jamhuri ya muungano wa tanzania wizara …...nyaraka zote muhimu kwa ajili ya uhakiki na baadae...
TRANSCRIPT
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA KATIBA NA SHERIA
MUONGOZO WA UTUMIAJI MFUMO WA USAJILI
WATOA HUDUMA YA MSAADA WA KISHERIA
Imeandaliwa na Alfred Chunga-0785998384 Aprili 10, 2019
UTANGULIZI
Mfumo wa Usajili na tathmini kwa watoa huduma ya msaada wa kisheria kwa
umma ni mfumo unaoratibu shughuli nzima ya usajili wa watoa huduma ya
msaada wa kisheria katika maeneo yao nchini kwa njia ya mtandao. Watoa
huduma wana wajibu wa kujisajili kupitia mfumo huu kwa kuambatisha
nyaraka zote muhimu kwa ajili ya uhakiki na baadae kupatiwa vyeti vya usajili.
Mfumo huu una sehemu mbili ambazo ni usajili na tathmini. Sehemu ya
kwanza usajili iko tayari na sehemu ya pili tathmini inaboreshwa.
Mfumo huu unapatikana kupitia https://legalaid.sheria.go.tz au kupitia tovuti
rasmi ya Wizara ya Katiba na Sheria www.sheria.go.tz katika sehemu ya
huduma za TEHAMA, Chagua Msaada wa Kisheria, bonyeza fungua hapa.
1. USAJILI WA TAASISI YA HUDUMA YA MSAADA WA
KISHERIA (LEGAL AID PROVIDER)
VIAMBATISHO MUHIMU;
a) Cheti cha usajili cha taasisi mfano NGO,CBO,FBO au kampuni
b) Taasisi inayotaka kuhudumia wilaya pekee inatakiwa kupata Barua
kutoka ofisi ya mkuu wa wilaya husika, Kwa Mkoa inatakiwa kupata
Barua kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kwa nchi nzima inatakiwa
kupata Barua kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi.
c) Orodha ya Mawakili/Wanasheria kama inavyotakiwa kwenye sheria
ya msaada wa Kisheria ambao wapo katika taasisi ikiambatana na
Vyeti vya taaluma (“Bachelor” kwa mwanasheria, “Practising
Certificate” kwa wakili). Kama taasisi ina paralegals pekee inatakiwa
kuambatisha “affiliation certificate/letter/declaration” kwa taasisi
iliyosajiliwa na yenye wakili.
d) Nakala halisi ya malipo ya ada ya usajili.
e) Fomu ya Maombi ya Taasisi ya inayotoa huduma ya Msaada wa
Kisheria “Application Form” kutoka kwenye kanuni.
f) Barua kutoka Mamlaka ya usajili wa Taasisi “Clearance Letter from
Registering Authority”.
g) Katiba au nyaraka ya kuanzisha taasisi (Mfano Katiba, MEMATS)
NB. Tafadhali hakikisha una viambatisho vyote na vimehifadhiwa katika pdf
ili mfumo uweze kukuruhusu kujisajili.
Kusajili taasisi katika mfumo huu bonyeza sehemu iliyoandika “REGISTRATION”
kisha chagua “REGISTER LEGAL AID PROVIDER”.
Katika sehemu hii utajaza taarifa za mtu aliyeteuliwa na taasisi kuwasilisha
nyaraka na taarifa zake katika mfumo. Jaza sehemu zote muhimu kama jina la
kwanza, jina la mwisho, barua pepe, neno siri na baada ya kujaza sehemu zote
bonyeza “REGISTER LAP”. Sehemu ya kuingia katika mfumo itafunguka na
utatakiwa kujaza barua pepe(e-mail) uliyoisajili na neno la siri ili kuingia katika
mfumo ambapo utatakiwa kuhakiki barua pepe yako kwa kutumiwa “Link”
kwenye barua pepe yako, Ukishabonyeza link hiyo mfumo utakupeleka
kuendelea na usajili.
Usajili wa taasisi umegawanyika katika sehemu kuu tano ambazo ni taarifa za
taasisi, huduma na eneo la kufanyia kazi,wafanyakazi,malipo na sehemu ya
kuwasilisha nyaraka muhimu.
i) Taarifa za taasisi- Tafadhali jaza na kuambatisha taarifa zote muhimu za
taasisi yako kama jina la taasisi, anwani,namba ya mlipakodi kama
ipo, chagua idadi ya chini kabisa ya wafanyakazi kama inavyotakikana
na sheria ya msaada wa kisheria. Iwapo utachagua Paralegals watatu
au Mwanasheria mmoja na Paralegals wawili inakupasa kuonyesha
“Affiliation” katika taasisi inayotoa msaada wa kisheria yenye Wakili
na kuambatisha Ushahidi wa “Affiliation” hiyo. Chagua Aina ya taasisi
yako kama ni NGO,FBO,CBO au Biashara na ambatisha nyaraka ya
usajili, bonyeza “NEXT” kuendelea na hatua inayofata.
ii) Chagua huduma utakazozitoa katika jedwali la kushoto kwa kubonyeza
“ADD” ambapo zitaonekana katika jedwali la kulia, kisha chagua eneo
utakalohudumia kama ni Wilaya,Mkoa au Taifa(Ikiwa utachagua
Wilaya ambatisha barua toka ofisi ya mkuu wa wilaya, ikiwa
utachagua mkoa ambatisha barua toka ofisi ya mkuu wa mkoa na
ikiwa utachagua Nchi nzima ambatisha barua toka Ofisi ya Rais
TAMISEMI). chagua sehemu uliyopo katika “Jurisdiction”. Jaza kata
na mitaa utakayofanyia kazi. Jaza taarifa zingine katika “Other
information” kama zipo. Bonyeza “NEXT” kuendelea na hatua
inayofuata.
iii) Katika sehemu ya tatu jaza kulingana na uchaguzi ulioufanya katika
hatua ya kwanza sehemu ya wafanyakazi. Kama ulichagua
“Paralegals” watatu basi inakupasa uwajaze kwa kubonyeza “Add
Paralegals” na kisha jaza taarifa zote zinazohitajika na kuambatisha
Ushahidi wa malipo na baada ya hapo bonyeza “Register Paralegal”
Fanya hivyo kwa idadi inayotakiwa. Hivyo hivyo kama ulichagua
mawakili wawili itakupasa kubonyeza “Add Lawyer/Advocate” na jaza
taarifa zote zinazotakiwa.
iv) Sehemu hii ni sehemu ya malipo hivyo utatakiwa kujaza taarifa za malipo
yako ya ada ya usajili. Unatakiwa kujaza jina la benki, tawi, umelipa
lini na kuambatisha nakala halisi ya malipo ya benki(Paying slip)
bonyeza kitufe cha “Save Details” kuhifadhi taarifa zako . Baada ya
kuhifadhi bonyeza kitufe cha “NEXT STEP” kuendelea na hatua
inayofuata.
v) Sehemu hii ni ya viambatisho muhimu. Angalia orodha ya viambatisho
vinavyohitajika katika jedwali la kushoto “Required Attachment” na
chagua kiambatisho kimoja kimoja katika orodha ya chini ya jedwali
la kushoto “Select Attachment File”. Bonyeza kitufe cha “Attach”
kuchagua kiambatisho katika kompyuta yako na bonyeza kitufe cha
“UPLOAD” kuhifadhi nyaraka hiyo. Rudia hatua hizi kwa nyaraka zote
zinazohitajika. Bonyeza kitufe cha “Finish & Submit your Application”
kuwasilisha maombi yako ya usajili baada ya kuhifadhi nyaraka zote
zinazohitajika.
2. USAJILI WA MTOA HUDUMA YA MSAADA WA
KISHERIA(PARALEGAL)
VIAMBATISHO MUHIMU;
a) Nakala Halisi ya cheti cha taaluma kilichothibitishwa na kamishna wa
viapo.
b) Nakala ya cheti cha mafunzo ya “Paralegal”
c) Barua kutoka katika taasisi yako kukuthibitisha “Letter from Institution
Supervisor”
d) Fomu ya Maombi ya mtoa huduma ya msaada wa Kisheria“Application
Form” kutoka kwenye kanuni.
e) Barua au cheti kutoka kwa Shahidi aliyehudumiwa na mtoa huduma ya
msaada wa kisheria “Witness Introduction Letter”.
f) Barua au cheti cha utambulisho kutoka eneo analoishi mtoa huduma ya
msaada wa kisheria “Hamlet leader Introduction Letter”.
g) Nakala halisi ya malipo ya ada ya usajili.
NB. Tafadhali hakikisha una viambatisho vyote na vimehifadhiwa katika pdf
ili mfumo uweze kukuruhusu kujisajili.
Mtoa huduma ya msaada wa kisheria anaweza kusajiliwa kwenye mfumo kwa
njia tatu ambazo ni;
i) Sehemu ya nje ya mfumo bonyeza “REGISTRATION” kisha “REGISTER
PARALEGAL”. Ambapo fomu ya usajili itaonekana. Utatakiwa
kuchagua Taasisi yako katika orodha “CHOOSE YOUR LEGAL AID
PROVIDER” na jaza taarifa zote muhimu ikiwemo majina yako,barua
pepe,neno siri n.k. kisha bonyeza “Register” kujisajili, Baada ya hapo
mfumo utakuhitaji kuingia kwa kujaza barua pepe na neno la siri ili
kuendelea, utahitajika kuhakiki barua pepe yako na baada ya
kubonyea kitufe cha uhakiki kwenye barua pepe yako mfumo
utaendelea sehemu ya na usajili.
NB. Taasisi lazima iwe imeshasajiliwa kwenye mfumo kabla ya
kumsajili mtoa huduma.
ii) sehemu ya ndani ya mfumo baada ya mtoa huduma kuingia kwenye
mfumo, bonyeza sehemu ya “Registration” iliyoko upande wa
kushoto kisha bonyeza “Register Paralegal”. Fomu ya usajili itatokea
na utatakiwa kujaza taarifa zote muhimu pamoja na kuambatisha
nyaraka muhimu.
3. Pia
unaweza kumsajili mtoa huduma “Paralegal” katika hatua ya tatu ya
usajili wa taasisi kwa kubonyeza kitufe kilichoandikwa “ADD
PARALEGAL”.