halmashauri ya wilaya ya kilosa - home | kilosa...
TRANSCRIPT
Graphic designer © Amandus Mtani -2016
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
HALMASHAURI YA WILAYA YA KILOSA
NINI MAANA YA UTAWALA BORA?
1:0 UTANGULIZI
Miaka ya hivi karibuni maneno " utawala" na
"utawala bora yamekuwa yakitumika sana
katika mazungumzo ya kila siku. Utawala
mbaya "Bad governance" ni neno ambalo pia
linatumika kama utawala mbaya na chanzo
cha uovu katika jamii. wahisani wakubwa na
taasisi za fedha za kimataifa hupendelea
kutoa misaada yao pale ambapo
kunaonekana kuwa kuna utawala bora.
Graphic designer © Amandus Mtani -2016
Utawala 'Governance' ni neno ambalo si jipya na
lilianza kutumika tangu ustaarabu wa kale kwa
kifupi likiwa na maana ya hatua au mchakato wa
kufanya maamuzi au uamuzi na kutekeleza
maamuzi yaliyofanywa au kutotekelezwa.
Neno utawala pekee linaweza kutumika katika fasihi
kadhaa, mfano utawala katika ngazi za taasisi
"corporate governance, utawala wa kimataifa '
international governance, utawala wa kitaifa
'national governance' lakini pia utawala wa mitaa '
local governance.
Graphic designer © Amandus Mtani -2016
Kwa kuwa utawala ni mchakato wa kufanya
maamuzi na kuyatekeleza, mchanganuo wa
utawala hulenga kote, watekelezaji rasmi na
wasio rasmi ( formal and informal actors) hawa
wote lazima wahusishwe katika maamuzi na
utekelezaji wake ambapo Serikali ni miongoni
mwa watekelezaji wa utawala.
Watekelezaji hawa ni pamoja na wafanyabiashara
wakubwa, vyama vya wakulima na wafanyakazi,
ushirika, NGOs, taasisi za utafiti, viongozi wa
dini, taasisi za fedha, vyama vya siasa, majeshi
n.k.
Graphic designer © Amandus Mtani -2016
2.0 UTAWALA BORA Utawala bora ni nini?
2.1.Utawala bora ni matumizi ya uwezo (mamlaka)
wa kiserikali katika jitihada za kuongeza na kutumia
rasilimali hizo ili kuboresha maisha ya wananchi
2.1.1 Utawala bora ni neno linalotumika na
maendeleo ya kimataifa kueleza namna taasisi za
umma zinavyofanya mambo yake kwa umma na
kusimamia rasilimali zao.
2.1.2 Kwa mujibu wa ripoti ya Utawala na
Maendeleo ya Mwaka 1992 iliyofanywa na Benki ya
Dunia, utawala bora ni matumizi sahihi katika
kusimamia uchumi wa nchi na rasilimali za
Jamii katika maendeleo.Graphic designer © Amandus Mtani -2016
Graphic designer © Amandus Mtani -2016
2.1.3 Shirika la Maendeleo Duniani la Umoja wa
Mataifa ( The United Nations Development
Programme (UNDP) lilitoa maana ya neno utawala
bora Mwaka 1997 katika ripoti yake ya sera iliyoitwa
“Governance for Sustainable Human Development”
kuwa ni utekelezaji wa uchumi, siasa na mamlaka ya
utawala katika kusimamia mambo ya nchi katika
ngazi zote.
2.2 MISINGI YA UTAWALA BORA
Misingi ya Utawala bora inatambulika kwa tofauti ya
idadi, mingine hutambulika kuwa ni ni mitano,
wakati mwingi misingi sita hadi nane hutajwa lakini
hata hivyo, misingi 15 nimeibaini katika mada yetu
hii.
Graphic designer © Amandus Mtani -2016
2.2.1 Utawala wa kidemokrasia, uchaguzi huru na haki
Kuhakikisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka unakuwa huru na wa
haki ili kuwawezesha wananchi kuitumia vyema haki yao ya
kidemokrasia kwa kuchagua viongozi wanaowataka.
Uchaguzi usiwe chanzo cha kuvurugika kwa amani ya nchi
hivyo ufanyike kwa amani na utulivu. Uwepo wa vipindi vya
uchaguzi wa viongozi na chaguzi zenye kuzingatia haki na
usawa
0
2.2.2 Ushirikishwaji wa umma
Kuhakikisha kuwa bila kujali jinsi, wanawake na
wanaume, wanashiriki katika ngazi zote za utawal
bora. Ushirikishwaji waweza kuwa wa moja kwa
moja au kwa njia ya uwakilishi kupitia taasisi
zinazotambuliwa. Ikumbukwe hata hivyo kwamba
ushirikishwaji si lazima uhusishe jamii isiyofikika
mfano, jamii inayokula mizizi na matunda lazima
ishiriki katika maamuzi. ushirikishwaji unahitaji
mtiririko wa taarifa na mipango, kwa maana nyingi
na hapa unazungumziwa uhuru wa kujieleza na
vyama vya kijamii 'civil society '.
Graphic designer © Amandus Mtani -2016
Graphic designer © Amandus Mtani -2016
2.2.3 Utawala wa kisheriaUtawala wa sheria yaani 'Rule of law' lazima uwepo
kwenye utawala bora. Sheria ziwe zinaongoza nchi
na asiwepo mtu aliye juu ya sheria. Miongoni mwa
waasisi wa Utawala wa sheria ni mwanafilosofia
Aristotle, ambaye aliandika "Law should govern".
yaani 'Sheria ni lazima iongoze'. Hii ni kuhakikisha
kwamba-;A. Serikali na maofisa wake wanawajibika chini ya sheria
B. Sheria ziko wazi, zinaeleweka kwa umma, haziyumbi na
zinalinda misingi ya haki ikiwemo usalama wa watu
na mali zao.
C. Mchakato unaoruhusu sheria kutendeka kwa wakati,
kusimamiwa na upatikanaji wa haki
D. Kuwa na uwezo wa kupata haki inayotolewa na wanasheria
mahiri na wenye maadili, mawakili, majaji, wawakilishi,
wanasheria na kwamba rasilimali sheria zinapatikana.
NUKUU"Nchi yetu inaongozwakwa sheria...Hatuwezikuchagua kiongoziasiyeheshimu sheriaakawa anaongoza nchikwa kushauriwa namkewe, maana hamjuikesho akiamkaatamshauri nini?"
JKN
2.2.4 Matarajio ya wananchi
Msingi au nguzo nyingine muhimu ni kuhakikisha
kwamba, matarajio ya wananchi yanafikiwa katika
kiwango cha kuridhisha, hii inaondoa malalamiko
lakini pia itawatia nguvu wananchi katika
kuendeleza shughuli za maendeleo.
2.2. 5 Kuheshimu haki za msingi za binadamu
Kuheshimu haki zote za msingi za binadamu
huleta usawa kwa watu wote, huondoa dhana ya
ubaguzi katika ngazi zote. Kuheshimu haki za
binadamu huleta heshima katika tamaduni za
watu na tofauti zao (diversity), kama uhuru wa
kuabudu, uhuru wa kushiriki n.k
Graphic designer © Amandus Mtani -2016
Graphic designer © Amandus Mtani -2016
2.2.6 Uwazi katika kuendesha shughuli za maendeleo
Mipango na Mgawanyo wa Rasilimali: Ni kiasi gani cha
fedha kilichopo? Nini kimepangwa kufanyika? Watoa
huduma wamepanga kuzitumia vipi? Mgawo wa
fedha/rasilimali za umma hutolewa kulingana na
Mpango Mkakati ulioainisha shughuli zote kwa kina na
kuidhinishwa.
Uwazi una maana kwamba uamuzi unafanyika katika
misingi ya sheria na taratibu lakini pia ina maana
mawasiliano au taarifa zinapatikana wakati wote kwa
watu watakaohusika ma maamuzi
Graphic designer © Amandus Mtani -2016
2.2.7 Uwajibikaji katika utendajiUwajibikaji ni msingi muhimu wa utawala bora na hii si tu
kwa taasisi za serikali lakini hata pia kwa taasisi binafsi.
Taasisi binafsi na za umma, mtu mmoja mmoja lazima
wawajibike. Rushwa za aina zote ni shurti zipigwe vita na
kusiwepo na mianya ya rushwa kwa muktadha huo. Je, watoa
huduma wanatekeleza wajibu wao kwa ufanisi? Watumishi wa
umma wanatoa huduma bora za jamii?
Kupokea kero na malalamiko na kuyatatua kwa wakati na
kuwajulisha wananchi hatua zilizochukuliwa. Kuweka
masanduku ya maoni ambayo yatamwezesha kila mwananchi
kuweza kutoa maoni yake kwa njia ya siri. Kuitisha Mikutano
ya maendeleo Mikutano Mikuu ya Kata, Vijiji na vitongoji ili
kuweza kujadili suala la Maendeleo kwa uwazi kwani kila
mmoja atakuwa na nafasi katika kutoa maoni katika Mkutano
huo wa Hadhara.
2.2.8 Uadilifu
Hii inashabihana na uwazi ambapo inahusiana sana
mgawanyo na utumiaji wa rasilimali za taifa kwa
minajili ambayo haibagui watu na haipendelei walio
katika madaraka. Katika kuzingatia uwepo wa uwazi,
uwajibikaji na uadilifu, mifumo tofauti
imetengenezwa na mashirika ya kijamii na serikali ili
iweze kutumika katika jamii zetu na kuhakikisha
ustawi wa jamii nzima.
Uwazi unaweza kuwepo katika nyanja mbalimbali
kama utendaji, fedha nk. mfano wa mifumo hiyo ni;
PETS (Public Expenditure Track System), PRA
(Participatory Rural Appraisal- Ushirikishaji wa jamii
ya vijijini katika tathmini).
Graphic designer © Amandus Mtani -2016
2.2.9 Ufanisi na tija ( Effectiveness and efficiency)
Utawala bora una maana mchakato na taasisi
kuzalisha matokeo ambayo yanakidhi mahitaji ya
jamii kwa wakati kwa kutumia rasilimali zilizopo
katika maeneo yao.
Dhana ya 'efficiency' katika muktadha wa utawala
bora ina maana kutumia rasilimali ipasavyo na
kulinda mazingira na neno effectiveness ni
kukamilisha majukumu kwa wakati.
Ufanisi na tija ni hali ya utendaji inayozalisha
matokeo yanayokidhi malengo na matarajio ya watu
na kuhakikisha matumizi mazuri ya rasilimali.
Ufanisi na Tija unajumuisha mambo yafuatayo:
Graphic designer © Amandus Mtani -2016
2.2.9 Ufanisi na tija ( Effectiveness and efficiency)
Utendaji wenye matokeo yanayokidhi malengo
na matarajio ya watu wote.
Graphic designer © Amandus Mtani -2016
Kutumia rasilimali kwa uangalifu na umakini
(Matumizi bora ya rasilimali).
Utumiaji endelevu wa rasilimali kwa ufanisi
Utunzaji wa mazingira.
Utoaji wa uhakika wa huduma za jamii na kwa
wakati
Graphic designer © Amandus Mtani -2016
2.2.10 Ujuzi na Uwezo kuboreshwa
Watu wenye ujuzi na uwezo katika makundi yote
wanapaswa kuendelea kuboreshwa kwa ajili ya
maendele ya taifa na wananchi wenyewe. Nchi
inayojali utawala bora hapana shaka dhana hii
inatekelezwa ipasavyo.
2.2.11 Utayari wa kubadilika
Huu ni msingi mwingine ya utawala bora, nchi
ambayo ina utayari wa kubadilika. Mfano kupokea
madiliko yenye tija, kuwahimiza wananchi kuwa
wabunifu na kupokea ubunifu, ubunifu ni kigezo
muhimu katika maendeleo ya nchi.
Graphic designer © Amandus Mtani -2016
2.2.12 Maendeleo ya endelevu (Sustainable Development)
Hii ni kuhakikisha kwamba maendeleo ya nchi
hayayumbi kiuchumi, maendeleo yanaboreshwa na nchi
inasonga mbele, kuepuka suala la, leo uchumi
unaanguka kesho uinuka keshokutwa unaanguka tena.
Uchumi wa nchi lazima uwe na mwendeleo wa kiuchumi
lakini pia uchumi wa mtu mmoja mmoja lazima
uonekane2.2.13 Mwitikio
'Responsiveness' au mwitikio ni hali ya kutoa huduma
kwa jamii kwa wakati na kwa kiwango kinachokidhi
matarajio ya watu. Mwitikio unajumuisha mambo
yafuatayo:
Kujali na kusikiliza matatizo ya watu.
Kutoa huduma kwa haraka na kwa kiwango bora.
Kukidhi matarajio ya watu.
Graphic designer © Amandus Mtani -2016
2.2.14 Ugatuaji wa madaraka
Ugatuaji wa madaraka yaani 'decentralization' ni
msingi mwingine muhimu kwa wananchi na
maendeleo ya taifa lenye misingi ya demokrasia ya
kweli.
Serikali inafanya ugatuaji wa madaraka kutoka
serikali kuu na kupeleka serikali za mitaa kwa lengo
la kuleta maendeleo nchini kuanzia ngazi ya vijiji
hadi serikali kuu, mfano Wizara ya Afya
inavyowajengea uwezo wananchi kupitia Serikali za
Mitaa namna yakujiongoza wenyewe kwenye masuala
ya afya ili kupunguza vifo.
Graphic designer © Amandus Mtani -2016
2.2.15 Maridhiano
Utawala bora unahimiza kukutanishwa kwa mawazo
mbalimbali ili kupata suluhu au maamuzi ya pamoja
ambayo yanazingatia matakwa ya jamii nzima.
Kwa muktadha huo basi, misingi hii ikizingatiwa na
kufanyiwa utekelezaji lazima mabadiliko yataonekana.
Ili utawala bora uwe na sifa za kupendeza na kupendwa
na wananchi, lazima uzingatie misingi yake
iliyoainishwa.
2.3 NGUZO ZA UTAWALA BORA
Dhana ya Utawala Bora ina nguzo kuu tano:
Katiba ya kidemokrasia
Ulinzi, ukuzaji na uzingatiaji wa haki za
binadamu;
Mgawanyo wa Madaraka
Uhuru wa Mahakama
Uhuru wa habari na uhuru wa vyombo vya
habari.
Graphic designer © Amandus Mtani -2016
2.3.1 Katiba ya Kidemokrasia
Katiba ni waraka wa kisiasa na kisheria wenye
muafaka wa kitaifa juu ya namna ya kuendesha
masuala ya nchi. Demokrasia ni mfumo wa kisiasa
wa kuchagua na kubadilisha serikali kwa njia ya
uchaguzi ulio huru na wa haki. Ni Ushirikishwaji wa
kweli wa wananchi katika maisha ya kiuchumi,
kisiasa na kijamii. Hivyo, Katiba ya Kidemokrasia ni
ile ambayo kuandikwa kwake kumetokana na ridhaa
na mwafaka wa wananchi.
Graphic designer © Amandus Mtani -2016
2.3.2 Ulinzi, Ukuzaji na Uzingatiaji wa Haki
za Binadamu
Utawala bora ni ule unaolenga kuboresha na
kujali maisha ya watu. Njia ya msingi ya kujali
maisha ya watu ni kulinda, kukuza na kuzingatia
haki za binadamu. Utawala bora unataka kuwe
na mfumo wa kisheria, kiutawala na utashi wa
kisiasa unaolinda, kukuza na kuzingatia haki za
binadamu.
Graphic designer © Amandus Mtani -2016
2.3.3 Mgawanyo wa Madaraka
Dhana ya mgawanyo wa madaraka inaeleza kuwa utawala
wa dola unapaswa kugawanywa katika vyombo vitatu
ambavyo ni Serikali, Bunge na Mahakama. Kila chombo kina
majukumu tofauti na chombo kingine. Kwa mujibu wa
dhana hii, mamlaka ya Serikali ni utendaji; mamlaka ya
Bunge ni kutunga sheria na kusimamia utekelezaji wa
shughuli za umma; na mamlaka ya Mahakama ni kutafsiri
sheria na kutoa haki.
Hapa nchini, dhana hii inatajwa kwenye Ibara ya 4 ya
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka
1977. Dhana hii inazuia chombo kimoja kutawala, kuingilia
na kufanya kazi za chombo kingine. Lengo la mgawanyo wa
madaraka ni kuongeza ufanisi na kuleta uwajibikaji wa
vyombo vya dola.
Graphic designer © Amandus Mtani -2016
2.3.4 Uhuru wa Mahakama
Uhuru wa Mahakama unamaanisha kuwa kila jaji au
hakimu yuko huru kuamua kesi iliyopo mbele yake
kwa mujibu wa sheria na ushahidi ulioletwa mbele
yake, na katika kutekeleza majukumu hayo,
hapaswi kuingiliwa, kushawishiwa, au kushinikizwa
na mtu au chombo chochote, ikiwemo Bunge na
Serikali kama inavyoelezwa katika Ibara ya 107B ya
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya
mwaka 1977.
Hivyo, dhana ya uhuru wa mahakama inaitaka
mahakama kutekeleza majukumu yake bila woga
wala upendeleo. Uhuru wa mahakama unahifadhiwa
na kulindwa katika maeneo manne ambayo ni:
Graphic designer © Amandus Mtani -2016
i) Kuzuia kuondolewa kwa Jaji au Hakimu katika ofisi
bila ya sababu za msingi na bila ya kufuata taratibu
zilizowekwa hata kama kuna sababu za kumuondoa,
ii) Kuweka kinga ya kutoshtakiwa kwa Jaji au Hakimu
kwa makosa yoyote, yawe ya jinai au madai kutokana na
maamuzi yake ya kimahakama aliyoyafanya,
iii) Kutopunguza au kuondoa mishahara na maslahi ya
Jaji au Hakimu, na
iv) Kutokuwa na vyeo kwenye vyombo vingine vya dola
au kushiriki katika shughuli za vyama vya siasa.
Hata hivyo, ni vema ikafahamika kwamba uhuru wa
mahakama sio kibali kwa jaji au hakimu kuamua kesi
kwa namna anavyojisikia yeye au kwa matakwa yake.
Graphic designer © Amandus Mtani -2016
2.3.5 Uhuru wa Habari na Uhuru wa Vyombo
vya Habari
Uhuru wa habari una maana ya watu kuweza
kuzungumza na kupashana habari na kuwa na haki ya
kupata habari kutoka katika vyombo vya umma na hata
binafsi ambavyo vinatekeleza wajibu wa umma.
Hili lazima liende sawia na kuwa na vyombo vya habari
vilivyo huru, kwa maana ya kuwa na uwezo wa kutafuta
na kuandika habari na kuzisambaza kwa watu ndani na
nje ya mipaka ya nchi bila ya kuingiliwa na bila ya
sababu maalum na Serikali.
Lengo ni kuwawezesha wananchi kufahamu namna
viongozi wanavyoendesha nchi na hatimaye kujadili na
kutoa maamuzi juu ya rasilimali za nchi yao.
MSISITIZO:
Dhana ya utawala bora ni pana sana ambayo
inahitaji umakini zaidi ili kuweza kuitekeleza hivyo
ni lazima watendaji tuwajibike ipasavyo katika
kuhakikisha wananchi wanapata huduma iliyobora
na yenye manufaa kwao, na hii si kufanya kazi kwa
nadharia bali kufanya kazi kwa vitendo.
Graphic designer © Amandus Mtani -2016
Graphic designer © Amandus Mtani -2016
2.2.4 NINI KIFANYIKE KUBORESHA UTAWALA BORA?
Kuongeza ushirikishwaji wa wananchi katika utendaji
wa shughuli za umma
Kujenga uelewa kwa kutoa elimu ya uraia ili kujenga
jamii iliyohabarishwa
Kufanya ushawishi ili kuboresha hali ya demokrasia
nchini
Kuandaa mihadhara ili jamii iweze kujadili masuala
ya kiutawala na kisiasa yanayoendelea nchini.
Graphic designer © Amandus Mtani -2016
2.2.4 FAIDA YA UTAWALA BORAUtawala bora unasaidia kuwa na mambo yafuatayo:
Matumizi mazuri ya rasilimali za nchi,
Maendeleo endelevu,
Kupungua kwa umasikini, ujinga na maradhi,
Kutokomea kwa rushwa,
Huduma bora za jamii,
Amani na utulivu,
Kuheshimiwa kwa haki za binadamu,
Utatuzi wa migogoro kwa wa sheria na taratibu,
Kuleta ustawi wa wananchi.
Graphic designer © Amandus Mtani -2016
2.2.5 UMUHIMU WA WANANCHI KUSHIRIKI
KATIKA UTAWALA:
Kukosoa matumizi mabaya ya fedha na viongozi kwa
misingi ya demokrasia
Kushirikishwa kupanga kusimamia miradi ya
maendeleo katika maeneo yao
Kuunga mkono jitihada za serikali katika kuchochea
ustawi na maendeleo kwa jamii
Kuhoji utendaji wa serikali kuanzia ngazi ya mtaa,
kata, kijiji, wilaya kuhakikisha uwazi, uadilifu na
uwajibikaji.
2.6.0 MISINGI YA UTOAJI WA HAKI
Uzingatiaji wa utawala bora hauhusu tu mhimili wa
serikali, bali pia unahusu vyombo vya kutoa haki.
Vyombo hivyo ni mahakama, mabaraza yenye asili ya
mahakama, kamati za nidhamu na vyombo vingine
vinayofanya kazi zenye asili ya kimahakama.
Hivyo, ili kuzingatia utawala bora katika utoaji wa
haki, Ibara ya 107A ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania ya mwaka 1977, pamoja na sheria
mbalimbali, imeweka misingi ambayo vyombo vya
kutoa haki vinatakiwa viifuate. Misingi hiyo ni kama
ifuatavyo:
Graphic designer © Amandus Mtani -2016
Kuzingatia Katiba na sheria za nchi;
Kutenda haki kwa wote bila ya kujali hali ya
mtu kijamii au kiuchumi;
Kutochelewesha haki bila sababu ya msingi;
Kutoa fidia stahiki kwa watu wanaoathirika
kutokana na makosa ya watu wengine;
Kukuza na kuendeleza usuluhishi baina ya
wanaohusika katika migogoro;
Kutenda haki bila kufungwa kupita kiasi na
masharti ya kiufundi yanayoweza kukwamisha
haki kutendeka;
Kuzingatia kanuni za haki ya asili (natural
justice).
Graphic designer © Amandus Mtani -2016
6.1 Kanuni za Haki ya AsiliKanuni za Haki ya Asili ni kanuni zinazoongoza
kufanya maamuzi ya utoaji wa haki yaliyo ya haki
na kwa kufuata utaratibu ulio wa haki. Wakati haki
na wajibu wa mtu yeyote vinahitaji kufanyiwa
uamuzi na mahakama au chombo kinginecho
kinachohusika, basi mtoa maamuzi ana wajibu wa
kufuata kanuni za haki ya asili. Kanuni hizo ni:
Haki ya Kusikilizwa
Wajibu wa kutopendelea
Wajibu wa kutoa sababu za uamuziVyanzo vya kanuni za haki ya asili ni Katiba, sheria
mbalimbali za nchi na maamuzi mbalimbali ya
mahakama. Ufafanuzi wa kanuni hizo ni kama
ifuatavyo:
Graphic designer © Amandus Mtani -2016
6.1.1 Haki ya Kusikilizwa
Haki ya kusikilizwa ina maanisha fursa ya
kusikilizwa kwa ukamilifu na kwa haki. Haki hii
inajumuisha kupewa taarifa ya kutosha na
yavmapema ya kesi ili kupata muda wa kuandaa
majibu ya kesi dhidi yake, kupewa nafasi ya kutoa
ushahidi wake kwa ukamilifu (ikiwani pamoja na
kuita mashahidi), kupewa fursa ya kuwauliza
maswali washitaki wake na kupewa fursa ya
kuwakilishwa, kama ilivyoelezwa kwenye Ibara ya
13 (6) (a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Graphic designer © Amandus Mtani -2016
6.1.2 Wajibu wa KutopendeleaKanuni hii inatamka kuwa, mtu hatakiwi kuwa
muamuzi katika kesi yake mwenyewe; na
inatokana na msingi kuwa mtoa maamuzi
hatakiwi kuwa na upendeleo na asihisiwe kuwa na
upendeleo. Upendeleo unaweza kusababishwa na
maslahi binafsi ya mtoa maamuzi, iwe moja kwa
moja au vinginevyo.
Graphic designer © Amandus Mtani -2016
6.1.3 Wajibu wa Kutoa Sababu za Uamuzi
Mtoa maamuzi ana wajibu wa kutoa sababu za
uamuzi wake. Hii ni kwa sababu kila upande
katika mgogoro una haki ya kujulishwa sababu za
uamuzi uliofikiwa na chombo cha kutoa haki.
Uamuzi wa chombo cha kutoa haki unatakiwa
uhalalishwe na sababu za kina na ushahidi. Sababu
za uamuzi zinausaidia kila upande kujua ni
kwanini umeshinda au umeshindwa. Sababu za
uamuzi zinaimarisha uwazi katika utoaji wa haki.
Graphic designer © Amandus Mtani -2016
7.0 HITIMISHO
Bila shaka umebaini kuwa utawala bora ni nyenzo
muhimu sana ya kufanikisha ajenda kuu za nchi
yetu na dunia ambazo ni amani, maendeleo
endelevu na ustawi wa mwanadamu na jamii kwa
ujumla.
Kwa kuwa sasa umejifunza kuhusu utawala bora,
inatarajiwa kuwa kwa nafasi yako utakuwa mdau
muhimu wa kujenga jamii ambayo misingi ya
utawala bora, demokrasia, haki za binadamu, utu
na ustawi wa mwanadamu inakuzwa, inalindwa,
inazingatiwa, inatekelezwa na kuhifadhiwa.