fataawa za shaykh muqbil kuhusu wanawake
DESCRIPTION
Fataawa Za Shaykh Muqbil Kuhusu WanawakeTRANSCRIPT
1
Fataawa Kuhusu
Wanawake
´Allaamah Muqbil bin Haadiy
al-Waadi´iy
Imefasiriwa Na:
Abu Bakr Khatwiyb al-Atrush
2
Fataawa zilizomo:
1) ´Allaamah al-Waadi´iy Kuhusu Mwanamke Kuwa Mbele Anapowaongoza Wenzio
Katika Swalah
2) ´Allaamah Muqbil Kuhusu Mwanamke Kunyoa Nywele Za Mwilini Mwake
3) Alikuwa Hatoi Zakaah Ya Dhahabu Kwa Ujinga Na Sasa Dhadhabu Yote Imekwisha
4) Anamnyonyesha Mtoto Mbele Ya Dada Zake
5) Baada Ya Kutwahirika Akakutana Na Mumewe, Damu Imejitokeza Tena?
6) Baadhi Ya Vitabu Ambavyo Mwanafunzi Mwanamke Anapaswa Kuwa Navyo
7) Dalili Kuwa Mwanamke Mwenye Hedhi Anaruhusiwa Kugusa Msahafu Na Kusoma
8) Damu Inayomtoka Mwanamke Kabla Ya Kujifungua
9) Haijuzu Kuoa Mwanamke Ambaye Mwanaume Kanyonya Kwa Mama Yake
10) Kajifungua Baada Ya Kuingia Swalah Ya Dhuhr, Ni Wajibu Kuilipa?
11) Katwaharika Na Hedhi Lakini Daktari Kamkataza Kukoga
12) Kauli Yenye Nguvu Ni Kuwa Mwanamke Kuonesha Uso Wake Ni Haramu
13) Kumnyonyesha Mtoto Baada Ya Miaka Miwili
14) Kumpasua Mwanamke Ambaye Kafariki Na Tumboni Mwake Kuna Mtoto Hai
15) Kunyonyesha Mbele Ya Wanawake Waislamu
16) Kutumia Dawa Ya Kuzuia Mimba Kutokana Na Uzito Anaoupata Mwanamke
17) Maandamano Ya Wanawake
18) Mama Wa Mwanamke Niliyemtaliki Atabaki Kuwa Mahram Kwangu?
19) Mavazi Ambayo Anapaswa Kuvaa Mwanamke Aliyefiwa Na Mume Wake
20) Mke Hana Haki Yoyote Ya Kumpa Talaka Mwanaume
21) Mke Hataki Kukoga Janaba Na Anajua Ni Wajibu
22) Mke Kumfanyia Mume Wake Maakulati Aina Mbali Mbali
23) Mke Kuomba Talaka Kwa Mume Wake Bila Ya Sababu Yoyote
24) Mke Kuwapa Zakaah Dada Zake Na Mume Wake
25) Mke Wake Alipotea Na Baadae Akampata Kishakuwa Na Mume Mwingine
26) Msimamo Wa Shaykh Muqbil Kuhusu Mwanamke Kufunika Uso
27) Mume Hataki Hijaab, Nifanye Nini?
28) Mume Kamtaliki Mke Wake Mara Sita Kisha Anasema Kuwa Hakumbuki
29) Mume Na Mke Wanatofautiana Katika Masuala Ya Dini
30) Mume Wake Kamtupa Miaka Miwili Na Kwenda Kutafuta Elimu
31) Mwanamke Alikuwa Hajui Kuwa Anajibika Kutoa Zakaah Ya Dhahabu Zake Na Sasa
Amejua
32) Mwanamke Anasafiri Kila Siku Na Kwenda Kwenye Masomo Ya Mchanganyiko
33) Mwanamke Anatakiwa Kuolewa Pale Anapofikisha Miaka 13, 14 Au 15
34) Mwanamke Anaweza Kusafiri Na Mwanamke Mwenzake?
35) Mwanamke Kufanya Kazi Ili Awapatie Watoto Wake Riziki
36) Mwanamke Kufanya Kazi Katika Idara Na Hospitali Za Mchanganyiko
37) Mwanamke Kumkogesha Mama Mzee Na Mwendawazimu Wasiojiweza
38) Mwanamke Kunyoa Nywele Za Mguuni Mwake
39) Mwanamke Kuondosha Nywele Za Kwenye Kidevu, Miguuni Na Mwilini
40) Mwanamke Kusafiri Na Mahram Mtoto Awezae Kupambanua
41) Mwanamke Kuvaa Mavazi Meupe
3
42) Mwanamke Kuvaa Suwali Mbele Ya Mume Wake Na Wanawake Wengine
43) Mwanamke Mwenye Hedhi Kuingia Msikitini Kutoa Darsa Kwa Wanawake Wenzio
44) Mwanamke Mwenye Hedhi Na Nifasi Kushika Msahafu Na Kuingia Msikitini
45) Mwanamke Wa Kiislamu Kutumia Vipodozi "Miquillaage"
46) Mwanaume Na Mwanamke Wote Ni Sunnah Kutahiriwa
47) Nasaha Za Shaykh Muqbil Kwa Mume Na Mke Ambao Ni Wanafunzi
48) Ni Wajibu Kwa Mwanamke Kuvaa Vifuniko Vya Mikoni (Gloves)
49) Ni Wajibu Kwangu Mke Kumhudumia Mama Wa Mume Wangu?
50) Ole Wako Mume Kumwacha Mke Wako Kwenda Kwa Wanawake Hizbiyaat
51) Shaykh Muqbil al-Waadi´iy Kuhusu Uke Wenza
52) Udugu Wa Kunyonya Wa Watoto Wa Mama Tofauti
53) Wamezini Katika Hali Ya Uchumba, Wanapigwa Mawe Au Wanauawa?
54) Yupi Bora Kati Ya Wanawake Hawa Wawili?
4
1) ´Allaamah al-Waadi´iy Kuhusu Mwanamke Kuwa Mbele
Anapowaongoza Wenzio Katika Swalah
Swali:
Mwanamke akiwaongoza wanawake katika Swalah, je, asimame mbele ya
wanawake au asimame katikati yao kama alivyofanya ´Aaishah (Radhiya
Allaahu ´anha). Aliswalisha watu, akasimama katikati yao. Kasema hili
Imaam al-Bayhaqiy? Je, hili limethibiti kwake? Na kama limethibiti, je inafaa
kuitumia kama hoja?
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Ndio limethibiti. Na kuna upokezi mwingine unaofanana na wa ´Aaishah ya
kwamba Ummu Salamah alifanya hivyo. Ingawa kitendo cha ´Aaishah na
Ummu Salamah vimethibiti, lakini si hoja. Kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu
´alayhi wa sallam) anasema:
"Swalini kama mlivyoniona nikiswali."
Na Hadiyth hii inamgusa mwanaume na mwanamke. Kama ilivyo katika
Kauli Yake (Ta´ala):
كاة لة وآتوا الز وأقيموا الص
"Na simamisheni Swalaah, na toeni Zakaah." (02:110)
Hii inamgusa mwanaume namwanamke. Lililo la dhahiri ni kuwa, Sunnah ni
mwanamke atangulie mbele ya wanawake kama afanyavyo Imamu.
Chanzo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=778
5
2) ´Allaamah Muqbil Kuhusu Mwanamke Kunyoa Nywele Za Mwilini
Mwake
Swali:
Je, mwanamke anaweza kuondosha nywele za usoni mwake na za mwili wake
wote isipokuwa tu za kichwani tu?
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Tunachomnasihi asiziondoshe, isipokuwa tu ikiwa kama yuko na ndevu.
Hakuna ubaya akaziondosha. Kwa kuwa akiziondosha kwa mara ya kwanza,
zitaongezeka na kuwa nyingi zaidi. Isitoshe zitakuwangumu na mbaya ilihali
angeliziacha zingekuwa laini. Tunamnasihi asifanye hivyo, na lau atafanya
hivyo hakuna neno. Hakuna dalili inayoharamisha na hili - In Shaa Allaah -
haliingii katika kubadilisha maumbile ya Allaah.
Chanzo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=1556
3) Alikuwa Hatoi Zakaah Ya Dhahabu Kwa Ujinga Na Sasa Dhadhabu Yote
Imekwisha
Swali:
Kuna mwanamke alikuwa na dhahabu na wala hatoi Zakaah kwa kutokujua.
Na kwa sasa hakubaki na kitu. Je, ni juu yake kutoa Zakaah sasa au afanye
nini?
6
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Ndio. Ni wajibu kwake kutoa Zakaah ikiwa yuko na uwezo wa kufanya
hivyo, la sivyo itabaki juu ya dhimmah yake. Kwa kuwa hii ni haki ya
mafukara. Huu ndio wajibu wake.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/default_ar.aspx?id=662
4) Anamnyonyesha Mtoto Mbele Ya Dada Zake
Swali:
Je, inajuzu kwa mwanamke kumnyonyesha mtoto wake mbele ya dada zake?
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Hakuna ubaya akamnyonyesha mtoto wake mbele ya dada zake.
Chanzo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=338
5) Baada Ya Kutwahirika Akakutana Na Mumewe, Damu Imejitokeza Tena?
Swali:
Mwanamke alikuwa na hedhi na baada ya masaa sita akatwahirika. Na baada
ya mume wake kumjamii, hedhi ikarudi. Afanye nini?
7
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Ikiwa siku zake za ada ni sita kwa mfano, na siku sita hizo zikapita, asijali kwa
hichi kilichodhiri. Isipokuwa tu ikiwa jambo hili litakariri, hapo kutatazamwa.
Au itatazamwa vile vile damu yake ni nyingi au ndogo, ikiwa ni damu ndogo
haidhuru. Na ikiwa ni damu nyingi, atachukulia damu ya siku zile kuwa ni
damu ya hedhi. Haruhusiwi kuswali wala kufunga. Na kwa kutumia fursa hii,
nimeambiwa kuwa baadhi ya wahubiri Hudaydah wametusemea uongo na
kusema kuwa mimi naamrisha mwanamke kulipa Swalah zake na asilipe
Swawm. Huu ni uongo. Mikanda ipo inayotolea ushahidi hilo. Anadai kuwa
kaambiwa na watu waaminifu. Ni watu gani waaminifu ambao
wamekwambia hivyo wewe masikini?
Chanzo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?sec_id=15
6) Baadhi Ya Vitabu Ambavyo Mwanafunzi Mwanamke Anapaswa Kuwa
Navyo
Swali:
Ni vitabu vipi ambavyo unamnasihi mwanamke wa Kiislamu kuwa nayo?
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Tunavyomnasihi navyo ni kwa mfano; "Riyaadh-us-Swaalihiyn", "Fath al-
Majiyd" ambacho ni Sharh Kitaab-ut-Tawhiyd, "al-Lu-ul wal-Marjaan" na
"Buluugh-ul-Maraam". Hivi ni kwa mwanamke ambaye anaweza kusoma na
kuandika. Ni vitabu ambavyo ni mukhtaswari. Hali kadhalika kitabu cha
ndugu yetu Muhammad "al-Qawl al-Mufiyd". Ama kwa mwanamke mwenye
uwezo wa kufanya utafiti na uhak-ikisho, inatakikana kwake kuwa na
Maktabah kubwa kadiri na atakavyoweza. Alhamdulillaah.
8
Chanzo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=1596
7) Dalili Kuwa Mwanamke Mwenye Hedhi Anaruhusiwa Kugusa Msahafu
Na Kusoma
Swali:
Je, inajuzu kwa mwanamke mwenye hedhi kugusa msahafu na kusoma ndani
yake?
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Sijui kama kuna makatazo yoyote ya kufanya hivi.
Ama Kauli Yake (Ta´ala):
ه إل المطهرون ل يمس
"Hawaigusi isipokuwa waliotwahara." (56:79)
Makusudio ni Malaika, kama Alivyosema (Subhaanahu wa Ta´ala) katika
Aayah ya ash-Shu´araa:
ياطين وما ينبغي لهم وما يستطيعون لت به الش وما تنز
"Na (wala) hawakuteremka nayo (hii Qur-aan) mashaytwaan. Na (wala)
haipasi kwao (kuteremka na Qur-aan) na wala hawawezi." (26:210)
Na amesema Imaam Maalik katika "al-Mu´attwah": "Kauli Yake (Ta´ala):
Inafasiriwa na Aayah ya ´Abasaa:
ها رة تذكرة فمن شاء ذكره فيكل إن طه رفوعة م مة م كر بأيدي سفرة كرام بررة صحف م
"Sivyo katu! Hakika (hizi Aayah za Qur-aan) ni ukumbusho. Basi atakaye
akumbuke. (Zimeandikwa) Katika swahifa zilizokirimiwa (Al-Lawh Al-
9
Mahfuwdh). Zimetukuzwa na zimetwaharishwa. (Zinazobebwa) Katika
mikono ya (Malaika) waandishi. Watukufu (na) watiifu." (80:11-16)
Yaani hawakuteremka nayo Mashaytwaan, isipokuwa imeteremka na
Malaika. "Katika mikono ya waandishi", nao ni Malaika. "Watukufu (na)
watiifu."
Na amepokea al-Bukhaariy katika Swahiyh yake:
"Ibn ´Abbaas alikuwa haonelei mwenye janaba tu kusoma Qur-aan."
Hakuna ubaya kwa hili In Shaa Allaah. Tumebakia na Hadiyth nyingine
inayosema:
"Haigusi Qur-aan isipokuwa aliye Twahara."
Hadiyth hii katika njia zake zote, kuna mtu dhaifu ndani yake naye ni Swaalih
bin Hujjiyah. Lakini hata hivyo, tunachukua kama alivyoif-asiri Imaam ash-
Shawkaaniy katika "an-Nayl al-Awtwaar":
Maana yake ni:
"Haigusi Qur-aan isipokuwa Muislamu."
Abu Hurayrah kapokea pia kuwa:
"Hakika ya Muislamu hajanasiki."
Hivyo, maana yake ni kuwa haigusi (Qur-aan) isipokuwa Muislamu tu. Kwa
dalili ya kwamba, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikataza
kusafiri na Qur-aan katika ardhi (miji) ya makafiri.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/default_ar.aspx?id=8107
8) Damu Inayomtoka Mwanamke Kabla Ya Kujifungua
Swali:
10
Mwanamke kabla ya kujifungua anakuwa na alama na anatokwa na maji maji.
Na wakati mwingine hali inaendelea namna hii siku mbili mpaka zaidi. Ipi
hukumu ya Swalah wakati wa hali hiyo?
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Ikiwa ni kabla ya kujifungua, haidhuru In Shaa Allaah. Anatakiwa kuswali.
Na ikiwa ni damu, huzingatiwa kuwa ni damu katika damu ya uzazi (nifasi).
Hapo Swalah itasimama kwake.
Chanzo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=2594
9) Haijuzu Kuoa Mwanamke Ambaye Mwanaume Kanyonya Kwa Mama
Yake
Swali:
Je, inajuzu kwangu kuoa mwanamke ambaye nilinyonya kwa mama yake
lakini yeye hakunyonya kwa mama yangu?
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Haijuzu kwa kuwa huyo huchukuliwa kuwa ni dada yake katika kunyonya.
Na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema:
"Ni Haramu kwa kunyonya kama yalivyo Haramu yanayopatikana katika
nasabu."
Chanzo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=533
11
10) Kajifungua Baada Ya Kuingia Swalah Ya Dhuhr, Ni Wajibu Kuilipa?
Swali:
Kuna mwanamke ambaye kajifungua baada ya kuingia kwa wakati wa Dhuhr.
Na kabla ya kujiwa na alama za kujifungua, kazaa. Je, ni juu yake kulipa
Swalah ya Dhuhr?
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Lililo la dhahiri ni kuwa hana juu yake kulipa, kwa kuwa kajifungua wakati
wa Dhuhr. Na Shari´ah haikumlazimu mtu kuswali pale mwanzo wa kuingia
kwa wakati.
Chanzo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=644
11) Katwaharika Na Hedhi Lakini Daktari Kamkataza Kukoga
Swali:
Kuna mwanamke mgonjwa aliyekuwa na hedhi sasa katwaharika. Afanye nini
baada ya kutwahirika naye amekatazwa kukoga?
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Baada ya kukatika damu yake atatayamamu. Mgonjwa akikhofia maradhi
yake yasizidi au kudumu, Allaah Kajaalia kutayamamu badala ya kutia
Wudhuu (kwa maji).
12
Chanzo: http://muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=450
12) Kauli Yenye Nguvu Ni Kuwa Mwanamke Kuonesha Uso Wake Ni
Haramu
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Uzuri wa mwanamke uko usoni mwake. Kauli yenye nguvu ambayo
imeegemea katika dalili ni kuwa, ni Haramu kwake kutoka ikiwa bado angali
ni mjane. Ama kama ameshakuwa mzee, kapewa rukhusa ya hilo. Anasema
Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):
جات بز والقواعد من الن تي ل يرجون نكاحا فليس عليهن جناح أن يضعن ثيابهن غير متبر ينة وأن ساء الل
يستعففن خير لهن
"Na Al-Qawaa’id (wanawake wazee wasiozaa tena au kutokwa hedhi)
miongoni mwa wanawake ambao hawataraji kuolewa, basi hakuna ubaya juu
yao kupunguza baadhi ya nguo zao bila ya kuonyesha mapambo yao (au
kujishaua). Na kama wakijisitiri (kwa kujifunika vyema) ni kheri kwao."
(24:60)
Ikiwa ni mama mwenye umri mkubwa na wala hakuogopwi kwake
kufitinisha watu, lau atatoka na uso wake kaufunua, hakuna neno kwa hilo.
Chanzo: http://muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=1203
13) Kumnyonyesha Mtoto Baada Ya Miaka Miwili
Swali:
13
Je, inajuzu kwa mwanamke kuomnyonyesha mtoto wake baada ya miaka
miwili?
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Sioni ubaya wowote wa hilo. Ama Kauli Yake (Ta´ala):
والوالدات يرضعن أولدهن حولين كاملين
"Na wazazi wa kike wanyonyeshe watoto wao miaka miwili kamili." (02:233)
Hii ndio aghlabu ya watoto wengi. Lakini lau mtoto atakataa, akamnyonyesha
mwezi mmoja, miwili, mitatu au minne, sioni ubaya wowote wa hili.
Chanzo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=756
14) Kumpasua Mwanamke Ambaye Kafariki Na Tumboni Mwake Kuna
Mtoto Hai
Swali:
Lau mwanamke anakufa na tumboni mwake ana kijusi (mtoto) ambaye yuko
hai. Je, inajuzu kwa tabibu kupasua tumbo lake?
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Sioni kama kuna makatazo yoyote ya hili, hakuna ubaya In Shaa Allaah
kupasua tumbo lake na kumtoa mtoto nje.
Muulizaji:
14
Baadhi yao (madaktari) wanawaua.
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Kuwaua haijuzu. Haijuzu kumuua mtoto.
Chanzo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=381
15) Kunyonyesha Mbele Ya Wanawake Waislamu
Swali:
Je, inajuzu kwa mwanamke kumnyonyesha mtoto wake mbele ya ndugu zake
wanawake katika Uislamu?
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Sioni ubaya wa kufanya hivyo.
Chanzo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=338
16) Kutumia Dawa Ya Kuzuia Mimba Kutokana Na Uzito Anaoupata
Mwanamke
Swali:
15
Kuna mwanamke ana mtoto mdogo ambaye ana miezi kumi na kwa sasa ana
ujauzito mwingine. Anahisi uzito wa kutazama watoto wake na ubebaji wa
mimba. Je, baada ya mimba hii mpya naweza kutumia dawa ya kuzuia
mimba?
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Tunachomnasihi, amkabidhi amri yake Allaah. Na akikhofia juu ya nafsi yake
maangamivu na akaambiwa na matabibu wenye fani hii huenda akafikwa na
maangamivu na akafa, hapo anaweza kutumia dawa hiyo. Tunachomnasihi ni
yeye amtegemee Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) na amkabidhi amri yake
Allaah (´Azza wa Jalla).
Chanzo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=3068
17) Maandamano Ya Wanawake
Swali:
Ni ipi hukumu ya maandamano ya wanawake?
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Maandamano yamezushwa, sawa ikiwa ya wanaume na wanawake.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=2151
18) Mama Wa Mwanamke Niliyemtaliki Atabaki Kuwa Mahram Kwangu?
16
Swali:
Mama wa mke wangu ambaye nimemtaliki anabaki kuwa Mahram au
hapana?
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Ndio. Anabakiwa kuwa Mahram.
Chanzo: http://muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=1501
19) Mavazi Ambayo Anapaswa Kuvaa Mwanamke Aliyefiwa Na Mume
Wake
Swali:
Mwanamke ambaye amefiwa na mume wake, je avae mavazi meusi au haya
ni maneno tu ya watu? Na je, atie wanja?
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Mwanamke ambaye amefiwa na mume wake, avae mavazi ambayo hayavutii
watu kwake, sawa mavazi hayo yakiwa ni meupe au meusi. Akae eda miezi
minne na siku kumi. Kama Alivyosema Allaah (Ta´ala):
والذين يتوفون منكم ويذرون أزواجا يتربصن بأنفسهن أربعة أشهر وعشرا
"Na wale wanaofishwa miongoni mwenu na wakaacha wake, (hao wake)
wangojee nafsi zao miezi minne na siku kumi (eda ya mfiwa)." (02:134)
Akae masiku haya naye yuko katika nyumba ya mume wake ambapo kafa
ndani yake.
17
Chanzo: http://muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=651
20) Mke Hana Haki Yoyote Ya Kumpa Talaka Mwanaume
Swali:
Je, inajuzu kwa mwanamke kumtaliki mume wake akishikwa na
wendawazimu au akakosa kuwepo kwa muda mrefu?
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Mwanamke hana haki ya Talaka. Lakini akidhurika kwa kukosa kuwepo
kwake, ataenda kwa kiongozi. Na ni wajibu wa kiongozi kukubali maombi
yake ya kutengana kisha awatenganishe. Inatakikana kuwa namna hii ikiwa
atadhurika, sawa kwa kukosa kuwepo mume au akiwa ni mwendawazimu.
Chanzo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=2730
21) Mke Hataki Kukoga Janaba Na Anajua Ni Wajibu
Swali:
Ipi hukumu ya mwanamke ambaye hakogi janaba naye anajua kuwa kukoga
ni wajibu?
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
18
Atazingatiwa kuwa ni mfanya madhambi na anafanya Haramu. Allaah (´Azza
wa Jalla) Anasema:
هروا وإن كنتم جنبا فاط
"Na mkiwa na janaba basi jitwaharisheni." (05:06)
Wajibu kwa Muislamu ni yeye kukimbilia kujitwahirisha kunapokuja wakati
wa Swalah. Ama lau maingiliano yatakuwa mwanzoni mwa usiku, mume
wake anaweza kutangulia kukoga kisha akafuata mke au wakakoga wote
wawili. Wanaweza vile vile kuchelewesha mpaka kabla ya Fajr. Hakuna
ubaya kwa hili. Katika hali hii itabidi watawadhe. Hakuna ubaya kufanya
hivi. Na kunapokuja wakati wa Swalah, ni wajibu kwake mwanamke
ajitwahirishe na aswali. Na kunapokuja wakati wa Swalah asijitwahirishe
wala kuswali, huku kutokuswali kwake anazingatiwa kuwa ni kafiri.
Chanzo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=2431
22) Mke Kumfanyia Mume Wake Maakulati Aina Mbali Mbali
Swali:
Mwanamke akimtengenezea mume wake vyakula aina mbalimbali, je,
kufanya hivi ni katika pumbao la dunia jambo ambalo limekatazwa?
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Hakuna ubaya kufanya hivi In Shaa Allaah. Na mume ni mtu bora. Anasema
Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):
ه لكم موا طي بات ما أحل اللـ ها الذين آمنوا ل تحر يا أي
"Enyi mlioamini! Msiharamishe vizuri Aliyokuhalalishieni Allaah." (05:87)
ه ل يحب المسرفين يا بني آدم خذوا زينتكم عند كل مسجد وكلوا واشربوا ول تسرفوا إن
19
"Enyi bani-Aadam! Chukueni mapambo yenu katika kila Masjid; na kuleni na
kunyweni; na wala msifanye israfu. Hakika Yeye (Allaah) Hapendi
wanaofanya israfu." (07:31)
Kunapobakia kitu katika chakula, asikimwage bali anatakiwa kukitoa awape
masikini na wanaohitaji. Jambo hili ni sahali. Ama mwenye kusema kuwa ni
Haramu au haijuzu, haitupasi kwetu kuwaharamishia watu kitu ambacho
Allaah Kawahalalishia. Allaah (Ta´ala) Anasema katika Kitabu Chake:
ه الكذب ول تقولوا ذا حرام ل تفتروا على اللـ ـ ذا حلل وه ـ لما تصف ألسنتكم الكذب ه
"Na wala msiseme yanayosifu ndimi zenu uongo; hii halaal na hii haraam ili
mumzulie Allaah uongo." (16:116)
بي لم تحر ها الن ه لك يا أي م ما أحل اللـ
"Ee Nabii! Kwa nini unaharamisha kile Alichokuhalalishia Allaah?" (66:01)
Chanzo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=555
23) Mke Kuomba Talaka Kwa Mume Wake Bila Ya Sababu Yoyote
Swali:
Je, inajuzu kwa mwanamke kuomba Talaka kwa mume wake na lini anaweza
kuomba?
´Allaamah Muqbil:
Imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
"Mwanamke yeyoye atakayeomba Talaka kutoka kwa mume wake bila ya
sababu yoyote, ni kaharamishiwa harufu ya Pepo."
Tunachomnasihi ni yeye kuwa na subira, na subira kwa mume wake na jamaa
zake huzingatiwa ni katika aina bora ya ´amali anazojikurubisha nazo mja
20
kwa Allaah. Kama jinsi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)
alivyomuamrisha mume kuwa naye na subira na akasema:
"Mwanaume asimchukie muumini mwanamke, akichukia tabia fulani kutoka
kwake atapenda nyingine alionayo."
Masuala haya ni lazima pande zote mbili kuwa na subira, la sivyo mwanamke
ambaye hana subira ataachika kila mwaka na kuolewa na mume mpya. Hali
kadhalika, mume ambaye hana subira hali itakuwa ni hii hii. Allaah (´Azza wa
Jalla) Anasema:
قوى ول تعاونوا على الثم والعدوان وتعاونوا على البر والت
"Shirikianeni katika wema na taqwa, na wala msishirikiane katika dhambi na
uadui." (05:02)
Allaah (´Azza wa Jalla) Anasema:
ه بعضهم على بعض وبما أنفقوا من أموالهم ل اللـ امون على الن ساء بما فض جال قو الر
"Wanaume ni wasimamizi juu ya wanawake kwa kuwa Allaah Amefadhilisha
baadhi yao kuliko wengine na kwa sababu ya (matumizi) wanayotoa katika
mali zao." (04:34)
تي تخافون نشوزهن ه والل الحات قانتات حافظات ل لغيب بما حفظ اللـ المضاجع فعظوهن واهجروهن فيفالص
واضربوهن فإن أطعنكم فل تبغوا عليهن سبيل
"Basi wanawake wema watiifu, wenye kuhifadhi (hata) wanapokuwa
hawapo (waume zao) kwa Aliyoyahifadhi Allaah. Na wale (wanawake)
ambao mnakhofu uasi wao, basi waonyeni na (wakiendelea uasi) wahameni
katika malazi (vitanda) na (mwishowe wakishikilia uasi) wapigeni.
Wakikutiini, basi msitafute dhidi yao njia (ya kuwaudhi bure)." (04:34)
Hali kadhalika, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema:
"Mwanamke ni mpungufu wa akili na Dini."
Na anasema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kama ilivyokuja
katika "Swahiyhayn", Hadiyth ya Abu Hurayrah:
"Ninawausia kuwatendea wanawake wema, hakika wao wameumbwa kwa
ubavu uliopinda... "
21
Tunachotaka kusema, ni lazima kuwa na subira kwa pande zote mbili sawa
mume na mke. Na kuna ndugu zetu hapa ya kuwa kuna mwanaume
aliyetalika wanawake watano katika siku moja. Alimtaliki wa kwanza. Akaja
wa pili na kumuuliza: "Alikufanya nini?" Akamwambia: "Na wewe
nimekutaliki."
Akaja wa tatu na kumwambia: "Wewe ni mwanaume mwenye khasira, kwa
nini umemtaliki?" Akamwambia: "Na wewe nimekutaliki."
Akaja mke wa nne na kutaka kumpa nasaha. Akamwambia: "Na wewe
nimekutaliki."
Na jirani wa nyumbani akamwambia: "Una nini wewe, wamekufanya nini?"
Akamwambia: "Na wewe nimekutaliki mume wako akipitisha hilo." Mume
wake akasema: "Nimepitisha hilo."
Baada ya hilo ni lazima kuwa na subira kwa mwanaume na mwanamke. Sote
ni wenye kughadhibika na tuna mapungufu mbalimbali. Ni lazima
tuvumiliane na tumche Allaah.
Chanzo: http://muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=757
24) Mke Kuwapa Zakaah Dada Zake Na Mume Wake
Swali:
Kuna mama anamiliki dhahabu na imefikisha Niswaab. Je, inajuzu kuwapa
Zakaah dada zake au mume wake ambaye ni mzee na hana mali zaidi ya
dhahabu hii anayomiliki?
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Ndio. Inajuzu kwake kuwapa Zakaah dada zake ikiwa ni mafukara. Na
mpaka wa ufukara ni kule kufikia daraja ya kuhitajia ikiwa hawana vya
22
kuwatosheleza. Inajuzu vile vile kumpa mume wake ikiwa ni fakiri. Kama
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivyomwambia Zaynab mke wa
´Abdullaah bin Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anha). Alipomuuliza:
"Je, ni Halali kwangu kumpa Swadaqah ya mali yangu?"
Akasema:
"Ndio."
Chanzo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=1645
25) Mke Wake Alipotea Na Baadae Akampata Kishakuwa Na Mume
Mwingine
Swali:
Kuna mwanaume kaoa mwanamke kisha akapotea na hakumpata.
Mwanamke huyo akaolewa na ndugu yake mwingine kisha akarejea mume
wa kwanza baada ya miaka kumi. Yule wa kwanza na huyu wa pili wote
wamezaa nae watoto. Ipi hukumu ya watoto?
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Ikiwa alimuacha na hakuwa ni mwenye kumpa matumizi au alikuwa ni
mwenye kumsubiri huku akitaraji atakuja, yule mwanamke akajivua katika
ndoa. Na baada ya kujivua, atakuwa sio Halali kwa yule wa kwanza na
atakiwa ni wa huyu wa pili. Ama ikiwa hakujivua, lakini mara nyingi
hupeleka mashtaka yake kwa hakimu na kujivua. Na Allaah (Ta´ala)
Anasema:
وهن ول تضار
"Na wala msiwadhuru." (65:06)
23
Akijivua, yule wa kwanza atakuwa hana njia nyingine. Anaweza kujivua
ikiwa anadhurika kwa matumizi, maisha na anaogopa kutumbukia katika
machafu. Katika hali hii, anaweza kujivua na atakuwa sio Halali kwa yule wa
kwanza.
Chanzo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=3083
26) Msimamo Wa Shaykh Muqbil Kuhusu Mwanamke Kufunika Uso
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Nawaelekeza katika kitabu cha ndugu yetu Mustwafah bin al-´Adawiy
(Hafidhwahu Allaah) kwa kuwa muda hautoshi kuzungumzia hilo [hukumu
ya kufunua uso]. Hii ni Radd kwa Shaykh al-Albaaniy (Hafidhwahu Allaah)
na kumbainishia ya kwamba ni wajibu kwa mwanamke kufunika uso wake.
Hali kadhalika kitabu cha Shaykh al-Answaar, hata kama kuna upetukaji wa
mipaka kwa Shaykh Albaaniy. Yasichukulie hayo, lakini faida zilizomo ndani
yake zichukuliwe.
Chanzo: http://muqbel.info/fatwa.php?fatwa_id=149
27) Mume Hataki Hijaab, Nifanye Nini?
Swali:
Mwamamke akitaka kujisitiri kwa Hijaab na mume wake au mmoja katika
ndugu zake anamkataza, pamoja na kuwa anayefanya hivyo ni katika
wanaoswali. Je, unamnasihi nini?
24
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Tunamchomnasihi mume huyu, anatakiwa kumshukuru Allaah (Subhaanahu
wa Ta´ala) ambaye Kamjaalia mke mwema ambaye anapenda Hijaab. Badala
yake, anatakiwa amshaji´ishe juu ya hili. Kuwaangalia wanawake ni fitina. Ni
fitina juu yao wanawake na vile vile ni fitina kwa yule mtazamaji. Na Mtume
(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema:
"Wanawake ni wapungufu wa akili na Dini... "
"Sijaacha fitina iliokuwa kubwa baada yangu kwa wanaume kuliko (fitina ya)
wanawake.”
Na anasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
Na ni Haramu kwake mume kumkataza. Hakika Mtume (Swalla Allaahu
´alayhi wa sallam) anasema:
"Mwanamke ni ´Awrah (uchi), Pindi anapotoka nje, matumaini ya Shaytwaan
huongezeka." (Kaipokea at-Tirmidhiy, Hadiyth ya ´Abdullaah bin Mas´uud
(Radhiya Allaahu ´ahu)
Haijuzu kwake kumkataza, kama tulivyotangulia kusema. Hali kadhalika,
mwanamke huyu haitakiwi kwake kumtii juu ya hili. Ajisitiri kwa Hijaab. Na
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema:
"Utiifu ni katika mema."
Chanzo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=1401
28) Mume Kamtaliki Mke Wake Mara Sita Kisha Anasema Kuwa
Hakumbuki
Swali:
25
Kuna mwanamke kumuacha mume wake na kwenda katika nyumba ya dada
yake hali ya kuwa yuko na watoto na baba yake. Mume wa dada yake akataka
kuwasuluhisha. Alipotaka kufanya hivyo, akasema mke kuwa hatorudi kwake
kwa kuwa ameshamtaliki mara sita na mimi kwake ni kama ajinabi. Na pindi
ninapomkumbusha (mume juu ya Talaka hizo) anasema kuwa hakumbuki. Je,
kufuatwe kauli ya mke au mume?
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Ni juu ya mwenye kudai abainishe na mwenye kukanusha ale yamini. La
dhahiri ni kuwa mume ndio mwenye kudai, kwa kuwa yeye ndio kamtaliki.
Kutokana na hili, ni juu yake kuleta mashahidi ya kuwa kamtaliki. Na kama
hakufanya hivyo, hana jengine ila kula yamini. Hili ndio la dhahiri. Ama
yaliyo baina yake (mke) na Allaah, akijua kweli kuwa kamtaliki zaidi ya mara
tatu, haijuzu kwake kumpa kitu. Kwa kuwa akifanya hivyo atazingatiwa
anazini nae.
Chanzo: http://muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=1644
29) Mume Na Mke Wanatofautiana Katika Masuala Ya Dini
Swali:
Mke katofautiana na mume wake katika jambo la Shari´ah. Yeye mke
anaamini kuwa ni Haramu na mume anaamini kuwa inaruhusiwa. Mume
anamuamrisha kukifanya. Je, mke amtii?
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Ikiwa kafikia daraja ya Ijtihaad, atakuwa ni mwenye kufanya ´Ibaadah kwa
ufahamu wake na Ijtihaad yake. Ama ikiwa ni mwanamke anayefuata
matamanio yake, ni juu ya mume kumpiga. Kwa mfano kamwambia:
26
"Usitoke, usijishauwe naye anajishaua na anasema kuwa kujishaua kunajuzu".
Hivyo, ikiwa ni ambaye kafikia Ijtihaad, hapana asimpige kwa kuwa atakuwa
ni mwenye kufanya ´Ibaadah kwa Ijtihaad yake na si juu yake mume
kumlazimisha. Na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema:
Miongoni mwa kuwatendea wema
"Nawausia kuwatendea wema wanawake."
Ni yeye mume kumshaji´isha juu ya kufahamu Kitabu cha Allaah na Sunnah
za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ama Kauli Yake
(Ta´ala):
ه بعضهم على بعض وبما أنفقوا من أموالهم ل اللـ امون على الن ساء بما فض جال قو االر تات لحات قان فالص
ه حافظات ل لغيب بما حفظ اللـ
"Wanaume ni wasimamizi juu ya wanawake kwa kuwa Allaah Amefadhilisha
baadhi yao kuliko wengine na kwa sababu ya (matumizi) wanayotoa katika
mali zao. Basi wanawake wema watiifu, wenye kuhifadhi (hata)
wanapokuwa hawapo (waume zao) kwa Aliyoyahifadhi Allaah." (04:34)
Aayah hii, makusudio yake ni katika jambo lisilokuwa hili ambalo ni masuala
ya Ijtihaad. Pengine akawa ni mtafutaji elimu, anajua kiarabu, Hadiyth za
Mtume wa Allaah, Kitabu cha Allaah na kwa mfano anaona kuwa kuweka
mkono wa kulia juu ya kifua baada ya Rukuu ni Sunnah, na yeye mume
anaona kuwa sio Sunnah, ni juu ya kila mmoja kufanya vile anavyoona na
yasiyokuwa hayo, hili linatumika hata ikiwa ni katika masuala ambayo mume
anaona kuwa ni Haramu na mke anaona kuwa inaruhusiwa kutokana na
Ijtihaad yake. Ikiwa mke ni mjinga, ni juu yake kumfunza na yeye mume
ataulizwa kwa alichokichunga.
"Kila mmoja wenu ni mchunga na ataulizwa kwa alichokichunga."
Muulizaji:
Ikiwa ni katika masuala ya kufunua uso. Mke anaona kufunua uso ni jambo
linajuzu. Je, mume amkataze?
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
27
Asimkataze [ikiwa mwanamke kafikia daraja ya Ijtihaad]. Akiweza
kumsubiria ni jambo zuri, la sivyo aachana nae. Ikiwa hawezi kuvum-ilia, si
juu yake kumkataza. Ingawa na sisi tunaona kuwa ni wajibu kwake kufunika
uso wake, kutokana na Hadiyth zilizotangulia:
"Mwanamke ni ´Awrah (uchi)."
Na Kauli ya Allaah (´Azza wa Jalla):
زواجك وبناتك ونساء المؤمنين يدنين عليهن من جلبيبهن بي قل ل ها الن يا أي
"Ee Nabii! Waambie wake zako, na mabinti zako, na wanawake wa Waumini
wajiteremshie jalaabiyb zao." (33:59)
Chanzo: http://muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=2595
30) Mume Wake Kamtupa Miaka Miwili Na Kwenda Kutafuta Elimu
Swali:
Afanye nini mwanamke ambaye mume wake kamtupilia zaidi ya miaka
miwili kwa hoja ya kwamba anatafuta elimu. Na mwanamke huyu kuna
khatari akatumbukia katika fitina kwa kumkosa mume wake. Ipi hukumu ya
hili?
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Mwanamke huyu akiweza kusubiri na ameachiwa matumizi na akapenda
mwenyewe kusibiri, basi afanye hivyo. Ama akikhofia nafsi yake fitina,
anaweza kuomba waachane.
Chanzo: http://muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=687
28
31) Mwanamke Alikuwa Hajui Kuwa Anajibika Kutoa Zakaah Ya Dhahabu
Zake Na Sasa Amejua
Swali:
Kuna mwanamke anamiliki dhahabu ambazo zimefikisha Niswaab. Na tokea
amiliki dhahabu hizi zimeshafanya Hawl sita na hakutoa Zakaah kwa kuwa
alikuwa hajui kuwa anawajibika Zakaah. Baada ya kujua alitoa Zakaah ya
miaka miwili na kumebaki miaka miwili mingine. Ipi hukumu ya hilo na
anawajibika nini?
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Miaka iliobaki iko juu ya dhimmah yake. Kwa kuwa ni haki ya mafukara.
Ataitoa pale ambapo Allaah Atamsahilishia. Katika dhimmah yake kumebaki
deni juu yake. Na pale ambapo Allaah Atamsahilishia ataitoa kuwapa
mafukara.
Chanzo: http://muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=1646
32) Mwanamke Anasafiri Kila Siku Na Kwenda Kwenye Masomo Ya
Mchanganyiko
Swali:
Baadhi ya wanawake wanasoma katika chuo kikuu cha mchanganyiko.
Wanapoambiwa wasifanye hivyo, wanasema kuwa wanajitengenezea
Mustaqbal wao. Isitoshe, mwanamke huyu anasafiri bila ya Mahram. Ni ipi
hukumu ya Kishari´ah kwa hilo?
29
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Mwanamke anayesoma katika chuo kikuu ambacho ni mchanganyiko,
huzingatiwa kuwa ni mwenye kukosea na anapata madhambi. Mtume (Swalla
Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema, katika Hadiyth ambayo imepotea
Usaamah bin Zayd (Radhiya Allaahu ´anhu):
"Sijaacha fitina iliokuwa kubwa kwa wanaume kama wanawake."
Na anasema tena (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
"Wanawake ni wenye akili na Dini pungufu."
Mwanaume anaenda na kutaka kumchumbia kwa familia yake, hapo
kafikisha miaka 25. Anaambiwa karibu, ila haitowezekana isipokuwa mpaka
baada ya kumaliza masomo yake. Lini atamaliza masomo yake chuo kikuu?
Baada ya miaka 52. Anamaliza masomo huku kishakuwa mzee na havutii
tena. Ilihali lau angeliolewa katika usichana wake, angelikuwa amekwishazaa
watoto watano, sita, saba n.k., kwa kiasi ambacho Allaah (Subhanaahu wa
Ta´ala) Atakuwa Amempa. Tunamnasihi kuacha masomo haya. Na Mtume
(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema:
"Yule mwenye kuacha kitu kwa ajili ya Allaah, Allaah Humpa kilicho bora
kuliko hicho alichoacha."
Muulizaji:
Kusafiri bila ya kuwa pamoja na Mahram?
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
"Sio Halali kwa mwanamke ambaye anamwamini Allaah na siku ya Mwisho
kusafiri bila ya kuwa pamoja naye Mahram."
Chanzo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=2303
30
33) Mwanamke Anatakiwa Kuolewa Pale Anapofikisha Miaka 13, 14 Au 15
Swali:
Ipi hukumu ya mwanamke kufanya kazi ya udaktari, ualimu na zisizokuwa
hizo?
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Haya ni mabalaa ambayo wamepewa majaribio kwayo Waislamu na kupotea
kwa sababu yake. Mwanamke anatakikana kuolewa naye ni msichana wa
miaka 13, 14 au 15. Namna hii ndivyo inavyotakikana. Lakini yeye anataka
kukamilisha masomo yake; Thanawiy, chuo kikuu, masta, Dr. kisha baada ya
hapo anatoka kama mwalimu na ikiwa ni mke wa mtu analeta mfanya kazi
nyumbani. Anashindwa kumpa mtoto malezi na maadili ya Kiislamu.
Muhimu ni kuwa, Waislamu hawahukumu kwa Shari´ah ya Allaah katika
jambo hili.
Na wajibu kwetu sote tuhukumu kwa Shari´ah ya Allaah. Mwanamke bora
kwake ni yeye kuwa nyumbani kwake. Na kutoka kwake, huzingatiwa ni
fitina kwake yeye au kwa wengine. Haitakikani kwa yeyote kutoa idhini ya
kufunza, isipokuwa tu ikiwa kama ni kufunzana Qur-aan na anajiwa na watu
nyumbani kwake au anatoka na wala hachanganyiki na wanaume. Ama
kufunza au kusoma katika masomo tulionayo na mchanganyiko kwenye chuo
kikuu, hili ni jambo lisilojuzu kwa hali yoyote ile, kwani huzingatiwa kuwa ni
fitina.
Chanzo: http://muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=1111
34) Mwanamke Anaweza Kusafiri Na Mwanamke Mwenzake?
31
Swali:
Mwanamke anaposafiri hali ya kuwa pamoja naye yuko na mwanamke
mmoja tu. Katika hali hii, Mahram anakuwa si wajibu kwake?
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Hapana. Uwajibu bado uko pale pale. Kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu
´alayhi wa sallam) anasema:
"Si Halali kwa mwanamke anayemwamini Allaah na siku ya Mwisho, kusafiri
isipokuwa awe pamoja naye Mahram."
Na makusudio ya Mahram, ni yule ambaye imeharamishwa kwake kumuoa.
Na makusudio hapa anaingia mume vile vile.
Chanzo: http://muqbel.info/fatwa.php?fatwa_id=639
35) Mwanamke Kufanya Kazi Ili Awapatie Watoto Wake Riziki
Swali:
Je, mwanamke kufanya kazi ni Haramu ilihali naye amelazimika ili awalishe
watoto zake na hakuna mwingine wa kuwalisha?
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Ikiwa hachanganyiki na wanaume, mudiri, tabibu au wasiokuwa hao, naye
isitoshe amelazimika, akafanya kazi naye anajiaminia nafsi yake, heshima
yake na Dini yake, In Shaa Allaah hakuna ubaya kwa hilo.
32
Chanzo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=729
36) Mwanamke Kufanya Kazi Katika Idara Na Hospitali Za Mchanganyiko
Swali:
Je, inajuzu kwa mwanamke kufanya kazi katika idara za serikali kwa hoja
hana ambaye atampa matumizi?
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Katika hali kama hii, haijuzu. Kwa kuwa atachanganyika na mudiri, raisi na
atachukua ujira kutoka kwake. Hili halijuzu. Mwanamke anazingatiwa kuwa
ni fitina. Na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema: "Mwanamke
ni ´Awrah (uchi), Pindi anapotoka nje, matumaini ya Shaytwaan huongezeka."
وإذا سألتموهن متاعا فاسألوهن من وراء حجاب
"Na mnapowauliza (wake zake) haja, waulizeni nyuma ya pazia." (33:53)
Hata kama Aayah hii inawahusu wake za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa
sallam). Hata hivyo, inawagusa wanawake wote, kama alivyosema Shaykh
ash-Shinqiytwiy (Rahimahu Allaah). Mimi ninawanasihi kina dada, bali
nasema kuwa haijuzu kufanya kazi katika idara kama hizi ambazo zina
mchanganyiko na fitina. Hali kadhalika Hospitali za mchanganyiko,
tunawanasihi kujiweka mbali na haya.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=3907
37) Mwanamke Kumkogesha Mama Mzee Na Mwendawazimu Wasiojiweza
33
Swali:
Je, inajuzu kwa mwanamke kumkogesha mwanamke ambaye ni
mwendawazimu ambaye yuko hai na mwanamke ambaye ni mzee ikiwa
hawawezi kujikogesha wenyewe?
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Akijiaminia kutopatwa na fitina na anayemuosha akawa na nguo zake,
hakuna ubaya wa hili. Ama akikhofia nafsi yake kupatwa na fitina, hapana
haijuzu, sawa kwake yeye na wengine.
Chanzo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=1827
38) Mwanamke Kunyoa Nywele Za Mguuni Mwake
Swali:
Kuna dada anauliza kama inajuzu kwake kunyoa nywele za mguuni kwa ajili
ya kujipamba?
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Tunachomnasihi aache kufanya hivyo. Kwa kuwa akishanyoa mara ya
kwanza itakuwa akijishughulisha kila wakati wake kunyoa nywele za mguu
wake. Ama kuhusiana na kuwa ni Haramu, sio Haramu. Lakini tunamnasihi
asianze kufanya hivyo, kwa kuwa asimtaabishe kunyoa.
Chanzo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=3050
34
39) Mwanamke Kuondosha Nywele Za Kwenye Kidevu, Miguuni Na
Mwilini
Swali:
Je, inajuzu kuondosha nywele zilizo kwenye mwili wa mwanamke au
miguuni mwake?
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Ama kama ni kujuzu, inajuzu. Ama kukipatikana dawa akaziondosha mara
moja, ni sawa. Ama nywele ambazo ziko miguuni mwa mwanamke sio
mbaya. Lakini nywele za kwenye kidevu, hakuna ubaya akaziondosha au
akatumia dawa ambayo itafanya zisijitokeze mara nyingine. Na kama
sikukosea nadhani ni an-Nawawiy ambaye amesema kuwa ni wajibu kwa
mwanamke kuondosha nywele za kwenye kidevu ili asijifananishe na
mwanaume. Ama nywele za kwenye miguu yake, hakuna ubaya
akaziondosha na si kama ndevu.
Chanzo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=3050
40) Mwanamke Kusafiri Na Mahram Mtoto Awezae Kupambanua
Swali:
Je, inajuzu kwa mwanamke kutoka mji kwenda mwingine akiwa pamoja na
mtoto wa kiume wa dada yake kwa ajili ya matibabu naye (mtoto huyo)
hajafikisha umri wa kuota ?
35
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Ikiwa mtoto huyo anaweza kupambanua mambo, hakuna ubaya kwa hili. Na
aghlabu ambaye kishafikisha miaka 10, 11 au 13 anakuwa ni mwenye kuweza
kupambanua. Hakuna ubaya kusafiri pamoja naye ikiwa kutaaminika fitina.
Na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema:
"Sio Halali kwa mwanamke ambaye anamwamini Allaah na siku ya Mwisho
kusafiri isipokuwa awe pamoja naye Mahram."
Chanzo: http://muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=1062
41) Mwanamke Kuvaa Mavazi Meupe
Swali:
Hadiyth ambayo imependekeza kuvaa mavazi meupe, je, ni kwa wanaume na
wanawake? Na je, ni jambo lililopendekezwa hata kwa wanaume?
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Lilio la dhahiri ni kuwa ni kwa wanaume. Kwa dalili ya Hadiyth ya ´Aaishah,
ya kwamba aliona wanawake wa Answaar wametoka kwa ajili ya Swalah ya
Fajr na walikuwa wamevaa mavazi meusi. Pamoja na haya, sio Haramu kwa
mwanamke kuvaa mavazi meupe. Jambo lililo la Haramu kwake ni
kujifananisha na wanaume. Kama ilivyokuja katika Swahiyh:
"Allaah Anamlaani mwanaume anayejifananisha na mwanamke; na
mwanamke anayejifananisha na mwanaume."
Chanzo: http://muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=650
36
42) Mwanamke Kuvaa Suwali Mbele Ya Mume Wake Na Wanawake
Wengine
Swali:
Ipi hukumu ya mwanamke kuvaa suruwali nyumbani kwake na mume wake
au mbele ya wanawake wenzake?
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Ni kujifananisha na maadui wa Uislamu. Suruwali ni kujifananisha na maadui
wa Uislamu. Na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema:
"Yule mwenye kujifananisha na watu, basi yeye ni katika wao."
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?id=6024
43) Mwanamke Mwenye Hedhi Kuingia Msikitini Kutoa Darsa Kwa
Wanawake Wenzio
Swali:
Je, inajuzu kwa mwanamke mwenye hedhi kuingia Msikitini kutoa mihadhara
kwa wanawake wenzake?
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Kumepokelewa Hadiyth kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)
amesema:
"Mimi sikuhalalisha Msikiti kwa mwenye hedhi wala janaba."
37
Lakini Hadiyth hii ni dhaifu.
Na imethibiti katika Swahiyh ya kwamba kuna mwanamke ambaye alikuwa
anafanya kazi Msikitini na analala Msikitini. Na mwanamke huyu ada yake na
tabia yake ilikuwa ni kama wanawake wengine (wanaopata hedhi). Alikuwa
anafanya kazi Msikitini na akiishi humo. Pamoja na hivyo hakuwahi (Swalla
Allaahu ´alayhi wa sallam) kumtoa wala kumkataza kutoingia humo.
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anamwambia vile vile ´Aaisha
(Radhiya Allaahu ´anha) hali ya kuwa alikuwa ni mwenye hedhi alipokuwa
katika Hajj:
"Fanya kama anayofanya mwenye kuhiji, lakini usitufu Ka´abah."
Anasema tena Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumwambia
´Aaishah pindi alipomwambia amsaidie kumpokeza kitu, akasema ´Aaishah:
"Mimi ni mwenye hedhi."
Akasema (´alayhis-Salaam):
"Hedhi yako haiko mikononi mwako."
Lililo la dhahiri ni kuwa, hakuna ubaya mwanamke mwenye hedhi kuingia
Msikitini kwa sharti asiuchafue Msikiti. Pengine akatokwa na kitu, ni lazima
ajisitiri na kitu vizuri ili asiuchafue Msikiti na awafanyie Darsa dada zake.
Chanzo: http://olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=3134
44) Mwanamke Mwenye Hedhi Na Nifasi Kushika Msahafu Na Kuingia
Msikitini
Swali:
Ipi hukumu ya mwanamke mwenye hedhi kugusa msahafu pasina kizuizi?
Na ni ipi hukumu ya mwanamke mwenye hedhi na nifasi kuingia Msikitini?
38
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Kugusa msahafu pasina kizuizi ni kwamba inajuzu kwa kukosekana dalili
sahihi zinazopinga hilo. Ama Kauli Yake (Ta´ala):
ه إل المطهرون ل يمس
"Hawaigusi isipokuwa waliotwahara." (56:79)
Makusudio hapa ni Malaika. Kama Alivyosema hilo Allaah (Subhaanahu wa
Ta´ala) katika Kitabu Chake Kitukufu:
لت به ياطين وما ينبغي لهم وما يستطيعون وما تنز الش
"Na (wala) hawakuteremka nayo (hii Qur-aan) mashaytwaan. Na (wala)
haipasi kwao (kuteremka na Qur-aan) na wala hawawezi." (26:210)
"Iliyoifasiri Aayah hii vizuri, ni Kauli nyingine ya Allaah (Subhaanahu wa
Ta´ala):
ها تذكرة فمن شاء ذكره في رة بأيدي سفرة كرام بررة كل إن طه رفوعة م مة م كر صحف م
"Sivyo katu! Hakika (hizi Aayah za Qur-aan) ni ukumbusho. Basi atakaye
akumbuke. (Zimeandikwa) Katika swahifa zilizokirimiwa (Al-Lawh Al-
Mahfuwdh). Zimetukuzwa na zimetwaharishwa. (Zinazobebwa) Katika
mikono ya (Malaika) waandishi. Watukufu (na) watiifu." (80:11-16)
Na makusudio hapa katika Aayah hii ni Malaika. Hivyo Aayah hii ya al-
Waaqi´ah makusudio ni Malaika. Na Allaah (Ta´ala) ndiye Mwenye Kujua
zaidi.
Ama mwanamke mwenye hedhi na nifasi kuingia Msikitini, sijui kama kuna
dalili yoyote katika Kitabu na Sunnah inayokataza hilo. Ama kuhusu Hadiyth:
"Mimi sikuhalalisha Msikiti kwa aliye na hedhi na janaba."
Hadiyth hii ni dhaifu.
Na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anamwambia ´Aaishah
(Radhiya Allaahu ´anha):
"Hedhi yako haiko mikononi mwako."
39
Na alimwambia tena (´alayhis-Salaam):
"Hapana! Fanya anayopasa kufanya mwenye kuhiji, isipokuwa tu usitukufu
kwenye Ka´abah."
Na katika zama za Mtume kulikowepo mwanamke ambaye anafanya kazi
Msikitini na anaishi Msikitini. Na mwanamke huyu alikuwa kishakuwa
mama, anajiwa na yanayowajia wanawake wengine. Mtume (Swalla Allaahu
´alayhi wa sallam) hakuwahi katu kumwambia:
"Unapojiwa na hedhi, toke nje (ya Msikiti)."
Hapa kuna dalili inaonesha kuwa, inajuzu kwa mwanamke kuingia Msikitini
naye yuko na hedhi au nifasi.
Chanzo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=284
45) Mwanamke Wa Kiislamu Kutumia Vipodozi "Miquillaage"
Swali:
Ipi hukumu ya vipodozi maquillage kwa mwanamke?
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Imethibiti ya kwamba ina madhara kama nilivyoona mwenyewe katika
maandiko ya kwamba inamdhuru mwanamke. Na huenda ikazeekesha uso
wake mapema. Ni Haramu hata kama itakuwa haina madhara. Na ni
kijifananisha na maadui wa Uislamu. Kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu
´alayhi wa sallam) anasema:
"Yule mwenye kujifananisha na watu, basi yeye ni katika wao."
40
Na mimi, bali hata nyie mnaamini kuwa mambo haya yalikuwa hayajulikani
mpaka yalipotujia kutoka kwa maadui wa Uislamu na tukajifananisha na
maadui wa Uislamu.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?id=6022
46) Mwanaume Na Mwanamke Wote Ni Sunnah Kutahiriwa
Swali:
Ipi hukumu ya mwanamke kutahiriwa katika Uislamu?
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Ni Sunnah ya kimaumbile. Na miongoni mwayo akatata kutahiriwa. Na hili ni
kwa wote wawili mwanaume na mwanamke.
Chanzo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=1463
47) Nasaha Za Shaykh Muqbil Kwa Mume Na Mke Ambao Ni Wanafunzi
Swali:
Ni katika mpaka upi ambao ni wajibu kwa mwanamke kumtii mume wake?
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
41
Ama masuala ya wajibu, anatakiwa kumtii katika yale mambo ambayo Allaah
Kamuwajibishia juu yake. Miongoni mwayo, ni pale ambapo atamwita
kitandani. Na ikiwa mume ni fakiri, inatakikana kwa mwanamke awe na
subira kwake kadiri na atakavyoweza.
Pamoja na hivyo, kuna jambo ambalo ni pana zaidi kuliko uwajibu huu. Na
jambo hilo sisi tunamnasihi amvumilie mume wake katika raha na shida,
asimkalifishe mume kwa asiyoyaweza na kununua mambo mapya. Akiona
gari na nguo mpya, anamuomba mume wake amnunulie mfano wa gari hii na
nguo hiyo. Inatakikana kwake awe na subira na mume wake, amtendee
wema, kuwalea watoto wake, amfulie nguo zake, amsaidie katika kheri na
amtengenezee chakula kizuri pale itapohitajika kufanya hivyo. Wawe ni
wenye kusaidizana na khaswa pale ambapo nyinyi nyote ni wanafunzi
wanaume na wanawake. Muda unaweza kuwa mfinyu kwa mwanamke na
hilo likasababisha akawa na mapungufu katika baadhi ya haki za mume wake.
Katika hali hii, inatakikana mume kuwa na subira kwa mke wake. Na muda
unaweza kuwa mfinyu kwa mume na akawa na mapungufu katika baadhi ya
haki za mke wake. Katika hali hii, inatakikana mke kuwa na subira kwa mume
wake.
Chanzo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=1733
48) Ni Wajibu Kwa Mwanamke Kuvaa Vifuniko Vya Mikoni (Gloves)
Swali:
Ipi hukumu ya vifuniko vya mikono (gloves) pindi mwanamke anapotoka
nyumbani?
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Ndio, tumeshatangulia kusema ya kuwa ni wajibu kwake kuufunika mwili
wake wote. Na Mtume (Swalla Allaahu ´alayh wa sallam) anasema:
42
"Mwanamke ni ´Awrah (uchi), Pindi anapotoka nje, matumaini ya Shaytwaan
huongezeka."
Huenda mwanaume akafitinishwa na mwanamke vile vile akafitinishwa,
kama livyosema mshairi ya kwamba chanzo cha yote ni mtazamo... Wajibu
kwa mwanamke ni yeye awe amejisitiri, na akiweza kubaki nyumbani ni bora
kwake. Uislamu umekuja kumhifadhia heshima yake, damu yake na mali
yake. Lakini Waislamu wengi leo, wao ndio ambao wamepuuza mafunzo
haya yenye baraka.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/default_ar.aspx?id=2972
49) Ni Wajibu Kwangu Mke Kumhudumia Mama Wa Mume Wangu?
Swali:
Kuna dada ambaye analazimishwa na mume wake kumhudumia mama yake,
pamoja na kuwa mwanamke huyo - yaani mama wa mume wake -
husababisha matatizo baina ya wanandoa. Na sasa dada muulizaji hawezi
kustahamili zaidi ya hayo. Afanye nini?
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Allaah Awajaze kheri kwa Da´wah na hima mnayoifanya juu ya Uislamu. Na
Allaah Awabariki kwa juhudi zenu na Allaah Aunufaishe Uislamu na
Waislamu kupitia kwenu. Ama kuhusiana kama ni wajibu, sio wajibu kwa
mwanamke huyu kumhudumia mama wa mume wake, khususan ikiwa
anaamiliana naye mu´amala mbaya. Ama nasaha zetu, tunamnasihi azidi
kusubiri zaidi na zaidi na zaidi ya alivyosubiri. Hakika ya Allaah (´Azza wa
Jalla) Anasema katika Kitabu Chake Kitukufu:
Hakika ya Allaah (´Azza wa Jalla) Anasema katika Kitabu Chake Kitukufu:
قوى ول تعاونوا على الثم والعدوان وتعاونوا على البر والت
43
"Shirikianeni katika wema na taqwa, na wala msishirikiane katika dhambi na
uadui." (05:02)
Pengine hayo (ya kutomhudumia) yakapelekea katika mfarakano na matatizo
baina ya mume na mke. Tunamnasihi, kwa njia ya nasaha na si kwa njia ya
uwajibu, amvumilie na asaidiane nae na amhudumie kwa mipaka
atakayoweza. Ama kuhusiana kama ni wajibu, sio wajibu kwake. Ni juu ya
mwanamke asimame kwa kufanya yale atakayoweza katika kazi za
nyumbani. Kama ilivyo katika Swahiyh, hakika ya Mtume (Swalla Allaahu
´alayhi wa sallam), wakati Faatwimah alipoja na kumshtakia uzito anaoupata
kutokana na kazi za nyumbani. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)
hakumwambia kuwa huu sio wajibu wako. Kinachotakikana na
tunachomnasihi awe na ustahamivu na asaidiane na mume wake.
Chanzo: http://muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=242
50) Ole Wako Mume Kumwacha Mke Wako Kwenda Kwa Wanawake
Hizbiyaat
Swali:
Je, inajuzu kwa mwanamke ambaye ameolewa kwenda katika mihadhara na
Darsa bila ya idhini ya mume pamoja na kujua kuwa mume wake
anamkataza?
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Haijuzu kwake kwenda. Lakini ikiwa ni mwanaume mwema na ashukuru
(afurahi) kwa hili. Tunamnasihi mwanaume huyu amchukue na kumpelekea
katika nyumba ambayo kunafanywa mihadhara na kwenda nae baada ya
kumalizika kwamuhadhara. Haijuzu kwake mume kumkataza ilihali naye
hamfunzi. Ole wako, ole wako kwenda na mke wako kwa wanawake
44
Hizbiyaat! Utarudi ukute yeye yuko upande huu na wewe uko upande
mwingine.
Chanzo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=1524
51) Shaykh Muqbil al-Waadi´iy Kuhusu Uke Wenza
Swali:
Tunaoma kalima kwa wanaume na wanawake kuhusu ukewenza?
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Hili ni jambo muhimu enyi ndugu zetu.
ن الن ساء مثنى وثلث ورباع فإن خفتم أل تعدلوا فواحدة فانكحوا ما طاب لكم م
"Basi oeni waliokupendezeni katika wanawake; wawili au watatu au wanne.
Mkikhofu kuwa hamtoweza kufanya uadilifu, basi (oeni) mmoja." (04:03)
Hapa ni pale ambapo mwanaume anaimania nafsi yake ya kuwa atafanya
uadilifu. Hili ni jambo la kwanza. Jambo lingine awe yuko na uwezo. Ama
hali yake ikiwa ni ile ya watoto wako ni wagonjwa na amekosa hata pesa za
matibabu, kisha baada ya hapo anataka kuoa mke wapili, watatu au wanne
naye isitoshe ni mwanafunzi, hili litamshughulisha enyi ndugu. Allaah
Akimfungulia milango ya riziki na akamrahisishia njia ya mali, hakuna ubaya
akafanya hivyo bali tunamnasihi kufanya hivyo. Hali kadhalika, awe ni
mwenye kujiaminia nafsi yake ya kutomili kwa mwanamke mmoja. Na wala
haijuzu kwa mwanaume wala mwanaume kuharamisha Aliyohalalisha Allaah
(Ta´ala).
Lakini inatakikana kama tulivyotangulia kusema, ajilazimishe kufanya
uadilifu na awe na uwezo wa kuongeza mke wapili, watatu au wanne. Na
tunamuomba Allaah (Ta´ala) Awawekee wepesi ndugu zetu ambao hawajaoa.
45
Tunamuomba Allaah Awawekee wepesi. Na ni kweli ya kuwa, kuna
wanawake Sunniy Dammaaj na nje ya Dammaaj na wanatamani kuolewa na
watafutaji elimu katika Ahl-us-Sunnah. Lakini pengine mama yake akawa
amtenza ndugu na kumwambia:
"Mume wa msichana wangu hatokuwa na mke isipokuwa mmoja tu. Atakuwa
na gari, makumbusho (museum) n.k."
Pengine wazazi wa msichana huyu wakawa wanamshaji´isha katika hili na
wakamwambia mwanafunzi aliyekuja kuchumbia: "Tunasikitika! Tumempa
fulani kwa utajiri wake na wewe umekosa kwa ajili wewe ni mwanafunzi."
Masikini, huenda mwanafunzi huyu hana lolote zaidi ya kilemba chake,
kanzu yake na suruwali yake. Wapi atatoa pesa zote hizi? Tunachowanasihi
ndugu zetu wasaidizane na ndugu zao ili kutengeneza familia njema na yenye
Imani. Na ni juu yako mzazi kumchagulia msichana wako mwanaume
mwema, akimpenda atamkirimu na akifikia kumchukia hatomdhulumu.
Chanzo: http://muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=2632
52) Udugu Wa Kunyonya Wa Watoto Wa Mama Tofauti
Swali:
Mwanamke ana watoto wanne ambao kila mmoja ana mama yake. Na yule
anayemnyonyesha ndio mtoto wake. Je, watoto hawa wawili huzingatiwa
kuwa ni ndugu wa kunyonya pamoja na kutofautiana kwa mama zao?
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Ndio. Huzingatiwa kuwa ni ndugu wa kunyonya hata kama kila mmoja ana
mama yake.
46
Chanzo: http://muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=12
53) Wamezini Katika Hali Ya Uchumba, Wanapigwa Mawe Au Wanauawa?
Swali:
Kuna mwanaume alichumbia mwanamke na alikuwa hajazini nae na baadae
kukatokea Zinaa katika kipindi hichi (cha uchumba). Je, asimamishiwe
adhabu ya bikira au adhahabu ya ambaye kishaingia katika ndoa?
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Lililo la dhahiri kwangu naona kuwa atasimamishiwa adhabu ya bikira. Kwa
kuwa alikuwa hajamuoa. Katika hali hii, wote wawili watasimamishiwa
adhabu ya bikira ikiwa ndo mara ya kwanza wanaingia katika ndoa.
Chanzo: http://muqbel.net/fatwa.php
54) Yupi Bora Kati Ya Wanawake Hawa Wawili?
Swali:
Ikiwa mwanamke anapenda kubaki nyumbani kwake na anaona ni bora
kubaki humo na hatoki hata kwenda Msikitini. Na mwanamke mwingine
ambaye anatoka kwenda kutafuta elimu na kwenda Msikitini. Yupi bora kati
ya hawa wawili?
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
47
Mwanamke ambaye anapenda kubaki kwake na kusoma nyumbani kwake
ndio bora. Kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema:
"Msiwazuia waja wa Allaah kwenda kwenye Misikiti ya Allaah. Na nyumba
zao ni bora kwao."
Chanzo: http://muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=557
Swalah na salaam ziwe juu ya Mtume wetu Muhammad, ahli zake na
Maswahabaha zake wote.