imaan newspaper issue 10

Download Imaan Newspaper issue 10

Post on 06-Jan-2016

2.114 views

Category:

Documents

10 download

Embed Size (px)

DESCRIPTION

Imaan Newspaper issue 10

TRANSCRIPT

 • ISSN 5618 - N0. 010 BEI: Sh800/- KSh80/- USh1,200/- 25 ShaaBaN 1436, IJUMaa, JUNI 12 - 18, 2015 www.islamicftz.org

  huwatoa watu gizani

  TOLEO MAALUMU LA RAMADHAN 1436

  Head office, Lumumba Street, Opp: Viwanja vya Mnazi Mmoja, P. O Box 779 Dar es Salaam, TanzaniaTell: 255 22 2182482/ 255 222184419, Fax: 255 22 2181424, E-mail: info@Binslum.com

  MTIHANI MGUMU: NANI ATAFAULU?

  RAMADHAN 1436

  HAbARi UK2

  MTIHANI MGUMU: NANI ATAFAULU?

  TIF KUTUmIa Tsh. mIl 200 KUFUTUrIsha-Uk 2

  25 shabaan

 • www.islamicftz.org

  25 Shaaban 1436, Ijumaa juni 12 - 18, 2015

  2 TOLEO MAALUMU LA RAMADHAN habarI / tangazo

  the Islamic Foundation kutumia tsh. mil 200 kufuturisha magereza 13 NA MWANDISHI WETU

  Taasisi ya The Islamic Founda-tion (TIF) yenye makao yake makuu mkoani Morogoro ina-tarajia kutumia zaidi ya Tsh. Milioni 216,000,000 kwa ajili ya kufu-turisha makundi mbalimbali ya Kiislam, wakiwemo wafungwa.

  Akizungumza na gazeti la Imaan, Katibu Mkuu wa taasisi hiyo, Sheikh Ally Ajirani amesema, fedha hizo zitatu-mika kusambaza futari nchi nzima.

  Aidha, Sheikh Ajirani alibainisha kuwa, makundi yatakayonufaika ni pamoja na misikiti zaidi ya 250, shule za sekondari na vyuo zaidi ya 50, pamoja na wafungwa katika magereza 13 nchini.

  Mbali na zoezi la kufuturisha, pia Sheikh Ajirani alizitaja shughuli ny-ingine zitakazofanywa na taasisi ya TIF katika mwezi mtukufu wa Ramadhan kuwa ni mafunzo ya darasa za Ramad-han yatakayotolewa na masheikh mbalimbali kutoka chuo cha Maahadil Imaan kilichopo wilaya ya Kilosa mkoa-ni Morogoro.

  Alisema, masheikh zaidi ya 100 kuto-ka chuo hicho kilicho chini ya The Islam-ic Foundation wanatarajiwa kutoa darsa katika baadhi ya misikiti hiyo.

  Aidha Sheikh Ajirani alisema, taasisi hiyo pia itashughulika na upokeaji wa zaka kutoka kwa wahisani mbalimbali

  na kugawa kwa watu waliokusudiwa kwa mujibu wa sharia ya Kiislam.

  Sheikh Ajirani aliongeza kusema kuwa, licha ya kugawa futari katika misikiti yake hapa nchini, Taasisi ya TIF pia inajishughulisha na ugawaji wa tende katika misikiti mbalimbali ya taa-sisi na isiyokuwa ya taasisi ndani ya mwezi huo wa Ramadhan.

  Kwa mujibu wa Sheikh Ajirani, mwa-ka huu taasisi ya TIF inatarajia kugawa tani 200 za tende zenye thamani ya Tsh. Milioni 700.

  Aliongeza kusema kuwa, taasisi pia inashughulika na kuwalipia baadhi ya wafungwa ambao walihukumiwa ku-fungwa magerezani kutokana na kushindwa kulipa faini.

  Katika hatua nyingine, Sheikh Ajirani alisema, Waislam na wasiokuwa Wais-lam wajiandae kunufaika na vipindi vya mafundisho sahihi ya dini ya Kiislam yenye kuhusiana na mwezi mtukufu wa Ramadhan kupitia radio na TV imaan pamoja na gazeti la Imaan.

  Sheikh Ajirani amewataka Waislam kufuatilia vipindi vya Ramadhan kupitia radio na Tv zao ili kupata mafundisho hayo sahihi ya Kiislam.

  Akizungumzia shughuli ambazo zili-fanywa na taasisi hiyo mwezi wa Ram-adhan kwa mwaka jana, Sheikh Ajirani alisema, taasisi ilifanikiwa kuwalipia faini wafungwa wapatao 25 na kuachiwa huru.

  NyAkAti zA swALANa. MJI aLFaJR DhUhUR aSR MaGhaRIB ISha 1 DAR ES SALAAM 11:16 6:22 9:44 12:15 1:25 2 zANzibAR 11:15 6:22 9:45 12:16 1:26 3 tANGA 11:17 6:26 9:49 12:22 1:32 4 MOROGORO 11:27 6:40 9:52 12:22 1:32 5 MtWARA 11:23 6:23 9:42 12:09 1:20 6 ARUSHA 11:22 6:35 10:00 12:34 1:44 7 DODOMA 11:27 6:35 9:58 12:29 1:39 8 MbEyA 11:43 6:47 10:08 12:37 1:47 9 kiGOMA 11:50 6:59 10:22 12:55 2:05 10 MWANzA 11:34 6:48 10:12 12:47 1:57 11 kAGERA 11:46 6:57 10:20 12:53 2:03 12 tAbORA 11:39 6:48 10:11 12:43 1:53 13 SHiNyANGA 11:36 6:47 10:11 12:45 1:55 14 SiNGiDA 11:33 6:41 10:04 12:36 1:46 15 iRiNGA 11:36 6:39 9:59 12:28 1:38

  08 jUNI - 14 jUNI, 2015

  Afyais natural source of sweet drinking water from under-

  ground stream which is blended

  with essential minerals to sup-port and aid per-fect metabolism.

  WATERCOM LIMITEDP.o. Box 20409, Plot N.4005, Kisarawe11 area

  Temeke,Daresalaam, Tanzaniawww.watercomtz.com, E-mail:info@watercomtz.com

  Katibu Mkuu The Islamic Foundation (TIF), Sheikh ally ajirani

 • www.islamicftz.org

  25 Shaaban 1436, Ijumaa juni 12 - 18, 2015

  3TOLEO MAALUMU LA RAMADHAN

  NA MWANDISHI WETU

  Balozi wa Marekani nch-ini Indonesia, nchi yenye Waislam wengi zaidi duniani, Robert O. Blake, amerudisha nyuma shere-he za uhuru wa Marekani kwa mwezi mmoja nyuma kutoka Ju-lai 4 hadi Juni 4.

  Sababu aliyoitoa, ni kuhesh-imu mwezi wa Ramadhan. Iwapo zingefanyika Julai 4, sherehe hizo zinazoambatana na muziki na mambo mengine yaliyo kinyume na Uislam, zingefanyika ndani ya mwezi huo mtukufu.

  Hapa nchini, zimebaki siku nne au tano mwezi wa Ramadhan uingie na tayari Watanzania wak-iwemo Waislam wako katika hek-aheka za kampeni za uchaguzi.

  Swaumu ya mwezi wa Ram-adhan mwaka huu ni mtihani mgumu kwa Waislam haswa wale wanaojihusisha na siasa za ucha-guzi, hususan wagombea au wa-pambe wao, mmoja wa wanasiasa wanaopigania nafasi ya udiwani jijini Dar es salaam, Karama Juma alisema.

  Mwezi wa Ramadhan ni mwezi mtukufu wa Waislam ambao nda-ni yake Mtume Muhammad (Re-hma na amani ziwe juu yake) ali-pewa utume pamoja na kuterem-shiwa Quran.

  Kwa mujibu wa Uislam, Mtume Muhammad (Rehma na amani ziwe juu yake) ametumwa kuwa Rehma kwa walimwengu wote na Quran imekusudiwa iwe mwongozo kwa watu wote.

  Mwezi wa Ramadhan ambao imeteremshwa ndani yake Quran

  mwongozo kwa watu wote na ki-pambanuzi katika miongozo (2:185).

  Nini utukufu wa Ramadhan? Utukufu ni tofauti na utakatifu. Ingawa mwezi wa Ramadhan ni mwezi mtukufu, lakini si mwezi mtakatifu. Miezi mitakatifu ni Muharram, Rajab, Dhul Qaadah na Dul Hijja. Utakatifu wao ni kwa kuwa Allah ameitaja miezi hii kuwa ni miezi mitakatifu (Quran 9:36)

  Ramadhan ni mwezi mtakatifu yaani wenye hadhi kubwa sana kwa sababu mbali na Mtume ku-pewa utume ndani ya mwezi huu na kuteremshwa Quran, ndani ya mwezi wa Ramadhan kuna usiku mmoja ambao Allah nasema Usiku wenye cheo ni bora kuliko miezi elfu moja (97:3)

  Mtume Muhamamd (Rehma

  na amani ziwe juu yake) anatu-dokeza moja ya sababu za mwezi wa Ramadhan kuwa mwezi mtukufu ni kwamba Allah ameii-ta ibada ya swaumu ifanyikayo ndani yake kuwa ni ibada yake.

  Imepokewa kutoka kwa Abu Huraira (Radhi za Allah ziwe juu yake), kuwa Mtume wa Allah al-isema: Allah Mwenye nguvu anasema kila tendo la mwanada-mu ni la kwake isipokuwa swau-mu, kwa hakika hiyo ni yangu na mimi ndiye nitakayeilipa.

  Swaumu ni ngao, kwa hiyo inapokuwa mmoja wenu katika siku ya swaumu ajiepushe na maneno machafu na ugomvi; na ikiwa mtu atamtukana na aseme hakika mimi nimefunga.

  Naapa kwa yule ambaye nafsi ya Muhamamd iko katika miliki yake, harufu ya kinywa cha aliye-

  funga inapendeza mbele ya Allah kuliko manukato ya miski. Mwenye kufunga ana furaha mbi-li, furaha pindi anapofungua na furaha pindi atakapokutana na mola wake atafurahi kwa (malipo) ya swaumu yake (Bukharin a Muslim).

  Ndiyo maana imeelezwa kuwa, mwezi wa Ramadhan kuangukia kipindi hiki cha uchaguzi, am-bacho wanasiasa na wapambe wao huzuliana, kufitiniana, huvu-rumishana makombora na hata kufikia kugombana ni mtihani mgumu sana.

  Kwa kuwa swaumu ni ya Allah basi mwezi wa Ramadhan ni mwezi wa Allah. Huu ndio utuku-fu wa mwezi wa Ramadhan. Ni kama vile Allah anasema miezi yote ya mwaka ni miezi yenu waja wangu, lakini mwezi wa Ramad-han ni mwezi wangu.

  Na hii ni kwa sababu ibada ny-ingine zote ni ibada ambazo watu wanaweza kusema huyu anaswali, anatoa sadaka, anasoma Quran, anatoa zaka au anahiji na kadha-lika. Lakini hakuna atakayesema kwa hakika nani amefunga.

  Kwanza kwa sababu swaumu si kuacha kula na kunywa pekee bali ni kufunga dhidi ya yale yote aliyoyakataza Allah na Mtume wake na pili ni kwa sababu uhaki-ka wa mtu kujizuilia na huko kula na kunywa aujuaye ni mwenye kufunga na Mola wake tu.

  Kwa hiyo, Waislam, kama ba-lozi wa Marekani anaamua ku-rudisha nyuma siku ya sikukuu yao ya taifa kwa heshima ya mwezi wa Ramadhani, naye si Muislam, sisi tunatakiwa tuuheshimu mwe-zi huu kiasi gani?

  Chonde chonde tusiuvunjie heshima mwezi huu mtukufu kwa kutanguliza mbele mambo ya ki-dunia, tukaangukia miongoni mwa wale ambao dunia yao ime-washughulisha hadi wakaisahau dini.

  Tujiandae kuukaribisha mwezi wa Ramadhan kwa kukithirisha uchamungu katika siku hizi chache zilizobaki na katu tusifan-ye ajizi tukapata hasara kama al-ivyosema Mtume Muhammad (Rehma na amani ziwe juu yake)

  .Amepata hasara atakayei-diriki mwezi wa Ramadhan na asisamehewe (Tirmidhy).

  habarI

  Swaumu ya

  mwezi wa Ramadhan

  mwaka huu ni mtihani mgumu kwa waiSlam haSwa wale

  wanaojihuSiSha na SiaSa za uchaguzi, huSuSan

  wagombea au wapambe wao

  mtIhanI mgumu: nanI ataFauLu?

  NA SELEMANI MAGALI

  Wakati Waislam waki-jiandaa kuukaribisha mwezi mtukufu wa R a m a d h a n , w a -nafunzi wa Kiislam wanaosoma katika shule za bweni wanakabili-wa na changamoto kubwa ya ku-kosa futari kufuatia shule hizo kushindwa kuwa na utaratibu wa kufuturisha.

  Hayo yamebainishwa na Rais wa Jumuiya ya Wanafunzi na Vija-na wa Kiislam Tanzania (TAM-SYA), Mohammedi Wage, wakati

  akizungumza na gazeti la Imaan juu ya mata-yarisho ya mapokezi ya

  mwezi wa Ramadhan kwa wa-nafunzi na vijana kwa ujumla.

  Mohammed Wage alisema, changamoto kubwa ambayo wa-nayo ni maombi mengi ya wa-nafunzi kutoka shule mbalimbali na vyuo kutaka kupatiwa msaada wa futari wakati wa mwezi wa Ra-madhan.

  Alisema changamoto hiyo bado hawajaweza kuipatia majibu yake.

  Wage aliongeza kusema kuwa, tatizo hilo lipo katika shule zote kuanzia zile za serikali na za watu binafsi, ambapo wanafunzi wa Ki-islam bado hawajui hatma yao, wakati wanaelekea kuupokea mwezi mtukufu wa Ramadhan.

  Wage ametaja changamoto ny-

  i