imaan newspaper issue 6

19
ISSN 5618 - N0. 006 BEI: SH800/- KSH80/- USH1,200/- 29 RAJAB 1436, JUMATATU, MEI 18 - 24, 2015 www.islamicftz.org huwatoa watu gizani Hatimaye Vatican yaitambua rasmi Palestina - Uk 2 Rais Nkurunziza ajitafakari Sh bil 1.3 zaokolewa Head office, Lumumba Street, Opp: Viwanja vya Mnazi Mmoja, P. O Box 779 Dar es Salaam, Tanzania Tell: 255 22 2182482/ 255 222184419, Fax: 255 22 2181424, E-mail: [email protected] Watu 446 wasilimu Mbeya, Rukwa Kamata kamata ya Masheikh yaendelea UK 5 UK 6 KHALID OMARY W atu zaidi ya 446 kutoka vi- jiji tisa vya mikoa ya Rukwa na Mbeya wamesil- imu baada ya kuufahamu ukweli kuwa Uislamu ndio dini sahihi na kuwa hakuna Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Allah na Mtume Mu- hammad (Rehma na amani ziwe juu yake) ni mjumbe wake. Hatua hiyo imekuja baada ya Amir Rais Jakaya Kikwete akimjulia hali mtoto aliyefanyiwa upasuaji wa moyo. (NA MPIGA PICHA WETU) UK 3 Ni kutokana na msaada wa matibabu Watoto 63 wafaidika Rais Kikwete apongeza

Upload: imaan-newspaper

Post on 05-Dec-2015

1.010 views

Category:

Documents


3 download

DESCRIPTION

Imaan Newspaper issue 6

TRANSCRIPT

Page 1: Imaan Newspaper issue 6

ISSN 5618 - N0. 006 BEI: Sh800/- KSh80/- USh1,200/- 29 RajaB 1436, jUmatatU, mEI 18 - 24, 2015 www.islamicftz.org

huwatoa watu gizani

Hatimaye Vatican yaitambua rasmi Palestina - Uk 2

Rais Nkurunziza ajitafakari

Sh bil 1.3 zaokolewa

Head office, Lumumba Street, Opp: Viwanja vya Mnazi Mmoja, P. O Box 779 Dar es Salaam, TanzaniaTell: 255 22 2182482/ 255 222184419, Fax: 255 22 2181424, E-mail: [email protected]

Watu 446 wasilimu Mbeya, Rukwa

Kamata kamata ya Masheikh yaendeleaUK 5

Uk 6

KHALID OMARY

Watu zaidi ya 446 kutoka vi-jiji tisa vya m i k o a y a

Rukwa na Mbeya wamesil-imu baada ya kuufahamu ukweli kuwa Uislamu ndio dini sahihi na kuwa hakuna Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Allah na Mtume Mu-hammad (Rehma na amani ziwe juu yake) ni mjumbe wake. Hatua hiyo imekuja baada ya Amir

Rais jakaya Kikwete akimjulia hali mtoto aliyefanyiwa upasuaji wa moyo. (na mpiga picha wetu)

UK 3

Ni kutokana na msaada wa matibabu Watoto 63 wafaidika Rais Kikwete apongeza

Page 2: Imaan Newspaper issue 6

www.islamicftz.org

29 Rajab 1436, jumatatu mei 18 - 24, 2015

2

NA MwANDIsHI wetu

Baadhi ya watuhu-miwa wa kesi ya ugaidi namba 29 ya mwaka 2014 inay-

owakabili viongozi wa Jumui-ya ya Uamsho na Waislamu wengine wamesitisha mgomo wa kula kufuatia kuombwa kufanya hivyo na uongozi wa Gereza la Segerea.

Kwa mujibu wa Katibu wa Kamati ya Maafa, Maalim Ally Mbaruk ambaye ambaye taasisi yake imekuwa ikipele-kea chakula watuhumiwa hao.

Ahadi ya Serikali ya kushu-ghulikia madai yao ifikapo Mei 25, ilitolewa kufuatia kikao cha dharura kati ya uon-

gozi wa Gereza la Segerea, vi-ongozi wakuu wa Jumuiya ya Uamsho pamoja na watuhu-miwa waliogoma.

Kwa mujibu wa Mbaruk, mpaka siku ya jumamosi ya Mei 16,2015 watuhumiwa wote waliokuwa wameanza mgomo juma moja lililopita walishakubali kusitisha mgo-mo wao isipokuwa wawili am-bao hata hivyo Amir wa ju-muiya ya Uamsho Sheikh Farid Hadi aliahidi kuwasihi

ili waweze kuungana na wen-zao.

Madai ya watuhumiwa hao ni pamoja na kufutiwa shtaka la ugaidi dhidi yao kwa kuwa ni la kubambikiwa, kupatiwa dhamana wakati shauri hilo likiendelea, kupangwa tarehe rasmi ya kusikilizwa kesi yao, kesi iendeshwe Zanzibar kwa kuwa ni nchi huru na pia ndio mahala panapodaiwa kosa kutendeka na dai lingine ni kupatiwa matibabu.

Kiongozi wa Uamsho, Sheikh Farid hadi

habaRi

Nchi ya Vatican imeitambua rasmi nchi ya Palestina katika mkataba mpya.

Mkataba huo ambao ulikami-lika siku ya Jumatano na ukiwa haujasainiwa, unaonesha dhahiri kuwa nchi ya Vatican ime-badili uhusiano wake wa kidiplomasia kutoka kukitambua chama cha ukombozi wa Palestina(PLO) na badala yake kuitambua nchi ya Palestina.

“Ni kweli, huo ni utambuzi wa kuwa nchi

ya Palestina ipo,” alisema msemaji wa Vatican mchungaji Federico Lombardi. Uamuzi wa Vatican umepongezwa na watu na taasisi mbalimbali duniani kote. Nchi ya Vatican im-ekuwa haiitambui rasmi nchi ya Palestina kwa mwaka sasa. Msemaji wa Waziri wa Mambo ya Nje, Monsignor Antoine Camilleri amekiri kuwa mabadiliko ya kihadhi ambayo awali makataba huo ulikihusu chama cha PLO, kwa sasa umehitimishwa kwa suala la nchi ya Pal-estina.

NA HAFswA MADIwA

Wanawake wa kiislamu wame-himizwa kuwatembelea wag-onjwa waliopo majumbani na wale waliolazwa hospitali kwani

kufanya hivyo ni ibada.Hayo yamesemwa hivi karibuni na Katibu

Mkuu wa taasisi ya Jamiyatul Akhlaq –ul - Is-lam kitengo cha Muhimbili, Ustadh Ramadha-ni Hassan alipowapokea kinamama kutoka madrasa za Tegeta, Mikocheni, Temeke, Mwa-nanyamala na Gongo la Mboto walioungana na taasisi hiyo kuwatembelea wagonjwa katika hospitali ya Muhimbili.

Wanawake hao wa Kiislamu walitembelea wadi ya watoto wenye matatizo ya vichwa vikubwa na kutoa misaada mbalimbali, ikiwemo sabuni za unga, sabuni za kuogea, dawa za meno, nguo za watoto, keki, katoni za maji, pempas na mafuta ya kupaka.

Ustadh Ramadhani alisema, Uislamu una-jali ustawi wa jamii na matatizo ya watu, na ndio maana Allah Ta’ala katika Suuratul-Baqara (2: 30) amemuita mwanadamu khalifa.

Naye mmoja kati ya viongozi wa madrasa zi-lizoshiriki ziara hiyo, Ustadha Ashura Bilali, ameshauri Waislamu kumshukuru Mwenyenzi Mungu (Subhaanahu Wataalah) kwa kutumia vizuri neema alizowajaalia, ikiwemo neema ya afya, mali na nguvu kabla hazijawatoka.

Kwa upande wake, Ustadha Farida Pembe kutoka Tegeta aliwataka Waislamu kudumisha kutekeleza ibada ya kutembelea wagonjwa, kwani ni miongoni mwa ibada zenye malipo makubwa.

“Unapotoka kwenda kumtembelea mgonjwa malaika sabini elfu wanakuombea msamaha kwa Mwenyezi Mungu”, amesema Farida akisisitiza Waislamu kutembelea wag-onjwa waliopo majumbani na wale wa hospita-lini.

Vatican yaitambua Palestina

Wanawake wa Kiislamu watembelea wagonjwa

“afya”is natural source of sweet drinking water from under-

ground stream which is blended

with essential minerals to sup-port and aid per-fect metabolism.

WATERCOM LIMITEDP.o. Box 20409, Plot N.4005, Kisarawe11 area

Temeke,Daresalaam, Tanzaniawww.watercomtz.com, E-mail:[email protected]

uamsho wasitisha mgomo

Na. mjI FajR DhUhUR aSR maGhaRIB IShaa 1 DSm(6.75 S, 39.25 e) 5:13 12:20 3:42 6:14 7:23 2 ZanZiBaR(6.17 S, 39.25 e) 5:12 12:20 3:42 6:15 7:23 3 tanga(5 S, 38.25 e) 5:15 12:24 3:47 6:20 7:29 4 mOROgORO(8 S, 37 e) 5:24 12:29 3:50 6:21 7:30 5 mtwaRa(10.67 S, 39 e) 5:19 12:21 3:41 6:09 7:19 6 aRuSha(3 S, 36 e) 5:21 12:33 3:56 6:32 7:41 7 DODOma(6 S, 36 e) 5:25 12:33 3:55 6:28 7:37 8 mBeYa(8.5 S, 33 e) 5:40 12:45 4:06 6:36 7:45 9 KigOma(5 S, 30 e) 5:48 12:57 4:20 6:53 8:02 10 mwanZa(2.75 S, 32.75 e) 5:33 12:46 4:09 6:46 7:54 11 KageRa (4.66 S, 30.67 e) 5:44 12:54 4:17 6:51 8:00 12 taBORa(5.5 S, 32.83 e) 5:37 12:46 4:08 6:41 7:50 13 ShinYanga(3.75 S, 33 e) 5:34 12:45 4:08 6:43 7:52 14 SingiDa(5.5 S, 34.5 e) 5:30 12:39 4:01 6:35 7:43 15 iRinga(9 S, 35 e) 5:33 12:37 3:58 6:28 7:37

nYaKati Za swala

Page 3: Imaan Newspaper issue 6

www.islamicftz.org

29 Rajab 1436, jumatatu mei 18 - 24, 2015

3

NA seLeMANI MAgALI

Serikali imeokoa jumla ya Tsh. bilioni 1.3 kufuatia msaada kutoka Shirika la Al-muntada Islamic Trust

la Uingereza wa matibabu ya moyo kwa watoto 63.

Upasuaji huo uliofanyika kwa siku nane kuanzia tarehe 8 hadi 15 Mei mwaka huu ambapo 23 kati yao walifanyiwa upasuaji mkubwa na 40 walizibwa matundu ya moyo, bila kufungua vifua.

Matibabu hayo, yaliyoratibiwa hapa nchini na Taasisi ya Dhi Nureyn Islamici Foundation wakishirikiana na Tampro na The Islamic Founda-tion, yalitolewa bure chini ya madak-tari bingwa kutoka Hospitali ya Prince Sultan Cardiac Centre iliyopo katika jiji la Riyadhi nchini Saudi Arabia.

Katika matibabu hayo yaliyodu-mu kwa siku nane, madakatari hao bingwa walitumia teknolojia mpya iitwayo Cathlet kuziba matundu ya moyo ya watoto 40 bila kuvungua vi-fua.

Kazi ya kuwatibu watoto hao ili-fanywa na timu ya watu 25 kutoka taasisi ya Almuntada Islamic Trust ya nchini Uingeleza ambapo kati yao 14 ni madaktari bingwa , sita (6) wakiwa wahudumu wa ICU na manesi watano (5) ambao walishiri-kiana vema na wenyeji wao wa Idara ya Tiba ya Upasuaji wa Moyo ya Hos-

pitali ya Taifa ya Muhimbili.Kwa mujibu wa Sheikh Said Abri

wa Dhi Nureyn, madaktari wageni waliohusika na matibabu hayo wal-itoka katika nchi za Saudi Arabia, Yemen, Sudan na Uingereza lakini wote wanafanyaka kazi nchini Saudi Arabia huku kiongozi wa msafara akiwa Dk. Jamil Al Attah.

Kikwete ashukuruRaisi wa Jamhuri ya Muungano

wa Tanzania, Dr. Jakaya Mrisho Kik-wete, alitembelea Muhimbili siku ya mwisho ya zoezi hilo na kushuhudia maendeleo ya zoezi hilo ambapo al-isifia na kushukuru Serikali ya Saudi Arabia, Al-Muntada, Dhi Nureyn na wataalamu wote waliofanikisha kazi hiyo.

“Kwetu sisi kupeleka watu 60 nje kwa ajili ya kutibiwa ni ngumu. Hatuwezi kupata pesa ya kuwezesha kufanya hivyo. Kwa hiyo kuna watu wengi ambao wanaugua na hata kufa. Asanteni, na tunatumai haita-chukua muda mrefu kabla hamjaleta timu nyingine”, alisema Dk. Kik-wete.

Kikwete alisema Tanzania haina wataalamu wa kutosha na hivyo basi inapopata kambi za matibabu kama hizi inasaidia sana. Kikwete alisema moja kati ya faida kubwa ya kambi ya matibabu kama hiyo ni wataala-mu wa Tanzania kujifunza kutoka kwa wenzao.

Historia ya juhudi za kuleta madakatari

Juhudi za kuwaleta madakatari bingwa kutoka Saudi Arabia zilianza na wazo la Mwenyekiti wa taasisi ya The Islamic Foundation, Aref Nahdi ambaye alikutana na Dk. Robert Mvungi wakati Mwenyekiti huyo akimuuguza mama yake mwaka jana na kumpa wazo Daktari huyo la kuleta madaktari wasaidie kufanya upasuaji wa moyo. Wakati huo, Dk. Mvungi alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Moyo cha Muhimbili.

Kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa Taasisi ya Dhi Nureyn Islamic Foundation ya Iringa, Sheikh Said Abri, Aref Nahdi na Tampro kwa pamoja walifanikisha ujio wa kion-gozi wa Al Muntada, Sheikh Khalid

Abdallah Al Fawaz. Wadau hao wa-likutana na Dr. Mvungi April 28, 2014 na kuanza mchakato wa kuan-daa zoezi hili.

Wadau wasifia Akizungumza mara baada ya ku-

fanikisha zoezi la kuhudumia wag-onjwa hao wa Moyo, Muasisi na mwenyekiti wa Taasisi ya Dhi Nureyn, Sheikh Said Abri, alishuku-ru kwa kumaliza kazi hiyo kwa ma-fanikio makubwa katika muda mfupi.

Alisema kutibu zaidi ya wagonjwa 60 ni mafanikio ya kujivunia kwa watanzania wote kwani taifa linge-ingia gharama kubwa kuwatibu wagonjwa hao lakini gharama hizo zimeokolewa kutokana na msaada wa wataalamu uliotolewa bure kwa walengo.

Akitoa mchanganuo wa gharama halisi ambazo taifa lingeingia kama huduma hiyo ingetakiwa malipo, Sheikh Abri alisema kwa upasuaji mkubwa ambao umehusisha wag-onjwa 23 ungeigharimu serikali dola 230,000 wakati matibabu ya kuziba

matundu kwa watoto 40 yangeghar-imu dola 280,000 huku jumla ikifi-kia dola 510,000 za kimarekani sawa na Shilingi za kitanzania bilioni 1.3.

Naye kiongozi wa msafara wa jopo la madaktari bingwa waliokuwa wanatoa huduma hiyo, Sheikh Kha-lid Abdallah Alfawaz alisema wame-farijika sana na mapokezi waliyoya-pata hapa nchini Tanzania na wame-farijika kuwa sehemu ya kuokoa maisha ya watoto waliokuwa wakis-umbuliwa na maradhi ya moyo.

Wakati zoezi la kuwatibu wag-onjwa likiendelea, siku moja kuliji-tokeza tatizo la damu ambalo lilisab-abisha zoezi hilo kusimama kwa muda. Hata hivyo Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa (JAI), Saad Ahmed Salim, Jumuiyyyat Akhlaaqil Is-laamiyyah (JAI) ilipeleka waislamu hamsini ambapo 37 kati yao walitoa damu na zoezi likaendelea.

Akizungumzia uwezekano wa zoezi hilo kuwa endelevu, Sheikh Al-fawaz alisema watafikisha salamu hizo kwa Mfalme Salman bin Ab-dulaziz wa Saudi Arabia ili ufadhili wa matibabu hayo yawe yanatolewa kila mwaka.

Naye, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dk. Hussein Kidanto, alisema ujio wa madaktari bingwa hao umeokoa maisha ya watoto wengi ambao huenda ingewachukua muda mrefu kutibiwa kutokana na wingi wa wag-onjwa.

Nao wataalamu kutoka idara ya upasuaji wa moyo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili waliozungumza na baadhi ya vyombo vya habari walise-ma tatizo la ugonjwa wa moyo ni kubwa ambapo mwaka jana pekee wagonjwa takriban 400 walipele-kwa India huku 200 kati yao wa-likuwa wakisumbuliwa na moyo.

Rais jakaya Kikwete akiingia chumba cha upasuaji muhimbili. (na mpiga picha wetu)

habaRi

Juhudi za kuwaleta madakatari bingwa kutoka Saudi arabia zilianza na wazo la

mwenyekiti wa the iSlamic Foundation, areF nahdi ambaye alikutana na dr. robert

mvungi wakati nahdi akimuuguza mama yake mwaka Jana

Sh bilioni 1 zaokolewa

Page 4: Imaan Newspaper issue 6

www.islamicftz.org

29 Rajab 1436, jumatatu mei 18 - 24, 2015

4

Waislamu visiwani Zanzibar wametakiwa kukuza imani zao pindi wanaposoma au kusomewa kisa cha Israa na Miraj ambapo Allah Taala alimpeleka mbinguni Mtume Muhammad (Rehma na amani ziwe juu yake)

Akihutubia mamia ya Waislamu katika swala ya Ijumaa katika msikiti wa Taqqiyu uliopo wilaya ya Micheweni, kisiwani Pemba, Maalim Ayoub Khamis amesema kama Waislamu watazingatia mafundisho ya kisa hicho yatawaongoza kujua ukubwa wa Allah na hivyo basi kutekeleza amri na kuacha makatazo yake.

Alisema wakati mwezi wa Rajab ukielekea ukin-goni, ni vema Waislamu wakazidisha kasi ya ibada za faradhi na sunna ikiwemo kuswali,kufunga na kuzidisha toba ili kunufaika na fadhila za mwezi huo. (Suleiman Masoud)

Israa, Miraj iwe somo kwa jamii ya waislamu

Waislamu nchini wameaswa kutenda uadilifu katika kutoa kwani amali hiyo imepandisha daraja za wengi katika wema waliotangulia.

Nasaha hizo zimetolewa na Sheikh Mussa Wangara, maarufu kama Mpalestina, wakati wa swala ya ijumaa iliyoswaliwa katika msikiti wa Mtoro uliopo Kariakoo jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa kutenda uadilifu ni miongoni mwa sifa za waja wa Allah.

Sheikh Wangara alisema mja hapaswi ku-fanya ubakhili katika kutoa. Pia aliwakumbusha waumini kuacha fujo katika kutoa kwani ni makosa katika dini. Sheikh Wangara alim-nukuu Allah Taala katika Qur’an 25:67: “Na wale ambao wanapo tumia hawatumii kwa fujo wala hawafanyi ubakhili, bali wanakuwa katikati baina ya hayo”. (Yusuph Amin)

sheikh wangara awasihi waislamu kutoa kwa uadilifu

KutOKa MIsIkItInI

Assalaam Alaykum na Idd Mu-baraka. Kwa niaba ya kamati ya maandalizi ya baraza la Idd napenda kuwakaribisha wote

waheshimiwa mliohudhuria hapa na wageni wetu katika hafla hii kwanza ya kujipongeza kwa kumaliza mwezi huu mtukufu wa Ramadhani na pia kush-erehekea sikukuu hii ya Idd-el-Fitri.

Kwa mara ya kwanza baraza hili la Idd limeandaliwa kwa pamoja kwa ush-irikiano wa madhehebu na jumuiya mbalimbali za Kiislamu zikiwemo Bak-wata, Bohora, Sunni,Ibadhi, Ismailia, Shia Ithnasheria, Dar es Salaam Islamic Club na Baraza Kuu la Jumuiya na Taa-sisi. Hii ni hatua moja kubwa ya kiju-muia kwa Waislamu kwa kuonyesha ushirikiano na mshikamano wa pamoja na Inshaallah Mungu audumishe umoja huu.

Mgeni rasmi na viongozi wa dini mliokuwepo hapa napenda kuwatam-bulisha kwamba mbele yenu ni wawak-ilishi wa madhehebu na jumuiya mbalimbali za Kiislamu. Pia wamo wawakilishi wa misikiti na vyuo vya Kiis-lamu toka katika wilaya za mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.

Tunawashukuru wote kwa kuhud-huria baraza hii leo. Kabla sijamkabidhi mwenzangu Alhaj Sheikh Suleiman Gorogosi kuendelea na ratiba nin-gependa kuwajulisha tu kwamba wakati sisi leo tunasherehekea hapa kuna bahati mbaya maafa kidogo yametokea katika msikiti wa Idrisa. Habari tulizozipokea ni kwamba kuna ukuta wa msikiti wa upande wa akina mama umeanguka na kwamba kuna akina mama karibu saba walioumia kuna mmoja amefariki kwa hiyo tumwombee dua huyo aliyefariki Mwenyezi Mungu ampeleke Peponi Amin. Na hao ambao wameumia waweze kupana haraka.

Kwa hiyo mpaka hapo hii niliyo soma siyo ndiyo spichi maalum hii ni utanguli-zi kuweza kuwajulisha wageni rasmi na kuwatambua viongozi waliokuwa hapa mbele yenu.

Audhubillah Minasheitwan Rajim. Bismillahir Rahmanir Rahiim. Alham-dulillah Rabil Alaminn Waswalatu Wasalaam Alaan Ashraful Mursaliim Waalaa Ahli Wasahbih Ajumayn.

Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bwana Ben-jamin William Mkapa, Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Mu-

ungano wa Tanzania Alhaj Dk. Omar Ali Juma, Mheshimiwa Mzee wetu Alhaj Rashid Mfaume Kawawa,waheshimiwa Masheikh wetu wakuu, Maimamu, wazee wetu na viongozi mbalimbali, wa-heshimiwa Mawaziri na Wabunge, wa-heshimiwa Mabalozi, waheshimiwa wageni waalikwa, mabibi na mabwana Assalaam Aleykum Warahmatullah Wabarakatuh.

Siku ya Idd kwetu sisi Waislamu ni siku tukufu sana, Waislamu duniani kote wanaosherehekea kumalizika kwa funga ya Ramadhani, nachukua fursa hii kwa niaba ya Waislamu wote kuwapongeza Waislamu na kumuomba Mwenyezi Mungu (s.w.) akubali funga yetu Amin.

Pamoja na Idd Waislamu tuna men-gine mengi ya kusherehekea wakati huu, kwanza tunasherehekea kuimarika kwa umoja wetu, viongozi wa Bakwata, Ju-muiya za Bohora, Ibadhi, Ismailia, Shia Ithinashiri na Sunni wamekubali kuun-gana na kushirikiana kwa yale wanay-okubaliana. Wamekubaliana kuwa na kamati ambayo ina mwakilishi kutoka kila madhehebu. Kamati hiyo sasa ndiyo itakayowakilisha Waislamu wa madhe-hebu tofauti. Ni nia yetu kuuendeleza umoja huu kwa ajili ya kuyakabili masu-ala mbalimbali yanayowaathiri Waisla-mu.

Kutokana na mshikamano huu, tarehe 8 Ramadhani waumini wa mad-hehebu mbalimbali tuliweza kukutana tukafuturu pamoja, pamoja na hata kuswali nyuma ya Imamu mmoja. Aid-ha Baraza la Idd mwaka huu limeandali-wa na kuhudhuriwa na waumini wa madhehebu zote. Imewezekana pia wa-heshimiwa, mimi kuteuliwa leo hii na kusimama hapa mbele yenu na kuyase-ma haya ninayoyasema kwa niaba ya Waislamu hao.

Mheshimiwa Rais; Waislamu pia tu-nasherehekea kuwa nawe katika hafla hii. Hii ni fursa ambayo hatuipati mara kwa mara. Na kama vile leo tumeipata ni vyema tuitumie kikamilifu kukueleza siyo tu ya furaha bali pia ya masikitiko. Matarajio yetu kwa Wakristo wema ni makubwa, kwao tunatarajia upendo kama Qur’an inavyosema katika sura ya tano (5) aya ya 82 kuwa walio karibu zai-di ya Waislamu kwa upendo ni Wakris-to.

Aidha, kwa uongozi mwema wa Kikristo tunatarajia uadilifu hata wal-ipozidi kuteswa na washirikina wa

Makkah Waislamu wa awali waliam-rishwa na Bwana Mtume (s.a.w.) wakim-bilie Abisinya ambako mtawala alikuwa Mkristo muadilifu.

Mheshimiwa Rais sisi tunaamini kwamba wewe ni Mkristo muadilifu, tu-naziona na tunazitambua juhudi zako katika kuyasikiliza matatizo ya Waisla-mu na kuyafanyia kazi. Kwa mfano ul-izivunja bodi za Parole pale ilipodhihiri kuwa hazikuwa na uwiano ulitoa picha sahihi ya jamii yetu. Tarehe za mitihani ya kidato cha nne zilibadilishwa ili zisian-gukie siku ya Idd ingawa bado mitihani hiyo iliendelea kufanyika katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, lakini sisi tu-naamini kwamba umeanza kuyatekele-za yale uliyoazimia kuyafanya na kwetu sisi tunaamini pia kwamba safari ya maili elfu moja siku zote huanza na hat-ua ya kwanza. Kwa hayo yote tunapenda kukushukuru na kukuombea kwa Mwenyezi Mungu (s.w.) azidi kukupa moyo wa ujasiri wa kuyakabili matatizo ya jamii yetu katika misingi ya usawa na haki.

Mheshimiwa Rais tunasema masua-la haya umeyasikia na umeanza kuyatat-ua, huku tukikushukuru wewe kwa hayo bado kuna masuala ya msingi inabidi tu-jiulize na yapatiwe majibu. Bado kuna mengine mengi yenye sura hii hii ya up-endeleo dhidi ya Waislamu ambayo bado hujayapatia uvumbuzi.

Kuna suala la Mwembechai ambalo liko mahakamani limechukua muda mrefu na bado halijatatuliwa. Waislamu bado wanaomba uchunguzi huru ufan-yike na ukweli ujulikane na haki itendeke. Kadhia ya Mwembechai ime-chukuliwa nisuala la fujo za Waislamu wenye udini na siasa kali wanaotaka ku-vuruga amani. Imedhihirika kwamba waliokamatwa katika kadhia ile hawakuwa Waislamu peke yao.

Vile vile waliohujumiwa hawakuwa Wakristo kwani pale Mwembechai sote tunafahamu kuna Makanisa mawili ambayo hata moja halikuathiriwa waka-ti wa kadhia ile, hakuna hata jiwe moja lililotupwa katika Makanisa hayo, kwa hiyo hili siyo suala la udini wa Waislamu, lakini bado vyombo vya dola viliwalenga Waislamu na kuwaona ndiyo walioleta uchochezi kwa lengo la kuleta vurugu (ee samahani) wanaoleta uchochezi kwa lengo la kuvuruga amani.

Hatuelewi hii ni kwanini. Hii imepe-lekea kuwa na hisia katika jamii kwamba

hiki ni kielelezo cha hitilafu iliyopo katika jamii katika kutafsiri sheria za msingi za nchi. Ili kuondoa hisia hizo hapana budi uchunguzi huru ufanywe, ukweli uju-likane, haki itendeke na pia ionekane kwamba inatendeka.

Aidha, Mheshimiwa Rais kuna suala la mahakama za Makadhi nalo bado li-nalaumiwa. Nchi jirani zenye Waislamu wachache kuliko Tanzania zina mahaka-ma hizo. Tanzania Visiwani pia ziko. Hapa bara zilikuwepo zikaondolewa. Mpaka leo Waislamu hawajapewa saba-bu wala mantiki ya kuondolewa ma-hakama za makadhi. Tunataka ieleweke kwamba suala la mahakama za Maka-dhi ni sehemu isiyomegeka na masuala ya sheria za Kiislamu. Sheria za Kiislamu ni mwongozo, maamrisho na makatazo ambayo yanagusa maisha ya kila siku ya muumini wa Kiislamu kama yalivyo ka-tika Qur’an na Sunnah za Bwana Mtume (s.a.w.). Zinatawala masuala ya kuratibu mwenendo, desturi, ndoa, mirathi, mavazi, utendaji kazi, uhusiano baina ya mtu na mtu, mahusiano ya kibiashara, majukumu kwa wazazi, viongozi na watawaliwa, mke, mume, watoto pamo-ja na jamii n.k. Kwa maneno mengine mfumo wa sheria za Kiislamu ni mfumo kamili wa maisha ya Waislamu. Kwa haya Muislamu hana hiyari. Tunaomba sheria za nchi zisipingane na maamrisho na makatazo ya sheria za Kiislamu kama zilivyo katika Qur’an na Sunnah za Mtume (s.a.w.).

Kuwepo mahakama za Makadhi pamoja na Makadhi waadilifu kutaisa-dia serikali kupata tafsiri sahihi ya masu-ala ya Waislamu.

Mheshimiwa Rais kuna suala la idadi ya Waislamu katika mashule ya sekond-ari ya umma, pamoja na vyuo vikuu na maofisi mbalimbali za serikali kuwa ndogo na idadi yao katika majela na miongoni mwa wazururaji kuwa kubwa.

Ni ukweli usiofichika kwamba vijana wetu wa Kiislamu hupata nafasi finyu katika kujiendeleza kielimu. Hatudhani kwamba vijana wa Kiislamu si waadilifu. Ni dhahiri kwamba mfumo wa kutahini, kuchuja na kuchagua wanafunzi kuen-delea na elimu una kasoro za msingi na hivyo hauna budi kurekebishwa. Mtu anapokosa elimu uwezo wake kimaen-deleo pia huwa mdogo. Uwezo wa kupa-ta ajira unatoweka, na uwezekano wa kujiingiza katika wizi, uzururaji, ujam-

bazi na uhalifu kwa ujumla huwa dha-hiri. Wakulaumiwa katika hali kama hii siyo vijana au wahalifu hao ingawa wen-gine wana makosa, bali ni jamii.

Aidha, kutokana na sababu za kihis-toria, nchi yetu imekuwa na uhusiano wa karibu zaidi na nchi ambazo si za Ki-islamu. Hivyo basi wawekezaji wengi hutoka nchi hizo hasa taasisi za kidini wamepata uhuru na fursa za kuwekeza katika elimu na huduma nyingine za jamii bila ya bughudha wala kero. Walengwa wamekuwa waumini wa dini zao.

Kwa upande mwingine wawekezaji wa kutoka nchi za Kiislamu wanapotaka kuwekeza katika huduma za jamii na hasa elimu, Waislamu wakiwa kama walengwa hukutana na vikwazo vingi, bughudha na kero, aghalabu wao huonekana kama ni wachochezi na wenye kutaka kuvunja amani. Tunacho-taka Waislamu ni uhuru wa Waislamu wenzetu pamoja na sisi wenyewe wana-otaka kuwekeza katika fani hizo wapewe fursa hiyo bila bughudha wala vikwazo visivyo kuwa vya msingi.

Isitoshe, Mheshimiwa Rais nchi yetu bado inachelea kuboresha uhusiano wake na nchi za Kiislamu. Nchi jirani kama vile Kenya, Uganda, Msumbiji zenye Waislamu wachache ukilingani-sha na Tanzania zimejiunga na Organi-zation of Islamic Conference (OIC) Tan-zania yenye Waislamu wengi bado hai-jajiunga bila ya kuwapo kwa sababu za msingi. Ni dhahiri kwamba ingejiunga ingestahili misaada mingi mbalimbali kutoka kwenye umoja huo na taasisi zake kama vile Islamic Development Bank.

Mheshimiwa Rais kwa kuwa vile leo ni siku ya Idd si vyema kuendelea kula-lamika na kusikitika. Malalamiko yetu ni mengi za hatuwezi kuyamaliza katika hafla hii. Leo ni siku ya furaha na ni siku ya kutembeleana na kupeana sikukuu. Sikukuu yetu kwako ni huu umoja wetu ambao lengo lake ni kuchangia katika harakati za kudumisha amani na kuleta maendeleo.

Kutoka kwako tunaomba sikukuu yetu kwanza tunaiomba serikali itambue umoja huu na ishirikiane nao. Kuwe na mawasiliano ya karibu na ya kudumu juu ya masuala yanayohusu maendeleo ya nchi yetu na ya jamii. Kisha tunaiom-ba serikali ilete usawa na uadilifu kwa wananchi wa dini zote.

tujiKumbuShe

Risala ya Waislamu kwa mgeni Rasmi, Rais mstaafu wa tanzania, benjamin mkapa, iliyosomwa kwenye baraza la idd Diamond jubilee, januari 19,1999

waislamu watakiwa kujiepusha na fitina Waislamu nchini wametakiwa kujiepusha na mambo mbalimbali yanayo mchukiza

Mungu hususan fitna ili kuweza kupata radhi za Muumba wao.Hayo yamesemwa na Imam Mkuu wa msikiti wa Haqi uliyopo mtaa wa Karume,

Manspaa ya Morogoro, Sheikh Ibrahimu Twaha katika hotuba ya swala ya ijumaa iliy-oswali wa katika msikiti huo.

Aidha Sheikh Twaha alisema kuwa miongoni mwa mambo yanayoweza kuwafitini-sha Waislamu ni pamoja na mali, watoto na wake zao hivyo Waislamu hawana budi kuzingatia uadilifu kwa lengo la kupata fadhila za Muumba wao. (Abeid, Morogoro)

Page 5: Imaan Newspaper issue 6

www.islamicftz.org

29 Rajab 1436, jumatatu mei 18 - 24, 2015

5

NA YusupH AMIN

Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam umetoa kibali kwa ajili ya upanuzi na maboresho ya jengo la msikiti la chuo hicho ili kusaidia

jamii ya Waislamu kufanya ibada kwa ukamil-ifu na nafasi.

Kwa mujibu wa barua ya Makamu Mkuu Msaidizi wa Chuo hicho (Utawala), Prof. Dav-id Mfinanga, kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyakazi wa Kiislamu wa Chuo hicho, (DUMT), Prof. Mussa Juma Assad, uongozi wa chuo umeruhusu ujenzi huo baada ya kutambua haja ya uwepo wa msikiti wa kisasa na mkubwa zaidi utakaokidhi mahitaji ya jamii ya Waislamu inayoongezeka.

Sehemu ya barua hiyo inasema: “Chuo ki-natambua haja ya msikiti kupanuliwa na ku-wekwa huduma za kisasa na za kutosheleza. Hivyo basi, Chuo kinaunga mkono jitihada zenu”, kisha, ”Hivyo basi, napenda kukujuli-sha ruhusa inatolewa kupanua msikiti”.

Hata hivyo, Chuo kimetoa masharti kadhaa ikiwemo msikiti mpya kujengwa katika eneo ambalo msikiti wa sasa upo, na si zaidi.

Kufuatia uamuzi huo wadau wakuu wa msikiti huo, DUMT na Jumuiya ya Wanafunzi wa Kiislamu (MSAUD) wameanza mchakato wa kusaka wafadhili. Wafadhili kadhaa wal-ishawahi kujitokeza kutaka kusaidia ujenzi wake ikiwemo ubalozi wa Saudi Arabia na

Iran. Hatua ya chuo hicho kuruhusu upanuzi wa msikiti imekuja baada ya manung’uniko ya muda mrefu ya Waislamu chuoni hapo wengi wakiamini msikiti haulingani na hadhi ya chuo hicho. Mchakato wa kutafuta kibali cha utanuzi ulianza miaka zaidi ya miaka 10 iliyo-pita, kwa mujibu Amir wa MSAUD, Said

Athumani . Imam wa msikiti huo, Hussein Juma

ameipongeza kamati iliyofuatilia suala hilo na kusema kuwa ujenzi wa msikiti mpya uta-wawezesha Waislamu kufanya ibada zao kwa nafasi kwani. Waumini wanaokadiriwa kusali katika msikiti huo ni 800.

Naye Naibu Mwenyekiti wa MSAUD anayemaliza muda wake, Japhari Mudhihiri amewashukuru viongozi waliotangulia kwa kuwa wameweka msingi mzuri na kushukuru chuo kwa kulipatia ufumbuzi suala hilo jambo ambalo linaonesha uongozi wa chuo hauna ubaguzi.

uDSm kujenga msikiti wa kisasa habaRi

DUMT, MSAUD wasaka wafadhili

NA MwANDIsHI wetu

Wakati Jeshi la Polisi nchini limewata-ka Waislamu wasitishe maanda-mano yaliyokuwa yafanyike wiki ili-opita, kwa hoja kuwa linayashuguli-

kia madai yao, baadhi ya masheikh katika wilaya ya Tunduru, mkoa wa Ruvuma wamekamatwa na kusafirishwa na Jeshi hilo hadi jijini Dar es sa-laam.

Akizungumza na gazeti hili, wakili anayefuatil-ia suala la masheikh hao, Rashid Kilindo, amese-ma kuwa, alipata taarifa za kukamatwa kwa watu hao na hivyo kufuatilia suala hilo ili kujua sababu za kukamatwa, hata hivyo hakupewa ushirikiano kutoka Jeshi la Polisi.

“Nimefuatilia ili kujua sababu za kukamatwa kwa masheikh hao. Bahati mbaya sikupata ushiri-kiano kutoka kwa maofisa wa polisi wa kituo cha Oysterbay jijini Dar es salaam wanakoshikiliwa watu hao,” alisema wakili Kilindo.

Kufuatia hali hiyo, wakili Kilindo amesema, watachukua hatua zaidi za kwenda Mahakamani ili itoe idhini masheikh hao washtakiwe au waachi-we.

Kwa mujibu wa wakili Kilindo, sababu alizozi-pata za kukamatwa kwa masheikh hao ambazo sio rasmi ni makosa ya ujangili.

Kuhusu idadi ya masheikh hao waliokamatwa na majina, wakili Kilindo amesema kuwa, taarifa sahihi bado hazijulikani, kwani jeshi la polisi hali-jampa ushirikiano wa kutosha.

Habari za kukamatwa kwa masheikh huko Tunduru zilithibitishwa pia na mkazi mmoja wa wilaya ya Tunduru ambaye alisema, mmoja kati yao aliachiwa na kuhadisia kuhusu mateso

makubwa wanayopata wanaoshikiliwa kituo cha Oysterbay.

Kamata kamata hii inaendelea wiki baada maimamu na viongozi wa misikiti kadhaa ya jijini Dar es salaam kukutana na kupokea taarifa za ma-zungumzo kati ya Waislamu na serikali, ambapo ilielezwa kuwa, yameendelea vizuri, huku Waisla-mu wakiombwa kusubiri utekelezaji.

Sheikh Mussa Kundecha alisema, serikali ime-omba maandamano ya April 15, 2015 yasifanyike, na badala yake wavute subra, kwani serikali imeji-zatiti kuyashughulikia madai yote yaliyotolewa.

Sheikh Kundecha alisema, ujumbe wa Waisla-mu katika mazungumzo na Serikali walikubali ku-sogezwa mbele kwa maandamano hayo hadi hapo itakapotangazwa.

Kufuatia rai hiyo ya Sheikh Kundecha, maima-mu hao kwa kauli moja walikubaliana kuyafuata maazimio yaliyofikiwa na uongozi wa juu na seri-kali, huku wakiazimia kufanya kongamano kubwa katika msikiti wa kichangani, ili kutoa mrejesho wa hatua zilizochukuliwa na serikali.

Hata hivyo, maimamu na viongozi wa taasisi za Kiislamu waliozungumza na gazeti la Imaan wal-isema, watafanya Kongamano Ijumaa ijayo litaka-lotoa sura ya nini cha kufanya, na kuweka mipango ya kufanya maandamano kama madai yao hayat-ashughulikiwa.

Nazo, taarifa kutoka Morogoro zinasema masheikh, maimam na waumini wengine zaidi ya nane wanaendelea kushikiliwa katika wilaya ya Kilosa na Kilombero.

Mmoja kati ya wanaoshikiliwa ni Imam Juma Salum wa msikiti wa Kisunna aliyekamatwa wiki iliyopita. Waislamu wengine wanaoshikiliwa na polisi walikamatwa katika vijiji vya Ruaha, Kidatu,

Mkamba na Msowero. “Kwa kweli hali inatisha. Hata hatujui tufanye

nini. Viongozi wa Kiislamu na waumini wengine wanaendelea kukamatwa kila kukicha na kushikil-iwa”, chanzo kimoja kiliarifu.

Watuhumiwa wa Mkoani Lindi:Akizungumzia kadhia ya masheikh na walimu

wa madrasa waliokamatwa katika mkoa wa Lindi, wakili Kilindo amesema kuwa, watuhumiwa hao kwa sasa wako nje kwa dhamana.

Kwa mujibu wa wakili Kilindo, watuhumiwa hao walisafirishwa hadi jijini Dar es salaam, makao makuu ya Jeshi la Polisi kitengo cha makosa ya ugaidi, kwa uchunguzi na mahojiano zaidi.

Wakili Kilindo alisema kuwa, mara baada ya uchunguzi wa vyombo vya ulinzi na usalama dhidi ya watuhumiwa hao, walipata taarifa kuwa masheikh hao hawakukutwa na hatia yoyote ila waliendelea kushikiliwa kinyume cha sheria. “Taarifa tulizozipokea kutoka katika vyanzo vyetu yakinifu ni kuwa masheikh wale hawakukutwa na hatia yoyote mara baada ya uchunguzi wa Polisi na usalama, lakini waliendelea kushikiliwa”, alisema wakili Kilindo.

Hata hivyo, baada ya mahojiano kati ya Jeshi la Polisi na wanasheria, watuhumiwa hao walirud-ishwa mkoani Lindi na kufikishwa katika ma-hakama ya wilaya mkoani hapo mbele ya hakimu Nzowana Laidha, ambapo Jeshi la Polisi liliomba wawekwe chini ya ulinzi wa kisheria kwa mwaka mmoja.

Watuhumiwa hao ambao inadaiwa kuwa wali-hojiwa na vyombo vya ulinzi na usalama kama wana mafungamano na kundi la wanamgambo wa Al-Shabaab na Alqaeda wanatarajiwa kuripoti mahakamani Mei 19, 2015.

Kamata kamata ya masheikh yaendelea licha ya ahadi ya Serikali

Hassan Jaibu pamoja na wenzake kufanya da’awa kupitia midahalo ili-yohusisha Waislamu na wale wasiokuwa Waislamu iliyochukua zaidi ya miezi mitatu katika mikoa hiyo ambayo inasifika kwa kuwa na wakazi wengi wasiokuwa Waislamu.

Vijiji ambavyo Amir Hassan Jaibu alifanya da’awa ni pamoja na Maleza, Kilya, Matundu, na Kilangawana vya mkoa wa Rukwa na Kamsamba, Kilulumo, Ivuna, Mpona, Masa-nyika na Itumbula vya mkoani Mbeya.

Hata hivyo, Amir Jaibu aliwataka Waisla-mu wote nchini kuwasaidia wale waliosilimu mahitaji muhimu katika maisha ya mwan-adamu kutokana na ukata unaowakabili, hali ambayo itawafanya wajisikie wako pamoja na ndugu zao.

“Waislamu wengi wapya hutengwa na ndugu zao wa damu na kwa sababu hiyo basi ni muhimu kuwaunga mkono”, alisema.

Vilevile amewaomba wale wenye uwezo wamsaidie usafiri wa kuzunguka katika mae-neo ya da’awa pamoja na walimu wa ku-wafundisha elimu ya dini ya Kiislamu kwa kuwa Waislamu wapya bado ni wageni hawa-jui lolote. Amir Jaibu alisema, kutokana na uzoefu, wapo ambao walisilimu katika miaka iliyopita na baadae kwa kukosa kufundishwa walirejea tena katika ukafiri.

Wimbi la watu kuingia katika Uislamu limezidi kuwa kubwa hapa nchini na duniani kwa ujumla licha ya mataifa mengi ya kima-gharibi kuupiga vita Uislamu kwa mbinu to-fauti tofauti.

Watu 446 wasilimu INatoKa UK 3

Page 6: Imaan Newspaper issue 6

hutoleWa na KuchaPiShWathe islamic Foundation, P.o. box 6011 morogoro, tanzania, e-mail: [email protected]

mhaRiRi mtenDaji: 0715 559 944, mhaRiRi: 0786 779 669, aFiSa maSoKo: 0785 500 502toVuti: www.islamicftz.org

29 Rajab 1436, jumatatu mei 18 - 24, 2015

tahaRiRi / uchambuzi6

Uislamu unatuusia kuwatendea haki siyo tu Waislamu b a l i h a t a w a -

siokuwa Waislamu. Na kubwa zaidi Waislamu

tunahimizwa kuwatendea wema hata maadui zetu “…Na wala kuwachukia watu kusi-wapelekee kutokuwafanyia uadilifu. Fanyeni uadilifu kwani huko ndiyo kujikurubi-sha zaidi na uchaMungu…” (Qur’an 5:8)

Hivi karibuni kumezuka mwenendo wa masheikh ku-rushiana makombora katika vyombo vya habari.

Tumeshuhudia au kusoma wakishutumiana na hata kuta-ja ‘aibu’ za wale wanaowaona kuwa wapinzani wao kwa sababu tu ya kutofautiana ka-tika mambo yahusuyo Waisla-mu kama vile mahakama ya kadhi, uchaguzi na maanda-mano.

Tunaamini mwenendo huu

ukiendelea utachangia sana katika kuugawa umma wa Waislamu kuliko kujenga. Hivi kuna faida gani kama Sheikh mmoja atataja anay-oyaona yeye ni aibu za Sheikh mwingine?

Hivi sio ninyi masheikh zetu ambao mnatuhubiria misikitini na kwingineko kusitiriana aibu zetu kwa sababu Muislamu nduguye ni Muislamu?

Iwapo Sheikh mmoja atao-

na Sheikh au kiongozi mwen-zake anapotoka au amekosea Uislamu unatuambia nini? Je na yeye aendeleze makosa kama alivyokosea mwenzake kwa kumshambulia hadharani au amfuata na kuongea nae?

Tunadhani si jambo jema mwenendo huu kuachiwa uendelee. Waislamu wanahi-taji kutoka kwa viongozi wao maelekezo na nasaha za ku-jenga au kuona masheikh wa-natofautiana lakini pasina

kubezana, kuabishana na kufedheheshana.

Wema waliotangulia wal-itofautiana sana katika masu-ala mbali mbali lakini kwa kuwa walikuwa na uchaMun-gu hawakufikia kushambulia haiba ya mtu binafsi.

Sisi katika gazeti Imaan tu-nasema, tunapaswa kuiga mwenendo wa wema walio-tangulia. Masheikh zetu ache-ni kutangaza aibu na makosa ya wengine.

Waislamu kwa mwendo huu tutafika?

Taarifa mbali mbali tuna-zoziona na kuzisikia kupitia vyombo vya habari vya ndani na nje

ni kuwa hali ya Burundi kwa sasa ni tete mno kufuatia watu kadhaa kufariki, kujeruhiwa na wengine kuyakimbia makazi yao nchini humo.

Kadhia hiyo imekuja kufuatia kauli ya Rais wa sasa wa Burundi, Pierre Nkurunzinza kusema atag-ombea tena nafasi hiyo kwa muhula wa tatu jambo ambalo limepingwa vikali na wapinzani na hata wanaharakati mbali mbali duniani.

Wakosoaji wa kauli ya Nkurun-zinza kuwa ‘atagombea tena kwa muhula wa tatu’ wanasema Rais huyo amekiuka mkataba wa ama-ni wa Arusha (Arusha peace ac-cord) ambao unamtaka Rais akae madarakani kwa mihula miwili tu.

Katika utetezi wake, Rais Nku-runzinza anasema anagombea tena kwa hoja kuwa kipindi cha kwanza cha utawala wake ali-chaguliwa na wabunge, hivyo hak-ihesabiki. Kinachohesabika ni kile kipindi cha pili kinachomalizika ambacho alichaguliwa na wa-nanchi. Ni baada ya kuhudumu kipindi cha pili cha kuchaguliwa na wananchi ndio atapoteza sifa ya kuongoza nchi hiyo.

Katika mahojiano na gazeti moja la kila wiki hapa nchini, Mwanasheria mkuu mstaafu wa Tanzania na aliyewahi kuwa mion-goni mwa viongozi waliopewa ju-kumu la kusimamia amani ya ku-dumu nchini Burundi, Jaji Mark Bomani amesema jambo hilo halipo na kuwa Rais Nkurunzinza anachokifanya kwa sasa ni ukiu-kaji wa mkataba wa amani.

“..kipengele cha saba cha mkataba huu kinazungumzia na-fasi ya Urais, kinasema Rais wa kwanza atachaguliwa na Bunge, kwa kuwa hapakuandaliwa utara-

tibu wa kupiga kura, wakaona kuwa rais wa kwanza achaguliwe na Bunge au Seneti na apate the-luthi mbili ya kura,” anasema Jaji Bomani

Jaji Bomani anaendelea kuse-ma kuwa “Lakini ni Rais kamili (kwa mujibu wa mkataba) kwa kipindi cha miaka mitano, baada ya hapo ndio akachaguliwa na wa-nanchi kwa ujumla.”

Katika mahojiano hayo Jaji Bomani anasisitiza kuwa mkataba huo unaposema Rais wa Burundi atatawala kwa mihula miwili, ni huo aliochaguliwa na Bunge na ule wa awamu ya pili aliochaguli-wa na wananchi inayokamilika kwa sasa.

Kutokana na uchambuzi huo wa Jaji Bomani ni kuwa Rais Nku-runzinza yuko kinyume na masharti ya mkataba, na kwa up-ande wangu mimi, naamini Rais huyo ndani ya nafsi yake anajua kuwa anaenda kinyume ila kuto-kana na hulka ya viongozi wetu wa bara la Afrika kulewa madaraka, ameamua kujifanya kiziwi.

Sawa, amekataa kuheshimu mkataba uliomtaka agombee kwa mihula miwili tu lakini je hawaoni wananchi wake wanaoteseka kid-halili, huku wengine wakikimbilia nchi za jirani na kuwa wakimbizi ikiwemo hapa Tanzania?

Hii haikubaliki. Kwa kuwa Rais Nkurunzinza anaonekana kabisa kushikilia msimamo wake wa kugombea awamu ya tatu licha ya

jaribio la kumpindua kushindwa, ni wajibu wa viongozi wenzake wa Afrika nzima wakamshawishi aachie ngazi.

Historia ya Burundi inajulika-na. Ni historia ya visasi vya kika-bila baina ya Watutsi na Wahutu. Ni historia ya mauaji. Ni historia ya ukimbizi kila kukicha. Anach-okifanya Rais Nkurunzinza ni kuibua upya historia hiyo iliy-okuwa imeanza kufutika vichwani mwa warundi wengi. Hapa in-aonekana Rais Nkurunzinza ame-sahau historia hiyo, historia am-bayo nae ni sehemu yake, amesa-hau kuwa yeye huko nyuma kabla hajawa Rais alikuwa kiongozi wa waasi wa CNDD-FDD akiongoza mapambano dhidi ya serikali.

Hivyo basi ni vema busara imu-ingie ndani ya kichwa chake. Nku-runzinza aache kung’ang’ania ma-daraka kwani wakati wake umei-sha. Ni vema apishe wengine watawale ili aishi kwa amani la sivyo anawaweka warundi katika chuki na visasi vya kila aina.

Nahitimisha nasaha hizi kwa kumnasihi Rais Nkurunzinza at-engue kauli yake hiyo ya kuwa ‘at-agombea tena’, awaangalie akina mama na watoto wanaoteseka ho-vyo, watoto, na wakubwa wanao-lia kwa sasa kwa kupoteza wazazi na wapendwa wao akumbuke damu hiyo itamuhukumu huko baadae.Naomba kuwasilisha!

Simu: 0658010594.

Kwa hali hii, Rais nkurunziza ajitafakarinaamini raiS huyo ndani ya naFSi yake anaJua

kuwa anaenda kinyume ila kutokana na hulka ya viongozi wetu wa bara la aFrika kulewa

madaraka, ameamua kuJiFanya kiziwi

YuSuFu ahmaDi

naSaha za WiKi

Page 7: Imaan Newspaper issue 6

www.islamicftz.org

29 Rajab 1436, jumatatu mei 18 - 24, 2015

7matuKio KatiKa Picha

Rais Kikwete akikaribishwa na mwenyekiti wa taasisi ya Dhin Nureyn Islamic Foundation , Sheikh Said abri.

Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya madaktari.

Rais jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na madaktari walioletwa na taasisi ya al muntada aid. aliyevaa suti nyeusi ni kiongozi wa madaktari hao, Dk Khalid al Fawadh.

mwenyekiti wa the Islamic Foundation, aref Nahdi akiwa na Dk abdulrahman al Radhiian katika hafla ya kuwaaga madaktari hao.

Rais Kikwete akiwa na na baadhi ya watoto waliofanyiwa upasuaji.

Page 8: Imaan Newspaper issue 6

www.islamicftz.org

29 Rajab 1436, jumatatu mei 18 - 24, 2015

8

Watoto wenye ulemavu wanakabiliwa na mti-zamo hasi kutoka kwa watu wanaowazun-

guka. Hali hiyo, inawapelekea kushindwa kukabiliana na mazin-gira yao kwa ufanisi.

Moja kati silaha zinazoweza kuwakomboa watu wenye ulemavu kifikra, kiuchumi, kijamii na hata kisiasa ni elimu. Elimu ni muhimu kwa walemavu kama ambavyo ili-vyo muhimu kwa binadamu yoyote.

Elimu humpa mtu uwezo wa kutawala mazingira na kujiletea maendeleo. Msisitizo wa elimu kwa watu wenye ulemavu, hususan wa-toto, unatakiwa uwe maradufu.

Kwa nini baadhi ya wazazi hu-wanyima watoto fursa ya kusoma?

Mwanzo, nimezungumzia kuhusu mitizamo hasi ya jamii kwa watu wenye ulemavu. Ni mitizamo hiyo hasi ndio inayopelekea baadhi ya wazazi na walezi kunyima watoto wenye ulemavu fursa ya elimu. Pia, wazazi huwaona watoto wenye ule-mavu kama mzigo, na hivyo kutow-apeleka shule. Baadhi ya wazazi huona aibu kumtoa mtoto nje.

Lakini, ukweli ni kwamba, elimu kwa mtoto mwenye ulemavu humpa nafasi mtoto kujiendeleza. Uzoefu unaonesha Allah hamnyimi mja wake kila kitu. Hata mtoto mle-

mavu hutokea kuwa na kipaji katika mambo fulani. Akipelekwa shule kipaji hicho kinaweza kuendelezwa na kumsaidia mtoto kujitegemea

katika kutafuta riziki na mambo mengine.

Unapomnyima mtoto mlemavu fursa ya kwenda shule, unamhuku-

mu kumtenga pekee mbali na jamii, yaani, akae nyumbani tu. Hali hii ya kutengwa, huku akiona wenzake wanaenda shule kunamfanya ahisi

ulemavu wake kwa uzito na kujiona kweli yeye ni tofauti.

Shime wanajamii, tuwapeleke shule watoto walemavu, sio tu kwa faida yao, bali pia, kwa faida ya fa-milia, jamii na taifa kwa ujumla. Usipomuelimisha mtoto mwenye ulemavu ujue kuwa, unamjengea utegemezi wa milele.

Muhimu zaidi ikumbukwe kuwa, Allah alipotuagiza tusome, hakubagua mtu mkamilifu wa vi-ungo peke yake, bali hata mtu mwenye ulemavu.

elimu kwa watu wenye mahitaji maalum

SheiKh taWaKKal juma

KutoKa KatiKa QuR’an’ na Sunnah

Katika makala iliyopita t u l i o n a w a s o m i mbalimbali hasa wana-sayansi wanapoamua

kuisoma Qur’an wanashangazwa sana pale wanapoikuta inazun-gumzia mambo ya elimu ya anga, jua, mwezi nk. Ndani ya Qur’an zimezungumziwa elimu au sayansi mbalimbali.

Juhudi, utafiti na ugunduzi anu-wai unaoonyesha ukweli wa Qur’an kisayansi ni kazi ndogo sana kulin-gana na maajabu ya kitabu hiki kitukufu, ambacho maajabu yake hayaishi wala hayataisha.

Wakati huo huo, mara kadhaa pamekuwa na matukio ya kutaka kuchomwa kwa kitabu kitukufu cha Qur’an na kundi jingine la wanaojii-ta wasomi, kama lilivyokaririwa tukio la mhubiri mmoja wa Florida nchini Marekani kutaka kuchoma moto maelfu ya nakala za Qur’an tukufu.

Mimi pamoja na wewe msomaji tunaweza kujiuliza, ni nani hasa huyu anayekariri mara kwa mara kutaka kuichoma moto Qur’an tukufu? Je anayetaka kufanya hivyo ni mhubiri kweli wa kikristo? Kwa nini hasa anataka kufanya hivyo? Ana akili timamu kweli?

Kwa upande wa Wakristo, hebu na wajiulize swali hili wakati wana-tafakari juu ya mhubiri huyo. Kama mtu anaweza kuandika jina la Yesu Kristo katika kipande cha karatasi mara 29, kisha akampa Mkristo ili

akichome, je atakichoma kweli kika-ratasi hicho?

Vile vile, lau ingetokea mtu akaandika jina la Nabii Mussa (Am-ani iwe juu yake) katika kipande cha karatasi, kisha akampa Myahudi akichome, atakichoma kweli kikara-tasi hicho?!

Nasema hivi kwa sababu ndani ya Qur’an, jina la Yesu Kristo limeta-jwa tena kwa heshima kubwa, mara 29, na jina la Nabii Mussa (Amani iwe juu yake) limetajwa mara 129! Wakati jina la Muhammad (Rehma na amani ziwe juu yake) limetajwa mara nne (4) tu!

Zaidi ya hapo, Mitume wote 24 waliotajwa ndani ya Qur’an wako katika Biblia. Kwa hakika wanaota-ka kuchoma Qur’an ni sawa na ku-taka kuchoma jina la Yesu Kristo, jina la Nabii Mussa na majina ya

Mitume wote 24 (Amani iwe juu yao).

Tatizo ni kuwa, kati ya wote hao wanaotaka kuichoma Qur’an, haku-na hata mmoja ambaye amewahi kuisoma Qur’an. Jambo la muhimu ni kuwashauri wasome walau tafsiri ya Qur’an kwa lugha zao, ambayo bila shaka kwa wakati wetu huu Qur’an inapatikana takriban katika lugha zote kuu za kila nchi.

Wakishaisoma, kwa hakika watajuta sana, na kuona ni jambo la kipumbavu kabisa kufikiria kuki-choma kitabu kama hiki.

Katika Qur’an, tuhuma zote za tabia mbaya, utovu wa nidhamu na maadili dhidi ya Maria, mama yake Yesu Kristo, na mitume wengine, zi-lizotajwa katika vitabu tofauti, zime-kanushwa na kukataliwa katu.

Tena Mama Maria amepewa

heshima ya juu kabisa ndani ya Qur’an, na kutajwa kuwa miongoni mwa wanawake wachache watuku-fu wa duniani.

Ukisoma Qur’an, utaona namna ilivyoeleza, tena kwa lugha ya heshi-ma, kuzaliwa kwa Nabii Mussa, na hata namna alivyooa. Hakuna hata neno moja la kejeli limetumika nda-ni ya Qur’an kwa yeyote miongoni mwa Mitume waliotajwa katika Biblia!

Kwa nini sasa Qur’an inataka ku-chomwa!? Mantiki inaonyesha pen-gine busara ya wachomaji hao inge-wapelekea kuvichoma vile vitabu ambavyo vimewatuhumu Mitume wa Allah kwa tuhuma zisizo na msingi wowote.

Pengine hapo wangeweza kuonekana kidogo kuwa wana akili. Sina shaka kuwa watu wanaotaka

kuichoma Qur’an, siku wakiisoma wataiona kuwa ni kitabu bora kuliko vitabu vyote duniani!

Kila neno la Qur’an ni la Mungu, Mungu wa Nabii Adamu, Mungu wa Nabii Ibrahimu, Mungu wa Na-bii Mussa na Yesu Kristo (Amani ya Allah iwe juu yao wote). Hakuna hata neno moja la Qur’an limebadi-lika kwa muda wa miaka zaidi ya 1400.

Qur’an ni kitabu pekee, ambacho bado kiko katika uasili na utimilifu wake. Tena kipo ambacho kimehifa-dhiwa katika uasili wake hadi leo, ikiwemo katika nchi ya Uturuki.

Kama tulivyoona katika makala zilizotangulia ni dhana potofu kabi-sa kudai kuwa Qur’an, iliandikwa na Mtume Muhammad (Rehma na amani ziwe juu yake).

Inawezekanaje kwa mtu kama Muhammad (Rehma na amani ziwe juu yake) ambaye alikuwa hajui kusoma wala kuandika aweze kuan-dika kitabu chenye kurasa zaidi ya 600 pasina kukosea, tena aelezee nadharia za juu kabisa za sayansi na mambo ya anga!?

Muhammad alikuwa hawezi hata kuweka saini yake katika barua alizokuwa akituma kwa watawala wa nchi mbalimbali wakati wake, bali alichokuwa akifanya ni kupiga muhuri wake uliokuwa na jina lake.

Endelea kufuatilia safu hii, uji-funze mengi kuhusu kitabu ki-tukufu cha Qur’an………

Mhubiri wa Kikristo anapotaka kuchoma moto Qur’an

habiib hamim

mahuSiano Ya KibinaDamu

ndani ya Qur’an, Jina la yeSu kriSto limetaJwa tena kwa heShima kubwa, mara

29, na Jina la nabii muSSa (amani iwe Juu yake) limetaJwa mara 129! wakati Jina la

muhammad (rehma na amani ziwe Juu yake) limetaJwa mara nne (4) tu!

elimu kwa mtoto mwenye ulemavu humpa

naFaSi mtoto kuJiendeleza.

uzoeFu unaoneSha

allah hamnyimi mJa

wake kila kitu

Page 9: Imaan Newspaper issue 6

www.islamicftz.org

29 Rajab 1436, jumatatu mei 18 - 24, 2015

9

Si jambo lenye kup-ingika kwamba s iasa na dini havitengani. Kwa

Waislamu neno siasa lina maa-na ‘jinsi ya kuongoza mambo ya watu’.

Neno hili lilitumiwa na Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) aliposema katika ha-dith iliyopokelewa na Abi Hurayrah (Radhi za Allah juu yake): “Wana wa Israili wa-likuwa wakiongozwa na mana-bii wao, kila alipokufa nabii (Al-lah) alimtumiliza nabii mwingine” (Bukhari).

Kwa hiyo siasa, nyumbani kwao ni katika Uislamu. Itashangaza akitokea Muislamu akasema Waislamu wasijihu-sishe na siasa. Jambo la kuzin-gatiwa ni kuwa siasa isiende kinyume na sharia.

Mtu anaweza kujiuliza, kati-ka nchi kama hizi zisizoongozwa kwa sharia itakuwaje? Wanawa-zuoni wa zama wametoa fat-wa kwamba, inajuzu kwa Waislamu katika nchi za kisekula kujihusisha na siasa, maadam kufanya hivyo kuna maslahi na Uislamu na Wais-

lamu.Tukijikita katika mada ya leo,

vyama vya siasa Tanzania vimew-ageuza Waislamu mawakala wao, pasina Waislamu kufaidika na vya-ma hivyo. Hali imekuwa hivi tangu wakati wa kudai uhuru wa nchi hii.

Tafakari, tangu uhuru, Waislamu wamefanywa nini na kwa nini? Ku-vunjwa EAMWS na kuundiwa Bak-

wata, kutaifishwa shule za Waisla-mu, kukataliwa mahakama ya ka-dhi.

Sakata la mabucha ya nguruwe, mauaji ya mwembechai, kukataliwa kujiunga na OIC, kamata kamata ya masheikh na kuwekwa ndani, huku wengine wakiuawa, sheria ya ugaidi inayowalenga Waislamu …orodha ni ndefu.

Kwa muda mrefu Waislamu wamekuwa wakiilalamikia serikali kuhusu kuwalazimisha mambo yao kusimamiwa na Bakwata. Hali ilivy-ofikia sasa ni kwamba, hata Waisla-mu wakitaka kusajili taasisi ni lazima wapate ‘clearance’ ya Bakwata.

Ingawaje kuna taasisi lukuki za Waislamu Tanzania zilizosajiliwa, serikali haijishughulishi nazo vya ku-tosha, kana kwamba hazipo.

Mawasiliano yote kutoka serika-lini kwenda kwa Waislamu, yanape-lekwa Bakwata, utadhani kuna makubaliano maalum baina ya Waislamu na serikali kwamba, mambo yao yapelekwe huko.

Hakuna mwenye ugomvi na Bakwata, kwani hiyo nayo ni taasisi ya Kiislamu.Tatizo ni pale serikali inapowalazimisha Waislamu kuwa chini ya Bakwata.

Kumbuka suala la muswada wa sheria uliokwama kuhusu Mahaka-ma ya Kadhi Tanzania, jinsi Bakwata ilivyokuwa ipewe mamlaka ya ku-teua na kusimamia makadhi, na ku-weka taratibu nyingine za mahaka-ma hiyo.

Laiti si busara za bunge kupitia Kamati yake ya Kudumu ya Sheria na Kanuni kuona umuhimu wa

kukutana na taasisi mbali mbali za Kiislamu kupata maoni yao, hilo lin-gepita na kuwaweka Waislamu kati-ka kitanzi cha Bakwata, tena safari hii kupitia sheria ya bunge.

Kwa serikali ya chama tawala ku-tojihusisha na taasisi mbali mbali za Waislamu na kuikumbatia Bakwata pekee ijue kuwa siyo tu inawanyima Waislamu wengine fursa ya kutoa mchango wao kujenga nchi, bali pia inajinyima yenyewe kupata fikra, maoni na mchango wa Waislamu.

Pamoja na hayo, Waislamu ha-wajabweteka, bali wameutumia uhuru wao wa kikatiba kwa kujiletea maendeleo yao wenyewe, huku wak-ipata ushirikiano kiduchu kutoka serikalini.

Kwa kiasi fulani, tunaweza kusema, hali hii ni kuto-kana na nchi kuwa chini ya chama kimoja cha sia-

sa kwa muda mrefu. Lakini je, kwa hali inavyokwenda, hivi vyama vingine vya siasa vina muelekeo wa kuwajali Waislamu?

Au navyo vikiingia madarakani vitaendeleza hali ya kutowajali Wais-lamu? Hadi hapa tulipofika, hakuna dalili yoyote njema kwa Waislamu kutaraji kwamba kwa kutawala vya-ma vya upinzani kutakuwa na nafuu yoyote kwa Waislamu.

Lakini pia, tunawezaje kuvilau-mu vyama hivi kama Waislamu wenyewe hatufanyi uraghibishi na kuwaeleza viongozi wa vyama hivyo madai yetu hata kabla havijaingia madarakani? Watajuaje mala-lamiko, madai na matarajiwa yetu kwao?

Mwaka 2007, Waislamu wa Kenya, baada ya kuona chama tawa-la hakiwasikilizi walifanya uraghibi-shi kwa vyama vya upinzani na hata kufikia kuingia navyo itifaki ya mari-dhiano (MoU), kwamba vikishika hatamu vitayashughulikia masuala ya Waislamu.

Kufanya hivyo si kuvunja ma-fundisho ya dini, kwani Mtume Mu-hammad (Rehma na amani ziwe juu yake) aliingia mikataba ya maridhi-ano (MoU) mingi iliyoweka mazin-gira mazuri kwa Waislamu. Kadha-lika, kufanya hivyo sio kuvunja kati-ba ya nchi, kwani ibara ya 20 (1) im-eweka wazi uhalali wa jambo hili.

Ibara ya 20 (2) inakataza chama kuundwa kwa misingi ya kidini. La-kini kutaka ushirikiano na vyama vya siasa kama walivyofanya Waisla-mu wa Kenya kwa maslahi ya Wais-lamu si kukibadili chama hicho kiwe cha kidini.

Je viongozi wetu wa taasisi mbali mbali za Kiislamu wanaliona hili? Au sira ya M tume tunaisoma kikas-uku tu? Umefika wakati Waislamu tukakumbuka wosia wa Profesa Kighoma Ali Malima aliposema, “Don’t’ moan, organize”, yaani Msila-lame, jipangeni.

Uchaguzi mkuu mwaka 2015 hauko mbali, kazi kubwa iliyo mbele ya Waislamu ni kuhakikisha kwamba, hatuwi mazulia ya kukan-yagwa na wengine ili waingie ma-darakani.

Katika kuwapima wanasiasa wa vyama mbali mbali, wafikishiwe madai ya Waislamu, kisha waeleze bayana watayashughulikia vipi

madai hayo wakiingia madarakani. Msikibague chama chochote, hata chama tawala kipeni madai yenu.

Lengo liwe kama walivyosema Waislamu wa Kenya katika MoU yao na vyama vya upinzani mwaka 2007 kwamba:

“…desire to see our country Ken-ya as a just, harmonious, peaceful and prosperous nation based on good governance, constitutionalism and rule of law, pro-poor policies….

positive upliftment of the status and welfare of Muslims in Kenya and the correction of historical and struc-tural injustices and marginalization meted on Muslims through deliber-ate policies and programmes.”

“…tunatamani kuona nchi yetu Kenya ikiwa nchi ya haki, utulivu, amani na taifa lenye ustawi ulioege-mezwa katika utawala bora, katiba na utawala wa sheria, sera za kuwa-jali masikini….

kuinuliwa chanya kwa hadhi na maslahi ya Waislamu wa Kenya na kusahihishwa kwa madhila ya kihis-toria na kimuundo na kubaguliwa kulikowafika Waislamu kupitia sera na mipango ya makusudi”.

Jamani watu wa vyama vya siasa hili nalo ni dhambi kufanyika nchini mwetu? Au ndiyo mtasema “litah-atarisha amani”? maana hiki sasa ndiyo kichaka cha kuwanyima watu haki zao siku hizi.

Tanzania ni yetu sote, tukinyama-za kimya wakati mambo hayaendi sawa tutakuwa watu waovu kabisa, kama Mwanafalsafa wa ki-Irish, Ed-mund Burke (1729 – 1797) alivyose-ma:

“The only thing needed for evil to thrive is for good people to remain si-lent” - “Kitu pekee kinachohitajika ili uovu ustawi ni watu wema kun-yamaza kimya”.

ncha Ya KalamuSheiKh muhammaD iSSa

Waislamu, tusilalame, tujipange Tukatae kuwa zulia la kufutia tope

taFakari, tangu uhuru,

waiSlamu wameFanywa

nini na kwa nini?

kuvunJwa eamwS na kuundiwa bakwata,

kutaiFiShwa Shule za

waiSlamu, kukataliwa

mahakama ya kadhi.

Page 10: Imaan Newspaper issue 6

www.islamicftz.org

29 Rajab 1436, jumatatu mei 18 - 24, 2015

10 www.islamicftz.org

29 Rajab 1436, jumatatu mei 18 - 24, 2015

11

Rajab, mwezi mtakatifu

makala maalum

makala maalum

NA ABUU MAYSARA

Ba a d a y a S a u d i a k u k at a a masharti ya Iran kuhusu ma-hujaji wake wanapokwenda nchini Saudia na kuendelea

kwa Iran kususia Hijja kwa mwaka wa tatu mfululizo, hatimaye mwaka 1990 mazungumzo kati ya nchi hizo mbili yal-ianza.

Waziri wa mambo ya nje wa Saudia, Sa’ud al-Faisal na mwenzake wa Iran, Ali Akbar Velayati wakakutana New York, Marekani kuzungumzia Hijja ya mwaka 1991.

Ni aibu iliyoje, hata mambo yahusuyo Hijja ya Waislamu yanakwenda kuzun-gumziwa New York, mji wa kikafiri. Vela-yati akatangaza:

“Mahujaji wetu wataweza kufanya ibada ya ‘Hijja-siasa’ (religious-political hajj ritual) mwaka huu” (Velayati, IRNA, 4 Oktoba 1990).

Baada ya mazungumzo hayo, kauli mbali mbali za viongozi wa pande zote mbili, Saudia na Iran, zikawa za kujenga zaidi kuliko kubomoa. Hijja ya mwaka 1991 ikaenda vizuri pasina tukio lolote na hata ile ya mwaka uliofutia.

Mwisho wa maandamano ya Iran Makka?

Mwaka 1993 msimu wa Hijja, kama ilivyo miaka yote, pande zote mbili zikakaa tayari kukabili changamoto za Hijja kwa mahujaji wa Iran.

Hakukuwa na dalili zozote za mabadi-liko kwa mahujaji wa Iran kufanya maan-damano yao ya ‘kulaani washirikina’ kama walivyoyaita.

Katika maandamano hayo yaliyotara-jiwa kufanyika Mei 27, 1993, mahujaji 115,000 wa Iran walitarajiwa kupaza sauti zao wakisema, ‘Kifo kwa Marekani, kifo kwa Israeli’.

Kwenye maandamano haya, kulito-kea sintofahamau kati ya polisi wa Sau-dia na mahujaji wa Iran katika eneo wal-ilopangiwa kufanya maandamano yao.

Polisi wakawaamuru waandamanaji kurejea walikotoka, jambo ambalo liliti-bua hali ya amani iliyotawala kwa miaka miwili nyuma.

Reyshahri, mwakilishi wa kiongozi wa Iran katika Hijja, haraka haraka akawakusanya mahujaji wa Iran huko Mina na kuwapa ujumbe wa Ali Khama-nei.

Reyshahri akaondoka Saudia huku akiulaumu utawala wa Saudia kwa ku-vunja mapatano ya awali.

Saudia haikujibu kitu juu ya shutuma hizo, bali ikaamua kupiga marufuku ka-bisa maandamano hayo ya mahujaji wa Iran wakati wa Hijja, kwa kuwa yanain-giza siasa katika ibada ya Hijja na kuon-doa utulivu kwa mahujaji wengine.

Saudia ilichukua uamuzi huo kwa maslahi ya utulivu katika msimu wa Hij-ja. Kiukweli, Saudia ilikuwa ikisubiri

fursa kama hiyo ili iyapige marufuku maandamano hayo ya mahujaji wa Iran.

Lakini ni kwa nini Iran ilishikilia ku-fanya maandamano haya ya kisiasa wakati wa ibada ya Hijja? Bila shaka Iran iliiona Hijja ambayo hukusanya Waisla-mu kwa mamilioni kutoka dunia nzima kama nyenzo muhimu ya kusambaza fikra zake za mapinduzi ya kishia.

Iran ingetamani iwe mahala pa Sau-dia ili ieneze ushia dunia nzima. Kwa hiyo kila inapopata fursa ya kuisham-bulia Saudia itafanya hivyo.

Wakati ikiituhumu Saudia kwa kuwa na uhusiano na mataifa ya magharibi, yenyewe ina uhusiano mzuri tu na matai-fa ya mashariki.

Waislamu wengi ni vipofu wa hili kwa sababu Iran ina mfumo mzuri wa propa-ganda na mikakati kuliko Saudia.

Tazama Yemen, Saudia imekuwa ikii-saidia Yemen kwa fedha nyingi, lakini kimkakati Iran iliizidi Saudia hadi ma-Hauthi wakaiteka nchi nzima.

Baada ya Saudia kuzuia maandamano hayo ya mahujaji wa kishia, Iran haikuanzisha mashambulizi ya maneno kwa Saudia kama awali, bali zikatoka kauli za kawaida tu, kama ile iliyotolewa na Spika wa Bunge la Iran, Ali Akbar

Nateq-Nuri, ambaye kwa kawaida ni mkosoaji mkali wa Saudia.

Alinukuliwa akisema: “Tunaamini ua-muzi wa Saudia unatokana na msukumo wa wengine kutoka nje kuzuia maanda-mano. Lakini hili halitovunja uhusiano wetu.

Kila siku tutaboresha mafungamanao yetu na nchi za ukanda huu na majirani zetu, na tutamaliza masuala yetu kwa ma-zungumzo ya pande mbili” (Nateq-Nuri, mahojiano na Middle East Insight, Julai-Agosti 1993).

Inaelekea Hijja ni moja ya maeneo am-bayo huathiri sana uhusiano wa Saudia na Iran. Mwaka 1994, Saudia ilipunguza idadi ya mahujaji wa Iran kutoka 115,000 hadi nusu ya idadi hiyo.

Iran haikulalamika sana. Huenda ni kwa sababu wakati huo ilikuwa ikikabili-wa na uhaba wa fedha za kigeni, hivyo wakaona kama ahueni kwao.

Hata katika wakati wa msimu wa Hijja wenyewe, Saudia ikachukua hatua ku-dhibiti maandamano ya mahujaji wa Iran na kupelekea kiongozi wa Hijja wa Iran kuachana na mpango huo na kuishia ku-wahutubia mahujaji katika viwanja vya Mina tu.

Kitendo cha Iran kukubaliana na hat-

ua zilizochukuliwa na Saudia ingawaje kwa shingo upande ilikuwa dalili kwamba Iran ilikuwa ikiona haja ya kuwa na uhu-siano mzuri wa kidiplomasia na Saudia.

Lakini hali hii haikujitokeza hivi hivi tu. Iran ilikuwa inakabiliana na tatizo la uasi wa masunni ndani ya nchi yao.

Idadi ya Masunni nchini Iran inaka-diriwa kuwa asilimia kumi hadi kumi na mbili ya wananchi wote wa Iran.

Januari mwaka 1994, mamlaka ya mji wa Mashhad nchini Iran iliamua kuvunja msikiti wa masunni kwa kile kilichoe-lezwa ni mradi wa upangaji mpya wa mji.

Febuari mosi mwaka huo, wakazi wa mji wa Zahedan ambao ni mji mkuu wa jimbo la Baluchistan lenye wakazi wengi masunni walisababisha vurugu kubwa ambazo ziliishia kwa watu kadhaa ku-uawa na wengine wakijeruhiwa.

Juni 20, bomu likalipuka katika jengo lenye kaburi la Imam Reza huko Mash-had, wakati wa sherehe za kishia za Ashu-ra na kuua watu ishirini na sita. Iran ika-watuhumu waasi wa kundi liitwalo Mu-jaadina e- Khalq.

Kuzuka huku kwa ghafla kwa vurugu za masunni nchini Iran kulidhihirisha kwamba vurugu za kidini kati ya Sunni na Shia katika maeneo yanayotembelewa na mahujaji haziepukiki hata huko Iran kwenyewe.

Eneo la Mashahad ni eneo takatifu sana kwa mashia, na mashia takriban milioni nane huzuru kila mwaka katika kile kiitwacho “Hijja ya watu masikini” kutofautisha na Hijja ya Makkah, kwani huko huenda watu wenye uwezo mkubwa kumudu gharama za safari.

“Karbala inapaswa iwe Qibla cha ulimwengu wa Kiislamu, Kwa sababu imam

hussein ameziKwa pale” - nuri al-maliKi

mGOGORO SauDIa Na IRaN: SIaSa au DINI? - 2Baada ya vurugu hizi za kidini nchini humo,

Iran ilipunguza mashambulizi kwa utawala wa Saudia na kujikita katika kujikuribisha kwa masunni kuliko kuchochea mitafaruku baina ya sunni na shia. Kipindi hiki kilitawaliwa na juhudi za eti mapatano kati ya Sunni na Shia.

Pamoja na kuonekana kwamba Iran ina uchun-gu sana na Makka na Madina kuwa mikononi mwa Saudia, ukweli ni kwamba kwa mashia Mak-ka si mahali patukufu kuliko Karbala au Najaf.

Ni imani ya mashia kwamba siku moja Makkah itaangamizwa na Karbala itachukua nafasi ya Makka kama inavyosimuliwa katika hii simulizi ya kishia ifuatayo.Imepokewa kutoka kwa Imam Ja-far Siddiq;

“Wakati fulani ardhi ya Ka’bah ilitangaza kwa kujisifu, ‘ni ardhi gani iko kama mimi? Allah ame-ijenga nyumba yake juu yangu. Watu kutoka sehe-mu mbali mbali za dunia huja kunizuru. Nimefan-ywa mtakatifu na Allah’.

Kusikia hivyo, Allah akasema, ‘nyamaza! Tafakari (kabla yakusema zaidi). Kwa nguvu zangu na utukufu wangu, ubora na umaarufu nilioipa ar-dhi ya Karbala ni zaidi ya nilivyokupa wewe.

Kulinganisha na Karbala, wewe ni kama tone sawa na kichwa cha sindano mbele ya bahari. Kama vumbi la Karbala lisingekuwa pale, nis-ingekupa wewe hadhi niliyokupa.

Kama yule aliyepumzika Karbala (Imam Hus-sein) asingeumbwa, nisingekuumba wewe, wala nyumba ambayo unajifakharisha kwayo.

Kuwa mnyenyekevu na mwenye haya na usiwe na kibri na majivuno, usijaribu kujikweza juu ya Karbala kwa umuhimu, vinginevyo nitakugha-dhibikia na kukutupa Jehannam.” (Kaamil al-Ziarat, uk. 267, hadith Na. 13, Al-Wasaail cha Al Hur Al-‘amiliy, uk. 403).

Kwa hiyo, si jambo la kushangaza kwamba, Desemba 27, 2013, aliyekuwa Waziri Mkuu wa Iraq, Nuri al-Maliki, alinukuliwa na vyombo vya habari vya Iraq akisema: “Karbala inapaswa iwe Qibla cha ulimwengu wa Kiislamu, kwa sababu Imam Hussein amezikwa pale.”

Yaani, mashia wanatamani siku Qibla cha Waislamu kitakapobadilika kutoka mji mtakatifu wa Makka kama alivyoagiza Allah katika Qur’an 2:244 kwenda Karbala, Iraq.

Huu ndio mkakati wa mashia na hatari ya ush-ia. Lakini ni vigumu kwa Muislamu wa kawaida kuyajua haya, kwani mashia ni mabingwa wa ku-ficha dhamiri yao kupitia “Taqiyyah,” ambayo ni nguzo katika dini yao.

Ndiyo maana Saudia inapinga Iran kumiliki si-laha za nyuklia, kwani iwapo Iran itamiliki silaha za nyuklia, na kwa kuwa mashia wanaamini kuwa Makka itakuja kuangamziwa, na kwamba, Karba-la ndiyo inayopaswa kuwa Qibla, kuna hatari kwamba, silaha hizo zitakuja kutumika kuian-gamiza Makka na Madina pia.

Kwa hiyo, mzizi wa fitna wa mgogoro baina ya Iran na Saudia siyo siasa, bali tofauti kati ya ushia na usunni, na sera ya Iran kueneza mapinduzi yake ya kishia mashariki ya kati na duniani kote.

Lebanon, Iraq, Syria, Bahrain na sasa Yemen ni nchi ambazo Iran inaona imefanikiwa lengo lake. Mpango huu wa Iran unaoitwa, “The Internation-al Islamic Awakening”, ulianza tangu enzi za Kho-meini.

Ukitilia maanani imani za kishia kuhusu Mak-ka kama tulivyoona hapo nyuma, ni taifa gani la mashariki ya kati liwezalo kuikabili Iran kama siyo Saudia?

Kwa hiyo, utaona kila mara malumbano ni kati ya Saudia na Iran, kwanza, kwa kuwa Saudia ndiyo msimamizi wa miji mitakatifu kwa Waislamu wote, yaani Makkah na Madina, na pili, ndiyo tai-fa la kisunni lenye nguvu miongoni mwa mataifa ya kisunni kwa sasa.

Ni bahati mbaya wasunni wasiojua yote haya, wamemeza propaganda za mashia dhidi ya Sau-dia, wakiiona Iran ndiyo mkombozi wa Waislamu duniani. Hata katika vita vya Yemen, ni Saudia ndiyo ya kulaumiwa na huku Iran wakionekana Waislamu wazuri.

Nahofia kuwa siku Waislamu hao wataka-potanabahi na kugundua kwamba, Iran haikuwa ikipigania Uislamu wa kweli, bali ushia wao, wa-takuwa wamechelewa sana.

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Iraq, Nuri al-Maliki akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Karbala kuwa Qibla cha waislamu, 2013.

Karbala inayodaiwa kuja kuwa Qibla kipya cha waislamu

Page 11: Imaan Newspaper issue 6

www.islamicftz.org

29 Rajab 1436, jumatatu mei 18 - 24, 2015

12

Namna ya kuoga janaba na tofauti kati ya kuoga janaba na hedhi:

Swali: Iliulizwa Kamati ya Ku-dumu ya Fat-wa, je kuna tofauti kati-ka kuoga janaba kati ya mwanaume na mwanamke? Je mwanamke hu-takiwa kufumua nywele zake au ata-jimwagia maji makonzi matatu kama hadith inavyoeleza? Na kuna tofauti gani kati ya josho la janaba na hedhi?

Jawabu: Hakuna tofauti ya jinsi kati ya josho la janaba la mwanamke na mwanaume, na wala hakuna yeyote kati yao anayetakiwa kufumua nywele zake kwa ajili ya josho, bali in-akidhi kujitiririshia makonzi matatu ya maji na kisha kujimiminia maji kwenye sehemu yote ya mwili.

Na hii ni kwa ushahidi wa hadith ya Ummu Salamah (Allah amridhie), aliyemwambia Mtume (Rehma na amani ya Allah ziwe juu yake): “Mimi ni mwanamke ninayesuka nywele zangu, je nizifumue wakati wa kuoga janaba?” Mtume akasema: “Usifum-ue, inakidhi kukitiririshia kichwa chako makonzi matatu, kisha jimim-inie maji, utasafika” (Muslim). Na endapo kama kwenye kichwa cha mwanamme au mwanamke kuna sidri au rangi inayozuia maji kufika kwenye ngozi, hapo italazimu kuon-doshwa. Na kama itakuwa hafifu kia-si cha kutozuwia maji kufika kwenye ngozi, hakuna lazima ya kuiondosha.

Ama kuhusu josho la hedhi la mwanamke, wanazuoni wametofau-

tiana katika suala la ulazima wa kufumua nywele wakati wa kuoga, ila sahihi ni kuwa, halazimiki kufumua ny-wele kwa ajili ya kuoga hedhi. Na hii inatoka-na na baadhi ya ri-waya z i l i zo-pokewa kutoka kwa Ummu Salamah na a m b a z o z i p o

k w e n y e Sahih Mus-lim.

Yeye alise-ma: “Mimi ni mw a n a m ke n i -nayesuka nywele zan-gu, je nizifumue waka-ti wa kuoga hedhi na janaba?” Akasema Mtume: “Usizifumue, inakidhi kukitir-irishia kichwa chako makonzi matatu, kisha jimiminie maji, utasafika”. Riwaya hii ndio hoja ya kutowajibisha kufumua nywele kwa ajili ya kuoga hedhi au janaba. Lakini kiasili, mwanamke atafumua nywele zake wakati wa kuoga hedhi kama se-

hemu ya tahadhari na kujiondoa kutoka katika khilafu na kuzi-

fanyia kazi dalili zote. (Fatawa Lajnatud Daimah 5/320).

Kufumua ny-wele wakati

wa kuoga hedhi:

Swali: Al-i u l i z w a

S h e i k h M u h a -mad bin

Ibrahim Alu Sheikh (Allah

amrehemu): Ni ipi hukumu ya ku-

f u m u a n y w e l e wakati wa kuoga hedhi?

Jawabu: Kauli sahihi na dalili yenye nguvu ni

kutofumua nywele wakati wa hedhi, kama ambavyo si wajibu

katika janaba, isipokuwa kufumua nywele wakati wa hedhi ni jambo li-

nalotakiwa kwa sababu ya kuwepo kwa uthibitisho.

Ummu Salamah Allah amridhie alimuuliza Mtume: “Mimi ni mwan-amke ninayesuka nywele zangu, je

nizifumue wakati wa josho la jana-ba?” Na katika riwaya na ‘hedhi.’ Akasema: “Usifumue inakidhi kuz-itiririsha makonzi matatu, kisha jimwagie maji, utasafika”. (Muslim). Na huu ndio uteuzi wa mwenye kita-bu kinachoitwa Al-inswaaf na Imam Zarkashiy. Ama katika kuoga janaba si sunna kufumua nywele, na ndivyo aonavyo Swahaba Abdallah bin Omar (Allah amridhie) na ndivyo al-ivyokuwa akisema Bi Aisha (Allah amridhie): “Kwanini nisiwaamuru wanawake wanyoe nywele zao”. Kwa kipengee hiki, kufumua nywele kati-ka janaba si jambo la kisharia, isipokuwa limesisitizwa wakati wa hedhi, na huko kutiliwa mkazo kwake kutatofautiana kulingana na wepesi na ugumu wa kufumua ny-wele. (Fatawa na Rasaailu za Sheikh Muhamad bin Ibrahim 2/81).

Je inalazimu kuyafiki-sha maji kwenye ngozi wakati wa kuoga jana-ba:

Swali: Aliulizwa Sheikh Muha-mad bin Saleh Uthaimin (Allah am-rehemu): Mwanamke anapokuwa na janaba na akaoga, je anapoziosha nywele zake hutakiwa kuyafikisha

maji mpaka kwenye ngozi?

Jawabu: Kuoga janaba na men-gineyo ni katika mambo ya wajibu katika josho, na ndani yake kuna kuyafikisha maji kwenye ukanda wa nywele kwa mwanaume au mwan-amke. Na hii inathibitishwa na neno la Allah: “Mkiwa na janaba jitwahari-sheni” (5: 6).

Wala haijuzu kwa mwanamke kuosha sehemu ya juu ya nywele pe-kee, bali ni lazima maji yafike kwenye vishina vya nywele na ngozi ya kichwa. Na ikiwa kasuka, halazimiki kufumua bali wajibu juu yake ni kufi-ka maji kwenye kila oteo la nywele. Anaweza akauweka msuko wa ny-wele kwenye mfereji wa maji na kisha akaziminya nywele zake mpaka maji yakapenya kwenye nywele zote. (Ra-sailu Sheikh Ibn Uthaimin 4/226).

Je hulinganishwa nywele ndefu za mwanamke zisizosukwa na za mwa-namke aliyesukwa:

Swali: Iliulizwa Kamati Ya Ku-dumu ya Fat-wa, je hulinganishwa mwanamke mwenye nywele ndefu zisizosukwa na za mwanamke ali-yesuka wakati wa kuoga janaba, au ni lazima azioshe nywele zake zote?

Jawabu: Inamlazimu mwan-amke mwenye janaba na aliyemaliza hedhi yake aeneze maji kwenye mwili na nywele zake kwa nia ya twahara, sawa nywele zake zikiwa ni fupi au ndefu, na sawa ikiwa zimesukwa au hazikusukwa. (Fataawa lajnatud Daimah 5/323).

NamNa ya kuoga

fat-wa kwa mwaNamKe wa KiiSlamsheikh shabani Mussa

Mwaka 2014, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Rais, Dk.

Jakaya Mrisho Kikwete, ilitangaza azma yake ya kuboresha hali ya lishe nchini. Azma hiyo ilikuja baada ya serikali kubainisha kuwa hali ya lishe nchini hairidhishi na tatizo la utapi-amlo (lishe duni) limeeendelea kuia-thiri jamii ya watanzania.

Serikali imefafanua kuwa tatizo la utapiamlo unaotokana na ulaji un-aozidi mahitaji ya mwili, linaendelea kuongezeka na linaathiri zaidi kwa wakazi wa mijini. Tatizo hilo hupele-kea magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama vile ugonjwa wa moyo, kisukari, kansa, shinikizo la juu la damu, unene na uzito kupita kiasi, upungufu wa nguvu za kiume na kike.

Ili juhudi hizi za serikali ziweze ku-leta matunda yanayotarajiwa, wa-nanchi ngazi ya familia lazima wajuwe wajibu wao na kuutekeleza.

Ugumu wa mafanikioKwa mujibu wa fani ya ulaji vyaku-

la, binadamu anahitaji nguvu za ziada ili kushinda matamanio yake ya ulaji mbaya. Ukiwatazama watu wengi wanaoishi katika miji wakiwemo wa-somi, viongozi wa aina na ngazi mbalimbali wakiwemo wale wa siasa na dini, na watu wenye kipato cha ku-mudu angalau milo mitatu kwa siku, nidhamu yao katika kufuata kanuni

za ulaji bora ni mbaya sana. Hata watalaamu wa

tasnia ya habari ambao kama wanavyooamini, ni muhimili wa nne wa dola wenye wajibu wa kufik-ishe elimu ya lishe katika jamii, bado wengi wao ha-waamini kama ulaji mbaya unadhuru afya na ni kikwazo kwa maen-deleo ya taifa.

U k i t a k a kupata uthibit-isho kuwa watu wen-gi hawali kwa nidhamu, andaa hafla yenye chakula cha bure, na kila mtu mruhusu ajiwekee kiasi anacho-taka. Watu wengi watajiwekea chaku-la kingi, watakula kupita kiasi na watabakiza chakula katika sahani zao. Ndio kusema, watu hao watafanya is-rafu. Katika Dini Tukufu ya Kiislamu, watu wanahimizwa kula vilivyo bora na kunywa vilivyo bora, lakini wana-katazwa kufanya israfu, kama tunavy-ojifunza katika aya ifuatayo.

“Enyi wanaadamu! Chukueni mapambo yenu wakati wa kila Sala; na kuleni (vizuri) na kunyweni (vizu-ri). Lakini msipite kiasi tu (msifanye israfu). Hakika yeye (Mwenyezi Mun-

gu) hawapendi wapitao kiasi”. (Qur’an. 7:31). Mtu anakumbuka kuchunga kanuni za ulaji unaofaa baada ya kupata ugonjwa, na kupewa angalizo na tabibu. Huu ndio ugumu wa kupa-ta mafanikio katika dhana nzima ya lishe bora, ambayo Mh. Rais Kikwete na serikali yake wameamua kuivalia njuga.

Hivi karibuni, daktari bingwa wa jijini Dar es Salaam, Dk. Ali Mzige, ali-wakumbusha watanzania kuwa mtu mzima anashauriwa kula nusu kilo ya nyama kwa wiki moja, mayai matatu kwa wiki moja. Na hivyo ndio viwango vinavyoshauriwa na nchi mbalimbali.

Lakini, baadhi ya watu kila siku wana-kula supu tena ya nya-ma nyekundu, chipsi-mayai na nyama cho-ma. Jiulize, kwa siku

saba za wiki wamekula

nyama na mayai kia-s i g a n i h a w a ?

Sasa tuta-nusurika v i p i n a m a -gonjwa ya m o y o , kansa, kis-

ukari, unene na uzito kupita kiasi, up-ungufu wa nguvu za kiume na kike, kama hatuna nidhamu katika ulaji wetu?

Ndio kusema, ratiba ya aina hii ni kinyume na utaratibu wa kula unao-himizwa na matumizi ya lishe bora. Lazima mtu mmoja mmoja, familia na taifa zitekeleze wajibu wao, kama kauli mbiyu ya kampeni ya uhama-sishaji wa matumizi ya lishe bora iliy-ozinduliwa na serikali mwaka jana ili-yohimiza: ‘Lishe Bora ni Msingi wa Maendeleo: Timiza Wajibu Wako’.

Ni kitendo cha aibu na cha ufaha-mu mbaya juu ya Uislamu kama tuta-

muona Muislamu hasa mwenye elimu japo kiasi ya Qur’an na Sunna, anakula bila nidhamu na kuzingatia kanuni za ulaji unaoleta siha bora. Kwa sababu, kwa mwislamu kula kwa kuzingatia kanuni za ujenzi wa afya bora ni wajibu wa kidini.

Ukubwa wa tatizo la lishe

Kwa mujibu wa takwimu za mwa-ka 2010 kama zilivyoelezwa na seri-kali hivi karibuni, asilimia 42 ya wato-to walio na umri chini ya miaka mi-tano wamedumaa, asilimia 16 wana uzito pungufu na asilimia tano wame-konda. Aidha, takwimu hizo zi-naonyesha kuwa asilimia 59 ya watoto wenye umri kati ya miezi sita hadi 59 wana upungufu wa damu, asilimia 33 ya watoto chini ya miaka sita wana upungufu wa vitamini A.

Pia, takwimu hizo zinabainisha kuwa asilimia ya wanawake walio ka-tika umri wa kuzaa yaani miaka 15 hadi 49 wanapata changamoto mbalimbali za kiafya zinazosababish-wa na lishe duni za upungufu wa damu, matatizo ya ukosefu wa madini joto mwilini, upungufu wa uzito na baadhi ya mama wajawazito kuwa na tatizo la ukosefu wa vitamini A.

Simu: 0655 654900

ugumu wa kupata mafaNikio ya lishe boRaPazi MwinyiMvua

afya yaKo

Page 12: Imaan Newspaper issue 6

www.islamicftz.org

29 Rajab 1436, jumatatu mei 18 - 24, 2015

13

Sifa njema na shukran anastahiki yule ambaye ametukamilishia dini yetu na akairidhia kuwa

mfumo kamili wa maisha yetu. Re-hma na amani zimfikie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Rehma na amani ziwe juu yake) kisha salam kwa wanaofuata muongozo.

Katika Makala yetu ya leo ndugu msomaji, In Sha Allah, tutadurusu juu ya Mushaarakah ambayo ni moja kati ya njia mbadala ya riba. Mushaarakah ni mkataba wa ku-shirikiana ambao unatokana na dhana nzima ya “Sharikah”. Shari-kah ina maana ya ushirikiano. Ush-irika umegawanyika katika matapo mawili yaani Sharikatul-Milk na Sharikatul -‘Aqd.

Sharikatul-Milk ni ushirika wa watu wawili au zaidi katika umiliki wa mali fulani. Ushirika huu un-aweza kuwa kwa namna nyingi. Un-aweza kuwa kwa maamuzi na rid-haa ya washirika. Kwa mfano, watu wawili wakikubaliana kununua ny-umba watakuwa na umiliki wa pamoja katika nyumba hiyo. Wakati mwingine unatokea bila washiriki kuamua hivyo. Kwa mfano, mtu ak-ifariki warithi wake wanaweza kuwa na umiliki wa pamoja katika baadhi ya mali zake. Ama kuhusu Shari-katul-‘Aqd, huu ni ushirikiano un-aoundwa kwa makubaliano yanay-owekwa kwenye mkataba baina ya washirika. Aidha kuna aina tatu za Sharikatul-‘Aqd ambazo ni Shari-katul-Amwaal, Sharikatul-A’amal na Sharikatul-wujuuh.

Sharikatul-Amwaal ni ushiriki-ano ambao kila mshiriki anawekeza kiwango fulani cha mtaji katika bi-ashara inayofanywa pamoja na wa-shirika. Sharikatul-A’amal ni ushiri-kiano katika kutoa huduma fulani ambapo washirika hugawana ada wanayotoza kwa uwiano walioku-baliana. Kwa upande mwingine, Sharikatul-wujuuh ni ushirikiano ambapo washirika hawana mtaji bali wananunua bidhaa kwa mkopo na hulipa deni baada ya kuuza kwa pesa taslimu na kugawana faida.

Musharaka hujumuisha Shari-katul-Amwaal na wakati mwingine Sharikatul-a’amal.

Kanuni za msingi za mushaarakah

Namna ya kugawana faida iain-

ishwe wakati wa kuingia mkataba wa ushirika katika biashara. Kwa mfano washirika wanaweza kuku-baliana kuwa mshirika mmoja ata-pata 40% ya faida na mwingine ata-pata 60% ya faida. Kutokuwa na makubaliano kabla ya kuanza bi-ashara yaani katika wakati wa ku-funga mkataba kutafanya mkataba huo wa ushirika usikubalike kishar-ia. Kwani kuanza biashara au ku-subiri faida ipatikane ndio washirika wakubaliane namna ya kugawana faida kunaweza kutoa mwanya kwa

washirika kugombana na hata kud-hulumiana.

Kiwango cha mgao wa faida ki-natakiwa kiende sawa na faida halisi iliyozalishwa na sio kiwango cha mtaji uliochangiwa na mshirika. Kwa mfano, hairusiwi kukubaliana mshirika kupata asilimia fulani ya mtaji wake kama faida, lakini in-aruhusiwa kukubaliana mshirika kupata asilimia fulani ya faida halisi itakayopatikana baada ya kufanya biashara kwani katika biashara kuna faida na hasara na kiwango cha faida

au hasara hubadilika mara kwa mara kulingana na hali ya kibiashara katika soko.Hivyo, kukubaliana ki-wango cha asilimia fulani cha faida juu ya mtaji wa mshirika ni kum-hakikishia mshirika huyo faida am-bayo wakati inaweza kupatikana au isipatikane na pia faida halisi inawe-za kuwa ndogo au kubwa zaidi ya ki-wango hicho.

Hivyo basi, ni lazima asilimia ya mgao wa faida iwe sawa na asilimia ya mtaji wa mshirika katika jumla ya mtaji wa biashara? Mathalani

mshirika wa kwanza ametoa asilim-ia 40% ya mtaji mzima wa biashara, je ni lazima apate 40% ya faida itakayopatikana?

Wanazuoni wametofautiana juu ya jambo hili. Kwa mtizamo wa Imam Malik na Imam Shafi’i, ni laz-ima kwa kila mshiriki apate kiwango cha faida kinachowiana na asilimia ya mtaji wake aliowekeza katika bi-ashara. Kwa upande mwingine, mti-zamo wa Imam Ahmad ni kuwa in-ajuzu mshirika kupata mgao wa fa-ida kwa kiwango kisichowiana na asilimia ya mtaji wake katika bi-ashara endapo patakuwa na maku-baliano ya kuridhiana bila kushu-rutishwa baina ya washirika. Hivyo inajuzu kwa mshirika aliyewekeza 40% ya mtaji wote wa biashara kupata mathalani 60% ya faida na mshiriki mwingine aliyewekeza 60% kupata 40% ya faida (Unaweza kurejea Ibn Qudamah, Al-Mughni, (Beirut: Dar al-Kitab al-Arabi, 1972), 5:140).

Rai ya Imam Abu Hanifah in-aweza kuchukuliwa kama njia ya kati ya mitizamo hiyo miwili kwani yeye mtizamo wake ni kuwa inajuzu katika hali ya kawaida mshiriki kupata asilima ya mgao wa faida isi-yowiana na asilimia ya mtaji alio-wekeza katika biashara. Ingawa, iki-wa mshirika amebainisha wazi hatoshiriki katika shughuli za kila siku za uendeshaji na usimamizi wa biashara hiyo, mgao wake wa faida hautozidi asilimia ya mtaji wake ka-tika biashara. Kwa mfano kama amewekeza 40% ya mtaji, hatoweza kupata zaidi ya 40% ya faida. (un-aweza kurejea Al-Kasani, Bada’i‘ al-Sana’i‘, 6:162–63).

Kwa upande mwingine wana-zuoni wote wamekubaliana juu ya mgawanyo wa hasara. Kila mshirika anatakiwa kubeba hasara kwa uwiano wa mtaji wake. Kwa mfano, mshirika aliyechangia 40% ya mtaji anatakiwa kuchukua 40% ya hasara tu bila kupunguza au kuongeza. Hivyo, kwa ujumla makubaliano juu ya mgawanyo wa faida bila kuz-ingatia uwiano wa mtaji yanakuba-lika lakini hakuna makubaliano ka-tika mgawanyo wa hasara nje ya mgawanyo unaozingatia uwiano wa mtaji wa washirika katika biashara.

+255713996031 [email protected] biashara na uchu-mi

uchumi na biashara JaMaL issa

watu maarufu wasiokuwa waislamu waSemavyo KUhUSU UiSlamU

mushaarakahKutoKuwa na maKubaliano Kabla ya

Kuanza biashara yaani KatiKa waKati wa Kufunga mKataba Kutafanya mKataba huo

wa ushiriKa usiKubaliKe Kisharia

reverend bosworth smith

Head of the State as well as the Church, he was Caesar and Pope in one; but he was Pope without the Pope’s pretensions, and Caesar without the legions of Caesar, without a stand-

ing army, without a bodyguard, without a police force, without a fixed revenue. If ever a man ruled by a right divine, it was Muhammad, for he had all the powers without their supports. He cared not for the dressings of power. The simplicity of his private life was in keeping with his public life.

Tafsiri: “mkuu wa dola pamoja na dini, alikuwa (kama) kaisari na Papa wakati mmoja; lakini alikuwa Papa pasina madoido ya upapa na kaisari pasina vikosi vya kaisari, pasina jeshi la kudumu, pasina mlinzi binafsi, pasina jeshi la polisi, pasina pato maalumu la kudumu. kama kuna mtu alipata kutawala kwa haki itokanayo na mwenyezi mungu, alikuwa muhammad, kwa sababu alikuwa na nguvu zote pasina mihimili yake. kamwe hakujali kujivika vazi la madaraka. ule wepesi wa maisha yake ya binafsi uliendana na maisha yake ya kijamii”. (muhammad and muhammadanism, london, 1874)

Page 13: Imaan Newspaper issue 6

www.islamicftz.org

29 Rajab 1436, jumatatu mei 18 - 24, 2015

14

sheikh abDallah bawaZiR

Juma lililopita, aliyekuwa Rais wa Yemen, Ali Abdal-lah Saleh aliibuka kutoka mafichoni na kutoa tamko

kali lililolenga kuchochea vita huko Yemen kufuatia kushtadi kwa op-eresheni kimbunga inayoongonzwa na Saudi Arabia iliyofanikiwa kuisambaratisha ngome ya Wa-houth katika jimbo la Sa’ada na kuli-vunja jumba la fakhari la Rais huyo aliyeng’olewa madarakani.

Hatua hiyo ya mashambulizi makali kwa upande wa Saudi Arabia ilikuja baada ya Wahouth kuisham-bulia kwa makombora miji ya mipa-kani mwa Saudi Arabia kwa upande wa kaskazini, Jezan na Najrani.

Rais aliyeng’olewa madarakani Ali Abdallah Saleh katika tamko hilo, aliwahimiza wananchi wa Yem-en wasimame imara dhidi ya ma-shambulizi hayo na kuwataka wa-pambane kufa na kupona, na wasi-jali hasara yeyote itakayojitokeza.

Aidha aliwaahidi wananchi wa Yemen kwamba, nyumba zilizovun-jwa, na silaha zote zilizoteketezwa zitafidiwa. Na mwisho aliwapongeza waliouwawa katika vita hivyo kuwa wamekufa shahidi na wale ambao ni majeruhi aliwaombea nafuu ya har-aka.

Ikumbukwe, huko nyuma nchi ya Yemen ilikuwa ni nchi ya Kifalme na ilikuwa ikitawaliwa kwa silsila ya Maimam. Mwaka 1962, serikali ya kifalme ya Yemen ilipinduliwa na al-iyekuwa Rais wa kwanza wa Yemen Jeneral Abdallah Yahya Sallal.

Katika kipindi hicho Saudi Ara-bia ilikuwa inaongozwa na Mfalme Feisal bin Abdulaziz ambae alikuwa anamuunga mkono Mfalme wa Yemen. Na Misri kwa wakati huo ilikuwa inaongozwa na Rais Jamal Abdu Nasser aliyekuwa anaungam-

kono mapinduzi ya Yemen.Rais aliyeng’olewa madarakani

Ali Abdallah Saleh aliingia madar-akani mwaka 1978 na kuanza kuion-goza Yemen baada ya mtangulizi wake Rais Ahmad Husein Al-ghash-imi kuitawala Yemen kwa muda wa miaka 33.

Ndugu msomaji, huyu Rais aliyeng’olewa madarakani Ali Ab-dallah Saleh, ni Rais wa sita wa Jam-huri ya Kiarabu ya watu wa Yemen. Naye alikaa madarakani kwa kipindi cha miaka 33 hadi alipong’olewa madarakani mwaka 2012 kwa ngu-vu ya umma.

Taarifa za mtandaoni za hivi kar-ibuni zilidokeza kuwa Rais Ali Ab-dallah Saleh ana uchu mkubwa wa kurudi tena madarakani baada ya kuondolewa kwa nguvu ya umma lakini mara hii ni kwa kupitia daraja la mapinduzi ya wana mgambo wa Houth na nguvu za askari waasi wa-naomuunga mkono.

Rais aliyeng’olewa madarakani alihamasisha vijana kwa lugha ya ki-naya kwenye mabaki ya nyumba yake, na kuwataka wapambane na mashambulizi ya Saudi Arabia aki-amini wangeweza kumrejesha ma-darakani akisahau kuwa ni vijana

hao hao ndio waliomng’oa madar-akani.

Mtume (Rehma na amani ya Al-lah iwe juu yake) alisema: “Ukikosa haya fanya ulitakalo”.

Eti leo ndio Ali Abdallah Saleh anawaahidi wa Yemen kwamba ma-jumba na miundo mbinu yao iliyo-vunjwa itajengwa, silaha zao zilizo-teketezwa zitafidiwa, lakini haelezi roho za wananchi zinazopotea na damu zinazomwagika kwa sababu yake zitafidiwa na nani?

Pia haelezi hao majeruhi anaow-aombea dua wapone haraka ni kwa matibabu gani na hospitali zipi,

wakati nchi hivi sasa haitawaliki na Wahouth wanashambulia kila kitu?

Ndugu msomaji, kama hali ya mashariki ya kati itaendelea hivi kwa mafahali wawili kushindwa kuishi kwenye zizi moja kwa kuvumiliana, ni dhahiri kwamba ipo katika ardhi ya volkano, na wakati wowote in-aweza ikalipuka.

Vita ya Yemen haitokani na ku-gundulika kwa kisima kikubwa cha mafuta kama inavyodaiwa na baa-dhi ya waandishi. Ikumbukwe mse-maji wa rasilimali ya mafuta na madini wa Yemen aliwahi kusema mnamo Januari 24, 2006 kuwa wamegundua kisima kikubwa cha mafuta kwenye mji wa Al-hudeidah.

“Kisima hiki kipo mahali pazuri na hakivuki mipaka ya Yemen, kina upana wa kilometer 250 X 70 na ki-nakadiriwa kuwa kinaweza kutoa mapipa bilioni 120”, msemaji huyo alisema.

Hiki ni kisima kinachojitegemea na wala hakianzii sehemu ya Iraq na Saudi Arabia kama inavyodaiwa. Ili kukuthibitishia kuwa hii haikuwa siri kubwa, rais wa wakati huo Ali Abdallah Saleh alitangaza: “Mapato yatakayopatikana katika kisima hi-cho yatatumika katika kuboresha huduma za afya, elimu na miundo mbinu”. (angalia: www.alternatehis-tory.com).

Ugomvi wa Yemen una mambo mawili tu. Iran inataka kujitanua ili kuikamata Mashariki ya Kati na hasa Saudi Arabia, ilipo misikiti mi-wili mitukufu na maeneo matakatifu kwa Waislamu. Saudi Arabia na wa-shirika wake wanalinda maslahi yao na mipaka yao na kujihadhari na vit-isho vya Iran na washirika wake.

Mwezi uliopita mshauri wa Rais wa Iran alijifaragua katika tovuti ya Al-arabia akisema: “Iran hivi sasa imeshakuwa enzi kuu (empire), na makao yake makuu yapo Baghdad”. Mshauri huyo aliendelea: “Iran haitasita kuendeleza himaya yake hadi Yemen na kwenye lango la Mandab bila ya kujali kipingamizi chochote kutoka kwa wenye siasa kali, Mawahabi na Mayahudi”.

Maneno haya yalileta mjadala mkubwa katika televisheni ya Al-jazira, na kusababisha watu kujiuli-za, ‘kulikoni?’ Na baada ya muda mfupi, ndipo operesheni kimbunga chenye ndege mia moja kutoka Sau-di Arabia zilipoelekezwa Yemen.

Sasa hivi Wahouth wame-takabari, hawataki kusikiliza la mtu, wanadharau makubaliano ya kusiti-sha vita na hawataki misaada ya kib-inaadamu iwafikie wahanga.

Kabla ya wiki mbili au tatu zilizo-pita Wahouth waliwashambulia na kuwauwa wananchi hamsini wa Yemen waliokuwa wanaikimbia nchi kwa boti. Tukio hili la kusikiti-sha lilisababisha Waziri wa Mambo ya Nje wa Yemen kulia hadharani wakati anatoa hotuba kwenye bara-za la Umoja wa Mataifa.

Tunamuomba Allah A’zza Wajal-la awasaidie ndugu zetu hawa wa Yemen na sisi tulio huku atuhifadhi na janga kama hilo.

Wabillahi tawfiq 0713215989

Vita vya yemen si mafuta ni uchochezi

makala ya kimataifa

Aliyekuwa Rais wa Yemen, Ali Abdallah saleh akiwa mbele ya mabaki ya kasri lake baada ya kushambuliwa na majeshi ya muungano.

Page 14: Imaan Newspaper issue 6

www.islamicftz.org

29 Rajab 1436, jumatatu mei 18 - 24, 2015

15

maPitio ya viTabU

mlango wa Nne – hadith zenye kukataliwa

Dhaifu: Ni hadith ambayo haina baadhi ya sifa za usahihi au haina sifa zote.

Munqatwi’u: Ni ile ambayo mtiririko wa upokezi wake (sa-nad) haikuungana kwa jinsi yoyo-te ile kukatika kutakavyokuwa.

3. mu’adhwalu: Ni hadith ambayo wamedondoka kutoka kwenye sanad yake (wapokezi) wawili au zaidi, katika nafasi yoy-ote, kwa sharti la kuzidiana na ku-fuatana kwa wadondokaji.

4. mursalu ya Taabi’iyyu: Ni hadith ambayo Taabi’I ameipe-leka hadi kwa Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake), kama kuse-ma Taabi’iyyu: “Alisema Mjumbe wa Allah (Rehma na amani ziwe juu yake). Kwa hakika ni dhaifu kwa wanawazuoni wa hadith kwa

kuchukulia kuwa mdondokaji pamoja na swahaba ni Taabi’ au mataabi’ wawili au zaidi.

5. mu’allaqu: Ni hadith am-bayo wameondoshwa toka mwan-zoni mwa sanad yake baadhi ya wapokezi wake au wote. Na ali-yeondoshwa iwapo anajulikana na ni mwenye kutegemewa hu-tolewa hoja (hadith hii) sahihi na iwapo si hivyo basi (hadith hii) ni dhaifu.

6. mu’an’an: Ni hadith am-bayo wanaisimulia baadhi ya wasimulizi wa sanad au wote kutoka kwa walio juu yao kwa tamko (Kutoka kwa) kama vile “Imesimuliwa kutoka kwa fulani (nae) kutoka kwa fulani…).

Basi kwa hakika hiyo ni yenye kuunganika na kukubalika kwa sharti la kusalimika na udangany-ifu hao wenye kupokelewa hadith

kutoka kwao (Almi’an’an) na kuthibiti kukutana baina yao (wasimulizi na wapokeaji kutoka kwao). Kama hili halipo, basi (ha-dith Mu’an’an) ni dhaifu na yenye kukataliwa.

7. Shaadhu: Ni ile ambayo ameipokea mwenye kutegemewa tofauti na hadith aliyoipokea mwenye kutegemewa zaidi kuliko yeye, pamoja na kukosekana uwezekano wa kukusanya (pamo-ja upokezi huo kuwa mmoja).

8. Ni ile hadith aliyoipokea mpokezi dhaifu tofauti na hadith aliyoipokea mpokezi aliye bora kuliko yeye miongoni mwa wana-otegemewa.

9. mu’allalu: Ni hadith am-bayo imeonekana ndani yake ina (kasoro) inayotia dosari usahihi wake ingawaje dhahiri yake huonekana imesalimika na dosari hiyo.

10. mudhtwaribu: Ni hadith ambayo imepokelewa mara hii kwa namna fulani na mara ny-ingine kwa namna nyingine to-

fauti na ile ya mwanzo kwa namna inayolingana (kwa usahihi) na isi-yumkinike kukusanya baina (ha-dith hizo mbili ili kuondoa mkan-ganyiko huo).

Hukumu yake ni kukubaliwa pindi mkanganyiko wake un-a p o k u w a k a t i k a w a p o k e z i wakutegemewa katika sanad yake, kama si hivyo huhukumiwa kuwa ni dhaifu na yenye kukatali-wa.

11. matruuku: Ni hadith ambayo haijulikani ila kutoka kwa mpokezi mmoja tu mwenye kutuhumiwa kwa urongo au ufaa-siq au mwenye kupindukia katika kukanganya mambo.

12. mudallasu: Ni hadith ambayo amedanganya ndani yake mpokezi kwa aina miongoni mwa aina za udanganyifu. Nayo ni ya aina mbili;-

- Udanganyifu katika sanad: Ni asimulie msimulizi wa hadith kutoka kwa mpokezi aliyekutana nae yale ambayo hakuyasikia kuto-ka kwake akisingizia kumsikia.

- Udanganyifu katika Masheikh wa hadith: Nako ni kusimulia kutoka kwa sheikh (wa hadith) hadith aliyoisikia kutoka kwake kisha akamtaja sheikh wake kwa yale ambayo hanayo ili asijulikane kutokana na udhaifu alionao au kwa udogo wa umri wake.

13. mursalu al-Khafiyyu: Ni msimulizi kusimulia kutoka kwa mtu aliyeishi nae zama moja yale ambayo hakuyasikia kutoka kwake kikauli, akasingizia kusi-kia.

14. mudraju: Ni hadith am-bayo msimulizi ameingiza katika matini yake matamshi yasiy-okuwa ya hadith hiyo pasi na ku-bainisha (kwamba hayo si katika hadith hiyo).

15. mawdhu’u: Ni habari ya kuongopa iliyonasibishwa kwa Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) kumsingizia. Haijuzu kuiinua hadi kwa Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) pasina kubainisha (kwamba hayo si maneno ya Mtume).

“Watu wema ni watu wema, wawe wa dini yoyote, na watu wao-vu ni waovu; wawe wa dini yoyote ile. Kama watu wema wenye ku-pendelea viumbe wenzao mema hawashikamani, basi waovu wenye kumfuata shetani watashinda na watatawala.” Prof. Ibrahim Noor Shariff

Prof. Ibrahim Noor Shariff, mwanachuoni wa Chuo Kikuu Cha Rutgers, New Jersey, Marekani. Ib-rahim, msomi wa Sanaa, Tarikh (Historia) na Fasihi ya Kiswahili ameandika kitabu kipya cha Kiswahili kuhusu ‘Udini na Uba-guzi’ Tanzania.

Mwandishi kakusudia kuandi-ka kitabu chake kwa Kiswahili ili ukweli uwafikie watu wengi ambao kila siku wanatiwa sumu za udini Tanzania. Hivyo basi, inawajibika kila mtanzania asome kitabu hiki, hususan wakubwa wa serikali, wa-nasiasa, mapadri na masheikh.

Makusudio ya kitabu hiki ni kuihifadhi nchi yetu na sumu za chuki za udini zinazopaliliwa kwenye masomo ya vijana wa leo ambao ni viongozi wa kesho.

Inatakiwa kila mwenye uwezo, afanye juhudi kuondoa propagan-da shuleni/ vyuoni mwetu, ili his-toria ya kweli ifundishwe. Kitabu hiki ‘Tanzania na Propaganda za Udini’ kina milango mitatu na sa-hifa 152.

Mlango wa Kwanza, unahusu ‘Taarikh ya kuwasili kwa Wabantu, Washirazi na Waarabu Pwani ya Afrika ya Mashariki.’ Hapa anawa-silisha ushahidi wa taarikh usioka-talika, kwamba, Waarabu walifika pwani ya Afrika Mashariki maelfu ya miaka iliyopita na Wabantu wamefika pwani hiyo katika karne ya 16 B.K. Makusudio ya mlango huu ni kuonesha kwamba, Waara-

bu si wageni, bali ni wenyeji, wenye haki sawa na wenyeji wengineo.

Mlango wa Pili, unazungumzia ‘Propaganda za siasa za chuki na athari zake’. Humo tunaona uovu wa propaganda za udini zilizo-watuhumu Waarabu na Waswahili Waislamu peke yao kukamata, ku-uza na kumiliki watumwa. Propa-ganda hizo zimepelekea kuuliwa maelfu ya Waislamu bila ya sababu Zanzibar, nchi yenye Waislamu wengi ilipovamiwa, na kumezwa na Tanganyika 1964.

Katika Mlango wa Tatu, ‘Tanza-nia na propaganda za udini shule-ni’, mwandishi ambaye ni Profesa wa Sanaa, anaonesha ubingwa wake wa kuchambua picha. Anatu-nakilia picha za kuchorwa kutoka-na na vitabu vya shule za Tanzania zinazoonesha Waarabu na Waswa-hili Waislamu wanawakamata, ku-wapiga na kuwauwa wanyonge wa Kiafrika ili kuwafanya watumwa.

Hapohapo Profesa Ibrahim, anaonesha uzushi wa picha hizo, zilizokopiwa na kubadilishwa kutoka picha za wauzaji watumwa wa Kizungu huko Amerika. Pia ameonesha kwamba, bila ya shaka picha nyingine zimebuniwa na wa-choraji na hazina ukweli.

Prof. Ibrahim Noor anakazia katika kitabu chake hiki kuyapitia na kuyatengeneza masomo ya taa-rikh (historia) katika shule za Tan-zania. Anataka masomo haya ya-jengwe kwenye misingi ya taarikh ya kweli na sio misingi ya uongo wa siasa za udini unaotokana na ukol-oni.

Prof. Ibrahim Noor anahad-harisha Watanzania wote na hatari ya kuendelea kupanda mbegu za chuki dhidi ya Waarabu, Wahindi na Waswahili na hasa Waislamu, katika mipango ya masomo Tanza-

nia. Hizi chuki za udini zitaleta ba-laa kubwa kuliko mauaji ya Zanzi-bar ya 1964. Watakaoumia na chu-ki hizi ni wafuasi wa kila dini na kila kabila nchini Tanzania.

Kitabu kinauzwa:

Dar es Salaam; Ibn Hazm Media Centre,

Msikiti wa Mtoro na Manyema, Simu: 0773 777 707

TAMPRO, Magomeni, bara-bara ya Morogoro, karibu na ofisi za Manispaa ya Kinondoni. Simu:

0714 151 532 Kalamu Education Founda-

tion (KEF), Magomeni, Dar es Sa-laam. Simu: 0776 525 268Zanzibar;

Masomo Bookshop, Zanzibar, Simu: 0242 232 652

kitabu: al Fusuul Fii mustwalahi hadiithi r-Rasuulimwandishi: haafidh Thanaau-llwaahi Zaahidymfasiri: Sheikh muhammad issa

kitabu kiPya: Tanzania na Propaganda za Udini mwandishi: Prof. ibrahim Noor Shariff

Page 15: Imaan Newspaper issue 6

www.islamicftz.org

29 Rajab 1436, jumatatu mei 18 - 24, 2015

16

Tanzania ni nchi ambayo ina-jipambanua kwa msimamo wake wa kutokuwa na dini. Inaelezwa kuwa suala la

dini limeachwa mikononi mwa raia, waamue upande wanaoutaka ili kuti-miliza malengo ya kuumbwa kwao na Allah.

Dhamira ya msimamo huo wa serikali ni kutaka kujiondoa na mi-gogoro ya kidini, ambayo ingeweza kujitokeza miongoni mwa raia wake.

Ukizingatia idadi ya dini zilizopo, ni dhahiri kama serikali ingejiingiza katika masuala ya dini ingejikuta ka-tika mtego wa machafuko.

Si kwa bahati mbaya serikali ime-fanya hivyo. Ilichukua uamuzi huo baada ya kutafakari kwa kina faida na hasara zake na ikaonekana ni vema raia wakapewa fursa na uhuru wa kuabudu, huku wakipewa sharti la kutovunja sheria za nchi.

Leo hii tunashuhudia jamii ya ki-tanzania wakijifaharisha na dini zao popote pale walipo. Kuna wanaoimba na kusifu. Kuna wanaovaa mavazi ya-nayojinasibisha na dini yao.

Watu wanaona fahari kudhihiri-sha hisia zao hadharani, kwani wa-naamini njia waliyopo ni salama na wana hakika watafika katika makazi yao ya mwisho wakiwa wenye kufani-

kiwa. Jambo la ajabu ni kuwa, kume-kuwa na uzito kwa Waislamu kujina-sibisha na dini yao. Wengi wetu tume-kuwa na hofu kubwa juu ya kujitan-gaza kuwa sisi ni Waislamu, na ku-waambia watu kuhusu mafundisho ya dini yetu.

Si vijana, si wazee, si wanawake, wala wanaume, wote tumekuwa kati-ka mkumbo mmoja, wa kuficha kile tunachokiamini. Matokeo yake, jamii inayotuzunguka haijifunzi ukweli un-aofundishwa ndani ya Uislamu. Kwa sababu hatuusemei Uislamu, wasio Waislamu wanabaki na dhana potofu, na hivyo kuharibu jina la Uislamu.

Umewahi kujiuliza, hivi hofu hii ya Waislamu inatoka wapi? Kwa nini kundi hili halina itikadi ya kujifahari-sha na Uislamu wao? Wapi tumeko-sea na kutoa mwanya kwa itikadi ny-ingine kuonekana ni zenye nguvu ku-liko Uislamu.

Bila shaka kuna tatizo. Masheikh, wasomi na wanazuoni wa Kiislamu wametoa maoni kuhusu suala hili ka-tika mahojiano na gazeti la Imaan, ambapo wengi wamesema, chanzo cha tatizo hilo ni hofu ya kutofikia malengo ya kidunia.

Kauli ya Baraza la vijana:Akizungumza na gazeti Imaan,

Amir wa Baraza la Vijana wa Kiislamu

Tanzania, Shabaani Mapeyo, amekiri uwepo wa tatizo hilo, hususan mion-goni mwa vijana.

Amir Mapeyo alisema, vijana wak-ishamaliza elimu yao ya sekula wame-kuwa wazito kudhihirisha imani yao, wakiogopa kukosa ajira.

Amir Mapeyo ameendelea kuse-ma, hata kwa wale ambao wamepata fursa ya kufanya kazi, bado wa-nashindwa kujinasibisha na dini yao wakihofu kutimuliwa kazi au kuto-pandishwa vyeo.

Mapeyo alisema: “Vijana wanaona kupata kazi ni kama bahati na kwamba, kitendo cha kuonesha ana-chokiamini, kitasababisha kuon-dolewa kazini, hoja ambayo ni nyepesi na haina mashiko”.

Kiongozi huyo wa vijana alisema, vijana lazima wafahamu riziki ina-pangwa na Allah (Subhanaahu Wataallah), na kwamba, hoja ya kupoteza kazi kwa kujifaharisha na kumtaja muumba wako pasi na ku-muonea soni haina mashiko.

Mapeyo aliwataka vijana ku-jiamini kwa ujuzi walioupata mafun-zoni na waamini kuwa wameajiriwa kutokana na utaalamu wao. Waki-fanya hivyo wataweza kuwa na uthubutu wa kupenda dini na kuitan-gaza kwa jamii na marafiki zao.

“Hivi sasa tuna tatizo. Tuna kundi kubwa la vijana wanamaliza vyuo, la-kini si mabalozi wazuri wa kutangaza Uislamu sehemu zao za kazi. Unakuta kijana anapata nafasi nzuri, anashindwa kutumia mwanya huo kuieleza kweli iliyomo ndani ya kitabu kitukufu”, alisema Hamisi Hussein, mhitimu wa shahada ya uhasibu, ak-iungana na mtazamo wa Amir Mape-yo katika swala hilo.

Wanawake watoa yao:Kwa upande wao, Baraza Kuu la

Wanawake wa Kiislamu Tanzania, nao wanaliona tatizo hilo kama la kimfumo, ambapo toka enzi za maba-bu zetu, Waislamu wamendelea ku-banwa hadi wanaogopa kujifaharisha na dini yao.

Naibu Katibu Mkuu wa Baraza hilo, Mayasa Sadallah alisema, hali hiyo ni janga la kiasili, ambalo kizazi cha sasa wanajaribu kupambana nalo.

Alisema, Waislamu wamekuwa wakionewa na kunyimwa uhuru kupitia mfumo uliopo, na kwamba, yeyote atakayethubutu kudhihirisha imani yake, atakumbana na misuko-suko.

Ametaja watu ambao walijaribu na kuishia pabaya kuwa ni pamoja na Waziri wa zamani wa Fedha, Marehe-

mu Kighoma Malima. “Lakini sio wote ni majasiri kama

Malima, na ndio maana wengine hu-ficha imani zao, na hata kutenda kama wasio Waislamu, ili tu wasiwekwe ka-tika kundi la waliopachikwa msamiati wa siasa kali,” ameeleza Mayasa na kuongeza kuwa:

“Hofu ya viumbe imekuwa kubwa kuliko ya Muumba, na hivyo basi watu wanaogopa. Lakini, lazima tumri-dhishe Mola wetu, kwa kuishi Kiisla-mu na kusema ukweli ili ujulikane, na Allah atatulipa.

Mayasa ametoa wito kwa jamii ya Kiislamu kuwaandaa vema vizazi vyao kwa kuwapatia elimu ya kutosha ili kujenga imani, uwezo wa kupam-banua mambo na kujenga hoja za ku-utangaza Uislamu popote pale walipo bila kuona haya.

Sheikh Hassani Chizenga, mmoja wa masheikh maarufu, aliyewahi kuwa kiongozi wa Bakwata, hakusita kutoa majumuisho ya nini cha kufan-ya ili kuweza kushinda vizingiti vina-vyowakabili Waislamu wa leo.

Sheikh anasema, fimbo nzuri ni umoja miongoni mwa waumini, ku-jiamini binafsi, kuamini mafundisho Uislamu na kufuata Sunna za Mtume Muhammad (Rehma na amani ziwe juu yake).

Pia, ameshauri Waislamu waache kupeana majina mabaya wenyewe kwa wenyewe, kwani hiyo ni mbinu ya kutugawa inayotumiwa na maadui, ambao huchukia kundi linalotekeleza Uislamu kiukamilifu.

Ni msiba unapoonea haya uislamu wakoseLeMani MaGaLi

mila na DeSTURi

Wakati Qur’an inaizun-gumzia safari ya Israa na Miraji, Mwenyezi Mungu alimsifu Mtume

wake (Rehma na amani ya Allah iwe juu yake) kwa nomino ya ‘Mtumwa wake’ (A’bdihi) na sio ‘Nabii wake’ (Nabiyyihi) au ‘mpenzi wake’ (Ha-bibihi).

Tunaweza tukajiuliza, je kuna hekima yoyote iliyopelekea kutumiwa kwa nomino hiyo kwa Mtume (Reh-ma na amani ya Allah iwe juu yake)?

Kwa mtu anayesoma taarifa za msafara huu wa ajabu na kuuzingatia umbali wake (Ni zaidi ya kilometre 1,200), na muda mfupi uliotumika (Ni kati ya Ishaa na Al-fajiri), bila shaka atapigwa na butwaa na kujiuli-za maswali mengi, na asipodhibiti utashi wake, anaweza akachupa mpaka, na kumtoa Mtume (Rehma na amani ya Allah ziwe juu yake) ka-tika utu, na kumvika daraja ya uun-gu/umwana wa Mungu n.k, kama walivyofitinika Manaswara kwa Issa mwana wa Maryam na mama yake.

Na ili hilo lisitokee kwa Waislamu, ndio Allah akaliweka wazi kupitia Qur’an, kwamba, pamoja na Mtume Muhammad kufikia daraja ya juu ka-tika utukufu, na kwenda mpaka mbinguni na kurudi ndani ya usiku mmoja, bado anabaki kuwa ni binaadamu na Mtumwa wa Allah.

Allah anasema: “Utukufu ni wake, Yeye aliyempeleka mja wake usiku (mmoja tu), kutoka Msikiti Mtukufu (wa Makkah) mpaka Msikiti wa mbali (wa Baytul Maqdis), ambao (tumeubariki na) tumevibariki vilivyo pembezoni mwake, tulimpeleka hivyo, ili tumuoneshe baadhi ya Ala-ma zetu. Hakika Yeye (Allah) ni Mwenye kusikia na mwenye kuona”.

(Al-israa: 1).Lugha hii iliyotumiwa na Qur’an

ni nyeti na imelenga zaidi kumtoa Mtume (Rehma na amani ya Allah ziwe juu yake) katika daraja ya Uun-gu/umwana wa Mungu na kumuacha na daraja yake ya Utume na Utumwa.

Na Mtume Muhammad (Rehma na amani ya Allah ziwe juu yake) vyo-vyote awavyo, bado anabaki kuwa ni binadamu, kama walivyo binadamu wengine, isipokuwa tofauti iliyopo kati yetu na yake ni Utume na Utumwa wa Allah.

Wanazuoni wanasema: “Lau kama Mtume (Rehma na amani ya Allah ziwe juu yake) angestahiki kuit-wa jina lingine tukufu zaidi kuliko hili, (Allah) angelimuita katika tukio hili tukufu” (Al-jamiu lia-hkamil-qur’an cha Imam Qur-tubiy:10/205).

Na Imam Al-qushayriy (Allah am-rehemu) anaeleza: “Allah alipom-pandisha Mtume wake (Rehma na

amani ya Allah ziwe juu yake) mpaka kwenye hadhara yake tukufu, na kumpandisha mpaka kwenye anga za juu, alimuacha na sifa ya utumwa ili kuonesha unyenyekevu kwa umma.” (Rejea Al-jamiu lia-hkamil-qur’an cha Imam Qur-tubiy:10/205).

Na hili ni fundisho kwetu, kwamba, hatutakiwi kuvuka mpaka katika kumsifu Mtume (Rehma na amani ya Allah ziwe juu yake), na kumtoa katika daraja ya utu na utumwa wa Allah, bali tunatakiwa tumsifu kama alivyosifiwa na Allah, au kama alivyojisifu mwenyewe, na si vinginevyo.

Kwa kuyazingatia hayo, Mtume (Rehma na amani ya Allah ziwe juu yake) anautahadharisha umma wake na kuutaka usichupe mpaka katika kumsifu kwa kusema:

“Msinisifu kama Manaswara wal-ivyomsifu Issa mwana wa Maryamu. Semeni Mtumwa wa Allah, kwani

Mimi ni Mtumwa wa Allah na Mtume wake.” (Bukhari: 3/543).

Mtume (Rehma na amani ya Al-lah ziwe juu yake) aliyasema hayo kwa kuuogopea umma wake usije ku-tumbukia kwenye dimbwi la mapenzi ya kijima, kama walivyotumbukia Manaswara, hata kumbatiza Issa mwana wa Maryam na Mama yake, daraja la uungu. Na kwa kuwa, utumwa wa Allah ni sifa adhimu kwa Mtume, ndio maana Allah akaitumia kwa Mtume wake katika matukio mbalimbali matukufu na nyeti, kama mifano ifuatayo inavyojieleza.

Allah anasema: “Utukufu ni wake, Yeye aliyempeleka mja wake usiku (mmoja tu), kutoka Msikiti Mtukufu (wa Makkah) mpaka Msikiti wa mbali (wa Baytul Maqdis), ambao

(tumeubariki na) tumevibariki vilivyo pembezoni mwake, tulimpeleka hivyo ili tumuoneshe baadhi ya Ala-ma zetu. Hakika Yeye (Allah) ni Mwenye kusikia na mwenye kuona (Al-israa: 1).

Na anasema: “Kuhimidiwa ni kwa Allah, ambaye amemteremshia mja wake Kitabu, wala hakukifanya kina upogo”. (Al-kahf: 1). Na anasema: “Ametukuka aliye teremsha Furqani kwa mja wake, ili awe mwonyaji kwa walimwengu wote.”( Al-furqan: 1).

Tanbih: Mja/Mtumwa ni mtu anayefuata na kutekeleza amri na maagizo ya bwana wake, kama inavy-ostahili, na kwa maana hiyo, ndio maana Mtume Muhammad (Rehma na amani ya Allah ziwe juu yake) akastahili kuitwa jina hili.

utumwa wa allah ni hadhi kwa mtumesafari ya iSRaa Na miRaJi na sheikh shabani Mussa

“utuKufu ni waKe, yeye aliyempeleKa mja waKe usiKu

(mmoja tu), KutoKa msiKiti mtuKufu (wa maKKah) mpaKa msiKiti wa mbali (wa baytul

maqdis), ambao (tumeubariKi na) tumevibariKi vilivyo pembezoni

mwaKe, tulimpeleKa hivyo, ili tumuoneshe baadhi ya alama

zetu. haKiKa yeye (allah) ni mwenye KusiKia na mwenye

Kuona”. (al-israa: 1).

Page 16: Imaan Newspaper issue 6

www.islamicftz.org

29 Rajab 1436, jumatatu mei 18 - 24, 2015

17makala ya kimataifa

na yusufu ahMadi.

MNAMO May 13, 2 0 1 5 , n c h i n i Marekani katika jiji la Texas, watu

wenye silaha za moto wanao-daiwa kuwa ni waumini wa dini ya Kiislamu walishambulia onesho la shindano la vibonzo (cartoons) vya Mtume Mu-hammad (Rehma na amani ziwe juu yake).

Pamoja na kuonesha vibon-zo hivyo, tukio hilo ambalo lil-iandaliwa na Taasisi ya Kutetea Uhuru ya Marekani (The American Freedom Defense Initiative) chini ya Rais wake, Bi. Pamela Geller, lililenga komkosoa Mtume Muham-mad (Rehma na amani ziwe juu yake) kuwa ni mchochezi.

Akiongea na kituo cha run-inga cha Fox News cha Mareka-ni na mtandao wa habari uit-wao Breitbart News baada ya shambulizi hilo, Geller ame-tetea onesho hilo kuwa lilikuwa ni sehemu ya uhuru wa kujiele-za na kuwa anaamini ni haki yake.

Kabla sijazungumzia dhana

hiyo tata ya uhuru wa kujieleza, ni vema wasomaji wakafahamu kuwa Geller ni mwanaharakati aliyejitolea kuupinga Uislamu na aliendesha kampeni ijulika-nayo kama ‘Zuia kusambaa kwa Uislamu nchini Marekani’ (Stop Islamization of America). Ni kwa sababu ya misimamo kama hiyo ndio maana Umoja wa Kupinga Udhalilishaji nchi-ni Marekani, (Anti-Defamation league), umelitaja kundi la Gel-ler kuwa ni la kueneza Chuki.

Turejee kwenye mada. Sawa ni dhahiri shahiri kuwa uhuru wa kujieleza anaoutetea Pamela ni nyenzo muhimu sana ya maendeleo ambapo watu ku-kosoana na kuelimishana. Hata tunaposikia watu wamehama dini moja kwenda nyingine (kusilimu) ni kwa sababu ya uwepo wa uhuru huo.

Lakini kuna maswali kad-haa lazima tujiulize na kuta-fakari. Je, uhuru huo wa ku-jieleza upo kwa watu au makundi yote? Je, ni watu au makundi yote yanayokubali changamoto za kukosolewa?

Miaka ya hivi karibuni, mpelelezi wa Marekani Bw. Ed-

tukio la texas, uhuru wa kujieleza au chuki za kidini?

ward Snowden alifichua siri za taifa hilo kuwa na tabia ya kudukua taarifa za watu katika barua pepe na simu, hali ambayo ilizua hofu duniani.

Jambo la kushangaza, uta-wala wa Obama ulitoa agizo Snowden akamatwe bila kuzin-gatia dhana nzima ya uhuru wa kujieleza wa Snowden kama ambavyo wamekuwa wak-iutetea. Leo hii Snowden yuko uhamishoni!

Lakini pia, dunia nzima ina-fahamu kuwa kuandika habari na kutoa maoni yanayowakosoa Wayahudi (Jews), ni kosa la jinai katika nchi za kimagharibi na utaambiwa unaeneza chuki dhidi yao (Anti-semitism).

Mfano, mwanahistoria wa nchini Uingereza, David Irving, aliwahi katika maandishi yake kuhoji usahihi wa idadi ya Waya-hudi waliouliwa enzi za Vita Kuu ya Pili ya Dunia na utawala wa Manazi wa Hitler, mauaji yaju-likanayo kama ‘The Holocust’.

Alichokifanya Irving ilikuwa ni kuhoji tu usahihi wa takwimu hizo zinazosema kuwa Wayahu-

di milioni sita waliuawa. Kiten-do hicho kilimfanya aonekana anakana mauaji yale (Holocust denial) na hivyo akachukiwa na Wayahudi. Irving alikamatwa na kufungwa jela kwa mwaka mmoja nchini Australia.

Kufuatia kufungwa kwa Irv-ing, hakuna hata mtu mmoja al-iyejitokeza kumtetea David Irv-ing kuwa alikuwa anatumia uhuru wake wa kujieleza hivyo haikuwa sahihi kwake kutiwa korokoroni.

Itakumbukwa pia nchini ufaransa mwaka 2011, mahaka-ma moja ilimtia hatiani mwana-mitindo John Gilliano kwa kosa la kutoa matamshi ya kuwadhi-haki Wayahudi. Je, uhuru wa kujieleza uko wapi hapo?

Wakati uhuru wa kujieleza kama huo wa kuwakosoa Waya-hudi umefanywa kuwa ni kosa la jinai na mwiko (taboo), lakini kudhihakiwa na kutukanwa kwa Uislamu na hususan kejeli dhidi ya Mtume Muhammad imekuwa ruksa.

Nasema ni ruksa kwa sababu hata pale Waislamu wanapoji-

tokeza na kuwakosoa kwa maneno wale wanaokashifu dini yao, kibao huwageukia wao na kuambiwa ‘lazima mkubali uhuru wa kujieleza’. Walioanzi-sha mashambulizi hawasemwi.

Ulimwengu ulishuhudia jin-si Salman Rushdie aliyeandika kitabu kinachokashifu Qur’an aliyoita kuwa ni aya za Shetani (Satanic verses) alivyotetewa na kupewa hifadhi nchini Uingere-za, na Waislamu waliolaani ki-tendo hicho wakaonekana ndio wakorofi.

Tukio la Texas linafanywa huku dunia ikifahamu kuwa kwa mujibu wa mafundisho ya dini ya Kiislamu ni makosa ku-chora picha za Mtume Muham-mad (Rehma na amani ziwe juu yake), ila kwa makusudi wanap-uuza hilo.

Bahati mbaya, dhana iliyo-jengeka miongoni mwa wako-soaji wa dini ya Kiislam ni kuwa dini hii ni ya kihafidhina (con-servatism), yaani haikubali ku-kosolewa, na pia ni dini ya vuru-gu tu.

Lakini huo si ukweli. Wana-chokipinga Waislam ni ukosoaji huo ambao umekaa kiudhalil-ishaji, dhihaka, kama inavyofan-ywa leo dhidi ya Mtume Mtuku-fu, Muhammad(Rehma na am-ani ziwe juu yake), kwani hata unaposoma maneno yanayoam-batana na katuni zile unaona kabisa lengo si kukosoa bali ku-dhihaki.

Kama ni ukosoaji wa ma-fundisho ya kiislamu hata mad-hehebu yenyewe ya kiislamu hukosoana lakini hufanya hivyo kwa kuangalia maudhui (con-tents) na sio kama wafanyavyo akina Geller. Ni sababu tu ya un-dumilakuwili (Double stand-ards) na chuki dhidi ya Uislamu, dunia imeendelea kuwaacha wale wanaodhihaki dini ya kiis-lam na kuupa Uislamu majina baya.

Siungi mkono shambulizi li-lilofanywa katika onesho la Tex-as ila watu kama akina Pamela Geller hatari sana/ Lengo lao ni kuifanya dunia iwachukie Wais-lamu tu jambo ambalo mus-takabali wake si mwema. Ni-likuwepo!

0658010594.

tuKio la texas

linafanywa huKu dunia iKifahamu Kuwa Kwa mujibu wa

mafundisho ya dini ya Kiislamu

ni maKosa Kuchora picha za

mtume muhammad (rehma na

amani ziwe juu yaKe)

Page 17: Imaan Newspaper issue 6

www.islamicftz.org

29 Rajab 1436, jumatatu mei 18 - 24, 2015

18 makala / taNgaZo

hukumu ya KUgoma KUla Na KUNywa

Wiki iliyopita tulisikia kwamba baadhi ya masheikh walioko ma-habusu wameanza

mgomo wa kutokula na kunywa ili kushinikiza kesi yao isikilizwe, na wengine wakidai kuonana na Mwa-nasheria Mkuu wa Serikali ya Mu-ungano na yule wa Zanzibar.

Kwanza, tuwape pole masheikh, maimamu, walimu na Waislamu wenzetu wote wanaoshikiliwa katika magereza mbali mbali nchini na hata wale wanaoshikiliwa katika magereza nchi mbali mbali duniani kwa sababu tu ya Uislamu.

Pili, kwa kuwa mahabusu wameg-

oma kula na kunywa hapa nchini, jambo ambalo tulikuwa tukilisikia nchi za wenzetu tu, tumeona iko haja kubwa ya Waislamu kujua hukumu ya Kiislamu kuhusu suala hili.

Tunafanya hivi ili iwe kama inavy-osema Qur’an: “…aangamie wa kuangamia kwa dalili zilizo dhaahiri, na asalimike wa kusalimika kwa dalili zilizo dhaahiri. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia Mwenye kujua.” ( 8:42).

Kugoma kula na kunywa katika historia ya Uislamu:

Kwa mujibu wa Dk. Abdulllahi bin Mubaarak bin Abdillahi Aalu Sayf, Mhadhiri msaidizi katika Idara

ya Fiqh, Kitengo cha Sharia cha Chuo Kikuu cha Riyadh nchini Saudi Ara-bia, mtu wa kwanza kugoma kula na kunywa katika Uislamu ni mama yake swahaba Sa’d ibn Abi Waqaas (Radhi za Allah ziwe juu yake).

Amesimulia Sa’d (Radhi za Allah ziwe juu yake): “Nilikuwa mtu mten-da mema kwa mama yangu. Nilipo-silimu akaniambia, “Ewe Sa’d, ima uache dini yako au sitakula wala kunywa mpaka nife ili waarabu wakulaumu, wasema, ewe mwenye kumuua mama yake”. Nikamwam-bia: “Ewe mama yangu, usifanye hivyo, kwani hakika mimi kamwe si-taacha dini yangu hii kwa kitu cho-

chote kile”.“Basi akakaa mchana mmoja na

usiku mmoja pasina kula. Akaamka amedhikika. Akakaa tena mchana mmoja na usiku mmoja na akadhiki-ka zaidi. Nilipoona hali hiyo nikase-ma: “Naapa kwa jina la Allah ewe mama yangu, laiti kungekuwa na roho mia moja mwilini mwako na ikawa inatoka moja baada ya moja, mimi nisingeacha dini yangu hii. Iki-wa unataka, kula na ikiwa unataka, basi usile”. Alipoona msisitizo wangu juu ya hilo, akaamua kula”. Allah akashusha aya ya 15 ya Sura Luqmaan (Sahihi Muslim).

Lakini katika karne ya 19, 20 na 21, matukio ya kugoma kula na kunywa yamekithiri sana hasusan kutoka kwa wanachama wa vyama vya siasa, kama njia mojawapo ya kushinikiza kupatiwa haki zao.

Hili ni suala lenye ikhtilaafu:Suala la kugoma kula na kunywa

ni katika masuala ambayo wanawa-zuoni wametofautiana. Kuna kauli tatu.

Kauli ya Kwanza: Ni haramu kati-ka ujumla wake kugoma kula na kunywa. Mfano ni tamko la Wizara ya Haki na Masuala ya Kiislamu ya Imarati, gazeti la Manar, toleo la 356, mwaka 1425 Hijriyya, ambapo hoja yao ni kwamba, kugoma kula na kunywa ni sawa na kujiua, jambo am-balo limekatazwa katika Qur’an na Sunna. Kauli ya Pili: Kugoma kula na kunywa inajuzu kwa ujumla wake pasina sharti lolote. Hii ni kauli ya Sheikh Taysiir At-Tamimy, Kadhi Mkuu wa Palestina na ikaungwa mkono na Kamati ya Fat-wa nchini humo.

Kauli ya Tatu: Kugoma kula na

kunywa inajuzu kwa sharti kwamba visipelekee katika kifo au madhara katika mwili. Na hii ni kauli ya jam-huri, na pia kasema Sheikh Ibn Uthaymiyn, Sheikh Fawzaan, Dk. Muhammad ibn Ibrahim Al-Gham-diy na wengineo.

Kila upande una hoja zake, lakini kauli ya walio wengi ni hiyo ya tatu, kwamba kugoma kunajuzu kwa sharti kwamba kusipelekee kwenye umauti au madhara katika mwili wa mwenye kugoma na kuwe na uhakika wa kufanikiwa lengo la mgomo wenyewe. Ikiwa hakuna uwezekano wa kufanikiwa, hapo haijuzu kugo-ma.

Amesema Shaykhul Islaami Ibn Taymiya (Allah amrahamu): “Na ama kauli yake nataka kuiua nafsi yangu kwa ajili ya Allah, basi haya ni maneno mazuri, kwani atakapofanya alilo-liamrisha Allah na likampelekea kuua nafsi yake basi huyu kafanya jema ka-tika hilo. Na kama kilichompelekea yule anayejitoma katika safu za adui peke yake ni manufaa ya Waislamu na huku ana uhakika kwamba atauawa, basi huyu katenda jema.

Ni katika mfano wake ikaterem-shwa aya: ‘Na miongoni mwa watu yuko aliyeiuza nafsi yake akitaka ra-dhi za Allah na Allah ni mpole kwa waja’ (2:207). Na mfano ni yaliyo-tokea kwa baadhi ya maswahaba ku-jitosa kuwakabili maadui na Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) aki-wa hadhiri…” (Majmu’u Fataawa Ibn Taymiyyah, Mjalada wa 25, uk.272).

Suala linabaki, je huyo mwenye kugoma kula na kunywa yuko katika jambo la haki? La sawa katika dini? Kama ni jambo la haki basi hukumu ya kujuzu itakuwa sawia kwake.

na sheikh MuhaMaMd issa

Page 18: Imaan Newspaper issue 6

www.islamicftz.org

29 Rajab 1436, jumatatu mei 18 - 24, 2015

19watoto / taNgaZo

zahRa ebRahiM kona ya waToTo

masafa ya imaan Fm

Kigoma

Moro

Arusha

Ruvuma

Dsm

Mtwara

Mwanza

Tabora

Mbeya1 Daresalaam 104.5 mhz2 Morogoro 96.3 mhz3 Arusha 90.8 mhz4 Mwanza 105.6 mhz5 Kigoma 92.5 mhz6 Tabora 101.6 mhz

7 Mbeya 90.3 mhz8 Dodoma 102 mhz9 Ruvuma 94.2 mhz10 Mtwara 90.9 mhz11 Zanzibar 104.5 mhz12 Pemba 104.5 mhz

Aisha (Radhi za Allah ziwe juu yake) alikuwa mke kipenzi cha Mtume Mu-hammad (Rehma na amani

ziwe juu yake), na pia amekuwa akiit-wa ‘Mama wa Waumini’.

Yeye pia ni mtoto wa Abubakar (Radhi za Allah ziwe juu yake) Khalifa wa kwanza wa Waislamu, ambaye ni rafiki kipenzi wa Mtume Muhammad (Rehma na amani ziwe juu yake).

Mtume Muhammad alimuoa Ai-sha akiwa katika umri mdogo. Kuto-kana na werevu wake na kumbukum-bu yake ya ajabu, kuolewa na Mtume kulimpa Aisha (Radhi za Allah ziwe juu yake) nafasi nzuri ya kujifunza na kuelewa kwa undani elimu ya mambo mbalimbali ya utekelezaji wa dini.

Hivyo basi, Aisha amesimulia ha-dith nyingi ambazo tumefaidika nazo.

Aisha alikuwa na uwezo wa kutatua mambo yanayotatiza kwa urahisi, na alikuwa mkarimu katika kusaidia masikini.

Kama mke, Aisha (Radhi za Allah ziwe juu yake) alikuwa mwenye basha-sha, tabia njema na liwazo la mumewe.

Nyumba yake ndio mahali al-ipozikwa Mtume Mtukufu (Rehma na amani ziwe juu yake). Alikuwa ni Muislamu aliyejitoa kwa moyo wote kuutumikia Uislamu, ikiwa ni pamoja na kuufundisha kwa wengine.

Zoezi:

Kwa nini baba yake Aisha (Radhi za Allah ziwe juu yao) ni mtu muhimu katika histioria ya Uislamu? .....................................................................................................................................................

Wake wa Mtume Mtukufu kwa

jina jingine wanajulikana kama ..............................................................................................................................................................

Nani alizikwa katika nyum-ba ya Aisha (Radhi za Allah ziwe juu yake)?.....................................................................................................

Chora ma – ‘apple’ manne yakiwa juu ya mti, na katika k i l a m o j a andika sifa m o j a (jumla 4) ya Aisha (Radhi za Allah ziwe juu yake).

aisha biNt abibakaR (Radhi za Allah ziwe juu yake)

Page 19: Imaan Newspaper issue 6

www.islamicftz.org

29 Rajab 1436, jumatatu mei 18 - 24, 2015

20 Uamsho wasitisha mgomo

Uk 2

29 Rajab 1436, jumatatu mei 18 - 24, 2015

hutolewa na kuchaPishwa na the islamic foundation, P.o. box 6011 morogoro, tanzania e-mail: [email protected]

na yusuPh aMin

Hakuna shaka yeyote kwamba Mitume wa Mwenyezi Mungu wali-letwa kwa lengo la ku-

waongoza watu katika uongofu. Hata hivyo, da’awa haikufaradhish-wa kwa Mitume pekee, bali kwa waislamu wote.

Allah Taala anasema katika Qur’an 3:110: “Nyinyi mmekuwa umma bora uliotolewa kwa ajili ya watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamua-mini Mwenyezi Mungu. Na lau kuwa Watu wa Kitabu nao wameamini in-gelikuwa bora kwao. Wapo miongo-ni mwao waumini, lakini wengi wao wapotovu”.

Kutokana na ushahidi huo, ni wazi kwamba jukumu la ulinganiaji ni la Waislamu wote, waume kwa wake. Kazi ya kulingania watu ku-ingia katika dini hufanywa na mtu mmoja mmoja lakini pia hufanywa na taasisi na makundi mbalimbali.

Msingi mkuu wa taaluma ya ul-inganiaji ni pamoja na ufahamu wa dini, tawhiid, na kustahamili misu-kosuko inayotokana na wapinzani wa dini. Uelewa usio sahihi wa wasio Waislamu kuhusu Uislamu ulipele-kea jumuiya ya Al-Markaz I’islamiyat Litanbihi Lilghaafilina fii Diin (AL-MALLID) ambayo hu-jishughulisha na kuwazindua watu walioghafilika na dini kuanzisha juk-waa la wahadhiri mwaka 1992 kwa lengo la kuwaelimisha watu juu ya Uislamu.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Maole Kuchilingolo, taasisi yake ilianza kama kikundi ki-dogo cha Waislamu cha kuwalinga-nia watu wa dini zote kwa kutumia vitabu vilivyotangulia Taurati, Injili, Zaburi na kitabu cha mwisho Qur’an kutokana na ukweli kwamba vitabu hivyo ni haki kutoka kwa Allah.

Maole alitaja lengo kuu la AL-MALLID kuwa ni kuwazindua watu wamtambue Mwenyezi Mungu na pia warudi kwenye dini ya Allah Taa-la kwa kufuata Qur’an na Sunna.

Kilele cha umaarufu wa AL-MALLID kilikuwa kati ya miaka 1998 hadi 2000 kutokana na waha-dhiri maarufu wa kipindi hicho wak-iwemo Dokta Sule, Sheikh Kipozeo, Said Ricco, Habib Bozza na Habib Mazinge kuvuma katika fani ya ulin-ganiaji kupitia mihadhara ya wazi.

Taratibu za daawaKatika utendaji wa shughuli za

kila siku taasisi huwafikia watu mbalimbali kupitia mihadhara ya wazi, semina na vyombo vya habari kama radio na televisheni ingawa njia ya mihadhara imekuwa na ma-fanikio zaidi kwani inawezesha wa-sio Waislamu ambao hawafiki misikitini kufikiwa na ujumbe kwa urahisi.

Njia zitumikazo kushawishi watu kuikubali dini ni tatu ambazo ni ku-fanya mihadhara ya moja kwa moja ambayo hujumuisha masomo ya tawhiid, njia ya maswali na kuelezea mapungufu ya vitabu vilivyotan-gulia. Kazi ya ulinganiaji hutumia

rejea za vitabu vitukufu vya Qur’an na Biblia ambavyo kwa kiasi kikubwa vimekusanya maelezo ya vitabu vya Taurati na Zaburi na kuongeza kuwa mapungufu ya vitabu hivyo ndio wa-nayoyatumia katika kueleza ukweli au uongo unaopatikana ndani yake.

Kutokana na asili na maudhui ya dini za Uislamu, Uyahudi na Unas-wara, wahadhiri hutumia njia za nukuu hasa katika mambo yenye utata kupitia vitabu hivyo jambo am-balo huwashangaza walio wengi.

Ziara kwa ajili ya kuwalingania watu zinafanywa zaidi katika mkoa wa Dar-es-salaam kwa kwa kuzin-gatia kuwa ndio makao makuu ya jumuiya na pia kuna wepesi kutoka-na na udogo wa gharama.

“Ikumbukwe kuwa shughuli hizi zinafanywa kwa kujitolea, kwa hiyo tunapohitajika mikoani huwa tuna-waomba wenyeji kuchangia nauli pamoja na gharama za kujikimu tut-akapo kuwa huko”, aliongeza Maole.

Kwa mujibu wa katibu huyo, ju-muiya imekuwa ikifanya ziara katika mikoa yote ya Tanzania. Hata hivyo,

taasisi hiyo imefungua matawi kati-ka mikoa ya Tanga,Mwanza,Morogoro,Rukwa,Kigoma,Iringa,Ruvuma na Mbeya ambako kuna wahadhiri wake wanaojitegemea.

Jumuiya ya Al-MALLID pia im-evuka mipaka na mara kwa mara wahadhiri hufanya ziara katika nchi za Burundi, Rwanda, Congo DRC, Zambia, Kenya na Uganda ambapo pia kuna matawi ya jumuiya. Ufun-guzi wa matawi hayo ulitokana na watu wa nchi hizo kuvutiwa na hoja madhubuti, mawaidha mazuri, lugha zenye mvuto na busara zinazo-tumika katika kulingania.

Ili kuhakikisha wahadhiri wana-fanya mahubiri kwa utulivu pasipo kubughudhiwa na vyombo vya dola, mihadhara hurekodiwa ili kuweka ushahidi endapo itatokea aina yeyote ya sintofahamu na hili lilisaida kwa kiasi kikubwa kwani hakuna mha-dhiri aliyewahi kushtakiwa kutoka-na na migongano ya kidini.

Njia zinazotumika kuwapata na kuwaandaa wahadhiri

Shughuli za ulinganiaji zilianza

muda mrefu chini ya baadhi ya taasi-si japo hazikuwa zimesajiliwa rasmi. Mara baada ya taasisi ya AL-MAL-LID kusajiliwa ilichukua wahadhiri kutoka taasisi nyingine waliok-wishaanza kazi hiyo muda mrefu.

Njia nyingine zilizotumika kupa-ta wahadhiri ni pamoja na kuchagua wanafunzi bora katika fani ya ulin-ganiaji kutoka vyuo mbalimbali na kutoka miongoni mwa wahudhuria-ji wa mihadhara hiyo kwani ilikuwa ni darasa tosha kwao. Njia nyingine ni kutambua watu wenye uwezo ka-tika elimu ya hoja kupitia majadil-iano ya wazi katika maeneo mbalim-bali.

ChangamotoTaasisi ya Al MALLID inakum-

bana na changamoto mbalimbali katika kazi zake. Moja kati ya changamoto hizo ni kupungua kasi ya kufanyika shughuli za mihadhara kutokana na wahadhiri wengi kua-mua kufanya shughuli nyingine kutokana na changamoto za kiuchu-mi. Kadhalika, Maole alisema kuan-

zia mwaka 2000 hadi 2004 kulito-kea tatizo la ukosefu wa viwanja kwa ajili ya kuendesha mihadhara na hali hiyo ilikwamisha juhudi za da’awa kwa kiasi kikubwa.

Kukosekana kwa viwanja vya ku-fanyia mihadhara kumetokana na hatua ya serikali kuagiza viwanja vyote vya shule hususan katika jiji la Dar es Salaam, kuzungushiwa uzio na kupiga marufuku viwanja hivyo kutumiwa kwa ajili ya mihadhara.

Changamoto nyingine ni baadhi ya watu kushindwa kujibu hoja na badala kuwashutumu wahadhiri hao kuwa wanatumiwa na watu wa nchi nyingine kuangamiza dini zao japo madai hayo hayana ukweli kwani katiba ya nchi ibara ya 18 na 19 inasema kila mtu ana uhuru wa kufuata dini anayotaka.

Pia watu wa dini nyingine wali-buni hoja, ‘mihadhara ya kashfa dhi-di yao’ kwa lengo la kupunguza makali ya da’awa yanayopelekea idadi kubwa ya watu kuingia katika Uislamu. Inakuwaje watu wakashi-fiwe dini zao kisha Wasilimu?

Suluhu ya changamotoYanapotokea madhila au tishio

lolote kwa wahadhiri yatokanayo na mgongano wa kisheria, jumuiya hu-fanya shura na kuwatafuta mawakili kwa ajili ya kufafanua hoja kisheria pindi wanapofikishwa mahakamani. Lakini walipoona mwenendo wa mawakili hauendani nao walijifunza wenyewe jinsi ya kutumia katiba na sheria za nchi kujtetea, alifafanua Maole.

Maole anasema Waislamu wana-paswa kuelewa kuwa suala la mja kuongoka hubaki kwa Allah kwani hakuna uwezekano wa watu wote kuifuata haki. Maole alimnukuu Al-lah Taala katika Quran 64:2, “Yeye ndiye aliye kuumbeni. Miongoni mwenu yupo aliyekafiri, na yupo ali-ye Muumini. Na Mwenyezi Mungu anayaona mnayoyatenda”.

Licha ya changamoto hizo jumui-ya imepata mafanikio kama vile ku-silimisha idadi kubwa ya watu am-bao baadae waliibuka kuwa waha-dhiri wakubwa katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.

Bwana Maole amewataja waha-dhiri hao kuwa ni pamoja na Mare-hemu Mchungaji Abubakar Mwai-popo, Issa John Luvanda, Marehe-mu Imani Petro, Wakili Issa John Maige, Michael Okelo, Mchungaji Manoni, Yahya Hosea Kyandu pamoja na Jamal Germanus.

Jumuiya ya AL-MALLID ilisajil-iwa rasmi Novemba 24, 1992 chini ya Sheria ya Usajili ya Wizara ya Mambo ya Ndani ambapo kwa sasa inaongozwa na Mwenyekiti Sheikh Othman Matata, Katibu Mkuu Maole Kuchilingolo,Naibu katibu mkuu Mahawiya Karenga,Mhazina Sheikh Rajab Katimba. Viongozi wengine ni pamoja na Mkurugenzi wa Dini, Sheikh Atiq Rashid; Mku-rugenzi wa Elimu da’awa, Sheikh Yusuf Omar; Mkurugenzi wa Fedha, Mipango na Uchumi; Sheikh Rajab Katimba pamoja na Mkurugenzi wa Akinamama, Mariam Willy.

al-malliD

Jumuiya ya mihadhara inayowaita watu kwenye nuru ya uongofu