hubiri-roho chafu

22
SOMO ROHO CHAFU NA MWISHO WA DUNIA. Fungu Kuu: 1 Yohana 4:1 “Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho,

Upload: injili-leo

Post on 04-Jan-2016

616 views

Category:

Documents


7 download

DESCRIPTION

Pata kufatilia fundisho la unabii unaotufundisha juu ya kutambua roho chafu,je ni zipi hizo na zinafanyaje kazi?

TRANSCRIPT

Page 1: Hubiri-Roho Chafu

SOMOROHO CHAFU NA

MWISHO WA DUNIA.

Fungu Kuu: 1 Yohana 4:1“Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo

roho, kwamba zimetokana na Mungu;

kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea

duniani.”

Page 2: Hubiri-Roho Chafu

ufunuo 16:12-15 12 Na huyo wa sita akakimimina kitasa chake juu ya mto ule mkubwa Frati; maji yake yakakauka, ili njia itengenezwe kwa wafalme watokao katika maawio ya jua. 13 Nikaona roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura, zikitoka katika kinywa cha yule joka, na katika kinywa cha yule mnyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uongo.

Page 3: Hubiri-Roho Chafu

14 Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi. 15 (Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake..

Page 4: Hubiri-Roho Chafu

ROHO TATU ZA UCHAFU. Joka,

Mnyama Na

Nabii Wa Uongo.

Page 5: Hubiri-Roho Chafu

JOKA (SHETANI)Alama ya upagani wa kirumi, umizimu. Roho hii inahamasisha mfumo wa maisha ulioundwa kwa technolojia, maisha yaliyojaa misisimuko na kuondoa uhalisia wa maisha.Roho hii inahamasisha miujiza, ishara, uponyaji na ibada za bandia ndani na nje ya kanisa, inahamasisha utajiri wa bure na haraka kimiujiza na vijana wengi waliomaliza masomo yao hutamani utajiri wa haraka kwa njia zinazogharimu ukristo wao. Utajiri si dhambi ila unaupataje na unautumiaje?

Page 6: Hubiri-Roho Chafu

Roho hii inahamasisha furaha, burudani na michezo inayovunja dhamira ya kuogopa dhambi. Mfano pornography, magazeti na majarida yenye hadithi chafu za ngono zinazochafua fikra, michezo ya maigizo inayochochea mihemuko ya kimapenzi i.e big brother, miss kisuraRoho hii inahamasisha muziki mbaya na maburudisho yenye mivuto mibaya, mapambo na vitu vinavyodhuru afya.

Page 7: Hubiri-Roho Chafu

E.G White GC 588 Umizimu unapouiga kwa karibu sana Ukristo wa jina tu wa siku hizi, unakuwa na nguvu kubwa sana ya kuwadanganya na kuwanasa watu mtegoni. Shetani mwenyewe ameongoka, anafuata utaratibu wa mambo ya kisasa. Atajitokeza katika tabia ya malaika wa nuru. Kwa njia ya imani hiyo ya mizimu, miujiza itatendeka, wagonjwa wataponywa, na maajabu mengi yasiyokanushika yatafanyika

Page 8: Hubiri-Roho Chafu

Mathayo 24:24-2824. Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu, wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule. 25. Tazama nimekwisha kuwaonya mbele.

Page 9: Hubiri-Roho Chafu

Na kwa vile yale mapepo yatakiri kwamba yana imani katika Biblia, na kuonyesha heshima yao kwa taasisi za kanisa, kazi yao itakubalika kama ni ishara [miujiza] ya uweza wake Mungu. Mstari unaowatofautisha wale wanaojiita Wakristo na wale wasiomcha Mungu kwa sasa ni shida sana kuonekana. Washiriki wa kanisa wanayapenda mambo yale yale wanayoyapenda walimwengu, tena wako tayari kujiunga nao, na Shetani amedhamiria kuwaunganisha katika shirika moja na kwa njia hiyo kuiimarisha kazi yake kwa kuwafagilia wote katika safu za jeshi la mizimu.

Page 10: Hubiri-Roho Chafu

E G White GC 557Wanakanusha kwamba Biblia haikutoka kwa Mungu, na kwa kufanya hivyo wanaubomoa msingi wa tumaini la Mkristo na kuizima nuru ile inayoonyesha njia ya kwenda mbinguni. Shetani anaifanya dunia hii isadiki kwamba Biblia ilikuwa ni hadithi za uongo tu, au kitabu kilichofaa kwa kizazi kile kichanga cha wanadamu [wale wa mwanzo], lakini kwa sasa kinafaa kuangaliwa kwa juu juu tu, au kutupiliwa mbali kama kitu kilichopitwa na wakati.

Page 11: Hubiri-Roho Chafu

MNYAMA (UPAPA) Hii ni roho inayopingana na kweli ya Mungu na za Biblia. Daniel 7:25, Yohana 8:32, Yohana 17:3 Roho hii inapingana na uhuru wa dini Roho hii inapingana na sabato na amri za Mungu ambazo ni tabia ya Mungu na kuwafanaya watu wa Mungu waikanyage sabato. Mfano watu wengi kutegeshewa mitihani siku ya sabato na kufanya kazi siku ya sabato.

Page 12: Hubiri-Roho Chafu

E.G White GC 584Po pote pale zinapokataliwa amri [kumi] za Mungu, dhambi inakoma kuonekana kwao kama ni dhambi, au haki kuweza kutamaniwa nao. Wale wanaokataa katakata kuitii serikali ya Mungu hawafai kabisa kujitawala wenyewe. Kwa njia ya mafundisho yao yenye madhara, roho ya kutotii inapandikizwa ndani ya mioyo ya watoto na vijana, ambao kwa kawaida hukosasubira wanapodhibitiwa; ndipo inatokea jamii iliyojaa uhalifu na uasherati.

Page 13: Hubiri-Roho Chafu

Roho hii inapingana na mpango wa Mungu wa ndoa. Waebrania 13:4 mfano katika jamii nyingi pamehalalishwa ndoa za mkataba, ndoa za jinsia moja na baya zaidi vijana wengi hawataki kuoa au kuolewa bali wanasema wanataka mtoto tu.Roho hii pia kwa siri inahamasisha watoto wa mipira (tube babies)Roho hii ndiyo inayohamasisha biashara ya ukahaba kwa njia ya mtandao na mandangulo ya kimataifa.

Page 14: Hubiri-Roho Chafu

E.G White 5T 450Wote wanaomcha Mungu hawawezi kuikubali taasisi inayovunja maagizo ya Amri kumi. Katika uwanja huu wa vita unatokea mgongano mkuu wa pambano la mwisho kati ya wema na uovu. Na hatujaachwa katika mashaka juu ya swala hili kama ilivyokuwa nyakati za Modekai Bwana atadhihirisha ukweli wake na watu wake.

Page 15: Hubiri-Roho Chafu

NABII WA UONGO (UPROTESTANT)Hii ni roho ya uasi wa kiprotestanti, iliyokinyume na uhuru wa haki ya dhamira. Ndani yake kumejaa dhana hatari iitwayo Rationalism. Warumi 1:32Roho hii inahamasisha dhana hatari kwa jamii husani vijana kuona dhambi kama kitu cha kawaida. (wanasema dhambi ni mtu mwenyewe anavyojisikia)Roho hii pia inadai tafsri ya dhambi inajengwa na sababu ya dhambi.

Page 16: Hubiri-Roho Chafu

Mf kama Mungu aliibariki sabato anaweza pia kubariki jumapili na watu wakasali (rationalize)Dhana hii imeingiza dini mpya ya kizazi cha karne ya 21 inayohusika na maisha ya kisasa.

Page 17: Hubiri-Roho Chafu

White GC Pg 592Makanisa ya Kiprotestanti yanapozikataa hoja hizo za Maandiko zinazoeleweka wazi ambazo zinaitetea Sheria ya Mungu [Amri Kumi], watatamani sana kuwanyamazisha wale ambao hawawezi kuipindua imani yao kwa kutumia Biblia.

Page 18: Hubiri-Roho Chafu

Ingawa wao wanajifanya wenyewe kuwa vipofu ili wasiweze kuuona ukweli huo [Eze. 22:26-29], hivi sasa wanaichagua njia ile itakayowafikisha katika kuwatesa wale ambao, kutokana na vile dhamiri zao zinavyowakataza, wanakataa kufanya kile ambacho Ulimwengu uliobaki wa Kikristo unafanya, na kukataa kuyakubali yale madai ya sabato ya papa [Jumapili].

Page 19: Hubiri-Roho Chafu

White GC Pg 588Waprotestanti wa nchi ya Marekani watakuwa mstari wa mbele kabisa katika kuinyosha mikono yao kupitia katika ghuba na kuushika mkono wa imani ya mizimu [kutoka India na mashariki ya mbali]; watanyosha mikono yao juu ya kilindi [cha bahari] ili kushikana mikono na mamlaka ile ya Roma; na chini ya utawala wa muungano huo wa utatu [Mizimu, Uroma, Uprotestanti Asi Ufu. 16:13,14], nchi hii itafuata katika nyayo za Roma kwa kuzikanyaga chini ya miguu yake haki za dhamiri za watu [kuzuia watu wasimwabudu Mungu kama mioyo yao inavyotaka].

Page 20: Hubiri-Roho Chafu

Sikia YESU anachosemaUfunuo 3:20-2220 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami. 21 Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi. 22 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.

Page 21: Hubiri-Roho Chafu

1 YOHANA 2:15-17Msiipende Dunia, Wala Mambo Yaliyomo Katika Dunia. Mtu Akiipenda Dunia, Kumpenda Baba Hakumo Ndani Yake. 16. Maana Kila Kilichomo Duniani, Yaani Tamaa Ya Mwili, Na Tamaa Ya Macho, Na Kiburi Cha Uzima, Havitokani Na Baba, Bali Vyatokana Na Dunia 17. Na Dunia Inapita, Pamoja Na Tamaa Zake, Bali Yeye Afanyaye Mapenzi Ya Mungu Adumu Hata Milele

Page 22: Hubiri-Roho Chafu

UPENDO WA

MUNGU

UKUFUNIKE