Transcript
Page 1: Imaan Newspaper issue 5

7/17/2019 Imaan Newspaper issue 5

http://slidepdf.com/reader/full/imaan-newspaper-issue-5 1/19

ISSN 5618 - N0. 005 BEI: SH800/- KSH80/- USH1,200/- 21 RAJAB 1436, JUMATATU, MEI11 - 17, 2015  www.islamicftz.o

huwatoa watu gizani

China yalazimisha Waislamu kuuza nguruwe, pombe - Uk 15

Sheikh Nassoro Bachu:Mhadhiri maarufu

 Afrika Mashariki 

Maandamanoya Waislamu 

Maandalizi yaiva Tamko la mwisho lasubiriwa

Head off ice, Lumumba Street, Opp: Viwanja vya Mnazi Mmoja, P. O Box 779 Dar es Salaam, TanzaniaTell: 255 22 2182482/ 255 222184419, Fax: 255 22 2181424, E-mail: [email protected]

Vituo vyakuandikisha

wapiga kuravyawekwamakanisani

Sheikh Pondaatoweka Moro

UK

UK 3

UK 7 

Page 2: Imaan Newspaper issue 5

7/17/2019 Imaan Newspaper issue 5

http://slidepdf.com/reader/full/imaan-newspaper-issue-5 2/19

www.islamicftz.

21 Rajab 1436,  JUMATATU Mei 11 - 17,

2

NA WAANDISHI WETU

Licha ya kiwango kidogocha ada kinachotozwakatika madrasa nyingizilizopo katika jiji la

Dar es Salaam, bado wazazi wengi wamekuwa wazito kuwa-himiza watoto wao kutafutaelimu ya dini.

Kadhalika, uchunguzi wagazeti la Imaan umeonyesha

kuwa wazazi wengi hawalipi adaza masomo za watoto wao, kuto-kana na kutothamani elimu hiyosawa na wanavyothamini shule.

 Waandishi wetu waliotembe- lea madrasa wamegundua kuwakiwango cha ada katika madrasanyingi jijini Dar es Salam ni kati

 ya Tsh. 1,000 hadi Tsh. 5,000kwa mwezi, lakini walimu wamadrasa waliozungumza nagazeti la Imaan wamesema wa-

zazi wengi wamekuwa hawalipiada hiyo.

Miongoni mwa madrasa walizozitembelea, ni pamoja naNurul-Islamiyyah na Azhari zili-zopo kata ya Mabibo, Tul-Tarbi-

 yyah iliyopo Kigogo na Is- tiqaamah ya Magomeni, ambazozote hutoza ada isiyozidi Tsh.3,000 kwa mwezi.

Hata hivyo, walimu wa ma-drasa hizo wamesema wanafun-

HABARI

NA KHALID OMARY

Taasisi ya Dhi Nureyn Islamic Founda-

 tion yenye makao makuu mkoani Ir-inga kwa kushirikiana na taasisi ya AlMuntada Islamic Trust ya nchini

Uingereza imefanikisha zoezi la kutibu watoto wenye magonjwa ya moyo bila ya kuwafanyiaupasuaji kwa kuziba matundu yaliyopo kwenyemoyo kwa kutumia kifaa maalum kiitwacho‘Cathlet’.

Tiba hiyo inafanyika kwa mara ya kwanzahapa nchini kupitia idara ya tiba ya upasuaji wamoyo ya Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ku-shirikiana na madaktari bingwa kutoka hospi-

 tali ya Prince Sultan Cardiac iliyopo katika jiji laRiyadh nchini Saudi Arabia.

 Zoezi hilo ambalo lilianza Jumamosi iliyopi- ta litakuwa ni la siku tisa hadi Ijumaa ya wiki hii.

Muasisi na Mwenyekiti wa taasisi ya Dhi

Nureyn, Sheikh Said Abri, amewahimizananchi kutumia fursa hiyo, kwa kuwapeleka

 toto wao kupata matibabu hayo yanayotol bure.

“Hakika ni furaha kutoa matumaini makwa watoto hawa wenye ugonjwa wa moyoni furaha zaidi kwa mzazi ambaye atamumtoto wake, kipenzi chake, anazaliwa upykuaga machungu ya maradhi yaliyoku

 yakimsumbua”, amesema Sheikh Said Abri.Naye Kaimu Mkurugenzi wa hospital

Taifa ya Muhimbili, Dk. Hussen Kidanto alma, huu ni mwaka mzuri kwa upande wa kwa Tanzania.

“Hadi kufikia mwezi April mwaka huu ju ya wagonjwa 453 wamefanyiwa upasuajmoyo na wagonjwa 110 wamefanyiwa uchguzi wa mishipa ya damu na utaratibu wa shirikiana na wataalam kutoka nje ya nchi

auendeleza”, ameeleza Dk. Kidanto.

Dhi Nureyn, Al Muntada wasaidia wagonjwa wa moyo

“Afya”is naturalsource of sweetdrinking waterfrom under-

ground streamwhich is blended

with essential

minerals to sup-port and aid per-fect metabolism.

WATERCOM LIMITED

P.o. Box 20409, Plot N.4005, Kisarawe11 area

Temeke,Daresalaam, Tanzaniawww.watercomtz.com, E-mail:[email protected]

zi wengi walioandikishwa hawahudhuriimadrasa ipasavyo na wazazi wengi ha-

 walipi ada. Ustadh Hussein Dilunga,

mwalimu wa madrasa ya Nurul-Islami- yyah iliyopo mtaa wa jitegemee, Mabiboamesema, mahudhurio hafifu na kutoli-pa ada kunasababishwa na mwamkomdogo wa wazazi pamoja na ratiba zashule ambazo hazitoi fursa ya muda kwa

 watoto kwenda madrasa.Ustadhi Dilunga, ambaye ameanza

kufundisha madrasa toka mwaka 1988alisema, kuzuka kwa elimu ya ziada muda

 wa jioni (tuition) inazuia watoto wa Kiis- lamu hususani wale walioanza sekondarikuhudhuria madrasa. “Zamani vijana

 walikuwa wanarudi kutoka shuleni saanane, wanapata riziki huko majumbani,kisha baadae wanakwenda madrasa ku-fundishwa dini, lakini siku hizi muda huohaupo kabisa”, alisema Dilunga akione-sha namna vijana wa Kiislamu wanavy-

okosa fursa ya kujifunza dini yao kutoka-na na mfumo wa kielimu uliopo.

“Hakuna ulazima wa kusoma maso-mo ya ziada. Enzi zetu tulikuwa tunasomandani ya masaa manane na tulifaulu, vipi

 leo ionekane mtoto hawezi kufaulu bila yamasomo ya ziada”, Dilunga alihoji.

 Akielezea sababu za mahudhuriomabovu, Ustadh huyo amesema, wazazihawaoni umuhimu wa kuhimiza watoto

 wao kusoma elimu ya dini kwa sababu wanaamini elimu ya dini haitawapatia vijana wao ajira na kipato.

Naye Ustadh Omari Jokoo wa Madra-sat Istiqama anasema, kuna hatari kubwa

 ya kizazi cha Waislamu wa sasa kupoteana kuingia katika majanga makubwa

kutokana na kushindwa kujifunza dini yao. Ustadh Jokoo anaamini wazazi na jamii ya Kiislamu kwa ujumla haitoi ush-irikiano wa kutosha kwa walimu, na hivyo

 walimu hao wanakumbana na changa-moto zinazorudisha nyuma maendeleo

 ya elimu.“Katika madrasa, mafundisho ya fiqhi,

qur’an, tabia, tajwid, tawhid, tafsiri yaqur’an, na sira ya Mtume (Rehma na am-ani ziwe juu yake) yanafundishwa. Katikahali hii, lazima uwe na walimu wasiopun-gua watatu, ambao wote wana mahitaji

 yao ya kimaisha, wanahitaji kulipwa. Bilaushirikiano wa wazazi, ni vigumu kwakweli kuendesha madrasa”, alisema Us-

 tadh Jokoo.Kwa upande wa madrasa za nje ya jiji

 la Dar es salaam, hali ni mbaya zaidi. Us-

 tadh Omari Kinumbi anayefundisha ma-drasa Daiyya Islamiyya wal Jihad iliyopokata ya masaki, tarafa ya Sungwi, katika

 wilaya ya Kisarawe amesema, walimu wa vijijini wanapata tabu kubwa katikautekelezaji wa jukumu lao la ufundishaji

 wa madrasa.

 Walimu wa madrasa wafungukaWataka elimu ya dini ithaminiwe

Na. MJI FAJR DHUHUR ASR MAGHARIB ISH

1 DAR ES SALAAM(6.75 S, 39.25 E) 5:13 12:20 3:42 6:15 7:232 ZANZIBAR(6.17 S, 39.25 E) 5:12 12:23 3:42 6:15 7:243 TANGA(5 S, 38.25 E) 5:15 12:24 3:46 6:21 7:294 MOROGORO(8 S, 37 E) 5:23 12:29 3:50 6:22 7:305 MTWARA(10.67 S, 39 E) 5:18 12:21 3:41 6:10 7:196 ARUSHA(3 S, 36 E) 5:21 12:33 3:56 6:32 7:407 DODOMA(6 S, 36 E) 5:25 12:33 3:55 6:29 7:378 MBEYA(8.5 S, 33 E) 5:40 12:45 4:06 6:37 7:469 KIGOMA(5 S, 30 E) 5:48 12:57 4:19 6:54 8:0210 MWANZA(2.75 S, 32.75 E) 5:34 12:46 4:09 6:46 7:5411 KAGERA (4.66 S, 30.67 E) 5:44 12:54 4:17 6:52 8:0012 TABORA(5.5 S, 32.83 E) 5:37 12:46 4:08 6:42 7:5013 SHINYANGA(3.75 S, 33 E) 5:34 12:45 4:07 6:44 7:52

14 SINGIDA(5.5 S, 34.5 E) 5:30 12:39 4:01 6:35 7:4315 IRINGA(9 S, 35 E) 5:32 12:37 3:58 6:29 7:37

NYAKATI ZASWALA

Page 3: Imaan Newspaper issue 5

7/17/2019 Imaan Newspaper issue 5

http://slidepdf.com/reader/full/imaan-newspaper-issue-5 3/19

www.islamicftz.org

21 Rajab 1436,  JUMATATU Mei 11 - 17, 2015

NA WAANDISHI WETU

Ikiwa zimebaki siku chache kabla

 ya maandamano makubwa yakushinikiza Serikali kutekelezamadai ya Waislamu, Serikali ime-

shauriwa kutumia busara ili kuepushamadhara yanayoweza kutokea kutoka-na na mgogoro huo.

Ushauri huo umetolewa na wau-mini wa dini ya Kiislamu waliozun-gumza na timu ya gazeti la Imaan iliyo-pitia misikiti 10 ya jijini Dar es Salaamili kukusanya maoni juu maandalizi yamaandamano hayo.

 Waislamu wengi waliohojiwa, hu-susan vijana, wamesema kama Serikalihaitafanyia kazi madai yao, ni wazimaandamano hayo hayaepukiki.

“Sisi tumeshajipanga na kuhama-sishana kujitokeza kwa wingi kufanyamaandamano ya amani kuelezea hisiazetu”, Halfani Abdallah, muumini kati-ka msikiti wa Idrissa, Kariakoo ameli-

ambia Imaan na kuongeza: “Tuna-wasikiliza viongozi wetu kwa sasa. Tu-

naamini kimya cha Serikali ni ishara yakutupuuza.

Msimamo huo wa Waislamu ume-kuja kufuatia Mwenyekiti wa Jumuiyana Taasisi za Kiislamu nchini, SheikhMusa Kundecha kutangaza kufanyikakwa maandamano nchi nzima May 15mwaka huu, iwapo madai ya Waislamuhayatopatiwa ufumbuzi.

Madai muhimu zaidi ya Waislamukwa sasa ni pamoja na kuachiliwa kwadhamana kwa viongozi wa Kiislamu

 walio magerezani, kusimamishwa kwazoezi la kamata kamata ya ‘uonevu’,ikiwemo kuwaachia masheikh, walimuna wanafunzi wa madrasa wana-oshikiliwa, na kushughulikiwa kwa su-ala la mahakama ya kadhi.

Hata hivyo, suala ambalo lililogusahisia za Waislamu wengi ni ufungajiholela wa madrasa na kamata kamata

 ya waumini wa dini ya Kiislamu.Uchunguzi wa gazeti Imaan ume-

 baini kuwa kutokana na kadhia ya ma-

drasa iliyoendeshwa na jeshi la Polisi, Waislamu wameingiwa na hofu na

 wanajihisi kama si raia halali wa nchihii, hali iliyopelekea kadhia hiyo kuwagumzo katika mikusanyiko mbalim-

 bali ya wananchi, hususan Waislamu.“Hili sasa ni suala la kufa na kupona.

Uhai na ustawi wa Waislamu na Uisla-mu unategemea jinsi tutakavyojitokezakuibana Serikali ili ishughulikie sualahili”, Mzee Hassan wa msikiti wa Tungi,Temeke alisema.

“Yapo mambo ya kufunika kombemwanaharamu apite, lakini sio hili.Ukicheza na mbwa utaingia naemsikitini”, alitahadharisha.

Suala jingine lililoamsha hasira za Waislamu ni kunyimwa dhamana kwa viongozi wa Kiislamu walioko magere-zani, wakihoji iweje Askofu JosephatGwajima awe nje kwa dhamana, lakini

 viongozi wa Kiislamu wanaozea mage-

reza, huku wakifanyiwa vitendokudhalilishwa?

Hamisi Kilongole wa msikitiChihota, Tandika alihoji: “Au ni um

 wa watu waliojitokeza kumuumkono Gwajima ndio ulioitisha Skali? Nasi tutajitokeza Ijumaa, hueSerikali itaelewa uchungu wetu”.

Kilongole pia aliasa Serikali kibali cha maandamano hayo, kw

 lengo si kufanya vurugu bali kuelehisia zao.

 Waislamu hao walisema, si hhata kidogo kuendelea kuwashikiliongozi wa Kiislamu huku sheria inmwanya kwao kupatiwa dhamhizo.

“Leo hii ni miaka miwili sasa ShePonda yuko gerezani, tena akiwmgonjwa. Cha ajabu hapatiwi dhana kisa Mkurugenzi Wa Mashtnchini hataki, hiyo sio haki hata kigo”, amelieleza Imaan, mmoja wa vgozi waandamizi wa Baraza la Vij

 wa Kiislamu nchini, akiongeamwandishi katika msikiti Kichangani, Magomeni.

Kiongozi huyo, akiongea kwa halisema, huenda hayo yanatokea kukana na vijana wa Kiislamu kukuonesha hisia zao juu ya mambonayojitokeza nchini.

 Waislamu wengi walioongea waandishi wa gazeti la Imaan walkuwa Serikali kwa muda mrefu imkuwa haiyatili manani madai yao, j

 bo ambalo wamesema, linajenga wira ya wao kubaguliwa.

“Madai ya Waislamu hapa nch yanapopelekwa Serikalini ni nasana kufanyiwa kazi, hapa dhana ilini kuwa Waislamu ni wakorofi tu, j

 bo ambalo si sahihi”, Maneno SaidBuguruni amelalamika.

Kuhusiana na suala la Mahaka ya kadhi, Waislamu hao wameseSerikali imepuuza suala hilo kmuda.

Mmoja wa waumini, mkazi

Kibaha, mkoa wa Pwani alisema, W lamu wamedai mahakama ya kakwa muda mrefu ila hawapewi sababu za msingi, hali inayoonekuwa bila kibali cha maaskofu Wamu wa Tanzania hawawezi kupata hzao.

Mahakama hiyo iliingizwa kailani ya chama cha Mapinduzi (CCmwaka 2005, kuwa kikiingia madakani kitawapatia Waislamu mahama hiyo, lakini hadi leo kimeshindkufanya hivyo.

 Wakati hayo yakijiri, viongozKiislamu walipotafutwa na gazetikuzungumzia mustakabali wa m

 yao na uwepo wa maandamano hSheikh Rajabu Katimba alisema: “Scha kueleza kwa sasa, tulishama

kwani hukupata tamko letu? Wamuafaka ukifika tutazungumza”.

Waislamuwakiwa katikamoja yamikusanyiko. (NA

MPIGA PICHA WETU)

HABARI

MSIMAMO HUO WA WAISLAMUUMEKUJA KUFUATIA

MWENYEKITI WA JUMUIYA NATAASISI ZA KIISLAMU NCHINI,

 SHEIKH MUSA KUNDECHAKUTANGAZA KUFANYIKAKWA MAANDAMANO NCHI

NZIMA MAY 15 MWAKA HUU,IWAPO MADAI YA WAISLAMUHAYATOPATIWA UFUMBUZI

Maandamano ya Waislamu

NA MWANDISHI WETU

Taharuki ilitanda mwisho-ni mwa wiki iliyopita juu

 ya hali na usalama wa Ka- tibu wa Jumuiya na Taasi-

si za Kiislamu Tanzania, SheikhPonda Issa Ponda baada ya kuibukakwa taarifa za kuhamishwa kutokaMorogoro na kupelekwa kusikoju-likana.

Hata hivyo, baada ya taarifa zamkanganyiko kutoka mamlaka zamagereza baadae ilithibitika kuwaSheikh Ponda amehamishiwaUkonga, ingawa sababu halisi badohazijajulikana.

Uthibitisho kutoka kwa mke waSheikh Ponda, Khadija Ahmad, jio-ni ya siku ya Jumamosi kuwa alion-ana na Sheikh Ponda na kuzun-gumza nae katika gereza la Ukongazilituliza kidogo nyoyo za Waisla-mu.

Kwa mujibu wa Khadija, baada ya ja na yake kuzu ngus hwa namaafisa wa gereza, Jumamosi ali-

omba kuonana na Mkuu wa Gereza la Ukonga ambaye alimruhusu kuo-

nana na mumewe.Khadija aliliambia gazeti la Im-

aan kuwa Jeshi la Magereza lilimwambi a m umewe ameham-ishiwa Dar es Salaam kwa usalama

 wake kwa sababu kat ika gereza laMorogoro kuna mgogoro wa

 wakulima na wafugaji.Mwanzo wa kadhia:Taarifa zilizosambaa awali na

kusababisha taharuki kubwa zilian-za siku ya Ijumaa baada ya wakili

 wa Sheikh Ponda, Juma Nassoro,familia yake na viongozi wa Kiisla-mu kugundua kuwa Sheikh Pondaalihamishwa kutoka Morogorokimya kimya.

Baada ya kugundua hilo, wakiliNassoro aliliambia gazeti la Imaankuwa wana wasiwasi mkubwakuhusu alipo na usalama wa SheikhPonda baada ya kutokuwepo taarifa

rasmi za kuhamishwa kutoka Mo-rogoro.

“Tulipata habari kwamba ShePonda hayuko tena Morogoro. kama mawakili wake hatukujul

 wa kuhusu kuhamishwa kwake wapi anakopelekwa ili tuweze fuatilia hali yake kama tulivyoku

 tukifanya tangu awekwe ndani.Tulipojaribu kufuatilia ni w

anaweza kuwa amepelekwa, tuli ta fununu kwamba huenda yuko

reza la Ukonga jijini Dar es Salaaalisema wakili Nassoro.

Sheikh Ponda atoweka Moro

U

Page 4: Imaan Newspaper issue 5

7/17/2019 Imaan Newspaper issue 5

http://slidepdf.com/reader/full/imaan-newspaper-issue-5 4/19

www.islamicftz.

21 Rajab 1436,  JUMATATU Mei 11 - 17,

4

Waislamu nchini wametakiwa kumuiga Mtume (Re

hma na amani ziwe juu yake) kwa vitendo kwa kuwa

yeye ni mwalimu wa dini ya Uislamu.

Wito huo umetolewa na Sheikh Muhammad

Mujahid katika ibada ya swala ya Ijumaa iliyoswaliwa

katika msikiti wa Umar bin Khatwab uliopo mtaa

wa Jangwani jijini Dar e salaam na akaonya kuwa ili

amali ihesabiwe kuwa ibada haina budi kutekelezwa

kwa mujibu wa alivyofundisha Mtume. Sheikh Muja-

hid alisema jamii ya Waislamu inapaswa kujiepusha

na ibada zisizothibiti katika dini, kwani kufanya hivy

kunapelekea mtu kuandikiwa madhambi mbele ya A

lah . Aidha, aIiwakumbusha Waislamu kufanya ibada

kwa kutegemea malipo kwa Allah katika mwezi huu

wa Rajab sanjari na kujiepusha kufanya maasi, kwan

kufanya hivyo ni kujidhulumu nafsi na pia ni makosamakubwa . (YUSUPH AMIN)

Waislamu watakiwa kumuigaMtume kwa vitendo

Serikali imetakiwa kuacha mara moja zoezi

linaloendelea la kufungia madrasa katika mae-

neo mbalimbali ya nchi, kwani kufanya hivyo

ni kuwanyima watoto haki yao ya elimu na

kuiangamiza dini ya Uislamu.

Hayo yalisemwa Ijumaa iliyopita, na Sheikh

Hussen Ismail, wakati akitoa khutba ya swala ya

Ijumaa katika msikiti wa Tungi, Temeke jijini Dar

es Salaam.

Sheikh Ismail alisema, sababu wanazozitoa za

kuzifungia madrasa hazina mashiko kwa sababu

serikali haijawahi kutoa muongozo wa kusajili

na kuendesha madrasa, na kusema kama suala

la mazingira mabovu ya madrasa, bado hawana

hoja, kwani zipo shule za serikali nazo hazina

mazingira mazuri. (KHALID OMARY)

Imam Tungi atahadharishaSerikali

KUTOKAMISIKITINI

NA MWANDISHI WETU

Madaraka yakachukuliwa namwanae, Nuuru d-DinZink ambaye naye alipam- bana na wapigan aji wa

crusade’ lakini hakufaulu kuwashinda.Hapo ndipo, hatimaye, Allah akamuin-ua kiongozi mpya kuja kuzikomboa ar-dhi za Waislamu, naye ni Salahud-DinAl-Ayyubiy au kifupi Saladin. Endeleana kisa hiki cha kusisimua:

Katika kipindi hiki, Misri ilikuwachini ya dola ya mashia Fatmiyyin (TheFatimid Dynasty). Watawala wa kishiawalikuwa wakishirikiana na wapiganajiwa “crusade” waliozikalia ardhi za Wais-lamu.

Pamoja na kushirikiana nao, mwaka1160 ma-crusaders wakaivamia Misrikujaribu kuiteka. Nuuru d-Din Zinkakatuma jeshi kwenda kuwahami ndu-gu zake Waislamu. Kiongozi wa jeshihili alikuwa Jemadari Mkurdi, Shirkuhhuku Salahud-Din Al-Ayyubiy, mpwawa Shirkuh, akiwa miongoni mwa wap-iganaji.

Shirkuh na jeshi lake wakafanikiwakuwashinda ma-crusaders na kuikom-boa Misri, lakini akafariki kwa homa yamatumbo muda mfupi baadae. Mpwawake Salahud-Din Al-Ayyubiy akashikahatamu za uongozi wa jeshi hilo la Wais-lamu. Na huo ukawa mwisho wa uta-wala wa mashia Fatmiyyin Misri.

Hivi ndivyo Allah alivyomuinuamkombozi wa ardhi takatifu BaitullMuqaddas, Salahud-Din Al-Ayyubiy,Mkurdi ambaye hata hakuwa mwara-bu, kuonesha kwamba Uislamu si dini

ya Waarabu kama makafiri wanavyo-penda ifahamike.Lakini ni nani huyu Salahud-Din Al-

Ayyubiy? Alikuwa kijana wa miaka 36wakati akishika hatamu za kuiongozaMisri, ikiwa sehemu ya dola ya Kiislamuikiongozwa na Wakurdi.

 Wanahistoria Waislamu na makafiriwanamuelezea kama mtu mnyenyeke-vu asiyependa makuu. Hakujali kuhusuanasa za dunia kama wafanyavyo watuwenye madaraka kama yake. Azma yakekubwa ilikuwa ni kuzikomboa ardhi zaWaislamu kutoka mikono ni mwamakafiri.

Inasemekana Salahud-Din Al-Ayy-ubiy alikuwa hacheki na daima akiwana uso usio na furaha. Alipoulizwa kwanini yuko hivyo, alijibu: “Nitawezajekucheka wakati Masjid al-Aqsa ikomikononi mwa wana msalaba?”. Wako wapi leo watawala wa nchi za Kiislamu wenye haiba, azma, na malengo kama ya Salahud-Din Al-Ayyubiy? Inaseme-kana washauri wake walilazimika ku-ficha kiasi fulani cha dhahabu kama ak-iba yake kwa kuwa laiti angeiona malihiyo angeitumia katika maandalizi ya wanajeshi tayari kuwakabili maadui. Watu walikuwa wakisema alikuwahajionei huruma, lakini akiwahurumia wengine.

Kwa sifa hizi, wako waliomlingani-sha Salahud-Din Al-Ayyubiy na makha-

 lifa wanne waongofu wa Kiislamu, in-gawa hawezi kufikia daraja yao kwasababu wale walikuwa maswahaba waMtume wa Allah (Rehma na amaniziwe juu yake).

Mara baada ya Salahud-Din Al-Ayy-ubiy kushika hatamu za Misri, watu walitegemea kwamba patazuka mvu- tano wa kugombea madaraka kati yakena Nuuru d-Din Zink.

Salahud-Din Al-Ayyubiy aliliepushahili, na akasisitiza kwamba, yeye ni mtu-mishi mtiifu kwa Zink na lengo lao nimoja, kuwashinda wana Msalaba. Uko wapi moyo kama huu kwa viongozi waKiislamu hivi leo?

Mwaka 1174 Miladia, Nuuru d-DinZink alifariki na kumuacha Salahud-Din Al-Ayyubiy akiwa mtawala wa dolampya ya Kiislamu iliyotangaa tokeaMisri hadi Syria, na kwa hali hiyo akawa

amewazunguka wana msalaba (crusad-ers) nchini Palestina.Kazi ya kwanza ya Salahud-Din Al-

 Ayyubiy baada ya kuwa mtawala mkuuilikuwa ni kuhakikisha kwamba Wais- lamu wameungana na wameandaliwa vya kutosha kuwashambulia wana

msalaba.Lakini, kwanza alilazimika kushu-

ghulikia masalia ya mashia Fatmiyyin walioleta chokochoko kwa lengo la ku- taka kuiteka tena Misri. Kulikuwa nakundi likiitwa ‘Hashaashiiyn’ (wazungu wakaitamka kama ‘Assassins’) ambalombinu yao kubwa ilikuwa ni kuendeshamauaji ya siri (assassinations) ya vion-gozi Waislamu na hata wana msalaba.Hili hatimaye lilishindwa.

Maandalizi ya Waislamu yalichukuamiaka kadhaa. Hadi kufikia mwaka1180 Miladia, Salahud-Din Al-Ayyubiyalikuwa amefanikiwa kuunganishanguvu za Waislamu tayari kuikomboaardhi takatifu ya Baitul Muqaddas (Je-rusalem).

 Wakati huo wana msalaba (crusad-

ers) walikuwa wameparaganyika, ha- wana uongozi mmoja na wakitofau- tiana wao kwa wao. Hii ndiyo hali waliy-okuwa nayo Waislamu wakati walipo-poteza ardhi zao kwa wana msalaba haomiaka 80 nyuma.

Mwaka 1182 Salahud-Din Al-Ayyu- biy alivuka kutoka Misri kwenda ardhizilizokaliwa na wana msalaba na kuanzamashambulizi dhidi ya wana msalaba wa “Franks” ambao asili yao ni Ujerum-ani. Tukumbuke hawa ndio waliomuuaImaad ad-Din Zengi.

Mpinzani mkubwa mwenye nguvuna katili katika wana msalaba alikuwani Reynald wa Chatillon, mmoja wakikosi cha wapiganaji waliojulikanakama ‘Knight Templers’. Hawa ndio waliokuja kuanzisha Umasonia dunianichini ya misingi ya ‘Hashaashiin’.

Huyu Reynald wa Chatillon alikuwa

akiwavamia Waislamu katika ardhi zili-zokaliwa na wana msalaba na kuwauana kushambulia misafara iliyokuwa ik-ienda Makka kwa ajili ya ibada ya hijja.Reynald hata alitishia kuishambuliamiji ya Makka na Madina.

Salahud-Din Al-Ayyubiy hakuvu-

milia vitendo hivi dhidi ya Waislamu naakaapa kumwadhibu Reynald kwamikono yake mwenyewe. Hili lilitimiakatika vita vilivyopiganwa Hittin, kaska-zini mwa Israeli ya leo, mwaka 1187.

 Wana msalaba wal ileta jeshi laokubwa la wapiganaji 20,000 kutoka Je-rusalem kwa ajili ya vita hivi vya Hittin.Jeshi la Salahud-Din Al-Ayyubiy lili- wakabili lilikwa na wapiganaji 30,000.

 Wana msalaba wakipigana kwa staili ya Ulaya walisonga mbele wakiwa wametanguliza wapiganaji waliovaliamavazi ya chuma, lakini walikabiliwa nauhaba mkubwa wa maji ya kunywa.

Hadi mapigano yanaanza, wapiga-naji wa msalaba walikuwa hawana ngu- vu ya kusimama mbele ya Waislamukwa kiu na kuelemewa na mavazi mazi- to ya chuma. Kwa muda mfupi vita vikamalizika kwa ushindi kwa jeshi la Waislamu, lilifanikiwa hadi kumtekaReynald.

Salahud-Din Al-Ayyubiy aliwapamsamaha mateka wote, lakini kama al-ivyoahidi alimuua Reynald kwa mikono yake mwenyewe, malipo stahiki kwamtu aliyewatesa na kuwaua Waislamukwa chuki kubwa.

Baada ya jeshi hilo kubwa la wanamsalaba kuteketezwa, Salahud-Din Al- Ayyubiy akasonga mbele na wapiganaji Waislamu kuelekea Baitul Muqaddasambayo kwa wakati huo haikuwa na ul-inzi madhubuti.

Oktoba 2, 1187 Miladia sawa namwezi Rajab mwaka 583 Hijriyyah,Salahud-Din Al-Ayyubiy aliingia nakuiteka Jerusalem ikiwa ni miaka 88,miezi 2 na siku 17 tangu itekwe na wanamsalaba. Kama Mtume (Rehma naamani ziwe juu yake) alivyowafanyia watu wa Makka, uungwana wa Sala-hud-Din Al-Ayyubiy ulionekana kuto-kana na jinsi alivyowafanyia Wakristo

 wa Jerusalem.Miaka 88 nyuma ya hapo, Wakristo wana msalaba toka Ulaya walipoitekaJerusalem, waliwaua wakazi wote Wais- lamu na Wayahudi mpaka inasemeka-na mitaa ya mji huo ilitiririka damu iliy-ofikia kiwiko cha mguu.(Wikipaedia,

History of Jerusalem During the Mid Ages).

 Waislamu waliposhinda, SalahDin Al-Ayyubiy aliwaruhusu wmsalaba kujikomboa kwa kulipa kkidogo cha pesa kama fidia na wale siomiliki kiasi hicho aliwaruhusu wadoke pasina kulipa. Uungwana ulkwa mshindi wa vita kuwatendea waliowashinda tena waliowaua ndzao hapo kabla?

 Wais lamu kuite ka Jer usakuliamsha ari ya vita vya tatu namwisho vya msalaba kati ya Wakr wa Ulaya dhidi ya Waislamu. Wapnaji wana msalaba walianza kuwardhi takatifu mwaka 1189, miaka  wili tu baada ya ushindi wa Waislam

Kiongozi wa jeshi hili la wana maba alikuwa Mfalme wa Uingerezachard the Lion Heart (Richard mwemoyo wa Simba). Baada ya mapigkadhaa kati ya majeshi ya Richardmajeshi ya Salahud-Din Al-Ayyu yakilinda ardhi takatifu, wana msa walilazimika kurudi Ulaya mikmitupu wakiiacha Jerusalem mikonmwa Waislamu.

Katika moja ya mapigano SalahDin Al-Ayyubiy aling’amua kuwa fa wa Mfalme Richard alikuwa ameuaKwa kutambua kwamba jemadar

 vita zama hizo hawezi kupiganisha j bila kuwa na farasi, Salahud-Din Ayyubiy alimpelekea farasi.

Kwa kitendo hiki, wema wa SalahDin Al-Ayyubiy umebaki kama simza mfano (legend) miongoni mwa w wa Ulaya hadi leo, na ingawa alikadui yao, wanamheshimu sana kukarimu wake hata kwa maadui zak

Uongozi wa Salahud-Din Al-Ay biy na kujitolea kwake muhanga ajili ya dini kulifungua ukurasa mpyumoja wa Waislamu.

Hata baada ya kufa kwake mnamwaka 1193 Miladia, dola ya Kiislaaliyoiasisi ambayo ilipewa jina la Dol Ayubi (Ayyubid Dynasty) na baadDola ya al-Amaalika (Mamluks) ildelea kupambana na uvamizi wa wmsalaba kwa muda mrefu.

 Ardhi takatifu ya Jerusalem na estina zilibaki mikononi mwa Waislhadi mwaka 1917 Miladia zilipotekna jeshi la Waingereza katika Vita K ya Kwanza ya Dunia kwa hadaa Waingereza walipowarubuni Waar wawasaidie vitani. Ardhi hizi sasnakaliwa kimabavu na Israeli.

Tunapoyatafakari matukio ya ki toria yaliyotokea ndani ya mwezi wa jab, hatupaswi kabisa kusahau kukilichonusuru Uislamu wakati uleuvamizi wa wana msalaba ni umoja wna ucha Mungu wa viongozi wao kSalahud-Din Al-Ayyubiy (Allah amhemu).

TUJIKUMBUSHE

Rajab, Mwezi wa Kumbukizi - 2 Vita vya kukomboa Jerusalem vilianza ndani ya Rajab

 Ilipiganwa zaidi ya miaka 100

HIVI NDIVYO ALLAH ALIVYOMUINUA MKOMBOZI WA ARDHI TAKATIFU BAITULL MUQADDAS, SALAHUD-DIN AL-

 AYYUBIY, MKURDI AMBAYE HATA HAKUWA MWARABU,KUONESHA KWAMBA UISLAMU SI DINI YA WAARABU

KAMA MAKAFIRI WANAVYOPENDA IFAHAMIKE

Waislamu wahimizwa kushikamana na itikadiWaislamu nchini wamehimizwa kushikamana na itikadi sahihi ya dini ya Kiislamu, kwani

kufanya hivyo kutawaepusha na misukosuko ya kimaisha na Allah (Subhanaahu Wataal-

lah) atakuwa pamoja nao. Akihutubia mamia ya Waislamu wakati wa swala ya Ijumaa,

hivi karibuni, katika msikiti wa Umar Bin Khatwaab uliopo mtaa wa Jangwani, Dar es

salaam, Sheikh Abuu Musa amewaasa Waislamu kushikamana na njia sahihi ya Uislamu,

kwani hakuna mafanikio pasipo kufanya hivyo. Alisema, ili wanadamu wasalimike na ma-

dhila ya dunia hawana budi kushikamana na ‘aqida’ sahihi, na kwamba fitna zitokanazo na

umiliki wa mali, watoto na madaraka zisiwadanganye, kwani hiyo ni mitihani kutoka kwaAllah ambayo huitoa katika mambo ya kheri na shari. (MWANDISHI WETU)

Page 5: Imaan Newspaper issue 5

7/17/2019 Imaan Newspaper issue 5

http://slidepdf.com/reader/full/imaan-newspaper-issue-5 5/19

www.islamicftz.org

21 Rajab 1436,  JUMATATU Mei 11 - 17, 2015

NA SELEMANI MAGALI

Waislamu wameelezea hofu

 ya kutengwa katika zoezi la uandikishwaji wa wapi-ga kura kwa mfumo wa

kielektroniki huko mikoani kutokana na baadhi ya vituo vya kuandikia kuwekwamakanisani.

Hofu ya Waislamu imekuja kufuatia taarifa ya waangalizi wa zoezi hilo kuwa baadhi ya makanisa yamegeuzwa kuwa vituo vya kuandikisha wapiga kura, jam-

 bo ambalo linakwaza uhuru Waislamukufika maeneo hayo na kuandikishwakutokana na msimamo wa kiimani.

Mmoja wa wananchi, Ustadh Mo-hammed Hamisi wa Kinondoni, jijiniDar es Salaam amesema: “Hili jambo

 limetushtusha sana. Tunashukuru li-meibuliwa mapema na waangalizi. Seri-kali iondoe hivyo vituo mara moja,

 vinginevyo Serikali itaingia katikamgogoro mwingine na Waislamu”.

 Waangalizi kutoka Mtandao wa Asasiza Kiraia wa Kuangalia Chaguzi Tanza-

nia (TACCEO) unaoratibiwa na Kituocha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC) wamesema, waliweza kushuhu-dia vituo vya uandikishaji vikiwa kwenyemakanisa mkoani Njombe.

Baadhi ya makanisa ambayo yalikuwana vituo vya kupiga kura ni pamoja naKanisa la Lutherani Ilembula na Kanisa

 la Pentekoste Ufwala, yote yakiwa Wilaya ya Njombe. Jingine ni Kanisa la KristoI so lway a, l i l i lopo wi lay a y a

 Wanging’ombe. Akizu ngumza na waandishi wa

habari ofisini kwake, Mwenyekiti TACEO, Martina Kabisama, amekiri kupo hali hiyo na kudai kuwa serikali ikiuka jukumu lake kwa kuruhusu vhivyo kuwekwa kanisani.

 Alisema, uwepo wa vituo hivyo kamakanisa ni kasoro kubwa inayohkufanyiwa marekebisho, vinginekunaweza kukasababisha kundi kub

 la waumini wa dini nyingine kuach bila kuandikishwa, hivyo kuwanyhaki yao ya msingi .

Kabisama ameongeza kuwa, kuw vituo hivyo makanisani kunaweza kuzuia watu wengi wakiwemo hata Wak

 to ambao kwa namna moja ama nyinhawapendi kufika katika makanisa hkutokana na sababu wanazozifaham

“Nadhani kuna haja ya kurekebkasoro hizi, kuacha makanisa au nyumnyingine za ibada kutumika kama v

 vya kuandikishwa wapiga kura si sahkwani waumini wa dini nying

 watashindwa kushiriki kutokana woga au kuwa na imani tofauti”, alieKabisama.

Ukiacha kasoro hiyo Kabisaametaja kasoro zingine ambazo zim

 bainika katika zoezi hilo kuwa ni pamna mwitikio mdogo wa wananchi ka

 vituo vya kuandikishwa kwa kile alich taja kuwepo elimu ndogo ya wapiga kinayotolewa juu ya umuhimu wa zohilo.

 Amesema, ili kukabiliana na chanmoto hizo tume ya taifa ya uchaguzi paswa kuongeza idadi ya asasi za kirazitoe elimu hiyo na kuwavutia wanan

 walio wengi kujitokeza kujiandikisha“Katika wilaya ya Ruangwa siku

za mwanzo watu wachache walijitokna hata kituo cha Kitandi Gulioni A27, 2015 tulishuhudia watu 44 peke y

 wakiandikishwa”, alisema KabisamaPia ametaja kasoro nyingine ka

zoezi hilo kuwa ni pamoja na zoezi ku tiliza muda wake hadi kufikia saa  watu kuandikishwa bila kuchukulalama za vidole, zoezi kushindwa ku

 yika kwa wakati kutokana na kukosna kwa mashine za kuandikishia (BVna kundi kubwa la watu kutoandikishkutokana muda kumalizika.

Kufuatia hali hiyo wameishauri tu ya taifa ya uchaguzi kuboresha mchak wa zoezi hilo na pia serikali itimize w bu wake wa kuipa fedha tume.

Zoezi la kuandikisha wapiga kura mfumo wa kielektroniki (Biometric ers registration-BVR) ulianza rasmi

 buari 23, 2015 katika HalmashaurMji wa Makambako mkoani Njombesha kuendelea katika mikoa ya LiMtwara, Ruvuma na Iringa.

Vituo vya kuandikisha wapigakura vyawekwa makanisani

 Wakili Nassoro

aliongeza: “Tulikwenda Ukonga ilikuongea nae atuambie kwa nini ali-hamishwa kutoka Morogoro kulet-wa Dar es Salaam, na kwa nini ape-lekwe gereza la wafungwa (Ukonga)na sio la mahabusu, lakini tuliambi-wa hayupo Ukonga.

“Tulipofika gerezani hapo tu-liones ha vit ambuli sho vyetu nawatu wa mapokezi waliingia ndani,wali poru di wal itu ambi a SheikhPonda hayuko pale”, Wakili Nassoroaliliambia gazeti la Imaan.

Kwa mujibu wa wakili Nassoro,majibu ya Jeshi la Magereza ya sikuya Ijumaa yaliongeza taharuki juuya hali ya Sheikh Ponda, hususanukizingatia kuwa huko nyuma Jeshila Mage reza lime kuwa likiwapa

ushirikiano mzuri tu kila walipota-ka kuonana naye.

 Wa kil i Na ss or o al is em a,hawakujua mabadiliko yale yanamaana gani, kwani mazingira yal-ionesha kuwa Sheikh yuko paleUkonga lakini hawakuwa na taarifarasmi na wahusika walikanushakuwa hayuko pale.

“ Ilitutia wasi wasi”, wakili Nas-soro aliliambia gazeti la Imaan siku

 ya Jumamosi (juzi).Katika hali ya kushangaza zaidi

katika kadhia hii, ndugu wa SheikhPonda walipofika gereza la Ukongasiku ya Ijumaa kumpelekea chakulana mahitaji mengine, chakula

kilipokelewa lakini hawakuruhusi- wa kumuona.

Kutojulikana alipo Sheikh Pondakuliwachanganya pia viongozi waJumuiya na Taasisi za Kiislamunchini, ambapo kupitia kwa Mse-maji wake, Sheikh Rajab Katiba,

 walielezea kuwa wameshtushwa na tukio hilo.

“Hatujui sheikh aliko na hali hiiinatuchanganya sana, inaelekea lol-ote linaweza kutokea kwa Sheikh

 wetu. Wahusika inabidi wawe wazi, Waislamu tunataka kujua SheikhPonda yuko wapi, maana katika his-

 toria ya nchi hi i wat u wam ewahikupotea katika mazingira ya kuta-

 tanisha”, alisema Katimba.

Mashataka ya Sheikh Ponda:Sheikh Ponda awali alikuwa

ameshtakiwa kwa kuvamia kiwanjacha Markaz Chang’ombe jijini Dares Salaam baada ya Bakwata wal-iokabidhiwa mali za iliyokuwa Ju-muiya iliyovunjwa ya Waislamu wa

 Afrika ya Mashariki (EAMWS) ku- wauzia wafanyabiashara kinyumena taratibu za kusimamia mali za

 waqfu.Kesi hiyo iliyokuwa imefunguli-

 wa mahakama ya Kisutu jijini Dares Salaam ilimalizika kwa SheikhPonda kufungwa kifungo cha nje

cha mwaka mmoja. Wakati akishughulikia rufaa ya

kesi yake na huku akitumikia kif

go hicho cha nje, Sheikh Ponda a wenda mji ni Morogo ro mw2013 kuhudhuria sherehe za I

 Adh’ ha ambako nus ura apotmaisha baada ya kupigwa risasi.

 Wakati akipatiwa matibabumajeraha ya risasi Hospitali ya TMuhimbili, Sheikh Ponda alitpingu na kafunguliwa mashitMahakama ya Hakimu Mkazi Mrogoro akituhumiwa kuvumasharti ya kifungo chake cha kesi ambayo ilikuwa inaendehadi sasa.

 Wakati kesi ya Morogoro ikiguruma, Sheikh Ponda alishinrufani yake Mahakama ya Kisuna siyo tu kuachiwa huru, balikuruhusiwa kuwashitaki walio

mali ya waqfu ya WaislaChang’ombe Markaz.

Sheikh Ponda atoweka

NATOKA UK 2

WAANGALIZIKUTOKA

MTANDAOWA ASASI ZA

KIRAIA WAKUANGALIA

CHAGUZITANZANIA(TACCEO)

UNAORATIBIWANA KITUO

CHA SHERIA

NA HAKI ZABINADAMU

(LHRC)WAMESEMA,WALIWEZA

KUSHUHUDIA VITUO VYA

UANDIKISHAJI VIKIWAKWENYE

MAKANISAMKOANINJOMBE

Mwenyekiti wa Tumeya Taifa ya Uchaguzi,

 Jaji Mstaafu DamianLubuva.

HABARI

Page 6: Imaan Newspaper issue 5

7/17/2019 Imaan Newspaper issue 5

http://slidepdf.com/reader/full/imaan-newspaper-issue-5 6/19

HUTOLEWA NA KUCHAPISHWA

The Islamic Foundation, P.O. Box 6011 Morogoro, Tanzania, E-mail: [email protected]

MHARIRI MTENDAJI: 0715 559 944, MHARIRI: 0786 779 669, AFISA MASOKO: 0785 500 502

TOVUTI: www.islamicftz.org

15 Rajab 1436,  JUMATATU May 4 - 10, 2015

TAHARIRI / UCHAMBUZI6

Tangu wiki iliyopita

kumekuwa na mfu- lulizo wa mvua nyingizinazoendelea kunye-

sha katika msimu huu wa mvuaza masika ambazo zimeletamaafa makubwa kwa wananchikatika mikoa ya Dar es Salaam,Mtwara, Lindi, Tanga, Pwani,Kagera, Zanzibar na maeneomengine ya nchi.

Ni kweli mvua ni neemakutoka kwa Mwenyezi Mungu,

 lakini zinapozidi zinaweza ku-sababisha maafa. Kutokana namvua hizo maafa mengi yame-

 jitokeza. Watu zaidi ya nane (8) waliarifiwa kufariki Dar es Sa- laam, huku familia zaidi ya 500zikipoteza makazi au mali zaokuharibika. Kadhalika, miun-dombinu ya barabara na ma-

daraja nayo imeathirika.

 Wat ab ir i wa na tu am bi akuwa mvua hizo zinatarajiwakuendelea kunyesha hadimwisho wa mwezi huu, na kwasababu hiyo basi, tunapaswakuchukua tahadhari. Ni kuto-ch ukua tah adh ar i ndiokumepelekea matatizo hayakujitokeza kila msimu nakuathiri hata maeneo ambayo

 yamepimwa.Hata hivyo, huu si wakati wa

kulaumiana bali kusaidiana, nandio maana sisi, gazeti la Im-aan tunawaasa Waislamu na

 wananchi wote kwa ujumla ku-saidiana katika maeneo yetu yamakazi pale miongoni mwetu

 tunapofikwa na maafa katikakipindi hiki cha mvua.

Mwenyezi Mungu anasema:

“Na saidianeni katika wema na

uchamngu. Wala msisaidianekatika dhambi na uadui. Namcheni Mwenyezi Mungu.Hakika Mwenyezi Mungu nimkali wa kuadhibu” (5:2).

Inaelezwa pia kuwa Uisla-mu ni kama mwili mmoja,kikiumwa kiungo kimoja

 vilivyobaki pia huathirika. PiaMtume (Rehma na amani ziwe

 juu yake) amesema Muislamundugu yake Muislamu.

Kutokana na ushahidi huo,ni wazi kuwa tunao wajibu kwakila mmoja wetu kumsaidiamwenzake mwenye tatizo. Sisi

 tunaamini kuwa wakati Seri-kali ikijipanga kuwasaidia

 waathirika wa maafa haya ya-nayoendelea; sisi wenyewe ka-

 tika maeneo yetu tuna wajibu

 wa kuwahami ndugu, jamaa na

majirani kwanza tatizo linapo- tokea kabla Serikali haijakuja.

Tunapenda pia kuwashauri wananchi wanaoishi mabonde-ni kuhama kwenye maeneohayo ili kuondokana na adhahizi za mafuriko na uharibifu

 wa mali za kila mwaka. Serikali yenyewe pia ina wajibu wa ku- wawezesha watanzania wen-zetu hawa kwa kuwatafutiamaeneo mengine, hususan

 wa le am ba o ha wa jaw ahikupatiwa viwanja hivyo hapokabla. Kwa upande wa Serikali,

 tunaishauri ijifunze kutokanana maafa haya, hususan up-ande wa miundo mbinu. Miun-do mbinu bora ni ile ambayoinaweza kutusitiri katika vipin-di vyote, kiangazi na masika.

Kwa hali tunayoiona sasa n

 wazi kuwa miundombinu yetuhaijawa rafiki. Katika jiji la Daes Salaam, ushahidi wa ubovu

 wa miundo mbinu uko dhahirkupitia foleni, mahandakmakubwa na mafuriko yanayosababisha foleni ndefu.

Kama tulivyotangulia kusem a, m vua ni neem a y aMwenyezi Mungu na jamii inapaswa kuelewa kuwa yote yanayojitokeza ni makadirio yakMuumba, hivyo tulichukulie‘janga’ hili kama ni sehemu yamaisha ya mwanadamu, kwanMola wetu hutahini waja wakekatika mambo ya kheri nashari.

Tunamuomba Allah atusitirkwa haya na mengineyo. Amiin.

Tusaidiane katika maafa ya mvua

Tangu vita vianze huko

 Yemen ukifwatilia sehemukubwa ya habari zinazo-andikwa na waandishi

 wetu katika vyombo vyetu vya Kiis- lamu nchini Tanzania utagunduakuwa ipo haja ya vyombo vyetukuwa makini zaidi katika kuripoti

swala hili.Namna vinavyoripoti inatia sha-

ka kama kweli vimefanya utafiti wakutosha juu ya kadhia hii, maana

 vimekuwa vikiulaumu na kuushu- tumu upande mmoja tu wa mgogorohuo pasina kutueleza chochotekuhusu upande wa pili.

Unapofwatilia vyombo hivi, waandishi wake wanatuaminishakuwa Saudi Arabia imekurupukakiwazimu wazimu na kuingia Yem-en kuanza kuuwa watu kiholela nakuharibu miundombinu ya nchihiyo na hivyo ndio upande pekee wamgogoro unaopaswa kubebeshwamzigo wa lawama.

Ukweli ni kwamba vita vya Yem-en si vya leo, vilianza muda mrefu,

 lakini wakati huo wahusika wa- likuwa ni Wahouth na Serikali ya Ali Abdallah Saleh, huku Serikali yaSaudi Arabia ikiwa msuluhishi wao.

Kwa sasa vita vimepanuka sana.Sababu za kupanuka vita hii ni tatu;Ushiriki wa askari waasi wanaomu-unga mkono rais aliyeondolewamadarakani kwa nguvu ya umma,

 Ali Abadal lah Saleh, Uwepo waaskari watiifu kwa Rais Abdo RabouMansour na kujiingiza nchi ya Irankwa kuwapatia silaha wanamgam-

 bo waasi wa Kihouth. Awali ugomvi wa Yemen ulikuwa

ni kupinga muungano na kutori-dhika kwa Wahouth na siasa ya nda-ni na nje ya Rais Ali Abdallah Saleh.

Taarifa za mitandaoni zinaone-

sha kuwa, mmoja kati ya viongozi

 wa Wahouth, Badruddin Al-houthni mshirika mkubwa wa serikali yaIran, na kupitia ushirika huo, mwa-ka 2009 Iran ilianza kupeleka she-hena za silaha kwa Wahouth kwanjia ya siri.

Na baada ya Ali Abdalah salehkuondolewa madarakani kwa ngu-

 vu ya umma, Urais wa nchi hiyoukashikwa na Abdo Rabboh Man-sour Hadi. Ali Abdallah Saleh haku-ridhika na uamuzi huo.

 Ali Abdallah Saleh alianza har-

akati za chini kwa chini na kufaniki-

 wa kuunganisha wanajeshi wa-naomuunga mkono na wale wanamgambo wa Kihouth waliokuwamaadui zake wakati wa utawala

 wake.Lengo la Ali Abdallah Saleh na

genge hili ni kuiondoa Serikali halali ya Abdo Rabboh Mansour madar-akani kwa mtutu wa bunduki.

Ikumbukwe, jeshi la serikali ta- wala lilidhoofishwa kwa ndani nahalikuwa na nguvu tena ya kuwezakupambana na makundi ya waasi

na hatimae Rais Abdo Rabboh

Mansour akatimuliwa na kukimbil-ia nchi jirani.Ni kukosa uadilifu kuilaumu

Saudi Arabia pekee katika balaa hii ya vita vya Yemen bila ya kusomakikamilifu sababu za vita hivi na wa-husika wakuu walioisababisha.

 Anayestahiki lawama kubwa ka- tika vita ya Yemen ni Ali AbdallahSaleh aliyesababisha fitna hii, na wapili ni Iran kwa kujiingiza katikamzozo wa Yemen ambao hausikinao kwa ndewe wala sikio.

Katika kipindi hiki cha vita, sila-ha zote walizonazo Wahouth wana-pata kutoka Iran.

 Wahouth ni waasi na kila mtuanalijua hilo. Sasa ni kwa nini tu-ibebeshe Saudi Arabia peke yake la-

 wama hii? Kwani ni lipi lengo la Iranna Houth katika sakata hili kama si

kutaka kueneza Ushia na kuchochea vita vya kiitikadi? Nini lengo la Irankama si kutaka kuleta vita baina ya

 Waarabu na Wafursi? Au nini lengo la Iran kama si ku-

 taka kuchochea ugaidi na kuleta vita vya Wayemen kwa Wayemen ili ha- timae Iran kidogo kidogo ipate na-fasi ya kuidhibiti Saudi Arabia nanchi za ghuba kwa kila upande, nahatimae kufikia lengo la kujitanuakidini, kisiasa na kiuchumi?

Nimalizie nasaha zangu kwakueleza sababu tano zilizoipelekeaSaudia Arabia na nchi za ghuba ku-ingia katika vita hii.

Mosi, hatari ya kujisogeza kwaIran kwenye mipaka ya nchi za ghu-

 ba. Pili, kuimarika kwa ushawishi wa Iran kusini mwa ghuba ya Uar-abuni.

Tatu, Wahouth kwenda kinyumena makubalianao ya Novemba 2011

 ya nchi za Kiarabu, kwa kuchukuahatua ya kuipindua Serikali iliyomadarakani kwa nguvu ya mtutu

 wa bunduki.Sababu ya nne ni kulinda masla-

hi ya nchi za ghuba yaliyo katika ar-dhi ya Yemen na tano, kuikwamuaBab al- Mandab kutoka kwenyeudhibiti wa Wahouth, kwani kim-kakati hili ni eneo nyeti kwa usalama

 wa mataifa ya ghuba na ndio njiakuu ya meli za mizigo na mafuta namaslahi mengine ya kiuchumi.

0773 215 898

 Vita vya Yemen, vyombo vyetuvinapaswa kuwa makini zaidi

UKWELI NI KWAMBA VITA VYA YEMEN SI VYA LEO,

 VILIANZA MUDA MREFU, LAKINI WAKATI HUO

WAHUSIKA WALIKUWA NI WAHOUTH NA SERIKALI

 YA ALI ABDALLAH SALEH

SHEIKH ABDALLAH BAWAZIR

NASAHA ZA WIKI

Page 7: Imaan Newspaper issue 5

7/17/2019 Imaan Newspaper issue 5

http://slidepdf.com/reader/full/imaan-newspaper-issue-5 7/19

www.islamicftz.org

21 Rajab 1436,  JUMATATU Mei 11 - 17, 2015

HAZINA YETU

NA YUSUFU AHMADI

Dhana iliojengeka kwa wengi ni kuwa uwezo wakuzungumzia masuala ya kitaalamu unatokana

na elimu kubwa ya ‘kisekula’.Lakini wapo baadhi ya watu

hawakusoma sana elimu ya kiseku- la lakini Allah amewabariki ufaha-mu mkubwa katika kuzungumzia

fani mbalimbali.Miongoni mwa hao ni Sheikh

mashuhuri Afrika Mashariki naKati, aliyekonga nyoyo za waumini wengi wa dini ya Kiislamu, mwenyeufasaha wa kuzungumza na kush-awishi, Marehemu Nassoro Bachu.

Sheikh Hamisi Yussuf, mwa-nafunzi wa Sheikh Bachu amese-ma Sheikh Bachu aliishia darasa lasaba, licha ya uwezo mkubwa waakili na ufahamu aliokuwa nao ka- tika masomo.

U p eo n a ufaham u w akemkubwa wa akili unadhihirikakutokana na uwezo wake wa ku-zungumzia fani mbalimbali,ikiwemo fani ya elimu ya viumbe(biology) na jiografia kwa umahirimkubwa sana.

 Ak iz un gu mz ia hi st or ia ya

mwalimu wake huyo, Sheikh Yus-suf alisema, Sheikh Bachu alizali- wa mwak a 195 1 kat ika ene o laFuoni nje kidogo ya mji wa Zanzi- bar.

Baada ya kuhitimu darasa lasaba, Sheikh Bachu hakuendeleana elimu ya kisekula kutokana na vikwazo mbalimbali, ingawa watu waliomfahamu enzi hizo wanase-ma alikuwa hodari sana darasani.

“Kwa watu ambao walisomanae walikuwa wanasema nafasi yaSheikh Bachu darasani ilikuwamtu wa kwanza na wa pili tu”, al-isema Sheikh Yussuf.

 Vikwazo vinavyotajwa kumzuiaSheikh Bachu kuendelea na maso-mo vilitokana na mambo mbalimbali ya kijamii, ikiwemo ubaguzi wa rangi ,anasema Sheikh Yussuf

ambaye anaamini Sheikh Bachualifelishwa kutokana na kuwa naasili ya Uhindi.

Kwa upande wa elimu ya dini,Sheikh Bachu alipata elimu yake visiw ani Zanz ibar na hakuwah ikwenda nje ya visiwa hivyo kwaajili ya kusoma.

Kuteuliwa kuwa Amir:Marehemu Sheikh Nassoro Ba-

chu ambae alibobea katika fani ya tafsiri ya Qur ’an aliteuliwa kuwa Amir wa Masjid Sunna akim rithimwalimu wake Sheikh Said Tum- ba ambaye alistaafu uongozi.

Baada ya Sheikh Tumba kus- taafu, alifwatwa na Mzee Othmani, Ally na Mzee Mwinyi na kumuom- ba ateue miongoni mwa wanafunzi wake kiong ozi (Amir) w a kuen-deleza Masjid Sunna.

Sheikh Tumba ambaye alipitiamisukosuko mingi kutoka Serika- lini alip endekeza Shei kh Bachuawe Amir kuanzia mwaka huo,1979.

Kwa mujibu wa Sheikh Yussuf,kustaafu kwa Sheikh Tumba kuli-changiwa na Serikali, enzi za uta- wala wa Rais Aboud Jumbe,mwaka1978, ambapo alimfungia kufanyashughuli za uongozi na da’awa.

Kufungiwa kwa Sheikh Tumbakulitokana na mahubiri yake yalio-zungumzia masuala tata ya mwan-damo wa mwezi, maulid, na uso-maji hitma.

Misukosuko toka Serikalini:Baada ya Sheikh Bachu ku-

chukua mikoba ya mwalimu wake

Sheikh Tumba, naye alipitia misu-

kosuko kama mwalimu wake. Alipokea vitisho kutoka Serika-

 lini na kwa baadhi ya makadhi waZanzibar waliotamani kumfungiashughuli zake.

“Kadhi wa wakati ule ambae si- tamtaja j ina alimuita Sheikh Ba-chu zaidi ya mara tatu ofisini kwakeakimtisha na kumpa changamotoasome na atafsiri Qur’an mbele yake kama yeye ni Sheikh kwel i”,amesimulia Sheikh Yussuf.

Kwa mujibu wa maelezo yaSheikh Yussuf, mahubiri ya mare-

hemu Sheikh Bachu ambayealikuwa na misimamo isiotetereka yal iin yim a usi ngi zi Serik al i yaMapinduzi ya Zanzibar na hivyomara kadhaa alijikuta mikononimwa jeshi la polisi, japo hakuwahikushtakiwa wala kufungwa.

“Wakati ule Zanzibar haikuwana mfumo wa vyama vingi vya sia-sa, hivyo yeye ndio alionekanakama chama cha upinzani na aduimkubwa wa Serikali, kwa kuwaalikuwa akisema ukweli”, Sheikh Yussuf alifafanua.

 Akitoa mfano, anasema, SheikhBachu aliwahi kutoa darsa kuhusuumuhimu wa waajiri kuwatendea vizuri wafanyakazi wao. Ilikuwa nikipindi cha kuelekea uchaguzi nahivyo akaonekana mbaya na kupa- ta misukokusuko ya Serikali.

Sheikh Nassoro Bachu na Sia-sa:

Miongoni mwa vitu ambavyoMarehemu Sheikh Nassoro Bachuna wanafunzi wake walijiepushanavyo ni siasa za kijahili (kijinga)na kibaguzi.

 Akifafanua hilo, Sheikh Yussufanasema: “Hatukuwahi kumsikiaakisema siasa ni haramu. Yeyemwenyewe alikuwa anasema,Mtume Muhammad (Rehma naamani ziwe juu yake) alikuwa nimwanasiasa.

Hata hivyo Sheikh Bachu alip-inga siasa za kijahili(kijinga) za ku-uana na kubaguana.

Sheikh Yussuf anaongeza,

“Sheikh Bachu alikwepa kuchukuaupande wowote kisiasa na kuwa- bagua watu, lengo likiwa ni kufiki-sha ujumbe wa Uislamu kwa watu wote”.

Kuhusu elimu ya kisekula,Sheikh Bachu alihimiza watu was-ome ikiwezekana hadi vyuo vikuu.

“Na hapa tulipo ni moja ya skulizake alizozijenga ili watu wasomeelimu ya kisekula”, anasema Sheikh Yussuf.

Urithi wake hapa duniani:Marehemu Sheikh Bachu ata-

kumbukwa kwa kuanzisha darsaza akina mama visiwani Zanzibarili kuwainua kielimu.

“Sheikh Bachu alianzisha darsaza akina mama na kuziendeleza. Wakati ule wanawake wa Kiislamu

hawakuwa na fursa nyingi za kuso-ma dini yao”, anasimulia Sheikh Yussuf.

Sheikh Yussuf anasema, Bachualisaidia sana wanawake kusoma,na baadhi ya walionufaika leo hii ni walimu katika vyuo vikuu mbalimbali vya kawaida na madrasa.

Kadhalika, Sheikh Yussuf alise-ma, miongoni mwa mambo ya ku-kumbukwa kwa Sheikh Bachu nipamoja na ushiriki wake katika ku- toa elimu ya uvaaji h ijab visiwaniZanzibar, mpango ambao ulifani-kiwa sana.

Katika uandishi, marehemuSheikh Nassoro Bachu kwa ushiri-kiano na wanafunzi wake wal-iandika kitabu cha ‘Muandamo wamwezi’.

Pia, Sheikh Bachu hakuwambinafsi wa elimu yake, aligawanaelimu na wanafunzi na Waislamukwa ujumla kupitia darsa na ma- waidha yake.

 Wanafu nzi wa Sheikh Bachu wametawanyika kila mahali dunianzima, ikiwemo nchi za Kimaghar-ibi na Saudi Arabia. Miongonimwa wanafunzi wake mashuhurini Sheikh Mselem Ally, Said Gwiji,Chichi na Hamadi Nassoro.

Kuugua na kifo chake:Mwaka 2004 katika mwezi wa

Ramadhani akiwa katika darsazake msikiti wa Raha Leo, Visi- wani, Sheikh Bachu alipatwa namaradhi.

Kwa mujibu wa Sheikh Yussuf,Sheikh Bachu alijiwa na kitu kisi-

cho cha kawaida wakiwa darasanihapo, ambapo walishangaa nakuhisi Sheikh alipata stroke (msh- tuko).

Sheikh Yussuf anasema, kuan-zia hapo hadi mauti yanamkutamarehemu Nassoro Bachu haku-fundisha tena darsa kubwaisipokuwa zile ndogo ndogo za ny-umbani tu.

Sheikh Bachu alifariki Febuari13, 2013 katika eneo la Chukwani,Zanzibar kwa ndugu yake - Abdal- lah Bachu na kuz ikw a ene o laDonge. Sheikh Bachu aliacha wake watatu na watoto 15.

Tunamuomba Allah Subhaana-hu Wataallah amrehemu SheikhNassoro Bachu, amsamehe pale al-ipokosea na ailaze roho yake ma-hali pema peponi.

SHEIKH BACHU Yungali ‘hai’ miongoni mwa Waislamu Mawaidha yake bado yanufaisha wengi

 SHEIKH BACHU HAKUWA MBINAFSI WA ELIMU YAKE, ALIGAWANA ELIMU NA WANAFUNZI NA WAISLAMUKWA UJUMLA KUPITIA DARSA NA MAWAIDHA YAKE.

Page 8: Imaan Newspaper issue 5

7/17/2019 Imaan Newspaper issue 5

http://slidepdf.com/reader/full/imaan-newspaper-issue-5 8/19

www.islamicftz.

21 Rajab 1436,  JUMATATU Mei 11 - 17,

8

Mambo ya msingi kwa

khatwibu wa IjumaaIlipoishia: Khatwibu aelewe

 kwamba kuna kundi la Waislamu hawajihus ishi na matuki o mbal imbali yanayouhusu umma na wala hawajali. Kundi hili linahita- ji kuzi ndul iwa ili wajue nini ki-naendelea katika kadhia za Wais- lamu . Mtu wa kari bu nao zaid iambaye watu hawa wanaweza kumtegemea ni khatwibu wa iju-maa…

Sita, kuoanisha mada na was- waliji : Khatwibu atoe mada am- bayo inae ndan a n a wana oswa likatika msikiti wake. Kwa mfano,iwapo waumini wengi katika

msikiti husika ni wageni, kutoamada ambayo itakuwa inahusumatatizo ya jamii ya mahala haposi sawa.

Na vile vile msikiti ambaohuswaliwa na wanafunzi wengi sihekima kutoa khutba inayohusumatatizo ya ndoa kwa sababu wa-nafunzi wengi watakuwa hawa-

 jaoa.Kwa hiyo ni wajibu wa khatwi-

 bu kuelewa vilivyo hali za waswali- ji katika msikiti wake na achaguemada ya khutba inayoendana nahali zao na yale wanayoyahitajia.

Saba, kuwa na elimu ya kuto-sha kuhusu khutba: Khatwibu waijumaa aepuke kufupisha madakwa sentensi fupi fupi pasina ku-

fafanua watu waelewe. Vile vile

asilete ufahamu au fikra zake baliaegemeze khutba yake katika dalili

za kisharia katika Qur’an na Sun-

na na kauli za wanawazuoni naahakikishe kwamba msikilizaji wa

khutba anakinai kwa maelezo yake

na ananufaika.Nane,  kuelezea kwa kina:

Khatwibu awe na ujuzi wa kuto-sha na sahihi kuhusu mada ai-

 toayo . Ujuzi wak e utokane nautafutaji (bahthi) wake katikaQur’an na hadith za Mtume zilizosahihi na wala asitumie hadithdhaifu (Dhu’afaau) au za kutunga(Mawdhu’u).

Kwa hiyo ni wajibu wa khatwi- bu ajue jinsi ya kuthibitisha hadithsahihi katika vitabu vya hadith zaMtume (Rehma na amani ziwe

 juu yake) au ajipambe na yale yali- yosemwa na wanawazuoni kuhusu

daraja ya kila hadith anayotakakuitumia katika khutba.

Tisa, kuepuka tetesi: hai- takikani khatwibu kurukia tetes iazisikiazo mtaani au katika vyo-mbo vya habari na kuegemeza aukusheheneza khutba yake nakhabari hizo pasina kuthibitishana kubaini ili kujua uhakika wake.

Kumi, masuala ya kitaalamu:Khatwibu anaweza kuzungumziakuhusu masuala ya utabibu aufani yoyote makhsusi. Mtu anapo-zungumzia jambo ambalo si fani

 yake , aweza kukosea sana . Kwahiyo khatwibu afanye juhudi ku-

 jua habari hizo kwa kina kutokakwa watu wa fani husika kuepukakusema maneno ya kushangaza

kwa watu ikawa fedheha kwake.

Kumi na moja, kunasibishmada na matukio, mahali n

 wakati: Kh atwibu anaweza akazungumzia fadhila za kudirik‘Laylatul Qadr’ usiku wa thelathi

 wa Ramad han , jambo amb alhalipo. Au panaweza kutoke

 tukio kubwa nchini, mjini au kij jini na waswaliji wakakaa kusubikhutba itazungumziaje tukio hilili wajue msimamo wa kisharukoje, na wasisikie kitu. Mifanhii ni kuonesha umuhimu wkhatwibu kunasibisha mada nmatukio, mahali au wakati.

Kumi na mbili, mada juu y

 jambo moj a: Hai tak ikani kwkhutba kuchanganya mambmengi, kiasi kwamba msikilizaasijue khutba imezungumzia ninhaswa. Si vema khutba kushehenkila kitu kinachomjia khatwibkichwani kuhusu matatizo yumma, hadi akamchanganymsikilizaji wa khutba.

Ni vizuri khutba ikawa juu ym a u d h u i m o j a m u h i minayoendana na mahali, wakati nmatukio katika wiki na ishehenhoja na ufafanuzi wa kisharia kwdalili kutoka katika Qur’an, sunnna kauli za wanawazuoni na mfano hai katika jamii juu ya maudhui hiyo.

 Itaendelea toleo lijalo.

Mpaka tutakapofaidika na Khutba za Ijumaa - 4

SHEIKH TAWAKKAL JUMA

KUTOKA KATIKA QUR’AN’ NA SUNNAH

Wa k a t i w a s o m i

 waku bwa na mab-ingwa wa sayansi wa-nashangazwa na

namna Qur’an inavyorandana na tafiti mbalimbali za kisayansi, hebu tuangalie walau maandiko kidogo ya vitabu vingine vya kidini ambavyo baadhi ya wasomi walidai eti ndikoMuhammad alikonakili Qur’an

 vinavyosema juu ya mambo yakisayansi.

Katika Mambo ya Walawi, 11:1-23, Biblia inataja sifa za wanyamambalimbali wanaoliwa na wale am-

 bao hawaruhusiwi kuliwa.Mambo ya Walawi 11:20 inase-

ma hivi: “Tena vyote vitambaavyo vyenye mabawa viendavyo kwa mig-uu minne, hivi ni machukizokwenu”. Katika Biblia ya Kiingereza“vitambaavyo vyenye mabawa vien-davyo kwa miguu minne”, vimeta-

 jwa kama “flying insects that walkon all fours”.Hapa Biblia inakataza kula

 wadudu au insects wenye miguuminne. Haijapatapo kutokea tangudunia kuumbwa hadi leo kuoneka-na au kuwepo mdudu au insectmwenye miguu minne!

Kwa mantiki hii, ni jambo mu-

hali na linalotia wasiwasi ufunuoueleze watu wasile kitu ambachohakijawahi kutokea, kwa sababu nirahisi kwa mfano, kwa wanasayansikulipinga hilo, maana wanatuam-

 bia kuwa katika wadudu, mdudumdogo sana ana miguu sita, walahapajawahi kutokea mdudumwenye miguu minne. Hivyo Mun-gu anawakataza watu wasile kituambacho hakiko au hajawahikukiumba!

Mfano mwingine, ni kile kifungukinachoeleza sababu ya kuumbwakwa upinde wa mvua au rainbow.

Ukisoma Biblia katika kitabu chaMwanzo 9:9-17 utaona Bibliainaeleza kuwa upinde wa mvuaumeumbwa na Muumba ili um-

kumbushe apunguze mvuainapokuwa kubwa ili isije ikazidi nakuleta maafa kama yale yaliyotokea

 wakati wa Nabii Nuh! Hivi ni kweliMungu ni msahaulifu kiasi ahitajikukumbushwa?

Ukweli ni kuwa upinde wa mvuahauna uhusiano na kuzidi au ku-pungua kwa mvua, bali ni mambo

 ya kupinda na kuak isiw a kwamwanga reflection and refraction of light! Hivi ndivyo wanasayansi wa-navyoeleza na ndiyo maana upinde

 wa mvua huonekana mchana!Ndani ya Qur’an kuna sura maa-

 lum inayoitwa Suratu Maryam yenye aya 98 ambayo pamoja namaudhui nyingine inazungumziana kutegua kitendawili cha BikiraMaria na mwanawe Issa au Yesu, ki-

 tendawili cha utatu mtakatifu nakuwa Yesu ni Nabii miongoni mwaManabii wa Allah, si Mungu wala siMwana wa Mungu na siku ya Qiya-ma atawakataa wale waliokuwa

 wakimwita Mungu au Mwana waMungu.

Kisa cha namna alivyozaliwa

 Yesu kinatajwa wazi katika sura hii ya 19 kuanzia aya ya 16 hadi 33. Ki-sha aya tatu zinazofuatia; yaani ya34, 35, na 36 zikasema hivi:

“Huyu ndiye Issa mwana waMaryam. Hii ndiyo kauli ya hakiambayo (Wakristo) wanaifanyiashaka. Haiwi kwa Allah Kufanyamtoto; Ametakasika, Anapolitaka

 jambo basi Huliambia kuwa; nalo likawa. Na hakika Allah ni Mola wangu na Mola wenu. Basi muabu-duni. Hii ni njia iliyonyooka”.

Nawaomba wakristo waisomesura hii ya Qur’an kisha walingan-ishe na yale yaliyomo katika Bibliakuhusiana na kuzaliwa kwa Yesu.Bila shaka watastaajabu kama alivy-okuwa akiistaajabu rafiki yangummoja niliyekuwa nikisoma nayekidato cha tano na sita nilipokuwanikimsomea sura hii. Kila siku alita-ka niirejee rejee huku akiniuliza kwamshangao mkubwa kuwa, kwelihaya yametajwa ndani ya Qur’an?!!!Qur’an ni chimbuko la elimumbalimbali na kwa hakika ni nuru

 yenye kumuongoza mwanadamu

katika maisha ya hapa duniani naakhera.Katika kitabu chake; “A Concise

Reply to Christianity, A Muslim View,” ukurasa wa 38, Gary Miller,raia wa Canada na mwanamahesa-

 bu aliyekuwa mfanyakazi wa Kan-isani na mtangazaji, ambaye alisil-imu, ameiita Qur’an: “The Amazing

Qur’an”, yaani Qur’an Yenye Kustaa- jabisha au Kushangaza.

Katika maelezo yake anasemakuwa, Qur’an haiwashangazi Wais-

 lamu tu, bali hata wasiokuwa Wais- lamu inawashangaza sana.

 Anaeleza kuwa, jambo moja am- balo huwashangaza sana wasiokuwa Waislamu ni pale wanapoisomaQur’an huikuta tofauti na walivy-okuwa wakitarajia; dhana yao nikuwa wanaposoma Qur’an wanaso-ma kitabu cha zamani kilichokujakarne 14 zilizopita, tena jangwani.

Kwa hiyo matarajio yao ni kuku- ta kimekaa kijangwa jangwa! Mara wanapoifungua na kuanza kuisoma wanakuta inazungumzia bahari nahata vilivyomo ndani ya bahari.

Mara wanakuta ndani mambohata ya sasa kabisa kama mabadi-

 liko ya tabia nchi au global warmingnk. Wanakuta pia inazungumzia

sayari, jua, mwezi, nk.Ndani ya Qur’an kuna elimu ausayansi mbalimbali. Juhudimbalimbali, tafiti na gunduzi zina-zoonyesha ukweli wa Qur’an kisay-ansi, ni kazi ndogo sana kulinganana maajabu mbalimbali ya kitabuhichi kitukufu, ambacho maajabu

 yake hayaishi wala hayataisha.

Qur’an, Biblia na sayansi

SHEIKH MUHAMMAD DUWAYSH

MLINGANIAJI

Page 9: Imaan Newspaper issue 5

7/17/2019 Imaan Newspaper issue 5

http://slidepdf.com/reader/full/imaan-newspaper-issue-5 9/19

www.islamicftz.org

21 Rajab 1436,  JUMATATU Mei 11 - 17, 2015

Katika ukuta mmojamjini Beghazi, Lib- ya kuna maandishi;“Get Free or Die

Trying”, yaani,“Kuwa huru aukufa ukijaribu”.Hii ndiyo kaulimbiu ya wale waitwao wahami-aji ‘haramu’ kutoka Afrika

kwenda Ulaya. Na kweli wengi wanafika huko wanakotaka ku-fika-Ulaya, lakini wengine wen-gi hufa njiani.

Kiongozi wa Chama cha Up-inzani, UKIP cha nchini Uinge-reza, Nigel Farage, alipoulizwanani wa kulaumiwa kwa wimbihili la wahamiaji ‘haramu’ lililoi-kumba Ulaya? Alijibu:

“Kwa kweli ni vitendo vyanchi za Ulaya vilivyosababisha

 tatizo hili, ni ulimbukeni waSarkozy na Cameron kuipigamabomu Libya na kuisambarati-sha kabisa”.

Huu ni mtazamo mmoja wa tatizo la wahamiaji ‘haramu’ kutoka

 Afrika kwenda Ulaya, ambapo wen-gi maisha yao hupotea kwa kufa maji baharini katika mitumbwi iliyoshe-heni watu wakiimba - ‘Kuwa huruau kufa ukijaribu’.

Bajeti za kugharamia huduma zauokoaji na za kibinadamu zime-ongezeka kwa majeshi ya baharini yaMalta, Italia, Ugiriki na Hispania.

Hivi sasa Bunge la Ulaya linajadi- li hatua za kuchukua, ambapo maaz-imio kumi (10) yamepitishwa kuka- bili hali hiyo, ikiwemo hatua zakijeshi za kuharibu mitumbwi inayo- tumika kuvushia wahamiaji.

Lakini wahamiaji hawa waliku- wepo kabla hata ya Libya kuvamiwa.Ni busara basi kujiuliza sababu za wimbi hili, uhuru upi wahamiaji wa-naoutafuta huko Ulaya na nani alau-miwe?

Katika kitabu, “The ImmigrationInvasion: How Third World Immi-

gration Is Destroying First World”,mwandishi Arthur Kemp anaandi-ka: “Ulimwengu wa tatu ni matokeo ya (matendo) watu wa ulimwengu wa tatu”.

Kwa maneno mengine, ni Afrika yenyewe inayostahili kujilaumu kwa wimbi hili la wahamiaji ‘haramu’ aukwa usahihi tuwaite wakimbizi,kwani kuhama gani huku anakoha-ma mhamaji mpaka kuhiari hatakufa?

Kwa upande wake mwandishi Walter Rodney, katika kitabu chake,“How Europe Underdeveloped Afri-ca”, anadai kwamba, mataifamakubwa yakiwemo yale ya Ulayandiyo sababu ya hali ya umasikini wakutupwa barani Afrika na kwingine-ko katika nchi za ulimwengu wa

 tatu.

Hapa, tunaona kila upande un-autupia lawama upande mwingine.Lakini swali la msingi ni je, wimbihili la wakimbizi kutoka Afrikakwenda Ulaya linasababishwa nauduni wa maendeleo?

Mbona hatukuwahi kuona halikama hii miaka kadhaa nyuma nauduni wa maendeleo ukiwa upo ka- tika nchi hizi? Ni lazima kuna jambo la ziada kando na uduni wa maen-deleo au hali ya maisha.

Katika kitabu “Migration andGlobalization: Challenges and Per-spectives for the Research Infrastruc- ture”, Klaus F. Zimmermann anase-ma: “Watu huhama kwa nia yakuboresha hali zao za kiuchumi, ku- jihakikishia mazingira salama zaidikuishi, kuungana na familia zao aukukimbia mateso katika nchi zao zaasili”.

Zimmermann anatupa fikra ny-ingine, kwamba inawezekana kabisahawa wanaoitwa wahamiaji ‘hara-mu’ si wahamiaji bali ni wakimbizi.

Kipo wanachokikimbia -hali ngumu ya maisha,kukosekana usalama namateso katika nchi zao.

Ni wazi hawaendi Ulaya kuunganana ndugu zao.

Hili la kuboresha hali zao za mai-sha haliwezi kuwa kweli, kwa sababuhali ngumu za maisha kwa Waafrikazilikuwepo hata kabla ujio wa wa-koloni. Kipindi hicho, hawakujazanakatika mitumbwi kukikabili kifo ili

kufika Ulaya. Waafrika waliendelea kukabili

mazingira yao duni kama watu wen-gine kwa sababu chambilecho cha waswahili ‘mtu kwao’.

Tofauti ni kwamba, walikuwa

 wakiishi katika hali ya usalama naamani, pasipo kuwepo mateso walakhofu kutoka kwa watawala, walamagenge ya wauaji na makundi ya waasi yenye kupigania madarakakatika nchi nyingi za Afrika kwamtutu wa bunduki baada yakushindwa katika uchaguzi wa ‘ki-demokrasia’ ya kimagharibi.

Nchi nyingi za Afrika baada yauhuru zilitawaliwa na wazawa wal-iosomeshwa katika mfumo wa elimu wa kimagharibi.

Mfumo huu haukuwa na lengo lakumuelimisha mwanafunzi kujakuitumikia Afrika, bali kuwa nyenzo ya kuingiza watu katika Ukristo nakuwaandaa kuwa watumishi wa ta- wala za kikoloni.

Mfumo huu wa elimu ulizalisha

 wasomi butu, wasiojua jinsi ya kuvi- tumia vipawa vyao kukabiliana namabeberu wa nchi za magharibi. Wengi wa wasomi hawa walihitimukatika nchi hizo hizo za Ulaya na ku-rudi kuja kuzitawala nchi zao.

Jinsi wasomi hawa wanavyota- wala utadhani walichosomea nikuiba mali ya umma, kuuza kwa beichee rasilimali za Afrika kwa wawekezaji wa nchi za kimagharibina kuwakandamiza Waafrika wen-

zao. Waafrika hatukuishia hapa,bali

 tawala za kidikteta zilizowekwa ma-darakani na wamagharibi zikai-kumba Afrika.

Naam, ubadhirifu wa mali yaumma, ufisadi, usimamizi mbovu wa rasilimali za mataifa ya Afrikana rushwa ni miongoni mwa saba- bu zinazopelekea wimbi la waha-miaji “haramu” kwenda Ulaya.

Kugombea madaraka ni chan-zo kingine, kwa kuwa kinasababi-sha ukabila, ukandamizaji wamakundi dhaifu katika jamii namachafuko ya kivita katika nchinyingi za Afrika.

Jambo moja la kufahamu hapani kwamba, katika nchi za Afrikazenye kukumbwa na machafukona ukosefu mkubwa wa usalamana amani ni nchi za magaharibi nakaskazini. Nchi za Chad, Niger,Gambia, Senegal, Bukina Faso, Af-rika ya Kati, Guinea, Mauritaniana Mali.

Matokeo ya machafuko katikanchi hizo ni kukosekana amani nausalama katika bara la Afrika, hivyo watu wanakimbia kutafuta palipona usalama na amani.

Kwa kuwa katika nchi za Afrikahakuna nchi isiyo na migogoro yake ya ndani, chaguo jepesi linakuwaUlaya, ulimwengu wa kwanza, penyemaisha ya raha na amani, ingawa wengi wakifika huko wamejikuta wakiishi maisha ya dhiki kubwa.

Lakini, wakimbizi hawa pia wa-natoka nchi za mashariki ya katizenye machafuko na vita, zikiwemo;Uturuki, Syria, Iraq, Afghanistan,Eritrea na Yemen.

Kwa hiyo sababu moja kuu ya wimbi hili la wakimbizi kwendaUlaya ni ukosefu wa usalama,mateso na vita kati nchi wanapotoka wakimbizi.

Kwa kiasi fulani maneno yamwandishi Athur Kemp yana uk- weli ndani yake, sisi wenyewe Waaf-rika na serikali zetu ndiyo wa kulau-

miwa kwa tatizo hili la wakimbizikutoka Afrika kwenda Ulaya.

Lakini kwa kiasi kikubwa piaUlaya na Marekani zinahusika. Tu-kumbuke maneno ya Nigel Faragekuhusu hatua ya Ulaya kuisambara- tisha Libya.

Marekani na washirika wake wa-natuhumiwa kutengeneza makundi ya kigaidi kufanikisha lengo lao lakubadili tawala wasizozitaka kuele-kea mfumo mpya wa dunia –New

 world Order. Wamasonia wanaamini kuwa

“Order comes from Chaos” yaanimpangilio au nidhamu huja kutoka-na na mparaganyiko. Dunia ilianzakwa “Chaos” waliyoiita Big BhangMlipuko mkuu. Baada ya mlipuko(chaos) ndiyo tukapata nidhamu yasayari, ikiwemo dunia tunayoishipenye mazingira ya nidhamu (Or-der).

Kwa hiyo katika kutengenezamfumo mpya wa ulimwengu, Wamarekani na washirika wake wameunda Al-Qaeda,ISIS, An-nus-ra, Boko Haram, Al-Shabaab n.k.

Na sisi Waafrika tumeunda Sele-ka, Anti-Balaka, Mungiki n.k. ma- tokeo ya makundi haya ni vita,mauaji, mateso na kupelekea vi-chocheo vikubwa vya wakimbizi.

Kwa upande mwingine, kunamagenge ya wavushaji wakimbizihawa yanayojitengenezea mabilion ya fedha.

 Watu hawa hufanikiwa kwasababu nchi zetu zimeoza kwarushwa, kwa hiyo wanachofanya nikuwalipa maafisa wa uhamiaji mi-pakani kuvusha “mizigo” yao. Hawa wanaitwa “human traffickers” au

 wasafirishaji wa binadamu.Mwaka 2011 pekee, zaidi ya was-afirishaji 9,000 nchini Uturuki wali- jilimbikizia Dola za Kimarekani mil-ioni 303 sawa na Shilingi za Kitan-zania 575,700,000,000 (Trilioni5.75).

kwa hiyo hili si tatizo la wakimbiz tu, lakini pia ni tatizo la biashara ya binadamu kinyume na sheria za ki-mataifa.

Kwa hili Waafrika si wa kulaumi- wa peke yao, bali pia magenge ya wazungu yanayowezesha kuwavusha wakimbizi kutoka Afrika kwendaUlaya. Bila magenge haya tatizo hili la wahamiaji “haramu” kwendaUlaya lisingekuwepo.

Suluhisho si kulaumiana, balikutafuta jinsi ya kuzuia sababu za Waafrika kukimbia na kwenda

Ulaya.Inaonekana sababu hizi ziko

ndani yetu, ndani ya nchi zetu. Seri-kali za Afrika zitende haki kwa raia wake, zisimamie rasilimali vizuri, zi jenge mazingira ya uwazi na uwa- jibikaji kwa viongozi.

 Waafrika wa makundi mbalimbali tuondoe fikra za kibaguzikama zinavyotokea huko Afrika yaKusini, hali ambayo inasababishaukosefu wa usalama na amani. Chu-ki za kidini kama zilivyotokea Afrika ya Kati na kupelekea mauaji ya raiana zinavyoanza kutokea hapa Tanza-nia, ni sababu tosha ya kuzalisha wakimbizi wa kesho kwenda Ulaya.

Tukumbuke kuwa tusipochukuahatua muwafaka kwa wakati muwa-faka, kila mmoja wetu ni mkimbizi

mtarajiwa.

NCHA YA KALAMUSHEIKH MUHAMMAD ISSA

 Wahamiaji

‘haramu’ auwakimbizi?

UBADHIRIFU WA MALI YA UMMA, UFISADI,

USIMAMIZI MBOVU WA RASILIMALI ZA MATAIFA

 YA AFRIKA NA RUSHWA NI MIONGONI MWA

 SABABU ZINAZOPELEKEA WIMBI LA WAHAMIAJI

“HARAMU” KWENDA ULAYA 

Wahamiaji wa Kiafrika wakiwa kwenye boti kuelekea Ulaya.

Page 10: Imaan Newspaper issue 5

7/17/2019 Imaan Newspaper issue 5

http://slidepdf.com/reader/full/imaan-newspaper-issue-5 10/19

www.islamicftz.org

21Rajab1436,  JUMATATU Mei11 -17, 2015

  www.islamicftz.org

21Rajab1436,  JUMATATU Mei11 -17, 2015

MAKALA MAALUM

AKALA MAALUM

NA ABUU MAYSARA

Miaka 35 ya mapinduzi ya Iran ya mwak a 197 9 ime ibuamengi katika umma wa Kiis- lamu. Badala ya k ujikita ka-

 tika kuleta mabadiliko (transfor mation) yanayolenga kuima risha imani, tawhidina maadili ya Waislamu, mapinduzi yaIran ya mechukua sura ya kisiasa na ki-mapambano zaidi (reactionary).

Katika kipindi hiki, ulimwengu wa Ki-islamu umeshuhudia vita vya wenyewekwa wenyewe kati ya Iraq na Iran, Syria,ISIS na Iraq, Yemen na kwingineko,kama ulivyoshuhudia pia vita mbili za

Ghuba kati ya Marekani na washiri-ka wake dhidi ya Iraq chini yaSaddam Hussein.

Mapinduzi ya Iran pia ya-meibua upya mitazamo inay-okinzana kati ya Shia na Sunnina kupelekea makundi haya

kupigana huko Syria, Iraq na Yemen.

Miji mitakatifu ya Wais- lamu, Makka na M adinaIlisukwasukwa na hadi ku-katokea mauaji. Misikitimaeneo mbalimbali ililip-uliwa kwa mabomu namaelfu ya Wai s lamukupoteza uhai.

 Wako wana oang aliamvutano unaoendeleakati ya Saudia na dola zaKisunni kwa upandemmoja na Iran kwa up-ande mwingine kama nimasuala ya kisiasa tu nakushindana kuhusuudhibiti wa mashariki ya kati.

Ki ukweli, kinach-oendelea ni zaidi yasiasa. Ni mvutano wakiitikadi kati ya Shia wakiongozwa na Iranna Ahlu Sunna walJamaa, Saudia iki- ta ng ul ia mb el ekutokana na kuwa

 wenyeji

 wa mah ujaji na hivyo wasimamiz i waMakka na Madina.

Kuupuuza ukweli huu ni kujidangan- ya na k uruhusu propaganda za itikad imoja kuipiku nyingine. Hii ni vita kati yau-Shia na u-Sunni.

Iwe haipendezi kusema hivi au inap-endeza, huu ndio ukweli na lazima use-mwe wazi Waislamu na walimwengu wajue.

Marekani kuunga mkono Sau-dia na washirika wake kush-ambulia ma-Houthi walio-ipindua Serikali ya Yemen ya

Rais Abdul Rabb Mansuri Hadi kuna- tafs iriwa kuwa Saudia inamt umik ia

Mmarekani.Lakini Marekani ana kila sababu za

kufanya hivyo; kwanza, kama mshirikamkubwa wa Saudia kibiashara na pili,kuhalalisha kitendo chake mwenyewecha kuchukua hatua za kuvamia na ku-piga nchi nyingine pasina kibali cha UN.

Ikiwa ushirika kati ya Saudia naMarekani kibiashara ni dhambi, kunanchi katika dunia ya leo itasalimika nadhambi hii? Iran yenyewe ni mshirikamkubwa wa China na Urusi kibiashara,kijeshi, kiteknolojia na hata kidiploma-sia. Nani asiyejua ukweli huu. Kwa niniisemwe Saudia tu?

Kwa kuwa Saudia na washirika wake wa dola za Kisunni wanafanya masham- bulizi Yemen pasina kupa ta kibal i chaUN, Marekani inachekelea kwa sababusasa ikichukua hatua mithili ya hizi zili-zochukuliwa na Saudia na washirika wake ni nani tena atainyooyesha k idolekuwa inajifanya ‘polisi’ wa dunia?

Tukirudi kwenye mada, je kinacho- tokea kati ya Saudia na Iran ni mgogoro wa kisiasa au kidini? Msingi wa mgogorokati ya Saudia na Iran ni tofauti za kii- tikadi kati ya u-Shia na u-Sunni, msingiambao umejengwa katika dhana nzima ya ‘al-Imaamiyyah’ au uimamu/uongozi.

Mashia wanaamini kwamba uimamuau uongozi wa Waislamu kufuatia kufa-riki Mtume Muhammad (Rehma naamani ziwe juu yake) ulipaswa kuchuku- liwa na kizazi cha M tume, wakati Ahl uSunnah wal Jamaa wakiamini kwamba yeyote mwenye s ifa za uongozi k atikamaswahaba alifaa kuchukua uongozi wa Waislamu.

Kwa mujibu wa ma-Shia, Makka naMadina zinapaswa kuwa chini ya

uongozi wao, kwani wao ndio vi-ongozi stahiki wa Waislamu

dunia nzima. Huu ndio msingimkubwa wa vita vya manenokati ya Iran na Saudia.

Historia ya uhusiano wa

sasa kati ya Saudia na Iran inaanzia mia-ka ta kriban 90 iliyopita, ambapo mna-mo 1925 Iran ilikuwa ikiongozwa naufalme wa Shah na Saudia ikiongozwana ufalme wa ukoo wa Sa’ud.

Kufuatia mapinduzi ya Iran ya mwaka1979, utawala wa kishia ulinyakua ma-daraka nchini humo na kufunga mlango wa uongozi wa kifalme, huku ukifunguamlango wa uimamu wa kishia.

Kwa upande wa Saudia, ukiachiliamabadiliko machache ya mwaka 2005katika mambo ya kisiasa, nchi hiyo ime- baki c hini y a uta wala w a kif alme un-aoongozwa na ukoo wa Sau’d, lakini uki- toa nafa si y a m aulam aa wa K isunni

kuongoza masuala ya kidini.Uhusiano kati ya Saudia na Iran un-

aweza kutazamwa katika ngwe (phase)mbili, Kabla ya mapinduzi ya Iran (mwa-ka 1929-1979) na baada ya mapinduzi yaIran (1979 hadi sasa).

Ngwe ya kwanza: 1929 -1979

Uhusiano kati ya Saudia na Iran ya l eo u lianza mwaka 1929kwa mkataba uliojulikanakama ‘Saudia-Iran Friendship

Treaty’ – Mkataba wa Urafiki kati ya Sau-dia na Iran. Katika mkataba huo, Iran il-itambua rasmi dola ya Saudia.

Hadi kufikia miaka ya 1960, nchi hizimbili majirani zilikuwa zikijishughuli-sha zaidi na kujenga miundo mbinu yao ya ndani. Kutoka 1 929 hadi 1968 ma- tukio mengi yalitokea k atika medani yakimataifa yaliyoathiri siasa za nje zamataifa hayo mawili.

 Vita vya pili vya dunia, kuundwa kwa taifa la Israeli, vita kati ya Waar abu naIsraeli na vita baridi ni miongoni mwamatukio makuu yaliyojiri katika kipindihiki.

Iran na Saudia, kila moja ilikuwa nasera tofauti na yenzake katika matukiohaya. Kuhusu Vita ya Pili ya Dunia, Iranilishambuliwa na Urusi na Uingerezazikilenga kudhibiti mafuta yake, ingawaIran haikuwa inaunga mkono upande wowote katika vita hiyo.

Mfalme wa Iran, Raza Shah akalaz-imika amwachie kiti cha ufalme mwa-nae, Muhammad Raza Shah kwa mkan-damizo wa mataifa ya kigeni.

Saudia kwa upande wake, nayo kama

Iran, mwanzo wa Vita haikuwa inaungamkono upande wowote. Kwa kuwa Sau-dia haikushambuliwa na mataifa ya ki-geni, baada ya vita ikaibuka ikiwa imarakuliko ufalme wa Iran.

Mwaka 1955, mkataba ulioitwa ‘TheBaghdad Pact’ ulisainiwa kati ya Uinge-reza na nchi tano za mashariki ya kati,

ikiwemo Iran.Nyingine zilikuwa Jordan, Uturuki,

Iraq na Pakistan. Saudi Arabia ilihofiamkataba huu wa kusaidiana kiulinzi ulio- waleta Waingereza karibu na dola za BaniHaashimu (waliokuwa watawala waMakka na Madina kabla ya utawala waSa’ud). Kwa hiyo Iran na Saudia zikaanzakutofautiana.

Mgogoro kati ya Waisraeli na Waarabuuliifanya Iran itofautiane na Saudia. Wakati mataifa ya kiarabu yakipigana naIsraeli katika vita ya mwaka 1956, Iranilikuwa na uhusiano kamili wa kibalozina Israeli.

Mwaka 1975, Mfalme Faisal wa Saudia

aliuawa. Khalid akashika hatamu za uon-gozi. Kwa upande wa Iran, sera za ShahMuhammad Reza Shah zilizojulikanakama ‘Shah’s white revolution’ zilikuwazikikasirisha wa-Iran na kupelekeaufalme wa Pahlavi kupinduliwa mwaka1979.

Ngwe ya Pili (1979 hadi sasa)

Kufuatia mapinduzi ya mwaka1979, ‘Jamhuri ya Kiislamu yaIran’ iliundwa chini ya itikadi ya ushia , ikiwa na sera mpya

kisiasa, kidini, kieneo na kimataifa.Ni sera hizi mpya za Iran chini ya Ayat-

ollah Khomein zilizoifanya Saudia naIran kuwa wapinzani wakubwa Masha-riki ya Kati.

Tayari dola hizi mbili zikawa zimes-imikwa katika itikadi mbili za kidini zina-zokinzana. Iran ikiongozwa na itikadi yaushia, isiyomtambua Khalifa Abu Bakar,Umar na Uthman na yenye chuki na mas- wahaba kadhaa wa Mtu me, na Saudiaikiongozwa na itikadi ya Ahlu Sunnah walJamaa.

Kuanzia hapo, yote yanayotokea kati ya Iran na Saudia ni muendelezo tu wa to-fauti za kiitikadi ambazo huchukua sura ya kisiasa. Mal umbano ya kidi ni kati yaMashia na Ahlu Sunnah yakaibuka upya tena kwa nguvu zaidi.

Tofauti na ilivyokuwa karne kadhaanyuma; kwa sasa, Mashia wanatumiambinu ya ‘wagawe uwatawale’ wakiwata-ka Waislamu wa Ahlu Sunna wajitengena ‘Mawahabi’ wanaoongozwa na wa-Saudia.

Mgogoro wa msingi wa kidini kati ya

Saudia na Iran unahusu uongozi –Nanianastahiki kuongoza Waislamu duniani?Nani anastahiki kuongoza ibada ya hijjana usimamizi wa misikiti miwili mitakat-ifu ya Makka na Madina?

Kwa mujibu wa Mashia, utawala waSaudia haustahiki kuongoza miji miwilimitakatifu ya Makka na Madina. Wanad-

ai utawala huo unapaswa kufukuzwakutoka katika ardhi takatifu na badala yake kuwe na kamati ya kimataifa ya kusi-mamia miji ya Makka na Madina.

 Wito huu ulitole wa mara ya kwanzamwaka 1926 huko Lucknow, India am- bako Waislamu dunia nzima walitak iwakuungana na kuwafukuza watawala waSaudia kutoka Hijaz. (Oriente Moderno6 91926): 310, 513-14, 610).

 Wito huu ukapamba moto tena baada ya mapinduzi ya Iran kufuatia mauaji yamahujaji 402 mwaka 1986 yaliyo-chochewa na mipango ya wa-Iran ambao waliandaa maandamano ya mahujaji yal-iyopelekea mapambano na polisi.

 Ayatollah Khomein alitoa kauli akise-ma: “Hawa mawahabi muflisi wa maadilina wasio wachaMungu ni kama jambiaambalo daima limeutoboa moyo wa Waislamu kutokea nyuma”.

 Ayatollah Khomein akaenda mbali za-idi kwa kusema: “Makka iko chini yamikono ya genge la walioritadi” (Kho-meini, Radio Tehran, 3 Agosti 1987, BBC,5 Agosti 1987).

Kilichofuatia ni kuharibika zaidi kwamahusiano kati ya Saudia na Iran. Kufua- tia kampeni kubwa ya Iran dhidi ya Sau-dia dunia nzima, Saudia ililazimika kuiti-sha mkutano mjini Makka Oktoba 1987uliofunguliwa na Mfalme Fahd ambapo wawakilish i wa Wai slamu k utoka nchi134 walihudhuria.

Mwezi mmoja baadae, Iran ikaitishamkutano wa kimataifa uliohudhuriwa na wawaki lishi kuto ka n chi 36 d uniani .Kauli mbiu ya mkutano huo ilikuwa ni‘Kulinda Utakatifu na Usalama wa Msiki- ti Mtakatifu’.

 Akizungumzia mkutano huo, Rais waIran wa wakati huo, Hashim Rafsanjani,alinukuliwa akitoa wito wa ‘kukom- bolewa Makka’ na ‘kuanzishwa kwa bara-za la kimataifa la Waislamu litakaloita- wala Makka kama mji huru’. (Rafsanjani,Radio Tehran, 26 Novemba 1987, FBIS,28 Novemba 1987).

 Ayatollah Husayn Ali Montazeri, al-ipokutana na waalikwa alisema: “Utawa- la wa Sa’ud ni genge la mawakala wa ma- jasusi wa Kii ngereza kutok a (ene o) laNajd ambao hawaiheshimu nyumba ya Allah, wala wageni wa Allah”.

Kisha Ayatollah Husayn akatoa unda-ni wa malengo ya Iran kwa Saudia akise-

ma:“Kama ambavyo Jerusalem itakavy-

okombolewa kutoka makucha ya wa- vamizi wa Israeli, hiv yo hivyo Makka naMadina zitakombolewa kutoka katikamakucha ya Sa’ud” (Kauli ya Montazeri,Radio Tehran, 27 Novemba 1987, FBIS,29 Novemba 1987).

Msomaji utakumbuka madai ya maa-dui wa Ahlu Sunna kudai kuwa harakatiza kisunna ziliasisiwa na Sheikh Muham-mad ibn Abdilwahab aliyetokea Najd nakwamba eti alifundishwa na jasusi wa Ki-ingereza Mr. Humphrey. Hizi ni propa-ganda za mashia walizozieneza duniani.

 Watawala wa Iran wakaenda mbali za-idi kwa kudai kuwa watawala wa ukoo waSa’ud unaotawala Saudi Arabia si Waara- bu bali ni Wayahudi.

Haya ni madai ya muda mrefu ya

Mashia walenga kutekaMakka, Madina WadaiKarbala ni bora kuliko Makka!

KWA MUJIBU WA MA-SHIA, MAKKA NAMADINA ZINAPASWA KUWA CHINI YA

UONGOZI WAO, KWANI WAO NDIO VIONGOZI STAHIKI WA WAISLAMU DUNIA NZIMA.

HUU NDIO MSINGI MKUBWA WA VITA VYAMANENO KATI YA IRAN NA SAUDIA.

MGOGORO SAUDIA NA IRAN: SIASA AU DINI?

Mfalme Sulaymanwa Saudia

Mashia wa Iran kama yalivyonukuliwa ksir al-Sa‘id, Tarikh Al Sa‘ud, vol. 1 ([Beihad sha‘b al-jazira al-arabiyya, n.d.): 392

Msomaji, pima mwenyewe manenokama haya yalivyoweza kuharibu uhusi ya Saudia na Iran. Serikali ya Saudia Aramapigo kwa kwanza, kupiga marufukumano ya mahujaji wakati wa hijja.

Pili, Saudia ilipunguza idadi ya mahuka Iran kutoka 150,000 kwa mwaka (idazaidi kuliko nchi yoyote ile) hadi 45,000

Saudia ilifanya hivyo ikitambua kuwapunguzwa idadi ya mahujaji wao Iran ita leta mahujaji, hivyo kuepuka kurudiwa kama lile la mwaka 1987.

Kwa muda wote wa mgogoro huu wa Saudia ilikuwa haijavunja uhusianopamoja na ubalozi wake kuvamiwa na watu wenye hasira na kuuawa kwa afisaubalozi.

 Aprili 1988, Sa udi Arabia ikak ata rasiano wake na Iran, isiwezekane kabisIran kupata visa za hijja.

Kama ilivyotazamiwa, Iran ilisusia hi1988, mwaka ambao pia Ayatollah Khomfariki. Iran iliendelea kususa hadi mwak

Pamoja na kutokuwapo mahujaji wa Ipuko miwili ilitokea mjini Makkah mw(1989) na kuua mahujaji wawili.

Polisi wa Saudia waliwatia nguvuni zahujaji 30 wa kishia kutoka Kuwait na m temba mwaka huo watu 16 kati ya hao whadharani kwa kosa hilo.

Ingawa walikiri kutumwa na maafisa zi wa Iran huko Kuwait, Serikali yhaikusema lolote kuhusu Iran kwa kukosdi madhubuti.

Mwaka 1990, wabunge 140 wa bun wakaandika barua ya wazi kwa Saudia wmasharti ya mahujaji wa Iran kurejea ten

Miongoni mwa masharti hayo ni Saud ba radhi, ilipe fidia damu za mahujaji waiokufa mwaka 1987 na pia ikubali idadi jaji 150,000 kama awa li na waruhusiwmaandamano ya kuwalaani ‘washirikina

Saudi Arabia ilikataa masharti yotehivyo kususia huku kukaendelea kwa m tatu. Wa kati wa msimu wa hijja , AyatKhamenei akasema:

“Makka iko salama kwa washauri wa na wamiliki wa makampuni ya mafuthaiko salama kwa Waislamu wenyewe” wa Khamene ’i kwa ma hujaji, Rad io TJuni 1990, FBIS, 2 Julai 1990).

Kiongozi wa kidiniIran - Ali Khamenei

Page 11: Imaan Newspaper issue 5

7/17/2019 Imaan Newspaper issue 5

http://slidepdf.com/reader/full/imaan-newspaper-issue-5 11/19

www.islamicftz.

21 Rajab 1436,  JUMATATU Mei 11 - 17,

12

 Je hutenguka udhu wamtu anayemuosha mwa-nawe najisi?

Swali: Aliulizwa Sheikh Mu-hamad bin Swaleh Al-uthaimin,

 Allah amrehemu: Mwanamke ali- ye na udh u anapomchambi shamwanawe hulazimika kuta-

 wadha?

 Jaw ab u :   Mwanamkeanayemuosha mwanawe wakike au wa kiume na akagusautupu halazimiki kutawadha,

 ba li anala zimika kuikosh amikono yake tu kwa sababukugusa utupu bila ya shaukuhakuwajibishi udhu, na inavy-ofahamika mwanamke anaye-

 wac ham bis ha wat oto wak ehawezi kuwa na fikra za ashikiakilini mwake.

Kwa maana hiyo, mwan-amke akimchambisha mwa-nawe wa kike au wa kiumeataosha tu mikono yake kwanajisi iliyomsibu, wala hawa-

 jibiki kutawadha. [Fataawana Rasailu za Sheikh Swaleh

 bin Uthaimin 4/203].

 Je kumgusa mwa-namke wa kandokunachanguaudhu?

  Swal i :   IliulizwaKamati ya Kudumu yaFat-waa, je kumgusa aukumpa mkono mwanam-

ke wa kando (ajnabiy) kunatenguaudhu (Wakati tunafahamukumpa mkono mwanamke wakando ni haramu), kwani tu-mekuta baadhi ya hadithkwenye vitabu vya fiqhi zina-zoashiria kuwa kumgusam w a n a m k e w a k a n d ohakutengui udhu, na kugusakunakozungumzwa walahakujafafanuliwa. Je huuujumla umewekewa ukomokwa kinacho-ruhusiwakuguswak w am w a n -amke au

 la?

 Jawabu:  Kauli sahihi mion-goni mwa kauli za wanazuoni nikuwa, kamwe kumgusa na kumpamkono mwanamke hakutenguiudhu, sawa akiwa ni mwanamke

 wa kando, mke au mahram, kwaniasili ni kubaki na udhu mpakaithibiti kutoka katika sharia kina-chofahamisha kuchangua, na hilohalijathibiti katika hadith sahihi.

 Ama kugusa kuliko ndan i yaneno la Allah:

“Enyi mlioamini! Mnaposima-ma ili mkasali basi osheni nyusozenu na mikono yenu”, mpakakwenye neno lake, “Na mkiwa wagon jwa au mmo safarini , aummoja wenu ametoka chooni aummeingiliana na wanawake, nahamkupata maji, basi kusudieniudongo ulio safi na kupaka nyu-so zenu na mikono yenu”; mu-

radi wa (kugusa) kwa kauli sa-hihi miongoni mwa kauli za

 wanazuoni ni jimai (kuingiliana).[Fataawa Laj-natud Daimah5/268].

 Je kuwatazama wan-awake na wanaumewalio uchi kunaharibuudhu?

Swali: Iliulizwa Kamati ya Ku-dumu ya Fat-waa: Je udhu unach-anguka kwa sababu ya kuwataza-ma wanawake na wanaume waliouchi? Na je udhu wa mtuhuchanguka kwa kuangalia utupu

 wake? Jawabu: Hauchanguki udhu

 wa mtu aliyetawadha kwa sababu ya kuwatazama wanawake na wa-naume walio uchi, wala kwa ku-

 jiangalia yeye mwenyewe, kwanihakuna ushahidi katika suala hili.[Lajnatud Daimah 5/270].

 Je huchanguka udhu wa

mkunga anayefanya kazya kuzalisha?

Swali: Iliulizwa Kamati ya Kudumu ya Fat-waa, je mkunga hu

 takiwa k uoga au udhu unamtosha?

 Jawabu: Mkunga hawajibikkuoga au kutawadha kwa sababu

 ya kusimamia taratibu za uzazi wmjamzito, isipokuwa mkunga anapotaka kuswali huwajibika kuiosha najisi iliyoingia kwenye nguau mwili wake.

Lakini mkunga hutengukudhu endapo atagusa utupu wmjamzito wakati wa kuzaa. [Fata

 wa laj-natud Daimah 5/316].

 Je malai ya nywele narangi ya mdomo inaten-gua udhu?

Swali: Aliulizwa Sheikh Muhamad bin Swaleh Uthaimin Al

 lah amrehemu: Je mwanamke ku tumia ‘cream’ ya nywele na rang ya mdomo (lipstic) kunachanguudhu?

 Jawabu: Mwanamke kujipa

ka ‘cream’ au mafuta ya aina yoyothakutengui udhu, na hata funghaiharibiki. Isipokuwa katikfunga, kama ‘lipstic’ itakuwa n

 ladha, na kama hiyo ladha ya ‘lipstick’ itakuwa inapenya tumbonkwake, hapo isitumike.[Fataawna Rasailu za Sheikh ibn Uthaimin4/201].

Maradhi mengi yanayomkabilimwanadamu yanachangiwa na uwe-po wa sumu au uchafu mwingi mwil-

ini (waste substances), kula kupita ki-asi, uchaguzi mbaya wa vyakula na

 vinywaji, kutokunywa maji ya kuto-sha, maisha ya kufanya kazi bila yakutoka jasho, kutokufanya mazoezina mtindo mbaya wa maisha kwaujumla.

Makala yetu ya leo inazungumziaumuhimu wa kufanya uchaguzi wa

 vile tunavyokula na kunywa.Kitabu Kitukufu cha Qur’an kiki-

 wa ni mwongozo kwa Waislamu na Wanadamu wote kwa ujumla, hak-ikuacha kutoa maelekezo kuhusuuchaguzi wa vyakula kama tunavyoji-funza katika aya mbalimbali.

“Enyi watu! kuleni vilivyomo kati-ka ardhi, halali na vizuri, wala msi-fuate nyayo za shet’ani. Hakika yeye ni

adui yenu aliye dhaahiri” (Qur’an:2.168).

“Enyi Mlioamini kuleni vizuri tu- livyokuruzukuni, na mumshukuruMwenyezi Mungu, ikiwa mna-muabudu Yeye Peke Yake”. (Qur’an:2:172).

“Na kuleni katika vile alivyokuru-zukuni Mwenyezi Mungu vilivyo vi-zuri na halali na mcheni MwenyeziMungu ambaye nyinyi mnamwa-mini” (Qur’an: 5: 88).

“...... na kuleni (vizuri) na kunyweni(vizuri). Lakini msipite kiasi tu. Haki-ka yeye (Mwenyezi Mungu) hawap-endi wapitao kiasi”. (Qur’an; 7:31).

Kwa mujibu wa aya tulizozirejeahapo juu, Mwenyezi Mungu kupitiaQur’an Tukufu anawataka Waislamu

na wanadamu wote kwa ujumla ku-fanya uchaguzi wa vyakula kwa kuzin-gatia vigezo viwili. Vigezo hivyo niuhalali na ubora (uzuri) wa vyakula.

 Vyakula vya haramu tunavyotaki- wa kuwa mbali navyo ni kama vile vyakula vya wizi, mali au vyakula vilivyopatikana kwa njia za rushwa,nyama iliyokufa bila ya kuchinjwa,mnyama aliyechinjwa kwa kutimizamasharti ya wachawi, na nyama yanguruwe.

Kama watu wangezingatia kula vya halali, dunia hii ingekuwa kisiwacha amani. Ndio kusema, tusinge-shuhudia watu wakiwaua albino nakuuza viungo vyao.

 Wala tusingewaona watu wenyedhamana ya kufanya kazi za umma au

katika sekta isiyokuwa ya umma wak-

ijilimbikizia mali kwa njia za haramukama wizi na rushwa.

 Waislamu wengi wanajitahidi ka- tika kufanya uchaguzi wa vyakula kwakigezo cha uhalali kama vile kutokulakibudu au nyama ya nguruwe. Msibaupo katika kufanya uchaguzi wa

 vyakula kwa kuzingatia kigezo chaubora.

Hata yule mwenye kiwango kizuricha elimu ya Qur’an na Sunna bado

 yuko mbali na utekelezaji wa ma-fundisho ya Uislamu wa uchaguzi wa

 vyakula kwa kigezo cha ubora. Waislamu wengine wanakwenda

mbali zaidi kwa kushangaa kuwa wa-fanye uchaguzi hata kwa vyakula vyahalali? Kabla ya kujibu swali hilikisayansi, vema kwanza turejee tena

Qur’an Tukufu pale ilipoeleza sababu

za kufanya uchaguzi.‘’Na katika ardhi muna vipande

 vinavyoungana (na kuzaa kwakenamna mbalimbali) na muna mabus-

 tani ya mizabibu, na mimea mingine,na mitende ichipuayo katika shinamoja na isiyochipua katika shinamoja. Vyote vinanoshelezwa(vinamiminiwa) na maji yale yale; na

 tunavifanya bora baadhi yake (kuliko) vyengine katika kula. Hakika katikahaya zimo ishara kwa watu wanaotiamambo akilini’’ (Raad, 13.3).

Katika aya hapo juu, MwenyeziMungu anatufundisha namna yauhodari wake wa kuumba. Ingawamaji ni yale yale na udongo ni ulele ule,

 lakini anaumba aina tofauti za mimeazenye ubora tofauti. Wanyama nao

ubora wao unatofautiana, ingawa wa-

naweza kula aina ile ile ya majaniKwahiyo, lazima tufanye uchaguzhata kwa vyakula vilivyo halali.

 Watu wengi, Waislamu na wasiokuwa Waislamu hawajishughulishkutafuta elimu ya kujua mambo y

 vyakula. Matokeo yake wanakula kilkinachopatikana. Hii ni hatari sankiafya.

Hebu tujiulize maswali haya Vyakula vya kukaanga na vile vykuchemsha vipi ni hatari kwa afya yamlaji, kama mtu anakula kila siku?

Ni kwa namna gani ulaji mbayunasababisha upungufu wa nguvu zakiume au upungufu wa nguvu za kike

 jambo ambalo kwa sasa ni tishio luhai wa ndoa nyingi.

Nyama nyekundu kama ng’ombembuzi na nyama nyeupe kama samaki, ipi bora zaidi kiafya? Kwaninmaziwa ya mama ni bora zaidi kuliko

 yale ya kopo kwa mtoto?Ni kwa sababu gani vyakula vya ki

 wandani vinachangia zaidi magonjwkama kisukari na shinikizo kubwa ldamu kuliko vyakula vya asilia.

Baadhi ya wafugaji wa kuku wakisasa wanawapa kuku vidonge vya

 ARV ili wakuwe haraka; nini madhara yake kiafya kwa walaji kuku?

Tuhitimishe makala yetu kwakuwakumbusha wasomaji wetu kuwmuumini mwenye afya bora anapendwa zaidi na Mwenyezi Mungu ku

 liko muumini mwenye afya dhaifu.Taifa imara linajengwa na watu

 wenye afya bora. Ujenzi wa afya borunamihimili yake. Ulaji wa vyakula

 vilivyo bora ni muhimili mmoja wapo.

UMUHIMU WA KUCHAGUA VYAKULA

PAZI MWINYIMVUA

AFYA YAKO

FAT-WA KWA MWANAMKE WA KIISLAMSHEIKH SHABANI MUSSA

Ukiyatizama baadhi ya maswali ya wiki hii, na ya toleo lililopita ni kamayanafanana kwa kiasi fulani, lakini kwa sababu ya nyongeza zilizomo namajibu tofauti kutoka kwa wanazuoni, tumeona tuyalete kama yalivyo kwalengo la kukuongezea faida. Karibu ndugu msomaji…….

Page 12: Imaan Newspaper issue 5

7/17/2019 Imaan Newspaper issue 5

http://slidepdf.com/reader/full/imaan-newspaper-issue-5 12/19

www.islamicftz.org

21 Rajab 1436,  JUMATATU Mei 11 - 17, 2015

A

m e t u k u k a

M u u m b ambingu na ar-dhi mwenye

kuhimidiwa na kushuku-riwa. Swala na salamzimfike mbora wa vi-umbe aliye mjumbe wamwisho wa Rahman kwa

 walimwengu wote, kishasalam kwa wenye kufuatamuongozo.

Ndugu mpenzi mso-maji karibu tena kwamara nyingine katikamfululizo wa makalazetu juu ya uchumi na bi-ashara katika Uislamu.Katika makala yetu ya leoIn Sha Allah tutadurusu

 juu ya aina za riba.Riba kwa ujumla ni

ziada au nyongeza inay-opatikana bila kufanyakazi. Riba katika lugha

 ya kiarabu maana yake niziada. Ama katika lugha

 ya elimu ya fiq-hi maana ya neno ‘Riba’, ni ile ziadaanayolipwa mdai juu yarasilimali yake.

Mwenyezi Munguanasema: “Enyi mlioamini! Mcheni Mwenye-zi Mungu, na acheni ribazilizobakia, ikiwa nyinyini Waumini. Basi msipo-fanya jitangazieni vita naMwenyezi Mungu na

Mtume wake. Na mkitu- bu, basi haki yenu ni ra-silimali zenu. Msidhulu-mu wala msidhulumiwe”

(2:278-279).

 Yaani msimdhulumumdaiwa kwa kumtakazaidi ya rasilimali; walamsidhulumiwe kwa ku-punguziwa rasilimali.

Mtume (Rehma naamani ziwe juu yake)amesema: “Jiepushenina mambo saba yanay-oangamiza”. Masahaba(Radhi za Allah ziwe juu

 yao) wakam uuliz a: “Ni yepi hayo ewe Mtume waMwenyezi Mungu?”

 Ak ase ma : “Ku m-shirikisha MwenyeziMungu, na uchawi, nakuiuwa nafsi iliyoharam-ishwa na Mwenyezi

Mungu isipokuwa ikiwakwa ajili ya haki (kwa ali-

 yefanya makosa yanayos- tahi ki kuh ukum iwaauawe), na kula riba, nakula mali ya yatima, nakurudi nyuma katika vita(ukawaacha wenzakopeke yao), na kuwasing-izia uongo wanawake

 wema wasio na makosa walioamin i (k uwa et i wamezini)” (Bukhari naMuslim).

Na Mtume (Rehmana amani ziwe juu yake)amewalaani wote wana-oshiriki katika Riba.Mtume (Rehma na ama-

ni ziwe juu yake) amese-ma: “Mwenyezi Munguamemlaani anayekulaRiba na anayelisha na

UCHUMI NA BIASHARA JAMAL ISSA

WATU MAARUFU WASIOKUWA WAISLAMU WASEMAVYO KUHUSU UISLAMU

mashahidi wake.” (Bukhari- Muslim naImam Ahmad).

Kuna aina kuu mbili za riba, ambazoni ‘Riba An Nasiyah’ na ‘Riba Al Fadhil’.Katika zama za ujahiliya aina ya kwanza

 tu ilijulikana kama riba, ingawa Mtume(Rehma na amani ziwe juu yake) al-

ipokuja alibainisha aina ya pili ya riba.Kwa kuwa Riba An Nasiyah ilikuwandio aina pekee ya riba inayojulika kati-ka kipindi cha ujahiliya (kabla ya Uisla-mu), hivyo aina hii ya riba huitwa Riba

 Al Jahiliya na kwa kuwa pia aina hii yariba ndio iliyokatazwa moja kwa mojakatika Quran, aina hii pia huitwa Riba

 Al Qur’an.Riba An Nasiyah ni ziada anayolipa

mtu aliyekopeshwa kwa kushurutishwana mdai. Kwa mfano, mtu akitaka ku-kopa shilingi elfu, anashurutishwa kuli-pa shilingi elfu na ziada ya mia moja.Sasa zile shillingi mia moja za ziada ndioriba yenyewe.

Mwenyezi Mungu anatuhimizakuwa, ikiwa mtu anataka kumkopeshamwenzake mwenye shida, basi amko-

peshe mkopo mwema bila ya ku-muongezea mwenzake dhiki, kwambakwa kufanya hivyo ndio baraka itokayokwa Mola wake huongezeka katika mali

 yake mtu. Ama unapomkopesha mwenye shida

kisha ukachukua faida ya riba, basihuko ni kumzidishia dhiki mwenzio napia ni kuiangamiza mali yako na kuion-dolea baraka. Riba hii pia inahusishaziada juu ya deni kwa sababu ya kua-hirisha kulipa pale ambapo mkopajiameshindwa kulipa kwa wakati. Hii piani haramu, kwani hukumu za mdaiwazipo wazi pindi muda wake unapokwi-sha.

Hukumu za mdaiwa ni ama kum-samehe au kumpa muda zaidi, na si

kuongeza deni. Allah anasema: “Na akiwa (mdaiwa)

ana shida, basi (mdai) angoje mpakaafarijike. Na mkiifanya deni kuwa nisadaka, basi ni bora kwenu, ikiwa mna-

 jua” (2:280). Aidha, ili kufunga mlango wa nyuma

 wa kula riba, katika hadith ya Anas ibnMalik (Radhi za Allah ziwe juu yake)Mtume (Rehma na amani ziwe juu

 yake) amekataza mkopeshaji kupokeazawadi kutoka kwa mkopaji.

Pia, katika hadith nyingine ya Anasibn Malik katika Sunan al-Bayhaqi,Mtume (Rehma na amani ziwe juu

 yake) amekataza mkopeshaji kuchukuachakula au kupanda kipando cha mko-paji kama haikuwa ada yao kabla ya ku-kopeshana. Ukweli ni kwamba aina hii

 ya riba imeshika hatamu katika wakati wetu huu na kuwa moja ya sehemu yamsingi ya uchumi na biashara.

Mfumo wote wa kifedha umejengwa juu ya riba, kutoka kwenye vyama vyakuweka akiba na kukopa mpaka benkizinazoitwa benki za kibiashara (com-

mercial banks). Taasisi zote hizi hu- jiendesha kwa riba kama chanzo mamacha mapato.

Kutoka kwa Abu Hurayrah: Mtume(Rehma na amani ziwe juu yake) amese-ma: “Kwa hakika itakuja zama kwamwanadamu ambapo kila mtu atakulariba na kama hatofanya hivyo vumbi

 lake litamfikia” (Abu Dawud, Ibn Ma- jah).

 Aina ya pili ya riba ni Riba Al Fadhil.Riba ya kufadhilisha ni ile ya kubadilis-hana pesa kwa pesa au chakula kwachakula na kuchukuwa zaidi.

Kwa mfano, mtu anapokwenda ku- badilisha dhahabu yenye uzito wa gramkumi kwa ajili ya kupata dhahabu ny-ingine iliyomvutia zaidi, akalipwa bada-

 la yake dhahabu yenye uzito wa gramsaba. Hiyo inahesabiwa ni riba.

Inavyotakiwa kwanza mtu aiuzedhahabu ile kwa thamani yake, kishaainunue dhahabu anayoitaka. Mtume(Rehma na amani ziwe juu yake) amese-ma: “Msiuze Dirham moja kwa Dirham

mbili kwani nakuogopeeni riba”.Na akasema: “Dhahabu kwa dhaha- bu, fedha kwa fedha, ngano kwa ngano,chumvi kwa chumvi, mkono kwa mko-no, atakayechukua zaidi au kutaka zai-di, kesha kula riba” (Ahmed naBukhari).

Mtu mmoja alikwenda kwa Mtume(Rehma na amani ziwe juu yake) akiwaamebeba tende. Mtume (Rehma naamani ziwe juu yake) akamwambia;

“Tende hii haipatikani kwetu hapa?”Mtu yule akasema; “Ewe Mtume waMwenyezi Mungu, tumebadilishana

 tende yetu pishi moja kwa pishi mbili za tende hizi”. Mtume (Rehma na amaniziwe juu yake) akamwambia; “Hiyo niriba, zirudishe, kisha uza tende yetu, ha-

 lafu nunua tende hizi” (Muslim).

Kwa ujumla ni haramu kuzidisha ka- tika kubadilishana kitu cha jinsi moja.Mtume (Rehma na amani ziwe juu

 yake) amebainisha bidhaa sita ambazoni ngano, dhahabu, fedha, tende, shairina chumvi, ambapo katika kubadilisha-na bidhaa ya namna moja hubadilishwakwa bidhaa ya namna hiyo hiyo kwakipimo cha ujazo au uzito ulio sawa bilakuzingatia tofauti ya ubora iliyopo.Mathalan, kilo moja ya tende ya daraja

 ya juu kwa ubora hubadilishwa kwa kilomoja ya tende ya daraja ya chini yenyeubora duni na si vinginevyo. Au anaye-hitaji tende za daraja ya juu auze tendezake zenye ubora duni katika soko naatumie thamani hiyo kununua tende zadaraja ya juu katika ubora. Na bidhaahizi hubadilishwa hapo kwa papo, mko-

no kwa mkono (spot transaction).

 [email protected] 0713 996

031

 Aina za riba

KUNA AINA KUU MBILI ZA RIBA, AMBAZO NI ‘RIBA AN NASIYAH’ NA

‘RIBA AL FADHIL’

THOMASCARLYLE(1795-1881):

The lies (Western slander) which the west has heapedround this man (Muhammad) are disgraceful to our-

 selves only. A silent great soul, one of that who can-not but be earnest. He was to kindle the world, the world’smaker had ordered so

Tafsiri: “Uongo (kashfa za Wamagharibi) ambazo Wamagharibi wamezirundika kumzunguka mtu huyu(Muhammad) ni fedheha tu kwetu wenyewe! (Ni) mtu mkimya mwenye moyo mkuu, mmoja miongonimwa wale ambao hawawezi kuwa vinginevyo ila waungwana. Alikusudiwa kuung’arisha ulimwengu,

Muumba wa ulimwengu aliamuru hivyo”.

 Je nisikujulisheni juu ya watu bora kuliko wote baa-da ya Mtume wa Allah? Ni Abuu Bakr, kisha baada

 ya Abuu Bakr ni Umar. Na laiti ningependa ningekujulish-eni kuhusu watatu wao

(Tuhfatu Swiddiyq Fiy Fadhwaaili Abii Bakr Swiddiyq, Mjalada 1, uk. 7)

ALI (r.a) ANAVYOWAZUN-GUMZIA ABUBAKAR,UMAR NA UTHMAAN (r.a):Imesimuliwa kutoka kwaAbi Muusa Al-Ash’ariy,Ali Bin Abi Twaalib (Radhiza Allah ziwe juu yake)alisema

Page 13: Imaan Newspaper issue 5

7/17/2019 Imaan Newspaper issue 5

http://slidepdf.com/reader/full/imaan-newspaper-issue-5 13/19

www.islamicftz.

21 Rajab 1436,  JUMATATU Mei 11 - 17,

14

NA IDDI JENGO

U

naweza ukaongopea watu wote kwa muda mchache,unaweza kuongopea watu wac hac he kwa muda

 wote, lakini huwezi kuongopea watu wote kwa muda wote.” (Abraham Lin-coln)

 Awali ya yote napenda nianze kwakumshukuru Mwenyezi MunguSub’hanahuu Wataala na nimtakierehma na amani Mtume wa mwisho(Rehma na amani ziwe juu yake) pianiwatakie rehma na amani wale wote wanaoshika mana na mwenendomwema mpaka siku ya mwisho .

Mwanadamu ni kiumbe wa ki- jamii anayetegemea mahitaji yakekutoka kwa wanajamii wenzake wakubwa kwa watoto wenye nia nzuriama nia mbaya, yawe mahitaji yoyote yawayo, ya kisiasa, kiuchumi, kiuta-maduni au kiimani.

Mambo haya yako hivi tangu enzina enzi, na imekuwa ni ada katikamaisha ya mwanadamu. Yapo mam- bo mawili ya msingi katika mengi am- bayo mwanadamu akiyakosa huwa nimwenye fazaa kubwa, kutengwa na jamii na kukosa taarifa sahihi .

Kukosa taarifa na kutengwa na jamii ni mambo ambayo yamewahikuikumba jamii ya Kiislamu, katikakile kipindi kigumu cha awali chaujenzi wa umma imara wa Kiislamupale Makka.

Mtume Muhammad (Rehma naamani ziwe juu yake) akiwa na mas- wahaba zake wachache waliomua-mini kikweli walitengwa katika lile bonde la shiib bin abi twalib na jamii ya kidhalimu ya Makka, na kupelekeakukosa taarifa na huduma za msingiza kijamii.

Kwa tukio hilo Waislam wengi walipoteza uhai wao. Ni tukio ambaloQur’an imeacha kumbukumbu kwetukama sehemu ya mafunzo. Allah Taa- la anasema katika Qur’an:

“Mnadhani kuwa mtaingiapeponi, bila ya kukujieni kama yaliyo wajia wale walio pita kabla yenu? Ili- wapata shida na madhara na waka- tikiswa hata Mtume na walio aminipamoja naye wakasema: Lini nusura ya Mwenyezi Mungu itakuja? Juenikuwa nusura ya Mwenyezi Munguipo karibu”( 2: 214).

Swali lililoulizwa (nusura yaMwenyezi Mungu itakuja lini?) ndo limenishajiisha kuja na mada hii. Nasi yatupasa tujiulize, zama za ukweli nauwazi zitafika lini? Katika maisha yetu tumepitia na tunaendelea kupitiazama za uongo na uwazi kama si uon-go na kificho.

 Watu wanakamatwa, wanapigwana wanafungwa kwa uwazi na un-asemwa uongo wa wazi, na watu wa-nakamatwa, wanapigwa, wanafun-gwa kwa kificho na unasemwa uongokwa lengo la kuthibitisha na kuhalali-sha dhulma hizo.

Moja ya jambo la msingi katikamaisha ya mwanadamu ni kujifaha-mu yeye mwanadamu ni nani naanalengo gani katika ulimwengu huuulio wazi lakini uliojaa kificho?

Kufahamu lengo la maisha, kuta-muwezesha mwanadamu kufanyamambo yake kwa namna iliyo kuwanzuri na kuwa na matarajio ya hakikakatika kila analolifanya .

Ukweli kuhusu lengo la maisha yamwanadamu ni jambo la msingi sana

ambalo kwa bahati mbaya halijulika-

ni na wengi miongoni mwetu. Nauongo kuhusu lengo la maisha ndiounatangazwa na kusimamiwa wazi- wazi utapelekea mwanadamu kuan-gamia.

T

anzania yetu ipo katikamchakato wa uchanguziunaotarajiwa kufanyikaOktoba, Mungu akipenda

ambapo tutampata Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano waTanzania. Awamu ya kwanza yaMwalim Julius Kambarage Nyerereilikuwa ngumu kwa wote lakini, kwa Waislamu ilikuwa ni ngumu zaidi.

 Awamu ile ilikuwa ngumu zaidikwa Waislamu kwa sababu ndio tu- likuwa tunatoka kutawaliwa na wa-koloni na kuwa Taifa huru na wapam- banaji (Waislamu) hawakuthamini- wa kiwango kinachostahiki. Kilikuwani kipindi cha kauli mbiu nyingiikiwemo Ujamaa, Azimio la Arushan.k. ambazo utawala ulijaribu kuzi-fanyia kazi (1963- 1985).

 Awamu ya Alhaji Ali HassanMwinyi (1985-1995) ilifuata ambapoTanzania ilipata neema kidogo kwa

 baadhi ya wanajamii lakini kwa Wais-

 lamu hali ilikuwa bado ngumu zaidi.Moja ya kauli mbiu iliyoshtadi kipindihicho ilikuwa ni awamu ya ‘rukhsa’.

Tukiachana na awamu hiyo, awa-mu iliyofuata ambayo ndio kiini chamada yetu ilikuwa kipindi cha Ben- jamini William Mkapa, awamu iliyo- batizwa, zama za ukweli na uwazi.Moja ya mambo aliyasema Rais Mka-pa kipindi cha utawala wake akili-hutubia bunge mjini Dodoma alise-ma: “miongoni mwa mambo yamsingi katika utawala bora lazimaujipambe na sifa ya ukweli na uwazikatika kufanya maamuzi, hii ni kwa viongozi wa siasa na watumishi wen-gine wa umma, katika masuala yaukusanyaji mapato na matumizi….”

Jambo la kuzingatia ni suala la uk- weli na uwazi (Trufullness and trans-parency ). Mambo haya ni katikamsingi wa uhuru, uadilifu wa maisha ya mwanadamu na viumbe wengine.Ukweli ni jambo zuri na kila mtu ana-penda aambiwe ukweli.

Kinyume cha ukweli ni uongo. Nahakuna mtu anapenda kuambiwauongo. Kwa kusimamia ukweli dhu-muni letu ni kuwa na uhuru kamili,

usawa na haki kwa njia yoyote itakay-

ohitajika. Zipo kauli nyingi kuhusuukweli baadhi ni hizi zifuatazo.

“Unaweza kuepuka ukweli lakinihuwezi kuepuka matokeo ya kuuk- wepa ukweli “( Ayn Rand,1905-1982).

“Ukweli upo katika upande un-aoonewa (Malcom X).”

“ Kweli haiachi kuwa kweli kwasababu watu wanaikataa”

“Ukweli huwa haudhuriki walahaunatijiki isipokuwa mtu/jamii ndoitafaidika kwa ukweli wake au itad-hurika kwa kupuuza ukweli”.

Kwa kuwa na kauli mbiu nyingihaimaanishi ndo mmefanikiwa kati-ka kauli mbio hizo, moja ya jambo li-nalotuangamiza kama taifa ni kuwana baadhi ya viongozi wetu waan-damizi ambao si wa kweli katikamaneno na vitendo, mpaka wanaji-danganya wenyewe.

Mfano, Juha yeye alikuwa anajita-hidi kuwa na ratiba zote za maeneo yenye sherehe katika mji wao. Sikumoja ikawa hana ratiba yoyote yasherehe. Kwa kuwa watu wake wana-pata taarifa kutoka kwake wakamfua- ta kumuuliza leo wapi? Juha alikuwa

hataki kuonekana hajui, akaamua

kutokuwa mkweli. Akawaambia leoni kwa mfalme!!!

Kweli wale watu wakaenda mpakakwa mfalme. Kwa bahati kwa mfalmehakukuwa na kitu. Wakaamua wakae wapumzike. Ikapita muda mrefu bilakurejea Juha akaona kimya nayeakaamini itakuwa kuna sherehe kwe- li, akafunga safari mpaka kwa mfalme lakini hakukuta kitu. Yapo matukiomengi ya nchi yanayotokea katikazama hizi za uhai wetu ambayo yame- litia Taifa letu katika janga la umasiki-ni ambao waathirika wakubwa ni raiamasikini wasiokuwa na hatia, ambao bado wana siasa wetu uchwara watatumia udhaifu wa wananchihawa na kuwaahidi kwa maneno yakijifedhuli na dhihaka katika kipindihiki cha uchaguzi unaokuja.

Chakusikitisha katika nchi yetumatukio makubwa ya kifisadi yalipoi- buka na mafisadi wakagundulika,hawakuonekana kwamba ni watu wa

ajabu na wabaya sana, bali wal-ioonekana ni mashujaa, ajabu sana!!Kwa mwenendo huu, tusitaraji

kwamba mtu anayetaka kufanyaufisadi ataogopa, kwani anajua Tan-zania bado hakuna hatua madhubutidhidi ya mafisadi wa kweli. Ukipimakwa vipimo vya sawa, utagunduakwamba bado Tanzania haijapata vi-ongozi wazalendo wa kweli.

Miongoni mwa mambo ambayo yanayoweza kumjengea mtu tabia yaukweli na uwazi ni mtu au jamii kuwana dhamira madhubuti katika kuy-aendea mambo. Jambo la kusikitishakwa baadhi ya viongozi wetu walio wengi hawana dhamira madhubutikwa jamii yetu ya Tanzania.

D

hamira ni jambo ambalomsingi wake ni uaminifu

na upendo wa kweli. Kwamaana nyingine, raia wa

Tanzania wanahuruma na upendo nanchi yao ndo maana huwa wanajita-hidi kwa kadri ya haja kutekeleza ma- jukumu kwa namna wanavyoweza, lakini wanakatishwa tamaa na baadhi ya viongozi.

Uislam umeipa dhamira kipaum- bele. Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) anasema: “Kila jambo/ten-do la mtu hukubaliwa kutokana nania/dhamira yake………”

Kwa kuwa na dhamira madhubu- ti, sote kwa pamoja viongozi na raia tutaiwezesha nchi yetu kupiga hatuakubwa na kuepusha mizozo namigongano isiyo ya msingi. Ukweli nauwazi utawezesha mambo yetu kuwamepesi, na Mwenyezi Mungu ata-

 tusamehe makosa yetu. Hayo ni ma-fundisho ya Qur’an, kitabu kilichomuongozo kwa wanaadamu.

“Hakika wale wanaoupotoa ukweliuliomo katika Ishara zetu hawatu-fichikii Sisi. Je! Atakaye tupwa motonini bora au atakaye kuja kwa amaniSiku ya Kiyama? Tendeni mpendavyo,kwa hakika Yeye anayaona mnayo ya- tenda. (41:40).

“Enyi mlioamini! McheniMwenyezi Mungu na semeni maneno ya kweli. Mwenyezi Mungu atakusa-hilishieni (kukutengenezeeni) mam- bo yenu na atakusameheni madham- bi yenu. Na anaye mt’ii MwenyeziMungu na Mtume wake, bila ya shakaamefanikiwa mafanikio makubwa.(33:70-71).

 [email protected] 0783

 174 730

Zama za ukweli na uwazi zitafika lini?

MAKALA

TANZANIA YETU IPO KATIKA MCHAKATO WA

UCHANGUZI UNAOTARAJIWA KUFANYIKAOKTOBA, AMBAPO TUTAMPATA RAIS WA

 AWAMU YA TANO. AWAMU YA KWANZA

 YA MWALIM JULIUS KAMBARAGE NYERERE

ILIKUWA NGUMU KWA WOTE LAKINI, KWA

WAISLAMU ILIKUWA NI NGUMU ZAIDI.

Page 14: Imaan Newspaper issue 5

7/17/2019 Imaan Newspaper issue 5

http://slidepdf.com/reader/full/imaan-newspaper-issue-5 14/19

www.islamicftz.org

21 Rajab 1436,  JUMATATU Mei 11 - 17, 2015

Kitabu: Al Fusuul Fii Mustwalahi Hadiithi r-RasuuliMwandishi: Haafidh Thanaau-ll-waahiZaahidyMfasiri: Sheikh Muhammad IssaMlangowaTatu – Hadith zenye kukubaliwa

1. Swahihu:Nazo zimegawikamafungu mawili;-

-Swahihu Lidhaatihii: Ni Hadith yenyeupokezi ambayo upokezi wake umeunganakuanzia mwanzo wake mpaka mwishowa ke kw a ku nu ku li wa na mw ad il if umwenye udhibiti kamili kutoka kwawapo kezi wa mfan o w ake na wala asip-wekeke wala kuwa na ila.

-Swahihu Lighayrihii: Ni hadith ambayo

upokezi wake umeungana kuanzia mwanzo wak e had i mwisho kwa kun uku liw a naMwadilifu ambaye udhibiti wake umekuwamdogo akinukuu kutoka kwa mwenyedaraja ya juu (kuliko yeye), lakini ikapatil-izwa kwa njia nyingine ya upokezi iliyo sawana hiyo au iliyo sahihi, na wala isiwe yakipekee au yenye ila. Nayo si kama Swahihu

 lidhaatihii kwa nguvu.

2. Al Hasan: Nayo imegawikamafungu mawili;

 - Hasanun Lidhaatihii: Ni Hadith am- bayo upokezi

 wa ke um eu ng an a kw a ku mn uk uumwadilifu ambaye udhibiti

 wake umepungua akinukuu kutoka kwa

mwenye daraja sahihi na wala asipwekeke wala kuwa na ila. Nayo ni ya 

hadhi ya chini kuliko Swahihu lighayri-hii.

-Hasanun Lighayrihii: Ni Hadith am- bayo mpokezi wake amedhoofishwa,si kwaUfaasiq wala urongo au niile ambayo up-okezi wake umekatika, lakini udhaifu wakeukaondoka kwa kupatilizwa au kuwekoushahidi (uliosahihi).

3.AlMahfuudhu:Ni hadith ambayoameisimulia aliyetegemewa zaidi, tofautina upokezi wa anayetegemewa kwa kuzidiau kupungua katika matini au Sanad yake.

4. Al Ma’ruufu: Ni hadith ambayo amei-simulia mwenye kutegemewa, tofauti na al-ichosimuliwa aliye dhaifu.

MAHUSIANO YA KIBINADAMUUSTAADH HABIB HAMIM

MAPITIO YA VITABU TOVUTI ZA KIISLAMU

Ulemavu wa akili ni nini?

Ulemavu wa akili ni hali ya matati-zo aliyonayo mtu kutokana na upun-gufu wa akili unaomzuwia kujifunza

na kutekeleza majukumu au kazi ana-zozifanya mtu wa kawaida asiyekuwana ulemavu, anaefanana naye kwaumri, kiutamaduni, kiuchumi, na ki-

 jamii.Kutokana na upungufu wa akili,

muathirika wa maradhi ya akiliatashindwa kutimiza mahitaji yakekama ilivyo kwa mtu wa kawaida.

Mahitaji hayo yanaweza kuwa ni ya kielimu, kisaikolojia, kimaisha,kikazi, kiuchumi na kiafya.

Jamii inatakiwa kutambuwa uwe-po wa watu wenye ulemavu, ku-

 wathamini kwa ubinadamu wao nakuwafanyia ihsani na wema kama Al-

 lah Ta’ala anavyotuamrisha ndani yaQur’an tukufu akisema:

 “…Na saidianeni katika wema nauchamungu. Wala msisaidiane katikadhambi na uadui. Na mcheniMwenyezi Mungu. Hakika MwenyeziMungu ni mkali wa kuadhibu” (5:2).

Katika hadith, Mtume anasema:Kwa hakika Allah ameandika thawa-

 bu za kutenda ihsani katika kila kitu.

Ikiwa suala la kutendewa wema naihsani linapaswa kutendewa watu

 wote bila kubaguwa, ni muhimu zaidikutendewa watu wanaohitajia, husu-san watu wenye mahitaji maalumkama ya ulemavu. Thawabu zinazo-patikana kwa kuwatendea ihsani nakuwatendea wema watu wenye mahi-

 taji maalum, ni nyingi ukilinganishana pale unapowatendea wema na ih-sani watu wa kawaida.

+255 718 561 149 habibmitwe@

yahoo.co.uk

ULEMAVU WA AKILI:

NA KHALID OMARY

Kila sifa njema anastahiki MwenMungu Muumba wa kila kitu, na hma na amani zimfikie kipenzi chMtume Muhammad pamoja na

naofuata muongozo mpaka siku ya mwisho.Baada ya kuiangazia tovuti ya Tanzil

naamini msomaji wa safu hii utakuwa umeipunaitumia na kuendelea kuelimika.

Leo tunaangazia tovuti nyingine yenye mafzo ya dini, iitwayo Alifta.com.

Tovuti ya Alifta ni tovuti iliyopo huko-Sa Arabia na imejikita kwenye ‘Fat-wa’ za mashembalimbali wa jopo maalum la masheikh wat

 linalojulikana kama ‘Wanachama wa KamatKudumu ya Wanazuoni ya IFTA’. Katika tovutunaweza kupata fat-wa mbalimbali, lakini w

 wamekwenda mbali zaidi kwa kuweka fat-wakila mwezi husika. Kwa mfano, katika mwezi

 wa Rajab kuna fat-wa zote za mambo yanayohdini katika mwezi husika. Kwa mfano utapata

 jua, swaumu katika mwezi huu imezungum vipi kwa mujibu wa Qur’an na Sunna, kadhamasuala ya umra na mengineyo. Vilevile utapkujifunza vitu vingi na dini yetu kwa ujumla ku

 tia vipengele vya mada tofauti tofauti,kamauchambuzi wa kina na kitaalamu wa kila moja

 tika nguzo tano za Uislamu.Kupitia tovuti hii ya Alifta.com, utaweza kup

khutba za Sheikh Abdul Aziz Ibn AbdullahMuhammad al Shaykh pamoja na Fat-wa zotSheikh Ibn Baz, bila kusahau historia na mai

 ya masheikh wanaochangia na kufanya kazi yauelimisha umma wa Kiislamu kupitia mtanhuu. Kupitia mtandao huu, unaweza kupekkutafuta na kusoma mada zote kwa lugha zaidnane tofauti, ikiwemo Kiarabu, Kiingereza,faransa, Kichina, Kihispania, Kiurdu, KiturKi-indonesia na Kifarsi.

 Wasimamizi wa mtandao huu hawakuwhau wale wenye matatizo ya macho, kwani unaza kubadilisha rangi ya nyuma ya muonekanomtandao ’background’ kwa rangi ambitaendana na uwezo wa macho yako ili isiwkukuumiza hata kama umekaa nayo kwa mmrefu.

Kwa ushahidi wa hayo unaweza ukatemb

kupitia www.alifta.com0683 110 006 

MWANDISHI WETU NA MASHIRI-

KA YA HABARI

Waislamu nchini wamelaani hatua yaSerikali ya China ya kulazimishandugu zao nchini humo kuuza vitu vya haramu kwa kisingizio cha

kupambana na Waislamu wenye siasa kali. Amir wa Shura ya Maima mu na Mwenyekiti

wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh MussaKundecha amesema kwamba suala hilo ni hara-mu, litaendelea kubaki haramu na halikubalikihuku akikielezea kuwa kitendo hicho ni uchokozina ukandamizaji wa haki za Waislamu.

Naye, Sheikh Muhammad Issa, Naibu Katibuwa Baraza la Sunna ameita hatua hiyo ya China

kuwa inalenga kudhoofisha Uislamu, lakini haita-fanikiwa.Kwa mujibu wa kituo cha habari cha Interna-

 tional Business Times, maduka na migawaha ya Waislamu nchini China iliamriwa kuuza pombena sigara ili kudhoofisha nguvu za Waislamu wen-gi katika mji wa Xinjiang.

Nacho kituo cha habari cha Radio Free Asiakimesema, wauzaji watakaokiuka amri hiyo watafungiwa maduka yao na kushtakiwa.

Kituo hicho kimeripoti kuwa, hali hiyo ni mfu- lulizo wa kampeni za kupinga dini ya Kiislamuinayoenedeshwa na utawala wa China kwa kising-izio cha kupambana na imani kali za kidini.

Hata hivyo, lengo halisi la Serikali ya China nikudhoofisha ushawishi wa Kiislamu kasikazinimagharibi mwa China.

Mamlaka za nchini humo katika mji waLaskuy umetoa tangazo kwa wakazi wa kijiji cha Aktash kuwa: “Migahawa na masoko katika kijijichetu lazima yaweke nembo mbali mbali zapombe na sigara katika maduka yao. Wenye

maduka pia wanaamriwa kutangaza bidhaa hizokatika maonesho”.

Mamlaka za nchini humo zimeonya kuwa:“Mtu yeyote atakaepuuza tangazo hilo nakushindwa kutii agizo, maduka yao yatafungwa, biashara zao zitasimamishwa na hatua za kisheriazitachukuliwa dhidi yao”.

Tangazo hilo linasema kuwa, amri hiyo ime- toka katika ngazi za juu za Chama cha Kikomunistkinachotawala nchini humo.

Kwa mujibu wa gazeti la The Washington Post la nchini Marekani linasema kuwa, maofisa waSerikali na watoto katika jimbo hilo la Xinjiang lenye idadi kubwa ya Waislamu wamezuiliwakuhudhuria misikitini au kufunga mwezi mtuku-fu wa Ramadhani, amri ambayo ilianza Junemwaka jana, huku katika maeneo mengine nchinihumo, wanawake wakizuiliwa kuvaa nikabu na wanaume kutokufuga ndevu ndefu.

China yalaaniwa kwakulazimisha Waislamu

kuuza nguruwe, pombe

Page 15: Imaan Newspaper issue 5

7/17/2019 Imaan Newspaper issue 5

http://slidepdf.com/reader/full/imaan-newspaper-issue-5 15/19

www.islamicftz.

21 Rajab 1436,  JUMATATU Mei 11 - 17,

16

G

azeti la Imaan limepatafursa ya kuhojiana na baa-dhi ya wasichana wali-

omaliza vyuo mbalimbali walioolewa na ambao hawajabahati-ka kupata nusra jijini Dar es Salaamkuhusiana mtazamo wao juu ya ndoa.

Kuhusu ndoa, Qur’an inatuambia:Na katika ishara zake ni kuwa ameku-umbieni wake zenu kutokana na nafsizenu ili mpate utulivu kwao. Nayeamejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shakazipo ishara kwa watu wanaofikiri.(30:21)

 Aidha, kwa mujibu wa MtumeMuhammad (Rehma na amani ziwe juu yake) ndoa ni katika sunna zakena yoyote asiyetekeleza sunna zakehana shirika naye (Sunan Ibn Majah).

Katika mjadala juu ya kwa nini vi- jana wengi wanachelewa kuoa, Ashu-ra Almasi amesema, moja wapo ya

sababu zinazopelekea hali hiyo ni

mmomonyoko wa maadili.Mmomonyoko wa maadili unaan-

zia katika ngazi ya familia. Watoto ha-

 wapelekwi madrasa kujifunza elimu ya dini na badala yake mtoto anapele-kwa shule za kikristo. Matokeo yakeanakua katika maadili ya kutokumjua Allah Ta’ala. Mtoto anayekulia maz-ingira ya kutokumjua Allah hatoonaumuhimu wa kuoa au kuolewa, bada- la yake ataendekeza uzinifu. Aidha Ashura aliongeza kwamba, vijana wengi hawana hofu ya MwnyeziMungu na hii inapelekea wao kuwambali na mafundisho ya Mtume wetuMuhammad (Rehma na amani ziwe juu yake). Katika Qur-an tunafaham-ishwa kuwa: “Hakika waumini ni wale ambao anapotajwa MwenyeziMungu nyoyo zao hujaa khofu, na wa-napo somewa aya zake huwazidishaimani, na wakamtegemea Mola waoMlezi”. (8:2)

Kama vijana tungekuwa na imani

 ya kweli tungekuwa na hofu ya Allahna tungeacha zinaa.

Katika mahojiano na mhitimu

mwingine wa chuo, Subira lymo al-isema kuwa, sababu nyingine inay-opelekea vijana wa Kiislamukuchelewa kuoa au kuolewa ni athariza utandawazi.

Utandawazi unaenda sambambana kuenea kwa tabia za kimagharibiambazo nyingi zinakinzana na Uisla-mu. Vijana wa Kiislamu wanaiga tabia na mitazamo hiyo bila kuzinga- tia kuwa zinaenda kinyume na ma-fundisho ya Allah. Vyombo vinavyo-chochea utandawazi ni pamoja namitandao ya kijamii na teknolojia ny-ingine za kisasa za mawasiliano.

Naye mhitimu mwingine wa chuoNeema Husein, akizungumzia up-ande wa wanawake, amesema wa-sichana wengi wanaogopa ndoa, hu-susan za wake wengi, wanapoangalia

 wenzao waliotangulia kuolewa wana-

 vyoishi katika maisha yao hayo yandoa.

Neema Husein amesema baadhi

 ya wanaume wamekosa uadilifu wan-apooa wake zaidi ya mmoja.

“Qur’an imeruhusu mwanammemwenye uwezo aowe mke zaidi yammoja kwa sababu tofauti tofauti, la-kini wanawake wengi waliopo kwenyendoa zenye mke zaidi ya mmoja wamepitia karaha na tabu nyingi siokwa sababu Allah alikosea, bali kwasababu wanaume wamekosa uadilfu”,alisema Neema.

Lakini kwa upande mwingine, vi- jana wa kiume nao wamelalamikakuwa wasichana wengi wa siku hizi wana tamaa ya mali na hivyo basi hu-penda kuolewa na wanaume wenyepesa, huku kigezo cha dini kikitupili- wa mbali. Ikitokea kijana hana malihawezi kumpata msichana aliyependakumuoa.

 AbdulQadir Oumar, mmoja kati

 ya vijana ambaye hajaoa, mkazi waMagomeni Makuti anasema: “Wakatifulani unataka kuoa, lakini msichanaanaweza kukupenda na akawa hata tayari kuzini na wewe, lakini siokuolewa nawe kwa sababu umaskini wako”. AbdulQadir anasema, kuto-kana na tamaa za wasichana, vijana wengi huamua kutafuta kwanza mai-

sha kabla ya kuingia katika ndoa.Kwa mujibu wa AbdulQadiri tam-aa za wasichana mara nyingi zimepe- lekea usaliti katika ndoa. “Tunaonahaya kwa wenzetu waliotangulia nandio maana nasi tu waoga”.

 AbdulQadir na wengine walio-changia mada walishauri kuwa vijana warudi katika misingi ya dini na waoemapema ili kujiepusha na maasi ya zi-naa na kupata radhi za Allah ambayeanasema katika Qur’an Tukufu: “Walamsikaribie uzinzi. Hakika huo niuchafu na njia mbaya (17:32).

 Aidha wameshauri vijana na wanandoa kwa ujumla wazingatie misingi ya ndoa ambayo kubwa zaidi ni hofukwa Mungu, upendo, kuvumiliana,ukarimu, kuheshimiana na kuyafum- bia macho matatizo madogo madogoambayo yanatokea kwa mmoja wa

 wanandoa.

Kwa nini vijana hawataki kuoa au kuolewa

HAFSWA MADIWA

MILA NA DESTURI

Katika toleo lililopita tulizun-gumzia kwa ufupi, maana ya Israa na Miiraji, aya ziliz-oizungumzia safari hiyo,

siku, mwezi na mwaka iliyotokea msa-fara huu. Tukio lililomtokea Mtumekabla ya safari, na tukahitimisha naaina ya usafiri uliyotumika katika safarihiyo.

Ndugu msomaji, andamana namikatika makala hii ili ubaini pamojanami kuwa, aya za Qur’an na hadith sa-hihi zinazoisimulia safari hii ya Israa naMi’iraj, zinabainisha kuwa; Safari mbilihizi zilifanyika kwa mwili na roho, naMtume akiwa hadhiri, kwa ushahidiufuatao:

Mosi: Allah ameanza kulisimulia tukio hili la msafara wa Israa na Mi’irajkwa tas-bih (Sub-hana): “Utakasifu ni wa Allah ………” Na kwa kawaida Waarabu na Waislamu wanapolistaa- jabu jambo au tukio lisilo la kawaidakatika maisha yao ya kila siku, husemaSub’hana Llah, kama ishara yamshangao kwa jambo lililoduwazakwa kukhalifu kawaida.

Pili: Surat Al-israa ilipoanza kwa

 tasbih “Utakasifu ni wa Allah aliyem-peleka mja wake”, bila ya shaka ilikuwainatoa taswira fulani kwa Waislamukuwa: Punde kuna jambo la ajabu litafuata na kuwashangaza wengi, na jambo lenyewe, ni safari ya Israa na Mi-iraj iliyouhusisha mwili na roho yaMtume Muhammad (Rehma na ama-ni ya Allah iwe juu yake).

Tatu: Kitenzi kilichotumika kwenyeaya ni ‘Asraa’. Kitenzi hiki hakitumikikwa mtu aliye usingizini/aliyelala nakilugha humaanisha safari iliyofanywana mtu nyakati za usiku ikijumuishamwili na roho sambamba na kumju-muisha anayepeleka na anayepelekwa.

Nne: Aya inaonesha Mtume (Reh-ma na amani ya Allah iwe juu yake)hakwenda mwenyewe katika safari hii ya ajabu, bali alipelekwa na aliyempe- leka ni Allah mwenyewe.

 Allah anasema: “Utakasifu ni wa Allah aliyempeleka mja wake”. Kupele-ka kunafahamika. Namna alivyompe- leka zaidi ya tulivyoelezwa hatujui.Kuhoji jinsi alivyompeleka ni uzushi na

kuamini kuwa alipelekwa na Allah ni

 wajibu.Tano: Neno ‘Mja wake’ popote linapotumika huwakilisha kiwiliwilisambamba na roho, na wala halitumikikwa kuiwakilisha roho pasi na kiwili- wili. Na lau Mtume angekwenda kiro-ho, Allah angesema: “Asraa biruuhia’bdihi”. Lakini fasaha ya Qur’an haine-ni hivyo. Tanabbahi !

Sita: Tumeelezwa katika hadithkadhaa zilizo sahihi kwamba (Rehmana amani ya Allah iwe juu yake) alisafirikwa mnyama wa peponi (Buraq) aliyena kimo cha kati ya punda na nyumbu. Wala hakuna hata sehemu moja katikahadithi panaposema kwamba Mtume(Rehma na amani ya Allah iwe juu yake) aliota amempanda Buraq wakatianakwenda Masjidul-aqswa!. Haliinayothibitisha alikwenda kwa mwilina roho.

Saba: Lau Safari ya Israa na Miirajiingefanyika kindoto hakungekuwa nasababu ya kuita safari hizo muujiza nahata washirikina wasingekuwa nasababu ya kumpinga Mtume (Rehma

na amani ya Allah iwe juu yake) kwani

kupitia ndoto mtu huweza kuona aukufanya vitu vingi vya ajabu.Lakini kilichosababisha mshangao,

ubishani na hata baadhi ya Waislamudhaifu wa imani kurtadi ni baada yakuambiwaMtume (Rehma na amani ya Allah iwe juu yake) aliifanya safarihiyo kwa mwili na roho na si ndoto, tena ndani ya muda mchache wa usikuna kuona kwa jicho yale aliyoyaona.

 Allah anasema: “Jicho halikupepesa wala halikuruka mpaka (uliowekewa)”.Jicho ni sehemu ya kiungo cha mwilina si roho. Imam Ibnu Qayyim anaele-za: “Jicho la Mtume halikuangalia kulia wala kushoto wala zaidi ya lilipopangi- wa”. Hii ni kuthibitisha jinsi Mtume al-ivyoiva na kukomaa kimaadili.

Na neno lake: “Tulimpeleka hivyoili tumuoneshe baadhi ya alama zetu”.

Na neno lake: “Kwa yakini aliona

mambo makubwa katika alama zaMola wake”. (Rejea: Annaj-mu: 17-18).

Nane: Kutajwa kutopepesa jicho,kupelekwa na kuoneshwa alama za Al- lah ni ishara kuwa Mtume alikuwa ha-

dhiri kwa mwili na roho wakati wa

 tukio na si ndoto. Tisa: Hadith kadhaasahihi zinaeleza kwamba Mtume (Re-hma na amani ya Allah iwe juu yake)alipofika kwenye Masjidul- aq-swaa al-iwaswalisha Mitume, na alikunywamaziwa, huu nao ni uthibitishomwingine wa kihadith kufanyika kwasafari hii kwa mwili sanjari na roho.

Hatuoni hata sehemu moja inayoe- leza kwamba Mtume (Rehma na ama-ni ya Allah iwe juu yake) aliota anawas- walisha Mitume wenzake kwenyeMasjidul- aqswa na kunywa maziwa !.

Kumi: Hadith zote sahihi za Mtume(Rehma na amani ya Allah iwe juu yake) zinathibitisha kwamba Mtumealisafiri kutokea Makka mpaka Mas- jidul aqswa kwa Buraq, hatujaona hatasehemu moja inayosema Mtume (Re-hma na amani ya Allah iwe juu yake),aliota amepanda Buraq. Na kifasihi

kiwiliwili na roho ndicho kinachopan-da mnyama na si roho pasi na kiwiliwi- li.

Kumi na moja: Ama dai la wana-osema, safari ya Israa na Miiraj ilifan-

 yika usingizini na kutoa ushahidi wneno la Allah: “Na hatukuyafany

maono yale tuliokuonesha ila ni kuw jaribu watu…”. (Al-israa: 60). Na kudkwamba; kilugha ‘Ru-uyaa’ hufanyikusingizini pekee, dai hili si sahihi nhalina mashiko ya moja kwa moja.

Neno ‘Ru-uyaa’ katika lugha ya Karabu huja baadhi ya nyakati likimaanisha maono ayaonayo mtu awapo usigizini, au ayaonayo awapo hadhiri, n wakati mwingine humaanisha kiakionacho mtu kwa njia ya wahyufunuo, hivyo kuing’angania maanmoja peke yake na kuziacha nyinginkunahitaji dalili na dalili hapa haipo.

 Ama neno ‘Ru-uyaa’ kwa maanaymaono anayoyaona mtu awapo hdhiri ni kama tukio hili lililomtokMtume katika usiku wa Israa na MiirImepokewa na Imam Bukhari (Allaamrehemu) kutoka kwa Swahaba Ibn Abbas (Allah amridhie), wakati anafasiri neno la Allah:

“Na hatukuyafanya maono yale tu liyokuonesha ila kuwajaribu wa(wataamini au hawataamini)”. [Al-iraa: 60]. Kisha akasema: “Huko kuona kwa jicho alikooneshwa Mtum(Rehma na amani ziwe juu yake), usikaliopelekwa mpaka ‘Beytul-maqd(Fat-hul baar: 8/218 na Zadul-masifiy I’lmit tafsiir: 5/35 na Sunanut Timidhiy 5/302).

Na Imam Bukhari ananukuu tenkutoka kwa swahaba Ibnu Abbas (A lah amridhie) akisema: “Huko ni kuna kwa jicho, na yawezekana hekim ya huko kuona kuitwa ‘Ru-uyaa’ ni kwsababu mambo ya ghaibu kimaonhutofautiana na maono ya asili, na ndmaana yakalinganishwa na yale yao wayo usingizini”. (Rejea Fat-hul baar

19/448 Mlango: Awwalu maa bud bihi rasulullah).Endelea kuandamana nami katik

 toleo lijalo ili upate faida insha Allah.

Safari ya Israa na Miiraji haikuwa ndoto

MAKALA YA DINI NA SHEIKH SHABANI MUSSA

Page 16: Imaan Newspaper issue 5

7/17/2019 Imaan Newspaper issue 5

http://slidepdf.com/reader/full/imaan-newspaper-issue-5 16/19

www.islamicftz.org

21 Rajab 1436,  JUMATATU Mei 11 - 17, 2015

MAKALA YA KIMATAIFA

NA YUSUFU AHMADI

Moja ya migogoro

mikubwa inayo- tikisa na kuugawaulimwengu kwa

kipindi kirefu ni ule wa Israel naPalestina. Ajenda ya mgogorohuu imejitokeza mara nyingikatika vikao vya Umoja waMataifa (UN) tangu ul-ipoundwa mwaka 1945.

Licha ya vikao vilivyolengakuushughulikia mgogoro huo,hali imebaki kama ilivyo, hukuwakazi wa Palestina wakiende-lea kuteseka chini ya utawala wakimabavu wa Kizayuni.

Pamoja na mgogoro huokuangazwa zaidi mara baada yakuundwa kwa taifa la Israelhapo mwaka 1948, sintofaha-mu ya eneo hili ilianza tangumwaka 1917 mara baada ya az-

imio la Balfour lililotangazamsimamo wa Uingereza wa ku-unga mkono uanzishawaji wataifa la Israel katika ardhi ya Pal-estina.

 Azimio hilo lilitolewa kupitiabarua ya Waziri Mkuu wawakati huo, kwenda kwa kion-gozi wa jamii ya Wayahaudi,Baron Rothschild.

Katika miaka ya 1920swenyeji walishaanzisha upinza-ni dhidi ya ujio wa Wayahudinchini Palestina, huku Israelinayo ikiunda vikundi vya siri vyakigaidi, vikiwemo Haganah naIrgan ili kukabiliana na wenyeji.

Kuundwa kwa Israel1948

 Wakati Umoja wa mataifa(United Nations) unaundwahapo Oktoba 24, 1945, Palesti-na ilikuwa miliki ya taifa laUingereza. Umoja wa Mataifawa wakati huo ukiitwa ‘Leagueof Nations’, ulioundwa January10, 1920 na kudumu kwa miaka26 ndio ulioipatia Uingerezamamlaka ya kuitawala Palestinamwaka 1922.

Kabla ya azimio lao la Bal-four, Waingereza walipendeke-za taifa hilo lianzishwe nchiniUganda, jambo ambalo lilip-ingwa na Wayahudi, walioitakaardhi ya Palestina tu.

Moja ya sababu zilizoifanyaUingereza kubadili uamuzi nakuruhusu Wayahudi kujengamakazi yao Palestina badala ya

Uganda ni woga wa baadhi yawanasiasa wa kukosa uungwaji

mkono toka kwa Waingereza wenye asili ya Kiyahudi.

Pili, Uingereza ilikubali

ombi la Wayahudi kwa sababu ya ushawishi wa Chaim Azriel Weizmann, mkemia aliyemilikikampuni ya Weizmann Insti- tute of Science ya kutengenezakemikali za acetoni ambazoUingereza ilizihitaji katikamambo ya silaha.

Sababu ya tatu, ni uhusiano wa dini ya Kikristo na ile ya Ki- yahudi, ambapo inaaminiwakurejea kwa Wayahudi katikaardhi ya Palestina walipokuwe-po karne kadhaa nyuma, kuna-safisha njia ya kurejea kwamkombozi wa Wakristo, Yesuambaye Waislamu wanamtam- bua kama Issa bin Maryam.

Hata hivyo, azimio la Waingereza la Balfour liliitakaIsrael kuzingatia haki zote za wenyeji bila kwabughudhi. Se-hemu ya tamko inasema “ ...naifahamike kuwa pasiwepo naunyanyasaji wowote wa haki zakiraia na kidini kwa Waarabu wa Palestina.” Kiyume na ma- tarajio ya Uingereza, ghasia zili-zuka mara kadhaa.

Mwaka 1947, Serikali yaUingereza ililipeleka suala laPalestina katika Umoja waMataifa (UN) kulitafutia ufum- buzi na kupelekea kuundwakwa kamati maalum ya wa- jumbe 11 walioenda Palestinakuchunguza tatizo.

 Wakati Wayahudi walishiri-kiana na kamati hiyo, uongozi wa Palestina waligoma kushiriki baada ya kubaini kamati hiyo il-

ielekea kuipendelea Israel.Kamati ilimaliza kazi yake Agosti 1947, ambapo katika az-imio namba 181(II) ilipendeke-za kugawanywa kwa Palestinana kuunda mataifa mawili, Pal-estina na Israeli, huku mji waJerusalem ukipewa hadhi maa- lum na kusalia chini ya uangalizi wa Umoja wa Mataifa.

Katika hali ya sintofahamu,May 14, 1948, Uingereza ilijion-doa kama msimamizi wa Pales- tina na kuondoa majeshi yake.Siku hiyo hiyo Wayahudi waka- tangaza rasmi kuundwa kwa taifa la Israeli.

Kuzuka kwa Vita Waarabu hawakuridhika na

kuundwa kwa taifa la Israel na

kupelekea kuzuka kwamgogoro. Mwaka 1948 vita ya

Mataifa yaMagharibi

yanavyosaidiadhulmaPalestina

kwanza baina ya Waarabu waki-iunga mkono Palestina dhidi yaIsrael ikazuka na kudumu hadi

1949, ambapo Umoja wa Matai-fa uliingilia kati na kufanikishakusainiwa kwa makubaliano yakusitisha vita.

Hata hivyo, kutokaa na vitahiyo, Wapalestina 750,000 wal-iondolewa katika ardhi yao nakuwa wakimbizi.

 Vita nyingine vilipiganwa1967 na 1973 huku Israeli ikien-delea kupora ardhi ya Warabu.Katika vita ya 1967 Israeli ilin- yakua maeneo ya Sinai, Ukanda wa Gaza, Ukingo wa Magharibiikiwemo mashariki ya Jerusale-mu na miinuko ya Golani ilioponchini Syria.

Ukiacha vita hivyo, Wapales- tina wameendelea kupinga uka- liaji wa ardhi yao kwa mabavu.Harakati hizo zinajulikana kama‘intifada’ neno la kiarabu lenyemaana ya mtikisiko.

Katika Intifada ya kwanzamwaka 1987 hadi 1993, Wapal-estina wa nyanja zote, vijana, wa-fanya biashara, wafanyakazi, wanawake na watoto, walianda-mana, waligoma kulipa kodi nakususia shughuli za kiuchumikupinga uvamizi wa kijeshi waIsraeli.

Katika maandamano hayo yaamani yaliyodumu kwa miakasita, zaidi ya Wapalestina 1,000 waliuawa huku maelfu wakije-ruhiwa na baadhi kuwekwa ki-zuizini.

Intifada ya kwanza ilisitishwamwaka 1993 kwa makubaliano ya Oslo baina ya kiongozi wa

Chama cha Ukombozi wa Pales- tina (PLO) hayati Yaseer Arafatna aliyekuwa Waziri Mkuu waIsraeli Yitzhak Rabin, ambapokila mmoja alitambua uwepo wa taifa la mwenzake.

Intifada ya pili iliyojulikanakama Al-Aqsa iliendeshwamwaka 2000 kufuatia Kiongozi wa upinzani na baadae wazirimkuu wa Israeli, Ariel Sharonkuzuru eneo la Haram al-Sharifkatika mji wa Jerusalem, hatuailiyopingwa na Wapalestina kwamaandamano.

Intifada ya pili ilidumu hadimwaka 2003, ambapo katikasiku tano za mwanzo Wapalesti-na 50 waliuawa na 1,500 walije-ruhiwa.

Baraza kuu la Usalama la

Umoja wa Mataifa lililaani ngu- vu kubwa iliotumiwa na utawala

 wa kizayuni kudhibiti maanda-mano katika azimio lake namba1322 la mwaka 2000.

Kuibuka kwa HamasMnamo 2005, Israeli ilion-

doka katika eneo la Gaza ambalo walilikalia kwa mabavu na kishaJanuari 2006, Chama cha Ha-mas kilishinda viti vingi vya bunge katika uchaguzi mkuu nahivyo Rais wa mamlaka ya Pales- tina Mahmoud Abbas wa chamacha Fatah alilazimika kuundaserikali mpya ya Palestina aki-shirikiana na aliyekuwa kiongozi wa Hamas Ismail Haniyeh.

Ushindi wa Hamas ulizika-sirisha nchi za magharibi zilizo-hofia msimamo wa chama hichoambacho tangu miaka ya 1980kimepinga kuitambua Israeli namakubaliano yote yalifanywahuko nyuma na kupendeleamapambano ya silaha zaidi ku- liko mazungumzo.

Hamas imeendelea kupam- bana na Israel katika eneo laGaza. Mwaka 2006 kulikuwa namapambano makali kati ya Junena Novemba baada ya Israel ku- vamia Ukanda wa Gaza kufuatiakutekwa kwa mmoja wa askari wake.

Mapambano ya Israel na Wa-palestina yamekuwa yakiendeleahuku karibu kila mwaka maelfu ya Wapalestina wakiuawa, kuje-ruhiwa na makazi na mali zaokuharibiwa.

Katika mapambano ya mwa-ka jana pekee takribani Wapal-estina 1,777 waliuawa na wen-gine wengi zaidi kujeruhiwa,

ambapo Israeli ilipoteza watu wapatao 68 tu.

Usugu wa mgogoroLicha ya jitihada mbali mbali

za kutafuta amani, mgogoro huouliodumu zaidi ya nusu karnehaujapatiwa uvumbuzi. Israeliinayoungwa mkono na mataifamengi ya magharibi ikiendeleakuyakalia kimabavu maeneokadhaa ya ardhi ya Wapalestina yakiwemo yale ya ukanda waGaza na ukingo wa Magharibi.

Suluhisho pekee linalotajwaili kumaliza uhasama baina yamataifa hayo ni kuhakikisha kilaupande unautambua mwenzakekama kama dola huru (Sover-eign), jambo ambalo Israeli haili- taki kulisikia, na hivyo Wapales-

 tina nao kukataa kuitambua Is-raeli. Mfano wa jitihada hizo za

kuwepo kwa mataifa mahuru, ni makubalianao ya mka 1995 yaliosainiwa kat

 Waziri mkuu wa Israeli wa w ti ule, Yitzhak Rabin na kion wa Palestina, Yasser Arafat,  bapo Israeli ilikubali kuonutawala wa kijeshi katika ar ya Palestina na kukabidhi daraka kwa serikali ya mpitPalestina ili ianze kujitaw yenyewe.

Jitihada hizo hazikuwafuhisha baadhi ya Wazayuni, kwhapo Novemba 4, mwaka 19 Waisraeli wenye msimamo m li wali muua Wazir i Mk Yitzhak Rabin, jijini Tel A tukio ambalo lililaaniwa dunzima.

Sio hivyo tu, hata pale baa ya mabunge ya nchi za U yanapojaribu kupiga kurkuitambua Palestina kamaivyofanya mabunge ya Ufarana Bunge la Umoja wa Ulmwaka jana, Israeli na mshi wake wa karibu Marekani zikuwa zikipinga juhudi hizohivyo kuzorotesha amani ehilo.

Wajibu wa Waislam kuiunga mkono Palestina

Suala la mgogoro wa Palena lina harufu ya ukiukwmkubwa wa haki za binadana ndio maana hata baadh viongozi wa nchi zisizo za Kimu kama hayati Rais Julius erere, Nelson Mandela, ukiambali Muamar Ghadaff na Amin walipaza sauti kuupiutawala wa kimabavu wa Isr

Kwa Waislamu, popote wipo duniani, ni wajibu kwkuiunga mkono Palestina khali na mali, dhidi ya uonevuIsraeli.

Ukiachia suala la kiutu, mujibu wa mafunzo ya Uisla Waislamu ni ndugu, bila kumipaka ya nchi. Katika mojmafundisho yake Mtume (Rma na amani ziwe juu yake) aufananisha Uislamu na mambao sehemu moja ikiugmwili wote hudhoofu. Ukiaudugu wa Kiislamu, kuna s la maeneo matukufu yaliymji wa Jerusalem iliyokuwa  la ya kwanza ya Waislamu (smu Waislamu waelekeayo wa ti wanaswali), kabla ya MakJerusalem ni miongoni mwa

mitakatifu duniani amb Waislamu wanaenda kuzuru

MOJA YA

 SABABU

ZILIZOIFANYAUINGEREZA

KUBADILI

UAMUZI NA

KURUHUSU

WAYAHUDI

KUJENGA

MAKAZI YAO

PALESTINA

BADALA YA

UGANDA NI

WOGA WA

BAADHI YA

WANASIASA

WA KUKOSAUUNGWAJI

MKONO

TOKA KWA

WAINGEREZA

WENYE ASILI

 YA KIYAHUDI.

Page 17: Imaan Newspaper issue 5

7/17/2019 Imaan Newspaper issue 5

http://slidepdf.com/reader/full/imaan-newspaper-issue-5 17/19

www.islamicftz.

21 Rajab 1436,  JUMATATU Mei 11 - 17,

18

Page 18: Imaan Newspaper issue 5

7/17/2019 Imaan Newspaper issue 5

http://slidepdf.com/reader/full/imaan-newspaper-issue-5 18/19

www.islamicftz.org

21 Rajab 1436,  JUMATATU Mei 11 - 17, 2015

1 WATOTO / TANGAZO

NAHIDA ESMAIL

KONA YA WATOTO

Masafa ya Imaan FM

Kigoma

Moro

Arusha

Ruvuma

Dsm

Mtwara

Mwanza

Tabora

Mbeya

1 Daresalaam 104.5 Mhz2 Morogoro 96.3 Mhz3 Arusha 90.8 Mhz4 Mwanza 105.6 Mhz5 Kigoma 92.5 Mhz

6 Tabora 101.6 Mhz

7 Mbeya 90.3 Mhz8 Dodoma 102 Mhz9 Ruvuma 94.2 Mhz10 Mtwara 90.9 Mhz11 Zanzibar 104.5 Mhz

12 Pemba 104.5 Mhz 

Uislam unatufundisha kuwa na huruma kwa wanyama na kuwatendea vizuri. Kuna wanyama wengi wametajwa katika Qur’an .

Swali: Unajua sura gani katika Qur’an in-amtaja mbwa?

Jawabu: Surat Kahf (Sura ya 18) – kisa cha watu wa pangoni.

“Nawe utawadhania wamacho, na hali wamelala. Nasi tunawageuza kulia na kushoto.Na mbwa wao amenyoosha miguu yake ya mbelekizingitini. Kama ungeli watokea hapana shakaungeli geuka kuwakimbia, nawe umejaa khofu”(18:18).

Unakijua kisa cha watu wapangoni?

Ni kisa ambacho ndani yake Allah (Sub-haanahu Wataallah) anataja waumini wazuriambao walijificha pangoni wakiwa na mbwa

 wao.Hapo zamani za kale, katika mji mdogo, ku- likuwa na kundi la vijana, ambao walimuaminiMwenyenzi Mungu. Hata hivyo, waliishi na watuambao walipotoka na waliosahau maana halisi ya kumuabudu Mungu mmoja.

 Watu hao waliopotoka, walitengeneza sana-mu ya mbao na mawe na kuanza kuyaabudu.Mfalme aliwalazimisha wale vijana wachaMun-gu kuabudu masanamu. Walipokataa, Mfalmealiwaagiza walinzi wake wawaadhibu vijana wale.

Hata hivyo Allah, kwa rehema zake aliwasaid-ia wale vijana waumini wakakimbia na kujifichapangoni. Allah akawafanya walale kwa miaka300! Mbwa pia alilala mlangoni mwa pangopamoja nao.

 Walipoamka, hawakujua walikuwa wamelalakwa muda gani. Walidhani walilala kwa ‘labdasiku moja au masaa kadhaa’.

 Walikuwa na njaa, kwa hivyo mmoja wao al-

ienda mjini na sarafu ya fedha kununua chakula.Hata hivyo, huyo aliyeenda mjini alikuta kila kitukilikuwa kimebadilika kabisa.

 Akakutana na mtu ambaye alikuwa akiuza

chakula na kumpa hiyo sarafu ya fedha. Muuzachakula hakuweza kuijua hiyo sarafu na akam-chukua mtu yule mpaka kwa mfalme wake.

Mjumbe yule aliyetumwa kununua chakulaakamhadithia mfalme kuhusu kisa chake na wenzake waliokuwa wamelala pangoni. Kishaaliongozana na mfalme na watu wa ule mji mpa-ka kule pangoni wakajionee.

Tunachojifunza: Lazima tumuabudu Mungu mmoja siku zote.Tumtegemee Allah. Tukimuabudu Yeye, Allah atatulipa na kutu-

saidia.

Ukimtii Yeye, Allah atakulinda.

Unajua kuwa kusoma SuratAl-Kahf kila ijumaa kuna faidakubwa?

“Yeyote atakayesoma Surat Al-Kahf siku yaIjumaa, atakuwa na nuru itakayong’ara kutokaIjumaa hadi Ijumaa inayofuata.”

Unajua kuwa Allah atatulipa kwa kuwaten-dea wanyama wema?

Mtume wa Allah amesema: “Kuna mtu waka- ti anatembea alisikia kiu na akaingia kwenye kisi-ma na kunywa maji.

 Wakati akitoka, aliona mbwa akihema kwkupaparika huku akila tope kwa sababu ya kikali. Yule mtu akasema: “Huyu (mbwa) anapatshida kama niliyoipata mimi”.

Hivyo basi (akaingia kisimani) akajaza majkwenye kiatu, akakibeba kwa kuking’ata kwmeno yake, akapanda na kumpatia mbwa yulmaji.

 Allah alifurahishwa kwa matendo yake mem

na kumsamehe dhambi zake. Watu wakauliza: “ Ewe Mtume wa MunguTutalipwa kwa kuwatendea wema wanyama? Akajibu: “Ndio, kuna malipo kwa kumtende wema kila kiumbe chenye uhai” (Bukhari).

MBWAUmewahi kusikia kuhusu mbwa aliyetajwa katika Qur’an?

Page 19: Imaan Newspaper issue 5

7/17/2019 Imaan Newspaper issue 5

http://slidepdf.com/reader/full/imaan-newspaper-issue-5 19/19

www.islamicftz.

21 Rajab 1436,  JUMATATU Mei 11 - 17,

20 MGOGORO

SAUDIA NA

IRAN: SIASA

AU DINI?

Uk 10

21 Rajab 1436,  JUMATATU Mei 11 - 17,

NA YUSUPH AMIN

Suala la elimu hupewa ki-paumbele katika maisha ya binadamu kwani ni ibadana hutamalaki na kila

kipengele cha uendeshaji wa maju-kumu ya kilimwengu na hata yale yaakhera.

Kumekuwa na tafsiri mbalimbalikutoka kwa wasomi wa dini ya Kiis- lamu na makundi tofauti kuhusianana dhana nzima ya elimu.

 Wapo wanaodhani kuwa elimu ya ‘k idu nia ’ amb ayo kwa kiasikikubwa imetokana na fikra, utashina falsafa za binadamu kuwa haifaikujifunza.

Lakini dini ya Uislamu ina mta-

zamo upi kuhusu elimu? Allah sub’hanahu wataala anase-

ma: “Soma kwa jina la Mola wakomlezi” (96:1) na hili ndilo agizo lakwanza kutoka kwa Allah kwaMtume Muhammad (Rehma naamani ziwe juu yake).

Pia Mtume Muhammad (Rehmana amani ziwe juu yake) ameamrisha Waislamu, waume kwa wake kutafu- ta elimu.

Hii inathibitisha kuwa, kwa up-ande wa dini ya Kiislamu suala lakuitafuta elimu yenye manufaa (yadunia na akhera) limepewa uzitomkubwa.

Kwa kuzingatia hilo, uongozi waJumuiya ya Wanafunzi wa Kiislamu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(MSAUD) unaendesha mpango

maalum wa kuwaandaa kitaaluma vijana wa Kiislamu wanaofikia 800ngazi ya sekondari kwa lengo la kut-anua wigo wa ufaulu. Mpango huounajulikana kama Msaud TuitionProgram (MTP).

Katika kuliangazia hili, gazeti laImaan limefanya mahojiano namwenyekiti wa jumuiya ya wanafun-zi hao, Ustadh Said Athuman ili ku- jua zaidi kuhusu harakati za jumuiyahiyo, hususan mpango wao wa mas-omo ya ziada kwa wanafunzi washule za sekondari.

Kwa mujibu wa Ustadh Said,MTP ni matokeo ya ajenda muhimuzilizopelekea kuundwa kwa jumuiyahiyo, na hiyo ilitokana na ukwelikwamba miongo kadhaa iliyopitakulikuwa na idadi ndogo ya Waisla-mu wanaojiunga na elimu ya juu.

Ustadh Said alitaja sababu zauchache wa vijana wa Kiislamu kati-ka vyuo vikuu kuwa ni pamoja na vi- jana hao kushindwa kumudu ghara-ma za masomo na mazingira magu-mu ya utafutaji elimu.

Katika kuhakikisha inafikia lengo la kuupe leka mbele Uislam u na Waislamu wenyewe, mwaka 1993 jumuiya ya MSAUD chini ya kamati ya wazee wa Kiislamu ilianzi shampango wa masomo ya ziada katikaShule ya Kiislamu ya Ridhwaa, Ki-nondoni, Dar es salaam.

Ustaadh Said alisema, jumuiya il-iazimia kuwanyanyua vijana kitaa- luma ndio maana masomo yote ya-nayotolewa na kituo hicho ni sawa na bure, isipokuwa kiasi cha shilingi30,000 ambacho mwanafunzi ata-

 ya mambo madogo madogo.Ustadh Said amesema, katika

kuendesha masomo MSAUD ime-kuwa ikishirikiana na walimu wafani mbalimbali kutoka vyuo vyaDIT, MUHAS, SUA, IMTU na Ar-dhi, hatua ambayo imesaidia kupam- bana na changamoto ya ukosefu wa wal imu wa say ans i na silaba sikushindwa kumalizika kwa wakati.

Ustadh Said alisema, pamoja nakufungua vituo vya MTP vilivyopokatika shule za Ridhwaa na Al-fur-qan, Tabata, Jumuiya pia huhamasi-sha walimu wa Kiislamu kufanyamazoezi ya kufundisha (TP) mikoa yen ye chang amo to ya wal imu,ikiwemo Pemba na Zanzibar pamojana mikoa ya kusini ya Lindi na Mt- wara.

 Aki zun gum zia mafanik io yampango huo, Ustadh Said amesema,kutokana na jitihada za walimu,athari imeonekana, kwani namba ya vijana wa Kiislam u kujiunga naelimu ya juu inaongezeka mwakahadi mwaka.

Mwenyekiti huyo, pia amesema,MSAUD inalea vijana kiimani kwakuwapatia elimu ya dini ili wawe

 wengi wao wanapopata elimu yadunia hudhani dini haina nafasi ka- tika maisha yao.

Ustadh Said alisema, katika somo la Qur’an wanafunzi hugawanywamadaraja manne (4), ambapo daraja la kwanza na pili huwa wanafundish- wa namna ya kusoma Qur’an, wakatidaraja la tatu na nne hufundishwahukumu za Qur’an, yaani ‘Ahkaami ttaj-wiid’.

Mbali na tuisheni za MTP kuwana mafanikio makubwa kwa umma wa vijana wa Kiislamu, pia jumuiyaimefanikiwa kutoa viongozi mbalim- bali wa kidini na kijamii katika nchi, wakiwemo viongozi wa sasa wa Cha-ma cha Wana Taaluma wa Kiislamu(TAMPRO) na wale wa TAMSYA.

Pia MSAUD imeweza kutungamtaala wa elimu ya dini kwa wale-mavu wa macho na wenye matatizo ya kutosikia. Mitaala hiyo hutumiwana vituo mbalimbali vya walemavuhao vilivyopo Temeke, Yombo jijiniDar-es-salaam.

Mwenyekiti huyo wa MSAUDamewataka vijana wa Kiislamu kuwamfano wa kuigwa ili kuacha atharikwa jamii kwa kutenda yaliyo mema

do wao. Amesema, ikiwa watatekele-za hilo wataweza kupandikiza fikrachanya kwa walio wengi ambao ha- wafikirii uwezekano wa mtu kuwamsomi na wakati huo huo kubakikuwa mcha Mungu kwa kuwatumi-kia Waislamu na Uislamu.

Gazeti la Imaan liliwatafuta baa-dhi ya viongozi wa zamani waMSAUD kupata maoni yao kuhusuUmoja huo na jinsi ulivyowasaidiakukua kitaaluma na kiuongozi.

Hussein Kapuya aliyekuwa Amirkati ya 2011-2012 ameizungumziaMSAUD kama taasisi iliyomjengakiimani, lakini pia kumtimiziamalengo yake kitaaluma.

 Akikumbuka enzi za uongoz i wake, Kapuya alisema, walifanikiwakulipia ada baadhi ya wanafunzi wenye shida na pia kuunganisha wa-nafunzi wa Kiislamu na Waislamu wa maeneo mengine ya dunia kwakujenga mahusiano na mataifa yaSudan, Kenya na India katika kufan- ya utafiti na kubadilishana uzoefukatika masuala ya dini na taaluma.

Kuhusiana na program ya MTPalisema, tofauti na awali, sasa zi-naendeshwa kwa ustadi mkubwa za-

Naye, Jumbe Ali ambaye naye ali- wahi kuongoza Jumuiya hiyo alise-ma, enzi zao walitoa fursa kwa vijanakufahamu elimu ya dini kwa uwazina urahisi kupitia misikiti, hususankwa wale waliokosa fursa ya kujifun-za elimu hiyo utotoni.

Kiongozi mwingine aliyepita am- baye hakutaka kutajwa jina lake,amesema, akilinganisha na sasa,kipindi cha uongozi wake Waislamuhawakuwa wenye kujiamini katikakutetea haki zao kutokana na sababuza kisiasa na ukosefu wa vyombo vyakuwasilishia matatizo yao.

 Aidha amefafanua kuwa MSAUD ya wakati huo haikuwa jumuiya ya wanafunzi tu, bali Waislamu wa nchinzima kutokana na kukosekana kwa watetezi wa dini, kinyume na sasaambapo kuna taasisi nyingi kama vile TAMPRO, TAMSYA na BarazaKuu la Jumuiya na Taasisi za Kiisla-mu. Rai hii pia iliungwa mkono namwalimu Sadick Gogo, mmoja wa viongozi waliopita wa MSAUD.

Jumuiya ya wanafunzi wa kiisla-mu wa chuo kikuu cha Dar-es-sa- laam (MSAUD) ilianzishwa miakaya 1960’s naumaarufu wake ulidhi-

KATIKAKUHAKIKISHA

INAFIKIALENGO LA

KUUPELEKAMBELE

UISLAMU NAWAISLAMU,

MWAKA 1993 JUMUIYA YAMSAUD CHINI YA KAMATI YA WAZEE

WA KIISLAMUILIANZISHA

MPANGO WAMASOMO YA

ZIADA KATIKA SHULE YA

KIISLAMU YARIDHWAA,

KINONDONI,DAR ES

 SALAAM.

MSAUD inavyoadhimisha wajibuwa elimu katika Uislamu nchini


Top Related