Transcript

www.uda.co.tz | 1

TUNAJIVUNIA MWANZO MPYA WA KITANZANIAISSN: 2453-5990 TOLEO NA. 01 HALIUZWI

LEOGAZETI

Mabasi ya BRT Ufunguo wa Maendeleo Dar

2 | www.uda.co.tz

4 | www.uda.co.tz www.uda.co.tz | 5

TUNAJIVUNIA MWANZO MPYA WA KITANZANIA TUNAJIVUNIA MWANZO MPYA WA KITANZANIA

Morogoro Mtendeni Street, Dar es Salaam. Email: salessmaishacomputers.com| Tel: ++++ ++ + ++

Mobile: ++++ + ++

, + ,

PRINT | COPY | SCANComplete office printer

Saves upto 40% Printing Cost

Project DirectorTumain Magila

Editor In ChiefIdrissa Kitwara

Marketing ManagerKhalifa Nyambi

Marketing Officer Annamaria Titus

Project OfficerAngelina Kanembe

ContributorsRaphael Mhilu

Lukuba Machibya

Creative DirectorsMichael Albert

Bakari Mkambo

KUCHAPISHA NA USAMBAZAJI

Plot No.2364/208 | Kamata ComplexJunction of Nyerere | Msimbazi Road

P. O. Box 872 | Dar es Salaam | Tanzania

Copyright © 2015UDA and SImon Media. No portion

of this magazine may be reproduced in any form without written consent of the publishers. The publishers are not

responsible for unsolicited material. UDA Leo magazine is published monthly by

SImon Media Reg: ISSN 2453-5990. The opinions expressed are not necessary

those of the UDA or Simon Media. All advertisements/advertorials and promotions have been paid for and

therefore do not carry any endorsement by UDA or the publishers.

© All rights reserved

LEO

www.uda.co.tz | 1

TUNAJIVUNIA MWANZO MPYA WA KITANZANIA

ISSN: 2453-5990

TOLEO NA. 01 HALIUZWI

LEOGAZETI

Mradi wa mabasi

yaendayo haraka

waanza rasmi www.uda.co.tz | 1

TUNAJIVUNIA MWANZO MPYA WA KITANZANIA

ISSN: 2453-5990 TOLEO NA. 01

HALIUZWI

LEOGAZETI

Mradi wa mabasi yaendayo haraka waanza rasmi

Awali, kabla ya mabasi hayo kuanza kutoa huduma hiyo, mabasi madogo maarufu kama

“vipanya” ndiyo yaliyotoa huduma hiyo kwa kiwango kikubwa katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam. “Vipanya” hivyo ambavyo havikukidhi haja ya usafiri viliondolewabaadaye na mamlaka husika na kutakiwa kuwepo kwa mabasi makubwa ya

“daladala” ambayo yalipunguza tatizo la usafiri Jijini hapa. Hata hivyo “daladala” hizo hazikuweza kumaliza tatizo la usafiri mpaka pale mabasi ya UDA yalipoingia nchini na kuanza kubeba abiria.

Mabasi ya UDA yameondoa adha kubwa ya usafiri jijini Dar es Salaam baada ya kuanza safari zake rasmi, ndani ya Jiji na kwenye maeneo ya pembezoni kama vile Mbezi, Kimara, Mbagala, Gongo la Mboto, Tegeta na kwingineko, ambapo tatizo hilo lilikuwa sugu.

Mbali na ujio huo wa mabasi ya UDA, kampuni hii imeongeza ajira kwa vijana wa jinsia zote, ambao sasa wanafanya kazi ya ukondakta ndani ya mabasi hayo na wamekuwa kivutio kwa abiria wanaotumia mabasi hayo mapya. Kuajiriwa kwa wanawake na wanaume, bila kujali jinsia, ni dhahiri kwamba Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) limejipanga kuhakikisha kwamba linatoa ajira kwa vijana wote. Tumezoea kuona mara nyingi jinsi ambavyo waajiri katika kampuni mbalimbali wamekuwa wakiajiriwanaume pekee na wanawake kuonekana kwamba hawawezi kazi kutokana na jinsia yao, bali kuonekanani watu wa kukaa nyumbani na kutunza familia.

Kwa upande wa UDA hali ni tofauti, kwani

kampuni hii imezingatia zaidi uwezo wa mtu binafsi, bila kuangalia jinsia, lengo likiwa kuinua maisha na mapato kwa kila mtu, jambo ambalo linapaswa sio tu kuigwa bali pia kupongezwa. Tunaamini kwamba sasa ni wakati ambapo kampuni nyingine za usafirishaji zinapaswa kujifunza kutoka kwa UDA ili kuhakikishakwamba wanawake wanapewa nafasikatika sekta hii muhimu kwa uchumi wa Tanzania.

Kwa upande wa mabasi ya mikoani baadhi ya wamiliki wameajiri wanawake wa kutoa huduma na madereva, jambo linalotia moyo na kuwahamasisha wanawake kujifunza udereva wa magari na kazi nyingine zinazofanywa na wanaume. Kuwepo kwa wanawake waajiriwa katika mabasi ya abiria kumeongeza nidhamu na uaminifu kwa mali za abiria ndani ya magari hayo. Tunapenda kutoa rai kwa wadau wote kwenye sekta ya usafirishaji kuzingatiaumuhimu wa kutoa fursa za ajira kwa kila mtu bila ubaguzi, kwa kuwa UDA tunaamini kwenye uwezo na kipaji binafsi, sio katika jinsia ya mtu mmoja mmoja.

Wanawake wana uwezo kama watu wengine. Wapewe nafasi!

Mchango wa UDA katika kupunguza tatizo la usafiri

Kuwepo kwa mabasi ya Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) kumepunguza tatizo la usafiri katika maeneo mbalimbali Jijini Dar es Salaam, likiwemo kero sugu ya “ukataji wa ruti” lililokuwa likifanywa na baadhi ya madereva wa mabasi ya “daladala” kabla ya mabasi hayo kuingia kwenye mchakato wa usafirishaji wa abiria.

• NA MWANDISHI WETU

6 | www.uda.co.tz

TUNAJIVUNIA MWANZO MPYA WA KITANZANIA

Mabasi yote 138 yamefika katika Bandari ya Dar es Salaam

Mabasi ya BRT Ufunguo wa Maendeleo Dar

SASA ni wazi kuwa kuanza kwa kipindi cha mpito cha mradi wa mabasi Yaendayo Haraka (BRT) ni halisi na si maneno tu.

Hii ni kwa sababu hatua muhimu katika utekelezaji wake umeshatokea baada ya kuwasili kwa mabasi 138 katika Bandari ya Dares Salaam kutoka China.

Mabasi hayo yamewasili ikiwa ni wiki chache tangu kuanza kwa mafunzo ya madereva wa mabasi hayo katika Jijila Dar es Salaam ambapo ndipo mradi huo utaanzia.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki alisema haya wakati akishuhudia kuwasili kwa mabasi hayo mapema mwezi Septemba “Tumefikia hatua nzuri na naipongezaKampuni ya UDA RapidTransit (UDA-RT) kwa kuleta mabasi hayo kwa ajili ya kuanza kutoa huduma hii ya usafiri, hii itasaidia kuondoa adha ya usafiri kwa wakazi wa jiji hili.”

Ni vyema ikakumbukwa kuwa kampuni hiyo ya wazalendo imepewa jukumu la

kuendesha kipindi cha mpito cha mradi huo kuanzia ‘mwezi wa 10, ili waweze kupata uzoefu na kuweza kushindana baada ya zabuni ya kuendesha mradi huo itakapotangazwa hapo baadaye.

Hivyo basi, UDA-RT taratibu wanaanza kuthibitisha uwezo na weledi wao katika mradi huo. Suala la kufanya kile wanachoahidi na kwa wakati si jambo dogo.

Aidha Msemaji wa Kampuni ya UDA-RT, Sabri Mabrouk anasema mabasi yote yamefika yakiwemo ya mita 12 .(101) na mita 18 (39) ‘na kwamba huduma ya usafiri kipindi cha mpito itaanza baada ya kukamilisha taratibu zote muhimu.

“Tuliahidi kuwa mwezi wa tisa mabasi yatakuwa yamewasili na ni kweli mabasi yalifika mwezi wa tisa”.anaseama

Anaeleza kuwa pamoja na mabasi ya kufundishia yaliyokuwa mawili, jumlayatakuwa mabasi 140. Anafafanua kwamba mabasi hayo yametokea kiwandani China na yanakidhi miundombinu ya barabara ya Mradi wa BRT kama walivyokubaliana na

mtengenezaji.

Kampuni ya UDA-RT imeundwa na Kampuni ya Usafiri Dares Salaam (UDA) na wamiliki wa daladala nchini. Ni vyema basi kampuni hii ikaendelea kujenga mshikamano ili kupata uwezo wa kushindana katika zabuni ya kuendesha huduma ya kudumu ya mradi huo baada ya kipindi cha mpito kuisha.

Mkataba huu wa kipindi cha mpito unaweka msingi na imani kwa wazawa kushiriki katika kuendesha huduma ya mabasi yaendayo haraka katika Jiji la Dares Salaam. Kuimarika kwa umoja huo wa wazawa utaweka msingi imara wa kushindanishwa na wawekezaji kutoka nje na ndani katika awamu zijazo za Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka.

Utekelezaji wa mradi huo katika Jiji la Dares Salaam umesanifiwa kutekelezwa katika awamu sita. Usanifu wa awamu ya pili na tatu katika barabara za Kilwa na Nyerere umekamilika na tayari Benki ya Maendeleo ya Afrika na Korea wameonyesha utayari wa kutoa fedha za ujenzi wa miundombinu. Katibu Mkuu wa Tamisemi Jumanne kutoa huduma za kipindi cha mpitoni pamoja na kuwapunguzia wananchi adha wanayopata kutokana na huduma duni ya usafiri.

“Lengo la pili ni kuwaandaa na kuwajengea uwezo wadau, hasa wadau wa ndani, kwa ajili yakutoa huduma kwenye mfumo mzima utakapozinduliwa”anasema.

ecobank.com

The future is pan-African

Send andreceive moneyacross Africa

Fast ConvenientReliable

• NA MWANDISHI WETU

8 | www.uda.co.tz www.uda.co.tz | 9

TUNAJIVUNIA MWANZO MPYA WA KITANZANIA TUNAJIVUNIA MWANZO MPYA WA KITANZANIA

KAMPUNI ya Bima ya UAP imeingia ubia na Kampuni ya Old Mutual ya nchini Kenya ambayo imenunua hisa asilimia 66.7 za kampuni hiyo kwa madhumuni ya kuimarisha huduma za bima nchini. Akizungumza na “UDA Leo”,Mkurugenzi Mtendaji wa UAP, Bw. Peter Mwangi amesema ushirikiano huo utasaidia kutoa huduma za bima zenye viwango nchini. Mwangi amesema kampuni ya Old Mu-tual ni imara zaidi katika masuala ya bima na itasaidia pia kuchangia uwekezaji katika huduma za kifedha hapa nchini. Kutokana na muungano huo kampuni hizo zitakuwa zikitoa huduma zake katika nchi sita zikiwemo Kenya, Tanzania, Rwanda, Kongo, Uganda pamoja na Sudan ya Kusini. “Malengo makuu ya kampuni hizi mbili ni kuima-risha huduma za bima na kutoa elimu kwa jamii ili ione umuhimu wa kujiunga na huduma za bima. “Kuna bima ambazo wananchi wengi bado hawajajiunga nazo kama vile bima ya mai-sha, watoto na rasilimali watu ambazo ni muhimu kwa jamii,” alisema. Bw. Mwangi alisema ni vema jamii ikawekeza katika bima mbalimbali kwa kuwa zitasaidia kuondoa changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo pindi wanapopata matatizo.

KAMPUNI ZA BIMA ZAINGIA UBIA

WANANCHI WATAKIWA KUTOHARIBU MIRADI YA BARABARA

WATANZANIA wametakiwa kutohu-jumu miradi ya barabara kwa kuibamafuta na vifaa vya ujenzi na pamojakuacha kutupa taka hovyo kwenyemiundombinu hiyo.Hayo yalisemwa na Meneja wa Mfuko

wa Barabara, Joseph Haule, alipokutanana waandishi wa “UDA Leo” mapemawiki iliyopita.Haule alisema kwamba barabaranyingi zimekuwa zikiathirika na kutakiwakukarabatiwa mara kwa mara kutokanana uharibifu unaofanywa na baadhi yawananchi katika sehemu mbalimbalihapa nchini.Haule amewataka wasafirishaji wamizigo na abiria kuzingatia sheriazinazodhibiti uzito wa magari ili barabarazidumu kwa muda mrefu kwa kuwakiwango cha tozo hakiwezi kufidiauharibifu unaofanywa na magari yawasafirishaji hao.Katika mahojiano hayo, Hauleamesema pia kwamba Serikali inapangakutenga fedha kwa ajili ya kuondoamalimbikizo ya matengenezo kwa kuwautafiti unaonesha uharibifu mdogousipofanyiwa matengenezo kwa mudaunaotakiwa kuna uwezekano mkubwawa barabara kuharibika na kuhitajikujengwa upya.“Serikali itaendelea kutenga fedha zamaendeleo ya barabara za halmashaurikwa kuanzisha mfumo maalumu na piainafanya juhudi zakupunguza barabaraza vumbi ambazo ni asilimia 91.5 yamtandao,” alisema Haule.Pamoja na hayo, Haule amesemakwamba Bodi hiyo imelenga kuhakiki-sha kwamba fedha za mfuko huozinatumika vizuri ili watumiaji wabarabara waone thamani ya fedha zao.

Bodi ya Mfuko wa Barabara imejivunia mafanikio katika kipindi cha Awamu ya Nne, ambapo imetumia takriban Bilioni 2.9 kuongeza mapato kuboresha bara-bara pamoja na kutengeneza ajira mpya 42,000 nchini. Hayo yalisemwa na Meneja wa Bodi hiyo, Bw. Joseph Haule alipozungumza na “UDA Leo” siku chache zilizopita. Haule alisema kwamba mapato ya Bodi hiyo yameongezeka kutoka Bilioni 73.1 kati-ka kipindi cha Mwaka wa Fedha 2005/2006 hadi kufikia Bilioni 641.5 katika Mwaka wa Fedha wa 2014/2015. Haule almeliambia “UDA Leo” kwamba barabara nyingi zimeboreshwa ikilinganishwa na kipindi cha awali, ambapo asilimia 86 ya barabara katika kipindi cha mwaka 2005/2006 zilikuwa nzuri na kufikia kuongezeka kufikia asilimia 89. Haule amesema kiasi kiku wa cha mapato kimepatikana kutoka kwe-nye tozo mbali mbali zinazotozwa kwenye mafuta, ambapo mapato hayo yalipanda kutoka Bilioni 69.5 hadi Bilioni 600.23 na kwa upande wa magari ya kigeni Mfuko ulikusanya Bilioni 1.6 hadi 7.9, na kwenye tozo zinazotokana na adhabu za magari yanayozidisha uzito wa mizigo mapato yamekuwa Bilioni 2.0 hadi 10.4 katika kipin-di hicho. Meneja huyo alisema suala la kuzidi kwa mizigo bado ni changamoto am-bayo wanaishghulikia na kwamba kutokana na uhaba wa fedha kwa ajili ya kutimiza majukumu yao wanapendekeza uandaliwe mfumo utakowawezesha kupata ush-uru wa magari yanayotumia gesi pindi yatakapoanza kutumika pamoja na kupata tozo za magari makubwa na shughuli zinazoendelea katika hifadhi ya barabara.

BODI YA MFUKO WA BARABARA YAJIVUNIA MAFANIKIO

SERIKALI imesema agizo la kuzuia vyombo vya usafiri kama Bajaj, bod-aboda na baiskeli liko pale pale. Akizungumza katika mafunzo ya Waandishi wa Habari juu ya kuripoti taarifa zinazohusu usalama bara-barani, mwanasheria wa Kikosi cha Usalama barabarani, Makao Makuu, Inspekta Deus Soko alisema hakuna sheria inayozuia bodaboda kuingia katikati ya jiji. “Bodaboda wamkuwa wakikamatwa kutokana na kushindwa kutii sheria za us-alama barabarani kama vile kuvaa kofia ngumu (helmet),”alisema.

“TUTAENDELEA KUZUIA BODABODA, BAJAJ, KUFIKA MJINI”

Msemaji wa Manispaa ya Ilala, Tabu Shaibu alisema agizo hilo linaeleweka na ndio maana hata baadhi ya waendesha bodaboda wanalielewa na hawaingii katikati ya jiji. Bi. Tabu alisema utaratibu huo wa kuzuia vyombo hivyo umetokana na Halmashauri ku-ruhusiwa kutunga sheria ndogon-dogo kutoka sheria mama.

• NA MWANDISHI WETU

•NA MWANDISHI WETU

10 | www.uda.co.tz www.uda.co.tz | 11

TUNAJIVUNIA MWANZO MPYA WA KITANZANIA TUNAJIVUNIA MWANZO MPYA WA KITANZANIA

mawasiliano ya moja kwa moja kati dreva na kituo kikuu maalumu na kumefungwa chombo maalumu kinacho saidia kurusha picha na sauti za matukio yote yanayo jiri kwenda kituo kikuu maalumu cha usalama chenye wataalamu waliobobea katika uchunguzi wa makosa ya jinai kilichopo makao makuu ya UDART tayari kwa kupambanua uhalifu na umilikaji halali wa vitu vinavyo sahaulika ndani ya basi.......Itaendelea Jarida lijaloImeandikwa na George Ntevi (Mtayalishaji na Mtangazaji wa Luninga) simu 0754 001 963

unastahili kuitwa hivyo kwani kwa kiasi cha asilimia sabini(70%) makutano yasio ya lazima yameondoshwa kabisa na kama haitoshi taa pamoja na alama za usalama barabarani zimetoa kipau mbele na upendeleo kwa barabara ya mwendo wa haraka.Nini faida kwa Taifa na watumiajiFaida ni kubwa kuliko inavyofikiliwa kwani mradi huu ni hazina ya Taifa wenye thamani kubwa na pia ni mradi mkubwa kuliko wote barani Afrika, utarahisisha usafirishaji wa abiria kwa kiwango cha kimataifa kuingia na kutoka Jijini na vitongoji vyake kwa usalama mkubwa na kasi ya haraka hivyo kila mtumiaji atakwenda na kurudi kwa muda mfupi hivyo kupelekea ufanisi wa makusudio kufikiwa kama vile shughuli kwa walioajiliwa, biashara,hospitali,shule na zile za kijamii.Lakini pia kodi ya tozo la nauri bima na leseni,na matozo mengine ya kila basi kama magari mengine binafsi yanavyolipa yata liongezea pato la kiuchumi la Taifa letu Usalama wa abiria na mali zake ni jukumu kubwa la mwendeshaji mradi aliepewa dhamana na Serikali UDART(Usafirishaji Dar es salaam Rapid Transit) kwa miaka miwili,na kwa kujua hilo UDART imeweka kamera maalum za rangi-dijitali (CCTV)ambazo zita rekodi matukio yote yanayojiri ndani na nje ya vituo vyote vya basi na pia ndani ya kila basi kumewekwa kamera 18 na skrini ya nchi saba mbele kwa dreva wa basi ikiwemo

NIUJUAVYO MRADI WA BASI YAENDAYO KWA HARAKA (UDART) JIJINI DAR ES SALAAM

Ukiuona ulimwengu ukipiga hatua mbalimbali za kiuchumi na maendeleo hapana shaka hizo ni harakati za binadamu na

sio binadamu wote bali hayo yote ni matunda dhahiri ya Wahandisi na wataalamu mbalimbali na wale wasio wahandisi ambao wana fikiri usiku na mchana na kufanya tafiti nyingi na wakati mwingine kuhatarisha hata usalama wa maisha yao.Miaka ya 1975 takribani miaka arobaini iliyopita nchini Brazil wazo la kuwa na mradi wa usafirishaji wa abiria mjini na vitongoji vyake ukitumia njia au barabara maalumu ilianza rasmi, kama ulivyo moto wa kichaka kiangazi mafanikio haya yalizagaa ulimwenguni kwa kasi ya ajabu hivyo kupelekea mataifa mengine kuiga mradi huo, kama wahenga walivyo nena ‘hakuna marefu yasio na ncha’ yakajitoteza mataifa mengine kutekeleza mradi huo kwa kina na mrefu hata kuliko Taifa bunifu. nalo si jingine ila ni Taifa jirani kaskazini mwa nchi ya Brazil liitwalo Colombia Jijini Bogota mradi huu ulifanikiwa kwa kiwango kikubwa sana hivyo kupelekea kuwa Taifa la kwanza ulimwenguni Jijini Bogota kujengwa na mradi huo nchini Colombia mradi huu ni lulu ya Taifa hilo lililo kusini mwa Taifa lenye nguvu za Kiuchumi na Kijeshi Ulimwenguni

kwazaidi ya asilimia 90(90%)unatarajiwa kukamilika rasmi asilimia mia moja(100%)mwaka 2017.Utakuwa na maswari mengi ya kujiuliza hivi mmiliki wa mradi huu ni nani na yuko wapi? Jibu ni rahisi nalo ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na unasimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) na DART, ili kuupa mradi huu nguvu za kitaalamu na usimamizi kitaaluma ukapewa kusimamiwa na Wizara ya Ujenzi kupitia idara maalumu BRT TANROADS.Nini sababu ya awamu ya kwanza kujengwa kwenye barabara ya Morogoro na sio barabara nyingine za Jiji la Dar akijibu kwa ufasaha Msemaji wa Kampuni ya UDART Bwana Sabri Mabrouk alibainisha umuhimu na wingi wa mahitaji ya usafiri kuingia na kutoka katikati ya ya Jiji la Dar Es Salaam ulipelekea kuanzwa kwa awamu ya kwanza ya ujenzi katikati ya barabara ya Morogoro kuanzia Kimara mpaka mpaka Kivukoni wenye urefu wa kilomita 20.9 na pia lingine muhimu katika barabara ya Morogoro ni kukidhi vigezo vya kitaalamu na kimataifa wa kuwa na upana usiopungua mita tatu kila upande....

Je hiyo inatosha mradi huu kuitwa ni wa kasi ya haraka wakati makutano ni yale yale? Jibu lake ni kweri kabisa mradi huu

yaani Muungano wa Mataifa ya Amerika (USA).Barani Afrika, Afrika Mashariki hususani nchini Tanzania miaka ya 2001 Mstahiki Meya Crest Sykes,Meya wa Jiji la Bandali ya Salama al maarufu Dar es Salaam alianzisha wazo hili usafirishaji wa abiria Jijini na vitongoji vyake wa haraka kama ulivyokuwa nchini Colombia Jijini Bogota na kulipeleka katika moja ya vikao vya Madiwani wa Halimashauri ya Jiji la Dar es Salaam bila ajizi ulijadiliwa kwa kina na kupokelewa kwa mikono miwili hivyo taarifa zikapelekwa Serikalini na Serikali ikaanza mkakati wa kutafuta fedha mara moja ukihusisha Wizara husika wakati huo, Wahenga walisema penye nia pana njia jitihada za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilizaa matunda ni baada ya Benki Kuu ya Dunia kuuafiki mradi na kukubari kuikopesha Tanzania ma-bilioni ya fedha ili kufanikisha mradi huu ulio mkubwa kuliko yote barani Afrika ambao ujenzi na miundo mbinu ulizinduliwa na Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania mwaka 2010 Kivukoni, hivyo kipenga cha kuanzwa rasmi ujenzi wa mradi huo kuanzwa. Pamoja na changamoto za hapa na pale mradi huu umeshakamilika

•NA GEORGE NTEVI

12 | www.uda.co.tz

TUNAJIVUNIA MWANZO MPYA WA KITANZANIA

ROBERT KISENAMfanyabiashara mwenye historia iliyotukuka

Robert Kisena ni mjasiriamali na mmiliki wa makampuni ya Simon Group yanayohusika na usafirishaji mizigo,

usafirishaji bidhaa, usafirishaji wa abiria na uuzaji wa mafuta.Kampuni ya Simon Group Limited ambayo hivi sasa ndiyo inayomiliki Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) ilianzishwa mwaka 1997 jijini Mwanza, ambayo ilimiliki viwanda vya Pamba na pia uzalishaji wa mafuta.Mwaka huo huo wa 1997 alianzisha ROBASICA ambayo iliendesha shughuli za usambazaji wa kemikali mbalimbali zitumikazo kwenye kilimo. Kisena alikuwa na ndoto ya kuwa mfanyabiashara mkubwa na maarufu nchini na mwenye kiu ya kutoa ajira kwa Watanzania wenzake.

Juhudi zake na matamanio ya kuongeza soko la ajira kwa Watanzania zilizidi kuonekana pale alipoanzisha kampuni ya Basic Elements kwa ajili ya kuendesha shughuli ya usafirishaji, mwishoni mwa miaka ya tisini.utokana na wingu zito la ukosefu wa ajira nchini hasa kwa vijana, Kisena aliona uwepo wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), kuwa likifufuliwa linaweza kuwa mkombozi wa ajira na pia kuwezesha wakazi wa Dar es Salaam kuwa na usafiri bora na wa uhakika. Ndipo mjasiriamali huyo wa siku nyingi alipoanza mazungumzo na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, ambao ndio walikuwa wamiliki wa UDA.

Mwaka 2009 mazungumzo yaliendelea na Halmashauri ya Juhudi zake na matamanio ya kuongeza soko la ajira kwa Watanzania zilizidi kuonekana pale

Kampuni ya Simon Group

Limited ambayo hivi sasa ndiyo inayomiliki Shirika la

Usafiri Dar es Salaam (UDA)

ilianzishwa mwaka 1997 jijini Mwanza,

ambayo ilimiliki

viwanda vya Pamba na pia uzalishaji wa

mafuta.

alipoanzisha kampuni ya Basic Elements kwa ajili ya kuendesha shughuli ya usafirishaji, mwishoni mwa miaka ya tisini.Kutokana na wingu zito la ukosefu wa ajira nchini hasa kwa vijana, Kisena aliona uwepo wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), kuwa likifufuliwa linaweza kuwa mkombozi wa ajira na pia kuwezesha wakazi wa Dar es Salaam kuwa na usafiri bora na wa uhakika. Ndipo mjasiriamali huyo wa siku nyingi alipoanza mazungumzo na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, ambao ndio walikuwa wamiliki wa UDA. Mwaka 2009 mazungumzo yaliendelea na Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam ili kuangalia uwezekano wa ubinafsishaji wa Shirika la UDA ili kampuni ya Simon Group iweze kununua hisa, kwa lengo la kuongeza ajira na kupunguza adha ya usafiri jijini Dar. Mwaka

2010 UDA ilibinafsishwa na idadi kubwa ya hisa kumilikiwa na Simon Group. Halmashauri ya Jiji la Dar-es-Salaam ilikabidhi uongozi wa UDA mikononi mwa kampuni hiyo ya mjasiriamali mzalendo aliyetoka mbali kibiashara ya Simon Group. Mwaka 2012 na 2013 kampuni ya Simon Group iliwekeza katika UDA kwa kununua mabasi 280 wakati ikiwa imeagiza mengine 720 kwa malengo ya kutimiza mabasi 1000 ifikapo katikati ya mwaka 2014. Mwaka 2013, kampuni za ZENONOil na Gesi, Simon Motors na Simon Media ziliungana ili kuleta nguvu zaidi katika makampuni hayo kwenye nyanja mbalimbali.

NAFASI YA SASARobert Kisena ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Simon Group, ambapo mwaka 2006 alikuwa miongoni mwa wafanyabiashara waliohudhur ia mafunzo kuhusu masuala ya Pamba nchini India yaliyoendeshwa na Taasisi iitwayo SITRA. Pia mfanyabiashara huyo alihudhuria semina ya ushindani katika biashara ya Pamba barani Afrika iliyofanyika Jijini Arusha September 2007. Mwaka 2014 Kampuni ya EicherBuses ilimtunukia cheti cha mfanyabiashara bora zaidi katika sekta ya Usafirishaji Afrika Mashariki.

Robert Kisena akizindua magari mapya ya UDA.

14 | www.uda.co.tz www.uda.co.tz | 15

TUNAJIVUNIA MWANZO MPYA WA KITANZANIA TUNAJIVUNIA MWANZO MPYA WA KITANZANIA

16 | www.uda.co.tz www.uda.co.tz | 17

TUNAJIVUNIA MWANZO MPYA WA KITANZANIA TUNAJIVUNIA MWANZO MPYA WA KITANZANIA

kuna baadhi ya wafanyakazi ambao sio waaminifu na wamekuwa wakiruhusu magari hayo kupita, hali inayosababisha uharibifu wa mradi huo. Mkumba amesema kwamba wafanyakazi hao wenye uchu wa fedha wamekuwa wakipewa kati ya shilingi 500 na 1000 ili kuruhusu magari hayo kupita na kwamba mpaka sasa kuna wafanyakazi ambao wamechukuliwa hatua za kisheria kwa kufikishwa katika kituo cha Polisi Mzimbazi. Mkumba alisema kwamba kuna watu ambao wamekuwa pia wakipitisha magari yao katika barabara hizo kwa kuamuru vijana wao ambao ni walinzi kuwaruhusu kupita na wanapokataliwa huanza kuwashambulia. “ Kwa mfano kuna wanajeshi walilazimisha kuruhusiwa kupita na walipokataliwa walishuka kwenye magari yao na kuanza kuwaangushia kichapo vijana wetu walinzi ambao tuliwaweka kulinda maeneo hayo,”alisema. Kuhusu

migogoro ya wafanyakazi, Mkumba alisema makubaliano kati ya Serikali na kampuni hiyo yalikuwa kwamba kima cha chini kiwe shilingi 80,000, lakini kampuni iliona kuwa kiwango hicho ni kidogo hivyo wakaamua kuwalipa kima cha chini cha shilingi 200,000 ambazo zilijumuisha fedha ya ziada ambayo haikuwemo kwenye makubaliano yao. Mkumba amesema kwamba tangu mwanzo kampuni hiyo imekuwa ikiwalipa kwa wakati wafanyakazi hao isipokuwa kipindi cha mabadiliko hayo ndio walichelewa na kisha wafanyakazi kuanza migomo na kwamba toka hapo hawajawai kupitiliza mshahara hata siku moja.

Yahya alisema kuwa barabara ni kwa ajili ya mabasi yaendeyo kwa kasi, hivyo kila mmoja anatakiwa kufuata sheria na kanuni zilizowekwa kwa kuwa mlinzi ka mwenzake pamoja na kuupenda mradi huo kwasababu ni mali yao.

zao,” alisema Mkumba. Mkumba alisema kwamba pamoja na kukaribia kufikia ukingoni mwa ujenzi huo, bado kuna wananchi wasiokua wahaminifu, ambao kwa kiasi kikubwa wamekuwa chanzo cha kutokukamilika kwa mradi huo mapema kutokana na wananchi hao kukaidi amri za wajenzi wa barabara hizo.

“Tumekuwa tukiweka uzio kwa ili kuzuia wananchi wasipite, lakini wanakahidi amri hiyo wanavunja uzio wanapita, hali hii imesababisha ajali kwa baadhi ya watu, ambapo wengine wamejikuta wakikanyagwa na makatapila. “Majuzi mwananchi mmoja alikanyagwa na katapila ambapo mguu wake ukavunjika kutokana na kukahidi amri ya wajenzi na matokeo yake alikwenda kutushtaki na kesi iko Msimbazi Polisi,” alisema. Mkumba amesema hivi sasa inatakiwa ifike mahali ambapo kila mwananchi anatakiwa kutambuwa kwamba huu mradi ni wake binafsi kwa kuwa utawasaidia wao wenyewe, hivyo kutakiwa kufuata masharti wanayopewa. Alisema mpaka sasa wanamalizia kukamilisha vituo na mabasi yanaweza kuanza kufanya kazi kutokana na vituo vingi kukamilika.

Akizungumzia changamoto ya magari kukatiza katika barabara iliyotengwa kwa mradi wa mabasi yaendayo kasi, Ofisa Uhusiano huyo amesema kwamba

TUMEPITIA CHANGAMOTO KUBWA

KAMPUNI ya Ujenzi kutoka Ujerumani, Strabarg International GmbH imesema kuwa tangu ilipoanza kazi ya mradi wa ujenzi wa barabara

mnamo Aprili 2012, imepitia changamoto kubwa ikiwemo kutozwa faini ya uharibifu wa miundombinu. Akizungumza na “UDA Leo”, OfisaUhusiano wa kampuni hiyo Yahya Mkumba alisema wakati wa ujenzi huo walijikuta wakiharibu miundombinu ya mabomba ya DAWASCO na nyaya za Kampuni ya Simu Tanzania TTCL zilizokuwa zimechimbiwa ardhini. Mkumba alisema kwamba kutokana na hali hiyo mara nyingi walishtakiwa na kutakiwa kulipa gharama za uharibifu huo, jambo ambalo lilikuwa

za TTCL ambazo zilichimbuliwa kwa bahati mbaya na wajenzi ziliibiwa, hali ambayo ilisababisha usumbufu mkubwa kwa TTCL. Alisema kuwa changamoto nyingine ambazo wamekumbana nazo zilitokana na wananchi ambao nyumba zao zilimegwa na mradi huo wa mabasi kuishtaki kampuni hiyo badala ya serikali ambayo ndiyo mmiliki na msimamizi mkubwa wa mradi huo.

“Tumekuwa tukishtakiwa mara kwa mara na wananchi ambao vipande vya sehemu yao vimekuwa vikimegwa na barabara wakidhani kwamba sisi ndio wasimamizi wa mradi huu, badala ya kuishtaki serikali,” aliongeza. “Changamoto nyingine ni kwamba tumekuwa tukiibiwa vifaa vya ujenzi kama vile mabomba, vitofali na vitu vingine, hali ambayo imesababishwa na wafanyakazi wasio waaminifu katika kazi

changamoto kubwa kwao wakati wa ujenzi huo.“Mabomba makubwa ya maji ambayo kwa asilimia kubwa yalichimbiwa barabarani na pembezoni yalipasuka na tulidaiwa mamilioni ya fedha,” alisema. Alisema DAWASCO imekuwa pia ikiwashtumu kutumia maji yao kwa njia ya wizi wakati jambo hilo si kweli na kwamba walilazimika kuchimba kisima chao cha maji kwa ajili ujenzi huo ni pamoja na kununua maji kutoka Sinza.

Mkumba alisema kwamba pamoja na wao kutotumia maji ya DAWASCO, Strabag walishangaa kuletewa ankara kubwa ya maji wakitakiwa kulipa kwa madai ya kutumia maji ya shirika hilo. Mkumba aliongeza kwamba nyaya

• NA MWANDISHI WETU

18 | www.uda.co.tz www.uda.co.tz | 19

TUNAJIVUNIA MWANZO MPYA WA KITANZANIA TUNAJIVUNIA MWANZO MPYA WA KITANZANIA

Minara ya DhahabuKanuni za mafanikio kupitia simulizi za Babu Kazwile:

Masomo yaliyomo ndani ya kitabu hiki yanalenga kutekenya akili yako ili itumike kujifunza juu ya ukweli halisi wa maisha, imedhamiliwa kukupa changamoto ya kutafakari, kuona na kutumia fursa uliyo nayo kujiletea mafanikio yako binafsi pamoja na jamii inayokuzunguka kwa ujumla. Imani yangu ni kwamba, hauwezi kufanikiwa bila kuisaidia jamii yako, historia inatuambia kuwa watu wote waliofanikiwa (iwe katika biashara, siasa, masomo,kilimo, tafiti) walifanya hivyo baada ya kuwa wametatua changamoto za jamii zao au kwa kugundua kitu kilichoisaidia jamii zao kurahisisha na kuboresha maisha ya watu wao. Mifano ni mingi mno kutosha kwenye kurasa hizi chache, tutajadiri michache tutakayojaliwa kuifahamu.

Mafanikio hayaji kwa bahati mbaya, huja kwa kufuata kanuni maalumu ama bila kujua au kwa kujua. Minara ya Dhahabu itakusaidia kujifunza kanuni wanazotumia watu wote waliofanikiwa, ambazo wewe pia unaweza kujifunza na kuzitumia ili uweze kuijenga minara yako ya dhahabu itakayokuwezesha kutoka hapo ulipo na kukupeleka kwenye maisha ya ndoto zako.

Sasa endelea…………..

Sura ya kwanza– Kukutana na Malaika wa Bahati

Waswahili husema mtembea bure si mkaa bure! Kama hali uliyo nayo sasa si ile unayoitamani au ile uliyokuwa unaiota wakati unakua haitabadilika mpaka pale utakapoanza kufikiri na kufanya tofauti na unavyofanya sasa, mabadiriko lazima yaletwe kwa jitihada madhubuti. Nchi za Kiafrika zingelikuwa bado makoloni ya wazungu kama babu zetu wasingedai Uhuru, kazi ya kudai Uhuru haikuwa lelemama; kuna waliouwawa au kupoteza kila walichokuwa nacho lakini walisimama kidete kuhakikisha kwamba wanapata walichokuwa wanahitaji. Vivyo hivyo kazi ya kudai Uhuru kutoka kwenye mikono ya umasikini si lelemama ni mapambano yanayohitaji kujinyima na kuwa tayari kuumia kama ilivyokuwa wakati wa kupigania Uhuru kutoka kwa wakoloni wa Kizungu ambao tunaojivunia sasa, matunda ya Uhuru ni matamu na yanasitahili kila jasho na nguvu inayohitajika kuupata. Umasikini lazima tuukabili kwa nguvu, ari na kasi inayostahili, lazima tutoke tulipo tukakutane na bahati, kama tumeisubiri siku zote na bado haijafika lazima tuifuate huko huko, aliye juu mfuate huko huko!

Kumbuka vita ya kupambana na umasikini haiwezi kushindwa kwa kuwategemea wengine wakupiganie, siyo serikali, mbunge wala Nabii yeyote atapigana vita hii kwa niaba yako; ni sawa na kufanya mazoezi ya viungo, hata ukiwa na mali kiasi gani huwezi kumwajiri mtu afanye mazoezi kwa niaba yako, lazima ufanye mwenyewe kama unataka kunufaika na mazoezi hayo. Bila jitihada binafsi utaendelea kubaki ulipo!

Ningependa kwanza tutazame historia za watu wawili ambao wameweza kulazimisha mpaka wamefanikiwa kuwa miongoni mwa matajiri wa dunia, ambao ni Chris Gadner na Robert Johnson, wote ni Wamarekani weusi.

Christopher Gardner alizaliwa Milwaukee, Wisconsin, Marekani Februari 9, 1954 ak iwa n i

mtoto pekee wa kiume kwenye familia ya watoto kumi na moja. Alilelewa na mama yake baada ya baba yao mzazi kuitelekeza familia, mama yake alikuwa mwalimu lakini ilimlazimu afanye kazi nyingine za vibarua ili aweze kuilisha familia yake, kwa ujumla maisha ya Gardner ya mwanzo yalikuwa ni magumu na ya kubangaiza. Ingawa alikuwa na uwezo mzuri darasani hakuwa na mapenzi sana na shule na badala yake alianza kujifunza tarumbeta kwa miaka tisa hivi akiwa na ndoto ya kuwa Miles Davis. Hata hivyo baadaye aligundua kuwa hakuwa na kipaji hicho na kwamba kulikuwa na Miles Davis mmoja tu na tayari alikuwa anaifanya kazi ambayo yeye alitaka kuifanya.

Baada ya kushindwa shule, Gardner ilibidi adanganye juu ya umri wake ili aweze kujiunga na jeshi la Marekani, alitarajia kuwa kujiunga nalo kungelimsaidia kuwa daktari ambapo angezunguka dunia yote, hata hivyo hilo alikomea North Calorina tu (Marekani kwao huko huko). Hata hivyo ujuzi alioupata ulimsaidia kwani alifanikiwa kuajiliwa na daktari bingwa mmoja wa moyo waliyekutana naye jeshini baada ya muda wao katika jeshi kuisha akimwajiri kama msaidizi wake kwenye

utafiti katika Chuo Kikuu cha California kwenye kitengo cha Utabibu mjini San Francisco. Gardner alifurahia kazi yake ingawaje ilikuwa inamlipa kiduchu, na chini ya matarajio yake.

Gardner alifikilia kusomea udaktari lakini hata hivyo gharama zikawa kubwa akaamua kuachana na wazo hilo na badala yake akapata kazi ya kuuza vifaa vya hospitali ambapo mshahara uliongezeka mara dufu. Ilikuwa siku moja wakati Gardner akipakia vifaa kwenye gari ilikuja kupaki gari aina ya Ferrari karibu na gari yake ambayo ilibadilisha maisha yake. Gari pamoja na ujumla wa maisha ya mtu aliyeweza kumiliki gari lile alivipenda na akaamua kumuuliza mwenye gari maswali mawili mhimu, moja “je unafanya kazi gani” na la pili “je kazi hiyo inafanyikaje”, bahati nzuri yote yalipata majibu.

Yule bwana mwenye gari alikuwa wakala kwenye soko la hisa. Gardner aliposikia juu ya mshahara a m b a o y u l e b w a n a alikuwa analipwa alipatwa

na wazimu, ingelimchukua miaka kumi na moja hivi kupata

mshahara wa mwezi mmoja wa yule bwana mwenye gari. Kuanzia hapo Gardner aliamua kuwa maisha yake yalikuwa yako kwenye uwakala katika soko la hisa na si kuuza vifaa, alijua yeye ni wa daraja la yule mwenye gari na si uchuuzi wa vifaa vya hospitali.

Baada ya kuamua kuwa angelifanya kazi ya uwakala wa hisa Gardner alianza kutafuta kampuni ya aina ile ambayo ingelikubali kumpa nafasi, akabahatika kupata kampuni moja ambao walikuwa wanafundisha watu wenye utashi wa Gardner kwenye kazi ile. Hata hivyo siku ya kwenda kuanza kazi akakuta meneja aliyekuwa amemwajiri amefukuzwa kazi na wala hapakuwa na taarifa zozote za kuajiriwa kwake, akaondoka akiwa amesononeka.

Hata hivyo bwana Gardner hakukata tamaa akaendelea kutafuta mpaka alipopata kampuni nyingine waliokubali kumchukua kwa masharti kwamba inabidi ajifunze kwa miezi kumi huku wakimtazama kabla hawajamwajiri. Ilikuwa ni miezi kumi ya mateso.

Katika kipindi hiki ambachokilionekana kifupi, mzazi mwenzie akatoroka na mtoto wao pamoja na vitu vyake vyote, matatizo hayakukomea hapo tu bali Gardner alijikuta hana hata senti na yuko jela. Baada ya ukaguzi

Tutakuwa tuk iku le tea mfu lu l i zo wa k i tabu cha Minara ya Dhahabu, kilichotungwa na Ndugu Charles Seleman Newe aka Babu Kazwile, wasiliana n a y e k u p i t i a + 2 5 5 7 6 9 3 3 5 8 6 4 a u m i n a r a y a d h a h a b u @ g m a i l . c o m .

wa kawaida wa trafiki iligundulika kuwa gari la Gardner lilikuwa na faini za maegesho ambazo hazijalipwa, alifungwa siku kumi, siku ya kuachiwa ikiwa siku moja tu kabla ya usaili wake wa Mwisho.

Gardner alikwenda kwenye usaili akiwa amevalia t-shirt na suruali chafu aliyosota nayo jela, angeliweza kudanganya lakini aliamua kusema ukweli. Gardner alimweleza aliyekuwa anamsaili kuwa amekimbiwa na mkewe na kwamba hakuwa na hata senti moja na kuwa jana yake alikiwa jela. Bahati nzuri aliyekuwa anamsaili alikuwa na yeye amemaliza kutalakiana na mkewe kwa hiyo alielewa mambo yanavyoweza kuwa mabaya na akampatia kazi.

Mara baada ya kupata kazi mkewe alilejea na mtoto wao, ingawaje hata hivyo aliondoka siku chache baadaye na kumtelekeza mtoto na baba yake. Kwa sababu nyumba aliyokuwa anakaa ilikuwa hairuhusu kukaa na watoto ilibidi Gardner na mwanaye wahamie mtaani (ingawaje hata kabla ya kuja mwanaye alikuwa hana makazi maalum kwa sababu alikuwa amefugwa kwa marafiki). Baadaye yeye na mwanaye walifanikiwa kuhamia kwenye nyumba ya kulala wageni ya uswazi, huku wakiendelea kubangaiza. Mwenyewe anasema kwenye autobiography yake kuwa “sikuwa na makao lakini sikupoteza mwelekeo”, anaendelea kusema “nilijuwa siku njema ziko mbele yangu”. Baadaye walipewa makazi kwenye nyumba ya akina mama wasiokuwa na waume hadi hapo Gardner alipopata leseni yake ya uwakala kwenye soko la hisa na kampuni za maana zikaanza

kumuona, baada ya safari na kazi ngumu safari yake ilianza kuonyesha mwelekeo.

Mwaka 1987 Gardner akaanzisha kampuni yake ya uwakala mjini Chicago, Gardner Rich. Kwa kutambua ugumu wa kuthaminiwa kwa biashara za weusi Marekani, aliamua kuhamia Chicago kwa sababu mji huu ulikuwa na historia nzuri kwa biashara za weusi kufanikiwa. Haikuchukua muda biashara yake ikaanza kukua na kupata wateja wakubwa wakubwa.

“Siyo historia ya maisha yangu tu, ni ya watu wengine pia” anasema kwenye kitabu chake cha maelezo ya maisha yake, kitabu ambacho kimewekwa kwenye mkanda wa sinema inayoitwa “The Pursuit of Happiness” sinema inayowashirikisha nguli kwenye tasinia hii kama akina Wil Smith, anasema ni historia ya maisha ya watu wengine wengi waliokuwa katika mazingira yangu waliopitia ugumu ambao mimi nimeuona na wakaamua basi, natafuta njia nyingine”. Leo hii Gardner anamiliki biashara Afrika Kusini na Marekani na anavaa saa mbili, moja ikiwa na majira ya Afrika Kusini na nyingine majira ya Chicago, kwa sababu anasema muda ni mali

Kabla hatujatafakari maisha ya Chris Gardner naomba uambatane na mimi katika historia fupi ya maisha ya mlalahoi mwingine bwana Robert Johson wa BET ambaye leo hii anahesabika kama milionea wa dola za Marekani, siyo milionea wa pesa za madafu.

“Tulikuwa tunaishi kwa mtindo wa mkono mdomoni kama ambavyo familia nyingi za kiafrika zilikuwa na zinaendelea kuishi”

anasema mwanzilishi wa Black Entertainment Television (BET) Robert Johnson.

Akizaliwa kwenye maisha ya kawaida jimboni Mississippi hadi kuwa milionea wa kujitengeneza Mmarekani Mweusi, Robert Johnson amejitengenezea jina kwa kujielekeza zaidi katika masoko bikira. Bila kuwa na uzoefu wa biashara amefanikiwa kuibadilisha $15,000 kuwa falme ya habari. Leo hii, BET, imevuka mipaka na kusambaa dunia kwenye biashara ya idhaa za TV za kulipia.

Johnson alizaliwa April 18, 1946 katika mji wa Hickory, Mississippi nchini Marekani, akiwa ni mtoto wa tisa kati ya watoto kumi wa Edna na Archie Johnson, waliokuwa wafanyakazi wa kiwanda cha betri. “Hatukuwa familia yenye ustawi mzuri, lakini tulijua kuwa kama ningelitaka baiskeli ili maanisha mtu mwingine kwenye familia lazima akose kitu fulani” anakumbuka Johnson. “Ama kama ulitaka kwenda chuo kikuu wazazi wako wasingelimudu kukulipia”

Wakati akiwa mdogo wazazi wake Johnson walihamia Freeport, Illinois Marekani, ambako baba yake alitarajia kupata kazi nzuri. Ilikuwa ni Freeport pia, ambapo Johnson naye alipata kazi nzuri-kazi yake ya kwanza. Johnson alianza kusambaza gazeti la Rockford Morning Star wakati akiwa na miaka kumi. Hata hivyo haikuwa kazi aliyoitarajia, “nilishindwa vibaya sana” anakumbuka. “Sikuweza kuamuka mapema, na bado siwezi kuamka mapema”

Itaendelea toleo lijalo...

20 | www.uda.co.tz www.uda.co.tz | 21

TUNAJIVUNIA MWANZO MPYA WA KITANZANIA TUNAJIVUNIA MWANZO MPYA WA KITANZANIA

Ubungo terminal and passenger bridge

KwANINI HUdUmA zA mpITO• Ili kuiwezesha jamii(abiria) kuzoea huduma hii

kutokana na kuwa mpya kwao.• Ili kuweza kuizoea miundombinu kikamilifu kabla

uendeshaji wa mradi huu hujaanza rasmi•KwANINI JINA lA UdA-RT• UdA inamaanisha USAFIRI dAR-ES-SAlAAm• RT inamaanisha RApId TRANSIT yaani Usafiri wa

Haraka• UdA ni neno lililozoeleka miongoni mwa wakazi

wa jiji la Dar Es Salaam na linatumika kumaanisha usafiri wa umma.

KwANINI UdA-RT ImEANzISHwA• Katika kuleta umoja rasmi kwa wote waendeshao

shughuli za daladala ili waweze kushiriki katika mradi huu wa DART

• Njia mojawapo ya kuwawezesha watanzania ili nao pia washiriki katika shughuli hii ya mradi wa DART.

mAdHARA YA FOlENI zA mAGARI NA mFUmO wA USAFIRI wA UmmA UlIVYO SASA• Zinapunguza uzalishaji kutokana na abiria kutumia

takribani saa 4 katika foleni barabarani• Taifa hupoteza kiasi cha shilingi bilioni 4 kila siku na

takribani trilioni 1.5 kwa mwaka kutoka na foleni za magari barabarani.

• Kupunguza mapato ya ziada katika ngazi ya mtu binafsi

• kutokana na matumizi yasiyo ya lazima gari binafsi

SIFA zA VITUO VYA mAbASI YA mwENdO wA HARAKA (bRT)• Vituo vya kisasa vilivyofunikwa• Sakafu ya kituo inalingana na ile ya basi (hii hupun-

guza ucheleweshaji katika kuingia na kuteremka kwenye basi pindi utumiapo ngazi).

• Nauli zinakusanywa nje ya basi kabla ya kupanda( hii hupunguza kuchelewa kupanda au kuteremka kama nauli ikiwa inalipwa kwa dereva).

• kamera za usalama kwa ajili ya vituo,raia na katika kudhibiti mapato.

• Mfumo wa matangazo kwa umma • Vituo vina alama mbalimbali zilizowekwa ili kutoa

taarifa na elimu kwa wateja

Mradi wa mabasi ya mwendo haraka na

mRAdI wA dART:• dART ni mradi wa mabasi yaendayo

haraka katika mji wa Dar-es-salaam • Dar es salaam imepitisha mfumo huu wa

bRT katika kukamilisha mpango wake wa muda mrefu wa mwaka 2003 wa mabadiliko katika usafirishaji.

• Mfumo huu utaboresha maisha kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam kutokana na kuwa na teknolojia bora.

mAlENGO YA mRAdI wA dART:• Kuongeza kiwango cha usafirishaji kwa

wakazi wengi ili kuimarisha kushiriki kwao katika shughuli mbalimbali.

• Kukabiliana na ongezeko la uhitaji mkubwa wa usafiri jijini.

• Kuboresha maendeleo ya mjini, mazingira na mipango sahihi ya matumizi ya ardhi pembezoni mwa bRT

bUS RApId TRANSIT (bRT) NI NINI?• Ni mfumo wa mabasi ya haraka

unaotumia mabasi yenye uwezo mkubwa na yatumiayo njia maalum ili kuepuka misongamano ya magari barabarani.

• Huduma ya mabasi yanayowachukua abiria pembezoni mwa barabara na kuwaleta katika mabasi makubwa yaliyo

katika barabara maalum ya mfumo wa BRT

mAmbO mUHImU KATIKA mFUmO wA bRT • Njia zake zipo katikati ya barabara za

kawaida• Nauli zinakusanywa nje ya basi kabla

ya kupanda (ili kuepuka kuchelewa wakati wa kupanda na kushuka kwenye basi)

• sakafu ya kituo inalingana na ile ya basi (hii hupunguza ucheleweshaji katika kuingia na kuteremka kwenye basi pindi utumiapo ngazi).

• Mabasi ya mwendo haraka yatakuwa na kipaumbele pindi yafikapo katika makutano ya barabara (yataruhusiwa kwanza na taa za barabarani )

UENdESHAJI KATIKA KIpINdI cHA mpITO• ni huduma ya mwanzo ambayo

itatumika kabla ya mradi huu kuanza kwa ukamilifu.

mRAdI wA dART UNA JUmlA YA AwAmU SITA

AwAmU YA KwANzA

• Awamu ya kwanza inajumuisha kilomita 20.9 ya barabara kuu inayotoka Kimara mpaka Kivukoni iliyo na matawi mawili Barabara ya Kawawa kutoka Morocco mpaka Magomeni na pia Msimbazi mpaka Kariakoo Gerezani.

• Kilomita 57.9 ni ya njia za pembezoni (ndogondogo)

• Vituo vikuu vitano vya mabasi;Kimara,Ubungo,Morocco,Kivukoni,Gerezani

• Jumla ya vituo vya njiani 27• Vituo vitano vya kupanda mabasi ya

kuunganishia• Depoti 1 ya jangwani

UdA-RT NI NINI?• Ni kampuni iliyoundwa kwa lengo

maalum la kutoa huduma za mabasi ya mwendo wa haraka. UdA-RT inaundwa na jumla ya kampuni tatu yaani;

• ( UdA) Shirika la Usafiri Dar-es-salaam

• (UwAdAR) Umoja wa Wamiliki wa Daladala Dar-es-salaam

• (dARcObOA) Dar-es-salaam Commuter Bus Operators Associationoperators association

www.uda.co.tz | 23

TUNAJIVUNIA MWANZO MPYA WA KITANZANIA

22 | www.uda.co.tz

UZINDUZI WA MAFUNZO YA MADEREVA WA MABASI YA MWENDO WA HARAKA DAR ES SALAAM

Msemaji wa Mradi wa UDA-RT, Sabri Mabruk, akizungumza (katikati) akizungumzakatika uzinduzi huo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Usafirishaji (UWADAR),

William Masanja.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Hawa Ghasia, akijaribu kuendesha moja ya basi la mwendo wa

haraka wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya madereva

Wakufunzi wa kutoa mafunzo kwa madereva hao kutoka China wakitambulishwa.

Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani Nchini, Mohamed Mpinga (kushoto),akibadilishana mawazo na wadau wa usafirishaji kabla ya uzinduzi huo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Hawa Ghasia, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mafunzo ya

madereva wa mabasi yaendayo haraka uliofanyika Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mh. Saidi Meck Sadiki akiongelea jambo katika uzinduzi wa mafunzo ya madereva wa magari ya mwendo kasi Ubungo,

Dar es Salaam

Matukio katika picha

Huduma Boraza Kibenkikwa Wote

24 | www.uda.co.tz

TUNAJIVUNIA MWANZO MPYA WA KITANZANIA

Wote tuna wajibu wa kuzingatia usalama barabarani

Manusura na majeruhi ndio wanaokuwa wa kwanza kulalamika kwamba “Dereva alikuwa anakimbiza basi...”? Ninakumbuka, takriban miaka 6 iliyopita nilisafiri kutoka Tanga kwenda Dar es Salaam, kwa mojawapo ya mabasi yanayosafiri kati ya miji hiyo mikuu. Dereva wa basi hili alikuwa anaendesha kwa mwendokasi, jambo ambalo binafsi nililitambua kuwa hatarishi kwa usalama wa abiria na mali zao.Hatua ya kwanza niliyochukua ilikuwa ni kusogea hadi mbele, alikokuwa dereva, na kumwomba apunguze mwendo wa gari, nikimtahadharisha uwezekano wa kutokea ajali. Hatua hiyo ya kwanza haikuzaa matunda, hivyo nikaamua kuirudia. Abiri waliokuwa wameketi viti vya mbele walianza kunikejeli na kunidhihaki. Kauli za “Sisi tuna haraka zetu, kama hutaki shuka

upande lingine...”Hali ikawa hivyo ili mradi kila aliyeweza kukejeli, kutusi, alifanya hivyo kadiri ya uwezo wake. Kisha hali ikatulia. Wao walidhani kwamba “yameisha”, kumbe ndio kwanza yalikuwa “yameanza”.Sikuridhishwa na hali hiyo, na kwa kuwa nilikuwa ninamfahamu mmoja wa viongozi wa Jeshi la Polisi, nilimtumia ujumbe mfupi wa simu kumweleza hali halisi. Bahati nzuri, namba ya basi iliandikwa kwenye tiketi. Nikatoa maelezo yote kikamilifu.Tulipofika Segera, basi lilisimamishwana Askari wa Usalama Barabarani alipanda ndani kufanya ukaguzi, akifuatilia taarifa niliyoitoa. Dereva na kondakta wake waliamriwa kushuka chini na walielezwa kuhusu kuwapokwa taarifa hiyo.Dereva alipewa onyo kali na kuambiwa kwamba iwapo kutakuwa na malalamiko tena, dereva, kondakta na mmiliki wa basi watawajibika kwa adhabu itakayotolewa kadiri ya maelekezo ya

kisheria. Japokuwa dereva alilalamika - na kuungwa mkono na abiria walionikejeli - aliporudi ndani ya basi, safari iliendelea salama kwa mwendo wa“kistaarabu”, hatimaye tukafika salama kwenye Jiji la Dar es Salaam. Wahenga walisema “Kawia ufike” na pia, “Mwendapole hajikwai, akijikwaa haumii.” Japokuwa methali hizi ni mojawapo ya nahau ambazo zimedumu kwenye utamaduni wetu kwa muda mrefu, mafunzo yake mpaka

Ni mara ngapi tumekuwa mashuhuda kuona ripoti kadha wa kadha, ambapo, mara tu baada ya ajali kutokea kwenye vyombo vya usafiri wa abiria.

dereva akipuliza mashine kuthibitisha anaendesha basi bila kilevi chochote

• IMEANDALIWA NA

26 | www.uda.co.tz www.uda.co.tz | 27

TUNAJIVUNIA MWANZO MPYA WA KITANZANIA TUNAJIVUNIA MWANZO MPYA WA KITANZANIA

DEREVA MAKINI AWARDS TANZANIA

Takribani watanzania milioni 4 mpaka milioni 5 husafiri kwa kutumia mabasi kila siku kiwango kinachotokana na idadi ya mabasi yapatayo zaidi ya

laki moja yaliyosajiliwa nakupewa leseni na SUMATRA kusafirisha abiria kutoka na kwenda sehemu mbalimbali za nchi kila siku.

Idadi hiyo kubwa ya wasafiri kwa upande mmoja imekuwa ni nyenzo muhimu katika kuleta maendeleo ya kiuchumi kutoka sekta ya usafirishaji na taifa kwa ujumla lakini hata hivyo usafiri wa mabasi umekuwa ni miongoni mwa vyombo vya usafiri vinavyochangia kupoteza nguvu kazi ya taifa kutokana na ajali za barabarani za kila siku.

Ni wajibu wa kila mtu kukabiliana na changamoto hiyo kwa kupunguza idadi ya watu wanaopoteza maisha kila siku kutokana na ajali za barabarani jambo ambalo limepukutisha maisha ya ndugu, jamaa na marafiki zetu waliokuwa tegemeo muhimu katika kuendesha maisha ya familia mbalimbali.

Kumekuwepo na juhudi mbalimbali zikifanywa na wadau mbalimbali wa usafiri katika kupunguza ajali, lakini harakati hizo zimekuwa na mafanikio ya muda mfupi

nakushindwa kubadilisha tabia na mwenendo mzima wa madereva wakiwa barabarani ambao wanatajwa kuwa chanzo kikubwa kwa kiwango cha asimilia 78 mpaka 80 za visababishi vya cha ajali hizo kutoka katika vyanzo vya tafiti mbalimbali.

Kampuni ya Transevents Marketing Limited imeanzisha shindano la kumtafuta kisha Kumtambua na kumtunuku TUZO ya Dereva Makini wa mwaka wa mabasi nchini linalolenga kubadilisha tabia na mwenendo mzima wa madereva kwa kutambua nafasi na mchango wao muhimu katika jamii kwa kulinda maisha ya abiria.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo bwana Peter George Nzunda anasema shindalo hilo pia linalenga kuhimiza uendeshaji salama likiwa na kauli mbiu ya “NI HAKI YAKO KUFIKA SALAMA”.

“Mashindano na tuzo ni moja ya chachu katika kuhamasisha utendaji kazi katika shughuli yoyote ile lakini madereva wa mabasi hawajapata fursa hiyo na ndiyo maana tunalitumia shindano hili kama chachu ya kubadili tabia na mwenendo wa madereva ambao ndiyo sababu kuu ya chanzo cha ajali” anasema Nzunda na kuongeza:

“Wamiliki wa mabasi wao wanataka faida na wengi wao hawatoi motisha kwa madereva wao, askari wa usalama barabarani wanasimamia sheria pekee,SUMATRA wanasimamia udhibit i wa huduma ya mabasi,NIT na Taasisi zingine wanatoa Mafunzo ,sasa unaweza kuona ni wakati gani madereva wanapata nafasi ya kutambuliwa hapa na kupewa motisha”

Anasema kuna madereva wengi ambao wanaendesha kwa uangalifu na kufuata sheria na kanuni zote wakati wote na kulinda vyombo vya matajiri wao ,lakini hata siku moja hawajatambuliwa na kutunukiwa tuzo kwa umakini wao huo hivyo kujiona hawana tofauti na wenzao ambao hawana weledi, walevi na wenye kusababisha ajali mara kwa mara.

Anasema shindalo hilo litawahusisha zaidi abiria ambao ndiyo walengwa, watahusika katika kupiga kura na kuwapendekeza madereva ambao wanasifa kwa kuendesha kwa kuzingatia kanuni ,taratibu na sheria na wenye mawasiliano mema kwa wasafiri kabla, wakati na baada ya safari.

Mchakato mzima wa shindanoMeneja Uhusiaono wa Transevents

Marketing Limited, Dotto Kahindi anasema

abiria watajulishwa juu ya shindano hilo kwa njia mbalimbali za matangazo kupitia vyombo vya habari na njia nyingine mbalimbali zitakazo weza kuwafikishia taarifa kwa wakati.

“Abiria watatakiwa kutuma ujumbe mfupi kupitia simu zao Kwa kumpigia Kura dereva ambaye wanaamini kawasafirisha na kuwafikisha salama kulingana na vigezo vitakavyokuwa vimetolewa, Ujumbe huu mfupi utakuwa na majina ya madereva, namba ya basi, jina la kampuni na namba ya usajiri ya basi” anasema Dotto

Aidha Dotto anasema mabasi yatakayoingia kwenye shindano hi lo yatabandikwa matangazo maalumu kwenye milango na

nyuma ya magari hayo, pia watatengeneza tiketi za mabasi makubwa na madogo pamoja na kuweka matangazo ya shindano hilo kwenye DVD ambazo zitaonyeshwa kwenye mabasi yenye televisheni.

Shindano hilo litawashirikisha kwa karibu jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani, ambao watasaidia katika kuhimiza uzingatiwaji wa sheria katika vituo vyote vya ukaguzi nchini ambapo pia wataweza kuwahimiza abiria kupiga kura.

Kwa upande wa habari Kampeni hii itaendeshwa na Clouds Entertainment Company Limited kwa Muda wa wiki 4 kupitia vipindi vyake vya Clouds FM vya Powebreakfast, XXL na Jahazi na kupitia mitandao yake ya kijamii ya facebook,tweeter,instagrams na WhatsApp.

Anasema pia matangazo hayo ya kupiga kura yatakuwa yakitangazwa kupitia vipeperushi na vipaza sauti kwenye vituo vikuu vya mabasi vikiwemo Ubungo, Mwanza, Mbeya, Arusha na kwingineko kuwasisitiza abiria kushiriki katika kuwapigia kura madereva wanaostahili kupigiwa kura.

Katika kuunga mkono jitihada za kupunguza ajali barabarani wakali katika muziki wa

bongo fleva Mr Blue, Amini, Banaba Boy na Dayna Nyange wameshiriki kurekodi wimbo wa “Dereva Makini” utakaotumika mfululizo kwenye kampeni hii kuhamasisha umakini kwa madereva wawapo barabarani .

Ambapo Mr Blue anasema “..kwa kweli hili janga limekuwa kubwa sasa hivi, ukiangalia idadi ya watu wanaofairiki au kupata matatizo kila mwaka imezidi kuwa kubwa janga, nawashauri madereva kuwa makini wanapoendesha magari”

Amin yeye anasema “familia nyingi zinapotea kutokana na ajali zikiwa pamoja safarini, na ajali nyingi zinasababishwa na madereva, kutokuwa makini wanapokuwa wanaendesha magari yao.”

Banaba Boy “Vizazi vingi tunavyotegemea ndiyo vije kuwa viongozi ndio vinavyo pata ajali, na vianvyooangamia kwakuwa havina upeo wa kuepuka mambo kama hayo”

Wimbo huo umerekodiwa na mtayarishaji wa muziki C9 na anasema “Mimi mwenyewe binafsi nimeshapoteza ndugu zangu, nimepoteza nguvu kazi nyingi sana za wasanii ambao nilikuwa nategemea wangekuja kurekodi na kunipatia kipato”

Dyna anasema “Tunandugu zetu, wasanii wenzetu wanapata ajali na ajali nyingi zinatokana na uzembe kabisa, kwa hiyo nimejitoa kwa hali na mali kwa uwezo wa mwenyezi Mungu kufikisha elimu ya dereva makini ili kupunguza ajali hizo”

Shindano hilo la kumtafuta na kumtambua dereva Makini limepokelewa kwa mikono miwili na madereva wa mabasi ambapo Mwenyekiti wa Chama Cha Madereva wafanyakazi Mzee Abdallah,anasema kuwa tangu aanze kuendesha basi miaka mingi iliyopita hajawahi kupata motisha ya kutambuliwa kwa mchango wake katika sekta ya usafirishaji abiria.

“Tunaona tu kuna tuzo za mfanyakazi bora, mwanamuziki bora, muigizaji bora,Bibi bomba ambapo wanaofadika na tuzo hizo ni wachache ukilinganisha na Tuzo ya Dereva Makini ambaye anabeba roho za watu wengi kila siku. Lakini nchi haijaweka utaratibu wowote wa kututambua sisi madereva na kero tunazokumbana nazo katika kazi zetu, tunachukuliwa kama watu tusio na mchango wowote katika uchumi wa taifa hili” anasema Ndimbo Manyoto.

Anasema kuwa kutokana na kukosekana utaratibu huo wa kutambuliwa na kupewa heshima imewafanya madereva wengi kutoiona tofauti yao na wale wanaovunja sheria za barabarani kwa kuwa hata wakitenda mema wote huwekwa kwenye kundi la watenda mabaya.

Ndimbo anasema shindano hilo litakuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa kila dereva atapenda kuibuka mshindi kwa kuzingatia sheria na kutoa huduma inayokidhi kwa abiria ambao ndio wateja wake na wapiga kura wake.

Akizungumzia juu ya tuzo hiyo bwana

Nzunda anasema kuwa Shindano hilo litatoa tuzo na zawadi mbalimbali kutoka kwa wadhamini wa shindano hilo kwa washindi kitaifa ambapo mshindi wa kwanza atapewa shilingi Milioni 5, huku mshindi wa pili akipata Shilingi Milioni 3.5 na mshindi wa tatu atapokea Shilingi Milioni 2.5 na zawadi mbalimbali kutoka kwa wadau wa sekta ya usafirishaji.

Anasema mshindi ataamuliwa kwa wingi wa kura kutoka kwa abiria na matokeo yatatolewa na majina na picha zao kuchukuliwa na kutatangazwa mara kwa mara kwenye redio, televisheni, magazeti, kwenye mabango makubwa barabarani na kwenye vituo vikuu vya mabasi ili kuwapa hamasa madereva wengine kuiga mfano wao.

“Hii itashawishi madereva wengine kufuata sheria za barabarani hivyo tutajikuta taratibu mwaka hadi mwaka tunaweza kubadili tabia na mienendo yao wawapo barabarani” anasema Nzunda.

Nzunda anasema wako katika hatua za mwisho za mchakato wa shindano hilo ambalo litaanza mwanzoni mwa mwezi Octoba mwaka huu ambapo anatoa wito kwa makampuni mbalimbali nchini kujitokeza na kudhamini shindano hilo ambalo lengo lake ni kupunguza ajali za barabarani ambazo zimekuwa ni mwiba mchungu kwa kuzolotesha uchumi wakifamilia wakijamii na taifa kwa ujumla, ambapo tumeona mara nyingi Wategemewa (wazazi) kubadilika na kuwa wategemezi (Kwa watoto) na pengine watoto kulazimika kukatisha masomo yao nakuanza kulea wazazi waliopata vilema vya kudumu kutokana na ajali hizo.

Wasiliana nasi kupitia +255 22 212 6007, +255 687 966 638

au [email protected], facebook;DerevaMakini

Tuzo za Dereva Makini wa mabasi zitapunguza ajali za barabarani?

28 | www.uda.co.tz www.uda.co.tz | 29

TUNAJIVUNIA MWANZO MPYA WA KITANZANIA TUNAJIVUNIA MWANZO MPYA WA KITANZANIA

Tanzania imepiga hatua kwenye muziki na filamu

T anzania imeonesha kupiga hatua katika tasnia ya filamu na

muziki, hii imethibitishwa na wasanii wenyewe kwa kuwa na maendeleo

makubwa yanayoonesha ni jinsi gani muziki na filamu

vinawaingizia kipato.

Hii imewafanya vijana wengi wa kitanzania kujiingiza katika tasnia hizo kwa lengo la kuwa

na mafanikio, wakivutiwa na mafanikio ya wanamuziki kama Sugu, Diamond Platnumz,Ali Kiba,Ney,Jay Dee na wengine wengi.Hii imeifanya jamii ya watanzania kuwaamini vijana wao ambao walikuwa wanamuziki na sasa ni wabunge,muziki sasa unaweza kuwa ni ajira kwa vijana kwani kumekuwa na mashindano mbalimbali ya kutafuta vipaji vya waimbaji ambao mwisho wa siku huwatoa vijana kimaisha,hii yote ni kwa sababu tasnia hii inazidi kukua kwa kasi sana hapa nchini,huku wengine wakivutiwa zaidi na tasnia ya filamu ambayo imezidi kuja kwa kasi katika jamii ya watanzania. Filamu hapo mwanzo haikuchukuliwa kwa umakini sana lakini baada ya waigizaji nguli wa Tanzania kufanya mapinduzi makubwa

kwa kuanza kutoa filamu badala ya maigizo yaliyokuwa yanarushwa hewani na vituo mbaimbali vya televisheni.Kukua kwa tasnia hii ya filamu kumeongeza soko

hili kuzidi kupenya afrika mashariki na kati na kujizolea mashabiki lukuki kutoka kila kona. Wanamuziki wa Tanzania kupenya mpaka

Afrika ya magharibi imeipa chachu tasnia hii kukua kwa kiasi kikubwa na kuifanya Tanzania kujitangaza zaidi kimataifa. Hii ni kwasababu wasanii wa kitanzania wameweza kushiriki

kwenye tuzo mbalimbali za muziki wa kimataifa, kama vile BET,AFRO MAMA,MTV na AMA.

Uhalisia utabaki palepale ya kuwa sasa watanzania wanafuatilia sana

filamu za kitanzania kuliko za nchi nyingine, siyo kama miaka ya nyuma ambapo filamu za Nigeria zilivyokuwa zimeteka soko hapa nchini. Kukua huku kwa filamu za kitanzania kumehamasisha hata vituo mbalimbali vya televisheni nchini kuwa na vipindi vya filamu za kitanzania. Filamu hizi sasa zimekuwa zikishindanishwa na zile za Nigeria kwenye tuzo mbalimbali zikiwemo tuzo maarufu za MA, na AMA zinazofanyika kila mwaka jijini Lagos Nigeria.Imeandaliwa na Lukuba Machibya

ALIKIBA

@PSPF TanzaniaPSPF Tanzania www.pspf-tz.org 0800 110 055 / 0800 780 060@PSPF TanzaniaPSPF Tanzania @PSPF Tanzania www.pspf-tz.org@PSPF Tanzania www.pspf-tz.org 0800 110 055 / 0800 780 060www.pspf-tz.org

Wakwanza kukuletea mikopo ya Nyumba, na ni wa kwanza tena kukuletea mikopo ya Viwanja.

Katika kudumisha dhana ya PSPF Pamoja Nawe Mfuko unatoa huduma ya Mikopo ya Viwanja vya Makazi kwa Wanachama wake. Lengo kubwa la huduma hii ni kuwawezesha wanachama wa Mfuko kumiliki viwanja vya makazi vilivyopimwa ili kuwaepusha dhidi ya ujenzi wa makazi holela, kwa kuwa makazi holela yana gharama kubwa zaidi kuliko makazi yaliyopangiliwa.

30 | www.uda.co.tz www.uda.co.tz | 31

TUNAJIVUNIA MWANZO MPYA WA KITANZANIA TUNAJIVUNIA MWANZO MPYA WA KITANZANIA

32 | www.uda.co.tz

TUNAJIVUNIA MWANZO MPYA WA KITANZANIA


Top Related