imaan newspaper issue 1

Download Imaan Newspaper issue 1

Post on 12-Feb-2018

1.599 views

Category:

Documents

2 download

Embed Size (px)

TRANSCRIPT

 • 7/23/2019 Imaan Newspaper issue 1

  1/19

  SSN 01 - 00005618 BEI: SH800/- KSH80/- USH1,200/- JUMATATU, APRIL 13, 2015 www.islamicftz.o

  huwatoawatugizani

  Hemed bin Jumaa:alinufaisha wengi kwa

  elimu yake - Uk 5

  Waislamu wadai usawa sera mpya ya elimu

  Tumeahidi, tumetimiza

  ni shahidi

  Kauli ya Mwenyekiti TIF Uk. 2

  ALLAHHead office, Lumumba StreetOpp: Viwanja vya Mnazi Mm oja, P. O Box 779 Dar es Salaam,

  Tanzania, Tell: 255 22 2182482/ 255 222184419Fax: 255 22 2181424, E-mail: info@Binslum.com

 • 7/23/2019 Imaan Newspaper issue 1

  2/19

  www.islamicftz.o

  24 Jumada Thani 1436, JUMATATUAprili 13 , 20

  2

  Shukrani zote anastahiki

  Allah Subhaanahuu waTaala na rehma na amaniziwe juu ya mjumbe wake

  Muhammad na maswahaba wakena wale wote wenye kufuata uon-

  gofu alokuja nao hadi siku ya mal-ipo. Ndugu msomaji, leo ni sikunyingine muhimu sana kwetu

  kama Waislam, Watanzania natasnia ya habari kwa ujumla kamailivyo muhimu kwa taasisi yetu yaThe Islamic Foundation (TIF).

  Hii ni kutokana na ujio wagazeti hili Imaan ambalo unaliso-ma hivi sasa. Hakuna asiyeelewaumuhimu wa vyombo vya habarikatika ulimwengu tunaoishi. Watu

  wasio na vyombo vya habari nisawa na mabubu kwa sababu ni

  vig umu wengi ne kuju a bubuanafikiria nini.

  Taasisi ya The Islamic Founda-tion, pamoja na huduma nyingineza kielimu, kiimani, kiafya na ki-

  jamii, il iahidi kuuhudumia um-mah katika nyanja ya habari, na

  tukaanza na redio mwaka 2003 namwaka 2013 kwa michango yenu

  ya hali na mali tukaanzisha tele-visheni Imaan.

  Gazeti Imaan ni mwendelezowa hatua ambazo The Islam icFoundation imezichukua katikahali ngumu ili kutimiza azma yetu

  ya kuanzisha na kuendesha vyo-mbo vya habari ambavyo, kwa uw-ezo wa Allah, tunataraji vitakidhi

  kiasi fulani mahitaji ya ummah ki-habari kwa kutoa habari za kwelina kwa uadilifu kwa kuzingatia

  imani sheria za nchi yetu na misin-gi ya Uislam.

  Tunawaomba kama tulivyow-aomba wakati wa kuzindua tele-

  visheni Imaan na kama tunavyow-aomba kila siku kuzidi kuliwezeshagazeti Imaan kwa kulinunua, kuli-soma na kuwezesha wengine wali-pate ili sote kwa pamoja tuwezekufikia malengo ya kuanzishwakwake ambayo ni kuwatoa watukatika giza na kuwapeleka katikanuru kwa uwezo wa Allah.

  Tunafahamu kuwa katikautekelezaji wa azma hii, kiubinad-amu upungufu na kasoro mbalimbali bila shaka zitakuwepo, lakini

  tutafanya kila tuwezalo kufikiamategemeo yetu.

  Nasaha zetu kwenu wasomajiwetu ni kuwaomba myatazamemazuri tutakayoyafanya kwa uwe-zo wa Allah na mzidi kutuombeadua na kutupa udhuru katika up-ungufu na kasoro mtakazozionahapa na pale, kwani hakika mka-milifu ni Allah subhaanahuu wa

  taala peke yake.Gazeti Imaan toleo la kwanza

  alhamdulilaa hilo hapo mikononimwenu hivi sasa. Tuliahidi, Tu-metimiza na Allah ni Shahidi.

  Shukran,Aref Nahd - MwenyekitiThe Islamic Foundation

  Kauli ya Mwenyekiti TIF

  NA YUSUFU AHMADI, DAR ES

  SALAAM

  Waislam nchini Tanzania wamesemamambo pekee yatakayositisha harakati zaoza kudai mahakama ya kadhi ni kupatikanakwa mahakama hiyo au kukoma kwa uhai

  wao na vizazi vyao.Aidha, Waislam wameukataa mpango

  wa Serikali wa kurasmisha na kuipa uhala-lali mahakama feki ya BAKWATA ambayowatendaji wanateuliwa na Mufti wa taasisihiyo.

  Katika tamko la taasisi za kitaifa 11 za Ki-islam lililosomwa na Sheikh Muhammad

  Issa, Waislam wamesema wamechoshwana hadaa za Serikali ambayo imekuwa iki-

  wapiga danadana tangu mwaka 2005 ili-poahidi kupitia ilani ya uchaguzi ya CCMkushughulikia suala hilo.

  Serikali iliendelea na hadaa zake katikaBunge Maalum la Katiba baada ya WaziriMkuu, Mizengo Pinda, kuahidi kuwa Seri-kali ingewasilisha suala la Mahakama yaKadhi kwenye kikao cha Bunge la Jamhuri

  ya Muungano cha Januari 2015 ili chombohicho kitambuliwe kisheria.

  Serikali ilifanya hivi ili kupoza wajumbe

  kutokana na baadhi yao kuhamasishanakuipigia kura ya kukataa Rasimu ya Katiba

  iwapo mahakama ya kadhi isingeingizwa.Pinda aliahidi kufanyia marekebisho

  Sheria ya Mahakimu, sura ya 11 na Sheria yaKiislam sura ya 375 ili kutambua Mahaka-ma ya kadhi kwa lengo la kuhakikisha umo-

  ja na mshikamano vinadumu kwa Watan-zania.

  Serikali ilishindwa kutekeleza ahadiyake Januari. Imeshindwa kutekeleza tenakatika kikao cha Machi mwaka huu.

  Tamko la Waislam limeelezea kusikit-ishwa kwao na udhaifu wa Serikali ili-

  yoonyesha kuwa haiwezi kufanya jambo

  mpaka kanisa litoe maelekezo, na kanisalikipinga, serikali nayo itapinga.

  Sehemu ya tamko hilo inasema: Wlam hatukubali kabisa mwenendo huu

  matamko ya maaskofu yenye kuingmambo ya Waislam kuachwa uendelee.Iwapo Serikali itakaa kimya na kur

  misha mwenendo huu wa kupokea makezo kutoka kwa maaskofu na kuyafankazi utapelekea makundi haya mawili kuna uhasama na hatimaye kuvunjika kamani iliyopo.

  Mwenyekiti wa Jumuiya na TaasisKiislam nchini, Sheikh Musa Kundeamesema kila unapojadiliwa muswadaKadhi, maaskofu hualikwa na kuulizwkwamba maaskofu huwa wa kwanza kataa, na hapo Serikali hupata uchoch

  wa kupita.Kundecha alisema:Serikali ha

  dhamira ya kweli ya jambo hili na inahaWaislam. Lakini pia inataka kuwavunatika katiba na uchaguzi, alisema She

  Kundecha.Sheikh Kundecha na wasomi weng

  wa Kiislam wanaowakilisha taasisi hizwameyaita madai ya maaskofu kuwa mhakama ya kadhi inakiuka katiba ya mw1977 kuwa yanatokana na husda na haymsingi wowote.

  Aidha, Waislam wamehoji kuwa, kamahakama ya kadhi inakiuka katiba knini Waislam walipopendekeza iwekndani ya katiba inayopendekezwaisikiuke katiba, maaskofu bado walipin

  Waislam wamesema mahakama ya kahaiwadhuru Wakristo na ndio maana hnchi za kisekula za Kenya na Uganda wazo.

  Hata hivyo, katika harakati za kumahakama ya kadhi, Waislam wameta

  baisha kuwa hawataikubali mahakam

  kadhi feki ya BAKWATA na kuitaka Skali irejeshe mchakati wa mazungumz

  Waislam kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu haka iwezekanavyo.

  Waislam wamesema si sahihi kwa Skali kuwalazimisha Waislam wote wchini ya BAKWATA ambayo ni moja tu

  ya taasisi nyingi za Waislam Tanzania. Tko la Waislam limetaja uamuzi huo wa Skali kuwa unaenda kinyume na KatIbara ya 19 (1) ya katiba ya Tanzania.

  Kifungu hicho cha Katiba kinaseKila mtu anastahili kuwa na uhuru wa m

  wazo, imani na uchaguzi katika mambdini, pamoja na uhuru wa mtu kubadildini au imani yake.

  Akijibu madai ya kuwa Waislam meikataa mahakama ya kadhi, Mwenye

  wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam nch

  Sheikh Kundecha alisema hakuna madhebu, hususan wahabi au ansari

  Mahakama ya Kadhi:Waislam wachoshwa na hadaa za Serikali

  Sheikh AliBaswaleh akitoanasaha zakekatika Kongamanoa jumuiya nataasisi za kiislam

  kuhusumahakama yakadhi na katibanayopendekezwaililiofanyika hivikaribuni katikamsikiti waKichanganiMagomeni jijiniDaresalaam. (PICHANA SELEMANI MAGALI)

  U

  HABARI

 • 7/23/2019 Imaan Newspaper issue 1

  3/19

  www.islamicftz.org

  24 Jumada Thani 1436, JUMATATUAprili 13 , 2015

  Waislamu wadai usawa sera mpya ya elimu

  NA WAANDISHI WETU

  Taasisi mbalimbali za kiislamzimeitaka serikali kutendahaki kwa kutumia vigezosawa katika usajili na ukagu-

  zi wa shule za Serikali na zile zisizo zakiserikali.

  Aidha, taasis i za kii slam piazimepinga Shirikisho la Wamiliki naMameneja wa Shule na Vyuo visivyovya serikali Tanzania (TAMONGSCO)kuitaja BAKWATA kuwa mwakilishiwa shule zinazomilikiwa na taasisi zakiislam katika uandaaji wa mchakatowa muswada wa elimu wa mwaka2015.

  Waislam walitoa kauli hizo katikakikao kilichowakutanisha wawakilishiwa shule zote zisizo za kiserikali nawakuu wa wizara kujadili sera mpya yaelimu 2014 na muswada wa sheria yaelimu 2015.

  Mkutano huo wa wadau ulihud-huriwa na Katibu Mkuu wa Wizara yaElimu na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Si-funi Mchome, Kamishna wa elimuProf. Eustella P.Bhalalusesa na maafisawengine waandamizi wa wizara hiyo

  wanaoshughulikia sera na sheria.Akiongea katika mkutano huo,

  Sheikh Muhammad Issa, aliyewakili-

  sha Baraza la Taasisi za Answar Sun-nah Tanzania (BASUTA) alisema,Serikali imekuwa ikizingatia kwa uka-milifu vigezo vyote kabla haijasajilishule zisizo za kiserikali lakini ime-kuwa ikilegeza vigezo kwa shule zaserikali. Sheikh Muhammad ametoamfano wa shule za kata ambazo ny-ingine zimesajiliwa bila kutimizamasharti ya vigezo vilivyowekwa.

  Kwa mujibu wa muswada huo waelimu kifungu cha 72 (1) kinacho-husika na usajili wa shule za msingi nasekondari, baadhi ya vigezo vinavyoz-ingatiwa ni pamoja na idadi ya kutosha

  ya walimu wenye sifa, vifaa vya ku-fundishia na kujifunzia, majengo ya

  kutosheleza idadi, jinsia na umri, maz-ingira na miundo mbinu minginemuhimu.

  Hali hii inafanya uwekezaji katikakuanzisha shule zisizo za kiserikalikuhitaji fedha nyingi, na hivyo kupele-kea kiwango cha juu cha ada kitaka-chofidia gharama za uwekezaji. Maranyingi kiwango hicho ni kikubwa kwamzazi, Sheikh Muhammad alisema.

  Sheikh Muhammad alisema ki-wango cha juu cha ada katika shule zi-sizo za serikali kimesababishamrundikano mkubwa wa wanafunzikatika shule za umma wakati mashule

  yasiyo ya serikali yana upungufumkubwa wa wanafunzi.

  Sheikh Muhammad alisema halihiyo pia inajitokeza katika ukaguzi washule ambapo Serikali mara nyingi in-

  achukua hatua haraka za kuadhibushule zisizo za kiserikali zisipokidhi vi-

  wango hata kwa kiasi kidogo, wakati ni

  nadra kwa Serikali kuadhibu shulezake ambazo nazo nyingi hazitimizi vi-wango. Kuhusiana na pendekezo laTAMONGSCO kwa Wizara ya Elimu

  linaloitaja BAKWATA kuwa ni mse-maji au mwakilishi wa shule za kiislam,Sheikh Muhammad amesema Bak-

  wata imesajiliwa chini ya RITA kamaambavyo taasisi