imaan newspaper issue 3

of 16 /16
Head off ice, Lumumba Street, Opp: Viwanja vya Mnazi Mmoja, P . O Box 779 Dar es Salaam, Tanzania Tell: 255 22 2182482/ 255 222184419, Fax: 255 22 2181424, E-mail: [email protected] nslum.com Tumekwisha! ISSN 5618 - N0. 003 BEI: SH800/- KSH80/- USH1,200/- 8 RAJAB 1436, JUMAT ATU , APRIL 27 - MEI 3, 2015  www.islamicftz.org huwatoa watu gizani Saudia yaboresha taratibu za Hijja - Uk 3 Sheikh Juma Poli: Ni muasisi wa  JA SU T A - Uk 5 Maafa Pemba: The Islamic Foundation yachangia zaidi ya milioni 10  Zaidi ya familia 100 zaathirika - Uk. 2  Vituo vya kulea yatima vyafungiwa Idadi kupunguzwa Machokoraa kuongezeka Tumekwisha!

Author: imaan-newspaper

Post on 06-Jan-2016

2.058 views

Category:

Documents


7 download

Embed Size (px)

DESCRIPTION

Imaan Newspaper Issue 38 Rajab 1436, Jumatatu, Mei 4 - 10, 2015

TRANSCRIPT

  • Head office, Lumumba Street, Opp: Viwanja vya Mnazi Mmoja, P. O Box 779 Dar es Salaam, TanzaniaTell: 255 22 2182482/ 255 222184419, Fax: 255 22 2181424, E-mail: [email protected]

    Tumekwisha!ISSN 5618 - N0. 003 BEI: Sh800/- KSh80/- USh1,200/- 8 RajaB 1436, jUmatatU, apRIl 27 - mEI 3, 2015 www.islamicftz.org

    huwatoa watu gizani

    Saudia yaboresha taratibu za Hijja - Uk 3

    Sheikh Juma Poli: Ni muasisi wa JasUta - Uk 5

    Maafa Pemba: The Islamic Foundation yachangia zaidi ya milioni 10 Zaidi ya familia 100 zaathirika - Uk. 2

    Vituo vya kulea yatima vyafungiwa Idadi kupunguzwa machokoraa

    kuongezeka

    Tumekwisha!

  • www.islamicftz.org

    8 Rajab 1436, jumatatu aprili 27 - mei 3 , 2015

    2

    Saudia yaipa Serikali ya tanzania tani 100 za tende

    Taasisi ya The Islamic Foundation imechangisha kutoka kwa wadau wake zaidi ya Tsh. Milioni 10 kupitia radio na Tv Imaan kwa ajili ya kusaidia wananchi walioathirika na upepo mkali uliovuma katika kisiwa Panza Wilaya ya Mkoani, Pemba usiku wa kuamkia Aprili 22 mwaka huu. Pichani juu ni baadhi ya nyumba zilizoathirika. Habari zaidi kuhusu tukio hili zitatoka toleo lijalo Insha-Allah.

    Mtumishi wa Wizara ya Mambo ya Fedha ya Saudi Arabia, Mohamed Alhajabani (wa kwanza kushoto) akimkabidhi tende Afisa Mwandamizi wa Serikali kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania, Leonce Bilauri (wa kwanza kulia). Anayeshuhudia (katikati) ni Kaimu balozi wa Saudi Arabia nchini Saad Al-asiri. Tende zilizotolewa ni tani 100 zenye thamani ya Tsh. Milioni 196.

    habaRi

    Na MwaNdishi wetu

    Serikali ya Saudi Ara-bia kupitia ubalozi wake hapa nchini umekabidhi msaada wa tani mia moja za tende zenye jumla ya Tsh. Milioni 196 (Tsh.196,000,000/=) kwa Serikali ya Tanzania ikiwa ni ishara ya mahusiano mema baina ya nchi hizo mbili.

    Makabidhiano hayo yame-fanyika hivi karibuni katika ubalozi wa nchi hiyo jijini Dar es Salaam kwa kuwakutanisha watumishi mbali mbali wa

    ubalozi huo na maafisa waan-damizi wa Serikali.

    Akizungumza mbele ya waandishi wa habari wakati wa kukabidhi msaada huo, mtu-mishi kutoka Wizara ya Mam-bo ya Fedha ya Saudia Arabia, Mohamed Alhajabani alisema kuwa, tende hizo ni zawadi ya Mfalme Salman bin Abdulaziz kwa Watanzania.

    ``Kiasi hiki cha tende ni za-wadi ya Mfalme Salman bin Abdulazizi wa Saudi Arabia kwa Watanzania wote; vilevile ni muendelezo katika mlolon-go wa misaada mingi iliyowahi

    kutolewa na Serikali ya nchi hiyo kwa taifa hili, alisema Alahajaban.

    Kwa upande wake, Afisa Mwandamizi wa Serikali, Le-once Bilauri ambaye alimwak-ilisha Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Balozi Has-san Simba alisema: Serikali ya Tanzania inatambua mchango mkubwa wa Saudi Arabia kati-ka kuchangia maendeleo nchi-ni, lakini pia niwahakikishie kuwa kiasi hiki cha tende zita-wafikia walengwa, kwani zitak-abidhiwa kwa taasisi zinazo-husika ili zisambazwe kwa wa-

    Afyais natural source of sweet drinking water from under-

    ground stream which is blended

    with essential minerals to sup-port and aid per-fect metabolism.

    WATERCOM LIMITEDP.o. Box 20409, Plot N.4005, Kisarawe11 area

    Temeke,Daresalaam, Tanzaniawww.watercomtz.com, E-mail:[email protected]

    MAAfA peMbA

    nanchi. Katika hatua nyingine

    Mwenyekiti wa Taasisi ya The Islamic Foundation, Aref Nahdi ambaye alia-

    likwa kushuhudia mak-abidhiano hayo, ameli-ambia gazeti hili kuwa watanzania wanatakiwa kushukuru kwa kupatiwa

    hidaya hiyo, ambapo pia alizitaka taasisi zitaka-zogaiwa amana hiyo ku-fanya uadilifu kwa ku-wafikishia walengwa.

  • Yusufu AhmAdi nA Yusufu Amini, dAr

    Serikali imeshauriwa kusi-mamisha mkakati wake wa kuvifungia vituo vya kulea watoto yatima badala yake iviongoze, ivilee, ivisaidie na kuvi-wezesha kutoa huduma bora zaidi kwa watoto kwa sababu ni bora mtoto alelewe katika mazingira duni kuliko kujilea mtaani.

    Akizungumza kwa niaba ya wami-liki wenzake ambao vituo vyao vime-fungiwa katika mikoa mbalimbali ya Tanzania, Bi Aminajati Kilemia, amezitaka mamlaka husika kufikiria mara mbili kabla ya kuchukua hatua, kwani vituo hivyo vinasaidia kupun-guza watoto wa mitaani na matukio ya uhalifu.

    Bi Aminajati ni mmiliki wa Kituo cha Kulea Watoto cha Hiari kilichopo katika Manispaa ya Temeke, jijini Dar es Salaam ambacho pamoja na vituo vingine kadhaa vilivyopo katika man-ispaa hiyo vilifungiwa hivi karibuni.

    Si sahihi kwa Serikali kuvifungia vituo hivi vinavyosaidia kutunza wa-toto walio katika mazingira magumu na kupunguza watoto wa mtaani am-bao huishia kuwa wahalifu, alisema Bi Kilemia.

    Bi Kilemia aliongeza kuwa, kulea watoto yatima ni kazi ya kujitolea

    inayotokana na huruma. Ni vigumu kujikamilisha kwa kila kitu kama Serikali inavyotaka, badala yake ni vema Serikali isaidie wamiliki wana-pokwama. Mimi kituo changu kimefungiwa kwa madai kuwa eneo ni dogo na mazingira yake si mazuri, sasa mimi hela ya kununua kiwanja cha mamilioni nazitoa wapi, nadhani katika hili Serikali haina budi kusaid-ia, alisema Bi. Kilemia.

    Naye Husna Abdul, ambaye ni msimamizi wa kituo kimoja cha wa-toto yatima kilichopo Tanga amese-ma, Serikali yenyewe haijaweza ku-wapatia makazi, chakula na malazi watoto waishio katika mazingira

    magumu mitaani, ingawa huo ni wa-jibu wake. Kisha Husna alihoji: Seri-kali inapata wapi utashi wa kuvifunga vituo vilivyowapa watoto makazi, chakula, malazi na uhakika wa mai-sha ambayo hawayapati mitaani.

    Husna amesifia na kupongeza uk-aguzi wa vituo vya kulelea watoto, vi-kiwemo vya mayatima na madrassah nchi nzima, lakini ameonya kuwa Serikali inapokuta upungufu iangalie hatua inazozichukua zisiwe na ma-tokeo hasi.

    Sababu za vituo kufungwa:

    Katika mkakati huo wa Serikali,

    baadhi ya vituo vya kulelea watoto ya-tima na vingine vya malezi ya kiroho (madrasa) vimefungiwa katika mikoa kadhaa, ikiwemo Kilimanjaro, Dar es Salaam na Dodoma.

    Sababu za kufunga vituo hivyo in-adaiwa ni kutokuwa na usajili, maz-ingira hatarishi, baadhi ya vituo ku-fundisha karate, watoto kukoseshwa elimu na wahusika kujinufaisha bin-afsi.

    Katika suala la usajili kuna mas-wali kadhaa ya kujiuliza katika sakata hili la kuvifungia vituo hivi. Je, kweli vyote ni vituo vya watoto/mayatima? Kama jibu ni ndiyo, wahusika wa-likuwa wapi miaka yote hii vituo vi-kiendeshwa pasina usajili?

    Kadhalika, je hatua zilizochukuli-wa zilizingatia madhara ya muda mrefu kwa watoto na walezi wao wal-iowapeleka katika vituo hivyo? Wa-zazi na walezi hao walipewa nafasi ya kusikilizwa kuelewa matatizo ili mambo yasije kujirudia tena?

    Wachambuzi wanasema in-

    gewezekana kwa Serikali kuvipa mwongozo jinsi ya kusajili, kuviende-sha na kisha kuwapa muda wahusika wa vituo hivi kufanya marekebisho.

    Wachambuzi wanasema, kuvi-fungia si ufumbuzi kwani tunaweza kujikuta tukiongeza idadi ya watoto wa mitaani. Mmoja wa wadau wa vi-tuo hivi, Jamal Kassim alihoji: Kama kuishi katika kituo kisicho na usajili ni mazingira hatarishi, tuseme nini kuhusu maelfu ya watoto waishio mi-taani? Yepi ni mazingira hatarishi?

    Serikali inajua ukubwa wa tatizo la watoto yatima ambao kwa tak-wimu zake yenyewe wanakadiriwa kufikia milioni 2.4. Kutokana na win-gi huo, wananchi wengi wanaamini Serikali ingepaswa kutoa msaada wa miongozo, usajili na jinsi ya kuende-sha vituo vya kulea watoto yatima na vile vya malezi vinavyoanzishwa na watu binafsi au taasisi pasina kufuata taratibu badala ya kuvifunga.

    Hoja nyingine iliyoshangaza wen-gi ni kituo kufungwa kwa sababu ya kufundisha watoto karate. Abdulka-dir Omar, mtaalamu wa sanaa za ma-pigano na mwalimu wa watoto wa mchezo huo, amehoji kuna kosa gani watoto wakijua karate?

    Abdulkadir anasema: Michezo ni moja ya mambo yanayohimizwa na Serikali katika mashule, kuna ubaya gani iwapo watoto wa kituo cha yati-ma wakifundishwa mchezo huo am-bao siyo tu mchezo, bali ni ulinzi bin-afsi (self defence)?.

    Katika wilaya ya Temeke Mratibu wa Ulinzi na Usalama wa mtoto kutoka ofisi ya Ustawi wa Jamii, Bi Subisya Kabuje, ambako vituo vilivy-ofungiwa katika wilaya ya Temeke vi-kikiuka miongozo na sheria ya mtoto namba 21 ya mwaka 2009.

    Ametaja sheria na kanuni zilizok-iukwa kuwa ni vituo kutosajiliwa na kutotoa taarifa kwa mamlaka husika pale wanapowachukua watoto. Bi Kabuje alisema kuwa, waliwaandikia wamiliki wa vituo hivyo kuwataka kufuata sheria na miongozo ya jinsi ya kuendesha vituo vyao pamoja na kurekebisha mazingira ya vituo vyao.

    Hata hivyo, madai hayo yote yalip-ingwa na wamiliki na watendaji wa vituo vya kulelea yatima na vile vya malezi. Katibu wa kituo cha malezi ya wajane na watoto yatima cha Safi-na kilichopo katika Manispaa ya Te-meke, Jijini Dar Es Salaam ambacho nacho kilifungiwa, Said Athumani amesema wao wamekuwa wakifuata sheria katika baadhi ya vipengele ikiwemo kufika kwa serikali za vijiji na kufanya makubaliano kabla hawa-jawachukua hao watoto.

    Kuvifungia vituo vya malezi ni kuongeza idadi ya watoto wa mitaani kama hawa..

    habariwww.islamicftz.org8 rajab 1436, jumatatu aprili 27 - mei 3 , 2015

    3habari

    Wachambuzi Wanasema ingeWezekana kWa serikali kuvipa mWongozo jinsi ya kusajili, kuviendesha na kisha kuWapa muda Wahusika Wa vituo hivi kufanya

    marekebisho

    tumekwisha!

    UK 14

    nA rAmAdhAni Ali mAelezo zAnzibAr

    Waislamu wa Zanzibar w a n a o t e g e m e a kutekeleza Ibada ya Hijja mwaka huu wameshauriwa kukamilisha mipan-go ya safari hiyo mapema ili kuzi-wezesha taasisi zinazosafirisha ma-hujaji kuweza kukamilisha taratibu mpya zilizowekwa na Serikali ya Saudi Arabia.

    Afisa katika Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana, Ustaadh Khalid Mrisho,ameliambia kongamano la mahujaji kuwa Serikali ya Saudi Arabia imebadilisha taratibu za maandalizi ya Hijjah kuanzia mwa-ka huu kufuatia malalamiko ya ma-

    hujaji kutokana na vitendo vya udanganyifu vya baadhi ya taasisi zinazosafirisha mahujaji kutoka mataifa mbali mbali duniani.

    Baadhi ya viongozi wa taasisi zi-nazosafirisha mahujaji walikuwa wakiwatoza fedha mahujaji wao kwa ajili ya kulipia viwanja vya ndege vya Makka na Madina lakini walikuwa hawalipi na kupelekea mahujaji ku-zuiliwa kwa saa kadhaa,alisema Us-taadh Khalid.

    Alisema taasisinyingine zilikuwa zinawaahidi mahujaji kuwakodia

    nyumba nzuri za karibu katika miji mitakatifu ya Makka na Madina la-kini wanapofika huko huwekwa kwenye nyumba mbovu, mbali na wengine hukosa huduma ya chaku-la. Alisema katika kukabiliana na matatizo hayo Serikali ya Saudia Arabia kuanzia sasa imeziagiza taa-sisi zinazosafirisha mahujaji kufan-ya taratibu zote za maandalizi ya sa-fari, makazi na matembezi kwa njia ya mtandao na kulipa gharama zote wakiwa nchini mwao.

    Alisema iwapo taratibu hizo haz-

    ikukamilika hujaji atakosa visa ya kuingia Saudi Arabia na atakosa kutekeleza ibada ya Hijjah kwa mwaka huo.

    Aliongeza Juni 27 ndio siku ya mwisho kukamilisha taratibu za mahujaji na baada ya tarehe hiyo mtandao huo utafungwa.

    Lengo la uwamuzi huo wa Saudi Arabia ni kuwaondoshea mahujaji usumbufu usiowalazima wakati wa kutekeleza ibada hiyo, alisisitiza Ustaadh Khalid.

    Aliwakumbusha mahujaji wa-

    tarajiwa kuwa waangalifu na mizigo yao wakati wa safari na wana-pokuwa nchini humo na wataka-porejea kuchukua kiwango cha mizigo kinachokubalika kwenye ndege.

    Akifungua kongamano hilo li-liloandaliwa na Umoja wa Taasisi za Hij ja Zanzibar (UTAHIZA) Mwenyekiti wa Bodi na kufanyika katika ukumbi wa Beit al Yamin Malindi, Sheikh Khamis Abdulha-mid amewasisitiza Waislamu wenye uweze kutekeleza ibada ya Hijja ili kukamilisha Uislamu wao.

    Mwaka huu Tanzania imepewa nafasi 3,000 za mahujaji watakaok-wenda kutekeleza ibada hiyo inayo-fanyika kila mwaka mwezi wa mfun-guo tatu.

    Saudia yaboresha taratibu za hijja

  • www.islamicftz.org

    8 Rajab 1436, jumatatu aprili 27 - mei 3 , 2015

    4 www.islamicftz.org8 Rajab 1436, jumatatu aprili 27 - mei 3 , 2015

    5

    Huu ni muendelezo wa hotuba ya alieku-wa Rais wa Uganda, Jenerali Idd Amin aliyoitoa wakati akiz-indua Baraza Kuu la Waislamu la Uganda (UMSC) katika Kituo cha Mikutano ya Ki-mataifa nchini humo, June 1, 1972, saa kumi jioni

    Yumkini moja ya vipengele nyeti v inavyosababisha migongano katika jumuiya za Kiislamu hapa Uganda ni ku-wepo kwa uelewa tofauti juu ya mafundisho ya Mtume Mu-hammad (Rehema na amani ziwe juu yake) jambo ambalo hutumiwa na wanaosaka ma-daraka ili kuwagawa Waisla-mu.

    Hali hii pia inatokana na walimu wasiofaa kabisa au wenye elimu ndogo kukabi-dhiwa jukumu la kuifundisha Quran na kwa sababu hii na-karibisha maoni yaliyotolewa katika hadhara ya dini mwaka jana kwamba ipo sababu ya kuanzishwa kwa taasisi moja inayohusika na mafundisho ya Kiislamu.

    Taasisi hiyo itahusika na kusahihisha baadhi ya mambo yaliyomo katika Uislamu yasi-yo sahihi. Hivyo, ninatarajia kwamba taasisi hiyo itafanya uchunguzi katika taasisi ny-ingine ambazo zinajishughuli-sha na mafundisho ya Kiisla-mu ili kuziboresha.

    Ninatambua kwamba baa-dhi ya watu hawajaridhika na jinsi Baraza kuu la sasa lilivy-oanzishwa. Wapo ambao ha-wajaridhishwa na muundo wake. Napenda kukumbusha kwamba moja ya mapendeke-zo yaliyotolewa na kamati inayojishughulisha na masuala ya Waislamu katika konga-mano la viongozi wa dini hapo mwaka jana lilikuwa kwamba Baraza Kuu linapaswa ku-undwa na watu watatu kutoka kila wilaya, akiwemo Kadhi wa wilaya hiyo.

    Wakati nilipokuwa nafunga kongamano la viongozi wa dini, niliomba msaada wa Seri-kali katika kuanzishwa kwa Baraza hilo.

    Mipango ilifanywa ili ku-wezesha kufanyika kwa ucha-guzi nchi nzima kwa mujibu wa mapendekezo niliyoyataja hapo juu; kwa bahati mbaya,

    baadhi ya viongozi wa Kiisla-mu walianza kufanya kampeni ili watu wao wachaguliwe kati-ka Baraza hilo.

    Watu hao sio tu walikuwa wakirejesha siasa hapa Ugan-da, vile vile walikuwa wakijari-bu kutoiwezesha jamii kubwa ya Waislamu wa Uganda kuwa na mwakilishi ndani ya Baraza hilo.

    Hali hiyo ilinifanya nikose njia mbadala, na hivyo kua-mua kusitisha uchaguzi huo, na nilitangaza juu ya suala hilo.

    Pia nilitambua kwamba, mwanzoni kabisa mwa uhai wa Baraza hili haitowezekana watu watatu pekee kutoka ka-tika wilaya ndio wawe wawak-ilishi. Ifahamike kuwa Waisla-mu wapo kila kona ya nchi hii, katika wilaya zote. Haitoleta maana kutegemea watu watatu kutosha kufahamu mi-tazamo na mahitaji ya Waisla-mu wote katika wilaya aliyopo. Ninaona kuna umuhimu wa kuhakikisha kila j imbo linakuwa na mwakilishi am-bae atayawasilisha matatizo ya watu wake katika Baraza Kuu.

    Hivyo basi, ninapanga kila wilaya kuwa na wawakilishi kumi na moja, ikizingatiwa kwamba kwa mujibu wa map-endekezo ya kongamano la dini, Baraza Kuu lenyewe linaweza kubadili idadi ya wa-n a c h a m a , k w a k a d r i litakavyoona inafaa.

    Muda mfupi kabla hamja-wasili katika mkutano huu, niliwaomba muwasilishe ma-jina ya Waislamu kumi walio na maarifa ya kutosha kutoka katika wilaya mbali mbali. Nil-iwaomba muwasilishe majina hayo ili kuwezesha Baraza hili liwe na Waislamu wenye elimu pana zaidi. Nina furaha wito

    wangu huo umepokelewa kwa moyo mkunjufu.

    Nyinyi wenyewe mme-waondoa wale waliokuwa wa-mechaguliwa hapo awali na badala yake kuwachagua vija-na wadogo wenye elimu kubwa. Ni jambo la faraja kuo-na baadhi ya wazee wamea-mua kwa hiari yao kuwaachia nafasi za kufundisha vijana ambao bado wana damu changa.

    Wanachama wa Baraza sasa ni mchanganyiko wa Masheikh wakubwa wenye uzoefu mzuri katika mambo ya Waislamu na vijana waliosoma wenye mtazamo wa kisasa.

    Lakini pia natambua, kuna idadi ya watu ambao hawa-jachaguliwa katika Baraza hilo ambao wanahisi walikuwa na haki zaidi ya kuwawakilisha Waislamu katika wilaya zao. Watu hao watambue kuwa Serikali haitomvumilia mtu yeyote yule atakaejaribu kuk-wamisha kazi za Baraza Kuu.

    Ikiwa Serikali itagundua shughuli za kulihujumu Bara-za Kuu italazimika kuchukua hatua kali ili kuhakikisha Baraza hilo linafanya kazi yake bila bughudha.

    Katika moja ya vikao vyan-gu na ndugu Nkambo-Mugerwa aliyeongoza kikao chenu cha mwaka jana na cha mwezi uliopita alizungumzia kutoridhishwa kwa baadhi ya vikundi katika uchaguzi wa baadhi ya viongozi wenu.

    Kumekuwa na shutuma kwamba kikundi kimoja cha Kiislamu kimefurahia ushindi wake dhidi ya vikundi vingine vya Kiislamu. Kama kuna kun-di lolote la Kiislamu linaona ushindi ni wake peke yake, basi napata hofu kuwa hatujafani-kiwa kuleta umoja kamili wa

    kitaifa miongoni mwa Waisla-mu hapa nchini.

    Unapotazama muundo wa Baraza Kuu, unathibitisha kuwa jumuiya na makundi yote ya Kiislamu ndani ya Baraza hilo yamewakilishwa vema.

    Suala hilo linatoa ishara njema kwa mustakabali wa Uislamu hapa Uganda. Kwa sasa ni wajibu wa Baraza zima, viongozi wake na mwanacha-ma mmoja mmoja al i-yechaguliwa kwa njia halali kuhakikisha kuwa vikundi vyote vya upinzani vinashaw-ishiwa kuungana na Baraza kwa faida ya Uislamu, ambao ndio sababu hasa ya kuanzish-wa hili Baraza na kamati zake.

    Mr. Nkambo-Mugwera ali-zungumzia pia matatizo na maombi yaliowasilishwa wakati wa mikutano yenu. Serikali itayazingatia matatizo na maombi yenu hayo pale yat-akapokuwa na faida kwa nchi nzima, ikiwemo nyinyi wenyewe.

    Ni katika muktadha huo Serikali itaendela kulitilia ma-nani jambo lolote lile litaka-lowasilishwa na Baraza kuu ama viongozi wake.

    Kuna uwezekano baadhi ya maombi yatafanyiwa kazi baa-da ya Serikali kuyapitia mazuri n a k u o n a k a m a y a n a umuhimu.

    Hata kama baadhi ya maombi yenu hayatafanyiwa, naomba mtuelewe kwa sababu maamuzi yoyote ambayo Seri-kali itachukua yatakuwa ni kwa manufaa ya taifa na ninyi pia.

    Nimepata fursa ya kuisoma katiba mliyoiunda ili kudhibiti na kuelekeza masuala ya Kiis-lamu hapa nchini. Nimeri-dhishwa kwa kiwango kikubwa na muundo wa kamati zilizo-mo ndani ya katiba hiyo. Ni katiba nzuri inayotokana na kazi kubwa, moyo wa kujitolea kwenye masuala yahusuyo Waislamu wa hapa Uganda, na nia njema itokayo kwa watu wote waliomo katika Baraza hili na walioshiriki katika kon-gamano la dini la mwaka jana huko Kabale na Kampala.

    Kwa sababu hiyo napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Waziri wangu wa Sheria na Mwanasheria Mkuu, Bwa-na Nkambo-Mugerwa kwa kujitolea kwake kiasi kikubwa ambapo ameweza kuwaongo-za Waislamu katika vikao mbalimbali tangu hapo mwezi wa tano mwaka jana.

    kutoka misikitini tujikumbushe

    hotuba ya Rais wa uganda - 2Jenerali Idi Amin Dada wakati akizindua Baraza Kuu la Waislamu la Uganda (UMSC) katika kituo cha mikutano ya kimataifa nchini humo, June 1, 1972.

    Yusufu Ahmadi, Zanzibar

    Wazazi na jamii kwa ujumla wameaswa kutowaita watoto wa-dogo kwa majina mabaya kwani ku-

    fanya hivyo ni kuwajengea tabia mbaya kinyume cha mafundisho ya dini ya kiislamu.

    Akikhutubu kabla ya sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Afraa Bint Issa(Shurbaa) ulioko eneo

    la Kidongo Chekundu katika mkoa wa mjini Magharibi Zanzibar, Mwalimu Moham-

    ad Soud amesema imejenge-ka tabia miongoni mwa jamii

    kuwaita watoto wadogo majina yasiyopendeza, jambo ambalo halifai.

    Mwalimu Soud ametoa mfano wa majina mabaya kama mjinga, mpumbavu na majina kadhalika majina ya utani yenye maana

    mbaya. Wakati huohuo, Mwalimu Soud

    ameutolea wito umma wa kiislam na jamii kwa ujumla kufanya mambo mema na kujiepusha na vitendo vina-vyozuia maombi (duwa) kupokelewa na Mwenyezi Mungu Subhanahu Wataala.

    Na Yusuph Amin

    Waislamu wametakiwa kuitendea haki miezi mitakati-fu kwa kufanya yaliyo mema ili kupata radhi za Allah.

    Akihutubia mamia ya Waislamu kwenye ibada ya swala ya ijumaa msikiti wa Kichangani jijini Da-es-salaam, Sheikh Omar Alhadi amesema ni wajibu wa kila Muislamu kutumia fursa katika mwezi huu wa Rajabu kuzidisha mambo mema na kufanya toba ili kupata msamaha wa Allah subhanahu wataala.

    Miongoni mwa mambo mema ambayo Sheikh Omary aliyowasihi Waislamu kuyafanya kuwasaidiaWaislamu walio magerezani na kusaidia wagonjwa walio hospitali kwani kufanya hivyo kunakumbusha faida ya kuwa na uzima. Katika ibada hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta Ghalib Bilal, Sheikh Omar amesema Waislamu wanaumizwa na madhila ya ndugu zao walio magere-zani na kutaka mamlaka husika kutenda haki katika kushughulikia kesi za masheikh.

    Na Khalid Omary

    Wislamu wamekumbushwa kuwafanyia wema wazazi wao ili kuweza kupata radhi za Mwenyezi Mungu ikiwa ni miongoni mwa sababu za kukubaliwa ibada zao na kupata baraka na mafanikio katika siku ya kiama zake.

    Ukumbusho huo ulitolewa na Sheikh Harif Suleiman wakati akitoa khutba ya siku ya Ijumaa, katika msikiti wa Masjid Hudaa uliopo Ilala Bungoni jijini Dar es salaam.

    Tunatakiwa tuwafanyie mema, tuwajali na tuzun-gumze nao kwa kauli nzuri, maneno laini na yenye hekima. Vilevile tujione bado hatujawafanyia jambo lolote kubwa hata kama unamlisha au umemjengea jumba. Kadhalika, tunatakiwa tuwaombee sana dua, Sheikh Harif alisema.

    Sheikh Harif alisema baadhi ya watu wanawatukana kuwadharau wazazi wao kwa sababu hawajui thamani na ukubwa wa wazazi wawili.

    Jamii yatakiwa kuita watoto majina mazuri

    Waislamu waitendee haki miezi mitakatifu

    Tuwafanyie wema wazazi wawili KumeKuwa na shutuma

    Kwamba KiKundi Kimoja cha Kiislamu Kimefurahia

    ushindi waKe dhidi ya viKundi vingine vya

    Kiislamu. Kama Kuna Kundi lolote la Kiislamu

    linaona ushindi ni waKe peKe yaKe, basi

    napata hofu Kuwa hatujafaniKiwa Kuleta umoja Kamili wa Kitaifa miongoni mwa waislamu

    hapa nchini.

  • www.islamicftz.org

    8 Rajab 1436, jumatatu aprili 27 - mei 3 , 2015

    4 www.islamicftz.org8 Rajab 1436, jumatatu aprili 27 - mei 3 , 2015

    5hazina zetu

    NA KHALID OMARY

    Ukiorodhesha Masheikh wa kupigiwa mfano kati-ka harakati za kutetea Sunnah za Mtume Mu-hammad (Rehma na amani ziwe juu yake) na kuuhuisha Uislamu hapa nchini, huwezi ukakosa kumtaja Sheikh Juma Poli.

    Sheikh Poli alizaliwa mwaka 1950 katika jiji la Dar es Salaam na kukulia katika jiji hilo. Wazazi wake ni wenyeji wa mkoa wa Pwani na ana-fahamika zaidi kama mmoja wa waasisi wa Jumuiya ya Ansaar Sun-nah hapa nchini.

    Kusoma KwaKe:Sheikh Poli alianza kutafuta elimu

    akiwa na umri wa miaka mitano ka-tika madrasa ya Kadiriya Al Aamudi-ya iliyopo mtaa wa Dodoma, Ilala ji-jini Dar es salaam. Hii ndio madrasa pekee aliyosoma ndani ya Tanzania.

    Mwaka 1963, Sheikh Poli alienda Pwani ya Afrika Mashariki katika miji ya Mombasa, Lamu, Malindi na katika visiwa vya Rasini Kizilitini ambako alisoma kwa Masheikh mbalimbali.

    Kiu ya elimu ya Sheikh Poli haiku-kaukia katika miji hiyo; akaendelea na safari yake ya kutafuta elimu se-hemu nyingine ndani na nje ya Afrika Mashariki.

    Katika jitihada zake za kutafuta elimu hakuwa peke yake. Sheikh Poli aliambatana na Masheikh kadhaa wengine ambao baadhi yao kwa sasa ni Masheikh wakuu wa mikoa. Miaka ya 1968-70 nilielekea Mach-akos, mji uliopo pembeni kidogo ya Nairobi nikiwa na Masheikh wen-gine kama Sheikh Nurdin Abdallah Mangochi wa Mtwara, Sheikh Ally Sariko wa Arusha na Sheikh Hassan Juma aliyekuwa mwenyeji wa Kon-doa na ambaye kwa sasa alishafariki, Sheikh Poli aliliambia gazeti la Im-

    aan. Baadae Sheikh Poli alibahatika

    kupata nafasi ya kwenda kusoma ka-tika Chuo Kikuu cha Madinah kwa miaka kumi na kupata Shahada ya Ulinganiaji.

    HaraKati za Kueneza sunna:

    Sheikh Poli ni miongoni mwa watu ambao wamefundisha Waisla-mu wengi na kushiriki katik kueneza dini ya Uislamu. Moja kati ya mae-neo ambayo athari ya kazi yake ikod-hahiri ni katika Chuo cha Alhara-main, jijini Dar es salaam.

    Sheikh Poli alijiunga na chuo hi-cho na kufanya kazi ya ualimu mara baada ya kurejea kutoka Madinah wakati huo kikiwa maeneo ya Mnazi Mmoja, jijini Dar es salaam. Chuo hi-cho kwa sasa kipo mtaa wa Lindi na Shaurimoyo, katika jiji hilo hilo la Dar es salaam.

    Kazi yangu kubwa ya msingi ili-kuwa ni kufudisha na kulea vijana katika mfumo sahihi wa mafundisho ya Uislamu. Mwaka 1995 tukaonge-za wigo kwa kujenga chuo kingine eneo la Buguruni tulichokipa jina la Al- Furqan, Sheikh Poli anaeleza.

    Sheikh Poli ambaye ni daktari wa kiroho anasema, pamoja na kufundi-sha, pia amekuwa akifanya kazi ya ulinganiaji (daaawah) kwa kukemea bidaa au uzushi katika dini, aki-maanisha mambo mapya yaliyoing-

    izwa katika dini ilihali hakuna usha-hidi kuwa Mtume wala maswahaba waliyafanya.

    Watu wengi wanapenda dini, la-kini hawaijui, utakuta mtu anafanya matendo akiamini kwamba anajiku-rubisha kwa Mwenyezi Mungu, laki-ni kiukweli matendo hayo yapo mbali na Allah, kuna tatizo kubwa la kutekeleza ibada kinyume na maele-kezo ya Quran na Hadith, alieleza Sheikh Poli akisisitiza umuhimu wa kazi ya kuwalingania Waislamu kati-ka mafundisho sahihi.

    Hali hiyo ndio iliyomsukuma

    Sheikh Poli kuunganisha nguvu za wadau mbalimbali kuanzisha chom-bo kitakachokuwa nembo ya kutan-gaza Sunna za Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake).

    Chombo hicho kilitambulika kwa jina la Jumuiya ya Answar Sunna Tanzania (Jamaat Answar Sunnah) huku Sheikh Poli akiwa Amir wake.

    Kwa mujibu wa Sheikh Poli, har-akati za kuanzisha chombo hicho zil-ianza mwanzoni mwa miaka ya 1980 maeneo ya Kinondoni, Da es salaam na kilitambulika rasmi na kupewa usajili mwaka 1985.

    Sheikh Poli anawakumbuka Masheikh wawili ambao walichangia kwa kiasi kikubwa katika kuunda chombo hicho; Sheikh Muhidin Kingaluna na Sheikh Ahmad Ham-za.Wote kwa sasa wamerejea kwa Mola wao. Baadae Jumuiya ya Ansar Sunna ilifungua matawi Kigoma, Mwanza, Singida na Morogoro.

    Akizungumzia kupotea kwa mi-hadhara baina ya Waislamu na Wais-lamu kwa ajili ya kufahamishana lipi sahihi na lipi si sahihi iliyokuwepo zamani ikihusisha masuala ya mwe-zi, maulid, khitma, uharamu wa ku-piga ramli iliyochukua nafasi katika maeneo mbalimbali ya nchi kama Kigoma,Unguja, Pemba, Dar es sa-laam, Sheikh Poli amesema hiyo sio sera ya Jumuiya ya Ansar Sunna.

    Katika jambo lolote hapakosi changamoto, lakini kwa Sheikh Poli

    magumu yaliyowakuta katika har-akati zao ni kama juisi kwani kwa al-iyeusoma Uislamu atakuwa anajua kuwa mazito zaidi yaliwakuta Wais-lamu waliopita. Kwa mujibuwa Sheikh baadhi ya watu waliwaita kundi la vijana, baadae walibadili na kuwaita watoto wanaofanya mageu-zi dhidi ya masheikh.

    Lakini Sheikh Poli anasema, kadri muda ulivyosogea waliungwa mko-no na baadhi ya wazee wa Tanga, Kigoma na Kondoa na likawa si tena kundi la vijana au watoto, bali watu wenye taaluma iliyo sahihi.

    Sheikh Poli anasema katika baa-dhi ya maeneo ikiwemo Kigoma baadhi yao walinyanganywa wake zao, walipigwa na hata kuondolewa misikitini.

    Changamoto hizo zilisukuma Ju-muiya ya Ansaar kujenga misikiti yao ambayo kwa sasa imeenea nchi nzi-ma. Kwa mujibu wa Sheikh, harakati za kueneza Sunna yaMtume Mu-hammad (Rehmana amani ziwe juu yake) zimefanikiwa na hivi sasa watu wengi wanafuata yale yaliyo sahihi kuliko hapo awali, ambapo watu wa-likuwa wakiburuzwa.

    Sheikh Poli akihitimisha maho-jiano, alitoa rai kwa waandishi wa habari, ambapo aliwataka watumie

    kalamu na ndimi zao kwa umaki-ni mkubwa, kwani kalamu zao ni si-laha hatari inayoathiri na yenye ngu-vu kubwa.

    Sheikh juma Poli

    Kutana na daktari wa kiroho

    Ni muasisi wa Jasuta

    Kazi yangu Kubwa

    ya msingi iliKuwa ni Kufudisha na Kulea

    vijana KatiKa mfumo

    sahihi wa mafundisho ya uislamu.

  • hutolewa na kuchapishwathe islamic Foundation, p.o. Box 6011 Morogoro, tanzania, e-mail: [email protected]

    Mhariri Mtendaji: 0715 559 944, Mhariri: 0786 779 669, aFisa Masoko: 0785 500 502toVuti: www.islamicftz.org

    8 rajab 1436, juMatatu aprili 27 - Mei 3 , 2015

    tahariri / uchaMBuzi6

    Moja kati ya habari zilizochapishwa katika toleo hili la gazeti la Imaan ni ile inayozungumzia maandalizi ya Hijja, ambapo Waislamu huko Zanzibar wametakiwa ku-jiandaa mapema kwa safari hiyo ya kutekeleza moja kati ya ngu-zo tano za Uislamu.

    Kwa kukumbushana tu, Uis-lamu umejengwa juu ya nguzo tano. Nazo ni Kushuhudia kuwa

    hapana Mola apasaye kuabudi-wa kwa haki ila Mwenyezi Mungu mmoja, Allah, kusi-mamisha swala tano za fardhi, kutoa zaka, kufunga mwezi Mtukufu wa Ramadhani na Hi-jja kwa mwenye kuwezeshwa na Allah.

    Imeelezwa kuwa Serikali ya Saudi Arabia imebadilisha tara-tibu za safari hiyo kufuatia ma-hujaji mara kwa mara kulalami-kia vitendo vya udanganyifu

    wanavyofanyiwa na baadhi ya taasisi zinazosafirisha mahujaji kutoka mataifa mbali mbali duniani. Kwa sasa, imeelezwa, taasisi zinazosafirisha mahujaji zinatakiwa kufanya taratibu zote za maandalizi ya safari, makazi na matembezi kwa njia ya mtandao na kulipa gharama zote wakiwa nchini mwao.

    Kufahamishwa haya kwa mahujaji wa Zanzibar, ndio pia kujulishwa kwa Waislamu wa

    nchi nzima. Kwa hiyo yafaa Waislamu wote, hususan wale ambao miongoni mwetu tume-tia nia ya kutekeleza ibada hii ya kipekee tujiandae mapema.

    Hatua hii ya Saudi Arabia in-alenga kutusaidia sisi mahujaji watarajiwa. Lakini ili tuweze kufaidika kwa hatua hii ni muhimu nasi tujisaidie kwa kutekeleza wajibu wetu ambao ni kujiandaa mapema.

    Kwa mujibu wa serikali ya

    Saudia mwisho wa kukamilisha taratibu za mahujaji (kwa msimu wa hijja, mwaka huu 1436 hijriyyah) ni tarehe 27 mwezi Juni na baada ya tarehe hiyo mtandao huo utafungwa.

    Shime Waislamu ambao tu-mewezeshwa na Allah tuji-tokeze kuchukua nafasi hizi 3,000 tulizotengewa na Serikali ya Saudi Arabia ili tukaitikie wito wa Muumba wetu, Allah Subhaanahu Wataala.

    waislamu tujipange mapema msimu wa hijja 1436

    Mwenyenzi Mungu al-ipomuumba Adam (Amani iwejuuyake) alimfundisha majina ya vitu vyote, ambayo ni lugha. Hii ilimpa Adam nafasi maalum kiasi kwamba Malaika wote walimsuju-dia.

    Katika sehemu nyingine ndani ya Quran Tukufu, imesemwa kati-ka Ayatul Qursiy (2:225) kwamba huwezi kufanikisha kupata elimu bila ruhusa (kibali) cha Allah.

    Allah anasema: Mwenyezi Mungu hapana Mungu ila Yeye Aliyehai, Msimamia mambo yote milele. Hashikwi na usingizi wala kulala. Ni vyake pekee vyote vilivy-omo mbinguni na duniani. Ni nani huyo awezaye kuombea mbele yake bila ya idhini yake? Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao; wala wao hawajui chochote katika viliopo katika ujuzi wake, ila kwa atakalo mwenyewe. Enzi yake imetanda mbinguni na duniani, na wala haemewi na kuvilinda hivyo. Na Yeye ndiye aliye juu, na ndiye

    Mkuu. (2:225). Elimu husambaa kupitia lugha. Nabii Musa alipo-tumwa kwa Firauni aliomba apewe ufasaha ili watu wapate kufahamu maneno yake:

    Na ulifungue fundo lililo katika

    ulimi wangu, Wapate kufahamu maneno yangu (20: 27 28). Kwa mara nyingine tena, umuhimu wa lugha unasisitizwa.

    Katika hadith ya Mtume (Reh-ma na amani ziwe juu yake); nifik-

    ishie walau aya moja (Sahih Al Bukhar). Unaweza kufikisha vipi kama hujui lugha?

    Mpenzi msomaji, ukweli ni kwamba katika miongo ijayo, yule ambaye anatawala lugha ndie atatawala dunia. Hata sasa mataifa yanayotawala yamechukua hatua kubwa katika kueneza lugha ya Ki-ingereza, ambayo ndio njia ya kuenezea fikra na nguvu zao.

    Kwa mujibu wa makadirio, kuna zaidi ya taasisi 70,000 zina-zojihusisha na kufasiri katika ul-imwengu wa nchi za Magharibi, wakati katika umma wa Kiislamu taasisi hizo zinahesabika.

    Tunawezaje kufidia huu upun-gufu? Hatua gani zichukuliwe? Na kwa hatua hizo tutakazochukua

    faida zake ni nini? Jawabu ni kwamba, kama am-

    bavyo tumetumia nguvu zetu ny-ingi kujifunza kiingereza na sayan-si na teknolojia, sasa yapaswa tu-weke mkazo wa sera za elimu kati-ka ufasiri wa Quran tukufu katika lugha zote kuu za dunia.

    Hatua hii si tu kwamba itatoa faida ya kisiasa na kiuchumi, lakini itatuwezesha kufikisha ujumbe wa Quran na Sunnah. Ni kupitia lugha pekee tunaweza kuwasil-iana, hivyo basi kuna haja kubwa ya kutengeneza walimu na kuwa na wanafunzi wakutosha katika ngazi zote, kuanzia msingi na kuendelea.

    Mwisho, napenda kutoa rai kwa viongozi walete mabadiliko makubwa katika sera zetu za elimu, ziweke msisitizo katika ku-jifunza lugha mbalimbali, kwani nawahakikishia kwa mara ny-ingine, tukijifunza na kutawala lugha basi umma wa Kiislamu utatawala dunia, Insha Allah. Al-lah anajua zaidi.

    umma wa kiislamu ujifunze lugha mbalimbali

    Elimu husambaa kupitia lugha. Nabii musa alipotumwa kwa FirauNi

    aliomba apEwE uFasaha ili watu wapatE kuFahamu maNENo yakE:

    MohaMMad khan

    nasaha za wiki

  • www.islamicftz.org

    8 Rajab 1436, jumatatu aprili 27 - mei 3 , 2015

    7

    Mambo ya msingi kwa Khatwibu wa Ijumaa

    Kwanza, yampasa khatwi-bu wa khutba ya Ijumaa achague mada mapema mwanzo wa wiki, kwani kuchelewa kuchagua mada humfan-ya akose muda wa kutosha wa ku-jiandaa na hivyo aamue kukhutubu mada yoyote ile atakayoiona rahisi kwake kuifikisha na hata kurudia mada aliyokwishaitoa huko nyuma.

    Kufanya hivyo hupelekea mada yake isisheheni yapasayo kuambiwa waumini siku ya Ijumaa au wakati mwingine kushindwa kuzungumzia tukio ambalo khutba lilipaswa kuli-zungumzia na kulitolea muongozo kwa wiki hiyo.

    Iwapo khatwibu atachagua mada mapema atapata muda wa kufanya rejea katika vitabu mbali mbali na kukusanya hakika za matukio katika jamii ambayo yanaingia katika mada yake ili aihudhurishe kwa wasikilizaji ikiwa inakwenda na wakati walion-ao.

    Pili, mada iwe huru na isiwe kwa shinikizo la mtu au kikundi fulani na wala isitokane na mihemko katika

    mitaa au tukio fulani. Matukio yawe sehemu tu ya ufafanuzi na mifano ndani ya khutba, lakini khutba yenyewe ijikite kufikisha aya au ha-dith fulani kwa lengo la kuongoza watu.

    Tatu, mada zibadilike zikigusa nyanja mbali mbali za maisha ya watu na zisijikite katika sekta moja ya maisha. Uislamu ni mfumo kamili wa maisha na kwa hiyo inatakikana khutba za ijumaa ziguse matatizo na changamoto zinazoikabili jamii ya Waislamu eneo husika au nchi husi-ka na jinsi ya kutatua matatizo hayo au kukabiliana na changamoto hizo.

    Khutba zielezee hali ya ummah kiimani, kimaadili, kiuchumi, kisia-sa, kielimu - makosa ya kitawhiid, matendo maovu tuyatendayo, njama za maadui wa Uislamu, kubainisha wanayoyahitaji watu kuhusu huku-mu za kishariah na ibada mbali mbali, kuwaandaa watu kwa siku ya mwisho na kadhalika.

    Khutba inaweza kuwa karipio, nasaha, mawaidha, mwongozo, ufa-

    fanuzi, fatwa, maelekezo, kuhimiza juu ya jambo fulani, ukumbusho, taalimu juu ya jambo fulani na men-gineyo.

    Kuna wakati unakuta khatwibu ameelekeza khutba zake zote upande mmoja tu - mawaidha na ukum-busho. Kifupi ni kwamba khutba zisheheni kila analolihitaji Muislamu katika maisha yake ya dunia na akhera.

    Ni makosa kwa khatwibu kuege-mea upande mmoja wa maisha ya Muislamu. Kwa mfano khutba juu ya masuala ya siasa pekee. Hii ni kwa sababu kuna watu hawana fursa ya kwenda madrasa kusoma na khutba za ijumaa kwao ndiyo fursa ya kuso-ma.

    Nne, kuhudhurisha mada vizuri ikiwa ni pamoja na kusoma aya za Quran na hadith za Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) vizuri kwa kiarabu kisha kuzitafsiri kwa kiswa-hili ili watu wafahamu. Si vizuri kwa makhatibu kusoma aya na hadith kwa kiarabu pasina kuzifasiri.

    Yampasa khatwibu afanye bahthi (uchunguzi) kuangalia vitabu vi-nasemaje, na pia atafute maarifa ya sasa ya kidunia yanasema nini. Khat-wibu apangilie khutba yake kwa kuandika katika karatasi ili aitoe kwa mtiririko mzuri.

    Mimbari ni amana na waswaliji wanasubiri wasikie mapya kutoka kwa khatwibu kila wiki. Hata awe ni msomi wa daraja gani, khatwibu hawezi kuepuka kufanya muraaa (kupitia vitabu) na kujiandaa kwa khutba kwa kuandika na kupangilia vizuri.

    Katika dhulma ya khatwibu ku-wadhulumu waswaliji na kuvunja amana ya mimbari, ni kutokujiandaa kwake na khutba ipasavyo na kuan-daa mada akiwa amechelewa na kuja msikitini mbio mbio pasina maan-dalizi.

    Tano, mada ya khutba iwe kuhusu yanayotokea sasa. Ulimwengu wa Kiislamu unapita katika matukio na changamoto nyingi. Akili ya Muisla-mu inahitaji kupatiwa maelezo na

    ufumbuzi wa matatizo mbali mbali.Waislamu wanahitaji kupatiwa

    maelezo juu ya yale wanayoyaona na kuyasikia katika vyombo vya habari kuhusu dini yao nchini na duniani kote ili kuwajengea ufahamu mmo-ja.

    Makhatwibu waelewe kwamba waswaliji wanasubiri kusikia ukweli kutoka katika khutba na ufafanuzi wa matukio kutoka kwa khatwibu ambaye wanamuamini kwa ayase-mayo kwa jina la Allah na anajua kwamba mimbari ni amana na anatekeleza wajibu wake kwa umma.

    Khatwibu aelewe kwamba kuna kundi la Waislamu hawajihusishi na matukio mbali mbali yanayouhusu umma na wala hawajali. Kundi hili linahitaji kuzinduliwa ili wajue nini kinaendelea katika kadhia za Wais-lamu. Mtu wa karibu nao zaidi am-baye watu hawa wanaweza kumtege-mea ni khatwibu wa ijumaa.

    Itaendelea toleo lijalo

    mpaka tutakapofaidika na Khutba za Ijumaa - 3

    Na sheIKh tawaKKal juma

    KutoKa KatIKa QuRaN Na suNNah

    Quran ni kitabu pekee ambacho k inapo -somwa huingiza hisia katika moyo wa mso-maji na wasikilizaji. Katika moja kati ya mashindano ya kimataifa ya kuhifadhi Quran yaliyofanyika Dubai kijana mdogo wa Kisomali kutoka Kenya alisababisha uku-m b i m z i m a urindime kwa vilio kutoka-na na uso-maji wake.

    Ni mtoto a m b a y e h a k u w a a n a j u a h a t a m a a n a ya neno moja la lugha ya kiarabu, l a k i n i

    alikuwa anapofikia katika aya zi-nazozungumzia adhabu akijikuta akilia pasina kujiliza au kudan-ganya kujiliza, jambo lilowafanya watu wengi wahisi ukubwa na utukufu wa Quran.

    Waislamu wanaamini kitabu hiki, hususan lugha yake, ni muu-jiza. Kwa upande mwingine hebu tuangalie walau kidogo kauli

    kuhusu Quran za wasiokuwa Waislamu na ambao walis-

    ilimu baada y a kuiso-

    ma Quran. Saifuddin Dirk Walter Mosig

    wa Marekani anasema: Nimeso-ma vitabu vitukufu vya kila dini, hakuna pahala nilipokuta mfano wa kile nilichokikuta katika Uisla-mu yaani Ukamilifu. Nikilingani-sha Quran na vitabu vingine nilivyosoma ni kama mwanga wa jua ulinganishe na mwanga wa njiti ya kibiriti. Naamini pasina shaka kila asomaye neno la Allah, (Quran) kwa moyo ambao hau-jafungwa kukubali haki, ni lazima atakuwa Mwislamu.

    Saifuddin ni msomi daktari wa falsafa, mwanasaikolojia, mwana-historia na mchambuzi wa vitabu

    aliyezaliwa Ujerumani na kui-shi miaka kadhaa Ajentina kabla hajahamia Marekani.

    Nakubaliana na msomi huyu na hii ndiyo sababu baadhi ya dini huwakataza wafuasi wao kuisoma Quran kwani wanajua fika kuwa atakayeisoma mwishowe laz-

    ima atasilimu. Msomi mwingine, Ali Selman

    Benoist, daktari Mfaransa anase-ma: Kitu kikubwa kabisa na muhimu sana kilichonifanya nisil-imu ni Quran. Nilianza kuisoma kabla ya kusilimu nikiwa na moyo halisi wa kisomi wa Kimagharibi wa kutafiti na kuchunguza mam-bo. Kuna baadhi ya aya za kitabu hiki (Quran) zikiwa zimeterem-shwa zaidi ya karne kumi na nne zilizopita miaka (1400) ambazo zinafundisha kile kile kinacho-fundishwa katika utafiti wa kisasa kabisa wa kisayansi. Hili lilinifan-ya nisilimu.

    Naye Gohann Wolfgang von Goethe, mwandishi na mwanadi-plomasia wa Kijerumani anasema: Kila mara nyingi tunapoigeukia (Quran) mwanzo huwa ikituudhi kila tunapoianza, mara mapema tu huanza kutuvutia, kutushanga-za na mwishowe hutupelekea kui-heshimuMtindo wake ni wa kipekee ukiendana na yaliyomo

    ndani yake na lengo lake ambalo ni kali, la kale, la kutisha, lakini hara-ka mno huamsha hisia za ndani. Kwa hiyo ni dhahiri kuwa kitabu hichi kina athari kubwa katika kila zama na kila nyakati.

    Kwa upande wake, msomi mwingine mkubwa G. Margo-liouth anasema:Quran kwa haki-ka inachukua nafasi muhimu miongoni mwa vitabu vikubwa vya dini za ulimwenguni. Pamoja na kuwa ndio cha mwisho kushuka katika daraja la vitabu vya aina hii, hakifikiwi na (kitabu) chochote kingine kwa upande wa athari ya ajabu kwa makundi ya watu.

    Anaendelea: Quran imeten-geneza awamu mpya na kamili ya fikra na tabia za mwanadamu. Kwanza imebadili makabila mbalimbali ya watu nchi za ma-jangwa katika ghuba ya Arabuni wakawa taifa la mashujaa na kisha ikaendelea kuunda taasisi kubwa ya kidini na siasa ya ulimwengu ambayo ni nguvu moja kubwa inayopaswa kutambuliwa na Ulaya na nchi za Mashariki.

    Itaendelea.

    waliosilimu baada ya kuisoma Quran

    Waislamu Wanaamini kitabu hiki, hususan lugha yake, ni muujiza. kWa

    upande mWingine hebu tuangalie Walau kidogo kauli kuhusu Quran

    kWa WasiokuWa Waislamu baada ya kuisoma Quran.

    Na sheikh muhammad Duwaysh

    mlINgaNIajI

  • www.islamicftz.org

    8 Rajab 1436, jumatatu aprili 27 - mei 3 , 2015

    8 www.islamicftz.org8 Rajab 1436, jumatatu aprili 27 - mei 3 , 2015

    9

    Na MwaNdishi wetu

    Alhamdulillahi, tuko ndani ya mwezi wa Rajab, moja kati-ka miezi mitakatifu aliyotu-julisha Allah (Subhaanahuu wa Taala) katika Surat At-Tawbah: 36 Hakika idadi ya miezi katika Ilmu ya Allah ni miezi kumi na miwili tangu siku aloumba mbingu na ardhi; katika hiyo minne ni mitakatifu, hiyo ndiyo dini ya sawa kwa hiyo msizidhulumu nafsi zenu ndani yake (miezi hiyo).

    Kuna tofauti kati ya mwezi mtakati-fu na mwezi mtukufu. Ramadhani ni mwezi Mtukufu lakini si Mtakatifu. Utakatifu ni wa Allah pekee na ana-pokiita kitu kitakatifu basi amekituku-za sana kitu hicho. Ni kwa nini miezi hii minne ni mitakatifu hatukujulishwa si katika Quran wala Sunnah.

    Miezi hii ni kwa mujibu wa mianda-mo ya Kiislamu iliyoegemezwa kwenye mwenendo wa mwezi na si jua kama zilivyo kalenda za kikafiri. Katika Quran hatukutajiwa majina ya miezi hii.Majina hayo yametajwa katika Sun-nah. Imesimuliwa na Abu Bakrah (Al-lah amridhie) kwamba Mtume (Reh-ma na amani ziwe juu yake) alitoa khutba yake ya kuaga akasema;

    Zama zimekamilisha mzunguko wake na imekuwa kama ilivyokuwa siku Allah alipoumba mbingu na ar-dhi. Mwaka una miezi kumi na miwili na katika hiyo minne ni mitakatifu, mi-tatu imefuatana-Dhul Qaadhah, Dhul Hijja na Muharram- na Rajab Mud-harr ulio kati ya Jumaada (aakhir) na Shaaban (Bukharin a Muslim).

    Mwezi wa Rajab ndio huu tulionao hivi sasa na umeitwa Rajab Mudharr yasemekana kwa sababu watu wa ka-bila la Mudharr katika Maqureysh wa-likuwa wakiutukuza sana tofauti na makabila mengine. Zama za jaahili-yyah, mwezi wa Rajab ukiitwa pia Mu-nassil al-Asinnah yaani wenye kusaba-bisha ncha za silaha kuondolewa.

    Abu Rajaa al-Ataaridi (Allah awe radhi nae) amenukuliwa akisema ulipofika mwezi wa Rajab, tulikuwa tukisema Munassil al-Asinnah na tu-likuwa hatuachi mkuki au mshale wowote uliokuwa na kipande cha chu-ma ila tuliondoa kichwa chake cha chuma na kukitupa wakati wa mwezi wa Rajab (Bukhari).

    Naam, mwezi wa Rajab ni mwezi mtakatifu na kama ilivyo miezi mi-takatifu, waumini tunakatazwa kuiv-unjia heshima iliyopewa na Allah. Al-lah (Subhaana huu wa Taala) anasema Enyi mlioamini, msivunje utukufu wa alama za Allah wala miezi mitakatifu(Maidah - 2).

    Kwa hiyo tujihimu kuitukuza miezi hii mitakatifu kwa sababu Allah (Sub-haanahuuw a Taala) ameiteua kwa kuipa hadhi maalum na katuusia kuto-kuzidhulumu nafsi zetu kwa kutenda maasi ndani yake ambalo ni kosa kubwa sana mbele ya Allah ingawa ku-

    Na aBuu MaYsaRa

    Katika sehemu ya kwanza, tuliona jinsi Wareno nchini Msumbiji walivy-ojenga khofu dhidi ya Uislamu na hata kuchukua hatua za kufunga misikiti na madrasa zao na baadae waligundua hili lisingeuzuia Uislamu kushamiri nchini humo.

    Wakaamua kuwadhibiti Waisla-mu kwa kuanzisha ukaribu nao hata kuanzisha programu maalum za ku-saidia kukarabati misikiti na madra-sa zao vilivyoachwa kama magofu. Mfuko Maalum wa Ureno kwa ajili ya Waislamu (Portugues Muslim Fund) ulianzishwa kufadhili miradi mbali mbali ya Waislamu.

    Hatimaye kikaja kipindi cha wa-pigania uhuru wa Msumbiji kuanzi-sha mapambano ya silaha dhidi ya utawala wa Wareno. Katika kipindi hiki, mikakati ya Wareno dhidi ya Waislamu ikabadilika.

    Harakati za mapambano dhidi ya Wareno zilishaanza kama tu-livyoona. Inaaminika kwamba wan-amgambo wa kimakua waliunda kilichoitwa Brotherhood of Muslim Makuas. Pia kaskazini mwa Msumbiji, Waislamu waliunda ju-muiya zao katika wilaya zote nne.

    Makundi yote haya yalisambara-tishwa kinyama na Wareno mwaka 1954-55, ingawa wenyewe Wareno hukanusha habari hizi. Unyama wa Wareno dhidi ya Waislamu hauku-zuia harakati za wapigania uhuru kuendelea na kuimarika.

    Kwa akili ya kawaida, huku wakikabiliwa na harakati za wapiga-nia uhuru zilizojumuisha makundi mbali mbali ya kijamii ya wanam-sumbiji, Wareno waliamua ku-waghilibu Waislamu wawe upande wao kupambana na nguvu ya Freli-mo. Na hiki ndicho kiini cha mada yetu.

    Je, ilikuwaje viongozi wa Waisla-mu wa Msumbiji kukubali kutumi-ka na Wareno dhidi ya wapigania uhuru wa Frelimo wakati ukoloni ulikuwa ni madhila kwao kama ili-vyokuwa kwa wananchi wengine wa Msumbiji ? Je, Waislamu wali-faidikaje au walipata hasara zipi kutokana na ushirika huu baina yao na Wareno?

    Kwa upande mwingine, wakati mapambano ya kudai uhuru yanaanza nchini Msumbiji, tayari Wareno walikuwa wanapambana na harakati za wapigania uhuru ka-tika makoloni yake mengine barani Africa.

    Mfano mzuri ni Guinea Bissau, ambako Wareno kwa kutumia ka-nuni ya wakati wa mapambano punguza maadui, waliwaorodhesha Waislamu wahafidhina katika kabila la Fula dhidi ya harakati za wapiga-nia uhuru. Huu ukawa mfano kwa mashirika yake ya kijasusi juu ya nini cha kufanywa katika makoloni men-gine yenye Waislamu kama Msumb-iji.

    Kwa hiyo, kuanzia katikati ya mi-

    Rajab, mwezi mtakatifu

    Rajab, mwezi mtakatifu

    makala maalum

    aka 1950, Uislamu ukaanza kuta-zamwa na Wareno kwa jicho jin-gine kabisa huku Adriano Moreira, ambaye alikuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi Jamii na Siasa za Kimataifa (Instituto superior de cincias sociais e poltica) akisisitiza umuhimu wa kudhibiti kuenea kwa kasi kwa Uislamu kaskazini mwa Msumbiji.

    Akihutubia katika chuo cha kijeshi kiitwacho Instituto de Altos Estudos Militares, Moreira, ali-himiza shughuli za wamishionari Wakatoliki katika eneo la Wama-konde ambao wengi wao walikuwa wameukwepa Uislamu na kubakia wapagani.

    Wareno walitekeleza sera yao ya siasa ya utangamano (politics of in-tegration) kinyume na ile ya Wa-faransa iliyojulikana kama siasa ya

    kumeza (politics of assimilation). Sera ya Ufaransa iliyotekelezwa Tu-nisia, Morocco, Mali na Ivory Coast ililenga kuhakikisha mila na desturi za Kiislamu hazitofautiani na zile za Kifaransa.

    Mwishoni mwa mhadhara wake siku hiyo, Bwana Moreira alishauri kwamba paundwe alichokiita kikosi cha utafiti cha ushawishi wa Waislamu Waarabu katika ma-koloni ya Ureno ili kufuatilia kwa karibu kuenea kwa Uislamu, kungamua kiwango cha mwamko wao kisiasa na kushauri mikakati inayostahiki kulinda maslahi ya koloni la Wareno dhidi ya Uislamu.

    Kutekeleza ushauri wa Moreira, Wareno mnamo mwaka 1960 wakaunda kikosi kazi kushughuli-kia Uislamu na Waislamu katika makoloni yake walichokiita Jumui-

    ya ya Jiografia ya Lisbon (Sociedade de Geografia de Lisboa).

    Ukiliangalia jina la kikosi kazi hiki huwezi kujua nini undani wa kazi au malengo yake. Hizi ndiyo mbinu za maadui wa Uislamu zilivyo. Hutoa majina yasiyoashiria malengo yao kuuzuga umma. Kufi-kia mwaka 1965, wigo mpana wa sera za wakoloni dhidi ya Uislamu ulikuwa umeshabadilika mno.

    Mwaka huo 1965, tawi la Shirika la Ujasusi la Wareno (Servios de Centralizao e Coordenao de In-formaes) kwa Msumbiji lilisam-baza maandiko yaitwayo Kuzishin-da nyoyo za waumini katika jamii.

    Andiko hili liliainisha mikakati ya kuzitawala nyoyo na akili za makundi mbali mbali ya jamii nch-ini Msumbiji likiwemo kundi jamii la Waislamu ili makundi haya yasi-unge mkono harakati za ukombozi wa Msumbiji zilizoongozwa na Fre-limo.

    Mfano, mwandishi alishauri kwamba Waafrika wanapenda sana ushawishi wa manabii kwa sababu akili zao zimetawaliwa na imani za mambo ya kufikirika. Ili kuikabili hali hii, ilishauriwa kwamba Serikali iwavute karibu vi-ongozi wa dini. Sehemu ya andiko hilo ilisomeka hivi:

    Mtazamo mpana kwa upande wa Serikali unawezekana kwa ajili ya kupata ushirikiano wao (viongo-zi wa dini) kama silaha muhimu ya mapambano dhidi ya vitendo vya kiuasi vinavyofanywa na baadhi ya wanadini ambao wanakuwa na mi-tazamo isiyo mizuri kwa maslahi ya taifa. Na pale vikundi kama hivyo (vya viongozi vibaraka) vinapoko-sekana, si vigumu kuvitengeneza na kuviingiza katika mioyo ya watu.

    Hatua iliyofuata kwa Wareno ni kukusanya taarifa za kutosha kuhu-su Waislamu nchini Msumbiji ili kuwezesha SCCIM na intelijensia ya jeshi kuchukua hatua muafaka dhidi yao.

    Kwa hiyo mwaka 1965, SCCIM ikaanda dodoso kuhusu Uislamu. Ilielekezwa kuwa maswali dodoso yajibiwe na viongozi wa Kiislamu wenye hadhi au ufahamu fulani kuhusu jamii yao. Wasimamizi wal-ionywa wasifanye vitendo vyovyote vile vitakavyowashtua Waislamu kuhusu lengo la dodoso hilo.

    Dodoso hilo liligawika sehemu nne zenye jumla ya maswali 28, mengi yakiambatana na namna ya ufuatiliaji wa watendaji kwa maja-wabu yatakayotolewa. Karatasi maalum iliandaliwa kwa ajili hiyo.

    Muundo wa maneno ya dodoso ulionesha kwamba waandaji wali-jua tofauti mbali mbali za kiaqida, kifiqh na kijamii zilizoko katika jamii ya Waislamu na waliuliza tu kupata undani kutoka kwa kila mlengwa.

    Muundo mzima wa zoezi hili ul-ilenga kuzielewa jamii za Waislamu nchini Msumbiji kwa kina kuanzia nini wanachokifanya misikitini, madrasa na katika mijumuiko yao, lugha itumikayo na uongozi wao unavyotambulika.

    Fuatana na mwandishi toleo lijalo kupata sehemu ya mwisho ya makala haya.

    Kwa aKili ya Kawaida, huKu waKiKabiliwa na haraKati za

    wapigania uhuru zilizojumuisha maKundi mbali mbali ya Kijamii

    ya wanamsumbiji, wareno waliamua Kuwaghilibu

    waislamu wawe upande wao Kupambana na nguvu ya Frelimo.

    Waislamu walivyotumika - 2tenda maasi muda wote ni dhambi lakini maasi katika miezi mitakatifu ni dhambi kubwa zaidi kutokana na utakatifu wake.

    Katika yaliyokatazwa ku-tendwa katika miezi mitakati-fu ni kupigana. Allah (Sub-haanahuu wa Taala) anasema Na wanakuuliza kupigana vita katka miezi mitakatifu, waambie (ee Muhammad) kupigana ndani yake ni (dhambi) kubwa (Al Baqa-rah: 217).

    Baadhi ya wanawazuoni wanasema katazo la kupigana vita ndani ya miezi mitakatifu ni mansuukh (lilifutwa) kwa aya ya 194 Suurat Al Baqarah Allah aliposema Miezi mi-takatifu kwa miezi mitakatifu na vilivyo vitukufu Qisasi, basi atakayechupa mipaka juu lenu nanyi chupeni mipaka dhidi yake, na mcheni Allah na jueni Allah yu pamoja na wachaMungu.

    Wengine wanasema, hau-ruhusiwi kuanzisha vita ndani ya miezi mitakatifu, lakini in-aruhusiwa kuendelea na vita iwapo vita ilianza nje ya miezi mitakatifu. Kwa hiyo iwapo Waislamu watashambuliwa na adui katika miezi mitakati-fu, wataruhusiwa kupigana kujilinda. Hawawezi kuacha kupigana eti kwa kuwa ni mie-zi mitakatifu.

    Dua ya Kuomba Mwanzo wa Rajab: Na katika yaliy-okithiri kuhusu mwezi wa Ra-jab ni watu kuomba kwa dua hii Allwaahumma baarik lanaa fiy Rajab wa shaa-b a a n , w a b a l -lighnaa Ram-adhwaan. Hii ni dua ili-

    yopokewa na Imam Ahmad. Lakini Sheikh Al Albaaniy ka-tika maelezo juu ya hadith hii anasema ni dhaifu. (Tazama Taliyq ya Al Baniy ya al-Mishkaat, Mujalada wa 1, uk. 306, hadithi ya 16).

    Funga katika mwezi wa Rajab:hakuna upokezi sahihi kutoka kwa Mtume wa Allah au kutoka kwa swahaba yeyo-te kuashiria kwamba kuna funga maalum ya mwezi huu wa Rajab. Funga katika mwezi wa Rajab ni funga za sunnah za kawaida kama vile ju-matatu na alhamisi, sunnah ya nabii Dawuud (alayhi sa-laam) na masiku meupe kama ilivyo katika miezi mingine yote.

    Amesimulia hadithi Imam Ahmad (Allah amrahamu) kutoka kwa Abii Bakrah kwamba Umar (Allah amridhie) alikuwa akipiga miko-n o

    ya waliofunga swaumu mwezi wa Rajab mpaka wachukue chakula na akisema, huu ni mwezi ulioabudiwa zama za Ujaahili. (Tazama Al Mugh-niy ya Ibn Qudamah Mjalada 3, uk. 167 na Sharh al-Kabiyr Mjalada wa 2 uk. 52).

    Na ametaja Shaykhul Is-laam Ibn Taymiyyah (Allah amrahamu) Kuadhimisha mwezi wa Rajab ni katika mambo ya uzushi ambayo yat-akikana kujiepusha nayo (Tazama Iqtidhwaau as-swiraatwal mustaqiym, mjala-da wa 2 uk. 624-625).

    Nae Imam Ibnul Qayyim al-Jawziyyah amesema, Mtume (rehma na amani ziwe juu yake) hakupata ku-funga swaumu miezi mitatu mfululizo-Rajab, Shaaban na

    Ramadhan-kama wafan-yavyo baadhi ya watu, na

    hakufunga mwezi wa Rajab kabi-

    s a

    na wala hakuwahimiza watu kufunga mwezi huu (Rajab) kama alivyopokea Ibn Majah (Tazama Zaad al-Maad, Mjalada wa 2, uk. 64).

    Kwa kusema haya hatum-katazi mtu kufunga swaumu zake za sunnah lakini asiseme kwamba kufanya hivi kaamri-sha Mjumbe wa Allah (rehma na amani ziwe juu yake) au ku-fanya hivyo kuna fadhila ma-khsusi kwa mwenye kufunga mwezi wa Rajab.

    Umrah mwezi wa Rajab: Hadith nyingi zinabainisha kwamba Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) haku-fanya Umrah ndani ya mwezi wa Rajab kama ilivy-o p o k e l e w a n a Um m u l Muminiyna Aisha (Radhi za Allah ziwe juu yake) Allah amrahamu Abu Abd al-Rah-maan, Mtume kamwe haku-fanya Umrah katika mwezi wa Rajab (Bukhari n a Muslim).

    Lakini kama mtu ataenda Umrah ndani ya mwezi wa Rajab pasina kuamini

    kwamba kufanya hivyo kuna fadhi-

    la fulani ma-khsusi na

    kwamba imetokezea ndio muda alioona ni fursa kwake kufanya hivyo, hapo hakuna ubaya kufan-ya hivyo.

    Baadhi ya Bida katika mwezi wa Rajab: miongoni mwa bida zinazofanywa na Waislamu nda-ni ya mwezi wa Rajab ni Swalaatu al-Raghaaib. Swala hii ilienea sana mnamo karne ya nne hijri-yyah. Swala hii huswaliwa usiku wa ijumaa ya kwanza ya mwezi Rajab. Shaykhul Islaam Ibn Taymiyyah (Allah amrahamu) anasema, Swalaat al-Raghaab ni bida kwa mujibu wa ijmaa ya wanawazuoni wa dini kama vile Maalik, Shaafii, Abu Hanifah, At-Thawriy, Al-Awzaaiy, Al-Laythiy na wengine. Hadith inay-osemwa kuhusu swala hii ni uzushi kwa mujibu wa wanawa-zuoni wa ilmu ya hadithi. (Taza-ma Majmuu Fataawa, mjalada wa 23, uk.132).

    Matukio yanayonasibishwa na Mwezi wa Rajab: Pametajwa ma-tukio kadhaa kuhusu Mtume wa Allah (Rehma na amani ziwe juu yake) kuwa yalitokea ndani ya Rajab lakini hakuna ukweli kuhusu matukio hayo kutokea ndani ya Rajab.

    Miongoni mwa matukio haya ni tukio la Israa na Miraaj. Ili-simuliwa na Al-Qaasim Ibn Mu-hamamd kwamba safari ya Israa ilikuwa usiku wa mwezi 27 Rajab. Usimulizi huu ukapingwa na Ib-rahim al-Harbi na wengine.

    Na kati ya yaliyozushwa ni ki-somo cha Miraaj mwezi 27 Rajab au kuuhuisha usiku huu kwa ma-tendo ya kiibadah na swaumu mchana wake na kufanya sherehe juu lake. Huu ni uzushi na kwa kuzingatia kuwa hakuna ithbaati kwamba Israa na Miraaj vilito-kea mwezi 27 Rajab.

    Na hata kama ingethibiti kuthibiti huko kwamba ilikuwa mwezi 27 Rajab kusingekuwa dalili ya kufanyika yote hayo maadam Mtume wa Allah wala maswahaba wake wala watu wema katika karne njema tatu hawakuyafanya haya.

    Swala ya Ummu Daawuud: Huu nao ni uzushi mwingine wa swala iitwayo swalaat Ummu Daawuud ambayo huswaliwa nusu ya mwezi wa Rajab kama ili-vyo uzushi kwa dua zinazosomwa makhsusi ndani ya mwezi wa Ra-jab na pia kutembelea makaburi siku maalum ndani ya Rajab ni bidah yafaa tujiepushe nazo.

    Twamuomba Allah (Subhaana huu wa Taala) atufanye tuvienzi vitu alivyovifanya vitakatifu na atuwezeshe kushikamana na Sunnah ya Mtume wake (Rehma na amani ziwe juu yake) kwa ku-fuata mwendo wa wema walio-tangulia, kwani Imam Malik ali-pata kusema Kamwe hawato-faulu wa mwisho wa ummah huu ila kwa yale waliyofaulu kwayo wa mwanzo wake (Minhaaj Sun-nah, mjalada wa 2, uk. 444).

    Na mwisho wa dua yetu- Al-

    naam, mwezi wa rajab ni mwezi mtaKatiFu na Kama ilivyo miezi

    mitaKatiFu, waumini tunaKatazwa Kuivunjia heshima iliyopewa na allah. allah (subhaana huu wa taala) anasema enyi mlioamini, msivunje utuKuFu wa alama za allah wala miezi mitaKatiFu

    (maidah - 2).

    Muumini wa dini ya Kiislamu akiwa msikitini mjini Maputo, Msumbiji

    Historia ya MsuMbiji

  • www.islamicftz.org

    8 Rajab 1436, jumatatu aprili 27 - mei 3 , 2015

    10

    Mlango wa udhu - 2

    Kutawadha (Kuchukua udhu)

    Namna ya mwanamke kupaka maji kichwani:

    Swali: Aliulizwa Sheikh Mu-hammad bin Swaleh Al-uthaimin (Allah amrehemu): Je ni Sunnah mwanamke anapopaka maji kichwa chake wakati anatawadha kuanzia kwenye maoteo ya nywele mpaka ki-chogoni kama anavyofanya mwa-naume?

    Jawabu: Naam, kwani asili kati-ka hukumu za kisharia ni kuwa kile kilichothibiti kwa mwanaume kime-thibiti pia kwa mwanamke na kiny-ume chake, isipokuwa kwa dalili. Nami siijui dalili inayomtofautisha mwanamke kwenye hili. Na kwa msingi huu mwanamke atapaka maji kuanzia kwenye maoteo ya nywele hadi kichogoni. Hata zikiwa nywele za singa haitoathiri, kwani aimaani-shi kuziminya nywele kwa nguvu mpaka zitote au aziinuwe hadi utosini. Kinachotakiwa ni kupaka maji polepole.

    Hukumu ya kupaka maji kwenye nywele zilizo-sukwa:

    Swali: Aliulizwa Sheikh Muha-mad bin Swaleh Al-uthaimin (Allah amrehemu): Ni ipi hukumu ya mwa-namke kupaka maji juu ya kilemba cha kichwa?

    Jawabu: Inaruhusiwa kwa mwanamke kupaka maji kwenye kichwa chake, sawa nywele zikiwa fupi au ndefu. Isipokuwa hatakiwi kuzirundika utosini (kufanya mnara), kwani naogopa asije kuingia kwenye neno la Mtume (Rehma na amani ya Allah iwe juu yake): Na wanawake wenye kuvaa wenda uchi, vichwa vyao kama nundu ya ngamia inayoyumba, hawatoingia peponi wala hawatoipata harufu yake, waka-

    ti harufu ya pepo hupatikana umbali kadhaa na kadhaa.

    Kupaka maji juu ya khofu zinazotokana na dhahabu au fedha:

    Swali: Aliulizwa Sheikh Muha-mad bin Ibrahim Alu Sheikh (Allah amrehemu): kuhusu khofu zi-napokuwa za dhahabu au fedha

    Jawabu: Haisihi kwa mwanam-ke au mwanamume kupaka maji kwenye khofu za dhahabu au fedha au vilivyochovywa na viwili hivyo, isipokuwa khofu zilizo na kiasi kido-go cha dhahabu na fedha, kama tut-akavyoeleza kwenye mlango wa vyo-mbo. Wanawake hawakuruhusiwa kutumia dhahabu na fedha isipokuwa kiwango kilichozoeleka kuvaliwa kidesturi, kwa lengo la ku-enziwa na waume zao. Ama zaidi ya hivyo hakuna lazima, na zaidi ya tu-livyoeleza kiasili hukumu yake ni ka-

    tazo. Kwa maana hiyo wanawake ku-vaa dhahabu na fedha ni ruhusa, ama zaidi ya tulivyoeleza hukumu yake ni kutoruhusiwa kuvaa na hata kupaka maji juu yake.(Fat-wa na Rasaailu za Sheikh Mohamad bin Ibrahim 2/67).

    Hukumu ya kupaka maji juu ya ushungi/ukaya:

    Swali: Aliulizwa Sheikh Muha-mad bin Swaleh Uthaimin (Allah amrehemu): Je inajuzu kwa mwan-amke kupaka maji juu ya ukaya wake?

    Jawabu: Kilicho mashuhuri kwenye madhehebu ya Imam Ah-mad, mwanamke anaweza kupaka maji kwenye ukaya wake kama ukaya umezungushwa mpaka kwenye koo, kwani kitendo kama hicho kime-thibiti kwa baadhi ya wanawake wa Kiswahaba (Allah awaridhie). Vyo-vyote iwavyo atapoona usumbufu,

    ima kwa sababu ya hali ya hewa ya baridi au usumbufu wa kuvua na ku-funga tena, si vibaya kupaka maji juu ya ukaya, ama bora nikutopaka. (Fat-wa na Rasaailu za Sheikh Ibn Uthaimin 4/171).

    Kupaka maji kwenye ma-pambo yaliyo kichwani:

    Swali: Aliulizwa Sheikh Moham-ed bin Ibrahim Alu Sheikh (Allah amrehemu): Kuhusu kupaka maji mapambo yaliyo kichwani.

    Jawabu: Hatakiwi kupaka maji mapambo yaliyo kichwani, kwani hayana maana inayolingana na kho-fu.

    Kupaka maji kichwa kilichosingwa mafuta mchanganyiko:

    Swali: Aliulizwa Sheikh Mo-hamed bin Ibrahim Alu Sheikh (Al-

    lah amrehemu) kuhusu kupaka maji kichwa kilichopakwa mchanganyiko wa mafuta mazito.

    Jawabu: Kichwa cha aina hiyo hakitopakwa maji juu yake, kwani hakilingani na khofu si kimaana wala kihisia. Mchanganyiko wa mafuta mazito hupakwa kwa ajili ya anasa, na wala hayapakwi kwa haja au dharura fulani.

    Kupaka maji kwenye ny-wele zilizo na rojo la hina:

    Swali: Aliulizwa Sheikh Mo-hamed bin Swaleh Uthaimin (Allah amrehemu): Mwanamke anapozi-paka hina nywele zake, je atapaka maji kwenye hina?

    Jawabu: Mwanamke atakapok-ipaka hina kichwa chake, atapaka maji kwenye hina, wala halazimiki kufumuwa nywele na kukwangua kilicho kichwani. Imethibiti kuwa Mtume (Rehma na amani ya Allah iwe juu yake) alipohirimia alikuwa amepaka hina kichwani. Hii ina maana kilichoganda kichwani ni se-hemu ya kichwa. Hii inaonyesha kuna unafuu wa aina fulani katika suala la kupaka maji kichwa. (Fat-wa na Rasaailu za Sheikh Muhamad bin Ibrahim 4/147).

    Kupaka maji nywele zilizo na mafuta:

    Swali: Aliulizwa Sheikh Muha-mad bin Swaleh Uthaimin (Allah amrehemu):

    Mwanamke anapokipaka mafuta kichwa chake na kupaka maji juu yake, je udhu wake ni sahihi au la?

    Jawabu: kabla ya kulijibu swali hili, napenda niweke wazi kuwa, Al-lah aliyetukuka amesema kwenye kitabu chake: Enyi mlioamini mnapoinuka ili kutaka kuswali, basi osheni nyuso zenu na mikono yenu mpaka kwenye visukusuku, na pake-ni maji kwenye vichwa vyenu na mu-oshe miguu yenu mpaka vifundoni (5:6).

    fat-wa kwa MwanaMKe wa KiiSlaMNa sheikh shabaNi Mussa

    Dini ya Kiislamu ni mfumo kamili wa maisha, ambayo haikuacha kutoa misingi ya mambo yote muhimu kwa maisha ya binadamu. Kuhusu manufaa ya chakula tunaona misingi yake katika Quran na Sunnah ya Mtume Muhammad (Rehma na amani ziwe juu yake).

    Kwa leo turejee aya zifuatazo: Hebu mwanadamu na atazame chakula chake. Hakika Sisi tumem-imina maji kwa nguvu. Tena tukai-pasuapasua ardhi. Kisha tukaotesha humo chembechembe. Na mizabibu na mboga. Na mizaituni na mitende. Na mabustani, yenye miti iliyosonga-na. Na matunda na malisho, kwa ajili ya kukustarehesheni nyinyi na wan-yama wenu. (80: 24-32).

    Enyi mlioamini kuleni vizuri tu-livyokuruzukuni, na mumshukuru Mwenyezi Mungu, ikiwa mna muabudu yeye peke yake. (2:172).

    Mwenyezi Mungu asingetuhimi-za kula vyakula tena vilivyo bora kama hakuna manufaa. Zaidi ya hayo, Mwenyezi Mungu anataka tufanye utafiti kuhusu vyakula ili tupate yaki-ni ya kuwepo kwake na nguvu zake.

    Chakula kinaweza kutazamwa au kufanyiwa utafiti kwa njia mbalim-bali kama vile kinavyozalishwa kwa kupitia ardhi na maji, aina ya vyakula vinavyozalishwa na ardhi nafaka, matunda, mbogamboga, wanyama, samaki, n.k. Namna chakula kinavy-ojenga au kuharibu afya ya mlaji, ni njia nyingine ya kukiangalia chakula.

    Makala haya yanajikita kujadili manufaa ya chakula katika ujenzi wa afya ya mlaji.

    Manufaa ya kwanza ni kuwa chakula kinakidhi mahitaji ya nishati ya kila siku ya mwili. Ili mtu aweze

    kuswali, kulima, kufikiri vizuri, kutembea, kusoma, kutazama, kusikiliza, ili dawa aliyokunywa ifan-ye kazi mwilini, ni lazima mwili wake upate nishati ya kutosha kutoka kati-ka vyakula anavyokula.

    Pia, nishati zaidi inahitajika ili kumwezesha mtoto tumboni na yule aliyezaliwa kukua vizuri.

    Vyakula vyenye wanga mwingi kama vile wali, ugali, ndizi, viazi, mi-hogo, mikate, chapati na maandazi ni vyanzo vizuri vya nishati mwilini.

    Vyakula hivyo vitumike zaidi ku-liko vyakula vya mafuta na sukari, in-gawa navyo vinaupa mwili nishati. Tunahitaji vyakula vya mafuta lakini viwe kwa kiasi kidogo.

    Manufaa ya pili ya chakula ni kuu-wezesha mwili kukua, kujikarabati na kuponya majeraha. Kati ya umri

    wa mwaka mmoja na umri wa ku-balehe au kuvunjaungo (adoles-cence), motto anakua kwa wasta-ni wa nchi 2.5 kwa mwaka. Ili kukua kwa kiwango hicho mi-fupa na misuli inahitaji chakula chenye protini, wanga, vitamini na madini.

    Kula kila siku vyakula vya protini, madini ya chuma na vi-tamini B ni muhimu sana ili mwili uweze kuwa na damu ya kutosha na kuwe-za kusafirisha virutubisho m u h i m u kutoka se-hemu moja kwenda se-hemu ny-ingine.

    Chakula kinavyonufaisha afya zetuPazi MwiNyiMvua

    afya yaKo

  • Shukran njema anastahiki Allah S u b h a n a h u Wataala na Re-hema na amani zimfikie Mtume wetu Muhammad (Rehma na amani ziwe juu yake), maswahaba zake na wale watakaofuata muon-gozo mpaka siku ya mwisho.

    Ndugu mpenzi mso-maji, katika makala yetu ya leo tutaangaaza juu ya ka-nuni za msingi zinazoon-goza biashara na uchumi wa Kiislamu.

    Biashara na uchumi wa Kiislamu umejengwa kati-ka msingi mama wa kuk-wepa riba. Miamala yote ya kibiashara inatakiwa isi-jihusishe na riba kwa nam-na yoyote ile. Katika Uisla-mu, biashara imehalalish-wa na riba imeharamish-wa.

    Allah anasema: Wale walao riba hawasimami ila kama anavyosimama ali-yezugwa na shetani kwa kumgusa. Hayo ni kwa kuwa wamesema: Bi-ashara ni kama riba. Lakini Mwenyezi Mungu amei-halalisha biashara na ameiharimisha riba. Basi aliyefikiwa na mawaidha kutoka kwa Mola wake Mlezi, kisha akajizuia, basi yake ni yaliyo kwisha pita, na mambo yake yako kwa Mwenyezi Mungu. Na

    wenye kurudia basi hao ndio watu wa motoni, h u m o w a t a d u m u (2:275).

    Kanuni ya msingi ya pili ni Al Gharar. Katika utara-tibu wa kibiashara un-aokubalika katika Uislamu ni kuhakikisha pande zi-nazoshiriki katika biashara kujiepusha na gharar am-bayo inajumuisha hiyana, hadaa, hatari, udanganyifu na ile hali ya kutokuwa na uhakika juu ya ya jambo fulani linalohusu muama-la ambalo huweza kusaba-bisha hasara na dhulma kwa upande mmoja wa washiriki katika biashara.

    Kutokana na kanuni hii, uwazi na utoaji wa taarifa sahihi na kamili juu ya bidhaa, huduma, masharti na vigezo baina ya muuzaji na mnunuzi vinapewa nafasi ya juu sana ili kuhakikisha mua-mala unafanywa katika hali isiyogubikwa na ujin-ga, ambapo pande zote zi-nakuwa na ufahamu na uhakika juu ya muamala wao.

    Swala la udanganyifu limekemewa na kunyimwa nafasi kabisa katika mua-mala, ambapo kila upande unatakiwa kutoa taarifa sahihi na kudumisha uk-weli, uadilifu na uaminifu katika biashara. Aidha, hadaa na upunjaji wa vipi-

    uchumi na biashara JAMAL ISSA

    Watu maarufu WasiokuWa Waislamu wasemavyo kuhusu uislamu

    www.islamicftz.org

    8 Rajab 1436, jumatatu aprili 27 - mei 3 , 2015

    11

    mo umekatazwa katika biashara. Allah anasema katika Quran

    tukufu: Na timizeni vipimo na mizani kwa uadilifu. (6:152), Ole wao hao wapunjao!Ambao wanapojipimia kwa watu hudai watimiziwe.Na wao wanapowapi-mia watu kwa kipimo au mizani hupunguza(83: 1-3).

    Katika aya nyingine Allah anasema: Na kwa watu wa Mady-ana tuliwatumia ndugu yao Shuaib. Akasema: Enyi watu wan-gu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna Mungu ila Yeye, wala msipunguze vipimo na miza-ni. Mimi nakuoneni mmo katika hali njema, nami nakukhofieni ad-habu ya Siku kubwa hiyo itakayo kuzungukeni. Na enyi watu wangu! Timizeni vipimo na mizani kwa uadilifu wala msiwakhini watu vitu vyao; wala msieneze uovu katika nchi mkafanya uharibifu. (11: 85-86).

    Kanuni muhimu ya tatu ni juu ya Al-Qimar na Al-Maisir. Uchumi katika Uislamu umejengwa juu ya

    msingi usiohusisha kamari (mche-zo wa bahati nasibu) kama sehemu ya biashara. Muamala wowote un-aohusisha kamari ambapo upande mmoja unaoshinda utanufaika kwa gharama/hasara ya upande mwingine unaoshindwa haukuba-liki katika Uislamu. Mbali na dhul-ma iliyopo katika kamari, pia kamari husababisha uvivu na uzembe wa kutojishuhulisha katika shuhuli za uzalishaji mali ambazo hujenga uchumi madhubuti na ha-timaye kuwa na wimbi la umaskini na watu tegemezi. Kamari husaba-bisha mtu kupata kipato bila ku-fanya kazi/kutolea jasho, kipato ambacho si halali (Al-Maisir).

    Allah ametuonya katika Quran: Enyi mlio amini! Bila ya shaka ul-evi, na kamari, na kuabudu masan-amu, na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya Shetani. Basi jiepush-eni navyo, ili mpate kufanikiwa.Hakika Shetani anataka kutia kati yenu uadui na chuki kwa ulevi na kamari, na akuzuieni kumkumbu-ka Mwenyezi Mungu na kusali.

    Basi je, mmeacha? (5:90-91). Kanuni ya nne muhimu ni kuji-

    husisha na sekta halisi ya kiuchumi. Mfumo wa kifedha katika Uislamu unatakiwa kuwa na uhusiano au kuambatana na rasilimali. Kwa maana mfumo wa kifedha unatak-iwa kuambatana na shughuli za uzalishaji mali na biashara na sio kuingiza fedha katika mzunguko bila kuzingatia uzalishaji mali na biashara au kuifanya fedha yenyewe kama bidhaa ambapo hubadilish-wa fedha kwa fedha ya aina moja kwa ziada kwa njia mbalimbali haswa mikopo ya riba.

    Mfumo wa kifedha usiojali na kuzingatia wapi fedha zinawekezwa pale zinapotolewa na taasisi za kifedha kwa wateja wake haukuba-liki katika Uislamu. Hivyo utarati-bu wa kifedha wa Kiislamu huzin-gatia fedha kuwekezwa katika sekta halisi ya uchumi na sio katika sekta za anasa, starehe na pumbao am-bazo hazijengi uchumi madhubuti wenye bidhaa na huduma halali. Miamala ya kifedha katika Uisla-mu huambatana na rasilimali am-bazo zitazalisha pato na mali halali.

    Kanuni ya msingi ya tano ni ushirika. Uislamu umesisitiza mfu-mo wa kibiashara wa kushirikiana katika mtaji, kuendesha na kusi-mamia biashara, na kugawana fa-ida na hasara.

    Utaratibu wa baadhi ya watu au taasisi za kifedha kuwapa watu mi-taji kama mikopo kwa riba hauku-baliki kwani hauleti tija zaidi ya un-yonyaji. Utaratibu huu pia hauzin-gatii matokeo ya biashara ambayo fedha hizo zimewekezwa, kwani al-iyekopeshwa kwa namna yoyote ile, hata kama amepata hasara, atalaz-imika kurejesha mkopo na riba. Hivyo mkopeshaji anakuwa ameji-hakikishia manufaa na kukwepa hatari ya kupata hasara.

    Katika utaratibu wa Kiislamu washirika hunufaika kutokana na matokeo ya biashara kwa kugawa-na faida au hasara. Na hii inaendana na dhana nzima ya kusaidiana kwa wema bila kunyonyana jambo am-balo tumeusiwa katika Quran;Na saidianeni katika wema na ucha-mngu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui(5:2).

    Ndugu mpenzi msomaji usiko-se makala ijayo In Sha Allah tutadurusu riba kwa undani. [email protected], +255713996031

    misingi ya Kiislamu ya uchumi na biashara

    Mfanyabiashara akiuza bidhaa sokoni.

    UtaratibU wa baadhi ya watU aU taasisi za kifedha kUwapa watU

    mitaji kama mikopo kwa riba haUkUbaliki kwani

    haUleti tija zaidi ya Unyonyaji.

    NapoleoN BoNaparte:alizaliwa august 15, 1769 naku-wa Generali wa jeshi na mfalme wa kwanza wa ufaransa. Vita vyake maarufu kama vita vya napoleon (napoleonic wars) vili-ubadili ulimwengu. anasema:

    I hope the time is not far off when I shall be able to unite all the wise and educated men of all the countries and estab-lish a uniform regime based on the principles of Quran which

    alone are true and which alone can lead men to happiness

    tafsiri: natumaini wakati hauko mbali pindi nitakapoweza kuunganisha watu wote wenye hekima na elimu wa nchi zote na kuanzisha utawala mmoja unaotokana na kanuni za Quran, kanuni am-bazo peke yake ndiyo za kweli na ambazo peke yake ndizo zinazoweza kuwaongoza watu kwenye furaha (ya kweli).imenukuliwa kutoka: christian cherfils, bonaparte et islam, Pedone Ed, Paris, france, 1914, pp. 105, 125. (original references: correspondance de napolon ier tome V pice n 4287 du 17/07/1799...)

  • www.islamicftz.org

    8 Rajab 1436, jumatatu aprili 27 - mei 3 , 2015

    12 www.islamicftz.org8 Rajab 1436, jumatatu aprili 27 - mei 3 , 2015

    13

    TAASISI YA KHIDMAT ISLAMIYA YENYE UZOEFU WA MIAKA 14 KATIKA SHUGHULI ZA HIJA NA UMRA, INAWATANGAZIA WAISLAM WOTE KUWA GHARAMA YA HIJA KWA MWAKA 2014/ 1435H NI DOLA 4750 TU AMBAZO ZINAWEZA KULIPWA KWA AWAMU (KIDOGO KIDOGO). AIDHA, GHARAMA YA KUFANYIWA IBADA YA HIJA (KUHIJIWA) NI DOLA 1450 TU.

    MALIPO YA HIJA YANAJUMUISHA GHARAMA ZIFUATAZO: NAULI YA NDEGE KWENDA NA KURUDI MALAZI MAKKA, HOTELI YA NYOTA 3*, MWENDO WA KUTEMBEA DAKIKA 7 TU MPAKA MASJID HARAM. MALAZI MADINA, HOTELI YA NYOTA 3* MWENDO WA KUTEMBEA DAKIKA 3 TU MPAKA MASJID NABAWY

    (NI UKWELI USIOFICHIKA KUWA KHIDMAT ISLAMIYA IMEKUWA IKIANDAA NYUMBA ZA MAHUJAJI KARIBU KABISA NA MASJID HARAM NA MASJID NABAWY).

    USAFIRI WA BASI JEDDAH MAKKA, MAKKA MADINA HUDUMA MAALUM (SPECIAL SERVICE) SIKU 5 ZA HIJJA MAHEMA YENYE VIYOYOZI (AIR CONDI TION), MAGODORO, MITO NA BLANKETI CHAKULA MILO MITATU, KUJIHUDUMIA MWENYEWE (BUFFET) CHAI, KAHAWA, JUISI, SODA, MAJI NA VITAFUNWA (SNACKS) VITAPATIKANA MASAA 24, SIKU 5 ZA HIJJA USAFIRI WA BASI KATI YA MAKKA MINA, MINA ARAFAT, ARAFAT MUZDALIFA, MINA MAKKA NGUO (IHRAM) KWA WANAUME NA HIJAB KWA WANAWAKE, GALONI MOJA YA MAJI YA ZAM ZAM (LITA 10) BEGI LA KUSAFIRIA, PAMOJA NA KILO 3 ZA TENDE KWA KILA HUJAJI ZIARA YA MAKKA KUTEMBELEA NYUMBA ALIKOZALIWA MTUME WETU MUHAMMAD (S.A.W), JABAL HIRA, JABAL THAWR, JABAL RAHMA, MASJID JINNI, MASJID KHEIF, MASJID NIMRAH, VIWANJA VYA ARAFAT, MINA, MUZDALIFA NA JAMARAT

    TAASISI YA YENYE UZOEFU

    MALIPO YA HIJA YANAJUMUISHA GHARAMA ZIFUATAZO:

    (NI UKWELI USIOFICHIKA KUWA KHIDMAT ISLAMIYA IMEKUWA IKIANDAA NYUMBA ZA MAHUJAJI KARIBU KABISA NA MASJID HARAM NA MASJID NABAWY).

    TAASISI YA YENYE UZOEFU

    MALIPO YA HIJA YANAJUMUISHA GHARAMA ZIFUATAZO:

    (NI UKWELI USIOFICHIKA KUWA KHIDMAT ISLAMIYA IMEKUWA IKIANDAA NYUMBA ZA MAHUJAJI KARIBU KABISA NA MASJID HARAM NA MASJID NABAWY).

    TAASISI YA YENYE UZOEFU

    MALIPO YA HIJA YANAJUMUISHA GHARAMA ZIFUATAZO:

    (NI UKWELI USIOFICHIKA KUWA KHIDMAT ISLAMIYA IMEKUWA IKIANDAA NYUMBA ZA MAHUJAJI KARIBU KABISA NA MASJID HARAM NA MASJID NABAWY).

    ZIARA YA MADINA KUTEMBELEA MSIKITI

    VILE VILE GHARAMA YA HIJJA INAJUMUI SHA ZIARA YA MADINA KUTEMBELEA MASJID QUBA, MASJID QIBLATAIN, MASJID JUMAA, SABA MASAAJID (MAHALI KULIPO FANYIKA VITA VYA KHANDAQ), NA JABAL UHUD. GHARAMA YA UCHINJAJI WA MNYAMA WA UDHHIYA CHAKULA MILO MITATU KUJIHUDUMIA MWENYEWE (BUFFET) SIKU ZOTE ZA SAFARI.

    SHEIKH HASHIM AHMED RUSAGANYA, SHEIKH JUMA RAJAB IKUSI NA SHEIKH HARUNA JUMANNE KAPAMA WATAKUWEPO NA KUTOA MWONGOZO KWA MAHUJAJI WAKATI WOTE. AL-HAJJ AHMED SALEH NAHDY (HAMAD) AL-HAJJ ZULFIKAR OSMAN (ZULLY) AL HAJJ ALTAF ABDU-LATIF NA AL HAJJ SIDIK VIONGOZI WENYE UZOEFU WA MUDA MREFU PIA WATAKUWEPO KUWAHU-DUMIA MAHUJAJI LENGO NI KUHAKIKISHA KILA HUJAJI ANATEKELEZA IBADA YAKE INAVYOTAKIWA. MADAKTARI DR. HAJI HAMDU NA DR. HAMISA THEREYA ( DAKTARI WA AKINA MAMA) WATAKUWEPO KATIKA MSAFARA NA MADAWA YOTE MUHIMU YATAPATIKANA WAKATI WOTE WA SAFARI.WAWEZA KUWAULIZA MAHUJAJI WALIOWAHI KUHUDUMIWA NA TAASIS HII, NA WATAKUHAKIK-ISHIA UWEPO WA HUDUMA ZA KURIDHISHA. ALHAMDULILAH DAIMA KHIDMAT ISLAMIYA TUMEWEZA KUTEKELEZA KILA TUNACHOKIAHIDI.

    TAHADHARI: NDUGU HUJAJI MTARAJIWA FANYA UCHUNGUZI WA KINA KABLA YA KUJISAJILI KWANI IBADA HII NI MOJAWAPO YA NGUZO TANO ZA UISLAM KWA HIYO HAKIKISHA UNAITEKELEZA INA-VYOTAKIKANA KWA NAFASI ULIYOJAALIWA, KWANI HUJUI KAMA UTAIPATA TENA NAFASI HIYO MAISHANI MWAKO. NDUGU MUISLAM KAMA UNAO UWEZO USISUBIRIE MWAKANI HUJUI KAMA UWEZO ULIONAO LEO WA AFYA NA MASURUFU UTAENDELEA KUWEPO NA PIA UJUE GHARAMA NAZO ZINAONGEZEKA KILA MWAKA.

    -

    -

    -

    TAHADHARI: NDUGU HUJAJI MTARAJIWA FANYA UCHUNGUZI WA KINA KABLA YA KUJISAJILI KWANI IBADA HII NI MOJAWAPO YA NGUZO TANO ZA UISLAM KWA HIYO HAKIKISHA UNAITEKELEZA INA-VYOTAKIKANA KWA NAFASI ULIYOJAALIWA, KWANI HUJUI KAMA UTAIPATA TENA NAFASI HIYO MAISHANI MWAKO. NDUGU MUISLAM KAMA UNAO UWEZO USISUBIRIE MWAKANI HUJUI KAMA UWEZO ULIONAO LEO WA AFYA NA MASURUFU UTAENDELEA KUWEPO NA PIA UJUE GHARAMA NAZO ZINAONGEZEKA KILA MWAKA.

    -

    -

    -

    TAHADHARI: NDUGU HUJAJI MTARAJIWA FANYA UCHUNGUZI WA KINA KABLA YA KUJISAJILI KWANI IBADA HII NI MOJAWAPO YA NGUZO TANO ZA UISLAM KWA HIYO HAKIKISHA UNAITEKELEZA INA-VYOTAKIKANA KWA NAFASI ULIYOJAALIWA, KWANI HUJUI KAMA UTAIPATA TENA NAFASI HIYO MAISHANI MWAKO. NDUGU MUISLAM KAMA UNAO UWEZO USISUBIRIE MWAKANI HUJUI KAMA UWEZO ULIONAO LEO WA AFYA NA MASURUFU UTAENDELEA KUWEPO NA PIA UJUE GHARAMA NAZO ZINAONGEZEKA KILA MWAKA.

    WA MTUME (SAW), MAKABURI YA BAQII (WALIPOZIKWA MASWAHABA, BAADHI YA WAKEZE NA WATOTO WA MTUME (S.A.W.) NA MAKABURI YA WALIOKUFA SHAHIDI KATIKA VITA VYA UHUD

    -

    -

    -

    TAHADHARI: NDUGU HUJAJI MTARAJIWA FANYA UCHUNGUZI WA KINA KABLA YA KUJISAJILI KWANI IBADA HII NI MOJAWAPO YA NGUZO TANO ZA UISLAM KWA HIYO HAKIKISHA UNAITEKELEZA INA-VYOTAKIKANA KWA NAFASI ULIYOJAALIWA, KWANI HUJUI KAMA UTAIPATA TENA NAFASI HIYO MAISHANI MWAKO. NDUGU MUISLAM KAMA UNAO UWEZO USISUBIRIE MWAKANI HUJUI KAMA UWEZO ULIONAO LEO WA AFYA NA MASURUFU UTAENDELEA KUWEPO NA PIA UJUE GHARAMA NAZO ZINAONGEZEKA KILA MWAKA.

    KWA MAELEZO ZAIDI NA UANDIKISHAJI WASILIANA NA: SHEIKH HASHIM AHMAD RUSAGANYA NAMBA YA SIMU 0715 915 008, 0784 915 008 SHEIKH ABDALLAH MOHAMED JUMA IMAM MSIKITI WA MTORO 0713 445 545 AL-HAJJ ZULFIKAR OSMAN 0777 411 020, 0713 530 036, 0786 411 020 AL-HAJJ HAFIDH SALIM 0655 616 623, 0682 535 319 SHEIKH HARUNA JUMANNE KAPAMA 0715 985 413 AL-HAJJ ALTAF ABDULLATIF AHMED 0789 373 222 AL-HAJJ OMAR AWADH KHAMIS - MSIKITI WA QIBLATAIN - 0715 210 666 ARUSHA: SHEIKH JUMA RAJAB IKUSI TAYSEER STORE DUKA NO.12 MKABALA NA NMB TAWI LA SOKO KUU NAMBA YA SIMU 0786 125 512, 0767 125 513, 0655 125 513 MOROGORO: AL-HAJJ AHMED SALEH NAHDY(AHMADO)- 0715 372 776, 0773 372 776 DODOMA & SINGIDA: AL-HAJJ YUNUSU RUGEIYAMU 0754 334 400, 0786 293 901 DODOMA & KONDOA: SHEIKH ESMAIL H. ALLIY 0713 677 683 MULEBA, BUKOBA & DAR AL-HAJJ MAULID ATHUMAN KYEJU 0655 883 573

    KUFUATANA NA SHERIA MPYA NCHINI SAUDIA, TAREHE YA MWISHO YA KUJISAJILI NA KUTUMA

    MAJINA YA MAHUJAJI KWA NJIA YA MTANDAO KWA MWAKA HUU NI TAREHE 8 JUNI2015 SAWA NA

    TAREHE 20 SHAABAN 1437

    MAHUJAJI WOTE MNAOMBWA KUJISAJILI MAPEMA ILI KUWA NA UHAKIKA WA SAFARI YA HIJJA

    0773 372 776

    RUGEIYAMU 0754 334 400,

    DODOMA & KONDOA: SHEIKH ESMAIL H. ALLIY 0713 677 683

    MAULID ATHUMAN KYEJU 0655 883 573

    KATIBU MTENDAJI MUHSIN MOHAMED HUSSEIN 0784 /0715 /0773 - 786 680,

    TAARIFA MUHIMUKUFUATANA NA SHERIA MPYA NCHINI SAUDIA, TAREHE YA MWISHO YA KUJISAJILI NA KUTUMA

    MAJINA YA MAHUJAJI KWA NJIA YA MTANDAO KWA MWAKA HUU NI TAREHE 8 JUNI2015 SAWA NA

    TAREHE 20 SHAABAN 1437

    MAHUJAJI WOTE MNAOMBWA KUJISAJILI MAPEMA ILI KUWA NA UHAKIKA WA SAFARI YA HIJJA

    Ushawishi wa marafiki wabaya na uhuru mkubwa vimetajwa kuwa sababu ya baadhi ya vijana wa kiislamu wanaojiunga na vyuo vikuu hapa nchini kutum-bukia katika maasi kama ulevi, ku-vaa mavazi yasiyo na stara na zinaa.

    Hayo yamebainishwa na baadhi ya walimu na wanafunzi wa kiislamu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam waliohojiwa na gazeti la Imaan hivi karibuni. Wengi kati ya waliohojiwa wamekiri kwamba kuna wimbi la vi-jana wa kiislamu, hususan wa kike kubadilika pindi tu wanapozoea mazingira ya chuo na kugundua wapo tofauti kitabia na vijana wengi.

    Hali hiyo ya upweke katika jamii ya wanafunzi ambao wengi wame-potoka hulazimisha vijana wa kiisla-mu kuiga ili kwenda na wakati, mwalimu Zuhura Selemani wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasil-iano ya Umma alisema.

    Zuhura anasema anazungumza

    kutokana na uzoefu ambapo yeye mwenyewe alikuwa mwanafunzi kutoka mwaka 2006 hadi 2009, na kisha kuajiriwa chuoni hapo mwaka 2010.

    Zuhura alisema, vijana wengi wa-nafwata mkumbo wa marafiki zao. Akitoa mfano, Zuhura alisema binti wa kiislamu aliyetoka kijijini na ku-ingia mjini anakuwa na ushamba wa mambo mengi, na anapokutana na watoto wa mjini atataka afanane nao kimavazi na tabia ili naye aonekane ameelimika na kustaarabika.

    Hoja ya Zuhura inaungwa mko-no na mmoja wa wanafunzi wa mwaka wa pili Rahma Muhajir, ali-yetaja msukumo wa marafiki kuwa moja ya sababu za mporomoko wa maadili, hususan kwa wanafunzi wa kike.

    Rahma alisema binti wa kiislamu mara nyingi hupangiwa chumba na vijana wasiokuwa Waislamu na hivyo huanza kuiga tabia za kusikili-za miziki, kuangalia picha za ngono, kwenda disko, ulevi na kadhalika.

    Rahma alisema:Vijana wengi wa kiislamu wanapofika Chuo huacha kabisa kujishughulisha na maswala ya dini kama vile kuswali kuhudhuria madarasa, semina za dini na badala yake kujihusisha na mambo ya kipuuzi kama vile pati, kutoka usiku na mahusiano ya ki-mapenzi.

    Upo Msikiti wa Chuo pale Msau-di, unafundisha madarasa na kuali-ka masheikh mbalimali kutoa daawa lakini wanafunzi wa kiislamu wan-aohudhuria ni wachache mno ukil-inganisha na idadi ya Waislamu chuoni hapo, Rahma aliongeza.

    Sababu nyingine iliyotajwa ya vi-jana kujiingiza katika maasi ni uhu-ru wa kupitiliza ukilinganisha na maisha yao kabla ya kujiunga na chuo.

    Akielezea hilo, Mwalimu Zuhura alisema baadhi ya mabinti wa kiisla-mu wanakuwa nje ya udhibiti wa wazazi kwa mara ya kwanza na baa-dhi yao huutumia uhuru huo vibaya kwa kujaribu anasa mbalimbali.

    Zuhura alisema kijana ambaye hakujengeka vizuri kimaadili na am-baye alikuwa anaishi kwa kumu-uogopa mzazi, katika hali mpya ya uhuru kamili nidhamu ya uoga huondoka na kuanza kufanya mam-bo apendavyo.

    Hata hivyo, Zuhura anasema sio wanafunzi wote wanabadilika na kuingia katika uovu. Wapo wa-nafunzi ambao wamedumu katika maadili mazuri kipindi chote cha masomo yao.

    Naye, Shekha Ally ambaye pia ni mwalimu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ametaja vishawishi kuwa ni moja ya sababu zinazoshu-sha maadili ya vijana wa kiislamu pindi wanapofika chuo.

    Shekha alisema wapo wanafunzi walioingia chuoni hapo wakiwa na maadili mema na misimamo mizuri ya kidini, wakivaa mavazi mazuri ya stara na kuswali lakini baada ya muda kwa sababu hakuna tena usi-mamizi wa wazazi hushawishika na kujiingiza katika vitendo visivyo-

    mpendeza Allah.Akikumbuka enzi zake za uwa-

    nafunzi, Shekha alisema yeye binafsi alikuwa akishauriwa na marafiki zake avue baibui ili avae gauni, sketi na bilauzi kwa kuwa angependeza zaidi, lakini hakuyumba.

    Kadhalika, Shekha alisema yeye hakuyumba kwa sababu alikuwa anajiamini na anaamini anachofan-ya ni sahihi, jambo ambalo baadhi ya mabinti wa kiislam wamekosa na hivyo kufwata mkumbo na kuigaiga kirahisi. Kuhusu kutojiamini, mwa-nafunzi wa mwaka wa tatu, Raiye Mkubwa, alisema mazingira ya uoga na udhaifu wa kiimani hupelekea kuporomoka maadili kwa vijana wa vyuo.

    Alifafanua kuwa baadhi ya vitivo vina wanafunzi wachache wa kiisla-mu wanaovaa hijab na wakati mwingine msichana anaweza kuogopa vitisho vya kufelishwa na walimu kwa madai ya ujahidina hali ambayo huweza kupelekea mwa-nafunzi kupunguza stara yake.

    uhuru, marafiki, chanzo mporomoko wa maadili vyuo vikuu Hafswa Madiwa

    mila na desturi

    mila na destuRi / tangazo

  • www.islamicftz.org

    8 Rajab 1436, jumatatu aprili 27 - mei 3 , 2015

    12 www.islamicftz.org8 Rajab 1436, jumatatu aprili 27 - mei 3 , 2015

    13

    Katika makala yake kwenye gaze t i Raia Mwema toleo namba 401 la tarehe 15 Aprili, 2015, mwandishi Joseph Mihangwa chini ya kichwa cha habari: Dini za Kigeni Tishio kwa Umoja Afrika aliuliza: Ni nchi ngapi za Afrika ya Kiarabu ziliwahi kushiriki katika ukombozi wa nchi za Afrika

    bila uswahiba wa kidini?Pengine ni kwa kutokujua

    au kwa kujifanya hajui, mwandishi ameupotosha umma uamini kwamba haku-na nchi za Afrika za Kiarabu zilizosaidia ukombozi wa Afri-ka dhidi ya minyororo ya ukol-oni isipokuwa ni kwa uswa-hiba wa kidini.

    Kabla hatujaonesha kwa ushahidi jinsi nchi za kiarabu zikiwemo Algeria na Libya zilivyoshiriki kwa hali na mali katika ukombozi wa Afrika, kwanza tumkumbushe kuwa ukombozi wa nchi za Afrika us-ingekuweko kama si kwa nchi za kizungu za kikristo kuivamia na kuikalia Afrika.

    Wazungu walikutana mjini Berlin, Ujerumani mwaka 1884-85 kugawana bara la Afri-ka lililokuwa linakaliwa na Waa-frika weusi, Wabantu weusi, Waarabu weusi na Waarabu we-upe.

    Mwandishi angepaswa kwanza kuwalaani wazungu kwa kuwad-halilisha waafrika lakini kama wal-ivyo waandishi mfano wake, hilo hawezi kulifanya kwa kuwa chuki yake ni kwa waarabu tu.Ndivyo walivyofundishwa katika shule zao za misheni-Mwarabu mbaya, mzungu mzuri.

    Tukirudi katika swali la mwandi-shi wa makala hayo, kama kuna nchi zilizosimama kidete na wapi-gania uhuru zikitoa fedha, silaha na mafunzo mbali na kuwaunga mko-no katika majukwaa ya kimataifa ni nchi za kiafrika za kiarabu.

    Algeria: Nelson Mandela alipata mafunzo yake ya kwanza ya kijeshi nchini Algeria. Mwaka 1961 Man-dela alitembelea vikosi vya ukom-bozi vya Algeria katika mji wa Oujda nchini Morocco.

    Katika kitabu cha maisha yake The Long Walk to Feedom Nelson Mandela alikiri kuhamasishwa na mapinduzi ya Algeria.

    Algeria ilitoa silaha, pasi za kusafiria na misaada mingine iliyo-fanikisha kungolewa kwa ubaguzi wa rangi.Alisema Lamtane Lamamra, Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria katika maombolezo ya kifo cha Mandela.

    Bwana Mihangwa, Mandela mwenyewe alisema: Nilijua kwamba wapiganaji wetu wa-nafanana na wapiganaji wa Algeria, na nilikuwa nataraji kwamba wata-pigana kishujaa kama wao (Walge-ria).

    Tangumwaka 1961 Algeria ili-

    popata uhuru, wapiganaji wengi wa ANC na vyama vingine vya ukom-bozi Afrika ya Kusini walipatiwa mafunzo yao ya kijeshi nchini Alge-ria.

    Baada ya Mandela kufariki, Rais wa Algeria, Abdulaziz Boutefliqa aliamuru bendera za nchi hiyo ku-pepea nusu mlingoti kwa heshima ya Mandela. Boutelfiqa alimuita Mandela: The loyal friend of Alge-ria- Rafiki mtiifu wa Algeria.

    Labda tumuulize mwandishi huyo, Mandela ni Mwarabu au Muislamu? Watu wa Algeria ni dini gani maana makala yake inadai: Dini za kigeni tishio kwa umoja wa Afrika. Kwanza hii dhana ya dini za kigeni anaipata wapi?

    Mgawanyo huu wa dini za kigeni na dini za kienyeji ni mabaki ya fikra za kikoloni? Wao ndio walitugawa tukawa natives wenye jina for-eigners wageni. Dini ni dini tu na hazipaswi kuitwa za kigeni wala

    kienyeji. Kwa ni dini ikiwa ya kienyeji ndiyo inakuwa dini ya kweli na si tishio?

    Kinachosababisha mauaji ya al-bino na vikongwe huko Shinyanga anakoishi mwandishi wa makala hayo ni dini gani, Uislamu au Ukris-to? Ni dini gani tishio kwa Afrika, za kigeni au kienyeji?

    Tukirudi kwenye swali lake, kwa taarifa yako msomaji Algeria ndiyo nchi ya kwanza aliyoitembelea Mandela mwaka 1990 mara tu baada ya kuachiwa huru na utawala wa kibaguzi kuonesha shukrani kwa kuungwa mkono na Algeria wakati wa mapambano.

    Libya: Hii ni nchi nyingine ya Kiafrika, ya Kiarabu, ya Kiislamu ambayo pasi na kigezo cha dini ili-saidia ukombozi wa Afrika ya Kusini. Mandela alipotangaza kutembelea Libya mwaka 1994 wakati Libya ikiwa imewekewa vikwazo na mataifa ya magharibi,

    alikumbana na upinzani wa Marekani.

    Mandela akawajibu akisema, Those who feel irritated by our friendship with President Gaddafi can go jump in the pool (Wale wa-naokerwa na urafiki wetu kwa Gaddafi, waende wakajitupe kwenye bwawa).

    Mandela akaongeza kusema: Those that yesterday were friends of our enemies have the gall today to tell me not to visit my brother Gadd-afi, they are advising us to be un-grateful and forget our friends of the past. Yaani: Wale ambao jana wa-likuwa marafiki wa maadui zetu leo wanathubutu kuniambia ni-simtembelee kaka Gaddafi, wana-tushauri tusiwe na shukrani na ku-wasahau marafiki zetu wa zamani.

    Si hivyo tu Afrika ya Kusini chini ya Mandela ilitoa nishani iitwayo Order of Good Hope kwa Gaddafi kama heshima kutambua mchango

    wa Libya na Gaddafi kwa Afrika Kusini. Yote hayo ni kwanini?

    Libya iliisaidia ANC kwa hali na mali ikitoa si tu mafunzo ya kijeshi bali silaha, pesa na kuiunga mkono kidiplomasia wakati wote wa vita vya ukombozi wa nchi hiyo.

    Labda tumuulize Mihangwa, Gaddafi ni dini gani na Libya ni nchi gani kama si ya kiarabu? Mandela naye alikuwa Muislamu mpaka Libya imsaidie yeye na wananchi wake? Bila shaka hiyo ni chuki tu dhidi ya Waarabu na Waislamu.

    Marekani na washirika wake waliendelea kumuona Mandela ni gaidi hata baada ya ukombozi wa Afrika ya Kusini. Ni mwaka 2008 ndiyo Bunge la Congress liliondoa jina la Mandela katika orodha ya magaidi duniani na walifanya hivyo si kwakuwa waligundua upumbavu wao, bali walitoa kama zawadi ya siku ya Mandela kutimiza miaka 90.

    Bwana Mihangwa, Waarabu walikukosea nini hata ukweli kama huu unajifanya huujui? Bahati mbaya ni kwamba si wewe tu, bali wapo Watanzania kadhaa hivi sasa wanawachukia Waarabu.

    Hata ule mshikamano ulioku-wepo baina yaWatanzania na Wa-palestina umetoweka. Sasa kuna Watanzania wengi wanaopendelea Israel. Ni kana kwamba dhulma na jinai zinazofanywa na Israel kwa Wapalestina hawazioni. Ni chuki kwa sababu Wapalestina ni Waara-bu.

    Mwalimu Nyerere kwa hili alikuwa mkweli. Kwake Waisrael walikuwa madhalimu na Wapales-tina wadhulumiwa.Kuko wapi kumuenzi kwenu Nyerere? Chuki dhidi ya Waarabu imejengeka kuanzia Zanzibar hadi bara, kana kwamba kuwa Mwarabu ni kosa.

    Watawala wengi waliotawala nchi zetu wawe Wareno, Waarabu, Wajerumani, Waingereza, Wa-faransa na kadhalika waliwatendea Waafrika vibaya. Lakini sisi wa ki-zazi cha leo, hatupaswi kuishi na chuki mioyoni mwetu hadi kuuka-na ukweli. Mazuri ya watu yat-haminiwe ipasavyo na mabaya yao yaelezwe pasi na upendeleo.

    Historia imepotoshwa pakubwa kiasi kwamba Waarabu hufanywa mashetani (demonized) na Wazun-gu malaika.

    Chuki dhidi ya Waarabu inayo-jengwa na watu kama akina