hotuba za kisasa - almokhtarone.com...muhammad na watu wake na masahaba zake na waliowafuata uongofu...

147
Jamhuri ya kiarabu ya Misri Wizara ya Wakfu Hotuba za kisasa Kutoka Wizara ya Wakfu ya Misri Kimetolewa na kusimamiwa Na Profesa \Muhammad Mukhtar Juma Mabrook Waziri wa Wakfu Mkuu wa Baraza Kuu la masuala ya Kiisilamu Na Mwanachama wa Jopu la Utafiti la Kiisilamu Kimefasiriwa Na Profesa\ Ayman Ibrahim Alaasar Kitivo cha Lugha na Ufasiri Chuo Kikuu cha Alazhar Kairo, Misri 6102 - 0341 H

Upload: others

Post on 06-Feb-2020

17 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Jamhuri ya kiarabu ya Misri

Wizara ya Wakfu

Hotuba za kisasa

Kutoka Wizara ya Wakfu ya Misri

Kimetolewa na kusimamiwa

Na

Profesa \Muhammad Mukhtar Juma Mabrook

Waziri wa Wakfu

Mkuu wa Baraza Kuu la masuala ya Kiisilamu

Na Mwanachama wa Jopu la Utafiti la Kiisilamu

Kimefasiriwa

Na

Profesa\ Ayman Ibrahim Alaasar

Kitivo cha Lugha na Ufasiri

Chuo Kikuu cha Alazhar

Kairo, Misri

6102 - 0341 H

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye

kurehemu

Utangulizi

Sukurani zote ni za Mwenyezi Mungu Mola wa ulimwengu, rehma

na amani zimshukie Mjumbe na Mtume wake wa mwisho, Mtume

Muhammad na watu wake na masahaba zake na waliowafuata

uongofu wake mpaka siku ya mwisho

Baada ya utangulizi:

Tuna furaha kubwa kwa kutoa kitabu hiki chenye mkusanyiko wa

hotuba za kisasa zilizochaguliwa kwa maimamu, wahadhiri,

wasomi na wenye kuhusika na masuala ya ulinganiaji ndani ya

Misri na katika ulimwengu wa kiarabu na wa kiisilamu. Kitabu

kilichoandaliwa na idara ya utafiti katika Wizara ya Wakfu chini

ya usimamizi na uhakiki wetu

Na tumezingatia kuwa hotuba za kidini ziwe katika muktadha wa usamehevu na

uadilifu wa dini ya kiisilamu ulio mbali na itikadi kali na kufanya inda na kuvuka

mipaka, na kwa ajili ya kufikisha ujumbe misikitini ambao utakuwa ukiwaweka

pamoja waumini na wala hauwatenganishi, na pia ukiwa na malengo ya kuleta

masilahi kwa waja kwa kuzingatia kuwa sheria ya Mwenyezi Mungu ipo kwa ajili

ya kusimamia masilahi haya. Na popote yawapo masilahi basi ni kwa kuwepo

sheria za Mwenyezi Mungu na kwa kufuatwa dini itakiwavyo na ipasavyo. Tuna

imani kuwa hotuba hizi zitakuwa ni maandalizi na marejeo kwa mwenye

kuhitaji hotuba kwa lugha ya kiswahili, sawa iwapo atakuwa anahutubu kwa

lugha mbili ya kiarabu na kiswahili au kwa kiswahili (pekee) na hii ni kwa mujibu

wa mazingira.

Mwenyezi Mungu ni mwafikishaji na ni mwenye kuombwa msaada…

Profesa: Muhammad Mukhtar Juma

Waziri wa Wakfu

Na Mkuu wa Baraza Kuu la masuala ya Kiisilamu

Uisilamu ni dini ya ujenzi na ya uimarishaji

32 Rabiu L awal 2548H. Sawa na 2 Januari 3127 A.D.

Imefasiriwa na profesa\ Ayman. I.Alasar

Kwanza: Vipengele

2. Kuimarisha ardhi ni jambo litakiwalo kisheria.

3. Wito wa uisilamu katika ujenzi na uimarishaji wa ardhi.

4. Kufanya vizuri kazi ni njia ya kuinuka kwa umma na raia

5. Uisilamu unakataa aina zote za uvivu.

6. Onyo la kubomoa na kufanya ufisadi katika ardhi.

Pili: Dalili

Ndani ya Kurani Tukufu

2. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: { Yeye ndiye aliye kuumbeni katika

ardhi, na akakuwekeni humo.}(Hud. 72)

3. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Yeye ndiye aliyedhalilisha ardhi kwa

faida yenu, basi tembeeni katika pande zake, na kuleni katika riziki zake. Na

kwake Yeye ndio kufufuliwa} (Almulk. 26)

4. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {na wengine wanasafiri katika ardhi

wakitafuta fadhila ya Mwenyezi Mungu} (Muzammil. 31)

5. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: { Na sema: Tendeni vitendo. Na

Mwenyezi Mungu, na Mtume wake, na Waumini wataviona vitendo vyenu. Na

mtarudishwa kwa Mwenye kujua siri na dhaahiri; naye atakuambieni mliyo

kuwa mkiyatenda} (Taubah. 216)

6. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {wala msifanye uharibifu katika nchi

baada ya kuwa imekwisha tengenezwa.. na muombeni kwa kuogopa na kwa

kutumai. Hakika rehema za ya Mwenyezi Mungu iko karibu na wanaofanya

mema} (Al Aaraf. 67)

7. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Basi malipo ya wale wanao mpiga

vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wakawania kufanya uchafuzi

katika nchi, ni kuuwawa, au kusalibiwa, au kukatwa mikono yao na miguu

yao kwa mabadilisho, au kutolewa nchi. Hii ndiyo hizaya yao katika dunia;

na katika Akhera watapata adhabu kubwa} (Al maidah. 44)

Ndani ya Hadithi za Mtume (Rehma na amani zimshukie juu yake)

2. Kutoka kwa Miqdam (Mwenyezi Mungu amwie radhi), kwamba Mtume

(Rehma na amani zimshukie juu yake) amesema: “ Hakula mtu chakula bora

kuliko alichochuma kwa kazi ya mikono yake, na hakika Mtume wa

Mwenyezi Mungu Daudi (juu yake rehma na amani) alikuwa akila kutokana

na kazi za mikono yake. (Imepokewa na Bukhari)

3. Na kutoka kwa Abdalla bin Abbas (Mwenyezi Mungu awawie radhi)

amesema: amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani

zimshukia juu yake) “ atakaepambazukiwa hali ya kuwa amejitosheleza

kutokana na kazi ya mkono wake basi amepambazukiwa hali ya kuwa

amesamehewa. (Muujam Alwasiyt).

4. Kutoka kwa Abi Hurayra (Mwenyezi Mungu amwie radhi) amesema:

amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani zimshukia juu

yake) kujifungia mmoja wenu mzigo wa kuni juu ya mgongo wake ni bora

kuliko kuomba mtu mwengine sawa ampe au amkatalie. (Imepokewa na

Bukhari)

5. Kutoka kwa Abi Hurayra (Mwenyezi Mungu amwie radhi) amesema:

amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani zimshukia juu

yake) “mwenye kumhudumikia mjane au masikini, hupata malipo sawa na

waipiganiao dini ya Mwenyezi Mungu, au anaesimama usiku kusali na

kufunga mchana. (Imepokewa na Bukhari)

6. Kutoka kwa Anas Bin Malik (Mwenyezi Mungu amwie radhi) amesema:

amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani zimshukia juu

yake) iwapo kitasimama kiama na kwenye mkono wa mmoja wenu ana

mche, kama ataweza kutosimama kabla ya kuipanda, basin a aipande.

(Imepokewa na Bukhari)

7. Kutoka kwa Ka`ab bin U`jrah (Mwenyezi Mungu amwie radhi). Kuna kijana

alipita mbele ya Mtume (Rehma na amani zimshukie juu yake), masahaba

wa Mtume (Rehma na amani zimshukie juu yake) wakaona kwenye ngozi

yake ukakamavu na ucheshi wake kitu ambacho kiliwavutia. Wakasema: “

ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu unaonaje lau kama kijana huyu

angelikuwa anapigania njia ya Mwenyezi Mungu!! Mtume (Rehma na amani

zimshukie juu yake) akasema: “ iwapo anawatafutia riziki watoto wake,

basi yupo katika njia ya Mwenyezi Mungu. Na iwapo ametoka kuwatafutia

riziki wazazi wake wawili watu wazima basi yupo katika njia ya Mwenyezi

Mungu. Na iwapo ametoka kwa ajili ya nafsi yake ili kujikinga na

haramu, basi yupo katika njia ya Mwenyezi Mungu, na ikiwa ametoka kwa

ajili ya kuitafutia familia yake riziki basi yupo katika njia ya Mwenyezi

Mungu. Na kama ametoka kutafuta riziki kwa ajili ya kujifaharisha na

kujilimbikizia basi atakuwa yupo katika njia ya shetani. (Imepokewa na

Attabari).

8. Kutoka kwa Anas bin Malik (rehma na amani zimshukia juu yake)

amesema: Mtume (Rehma na amani zimshukie juu yake) alikuwa akisema

“Ewe Mola angu, hakika mimi ninajilinda kwako kutokana na kushindwa,

uvivu, woga, ukongwe, ubakhili. Na ninajikinga kwako na adhabu za kaburi

na fitina za uhai na umauti.” (Imepokewa na Muslim).

Maudhui

Hakika Mwenyezi Mungu amemuumba mwanadamu katika umbile bora zaidi,

akamtukuza kuliko viumbe wengine, na kumdhalilishia ulimwengu kila kilichopo

ulimwenguni. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema {Na hakika tumewatukuza

wanaadamu, na tumewapa vya kupanda nchi kavu na baharini, na tumewaruzuku vitu

vizuri vizuri, na tumewafadhilisha kwa fadhila kubwa kuliko wengi miongoni mwa

tulio waumba} Al Israa, 81. Pia amesema: {Yeye ndiye aliye kuumbieni vyote

vilivyomo katika ardhi.} Al baqara 3:.

Na ikapelekea ukarimu huu na neema hii kuwa ndio sababu ya ukhalifa katika

ardhi. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema {Na pale Mola wako Mlezi alipo

waambia Malaika: Mimi nitamweka katika ardhi Khalifa (mfwatizi), wakasema:

Utaweka humo atakaye fanya uharibifu humo na kumwaga damu, hali sisi

tunakutakasa kwa sifa zako na tunakutaja kwa utakatifu wako? Akasema: Hakika

Mimi nayajua msiyo yajua} (Al baqara 41). Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu

akamwekea mwanadamu mipaka na kumpa jukumu kubwa kuhusu ibada nalo ni

kumtaka aiimarishe ardhi, na atowe hazina zake na vyenye thamani. Akasema {

Yeye ndiye aliye kuumbeni katika ardhi, na akakuwekeni humo. } (Hud, 72.) Ikiwa na

maana, amewatakeni kuijenga ardhi na kuiimarisha, na kuangalia vile alivyokupeni

katika kheri na katika vyakula.

Mwenyezi Mungu amemuamrisha mwanadamu atafute na awe na sababu ya

kutafutia riziki, na kuacha kujibweteka na kupiga uvivu kwa ajili hiyo Mwenyezi

Mungu amesema { Yeye ndiye aliyedhalilisha ardhi kwa faida yenu, basi tembeeni

katika pande zake, na kuleni katika riziki zake. Na kwake Yeye ndio kufufuliwa}

(Almulk.26).

Na katika kufanya kazi hakuna wakati maalumu, mwanadamu hana budi kufanya

kazi hadi mwisho wa pumzi zake, kuthibisha hilo, Mtume (Rehma na amani

zimshukie juu yake) anasema katika hadithi aliyoipokea Anas Bin Malik

(Mwenyezi Mungu amwie radhi) amesema: amesema Mjumbe wa Mwenyezi

Mungu (rehma na amani zimshukia juu yake) Kutoka kwa Anas Bin Malik

(Mwenyezi Mungu amwie radhi) amesema: amesema mjumbe wa Mwenyezi

Mungu (rehma na amani zimshukia juu yake) iwapo kitasimama kiama na kwenye

mkono wa mmoja wenu ana mche, kama ataweza kutosimama kabla ya kuipanda,

basi na aipande. (Imepokewa na Bukhari). Dini ya kiisilamu inatukuza sana ujenzi,

na kuimarisha na inalingania hasa vitu hivi, hata iwapo katika wakati wa dhiki,

kwani kuimarisha ni miongoni mwa sababu kuu za maendeleo ya umma na jamii.

Uisilamu unazingatia sana elimu na mafunzo yote yanayoshikamana na kuijenga

ardhi na kuimarisha dunia, ikawahimiza wafuasi wake kutembea katika pembe

zake, na kujitafutia riziki zao baharini na nchi kavu pia, pamoja na kuhimizwa

kufanya kazi. Inathibiti haya kutoka kwa hadithi ya Miqdam (Mwenyezi Mungu

amwie radhi), kwamba Mtume (Rehma na amani zimshukie juu yake) amesema: “

Hakula mtu chakula bora kuliko alichochuma kwa kazi ya mikono yake, na hakika

Mtume wa Mwenyezi Mungu Daudi (juu yake rehma na amani) alikuwa akila

kutokana na kazi za mikono yake”. (Imepokewa na Bukhari).

Uisilamu ni wito ulio wazi wa kufanya kazi ambazo zitapelekea kuimarisha na

kujenga ili manufaa yarudi kwa ulimwengu mzima.

Kwa ajili hiyo: Uisilamu umeingalia kazi kwa mtazamo usio na mzaha na

kuitukuza pia, na kunyanyua thamani ya kazi na kuifanya kuwa ndio sababu ya

maeneleo. Na pia kuifanya kuwa ni ibada ambayo mtu hupata malipo. Aya za

Kurani Tukufu zimehimiza kufanya kazi na kuishi. Likaja agizo la kutaka watu

watawanyike katika ardhi kwa ajili ya kutafuta riziki baada ya amri ya kusali.

Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema {Na itakapokwisha sala, tawanyikeni katika

nchi mtafute fadhila za Mwenyezi Mungu, na mkumbukeni Mwenyezi Mungu kwa

wingi ili mpate kufanikiwa} Jumaa, 21.

Na Sayyidna I`rak Bin Malik (Mwenyezi Mungu amwie radhi) akishasali sala ya

Ijumaa husimama mbele ya mlango wa msikiti, kisha husema “ewe Mola wangu

hakika nimeitikia wito wako na nimekishasali faradhi yako, na ninaondoka kama

ulivyoniamrisha, niruzuku katika fadhila zako kwani wewe ni mbora wa

wanaoruzuku.”

Na kwa kutokana na umuhimu wa kazi kwa ajili ya kuimarisha na kujenga, aya

nyingi ndani ya Kurani Tukufu zimezungumzia kuhusu kazi, vilevile hadithi za

Mtume (Rehma na amani zimshukie juu yake) zipo nyingi zilizoweka wazi jambo

hili na kuhimiza na kutia shime kuhusu kazi, na kuacha kupiga uvivu na

kujibweteka. Na kuweka wazi kuwa kufanya kazi ni kijiondoshea udhalilifu na

kuwa na heshima na utukufu. Imepokewa na Abi Hurayra (rehma na amani

zimshukia juu yake) amesma: amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu (rehma na

amani zimshukia juu yake) “kujifungia mmoja wenu mzigo wa kuni juu ya

mgongo wake ni bora kuliko kuomba mtu mwengine sawa ampe au amkatalie.

(Imepokewa na Bukhari). Na Sufyan Thawriy (Mwenyezi Mungu amrehemu)

akipita kwa baadhi ya watu wakiwa wamekaa ndani ya msikiti wa mtukufu,

huwaambia: “ ni nini kilichowafanya mukae? Nao hujibu: “Tufanye nini sasa!?

Nae husema: tafuteni fadhila za Mwenyezi Mungu na wala musiwe waombaji kwa

waisilamu.

Uisilamu umeweka wazi kuwa, yeyote atafutae maisha ya halali kwa ajili ya

wanawe anahesabiwa kuwa yupo katika mashahidi na aliyefungamana na njia ya

Mwenyezi Mungu. Imepokewa na Kutoka kwa Ka`ab bin U`jrah (Mwenyezi

Mungu amwie radhi). Kuna kijana alipita mbele ya Mtume (Rehma na amani

zimshukie juu yake), masahaba wa Mtume (Rehma na amani zimshukie juu yake)

wakaona kwenye ngozi yake ukakamavu na ucheshi wake kitu ambacho

kiliwavutia. Wakasema: “ ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu unaonaje lau kama

kijana huyu angelikuwa anapigania njia ya Mwenyezi Mungu!! Mtume (Rehma na

amani zimshukie juu yake) akasema: “ iwapo anawatafutia riziki watoto wake,

basi yupo katika njia ya Mwenyezi Mungu. Na iwapo ametoka kuwatafutia riziki

wazazi wake wawili watu wazima basi yupo katika njia ya Mwenyezi Mungu. Na

iwapo ametoka kwa ajili ya nafsi yake ili kujikinga na haramu , basi yupo katika

njia ya Mwenyezi Mungu, na ikiwa ametoka kwa ajili ya kuitafutia familia yake

riziki basi yupo katika njia ya Mwenyezi Mungu. Na kama ametoka kutafuta riziki

kwa ajili ya kujifaharisha na kujilimbikizia basi atakuwa yupo katika njia ya

shetani. (Imepokewa na Attabari).

Na uisilamu haukutosheka kuwalingatia wafuasi wake kufanya kazi tu pekee kama

ndio njia ya maendeleo, bali pia umewataka wafanye kazi kama itakiwavyo –wawe

na ikhlasi- kwa ajili ya kupata mapenzi ya Mwenyezi Mungu na rehema zake.

Imepokewa kutoka kwa Aisha (rehma na amani zimshukia juu yake). Kwamba

Mtume (Rehma na amani zimshukie juu yake) amesema: “ Hakika Mwenyezi

Mungu – Mtukufu – anapenda mmoja wenu akifanya kazi aifanye vizuri.”

(imepokewa na Tabbariy).

Kufanya kazi itakiwavyo na kuijali na kuihifadhi ni katika misingi ambayo

uisilamu unataka ifuatwe, nayo ni lengo miongoni mwa malengo ya dini,

humtukuza muisilamu kupata radhi za Mwenyezi Mungu, kwa sababu Mwenyezi

Mungu huwa hakubali kazi isipokuwa ile iliyofanywa kwa ajili yake, kwani

Mwenyezi Mungu ameumba kila kitu kwa uangalifu sana, Mwenyezi Mungu

Mtukufu anasema {Huo ndio ufundi wa Mwenyezi Mungu aliye tengeneza vilivyo kila

kitu. Hakika Yeye anazo khabari za yote myatendayo} (Annaml, 99).

Na uisilamu ukahimiza kufanya vizuri na ipasavyo na kukataza kufanya ufisadi,

Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema { Na fanyeni wema. Hakika Mwenyezi Mungu

huwapenda wafanyao wema} (Al baqara.2:6). Na akasema {Nawe fanya wema

kama Mwenyezi Mungu alivyo kufanyia wema wewe. Wala usitafute kufanya ufisadi

katika ardhi. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi mafisadi.} (Al qasas.88).

Aya nyingi za Kurani Tukufu zimetaka mtu akifanya kazi basi aifanywe katika njia

sahihi hii kwa ajili ya kupata radhi za Mwenyezi Mungu, kusaidiana katia ya mtu

na jamii, na akaahidi malipo makubwa sana na kumsifia sifa njema hapa duniani

na kesho akhera. Na akaweka wazi kuwa mwanaadamu hatoacha kuwa anafanya

kazi ilivyokuwa yupo chini ya ulinzi wa Mwenyezi Mungu, mjuzi wa

vilivyofichikana kifuani, Naye kwake hakifichiki hata kilicho kidogo sana katika

matendo ya waja. Mwenyezi Mungu tawadhihirishia kwa kuwa amekisajili na

atawalipa kwa hicho siku ya watakayokutana. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema

{Na huwi katika jambo lolote, wala husomi sehemu yoyote katika Qur'ani, wala

hamtendi kitendo chochote ila Sisi huwa ni mashahidi juu yenu mnapo shughulika

nayo. Na hakifichikani kwa Mola wako Mlezi chenye uzito hata wa chembe katika

ardhi na katika mbingu, wala kidogo kuliko hicho wala kikubwa ila kimo katika

Kitabu kilicho wazi} (Yunus. 72).

Mwenyezi Mungu Mtukufu ndie anayemchunga mwanadamu katika kazi zake, na

humuona akiwa kiwandani, kondeni na hata katika biashara zake sehemu ambazo

hufanyia kazi. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema { Na sema: Tendeni vitendo. Na

Mwenyezi Mungu, na Mtume wake, na Waumini wataviona vitendo vyenu. Na

mtarudishwa kwa Mwenye kujua siri na dhaahiri; naye atakuambieni mliyo kuwa

mkiyatenda.} (Tawbah. 216). Amri ya hapa ni kama walivyosema wafasiri: kuna

kuogopesha: ikiwa na maana: matendo yenu hayafichikani mbele ya Mwenyezi

Mungu na wala kwa Mtume wake wala kwa waumini, basi harakisheni kutenda

mema, na fanyeni kazi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Na pia kuna - katika aya hii

– bishara na kuhamasishwa, kwani iwapo mtu ataelewa kuwa matendo ayatendayo

sawa ni mabaya au mazuri Mwenyezi Mungu ndie ayaonae, basi atakuwa na shime

ya kuyakimbilia matendo mema, na kujiepusha na mabaya, na maneno mazuri

yaliyoje ya mshairi Zuhayri:

“Mtu akiwa na tabia ya aina yoyote * hata kama ataificha, basi watu wataijua”

Pia imekuja katika hadithi za Mtume (Rehma na amani zimshukie juu yake) zenye

kuhimiza kufanya kazi kama itakiwavyo na kuimarisha kwa ajili ya kufikia kilicho

bora na kizuri. Kwa mfano katika upande wa kuabudu kupitia ibada ya sala

ambayo ninguzo kati ya mja na Mola wake, inatakiwa imamu wao awe mwenye

ujuzi kuliko wote na awe anaisoma Kurani Tukufu vizuri, pia awe anaisoma kwa

kuizingatia, ili ajumuike na wale waliobashiriwa na Mtume (Rehma na amani

zimshukie juu yake) kuwa atakuwapo pamoja na malaika wakarimu. Na vilevile

kwa asimamiaye masuala ya maiti, Mtume (Rehma na amani zimshukie juu yake)

anasema: “ Mmoja wenu akimveka sanda maiti basin a amvike vizuri”

(Imepokewa na Muslim).

Kutoka kwa A`swim Bin Kulayb Al jaramiy amesema: Baba yangu Kulayb

amenihadithia kwamba yeye amehudhuria jeneza pamoja na baba yake

alipokuwepo Mtume na mimi kipindi hicho ni mdogo mwenye akili na ufahamu,

wakamaliza kusalia jeneza wakaenda makaburini walipomlaza, akasema, Mtume

(Rehma na amani zimshukie juu yake) akawa anasema “uwekeni vizuri

mwanandani huu”. Mpaka watu kakadhania kuwa ni sunna, nikawageukia,

akasema: “ Ama huu haumfai maiti na wala haumdhuru, isipokuwa Mwenyezi

Mungu hupenda kwa mtenda kazi akifanya kazi basi aifanye vizuri.” (Imepokewa

na Bayhaqiy).

Kazi yoyote aitendayo mwanadamu ni lazima aifanye vile itakiwavyo, amchunge

Mwenyezi Mungu katika kazi hiyo, kwani Yeye Mwenyezi Mungu humuona mja

huyo na kilichomo ndani ya moyo wake na atawahesabu juu ya matendo yao

makubwa au madogo, mengi au machache.

Ama kwa wale ambao hawafanyi itakiwavyo kazi zao na wala hawamchungi

Mwenyezi Mungu, hupata madhambi mengi kwa kadiri ya madhara

atakayoyasababisha ya kupoteza mali na nguvu. Mfanya kazi ambaye hatimizi

wajibu wake na huzembea na wala hafanyi kazi kama alivyoagizwa na akatosheka

kujiridhisha yeye mwenyewe na akawa anapokea mshahara, huyu huwa anapokea

mshahara wa haramu na watu watakwenda kudai madai yao siku ya kiama. Na

yeyote ambae hii ndio sifa yake basi aelewe kuwa anabeba jukumu la

kutokuendelea kwa umma na kuonekana kuwa upo nyumba kimaendeleo.

Hatutoacha kumshtakia mbele ya Mwenyezi Mungu. Sayidna Omar (Mwenyezi

Mungu amwie radhi) anasema: “namshtakia Mwenyezi Mungu kutokana na

udhaifu wa kiongozi na ukhaini wa mwenye nguvu.”

Hakika uisilamu umepiga vita aina zote za kukata tama na uvivu ambao hausaidii

kitu katika kujenga na kuimarisha. Na ukaifanya sifa ya uvivu kuwa ni sifa chafu,

Mwenyezi Mungu amewakashifu wavivu kwenye kitabu chake kitukufu na kusema

kuwa ni sifa za wanafiki, akasema {wala hawaji kwenye Sala ila kwa uvivu, wala

hawatoi michango ila nao wamechukia} (Atawba. 65).

Uvivu ni njia mbaya na ni maafa makubwa yenye kuangamiza yenye kuharibu

taifa na raia zake na pia hupelekea kutoendelea na kuonekana taifa lililo nyuma

kimaendeleo. Nao ni ugonjwa hatari, mtu akiwa nao basi anaweza hata kupoteza

utu wake. Imamu Raghib amesema: “ajiewekae bila kazi hujivua ubinaadamu na

kujiweka kuwa mnyama, na hufikia pia kuwa kama maiti”.

Kwa ajili hiyo Mtume (Rehma na amani zimshukie juu yake) akajikinga kwa

Mwenyezi Mungu kutokana na uvivu na unyongonyevu, imepokewa kutoka kwa

Anas bin Malik (rehma na amani zimshukia juu yake) amesema: Mtume (Rehma

na amani zimshukie juu yake) alikuwa akisema “Ewe Mola angu, hakika mimi

ninajilinda kwako kutokana na kushindwa, uvivu, woga, ukongwe, ubakhili. Na

ninajikinga kwako na adhabu za kaburi na fitina za uhai na umauti.” (Imepokewa

na Muslim).

Na Mtume (Rehma na amani zimshukie juu yake) amelinganisha kati ya uvivu na

ukongwe kwa sababu kila moja katika hivi viwili humfanya mtu kuwa mzito wa

kutimiza wajibu aliotakiwa autimize.

Uvivu ni maafa yatokayo moyoni, na kizuizi chenye kuzuia kutimiza wajibu,

hudhoofisha utashi, hupelekea kwenye ufakiri, na ni vimelea vyenye kuua, maradhi

yenye kuangamiza, hudhoofisha ukuaji wa taifa na watu wake, na huzuia watu

wasifanye kazi kwa bidii na kuyatafuta manufaa.

Uisilamu umeutia dosari uvivu na kutahadharisha kutokuwa nao, kwani una

kuzembea katika mambo yasiyopasa kuzembewa, na kupelekea kujiweka mbali na

yaliyo muhimu na kuhisi kama kwamba ni sumu au kitu cha kuchukiza Mwenyezi

Mungu atuepushe nao. Na –uvivu- humfanya mtu achukie mazuri kutokana na

udhaifu wake wa kufuatilia, na humfanya aache yaliyo wajibu, kweli ni maafa

yasiyoleta mafanikio, humsambaratisha kila aliye nao, na humfanya mvivu kuwa

mwenye kutegemea wengine, asiye na uwezo wa kuchukua jukumu kama mtu

kamili. Na hatari yake huenea kwa mmoja moja na hata kwa jamii nzima. Imamu

Ali (Mwenyezi Mungu amwie radhi) anasema: “Kuzembea ni ufunguo wa kukatisha

tamaa, ulegevu na uvivu huleta maafa, na huzalisha maangamizo, asiyetafuta huwa

hapati na pia hupelekea katika maovu.”

Uvivu si katika mambo yatakiwayo katika uisilamu na wala hauna thamani, kwani

uisilamu hufukuzia mema na kuimarisha ulimwengu, ama wavivu wao hubomoa

ustaarabu na huharakisha kubomoa aina zote nyengine za ustaarabu.

Haya ni miongoni mwa mambo ambayo uisilamu umeyapiga vita, na ambayo katu

hayajengi na kuimarisha ulimwengu na huleta ufisadi katika ardhi na kuiharibu nayo

ni tabia yenye kudhalilisha iwapo atakuwa nayo mwanadamu. Tabia hii huwa hawawi

nayo isipokuwa wanafiki pekee ambao Mwenyezi Mungu amesema. {Na

wanajitahidi kuleta uharibifu katika ardhi. Na Mwenyezi Mungu hawapendi

waharibifu} (Al maida 75). Na anasema {wala msiasi katika nchi mkafanya

uharibifu} (Al baqara. 71).

Ufisadi upo wa aina nyingi, na ulio mbaya zaidi ni ule unaotumia jina la dini,

umma umefikwa na mitihani kwa sababu ya ufisadi hali ya kuwa dini haihusiki

kabisa. Huuwa, hujihalalishia mali na kuvunja heshima kwa jina la dini. Watu

hawa Mwenyezi Mungu amewakashifu ndani ya kitabu chake akasema {Na katika

watu yupo yule ambaye maneno yake kwa maisha ya kidunia hukufurahisha; naye

humshuhudisha Mwenyezi Mungu kwa yaliyomo moyoni mwake, na hali yeye ndiye

mkubwa wa ukhasimu 316. Na anapo tawala hufanya juhudi katika nchi kwa kufisidi

humo na kuteketeza mimea na viumbe. Na Mwenyezi Mungu hapendi ufisadi. 317. Na

akiambiwa: Mwogope Mwenyezi Mungu, hupandwa na mori wa kutenda madhambi.

Basi huyo inamtosha Jahannam. Paovu mno hapo kwa mapumziko.} (Al baqara

315-317).

Ufisadi kwanamna zake zote huyumbisha ukuaji na maendeleo ya taifa, na hueneza

mabaya na kupelekea kutojali majukumu. Kwa ajili hiyo, hakuna budi kupinga

ufisadi na wafanyao ufisadi. Kuupinga ufisadi ni kwa manufaa ya jamii nzima. Na

kuzembea bila ya kuupinga ni maangamizo kwa jamii nzima. Imepokewa kutoka

kwa Nuuman Bin Bashir (Mwenyezi Mungu awawie radhi), kwamba Mtume

(Rehma na amani zimshukie juu yake) alikuwa akisema: “Mfano wa asimamiaye

mipaka ya Mwenyezi Mungu na aliyeivuka ni mfano wa watu waliojazana kwenye

marikebu, wengine wakawa wapo juu na wengine chini, wale waliopo chini

wakiwa wanataka maji huwafuata wale waliopo juu, kisha huwaambia lau kama

sisi tungelichukua fungu letu na wala tusingelikukereni mliopo juu. Iwapo –wa

juu- wangeliwaacha na kile watakacho basi wangelizama wote na wangeliwapa

watakacho basi wangeliokoka wote pamoja.” (Imepokewa na Bukhari).

Hakuna budi kusaidiana, kuwa pamoja na kushikamana kati ya waisilamu ili imani

ipatikane pamoja na undugu wa kiisilamu.

Kuisafisha ardhi na wafanyao ufisadi , na kulinda njia na taasisi ni katika mambo

mema na mazuri. Mwenyezi Mungu huwakinga wafanyao ufisadi kwa kuwepo

watu wema, amesema {Basi mbona hawakuwamo katika watu wa kabla yenu wenye

vyeo na wasaa wanao kataza uharibifu katika nchi, isipo kuwa wachache tu, ambao

ndio tulio waokoa? Na walio dhulumu walifuata starehe zao, na wakawa ni

wakosefu} (Hud. 227). Kwani ufisadi ni ubomoaji wa jamii na hakuna njia ya

kujiokoa nao isipokuwa kuuzuia.

Na umma wa kiisilamu kwa fadhila zake Mwenyezi Mungu una kheri nyingi

kutoka kwa Mwenyezi Mungu, Kuna bahari, maziwa, mito mikubwa, ndani ya

ardhi muna madini yanayoitajika katika ulimwengu wetu wa kisasa, pia unamiliki

hazina kubwa ya mafuta ulimwenguni, ukizidisha thamanikubwa ya akili na fikira

na watendaji kazi. Kwa ajili hiyo umma hauna budi kuweka vitega uchumi vilivyo

bora, na pia kutumia wakati katika yenye kuleta manufaa kwa watu, na kwa njia ya

kuinua ustaarabu na maendeleo ya kielimu.

Umma wetu ni wa kazi na si wa kupiga uvivu, umma wa kujenga si wa kubomoa

na kuharibu, umma wenye ustaarabu, na kutoendelea si sifa isifikayo katu kwa

umma huu, ni juu ya kila muisilamu mwenye kuipenda dini yake na kujifaharishia

nayo atende kwa ajili ya kuiinua dini yake na kuliinua taifa lake.

Ubora wa maadili katika ujumbe wa Muhammad

25 Rabi`u awal 2548H. Sawa na 36 Disemba 3126 A.D

Kwanza :Vipengele

Uisilamu ni dini ya maadili mema.

Kuporomoka kwa maadili ni kuporomoka kwa umma.

Maadili ni matunda ya matendo sahihi.

namna gani tutatukuka kupitia maadili yetu?

Pili: Dalili

Katika Kurani Tukufu:

Mwenyenzi Mungu Mtukufu anasema { Na hakika wewe una tabia tukufu. }

Alqalam, 5.

Mwenyenzi Mungu Mtukufu anasema {Shikamana na kusamehe, na amrisha

mema, na jitenge na majaahili} Al aaraf, 2::.

Mwenyenzi Mungu Mtukufu anasema {Na ni nani mbora wa kusema kuliko aitae

kwa Mwenyezi Mungu, na akasema: hakika mimi ni katika Waisilamu 45. Mema

na maovu hayalingani. Pinga uovu kwa lililo jema zaidi. Hapo yule ambaye baina

yako naye pana uadui atakuwa kama rafiki jamaa wa kukuonea uchungu. 46. lakini

hawapewi wema huu ila wanao subiri, wala hawapewi ila wenye bahati kubwa.}

Fuswilat 44 -46.

Mwenyenzi Mungu Mtukufu anasema { Na waja wa Arrahman Mwingi wa

Rehema ni wale wanao tembea ulimwenguni kwa staha, na wajinga wakiwasemeza

hujibu: Salama! } Alfurqaan, 74.

Mwenyenzi Mungu Mtukufu anasema { Ewe mwanangu! Shika Sala, na amrisha

mema, na kataza maovu, na subiri kwa yanayo kupata. Hayo ni katika mambo ya

kuazimiwa. 29. Wala usiwabeuwe watu, wala usitembee katika nchi kwa maringo.

Hakika Mwenyezi Mungu hampendi kila anaye jivuna na kujifakhirisha. 2: Na

ushike mwendo wa katikati, na teremsha sauti yako. Hakika katika sauti mbaya

zote bila ya shaka iliyo zidi ni sauti ya punda.} Luqman, 28-2:.

Mwenyenzi Mungu Mtukufu anasema {Soma ulivyofunuliwa katika kitabu, na

ushike sala, hakika sala inazuilia mambo machafu na maovu. Na kwa yakini

kumdhukuru Mwenyezi Mungu ni jambo kubwa kabisa. Na Mwenyezi Mungu

anayajua mnayoyatenda. 57. wala msijadiliane na watu wa kitabu ila kwa njia iliyo

nzuri kabisa, isipokuwa wale walio dhulumu miongoni mwao. Na semeni:

tumeyaamini yaliyo teremshwa kwetu nayaliyo teremshwa kwenu. Na Mungu

wetu na Mungu wenu ni mmoja. Na sisini wenye kusilimi kwake. } Al ankabuut,

56-57.

Mwenyenzi Mungu Mtukufu anasema {Hija ni miezi maalumu. Na anaye kusudia

kufanya Hija katika miezi hiyo, basi asiseme maneno machafu wala asifanye

vitendo vichafu wala asibishane katika Hija. Na kheri yoyote mnayo ifanya

Mwenyezi Mungu anaijua. Na jitengezeeni zawadi. Na hakika bora ya zawadi ni

uchamngu. Na nicheni Mimi, enyi wenye akili !} Al baqarah, 2:8.

Mwenyenzi Mungu Mtukufu anasema {Wala usimt'ii kila mwingi wa kuapa wa

kudharauliwa, 22. Wanatamani lau unge lainisha ili nao

wakulainishie. 23. Mwenye kuzuia kheri, dhaalimu, mwingi wa

madhambi, 24. Mkavu, na juu ya hayo, mshari, amejipachika tu. 25. Ati kwa kuwa

ana mali na watoto! 26. Anapo somewa Aya zetu, husema: Hizi ni simulizi za

uwongo za watu wa zamani! 27. Tutamtia kovu juu ya pua yake.} Alqalam 21-27.

Katika hadithi za Mtume (Saw)

Kutoka kwa Nawaas bin Sama`n Al-answaary (Mwenyezi Mungu amwie radhi)

kwamba yeye amesema: Nilimuuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na

amani zimshukie juu yake) kuhusu wema na ubaya? Akasema: “wema ni tabia

njema, na ubaya ni uliopo ndani ya moyo wako na ukachukia watu wengine

wasikione.” (Sahihi Muslim).

Kutoka kwa Abi Dardai (Mwenyezi Mungu amwie radhi), kwamba Mtume wa

Mwenyezi Mungu (Rehma na amani zimshukie juu yake) amesema: “ Hakuna kitu

cha muumini ambacho kitakuwa kina uzito kwenye mizani yake siku ya kiyama

kuliko tabia njema, na hakika ya Mwenyezi Mungu anamchukia muovu mwenye

tabia chafu.” (kitabu cha Tirmidhy).

Kutoka kwa Abi Hurayra (Mwenyezi Mungu amwie radhi), amesema: amesema

Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na amani zimshukie juu yake) “ Hakika

mimi nimetumwa ili kutimiza matendo mema” (Imepokewa na Imam Ahmad).

Kutoka kwa Abi Durrin (Mwenyezi Mungu amwie radhi), amesema, Mtume wa

Mwenyezi Mungu (Rehma na amani zimshukie juu yake) ameniambia: “ Mche

Mwenyezi Mungu popote ulipo, na fuatishia jema kwa baya ili ulifute, na ishi na

watu kwa tabia njema.” (Imepokewa na Tirmidhiy).

Kutoka kwa Abi Hurayra (Mwenyezi Mungu amwie radhi), amesema: amesema

Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na amani zimshukie juu yake) “Muumini

aliyekamilika imani ni yule mwenye tabia njema, na mbora wenu ni yule aliye

mbora kwa wake zake.” (Imepokewa na Ahmad).

Kutoka kwa Saa`d bin Hisham bin Amir Al answaari (Mwenyezi Mungu amwie

radhi), amesema: Nilisema “ewe mama wa waumini –yaani Aisha (Mwenyezi

Mungu amwie radhi), - nieleze kuhusu tabia za Mtume wa Mwenyezi Mungu

akasema “ kwani wewe si unasoma Kurani? Nikamwambia ndio, akasema: “Basi

hakika tabia ya Mtume (Rehma na amani zimshukie juu yake) ilikuwa ni Kurani.”

(Imepokewa na Muslim).

Kutoka kwa Aisha (Mwenyezi Mungu amwie radhi), amesema: “ nilimsikia

Mtume wa Mwenyezi Mungu akisema: “ hakika ya muumini hujulikana kwa uzuri

wa tabia zake na kwa vyeo vya kusimama usiku na kufunga mchana.” (Imepokewa

na Abu Daudi.)

Kutoka kwa Jabir (Mwenyezi Mungu amwie radhi), hakika ya Mtume wa

Mwenyezi Mungu (Rehma na amani zimshukie juu yake) amesema: “ hakika ya

nimpendae kati yenu na atakaekuwa karibu nami kwenye kikao siku ya kiama ni

yule mwenye tabia njema, na hakika ya nimchukiae kati yenu na atakaekuwa mbali

nami kwenye kikao siku ya kiama wenye kuropokwa, wenye kusema sana na

wenye kujigamba” Masahaba wakamuuliza ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu

tumekwishamuelewa ni nani mropokwaji na msema sana lakini ni nani huyo

mwenye majigambo ? Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na amani zimshukie

juu yake) akasema ni wenye kiburi.” (Amepokea Tirmidhy.)

Tatu: Maudhui

Hakuna shaka ya kuwa namna ya kuupata utukufu ndani ya uisilamu ipo za aina

tofauti, na katika utukufu wake ni kuwa ni dini ya sheria na tabia, inayokusanya

maadili na utu wa hali ya juu, ambau unaweka pamoja sura ya kipekee ya tabia

njema. Na dini hii inatukuka kwa kuwa imekusanya njanja zote za maisha,

haikuacha jema miongoni mwa mambo mema isipokuwa imekusanya na

kulilingania na kuhimiza kulishikilia, wakati huo huo haikuacha ovu isipokuwa

imeliweka wazi na kulitahadharisha na kuamrisha kuliepuka.

Na katika mambo mazuri ambayo yamelinganiwa na kupendezeshwa kwa kuwa

nayo ni: Kujipamba na tabia njema kama subira, upole, huruma, ukweli uaminifu,

kutimiza ahadi, ukarimu, haya, kunyenyekea, ushujaa, uadilifu, wema, kusaidia,

kuweka macho chini, kuondoa uchafu, ubashasha wa uso, maneno mazuri, dhana

nzuri, kumheshimu mkubwa, kusuluhisha kati ya watu, athari njema, kuchunga

hisia za wengine na tabia njema nyenginezo. Na haya yote ni kama ilivyoashiriwa

katika aya ya Kurani Tukufu {Hakika hii kuran inaongoa kwenye yaliyo nyooka

kabisa, na inawabashiria Waumini ambao wanatenda mema ya kwamba watapata

malipo makubwa.) Al israa :.

Na kwa jambo hili kuna aya na hadithi za Mtume wa Mwenyezi Mungu nyingi

sana, kwa mfano Mwenyezi Mungu anamuamrisha Mtume wake kwa kusema

{Shikamana na kusamehe, na amrisha mema, na jitenge na majaahili} Al a`raf 2::.

Pia anasema {na semeni na watu kwa wema} Al baqara 94. Anaongeza kusema

tena { Hakuna kheri katika mengi ya wanayo shauriana kwa siri, isipo kuwa kwa

yule anaye amrisha kutoa sadaka, au kutenda mema, au kupatanisha baina ya watu.

Na mwenye kufanya hayo kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu, basi tutakuja

mpa ujira mkubwa} Alnisa 255. Na aya zenye ujumbe kama huu ziko nyingi.

Na kwa kila mwenye kuzingatia aya a Kurani na akachuguza kwa kina atagundua

ya kuwa muna aya nyingi sana zenye kulingania katika tabia njema na kuhimiza

watu wawe nazo. Na si kwa chochote zaidi ya kuwa tabia ni kama mizani ya

kisheria yenye kumpima mtu na kumpandisha mtu daraja za ukamilifu.

Na kama hadithi za Mtume wa Mwenyezi Mungu zilivyosisitiza juu ya umuhimu

wa tabia katika maisha ya mwanadamu. Kwa kuweka wazi malipo kwa mwenye

kuwa nazo, kwa mfano Mtume wa Mwenyezi Mungu anasema: “wema ni tabia

njema” (imepokewa na Imam Muslim.) na wema ni neno lenye kumaanisha kila

lililo zuri. Na hadithi nyengine ya Mtume wa Mwenyezi Mungu: “ Hakuna kitu

cha muumini ambacho kitakuwa kina uzito mkubwa kwenye mizani kushinda tabia

njema” na katika mapokezi mengine: “ Hakuna kitu cha muumini ambacho

kitakuwa kina uzito mkubwa kwenye mizani siku ya kiyama kuliko tabia njema, na

hakika ya Mwenyezi Mungu anamchukia muovu mwenye tabia chafu.”

(imepokewa na Tirmidhy katika kitabu chake kutoka kwa Abi Dardai.)

Na hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuwa akihimiza watu wawe na tabia

njema, kwani baadhi ya wakati huwa anasema “Muumini aliyekamilika imani ni

yule mwenye tabia njema, na mbora wenu ni yule aliye mbora kwa wake zao.”

(Imepokewa na Ahmad).

Na akaulizwa Mtume wa Mwenyezi Mungu: “ Ni muumini gani aliye bora?

Akasema: “ Mwenye tabia njema kuliko wote” (imepokewa na Ib Maajah.

Na Mtume wa Mwenyezi Mungu alipoulizwa kuhusu kitu ambacho kitawaingiza

kwa wingi watu peponi akasema: “ucha Mungu na tabia njema.” (Kitabu cha

Tirmidhy.)

Kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na amani zimshukie juu yake)

akafanya kuwa miongoni mwa mapenzi ya kumpenda yeye ni kuwa na tabia

njemaakasema: “hakika ya nimpendae kati yenu na atakaekuwa karibu nami

kwenye kikao siku ya kiama ni yule mwenye tabia njema.” (Kitabu cha Tirmidhy.)

Maadili yana nafasi yake kubwa sana ndani ya uisilamu, kwani ni kiini cha dini na

johari yake. Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na amani zimshukie juu yake)

alipoulizwa: “ dini ni nini? akasema: “tabia njema” (Imepokewa na Muslim.)

Si hivyo tu bali pia Mtume wa Mwenyezi Mungu amezipa tabia umuhimu wa hali

ya juu pale alipotangaza kwa kusema kuwa, lengo kuu la kutumwa kwake na la

ujumbe wake ni kutimiza maadili mema akasema: “ hakika nimetumwa kwa ajili

ya kutimiza tabia njema.” (Imam Buhkari.)

Na hata kabla utume watu walikuwa wakimuita mkweli muaminifu. Hizo ndizo

tabia njema za kiisilamu ambazo zinakwenda sambamba na imani ya ukweli,

kwani Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na amani zimshukie juu yake)

alikuwa ni mfano wa hali ya juu kabisa wa tabia njema, kwa ajili hiyo Mwenyezi

Mungu Mtukufu Mola wake akamsifu kwa kusema {Na hakika wewe una tabia

tukufu} Al qalam 5.

Na huu ni ushahidi mkubwa sana kutoka kwa Mkuu Alietukuka kwa Mtume wake

(Rehma na amani zimshukie juu yake), kwa uzuri wa tabia yake na wema wa

maadili yake. Hakika ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na amani

zimshukie juu yake) alikuwa ni mwenye tabia njema kuzidia wote, kwani tabia ya

Kurani yote aliikusanya yeye na akawa anaifuatisha na kujiepusha na makatazo

yake, hapo ubaora ndipo ulipojikusanya na haya yanathibitishwa na mama wa

waumini Aisha (Mwenyezi Mungu amwie radhi), alipoulizwa kuhusu tabia ya

Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na amani zimshukie juu yake) akasema: “

tabia yake ilikuwa ni Kurani.”

Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuwa ni mfano wa kimatendo katika kuifuata

Kurani, alikuwa ni mwenye tabia bora zaidi kuliko watu wote, na pia alikuwa na

upendo, huruma, ucheshi, msamaha kuzidi wote, mkweli anapozungumza,

anapotoa ahadi, na mkarimu kwenye familia, na ni mfano katika unyenyekuvu

pamoja ya kuwa yeye ni bwana wa viumbe, amuonae ni lazima amtukuze,

ukiungana nae basi utampenda.

Mama wa waumini Khadija (Mwenyezi Mungu amwie radhi), amemtakasa Mtume

wa Mwenyezi Mungu kwa kumwambia: “ hakika wewe utaunga koo, utavumilia

vishindo, utampata asiyekuwepo na utakuwa ni mwenye kuwarudisha watu katika

haki.”

Na Mola wake pia akamsifu kwa kusema {Basi ni kwa sababu ya rehema itokayo

kwa Mwenyezi Mungu ndio umekuwa laini kwao. Na lau ungeli kuwa mkali,

mwenye moyo mgumu, bila ya shaka wangeli kukimbia. Basi wasamehe, na

waombee maghfira, na shauriana nao katika mambo. Na ukisha kata shauri basi

mtegemee Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanao

mtegemea} Al imraan 26:. Na kwa tabia hii basi Mtume wa Mwenyezi Mungu

(Rehma na amani zimshukie juu yake) ameweza kuathiri nyoyo na akili.

Mtume (Rehma na amani zimshukie juu yake) aliwalea masahaba zake katika tabia

njema na kuwaamrisha kujipamba nayo na kuishikilia, na haya ni kama alivyosema

kumambia Abi Dhari (Mwenyezi Mungu amwie radhi), “ mche Mwenyezi Mungu

popote ulipo na fuatishia jema kwa baya ili ulifute, na ishi na watu kwa tabia

njema.” Wakajifunza upole, msahama na hisani na kujiepusha na maasi na hasira

wakawa ni wema na wavumilivu, wakawa pia ni mfano wa hali ya juu katika tabia

na muamala na ukarimu sawa kwa mtu mmoja mmoja au kwa pamoja.

Mtume wa Mwenyezi Mungu alipohama kutoka Makka kwennda Madina na

kuwaunganisha undugu kati ya muhajirina na Maanswari, Ansari alikuwa

akimuunga mkono ndugu yake muhajirina kwa nusu ya mali yake, kwani tabia ya

mwanadamu hujulikana kwa kadir ya utoaji wake, na kurani metupa mfano mzuri

ambao haukusudii kumlenga mtu maalumu, isipokuwa ni sifa kwa waumini wote,

Mwenyezi Mungu anasema {bali wanawapendelea kuliko nafsi zao ingawa

wenyewe ni wahitaji} Al hashri :.

Kwa ajili ya tabia hizo umma ukaongoza, ukawa unaangaliwa kuwani igezo kwa

kule kushikamana na tabia njema iliyotukuka. Na watu walikuwa wakiingia katika

dini ya Mwenyezi Mungu kwa makundi kwa kuona tabia na muamala mzuri, na

maadili mema. Ama wakati tabia zilipoanza kubadilika na maadili ya watu kuanza

kupotea; kigezo chema kikatoweka na ufahamu ukabadilika, hakika amesema

kweli imamu Malik (Mwenyezi Mungu amwie radhi), aliposema “Umma huu wa

mwisho hautopata kuwa mzuri isipokuwa kwa kufuata umma wa mwanzo.”

Maadili ni kitu bora ambayo jamii kujikinga na upotovu, na kuihifadhi na

misukosuko na kupotea, amani ya umma na nguvu za ujenzi wake na kuimarika

nafasi yake ipo katika maadili mema. Na kama ilivyo kuwa kuenea kwa uchafu na

maovu ni kwa sababu ya kujiweka mbali na maadili mema na vitendo vizuri.

“Tengeneza tabia yako kwa matendo mazuri * ijenge nafsi yako kwa maadili ili

isiyumbe.

Ipe nafsi ubora naa fya njema * kwani nafsi kwa maovu huwa duni.

Kwa ajili hiyo, kuwa na hadhari juu ya kuporomoka kwa maadili ni jambo la

kusisitizwa. Kutoka kwa Sahli bin Saa`d Saa`idi (Mwenyezi Mungu amwie radhi),

kwamba yeye amemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na amani

zimshukie juu yake) akisema: “ Hakika ya Mwenyezi Mungu ni Mkarimuna

anawapenda wakarimu na hupenda tabia njema na huchukia mambo machafu.”

Maadili hulifanya taifa kukua na athari zake hubakia milele, na kwa kutokuwa na

maadili mema taifa husambaratika na huanguka. Ni Staarabu ngapi zimeporomoka

na si kwa sababu ya hali mbaya ya kiuchumi au nguvu zake za kijeshi lakini ni

kwa sababu ya kuwa na maadili maovu. Mwenyezi Mungu amrehemu kiongozi wa

mashairi. Aliposema:

Hakika umma utabakia kwa kubaki maadili * wakikosa maadili basi na umma

hutoweka.

Na ukizingatia ibada ndani ya kurani na hadithi za Mtume tutagundua kuwa

malengo hasa makuu ni: kuijenga tbia njema ya muisilamu na kumpamba kwa

maadili, hakuna ibada ambayo Mwenyezi Mungu ameiamrisha mfano; sala,

saumu, zaka, na kuhiji isipokuwa ina athari ambayo inaonekana ndani ya tabia ya

mtu, si hivyo tu, bali tabia hii huathiri mtu hadi jamii kwa ujumla. Uisilamu si

kufanya ibada zisizo na natija ndani ya msikiti ambazo hazina mfungamano na

maisha ya nje (ya msikiti), ikawa aliyesali baada ya sala atoke kisha afanye ghoshi,

adanganye, amuudhi jirani yake, si hivyo. Lakini ibada zimeletwa kwenye dini

zote ili mwanadamu awe na utu na tabia iwe njema. Kwa mfano sala, Mwenyezi

Mungu ametuwekea wazi hekima yakusaliwa. Akasema {Soma ulivyofunuliwa

katika kitabu, na ushike sala. Hakika sala inazuilia mambo machafu na maovu. Na

kwa yakini kumdhukuru Mwenyezi Mungu ndio jambo kubwa kabisa. Na

Mwenyezi Mungu anayajua mnayoyatenda.} Al ankabuut 56. kujiepusha na maovu

na kujitakasa na kauli chafu na matendo mabaya hivi ndivyo sala itakiwavyo.

Kutoka kwa Ibn Abass (Mwenyezi Mungu awawie radhi), amesema: Mtume wa

Mwenyezi Mungu (Rehma na amani zimshukie juu yake) amesema: “amesema

Mwenyezi Mungu Mtukufu: hakika ninaikubali sala kwa anaenyenyeyekea kwa

utukufu wangu, na akawa hajitukuzi mbele ya waja wangu, na wala haendelei

kuniasi, na akawa naumaliza mchana wake kwa kunitaja, na kuwahurumia

masikini, na wapiti njia na wajane, na kuwahurumia wenye matatizo..”

(Imepokewa na Bazaz.)

Na kutoka kwa Ib Masu`ud (Mwenyezi Mungu amwie radhi): “ Yule ambaye sala

yake haimuamrishi kutenda mema na wala haimkatazi kuacha mabaya

hatozidishiwa kwa Mwenyezi Mungu isipouwa kutengwa mbali.” (Imepokewa na

Twabari). Basi yule ambaye sala yake haimuweki mbali na maovu sawa iwe ya

maneno au matendo, mtu huyu basi sala yake itakuwa haimfikishi katika lengo

miongoni mwa malengo makubwa ya sala.

Na namna hiyo hiyo kwa upande wa utoaji wa zaka, kufunga, kuhiji na kwa

upande wa ibada nyengine, utaona kuwa zimewekwa kwa kuitakasa nafsi na

kumfanya mja atukuke kimaadili, na Mwenyezi Mungu anasema khusu zaka:

{Chukua sadaka katika mali zao, uwasafishe na uwatakase kwazo, na uwaombee

rehema. Hakika maombi yako ni utulivu kwao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye

kusikia Mwenye kujua.} Al taubah 214.

Hivyo basi Mtume wa Mwenyezi Mungu akalipambanua zaidi neno sadaka

ambayo ni inampasa muisilamu kuitoa, imepokewa kwa Abi Dhari (Mwenyezi

Mungu amwie radhi) amesema, amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (Rehma

na amani zimshukie juu yake) “kutabasamu mbele ya uso a mwenzako ni sadaka,

na kuiweka tupu ndoo yako na kuijaza ya mwenzako ni sadaka, kuamrisha mema

na kukataza mabaya pia huandikiwa sadaka, kuondoa mwiba na jiwe njiani ni

sadaka, kumuongoza aliyepotea njia pia ni sadaka.” (Imepokewa na Bazaz).

Na swaumu ni ibada miongoni mwa ibada alizozifaradhisha Mwenyezi Mungu

kwa ajili ya kufanikisha uchamungu, matunda na malengo ambayo Mwenyezi

Mungu anayataka yafikiwe na mja ni uchaji Mungu, akasema Mwenyezi Mungu

Mtukufu: {Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyo andikiwa walio

kuwa kabla yenu ili mpate kuchamngu} Albaqara 294.

Kwa kupitia funga utashi wa muumini huwa na nguvu na anakuwa na uwezo wa

kuidhibiti nafsi yake na matamanio yake, kwani imepokewa kutoka kwa Abi

Hurayra (Mwenyezi Mungu amwie radhi), hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu

amesema: “ Funga ni kinga, basi asisema maneno mabaya wala kutenda mabaya,

na iwapo mtu amempiga au kumtusi basin a aseme; mimi nimefunga.”

(Imepokewa na Bukhari). Hii inamaanisha kuwa funga yake inabidi imlinde na

kuwa na tabia chafu na matendo maovu, funga ni lazima iache athari za tabia

njema kwa muisilamu na katika maadili yake.

Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Hija ni miezi maalumu. Na anaye kusudia

kufanya Hija katika miezi hiyo, basi asiseme maneno machafu wala asifanye

vitendo vichafu wala asibishane katika Hija. Na kheri yoyote mnayo ifanya

Mwenyezi Mungu anaijua. Na jitengezeeni zawadi. Na hakika bora ya zawadi ni

uchamngu. Na nicheni Mimi, enyi wenye akili!} Albaqara 2:8. Na kutoka kwa Abi

Hurayra (Mwenyezi Mungu amwie radhi), amesema: amesema mjumbe wa

Mwenyezi Mungu (Rehma na amani zimshukie juu yake): “ atakaeijia nyumba hii

akawa hajanena upuuzi, na wala kufanya uchafu basi atakuwa amerejea kama

kwamba amezaliwa na mama yake”. (Imepokewa na Muslim.)

Kwa upande wa ibada ni lazima iache athari njema kwa mtu na kwa jamii, na

iwapo ibada hazitoleta athari yoyote kwa mtu na maadili yake na nyenendo zake

huwa haina thamani yoyote siku ya kiyama, kwa sababu matendo maovu hula zile

ibada na mema kama ambavyo moto unavyokula kuni. Imepokewa na Abi Hurayra

(Mwenyezi Mungu amwie radhi), Kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma

na amani zimshukie juu yake) amesema: “ Munamjua ni nani muflisi? Wakamjibu,

mtu aliyefilisika miongoni mwetu ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni yule asiye

na dirhamu wala starehe, akasema (Rehma na amani zimshukie juu yake) “ Mtu

aliyefilisika katika umma wangu ni yule atakaekuja siku ya kiama na sala zake,

funga zake, na zaka zake, na atakuja hali ya kuwa kamtukana huyu, kamzulia

huyu, amekula mali ya huyu na kumwaga damu ya huyu na amempiga huyu,

atakaa na kupunguzwa katika mema yake, n kwa huyu yatachukuliwa mema yake,

na yatakapomalizika mema yake, kabla ya kumaliza kuhesabiwa huchukuliwa

madhambi yao na kupewa yeye kisha hutumbukizwa motoni.” (Imepokewa na

Tirmidhy.)

Na alipoulizwa (Rehma na amani zimshukie juu yake) ewe mjumbe wa Mwenyezi

Mungu; “ hakika ya fulani hutajwa kwa kuwa anasali sana, anafunga sana, na

anatoa sadaka sana isipokuwa anawakera majirani zake kwa ulimi wake, akasema;

“yeye ataingia motoni”. Akasema: “ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika ya

fulani hutajwa kuwa ni mchache wa kufunga, na sadaka zake, na sala zake naye

hutoa sadaka kwa, isipokuwa hawakeri majirani zake kwa ulimi wake; akasema

“yeye ataingia peponi.” (Imepokewa na Ahmad).

Hakika tabia njema (maadili mema) inakusanya kwa viumbe vyote, hakuna tafauti

kati ya muisilamu na asiye muisilamu, wote ni ndugu kwa ubinaadamu, Mwenyezi

Mungu Mtukufu anasema {Na hakika tumewatukuza wanaadamu, na tumewapa

vya kupanda nchi kavu na baharini, na tumewaruzuku vitu vizuri vizuri, na

tumewafadhilisha kwa fadhila kubwa kuliko wengi miongoni mwa tulio waumba}

Israa 81.

Na Mtume wa Mwenyezi Mungu aliposimama lilipopitishwa, akaambiwa: ni

jeneza la Myahudi, mtume (Rehma na amani zimshukie juu yake) “je kwani si

nafsi? (imepokewa na Bukhari).

Na Mwenyezi Mungu {wala msijadiliane na watu wa Kitabu ila kwa njia iliyo

nzuri kabisa, isipokuwa wale walio dhulumu miongoni mwao. Na semeni:

Tumeyaamini yaliyo teremshwa kwetu na yaliyo teremshwa kwenu. Na Mungu

wetu na Mungu wenu ni Mmoja. Na sisi ni wenye kusilimu kwake.} Al ankabuut

57. Na kutoka kwa Mujahid, kwamba Abdallah bin Amru (Mwenyezi Mungu

amwie radhi), amechinjiwa mbuzi na familia yake, alipofika akasema: je

mumempa jirani yetu myahudi? Je mumempa jirani yetu myahudi? Nimemsikia

Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na amani zimshukie juu yake) akisema: “

Jibrilu hakuacha kuniusia kuhusu jirani mpaka nikadhani kuwa anaweza kumrithi”

(Imepokewa na Tirmidhy.)

Na tabia njema si kwa wanaadamu tu pekee, isipokuwa inakusanya hata wanyama

pia, kwani Mwenyezi Mungu amemuingiza kijana peponi kwa sababu ya mbwa

aliyemyweshelezea maji. Kutoka kwa Abi Hurayra (Mwenyezi Mungu amwie

radhi), “hakika ya kijana alimuona mbwa anakula mchanga kutokana na kiu, kijana

akachukua khofu yake akawa anamchotea kwayo maji mpaka akamywesha,

akamshukuru Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu akamuingiza peponi”

(Imepokewa na Bukhari). Na namna kama hiyo Mwenyezi Mungu amemuingiza

mtu motoni kwa sababu ya paka, imepokewa na Ibn Umar (Mwenyezi Mungu

awawie radhi), hakika ya Mwenyezi Mungu amesema “mwanamke ameadhibiwa

kwa sababu ya paka amemfunga na wala hakumuacha huru akila masalia ya

ardhini.” (Imepokewa na Bukhari).

Iwapo tunataka kujiimarisha kitabia na kuinuka kwa jamii yetu hatuna budi kufuata

vigezo vyema. Vigezo ni kitendea kazi muhimu katika kujenga maadili, Mwenyezi

Mungu anasema {Hakika nyinyi mnayo ruwaza njema kwa Mtume wa Mwenyezi

Mungu kwa anaye mtaraji Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na

akamkumbuka Mwenyezi Mungu sana } Al Ahzab 32. Kwani mzazi anatakiwa

kuwa ni kigezo kwa mwanawe, na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na amani

zimshukie juu yake) ametueleza kwamba ya mtoto huzaliwa katika maubile safi,

maumbile ya Mwenyezi Mungu aliyowaumbia watu, kisha tena kigezo ndicho

kitakachombadilisha ima kizuri au kibaya. Kutoka kwa Abi Hurayra (Mwenyezi

Mungu amwie radhi), amesema, amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu (Rehma

na amani zimshukie juu yake) “ hakuna kizaliwacho isipokuwa huzaliwa katika

maumbile (uisilamu), ima baba yake humfanya kuwa myahudi, au mnasara au

mmajusi...” Kisha akaendelea kusema Abu Hurayra (Mwenyezi Mungu amwie

radhi), {Basi uelekee uso wako sawasawa kwenye dini – ndilo umbile la

Mwenyezi Mungu alilowaumbia watu. Hapana mabadiliko katika uumbaji wa

Mwenyezi Mungu. Hiyo ndiyo dini iliyoonyoka sawa.} Ruum 41. (Imepokewa na

Bukhari).

Vile vile mwalimu ni kigezo kwa wanafunzi kwa mwenendo wake na tabia zake,

wanafunzi inabidi wawe kama yeye kitabia. Siku moja imam Shafii ameingia kwa

Harun Rashid pamoja na kijana Siraj, akawakaribisha na kuwaambia wakae kitako

mbele ya Abdul-swamad ambae ni mwalimu wa watoto wa Rashid. Siraj akasema

kumwambia Shafii: ewe Abu Abdallah! Hawa ni watoto wa Amir Muuminina,

naye ni wanafunzi wake, unaonaje lau kama ungeliwausia.. Imam Shafii

akamwelekea Abi Abdul-swamad akamwambia, “iwe kwako ewe kiongozi wa

waumini ukitaka kuwarekebisha wanao ni itakubidi kuirekebisha nafsi yako

kwanza, kwani macho yao yanaangalia macho yako, zuri kwao ni lile

utakalolipenda wewe, na baya kwao ni lile uliachalo…” (Kitabu cha Hilliya

Awliyaa. Abi Na`im).

Na jambo lililo muhimu kukumbushia ni kwamba, tabia za mtu binafsi ambazo

hujilazimisha kuacha na kujikataza na kitu, n.k. na kuna tabia za kifamilia kati ya

mtu na mkewe na kati ya mtu na wanawe na wazazi wake na watu wa karibu nae

na ukoo wake na mfano wake. Pia kuna tabia za kijamii kwa mfano katika kuuza,

kununua, ujirani, urafiki, kazini, … n.k. na pia kuna tabia za kimataifa kati ya nchi

na nchi, na tabia za wakati wa vita na wakati wa usalama.

Na katika mambo ambayo humsaidia mja katika kuwa na tabia njema ni: kufanya

kitu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kisha kuomba awe na tabia njema, na pia

kujitahidi ndani ya nafsi yake ili ashinde matamanio, na kuihesabu nafsi kila siku

pamoja na kuzingatia mwisho wa kuwa na tabia mbaya na kwa yaliyowafika watu

walioishi kwenye jamii mbaya.

Miongoni mwa aliyokirimiwa Mtume Muhammad

(Saw)

1 Rabiul awwal, 0341 H. Sawa na 01 Disemba 6102 A.D.

Kwanza: Vipengele

1. Kukirimiwa kwake Mtume Muhammad (Saw) tangu mwanzo wa

kuumbwa.

2. Kukirimiwa kwake Mtume Muhammad (Saw) kabla ya kuzaliwa.

3. Kukirimiwa kwake Mtume Muhammad (Saw) kwa kuwemo katika na

familia njema.

4. Kutajwa jina lake Mtume Muhammad (Saw) kunaendana sambamba

na utukufu wa utume na ubora wa risala.

5. Wajibu wa kumpenda na kumtii Mtume Muhammad (Saw).

6. Kukirimiwa kwake Mtume Muhammad (Saw) kwa kupata ulinzi

utokao kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.

7. Ujumbe wake ni kwa walimwengu wote.

8. Ujumbe wake ni rehem kwa walimwengu wote.

Pili: Dalili

Dalili ndani ya Kurani Tukufu

1. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Na pale Mwenyezi Mungu alipo

chukua ahadi kwa Manabii: Nikisha kupeni Kitabu na hikima, kisha

akakujieni Mtume mwenye kusadikisha mliyo nayo, ni juu yenu mumuamini

na mumsaidie. Akasema: Je, mmekiri na mmekubali kushika agizo langu juu

ya hayo? Wakasema: Tumekubali. Akasema: Basi shuhudieni, na Mimi ni

pamoja nanyi katika kushuhudia.} (Al Imraan aya ya 81).

2. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: { Ewe Mola Mlezi wetu! Waletee

Mtume anaye tokana na wao, awasomee Aya zako, na awafundishe Kitabu

na hikima na awatakase. Hakika Wewe ndiye Mwenye nguvu, Mwenye

hikima.} Albaqarah aya 129.

3. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: { Na Isa bin Mariamu alipo sema: Enyi

Wana wa Israili! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu,

ninaye thibitisha yaliyo kuwa kabla yangu katika Taurati, na mwenye

kubashiria kuja Mtume atakaye kuja baada yangu; jina lake ni Ahmad!

Lakini alipo waletea hoja zilizo wazi, walisema: Huu ni uchawi ulio

dhaahiri! } Assa`f aya 2.

4. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Mwenye kumt'ii Mtume basi ndio

amemt'ii Mwenyezi Mungu. Na anaye kengeuka, basi Sisi hatukukutuma

wewe uwe ni mlinzi wao } Al nisaa aya 11.

5. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: { Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda

Mwenyezi Mungu basi nifuateni mimi, Mwenyezi Mungu atakupendeni na

atakufutieni madhambi yenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta

madhambi na Mwenye kurehemu.} Al Imraa aya 31.

6. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Ewe Mtume! Fikisha uliyo

teremshiwa kutoka kwa Mola wako Mlezi. Na ikiwa hukufanya hayo basi

hukufikisha ujumbe wake. Na Mwenyezi Mungu atakulinda na watu. Hakika

Mwenyezi Mungu hawaongoi watu makafiri} Al maidah aya 21.

7. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Na hatukukutuma ila kwa watu

wote, uwe mbashiri, na mwonyaji. Lakini watu wengi hawajui } Sabaa 61.

8. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Nasi hatukukutuma ila uwe ni

Rehema kwa walimwengu wote} Al anbiyaa aya011.

9. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika

wake wanamsalia Nabii. Enyi mlio amini! Msalieni na mumsalimu kwa

salamu } Al ahzaab 22.

11. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Msifanye wito wa Mtume baina yenu

kama wito wa nyinyi kwa nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu anawajua

miongoni mwenu wanao ondoka kwa uficho. Basi nawatahadhari wanao

khalifu amri yake, usije ukawapata msiba au ikawapata adhabu chungu} Al

nuur aya 24.

Dalili ndani ya hadithi

1. Kutoka kwa Waathila bin Asqa`a (Mwenyezi Mungu amwie radhi)

amesema: nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu akisema: “ hakika ya

Mwenyezi Mungu amechagua Kabila la Kinana kutoka katika kizazi cha

Ismaili, na akawachagua Maquraishi kuwa ndio kutoka kwa Kabila la

Kinana, na katika maquraishi ukachagulia ukoo wa bani Hashim, na katika

ukoo wa bani hashim akanichaguwa mimi”. (Imepokewa na Muslim).

6. Kutoka kwa Irbaadh bin Saariya Salamiy amesema: nimemsikia Mtume

wa Mwenyezi Mungu akisema: “ … mimi ni kutokana na maombi ya baba

yangu Ibrahim, na bishara ya Isa kwa watu wake, na nikutokana na ndoto

ya mama yangu ambaye ameona nuru imechomoza na kuangaza

majumba ya Sham.” (Kitabu cha Imam Ahmad).

4. Kutoka kwa Abi Saaed (Mwenyezi Mungu amwie radhi), kutoka kwa

Mtume (Saw) kwamba yeye amesema: “Jibrilu alinijia akaniambia: hakiak

mola wako na mola wangu anasema: Ni namna gani nimenyanyua utajo

wako? Mtume akajibu: Mwenyezi Mungu ndie ajuae: Jibrilu akasema:

nitajwapo mimi nawe hutajwa pamoja nami”) (Kitabu cha Zawaed cha

Imam Haytham).

4. Kutoka kwa Abi Hurayra (Mwenyezi Mungu amwie radhi) amesema,

hakika mjumbe wa Mwenyezi Mungu amesema “yeyote atakaenitii mimi

basi kwa hakika amemtii Mwenyezi Mungu, na atakaeniasi basi kwa

hakika amemuasi Mwenyezi Mungu” (Imepokewa na Muslim na

Bukhari).

5. Kutoka kwa Anas (Mwenyezi Mungu amwie radhi) amesema, amesema

mjumbe wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani zimshukie) “hatoamini

mmoja wenu mpaka niwe ananipenda zaidi kuliko wazazi wake watoto

wake na watu wote.” (Imepokewa na Muslim na Bukhari).

6. Kutoka kwa Abi Hurayra (Mwenyezi Mungu amwie radhi) amesema,

amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani zimshukie),

“hakika mimi ni rehema yenye kuongoa” (Imepokewa na Imam Hakim

katika kitabu cha Mustadrik).

1. Kutoka kwa Jabir bin Abdi Llah (Mwenyezi Mungu awawie radhi

amesema: amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani

zimshukie): “ nimepewa mambo matano hakuna nabii yeyote aliyepewa

kabla yangu: nimepewa ushindi wa kuwahofisha maadui kwa mwendo wa

mwezi, nikafanyiwa ardhi kuwa ni msikiti na ipo safi na mtu yeyote katika

umma wangu akifikwa na swala basi na aswali, na nimehalalishiwa

ngawira, na ilikuwa nabii akipelekwa (akitumwa) kwa watu wake

maalumu, ama mimi nimetumwa kwa watu wote, na nimepewa uombezi.

((Imepokewa na Bukhari).

Tatu: Maudhui

Hakika Mwenyezi Mungu amemkirimu mtume wake, ukarimu ambao

hajawahi kumpa yeyote katika waja wake, mwanzo wa kuumbwa kwake

(rehma na mani ziwe juu yake), kabla ya kuzaliwa kwake (rehma na amani

ziwe juu yake), baada ya kuzaliwa kwake (rehma na amani ziwe juu yake),

dani ya maisha yake na baada ya kufariki kwake (rehma na amani ziwe juu

yake).

Ama ukarimu aliokirimiwa na Mwenyezi Mungu mwanzo wa kuumbwa ni;

Mwenyezi Mungu ameuinua utajo wake kwa waliotangulia (umma wa

mwanzo) na waliochelewa (umma wa mwisho), kwani hakuna Mtume yeyote

aliyetumwa na Mwenyezi Mungu – kabla yake (rehma na amani ziwe juu

yake) isipokuwa amechukua ahadi na utiifu iwapo atakutana na Mtume

rehma na amani ziwe juu yake) basi atamuamini na kumnusuru, Mwenyezi

Mungu mtukufu anasema: {Na pale Mwenyezi Mungu alipo chukua ahadi

kwa Manabii: Nikisha kupeni Kitabu na hikima, kisha akakujieni Mtume

mwenye kusadikisha mliyo nayo, ni juu yenu mumuamini na mumsaidie.

Akasema: Je, mmekiri na mmekubali kushika agizo langu juu ya hayo?

Wakasema: Tumekubali. Akasema: Basi shuhudieni, na Mimi ni pamoja nanyi

katika kushuhudia} (Al imraan aya 81). Mwenyezi Mungu Mtukufu

akamzidishia Mtume wake rehma na amani ziwe juu yake) ubora na heshima

kwa ahadi hii ambayo imeshuhudiwa na Mitume wengine pia.

Na mitume waliotangulia pia walimbashiria, kutoka kwa Irbaadh bin sariyata

Salamiy amesema: nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu akisema: “mimi

ni kutokana na maombi ya baba yangu Ibrahim, na bishara ya Issa kwa watu

wake, na nikutokana na ndoto ya mama yangu ambaye ameona nuru

imechomoza na kuangaza majumba ya Sham.” (Kitabu cha Imam Ahmad).

Na maombi ya sayidna Ibrahim (A.S) ni pale aliposema { Ewe Mola Mlezi

wetu! Waletee Mtume anaye tokana na wao, awasomee Aya zako, na

awafundishe Kitabu na hikima na awatakase. Hakika Wewe ndiye Mwenye

nguvu, Mwenye hikima.} Albaqara 061. Ama bishara ya sayidna Isa (A.S) ni

pale aliposema Mwenyezi Mungu { Na Isa bin Mariamu alipo sema: Enyi

Wana wa Israili! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu, ninaye

thibitisha yaliyo kuwa kabla yangu katika Taurati, na mwenye kubashiria kuja

Mtume atakaye kuja baada yangu; jina lake ni Ahmad! Lakini alipo waletea

hoja zilizo wazi, walisema: Huu ni uchawi ulio dhaahiri} Assa`f 6).

Na kuhusu kukirimiwa kwake Mtume Muhammad (rehma na amani ziwe juu

yake) na Mwenyezi Mungu kabla ya kuzaliwa kwake, ni kule kuitwa

Muhammad. Amina bint Wahab alipokuwa akielezea namna alivyomzaa

Mtume (rehma na amani ziwe juu yake). Nimewasikia waliokuwa

wakimbwambia; “ wewe umebeba mamba ya bwana wa umma huu,

utakapomzaa tu basi sema: ninamrudisha kwa aliye Mmoja na aepukane na

kila shari ya mwenye husuda, kisha umpe jina la Muhammad, kwani jina lake

ndani ya kitabu cha Taurati ni Ahmad, atashukuriwa na wakazi wa ardhini na

wa mbinguni. Na jina lake ndani ya kitabu cha Injili ni Ahmad atashukuriwa

na wakazi wa ardhini na wa mbinguni.. na jina lake ndani ya Kurani ni

Muhamad basi umwite kwa jina hilo. (Imam Bayhaqiy).

Hivyo basi, ukoo wake katika koo njema zaidi ya koo nyengine, kwani yeye

rehma na amani ziwe juu yake) ni katika kizazi cha familia iliyo bora zaidi,

imesemwa hayo na Mwenyezi Mungu { Na mageuko yako kati ya wanao

sujudu } Ashuaraa aya 601, amesema Ibn Abbas, kinachokusudiwa ni katika

migongo ya mababu, Sayidna Adam (A.S), Sayidna Nuh (A.S) na Sayidna

Ibrahim (A.S) mpaka akazaliwa mtume wetu rehma na amani ziwe juu yake).

(Tafsiri Ibn kathir).

Familia yake ni bora, na ni nyumba njema katika nyumba za waarabu, kwani

Mwenyezi Mungu ameihifadhi na maovu ya kijahilia, na akamtoa katika

migongo mitukufu mpaka kwenye tumbo jema kutoka kizazi hadi kizazi.

Mwenyezi Mungu amechagua Kabila la Kinana kutoka katika kizazi cha

Ismaili, na akawachagua Maquraishi kuwa ndio kutoka Kinana, na katika

maquraishi ukachaguliwa ukoo wa bani Hashim, naye Mtume (rehma na

amani ziwe juu yake) ni katika uchaguzi ulio bora na mwema. Imepokewa na

Waathila bin Asqa`a (Mwenyezi Mungu amwie radhi) amesema: nimemsikia

Mtume wa Mwenyezi Mungu akisema: “ hakika ya Mwenyezi Mungu

amechagua Kabila la Kinana kutoka katika kizazi cha Ismaili, na akawachagua

Maquraishi kuwa ndio kutoka Kinana, na katika maquraishi ukachagulia ukoo

wa bani Hashim, na katika ukoo wa bani hashim akanichaguwa mimi”.

(Imepokewa na Muslim).

Ama kukirimiwa kwake na Mwenyezi Mungu katika maisha yake rehma na

amani ziwe juu yake). Jina na utajo wake umenyayuliwa duniani na akhera,

kwani jina la Mwenyezi Mungu huwa halitajwi isipokuwa na jina la Mtume

rehma na amani ziwe juu yake) hutajwa pamoja nae. Hakika amesema kweli

Mwenyezi Mungu: {tukaunyajua utajo wako}.

Kutoka kwa Abi Saaed (Mwenyezi Mungu amwie radhi), kutoka kwa Mtume

(Saw) kwamba yeye amesema: “Jibrilu alinijia akaniambia: hakika mola wako

na mola wangu anasema: Ni namna gani nimenyanyua utajo wako? Mtume

akajibu: Mwenyezi Mungu ndie ajuae: Jibrilu akasema: nitajwapo mimi nawe

hutajwa pamoja nami”) (Kitabu cha Zawaed cha Imam Haytham).

Na Mwenyezi Mungu ameliweka pamoja jina lake na jina la Mtume wake

rehma na amani ziwe juu yake) katika sehemu nyingi, kwani hata shahada ya

anaesilimu huwa haikubaliwi mpaka amshuhudie kuwa yeye ni mjumbe

mtume na upweke wa Mwenyezi Mungu.

Amesema Hassan bin Thabit (Mwenyezi Mungu amwie radhi):

Jina la Mwenyezi Mungu lipo na la mtume * pindi Muadhini akisoma adhana.

Hutaja jina hilo kwa utukufu * kwenye arshi ni Mahmud na huyu hapa ni

Ahmad.

Jina la Mtume (rehma na amani ziwe juu yake) hutajwa atajwapo Mwenyezi

Mungu kwenye shahada mbili, kwenye hutuba ya Ijumaa, ndani ya Kurani

Tukufu. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ameweka sambamba utiifu wa

mtume kua ndio utiifu wa Mwenyezi Mungu, akasema: {Mwenye kumt'ii

Mtume basi ndio amemt'ii Mwenyezi Mungu. Na anaye kengeuka, basi Sisi

hatukukutuma wewe uwe ni mlinzi wao} Al nisaa 11.

Ibnu Abbas (Mwenyezi Mungu awawie radhi) alikuwa akisema: Aya tatu

zimeteremshwa na kuambatana sambamba na aya tatu, hakuna aya hata

moja yenye kukubalika bila ya aya nyengine (iliyo sambamba nae).

Ya kwanza: { Na shikeni Sala, na toeni Zaka, na inameni pamoja na wanao

inama } Albaqarah 34.

Ya pili : { Nishukuru Mimi na wazazi wako} Luqman 14.

Ya tatu: {Enyi mlio amini! Mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume} Al

nisaa 59. kwani atakaemtii Mwenyezi Mungu na kuacha kumtii Mtume

(rehma na amani ziwe juu yake) mtu huyo haikubaliwi ibada yake.

Pia Mwenyezi Mungu ameweka sambamba uteuzi (uchaguzi) wa kumteua

mtume (rehma na amani ziwe juu yake) kuwa sana na kumteua Yeye

Mwenyezi Mungu. Amesema {Bila ya shaka wanao fungamana nawe, kwa

hakika wanafungamana na Mwenyezi Mungu.} Al fathi aya 01. a kufanya

kuwa, kumtii Mtume (rehma na amani ziwe juu yake) kuwa ni moja ya

mafanikio ya kuingia peponi, akasema { Na anaye mt'ii Mwenyezi Mungu na

Mtume wake, bila ya shaka amefanikiwa mafanikio makubwa.} Al ahzaab

aya 10. Na aya nyenginezo.

Na imekuja katika hadithi kutoka kwa Abi Hurayra (Mwenyezi Mungu amwie

radhi) hakika mjumbe wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani ziwe juu yake)

amesema: “ watu wote katika umma wangu wataingia peponi isipokuwa

atakaekataa”, akaulizwa: na ni nani atakaekataa ewe mjumbe wa Mwenyezi

Mungu? Akasema: “ atakaenitii mimi ndie atakaeingia peponi, na atakaeniasi

mimi huyo ndie aliyekataa.” ( imepokewa na Bukhari).

Na hadithi ya Umar (Mwenyezi Mungu amwie radhi), wakati alipoliendea

jiwe jeusi na kulibusu akasema: “hakika mimi ninaelewa wazi kuwa hili ni jiwe

halidhuru wala halinufaishi, na lau kama nisingelimuona Mtume anakubusu

basi nisingelikubusu”. (Imepokewa na Bukhari). Utiifu kwa Mwenyezi Mungu

hautokamilika katu isipokuwa kwa kumtii mtume wake (rehma na amani

ziwe juu yake).

Na vile vile katika kukirimiwa kwake Mtume (rehma na amani ziwe juu yake)

na Mwenyezi Mungu ni kufanywa mapenzi yake kuwa ni sehemu ya imani ya

kumuamini Mwenyezi Mungu, namapenzi a Mwenyezi Mungu ni mapenzi ya

Mtume wake (rehma na amani ziwe juu yake). Kumfuata Mtume (rehma na

amani ziwe juu yake) ni alama ya upendo kwake, Mwenyezi Mungu

amesema: { Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu basi nifuateni

mimi, Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakufutieni madhambi yenu. Na

Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta madhambi na Mwenye kurehemu. } Al

Imraan 31. Kumpenda mtume (rehma na amani ziwe juu yake) ni jambo la

lazima kwa kila muisilamu. Imekuja katika hadithi Kutoka kwa Anas

(Mwenyezi Mungu amwie radhi) amesema, amesema mjumbe wa Mwenyezi

Mungu (rehma na amani zimshukie) “hatoamini mmoja wenu mpaka niwe

ananipenda zaidi kuliko wazazi wake watoto wake na watu wote.”

(Imepokewa na Muslim na Bukhari).

Si hivyo tu, bali hata imani ya mja huwa ni pungufu ndani ya moyo wake

iwapo hatotanguliza mapenzi ya Mtume (rehma na amani ziwe juu yake)

zaidi ya nafsi yake, wazazi wake, na watu wote kwa ujumla.

Imepokewa na Abdallah Bin Hisham (Mwenyezi Mungu amwie radhi),

amesema: “ tulikuwa pamoja na Mtume (rehma na amani ziwe juu yake)naye

ameushika mkono wa Umar bin Khatwab akasema kumwambia Umar: ewe

mjumbe wa Mwenyezi Mungu hakika wewe ninakupenda sana isipokuwa

nafsi yangu ninaipenda zaidi, Mtume (rehma na amani ziwe juu yake)

akasema: “ hapana, naapa kwa yule ambae nafsi yangu ipo mikononi mwake

mpaka niwe unanipenda kuliko nafsi yako”. Umar kamwambia Mtume

(rehma na amani ziwe juu yake) “ hakika kuanzia hivi sasa na ninaapa kuwa

wewe ninakupenda zaidi kuliko nafsi yangu, Mtume (rehma na amani ziwe

juu yake) akamwambia: “ Hivi sasa ewe Umar.” (Imepokewa na Bukhari).

Na inatosha kwa ampendae Mtume (rehma na amani ziwe juu yake)

Kuwa na ubora na bahati ya kufufulia pamoja nae mpenzi wake Mtume

(rehma na amani ziwe juu yake) siku ya kiama, na nii ni fadhila kubwa sana na

ukarimu wa hali ya juu. Imepokewa na Anas Ibn Malik (rehma na amani ziwe

juu yake) amesema: “tulipokuwa mimi na Mtume (rehma na amani ziwe juu

yake) tunatoka msikitini tukakutana na mtu kwenye mlango wa msikitini,

akasema: ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu, kiama kitakuwa lini? Mtume

(rehma na amani ziwe juu yake) akasema “ je umejiandaa nacho? Kama

kwamba yule mtu alikuwa amejawa na unyenyekevu “kisha akasema: ewe

mjumbe wa Mwenyezi Mungu sikujiandaa kwa kufunga sana, wala kwa

swala, wala kwa sadaka lakini mimi ninampena mwenyezi mungu na Mtume

wake, akasema: ‘ wewe basi utakuwa na umpendae”. (Imepokewa na

Bukhari).

Na katika hali ya juu zaidi ya kukirimiwa Mtume (rehma na amani ziwe juu

yake) ni kuwa Mwenyezi Mungu anapomzungumzia huwa hamtaji jina lake

kikawaida kama anavyowataja mitume wengine wa kabla yake. Mitume

wengine walikuwa wakiitwa majina yao kikawaida tu, mfano kauli yake

Mwenyezi Mungu Mtukufu: { Na tulisema: Ewe Adam! Kaa wewe na mkeo

katika Bustani,} Al baqarah 42.

{Ewe Isa! Mimi nitakufisha, na nitakunyanyua kwangu,} Al Imraan aya 22.

{Ewe Nuhu! Shuka kwa salama itokayo kwetu } Hud aya 31.

{Ewe Musa! Hakika Mimi ni Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu

wote } Al qaswas 41.

{ Ewe Yahya! Kishike Kitabu kwa nguvu!} Maryam 06.

{ Basi alipo ufikia akaitwa: Ewe Musa! 12. Hakika Mimi ndiye Mola wako

Mlezi! Basi vua viatu vyako. Kwani upo katika bonde takatifu la T'uwa.} Taha

00-06.

{ Tulimwita: Ewe Ibrahim! 115. Umekwisha itimiliza ndoto. Hakika hivi ndivyo

tunavyo walipa wanao tenda mema. } Aswaafat 013-012.

{(Akaambiwa): Ewe Zakariya! Hakika Sisi tunakubashiria mwana; jina lake ni

Yahya. Hatujapata kumpa jina hilo yeyote kabla yake.} Maryam aya 1.

Lakini anapomzungumzia mtume wa mwisho (rehma na amani ziwe juu yake)

anamtaja kwa cheo chenye kujuulisha utukufu wake na nafasi yake na

ukubwa wa risala yake, Mwenyezi Mungu anasema {Ewe Nabii! Hakika Sisi

tumekutuma uwe shahidi na mbashiri na mwonyaji,} Al ahzaab 32.

Pia anasema {Ewe Mtume! Fikisha uliyo teremshiwa kutoka kwa Mola wako

Mlezi. Na ikiwa hukufanya hayo basi hukufikisha ujumbe wake. Na Mwenyezi

Mungu atakulinda na watu. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu

makafiri} Al maidah aya 21.

Si hivyo tu, bali pia Mwenyezi Mungu amewakataza wafuasi wa umma huu

kutomwita jina lake kikawaida kama walivyokuwa wakiita wafuasi wa umma

ziliizopita mitume yao. Na akaahidi kumpa adhabu kali atakaehalifu agizo

hili. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu { Msifanye wito wa Mtume baina

yenu kama wito wa nyinyi kwa nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu anawajua

miongoni mwenu wanao ondoka kwa uficho. Basi nawatahadhari wanao

khalifu amri yake, usije ukawapata msiba au ikawapata adhabu chungu. } Al

nuur aya 24.

Vile vile kukirimiwa kwa Mtume (rehma na amani ziwe juu yake) ni wajibu wa

kumfanya kuwa ni kigezo, Mwenyezi Mungu amesema { Hakika nyinyi mnayo

ruwaza njema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa anaye mtaraji

Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na akamkumbuka Mwenyezi Mungu

sana } Al ahzaab 60.

Aya hii ina umuhimu mkubwa sana kwani chimbuko la wajibu wa kumfuata

Mtume (rehma na amani ziwe juu yake) kimaneno, kivitendo na kihali, je,

tunamfuata na kuigiza kama alivyokuwa (rehma na amani ziwe juu yake).?

Na pia katika kukirimiwa kwake na Mwenyezi Mungu ni kuwa. Mwenyezi

Mungu Mtukufu amemtakia rehema ndani ya kitabu chake pia na malaika

wakamtakia rehema na kuwahimiza waumini nao wamswalie (wamuombee

rehma), Mwenyezi Mungu amesema { Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika

wake wanamsalia Nabii. Enyi mlio amini! Msalieni na mumsalimu kwa

salamu} Al ahzaab aya 22.

Na pia katika kukirimiwa kwake ni kwamba Mwenyezi Mungu mwenyewe

ndie aliyeshika jukumu la kumlinda (rehma na amani ziwe juu yake), tna

mitume wengine, wao ilikuwa wakituhumiwa kwa tuhuma sizo huwa

wanajitetea wenyewe, mfano nabii Nuh (A.S.), watu wake wamemtuhumu

kwa upotofu kama inavyosimulia Kurani Tukufu, inasema {Wale watukufu

katika kaumu yake wakasema: Hakika sisi tunakuona wewe umo katika

upotofu ulio dhaahiri.} Al aaraf 21. Naye anajitete mwenyewe kwa kusema

{Akasema: Enyi watu wangu! Mimi simo katika upotofu, lakini mimi ni

Mtume nitokaye kwa Mola Mlezi wa viumbe vyote. 62. Nakufikishieni

Ujumbe wa Mola Mlezi wangu, na ninakunasihini; na ninayajua kwa

Mwenyezi Mungu msiyo yajua nyinyi} Al aaraf 20-26.

Mfano mwengine nabii Hud (A.S.) watu wake walimtuhumu kwa uzembe na

wendawzimu na uongo walipomwambia {Wakasema watukufu wa wale walio

kufuru katika kaumu yake: Sisi tunakuona umo katika upumbavu, na hakika

sisi tunakufikiria kuwa wewe ni katika waongo} Al aaraf aya 22. Naye

anajitetea mwenyewe kwa kusema. {Akasema: Enyi watu wangu! Mimi sina

upumbavu. Lakini mimi ni Mtume niliye toka kwa Mola Mlezi wa viumbe

vyote. 68 Nakufikishieni ujumbe wa Mola wangu Mlezi. Na mimi kwenu ni

mwenye kukunasihini, muaminifu} Al aaraf 21-21.

Lakini kwa mtume wa mwisho (rehma na amani ziwe juu yake) kila

anaposingiziwa uongo na kumzushia uzushi Mwenyezi Mungu ndiye

anaesimama kumtetea, watu wake walimtuhumu kuwa yeye ni mshairi, {

Lakini wao walisema: Hizo ni ndoto za ovyo ovyo, bali amezizua tu, bali huyo

ni mtunga mashairi. Basi atuletee miujiza kama walivyo tumwa wale wa

mwanzo.} Al anbiya 2. Mwenyezi Mungu akawarudi kwa kusema { Wala

hatukumfundisha (Muhammad) mashairi, wala hayatakikani kwake hayo.

Haukuwa huu ila ni ukumbusho na Qur'ani inayo bainisha} Yasin 21.

Wakamwambia kuwa yeye ni kuhani, anayasema aambiayo na shetani…

Mwenyezi Mungu akawarudikwa kusema { Basi kumbusha! Kwani wewe, kwa

neema ya Mola wako Mlezi, si kuhani wala mwendawazimu.} Al Twuur 61.

Na Mwenyezi Mungu anaapa kiapo – na hakuna kiapo kikuba kkuliko cha

Mwenyezi Mungu - kwa ajili ya kumlinda mtume wake (rehma na amani ziwe

juu yake) na kuthibitisha ukweli wa wahyi na kurani na kuvunja hoja na

uzushi wao, Mwenyezi Mungu anasema { Basi naapa kwa mnavyo viona

41. Na msivyo viona, 31. Kwa hakika hii ni kauli iliyo letwa na Mjumbe

mwenye hishima. 30. Wala si kauli ya mtunga mashairi. Ni machache sana

mnayo yaamini. 36. Wala si kauli ya kuhani. Ni machache mnayo

yakumbuka. 34. Ni uteremsho utokao kwa Mola Mlezi wa walimwengu

wote.} Al haqah aya 41-34.

Baadhi ya nyakati walikuwa wakimwambia kuwa yeye ni mchawi. Mwenyezi

Mungu akawajibu { Basi ndio hivyo hivyo, hakuwajia kabla yao Mtume ila

walisema: Huyu ni mchawi au mwendawazimu.} Al dhariyaat 26. Na baadhi

ya nyakati walikuwa wakimwambia amerogwa, Mwenyezi Mungu akawajibu

aliposema { Au akaangushiwa khazina juu yake, au akawa na bustani ale

katika hiyo? Wakasema madhaalimu: Nyinyi hamumfuati ila mtu aliye rogwa

9. Tazama jinsi wanavyo kupigia mifano. Basi wamepotea, wala

hawataiweza Njia.} Al furqan 1-1.

Wakasema ni mwendawazimu, nae Mwenyezi Mungu akawarudi kwa

kusema {Au wanasema: Ana wazimu? Bali amewajia kwa Haki, na wengi wao

wanaichukia Haki.} Al muuminuun aya 11. Na kauli yake aliposema { Nuun.

Naapa kwa kalamu na yale wayaandikayo. 6. Kwa neema ya Mola wako

Mlezi wewe si mwendawazimu. 4. Na kwa hakika wewe una malipo yasiyo

katika. 3. Na hakika wewe una tabia tukufu.} Al qalam aya 0-3.

Wakamtuhumu kwa upotofu na kuchanganyikiwa , naye Mwenyezi Mungu

akawajibu, aliposema {0. Naapa kwa nyota inapo tua . 6. Mwenzenu huyu

hakupotea, wala hakukosea. 4. Wala hatamki kwa matamanio. 3. Hayakuwa

haya ila ni ufunuo ulio funuliwa.} An najm 0-3.

Si hivyo tu bali Mwenyezi Mungu amejitolea kumkinga na kumlinda juu ya

washirikina, akasema, {Ewe Mtume! Fikisha uliyo teremshiwa kutoka kwa

Mola wako Mlezi. Na ikiwa hukufanya hayo basi hukufikisha ujumbe wake.

Na Mwenyezi Mungu atakulinda na watu. Hakika Mwenyezi Mungu

hawaongoi watu makafiri.} Al maidah 21.

Na vile vile katika kukirimiwa kwa Mtume (rehma na amani ziwe juu yake)

kwa kule kupewa ujumbe kwa walimwengu wote na si kwa kizazi maalumu

au watu maalumu, ulinganio wake ni kwa watu wote. Kwani Mwenyezi

Mungu aliwatuma kila mtume kwa watu wake ama Mtume (rehma na amani

ziwe juu yake) yeye ni kwa watu wote. Kurani tukufu imeweka wazi jambo

hili, Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema { Na hatukukutuma ila kwa watu

wote, uwe mbashiri, na mwonyaji. Lakini watu wengi hawajui} Saba`a 61.

Na Kutoka kwa Jabir bin Abdi Llah (Mwenyezi Mungu awawie radhi

amesema: amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani

zimshukie): “ nimepewa mambo matano hakuna nabii yeyote aliyepewa

kabla yangu: nimepewa ushindi wa kuwahofisha maadui kwa mwendo wa

mwezi, nikafanyiwa ardhi kuwa ni msikiti na ipo safi na mtu yeyote katika

umma wangu akifikwa na swala basi na aswali, na nimehalalishiwa ngawira,

na ilikuwa nabii akipelekwa (akitumwa) kwa watu wake maalumu, ama mimi

nimetumwa kwa watu wote, na nimepewa uombezi. ((Imepokewa na

Bukhari).

Na miongoni mwa kukirimiwa ni kufadhilishwa kwake (rehma na amani ziwe

juu yake) na Mwenyezi Mungu zaidi ya mitume wengine, Mtume (rehma na

amani ziwe juu yake) amepewa ubora zaidi na hii ni kama ilivyoeleza Kurani

Tukufu { MITUME hao tumewatukuza baadhi yao juu ya wengineo. Katika

wao wapo ambao Mwenyezi Mungu alisema nao, na wengine

akawapandisha vyeo} Al baqara aya 624. Na kama walivyoeleza baadhi wa

wafasiri pale aliposema { Katika wao wapo ambao Mwenyezi Mungu alisema

nao, na wengine akawapandisha vyeo..} anaekusudiwa hapa ni mtume wetu

(rehma na amani ziwe juu yake), kwani yeye ndie mwenye vyeo vya juu, na ni

mwenye mwujiza wa kudumu nayo ni Kurani Tukufu na ni mwenye risala

iliyokusanya mambo yote mazuri yaliyotajwa katika umma zilizotangulia.

Na katika hadithi ambayo imepokewa na imam Muslim na Tirmidhy kutoka

kwa hadithi ya Abu Hurayra, kwamba Mtume (rehma na amani ziwe juu

yake) amesema, “ nimefadhilishwa zaidi ya mitume wengine kwa mambo

sita: nimepowa ufupisho wa maneno, nimenusuriwa kwa kuwapa hofu

maadui – na katika mapokezi ya ya Bukhari: nimpewa nusura ya

kuwaogopesha maadui kwa mwendo wa mwezi – na nimehalalishiwa

ngawira, na ardhi ikafanywa kwangu kuwa ni msikiti na ni safi, n nimetumwa

kwa viumbe wote na unabii ukaishia kwangu.”

Na katika kukirimiwa kwake (rehma na amani ziwe juu yake) ni kuwa

Mwenyezi Mungu akiapa basi huapa kwa kupitia jina lake na wala hatumii

jina la viumbe vyake, na Mwenyezi Mungu akiapia juu ya vitu basi ni kwa

kuvitilia mkazo, na anaapia vitu vingi mbali mbali, kama visivyo na uhai,

wanyama, malaika, maeneo, nyakati, na hali ya kilimwengu. Mwenyezi

Mungu hakupa ndani ya Kurani kumuapia mwanadamu isipokuwa Mtume

(rehma na amani ziwe juu yake), aliposema { Naapa kwa umri wako! Hakika

hao walikuwa katika ulevi wao, wakihangaika ovyo} Al hajar 16. akikusudia,

kupitia uhai wako ewe Muhamad hakika wao wamo katika upotofu mkubwa,

na wamo katika kutojua njia wala haki wala uongofu… Na washirikina

waliposema kuwa Mwenyezi Mungu amemuacha mkono Mtume Mtume

(rehma na amani ziwe juu yake), na amemtenga, Mwenyezi Mungu Mtukufu

akapa kuwa yeye hakumuacha na wala hakumuacha mkono, akasema

{0. Naapa kwa mchana! 6. Na kwa usiku unapo tanda! 4. Mola wako Mlezi

hakukuacha, wala hakukasirika nawe. 3. Na bila ya shaka wakati ujao

utakuwa bora kwako kuliko ulio tangulia. 2. Na Mola wako Mlezi atakupa

mpaka uridhike.} Adhuha 0-2.

Na kwa upande wa kukirimiwa kwake (rehma na amani ziwe juu yake) baaya

ya kufariki, ni kuwa Mwenyezi Mungu amempa uombeaji mkubwa siku ya

kiama. Kwani katika hadithi mbayo ameipokea Bukhari na Muslim kutoka

kwa Abi Hurayra (Mwenyezi Mungu amwie radhi), hakika mtume (rehma na

amani ziwe juu yake) amesema, “ mimi ni bwana kati ya watoto wa Adam

siku ya kiama, na ni wa mwanzo atakaepasukiwa na kaburi na ni mwombezi

wa mwanzo na wa mwanzo atakae ekubaliwa maomi yake.”

Na katika aya tukufu, Mwenyezi Mungu Mtukufu amemfanya (rehma na

amani ziwe juu yake) kuwa ni rehema kwa walimwengu wote, amesema {

Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote.} Al anbiyaa

117.

Kutoka kwa Abi Hurayra (Mwenyezi Mungu amwie radhi) amesema,

amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani zimshukie),

“hakika mimi ni rehema yenye kuongoa”. Na katika mapokezi mengine

nimetumwa kuwa ni rehema yenye kuongoa.

Wajibu wetu kwa upande wa Kurani tukufu

3 jamad-Awal 7331H. / 71-1-1172AD

Kwanza: Vipengele

Kurani Tukufu ni miujiza wa kiisilamu wa milele.

Nafasi ya Kurani Tukufu na fadhila zake.

Nafasi za wenye kuitendea Kurani Tukufu hapa duniani na akhera.

Wajibu wa waisilamu kwa upande wa Kurani Tukufu.

a. kuitukuza na kuisoma na kuzingatia aya zake.

b. Adabu tuwapo na Kurani Tukufu na kujiweka kitabia za Kurani Tukufu.

c. kuzifanyia kazi amri zake na makatazo yake.

Pili: dalili ndani ya Kurani Tukufu na hadithi

Dalili ndani ya Kurani Tukufu

Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema {Mwenyezi Mungu ameteremsha hadithi

nzuri kabisa, Kitabu chenye kufanana na kukaririwa; husisimua kwacho ngozi za

wenye kumkhofu Mola wao Mlezi. Kisha ngozi zao na nyoyo zao hulainika kwa

kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Huo ndio uwongofu wa Mwenyezi Mungu, na

kwa huo humwongoa amtakaye. Na ambaye ameachwa na Mwenyezi Mungu

kupotea, basi hapana wa kumwongoa }Zumar. 13.

Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema { Lau kuwa tumeiteremsha hii Qur'ani juu ya

mlima, basi bila ya shaka ungeli uona ukinyenyekea, ukipasuka kwa khofu ya

Mwenyezi Mungu. Na hiyo mifano tunawapigia watu ili wafikiri }Al hashri. 17.

Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema {Na namna hivi tumekufunulia Qur'ani kwa

amri yetu. Ulikuwa hujui Kitabu ni nini, wala Imani. Lakini tumekifanya kuwa ni

Nuru ambayo kwayo tunammwongoa tumtakaye katika waja wetu. Na hakika

wewe unaongoa kwenye Njia Iliyo Nyooka 35. Njia ya Mwenyezi Mungu ambaye

ni vyake Yeye tu viliomo mbinguni na katika ardhi. Jueni kuwa mambo yote

yanarudi kwa Mwenyezi Mungu }Ash shuraa 21-23.

Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema { Hakika hii Qur'ani inaongoa kwenye ya

yaliyo nyooka kabisa, na inawabashiria Waumini ambao wanatenda mema ya

kwamba watapata malipo makubwa }Al israa. 3.

Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema { Hakika Sisi ndio tulio teremsha

Ukumbusho huu, na hakika Sisi ndio tutao ulinda }Al hijri.3.

Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema { Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur'ani

iwe nyepesi kufahamika. Lakini yupo anaye kumbuka? }Al qamar. 71.

Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema { Na tunateremsha katika Qur'ani yaliyo ni

matibabu na rehema kwa Waumini. Wala hayawazidishii madhaalimu ila khasara.

}Al israa. 21.

Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema { Na ikiwa mna shaka kwa hayo tuliyo

mteremshia mja wetu basi leteni sura moja ya mfano wake, na muwaite mashahidi

wenu badala ya Mwenyezi Mungu, ikiwa mnasema kweli }Al baqara.13.

Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema {Na hiki Kitabu, tumekuteremshia wewe,

kimebarikiwa, ili wazizingatie Aya zake, na wawaidhike wenye akili.} S`aad. 13.

Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema { Sema: Wangeli kusanyika watu na majini

ili walete mfano wa hii Qur'ani basi hawaleti mfano wake, hata wakisaidiana wao

kwa wao }Al Isaraa. 22

Dalili ndani ya hadithi

Kutoka kwa Aisha (radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie) alipoulizwa kuhusu

tabia za mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) amesema: “Tabia zake

zilikuwa ni kurani.” (Imam Ahmad).

Kutoka kwa Aisha (radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie) kutoka kwa mtume

(rehma na amani zimshukie juu yake) amesema: “ambae husoma kurani naye

anaijua vyema basi huwa na malaika wema, na ambaye huisoma kurani hali ya

uzito basi ana malipo mara mbili.” (Imam Abi Daudi)

Kutoka kwa Anas bin Malik (radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie) amesema;

amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani zimshukie juu yake)

“Mwenyezi Mungu ana watu wa aina mbili, wakasema, ni akina nani hao ewe

mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: “hao ni watu wa kurani, watu wa

Mwenyezi Mungu na ndio aliowatenga maalumu.” (Ibn Majah)

Kutoka kwa Ibn Masuud (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) amesema;

amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu(rehma na amani zimshukie juu yake)

“mwenye kusoma herufi moja ndani ya kitabu basi atapatwa kwayo jema, na jema

moja ni huzidishwa mfano wake mara kumi, sisemi Alif Laam miim ni herufi,

lakini Alif ni herufi, Laam ni herufi na Miin ni herufi. (Imam Tirmidhy)

Kutoka kwa Ibn Masuud (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) amesema;

mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) ameniambia: “Nisomee” akasema:

nikamwambia nikusomee na kwako imeteremshwa? Akasema “ hakika mimi

ninapenda kuisikia ikisomwa na mwengine. Akasema: nikasoma Annisai mpaka

nilipofika: { itakuwaje tutakapouleta kila umma na shahidi, kisha ukaja wewe

kama ni shahidi wa hawa} akaniambia inatosha. Nikayaona macho yake

yanatokwa na machozi.” (Imam Bukhari na Muslim)

Kutoka kwa Abi Malik Al ashaariy (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake)

amesema: amesema mjumbe (rehma na amani zimshukie juu yake) “… kurani ima

ni hoja kwako au dhidi yako… (Imam Muslim)

Na kutoka kwa Abi Mussa Al ashariy (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake)

amesema: amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani zimshukie juu

yake) “mfano wa muumini asomae kuran ni mfano wa mtunda harufu yake ni

nzuri na ladha yake ni nzuri. Na mfano wa muumini ambae hasomi kurani ni

mfano wa tende, haina harufu (lakini) ladha yake ni tamu. Na mfano wa mnafiki

ambae anasoma kurani ni mfano wa mrehani harufu yake ni nzuri na ladha yake ni

chungu. Na mfano wa mnafiki ambae hasomi kurani ni sawa na mfano wa mtango

mwitu halina harufu na ladha yake ni chungu.” (Bukhari na Muslim)

Na kutoka kwa Ukubah bin Amir Aljuhaymiy amesema: mtume wa Mwenyezi

Mungu (rehma na amani zimshukie juu yake) alitujia tulipokuwa tumekaa kivulini

akasema: “ hivyo ni nani kati yenu angependa kwenda Kuthan au Al akiyk

akachukua ngamia wawili walio wazuri bila ya kupata madhambi kutoka kwa

Mwenyezi Mungu na wla kukata ukoo?” wakasema: sote tunataka ewe mjumbe wa

Mwenyezi Mungu. Akasema: “ aendapo mmoja wenu msikitini kila siku

akajifunza aya mbili ndani ya kitabu cha Mwenyezi Mungu ni bora kwake kuliko

ngamia wawili, na akisoma aya tatu (basi bora kwake) kuliko ngamia watatu na

mfano wa idadi za aya kwa idadi za ngamia.” (Abi Daudi)

Kutoka kwa Abi Umamah (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) amesema:

nimemsikia mjumbe wa Mwenyezi Mungu akisema: “Kurani italetwa siku ya

kiyama na watu wake ambao walikuwa wakiitendea, itatangulia sura ya Al baqara

na Al imran.” Na mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) akazipigia mfano

sitoisahau milele, akasema: mfano wake (hizo sura) ni kama mawingu mawili au

vivuli viwili vyeusi kati yao ni mwanga kama kwamba ni makundi ya ndege

waliopiga safu zitamuombea shifaa waliokuwa wakizisoma.” (Muslim)

Na kutoka kwa maneno ya wanazuoni (waliotangulia)

Abu Abdulrahman Assalamiy (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake)

anasema: “tulikuwa tukijifunza aya kumi za kurani na wala hatukuwa tukijifunza

aya kumi (nyengize) zijazo isipokuwa baada ya kujifunza halali zake na haramu

zake na amri zake na makatazo yake.” (Utunzi wa Abdu Razak)

Tatu: Maudhui

Kurani Tukufu ni mwujiza mkubwa wa kiisilamu kwa nyakati zote, majini na

wanadamu walishindwa kuileta kama hiyo. Akasema Mwenyezi Mungu { Sema:

Wangeli kusanyika watu na majini ili walete mfano wa hii Qur'ani basi hawaleti

mfano wake, hata wakisaidiana wao kwa wao }Al Isaraa. 22. bali pia

wameshindwa kuleta sura kumi tu mfano wake au sura moja mfano wake,

Mwenyezi Mungu amesema {Au wanasema: Ameizua? Sema: Basi leteni Sura

kumi zilizo zuliwa mfano wa hii, na waiteni muwawezao badala ya Mwenyezi

Mungu, ikiwa mnasema kweli.} Hud.73. na akasema Mwenyezi Mungu { Na

ikiwa mna shaka kwa hayo tuliyo mteremshia mja wetu basi leteni sura moja ya

mfano wake, na muwaite mashahidi wenu badala ya Mwenyezi Mungu, ikiwa

mnasema kweli }Al baqara.35.

Mwenyezi Mungu Mtukufu ameiteremsha ndani ya moyo wa mtume (rehma na

amani zimshukie juu yake) iwe ni uongofu kwa watu katika njia iliyonyooka,

iwaangazie maisha, na kuongoa wasiokuwa na uongofu. Ni katiba ya waislamu

kwani kwayo nyoyo huuishwa pia nafsi hufanywa kuwa safi na kwayo tabia huwa

njema, Mwenyezi Mungu anasema {7. Alif Lam Mim. 1. Hiki ni Kitabu

kisichokuwa na shaka ndani yake; ni uwongofu kwa wachamungu 3. Ambao

huyaamini ya ghaibu na hushika Sala, na hutoa katika tuliyo wapa} Albaqara. 7-3.

na Mwenyezi Mungu anasema { Hakika hii Qur'ani inaongoa kwenye ya yaliyo

nyooka kabisa, na inawabashiria Waumini ambao wanatenda mema ya kwamba

watapata malipo makubwa }Al israa. 3. mwenye kushikamana nayo ataokoka na

fitina, kwani ni mwanga kwa waumini na ni roho ya uongofu wake. Mwenyezi

Mungu anasema {Na namna hivi tumekufunulia Qur'ani kwa amri yetu. Ulikuwa

hujui Kitabu ni nini, wala Imani. Lakini tumekifanya kuwa ni Nuru ambayo kwayo

tunammwongoa tumtakaye katika waja wetu. Na hakika wewe unaongoa kwenye

Njia Iliyo Nyooka 23. Njia ya Mwenyezi Mungu ambaye ni vyake Yeye tu viliomo

mbinguni na katika ardhi. Jueni kuwa mambo yote yanarudi kwa Mwenyezi

Mungu }Ash shuraa 21-23.

Na kutokana na uzuri wake kundi la majini walipoisikia waliiamini na kuitukuza,

wakapata uongofu wa njia iliyonyooka, kisha wakaenda kuwaonya wenziwao, na

hivi ni kama alivyosimulia Mwenyezi Mungu Mtukufu, {Na wakati tulipo waleta

kundi la majini kuja kwako kusikiliza Qur'ani. Basi walipo ihudhuria walisema:

Sikilizeni! Na ilipo kwisha somwa, walirudi kwa kaumu yao kwenda kuwaonya.

31. Wakasema: Enyi kaumu yetu! Sisi tumesikia Kitabu kilicho teremshwa baada

ya Musa, kinacho sadikisha yaliyo kuwa kabla yake, na kinacho ongoza kwenye

Haki na kwenye Njia Iliyo Nyooka. 37. Enyi kaumu yetu! Muitikieni Mwenye

kuitia kwa Mwenyezi Mungu, na muaminini, Mwenyezi Mungu atakusameheni, na

atakukingeni na adhabu chungu. 31. Na wasio mwitikia Mwitaji wa Mwenyezi

Mungu basi hao hawatashinda katika ardhi, wala hawatakuwa na walinzi mbele

yake. Hao wamo katika upotovu ulio dhaahiri.} Al ahqaf 13-31.

Na iwapo hii ndio ilivyokuwa hali ya majini juu ya Kurani Tukufu basi na malaika

ni hivyo hivyo. Kutoka kwa Usayd bin Hudhayr, amesema: alipokuwa yeye

akisoma usiku sura albaqara na farasi wake amemfunga pembeni mwake, farasi

wake akataharaki naye akanyamaza (kusoma), akaendelea kusoma, farasi wake

akataharaki, akanyamaza kusoma naye (farasi) akaacha kutaharaki, kisha

akaendelea kusoma nae farasi akataharaki baadae akaondoka zake. Na mwanawe

yahya alikuwa karibu naye akaogopa asijwe kufikwa na tatizo na alipocheua (farasi

wake) alinyanyua kichwa chake juu kuangalia. Ilipofika asubuhi nikamueleza

mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) akasema: Soma ewe ibn Hudhayr,

akasema niliogopa ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu asije kumkanyaga yahya

kwani alikuwa nae karibu, nikanyanyua kichwa changu na kumuondoa kisha

nikanyanyua kichwa juu mbinguni, tahamaki mfano wa kivuli mifano ya taa,

nikaondoka ili nisiendelee kutazama, akasema “Unafahamu hicho kilikuwa ni kitu

gani?” akasema: “hapana”. Akasema “ hao ni malaika walikaribia kwa sababu ya

sauti yako na lau kama ungeliendelea basi watu wangeliwaona bila ya kificho.”

(Bukhari). Na namna hii ndio huwa athari ya kurani inaposomwa.

Ni maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ambae maajabu yake hayapungui, naye

amedhamini kuitunza kuepukana na kuharibiwa na kubadilishwa, akasema : {

Hakika Sisi ndio tulio teremsha Ukumbusho huu, na hakika Sisi ndio tutao ulinda

}Al hijri.3.

Asemae kupitia kurani basi amesema kweli, aitendeaye basi hulipwa, afanyae

hukumu kupitia kurani basi hufanya uadilifu, na ailinganiaye basi huongozwa

katika njia iliyonyooka nae Mwenyezi Mungu ameifanya kuwa ni tiba na rehema

akasema: { Na tunateremsha katika Qur'ani yaliyo ni matibabu na rehema kwa

Waumini. Wala hayawazidishii madhaalimu ila khasara. }Al israa. 21.

Kutoka kwa Abdillah (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) kutoka kwa

mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) amesema: “hakika kurani hii ni

karamu ya Mwenyezi Mungu basi ipokeeni karamu hii kadiri muwezavyo, hakika

kurani hii ni kamba ya Mwenyezi Mungu, na nuru iliyo wazi na matibabu yenye

manufaa na ngao kwa wanaoshikamana nayo, uokovu kwa waifuatayo, haipotoshi

na wala haiendi kombo na maajabu yake hayaishi na wala haina majibizano.

Isomeni kwani Mwenyezi Mungu hukulipeni kwa kuisoma kwake kwa kila herufi

thawabu kumi kwani mimi sisemi Ali Laam Miin ni herufi lakini Alif ni herufi

Laam ni herufi na Miim ni herufi. (Alhakim)

Mwenyezi Mungu ameinyanyua cheo na kuisifu kwa sifa njema na kuitaja kwa

majina mazuri sana ili watu waelewe nafasi na cheo chake, Mwenyezi Mungu

akaisifia kwa kusema { Hiki ni Kitabu ambacho Aya zake zimewekwa wazi, kisha

zikapambanuliwa, kilicho toka kwa Mwenye Hikima na Mwenye Khabari} Hud. 7.

na aliposema { na haya bila ya shaka ni Kitabu chenye nguvu na utukufu.

23. Hautakifikia upotovu mbele yake wala nyuma yake. Kimeteremshwa na

Mwenye hikima, Msifiwa.} Fusilat37-31. na sifa nyengineze zenye kujuulisha

cheo na nafasi yake iliyotukuka.

Na mtume wetu (rehma na amani zimshukie juu yake) ametueleza fadhila nyingi

sana juu ya Kurani Tukufu ambazo manufaa yake humrudia yeye mwenyewe

mwanadamu hapa duniani na kesho akhera, na katika fadhila hizo ni:-

Ubora kwa mwenye kuisoma: Hadithi ya Othmani Bin Affan (radhi za Mwenyezi

Mungu ziwe juu yake) kutoka kwa mtume (rehma na amani zimshukie juu yake)

amesema: “mbora wenu ni mwenye kujifundisha kurani na kuifundisha”

(Bukhari?)

Kupandishwa cheo: imepokewa hadithi kutoka kwa Amru (Mwenyezi Mungu

awawie radhi) amesema, amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani

zimshukie juu yake) “itasemwa kuambiwa msomaji wa kurani: soma na panda

cheo, na soma kama ulivyokuwa ukiisoma duniani, kwani cheo chao ni mwisho wa

aya utakayoisoma) (Abi Daudi)

Kumuombea msomaji: imepokewa hadithi kutoka kwa Umama Albahiliy (radhi

za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) amesema: nimemsikia mjumbe wa Mwenyezi

Mungu (rehma na amani zimshukie juu yake) akisema: “ someni kurani kani hiyo

itakuja siku ya kiyama kama ni mwombezi kwa wasomaji wake” (Muslim)

Malipo makubwa kwa msomaji wake: imepokewa hadithi kutoka kwa Ibn Mas

uud (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) amesema: amesema mjumbe wa

Mwenyezi Mungu (rehma na amani zimshukie juu yake) “Mwenye kusoma herufi

moja ndani ya kitabu basi atapatwa kwayo jema, na jema moja ni huzidishwa

mfano wake mara kumi, sisemi Alif Laam miim ni herufi, lakini Alif ni herufi,

Laam ni herufi na Miin ni herufi.” (Imam Tirmidhy)

Kuhifadhiwa nyumba zisomwazo kurani: imepokewa na Abi Hurayra (radhi za

Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) kwamba mtume (rehma na amani zimshukie juu

yake) amesema: “ musizifanye nyumba zenu makaburi, hakika ya shetani hukimbia

nyumba ambayo husomwa ndani yake sura ya Albaqara.” (Muslim) na fadhila

nyenginezo ambazo hazimaliziki. Kwa mfano hadithi ya Ibn Siyriyn, amesema:

“nyumba ambayo husomwa ndani yake kurani malaika huwa wanahudhuria na

mashetani hutoka, na wasomi wake huombewa na kheri zake huzidi. Na nyumba

ambayo kurani haisomwi, huhudhuria mashetani na malaika hutoka na huwapo

katika simanzi waktu wake na kheri zake huwa ni chache.” (Ibn Abi Shaybah)

Na tukizingatia hali za masahaba wakarimu (Mwenyezi Mungu awawie radhi)juu

ya kurani tukufu tutaona kuwa wao hawakutosheka kuisoma tu na kuisikiliza,

lakini waliisoma na kuizingatia nyonyo na nafsi zao zikashikamana nayo, wakawa

wanaitekeleza kimaneno na kimatendo na kufuata amri zake na kujiepusha na

makatazo yeke. Kwa ajili hiyo wakafikia vyeo vikubwa sana walivyofikia kwa

sababu ya kuitikia wito wa Kurani Tukufu. Sayidna Omar aliihifadhi sura ya

Albaqara kwa muda wa miaka minane si kwa sababu ya uzito wa kuhifadhi

isipokuwa alikuwa na pupa ya kupata elimu na kuitendea elimu hiyo. Abu Abdu

rahman As salamiy (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) anasema:

“tulikuwa tunapojifunza aya kumi ndani ya Kurani Tukufu huwa hatujifunzi aya

kumi nyengine zijazo mpaka (tunahakikisha) tumejifundisha halali yake na haramu

na amri zake na makatazo yake” (Abdu Razzak)

Na kwa kuwa masahaba (Mwenyezi Mungu awawie radhi) walikuwa

wakijielimisha na kisha kuitendea kwa ajili hiyo wakawa wako mbele katika

kumtii Mwenyezi Mungu Mtukufu na kujiepusha na makatazo yake. Na wakati

zilipoteremshwa aya za makatazo ya kunywa ulevi, muitaji akaita: “ Tambueni

kuwa ulevi umeharamishwa”, basi wote wakaitikia wito wa kurani. Aliyekuwa na

ulevi mkononi basi akaurembea, na aliyekuwa ulevu imo kinywani akaucheua, na

aliyekuwa na ulevi kwenye chombo akaumwaga hii yote ni kwa ajili ya kuitikia

wito wa Mwenyezi Mungu, - na mpaka njia za mji wa Madina zilijaa pombe-

wakawa wanasema “tumeacha ewe Mola wetu”. Na kwa namna hiyo ilipoteremka

aya { Kabisa hamtafikia wema mpaka mtoe katika vile mnavyo vipenda. Na kitu

chochote mnacho kitoa basi hakika Mwenyezi Mungu anakijua} Al imran 31.

Sayidna Abu Dahdah alisimama kwenye bustani aipendayo zaidi akaitoa sadaka.

Kwa hivyo, masahaba (Mwenyezi Mungu awawie radhi) waliweza kuhifahi kitabu

cha Mwenyezi Mungu kwani kao hakikua kama kitabu cha kawaida, lakini ni

mwongozo wa kimalezi, kimaadili na kiimani iliyodhihiri katika maisha yao ya

kila siku na kwa wengine.

Kwa ajili hiyo cheo ambacho Mwenyezi Mungu amewapa wasomao Kurani

Tukufu na kuitendea kazi ni kikubwa mno. Imepokea kutoka kwa Anas bin Malik

(radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) amesema: amesema mjumbe wa

Mwenyezi Mungu ““Mwenyezi Mungu ana watu wa aina mbili, wakasema, ni

akina nani hao ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: “hao ni watu wa

kurani, watu wa Mwenyezi Mungu na ndio aliowatenga maalumu.” (Ibn Majah).

Asomae Kurani Tukufu amenasibishwa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na ni

cheo kikubwa kilichoje!

Ama wajibu wetu kuhusu kurani inakusanya:-

* Kujifundisha na kuifundisha, na kuendelea kuisoma na kuifundisha, kwani walio

bora ni wale wenye kujifundisha na kuifundisha, imepokewa katika hadithi (mbora

wenu ni yule ajifundishae kurani kisha kuifundisha. Na mtume wetu (rehma na

amani zimshukie juu yake) ametuamrisha kuisoma na kuishikilia akasema:

“shikamaneni na kurani ninaapa kwa yule ambaye nafsi yangu ipo mikononi

mwake ni rahisi sana kuponyoka kuliko ngamia aliye katika kamba yake.”

(Bukhari)

Kurani Tukufu ni chanzo madhubuti chenye kutengeneza nafsi ya mwisilamu,

kupitia Kurani Tukufu hupata mafunzo na tabia njema. Hivyo basi, juu ya

muisilamu awe na pupa katika kuisoma vizuri, na jambo hili si gumu, kwani

tunakutia watu huwa wanajifunza lugha za kigeni, na hutumia juhudi za namna

tafauti ili wawe na maarifa mengi kwa ajili ya kupata kipato kingi. Itakuwaje basi

kuzembea katika kujifunza maneno ya Mwenyezi Mungu mtukufu iwe ndio tabu?

Imepokewa kutoka kwa Aisha (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) kutoka

kwa mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) amesema: “ambae husoma

kurani naye anaijua vyema basi huwa na malaika wema, na ambaye huisoma

kurani hali ya uzito basi ana malipo mara mbili.” (Imam Abi Daudi) na Mwenyezi

Mungu Mtukufu ametuahidi kuwa ametufanyia kuwa ni chepesi kwa kukisoma na

kwa kuabudia akasma { Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur'ani iwe nyepesi

kufahamika. Lakini yupo anaye kumbuka? } Alqamar;71.

Kuzingatia aya zake kama kwamba bdio zinashuka kwa msomaji wake, kwani

katika wajibu wetu juu ya Kurani Tukufu isiwe ni kuisoma tu lakini hakuna budi

kuizingatia ili tupate ladha yake na kuihisi utukufu wake, Mwenyezi Mungu

anasema { Je! Hawaizingatii hii Qur'ani? Au kwenye nyoyo (zao) zipo

kufuli?}Muhhamad;13. na akasema pia, { Hebu hawaizingatii hii Qur'ani? Na lau

kuwa imetoka kwa asiye kuwa Mwenyezi Mungu bila ya shaka wangeli kuta ndani

yake khitilafu nyingi} Anisaa;21.

Kwa wasomi wa Kurani Tukufu wanaopata malipo makubwa sana ni wale

waisomao kwa ndimi zao na kuzingatia nyoyoni mwao na akilini mwao,

Mwenyezi Mungu anasema, { Na hiki Kitabu, tumekuteremshia wewe,

kimebarikiwa, ili wazizingatie Aya zake, na wawaidhike wenye akili } Saad;13. na

Mwenyezi Mungu amemsifu asomaye aya zake kwa kuzingatia zikawa

zinamzidishia imani akasema, { Hakika Waumini ni wale ambao anapo tajwa

Mwenyezi Mungu nyoyo zao hujaa khofu, na wanapo somewa Aya zake

huwazidisha Imani, na wakamtegemea Mola wao Mlezi }Al anfaal;1. Ibn Abbas

amesema: “Mwenyezi Mungu amechukua dhamana kwa aisomae Kurani Tukufu

kuwa hatapotea hapa duniani na wala hatokuwa na tabu kesho akhera, na dalili ya

hayo ni kauli yake Mwenyezi Mungu, {basi atakaye ufuata uwongofu wangu,

hatapotea wala hatataabika 432. Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi

kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya

kuwa kipofu 433. Aseme: Ewe Mola wangu Mlezi! Mbona umenifufua kipofu,

nami nilikuwa nikiona? 434. (Mwenyezi Mungu) atasema: Ndivyo vivyo hivyo.

Zilikufikia ishara zetu, nawe ukazisahau; na kadhaalika leo unasahauliwa }

Taha;713-712.

Na mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) ametupigia mfano kwa mwenye

kuathirika na Kurani Tukufu na kutekeleza kama aya zake zisemavyo. Siku moja

alisema kumwambia Abdullah bin Masuud (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu

yake): “Kutoka kwa Ibn Masuud (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake)

amesema; mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) ameniambia: “Nisomee”

akasema: nikamwambia nikusomee na kwako imeteremshwa? Akasema “ hakika

mimi ninapenda kuisikia ikisomwa na mwengine. Akasema: nikasoma Annisai

mpaka nilipofika: {itakuwaje tutakapouleta kila umma na shahidi, kisha ukaja

wewe kama ni shahidi wa hawa} akaniambia inatosha. Nikayaona macho yake

yanatokwa na machozi.” (Imam Bukhari na Muslim). Fahari ya muumini ni kuenda

sambamba na neno la Mwenyezi Mungu Mtukufu, Mwenyezi Mungu anasema

{Mwenyezi Mungu ameteremsha hadithi nzuri kabisa, Kitabu chenye kufanana na

kukaririwa; husisimua kwacho ngozi za wenye kumkhofu Mola wao Mlezi. Kisha

ngozi zao na nyoyo zao hulainika kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Huo ndio

uwongofu wa Mwenyezi Mungu, na kwa huo humwongoa amtakaye. Na ambaye

ameachwa na Mwenyezi Mungu kupotea, basi hapana wa

kumwongoa}Azzumar;13.

Adabu (heshima) za kuwa na Kurani Tukufu na kujipamba kwa tabia zake,

miongoni mwa wajibu wa msomi wa Kurani Tukufu ni kuwa na heshima na

kujipamba kwa mwenendo wa Kurani Tukufu, ashikamane na mafunzo yake.

Kwani kupitia tabia za kurani mwanadamu anajikinga na ufuataji wa matakwa

yake na matamanio yake na nafsi yake huwa madhubuti katika maadili mema,

Mwenyezi Mungu anasema, { Hakika hii Qur'ani inaongoa kwenye ya yaliyo

nyooka kabisa, na inawabashiria Waumini ambao wanatenda mema ya kwamba

watapata malipo makubwa }Al israa;3. na kigezo chetu juu ya hili ni bwana mtume

(rehma na amani zimshukie juu yake) kwani alikuwa kama kurani ikitembea juu ya

mgongo wa ardhi, alijipamba kitabia kama kurani itakavyo, akiridhia kile ambacho

Kurani Tukufu imeridhia,na kuchukia kile kilichochukiwa na Kurani Tukufu. Bibi

Aisha (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) aliulizwa kuhusu tabia za mtume

(rehma na amani zimshukie juu yake) akasema: “tabia zake ni kurani.” (Ahmad)

* kufuata maamrisho yake na makatazo yake, wajibu wetu juu ya Kurani

Tukufu hautakiwi uwe ni vifuani au hata kuizingatia pekee lakini itabidi kufuata

maamrisho yake na makatazo yake. Ili tabia na matendo yetu yaonekane kama

alivyokuwa mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) na masahaba wake.

Hivyo, wajibu wa muisilamu afuate amri za kurani na kuacha makatazo yake

kwani mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) anasema: “kurani ima ni

hoja kwako au dhidi yako.” (Muslim) Itakuwa ni hoja dhidi yako pindi iwapo

haitofika masikioni mwako na wala haitoathiri kitu katika mwenendo wa

maisha yako na huenda msomaji wake ikawa inamlaani.

* Na miongoni mwa wajibu wetu juu ya Kurani Tukufu ni kupambana na

wanaoipotosha na kuifasiri visivyo na kuizungumzia kisiasa au kiitikadi (sizo)

ili kupata manufaa na chumo. Kurani Tukufu inabidi ielezwe kimaneno na

kimaana kwa wasomi wake wa umma wenye kuamninika na waliobobea katika

fani hiyo, wawafundishe watu mafunzo sahihi na itikadi ndiyo ya kiisilamu ama

kwa wale wasioijua hawatakuwa na cha kufanya zaidi ya masilahi yao na

matamanio yao.

* Na ulimwengu wetu wa sasa unahitajia zaidi uongofu wa Kurani Tukufu,

matatizo yaliyopo sasa ni matatizo ya kimaadili na hakuna kitabu

kilicholingania maadili kwa watu wote mfano wa Kurani Tukufu. Na iwapo

kosa la waislamu kwa wakati huu kujiweka mbali na mwenendo wa Kurani

Tukufu sasa itawalazimu wairudie na kufuata mifano ya kivitendo ya Kurani

Tukufu na kwa aliyeteremshiwa hii kurani (mtume Muhammad rehma na amani

zimshukie juu yake). Kwani yeye ndiye aliyesifiwa na Mola wake kuwa ni

mwenye tabia njema kabisa kwakuwa tu ameifuata kurani kimarefu na mapana.

Alikuwa ni kiumbe mwenye tabia nzuri kwa kule kuifuata katika nyanya zote,

Mwenyezi Mungu anasema {Hakika wewe ni mwenye tabia nzuri} Alqalam,3.

na kama ilivyoelezwa katika hadithi ya Aisha (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe

juu yake) akasema “tabia zake ni kurani.”

* Nasi hatutoacha kuelezea Kurani Tukufu ili iwe ni mwongozo mwema

utakaotukinga siku ambayo hatutokuwa na mkingaji wala muokoaji,

imepokewa kutoka kwa Abi Umamah (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu

yake) amesema: “nimemsikia mjumbe wa Mwenyezi Mungu akisema: “Kurani

italetwa siku ya kiyama na watu wake ambao walikuwa wakiitendea, itatangulia

sura ya Al baqara na Al imran.” Na mtume (rehma na amani zimshukie juu

yake) akazipigia mfano sitoisahau milele, akasema: mfano wake (hizo sura) ni

kama mawingu mawili au vivuli viwili vyeusi kati yao ni mwanga kama

kwamba ni makundi ya ndege waliopiga safu zitamuombea shifaa waliokuwa

wakizisoma.” (Muslim)

Waisilamu wakiendelea kuisoma, kuzingatia maana yake na kuitendea pia

kujifunza na kuifundisha watakuwa na manufaa makubwa sana, kwani rehema

na uadilifu utaenea, nyoyo zitakuwa njema kheri zitakuwa nyingi na shari na

maafa yatatoweka.

Wito wa Manabii na Mitume katika urekebishaji kwa

mtazamo wa kurani tukufu 71 Rabiu Akhar 7331H. 11 Januari 1172A.D

Kwanza: Vipengele

7. Uisilamu ni dini ya wema na marekebisho

1. mifano ya ulinganio wa Manabii na mitume katika kurekebisha kwa kupitia

Kurani Tukufu

3. Umuhimu wa kuzirekebisha nafsi zetu kwanza.

3. Athari ya marekebisho kwa mtu mmoja mmoja na kwa jamii

2. Madhara ya kuacha kujirekebisha.

Pili: Dalili

Ndani ya Kurani Tukufu

7. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema { Na hatuwatumi Mitume ila huwa ni

wabashiri na waonyaji. Na wenye kuamini na wakatenda mema haitakuwa khofu juu yao,

wala hawatahuzunika} [Al anaam; 24]

1. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema kwa kupitia ulimi wa Nabii Shuaib (

Rehema na amani zimshukie juu yake) {Akasema: Enyi watu wangu!

Mwaonaje ikiwa ninayo dalili wazi inayo tokana na Mola wangu Mlezi, na

ikawa Yeye ameniruzuku riziki njema kutoka kwake? Wala mimi sipendi

kukukhalifuni nikafanya yale ninayo kukatazeni. Sitaki ila kutengeneza kiasi

ninavyo weza. Na sipati kuwezeshwa haya ila na Mwenyezi Mungu. Kwake

Yeye ninategemea, na kwake Yeye naelekea} [Hud; 44]

3. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema kwa kupitia ulimi wa Nabii Shuaib (

Rehema na amani zimshukie juu yake) { Timizeni kipimo sawa sawa, wala msiwe

katika wanao punja. 443. Na pimeni kwa haki iliyo nyooka; 445. Wala msiwapunje watu

vitu vyao, wala msifanye jeuri kwa ufisadi} [Ashuaraa; 444-445]

3. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema {Wala msifanye uharibifu katika nchi

baada ya kuwa imekwisha tengenezwa. Na muombeni kwa kuogopa na kwa

kutumai. Hakika rehema ya Mwenyzi Mungu iko karibu na wanao fanya

mema.} [Alaaraf; 34]

2. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema { Na Musa akamwambia nduguye

Haarun: Shika mahala pangu kwa watu wangu na utengeneze wala usifuate

njia ya waharibifu} [Al aaraf; 423]

2. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema {Sema: Njooni nikusomeeni aliyo

kuharimishieni Mola wenu Mlezi. Nayo ni kuwa, msimshirikishe Yeye na chochote. Na

wazazi wenu wafanyieni wema. Wala msiwauwe watoto wenu kwa sababu ya umasikini.

Sisi tunakuruzukuni nyinyi na wao. Wala msikaribie mambo machafu, yanayo onekana,

na yanayo fichikana. Wala msiuwe nafsi ambayo Mwenyezi Mungu ameharimisha

kuiuwa, ila ikiwa kwa haki. Hayo amekuusieni ili myatie akilin} [Al anaam; 434]

7. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema { Wala hakuwa Mola wako Mlezi wa

kuihiliki miji kwa dhulma tu na hali watu wake ni watenda mema } [Hud;

447]

4. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema {Na Mola wako Mlezi haangamizi miji

mpaka ampeleke Mtume katika miji yake mikuu awasomee Ishara zetu. Wala

hatuiangamizi miji mpaka watu wake wawe madhaalimu.} [Al qasas; 35]

3. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema { Na kina Thamud tuliwapelekea ndugu

yao Saleh. Akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi

hamna Mungu ila Yeye. Yeye ndiye aliye kuumbeni katika ardhi, na

akakuwekeni humo. Basi mwombeni msamaha, kisha mtubu kwake. Hakika

Mola wangu Mlezi yupo karibu, anaitikia maombi.} [Hud; 44]

71. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema { Hakuna kheri katika mengi ya

wanayo shauriana kwa siri, isipo kuwa kwa yule anaye amrisha kutoa sadaka, au

kutenda mema, au kupatanisha baina ya watu. Na mwenye kufanya hayo kwa kutaka

radhi ya Mwenyezi Mungu, basi tutakuja mpa ujira mkubwa} [Nisaa; 442]

44. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema {Wanakuuliza juu ya Ngawira.

Sema: Ngawira ni ya Mwenyezi Mungu na Mtume. Basi mcheni Mwenyezi

Mungu na suluhisheni mambo baina yenu, na mt'iini Mwenyezi Mungu na

Mtume wake ikiwa nyinyi ni Waumini} [Al anfaal; 4]

Dalili kwa hadithi za Mtume ( Rehema na amani zimshukie juu yake)

7. Kutoka kwa Zayd Bin Milha (Mwenyezi Mungu amwie radhi), hakika ya

mtume ( Rehema na amani zimshukie juu yake) amesema: (… hakika ya

dini imeanza ngeni na itarudi hali ya kuwa ni ngeni, basi uzuri ulioje kwa

wageni (nao ni) ambao wanarekebisha yale waliyoyaharibu watu baada

yangu katika mwenendo wangu (sunna zangu). (Tirmidhiy)

1. Kutoka kwa Abi Dardai (Mwenyezi Mungu amwie radhi) amesema:

amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani zimshukie juu

yake), “Je nikuelezeni lililo bora kuliko thawabu za kufunga na s;a na

sadaka? Wakasema: “Ndio, akasema, kuwarekebisha jamaa , kwani

kuharibika kwa jamaaa ni kuifuta dini miongoni mwa watu . (Tirmidhy)

3. kutoka kwa Abi Hurayra (Mwenyezi Mungu amwie radhi) amesema:

Mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) alikuwa akisema: “ewe

Mola nirekebishie dini yangu ambayo ni hifadhi ya mambo yangu, na

unirekebishie dunia yangu ambayo ni maisha yangu, na unirekebishie

akhera yangu ambayo ni mareleo yangu, na nifanyie maisha kuwa na kila

la kheri, na nifanyie umauti wangu yawe ni starehe kwa kila ovu.”

(Muslim).

3. kutoka kwa Abi Hurayra (Mwenyezi Mungu amwie radhi) amesema;

amesema mtume wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani zimshukie juu

yake) kila kiungo cha mwanadamu kina sadaka, kila siku ichomozayo

jua, akipatanisha kati ya watu waili ni sadaka, kumsaidia mtu katika

kumpandisha kipando cha mnyama wake ni sadaka au kumsaidia mtu

kupandisha mzigo wake juu ya mnyama ni sadaka, neno zuri ni sadaka,

na kila hatua apigayo kwenda kusali ni sadaka, kuondoa uchafu njiani ni

sadaka.” (Bukhari na Muslim)

2. Kutoka kwa Ubada Bin Umayr Bin Auf, amesema, Abu Ayubu

(Mwenyezi Mungu amwie radhi) aliniambia: Mtume (rehma na amani

zimshukie juu yake) aliniambia ewe Aba Ayubu, je nikujuulishe sadaka

ambayo Mwenyezi Mungu na mtume wake wanaipenda? Suluhisha kati

ya watu wakikasirikiana na kuharibiana.” (Muujam kabiir, Twabarani)

2. Kutoka kwa Anas Bina Malik amesema: amesema mtume wa Mwenyezi

Mungu (rehma na amani zimshukie juu yake) “ iwapo kiama kitasimama

na kwenye mkono wa mmoja wenu ana mbegu basi akiweza kuipanda na

aipande.” (Bukhari)

Tatu: Maudhui

Miongoni mwa maadili ya uisilamu ambayo dini yetu imehimiza na kulingania

sana ni maadili ya wema na usuluhishaji (urekebishaji). Kwani ni tabia njema

ambayo nafsi ya mtu hupenda na kuitamani. Ni maadili ambayo kila mtu inapasa

awe nayo kwa ajili ya kuimarisha ulimwengu. Na ni kitu kitakiwacho katika sheria

kwa kuwa kinaondosha sababu za ufisadi na mipasuko, huharakisha uwepo wa

ukaribu kati ya watu kwa lengo la kuleta usawa wa hali zao ndani ya maisha.

Hapana shaka kuwa wema na usuluhishaji ni upeo utakiwao kwa waja katika

ibada zao na katika kazi zao, bila ya wema ibada haikubaliki, kwa hivyo, hakuna

budi kwa mwanadamu awe mwema katika nafsi yake kimatendo na kimaneno

mwenye kusuluhisha matatizo ya wengine na kutenda kwa ajili ya kuwarekebisha.

Na mwenye kuzingatia aya za Kurani Tukufu ataona kuwa zimeweka mkazo

mkubwa sana katika suala hili – la maadili ya urekebishaji-. Neno kurekebisha

limetajwa ndani ya Kurani Tukufu karibuni mara mia moja na sabini, n kila

kinapotajwa kitu kwa wingi huwa ni dalili ya umuhimu wake na ukubwa na nafasi

yake. Hivyo neno hili (urekebishaji - usuluhishaji) limkuja kwa maana tafauti na

katika mana zote hizi inajulisha kuwa uisilamu ina lengo kusawaziha wanadamu

katika itikadi zao, ibada zao, matendo yao na nyanja nyengine za maisha yao.

Kurani Tukufu imeweka sambamba kati ya imani ya kumuamini Mwenyezi

Mungu na kurekebisha – kusuluhisha, katika aya nyingi, kama ni ishara ya mja

kuwa na imani ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu anasema {Na wenye kuamini

na wakatenda mema haitakuwa khofu juu yao, wala hawatahuzunika} [Al anaam; 32] na

amesema Mwenyezi Mungu {Wanakuuliza juu ya Ngawira. Sema: Ngawira ni ya

Mwenyezi Mungu na Mtume. Basi mcheni Mwenyezi Mungu na suluhisheni mambo

baina yenu, na mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume wake ikiwa nyinyi ni Waumini}

[Al anfaal;4]

Vile vile Kurani Tukufu imeweka sambamba kati ya uchaji Mungu na kurekebisha

– kusuluhisha, Mwenyezi Mungu amesema {basi watakao mchamngu na

wakatengenea haitakuwa khofu kwao, wala hawatahuzunika} [Al aaraf; 53]. Na pia

kufungamanisha kati ya kutubu na kurekebisha – kusuluhisha akasema Mwenyezi

Mungu { Ila wale walio tubu na wakatengeneza na wakabainisha,} [Al baqara;

441]. Na pia akasema { Na wakitubia wakatengenea }[Anisaa; 44]. Na akasema pia {

Isipo kuwa wale walio tubu baada ya hayo na wakatengenea; kwani bila ya shaka

Mwenyezi Mungu ni Msamehevu, Mwenye kurehemu} [Anuur; 3]. Hivyo basi,

kurekebisha – kusuluhisha ni matunda ya imani ya kumuamini Mwenyezi Mungu

Mtukufu na uchaji na ni toba ya kweli kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mola wa

walimwengu wote.

Na Kurani Tukufu imependezesha kurekebisha – kusuluhisha kwa kuwa kuna

malipo makubwa, Mwenyezi Mungu anasema { Hakuna kheri katika mengi ya wanayo

shauriana kwa siri, isipo kuwa kwa yule anaye amrisha kutoa sadaka, au kutenda mema, au

kupatanisha baina ya watu. Na mwenye kufanya hayo kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu,

basi tutakuja mpa ujira mkubwa} [Anisaa; 442].

Na tukifuatilia habari za manabii na mitume pamoja na watu wao tutaona kuwa

wametumwa kwa lengo la kurekebisha yale waliyoyaharibu watu katika dunia. Na

kwa ajili hiyo ujumbe wa kila nabii ulikuwa ni mmoja, nao ni kurekebisha

ulimwengu kutokana na maasi na magonjwa ambayo yameenea kati yao, na kila

mtume akapelekwa kwa watu wake ili kuondoa ufisadi ambao umeenea katika

zama zake, Mwenyezi Mungu akawatuma kwa waja wake ili wawe wabashiria

mema na waonyaji wa itikadi na sheria pamoja na maadili ya kuisawazisha nafsi na

kuiepusha na uchafu wa ushirikina. Mwenyezi Mungu anasema {Na hatukumtuma

kabla yako Mtume yeyote ila tulimfunulia ya kwamba hapana mungu isipo kuwa Mimi. Basi

niabuduni Mimi tu.} [Al anbiya; 33] na wito wao mitume umekuja kwa ajili ya

kuwarekebisha waja duniani ili wakapate radhi za Mola wao huko akhera.

Mfano sayidna Nuh (rehma na amani zimshukie juu yake) hakika aliwalingania

watu wake kwa ajili ya kuwarekebisha ndani ya dini ya Mwenyezi Mungu ili

wapate kumuabudu Yeye (Mwenyezi Mungu) na wasimshirikishe na chochote na

waachane na ibada ya masanamu ambayo hayadhuru wala hayanufaishi, Mwenyezi

Mungu anasema { Na wakasema: Msiwaache miungu yenu, wala msimwache Wadda

wala Suwaa' wala Yaghutha, wala Yau'qa, wala Nasra 32. Na hao walikwisha

wapoteza wengi, wala usiwazidishie walio dhulumu ila kupotea.} [Nuh; 35-32]. Na

akawa anawapenezeshea katika kujirekebisha ili wapate riziki nyingi, na

Mwenyezi Mungu awaneemeshe kwa mali na watoto. Mwenyezi Mungu anasema

{Nikasema: Ombeni msamaha kwa Mola wenu Mlezi; hakika Yeye ni Mwingi wa

kusamehe. 44. Atakuleteeni mvua inyeshe mfululizo. 43. Na atakupeni mali na wana,

na atakupeni mabustani na atakufanyieni mito. 45. Mna nini hamweki heshima ya

Mwenyezi Mungu?} [Nuh;41-45]

Na mfano mwengine ni nabii Shuaibu (rehma na amani zimshukie juu yake)

anatibu ufisadi wa itikadi na kila lililoambatana na uharibifu wa uchumi kwa watu

wake, akawa anawalingania waache kupunguza vipimo na mizani, na tabia hii

mbaya ilikuwa imeenea sana kati ya watu wake, akaja kuwalingania katika

marekebisho ya kuhifadhi haki ya muuzaji na mnunuzi. Mwenyezi Mungu

anasema kwa ulimi wa nabii Shuaib (rehma na amani zimshukie juu yake) { Na

kwa watu wa Madyana tuliwatumia ndugu yao Shua'ib. Akasema: Enyi watu wangu!

Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna Mungu ila Yeye, wala msipunguze

vipimo na mizani. Mimi nakuoneni mmo katika hali njema, nami nakukhofieni adhabu

ya Siku kubwa hiyo itakayo kuzungukeni. 43. Na enyi watu wangu! Timizeni vipimo

na mizani kwa uadilifu wala msiwakhini watu vitu vyao; wala msieneze uovu katika

nchi mkafanya uharibifu.} [Hud; 42-43]. Kisha akawawekea wazi kuwa lengo la

ulinganio wake ni kurekebisha akasema { Sitaki ila kutengeneza kiasi ninavyo weza.

Na sipati kuwezeshwa haya ila na Mwenyezi Mungu. Kwake Yeye ninategemea, na

kwake Yeye naelekea.} [Hud;44]. Na katika sehemu nyengine anasema kuwa

dhumuni ni kurekebisha tabia mbovu ya watu ya kupunguza mizani na vipimo

akawa anawaambia {Timizeni kipimo sawa sawa, wala msiwe katika wanao punja. 443. Na

pimeni kwa haki iliyo nyooka; 445. Wala msiwapunje watu vitu vyao, wala msifanye jeuri kwa

ufisad.} [Ashuaraa; 444-445].

Na tuzingatie kitu muhimu sana pale Sayidna Shuaib (rehma na amani zimshukie

juu yake) aliposema wakati anawalingania watu wake {Na sipati kuwezeshwa haya

ila na Mwenyezi Mungu. Kwake Yeye ninategemea, na kwake Yeye naelekea} [Hud;

44]. Hapa amebainisha kuwa pana dhumuni kubwa ambalo hapana budi

kuchungwa kwa kila mwenye kutaka kurekebisha, nalo ni kufanya marekebisho

kwa ajili ya Mwenyezi Mungu pekee.

Nayo marekebisho hayahitaji masilahi na wala mapendekezo ya mtu binafsi, ni

marekebisho yenye kurekjelea manufaa yake kwa wana jamii wote na kwa kila

mtu.

Mfano mwengine ni Nabii Saleh (rehma na amani zimshukie juu yake) anawaita

watu wake kwa kusema {Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi. 434. Wala msit'ii

amri za walio pindukia mipaka, 433. Ambao wanafanya ufisadi katika nchi, wala

hawatengenezi} [Ashuaraa 431-433]

Na wakati sayidna Mussa (rehma na amani zimshukie juu yake) alipomachilia

madaraka mdogo wake sayidna Harun (rehma na amani zimshukie juu yake) juu ya

watu wake alimuusia kuwarekebisha na kuacha kufuata njia za waharibifu.

Mwenyezi Mungu amesema {Tulimuahidi Musa masiku thalathini na tukayatimiza

kwa kumi; ikatimia miadi ya Mola wake Mlezi masiku arubaini. Na Musa

akamwambia nduguye Haarun: Shika mahala pangu kwa watu wangu na utengeneze

wala usifuate njia ya waharibifu.}[Al aaraf 423].

Kisha akaja mtume wa waisilamu (rehma na amani zimshukie juu yake)

kukamilisha marekebisho katika nyanja zote za maisha ya kidunia, kijamii

kiuchumi na kisiasa ambayo hata watume waliomtangulia walilingania pia. Na kwa

kutazama kwa undani kabisa kuhusu maisha yake tutaona kuwa mtume (rehma na

amani zimshukie juu yake) ametengeneza tamaduni za kiisilamu zenye

kushikamana na maadili na tabia. Baada ya kuwa jamii ilikuwa imejaa uharibifu

wa kitabia kama uzinifu, wizi, mauaji, riba, kula mali za watu kwa dhuluma na

kula mali za mayatima na mengineyo katika maovu na mambo ya kuchukiza.

Lakini mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) aliyakabili haya yote kwa

mfumo wa kuyarekebisha, na wito wake ukawa ni wito wa urekebishaji wa mtu na

jamii. Mwenyezi Mungu anasema {Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na

Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.}[Al anfaal 32]. Na kwa

upande wa dini, ulinganio wake umekuja kwa kuirekebisha nafsi kupitia dini,

akaweka wazi ya kuwa Mwenyezi Mungu ni mmoja na hana mshirika, na

akasimamisha dalili za kumpwekesha. Na pia kwa upande wa kurekebisha tabia

alilingania kuwa na tabii njema ambayo ndio chimbuko la ulinganiaji. Imepokewa

kutoka kwa Al bayhaqi (Mwenyezi Mungu amwie radhi) katika kitabu chake

kwamba mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) amesema: “ hakika mimi

nimetumwa kuja kukamilisha tabia njema.”

Na kama ambavyo mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) alilingania katika

misingi ya maadili mema ya kiutu ambayo kwayo jamii hutengenea, na huhifadhi

umoja wake na nguvu zake pia mshikamano wake kwa ajili ya kushi maisha yaliyo

salama na mazuri, yasiyo na machafuko wala mipasuko wala fujo na matendo ya

kigaidi kinyume na tuonavyo hivi sasa kuhusu mambo ya uharibifu, mauaji na

ubomoaji.

Na katika maadili ambayo sheria ya mbinguni imekusaya kuhusu urekebishaji ni

uadilifu, usamehevu, kutelekeza ahadi, kutimiza amana, ukweli katika maneno na

matendo, kuwafanyia wema wazazi wawili, kuacha mali ya mayatima, kuchunga

haki za jirani na maneno mazuri hii ni kwa sababu chimbuko la sheria za mbinguni

ni moja, na kwa ajili hii mtume (rehma na amani zimshukie juu yake)amesema: “

manabii ni ndugu kwa aila za mama tafauti (lakini) dini yao ni moja.” (Bukhari).

Sheria zinaweza kutafautiana katika ibada na namna ya kuifanya kwa mujibu wa

zama na nyakati, lakini maadili na tabia za kiutu ambazo ni msingi wa kuishi hizi

huwa hazitafautiani katika sheria yoyote. Mtume (rehma na amani zimshukie juu

yake) “ katika yale waliyopata watu katika maneno ya mitume wa mwanzoni ni

kuwa utakapokuwa huna haya basi fanya utakacho.” Basi ni sheria gani

iliyohalalisha kuua nafsi ambayo Mwenyezi Mungu ameiharamisha kuuliwa

isipokuwa kwa haki au imehalalisha kuwatenga wazazi wawili, au kula haramu au

kula mali ya mayatima au kula mali za wafanyakazi?

Na ni sheria gani iliyohalalisha uongo, kuvunja ahadi, khiana, au kulipa mabaya

kwa wema? Yote haya ni kinyume, kwani sheria za mbinguni zimelingana na

kujikita katika maadili ya kiutu, na yeyote ambae ataziacha tabia hizi basi huwa

hajatoka tu katika sheria bali pia atakuwa ametoka katika mzunguko mzima wa

maadili na kujivua maumbile ya uanadamu wake ambayo Mwenyezi Mungu

amemuumbia.

Kwa ajili hiyo, Ibn Abas (rehma na amani ziwashukie juu yao) amesema kuhusu

kauli yake Mwenyezi Mungu {Sema: Njooni nikusomeeni aliyo kuharimishieni Mola wenu Mlezi.

Nayo ni kuwa, msimshirikishe Yeye na chochote. Na wazazi wenu wafanyieni wema. Wala msiwauwe

watoto wenu kwa sababu ya umasikini. Sisi tunakuruzukuni nyinyi na wao. Wala msikaribie mambo

machafu, yanayo onekana, na yanayo fichikana. Wala msiuwe nafsi ambayo Mwenyezi Mungu

ameharimisha kuiuwa, ila ikiwa kwa haki. Hayo amekuusieni ili myatie akilini. 026. Wala msiyakaribie

mali ya yatima ila kwa njia ya wema kabisa, mpaka afikilie utu-uzima. Na timizeni vipimo na mizani kwa

uadilifu. Sisi hatumkalifishi mtu ila kwa kadiri ya uwezo wake. Na msemapo semeni kwa uadilifu ingawa

ni jamaa. Na ahadi ya Mwenyezi Mungu itekelezeni. Hayo amekuusieni ili mpate kukumbuka 024. Na

kwa hakika hii ndiyo Njia yangu Iliyo Nyooka. Basi ifuateni, wala msifuate njia nyingine, zikakutengeni na

Njia yake. Haya amekuusieni ili mpate kuchamngu} [Al anaam 151-153]. Aya zenye

kuzungumzia hukumu hazikufuta chochote katika vitabu vyote, kwani nimambo

yaliyoharamishwa ka watu wote, nayo ni asili ya maandiko, yeyote atakayetenda

kwa mujibu wa aya hizo basi ataingia peponi na mwenye kuacha ataingia motoni.

Na mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) ametupigia mfano wa hali ya

juu katika kurekebisha – kusuluhisha kimaneno na kimatendo, na dua yake

ilikuwa ni kutaka marekebisho katika kila jambo, alikuwa akiomba ““ewe Mola

nirekebishie dini yangu ambayo ni hifadhi ya mambo yangu, na unirekebishie

dunia yangu ambayo ni maisha yangu, na unirekebishie akhera yangu ambayo

ni mareleo yangu, na nifanyie maisha kuwa na kila la kheri, na nifanyie umauti

wangu yawe ni starehe kwa kila ovu.” (Muslim).

Na alikuwa akisuluhisha kati ya watu, pia alikuwa na pupa ya kuondosha fitina

na hitilafu. Imepokewa kutoka kwa Sahli bin Saad (rehma na amani zimshukie

juu yake) “ kuwa watu wa Kubaa walipigana nakurembeana kwa mawe, mtume

akaelezwa jambo hilo, basi akasema: nipelekeni ili nikawasuluhishe.” (Bukhari)

Hakika ya wema na usuluhishaji ni nguzo madhubuti za kubaki kwa jamii na

kuendelea kwake, nasi tuna haja ya kurekebisha nafsi zetu kwanza na

kuzisafisha katika nyanja zote za kimasiha kama za kisiasa, kijamii kiuchumi na

kielimu pia. Kuirekebisha nafsi ni jambo litakiwalo na sheria na ni wajibu wa

kidini, na hasa katika wakati huu tulionao ambao imani imekuwa ni dhaifu na

uharibifu wa tabia na kupotea kwa haki na wajinu, watu wengi wakawa

hawaelewi haki ya mkubwa wala za jamaa, wazazi na za taifa.

Na katika kurekebisha ni kujichunga mtu juu ya haki yake na za wenzake,

asifnye uadui katika haki za wengine, na kila mtu aelewe wajibu wake na

autekeleze ipasavyo, kwani kufanya hivyo ni kutekeleza maadili mazuri na

kujiweka mbali na uharibifu na ufisadi katika ardhi na dhuluma na kuujaza

moyo chuki na hasada. Kwani hiki ni kiini cha urekebishaji, kila mtu

ajirekebishe yeye mwenyewe kwa ajili ya Mola wake na kwa ajili ya wenzake

na kwa ulimwengu mzima, kufanya hivyo atakuwa mtu mwema mwenye

kuweza kurekebisha na mwengine. Yaani kama kwamba kujirekebisha ni

kuitakasa nafsi kwa kuipamba kwa tabia njema na kuizuia na dhuluma na

madhambi na kutenda yaliyokatazwa na Mwenyezi Mungu, na kuiimarisha

ardhi pia kutoa hazina na siri zake ambazo manufa yake huwa kwa wote.

Kurekebisha huwa kwa mshikamano na si kwa mgawanyiko nao ni ule

unaolinganiwa na Kurani Tukufu, wema na usuluhishaji huakisi upendo na

usamehevu kati ya wana jamii kisha kwa umma mzima, na kwa kupitia

marekebisho vyanzo vya ugomvi hutoweka na chuki pamoja na husuda.

Nayo marekebisho hayana wakati maalumu, lakini mtu huwa hana budi

kuendeleza suluhisho hadi mwisho wa uhai wake na kwa ajili hiyo mtume

(rehma na amani zimshukie juu yake) ameashiria katika hadithi aliyoipokea

Anas bin Malik (Mwenyezi Mungu amwie radhi) “iwapo kiama kitasimama

na kwenye mkono wa mmoja wenu ana mbegu basi akiweza kuipanda na

aipande.” (Bukhari)

Na la muhimu kulitaja hapa ni kuwa suluhisho – marekebisho hayawezi

kuonekana mattund yake mpaka mtu aanze yeye mwenyewe kisha ndani ya

familia yake na kwa jamii yake. Marekebisho ni kitu cha lazima ili jamii iwe

sawa n taifa linufaike kwa usalama na kwa kazi na maendeleo na kueneza

upendo kati ya watu. Na yeyote afanyae juhudi kwa mali yake ili asuluhishe

kati ya watu waliohaimiana ajue kuwa mtume (rehma na amani zimshukie

juu yake) ameshamuombea dua akasema “hakika ya dini imeanza ngeni na

itarudi hali ya kuwa ni ngeni, basi uzuri ulioje kwa wageni (nao ni) ambao

wanarekebisha yale waliyoyaharibu watu baada yangu katika mwenendo

wangu (sunna zangu). (Tirmidhiy).

Suluhisho lina athari kubwa sana kwa mtu na kwa jamii, nazo: kuwezesha

maisha mazuri, Mwenyezi Mungu anasema {Mwenye kutenda mema,

mwanamume au mwanamke, naye akawa ni Muumini,tutamhuisha maisha

mema; na tutawapa ujira wao kwa bora ya waliyo kuwa wakiyatenda.}

[Anahl; 57]

Pia, kuokoka na maangamizo na uharibifu, Mwenyezi Mungu anasema {

Wala hakuwa Mola wako Mlezi wa kuihiliki miji kwa dhulma tu na hali watu

wake ni watenda mema} [Hud 447].

Na pia kuirithi ardhi, kwani kuirithi kwake kumeshartishwa kwanza kuweko

namarekebisho, Mwenyezi Mungu anasema {Na hakika tulikwisha andika katika

Zaburi baada ya Kumbukumbu, ya kwamba nchi watairithi waja wangu walio wema} [al

anbiya 413].

Vile vile kuwepo uongozi wa Mwenyezi Mungu na hifadhi yake kwa yule

aliyeshikamana na misingi sahihi ya marekebisho, Mwenyezi Mungu

amesema {Hakika Mlinzi wangu ni Mwenyezi Mungu aliye teremsha Kitabu.

Naye ndiye awalindae walio wema} [Al aaraf 454].

Pia kuna kuhifadhi kizazi, Mwenyezi Mungu {Na ama ukuta, huo ulikuwa ni

wa vijana wawili mayatima kule mjini. Na chini yake ilikuwako khazina yao;

na baba yao alikuwa ni mtu mwema. Basi Mola wako Mlezi alitaka wafikie utu

uzima na wajitolee khazina yao wenyewe, kuwa ni rehema itokayo kwa Mola

wako Mlezi. Wala mimi sikutenda hayo kwa amri yangu. Hiyo ndiyo tafsiri ya

hayo ambayo wewe hukuweza kuyasubiria}[Kahf; 43], kisa cha kujengwa

ukuta wa watoto waili mayatima kwenye kisa cha nabii Mussa (rehma na

amani zimshukie juu yake) kisa hiki kinajulikana, na kazi ya kujenga

haikuya ya bure lakini ilikuwa na athari ya wema ya mzazi wao. Imepokewa

kutoka kwa Abbas (Mwenyezi Mungu amwie radhi) ilikuwa ni kwa sababu

ya wema wa mzazi wao lakini haukutajwa wema wa watoto hao.

Pia suluhisho huleta usalama wa kutoogopa dunia na akhera, Mwenyezi

Mungu anasema { Na hatuwatumi Mitume ila huwa ni wabashiri na waonyaji. Na

wenye kuamini na wakatenda mema haitakuwa khofu juu yao, wala hawatahuzunika.}

[Al anaam; 24] pia huleta msamaha na upendo, Mwenyezi Mungu anasema

{. Na mkisikizana na mkamchamngu basi Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira na

Mwenye kurehemu} [Anisaa; 435]

Marekebisho yakifanyika juu ya kitu basi huwa kimepambika na ni tabia

ipendwayo na Mwenyezi Mungu na mtume wake (rehma na amani

zimshukie juu yake) kwani kupitia hayo maisha huenda itakiwavyo, na

umma unakuwa umeshikamana, myonge huwa na nguvu, waisilamu huwa

wamoja na neno lao huwa moja na huondosha mgawanyiko, na kueneza

upendo nayo ni dalili ya imani, mwenyezi mungu anasema {Hakika Waumini

ni ndugu, basi patanisheni baina ya ndugu zenu, na mcheni Mwenyezi Mungu

ili mrehemewe. }[Alhujraat; 41].

Na tukosapo thamani ya suluhisho basi umma utaharibika, familia

zitaporomoka, fujo zitaenea, ufisadi nao utashika nafasi na haki za

Mwenyezi Mungu zitavyunywa, maovu yatatendwa hapo ndipo jamii, taifa

na ustaarabu utakaposambaratika, kuacha kusuluhisha hupelekea kuenea

kwa adhabu hapa duniani na maangamizo ya kinafsi kama ufakiri, udhalili

na fedheha.

Sifa za waumini ndani ya kurani

17 jamad uwla 1437 H. 26022116

Imefasiriwa na

Profesa\ Ayman Ibrahim Alaasar

Kwanza: vipengele

Kumjua Mweneyzi Mungu ni njia ya imani

Imani na matendo mema ni mambo yenye mshikamano

Sifa za waumini

Kumuogopa Mwenyezi Mungu.

Kumtegemea Mwenyezi Mungu ipasavyo.

Kuhifadhi sala na kunyeyekea ndani yake.

Kutoa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.

Ukweli, uaminifu, kutimiza ahadi, haya na tabia njema.

Neema alizoziandaa Mwenyezi Mungu kwa waumini.

Pili: Dalili:

Dadili ndani ya Kurani tukufu

Mweneyzi Mungu Mtukufu anasema {1. Hakika wamefanikiwa Waumini,2.

Ambaoni wanyenyekevu katika Sala zao, 3. Na ambao hujiepusha na mambo

ya upuuzi, 4. Na ambao wanatoa Zaka. 5. Na ambao wanazilinda tupu zao, 6.

Isipo kuwa kwa wake zao au kwa iliyo wamilikimikono yao ya kulia. Kwani

hao si wenye kulaumiwa. 7. Lakini anaye taka kinyume cha haya, basi hao

ndiowarukao mipaka. 8. Na ambao wanazitimiza amana zao na ahadi zao, 9.

Na ambao Sala zao wanazihifadhi 11. Hao ndio warithi,} Almuuminun 1-11.

Mwenyezi Mungu anasema: {Hakika Waumini ni wale ambao anapo tajwa

MwenyeziMungu nyoyo zao hujaa khofu, na wanapo somewa Aya

zakehuwazidisha Imani, na wakamtegemea Mola wao Mlezi. 3. Hao ambao

wanashika Sala na wanatoa katika yale tunayo waruzuku 4. Hao kweli ndio

Waumini. Wao wana vyeo, na maghfira,na riziki bora, kwa Mola wao Mlezi.

}Al anfal, 2-4.

Mwenyezi Mungu anasema: {Kwa hakika hao ambao kwa kumwogopa Mola

wao Mleziwananyenyekea, 58. Na wale ambao Ishara za Mola wao

Mleziwanaziamini, 59. Na wale ambao Mola wao Mlezi hawamshirikishi,61.

Na wale ambao wanatoa walicho pewa, na hali nyoyo zao zinagopa kwa

kuwa watarejea kwa Mola wao Mlezi, 61. Basi wote hao ndio wanao kimbilia

katika mambo yakheri, na ndio watakao tangulia kuyafikia.} Almuuminun 57-

61.

Mwenyezi Mungu anasema {Na ukisha kata shauri basi mtegemee Mwenyezi

Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanao mtegemea.161.

Akikunusuruni Mwenyezi Mungu hapana wakukushindeni, na akikutupeni ni

nani, basi, baada yakeYeye ataye kunusuruni? Na Waumini wamtegemee

Mwenyezi Mungu tu} Al imran. 159-161.

Mwenyezi Mungu anasema: {Na waja wa Arrahman Mwingi wa Rehema ni

wale wanaotembea ulimwenguni kwa staha, na wajinga

wakiwasemezahujibu: Salama! 64. Na wale wanao kesha kwa ajili ya Mola

wao Mlezi kwa kusujudu na kusimama. 65. Na wale wanao sema: Mola wetu

Mlezi! Tuondolee adhabu ya Jahannamu. Hakika adhabu yake ikimpata

tuhaimwachi. 66. Hakika hiyo ni kituo na makao mabaya. 67. Na wale ambao

wanapo tumia hawatumii kwa fujo wala hawafanyi ubakhili, bali wanakuwa

katikati baina ya hayo.} Alfurqan 63-67.

Mwenyezi Mungu anasema: {Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na

kuweni pamoja na wakweli} Atawba,119.

Mwenyezi Mungu anasema: { Enyi mlio amini! Timizeni ahadi.

Mmehalalishiwawanyama wa mifugo, ila wale mnao tajiwa.

Lakinimsihalalishe kuwinda nanyi mmo katika Hija. HakikaMwenyezi Mungu

anahukumu apendavyo} Almaida,1.

Dalili ndani ya hadithi.

Kutoka kwa Ibn Umar (Mwenyezi Mungu amwie radhi) amesema: siku moja

tulipokuwa tumekaa pamoja na mtume (rehma na amani zimshukie juu yake)

akatutokezea mtu amevaa nguo myeupe sana ana nywele nyeusi

haikuonekana athari yoyote ya safari na hakuna yeyote kati yetu aliyemjua

mpaka akakaa mnele ya mtume (rehma na amani zimshukie juu yake)

akakutanisha magoti yake na magoti ya mtume na kuweka bega lake katika

bega la mtume kisha akasema: “ewe Muhammad nieleze kuhusu uisilamu.”

Mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) akasema: “ uisilamu ni

kushuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa

Mwenyezi Mungu na hakika Muhammad (rehma na amani zimshukie juu

yake) ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na kusimamisha sala, na kutoa zaka

na kufunga ramadhani na kuhiji nyumba ukiwa na uwezo. Akasema:

“umesema kweli.” Akasema: “ nieleze kuhusu imani.” Akasema: “kumuamini

Mwenyezi Mungu na malaika wake na vitabu vyake na siku ya mwisho na

kuamini kadari kheri yake na shari yake. Akasema: “ umesema kweli.”

Akasema: “ nieleze kuhusu ihsani. Akasema: “ni kumuabudu Mwenyezi kama

kama kwamba unamuona na iwapo humuoni basi yeye anakuona. Akasema:

“Umesema kweli.” Akasema: “ nieleze kuhusu kiama. Akasema: “huenda

muulizaji akawa anaelewa zaidi kuliko anaeulizwa. Akasema: “ nieleze ishara

zake” akasema: “ mtumwa kuzaa bwana wake na kuwaona wachungaji

watembeao miguu peku wanashindana katika ujenzi wa majumba makubwa.

Akasema, kisha akaondokam nikabaki hali ya kufikiria, kisha nikamuuliza ewe

Umar unamjua ni nani huyo muulizaji? Akasema: “ Mwenyezi Mungu na

mtume wake wanaju. Akasema Yule ni Jibrilu amekujieni kukufundisheni dini

yenu.” (Muslim)

Kutoka kwa Anas bin Malik (Mwenyezi mungu amwie radhi)hakika ya mtume

(rehma na amani zimshukie juu yake siku moja alitoka na akakutana na kijana

wa kianswar anaitwa Haritha bin Nuuman, akamwambia: “ umeamkaje ewe

Haritha? Akasema: nimeamka hali ya kuwa ni muumini wa kweli. Akasema

mtume wa Mweneyzi Mungu (Rehma na amani zimshukie juu yake) angalia

usemacho, kwani kila haki ina kithibitisho, basi ni upi huo uthibitisho wa

imani yako? Akasema: Najizoea nafsi yangu kujiepusha na ya dunia,

nikakesha usiku wangu na kufunga mchana wangu, nami kama kwamba

naagalia Arshi ya Mola wangu iliyo wazi na kama kwamba naagalia watu wa

peponi namna wanavyotembeleana, na kama kwamba naangalia watu wa

motoni na namna wanavyofanyiana uadui ndani yake. Mtume rehma na

amani ziwe juu yake akamwambia. Umeona (umesema kweli) basi

jilazimishe. Kasema hivi mara mbili, mja Mwenyezi Mungu amenawirisha

imani ndani ya moyo wake.” (sehemu ya imani).

Kutoka kwa Abi Hurayra (mwenyezi Mungu amwie radhi) amesema:

amesema mjumbe wa Mweneyzi Mungu (rehma na amani zimshukie juu

yake) imani ni sehemu sabini au sitini ya mafungu na bora ya (mafungu haya)

ni kauli ya “Lailaha illa llahu” (hapana wa kuabudiwa kwa haki isipokuwa

Mwenyezi Mungu na kuondosha uchafu njiani na kuona haya ni sehemu ya

imani.” (Muslim)

Kutoka kwa Umar (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) amesema,

nimemsikia mjumbe wa Mweneyzi Mungu (rehma na amani zimshukie juu

yake) akisema: “ lau kama mungelimtegemea Mwenyezi Mungu kama

ipasavyo basi angelikupeni riziki kama ampavyo ndege, huondoka asubuhi

ana njaa na kurudi jioni ameshiba.” (Tirmidhi).

Kutoka kwa Ibn Abbas (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao) amesema,

mtume alikwenda kwa Umar alipokuwa yupo na masahaba zake, akasema:

“je nyinyi ni waumini?” hawakujibu. –akawauliza mara tatu- kisha mwishoni

Umar akasema. “ndio, tunaamini kile ulichotuletea, na kushukuru juu ya hali

nzuri na kusubiri juu ya balaa, na tunaamini kadari. Mtume (rehma na amani

zimshukie juu yake) Akasema: “hakika mumeamini kwa jina la Mola wa

Alkaba.” (Tabari).

Tatu: maudhui

Miongoni mwa rehema za Mwenyezi Mungu ni na upendo wake kwa waja

wake ni kuwapelekea mitume ili wawaongoze katika njia ya haki, na katika

njia iliyonyooka, ili isije ikapatikana hoja kwa mja yeyote mbele ya Mwenyezi

Mungu. Mwenyezi Mungu anasema { Mitume hao ni wabashiri na waonyaji,

ili watuwasiwe na hoja juu ya Mwenyezi Mungu baada ya kuletewaMitume.

Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima }Anisaa 165.

Kumuamni Mwenyezi Mungu ni katika ilaka kubwa walizokuja nazo mitume,

ikiwa na maana kuthibiti imani ya Mwenyezi Mungu –itikadi- ndani ya moyo

wa mja, na kuamini malaika wake, vita vyake, mitume wake, na siku ya

mwisho na kadari kheri zake na shari zake. Na waumini itawalazimu watimize

wajibu wa imani nao ni kutimiza yale waliyokalifishwa ambayo yana uongofu

kutoka kwa Mwenyezi Mungu yaliyoletwa kutoka kwa mtume wetu (rehma

na amani zimshukie) katika makatazo na mahimizo.

Na kumjua Mwenyezi Munguni njia ya kwanza ya imani, Mwenyezi Mungu

anasema { Basi jua ya kwamba hapana mungu ila Mwenyezi Mungu, na omba

maghufira kwa dhambi zako na za Waumini wanaume na Waumini

wanawake. Na Mwenyezi Mungu anajua mahali penu pa kwenda na kurudi,

na mahali penu pakukaa.} Muhammah, 19.

Na kitu kijulikanacho ni kuwa imani ya Mwenyezi Mungu imeshikamana na

matendo mema, na wala havitengani, imekuja katika kurani tukufu ndani ya

aya nyingi, kwa mfano, { Na wale walio amini na wakatenda mema, hao

ndiowatu wa Peponi, humo watadumu }Albaqara 82. Na { Hakika walio amini

na wakatenda mema, Mola wao Mlezi atawaongoa kwa sababu ya Imani yao.

Itakuwa inapita mito kati yao katika Mabustani yenye neema }Yunus 9. Na

aliposema { Hakika wale walio amini na wakatenda mema mashukio yao

yatakuwa kwenye Pepo za Firdausi }kahf 117. Na aya nyeginezo zilizo tukufu.

Imani huzidi kwa kutii na hupungua kwa maasi, na kuna sehemu (makundi)

tafauti za waumini kwa mujibu wa imani zao kwa Mwenyezi Mungu. Kutoka

kwa Abi Hurayra amesema: amasema mjumbe wa Mwenyezi Mungu (rehma

na amani zimshukie juu yake) imani ni sehemu sabini au sitini ya mafungu na

bora ya (mafungu haya) ni kauli ya “Lailaha illa llahu” (hapana wa kuabudiwa

kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na kuondosha uchafu njiani na kuona

haya ni sehemu ya imani.” Na matendo mema ni sehemu ya imani.

Na imekuja katika hadithi ya Jibrilu – juu yake rehema- iliyo mashuhuri

inayoweka wazi ukweli wa imani ambayo inapaswa kuwepo ndani ya nyoyo

ya kila muumini, hadithi yenyewe, anasema umar (Mweneyzi mungu amwie

radhi) amesema: siku moja tulipokuwa tumekaa pamoja na mtume (rehma

na amani zimshukie juu yake) akatutokezea mtu amevaa nguo myeupe sana

ana nywele nyeusi haikuonekana athari yoyote ya safari na hakuna yeyote

kati yetu aliyemjua mpaka akakaa mnele ya mtume (rehma na amani

zimshukie juu yake) akakutanisha magoti yake na magoti ya mtume na

kuweka bega lake katika bega la mtume kisha akasema: “ewe Muhammad

nieleze kuhusu uisilamu.” Mtume (rehma na amani zimshukie juu yake)

akasema: “ uisilamu ni kushuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa

kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na hakika Muhammad (rehma na

amani zimshukie juu yake) ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na kusimamisha

sala, na kutoa zaka na kufunga ramadhani na kuhiji nyumba ukiwa na uwezo.

Akasema: “umesema kweli.” Akasema: “ nieleze kuhusu imani.” Akasema:

“kumuamini Mwenyezi Mungu na malaika wake na vitabu vyake na siku ya

mwisho na kuamini kadari kheri yake na shari yake. Akasema: “ umesema

kweli.” Akasema: “ nieleze kuhusu ihsani. Akasema: “ni kumuabudu

Mwenyezi kama kama kwamba unamuona na iwapo humuoni basi yeye

anakuona. Akasema: “Umesema kweli.” Akasema: “ nieleze kuhusu kiama.

Akasema: “huenda muulizaji akawa anaelewa zaidi kuliko anaeulizwa.

Akasema: “ nieleze ishara zake” akasema: “ mtumwa kuzaa bwana wake na

kuwaona wachungaji watembeao miguu peku wanashindana katika ujenzi wa

majumba makubwa. Akasema, kisha akaondokam nikabaki hali ya kufikiria,

kisha nikamuuliza ewe Umar unamjua ni nani huyo muulizaji? Akasema: “

Mwenyezi Mungu na mtume wake wanaju. Akasema Yule ni Jibrilu

amekujieni kukufundisheni dini yenu.” (Muslim).

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ameweka wazi katika kitabu chake kitukufu

sifa nyingi za waja wake waumini,kwa mfano, unyenyekevu kwa ajili ya

Mwenyezi Mungu, kwa kuwa unyenyekevu ni vyeo vya juu kabisa, Mwenyezi

Mungu anasema { Hakika Waumini ni wale ambao anapo tajwa

MwenyeziMungu nyoyo zao hujaa khofu, na wanapo somewa Aya

zakehuwazidisha Imani, na wakamtegemea Mola wao Mlezi. 3. Hao ambao

wanashika Sala na wanatoa katika yale tunayo waruzuku 4. Hao kweli ndio

Waumini. Wao wana vyeo, na maghfira,na riziki bora, kwa Mola wao

Mlezi.}Al anfal 2-4. Na anasema { Kwa hakika hao ambao kwa kumwogopa

Mola wao Mleziwananyenyekea, 58. Na wale ambao Ishara za Mola wao

Mleziwanaziamini, 59. Na wale ambao Mola wao Mlezi hawamshirikishi,61.

Na wale ambao wanatoa walicho pewa, na hali nyoyo zao zinagopa kwa

kuwa watarejea kwa Mola wao Mlezi, }Al muuminuun 57-61. Na anasema pia

{ Hakika wewe unamwonya mwenye kufuata ukumbusho, naakamcha

Arrahman, Mwingi wa Rehema, kwa ghaibu. Basimbashirie huyo msamaha na

ujira mwema.} Yasini, 11.

Na mtume (rehma na amani zimshukie juu yake ametupigia mfano wa hali ya

juu ya unyenyekevu. Kutoka kwa Mutarif kutoka kwa baba yake amesema:

nimemuona mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) akisali na katika

kifua chake kuna mgurumo kama mgurumo wa chombo .” (Ibn Khuzayma).

Na mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) alikuwa akimuomba

Mweneyzi Mungu ampe unyenyekevu, kutoka kwa Abi Mijlaz (radhi za

Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) amesema: Umar alitusalisha sala,

akaifupisha, na akapinga (kuwa hakufupisha) akasema, kwami sijatimiza

rukuu na sujudu? Wakasema: ndio” akasema: “kwa kuwa mimi nimeomba

kwakati wa sujudu na kurukuu dua aliyokuwa akiomba mtume (rehma na

amani zimshukie juu yake) akiomba “ewe Mola kwa elimu yako ya

visivyojulikana na kudura zako kwa viumbe nihuishe iwapo uhai una kheri

nami na unifishe iwapo kifo kina kheri nami, nakuomba unyenyekevu wako

kwa nikionacho na nisichokiona na neno la kweli niwapo na hasira na

kuridhia, na lengo wakati wa umasikini na utajiri, na kadha ya kuona uso

wako na hamu ya kukutana nawe na najikinga kwako kutokana na madha

yenye kudhuru na fitina zenye kupoteza, ewe Mola zipambe nyoyo zeteu kwa

imani na utufanye katika walioongoka.” (Ahmad).

Mshairi anasema:

Muogope mola na tarajia kila zuri * usiitii nafsi kwa maasi utajuta.

Kuwa na khofu na matarajio * na jibashirie msamaha wa Mungu iwapo ni

muisilamu.

Namiongoni mwa sifa za waumini ni kumtegemea Mwenyezi Mungu, ikiwa

na maana kuufanya moyo umtegemee Mwenyezi Mungu katika kuleta

masilahi na kuondoa madhara, na kumuachia mambo yote Yeye pamoja na

kuitakidi kuwa hakuna atoaye wala azuiaye na anayedhuru na kunufaisha

isipokuwa Yeye pekee. Muumini humtegemea Mwenyezi Mungu na hutenda

sababu zenye kupelekea kutimia matendo bila ya kutegemea matendo hayo.

Kufanya sababu haina maana kuwa humtegemei Mwenyezi Mungu, kutoka

kwa Umar (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) amesema, nimemsikia

mjumbe wa Mweneyzi Mungu (rehma na amani zimshukie juu yake) akisema:

“ lau kama mungelimtegemea Mwenyezi Mungu kama ipasavyo basi

angelikupeni riziki kama ampavyo ndege, huondoka asubuhi ana njaa na

kurudi jioni ameshiba.” (Tirmidhi).

Ama kwa wale wanaodai kuwa kumtegemea Mwenyezi mungu bila ya

kufanya kazi huku hakuitwi kumtegemea Yeye bali huko ni kuzembea na

kuzembea ametukataza mtume (rehma na amani zimshukie) na pia kukataza

sababu zinazopelekea kuzembea, kutoka kwa Muadh bin jabal ( Mwenyezi

Mungu amwie radhi) amesema; nilikuwa nyuma ya punda wa mtume (rehma

na amani zimshukie) akiitwa Ukayr. Akasema (mtume) ewe Muadh hivyo

unafahamu haki ya Mwenyezi Mungu juu ya waja na haki za waja kwa

Mweneyzi Mungu? Akasema: Mwenyezi Mungu na mtume wake wanajua.

Akasema: “haki ya Mwenyezi Mungu juu ya waja ni kumuabudu Mwenyezi

Mungu na wala wasimshirikishe na chochote na haki za waja kwa Mwenyezi

Mungu ni kutomwadhibu Yule asiyemshirikisha na chochote.” Akasema: ewe

mjumbe wa Mwenyezi Munguje niwaambie watu hivyo? Akasema:

“usiwaambie ili wasije kuzembea” (muslim). Kumtegemea kunakotakiwa

kunashikamana na maisha ya muumini, manufaa hayatopatikana au madhara

isipokuwa kwa utegemezi ulio mzuri.

Na miongoni mwa sifa za waumini ni kuhifadhi sala na kunyeyekea ndani

yake. Mwenyezi Mungu anasema { Hakika wamefanikiwa Waumini,2. Ambao

ni wanyenyekevu katika Sala zao,}. Sala ni alama ya uisilamu na imeamrishwa

kupitia aya nyingi Mwenyezi Mungu anasema{Na shikeni Sala, na toeni Zaka,

na inameni pamoja na wanao inama}Albaqara 43. Na mtume (rehma na

amani zimshukie) akaifanya ni moja ya nguzo tano za kiisilamu, kutoka kwa

Ibn Umar (Mwenyezi Mungu awawie radhi) amesema; amesema mjumbe wa

Mwenyezi Mungu (reahma na amani zimshukie) “ uisilamu umejemngea juu

ya nguzo tano: kushuhudia kuwa hapana Mola wa haki isipokuwa Mwenyezi

Mungu, na Muhammad ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu nakusimamisha

sala, na kutoa zaka, na kuhiji nyumba na kufunga Ramadhani.” (Bukharin a

Muslim).

Na watu wametafautiana kidaraja za unyenyekevu ndani ya sala, wapo

wapatao malipo kamili, na wengine hawana wapatacho zaidi ya

kujihangaisha na tabu, kutoka kwa Abi Hurayra (Rehma na amani ziwe juu

yake) amemsikia mjumbe wa Mwenyezi Mungu akisema: “ huenda

anaesimama usiku kusali fungu lake likawa ni kukesha tu usiku, na huenda

anaefunga fungu lake likawa ni kukaa na njaa na kiu.” (Albaihaqi). Sala ni

sababu za kuifunza nafsi tabia na nyendo na kujiweka mbali na yenye

kuchukiza, mwenye kusali huwa yuko mbali sana na sababu za kuingia katika

maasi na maovu. Mwenyezi Mungu anasema { na ushike Sala.Hakika Sala

inazuilia mambo machafu na maovu.}Al ankabuut 45. Na katika yenye

kuthibitisha kuwa ni lazima sala iwe na unyenyekevu ni hadithi iliyopokelewa

na Anas bina Malik (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake)amesema;

amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani zimshukie juu

yake) inakuwaje watu hunyanyua macho yao juu (mbinguni) ndani ya sala

zao, akasisitizaneno lake hili mpaka akasema: waache hivyo au Mwenyezi

Mungu atapofua macho yao.” (Bukhari).

Na miongoni mwa sifa za waumini ni kutoa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kwa

maana ya utoaji wa zaka iliyolazimishwa na sadaka za kujitolea, kutoka kwa

Ibn Umar (Mwenyezi Mungu amwie radhi) amesema: “mkono wa juu (utoao)

ni bora kuliko wa chini (usiotoa), na anza kwa unaowalisha, na sadaka iliyo

bora ni ile itolewayo kwa kificho na anayeacha kuomba Mungu atamsaidia na

anayejitosheleza basi Mungu atamtoshelezea.” (Bukhari). Kutoka kwa Ibn

Masuud (Mwenyezi Mungu amwie radhi) amepokea kutoka kwa mtume

(rehma na amani zimshukie juu yake) amesema: “ mtu akitoa kwa ajili ya

watu wake huhesabiwa ni katika sadaka.” (muslim). Muumini huamini kuwa

mali aliyonayo ni kama dhamana kwake, na fadhila zipo mikononi mwa

Mwenyezi Mungu. Kutoka wa Abi Hurayra (Mwenyezi Mungu amwie radhi)

kwamba mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) amesema: “ kijana

mmoja alipokuwa akitembea jangwani akasikia sauti utoka mawinguni,

nyoshelezea bustani ya Fulani, mawingu yale yakasogea kachota maji yake

katika chombo, tahamaki kile chombo kikajaa maji chote, mara kuna mtu

mwengine amemsimama kwenye bustani yake akijaribu kunyoshelezea maji,

akamwambia: ewe mja wa Mweneyzi Mungu, unaitwa nani? Akasema, ni

Fulani lile jina alililisokia kutoka katika mawingu, akamwambia, kwa nini

unaniulia jina langu, akamwambia: “ nimesikia sauti kutoka mawinguni

ambayo yamenipa maji yake, yakisema “ nyosheleza bustani ya Fulani kwa

kutaja jina lako, wewe kwani unafanya nini ndani ya bustani hiyo? Akajibu:

“kwa kuwa umeuliza basi mimi huwa matunda yakiwa tayari basi hutoa

sadaka thuluthi na mimi mwenyewe na wanangu hula thuluthi najirudisha

thuluthi yake.

Na kurani imeashiria sifa za waumini kama ifuatavyo kwa mfano,

wanajiepusha nay a upuuzi, na huchunga amana, Mwenyezi Mungu anasema

{1. Hakika wamefanikiwa Waumini,2. Ambaoni wanyenyekevu katika Sala

zao, 3. Na ambao hujiepusha na mambo ya upuuzi, 4. Na ambao wanatoa

Zaka. 5. Na ambao wanazilinda tupu zao, 6. Isipo kuwa kwa wake zao au kwa

iliyo wamilikimikono yao ya kulia. Kwani hao si wenye kulaumiwa. 7. Lakini

anaye taka kinyume cha haya, basi hao ndiowarukao mipaka. 8. Na ambao

wanazitimiza amana zao na ahadi zao, 9. Na ambao Sala zao wanazihifadhi

11. Hao ndio warithi, 11. Ambao watairithi Pepo ya Firdausi, wadumu humo}

Almuuninuun 1-11. Aya zikaweka wazi kuwa mafanikio na kufuzu ni kwa

atakayesifika kwa sifa hizi za unyenyekevu ndani ya sala, kujiepusha na

upuuzi, kutoa zaka, kuhifadhi tupu, kuhifadhi amana na kuzifikisha kwa

wenyewe, kutimiza ahadi na yote hayo yametajwa ndani ya kurani kama ni

sifa kwa waumini na tabia zao.

Kwa waumini ni lazima wawe na tabia ya kutimiza ahadi kama ilivyokuja

ndani ya kurani ili ajidhaminie mafanikio duniani na akhera, ikipatikana imani

ndani ya moyo wa mja kama itakiwavyo basi itamuhifadhi na chuki na itikadi

kali na kutenda yaliyokatazwa na itamfanya ampendelee mwengine zaidi

kuliko hata nafsi yake na atajiepusha na kauli za uongo na kukaa vikao vya

kipuuzi, na atakuwa na pupa ya kufanya mema kwa ajili ya manufaa ya jamii

na taifa lake. Ama kwa wanaojidai kuwa ni wauminina tabia zake zikawa ni

mbaya na mwenendo wake ukawa si mzuri basi imani yake huwa ni pungufu.

Kwani imani ahihi hujulikana, Kutoka kwa Anas bin Malik (Mwenyezi mungu

amwie radhi)hakika ya mtume (rehma na amani zimshukie juu yake siku moja

alitoka na akakutana na kijana wa kianswar anaitwa Haritha bin Nuuman,

akamwambia: “ umeamkaje ewe Haritha? Akasema: nimeamka hali ya kuwa

ni muumini wa kweli. Akasema mtume wa Mweneyzi Mungu (Rehma na

amani zimshukie juu yake) angalia usemacho, kwani kila haki ina kithibitisho,

basi ni upi huo uthibitisho wa imani yako? Akasema: Najizoea nafsi yangu

kujiepusha na ya dunia, nikakesha usiku wangu na kufunga mchana wangu,

nami kama kwamba naagalia Arshi ya Mola wangu iliyo wazi na kama

kwamba naagalia watu wa peponi namna wanavyotembeleana, na kama

kwamba naangalia watu wa motoni na namna wanavyofanyiana uadui ndani

yake. Mtume rehma na amani ziwe juu yake akamwambia. Umeona

(umesema kweli) basi jilazimishe. Kasema hivi mara mbili, mja Mwenyezi

Mungu amenawirisha imani ndani ya moyo wake.” (sehemu ya imani).

Inatakiwa muumini asifike kwa sifa njema za ukweli, uaminifu, kutekeleza

ahadi, ukarimu, haya, msimamo, upole, msamaha, unyeyekevu, uadilifu,

hisani, kuathiri na tabia nyengine njema ambazo kurani imehimiza, Mwenyezi

Mungu anasema {Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na kuweni

pamoja na wakweli}At tawbah 119. Na akasema { Na ambao wanazichunga

amana zao na ahadi zao } Al maarij 32. Na akasema kuhusu alama za wakweli

wacha Mungu. { na wanao timiza ahadi yao wanapo ahidi, na wanaovumilia

katika shida na dhara na wakati wa vita; haondio walio sadikisha, na hao ndio

wajilindao } Al baqara 177.

Na Mwenyezi Mungu amewandalia waumini wenye kusifika kwa tabia njema

kwa malipo mazuri na thawabu njema, akasema { Hakika wale walio amini na

wakatenda mema mashukio yao yatakuwa kwenye Pepo za Firdausi118.

Watadumu humo; hawatataka kuondoka.} Kahf 117-118.

Uhusiano wa kifamilia ulio bora

23 Jamad Akhir 1437 H. sawa na 1 Aprili 2116 AD

Vipengele

Nafasi ya familia katika uisilamu.

Njia za uongofu katika kuwepo kwa utulivu wa kifamilia.

Uchaguzi bora

Kuchunga ya haki na yaliyo lazima

Kuwepo kwa upendo na huruma

Kuishi kwa salama

Uadilifu kati ya watoto.

Athari za kuwepo kwa utulivu wa familia katika jamii.

Pili: dalili

Ndani ya Qurani Tukufu.

Mwenyezi Mungu anasema {Na katika Ishara zake ni kuwa amekuumbieni

wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao.Naye amejaalia

mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara

kwa watu wanaofikiri} (Aruum. 21).

Mwenyezi Mungu anasema { Na Mwenyezi Mungu amekuumbieni mwake

katika jinsi yenu, na akakujaalieni kutoka kwa wake zenu wana na wajukuu,

na akakuruzukuni vitu vizuri vizuri. Basi je, wanaamini upotovu na

wanazikataa neema za Mwenyezi Mungu?}(An hahl. 72)

Mwenyezi Mungu anasema { Na waozeni wajane miongoni mwenu na wema

katika watumwa wenu na wajakazi wenu. Wakiwa mafakiri Mwenyezi Mungu

atawatajirisha kwa fadhila yake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa

Mwenye kujua.}(An nuur 32)

Mwenyezi Mungu anasema { Nao wanawake wanayo haki kwa Sharia kama

ile haki iliyo juu yao. }(Al baqara 228)

Mwenyezi Mungu anasema { Na kaeni nao kwa wema, na ikiwa

mmewachukia, basi huenda mkakichukia kitu, na Mwenyezi Mungu ametia

kheri nyingi ndani yake.}(Anisaa 19.)

Mwenyezi Mungu anasema {Na mkichelea kutakuwapo mfarakano baina ya

mke na mume basi pelekeni muamuzi kutokana na jamaa za mume,na

muamuzi kutokana na jamaa za mke. Wakitaka mapatano Mwenyezi Mungu

atawawezesha. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye khabari}(Anisaa

35)

Mwenyezi Mungu anasema { Mwenye wasaa atoe kadiri ya wasaa wake, na

mwenye dhiki atoe katika alicho mpa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu

hamkalifishi mtu ila kwa kadiri ya alicho mpa. }(Atalaak.7)

Dalili katika hadithi

Kutoka kwa Abdallah bin Masuud (radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie)

amesema: Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani

zimshukie) “ enyi vijana mweneye kuweza miongoni mwenu kuoa basi na

aowe, kwani hivyo ni kuinamisha macho na kuhifadhi tupi. Na asiyeweza basi

afunge kwani hiyo ni kinga.” (Bukhari na Muslim).

Na kutoka kwa Abi Hurayra (radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie) amesema:

Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani zimshukie) :

“mwanamke huolewa kwa mambo manne; kwa mali yake na nasaba (ukoo)

yake na uzuri wake na dini yake, chagua aliye na dini ili ubarikiwe mikono

yako.” (Bukhari).

Kutoka kwa Anas (radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie) amesema: Wageni

watatu walikuja katika nyumba za wake wa Mtume (rehma na amani

zimshukie) kuja kuuliza kuhusu ibada ya Mtume (rehma na amani zimshukie)

na walipoelezwa wakawa kama kwamba wamejiona ni wadogo wakasema:

“tuko wapi sisi na Mtume? Amekwishasamehewa madhambi yaliyotangulia

na yaliyochelewa. Na mmoja wao akasema: “ ama mimi nitasali sala za usiku

milele. Mwengine akasema: “ mimi nitafunga na wala sitofuturu. Na wa

mwisho akasema: “ama mimi nitajiepusha na wanawake na sitaoa milele.

Mtume (rehma na amani zimshukie) akawaendea akasema: “ni nyinyi

muliosema hivi na hivi, ama mimi naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu

ninamuogopa Mweneyzi Mungu kuliko nyinyi nyote lakini ninafunga na

kufuturu, ninasali na kulala na ninaoa wanawake, na mwenye kujiweka mbali

na mwenendo wangu basi hayuko nami.” (Bukhari.)

Kutoka kwa Abi hatim Almuzaniy amesema: amesema Mjumbe wa Mwenyezi

Mungu (rehma na amani zimshukie): atakapokujieni Yule munayemridhia dini

yake na tabia zake basi muozesheni, na musipofanya hivyo itakuwa ni fitina

duniani na ufisadi. Wakasema: “ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu na akiwa

naye? “ akasema: “atakapokujieni Yule munayemridhia dini yake na tabia

zake basi muozesheni, mara tatu. (Tirmidhi) na katika kitabu cha Bayhaqi

(atakapokuja yule munayemridhia dini yake na tabia zake basi muozesheni,

na musipofanya hivyo itakuwa ni fitina katika dunia na ufisadi mkubwa mno.)

Kutoka kwa Umar (Mwenyezi Mungu amwie radhi) hakika Mtume (rehma na

amani zimshukie juu yake) amesema: nyote ni wachungaji, na nyote

mutaulizwa juu ya mulivyovichunga. Imamu ni mchungaji naye ataulizwa juu

ya aliowachunga, mume ni mchungaji juu ya watu wake naye ataulizwa juu

ya aliowachunga, mke ni mchungaji katika nyumba ya mumewe naye

ataulizwa juu ya aliowachunga, mtumishi ni mchungaji juu ya mali ya bwana

wake naye ataulizwa juu ya alichokichunga.” Mpokezi akasema nadhani

alisema: “kijana ni mchungaji wa mali ya baba yake naye ataulizwa juu ya

alichokichunga, nyote ni wachungaji na mutaulizwa juu ya mulichokichunga.”

(Bukhari)

Kutoka kwa Abdallah bin Amru bin Al`as (Radhi za mwenyezi Mungu ziwe juu

yao) amesema: nimemsikia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu akisema:

“inatosha mtu kuwa na madhambi kwa kukizembea kile

anachokilisha.”(Ahmad). Na katika mapokezi ya Hakim (inatosha mtu kuwa

na madhambi kwa kukizembea kile anachokilea.)

Maudhui

Uisilamu umejali sana familia kwani ni nguzo ya kwanza ya kujenga, jamii

familia ikitengemea na jamii nayo hutengemea na ikiharibika na jamii pia

huharibika. Kwa ajili hiyo uisilamu ukaweka shuruti na vipimo

vitakavyosimamia jambo hili, kwa ajili ya kuwepo na utulivu na usalama kwa

lengo la kuhifadhi watu na jamii nzima, kwani utulivu wa familia ni utulivu wa

jamii.

***********************

Uisilamu umefuatilia uhumimu wa familia hata kabla ya makutano (ndoa)

katika wa wanajamii kwa kutaka kuwepo upendo, huruma na ushirikiano na

kupunguza kila kinachopelekea uharibifu wa jengo hilo. Na ukawataka

wafuasi wake kutengeneza familia kwa njia zinazokubalika zenye kuhifadhi

utu na heshima ya mwanadamu yenye kwenda sambamba na maumbile yake

na njia hiyo ni ya kuozana ambayo ni mojawapo ya mwenendo wa Mwenyezi

Mungu kwa viumbe vyake vyote. {na kila kitu tumekiumba viwiliviwili ili

mupate kukumbuka} (Adhariyat. 49). Na anasema pia {utukufu ni wake

aliyeumba kike na kiume katika vile viotavyo katika ardhi na katika nafsi zenu

na katika vile musivyovijua} Yaasin. 36). Ndoa ni mwenendo wa kimaumbile.

Na mwenyezi Mungu akaifanya kuwa ni mojawapo ya ishara za utukufu wake

na nguvu zake na miujiza yake mikubwa yenye kushangaza, akasema { Na

katika Ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu

ili mpate utulivu kwao.Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu.

Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanaofikiri.}(Ruum.

21).

Na kama uisilamu ulivyopendekezesha kutengeneza familia na utulivu wake

kuwa ni kuijenga ardhi na kuleta masilahi kwa jamii na ujenzi wa taifa na

kuwa ni njia ya kufikia katika lengo lililokusudiwa: nalo ni kueneza heshima

na utu na kuilinda jamii kutokana na aina zote za uchafu na maovu, na

kuunganisha familia kwa njia ya kuozana, pamoja na hekima nyengine na

malengo yaliyo mazuri. Mwenyezi Mungu anasema { Na waozeni wajane

miongoni mwenu na wema katika watumwa wenu na wajakazi wenu.

Wakiwa mafakiri, Mwenyezi Mungu atawatajirisha kwa fadhila yake. Na

Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa Mwenye kujua. 33. Na wajizuilie na

machafu wale wasio pata chakuolea, mpaka Mwenyezi Mungu awatajirishe

kwa fadhila yake. Na wanao taka kuandikiwa uhuru katika wale ambao

mikono yenu ya kulia imewamiliki, basi waandikieni kama mkiona wema

kwao. Na wapeni katika mali ya Mwenyezi Mungu aliyo kupeni. Wala

msiwashurutishe vijakazi vyenu kufanya zina kwa ajili ya kutafuta pato la

maisha ya dunia, ilhali wao wanataka kujihishimu.Na atakaye walazimisha

basi Mwenyezi Mungu baada ya kulazimishwa kwao huko, atawasamehe,

kwani Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.} (Anuur

32.33). bali pia Mtume (rehma na amani zimshukie) amewahimiza vijana

wafikie lengo la kuona kwa kuweka wazi manufaa yake na faida zake

akasema: ““ enyi vijana mwenye kuweza miongoni mwenu kuoa basi na

aowe, kwani hivyo ni kuinamisha macho na kuhifadhi tupi. Na asiyeweza basi

afunge kwani hiyo ni kinga.” (Bukhari na Muslim).

Kinyume na hivyo, uisilamu umekataza mambo yenye kupingana na

uimarishaji wa ulimwengu, mfano kukaa bila ya kuoa na kujiweka mbali na

wanawake (kukataa kuoa), mtme (rehma na amani zimshukie) amekataza

kukaa bila ya kuoa, Saad bin abi Waqas (radhi za Mwenyezi Mungu

zimshukie) amesema, hali ya mtume (rehma na amani zimshukie) kumjibu

Othman bin Mad ghun kuhusu kuacha kuoa, na lau kama angeruhusiwa basi

nasisi tungelihusika pia.” (Muslim). Na kutoka kwa Anas (radhi za Mwenyezi

Mungu zimshukie) amesema wageni watatu walikuja katika nyumba za wake

wa Mtume (rehma na amani zimshukie) kuja kuuliza kuhusu ibada ya Mtume

(rehma na amani zimshukie) na walipoelezwa wakawa kama kwamba

wamejiona ni wadogo wakasema: “tuko wapi sisi na Mtume?

Amekwishasamehewa madhambi yaliyotangulia na yaliyochelewa. Na mmoja

wao akasema: “ ama mimi nitasali sala za usiku milele. Mwengine akasema: “

mimi nitafunga na wala sitofuturu. Na wa mwisho akasema: “ama mimi

nitajiepusha na wanawake na sitooa milele. Mtume (rehma na amani

zimshukie) akawaendea akasema: “Ni nyinyi muliosema hivi na hivi, ama

mimi naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu ninamuogopa Mweneyzi Mungu

kuliko nyinyi nyote lakini ninafunga na kufuturu, ninasali na kulala na ninaoa

wanawake, na mwenye kujiweka mbali na mwenendo wangu basi hayuko

nami.” (Bukhari.)

Na ilivyokuwa utulivu wa familia ni kitu kitakiwacho kisheria na hata kidunia

basi usilamu ukaweka nguzo madhubuti na misingi imara ili ukoo na familia

idumu kati ya wanandoa na upatikane utulivu unaotakiwa, na miongoni mwa

misingi hiyo ni:-

Uchaguzi mwema kwa kila mwanandoa kwa mwengine, Mtume (rehma na

amani zimshukie) aliusia wakati wa kuchagua mke kuwa uchaguzi uwe

mwema kwani una masilahi na unahifadhi mali na heshima na ni starehe

nzuri duniani. Kutoka kwa Abdalla bin Amruu (radhi za Mwenyezi Mungu

ziwashukie) amesema: amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (rehma na

amani zimshukie): “ dunia ni starehe na starehe iliyo bora zaidi ni mke

mwema.” Na familia inapojengwa kwa uchaguzi uliobora basi ndipo utulivu,

mapenzi ya kudumu, kuoneana huruma kunapatikana, na hapo tena ndoa

inakuwa ni yenye Baraka na kuwa na athari.

Na katika uchaguzi hakuna budi iwe ni kwa misingi ya dini na tabia,

imepokewa na Abi Hurayra (radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie) Amesema

Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani zimshukie) : “mwanamke

huolewa kwa mambo manne; kwa mali yake na nasaba (ukoo) yake na uzuri

wake na dini yake, chagua aliye na dini ili ubarikiwe mikono yako.” (Bukhari).

Na katika mapokezi ya Imam Ahmad kutoka kwa Abi Saad Alkhudriy (radhi za

Mwenyezi Mungu zimshukie) amesema: amasema Mjumbe wa Mwenyezi

Mungu (rehma na amani zimshukie) “mwanamke huolewa kwa moja ya

mambo matatu; huolew mwanamke kwa mali zake, huolewa mwanamke

kwa uzuri wake, na huolewa mwanamke kwa dini yake, chukua mwenye dini

na tabia ubarikiwe mkono wako. (Ahmad)

Mke ana nafasi kubwa katika kulea familia, akiwa mwema basi nayo huwa

njema na jamii itakuwa na utulivu na kama si mwema basi familia

huporomoka.

Mshairi anasema:

Mama ni shule pindi ikiandaa * itaandaa watu weney asili njema.

Pia Mtume (rehma na amani zimshukie) ameusia wakati wa kuchagua mke

kuwa uchaguzi uambatane na dini na tabia. Kutoka kwa Abi Hatim Almuzaniy

(radhi za mwenyezi Mungu zimshukie) amesema Mjumbe wa Mwenyezi

Mungu (rehma na amani zimshukie): atakapokujieni Yule munayemridhia dini

yake na tabia zake basi muozesheni, na musipofanya hivyo itakuwa ni fitina

duniani na ufisadi. Wakasema: “ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu na akiwa

naye“ akasema: “atakapokujieni Yule munayemridhia dini yake na tabia zake

basi muozesheni, mara tatu. (Tirmidhi). Mtume akafanya kuwa dini na tabia

kuwa ndivyo sifa muhimu za ndoa njema, kwa ajili hiyo, uchaguzi sahihi ni

misingi ya dini ambayo utulivu wa familia utapatikana ambao utakuwa ni

sababu ya kuendelea kwa jamii.

Na miongoni mwa utulivu ni; kila mmoja katika wanafamilia achunge wajibu

na haki. Kwani Uisilamu umetoa haki na wajibu ulio sawa kwa wanandoa

wote, Mwenyezi Mungu akasema { Nao wanawake wanayo haki kwa Sharia

kama ile haki iliyo juu yao.}(Al baqara 128). Mwanafamilia hatotakiwa

kutekeleza haki ya mwengine kabla ya kutekeleza haki aliyonayo yeye

kwanza ili upendo na utulivu upatikane vitu ambavyo vinaituliza familia.

Uisilamu ukaweka wazi wajibu na haki hizi, na ukazigawa kwa wanandoa na

kutaka kila mmoja kujilazimisha na kuzihifadhi, kwani kuna haki za kimali na

za kiroho na kimalezi, pia kuna haki za kushirikiana katika ujenzi wa

kutekeleza majukumu. Na umuhimu wa kusaidiana kati ya wanafamilia

kutokana na mahitajio ya maisha. imepokewa katika hadithi ya Abdallah bin

Amru (radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie) kwamba yeye amemsikia

Mjumbe wa Mweneyzi Mungu akisema nyote ni wachungaji, na nyote

mutaulizwa juu ya mulivyovichunga. Imamu ni mchungaji naye ataulizwa juu

ya aliowachunga, mume ni mchungaji juu ya watu wake naye ataulizwa juu

ya aliowachunga, mke ni mchungaji katika nyumba ya mumewe naye

ataulizwa juu ya aliowachunga, mtumishi ni mchungaji juu ya mali ya bwana

wake naye ataulizwa juu ya alichokichunga.” Mpokezi akasema nadhani

alisema: “kijana ni mchungaji wa mali ya baba yake naye ataulizwa juu ya

alichokichunga, nyote ni wachungaji na mutaulizwa juu ya mulichokichunga.”

(Bukhari). Na kutoka kwa Abdallah bin Amru bin Al`as (Radhi za mwenyezi

Mungu ziwe juu yao) amesema: nimemsikia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu

akisema: “inatosha mtu kuwa na madhambi kwa kukizembea kile

anachokilisha.”(Ahmad).

Mmoja wa masahaba alimuuliza Mtume (rehma na amani zimshukie)

akasema: “ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni ipi haki ya mke wa mmoja

wetu kwake?” akasema: “kumlisha unapokula, kumvisha unapovaa au

unapopata, usimpige usoni, wala usimnange (usimwambie kama ni mbaya)

na wala usimkimbie isipokuwa ndani ya nyumba.” (Abi Daudi).

Mfano huu wa Asmaa bint Yazid Al ansareyyah anamuuliza Mtume (rehma na

amani zimshukie) anasema: “ Kwa hakika sisi wanawake kuna wengi wetu

wamefungwa na kuwekwa ndani katika misingi ya nyumba zenu na kumaliza

matamanio yenu na kubeba mimba za watoto wenu. Nyinyi wanaume

mumefadhilishwa sana kuliko sisi kwa kusali sala ya Ijumaa na sala za

pamoja, kuwatembelea magonjwa, kushindikiza jeneza, kuhiji tena na tena,

na bora kuliko yote ni kuwa munapigana jihadi katika njia ya Mwenyezi

Mungu, na mtu yeyote miongoni mwenu akitoka na kwenda kuhiji au

kufanya umra tunakuhifadhieni mali zenu na kukutengeeni nguo na kuwalea

watoto wenu, hivyo ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu hatushirikiani nanyi

katika malipo? Akasema: “Mtume (rehma na amani zimshukie) akawageukia

sawa sawa (kwa uso wake) masahaba zake kisha akasema: “ mmesikia

masuala ya mwanamke hakuna mazuri kama hayo katika masuala ya dini

yaliyoulizwa, ni nani muulizaji?wakasema: “ewe Mjumbe wa Mwenyezi

Mungu hatukuwa tukidhani kwamba mwanamke angeweza kuuliza kama

hivi. Mtume (rehma na amani zimshukie) akamgeukia mwanamke na kisha

akasema: “ ondoka ewe mwanamke, na waeleze wanawake walio nyuma

yako kuwa, mwanamke akiwa mwema kwa mumewe na kutaka radhi zake na

kumtii basi hupata malipo sana na hayo yote.” Akasema: “mwnamke

akaondoka hapo hali ya kusema “Lailahailla llah na Allahu Akbar, hali ya

kujibashiria mema. (Mlango wa sehemu ya imani).

Kwa ajili hiyo kufanikiwa kwa familia ya kiisilamu ipo katika kuhifadhi haki na

wajibu kati ya wanandoa na kujiepusha na uzembe na kukiuka mipaka.

Na miongoni mwa mambo yenye kusaidia kuleta utulivu ndani ya familia; ni

kuenea kwa upendo kati ya wanafamilia, kwani upendo ni nguzo muhimu

ndani ya nyumba na ni chanzo cha mafanikio yote ndani ya familia yenye

njema. Nao ni muhimili mkubwa ambao unapaswa kwa kila mwanafamilia

kuwa nao ili familia ineemeke kwa utulivu, upendo na msimamo, Mwenyezi

Mungu anasema { Na katika Ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu

kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao.Naye amejaalia mapenzi na

huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu

wanaofikiri} (Ruum.21). Upendo kwa wanajamii wote umewekewa rehani

kwa kuwepo katika familia. Na tuna kigezo kizuri kwa Mtume (rehma na

amani zimshukie) kwani alikuwa ni mfano wa upendo kwa watu wa familia

yake wote bila kubaguwa, wake zake, watoto wake na hata wajukuu wake na

mtumishi wake kwani yeye (rehma na amani zimshukie) alikuwa ni mbora

kwa watu wake.

Na iwapo nyumba haina upendo basi maisha ya familia huwa ni mabaya na

magumu, hivo, ni wajibu wa kila mwanafamilia awe makini katika kuhakikisha

kuna upendo.

Na miongoni mwa utulivu wa familia: ni kuishi kwa wema, na hili nalo

ametuamrisha Mola wetu na Mtume wetu nae ametuusia. Mwenyezi Mungu

anasema Na kaeni nao kwa wema, na ikiwa mmewachukia, basi huenda

mkakichukia kitu, na Mwenyezi Mungu ametia kheri nyingi ndani

yake.}(Anisaa 19.) kila mwanandoa anahitajika kuwa na mawasiliano na

mwengine ili upendo uenee na ushirikiano uzidi hapo ndipo lengo la ilaka-

uhusiano- litapatikana. Mwenyezi Mungu anasema { Wao ni vazi kwenu, na

nyinyi ni vazi kwao.}(Al baqara 187) na akasema pia { Na katika Ishara zake ni

kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu

kwao.Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila

ya shaka zipo Ishara kwa watu wanaofikiri.}(Ruum. 21). Na akasema { na

katika hiyo hiyo akamfanya mwenzi wake, ili akae naye kwa utulivu. } (al

araaf. 189).

Na katika yaletayo uhusiano mwema ni pamoja na maneno mazuri vitendo

vyema, kusameheana, kusaidiana, kuheshimiana, kushauriana, kulinda siri,

kujiepusha na mzozo na matatizo na mambo mengineyo yaliyo mazuri.

Na Mtume (rehma na amani zimshukie) pamoja na masahaba zake

wametuwekea mifano mizuri kuhusu uhusiano wa kuishi na familia zao.

Imepokewa kutoka kwa Aswad, amesema,: nimemuuliza Aisha (rehma na

amani zimshukie) Mtume alikuwa akifanya nini nyumbani kwake? Akasema:

“alikuwa akifanya kazi za watu wake- yaani alikuwa akiwasaidia wakeze -

muda wa sala ukifika alikuwa akitoka na kwenda kusali. (Muslim). Na kutoka

kwa ibn Abbas (radhi za Mwenyezi Mungu awawie radhi) amesema: Mimi

ninapenda kujipamba kwa mwanamke (mke wangu) kama nipendavyo yeye

ajipambe kwa ajili yangu, kwani Mwenyezi Mungu anasema { Nao wanawake

wanayo haki kwa Sharia kama ile haki iliyo juu }(Al baqara 228). Na nipendalo

ni usafi kwa haki zangu zote, kwani Mwenyezi Mungu anasema { Na

wanaume wana daraja zaidi kuliko wao.} (Albaqara 228) (kitabu cha Ibn Abi

Shayba).

Na miongoni mwa uhusiano mwema kati ya wanandoa; ni kumuachilia

mmoja wapo matatizo yote ya ndani ya ndoa, uhusiano mwema unakusanya

maana zote zinazoshikamana na uhai wa wanandoa. Hakina ya uisilamu

unahimiza sana kuwepo kwa uhusiano wa mapenzi, kufahamiana na kuwa

pamoja na hii ni hatua nzuri ya kujenga jamii.

Na miongoni mwa mambo ambayo yatasaidia kuendeleza familia: ni

kushauriana kati ya wanandoa, kwani katika kushauriana kunaleta upendo

kati yao. Hata katika mambo ambayo yataonekana kwa baadhi ya watu kuwa

ni madogo mfano suala la kumnyonyesha mtoto miaka miwili, Mwenyezi

Mungu anasema {Na kama wote wawili wakitaka kumwachisha ziwa kwa

kuridhiana na kushauriana, basi si vibaya kwao.} (Al baqara. 233).

Mashauriano kati ya wanandoa na hata wanafamilia hujenga muongozo wa

maisha ya dini yetu tukufu ya kiisilamu. Na amri iliyokuja katika aya hii ni kwa

ujumla aliposema { Na wanao mwitikia Mola wao Mlezi, na wakashika Sala,

na mambo yao yakawa ni kwa kushauriana baina yao, na kutokana na tulicho

waruzuku wakawa wanatoa }(Ashuraa.38). na jambo hili ndilo alilolofanya

Mtume (rehma na amani zimshukie) kimatendo. Na katika mienendo

mengine ya kushauriana kwake na wakeze, mfano; kama ilivyotokea kati

yake (rehma na amani zimshukie) na mkewe bibi Umu Salama (radhi za

Mwenyezi Mungu zimshukie) siku ya Hudaibiya. Baada ya Mtume kumaliza

kuweka ahadi za suluhu kati yake na watu wa Makka, akawaambia masahaba

zake: “ simameni na chinjiyeni kisha nyoeni”. Mpokezi wa hadithi akasema:

naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu hajasimama mtu yeyote mpaka akarudia

kusema tena hivyo mara tatu. Na ilivyokuwa hajasimama yeyote Mtume

(rehma na amani zimshukie) akaingia hemani kwa Ummu salama akamueleza

yaliyotokea kati yake na watu wake. Ummu salama akamwambia: “Ewe

Mjumbe wa Mwenyezi Mungu unataka wakusikilize kuhusu hilo? Toka kisha

usizungumze na yeyote mpaka utakapochinja mnyama wako na kumuita

kinyozi wako na kukutaka nywele. Mtume akatoka na hakumsemesha yeyote

mpaka akachinja mnyama akamwita kinyozi na kumnyoa, na watu

walipomuona wakasimama na kunyoa na wengine wakanyoana mpaka

wakakaribia kusongamana.) (Muslim) Hassan Basriy (radhi za Mwenyezi

Mungu zimshukie) amesema; “ijapokuwa Mtume hakuwa na ulazima wa

kufuata ushauri wa Ummu Salama isipokuwa amefanya hivyo ili watu wapate

kumfuata na wala mwanamme asihisi kuwa kuna kasoro katika kufuata

ushauri wa mwanamke.

Pia miongoni mwa misingi ya utulivu wa familia: ni kutoa mahitajio kwa

wanafamilia wote, kwani ni haki ambayo sheria ya kiisilamu imewajibisha.

Mwenyezi Mungu anasema { Wanaume ni wasimamizi wa wanawake, kwa

kufadhiliwa na Mwenyezi Mungu baadhi yao juu ya baadhi, na kwa mali yao

wanayo yatoa. }(Anisaa 34). Na kusema { Na juu ya baba yake chakula cha

kina mama, na nguo zao kwa mujibu wa ada. Wala halazimishwi mtu ila kwa

kadiri ya uwezo wake. Mama asitiwe taabuni kwa ajili ya mwanawe, wala

baba kwa ajili ya mwanawe. Na juu ya mrithi mfano wa hivyo. }(Albaqara

233). Na akasema pia {7 Mwenye wasaa atoe kadiri ya wasaa wake, na

mwenyedhiki atoe katika alicho mpa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu

hamkalifishi mtu ila kwa kadiri ya alicho mpa.} (Atalaq. 7).

Na miongoni mwa mambo yenye kusaidia kuwepo kwa utulivu ndani ya

familia: kuwepo kwa uadilifu kwa wanafamilia, malezi mema ya kidini kwa

watoto na kuwafundisha mambo ya dini. Uadilifu ni nguzo muhimu sana

katika kuendelea kwa familia, Mtume (rehma na amani zimshukie)

ametuhadharisha kuwatafautisha watoto katika kuwa nao kwa ajili ya

kuhifadhi ushirikiano na kuwa pamoja kwa wnafamilia. Imepokewa na

Nuuman bin Bashiir (radhi za Mwenyezi Mungu ziwashukie) amesema: baba

yangu alinitolea sadaka kwa baadhi ya mali zake. Ummu Umra bint Rawaha

akasema: “ sikubali mpaka tumuweka Mtume kuwa ni shahidi, baba yangu

akaondoka mpaka kwa Mtume (rehma na amani zimshukie) ili awe ni shahidi

wa sadaka yangu. Mtume (rehma na amani zimshukie) akamuuliza, je,

umefanya hivyo kwa wototo wako wengine? Akasema: “hapana” akasema: “

Muogopeni Mwenyezi Mungu na wafanyieni uadilifu watoto wenu.” Baba

yangu akarudi na kuirudisha ile sadaka. (Muslim).

Uisilamu umeiangalia familia kwa mtazamo wa heshima na kuitukuza, kwani

ni mfungamano uliosafi na ni malengo yaliyo matakatifu, na ukataka familia

ibakie kuwa ni madhubuti yenye kushikamana. Ifikie malengo yake na

isimame imara penye matatizo. Kwa ajili hii, uisilamu ukaiangalia kwa

umakini zaidi na kuweka adabu ambazo zitakuwa ni msingi wa kujenga

familia iliyoshikamana na yenye nguvu. Na yenye kuhifadhi utulivu wa jamii

na kuweko mbali na aina zote za kiugaidi na utumiaji wa nguvu.

Jamii itakapokuwa na utulivu wa watu wote watahisi usalama katika nyanja

zote, kinafsi, kimwili kijamii na kiuchumi, kitu ambacho kitaakisi jamii ya

kiisilamu na uwepo wake wa amani na utulivu. Uisilamu umezingatia utulivu

wa familia ni njia mojawapo ya kuhakikisha usalama wa kijamii kwa

kuepukana na ufisadi na mizozo, mwanzo wa usalama wa jamii unatokana na

familia, kisha shuleni na baadae katika jamii nzima.

Familia ni shule ya kwanza ambayo mtoto huelimishwa zuri na baya, kheri na

shari, na kujifunza kutimiza majukumu na uhuru wa maoni. Familia ndio

imjengayo mtoto na kujulikana nini akitakacho na iwapo atakuwa ni raia

mwema ndani ya jamii yake.

Usalama hauletwi kwa nguvu, hutetwa na wanajamii weneywe, kupitia

dhamiri zao na kwa nafasi kuu ya familia katika kutengeneza dhamiri na

kuikuza katika nafasi za watu wake.

Fadhila za masahaba (radhi za Mwenyezi Mungu

ziwashukie)

na mifano ya historia yao njema 44 Jamad Akhar 4257H. sawa na 33/5/3144

Kwanza: vipengele

7. Nafasi za masahaba na kupanda vyeo vyao.

1. Fadhila za masahaba ndani ya Qurani Tukufu.

3. Kuwapenda masahaba ni katika imani.

3. Mahimizo ya kuwaiga masahaba watukufu.

2. Makatazo ya kuwatusi au kuwasema vibaya.

2. Mifano katika historia yao.

Pili: dalili

Ndani ya Qurani Tukufu

7. Mwenyezi Mungu anasema { Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu.

Na walio pamoja naye wana nguvu mbele ya makafiri, na wana hurumiana

wao kwa wao. Utawaona wakiinama na kusujudu wakitafuta fadhila na

radhi za Mwenyezi Mungu. Alama zao katika nyuso zao, kwa athari ya

kusujudu. Huu ndio mfano wao katikaTaurati. Na mfano wao katika Injili ni

kama mmea uliotoa chipukizi lake, kisha ukalitia nguvu, ukawa mnene,

ukasimama sawa juu ya ubuwa wake, ukawafurahisha wakulima, ili

kuwakasirisha kwa ajili yao makafiri. Mwenyezi Mungu amewaahidi walio

amini na wakatenda mema katika wao msamaha na ujira mkubwa.}(Alfathi.

13)

1. Mwenyezi Mungu anasema { Na wale walio tangulia, wa kwanza,

katikaWahajiri na Ansari, na walio wafuata kwa wema,Mwenyezi Mungu

ameridhika nao, na wao wameridhika naye; na amewaandalia Bustani

zipitazo mito kati yake,wadumu humo milele. Huko ndiko kufuzu

kukubwa.}(Atawba. 711).

3. Mwenyezi Mungu anasema {Na wa mbele watakuwa mbele. 77. Hao ndio

watakao karibishwa 71. Katika Bustani zenye neema. 73. Na wachache

katika wa mwisho. 73. Fungu kubwa katika wa mwanzo, }(alwaqia. 71-73)

3. Mwenyezi Mungu anasema { Basi wale walio muamini yeye, na

wakamhishimu, na wakamsaidia, na wakaifuata nuru iliyo teremshwa

pamoja naye - hao ndio wenye kufanikiwa.}(Alaaraf. 721).

2. Mwenyezi Mungu anasema {Mwenyezi Mungu amekwisha pokea toba ya

Nabii na Wahajiri na Ansari waliomfuata katika saa ya dhiki, pale baada ya

kukaribia nyoyo za baadhi yao kugeuka. Basi akapokea toba yao, kwani

hakika Yeye kwao wao ni Mpole na ni Mwenye

kuwarehemu}(Atawaba.771)

2. Mwenyezi Mungu anasema {Lakini Mtume na wale walio amini pamoja

naye waliwania Jihadi kwa mali zao na nafsi zao. Hao ndio watakao pata

kheri nyingi, na hao ndio wenye kufanikiwa.23. Mwenyezi Mungu

amewatengenezea Bustani zipitazo mito kati yake, wadumu humo. Huko

ndiko kufuzu kukubwa.}(Atawaba.22-23)

1. Mwenyezi Mungu anasema { Kwa hakika Mwenyezi Mungu amewapa radhi

Waumini walipo fungamana nawe chini ya mti, na alijua yaliyomo nyoyoni

mwao. Basi akateremsha utulivu juu yao, na akawalipa kwa ushindi wa

karibu.}(Alfathi.72)

2. Mwenyezi Mungu anasema {Wapewe mafakiri Wahajiri walio tolewa

majumbani mwao na mali yao kwa ajili ya kutafuta fadhila kutoka kwa

Mwenyezi Mungu na radhi zake, na wanamsaidia Mwenyezi Mungu na

Mtume wake. Hao ndio wa kweli. 3. Na walio na maskani zao na Imani yao

kabla yao,wanawapenda walio hamia kwao, wala hawaoni choyo katika

vifua vyao kwa walivyo pewa (Wahajiri), bali wanawapendelea kuliko nafsi

zao, ingawa wao wenyewe ni wahitaji. Na mwenye kuepushwa uchoyo wa

nafsi yake,basi hao ndio wenye kufanikiwa.} (Alhashri.2-3)

Ndani ya hadithi

7. Kutoka kwa Abdala bin Masud (radhi za Mwenyezi Mungu

zimshukie) kutoka kwa Mtume (rehma na amani zimshukie)

amesema: “bora ya watu ni waliopo katika wakati wangu, kisha

wanaowafuatia, kisha wanaowafuatia, kisha watakuja watu shahada

ya mmoja wao itatanguliwa na kiapo na kiapo chake kwa shahada

yake.” (Muslim na Bukhari).

1. Kutoka kwa Abi hurayra (radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie)

amesema: amaesma Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani

zimshukie): “ Msiwatusi masahaba zangu, msiwatusi masahaba

zangu, naapa kwa yule ambaye nafsi yangu imo mikononi mwake lau

kama mmoja wenu angelitoa dhahabu mfano wa jabali la Uhud basi

asingelifikia kwa utoaji huo wala nusu yake.” (Bukhari na Muslim).

3. Mtume (rehma na amani zimshukie) anasema: “Tahadharini,

tahadharini kuhusu masahaba wangu. Tahadharini, tahadharini kuhusu

masahaba wangu. Msiwavunjie heshima baada yangu, mwenye

kuwapenda basi kwa mapenzi yangu nitampenda, na mwenye

kuwachukia basi kwa chuki yangu nitamchukia, na mwenye kuwakera

basi kwa hakika amenikera mimi, na anikeraye hakika huwa

amemkera Mwenyezi Mungu, na amkeraye Mwenyezi Mungu pana

wasiwasi wa kuchukuliwa.” (Ahmad).

3. Kutoka kwa Abi Hurayra (radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie)

amesema: amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani

zimshukie) nani kaamka hali ya kuwa amefunga? Abu Bakar

akasema: “Mimi”. Akasema: “Ni nani kati yenu aliyeshindikiza

jeneza?” Abu Bakar akasema: “Mimi” akasema: “Ni nani kati yenu

aliyelisha masikini?” Abu Bakar akasema: “Mimi” akasema: “Ni nani

kati yenu aliyetembelea mgonjwa?” Abu Bakar akasema: “ Mimi”

Mtume (rehma na amani zimshukie) akasema mambo haya

yakikusanyika kwa mtu basi ataingia peponi.” (Muslim).

Tatu: maudhui

Mwenyezi Mungu Mtukufu amemchagulia Mtume wake (rehma na amani

zimshukie) watu wasafi, masahaba walio wema, waliomuamni na kumuunga

mkono na kumnusuru, waliosoma na kupasi kutoka katika chuo cha Nabii

Muhammad (rehma na amani zimshukie), waliolelewa katika mikono yake,

waliokunywa kinywaji cha chemuchemu safi ambayo inatoa maji ya imani,

wakawa watu wenye imani ya kweli, na wenye elimu kubwa, na ufahamu wa kina,

na matendo mema zaidi. Waliibeba bendera ya dini katika ulimwengu wote,

hawakuwa wakiogopa lawama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kwa ajili hiyo,

wakafanikiwa kupata radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu. Naye akawasifu ndani

ya Qurani Tukufu kwa kusema { Na wale walio tangulia, wa kwanza, katika

Wahajiri na Ansari, na walio wafuata kwa wema,Mwenyezi Mungu ameridhika

nao, na wao wameridhikanaye; na amewaandalia Bustani zipitazo mito kati

yake,wadumu humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa.}(Atawbah. 711). Hao

ndio masahaba wa Mtume (rehma na amani zimshukie) ambao Mwenyezi Mungu

amewateua kwa Mtume wake wa mwisho.

Kizazi kilichoweza kubadilisha mwenendo wa maisha, waliibeba nuru aliyokuja

nayo bwana wetu, Mtume Muhammad (rehma na amani zimshukie) kwa

ulimwengu wote. Na kadiri tutakavyojaribu kuwafukuzia basi hatutaweza, na

inatosha kuelewa kuwa lau kama tutatoa sadaka ya dhahabu kila siku mfano wa

jabali la Uhudi hatofikia mmoja wenu thamani ya kile walichokitoa masahaba wala

nusu yake. Hivi ni kama alivyoashiria Mtume (rehma na amani zimshukie)

aliposema… “Naapa kwa Yule ambaye nafsi yangu imo mikononi mwake lau

kama mmoja wenu angelitoa dhahabu mfano wa jabali la Uhud basi asingelifikia

kwa utoaji huo wala nusu yake.” (bukhari na Muslim). Na hii ni kwa sababu

walihimili matatizo ya kueneza hii dini na kufikwa yaliyowafika, wakajitolea

kinafsi zao, roho zao na mali zao katika njia ya kuinusuru dini ya Mwenyezi

Mungu na kumnusuru Mtume wake (rehma na amani zimshukie), akasema

Mwenyezi Mungu { Hakika Mwenyezi Mungu amenunua kwa Waumini nafsi zao

na mali zao kwa kuwa wao watapata Pepo. Wanapigana katika Njia ya Mwenyezi

Mungu - wanauwa na wanauwawa. Hii ni ahadi aliyo jilazimisha kwa Haki katika

Taurati na Injili na Qur'ani. Na nani atimizae ahadi kuliko Mwenyezi Mungu? Basi

furahini kwa biashara yenu mliyo fanya naye. Na huko ndiko kufuzu

kukubwa,}(Atawbah.777).

Na iwapo ni katika haki zetu kwa Mtume (rehma na amani zimshukie) kuisoma

historia yake na mwenendo wake na kufuata uongofu wake na kutenda kwa mujibu

wa sheria yake, basi pia katika haki zetu kwa upande wa masahaba ni kuelewa

ubora wao na nafasi zao na kusoma historia zao ili tuweze kufanana nao katika

kuwa na maadili mazuri, katika kumtii na kumuabudu Mwenyezi Mungu Mola wa

ulimwengu wote, na tuchukue mazingatio na mawaidha katika maish yao. Kwani

wao wamechaguliwa na Mwenyezi Mungu ili wawe pamoja nae (rehma na amani

zimshukie) na kueneza ujumbe baada ya kuondoka kwake, kwani wao ni watu bora

katika umma huu kwa kuwa Mwenyezi Mungu amewasifu kwa sifa za ukamilifu

na kuwasafisha, hakuna katika watu aliyeweza kuelewa mfano wa uchaji Mungu

kama walivyokuwa hawa wakimcha Mungu . Mwenyezi Mungu amewasifu na

akaweka wazi ni kipi alichowaandalia katika malipo makubwa, akasema { Na wa

mbele watakuwa mbele. 77. Hao ndio watakao karibishwa 71. Katika Bustani

zenye neema. 73. Na wachache katika wa mwisho. 73. Fungu kubwa katika wa

mwanzo,}(Alwaqiah. 71-73).

Na kwa kuweka wazi nafasi zao na kupanda kwa cheo chao Mwenyezi Mungu

akawapa sifa miongoni mwa sifa zake ndani ya Qurani Tukufu, si hivyo tu, bali pia

wamesifiwa katika Taurati na Injili akasema { Muhammad ni Mtume wa

Mwenyezi Mungu. Na walio pamoja naye wana nguvu mbele ya makafiri, na wana

hurumiana wao kwa wao. Utawaona wakiinama na kusujudu wakitafuta fadhila na

radhi za Mwenyezi Mungu. Alama zao katika nyuso zao, kwa athari ya kusujudu.

Huu ndio mfano wao katikaTaurati. Na mfano wao katika Injili ni kama mmea

uliotoa chipukizi lake, kisha ukalitia nguvu, ukawa mnene, ukasimama sawa juu ya

ubuwa wake, ukawafurahisha wakulima, ili kuwakasirisha kwa ajili yao makafiri.

Mwenyezi Mungu amewaahidi walio amini na wakatenda mema katika wao

msamaha na ujira mkubwa} (Alfathi.13). Mwenyezi Mungu akawasifu kuwa wao

ni wenye nguvu mbele ya makafiri pasi na kudhulumu na weney kuoneana hurumu

kati yao, wakimuabudu Mwenyezi Mungu mmoja bila ya kumshirikisha na

chochote, wakirukuu na kusujudu, hawatafuti fadhila na radhi isipokuwa zitokazo

kwa Mwenyezi Mungu, na ibada imewaathiri mpaka ikadhihiri alama zake katika

viungo vyao, ukimuona mmoja wapo basi utaelewa tu ni katika wale wamuogopao

Mwenyezi Mungu na kumcha. Hivyo, masahaba (radhi ziwe juu yao) ni neema

kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa waja wake, akasema { Kwa hakika Mwenyezi

Mungu amewapa radhi Waumini walipo fungamana nawe chini ya mti, na alijua

yaliyomo nyoyoni mwao. Basi akateremsha utulivu juu yao, na akawalipa kwa

Ushindi wa karibu.}(Alfathi 72) .

Na tukiusoma mwenendo wa Mtume (rehma na amani zimshukie) tutaona kuwa

umejaa masimulizi yenye kuonyesha ubora wao na kukuwa kwa nafasi zao, kwa

mfano, kukiri kwake Mtume (rehma na amani zimshukie) kuwa wao ni katika watu

wa karne (wakati) bora na bora ya umma. Kutoka kwa Abdala bin Masud (radhi

za Mwenyezi Mungu zimshukie) kutoka kwa Mtume (rehma na amani zimshukie)

amesema: “bora ya watu ni waliopo katika wakati wangu, kisha wanaowafuatia,

kisha wanaowafuatia, kisha watakuja watu shahada ya mmoja wao itatanguliwa na

kiapo na kiapo chake kwa shahada yake.” (Muslim na Bukhari). Na wamekuwa

watu bora kwa kuwa walimuamini Mtume (rehma na amani zimshukie) wakati

watu wengine walipomkanusha, na kumsadiki wakati wengine walipomuona

muongo, na kumnusuru kwa mali zao na nafsi zao kwa ajili ya Mwenyezi Mungu .

imepokewa katika kitabu cha imam Ahmad, kutoka kwa Abdalla bin Masud (radhi

za Mwenyezi Mungu zimshukie) amesema: “Mwenyezi Mungu ameangalia katika

nyoyo za waja akaona moyo wa Muhammad (rehma na amani zimshukie) ni bora

kati ya nyoyo za waja, akamchagua yeye, na akampa ujumbe wake, kisha

akaangalia nyoyo za waja baada ya moyo wa Muhammad akaona nyoyo za

masahaba ni nyoyo bora kati ya nyoyo za waja, akawafanya kuwa ni mawaziri wa

Mtume wake (rehma na amani zimshukie) wenye kuipigania dini yake, na kile

waonacho waisilamu ni jema basi na kwa Mwenyezi Mungu pia ni jema, na

walionalo kuwa si jema basi kwa Mwenyezi Mungu pia si jema.”

Pia katika ubora wa masahaba ni kama alivyosema Mtume (rehma na amani

zimshukie) kuwa wao ni amana ya umma, Mtume (rehma na amani zimshukie)

anasema: “nyota ni amana kwa mbingu, na nyota ziondokokapo basi mbigu huleta

kile kilichoahidiwa, na mimi ni amana kwa masahaba zangu nikiondoka basi

masahaba zangu wanaleta kile walichoahidiwa, na masahaba zangu ni amana kwa

umma wangu wakiondoka basi umma wangu wataleta kile walichoahidiwa.”

(Muslim) . Ikawa kuwepo kwa masahaba (radhi za Mwenyezi Mungu ziwashukie)

ni amana kwa umma ya kutokuwepo kwa uzushi, lakini pia kutokana na Baraka

zao zimeenea na kufika hadi katika kizazi cha pili baada yao. Kutoka kwa Saad

Alkhudriy (rehma na amani zimshukie) kwamba Mtume (rehma na amani

zimshukie) amesema: “watakuja watu watawapigana vita na kundi jengine,

watasema: “yupo katika nyie aliyekuwa na Mtume (rehma na amani zimshukie)?”

watasema: “ ndio” basi watafunguliwa. Kisha watakuja watu watapigana vita na

kundi jengine, itasemwa ““yupo katika nyie aliyekuwa na waliokuwa na Mtume

(rehma na amani zimshukie)? Watasema: “ndio” watafunguliwa. Kisha watakuja

watu watapigana vita na kundi jengine, itasemwa, “yupo katika nyie aliyekuwa na

waliokuwa pamoja na waliokuwa na Mtume (rehma na amani zimshukie)?

Watasema “ndio” watafunguliwa. (Bukhari naMuslim).

Pia Mwenyezi Mungu amewashuhudia kuwa ni watu waliokuwa na moyo wa

kujitolea, ukarimu na juhudi za kutafuta radhi na mafanikio kwa Mwenyezi

Mungu. Naye akawaandalia kutokana na hili pepo ya milele yenye neema.

Akasema {Lakini Mtume na wale walio amini pamoja naye waliwania Jihadi kwa

mali zao na nafsi zao. Hao ndio watakao pata kheri nyingi, na hao ndio wenye

kufanikiwa 23. Mwenyezi Mungu amewatengenezea Bustani zipitazo mito kati

yake, wadumu humo. Huko ndiko kufuzu kukubwa. }(Atawbah22-23). Umar

(radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie) anasema: “siku moja Mtume (rehma na

amani zimshukie) alituamrisha tutoe sadaka, ikawa ninazo mali, nikasema: “ leo

nitamshinda Abu Bakar nikishindana naye, nikaja na nusu ya mali yangu. Mtume

(rehma na amani zimshukie) akasema: “ watu wako umewabakishia kitu gani?

Nikasema: “mfano wake. Akasema: “akaja Abu Bakar (radhi za Mwenyezi Mungu

zimshukie) na kila alichonacho, Mtume akamwambia. “watu wako umewabakishia

kitu gani? Akasema: “nimeaachilia Mwenyezi Mungu na Mtume wake, nikasema

(Umar) siwezi kushindana na wewe kwa kitu chochote milele..” (Tirmidhi).

Na iwapo hii ndio nafasi ya masahaba wa Mtume (rehma na amani zimshukie) basi

kuwapenda kwao (radhi za Mwenyezi Mungu ziwashukie ) na kukiri ubora wao

kuliko wengine ni katika imani ya lazima juu ya kila muisilamu. Kwani ni ishara

ya kumpenda Mtume (rehma na amani zimshukie) ambaye aliwapenda na

kuwachagua kuwa ni masahaba wake. Muumini hupenda kila apendacho Mtume

(rehma na amani zimshukie) wakiwemo masahaba zake. Imepokewa na Abdalla

bin Mugh-qal (radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie) amesema: amesema Mjumbe

wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani zimshukie) “tahadharini, tahadharini

kuhusu masahaba wangu. tahadharini, tahadharini kuhusu masahaba wangu.

Msiwavunjie heshima baada yangu, mwenye kuwapenda basi kwa mapenzi yangu

nitampenda, na mwenye kuwachukia basi kwa chuki yangu nitamchukia, na

mwenye kuwakera basi kwa hakika amenikera mimi, na anikeraye hakika huwa

amemkera Mwenyezi Mungu, na amkeraye Mwenyezi Mungu pana wasiwasi wa

kuchukuliwa.” (Ahmad). Na katika kitabu cha imam bukhari na muslim kutoka

kwa Bara`a ibn A`zib, kutoka kwa Mtume (rehma na amani zimshukie) amesema

kuhusu Maanswar; hawapendi hao (Maanswar) isipokuwa ni muumini, na wala

hawachukii isipokuwa ni mnafiki, atakaewapenda basi atapendwa na Mwenyezi

Mungu, na mwenye kuwachukia atachukiwa na Mwenyezi Mungu. Kuwapenda ni

dalili ya imani na ni kumtii Mwenyezi Mungu, na kuwachukia ni unafiki na uasi.

Imepokewa na Anas bin malik (radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie) kutoka kwa

Mtume (rehma na amani zimshukie) amesema: “dalili ya imani ni kuwapenda

Maanswari, na dalili ya unafiki ni kuwachukia Maanswari.” (Bukhari).

Uisilamu umeharamisha kuwasema vibaya masahaba (radhi za Mwenyezi Mungu

ziwashukie) kwani aliowachagua ili wawe na Mtume –naye ni Mwenyezi Mungu –

amewasifu na kuwaridhia. Na kama alivyotukataza Mtume (rehma na amani

zimshukie) juu ya kuwatusi. Kutoka kwa Abi Hurayra (radhi za Mwenyezi Mungu

zimshukie), hakika ya Mtume (rehma na amani zimshukie) amesema: Musiwatusi

masahaba wangu, musiwatusi masahaba wangu naapa kwa Yule ambaye nafsi

yangu imo mikononi mwake lau kama mmoja wenu angelitoa dhahabu mfano wa

jabali la Uhud basi asingelifikia kwa utoaji huo wala nusu yake.” (Muslim). Na

kutoka kwa Abdalla bin Umar (radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie) amesema.

Musiwatukane masahaba wa Mtume Muhammad (rehma na amani zimshukie),

kwani kisimamo cha ibada ya mmoja wao cha saa moja ni bora kuliko ibada ya

miaka arobaini ya mmoja wenu.” (ubora wa masahaba, Imam Ahmad). Kwa ajili

hiyo ni wajibu wetu kuwapa heshima na kuelewa vyeo vyao.

Na mwenye kuangalia maisha ya masahaba (radhi za Mwenyezi Mungu

ziwashukie) ataona kiwango kikubwa sana cha imani waliyokuwa nayo, na kufuata

amri za Mwenyezi Mungu na Mtume wake (rehma na amani zimshukie), atakutia

kuwa kuna ufasiri wa kiuhakika wa utendaji matendo mazuri, walikuwa ni

viongozi wema walioonyesha mfano wa utoaji, elimu, utendaji, kujitolea muhanga

kwa ajili ya kuinusuru dini ya Mwenyezi Mungu, mpaka wakateremshiwa aya {

Wapewe mafakiri Wahajiri walio tolewa majumbani mwao na mali yao kwa ajili

ya kutafuta fadhila kutoka kwa Mwenyezi Mungu na radhi zake, na wanamsaidia

Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hao ndio wa kweli.}(Alhashri.2) .

Na mfano wa wazi kabisa ni, sahaba Ali bin Abi Twalib (radhi za Mwenyezi

Mungu zimshukie) alipojitolea kulala katika kitanda cha Mtume (rehma na amani

zimshukie) usiku wa kuhama kwa Mtume ili ajitoe muhanga kwa nafsi yake na

roho yake hali ya kuelewa kuwa washirikina wanamsaka kwa mapanga kwa ajili

ya kumuua.

Pia sahaba Suhayb Ruumi alijitolea muhanga wa mali zake kwa ajili ya kuinusuru

dini ya Mwenyezi Mungu, na kumnusuru Mtume (rehma na amani zimshukie)

wakati alipotaka kuhamia Madina. Makafiri wa kikuraish wakamwambia: “ulikuja

kwetu huna kitu, ukaupata utajiri kutoka kwetu, na kufikia ulipofikia kisha unataka

kutoka wewe na nafsi yako, hiyo haiwezekani. Akawaambia: “Mnaonaje iwapo

nitakupeni mali zangu mutaniachia? Wakasema: “ ndio” akasema: “ninakuwekeni

mashahidi kuwa mali yangu nimewaachilia nyinyi.” Ikamfika hilo Mtume (rehma

na amani zimshukie) akasema: Suhayb amepata faida, suhayb amepata faida.” (Ibn

Haban).

Mfano mwengine ni Abu bakar (radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie) anatupa

mfano mzuri wa maadili mema, na sifa nzuri mpaka akawa ni kigezo cha kila

jema. Na Mtume akamshuhudia kwa hili kuwa ni katika watu wa peponi. Kutoka

kwa Abi Hurayra (radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie) amesema: amesema

Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani zimshukie) nani kaamka hali ya

kuwa amefunga? Abu Bakar akasema: “mimi”. Akasema: “ni nani kati yenu

aliyeshindikiza jeneza?” Abu Bakar akasema: “mimi” akasema: “ni nani kati yenu

aliyelisha masikini?” Abu Bakar akasema: “mimi” akasema: “ni nani kati yenu

aliyetembelea mgonjwa?” Abu Bakar akasema: “ mimi” Mtume (rehma na amani

zimshukie) akasema mambo haya yakikusanyika kwa mtu basi ataingia peponi.”

(Muslim).

Nae sahaba Umar (radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie) siku moja alikuwa

akitembea usiku, tahamaki kuna mwanamke ana watoto na chungu kipo motoni na

watoto wamejikunyata. Umar akasema: Amani juu yenu enyi watu wa mwangani,

alichukia kusema enyi watu wa motoni, mwanamke akasema: “nawe amani iwe

juu yako”. Akasema (Umar) je nikaribie? Akasema (mwanamke) ikiwa kwa heri

karibia na kama kwa shri usikaribie, akakaribia, akasema: “ muna nini? Akajibu:

“usiku umekuwamfupi kwetu pamoja na baridi. Akasema: “na hawa watoto wana

nini mbona wamejikunyata? Akasema: „ni njaa. Akasema: “ndani ya chungu hiki

muna kitu gani?” Akasema: “cha kuwadanganyia mpaka walale, na Mwenyezi

Mungu yupo pamoja nasi juu ya Umar. Akasema “Mungu akurehemu, munamjuaje

Umar?” akasema: “Umar unatuongoza kisha anatusahau.” Zaid – mpokezi wa

hadithi- anasema: “ akanikabili kisha akaniambia tuondoke, tukaondoka huku

tunakazana mpaka tukafika nyumba ya unga (nyumba ya hazina), akatoa kiwango

cha unga na kopo la mafuta, akasema: “ nibebeshe: “ nikamwambia: “ mimi

nitakubebea: “je nawe utanibebe mzigo wa madhambi yangu siku ya kiyama?

Nikambebesha, akaondoka nami nikaondoka nae hali yakukazana. Tulipofika kwa

Yule mwanamke tukautua akampa unga, akawa anamwambia tupa juu yangu na

ninakutetemeka mimi mwenywe, akawa anapuliza chungu. Akasema: “ nipe kitu

chochote (cha kupakulia) akapewa na kupakuwa ndani yake huku akisema:

“walishe na mimi nitawashikia, akawa katika hali hiyo mpaka wakashiba, na

baadae wakamuacha akaondoka nami (Zaid) nikaondoka nae. Naye Yule

mwanamke akawa nasema Mungu akulipe kila la kheri, jambo hili ulilolifanya ni

jema kuliko afanyavyo kiongozi wa waumini: „nikamwambia “ sema mema pindi

kiongozi wa waumini atakapokujia, na nisimulie kuhusu yeye akipenda Mungu,

kisha akajiweka upande na baadae akamsogelea na kukaa kitako ,na kumpokea

tukamwambia: “ tuna jambo jengine lisilo hili na akawa hatuzungumzishi mpaka

nilipowaona watoto wamelala na kutulizana, akasema : amani, hakika njaa

imewafanya wasilale na kuwafanya walie na nilipendelea kuwa nisiondoke mpaka

nione niliyoyaona. (ubora wa masahaba, imamu Ahmad).

Na hata masahaba wa kike (radhi za Mwenyezi Mungu ziwashukie) nao wana

fadhila na misimamo ya kujitolea muhanga kwa ajili ya dini ya Mwenyezi Mungu,

kwa mfano: -

Msimamo wa Mama wa waumini Khadija (radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie)

alivyokuwa na msimamo wa kueneza dini ya Mwenyezi Mungu pale aliposimama

wima na mumewe na kujitolea muhanga kwa mali zake na nafsi yake, na

kumtuliza kutokana na hofu aliyokuwa nayo (rehma na amani zimshukie) wakati

alipoteremshiwa wahyi katika jabali la Hiraa,na kumwambia kwa kujiamini, na

wala kutetereka: “ hakika Mwenyezi Mungu hakuhuzunishi katu, wewe utaunga

ukoo, na kubeba yote na kumpata asiyekuwepo, na kumtuliza mgeni na kusaidia

kwenye haki. (Bukhari) akawa ni katika wake wema sana mwenye kujua wajibu

wake na haki. Vilevile Mtume (rehma na amani zimshukie) alikuwa akimtaja sana

na kumsifia, kutoka kwa Aisha (radhi za Mwenyezi Mungu) amesema: Mtume

(rehma na amani zimshukie) alikuwa akitajwa Khadija huwa anamsifia,, akasema:

“ nikawa na wivu siku moja, nikasma: “mbona unamtaja sana huyu mwenye uso

mwekundu yaani khadija ,na Mwenyezi Mungu amekubadilishia mbora kuliko

yeye. Mtume akasema (rehma na amani zimshukie) Mwenyezi Mungu

hajanibadilishia mbora zaidi yake, kwani yeye aliniamni wakati watu wakinipinga,

na kuniona ni mkweli wakati watu wakiniona ni mwongo, na kuniliwaza kwa mali

zake wakati watu walinitenga, na Mwenyezi Mungu amenipatia kutoka kwake

watoto wakati sikupata watoto kutoka kwa wanawake wengine.” (Ahmad)

Na mfano mwengine mwema na wa kuigwa wa masahaba wa kike (radhi za

Mwenyezi Mungu ziwashukie) ni Mama Umarah nasiybah bint Ka`ab Al answari

ambaye Mtume (rehma na amani zimshukie ) alisema kuhusu yeye: “ mimi katika

vita ya Uhud sikuwa nikigeuka upande wa kulia wala wa kushoto isipokuwa

nilikuwa nikimuona Umu Umarah akipigana pamoja nami.” Mpaka mtu akitaka

kumuua Mtume (rehma na amani zimshukie) anamuona Umu Umrah yupo mbele

yake, na hupigana naye kwa panga mpaka bega lake likajawa na damu kutokana na

mapigo ya mapanga. Mtume akamwambia: “ ni adhabu gani uipatayo ewe umu

umarah, akajibu”: “lakini ninaweza kuivumilia, ninaweza, ninaweza ewe Mjumbe

wa Mwenyezi Mungu. Mtume (rehma na amani zimshukie) niombe ewe Umu

Umarah” akasema: “naomba niwe nawe peponi ewe Mjumbe wa Mwenyezi

Mungu. Mtume (rehma na amani zimshukie) akasema sio wewe peke yako bali na

watu wa nyumba yako pia. Akasema (radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie) sijali

kwa yanipatayo duniani.” Kitabu cha Siyra A`alam Anubalaa)

Na iwapo tunataka kuendelea na kuokoa na matatizo na kufanikiwa kwa kupata

radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu hapa duniani na kesho akhera, basi hatuna

budi tufuate mwangaza tuliomurikiwa kwa nuru ya masahaba wa Mtume (rehma

na amani zimshukie) na kufuata mwenendo waona tabia zao, wao ni kigezo cha

waumini na waislamu wote. Mtume (rehma na amani zimshukie ) katuhimiza

kuwafuata na kushikamana na mwenendo wao pia, kutoka kwa Urbaadh bin

Sariyah kuwa Mtume (rehma na amani zimshukie) amesema: “ jilazimisheni

kufuata mwenendo wangu na mwenendo wa makhalifa walioongoka, na chukueni

kwa kukaza magego, na tahadharini na yenye kuzuka, kwani kila la uzushi ni

upotofu.” (Ibn Majah).

Na juu yetu kujifunza na watoto wetu na wake zetu juu ya mwenendo wa

masahaba watukufu, ni namna gani walikuwa wakimfuata Mtume (rehma na amani

zimshukie) na kujitolea kwao muhanga kwa ajili ya kuinusuru dini na kumnusuru

Mtume (rehma na amani zimshukie) kwani waliziuza nafsi zao kwa ukweli na kwa

uyakini hii yote ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu mtukufu.

Haki ya mtoto katika ukuaji mzuri na maisha bora na

maandalizi mazuri kwa ajili ya mustakbali

Prof. Muhammad Mukhttar Juma

Waziri wa wakfu

Kimefasiriwa na

Prof. Ayman Ibrahim Al-Asar

11 jamad Uwla 1437 H. Sawa na 19-2-2116 A.D.

Kwanza : Vipengele

Watoto ni neema kutoka kwa Mwenyezi Mungu inapaswa kuishukuru.

Huduma ya uisilamu kwa watoto

Nguzo muhimu za ukuzaji mzuri wa watoto.

Kumchagulia jina zuri.

Kumnyonyesha kidesturi.

Kuwafanyia wema na kuacha kutumia nguvu na ukali

Uadilifu na usawa kwa watoto wote.

Ulazima wa kuwahakikishia watoto maisha bora.

Umuhimu wa kuwa na tama maishani mwetu.

Dalili: ndani ya Kurani tukufu na hadithi

Mwenyezi Mungu anasema: { Ufalme wa mbingu na ardhi ni wa Mwenyezi

Mungu anaumba apendavyo, anamtunukia amtakaye watoto wa kike, na

anamtunukia amtakaye watoto wa kiume. 51 Au huwachanganya wanaume

na wanawake, na akamfanya amtakaye tasa. Hakika Yeye ni Mjuzi Mwenye

uweza.}Ashura, 49-51.

Mwenyezi Mungu anasema: { Na Mwenyezi Mungu amekuumbieni wake

katika jinsiyenu, na akakujaalieni kutoka kwa wake zenu wana nawajukuu, na

akakuruzukuni vitu vizuri vizuri. Basi je, wanaamini upotovu na wanazikataa

neema za MwenyeziMungu?} Anahl, 72.

Mwenyezi Mungu anasema: { Na wazazi wanawake wawanyonyeshe watoto

wao miaka miwili kamili kwa anaye taka kutimiza kunyonyesha. Na juu ya

baba yake chakula cha kina mama, na nguo zao kwa mujibu wa ada. Wala

halazimishwi mtu ila kwa kadiri ya uwezo wake. Mama asitiwe taabuni kwa

ajili ya mwanawe, wala baba kwa ajili ya mwanawe. Na juu ya mrithi mfano

wa hivyo. Na kama wote wawili wakitaka kumwachisha ziwa kwa kuridhiana

na kushauriana, basi si vibaya kwao. Na mkitaka kuwapatia watoto wenu

mama wa kuwanyonyesha basi hapana ubaya kwenu mkitoa mlicho ahidi

kwa mujibu wa ada. Na mcheni Mwenyezi Mungu, na jueni kwamba

Mwenyezi Mungu anayaona yote mnayo yatenda.}Albaqara, 233.

Mwenyezi Mungu anasema: { Na wale wanao sema: Mola wetu Mlezi! Tupe

katikawake zetu na wenetu yaburudishayo macho, na utujaalietuwe

waongozi kwa wachamngu }Alfurqan, 74.

Mwenyezi Mungu anasema: { Na walio amini na dhuriya zao wakawafuata

kwaImani tutawakutanisha nao dhuriya zao, na walahatutawapunja hata

kidogo katika vitendo vyao. Kilamtu lazima atapata alicho kichuma.}At tuur,

21.

Mwenyezi Mungu anasema: {Na Luqman alipo mwambia mwanawe kwa

kumpa mawaidha: Ewe mwanangu! Usimshirikishe Mwenyezi Mungu. Kwani

hakika ushirikina bila ya shaka ni dhulma iliyo kubwa. 14 Na tumemuusia mtu

kwa wazazi wake wawili. Mamayake ameichukua mimba yake kwa udhaifu

juu ya udhaifu, na kumwachisha ziwa baada ya miaka miwili. (Tumemuusia):

Nishukuru Mimi na wazazi wako. Ni kwangu Mimi ndiyo marudio. 15 Na pindi

wakikushikilia kunishirikisha na ambayo huna ilimu nayo, basi usiwat'ii. Lakini

kaa nao kwa wema duniani, nawe ishike njia ya anaye elekea kwangu. Kisha

marejeo yenu ni kwangu Mimi, na Mimi nitakuambieni mliyo kuwa

mkiyatenda. 16 Ewe mwanangu! Kikiwapo kitu cha uzito wa chembe

yakhardali kikawa ndani ya jabali au ndani ya mbingu au ndani ya ardhi, basi

Mwenyezi Mungu atakileta. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa

yaliyofichika, Mwenye khabari za yote. 17 Ewe mwanangu! Shika Sala, na

amrisha mema, na kataza maovu, na subiri kwa yanayo kupata. Hayo ni

katika mambo ya kuazimiwa. 18 Wala usiwabeuwe watu, wala usitembee

katika nchi kwa maringo. Hakika Mwenyezi Mungu hampendi kila

anayejivuna na kujifakhirisha. 19 Na ushike mwendo wa katikati, na

teremsha sauti yako. Hakika katika sauti mbaya zote bila ya shaka iliyo zidi ni

sauti ya punda.}Luqman 13-19.

Mwenyezi Mungu anasema: {Enyi mlio amini! Jilindeni nafsi zenu na ahali

zenuna Moto ambao kuni zake ni watu na mawe. WanausimamiaMalaika

wakali, wenye nguvu, hawamuasi Mwenyezi Mungu kwa anayo waamrisha,

na wanatenda wanayoamrishwa} At tahriim, 6.

Dalili za hadithi

Kutoka kwa Umar (Mwenyezi Mungu amwie radhi) hakika Mtume (rhma na

amani zimshukie juu yake) amesema: nyote ni wachungaji, na nyote

mutaulizwa juu ya mulivyovichunga. Imamu ni mchungaji naye ataulizwa juu

ya aliowachunga, mume ni mchungaji juu ya watu wake naye ataulizwa juu

ya aliowachunga, mke ni mchungaji katika nyumba ya mumewe naye

ataulizwa juu ya aliowachunga, mtumishi ni mchungaji juu ya mali ya bwana

wake naye ataulizwa juu ya alichokichunga.” Mpokezi akasema nadhani

alisema: “kijana ni mchungaji wa mali ya baba yake naye ataulizwa juu ya

alichokichunga, nyote ni wachungaji na mutaulizwa juu ya mulichokichunga.”

(Bukhari)

Kutoka kwa Maaqil bin Yasaar (Mwenyezi Mungu amwie radhi) kutoka kwa

mjumbe wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani zimshukie juu yake)

amesema: “hakuna mja ambaye Mwenyezi Mungu humpa wa kumchunga,

akafariki mchungaji hali ya kuwa amefanya hadaa basi Mwenyezi Mungu

atamuharamishia pepo.” (Bukharin a Muslim).

Kutoka kwa Ibn Abbas (Mwenyezi Mungu awawie radhi) amesema: “siku

moja nilikuwa nyuma ya mtume (rehma na amani zimshukie juu yake)

akasema: “ ewe kijana mimi nitakufundisha maneno, muhifadhi Mwenyezi

Mungu naye atakuhifadhi, muhifadhi Mwenyezi Mungu utamkuta mbele

yako, na pale uombapo basi muombe Mwenyezi Mungu, na pale utakapo

msaada basi taka msaada kutoka kwa Mwenyezi Mungu, tambua kuwa lau

umma utakusanyika juu ya kutaka kukunufaisha kwa kitu basi hawataweza

kukunufaisha isipokuwa kile alichokuandikia Mwenyezi Mungu. Na lau

wakikusanyika juu ya kutaka kukudhuru kwa kitu basi hawataweza

kukudhuru kwa kitu isipokuwa kile alichokuandikia Mwenyezi Mungu,

kalamu zishanyanyuliwa na kurasa zishakauka.” (Tirmidhi).

Kutoka kwa Abdalla Bin Amru bin A`s (Mwenyezi Mungu awawie radhi)

amesema: nimemsikia mjumbe wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani

zimshukie juu yake) akisema: “mtu inatosha kuwa na madhambi kwa kule

kutomjali anaye mlea.” (Kitabu cha Hakim).

Kutoka kwa Saad Bin Abi Waqas (Mwenyezi Mungu awawie radhi) amesema:

“mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) alikuwa akinitembelea mwaka

wa hija ya kuagana, kutokana na maumivu yaliyonizidi, nikasema: “

nimefikwa na maumivu, nami nina mali, na hakuna atakayeirithi isipokuwa

mwanangu wa kike, je nitoe sadaka thuluthi mbili za mali yangu? Akasema :

“hapana,” nikasema: “nusu? Akasema: “Hapana”, kisha akasema: “ thuluthi,

na thuluthi ni nyingi, kwani wewe ukiacha kizazi chako matajiri ni bora kuliko

kuwaacha ni watu waombao wengine, kwani (pia) hutumii matumizi yoyote

aikawa uanataka radhi za Mwenyezi Mungu isipokuwa utalipwa kwayo.”

(Bukhari).

Kutoka kwa Thauban (Mwenyezi Mungu amwie radhi) amesema, amesema

mjumbe wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani zimshukie juu yake) “Dinari

bora aitoayo mtu ni ile dinari anayoitoa kwa ajili ya familia yake, na dinari

aitoayo kwa ajili ya kipando chake katika njia ya Mweneyzi Mungu na dinari

aitoayo kwa wenzake katika njia ya Mweneyzi Mungu.” Abu Qalabah

akasema “ akaanza kwa watoto, kisha akasema Abu Qilabah: na hakuna mtu

mwenye kupata malipo mazuri kama Yule anayetoa kwa ajili ya watoto ili

kuwazuilia wasiombe au kuwanufaisha kwa ajili ya Mweneyzi Mungu na

kuwatosheleza.” (Muslim).

Kutoka kwa Athman Hatabiy amesema: nimemsikia Ibn Umar (Mwenyezi

Mungu amwie radhi) akimwambia kijana: “ mfunze heshima (adabu)

mwanao, kwani wewe utaulizwa juu ya mwanao, ni kitu gani umemfunza? Na

yeye ataulizwa juu ya wema wako na kukutii kwako.” (Imam Albayhaqiy –

Sunan Kubra).

Kutoka kwa Abi Dardai (Mwenyezi Mungu amwie radhi) amesema: amesema

mjumbe wa Mweneyezi Mungu (rehma na amani zimshukie juu yake) “hakika

nyinyi mtaitwa siku ya kiama kwa majina yenu na majina ya baba zeni, basi

majina yenu yafanyeni kuwa mazuri.” (imepokewa na Daud).

Kutoka kwa Aamir, amesema: nimemsikia Nuumaan bin Bashiir (Mweneyzi

Mungu awawie radhi) naye yuko juu ya membari akisema: “Baba yangu

amenipa zawadi, Umrah bint Rawaha akasema: sikubali mpaka mtume

(rehma na amani zimshukie juu yake) aishuhudie. Mtume (rehma na amani

zimshukie juu yake) akaja, akasema: “mimi nimempa mwanagu kutoka kwa

Umrah bint Rawaha zawadi, akaniamrisha kuwa nikufanye wewe kuwa ndiye

shahidi ewe mjumbe wa Mwenyezi mungu, akasema: “je wanao wengine

umewapa kama hiki?” akasema: “ hapana.” Akasema “ muogopeni Mwenyezi

Mungu na fanyeni uadilifu juu ya watoto wenu.” Akasema, akaichukua

zawadi yake. (Bukhari).

Kutoka kwa Umara Bin Salama (Mwenyezi Mungu awawie radhi) amesema:

nilikuwa katika chumba cha mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) na

mkono wangu ulikuwa ukitangatanga ndani ya sahani akaniambia “ewe

kijana taja jina la Mwenyezi Mungu ( sema Bismillahi) na kula kwa mkono

wako wa kulia na kula kilicho mbele yako.”

Tatu: Maudhui

Miongoni mwa neema kubwa sana ambazo Mweneyezi Mungu

amemneemesha mwanadamu baada ya imani ya Mweneyezi Mungu

Mtukufu ni neema ya mtoto ambayo huhifadhi kizazi na hutuliza moyo.

Watoto ni neema ya Mwenyezi Mungu, ni zawadi kutoka kwake humpa

amtakae katika waja wake, Mwenyezi Mungu anasema: { Ufalme wa mbingu

na ardhi ni wa Mwenyezi Mungu anaumba apendavyo, anamtunukia

amtakaye watoto wa kike, na anamtunukia amtakaye watoto wa kiume. 51

Au huwachanganya wanaume na wanawake, na akamfanya amtakaye tasa.

Hakika Yeye ni Mjuzi Mwenye uweza }Ashuura, 49-51. Watoto huyafanya

maisha kuwa ni ya furaha na ucheshi, huondoa kiza ndani ya nyumba na

huingiza mwanga, wao ni taa za nyumba, utulivu wa macho na ni vipenzi vya

nyoyo, wao ni pambo la maisha ya dunia, kama alivyosema Mola wetu ndani

ya Kuran Tukufu {Mali na wana ni pambo la maisha ya dunia. Na

memayanayo bakia ni bora mbele ya Mola wako Mlezi kwamalipo, na bora

kwa matumaini.} Kahf 46.

Hivyo basi, neema hii – ya watoto – inapasa kushukuriwa Mwenyezi Mungu

Mtukufu, kipenzi cha Mwenyezi Mungu mtume Ibrahim (rehma na amani

zimshukie juu yake) baaya ya kupewa mwana na Mwenyezi Mungu alisema:

{Alhamdulillahi! Himdi zote ni za Mwenyezi Mungu aliye nipa juu ya uzee

wangu Ismail na Is-haq. Hakika Mola wangu Mlezi ni Mwenye kusikia

maombi. 41. Mola wangu Mlezi! Nijaalie niwe mwenye kushika Sala, na

katika dhuriya zangu pia. Ewe Mola wetu Mlezi, na ipokee dua yangu.}

Ibrahim 39-41. Kuishukuru neema ni kuihifadhi, Mwenyezi Mungu Mtukufu

anasema { Na alipo tangaza Mola wenu Mlezi: Mkishukuru nitakuzidishieni;

na mkikufuru, basi adhabu yangu ni kali } Ibrahim, 7. Na inapasa

kuwahudumia ili akue katika kizazi kitakachomtambua Mwenyezi Mungu,

kujua haki za wazazi wake, haki za jamii na taifa.

Uisilamu umetoa huduma kubwa sana kwa watoto na kwa kuwalea vyema

basi hupatikana furaha duniani na akhera kwa watoto na wazazi. Uisilamu

ukamjali mtoto kabla hata ya kuja duniani ukamtaka mwenye kutaka kuoa

achague mke mwema, kwani nyumba itakapokuwa imezingirwa na mazingira

ya imani athari zake njema huenea kwa waliomo, na hivi ni kama alivyosema

Mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) aliposema: “ ..mchague aliye na

dini mikono yako ipate kubarikiwa” (Muslim).. na uisilamu umejali mtoto

kabla ya hata kuanzishwa kwa taasisi za kimataifa zeneye kujali haki za

watoto, kwa kuwa kipindi hiki ni hatari na chenye misukosuko katika maisha

ya mwanadamu. Utoto ni kipindi kigumu na uhimu ambacho kila mtu ni

lazima apitie kisha apitea ujana. Hivyo, uisilamu ukajali sana utoto ili wawe

ongezeko zuri na chanzo chenye kuwa na faida katika jamii. Ukawapa

hukumu (sheria) nyingi kuhusu wao ambazo zinarudi kwa mtoto, familia,

kisha jamii kwa manufaa na faida njema.

Uisilamu umechunga kuhusu watoto tokea yupo tumboni mwa mama yake,

ukaweka hukumu na sheria zenye kumkinga na kumlinda uanadamu wake

katika kumchunga na kumpa malezi yote anayostahiki., hiki ni kipindi cha

mwanzo ambacho pia anastahiki kutunzwa na kuchungwa. Kwa maana hiyo,

uisilamu umedhamini haki ya maisha yake hali ya kuwa bado yu tumboni

mwa mama yake. Ukaharamisha utoaji wa mimba kwa makusudi, na

kuwajibisha kutunzwa kwa mama mja mzito, na ukaruhusu kwa mama mja

mzito kutofunga katika mwezi wa Ramadhani pindi akihofia mtoto wake

tumboni, mpaka akue kama kawaida. Kutoka kwa Anas (Mwenyezi Mungu

amwie radhi) kwamba mtume (rehma na amani zimshukie juu yake

amesema: “ hakika ya Mweneyzi Mungu ameondosha kwa msafiri nusu sala

na funga na kwa mja mzito na mwenye kunyonyesha.” (Nisai).

Vilevile katika yanayohusu kutunzwa kwa watoto: kumchagulia jina zuri,

wazazi waliotangulia walikuwa wakijilazimisha kuwachagulia wana wao

majina mazuri watakayoitwa, kwani jina zuri huleta furaha nyoyoni na utulivu

tafauti na jina baya. Kutoka kwa Abi Dardai (Mwenyezi Mungu amwie radhi)

amesema: amesema mjumbe wa Mweneyezi Mungu (rehma na amani

zimshukie juu yake) “hakika nyinyi mtaitwa siku ya kiama kwa majina yenu na

majina ya baba zenu, basi majina yenu yafanyeni kuwa mazuri.” (imepokewa

na Daud). Wazazi wawili wanaporuzukiwa mwana basi wameamrishwa

wamchagulie jina zuri, mtume (rehma na amani zimshukie juu yake)

amesema “mtoto anakuwa katika rehani kwa akika yake, atachinyiwa siku ya

saba, atapewa jina, na kunyolewa kichwa chake.” (Tirmidhi).

Mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) amependelea kwa umma wake

wachague majina ayapendayo Mwenyezi Mungu, kutoka kwa Naafi`, kutoka

kwa Ibn Umar (Mwenyezi Mungu awawie radhi) amesema: “ majina

yapendwayo na Mwenyezi Mungu ni Abdullah na Abdulrahman.” (Abu

Daudi). Nakatika mapokezi ya imamu Muslim, kutoka kwa Umar, amesema:

amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani zimshukie juu

yake): “ hakika majina yenu yapendwayo sana na Mwenyezi Mungu ni

Abdullah na Abdulrahman.” Na mtume (rehma na amani zimshukie juu yake)

alikuwa akikataza kuwaita wana majina mabaya, akasema “ usimwite mtoto

wako jina la Rabaha wala Yasara wala Aflaha wala Naafia` (Muslim).

Na sababu ya kukatazwa kuitwa majina mabaya ni kwa upande wa nafsi ya

mtoto, ili isije kumsababishia aina Fulani ya makero ya nafsi. Mzee mmoja

alikuja kwa Umar bin Khatwab (Mwenyezi Mungu amwie radhi) akimshtakia

kuhusu mwanawe, Umar akawita mzazi na mwanawe na kumlaumu mwana

juu ya haki ya mzazi wake na kwa kusahau kwake haki hizo, mtoto akasema,

ewe kiongozi wa waumini, kwani mtoto hana haki kwa wazazi wake?

Akasema: “anazo.” Akamuuliza: “ ni zipi haki zenyewe? Akasema Umar: “ ni

kuwa mwema mama yake, kumchagulia jina zuri, kumfundisha kitabu

(kurani). Mtoto akasema: “ewe kiongozi wa waumini hakika baba yangu

hakufanya hata moja katika hayo, mama yangu alikuwa mtu mweusi

aliyekuwa akimilikiwa na mwenye kuabudu moto na ameniita kombamwiko

(mbawakawa) na wala hakunifundisha hata herufi moja ndani ya kitabu.

Umar akamgeukia mzee akamwambia, “wewe umekuja kwangu kumshtakia

mwanao juu ya haki yako, lakini wewe umekeuka haki zake kabla ya yeye

kukeuka haki zako na umemtendea sivyo kabla ya yeye kukutendea sivyo.”

(Malezi ya watoto katika uisilamu).

Sufyan Thauri amesema: “ haki ya mtoto kwa wazazi wake ni kuitwa jina zuri,

kumuoza pindi akibaleghe, na kumfunza heshima (adabu) njema.” Kwani

kumchagulia jina zuri humsaidia katika kuishi maisha mazuri atakayoweza

kuepukana na kutaniwa na kufanyiwa kujeli, pia atapata raha na utulivu wa

nafsi pale atakapoitwa kwa jina lake, jina ni kitambulisho cha mtu.

Na katika matunzo ya uislamu kwa mtoto: inatakiwa kumyonyesha iwe ni

haki yake inayotambulika, Mwenyezi Mungu anasema: { Na wazazi

wanawake wawanyonyeshe watoto wao miaka miwili kamili kwa anaye taka

kutimiza kunyonyesha. Na juu ya baba yake chakula cha kina mama, na nguo

zao kwa mujibu wa ada. Wala halazimishwi mtu ila kwa kadiri ya uwezo

wake. Mama asitiwe taabuni kwa ajili ya mwanawe, wala baba kwa ajili ya

mwanawe. Na juu ya mrithi mfano wa hivyo. Na kama wote wawili wakitaka

kumwachisha ziwa kwa kuridhiana na kushauriana, basi si vibaya kwao. Na

mkitaka kuwapatia watoto wenu mama wa kuwanyonyesha basi hapana

ubaya kwenu mkitoa mlicho ahidi kwa mujibu wa ada. Na mcheni Mwenyezi

Mungu, na jueni kwamba Mwenyezi Mungu anayaona yote mnayo

yatenda.}Albaqara, 233. Katika aya hizi tukufu wazazi wa kike

wameamrishwa kama kwamba wameambiwa. “enyi wazazi wanyonyesheni

watoto wenu kwa miaka miwili kamili, kani mtoto kipindi hiki huwa anahitaji

maangalizi muhimu ya chakula ambayo yatamsaidia katika kukuza mwili

wake na hakuna chakula kilicho bora kama maziwa ya mama yake ambayo

Mwenyezi Mungu ameyaandaa kwa ajili hiyo. Na amesema kweli Mwenyezi

Mungu: { Asijue aliye umba, naye ndiye Mjua siri, Mwenyekhabari?} Almulk

14. Ama iwapo mama ana matatizo ambayo kisheria ameruhusika

kutonyonyesha au mtoto kajizuilia kunyonya au mzazi kufariki basi hapa

sheria ya kiisilamu imelazimisha kwa mzazi wa kiume kumtafuta myonyeshaji

wa huyu mwana kwa malipo ili mwana apate usalama wake.

Na elimu za kiafya na nafsi zimethibitisha kuwa kipindi cha kunyonyesha

mtoto kilichotajwa kisheria cha miaka miwili ni lazima kwa ajili ya ukuaji wa

mtoto ukuaji unaohitajika nayo ni kwa pande mbili:- kisiha na kinafsi. Na

kumkuza mtoto katika mazingira ya upendo, utulivu na amani nayo haya yote

hayapatikani isipokuwa kwa mama ambaye atamsaidia mwana kukua katika

ukuaji bora na kumfanya aishi maisha mazuri.

Na miongoni mwa misingi ya ukuzaji wa mtoto: kumtendea wema na kuacha

kutumia nguvu na ukali. Kwani hujulikana kisheria kuwa upendo hauleti

isipokuwa jema. Kutoka kwa mama wa waumini Aisha (Mwenyezi Mungu

amwie radhi) hakika mjumbe wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani

zimshukie juu yake) amesema: “ewe Aisha Mwenyezi Mungu ni mpole naye

hupenda upole, humpa mwenye mpole kile ambacho hampi (humnyima)

asiyekuwa na upole (mwenye kutumia mabavu) na kile ambacho hawapi

wengineo.” (Muslim). Nguvu na ukakamavu katika malezi na kutumia

mabavu katika malezi hupelekea kumfanya mtoto mara nyingi kuharibika

kitabia na kumfanya amchukie mzazi wake (mlezi) na kutosikia maneno yake.

Imepokewa katika hadithi tukufu kwa mba mtume (rehma na amani

zimshukie juu yake) alikuwa akimbeba Hassan na Hussein (Mwenyezi Mungu

awawie radhi) juu ya mabega yake na akicheza nao. Na katika misingi

aliyotumia mtume mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) ilikuwa ni

upole na ulaini. Kutoka kwa Burayda kapokea kutoka kwa baba yake

amesema: “mtume alipokuwa juu ya mimbari akihutubia, mara Hassan na

Hussein wakaingia hali ya kusota na walikuwa wamevaa nguo nyekundu,

mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) akashuka akawabeba kisha

akasema: “Mwenyezi Mungu amesema kweli { Hakika mali yenu na watoto

wenu ni jaribio} Ataghaabun,15. Nami nimewona hawa wakitembea na

kusota sikuweza kusubirio bali nikashuka na kuwabeba (Nisai).

Mlezi mwema- sawa ni mzazi au mwalimu – yeye ndie achungae misingi hii

mikubwa ya malezi nayo ni matendo ya upole na laini. Na kujiepusha na

maguvu na ukakamavu, hutibu tatizo kwa hekima na upole, maguvu

husababisha hofu ndani ya nyoyo ya mtoto na woga ukiachana na wasiwasi

wa kinafsi na kuona haya na kutojiamini. Ahnaf bin Qiys amesema katika

moja ya nasaha zake: “ usiwe kwao kufuli ili wasije wakatamani kifo chako na

wakachukia kukuona upo karibu nao na kuyachukia maisha yako.”

Kuwatendea upole haina maana kuwa usitumie adhabu wakati inapobidi,

lakini ni lazima tukumbushe kuwa adhabu ni lazima iwe kwa hekima na wala

isiwe kwa kila kosa alikosalo (alitendalo).

Na vilevile miongoni mwa malezi bora kwa watoto: ni uadilifu na usawa kati

yao. Uadilifu kwa viumbe vyote ni haki ya lazima katika sheria ya kiisilamu,

Mwenyezi Mungu anasema {Enyi mlio amini! Kuweni wasimamizi madhubuti

kwa ajili ya Mwenyezi Mungu mkitoa ushahidi kwa haki. Wala kuchukiana na

watu kusikupelekeeni kutofanya uadilifu. Fanyeni uadilifu. Hivyo ndio kuwa

karibu mnona uchamngu. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika

MwenyeziMungu anazo khabari za mnayo yatenda}Almaida, 8. Na jambo hili

linapasa kwanza lianze kwa mzazi na watoto wake.

Mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) ameelekeza wazazi wa kike na

wa kiume misingi ya lazima ambayo ni lazima waifuate, si hivyo tum bali pia

ameambatanisha na uchaji wa Mungu Mtukufu, kutoka kwa Amir, Kutoka

kwa Aamir, amesema: nimemsikia Nuumaan bin Bashiir (Mweneyzi Mungu

awawie radhi) naye yuko juu ya membari akisema: “Baba yangu amenipa

zawadi, Umrah bint Rawaha akasema: sikubali mpaka mtume (rehma na

amani zimshukie juu yake) aishuhudie. Mtume (rehma na amani zimshukie

juu yake) akaja, akasema: “mimi nimempa mwanagu kutoka kwa Umrah bint

Rawaha zawadi, akaniamrisha kuwa nikufanye wewe kuwa ndiye shahidi ewe

mjumbe wa Mwenyezi mungu, akasema: “je wanao wengine umewapa kama

hiki?” akasema: “ hapana.” Akasema “ muogopeni Mwenyezi Mungu na

fanyeni uadilifu juu ya watoto wenu.” Akasema, akaichukua zawadi yake.

(Bukhari). Na imepokewa na Abdulrazaak katika kitabu chake kwamba

mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) alimuita kijana mmoja wa

kianswar, akaja (mbele ya mtume) kisha mtoto wake wa kiume akaja na

akambusu na kumbeba na kumkumbatia na kukaa nae, kisha (baadae) akaja

mtoto wake wa kike akamshika mkono akammkalisha chini, mtume rehma na

amani zimshukie juu yake) “lau ungeliwafanyia uadilifu ingelikuwa ni bora

kwako, jikurubisheni kwa watoto wenu hata pale munapowabusu.”

Na katika kufanya uadilifu kwa wote kuna faida kubwa mno na huwasaidia

ndugu kusaidiana katika mema na pia huwasaidia katika kutengeneza kizazi

chema ndani ya jamii kama inavyosaidia kujenga undugu wa ukweli kati ya

jamaa.

Kinyume na haya tunaona mtafaruku kati ya wanandugu ambayo ni sababu

kubwa sana ya kuasi wazazi, kuwakimbia na kuwachukia na pia ni sababu ya

kupandikiza chuki kati ya wanandugu.

Baadhi ya matukio ya wanaelimu ya nafsi yamethibitisha kuwa mtoto mara

nyingi humili kuhisi kufanya mabaya kwa sababu ya dhuluma na

kutotendewa usawa ndani ya familia. Na mfano mzuri sana ni kisa cha nabii

Yussuf (rehma na amani ziwe juu yake) kwa kuboreshwa kwake zaidi yao,

Mwenyezi mungu anasema {Kwa yakini katika Yusuf na nduguze ziko ishara

kwawanao uliza 8.Pale walipo sema: Hakika Yusuf na nduguyewanapendwa

zaidi na baba yetu kuliko sisi, hali sisini kikundi chenye nguvu. Hakika baba

yetu yumo katika upotofu wa dhaahiri. 9. Muuweni Yusuf, au mtupeni nchi

mbali ili uso wababa yenu ukuelekeeni nyinyi. Na baada ya haya

mtakuwawatu wema.} Yusuf 7-9.

Vilevile katika misingi ambayo uisilamu umeiweka kwa ajili ya kudhibiti ukuaji

bora wa mtoto: ni malezi na mafundisho ya sheria. Mwenyezi Mungu

mtukufu amewamrisha wazazi wa kike na wa kiume ndani ya kurani tukufu

umuhimu wa kuikinga nafsi na jamaa ili wasiingia katika maangamizi,

akasema {Enyi mlio amini! Jilindeni nafsi zenu na ahali zenuna Moto ambao

kuni zake ni watu na mawe. WanausimamiaMalaika wakali, wenye nguvu,

hawamuasi Mwenyezi Mungu kwa anayo waamrisha, na wanatenda

wanayoamrishwa}At tahrim, 6. Na kumlea mtoto na kumfundisha adabu ni

misingi itakiwayo na sheria nazo pia ni haki miongoni mwa haki za mtoto kwa

wazazi wake. Kutoka kwa Ibn Abass (mwenyezi Mungu awawie radhi)

wamesema: ewe mjumbe wa Mweneyzi Mungu, tumekwisha elewa haki ya

mzazi kwa mwanawe, lakini ni zipi haki za mwana kwa mzazi? Akasema;

“kumfundisha adabu njema na kumlea vizuri.” (Sehemu ya imani. Kitabu cha

Bayhaqiy) na amepokea Tirmidhi katika kitabu chake kwamba mtume (rehma

na amani zimshukie juu yake amesema: “hakuna wema autendao mzazi kwa

mwana kuliko wema wa kumlea malezi mema.”

Na miongoni mwa misingi muhimu ya ukuzaji watoto ni kuwaelekeza na

kuwalea malezi bora, malezi na maelekezo yanatakikana yawe kwa utaratibu

na si mbele ya wengine, na hivi ndivyo alivyokuwa akifanya mtume (rehma

na amani zimshukie juu yake) Kutoka kwa Ibn Abbas (Mwenyezi Mungu

awawie radhi) amesema: “siku moja nilikuwa nyuma ya mtume (rehma na

amani zimshukie juu yake) akasema: “ ewe kijana mimi nitakufundisha

maneno, muhifadhi Mwenyezi Mungu naye atakuhifadhi, muhifadhi

Mwenyezi Mungu utamkuta mbele yako, na pale uombapo basi muombe

Mwenyezi Mungu, na pale utakapo msaada basi taka msaada kutoka kwa

Mwenyezi Mungu, tambua kuwa lau umma utakusanyika juu ya kutaka

kukunufaisha kwa kitu basi hawataweza kukunufaisha isipokuwa kile

alichokuandikia Mwenyezi Mungu. Na lau wakikusanyika juu ya kutaka

kukudhuru kwa kitu basi hawataweza kukudhuru kwa kitu isipokuwa kile

alichokuandikia Mwenyezi Mungu, kalamu zishanyanyuliwa na kurasa

zishakauka.” (Tirmidhi).

Kisha tena mtume (rehma na amani zimshukie juu yake analea na kufunza na

kuelekeza adabu njema kwa kupigia mifano mizuri juu ya mtoto, imepokewa

Kutoka kwa Umara Bin Salama (Mwenyezi Mungu awawie radhi) amesema:

nilikuwa katika chumba cha mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) na

mkono wangu ulikuwa ukitangatanga ndani ya sahani akaniambia “ewe

kijana taja jina la Mwenyezi Mungu ( sema Bismillahi) na kula kwa mkono

wako wa kulia na kula kilicho mbele yako.”(Muslim). Imam ghazali (Mweyezi

Mungu amrehemu) “mtoto ni amana mbele ya wazazi wake, moyo wake uko

safi suio na dosari, pindi ukizoweshwa mazuri na kufundishwa mema basi

atafurahia duniani na akhera.”

Juu ya mlezi awe kiongozi kwa watoto wake, ajiweke katika tabia njema kabla

ya kuwaamrisha, kwani watoto huiga.

Ana haki aliyesema:

Watoto wetu hukuwa kutoka kwetu * kama vile wazazi wake

walivyomzowesha

Na la msingi kulitaja ni kuwa, malezi hayawi kwa wazazi peke yaolakini pia

kwa mwalimu. Mwalimu ni sehemu katika jamii na ana umuhimu na ulazima

wa kukuza kizazi kwa kuzingatia tamaduni za jamii anayoishi. Watoto

niamana inayobebwa na jamii kwa ujumla na ni jukumu lililo katika shingo

zao, na inapasa kuwalea ipasavyo.wote pamoja wafahamu jukumukubwa

walilolibeba kuhusu watoto, na hakuna mfano wa wazi zaidi ya kauli ya

mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) Kutoka kwa Umar (Mwenyezi

Mungu amwie radhi) hakika Mtume (rehma na amani zimshukie juu yake)

amesema: “nyote ni wachungaji, na nyote mutaulizwa juu ya

mulivyovichunga. Imamu ni mchungaji naye ataulizwa juu ya aliowachunga,

mume ni mchungaji juu ya watu wake naye ataulizwa juu ya aliowachunga,

mke ni mchungaji katika nyumba ya mumewe naye ataulizwa juu ya

aliowachunga, mtumishi ni mchungaji juu ya mali ya bwana wake naye

ataulizwa juu ya alichokichunga.” Mpokezi akasema nadhani alisema: “kijana

ni mchungaji wa mali ya baba yake naye ataulizwa juu ya alichokichunga,

nyote ni wachungaji na mutaulizwa juu ya mulichokichunga.” (Bukhari)

Dini ya kiisilamu inambebesha mzigo wazazi wa kuhifadhi watoto kwani

imepokewa Kutoka kwa Umar (Mwenyezi Mungu amwie radhi) hakika

Mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) amesema: hakika yaMweneyzi

Mungu atamuuliza kila mchungaji kwa kile alichokichunga je amekihifadhi au

amezembea, mpaka atamuuliza pia mume juu ya watu wa nyumba yake.”

(imepokewa na Ibn Haban.) na tumuangaliapo mtoto basi tumuangalia kama

mtu aliyekamilika na kuwa na haki zote za kimwili, kinafsi, kimali, kielimu, na

malezi na ni wajibu kuzihifadhi ili awe na maisha mema na bora na ili jamii

iwe na ustaarabu na kuenea upendo, mapenzi na huruma.

Na tunasisitiza umuhimu wa kuwa na tama juu ya watoto wetu kwa kuwa

mwanadamu hawezi kuishi bila ya tama. Hakuna maisha iwapo tamaa haipo,

na ikikosekana tamaa maisha hupotea. Wasomi wameeleza ya kuwa “kukata

tamaa ni kuchanganyikiwa na kujichanganya huwa ni katika makosa

makubwa.” Abdallah Bin Abass (Mweneyzi Mungu awawie radhi) anasema:

“kuna kijana kasema: “ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni yepi madhambi

makubwa: akasema: “kumshirikisha Mwenyezi Mungu, kupoteza matumaini

kwa Mweneyzi Mungu. kukata tamaa katika rehema za Mwenyezi Mungu, na

atakaeepushwa na Mwenyezi Mungu na hayo basi amedhaminiwa kuingia

peponi.”

nyote ni wachungaji, na nyote mutaulizwa juu ya mulivyovichunga. Imamu ni

mchungaji naye ataulizwa juu ya aliowachunga, mume ni mchungaji juu ya

watu wake naye ataulizwa juu ya aliowachunga, mke ni mchungaji katika

nyumba ya mumewe naye ataulizwa juu ya aliowachunga, mtumishi ni

mchungaji juu ya mali ya bwana wake naye ataulizwa juu ya alichokichunga.”

Mpokezi akasema nadhani alisema: “kijana ni mchungaji wa mali ya baba

yake naye ataulizwa juu ya alichokichunga, nyote ni wachungaji na

mutaulizwa juu ya mulichokichunga.” (Bukhari)

Hatari za ulinganio potofu na umuhimu wa kuuzuia

kwa ajili ya upatikanaji wa amani na utulivu

29 Safar 1437 H.

Sawa na 11 Disemba 2115 A.D

Kwanza: Mambo muhimu

Neema ya amani na utulivu.

Utulivu wa nchi ni katika mambo ya lazima kisheria na kitaifa.

Vitendea kazi vya utulivu katika taifa.

Raia kuipenda nchi yake.

Kueneza upendo na msaada kati ya watu.

Kuwasikiliza na kuwatii viongozi wa nchi kwa lile atakalo Mwenyezi Mungu,

na kulitumikia taifa.

Kujiepusha na fitina.

Hatari ya ulinganio potofu kwa mtu mmoja mmoja na kwa jamii.

Ulazima wa kuzuia ulinganio huu.

Pili: Dalili

Ndani ya Kurani Tukufu

Mwenyezi Mungu anasema : { Na alipo sema Ibrahim: Ee Mola wangu Mlezi!

Ufanye huu uwe mji wa amani, na uwaruzuku watu wake matunda.. }

Albaqara aya ya 126.

Mwenyezi Mungu anasema : { Na Ibrahim alipo sema: Ewe Mola wangu

Mlezi! Ujaalie mji huu uwe wa amani, na uniepushe mimi na wanangu na

kuabudu masanamu.} Ibrahim aya ya 35.

Mwenyezi Mungu anasema : {Wale ambao wameamini, na

hawakuchanganya imani yao na dhulma - hao ndio watakao pata amani na

wao ndio walio ongoka. } Al an aam aya ya 82.

Mwenyezi Mungu anasema : {1. Kwa walivyo zoea Maqureshi. 2. Kuzoea

kwao safari za siku za baridi na siku za joto. 3 Basi nawamuabudu Mola Mlezi

wa Nyumba hii, 4. Ambaye anawalisha wasipate njaa, na anawalinda na

khofu.} Quraish aya ya 1-4.

Mwenyezi Mungu anasema : { Je! Kwani Sisi hatukuwaweka imara katika

pahala patakatifu, penye amani, ambapo huletewa matunda ya kila aina

kuwa ni riziki itokayo kwetu? Lakini wengi wao hawajui.} Al qaswas aya ya 57.

Mwenyezi Mungu anasema : { Je! Hawaoni ya kwamba tumeifanya nchi

takatifu ina amani, na hali watu wengine wananyakuliwa kote kwa majirani

zao? Je! Wanaamini upotovu, na neema za Mwenyezi Mungu wanazikataa? }

Al ankabuut aya ya 67.

Mwenyezi Mungu anasema : { Na baina yao na miji mingine tuliyo ibariki

tuliweka miji iliyo dhaahiri, na tukaweka humo vituo vya safari.

Tukawaambia: Nendeni humo usiku na mchana kwa amani } Sabaa aya 18.

Mwenyezi Mungu anasema : { Walio ambiwa na watu: Kuna watu

wamekukusanyikieni, waogopeni! Hayo yakawazidishia Imani, wakasema:

Mwenyezi Mungu anatutosha, naye ni mbora wa kutegemewa } Al imraan

173.

Mwenyezi Mungu anasema : { Na jikingeni na Fitna ambayo haitowasibu

walio dhulumu peke yao kati yenu. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu ni Mkali

wa kuadhibu. } Al anfaa aya 25.

Mwenyezi Mungu anasema : { Kwa hakika wale wanao penda uenee uchafu

kwa walio amini, watapata adhabu chungu katika dunia na Akhera. Na

Mwenyezi Mungu anajua na nyinyi hamjui.} Al nuur aya 19.

Mwenyezi Mungu anasema : { Enyi mlio amini! Mt'iini Mwenyezi Mungu, na

mt'iini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi. Na mkizozana katika jambo

basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa mnamuamini

Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Hayo ndiyo bora zaidi na ndiyo yenye

mwisho mwema.} Al nisaa 59.

Mwenyezi Mungu anasema : {Na linapo wafikia jambo lolote lilio khusu

amani au la kitisho wao hulitangaza. Na lau kuwa wangeli lipeleka kwa

Mtume na kwa wenye mamlaka kati yao, wale wanao chunguza wangeli lijua.

Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema yake mngeli

mfuata Shet'ani ila wachache wenu tu.} Al nisaa 83.

Hadithi za Mtume (Saw)

Kutoka kwa Ibnu Ubayd llah bin Mehsan Al-hatmiy, kutoka kwa baba yake,

amesema, amesema Mtume (Saw): “ atakaeamka hali ya kuwa yupo salama

katika nafsi yake, ana siha katika mwili wake, na ana chakula cha siku yake

basi kama kamba amemilikishwa dunia”. (Imepokewa na Tirmidhy).

Kutoka kwa Ibn Abbas (Mwenyezi Mungu amwie radhi), amesema,

amemsikia Mtume (Saw) anasema: “ macho mawili hayataguswa na moto;

jicho lililolia kwa ajili ya kumuogopa Mwenyezi Mungu na jicho lililokesha

kulinda kwenye njia ya Mwenyezi Mungu”.

Kutoka kwa Abdullah bin Ady bin Hamraa, amesema: nimemuona Mtume

(Saw) amesimama katika eneo la Haz-wara akasema: “ hakika eneo hili ni

eneo bora katika maeneo ya ardhi ya Mwenyezi Mungu, na eneo lipendwalo

na Mwenyezi Mungu, na lau kama nisingelikuwa nimefukuzwa hapa, basi

nisingelitoka”. (Kitabu cha Ahmed na Tirmidhy). Haz-wara hili ni eneo lililopo

nchini Makka.

Kutoka kwa ibn Abbas (Mwenyezi Mungu awawie radhi) amesema: amesema

Mtume (Saw) kuhusu Makka: “Mji bora ulioje na niupendao na lau kama

watu wangu hawakunifukuza basi nisingelikaa katika mji mwengine”

(Imepokewa na Tirmidhy).

Kutoka kwa Aisha (Mwenyezi Mungu amwie radhi) amesema: Mtume (Saw)

amesema: “Ewe (Mwenyezi Mungu tupendezeshe kuupenda mji wa Madina

kama ulivyotupendezesha kuupenda mji wa Makka. (Imepokewa na Bukhari).

Kutoka kwa Abi Hurayra (Mwenyezi Mungu amwie radhi) amesema:

amemsikia Mtume (Saw) akisema: “atakaenitii mimi basi hakika amemtii

Mwenyezi Mungu, na atakaeniasi basi hakika amemuasi Mwenyezi Mungu,

na atakaemtii kiongozi basi amenitii mimi, na atakaemuasi kiongozi basi

ameniasi mimi, kwani kiongozi ni kizuizi hupambana kwa ajili yao na

humuogopa Mwenyezi Mungu kwa ajili yao, na pindi akiamrisha kumtii

Mwenyezi Mungu na kufanya uadilifu atapata malipo mema kwa hilo, na

iwapo atakuwa kinyume na hivyo basi mzigo huwa ni wake. (Imepokewa na

Bukhari).

Kutoka kwa Abi Hurayra (Mwenyezi Mungu amwie radhi), kutoka kwa

Mtume (Saw) amesema: “atakaejitoa katika utiifu na kuachana na kundi

(umoja) kisha akafariki, basi huwa kafariki katika kifo cha kijahilia, na yeyote

atakaepigana chini ya bendera ya upofu, hukasirika kwa ajili ya koo yake au

huendeleza chuki au kutaka ushindi kwa koo yake kisha akafariki, basi huwa

kafariki katika kifo cha kijahilia. Na yeyote katika umma wangu akatoka

akawa anawapiga wema na waovu na wala hakuna anaesalimika nae na wala

hatimizi ahadi kwa wenye ahadi ya ulinzi, basi huyo si katika mimi na mimi si

katika yeye. (Imepokewa na Muslim).

8. Kutoka kwa Abi Hurayra (Mwenyezi Mungu amwie radhi) amesema:

“amesema Mtume (Saw): “ Itakujakuwa fitina kiasi ambacho fitina ya aliyekaa

ni bora kuliko fitina ya aliyesimama. na fitina ya aliyesimama ni bora kuliko ya

anaetembea. na fitina ya anaetembea ni bora kuliko fitina ya anaeieneza.

Yoyote mwenye kutafuta utukufu kutokana na fitina hiyo basi ataupata. Na

mwenye kupata kimbilio basi ajilinde kwa kimbilio hilo. (Imepokewa na

Bukhari na Muslim).

Tatu: Maudhui

Hakika miongoni mwa neema kubwa za Mwenyezi Mungu kwa mwanadamu

ni neema ya usalama na utulivu, bila ya hizo akili na nafsi ya mwanadamu

hautulizani, na katu hatopata furaha ulimwenguni hata kama atakuwa

anamiliki dunia na vilivyomo, kwani bila shaka furaha na neema ya

ulimwengu ni kuwepo kwa amani na utulivu, kwani katika hadithi ya Mtume

(Saw) : “ atakaeamka hali ya kuwa yupo salama katika nafsi yake, ana siha

katika mwili wake, na ana chakula cha siku yake basi kama kwamba

amemilikishwa dunia”. (Imepokewa na Tirmidhy).

Neema ya amani na utulivu ni matakwa ya kila kiumbe ulimwenguni, hata

nabii ibrahim (amani iwe juu yake) aliwaombea watu wake aliposema. {Na

alipo sema Ibrahim: Ee Mola wangu Mlezi! Ufanye huu uwe mji wa amani, na

uwaruzuku watu wake matunda, wale wanao muamini Mwenyezi Mungu na

Siku ya Mwisho.} Albaqara aya 126.

Hapa nabii Ibrahim (amani iwe juu yake) anamuomba Mwenyezi Mungu

aibariki Makka kwa amani na pato (rizki), na katanguliza kuomba amani kabla

ya rizki kwa sababu rizki haitokuwa na utamu wake pindi ikikosekana amani,

kupitia amani mwanadamu hupata utulivu na anahisi umuhimu wa maisha.

Naye Mwenyezi Mungu akamuitikia mtume wake na kipenzi chake kwa

kuifanya Makka kuwa ni sehemu tulivu kwa uwezo wake na utashi wake, na

kuifanya nchi ya uisilamu, na hii yote ni kwa baraka za maombi ya nabii

Ibrahim (amani iwe juu yake). Si hivyo tu bali nabii Ibrahim (amani iwe juu

yake) ametanguliza neema ya usalama –amani – kabla ya tauhidi, akasema

{Na Ibrahim alipo sema: Ewe Mola wangu Mlezi! Ujaalie mji huu uwe wa

amani, na uniepushe mimi na wanangu na kuabudu masanamu.} Ibrahim aya

35.

Na kama Mwenyezi Mungu mtukufu alivyowaneemesha makuraish kwa

neema hii kubwa, akawapa maisha mazuri na utulivu katika nchi, Mwenyezi

Mungu amesema :{3.Basi nawamuabudu Mola Mlezi wa Nyumba hii. 4.

Ambaye anawalisha wasipate njaa, na anawalinda na khofu.} Quraesh aya 3-

4.

Na kama alivyowaneemesha kwa kuifanya Al kaaba kuwa ni mahala pa

utulivu, Mwenyezi Mungu anasema {Je! Hawaoni ya kwamba tumeifanya

nchi takatifu ina amani, na hali watu wengine wananyakuliwa kote kwa

majirani zao? Je! Wanaamini upotovu, na neema za Mwenyezi Mungu

wanazikataa?} Al ankabuut 67.

Kupitia amani na utulivu taifa hukua na watu hupata utulivu wa maisha yao

na utafutaji wa riziki zao, taifa nalo huendelea pamoja na jamii, uchumi pia

hukua, na haya tayari Mwenyezi Mungu ameshayaeleza katika Kurani tukufu

wakati alipowaneemeha watu wa Saba-a kwa neema ya amani na utulivu,

akasema {Na baina yao na miji mingine tuliyo ibariki tuliweka miji iliyo

dhaahiri, na tukaweka humo vituo vya safari. Tukawaambia: Nendeni humo

usiku na mchana kwa amani.} Saba-a aya 18.

Hakuna taifa lililotangulia miongoni mwa mataifa, na wala jamii miongoni

mwa jamii isipokuwa amani na utulivu upo kwa raia zake.

Kuyumba kwa amani na utulivu huathiri pakubwa taifa na raia hata katika

ibada – ambayo ni lengo kuu la kuumbwa wanadamu – kwa ajili hiyo, hata

sala isaliwayo wakati wa wasiwasi (sala ya hofu) ipo tafauti na sala isaliwayo

wakati wa amani kimuundo na kimatendo. Na hata ibada ya kuhiji pia

inashurutishwa kuwepo na amani njiani, na kama njia itakuwa haina amani

basi ibada ya hijja huwa si lazima kuitimiza, hapa tunafahamu kuwa, hata

ibada haitokamilika kama itakiwavyo pindi tu pakiwa na ukosefu wa amani na

utulivu.

Amani na utulivu ukiwepo katika taifa na ikawa kila mmoja yupo salama yeye

mwenyewe, mali zake, heshima yake, bila shaka jamii hii wataishi katika

utulivu wa hali ya juu kabisa, pasi na hofu wala wasiwasi, na jamii itanufaika

kwa maendeleo na ukuaji, na maendeleo ni vitu vya lazima kisheria na ni

matakwa ya taifa pia ni lengo kuu na muhimu miongoni mwa malengo ya dini

tukufu.

Vitendea kazi vya kuleta utulivu: raia inamlazimu aipende nchi yake ambayo

anaishi kwa uhuru unaokubalika, na ahisi umuhimu wa taifa ambalo amekulia

katika mchanga wake, na hivi ndivyo alivyopiga mfano Mtume (Saw)

kivitendo, wakati anahama Makka Tukufu na kuhamia Madina Munawara,

kwani Mtume (Saw) ametufundisha mapenzi ya taifa na ubora wa

kujifaharisha nalo, na mapenzi yake (Saw) juu ya nchi yake ya Makka na hisia

zake juu ya taifa hilo ilikuwa ni jambo kubwa, pamoja na ubaya wa watu

wake, akasema ingawa ameathirika kuliacha: {Hakika hii ni ardhi bora ya

Mwenyezi Mungu na ni ardhi ya Mwenyezi Mungu niipendayo na lau kama

watu wangu hawakunifukuza basi nisingelitoka.” (Kitabu cha Ahmad na

Tirmidhy).

Na katika mapokezi ya Ibni Abbas (Mwenyezi Mungu awawie radhi)

amesema: amesema Mtume (Saw) kuhusu Makka” (“ Mji bora ulioje na

niupendao na lau kama watu wangu hawakunifukuza basi nisingelikaa katika

mji mwengine” (Imepokewa na Tirmidhy).

Na alipohamia Mtume (Saw) katika mji wa Madina akaanza kujenga taifa la

kisasa kwa lengo la kuwafundisha masahaba zake na ulimwengu kwa ujumla

ya kuwa taifa halijengwi isipokuwa kwa wale wenye kulipenda, na dua yake

kubwa ilikuwa kama ilivyokuja kutoka kwa mama wa waumini Aisha

(Mwenyezi Mungu amwie radhi) amesema: amesema Mtume (Saw) “ Ewe

Mwenyezi Mungu tupendezeshee mji wa Madina kama ulivyotupendezeshea

mji wa Makka au zaidi”. (Imepokewa na Bukhari)

Na Mtume (Saw) hakuwa akitaka kuonesha upendo wa taifa isipokuwa

kutaka kuwepo kwa amani na utulivu ili kila mmoja awe na usalama.

Kwa ajili hiyo ni lazima kwa kila raia ahifadhi taifa lake na alipende na alilinde

pia alitetee, na asimamie wajibu wake na majukumu yake kwa ajili ya taifa.

Taifa kwa mtazamo wa kiisilamu ni kitu kikubwa sana na kuzembea kuhusu

haki ya taifa ni hatari sana, kwa ajili hiyo, Mtume (Saw) amempa cheo kila

ambae atahifadhi utulivu wa taifa lake na kujitolea muhanga kwa ajili yake,

kwani Mwenyezi Mungu hatomuadhibu na wala moto hautogusa macho

yake, kwani malipo huwa sana na matendo.

Imepokewa na Ibn Abbas (Mwenyezi Mungu awawie radhi amesema:

nimemsikia Mtume (Saw) akisema; “ macho mawili hayataguswa na moto;

jicho lililolia kwa ajili ya kumuogopa Mwenyezi Mungu na jicho lililokesha

kulinda kwenye njia ya Mwenyezi Mungu”. (Imepokewa na Tirmidhy).

Kulipenda taifa ni katika mambo muhimu sana yaletayo utulivu nchini kwa

jamii yoyote, kwani mtu akilipenda taifa lake na akihisi jukumu lake la

kuhifadhi amani na utulivu na wala hayuko pamoja na wanaoliharibu katika

wenye kuhubiri, kwani mwanadamu akipata utulivu ndani ya nchi yake basi

pia utulivu wa nafsi yake utakuwepo na ataleta mafanikio katika kazi zake na

chumo lake.

Na katika vitendea kazi vya utulivu: ni kueneza upendo, ushirikiano kati ya

watu, Mtume (Saw) anasema “ Muumini kwa muumini mwenziwe ni sawa na

jengo hushikana wenyewe kwa wenyewe na kisha akagandisha vidole vyake”

(imepokewa na Bukhari na Muslim).

Na kujiepusha na tofauti na migongano, kwani hiyo ni shari inayowapelekea

kwenye mgawanyiko na upotevu, Mwenyezi Mungu anasema (Na mt'iini

Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala msizozane mkaingiwa woga, na

zikapotea nguvu zenu. Na subirini. Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na

wanao subiri) Al anfaal 46.

Tujiepushe sana na ushabiki au vikundi vikundi kwani hivyo ni shari

ipelekeayo kusambaratika kwa jamii, na inapasa kuunga jamii na kuwepo

ushirikiano ili amani na utulivu uwepo na hivi ndivyo alivyoamrisha Mwenyezi

Mungu {Na saidianeni katika wema na uchamungu. Wala msisaidiane katika

dhambi na uadui. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni

Mkali wa kuadhibu. } Almaaidah aya 2.

Na katika mambo muhimu ambayo husaidia kuleta utulivu nchini: ni kuwatii

wenye madaraka bila ya kuasi Mwenyezi Mungu, kwani Mwenyezi Mungu

anasema {Enyi mlio amini! Mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume na

wenye madaraka katika nyinyi. Na mkizozana katika jambo basi lirudisheni

kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa mnamuamini Mwenyezi Mungu na

Siku ya Mwisho. Hayo ndiyo bora zaidi na ndiyo yenye mwisho mwema}

Alnisaa 59.

Kwani wenye madaraka ni kama kivuli cha Mwenyezi Mungu katika ardhi,

kama alivyosema Mtume (Saw) “viongozi ni kivuli cha Mwenyezi Mungu

katika ardhi, yeyote atakaewakarimu naye atakirimiwa na Mwenyezi Mungu

na atakaewadhalilisha, nae atadhalilishwa na Mwenyezi Mungu”. Imepokewa

na Tabariy na Bayhaqiy.

Na pia Mtume (Saw) amesema, “yeyote atakaemkirimu kiongozi atendae kwa

ajili ya Mwenyezi Mungu duniani, basi naye Mwenyezi Mungu atamkirimu

siku ya kiyama, na yeyote atakaemdhalilisha kiongozi atendae kwa ajili ya

Mwenyezi Mungu basi naye atadhalilishwa siku ya kiyama”. (Imepokewa na

Ahmad)

Hakika kumtii kiongozi ni kwa kumtii Mwenyezi Mungu na kwa masilahi ya

taifa na kwa imani ya waisilamu, na kiongozi akimrisha au kukataza itapasa

kumtii pindi tu si katika maasi ya Mwenyezi Mungu. Imepokewa na Abi

Hurayra (Mwenyezi Mungu amwie radhi) amesema, amemsikia Mtume

(Saw): “ yeyote atakaenitii mimi basi amemtii Mwenyezi Mungu, na yeyote

atakaeniasi basi amemuasi Mwenyezi Mungu, na yeyote atakaemtii kiongozi

basi amenitii mimi, na yeyote atakae muasi kiongozi basi ameniasi mimi,

kwani kiongozi ni kizuizi hupambana kwa ajili yao na humuogopa Mwenyezi

Mungu kwa ajili yao, na pindi akiamrisha kumtii Mwenyezi Mungu na kufanya

uadilifu atapata malipo mema kwa hilo, na iwapo atakuwa kinyume na hivyo

basi mzigo huwa ni wake.” (Imepokewa na Bukhari). Kinachokusudiwa ni

kumtii kiongozi bila ya kumuasi Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kutengeneza

dini na dunia.

Kwa ajili hiyo ni wajibu wa raia kusikia na kutii viongozi, na wala asitengane

na kundi la waisilamu, imepokewa kutoka kwa Abi Hurayra, kutoka kwa

Mtume (Saw) kwamba yeye amesema: “atakaejitoa katika utiifu na kuachana

na kundi (umoja) kisha akafariki, basi huwa kafariki katika kifo cha kijahilia,

na yeyote atakaepigana chini ya bendera ya upofu, hukasirika kwa ajili ya koo

yake au huendeleza chuki au kutaka ushindi kwa koo yake kisha akafariki,

basi huwa kafariki katika kifo cha kijahilia. Na yeyote katika umma wangu

akatoka akawa anawapiga wema na waovu na wala hakuna anaesalimika nae

na wala hatimizi ahadi kwa wenye ahadi ya ulinzi, basi huyo si katika mimi na

mimi si katika yeye. (Imepokewa na Muslim).

Na huenda sababu ya kulazimika kuwatii na kuwasikiliza viongozi ni kwa vile

iwapo wataacha mema basi hapo ndipo italazimu kutowatii kwani kufanya hivyo

kutapelekea kuzidi uasi, na kitakiwacho ni kunasihiana ambako kuko kwa njia

tofauti zilizo salama na za kidemokrasia, na hii ni kwa ajili ya kufanya neno la

umma liwe ni moja, na kuzuia mipasuko na makundi, ambayo huenda

yakasababisha mauaji, umwagaji wa damu, kuvunjiana heshima, kufanya

yaliyoharamishwa, kuangamiza taifa, kupoteza mali, kudhoofisha ushirikiano na

haya yote yapo wazi kwa kila mtu kwa sababu ya matatizo yaliyosababishwa kwa

kutowasikiliza viongozi.

Na katika mambo makubwa yanayoondosha utulivu wa taifa: ni kueneza

fitina ambazo zinapelekea kuondoka kwa neema na kuleta maafa, na kukata

ushirikiano kati ya mataifa na mengine, na kueneza machafu na kuondosha

mazuri, na kutangaza roho ya uadui na chuki na kuacha kueneza roho ya

upendo na undugu.

Fitina ni moto wenye kuangamiza kikavu na kibichi, yenye kutenganisha kati

ya mtu na mwengine, mama na mwanawe, mtu na mkewe, na inampelekea

mja kuacha kumtii Mola wake. Na yeyote anaechochea fitina ni amelaanika,

na muenezaji wake ni mtu fitina mwenye kuharibu hali njema na kuzifanya

kuwa mbaya, ama muuaji na aliyeuliwa wote watafikia motoni na ni makazi

mabaya yaliyoje.

Kwa ajili hiyo, uisilamu umefanya pupa kubwa zaidi ili kuepukana na fitina, na

Mtume (Saw) ametuelekeza maelekezo ya kuweza kuepukana na fitina, na

kumfundisha muisilamu ni namna gani ataweza kutaamali na fitina. Kwani

imepokewa kutoka kwa Abdallah Bin Amru bin Al-as (Mwenyezi Mungu

awawie radhi), hakika ya Mtume (Saw) amesema: “ itakuwaje pindi

mukifikwa na wakati, ambao watu watapetwa na wakabaki wabaya kati yao

wametimizi ahadi zao na amana zao, kisha wakahitilafiana hata wakawa

kama hivi” akakutanisha vidole vyake, masahaba wakasema, unatuamrisha

nini ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Akasema: “ Kichukueni mukijuacho

kuwa ni haki, na kiacheni mukichukiacho, na mukubali jambo mulionalo ndilo

na kuacha mambo (mabaya) yatendwayo na wengi.

Shime tena shime kuhifadhi umoja wa taifa. Na tahadhari kisha tahadhari na

fitina zilizo wazi na zilizo jificha, kwani hata Mwenyezi Mungu

ametuhadharisha nazo katika sehemu nyingi ndani ya Kurani, na katika hizo

ni kama alivyosema kuwa fitina ikifika mahala huwa haibagui katia ya aiungae

mkono na aipingae, akasema { Na jikingeni na Fitina ambayo haitowasibu

walio dhulumu peke yao kati yenu. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu ni Mkali

wa kuadhibu.} Al anfaal 25.

Pia naye Mtume (Saw) ametuhadharisha sana, imepokewa kutoka kwa

hudhaifa (Mwenyezi Mungu amwie radhi, amesema, amemsikia Mtume

(Saw) akisema: “ fitina hupita nyoyoni kama nyoyo za mkeka wenye nyuzi

nyuzi wazi, nyoyo yoyote itakayoikubali, basi huwekewa kidoto cheusi na

nyoyo yoyote itakayoikataa huwekewa kidoto cheupe hata huwa cheupe

mfano wa almasi, mtu huyo hatodhuriwa na fitina kwa muda wote wa

kuwepo mbingu na ardhi. (Imepokewa na Muslim)

Kutoka kwa Abi Hurayra (Mwenyezi Mungu amwie radhi) amesema:

“amesema Mtume (Saw): “ Itakujakuwa fitina kiasi ambacho fitina ya aliyekaa

ni bora kuliko fitina ya aliyesimama. na fitina ya aliyesimama ni bora kuliko ya

anaetembea. na fitina ya anaetembea ni bora kuliko fitina ya anaeieneza.

Yoyote mwenye kutafuta utukufu kutokana na fitina hiyo basi ataupata. Na

mwenye kupata kimbilio basi ajilinde kwa kimbilio hilo. (Imepokewa na

Bukhari na Muslim).

Hakika ni wajibu kwa mwisilamu mwenye akili ajiepushe na fitina na kiali

lenye kupelekea fitina, na ataamali na fitina kwa hadhari sana, kwani

imepokewa na Anas (Mwenyezi Mungu amwie radhi) amesema; amesema

Mtume (Saw) kuwambia Maanswari: “ Mutakuja kuona baada yangu athari,

basi kuweni na subira mpaka mutakapokutana nami, na ahadi yenu ni

kunywa katika hodhi. Hapa Mtume (Saw) anakusudia kuwa wataona athari za

mambo ya kuliwaza ya kidunia, na wasio wema watafadhilishwa zaidi wa

walio wema,na hawatokuwa na nafasi.

Kufunga njia zinazopelekea katika fitina na kujikinga nazo ni kitu kitakiwacho

kwa muisilamu ambae anataka kufanikiwa duniani na akhera, na hivyo

ndivyo Mtume (Saw) anamsifia anaechukua hadhari na kujiepusha kuzama

katika fitina kadiri ya uwezo wake.

Kutoka kwa Abi Hurayra (Mwenyezi Mungu amwie radhi) amesema:

“amesema Mtume (Saw): “ Itakujakuwa fitina kiasi ambacho fitina ya aliyekaa

ni bora kuliko fitina ya aliyesimama, na fitina ya aliyesimama ni bora kuliko ya

anaetembea, na fitina ya anaetembea ni bora kuliko fitina ya anaeieneza,

yoyote mwenye kutafuta utukufu kutokana na fitina hiyo basi ataupata, Na

mwenye kupata kimbilio basi ajilinde kwa kimbilio hilo. (Imepokewa na

Bukhari na Muslim).

Na kujikinga na fitina kutatokana na kufuata maamrisho ya Mwenyezi Mungu

na maamrisho ya Mtume wake (Saw), na kuwa pamoja na jamaa na kuwatii

viongozi kwa wema. Na kwa ajili ya masilahi ya taifa, hivyo basi, Mwenyezi

Mungu amemtahadharisha mwenye kuacha jamaa na kuzama katika fitina

duniani ya kuwa atakumbana na adhabu iliyo kali. Mwenyezi Mungu

anasema {Basi nawatahadhari wanao khalifu amri yake, usije ukawapata

msiba au ikawapata adhabu chungu} Alnuur 63.

Ni wajibu wa kila mmoja wetu kusaidiana kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu

lilobarikiwa, kujitahidi kulitukuza kwa kufaya juhudi na kuhifadhi mali zake na

kuzingatia tabia na maadili yake, kanuni na sheria zake ili tupate kujiinua kwa

kuhifadhi usalama wetu na utulivu wetu. Raia mwema ni yule mwenye

kujenga nchi yake na kuleta utulivu na kuuhifadhi na wala hawi pamoja na

watu wenye nyoyo za msilahi yao ya kibinafsi, na wenye ulinganio potofu

wenye kubomoa na ambao wanafanya kazi ya kuliharibu taifa na kueneza

fujo.

Mwenyezi Mungu anasema, {Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi

Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi

Mungu iliyo juu yenu: vile mlivyo kuwa nyinyi kwa nyinyi maadui naye

akaziunganisha nyoyo zenu; kwa neema yake mkawa ndugu. Na mlikuwa

ukingoni mwa shimo la Moto, naye akakuokoeni nalo. Namna hivi Mwenyezi

Mungu anakubainishieni Ishara zake ili mpate kuongoka.} Al imran aya ya

113.

Na miongoni mwa fitina kubwa zenye kupoteza amani na utulivu ndani ya

jamii: ni ulinganio potofu ambao unaotolewa na wenye imani dhaifu, ambao

hawana upendo na taifa lao na wenye misimamo mikali ambao kazi yao ni

kuhakikisha kuisambaratisha jamii na kuleta hali ya misukosuko ndani yake,

na kubomoa nguzo zake na kuharibu vyanzo vyake. Na pia hawatosheki na

mipango yao miovu ya kuangamiza ambayo lengo kuu ni kuliangusha taifa na

kupoteza utulivu wake.

Na hatari kubwa iliyoje ndani ya taifa ambayo hupelekea kuwepo mtafaruku

ni kule kuitumia dini vibaya, na kuzidisha yasiyokuwemo na matumizi mabaya

ya ulinganio usio na malengo au kwa hutuba za midomoni tu au kwa

majadiliano mengi yasiyo na matokeo yoyote muhimu. Na hivi karibuni sauti

nyingi potofu na zenye kuharibu zimesikika ambazo zinaita bila ya hata haya

kuharibu taifa, kumwaga damu, na kuwahofisha walio katika usalama na

kueneza machafu. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema katika kitabu chake

kitukufu {Kwa hakika wale wanao penda uenee uchafu kwa walio amini,

watapata adhabu chungu katika dunia na Akhera. Na Mwenyezi Mungu

anajua na nyinyi hamjui.} Al nuur 19.

Ulinganio huu potofu ambao wenye wana malengo ya kuiharibu jamii na

kueneza fujo na kupoteza umuhimu wa kuwepo kwa sheria ni moja wapo ya

hatari kubwa tena sana za kupoteza usalama ndani ya taifa, na ni moja wapo

wa umuhimu wa kuamsha moto za kuwepo vitndo vya kigaidi, na huifanya

jamii isifike kwa sifa zisizostahiki. Hakika ulinganio huo ambao wanaoueneza

unapelekea kuwepo fitina kubwa ambayo itayumbisha taifa na waja pia kwa

kuwepo mauaji, uharibifu, kuyumbisha hali ya usalama kati ya mtu mmoja

mmoja na kwa jamii nzima, na kuna mifano ya kuanguka na kuporomoka

mataifa mbali mbali kutokana na hali ya kukosa usalama. Dini yetu tukufu ya

kiisilamu inalingani yote yaletayo usalama na utulivu na kupinga vikali aina

zote za uadui na ugaidi.

Amana ya neno na majukumu yake

1 Rajab 1437H. sawa na Aprili 2116 A.D

Kwanza: vipengele:

1. Nafasi ya neno katika uisilamu. 2. Kuhifadhi ulimi ni katika dalili za kuwa na imani. 3. Amana ya neno na majukumu yake ni jambo la lazima kisheria na kimaadili. 4. Hatari ya neno na athari zake kwa mtu na kwa jamii.

Pili:Dalili

Ndani ya Kurani Tukufu

7. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema : { Enyi mlio amini! Mcheni

Mwenyezi Mungu na semeni maneno ya sawasawa 17. Apate

kukutengenezeeni vitendo vyenu na akusameheni madhambi yenu. Na anaye

mt'ii MwenyeziMungu na Mtume wake, bila ya shaka amefanikiwa

mafanikio makubwa.} (Al ahzab. 11-17)

1. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema : {.. na semeni na watu kwa wema, }

(Albaqara. 23)

3. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema : { Waambie waja wangu waseme

maneno mazuri, maana Shet'ani huchochea ugomvi baina yao. Hakika

Shet'an ini adui aliye dhaahiri kwa mwanaadamu } (Israa. 23)

3. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema : { Mema na maovu hayalingani. Pinga

uovu kwa liliojema zaidi. Hapo yule ambaye baina yako naye pana uadui

atakuwa kama rafiki jamaa wa kukuonea uchungu.} (Fussilat. 33)

5. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema : {Arrah'man, Mwingi wa Rehema 2. Amefundisha Qur'ani. 4. Akamfundisha kubaini. 3. Amemuumba mwanaadamu,} (Arahman.1-4)

6. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema : {Hebu hukuona vipi Mwenyezi Mungu alivyo piga mfano wa neno zuri? Ni kama mti mzuri, mizizi yake ni imara,na matawi yake yako mbinguni. 25. Hutoa matunda yake kila wakati kwa idhini ya Mola wake Mlezi. Na Mwenyezi Mungu huwapigia watu mifano ili wapate kukumbuka. 26. Na mfano wa neno ovu ni kama mti muovu, uliong'olewa juu ya ardhi. Hauna imara.} (Ibrahim.24-26)

7. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema : { Kauli njema na usamehevu ni bora kuliko sadaka inayo fuatiliwa na maudhi. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujitosha na Mpole } (Albaqara. 263)

8. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema : { Wala msiseme uwongo, kwa kuropokwa na ndimi zenu:Hichi halali, na hichi haramu - mkimzulia uwongo Mwenyezi Mungu. Hakika wanao mzulia uwongo Mwenyezi Mungu hawatafanikiwa.} (Anahl.116)

9. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema : {. Nendeni kwa Firauni. Hakika yeye amepindukia mipaka. 44. Mwambieni maneno laini, huenda akazingatia au akaogopa.} (Taha.43-44)

Dalili ndani ya hadithi

1. Kutoka kwa Abi Hurayra (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) kutoka kwa Mtume (rehma na amani zimshukie) amesema: “hakika ya mja hunena neno la kumridhisha Mwenyezi Mungu Mtukufu na akawa hajalizingatia isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu humnaynyua kupitia neno hilo daraja. Na hakika ya mja hunena neno la kumkasirisha Mwenyezi Mungu Mtukufu na akawa hajalizingatia basi huingia kupitia neno hilo katika moto wa jahannamu.” (Bukhari na Muslim).

2. kutoka kwa Abi Hurayra (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) amesema: amasema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Mtukufu (rehema na amani zimshukie) “ kila salamu ni sadaka, kila siku ichomezewayo jua akawa anafanya uadilifu kati ya watu wawili ni sadaka, na kumsaidia mtu katika kipando au kumsaidia kupandisha mzigo juu ya kipando ni sadaka. Neno zuri ni sadaka. Na hatua aipigayo kuelekea msikinitini ni sadaka. Na uchafu auondoshao njiani ni sadaka.” (Bukhari na Muslim)

3. Kutoka kwa Abi Hurayra (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) hakika ya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Mtukufu (rehema na amani zimshukie) amesema: “ dalili za mtu mnafiki ni tatu, asemapo huongopo. Akiahidi hatimizi ahadi. Na akiaminiwa hufanya khiyana.”

4. Kutoka kwa Abi Hurayra (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) amesema: amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Mtukufu (rehema na amani zimshukie ):“ anaeamini Mwenyezi Mungu Mtukufu na siku ya mwisho basi asimuudhi jirani yake. Na anaeamini Mwenyezi Mungu Mtukufu na siku ya mwisho basi amkirimu mgeni wake. anaeamini Mwenyezi Mungu Mtukufu na siku ya mwisho basi aseme neno zuri au anyamaze.” (Bukhari na Muslim)

5. Kutoka kwa Ibn Abass ((radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao) kuna mtu nguo (shuka) yake ilipeperushwa kwa upepo katika zama za Mtume (rehema na amani zimshukie ) akaulaani upepo. Mtume (rehema na amani zimshukie ) akamwambia: “ usiulaani kwani umetumwa, kwani yeyote mwenye kukilaani kitu pasi na haki basi laana ile humrudia mwenyewe.” (Abu Daudi)

6. Kutoka kwa Muadh bin Jabal (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) amesema: nilikuwa safarini na Mtume (rehema na amani zimshukie )nikawa karibu naye … kasha akasema: “je, nikueleze juu ya umiliki wa hayo yote? Akasema: “ nikasema: “ndio ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Mtukufu: akaashiria katika ulimi wake na kusema: “jizuie na huu”. Nikasema: “ kwani sisi tunahesabiwa kwa tukisemacho? Akasema: “ ewe Muadhi,mama yako akupotea hivyo unadhani watu wataingia motoni kwa sababu ya nyuso zao –au amesema- kwa pua zao – huoni kuwa wataingia motoni kwa sababu ya ndimi zao..” (Tirmidhiy)

Tatu: Maudhui

Mwenyezi Mungu Mtukufu amemneemesha mwanadamu kwa neema nyingi

zisizohesabika akasema: { Na mkizihisabu neema za Mwenyezi Mungu,

hamwezi kuzidhibiti. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghfira,Mwenye

kurehemu.} (Anahl.18) Na miongoni mwa neema kubwa sana ni ulimi akasema

{Kwani hatukumpa macho mawili? 9. Na ulimi, na midomo miwili?} (albalad.8-

9) na kasha akaupa ulimi neema nyengine nayo ni kuweza kutamka ambayo

humtenganisha mwanadamu na viumbe wengine, akasema Mwenyezi Mungu

Mtukufu anasema : {Arrah'man, Mwingi wa Rehema 2. Amefundisha Qur'ani.

4. Akamfundisha kubaini. 3. Amemuumba mwanaadamu,} (Arahman.1-4).

Neno ni anuani ya ulimi na ni njia ya kuwasiliana na mwengine na kupitia

maneno maisha huendelea, na hakuna sheria yoyote iliyojali neno kama sheria

ya kiisilamu, imejali kwa hali zote sawa iwe kweli au matani. Kuna maneno

hufutahisha watu na mengine hukasirisha, na kwa neno heshima na umwagaji

wa damu huhifadhika.

Na kutokana na hatari ya neno Mwenyezi Mungu Mtukufu ameleta amri ya

kutaka ulimi uhifadhiwe, na kuacha kutamka lenye kuondoa heshima za watu,

na kuzungumzia yasiyohusu wala yasiyo na faida, akasema { Hatamki neno ila

karibu yake yupo mwangalizi tayari } (Qaf.18). viungo vyote vya mwanadamu

vimeshikamana na ulimi, ulimi ukiwa mwema navyo huwa vilevile na ukiwa

mbaya navyo huwa vibaya. Kutoka kwa Abi Said Alkhudriy (radhi za Mwenyezi

Mungu ziwe juu yake) amesema: mwanadamu afikapo asubuhi viungo vyote

husemeza ulimi na kuuambia: muogope Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa ajili

yetu kwani ukiwa sawa nasi tutakuwa sawa na kama utapinda nasi tutapinda.”

(Tirmidhi).

Na Mtume (rehema na amani zimshukie ) ameweka wazi kwa kumwambia

Muadh kuwa ulimi ni sababu ya kumfanya mtu aingie peponi au motoni.

Akasema : nilikuwa safarini na Mtume (rehema na amani zimshukie )nikawa

karibu naye … kasha akasema: “je, nikueleze juu ya umiliki wa hayo yote?

Akasema: “ nikasema: “Ndio ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Mtukufu:

akaashiria katika ulimi wake na kusema: “jizuie na huu”. Nikasema: “ kwani sisi

tunahesabiwa kwa tukisemacho? Akasema: “ Mama yako akupotea ewe

Muadhi, hivyo unadhani watu wataingia motoni kwa sababu ya nyuso zao –au

amesema- kwa pua zao – huoni kuwa wataingia motoni kwa sababu ya ndimi

zao..” (Tirmidhiy)

Neno ni amana na inabidi kwa atamkaye amuogope Mwenyezi Mungu

Mtukufu kwalo, kwani lina madhara na hatari kubwa pia lina faida na

mafanikio mengi. Imepokewa kutoka kwa Abi Hurayra (radhi za Mwenyezi

Mungu ziwe juu yake) kutoka kwa Mtume (rehma na amani zimshukie)

amesema: “ hakika ya mja hunena neno la kumridhisha Mwenyezi Mungu

Mtukufu na akawa hajalizingatia isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu

humnaynyua kupitia neno hilo daraja. Na hakika ya mja hunena neno la

kumkasirisha Mwenyezi Mungu Mtukufu na akawa hajalizingatia basi huingia

kupitia neno hilo katika moto wa jahannamu.” (Bukhari na Muslim).

Na ilivyokuwa neno zuri ni dalili ya imani ya mtamkaji kama alivyotueleza

Mtume (rehema na amani zimshukie) pale aliposema: “anaeamini Mwenyezi

Mungu Mtukufu na siku ya mwisho basi aseme neno zuri au anyamaze.” Na

Mwenyezi Mungu Mtukufu ametuamrisha kusema neno la kweli kwa yeyote

bila ya kutafautisha na wala tusitamke isipokuwa tamshi jema ambalo hujenga

na wala halibomoi, huimarisha na si kuporomosha, akasema (na semeni na

watu kwa wema, } (Albaqara. 83). Pia akasema {Waambie waja wangu waseme

maneno mazuri, maana Shet'ani huchochea ugomvi baina yao. Hakika Shet'ani

ni adui aliye dhaahiri kwa mwanaadamu } (Israa. 53)na akasema pia {Enyi mlio

amini! Mcheni Mwenyezi Mungu na semeni maneno ya sawasawa 71. Apate

kukutengenezeeni vitendo vyenu na akusameheni madhambi yenu. Na anaye

mt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, bila ya shaka amefanikiwa mafanikio

makubwa.} (Al ahzab. 71-71). Kutengemea kwa matendo na kupata msamaha

wa madhambi upo kupitia matamshi mema na kwa maneno mazuri. Kwa ajili

hiyo maelekezo ya uisilamu ni kuchunguza na kuwa na uhakika wa

ukisemacho, Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema {. Enyi mlio amini! Akikujieni

mpotovu na khabari yoyote, ichunguzeni, msije mkawasibu watu kwa kutojua,

na mkawa tena wenye kujuta kwa mliyo yatenda.}(Alhujuraat.6).

Kwa ajili hiyo itafahamika kuwa kuhifadhi ilimi ni dalili ya imani, na ni katika

uisilamu mzuri na ni njia ya kufikia pepo ya Firdausi ya juu, Mwenyezi Mungu

Mtukufu anasmea { Na ambao hujiepusha na mambo ya upuuzi,}

Almuuminuun.3) mpaka aliposema {Hao ndio warithi,11. Ambao watairithi Pepo

ya Firdausi, wadumu humo.} (Almuuminuun11.11). na kutoka kwa Saad bin

Muadh (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) kutoka kwa Mtume (rehema na

amani zimshukie) amesema: “yeyote atakayenipa dhamana ya kuhifadhi kilichopo

kati ya ulimi wake na kilichopo kati ya miguu yake miwili basi nami ninampa

dhamana ya kuingia peponi.” (Bukhari).

Na amana ya neno na majukumu yake ni jambo la lazima kwa upande wa sheria

na kimaadili, kwani huufanya umma uwe pamoja na kuwa na nguvu na kuweza

kumbadilisha adui kuwa rafiki na chuki kuifanya kuwa ni upendo na kuondoa

matendo na vitimbi vya shetani, Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema {34 Mema

na maovu hayalingani. Pinga uovu kwa liliojema zaidi. Hapo yule ambaye baina

yako naye pana uadui atakuwa kama rafiki jamaa wa kukuonea uchungu.}

(fussilat.34). na kama ilivyokuwa neno zuri hukutanisha nyoyo na kurekebisha

nafsi na kuondosha huzuni na hasira na kufanya kuhisi kuridhia na furaha hasa

hasa linapoambatanishwa na tabasamu. Imepokewa kutoka kwa Abi Dhari (radhi

za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake)amesema: amesema Mjumbe wa Mwenyezi

Mungu Mtukufu (rehma na amani zimshukie) “kutabasamu katika uso wa ndugu

yako ni sadaka.” (Bukhari).

Na kama ilivyokuwa amana ya neno linahitaji kwa msemaji kuwa asiseme

isipokuwa kwa kheri na ukweli, asiseme uongo wala kwa hadaa au kwa kutoa

ushahidi wa uongo na kugeuza ukweli na wala asizungumze bila ya kujua.

Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema Wala msiseme uwongo, kwa kuropokwa na

ndimi zenu: Hichi halali, na hichi haramu - mkimzulia uwongo Mwenyezi Mungu.

Hakika wanao mzulia uwongo Mwenyezi Mungu hawatafanikiwa.} (Anahl.116).

Pia katika amana za neno ni kutoa nasaha na ushauri mwema, kwani dini ni

kushauriana kama alivyotueleza Mkweli Muaminifu (rehema na amani zimshukie)

kutoka kwa Tamim Aldaramiy (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) kuwa

Mutume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu (rehema na amani zimshukie ) amesema:

“ dini ni nasaha”. Tukasema: “ ni kwa nani.? Akasema: “ ni kwa (ajili) ya Mwenyezi

Mungu Mtukufu na Mtume wake na kwa viongozi wa waumini na wengineo.”

(Muslim). Na kutoka kwa Abi hurayra (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake)

amesema: amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Mtukufu (rehema na amani

zimshukie ) “mweney kutaka ushauri basi amesalimika.” (Daudi). Hivyo basi,

nasaha na ushauri wa ukweli mambo mengi hutengemea ikiwemo amani na ,

upendo katika taifa.

Neno ni silaha ya hatari sana yenye pande mbili, linaweza kuwa ni sababu ya

kuimarika kwa taifa pindi ni zuri na la ukweli na linaweza pia kuwa ni sababu ya

kuporomoka, ufisadi na uharibifu pindi liwapo si la ukweli. neno si kitu kidogo lina

umuhimu mkubwa sana katika maisha ya watu, na kwa yale wafanyiayo mfano wa

kuuziana, ahadi na makubaliano na mifano mwngine yenye kuhitaji ukweli katika

mazungumzo.

Haifichikani kuwa neno zuri lina athari nzuri kati ya watu, wema kwa jirani kupitia

neno zuri huenda ikawa ndio sababu ya kuingia peponi, na ubaya wake kwao

ikawa ndio sababu ya kuingia motoni. Imepokewa kutoka kwa Abi Hurayra

amesema: Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Mtukufu (rehema na amani zimshukie )

aliambiwa: “ ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Mtukufu kuna mwanamke Fulani

anasali usiku na kufunga mchana, na hufanya (mema) na hutoa sadaka na

huwakera majirani zake kwa ulimi. Mtume (rehema na amani zimshukie )

akasema: hana jema huyo yeye ni katika watu wa motoni.” Akaambiwa:“na kuna

mwanamke fulani husali sala za lazima tu na hutoa sadak ، lakini hamkeri mtu.

Mtume (rehema na amani zimshukie ) akasema yeye nikatika watu wa peponi.”

(Bukhari).

Vilevile neno lina athari kubwa katika mahusiano kati ya muisilamu na asiyekuwa

muisilamu, hata pamoja na maadui zetu Mwenyezi Mungu Mtukufu

ametuamrisha tuseme nao kwa maneno mazuri, Mwenyezi Mungu Mtukufu

anasema { Nendeni kwa Firauni. Hakika yeye amepindukia mipaka. 44.

Mwambieni maneno laini, huenda akazingatia au akaogopa.} (Taha. 43-44)

Na katika jambo la msingi kulitaja hapa ni kuwa neno lililoandikwa linaweza kuwa

na maafa na madhara makubwa ya kuangamiza taifa na halina tafauti na neno

litamkwalo, aina zote hizi ni amana, na ni wajibu wa kila ashikae kalamu aipe haki

yake kama itakiwavyo na awe na pupa na kujiepusha na makosa kwani ni kalamu

ndio itakayomuweka wazi juu ya misimamo yake na inahitajika aitumie kwa

kunusuri haki na kuilingania pia. Imam Jahidh anasema “kalamu ni ndimi mbili

nayo ni yenye kubakisha athari.” Si hivyo tu bali ni upanga mkali sana na weney

nguvu na unafika mbali kuliko hata upanga wenyewe.

Kwa ajili hiyo kila mwandishi amuogope Mwenyezi Mungu Mtukufu aache

kueneza habari za uongo na kuupotosha ukweli pia kuzungumzia heshima za watu

na kuacha kabisa kila lenye kuleta madhara kwa jamii kwani jambo hili huwa ni

khiyana ya neno.

Mshairi anasema:

Mwandishi yeyote atatoweka * na alichokiabdika kitabakia

Basi mkono wako usiandike kitu isipokuwa * siku ya kiama ukikiona utafurahi

Kila mtu aelewe jukumu la neno na kuwa atasimamishwa mbele ya Mwenyezi

Mungu Mtukufu na mbele ya dhamira yake kwa kila alichokizungumza, ili isije

ikawa ndio sababu ya kutengana na kukimbiana kati ya wanajamii na mtu na

mwengine na kutengana kati ya mwanfamilia na kuharibu mahusiano kati ya

watu.

Tunahitajia sana maneno mazuri ya kweli kati ya watu na jamii ili kueneza

mapenzi na ukaribu na kuondosha mtengamano na mfarakano. Neno zuri lina

athari nzuri na yenye kuleta masilahi mazuri na pia huleta msamaha wa makosa.

Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu

na semeni maneno ya sawa sawa 71. Apate kukutengenezeeni vitendo vyenu na

akusameheni madhambi yenu. Na anaye mt'ii MwenyeziMungu na Mtume wake,

bila ya shaka amefanikiwa mafanikio makubwa.} (Al ahzab. 71-71).

Index

2 Utangulizi 3

3 Uisilamu ni dini ya ujenzi na ya uimarishaji 5

4 Ubora wa maadili katika ujumbe wa Muhammad 29

5 Miongoni mwa aliyokirimiwa Mtume Muhammad (Saw) 42

6 Wajibu wetu kwa upande wa Kurani tukufu 57

7 Wito wa Manabii na Mitume katika urekebishaji kwa mtazamo

wa kurani tukufu 72

8 Sifa za waumini ndani ya kurani 83

9 Uhusiano wa kifamilia ulio bora 95

: Fadhila za masahaba (radhi za Mwenyezi Mungu

ziwashukie)

:8

21 Haki ya mtoto katika ukuaji mzuri na maisha bora na maandalizi mazuri kwa ajili ya mustakbali

219

22 Hatari za ulinganio potofu na umuhimu wa kuuzuia kwa ajili ya upatikanaji wa amani na utulivu

234

23 Amana ya neno na majukumu yake

248