first page ilo.fm

178
MUHTASARI WA RIPOTI ya mradi wa utafiti uliofanywa na Shirika la Leba la kimataifa (ILO) na Tume ya Afrika ya kushughulikia haki za Kibinadamu na Haki za Watu, kuhusu ulinzi wa kikatiba na kisheria wa haki za watu wa kiasili katika mataifa 24 ya Afrika

Upload: haanh

Post on 29-Jan-2017

1.066 views

Category:

Documents


15 download

TRANSCRIPT

Page 1: First page ILO.fm

MUHTASARI WA RIPOTI

ya mradi wa utafiti uliofanywa na

Shirika la Leba la kimataifa (ILO)

na Tume ya Afrika ya

kushughulikia haki za Kibinadamu

na Haki za Watu, kuhusu ulinzi wa

kikatiba na kisheria wa

haki za watu wa kiasili katika

mataifa 24 ya Afrika

Page 2: First page ILO.fm

© Haki miliki 2009, Shirika la Kimataifa la Leba na Tume ya Afrika yaKutetea haki za kibinadamu na watu. Chapa ya kwanza mwaka wa 2009

Ili kupata haki ya kuchapisha tena au kutafsiri, lazima kupata idhini kutokakwa ILO publications (Haki na idhini), Ofisi ya Kimataifa ya Leba, CH-1211 Geneva 22, Uswizi au kwa barua pepe; [email protected] , na Kituocha Habari na Stakabadhi, Tume ya Afrika kuhusu Haki za kibinadamu naHaki za watu S.L.P 673, Banjul, Gambia, au kwa barua pepe:[email protected] <barua kwa: [email protected]>.

ILO/ACHPR Muhtasari wa ripo ya utafiti uliofanywa na shirika la Leba laKimataifa na Tume ya Afrika kuhusu Haki za Kibinadamu na Haki zaWatu kuhusu ulinzi wa kikatiba na kisheria wa haki za watu wa kiasilikatika mataifa 24 ya Afrika / Ofisi ya Leba ya kimataifa. – Geneva, ILO,2009 xv   155 p.

ISBN: 978-92-2-122512-6 (chapa) ISBN: 978-92-2-122513-3 (web pdf)

Watu wa kiasili / haki za kijamii na kiuchumi / haki za kitamaduni / sheriaya kimataifa / sheria ya katiba / uundaji wa sheria / maoni / matumizi /Afrika 14.08

Pia inapatikana kwa Kifaransa: Aperçu du Rapport du Projet de Recherche par l'Organisation Internationale duTravail et la Commission Africaine des Droits de l'Homme et des Peuples relatifà la protection constitutionnelle et législative des droits des peuples autochtonesdans 24 pays africains (ISBN 978-92-2-222512-5), Geneva, 2009 kwaKiarabu:

(ISBN 978-92-2-622512-1), Geneva, 2009.

Uteuzi uliotumika katika chapisho hili na uwasilishaji wa yaliyomo,haudhihirishi maoni yawayo yoyote kwa upande wa Ofisi ya Leba yakimataifa na Tume ya Afrika Kuhusu Haki za Kibinadamu na Haki za Watujuu hadhi ya kisheria ya nchi yoyote, eneo au himaya wala serikali zake aukuhusu uwekaji wa mipaka yake.

ILO pamoja na Tume ya Afrika Kuhusu Haki za Kibinadamu na Haki zaWatu haitawajibika kwa hitilafu, kasoro, au kosa lolote linalotokana nakutumia data hii.

Ilichapihswa katika Jamuhuri ya Afrika Kusini.

Page 3: First page ILO.fm

iii

DIBAJI

Wakati Tume ya Afrika ya kushughulikia haki zakibinadamu na haki za watu (ACHPR) (Tume yaAfrika) ilipoanzishwa zaidi ya miongo miwiliiliyopita, swala na dhana yenyewe ya watu wakiasili barani Afrika haikutiliwa maanani. Kwahakika, ilikuwa hivyo hadi mwaka wa 1999 ndiposuala la haki za watu wa kiasili lilitokeza kwa maraya kwanza katika ajenda za Tume ya Afrika. Hukukuonekana kukosa nia hakukuwa kwa makusudibali kulikuwa ni kielelezo cha mwelekeo,mtazamo au uelewa wa umma kwa jumla na ulewa wa viongozi wa Afrika kuhusu suala la watuwa kiasili barani. Huku kuonekana kukosa habarina maandishi ya kutosha kuhusu watu wa kiasilipamoja na pingamizi kali kutoka kwa Mataifa yaAfrika katika kukubali wazo hili barani,kulimaanisha kwamba Mashirika yasiyo yakiserikali Afrika hayakuwa na nafasi kujielezakikamilifu kuhusiana na suala hili.

Tume ya Afrika iliangaliwa na mashirika yaumma barani kama baraza mwafaka la kuwasilishamasaibu ya watu asili. Kwa hivyo, kwa takribanivikao vyake vine, Tume ya Afrika ilikumbushwakila mara na mashirika yasiyo ya kiserikali yaAfrika na ya ulimwengu kuhusu masaibu ya watuwa kiasili barani, walio na wasifu wakupembezwa, kunyonywa na kunyang’anywa mali,kunyanyaswa , umasikini, kutojua kusoma nakuandika n.k. Tume ya Afrika haingeweza tenakupuuza masaibu yanayowakumba watu asilibarani na hivyo ikaamua kuunda Kamati Teulekushughulikia haki za watu wa kiasili, pamoja namengineyo, kuchunguza dhana ya watu/ jamii asilibarani Afrika.

Baada ya miaka miwili ya utafiti, mnamomwaka wa 2003 tume ya Afrika ilitumia ripoti yaKamati hiyo teule katika stakabadhi iliyoitwaRipoti ya Kamati Teule ya Wataalamu wa Tume yaAfrika Kuhusu watu/ jamii za kiasili katika Afrika.Ripoti hii imedumu kwa muda murefu naikatumikia hadhira za kitaifa, kimaeneo nakimataifa katika nyanja ya haki asili, yakiwemomashirika ya wanafunzi, wahadhiri, watafiti,wafanyikazi wa huduma za jamii, wanaharakati wakutetea na kulinda haki za kibinadamu, Umoja waAfrika pamoja na Shirika la Umoja wa Mtaifa.

Mojawapo ya mapendekezo ya kamatihiyo teule lilikuwa ni kuanzisha kamati ya kudumuinayoshughulikia watu/jamii asili katika Afrika

(Kamati Teule ya Tume ya Afrika), itakayohusishawanachama wa Tume na wataalamu huru ilikufanya uchunguzi na utafiti kuhusu masuala yawatu asili barani, kati ya majukumu mengineyo.Tangu kuanzishwa kwake mnamo mwaka wa2003, Kamati Teule ya Tume ya Afrika imefanyaziara katika mataifa manne, Namibia, Botswana,Niger na Burkina Faso, na ziara sita za utafiti nahabari katika nchi ya Kongo, Burundi, Uganda,Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Gabon na Libya. Ziarahizi zimedokeza kwamba, huku kukiwa namaendeleo ya polepole katika jinsi kuwachukuliawatu asili katika baadhi ya nchi, hali katika nchinyingine ingali ile ile ya kuzua wasiwasi. Aidhazinadokeza hitaji la kuwepo kwa jitihada zapamoja ili kuwahushisha washikadau wote ilikutafuta mbinu za kusaidia kuendeleza na kulindahaki za watu wa kiasili barani.

Ni katika misingi hii ndipo Shirika la Lebala kimataifa (ILO) likishirikiana na Tume yaAfrika, kupitia kwa Kituo cha kutetea Haki zaKibinadamu cha Chuo Kikuu cha Pretoria-nchiniAfrika Kusini- kama taasisi ya utekelezaji, liliamuakufanya utafiti wa kina zaidi, hususan likitiliamaanani vipengele vya kikatiba, kisheria na vyakiutawala vinavyohusikana na watu asili katikamataifa 24, kwa kusudi la kulinganisha nakubadilishana kaida zilizo bora. Uchunguzi huuuliopewa mada, Muhtasari wa Ripoti ya mradi wautafiti uliofanywa na ILO na Tume ya Afrika kuhusuulinzi wa kikatiba na kisheria wa haki za watu waasili katika mataifa 24 ya Afrika, miaka mitatu naulihusisha watafiti wa kudumu waliofanya utafitiwa kikao pamoja na utafiti nyanjani. Matokeoyake yalithibitishwa kwenye warsha iliyofanyikaMei 2009, kabla ya Kikao cha Kawaida cha 45chaTume ya Afrika ambapo wengi wa watafiti,wawakilishi kutoka ILO, wanachama wa Tume yaAfrika, Taasisi ya utekelezaji- kituo cha Haki zaKibinadamu- pamoja na washikadau wenginewalihudhuria. Baadaye, uchunguzi huu ulijadiliwana kukubaliwa na Tume katika Kikao chake chakawaida cha 45.

Kamishna Musa Ngary BitayeMwenyekiti, Kamati Teule ya Tume ya Afrikakuhusu Haki za Watu / Jamii za Kiasili BaraniAfrika (WGIP)

Page 4: First page ILO.fm
Page 5: First page ILO.fm

MUHTASARI RASMI

A Utangulizi

Kote ulimwenguni, watu wa kiasili wanakumbwana unyanyasaji kama vile kunyang’anywa ardhi naraslimali za kihistoria na kulazimishwa kufuatadesturi za makundi makubwa. Watu asili baraniAfrika wanakumbana na changamoto hata kubwazaidi kutokana na hali kwamba mataifa ya Afrikahayajataka kutambua kuwepo kwa makundi yawatu wa kiasili katika himaya zao.

Ripoti hii inatoa matokeo ya mradi wautafiti uliofanywa na Shirika la Leba la Kimataifa(ILO) na Kamati teule ya Tume ya Afrika yakushughulikia haki za watu /jamii za kiasili katikaAfrika (kamati teule ya Tume ya Afrika), pamojana Kituo cha Kutetea haki za Kibinadamu (CHR)-Chuo Kikuu cha Pretoria kikifanya kazi kamataasisi ya utekelezaji. Mradi huu ulichunguzakiwango kilichofikiwa na mifumo ya kisheria yamataifa 24 yaliyoteuliwa katika kuathiri na kulindahaki za watu asili. Malengo makuu ya mradi huuyalikita kuwili: kwanza, kuchangia katikakuendeleza sera na mifumo ya kisheria inayofaakatika kulinda haki za watu wa kiasili. Pili nikujenga uwezo na kuinua kiwango cha ufahamuwa wahusika muhimu baina ya watu asili na taasisiza kiserikali ili kuimariha uendelezaji na ulinzi wahaki za watu asili katika mataifa ya Afrika. Ainambili za uchunguzi zilifanywa kama sehemu yautafiti, yaani; utafiti wa kikao na utafiti nyanjani.Mataifa ishirini na manne yalichunguzwa katikautafiti huu na tafiti kumi nyanjani zilifanywa.Mataifa haya yaliteuliwa kulingana na vigezovilivyojadiliwa na kuafikiwa katika warsha yauzinduzi wa mradi mjini Yaounde mwaka wa2006. Nakala kamili meme za ripoti hizi, ripoti yamaoni na stakabadhi za msingi za kisheriakuhusiana na watu asili zimo katika databenkiiliyoundwa kama sehemu ya utafiti.(www.chr.up.ac.za/indigenous)

Elementi tatu zilitumika sana katikakutambulisha watu wa kiasili katika utafiti huu.Nazo ni; kiwango kikubwa cha upembezwajiunaowakumba, kujibainisha wenyewe pamoja nautegemezi wao kwenye mashamba ili kujikimukwa pamoja kama watu. Ripoti hii inahitimishakwamba ni ukweli usiokanika kwamba watu asiliwapo katika mataifa mengi ya Afrika na katikamaeneo yote barani.

Kupitia kwa Mkataba wa 169 wa ILO,pamoja na Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusuHaki za Watu wa Kiasili (UNDRIP), sheria yakimataifa kuhusu haki za kibinadamu inatoaviwango muhimu kuhusiana na haki za watu asili.Hata hivyo, hakuna nchi yoyote ya Afrika ambayoimetia sahihi Mkataba wa 169 wa ILO, na walaUNDRIP sio chombo cha lazima kwao.Ijapokuwa hivyo, mataifa ya Afrika ni wanachamawa vyombo vingi vya kimataifa ambavyo nimuhimu sana kwa watu wa kiasili. Hivi ni kama;Mapatano ya Kimataifa kuhusu Haki za Kiraia nakisiasa (ICCPR), Mapatano ya kimataifa kuhusuHaki za Kiuchumi, Kijamii na Kitamaduni(ICESCR), Mkataba wa kukomesha aina zote zaUbaguzi wa kimbari (CERD), Mkataba waKukomesha aina zote za Ubaguzi Dhidhi yaWanawake (CEDAW), Mkataba wa Haki zaMtoto (CRC) na Mkataba kuhusu Watu waKiasili na wa Makabila, mwaka1957 (mkataba wa107) na mkataba wa 111 (1958) wa ILO kuhusuUbaguzi (wa ajira na kazi). Mashirikayanayofuatilia mikataba hii imeendelea kufanyamasilahi ya watu wa ki asili kuwa sehemu ya mojakwa moja ya majukumu yao. Hasa, maoni yakuhitimisha ya hivi karibuni yaliyokubaliwa baadaya kuzichunguza ripoti za Mataifa, yanatoamapendekezo muhimu yanayohusiana na watuwa kiasili katika mataifa ya Afrika.

Kwenye kiwango cha kimaeneo,kuhusishwa kwa ‘watu wa kiasili’ katika Mkatabawa Afrika kuhusu Haki za Kibinadamu na Haki zaWatu (makataba wa Afrika), ambao umetiwasahihi na mataifa yote ya Afrika isipokuwaMoroko, kunatumika kama msingi wa kuhusishawatu asili katika mawanda yake ya ulinzi. Tume yaAfrika Kuhusu Haki za Kibinadamu na Watu(Tume ya Afrika) iliunda Kamati Teule yaWataalamu kuhusu Watu/Jamii Asilikushughulikia suala hilo. Kwa kukubali ripoti yaKamati yake Teule, Tume ya Afrika imekubalikwamba watu asili wapo katika mataifa mengi yaAfrika na kwamba wana haki ya kulindwa chini yaMkataba wa Afrika

Hata hivyo, kutokana na kutoibinafsisha nakufuatilia sheria ya kimataifa, athari zake katikanchi mblimbli binafsi zimebaki finyu.

v

Page 6: First page ILO.fm

B Muhtasari wa matokeo yautafiti

Muhtasari wa jumla

Mbali na vighairi vichache vinavyowezakuonekana, kama elementi fulani katika Katiba zaAfrika Kusini na rasimu ya sheria nchini Kongo,mataifa bado hayajakubali kirasmi kuwepokisheria kwa watu wa kiasili. Sababu mahususi zakuwepo kwa ulegevu huu wa kutambua kuwepokwa watu asili zinatofautiana kutoka taifa mojahadi lingine, lakini kwa usawa zinahusiana nalengo la kutotaka kudhoofisha ujenzi wa taifa nakudumisha umoja wa kitaifa katika jamii zamakabila mengi zilizo na wasifu wa kushindaniaraslimali chache. Tokeo muhimu la kukana hukuni kwamba rekodi za serikali kama sensa yakitaifa, hazidhihirishi kuwepo kwa makabila nalugha mbalimbali, wakiwemo watu asili, katikanchi hiyo.

Hata hivyo mifumo ya kisheria ya mataifamengi ina vipengele kadhaa vya kisheria ambavyovinaweza kuwa kama vyanzo vya ulinzi wakutosha wa haki za watu asili. Mataifa yote yanavipengele kadhaa vya kisheria, sera na mipangoambavyo vinaweza kutumiwa kulinda nakuendeleza hali za watu wa kiasili. Hilihalijafanywa kikamilifu, kwa kiasi fulani kutokanana vizuizi vinavyozuia uwezekano wa watu wakiasili kupata haki, na kwa kiasi kwa sababumaafisa wa serikali pamoja na washirikadauwengineo hawajaelimishwa kuhusu masaibu yawatu asili. Vivyo hivyo, majukumu na kaida zataasisi za kitaifa kama vile Taasisi za kitaifa zakupigania haki za kibinadamu, ofisi ya Mrajisi naya upatanishi hazijarekebishwa ili kuhusishauwakilishi na mahitaji ya watu asili. Hizi pamojana taasisi nyinginezo zina uwezo wa kushughulikiamasuala ya watu asili, kama ambavyo Tume yakutetea Haki za Binadamu nchini Kenya imefanya.Ni taasisi chache tu za kitaifa zimeanzishwakushughulikia masuala mahususi ya hali za watuwa kiasili

Huku ikiwa ni sahihi kwamba sheria nasera za baadhi ya mataifa zinarejelea hali na hakiza jamii nyonge na zilizopembezwa, baadhi yamatakwa mahususi ya watu asilia yanawezakupuuzwa iwapo tahadhari haitachukuliwa ilikuyashughulikia kimahususi katika muktadha huu,badala ya kuyashulikia kama matakwa ya sehemuya kundi pana lililo na mahitaji na changamototofauti.

Huku utafiti huu ukiwa umetilia maananimajukumu ya mataifa, lazima isisitizwe kwambawashirika wasio wa kiserikali pia wana sehemuyao katika kutumia utawaala wa kisheria uliopokufaidi watu asilia, kubadilisha sheria, sera nautekelezaji, ili kuenda sambamba na mahitajimaalum ya watu asilia. Mfano wa shirika lisilo lakiserikali ambalo limetoa mchango kama huu ni;Kamati Teule ya Watu wa Kiasili waliowachachekusini mwa Afrika (WIMSA) la nchini Namibia..

Jamii asili zenyewe zimeonyesha umuhimuwa kuungana na kutangaza mahitaji yaohadharani. Wakati mwingine kumekuwepo faidakubwa zinazofuatia vipindi au matukio ya maasi yaumma na malalamiko yanayofanywa na watu wamakundi haya asilia. Matokeo kina kabisa ya ripotihii yamejadiliwa chini ya mada kumi na mojatofauti, kila moja wapo ikishughulikia kipengelekimoja kuhusiana na mahitaji maalum ya watuasili.

1 Kukubaliwa na kutambuliwa.

Kuna vipengele rasmi vichache sana vya kikatibaau vya kisheria kuhusu watu wa kiasili katikasheria za mataifa ya Kiafrika. Matumizi ya ainaainati za istilahi katika sheria na sera za kiafrikakuwarejelea watu wa kiasili, hayalingani. Hatahivyo kuna baadhi ya mataifa ambayo yameanzakukubali upekee na mahitaji mahsusi ya watu wakiasili na kuunda sheria na kujenga sera namifumo inayolenga makundi haya mahsusi.

Ijapokuwa istilahi “watu wa kiasili”haitumiki kirasmi katika sheria za kitaifa katikanchi zilizotafitiwa, mwelekeo chanya unawezakuonekana katika nchi nyingi za kiafrikazinazoendelea. Sheria kama hizi, sera na mipango,ingali ya kidharura na katika hali zotezilizochunguzwa, haitoi mpangilio wowotemwafaka wa kuwatambua na kuwakubali watuasilia na kulinda haki zao katika mawanda yakekama zinavyotambulika katika sheria za kimataifa.Ijapokuwa hivyo, hii ni hatua ya taratibu yakukubali ukweli kwamba katika jamii nyingi zakiafrika pana makukundi maalum ambayo yamokatika hali ya kudhalilishwa au kupembezwa, nakwamba makundi haya yanahitaji mikakatimaalumu ili kuweza kufaidika kutokana na haki zakibinafsi ambazo zinatolewa kiswa kwa ummamzima. Takriban katika hali zote, kuna ukosefuwa vigezo vinavyotumiwa kutambua makundiyanayorejelewa kwa kiasi kipana sana chamisamiati inayotumiwa kutaja watu asilia katikavyombo vya kisheria na sera. Kighari kimojawapo

vi

Page 7: First page ILO.fm

ni rasimu ya sheria haki za watu asilia nchiniKongo

2 Kutobaguliwa

Mojawapo ya matakwa ya kimsingi ya watu wakiasili ni kutobaguliwa kwa haki zao. Mataifamengi yanahukumika kila mara kwa ubaguzi waokatika kutekeleza haki za kitamaduni za watu wakiasili na katika ugavi wa raslimali. Hali ambayohusababisha wao kukosa kupata ardhi, huduma zaafya na elimu. Pengine chanzo cha ubaguzi huu siserikali hasa, lakini inaweza pia kuwa watu binafsina makundi ya watu. Watu wa jamii asiliaaghalabu hukumbwa na ubaguzi kutokana nashutuma na mitazamo hasi ya kijami. Mataifa badoyana jukumu la kuchukua hatua za kulinda haki zawatu asilia, kwa mfano sheria inayopinga ubaguziili kutilia ging’izomajukumu yao ya kulinda haki zawananchi wake wote. Ingawa baadhi ya mataifayanatumia sheria kama hizi, bado sheria hizohazilengi hasa kulinda haki za watu asilia.

Licha ya athari hasi za ubaguzi uliokithirina wa muda mrefu dhidi ya watu wa kiasili,hakuna taifa ambalo limechukua hatua maalumkurekebisha hali hii mbaya. Pale ambapo hatuamaalum zimechukuliwa kukabiliana na ubaguzi,mara nyingi huwa zinalenga makundi Fulani katikaumma kwa jumla, lakini ni nadra sana zikalengawatu asilia. Aidha, nyingi ya hatua hizi huwa ni zadharura tu na wala haziwakilishi hatua pana zakisera. Hata hivyo zinaweza kuwakilisha misingiambayo kwayo, haki za watu wa kiasili zinawezakulindwa au kutalii njia za kuboresha na kupangavizuri mikakati iliyopo.

3 Kujitawala, mashauriano naKushirikishwa

Kuna mifumo kadhaa ya kisheria katika kanda yaAfrika ambayo inatoa nafasi kwa umma mzima aumakundi maalum ya watu, yakiwemo makundiyaliyopembezwa, kushiriki na kufanyamashauriano. Ijapokuwa ni michache tu kati yamifumo hii ambayo hutoa fursa hususan kwawatu wa kiasili, baadhi inaweza kutumiwa kamamisingi kuendeleza kushirikishwa kwa watu wakiasilia katika kuunda sera. Pale ambapo kunasheria zinazotoa nafasi kwa watu wa kiaasili,huwa zinahusiana tu na hali fulani mahsusi. Maranyingi haipo mikakati kabisa na aghalabu hatuazaidi hazichukuliwi kukabiliana na ugumuwalionao watu wa kiasili katika kutumia haki hizo.Licha ya kwamba mataifa mengi ya Afrika yanavipengele vya haki za wananchi wote kupiga kura,

kwa jumla sheria hizo hazizingatii hali kwambamasharti ambayo ni lazima yakatimizwe na watubinafsi ili kupiga kura ni magumu sana kuafikiwahasa na watu asili. Mfano, ukosefu wa stakabadhiza uraia.

Kwa upande wa kujitawala, baadhi yamifumo ya kisheia inatoa fursa ya kushirikishwa.Katika maeneo ya misitu katika Afrika ya kati,sheria hazitoi kibali cha utumizi na usimamizi waraslimali kwa jamii wenyeji. Hata hivyo, halikwamba vijiji asilia havitambuliki kivyao kama“jamii wenyeji” bali kama vijisehemu vya vijijijirani, inamaanisha kwamba watu asilia wanaugumu zaidi katika kudai haki zao za ardhi namali-asili kama watu. Katika nchi nyingi zaKiafrika, sheria inatambua sheria za kimila namachifu au mamlaka za kitamaduni. Hii ni nafasimuhimu sana ya kushirikishwa kwa watu asiliapamoja na wawakilishi wao katika kufanyamaamuzi. Mikakati ya kushirikishwa kama huku nihafifu na mara nyingi haifai kwa kuhusishwakikamilifu kwa watu asilia katika kuunda,kutekeleza na kuiangalia mikakati kama hii.

4 Kupata haki

Ili kupata haki, inahitajika kwamba pana mawakiliwa kuwasaidia watu wanaowahitaji, kwambakorti hazipo mbali na haziwezi kufikiwa ilikutumiwa na kwamba lugha ya kisheriainaeleweka na watu wanaohitaji kutegemeasheria. Ingawa ufikiwaji wa sheria na watu wengiwanaoishi katika nchi za Afrika ni finyu mno,shida zinazonga umma kwa jumla zinafanywakubwa zaidi kwa watu asilia. Korti pamoja namabaraza mengine ya kisheria aghalabu huwakatika maeneo yasiyofikika, kwa sababu wanaishimashambani au watu hawa huishi maisha yakuhamahama. Kutokana na viwango vilivyokithirivya umasikini na kukosa elimu baina yao, watuasili hawana uwezo wa kugharamia huduma zakisheria au hata kufahamu haki na uwezekano wakupata msaada wa kisheria- iwapo vipo.Kutambulika kwa sheria ya kimila ya wabantukama aina moja ya mfumo wa kitamaduniuliotambulika kumemomonyoa zaidi uwezo wakupata haki kwa watu asili. Kando na vighairivichache tu kama korti tamba kwa baadhi ya jamiiasili nchini Afrika Kusini, mataifa mengihayajachukua hatua kushughulikia suala hili.

5 Utamaduni na lugha

Kulindwa kwa utamaduni na lugha yao ya kipekeeni suala muhimu sana kwa kuendelea kuwepo

vii

Page 8: First page ILO.fm

kwa watu wa kiasili. Kwa makundi haya, lugha nautamaduni aghalabu vinategemeana nahaviwezitenganishwa. Mataifa hayajatilia maananisana thamani wanayoweka kwenye udumishaji wautamaduni kama arki muhimu ya kujitambulishakwao. Mataifa yote yaliyochunguzwa yanathaminisana umoja wa kitaifa kuliko uwingi wautamaduni, licha ya majuumu yao ya kitaifa nakimataifa. Vivyo hivyo, lugha asili hazijatambulikakirasmi na hivyo hazitumiki katika vyombo vyahabari vya serikali na shule. Na kutokana na haya,baadhi ya lugha asili zimepotea tu na nyinginezokama Kitamazi (Tamazight) na Khoi zinazongwamno. Hali hii si mbaya kwa urithi wa kitaifa nauanuwai wa utamaduni lakini pia hupelekeakuangamizwa kwa makundi hayo asili yenyewe.Utafiti huu uligundua kuwa kutotekelezwa kwasheria, sera na udhamini wa kikatiba pia ni hali yakawaida katika mataifa mengi.

Baadhi ya mataifa (hususan Jamuhuri yaKidemokrasia ya Kongo (DRC) na Gabon)yamechukua hatua za kupamabana na hali hii yamambo, zikiwemo hatua za kikatiba, kisheria nakisera. Vilevile mataifa yameunda katiba mpyakushughulikia masuala ya utamaduni wa watuasili. Mifano ni kama Tume ya Kudumisha naKulinda haki za Jamii za Kitamaduni, Kidini naKilugha, ya Afrika Kusini, Ubalozi wa Wa-amazighnchini Algeria na Taasisi ya kifalme ya utamaduniwa Wa- amazigh nchini Morocco (Royal institutefor Amazigh – IRCAM).

6 Elimu

Elimu ni muhimu sana kwa watu wa kiasilikujiendeleza wenyewe na kuwapa uwezo wakupigana dhidi ya kutawaliwa pamoja na athari zakutawaliwa huku. Hata hivyo, licha ya kuwepokwa juhudi za kikaiba na kimataifa zakuwaelimisha watu asili, elimu ya watoto asilikihalisia si ya bure wala ya lazima. Ingawa haki zakupata elimu katika takriban mataifa yote yaAfrika zimehakikishwa, watoto wa kiasili badowanakumbwa na ugumu wa kupata haki yao yaelimu, hasa elimu inayoafikiana na mahitaji nautamaduni wao. Mango wa Elimu Badala yaKimsingi kwa Wakaramajong (ABEK), wa nchiniUganda, ambao umeundwa kutoa mtaala nambinu za kufundisha ambazo zinafaa kwa maishaya kuhamahama, ni mfano bora wa hatuazinazozingatia mahitaji ya jamii asili. Zaidi ya hayo,upande wa elimu ya msingi, udhamini wa kikatibana kisheria haujakuwa wa kutosha kuzungumziamahitaji maalum na changamoto za watu asili.

Viwango vya elimu kwa watu wazima piavimebaki chini.

7 Ardhi, maliasili na mazingira

Kwa watu wengi wa kiasili, ardhi haitoi tu namnaya kujikimu kiuchumi, lakini pia huwa msingi wakutambulika kwao kitamaduni, kiroho namasilaha ya kijamii. Ardhi ya jadi hupoteakutokana na mipango ya uhifadhi wa mazingira,ukuzaji wa utalii na ukataji wa miti. Athari naupotezaji huu wa ardhi vinazidishwa na kukosakuwapa ardhi badala na kuwafida. Baadhi yamataifa yaliyochanganuliwa katika utafiti huu yanavibali ama vya kikatiba au vya kisheriavinavyotambua haki ya pamoja ya umiliki wa malina mashamba. Hitaji kwamba ni lazima jamii zakiasili ziwe na idhini ya kisheria kabla ya kudaihaki zao za pamoja za umiliki wa ardhi, linazizuiajamii nyingi asili zisifurahie haki zinazopatikanakatika sheria. Zaidi ya hayo, kutokana na halikwamba mbinu za utumizi wa ardhi za watu wakiasili aghalabu huangaliwa kama zilizopitwa nawakati, inaweza kuchuliwa kuwa ardhi ya watuasili haitumiki ipasavyo (kiuzalishaji). Hali hiiinaweza kuangaliwa kama aina fulani ya ubaguzidhidi ya njia za utumizi wa ardhi za watu asili naumiliki wao wa kitamduni. Katika hali nyingi,uwezekano wa watu asili kudai haki zao zapamoja za kumiliki ardhi hutegemea waokuonyesha “matumizi zalishi” ya ardhi hiyo.

Hali kama ukosefu wa katiba, kutolipwafidia na kushindwa kutoa ardhi badala,zimechangia kuongezeka kwa athari ya kupotezaardhi. Kuasisiwa kwa haki za kibinafsi za kumilikiardhi pamoja na kutia ardhi inayomilikiwa nawatu kimila chini ya serikali,au kudhoofisha hakiza umiliki wa ardhi kijamii, kumekuwa na atharikubwa sana kwa haki za watu wa asili. Mifumomipya ya ardhi kama hii pia ilivipa hadhi kilimo naumiliki wa ardhi wa kibinafsi, kuliko utumizi waardhi wa kuhamahama, pamoja na ufugaji nauwindaji-ukusanyaji. Zaidi ya hayo, pamoja nakuanzishwa kwa hatua za uhifadhi wa maeneo namazingira, nafasi ya watu asili katika kuhifadhi nakusimamia ardhi kama hizi ilidunishwa. Uongozipia ni suala muhimu linalofungamana moja kwamoja na haki walizo nazo watu asili kwamashamba yao.

Mataifa mengi ya Afrika yanatambua hakiza kimila kama namna ya haki za kumiliki ardhi.Huu ungekuwa msingi mzuri kwa watu asili. Zaidiya hayo, katika hali chache zilizoko, kanuni zakimila (kitamaduni) zilizosambamba na sheria ya

viii

Page 9: First page ILO.fm

kitaifa na zinatambuliwa katika sheria, zinaruhusukuwepo kwa haki za pamoja na za kibinafsi zakumiliki ardhi. Ingawa mara nyingi haki kama hizisi za umiliki mkamilifu na ni haki za kutwaa au zakimatumizi tu.

8 Haki za uchumi wa jamii

Kupuuzwa kwa haki za uchumi wa jamii ni kiinicha kupembezwa kwa watu wa kiasili. Watu wakiasili aghalabu hukumbwa na unyimwaji wa hakiza kibinadamu za uchumi wa kijamii. Ingawaishara za kuaminika mara nyingi huwa hazipo,taswira ya kunyimwa haki zinazohusiana na elimu,huduma za afya, umiliki wa mali na ajira,inajitokeza. Baadhi ya ibara za sheria za kimataifa,kilimwengu na kieneo , zinaweza kutambulikakama zinazodhamini haki za uchumi wa kijamii zawatu wa kiasili. Katika juhudi za kutekelezamajukumu yao, baadhi ya mataifa ya Afriakayameishia kukubali baadhi ya hatua, zikiwemo zakikatiba, kisheria hata za kiutawala, kwa lengo lakudumisha hususan haki za uchumi wa kijamii zawatu wa kiasili. Haki hizi ni pamoja na, haki zakupata chakula, huduma za afya, usalama wa jamii,haki za kuwa na makao, haki za kielimu, haki zakupata ardhi, kumiliki mali yakiwemo mali yakiusomo. Kama kutoa mfano wa maendeleochanya ya kisheria, Jamuhuri ya Afrika ya Kati(CAR) ilipitisha sheria kuharamisha matumizi yatamaduni simulizi za jamii za waliowachachekatika nchi hiyo. Kuhusishwa kwa maslahi yaWabatwa katika Waraka wa Mikakati yaKupunguza Umasikini wa Burundi ni mfano zaidiambao ndio msingi wa maendeleo zaidi ya halafu.

9 Usawa wa kijinsia

Usawa wa kijinsia unahusiana haswa na usawakatika namna mtu anachukuliwa chini ya sheria nausawa wa nafasi. Suala la jinsia ni muhimu sanakwa watu wa kiasili na hususan wanawake wajamii asili kwa sababu masuala ya ubaguzi pamojana matatizo ya sera za utamaduni wa kijamiihuifanya hali ya wanawake katika jamii asili kuwambaya zaidi. Usawa wa jinsia, kutobaguliwa nakuimarisha haki za wana wake, ni mambo ambayoyanahusiana kwa karibu sana. Ijapokuwa mataifamengi ya Afrika yametilia sahihi vyombo kadhaavya kimataifa vinavyopinga ubaguzi kwa misingi yajinsia, wanawake bado ukosefu wa usawa kwaupana. Wanawake na wasichana katika jamii asiliwanakumbwa na matatizo mengi na makubwa

zaidi kutokana na miktadha ya uchumi wa kijamiina ya kitamaduni wanamojikuta, na ambayoinawatia katika ndoa za mapema na zakulazimishwa, dhuluma na tamaduni mbaya.Viwango vyao vya elimu ni duni ikilinganishwa nawanaume; wamo katika hatari zaidi kuambukizwavirusi vya ukimwi. Wamebaguliwa katika kufaidihaki za kurithi. Mataifa yamechukua hatua chachesana kushughulikia hali maalum za unyonge zawanawake wa asili. Hii haswa inatokana na halikwamba nafasi ya jumla ya kisheria inatilia nguvuukosefu wa usawa baina ya wanaume nawanawake, aghalabu ikiendeleza mitazamo yakijamii na kidini. Mataifa ya Afrika yamechukuahatua chache sana kushughulikia hali maalum zaunyonge za wanawake masikini wa asili. Idhini zakijumla zinazohusu haki za wanawake kama vileulinzi wa kikatiba dhidi ya ubaguzi kwa misingi yajinsia, sheria kuhusu dhuluma za kinyumbani, nahatua maalum, hazijazingatia mahitaji maalum yawanawake wa asili na hazijatumiwa kushughulikiamahitaji yao.

10 Watoto wa asili

Sheria katika mataifa mengi yalichunguzwahazigusii hasa masuala ya watoto asili. Sababu yakutohusishwa kwa suala hili inatokana nachukulizi kwamba sheria zinazoshughulikiawatoto tayari zinagusia kategoria maalum yaunyonge katika umma mzima. Watoto wotewanakumbwa na kunyanyaswa na wanahitajiulinzi spesheli wa kisheria. Mara nyingi, mahitajiya watoto asili yanaingiliana nay ale ya watotowengine waliohatarini. Hata hivyo inaonekanakwamba pana maelewano fulani kuhusu kiwangocha dhuluma ambazo watoto, hususan wa asili,wanakumbana nazo. Licha ya kuwepo kwauwezekano kwamba watoto asili wanaezakufaidika kutokana na idhini za kijumla zakisheria, pana ushahidi mdogo sana kwambakwahakika wanafaidika. Kwa kweli, kuna ishara zawazi kabisa kwamba mambo ni kinyume. Watotoasili wamo katika kikundi fulani kidogo kilichohatarini kutokana zaidi na ukweli kwambawanaishi katika maeneo ya mashambani au katikahali za uhamaji ambapo huduma za kijamiihaziwafikii ipasavyo au hata hazipo. Baadhi yamapendekezo yanatolewa kwamba, kwa mfano,serikali zihakikishe kwamba data zilizopakaazinazohusu watoto zikusanywe ili kubainishamapengo na vizuizi vilivyopo vinavyowazuiawasifurahie haki zao za kibinadamu.

ix

Page 10: First page ILO.fm

11 Watu wa kiasili wanaoishimaeneo ya mipakani na hali zang’mbo ya mipaka

Watu wa kiasili aghalabu wametawanyika katikamaeneo yote ndani ya mipaka ya kitaifa.Kutokana na hali hii, makundi ambayo yanafananakijamii yanaishai kuchukuliwa kama yaliyo nauraia tofauti kisheria. Mipaka inakuwa kamavizuizi vinavyowapinga au kuzuia maingiliano yakijamii na kitamduni na kudhoofisha mshikamanobaina ya kundi hilo. Hususan yale makundi yawatu wanaoishi maisha ya makazi ya muda namaisha ya kuhamahama kama vile Watuareg naWambororo, mara nyingi huvuka mipaka kamasehemu ya kujikimu kwao. Mataifa yaliyoathiriwa,hayajashughulikia hali ya uhamaji wa watu asili njeya mipaka rasmi katika mifumo yao ya kisheria.Mahitaji maalum ya watu hawa yanapaswakuchunguzwa na matokeo ya mikondo yao yauhamaji na uhalisia wao wa pamoja uwekwekatika mipaka ya sheria.

C Mapendekezo

Kwa msingi wa matokeo haya, ripoti hii inatoa yamapendekezo kadhaa kwa mataifa, jamii yakimataifa, umma na vyombo vya habari. Baaddhiya mapendekezo muhimu yametolewa hapakimuhtasari.

(a) Kwa mataifa ya Afrika

Inafaa tume za kitaifa za uchunguzi zinazohusishawataalamu wa kitaifa na kimataifa ziundwe ilikuchunguza na kutoa ripoti kuhusiana na nafafi yawatu asili katika kila nchi. Uchunguzi huo unafaakubainisha watu asili katika taifa hilo (ikiwa wapo)

Hatua za ukusanyaji data zitafaa sanakatika kusaidia serikali katika kubainisha mahitajimaalum ya watu asili (pamoja na makabilamengineyo) nchini, ambazo pia zitasaidia katikakubuni hatua zitakazosaidia kuhakikisha kwambakuna usawa baina yao. Yafaa kupatikane datainayohusu hali zao zote za kimaisha, ikiwemokiwango chao cha elimu, viashiria vya afya, kupatahuduma za uchumi wa kijamii kama vile hudumaza kiafya na maji safi ya kunywa na hata fursa yakupata haki. Data hii yafaa kutengwa sana kamaiwezekanavyo kulingana na umri na jinsia, naitolewe baada ya kushauriana na watu asili ilikuhakikisha kwamba inawakilisha mahitaji yaomuhimu na mitazamo yao wenyewe.

Iwapo watu wa asili wapo katika nchifulani, ni lazima Mataifa yahakikishewanatambulika kisiasa na kisheria kwa kutumiavigezo vya kimataifa na kimaeneo. Lazima serikalizihakikishe kwamba pana ukusanyaji wa data zakutegemewa kwa kubainisha mahitaji maalum yawatu asili (pamoja na makabila mengineyo) katikanchi.

Katika hali ambapo kunakosekana sheriapana inaolenga watu asili katika nchi, sheriailiyopo yafaa kutumiwa kikamilifu kulinda haki zawatu wa asili. Hata hivyo mataifa yanafaa kuwaziakutumia sheria ambayo inashughulikia haki zawatu asili kwa upana, kama inavyofanywa nchiniKongo.

Katika mambo yote yanayowaathiri watuasili, kama vile hatua za kisheria, sera zakimaendeleo au ya uhifadhi, mipango na miradi,masuala ya uongozi na utawala, ni lazima serikalizishauriane nao wenyewe.

Kutokana na kukosa uzoevu wa mifumoiliyopo ya kulinda pamoja na matokeo ya miakamingi ya kutawaliwa, kupembezwa na kutngwa,watu wa asili wanahitaji hatua maalum kulindamasilaha yao. Kwa hivyo mataifa yanafaa kutwaana kutekeleza hatua maalum kushughulikia hali yakupembezwa na kubaguliwa iliyokita mizizi na yamuda mrefu ya watu asili inayotokana na upekeewao.

Taasisi za kitaifa zilizoko, kama taasisi zakutetea haki za kibinadamu, zinapaswakushughulikia hali ya watu asili. Ikihitajika,majukimu ya taasisi kama hizi zinapaswakudurusiwa ili kuhusisha masuala asilia, na watuwa asili wahusishwe kama wanachama wa taassisihizi. Zaidi ya hayo, mataifa yanapaswa kuzingatiakuazisha taasisi ya kitaifa inayolenga hususankuhakikisha kuwa kuna kulindwa kwa haki zajamii za asili.

Mataifa yanapaswa kutia sahihi mkatabawa 169 wa ILO, ambao unafafanua majukumu yamataifa kwa watu asili.

(b) Kwa Umoja wa Mataifa,Muungano wa Afrika namashirika mengine ya kimataifa

Mashirika ya mikataba ya haki za kibinadamu yaUmoja wa mataifa na Muungano wa Afrikayameonekana yenye utoshelevu katika matukiokadhaa ya uchunguzi wao wa matakwa ya watu

x

Page 11: First page ILO.fm

asili. Uwekaji wa uchunguzi huu wa hali za watuwa asili katika muktadha wa uchunguzi wa ripotiza kitaifa utawezesha mashirika kama hayakujiingiza katika mazungumzo yanayoendeleabaina ya mataifa, na kufuatilia majadiliano ya awaliili kuangalia maendeleo ya utekelezwaji wa hakizilizohifadhiwa katika mikataba ya uanzishaji wakekwa watu wa asili. Hususan, kuakisiwa kwa hayakatika maoni yoyote ya uhitimisho lazimakusambazwe kwa upana iwezekanavyo

Uwezo wa Utaratibu wa Udurusiaji Bia waKimuhula (Universal Peridic review) Udurusiajiwa masuala ya rika wa Afrika (African PeerReview) katika kushughulikia mahitaji ya watu waasili wapaswa kuchunguzwa kikamilifu.

Umoja wa mataifa pamoja na mashirikamengine ya muungano wa mashirika mengi aumawili yaliyo na mipango kwenye kiwango chanchi yatakuwa ya muhimu sana katika kusaidiaserikali za Kiafrika katika utekelezaji wamapendekezo yaliyoorodheshwa hapo juu.

(c) Kwa Umma

Mashirika ya umma yapaswa kupigania kuwepokwa mashauriano na watu wa asili kuhusumambo yote yanayowahusu, na kwa kuhusishwakwa matakwa ya watu asili katika sheria, sera namipango yote. Kuhusishwa kwa matakwa ya watuwa asili katika shughuli za kufundisha na utafiti wataasisi za elimu kutahakikisha kuwepo kwakiwango kikubwa cha ujenzi wa uwezo kuhusianana masuala ya ukanda wa Afrika

(d) Kwa vyombo vya habari

Vyombo vya habari vinapaswa kuufahamishaumma mzima kuhusu dhana ya watu wa kiasili,mahitaji na haki zao maalumu, na dharura yakushughulikia mahitaji yao. Pia, yanapaswakuchangia katika kudidimiza mitazamo hasi dhidiya watu wa kiasili kupitia kwa kutoa taarifa sahihi.

xi

Page 12: First page ILO.fm
Page 13: First page ILO.fm

Yaliyomo

Shukurani xvOrodha ya vifupisho xvi

A Utangulizi 11 Asilia, lengo na mbinu za utafiti 12 Mipaka ya utafiti 33 Dhana ya watu wa kiasili 44 Sheria ya kimataifa 7

B Muhtasari wa matokeo ya utafiti 15

1 Kukubaliwa na kutambuliwa 151.1 Utangulizi 151.2 Utambuzi wa kisheria na wa kikatiba wa watu wa kiasili 17

katika Afrika1.3 Sera na mipango ya kitaifa 221.4 Taarifa na stakabadhi za mabaraza ya kimataifa 241.5 Uraia 251.6 Hitimisho 27

2 Kutobaguliwa 292.1 Utangulizi 292.2 Sheria ya kimataifa 292.3 Mielekeo ya Kitaifa 312.4 Hitimisho 37

3 Kujitawala, Mashauriano na kushiriki 393.1 Utangulizi 393.2 Muundo wa serikali na utawala mkuu 403.3 Muundo wa vyombo vya kufanya maamuzi 423.4 Utawala wa mitaa 443.5 Uongozi wa kitamaduni na sheria ya kimila 473.6 Kushiriki katika uchaguzi 493.7 Kushiriki katika usimamizi wa ardhi na maliasili na kufanya 52

maamuzi3.8 Kushauriwa na kushiriki katika uundaji wa sera na 55

mipango ya maendeleo3.9 Hitimisho 58

4 Kupata Haki 604.1 Utangulizi 604.2 Viwango vya kimataifa 604.3 Mielekeo muhimu ya kitaifa 614.4 Hitimisho 66

5 Utamaduni na Lugha 685.1 Utangulizi 685.2 Sheria ya kimataifa 685.3 Mielekeo ya Kitaifa 705.4 Hitimisho 75

6 Education 776.1 Utangulizi: Umuhimu wa Elimu kwa watu wa kiasili 776.2 Viwango vya kimataifa 77

xiii

Page 14: First page ILO.fm

6.3 Mielekeo ya Kitaifa 796.4 Hitimisho 83

7 Ardhi, maliasili, na mazingira 857.1 Utangulizi: Viwango vya kimataifa 857.2 Umilikaji, Utwaaji, haki za matumizi, na masula ya 87

masharti ya kumiliki ardhi7.3 Namna za matumizi ya ardhi ya watu wa kiaisili na sheria 92

ya kitaifa7.4 Haki za pamoja na za kibinafsi na Sheria ya Kimila 987.5 Maliasili 1047.6 Hitimisho 114

8 Haki za uchumi wa jamii 1188.1 Utangulizi 1188.2 Sheria ya kimataifa 1188.3 Mielekeo ya kitaifa 1208.4 Hitimisho 124

9 Usawa wa kijinsia 1269.1 Utangulizi 1269.2 Sheria ya kimataifa 1269.3 Mielekeo ya kitaifa 1279.4 Hitimisho 137

10 Watoto wa kiasili 13910.1 Utangulizi: Umuhimu na mahitaji maalumu ya watoto 139

wa kiasili10.2 Sheria ya kimataifa 13910.3 Mielekeo ya kitaifa 14110.4 Hitimisho 145

11 Watu wa kiasili katika maeneo ya mipakani na 147hali za uvukaji mipaka1

11.1 Utangulizi: Watu wa kiasili wenye makaazi ya muda ya 147wahamahamaji

11.2 Sheria ya kimataifa 14811.3 Mielekeo ya kitaifa 14911.4 Hitimisho 150

C Mahitimisho na Mapendekezo 1511 Mahitimisho 1512 Mapendekezo 157

Kiambatisho A: Orodha za tafiti za nchi mbalimbali 161

xiv

Page 15: First page ILO.fm

Shukurani

Muhtasari wa ripoti hii umekusanywa hasa na Francesca Thornberrywa ILO na Frans Viljoen wa Kituo cha kutetea Haki za Kibinadamu,Chuo Kikuu cha Pretoria. Usaidizi wa Solomon Ebobrah, ClementMavungo na Sekai Saungweme katika kukusanya Muhutasari waRipoti; usaidizi wa Annelize Nienaber na Serges Allain katika kuhaririMuhtasari na ripoti za nchi mbalimbali; na usaidizi wa wanafunzi wakituo hiki – Alexander Prezanti, Divina Gomez, Anne Schuit,Cuthbert Tumusime Kazora na wa Belkacem Boukherouf,mwanafunzi wa Mpango wa ILO wa Kuendeleza Mkataba wa ILOnambari 169 (PRO 169) – katika kuhariri na kufannyia kazi tenabaadhi ya ripoti za nchi, unapokelewa kwa shukrani nyingi. Katikawakati wake wa mafunzo kwenye CHR, Alaric Van den Berghealisaidia katika masuala mbalimbali, ikiwemo kutafsiri stakabadhimuhimu. Msaada wake wa ukarimu utakumbukwa daima. Usaidizi wadakika za mwisho wa Belkacem Lounes, Mohammed Khattali,Genevieve Rose, Stefania Errico na Valery Couillard katika kufanyautafsri unatambulika kwa shukrani.

Muhtasari huu wa ripoti umejikita katika tafiti za kikao nanyanjani zilizoandaliwa na watafiti walioonyeshwa katika kiambatishoA. Michango yao usiokifani na ile ya wasomaji wa kitaalamuinatambulika kwa shukrani kubwa.

Wanachama wa Kamati Andalizi ya mradi huu, Kamati Teule nawasomaji wote wanatambulika kwa shukrani.

Usaidizi wa Yolanda Booyzen katika kuunda databenki na arkiza muundo, na usaidizi wa Waruguru Kaguongo katika kukusanyastakabadhi unatambuliwa kwa shukrani. Michango ya kibunifu yaLizette Besaans, ambaye ndiye aliyeshughulika na mpangilio waripoti, pia umetambulika.

Michango ya watu wafuatao kutoka ILO inatambuliwa kwataadhima: Cecile Balima, Christina Holmgren, Birgitte Feiring, MartinOelz, Stefania Errico, Benoit Guiguet, Serge Bouopda na BoshigoMatlou.

Kazi hii ilifanikishwa na kutokana na mchango wa kifedha waChombo cha Ulaya cha Demokrasia na Haki za kibinadamu (EIDHR)cha Ubalozi wa Ulaya na Wizara ya Mambo ya Nje ya Denish(Danida).

xv

Page 16: First page ILO.fm

Vifupisho na Akronimi

ABEK Elimu badala ya msingi kwa WakaramojaACHPR Mkataba wa Afrika kuhusu haki za kibinadamu na

haki za watuAIDS Ukimwi APRM Mkakati wa kiafrika wa kuchunguza masuala ya rikaARV Dawa za kupunguza makali ya ukimwiAU Umoja wa AfrikaCAR Jamuhuri ya Afrika ya KatiCAT Maafikiano dhidi ya matesoCBNRM Mpango wa kijamii wa kusimamia raslimali za

kitaifaCEDAW Mkataba wa kukomesha kila aina ya ubaguzi dhidi

ya wanawakeCERD Mkataba wa kukomesha kila aina ya ubaguzi wa

kikabilaCHR Kituo cha haki za kibinadamuCIB Congolaise Industrielle des BoisCKGR Mbuga ya wanyama ya Kalahari ya KatiCRC Mkataba kuhusu haki za mtotoDRC Jamuhuri ya Kidemokrasia ya KongoEID I’Espace d’Interpellation DemocratiqueFGM Ukeketaji wa wanawakeGEF Nyenzo ya Ulimwengu kuhusu mazingiraHIV Virusi vya Ukimwi (VVU)HRC Kamati kuhusu haki za kibinadamuICCPR Maafikiano ya kimataifa kuhusu haki za kiuchumi,

kijamii na kitamaduniIWGIA Kamati Teule ya kimataifa kuhusu masuala ya kiasiliILO Shirika la Leba la kimataifaIPDP Mpango wa maendeleo wa watu wa kiasiliIRCAM Taasisi ya Kifalme ya Utamaduni wa WaamazighNEPAD Ushirikiano mpya wa maendeleo ya AfrikaNGO Shirika lisilo la kiserikaliNDDC Tume ya maendeleo ya Nijaa DeltaOAU Shirika la umoja wa AfrikaOHCHR Ofisi ya Balozi wa umoja wa mataifa kuhusu haki za

kibinadamuPASDEP Mpango wa maendeleo ya haraka na ya kudumu ya

kuukomesha umasikiniRADP Mpango wa wakaaji wa maeneo ya mashambaniSADC Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa AfrikaSASI Taasisi ya Wasan ya Afrika KusiniSASC Baraza la Wasan la Afrika KusiniSPRP Makala ya mikakati ya kupunguza umasikiniUN Umoja wa MataifaUNDRIP Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu watu wa kiasiliUNDP Mpango wa maendeleo wa Umoja wa MataifaUNIPOBRA Unisson-nous pour la Promotion des BatwaUSA Muungano wa Mataifa ya Marekani (Marekani)WHO Shirika la afya UlimwenguniWIMSA Kamati Teule ya watu wa kiasili waliowachache

kusini mwa Afrika

xvi

Page 17: First page ILO.fm

Kwa miaka michache iliyopita masaiibu ya watu wa kiasilia yameendeleakutiliwa maanani ulimwenguni kote. Imekubaliwa kijumla kwamba watu wakiasili ni kati ya watu walio maskini na walio katatika hali ya unyonge zaidi.Kutokana na kutambulika kwao kwa kipekee na mshikamano wao kwenyehistoria zao, mazingira, tamaduni, mifumo yao ya kisiasa au lugha, watu wakiasili wameteseka na bado wanakabiliwa na upembezwaji, kushutumiwa nakubaguliwa. Kushikamana kwao kwenye upekee wa siasa za jamii au wakiuchumi, kumesababisha kuwepo kwa mitazamo kwamba watu wa kiasili nitofauti au ni ‘duni’, kote ulmwenguni. Kutokana na haya, ama kwa sababu yaukoloni au kutawaliwa na makundi ya waliowengi au uundaji wa serikali zamataifa, watu asilia aghalabu wamekumbwa na kila namna ya dhuluma kuanziakunyang’anywa ardhi yao ya jadi na raslimali, hata kusilimishwa katika hali zamaisha za makundi ya waliowengi. Kwa watu wa kiasili, changamoto basizimekuwa kuzimaliza dhuluma hizi huku wakidumisha upekee wao.

Watu wa kiasili barani Afrika wanaonekana kukabiliwa na changamotokubwa zaidi kutokana na hali kwamba mataifa ya Afrika yamekuwa malegevukukubali kuwepo kwa makundi ya kiasili katika maeneo yao. Kwa hivyo, zaidihali ya kijumla ya haki za kibinadamu barani Afrika, kutokana kutotambuakuwepo kwao, watu wa kiasili wana mahitaji maalumu ya haki za kibinadamukatika baadhi ya mambo kama, kuwakilishwa na kushirikishwa kisiasa,kubaguliwa, ukosefu wa ardhi na raslimali, kiwango cha chini cha kupatamiundomisingi, kunyimwa haki za kibinadamu na kuharibiwa kwa mazingirayao. Ijapo maendeleo katika haki za kibinadamu kimataifa yameinua kiwangocha ufahamu kuhusu umuhimu wa kuwapa uwezo wahanga wa dhuluma iliwaweze kudai haki zao, hali hii pekee yake haijatosha kushughulikia mahitajiya watu asilia. Kutokana na kukosa uzoefu wa mbinu zilizopo za kuwalindapamoja na matokeo ya kutawaliwa kwa miaka mingi, kupembezwa nakutengwa, watu asilia wanahitaji mikakati maalum ya kulinda maslahi yao.

1 Asilia, lengo na mbinu za ripoti

Kutokana na asilia hii, mradi huu umehusisha utafiti wa miaka mitatu washirika la wafanyikazi la kimataifa (ILO) na jopokazi la Tume ya Afrika kuhusuwatu asili (African commission working group). Utafiti ulilenga kuchunguzakiwango ambacho mifumo ya kisheria ya nchi za kiafrika inaathiri na kulindahaki za watu asili. Kituo cha kushughulikia haki za kibinadamu (CHR) - ChuoKikuu cha Pretoria kilifanya kazi kama taasisi tekelezi. Kamati ya uendeshajiwa mradi, iliyohusisha mwakilishi mmoja wa ILO, jopokazi la tume ya Afrika(ACWG), kituo cha kushughulikia haki za kibinadamu (CHR), na mtaalamuwa kujitegemea kutoka shirika lisilo la kiserikali- shirika la kazi la kimataifa lakushughulikia masuala ya kiasili (IWGIA) ilifawidhi mradi.

Malengo makuu ya mradi huu yalikita kuwili: lengo la kwanza lilikuwakuchangia katika kuendeleza sera na mifumo ya kisheria inayofaa kulinda hakiza watu asili. Pili, ilikuwa ni kujenga uwezo na kuleta ufahamu kwa wahusikakutoka katika watu asili na taasisi za kiserikali ili kuimarisha harakati zakuendeleza na kulindsa haki za watu asili katika mataifa ya Afrika.

A Utangulizi

1

Page 18: First page ILO.fm

Kwa kutumia kanuni za mkataba wa ILO kifugu 169 na mwafaka wa Afrikakama mfumo rejelezi, utafiti huu ulikadiria kiwango ambacho haki za watu asilizimelindwa kwenye kiwango cha kimataifa. Utafiti unahusisha, uchunguzi pevuwa viwango vinavyofaa vya kimataifa, kimaeneo na kitaifa, katiba, utunzi washeria, sheria za desturi, mikakati ya kiutawala na sera za kiserikali namaelekezo, kati ya mengineyo, katika nchi zilizotafitiwa, kwa lengo lakukadiria kiwango ambacho haki za watu asili zimelindwa katika mifumo yaoya kisheria. Hitaji la kufanya utafiti huu limejengwa kwenye hali kwamba haki,ambazo ni za lazima katika mkataba wa ILO kifungu nambari 169, na mwafakawa Afrika, za ulinzi wa watu asili hazitakuwa na maana ikiwa hazitahakikishwana kutekelezwa katika mifumo ta kisheria ya kitaifa.

Mradi ulianza kwa warsha iliyofanyika kuanzia tarehe 18 hadi 20 Septemba2006. warsha hiyo ilifanywa kwa ushirikiano wa ILO na Tume ya Afrika. Lengola warsha hiyo lilikuwa kuzichambua mbinu za utafiti na michakatoitakayofuatwa katika mradi wa utafiti. Warsha ulifanyiwa Yaoundé nchiniKameruni, na washirika wake walikuwa ni pamoja na wanachama wa Tume yaAfrika, ILO, CHR, IWIGA, wataalamu wa kiasili, wataalamu wengine pamojana watu asili na mashirika yasiyo ya kiserikali yanayofanya kazi baina ya watuasili.

Aina mbili za uchunguzi zilifanywa kama sehemu ya utafiti. Nazo ni;uchunguzi wa kikao na uchunguzi wa kina (pevu)

• Utafiti wa kikao ulilenga kutoa taarifa nyingi iwezekenavyo kutokakatika stakabadhi zilizopo kuhusu mifumo ya kisheria inayoathiri nakulinda watu asili katika nchi mahsusi.

• Tafiti za kina zilifanywa kwenye msingi wa utafiti wa awali wa kikao,lakini kwa kuongezea ulilenga kutoa uchanganuzi tekelezi na pevuwa kiwango cha utekelezwaji wa mifumo ya kisheria na kiserailyopo inayohusiana na watu asili. Tafiti hizi zililenga kutambulishana kupima mikakati halisi, kama ipo, katika nchi zailizotafitiwa.Aidha zililenga kuthibitisha (kutekeleza) mifumo ya kisheriainayolinda haki za watu asali. Tafiti za kina zilihusisha ziara katikanchi Fulani ambapo watafiti walihojiana na kutangamana namashirika na taasisi za kiserikali, ILO, Umoja wa Mataifa (UN),mashirika ya watu asilia na mashirika ya watumishi wa umma ilikutekeleza ziara za utafiti.

Nchi ishirini na nne zilichunguzwa katika utafiti kwa njia ya uchunguzi wakikao. Nazo ni;1 Aljeria, Botswana, Burundi, Burkina Faso, Kameruni,Jamuhuri ya Afrika ya kati (CAR), Chad, Kongo, Jamuhuri ya Kidemokrasia yaKongo (DRC), Misiri, Ethiopia, Gabon, Kenya, Mali, Moroko, Namibia, Nija,Naijeria, Rwanda, Tanzania, Afrika Kusini, Sudan, na Uganda. Vilevile utafitiwa kina ulifanywa katika nchi nane kati ya hizi zilizotajwa: Aljeria, Burundi,CAR, Ethiopia, Kenya, mali, Nija, na Afrika Kusini. Nchi hizi ziliteuliwa kwamsingi wa vigezo vilivyojadiliwa na kukubaliwa katika warsha ya uzinduzi wamaradi ilyofanyika mjin Yaoundé mwaka wa 2006. vigezo hivi vilihusishavifuatavyo; 1

• Uwakilisho wa kieneo.• Hitaji la kuhusisha nchi ambamo masuala ya watu asili hayajafanyiwa

utafiti kikamilifu.• Kujitambulisha kwa makundi kibinafsi kama makundi asilia.

1. Angalia kiambatanisho A mwishoni mwa ripoti ili kupata orodha kamili ya waandishi.

2

Page 19: First page ILO.fm

Kulingana na kufanya ziara za kina, ufikiwaji wa nchi ya kufanyiwa ziara yautafiti wa kina uliangaliwa. Licha ya Moroko kutokuwa mwanachama waMuungano wa Afrika (AU), ilikubalika kwamba itahusishwa katika utafiti wakikao kutokana na maendeleo endelevu yanayofanyika huko pamoja na dhimayake kubwa katika ukanda kaskazini mwa Afrika kuhusiana na masuala ya watukiasili.

Watafiti waliofanya utafiti wa kikao, waliteuliwa kwa ajili ya kila nchi.Baada ya marakebisho ya baadaye ya watafiti, ripoti ilidurusiwa na msomaji wanchi. Kwa nchi nyingi, mtu aliye na ujuzi wa kutosha kuhusu sheria na anaufahamu wa hali ya juu kuhusu hali ya watu asili katika nchi inayotafitiwaalichaguliwa. Baada ya kuhusishwa kwa maoni na marekebisho ya wasomaji,ILO na Kamati ya uendeshaji viliwasilisha mapendekezo yao pamoja namaidhinisho ya baadaye. Muhtasari wa ripoti hii ulitayarishwa kwa msingi wahizi ripoti za nchi, ukawasilishwa na kutolewa maoni na wahusika na taasisianuwai, kisha ukawasilishwa kwa Tume ya Afrika ili kuidhinishwa. Kamatiilikubali muhtasari huu wa ripoti kwenye kikao chake cha 46 Mei 2009kilichofanyika katika mji mkuu wa Gambia, Banjul.

Ripoti ya kila nchi imepangiliwa katika sehemu tatu kuu: Sehemu yakwanza imedokeza kwa kifupi hali ya watu asili pamoja na usuli wa nchi kamainvyohusiana na masuala asilia. Sehemu ya pili inachunguza ulinzi wa kwa watuasilia katika nchi kulingana na orodha ya maudhui. Sehemu ya tatu inatoahitimisho na kutoa maoni.

Makala ya muhtasari huu yamepangiliwa kulingana na ripoti za nchi.

Databenki ya kielektroniki (meme) yenye nakala kamili ya ripoti za nchi,nakala ya mwisho ya muhtasari wa ripoti pamoja na stakabadhi zinazohusuwatu asili kulingana na nchi hizi, pia imetayarishwa2

2 Mipaka ya utafiti

Vipengele vya kikatiba pamoja na vya kisheria vinjihusisha hususan na watu wakiasilia kwa nadra sana. Kwa upande mmoja, ukosefu huu wa umahususiunatokana na kukana kuwepo kwa watu wa kiasili. Kwa upande mwingineinaweza kuchukuliwa kwamba ulinzi wa watu wa kiasili umewekwa chini yamikakati ya ulinzi inayolenga umma mzima au makundi mengine manyonge.Kwa hivyo mradi wa utafiti ulihitaji kupatanisha ufafanuzi wa mifumo yakisheria kijumla na kuonyesha umuhimu na uamilifu wa vipengele hivi kwawatu asilia. Iliwezekana katika hali chache tu, kurejelea sheria zilizolengahususan watu wa kiasili.

Ukosefu wa data rasmi ya kiserikali au takwimu zisizoungwa pamoja, naukosefu taarifa ya kiserikali juu ya matumizi ya sheria (badala ya utungajipekee) - vilevile iliathiri utafiti. Kwa kuwa mipaka ya utafiti haikuruhusuukusanyanyaji wa kimsingi wa data kiamali kuhusu hali za watu asilia nautekelezaji wa sheria, ilibidi kutegemea data tanzu (ya pili) ambayo aghalabuhaikuwepo au haingetegemewa.

Pamoja na nchi ishirini na nne kutoka kwenye maeneo madogoyaliyotafitiwa, utafiti unaweza kudaiwa kihalali kwamba uanatoa taswirakielelezo ya hali ya watu kiasili. Hata hivyo, kwa wazi kabisa uchunguzi huu si

2. Pia tazama www.chr.up.ac.za/indigenous; data hii imepangiliwa kulingana na nchi, aina yastakabadhi na maudhui.

3

Page 20: First page ILO.fm

mkamilifu, kwani umeacha nje kama ilivyokawaida, tajriba ya takribani zaidinusu ya bara. Kama kuwepo kwa makundi yanayojitambulisha yenyewe kamamakundi asilia ilivyokuwa kigezo kilichopelekea kuteuliwa kwa nchi fulani,utafiti pia ulifanywa kwa kuegemea tajriba fulani ya watu asilia.3

Ubora wa ripoti kutoka nchi mbalimbali unatofautiana, hali inayoonyeshachangamoto katika ukusanyaji wa taarifa, vile vile ukosefu wa uwezo wakutosha wa kushughulikia masuala asilia kwa mkabala wa haki za kibinadamukatika ukanda wa Afrika. Kivyake, haya yanaweza kuchukuliwa kamamahitimisho ya awali kutokana na tajriba zilizopatikana katika kufanya mradihuu.

3 Dhana ya watu wa kiasili

Ukosefu wa kuwepo kwa fasili ya dhana ya “watu wa kiasili” iliyokubalikakijumla, pamoja na kukubaliana kwa jumla kwamba, kwa hakika, fasili bia ya‘watu wa kiasili yaweza kuwa si mbinu ifaayo na inaweza kusababishakutengwa kwa makundi fulani, katika warsha ya Yaounde, uteuzi wa vigezoambavyo vingesaidia katika kutambulisha makundi yanayolengwa katika utafitiulijadiliwa kama mbinu mwafaka kwa utafiti huu. Ijapo mfumo mmojaunafuatwa, ripoti ya kila nchi inabainisha watu asilia kwa misingi ya kpekeekwa kuwa nchi mbalimbali zinachukulia suala hili kitofauti. Vigezo vifuatavyoambavyo vilibainishwa katika warsha ya Yaounde, vinalenga kutoa mwelekeojuu ya makundi yanayojitambulisha yenyewe kama watu asilia barani navinatumiwa kwa makusudi ya utafiti4

• Watu asili ni bainifu kijamii, kitamaduni na kiuchumi.• Tamaduni zao pamoja na hali zao za maisha ni tofauti kwa kiasi

Fulani na zile za jamii za waliowengi na tamaduni zao aghalabuzimehatarishwa sana na hata katika hali zingine kutishiwakutoweka.

• Wana mashikamano wa aina Fulani kwenye mashamba yao aumaeneo yao. Sifa moja kuu ya watu asili ni kwamba kuendeleakuwepo kwa namna yao ya kuishi kunategemea upataji na haki yakutumia mashamba yao ya kitamaduni pamoja na mali-asili yaliyokokwenye masmba hayo.

• Wanakumbwa na kubaguliwa kutokana na kutazamwa kama“wasioendelea” na ‘walionyuma’ kuliko vitengo vingine vikubwa vyakijamii.

• Aghalabu wao huishi katika maeneo yasiyofikiwa, ambayo maranyingi yametengeka kijiografia na yanakumbwa na upembezwaji waaina nyingi ikiwemo wa kisiasa na kijamii.

• Wanapitia katika kutawaliwa na kunyonywa kwenye mifumo yakitaifa ya kisiasa na kiuchumi ambayo kwa kawaida imeundwakuonyesha matakwa na shughuli za waliowengi kitaifa.

• Zaidi ya vigezo vilivyoorodheshwa hapo juu, washirika kwenyewarsha pia waliangazia dhima ya kimsingi ya kujitambulisha kibinafsi,ambapo watu wenyewe wanatambua upekee wao wa kitamadunina namna ya maisha yao, wakiwa na lengo la kukuza na kudumishaupekee wao.

3. Kwa kuwa utafiti huu ulifanywa kwa kipindi kirefu, kwa kipindi cha miaka mitatu, ilikuwavigumu kuhusisha maendeleo yote ya hivi karibuni kuhusiana na nchi zilizotafitiwa, hasawakati baada ya utafiti wa kikao kutangulia kufanywa mapema katika kipidi cha utafiti.

4. Pia tazama ripoti ya Kamati Teule ya wataalamu ya Tume ya Afrika kuhusu Watu / JamiiAasilia, ambayo iliwasiishwa kulingana na ‘Azimio kuhusu watu / jamii asilia Afrika’ IWGIA(Copenhagen) na ACHPR (Banjul, 2005) na Mkataba wa ILO nambari 169 sehemu ya 1.

4

Page 21: First page ILO.fm

Arki tatu ambazo zilitumika sana katika kuwatambulisha watu asili katikautafiti huu ni; kiwango kikubwa cha kupembezwa kunakowakumba,kujitambulisha wenyewe na kutegemea kwao mashamba na raslimali ili kuishi.Ikumbukwe kwamba vigezo vingine vinaweza kutumiwa kwenye kiwango chakitaifa.

Serikali za baadhi ya nchi zilizofanyiwa utafiti hazitumii istilahi ‘watu asili’.Nchini Rwanda kwa mfano, ‘jamii za kitaifa ambazo zimepembezwa sanakihistoria’ (‘la communauté nationale historiquement marginales’) inatumika.Zingine huwarejelea kama ‘populations marginale’ (watu waliopembezwa) au‘amii nyonge”. Wakati mwingine jina la kabila Fulani hurejelewa, kama ‘Batwa’badala ya kategoria ya umma. Hata hivyo, kuunga pamoja watu asili katikakategoria mbalimbali kwa msingi wa maana au upeo mpana, uleta hatari yakutoshughulikia kikamilifu upekee wao na haki zao zinazotambuliwa kimataifa.

Lengo la utafiti huu si kutoa orodha kamilifu ya watu wa kasili waliomo katikanchi zilizotafitiwa. Makundi makuu ya watu kiasili katika kila eneo ni kamayafuatayo, lakini hii haipuuzilii mbali kuwepo kwa makundi mengine, na siyomakundi yote yaliyoangaziwa katika tafiti za nchi yameorodheshwa hapa:

• Eneo la kaskazini na magharibi mwa Afrika: Kundi la Wa-Amazigh (au Berber) ndilo kundi kubwa la watu asili barani. Ndiowatu walio wengi nchini Moroko, (ambapo ni baina ya asilimia 30na 60 ya watu wote)5 na nchini Aljeria ambako wanachukuatakribani asilimia 15 ya watu wote.6 Pia Wa- Amazigh wakoTunisia, Libya and Misri (karibu na Oasisi la Siwa), watu wa mbariya Tuareg, ambayo ni kundi dogo la Wa-Amazigh, ambao huishimaisha ya kuhamahama yanahusiana na ufugaji wa ngamiawanapatikana nchini Nija, Mali, Burkina faso, Aljeria na Libya.Kutokana na kampeni za pamoja katika mataifa yote ya kaskazinimwa Afrika za kuwatia uarabu na kuwaslimu katika eneo zima lakaskazini mwa Afrika, upekee wa Wa-Amazigh ni tata na uliotiwaukungu na kupanuka. Kwanza, Wa-Amazigh wanajibainisha kwakutumia lugha ya Kitamazi (Tamazight). Utambulisho dhahiri wakiisimu na ufahamu wa kihistoria unahakikisha kwmbakujitambulisha kwao wenyewe kama ‘asilia’ ni dhabiti mno. Ingawabaadhi ya watu wa kundi hili wameingia mijini, wengi wao badowanaishi katika maeneo ya vijijini wakishikilia maisha yakuhamahama kwa kiasi (kama Wa-Amazigh wa nchini Moroko) aumaisha makazi ya muda (Watuareg). Nchini Sudan makundiambayo yanaweza kuchukuliwa kama asilia ni kama Wadinka,Wanuer, Azake na Wanubi.

• Magharibi na katikati mwa Afrika: Watu wa kabila la Peul,ambao wanaweza kuelezwa kama wafugaji wa kuhamahama, ndiowatu asilia waliowengi sana katika eneo hili. Wanaweza kugawikakatika; Wafelbe (Fulani), ambao ni wazalishaji wa n’gombe naWambororo, ambao sanasana ni wafugaji wa kuhamahama na waliona makazi ya muda na ambao maisha yao aghalabu yamefungamanakiroho na yale ya n’gombe wao (mafahali) na wala hayawezikutengeka kutoka kwao. Kijumla wao ni watu wanaomini katika

5. Tazama mfano wa Middle East Encyclopedia, http://www.mideastweb.org/Middle-East-Encyclopedia/amazigh.htm; baadhi ya ukadiriaji ni wa juu kiasi cha asilimia 80(http://phoenicia.org/berbe.html).

6. Tazama Middle East Encyclopedia, http://www.mideastweb.org/ Middle-East-Encyclopedia/amazigh.htm.

5

Page 22: First page ILO.fm

vitu vya kimaumbile na wanajihusisha na ibada za mizimu, lakiniwengi sasa wanakiri dini ya kiislamu. Kitamaduni, wambororowalikuwa wafugaji wakuhamahama kindakindaki waliosonga kutokamahali pamoja hadi kweingine kutafuta malisho ya mifugo wao. Sikuhizi wengi wao ni wale ambao huweka makaazi ya muda. Wa-peulwanaweza kupatikana kote katika Afrka magharibi, ikiwemoBurkina Faso, Kameruni, Jamuhuri ya Afrika ya kati, Chadi, Mali,Mauritania, Nija na Senegali. Kisiasa, wametengwa nawamepembezwa kiuchumi na kijamii. Makundi madogo ya watuasilia kama Ogoni na Waijau (Ijaws), pia yanaishi Naijeria.

• Afrika ya kati: kundi mojawapo muhimu zaidi la watu asiliwanaoishi katika maeneo ya misitu hasa karibu na maeneo yaMaziwa Makuu, ni ‘mbilikimo’7 watu wa kundi hili sanasanawanachukuliwa au hujichukulia wenyewe kama walio na madaihalali kuwa ndio wakazi asilia wa maeneo ya misitu ya Afrika yakati. Makundi mbalimbali madogo yanaishi katika na baina ya nchiza eneo hili, kama Batwa, wanaoishi Burundi, kongo, Jamuhuri yaKidemokrasia ya Kongo, Rwanda na Uganda. Makundi mengine nipamoja na, Baka, Bayeli na Bedzan wa Kameruni; Babisi, Babongo,Bakola, Mikaya, Mbenzele, Baka na Bagombe wa nhini Kong;Bakongo, Bakoya, Baaka, Barimba,Bagama na Bakoyi wa Gabon; naWa- Aka katika CAR, na Bambuti na Bakwa katika DRC.Kwakutegemea usasi, ukusanyaji, uvuvi, na ufinyanzi, makundi hayakiasili walikuwa na mshikamano wa karibu sana na mazingira yao yakimaumbile. Pia wanashiriki kupuuzwa na kupembezwa kumojaambako aghalabu hupelekea kutishiwa kufilia mbali.

• Afrika mashariki na upembe wa Afrika: Watu wa kiasiliwanatofautiana sana na ni wengi sana katika nchi za afrika masharikina upembe wa Afrika. Katika nchi ya Eritrea kwa mfan, watu wajamii ya Kanama na Nara wanaafiki vigezo vya makao ya awali,kutengwa kijamii na upembezwaji wa kiuchumi. Hata hivyo maishayao ya kipekee ya kitamaduni ya kutegemea mashamba kujikimu,yamemomonyoka kwa kiasi Fulani, kutona na kuingiliwa kwenyeardhi yao. Nchi Ethiopia kuna makundi mbalimbali ya wafugaji kamavile Wasomali, Waafari, Waboran, Wakarayu, Wahameri, Tsemei,na Waebore, wanao kumbwa na viwango tofauti vya athari kutokanje, lakini wengi wao wamevuka mipaka na kuishi katika nchi zaeneo hilo. Pia kuna jamii nyingi za wafugaji wanaoishi katika sehemufulanifulani nchini Sudan. Nchini Kenya, kuna idadi kubwa yamakundi yanayojitambulisha kama asilia na hutegemea ufugaji nausasi-ukusanyaji kujikimu. Makundi haya ni pamoja na Anweri,Borana, Elimolo, Enderois, Gabra, Maasai, Wamunyayaya,Waogiek, Wapokoti, Warendile, Wasamburu, Wasengwer,Wasomali Waturkana, na Wayaaku. Nchini Uganda makundimatatu makuu ni Basongora, Wakaramajong’o na Batwa.Wabasongora ni jamii wafugaji wanaoishi maisha ya kuhamahama.Majanga ya kimaumbile, kuhamishwa na kufukuzwa kwao kwasababu ya maeneo yao kutangazwa kuwa hifadhi za maumbile,vimewatilia msukumo mkubwa na kuhatarisha maisha yao yakitamaduni. Wakaramajong ni jamii ya wapiganaji wahamahamajiwa kadiri ambao maisha na utamaduni wao vimo katika hatari

7. Neno mbilikimo (pygmy) hata hivyo linachukuliwa na watu husika kama matusi, ambaohupenda kuitwa kwa majina ya makundi yao (Baka, Batwa, nk).

6

Page 23: First page ILO.fm

kubwa sana kutokana na mabadiliko ya kimazingira na kuongezekakwa uwaniaji wa ardhi. Wabatwa ni wasasi na wakusanyaji ambaowanahusiana na makun dim engine sawia ya wabatwa wa nchiniRwanda, Burundi na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. NchiniTanzania, kuna jamii za wasasi-wakusanyaji, kama Wa-hadzabe,vilevile wafugaji kama vile Wabarabaig na Wamaasai, ambao wotewanaishi Kaskazini mwa nchi.

• Afriaka ya kusini: Wasan ndio kundi kubwa zaidi katika sehemuhii. Wao wanaishi katika maeneo ya jangwa ya kusini mwa Afrika.Makundi madogo ya Wamaasai (au Basarwa, kama wanavyojulikananchini Botswana) ni pamoja na ju/’hoansi, Bugakhwe, Anikhwe,Tsexakhwe,!Xoo, Naro, G/wi, G//ana, kua, Tshwa, Deti, Khomani,Hoa, =kao//’aesa, Shua, Danisi,na /Xaisa (nchini Botswana)Wakhure na Wakomani (Afrika Kusini) na Ovatue, Ovatjimba naOvazemba (Namibia). Makundi haya yanajichukulia nayanachukuliwa zaidi na wengine kama ‘wakaazi asilia’ wa seheemuwanazoishi na wanajitambulisha wenyewe kama wa kiasili. Ijapowameekuwa sehemu ya utamaduni na uchumi wa kisiasa wawaliowengi kwa viwango vinavyotofautiana, wanaelekea kuishimaisha ya kuhamahama yanayohusisha usasi na ukusanyaji. Mbinuhizi za uzalishaji zinawafanya kutegemea sana maliasili. Licha yakuwepo kwa lugha bainifu ya San, hata hivyo imejifilia katikasehemu kadha wa kadha.

Zaidi ya makundi haya makuu (pamoja na makundi yake madogo), kunaidadi fulani ya makundi ya ziada, madogo na ya nchi mahususi. Mifano ni kama,Wa-Ovahimba wanaoishi kaskazini mwa Namibia, ambao wanaishi maisha yakitamaduni ambayo mashikamano wao kwenye ardhi unachukua nafasimuhimu. Maisha kama haya yanawatenga na maisha ya watu wengi katika jamiina kuwasukuma pembezoni.

4 Sheria ya kimataifa

Ingawa matokeo ya kina ya utafiti huu yamejadiliwa katika sehemu ya B hapochini, mojawapo ya matokeo yake ya muhimu sana linaweza kudokezwa hapa:Mataifa ya Afrika hupinga au hupuuza haki za watu wa asili katika sheria zakena utekelezaji wa sheria hizo. Ugunduzi huu unamulika jukumu muhimu laviwango vya kimataifa kama kioleza cha kuelekeza upande ambakomarekebisho ya kisheria na utekelezaji katika mataifa haya, yanafaakuelekezwa. Ni chini hasa ya hali hizi ndipo jukumu la sheria za kimataifalinabainika zaidi na la maana zaidi. Kwahivyo ni muhimu kwamba utafiti huuunachunguza jinsi haki za watu asili zinaweza kuboreshwa (kuendelezwa)kupitia utekelezaji wa sheria za kimataifa kuhusu haki za kibinadamu, na haswaMkataba wa ILO kifungu nambari 169, Azimio la Umoja wa kimataifa kuhusuhaki za watu asili (UNDRIP) na Mkataba wa Afrika kuhusu haki za kibinadamuna haki za watu (mkataba wa Afrika).

Vyombo viwili vya kimataifa vinavyolenga watu asilia- Mkataba wa ILOnambari 169 kuhusiana na watu wa kiasili na Watu wa makabila katika nchihuru na UNDRIP- vinafaa sana kufanya majadiliano ya kuboresha na kulindahaki zao.

7

Page 24: First page ILO.fm

Mkataba wa 169 wa ILO

Mkataba wa 169 wa ILO uliokubaliwa mnamo mwaka wa 1989, ulianzakutumika mwaka 1991. Ndio chombo cha lazima cha kimataifa ambachokinashughulikia hususan haki za watu asili. Hata hivyo, hamna nchi ya Afrikaimetia sahihi mkataba huu. Mkataba wa 169 wa ILO unachukua nafasi yamkataba wa 107 wa ILO- mkataba kuhusu watu wa kiasili na wa makabila,uliokubaliwa mnamo mwaka wa 1957- ambao ulitiwa sahihi na mataifa sita yaAfrika8 na unabaki wa lazima kwa mataifa haya yaliyoutilia sahihi lakini ambayobado hayajatia sahhihi kwenye mkataba wa 169.

Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Watu Asili

Baada ya mchakato mrefu wa kuunda rasimu kwenye Umoja wa Kimataifa,Baraza la Haki za Kibinadamu lilikubali UNDRIP, Juni 2006. kati ya nchiwanachama kumi na sita wa Baraza la Haki za Kibinadamu, ni nne tu(Kameruni, Mauritius,Afrika Kusini na Zambia) yaliipigia kura UNDRIP.Mataifa ya Afrika yalionyesha wasiwasi wao na kuchangia kuhairishakukubaliwa kwa UNDRIP na Barasa Kuu la Umoja wa Mataifa.9 Muungano waAfrika ulichukua msimamo wa pamoja kuonyesha wasiwasi wao kuhusiana naUNDRIP10 na kukubali kuhairishwa kwa mjadala wa Umoja wa Mataifakuhusu UNDRIP. Muungano wa Afrika ulilipa kundi la Afrika jukumu lakulinda masilahi na mahitaji ya Afrika kuhisu athari za UNDRIP11 kisiasa,kiuchumi, kijamii na kikatiba. Kikundi cha Afrika kilitoa taarifa likielezamahitaji12 yao na kupendekeza kwamba marekebisho zaidi yafanyiweUNDRIP.13 Katika mwezi wa Machi mwaka 2007, kikundi cha wasomi kutokaAfrika lilitoa majibu ya kupinga ardhihali14 ya kikundi cha Afrika. Katika kikaochake cha 41, Mei 2007, Tume ya Afrika iliitikia kwa kukubali Wazo laUshauri kuhusu Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu haki za Watu wa Asili,ambamo ilijaribu ‘kutuliza wasiwasi ulioonyeshwa kuhusiana na haki zakibinadamu za watu wa asili’ na kutaja tena ‘utayari wake kwa mapatanoyoyote baina yake na Mataifa ya Afrika kwa lengo la kuharakisha kukubaliwakwa Azimio’

Baada ya kushinda pingamizi hizi za awali, na baada ya marekebisho kadhaakufanyiwa matini ya awali, Baraza kuu la lilikubali UNDRIP mnamo Septemba7, 2007. Mataifa thelathini na tano ya Afrika yalikuwa kati ya mataifa 143yalipiga kura ya kuunga mkono UNDRIP; matatu yalisusia (Burundi, Kenyaand Nigeria); na kumi na tanoi (Chad, Côte d’Ivoire, Equatorial Guinea,Eritrea, Ethiopia, Gambia, Guinea-Bissau, Mauritius, Morocco, Rwanda, São

8. Angola, Misri, Guinea-Bisau, Malawi, na Tunisia.9. Tazama k.f ‘Rasimu ya Kumbukumbu ya Msaada’ (Draft Aide Memoire) ya Jopo la Afrika

kuhusu asimio ya tarehe 9 Novemba 2006, New York, ambamo Jopo hilo lilionyeshawasiwasi wake kuhusu k.m kukosekana kwa fasili; kuhusishwa kwa haki ya kujibainisha; nakuitisha uhairishaji wa kutumiwa kwa azimio hili’ (ukurasa wa 9.1).

10. Angalia pia Uamuzi wa Muungano wa Afrika kuhusu Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusuHaki za Watu wa Asil, Doc Assembly/AU/Dec.141 (VIII) (Januari 30 2007).

11. AU Doc Assembly/AU/Dec.141 (VIII), ukurasa 3.12. Rasimu ya ardhihali ya kikundi cha Afrika: Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu haki za

Watu wa Kiasili (Novemba 9, 2006).13. Rasimu ya Matini Pendekezwa ya Azimio la Umoja wa Mataifa iliyotolwa na Kikundi cha

Afrika kuhusu Haki za Watu wa Kiasili (Mei 8 2007), inapatikana kwenye http://www.ishr.ch/hrm/nymonitor/new_york_updates/african_text_draft_8_may_2007.pdf(yaliangaliwa September 24, 2007).

14. Waraka wa Itikio la Wataalamu wa Kikundi cha Afrika kwa ‘ Rasimu ya Ardhihali yakikundi cha Afrika kuhusu Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Watu waKiasili’(Machi 21, 2007). Ujumbe huu ulitiwa saihihi na Wataalamu wanaoongoza kumi nasaba wa haki za kiasili kutoka katika maeneo kadhaa tofauti.

8

Page 25: First page ILO.fm

Tomé e Principe, Seychelles, Somalia, Togo, and Uganda) yalipiga kura mkonojapo hayakuhudhuria. Ni mataifa manne tu ndiyo yaliyopinga UNDRIP:Marekani, Kanada; New Zealand na Australia.

Mikataba ya Umoja wa Matifa kuhusu Haki za Kibinadamu

Ijapokuwa hakuna mkataba wowote kati ya ile muhimu ya Umoja waMtaifa unashughulikia hususan haki za watu wa kiasili, kuna baadhi ya mikatabahii hasa Mkataba wa kimataifa kuhusu Haki za Kiraia na Kisiasa (ICCPR),Mkataba wa kimataifa kuhusu Haki za Kiuchumi Kijamii na kitamaduni(ICESCR), mapatano ya ya kuondoa kila aibaguzi wa kikabila (CERD)napatano kuhusu Haki za Watoto (CRC), ina viwango vya haki za kibinadamuvinavyofaa watu wa asili. ICCPR (katika kifungu cha 24) na CRC (Kifungu30)15 ina idhini ambazo zinahusiana kwa karibu na mahitaji ya watu wa kiasili.Baadhi ya mashirika angalizi yamefafanua baadhi ya mikataba inayowafaa watuwa kiasili. Kamati ya CERD, kwa mfano, ilikubali Mapendekezo ya Jumla,manane kuhusu kujitambulisha (mwaka wa 1990), na 23 kuhusu haki zakibinadamu (mwaka 1997). Kamati ya CRC wakati Fulani pia imehusishamahitaji ya watu wa kiasili katika Maoni yake ya Jumla.16

Mataifa yaliyotafitiwa hapa yametii mingi ya mikataba ya Umoja wa Mataifakuhusu haki za kibinadamu. Hata hivyo mataifa machache yamekubali kutumiataratibu badala za kushughulikia malalamiko ya kibinafsi. Ni idadi ndogo tu yamalalamiko haya ya kibinafsi imewasilishwa. Ni katika arifa moja tu ya kibinafsiiliyowasilishwa dhidi ya taifa la Afrika, Namibia17 ambapo Kamati ya KuteteaHaki za kibinadamu (HRC) iliamuru jambo la umuhimu kwa watu wa kiasili,yaani, haki ya kutumia lugha ya waliowachache katika mawasiliano rasmi naserikali.

Kuhusu sharti la mataifa yaliyoko chini ya mikataba hii kuwasilisha ripoti zakila baada ya kipindi Fulani, kijumla sharti hili limetimizwa kulingana naCRC.Rekodi ya mataifa mengine ya Afrika yaliyo chini ya mikataba mingine, hususanICESCR, haivutii sana. Mashirika ya mikataba yanapopewa nafasi, mara kwamara yametoa mapendekezo kwa mataifa kuhusiana na watu wa Kiasili wakatiwa kukubali maoni ya mwisho ya ripoti za Mataifa.

Kamatai ya CERD, katika miaka ya hivi karibuni imetilia maanani sana sualala watu wa kiasili wakati wa kuzikagua ripoti za mataifa wanachama, kamailivyo mfano wa ukaguzi wa ripoti za hivi karibunisa sana za Namibia,Botswana, na Tanzania

Katika kukagua ripoti ya hivi karibuni ya Namibia, Kamati ya CERDilionyesha wasiwasi wake kuhusu ukosefu wa kutambulika kwa haki za jamii zakiasili kumiliki ardhi ambazo ziliyamiliki kitamaduni, na kupendekeza kwambaTaifa libainishe ardhi hizi na kuunda taratibu za kisheria za ndani kusuluhishamadai ya jamii za kiasili18 kuhusu ardhi. Kamati iliendelea kuhimiza serikalikuhakikisha kwamba mbuga kitaifa zilizowekwa katika ardhi za mababu zajamii za kiasili, zinawaruhusu kujiendeleza kiuchumi na kijamii na kwambaserikali irejeshe zile ardhi na himaya zao au kutoa mikakati ya kutosha ya

15. Angalia pia kifungu cha 17 na 19 cha Tume ya kutetea haki za watoto (CRC).16. Tazama k.m Wazo la Jumla Namb. 9, ‘Haki za watoto walio na ulemavu’ (2006) uk. 79 na

80; na Wazo la Jumla Namb.11, ‘watoto wa kiasili na haki zao chini ya mkataba’ (2009). 17. Diergaardt v Namibia, Arifa ya 760/1997, UN Doc CCPR/69/D/760/1997 (Septemba 6

2000). Angalia pia UN Doc CCPR/CO/81/NAM.18. Ripoti ya Kamati kuhusu Uondoaji wa Ubaguzi wa Kikabila. Stakabadhi ya Umoja wa

Mataifa A/63/18 (2008), Uk 299.

9

Page 26: First page ILO.fm

kufidia pale ambapo jamii hizo zimenyang’anywa ardhi/ mashamba yao.19 Piailiuliza serikali kushughulikia hali ya umasikini uliokithiri ambamo watu wakiasili hujikuta ndani yake na kuchochea ukuaji wa kiuchumi na maendeleo yajamii hizo, hasa kuhusiana na elimu na afya. Hasa, kamati ilionyesha wasiwasiwake kuhusu kiwango kikubwa cha maambukizi ya virusi vya HIV baina yaWa-san, kushindwa kupata stakabadhi za kujitambulisha, kiwango chao chachini cha kuhudhuria shule na muda wa maisha wa chini kiasi. Ikizungumziashida ya visa vingi vya kubakwa kwa wanawake Wa-San na watu wa jamiizingine, kamati ilipendekeza kwamba serikali ichukue zote muhimukuhakikisha kwamba uchunguzi wa haraka, wa kina na huru unafanywa kuhusumadai ya ubakaji wa wanawake Wa-San na kwamba kuzidishe juhudi zakezinazolenga kupigana na ubaguzi dhidi ya Wa-San.20

Ripoti pamoja ya Botswana ya kumi na sita na kumi na saba,iliyochunguzwa mwaka wa 2005, inatoa mfano mwingine.21 kamati ya CERDiligundua kuhamishwa kwa Baraswa kutoka kwenye mbuga ya wanyama yaKalahari ya Kati na kupendekeza kwamba serikali iache kuchukua hatuaambayo athiri matokeo ya kesi ya kortini ambayo ilikuwa ikiendelea wakatihuo.22 Sehemu nyingine ya kutilia shaka ambayo kamati ilibainisha ni ukosefuwa kupata haki kwa ‘watu masikini ambao wengi wao ni wa makundi ya San/Baraswa na wengine wasio wa makabila ya Tswana’. Kwa hivyo kamatiilipendekeza kwamba serikali itoe msaada wa kutosha wa kisheria na hudumaza ufasili, hasa kwa makundi ya makabila yanayokumbwa na hali ngumu zaidi,ili kuhakikisha kwamba wanapata haki kikamilifu.

Kuhusu ripoti ya Tanzania iliyokaguliwa hivi karibuni,23 kamati ya CERDiligundua kuwepo kwa ukosefu wa habari kuhusu makabila yaliyohatarini, sanasana watu wa kuhamahama, wakiwa Barbaig, Maasai na Hadzabe 24 kati yawengineo, na kupendekeza kwamba chama cha serikali kitoe taarifa ya kinakuhusu hali yao.

Kwenye maoni yake ya mwisho kuhusu ripoti ya Algeria, Tume ya KuteteaHaki za kibinadamu (HRC) ilirejelea kutotambulika kwa Wa-Berber25(mnamomwaka wa 1992)26 na ikaonyesha wasiwasi wake kwa kina kuhusu ‘sehemukubwa watu, wakiwemo Waberber ambao haki za lugha zimezuiliwa kutokanana Amri ya lugha ya Kiarabu, ambayo inakifanya kiarabu lugha ya pekee yaumma (mwaka wa 1998).27 Katika maoni yake ya mwisho ya hivi karibuni,HCR, haikushughulika na masuala ya kiasili wala mengine ya waliowachache.28

Pengine masuala haya yalifunikwa na masuala ya dharura na dhahiri sana yaukiukaji wa haki zakibinadamu kuhusiana na kupotea, mateso, kufungwakusiko halali na harakati za kupigana dhidi ya ugaidi. Kwahivyo tume yakutetea haki za kibinadamu- HCR- haina utekelezaji thabiti wa kuchunguzaiwapo serikali zinatii kifungu nambari 27, ambacho kinashughulikia haki zawaliowachache.

19. Ripoti ya kamati kuhusu uondoaji wa Ubaduzi wa ubaguzi wa kikabila UN Doc A/63/18(2008), uk. 300.

20. Ripoti ya kamati kuhusu uondoaji wa Ubaduzi wa ubaguzi wa kikabila UN Doc A/63/18(2008), uk.303.

21. UN Doc CERD/C/BWA/CO/16, Aprili 4, 2006.22. Ukurasa wa 12.23. UN Doc CERD/C/TZA/CO/16, 27 Machi 2007.24. Ukurasa wa 16.25. Istilahi ‘Waberber’ inachuliwa na makundi inayoyarejelea kama ya kuwashusha hadhi.

Istilahi hii haitumiki sana, na watu inaowarejelea ni Amazigh wa kaskazini mwa Afrika. 26. Un Doc CCPR/C/79/Add.1, ya tarehe 25 Septemba 1992, uk. 6.27. UN Doc CCPR/C/79/Add.95, ya tarehe 18 Agosti 1998, uk. 15.28. UN Doc CCPR/C/DZA/CO/3, ya tarehe 12 Disemba 2007.

10

Page 27: First page ILO.fm

Kamati ya CRC ilipozingati Ripoti ya seriakali ya Algeria mnamo mwakawa 2005, kamati ilitilia maanani sana watoto wa kiasili. Iligundua kwambamahitaji ya awali kuhusiana na watoto wa jamii za kuhamahamahayajashughulikiwa ipasavyo. Kisha kamati ilirudia na kufafanua zaidi wasiwasiwake ulioonyeshwa awali kuhusiana na usajili wa watoto wanaozaliwa, elimuna lugha.29 Kamati iliendelea na kuiliza Algeria kutoa data ya takwimuzisizojumlishwa pamoja hususan kuhusu makundi yaliyohatarini, yakiwemo yawatoto wa Amazigh30 na kueleza ni ulinzi gain unapewa watoto walio katikamakundi ya waliowanyonge, hasa ili kulinda utambulisho wa watoto waKiamzigh.31 Ikumbukwe kuwa, hata kama kamati inarejelea kifungu nambari30 cha CRC ambacho kinazungumzia haki za waliowachache na watoto wakiasili, kamati haitumii neno ‘Asili’ badala yake ilichagua kutumia‘waliowachache’ mfano mwingine ambapo kamati inajihusisha na suala lawatoto wa kiasili ni kuzingatia kwake kwa ripoti ya Kongo mwaka wa 2006.32

Uchunguzi Bia wa Kimuhula

Uchunguzi Bia wa Kimuhula unaofanywa na Baraza la kutetea haki zaKibinadamu lililoanzishwa mwaka wa 2006, linatoa nafazi zaidi ya uchunguziwa kimataifa wa kujitolea kwa Serikali kuhusiana na haki za watu wa kiasili.Kwa mujibu wa Afrika, kwa sasa uchunguzi Botswana na Algeria umeibuawasiwasi kuhusiana na masuala ya watu wa kiasili. Kuhusu Botswana, baadhiya mataifa yaliuliza maswali kuhusiana na utekelezwaji kamili wa hukumukuhusu Basarwa katika Mbuga ya wanyama ya Klahari ya Kati. Katika wasilisholake, Algeria ililiambia Jopokazi kwamba tangu mwaka wa 2002, katiba iliwapaKitamazi (Tamazight) hadhi ya kuwa lugha ya taifa na kwamba zaidi yawanafunzi 100,000 hadi kufikia wamesoma Kitamazi katika shule za kiserikali,na kwamba mpango maalumu wa kufunza walimu umeanzishwa ili kuendeleakufunza Kitamazi.33 Hali ya kidharura tu ya mpango na ukosefu wamapendekezo maalum unaibua maswali kuhusu ufaafu wa mchakato wauchunguzi.

Katibu maalum

Mnamo mwaka wa 2001, Ofisi ya Katibu Maalum wa Umoja wa mataifakuhusu hali ya haki za kibinadamu na uhusru wa kimsingi wa watu wa kiasiliilianzishwa. Ofisi ya katibu maalum imefanya kazi maalumu nyanjani katikamataifa matatu ya Afrika- Afriaka Kusini (mwaka wa 2005),34 Kenya (2006),35

na maajuzi kabisa, Machi 2009, katika nchi ya Botswana. Katika ripoti kuhusuKenya, ofisi ya katibu maalum ilependekeza kwamba haki za ‘wafugaji wakiasili na jamii za wawindaji-wakusanyaji’ zinapaswa kujikita katika katiba nakwamba ‘sheria maalum iwekwe, hata ‘uteuzi maalum ikibidi’.36 KuhusuBotswana, ukatibu maalum ulitambua kuboreka kwa hali za watu wa kiasilikutokana na kuongezeka kwa upatikanaji wa huduma muhimu, lakini piaugundua kuwa utekelezwaji wa mipango mara nyingi ‘hauzingatii lugha,utamaduni na urithi wa wale wanaohusika zaidi.37

29. UN Doc CRC/C/15/Add.269, ya tarehe 12 Octoba 2005.30. Ukurasa wa 20 na 21.31. Ukurasa wa 83 na 84.32. Stakabadhi ya Umoja wa Mataifa CRC/C/COG/CO/1, ya tarehe 20 Octoba 2006 33. UN Doc A/HRC/8/29 (23 Mei 2008).34. UN Doc E/CN.4/2006/78/Add.2.35. UN Doc A/HRC/4/32/Add.3.36. UN Doc A/HRC/4/32/Add.3, uk. 91.37. Umija wa Mataifa (Habari motomoto kutoka Umoja wa Mataifa), Wataalamu wa Umoja

wa Mataifa kuhusu watu wa Kiasili wazuru Botswana.

11

Page 28: First page ILO.fm

Mikataba mingine ya ILO

Kando na mkataba wa 169 wa ILO, mikataba mingineyo ya ILO ni muhimukwa mjadala huu. Muhimu sana ni mkataba wa ILO wa 111 unaohusu Ubaguzikwa mujibu wa Ajira na Kazi (mkataba wa Ubaguzi katika ajira), Mkataba waILO wa 138 kuhusu umri wa chini sana wa kuajiriwa kazi (Umri wa chini ) naMkataba wa ILO wa 182 kuhusu Kupigwa marufuku na Hatua ya Harakakatika Kukomesha Aina Mbaya zaidi za Ajira ya Watoto (Aina Mbaya zaidi zaAjira ya Watoto). Mataifa yote ya Afrika ni wanachama wa mkataba wa 111wa ILO, 47 yametia sahihi mkataba wa 138 na hamsini ni wanachama wamkataba wa 182. Mikataba ni umuhimu mkubwa si kwa sababu tu yayaliyomo, lakini pia kwa sababu ya ukweli kwamba imetiliwa sahihi kwa wingimno. Katika Mwongozo wa ILO kwa Mkataba wa 111-‘Ukomeshaji waUbaguzi dhidi ya watu wa kiasili na wa makabila katika ajira na kazi’(Mwongozo), imeonyeshwa mjinsi mkataba huo unaendeleza upatikanaji sawawa kazi ya heshima kwa watu wa kiasili na wa makabila. Mkataba dhidi yaUbaguzi Kazini unafasili kanuni ya usawa wa nafasi za kazi na jinsi yakuchukiliwa katika muktadha wa kazi na pia unatoa hatua na tararibu kadhaaambazo ni lazima mataifa yanayoutia sahihi kuzingatia ili kuheshimu,kuendeleza na kufanikisha kanuni hii. Mwongozo huu unadhamiria kubainishahali ambazo zinaweza kuhusisha ubaguzi dhidi ya watu wa kiasili. Una orodhambili za kukugaulia, moja ikitoa maelekezo ya kuchunguza hali thabiti kwalengola kubainisha ubaguzi uliopo kinyume na mkataba; na orodha nyingineinasaidia watu wa kiasili na wa makabila pamoja na washikadau muhimu katikakuchunguza sera za kitaifa ili kuimarisha usawa wa nafasi za kazi na jinsi yakuchukuliwa kazini katika nchi zao. Kwa kushauri kuhusu umri wa chini kabisakuajiriwa kazi kuwa ni miaka kumi na tano, Mkataba Kuhusu Umri wa Chiniunadhamiria kushughulikia suala ajira ya watoto.

Mkataba huu pamoja na mkataba kuhusu Aina mbaya zaidi za ajira yawatoto, unazungumzia suala linaloathri watoto wa kiasili kwa namnaisiyolingana. Watoto wa kiasili aghalabu wamo katika hatari ya aina mbayazaidi za ajira ya watoto, haswa wakati ambapo mazao ya ufugaji yanapopunguana kuwepo na uwewezekano mkubwa kufanya kazi mijini, ikiwemo kufanyakazi katika nyanja za utalii na ukahaba. Mkataba dhidi ya ajira ya watotoiliyombaya zaidi unayauliza mataifa kukomesha vitendo hivi, pamoja na‘utumwa wa madeni’ na ‘utwana’, ambavyo ndivyo wasifu wa watoto wakiasili. Kwa kutumia mbinu pana kwa misingi ya haki, Mwongozo wa ILO waKupigana na Ajira ya watoto baina ya watu wa Kiasili na wa Makabilaunaambatanisha dhana ya ajira ya watoto na mambo mengine yanayochangiakama kupataji wa elimu na umasikini. Mikataba mingine muhimu ni pamoja naMkataba wa 29 Dhidi ya Ajira ya lazima wa mwaka 1930.

Mkataba wa Afrika

Ijapokuwa mkataba wa Afrika haushughulikii haki za watu wa Kiasili kwawazi, imekubaliwa kijumla kwamba dhana ya ‘watu’ katika Mkataba inatumikakwa na inahusisha watu wa kiasili. Haya pia ndiyo maoni ya Jopokazi laWataalamu la Tume ya Afrika kuhusu watu/jamii za kiasili(jopokazi kuhusuWatu wa Kiaasili). Awali, Tume ilikuwa ikipinga dhana ya watu wa kiasilibarani Afrika hadi pale ilipofanya kikao chake cha 29 kwa masaada wakamishna wa zamani BarneyPityana ndipo Tume iliposikiliza suala hili. Tanguhapo suala hili limekuwa kwenye ajenda za vikao vya kawaida vya Tume yaAfrika. Kamati Teule ya Tume hii liundwa baadaye (mwaka wa 2001) ilikuchunguza dhana ya watu/jamii za kiasili barani Afrika, kuchunguza athari zaMkataba wa Afrika kwenye masilahi ya jamii za kiasili na kuangalia

12

Page 29: First page ILO.fm

mapendekezo mwafaka ya kusaidia katika kuchunguza na kulinda haki za watu/jamii za kiasili. Hata ingawa mataifa ya Afrika yamebisha sana kwamba dhanaya watu wa kiasili haina maana katika Afrika, hii hurejelea uelewa mwinginetofauti wa dhana ya watu asilia na jinsi inavyoeleweka kwenye sheria yakimataifa. Maendeleo kwenye kiwango cha kimaeneo,hususan yaliyo chini yamfumo wa haki za kibinadamu wa Afrika, yanaonyesha hatua fulani za kutajikaambazo zimechukuliwa na mataifa ya Afrika kwa masilahi ya watu wa kiasili.Maendeleo haya yalifikia kilele katika ripoti ya Tume ya Afrika, -Ripoti yaKamati Teule ya Wataalamu wa Tume ya Afrika kuhusu haki za kibinadamu nawatu ya mwaka 2005 kuhusu watu/ jamii za kiasili,38- ambayo inayakubalikikamilifu makundi fulani kama watu wa Kiasili na kupendekeza kuwepo kwamfumo wa kisheria wa kulinda haki za makundi haya ya kiafrikayaliyopembezwa.

Mataifa yote ya Afrika isipokuwa Morocco, ni wanachama katika Mkatabawa Afrika. Baada ya kuwa mwanachama, mataifa moja kwa moja yanakubalihaki za watu binafsi kuwasilisha malalamiko (‘arifa’) yao kwa Tume ya Afrika.Hakuna hata moja ya arifa zinazohusu haki za watu iemkamilishwa kamainavyostahili. Kesi ya kwanza, kati ya Kamati ya madai ya Ardhi ya Bakweri nacameroon,39 iliyowasilishwa kwa niaba ya ‘watu wa kiaasili waliowachache’nchini Cameroon- Wabakweri, iliamuliwa kuwa isiyokubalika kwa sababu yakutotumia kikamilifu suluhu zote zilizomo katika nchi hiyo. Ijapokuwamalalamiko haya yalishutumu ukiukaji wa haki za kibinafsi na za watu, uamuziwa kutegemea ukubalifu wake hauonyeshi majaribio yoyote ya kufasiliWabakweri kama ‘watu wa kiasili’. Katika kesi ya pili baina ya Baraza la Hakiza Wanuak na Ethiopia, Wanuak-ambao wanajitambulisha kama mojawapo wa‘kundi la watu kiasili waliowachache’, walidai kuwepo kwa ukiukajiunaotokana na mauaji ya kinyama, kupotea kwa watu, kuzuiliwa bilakuhukumiwa na uharibifu wa mali. Wasilisho la tatu- baina ya Kituo chaMaendeleo ya Haki za waliowachache (CEMIRIDE) (kwa niaba ya jamii yaEndorois) na Kenya,40 lililo wasilishwa mwaka wa 2003 na ambalo badohalijashughulikiwa, limefungamanishwa sana na uanachama wa waathiriwahawa katika kikundi cha watu wa kiasili. Wa-Endorois, ambao ni jamii yawafugaji nchini Kenya wenye idadi ya takriban watu 60 000, wanadai kwambakuhamishwa kwao kutoka kwenye ardhi ya mababu zao ili kutoa nafasi yakuweka mbuga ya wanyama (Mbuga ya wanyama ya Ziwa Bogoria) kunakiukahaki zao kama watu binafsi (kwa mfano haki yao ya kuendeleza dini yao) nahaki zao kama ‘watu’ (kama haki kuuza mali na haki ya kujiendeleza).

Ni vigumu kuchanganua maoni ya kuhitimisha ya Tume yaliyokubaliwabaada ya kuchunguza Ripoti za Mataifa, kwa sababu hayajachapishwa kwamfululizo. Hata hivyo, kutokana na taarifa zilizopo inaonekana kuwa Tume yaAfrika huwasiliana na mataiafa yanayoripoti kuhusu masuala ya kiasili baadakuazishwa kwa Jopokazi linalohusika na Jamii za Kiasili. Katika kikao chake cha29 cha mwaka wa 2001, kwa mara ya kwanza, Tume ili ilizua maswali kuhusuhali za watu wa kiasili katika mataifa yaliyotoa ripoti.41 Tangu hapo kipengelehiki kimeibuka mara kwa mara wakati wa kuzichunguza ripoti za Mataifa namara nyingine kikwa kama sehemu ya maoni ya kuhitimisha. Kufuatiakuzingatiwa kwa ripoti yake kwanza ya kimuhula katika kikao hicho, Namibiailitokea kuwa nchi ya kwanza kulengwa na maoni ya kuhitimisha kuhusiana na

38. Tume ya Afrika ya kushughulikia haki za kibinadamu na watu- Ripoti ya Kamati Teule yaWataalamu ya Tume ya Afrika kuhusu Watu/jamii za kiasili (2005).

39. Arifa ya 260/02, iliyoamuliwa katika kikao cha Tume cha 36, Nov-Des 2004, bado haimokatika Ripoti ya Matukio ya Tume.

40. Wasilisho la 276/2003.41. Ripoti ya Kamati Teule inayojishughulisha na jamii za kiasili (2005) 78.

13

Page 30: First page ILO.fm

watu wa kiasili.42 Katika mfano mwingine, maoni ya kuhitimishayaliyokubaliwa baada ya kukagua ripoti ya pili ya Afrika Kusini mwaka wa2005, yalipendekeza kwamba Afrika Kusini ‘ichukue hatua zote mwafakakuhakikisha kuwa haki za watoto wa makundi ya waliowachache-wakiwemoWakhoi-khoi na Wasan- zimehakikishwa, hasa zile zinazohusiana nautamaduni, dini, na kupata habari.43 Mataifa bado hayazingatii sana kipengelehiki katika Ripoti zao, japo, kama ilivyo mfano wa ripoti ya Uganda, ambayoinataja tu kwamba Uganda ‘ina jamii za kiasili 56 tofauti’ ambazo zimegawikachini ya makabila manne makuu; Wabantu, Wanailoti, Wanailo-Hemiti nawaluo.44 Katika mfano huu, kama ilivyo katika mingine mingi, mashirika yasiyoya kiserikali yaliandaa na kuwasilisha ripoti za kisiri au ripoti sambambakwanjia isiyo rasmi45 ambazo aghalabu ziliarifu maswali yaliyoulizwa namakamishana kwa wawakilishi wa serikali.

Vyombo vingine vya Kiafrika

Vyombo vingine vya Muungano wa Afrika, kama Mkaba wa Afrika kuhusuMaumbile uliofanyiwa marekebisho, vinaweza kuwa vya umuhimu kwa watuwa kiasili. Kulingana na Mkataba huu, ni lazima mataifa kuheshimu ‘haki zakitamaduni na haki za mali ya kiusomi za jamii za maeneo husika zikiwemohaki za wakulima’.46 Utaratibu wa Kiafrika wa kuchunguza masuala ya Rika(APRM) haulazimu hasa kwamba nchi zinzoshiriki kuripoti hususan kuhusuulinzi wa watu wa kiasili. Lengo nambari 9 chini ya mada ya jumla ‘Demokrasiana Utawala wa Kisiasa, linaloshughulikia haki za ‘makundi yaliyohatarini’ nimada mwafaka zaidi ambayo ingeweza na lazima ishughulikie suala hilimuhimu. APRM ya Kenya hairejelei ‘watu wa kiasili’. Ripoti inakosoa‘mtazamo na mwelekeo wa kutenga’ makundi mbalimbali ambayo hayanaufahamu wowote wa matatizo yanayokabili makundi mengine au jinsi yakushughulikia kwa pamoja masuala yanayofanya tao juu ya matatizo yakimuundo yanayowakabili makundi binafsi.47 Vilevile ripoti ya APRM ya nchiniRwanda haitumii istilahi‘asili’ lakini badala yake ikachagua kutumia ‘Wabatwawaliowachache’ Ripoti za Uchunguzi za APRM ya Ghana na Afrika Kusinizimebaki kimya kuhusiana na masuala ya watu wa kiasili.

42. Tume ilisisitiza kwamba ‘kujitolea katika haki za kibinadamu kutazaidia nchi kukabilana nawasiwasi ...’. Pia iliona ‘hatua ambazo hazitoshi za kushughulikia mahitaji maaalum yaw amakundi yaliyomo hatarini kama Wahimba na Wasan’ na ikapendekeza kwamba serikali yaNamibia ‘ianzishe hatua za kusaidia makundi haya kufurahia haki zilizomo katika Mkatabaharaka iwezekanavyo, kwa msingi wa kuweko kwa usawa na makundi mengine nchini(maoni ya kuhitimisha kwa ripoti ya Namibia, kikao cha 29 -2001).

43. Mahitimisho na mapendekezo ya Ripoti juu ya kwanza ya kimuhula ya Jamuhuri ya AfrikaKusini, kikao cha 38 cha Tume hii,21 Novemba–5 Disemba 2005 (iko kwenye faili yamwandishi), aya 34.

44. Ripoti ya kimuhula ya Uganda <http://www.achpr.org/english/state_reports/ 40_Uganda%20periodic%20report_Eng.pdf> (alingaliwa  Disemba 2008) uk. 3.

45. Tazama ‘Ripoti Badala kuhusu Ripoti ya Kimuhula ya nchi ya Uganda kwa Tume ya Afrikaya kushughulikia Haki za kibinadamu na haki za watu, iliyowasilishwa na Shirika la Umojawa Wabatwa nchini Uganda (UOBDU), Mpango wa watu wa maeneo ya misitu (FPP) naKamati Teule ya Kimataifa inayoshughulika na masuala ya kiasili (IWGIA).

46. Revised African Nature Convention, Art XVII(1) & (2). 47. Kama hapo juu.

14

Page 31: First page ILO.fm

1 Ukubalifu na Utambuzi

1.1 Utaangulizi

Sehemu ya kwanza ya ripoti inaorodhesha baadhi ya vigezo muhimuvinavyotumika- na watu wa kiasili na wengine- kuta kutambua watu wa kiasilibarani Afrika. Kwa kurejelea uelewa wa dhana ya watu wa kiasili kama ilivyokatika mfumo wa kimataifa na kimaeneo wa kutambua watu hawa, Sura hiiinatalii baadhi ya mbinu zinazotumiwa kwenye kiwango cha kitaifa- katika nchi24 zilizotafitiwa- kwa utambulishaji na kuwakubali watu wa kiasili kisheria.Mijawapo ya changamoto zinazowakumba watu wa kiasili katika kuzilinda hakizao za kimsingi na uhuru, ni kukosa kutambuliwa kirasmi na serikali kamamakundi yaliyo na mahitaji, utamaduni na hali za maisha maalum.

Mfumo wa kimataifa na kimaeneo wa kutambulisha watu wa Kiasili

Kabla ya kueleza hali na mielekeo katika utambuzi wa kisheria wa watu wakiasili katika mataifa ya Kiafrika zilizotafitiwa, ni faradhi kutoa muhtasariwamifumo ya kisheria na kidhahania ya kimataifa na kimaeneo inayotumika katikakuwatambulisha watu hawa.

Jamii ya kimataifa haijakubali fasili yoyote ya watu wa kiasili. Kwa hakika,msimamo wa mashirika mengi ya kimataifa yaliyopewa jukumu la kuchunguzaau kushughulikia haki za watu wa kiasili (ukiwemo msimamo wa vyombo vyakimataifa vilivyopo, kama Mkataba wa 169 wa ILO ambao hususan unazilindahaki za watu hawa, poamoja na msimamo wa Tumre ya Afrika ya kutetea hakiza Kiabinadamu na watu) ni kwamba fasili kamili ya watu wa kiasili si muhimuwala haihitaajiki. Ni jambo la maana na la kujenga kujaribu kueleza kimuhtasarisifa kuu ambazo zinaweza kutusaidia kubainisha watu na jamii za kiasili ni kinanani Afrika. Zaidi ya hayo, kukosekana kwa fasili hakufai kuwa kizuizi katikakushughulikia masuala halisi yanayowakumba watu wa kiasili.

Katika mwaka wa 1986, Utafiti kuhusu ubaguzi dhidi ya watu wa kiasili(utafiti wa Martínez Cobo) ulipendekeza fasili toshelevu ya awali ya watu wakiasili.48 Hata hivyo, mtindo wa kimsingi wa kuwatambulisha watu wa kiasiliumekuwa ule wa kutumia vigezo kufafanua makundi kama hay, na sio kutumiafasili iliyokwisha amuliwa. Makala tendaji kuhusu dhana ya ‘watu wa kiasili’ yaKamati Teule ya Umoja wa mataifa inayohusika na watu wa kiasili,inaorodhesha baadhi ya mambo yanayochukuliwa kuwa muhimu kwakueleweka kwa dhana ‘asili’ na mashirika ya kimataifa na wataalamu wa

48. Jamii, watu na nchi za kiasili ni zile ambazo, kutokana na mwendelezo wao wa kihistoria najamii za kabla ya uvamizi na kabla ya ukoloni ambazo zilikuweko katika himaya zao,zinajichukulia kuwa ni tofauti na vitengo vingine vya jamii ambazo kwa sasa zinatawalakatika himaya hizo, au kama sehemu ya jamii hizo. Zinaunda vitengo vya jamii vya sasavisivyo na nguvu na zimeazimia kudumisha, kuendeleza na kupitisha himaya zao za jadi naupekee wa kabila lao kwa vizazi vijavyo, kama msingi wa kuendelea kuwepo kama watu,kulingana na mitindo yao ya kitamaduni, asasi za kijamii na mifumo yao ya kisheria’ Utafitiwa tatizo la ubaguzi dhidi ya watu wa kiasili. (UN Doc E/CN.4/Sub.2/1986/7).

B Muhtasari wa matokeo ya utafiti

15

Page 32: First page ILO.fm

kisheria.49 Zaidi ya hayo, Kifungu nambari 33 cha Azimio la Umoja wa Mataifakuhusu Haki za Watu wa Kiasili (UNDRIP) kinarejelea haki za watu asilikujiamulia utambulisho wao na taratibu za kuwa watu wa kundi hilo.

Mkataba wa 169 wa ILO hauelezi watu wa kiasili ni kina nani; badala yakeuna vigezo vinavyotumika kuwatambulisha hawa watu katika nchi wanamoishi.Wakati wa kurasimu Mkataba huu, ilionelewa kuwa kutoa fasili ya watu waKiasili kungepelekea kuachwa nje kwa makundi ambayo yangefaidika kutokanana haki zilizoafikiwa katika Mkataba. Vigezo vilivyo katika taarifa ya matukiokatika Mkataba wa 169 ni halisi na vya kidhahania:

• Vigezo halisi ni pamoja na watu katika nchi huru ambaowanachukuliwa kuwa wa kiasili kwa misingi ya utangulizi wakihistoria; na watu waliobaki na baadhi au asasi zote za kijamii,kiuchumi na kisiasa, ambao hali zao za kitamaduni na kiuchumizinawatofautisha kutoka kwa sekta zingine za jamii ya kitaifa, auambao hadhi yao inathibitiwa kikamilifu au kwa kiasi na mila zaowenyewe au desturi au na sheria au taratibu maalum.50 Hapa,utangulizi wa kihistoria tu sio kigezo cha pekee cha kutumikakuwatambulisha watu wa kiasili.

• Kuongezea kwa vigezo hivi halisi, mkataba huu pia unataja katikakifungu cha 1(2), kwamba kujitambulisha kwa watu wenyewe kamawa kiasili au wa makabila kutachukuliwa kama kigezo msingi chabainisha makundi wanahusishwa na vibali vya Mkataba.

Kamati Teule inayohusika na watu/ jamii asili ya Tume ya Afrika ya kuteteahaki za Kibinadamu na za watu (Kamati Teule ya Tume ya Afrika) ilipewajukumu na Azimio kuhusu Haki za Watu/ Jamii za Kiasili barani Afrika,likapitishwa na Kikao cha Kawaida 28 cha Tume hii mwaka wa 2000,kuchunguza dhana ya watu/jamii za kiasili Afrika na kufanyia uchunguzimatokeo Mapatano ya Afrika kwa hawa watu, kati ya majukumu mengineyo.Kati ya makadirio ya Jopokazi la yalikuwa yale yanahusika na Vifungu vyaMapatano ya Afrika ambavyo vingetumiwa kulinda haki za watu wa kiasili.Hivi, kati ya vinginevyo, vilihusu sehemu zifuatazo:

• Haki za watu/ haki za pamoja. Maisha ya watu wengi wa kiasiliyamo hatarini- hasa yale ya jamii za wawindaji-wakusanyaji. Katikaripoti yake, jopokazi lilihusisha haki za pamoja za watu wa kiasili nahaki za watu kama zilivyo katika Mapatano ya Afrika.51 Mapatanoya Afrika yanatambua na kulinda haki za watu wa kiasili moja kwamoja.

• Vifungu nambari 20 na 22 vya Mapatano Inatumia istilahi ‘watu’katika idhini zake, hata kwenye dibaji yake. ya Afrika vinasisitizakwamba watu wote watakuwa na haki ya kuishi na haki yamaendeleo ya kijamii, kiuchumi na kitamaduni wanyaopendelea nakulingana na upekee wao. Haki za pamoja za kimsingi kama hizizimenyimwa watu wa kiasili kwa kiwango kikubwa.52

49. Haya ni: aula kwa wakati, kuhusiana na kumiliki na kutumia eneo Fulani mahususi;Uendelezaji wa upekee wa kitamaduni kwa hiari, ambao unaweza kuhusisha masuala yalugha, muundo wa kijamii, dini na maadili ya kiroho, mbinu za uzalishaji, sheria na asasi;kujitambulisha, pamoja na kutambuliwa na makundi mengine, au na mamalaka za taifa kamaumoja wa kipekee; tajriba ya kutiishwa, kupembezwa, kunyang’anywa mali, kutengwa aukubaguliwa, hata ikiwa hali hizi zinaendelea au la.

50. Mkataba wa ILO wa 169, vifungu 1(1)(a) and 1(1)(b).51. Ripoti ya Kamati Teule ya wataalamu ya Tume ya Afrika kuhusu watu/jamii za kiasili,

iliyowasilishwa kulingana na Maazimio kuhusu Haki za watu/jamii za Kiasili Afrika; IWGIA(Copenhagen) na ACHPR (Banjul), 2005, 20.

52. Kama hapo juu, 57.

16

Page 33: First page ILO.fm

• Haki na uhuru wa watu bila mipaka ya aina yoyote kama vile yakimbari, kikabila, rangi, jinsia, lugha, dini, siasa au maoni yoyote,taifa au chimbuko la kijamii, mali, kiuzao au hadhi nyingineyo.

Kamati Teule ilitja kuwa istilahi ‘watu wa kiasili’ imeondokea kuwa navidokezi na maana zilizopana zaidi kuliko swali la ‘ni yupi wa kwanza’. Zaidi yahayo liliibua vipengele vifuatavyo:

• Uelewa wa istilahi ‘watu wa kiasili’ kulingana na ukoloni waUingereza tu si jambo la mgeuko katika mjadala huu.

• Mifumo ya kijumla ya kileo ulimwenguni inayohusiana na watu wakiasili lazima ikubaliwe kama jambo la mgeuko.

• Mwelekeo wa kutambulisha unafaa kutumiwa, pamoja na vigezovya kutambulisha watu wa kiasili badala ya kutoa fasili tu.53

• Kanuni ya watu kujitambulisha wenyewe kama ilivyoelezwa katikaMkataba wa 169 wa ILO na Jopokazi la Umoja wa mataifalinalohusika na watu wa kiasili, ni kanuni muhimu inayofaakuelekeza mashauriano ya baadaye ya Tume ya Afrika.54

Inahitimisha zaidi kwamba ‘ ... ikiwa dhana ya watu wa kiasiliitafungamanishwa kabisakabisa na hali hali ya kikoloni, inatuacha bila dhanainayofaa kuchanganulia mifumo ya kindani ya mahusiano yasiyo na usawaambayo yamedumu baada ya kujikomboa kutoka kwa utawala wa kikoloni’.55

1.2 Utambuzi wa Kishria na Kikatiba waWatu waKiasili Barani Afrika

Tangu mwanzo, ni wazi kuwa katika Afrika kuna utambuzi mdogo sana rasmiwa kikatiba au kisheria wa watu wa kiasili katika sheria. Hata hivyo,kiutekelezi, wakati mwingine, makundi haya yanarejelewa kwa kutumiamakabila yao katika nchi nyingi, na aghalabu kwaweza kuwepo na ukubalifudhabiti kwamba baadhi ya makundi ndani ya mipaka ya kitaifa yanajitambulishakama watu wa kiasili kulingana na uelewa wa kimataifa wa istilahi yenyewe.Baadhi ya mataifa kama vile Eritrea na Ethiopia, yatambua kirasmi makabilambalimbali yaliyo ndani ya mipaka ya kitaifa. Katika nchi ya Ethiopia kwamfano, ‘mataifa, uraia, na watu’ katika taifa lenyewe wanatambulika katiba nakupewa haki maalum za kikatiba; lakini aghalabu hali ni kwamba utambuzi huurasmi haufasiriki kuwa utekelezaji halisi wa haki kulingana na mahitajiyanayotofautiana ya makundi tofauti. Zaidi ya hayo, ni kawaida katika halinyingi kwa kabila Fulani dogo lisihusishwe katika utambuzi rasmi, lichukuliwekuwa ndani ya kabila jingine kubwa, kama kwa mfano hali ya Watukurir naWajeberti nchini Eritrea, makundi ya San ya Botswana, na jamii kadhaa zakiasili nchini Kenya.

Kwa upande mwingine wa kigezo, baadhi ya katiba na sheria za mataifa,hazionyeshi vijenzi vya kikabila kayika nchi (kama ilivyo mfano wa Misriambayo katiba yake inarejelea Wamisri kama Taifa la Kiarabu, hivyoikionyesha kwamba inajiona kama ya jinsi moja, na kushindwa kutambuakirasmi kuwepo kwa makundi ambayo kwa hakika ni tofauti na watu waKiarabu waliowengi). Ni katika kifungu cha usawa tu katika Katiba ndipokumeonyeshwa kiwazi kuwepo kwa tofauti za kilugha, kikabila au za kidini kati

53. Kama hapo juu,88.54. Kama hapo juu, 101.55. Kama hapo juu 92.

17

Page 34: First page ILO.fm

ya Wamisri.56 Ijapokuwa hivyo, Misri imetia sahihi Mkataba wa 107 wa ILOkuhusu Watu wa Wiasili na wa Makabila, ambao hadi kufikia sasa umetumikakwa Wabedouin, inagawa kwa kiwango kikubwa mwelekeo umekuwakimchanganyiko.57 Katika namna ileile kama katiba ya Misri, Katiba ya Algeriainashindwa kutambua kundi lingine lolote kando na Waarabu. Haitambuuasilia wa Waamazigh. Katiba inaambatanisha tu taifa na dini, na kutambulishaAlgeria kama ‘Algeria, ardhi ya Uislamu, sehemu muhimu ya nchi tukufu yaMaghreb, Kiarabu, ya Mediterenia nay a Kiafrika’ (L'Algérie, terre d'Islam, partieintégrante du Grand Maghreb, pays arabe, méditerranéen et africain ...)’58 na diniya kiislamu kama Dini ya Kitaifa59 na kiarabu kama lugha rasmi ya kitaifa.60

Utamaduni na dini ya Kiislamu vinachukuliwa kuwa ndivyo vihalisi vya pekee‘thabiti vya utambulisho wa kitaifa wa Algeria’. Kwa hivyoutambulisho waWaamazigh kwa hakika umepembezwa san akwsenye kiwango cha kitaifa.Licha ya kutambulika kwa Kitamazi (Tamazight) kama lugha ya taifa mnamomwaka wa 2002, hakujakuweko mabadiliko makubwa katika sheriazilizotungwa au utekelezaji wake kuonyesha haya.

Baadhi ya katiba zinapioga marufuku kabisa kurejelea kabila lolote. Mfanowake ni katiba ya rwanda. Hakuna matini yoyote ya kisheria nchini Rwandainatumia neno ‘asilia’ na serikali haitambui istilahi ‘ watu wa kiasili’. Hata hivyoWabatwa wa nchini Rwanda na Mbilikimo wa Afrika ya Kati wamnatambuliwasana kwa jumla kama wakaazi wa kwanza wa eneo hilo. Hatahivyo, hasa nchiniRwanda, suala la kabila ni nyeti mno, na linalopigiwa siasa sana na serikalihaiwatambui Wabatwa kwa msingi wa wazo kwamba kufanya hivyo kunawezakuzua ukabila. Badala yake Wabatwa wanatajwa kirasi kama ‘jamiizilizopembezwa kihistoria’. Kifungu cha 82 cha Katiba, kwa mfano, kinaruhusuuwakilishi maalum katika Senati ambayo inaundwa kwa wanachama ishirini nasit, ambapo wanane lazima watoke katika jamii zilizopembezwa kabisakihistoria.

Baadhi ya katiba zina vipengele vya wazi vinavyohusu usawa wa wananchiwote mbele ya sheria pamoja na vipengele vipengele vya kijumla dhidi yaubaguzi, na kutambua kuwepo kwa tamaduni anuwai katika nchi au kutambuauanuwai wa makabila katika Taifa. Katiba ya Mali inatangaza ulinzi wa uanuwaiwa tamaduni na lugha wa jamii ya kitaifa.61 Hata hivyo hakuna utambuzi wawatu wa kiasili katika sheria ya kitaifa, licha ya Watuareg na Peul kutambuliwana jopokazi la Tume ya Afrika linaloshughulika na watu/jamii za kiasili, kamawatu wa kiasili, wao wenyewe kujitambulisha kama watu wa kiasili.

Baadhi ya katiba za Afrika zinahakikisha kuwepo kwa ulinzi wawaliwachache, na baadhi yazo zinaruhusu uwakilishwaji wa makabila fulanimaalum katika mashirikwa yaliyoteuliwa kitaifa (kama Burundi, ambayo inasehemu ya haki kwa makabila wakiwemo Wabatwa, katika Bunge na Seneti).Hata hivyo hakuna katiba ya Kiafrika ambayo hususa inatambua istilahi ‘watuwa kiasili’, mbali na Katiba ya Kameruni ya Januari 18,1996, ambayo inataja

56. Ibara ya usawa chini ya kifungu cha 40 kinasema:’ Raia wote ni sawa mbele ya sheria. Wanahaki na majukumu sawa ya kiraia bila mapendeleo baina yao kutokana na mbari, chimbuko lakikabila, lugha, dini au imani’ (msisitizo umeongezwa).

57. Kamati ya wataalamu ya ILO kuhusu Utumizi wa Mapatano na Mapendekezo. Ombi laKinafsi la Moja kwa moja kuhusiana na mkataba wa 107. Watu wa Kiasili na wa Makabila.1957 Misri(sahihi: 1959) 2005.

58. Dibaji ya katiba Algeria (Algeria, ardhi ya Uislamu, sehemu muhimu ya nchi tukufu yaMaghreb, Kiarabu, ya Mediterenia nay a Kiafrika).

59. Kifungu cha 2 cha katiba.60. Kifungu cha 3 cha katiba.61. Dibaji ya katiba ya Mali.

18

Page 35: First page ILO.fm

kwenye dibaji kwamba Serikali itahakikisha ulinzi wa waliowachache naitatunza haki za watu wa kiasili kulingana na sheria.62

Katiba ya Burundi kwa mfano, unatambua Wabatwa kirasmi, hivi kwambainatambua kuwepo kwa makabila na dini anuwai katika nchi na hususaninaruhusu uwakilishwaji wa Waabatwa katika Bunge na Senati.63

Katiba inaenda hatua zaidi kwa kuanza kwa maneno ‘Sisi Taifa, Uraia, naWatu wa Ethiopia …’ na zaidi pia kwa kutaja kwamba ‘Uwezo wote wamamlaka umo katika Taifa, Raia na Watu wa Ethiopia’.64 Kulingana na katiba;

Taifa, Raia au Watu’ kwa kusudi la katiba, ni kikundi cha watu ambao wanaau wanashriki kiwango kikubwa cha utamaduni mmoja au milazilizosawa,ujuzi sawa wa lugha, imani katika utambulisho sawa auunaokaribiana, hulka sawa ya kisaikolojia na wale wanaokaa katika eneolinaloweza kubainika na lilowaathiri pakubwa.65

Kuna idadi Fulani ya viti bungeni vilivyotengwa na katiba ya Ethiopia kwaajili ya makabila ya wachache katika nchi bila kutaja hasa makundi haya yawaliowachache ni kina nani, ikiacha watambuliwe kwenye kiwango chautekelezaji. Kinyume na nchi nyingi, zinazoweka mkazo mtu binafsi, Ethiopiailichagua kurasimu katiba yake kutumia mbinu ya upamoja. Katiba inatambuawingi wa makabila yaliyoko nchini Ethiopia, lakini haitofautishi baina ya ‘taifa,raia au watu’ wala haitambui waziwazi waliowachache kitaifa, kikabila nakilugha au hata hadhi ya uasili’.66 Katiba ya Ethiopia inazipa lugha na tamadunizote utambuzi ulio sawa, na kila kabila ‘lina haki ya kuendeleza na kukuzautamaduni wao na kutunza historia yao’.67 Haki za wafugaji vilevile hususanzimetajwa katika katiba.

Kuhusiana na uundaji wa sheria kitaifa, ni nchi moja tu katika eneo laAfrika imetoa rasimu (lakini haijapitishwa) ya sheria ya kitaifa kuhsu watu wakiasili pekee. Jamuhuri ya Kongo, imerasimu sheria pana kuhusu haki za watuwa Kiasili, ikirejelea hususan ‘Mbilikimo’ kama watu waliolinwa na sheria.Exposé des Motifs ya rasimu ya sheria inaweka sheria katika mfumo wa kifungucha 4(6) cha katiba ya kitaifa, ambayo inaruhusu ulinzi wa makabila yawachache. Sheria inarejelea vipengele vya kikatiba vya kutokuwepo na ubaguzina usawa wa raia wote, japo inatoa inaonyesha hitaji la kuweko kwa hatuamaalum ili kushughulikia hali mahsusi ya ‘Mbilikimo.’ Vigezo vinavyotumikakatika rasimu ya sheria katika kutambulisha makundi inayoyarejelea ni,utambulisho a kitamaduni na asasi, na mila na destruri ambazo zinawabainishakutoka kwa makundi mengine, na hali kwamba ‘Mbilikimo’ wanajibainishakutoka kwa makundi mengine kulingana na vigezo hivi.

62. Dibaji, Katiba ya Kameruni, mwaka 1996. kutokana na kifungu cha 65 cha katiba ‘Dibajiitakuwa sehemu muhimu ya katiba hii.’ Hata hivyo, hakuna ufasiri rasmi wa maana yamatumizi ya istilahi ‘Aisili’ katika Dibaji. Kuwanaweza kuweko na shaka kuhusi iwapomatumizi ya istilahi ‘asili’ katika hali hii yanarejelea kile kinachoeleweka chini ya UNDRIP.

63. Arts 164, and 180, respectively, of the Burundian Constitution.64. Katiba ya Ethiopia kifungu nambari 8(1)65. Katiba ya Ethiopia kifungu cha 39(5).66. Baraza la umoja wa mataifa la Kutetea Haki za Kibinadamu, Utekelezaji wa Azimio la 60/

251 la Bunge la tarehe 15 Machi 2006 lenye mada ‘Baraza la kutetea Hai za Kibinadamu’ -Ripoti ya mtaalamu huru kuhusu masuala ya waliowachache, Gay McDougall, Ujumbe wanchini Ethiopia, UN Doc A/HRC/4/9/Add.3, aya ya 7, Februari 28, 2007.

67. Baraza la Umoja wa Mataifa la kutetea haki za kibinadamu, Utekelezaji wa Azimio la Bungela 60/251 la Machi 15, 2006 lenye kichwa ‘Baraza la Kutetea Haki za kibinadamu’ Ripoti yamtaalamu huru kuhusu masuala ya kiasili, Gay McDougall, Ujumbe wa nchini Ethiopia UNDoc A/HRC/4/9/Add.3, aya ya. 8, 28 Februari 2007.

19

Page 36: First page ILO.fm

Au sens de la présente loi, on entend par populations autochtones, appelésPygmées, les populations qui se distinguent des autres groupes de la populationnationale par leur identité culturelle, leurs institutions et qui sont régies par descoutumes et traditions qui leur sont propres.68

Nchini Kongo kwa jumla zaidi, istikahi ‘asili’ na ‘mbilikimo’ zinatumiwakama visawe, kwa maana kwamba inakubalika bila kutaja kuwa ‘Mbilikimo’ niwatu wa kiasili katika nchi hiyo. Kwa hakika matumizi kubadilishana yamaneno ‘mbilikimo’, ‘asili’ na ‘waliowachache’ ni ya kawaida katika nchi nyingiza Afrika ya Kati katika sera na matini, kama sio katika uundaji wa sheriakitaifa ambapo istilahi mbili za mwisho zinatumika wala sio iastilahi ‘asili’

Katika hali zingine, watu wa kiasili wanatambulika kimahususi katika sheriaya kitaifa, au wakati mwingine katika taarifa rasmi kama makundi‘yaliyohatarini’ au yaliyopembezwa. Mpango wa miaka mita wa kuharakisha nakudumisha maendeleo ili kumaliza umasikini wa nchini Ethiopia [Programmefor Accelerated and Sustainable Development to End Poverty (PASDEP)] unawezakutajwa kama mfano mzuri. Wanaweza pia kurejelewa katika hali kama hizi,kwa kutumia makabila yao, kama ilivyo ilivyo mfano wa Burundi. NchiniKameruni watu wa kiasili wanachukuliwa chini ya kichwa jumulishi cha ‘ watuwaliopembezwa’ na sheria inaundwa kwa sasa kuyalinda makundi kama haya.Huku ikiwa kwamba uundaji wa sheria kama hii bila shaka yoyote ni hatuachanya, kuyaunganisha makundi ambayo yanajitambulisha kama asilia nakutimiza vigezo vilivyotolewa katika mifumo ya kisheria ya kimataifa kwa ajiliya haki za watu wa kiasili, pamoja na makundi mengine ambayo hayajafanyahivyo, kunaweza kufanya uundaji wa sheria kama hii kupungukiwa katikakuwapa watu wa kiasili haki za kutosha. Zaidi ya hayo, kukosekana kwa vigezovyovyote rasmi vya kutambulisha yale makundi yanayofaa kulindwa na sheriailiyopendekezwa kuna maana kwamba, kwa kweli, itahusisha makabila kadhaayaliyotajwa yaliyo na kiasi kikubwa cha madai tofauti ya mahitaji na haki. Hililinaweza kuwa jambo gumu kiasi kushughulikiwa katika mfumo wa sheriamoja. Ijapokuwa hivyo, kuundwa kwa sheria kuhusiana na suala la misitu naraslimali, kama Sheria ya Misitu ya mwaka 1994, inatumia istilahi ‘watu wakiasili’ na ‘jamii za vijijini’ kwa kubadilishana katika baadhi ya sehemu.

Katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kanuni ya Misitu inarejeleajamii wenyeji ambazo zina haki maalumu chini ya kanuni hiyo. Kanuni hiyoinafasiri ‘jamii wenyeji’ kama ‘une population traditionnellement organisée sur labase de la coutume et unie par des liens de solidarité clanique ou parentale quifondent sa cohésion interne. Elle est caractérisée, en outre, par son attachement àun terroir determine’.69 Ingawa neno ‘asili’ halitumiki, inarejelea watu wa kiasilikwa wazi. Vilevile kanuni ya misitu (sheria ya kifungu nambari 004/74) yaJamuhuri ya Kongo, na Jamuhuri ya Afrika ya Kati (kifungu 90/003 ya 1990)hazitumii istilahi ‘watu wa kiasili’, lakini inazungumzia ‘wenyeji’ au ‘populationsriveraines’ badala yake.

Aina nyingine za utambuzi katika makatiba na uundaji wa sheria kitaifazinaweza kuwa ni utambuzi wa lugha za kiasili. Nchini Afrika Kusini, katiba

68. ‘Kwa ajili ya sheria iliyoko sasa, istilahi ‘watu wa kiasili’ wanaojulikana pia kama ‘Mbilikimo’inaeleweka kuwa inahusisha watu ambao hujibainisha wenyewe kutoka kwa makundimengine ya umma wa kitaifa. Kwa misingi ya uambulizi wao wa kitamaduni, asasi zao nakama watu wanaoongozwa na mila na desturi zao.

69. Kifungu cha 17 cha Code Forestier Congolais (jamii ya watu ambao wamejipangiliakitamaduni kwa msingi wa mila na kuunganishwa na uhusiano wa kimbari au wa kifamilia,ambao kwao mshikamano wake wa ndani wa kijamii umejengekeka. Pia ina wasifu wamsikamano wake kwa sehemu Fulani ya ardhi yenye mipaka Fulani).

20

Page 37: First page ILO.fm

inataja waziwazi lugha za kiasili.70 Huku ikiwa kwamba hizi lugha tatu za kiasilihazipewi hadhi rasmi sawa na lugha zingine za Kibantu zenye nguvu za Afrika,ukweli kwamba zinatajwa katika katiba ni ishara kwamba serikali inatambuafaida zake. Kifungu cha 6(2) cha katiba ya Afrika Kusini kinataja ‘utambuzi wahadhi iliyodidimia kihistoria ya lugha za kiasili za watu wetu’. Kifungu nambari30 na 31 cha Katiba (kinachohusu lugha na utamaduni pamoja na jamii zakitamaduni, kidini na za lugha mtawalia) vina hakikisho muhimu kuhusu baadhiya haki za kimsingi za watu wa kiasili, kwani vipengele hivi vinazungumziawaliowachache na jamii za kitamaduni moja kwa moja.

Katika hali zingine, watu wa kiasili wanaweza kutambulika, au kujibainishawenyewe, kama waliowachache kitaifa. Hivi ndivyo ilivyo nchini Kenya,ambapo utambuzi rasmi wa watu wa kiasili ungali tata. Hata hivyo, hivikaribuni Serikali imekubali kuwa ‘kuwemekuwepo na kukubali kwa hadhi yaopolepole na kuna juhudi zinazofanywa sio tu kuwatambua hawa watuwaliowachache, lakini pia kuimarisha maisha yao na ulinzi’, ambapo awaliserikali haikuchua hatua muhimu kuhifadhi na kuwalinda waliowachachenchini.71 Hata hivyo, kwa upande wa Kenya, mwelekeo wa kuyatambuamakabila arobanne na mawili yanayotambulika kirasmi ‘kumetokana na seraya kikoloni ya kuendeleza kumezwa kwa makabila madogo ndani ya makabilamengine makubwa’.72 Hii imekuwa na athari ya kupunguza au kuziondoakabisa jamii ndogondogo za wafugaji na wawindaji-wakusanyaji kutokakwenye uundaji wa sera za kitaifa na ugavi wa bajeti ya kitaifa.73

Kwa kiwango kikubwa, watu wa kiasili nchini Nigeria wanajibainisha kamawaliowachache kutokana kutokuwepo na utambuzi rasmi, au hata mjadala wakitaifa kuwahusu wao kama watu wa kiasili. Baadhi ya sheria za kitaifa katikanchi mbalimbali pia zinayarejelea makundi, ambayo kwa kweli yangejibainishakama watu wa kiasili, kama waliowachache. Dibaji ya katiba ya Jamuhuri yaAfrika ya Kati ya mwaka 2004, kwa mfano, inaonyesha kuwa nchi ya CAR ni‘Taifa lililojengwa kwenye sheria, na msingi wa uwingi wa kidemokrasia,ambao unahakikisha ulsalama wa watu na mali usalama wa waliohatarini sana,hasa waliowachache na utekelezaji mkamilifu wa uhusru na haki za kimsingi.’74

Badala ya kurejelea watu wa kiasili, inazungumzia ‘waliowachache’ na ‘watuwaliohatarini.’ Katika ripoti yake ya mwaka 2006 kwa Kamati yaKushughulikia Haki za Kibinadamu, nchi ya Jamuhuri ya Afrika ya Katiinawataja ‘Mbilikimo waliowachache’ lakini sio katika muktadha wa kifungucha 27 cha ICCPR ambacho kinashughulika na haki za waliowachache. Katikamaoni yake ya kuhitimisha, kamati hiyo haikutia mjadala huu katika muktadhawa mfumo wa kifungu cha 27.

Huku ikiwa kwamba kutambuliwa kama waliowachache kunaweza kuletakiwango Fulani cha ulinzi, haki wanazopewa waliowachache katika mfumo washeria ya kimataifa ni tofauti, katika sehemu nyingi sana, na zile wanazopewawatu wa kiasili.

70. Sehemu ya 6(2) ya Katiba ya Afrika Kusini inalazimu seriakali kuchukua hatua tekelezi nazilizochanya ili kuinua hadhi na kuendeleza matumizi ya lugha za kiasili. Sehemu ya 6(5) yakatiba inaendeleza ulinzi wa lugha za Kikhoi, Kinama na Kisan.

71. Ripoti ya pili ya kimuhula ya Kenya iliyotolewa kwa Kamati ya Umoja wa Mataifa yakutetea haki za kibinadamu, ukurasa wa 212.

72. Ripoti ya Ofisi ya Katibu maalum wa Umoja wa Mataifa inayohusika na watu wa kiasilinchini kenya, ubeti wa 21.

73. Kama hapo juu.74. ‘Etat de droit fondé sur une démocratie pluraliste, garantissant la sécurité des personnes et des

biens, la protection des plus faibles, notamment les personnes vulnérables, les minorités et leplein exercice des libertés et droits fondamentaux’.

21

Page 38: First page ILO.fm

1.3 Sera na Mipango ya Kitaifa

Sera na mipango ya maendeleo ya kitaifa mara nyingi hulenga watu wa kiasilihasa kwa sababu ama wanaishi katika maeneo yaliyo na utajiri wa raslimalizina dhamani ya moja kwa moja kiuchumi au kwa sababu ni kati ya sekta zaumma wa kitaifa zilizopembezwa sana na zilizomasilikini zaidi. Mikakati yaKupuguza Umasikini (PRSs) ni sehemu muhimu sana kwa watu wa kiasili nabaadhi ya Mikakati hii katika Afrika kwa kweli inalenga watu wa kiasili mojakwa moja- hususan zile nchi zilizo katika kanda ya Katikati mwa Afrika. PRS yaKongo DRC katika mwaka wa 2006 na 2007 ilitambua kuwepo kwa watu wakiasili:

La RDC est le premier pays d’Afrique du point de vue de l’étendue de ses forêts etle plus important dans la préservation de l’environnement mondial. La forêt estessentielle à la survie et au développement d’au moins 40 millions de Congolais.Au sein de cette population, il faut mentionner particulièrement les peuplesautochtones qui vivent à la lisière de la forêt et principalement des produitsnaturels de la biodiversité forestière, tant pour leur alimentation, leur habitat etleur santé que pour l’énergie bois (80% de toute l’énergie consommée dans lepays).75

Baadhi ya stakabadhi zingine za PRS zinarejelea ‘makundi yaliyohatarini’,‘waliowachache’ au makundi ya kiasili kwa kutumia majina ya makabila yao,lakini bado zinawashughulikia watu wa kiasili. Mifano yake ni pamoja naJamuhuri ya Kongo (ambayo inatumia ‘mbilikimo’, ‘makundi yaliyohatarini’ na‘waliowachache’ kwa kubadilishana), stakabadhi za muda za PRS za Jamuhuriya Afrika ya Kati, na Stakabadhi za PRS za mwaka 2008-2010, ambazozinayarejelea ‘makabila ya waliowachache’ inagawa zinawataja ‘Mbilikimo’ naWambororo kama makundi mawili ambayo yameathirwa sana na umasikini.Nchini ethiopia, mpango wa maendeleo (PASDEP) wa mwaka 2005 unatajakwamba ‘vigezo vya maendeleo ya kibinadamu na umasikini baina ya kikundicha wafugaji ni ni vibaya zaidi kwa kiwango sawa kuliko mahali kwinginekonchini, na vimeonekana vigumu kufikiwa na huduma za kimapokeo’.76

Baadhi ya mataifa ya Afrika yameunda Mipango ya Kimaendeleo kwa Watuwa Kiasili- zaidi katika mfumo wa PSR, mipango ya sekta (kwa mfano Mipangoya sekta ya Misitu na Mazingira nchini Kameruni na Gabon) na mipango yamiundomisingi kama vile mpango wa ukarabati wa barabara katika Jamuhuriya Kidemokrasia ya Kongo. Hii ni kutokana na masharti ya Sera ya Utendaji yanambari 4.10 ya Benki ya Dunia inayohitaji hatua maalum iwapo uwekezaji waBenki ya hiyo na Nyezo za Mazingira Duniani (GEF) vinaadhiri uwezo wa watuwa kiasili, makabila ya wachache au makundi mengineyo katika kulindamasilahi na haki zao zinazohusiana na ardhi na maliasili. Mpango waMaendeleo ya Watu wa Kiassili wa nchini Gabon kwa mfano unamnukuuWaziri Mkuu:

75. ‘Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ni ya kwanza kabisa kuhusiana na misitu yake nailiyomuhimu zaidi katika kuhifadhi mazingira ulimwenguni. Misitu ni ya muhimu sana kwamaisha na maendeleo ya zaidi ya Wakongo milioni arobanne. Kati ya watu hawa, watu wakiasili, -ambao wanaishi kingoni mwa misitu na wanategemea mazao ya kiasili ya viumbehaianuwai vya msituni kwa kupata chakula, mazingira wanamoishi na afya yao na kawikutokana na kuni (ambayo ni asilimia 80 ya kawi inayotumiwa kitaifa)- wanahitaji kutajwakwa njia ya pekee.’ République Démocratique du Congo, Document de la stratégie decroissance et de réduction de la pauvreté (DSCRP), juillet 2006, para.111, p.34 voir sur lesite : http://siteresources.worldbank.org/INTPRS1/Resources/Democratic-Rep-of-Congo-French(July2006).pdf.

76. PASDEP, uk. 50.

22

Page 39: First page ILO.fm

Les premiers habitants de notre pays, les pygmées, sont effectivement absents àl’occasion par exemple des échéances importantes. Non pas parce qu’ilsrefuseraient d’y prendre part; mais tout simplement en raison de ce que, d’unepart ils n’ont pas de moyens et, d’autre part, ils n’ont pas de cartes d’identité.77

Kwa hivyo mpango wa watu wa kiasili wa Gabon kwa wazi unatambuawatu wa kiasili (Mbilikimo) kama kikundi kilicho na mahitaji maalum, na wajibukwa watu hawa katika masuala yanayohusiana na misitu. Utambuzi katika halihii imeambatanishwa na kigezo cha kihistoria. Sheria ya kitaifa katika hali hii,hata hivyo, inasema mengine. Sheria ya 0016101 kuhusu misitu yaDisemba 31, 2001 (Code Forestier), kwa mfano inarejelea ‘communautésvillageois’ (jamii za vijijini) ingawa hizi zinahusisha watu wa kiasili. NchiniKongo(DRC), katika muktadha wa mpango wa ujenzi wa barabara (sehemu ya3 ya mpako wa Benki ya Dunia wa kusaidia kuunganika tena kwa uchumi najamii), Mpango wa Watu wa Kiasili hautumii tu neon ‘asili’ bali pia unaonyeshakwamba Mbilikimo ni watu wa kiasili wanaokaa nchini humo.78

Nchini Afrika Kusini ‘baraza la mawaziri lilikubali maafikiano katika mwakawa 2004 yanayoeleza mchakato wa sera ya kuwatambua za Wakhoi na Wasankama jamii za kiasili zilizohatarini’.79 Hii ni hatua chanya ya kuwatambulishawatu wa kiasili nchini Afrika Kusini, na kama ilivyodhihirishwa na taarifambalimbali za kiserikali na za kirasmi, Wakhoi na Wasan wanachukuliwa naserikali kama ‘watu wa kiasili ambao wanepembezwa sana na wanahitaji ulinzimaalum. Hata hivyo, maafikiano na taarifa za maafisa wa umma havijafanywakuwa sera rasmi zinazowatambua Wakhoi na Wasan kama watu wa kiasili waAfrika Kusini.80

Nchini Uganda, licha ya kutokuwepo kwa sera rasmi ya kiserikaliinyotambua watu wa kiasili kama inavyoeleweka kimataifa, kuna mwelekeo wakuyatambua makundi fulani yaliyopembezwa na yaliyohatarini au kama yawaliowachache. Wizara ya Jinsia, Leba na Maendeleo ya Kijamii, hivi karibuni,kwa mfano imeanza shughuli ya kuunda detabenki ya kutoa taarifa kuhusumakabila ya waliowachache.81 Wakat Wizara inatumia istilahi ‘watu wa kiasili’,pamoja na ‘waliowachache’, ni wazi kutokana na utafiti wake mzima kwambamakundi ya waliowachache ndiyo yanayorejelewa na sio ‘watu wa kiasili’ kamainavyoeleweka kimataifa. Nchini Rwanda, licha ya kutokuwepo kwa utambuzirasmi wa watu wa kiasili, Tume ya Kitaifa ya Umoja na Mapatanoilitambua(katika mwaka wa 2006) kwamba Wabatwa walikuwawamesahaulika au kupuuzwa na walifaa kupewa uangalifu maalum,

77. ‘Wakaazi wa kwanza wa nchi yetu, Mbilikimo, hawaonekani kabisa katika hafla muhimu,kati ya nyinginezo. Si tu kwa sababu wanakataa kushiriki, lakini tu ni kwa sababu, kwaupande mmoja wanakosa njia ya kufanya hivyo, na kwa upnade mwingine, kwa sababuhawana vitambulisho’. République Gabonaise, Ministère de l’Economie Forestière, des Eaux, dela Pèche, de l’Environnement chargé de la Protection de la Nature, Plan de Développement dePeuple Autochtones du Programme Sectoriel Forêts Environnement, Rapport Final préparé parDr. Kai Schmidt-Soltau, juillet 2005, 4.

78. République Démocratique du Congo, Plan des peuples autochtones, Composante 3 du Projetd'urgence et de soutien au processus de réunification économique et sociale (PUSPRES), Rapportfinal 2006. tazama http://wwwwds.worldbank.org/external/default/WDSContentServer/WDSP/IB/2007/10/09/000020953_20071009141319/Rendered/PDF/IPP248.pdf.

79. Angalia IWGIA, The Indigenous World (2006) 516. Serikali pia imeanzisha Jopokazi la Idaraya kushughulika na masuala ya Wakhoi na Wasan.

80. Angalia Ripoti ya Ujumbe wa Katibu Maalum wa Umoja wa Matifa kuhusu watu wa kiasilinchini Afrika Kusini, aya ya 81.

81. Wizara ya Jinsia, 2007.

23

Page 40: First page ILO.fm

ikapendekeza hatua maalum kuchuliwa kwa maslahi ya Wabatwa kwa namnaya masuala ya elimu na afya.82

1.4 Taarifa na stakabadhi katika katika mabaraza yakimataifa

Wakati mwingine mgeuko wa mwelekeo wa serikali kuhusu watu wa kiasiliunaweza kudodoswa kutoka katika ripoti ripoti na taarifa zake kwamashikrika anagalizi ya mikataba au katika mabaraza mengine ya kimataifa.Kura ziliyopigwa na Bunge ili kukubali azimio la Umoja wa mataifa kuhusuHaki za Watu wa kiasili mwezi wa Septemba 2007, zilipelekea kura 143kupigiwa kwa kukubali na nne pekee kupigwa dhidi yake (Australia, Canada,na New Zealand). Burundi, Kenya, na Nigeria ndiyo mataifa ya kiafrikayaliyokwepa kupiga kura hiyo. Benini ndiyo nchi ya pekee kutoka Afrikailiyohusika katika mjadala kabla ya kupiga kura, ikionyesha kwamba imekuwamdhamini wa rasimu hii tangu mwanzo, pamoja na ushawishi wake kwambainawakilisha maendeleo katika uwanja wa haki za kibinadamu na hasa haki zawatu wa kiasili. Hata hivyo, ilieleza ukweli kwamba iliiona matini hiyo kuwailikuwa na ‘kasoro nyingi, lakini kwamba inagali inaikubali itekelezwe kwamuda huku marekebisho yakianzishwa ili baadaye iidhinishwe na wajumbewote.’83

Katika baadhi ya nchi kuna utambuzi unaoitokeza, wakati mwingine namaafisa fulani binafsi, kwamba ukosefu wa kuwatambua watu wa kiasilikunaweza kuwa kizuizi katika kuimarisha hali yao. Kutokana na ziara yakenchini Burundi, kwa mfano, Jopokazi la Tume ya Afrika Kuhusu Haki zakibinadamu na haki za watu(ACHPR’s) ilikutana na Waziri wa Haki zaKibinadamu, ambayo alidhihirisha msimamo kama huu.84

Mataifa mengi hata hivyo, ni malegevu kuwatambua watu wake wa kiasili.Kulingana na vipengele vyake vya kikatiba, Misri- katika ripoti yake yakimuhula kwa Kamati inayohusika na Kuondoa Ubaguzi wa Kikabila- kwamfano ilitaja kwamba;

Misri haina makabila yoyote ya waliowachache. Kuhusiana na wahamahamaji,Waberber, na Wanubi, pana urejelezi uliofanywa … kutokana na ukwelikwamba pana mfanano kamili baina ya makundi na jamii zote zilizomo nchiniMisri kwani wote wanazungumza lugha moja, Kiarabu, ambayo inatawalakatika maeneo yote ya nchi, ya jangwa na ya Pwani.85

Katibu Maalum wa Nchi, Bw. Diaconu, wakati wa kuchunguza Ripoti yaNchi aliona kisawa kwamba ‘hakukuweko na sheria au hatua iliyopangwailiyolenga kuzuia au kuondoa ubaguzi au kulinda lugha au utamaduni wamakundi hayo yote, kwa mfano, kwa kudhamini elimu ya lugha ya mama au yalugha nyingi’.86

Au, mataifa yanaweza kudai, kama yanavyofanya mengi, kwamba watuwote wanaoishi ndani ya mipaka yake ni ‘wa kiasili’ kwa dhana kwamba wao ni

82. CAURWA, Convention relative aux droits de l’enfant, Contre rapport présenté par CAURWA,Kigali, 2004, 7.

83. Kikao cha sitini na moja cha bung, Ripoti ya kikao cha 107 cha jumla, Septemba 13, 2007,New York, UN Doc A/61/PV.107, 16.

84. Ripoti ya Jopokazi la Tume ya Afrika kuhusu watu/jamii za kiasili, Ziara ya utafiti na habarinchini Burundi, Machi- Aprili 2005, 19.

85. CERD Ripoti ya 16 ya Kimuhula (n 20 hapo juu) aya ya 362.86. CERD, Rekodi ya muhtasary ya sehemu ya kwanza ya mkutano wa 1484, Misri UN Doc

CERD/C/SR.1484 17/09/2002 aya ya 9.

24

Page 41: First page ILO.fm

asili kwa Afrika, kwa kulinganuliwa na walowezi wa kikoloni. Uelewa huu nihatua ya mgeuko katika mjadala huu, kama ilivyothibitishwa na Jopokazi laTume ya Afrika kuhusu watu/jamii za kiasili. Katika mataifa mengine imedaiwakuwa athari limbikizi za kuwachukulia makabila yote kama watu wa kiasili nikwamba watu wa kiasili hawajaweza kufuraihia haki zao za pamoja kama watuwa kiasili na kupata suluhu kwa kunyimwa kwa haki kama hizi. Hii ndiyo hojailiyotolewa katika ripoti badala iliyoandaliwa Tume ya Afrika kuhusuUganda.87

Kunaonekana hali ya maendeleo katika kuwatambua watu wa kiasilikwenye kiwango cha kitaifa ambayo inaweza kudodoswa kutoka kwenyemataifa yaliyotoa ripoti kwa mashirika au mabaraza angalizi ya kimataifa nakimaeneo yanayohusika na masuala ya kiasili. Baadhi ya serikali za kiafrikahushiriki kwenye vikao vya Baraza la Kudumu la Umoja wa Mtaifa kuhusumasuala ya asili (DRC, kongo, na Afrika Kusini ni nchi zinazojitokeza sana) nakatika mabaraza mengine muhimu ya Umoja wa Mtaifa. Afrika kusini ilimteuamtu wa kiasili, Dkt. William Langeveldt (Mkorana) kuwakislisha taifa katikaBaraza la Kudumu kuhusu masuala ya kiasili. Katika ripoti yake ya mwishokwa Kamati ya kushughulikia Haki za watoto, Gabon ilitumia neon ‘asili’ naikawatambua moja kwa moja ‘Mbilikimo’ kama watu wenye hadhi hii:

Kwa kweli, kuna makabila 40, yakiwemo machache ya waliowachache, lakinihali hii haizuii watu wa kiasili wasifurahie maisha yao ya kitamaduni,kutekeleza dini yao au kutumia lugha yao pamoja na wenzao katika kikundihicho. Tukizungumza kiusomi, watoto wa waliowachache wanaendeleakutekeleza utamaduni wao kwa uhuru wanapohudhuria masomo katikashule za umma. Kuhusiana na taratibu za kesi za jinai, huduma za utafsirizimeidhinishwa.

Kwa nchi ya Gabon, hii inaonekana kuwakilisha mgeuko katika dhana yaongezeko la polepole katika kuwatambua watu wa kiasili, hata kama hilihalijafanywa kuwa utambuzi wa kisheria, hasa ikiwa kwamba katika ripoti yakekwa Kamati ya Haki za Kibinadamu mwaka wa 2002, ilikuwa imekana kuwepokwa waliowachache katika nchi.88

Baadhi ya mataifa katika eneo la Afrika ya Kati na eneo la Maziwa Makuupia yamerejelea hali ya ‘Mbilikimo’ katika ripoti zao kwa mashirika yamikataba ya Umoja wa Mataifa- hasa, katika ripoti zilizochini yaTume yaKushughulikia haki za watoto (CRC), ambayo ina vipengele vinavyohusuwatoto wa kiasili. Mara nyingi, ripoti zao hutumia neno ‘mbilikimo’, ‘asili’ na‘jamii wenyeji’ kwa njia ya kubadilishana.

1.5 Uraia

Suala la utaambuzi wa kisheria ni muhimu kwa kuwa linahusiana na haja yakuwa sehemu ya kundi Fulani na uwezo wa kutumia haki zinazotokanautambulisho huo. Katiba kijumla huwa na vipengele kuhusu aina tatu za uraia.Hivi ni Uraia kwa kuzaliwa, uraia wa kujisajili na uraia wa kujiandikisha. Hivindivyo ilivyo hali ya Uganda na Kenya kwa mfano. Sura ya sita ya katiba yasasa ya Kenya inakipengele cha uraia wa kuzaliwa, kujisajili na wakujiandikisha. Sheria ya Kenya Kuhusu Uraia sehemu ya 170 inatawala upewa

87. Mpango wa watu waishio misituni, Shirika la Umoja wa Maendeleo ya Wabatwa nchiniUganda (UOBDU) na shirika la kazi la kimataifa kwa masuala ya kiasili. Repoti Badalakuhusu Ripoti ya kwanza ya Muhula ya Uganda kwa Tume ya Afrika kuhusu haki za kibinadamuna haki za watu’ Mei 9, 2006.

88. Maoni ya kuhitimisha ya Kamati ya kutetea haki za kibinadamu kwa Gabon, UN DocCCPR/CO/70/GAB, Novemba 2000.

25

Page 42: First page ILO.fm

na unyan’ganywaji wa uraia. Sehemu ya 11 ya sheria kuhusu watoto ya 8 yamwaka wa 2001 inakibali kwamba kila motto atakuwa na haki kupata jina nauraia na pale ambapo motto ananyang’anywa utambulisho wake,serikali itatoausaidizi na ulinzi uanofaa kwa lengo la kuiweka utambulisho wake. Sheria yaKuweka saji ya Kuzaliwa na vifo sura ya 149 pia inasisitiza kwamba kilaaliyezaliwa Kenya ni sharti asajiliwe hata pia anapokufa. Cheti cha kuzaliwapamoja na jina linalohusiana na utambulisho wa mtu husika vinapeanwa baadaya kusajiliwa kama huku.

Hata hivyo, jamii Fulani, hasa zile zinazoishi sehemu zisizifikika nazilizombali, aghalabu hushindwa kusajilisha watoto wanaozaliwa kwa sababuvituo vya kujisajili vimewekwa mahali pamoja. Haya ni kweli hasa ikiwa mtuhazaliwi hospitalini kama ilivyo hali za watu wengi kutoka maeneo ya vijijini.89

Cheti cha kuzaliwa ni cha maana kwani ndiyo stakabadhi inayothibitishamahali pa kuzaliwa, ukoo na eneo na kisha baadaye kinatumika kupatakitambulisho cha kitaifa na cheti cha usafiri. Wasomali, kwa mfano-kikundikinachojitambulisha kama asilia nchini Kenya, ni kikundi moja wapo ambachokimekuwa na matatizo kupata stakabadhi za kujitambulisha. Hali inatokana nakupembezwa kwa kihistoria kwa jamii hiyo na kupenyeza kwa Wasomalikutoka Somalia. Kwahivyo wamenyimwa haki kamili za uraia amzozingehusisha haki za kupiga kura, kusafiri, kufanya kazi na haki na majukumu yakijumla ya wananchi.90

Katika kukubali imuhimu wa utambulisho, Katiba ya Afrika Kusini inavipengele vya haki za uraia. Sehemu ya 3 ya Katiba ya Afrika Kusini inavipengele vinanyohusu uraia uliosawa kwa raia wote wa Afrika Kusini. Zaidiya hayo katiba hiyo ina vipengele kwamba raia wote ni sawa katika kupatahaki, tunu na faida za uraia, lakini pia wako sawa katika kazi na majukumu yauraia. Sheria ya Afrika Kusini inayohusu Uraia91 Seria ya Bunge ya Kurejeshana Kuendeleza uraia92 zinaidhini ya kupata, kupoteza na kurejesha uraia.Sheria ya bunge ya Afrika kusini ya Kurejesha na kuuendeleza uraia inahusikana watu ambao walipokonywa au hawakupata uraia kutokana na sera yaubaguzi wa rangi ya kuunda himaya za Kibantu za Transkei, Bophuthatswana,Venda na Ciskei.

Sheria za uraia aghalabu hutambua kanuni ya jus sanguini(uraia wa asili),ambayo ingewahusisha watu wa kiasili. Utambuzi wa kisheria ni muhimu sanakwa watu wa kiasili, kwa maana hautoi tu haki za uraia bali pia unawezakutumika kuhakikisha kwamba makundi yaliyobainishwa yanafaidika kutokanana sera za serikali. Kwa watu wa kiasili, suala la utambuzi linaenda zaidi yauraia. Kutambulika kisheria kama watu wa kiasili kunafaa kupekelee kupewahaki ambazo zinahusiana na watu wa kiasili, kama vile haki za ardhi, maeneona raslimali, utamaduni na desturi, ushauri na kushirikishwa.

Hatahvyo, hata pale ambapo pana utambuzi usiowazi au hata wa dhahiriwa makabila maalum au watu wa kiasili katia sheria yakitaifa kuhusiana nauraia, hii haimaanishi moja kwa moja kwamba kuna utekelezaji wa haki zakimsingi. Kwa mfano, kukosekana kwa cheti cha kuzaliwa, stakabadhi navitambulisho kunabako changamoto iliyosambaa baina ya watu wa kiasili

89. Uchunguzi wa ripoti zilizowasilishwa na mataifa wanachama chini ya kifungu cha 44 chaMkataba: Maoni ya Kuhitimisha ya Kamati inayohusika na Haki za watoto: Kenya, UN DocCRC/C/15/ADD.160 (CRC, Kenya 2001) aya ya 31.

90. Ona Ripoti ya Katibu maalum wa Umoja wa mataifa kuhusu watu wa kiasili nchini Kenya,aya ya 21.

91. Sheria ya bunge ya 88 ya mwaka 1995.92. Sheria ya bunge ya 196 mwaka wa1993.

26

Page 43: First page ILO.fm

katika bara zima na aghalabu hualemaza uwezo wao wa kupata huduma zajamii kati ya mambo mengineyo. Haki ya kuwa na jina na uraia ni suala lakawaida katika katiba nyingi Afrika, ikisaidiwa na sheria kuhusu uraia na usajili.Mara nyingi kutekelezwa kwa sheria kama hizi huzuiliwa, hasa katika upandwa watu wa kiasili, na kutofikiwa kwa maeneo wanamoishi watu wa kiasili,kutokana na hali kwamba mara nyingi, vituo vya kuwasajili viko mahali pamoja(kama ilivyo Kenya) au kama vimegatuliwa, watu wa kiasili huenda hawajuihatua zinazohitajika kwa kujisajili kutokana umbali huo au ujinga wakutosoma. Katika hali zingine, mtazamo wa kibaguzi wa kiutawala kuwaelekeapia ni changamoto nyingine. Hata pale ambapo pamewekwa mipango ya kutoavyeti vya kuzaliwa na aina nyingine za stakabadhi za kujitambulisha bila malipokwa watu wa kiasili, pana changamoto zingine nyingi. Pia ni nadra sana waokuzaliwa hospitalini, na kwa hivyo kusajiliwa kwao si jambo la moja kwa mojawakati wanapozaliwa. Katika hali nyingi ubaguzi na upembezwaji wa kihistoriahuchangia saana katika kutosajiliwa kwa watu wa kiasili. Zadi ya hayo, baadhiya makundi ya kiasili wanaoishi maeneo yanayovuka mipaka ya nchi moja auzaidi, wanaweza kukumbwa na changamoto zaidi za kiraia, hasa ikiwa wanaishimaisha ya kuhamahama. Huu ni mfano ulioko nchini Kongo

La délivrance de cartes d’identité à des personnes autochtones est peusatisfaisante. L’éloignement des centres hospitaliers, des campements ou villagesdes peuples autochtones ne favorise pas l’accouchement des femmes autochtonesdans les hôpitaux ou les centres de santé. Ce qui ne permet pas d’obtenir ladéclaration de naissance qui est l’élément fondamental pour l’obtention de l’actede naissance. Cette question, qui se pose aussi bien au niveau des populationsbantoues des villages enclavés, se pose avec plus d’acuité en milieu autochtone.93

Katia Afrika ya Kati nzima, wale wanaojulikana kama Mbilikimowaqnakumbana na changamoto za kupaata stakabadhi za kujitambulisha. Hatakatika mataifa kama Rwanda- ambako sheria inatambua hali ya nafasi yambelekama msingi wa uraia-, usajili wa watoto na umiliki wa stakabadhi zakujitambulisha unabaki changamoto kubwa.

1.6 Hitimisho

Tangu mwanzo ni wazi kwamba kuna utambuzi rasmi mchache sana wakikatiba au wa kisheria kwa watu wa kiasili katika sheria za Afrika. Ni wazikwamba matumizi ya misamiati ya aina aina mbalimbali katika sheria na sera zakiafrika kuwarejelea wale wanofahamika katika sheria ya kimataifa kuwa niwatu wa kiasili kwa kiasi fulani hayalingani na ni kinzani. Hata katika mfumowa kisheria wa mataifa binafsi, istilahi katika sheria na sera zinatumiwa kwakubadilishana na aghalabu inadokeza ukubalifu usiodhahiri kwamba angalauwatu wa kiasilia ni makundi yanayohitaji haki Fulani maalum ili kushughulikiahali zao maalum. Au, katika upande mwingine, baadhi ya mataifa yangalimalegevu zaidi kukubali hata ukweli huu wa kimsingi kama. Hata hivyo baadhiya mataifa yameanza sio tu kutambua upekee na mahitaji ya pekee ya watu wakiasili, lakini pia kuunda sheria na kuunda sera na mipango inayolenga makundihaya maalum. Licha ya ukweli kwamba istilahi ‘watu wa kiasili’, peke yake,haitumiki kirasmi katika sheria ya kitaifa katika mataifa yaliyotafitiwa (kando

93. ‘Utoaji wa vitambulisho kwa wayu wa kiasili hauridhishi kabisa. Miendo mirefu baina yahospitali (vituo vya afya) na kambi au vijiji vya watu wa kiasili inawazuia wanawake wakiasili kujifungulia hospitalini au katika vituo vya afya. Hii haiwaruhusu kupata taarifa za yakuzaliwa kwa watoto wao, ambazo ni sharti muhimu la kupata cheti cha kuzaliwa. Sualahili, ambalo pia linawaathiri Wabantu wanaoishi katika vijiji vilivyojitenga, linatokea zaidikwa watu wa kiasili.’ Wakifu wa Misitu ya Mvua/UKna OCDH, 2006, haki za watu wakiasili katika Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo, London, p.69. tazama:www.rainforestfoundationuk.org/files/droits_autochtones_final.pd.

27

Page 44: First page ILO.fm

na rasimu ya sheria katika nchi moja ya Afrika), mwelekeo chanya katikauundaji wa sheria au kuunda sera na mipango inayohusu yale makundi ambayoyangechukuliwa kuwa ya watu wa kiasili, unaweza kuonekana katika nchinyingi za Afrika.

Uundaji wa sheria, sera na mipango kama huu ungali wa kijumla tu nakatika hali zote zilizochunguzwa hautoi mfumo wa kina wa kuwatambua nakuwabainisha watu wa kiasili na ulinzi wa kiwango kipana cha hakizinazotambulika kwatika sheria ya kimataifa, kwa mfano. Hata hivyo, ni isharaya kuwepo kwa kuna kukubali polepole ukweli kwamba katika jamii nyingi zakiafika kuna makundi maalum yaliyokatika hali ya kudunishwa na kupembezwana kwamba yanahitaji hatua maalum ili kuweza kufaidika kutokana na haki zakibinafsi zinazotolewa kwa usawa kwa watu wote wa umma wa taifa.

Takriban katika hali zote, kuna ukosefu wa vigezo maalum vyakuyambulisha yale makundi yanayorejelewa na kiasi kikubwa cha istilahizinazotumika katika vyombo vya kisheria na sera kuwarejelea watu wa kiasili.Kighairi mojawapo ni rasimu ya sheria kuhusu haki za watu wa kiasili ya nchiniKongo. Huku ikiwa kwamba kukosena kwa fasili rasmi au utambuzi wakisheria wa watu wa kiasili hakutakikani kuzuia juhudi za kuziundia sheria hakizao kama makundi maalum au kuunda sera na mipango kushughulikia hakizao- na kweli imeonyeshwa katika uchunguzi huu mzima kwamba kukosekanakwa utambuzi wa kisheria wa watu wa kiasili haujazuia juhudi kufanywa ilikushughulikia haki zao- lakini kukosekana kwa kutambua upekee makundihaya, na haki zinazoambatana nao kama watu wa kiasili- kunaweza kuzuiajuhudi kama hizi.

Zaidi ya miaka kumi hadi ishirini iliyopita, kumekuweko na ongezeko laidadi ya jamii barani Afrika ambazo zimejitambulisha zenyewe kama watu wakiasili. Kujitambulisha wenyewe ni muhimu katika mjadala kwenye viwangovya kitaifa na kimaeneo kuhusu utambuzi wa kisheria wa watu wa kiasili.Kutokana na athari za hatua za kihistoria, hawa watu wamepembezwa katikanchi zao wenyewe na wanahitaji utambuzi na ulinzi wa haki zao za msingi zakibinadamu.

28

Page 45: First page ILO.fm

2 Kutobaguliwa

2.1 Utangulizi

Mojawapo ya matakwa ya kimsingi ya watu wa kiasili ni kutobaguliwa kwa hakizao. Ni hadi pale tu ambapo wamehakikishiwa ulinzi wa kutosha dhidi yaubaguzi ndipo watu wa kiasili wanaweza kufurahia haki muhimu za kibinadamukwa kiwango sawa na watu wengine katika jamii. Ili kufikia usawa uliobora nakuhakikisha kwamba hakuna ubaguzi dhidi ya makundi yaliyopembezwakihistoria, wakiwemo watu wa kiasili, serikali ina jukumu la ‘kuchukua hatuamaalum’

2.2 Sheria ya Kimataifa

Kanuni ya kutokuwepo na ubaguzi inatambuliwa katika vyombo vya kimataifana kitaifa na inatoa mfumo ambao kwao watu wa kiasili wanaweza kutafutaulinzi dhidi ya mapendeleo, kupuuzwa na kupembezwa. Kanuni hii imepewahadhi ya kimila kimila kimataifa94 na jus cogens.95 Mifano ya mikataba mikuu yakimataifa kuhusu haki za kibinadamu iliyo na vipengele vinavyopinga ubaguzi nipamoja na ICCPR na ICESCR. Vipengele vya CERD ni mahsusi zaidi, hivikwamba kifungu chake cha 2(1)(a) kinalazimu Mataifa wanachama yasijihusishekatika kitendo chochote ubaguzi wa kikabila dhidi ya watu au kikundichochote cha watu. Chini ya CERD, ubaguzi wa kikabila unamaanisha mipikayoyote inayowekwa au kutengwa kwa misingi ya kabila, rangi, uzao auchimbuko la kijtaifa au la kikabila la mtu fulani, kwa lengo la kumzuia mtu huyoasifurahie haki yake sawa na mtu mwingine yeyote.96

Mkataba wa 169 wa ILO hasa unawahakikishia watu wa kiasili na wamakabila haki ya ‘kufurahia haki za kibinadamu na uhuru wa kimsingi kikamilifubila kizuizi wala ubaguzi’ na unataja tena vipengele vya kwamba vipengele vyaMkataba uatumika ‘bila ubaguzi kwa watu hawa,waume kwa wake.’97 Kanuniya kutokuwepo na ubaguzi kama ilivyo katika mkataba huu pia imeingizwakatika taratibu za uteuzi na kuajiri kunakohusisha wait wa kiasili.98 Katikakuyatambua matatizo ya kihistoria na yaliyopo ambayo watu wa kiasiliwanakumbana nayo, Mkataba vilevile unaitisha kuchukuliwa kwa ‘hatuamaalum’99 ambazo zitafanywa kuwa sheria na kutekelezwa ili kufaniksha hadhiya uasawa baina ya watu, hasa kuhusiana na wale ambao wamekumbwa namatatizo yanayohusiana na sheria na vitendo vya kibaguzi. Makataba wa 111wa ILO unawalinda wafanyikazi wote dhidi ya ubaguzi kwa misingi ya mbari,rangi, dini, msimamo wa kisiasa, asili ya taifa Fulani, asili ya kijamii na vigezovingine kulingana na taifa lililoutilia sahihi baada ya kushauriana na mashirikayanayowawakilisha waajiriwa na wafanyikazi. Ubaguzi wa moja kwa mojana usio wa moja kwamoja umeshughulikiwa kwenye mkataba, ambaounalazimu mataifa kuchukua hatua za kukomesha ubaguzi kwa misingi ya

94. Imebainishwa na kukuliwa kwake ulimwenguni na mfululizo wa matumizi yake na mataifa.95. Hakuna kudunishwa kunakunakubaliwa kulingana kaida ya jus cogens, kama ilivyowekwa na

kifungu cha53 cha Mkataba wa Vienna wa mwaka wa 1969 kuhusu Sheria ya Mikataba.96. Kifungu cha 1(1) cha CERD.97. Kifungu cha 3 cha Mkataba wa 169 wa ILO.98. Kifungu cha 20 cha Mkataba wa 169 wa ILO kinasema ‘serikali zitafanya kila

kiwezekanacho kuzuia ubaguzi baina ya wafanyikazi wanaotoka kati ya watu husika nawafanyikazi wengine’.

99. Kifungu cha 4(3) cha Mkataba wa 169 wa ILO.

29

Page 46: First page ILO.fm

kabila, ‘asili ya taifa Fulani au chimbuko la kijamii’100 kati ya mambomengineyo. Ulinzi wa Mkataba wa 111 unafaa kwa hali zote za ajira na kazi, yaumma au ya kibinafsi na kuenea hadi kwenye elimu, mafunzo, ajira kazi(zikiwemo kazi/shughuli za kitamaduni za watu wa kiasili), usalama wa mudawa kazi na malipo sawa kwa viwango sawa vya kazi, kati ya mambomengineyo. Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu watu wa kiasili lililokubaliwahivi karibuni linathibitisha kuwa watu wa kiasili wako sawa na watu wenginewote, huku wakitambua kuwa haki za watu wote ni tofauti, wajichukulie kuwatofauti na waheshimiwe hivyo.101

Kanuni pacha za usawa na kutobaguliwa zimeimarishwa katika falsafa yakimataifa ya sheria za kibinadamu ya Afrika, ukiwemo mkataba wa Afrika.Mkataba wa Afrika unataja kwamba kila ‘ mtu atakuwa na haki ya kufurahiahaki na uhuru unaotambuliwa na kuhakikishwa katika Mkataba wa sasa bilamipaka ya aina yoyote kama ya kimbari, kikabila, rangi, jinsia, lugha, dini,maoni ya kisiasa au mengine yoyote, chimbuko la kitaifa au kijamii, mali, uzao,au hadhi nyingine yoyote’.102 Kurerejelea kwake kwa istilahi ‘bila mpaka’kimantiki unasema kwamba haki zipo kwa kila mtu watu binafsi wa jamiizinazojitambulisha kama watu wa kiasili. Katika kifungu cha 19, Mkataba waAfrika una vipengele hususan kuhusu usawa wa ‘watu’ wote kupiga marufukukutawaliwa kwa watu na watu wengine.katika Muungano wa Kiafrika waMalawi na wengineo dhidi ya Mauritania,103 Tume ya Afrika ilishikilia kwambadhuluma dhidi ya Wamauritania weusi kutokana na kutanguliwa kwa kanunimuhimu ya usawa kulingana na kifungu cha 19 ilikuwa ni kukiuka kifunguhicho. Ugunduzi huu inatufikisha kwenye hitimisho kwamba sheria yoyoteinayowabagua watu au kabila Fulani itakuwa imekiuka kifungu nambari 19.

Ikiangaliwa kutokana na mkabala wa aina ya ‘mbaguzi’, ubaguzi unawezakuwa wa aina mbili; ubaguzi wa kiwima na wa kimlalo. Ubaguzi wa kiwima niubaguzi unaotokana na serikali dhidi ya watu binafs, na unachukua namna yasheria, sera au mipango ya kibaguzi. Ubaguzi wa kimlalo uatokea baina yawahusika wasio wa kiserikali (kama watu binafsi au mashirika ya kibinafsi) naunachukua namna ya mitazamo, utambuzi au tabia za kibaguzi ya watu auvikundi dhidi ya mtu binafsi au kikundi cha watu.

Tukilenga kwenye namna na athari ya ubaguzi, mpaka unaweza kuwekwakati ya ubaguzi wa moja kwa moja na usio wa moja kwa moja.104 Ubaguzi wamoja kwa moja (de jure) unarejelea kutengwa au hali ngumu ambayoimejijenga dhahiri kwenye jambo kama hadhi ya kiasili, kwa mfano sheriainayoruhusu malipo ya mishahara duni kwa waajiriwa wote wa kiasili. Ubaguziusio wa moja kwa moja (de facto) unarejelea kutenwa kulikofichika aukusikotambulika kwa urahisi au hali ngumu na aghalabu inajitokeza tu katiautekelezaji halisi au athari mbaya ya sheria na wala sio kutoka kwenyevipengele vya sheria hasa. Mfano ni kama sharti kwamba wote wanaoombakazi lazima waweze kuandika vizuri katika kiingerez, Kifaranza au Kiasrabu.Kutokana na kufungamana kwao na lugha yao ya asili, na kiwango kikubwa chakutosoma, uwezekano wa kutimiza sharti hili unaweza kuwa wa chini mnobaina ya watu wa jamii za kiasii, na hivyo kusababisha ubaguzi dhidi yao.

100. Kifungu cha 2 cha Mkataba wa 111 wa ILO; anagalia pia ILO (2007)Mwongozo wa Mkatabawa 111 ILO, Uondoaji wa ubaguzi dhidi ya watu wa kiasili na watu wa makabila katika ajira nakazi.

101. Vifungu, 2 na 3 vya Azimio la Umoja wa Wataifa.102. Kifungu cha 2 cha Mkataba wa Afrika.103. (2000) AHRLR 149 (ACHPR 2000) 174.104. Angalia ILO (2007) Mwongozo wa Mkataba wa 111 wa ILO, Uondoaji wa ubaguzi dhidi ya

watu wa kiasili na wa makabila katika ajira na kazi,11.

30

Page 47: First page ILO.fm

2.3 Mielekeo ya kitaifa

Vipengele vya kikatiba na vinginevyo vya kisheria

Sheria nyingi, sera za serikali na utendaji ambavyo hivi leo vinaathiri haki zawatu wa kiasili moja kwa moja vilitangazwa kirasmi enzi za ukoloni. Botswanana Kenya ni mifano mizuri.

Mfano wa sheria kama hii ni Sheria ya Bunge la Botswana kuhusuUtemi.105 Iliyokubaliwa wakati wa utawala wa kikoloni. Sheria hii inatambuatu machifu/watemi wa kile kilichoitwa ‘makabila manane makuu’ kamawatemi. Athari ya moja kwa moja ya Sheria hii ni kwamba wale wasio wamakabila ya Watswana, wakiwemo Basarwa, wanachukuliwa kama wasio nawatemi kama wale watemi wa wenzao Watswana.

Vile vile, ukosefu wa usawa baina ya makabila mbalimbali nchini Kenyaunaweza kufuatiliwa kutoka nyuma kwenye sera na sheria za kikoloni navitendo vya baada ya ukoloni ambavyo viliimarisha ubaguzi wa kikoloni, kamavile Sheria Maalum ya (Utawala ) Kiwilaya ya 1934, Sheria ya Wizi wa mifugona Mazao ya 1933, sehemu ya 19 ya Amri ya Kujitawala kwenye Baraza ya1963, ambayo Gavana mkuu uwezo mkubwa wa kupitisha kipengele chochotecha kisheria ili kuhakikisha kuwa kuna utawala unaofaa, ambao kwa mujibu waeneo la Kaskazini Mashariki ulihusisha kutangazwa kwa hali za hatari ambzozilisababisha mauaji ya watu wengi na watu wengine wa kiasili kupotezamakaazi yao.

Leo hii, katiba nyingi za kiafrika za baada ya ukoloni zinashikilia kanuni yakutokuwepo kwa ubaguzi. Ingawa hakuna katiba yoyote inayopinga ubaguzidhidi ya watu wa kiasili moja kwa moja, karibu zote zinahusisha ‘mbari’ na‘ukabila’ (au hadhi ya ‘kikabila’ au ‘chimbuko’) kati ya sababu za kutokuwepona ubaguzi. Nyingi ya orodha hizi za sababu hazijatangazwa hasa kuwa wazi,hali inayoibua maswali ya iwapo kila mojawapo ya orodha hizi za sababu nikamilifu au zinahitaji fasili ya jumla zaidi. Korti ya Kikatiba ya Misri, kwa mfano,iliamuru kwamba sababu za ubaguzi zilizokataliwa ambazo zimeorodheshwakatika kifungu cha 40 cha katiba hazikuwa zimekamilika.106 Kifungu cha 40 chaKatiba kinakataza ubaguzi baina ya wananchi kulingana na haki wanazofurahiakwa misngi ya kuzaliwa, hadhi ya kijamii au tabaka, chama, mwegemeo wakisiasa na uhusiano wa kimbari au wa kikabila. Korti iliamua kwambakulikuweko na aina nyingine mbaya za ubaguzi ambao haujarejelewa wazi wazikatika vipengele vya kikatiba. Mwelekeo kama huu ungeruhusu sababu kamahadhi ya kiasili ‘kusomeka kwenye’ mipaka ya ulinzi wa kikatiba.

Katiba tatu za hivi karibuni kabisa, za Burundi, Kongo na Kongo DRC,zimechukua hatua za kuyahusisha makundi ya kiasili kwa kusisitiza kuwepokwa ulinzi wa waliowachache na dhamani ya stahaamala. Katika Dibaji yake,Katiba ya Burundi ya mwaka wa 2005 inatangaza kwamba vyama vya kisiasavya waliowachache na ulinzi wa makabila na utamaduni wa waliowachache nisehemu muhimmu ya uongozi mzuri. Aidha, katiba inalazimu kuwaWaburundi wote waishi kwa utangamano na stahamala na wenzao.107 Vilevile kila Mburundi ana jukumu la kuendeleza stahamala katika mahusiano yake

105. Kifungu cha 41:01 cha sheria za Botswana.106. Kesi ya Kikatiba ya nambari. 17, mwaka wa 14 mahakama, kikao cha Januari 14, 1995,

uamuzi uliochapishwa kwenye Gazeti Rasmi nambari 6 la mwaka wa 1995 tarehe 9Februari.

107. Kifungu cha 14 cha katiba ya 2005 ya Burundi.

31

Page 48: First page ILO.fm

na wengine.108 Katiba ya Kongo ya mwaka wa 2002 iliharamisha uchocheziwa kuleta chuki ya kikabila na pia kutoa wajibu kwa watu binafsi kukuzastahamala kati yao. 109 Katiba ya Kongo DRC ya mwaka 2006 inasonga hatuazaidi kuhusisha uanachama wa ‘utamaduni na lugha ya wachache’ kama msingiwa kutobaguliwa kulingana na ‘mbari’ na ‘kabila’110 zaidi ya hayo serikali inawajibu wa kukusa maisha ya utangamano baina ya makabila yote nchini nakulinda makundi yote ‘yaliyohatarini nay a wachache’.111

Baadhi ya nchi pia zimechukua hatua za kisheria za kuharamisha ubaguzi nachuki ya kimbari na kikabila. Mojawapo ya hatua kama hizi ni kupiga marufukuvyama vya kisiasa na uundaji wa vyama vya kisiasa kwa misingi ya kimbari, aukabila (nchini Rwanda na Niger). Katiba ya Rwanda haiharamishi tu kuundajiwa vyama vya kisiasa vinavyojibainisha kwa misingi ya ‘mbari moja, kabila,ukoo, eneo, au dini’, lakini pia inaelekeza kuwa vyama vya kisiasa vitii kanuniya umoja wa taifa katika shughuli zake zote.112 Huku kanuni za kikatiba za‘kuondoa migawanyiko ya kikabila’ na ‘kukuza umoja wa taifa’ zikiwa wazi nazimehalalishwa na mauaji ya halaiki ya mwaka 1994, hatari kubwa inayovizia nikwamba zinaweza kuwa shuruti za kikatiba za umuhimu wa kipuuzi hivikwamba hata sauti waliowachache kihalali zinazimwa na mahitaji yaokupuuzwa- hasa yale ya Wabatwa. Katika muhtsari waripoti yake, ujumbe waAPRM wa nchini Rwanda uligundua kwamba mwelekeo wa serikali ‘umejikitakwenye sera ya usilimisho’ na kwamba ‘inaonekeana kuna haja ya kufutiliambali utambulisho bainifu na kuwaunganisha watu wote katika mfumo mmojamkuu wa uchumi wa kijamii.’113 Kulingana na katiba ya Niger yamwaka 1999,‘vyama vya kikabila, kimaeneo, na kidini’ vimepigwa marufuku, na ‘propagandazote za wasifu wa kieneo, kimbari au kikabila’ na ‘aina yoyote ya ubaguzi wakimbari, kikabila, kisiasa au kidini’ vimepwa adhabu ya kisheria.114 Marufukukama haya pia yametolewa chini ya Kanuni ya Adhabu ya nchi ya Mali.115

Vipengele hivi vinaweza kuwa na athari sawa ya kuzima kumka kwa mahitajiwatu wa kiasili.

Ubaguzi wa kiwima na wa kimlalo

Ubaguzi wa kiwima unatokana na sera za kibaguzi zinazodhaminiwa naserikali, kama ilivyodhihirishwa kwa mofano mingi katika muhtasari huu.Ubaguzi wa kimlalo ambao aghalabu huwa umesambaa sana laki ambaohauonekani kwa urahisi, hautokani na sheria, sera au taasisi za Serikali lakiniunaoendelezwa na watu binafsi au na kikundi kimoja dhidi ya kingine. Katikakuonyesha wasiwasi unaohusiana na haya, Kamati ya CERD kuhusiana naEthiopia imeonyesha wasiwasi mkubwa juu ya ugomvi wa kikabila kote nchiniambao umesababishwa na ubaguzi wa kimbari na ‘mivutano ya kisiasa naukiukaji wa haki za kimsingi za kiuchumi, kijamii na kitamaduni, na kuzidishwakutokana na kushindania maliasili, chkula, maji safi na ardhi ya kilimo.’116

108. Kifungu cha 67 cha Katiba 2005 ya Burundi.109. Kifungu cha 11 na 14 cha katiba ya Kongo ya mwaka 2002.110. Vifungu vya nambari 11,12 na 13 vya katiba ya Kongo (DRC) ya mwaka wa 2002111. Kifungu cha 51 cha katiba ya Kongo DRC ya mwaka wa 2006.112. Kifungu cha 54 cha Katiba ya Rwanda.113. APRM ya Ripoti ya Uchunguzi ya Review aya ya 153.114. Kifungu cha 8(3) na 9(3) cha katiba ya Niger.115. Kifungu 55 cha sheria Nambari 61-99 AN-RM ya tarehe 3 Agosti 1961 kuhusu Kanuni ya

Adhabu.116. Kamati inayoshughulikia Kuondoa ubaguzi wa Kimbari, UN Doc CERD/C/ETH/CO/15,

aya ya 12, Juni, 20, 2007.

32

Page 49: First page ILO.fm

Ubaguzi wa kimlalo dhidi ya watu wa kiasili katika nchi nyingi unajitokezakatika aina kadhaa. Mahali kwingi, kwa mfano, watu wa kiasili kama Wabatwanchini Uganda wanetengwa na majirani zao; wanaepukwa na makabilamengine kama wapenzi; na wanachukuliwa kama wasiokomaa na walionyumakimaendeleo na kwa hali Fulani kama nusu-watu (wasio kamili). Hali kama hiipia inawakumba watu wengine wa makundi ya ‘Mbilikimo’ katika nchi kamaKameruni na Jamuhuri ya Afrika ya Kati. Aina mbaya zaidi ya mtazamo huuinadhihirika katika vitendo vinavyofanana na utumwa na ajira ya lazima kwa‘Mbilikimo’ vinavyofanywa na Wabantu wenye nguvu.117 Watu wengi katikanchi kama Burkina Faso, Kameruni na Chad wanawachukulia Wambororokama ‘wasiostaarabika’. Hasa wasichana wa Kimbororo wanakejeliwa nakubezwa, hali inayowafanya wasiende shuleni.

Katika hali hizi ni wajibu wa serikali kulinda haki za watu hawa wa kiasiliwaliohatarini. Mfano ambapo taifa limetekeleza wajibu huu unapatikana katikaKatiba ya Chad, am bayo inaharamisha mila zote zinazokuza ukosefu wauasawa baina ya wananchi. Huku ikiwa kweli kwamba utumwa na ajira yalazima vimeondolewa, mataifa husika hayafanyi chochote kuhakikisha kuwahizi sheria zinatekelezwa mkikamilifu, hasa uwanja wa kinyumbani (ndani yanchi yenyewe).

Ili kuhakikisha kuwa kuna usawa na hakuna ubaguzi, hasa kwa kiwango chakimlalo, serikali ya Uganda ilianzisha Tume Usawa wa Nafasi.118 Hata hivyo,watu wa kiasili hawajawakilishwa kweny Tume hiyo na haina vipengelevyovyote vinavyoshughulikia mahitaji maalum ya watu wa kiasli kwa njia yamoja kwa moja. Kulingana na waliomo katika tume, ni vijana, wanawake, nawatu walio na ulemavu tu ndio waliowakilishwa.119 Nchini Afrika Kusini, kortiza kushughulikia masuala ya usawa zilizoanzishwa chini Sheria ya Bunge yaKukuza Usawa na Kuzuia Ubaguzi usiofaa, pia zimeshughulikia suala la ubaguziwa kimlalo bila kuzingatia watu wa kiasili.

Mataifa yanaweza kutumia sheria ya jinai katika juhudi za kuondoa dalili zaubaguzi (kama vile matamshi ya chuki) baina ya watu binafsi. Nchini Botswanakwa mfano, sehemu ya 92(1) ya Kanuni ya Adhabu inachukulia kuwa ni kosa lajinai kutamka au kuchapisha maneno yanayodhihirisha chuki, kejeli aumadarau kwa mtu yeyote kwa misingi ya mbari yake, kabila au mahali pachimbuko lake, kati ya mengineyo.120 Sehemu ya 94 (1) ya inaufanya ubaguzikuwa ni uhalifu na ubaguzi kwa malengo hayo ina maana ya kumchukulia mtumwingine kwa njia isiyopendeza au kwa namna tofauti na ile ambayo mtuangemchukulia mtu mwingine yeyote kwa msingi wa mbari, rangi, uraia auimani yake. Tatizo ni kwamba adhabu kwa makosa haya ni ya P 500.00ambayo haitoshi (chini kidogo ya $US 100). Hata kama vipengele hivihavitumiki sana kuthibitisha haki za watu wa kiasili nchini Botswana,vinaongeza uzito wa kisanifu kwenye dhana kwamba hadhi yao lazimaiheshimiwe na watu wengine na vinatengeneza njia nzuri ya marekebisho.Nchini Niger, propaganda zote zenye sifa ya ‘umaenoe’ au zilizojikita kwenyeukabila au mbari na ubaguzi wote kwa misingi hii, vimeharamishwa (chini yakifungu cha 8 cha Katiba).

117. Angalia sehemu ya 8 na 9 hapo chini kwa mjadala wa kina.118. Katiba ya Uganda kifungu cha 32(3) na (4). Iliyo na jukumu ka kuondoa ubaguzi na ukosefu

wa usawa dhidi ya watu binafsi na vikundi.119. Sehemu ya 5(1).120. Sura ya 08:01 ya sheria za Botswana.

33

Page 50: First page ILO.fm

Ubaguzi wa moja kwa moja na usio wa moja kwa moja

Ubaguzi wa moja kwa moja unatokea pale ambapo upokezi wa kitofautiumehalalishwa waziwazi, kwa mfano kwa kurejelea watu wa kiasili kijumla aukwa kurejelea kikundi mahususi cha watu wa kiasili. Licha ya ulinzi wa kisheri,ukweli ni kwamba watu wa kiasili wanakumbwa n ubaguzi uliokita mzizi sanana ambao aghalabu umefichika (usio wa moja kwa moja). Hali hii inaonekanasana katika kiwango kikubwa cha umasikini na kutengwa kwa kijamii ambamowengi wa kiasili wanajikuta. Wakati mwingine athari yake ni ile ya kupuuzwana serikali kijumla.

Katika hali zingine matumizi ya sheria ambazo zinaonekana kuwa hazinamapendeleo yanaweza kuwa na athari mbaya, kwa mfano, kwa watoto wakiasili. Nchini Botswana, kwa mfano, matumizi ya adhabu ya kupigwa vibokohususan yanachukiwa na wazazi na wanafunzi wa Kibasarwa kwa kuiona kamakujiwekelea ugeni unaokinzana na utamaduni wao. Desturi iliyopo nchiniAlgeria inawazuia wazazi kuwapa watoto wao majina ya kienyeji au ya‘kitamaduni.’ Sera ya kitaifa kuhusu elimu inawalazimisha watoto wawaliowachache kusoma na kukariri vifungu vya Kurani bila hata kuelewakwani wao si Waislamu.

Nchini Algeria, matokeo ya baadhi ya sera za kiserikali ni kukwamizaukuaji wa utamaduni wa tamaduni zisizo za Kiislamu wala Kiarabu. Ikichuliwakwamba ubaguzi huu haukulengwa hasa dhidi ya Waamazigh, unawezakuonekana kama ubaguzi usio wa moja kwa moja. Katika Burkina Faso, sheriakuhusu wanyama wanaorandaranda unasabaisha kupotea kwa ng’ombe wengiwa Wambororo amboo ni muhimu kwa kujikimu kwao kimaisha. Kuhusujamii ya wafugaji ya Fulani, imeonekana kwamba jamii hiyo ya wafugaji ni katiya makundi yaliyopuuzwa sana nchini Naijeria. Iro iligundua kuwa sera zaserikali zimelenga kuendeleza mtaji wa mifugo jambo linalozidhuru jamii zakuhamahama.121 Kwa mfano pesa nyingi zinatumiwa katika kuchanja ng’ombebadala ya kuwapa kinga watoto wa wafulani wahamahamaji dhidi ya maradhi.Wafulani wahamahamaji pia wanakumbana na ubaguzi katika mikono ya jamiiwenyeji wanaohisi kwamba Wafulani wanaingilia himaya zao. Sehemu yamaitikio ya serikali kwa masaibu ya Wafulani wahamahamaji ni Mpango waElimu kwa Wahamahamaji uliodhaminiwa na shirikisho, unaowalenga wao.Nchini Mali, sheria kuhusu ndoa ya mwaka wa 1962 - iliyotumiwa kukomesha‘baadhi ya desturi zilizopitwa na wakati ambazo zinafaa kuondolewa katikajamii’122 - ilipunguza muda wa sherehe za harusi hadi siku moja na gharama zamaandalizi yake hadi kisichozidi 20 000 CFA (40$).123 Sheria hii ilichukuliwana makundi ya kiasil, hasa Watuareg, kama ya kinasibu tu na ni kuingiliwakusikokubalika katika imani zisizo za kidini zinazohusu dhamani ya ndoa nasherehe za harusi.

Sheria ya nchi ya Sudan in vipengele ambavyo vinaadhiri sana haki nadesturi za kitamaduni za watu wa kiasili, ijapokuwa sheria hizi zimeelezwakatika mtindo wa kutobagua, na haziwalengi hasa watu wa kiasili. Vipengelevya Sheria ya Jinai ya mwaka wa 1991 ambavyo vina umuhimu sana katika halihii ni pamoja na;

• Kupigwa marufuku unywaji wa pombe(kifungu cha 78)

121. Angalia Iro, ‘Elimu ya wahamahamaji na Elimu kwa Wafulani wahamahamaji’, online: <http://www.gamji.com/fulani7.htm> (accessed 6 August 2007).

122. P Boilley (1999) Les Touaregs Kel Adagh. Dépendances et révoltes: du Soudan français au Malicontemporain, p 311.

123. Loi No 63-19 AN-RM ya Januari 25, 1963 iliyorekebisha vifungu 10, 24 et 43 vya Loi No 62-17 ANRM du 3 février 1962 kuhusu Kanuni ya Ndoa ya Mali.

34

Page 51: First page ILO.fm

• Uuzaji wa pombe(kifungu cha 79)• Kupigwa marufuki kwa vitendo vya aibu na viovu (kifungu 152) na• Kupigwa marufuku kwa ukahaba na uasherati (kifungu cha 145-

146)

Upikaji wa pombe, unywaji na uuzaji wa pombe aghalabu huwa ni sehemuya utamaduni na maisha ya jamii za watu wasiowaislamu wasio na makaazikutoka Kusini mwa Sudan, wakiwemo watu wa kiasili, lakini sio walewanaotoka Kaskazini ambao san asana huwa ni Waislamu. Kwa hivyo sheriamara nyingi inawaathiri watu wasio na makao kutoka kusini ambao siWaislamu. Vivyo hivyo, kwa kuwa ndoa za kiasili hazitambuliwi na mamlakakwa sababu hazifuati taratibu zanazotolewa na sheria na badala yakezinaambatana na mambo ya kimila, wanandoa wanaweza kuhukumiwa kwauasheratu na tabia chafu au wanawake wahukumiwe kwa ukahaba ingawakihalisia wamefungamanishwa kwa pingu za kifamilia kama mke na mume.

Ubaguzi usio wa moja kwa moja pia unaweza kutokana na upuuzaji aukutofanya chochote kwa upande wa serikali. Kwa sasa hakuna sheria yoyotenchini Misri (na nchi nyingi nyinginezo)ambayo inashughulikia na kutekelezakikamilifu hatua za kutimiza haki za watu wakiasili (na wenginewaliopembezwa) kama inavyodokezwa katika Katiba ya Misri. Kutokana nahaya, makundi ya kiasili (na mengine yaliyopembezwa) wanakumbwa naubaguzi na mapendeleo kutokana na sheria na sera za serikali zilizopo ambazozinashindwa kuzingatia hali maalum za makundi haya.

Dhana ya ‘hatua maalum’

Sera za hatua maalum au za uteuzi maalum zanatambuliwa kama mbinumuhimu ambazo kupitia kwazo mataifa yanaweza kufidia dhuluma na ukosefuwa uasawa wa awali au wa sasa, hasa kwa watu wa kiasili. Pale ambapo kunatakwimu sahihi, mara nyingi zinafunua matokeo ya ubaguzi, kupuuzwa nakutowajali watu wa kiasili katika mataifa. Nchini Mali kwa mfano, takwimuzilizopo zinaonyesha tofauti ya wazi kabisa ilyopo baina ya wanaojua kusomana kuandika katika umma mzima ya asilimia 23 kwa wastani, na takribaniasilimia 14 kwa wastani katika maeneo matatu ya nchi wanamopatikana watuwa kiasili. Tofauti hii pia ipo kwa upande wa kiwango cha kuhudhuria shule(asilimia 47 kwa wastani kitaifa ikilinganishwa na asilimia 31 kwa wastanikimaeneo).

Katika kifungu cha 23(2), Katiba ya Namibia inatambua hitaji la kuwepo nahatua maalum (uteuzi maalum) kutokana na dhuluma na kukiukwa kwa haki zakibinadamu chini ya utawala wa ubaguzi wa rangi:

Hakuna kitu chochote kilichoko hapa kwenye kifungu cha 10 (kipengele chausawa) kitazuia Bunge lisitekeleze sheria iliyo na vipengele ambavyo, kwa njiaya moja kwa moja au isiyo ya moja kwa moja, ni vya maendeleo ya watundani ya Namibia ambao wamedhulumiwa kijamii, kiuchumi au kielimukutokana na sheria au vitendo vya kibaguzi au vya utekelezwaji wa sera namipango inayolenga kurekebisha hali ya kukosekan kwa usawa kijamii,kiuchumi,au kielimu katika jamii ya Namibia kunakotokana na sheriana auvitendo vya kibaguzi au vya kupatikana kwa usawa wa mipangilio ya hudumaza umma, kikosi cha polisi, jeshi na huduma za magereza.

Kwa kurejelea hususan, hali ngumu za kijamii, kiuchumi na kielimu,vipengele hivi vinafungua mlango kwa watu wa kiasili nchini Namibia kufaidikakutokana na utekelezwaji wake (vipengele hivi). Hata hivyo, katika uhalisiamambo hayajakuwa hivyo.

35

Page 52: First page ILO.fm

Katiba ya Ethiopia, chini ya kifungu cha 89(40) inatoa wajibu kwa serikali,katika viwango vyote, kutoa usaidizi maalum kwa makundi yasiyobahatikakatika maendeleo ya uchumi wa kijamii. Chini ya Katiba ya Botswana, serikaliiliruhusu kuwapa heshima au nafuu kwa wanachama wa makundi yoyoteyaliyotajwa kwenye ibara ya usawa (sehemu ya 15) ikiwa- kulingana na halimaalum za wanachama wa kikundi hicho- kufanyiwa hivyo ‘kunahalisi katikajamii ya kidemokrasia.’124 Upekee huu unaruhusu kuchukuliwa kwa hatuaambazo zinaweza kufanikisha urekebishaji wa ukosefu wa usawa wa awali naunaoendelea ili kuzileta jamii zilizopembezwa kama vile watu wa kiasili katikakiwango ambacho wanaweza kuishi kwa usawa kama jamii nyinginezo. Kwabahati mbaya, kipengele hiki hakijatumiwa kikamilifu na serikali. Baadhi yawatu wa kiasilihufaidika kutokana na sera ya maendeleo ya serikali inayoitwaMpango kwa Wakaaji wa Maeneo Yaliyombali (Remote Area DwellersProgramme- RADP), ambao awali uliitwa Bushman DevelopmentProgramme(Mpango wa Watu wa Mwituni). Mpango huu unalenga kuletanyenzo kama shule na huduma za afya karibu na watu wanaoishi maeneo yambali- ikimaanisha pia watu wa kiasili.125 Hata hivyo, mpango huuumedhoofishwa kutokana na sera ya kiserikali ya kutokuwepo na ukabila,inayopelekea watu wa kiasili kushindana, na kushindwa, na makabila menginekatika sehemu zilizombali.

Ili kuhakikisha kwamba kuna haki, usawa na hata kuwakilishwa, Katiba yaNigeria ina vipengele vya matumizi ya kanuni ya ‘hulka ya shirikisho’ katikauteuzi wa maafisa wa umma ili kukuza umoja wa kitaifa na kuendeleza fahiwaya kuwa sehemu ya wengine baina ya raia.126 Hii hufanya kazi kama aina yahatua ya uteuzi maalum. Kanuni ya hulka ya shirikisho husambaa kwa usawakwa serikali zote kwenye kiwango cha kitaifa na mashinani.127 Kutokana nahayo, kuna mfumo wa majimbo unaotumika kwa ajili ya kuajiri kwenyeutumishi wa umma, uteuzi katika taasisi zinazomilikiwa na serikali,128 uteuziwa makurutu katika kikosi cha polsi, jeshi na vikosi vingine vya usalama. Hatahivyo, watu wa kiasili kama vile Wa-Ogonis na Ijaws, wametengwa waziwazi,hasa kutoka kwenye vyeo katika kampuni za mafuta zinatawaliwa na serikaliambazo zimo katika makaazi yao ya tangu jadi.129

Katika nchi ambamo mna ‘uteuzi maalum’, manufaa yake aghalabuhayajasambazwa kikamilifu kuwahusisha watu wa kiasili- au kwa kweli, hatuahizi zimekuwa za kijumla tu na haziwakilishi sera yoyote pana ya kushughulikiaubaguzi dhidi ya watu hawa. Katiba ya Afrika Kusini ina ikibali kwamba,kutokana na ukosefu wa usawa wa awali, hatua ya uteuzi maaluminakubalika.130 Hatua kama hizi zinalenga ‘Waafrika kusini weusi’, wanawakena walemavu. Watu wa kiasili hawalengwi katika sheria wala utekelezaji wake.Katiba ya Uganda pia ina idhini za hatua ya uteuzi maalum kwa minajili yawanawake, watoto na walemavu, lakini pia kwa makundi yaliyopembezwa kwa

124. Sehemu ya (4)(e).125. M Bolaane na S Saugestad ‘Mother-Tongue: Old Debates and New Initiatives in San

Education’ Indigenous Affairs, IWGIA, 1/06, 48.126. Sura ya II sehemu ya 14(3) ya Kati ba yaNigeria.127. Sehemu ya 14(4) ya Katiba ya Nigeria.128. Mfuno wa kimajimbo, wa Wizara ya Elimu ya Shirikisho, wa kusajili wanafunzi unatumika

kwenye shule za upili na taasisi za elimu za serikali ya shirikisho. Angalia C Nwagw, ‘TheEnvironment of Crisis in the Nigerian Education System’ (1997) 33 Comparative Education92. (‘Mazingira ya Mgogoro kwenye Mfumo wa elimu wa Nigeria’ (1997)) 33 ElimuLinganishi 92).

129. A. Onduku, Towards a culture of peace in the Niger Delta, kutoka http://www.waado.org/NigerDelta/Essay/ResourceControl/Onduku.html (accessed 21 July2007).

130. Sehemu ya 9(2) ya Katiba ya Afrika Kusini.

36

Page 53: First page ILO.fm

misingi ya ‘sababu zozote zilizoletwa na historia, desturi au mila.131 Jukumu lakuchukua hatua ya uteuzi kwa faida ya makundi yaliyopembezwa pialimepanuliwa kikatiba hadi kwenye mabaraza ya serikali za mitaa. Katibainalazimu kuwa sheria inayotumiwa na serikali kudhibiti mabaraza ya mitaairuhusu kuwepo kwa uteuzi maalum kwa makundi yote yaliyopembezwaambayo yatajwa kwenye kifungu cha 32.132 hata hivyo, mbali na wanawake,vijana na watu wenye ulemavu, sheria za serikali ya mitaa haina vipengelevyovyote vya kuwafaidi watu wa kiasili. Wala sheria haiweki mipangilio yakuhakikisha kuwa watu wa kiasili wanashiriki kikamilifu katika michakato yakufanya maamuzi.

2.4 Hitimisho

Ijapokuwa katiba zao zinahusisha kanuni ya kutobaguliwa, mifumo ya kisheriaya mataifa mengi ya Afrika yanashindwa kuzuia kikamilifu ubaguzi dhidi yawatu wa kiasili. Huku ikiwa ni jambo la muhimu na la kutia moyo kwambabaadhi ya mataifa (kama Burundi, Kongo na Kongo DRC) yameipa umuhimuwa kikatiba dhamani ya stahamala kwa waliowachache, kupiga marufukuuhamasishaji wa umma kwa misingi ya kikabila au mbari (kama ilivyo nchiniRwanda) kunaweza kuzima utamkaji wa madai ya watu wa kiasili. Kuzuiaubaguzi wa watu binafsi au vikundi dhidi ya watu binafsi wa kiasili au umma,baadhi ya mataifa (kama Botswana) yameharamisha maneno ya chuki kwamisingi ya kikabila, mbari au chimbuko. Hakuna taifa linalotumia sheriainayopinga ubaguzi ili kutekeleza jukumu lake la kulinda haki za watu wa kiasili.

Ubaguzi uanaofanywa na taifa aghalabu huwa ni wa aina ya upuuzaji, naunaonekana sana kwenye kiwango cha unyimwaji wa aina Fulani kwa mujibuwa ardhi, afya na elimu. Kusipokuwepo na takwimu za kutegemewa, mitindoya ubaguzi huelekea kubakia fiche. Hata hivyo, takwimu na data zinazohitajikahaipo katika mataifa yote, na hivyo kufanya utambuzi wa kiwango ambachoshida hii imefikia kuwa mgumu sana.

Licha ya athari mbaya zaidi za ubaguzi uliojikita sana na wa muda mrefudhidi ya watu wa kiasili, mataifa machache yamechukua hatua maalumkushughulikia hali hii mbaya. Katika hali ambapo hatua maalum zimefanywa,zimekuwa za kijumla sana, na hazilengwi watu wa kiasili, na wala haziambatanina hatua za kuhakikisha pana ujenzi wa uwezo wa makundi ambayo awaliyalikuwa katika hali ngumu,wakiwemo watu wa kiasili.

131. Kifungu cha 32(1) Licha ya kitu chochote katika Katiba hii, serikali itachukua hatua yauteuzi maalum kwa minajili ya makundi yaliyopembezwa kwa misingi ya jinsia, umri,ulemavu au sababu nyingine ya kihistoria, desturi au mila, kwa kemgo la kurekebishaukosefu wa usawa uliopo dhidi yao.

132. Kifungu nambari 180(2)(c).

37

Page 54: First page ILO.fm
Page 55: First page ILO.fm

3 Kujitawala, mashauriano na kushiriki

3.1 Utangulizi

Kujitawala, mashauriano na kushiriki ni baadi ya haki muhimu sana za watu wakiasili. Haki ya radhi iliyohuru, ya awali na baada ya kupata habari za kutosha,imo kwenye UNDRIP, na haki ya watu wa kiasili kushiriki na kushauriwa imokatika Mkataba wa 169 wa ILO. Dhana zote zinafanana kwa yaliyomo. Kiinicha mashauriano na kushiri ni sehemu ya mhimili wa mkataba wa 169 wa ILO.Kifungu cha nambari 6 cha mkataba kina kinasema kuwa ni lazima watuwashauriwe kupitia kwa taratibu zinazofaa na kupitia kwa taasisizinazowawakilisha. Pia kinasema kuwa ushauri huo lazima ufanywe, kwa nianzuri kwa namna inayolingana na hali na lengola kuafikia makubaliano au radhi yahatua zilizopendekezwa. Kiungo kingine cha dhana ya mashauriano ni ile yauwakilisho wa kutosha - wale wanaoshauriwa lazima wawe wawakilishi wakweli wa watu wa kiasili. Zaidi ya hayo, haki ya watu wa kiasili kushauriwalazima izingatiwe kutokana na haki yao ya kujiamulia mambo muhimu yamaendeleo yao, kama ilivyo katika kifungu cha 7(1) cha Mkataba wa 169 waILO.133 Ili kufanikisha kushiriki huku, Mkataba pia unalazimu kuanzishwa kwambinu za maendeleo taasisi na miradi ya watu wa kiasili na wa makabila.

Haki za kushauriwa, kushiriki na kujitawala, zinaweza pia kuchukuliwakama viungo vya haki ya kujiamulia mambo. Mkataba wa 169 wa ILOhaushughuliki na haki ya kujiamulia mambo, lakini haki hii inathibitishwa naUNDRIP, ambayo inafasili kuwa haki ya kujiamulia inahusisha haki ya kuwahuru au kujiamulia katika masuala yanayohusiana na ‘mambo ya ndani au yakienyeji’ ya watu wa kiasili.134 Zaidi ya vyombo hivi, Mapatano ya Kiafrikakuhusu Haki za Kibinadamu na Haki za Watu yanahakikisha haki ya kuishi nakujiamulia kwa watu wote, ambayo inahusisha haki ya kuamua hadhi yao yakisiasa na kufuatilia maendeleo yao ya kiuchumi na kijamii.135 Zaidi ya hayo,Mapatano yanaeleza kuwa watu wote watkuwa huru kuondosha mali namaliasili yao.136 Katika maoni yake ya kisheria kuhusu Azimio la Umoja waMataifa kuhusu haki za watu wa kiasili, Tume ya Afrika kwa wazi inazitia hakiya watu wa kiasili kujiamulia, katika muktadha hadhi ya kieneo ya Mataifa,ikitaja yafuatayo:

…Tume ya Afrika kuhusu Haki za Kibinadamu na Haki za watu, inaoneleakuwa haki ya kujiamualia katika matumizi yake kwa watu na jamii za kiasili,kwa kiwango cha Umoja wa Mataifa na cha Kimaeneo, zafaa zieleweke kuwazinahusisha msururu wa haki zinazohusiana na kushiriki kikamilifu katikamasuala ya kitaifa, haki ya kujiamulia mambo ya kienyeji, haki ya kutambulikaili kushauriwa wakati wa kurasimu sheria na mipango inayowahusu,kutambua mifumo na desturi za maisha yao pamoja na uhuru wa kutunza nakuendeleza utamaduni wao. Kwa hivyo ni mkusanyiko wa mambo tofautikatika kutekeleza haki za kujiamulia, ambayo yanakubaliana na umoja nahadhi ya kimaeneo ya Vyama vya Kitaifa.137

133. Ripoti ya Kamati ya watu watatu iliyoundwa kuchunguza Uwakilisho kwa tuhuma zaEcuador kukataa kutii mkataba wa 1989 (nambari 69) kuhusu watu wa kiasili na wamakabila uliofanywa chini ya kifungu cha 24 cha mkataba wa ILO na ConfederaciónEcuatoriana de Organizaciones Sindicales Libres (CEOSL) aya ya 44.

134. Kifungu nambari 4.135. Kifungu nambari 20.136. Kifungu nambari 21.137. Maoni ya ushauri ya Tume ya Afrika ya kushughulikia haki za kibinadamu na Haki za Watu juu

ya Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watu wa kiasili, Banjul, 2007, aya ya. 27.

39

Page 56: First page ILO.fm

Vipengele muhimu vya haki za watu wa kiasili za kushauriwa na kushiriki nipamoja na haki ya kupiga kura na haki za kisiasa zinazohusiana nayo, haki yakushauriwa katika upana wa hatua uundaji wa sheria na utawalazinazowaathiri, ikiwemo marekebisho ya kisheria na urasimu na utekelezajiwa sera mipango na miradi ya maendeleo. Pia idadi ya haki nyinginezo,ikiwemo heshima ya matumizi ya ardhi na maliasili, imehusishwa. Mkataba wa169 wa ILO138 na UNDRIP139 vyote ninashughulikia masuala haya. Watu wakiwasili pia hutilia mkazo kwenye haki ya kujitawala na haki ya kushriki katikauongozi wa jamii pana. Kujitawala kunachangia katika kuzitia nguvu desturi zakiafrika na inaweza kuonekana kulingana na Vifungu vya 21 na 22 vya Mkatabawa Afrika ambavyo vinashughulikia na haki za watu au jamii za kuwa hurukuuza maliasili yao na haki ya jamii hizi kwa maendeleo ya kiuchumi, kijamii nakitamaduni. Baadhi ya masuala ya kujitawalia maliasili yameshughulikiwa katikasira hii, pamoja na sura juu ya ardhi, maeneo na raslimali.

Vyombo kadhaa vya kimataifa vya haki za kibinadamu vina vipengelekuhusu haki ya kushiriki katika siasa, ingawa kwa namna tofautitofauti. Katikakifungu cha 23 cha Mkataba wa Afrika kinahakikisha haki za wananchi kushirikikatika kusimamia masuala ya umma, na kuhudhuria sherehe za hadhara kati yamambo mengine. Kifungu cha 25 cha ICCPR kinasema kwamba kilamwananchi ana haki na nafasi, bila kubaguliwa kushiriki katika kuendeshamasuala ya umma kupiga kura na kuchaguliwa kwenye uchaguzi halali wakimuhula ambao utafanywa kwa haki ya kupiga kura iliyobia na sawa na kupatahuduma za umma nchini mwao kwa viwango sawa.

3.2 Muundo wa Serikali na Utawala mkuu

Baadhi ya katiba sheria na miundo ya serikali za Kiafrika zilizochunguzwakatika muktadha wa wa utafiti huu zinavipengele vya uongozi wakushirikishwa, na hata zingine zinasonga mbele kuzungumzia swala lakujiamulia. Miundo ya kiserikali inatofautiana kwanzia ile ya ilyogatuliwa,auhata ya serikali za shirikisho, hadi zile za amabapo uwezo wa kufanya maamuziuko kwenye makao makuu. Hata hivyo mifumo michache sana ya kisheria aumiundo ya utawala, ikiwa ipo, imerasimisha kushiriki kwa watu wa kiasili kwanamana ya kimfumo, licha ya ukweli kwamba mifumo na miundo kama hiiinatoa nafasi ya kuweka mifumo kama hii.

Kipengele cha pekee cha Katiba ya Ethiopia ni haki ya kujiamulia.140

Kifungu cha 39 kinasema kuwa ‘kila Taifa, raia na watu nchini Ethiopia wanahaki ya kujiamulia bila vikwazo’. Vilevile, katiba inakipa kila kikundi haki ya‘kujitawala kikamilifu amabayo inahusisha haki ya kuanzisha taasisis za utawalakatika eneo kinamokaa na uwakilishwaji uliosawa katika taifa na Serikali zashirikisho.141 Ingawa vipengele hivi vinaelekea kulipa kila kabila haki sawa zakujitawala na kujiongoza, serikali nchini Ethiopia kijumla zinatawaliwa namakabila yaliyo na nguvu hivi kwamba makabila madogo, wakiwemo watu wakiasili, hayana ushawishi mkubwa.142

Dhana ya ya watu kujiamulia pia inajitokeza kwenye katiba ya Burundi,ambayo inataja kwamba:

138. Vifungu vya 6 na 15, kati ya vinginevyo.139. Vifungu vya 19, na 10, mtawalia.140. Katiba ya Ethiopia kifungu cha 39(1).141. Katiba ya Ethiopia,kifungu cah 39(3).142. Kjetil Tronvoll, Minority Rights Group International, Ethiopia: A New Start? 19 (2000).

40

Page 57: First page ILO.fm

Kila mtu ana haki ya kuishi. Kila mtu ana haki isiyotengeka ya kujiamulia bilakuelekezwa. Wako huru kujiamulia maendeleo yake ya kiuchumi na kijamiikwa namna waliyoichagua wenyewe.143

Katiba ya Afrika Kusini inazungumzia haki ya kujiamulia katika mfumo wahadhi ya himaya ya taifa. Serikali imetoa idhini ya jamii mbalimbali kujitawalakupitia kwa kanuni yake ya utawala wa ushirika.144 Kwa hivyo, kinadharia,watu wa kiasili lazima wawe na ushawishi na kutekeleza wajibu muhimu katikanyanja za uongozi. Hata hivyo, kutokan na sababu kwamba mara nyingi huwawachache na wenye uwezo mdogo wa kiuchumi, wanaendelea kupembezwa.

Ni kanuni ya kimsingi ya katiba ya Eritrea kuhakikisha kuwa wanachi wakewanashirikishwa katika hali za kisiasa, kiuchumi, kijamii na kitamaduni za nchiyao.145 Zaidi ya hayo katiba inadai kuwepo kwa taasisi zinazofaa kuhimiza nakuimarisha ari na kushiriki kwa watu katika jamii zao.146 Hata hivyo, si dhahirini vipi watu wa kiasili kwa kweli hufaidika kutokana na vipengele hivi. Hukuvipengele vya kikatiba vikiwa bado havijatekelezwa, havijaweza kutumikakatika baraza lolote kwenye kiwango cha kitaifa, ikiwemo idara ya mahakama.

Nigeria inaendesha mfumo wa serikali ya shirikisho. Huu ni mkakati wakikatiba wa kuhakikisha kuwa kuna uwakilisho na kushirikishwa sawa kwaWanaijeria wakiwemo watu wakiasili na wa makabila ya wachache, katikautawala.147 Ili kukuza kushiriki kwa watu wa kiasili katika sera ziznzowaathiri,serikali imezindua mipango kama vile Baraza la Muungano wa Maendeleo yaUchumi wa Kijamii wa Serikali ya Kikatiba ya Niger Delta, unaohusishawawakilishi wa seriklai na wanajamii, unaolenga kuziinua jamii zinazozalishamafuta.148

Kinyume na haya, Kenya ni Taifa la umoja lillilo na serikali kuu kulingana naKatiba yake. Majaribio ya kutia vipengele kuhusu serikali gatuzi(ya shirikisho)kwenye mchakato wa marekebisho ya kikatiba yalizua pingamizi nyingi.Kwenye stakabadhi ya mwisho iliyowasilishwa wakati wa kura ya maoni yakitaifa, hili lilikuwa mojawapo ya masuala nyeti mno.149 Serikali kuu imepewamamlaka makubwa katika kuitawala nchi. Rais (ambaye ndiye mkuu waserikali) anawateua Wakuu wa Mikoa ambao ni watumishi wa umma nahawana usemi kuhusiana na jinsi masuala ya kimkoa yanavyoendeshwa. Hukukukiwa hakina vipengele vya moja kwa moja Katiba ya Kenya kuhusukushirikishwa na kushauriwa kwa watu watu wa kiasili juu ya masuala yakufanya maamuzi, katiba inaruhusu kushiriki katika siasa kupitia kwa vipengelevilivyomo katika Sheria ya Haki za kibinadamu (Bill of rights) kama vile haki ya

143. ‘Tout peuple a droit à l'existence. Tout peuple a un droit imprescriptible et inaliénable àl'autodétermination. Il détermine librement son statut politique et assure son développementéconomique et social selon la voie qu'il a librement choisie.’

144. Katiba ya Afrika Kusini sehemu ya 40-41.145. Kifungu nambari 7(1).146. Kifungu cha 7(3).147. Sehemu ya 14(4) ya katiba ya Naijeria.148. Uanachama wa baraza hili umekosolewa kutokana na serikali kuonekana kushindwa

kuwachagua wawakilishi wa umma wanaofaa kuwa kama wanachama wa kamati. Angalia:International Crisis Group ‘Nigeria’s Faltering Federal Experience’ (2006) 1 African Report..

149. Angalia Rasimu ya Katiba ya Wako iliyowakilishwa wakati wa kura ya maoni mnamoNovemba 2005 (ilikuwa Rasimu ya Katiba iliyoungwa mkono na serikali ya sasa kinyume naRasimu ya Bomas ambayo iliyokuwa na vipengele vya serikali ya ugatuzi na kukubaliwa nawajumbe katika Kongamano la Kitaifa kuhusu Katiba). Rasimu ya Wako baadaye nawakenya wengi na hadi kufikia sasa hakuna katiba ambayo imekubaliwa na nchi badoinaendeshwa kwa Katiba ya tangu Uhuru ya mwaka wa 1963 iliyo na marekebisho anuwaiambayo yammempa rais na serikali kuu mamlaka makubwa zaidi.

41

Page 58: First page ILO.fm

kukutana, kuungana na kujieleza pamoja na kufanya uchaguzi wa mara kwamara.

Kifungu cha 55 cha Katiba ya Misri kina vipengele kuhusu haki ya kilamwananchi kuunda vyama kulingana na sheria. Vipengele hivi vinaelekea kutoamfumo wa jumla wa kisheria ambao unawapa watu wa kiasili nchini Misri hakiya kuungana na kushindania uwezo wa kisiasa, hasa kwenye kiwango chamashinani. Hata hivyo, haonekani kuwa ndivyo ilivyo. Njia nyingine tu yapekee ambayo watu wa kiasili wanaweza kuwa na sauti katika uendeshaji waofisi ya umma katika maeneo yao ni kupitia kwa kugmbea kura ama kamawatu binafsi au kama mwanachama wa chama kingine. Shida iliyopo nikwamba watu wa kiasili kijumla hawajahamasishwa vilivyo. Wanaishipembezoni mwa michakato ya kisiasa wakiwa na ushawishi mdogo wa kisiasaau bila.

3.3 Muundo wa mashirika ya kufanya maamuzi

Katika mipaka ya miundo ya Serikali mbalimbali kama ilivyoelezwa hapo juu, nivizuri kuchanganua ushiriki wa watu wa kiasili katika vyombo vya kufanyamaamuzi kwenye kiwango cha kitaifa. Kama inavyoonekana hapo chini, baadhiya mataifa yamejaribu kuanzisha vyombo vya kuwakilisha masuala ya watu wakiasili, au hatua za uteuzi maalum ili kushughulikia hali ya ukosefu wa watu wakiasili kushirikishwa katika vyombo vya kitaifa kama vile Bunge. Hata hivyo,hatua kama hizi zinatofautiana katika kimawanda, na changamoto zipo katikautekelezwaji wake. Zaidi ya hayo, kama inavyoonekana kwenye mifano yahapo chini, mikakati ilyowekwa ni ya jumla na wala haijaambatana hasa na serapana au mikakati ya hatua kwa hatua iliyopo kwa watu wa kiasili kwenyekiwango cha kitaifa.

Nchini Uganda, muundo wa Bunge unahusisha watu wanaowakilishamaslahi maalum. Wanawake, watoto, na watu walio naulemavu ndiowanaofadika kutokana na uteuzi maalum kama huu. Kabila, kwa mfano, siosababu maalum ya kuwakilishwa. Maeneobunge hayawekwi kwa misingi yamakabila, ila ni jambo la kawaida kwamba wabunge kutoka eneo Fulani niwatu wa makabila yaliyomengi katika sehemu hiyo.150 Hakuna mbunge hatammoja wa Kimutwa bungeni. Hii ni kwa sababu Batwa wamebaguliwa katikawilaya wanakoishi; na pia wengi wao hawajasoma na hivyo hawana kiwangokizuri cha elimu kinachhitajika kugombea kiti katika bunge. Katika Jamuhuri yaKongo, kama ilivyo katika nchi nyingine kadhaa, ambako jamii asili ya‘Mbilikimo’ inaishi, hakuna wawakilishi wa kiasili katika vyombo vya kitaifa vyakufanya maamuzi ikiwemo Bunge; wala katika vyombo vya utawala. Zaidi yahayo, hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kuhakikisha kuwa wanawakilishwa.Tena, nchini Gabon, Seneti inachaguliwa kwa msingi wa uwezo wakuwakilishwa wa jamii wenyeji. Hata hivyo, hakuna majimbo kwa makundifulani maalum nahadi sasa, bunge la seneti halina mwakilishi wa kiasili.Viwango vya kutojua kusoma na kuandika vya watu wa kiasili nichangamotokubwa katika kuingia kwenye mabaraza ya kufanya maamuzi.

Nchini Burundi, hali ni tofauti, na hatua mahususi zameanzishwa kwa ajiliya uwakilishi wa Batwa Bungeni. Kifungu cha 16 cha Katiba ya Burundikinasisitiza kuwa serikali ya Burundi itaundwa kwa namna inayowakilishaWarundi wote na kwamba wote watakuwa na nafasi sawa ya kushiriki katikaserikali. Vilevile, inasisitiza kwamba matendo na maamuzi ya serikali lazima

150. Ona orodha ya wabunge kwenye: www.parliament.go.ug/index/php?option+com_wrapper&Itemid=37 (iliangaliwa Januari 30, 2008).

42

Page 59: First page ILO.fm

yaweze kuungwa mkono na umma kwa kiwango kikubwa iwezekanavyo.Kulinga na katiba, wawakilishi watatu wa Batwa wamechaguliwa katika Bungela Taifa151 na Seneti.152 Wawakilishi hawa ni pamoja na Rais wa Shirika lisilola kiserikali la kitaifa linalotetea haki za watu wa kiasili- UNIPROBA.153 Hatahivyo kwenye viwango vya chini vya uongozi, ukosefu wa kushirikishwa kwawatu wa kiasili bado ni changamoto kubwa. Kando na ushawishi finyuwalionao Batwa nchini Burundi- kupitia kwa uwakilishi wao katika Seneti naBunge- kihalisia, Batwa wana uwezo mdogo sana, au hata hawana, wakuyanendesha maendeleo yao wenyewe. Hakuna sheria wala sera zakuhakikisha kuwa wanawakilishwa katika sekta zingine kitaifa.154

Vivyo hivyo, nchini Rwanda zipo hatua ambazo zimechukuliwa kuhakikishakuwa kuna kushirikishwa kwa makundi yasiyobahatika. Kifungu cha 45 chakatiba ya Rwanda kunasema kuwa wananchi wote wana haki ya kishiriki katikauendeshaji wa masuala ya umma- moja kwa moja au kupitia kwa wawakilishiwao waliochaguliwa kwa nchia huru. Hata hivyo Batwa hawamo kabisa karibukatika vyama vyote vya kisiasa, na wamezuiliwa kuchukua nafasi katika vyamahivyo kutokana chuki wanayokumbana nayo kijumla. Kifungu cah 82 chaKatiba ya Rwanda kinashughulikia uanachama wa Seneti. Kando nakuhakikisha kuna asilimia 30 ya uwakilishi wa wanawake, pia idhinishawanachama wanane wa Seneti kutoka ‘jamii zisizopendelewa kihistoria’kuchaguliwa na Rais wa jamuhuri kuingia kwenye seneti. Hii imehakikishakuhusishwa kwa mwanachama mmoja wa Batwa kwenye Seneti.

Hatua maalum pia zimechukuliwa nchini Afrika Kusini kulingana namashauriano na watu wa kiasili kwenye kiwango cha kitaifa. Baraza lisilo lakisheria lakini linalodhaminiwa na serikali la National Khoi-San Council(NKSC) lilianzishwa mnamo mwaka wa 1999, likiwa na wanachama 21. kati yavitu vingine, limepewa wajibu wa ‘ kuchunguza yaliyomo kwenye Ripoti yaHali ya mambo ilivyo (status quo) ya serikali juu ya wajibu wa viongozi wakitamaduni katika serikali ya mitaa, na kutoa ushauri kuhusu masula yakiasili.’155 Mashauirano yanaendelea katika mukatadha wa Idara ya Serikali yaMikoa ya Serikali ya Mitaa.156 Ingawa watu wa kiasili wameonyessha‘kutoridhishwa kwao kuhusu mwendo wa polepole wa mchakato na kwambaumewekwa chini ya maajadiliano ya kijumla yanayohusiana na hali ya mamlakaya kienyeji,’ mchakato huu unawapa watu wa kiasili nafasi kushirikiana mojakwa moja na serikali kuhusu masuala yanayowaadhiri.157

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 1999 nchini Namibia, Mbunge wakwanza kabisa wa Ki- San alichaguliwa kuingi bungeni kwa tiketi ya chamaTawala.158 Hata hivyo, Mbunge wa Ki- San anatoka katika jamii ya Nyae Nyae,ambayo ina jamii moja tu ya San (jamii ya Ju/’hoansi) na ingawa hii bila shaka nihatua moja chanya, uchaguzi hauwakilishi hatua mahususi zilizochukuliwa na

151. Kifungu cha 164.152. Kifungu cha 180.153. IGWIA (2007) The Indigenous World 500.154. Ripoti ya ziara ya Jopokazi la Tume ya Afrika nchini Burundi 32.155. Mkataba wa ILO kuhusu Watu wa kiasili na Watu wa Makabila, 1989 (wa. 169), Mwongozo

(2003) 20.156. R Chennells na A Du Toit ‘Haki za watu wa kiasili nchini Afrika Kusini’ katika in RK

Hitchcock na D Vinding (eds) Indigenous peoples’ rights in Southern Africa, IWGIA (2004)103.

157. C Daniels ‘ Haki Za watu wa kiasili nchini Namibia’ kwenye RK Hitchcock Robert & DVinding, (eds) Indigenous peoples’ rights in southern Africa IWIGA (2004) 48- 49.

158. Kamati ya Uondoaji wa Ubaguzi wa Kikabila, UN Doc CERD/C/407/Add.2, 10 June 2002,21 (Ripoti ya uchunguzi wa hali ya Mali’s).

43

Page 60: First page ILO.fm

serikali kuhakikisha kuna ushiriki wa kutosha wa watu wa kiasili katikavyombo vya kufanya maamuzi kitaifa.

Maendeleo ya kuvutia nchini Mali ni kuundwa kwa ‘l’Espace d’InterpellationDémocratique (EID)’. Kikao cha kila mwaka kinachotoa nafasi kwa raia,yakiwemo mashirika ya kutetea haki za kibinadamu na mengineyo, kusailiuongozi hadharani kuhusiana na masuala yanayowahusu, hasa maswala ya hakiza kibinadamu.159 EID iliundwa kutokana na Agizo la 159/P-RM katika mwakawa 1996, na ingeweza kutona nafasi muhimu sana ya kujadili masuala ya kiasilikwenye kiwango cha kitaifa, ingawa hadi kufikia sasa haijashughulikia masualayanayohusiaana na watu waliowachache au wa kiasili. Maafikiano ya Kitaifa yamwaka wa 1992 yalikua ni hatua muhimu ya kutambua upekee wa sehemuwanakoishi Wa-Tuareg nchini Mali na yanabashiri hadhi mahsusi kwa maeneohaya. Haya yangeangaliwa zaidi, hata hivyo, kwa upande wa utekelezaji, nakama hatua ya kutambuliwa zaidi kwa watu wa kiasili nchini Mali. Taasisinyingine zinazolenga kuvihusisha vikundi mbalimbali husika katika kusimamiamasuala ya kitaifa ni pamoja na Baraza la Uchumi, Jamii na Utamaduni naBaraza Kuu la Jumuia Wenyeji (Haut Conseil des collectivités locales). Watu wajamii ya Tuareg wanawakilishwa katika Haut Conseil des collectivités locales.Kwa kweli, kwa sasa Baraza hili liko chini ya uangalizi wa mtu wa jamii yaTuareg, Oumarou Haidara. Uanachama wa Baraza la Uchumi, Jamii naUtamaduni linadhibitiwa na kifungu cha 110 cha Katiba. Uanachama kama huuunahusisha wanachama kutoka kwenye vyama vya wafanyikazi, wasomimbalimbali waliochaguliwa na mashirika yao na makundi yenye asiilimbalimbali za kijamii. Kwa hivyo, kwa kuwepo ukosefu wa utambuzi rasmi wawatu wa kiasili kama kategoria mahususi, hakuna wanachama walioko kwenyeBaraza kwa uwezo wao kama watu wa kiasili. Hata hivyo, Rais wa Barazapamoja na wanachama wengine, ni Mtuareg Baraza Kuu la Jumuia Wenyejilinalenga kuhakikisha kuwa kuna ushirikisho wa watu mbalimbali wanaoishikatika jamii mbalimbali wenyeji nchini Mali, na lina wajibu wa kutoamapendekezo kwa serikali katika sehemi zinazohusu mazingira, na dhamani yamaisha ya wananchi walio katika jamii hiyo wenyeji.160 Hii ingetoa nafasimuhimu sana kwa watu wa kiasili kueleza wasiwasi wao.

Nchini Ethiopia, bunge la pili lianzisha Kamati ya Muda ya kushughulikiaMaslahi ya Wafugaji yenye wawakilishi bungeni hasa kutoka jamii za wafugaji.Kamati hii inasimamia ukuzaji na ulinzi wa maslahi ya jamii za wafugaji kwenyemaamuzi, sera na sheria zinazopitishwa na Bunge. Lakini bado mengiyanahitajika kufanywa kitekelezi, hasa kuhusu uwakilishi wa vikundi vya jamiiza waliowachache.

3.4 Utawala wa mitaa

Njia ya pekee ya watu wa kiasili kushauriwa na kushiriki katika kufanyamaamuzi ni kupitia utawala wa mitaa. Baadhi ya mataifa yaliyochunguzwayanatawaliwa na serikali kuu, yakiachia nafasi ndogo sana ushawishi kutokaviwango vya mashinani kwa sera na mipango ya kitaifa. Kuhusiana na yalemataifa yaliyogatuliwa kwa viwango mbalimbali, viwango vya kushirikishwakikamilifu kwa watu wa kiasili katika michakato ya kwao vinatofautiana kiasi.

Mataifa yaliyogatuliwa ni pamoja na Uganda, ambapo mfumo wa serikali yamitaa unadhibitiwa na Sura ya Kumi na moja ya Katiba na Sheria ya Serikali ya

159. Kamati ya Uondoaji wa Ubaguzi wa Kikabila, UN Doc CERD/C/407/Add.2, 10 June 2002,21 (uchunguzi wa Ripoti ya kitaifa ya Mali).

160. Kifungu cha 99 cha Katiba.

44

Page 61: First page ILO.fm

Mitaa.161 Sheria hii inashughlika na vitengo vya serikali vilivyoundwa kwenyeviwango vya kijiji, jimbo, mkoa, mkoa mdogo na wilaya.162 Kando namabaraza ya wilaya yaliyo na uwezo wa utawala na wa kisheria pekee yake,viwango vingine pia vina uwezo wa kimahakama.163 Hata hivyo, vikundi vyapekee vyenye mahitaji maalum vilivyowakilishwa ni vijana, wanawake na watuwalio na ulemavu. Muundo wa vitengo vya utawala vya kimajimbo na kijiji niule ambao kabila lililo na nguvu linahakikishiwa kuwakilishwa. Batwahawatawali vjiji vingi na hivyo wana ushiriki finyu mno.164

Nchini Mali, ugatuzi umelengwa kwenye kuongeza uhuru wa kujitawalakwa miungano ya kimaeneo, na umeungwa mkono na wafadhili kadhaa. Hatahivyo, mchakato huu unakumbwa na changamoto kadhaa, zikiwemo uhamishowa umiliki wa maendeleo ya mahali fulani na ya eneo hadi kwa mamlaka yamitaa, na kuhakikisha kuwepo kwa urari baina mikakati ya sekta kwenyekiwango cvha kitaifa na maamuzi na mambo yanayopewa kipaumbele yamamlaka ya mitaa na maeneo.165 Zaidi ya hayo, haitikii hasa mahitaji yakujiamulia ya watu wa kiasili. Uwekeaji mipaka kwa jamii za maeneo na kutiliamkazo miundo ya vijiji vyenye maeneo mahususi ya kijiografia vimewatiawafugaji wa kuhamahama katika hali ngumu katika sehemu ya kushirikishwakatika utawala wa mitaa pamoja na haki za mali na kupata ardhi.166

Awali, Rwanda ilikuwa imegatuliwa na vyombo vya utawala vyenye hulkaya kisheria na uhuru wa namna Fulani.167 sheria zinazozungumzia nguvu zamamlaka ya wilaya zingekuwa za maana kwa watu wa kiasili, ingawa hadikufikia sasa hazijatumika hadi hapo. Kwa mfano, Sheria Nambari 08/2006kuhusu uundaji na kazi ya Wilaya inasema kwamba mamlaka ya Wilaya yafaakuunga mkono juhudi za wenyeji, na kuzingatia matamanio yao katika kupangashughuli za maendeleo.168 Hata hivyo, licha ya kuwepo kwa vipengelemuhimu vilivyo na uwezo wa kisheeria, ubaguzi na mitazamo hasiwanayokumbana nayo watu wa kiasili, vinazuia uwezekano wa kuchukuahatua kwa maslahi yao kwenye kiwango cha maashinani, ingawa kuna vighairikadhaa. Suluhu za shida zao zinapokelewa mijini, aghalabu kwa misingi yamitazamo kwamba hali za maisha yao ni ‘kizuizi kwa maendeleo.’

Uwezo wa kufanya maamuzi nchini Misri ni wa makao makuu, inagwaKatiba inadokeza uanzishaji wa utawala wa mitaani chini ya vifungu vya 161hadi 163- ikiwemo majimbo (governorates),miji na vijiji. Kwa sasa Misri inamajimbo ishirini na sita (muhafazat). Haya yaligawanywa zaidi katika wilaya(marakaz) na vijiji (qura) au miji. Pale ambapo mipaka ya vitengo vya kiutawalainakutana na maeneo yanayokaliwa na watu wa kiasili, kuna uwezekanomkubwa kwamba watu wa kiasili wataweza kuwa na uwezo fulani juu yaserikali ya mitaa. Hata hivyo, kuna satua ndogo sana ya haya kutendeka- sio tukwa sababu ya tofauti uliyoko baina ya mipaka ya utawala na himaya za watuwa kiasili- lakini pia kutokana kiwango cha juu cha mamlaka yasiyogatuliwa yamfumo wa serikali.

Baadhi ya mataifa yaliyoko katikati mwa Afrika yanafuata muundo uo huokulingana na utawala mkuu, wa wilaya na wa kimitaa, na changamoto za watu

161. Sura ya 243, Sheria za Uganda 2000.162. Angalia sehemu ya 10 – 48 ya Seheria kuhusu Serikali ya Mitaa.163. Angalia Sheria kuhusu Korti za Mabaraza ya Mitaa.164. Kamati ya Bunge, 2007, 11.165. Serikali ya Mali (2006) Mali: Poverty Reduction Strategy Paper, 44.166. MAA Hamana ‘La charte pastorale malienne: Entre droits coutumiers et décentralisation’

(June 2006) Regards Croisés, Revue trimestrielle, 17, 29. 167. Kifungu cha 3 cha katiba.168. Kifungu cha 6.

45

Page 62: First page ILO.fm

wa kiasili za kuhusika katika kufanya maamuzi mashinani ni zilezile.Changamoto mojawapo ni kutotambuliwa kwa vijiji vya kiasili kama vilivyohaki yao. Kama ilivyofafanuliwa katika sura za baadaye kuhusiana na haki zaardhi, kwa mfano, vijiji vya kiasili vya ‘Mbilikimo’ aghalabu hutambuliwa tukama kambi ambazo vimeshikamana na vijiji vya jamii za Kibantu au vya jamiinyinginezo jirani. Pale ambapo kuna vijiji vya kiasili, ni nadra sana vikaongozwana Mtemi wa kijiji wa kiasili. Nchini Gabon, kwa mfano, sheria zinazohusuhadhi ya Watemi169 hazina vipengele vyovyote maalum kuhusiana na watu wakiasili. Uwakilishi kwenye kiwango cha kimkoa, Mtemi wa mkoa, anafuatiwana mtemi wa kikundi cha vijiji ambaye chini yake kuna machifu wa vijiji. NchiniGabon kuna vijiji kadhaa ambavyo vinakaliwa na watu wa kiasili pekee. Hatahivyo, ni nadra sana vijiji hivi vikatawaaliwa na watemi wa kiasili. Kijumla, vijijivya ‘mbilikimo’ vinazingatiwa tu mradi viwe ni sehemu ya kijiji kukubwa chaWabantu. Kuna mfano mmoja tu uanaonekana (katika la Lopé) ambapoMtemi wa kikundi cha vijiji ni ‘Mbilikimo’.170 Pia katika Jamuhuri ya Afrika yaKati (CAR) kuna juhudi zinazoendelea za kutambua vijiji vya kwanza vyakiasili. Katika mwaka wa 2006, kwa mfano, vijiji vya kwanza kabisa vya kiasilivilitambuliwa huko Ngouma, Bakota1 na Bakota2 katika Wilaya ya La Lobaye.Vijiji vinaongozwa na viongozi wa Ki-Aka.

Vifungu vya 174 na 175 vya Katiba ya Jamuhuri ya Kidemokraasia yaKongo vinasistiza kwamba jamii wenyeji imeundwa kwa Idara na Jumuia. Hivivinatawaliwa na mabaraza yaliyochaguliwa, hasa katika maeneo ya ujuziwao,na raslimali zao. Sheria nambari 3-2003 kuhusu ugatuzi inachukuli kijijikama chombo cha utawa cha chini kabisa.171 Amri ya Nambari 2003-20inasisitiza kuwa kijiji kinaundwa na arrêté du préfet ambaye humteua Mtemi wakijiji nakumwonyesha kazi yake.172 Watu wa kiasili nchi Kogo moja kwa mojawanaunda sehemu ya vijiji jirani, ambavyo huwazuia kabisa wasiwe na uwezowowote wa kufanya maamuzi katika kiwango chochote. Hadi sasa, hakunakijiji chochote cha kiasili kina hadhi rasmi ya kuwa kijiji, na hali ni ileile katikanchi zingine katikati mwa Afrika, ingawa baadhi ya mashirika yasiyo yakiserikali yafanya juhudi za kuvitambulisha, hasa nchini Kameruni. Kupahahadhi ya kuwa vijiji inaweza kuwa njia nzuri ambayo kupitia kwayo jamii asilinyingi zilizo kanda ya Afrika ya Kati nzima zinaweza kutumia haki yao yakujiamulia, kushauirwa na kushiriki, vizuri.

Zaidi ya hayo, dhana ya kuwa na Mtemi wa kijiji ni ajinabia kwa tamaduninyingi za makundi ya Mbilikimo wa kiasili ambayo, kwa kiasili kikubwa, hawanamfumo wowote wa tabaka za utawala unaoweza kutambuliwa. Nchini Kongokwa mfano,

Traditionnellement, les sociétés égalitaristes des peuples autochtones ne sont passtructurées autour de chefs et de représentants puissants. Les relations se basentsur le principe d’égalité. Il n’existe pas d’organigramme précis. Cependant, ilsreconnaissent une autorité morale que l’on consulte souvent lors des situationsconflictuelles. Cette autorité est le patriarche de la famille, ayant une connaissance

169. L'arrêté n°0058/ML-SG-DPRH du 20 mars 1996 et l'arrêté n°0031/ML du 21 juillet 1998portant statut des chefs de quartier.

170. République Gabonaise, Ministère de l’Economie Forestière, des Eaux, de la Pèche, del’Environnement chargé de la Protection de la Nature, Plan de Développement de PeupleAutochtones du Programme Sectoriel Forêts Environnement, Rapport Final préparé par Dr. KaiSchmidt-Soltau, juillet 2005, 21.

171. Kifungu cha 30 hadi 34 de la Loi du 17 janvier 2003.172. Kifungu cha 126 cha Amri nambari 2003-20 cha Februari 6, 2003(décret No. 2003-20 du 6

février 2003.)

46

Page 63: First page ILO.fm

infuse des pratiques coutumières et rituelles; ou encore une personne choisie poursa sagesse et son âge avancé.173

3.5 Uongozi wa kitamaduni na Sheria ya Kimila

Viongozi wa kimila wanambulika katika nchi kadhaa za kiasfrika. Wajibu nauwezo wao vinatofautiana, lakini katika nchi nyingi, kutambuliwa kwaokungekuwa nafasi nzuri ya kushauriwa na kushirikishwa kukamilifu kwa watuwa kasili, ingawa changamoto kadhaa zingalipo katika kushughulikia swala hili.Kwa upande mwingine, baadhi ya nchi hazitambui uongozi wa kitamadunikatika mifumo yao ya kisheria, na uundaji wa sheria kitaifa hauna vipengelevinavyotambua sheria ya kimila, na uwiano wake na sheria iliyoandikwa.

Uongozi wa kitamaduni haujatambuliwa kirasmi katika mfumo wa kisheriawa Kenya na Nigeria kati ya nchi nyinginezo. Katiba ya Nigeria ya mwaka1999 haionekani kutambua uongozi wa kitamaduni. Mabaraza ya serrikali zamitaa yamepewa majukumu ya kutoa mamlaka kwa miungano ya kitamadunina kwa maslahi ya pamoja ya jamii husika.174 Msimamo wa kikatiba hata hivyoutekelezaji wenyewe hivi kwamba serikali zote za shirikisho la Nigeria, kunasheria zinazotambua viongozi wa kitamaduni na wajibu wao katika jamiimbalimbali. Viongozi wa kitamaduni wamepewa wajibu tofauti katika kutawalajamii wenyeji na wamehusishwa katika utawala wa serikali za mitaa ingawa niwajibu finyu sana.175 Japo kwa njia isiyorasmi, viongozi na taasisi zakitamaduni zina ushawishi mkubwa katika utawala wa Nigeria.

kwa upande mwingine, kama ilivyotajwa hapo juu, baadhi ya mifumo yakisheria inatambua kuwepo kwa sheria ya kimila na taasisi za viongozi wakitamaduni- ingawa haya ni kwa viwango vinavyotofautiana na athari nachangamoto zinazotofautiana kwa watu wa kiasili. Katiba ya Uganda kwamfano, ina vipengele kuhusu taasisi za kitamaduni au viongozi wa kitamaduni,ambao wanaweza kuwepo katika sehemu yoyote Uganda kulingana natamaduni, mila na desturi au matakwa na matarajio ya watu ambao taasisi hizozinawahusu.176 Vipengele hivyo hata hivyo, kwa jumla vinafanikiwa tu kwayale makundi ambayo idadi nzuri na ushawishi fulani wa kisiasa. Jamii kama vileBatwa ambao hawana miundo dhahiri ya uongozi wa kitamaduni zimekumbwana ugumu wa kutumia kipengele hiki, na kwa hivyo hawajafaidika kutokana nampangilio huu wa kitaasisi.

hali ni ile ile katika mataifa yaliyo na ‘Mbilikimo’. Katiba ya Kongo DRC,kwa mfano, inatambua uanzishaji wa ‘mamlaka ya kimila’, na inabashirikuanzisha sheria ya kuyadhibiti mamlaka haya. hata hivyo hadi kufikia sasahakuna sheria yoyote ambayo imetumika.177 Pia, watu wa kiasili hawajaungana

173. Kama hapo juu 44: ‘kidesturi, jamii za watu wa kiasili zinazopenda usawa hazijaundwakwenye viongozi wa kitamaduni na wa mamlaka ya maadili ambayohushauriwa kila marawakati wa mizozo. Kielezo hiki cha Mamlaka ni mkuu wa familia aliye na ufahamu wa kinawa shughuli za kimila na matambiko au pia anaweza kuwa mtu aliyechaguliwa kwa misingiya hekima yake na umri mkubwa.

174. Sehemu ya 7 ya Katiba ya Nigeria.175. O Agbese ‘Chiefs, Constitutions and Policies in Nigeria’ (2004) 6 West African Review.

Watawala wa kitamaduni katika Niger Delta, wakiwa chini ya uangalizi wa Muungano waWatawala wa Kitamaduni wa Jamii zinazozalisha Madini ya Mafuta nchini nigeroia(ATROMIPCON)- inahusisha watawala wa kitamaduni kutoka jamii za Ijaw na Ogoni-huungana na serikali kuhakiisha kuna amani na maendeleo ya kudumu katika eneo hilo.Angalia Ogbu, Niger Delta yapokea N3.07 Trillion kwa miaka Ilitolewa kwenye http://www.legaloil.com/NewsItem.asp?DocumentIDX=1174818064&Category=news (accessed10 July 2007).

176. Kifungu cha 246(1).

47

Page 64: First page ILO.fm

kwa namna inayoambatana na kuanzishwa kwa mamlaka makuu.178 Muunganowa Watemi wa Kimila hauna wanacha wa kiasili kutokana na sababu kwambavyama vya watu wa kiasili havijapangiliwa kwa namna ya kitabaka nahavitambui mamlaka makuu. Kwa hivyo, kuwazia tena kwa dhana ya uongozikwa jamii kama hizi kunahitajika ndipo sheria za kitaifa zizingatie hitaji la waokuhusishwa katika shughuli za kufanya maamuzi, na wakati huo huo kutambuakuwa michakato yao ya kufanya maamuzi inaweza kuwa tofauti na ile ya watuwengine.

Nchini Kameruni, kuna juhudi ambazo zimefanywa na mashirika yasiyo yakiserikali kukuza na kuwa na utemi wa kitamaduni unaotambulika kwa watuwa kiasili. Hizi zinadhibitiwa na amri ya 77/245. Namna za uandalizi nausimamizi wa utemi kama huu zinadhibitiwa ba sheria ya kimila ya jamii husika,na mamkala ya mitaa imeonyesha nia nzuri kuhusu uanzishaji wake, haliambayo inatoa mfumo wa kisheria wa kujiamulia.

Vipengele vya kikatiba kuhusu uongozi wa kitamaduni uanofanya kazikulingana na mila na desturi, ni pamoja na Sura ya 12 ya katiba ya AfrikaKusini.179 Uongozi wa kitamaduni na Sheria ya Mfumo wa Utawala180 inavipengele kuhusu utambuzi wa jamii za kitamaduni ambazo mila zaozinatambua uongozi wa kitamaduni na kutii sheria ya kimila.181 Kinadhariavipengele hivi vinaacha nje jamii nyingi za San na Khoe ambazo hazionyeshimiundo iliyowekwa ianyotambua uongozi wa kitamaduni.182 Ijapokuwaserikali ingali katika harakati za kutambua miundo hii, watu wa kiasiliwanafanya juhudi kuhakikisha kuwa wanatambuliwa katika mifumo ya uongoziwa kitamaduni kama inavyodhihirishwa na Sheria ya bunge.183 Bunge la kitaifala Viongozi wa Kitamaduni lililoidhinishwa katika Sura ya 12 ya Katiba,linafanya kazi kama shirika la ushauri kwenye kiwango cha kitaifa, pamoja naMabunge ya Kimkoa ya Viongozi wa Kitamaduni. Hata hivyo mabunge hayahayahusishi jamii za Khoi-San.184 Huku baadhi ya jamii na mabaraza yakitamaduni yakiwa yametambulia katika mikoa kadhaa nchini Afrika kusini,hakuna yaliyotambuliwa kukidhi watu wa kiasili kama vile Wakhoi naWasan.185 Changamoto inashidishwa na ukosefu wa matabaka maalum yauongozi katika tamaduni zao.

Kifungu cha 66 (1) cha Katiba ya Namibia pia inatambua sheria ya kimila namamlaka ya kitamaduni kama sehemu ya mfumo wa kisheria. Sheria yamamlaka ya kitamaduni Nambari 25 ya mwaka wa 2000 ina vipengele kuhusukuanzishwa kwa mamlaka za kitamaduni zinazohusisha watemi au wakuu wajamii za kitamaduni na madiwani wa kitamaduni.186 Hawa wana jukumu lakutekeleza sheria za kimila na kusuluhisha ugomvi. Ili kutambuliwa lazimawasilishe ombi kwa serikali,187 kwa hivyo mamlaka ya kuwatunuku utambuzihuo au kuwanyima viongozi wa kitamaduni uko mikononi mwa serikali. Hata

177. Sehemu ya 3 de la Constitution de février 2006.178. Nkoy Elela (2005) Situation des autochtones pygmées (Batwa) en République Démocratique du

Congo: enjeux des droits humains 42.179. Katiba ya Afrika Kusini sehemu ya 211-212.180. Sheria ya 41 ya 2003.181. Kama hapo juu sehemu ya, Sec 2.182. N Crawhall (1999) 19; angali pia Ripoti ya Katibu Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu

Ujumbe wa watu wa kiasili nchini Afrika kusini aya ya 49-54 (Report of the UN SpecialRapporteur on Indigenous Peoples Mission to South Africa, paras 49-54.).

183. Kama hapo juu.184. Ripoti ya Katibu Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ujumbe wa Watu wa kiasili nchini

Afrika Kusini, aya ya 51.185. Kama hapo juu.186. Sehemu ya 2(1).187. Sehemu na 4 - 6 za sheria hiyo.

48

Page 65: First page ILO.fm

hivyo ni watemi wawili tu wa Kisan kati ya wale waliochaguliwa na watu waowametambuliwa na serikali. Kamati ya CERD, kati ya nyinginezo, imetiliashaka ukosefu wa vigezo dhahiri vya kutambua viongozi wa kitamaduni, naukweli kwamba hakuna taasisi yoyote ya kukagua maombi ya kutambuliwa bilakuingiliwa na serikali.188 Hata hivyo, baadhi ya mashirika yasiyokuwa yakiserikali yaiona Sheria ya Mamlaka za Kitamaduni kana satua ya watu wakiasili kushiriki kikamilifu katika kufanya maamuzi, pamoja na changamotokadhaa, ikiwemo mafunzo yanayohitajika katika ujuzi wa kiutawala na uongoziambao ungeweza kudokezwa na utekelezaji kamili wa Sheria kuhusu watu wakiasili.189

Nchini Botswana pia kuna sheria ambazo zina vipengele kuhusu taasisi zakitamaduni au za kimila ambazo zingeweza kufanikisha kushirikishwa kwawatu wa kiasili. Katiba ya Botswana ina kipengele kuhusu Bunge la Watemiambalo ni sehemu ya Bunge la Kitaifa. Chini ya Kifungu cha 88 cha Katiba,Bunge la kitaifa linapaswa kushauriana na Bunge la Watemi kabla ya kupitishasheria yoyote kuhusiana na muundo wa kikabila au mali ya kikabila, mpangilio,usimamizi na uwezo wa korti za kimila na sheria ya kimila. Hata hivyo panachangamoto za msingi zinazowakumba watu wa kiasili kuhusiana na Bunge laWatemi. Ina uanachama wa kitabaka ambapo uanachama wa kudumuumetengewa watemi wa makabila ya Tswana.190 Hadi sasa, ni mwakilishimmoja tu wa kiasili amechaguliwa kuingia katika Bunge la Watemi. CERDimeona kuwa hali iliyopo kwa sasa inazalisha nafasi ya kibaguzi kuhusiana namigawanyo ya makabila katika Bunge la Watemi.191

Kutokana na hayo, Jopokazi la watu wa Kasili Waliowachache Kusini mwaAfrika (WIMSA) na Wasan Kusini mwa Afrika yalianzisha dhana ya Mabarazaya Wasan.192 Mabaraza ya Kitaifa ya Wasan huenda yasiwe taasisi za watu wakiasili lakini ni maitikio halisi ya kukabiliana na uhalisia wa jamii na nyakatiwanamoishi.193 Nchini Afrika Kusini Baraza la Wasan la Afrika kusinililijihusisha katika majadiliano ili kuwa sehemu ya Bunge la Watemi nchiniAfrika kusini, jambo ambalo lingekuwa kama kielelezo cha hali kama hizi nchini Afrika Kusini194

3.6 Kushiriki katika uchaguzi

Kushiriki katika chaguzi ni jambo muhimu la kuchunguzwa chini ya mada yakushiri. Haki ya kupiga kura ni haki muhimu ya kibinafsi, na pia ina atharikwenye haki za pamoja za watu wa kiasili. Mifumo yote ya kisheria ya kitaifainashughulikia haki ya kupiga kura, na kuanzishwa kwa vyama vya kisiasa,

188. CERD, Maoni ya Kuhitimisha: Namibia, Agosti 2008, UN Doc CERD/C/NAM/CO/12 ayaya 16.

189. R Kappleca & WIMSA ‘Civil Rights In Legislation and Practice: A Case Study fromTsunkwe District West, Namibia’ in RK Hitchcock and D Vinding (eds) Indigenous Peoples’Rights in Southern Africa (2004) 91.

190. Muundo wa Bunge la Watemi ulipingwa katika kesi ya Kamanakao kwa msingi kwambailikuwa ya kibaguzi na ilikiuka kifungu cha 3 na 15 cha Katiba ya Botswana. Mahakama kuuilikubali lakini ikashikilia kwamba, kwa kuwa muundo wa kibaguzi wa Bunge la Watemiulikuwa katika Katiba, Mahakama kuu isingeweza kuitangaza kuwa haikuwa ya kikatiba.

191. Ripoti ya CERD ya Botswana ya 2006 aya ya 10.192. Kama hapo juu.193. Nchini Afrika Kusini kwa mfano, Baraza la Wasan la Afrika Kusini (SASC) lilianzishwa

mwaka wa 2001. malengo yake muhimu yaliyowekwa mwaka wa 2004 yalikuwa niuanzishaji wa ofisi za mashinani, kutoa magunzo kwa wanachama wa SASC, kupata haki yakutembelea maeneo ya urithi kwa Wasan, kujenga miungano na makavazi na mbuga zawanyama, kubainisha makundi mengine ya Wasan kusini mwa Afrika na kufanyamashauriano ya kuingia katika Bunge la Watemi nchini Afrika kusini; kama hapo juu.

194. Kama hapo juu.

49

Page 66: First page ILO.fm

pamoja na suala la ugombeaji wa uchaguzi. Suala la kutobaguliwa katikasehemu hii pia ni arki muhimu ya mifumo ya kisheria kitaifa. Hata hivyo, kamaitakavyoonekana hapo chini, kwa watu wa kiasili, kuna changamoto nyingizinazohusiana na kutekeleza haki zao katika sehemu hii.

Sheria ya 06/006 ya Jamuhuri ya Kdemokrasia ya Kongo inahusumaandalizi ya uchaguzi wa urais, ubunge, wa miji, manispaa na wa mitaa. Hatahivyo imeonyeshwa kwamba masharti na taratibu za kuandikwa katika sajili zawapigakura ni chanagamoto kubwa kwa watu wengi wa kiasili, ambaokutokana na haya hushiriki katika chaguzi kwa idadi ndogo sana. Ilikujiandikisha kupiga kura, watu wanahitaji kuwa na kitambulisho cha kitaifa,cheti cha kusafiria au cheti cha uraia. Vivyo hivyo katiba ya Jaamuhuri yaAfrika ya Kati inazungumzia haki za kiraia na kisiasa, na haki za wanaume nawanawake walio na umri wa miaka kumi na minane au zaidi kupiga kura.Kifungu cha 28 cha Sheria ya Uchaguzi kinafafanua kuhusu taratibuzinazohitajika kitimizwa kabla ya kujiandikisha kupiga kura. Hizi ni pamoja nakwamba ni lazima watu wawe na kitambulisho cha kitaifa, cheti cha kuzaliwana stakabadhi zingine kama vile leseni ya kuendesha gari na kadhalika. Bilakuwa na stakabadhi kama hizi, maelezo ya ushahidi yanahitajika. Ripoti yashirika lisilo la kiserikali tangu mwaka wa 2006 inaonyesha kwamba Wa-akahawafurahii hata haki za kimsingi kabisa zinazohusiana na kushiriki,kushauriwa, uraia na uwakilishi wa kisiasa. Mara nyingi wanakosa stakabadhiza kujitambulisha, na hivyo hawana haki ya kupiga kura, jambo linalopelekeawao kukaribia kutengwa kutengwa kabisa kutoka maisha ya hadhara.195

Katika nchi zote mbili, watu wa kiasili wengi, kama sio wote, hawanastakabadhi kama hizi. Vile vile, vtuo vya usajili aghalabu huwa kwenye vituovya utawala, ambavyo mara nyingi huwa mbali zaidi na vijiji vya watu wa kiasili.Zaidi ya hayo, viwango vyao vya chini vya kujua kusoma na kuandika ni kizuizikikubwa kwao kushiriki katika kirasmi katika kupiga kura.

Hali ni ile ile nchini Kongo, ambapo Sheria ya Uchaguzi inahakikisha hakiya Wakongo kushiriki katka uchaguzi au kugombea ofisi,196 na bado mashartiya kusajiliwa katika sajili ya wapiga kura chini ya Kifungu nambari 10 chaSheria nambari 04/028, ambayo ni sawa na yale yaliyotajwa hapo juu kuhusuJamuhuri ya Afrika ya Kati na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, yanafanyamambo kuwa magumu zaidi kwa watu wa kiasili ama kujiandikisha kupiga kuraau kugombea uchaguzi.

La non jouissance du droit de citoyenneté des peuples autochtones au même titreque le reste de la population est un véritable obstacle à leur participation à la vienationale. Car, en dépit de la gratuité de l’acte de naissance, plusieurs enfants‘pygmées’ ne jouissent pas de ce document, notamment à cause de l’inaccessibilitéde leurs parents aux bureaux de l’état civil, l’adaptabilité des procédures mises enplace au mode de vie, l’éloignement de ces communautés. De plus des frais sontexigés aux ‘pygmées’ qui veulent acquérir un document d’état civil.197

195. A Giolitto (2006) Etude des cas de discrimination, abus et violations des droits de l’hommeenvers les pygmées Aka de la Lobaye République Centrafricaine, Etude faite pour COOPI, Caritaset OCDH, Bangui 17.

196. Art 4 de la Loi n 06/006 portant organisation des élections présidentielle, législatives, provinciales,urbaines, municipales et locales.

197. ‘Kukosa kufurahia haki ya uraia kwa watu wa kiasili kwa msingi sawa na watu wengine nikizingiti kikubwa kwa kushiriki kwao kikamilifu katika serikali ya kitaifa. Kwa sababu, lichaya umuhimu wa cheti cha kuzaliwa, watoto wengi wa ‘kimbilikimo’ hawana stakabadhi hii,hasa kutokana na wazazi wao kukosa uwezo wa kufikia ofisi za serikali, kukosekana kwamarekebisho ya taratibu ili kuakisi hali zao za maisha, na kutengeka kwa kijiografia kwajamii hizi. Zaidi ya haya malipo yanatozwa wakati Mbilikimo wanapotaka kupata stakabadhizinazohusiana na hadhi yao ya kiraia.’ Rainforest Foundation et OCDH, 2006,www.rainforestfoundationuk.org/files/droits_autochtones_final.pdf (accessed 30November 2008).

50

Page 67: First page ILO.fm

Vile vili, ishara nzuri ya changamoto kama hizi ni ukweli kwamba hakunamtu wa kiasili hata mmoja kati ya makaimu 500 na maseneta 108 kwenyekiwango cha kihtaifa nchini Kongo. Vivyo hivyo, nchini Gabon ambapo Sherianambari 24/96 kuhusu vyama vya kisiasa inawasilisha sheria ya kutobaguliwana kuihakikisha haki ya Wagaboni wote kujiunga na chama cha kisiasawanachokipenda, na sheria nambari 7/96 kuhusu uchaguzi inahakikisha haki yakufurahia haki za kiraia na za kisiasa kama wapiga kura na wagombeaji wauchaguzi, kupata ya haki ya kimsingi ya kushiriki katika uchakuzi kunabakochangamoto kubwa kwa watu wa kiasili. Sheria ya uchaguzi ya Gabonhaizingatii changamoto anuwai wanazokumbana nazo watu wa kiasili. Kamamatokeo ya haya, hakuna, kama ilivyo katika nchi nyinginezo kama Burundi,hata majimbo ya uwakilishi wa watu wa kiasili katika vyombo vya kiasiasa.

Chini ya katiba ya Misri ya mwaka wa 1971, kuna baadhi ya masuala yahaki ya kushiriki. Sheria nambari 73 ya mwaka 1956 inasisitiza kwamba baadaya kufikia umri wa miaka 18, kila mmisri ana wajibu wa kutumia haki yake yakisiasa kibinafsi kwa kutoa maoni yake kwenye kura za maoni zinazopigwakulingana na katiba. Kwa mkabala wa watu wa kiasili, mtu anaweza kuonakwamba sheria haina kipekele kuhusu kuwakilishwa kwa makundiyaliyopembezwa kama vile Wanubi, Waberber na Wabedouini katika vyamavilivyochaguliwa. Kutokana na uhamasisho finyu wa kiasiasa baina ya jamii hizi,kutokuwepo kwa vipengele kama hivi kunamaanisha kuwa watatiwa katikanafasi ngumu.

Katiba ya Botswana inahakikishia kila raia ambaye ametimu umri wa miaka18 haki ya kupiga kura, bila kutofautishwa kwa msingi wa kimbari au chmbukola kikabila.198 Sheria ya uchaguzi inashughulika na uendeshaji wa shughuli zaupigaji kura za bunge na mabaraza ya mitaa. Kati ya changamotozinazihusishwa na sheria za uchaguzi ni sharti la kuzungumza kwa kiingereza ilikugombea uchaguzi. Basarwa kabila la watu walio na kiwango cha chini chamasomo nchini Botswana, jambo linalomaanisha kwamba ni wachache sanakati yao watatimiza sharti hili.199 Tangu uhuru, hakujawahi kuweko nambunge wa kabila la Basarwa bungeni. Nafasi nzuri zaidi ya watu wa kiasili nikifungu cha 58 (b) cha Katiba, ambacho kinatoa nafasi kwa wabunge maalumwane walioteuliwa na rais na kupigiwa kura na Bunge.200 Hata hivyo, kihalisiakipengele hiki hakijatumiwa kuhimiza uteuzi wa makundi yaliyopembezwa.

Katiba ya Afrika Kusini inakubalisha Tume Huru ya Uchaguzi,201 ambayomajukumu na kazi yake yamefafanuliwa na Sheria Tume ya Uchaguzi ya1996.202 Tume hiyo inasimamia ushiriki huru na wa haki wa kila mpigakuraaileyesajiliwa katika uchaguzi au kugombea uchaguzi. Katibu maalum waumoja wa Mataifa anayehusika na watu wa kiasili ameviomba vyama vya kisiasanchini Afrika kusini ‘kuchukua msimamo wa kuwatambulisha watu wa kiasilikikatiba’, kwa maana ya kushiki kwao kikamilifu katika masuala ya vyama vya

198. Sehemu ya 67(b) kama ilivyorekebishwa na Sheria nambari 18 ya mwaka 1997 (yamarekebisho) ya katiba; vivyo hivyo, kila mwanchi ana haku ya kugombea kiti cha ubungemradi tu awe anaweza ‘kunena na, pengine tu ikiwa hana uwezo wa kuona au kuna sababunyine yoyote ya kimwili, kusoma kwa kiingereza kwa kiwango kinachomwezesha kushirikikikamilifu katika vikao vya Bunge. Sehemu ya 61 ya Katiba.

199. I Mazonde ‘Equality and ethnicity: How equal are San in Botswana’ in RK Hitchcock and DVinding (eds) Indigenous peoples’ rights in Southern Africa (2004) IWGIA Document 110,140.

200. Ripoti ya CERD ya Botswana 2006 aya ya 221.201. Katiba ya Afrika Kusini vifungu 190-191.202. Sheria ya 51 ya 1996.

51

Page 68: First page ILO.fm

kisiasa ambako kutapelekea kuteuliwa katika nyadhifa za kupigiwa kura nakatika kuunda sera.203

Mfumo wa uchaguzi wa kenye unategemea haki yak kupiga kura kwa wote,na kwa kutegemea mahali ziliko jamii fulani waliowengi watashinda katikauchaguzi.204 Kunapokosekana vipengele dhahiri na mikakati maalum yauwakilishi, watu wa kiasili na waliowachache wanaendelea kuoembezwakatika siasa za uchaguzi. Sehemu 42 ya Katiba inakubalisha Tume ya Uchaguziya Kenya, chombo kilichopewa wajibu wa kusimamia na kuandaa uchaguzi kilabaada ya miaka mitano. Kenya imegawika katika maeneobunge 210 yenyemipaka iliyowwekwa na Tume ya uchaguzi. Hata hivyo, maoni na mahitaji yawatu wa kiasili kila mara hayawakilishwi katika shughuli hii, kamailivyoonyeshwa kwenye kesi ya Il Cham.205 Jamii ya Il Chamus ilitaka tangazoya Mahakama ya ya Kikatiba kwamba takwimu za uwezekano wa mgombeziwa Il Chamus kuchaguliwa kama mbunge katika eneobunge la Baringo yaKati206 mdogo sana kiasi cha kuwanyima kabisa nafasi ya kuwakilishwaBungeni la kitaifa. Mahakama ilishikilia kwamba watu walowachache kama IlChamus wana haki ya kushiriki na kushawishi uundaji na utekelezaji wa seraza umma, na kuwakilishwa na watu wanaotoka katika miktadha ya utamaduniwa jamii na kijuchumi kama yao. Uamuzi hii ulikuwa ndio mwanzo wa mgeukochanya katika mahaka ya Kenya katika kuzitambua haki za watu wa kiasili.

3.7 Kushiriki katika usimamizi wa ardhi na maliasilina kufanya maamuzi

Kwenye kiwango cha mashinani, taratibu za kusimamia ardhi na maliasili zinaumuhimu wa moja kwa moja kwa suwala la kujiamulia kwa jamii za kiasili.Kuna vipengele vingi, hasa kuhusiana na usimamizi wa raslimali ya misitu,amabvyo vinewapa watu wa kiasili nafasi ndogo ya kujiamulia pamojakushauriwa katika masuala ya kufanya maamuzi kuhusu ardhi na raslimali.Hata hivyo, kama inavyoweza kuonekeana hapo chini, nafasi kama hizi nichache, na aghalabu hazizingatii upekee wa maisha ya watu wa kiasili. Ijapokuwa hivyo, ni dhahiri kutokana na mifano iliyotolewa kwamba baadhi yavipengele vya kisheria vinaweza kuwa msingi bora wa watu wa kiasilikushauriwa na kujitawala, au kama hatua ya kwanza kwa kushughulikia wajibuwa watu wa kiasili katika usimamizi wa ardhi na maliasili, hatua kwa hatua.

Sheria ya Misitu ya Jamuhuri ya Afrika ya Kati (sheria ya 90-003) inavipengele kadhaa ambavyo kinadharia vinafaa kuziwezesha jamii za kiasili kuwana kiwango fulani cha kujitawala wenyewe kwa muhibu wa haki ya matumizi.Kifungu cha 15 na 16 kwa mfano, vinahusika na haki za matumizi za kibinafsina za pamoja, kwa maana kwamba wanajumuia wanaweza kutumia raslimali zamisitu kulinga na mila zao. Kifungu cha 53 cha Sheria ya Misitu kinafasili misituya jumuia kama zile sehemu ambazo zimegawika kwa amri, na zina misitu nazimehifadhiwa na jumuia husika. Jumuia kwa mujibu wa sheria hii ni, maeneo,au makundi ya watu wanaokaa pamoja katika eneo fulani. Kwa hivyo,kutokana na ukweli kwamba hakuna jamuia ya Aka iliyopo, na vijiji vyao nisehemu tu ya vijiji jirani vya jamii nyinginezo, hakuna uwezekano wa watuhawa kusimamia sehemu zao za misitu moja kwa moja. Kama ilivyojadiliwa

203. Ripoti ya Katibu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu ujumbe wa watu wa kiasili wanchini Afrika Kusini, aya ya 103.

204. Angalia Sheria ya serikali ya Mitaa (Kifungu cha 265) ya Sheria ya Kenya.205. Rangal Lemeiguran & wengine v Mkuu wa sheria & wengine (kesi ya Il Chamus).206. Angalia hapo juu. Wilaya ya Baringo ina makabila matatu: Wapokoti, IL Chamus na

Watugen. Ina maeneo ya uwakilishibunge matatu. Ilidaiwa kuwa Jamii ya IL Chamus hainauwakilishi mzuri katika kupitia kwa haya maeneo ya uwakilishibunge.

52

Page 69: First page ILO.fm

hapo juu, utambuzi wa vijiji vya kiasili kwa uhalali wake ni njia muhimu yakuwahakikishia watu wa Afrika ya Kati haki zao za raslimali.

Sheria ya misitu ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo pia ina vipengelekadhaa ambavyo vingetoa nafasi kushauriwa na kushiriki kwa watu wa kiasili.Kifungu cha 84 kinasema kwamba mapatano yoyote ya umiliki wa misitulazima yatanguliwe na kutafuta habari kutoka kwa umma. Kihalisia utafutaji wahabari kama huu unahusisha matangazo na ziara za nyanjani. Watu wa kiasilihuudhuria mikutano kama hii kwa nadra, na kama watahudhuria, kijumlahashiriki kikamilifu kwa sababu ya ubaguzi wanaokumbana nao kutoka kwajamii jirani. Kwa hivyo, licha ya kuweko kwa vipengele vya kisheria ambavyokinadharia vingewapa nafasi ya kushiriki, kihalisia, hali ni tofauti kabisa.

Hali ni ile ile nchini Kongo, ambapo sheria ya nambari 16-2000(sheria yamisitu) ina vipengele kuhusu kushirikishwa katika usimamizi wa misitu.Kifungu cha24 na 25 cha Sheria kinasisitiza kwamba jamii za kiasili zinafaakushauriwa kabla ya kuweka mipaka ya maeneo ya misitu ya kudumu.Kihalisia, shughuli ya ‘kushauri’ inahusisha kusambaza habari katika ofisi zakuandaa mikutano ya hadhara katika vijiji viilivyo jirani na maeneo ya misituhusika. Tena, viwango vya ujinga wa kutojua kusoma na kuandika na vikwazovingine pia vitoa changamoto kubwa. Zaidi ya hayo, ukweli kwambahawawasiliani na ofisi za utawala pia ina maana kuwa habari zinazotumwakatika ofizi hizo, kwa nadra, hutimiza lengo, ikiwa kweli hufanya hivyo, lakuwafahamisha watu wa kiasili kikamilifu kuhusu hatua zilizopendekezwa.Vivyo hivyo, nchini Kameruni, chini ya agizo la mwaka wa 1995 kuhusu Sheriaya Misitu, wanyamamwitu na Sehemu za uvuvi (Amri nambari 95/59),207

usambazaji wa ilani za uainishaji wa misitu na sehemu zilizohifadhiwa ndio njiainayopendelwa ya kusambaza habari. Mbuga za kitaifa za Campo Ma’an,Benoue, Boumbek Nki, Dja na Lobeke ni mifano mizuri. Kuanzishwa kwaHifadhi hii ilipelekea kuongezeka kwa chakula katika makaazi jirani, yakiwemomakaazi ya watu wa kiasili. Kutokana na shughuli ya kuweka ramani yakushirikishwa iliyofanywa na CED, na majadiliano na Benki ya Dunia, hatahivyo, kiasi Fulani cha kupata haki kimeweza kuonekana kwa jamii yaBagyeli.208

Vifungu nambari 63 na 64 vya Sheria ya Viumbehai (Organic Law) ya 04/2005 kuhusu taratibu za kulinda, kuhifadhi na kukuza mazingira nchini Rwandavinafafanua wajibu mahususi kwa watu husuika katika usimamizi wa mazingira.Watu wanaohusika wana haki ya kupata habari bila vikwazo,kueleza maoniyao kuhusiana na masuala ya mazingira, kuwakilishwa katika vyombo vyakufanya maamuzi vinavyojihusisha na masuala ya mazingira, pamoja na kupatamafunzo. Haya yangekuwa nafasi nzuri sana kwa watu wa kiasili kushirikikatika shughuli ya kuunda sera na mipango kuhusu masuala ya mazingira- hasayale muhimu kwani wana maarifa ya kina juu ya mazingira na namnakuyahifadhi- ambayo yamelimbikwa kwa miaka mingi.

Kuongezea kwenye vipengele vinavyohusu kushiriki katika usimamizi waraslimali za misitu, pia kuna nafasi kadhaa za aina za kushiriki katika usimamiziwa raslimali zingine. Kwa jamii ya Mbororo katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati,kuundwa kwa vyombo vya kimaeneo kunaonekana kuwa nafasi ya kuwa na

207. Kifungu cha 18(3) kinasema kuwa ilani kuhusu uainishaji wa mistu zinafaa kusambazwakote katika ofisi zote za serikali, kumbi za miji na huduma za kiutawala zinazohusika namisitu katika maeneo ambako uainishaji huo unafanywa.

208. Kituo cha Mazingira na Maendeleo kimeanzisha mafunzo ya kushiriki katika usanifu ramanibaina ya jamii za ‘Mbilikimo’. Shughuli hii ilizalisha ramani ya ardhi ya kitamaduni yaWabaka, ambayo ilikuwa muhimu sana wakati wa majadiliano.

53

Page 70: First page ILO.fm

kiwango fulani cha kujiamulia wenyewe. Hii inahusiana na Sheria nambari 64/32 and 64/33 kuhusu kuanzisha na kuunda jumuia hizi, pamoja na Sherianambari64/32 inayohusu kuanzishwa kwa jamii za vijijini katika maeneo yaufugaji, uteuzi wa mameya na mabaraza ya usimamizi ya manispaa, kuongezeakwenye Sheria ya 65/61 kuhusu kudhibiti wa uzalishaji wa wanyama,inaruhusu uundaji wa jumuia za ukulima wa mifugo. Tangu miaka ya 1960,jumuia saba zimeundwa na mabaraza ya huru ya manispaa. Licha ya ukwelikwamba ziliundwa kuwafanya wambororo wakae mahali pamoja, ukwelikwamba jamii hizi zina mabaraza yao huru yaliyochaguliwa ungekuwa nafasinzuri ya kuimarisha kushiriki kwao katika shughuli za kila siku za kusimamiamaslahi yao wenyewe. Wafugaji pia wameanzisha Shirikisho la Kitaifa lawafugaji, ambalo lina kiwango fulani cha uwezo katika maamuzi yanayowahusuwafugaji. Katika mkumbo huu huu, serikali ya Ethiopia imetwaa mbinu mpiakuhusu maendeleo ya ufugaji, ambayo imeongeza kiwango cha ushirikianobaina ya wafugaji na serikali za kimaeneo.209 Kwa kufuata mwongozo waserikali ya shirikisho, serikali za mitaa za Oromiya, Afar na za Watu wa Kusinizimeunda jumuia za wafugaji.210

Kwa mujibu wa Sheria ya Misitu ya Kameruni, Waziri wa Misitu,wanyamapori na Uvuvi anaweza, kwa maslahi ya umma na kwa kushauriana nawatu wanaohusika, kusitisha utekelezaji wa haki za matumizi kwa kipindi fulanikifupi, inapohitajika hivyo (kifungu 8(2)). Licha ya sharti la kufanyamashauriano, maafisa wa serikali walioidhinishwa chini ya sheria ndiowapatanishi wa pekee wa kuamua iwapo kuna hitaji la kusitisha haki yamatyumizi. Kutokana na unyonge wao, jamii za ‘Mbilikimo’ ni wahasiriwa wamsingi wa hatua za aina hii. Pamoja na uasisi wa Mbuga ya Wanyama ya kitaifaya Campo, kuzuiwa kwa nguvu na kwa ghafla kwa haki za ya matumizi ya jamiihii, ambako kulisababisha kudorora kwa hali za maisha yao, kumeanzishwa.

Nchini Burkina Faso, Sheria nambari 034-2002/an kuhusu ufugajiinashughulika na matumizi ya maliasili. Katika muktadha huu serikali na jumuiaza kitaifa vimepewa jukumu la kutambulisha, kulinda na kuhifadhi sehemuambazo ufagaji hufanyika. Miungano ya wafugaji, kwa kushauriana na mamlakaza kimila, inafaa kushughulikia masuala ya kutambulisha, kuhifadhi nakusimamia sehemu zinazotumiwa kwa ufugaji, vyanzo vya maji na kadhalika.

Nchini Botswana, serikali imeanzisha mipango na sera ambazo zinatoahaki za kujitawala kiasi kiuchumi. Mpango wa kijamii wa kusimamia raslimali zanchi (CBNRM) ulianza mwaka wa 1993.211 Unaruhusu jamii zilizo halali kuwana haki za kusimamia ardhi inayozidi hekta100,000.212 Imetambuliwa kijumlakwamba jamii ambazo zinaweza kuwa halali ni Basarwa na takwimuzinaonyesha kwamba vijiji vilivyochagua CBNRM sana sana ni za Basarwa.213

Mpango huu haikabidhi jamii haki ya kumiliki kwa jamii bali unaitunukia tujamii haki ya kusimamia na kufaidika kutokana na umiliki wa raslimali za ardhikatika kipand mahususi cha ardhi.214 Hata hivyo, kati ya changamoto

209. Ripoti ya kamati teule, 33.210. Ripoti ya kamati teule, 50.211. Angalia kwa jumla; JW Arntzen ‘An Economic View of Wildlife Management Areas in

Botswana’ Mpango unaodhminiwa na CBRM.212. M Taylor ‘The Past and Future of San Land Rights in Botswana’ katika Hitchcock, R.K na

Vinding, D (eds) (2004) Indigenous Peoples’ Rights in Southern Africa 152.213. M Taylor ‘CBNRM na Maendeleo ya Ufugaji nchini Botswana: Makala kuhusu Haki za

Ardhi ya kuwasilishwa kwenye warsha kuhusu mazingira, Utambuzi na Usimamizi wamazingira wa kijamii: Wanayopita Wasan nchini Afrika Kusini, Ijumaa Disemba 1, 2006Kituo cha Uchunguzi wa Afrika na Mpango wa 9 wa Afrika kuhusu mazingira Chuo Kikuucha Oxford.

214. Taylor (n 212hapo juu) 162.

54

Page 71: First page ILO.fm

zinazohusishwa na mpango huu ni kwamba CBNRM haitumii taasisi zakitamaduni, kisasa, za kijamii za watu wa kiasili wenyewe. Kwa hivyo, kwamfano, wanalazimika kuunda na kusajisha taasisi za kisheria zinazotambulikazinazofanana na mashirika.215 Pili, kukosekana kwa wanajamii waliosomakutoka jamii hizi kunamaanisha kwamba hawana uwezo wa kuthaminimasharti tatanishi ya kisheria ili kutumia CBNRM.

Nchi ya Nigeria inaendesha mfumo wa serikali ya shirikisho na kama ilivyoudhibiti na usimamizi wa maliasili ni majukumu ya serikali ya shirikiso. Mnamomwaka wa 2000 Tume ya Maendeleo ya Niger Delta (NDDC) iliundwa kwalengo la kupata mafanikio makubwa na yenye kufaa katika ‘matumizi ya pesazilizopokelewa kutoka katika hazina ya shirikisho ili kusuluhisha matatizo yakiikolojia yanayotokana na uchimbaji wa madini ya mafuta katika eneo laNiger Delta na kwa malengo yanayofungamana na haya. 216 Mpango Mkuu wamaendeleo ya eneo la Niger Delta linadhamiriwa kushughulikia suala laumasikini na uharibivu wa mazingira na kuwapa watu wa kiasili nafasi yakushiriki kikamilifu katika shughuli za kufanya maamuzi.217 Hata hivyokiwango cha kushiriki, licha ya kuwepo kwa mpango huu, ni cha chini. Katikasiku za hivi majuzi, serikali ya shikisho ya Nigeria ilianzisha Wizara yaShirikisho kwa ajili ya Niger Delta. Wizara hiyo inaongozwa na mrasimukutoka Niger Delta. Imelengwa kwa uratibu bora na kusuluhisha shida zilizoza kipekee kwa Niger Delta chini ya viwango vya bageti ya serikali yashirikisho.

3.8 Kushauriwa na kushiriki katika uundaji wa sera namipango

Wasiwasi mkubwa wa watu wa kiasili ni kwamba miradi ya maendeleoinayowaathiri mara nyingi huandaliwa bila mchango wa makundi lengwa nakwa njia hii huelekea kutozingatia upekee wa kitamaduni wa watu wakiasili.218 Kukosekana kwa mashauriano na watu wa kiasili kila marakumesababisha kutwaliwa kwa sera na mipango ya maendeleo ambayohailingani na mahitaji yao halisi. Kulingana na utafiti uliofanywa na ILO, kati yawengineo, watu wa kiasili aghalabu wana utambuzi tofauti sana wa umasikinina mali, pamoja na vipaumbele katika kupunguza umasikini, kuliko sehemunyinginezo za umma kitaifa.219 Ijapokuwa hivyo, serikali nyingizilizochunguzwa wakati wa kufanya utafiti huu zinaendelea kutambuaumuhimu wa kushughulikia masuala ya kiasili hasa katika mikakati yao yakupunguza umasikini na ya maendeleo kwa jumla.

215. T Gujadhur ‘”Ni vizuri kuhisi kama tunaimiliki ardhi”: Mtazamo wa watu kuhusu Haki zaardhi za jamii chini ya CBNRM nchini Botswana’ Makala ya 3, 3 ya Mpango saidizi wa.

216. Serikali ya shirikisho pamoja na NDDC inahitaji zaidi ya N400BN ili kutekeleza mpangomkuu. angalia http://www.projectnddc.com/ (iliangaliwa 24 Machi 2007). Ingawakuanzishwa kwa mashirika haya na ugawaji upya wa kikatiba wa takriban asilimia 13 (13%)ya ushuru wa mafuta na gesi, uliokusanywa na ofisi kuu, kwa majimbo yanayozalisha mafutakumepongezwa kama hatua nzuri kwa upande wa serikali ya Nigeria, bado kuna kunamakubaliano dhabiti kitaifa kwamba serikali ya Nigeria inahitaji kufanya mengi zaidi yahayo. Angalia T Suberu, Reconstructing the architecture of federalism in Nigeria: The option ofnon-constitutional renewal, yalitolewa kwenye; www.darthmouth.edu/jcarey/suberu.pdf(Oktoba 30, 2006).

217. Mnamo tarehe 27 machi 2007, Rais wa Nigeria alizindua mpango mkuu wa NDDC.Angalia; http://www.thenationonlineng.com/dynamicpage.asp?id=14678 (28 Machi 2007).

218. S Saugestad; ‘Developing Basarwa Research and Research for Basarwa Development’(1994) 10 Anthropology Today 20-22.

219. B Tcoumba, Peuples Indigènes et Tribaux et Stratégies de Réduction de la Pauvreté auCameroun (2005, ILO).

55

Page 72: First page ILO.fm

Katika mukta wa mpango wa kitaifa wa kushirikishwa katika maendeleonchini Kameruni, kuna juhudi ambazo zimefanywa kushughulikia mahitaji yawatu wa kiasili, lakini mipango mahususi iliyoendelezwa kufikia sasa badohaifai na haiambatani na mahitaji ya watu wa kiasili. Kutokana na haya atharizake chanya ni ndogo mno. Wakati wa kuchanganua Makala ya Mikakati yakitaifa ya Kupunguza umasikini (PRSP), watu wa kiasili hawakushauriwa lichaya methodolojia ya kushirikishwa iliyokubaliwa na serikali katika muktadhahuu.220 Na licha ya kuwepo kwa mpango wa maendeleo ya watu wa kiasilikatika mfumo wa PRSP, PRSP haizingatii aula na mahitaji ya watu wa kiasilikatika mkakati wa jumla, au katika mikakati ya sekta zinazohusiana na mfumowa matumizi ya pesa ya muda wa kadiri. Katika mfumo wa mchakato wakudurusia PRSP, uliokuwa unaendelea mnamo mwaka wa 2007 na 2008,serikali ilifanya mashauriano na vitengo mbalimbali vya jamii ya Kameruni,zikiwemo jamii za Wambororo na ‘Mbilikimo’. Hata hivyo, linabakia jambo lakuangaliwa iwapo stakabadhi iliyofanyiwa marekebisho na mitindo yautekelezwaji wake itazingatia na kushughulikia haki za watu wa kiasilikikamilifu.

Juhudi pia zimefanywa na serikali ya Kenya ili kufanikisha ushirikishwaji wajamii na kufanya mashauriano nao katika ajenda za maendeleo. Inaweza, kwamfano, kuhisika kupitia kwenye Sheria ya Hazina ya Maendeleo ya MaeneoBunge na Sheria mwaka 1999 ya Hazina ya Uhawilishaji ya Mamlaka ya Mitaa, ‘ambayo inakuza utambuzi unaunga mkono masikini na utekelezaji wa miradiya maendeleo katika viwango vya mashinani,221 kwamba jamii wenyejiwangeweza kuhusishwa katika kuamua mipango ya hatua zilizopewakipaumbele. Hata hivyo, kuna ukosefu wa mikakati na hatua mwafaka yaugatuzi mkamilifu na uwezo wa kusimamia raslimali hizi kwa faida ya jamiizinazolengwa.222

PRSP ya Kongo inatilia mkazo kushiriki kama arki muhimu ya uongozimzuri. Stakabadhi hii inabashiri mchakato wa kushiriki katika hatua tatu, yakwanza ikiwa ni kuleta ufahamu wa mchakato huo kupitia kampeni nakushauriana, ikiwemo na watu wa kiasili. Ya pili inahusisha mashauriano yakushiriki ya kiwamgo kikuu na mashauriano na jamii katika idara kumi na mojanay a tatu inahusisha mashauriano ya kushiriki ili kuhusisha matazamio yakisekta kwenye rasimu ya I-PRSP.223 Hata hivyo, moja wapo ya malengoinayoyaingiza kuhusiana na watu wa kiasili ni ‘ kuanzisha hazina ya kusaidiakuleta ufungamano kwa ajili ya ‘Mbilikmo’.224 Hadi leo, haya hayajafanyika, nani wazi kwamba lengo la ufungamano lililoelezwa hapa linakinzana na rasimuya sheria kuhusu haki za watu wa kiasili nchini Kongo, ambayo inachukuliaaula za watu wa kasili wenyewe na ulinzi wa utamaduni wao kama hatua yakeya kwanza.

Wakati wa kuyaangalia masuala ya mashauriano na kushiriki, ni muhimukuzingatia muundo wa jamii na dhana za uwakilishaji wa watu wa kiasili. Jamiiya ‘Mbilikimo’ kwa mfano, inajulikana kutokana na ukosefu wa mpangilio wakitabaka na ukosefu wa msemaji aliyetuliwa ikilinganisha na zingine. Mwakilishiwa société d’exploitation forestière en République du Congo (CIB)- (shirika lamatumizi ya misitu la Jamuhuri ya Kongo) alifafanua kwa mfano- katikamuktadha wa kuanzisha kipindi kwenye redio ya kijamii, kwamba.

220. B Tchoumba, Peuples Indigènes et Tribaux et Stratégies de Réduction de la Pauvreté auCameroun (2005, ILO).

221. Ripoti ya 57 ya APRM ya Kenya.222. Ripoti ya 75 ya APRM ya Kenya. 223. Kama hapa juu aya ya 23.224. Kama hapa juu, aya ya 216.

56

Page 73: First page ILO.fm

Jamii yao ni yenye usawa; kutokana na hayo mtu hawezi tu kuzungumza namtemi wa kijiji lakini inafaa azungumze na jamii. Ni vigumu sana kupita vikwazihivi na kuziba pengo lililosababishwa na kutojua kusoma na kuandika baina yawatu hawa. Kwa hivyo tulishauriana na wataalamu walio na ufahamu wa kinakuhusu jamii za ‘Mbilikimo’ ambao walipendekeza kuwa tuanzishe kuituo charedio. Nasi tulijibu, ‘wacha tujaribu’.225

Kwa kweli, stakabadhi nyingi za PRSP (ikiwemo ile ya Jamuhuri ya Afrikaya Kati, na nyinginezo kadhhaa zilizokaguliwa katika utafiti huu) zinatiamsisitizo maalum katika kufanya mashauriana na jamii wenyeji. Hata hivyo, nichache mno kwa kweli zinabashiri mikakati yoyote mahususi ya kushaurianana watu wa kiasili. Na kwa zile stakabadhi zinazobashiri mashauriano kamahaya- kama vile shughuli ya sasa kurasimu upya stakabadhi ya PRSP yaKameruni- mashauriano yanayofanyika si ya kushirikisha kikamilifu auyaliyotoholewa katika mbinu za kufanya maamuzi za watu wa kiasili wenyeweili kuhakikisha kuna matokeo yanayodhihirisha mahitaji yao wenyewe.

Mfumo wa kimkakati wa kupunguza umasikini nchini Burkina Fasounatangaza maendeleo fulani yaliyopewa vipaumbele ambayo ambayoyangeunda mfumo unaofaa kwa watu wa kiasili kueleza aula zao wenyewe.Ufafanuzi wa stakabadhi hii ulitanguliwa na kushirikishwa kwa makundi kadhaahusika. Hata hivyo, matumizi ya methodolojia ambazo hazikuzoeleka na watuwa kiasili, pamoja na kutumia lugha ya Kifanza amabayo watu wengi wa kiasilihawaielewi vizuri wakati wa kufanya mashauriano, viliathiri sana kiwangoambacho watu wa kiasili wameweza kuchangia katika ufafanuzi wa stakabadhihii. Zaidi ya hayo, kwa kuwa baadhi ya watu wa kiasili wanaishi katika maeneoyaliyojitenga, habari zilizotolewa katika mikutano mbalimbali hazikuwafikiaumma huu uliojitenga.

Kwa upande mwingine baadhi ya mifumo ya PRSP haibashiri kushirikikwokwote kwa watu wa kiasili,au ikaitikia aula zao. Hivi ndivyo ilivyo, kwamfano, na stakabadhi ya PRSP ya Uganda. Nchini Algeria, hakuna mikakatirasmi ya kufanya mashauriano na watu wa kiasili. Hususan katika kuendelezamiradi mikubwa ya miundomisingi kama vile Bwawa la Taksebt la Kabylie,kukosekana kwa mashauriano na watu wa kiasili wenyeji kumesababisha majikuchepuliwa (kugeuzwa mkondo) kutoka kutoka kwenye sehemu hiyo hadikwenye mji wa Alger, na hivyo kuwanyima wenyeji raslimali walizotumiaawali. Katika hali zingine, wakati ambapo mikakati ya kitaifa ya kupunguzaumasikini na ya kimaendeleo huenda isiwe na makini hususa na masuala yakiasil, hitaji la kushughulikia mahitaji maalum ya watu wa kiasili linawezakushughulikiwa katika muktadha mwingine. Ingawa mikakati ya jumla yaNamibia ya kupunguza umasikini hazingatii watu wa kiasili,226 kufuatia ziara zaNaibu wa Waziri Mkuu katika jamii za Wa-san katika nchi zima ya Namibia,mpango wa maendeleo ya Wa- san ulianzishwa upya.227 Ziara hizi zililenga

225. ‘Leur société est égalitaire, par conséquent on ne peut pas seulement parler au chef du village,mais il faut parler à tout le monde. Il est très difficile de surmonter tous ces obstacles et decombler le fossé créé par l'analphabétisme de ces populations. Nous avons donc consulté desexperts qui connaissent très bien les communautés pygmées et nous ont recommandé de monterune station radio. Nous avons répondu, d'accord, essayons cela.’ Taarifa ya M Poynton kwaCIB/Congo, angalia tovuti ya Benki ya Dunia http://web.worldbank.org/WBSITE/EXTERNAL/COUNTRIES/EASTASIAPACIFICEXT/EXTEAPREGTOPSOCDEV/0,,contentMDK:20539995~isCURL:Y~menuPK:502986~pagePK:34004173~piPK:34003707~theSitePK:502940,00.html (ilipatikana 30 Novemba 2008).

226. Malengo ya Maendeleo ya Milenia ya Namibia, 2004; Serikali ya Nmibia (Agosti 2004),yanapatikana kwenye; www.undg.org/documents/5307-Namibia MDG Report 2004.pdf(yaliangaliwa 31 Juai 2007).

227. Angalia, Ripoti ya Mpango wa Maendeleo ya Wa-san 2007/2008.

57

Page 74: First page ILO.fm

kufanya mashauriano na watu wa kiasili juu ya mahitaji yao na mitazamo yaoya changamoto nzito zinazowakumba. Mpano huo uliundwa kutokana naugunduzi wa mashauriano kuhusiana na masaibu ya Wa-san. Hata hivyo,Mpango huu unadumisha kwa kiasi fulani mwelekeo wa kimchanganyo, kwamaendeleo ya Wa-san, ambao unaibua maswali kuhusu ufaafu wamashauriano yaliyofanywa pamoja nao.

3.9 Hitimisho

Baadhi ya mifumo ya kisheria katika kanda ya Afrika ina vipengele vya kushirikina kushauriwa kwa umma kijumla au watu mahususi, yakiwemo makundiyaliyopembezwa. Michache sana kati ya mifumo hii kwa hakika ina vipengelemahususi vinavyohusu watu wa kiasili, lakini baadhi yayo inaweza kuwa kamanafasi ya kukuza kushirikishwa kwa watu wa kiasili katika kufanya maamuzi.Hata hivyo, mikakati ya utekelezwaji wa mifumo hii ya kisheria aumashauriano au kushiriki kwingine kunakohusiana nayo kwa jumla ni dhaifu,na haizingatii makadirio mahususi yanahitaji kufanywa wakati wa kushaurianana watu wa kiasili. Kwa upande mwingine, baadhi ya mifumo ya kisheria hainavipengele viwavyo vyovyote kwa ajili ya mahitaji ya makundi yaliyopembezwana makundi mengine mahususi katika jamii ya kitaifa.

Pale ambapo pana vipengele kama hivi, sheria zilizo na vipengele kuhusuwatu wa kiasili, au vifungu vya uteuzi maalum, mara nyingi huhusu matukiomahususi tu na wala sio sera pana ya kuwahusisha watu wa kiasili. Zaidi yahayo, juhudi za kuhusisha na kushauriana na watu wa kiasili aghalabu huwa zakijumla sana. Katika hali mbaya zaidi, hakuna mikakati kabisa, na pale ambaposheria ina vipengele kuhusu usawa wa kupata huduma fulani na haki sawakatika sehemu mahususi, aghalabu hali ni kwamba hamna hatua zaidiinayochukuliwa kushughulikia ugumu walio nao watu wa kiasili katikakuzitekeleza haki hizo. Taratibu kuhusu kushiriki katika uchaguzi ni mfanomzuri. Wakati ambapo uundaji sheria nyingi za kitaifa huwa na vipengelekuhusu haki ya raia wote kupiga kura, kijumla hauzingatii kwamba mashartiambayo watu binafsi wanapaswa kutimiza ili kupiga kura ni magumu sana kwawatu wa kiasili kuyatimiza. Haya ni pamoja na ukosefu wa stakabadhi msingi zauraia. Katika hali fulani, kuweka mipaka ya maeneo ya kupiga kura kunawezakuyafaidi makundi yaliyo na nguvu zaidi, na kupelekea kupunguka kwauwezekano wa watu wa kiasili kutumia uashawishi wao kwa kupiga kuga kura.

Kuhusiana na kushiriki katika vyombo vya kitaifa vya kufanya maamuzi,hatua kama hizi za uteuzimaalum, kando na Burundi, znatoa nafasi kwamakundi mahususi yanayohusika lakini hazihusishi watu wa kiasili. Paleambapo pana mifano chanya ya uteuzi maalum kwa watu wa kiasili, kamailivyo nchini Burundi, haifungamani na sera pana ya kuhakikisha kushiriki kwawatu wa kiasili katika uongozi, ila inafungamana tu na mifano mahususi yaBunge na Seneti. Mifano kadhaa chanya ya juhudi za kuanzisha vyombo vyakitaifa kujadili na kutoa ushauri kuhusu masuala ya kiasili, kama vilevilivyozinduliwa nchini Afrika Kusini, inaweza kupatikana, ingeonekana kamamianzo ya makadirio mapana ya mahitaji yao katika sera na sheria.

Kwa upande wa kijitawala wenyewe, baadhi ya mifumo ya kisheriainaruhusu kushiriki, kwa mfano katika kusimamia maliasili. Suala la usimamiziwa maliasili limefungamanishwa na uongozi. Katika maeneo ya misitu katikaAfrika ya Kati kwa mfano, ingawa sheria hazina vipengele kuhusu matumizi nausimamizi kwa jamii wenyeji, ukweli kwamba vijiji vya kiasili havitambuliwikama ‘jamii wenyeji kama vinavyostahili- ila kama viambatisho tu vya vijijijirani, inamaanisha kwamba watu wa kiasili wana ugumu zaidi katika kudai haki

58

Page 75: First page ILO.fm

zao za ardhi na maliasili kama wanavyostahili. Pia inamaanisha kwambakushiriki kwao wenyewe katika kufanya maamuzi na katika utawala wa mitaani finyu, sio tu kwa sababu jamii zao hazitambuliki na hivyo ‘kuwakilishwa’ nawatemi wa jamii zilizojirani nao.

Kwa kufungamana na suala hili, ni utambuzi wa sheria za kimila namamlaka za kitamaduni kwenye viwango vya kitaifa na mashinani. Sheria nyingiza mataifa ya Afrika zinatambua sheria za kimila na machifu (watemi) aumamlaka za kitamaduni. Hii ni nafasi muhimu ya kushiriki kwa watu wa kiasilina wawakilishi wao katika kufanya maamuzi. Hata hivyo, changamoto zimokatika zile sehemu ambapo huenda watu wa kiasili hawana muundo au mfumowa ngazi za madaraka unaoweza kuonekana wa kufanya maamuzi katika jamiizao. Hivi ndivyo ilivyo na Wa-san na watu ‘Mbilikimo. Hali zingine kama vilekutumia lugha mahususi, mara nyingi pia husababisha kuzuiwa watu wa kiasiliwalio na uwezo. Changamoto zaidi kwa uongozi na kushiriki katika kufanyamaamuzi zimo katika ukweli kwamba utambuzi rasmi wa mamlaka zakitamaduni unatenga mamlaka za kitamaduni za yale makundi ambayoyameshikamana kwenye maeneo fulani mahususi. Kama inavyoonekana hapojuu, hatua ambazo zimechukuliwa kwa mfano, kuwahususha wafugaji wakuhamahama katika shughuli za kufanya maamuzi, aghalabu zimetawaliwa nakuwatuliza mahali pamoja tu, badala ya kuirebisha (kuitia) hali hii katikamiundo ya kufanya maamuzi. Uundaji wa sheria kuhusu mamalaka za kimila auza kitamduni zinahita unahitaji kuzingatia tofautu kama hizi iwapo utakuwa wakuleta faida nzuri kwa watu wa kiasili.

Serikali katika nchi kadaa zilizokaguliwa wakati wa kufanya utafiti huuzinaendelea kutambua hitaji la kushughulikia masuala ya kiasili hususan katikamikakati yake ya kupunguza umasikini na ya maendeleo kijumla. Haya nimaendeleo muhimu katika eneo ambapo masuala ya kiasili yamekuwa kwenyeajenda kwa nadra sana hapo awali. Lakini tena, mikakati ya kushiriki kamahuku ni dhaifu na mara nyingi haifai katika kuwahusisha kikamilifu watu wakiasili katika kuunda, kutekeleza na kufuatilia mikakati kama hii.

59

Page 76: First page ILO.fm

4 Kupata haki

4.1 Utangulizi

Kufikia haki kunahitaji, kwanza, kwamba mawakili wapo kuwasaidia watuambao wanawahitaji. Zaidi kunahitajika kwamba mahakama haziko mbali sanana zisizofikika ili kutunika, na kwamba lugha ya kisheria iwe ya kueleweka kwawatu ambao wanategemea sheria. Zaidi, kupata haki kuhahusisha nafasi nzuriya kupata habari inayohitajika kuhusu utendakazi wa mfumo wa mahakama.Kunahitaji mfumo wa kisheria unaofanya kazi, ukiruhusu hukumu za haki,ambazo zinahusisha-kati ya mengineyo, kusuluhisha ugomvi kwa wakatiunaofaa, gharama ya kumudu, uwazi, haki, zenye ufaafu, na ubora.

4.2 Viwango vya kimataifa

Kifungu cha 17 (2) cha ICCPR kinasema kwamba ‘kila mtu ana haki yakulindwa na sehria’. Katika kifungu nambari 7, Mkataba wa Afrikaunahakikisha vipengele yanayohusiana na kupata haki:

1. Kila mtu atakuwa na haki ya daawa yake kusikizwa. Hii inahusisha;

(a) Haki ya kukata rufaa kwa vyombo vya kitaifa vya sheria vya kuridhishadhidi ya vitendo vya ukiukaji wa haki zake muhimu kama zinavyotambulika nakuhakikishwa na mikataba, sheria, kanuni na mila zinazotumika;

(b) Haki ya kuchukuliwa kuwa hana hatia hadi akathibitishwe kuwa nahatia na mahakamaya kisheria au baraza la hukumu;

(c) Haki ya kujitetea, ikiwemo haki ya kutetewa na wakili anayependa;

(d) Haki ya kuhukumiwa katika wakati unaofaa na kuti au baraza lahukumu lisilo na mapendeleo.

Kinyume na Mkataba wa Afrika, Mkataba wa 169 wa ILO unashughulikakikamilifu na haki za watu wa kiasili peke yake, vikiwemo vipengele vya kupatahaki. Kwa mfano, kifungu cha 2 kitwika Serikali wajibu wa kuhakikisha kuwawatu wa kiasili ‘wanafaidika kwa kiwango sawa kutokana na haki na nafasiambazo sheria na kanuni za kitaifa zinawapa watu wengine katika umma’,ikiwemo kwa maana hiyo, haki ya kupata haki. Vilevile, kifungu cha 12kinazilazimu serikali kuwalinda watu wa kiasili ‘dhidi ya ukiukaji wa haki zao’na kuhakikisha kuwa ‘wanaweza kwenda mahakamani, ama kibinafsi au kupitiavyombo vyao vya kuwawakilisha, kwa ulinzi bora wa haki hizi’. Zaidi ya hayo,kinataja kwamba ‘hatua zitachukuliwa kuhakikisha kwamba watu hawawanaweza kuelewa na kueleweka katika mashtaka, ikiwezekana kuwepo nautafsiri au kwa njia nyinginezo zinazofaa’.

Chini ya kifungu cha 13(2) cha UNDRIP, mataifa yatachukua hatua zifaazokuhakikisha kuwa watu wa kiasili ‘wanaweza kuelewa na kueleweka katikamashtaka ya kisiasa, kisheria, nay a kiutawala ikiwezekana kupitia utafsiri aunjia nyinginezo zinazofaa’. Kifungu cha 34 cha Azimio kinawezesha watu wakiasili kudumisha mifumo yao ya kisheria. Kifungu cha 40 kinatambua haki zaoza ‘kupata uamuzi wa haraka kupitia kwa taratibu za haki na zisizo namapendeleo kwa kusulihisha ugomvi na mizozo kati yao na serikali aumakundi mengine, sawa na kupata suluhu bora kwa aina zote za kuingiliwakwa haki zao za kibinafsi na za pamoja’, huku ikihitaji kwamba ‘uamuzi kamahuu utazingatia ifaavyo mila, desturi, amri na mifumo ya kisheria ya watu wakiasili wanaohusika na haki za kimataifa za haki za kibinadamu.’ Kwa hivyoAzimio la Umoja wa Mataifa linaendeleza utawala wa kisheria uliokuwepo

60

Page 77: First page ILO.fm

kabla ya sasa; watu wakiasili hawana haki ya kupata haki tu, lakini mataifa piayafaa kuhakikisha kuwa mizozo yao inasuluhishwa kulingana na desturi zao zakisheria.

4.3 Mielekeo muhimu ya kitaifa

Kutona na muhtasari huu mfupi wa vyombo muhimu vya kisheria, uchunguziunageukia vikwazo vikuu vinavyohitaji kupitwa na watu wa klasili kiutendaji,na jinsi vinavyotatuliwa na mataifa ya Afrika.

Umbali wa kijiografia

Kizuizi cha kwanza ambacho watu wa kiasili watakikana kukumbana nachowanapojaribu kupata haki ni cha namna ya kiutendaji. Watu wa kiasiliwanaelekea kuishi katika maeneo ya mbali, yaliyotengeka sana kutoka kwamiji muhimu na kwa hivyo kutoka kwa korti rasmi. Ingewagharimu watuwengi wa jamii ya ‘Mbilikimo’, wanaoishi katika maeneo ya mbali ya misitukatika nchi kama Gabon na Kongo DRC, siku nyingi sana za kutembea ilikufikia kituo kilichokaribu cha polisi au korti. Nchini Kongo, kutokana naukosefu wa korti katika sehemu nyingi ambako idadi ya watu wa kiasili nikubwa zaidi, haki hutolewa na polisi badala ya mahakama. Hali hii ya mamboinaongeza udhalimu ambao watu wa kiasili wanakumbana nao.

Gharama ya mashtaka

Gharama ya mashtaka ni jambo jingine linalowazuia watu kupata haki. NchiniGabon, kwa mfano, kuanzisha kesi kutagharimu takriban Dola 20 za Marekani,ambapo mtu atahitaji kuongeza kiasi kisichopungua Dola 100 za Marekani zakumlipa wakili, ilihali mapato ya kila mwaka ya watu wa kiasili katika nchi hiyoyamekadiriwa kuwa Dola 60 za Marekani. Gharama ya juu ya kuwakilishwakisheria katika korti rasmi za nchi zote zilizochunguzwa, inafanya upataji wahaki kubakia kuwa wa matajiri, waliosoma na wale walio na uwezo wa kisiasa.Masikini, ambao ni pamoja na watu wa kiasili, hawamudu malipo ghali yakisheria.

Sheria za nchingi nyingi, zikiwemo Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Kongo,Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Gabon, zinaimarisha haki ya usaidi wakisheria wa bure kulingana na uzito wa hukumu inayomkmba mtu masikini.Vikwazo vinavyofanya usaidizi huu wa kisheria usifikiwe na hususan watu wakiasili ni;

• Watu wa kiasili hawazungumzi vizuri sana lugha ambayo imetumikakuandika sheria (sana sana kiingereza, Kifaranza na Kiarabu). Wanaufahamu mdogo sana wa kialfabeti na kwa hivyo huenda maranyingi wasizielewe haki zao vizuri.

• Hawajui jinsi ya kufikia mipango hii.• Wanaishi katika maeneo yaliyombali ambako usaidizi kama huu

kiutendaji haupo.

Nchini Eritrea kila eneo lina mahakama kadhaa za kieneo ambako watuwanaweza kuendea. Afrika Kusini pia imepata suluhisho kwa tatizo lakutofikiwa kwa maeneo kijeografia kwa kuzindua mahakama tamba (za‘mzunguko’) katika jamii za mashambani na yaliyojitenga hasa katika Juba yaKaskazini ambako Wasan wengi wanaishi. Mahakama hizi zinashughulikiakesi za uhalifu na za madai.

61

Page 78: First page ILO.fm

• Wanaweza kushindwa kuthibitisha hali yao ya umasikini kulinganana kanuni zilizoelezwa na mamlaka, au wanaweza kung’ang’anakushinda vizuizi vingine vya urasimu. Ukosekana, karibu wa namnamoja, wa vyeti vya kuzaliwa na vitambulisho vya kitaifa kwa watuwa kiasili ni kizuizi kikubwa katika kufanikisha upataji wao wamsaada wa kisheria.

• Katika nchi nyingi, msaada wa kisheria upo tu kwa watuwanaokumbana na kezi mbaya zaidi. mipango ya msaada wakisheria za Botswana, Kenya na Uganda, kwa mfano, inapatikana tukwa watu ambao wameshtakiwa kwa makosa ambayo hukumuyake inaweza kuwa kifo au kifungo cha maisha.

• Malipo kwa kazi ya msaada wa kiasheria yanaweza kuwa ya chinikabisa kiasi cha kusababisha ulegevu baina ya mawakili kujihusishakatika kesi kama hizo, kama ilvyo nchini Botswana.

Kamati ya CERD mnamo mwaka wa 2006 ilionyesha wasiwasi wakekuhusu hali ngumu zinazowakumba watu masikini,’ ambao wengi wao ni wamakundi ya San/ Basarwa na mengineyo ya wasio wa makabila ya Tswana,katika kutumia korti za sheria za kawaid, hasa kutokana na malipo ya juu,kukosekana kwa msaada wa kisheria mara nyingi, pamoja na kupata hudumaza kutosha za utafsiri.228 Kamati ilipendekkeza kwamba taifa litoe msaada wakutosha wa kisheria na huduma za utafsiri, hasa kwa watu wa makabilayanayokumbwa na hali ngumu sana, ili kuhakikisha kuwa wanapata halikikamilifu.

Ili kuwahudumia watu wasioweza kumudu huduma za kisheria, nchi yaAfrika kusini ilizindua mpago wa kitaifa wa kutoa huduma za kisheria.Kinyume na ilivyo katika masuala ya uhalifu, hayapo majukumu ya kikatibayaliyowekewa serikali kutoa huduma za mwanasheria kwa wadai katikamasuala ya madai. Nchini Kameruni, msaada wa kisheria upo na unaruhusuuhuru wa kupata haki, lakini, ili kuanzisha kesi, kila upande unapaswa kulipakiasi fulani cha pesa. Sharti hili kwa hivyo linaonekana kama kizingiti kwa watuwa kiasili na kwa mafukara kwa jumla, kupata haki. Zaidi ya hay, ili kupata hakinchini Kameruni, lazima mtu awe na kitambulishi cha kitaifa, kitu ambachoaghalabu watu wa kiasili hawana.

Mfumo wa sheria ambao kwa jumla haufanyi kazi vizuri

Kupata haki kwa watu wa kiasili kunaendelezwa na kutofanya kazi kwamifumo ya kisheria kwa jumla na mambo men gine kama vile majaji kukosatajiriba au uwezo, na ukosefu wao wa uhuru. Katika nchi nyingi za Afrika,majaji hawana ufahamu au mafunzo ya kutosha- hasa katika sehemu zamashambani. Jambo hili, pamoja na ukosefu wa miundombinu ya idara yamahakama na taratibu zake, vinaelekea kufanya mambo kuwa magumu sanakwa watu waliopembezwa na walio masikini kupata haki. Nchini Uganda kwamfano, mara kwa mara majaji hutumia sheria zisizofaa au zilizopitwa nawakati. Nchini Ethiopia, huku kukiwa na vipengele vya kitaifa na kimataifadhidi ya ubaguzi ambavyo vingetumiwa mbele ya mahakama, hajijachapishwakwatika gazeti rasmi la serikali. Kwa hivyo ni mawakili au majaji wachache tuwana ufahanu kuhusu njia hizi za kisheria. Makala ya Taratibu za kupunguzaumasikini ya Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo (SPRP) inabaini kuwa mfumowa mahakama wa nchi hii haufanyi kazi vizuri, na wenye wasifu wa ukiukajimwingi wa kanuni ya kuwa na haki sawa mbele ya sheria, usimamizi mbaya waidara ya wafanyikazi, na kutokuwepo kwa kampeni zozote za kufahamisha

228. UN Doc CERD/C/BWA/CO/16, 4 Aprili 2006.

62

Page 79: First page ILO.fm

watu kuhusu mfumo wa mahakama, mambo ambayo yanaadhiri watuwanyonge kwa njia mbaya.229

Ufisadi ni mojawapo wa vizuizi zaidi vya umma kupata haki. Nchini Kenya,kwa mfano, ufisadi pamoja na matumizi ya sheria kimapendeleo, kutokana nakutokuwepo na uhuru wa majaji kutoka kwa Serikali, vimetambuliwa kamavizuizi katika utekelezaji bora wa sheria na amani, vikiwa na matokeomakubwa hasi kwa madai ya watu wa kiasili.230 Nchini Eritrea idara yamahakama ni hafifu. Ingawa idara hiyo inachukuliwa kuwa na uwezo na ikohuru kwa mujibu wa masuala ya ogomvi kati ya au baina ya watu binafsi,umma hauna imani na masuala ambapo serikali inahusuka. Mawakili katikanchi hii hawakosoi vitendo vya serikali mbele ya mahakama. Tume ya Afrikapia imeshutumu ukosefu wa uhuru wa majaji nchini Sudan. Nchini Uganda,mfumo wa idara ya mahakama ina wasifu wa kiwango kikubwa cha kuingiliwana serikali na vitisho dhidi ya uhuru wa idara ya mahakama. Ufisadi ni sualakubwa vilevile. Nchini Burundi, serikali za mitaa aghalabu huwa upande wawakulima katika juhudi zao kuwataifisha watu wa kiasili (Batwa). Ukosefu waowa hadhi rasmi pia ni njia moja bora ya msukumo kutoka kwa watu wengine.Nchini Kongo, kutokana na kutofikia mifumo ya mahakama, watu wa kiasiliwanakumbwa na ufisadi kwa upande wa polisi.

Matatizo yanayohusiana ujuzi na uadilifu kinyume na matarajio linawezakuwa suala kubwa sana wakati ambapo sheria inatoa mikakati au mamlakamaalum kusuluhisha mizozo baina ya watu wa kiasili na wanakijiji. NchiniBurkina Faso, mizozo mingi hutokea baina ya wakulima na wafugaji kwasababu shughuli zao hutumia maliasili sawa. Kabla ya kuleta mambo hayambele ya mahakama, makarani wa kiutawala hujaribu kusaidia pande zotembili ili kupata mapatano ya amani. Hata hivyo, wafugaji hudai kwambamakarani hawa, wanaotoka katika jamii za wakulima, si waadilifu. NchiniBotswana, watu wa kiasili huishi katika vijiji ambako wanakumbana na sheriaya uhalifu ya mahakama za kimila kwa makosa kama ya wizi, uvamizi namakosa mengine madogo madogo. Shida iliyoko ni kwamba machifuwanaosimamia mahakama hizi hawana mafunzo yoyote ya sheria na mawakilihawana haki ya kusikizwa mbele ya mahakama hizi.

Ukweli wa kutoadhibiwa kwa wale wanaokiuka haki za watu wa kiasiliunadunisha uhalali wa mfumo wa kisheria machoni mwa makundi ya kiasili.Nchini Niger, hususan, dhuluma dhidi ya watu wa kiasili zimekuwa mbaya nana kuenea hivi kwamba zinaweza kuchukuliwa kama uhalifu dhidi ya binadamuau uhalifu wa mauaji ya halaiki. Mauaji ya watu wengi yametokea mara kadhaana hadi leo uhalifu huu mwingi bado haujaadhibiwa. Makosa haya mengi yauhalifu yameruhusiwa kwa werevu mno hivi kwamba waanzilishi wakewanaepuka kwa kupatikana na hatia ndogo, hivyo kuchochea urudiaji wake.

229. DRC, ‘Document de stratégie de croissance et de réduction de la pauvreté’, Julai 2006,aya ya 93 - 95.

230. Anagalia k.m Makadirio ya ripoti zilizowasilishwa na mataifa wanachama chini ya Kifungucha 40 cha Mapatano: Mapatano ya Kimataifa kuhusu haki za kiraia na kisiasa: Maoni yakuhitimisha ya Kamati ya Tume ya Kutetea haki za Kibinadamu: Kenya, CCPR/CO/83/KEN (HRC, Kenya 2005), aya ya 20; angalia pia Ripoti ya 68 ya APRM; angalia pia Maoni yakuhitimisha ya Kamati kuhusu haki za kiuchumi, kijamii na kitamaduni kuhusu Ripoti yaawali ya kenya kuhudu haki za ECOSOC katika kikao cha 41 Geneva, 3-21 Novemba2008, UN Doc E/C.12/KEN/CO/1, aya ya 10.

63

Page 80: First page ILO.fm

Kukosa ufahamu wa sheria na lugha ya sheria

Jambo lingine linalowazuia watu wa kiasili wasipate haki ni ukosefu waufahamu na maarifa ya sheria sheria, aghalabu kutokana lugha na utata washeria. Sehemu ya kwanza ya suala hili imefungamana kwa karibu na swala lawatu wa kiasili kupata elimu. Lugha inayotumiwa mahakamani kila wakatihuwa lugha rasmi ya nchi, sana sana Kiarabu, Kiingereza au Kifaransa. Watuwengi wa kiasili hawazungumzi lugha hizi rasmi. Kutoweza kwao kuelewalugha inayotumiwa mahakamani huhatarisha uwezo wao wa kupata haki bilamapendeleo na hata kunaweza kuzima nia yao ya kwendea korti. NchiniGabon, uamuzi hotolewa kwa kifaransa na majaji hawalazimiki kutumia lughainayozungumzwa na mtu aliyeletwa mahakamani. Ilihali sheria ya Gaboninampa kila mtu haki ya kupata mkalimani kama mtu huyo haelewi Kifaransa.Hata hivyo, ili kuweza kudai haki hiyo, inapasa mtu ajue kuwa ipo. Ikiwa watuwa kiasili hawaelewi lugha ilyotumika kuandika sheria, hawazijui haki zao najinsi ya kuzitambulisha. Mfumo ya Algeria hata unazidi ule wa Gabon. NchiniAlgeria, malalamishi, ushahidi, maandishi rasmi ya utetesi na hukumuhufanyika tu kwa Kiarabu. Sheria haina nafasi ya kuomba mkalimani, kwaniWaaljeria wote wanapasa kuzungumza Kiarabu. Kwa hivyo Waamazighambao hawawezi kuizungumza lugha hii hawawezi kupata haki. Nchi yaKameruni imechukua nafasi kama hii. Uchunguzi wa ILO wa mwaka wa 1999kuhusu Afrika Kusini uligundua kwamba ‘wawakilishi wengi wa serikali, nahususan mahakama, wanapuuza dhamana ya katiba kikatika kifungu cha 35 chaKatiba ya Afrika Kusini ambacho kinataka washtakiwa kufahamishwa katikalugha wanayoielewa’.

Mataifa mengi ya Afrika yamejaribu kusuluhisha tatizo hili kwa kutekelezahatua za utafsiri kama sehemu ya mpango wao mpana wa msaada wa kisheria.Nchini Chad, Kameruni, Namibia na Uganda, kwa mfano, sheria inatajabayana kuwa wakalimani watateuliwa wakati amabapo upande mmoja aupande zote hazielewi au hazizungumzi lugha inayotumika katika mahakama.Nchini Botswana, ukalimani unatolewa bure unapohitajika katika kesi zote zauhalifu. Hata hivyo, katika kesi za madai, pande zote mbili zinaweza kuhitajikakubeba gharama kiasi au kamili ya ukalimani iwapo lugha inayoeleweka napande zote au mashahidi haizungumzwi kwa kawaida katika mipaka yamamlaka ya mahakama. Nchini kongo uteuzi wa wakalimani ni lazimawanapohitajika katika kesi za uhalifu iwapo mshtakiwa hazungumzi walakuelewa kifaransa. Kifungu cha 19 cha katiba ya Ethiopia kinahitaji kwambamtu aliyekamatwa lazima afahamishwe kwa haraka, katika lugha anayoielewa,sababu ya kukamatwa kwake na kuhusu mashataka yoyote dhidi yake. Katibavilevile inahakikisha usaidizi wa mkalimani kwa gharama ya serikali iwapomshitakiwa haelewi lugha ya mahakamani. Katika Jamuhuri ya Kidemokrasiaya Kongo, serikali zina jukumu la kutimia lugha ambaayo mshutumiwaanaielewa wakati anapokamatwa. Kwa hivyo Sheria ya Taratibu za Adhabuinawapa washutumiwa wote huduma za bure za ukalimani. Ripoti kuhusuJamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) haionyeshi iwapo majukumu hayani ya lazima kwa serikali katika kesi za madai.

Sheria ya kimila231

Watu wengi wa kiasili wangali wanaendeleza mila zao (sheria za kimila) nawanazijua vizuri. Suala la mataifa mbalimbali kutambua mbinu za kimila za

231. Kwa mjadala zaidi kuhusu sheria ya kimila, tafadhali rejelea Chs 3 (kujitawala, kushauriwana kushiriki) na 7 (ardhi na maliasili).

64

Page 81: First page ILO.fm

watu wa kiasili kusuluhisha mizozo ni la umuhimu mkubwa kwa watu hawakupata haki ipasavyo. Nchini Rwanda, mbinu ya kusuluhisha mizozo kwamisingi ya uelewa na michakato ya kitamaduni, yaani Korti za gacaca,ilifufuliwa na kufanywa sheria ili kushughulikia kesi nyingi zinazotokana namauaji ya halaiki ya mwaka wa 1994. katika baadhi ya nchi, watu wa kiasiliwanaoishi mbali na miji au miji mikuu ya maeneo yao wana mfumo wao wamahakama ya kitamaduni unaotawaliwa na mila zao wenyewe. Maamuziyanafanywa na ‘watemi wa maeneo yao’ hasa katika mizozo kindoa, ujirani,mashamba na urithi.

Katika hali kadhaa, mifumo ya sheria za kimila haina au ina utambuzi naulinzi mchache sana chini ya sheria. Nchini Misri, kwa mfano, sheria ya kimilana taasisi za kitamaduni za Wabedui, Amazigh (Waberber) na Wanubizimelindwa almradi ziwe zimejikita katika sheria ya Kiislamu. Hata ingawamataifa ya Afrika yanatambua mila kama chanzo cha sheria, sheria hizi huwana wajibu mdogo sana. Nchini Kenya kwa mfano, sheria za kimila na desturizinazuiliwa na ‘ibara ya ukinzani’, iliyorithiwa kutoka siku za ukoloni,inayohitaji kuwepo kwa ulinganifu baina ya sheria ya kimila, sheriazilizoandikwa na katiba. Hali hii ya mambo imemchochea katibu maalum waUmoja wa Mataifa kuhusiana na watu wa kiasili kutangaza kwamba ‘mbali naKorti za Kadhi (koeti za kiislamu), kuna utambuzi mdogo tu wa mfumo wawahakama wa kitamaduni au kimila nchini Kenya’.232 Chini ya sheria yaKongo, mfumo wa sheria ya ardhi unadhamini sheria ya kimila muradi tuhaikinzani na vyeti vya umiliki wa mashamba vilivyosajiliwa.

Katika mataifa mengi, sheria anuwai za kimila zipo kwa pamoja. Utambuzirasmi wa mfumo mmoja wa sheria ya kiasili- ule wa makundi yenye nguvu,hasa mifumo ya sheria za kimila za Waislamu wabantu – unazua kizuizikikubwa kwa matumizi ya mila za watu wa kiasili. Nchini Aljeria, kwa mfano,kutawala kwa sheria ya Kiiislamu kunasababisha kupuuzwa kabisa kwa sheriaya kitamaduni ya na taasisi za mahakama za kitamaduni za Waamazigh.Tajmaat, baraza lililo na uwezo za kimahakama katika utamaduni waWaamazigh, halitambuliki. Kwa hivyo Waamazi hawahukumiwi kulingana nasheria wao wenyewe, lakini kulingana na kanuni na mila za sheria ya Kiislamu,na katika Korti za kiislamu. Nchini Sudan pia, uislamu una athari kubwa sanakwa sheria na Sharia(sheria ya kiislamu) ingali inatumika kwa watu wa kiasiliwasio Waislamu. Katika mataifa wanamoishi, kama vile Kongo na Gabon,mifumo ya mahakama za kiasili za ‘Mbilikimo’ haitambuliwi. Wengi wa watemiwa vijiji si wa kiasili na ‘kambi’ za watu wa kiasili zinatambulika almuradi ziwesehemu ya vijiji vya Wabantu na wala ziziwepo kwa khiari yao tu. Hii inamaana kwamba watu wa kiasili wako chini ya mifumo ya kisheria ya majiranizao wa kibantu. Kwa hivyo mizozo yao inasuluhishwa kulingana na sheria yakimila ya Wabantu – sio mila za watu wa kiasili. Nchini Botswana, kiutendaji,sheria ya kimila inayotambulika ni ile ya makabila ya Tswana, kwa sababu watuwa kiasili walichuliwa na wangali wanachukuliwa kama sehemu za makabila yaTswana au jamii za makabila. Zaidi ya hayo, sheria ya kimila, ambayoimeandikwa, inatekelezwa na machifu na manaibu wa chifu, ambao wengi waowanatoka katika makabila ya Tswana. Kulingana na haya sheria za watu wakiasili hazitambuliki katika kiutendaji.

Hata wakati ambapo mila za kiasili zinatambulika, inaweza kuwa vigumukuthibitisha yaliyomo. Nchini kameruni, kwa mfano, sherria ya kimmilainakubalika kirasmi kama chanzo cha sheria. Hata hivyo kiutendaji, maafisa

232. Ripoti ya Katibu Maalum wa Umoja wa Mataifa anayehusika na watu wa kiasili nchini kenyaaya ya 64.

65

Page 82: First page ILO.fm

wasimazi kwa nadra sana hurejelea mila za watu wa kiasili kutokana nakutokuwepo kwa wazee wa mabaraza wenye maarifa ya kuaminika juu ya milahizi, na kutokuwepo na wakalimani wanaojua lugha za Baka, Bakola na Bagyeli.Nchini Uganda Mahakama za Mabaraza ya Miji zimeundwa ili kutoa namnafulani ya haki ya umma. Hazima mamlaka ya kushughulikia jinai, lakini zinauwezo wa kuamua kesi za madai na masuala yanayotawaliwa na sheria yakimila. Sheria ya kimila inayotumiwa na watu wa kiasili kwa hivyo inatumikakatika mahakama hizi. Aidha, watu wa kiasili ni wachahe katika takribansehemu zote na hivyo hawatawali jamii wanamoishi. Kwa hivyo huendawasiwe wenye idadi ianyohitajika kutawala mahakama; kwa sababu hii daawana sheria zao zinaweza kupuuzwa. Jambo hili limewalazimu watu wengikuacha sheria zao za kimila na kutafuta kulinda haki zao kwa kutumia sheriailiyoandikwa, ambayo imeunyima mfumo wa kisheria faida zinazotokana nasheria ya kimila. Nchini Ethiopia, sheria ya kimila na mifumo yake ya mamlakaya kisheria inatambulika kikatiba, lakini kwa kiwango tu kitakachokubalika napande zinzozozana. Mfumo wa kimila ungali na nguvu baina ya jamii nyingi zakiasili za nchi hii.

Maswali fulani yanaweza kuulizwa kuusu utambuzi na ubora wawafanyikazi wa mahakama hizi. Nchini Chad, sheria ya kimila inatambulika nainatumiwa katika mahakama za kitaifa. Mahakama hizi zina chumba cha jaji wakiseriakali na cha jaji wa kimila. Wakati wa kuamua kesi za masuala ya kiraia,majaji huteua wazee wa baraza wanaowakilisha mila za pande zote, hatawakati ambapo mila za kiasili zinahusika. Aidha, asasi za kitamadunizimelindwa na Katiba, na Wachadi wengi wanazitumia. Asasi hizi husuluhishamizozo kulingana na sheria ya kimila ya pande husika. Jamuhuri yaKidemokrasia ya Kongo inatambua sheria ya kitamaduni na mahakama. Hatahivyo, kwa sasa hakuna majaji wa kiasili kuamua mambo haya, kwaniWakongo wengi wanawachukulia watu kutoka jamii hizi kama ‘wananchi watabaka la pili’ na hawafai kutimiza wajibu muhimu kama huu.

Asasi badala za kufanikisha ufikiaji upataji wa haki

Kwa kufahamu mapengo yaliyopo katika mifumo yao ya kisheria, hasa utata naurefu wa taratibu zake, baadhi ya mataifa yamebuni Wachunguzi Maalum ilikufanikisha fursa ya umma kufikia mifumo ya kisheria kunapokuwa na ukiukajiwa haki zao za kibinadamu nchini Namibia, kazi ya Mchunguzi Maalum nipamoja na uchunguzi wa ‘malalamishi kuhusu shutuma au visa dhahiri vyaukiukaji wa haki za msingi za kibinadamu’. Wachunguzi Maalum wamewekwakuendeleza dhana ya haki za kibinadamu baina ya umma; kuangalia ukiukaji wahaki za kibinadamu; na kuchukua hatua za kuondoa dhuluma. Shida ni kwambahawafaidiki sana kutokana na njia zifaazo kutimiza wajibu wao. Aidha, mfanowa Namibia unaonyesha kuwa, tangu kuteuliwa kwake, Mchunguzi Maalumamepokea malalamishi machache sana labda kutokana na wahasiriwa kukosahabari kuhusu haki zao na jinsi ya kupata suluhu za kisheria. Nchini Burundihuduma ya Mchunguzi maalum ilyowekwa na katiba mnamo mwaka wa 2005haifanyi kazi kwani mfumo wa sheria unaohitajika bado haujakubaliwa.

4.4 Hitimisho

Kupata haki kunahitaji kwamba mawakili wapo ili kuwasaidia watuwanaowahitaji, kwamba mahakama haziko mbali sana na zisizofikika ilikutumiwa na kwamba lugha ya sheria inaeleweka na watu wanaohitajikutegemea sheria. Huku ikiwa kwamba mfumo wa kisheria wa nchi zotezilizochunguzwa unadhamini upataji wa haki kwa wote, ukweli uliopo kwa

66

Page 83: First page ILO.fm

watu wa kiasili unasawiri picha tofautu sana. Katika nchi nyingizilizochunguzwa, kutofikia mifumo ya kisheria hakuwaadhiri watu wa kiasilipekee yake. Ingawa kupata haki kwa watu wengi wanaoishi katika mataifa yaAfrika ni finyu sana, shida zinazowakumba watu kwa jumla zinazidishwa kwawatu wa kiasili. Korti na mabaraza mengie ya kimahakama mara nyingihavifikiki kijiografia, kwa sababu watu hawa wanaishi katika maeneo ya mbaliya mashambani sana au wanaishi maisha ya kuhamahama. Kutokana naviwango vikubwa vya umasikini na kutojua kusoma na kuandika baina yao,watu wa kiasili huenda wasiweze kulipia huduma za kisheria, au wasijue hakizao na uwezekano wa kupata msaada wa kisheria, kama upo. Kutambuliwakwa sheria ya kimila ya Wabantu kama aina moja tu ya mfumo wa‘kitamaduni’ unaotambulika kumemomonyoa zaidi fursa ya watu wa kiasilikupata haki. Mbali na mambo machache tu, kama vile korti tamba kwa jamiikadhaa za kiasili nchini Afrika Kusini, mataifa hayajachukua hatua yoyotekusghulikia hali hii. Huku mataifa kadhaa yakiwa yamefaulu kusuluhisha tatizola jumla la kutofikika kwa njia ambayo inaweza kuwafaa watu wa kiasili pia,machache yamechukua hatua inayolenga hususan watu wa kiasili.

67

Page 84: First page ILO.fm

5 Utamaduni na Lugha

5.1 Utangulizi

Ulinzi wa utamaduni na lugha yao ya pekee ni elementi muhimu kwa maishaya watu wa kiasili. Kwa makundi haya, lugha na utamaduni mara nyingihutegemeana na haviwezi kutengeka. Vivyo hivyo, imani na dini sawa aghalabuhuwa sifa muhimu ya utamaduni, ambavyo vinaweza tu kudhihirishwa nakufafanuliwa kikamilifu kwa lugha ya kiasili ya jamii hiyo. Kuinyima jamiimojawapo ya vitu hivi kwa hakika kutatishia utambulisho wa jamii hiyo. Aidha,kwa sababu makundi ya kiasili huwakilisha waliowachache katika umma wakitaifa, kuwanyima haki ya lugha, utamaduni au imani pia kunaweza kudhihirikakatika kushindwa kulinda na kuendeleza haki hizo. Hakuna sifa zingine zamakundi ya wachache ambazo zinahatarishwa na ‘udhalimu wa waliowengi’kama ilivyo utamaduni na lugha yao. Kando na lugha, vipengele vinginemuhimu vya utamaduni ni sifa zake za kiubunifu na za kisayansi. Heshima kwautamaduni za kiasili kila mara itategemea heshima kwa ulimwengu wakehalisia, ikiwemo ardhi wanamoishi na maliasili ambayo maisha yaoyanayategemea.

Sheria ya kimataifa na stakabadhi nyingi za kitaifa za katiba zinatambuamatatizo haya na kudhamini haki ya utamaduni, imani na wakati mwingine yakutumia lugha kama haki muhimu. Baadhi ya udhamini huu umetiwa nguvu nastakabadhi za sheria na sera pamoja na mifumo ya kitaasisi.

5.2 Sheria ya kimataifa

Kuna vipengele kadhaa katika sheria ya kimataifa vinavyolenga kuzilinda hakiza lugha na utamaduni za watu wa kiasili.

Azimio la umoja wa mataifa kuhusu haki za watu wa kiasili lina vipengeleanuwai vya maana kwa utamaduni na lugha ya watu wa kiasili, vikisisitizaumuhimu wa utamaduni katika madai ya makundi asiili. Kifungu cha 8kinasema kuwa watu wa kiasili wana haki ya ‘kutotiwa katika usilimisho walazima au kuharibu utamaduni wao’. Watu wa kiasili wana haki ya kutekelezana kutia nguvu tena desturi na mila za utamaduni wao, ikiwemo haki yakuhifdhi maeneo yao ya kitamaduni.233 Mataifa yanapasa kutoa fidia na njiazingine za kurekebisha hali ya kuchukua mali ya kitamaduni, kiakili, kidini nakiroho ya watu wa kiasili,234 na kurejesha kwao vifaa vya kimila na mabaki yabinadamu.235 Kulingana na kifungu nambari 13, watu wa kiasili wana haki yakuhuisha, kutumia kuendeleza na kupisha kwa vizazi vya baadaye historia zao,lugha, tamaduni simulizi, falsafa, mifumo ya maandidshi yao na fasihi, na kuteuana kudumisha majina yao wenyewe ya jamii, mahali na watu. Ili kushughulikiamasuala ya shutuma na ukosefu wa stahamala, mataifa yanapasa kuchukuahatua zifaazo kukabiliana na chuki na kuondoa ubaguzi na kuendelezastahamala, maelewano na uhusiano bora baina ya watu wa kiasili na tanzunyingine zote za jamii.236 Kazi ya vyombo vya habari ni muhimu katikakuwepo kwa utamaduni. Watu wa kiasili vivyo hivyo wana haki ya kuanzishavyombo vya habari vyao wenyewe. Zaidi ya hayo, inapasa serikali zichukue

233. Kifungu cha 11(1) na 12(1).234. Kifungu cha 11.235. Kifungu cha 12(2).236. Kifungu- 15(2).

68

Page 85: First page ILO.fm

hatua mwafaka za kuhakikisha kuwa vyombo vya habari vinavyomilikiwa naserikali vinadhirisha uwingi wa utamaduni.237

CERD inashurutsha mataifa kuondoa ubaguzi wa kikabila katika kufurahia‘haki ya usawa wa kushiriki katika shughuli za kitamaduni’.238 Katika mwakawa 2006 Kamati ya CERD ilionyesha wasiwasi wake kwamba lengo laBotswana la kujenga taifa kwenye msingi wa kanuni ya usawa kwa wotelilikuwa limetekelezwa kwa njia inayoleta madhara kwa ulizi wa uwingi wamakabila na tamaduni, na ikaomba serikali kuheshimu na kulinda maisha nautambulisho wa kitamduni wa makabila yote katika himaya yake. VilevileKamati ilialika chama cha kitaifa kurekebisha sera ya kuhusu watu wa kiasilina, kwa njia hiyo, kuzingatia namna makundi husika yanavyojiona nakujibainisha wenyewe.

Kwa njia ya moja kwa moja zaidi, ICCPR inayolazimu kisheria inahakikishakatika kifungu cha 27 kama ifuatavyo: ‘Katika yale mataifa ambako kunamakabila, dini au lugha za wachache, watu wanaotoka katika jamii zawachache kama hizi hawatanyimwa haki, katika jamii pamoja na wanajamiiwengine wa kundi lao, kufurahia utamaduni wao wenyewe, kukiri nakutekeleza dini yao wenyewe, au kutumia lugha yao wenyewe.’ Kamati yakutetea haki za kibinadamu iligundua uhusiano wa karibu, hasa kuhusiana najamii za kiasili, baina ya haki ya mtu kufurahia utamaduni wake mwenyewe nauhifadhi wa hali za maisha yao kwa kutegema ardhi na maliasili.239 Mapatanomengine menza, ICESCR, yanalinda jamii za kitamaduni kutokanakunyanyaswa kitamaduni kwa ajili ya sekta ya utalii, pamoja na kulinda hakizao za mali yaokiakili kwa minajili ya maendeleo yao ya kitamduni nakisayansi.240 Kwenye kiwango cha ulimwengu ni muhimu pia kutaja dhamanazilizokubaliwa katika Azimio la Umoja wa mataifa kuhusu Uwingi waTamaduni (2001), Mkataba wa Hague wa 1954 (juu ya ulinzi wa mali yakitamaduni wakati wa mzozo) na itifaki yake ya pili, pamoja na bila shakavipengele vya Mkataba wa 169 wa ILO. Cha muhimu kutajwa katika Mkatabahuo ni umuhimu wa mwelekeo wa mageuzi kwa upande wa serikali ili kulindakwa bidii haki za watu wa kiasili.

Kifungu cha 22 cha Mkataba wa Afrika ni hatua muhimu hivi kwambaunasisitiza umuhimu wa kutilia maanani usawa, uhuru na upekee wa watuwakati wa kutekeleza sera za skiuchumi na maendeleo. Pia unatia wajibu kwamataifa kukuza na kulinda heshima na maadili ya jamii.241 Ripoti ya Kamatiteule ya Tume ya Afrika inayohusika na watu wa kiasili inaonyesha kwambakutotambua haki za kiasili, kitamaduni, na za lugha ili kulinda umoja wa taifa,kunadunisha thamani ya kutambua haki za kitamaduni na lugha kama raslimaliya kitamaduni, ambayo inaweza kutumika kufaidi kila mtu katika jamii.242

Vile vile cha kukumbukwa ni Mkataba wa Kitamaduni kwa Afrika, waMuungano wa Afrika, na hasa kudhihirisha uelewa wa umuhimu wautambulisho wa kitamaduni kwa jamii za kiasili za Afrika kwenye dibaji,pamoja na umuhimu wa kuwa na tamaduni anuwai na mwingiliano wake nautambulisho wa taifa katika Sehemu ya II ya Mkataba huu. Shabaha, malengona kanuni za Mkataba huu ni pamoja na ‘ukarabati, urejesho, uhifadhi na

237. Kifungu cha 16. 238. Kifungu cha 5(e)(vi) cha CERD. 239. Maoni ya jumla nambari 23. (1993).240. Kifungu cha 15(1)(c) cha ICESCR.241. Kifungu cha 17(3) cha mkataba wa Afrika.242. Ripoti ya Kamati Teule ya Wataalamu wa Tume ya Afrika kuhusu watu/ jamii za kiasili 28-

29.

69

Page 86: First page ILO.fm

uendelezaji urithi wa utamaduni wa Afrika’. Haya ni ya kongezea kwenye‘utetezi wa heshima ya mwafrika na misingi pendwa ya utamaduni wake’.243

Mkataba unashurutisha wanachama kukubali sera ya kitamaduni iliyoundwakama njia ya kufanya kuwa kanuni desturi za jamii na shughuli za pamojazinazotosheleza mahitaji ya kitamaduni244 mojawapo ya vipaumbelevilivyowekwa na Mkataba wa Kitamaduni ni kuendeleza lugha za kitaifa; hii nikwa kuongezea kwenye maeneleo ya utafiti na kustawishwa kwa vituo vyakudumu vya utafiti katika nyanja za utamaduni.245

5.3 Mielekeo ya kitaifa

Ijapokuwa karibu kila taifa la Afrika lina muundo tofauti wa kikabila na halizisizofanana za kisiasa na kiuchumi ambazo zinasababisha serazinazotofautiana kuhusiana na ulinzi wa haki za lugha na utamaduni, kunamielekeo fulani inayoweza kubainika inayoweza kutoa tathmini ya jumlakuhusu hali za haki hizi barani Afrika.

Utamaduni kama kawaida ya maisha

Utamaduni ni istilahi pan asana. Inarejelea njia fulani ya maisha ambayoinahusisha aina ya kazi na mbinu za kujikimu kimaisha za kikundi fulani. Kwasababu maisha ya watu wa kiasili yamefungamana sana kwenye mazingira yaoasili, utamaduni wao aghalabu unahatarishwa na kuingiliwa katika himaya zao,kunakosabibishwa na miradi ya kimaendeleo, ukataji wa miti na ubainishaji wahifadhi za maumbile au mbuga za wanyama.

Mradi mmoja wa maendeleo nchini Namibia, uliolenge kujenga bwawa lauzalishaji umeme chini ya maporomoko ya maji ya Epupa (Epupa Falls)yalitishia makaburi ya mababu wa Ovahimba kwa mafuriko na ungewezakuathiri vipengele vingine vya utamaduni wao. Kupotezwa kwa raslimali zaokungewaathiri vibaya, hivyo kuwanyima haki ya kudumisha maisha ya chafuolao na kuweka na kuendeleza utamaduni na utambulisho wa utamaduni kamawanavyopenda. Hadi sasa, uhamasishaji wa jamii, pamoja na shinikizo la nchinina la kimataifa, vilisimamisha shughuli hiyo isiendelee. Wasiwasi mkubwaumekuwa ni kukosa kuwashirikisha jamii za kiasili katika mradi huu unaoathiriutamaduni wao. Suala hili lilikuwa maudhui katika kesi baina ya Kapica naserikali ya Namibia, ikidhihirisha jinsi mchakato wa mahakama unawezakutumiwa kufaidi daawa ya watu wa kiasili.

Ustawishaji wa mbuga za asili aghalamu husababisha kuwaondoa watu wakiasili kutoka kwenye makaazi yao na kuathiri tamaduni zao vibaya. Sheria yaGabon ya mwaka 2007 (sheria ya 32007 ya Septemba 11, 2007) inaamurukuwa taasisi zinazohusika na usimamizi wa mbuga ziheshimu umuhimu wakulinda urithi wa asili na wa kitamaduni.

Hata hivyo dhamana kama hizi za taasisi aghalabu huja na ibara yakuziwekea mipaka, kama vile kifungu cha 31(2) cha katiba ya Afrika Kusini:

Haki katika kifungu kidogo cha (1) huenda zisitekelezwe kwa namnainayolingana na kipengele chochote cha Sheria ya Haki za Kibinadamu.

243. Kifungu cha1.244. Kifungu cha 6(a).245. Kifungu cha 6.

70

Page 87: First page ILO.fm

Hata hivyo, ushaidi wa kutengwa na kubaguliwa kijamii kwa watu wa kiasilikunabaki sababu ya kutia wasiwasi nchini Afrika Kusini licha ya mfumo wakisheria.246

Baadhi ya katiba, kama ile ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, zinatajawaziwazi ‘utamaduni na lugha ya wachche’ kama sababu ya kupiga marufukuubaguzi.247 Nchini Ethiopia, kifungu cha 39 cha katiba kinadhamini haki zakitamaduni za ‘mataifa, raia na watu’, zaidi ya wajibu wa serikali kuhifadhiurithi wa kitamaduni na wa kihistoria wa watu.

Katiba nyingi za kitaifa zina ibara inayoruhusu kuwepo kwa pamoja kwasheria ya kimila sambamba sheria ya kitaifa, kama vile kifungu cha 115(2) chaKatiba ya Kenya, ambacho kinaruhusu utambuzi wa kisheria uwezo wa sheriaya kimila juu ya masuala kama uasili, ndoa, talaka, mazishi na ugavi wa malibaada ya mtu kufariki. Hata hivyo, mamlaka na ufaafu wa sheria ya kimilavimemomonyoka sana kupitia kwa ‘ibara ya ukinzani’, ambapo kulingana nayosheria ya kimila inatiishwa kwa sheria zilizoandikwa. Kesi ya Naijeria baina yaOyewumi na Ogunesan inadhihirisha kuwa utambuzi wa kikatiba wa sheria yakimila ni muhimu sana kwa kuwepo kwa tamaduni na lugha za kiasili katikaAfrika. Sheria ya kimila imefungamanika na matambiko, na usimamizi wa ardhi,kipengele muhimu sana cha utamaduni wa kiasili.

Katika baadhi ya nchi kumekuweko na stakabadhi kadhaa muhimu kujalizaau kutilia nguvu udhamini wa kikatiba. Mfano wa kuvutia ni sheria ya 06.002 yaJamuhuri ya Afrika nya Kati, inayohusu Mktaba wa Kitamaduni wa nchi hiyo,ambayo inasisitiza umuhimu wa kulinda urithi wa utamaduni wa taifa nahususan pia ‘utamaduni wa waliowachache umerejelewa’. Vile vile, Sheria yaJamuhuri ya Afrika ya Kati ya mwaka wa 2003 (arrêté ministerial) inapigamarufuku utumizi na utaifishaji wa utamaduni simulizi na desturi nyinginezo zautamaduni wa waliowachache kwa malengo ya kibiashara. Msururu mwinginewa sheria za kuvutia unapatikana katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongokama Sheria za misitu na Uchimbaji wa madini, ambazo zinatilia mkazokwamba hatua zinazochukuliwa katika maeneo haya lazima zifanywe kwakuangalia sana ulinzi na uhifadhi wa mali ya kitamaduni. Sheria ya misituinalenga kulinda matumizi ya kimila ya misitu ya kiasili, ikiwemo heshima kwamaeneo yao ya dhati.

246. Kwa jumla tazama Ripoti ya ziara ya Katibu Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu watuwa kiasili nchini Afrika Kusini; Maoni ya mwisho ya CERD mwaka wa 2006, aya ya 19; piatazama Channels R na du Toit A Ibid, 101, zikinukuu ripoti ya ILO inayohifadhi kampeni zausilimishaji wa watoto wa Kinama na Kisan waliotandikwa kwa kukiri utambulishi wao aukuzungumza lugha yao.

247. Kifungu cha 13 cha katiba ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Ama kweli dhamana za kikatiba zinazolinda haki za kitamaduni ni hatuanzuri ya kuanzia. Mfano wake mzuri ni kifungu cha 31(1) cha katiba yaAfrika kusini:

Watu wa jamii za kitamaduni, kidini au kilugha hawatanyimwa haki, nawatu wengine katika jamii hiyo

(a)ya kufurahia utamaduni wao, kuendesha dini yao au kutumia lughayao; na

(b)kuunda, kujiunga na kudumisha miungano ya kitamaduni, kidini nakilugha pamoja na mashirika mengine ya umma.

71

Page 88: First page ILO.fm

Kuhusiana na vyombo vya kuunda sera, pana vitendo kadhaa ambavyovinaweza kubainika. Mpango wa maendeleo kwa watu wa kiasili wa nchiniGabon (Plan de Developpement des peuples autochtones), ulioanzishwa kamasehemu ya mpango sekta ya misitu na mazingira, ni mfano muhimu. Shabahakuu ya Mpango huu, iliyowekwa wazi, ni kuhakikisha uhifadhi na kuwepo kwahesima kwa utamaduni wa ‘Mbilikimo’ (‘la culture des populations pygmées auGabon’). Mfumo wa ruwaza ya muda mrefu kwa nchi ya Botswana (Ruwaza yamwaka 2016), kwa mfano, unatambua uwingi wa utamaduni na kushirikishaserikali katika kuendeleza utamaduni wa wachache. Hadi hii leo, hata hivyokutawala kwa Kiingeresa na Kitswana juu ya lugha nyingine zote m kunawezatu kuelezwa kama mamlaka ya kitamaduni. Wakati mwingine, kama ilivyo Seraya Kitaifa ya Uganda iliyokubaliwa mwaka wa 2006, sera ya serikali hubakiakimya kuhusiana na tamaduni asili. Hata hivyo, ni sahihi pia kutaja kwambawasiwasi ulioonyeshwa na serikali kuhusu tamaduni umeunda chomboambacho kinaweza kuhusisha mahitaji ya watu wa kiasili.

Uhifadhi wa vyombo vya kitamaduni mara nyingi hauendi zaidi yakuhusisha vyombo vichache asili vya kitamduni kwenye makavazi ya kitaifa.

Maonysho ya utamaduni, kama vile densi za ‘Mbilikimo’, agalabu hukuzwakwa njia illyobora zaidi nje ya mipaka ya serikali. Mifano ni Tamasha za muzikiza Afrika nzima, zilizoandaliwa mjini Brazzaville (Julai 2007), ambakokulibadilishanwa maonyesho ya utamaduni, na tamasha za kitamaduni zakawaida za Waamazi (Amazigh).

Dini

Shughuli za kidini pia zinaweza kuwa na wajibu muhimu katika maisha yakitamaduni ya jamii za kilasili. Shughuli hizi kijumla zinaweza kuelezwa kamazenye ‘imani katika uroho wa vitu vya kimaumbile’, zikisisitiza uhusiano bainaya binadamu na mazingira ya kiasili, na baina ya kizazi kimoja na kingine. Sifanyingine ya kawaida ya katiba nyingi ni ulinzi wazo wa uhuru wa dhamiri,pamoja na uhuru wa kuabudu. Haki ya uhuru wa kutanbgamana piaimehakikishwa. Hata hivyo, kwa miaka kadhaa mmifumo ya imani ya watu wakiasili umetiwa na ungali ukitiwa chini ya mvutano mkali kwa kuja kwaUislamu na Ukristo. Matambiko ya kidini ya watu wa kiasili yamechukuliwakama za kishetani kulingana na Ukristo, au nafasi yake imechukuliwa namwonoulimnwengu wa kiiaslamu. Baadhi ya makundi ya kiasili, kama vileWafulani wa nchini Nigeria, wamesilimishwa sana; na, pengine kwa kinyumena inavyotarajiwa, wanatazamwa kama tisho kwa dini za makundi menginekatika Nigeria ya kati.

Lugha

Kuhusiana na haki za kilugha, mwelekeo wa kawaida ni ubainishaji wa lugharasmi ya serikali, pamoja utambuzi wa lugha kadhaa za taifa. Hata hivyo, niwazi kwamba lugha rasmi na za taifa zilizotambuliwa na katiba huwahazihusishi lugha za kiasili za wachache, jambo ambalo loinaweza kuwa naathari mbaya kwa kuwepo kwa lugha hizo kwani shughuli zote za serikali,mawasiliano na aghalabu elimu zitafanywa kwa zile lugha zilizotambuliwa nakatiba. La kutajwa ni katiba ya Eritrea, ambayo kinyume na zinginezo nyingihaibainishi lugha rasmi, lakini badala yake inadhamini usawa wa lugha zote zaEritrea katika kifungu cha 4(3). Ijapokuwa hivyo, kiutendaji, Kiarabu naKitigriyna (pamoja na kudhihirika kuwa kuwa Kitigriyna kina nguvu zaidi), ni

72

Page 89: First page ILO.fm

lugha za sherhe rasmi, mikutano ya kitasifa na matan gazo ya kiserikali, hukulugha za wachache (zikiwemo lugha asili) zikiachwa nje.

Lugha ya Waamazi, Kitamazi, Kaskazini mwa Afrika iko hatarani. Katikanchi tatu zilizochunguzwa, Aljeria, Misri, na Moroko, kuanzisha Kiarabu kuwakama sehemu muhimu ya utamaduni wa Kiislamu kumepelekeakukandamizwa na kupungua kwa lugha amabazo si za Kiarabu, hususanKitamazi. Kukandamizwa kwa Kitamazi pia kuna mwelekeo wa kisiasa, hivikwamba kufufuliwa kwake tena kunatazamwa kama tisho kwa mamlaka yautamaduni wa kitaifa (na kisiasa).

Nchini Aljeria, Kitamazi kimekuwa mhanga wa mchakato, kuanzia uhurumwaka wa 1962, wa kubadilisha nafasi ya Kifaranza pamoja na utamaduniwake na utamaduni wa Kiarabu-kiislamu. Kirabu likuwa na kingali lugha rasmiya Aljeria. Kwa hakika, Sheria ya 91-05 ya mwaka wa 1991 inasisitiza kwambataasisi za umma zinaweza tu kutumia Kiarabu kama lugha ya mawasiliano; nainaeleza kwamba stakabadhi zote rasmi zikiwemo kumbukumbu zamahakamani lazima ziandikwe kwa Kiarabu. Pamekuwepo na maendeleofulani katika karibu mwongo mmoja uliopita. Mnamo mwaka wa 1996, wakatiambapo katiba mpya ilikubaliwa, maadili ya msingi ya taifa la Algeria yaliendazaidi ya ‘Kiarabu’ na ‘uislamu’ na kuhusisha ‘Kiamazi’. Mnamo mwaka wa 2002,Bunge la Algeria liliidhinisha marekebisho ya Katiba kwa kuipitia lugha yaKiamazi hadhi ya ‘lugha ya kitaifa’. Maendeleo haya muhimu yalitokana nashinikisho kubwa lajamii ya Waamazi kwa serikali.

Mnamo mwaka wa 1995 wanafunzi walisusia kwenda shule, na katikamwaka wa 2001, kulizuka maandamano huko Kabylie baada ya kijana mmojakuuawa na polisi. Vikosi vya usalama viliitikia kwa njia isiyofaa na wakaua nakujeruhi watu wengi, kitendo kilichokuja kuitwa ‘matukio ya Kabylie’. Baadaya matukio haya, vuguvugu la Waamazi lilipata nguvu zaidi na kuishia katikamaandamano ya waamazi milioni mbili nchini Aljgers. Hata hivyo, viongozi waWaamazi wanakubali kwamba mabadiliko ya kisheria huwa hayaendi mbalikama invyopasa. Kuhusishwa kwa ‘kiamazi’ ni kwenye Dibaji ya katiba tu, nahakuna umuhimu zaidi; na Kitamazi kinaelezwa kama lugha ya taifa pia, ikitilianguvu Kiarabu kama lugha rasmi na lugha ya taifa. Kitamazi bado kinakumbwana ukosefu wa kuwekwa wazi na uungwaji mkono na serikali. Kinatumika tukatika vipindi vya televisheri vya nyakati fulanifulani na kwa kuwa ni lugha yahiari shuleni, inatazamwa kama iliyo na matumizi finyu katika jamii, idadi yashule zinazofunza lugha hii inaendelea kudidimia. Matatizo haya yanzidishwakutokana na kupunguzwa kwa nafasi za ualimu zinazodhaminiwa na serikali.

Kitamzi kimekumbwa na kinaendelea kukumbwa na hali ii hii nchini Misrina Moroko. Nchini Misri, Kiarabu ndiyo lugha rasmi ya pekee. Lugha za kiasiliza Wanubi na Waberber (Kitamzi) hazina hadhi rasmi na hazitambuliki kwashughuli yoyote ya umma. Kuhusiana na hali ilivyo nchini Misri, Kamati yaCERD iligundua kwamba ‘hakuna mkakati wa kisheria au uliopangwaunaolenga kuzuia au kukomesha ubaguzi au kulinda lugha au utamaduni wamakundi hayo, kwa mfano kwa kudhamini elimu ya lugha ya kwanza au yalugha mbili’.248 Nchini Moroko pia, Kiarabu pekee ndicho lugha rasmi nalugha ya taifa. Tangazo la hadhara la Mfalme mohammed wa VI mnamomwaka wa 2001 la kukubali ‘Kiamazi’ kama sehemu ya utamaduni wa kitaifa,ndilo lilikuwa utambuzi wa kwanza wa ukweli kwamba kuna lugha natamaduni anuwai.

248. CERD, muhtasari wa kumbukumbu za awamu ya kwanza ya mkutano wa 148: Misri. UNDoc CERD/C/SR.1484 17/09/2002 aya ya 9.

73

Page 90: First page ILO.fm

Alfabeti za Kitifina, zinazotumika na baadhi ya Waamazi, zina uhumuhimumkubwa kwa Watuaregi, ambao maandishi haya ni kama sifa muhimusana yautambulisho wao. Ingawa imeendelezwa na kufunzwa katika baa dhi ya nchi zaMaghreb kama vile Moroko, lugha ya Tifinagh ingali inepuuzwa sana n chiniMali na Niger, ambapo inatumika tu sana sana katika tamasha za kisanaa aukwa mapambo.

Nchni Sudan, Katiba ya mwaka wa 2005 inaonyesha utambuzi mkubwa wauwingi wa kitamaduni na kilugha kuliko katiba zilizotangulia. Ingawa Kiasrabuna Kiingereza kinafaidi fursa ya ‘kuwa ya lugha ya taifa inayozungumzwa kwawingi na ‘lugha rasmi ya kazi’ mtawalia, jamii za makabila na tamadunimbalimbali zimepewa ruhusa kikatiba kutumia lugha zao, na ‘lugha zote zakiasili za nchini Sudan ni lugha za kitaifa’ na lazima zika’249 lindwe na kukuzwa.

Nafasi ya lugha za kiasili za makundi mbalimbali ya ‘Mbilikimo’ ni mbayahata zaidi. Lugha hizi zinawania kutambuliwa sio tu pamoja na lugha yakikoloni ya umoja wa kitaifa (Kifaransa), lakini pia pamoja na lugha zi9ngine zakitaifa zinazozungumzwa na makundi yenye nguvu ya Wabantu. Hakuna nchiyoyote katika kanda ya Afrika ya Kati inayotambua lugha yoyote ya kiasilikama lugha ya taifa wala lugha rasmi. Kulingana na takwimu rasmi zilizopo, niasilimia ndogo sana ya umma mzima unazungumza lugha ya kiasili. Hali hiiinafanywa mbaya zaidi na kiwango ambacho watu wa kiasili wamebwiamtazamo uliopo kwamba lugha yao ni dini, iliyonyuma na isiyo na matumizi yaamilifu katikauchumi wa kisasa. Katika Jamuhuru ya Afrika ya Kati kwa mfano,wengi wa Waaka na Wambororo wanazungumza Kisango, mojawapo ya lughaza kibantu iliyotambulika kama lugha rasmi. Lugha hizi za kiasili hazitumiki kwamakusudi yoyote ya umma kama vile elimu au katika mfumo wa idara yamahakama.

Kando na Afrika kusini, nafasi ya kusini mwa Afrika si tofauti sana vile.Mfano mzuri ni ule wa Botswana, ambapo Kistwana na Kiingereza ndizo lughapekee zinazotambulika kama lugha za kitaifa na lugha rasmi; pia zinatumikakama nyenzo rasmi ya pekee ya kufundishia katika shule za kiserikali nchiniBotswana. Nchini Afrika kusini, haki ya mtu kutumia lugha yake imelindwakikatiba.250 Katiba ya Afrika hususan inataja lugha za kiasili kwa jina, nainaamuru kwamba serikali ikuze lugha za Kikhoi Kinama, na Kisan.251

Upitishaji wa sheria252 pia umetumiwa nchini Afrika Kusini kulinda na kukuzalugha za kiasili kupitia kwa uanzishaji wa taasisi mahususi.

Vyombo vya habari

Vyombo vya habari vina nafasi muhimu katika kukuza haki za kitamaduni na zakilugha. Idhaa ya Utangazaji ya Misri (Egyptian Broadcasting Authority) kwamfano, ina wajibu wa kufanya shughuli zinazounga mkono tamaduni zamakundi yasiyo na nguvu, wakiwemo watu wa kiasili. Haya pia yanatendekanchini Naijeria na mataifa mengine machache. Hata hivyo, mwelekeo wa jumlabarani Afrika ni kuwa mashirika ya vyombo vya habari ya umma na ya kibinafsiyanatangaza (au kuchapisha) habari na matangazo ya utamaduni kwa lughazenye nguvu, yakiacha tamaduni za wachache nje ya mawanda ya njia za kisasaza utangazaji. Kwa wingi, vipindi vinavyopeperushwa kwa lugha zenye nguvu

249. Ingeonekana kwamba ‘lugha za kiasili’ hapa inarejelea lugha zote mbali na Kiarabu nakiingereza, na wala sio tu lugha za watu wa kiasili kama vile istilahi hii inavyotumika katikautafiti huu.

250. Sehemu ya 6(2) ya Katiba ya Afrika Kusini. 251. Sehemu ya 6(5).252. Sheria ya Lugha ya mwaka wa 1995, Sehemu ya 5(b)ii.

74

Page 91: First page ILO.fm

vinaweza kufungwa kwa masuala yanayohusiana na watu wa kiasili, au wakatimwingine kunaweza kuwepo na vipindi vinavyopeperushwa kwa lugha zakiasili. Mfano mmoja kama huu ni televisheni moja tu inayomilikiwa na serikalinchini Algeria, ambayo ina nafasi ya dakika 20 kila siku kutangaza kwaKitamazi. Hata hivyo vipindi hivi vina wasifu wa kuwa na mwelekeo mmoja nakuwasilisha utamaduni kama sanaa ya jadi.

Asasi mbalimbali

Baadhi ya sheria za kisheria hata zimesonga mbele kuanzisha asasi maalum zakitaifa zinazolenga kulinda haki za kitamaduni na lugha. Asasi za kawaida nipamoja na makavazi na vituo vya utamaduni, ndani ya jamii za kitamaduni nakatika miji mikuu. Mataifa mengine yanalenga kulinda haki za kitamaduni nalugha kwa njia ya mifumo rasmi zaidi ya kiserikali, kama vile Wizara ya jinsia,michezo, tamaduni na huduma za jamii nchini Kenya. Ijapokuwa hivyo,kutumia asasi iliyo na uwezo mpana kama huu aghalabu husababishaunyanyasaji, badala ya kuzilinda tamaduni asili, kwani jamii nyingi za kitamaduninchini kenya zimetiwa katika kampeni za matangazo ya utalii huku zikipatafaida ndogo sana kutokana na shughuli hii yenye faida kubwa. Asasi mahususizaidi zinazohusika na ufundi (kama vile Baraza la Kitaifa la Ufundi nchini AfrikaKusini) au lugha (Halmashauri ya Lugha ya Afrika Kusini nzima) zinafaa zaidikushughulikia mahitaji maalumu ya jamii asili. Mfano mzuri zaidi ni Tume yaUkuzaji na ulinzi wa haki za Jamii za kitamaduni, kidini, na za lugha nchiniAfrika Kusini, ambayo baadaye ilianzishwa mwaka wa 2002.

Umma unaweza kuchangia katika kumulika masuala ya usambazaji wavyombo vya habari, kama ilivyo mfano wa Mwongozo juu haki za mali yakimaarifa ya Wasan wa Namibia ulioundwa na WIMSA, ambao una shughulikiamasuala kama vile matumizi ya picha za Wasan na unalazimu vyombo vyahabari na watafiti kuwaheshimu na kushauriana nao.

5.4 Hitimisho

Ulinzi wa utamaduni na lugha maalumu ya watu wa kiasili ni elementi muhimukwa maisha yao. Kunyima jamii mojawapo ya mambo haya bila shakakutatishia utambulisho wa jamii husika. Nchi zote zilizochunguzwazinadhamini umoja wa kitaifa, kwa njia ya wazi au isiyo ya wazi,kuliko uwingiwa utamaduni, licha ya wajibu wao wa kitaifa na kimataifa. Sera kama hizitaratibu zinasababisha usawashaji wa utamduni na lugha na kupotea kwadesturi, maarifa na tamaduni za waliowachache. Hii haina madhara tu kwaurithi wa kitaifa na uwingi wa lugha, bali pia inasababisha uharibifu wa makundiya kiasili yenyewe, kwani michepuo ya kilugha na kitamaduni ni sifa muhimu zautambulisho wao wa kipekee. Kuna mwelekeo zaidi wa kuuangalia usilishajiwa utamaduni wa kiasili kama wa sanaa jadi tu au wa kisherehe, aghalabu kwakusudi la kupata soko la utalii.

Katika Afrika yote, nafasi ya mamlaka ya lugha zilizorithiwa kutoka kwawakoloni Kiingereza na Kifaransa na Kiarabu kama lugha rasmi, inatishia lughazote za kiafrika na imesababisha lugha nyingi za kiasili kujifilia mbali au kuwakatika hayari ya kujifilia mbaliu. Kutotekelezwa kwa sheria, sera na dhmana zakikatiba pia ni jambo la kawaida katika mataifa mengi. Mwelekeo wa kijumlabarani Afrika ni wa kutamausha, kwani kiutendaji, serikali nyingi hazifanyijuhudi za kutosha kutekeleza hatua zinazolenga kulinda na kukuza lugha natamaduni za kiasili, jambo linalosababisha kupotea kwa jamii za kiasilizenyewe.

75

Page 92: First page ILO.fm

Hata hivyo, pana maendeleo kadhaa chanya, kama vile ulinzi wa kikatibawa haki za utamaduni (nchini Afrika kusini); ulinzi wa kisheria wa urithi wakitamaduni kama sehemu ya uhifadhi na usimamizi wa maumbile ya asili(Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Gabon), sera ya serikali kutaja ulinziwa utamaduni wa ‘Mbilikimo’ na kuzilinda sheria za kimila kupitia kwa uundajiwa sheria zinazoruhusu kushirikishwa kwa jamii katika kuzikagua nakuziandika sheria hizi, katika sera ya serikali ya Gabon kwa sheria hizi (nchiniNamibia). Kama daawa ya nchini Namibia baina ya Kapika na serikali yaNamibia, inavyodhihirisha, mchakato wa mahakama unaweza kutumiwakulinda utamaduni wa watu wa kiasili. Ijapokuwa asasi hizi hazifanyi kaziipasavyo (kwa sasa), baadhi yazo kama vile Haut Commissariat á l’Amazighité(Ubalozi wa Amazigh) na Taasisi ya kifalme kuhusu utamaduni wa Waamazigh(IRCAM) na Tume ya kukuza na kulinda haki za jamii za kitamaduni, kidini nalugha ya Afrika Kusini, pia zimeanzishwa.

76

Page 93: First page ILO.fm

6 Elimu

6.1 Utangulizi; Umuhimu wa elimu kwa watu wakiasili

Ufaafu wa elimu kwa maendeleo ya kibinafsi nay a jamii hauwezi kusisitizwakupita kiasili. Elimu ni muhimu kwa kujiendeleza kwa watu wa kiasili nakuwawezesha kupambana na kutawaliwa na matokeo ya kutawaliwa kamahuku. Ukweli kwamba elimu ni muhimu kwa maisha ya makundi ya kiasilihauwezi kukanika. Kwa hivyo haki ya kupata elimu kwa watu wa kiasili nimuhimu sana kuhusiana na elimu ya msingi na ya malezi kama tu ilivyomuhimu kwa elimu rasmi na isiyo rasmi na hata elimu kiufundi. Kwa hivyo,kupata elimu ya msingi kwa watoto na hasa motto msichana, kupata elimu yajuu ikiwemo elimu ya shule ya upili, ya ufundi na vyuo vilevile na mafunzo yakusoma na kuandika kwa watu wazima ni vijenzi muhimu vya haki za watu wakiasili kupata elimu.

Kuhusiana na haki za elimu kwa watu wa kiasili, chunguzi zinaendelakuonyesha viwango vya chini sana vya watoto wa kiasili wanaoingia shuleni(hasa motto msichana) na kiwango cha juu sana cha watoto wa kiasiliwanaoacha masomo. Haya ni kwa sababu ya mambo kama ukosefu wa shulekatika maeneo yaliyokaribu na jamii za kiasili, gharama za juu za elimuikilinganishwa na kiwango cha watu wa kiasili, ukosefu au kutokuwepo kwamiundomisingi maalumu na waliimu wakutosha, kubagua au kutohusishwakwa mahitaji ya kiasili katika mtalaa. Kijumla, pana ukosefu wa utoshelevukatika mifumo ya masomo ya kitaifa kwa mujibu wa kushughulikia mahitajimahususi, njia za maisha na utamaduni wa watu wa kiasili. Hizi pia ni baadhi yasababu za kutaka kuwepo na hatua maalum za kulinda haki za kielimu za watuwa kiasili. Utambuzi wa ukweli huu pia unaweza kuonekana katika vyombofulanifulani vya haki za kibinadamu vya kimataifa. Huku ikiwa kwamba sivyombo vyote kama hivi ni vya lazima kwa mataifa yaliyotathminiwa katikauchunguzi huu, vipengele muhimu katika vyombo kama hivi vinawezakuelezwa kama viwango vya kutathmini mikakati ya kitaifa katika muktadhahuu.

6.2 Viwango vya kimataifa

Viwango vya ulinzi wa haki za kupata elimu kwa ajili ya watu wa kiasilivinaweza kupatikana katika vyombo vya kimataifa vya haki za kibinadamu vyalazima na visivyo vya lazima. Vyombo kama hivi huenda zaidi ya hakikisho lajumla la kaki ya kupata elimu na kuakisi haki ya watu wa kiasili za kuwepo kwahatua maalum zinazohitajika kwa ulizni wa haki zao za kielimu. CRC, kwamfano ina taarifa muhimu sana kuhusu ulinzi wa haki za kielimu za watoto wakiasili. Zaidi ya kutambua haki ya jumla na ya usawa wa watoto wa kiasilikupata elimu ya lazima na ya bure ya msingi iliyo katika Kifungu cha 29, CRCinanakili haki ya watoto wa waliowachache au wa kiasili kufurahia elimumahususi kuhusu utamaduni wao, dini na lugha katika jamii pamoja na watuwengine baina ya makundi ya kiasili.253 Kulingana na Maoni ya Jumla ya CRCnambari 11, serikali zinapasa kuhakikisha kuna hatua maalum ili kuhakikishakwamba watoto wa kiasili wanafurahia haki yao ya kupata elimu kwa usawa nawatoto wengine wasio wa kiasili. Inashurutisha zaidi kwamba serikali ‘zitengeraslimali mahususi za kifedha, vifaa, na za kibinadamu ili kuweza kutekelezasera na mipango ambayo hususan inalenga kuimarisha upataji wa elimu kwa

253. Kifungu cha 28 na 30 vya CRC.

77

Page 94: First page ILO.fm

watu wa kiasili’. Kulingana na kifungu cha 27 cha Mkataba wa 169 wa ILO,mipango na huduma za elimu vyafaa kuendelezwa na kutekelezwa kwaushirikiano na watu wanaohusika ili kushughulikia mahitaji yao maalumu. Zaidiya hayo, lazima serikali zitambue haki ya watu wa kiasili kuanzisha taasisi nazao za kielimu, mradi taasisi hizi zinaafiki viwango vilivyowekwa na mamlakainayofaa kwa baada ya kushauriana na watu hawa.254

Mataifa vilevile yanafaa kuhakikisha kuwa shule zinafikiwa kwa urahisikatika maeneo wanakoishi watoto wa kiasili, na kipindi cha masomo lazimakizingatie na kuweza kurekebishwa kulingana na shughuli za kitamaduni,misimu ya kilimo na vipindi vya sherehe mbalimbali.

Kifungu cha 30 cha Mkataba huu kinaweka haki ya mototo wa kiasilikutumia lugha yake. Ili kuitekeleza haki hii, masomo yanayofanywa katikalugha ya motto husika ni muhimu. Kifungu cha 28 cha mkataba wa 169 wa ILOkinatilia mkazo kwamba watoto wa kiasili lazima wafunzwe kusoma nakuandika katika lugha yao wenyewe kando na kupewa nafasi ya kupata ufasahawa lugha rasmi za nchi yao.255 Walimu wa watoto wa kiasili kwa vyovyotevile wafaa kuteuliwa kutoka katika jamii za kiasili na kupewa uzaidizi namafunzo ya kutosha.

Mkataba wa 169 wa ILO unashughulikia swala la haki ya watoto wa kiasilikupata elimu kwa kuyashurutisha mataifa kufanya juhudi za kuhakikishakwamba watu wa kiasili wanafurahia haki ya jumla ya kupata elimu kwaviwango vyote sawa na wanajamii wengine kitaifa.256

Azimio la Umoja wa mataifa kuhusu haki za watu wa kiasili linatambua hakiya watu wa kiasili, hasa watoto wa kiasili, kuendelea na kila aina ya elimu kwaviwango vyote bila kubaguliwa.257 Kwa kutambua kuwa huenda serikali zisiwena raslimali za kutosha kutoa aina za elimu zinazohitajika na watu wa kiasili,Azimio hilo tena linathibitisha haki ya watu wa kiasili kuanzisha na kusimamiamifumo na taasisi za kielimu zao wenyewe kwa makusudi ya elimu mahususiinayoshughulikia mahitaji yao maalum, ikiwemo kufunza na kusoma katikalugha za kiasili. Kwa hivyo mataifa yanahitajika kushirikiana na makundi yakiasili ili kuhakikisha kwamba kwa kadiri iwezekanavyo, watu wa kiasiliwanapata elimu katika utamaduni na lugha yao, hata ikiwa nje ya jamiimahususi ya kiasili.258 Katika kutekeleza kifungu nambari 14 kinachohusianana elimu chini ya UNDRIP, kuna sharti kwamba lazina kuwepo na makini sanakuhusu mahitaji ya sekta mbalimbali za makundi ya kiasili.259 Kifungu cha15(1) pia kinaamuru kuwa heshima na uwingi wa tamaduni, desturi, historiana matarajio ya watu wa kiasili yanajitokeza kama ipasavyo katika elimu nataarifa za hadhara.

Vipengele katika vyombo hini vinawakilisha viwango vya kiulimwengu vyakulinda haki za watu wa kiasili kupata elimu. Ikumbukwe kwamba kwa pamoja,vipengele hivi vinalazimu kuwepo na hakikisho la kupata elimu ya jumla kwausawa kwenye kiwango cha kitaifa, kuyahusisha makundi ya watu wa kiasilikatika maamuzi yanayoathiri mikakati maalum inayowahusu na msaada kwawatu wa kiasili kuanzisha taasisi za kuhifadhi tamaduni, dini na lugha za kiasilikwa mujibu wa kanuni zilizowekwa.

254. Mkataba wa ILO Nambari 169, kifungu cha 27.255. Mkataba wa 169 wa IL, kifungu cha 28.256. Mkataba wa 169 wa IL, kifungu cha 26.257. Kifungu cha 14(2) cha Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watu wa kiasili(2007).258. Kifungu cha 14(1)(2) cha UNDRIP (2007).259. Kifungu cha 22 cha UNDRIP (2007).

78

Page 95: First page ILO.fm

Kwenye kiwango cha kimaeneo, baadhi ya vyombo vya mifumo ya kiafrikahaki za kibinadamu pia vinaweka viwango vya kulinda haki za watu wa kiasilikupata elimu. Haki ya jumla ya kupata elimu katika mifumo ya kiafrka ya hakiza kibinadamu imo kwenye Kifungu cha 17 cha Mkataba wa Afrika. Hukukikitaja haki ya watu wote kupata elimu, kifungu nambari 17 pia kinatambuahaki za watu kushiriki katika maisha ya kitamaduni ya jamii zao wenyewe. Hikikinafanya kazi kwa faida ya watu wa kiasili kwani kinalinda haki zao zakuelimishwa katika tamaduni zao mahususi. Zaidi ya haki hii ya jumla, Mkatabawa Afrika kuhusu Haki na Maslahi ya Mtoto (Mkataba wa Afrika kuhusuwatoto) una taarifa kuhusu haki za watoto kufurahia usawa wa kupata elimuya msingi ya bure na ya lazima.260 Vile vile mkataba wa Afrika Kuhusu watotounashurutisha mataifa kuchukua hatua za kushughulikia viwango vya wanafunziwanaoacha masomo na hatua maalum kwa ajili ya watoto wasiobahatika.261

Vipengele hivyo vya mwisho vinashughulikia hali ya watoto wa kiasili katikakufurahia kwao kwa haki ya kupata elimu. Zaidi ya hayo, hati kwa Mkataba waAfrika kuhusu haki za kibinadamu na haki za watu kuhusu Haki za Wanawakekatika Afrika (Itifaki ya wanawake wa Afrika) inayapa wajibu mataifawanachama kuchukua hatua za kuondoa ubaguzi dhidi ya wanawake kuhusianana kupata elimu na kushughulikia viwango vya chini vya wasichanawanaosajiliwa sajili na wanaobakia katika shule.262 Tena, hali za kipekee zawanawake wa kiasili, hasa motto msichana, zimeshughulikiwa na vipengelehivi. Ni kulingana na viwango hivi ndipo hatua za kulinda haki za watu wakiasili kupata elimu zinapaswa kukaguliwa.

6.3 Mielekeo ya kitaifa

Utoshelezi wa dhamana rasmi za kisheria

Kama ilivyotajwa awali, haki ya elimu imedhaminiwa kikamilifu katika vyombombalimbali vya kimataifa kuhusu haki za kibinadamu. Kwenye kiwango chakitaifa, hata hivyo, haki ya elimu haijadhaminiwa kwa usawa. Huku baadhi yamataifa yakidhamini haki za elimu katika katiba zao, mengine hutoa tu haki hiikatika vyombo vya sheria. Dhamana za kikatiba na kisheria za haki za elimumaranyingi huwa za jumla na hulinda haki za wananchi wote kupata elimu yamsingi. Dhamana ya chini kabisa aghalabu huwa ni ya elimu ya msingi ya burena ya lazima.263 Hata hivyo, pale ambapo katiba inatoa nafasi ya uteuzimaalum kwa ajili ya makundi ambayo awali hayakubahatika, nafasi ya kuchukuahatua za kisheria na kiutawala huundwa ili kuendeleza mikakati inayohusuwatu wa kiasili.264

260. Kifungu cha 11 cha mkataba wa Afrika kuhusu watoto.261. Kifungu cha 11(3)(d)(e) cha mkataba wa Afrika kuhusu watoto.262. Kifungu nambari12 cha Itifaki ya Wanawake wa Afrika.263. Uchunguzi kuhusu Ethiopia unaonyesha kuwa elimu katika kiwango chochote kile si ya

bure wala ya lazima nchini humo. Afrika kusini pia haionekani kuwa na kipengele chakikatiba kuhusu elimu ya msingi ya bure.

264. Kwa yale mataifa yanayotoa dhamana za kikatiba, baadhi yao yanatambua haki hii kamahaki inayoweza kutekelezeka chini ya seria ya haki za kibinadamu katika katiba ilihalimengine yanataja tu haki ya kupata elimu kama maelekezo ya kanuni isiyo ya kisheria yasera ya kitaifa. Matokeo yake ni kwamba katika yale mataifa ambapo haki ya kielimuinaonekana kama haki halali ya kikatib, pana nafasi kubwa ya marekebisho ya kimahakamaya hatua za kisheria na kiutawala kwa ajili ya utelezaji ingawa vipengele vya kisheria piavinatoa nafasi ya kutekelezaji wake kupitia mahakama. Lakini hata kukiwepo na udhaminihalali wa kikatiba kama huu, bado pana ishara za ukosefu wa nia ya kisiasa kutimiza haki zakupata elimu.

79

Page 96: First page ILO.fm

Jamuhuri ya Afrika ya Kati ilikubali Mpango wa Kitaifa wa Elimu kwa watuwote (‘Plan National d’Action de l’Education Pour Tous’ (PNA-EPT)) ili kuongezakiwango cha upataji wa elimu wa ‘makundi ya wachache (‘Mbilikimo’,Mbororo, na watoto walemavu, na watoto wanaoishi katika maeneo yauchimbaji magodi n.k) kati ya umri wa miaka kumi na mitano kutoka asilimia10 hadi 80.265

Ukosefu wa makini ya kutosha kuhusu mahitaji maalum ya kielimu ya watoto wa kiasili

Hitaji la kuwepo na mikakati maalumu za kukuza haki za watu wa kiasilikupata elimu linazuka kwa sababu vipengele vya jumla kuhusu haki za haki zaelimu vinashindwa kushughulikia kikamilifu mahitaji ya watu wa kiasili. Ukaguziwa mataifa yaliyochunguzwa katika utafiti huu unaonyesha upungufu wadhamana hizi za jumla za haki za kupata elimu. Hivyo, kuna masuala yaviwango vya chini sana vya kujua kusoma na kuandika baina ya makundi yakiasili, viwango vya chini vya wale wanaojisajili shuleni, viwango vya juu vyawale wanaoacha masomo na mikakati isiyotosha ya kushughulikia mahitajihalisi ya watu wa kiasili. Haya ni dhihirisho la matatizo ya kina sana yaupembezwaji, chuki na umasikini. Familia za kiasili huenda zisiweze kulipa hatakaro ya chini kabisa ya shule au hata kumudu gharama ndogo ndogo za bidhaakama vile vifaa vya kuandikia au nguo. Mnamo Januari 2006, serikali yaBotswana ilianzisha ulipaji wa karo ya shule.266 Kwa kuwa watu wa kiasiliwako chini kwenye tabaka la kiuchumi kuna uwezekano kwamba viwango vyakutojua kusoma na kuandika baina ya Wasan vitaendelea kupanda hata zaidi.

Vilevile, mifumo ya elimu ya mataifa yaliyokaguliwa haizingatii kwambawengi wa watu wa kiasili ni wafugaji na wawindaji-wakusanyaji, na wanajamiiwa jamii za wahamahamaji na za makaazi ya muda. Kwa kutotoa sababu zautata unaotokana na upekee huu, serikali zinazuia uwezekano wa waokuendelea kusoma. Kushindwa kurekebisha mfumo wa elimu ili luakisi upekeehuu kunafanya iwe vigumu kwa makundi haya kuoanisha njia zao za kujikimuna mahitaji ya elimu inayofaa. Baadhi ya madai na vipengele vinavyorejelewawakati wa kushughulikia hususan haki za elimu vinaweza kutajwa hapa:

265. Gouvernement de la République Centrafricaine, Plan National d’Action de l’Education Pour Tous(PNA-EPT, portal.unesco.org/education/en/file_download.php/08809d2e13a118ddc8df9f6113081c3bPNA-EPT-RCA.doc – (iliangaliwa 30 Novemba 2008).

266. Ripoti ya CRC ya Botswana uk. 275.

Haki ya kupata elimu ni jambo ambalo siku zote limo katika katiba zakitaifa, lakini ni nadra sana kupata haki ya kupata elimu ambayo inahusikana haki ya mtu kuelimishwa katika lugha yake ya waliowachache aukufunzwa kwa kutumia mtaala unaofungamana na mila za tamaduni za mtuhusika. Mojawapo wa mfano wa nadra sana wa hali hii ni kifungu cha 32cha katiba ya Afrika Kusini, ambayo inamhakikishia ‘kila mtu ... haki yakufundishwa katika lugha anayoichagua yeye pale inapohalisi’. Kwakiwango cha utendaji, Mradi wa Schmidtsdrift San Combined school katikaMkoa wa juba ya Kaskazini (Northern Cape province) nchini AfrikaKusini, ambao ulianzisha mipango badala ya elimu ili kuwarahisishiamasomo watoto wa kiasili, ni mfano mfano wa kitendo bora zaidi japo nimradi finyu. Kuanzishwa kwa Mpango changamano wa kitaifa wa lishe naMtaala katika shule za msingi mwaka 2005 kulilenga kurekebisha tofautizilizopo katika kupata elimu, pia ni mpango muhimu wa hatua maalum.

80

Page 97: First page ILO.fm

umuhimu wa elimu za malezi, mafunzo ya lugha mbili na upatanifu wa ratiba zadarasani na mfuatano wiano wa jamii kama unavyoamuliwa na sababu zakimisimu.

Mitalaa ya shule pia haina makala ya kuhamasisha jamii pana kuhusu masulaya watu wa kiasili wala haina vipengele vya utamaduni na mifumu ya maarifa yawatu wa kiasili. Mtalaa wa elimu wa Botswana ni mfano mzuri, kwaniumelengwa kwenye kuwastaarabisha watoto wasio Watswana.

Ikishirikiana na mashirika ya umma kama vile Children-Norway, serikali yaUganda ilianzasha mpango wa Elimu ya Maingi Badala kwa Wakaramoja(ABEK). ABEK imeundwa kutoa mtalaa na mbinu zinazofaa maisha yakuhamahama. Pia inahakikisha kuwa kuna kushirikishwa kwa jamii katika elimuya watoto wao. Wafawidhi wanateuliwa kutoka kwa wanajamii, hasa wazeewa jamii. Mtalaa unalenga masomo ambayo yanayohusika moja kwa moja nanjia za maisha kama vile uzalishaji wa mimea, mifugo, afya, amani na usalama.

Mpango wa elimu badala wa nchini Ethiopia ulnaolenga jamii za wafugajinchini humo ni kitendo chanya ambachohmiza makundi ambayo bila yachoyangekuwa katika hali ngumu, kujiunga na shule. Aidha Ethiopia ina mpangowa maendeleo ya sekta ya elimu ulioanzishwa mwaka wa 1997, na kishakurekebishwa mwaka wa 2005 kwa lengo la kuzidisha upataji, ubora na usawakatika elimu kwa wasichana na watoto kutoka katika maeneo ya mashambani.Watoto wa kiasili katika sehemu za mashambani na watoto wasichana wakiasili wanaweza kunufaika kutokana na mpango huu. Hata hivyo, utekelezawake wenyewe umeanza juzijuzi tu na mpango huu umetumika kwenyekiwango cha mradi wa kimajaribio katika sehemu chache sana.

Lugha za kiasili zimepuuzwa

Watoto wa kiasili mara nyingi wamepata ugumu kufuatilia masomo ambayoyanafunzwa katika lugha zingine mbali na lugha zao za kwanza, jambo

Nchini Chad, elimu ni wajibu wa pamoja baina ya serikali pamoja namamlaka za mitaa. Kwa sasa hata hivyo, si taasisi zote za mashinanizilizohusishwa katika katiba na sheria zingine za ugatuzi zisitawishwa. Dhanaya ‘shule za jamii’ ilizalika kutokana na kuonekana kushindwa kwa serikalikutoa huduma zote za kielimu. Shule hizi zinaendeshwa na jamii, kwamsaada wa serikali. Ijapokuwa hazihusika hasa hasa na watu wa kiasili, shuleza kijamii ni vyombo muhimu ambavyo vinaweza kuwaathiri kwa njiachanya. Katika shule hizi upekee wa jamii fulani unatiliwa maanani, kwamfano, kwa kusaidia mtaala rasmi kwa masuala fulani yenye manufaa kwawatu wa jamii hiyo husika. Serikali ya Chad ilipitisha sheria ya kuanzishaShirika la Kuendeleza Juhudi za jamii katika elimu (Agence pour des initiativescommunautaires en education (APIDEC) ili kuthibiti ruzuku inayotolewa kwamiungano ya wazazi, hivyo kuwawezesha kuteua waalimu katika jamii hiyo.Vile vile Chad imeanzisha shule za wahamahamaji, kwa msaada wa UNICEFna GTZ. Hizi jamii za wahamahamaji ndizo zinasimamia shule hizi kwakusaidiwa na serikali. Lengo la shule hizi linaelezwa kama ‘elimu pamoja namasuala mengineyo ya manufaa kwa watoto wa jamii za kuhamahama’. Kwaupande wa maudhui ya elimu, sheria ya mwaka wa 2006 inahusisha ukuzajiwa stahamala na heshima kwa tamadnuni zingine kama shabaha ya mfumowa elimu.

81

Page 98: First page ILO.fm

linalowafanya kuchukiwa na waalimu na wanafunzi wenzao. Nchini Botswana,pana kumbukumbu ya himizo la serikali la kutumia kiingereza na Kisetswanapekee yake kama lugha za kufundishia katika shule za msingi. Ingawa kunamarekebisho ya sera yanayopendekeza matumizi ya lugha ya mama katikamaeneo ambako lugha hii inatumika kwa wingi, bado yanaleta ugumu kwawatoto wa kiasili ikiwa masomo ya kwanza yanafanywa katika lugha nyinginetofauti. Kitendo cha serikali ya Misri ya kukataza maandishi katika lughazingine mbali na Kiarabu pia ni kizingiti kwa masomo ya watoto wa kiasili.Mfano mwingi wa kitendo kisichofaa ni kufungwa kwa shule za kibinafsi 42mnamo mwaka wa 2006 nchini Aljeria kwa kutofuata mtalaa wa shule wenyemwelekeo wa Kiarabu. Vitendo hivi ni hasi hivi kwamba vinajenga vikwazo vyakiakili na kilugha kwa watu wa kiasili wanaotaka kusoma. Huku ikiwa kwambaKamati ya CERD ilitambua maendeleo yanayoruhusu ufundishaji wa Kitamazikatika shule na vyuo vikuu,267 Kamati ya CESCR inapendekeza kuwa serikaliiweke mipango ya kufunza kusoma na kuandika katika lugha ya Kitamazi nakuiuliza serikali kutoa masomo ya bure katika Kitamazi katika viwangovyote.268

Katika eneo la Ngorongoro nchini Tanzania, kuna hitilafu baina ya idhiniiliyotolewa kwa ujenzi wa mahoteli ya anasa katika yaliyomuhimu kiekolojia,na kukataa kuruhusu ujenzi wa shule katika eneo halo halo.

Ingawa Kifaransa na Kiarabu ni lugha za kufundishia katika shule za nchiniChad, ‘lugha za kitaifa’ huenda zisitumiwe.

Kutozingatia elimu ya watu wazima baina ya watu wa kiasili

Elimu ya kimsingi ni muhimu ili kuelewa ulmwengu wa sasa na kuwasiliana kwanjia bora na sehemu zingine za ulimwengu na kufikia maisha bora nakupatanisha uhalisia wa masiha mbalimbali ambamo wamejikita. Elimu ya watuwazima baina ya watu wa kiasili ni ya kiwango cha chini. Licha ya hitaji hilikubwa, pana ushahidi mchache sana wa kuwepo kwa mipango serikaliinayolenga kuboresha elimu baina ya watu wazima wa kiasili.

267. UN Doc CERD/C/304/Add.33, tarehe 18 Septemba 1997, aya ya 8.268. Kamati ya CESCR UN Doc E/C.12/MAR/CO/3, 4 Septemba 2006, aya ya 58.

Kuhusiana na sera ya serikali ya Namibia ya kutoa elimu kwa lugha yakwanza katika darasa la kwanza hadi la tatu, Mradi wa Shule wa kijiji chaNyae Nyae (almaarufu VSP), ambao ni ufungamanishaji wa elimu ya kimila,inayolingana na utamaduni kwa lugha ya mama na elimu rasmi, imeletautofauti katika maisha ya watu wa kiasili. Mradi huu ilianzishwa kwaushirikiano wa mashirika yasiyo ya kiserikali nchini humo na Wizara yazamani ya Elimu na Utamaduni mapema ya miaka ya 1990 kwa kuitikiaukosefu wa kushiriki kwa watoto wa Kiju’hoansi katika shule za serikali zaMashariki mwa Wilaya ya Tsumkwe. Aidha, shule ya msingi ya Gquainainahimiza kuwepo kwa uwingi wa kitamaduni na inaajiri walimuwanaozungumza lugha ya Ju’hoansi na kuwapa masomo wanafunzi waKiju’hoansi kwa lugha ya kwanza katika darasa la kwanza.

82

Page 99: First page ILO.fm

Upungufu wa mikakati maalum

Baadhi ya mataifa haina miradi mahususi inayolenga hatua maalum (uteuzimaalum). Hata hivyo kupigwa marufuku kwa ubaguzi katika elimu kunamatokeo chanya kwa elimu ya kiasili. Katika kategoria hii, inawezekanakubainisha mfumo wa kisheria nchini Niger unaotambua haki ya makundi yotekutumia lugha zao wenyewe, unahimiza kuheshimu kila lugha na kupinga serana hatua zinazojikita kwenye misingi ya kieneo, kikabila, kidini au ya migaomingine. Katika hali zingine, kama vile nchini Kongo, serikali inahimiza auangalau inaruhusu washiriki wa serikali mbalimbali na wasio wa kiserikalikuingilia kati ili kukuza hatua za utuzi maalum. Katika sehemu hii baadhi yamataifa kama vile Chad yanashirikiana na washirika wasio wa kiserikali kutoamipango ya uteuzi maalum.

Mpango wa elimu kwa wahamahamaji wa nchini Nigeria, ulioanzishwa kwaamei ya kijeshi manamo mwaka wa 1989, unaweza kuwa kama mfano wa Taifakuchukua ‘hatua maalum’ kwa ajili ya haki ya watoto wa kiasili kupata elimu.Tume ya kitaifa ya elimu kwa wahamahamaji iliundwa kwa Amri ya 41 yamwaka wa 1989, ikiwa na wajibu wa kuunda sera za masomo yawahamahamaji nchini Nigeria na halafu utekelezwaji wa Mpango wa elimu kwawahamahamaji (NEP). Hizi ni pamoja na madarasa ya kukunjika wakati wakuhama na vipindi vya redio na televisheni kwa ajili ya watu wa wanaoishimaisha ya kuhamahama nchini Nigeria. Hata hivyo, kuendelea kwa mpangohuu kunakatizwa na ukosefu wa miundomisingi, walimu wasiohitimu namalipo duni.

6.4 Hitimisho

Licha ya matumizi ya katiba na sheria ya kimataifa, elimu kwa watoto wa kiasilikiutendaji si ya bure wala si ya lazima. Uchunguzi wa shughuli za kitaifa zakikatiba, kisheria na kiutawala unaonyesha kuwa, katika mataifa mengidhamana za kikatiba za haki ya kielimu hazizidi dhamana za kijumla za kupataelimu ya msingi. Tokeo moja la ukweli huu ni kwamba viwango vya elimu yawatu wazima vimebaki chini. Hata katika sehemu ya elimu muhimu ya msingi,dhamana za jumla za kikatiba na sheria hazijatosha kushughulikia mahitaji nachangamoto maalum za watu wa kiasili. Kwa hivyo, ni katika yale mataifaambako kuna hatua maalum ndiko watu wa kiasili wamekuwa na nafasi kubwakufurahia haki ya kupata elimu. Hali hii inabatili faida ambazo hakikisho lakupata elimu ya msingi lingeleta. Ni wazi pia kwamba wakati kuna ukosefu waraslimali za kutosha, mataifa yanaweza kuungana na washiriki wasio wakiserikali kuendeleza haki ya watu wa kiasili kupata elimu. Kwa hivyo nimuhimu kuwa mataifa yaendeleze nia ya kisiasa kwa ajili ya watu wa kiasili.

Kwa mujibu wa hitimisho lililofikiwa kutokana uchunguzi wa sheria, serana shughuli za kitaifa, inafaa kupendekezwa kuwa mataifa yahimizwe kutumiasheria na sera zilizo na shabaha zilizowazi ili kukuza haki ya elimu kwa watuwa kiasili. Aidha inapendekezwa kuwa mataifa yaanzishe miradi ya kukuzamatumizi ya lugha za kiasili kama nyezo za kufunzia katika kiwango cha shuleya msingi, pamoja na lugha rasmi.

Kwa kipindi kifupi, mataifa yafaa sio tu kuhakikisha kuwa haki ya elimu yamsingi ya lazima na ya lazima imetiwa katika katina na sheria, lakini pia hakihiyo inafanywa kuwa uhalisia kwa watoto wote, wakiwemo watoto wa kiasili.Kwenye kiwango ambapo mahitaji maalum ya hawa watoto yanahitaji hatuamaalum, lazima hatua hizo zitekelezwe na kutafitiwa. Hata ingawa watoto wa

83

Page 100: First page ILO.fm

kiasili wanafaa kufaidika kwa kiwango sawa kama watoto wengime kutokanana haki ya kupata elimu, elimu yao yafaa kuelekezwa kwenye kudumisha nakukuza lugha, utamaduni na namna zao za maisha.

84

Page 101: First page ILO.fm

7 Ardhi, aliasili na mazingira

7.1 Utangulizi: Viwango vya kimataifa

Kwa watu wa kiasili, ardhi ni muhimu zaidi yaidi ya kuwa mali ya kiuchumi.269

Haiwapi tu njia ya kujikimu kiuchumi lakini pia ni msingi wa utambulishi waowa kitamaduni na maslahi yao ya kiroho na kijamii. Kwa kuwa kuishi kwaokama watu kumefungamana sana ardhi ya mababu zao, kunyag’anywa ardhiwanayoimiliki au kuharibu mazingira yao ya asili kupitia kwa shughuli za‘maendeleo’ kama vile uchimbaji madini, ukataji wa miti na ujengaji wamabwawa, au kwa kupitia uanzishaji wa mbuga za kitaifa na maeneoyaliyohifadhiwa katika ardhi yao, kuna madhara makubwa sana maisha yao.Katika nchi nyingi za kiafrika, sheria za za kikoloni zilileta dhana mpya zaumiliki wa ardhi, ambazo nyingi yazo hazikujulikana na watu wa kiasili vilevilena Waafrika wengi. Baadhi ya sheria hizi zilileta dhana ya umiliki wa kibinafsi,na zikapuuza sheria za kimila. Dhana za umiliki wa kibinafsi zilitumika vilevilekatika sehemu nyingi ambapo sheria ya kimila ilikuwa imedumishwa kwa kiasifulani. Baada ya uhuru watu wa kiasili wangali wanakumbwa na changamotonyingi kuhusianan na haki zao za ardhi na maliasili. Vyombo vya sheria vyakimataifa na kimaeneo vinatoa mfumo mpana wa kulinda haki za ardhi za watuwa kiasili na haki zao za maliasili kuhusiana na ardhi zao.

Kifungu cha 26(i) cha UNDRIP kinasema kuwa watu wa kiasili wana hakiya kumiliki ardhi, maeneo na raslimali ambazo wamemiliki, wamekalia au hatakutumia kitamaduni. Zaidi ya hayo kinataja haki za watu wa kiasili kutawala,kuendeleza au kutumia ardhi na kushurutisha mataifa kutoa utambuzi wakisheria kwa mashamba, maeneo na raslimali kama hizi kwa kuheshimu mila,tamaduni na mifumo ya umiliki wa ardhi ya watu wa kiasili.270 Kifungu cha 27kinashurutisha mataifa kuanzisha taratibu za kutambua mila na mifumo yaumiliki wa ardhi kwa kushirikisha watu wa kiasili. Kifungu cha 28kinashughulikia suala la kufidia ardhi ambazo watu wa kiasiliwamenyang’anywa. Umuhimu wa pamoja wa vingu vya 26, 27, na 28 haupokatika kuzitambua haki zao za ardhi, maeneo na maliasili lakini pia katikakulinda na kuzitambua tamaduni, mila na mifumo ya matumizi ya Ardhi ya watuwa kiasili.

Mktaba wa ILO wa 169 unatambua haki ya watu wa kiasili kumiliki ardhiwanayoikalia au hata kuitumia,271 na vifungu vinginevyo kadhaa vinalazimumataifa kuheshimu mila, sheria ya kimila na asasi za watu wa kiasili272 navinabashiri hatua za kukuza haki, kati ya nyinginezo, zakijamii na kiuchumi zawatu wa kiasili pamoja na heshima kamili kwa mila na tamaduni zao.273 Hili nijambo la maana kwani haki za ardhi zilizotambulika katika nchi nyingizilizopata uhuru mara nyingi hazitambui tamaduni, mila na dhana za umiliki.

269. Tazama ripoti ya JR Martinez Cobo, Katibu maalum wa Tume ndogo inayohusika naKuzuia Ubaguzi na kuwalinda waliowachache: Study on the Problem of Discrimination AgainstIndigenous Populations. UN Doc E/CN.4/Sub.2/1986/7/Add.1, aya ya 196 na 197.

270. Kifungu cha 26(2) kinayataka mataifa kutanbua na kuzilinda ardhi, maeneo na raslimali hizikwa kuheshimu mila, sesturi na mifumo yao ya kumiliki ardhi kama inavyopasa. Vifun guvya 27 na 28vinalenga kutoa mikakati ya kuamua madai ya ardhi na kurejeshea watu ardhizao. Kifungu cha 28 kinawapa watu wa kiasili haki ya kurekebisha kwa njia ya kurejeshewana kufidiwa ardhi katika hali ambapo ardhi, maeneo, na raslimali za watu wa kiasilizimechukuliwa, kutumiwa au kutwaliwa bila wao kukubali. Kwanza.

271. Kifungu cha 14.272. Kifungu cha 8.273. Kifungu cha 2(2)(b).

85

Page 102: First page ILO.fm

Kifungu cha 13 cha mkataba wa 169 wa ILO kinatambua dhana ya upamojaya uhusiano wa watu wa kiasili kuhusiana na ardhi yao. Dhana ardhi inahusishaardhi ambayo jamii au watu fulani wanatumia na kuitunza kwa pamoja. Piainahusisha ardhi inayotumiwa na kumilikiwa kibinafsi. Ardhi pia inawezakugawanywa baina ya jamii au hata watu mbalimbali. Hii hasa ndiyo hali ilivyokwa ardhi ya malisho ya mifugo, uwindaji na maeneo ya ukusanyaji na misitu.Hali ya watu wa kuhamahama na wakulima wa kubadilisha mashamba yafaakuzingatiwa, kulingana na kifungu cha 14 cha Mkataba huu. Vile vile, UNDRIPkatika Dibaji yake inatambua haki ya pamoja ya watu wa kiasili na vilevilekatika kifungu cha 1.

Athari ya pamoja ya vifuungu vya nambari 14 (haki ya kumiliki mali) na 21(haki ya watu kuwa huru kuuza mali na raslimali yao) vya ACHPR, nikudhamini aina zote za mali, ikiwemo ardhi, na kutoa njia ambazo mali hayoyanaweza kurejeshwa na fidia kulipwa wakati ambapo haki hiyo inaingiliwa.Huku ikiwa kwamba kifungu cha 14 hakirejeli hususan haki ya kumiliki malikama haki ya pamoja, vifungu vya ACHPR vinatia wajibu kwa serikalikudhamini haki za pamoja za kumiliki mali. Pia, kifungu cha 21 kinalinda haki zapamoja kwa maliasili. Aidha, kifungu cha 22 cha ACHPR, kina haki za watukujuendeleza, ambayo aghalabu imefungamanishwa na haki za ardhi katikamijadala ya kimataifa na kitaifa.

Maoni ya Jumla ya CERD nambari 23 kuhusu watu wa kiasili kinaombamataifa kuwapa watu wa kiasili hali zinazowawezesha kupata maendeleo yakudumu ya kiuchumi na kijamii yanayopatana na sifa za utamaduni wao, vilevile kutambua na kulinda haki za watu wa kiasili za kumiliki, kuendeleza,kutawala na kutumia ardhi, maeneo na raslimali za kijamii.274 Zaidi ya hayo,kwenye kiwango cha kimataifa UNDRIP inatambua na kuthibitisha kuwa watuwa kiasili bila kubaguliwa wana haki zote za kibinadamu zinazotambuliwakatika sheria ya kimataifa na kwamba watu wa kiasili wana haki za pamojaambazo ni za lazima kwa maisha yao, maslahi na maendeleo ya pamoja kamawatu.275 Aidha, katika vifungu juu ya haki za ardhi za watu wa kiasili, UNDRIPinatumia istilahi ‘watu’, ikidhihirisha wazi kwamba watu wa kiasili wana haki zapamoja za ardhi. maoni ya Jumla nambari 23 ya Tume ya Kutetea haki zaKibinadamu inaweka kiungo dhahiri baina ya maeneo na maliasili na haki yamtu kufurahia utamaduni wake.

Kifungu nambari 15(1) cha Mkataba wa 169 wa ILO kilinuiwa kulinda hakiza watu wa kiasili juu maliasili kuhusiana na mashamba yao, ikiwemo haki yawatu hawa kushiriki katika matumizi, usimamizi na uhifadhi wa raslimali hizi.Katika hali ambapo taifa libakia na umiliki wa madini au raslimali za chini yaardhi au haki juu ya raslimali nyinginezo kuhusiana na ardhi, serikali zinapasakuweka au kudumisha taratibu ambazo kupitia kwazo zinaweza kushauriana nawatu hawa, kwa lengo la kuthibitisha iwapo mahitaji yao yatabaguliwa na kwakiwango kipi, kabla ya kutekeleza au kuruhusu mipango yoyote ya utafiti auutumizi wa raslimali kama hizi kuhusiana na ardhi zao. Watu husika wanapasa,pale panapowezekana, kushiriki katika faida za shughuli kama hizi, na lazimawapate fidia ya haki kwa madhara yoyote wanayoweza kupata kutokana nashughuli kama hizi.

274. Kamaiti kuhusu Uondoaji wa ubaguzi wa kikabila, General Recommendation No. 23:Indigenous Peoples: 18/08/97, kur 4(c) na 5, mtawalia.

275. Dibaji na kifungu cha 7.

86

Page 103: First page ILO.fm

7.2 Umilikaji, utwaaji, haki za matumizi na masualaya masharti ya Umiliki wa ardhi

Mfumo wa kijumla

Kuja kwa ukoloni barani Afrika aghalabu kulikuwa na maana ya unyang’anywajimkubwa wa ardhi za watu wa kiasili, vile vile na kuanzishwa kwa taratibumpya kuhusiana na umiliki na utumizi wa ardhi ambazo hata zinaathiri sera nasheria za sasa. Katika baadhi ya nchi za Afrika, utaratibu wa umiliki wa ardhiuliowekwa wakati wa ukoloni umebakia vivyo hivyo au kuathtiri utaratibu waumiliki wa ardhi wa baada ya uhuru. Jambo hili limezua matatizo kadhaa baadaya uhuru. Katika hali nyingi, sheria na taratibu za kumiliki wa ardhi ambazokimsingi zilikuwa ni sheria za kimila za pamoja zilibadilishwa na dhana yakibinafsi kabisa ya kumiliki kutwaa ardhi, au kwa kweli, ardhi ambazo awalizilichukuliwa kuwa za watu wa kiasili chini ya sheria ya kimila, ziligeuka kuwaardhi zilizolindwa na serikali (za umma au kibinafsi) au zinazomilikiwa na watuwa kibinafsi, hali ambayo aghalabu inapelekea kupoteza haki ya utumizi kwajamii ambazo awali zilimiki au kutumia ardhi hiyo.

Elementi iliyotiwa katika taratibu za haki za ardhi katika nchi kadhaawakati wa ukoloni na baada ya ukoloni ni ile ya ardhi za amana. Hii haswa nihali ilivyo katika nchi zilizokuwa chini ya ukoloni wa Uingereza, ambapo baadaya uhuru, serikali ilibadilisha utawala wa kifalme kama mdhamini. Katikamifumo kadhaa ya sheria za kuitaifa, ambapo mashamba ya amana ni sehemuya utaratimu wa haki za ardhi, zile ardhi zinazomilikiwa kwa amana zinachukuasehemu wanakoishi watu wa kiasili, hii ikiwa na maana kuwa uwezekanao wawatu wa kiasili kupata umiliki wa ardhi hizi ni mdogo sana. Mashamabayanayomilikiwa kwa amana hazidumu, na zimo katika hatari ya madiliko nasibuya hadhi na hata kutwaliwa kutoka kwa wenye ardhi hizo.

Nchini Botswana kwa mfano, sera ya jumla ya kikoloni ilikuwa ni kuhimizaumiliki wa ardhi kibinafsi na kugeuza mashamba kuwa ya kibiashara.276

Matumizi ya ardhi kitamaduni na kijamii yalichukuliwa kuwa ya uharibifu nayaliyokinyume na maendeleo ya kiuchumi.277 Mfumo mpya uligawanya ardhikatika aina tatu, yaani, ardhi ya kikabila, ardhi ya kifalme (ardhi ya serikalibaada ya ukoloni) na ardhi huria. Ardhi ya kikabila ilikuwa ya kabila zima nailiwekwa kwa amana na machifu. Wakati wa kupata uhuru, tume ya ardhiilichukua nafasi ya machifu kuhusiana na ardhi za kikabila, iliyokuwaimewekewa dhamana kwa makabila na kupeanwa na kugawanywa na Tume zaArdhi278 kwa ajili ya makaazi, ukulima, malisho ya mifugo au biashara.279

Tume za mashamba kitaifa, ni mashirika huru. Hata hivyo, kuna ripoti nyingikutoka kwa watu wa kiasili kuwa maombi yao ya kutaka kugawiwa ardhihayakubaliwi au kwamba michkato ya kutuma maombi inajikokota kuliko ileya kabila la Watswana wa eneo hilo.280

Nchini Kenya, tangu siku za ukoloni sheria zimesababisha watu wa kiasilikunyang’anywa ardhi zao za kitamaduni. Sheria kifalme ya ardhi ya mwaka wa1915281 na sheria na sera za kikoloni za baadaye kuhusu ardhi zililenga

276. I Schapera (1943) Native Land Tenure in Bechuanaland Protectorate.277. JC Smuts (1930) Africa and Some World Problems 82.278. Sheria ya ardhi ya kikabila na sheria ya ardhi ya serikali.279. Sheria ya ardhi ya kikabila na sheria ya ardhi ya serikali.280. Kituo cha haki za kibinadamu cha Botswana ‘Haki za Ardhi’ <http://

www.ditshwanelo.org.be/land_rights> (ilifunguliwa mnamo 30 Novemba 2008).281. Sheria ya ardhi ya kifalme ya mwaka wa 915 sehemu ya 5; angalia Ghai YP na Mac Auslan

JPWB, Public Law and Political Change in Kenya (1970) 28.

87

Page 104: First page ILO.fm

kuwanyang’anya waafrika uridhi wao na kuwapembeza zaidi.282 Baadaye’kupitia kwa Mpango wa RJM Swynnerton mwaka wa 1955, mamlaka zakikoloni ziliamua kufanya umiliki wa ardhi wa ardhi kuwa wa kibinafsi. Sera hiiilitwaliwa na kuwekwa na taifa huru la Kenya.283 Katiba ya sasa ya Kenyainashughulikia ardhi kama mali na kama ardhi za amana. Ardhi kama maliimelindwa na sehemu ya 75 ya katiba. sura ya 9 ya katiba ya Kenya inahusuardhi za amana. Sura hii ina vipengele kuhusu ardhi za amana zinazosimamiwana Mabaraza ya Miji, ambayo usimamizi wake wa ardhi za amana unathibitijwana Sheria ya ardhi ya amana.284 Hata hivyo kutia usimamizi na uendeshaji waardhi kama hizi mikononi mwa serikali za mitaa wakati mwingi kumechangiakutwaliwa kwa ardhi hizi na watu binafsi au mashirika. Sheria ya ardhizilizosajiliwa ilitakasa mfumo wa umiliki wa ardhi wa kibinafsi nchini Kenya nawala haitumiwi kwa ardhi ya kijamii.285 Kwa hivyo ardhi za wafugaji na ardhizingine za kiasili za pamoja hazijalindwa na ulinzi wa aina hii.

Mwelekeo chanya ni kwamba serikali imebuni rasimu ya Sera ya kitaifakuhusu ardhi, ilyochapishwa Desemba 2005,286 inayokusudia kushughulikiabaadhi ya masuala nyeti kuhusu haki za ardhi nchini Keny, kama vile kupataardhi, matumizi ya ardhi, umiliki, mipango, kufidia dhuluma za kihistoria,uharibifu wa mazingira, mizozo, kuenea ovyoovyo kwa maakazi duni ya mijini,mifumo ya kisheria iliyopitwa na wakati, mifumo ya taasisi na utunzaji wahabari. Sera hii ni muhimu kwa watu wa kiasili kwani inatambua haki na ainaza umiliki wa ardhi za jamii za wafugaji na makundi mengineyaliyopembezwa.287 Hata hivo, sera hii imetiwa lawama kwa kutoshughulikiakikamilifu suala la haki za pamoja za kumiliki ardhi.288 kwa mujibu wa ripoti yaIWGIA ya mwaka wa 2007 ‘huku baadhi ya sehemu kwenye rasimu (Sera yakitaifa kuhusu ardhi) ni nyeti sana kuhusiana na masuala ya ardhi na raslimali(masuala yanayohusiana moja kwa moja na maisha ya watu wa kiasili), inakosakutambua haki. Mnamo mwaka wa 2008, Kamati ya Umoja wa Mtaifa kuhusuhaki za kKiuchumi, Kijamii na Kitamaduni iligundua kuwa ‘kuwepo kwa tofautikatika kufurahia haki za kiuchumi, kijamii na kitamaduni, ikiwemo haki yakupata ardhi, kumesababisha mivutano baina ya makabila na fujo za baada yauchaguzi ambapo takriban watu 1,500 waliuawa mapema mwaka wa 2008.289

kamati inapendekeza kuwa, kati ya mambo mengineyo, Kenya ianzishemashirika ya ukaguzi wa ardhi kuchunguza ugavi wa kibaguzi wa ardhi nakutekeleza mapendekezo ya Tume ya uchunguzi ya Ndung’u kuhusu ugaviharamu/ usiosawa wa ardhi ya umma.290

282. Angalia k.m sheria ya amana ya ardhi za asili ya 1930, sheria ya amana ya ardhi ya asili(yamarekebisho) ya mwaka wa 1934; sheria (ya marekebisho)ya Kifalme kuhusu ardhi yamwaka wa 1938; sheria ya ardhi za asili ya mwaka wa 1938; Amri (ya maeneo ya wenyeji)*Kenya (maeneo ya wenyeji) Order in Council 1939 na Kenya (nyanda za juu) Order inCouncil.*

283. HWO Ogendo Tenants of the Crown, Evolution of the Agrarian Law and Institutions in Kenya,Acts 1991 70.

284. Sheria ya ardhi za Amana (kifungu cha 288) Sheria za kenya.285. SC Wanjala ‘Land ownership and use in Kenya: past present and future’ in SC Wanjala

(ed) Essays on land law, the reform debate in Kenya Faculty of Law, University of Nairobi(2000) 34; See also SC Wanjala ‘Problems of land registration and titling in Kenya’ in SCWanjala (ed) Essays on land law 97.

286. Rasimu ya Sera ya kuitaifa ya Kenya kuhusu ardhi ya mwaka 2005.287. Kama hapo juu.288. Tazama IWGIA (2007) The Indigenous World 470.289. Tazama maoni ya mwisho ya Kamati kuhusu haki za Kiuchumi, Kijamii na Kitamaduni

kuhusu Ripoti ya awali ya Kenya kuhusu haki za ECOSOC katika kikao cha 41 mjiniGeneva, 3-21 Novemba 2008, 2008, UN Doc E/C.12/KEN/CO/1 aya ya 12.

290. Angalia maoni ya kuhitimisha ya Kamati ya Haki za kiuchumi, kijamii na kitamaduni kuhusuripoti ya awali ya kenya kuhusu haki za ECOSOC kwenye kikao cha 41 mjini Geneva, 3-21Novemba 2008, UN Doc E/C.12/KEN/CO/1 ubeti wa 12.

88

Page 105: First page ILO.fm

Katiba ya Ethiopia imetambua haki za raia wakiwemo watu wa kiasilikuhusu ardhi, ijapokuwa umiliki wa ardhi ni suala lenye utata. Kifungu cha439(5) cha katiba kinasema kuwa wafugaji wana haki ya kutofukuzwa kutokakwenye ardhi zao. Vijisehemu kadhaa vya sheria za usimamizi wa ardhivimetekelezwa tangu mwaka wa 1997. ingawa baadhi ya vipengele vya sheriahizi vinazungumzia haki za pamoja za jamii kuhusu ardhi (hasa zile za wafugaji),vilishindwa kuanzisha vyombo dhahiri na vya kutekelezeka vya haki za pamojakuhusu ardhi za jamii za kitamaduni.

Kutokana na ukoloni wa ufaransa nchini Algeria katika mwaka wa 1930,kulitokea upokonywaji wa ardhi kutoka kwa watu wakiasili kwa kiwangokikubwa. Baada ya uhuru katika mwaka wa 1982, serikali ilijitwalia ardhi hiilakini haikuwarudishia wamiliki wake halisi. Zaidi ya hayo, katika utamaduniwa Waamazi, hakuna dhana ya mali yanayomilikiwa kibinafsi, na Waamaziwengi wamepoteza mashamba yao kutokana na hali kwamba ukosefu wa hatiya kumiliki ardhi hiyo umeipa serikali nafasi ya kuwapokonya ardhi zao.

Nchini Afrika kusini, swala la umiliki wa ardhi limekuwa kwenye ajendakuu katika kujaribu kufanikisha urekebishaji wa makosa ya awali yaliyofanywana utawala wa ubaguzi wa rangi. Kando na katiba kuwa na vipengele kuhusumarekebisho mambo ya mashamba,291 baadhi ya sheria zilizotekelezwavilevile, ikiwemo sheria ya 28 ya Mali ya kibiashara ya ushirika (CommercialProperty Association Act ) ya mwaka wa 1996,292 kutambua umiliki wa ardhiza kiasili pamoja na kushughulikia masuala ya kunyang’anywa ardhi. sheria hiiimekuwa ya muhimu katika kuwapa watu wa kiasili haki ya kumiliki na kutumiaardhi zao kwa pamoja (angalia mjadala juu ya haki za pamoja hapo chini)

Kifungu cha 237 cha katiba ya Uganda kinasema kwamba mashamba ni yaraia.293 Kinaeleza aina nne za mifumo ya haki kuhusu ardhi inayotumika nchiniUganda: (a) za kimila (b) umilikaji wa ardhi usio na masharti (c) mailo na (d) zakukodisha.294 Sheria kuhusu ardhi295 inafafanua haki na wajibu wa wanajamiiwanaotumia ardhi ya pamoja.296 Wana haki ya ‘kutumia ipasavyo’ ardhipamoja na wengine, kukusanya kuni na vifaa vya ujenzi na kuvuna raslimali zamashambani, na kuwatenga wasiowanachama kutumia ardhi. shida tu hatahivyo, imekuwa ni kwamba katika hali za ardhi hiyo kutwaliwa na mtu binafsiau serikali, hakuna njia nyingine ya kuonyesha umiliki wa ardhi hiyo kwanimifumo ya kisheria ya kutoa vyeti vya umilikaji wa kimila haujatekelezwasana.297 Pia kuna ubaguzi dhidi ya mfumo wa kimila wa umiliki wa ardhi, kwaniunachukuliwa kuwa kizuizi kwa maendeleo ya kiuchumi.298

Sifa nyingine ya kawaida sana ya tawala kuhusu ardhi za baada ya uhuru nikwamba ziliwekeza ardhi yote au sehemukubwa ya ardhi katika serikali.Wakati mwingi zile sehemu zilizowekezwa katika serikali ni ardhi

291. Katiba ya Afrika kusini kifungu cha 25(4) - 25(9).292. Sheria hii inawezesha jamii mashirika ya kisheria, yatakayojulikana kama ushirika wa Mali ya

kijamii ili kupata, kumiliki na kisimamia mali kwa msingi uliokubaliwa wanajamii kwa katibailiyoandikwa.

293. Kifungu cha 237(1).294. Kifungu cha237(3).295. Sura ya 277, sheria za Uganda 2000.296. Kifungu cha 26.297. Kifungu cha 4 cha sheria kuhusu ardhi.298. Ripoti ya Tume ya Katiba: Uchanganuzi na mapendekezo (1992) kama inavyonukuliwa na

Mugambwa (2007) 53. angalia pia, SB Tindifa Land rights and peace-building in Gulu District,Northern Uganda: Towards a holistic approach Human Rights and Peace Centre WorkingPaper No. 7 (May 2007) 11.

89

Page 106: First page ILO.fm

zinazotumiwa au kukaliwa na watu wa kiasili. Kifungu cha 40 cha Ktiba yaEthiopia kwa mfano inakabidhi serikali ardhi yote.

Katiba ya Jamuhuri ya Kongo ina vipengele fulani ambavyo vinawezakuwafaidi watu wa kiasili kwa upande wa masuala ya ardhi za mababu zao,maliasili na mazingira. Kifungu cha 17 kinahakikisha haki ya kumiliki mali nainaruhusu hatua za kufidia iwapo kuna utaifishaji kwa maslahi ya umma.Kifungu cha 36 cha katiba ya Burundi inadhamini haki kuhusu mali. Sheria yaardhi ya nchini Burundi,299 inabainisha kategoria mbili za ardhi: ardhi yaserikali (ikiwemo misitu na ardhi inayochukuliwa kuwa haimilikiwi na mtu) naardhi isiyo ya serikali (ikiwemo inayomilikiwa na watu binafsi).300 Kwakusisitiza umiliki wa ardhi unaoweza kuonekana, sheria hii hazingatii hali yaWabatwa.301 Mbali na vipenegele hivi, Wabatwa kadhaa nchini Burundiwamefaulu kupata ardhi kutokana na Wabunge wa Wabatwa na baadhi yaserikali za mitaa.302 Pia Burundi inachukua hatua nzuri za kushughulikia sualala ardhi kwenye kiwango cha kitaifa.

Kulingana na kifungu cha 100 cha katiba ya Namibia, ardhi zotezisizomilikiwa na watu binafsi na maliasili vimo mikononi mwa serikali, jamboambalo pia linaonyesha umuhimu unaopewa haki za umiliki wa kibinafsi kulikoumiliki wa pamoja. Umiliki wa serikali unahusisha pia ardhi za jumuiya,ambazo ndizo za umuhimu mkubwa watu wa kiasili. Kifungu cha 17(1) chaSheria ya marebisho Kuhusu ardhi ya Kijumuia kinasema hivi:

299. Loi 1/1008 du 1er septembre 1986.300. IWGIA The indigenous world (2007) 502.301. Rapport de la Visited u Groupe de travail, 30.302. IWGIA The indigenous world (2007) 502.302. IWGIA The indigenous world (2007) 502.

Serikali ya Burundi imeanzisha tume inayojulikana kama ‘Commission Terreset Autres Biens’ zaidi ya sheria iliyopitishwa na Bunge mnamo mwaka wa2006. Wajibu wa tume hii ni:

• Kuchunguza mizozo ya ardhi• Kubainisha na kurejesha ardhi za serikali ambazo zimetolewa

visivyo• Kuchunguza masuala yote yaliyowasilishwa kwa Tume hii na

waathiriwa kwa nia ya kurejesha ardhi zao• Kutoa msaada wa kiufundi na nyenzo kwa wathiriwa ili

kuwasaidia waweze kufurahia haki zao za mali; na• Kuchunguza maswala ya ugawaji wa ardhi na kuwafidia

hathiriwa.Tume hii inakusudiwa kushughulikia maswala yanayotokana na kupotezaardhi wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe, lakini pia inaweza kuwanjia ambayo madai ya ardhi ya watu wa kiasili yanaweza kuangaliwa. Sheriainayothibiti Tume hii inasisitiza kuwa mmoja kati ya wanachama 23 watume hii lazima awe Mutwa. Kwa hivyo, mnamo mwaka wa 2006,mwanachama wa shirika la watu wa kiasilli (Unissons-nous pour la Promotiondes Batwa) aliteuliwa kuwa mwanachama katika tume hii. Ijapokuwa nimapema sana ikiwa hii itapelekea katika kuimarisha hali ya haki za kiardhiya watu wa kiasili nchini Burundi,lakini ni hatua ya mwelekeo mzuri, namojawapo wa matukio machache sana katika kanda ya Afrika ambapowawakilishi wa kiasili wanahusishwa katika vyombo vilivyo na wajibu wakushughulikia masuala muhimu kwa watu wa kiasili kama haya.

90

Page 107: First page ILO.fm

Kwa mujibu wa yaliyomo kwenye Sheria hii, ardhi zote za kijumuia zimo katikamamlaka ya serikali kama amana kwa faida ya jamii za kitamaduni zilizokatikasehemu hizo kwa kusudi la kukuza maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya watu waNamibia, hususan wale wasio na ardhi na wale wasio na uwezo wa kupata ardhiwasio na ajira au wanajihusisha na biashara zisizohusiana na kilimo.

Ni wazi kutona na kipengele hiki kwamba kuna vikwazo juu ya uwezekanowa watu wa kiasili kumiliki ardhi hasa ardhi ya kijumuia, na hata kutawalaardhi wanazomiliki au kutumia kulingana na viwango vya kimataifa. zaidi yayaliyomo katika katiba, Sheria nambari 5 ya Marekebisho kuhusu ardhi zajumuiya ya mwaka wa 2002 nchini Namibia inakusudiwa ‘kuruhusu upewajiwa haki za ardhi katika maeneo ya jumuiya, kuanzisha tume za ardhi na kutoamaelezo kuhusu uwezo wa machifu na serikali na tume za kitamadunikuhusiana na ardhi zinazomilikiwa kijumuiya.’ Sheria hii inalenga kuthibitiuhusiano wa umiliki wa ardhi baina ya serikali na wale wanaokaa katika ardhiza jumuiya zinazomilikiwa na serikali. Inatambua kuwepo kwa tume zakijumuia za kuhifadhi maliasili ya eneo husika na wajibu wazo. Kati ya Jamii sitapana za Wasan wa Namibia, ni mbili tu- yaani !Kung na Ju/’hoansi za Wilaya yaTsumkwe, kwa sasa wana usemi katika masuala yanayohusiana na ardhi zao zamababu. Hifadhi za maliasili zilizo katika ardhi zao na ambazo zinasimamiwana wao wenyewe zimewawezesha kutumia wanyamapori na maliasilimengineyo. Kwa mujibu wa sheria hii, watu binafsi na jamii wanaweza tukufurahia namna fulani za haki za kumiliki ardhi.303 Sheria kuhusu ardhi hatahivyo, inatambua haki za kimila kuhusu ardhi, ambazo zinashughulikiwabaadaye katika sura hii. Vile vile, sawa na baadhi ya mifumo ya sheria ya kitaifailiyochanganuliwa katika ripoti hii, ardhi inayochukuliwa kuwa ‘wazi’inarejeshwa kwa serikali ambayo inaweza kutimia kwa shughuli zingine.

Hali hii ni sawa na kama ilivyo nchini Gabon, ambapo sheria inatambuahaki za kumiliki ardhi kibinafsi na za pamoja. Hiki ni kipengele muhimu chamkikatiba kinachotoa mawanda ya ulinzi wa haki za watu wa kiasili kuhusuardhi, hasa kwa sababu ya kutaja haki za pamoja. Hata hivyo, kwa mujibu wahaki za ardhi, sheria ya mwaka wa 1963 inatangaza serikali kuwa ndiyo mmilikiwa pekee wa ardhi. Tangu enzi za ukoloni, watu wa kiasili wamepotezatakriban ardhi zao zote kwa serikali au kwa miliki kubwa za kigeni. Ijapokuwahivyo, matumizi ya ardhi kimila yanatambuliwa, na utambuzi huu unawapawatu wa kiasili uwezo wa kusajili mashamba yao chini ya sheria ya kimila. Hatahivyo, changamito nyingine ni sharti kwamba, ili kusajiliwa, ni lazima ardhi iweinakaliwa au inatumika. Sheria nambari 25/PR na 1/76/PR inaruhusu serikalikutwaa zile ardhi ambazo hazitumiki wala kukaliwa. Kwa hivyo, watu wa kiasiliwanaweza kuwa wahanga wa kupokonywa ardhi zao na serikali au wamilikiwa mashamba makubwa.

Sheria ya Rwanda inatoa hatoa haki za umiliki wa ardhi kibinafsi na zapamoja vile.304 Vipengele hivi vinasaidiwa na Sheria ya Ogani, nambari 08/2005 kuhusu utaratibu wa ardhi nchini Rwanda. Hii inathibitisha haki za ardhiza watu halisi vilevile na haki za kimila kuhusu ardhi.305 Vifungu nambari 54 na56 vya sheria hiyo hiyo vinalinda wenye mashamba dhidi ya kufukuzwa, ila tukatika hali ambapo wanahamishwa kwa masiliahi ya umma. Hata hivyo, kwakuwa watu wa kiasili hawana haki rasmi za kumiliki mali, vipengele hivihavitekelezwi katika sehemu wanazoishi, na watu wa kiasili aghalabuhufukuzwa kutoka katika ardhi zao za kitamaduni. Inakadiriwa kuwa takribaniasilimia 40 ya Wabatwa wamelazimishwa kubadilisha makao kutoka katika

303. Kifungu cha 57 cha sheria ya Ardhi.304. kifungo 20 hadi 30.305. Kifungu nambari 5 na 6.

91

Page 108: First page ILO.fm

maeneo yao asili.306 Licha ya kuwepo kwa vipengele kuhusu haki za ardhi zakimila, vipengele kuhusu raslimali za misitu havifuati mfano uu huu.

7.3 Aina za utumizi wa ardhi wa watu wa kiasili nasheria ya kitaifa

Ufugaji

Watu wa asili wengi katika Afrika ni wafugaji, shughuli ambayo inatumia ardhikubwa, na kuhamahama kulingana na misimu mbalimbali kwa minajili yakutafutia mifugo wao malizho. Aina hii ya utumizi wa ardhi unawakilishachangamoto katika hali nyingi hasa pale ambapo madai yanayopinganayanapozuliwa kuhusu maeneo ambayo yanatumiwa na jamii fulani ya wafugaji.Mara nyingi, lutokana na kutotambua haki za pamoja za kumiliki ardhi aushughuli za kitamaduni za watu wa kisili, utekelezaji wa shughuli kama hii nichangamoto tata na kubwa kwa watu wa kiasili. Mitazamo kuhusu ufugajikatika nchi mbalimbali za Afrika inatofautiana kwanzia uadui mkali, hisia zaukinzani hadi utambuzi na sheria kuhusu ufugaji na haki kuhusu ardhizinazofungamana na haya.

Ijapokuwa haki ya wafugaji kulisha mifugo yao na kulima mashamba bilakupingwa imo katika Katiba ya Ethiopia, sawa na haki ya kutofukuzwa kutokakatika ardhi zao,307 pana mvutano kutokana na wafdugaji wanaoigilia ardhi zawafugaji.308 Kama watu wa kiasili wengine wengi, wafugaji wamehamishwakwa nguvu kutoka katika ardhi za mababu zao ili kuunda nafasi ya mashambaya kibiashara, mashamba ya serikali, hifadhi za wanyamapori na mbuga zawanyama.309 Ijapokuwa imekadiriwa kuwa hekta 1.9 za mashamba ya malishoya mifugo yametwaliwa kwa ajili ya ukulima na hekta 466, 000 kwa mbuga zakitaifa za wanyama,310 haki ya kufidiwa ‘kulingana na dhamani ya mali,haijatekelezwa’.311 Kutokana na haya, jamii hizi zinanyang’anywa ardhi zao312

na kukosa kuchukua hatua kumesababisha kuharibika kwa maliasili ambayoufugaji hulinda.313

Serikali ya Tanzania imeonyesha mtazamo hasi dhidi ya wafugaji na watuwa kiasili.314 Sera yake kuhusu ardhi kwa mfano inapiga marufuku ‘maisha yakuhamahama’. Sheria ya uhifadhi wa wanyamapori ya mwaka 1974,315 ambayoinaruhusu uundaji wa Hifadhi za wanyama, Sehemu zaUwindaji uliothibitiwana hifadhi kiasil za wanyama, ndiyo sheria kuu kuhusu uhifadhi wawanyamapori nchini Tanzania. Sheria hii imetumiwa kutangaza ardhi za vijijivya wafugaji wa kiasili kuwa kama sehemu za uwindi uliothibitiwa na hifadhi zawanyama, kwa mfano Sehemu za uwindaji uliothibitiwa ni kama Loliondo naLongido kaskazini mwa Tanzania. Mnamo Novemba 2008, Tanzania ilitoamswada mpya wa uhifadhi wa wanyamapori ili kusikizwa ili kufuta na

306. Tazama kwa mfano mfano wa Wabatwa waliofukuzwa kutoka ardhi inayohusisha Mbugaya kitaifa ya Virguna, Mbuga ya milimani inayosifika kwa nyani wa mlima huo upande waKaskazini; Wabatwa waliofukuzwa kutoka msitu wa zamani wa Gishwati wakati wa vitavya mwaka wa 1990-1994, na mfano wa Wabatwa wanaoishi katika msitu wa sasa waNyungwe kusini Magharibi mwa Nchi hiyo.

307. Katiba ya ethiopia kifungu cha 40(5).308. Kjetil Tronvoll, Minority Rights Group International Ethiopia: A New Start? 27 (2000).309. IWGIA (2006) The indigenous world 434.310. Pastoralist Forum Ethiopia, Strategic Plan 2004-2008, 2.2, May 2004.311. Katiba ya ethiopia kifungu cha 40(8).312. IWGIA (2006) The indigenous world 434.313. Kama hapo juu.314. IWGIA, Indigenous Peoples Yearbook 2008, ‘Tanzania’.315. Kifungu cha 282, R.E 2002.

92

Page 109: First page ILO.fm

kubatiliza sheria ya mwaka wa 1974. Mswada wa 2008 unasema kuwa baadaya Rais kushauriana na serikali za mitaa husika anaweza, kwa kutoa amrikwenye gazeti la serikali, kutangaza sehemu yoyote ya Tanzania kuwa hifadhiya wanyama; bila kuwatenga watu ambao awali waliishi katika masneo hayokupata leseni.316 Mswada huu aidha una vipengele mahususi vinavyokatazaulishaji wa mifugo kwenye hifadhi za wanyama bila ya kuwa na leseni, jamboambalo linageuza msimamo wa Sheria ya uhifadhi wa wanyamapori ya mwakawa 1974 ambayo hailazimu watu waliozaliwa au ambao mahali pao pa kuishikikawaida yamo kwenye maeneo ya uwindaji uliothibitiwa, kupata ndiposawaishi (na kulisha mifugo wao) katika sehemu hizo.

Nchini Eritrea, kuna mfumo wa kulinda ardhi za wafugaji, jambo ambalo sila kawaida katika muktadha wa Afrika, lakini kuna changamoto kuhusiana nauelewa wa sheria kuhusu ufugaji na kulingana na ulinzi wa haki zawahamahamaji. Kama ilivyo kwingineko, katiba ya Eritrea inatia umiliki waardhi na maliasili yote, chini na juu ya ardhi ya himaya yake katika serikali.Katika mfumo wake wa kisheria, haki za kutumia ardhi bila kuimiliki ndizohaki zenye nguvu sana ambazo wafugaji wa kiasili wanaweza kutimainia kuwanazo juu ya ardhi zao. Ilani nambari 58/1984 kuhusu ardhi inathibitisha kuwaardhi zote zinamilikiwa na serikali (kifungu cha 3(1)). Serikali inawezakuruhusu utoaji wa haki za kutumia ardhi bila kuimiliki au haki sawa na hizikuhusu ardhi na inaweza kuweka masahrti na vigezo vya kutumia nakusimamia radhi (kifungu cha 3(3) na (4)). Hata hivyo, imeruhusiwa katikasheria kwamba kila raia wa Eritrea317ana haki ya kutuma ardhi bila kuimiliki(kifungu cha 6(3)). Nyingine ni haki ya kupata ardhi kwa ajili ya ujenzi wanyumba au ukulima au shughuli zote mbili katika vijiji vilivyopo, ama vijiji aumaeneo mengine ambayo yangeweza kuanzishwa halafu (kifungu cha 4(20)).

Serikali pia imepewa uwezo wa kugawa ardhi kwa ajili ya shughuli za ujenziwa nyumba na ukulima.318 Ubainishaji wa ardhi unafasili ‘ shughuli za ukulima’kuwa unahusisha ukulima na ufugaji (kifungu 2(6)). Hata hivyo kuna vikwazovikubwa kuhusiana na uelewa wa suala la ufugaji. Haki za mtu kutumia ardhiasiyoimiliki kwa kilimo (ikiwemo shughuli za ufugaji) katika maeneo ya vijiji yaEritrea zinakubaliwa tu kwa raia wa Eritrea ambao ni wakaazi wa kudumukatika vijiji vya nchini humo na maisha yao yanategemea ardhi, na kwa raia waEritrea ambao wamepewa ruhusa na serikali kuishi katika vijiji na kutumiaardhi hiyo (kifungu cha 6(2)). Wakisha pewa makao, hawaendelezi tena ufugajiwa kuhamahama.319 Kwa njia hii, kubainishwa kwa ardhi kunawalazimuwafugaji kugeukia ukulima wa kuishi mahali pamoja.

Nchini Burkina Faso, juhudi dhahiri zimefanywa katika kushughulikiaufugaji. Sheria nambari 034- 2002/an kuhusu ufugaji inahusika na utumiaji wamaliasili. Katika muktadha huu, serikali na wanajamii wa maeneo fulani wanawajibu wa kubainisha, kulinda na kuhifadhi maeneo ya ufugaji. Haki za pamojakuhusu ardhi husika zinatambulika kwa wa watu wa uzao fulani au kabila.Aidha inatambuliwa na sheria kwamba wafugaji wanafaa kutumia maliasilikulingana na mfumo wa sheria, hasa sheria inayohusu mazingira. Miungano yawafugaji, kwa kushauriana na serikali za kimila, yanahitaji kushughulikia

316. Sehemu ya 14(1) na 17(2) na (3) ya Mswada ya uhifadhi wa wanyama pori.317. Mtu yeyote ambaye amefikisha umri wa wengi au ambaye anaonekana kuwa

amekombolewa kulingana na vifungu nambari 329-334 vya Sheria ya Mpito eritrea kuhusuumma, ana haki ya ardhi (kifungu cha 7 cha ubainishaji wa ardhi).

318. Mkazo umewekwa.319. Kwa uchanganuzi wa kina wa kipengee hiki angalia JR Wilson ‘Eritrean land reform: The

forgotten masses’ (1999) 24 North Carolina Journal of International Law and CommercialRegulation 498 na SF Joireman, ‘The minefield of land reform: Comments on the Eritreanland proclamation’ (1996) 95 African Affairs 273, 275.

93

Page 110: First page ILO.fm

masuala ya kubainisha, kuhifadhi na kusimamia maeneo ambayo yanatumiwakwa ufugaji, vyanzo vya maji na kadhalika. Nchini Mali, utekelezaji wa mkatabaunaolenga kuthibiti ufugaji na utumizi wa maji na malisho ya mifugo mnamomwaka wa 2001, kwa kiasi, ulikuwa jaribio la kushughulikia mivutano baina yawakulima na wafugaji.320 Hata hivyo mkataba huu unaacha swala laupokonywaji wa ardhi za ufugaji na watu wengine bila kushughulikiwa, nabadala yake unashughulikia haki za utumizi tu katika hali hii.

Kwa Wambororo wa Jamuhuri ya Afrika ya kati, uundaji vyombo vyakimaeneo unaonekana kuwa kama chanzo cha kiwango fulani cha kutambuaufugaji kupitia kwa sheria nambari 64/32 na 64/33 zinazohusu uanzishaji naupangiliaji wa jamii hizi, aidha sheria nambari 64/32 kuhusu uanzishaji wa jamiiza mashambani katika maeneo ya ufugaji, uteuzi wa mameya na usimamizi wamabaraza ya miji. Sheria ya nambari 65/61 kuhusu kuthibiti uzalishaji wawanyama inaruhusu uanzishaji wa jumuiya za wakulima wa mifugo. Jumuiyakama hizi ziliundwa katika miaka ya 1960 kwa lengo la kuwatuliza wafugajimahali pamoja. Tangu hapo, jumuiya saba zimeanzishwa zikiwa na mabaraza yamiji iliyohuru.

Nchini Niger, Sheria ya Maeneo ya mashambani (ya maji, mwaka wa 1983kama ilivyorekebishwa mwaka wa 1998) inayo mikakati ya kuhakikisha kuwawatu wote wana hakika ya kupata maji kama haki isiyotengeka, kupitia kwaumiliki wa serikali (umma) na uundaji wa ‘shoroba za mpito’ (couloirs depassage) ambazo ni za umuhimu mkubwa kwa watu wa kuhamahama.

Wawindaji-waokotaji

Kuhusiana na wawindaji na waokotaji, ukweli kuwa kuishi kwa watu wa kiasilikatika misitu hakujatambulika sana katika sheria ya kimila au sheria ya bungekunaelza ukweli kwamba ni wachache sana, kama wapo, wana vyeti vyakumiliki ardhi.321 Katika Afrika ya kati, suala jingine kuhusu haki ya kuwindana kukusanya ni kwamba makaazi ya watu wa kiasili mara nyingi huwayameungana na vijiji vya makabila makubwa zaidi na yanatambuliwa tu kamasehemu za vijiji hivyo, jambo linalomaanisha kuwa haki zozote kuhusu ardhizinazohusishwa na jamii za mashinani kwa jumla huwa haziwahusu watu wakiasili.

Nchini Gabon, mijadala inayoendelea kuhusu Mpango wa Kisekta kuhusumisitu na mazingira na Mpango wa maendeleo ya watu wa kiasili (IPDP)inaweza kutumiwa kama hatua za awali za kuanza kufikiria kurekebishaunyanyasaji ambao watu wa kiasili wamepata kuhusiana na haki zao kuhusuardhi. Katika mfumo uliotolewa na Sera ya Utendaji ya 4.10 ya Benki yaDunia, IPDP inapendekeza, kati ya mambo mengineyo; kuhakikisha kuwa kunautambuzi wa kiasheria (vitambulisho) kwa Babongo, Bagoya, Baka, Barimba,Bakouyi na Waakoa; kushughulikia masuala ya kisheria na usawayanayohusiana na swala la ‘kambi’ za watu wa kiasili; kuanzishwa kwa misitu yakijamii (kilomita mija mraba kwa mtu mmoja, kwa kiwango cha chini) kwa ajiliya jamii zilizotajwa hapo juu; kutambua rasmi na kulinda maeneo ya ardhizinazotumiwa na watu wa kiasili, zikiwemo mbuga za kitaifa za wanyama namaeneo yaliyolindwa; na kurasimu sera ya kitaifa kuhusu watu wa kiasili.322

320. Angalia Loi No 01-004 du 27 février 2001 portant charte pastorale du Mali. 321. Jackson Twa Women, Twa Rights in the Great Lakes of Africa 8.322. République Gabonaise, Ministère de l’Economie Forestière, des Eaux, de la Pèche, de

L’Environnement chargé de la Protection de la Nature, Plan de Développement de PeupleAutochtones du Programme Sectoriel Forêts Environnement, Rapport Final préparé par Dr KaiSchmidt-Soltau, juillet 2005 5.

94

Page 111: First page ILO.fm

Kulingana na Sheria kuhusu ardhi za kikabila nchini Botswana, ardhiinaweza kukubaliwa tu kwa makusudi ya kuishi, kilimo, malisho ya mifugo aubiashara. Matumizi mengine ya ardhi yanayotambulika kama vile uwindaji naukusanyaji wa chakula cha mwituni yakuwa wajibu wa serikali kuu, ikimaanishakuwa mifumo ya matumizi ya ardhi kitamaduni ya watu wa kiasili wa nchi hiihaitambuliki. Zaidi ya hayo, ardhi inaweza tu kupewa kwa mtu binafsianahitimu kama mtu wa kabila fulani. Kwa kuwa uanachama wa kabila fulanimara nyingi ulishindaniwa, Basarwa walibaguliwa katika kutuma maombi yakupata ardhi kwa msingi kuwa hawakuwa wa kabila moja.323 Katika mwakawa 1993, sheria kuhusu ardhi ya kikabila ilirekebishwa ili kuruhusu ugawaji waardhi kwa msingi wa uraia na wala sio uhusiano wa kikabila.324 Hata hivyo,ingawa msimamo rasmi ni kwamba hakuna kabila litamiliki eneo lolote,ushahidi ni uliopo nikwamba unaonyesha kutambulika kwa umiliki wa kikabilawa ardhi, au kitu kinachohusiana na ardhi. kwa mfano, mabaraza ya ardhiyanayosimamia ardhi inayohusika kwa amana yamepewa majina kulingana namaeneo yanayosimamia. Haya yote yana majina ya makabila makubwa yaTswana. Kwa hivyo watu wa kiasili hawana maeneo yanayotambulika nje yamakabila ya Tswana wanayochukuliwa kuwa sehemu yake.325

323. Wily, EA (1979) Official Policy Towards San (Bushmen) Hunter-Gatherers in Modern Botswana:1966-1978 Gaborone: National Institute of Development and Cultural Research 33.

324. Sehemu ya 10(1) ya Sheria kuhusu ardhi za kikabila ya mwaka wa 1993 (iliyofanyiwamarekebisho I Mazonde ‘Equality and ethnicity: How equal are San in Botswana’ in RKHitchcock na D Vinding (eds) Indigenous Peoples’ Rights in Southern Africa (2004) IWGIADocument 110, 138.

325. I Mazonde ‘Equality and ethnicity: How equal are San in Botswana’ in RK Hitchcock na DVinding (eds) Indigenous Peoples’ Rights in Southern Africa (2004) IWGIA Document 110,138.

95

Page 112: First page ILO.fm

96

Page 113: First page ILO.fm

Mfano: Daawa ya Kamanakao, Mbuga ya wanyama ya Kalahaya Kati, Botswana

Daawa ya Kamanakao inawakilisha uamuzi mkubwa kuwahikutolewa ambaounaonyesha umuhimu wa suala la seriakali ilikuwa imejiingiza katika mjadala kwamuda wa zaidi ya miaka kumi na mitano kabala ya kukubali baadaye kuwahamishawalalamishi. Kwa hivyo, wali ilionekana kwamba waliotuma maombi walikuwawameulizwa ha kwa hivyo walikuwa wamekubali kwa hiari kuhamishwa. Hatahivyo, mahakama iligundua kwamba hakukuwa na ridhaa huru na yenye ufahamukwani serilkali ilishindwa kuzingatia hali maalumu za uchumi wa kijamii za walalamishiHii ilihusisha ukweli kwamba watu husika kijumla walikuwa masikini sana, jamiizilizopembezwa zenye kiwango kidogo cha elimu na zilizozungumza na kukielewaKitswana kwa viwango tofautitofauti. Pia walikuwa watu wenye utamaduni ambaoulikuwa tofauti sana na utamaduni wa Watswana. Hivyo, aina za mikutanoiliyotumiwa kwa makundi ya Tswana huenda isiyafae makundi yasiyo ya Kitswana.

Mnamo mwaka wa 1986 serikali ya Botswana ilipitishwa sera ambayo kwayoWabasarwa wanaoishi katika Mbuga ya wanyama ya Kalahari ya Kati(CKGR)wangeweza kuhamishiwa katika makaazi yaliyonje ya mbuga hiyo. Sababuzilizotolewa na serikali kuhusu jambo hili zilikuwa: haja ya kuzileta jamii hizi karibuna ‘maendeleo’; na kwamba kuwepo kwao katika mbuga hiyo kulikuwa ‘tishio kwawanyamapori walio katika mbuga hiyo’. Uamuzi wa kuendelea na uhamishaji huoulifanywa katika mwaka wa 2002. Serikali ilichukua hatua za kutekeleza uamuzi wakuwahamisha, ambao, ilisisitizwa, ulikuwa wa makubaliano. Baadhi ya wakaaji wambuga hiyo walitaka amri ya Mahakama Kuu kutangaza hatua ya serikalikuwahamisha kuwa haramu. Jibu la swala hili lilitegemea, kwa mujibu waMahakama Kuu, iwapo Wabasarwa walikuwa wakikalia mbuga hiyo kihalaliwalipoondolewa mwaka wa 2002 au la. Kwa upande mmoja, hoja ilikuwa kwambambuga ya wanyama ya Kalahari ya Kati ilikuwa ya serikali, na kwa hivyo, kihalalikabisa, haki za Basarwa katika hali hii zingekuwa zile za kukalia na wala sio zaumiliki. Kwa upande mwingine walalamishi walidai kwamba walikuwa na hati milikiya asili kwa Mbuga hiyo.

Mahakama ilishikilia kwamba ili utawala wa kikoloni kupata umiliki wa ardhilazima kuwepo na sheria mahsusi ya upataji huo ambayo ni tofauti na sheria yakikoloni. Aidha ilishikilia kwamba wakati uhuru ulipotangazwa, Wabasarwawalikuwa na hati za umiliki ya kiasili kwa Mbuga hiyo na kwamba haki za kiasilizingeweza tu kubainishwa na sheria mahususi ya kuachilia kwa mtu wa tatu. Zaidiya hayo, mahakama ilishikilia kwamba hati miliki ya asili haingeweza kufutiliwambali kwa tangazo la haki za kumiliki ardhi na utawala wa kikoloni, ila pale ambapoutumizi wa ardhi husika (kwa mfano, iwapo ardhi hiyo ilikuwa imeachiliwa kwawatu wengine, au kutumiwa kama makaazi) haukulingana na kuwepo kwa haki asili.Kwa hivyo mahakama ilishikilia kwamba:

• Hatimiliki ya asili ya Basarwa kwa Mbuga ya wanyama ya Kalahari yaKati haikuathiriwa kwa kuwa serikali ya kikoloni ya Uingerezailiwaruhusu kuishi na kuwinda katika mbuga hiyo bila kuingiliwa.

• Kuanzishwa kwa Mbuga ya Wanyama ya Kalahari ya Kati hakukufutiliambali hatimiliki ya asili kwa kuwa kifungu cha 3 cha uhifadhi wawanyama kilikuwa na ibara ya haki za uwindaji kwa wale ambaokimsingi walitegemea uwindaji.

Kutokana na haya ilishikiliwa kuwa Basarwa waliishi kihalali katika Mbuga yaWanyama ya Klahari ya Kati katika mwaka wa 2002. Kasha mahakama ilifikiauamuzi kwamba Wabasarwa walipokonywa umiliki huu kinyume na sheriakutokana na sababu kadhaa ikiwemo kuharibiwa kwa nyumba zao, kukomeshwakwa kutolewa kwa huduma kama maji na leseni za uwindaji na kutengwa kwafamilia. Mambo haya yote yalikuwa ushahidi fika kwamba walalamishi katika kesi hiihawakutoa hiari ipasavyo kwa kuhamishwa kwao.

97

Page 114: First page ILO.fm

7.4 Haki za pamoja na za kibinafsi na sheria ya kimila

Ulinzi wa haki za pamoja kuhusu ardhi na maliasili ni muhimu sana kwa kuwakutumia ardhi na maliasili yanafungamana sana na utambulisho na maisha yawatu. Zaidi ya hayo, ardhi pamoja na maliasili aghalabu vimefungamanishwa namaisha ya kitamaduni na ya kimila ya watu, na haki za pamoja kuhusu ardhi nimoja wapo ya haki muhimu za watu wa kiasili.

Kifungu cha 29 cha katiba ya Rwanda kinatambua haki za kibinafsi na zapamoja kuhusu ardhi. katika Jamuhuri ya Kongo, sheria ya mwaka wa 2004kuhusu ardhi inatambua sifa ya haki za kibinafsi za pamoja kuhusu mali yakimila.326 Nchini Chad, mali ya pamoja inatambuliwa pia, kwa masharti kuwajamii ina hadhi ya kisheria. Sheria kuhusu raslimali ya umma ya Julai 1967327

jinasema kuwa ardhi ambazo zinatumika kiuzalishaji kiujima itapewa ikibalimaalum ikiwa ni pamoja na usajili wa ardhi kwa jina la jamii ikiwa jamii hiyo inahadhi ya kisheria, au kwa jina la serikali, ambapo itaipa jamii hiyo haki juu yaardhi hiyo bila gharama.

Kama ilivyotajwa awali katika sura hii, kulingana na kifungu cha 29 chakatiba ya Misri ya mwaka wa 197, aina tatu za umiliki zinatambuliwa: umilikiwa umma, wa ushirika na umiliki wa kibinafsi. Kuhusiana na haki za pamoja,inapendekeza kuanzishwa kwa vyama ushirika ambavyo vinaweza kufurahiakwa pamoja umilikaji wa pamoja ambao umehakikishwa kwa mujibu wakifungu cha 31 cha katiba. ingawa umiliki wa ushirika unaweza kuchukuliwakuwa kama namna ya umilikaji wa pamoja, sio mfumo wa kimila wa umilikaji.Pale ambapo kikundi fulani cha watu hakijapangiliwa katika vyama vya ushirikana shughuli zake na utumizi wa ardhi havijasajiliwa kama umilikaji wa kibinafsi,ardhi yake itachukuliwa kirasmi kuma ardhi ya umma. Pale ambapo watu wakibinafsi wanalazimishwa kuingia katika vyama vya ushirika, wanawezakulazimishwa kutumia njia ya uzalishaji ambayo inadunisha mfumo wao wakitamaduni na maisha yao. Baada ya kuhama na kuishi kwingine mbali nabonde la Nubi, kwa mfano, wanajamii wa jamii ya Nubi waliunda chama chaushirika na kwa sababu ya hayo wakaanza kulima miwa- mmea ambaohaukuwa sehemu ya desturi ya utamaduni wao.328

Nchini Kenya, rasimu ya Sera ya kitaifa kuhusu ardhi imetiliwa shaka kwakutoshughulikia ipasavyo swala la haki za pamoja kuhusu ardhi.329 kulinganana ripoti ya IWGIA ya mwaka wa 2007, huku baadhi ya sehemu za rasimu hii(Sera ya Kitaifa kuhusu ardhi ) zikiwa zinahusu sana masuala yanayohusiana naardhi na maliasili (masuala yanayogusia maisha ya watu wa kiasili moja kwamoja), inashindwa kutambua haki za pamoja kuhusu ardhi.

Nchini Afrika kusini, sheria ya 28 ya mwaka wa 1996 kuhusu ushirika wamali ya jumuiya330 ina uwezo wa kulinda haki za watu wa kiasili kuhusu ardhikwa kuwa imetengenezwa kushughulikia dhuluma za kihistoria zainazohusianana utumizi na umilikaji wa ardhi. sheria ya ushirika wa mali ya jumuiyaimekuwa ya maana sana katika kuwapa watu wa kiasili haki ya kumiliki nakutumia ardhi yao kwa pamoja, hasa baada ya kurejeshwa kwa ardhi yao ya

326. Kifungu cha 31 cha Sheria nambari 10-2004 ya 26 Machi 2004 kuhusu Kanuni za Jumlazainazotumika kwa umma na Taratibu za ardhi.

327. Kifungu cha 20 cha sheria nambari 24 ya 22 Julai 1967.328. Uchunguzi wa Maktaba ya Kongresi kuhusu nchi http://lcweb2.loc.gov/cgi-bin/query/r?frd/

cstdy: @field(DOCID+eg0069) (iliangaliwa 2 Disemba 2006).329. Angalia pia IWGIA (2007) The indigenous world 470.330. Sheria hii inaziwezesha jamii kuunda miungano halali itakayojulikana kama Muungano wa

kumiliki Mali kwa Jumuia ili kupata, kumiliki na kusimamia mali kama itakavyokubaliwa nawanajamii kwa mujibu wa katiba iliyoandikwa.

98

Page 115: First page ILO.fm

kitamaduni kama inavyojadiliwa hapa chini. Hata hivyo, masharti yaliyotolewana sheria hii yanayolazimu kuchaguliwa kwa viongozi wa kuwakilisha jamiiwakati mwingine yanakinzana na mifumo ya uongozi wa kitamaduni uliopo wajamii za,kitamaduni, na kuzua mivutano na kuchelewesha usimamizi nautekelezaji wa uamuzi.

Sheria ya kimila ipo katika nchi nyingi na sheria ya kitaifa inatambuakuwepo kwake sambamba na sheria iliyoandikwa. Baadhi ya sheria za kitaifa,kama tutakavyoona hapo chini, zina nafasi kwa watu wa kiasili kudai haki zaoza kimila kwa ardhi, ingawa bado kungali na changamoto kadhaa.

Katika nchi nyingi za ukanda wa Afrika ya Kati, sheria za kitamaduni zawabantu ni tofauti na zile za ‘Mbilikimo’, kwani maeneo ya mbilikimo nisehemu kubwa za ardhi au maeneo ambamo wanafanyia uwindaji, ukusanyaji,uvuvi na shughuli nyinginezo. Ardhi hizi zinachukuliwa kuwa mali ya jamiinzima. Dhana hii ni sawa kwa Wambororo wa Afrika ya kati nay a Magharibiambao wanachukulia kuwa sehemu za malisho ya mifugo ni ya jamii nzima.Haiyumkini mtu mmoja au familia moja katika jamii hizi kudai sehemu moja yaardhi pamoja kwa matumizi ya kibinafsi. Katika sehemu nyingine za Afrika, halini ile ile, na dhana za kiasili kuhusu utumizi wa ardhi na haki za kimila, pamojana usimamizi wa kitamaduni na mifumo ya kufanya maamuzi inatifautiana sanana kwa umma mzima.

Kifungu cha 237 cha katiba ya Uganda inasema,kuwa ardhi ni ya wananchiwake.331 Katiba inaeleza aina nne za mifumo ya umiliki wa ardhi, ikiwa nipamoja na umiliki wa kimila.332 Sheria kuhusu ardhi,333 ambayo ni sheria kuuinayozungumzia masharti ya kumiliki, umilikaji, utumizi na usimamizi wa ardhi,inafafanua aina mbalimbali za mifumo ya umiliki wa ardhi inayoelezwa katikakatiba, ikiwemo umiliki wa kimila. Kifungu cha 3(1) cha sheria kuhusu ardhikinafasili mfumo wa kimila kama namna ya umilikaji. Kwa kusoma kipengelehiki kwa mara ya kwanza, hata hivyo, ni wazi kwamba haki za kimila katika hiizinatumika kwa watu binafsi na familia, hali ambayo kwa kweli haifuatani nauelewa wa kimila wa watu wa kiasili kuhusu haki za pamoja kuhusu ardhiambao unapita mipaka ya watu binafsi na familia na kuhusisha jamii kwa jumla.Sheria kuhusu ardhi aidha inafafanua haki na wajibu wa wale wanaotumiaardhi ya pamoja.334 Wana haki ya kutumia ardhi vizuri pamoja na watuwengine, kukusanya kuni na vifaa vya ujenzi na kuvuna raslimali zilizokokwenye ardhi hiyo na kuwatenga wale wasiokuwa wa jamii husika wasitumieardhi hiyo. Tatizo moja hata hivyo, limekuwa ni kwamba wakati ambapo ardhiya jumuiya inapochukuliwa na mtu binafsi au serikali, hakuna njia yakuthibitisha umiliki wa ardhi hiyo kwani mikakati ya kisheria ya kutoa hati zaumiliki wa kimila haijatekelezwa kabisa.335 Vile vile pana ubaguzi dhidi yamifumo ya kimila ya kumiliki ardhi kwa kuwa inaonekana kuwa inazuiamaendeleo ya uchumi.

Vipengele mbalimbali katika sheria kuhusu ardhi inarahisisha ugeuzaji waumilikaji wa ardhi kimila kuwa ule usio na masharti.336 Mtazamo huu piaumesambaa sana barani Afrika na unaonyesha vizuri sana umuhimu ambao

331. Kifungu cha 237(1).332. Kifungu cha237(3).333. Sura ya 277, Sheria za Uganda 2000.334. Sehemu ya 26.335. Sehemu ya 4 ya Sheria kuhusu ardhi.336. Sehemu ya 9.

99

Page 116: First page ILO.fm

mifumo ya kisheria ya Afrika inaupa umiliki wa ardhi wa kibinafsiukilinganishwa na ule wa kimila.337

Ni kawaida ya vipengele vinavyohusiana na haki za kimila kuhus ardhikupuuza mila za watu wa kiasili. Haki za kimila mara nyingi huwa zimejikitakwenye uelewa wa aina za utumizi wa ardhi ambao ni wa mahali pamoja tu,ambazo zinaacha nje jamii za wahamahamaji, wafugaji na wawindaji-wakusanyaji – ambazo ni pamoja na watu wengi wa kiasili katika kanda hii nahata Afrika kwa jumla. Uhamaji wa mara kwa mara wa Wafulani, kwa mfano,unawafanya ‘wageni’ kulingana na mfumo wa umiliki wa ardhi kimila nchiniNigeria.338 Mfumo wa kumiliki ardhi kimila unashikilia kuwa ardhi ingaliinamilikiwa iwe inalimwa au imekaa bure.339 Kutokana mfumo huu, Wafulaniwahamahamaji hukopeshwa mashamba kwa makusudi ya malisho na maji nabadaye hurejeshwa kwa wamiliki wa kimila baada ya wahamahamaji hawakupita.340

Mahakama za sheria aimetoa uamuzi unaokinzana zinapoamua masuala yaardhi kwa kulingana na haki za kimila kuhusu ardhi. wakati mwinginemahakama zimeshikilia kuwa usajili wa ardhi unafisha haki za kimila kuhusuardhi na kisha kuweka haki zote katika mmiliki aliyesajiliwa.341 Kwa upandemwingine, pia zimeshikilia kwamba usajili wa haukukusudia kuwanyang’anyauridhi watu ambao ndio wangekuwa wamiliki halali wa ardhi yao.342 Uamuziunaokinzana kama huu kutoka kwa mahakama zile zile unazua mawali kuhusuupana wa utata washeria kuhusu ardhi nchini ambao unawanyang’anya uridhina kuathiri haki walizo nazo watu kwa ardhi zao. Baadhi ya kesi ambazozimewasilishwa mbele ya mahakama za Kenya kujaribu kutetea haki za watuwa kiasili kuhusu ardhi, bila kufanikiwa, ni kama kesi ya Ogiek343 ambayoilijadiliwa hapo awali, na kesi ya Endoroi,344 ambayo kwa sasa imewasilishwambele ya Tume ya Afrika kuhusu haki za kibinadamu na watu.345

337. Angalia Sehemu ya 115(2) ya katiba ya Kenya.338. C Ezeomah, Land tenure constraints associated with some recent experiments to bring formal

education to nomadic Fulani in Nigeria. Iliyotolewa kwa http://www.odi.org.uk/pdn/papers/20d.pdf (iliangaliwa 15 Juni 2007).

339. Kama hapa juu.340. Kama hapa juu.341. Obiero v Opiyo (1972) EA 227; and Esiroyo v Esiroyo (1972) EA 388.342. Wanjala Ibid;angalia Muguthu v Muguthu HC Civil case No 377 ya 1968 (haikuripotiwa).343. Francis Kemai and Others v the AG and others HCC 238/1999.344. High Court Misc. Civil Case No. 183 of 2002. katika kesi hii jamii ilijitetea mbele ya

Mahakama kuu ya Nakuru kwamba, kwa kuanzishwa kwa mbuga ya wanyama kwenyeardhi yao ya jamii na bila kuwauliza na hivyo kuwafukuza na kuwazuia wasiingie kwenyeardhi zao, baraza la jiji la Baringo lilikiuka haki na uhuru wao muhimu vile vile na vipengeevya kikatiba kuhusu ardhi za amana. Mahakama Kuu ya kenya mjini Nakuru uliamua kesihiyo dhidi ya jamii.

345. Katiba 276/2003, CEMIRIDE (kwa niaba ya jamii ya Endorois) v Kenya.

100

Page 117: First page ILO.fm

Utambuzi wa sheria asili ya kimila – daawa ya Richtersveld

‘Rchtersveld ni eneo pana la ardhi lililoko katika pembe ya Kaskazini-magharibimwa juba ya kaskazini ya Cape province ya Afrika Kusini na kwa karne nyingilimekaliwa na jamii ambayo kwa leo inajulikana kama Jamii ya Richtersveld’.Jamii hii ilikuwa ikiishi katika ardhi hii kabla ya kutwaliwa na utawala waUingereza mwezi Disemba mwaka wa 1847. Hata baada ya kutwaliwa hukujamiihii iliendelewa kuishi katika ardhi hii hadi katika miaka ya 1920 ambapo madiniya Almasi yaligunduliwa. Baada ya kuzinduliwa kwa shughuli za uchimbaji wamadini katika miaka ya 1920, Jamii ya Richtersveld ilinyimwa ruhusa ya kuingiakatika ardhi zake hadi kufikia mwaka wa 1994, serikali ilikuwa imekabidhiumiliki wa ardhi husika kwa kampuni ya uchimbaji madini. Kwa kuchochewa naibara za Sheria ya kufidiwa, jamii hii iliwasilisha dai la haki zao za ardhi pamojana madini ya dhamnani yanayoambatana nayo katika eneo kubwa la ardhi yenyeutajiri wa madini ya Almasi katika juba ya Barren Northern Cape.

Kufuatia dai ambalo halikufaulu lililowasilishwa katika Mahakama ya Madai,jamii ilifaulu kuwasilisha kesi hiyo katika Mahakama kuu ya Rufaa, ambayoilisema kuwa ‘Jamii ya Richtersveld ina haki kulingana na Sehemu ya 2(1) yaSheria ya 22 ya Kurudishiwa Haki za ardhi ya mwaka wa 1994, kurejeshewahaki ya umiliki na utumizi mkamilifu wenye manufaa, kama ule uliomo katikasheria ya kawaida ya umiliki, wa ardhi husika (ikiwa ni pamoja na madini namawe ya dhamani yaliyomo)’. Mahakama iligundua kuwa upokonywaji huoulikuwa unabagua dhidi ya kabila ‘kwa kuwa ulijikita katika kwa kigezo thabitikwamba kutokana kutokana na kabila na kutostaarabika kwa jamii ya Richtersveld,haki yake ya kiardhi ilikuwa imepotea kutokana na kutwaliwa kwa ardhi zao’.

Kampuni ambayo ilikuwa imepewa umiliki wa ardhi husika ilikata rufaa kwamahakama ya juu zaidi nchini Afrika Kusini – Mahakama ya kikatiba – iliteteahaki ya Jamii ya Richtersveld kurejeshewa haki za utumizi na umiliki makamilifuwenye mannufaa wa ardhi hiyo ikiwa ni pamoja na madini na mawe ya dhamaniyaliyomo. Katiba ya Kikatiba ilizidi kugundua kwamba jamii ya Richtersveldilimiliki ardhi hiyo chini ya sheria ya kiasili, vile vile ikathibitisha hadhi ya uhuruya sheria ya kimila chini ya katiba ya Afrika Kusini:

Wakati sheria ya kiasili iliangaliwa katika lensi ya sheria ya kawaida hapoawali, yapasa sasa ionekane kama sehemu ya sheria yetu. Kama sheriazote inategemea katiba kwa uwezo na ufaafu wake. Ufaafu wake sasalazima ukadiriwe kwa kurjelea si kwa sheria ya kawaida bali kwenye katiba... Katiba inatambua uasilia na upekee wa sheria ya kimila kama chanzohuru cha kaida katika mfumo wa sheria ... Sheria ya kiasili inaigia ndani ya,inainawirisha, inafungamana na kuwa sehemu ya mchanganyiko wa sheriaya Afrika Kusini.

Ijapokuwa ilikuwa miaka kadhaa tu baadaye ambapo makubaliano kuhusukufidiwa kwa jamii hii na kuhusu kushiriki faida ya nadini yaliyochimbwa katikaeneo hilo yaliafikiwa, daawa ya Richtersvelt ilidhihirisha kwamba sheriamwafaka ni chombo muhimu cha kupata haki za watu wa kiasili. Kwa kweli,huku ibara za moja kwa moja katika katiba na sheria nchini Afrika Kusini vikitoanjia wazi ya kurejesha ardhi kupitia kwa mahakama, jamii pia ilitumia mbinubadala za kupata suluhisho. Dhana hii ya hatimiliki ya asili inatoa njia badala yakuchukua hatua ambayo inaweza kutumiwa pale ambapo dai linawezakushindwa kufuzu chini ya ibara za kufidiwa, au pale ibara kama hizi hazipokabisa.

101

Page 118: First page ILO.fm

Haki za pamoja na sheria ya kimila katika daawa ya Jamuhuri yKidemokrasia ya Kongo, na kutoonekana kwa mbinu za kutumardhi za watu wa kiasili

Kifungu cha 34 cha Katiba ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kinalinda hakiza mali ya kibinafsi na pamoja:

La propriété privée est sacrée. L’Etat garantit le droit à la propriété individuelleoucollective, acquis conformément à la loi ou à la Coutume. (Mali ya kibinafsihaiwezi kukiukwa. Serikali inadhamini haki mali ya kibinafsi au ya pamoja,yaliyopatikana kulingana na sheria au mila.

Sheria ya Kongo ina wasifu wa uwili kwa kuhusiana na haki za mali. Sheriailiyoandikwa iko sambamba na sheria ya kimila. Kwa watu wa kiasili nchiniKongo (DRC), njia za kutumia na kusimamia ardhi ni zenye wasifu wa pamoja,kwa hivyo, dhana ya mali ya pamoja inaweza kuwa umuhimu mkubwa. Zaidi yahayo katiba pia inatambua kwa wazi dhma ya sheria ya kimila katika masuala yahaki za mali. Kinadharia, ibara hizi zinaweza kuwa za muhimu kwa watu wakiasili.

Sheria kuhusu ardhi (Loi n° 73-021 du 20 juillet 1973 portant régime généraldes biens, régime foncier et immobilier et régime des sûretés, telle que modifiée etcomplétée par la Loi n° 80-008 du 18 juillet 1980) pia inatambua sheria ya kimilakuhusu ardhi:

Les terres occupées par les communautés locales sont celles que ces communautéshabitent, cultivent ou exploitent d’une manière quelconque – individuelle ou collective– conformément aux coutumes et usages locaux. Les droits de jouissancerégulièrement acquis sur ces terres seront réglés par une Ordonnance du Présidentde la République.

Agizo la Rais wa Jamuhuri, kama inavyobasiriwa katika sheria bado halijatolewa.Kwa hivyo kwa mujibu wa sheria ya kimila, masuala ya mali na radhiyanachukuliwa kulingana na kanuni za kila jamii husika mabazo hutofautiana kwakiasi Fulani. Katika sehemu zingine, haki za ardhi zinathibitishwa kupitia kwamatumizi na ukaliaji wa sehemu Fulani ya ardhi unaoonekana. Halii hii inaitwa‘umiliki wa kimila’ – ardhi ambayo imekaliwa au kutumika kwa muda mrefukadiri ya mtu anavyoweza kukumbuka. Dhana hii ni sawa na wazo la ‘tangu kale’katika sheria ya kimataifa. Katika sehemu zingine mtemi wa kitamadunihugawanya ardhi baina ya wanajamii wa jamii yake. Kwa watu wa kiasili, ardhi yapamoja ni pamoja na ardhi ya uwindaji na uokotaji, zaidi ya maeneo mbalimbaliya kiroho na kitamaduni. Ardhi hizi ni za jamii yote. Maisha yao ya kuhamahamahuacha ishara ndogo sana ya ukaliaji au utumizi wa ardhi. Kutokana na hayo,umiliki wa ardhi wa watu wa kiasili unaingiliana na ule wa jamii zingine. Kulinganana sheria iliyoandikwa, usaji wa ardhi za mashambani lazima utanguliwe naudadisi ili kuhakikisha kuwa ardhi husika haijakaliwa tayari kimila. Kinadharia,huu ni mkakati muhimu wa kulinda haki za radhi za watu wa kiasili. Hata hivyo,utumizi wa ardhi kimila wa watu wa kiasili bado haujawahi kuzingatiwa katikaudadisi kama huu, ambao kwa jumla unahusisha kutundika mabango na ilanihadharani, pamoja na ziara za nyanjani ili kuangalia kama kuna isharazinaoonekana za ardhi husika kukaliwa au kutumiwa. Kwa kuwa ardhi ya watuwa kiasili aghalabu kwa watu wanje huonekana kama isiyokaliwa, hii imekuwasababu ya kuptea kwa sehemu kubwa ya radhi za watu wa kiasili – ama kupitiakwa ardhi hizo kugeuzwa kuwa maeneo yaliyolindwa, au kupitia kwa kutwaliwana watu binafsi au jamii zingine.

102

Page 119: First page ILO.fm

Changamoto zaidi katika kutekeleza haki za kimila za watu wa kiasilikuhusu ardhi Afrika ni utumizi wa dhana ya ardhi zinazotumika ‘kiuzalishaji’.Wakati ambapo katika nchi nyingi haki ya kimila kuhusu ardhi inaonekanakama kweli, sehemu kubwa ya sharti hili ni kwamba ardhi hizo lazima ziwe‘zalishi’. Dhana ya uzalishaji inayotumika hapa aghalabu inakinzana na mbinu namkondo wa utumizi wa ardhi za watu wa kiasili, hasa kuhusiana na watu wakuhamahama. Nchini Chad kwa mfano, haki za kimila kuhusu ardhizinatambuliwa kwa mujibu wa sheria ya nambari 24 ya Julai 24, 1967. kifungucha 15 cha sheria hii kinasema kikamilifu kuwa haki kuhusu ardhi ambazohazitumiki vizuri zinaweza kupokonywa na serikali, na kubatilishwa na amakulipwa fidia au na aina nyinge za haki.

Katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, uanzishaji wa maeneoyaliyolindwa, hivi karibuni (Réserve de Faune de Lomako-Yokokala) ulifuatiauchunguzi uliofanywa kuhusu ‘ardhi ambazo hazina mtu’ ambazo hazikutiwasahihi na jamii wenyeji, bali na mawakala wa serikali za mitaa. Amri yaWizara346 ambayo iliyoanzisha maeneo yaliyolindwa haitaji kama jamiizinazoathiriwa zilishauriwa. Mara tu zinapotangazwa kuwa wazi, ardhi za watuwa kiasili zimegeuzwa kwa matumizi mengine bila wao kufidiwa.347

Masharti yanayofaa kutekelezwa ili kusajilisha ardhi ni magumu sana kwawatu wa kiasili nchini Kameruni kwani hawawezi kupata kibali za chakusajilisha ardhi zao iwapo ‘hazitumiki kiuzalishaji’.348 Jambo hili, kwa Wabakana Banyeli wa Kameruni, linamaanisha kuwa wana nafasi ndogo sana yakuhitimu kwa haki za kusajilisha ardhi tukizingatia maisha yao ya kuhamahama.Hata kama Agizo nambari 74/1349 linatoa uwezekano wa kikundi cha watukuwa kama kitu halali, bado ni vigumu kwa watu wa kiasili kutekeleza mashrtiili waweze kuwasilisha maombi ya kusajilisha ardhi. kwa hivyo, si mchakato,ambao ni mrefu sana na unahitaji kutolewa kwa taarifa nyingi ya kitaalamu,wala haki inayotolewa na sheria hii vinashughulikia kikamilifu mahitaji ya watuwa kiasili.

Vile vile, wakati ambapo sheria iliyoandikwa inagawa ardhi kama zaseriakali za ardhi zisizo za umma nchini Burundi, baadhi ya utumizi wa kimilaunavumiliwa. Msisitizo, hata hivyo, ni juu ya umiliki dhahiri wa ardhi, na utumiziwa kiuzalishi wa ardhi ambazo zimependekezwa kusajiliwa. Katika mkumbouu huu, Sheria Kuhusu ardhi ya Jamuhuri ya Kedemokrasia ya Kongoinatambua haki za kumiliki na kutumia ardhi, kulingana na mila na utumizi wawenyeji, za jamii wenyeji wanaoishi, wanaolima au kutumia sehemu maalumya ardhi – kibinafsi au kwa pamoja.350 Hata hivyo, sheria pia inasema kuwazile ardhi zinazochukuliwa kama ziko wazi zafaa kupewa kwa serikali.

Kifungu cha 7 cha sheria ya asili kuhusu usimamizi wa ardhi nchiniRwanda351 kinakubali utambuzi wa umiliki wa kimila wa ardhi ya wale ambaowameirithi kutoka kwa wazazi wao, wameipokea kutoka kwa mamlaka

346. Nambari. 024/CAB/MIN/ECN-EF/2006 ya 26 Juni2006.347. R Busane (2006) Gestion des aires protégées et conflictualité. Recherche sur l’impact de la

domanialité publique sur les activités socioéconomiques des terroirs villageois du Sud Kivu, UCB10.

348. Kifungu cha 11(3) cha amri nambari. 2005/481 (16 Disemba 2005), kikirebisha vipengeeFulani katika Amri nambari 75/165 (27 Aprili) 1976 na kuorodhesha masharti ya kuoatahati ya umiliki wa ardhi na kupiga marufuku kabisa kuandikisha hati ya umiliki wa ardhiambazo hazimilikiwi wala kutumiwa.

349. Kifungu cha15.350. Vifungu 388 na 389 vya Sheria ya Ardhi.351. Loi organique no. 08/2005 du 14/07/2005 portant régime foncier.

103

Page 120: First page ILO.fm

yanayofaa, au kwa njia nyinginezo zinazotambuliwa, ikiwa ni pamoja naubadilishanaji na kuuza.

Sheria ya kimila inaendelea kuwa na umuhimu mkubwa kwa mujibu wahaki kuhusu ardhi katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati. Utawalwa umejengwakwa kanuni kwamna wale wanao tangulia kufyeka sehemu ya ardhi kwa ajili yakulima wako na haki ya sehemu hiyo.352 Sheria iliyoandikwa ina nguvu paleambapo kunatokea utata katika kanuni za kimila. Umiliki wa kimila, hata hivyo,una uzito fulani katika kusuluhisha migogoro kisheria. Tangu zamani kanuni yautumizi na umiliki inaweza kusababisha haki za umiliki zinazotambulikakisheria. Kanuni hii imewafaidi raia wengi, lakini kutokana na ubaguzi na chukidhidi ya watu wa kiasili, ni wachache sana wamefaidika.

Sheria kuhusu Kanuni za jumla zinazotumika katika upande wa umma nataratibu kuhusu ardhi,353 ya Jamuhri ya Kidemokrasia ya Kongo ina uvumbuzikadhaa ambao unaweza kufaa katika kukuza haki za watu wa kiasili:

Wa kwanza ni utambuzi wa haki za kimila ambazo zimekuwepo kwanziakitambo (le régime foncier garantit la reconnaissance des droits coutumierspréexistants non contraires ou incompatibles avec des titres dûment délivrés etenregistrés).354

Wa pili ni utambuzi wa hulka ya upamoja na kibinafsi ya haki za kimilamkuhusu ardhi (Ce régime fixe les modalités de constatation et d’établissement desdroits fonciers coutumiers, qu’ils relèvent d’appropriation individuelle oucollective).355

Wa tatu ni utoaji wa hati za umiliki za ardhi zinazotambulika kuwazinamilikiwa kimila.356 Ni muhimu pia kutaja hapa kuwa, kinyume na sheriazingine katika nchi za Afrika zinazozungumzia utumizi ‘zalishi’ wa ardhi, hiihaifanyi hivyo.

Nne, sheria pia inazungumzia hati za umiliki ambazo zimepeanwa kwawatu wanaowakilisha jamii zao.357 Hata hivyo, hii inaweza kuwakilishachangamoto hivi kwamba hususan Mbilikimo wa kiasili hawana mfumowowote wa kijamii ambapo mtu kama huyu anaweza kuteuliwa ili kupewahazi za mashamba kwa niaba ya jamii.

7.5 Maliasili

Kama tunavyoona hapo juu, pana mifano mingi ambapo katiba ya taifa inasemakuwa serikali pekee yake ndiyo inayomiliki madini na raslimali zingine naumiliki hasa wa raslimali zilizochini ya ardhi ndiyo hali ya mifano yoteiliyochunguzwa katika utafiti huu. Mfumo wa kimataifa wa kulinda haki zawatru wa kiasili unatambua hali hii huku ukiruhusu watu wa kiasili na makabila

352. NEPAD et FAO, République Centrafricaine: Programme national d’investissement à moyenterme (PNIMT), TCP/CAF/2905 (I), (NEPAD Ref. 05/43 F), Disemba 2005.

353. Loi No. 10-2004 du 26 mars 2004 fixant les principes généraux applicables aux régimesdomanial et foncier.

354. Kifungu cha 31 cha Sheria kuhusu Kanuni za Jumla zinazoweza kutumika kwa Umm naTaratibu za Ardhi: ‘utaratibu wa kumiliki ardhi unatambua haki ya kitamaduni ambayoimekuweko tangu kitambo ambayo haiendi kinyume hati ya kumiliki ardhi ambayoimekwisha kupeanwa na kusajiliwa’.

355. Kama hapa juu: ‘utaratibu huu unaweka mtindo wa kutambua na kutekeleza haki za kimilakuhusu ardhi, ziwe zinahusu umiliki wa kibinafsi au wa pamoja’.

356. Kama hapa juu, kifungu cha 23.357. Kama hapa juu, kifungu cha 34.

104

Page 121: First page ILO.fm

kuwa na usemi kuhusiana na jinzi raslimali hizi zinafaa kutumika. Kanuni yakwanza ni ile ya mashauriano. Mashauriano yafaa kuwepo hata kabla yakutumia raslimali zilizoko kwenye ardhi za watu wa kiasili, shughuli ambayoinaweza kuwa yenye kuharibu. Katika hali nyingi, kama inavyoonekana katikamifano mingi katika sura hii, serikali pia inamiliki ardhi yote ndani ya mipaka yakitaifa, au inamiliki sehemu maalmu za ardhi – sehemu ambazo nyingizinakaliwa na watu wa kiasili. Yote haya yana athari kadhaa kwa watu wakiasili, hususan pale inpohusu raslimali za chini ya ardhi. ijapokuwa hivyo,kama inayoelezwa hapa chini, pana nafas ya watu wa kiasili kupata, kutumia nakusimamia maliasili zilizo katika ardhi zao na kushiriki katika faida za kutumiahatika hali zingine.

Mfumo wa sheria kwa jumla

Kuhusiana na mifumo ya mkisehria kwa jumla, katiba ya Chad inathibitishaumiliki wa maliasili na serikali pekee. Kifungu cha 57 cha katiba kinasemakuwa:

L’Etat exerce sa souveraineté entière et permanente sur toutes les richesses et lesressources naturelles nationales pour le bien-être de toutes la communauténationale. Toutefois, il peut concéder l’exploration et l’exploitation de cesressources naturelles à l’initiative privée.358

Hiki kinasaidiwa na kifungu cha 3 cha sheria kuhusu uchimbaji madini,359

ambayo inasema kuwa:

Les gîtes naturels de substances minières contenues dans le sous-sol ou existanten surface sont, sur le territoire de la République du Tchad, la propriété de l’Étatet, sous réserve du Code minier, ne peuvent être susceptibles d’aucune formed’appropriation privée.

Sheria kuhusu migodi na madini ya nchini Botswana360 pia katika kifungucha 3 inasema kuwa haki zote kuhusu madini niko katika serikali. Katikamwaka wa 1969 ya Petroli (Kanuni za uchimbaji na uzalishaji) ya nchiniNigeria inaruhusu uchimbuaji wa mafuta kutoka katika maji ya taifa na katikaardhi ya Nigeria na kutia umiliki wa mapato yote ya raslimali za pwani na barakutokana katika serikali ya shirirkisho na mambo mengineyo yanayoambatananayo. Waogoni, Ijau na wachache wanaoathiriwa pamoja na makundi ya kiasiliwanadai kuwa sheria hii inawatenga na utajiri wao wa mafuta, dai ambalo kwakiasi limesababisha kuwepo kwa mpango wa mgao wa asilimia 13 ya mapatokutokana na mafuta. Baina ya kituo cha haki za kijamii na kiuchumi SERAC) naKituo cha haki za kiuchumi kwa haki za kiuchumi na kijamii (CESR) dhidi yaNigeia, Tume ya Afrika ilishikilia kwamba serikali ya nigeria imekiuka haki zajamii ya Ogoni za kuuza mali na maliasili yao.361

358. Serikali inatumia mamlaka yake yote nay a kudumu juu ya mali raslimali zote za kitaifa kwaajili ya ustawi wa jimii ya kitaifa kwa jumla. Hata hivyo, serikali inaweza kuruhusu wahusikawa kibinafsi kugundua na kutumia maliasili.

359. ‘mashapo ya madini chini ya ardhi au juu ya ardhi, ndani ya mipaka ya Jamuhuri ya Chad nimali ya serikali na, ila iwe tu imeidhinishwa kivingine katika Sheria kuhusu madini,yanaweza kumikiwa kibinafsi bila vikwazo’. (Loi n°011/PR/1995 du 20 juin 1995).

360. Sheria ya nambari 17 ya Julai 1999.361. Angalia Arifa ya 155/96, angalia pia J Nwobike ‘The African Commission on Human and

Peoples’ Rights and the Demystification of Second and Third Generation Rights under theAfrican Charter: Social and Economic Rights Action Center (SERAC) and Economic Rights ActionCenter for Economic and Social Rights (CESR) v Nigeria’ (2005) 2 African Journal of Legal Studies129-146.

105

Page 122: First page ILO.fm

Wakati mwingine, umiliki wa raslimali unaenda hatua zaidi hivi kwambamfumo wa sheria ya kitaifa unaweza kuruhusu kwamba taifa lishikilie umilikiwa raslimali zingine za kiasili. Katiba ya Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo,kwa mfano inasema kwamba:

L’Etat exerce une souveraineté permanente notamment sur le sol, le sous-sol, leseaux et les forêts, sur les espaces aérien, fluvial, lacustre et maritime congolaisainsi que sur la mer territoriale congolaise et sur le plateau continental.362

Kifungu cha 23(2) cha katiba ya Eritrea inasema kuwa ardhi na maliasiliyote chini na juu ya ardhi ya taifa ya eritrea ni ya serikali na hisa za raia katikaardhi zitaamuliwa na sheria. Kifungu cha 8(3) kinasema kuwa serikali inawajibu wa kuasimamia ardhi, maji, hewa na maliasili yote na kuhakikisha kuwavinasimamiwa kwa njia sawa na ya kudumu ; na kuunda hali nzuri kuhakikishakushiriki kwa watu katika kulinda mazingira. Kulingana na shughuli hizi zauchimbaji madini, hasa kwa upande wa maeneo yanayohusu maslahi yakihistoria, kitamduni au kidini.363 Leseni haiwezi kutolewa kwa sehemuyoyote ambayo imo katika eneo la mita 100 la eneo muhimu kiakiolojia,kitamduni au kijamii isipokuwa kama Mamlaka ya kutoa leseni imeamua(kifungu cha 13(1)) hivyo.

Katiba ya sasa ya Kenya haizungumzii sana kuhusu maliasili. Hata hivyo,kwa mujibu wa sheria, maliasili ambayo ni pamoja na madini, wanyamapori,maji, misitu ya kitaifa ni vya serikali.364 Sehemu kadhaa za sheria zinathibitiupataji usimamizi na, utumiaji wa maliasili nchini Kenya.365 Raslimali za kitaifaambazo kwa sasa ziko katika maeneo ya watu wa kiasili ni pamoja na mbugaza kitaifa, hifadhi za wanyamapori na raslimali za madini. Watu wa kiasiliwanataka kushauriwa na kuhusishwa katika kusimamia raslimali na kushirikifaida zinazotokana nazo. Mbali na mbuga ya wanyama ya Maasai Mara ‘ambapoinasemekana kuwa asilimia 19 ya ushuru unaokusanywa unawekezwa kwa ajiliya jamii ya Wamaasai’, watu wengi wa kiasili wanadai kuwa hawahusishwi naserikali haishiriki nao mapato yanayotokana na raslimali zilizoko katikamaeneo yao.366 Kulingana na ripoti ya katibu maalum wa umoja wa mataifakuhusu athari za miradi mikubwa kwa haki za watu wa kiasili, watu wa kiasilinchini Kenya wamelalamika kuwa ‘kuanzishwa kwa mbuga za wanyama auhifadhi za wanyama kumewalazimu watu hawa kutoka kwenye ardhi zao.367

Ripoti hii inatoa mfano wa Waborana ambao wameshuhudia kuwa hifadhi nneza wanyama zilizoanzishwa kule Isiolo zilianzishwa kwa nguvu hivyo kuathirimaeneo muhimu ya malisho na maji ambayo awali yalitumika na wafugaji.368

Nchini Algeria, raslimali nyingi za kiasili zainapatikana katika maeneo ya

362. Kifungu cha 9cha katiba ya DRC: ‘serikali ina uwezo juu ya mchanga juu ya ardhi, chini yaardhi, maji, misitu, anga ya Kongo, mito yake, maziwa na sehemu za majini pamoja nabahari ya nchi ya Kongo na nchi kavu’.

363. Tangazo la kukuza maendeleo ya raslimali za madini, Tangazo nambari No. 68/1995,kifungu cha 6.

364. Tazama sehemu ya 115(1) ya Katiba ya Kenya.365. Sheria kama hii ni pamoja na Sheria kuhusu (uhifadhi na usimamizi wa) wanyama pori

(kifungu cha 376), Sheria kuhusu Uchunguzi na Uzalishaji wa Mafuta (kifungu cha 308),Sheria ya Usimamizi wa Mazingira (kifungu cha 8 cha mwaka wa 1999, Sheria ya misitu yamwak wa 2005, sheria kuhusu maji ya mwaka wa 2005, Sheria mamlaka ya maendeleo yaBonde la Kerio (kifungu cha 441), Sheria ya Mamlaka ya maendeleo ya Lake Basin (kifungucha 442), Sheria ya maendeleo ya Mto Tana na Athi (kifungu cha 444), Sheria yaMaendeleo ya eneo la Mto Ewaso Ng’iro kaskazini (kifungu cha 448) na Sheria yaMaendeleo ya Pwani (kifungu cha 449).

366. Angalia Ripoti ya Katibu maalumu wa Umoja wa mataifa kuhusu watu wa kiasili nchiniKenya, aya ya 48-54.

367. Anagalia Ripoti ya Katibu maalumu wa Umaoja wa Mataifa kuhusu watu wa kiasili juu yaathari ya Miradi mikubwa mikubwa, aya ya 23.

368. Kama hapa juu.

106

Page 123: First page ILO.fm

Waamazi. Hata hivyo, hawafaidiki sana kutokana na raslimali hizi. Kwa mfano,mabwawa kadhaa yameundwa katika makaazi ya Waamazi ili kuhudumiasehemu za miji. Kwa hivyo jamii za maeneo hayo yanapata faida ndogo sana auhata hawafaidiki kabisa kutokana na raslimali hii.

Kifungu cha 35 cha katiba ya Burundi kinazungumzia utumizi kiasi wamaliasili, uhifadhi wa mazingira na uhifashi wa raslimali kwa ajili ya vizazivijavyo. Kulingana taarifa ya waziri anayehusika na uhifadhi, ardhi katikamaeneo yanayotazamiwa kuwa hifadhi za kiasili yanafaa kutwaliwa na serikalina wakaaji wake kuhamishiwa kwingineko.369 Kulingana na haya haielekeikuonyesha kuwa maslahi ya watu wa kiasili yamefikiriwa kwa njia yoyote.Sheria nambari 04/2005 kuhusu taratibu za kulinda, kuhifadhi na kukuzamazingira nchini Rwanda inazipa jamii wenyeji wajibu wa kulinda mazingira.370

Wajibu wa kufanya uchunguzi kuhusu athari za kimazingira umo kwenyesheria,371 lakini hazungumzii taratibu zozote za kufanya mashauriano aukushirikisha jamii za wenyeji katika mchakato kama huu.

Katika nchi ambazo tayari kuna utambuzi mchache wa haki za watu wakiasili kumiliki au kutumia ardhi, kuna athari hasi kwa uwezekano wa watuhawa kupata na kutimia maliasili yaliyo kwenye ardhi wanakalia au kutumia.Katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Amri nambari 84.045 kuhusu ulinzi wawanyama wa mwitu na uthibiti wa uwindaji inasema kuwa maliasiliyanayopatikana katika ardhi inayomilikiwa na serikali ni ya serikali. Leseni yakuwinda inahitajika ili kuwinda, isipokuwa kwa wale walio na haki ya kimila.Katika mfano huu wa pili, wale walio na haki kimila wanakumbana na vikwazokadhaa kuhusiana na aina ya wanyama wanaofaa kuwinda na silahawanazoruhusiwa kutimia.372

Raslimal za misitu

Kuhusiana na raslimali za misitu, sheria ya misitu ya Jamuhuri ya Afrika yaKati373 inatofautisha ya misitu ya kijumuiya nay a kibinafsi kutoka kwa misituya serikali. Misitu ya serikali inahusisha hifadhi za wanyama na aina nyinginezoza misitu iliyolindwa, sura ya II ya sheria hii inataja waziwazi kwamba jamii zinahaki za utumizi za kimila pekee kwa ardhi zao ili kukimu mahitaji yao – kwamaliasili bali si kwa raslimali zilizochini ya ardhi:

Les populations locales continuent d'exercer leurs droits coutumiers d'usagegratuitement en se conformant aux dispositions de la présente loi, de laréglementation en vigueur et des règles coutumières. L'exercice des droitscoutumiers d'usage est strictement limité à la satisfaction des besoin personnels,individuels ou collectifs des usagers.374

369. Groupe de travail d’experts de la Commission africaine sur les populations/communautésautochtones, Rapport de la Visite de recherche et d’information en République du Burundi : 27mars – 9 avril 2005 (2007) 24.

370. Kifungu cha 64. 371. Kifungu cha 67.372. Vifungu 34, 37 et 38 vya Ordonnance n°84.045 du 27 Juillet 1987 portant protection de la

faune sauvage et réglementant l’exercice de la chasse en République Centrafricaine.373. Sheria namabari. 90/003, 9 Juni1990. 374. Code forestier: ‘Wenyeji wanaendelea kutumia haki zao za kimila za utumizi huru maadamu

wanafanya hivyo kulingana na vipengele vya sheria iliyopo, kanuni za sasa na za kitamaduni.Kutumia haki za utumiizi wa raslimali za misitu kitamaduni kunajifunga kwenye haja yakutosheleza mahitaji watumizi, ya mtu binafsi au ya pamoja.’

107

Page 124: First page ILO.fm

Aidha, haki za kimila zinazotolewa na sheria hii zinatoa tu ainafulani za hakiza utumizi, yaani: kukusanya kuni kavu, kuokota matunda au mimea ya tiba,kutumia miti kwa ajili ya kujengea nyumba au kuunda vyombo fulanifulani.375

Zaidi ya hayo, kifungu cha 12 cha sheria ya misitu kinazuia jamii za wenyejikuishi katika ardhi ambazo zimegeuzwa kuwa mbuga za kitaifa za wanyama.Aidha, sheria hii inazuia shughuli zozote kando na zile zinazolenga uhifadhi wamisitu katika maeneo hayo.

Mtu haruhusiwi kuishi katika m buga za kitaifa na misitu ya burudani nahakuna shughuli yoyota inaweza kufanywa mbali na zile shughuli muhimukwa usimamizi, uhifadhi au kwa kurejeshwa kwa mali ya kiasili, ambayo ndiyoshabaha ya kuanzishwa kwa mbuga hizi za wanyama. (Dans les parcsnationaux et les forêts récréatives, nul n'est admis à résider de façonpermanente et aucune activité autre que celles nécessaires àl'aménagement, à la conservation ou à la restauration des richessesnaturelles, objet de la création, ne peut être entreprise.)

Uamuzi wa baraza la mawaziri nchini Rwanda376 linaonyesha mipaka yambuga ya kitaifa ya Akagera, zaidi ya kurejesha na mahitaji ya ardhi ya watuwaliofidiwa. Rasimu ya sheria ambayo itaonyesha mipaka mipya iliyopunguzwaya mbuga hiyo, inaundwa.377 Hata hivyo, hakuna hatua yoyote ambayoimechukuliwa kuhakikisha kuwa Wabatwa wanahusishwa katika mipangoyoyote inayohusiana na Mbuga hiyo, licha ya wao kutegemea maliasiliyaliyomo katika mbuga hiyo na kuishi kwao katika eneo hili tangu kale.

Sheria ya misitu ya Jamuhuri ya Afrika ya Kati inafasili misitu tu kuwa ni ileambayo imegawanywa kwa njia ya amri kwa niaba ya jumuiya fulani auimepndwa miti upya au kuhifadhiwa na jumuiya husika. Misitu ya kibinafsi ni ileambayo imepandwa na watu binafsi kwenye ardhi yao kulingana na sheria.Kulingana na uelewa huu, jumuiya ni maeneo, wilaya, kata na jamii. Vijijihavihesabiwi kama jumuiya kulingana na haya, jambo ambalo linaondoauwezekano wa jamii yoyote ya kiasili kudai au kusimamia msitu wa jumuiya.Hata hivyo, hali ni tofauti kabisa katika nchi zingine katika kanda hii kama vileKameruni, na DRC. Hapa, hata kama watu wa kiasili hawana sheria kama zilezilizomo kwenye sheria ya kimataifa inayowafaa kuhusiana na maliasili, kunataratibu za misitu ya kijamii ambazo zinawazadia kufikia na kuwa na haki kidogokwa raslimali fulani.

Katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, taratibu za kijamii kuhusumisitu pia zinabashiriwa kama njia ya jamii za wenyeji kutumia raslimali katikamaeneo ya misitu. Kifungu cha 22 cha sheria ya misitu kinasema:

Jamii ya wenyeji, ikiomba, inaweza kupata sehemu au msitu mzima ambaowanaoumiliki kila mara kidesturi kwa kupata ridhaa ya kumiliki. (Unecommunauté locale peut, à sa demande, obtenir à titre de concession forestièreune partie ou la totalité des forêts protégées parmi les forêts régulièrementpossédées en vertu de la coutume.)

Utaratibu wa misitu ya kijamii unaruhusu kutumia raslimali ambazozinaweza kuwa na umuhimu mkubwa kwa watu wa kiasili na kisha unawezakutumika kama msingi wa kuimarisha haki zao za ardhi. hata hivyo kuna misituya kijamii michache sana katika Afrika ya Kati, kwa mfano, ambayoimetengewa jamii ya kiasili na nchi kadhaa zilizo na sehemu kubwa za misitu

375. Vifungu nambari 20 et 21 vya Code forestier.376. 29 Julai 1997.377. Rwanda, Ministère des terres, de la Réinstallation et de l’environnement, Stratégie nationale et

plan d’action pour la conservation de la biodiversité au Rwanda, Kigali, avril 2003, 28-30.

108

Page 125: First page ILO.fm

bado hazijaanzisha taratibu kama hizi. Changamoto anuwai badozinawakumba watu wa kiasili wasiweze kufaidika kutokana na nafasi hii, ikiwani pamoja na namna ambavyo msitu hii inasimamiwa, na njia za kuzuiaunyakuzi wa sehemu kama hizi na watu walio na uwezo katika jamii, nimasuala ambayo bado hayajapata suluhisho.

Kifungu cha 5 cha Sheria ya Misitu ya nchini Gabon inashughulikia misituya kijamii, ambayo inaifasili kama eneo la msitu ambalo limeten gewa jamii yakijiji fulani kwa nia ya kufanya shughuli za kuleta usimamizi unaofaa wamasliasili kwa msingi wa mpango sahili wa usimamizi.378 Ombi la kutakakuunda msitu wa kijamii lazima lihusishe stakabadhi kuhusiana na ombi lajamii, ikiwa ni pamoja na ramani ya eneo husika.379 Masharti haya yanawezakuwatenga watu wa kiasili tukizingatia viwango vya chini vya kujua kusoma nakuandika kati yao na tofauti za dhana ya uwakilishi wa jamii baina ya watu wakiasili na watu wengine, pamoja na aina mbalimbali za ubaguzi.

Jamii zina haki chini ya sheria hii, cha kukusana baadhi ya mazao ya misitubila kuruhusiwa, ingawa mazao kama haya yanapasa yawe ya matumizi yakibinafsi au ya kijamii. Kwa watu wa kiasili hususan, ikichukuliwa kuwa mapatowanayoyapata hasa ni kutokana na kuuza mazao ya misitu kama vile kuni,mawindo, Njansang (Ricinodendron heudelotii), asali, mianzi na mimea ya tiba,kupiga marufuku uuzaji wa vitu kama hivi unazua matatizo makubwa.

Katika muktadha wa mradi wa kuhifadhi maliasili wa Jamuhuri ya Afrika yaKati, ambao umechangia kuanzishwa kwa hifadhi maalum ya msitu mzito waDzanga Sangha, majiribio yamefanywa kuhusisha jamii wenyeji na wa kiasili.Sheria ya 93/13, kwa mfano, ambayo ilianzisha ukanda wa kimajaribio waSangba haitaji jamii wenyeji katika kifungu cha 3:

Ukanda wa majaribio wa Sangba una shabaha ya kubainisha, kufanyiamajaribio na kuendeleza mbinu anuwai za utumizi unaofaa wa maliasili ilikuhakikisha kuwa – kwa mkabala wa maendeleo ya kudumu – kuna manufaathabiti kwa manufaa ya umma kutokana na harakati za uhifadhizilizoanzishwa katika ukanda wa kaskazini (La Zone Pilote de Sangba a pourbut d'identifier, de tester et de promouvoir les modes divers d'utilisation rationnelledes ressources naturelles renouvelables afin de garantir, dans une optique dedéveloppement durable, les retombées concrètes au bénéfice des populations à lasuite des actions de préservation mises en place dans la région Nord.)

Kifungu cha 4 cha Amri hii kinasema ifuatavyo:

Shughuli zilizopendekezwa zitafanywa kwa ushirikano na jamii zinazoishikatika maeneo ya maji ili kupata kibali chao na kushirikishwa katika shughuliza maendeleo katika eneo hilo. (Les activités proposées seront menées enétroite collaboration avec les populations riveraines afin d'obtenir leur adhésion etleur participation aux actions de développement de ladite région.)

Moja wapo ya malengo mahususi ya Hifadhi maalum ya Dzanga Sangha,ambalo ni nadra sana katika muktadha wa Kiafrika, ni kushughulikia mahitaji yajamii za wenyeji kuhusiana na utumizi mzuri na wa kudumu wa maliasili.Kamati ya maendeleo ya Bayanga iliundwa kwa nia ya kuwakilisha maslahi yajamii wenyeji katika mpangilio mzima wa hifadhi hii. Hata hivyo, ... ‘Kamailivyomafano wa zones cynégétiques villageoises, comité de développement (kamati yamaendeleo) ya Bayanga inabakia kuwa zao la uzimamizi wa hifadhi ya msituambao unapangilia na kuifanya kuendelea kufanya kazi.’380

378. Kifungu cha 156 cha Code forestier.379. Kifungu cha 162 cha sheria kuhusu misitu.

109

Page 126: First page ILO.fm

Nchini Kameruni, kama ilivyo katika nchi zingine, jamii za kiasilizinategemea sana maliasili kujikimu. Sera kuhusu Misitu ya mwaka wa 1993,inabashiri kiwango kikubwa cha kushirikishwa kwa jamii za wenyeji katikauzimamizi wa misitu. Sheria kuhusu misitu ya mwaka wa 1994 ina vipengelevinavyohusu namna ya kuhusishwa kwa jamii za wenyeji hadi kiwango hiki,pamoja na kuhusiana na misitu ya kijamii na uwindaji na ushuru kwa matumiziya kiviwanda ya misitu.

Hata hivyo, wakati mwingi imegundulika kuwa vipengele hivi vilivyowekwakuzilinda haki za jamii wenyeji za kusimamia baadhi ya raslimali havifanyi kazi,

380. ‘… comme dans le cas des zones cynégétiques villageoises, le comité de développement de Bayangareste une création de l’administration de la réserve qui l’organise et le fait fonctionner’ (GTZ, Étuderessources naturelles 24).

Misitu ya kijamii nchini Kameruni

Ibara za kisheria nchini Kameruni kuhusu misitu ya kijamii ni mfano wa jinsimara nyingi sheria haizingatii hali maalumu ya watu wa kiasili, na wakatimwingine, kuonyesha mtazamo wa kibaguzi dhidi ya njia za maisha yao, haliinayofanya kuwa vigumu kwao kufaidika kutokana na sheria hiyo. Tangukupitishwa kwa Sgeria ya Misitu mnamo mwaka wa 1994, jamii za vijijinizilizoishi katika ardhi inayochukuliwa kuwa ni sehemu ya himaya ya kitaifanchini Kameruni zina haki ya kuwa na misitu ya jamii. Msitu wa jamii nikipande cha msitu wa himaya kitaifa, ambao hauhitaji aina yoyote ya ridhaaya kutumia, wenye eneo lisilozidi hektari 5000 ambao unamilikiwa naserikali lakini inaweza kutoa haki za usimamizi kwa jamii ya kijiji kwa kipindicha miaka 25 kinachoweza kuandikishwa tena. Makubaliano baina ya jamiiinayopokea na serikali ambayo yanaandamana na mpango sahili wausimamizi kulingana ambao shughuli zote katika msitu wa jamii zitafuata.

Mazao yote yam situ wa jamii ni mali ya jamii hiyo (kifungu cha 37 (3) na67 (2)). Utumizi wa mazao hayo uanweza kufanywa moja kwa moja aukupitia kwa aina ya kufanya kandarasi ya muda (kifungu cha 54). Licha yakuwepo kwa vipengele hivi, mfumo wa kidhahania, kisheria na kiutendaji wamsitu wa jamii una matatizo kwa watu wa kiasili kwa sababu zifuatazo:

• Mojawapo ya masharti yaliyokwisha wekwa kabla ya kupata msituwa jamii ni kuteua taasisi wakilishi ya jamii hiyo. Aidha, ombi lakutaka msitu wa kijamii ni tata na ina masharti kadhaa ya kiufundi,yakiwemo ramani ya eneo hilo na mpango wa usimamizi. Jamii za‘Mbilikimo’ kwa jumla huwa hazina elimu ya kutosha ili kuwezakutosheleza mashari haya.

• Misitu ya jamii haiwezi kupatikana ila mpaka jamii inayowasilishaombi hili iwe na haki za kimila za kiardhi ambazo zimekuwekokwanzia kitambo. Kijumla, jamii za ‘Mbilikimo’ zinazoishi kandokando mwa mabarabara hawana haki yoyote ya kimila kuhusuardhi, kwani ni jamii za kibantu ndizo zilizo na haki hizi. KatikaHifadhi ya misitu ya Kudumu, ambako ‘Mbilikimo wangekuwa nauwezekano mkubwa wa kudai haki za kimila, sheria haihalalishimisitu ya jamii. Kwa hivyo, ‘Mbilikimo wametengwa sana kutokakwa wale wanaofaidika na haki kama hizi.

• Kiwango kikubwa zaidi cha msitu wa jamii ni hekta 5000. Hikihakitoshi jamii za ‘Mbilikimo’ ambao aghalabu hutumia sehemukubwa kwa shughuli zao za kutafuta riziki na ni wahamahamaji.

110

Page 127: First page ILO.fm

hasa kuhusiana na Mbilikimo, kwani havizingatii upekee wa utamaduni wao nawamepuuzwa sana katika hatua zote za mchakato mzima. Ubainishaji wa kiasicha eneo lililopo kutumiwa hauzingatii maeneo yao ya uwindaji, au maeneoyao ya kuhamia kwa muda. Vigezo vya pekee vinavyotumiwa katika kubainishamaeneo ya ardhi vinategemea makadirio ya kiuchumi na sio ya kijamii wala yakitamaduni.

Katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,381 sheria kuhusu misituinaruhusu haki za kimila za utumizi wa maliasili, ijapokuwa ni finyu:

les droits d’usage forestier des populations vivant à l’intérieur ou à proximité dudomaine forestier sont ceux résultants de coutumes et traditions locales pourautant que ceux-ci ne soient pas contraires aux lois et à l’ordre public.382

Hii ingeweza kuwa nafasi nzuri kwa watu wa kiasili, kama hawangekuwapia wanakumbwa na changamoto ya kutaka vijji vyao kutambulika kama hakiyao. Kwa jumla, vijiji hivi vinachukuliwa tukama sehemu ya vijiji vya Wabantuvilivyopo, na wazo la kuwa na kijiji halifai katika maisha ya watu wa kiasili. Kwahivyo, hawawezi kufaidika kikamilifu kutokana na vipengele vilivyo katikasheria ya misitu.

Sheria kuhusu misitu inatofautisha baina ya misitu ilyoanishwa, misituiliyolindwa na misitu ya uzalishaji wa kudumu. Misitu iliyolindwa ni ile ambayohaijatengwa kwa ajili ya jukumu mahususi, na haijaainishwa. Ni katika maeneohaya ndiko kuna haki za utumizi kwa wingi kwa ajili ya jamii za wenyeji(zikiwemo jamii za watu wa kiasili). Ubainishaji baina ya aina hizi mbili zamisitu ni muhimu kwa watu wa kiasili kwa upande wa kuhakikisha kuwa ardhizao za kitamadunu hazigeuzwi kuwa misitu iliyoainishwa na hivyo kuwanyimahaki zao. Misitu ya uzalishaji wa kudumu ni sehemu ya misitu iliyolindwaambayo imetolewa baada ya kuudadisia umma, na kuamuliwa kuwa inawezakutumiwa. Maeneo mengi kama haya ni miliki, pamoja na haki za utumizi kwakufuatana na mipaka fulani. Kulingana na kifungu cha 84 cha Sheria kuhusumisitu kandarasi ya kumiliki msitu lazima itanguliwe na uchunguzi wa umma.Hata hivyo chunguzi za umma zinazohusiana na mchakato huu hazizingatiikikamilifu utumizi na umiliki wa ardhi na watu wa kiasili au hata suala la kulipafidia wakati ardhi zao zinapotolewa.

Haki ya kufaidika kutona na ushuru kutoka kwa utumizi wa misitu ni sualajingine ambalo linafungamana na haki ya kutumia raslimali za misitu. Sheriakuhusu misitu haishughulikii hali mahususi za watu wa kiasili, lakini inaruhusuhaki fulani kwa watu wa kiasili kuhusiana na suala hili:

Ujenzi na usimamizi wa njia, upeanaji wa chakula, uwekaji wa nyenzozinazohitajika mahospitalini na za kijamii, vifaa vya usafirishaji wa watu na vitu(la construction, l’aménagement des routes, la réfection, équipement desinstallations hospitalières et sociales; les facilités en matière de transport despersonnes et des biens.)

Suala jingine la kuzua wasiwasi kwa watu wa kiasili ni namna ambamoushuru na riba zinazotokana na misitu zinagawanywa. Kwa mujibu wa Sheriaya misitu, asilimia 40 ya mapato kama haya yanatolewa kwa vyombo vyautawala vilivyogatuliwa, na asilimia 60 kutolewa kwa hazina ya serikali.Asilimia 30 ya asilimia hiyo 40 inayotolewa kwa vyombo vya utawalavilivyogatuliwa, inaenda kwa Mkoa, na asilimia 15 kwa serikali za mitaa katika

381. Sheria ya Nambari. 011/2002 ya Tarehe 29 Agosti 2002.382. Kifungu cha 36 cha Code forestier: ‘haki za kutumia misitu za watu wanaoishi ndani au

maeneo ya karibu na misitu ni matokeo ya mila na desturi mradi mila na desturi hizihazipingani na sheria au utulivu wa umma.’

111

Page 128: First page ILO.fm

sehemu inamopatikana misitu inayotumiwa. Kwa kuwa hakuna eneo rasmi lawatu wa kiasili, na watu hawa hawajawakilishwa kwa kiwango cha jumuiya,huenda watu wa kiasili wasifaidike kutokana vipengele hivi, au vipengele hiviviziafikie shabaha iliyotajwa ya kupunguza umasikini katika maeneo ya misitu,ikiwa jamii masikini kabisa hazitatiliwa maanani.383

Katika Jamuhuri ya Kongo, sheria ya ardhi ya mwaka wa 2004 haitambuihaki za kimila za umiliki isipokuwa haki za utumizi tu, ambazo zinatawaliwa nakifungu cha 41. kama ilivyo na vipengele vya kisheria kuhusu haki za utumizikatika nchi zingine kadhaa, haki ya kugeuza bidhaa za utekelezaji wa haki hiziza utumizi kuwa za kibiashara, inahusiana tu na haki za utumiaji za kibinafsi nakufanyia biashara bidhaa hizi kumepigwa marufuku kulingana na kifungu cha 37cha sheria ya DRC kuhusu misitu.

Kisheria, pana vipengele kadhaa kuhusu haki za utumizi kamainavyobashiriwa katika sheria ya misihtu ambavyo si dhahiri. Kwanza, sheriahii haibainishi wazi ni nani aliye na haki kama hizi. Sheria hii inazungumzakuhusu wenyeji bila kubainisha hasa hii inamaanisha nini, suala ambalolinaweza kuleta wasiwasi kwa jamii asili kama vile watu wa kiasili nchini Kongoambao wanategemea sana raslimali za misitu. Pili, haki za kutumia misitu nifinyu mno na zinatumika tu kwa bidhaa fulani zinazotokana na misitu ambazozinakadiriwa na serikali, ambazo haziwezi kuuzwa na kwa kufanya hivyokunakuwa ni hatia kiulingana na kifungu cha 143. Tatu, sheria hii haionyeshikushirikishwa kwa jamii wenyeji katika faida zozote zinazotokana na utumiziwa misitu.384 Wala hakuna mikakati inayobashiriwa kuhakikisha kuwa kunaajira inayotokana na utumizi wa misitu. Kampuni za kukata miti huingilia katikakatika masuala ya uchumi wa jamii ili kuwafaidi wenyeji, lakini hapana lazima yamambo haya kulenga hususan watu wa kiasili, na matokeo yake ni kwambawatu wa kiasili wanapuuzwa kwa ajili ya mikakati ya kuunda vijiji vya wabantu,ambavyo jamii hizi huwa sehemu yake.

Sheria nambari 48/83 kuhusu uhifadhi na utumizi wa wanyama wa poriinathibiti shughuli za uwindaji. Mfumo huu unaweka vikwazo kuhusu aina zawanyama wanaofaa kuwindwa, licha ya ukweli kwamba kunaweza kuwepo nasababu fulani za kitamaduni za kufanya hivyo. Mfumo huu vilevile unapuuzamethodolojia zilzopo na ujuzi mabao watu wa kiasili wametumia kwa karnenyingi kwa ajili ya kuhifadhi mazingira yao. Hata Sheria ya bunge ya mwaka wa1993 ambayo iliruhusu kuanzishwa kwa mbuga ya kitaifa ya Nouabalé-Ndokiinasema kuwa haki zote katika eneo hilo zimefutiliwa mbali, ikiwa ni pamojana ufyekaji wa mashamba, ukataji wa ‘bois vivants’, uokotaji wa kuni nauwindaji wa kitamaduni.385

Sheria ya misitu ya Gaboni inasema kuwa maeneo yote ya misitu ya kitaifani mali ya serikali.386 Misitu kama hii imegawika katika kategoria mbili: (1)Misitu ya kudumu – ikiwa ni pamoja na ile misitu ambayo imetengwa kwamatumizi, au kuhifadhiwa na serikali; na (2) misitu ya sehemu za mashambani– ambayo ni pamoja na misitu ambayo inaweza kutumika kwa mambo anuwai,ikiwemo misitu ya kijamii. Kwa hivyo, sheria inatambua tu haki za utumizi nawala haitambui haki zozote mali walizo nazo wenyeji kuhusu misitu ya tangu

383. AK Barume 2003, Le nouveau code forestier congolais et les droits des communautés des forêts,Rainforest Foundation www.rainforestfoundationuk.org/files/DRC%20Code%20and%20communities.pdf (accessed 30 November 2008).

384. Kifungu cha 92 cha Sheria hiyo.385. Rainforest Foundation et OCDH, 2006, p. 6 angalia : www.rainforestfoundationuk.org/files/

droits_autochtones_final.pd (iliangaliwa 30 Novemba 2008).386. Kifungu cha 13cha Code forestier gabonais – Sheria Namb. 0016/01.

112

Page 129: First page ILO.fm

mababu zao. Haki za utumizi zinategemea masharti kadhaa387 na kifungu cha252 cha sheria kwa mfano, kinaruhusu haki za utumizi kuhusisha miti yaujenzi, kuni, bidhaa za misitu ambazo si mbao, ulimbo, uwindaji na uvuvi kwaminajili ya shughuli za mila (za kisanaa) na bidhaa zilizobainishwa ambazozinatokana na misitu. Kwa hivyo, pia haki za utumizi finyu, kama ilivyomawanda ya utekelezaji wake. Haki za utumizi, kwa mfano, katika maeneo yamashambani ni huru, lakini zimezuiliwa sana katika misitu ya kudumu.388 Zaidiya hayo, kutekelezwa kwake kunaweza kuzuiliwa na uamuzi wa wizara, haliinayoonyesha ukosefu wa usalama wa kisheria ambao watumizi wa bidhaazinazotokana na misitu wanakumbana nao.

Nchini Gabon, kama ilivyo katika nchi zingine katikati mwa Afrika, ardhi zakitamaduni za watu wa kiasili ni misitu. Gabon imeonyesha nia yake yakupanua uchumi wake kwa kuongeza ushuru unaotozwa kwa misitu.389

Katika muktadha huu, Gabon imekubali mpango wa maendeleo ya watu wakiasili, ambao kati ya mambo mengine, unaonyesha nia ya kuwekea mipakaardhi za watu wa kiasili na kuwalipa fidia kwa ardhi walizopoteza zaidi yakuhahakikisha kuwa wanasgiriki katika kusimamia misitu hiyo.

Uchimbaji wa madini

Katiba za kitaifa aghalabu husema kuwa raslimali zilizochini ya radhi ni zaserikali. Mojawapo ya changamoto kwa watu wa kiasili, na kwa mfumowowote wa kisheria wa kulinda haki zao, ni kuhakikisha kuwa wanahusishwakatika mashauriano kabla ya kuzingatia shughuli yoyote ya kuchimba raslimalikama hizi, na kushiriki kwao faida zinazotokana na shughuli kama hii.

387. Kifungu cha 14 cha Code forestier gabonais.388. Kifungu cha 253 sheria ya misitu. 389. Ili kuendelea na marekebisho haya na kuendesha uingiliaji kati wa washirikadau, mamlaka

za Gaboni ziliamua kuanzisha Mpango wa sekta ya misitu, Uvuvi na Mazingira (SFFE).Mpango huu ni elementi muhimu ya mkakati wa kitaifa wa kupunguza umasikini. Mpangowa SFFP, unatarajiwa kuongeza mchango wa sekta kama sekata ya misitu, uvuvi, uhifadhiwa maumbile na mazingira kwa uchumi wa Gabon.

CIB (Congolaise Industrielle des Bois) ni mojawapo ya kampuni kubwasana za kukata miti na kwamba ina milki kubwa sana za ukataji miti katikaJamuhuri ya Kongo na kwamba milki zake kadhaa zimepewa kibali nabaraza la FSC (Forest Stewardship Council) kwa ukataji miti wa kudumuna hivyo kuitoa CIB kuheshimu haki za watu wa kiasili. Juhudi mpyazinazofanywa na CIB ni pamoja na kushughulikia masuala ya umiliki nautumizi wa ardhi wa watu wa kiasili wa jamii ya Mbendjelle, katikamuktadha wa mipango ya uhifadhi wa misitu. Ijapokuwa shughuli hii badohaijafikia kiwango cha haki za ardhi za kundi hili la watu wa kiasilikudhaminiwa kisheria, maeneo matakatifu, pamoja na himaya zinginemuhimu kitamaduni zimebainishwa katika muktadha wa mpango wa CIB,na zinaweza kuhifadhiwa zizitumike kwa shughuli za kiviwanda. Kulinganana mpango wa Uhifadhi wa UFA kule Kabo, hekta 296,000 zimetengwakwa matumizi ya watu wa kiasili wa jamii ya Mbenzélé pekee pamoja namaeneo yao matakatifu. Hikikaribu ni kitendo cha kipekee katika kandahii, na kinaweza kuleta utambuzi thabitu wa kisheia wa haki zao za ardhina raslimali.

113

Page 130: First page ILO.fm

Sheria za uchimbaji madini za Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongozinaruhusu kufaidika kwa serikali, wilaya, na eneo linalohusika na uchimbajihuo, moja kwa moja kutokana na mapato yanayotokana na uchimbaji wamadini yoyote. Hata hivyo, pia hii haidokezi hasa kuwa watu wa kiasiliwatapata faida yoyote kutokana na shughuli hii kwani hawawakilishi kwenyekiwango cha jumuiya. Hata hivyo, sheria hii ina vipengele ambavyo vingewezakuchukuliwa kama nafasi ya watu watu wa kiasili, kwani ardhi kadhaa zamababu zao zina madini, kama ilvyo mfano wa mbuga ya kitaifa ya KahuziBiega.

Kifungu cha 63 cha sheria za uchimbaji madini za Jamuhuri ya Afrika yaKati390 inazungumzia kanuni ya sheria ambazo zinatolewa kutegemea naumuhimu wa kwanza, zikiwemo zile haki za jamii za wenyeji. Vile vileinazungumzia hitaji la kushauriana na serikali za mitaa na jamii wenyejikuhusiana na haki muhimu kabla ya kutoa leseni ya kuchimba madini.

Nchini Chad, hakuna vipengele vya kisheria vinavyobashiri kuwepo kwamashauriano na wenyeji ambao wanaweza kuathiriwa na shughuli za uchimbajiwa madini, hata utumiaji wa maliasili kwa jumla. Ni sheria kuhusu usimamiziwa mapato yanauotokana na petroli pekee ndiyo inaoonyesha kuwa asilimia 5ya faida kwa wenyeji wa eneo la uzalishaji.391 Pia ni vizuri kutaja kuwa watuwalio katika maeneo ya uzalishaji wa mafuta katika nchi hii hawawakilishwikatika shirika linalohusikana na uangalizi wa mapato ya petroli.392

7.6 Hitimisho

Sheria ya kikoloni ilianzisha aina mpya za taratibu na sheria kuhusu ardhiambazo zilikuwa ngeni kwa waafrika. Hususan, kuanzishwa kwa haki zakibinafsi za kumiliki ardhi, pamoja na kukabidhi serikali ardhi ambazozinamilikiwa na watu wa kiasili kidesturi, au kugatuliwa kwa haki za jumuiyakuhusu ardhi kulikuwa na athari kubwa kwa haki za watu wa kiasili. Taratibumpya kama hizi kuhusu ardhi vilievile ziliinua kilimo na umiliki wa ardhi nawatu binafsi zaidi ya utumizi wa ardhi kwa pamoja, umiliki wa ardhi wakuhamahama, ikiwemo ufugaji na uwindaji-uokotaji. Maadili na taratibu nyingikama hizi zilikubalika, baada ya kufanyiwa marekebisho kadhaa, baada yakupata uhuru. Zaidi ya hayo, baada ya kuanzishwa kwa mikakati ya kuhifadhimaneo yaliyolindwa pamoja na mazingira, wajibu wa watu wa kiasili katikakuhifadhi na kusimamia ardhi kama hizi haukudhaminiwa. Baadhi ya masualana changamoto muhimu kwa haki za watu wa kiasili, yanayohusiana nataratibu za ardhi katika nchi za Afrika ni:

• Haki za watu binafsi kumiliki ardhi kuwa na nguvu kuliko haki zapamoja

• Mitazamo kuhusu namna za utumizi wa ardhi – hususan ufugaji wakuhamahama na uwindaji na uokotaji, ama uhamahamaji au makaaziya muda – kijumla ni kwamba namna kama hizi hazina faida na hivyohazifai hata kudai haki za kumiliki ardhi, hali inayopelekea juhudi zakuwatuliza wafugaji mahali pamoja na kubinafsisha ardhi zao. Hatahivyo, wakati mwingine hali si mbaya sana kwa wafugaji wachache,ambapo dhamani ya shughuli za ufugaji zainatambuliwa na wafugaji

390. Amri ya nambari. 04/001.391. Kifungu cha 8 de la Loi n°001/PR/99 du 11 janvier 1999 (modifiée par la Loi n°016/PR/2000

du 1er août 2000).392. Le Collège de Contrôle et de Surveillance des Revenus Pétroliers (CCSRP). Art 16 de la

Loi n°001/PR/99 du 11 janvier 1999 (modifiée par la Loi n°016/PR/2000 du 1er août2000).

114

Page 131: First page ILO.fm

wanauwezo fulani katika kufanya uamuzi katika masualayanayoathiri ardhi zao, kama tunavyoona hapo juu.

• Uongozi ni suala muhimu ambalo ninafungamana moja kwa moja nahaki za watu wa kiasili kuhusu ardhi zao. Kama inavyoonekanakatika mjadala wa hapo juu, katika hali nyingi, vyombo vilivyo katikamaeneo fulani ambavyo vimekabidhiwa haki wa watu wa kiasilikuhusu ardhi, au vile vyombo (vijiji au mamlaka za kitamaduni)ambavyo vina haki maalumu za radhi, aghalabu huvihusishi watu wakiasili au mamlaka zao za kitamaduni. Katika nchi kadhaa, vijiji vyawatu wa kiasili havitambuliki kama inavyostahili, lakini kamasehemu tu ya vijiji vingine, hivyo kuwekea vikwazo uwezo wao wakumiliki na kutumia ardhi.

Nchi nyingi za Kiafrika zinatambua haki za kimila kama aina za haki zaardhi. hii ni nafasi muhimu kwa watu wa kiasili. Sheria ya kitamduni aghalabuhuwepo sambamba na sehria iliyoandikwa, na mara nyingi sheria za kitaifahuzingatia kanuni za kitamaduni kuhusiana na haki za ardhi. zaidi ya hayo,katika hali chache, kanuni za kitamaduni zilizopo sambamba na sheria ya kitaifana zinatambuliwa katika uundaji wa sheria zinatoa nafasi kwa haki za pamojana za kibinafsi kuhusu ardhi, ingawa wakati mwingi haki kama hizi si za kamiliza umiliki wa ardhi, na zinahusisha tu haki za kukalia au kutumia ardhi. hivindivyo hasa ilivyo katika nchi za kanda ya Afrika ya Kati.

Baadhi ya nchi zilizochunguzwa katika muktadha wa utafiti huu zina amavipengele vya kikatiba au vipengele vingine vya kisheria ambavyo vinatambuahaki fulani za pamoja kuhusu mali na ardhi. Katika mingi ya mifano hii, panauhusiano wa moja kwa moja na sheria ya kitamaduni, pale ambapo kunamfumo wa uwingi uanaotambua sheria iliyoandikwa na ile ya kitamduni. Hatahivyo. Hata hivyo, kutokana na ukweli kwamba mbinu za watu wa kiasili zakutumia ardhi aghalabu huchukuliwa kama zilizopitwa na wakati, kwa mfanokukiwa na msisitizo wa kitaifa katika kuimarisha kilimo kinyume na kutambuashughuli kama vile ufugaji na uwindaji-uokotaji, na kunaweza kuwepo naushahidi wa umiliki dhahiri wa eneo fulani, inaweza kuchukuliwa kuwa ardhiza watu wa kiasili hazitumiki ‘kwa namna ya kuleta faida’. Hii inawezakuonekana kama ubaguzi dhidi aina za utumizi wa ardhi na umiliki wakitamaduni wa watu wa kiasili. Aidha, huwa hakuna haki ya kisheria iliyothabitiya kumiliki ardhi kwa pamoja. Pale ambapo pana mipango ya kuwa na haki zapamoja kuhusu ardhi, huwa ni haki hafifu.

Kwa watu wa kiasili hasa, ambao mara nyingi hawana vyeti vya kumilikiardhi – kama watu binafsi au jamii – sheria ya kimila inaweza kuwa njiaambayo baadhi ya haki zao za ardhi zingeshughulikiwa. Kwa hakika, kunamifumo na vipengele vya kisheria katika nchi nyingi ambavyo vingekuwa vyafaida ya moja kwa moja kwa watu wa kiasili. Hata hivyo, faida zinazotarajiwakama hizi aghalabu hupunguzwa na mambo kama haya yafuatayo:

• Katika miktadha mingi ya kitaifa, ambapo umiliki au utumizi waardhi kimila unawapa haki watu binafsi au jamii, ni nadra haki hizokuwa katika aina za haki za umiliki, na zimefika mwisho, jambolinalomaanisha kuwa jamii au watu husika wanaendelea kubakikatika hali ya hatari kwa mujibu wa usalama wa ardhi.

• Mara nyingi, sharti kwamba ni lazima ardhi iwe inamilikiwa kwa njiainayoonekana au itumike kiuzalishaji ndipo madai kuhusiana nautumizi au umiliki wa kimila yawezekane, linawaweka watu wakiasili katika hali ya hatari kwani sehemu kubwa ya watu hawa ni wakuhamahama, bila kuacha ishara yoyote ya utumizi wa ardhi. panahaja sana ya kushughulikia upungufu wa sheria na kanuni kitaifa

115

Page 132: First page ILO.fm

kuhusiana na utambuzi wa umiliki na utumizi wa ardhi kimila nakuhakikisha kuwa mbinu watu wa kiasili za kutumia ardhizinatambuliwa ipasavyo.

Kwa hiyo changamoto za kisheria na za kiutendaji za kupata haki zapamoja za kumiliki ardhi kwa watu wa kiasili zinaweza kuelezwa kwamuhtasari kama ifuatavyo:

• Sharti kuwa ni lazima jamii za kiasili ziwe na hadhi ya kisheria kablaya kudai haki za pamoja kuhusu ardhi linazizuia zisiweze kufurahiahaki zilizomo kwenye sheria ya kitaifa. Iwapo watu wa kisheriahawezi kuunganika kuunda vyombo vinavyotambulika kisheria, inamaana kuwa hawawezi kuwa na haki za ardhi za pamoja. Wakatimwingine njia ya pekee ambayo jamii za kiasili zinaweza kujisajilishakama vyombo halali ni kwa kuunda mashirika au miunganomingineyo ambayo haionyeshi asasi au miundo ya tamaduni zaokama jamii.

• Katika hali nyingi, uwezekano wa kudai haki za pamoja za kumilikiardhi unategemea uwezo wa watu wa kiasili wa kudhihirishautumizi wa ardhi wenye kuleta faida. Dhana ya uzalishaji imejikitakwenye wazo la kuwa na kilimo cha mahali pamoja na inashindwakuzingatia mbinu za watu wa kiasili za kutumia ardhi pamoja nawajibu wao muhimu katika kulinda raslimali zilizo kwenye ardhiwanazomiliki au kutumia.

• Wakati mwingi, aina za haki zilizoko kuhusu haki za pamoja si zaumiliki kamili wa ardhi. Ni haki ambapo ardhi ama imetiwa chini yashirika, mtunzaji halali au mwakilishi wa jamii. Hali hii inakinzana nausimamizi na mifumo ya kitamaduni ya kufanya maamuzi katikajamii za kiasili.

Kuhusiana na maliasili, katiba nyingi huyaweka maliasili haya katika serikalina haki za utumizi wa ardhi ndizo kuu ambazo jamii za kiasili zinawezakutumia. Katika maeneo ya misitu, haki za utumizi pia zimethibitiwa sana,kama zilivyo haki za kuwinda wanyama. Kwa msingi wa utambuzi wa umilikajina utumizi wa ardhi na raslimali kitamduni katika mataifa mengi, hata hivyo,wakati mwingi huwa ni vigumu kuthibitisha umiliki kama huu.

Hata hivyo, kama ambavyo imeonyeshwa, nafasi chanya zinawezakupatikana ambapo watu wa kiasili wanaweza kutumia madai yaliyopo yakimila kama msingi wa kuwa na haki rasmi zaidi kuhusu ardhi na raslimalibaadhi ya mifano ni:

• Mipango ya kutambua ufugaji katika baadhi ya nchi. Nchini BurkinaFaso na Jamuhuri ya Afrika ya kati, kwa mfano, sheria kuhusu jamiiza maeneo mbalimbali au msisitizo katika sheria kwamba lazimapawepo na mashauriano na mashirika ya wafugaji, vinaweza kuwanafasi za kuwepo kwa ulinzi zaidi wa ardhi zao. Rasimu ya Sheria yakitaifa kuhusu ardhi nchini Kenya pia inatambua haki fulani zaumiliki kwa wafugaji, kama ilivyo pia rasimu ya Sheria kuhusu ufugajinchini Niger, ambayo mashirika ya umma – yakiwemo mashirika yawafugaji – yamesaidia sana kuifafanua.

• Mikakati kuhusu misitu ya kijamii nchini Kameruni, Jamuhuri yaAfrika ya Kati, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Gabon, kwamfano, imekuwa ya muhimu kwa watu wa kiasili na inawezakutumiwa baadaye kama msingi wa kuimarisha haki zao za ardhi.

• Pia kuna mipango ya kugawana faida, hususan katika maeneo yamisitu, ambayo inaweza kutumiwa kama mifano ya kuigwa katika

116

Page 133: First page ILO.fm

nchi zingine. Hii ni pamoja na mipango ya CIB ya kugawana faida najamii za wenyeji nchini Kongo.

117

Page 134: First page ILO.fm

8 Haki za uchumi wa kijamii

8.1 Utangulizi

Watu wa kiasili ni sehemu ya makundi kadhaa katika bara zima la Afrikaambao wamekumbwa na wanaendelea kukumbwa na ukiukaji mkubwa wahaki za kibinadamu za uchumi wa kijamii. Baadhi yao wamefukuzwa kutokakatika ardhi wanazozichukulia kama makao yao ya kiasili na ambazo wanaufungamano maalum nazo. Kwa miaka michache ya hivi karibuni, sheria nawahusika wa kimataifa wameitikia masaibu na mahitaji ya watu wa kiasiliulimwenguni kote, hasa wale kutoka Afrika. Uitikaji huu umesisitizwa kwakukubali chombo maalum cha sheria inayolenga katika kuendeleza na kulindahaki za watu wa kiasili. Kati ya haki hizo, haki za uchumi wa kijamii ndizomuhimu kwa maisha na maslahi ya watu wa kiasili wa Afrika.

8.2 Sheria ya kimataifa

Vipengele kadhaa ya sheria ya kimataifa, kiulimwengu na kimaeneo, vinawezakubainishwa kama vinavyodhamini haki za watu wa kiasili.

ICESCR inaruhusu haki ya watu kujiamulia.393 Ijapokuwa hakizinazozungumziwa katika ICESCR zinafaa kutekelezwa hatua kwa hatua,ICESCR inatia wajibu maalum kwa serikali chini ya uangalizi wa CESCR.Mfumo wa ICESCR unatiwa nguvu zaidi na CRC394 na CEDAW,395 ambazozinahusu haki maalum za uchumi wa kijamii za watoto na wanawake,wakiwemo wale wanaotoka katika jamii asili za kiafrika.

Zaidi ya hayo, CERD ina kipengele muhimu ambacho kinawezakuchukuliwa kuwa muhimu kwa ulinzi wa haki za uchumi wa kijamii za watuwa kiasili.396 Kifungu cha 5(e) cha CERD kinaomba mataifa kupiga marufukuna kuondoa ubaguzi wa kikabila wa aina zote na kumhakikishia kila mtu hakiyake bila kubagua kwa mujibu wa kabila au rangi mbele ya sheria, hasa katikakufurahia haki za kiuchumi, kijamii na kitamaduni. Ijapo kuwa CERD haitoifasili ya istilahi ‘kabila’, ambayo ni muhimu katika kutafuta haki za kiasilikuhusu uchumi wa kijamii, kamati ya CERD katika Pendekezo la Jumlanambari 8 inajaribu kubainisha uanachama wa kikundi fulani kwa msingi wa‘kujitambulisha kwa watu husika wenyewe’ kuwa ni wa kikundi fulani. KatikaPendekezo la jumla nambari 3, Kamati ya CERD ilionyesha uhusiano baina yahali ya uchumi wa kijamii wanamojikuta watu wa kiasili na kunyang’anywaardhi na maeneo yao na kutokana na shughuli za biashara za kiserikali namakampuni ya kibiashara. Aidha inahitaji kwamba serikali iwape watu wakiasili ‘hali nzuri zinazowawezesha kupata maendeleo ya kudumu ya kiuchumina kijamii inayofuatana na wasifu wao wa kitamaduni.’397

Mkataba wa uliomuhimu sana ni ule wa Shirika la Leba la kimataifa nambari169, ambao unatoa mfumo sanifu na majukumu ya serikali wakati wakutekeleza miradi ya maendeleo ambayo inaathiri watu wa kiasili. Mataifayanaombwa kuchukua hatua maalum kuhakikisha kuwa haki za usalama wa

393. Kifungu cha 1 cha ICESCR.394. Angali vifungu nambari23, 24, 25, 26, 27 na 28.395. Angalia vifungu nambari 11, 12, 13, 14, 15 na 16.396. Kifungu cha 5(e).397. Kamati ya CERD, Pendekezo la jumla la 23, haki za watu wa kiasili, (kikao cha hamsini na

moja, 1997) UN Doc A/52/18 kiambatisho cha V kwenye 122 (1997) aya ya 4(c).

118

Page 135: First page ILO.fm

kijamii, afya na elimu ya watu wa kiasili vinaafikiwa. Aidha mkataba huuunatambua kuwa, kwa kadiri iwezekanavyo, watu wa kiasili wanafaakuruhusiwa kutawala maendele yao ya kiuchumi, kujamii na kitamaduni.398

Ijapokuwa hakuna taifa lolote la kiafrika hadi kufikia sasa limetia sahihismkataba huu, ukweli uliopo ni kwamba chombo hiki ni himizo nakinadhihirisha mwelekeo wa kulinda haki za kiasili ulimwengu mzima naBarani Afrika. Ukweli kwamba maazimio na mielekeo hii kwa leo ni sawaulimwenguni kote, umethihirishwa na kukubaliwa kwa UNDRIP.399 Mkabamwingine muhimu katika muktadha huu ni ule mkataba wa ILO dhidi yaubaguzi (wa ajira na kazi) wa mwaka wa 1958 (nambari 111), ambao unahusuubaguzi katika ajira na kazi ikiwa ni pamoja na shughuli za kitamaduni za watuwa kiasili, na unaweza pia kuhusisha upataji wa elimu pamoja na masuala yaardhi yanayohusiana na utekelezaji wa shughuli zao za kitamaduni. Mkatabadhidi ya ajira ya lazima wa mwaka wa 1930 (nambari 29) vile vile ni waumuhimu wa moja kwa moja.

Mkataba wa Afrika ambao umeundwa kutatua masuala maalumuyanayohusu Afrika ukizingatia muktadha wa utamaduni wa kiafrika,unatambua na kulinda haki za pamoja kwa kutumia neno ‘watu’linalowahusisha watu wa kiasili. Kwa hivyo, haki za uchumi wa kijamiizinazozungumziwa katika Mkataba wa Afrika zinaweza kudaiwa na watu wakiasili, hasa zile zinazorejelea watu wa kiasili na maendeleo ya kudumu.400

Mbali na haki ya kujiamulia,401 ambayo imefafanuliwa na Tume ya Afrika kwanjia finyu,402 Mkataba wa Afrika una hifadhi ya nguvu ya haki za uchumi wakijamii katika kifungu cha 14 hadi 25, ambazo ni muhimu sana kwa watu wakiasili kibinafsi na kama jamii kwa jumla. Hizi ni pamoja na haki ya watu kuuzamali yao ya asili bila kupingwa, pale ambapo wamenyang’anywa warudishiwena kupata fidia kamili nay a kutosha, na kufaidika kwa faida zinazotokana nayo.Kifungu muhimu sana ni kifungu cha 22, ambacho kinadhamini haki yawatukujiendeleza kiuchumi, kitamaduni na kijamii pamoja na haki za kumiliki mali(kifungu cha 14), ambazo zinaweza kuhusisha mali ya maarifa ya kitamaduni,haki ya kufanya kazi katika mazingira sawa na ya kutosheleza (kifungu cha 15),haki ya kupata hali nzuri ya afya kimwili na kiakili (kifungu cha 16) mbayoinafafanuliwa kuwa inahusisha haki za kupata chakula, nyumba na mazingirasalama pamoja na haki ya elimu ya bure na maisha ya kitamaduni (kifungu cha17).

Mkataba wa Afrika unasaidiwa na kutiwa nguvu na vipengele vya hati yaawali kwa Mkataba wa Afrika kuhusu haki za wanawake barani Afrika,403 naMkataba wa Afrika kuhusu Haki na Maslahi ya Mtoto,404 ambavyo vinazingatiamahitaji na wasiwasi wa wanawake kiafrika mtawalia, kuhusu uchumi wakijamii, wakiwemo wanawake kutoka katika jamii za kiasili.

Mkusanyo huu wa haki za uchumi wa kijamii, hasa zile za watu wa kiasili,kimsingi zinakusudiwa kutekelezwa kwa kiwango cha kinyumbani (nchihusika), pamoja na mambo mengine, kupitia kwa hatua za kikatiba, kisheria na

398. Kifungu cha 7(1) cha Mkataba wa ILO nambari. 169. 399. Ilikubaliwa na Bunge la Umoja wa Mataifa tarehe 13 Septemba 2007.400. Angalia vifungu vya 21, 22, 23 & 24.401. Angalia kifungu cha 20.402. Arifa ya nambari 75/92 Katangese Peoples’ Congress v Zaire (2000) AHRLR 72 (ACHPR

1995).403. Angalia kifungu cha 12 (elimu), 13 (maslahi ya kiuchumi na kijamii), 14 (Haki kuhusu afya na

uzazi), 15 (usalama wa chakula), 16 (makao mazuri), 17 (mazingira mazuri ya kitamaduni),18 (mazingira salama na ya kudumu) na 19 (maendeleo ya kudumu).

404. Angalia kifungu cha 11 (Elimu), 12 (wasaa wa kupumzika, burudani, burudani na shughuli zakitamaduni), 13 (Msaada maalumu kwa watoto walemavu) & 14 (Afya na huduma za afya).

119

Page 136: First page ILO.fm

kiutawala. Hata hivyo, viwango hivi vya kimataifa havijatekelezwa kwa usawakatika nchi zote za Afrika. Hali hii imesababisha ukosefu wa usawa katikakufurahiwa haki za uchumi wa kijamii, zinazodhaminiwa ulimwenguni kote nakimaeneo, na watu wa kiasili Afrika.

8.3 Mielekeo ya kitaifa

Wakati wa kutekeleza viwango vya kimataifa kuhusu haki za kiasili za uchumiwa kijamii kupitia kwa hatua za kikatiba, kisheria na kiutawala, kila nchi yakiafrika huelekea kuitikia muktadha wake wenyewe wa kisiasa, kijamii,kiuchumi na kitamaduni. Huku ikiwa kwamba miktadha hii inatofautianakutoka nchi moja hadi nyingine, kiwango cha kutekeleza viwango vya kimataifakinaweza pia kutofautiana kutoka nchi moja hadi nyingine. Hata hivyo,inawezekana kubainisha mielekeo fulani katika kulinda haki za uchumi wakijamii za watu wa kiasili barani Afrika.

Kukosa vitu muhimu vya msingi maishani

Katika nchi nyingi za Afrika, watu wa kiasili wanachukuliwa kamawasioendelea na walionyuma kuliko makundi mengine ya kijamii nakitamaduni, na wasiozalisha kiuchumi. Mitazamo hii inawatia katikakubaguliwa, kutawaliwa na kunyonywa katika mifumo ya siasa na uchumi wakitaifa ambayo aghalabu huwa imeundwa kudhihirisha maslahi na shughuli zawaliowengi katika taifa. Kiutendaji, watu wa kiasili ni kati ya vitengo masikinina vilivyonyanyaswa sana kiuchumi-jamii katika jamii wanamoishi. Watu wakiasili karibu ndio masikini zaidi kuliko wanajamii wa makabila mengine yamataifa ya kanda hii. jamii za kuhamahama kama vile Tuaregi, hazina hospitalina huduma za tiba ya mifugo kwa ngamia wao, ambao wanawategemea sanakujikimi, na wametengwa kutoka katika mipango ya maendeleo. Masuala yoteya maendeleo ya watu wa kiasili yanalemazwa na hali za kiwango kikubwa chakunyonywa na kutengwa. Hata hivyo, ni lazima itajwe kwamba mataifa mengiya Afrika yanaendelea kukubali kuwa watu wao wa kiasili ni kati ya makundi‘yaliyopembezwa’ na ‘yaliyohatarishwa’ katika uchumi wa kijamii yanayohitajikutiliwa maanani sana na kulindwa, ingawa mbinu zao maalumu kuhusiana naswala hili zinatofautiana sana.

Utambuzi wa unyonge wa kiuchumi pamoja na hatua maalumu za ulinzivinaonekana nchini Kameruni, Namibia (zahanati za kutembea), Nigeria(Elimu ya kuipa jamii uwezo), nchini Namibia (mpango wa maendeleo yaWasan) na nchini Misri (kukubaliwa kwa sheria ya usalama wa kijamii nambari30 ya mwaka wa 1977 iliyoweka usaidizi kiasi wa kifedha kwa jamii masikinihasa ikiwa ni pamoja na jamii za kiasili). Nchini Ethiopia, mpango wamaendeleo wa PASDEP wa mwaka wa 2005 unatambua wazi kuwa ‘viashiriavya maendeleo ya kibinadamu na umasikini baina ya makundi ya [wafugaji] nivibaya sana kuliko kwingineko nchini na imekuwa vigumu kufikia makundihaya na huduma za kawaida.’

Aidha, huku mikakati maalum ya hapo juu ikiwa imeundwa kutoa ulinzimaalumu kwa watu wa kiasili kwa sababu ya hali yao ya kiuchumi, kupata hakizao zinazohusiana na uchumi wa kijamii kuna kumelindwa kwa sawa chini yakanuni inayopinga ubaguzi. Angalau kwenye kiwango cha kisheria na sera, nisharti kuwa taifa halifai kubagua kikundi chochote cha wananchi wake, hasawatu wa kiasili, katika kutoa huduma za afya ya umma, maji safi, nyumba,chakula na usalama wa kijamii. Kanuni inayopinga ubaguzi pia inalinda uhuru

120

Page 137: First page ILO.fm

wa mtu kushiriki katika shughuli za kiuchumi na kuishi maisha ya anayopenda,na hivyo kuhakikisha kuwa serikali haiingilii maisha ya watu wa kiasili.

Athaei moja dhahiri watu wa kiasili kunyanyaswa katika kiuchumi wa jamiini kiu na ukosefu wa lishe bora. Baadhi ya nchi ambazo zimeathiriwazimerasimu Hati za mbinu za kupunguza umasikini (PRSP), ambapo hatua zakukomesha umasikini unaohusiana na ukosefu wa lishe borazimependekezwa. Ingawa watu wa kiasili ni sehemu ya watu waliofukara zaidiwaliotajwa katika nyinngi ya hizi Hati za mbinu za kupuguza umasikini,wanatajwa kwa wazi mara chache tu kama sehemu ya tabaka la waliomasikinisana katika jamii.

PRSP ya Burundi inataja wabatwa kwa jina, kuwatambua kuwa wanaishikatika hali ya kunyanyaswa na kutengwa kijamii na kitamaduni. PRSP iliundwabaada ya kufanya mashauri pamoja na wawakilishi wa watu nasikini zaidi katikajamii, wakiwemo Wabatwa.

Kanuni ya kuhalalisha haki za uchumi wa kijamii unaziruhusu haki hizikutumiwa moja kwa moja mahakamani. Ingawa kanuni hii bado haijatambuliwakatika Mataifa mengi, inaweza kuwezesha utekelezaji wa haki za uchumi wakijamii za watu wa kiasili. Katiba ya Afrika kusini, ikisaidiwa na maarifa ya awaliya sheria,405 ni wazi kuhusiana na uhalalishaji wa haki za uchumi wa jami, nakatiba ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inasisitiza mwelekeo waMkataba wa Afrika wa kutogawanya haki za kibinadamu katika vizazi viwilikama desturi. msimamo huu inatoa uwezekano wa kuwepo kwa utekelezajiwa kimahakama wa haki za uchumi wa kijamii za watu wa kiasili. Hii inawezakutumika pia katika nchi zenye sheria ya kiraia ambapo vipengele vya Mkatabawa Afrika vinaweza kutekelezwa moja kwa moja katika mahakama za nchinihumo kupitia kwa mkakati wa utumizi wa moja kwa moja. Hata katika zilenchi ambapo haki za kiuchumi wa jamii zimeonyeshwa moja kwa moja chini yakifungu kuhusu malengo ya msingi yasiyotekelezeka na kanuni ya amri ya seraya serikali, pamekuwepo na maendeleo chanya ya kufurahisha ya utekelezajiwa kimahakama wa haki za kiuchumi wa jamii kwa msingi wa wajibu wakimataifa wan chi hiyo.

Makao

Katika utamaduni wa jamii za kiasili, suala la makao na nyumba halikuwa lakuzua wasiwasi. Watu wa kiasili walipopoteza ardhi zao za kitamadunu, nauwezo wa kutimia maliasili ukawekewa vikwazo sana, tatizo la kutokuwa nanyumba za kutosha likaanza kuibuka. Kwa kiwango cha kanuni, ni katiba zaNamibia (kifungu cha 95), Burkina Faso (kifungu cha 18), Afrika kusini (kifungucha 26) na Ethiopia (kifungu cha 90(1) pekee ndizo zinazohusisha haki yakupata makao mazuri kwa wanchi wote. Katiba ya Afrika kusini (kifungu cha27) inaelekea kuhusisha masuala yote yanayodhamini haki ya watu wa kiasilikupata makao hivi kwamba haidhamini tu haki ya kuwa na nyumba bali piaulinzi dhidi ya kufukuzwa kutoka katika makao yao kusiko halali. Hata hivyo,hakuna hatua zozote za kisera ambazo zimekubaliwa nchin Afrika kusini ilikutekeleza kikamilifu vipengele vya kikatiba vilivyotajwa hapo juu.

Kuna mifano kadhaa ya mipango inayoshughulikia matatizo ya nyumba kwawatu wa kiasili, hasa wakati wanapofukuzwa kutoka katika makao yao ya

405. Angalia, inter alia, Government of the Republic of South Africa v Grootboom & Others (1) SA 46(CC); Soobramoney v Minister of Health, Kwazulu-Natal 1998 (1) SA 765 (CC); TreatmentAction Campaign v Minister of Health and Others 2002 4 BCLR 356 (T).

121

Page 138: First page ILO.fm

kitamaduni. Serikali ya Namibia imelifanya suala la nyumba kuwa mojawapo yamasuala ya maendeleo yake yaliyopewa kipaumbele ili kuleta maendeleokupitia kwa mpango wa ujenzi wa nyumba wa Build Together HousingProgramme, ambao unashughulikia suala la kupanuka kwa miji na uhamiaji wamijini kwa kuanzisha maeneo ya upokezi wa wale wanaohamia mijini. Faida zampango huu zimo katika juhudi za serikali za shughulikia hitaji la nyumba kwawasiojiweza nchini humo. Vile vile, Mpango wa Wakaaji waMaeneo yaMashambani (RADP) ulioanzishwa nchini Botswana ili kusaidia wananchi wotewanaoishi katika sehemu za vijijini, wakiwemo watu wa kiasili, kwa kuanzishamakaazi yenye utaratibu mzuri, utoaji wa elimu ya msingi na ugawaji waardhi.406 Mifano hii miwili, ambayo inaweza kuigwa na mataifa mengine yaAfrika inadhihirisha wazi nia ya serikali kuendeleza upataji wa haki za uchumiwa kijamii za watu wa kijamii kuhusu makao mazuri. Hata hivyo mipangokama hii haitambui watu wa kuhamahama na wakaaji wa misituni. Mahitaji yaoya nyumba ni aina nyingine ya matatizo.

Huduma za Afya

Kadiri ya inavyoweza kuthibitishwa, vishirio vya afya kwa watu wa kiasili niduni kuliko vile vya wanajamii wengine. Viashirio hivi ni pamoja na viwangovya vifo vya kinamama; viwango vya vifo vya watoto wachanga na viwango vyakupata chanjo. Kwa kuwa watu wa kiasili wanaishi katika sehemu zamashambani, kwa jumla hawawezi kupata maji safi ya kunywa. Kutegemeavyanzo vya maji kume kumehatarishwa na miradi ya maendeleo, ikiwa nipamoja na ukataji wa miti na kuharibu misitu, athari za mabadiliko ya hali yahewa, kama ilivyomfano wa kuzuka kwa jangwa la Sahel. Hali hii aidhainawaweka watu wa kiasili hasa watoto katika hatari ya kupata magonjwa.

Nchi chache zinadamini haki za zinazohusiana na afya. Kifungu cha 95(a) na(e) cha katiba ya Namibia kinailazimu serikali kutekeleza sheria zilizoundwakuhakikisha kuwa mahitaji ya kiafya ya watu na kumwezesha kila mwananchikutumia vifaa vya umma ikiwa ni pamoja na vifaa vya afya. Kwa mkumbo huuhuu, kifungu cha 27 cha katiba ya Afrika kusini kinasema kuwa kila mtu anahaki ya kupata huduma za afya, zikiwemo huduma za afya ya uzazi. Kipenegelehiki kirudia yaliyosemwa katika kifungu cha 26 cha katiba ya Burkina Faso; nakama sehemu ya kanuni za amri ya sera ya serikali katika katiba ya Nigeria.Nchini Kenya, kama ilivyo nchi nyinginezo, ulinzi halali wa afya umejikitakatika sheria kadhaa ikiwemo sheria ya afya ya umma (kifungu cha 242),Sheria kuhusu afya ya kiasili (kifungu cha 248 ) na sheria kuhusu kuzuia malaria(kifungu cha 246).

Kwa mujibu wa utekelezaji halizi wa hivyo vipengele vya kisheria, ni nchichache sana za Afrika zimekubali sera ya kimatibabu inayolenga kuwapa watuwake wa kiasili huduma za matibabu za mara kwa mara.

Katika kanda ya kusini mwa sahara, yakiwemo maeneo wanamoishi watuwa kiasili, suala la afya linahusiana sana na lile la virusi vya kusababisha ukimwi(VVU). Kutokana na njia nyingi za kuambukiza, watu wa kiasili wanawezakuwa katika hatari kubwa ya kuambukizwa. Mara nyingi wanawake wa kiaslihuwa wahanga wa mapenzi bila hiasri, kunajisiwa na ubakaji. Kiasi kikubwa chaumasikini unaowakumba kinaweza kuwalazimu kujihusisha na ukahaba.Uchunguzi wa hivi karibuni aidha umeonyesha kwamba ueneaji wa virusi vya

406. L Tshireletso ‘Participatory Research: A Development World Research Paradigm forChange’ in S Saugestad (ed) Indigenous Peoples in Modern Nation-States Occasional PapersSeries A No. 90. 141-147.

122

Page 139: First page ILO.fm

ukimwi kati ya jamii za kiasili unazidishwa na ukataji wa miti katika misitu yaeneo la istiwahi la katikati mwa Afrika.407 Licha ya ishara hizi za hatari kubwa,pana data chache sana kuhusu viwango vya juu vya uambukizaji wa Virusi vyaukimwi baina ya makundi haya katika taifa lolote lililochunguzwa. Ingawamataifa yote yana mipango na mikakati ya kitaifa kuhusu VVU na Ukimwi,nafasi ya kipekee ya watu wa kiasili aghalabu imesahauliwa sana.

Zahanati za kutembezwa zinapatikana nchini Namibia, Kameruni naKenya. Watu wa kiasili aidha wamepewa maarifa yanayofaa kuhusiana na jinsiya kukabiliana vyema na magonjwa hatari kama vile VVU na UKIMWI, kifuakikuu na malaria. Uhamazishaji unahusisha hatua za kukinga, kama vile zilezilizozinduliwa na serikali ya Uganda kukabiliana na tatizo la VVU naUKIMWLI baina ya Wabatwa. Serikali ya Botswana imetumia mbinu hiikupitia kwa matangazo ya redio.

Kushindwa kulinda haki za wafanyikazi na ajira ya lazima

Pamoja na kuendelea kutishiwa kwa mbinu zao za kimila za uzalishajikutokana na mikasa ya kimaumbile na shinikizo la kugeuza uchumi upya, watuwengi zaidi wa kiasili wanaingia katika ajira zisizo za utamaduni wao. Hivindivyo hasa ilivyo kwa Wabatwa na ‘Mbilikimo’ wengine katika kanda yaAfrika ya Kati. Wafanyikazi ‘Mbilikimo’ karibu wote wanafanya kazi katikasekta ya juakali, bila uthabiti wa kandarasi, na mara nyingi hupewa malipokidogo kuliko wafanyikazi wengine na aghalabu hutarajiwa kufanya kazi kwamasaa mengi. Uhusiano wa deni la kibinafsi (‘ufungwa’), ambalo mara nyingihudumu kwa vizazi vingi, wakati mwingine husababisha hali za ajira ya lazimaau utumwa. Hii hasa ndiyo hali ilivyo kuhusiana na vijana, wanaume nawanawake wanaofanya kazi katika mashamba makubwa ya majirani zao wakibantu. Hali ya kutia wasiwasi ni ile ya nchini Kongo, Kameruni, DRC naGabon, ambapo jamii za wabantu zinajulikana kwa kutumia vibaya hali nduniya uchumi wa watu wa kiasili. Watoto wa kiasili wanakumbwa pakubwa nahali za hatari kazini

Mwelekeo mkuu kuhusu haki za wafanyikazi ni kupingwa kwa kauli mojaajira ya lazima na ajira hatari kwa watoto. kwa hivyo nchi hizi pamoja nanyinginezo zimepiga marufuku ajira ya lazima na ajira hatari kwa watoto.katika baadhi ya nchi, marufuku haya yamo katika katiba. kwa mfano: kifungucha 25 cha katiba ya Uganda, kifungu cha 13 cha katiba ya Afrika kusini nakifungu cha 26 cha katiba ya Kongo kinasema kuwa hakuna mtu yeyeoteatakayelazimishwa kufanya kazi.

Katika nchi zingine, sheria inayohusu suala hili imekubaliwa. Kifungu cha2(3) cha Sheria ya Leba ya Kameruni kinapinga ajira ya lazima kabisa (de façonabsolue). Sheria ya Leba ya Kongo ya mwaka wa 1975 pia inapiga marufukuajira ya lzima,408 kama ilivyo Sheria ya leba ya Gabon.409 Kifungu cha 3 chasheria ya leba ya Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo kinaidilisha sheria yakimataifa kwa kupiga marufuku aina mbaya za ajira za watoto.

Hata hivyo, vipengele hivyo vya kikatiba na kisheria havijatekelezwaipasavyo katika mataifa haya. Sheria ya kimataifa au ya sheria ya nchi hizi

407. C Laurent, A Bourgeois, M Mpoudi, C Butel, M Peeters, E Mpoudi-Ngolé et al‘Commercial logging and the HIV epidemic, rural Equatorial Africa’ Emerg Infect Dis (2004)Nov Available from http://www.cdc.gov/ncidod/EID/vol10no11/04-0180.htm (iliangaliwa30 Novemba 2008).

408. Kifungu cha 4, soma pia kifungu cha 257.409. Kifungu cha 4 cha Sheria ya Leba ya mwaka 1994.

123

Page 140: First page ILO.fm

haijatumika kama njia ya kurekebisha maovu makubwa ya jamii. Mojawapo yasababu ya tatizo hili linalojirudia ni kukana kuwepo kwa tatizo lenyewe,aghalabu kwa msingi wa kutokuwepo kwa habari ya kutegemewa. Aidha, nahasa kwa ‘Mbilikimo’, suala la ajira ya lazima linafungamana moja kwa moja nakubaguliwa na kupembezwa na makundi mengine, hivyo kusababisha haliambayo wale wanaokumbwa na kitendo hiki hawana uwezo kabisa wakukabiliana nacho. Sababu nyingine inahusiana na uwezekano mdogo wakupata haki, mada ambayo inajadiliwa kikamilifu kwingineko.

Haki za mali ya kitaaluma

Kwa miaka ambayo imepita, watu wa kiasili wa Afrika wamekumbwa na‘utekwaji nyara kitaaluma’ wa maarifa yao ya kitamaduni kutokama na wizi wamali ya kitaaluma unaofanywa na watu binafsi na mashirika ya kibinafsiyanayojihusisha na vyombo vya habari, viwanda vya uzalishaji, vya utengenezajiwa dawa na viwanda vinginevyo.

Kwa kuitikia haya, juhudi kadhaa za kiserikali zimefanywa kuhusiana nafenomena hii kwa kutekeleza sheria au kusambaza habari au labda kwakuanzisha mashirika maalumu ya kukuza na kulinda haki za kitaaluma za watuwa kiasili. Hivi ndivyo ambavyo imekuwa katika Jamuhuri Afrika ya Katiambapo sheria nambari 06/002, sheria kuhusu Mkataba wa kitamaduni waJamuhuri ya Afrika ya Kati, inadokeza kanuni ya kupiga marufuku kutumia aukuuza nje tamaduni simulizi za waliowachache wa Jamuhuri ya Afrika ya Katikwa malengo ya kibiashara (interdiction d’exploitation et/ou d’exportation destraditions orales des minorités culturelles de Centrafrique à des fins commerciales).Kwa kupiga marufuku utumizi au uuzaji wa tamduni simulizi za waliowachachekatika Jamuhuri ya Afrika ya Kati, taifa hili linalenga kulinda maarifa yakitamaduni. Maendeleo mengine ya kutia moyo ni pamoja na yafuatayo: kandona haki ya afya katika sheria ya haki za kibinadamu, Rasimu ya Katiba ya Wakoinatambua pia maarifa ya kiasili na haki za mali ya kitaaluma na inatafutakuziunga mkono na kuzikuza.410 Mpango kuhusu Dawa za kiasili (2004) piaumekubaliwa kwa lengo la kutambua na kulinda waganga wa kienyeji. Vivyohivyo serikali ya Gabon imeanzisha taasisi ya kitaifa iliyo na jukumu la kukuzatiba na dawa za kienyeji.

8.4 Hitimisho

Nafasi ya uchumi wa kijamii wa watu wa kiasili aghalabu huwa mbaya sana.Kuna haja kubwa ya kutambua kwa wazi na kushughulikia wasiwasi waokuhusiana na nafasi yao na kuushughulikia kama sehemu muhimu ya mikakatina mipango ya kimaendeleo. Muhimu ni hatari waliyomo watu wa kiasili yakuambukizwa virusi vya ukimwi; na vitendo vinavyofanana na ajira ya lazima nautumwa vinavyohusisha ‘Mbilikimo’ walioko katikati mwa Afrika.

Katika juhudi za kutekeleza wajibu wao wa kimataifa, nchi kadhaa zaAfrika zimeishia kukubali mikakati kadhaa, kuanzia kwa ile ya kikatiba, kisheriahadi ile ya kiutawala, kwa lengo la kudumisha hususan haki za kiuchumi wajamii za watu wa kiasili. Haki hizi ni pamoja na haki ya kupata chakula, afya,usalama wa jamii, makao, haki ya elimu, ardhi na haki ya kumiliki mali ikiwemomali ya kitaaluma. Kama mfano wa maendeleo chanya ya kisheria, Jamuhuri yaAfrika ya Kati ilitoa sheria ya kupinga utumizi wa utamaduni simulizi wawaaliowachache katika jamii nchini humo kwa sababu za kibiashara. Licha ya

410. Rasimu ya katiba ya Wako. Kifungu cha 26(2).

124

Page 141: First page ILO.fm

kuwepo kwa maendeleo fulani kwa miaka mwongo mmoja uliopita, watu wakiasili katika Afrika wanaendelea kuishi maisha magumu na yenye hatarikutokana na ukosefu wa nia ya kisiasa ya kutekeleza mifumo ya kisheriainayofaa kwa kukuza na kulinda haki za uchumi wa kijamii za watu wa kiasili.Kuhusishwa kwa mahitaji ya Wabatwa katika Hati ya mpango wa kupunguzaumasikini ya nchini Burundi ni mfano mzuri wa kile kinachohitaji kutumiwakama msingi.

125

Page 142: First page ILO.fm

9 Usawa wa kijinsia

9.1 Utangulizi

Usawa wa kijinsia unahusu hasa usawa wa kuchukuliwa kwa namna sawa chiniya sheria na kupewa nafasi sawa. Usawa wa kijinsia hujengwa kupitia kwasheria na amri rasmi za kijamii na kupitia kwa kaida na mitazamo yakidhahania kuhusu ni nini nafasi ya mwanamke katika jamii. Swala la jinsia nimuhimu sana kwa watu wa kiasili na hasa kwa mwanamke wa kiasili kwa kuwambali na suala la kubaguliwa na kupembezwa kunakowakumba wanawake,wanawake wa kiasili aidha wamewekwa katika hali mbaya na utamaduni namila za jamii pamoja na seria na sheria za kitaifa ambazo zinawabagua kamawatu na kama wanawake kwa njia ya moja kwa moja au isiyo ya moja kwamoja.

9.2 Sheria ya Kimataifa

Usawa wa kijinsia, kutobaguliwa na kuendeleza haki za wanawake ni mamboyanayohusiana kwa karibu. Vyombo vingi vya kimataifa vina vipengele vyakijumla vinavyopinga ubaguzi, kwa misingi ya jinsia. Kifungu cha 3 cha mkatabawa ICCPR (Mkataba wa kimataifa kuhusu haki za umma na kisiasa) kwa mfanokinalinda haki za wanaume na wanawake kufurahia haki zote za umma nakisiasa kama zinavyoelezwa katika ICCPR. Kifungu cha 26 cha chombo hikikinatilia mkazo ulinzi sawa wa kisheria, ambao pia unaelezwa katika kifungucha 3 cha mkataba wa Afrika. Kifungu cha 18 cha Mkataba wa Afrika aidhakinataka mataifa ‘yahakikishe kuwa yanaondoa kila aina ya ubaguzi dhidi yawanawake na kuhakikisha kuwa haki za wanawake na watoto zimelindwakama inavyosisihtizwa katika maazimio na mikataba ya kimataifa’. Katika kifungu cha 10(2) cha ICESRCR kinazungumzia hasa ulinzi wa kinamama kwakipindi fulani kizuri kabla na baada ya kujifungua.

Mkataba kuhusu ukomeshaji wa kila aina ya ubaguzi dhidi ya wanawake(CEDAW) unadhamini haki za wanawake kijumla tu na wala hautajiwanawake wa kiasili. Katika maoni yake ya jumla nambari 24, kamati yaCEDAW ilidhihirisha kuwa kuna masuala mengi ya kijamii ambayo yanawezakuathiri haki mbalimbali za wanawake kuhusu afya. Kwa sababu hii, inafaakuzingatia zaidi makundi mahususi ya wanawake, wakiwemo wanawake wakiume. CEDAW inapinga tamaduni mbaya, dhuluma za kinyumbani nadhuluma dhidi ya wamawake.

Kifungu cha 3 cha Mkataba wa 169 ILO kinapiga marufuku ubaguzi kwamsingi wa jinsia. Makataba wa 100 wa ILO unathibitisha wajibu kwa mataifawa kuhakikisha kuwa wafanyikazi wa kike wanapewa malipo sawa kulingana nakazi wanayofanya. Kwa mujibu wa uteuzi na masharti ya kazi, Mkataba wa 111wa ILO unayapa mataifa wajibu wa kuondoa ubaguzi kwa misingi mbalimbali,ikiwa ni pamoja na ‘jinsia’. Aidha inakubali kanuni kwamba hatua zinazolen ga‘uteuzi maalum’ zinaweza kutumiwa kushughulikia mahitaji ya makundiyanayohitaji ‘ulinzi au uzaidizi maalum’.

Itifaki ya wanawake wa Afrika ni mfumo wa kisheria wa kutumiwa nawanawake katika Afrika katika kutekeleza haki zao. Ni kijalizo cha Mkatabawa Afrika. Kama vile CEDAW, itifaki hii hairejelei kabisa wanawake wa kiasili.

126

Page 143: First page ILO.fm

Hata hivyo, haki nyingi ambazo zimeelezwa humo zinaweza kuwa na athari yamoja kwa moja kwa wanawake wa kiasili.411

Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watu wa kiasili linathbitishakwamba haki na uhuru wote uliondani yake unadhaminiwa kwa watu wakiasili, waume kwa wake.412 Katika vipengele viwili muhimu, wanawakewamewekwa katika kategoria moja na watoto pamoja na makundi mengine‘manyonge’. Mataifa yanafaa kuzingatia sana ‘haki na mahihtaji maalumu yawazee, wanawake, vijana, watoto na walemavu wa kiasili’.413 Suala moja lakutia wasiwasi sana, dhuluma dhidi ya wanawake (na watoto) limezungumziwakimahususi: ‘mataifa yatachukua hatua, kwa kushirikiana na watu wa kiasili,kuhakikisha kuwa wanawake na watoto wa kiasili wanafurahia ulinzi nahakikisho kamili dhidi ya kila aina ya dhuluma na ubaguzi.’414

9.3 Mielekeo ya kitaifa

Taswira ya ubaguzi kwa jumla na madhara yake maradufu

Hata pale ambapo haki za wanawake zimedhaminiwa kirasmi, ukweli uliopokatika kila nchi iliyotafitiwa ni kwamba wanawake bado wanakumbwa na ainanyingi za ubaguzi na upembezwaji. Kama walezi wa msingi, hasa maeneo yamashambani, wanawake ndio wanaokumbwa na kiasi kikubwa cha umasikini,ukosefu wa huduma za kijamii na magonjwa kama vile VVU na Ukimwi. Ulinzirasmi aghalabu humezwa na desturi namila. Wanawake wa kiasili hukumbwana madhara maradufu na ubaguzi: kwanza wanakumbwa na ubaguziunaowakumba wanawake wengine, na pili wanakumbwa na mitazamo nadesturi hasi kuhusu watu wa kiasili.

Katika kushughulikia haja ya kuhakikisha kuwepo kwa usawa wa kijinsia,katiba nyingi za mataifa yaliyohusishwa katika utafiti huu zinalinda haki yausawa na kutobaguliwa kama sehemu sehemu muhimu ya usawa wa kijinsia.Ubaguzi kwa misingi ya jinsia umekataliwa kwa jumla katika katiba nyingi.Wakati mwingi, ‘jinsia’ au sababu nyinginezo muhimu kama vile ‘hadhi yakindoa’ pia huhusishwa. Katiba za Misri, Kenya, Namibia na Uganda zinakatazaubaguzi kwa misingi ya jinsia, lakini katiba ya Afrika kusini inasonga mbele zaidikatika kusughulikia na kupinga ubaguzi kuhusu masuala yahusiana na jinsiakama vile ujauzito na ndoa.415

Ili kushughulikia hali ya wanawake wa kiasili kikamilifu, sheria inafaakutambua kuwa kutumikishwa kwao ni kubaya zaidi na hatua ‘mikakatimaalum’ inafaa kutumiwa. Hata hivyo, uwezekano wa kuwepo kwa mikakatikama hii ni mdogo sana ikizingatiwa kuwa mataifa mengi hata hayana mipangoya kuwaendeleza wanawake. Pana vighairi vichache. Katiba ya Ethiopia inakifungu ambacho kinakusudia kukuza usawa wa wanawake na kinachotambuahistoria ya ubaguzi wa kijinsia.416 Katiba ya Namibia inahusisha mikakatimaalum katika kutambua ubaguzi maalumu ambao umewakumbawanawake417 na hivyo kuhitaji kwamba sheria iundwe.418 Kutokana na haya

411. Tazama kwa fano, vifungu vya 2, 5 na 17 ambavyo vinaweza kuhusishwa hususan nawanawake wa kiasili.

412. Kifungu cha 44 cha UNDRIP.413. Kifungu cha 21(2).414. kifungu cha 22(2).415. Kama hapo juu.416. Kifungu cha 35 1-7.417. Kifungu cha 23(3).418. Kifungu cha 95(1).

127

Page 144: First page ILO.fm

inahitaji kwamba kuundwe sehria ambayo itazuia kutokea tena kwa ubaguziusiofaa dhidi ya wanawakwe.419 Katiba ya Uganda inaunga mkono usawawanawake kwa jumla na katika kutambua ukosefu wa usawa wa kihistoriainaruhusu haki ya kuwepo kwa uteuzi maalum, kama tu ilivyo Afrika kusini,Namibia na Ethiopia.420

Ndoa ya mapema na ya lazima

Usawa wa kijinsia huwa umetiwa ndani ya muktadha wa ndoa na uhusiano wakifamilia. Wanawake wa kiasili hukumbana na aina nyingi za unyanyasaji nakudhalilishwa katika muktadha wa sheria ya familia na hususan katika ndoa.Hali hii inasababishwa na tamaduni za kijadi, ambazo zimekuwa na wasifu wavitendo vibaya vya ndoa za mapema na za lazima kwa muda mrefu. Kati yaWamaasai wa Tanzania, kwa mfano, wanawake hulazimishwa kuingia katikandoa zilizopangwa, aghalabu wakiwa wa umri mdogo wa chni ya miaka 18, namara nyingi wakiozwa kwa wanaume wakubwa kwa umri kuwashinda.

Katiba nyingi zinawalinda watu binafsi kutokana na ubaguzi kwa misingi ya‘jinsia’, ijapo kwa mara fulani tu katika hali ya kindoa. Katiba ya Afrika kusiniinatoa mfano wa upigaji marufuku wa ubaguzi kwa misingi ya ndoa. Hatahivyo, kwa mujibu wa sheria ya kimila ya kiafrika, wanawake kijumlahawafaidiki kwa hadhi sawa na wanaume kutokana na ubabedume hasa katikandoa za kitamaduni. Suala hili limeshughulikiwa na sheria ya 120 kuhusuUtambuzi wa ndoa za kitamaduni ya mwaka wa 1998 ambayo inahusishakutambuliwa kwa ndoa za kimila. Kifungu cha 3 cha sheria hiyo kinaruhusumakubaliano ya watu wawili walio na umri wa zaidi ya miaka 18, kabla ya ndoahalali ya kimila kufanywa. Suala hili ni muhimu kwa watu wa kiasili kwa kuwawao hutegemea sana mila na desturi, na hivyo sheria kama hii inawapawanandoa wa kiasili kibali cha kisheria kwa ndoa zao. Kwa hivyo sheria hiiinahakikisha kuwa ndoa hata baina ya watu wa kiasili zinatokana namakubaliano baina yao na kupinga ndoa za mapema. Kifungu cha 6, ambachokinahusu hadhi na uwezo sawa wa mume na mke ambao wameoana kimila, nikipengele muhimu ambacho kinadhamini usawa wa kijinsia baina ya wanandoakiasili. Hii inahusisha uwezo wa mke kununua mali na kuuza, kuchukuakandarasi na kufungua kesi mahakamani, mbali na haki nauwezo wowoteambao anaweza kuwa nao chini ya sheria ya kimila.

Sheria kuhusu familia ya nchini Ethiopia (Tangazo la 213/2000) ina athariya moja kwa moja kwa haki pamoja na ulinzi wa wanawake walioolewa.Ingawa serikali imefanyia marekebisho vipengele vyake kuhakikisha kuwa kunausawa baina ya jinsia mbili, sheria hii inabakia ya Sheria ya Shirikisho kwenyekiwango cha kitaifa. Katika sehemu nyingi za mashambani, hasa kati yawafugaji, mifumo wa kitamduni na kidini unaotawala masuala ya familia ingalina nguvu na sheria mpya kuhusu familia zinaathari ndogo sana.

Wanawake wanaoishi katika nchi zenye familia zinazotawaliwa na Shari’ahaghalabu huwa na migogoro katika maisha yao ambayo huwa yenye usawa.Nchini Algeria kwa mfano, sheria ya kifamilia (Code de la Famille) inaruhusundoa za mitala, kwa wanawake wachache, na kukataza watu kuoa wanawakewasio Waisilamu. Mambo haya ni kinyume cha utamaduni wa Waamazigh.Wakati mwingine sheria yenye nguvu yaweza pia kupunguza makali ya sheriaya kiislamu (Shari’ah). Sheria kuhusu familia ya nchini Moroko, iliyokubaliwamnamo mwaka wa 2004, kwa mfano inatambulisha usawa wa kijinsia kama

419. Sehemu ya 9(4).420. Kifungu cha 33.

128

Page 145: First page ILO.fm

kanuni moja muhimu. Kulingana na sheria ya Sudan, wanaume na wanawakewana haki ya koana kwa makubaliano huru na kamilifu baina yao.421

Haki kuhusiana na mali na urithi

kwa kuwa maisha ya wanawake wa kiasili yanategemea ardhi, kutengwa kwaokutoka kwa utumizi wa ardhi kuna athari mbaya sana kwao. Kulingana nautamaduni wa Batwa, mali hupokezwa kinababa au wana wa kiume. Wakatimume wa mwanamke Mbatwa anapofariki, mjane huyo hana haki ya kudaimali ikiwa ni pamoja na ardhi.

Sheria ya Namibia kuhusu Usawa katika ndoa inakipengele kuhusu ndoakatika jamii yenye. Sheria hii, pamoja na Sheria kuhusu marekebisho ya Sjili yaHati ya Makubaliano, ilizuia uuzaji wa ardhi ya biashara na mume au mke bilakibali cha mwenzake. Zaidi ya hayo, Marekebisho ya sheria ya ardhi nambari 5ya mwaka wa 2002 inawapa wanawake haki sawa wakati wa kusilisha maombiya kupata haki ya ardhi ya jumuiya. Ingawa sheria haishughulikii wanawake wakiasili pekee yake, wanawake wote wakiwemo wa kiasili wamewekwa chini yasheria hii. sheria inapiga marufuku vitendo vya kibaguzi dhidi ya wanawakewalioolewa chini ya sheria ya kitaifa, lakini wanawake walioolewa kulingana nasheria ya kimila wanaendelea kukumbana na ubaguzi wa kisheria nakitamaduni. Mila zinazoruhusu watu wa familia kutwaa mali ya mumealiyefariki kutoka kwa wajane wao na yatima zingalipo.

421. Kifungu cha 15(1) cha katiba ya Sudan.

129

Page 146: First page ILO.fm

Akimalizia ziara yake nchini Kenya, Katibu maalum wa Umoja wa Mataifaanayehusika na watu wa kiasili aliiomba serikali kurekebisha na masharti yakibaguzi yaliyopo zinazoathiri haki za wanawake wa kiasili za kumiliki mali hasazile za wajane na waliotalakiwa.422

Sheria ya ardhi ya nchini Uganda inatoa vipengele ambavyo vinakusudiakufanikisha maslahi ya kiuchumi ya wanawake, hasa wale walioolewa. Sheriahii inakataza uuzaji wa ardhi ambamo mtu anaishi pamoja na mume au mkewake na ambamo wanapata riziki yao, bila ya ridhaa ya mmoja waoiliyoandikwa.423 Mapatano yoyote yanayofanyika bila rdhaa kama hiiyanafanywa kama yasiyofaa kisheria.424 Ni vyema kutajwa kuwa kuwautendakazi mkamilifu wa sheria hii umedhoofishwa na hali ya wanawakekukosa uwezo katika familia.425 Kama ilivyo na makabila mengi ya Uganda,urithi wa ardhi baina ya Wabatwa ni kutoka kwa baba hadi kwa mtoto wakiume.426 Nchini Ethiopia Uainishaji wa ardhi za mashambani wa mwaka wa2005 pamoja na sheria za ardhi zilizotolewa baadhi ya majimbo nchini Ethiopiazina vipengele vinavyodhamini haki za wanawake kumiliki ardhi na kuwapahaki sawa juu ya ardhi kama waume zao. Vipengele hivi vya sheria ya ardhivimetekelezwa katika maeneo fulani nchini, lakini wanawake wafugaji badohawajatumia haki kama hizi.

422. Ripoti ya Katibu maalum wa Umoja wa Mataifa anayehusika na watu wa kiasili nchinikenya, aya ya 119.

423. Kifungu cha 39(1)(a).424. Kifungu cha 39(4).425. Tazama M Nabacwa Working in gender and development in the Ugandan context. Makala

waliyopewa wanafunzi wa Sera ya Jinsia ya Maendeleo. Chuo Kikuu cha Wales Swansea, 4Disemba 2002, yalifanyiwa marekebisho April 1 2004, 4.

426. D Jackson (2003) Twa women, Twa rights in the Great Lakes region of Africa Minority RightsGroup 7.

Imedaiwa kuwa serikali ya Botswana hushindwa kutumia mbinu inayojaliutamduni kuhusu masuala ya usawa wa kijinsia, hali ambayo, kamainavyodaiwa, inaonekana lupitia kwa sera zake kuhusu watu wa kiasili. Kwamfano, ijapokuwa kuwapa Wabasarwa makao mapya kulikuwa na atharihasi kwa wanaume na wanawake, kulielekea kuwaathiri wanawake zaidi.Baina ya familia za Wabasarwa, wanawake walielekea kumiliki mifugowachache waliowanunua kutoka kwa mapato yaliyotokana na mauzo yavifaa walivyotengenza kwa mikono yao. Hata hivyo, wakati serikaliilipozilipa familia fidia kwa kuhamishwa kutoka katika Mbuga ya wanyamaya Kalahari ya Kati, ilielekea kuwapa wanaume mifubo kwa kuwa kulinganana utamaduni wa Watswana mifugo ilikuwa ya wanaume. Vivyo hivyo,wakati wa kugawanya ploti za ardhi baada ya kuwahamisha WatswanaHalmashauri za ardhi zilikuwa legevu kutoa vyeti kwa wanawake kwasababu katika utamaduni wa Kitswana wanaume ndio waliokuwa na haki yaardhi. Haya yalifanywa kwa kupuuza kaida za utamaduni wa Wabasarwaambapo wanaume na wanawake walikuwa sawa kinadharia. Katikamkumbo uu huu, Tangazo nambari 58/1994 la Eritrea linampa kila raia hakiya kutumia ardhi bila ubaguzi, ingawa shabaha finyu ya tangazo hili kuhusuhaki za ardhi za jamii zinazokaa mahali pamoja inaweza kuwaacha baadhi yawanawake wa kiasili bila ya msaada.

130

Page 147: First page ILO.fm

Dhuluma dhidi ya wanawake, ikiwa ni pamoja na ubakaji

Dhuluma za kimapenzi, ikiwa ni pamoja na ubakaji, dhidi ya wanawake wakiasili zinazofanywa na wanaume wabantu zimeonekana katika mataifawanamoishi wanawake ‘Mbilikimo’. Mambo, kama vile, uwezekanao mdogowa kupata haki pamoja na kukubali hali hizi kimya kimya, yanachangia ukosefukuhukumiwa kwa maovu haya. wakati wa migogoro, kama ilivyo masharikimwa Jmuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wanawake wa kiasili ndiowameathiriwa sana. Kusthiriwa kwao kunazidishwa na imani kwamba kufanyangono na wanawake ‘Mbilikimo’, ambao wamejaa sifa nyingi za kikale,kunaponya maradhi, ikiwemo virusi vya ukimwi.

Katiba ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inalipa kipaumbele suala ladhuluma za kimapenzi kwa kueleza kwamba ‘serikali za mitaa’ zinafaakuhakikisha kwamba suala hili limeondolewa. Kipengele huki kinasaidiwa nautekelezwaji wa vipengele katika Sheria ya Taratibu za kughulikia kesi za jinaina sheria inayohusisha kanuni za sheria ya kimataifa ya haki za kibinadamukuhusu dhuluma za kimapenzi. Sheria ya nchini Kongo ya mwaka wa 1998inayohusiana na ubainishaji na adhabu ya mauaji ya halaiki, uhalifu wa kivita najinai, inabainisha na kuvifanya vya ‘ubakaji’ na ‘utumwa wa ngono’ kuwa‘uhalifu dhidi ya binadamu’ na vinafaa kuadhibiwa.

Nchi kadhaa zimekubali Sheria kuhusu dhuluma za kinyumbani. NchiniAfrika Kusini Sheria ya 116 kuhusu dhuluma za kinyumbami ya mwaka wa1998 inasema kuwa mtu yeyote anaweza kuiomba mahakama kutoa agizo lakulindwa. Iwapo mahakama itathibitisha kuwa kuna ushahidi wa kutoshakwamba mshitakiwa anatekeleza au ametekeleza kitendo cha dhuluma zakinyumbani na mlalamishi kukumbwa na mateso yasiyofaa kutokana nadhuluma hiyo ikiwa agizo la serikali halitatolewa mara moja, lazima mahakamaitoe agizo la ulinzi wa muda kwa mshtakiwa. Ijapokuwa sheria hii haiwalengiwanawake wa kiasili pekee, inabakia kuwa njia nzuri ya wao kudai haki zao.Kama ilivyo na suluhu nyinginezo za kisheri, ufaafu wake utategemea kuwepokwake kijutendaji na uhalisi wa kupata haki. Afrika Kusini aidha ilianzishaMahakama za Usawa chini ya Sheria 4 ya kukuza Usawa na Kuzuia Unyanyasajiya mwaka wa 2000. Mahakama hizi zinatarajiwa ifanikishe ufikiwaji wawahasiriwa wa ubaguzi kwa msisingi yoyote ikiwemo jinsia. Hata hivyo,matukio ya dhuluma dhidi ya wanawake nchini Afrika Kusini, hasa kutoka kwamakabila yasiyobahatika na yaliyomasikini, yangali mengi.427 Kwa hakikaCERD imeiuliza Afrika Kusini kuchukua hatua madhubuti ‘kushughulikia haliya kubaguliwa maradufu, hasa kuhusiana na wanawake na watoto katikamakabila masikini na yasiyobahatika.’428

Namibia pia iliunda sheria dhidi ya dhuluma za kinyumbani. Hata hivyo,dhuluma dhidi ya wanawake yanabakia sula kubwa la kutia wasiwasi.. mnamomwaka wa 2008, CERD ilionyesha wasiwasi wake kuhusu vitendo vingivyaubakaji wa wanawake Wasan na watu wa jamii zingine, vitendo ambavyovinasababishwa na mitazamo hasi, na kupendekeza kuanzishwa kwa uchunguziwa madai hayo, na hivyo kuzidisha juhudi za kupambana na chuki.429

Nchini zingine haziendi ndani sana, na hivyo kuiachia sheria ya uhalifu kwajumla kukabilana na madai ya dhuluma za kimapenzi na kinyumbani. Kanuni ya

427. Angalia Maoni ya mwisho ya CERD (2006), aya ya 16.428. Kama hapo juu.429. Maoni ya mwisho ya CERD: Namibia, Agosti 2008, UN Doc CERD/C/NAM/CO/12.

131

Page 148: First page ILO.fm

adhabu ya Misri (Sheria ya mwaka wa 1937) inatoa vipengele mbalimbaliambavyo vinatia adhabu kwa dhuluma za kimapenzi dhidi ya wanawake.

Nchi nyingi, zikiwemo Botswana, Kenya na Nigeria, hazina sheriainayopinga Dhuluma za kinyumbani. Serikali ya Eritrea haijaunda seria zozotewala sheria inayopinga dhuluma dhidi ya wanawake.

Dhuluma dhidi ya wanawake, ikiwa ni pamoja na ubakaji

Dhuluma za kimapenzi, ikiwa ni pamoja na ubakaji, dhidi ya wanawake wakiasili zinazofanywa na wanaume wabantu zimeonekana katika mataifawanamoishi wanawake ‘Mbilikimo’. Mambo, kama vile, uwezekanao mdogowa kupata haki pamoja na kukubali hali hizi kimya kimya, yanachangia ukosefukuhukumiwa kwa maovu haya. wakati wa migogoro, kama ilivyo masharikimwa Jmuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wanawake wa kiasili ndiowameathiriwa sana. Kusthiriwa kwao kunazidishwa na imani kwamba kufanyangono na wanawake ‘Mbilikimo’, ambao wamejaa sifa nyingi za kikale,kunaponya maradhi, ikiwemo virusi vya ukimwi.

Katiba ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inalipa kipaumbele suala ladhuluma za kimapenzi kwa kueleza kwamba ‘serikali za mitaa’ zinafaakuhakikisha kwamba suala hili limeondolewa. Kipengele huki kinasaidiwa nautekelezwaji wa vipengele katika Sheria ya Taratibu za kughulikia kesi za jinaina sheria inayohusisha kanuni za sheria ya kimataifa ya haki za kibinadamukuhusu dhuluma za kimapenzi. Sheria ya nchini Kongo ya mwaka wa 1998inayohusiana na ubainishaji na adhabu ya mauaji ya halaiki, uhalifu wa kivita najinai, inabainisha na kuvifanya vya ‘ubakaji’ na ‘utumwa wa ngono’ kuwa‘uhalifu dhidi ya binadamu’ na vinafaa kuadhibiwa.

Nchi kadhaa zimekubali Sheria kuhusu dhuluma za kinyumbani. NchiniAfrika Kusini Sheria ya 116 kuhusu dhuluma za kinyumbami ya mwaka wa1998 inasema kuwa mtu yeyote anaweza kuiomba mahakama kutoa agizo lakulindwa. Iwapo mahakama itathibitisha kuwa kuna ushahidi wa kutoshakwamba mshitakiwa anatekeleza au ametekeleza kitendo cha dhuluma zakinyumbani na mlalamishi kukumbwa na mateso yasiyofaa kutokana nadhuluma hiyo ikiwa agizo la serikali halitatolewa mara moja, lazima mahakamaitoe agizo la ulinzi wa muda kwa mshtakiwa. Ijapokuwa sheria hii haiwalengiwanawake wa kiasili pekee, inabakia kuwa njia nzuri ya wao kudai haki zao.Kama ilivyo na suluhu nyinginezo za kisheri, ufaafu wake utategemea kuwepokwake kijutendaji na uhalisi wa kupata haki. Afrika Kusini aidha ilianzishaMahakama za Usawa chini ya Sheria 4 ya kukuza Usawa na Kuzuia Unyanyasajiya mwaka wa 2000. Mahakama hizi zinatarajiwa ifanikishe ufikiwaji wawahasiriwa wa ubaguzi kwa msisingi yoyote ikiwemo jinsia. Hata hivyo,matukio ya dhuluma dhidi ya wanawake nchini Afrika Kusini, hasa kutoka kwamakabila yasiyobahatika na yaliyomasikini, yangali mengi.430 Kwa hakikaCERD imeiuliza Afrika Kusini kuchukua hatua madhubuti ‘kushughulikia haliya kubaguliwa maradufu, hasa kuhusiana na wanawake na watoto katikamakabila masikini na yasiyobahatika.’431

Namibia pia iliunda sheria dhidi ya dhuluma za kinyumbani. Hata hivyo,dhuluma dhidi ya wanawake yanabakia sula kubwa la kutia wasiwasi.. mnamomwaka wa 2008, CERD ilionyesha wasiwasi wake kuhusu vitendo vingivyaubakaji wa wanawake Wasan na watu wa jamii zingine, vitendo ambavyo

430. Angalia Maoni ya mwisho ya CERD (2006), aya ya 16.431. Kama hapo juu.

132

Page 149: First page ILO.fm

vinasababishwa na mitazamo hasi, na kupendekeza kuanzishwa kwa uchunguziwa madai hayo, na hivyo kuzidisha juhudi za kupambana na chuki.432

Nchini zingine haziendi ndani sana, na hivyo kuiachia sheria ya uhalifu kwajumla kukabilana na madai ya dhuluma za kimapenzi na kinyumbani. Kanuni yaadhabu ya Misri (Sheria ya mwaka wa 1937) inatoa vipengele mbalimbaliambavyo vinatia adhabu kwa dhuluma za kimapenzi dhidi ya wanawake.

Nchi nyingi, zikiwemo Botswana, Kenya na Nigeria, hazina sheriainayopinga Dhuluma za kinyumbani. Serikali ya Eritrea haijaunda seria zozotewala sheria inayopinga dhuluma dhidi ya wanawake.

Tamaduni mbaya

Ukeketaji wa wanawake unabakia kuwa kikwazo kwa haki za kibinadamu zawanawake. Tatizo hili linasambaa kwa wanawake wa jamii za kiasili. Kulinganana utafiti kuhusu hali ilivyo nchini Nigeria, kwa mfano, ni Wafulani pekee ndiohawawakeketi wanawake, Waijau – kutegemea jamii wenyeji – wanafanyaukeketaji wa wanawake kwa kiasi fulani. Ukeketaji wa wanawake piaunafanywa sana kati ya makundi ya wafugaji katika Afrika mashariki, upembewa Afrika na kati ya makundi kadhaa wafugaji Magharibi mwa Afrika. NchiniNigeria, pia kuna sheria za serikali ya shirikisho zinzopiga marufuku ukeketajiwa wanawake. Baadhi ya mataifa kama vile Eritrea, katika siku za hivi karibunizimepiga marufuku shusghuli hii, lakini kufuatilia utekelezaji wake nichangamoto kubwa.

Tamaduni nyingine pia zinaharibu hadhi ya wanawake wa kiasili. NchiniKongo kwa mfano, mojawapo ya kitendo cha kudhalilisha ni kile chamwanamume wa kibantu ‘kumkomboa’ mwanamke wa kiasili kwa ajili yakuzaa mtoto na kisha baadaye mwanamke huyo kurejeshwa kwa jamii yake.

Haki za wanawake wa kiasili zimo katika hatari kutokana na vitendo vyandoa za mitala na wanawake wamo katika hatari ya kuambukizwa ukimwikwani hawana usemi katika masuala ya kimapenzi yao wenyewe wala yawaume zao. Nchini Ethiopia, ndoa za mitala katatika maeneo ya mashambani,ambako wanawake wengi wa kiasili huishi, zingali zainaruhusiwa sana serikaliza majimbo. Nchini Nigeria, ndoa za mitala ni nyingi sana baina ya jamiizakiasili; aghalabu wanawake kutelekezwa na waume zao wenye wake wengina kuachiwa majukumu ya kuwalea watoto. ndoa za mitala zimeharamishwakwa ambao kwanza wanaoa chini ya mtindo wa kimagharibi wa sheria yakikoloni kuhusu ndoa, lakini hakuna kumbukumbu yoyte ya walewalioshtakiwa. Katika kutoa mfano wa hatua ya kisheria, katiba ya Sudaninawekea serikali jukumu la ‘kukabiliana na mila na desturi mbaya ambazozinadhalilisha heshima na hadhi ya wanawake’.433

Haki ya kushiriki katika michakato ya kisiasa na ya kufanya maamuzi

Kama kanuni ya jumla, wanawake wa kiafrika wamewekwa faraghani tu nahawana wajibu wowote muhimu katika maisha ya faragha, ikiwemo siasa zavyama. Ijapokuwa hali hii inabadilika haraka, bado ingalipo kwa wanawake wakiasili. Ingawa wawakilishi wa wanawake katika bunge la Moroko iliongezekakutoka asilimia 0.6 hadi 10.8 mwaka wa 2007, hakuna ishara yoyote yakuimarika kwa uwakilishi wa wanawake wa kiasili.

432. Maoni ya mwisho ya CERD: Namibia, Agosti 2008, UN Doc CERD/C/NAM/CO/12.433. Kifungu cha 32(3) cha katiba ya Sudan.

133

Page 150: First page ILO.fm

Sheria ya kimila inaweza kuwa jambo linalochangia hali hii. sheria ya kimilaya watu wa kiasili ni tofauti na yaw engine, na inagawanywa baina ya zile ainazinazowaona wanawake kama watu duni katikasehemu fulani za maisha, lakinisio sehemu zingine, aina ambapo wanawake wanatawala katika sehemu fulaniza maisha na aina ambapo jamii haina matabaka. Wakati mwingine wanawakewa kiasili hutiishwa chini ya sheria ya kimila ya makundi ya wabantu wenyenguvu na hawana haki sawa kunena katika mikutano ya kgotla kama wanaume,kama inavyolazimishwa na mifumo hii. hata hivyo pana mwelekeo wa kukubaliusawa mkubwa zaidi kwa wanawake.

Nchini Afrika kusini, suala jingine linaloathiri usawa wa kijinsia kwawanawake wa kiasili ni wajibu na kushiriki kwa wanawake wa kiasili katikamaendeleo. kwa sasa, wanawake wengi wa kiasili hawajawakilishwa katikakuanzisha na kushiki katika mapatano na mikakati ya kuinua maslahi ya jamii.Hata hivyo, kwa wakati ambao umepita baadhi ya jamii hizi zimetambuamchango na wajibu mhimu wa wanawake katika maendeleo. kwa mfano. Jamiiya Riemvasmaak Namas imefanya juhudi za kuhakikisha kuwa wanawakewako mstari wa mbele katika mafunzo ya utetezi na mashauriano na serikali.Wanawake wa ‡Khomani huunda vikundi vya kufanya kazi vyao wenyewenhyakati za kupanga nkuhakikisha kuwa michango inayohusu jinsia yaoinazingatiwa.434 Ingawa hatua hizi hazijatumika kikamilifu, inatazamiwa kuwazitachochea mifumo inayofaa zaidi siku zijazo.

Katika nchi ambapo ‘hatua maalum’ zimechukuliwa kuhakikisha kunauwakilishi sawa wa wanawake katika nyanja ya siasa ya taifa, kama vile Rwandana Uganda, wanawake wa kiasili hawajalengwa moja kwa moja. katiba yaUganda inataka kila wilaya iwakilishwe na mwanamke mmoja kama mwakilishimaalum wa wanawake.435 Kipengele hiki kimeongeza idadi ya wanawakebungeni: idadi imekuwa ikiongezeka kwani wilaya nyingi zimeundwa ambaposasa zimefikia zaidi ya 70. kwenye kiwango cha mashinani, sheria ya serikali zamitaa inaruhusu thuluthi moja ya viti vya kila baraza la wilaya na mabarazamadogo vitengewe wanawake.436 Hata hivyo, kati ya Wakaramajong,wanawake bado hawahusishwi katika maamuzi. Wajibu wao muhimuunachukuliwa kuwa ni kulima na kuzaa watoto tu.437

Mojawapo ya sera ya serikali katika katiba ya Namibia ni kutoa sheriaitakayohakikisha kuwa pana usawa wa nafasi kwa wanawake ili kuwawezeshawanawake kushiriki kikamilifu katika kila nyanja ya jamii ya Namibia. Sera yakitaifa ya Namibia kuhusu jinsia ya mwaka wa 1997, inapigania usawa baina yawanaume na wanawake katika kila zote za maisha ya umma. Kufaulu kwalengo hili kunahitaji juhudi za pamoja ili kuondoa tofauti za kihistoria ambazozilikuwepo baina ya wanaume na wanawake hasa kutokana na sheria za kimilana desturi. kwenye kiwan go cha kitaifa, hatua kubwa zimefanywa kamainavyoshuhudiwa na kuwepo kwa mawaziri kadhaa wa kike akiwepo Naibuwa Waziri Mkuu, wabunge wa kike, makatibu wa kudumu na watu wenginewakuu serikalini. Kuteuliwa kwa mwanamke Mhimba kama naibu wa wazirikuliweka mwanzo mzuri wa kuwapa wanawake wa kiasili uwezo wa kisiasa.Chini ya Mpango wa maendeleo ya Wasan, miradi mbalimbali ya maendeleo

434. N Crawhall (1999) Indigenous Peoples of South Africa: Current Trends, Project to PromoteILO Policy on Indigenous and Tribal Peoples / South African San Institute, InternationalLabour Office, Geneva 33.

435. Kifungu cha 78(1)(b).436. Tazama sheria ya Serikali za Mitaa, kifungu cha 10(e) na 23(1)(e).437. Uganda Wildlife Authority (2004) Environmental Impact Statement of Land use change of

Pian-Upe Wildlife Reserve. Ripoti iliyoandaliwa na Ema Consults (Agosti 2004) inapatikanakwenye http://www.nemaug.org/UPLOADS/eian/, Sura ya 7.

134

Page 151: First page ILO.fm

kwa wanawake wa kisan imeanzishwa. Miradi ya Ushoni imeanzishwa katikamajimbo ya Omaheke na Oshikoto kwa usaidizi wa Wzara ya Jinsia, Usawa naMasilahi ya Watoto. Maandalizi ya mradi wa uokaji wa mikate katika jimbo laTsumkwe karibu yanakamilika. Zaidi ya hayo, ofisi ya Waziri Mkuu na Wizaraya Jinsia, Usawa na Maslahi ya Mtoto inshughulikia kuandaa uzinduzi waMuungano wa Wanawake wa Kisan. Kamati za wanawake wa Wasan tayarizimeanzishwa katika majimbo saba ya nchi ambamo jamii za San zinaishi, yaanimajimbo ya Oshana, Otjozondjupa, Omusate, Oshikoto, Kavango, Caprivi naOmaheke. Kongamano la wanawake wa San kuhusu maendeleo ambapochangamoto mbalimbaloi zinazowakumba wanawake wa Kisan zitajadiliwakama ilivyopangwa na litaongozwa na Wizara ya Jinsia, Usawa na Maslahi yaMtoto.

Haki za kiafya na uzazi

Kadiri na inavyoweza kuthibitika, kiwango halisi cha vifo vya kinamama bainaya wanawake wa kiasili ni vya juu sana katika nchi zote katika kanda hii.Wanawake wa mashambani, ambao ni pamoja na wanawake wa kiasili kamavile ‘Mbilikimo’, aghalabu hawapati huduma chache tu za afya, ikiwa ni pamojana huduma zinazohusiana na afya ya uzazi. Hali hii ndiyo kubwa zaidikuhusiana na wanawake wanaoishi katika maeneo ya jangwani yaliyotenwa,kama vile baadhi ya wanawake wa Amazigh. Wanawake wa kiasili wanaoishimaisha ya kuhamahama hawafaidiki kutokana na huduma za afyazinazopatikana.

Kifungu cha 12 cha CEDAW kinayapa mataifa wanachama jukumu la‘kuchukua hatua zinazofaa kuondoa ubaguzi dhidi ya wanawake, kupatahuduma za afya, zikiwemo zile zinazohusiana na upangaji uzazi’. Hata hivyo,ijapo kiwango cha wanawake wanaopata uzaidizi wa wakunga wenye ujuziimeongezeka katika miaka ya hivi karibuni, bado kuna tofauti kubwa zakimaeneo. Watu wa kiasili wanaishi katika maeneo ya mashambani ambapokuna viumba vya kutoa huduma za dharura kwa wanawake walio na matatizoya kujifungua, wakunga wachache wa kitamaduni na waliohitimu na miendomirefu wanayopasa kutembea ili kupata huduma za afya. Kwa hivyo chukuliziiliyopo ni kwamba vifo vya kinamama wanaojifungua ni vingi kati ya jamii zakiasili.

Wizara ya Afya na idadi ya watu ya Misri ina mipango mingi inayolengakutoa huduma za afya kwa kinamama na watoto na kupanga masuala ya afyaya jamii na ya kinamama ili kuhakikisha kuwa wanawake wanapata huduma zaafya, kuhakikisha kuna usalama wa kiafya kwa kinamama na watoto wao, nakupunguza vifo vya kinamama wanaojifungua. Mipango hii ni pamojana,mpango wa kuangalia masuala ya vifo vya kinamama wanaojifungua,mpango wa huduma za afya kwa kinamama wajawazito, mpango wa kutoahuduma kwa kinamama wakati wanapojifungua na mipango ya upangaji uzazina afya kwa kinamama.438 Kulingana na nafasi wanayoichukua wanawake, faidawanayopata inategemea kuwepo kwa vituo vinavyotoa huduma hizi katikamaeneo ya mashambani. Aidha, kwa kuwa mipango hii huwa imetayarishiwawanawake katika jamii pana, kuna shaka ikiwa kweli vituo hivi vipo hususankwa wanawake wa jamii ya Berber wanaoishi katika ardhi zilizojitenga zajangwa la magharibu na kwa wanawake wa jamii ya Bedouin, ambao kwamujibu wa maisha yao ya kuhamahama hawatulii mahali pamoja.

438. Tazama pia Ripoti ya ACHPR, 119-122.

135

Page 152: First page ILO.fm

Nchini Nigeria, kuna matukio mengi ya ugonjwa wa Vesicovaginal Fistula(VVF) kati jamii asili za Fulani kutokana na ukweli kwamba wasichana huozwawakiwa na umri mdogo. Serikali imefanya juhudi za kushughulikia suala hilikwa kutekeleza Sheria kuhusu Haki ya Mtoto ya mwaka wa 2003 kwa lengoka kupinga kuozwa kwa motto msichana na kuchumbiwa kwa wato.439

Ajira na kazi

Suala la ajira ya lazima limeshughulikiwa kwingineko. Katika muktadha wausawa wa kijinsia, inaweza kusemwa kuwa kuondolewa kwa ‘mifumo yakijamii ya usawa’ baina ya ‘Mbilikimo’ na nafasi yake kuchukuliwa na mifumomipya ya kijamii, inayokurubiana na mifano ya kibabedume ya Wabantu,kumesababisha mabadiliko ya majukumu ya jinsia mbalimbali. Wajinbu wakuhakikisha maslahi ya watoto na utoaji wa chakula kwa familia sasa hiviunawaangukia wanawake Wabatwa, ilihali kwa mila za jamii zinazokaa misitunimajukumu haya yaligawanywa baina ya wanaume na wanawake.440 Licha yahaya, tofauti katika za kiwango cha mapato kati ya wanaume na wanawake nidhahiri katika jamii za Kibantu. Kwa jumla wanawake wanapata asilimia 50chini kuliko wanaume;441 hali hii inalemaza uwezo wao wa kukimu familia zaoiapasavyo. Zaidi ya hayo, inaleta utofauti katika viwango vya ustawi wa uchumiwa kijamii baina ya wanaume na wanawake. Tatizo hili, kati ya mengineyo,linasababishwa na tofauti za kimuundo ambazo zipo baina ya wanaume nawanawake zinazosababishwa na tofauti za ujira kulingana jinsia.442

Mifumo ya kisheria katika nchi nyingi imepuuza kushughuliki masuala haya.

Ukosefu wa usawa kwatika elimu

Viwango vya kutojua kusoma na kunadika baina ya wasichana, kama vileWasan, Wabatwa, na makundi mengine ya ‘Mbilikimo’, Mbororo naWaamazigh, ni vya juu kuliki vile vya wavulana katika jamii hizi. Viwango vyawale wanaoacha shule pia viko juu, hata kwenye kiwango cha shule ya msingi,kwa sababu wasichana wa kiasili wanakumbwa na aina nyingi zaidi zaunyanyasaji kuliko wenzao wa kiume. Muda mrefu wa kutokuwa nyumbaniwakati wa mihula ya masomo na hali za mabweni vinawatia wasichana waKisan katika hatari ya kushambuliwa na visa vya upataji mamba kwa vijana, haliambayo inasababisha viwango vikubwa vya wasichana wa Kisan wanaoachamasomo.443

Mitazamo fulani ya ndani kwa ndani hata baina ya jamii za kiasili zenyeweinaweza kuzuia elimu ya wasichana wa kiasili. Kulingana na Katibu maalum waUmoja wa Mataifa anayeshughulika na watu wa kiasili, kati ya jamii yaWamaasai wa Kenya, wasichana huchukua nafasi ya kitamaduni baina yafamilia ya wazazi wao na ile ya waume zao. Katika muktadha unaotawaliwa naubabedume, hitaji la kuwaelimisha wasichana halichukuliwi kuwa muhimu,

439. http://www.un.int/nigeria/docs/GA_Docs/s_m-c_10_12_05.htm (accessed 24 January2007).

440. D Jacksoon ‘The health situation of women and children in Central African Pygmypeoples’ 1/06 Indigenous Affairs 38 40 – 41.

441. F Banda and C Chinkin ‘Gender, Minorities and Indigenous Peoples’ (2004) Minority RightsGroup International 24.

442. Tazama P Kagundu na O Pavlova ‘Gender wage differentials in Uganda: Evidence from theUganda National Household Survey’ Andrew Young School of Policy Studies, Workingpaper 07-26.

443. M Bolaanena S Saugstad ‘Mother-Tongue: Old Debates and New Intiatives in SanEducation’ IWGIA 1/06 46 59.

136

Page 153: First page ILO.fm

kwani familia nyingi huhisi kuwa hakuna maana ya kufanya uwekezaji wakiuchumi katika elimu ya mwanamke iwapo matunda ya uwekezaji huoyatafurahiwa tu na familia ya mume.

Licha ya juhudi za kuondoa tofauti kufanywa, ukosefu wa usawa bado upo.Namibia iliidilisha lengo nambari 3 la Malengo ya Maendeleo ya Milenia yaKukuza Usawa wa kijinsia na Kuwapa wanawake uwezo kwa kuondoatofautiza kijinsia katika elimu. Hata hivyo, zipo tofauti za kimsingi za kimaeneo bainaya wavulana na wasichana wakati wa kuchanganua kujua kuandika na kusomapamoja na viwango vya wanaojiunga na shule katika maeneo yaliyo na watuwa kiasili.

9.4 Hitimisho

Licha ya kuwepo kwa vipengele vya kisheria kuhusu usawa wa kijinsia katikamataifa mengi, wanawake wangali wanakumbwa na ukosefu wa usawa kwaupana. Wanawake wa kiasili aghalabu hukumbwa na ubaguzi maradufu,kwanza kwa kuwa wa kiasili, na pili kwa kuwa watu wa kike. Kutokana namiktadha fulani ya uchumi wa kijamii na kitamaduni wanamojikuta, wanawakewa kiasili hukumbwa na halimbaya zaidi katika masuala kama ndoa ya mapemanay a lazima, dhuluma za kinyumbani, ubakaji, tamaduni mbaya kama vileUkeketaji, pamoja na kutengwa katika elimu na kufanya uamuzi kisiasa.Matokeo ya haya ni kuwa viwango vyao vya elimu ni duni ikilinganishwa nawanaume wa kiasili. Wanawake wa kiasili pia wamo katika hatari kubwa yakuambukizwa virusi vya ukimwi. Aidha wametengwa katika kufurahia haki zakumiliki mali na haki ya kurithi.

Mataifa hayajachukua hatua sana kushughulikia hali mahususi za unyongewa wanawake wa kiasili. Vipengele vyote vinavyohusu haki za wanawake –kama vile ulinzi wa kikatiba dhidi ya kubaguliwa kwa misingi ya jinsia, sheriadhidi dhuluma za kinyumbani, na hatua maalum – havijazingatia mahitajimaalumu ya wanawake wa kiasili na havijatumika kushughulikia wasiwasi wao.

137

Page 154: First page ILO.fm
Page 155: First page ILO.fm

139

10 Watoto wa kiasili

10.1 Utangulizi: Umuhimu na mahitaji maalum ya watoto wa kiasili

Huku maisha hasa ya watu wengi wa kiasili yakiendelewa kuwa hatarini,inafuatia kuwa haki za watoto, ambao ndio tegemeo la siku zijazo, zinahitajikulindwa. Kwa kuwa watu wa kiasili wanaendelea kupembezwa, kunauwezekano kwamba watoto wao watashawishiwa kutoka kwenye desturi zaza kiasili. Kutokana na kukosekana kwa ulinzi wa kisheria wa kutosha,uwezekano wa watoto wa kiasili kulazimishwa kuacha utamduni wao nakupata ajira au kufuatilia masomo kutokana na ushawishi wa usasa au hasauraia wa kushurutishwa.

10.2 Sheria ya kimataifa

Kifunbgu cha 22 cha UNDRIP kinayapa mataifa wajibu wa kuzingatia sanamahitaji na haki maalum za makundi fulani wakiwemo watoto na vijana wakiasili. Aidha mataifa yanahitajika kushirikiana na watu wa kiasili ili kuwekamikakati ya kuwalinda watoto wa kiasili dhidi ya dhuluma na ubaguzi. Wakatifulani kabla ya kukubaliwa kwa UNDRIP, mnamo mwaka wa 2002, Baraza kuula Umoja wa Mataifa lilikuwa limehimiza mataifa kutoa msaada maalum nakuhakikisha kuwa watoto wa kiasili wanaweza kupata huduma kwa usawa.444

Vipengele vya hapa juu ni seehemu ya viwango visivyo vya lazima vya ulinzi wawatoto wa kiasili.

Ijapokuwa vipengele fulani katika sheria ya kimataifa kuhusu haki zakibinadamu haviwalengi hususan watoto wa kiasili, vinayataka mataifawanachama kuhakikisha kuwepo kwa ulinzi maalumu wa haki za watoto kwajumla. Kifungu cha 10(3) cha ICESCR hususan kinayataka mataifa kuchukuahatua maalumu za kulinda watoto na vijana bila ubaguzi. Aidha kifungu hikikinahitaji kwamba watoto na vijana walindwe dhidi ya unyonyaji wa kiuchumina kijamii, na dhidi ya ajira mbaya. Kifungu cha 24 cha ICPPR vile vilekinadhamini haki za watoto dhidi ya kila aina ya ubaguzi na kulinda haki zao zakusajiliwa kuzaliwa kwao, jina na uraia.

Vipengele vingine vya jumla kuhusu ulinzi wa watoto vinaweza kupatikanakatika Mkataba wa ILO nambari 138, ambao unapiga marufuku kuajiriwa kwawatoto chini ya umri wa miaka 15 katika kazi fulani.445 Mkataba wa ILO wanambari 182 pia kinahimiza kupigwa marufuku na kuondolewa kwa ajira yawatoto, hasa aina mbaya kabisa za ajira.446 Mkataba kuhusu haki za Mtoto(CRC) pia unavipengele fulani muhimu kuhusu ulinzi wa haki za watoto kwajumla. Hata hivyo, vipengele mahususi kabisa kuhusu ulinzi wa haki za watotowa kiasili vinaweza kupatikana katika vipengele fulani vya CRC na kwenyeMkataba wa ILO nambari 169.

Katika kifungu cha 17(d), 29(1)(c)(d) na 30, Mkataba kuhusu haki zawatoto moja kwa moja unabainisha watoto kama ndio wenye haki. Vipengelehivi kwa pamoja vinatambua haki za watoto wa kiasili kufurahia utumizi wa

444. Aya ya 20 ya A World Fit For Children (stakabadhi ya kikao maalumu cha UNGA kuhusuwatoto.

445. Kifungu cha 2 cha Mkataba wa 138 wa ILO. Kifungu cha 3 cha Mkataba huu kinaeleza umriwa kuajiriwa kwenye kazi hatari kama miaka 18.

446. Kifungu cha 1 na 3 cha Mkataba wa ILO nambari182.

Page 156: First page ILO.fm

140

lugha zao katika vyombo vya habari na haki ya kusoma na kuendeshautamaduni na dini zao katika jamii pamoja na wanajamii wengine. IngawaKamati ta CRC katika maoni yake ya mwisho ilimulika sana wasiwasi wakekuhusu watoto wa kiasili, undendaji wake bado si thabiti. Katika hali zingine,kama ilivyo ripoti ya Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Kamati ya CRC haikugusiawatoto wa kiasili katika maoni yake ya mwisho. Katika Maoni ya Jumlanambari 11 kuhusu ‘watoto wa kiasili na haki zao chini ya Mkataba huu’,yaliyokubalika hivi karibuni, Kamati ya CRC inayapa mataifa maagizo ya kinakuhusu jinsi ya kutekeleza wajibu wao chini ya mkataba wa CRC kuhusiana nawatoto wa kiasili. Kwa hali hii, huweza kuimarisha vipengele au mwelekeo waMkataba wa ILO nambari 169 na Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusuhaki zawatu wa kiasili. Kwa kueleza matumizi ya kila mojawapo wa vipengele vyaCRC kwa watoto wa kiasili, Mkataba huu unataja kwa mfano kwamba watotowa kiasili, hasa kuliko wale wasio wa kiasili, bado hawajasajiliwa kuzaliwakwao; kwa hivyo mataifa yanafaa kuhakikisha kuwa hususan watoto wa kiasili,wanasajiliwa maratu baada ya kuzaliwa na kwamba wapewe uraia kamasehemu yao mchakato huru na uanaopatikana.447

Kwa upande wake, kipengele cha 28 na 29 cha makataba wa 169 waShirika la leba la kimataifa (ILO), pia vinashughulikia haki za watoto wa kiasilikufundishwa katika lugha, utamaduni na dini yao. Vipengele hivi vinaimarishwana vipengele vyote vilivyomo kwenye vyombo vyote vya haki za kibinadamuvinavyopinga ubaguzi kwa msingi wa kabila au hali alimozaliwa mtu.

Kwenye kiwango cha kimaeneo, vipengele vya jumla katika kifungu cha 18cha Mkataba wa Afrika na vipengele vyote vya Mkataba huu kuhusu haki namaslahi ya mtoto kwa pamoja vinadhamini ulinzi wa watoto kwenye kiwangocha jumla. Hata hivyo, hamna mtajo mahususi kuhusu watoto wa kiasili. Kwakweli, dhana yenyewe ya ‘watu’ ambayo ndiyo mojawapo ya sifa bainifu zaMkataba wa Afrika, haimo kwenye Mkataba wa Afrika Kuhusu watoto. dibajiya Mkataba wa Afrika kuhus Watoto unatambua hitaji la ulinzi na ulenzimaalum wa watoto. inaweka wazi haki ya kupata elimu ili kukuza nakuendeleza hulka, vipaji na uwezo wa watoto wa kiakili na kimwili kwaukamilifu wake (kifungu cha 11), haki yao kupumzika na kujiburudisha (kifungucha 12) na kufurahia kufikia hali bora ya afya kimwili, kiakili na kiroho (kifungucha 14). Watalindwa dhidi ya kila aina ya unyanyasaji wa kiuchumi (katikasektarasmi na zisizorasmi, kifungu cha 15), kuwapa haki ya kufurahia ulezi naulinzi wa wazazi (kifungu cha 19): wazazi wana wajibu wa kimsingi wa kuwaleana kuwakuza watoto. kifungu cha 31 cha Mkataba wa Afrika kuhusu watotopia unawapa watoto wajibu kwa familia na jamii, kulingana na umri na uwezowao(na kulingana na mipaka fulani). Haki hizo zote zitafafanuliwa chini yakanuni ya maslahi bora ya mtoto: maslahi ya mtoto ndio kanuni elekezi. Chiniya Mkataba wa Afrika kuhusu Watoto, mtoto ina maana kuwa kila binadamuyeyote aliyechini ya umri wa miaka 18 (kifungu cha 2). Unaeleza hususan ulinziwa mtoto dhidi ya mila mbaya ambazo zinadhuru afya yake, na kupigamarufuku ndoa za watoto. Mkataba huu umetiwa sahihi na nchi 43 za Afrika.

447. Aya ya 41 na 42.

Page 157: First page ILO.fm

141

10.3 Mielekeo ya kitaifa

Hali mahusuzi za unyonge zilizofunuliwa

Watoto wa kiasili wanakumbwa na hali mbaya sawa na wanakumbana ukiukajisawa wa haki za kibinadamu kama zilivyo familia na jamii wanamotoka, kamavile kutengwa kijamii, kutopata huduma za afya za kutosha na elimu, umsikinina shutuma za kijamii. Vipengele vilivyojadiliwa kwingineko katika ripoti hii,kama vile kutobaguliwa au elimu, bila shaka ni vya maana sana kwa watoto.bado watoto wa kiasili wamokatika hatari fulafulani ambazo baadhi yazozimetajwa hapa:

Kuzaliwa kwao mara nyingi huwa hakusajiliwi, hali inayowaweka katikahatari wakati wanapokumbana na urasimu wa serikali.

Wanakumbana na ajira ya lazima. Mojawapo ya mambo yanayotia wasiwasiambayo yamefunuliwa katika ripoti za nchi ni suala la ajira ya watoto (hasaaina mbaya zaidi za ajira, kama vile utumwa, ajira ya lazima, ukahaba nautwana au ujakazi), ambalo linatishia ustawi wa mtoto kimwili, kiakili nakimaadili. Ufanyikazi huu usio na malipo kwa jumla unahusiana kwa karibusana na umasikini na kukosa elimu. Hali hii hatari na isiyothabiti ambamowatoto w kiasili wanaishi, inawalazimu kujiingiza katika vitendo hivi vyakunyanyaswa kiuchumi na kimapenzi.

Watoto wa kiasili wako katika hatari ya kuwa kama wanajeshi watoto aukuwa wahasiriwa wa mapigano. Hivi haswa ndivyo ilivyo katika Afrika ya Katiambapo makundi ya ‘Mbilikimo’ wanaishi ndani au karibu na maeneoyanayowaniwa sana na yaliyo na utajiri wa madini. Watoto wanawezakulazimishwa au kushawishiwa kwa urahisi kuwa wanajeshi katika mojawapoya majeshi na wasichana kulazimishwa au kushawishiwa kujiingizakatikauhusiano wa kimapenzi na wanjeshi.

Tamaduni zinaweza kuathiri vibaya matarajio yao maishani. Mifano yake nikama, ndoa zinazopangwa na wazazi, ndoa za mapema na za lazima;ukekeketaji wa wanawake.

Maoni ya Jumla ya nambari 11 (2009) yanasisitiza kuwa mataifa yanafaakushirikiana pamoja na jamii za kiasili ili kuhakikisha kwamba tamaduni mbayakama vile ndoa za mapema na ukeketaji wa wanawake zimeondolewa. Kamatiinayahimiza sana mataifa wanachama kuunda na kutekeleza kampeni zauhamazishaji, mipango ya elimu na sheria zinazolenga kubadilisha nia nakushughulikia masuala ya majukumu ya jinsia na mitazamo inayochangiavitendo vibaya.448 Nchini Eritrea, Tangazo nambari 158/2007 lilipiga marufukuukeketaji wa wanawake, kitendo ambacho pia kinawaathiri wasichana wengiwa kiasili. Nchini Ethiopia, hatua zilichukuliwa kulinda mtoto msichana kwakuharamisha ukeketaji wa wanawake katika Kanuni ya Adhabu na kuinuakiwango cha umri wa chini kabisa wa mtu kuhiari kuolewa. Hata hivyo, sheriahaijatekelezwa kabisa na haijaambatana na kushirikishwa kwa jamii kikamilifu.

Wasichana hususan wamo hatarini, hasa kutokana na dhuluma zakimapenzi na ubakaji. Watoto wa kiasili wanachukuliwa na baadhi baadhi yadesturi kama wasiobahatika na wanyonge, kategoria ambayo inahusisha;mayatima, walemavu watoto waliotelekezwa na wa mitaani kati ya wengineo.

448. Aya ya 22.

Page 158: First page ILO.fm

142

Wanakumbana na ubaguzi wa hali ya juu, hali ambayo inaonengezekakutokana na dhiki ya kitamaduni na kijamii zinamoishi jamii zao. Ubaguziwanaouvumilia watoto wa kiasili kama sehemu ya makundi ya kiasiliuanzidishwa kwa upande wa watoto wasichana. Wanakumbwa na ubaguziaina tatu, kwa kwa msingi wa kuwa wa kiasili, wanawake na pia kuwa niwatoto. mambo mengine yanayohusiana na ubaguzi wanaokumbana naoyanaweza kuelezwa kwa kurejelea afya na lishe na ukosefu wa huduma namisaada ya kutosha za matibabu (ukosefu wa chanjo na viwango vya juu vyavifo), vile vile kwa upande wa nyumba, ukosefu wa chakula na maji ya kunywa.Kutokana na hali hii, mtoto msichana anakumbwa na hatari nyingi mbali nazile ambazo zimekwisha tajwa. Hatari hizi ni pamoja na dhuluma, biashara yabinadamu, utekaji nyara mila na desturi mbaya (yaani ukeketaji wa wanawakendoa za mapema na za lazima). Hali hizi zote zinadunisha hadhi yao nakusababisha hali ya kuhisi kuwa wamepembezwa, na hivyo kuzuiakuchanganyika kwao katika utamaduni mkubwa vile vile na uwezekano wakupanua nafasi zao na kuwa na maisha bora.

Mengi ya mambo haya yanaungana na kuwaacha watoto wa kiasiliwasiandaliwe vizuri kwa masomo na kuwafanya wasihudhurie shule. Kutokanana hayo, kiwango cha kutojua na kuandika na viwango vya kuhudhuria shuleviko chini sana baina ya watoto wanaotoka katika jamii hizi.

Kimya cha sheria

Licha ya hitaji hili dhahiri la kushusghulikia masuala haya, mifumo ya kikatiba,sheria na sera haitaji watoto wa kiasili kama kikundi hasa kilichohatarini.

Katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwepo na kuongezeka kwa idadi yakatiba zilizo na vipengele ambavyo hususan vinadhamini haki za watoto.kufuatana na mwelekeo wa jumla wa katiba hizi, hamna katiba yoyote baina yahizi inataja watoto wa kiasili.

Baadhi ya haki za jumla za watoto katika mifumo ya katiba ambazozinaweza kuwafaa watoto wa kiasili lakini haziwarejelei kwa uwazi ni kamavile: kifungu cha 24 cha katiba ya Burkina Faso ina kipengele kuhusu ulinzisawa wa watoto. katiba ya Burundi, katika kifungu chake cha 44 inadhaminiafya, ustawi na usalama wa mtoto. Kifungu cha 36 cha katiba ya Ethiopiakinalinda haki za watoto zilizomo kwenye Mkataba kuhusu Haki za watoto(CRC), ikiwa ni pamoja na haki ya kuishi, kupewa jina na uraia; na kulindwadhidi ya unyanyasaji na kudhulumiwa.449 Kifungu cha 95 (b) cha katiba yaNamibia kinaitaka serikali kuhakikisha kuwa ‘watoto hawadhulumiwi nakwamba raia hawalazimishwi na uhitaji wa kiuchumi kujiingiza katika kaziambazo haziafikiani na umri na nguvu zao.’ Katiba za Jamuhuri yaKidemokrasia ya Kongo, Afrika Kusini na uganda zina orodha ya kimili ya hakiza watoto.

Mataifa mengi zaidi pia yanatumia sheria zinazolenga watoto. Hamnamahali katika matini hizi ambapo watoto wa kiasili wametajwa. Maoni ya Jumlaya nambari 11 ya kamati ya Mkataba kuhusu Haki za Watoto (CRC)yanasisitiza kuwa mataifa yanahitaji kutumia sheria mwafaka kulingana na CRCili ‘kutekeleza kikamilifu haki zilizomo kwenye Mkataba kuhusu watoto wakiasili’.450 Idadi kubwa ya mataifa ya Afrika, hasa yaliyoko Kusini na Mashariki

449. Kamati inayohusiana na Haki za Mtoto, Ethiopia, UN Doc CRC/C/129/Add.8, aya ya 21,31, 28 Oktoba 2005.

450. Aya ya 80.

Page 159: First page ILO.fm

143

mwa Afrika, yametwaa sheria zinazolenga watoto. Hata hivyo, kwa kuwawatu wa kiasili (pamoja na watoto wao wa kiasili) hawajatambuliwa ipasavyo,ulinzi a wa haki za watoto wa kiasili unabakia finyu, wa dharura na mdogokuhusiana na ulinzi wa watoto kwa jumla. Hakuna juhudi zozote zimefanywaama kwa kuunda au kutumia sheria hizi ili kushughulikia mahitaji maalum yawatoto wa kiasili. Ifuatayo ni mifano ya sheria kuhusu watoto ambazozinafumbata uwezo mkubwa ambao haujatambuliwa kwa watoto wa kiasili:

Kenya imeunda sheria inayoshughulikia haki za watoto na kupinga ubaguzidhidi ya watoto kama vile Sheria ya Watoto nambari 8 ya mwaka wa 2001,ambayo inaidilisha Mkataba wa Umaja wa Mataifa kuhusu haki za Mtoto naMkataba wa Afrika kuhusu haki na maslahi ya mtoto. Sheria ya watoto katikakifungu cha 5 kinasisitiza kwamba hakuna mtoto yeyote atakayebaguliwa kwamsingi wa asili, jinsia, dini, imani, mila, lugha, maoni, dhamiri, rangi, kuzaliwa,hadhi ya kijamii, kisiasa, kiuchumi au hadhi nyingineyo,, ulemavu, mbari, kabilamakaazi au uhusiano uliopo. Namibia ilikubali Sheria ya watoto (nambari 33ya mwaka wa 1960). Hata hivyo, kwa kuwa serikali haiwatambui watu wakiasili hasa, ulinzi wa haki za watoto wa kasili unabakia wa dharura na mdogosana kulingana na ulinzi wa haki za watoto kwa jumla. Sheria ya Jamuhuri yaKidemokrasia ya Kongo ya mwaka wa 2002 ilipiga marufuku aina mbaya zaidiza ajira ya watoto.

Hata rasimu ya Sheria ya Kongo kuhusu uendelezaji na ulinzi wa haki zawatu wa kiasili, ambayo inahusu masuala mengi ya haki za watu wa kiasili,haitaji watoto wa kiasili kwa wazi.

Nyingi ya sheria hizi zinazingatia sana watoto waliohatarini au watoto‘walio katika hali ngumu,’ hasa watoto wanaorandaranda barabarani, walio naulemavu, mayatima, watoto walio weknye mzozo na sheria. Watoto wa kiasilihawamo kwenye orodha hii, pengine kutokana na kutotambulika kwa watuwa kiasili kama watu katika mengi ya mataifa haya. wakati wowote ule, hatakama sheria zinatumika kuhusiana na watoto wa kiasili, suala hili halitakuwadhahiri iwapo hakuna takwimu ambazo zimegawanywa kulingana na umri, asiliya kikabila, wakiwemo watu wa kiasili.

Asasi nyingi zaidi zinazolenga hasa haki za watoto pia zinaundwa. Mtindoule ule unajirudia hapa: hamna nafasi ya masuala ya kiasili katika mawanda yashughuli za mashirika haya. Kwa mbfano: mnamo mwaka wa 1990, Kameruniilianzisha Tume ya Kitaifa ya Kuwalinda watoto walio hatarini kimaadili,wahalifu na wale waliotelekezwa (Commission Nationale pour la protection del’enfance en danger moral, délinquante et abandonee. Mwelekeo wa kuundabunge za watoto (kwa mfano nchini Burkina Faso na Jamuhuri ya Afrika yaKati) haujahusisha watoto wa kiasili katika mabaraza haya, wale hakunakipengele chochote kimewekwa kuhusu kuhusishwa kwao. Kenya imeanzishamfumo wa kitaasisi wa kulinda haki za watoto, mfumo umbao unahusishaBaraza la Kitaifa kuhusu watoto, Idara ya Huduma za Wtoto, ilio katika ofisiya makamu wa rais, serikali za mihtaa na mahakama za watoto.451

Hata wakati ambapo mataifa hutoa ripoti kulingana na Mikataba ya haki zakibinadamu ya Umoja wa Mataifa, hususa ule mkataba wa Haki za watoto(CRC), aghalabu huwa hayatilii maanani yoyote masaibu ya watoto wa kiasili.Wakati Jamuhuri ya Afrika ya Kati ilipowasilisha ripoti yake ya muhula kwaCRC, haikutaja kabisa masuala mahususi yanayowakumba watoto wa kiasili.

451. African Peer Review Mechanism, Country Review Report of the Republic of Kenya, May2006, African Socialism and its Application to Planning in Kenya, Sessional Paper No 10,Government Printer, 1966, 108.

Page 160: First page ILO.fm

144

Ni faradhi kuongeza kuwa Kamati ya CRC, katika uchunguzi na maoni yake yamwisho mnamo mwaka wa 1999 pia haikurejelea suala hili. Kama ambavyoimeelezwa kwingineko, kwa sasa kuna ufahamu zaidi juu ya umuhimu wa sualahili baina ya wanakamati wa kamati ya CRC. Kukubaliwa kwa Maoni ya Jumlanambari 11 bila shaka pia kutaimarisha mkondo huu.

Hakuna mikakati maalum kwa watoto wa kiasili

Kwa hivyo uwezekano wa taifa loloto kuweka mikakati ‘chanya ‘ au ‘maalum’kushughulikia hali ya watoto wa kiasili ya kutobahatika iliyokita mizizi nimdodo sana.

Kwa,kiwango fulani, sheria ya kimataifa inavipengele mahususivinavyotambua haki za waoto wa kiasili. Licha ya utambuzi huu rasmi na wamoja kwa moja, katiba nyingi za nchi zilizochunguzwa hazina vifungu mahususivinavyoshughlikia matatizo au haki za watoto wa kiasili, na hata hazidhihirishiulinzi uliodhaminiwa na Mikataba iliyotajwa hapo juu, ambayo nchi hizi niwanachama. Huku ulinzi wa jumla wa watoto ukiwa umehakikishwa katikanchi nyingi, haitambuliki kwamba watoto wa kiasili wana matatizo maalumu namahususi yanayohitaji kushughulikiwa.

Baadhi ya sera na mipango inayoleta matumaini

Katika nyanja ya sera na mipango, hali ya watoto wa kiasili angalau wakatimwingine hushughulikiwa kwa wazi kuliko ilivyo kwenye katiba, sheria namifumo ya taasisi. Hii inadokeza mwelekeo wa ongezeko la ufahamu kwenyekiwango cha sheria ‘hafifu’ (isiyofunga).

Tangu Kamati Teule ya Tume ya Afrika kuhusu Watu/ jamii za kiasili ifanyeziara nchini Namibia (mnamo July/Agosti 2005), seriakali ya Namibiaimezindua Mpango wa Maeneleo kwa Wasan. Mpango huu ambaoulipendekezwa na Naibu wa Waziri Mkuu na kuidhinishwa na Baraza lamawaziri Septemba 29 mwaka wa 2005, lengo lake ni kuhakikisha kuwa kunakuhusishwa kwa Wasan katika mpangilio mpana wa uchumi wa kijamiikikamilifu. Huku mipango kadhaa ikiwa imezinduliwa kwa ajili ya Wasan, raisPohamba pia alimshauri Naibu wa Waziri Mkuu kuhakikisha kuwa jamii zawahamahamaji za Ovatue na Ovatjimba wa eneo la Kunene wamepewamakaazi mapya. Chini ya mpango wa Elimu kwa Wasomi wa Kisan (udhaminiwa masomo), Ofisi ya Naibu wa Waziri Mkuu ilizindua kampeni za ‘Rudishuleni na Udumu shuleni kwa watoto wa Kisan’. Msaada wa kifedhaumetolewa kwa watoto wa San kwanzia masomo msingi hadi chuoni.

Nchini Uganda, Wizara ya Jinsia, Leba na Maendeleo ya kijamii ilitwaasera ya kushughulikia mahitaji ya mayatima na watoto wenginewasiojiweza.452 Lengo la sera hii ni kutimiza haki za watoto mayatima nawasiojiweza na kuhakikisha kuwa wajibu kuhusu watoto hawa umetimizwa. Ilikuafikia lengo lake, NSPPI inabainisha kanuni 13 zinazoelekeza mpango huu.Ijapokuwa sera hii haikusudiwi watoto wa kiasili, inaweza kupanuliwakuhusisha watoto kama hawa. Mojawapo ya mpango wa pekee wa serikaliambao hususan unawahusisha watoto wa kiasili ni mpango wa elimu maalumu,

452. Tazama; Mpango wa Mikakati ya kitaifa wa Wizara ya Jinsia, Leba na Maendeleo ya jamii,wa kuwasaidia watoto mayatima na watoto wengine wasiojiweza,Mwaka wa kifedha wa2005/6 – 2009/10.

Page 161: First page ILO.fm

145

ABEK, kwa watoto katika Karamoja. Hata hivyo mpango kama huuhaujafanywa kwa ajili ya watoto wengine wa kiasili kama vile Batwa.

Hata hivyo, sehemu kubwa ya sera – hata hati za mikakati ya kupunguzaumasikini – hazitoi umuhimu wowote kwa nafasi ya watoto wa kiasili. Mfanomwingine ni mfumo wa msaada wa kiufundi kuhusu ajira ya watoto – mfumounaolenga kuondoa kila aina mbaya ya ajira ya watoto (almaarufu TECL) –unaoendeshwa katika mataifa kadhaa ya kusini mwa Afrika, kwa kushirikianana ILO. Fasili ya ‘watoto wasiojiweza’ katika rasimu yake, Mpango kuhusuuondoaji wa ajira ya watoto (APEC) hautambui kwamba watoto wa kiasiliwamo kwenye kategoria hii.

10.4 Hitimisho

Kutokana na mambo yaliyoelezwa hapa juu, tunaweza kubainisha hali yakushindwa kuchukua hatua mahususi za kulinda haki za watoto wa kiasili.Kushindwa kwa jumla kukubali ukosefu wa watoto kujitetea na hatari za ajiraya watoto, pamoja na ukosefu wa nia ya kisiasa kupambana na hali yakutojiweza inayowaathiri watoto, kunaeleza ukosefu huu wa ukosefu waulinzi. Kuidilishwa kwa vipengele vilivyotajwa kwenye vyombo vya kimataifana kimaeneo kunafaa kuafikiwa ili kuwepo na sera nzuri kuhusu watoto, na ilikutekeleza hatua madhubuti za ulinzi, zinazolenga watoto kufikia maendeleomazuri katika kila hali; uhuru, heshima na ubinadamu. Licha ya hitaji hili, sheriakatika nchi nyingi zilizochunguzwa hasa haisemi chochote juu ya masuala yawatoto wa kiasili. Sababu ya kutohusisha masuala haya inaweza kuwa kwenyeuchukulizi kwamba sheria zinazohusu watoto tayari zinashughulikia kategoriamaalum ya kutojiweza kati ya umma kwa jumla. Watoto wote wamo katikahatari ya kunyanyaswa na katika hitaji ya kupewa ulinzi wa kisheria. Maranyingi, mahitaji ya watoto wa kiasili huweza kuhusisha yale mahitaji ya watotowengine wasiojiweza. Hata hivyo inaonekana kuna uelewa mchache sana wakiwango cha dhuluma zinazowakumba hususan watoto wa kiasili. Licha yakuwepo na uwezekano kwamba watoto wa kiasili wanaweza kufaidika navipengele vya jumla vya kisheria, pana ushahidi mdogo sana kwamba waohufaidika kweli. Kwa kweli, pana ishara dhahiri kwamba kinyume cha haya nikweli. Watoto wa kiasili ni sehemu ya kikundi kidogo hasa cha wasiojiweza,kwa kiasi kikubwa kutokana na ukweli kwamba wanaishi katika sehemu zamashambani au katika hali za uhamaji ambapo hawafikiwi vya kutosha nahuduma za kijamii au huduma hizi hazipo.

Yafutayo ni mapendekezo yanayoweza kutolewa:

Serikali inafaa kuhakikisha kwamba data changanuzi kuhusu watotoinakusanywa ili kubainisha mapengo yaliyopo na vizuizi vya wao kufurahiahaku za kibinadamu, na kulenga kuunda sheria, sera na mipango ilikushughulikia vikwazo hivyo. Kamati ya CRC, katika kuitikia kushindwa kwaserikali ya Gabon, katika ripoti yake ya mwaka wa 2001 kwa CRC, kutambuakwamba watoto wa kiasili wanastahili kuzingatiwa kipekee, ilieleza hali mbayawaliyomo watoto Mbilikimo nchini humo.453 Kamati hiyo ilipendekezakwamba serikali ifanye uchunguzi ili kubainisha mahitaji ya watoto hawa nakufafanua mpango wa kuhusishwa kwao kijamii katika mashauriano naviongozi wa jamii ya mbilikimo. Aidha ilisisitiza hitaji la kuwawezesha watotohawa kusajiliwa wanapozaliwa na kupata huduma za kijamii.

• Kushiriki kikamilifu kwa watoto na vijana waliobaleghe pamoja najamii za wenyeji katika kuwalinda watoto na utekelezaji wa haki

453. UN Doc CRC/C/15/Add.171, aya ya 69 na 70.

Page 162: First page ILO.fm

146

zao. Kwa kusudi hilo, ni muhimu kuhakikisha kuwa kuna mikakatiitakayowezesha na kufanikisha kushiriki kwa jamii, pamoja nakupewa uwezo kwa lengo la kuafikia wajibu muhimu katikakutengeneza mustakabali wao.

• Lazima hatua maalumu zichukuliwe kwa ajili ya watoto wa kiasili,kama yanavyofanyiwa makundi mengine ya wasiojiweza, kama ilivyomfano wa hatua maalum zilizochukuliwa kwa ajili ya watoto waliona ulemavu katika Sheria kuhusu Watoto nchini Uganda.

• Baadhi ya mikakati inayoweza kuimarisha hali ya watoto wa kiasiliinaona tatizo hili kwa mkabala wa kiuchumi tu, ikilishughulikia kwakuchukua hatua zitakazoimarisha hali yao ya kiuchumi tu. Sababu zakimsingi za hali yao, yaani ubaguzi na kutojiweza, zinalazimukutumiwa kwa sheria mahususi ambayo inalinda na kukuza haki zawatoto wa kiasili.

Kutokana na asilimia zao kubwa za idadi ya watu, mataifa mengiyametambua vijana kama raslimali moja muhimu na iliyo na umuhimu mkuwakwa maendeleo ya taifa. Mataifa yanafaa kukutambua kuwa kulinda na kukuzahaki za watoto wa kiasili ni muhimu pia kwa mustakabali wa watu wa kiasilikatika himaya zao.

Page 163: First page ILO.fm

147

11 Hali za watu wa kiasili katikamaeneo ya mipakani

11.1 Utangulizi: watu wa kiasili wenye makaazi ya muda na wahamahamaji

Watu wa kiasili aghalabu huwa wamesambaa ndani ya miapaka yote ya taifa.Kuwepo kwa watu wa jamii moja katika nchi mbalimbali na mizunguko yaokupita mipaka kunaweka wazi kabisa ubandia wa mipaka uliyowekwa naukoloni. Kutokana na hayo, makundi ambayo yanayofanana kijamii huishiakupewa uraia rasmi tofauti. Hata hivyo, ukweli wa maisha ya watu hawaaghalabu huwa tofauti kabisa, kwani maisha yao hayaathiriwi na (‘hati’) mipakarasmi na hubakia zimebainishwa na uhusiano wa kifamilia na kikabila ambaoumedumu karne nyingi.

Hadi kiwango kwamba mipaka ni sehemu ya vikwazo vianapinga au kuzuiamwingiliano wa kijamii na kitamaduni, inadunisha muwala baina ya kikundihusika na hivyo kuathiri uwezo wa kikundi hicho kuhifadhi upekee wao. Kwamfano, familia za Amazigh zinazoishi katika pande zote mbili za mpaka bainaya Aljeria na Moroko zimetengana tangu kufungwa kwa mpaka huo mnamomwaka wa 1994 na kuzuia kutembea kwao na uhusiano wa kibiashara.

Hususan vile vikundi vya watu vinavyoishi maisha ya makaazi ya muda naya kuhamahama aghalabu huhamia upande mwingine wa mipaka kama sehemuya maisha yao. Utofauti baina ya jamii zenye makaazi ya muda,zinazohama kwamisimu fualani na kisha kurejea mahali pao, na zile za wahamahamaji, ambaohutangatanga daima, umeendelea kudidimia. Wanavyofanya hivyo katikamaeneo ya mbali ya jangwa la Sahara au katika sehemu za misitu mikubwakatika Afrika ya Kati, kutembea kwao aghalabu huwa hakujulikani walakuthibitiwa. Hali hii ni kweli kwa mujibu wa Watuaregi wa Afrika Kaskazini,wanao patikana na kutembea baina ya Burkina Faso, Mali, Nijaa na Mauritaniakatika Afrika Magharibi; na baina ya Aljeria na Libya Kaskazini mwa Afrika.Wambororo (sehemu ya Wapeul) wahamaji wa muda wanaofuga mifugo naaghalabu huhama kwa misimu fulani baina ya Kameruni, Jamuhuri ya Afrika yaKati, Chad, Burkina Faso, Mali na Nijaa. Makundi ya ‘Mbilikimo’ yanapatikananchini Burundi, Kameruni, Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Kongo, Jamuhuri yaKidemokrasia ya Kongo, Gabon, Rwanda na Uganda. mwingiliano wa makundiya ‘Mbilikimo’ katika eneo kati ya Gabon na Kongo; na mwingiliano wa jamiiya Aka katika eneo kati ya Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Kongo na DRC nimifano mwafaka ya uhusiano wa karibu baina ya jamii za mipakani. Sawa naWamaasai wanaoishi nchini Kenya na Tanzania na huzunguka katika nchi zotembili.

Vile vile kuna mfano wa pekee wa Wakunama wanaoishi pande zote zampaka baina ya Ethiopia na Eritrea. Ikumbukwe kwamba Eritrea ilipata uhuruwake kutoka kwa Ethiopia mnamo mwaka wa 1993 tu. Walipojikuta katikatiya vita vya mwaka wa 1998 baina ya nchi hizi mbili, Wakunama hawakujuawako upande gain baina ya nchi hizi zinazopigana. Kwa kuchukuliwa kumawalioasi serikali ya Eritrea, wakunama waliangaliwa kwa tuhuma. Baada yavita, wengi wao waligura Eritrea ili kuepuka kusajiliwa katika jeshi kwa lazima.Wakiwa wamekaa kwenye ardhi ya Ethiopia kwa muda, watu hawa wasio namakaazi wanakumbana na matatizo anuwai, ikiwa ni pamoja na kuchomwakwa nyumba zao, uhaba wa maji na ukosefu wa usafi. Huku suala la kuwapamakao likiwa si chaguo linalofaa, watu hawa wanajikuta kwenye pengo lakisheria. Hata hivyo imegundulika kwamba Wakunana huchochewa na kikundi

Page 164: First page ILO.fm

148

wapiganaj kutoka Ethiopia na hili limechangia katika hali yao kunyanyaswanchini Eritrea.

Hali kama hii imewakumba wafugaji wa Kibasongora, waliohama kutokakatika maeneo yao ili kutafuta maji na malisho ya mifugo wao katika Mbuga yakitaifa ya Virunga katika DRC, na nchini Tanzania. Baada ya kufukuzwa nakulazimishwa kurudi Uganda, walikumbana na taharuki ya kisheria ya kutofaakuitwa wakimbizi (kwani wanajiona kama Waganda) wala kama wakimbizi wandani kwa ndani (kwani walifuga mipaka ya kitaifa).

11.2 Sheria ya kimataifa

Sheria ya kimataifa inadhihirisha ufahamu mdogo sana wa hali hii ya kuhofishaau masaibu ya watu wa kiasili ambao mitindo ya maisha yao inapuuza mantikiya mipaka rasmi. Mkataba wa ILO wa 169, kwa mfano, unazitaka serikalikuchukua hatua mwafaka, na pia kupitia kwa makubaliano ya kimataifa,kufanikisha utangamano na ushirikiano baina ya watu wa kiasili wamipakani.454 Hatua hizi zinafaa kulengwa kwenye shughuli katika nyanja zakiuchumi, kijamii, kitamaduni, kiroho, kimazingira na katika nyanja nyinginezo.

Kwenye dibaji yake na katika matini yake nzima, UNDRIP haihusishi ulinziwa watu wa kiasili na au kuwachukulia kuwa tegemezi kwa utaifa au uraia.Badala yake, uhusiano baina ya watu wa kiasili na ardhi, himaya naraslimali zaohupewa kipaumbele. Kifungu cha 36 cha UNDRIP ni kipana sana katikakushughulikia watu wa kiasili walioko katika maeneo ya mipakani, hivikwamba kinasema kuwa watu wa kiasili, hasa wale waliogawanywa kwamipaka ya kimataifa, ‘wana haki ya kudumisha na kuendeleza mawasiliano,uhusiano na ushirikiano, zikiwemo shughuli za kidini, kitamaduni, kisiasa,kiuchumi na kijamii, baina yao na wanajamii wenzao pamoja na watu wenginenje na ndani ya mipaka’. Mataifa yanahitajika, kwa kushauriana na kushirikianana watu wa kiasili, kuchukua ‘hatua madhubuti ili kufanikisha shughuli hii nakuhakikisha utekelezaji wa haki hii’

Kwenye kiwango cha ukanda wa Afrika, Mkataba huu katika kifungu cha12 kunaruhusu haki ya mtu kutoka na kurudi nchini kwake. Hata hivyo haki hiiinaweza kuwekewa vikwazo vinavyohusiana na usalama wa taifa, sheria nautulivu, afya ya umma na maadili.

Kwa kuwa suala la kutembea kwa watu wa kiasili nje na ndani ya mipakabaina ya mataifa hutendekeka kwenye kiwango cha kieneo baina ya mataifaambayo pia ni wanachama wa jumuiya ya kiuchumi ya eneo hilo, ingetarajiwakuwa sulihu zingetafutwa katika uhusiano huu. Mifano kadhaa ya hatua zakimajaribio zimeonekana.

Maafikiano ya Umoja wa kiuchumi na kifedha wa Afrika ya Kati(Communauté Economique et Monétaire de l’Afrique Centrale (CEMAC)),ikishirikisha mataifa ya Kameruni, Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Chad naEquatorial Guinea, yanakubali ubadilishaji wa watu na mali baina ya mataifawanachama. Tume ndogo imeundwa ili kufuatilia mzunguko wa kila mwakawa wahamaji wa muda pamoja na njia zao.

Sio mataifa peke yake bali pia umma umejiandaa na kujihamasha kieneo ilikushughulikia suala hili. Wakati mwingine juhudi hizi zimekuwa za pamoja.Kwa msaada wa CEFDHAC, ambao ni mfumo wa kanda ya Afrika ya Kati,

454. Kifungu cha 32

Page 165: First page ILO.fm

149

ambao huunganisha mataifa anuwai katika kanda hii pamoja mwakilishi waMbilikimo kutoka kwatika kila nchi, shirika la Réseau des PopulationsAutochtones et Locales pour la Gestion Durable des Eco-systèmes Forestiersd’Afrique Centrale (REPALEAC) liliundwa na kuwa kama Shirika lisilo lakiserikali la kanda hii kwa ajili ya watu wa kiasili.

Maendeleo chanya kama haya mnamo mwaka wa 2007, yaliyoanzishwa naserikali ya kitaifa, yalikuwa kuandaliwa kwa hafla ya kwanza ya kimataifa yawatu wa kiasili wa Afrika ya Kati, na serikali ya Kongo (Forum International desPeuples Autochtones de l’Afrique Centrale, FIDAC). Lengo la shughuli hii lilikuwani kuhakikisha kuwepo kwa kushirikishwa kwa watu wa kiasiili katikamaendeo yanayofaa ya misitu na mifumo ya ikolojia katika kanda hiyo. Mataifamengine katika kanda ya Afrika ya Kati yalishiriki, pamoja na mashirika yakimataifa kama vile UNICEF,WWF na Benki ya Dunia.

11.3 Mielekeo ya kitaifa

Mataifa men gi katika katiba zao, huwapa raia wote haki ya kutoka na kuingianchini. Katika njia moja au nyingine, aghalabu kwa kurejelea sheria za kitaifazilizopo, mtu hufaa kuhitimu kupata haki hii. kuhitimu kwa kawaida kabisa ilikuwa huru kutumia haki hii ni sharti la kupata na kusafiri akiwa na pasipoti,kama inavyosisitizwa katika sheria kuhusu uraia. Kwa namna ya pekee, haki iihii hupeanwa kwa kila mtu aliye katika mipaka ya taifa.

Watu wa kiasili huishi pembezoni mwa vyombo rasmi vya utawala.Kutembea kwao hasa huwa nje ya vigezo vya sheria. Wachache hutoka nakuingia tena kwenye vituo vya kuvukia mipaka, na sio wengi wanaobebapasipoti. Kirasmi, wanahitaji kutimiza kanuni rasmi za mpakani. Hamna nchiyoyote ambayo Watuaregi hupitia katika kuhama kwao ina sheria auinaruhusu kuwepo kwa mikakati maalum ya kuwawezesha kutembea kwauhuru.

Sheria kuhusu misitu ya Burkina Faso (Code Forestier) inatoa mfano mzuriwa kukubali ukweli wa kuwepo kwa uvukaji wa mipaka wa wafugaji wakuhamahama, kama vile Wapeul (Fulbé).455 Kwa sharti la mapatano, mifugowa kigeni wanaruhusiwa kuvuka mipaka nchi katika muktadha wa uhamaji wamuda. Mzunguko au uvukaji kama huu unatengemea yafuatayo: (1) lazimawachungaji wafuate sheria inayohusiana na usafi wa wanyama na lazima wawena stakabadhi rasmi kuhusiana na usafi; (2) lazima wawe na vyeti vya uhamajiwa muda vinavyohihtajika na utawala. Aida, kundi la mifugo linafaakuandamana na kuangaliwa na wachungaji wazima wanaotosha.

Kwa upande wa sera, Wizara ya kilimo na mifugo (Elevage) ya Jamuhuri yaAfrika ya Kati mra kwa mara huweka ‘couloirs de la transhumance’ nahuwapasha haya wachungaji na wazalishaji wa ng’ombe (éleveurs).

Aghalabu, tatizo kubwa la makundi haya yanahusiana sana na uhuru wakutembea katika taifa lao wenyewe, kwa mfano wanapojikuta katika maeneoyaliyohifadhiwa kama vile mbuga za kitaifa.

455. Tazama kifungu cha 36-42 cha Loi no. 006/97/ADP, du 31 janvier 1997 portant Code Forestier.

Page 166: First page ILO.fm

150

11.4 Hitimisho

Hali ya watu wa kiasili kuhama na kuishi pande zote za mipaka rasmihaijashughulikiwa kikamilifu. Uwezo zaidi wa kubalika unafaa kuingizwa katikautawala wa kisheria ili kushughulikia ukweli huu. Mahitaji mahususi yamakundi haya yanafaa kukaguliwa na matokeo ya mitindo ya uhamaji wao naukweli wa pamoja lazima vitiwe katika mipaka ya sheria.

Sehemu hii inatoa mahitmisho na mapendekezo kadhaa ya jumla kuhusianana utafiti huu kwa jumla. Mahitimisho na mapendekezo mahususi kuhusumada kumi na moja yanashughulikiwa katika ripoti, ya hapo juu, mwishonimwa kila sehemu ya mada.

Page 167: First page ILO.fm

151

Mahitimisho

Kuwepo kwa watu wa kiasili ni uhalisia

Kwa kukubali uelewa kwamba watu wa kiasili ni zile jamii zinazokumbwa naupembezwaji wa kiwango cha juu, ambazo zinajibainisha zenyewe kama ‘zakiasili’ aghalabu kwa misingi ya madai ya makazi yao ya kihistoria, nazinazotegemea ukuruba wao mkubwa na ardhi na raslimali zao kwa ajili yakuishi, ni ukweli usiokanika kwamba watu wa kiasili wamo katika mataifamengi ya Afrika. Makundi haya yanahusisha makabila, desturi, tamaduni nalugha mbalimbali.

Ijapokuwa kuna tofauti nyingi kulingana na kila nchi kuhusu jinsiwanavyochukuliwa na suala la ulinzi wa kisheria kwa watu wa kiasili, taswirahii iliyopo ni ile ya serikali kupuuza na kukana masaibu yanayowakumba watuhawa. Watu wa kiasili wametengwa kutoka kwa jamii pana katika hali yakiuchumi, kijamii na kisiasa. Wametengwa na kubaguliwa kwa misingi yamakabila yao na desturi za maisha.

Hatahivyo, licha ya kutokuwepo na utambuzi wa watu wa kiasili kamainavyoelezwa chini ya sheria ya kimataifa, katika sheria za Afrika, kuna nafasinzuri za kulinda watu hawa katika muktadha wa mifumo ya kisheria ilyopokatika baadhi ya nchi za kiafrika (ingawa baadhi ya mifumo ya kisheria ingalihafifu). Jambo hili limedhihirishwa katika ripoti hii nzima na linahusikana nahatua maalum katika sehemu kadhaa kwa makundi yasiyobahatika auyaliyotengwa au makundi mengineyo mahususi katika jamii, na vipengelekuhusu uongozi wa kitamaduni na sheria y akimila na utawala wa kimitaa,linahusikana na vipengele kuhusu usimamizi wa ardhi na raslimali na sera zamaendeleo, vile vile na sehemu nyinginezo kadhaa. Hata hivyo, changamotokubwa ni ukosefu wa mikakati ya kutosha kwa ajili ya kutekeleza vipengelekama hivi kwa faida ya watu wa kiasili, ukosefu wa uwewzo wa kushughulikiamasuala ya kiasili kwa namna inayofaa na ya mashauriano/ushirikishi, vile vilena mitazamo ya kijumla dhidi ya watu wa kiasili, kati ya mambo mengineyo.

Sheria ya kimataifa

Kupitia kwa mkataba wa ILO wa 169 na UNDRIP, sheria ya kimataifa kuhusuhaki za kibinadamu inatoa viwango muhimu kuhusu haki za watu wa kiasili.Mataifa ya kiafrika yamekuwa wanachama wa vyombo vingi vya kimataifaambavyo vina umuhimu mkubwa kwa watu wa kiasili, kama vile CERD,CEDAW na CRC na Mikataba ya ILO nambari 107 na 111. Mashirikayanayoangalia Mikataba hii yamezidi kufanya mahitaji ya watu wa kiasilisehemu ya moja kwa moja ya majukumu yake. Hususan, maoni yaliyokubalikabaada ya kuchunguza ripoti za mataifa yanatoa mapendekezo muhimuyanayohusiana na watu wa kiasili kwa mataifa ya Kiafrika.

C Mahitimisho na mapendekezo

Page 168: First page ILO.fm

152

Kwenye kiwango cha kimaeneo, kuhusishwa kwa ‘haki za watu’ katikaMkataba wa Afrika kunawweka msingi wa kuhusisha watu wa kiasili katikamawanda ya ulinzi wake. Baada ya pingamizi na kusitasita fulani kwa awali,Tume ya Afrila ilizindua Kamati Maalumu kushughulikia suala hili. Kwakukubali ripoti ya Kamati yake Teule, Tume hii imekubali kwamba watu wakiasili wapo katika mataifa mengi ya Kiafrika, na kwamba wana haki yakulindwa kwa mujibu wa Mkataba huu.

Hata hivyo kutokana na ukosefu wa kuidilisha na kufuatilia, athari za sheriaya kimataifa katika kila nchi zimebaki finyu mno.

Sheria ya nchini

Kwa mujibu wa sheria ya nyumbani (nchini), pana vipengele anuwai vyakisheria ambavyo vinaweza kutoa nafasi kwa ulinzi wa kutosha zaidi wa hakiza watu wa kiasili. Hata hivyo, kwa upana, kando na vighairi vichachevinavyoonekana, kama vile elementi fulani katika Katiba za Burundi na AfrikaKusini na rasimu ya sheria ya Kongo, mataifa hayajakubali kirasmi kuwepokwa watu wa kiasili kwa halali. Sababu kuu za ulegevu huu wa kukubalikuwepo kwa watu wa kiasili zinatofautiana toka nchi moja hadi nyingine, lakinikaribu kwa sawa zinahusiana na lengo la kutopuuza ujenzi wa taifa nakudumisha umoja wa kitaifa katika jamii ya makabila mengi yenye wasifu wakung’ang’ania raslimali chache. Kutokana na haya kuwepo kwa utajiri wauwingi wa kitamaduni kunapingwa na kufinyiliwa chini. Kinachotawala sera hizini falsafa ya kutawala kwa makundi yenye nguvu, ambayo aghalabu hutokanana miundo na mipangilio ya kikabila ya kabla ya ukoloni, ambayo kulingananayo, tamaduni, mila na historia za makabila fulani zilipendelewa. Tokeomuhimu la kukana huku ni kwamba rekodi za serikali, kwa mfano, senza yakitaifa, hazidhihirishi makabila na lugha mbalimbali – pamoja na zile za watu wakiasili – zilizopo katika nchi.

Huku ikiwa ni kweli kwamba sheria na sera za baadhi ya mataifazinarejelea hali ya na haki za jamii au makundi ‘yasiyojiweza’ na‘yaliyopembezwa’, mahitaji mahujsusi ya watu wa kiasili yanaweza kupuuzwakwa urahisi iwapo tahadhari haitachukuliwa ili kushughulikia upekee waokatika muktadha huu, badala ya kuwashughulikia kama sehemu ya kundi panalililo na mahitaji na changamoto tofauti. Aidha, mataifa yote yana vipengelekadhaa vya kisheria, sera, na mipango ambayo inaweza kutumiwa kulinda nakuendeleza haki za watu wa kiasili. Hili halijafanywa kikamilifu, kiasi kutokanana vizuizi vinavyozuia uwezo wa watu wa kiasili kupata haki, na kiasi kwasababu maafisa wa serikali pamoja na washirikadau wengine muhimuhawajahamazishwa kuhusu masaibu ya watu wa kiasili.

Vivyo hivyo, wajibu na vitendo vya asasi za serikali, kama vile taasisi zakutetea haki za kibinadamu, ofisi ya mrajisi na ‘mpatanishi’, hazijarekebishwaili kuhusisha uwakilishwaji na haja za watu wa kiasili. Asasi hizi pa,oja mamyinginezo zina uwezo wa kuhusisha masuala ya watu wa kiasili kama vileambavyo Tume ya Kenya ya Kutetea haki za kibinadamu imefanya. Asasichache zimeanzishwa kushughulikia masuala mahususi ya hali ya watu wakiasili.

Aghalabu watu wa kiasili hubaguliwa na serikali, hasa katika upande wakufanya utamaduni wao na ugavi wa raslimali. Pengine mara nyingi chanzo chaubaguzi si serikali vile, lakini ni watu binafsi na vikundi vingine. Wanajamii wajamii za kiasili hukumbwa na ubaguzi unaotokana na shutuma na mitazamohasi. Mataifa yangali na wajibu wa kuchukua hatua za kulinda haki zao. Pale

Page 169: First page ILO.fm

153

ambapo hatua maalum zimechukuliwa kupambana na ubaguzi, huwa maranyingi huwa zimelenga makundi fulani mahususi katika umma wa kitaifa lakinikwa ndara sana zikalenga watu wa kiasili. Aidha nyingi za hatua hizi huwa zadharura tu na hazihusishi mikakati mipana ya kisera. Hata hivyo, zinawezakuwakilisha nafasi ambazo kupitia kwazo haki za watu wa kiasili zinawezakulindwa kwa njia bora, au kutalii njia ambazo zinaweza kutumiwa kuimarishana kupangilia vizuri mikakati iliyopo.

Mifumo kadhaa ya kisheria katika kanda ya Afrika inakubali kushiriki nakushauriana kwa umma kwa jumla au makundi mahususi ya watu, yakiwemomakundi yaliyopembezwa. Hata hivyo, mifumo hii,michache sana, kama ipo,ina vipengele mahususi kwa watu wa kiasili. Ijapokuwa hivyo, vichachevinaweza kutumiwa kama nafasi za kuendeleza kushiriki kwa watu wa kiasilikatika kufanya maamuzi. Aidha, mikakati ya kutekeleza mifumo hii ya kisheriaau kwa mashauriano yanayohusikana nayo au kushirikishwa, kwa jumla nihafifu, na haitilii maanani mamno muhimu yanayofaa kuzingatiwa wakati wakushauriana na watu wa kiasili. Kwa upande mwingine, baadhi ya mifumo yakisheria haina vipengele vyovyote hata kuhusu mahihtaji ya makundiyaliyopembezwa na makundi mengineyo mahususi katika jamii ya kitaifa. Paleambapo pana vipenge kama hivi, sheria zilizo na vipengele kuhusu makundimahususi au hatua maalum (uteuzi maalum), aghalabu kuhusiana tu na halimahususi, wala sio sera pana ya kuhusishwa kwa watu wa kiasili.

Kwa mujibu wa kupata haki, ingawa kupata haki kwa watu wengiwanaoishi katika mataifa ya Afrika ni finyu sana, matatizo yanayokumba ummamzima yanazidishwa inapokuja kwa upande wa watu wa kiasili. Korti pamojana mabaraza mengine ya kimahakama aghalabu huwa havikiki kijiografia, kwakuwa watu hawa wanaishi mbali katika maeneo ya mashambani au wanaishimaisha ya kuhamahama. Kutokana na viwango vikubwa vya umasikini nakutojua kusoma na kuandika kati yao, kuna uwezeikano mdogo wa watu wakiasili kuweza kulipia huduma za kisheria au hata kujua haki zao na uwezekanowa kupata msaada wa kisheria, kama upo. Kutambuliwa kwa sheria ya kimilaya Kibantu kama aina moja ya mfumo ‘wa kitamaduni’ kumemomonyoa zaidiufikiaji wa haki kwa watu wa kiasili. Mbali na vighairi vichache kama vilemahakama za kutembea kwa ajili ya jamii fulani za kiasili nchini Afrika Kusini,mataifa hayajachukua hatua za kushughulikia hali hii.

Mataifa hayajakuwa makini sana kuhusiana na umuhimu amabao watu wakiasiili wanaambatanisha na uhifadhi wa utamaduni kama arki muhimu yakutambulishwa kwao. Hali hii ya mambo ni mojawapo ya matokeo ya shughulimuhimi zilizoshamiri za ujenzi wa taifa na kukana kuwepo kwa watu wa kiasili.Vivyo hivyo, lugha za kiasili hazijatambulika kirasmi na kwa hiuvyo hazitumikikatika vyombo vya habari na shule zinazomilikiwa na serikali. Pia makundi yakiasili hayachukuliwi kwa sawa katika mashirika ya kuwawakilisha haliinayoathiri vibaya uwezo wao wa kushiriki katika mchakato wa kufanyamaamuzi yanayowahusu. Kutokana na haya, baadhi ya lugha za kiasilizimetoweka na nyingine kama Kitamazigh na Khoi zimewekwa chini yashinikizo kubwa.

Mataifa kadhaa yamechukua hatua fulani ili kupambana na hali hii, aghalabukwa njia ya kuanzisha taasisi mpya. Mifano mizuri ni Tume ya Afrika kusini yakukuza na kulinda haki za jamii za kitamaduni, kidini na lugha, Ubalozi waAmazigh nchini Aljeria, na Taasisi ya kifalme ya Utamaduni wa Waamazigh(IRCAM) nchini Moroko. Kwa kuwa taasisi hizi zingali changa, inabakia kuonajinsi ambavyo matatizo ya uwakilishwaji wa kutosha wa watu wa kiasili naugavi wa raslimali yatakavyotatuliwa.

Page 170: First page ILO.fm

154

Viwango vya uhudhuriaji wa shule na viwango vya kujua kusoma nakuandika baina ya watu wa kiasili ni vya chini sana. Ingawa haki ya kupataelimu imehakikishwa katika takriban mataifa yote ya Afrika, watoto wa kiasiliwangali na ugumu wa kupata haki yao ya kielimu, hasa elimu inayofaa kwamahihtaji na utamaduni wao. Mpango serikali ua uganda wa Elimu Badala yamsingi kwa Wakaramajong (ABEK), ambao umeundwa kutoa mtaala na mbinuza kufunza zinazofaa maisha yao ya kuhamahama, unatoa mfano wa hatuainayozingatia mahitaji ya jamii ya kiasili.

Uhusiano wa karibu na utegemeaji wa ardhi na maliasili si tu sehemumuhimu ya utambulizho wa watu wa kiasili, lakini pia shemu ya maisha yaoyenyewe. Sababu kubwa ya kupuuza na kukiuka haki zao anuwai inatokana nakupotea kwa ardhi ya mababu zao kutokana na mipamgo ya uhifadhi, ukuzajiwa utalii, ukataji wa miti, pamoja na uharibifu wa misitu na kuenea kwa jangwakunakotokana na mabadiliko ya tabianchi.mambo kama vile ukosefu wakufanya mashauriano, kukosa kulipwa fidia na kushindwa kutoa ardhi badalayamezidisha athari za kupoteza ardhi. kuanzishwa kwa haki za kumiliki ardhikibinafsi vile vile na kutia ardhi zinazomilikiwa kitamaduni na watu wa kiasilikatika serikali, au kuzipuuza haki za umiliki wa ardhi kwa jumuiya kumeathiripakubwa haki za watu wa kiasili. Taratibu mpya kama hizi kuhusu ardhi piazimeinua kilimo na umiliki wa ardhi kibinafsi juu ya utumizi wa ardhi kijumuiya,wa kuhamahama pamoja na ufugaji na uwindaji-uokotaji. Aidha, kutokana nakuanzishwa kwa mikakati ya kuhifadhi maeneo na mazingira yaliyolindwa,wajibu wa watu wa kiasili katika kuhifadhi na kusimamia ardhi kama hiziumedunishwa. Uatawala pia ni suala muhimu ambalo linahusiana moja kwamoja na haki walizo nazo watu wa kiasili kwa ardhi zao.

Mataifa mengi ya Afrika yanatambua haki za kimila kama aina ya haki zakiardhi. Hii inaweza kuwa nafasi muhimu kwa watu wa kiasili. Zaidi ya hayo,katika mifano michache, kanuni za kimila zilizopo sambamba na sheria yakitaifa na zinatambuliwa katika uundaji wa sheria, zinaruhusu kuwepo kwahaki za pamoja na za kibinafsi za kumiliki ardhi. hata hivyo, katika hali nyingi,haki kama hizi si haki kamili za umilikaji na huhusisha tu ama haki za kukalia auutumizi.

Kunyimwa kwa haki za uchumi wa kijamii ndiko kiini cha kutengwa kwawatu wa kiasili. Ingawa ishara za kuaminika aghalabu huwa hazipo, taswira yakunyimwa haki za kielimu, haki za kupata huduma za afya, haki za mali na ajirainajitokeza.

Pia inaweza kuonekana kwamba baadhi ya vikundi baina ya watu wa kiasili,kama vile wanawake na watoto viko katika hali mbaya hata zaidi. Wanawakena wasichana wa kiasili hukumbwa na hali ngumu nyingi. Hii hasa ni kwasababu ya ukweli kwamba nafasi ya kisheria kwa jumla inatilia nguvu ukosefuwa usawa baina ya wanaume na wanawake, na aghalaabu ikiendeleza dhana zakitamaduni na za kidini. Ingawa serikali imechukua hatua za kuhakikishakuwepo kwa usawa na ulinzi wa haki za watoto, hakuna chochote ambachokimefanywa kabisa kushughulikia mkondo wa kikabila wa ubaguzi wa kijinsiana ukiukaji wa haki za watoto.

Aghalabu watu wa kiasli wametawanyika katika sehemu zote ndani yamipaka ya kitaifa. Mipaka ni sehemu ya vizujizi vinavyo zuia maingiliano yaokijamii na kitamaduni, na kudhoofisha muwala baina ya watu hawa. Hasa yalemakundi ya watu wanaoishi maisha ya makaazi ya muda nay a kuhamahama,kama vile Watuaregi na Wambororo, mra nyingi huhamia nje ya mipaka kama

Page 171: First page ILO.fm

155

sehemu ya kuishi kwao. Mataifa husika hayajashughulikia suala la uhamiaji wawatu wa kiasili nje ya mipaka rasmi katika mifumo yake ya sheria.

Huku mkazo katika uchunguzi huu ukiwekwa kwenye majukumu yaserikali, ni faradhi kusisitizwa kwamba sekta zisizo za kiserikali pia zina wajibuwa kutimiza katika kutumia taratibu za kisheria zilizoko ili kuwafaidi watu wakiasili, na kuziweka sheria, sera na utendaji sambamba na mahitaji mahususi yawatu wa kiasili. Mfano wa shirika lisilo la kiserikali ambalo limefanya mchangokama huu ni WIMSA nchini Namibia. Jamii za kiasili zenyewe zimeonyeshaumuhimu wa kuungana na kuweka wazi matakwa yao. Wakati mwingine, faidakubwa zimefuatia vipindi au matukio ya uasi na tetezi za kiraia zinzofanywa nawanajamii wa kiasili.

Page 172: First page ILO.fm
Page 173: First page ILO.fm

157

Mapendekezo

Masomo dhahiri na mikondo mipana ya hatua kadhaa za kuchukuliwazinaweza kupendekezwa kwa msingi wa mahitimisho ya uchanganuzi huu washeria kuhusiana na watu wa kiasili katika Afrika. Kama vile ambavyoimeonyeshwa, jinsi ambavyo watu wa kiasili na masuala ya kiasiliyanavyochukuliwa inatofautiana katika kanda nzima – kutoka kwa kupuuzwana kubaguliwa kabisa hadi kwa kuanzishwa kwa juhudi za kuanza kushughulikiamasuala mahususi yanayowaathiri watu wa kiasili katika maeneo kadhaa. Pananafasi katika sheria, na sera za kitaifa zilizopo na changamoto za kutekelezwakwazo, pamoja na mahitaji makubwa ya kuchunguza na kushughulikia haki zawatu wa kiasili kwa mpangilio mzuri. Mapendekezo yalitolewa hapo chiniyamejikita kwenye makadirio haya mapana na yanakusudiwa kuwamapendekezo ya hatua mwafaka zinazoweza kuchukuliwa na serikali, watu wakiasili, mashirika ya kimataifa na mashirika ya habari na umma kujenga msingiwa mpangilio kama huu na kujenga na kutosheleza jukwaa la maarifa, nasheria, sera na msingi wa kitaasisi kwa ajili ya kushughulikia kikamilifu haki zawatu wa kiasili katika Afrika.

Kwa mataifa ya Afrika:

Chunguzi za kitaifa

Tume za kitaifa za uchunguzi au mashirika mengine kama haya, zilizo nawataalamu wa kitaifa na wa kimataifa zingekuwa njia nzuri sana ya kuwekamawanda na kuweka rekodi ya taswira pana kuhusu hali ya watu wa kiasilikwenye kiwango cha kitaifa na hivyo, kukusanya shabari muhimu ili kuwekamsingi wa dira ya hatua zitakazochukuliwa. Mashirika kama haya yangechun-guza na kutoa ripoti kuhusu nafasi ya watu wa kiasili nchini. Uchunguzi wakeungelenga kuthibitisha iwapo watu wa kiasili, kama inavyoeleweka na Tume yaAfrika na vyombo na mashirika mengineyo, wapo katika nchi husika (iwapokuna shaka yoyote kuhusiana na suala hilo), ni matatizo yapi yanazikumbajamii hizi (iwapo zipo), ni ilinzi upi wa moja kwa moja na halali kisheria wana-furahia, na marekebisho yapi ya sheria yanahitajika kufanywa ili kuboresha haliyao.

Ili mchakato wa uchunguzi kama huu na hatua zinazotokana nao kudumu,kunahitajika kuwepo kwa kujitolea kisiasa kwa mataifa husika. Baadhi yamataifa yameonyesha mwelekeo katika kanda ya Afrika kwa kuwa kati yamataifa ya kwanza kushughulikia masuala ya kiaisili katika rasimu za sheria aukupitia kwa mipango maalum – haya ni kama Namibia na Kongo.

Data na takwimu

Mikakati ya ukusanyaji wa data unaweza kuwa wa muhimu katika kusaidiaserikali kubainisha mahitaji maalumu ya watu wa kiasili (na makabila mengine)katika nchi, ambayo nayo yangesaidia katika kuchukua hatua ambazo zinawezakuleta usawa baina yao. Data inafaa kukusanywa kuhusiana na masuala yotekuhusu maisha yao, ikiwemo kiwango chao cha elimu, viashirio vya afya,kupata huduma za uchumi wa kijamii kama vile huduma za afya na maji yakunywa, na kupata haki. Data hii inafaa kugawiga zaidi iwezekanavyo kulinganana umri, jinsia, kutolewa baada ya kushauriana na watu wa kiasili ilikuhakikisha kuwa inaonyesha kikamilifu mambo yaliyomuhimu kwao namitazamo yao. Michakato ya kimataifa na kimaeneo iliyopo ya kuzalisha datainafaa kurekebishwa na viashirio vya nafasi ya watu wa kiasili kuanzishwa ilikushughulikia hitaji la kuwa data na takwimu zinazofaa.

Page 174: First page ILO.fm

158

Utambuzi

Ikiwa watu wa kiasili wamo katika nchi fulani, mataifa yanapaswa kuhakikishakuwa wanatambuliwa kisiasa na kisheria, kwa kutumia vigezo vya kimataifa nakieneo. Katika muktadha huu, istilahi ‘watu wa kiasili’ inafaa kueleweka nje yamipaka ya uasili. Utambuzi na ubainishaji kama huu utaunda njia ya kuwalindawatu wa kiasili. Hii itahusisha utambuzi wa urithi wao wa kitamaduni, ikiwemolugha na sheria za kimila, na haja ya kuwapa ulinzi maalum. Mataifa yanapasakuweka mikakati inayofaa kuhakikisha kuwa watu wa kiasili wanapata vyeti vyakuzaliwa, stakabadhi za uraia, vitambulisho na stakabadhi zingine rasmizinazofaa ambazo zitawaruhusu kutekeleza haki zao kikamilifu.

Sheria na sera katika nchi

Serikali zapaswa kuzingatia kutumia sheria inayoshughulikia haki za watu wakiasili kikamilifu, kama inavyofanywa nchini Kongo. Sheria iliyopo, kamahakuna sheria ya kina inayolenga watu wa kiasili nchini, inapasa kutumiwakikamilifu ili kutoa ulinzi kwa watu wa kiasili. Taratibu na mipango yote yakitaifa ya kutetea haki za kibinadamu inapasa kushughulikia suala la haki zawatu wa kibinafsi.

Hatua maalumu

Mataifa yanafaa kuhakikisha kuwa watu wa kiasili wanatambuliwa kamamakundi maalumu ili kutekeleza hatua maalumu katika sehemu za maisha yakijamii, kiuchumi, kitamaduni, kiraia au kisiasa zinazofaa. Hatua maalumu kamahizi zingeweza kushughulikia hali za upembezwaji na ubaguzi zinazowakumbawatu wa kiasili kutokana na upekee wao, na ziundwe na kutekelezwa kwakushauriana na watu wa kiasili ili kuhakikisha kuwa zinapatana na maazimio yawatu wa kiasili. Lazima kuwepo na makini katika kushughulikia mahitajimahususi na unyonge wa wanawake na watoto wa kiasili. Pana mafunzo fulanikutokana na hatua maalumu zilizopo ambazo zimetekelezwa katika nchikadhaa za Afrika, ambazo zinaweza kuwa msingi wa kuunda sera pana.

Asasi

Asasi za kitaifa, kama vile asasi za kitaifa kuhusu haki za kibinadamu, zikokatika nafasi nzuri ya kushughulikia hali ya watu wa kiasili kwani tayarizimetiwa katika mifumo ya serikali au zinatumika katika asasi huru. Ilikufanikisha hili, marekebisho ya majukumu ya asasi kama hizi ili kuhusishamasuala ya kiasili yatakuwa ya maana. Watu wa kiasili wanafaa kuhusishwakama wanachama wa asasi kama hizi.

Kuanzishwa kwa asasi za serikali zilizo na jukumu la kulinda haki za watuwa kiasili, pale ambapo asasi kama hizi hazipo, kutahakikisha kuwa kunamwelekeo mzuri kuhusu masula ya kiasili. Mataifa yanafaa kufikiria kuanzishaasasi ya serikali yenye jukumu la kuhakikisha kuna ulinzi wa haki za jamii zakiasili. Watu wa kiasili wanafaa kuhusishwa kama wanachama wa asasi hizi.

Mashauriano na kushirikishwa

Katika masuala yote yanayowahusu, kama vile hatua za kisheria na kiutawala,sera za maendeleo au za uhifadhi, mipango na miradi na mambo mengine

Page 175: First page ILO.fm

159

yanayoweza kuwaathiri watu wa kiasili, yakiwemo afya na elimu, kufanyamashauriano ni muhimu ili kuhakikisha kuwa hatua za kisheria, kisera au zakimipango zinazochukuliwa zinaitikia mahitaji ya watu wa kiasili kamayalivyotajwa na wao wenyewe. Mashauriano kama haya yanafaa kufanywakupitia kwa kuwepo kwa taasisi mahususi, kama ilivyopendekezwa hapo juu,au kupitia kwa kuweka mifumo madhubuti ya kufanya mashauriano nakuifanya kuwa mipango na sera zenye kiini fulani. Tajiriba kutoka ulimwengunikote imeonyesha kuwa mifumo ya kufanya mashauriano ni mwafaka sanaiwapo imeundwa baada ya kushauriana na watu wa kiasili – na kufumbatwakatika muundo wa utawala wa taifa – katika viwango vyote vya utawala. Nilazima watu wa kiasili waruhusiwe kushiriki kikamilifu katika kufanya uamuzikatika asasi za uchaguzi na katika miundo ya utawala kwa viwango vyote.Mataifa yanafaa kurekebisha michakato ya uchaguzi ili kutosheleza upekee wawatu wa kiasili, hasa watu wa kuhamahama, ili kuhakikisha kuwa wanashirikikikamilifu katika siasa.

Sheria ya kimataifa

Kutiwa sahihi kwa Mkataba wa ILO nambari 169, ambao unafafanua wajibu wamataifa kuhusu watu wa kiasili, kutayawezesha mataifa ya Afrika kufaidikakutokana na ujuzi na michakato ya kimataifa kuhusu utekelezaji wa haki zawatu wa kiasili. Kwa kuwa kutiwa sahihi kwa Mkataba huu kutamaanisha kuwakutakuwepo na kufuatilia kutekelezwa kwake mara kwa mara na shirika hurula wataalamu, kutayasaidia mataifa na watu wa kiasili kufanya majadilianokuhusiana na njia mwafaka ya kutekeleza vipengele vya Mkataba huu.Uidilishaji wa mkataba huu ungeupatia athari ya kisheria katika kila taifa.UNDRIP pia inatoa mwelekeo muhimu katika kulinda haki za watu wa kiasili.

Mataifa yanafaa kuhusisha habari na maelezo kuhusu watu wa kiasili katikaripoti zake kwa mabaraza Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika yakufanya mikataba kuhusu haki za kibinadamu ya. Aidha yanafaa kutekeleza nakufuatilia mapendekezo yaliyomo katika maoni ya mwisho yaliyotolewa baadaya kuzichunguza ripoti zao za kitaifa yalizotoa kwa mabaraza haya.

Kwa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika na

mashirika mengine ya kimataifa:

Mabaraza ya kufanya mikataba ya Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrikayamethibitisha kuwa na uwezo wakati mwingine katika uchunguzi wakekuhusu matakwa ya watu wa kiasili. Kuweka vizuri chunguzi kama hizi kuhusuhali za watu wa kiasili katika muktadha wa uchunguzi wa ripoti za mataifakunaweza kusaidia mashirika kama haya kujiunga pamoja na mataifa katikamjadala unaoendelea kufuatilia majadiliano ya awali ili kuangalia maendeleo yamataifa katika kutekeleza haki zilizoko katika mikataba kuhusu watu wa kiasili.Kudhihirika kwa haya hasa, katika maoni yoyote ya mwisho kunahitajikusambazwa kwa upana iwezekanavyo. Tume ya Afrika inafaa kuhuisha tenamasharti kuhusu Utoaji wa habari za mataifa ili kushghulikia kabisa masualayanayohusu ulinzi wa haki za watu wa kiasili.

Pale zinapofaa, taratibu maalumu za Tume ya Afrika, kama vile Katibumkuu wa kushughulikia haki za wanawake katika Afrika, Katibu maalum wamasuala ya Wakimbizi, watafutaji wa hifadhi, wahamiaji na wakimbizi wa ndanikwa ndani Barani Afrika, na Kamati Teule kuhusu Haki za Kiuchumi, Kijamii

Page 176: First page ILO.fm

160

na Kitamaduni katika Afrika, zinahitaji kuzingatia mahitaji na matakwamaalumu ya watu wa kiasili kama sehemu ya wajibu wake.

Uwezo wa Uhakiki bia wa Kimuhula na Taratibu za uchunguzi wa masualaya rika barani Afrika, kushughulikia matakwa ya watu wa kiasili unafaakutumiwa kikamilifu.

Umoja wa mataifa pamoja na mashirika yanayohusisha mataifa mengi nayale yanayohusisha mataifa mawili yaliyo na mipango kwenye kiwango chanchi yangekuwa na umuhimu mkubwa katika kusaidia serikali za Afrikakutekeleza mapendekezo yaliyoelezwa hapo juu. Kupitia kwa uongoziunaotolewa na Mfumo wa Umoja wa mataifa kwa namna ya viwango namwongozo wa kimataifa, mashirika kama haya yanafaa kuhusisha maslaha yawatu wa kiasili katika mipango yake pana na kuhakikisha kuwa wafanyikaziwake wanafunzwa na kufahamu masuala ya watu wa kiasili. Mashirika hayayanafaa kuzua mbinu za kufanya mashauriano ya kutosha na yenye utaratibumzuri na watu wa kiasili kuhusiana na shughuli zao wenyewe zinazowezakuwahusu, na pia yawe katika nafasi nzuri ya kupiga jeki juhudi za serikali kwakufanikisha michakato ya kufanya mashauriano.

Tume ya Afrika kupitia kwa Kamati yake teule kuhusu watu/jamii za kiasili,ILO pamoja na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa yanafaa kutoa usaidiziwa kitaalamu na kufanya shughuli za kuwapa uwezo na kuwahamazishamaafisa wa serikali, maafisa wa idara ya mahakama na wabunge, pamoja naumma kuhusu masuala ya watu wa kiasili katika Afrika.

Kwa umma:

Kuhusishwa kwa maslaha ya watu wa kiasili katika ufundishaji na utafiti katikataasisi za elimu kutasaidia kuhakikisha kuwa watu wanapewa mafunzo yakutosha kuhusu suala hili katika kanda ya Afrika.

Makundi ya umma, ikiwemo miungano ya watu wa kiasili, yanafaa kupiganiakuwepo kwa mashauriano mazuri na watu watu wa kiasili katika mambo yoteyanayowahusu, na kuhusishwa kwa maslaha ya watu wa kiasili katika sheria,sera na mipango. Yanafaa kuhakikisha kuwa mipango yake kuhusu masuala yakiasili inafasiliwa na kutekelezwa kikamilifu kwa kufanya mashaurianokikamilifu na watu wa kiasili na kuhakikisha kuwa mipango ambayo haiwalengihususan watu wa kiasili inazingatia matakwa mahususi ya watu wa kiasili, nakuhusisha au kushirikiana moja kwa moja na watu wa kiasili katika sehemuzote za maudhui yaliyomuhimu. Pale inapowezekana, mashirika ya ummayanafaa kujihusisha na kuwapa mafunzo wafanyikazi wake kuhusu masualakiasili.

Kwa vyombo vya habari:

Vyombo vya habari vina wajibu muhimu wa kutoa habari kwa umma mzimakuhusu dhana ya watu wa kiasili, mahitaji na haki zao maalumu, na dharura yakutatua wasiwasi wao. Vyombo vya habari pia vinaweza kuchangia pakubwakatika kupunguza mitazamo hasi kuhusu watu wa kiasili kwa kutoa habarisahihi, pamoja na kushirikiana na mashirika ya watu wa kiasili ili kutoa mkabalawa kiasili kuhusiana na maudhui husika.

Page 177: First page ILO.fm

161

Kiambatisho A: Orodha chunguzi zanchi mbalimbali

Algeria: B Lounes Protection constitutionnelle, legislative et administrative despeuples autochtones en Algerie

Botswana: K Bojosi (maoni yaliyofanywa na Alice Mogwe yakiwa yamehu-sishwa), Botswana: Constitutional, legislative and administrative provisions concerningindigenous peoples

Burundi: Albert Kwokwo Barume, Protection constitutionnelle, legislative etadministrative des peuples autochtones au Burundi

Burkina Faso: S Aboubacrine & A Hamady Sow, Protection constitutionnelle,legislative et administrative des peuples autochtones au Burkina Faso

Cameroon: Samuel Nguiffo, Nadine Mballa & P Bigombe Logo, Protectionconstitutionnelle, legislative et adminstrative des peuples autochtones au Cameroun

Central African Republic (CAR): Albert Kwokwo Barume, Protectionconstitutionnelle, legislative et administrative des peuples autochtones en RepubliqueCentrafricaine

Chad: F N Ngarhodjim, Protection constitutionnelle, legislative et administrativedes peuples autochtones au Tchad

Congo: Albert Kwokwo Barume, Protection constitutionnelle, legislative et admi-nistrative des peuples autochtones en Republique du Congo

Democratic Republic of Congo (DRC): Albert Kwokwo Barume, Protec-tion constitutionnelle, legislative et administrative des peuples autochtones en Republi-que Democratique du Congo

Egypt: S Dersso, Egypt: Constitutional, legislative and administrative provisionsconcerning indigenous peoples

Eritrea: S Mebrahtu (yakiwemo maoni ya Zerisenay) Eritrea: Constitutional,legislative and administrative provisions concerning indigenous peoples

Ethiopia: Mohammud Abdulahi (maoni ya Melakou Tegegn yakiwa yamehu-sishwa), Ethiopia: Constitutional, legislative and administrative provisions concerningindigenous peoples

Gabon: Albert Kwokwo Barume, Protection constitutionnelle, legislative et admi-nistrative des peuples autochtones au Gabon

Kenya: G Wachira Mukundi, Kenya: Constitutional, legislative and administrativeprovisions concerning indigenous peoples

Mali: P Eba & S Aboubacrine, Protection constitutionnelle, legislative et adminis-trative des peuples autochtones au Mali

Morocco: Mohammed Amrhar (pamoja na Divinia Gomez na Anne Schuit),Morocco: Constitutional, legislative and administrative provisions concerning indigenouspeoples

Namibia: Andrew Chigovera (pamoja na maoni ya Clement Daniel), Namibia:Constitutional, legislative and administrative provisions concerning indigenous peoples

Niger: Oumarou Narey & Gandou Zakara, Protection constitutionnelle, legisla-tive et administrative des peuples autochtones au Niger

Nigeria: B Fagbayibo (pamoja na maoni ya Chidi Oguamanam), Nigeria: Consti-tutional, legislative and administrative provisions concerning indigenous peoples

Rwanda: Z Kalimba Protection constitutionnelle, legislative et administrative despeuples autochtones en Republique du Rwanda

Tanzania: W Olenasha & R Kapindu, Tanzania: Constitutional, legislative andadministrative provisions concerning indigenous peoples

South Africa: G Wachira Mukundi, South Africa: Constitutional, legislative and

Page 178: First page ILO.fm

162

administrative provisions concerning indigenous peoples

Sudan: C Doebbler, Sudan: Constitutional, legislative and administrative provi-sions concerning indigenous peoples

Uganda: C Mbazzira, Uganda: Constitutional, legislative and administrative provi-sions concerning indigenous peoples