jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya rais, ikulu · • serikali imepitisha marekebisho ya...

41
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS, IKULU MADA KUHUSU MPANGO WA UENDESHAJI SHUGHULI ZA SERIKALI KWA UWAZI (OPEN GOVERNMENT PARTNERSHIP - OGP) NA UTUMISHI WA UMMA ILIYOTOLEWA KATIKA KONGAMANO LA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA-UKUMBI WA MIKUTANO WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE,DAR ES SALAAM TAREHE 17 JUNI, 2015 _______________ _ IMETOLEWA NA KITENGO CHA UTAWALA BORA OFISI YA RAIS, IKULU

Upload: others

Post on 05-Feb-2020

43 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS, IKULU

MADA KUHUSU MPANGO WA UENDESHAJI SHUGHULI

ZA SERIKALI KWA UWAZI (OPEN GOVERNMENT PARTNERSHIP - OGP) NA UTUMISHI WA UMMA ILIYOTOLEWA KATIKA KONGAMANO LA WIKI YA

UTUMISHI WA UMMA-UKUMBI WA MIKUTANO WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE,DAR ES SALAAM TAREHE 17 JUNI, 2015

_______________ _

IMETOLEWA NA KITENGO CHA UTAWALA BORA

OFISI YA RAIS,

IKULU

YALIYOMO

• Utangulizi

• Maeneo Makuu ya OGP

• Faida za Mpango wa OGP

• Utekelezaji wa Mpango

• Maeneo ya Kipaumbele

• OGP na Utumishi wa Umma

• Mafanikio na Changamoto

• Mpango Kazi Awamu ya Pili (2013/14-2015/16)

• Hitimisho

1. UTANGULIZI

• Mpango wa Uendeshaji wa Shughuli za Serikali kwa Uwazi(Open Government

Partnership-OGP) ni Mpango wa Kimataifa uliobuniwa na wadau mbalimbali zikiwemo Serikali na Asasi za Kimataifa zisizo za kiserikali.

• Mpango huu ulizinduliwa mjini New York,Marekani 20 Sept, 2011. Kimsingi, mwanzilishi wa wazo hili ni Serikali ya Marekani na kuungwa mkono na Serikali ya Brazil. Nchi nyingine anzilishi ni Indonesia,Mexico,Norway,Phillipenes,Afrika Kusini na Uingereza. Hadi sasa nchi 65 zimejiunga na Mpango huu. Tanzania ilijiunga 21 Septemba, 2011

• Barani Afrika nchi wanachama ni Tanzania, Afrika ya Kusini, Kenya, Liberia,Tunisia, Ghana, Malawi na Sierra Leone.

• Uendeshaji unasimamiwa na “Multi-Stakeholder International steering committee”. wajumbe ni serikali za nchi 11 na Asasi za kiraia 11. Serikali ya Tanzania na TWAWEZA ni wajumbe

• Mwenyekiti ni Mexico na Mwenyekiti mwenza Afrika ya Kusini.

2. MAENEO MAKUU YA OGP

• Mpango wa OGP unajikita katika maeneo makuu manne:-

– Kuweka Uwazi zaidi katika uendeshaji wa shughuli za Serikali

– Ushirikishwaji wa wananchi katika kuweka mipango na utekelezaji wa shughuli za Serikali.

– Kuimarisha uwajibikaji na maadili ya utendaji.

– Kuweka umuhimu katika matumizi ya teknolojia na ubunifu.

3. FAIDA ZA MPANGO

• Kutoa huduma bora kwa Wananchi

• Kuongezeka kwa uwajibikaji na uadilifu na kupungua kwa rushwa

• Usimamizi mzuri wa matumizi ya rasilimali za umma

• Kujenga uhusiano wa kidiplomasia kwa nchi zenye malengo sawa kwa kutengeneza mitandao ya mashirikiano na pia kupata uzoefu wa nchi nyingine

• Kujenga Amani na Usalama miongoni mwa Nchi wanachama

4.UTEKELEZAJI WA OGP TANZANIA

• Serikali ya Jamhuri ya Muungano ilijiunga na Mpango wa OGP tarehe 21 Septemba,2011

• Madhumuni ya kujiunga na Mpango huu ni kuiwezesha Serikali kuwa wazi zaidi kwa wananchi wake katika utekelezaji wa shughuli zake.

• Lengo ni kuboresha utoaji huduma,kuwajibika kwa wananchi,kupambana na rushwa na kuongeza imani ya wananchi kwa Serikali yao.

• Misingi ya Mpango wa OGP inaendana na hatua mbali mbali ambazo Serikali ilichukua katika kutekeleza misingi ya Utawala Bora ambayo inasisitiza pia Uwazi,ushirikishwaji wa wananchi, uwajibikaji na uadilifu na matumizi ya teknolojia. Programu hizo ni PSRP,LGRP,LSRP,PFMRP na NACSAP.

5.MAMBO YALIYOFANYWA NA SERIKALI KATIKA KUBORESHA

UTUMISHI WA UMMA 5.1 UWAZI

• Serikali ilichukua hatua zifuatazo katika kuimarisha uwazi Serikalini:-

• Mikutano ya Bunge huonyeshwa kwenye Tv na wananchi kufuatilia mijadala na kusikia majibu ya utekelezaji wa shughuli za serikali.

• Uhuru wa kupata habari.

• Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG)kuwekwa wazi.

• Sheria ya kuzuia na Kupambana na Rushwa kuwa pana zaidi kawa kuongeza makosa yanayohusiana na rushwa.

• Tanzania ni mwanachama wa Mpango wa Afrika wa wa Kujitathmini Wenyewe (APRM) na Mpango wa Uwazi katika Uvunaji wa Rasilimali(EITI).

5.2 USHIRIKISHWAJI WA WANANCHI

• Kuanzishwa kwa tovuti ya wananchi mwaka 2007.

• Uandaaji na upitishaji wa bajeti za Serikali za mitaa kwa kuwashirikisha wananchi.

• Mfumo wa ugawaji wa ardhi katika ngazi ya kijiji unaofanyika katika mkutano wa kijiji(Village Assembly).

• Kusambazwa kwa Mwongozo katika Wizara zote, Taasisi na Wakala wa Serikali unahusu kushirikisha Asasi zisizo za Serikali katika kutekeleza shughuli za Serikali.

5.3UWAJIBIKAJI NA UADILIFU

• Matumizi ya Kanuni za Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma inayosisitiza uwazi na uwajibikaji katika utumishi wa umma.

• Kuanzishwa kwa Mkakati wa Kupambana dhidi ya Rushwa. Mkakati unaelekeza Taasisi za Umma kuchukua hatua katika kuzuia na kupamabana na rushwa katika Taasisi zao.

• Kuanzishwa kwa Kamati za Maadili katika Wizara na Halmashauri.

• Kuanzishwa kwa Intergrated Finacial Management System kwa ajili ya usimamizi wa matumizi ya fedha za Umma kutokana na Bajeti iliyopitishwa.

5.4 TEKNOLOJIA NA UBUNIFU

• Uwekezaji katika teknolojia na ubunufu ni jambo la msingi katika kufanya shughuli za Serikali kuwa wazi. Mambo mbalimbali yamefanika kama ifuatavyo:-

• Kupitisha na kutumika sera ya Habari na Mawasiliano,2003( National and Communication Technology Policy.

• Kuanzishwa kwa mfumo wa taarifa za visima vya maji unao saidia kupanga na kufuatilia mgawanyo wa huduma ya maji( Water Sector Management Information System.

• Kuanzishwa kwa Telemedicines services iliyolenga kupeleka huduma hiyo kwenye vituo vya Afya vilivyokua mbali.

6.OGP TANZANIA

• OGP nchini inasimamiwa na WN OR UB

• Serikali iliunda Kamati ya Kitaifa ya Uendeshaji (Task Force) ili kusimamia, kuratibu na kufuatilia utekelezaji Mwenyekiti ni Naibu Katibu Mkuu- Ikulu.

• Wajumbe wanatoka kwenye Sekta zinazotekeleza Mpango ambazo ni, Ofisi ya Waziri Mkuu- TAMISEMI, Wizara za Elimu, Afya, Maji, Fedha, Ardhi,eGA na Nishati na Madini na kutoka Asasi za Kiraia/Taasisi zisizo za Serikali ni TWAWEZA,REPOA , The Foundation for Civil Society Ltd na Tanganyika Law Society

• Mpango Kazi Awamu ya Kwanza uliandaliwa na Kamati kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali na ulitekelezwa mwaka 2012/13.

• Vipaumbele vya Awamu hii vilikuwa 25 ambavyo vililenga kuongeza Uwazi na Uwajibikaji Serikalini.

7. MAENEO YA KIPAUMBELE

• Kwa kuanzia, Serikali iliamua kutekeleza Mpango wa OGP na kuweka mkazo katika Sekta tatu (3) za huduma za jamii ambazo ni Elimu, Maji na Afya.

• Maeneo mengine ni katika masuala ya fedha, data huria (open-data), Sheria ya Haki ya kupata Habari na maadili (asset disclosure)

• Mkazo mkubwa ni kutoa taarifa kwa uwazi kwa kushirikisha Wananchi ili waweze kuifuatilia Serikali.

• Maeneo mahsusi kwa kuzingatia maeneo makuu manne ya OGP kwa kila eneo ni kama ifuatavyo:-

7.1 UWAZI

• Kuweka kwenye mitandao na vituo vya kutolea huduma taarifa za uagizaji, usambazaji na upokeaji wa dawa na vifaa vya tiba unaofanywa na Bohari Kuu ya Madawa;

• Kuanzisha na kuimarisha tovuti na kuweka taarifa isipokuwa zile zinazohatarisha usalama wa nchi;

• Kuchapisha vitabu vya bajeti kwa mfumo na lugha rahisi;

• Kuhuisha mfumo wa ugawaji wa ruzuku kwa fomula maalum kukidhi mahitaji ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa na kuchapisha migao ya ruzuku katika mtandao;

• Kutangaza taarifa ya mgao wa fedha wa kila robo mwaka katika tovuti ya Wizara ya Fedha;

• Mamlaka za Serikali za Mitaa kubandika taarifa za bajeti na matumizi yake

7.2. USHIRIKISHWAJI WA WANANCHI

• Kuboresha Tovuti ya Wananchi ili kuifanya iwe na mvuto zaidi kwa watumiaji wanaoshiriki kutoa maoni yao;

• Kuhakikisha ushirikishwaji mpana zaidi wa wananchi kwa kupitia simu za mkononi;

• Kuanzisha utaratibu wa mikutano na mijadala ya wazi kwa kushirikiana na Asasi za Kiraia mara mbili kila mwaka kuhakiki ubora, uadilifu na kasi ya utekelezaji wa maazimio ya OGP;

• Kuwa na Ofisi na anuani kwa ajili ya mawasiliano ya shughuli za OGP kati ya Serikali na Wadau;

• Wananchi website

7.3. UWAJIBIKAJI NA UADILIFU

• Kuhuisha na kusimamia Mikataba ya Huduma kwa Mteja;

• Kuhuisha daftari la malalamiko. Yale yaliyopokelewa yapatiwe majibu

na hatua zilizochukuliwa kuwekwa kwenye tovuti ;

• Kuboresha Bodi na Kamati za Huduma za Mamlaka ya Serikali za

Mitaa kuleta ufanisi zaidi

• Kuboresha tovuti ya Ofisi ya CAG ili itumike kwa uwazi zaidi

• Kurekebisha Sheria ya Maadili ya Utumishi wa Umma kuweka uwazi

zaidi masuala ya mali za Viongozi wa umma;

7.4. TEKNOLOJIA NA UBUNIFU

• Kukamilisha Mfumo wa kubaini hali ya upatikanaji wa maji kwa kutumia mitandao ya Mamlaka za Serikali za Mitaa na kuchapisha data kwenye tovuti; (water point mapping).

• Kuimarisha matumizi ya mifumo ya habari na kuweka wazi na kwenye mitandao taarifa kuhusu masuala ya zahanati, shule nk

• Kufanya utafiti kuhusu uanzishwaji wa tovuti ya ‘Nifanyeje?’ itakayowezesha wananchi kupata taarifa kuhusu namna ya kupata huduma mbalimbali zitolewazo na Serikali;

8.OGP NA UTUMISHI WA UMMA

• Maeneo Makuu ya OGP uwazi,ushirikishwaji wa Wananchi,uwajibikaji na Maadili ya Utendaji na matumizi ya teknolojia yanasisitiza Kanuni za maadili katika utumishi wa umma.

• Kanuni hizi zinasisitiza kutoa huduma bora kwa Wananchi,kuwajibika kwa Umma,uadilifu katika kazi na kutokuwa na upendeleo.

• Kuendeleza uwajibikaji Serikalini ndiyo shabaha kuu ya Mpango wa uwazi katika Serikali.

• Ili mtumishi wa Umma aweze kutoa huduma bora kwa mwananchi,yampasa kutimiza majukumu yake kutokana na Sheria,Taratibu na Kanuni za Utumishi wa Umma.

• Kuhudumia Umma kwa usawa,uaminifu,uadilifu na kujiepusha na ubadhilifu na wizi wa mali ya Umma,

hupelekea kupungua kwa Rushwa.

• Ili kujenga msingi wa Uwazi,mtumishi wa Umma anatakiwa kutekeleza majukumu yake kwa uwazi.

• Uwazi unawawezesha wananchi kudai haki zao au kuwakumbusha viongozi na watendaji Serikalini kutimiza wajibu wao kwa wananchi wanaotakiwa kuwahudumia.

• Mtumishi wa Umma anatakiwa kutoa taarifa sahihi kwa wakati na zilizo wazi kwa wadau/wananchi kuhusu utekelezaji wa majukumu pale inapotakiwa kufanya

hivyo.

• Kuwashirikisha wananchi katika kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo ya maeneo yao.

• Kuwepo kwa utaratibu huu utawezesha wananchi kupima na kuamua kuhusu ufanisi wa Watumishi wa Umma.

8. MAFANIKIO

• Serikali imepitisha marekebisho ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

• Tovuti za Wizara ya Elimu, Afya ,Maji, Fedha, TAMISEMI pamoja na baadhi za Ofisi za Sekretarieti za Mikoa zimeimarishwa na kuwekwa kwa lugha za Kiswahili na Kiingereza.

• Taarifa mbali mbali kama vile nyaraka, hotuba za viongozi zinawekwa katika Tovuti za Wizara husika;

– Bajeti ya Wananchi (citizens budget) ya 2013/2014 iliandaliwa na kuwekwa kwenye tovuti ya Wizara ya Fedha.

– Wizara za Maji na Afya zimehuisha Mikataba ya Huduma kwa Wateja (Client Service Charters)

– Wizara ya Maji imeweka kwenye ramani vituo 75,777 vya maji katika vijiji (Water Point Mapping) - Taarifa zaidi kuhusu vituo hivi angalia wpm.maji.go.tz.

– Mpango wa Kitaifa wa Ujumbe Mfupi wa Simu (SMS) unaolenga katika kuboresha afya ya Mama, Mtoto na Familia umefanikiwa zaidi ujumbe mfupi milioni 13 zimepokelewa na kufanyiwa kazi.

– Tovuti kwa ajili ya wananchi kupata taarifa kuhusu namna ya kupata huduma mbalimbali serikalini imeanzishwa. Tovuti hii itakayojulikana kama “Nifanyaje”, inaendelea kukamilishwa.

– Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Dunia imefanya zoezi la tathmini la kubaini utayari wa Serikali kuanzisha mfumo wa Takwimu Huria (Open Data Readiness Assessment).

– Tovuti ya Takwimu Huria imeanzishwa ipo katika majaribio

9. CHANGAMOTO: • Uelewa mdogo wa wananchi kuhusu Mpango. Mkakati wa

Mawasiliano wa kuutangaza Mpango umeandaliwa

• Tovuti ya OGP ya awali kutofanya kazi kwa ufanisi. Tovuti

mpya www.opengov.go.tz inafanya kazi vizuri.

• Baadhi ya sekta kutoelewa vizuri majukumu yao hivyo kasi

ya utekelezaji kutoenda sambamba na Mkakati wa

Utekelezaji.

• Ushiriki mdogo wa Asasi zisizo za Kiserikali na Sekta

Binafsi katika kutekeleza Mpango huu.

• Mpangokazi Awamu ya Kwanza kuwa na ahadi (commitments) nyingi baadhi kutokamilika au kutotekelezwa kabisa

• Mifumo ya uratibu na upataji wa habari hasa kutoka kwenye Asasi za Kiraia kuhitaji kuangaliwa upya

• Tovuti nyingi za Serikali kutofanya kazi kwa ufanisi na kutokuwepo kwa utaratibu wa kujibu hoja za wananchi (feedback mechanism)

• Mikataba ya Huduma kwa Mteja kutozingatiwa

• Upungufu wa fedha za utekelezaji

10. MPANGOKAZI AWAMU YA PILI

• Mpango kazi wa Awamu ya Pili umepangwa kutekelezwa

kwa miaka miwili (2014/15 - 2015/16) kwa kushirikisha Asasi za Kiraia, Serikali itatekeleza vipaumbele vichache

• Uandaji wa Mpango kazi awamu ya pili umezingatia maoni na mapendekezo ya taarifa ya SAR( Self Assessmemt Report) na IRM( Independent Reporting Mechanism)

• Serikali iliandaa vikao vya majadiliano katika ngazi ya sekta kwa ajili ya kuandaa Mpango

• Asasi zisizo za Kiserikali takribani sitini zilishirikishwa

Vipaumbele vya Awamu ya Pili ni 5 vifuatavyo :- • Kutunga kwa Sheria ya Haki ya Kupata Habari • Kukamilisha mfumo wa Open data. • Kuweka wazi mipango na matumizi bora ya ardhi,

umiliki wa ardhi na maeneo ya ardhi yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji mkubwa

• Kuweka wazi ripoti muhimu za Bajeti za Serikali kwa ajili ya matumizi ya wananchi na misamaha ya kodi

• Kuweka wazi mikataba na makubaliano ya maendeleo ya utafutaji na uchimbaji wa madini, mafuta na Gesi kwa mujibu wa EITI.

11. UTEKELEZAJI WA MPANGO KAZI AWAMU YA PILI

• Kamati mpya ya Kitaifa ya Uratibu wa Mpango huu iliteuliwa • Utekelezaji unafanywa na Wizara na Taasisi husika. • Wizara na Taasisi zimeandaa Mpango Mkakati wa Utekelezaji

unaoainisha shughuli,muda wa kutekeleza,wahusika wa utekelezaji na bajeti.

• Utekelezaji unaendelea kuratibiwa na Kamati ya Kitaifa ya uratibu

• Wizara/Taasisi husika huwasilisha taarifa za utekelezaji kwa kila robo mwaka.

• Tathmini ya utekeleaji zitafanywa SAR na IRM

12. MATARAJIO

• Ushirikiano kutoka kwa wadau katika kutekeleza Mpango huu,

• Kufikiwa kwa Malengo ya Mpango wa OGP kutokana na kuongezeka kwa uwazi,uwajibikaji,ushirikishwaji wa wananchi,mapambano dhidi ya rushwa,kupatikana kwa teknolojia mpya na kuimarika kwa utoaji wa huduma kwa wananchi.

• Kuimarika kwa Mpango wa BRN • Kuzingatia matakwa mapana ya misingi ya OGP

iliyowekwa kimataifa.

12. MAPENDEKEZO

• Mpango wa OGP umeharakisha utekelezaji wa baadhi ya mambo kama vile utungwaji wa Sheria ya Haki ya Kupata Habari,matumizi ya data huria n,k.

• Tuendelee kuutekeleza Mpango huu ipasavyo ili kuleta uwazi na uwajibikaji kwa wananchi.

• Kuhuisha na kusimamia clients charter ipasavyo.

• Kuimarisha matumizi ya teknolojia katika kutoa huduma kwa wananchi.

• Kutoa elimu kwa Umma katika kutekeleza uwazi na uwajibikaji

• Kusimamia maadili ya utumishi wa Umma.

13. HITIMISHO

• Mpango wa OGP umeipa heshima nchi kimataifa

• Unaongeza uwazi na uwajibikaji wa Serikali kwa wananchi.

• Unashirikisha wadau nje na ndani ya Serikali

• Unaimarisha juhudi za Serikali katika uwajibikaji

• Dhana hii si mpya sana lakini bado kuna hofu miongoni mwa watendaji kutoa taarifa

• Tukubali kubadilika, utendaji utaimarika na kuleta maelewano kati ya Serikali na wadau wote wakiwemo wananchi wenyewe na hivyo kupunguza migogoro isiyo ya lazima.

ASANTENI KWA KUNISIKILIZA