamii kwa ujumla kui-shi maisha ya furaha na amani. Uis-lamu pia ni mfumo ambao umeweka mifumo ya kijamii kama vile siasa, uchumi, utamaduni, na kadhalika juu ya misingi ya haki na uadilifu.

Katika toleo lijalo tutaanza kuu-dadisi Uislamu kuujua asili yake namna ulivyopangwa katika kurati-bu maisha ya mwanadamu na kama alivowahi kuandika bwana Hofman Murad kwamba, “Uislamu ndio mbadala” (Islam the alternative).

[email protected] 0714135201

uislamu ni dini ya

kusimamia haki, usawa na uadiliFu

katika jamii. miongoni

mwa mambo yanayo Vuruga amani

ulimwenguni ni kuwepo

kwa dhulma katika jamii na dhulma haiondoki

mpaka haki iwepo katika

jamii

kwa nini uislamu ni dini ya asili?Asili yetu ni dini yA Asili – (7)

Page 17: Imaan Newspaper issue 33

www.islamicftz.org

6 muharram 1437, jumatatu oktoba 19 - 25, 2015

18

sababu unaweza kumuona Muislamu akaamini lisemwalo na chombo cha mawa-siliano hata likiwa na uharamu ndani yake. Wakati mwingine tu-nachupa mipaka ya dini ambapo mtu hufikia kuamini na kufuata falsafa za kilimwengu ambazo zi-napingana na mafundisho ya dini. Imefikia hatua hata sifa za wake au waume tunaopaswa kuishi nao ka-tika ndoa tunatengenezewa na ku-tangaziwa kupitia televisheni, nasi bila wasiwasi tumekuwa tukiku-baliana nazo pasipo kujitambua.

Kuhusiana na hilo, katika ha-dithi iliyopokelewa na Swahaba Abu Huraira (Allah amridhie), Mtume (Rehma na amani ya Allah ziwe juu yake) amesema: “Mwan-amke huolewa kwa mambo manne (4), kwa mali yake, kwa ukoo wake, kwa uzuri wake na kwa mapenzi yake ya dini, jishindie kwa kumpa-ta aliyeshika dini, mikono yako ita-barikiwa” (Bukhari na Muslim).

Pamoja na mafundisho mazuri ya hadithi hiyo, jamii ya Kiislamu bado imejikuta ikianguakia pua kutokana na baadhi yetu kuacha

kufuata mafundisho ya hadithi pindi wanapotaka kuchagua mchumba na hatimae kujikuta wanashindwa kudumu katika maisha ya ndoa.

Hii ina maana kwamba watu hubainishiwa sifa za mwanamke anayefaa kwa ajili ya maisha ya ndoa kupitia vipindi vya televishe-ni na mitandao ya inaneti na si kwa mujibu ya maelekezo ya dini. Hivyo basi, kwa kuwa televisheni imese-ma, wengi huamini kilichosemwa kwa asilimia mia moja.

Sheikh Bin Taymiya (Allah am-rehemu) anasema: “Ni kitabu tu kutoka mbinguni kinachoweza ku-tatua matatizo ya watu. Lau kama watu wangeachwa kufuata rai zao basi kila mmoja kati yao bila shaka angekuwa na rai (yake)”. Sheikh Taymiya anaendelea kusema: “Ku-fuata matamanio katika masuala ya dini ni kubaya zaidi kuliko ku-fuata mambo mengine ya starehe.Hiyo ilikuwa ndio hali ya wasio-amini miongoni mwa washiriki-na”.

Ni kweli vyombo vya mawasil-iano vina athari kubwa katika

muktadha wa kuiongoza au kuipo-tosha jamii kutokana na nguvu yake yake ya kufikia kundi kubwa la watu kwa wakati mmoja. Lakini hiyo haina maana jamii ipum-bazike kwa sababu za ajenda buni-fu zitokanazo na fikra huru za kib-inadamu.

Pamoja na vipindi bunifu za vy-ombo vya mawasiliano kulenga maslahi ya kiuchumi kwa wa-naoziandaa lakini pia vipindi hivyo ni mojawapo ya mikakati ya dini ya umasonia ambayo inawataka watu wa dunia kuishi mfumo mmoja katika kumtumikia shetani.

Katika hili niwakumbushe Waislamu wanaojihusisha na vipindi vya televisheni zinazojikita katika kubuni mitindo ya maisha ambayo ni kinyume na Uislamu kujihadhari na adhabu iumizayo siku ya kiyama kama anavyobaini-sha Allah Taala: “Na atakayechagua dini isiyokuwa ya Uislamu haitaku-baliwa kwake. naye akhera atakuwa katika wenye kupata hasara” (3:85).

Na kama al ivyobainisha Mtume, (Rehma na amani ya Al-

lah ziwe juu yake): “Atakayefanya kitendo chema katika uislam atap-ata ujira wake na ujira wa yule atakayekitenda baada yake bila ya kupungukiwa thawabu zao.Na atakayetenda kitendo kibaya kati-ka Uislamu atabeba dhambi zake na dhambi za yule atakayetenda wala hapungukiwi kitu katika dhambi hizo”(Muslim).

Hakuna haja kwa jamii ya Kiis-lamu kuanzisha mijadala kuhusi-ana na mitindo ya maisha ya kisasa (modernazitaion) kwani jambo hili limeleta athari kubwa tangu vyo-mbo vya mawasiliano vikiwemo televisheni, na mitandao ya inta-neti kuwa chanzo cha kuporomoka kwa maadili ya jamii.

Mtume (Rehma na amani ya Allah ziwe juu yake) amesema: “Watu watazuka kutoka katika umma wangu ambao watakuwa wamejaa matamanio kama ugonjwa wa kuambukizwa na mn-yama unavyozagaa mwili mzima na kuathiri mishipa na viungo vyo-te” (Abu Dawud).

Kwa bahati, sisi Waislamu tu-mependelewa na Allah Taala kwa

kuletewa dini ya sawa sawa, isiyo na shaka ndani yake na kwa saba-bu hiyo hakuna nafasi kwa akili au maamuzi ya mtu binafsi mbele ya ushahidi wa maandiko yaliyotoka-na na Allah Taala na Mtume wake.

Katika kuhitimisha napenda kutahadharisha jambo ambalo pia Mtume (Rehma na amani ya Allah ziwe juu yake0 ametutahadharisha kupitia hadithi iliyopokelewa na Swahaba, Jaabir bin Abdullah (Al-lah awe radhi nae) aliposema: “Nimemsikia Mtume wa Mwenye-zi Mungu akisema: “Kila mja atafufuliwa katika hali aliyofia nayo”(Muslim).

Hadithi hii inatoa ishara ya mtu kufufuliwa kutokana na kile ali-chokipenda zaidi katika maisha ya dunia. Swali ni je,ndugu yangu Muislamu umejiandaaje kwa siku hiyo hali ya kuwa mtindo wa mai-sha uliochagua haukubalini na matakwa ya dini ?

Tunamuomba Allah Taala atu-jaalie, atuoneshe haki tuweze kui-fuata na pia atuoneshe batili tu-weze kuiepuka ili kubaki katika ra-dhi zake. Allah ni mjuzi zaidi.

Qur’an, Sunna rejea yetu; siyo vyombo vya habariinatoka Uk 20

darasani wiki hii kagiMu Mk. (Science teacher) 0752 224 550

GET READY FOR MATHEMATICS

Page 18: Imaan Newspaper issue 33

www.islamicftz.org

6 muharram 1437, jumatatu oktoba 19 - 25, 2015

19

Wanafunzi wa shule ya msingi Jitegemee iliyopo wilayani Bagamoyo wakipata huduma ya maji katika kisima kilichochimbwa na tiF.

katibu mkuu wa tiF ustadh ally ajirani (kulia) akibadilishana mawazo na mkurugenzi wa Radio Fadhila iliyopo katika mji wa Conakry nchini Guinea Sheikh Muhammad alhaafedh Sow wakati alipotembelea ofisi za tiF mjini Morogoro.

Mwanafunzi Juma Yasim kapilimbi akiwa katika uwanja wa ndege wa J.k nyerere akiwa safarini kuelekea afrika kusini kwenda kujiunga na chuo cha kuhifadhisha Qur’an, kilichoko Johannesburg afrika ya kusini.

Mkazi wa kijiji cha Maji Mapana, wilayani Bagamoyo akichota maji katika moja ya visima vilivyochimbwa na tiF wilayani humo.

Mkurugenzi mtendaji wa tiF akijaribu kisima kilichopo makazi ya polisi Bagamoyo

matukio katika picha

Mwenyekiti wa taasisi ya the islamic Foundation (tiF) aref nahdi (kushoto) akiwa katika kipindi maalum cha kuhamasisha amani katika tv imaan katikati ya wiki,kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo Sheikh ibrahim twaha na katikati ni mwendesha kipindi hicho ambaye pia ni Msimamizi Mkuu wa tv hiyo Sheikh Chembea.

Page 19: Imaan Newspaper issue 33

www.islamicftz.org

6 muharram 1437, jumatatu oktoba 19 - 25, 2015

20 Tariq bin Ziyad: shujaa wa kiislamu aliyeiteka

Uk 14

6 muharram 1437, jumatatu oktoba 19 - 25, 2015

yuSuPh aMin

Miongoni mwa maafa yanayoikabili jamii katika karne tuliyo-n a y o n i w a t u

kuathiriwa na maudhui yatoka-nayo na vipindi vya televisheni, matangazo ya biashara na sine-ma huku maudhui yatokanayo na vipindi hivyo yakitumika kama rejea ya suluhu ya changa-moto na matarajio yanayojitoke-za katika maisha ya mwanada-mu.

Mfumo wa kutegemea vyo-mbo vya mawasiliano kama rejea umepata umaarufu mkubwa ka-tika nchi za Marekani na Ulaya ambako vituo fulani vimetenga vipindi maalum vya muongozo wa mambo ya kijamii na men-gineyo.

Mfumo huo pia umeenea kwa kasi katika nchi zinazoendelea, ikiwemo Tanzania, kutokana na kasi ya maendeleo ya utandawazi hatua inayopelekea kuwepo kwa wimbi la vituo maalum vyenye maudhui pacha na zile za wama-gharibi zikiwa na malengo ya kuelekeza jamii mitindo ya mai-sha (life styles).

Ingawa katika dini ya Kiisla-mu ni wajibu kwa mja kufuata amri za Allah mlezi na Mtume wake sambamba na kujiepusha kufuata matamanio ya nafsi, wapo baadhi wamekiuka hilo kama ilivyokuwa kwa watu wa kitabu (Mayahudi na Manas-wara) ambao ni wenye kulaaniwa na Allah Taala.

Amesema Allah Taala: “Ha-watokuwa radhi Mayahudi na Manaswara mpaka mfuate mila yao. Sema: Hakika uongofu wa Mwenyezi Mungu ndio uongofu. Na kama ukifuata matamanio yao baada ya ujuzi ulio kwisha kujia, hutapata mlinzi wala msaidizi kwa Mwenyezi Mungu” (2:120).

Wakati tukitafakari ma-fundisho ya aya hiyo tutambue ya kuwa mafundisho yanayopatika-na kupitia vipindi vya vyombo vya mawasiliano ambavyo ndio msingi wa malezi ya jamii ya wamagharibi yametawaliwa zai-

di na matamanio ya nafsi na uharibifu kwani lengo lake ni ku-tangaza na kueneza vitu vya anasa kwa sura ya usasa.

Kwa mfano, vipo vipindi maa-lum vya televisheni na maudhui katika mitandao ya intaneti vina-vyotangaza mitindo ya mavazi ya kike na kiume isiyokubalika si tu kwa mujibu wa dini ya Uislamu bali hata katika tamaduni zetu za kiafrika. Bahati mbaya ilioje kuwa jamii imekuwa inaiga mitindo hiyo ya mavazi kwa

malengo ya kutaka kufanana na watu fulani maarufu.

Hata hivyo, suala la vyombo hivyo kugeuka mwalimu wa mi-fumo ya maisha ya watu hal-ionekani kuwa tishio kwa jamii kutokana na kuzoeleka. Kwa sababu hiyo basi, viongozi wa makundi ya jamii wakiwemo wa dini wanawajibika kufanya kazi ya ziada katika kuwaelimisha wafusi wao kuchuja mambo yasi-yofaa tunayoletewa kutokana na maendeleo ya utandawazi.

Hali ya jamii kutegemea vyo-mbo vya mawasiliano kama rejea ya maisha badala ya miongozo ya dini ni ishara ya shetani na wafuasi wake kushika hatamu ya kuwaongoza wanadamu katika njia ya upotovu badala ya ile ya uongofu iliyoamriwa na mola wao mlezi.

Maendeleo ya utandawazi pia yameathiri kwa kiasi kikubwa jamii ya Kiislamu hasa rika la vi-jana wa kike na kiume na hakika tumeshuhudia baadhi yao wakii-

ga mifumo isiyokubaliana kidini kama ile ya kuchanganyika wa-naume na wanawake wakati wa utekelezaji wa shughuli za ki-jamii kama vile harusi na misiba ambayo ni katika mienendo ya Wamagharibi.

Licha ya Qur’an na Sunna kuwa miongozo sahihi katika maisha ya Waislamu, jambo la kusikitisha ni kwamba baadhi yetu tumekuwa na mashaka na viwili hivyo kwa kukosa yakini. Na hii ndio

hutoleWa na kuchapishWa na the islamic foundation, p.o. box 6011 morogoro, tanzania e-mail: [email protected] na kuchapishWa na the islamic foundation, p.o. box 6011 morogoro, tanzania e-mail: [email protected]

MOROBEST BUS SERVICEMOROBEST BUS SERVICEKWA MAHITAJI YA USAFIRI WA UHAKIKA, SAFIRI NA KAMPUNI YA MABASI YA MORO BESTKILOMBERO – DAR, NA DAR - KILOMBEROKILOSA – DAR, NA DAR - KILOSASAFIRI NA MORO BEST KWA SAFARI ZA AMANI, UTULIVU NA UHAKIKAMORO BEST BUS SERVICE NI KWA AJILI YAKO NA FAMILIA YAKO

inaendelea Uk 18

Qur’an, Sunna rejea yetu; siyo vyombo vya habari


Top Related