je uko tayari? - fargo, nd · . kuwa macho kwa kuangalia hali ya hewa inayobadilika na epukana na...

24
Mwongozo wa dharura wa majimbo ya Cass na Clay umewezeshwa kutokana na ushirikiano wa dharura wa Cass na Clay. Swahili (Kiswahili) Je Uko Tayari?

Upload: others

Post on 21-Jan-2021

10 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: Je Uko Tayari? - Fargo, ND · . Kuwa macho kwa kuangalia hali ya hewa inayobadilika na epukana na usafiri usiohitajika. Onyo ya dhoruba inamaanisha kwamba dhoruba inaelekea kuonekana

Mwongozo wa dharura wamajimbo ya Cass na Clay

umewezeshwa kutokana na ushirikiano wa dharura wa Cass na Clay.

Swahili (Kiswahili)

Je

Uko

Tayari?

Page 2: Je Uko Tayari? - Fargo, ND · . Kuwa macho kwa kuangalia hali ya hewa inayobadilika na epukana na usafiri usiohitajika. Onyo ya dhoruba inamaanisha kwamba dhoruba inaelekea kuonekana

Wakati dharura inatokea, inawezakukulazimisha kuondoka katika ujiraniwako au kukuzuia nyumbani pako.

Kama dhoruba haribifu itakata umemewako, simu au huduma nyinginezo zakila siku kwa siku kadhaa, au kuvujakwa kemikali na ukalazimika kukaanyumbani pako, utafanya nini?

Familia yako itadhibiti vyema zaidi halihii kwa kujitayarishia janga hili kablahalijatokea.

Page 3: Je Uko Tayari? - Fargo, ND · . Kuwa macho kwa kuangalia hali ya hewa inayobadilika na epukana na usafiri usiohitajika. Onyo ya dhoruba inamaanisha kwamba dhoruba inaelekea kuonekana

Maelezo muhimu 1

Fanya mpango na ufanyie mazoezi 2

Unda mkoba wa kujitayarishia dharura 3

Taarifa ya kibinafsi ya Mawasiliano 4

Mifugo ya kibinafsi na janga 5

Kujihifadhi mahali maalum 6

Onyo na tahadhari 7

Ving’ora & CodeRED 7

Hifadhi za kuondolewa na jamii 8

Aina za dharura:

Usalama wa moto nyumbani 9

Mafuriko na gharika za ghafula 10

Mimweso na radi 11

Vimbunga 12

Nyaya za umeme zilizoanguka 13

Mawimbi ya joto 14

Dhoruba za msimu wa baridi na kipupwe 15

Moto wa kichakani 16

Kupotea kwa umeme 17

Dharura za mafuta ya kimaumbile 18

Dharura za kemikali 19

Dharura za afya ya umma 20

Yaliyomo

Page 4: Je Uko Tayari? - Fargo, ND · . Kuwa macho kwa kuangalia hali ya hewa inayobadilika na epukana na usafiri usiohitajika. Onyo ya dhoruba inamaanisha kwamba dhoruba inaelekea kuonekana

Kama utahitaji msaada katika dharura, piga simu 911. Maelezo yaliyopohapa chini yametolewa ili kukusaidia katika kujipanga kwa dharura.

Maelezo muhimu

Minn-Kota Chapter, American Red Cross: 701-364-1800 www.minnkotaredcross.org� Disaster planning resources� CPR and first aid courses� Educational presentations

City of Dilworth: 218-287-2313Dilworth Fire: 218-287-2313Dilworth Police: 218-287-2666

City of Fargo: 701-241-1310www.cityoffargo.comFargo Fire: 701-241-1540 Fargo Police: 701-241-1437

City of Moorhead: 218-299-5166www.cityofmoorhead.com Moorhead Fire: 218-299-5434Moorhead Police: 218-299-5120

City of West Fargo: 701-433-5300www.westfargo.orgWest Fargo Fire: 701-433-5380West Fargo Police: 701-433-5500

Cass Fargo Emergency Management: 701-476-4068 www.cassfargoemergency.comwww.cityoffargo.com/emergencies

Clay County EmergencyManagement: 218-299-7357

Fargo Cass Public Health: 701-241-1360www.cityoffargo.com/health

Clay County Public Health: 218-299-5220www.co.clay.mn.us/Depts/Health/Health.htm

Statewide Information andReferral: (Minnesota and North Dakota): Piga simu 211

“Call before you dig:”Minnesota and North Dakota:Piga simu 811

North Dakota Department ofEmergency Services: 701-328-8100www.nd.gov/des

Minnesota Homeland Securityand Emergency Management:651-201-7400

Department of HomelandSecurity: www.dhs.gov

Poison Center:1-800-222-1222

1

Page 5: Je Uko Tayari? - Fargo, ND · . Kuwa macho kwa kuangalia hali ya hewa inayobadilika na epukana na usafiri usiohitajika. Onyo ya dhoruba inamaanisha kwamba dhoruba inaelekea kuonekana

Kwa kujitayarishia dharura, watu binafsi, familia na biashara, vyotevinaweza kupunguza kupoteza mali na kupata majeraha na hata kufanyahali hiyo ya kupata nafuu kuwa rahisi zaidi. Soma kijitabu hiki ili uzoeanena baadhi ya hatari za kila siku katika majimbo ya Cass na Clay. Kisha undampango wa kibinafsi ambao unajumuisha:

Njia za kukimbilia—Chora mpango waghorofa la nyumbani kwako au mahali pabiashara na uweke njia mbili za kukimbiliakutoka katika kila chumba.

Mahali pa kukutania—Teua mahalimaalumu pa kukutania mbali na nyumbanipako au mahali pa biashara; jumuishamifugo ya kibinafsi katika mipango hii.

Mawasiliano ya dharura—Familia yako auwafanyi kazi huenda wasiwe pamoja wakatijanga linatokea, kwa hivyo panga jinziambavyo mtakavyo wasiliana, chagua mtualiye kando ya muji ambaye anawezakuwasilisha ujumbe huo. Hakikishakwamba kila mtu anayo majina, namba pamoja na baruapepe za wenginekwa kuwasiliana nao.

Rekodi muhimu na za bima—Chukua na uangalie upya bima ya mali,afya na maisha. Pitia upya sera zilizoko kuhakikisha kwamba umelindwakikamilifu katika kukidhi mahitaji yako.

Mahitaji spesheli—Kama wewe au mtu aliye karibu nawe anao ulemavu au hitaji spesheli, unda mtandao wa jirani, watu wa ukoo, rafiki nawafanyikazi wenza ambao wanaweza kusaidia wakati wa dharura.

Chunguza na pitia upya kila mwaka—Tekeleza marekebishoyanayohitajika katika tanuu lako, kipatia maji joto, bomba la sump namfumo wa kuweka hewa safi kila mwaka. Pitia upya mpango wa dharurakuhakikisha kwamba njia yako ya watu wa kuwasiliana nao pamoja na njiaza kukimbilia ziko sawa. Chunguza Mkoba wako ya kujitayarisha kwadharura na uhakikishe kwamba vitu vyote viko katika hali nzuri.

Fanya mpango na ufanyie mazoezi

2

Page 6: Je Uko Tayari? - Fargo, ND · . Kuwa macho kwa kuangalia hali ya hewa inayobadilika na epukana na usafiri usiohitajika. Onyo ya dhoruba inamaanisha kwamba dhoruba inaelekea kuonekana

Majanga yanaweza kufanyika haraka bila ya onyo. Weka pamoja mkobaunaolenga kukusaidia kudhibiti mseto wa dharura.Vitu katuka mkoba wako:� Mkoba wa huduma ya kwanza, dawa muhimu zaidi na asili ya ziada yaumeme endapo ule wa kawaida utapotea ili kusaidia mtambo wowote wamatibabu unaohitajika kama vile tangi la oksijeni.

� Redio inayotumia betri, kurunzi,betri za ziada

� Chakula cha mkebeni, kizibuomkebe cha mkononi

� Maji ya chupa (Galani 1 kwa kilamtu kila siku kwa siku tatu)

� Mavazi ya ziada yenye jotopamoja na buti, miteni na kofia

� kitamba chekundu ama chenyerangi ya kuonekana haraka

� Redio ya hali ya hewa ya NOAA

Redio ya hali ya hewa ya NOAAinayonya umma kuhusu hali ya hewa mbaya zaidi pamoja na hatari zakimaumbile na za kibinadamu kama vile, mafuriko, moto wa misitu nakuvuja kwa kemikali. Redio za hali ya hewa za NOAA zinaweza kununuliwakutoka katika maduka ya idara maalumu, wauzaji rejareja wa vifaa vyaelektroniki na wauzaji wa mtandaoni.

Tilia maanani kuweka mkoba wa kujitayarisha katika gari lako, mashuana RV au kampa Kuongezea vitu vilivyotajwa hapo juu, mkoba wagarini unafaa kujumuisha:� kizima moto.� nyaya za kuunga mkono pamoja na kamba ya kuvuta.

� dira na ramani za barabara� pakio� mkoba wa kurekebisha gurudumu na bomba.

Kwa taarifa zaidi kuhusu uundaji wa mikoba ya dharura, wasiliana na Minn-kota chapter ya Msalaba Mwekundu wa Marekani katika 701-364-1800.

Unda mkoba wa kujitayarishia dharura

Kumbuka. Mkoba wako wa dharuraunafaa kujumuisha maji ya chupa,chakula cha mkebeni na kurunzi iliyo na betri za ziada

� mavazi ya ziada ya kukufanyakuwa mkavu

� mwake wa barabarani� mkoba mdogo wa zana.� kitilita au changarawe kwakushikilia gurudumu

3

Page 7: Je Uko Tayari? - Fargo, ND · . Kuwa macho kwa kuangalia hali ya hewa inayobadilika na epukana na usafiri usiohitajika. Onyo ya dhoruba inamaanisha kwamba dhoruba inaelekea kuonekana

Taarifa ya kibinafsi ya MawasilianoKwa dharura, piga simu katika 9-1-1.

Taarifa YakoAnwani: (Nyumbani au Mahali pa Biashara)

______________________________________________________Anwani ya Barabara karibu na unapoishi Mji Jimbo Msimbo Zipu

Nambari ya simu: (Nyumbani au Mahali pa Biashara) __________________Simu ya mkononi: ________________________________________Daktari: (Jina na nambari ya simu)________________________________Famakia: ________________________________________________Maagizo ya Dawa:__________________________________________Mizio: __________________________________________________

Anwani za Dharura(majina na nambari za simu)

Mtu wa ukoo: ____________________________________________Rafiki: __________________________________________________Jirani: __________________________________________________Ambalanzi 9-1-1Daktarimifugo: ____________________________________________Udhibiti wa Sumu (au 800-222-1222): ________________________Hospitali/Zahanati: ________________________________________Afya ya umma ya eneo lako: __________________________________Kampuni ya umeme:________________________________________Gesi/mafuta ya gari: ________________________________________Simu ya Kampuni: ________________________________________Maji/maji taka: ____________________________________________Takataka: ________________________________________________Idara ya Moto na Utekelezaji Sheria: 9-1-1

4

Page 8: Je Uko Tayari? - Fargo, ND · . Kuwa macho kwa kuangalia hali ya hewa inayobadilika na epukana na usafiri usiohitajika. Onyo ya dhoruba inamaanisha kwamba dhoruba inaelekea kuonekana

Kama utaondoka mahali, njia bora zaidi ya kuilindamifugo yako ya kibinafsi ni kuondoka mahali hapopamoja nayo pia. Kuiacha mifugo yako ya kibinafsihata kama utajaribu kuunda mahali salama kwayo,kunaweza kusababisha mifugo hiyo kujeruhiwa,kupotea au kupatwa na makubwa zaidi.Kuwa na mahali salama pa kupelekamifugo yako ya kibinafsiHifadhi za janga za Shirika la Msalaba Mwekunduhaziwezi kukubali mifugo ya kibinafsi. Wanyama wahuduma (wanyama wanaosaidia watu wenyeulemavu), ndiyo wanyama pekee wanaoruhusiwakatika hifadhi za Shirika la Msalaba Mwekundu.Chama cha Kibinadamu hakiwezi kuichukua mifugoya kibinafsi wakati wa janga.� Weka orodha ya sehemu ambazo ni za “kupokeamifugo ya kibinafsi” pamoja na nambari za simu. Ulizia kama sera za“hakuna mifugo ya kibinafsi” zinaweza kuondolewa wakati wa dharurakwenye hoteli, mikahawa ya barabarani au maskani ya rafiki.

� Mwulize mtu wa ukoo, rafiki au wengine walio nje ya eneo lililoathiriwakama wanaweza kuhifadhi wanyama wako katika nyumba zao.

� Ilete mifugo yote ya kibinafsi wakati dharura inapoanza ili usije ukaitafutaendapo itabidi uondoke kwa haraka.

� Hakikisha kwamba mbwa wote na paka wamevalia ukosi na kwambaumewakaa vizuri shingoni na wanao utambulisho bora zaidi.

Ndege wanafaa kusafirishwa kwenye kichukuzi chao cha usafiri kwa usalama.Wapatie slaisi kadhaa za matunda na mboga zilizo na kiwango kingi cha maji.Kuwa na picha kwa minajili ya utambulisho na vibandiko kwenye miguu.Beba shashi nyingi au magazeti ya kukusanyia kinyesi chao kwenye sehemuya chini ya kiota hicho cha ndege.Nyoka wanaweza kusafirishwa kwenye foronya lakini lazima wahamishwehadi katika maskani mengine yenye usalama zaidi watakapofika katika eneola kuondokea. Beba bakuli kubwa zaidi la maji litakalotoshea kujirowekeandani pamoja na padi ya kujipatia joto.Wakati wa kusafirisha mijusi wa nyumbani au wajusi wa nyumbani fuatamaagizo sawa kama yale ya ndege.Mamalia wadogo (hamsta, gebili, nk) wanafaa kusafirishwa kwenye vichukuzivyao salama. Chukua vifaa vya malazi, mabakuli ya chakula na chupa za maji.

Mifugo ya kibinafsi na janga

5

Page 9: Je Uko Tayari? - Fargo, ND · . Kuwa macho kwa kuangalia hali ya hewa inayobadilika na epukana na usafiri usiohitajika. Onyo ya dhoruba inamaanisha kwamba dhoruba inaelekea kuonekana

Mojawapo ya maagizo ambayo unawezakupewa wakati ambapo vifaa hatari huendavimetolewa katika anga ni kujihifadhi “mahalimaalum”. Tahadhari hii inalenga katikakukuweka salama kwa kukuweka ndani kwandani. (Hali hii si sawa na kuenda katikahifadhi ya umma kwenye shule au mahalipengine.) Kuhifadhiwa mahali maalumkunamaanisha kuteua chumba kidogo chandani kwa ndani kilichopo na madirishamachache au hata bila madirisha nakujihifadhi hapo. Haimaanishi kuzuia kabisanyumbani pako pote au jengo la ofisi.

Huenda ukahitaji mahali maalum pakuhifadhi vitu kama vile kemikali, vyakibiologia au vya kiradiolojiavitakavyotolewa kwenye mazingira. kama hali hii itafanyika, mamlaka yaumma yatatoa maelezo kwenye vituo vya televisheni na redio ilikukusaidia kujilinda pamoja na familia yako. Washa redio au televishenimahali pako pa kazi ili uweze kutaarifiwa kuhusu hali zozote haribifumara moja.Jua jinsi ya kujihifadhi mahali maalum� Yarudishe na uyafunge madirisha yote na milango ya kutoka nje.� Kama utaambiwa kwamba kuna hatari ya mlipuko, ifunge pia miinukoya dirisha, masanduku ya madirisha na mapazia.

� Zima mapankaboi yote, pamoja na mifumo yote ya joto, na kusambazahewa safi.

� Funga kiowevu cha mahali pa moto.� Tafuta kijisanduku chako cha kujitayarishia dharura pamoja na redio � Nenda katika chumba cha ndani kisichokuwa na madirisha ambachokiko katika kiwango cha juu zaidi na ardhi. Beba pia mifugo uipendayopale nyumbani.

� Tumia tepu ya bomba pamoja na bati la plastiki (ni nene zaidi kulikokifungaji cha chakula) ili kuziba mianya ya joto iliyoko karibu na mlangopamoja na venti zozote zinazoingia chumbani.

� Endelea kusikiliza redio au televisheni mpaka utakapoambiwa kwambakila kitu ni salama.

Funga mapazia na uyafungemadirisha yako na milango,kama mamlakawatakushauri kujihifadhimahali maalum.

Kujihifadhi mahali maalum

6

Page 10: Je Uko Tayari? - Fargo, ND · . Kuwa macho kwa kuangalia hali ya hewa inayobadilika na epukana na usafiri usiohitajika. Onyo ya dhoruba inamaanisha kwamba dhoruba inaelekea kuonekana

Tahadhari ya dhoruba inamaanisha dhorubahuenda ikawezekana kupatikana katika eneolako. Wakati tahadhari inatolewa, visikilizevituo vya redio pamoja na televisheni kwamaelezo zaidi au tembelea tovutiwww.weather.gov.

Kuwa macho kwa kuangalia hali ya hewainayobadilika na epukana na usafiriusiohitajika.

Onyo ya dhoruba inamaanisha kwambadhoruba inaelekea kuonekana au tayari ipokatika eneo lako. wakati ambapo onyo yadhoruba inatolewa, wataalamu wa usalamawanapendekeza kwamba ukae ndani yanyumba; ndipo mahali bora zaidi pakujilinda wewe mwenyewe.

Onyo na tahadhari

Kumbuka: Onyo yadhoruba inamaanishakwamba dhoruba inaelekeaau iko katika eneo lako.

Vingora vya onyo vya nje ya nyumba vinatufanya kuwa macho kuhusukuvuja kwa kemikali, hali mbaya ya hewa na dharura nyinginezo za njeya nyumba. Wakati ambapo ving’ora vinatolewa, nenda ndani ya nyumbana uiwashe televishseni yako au redio ili kupata kujua ni hali gani na jinsigani unavyoweza kujilinda.

Usichukulie vivihivi kwamba hakuna dharura kwa sababu mbingu ziwazi.

Majaribio ya ving’ora hufanyika kila Jumatano ya kwanza ya mwezi saa sabaadhuhuri kule Fargo, Dilworth na Moorhead. Jiji la Fargo Magharibihujaribu ving’ora vyake kila siku saa sita adhuhuri.

Ving’ora

7

Mfumo mwekundu ni mfumo atomatiki wa kutaarifu ambao unawezakuwasiliana na nyumbani, biashara, au hata simu za mkononi kwa ujumbewa dharura uliorekodiwa na maofisa wa eneo lako. CodeRED unapatikanakwa wakazi wote wa jimbo la Cass na Clay. Tembelea Tovuti ya mji wako au jimbo ili kujisajili au piga simu 476-4068 (Jimbo la Cass) au 299-5151(Jimbo la Clay).

Mfumo wa tahadhari wa CodeRED

Page 11: Je Uko Tayari? - Fargo, ND · . Kuwa macho kwa kuangalia hali ya hewa inayobadilika na epukana na usafiri usiohitajika. Onyo ya dhoruba inamaanisha kwamba dhoruba inaelekea kuonekana

8

Maofisa wa serikali wa eneo lako hutoka amri ya kuondoka mahali wakatiambapo janga hutishia. Zisikilize ripoti za redio yako na televisheni wakatiambapo dharura hutokea. Kama ofisa wa eneo lako watakuomba uondoke,fanya hivyo mara moja!

Kama una muda mfupi tu wa kuondoka, chukuavifuatavyo:

� Vitu vya kimatibabu-maagizo ya kimatibabu, tepe za majaribio za bolisukari, n.k.

� Miwani ya machoni au lensi za machoni namajimaji ya kusafisha.

� Kijisanduku cha kujitayarishia dhoruba (tazama ukurasa 3)

� Nguo na malazi� Funguo za gari

Kama wajumbe wa eneo lako hawajashaurikuondoka kwa mara moja, chukua hatua hizi ilikupalinda nyumbani pako kabla ya kuondoka:

� Zima umeme kwenye kiwambo kikuu au kikatizina uyafunge maji kwenye valvu kuu.

� Wacha gesi ya kimaumbile ikiwa imewashwaisipokuwa tu kama wajumbe wa eneo lakowatakushauri vinginevyo.

� Kama pepo kuu zinatarajiwa, funika sehemu ya juu ya madirisha yote.� Kama mafuriko yanatarajiwa, unaweza kufikiria kutumia sandibagi ilikuzuia maji kuingia.

� Zichukue nyaraka muhimu pamoja nawe, leseni ya dereva, kadi yausalama ya kijamii, sera za bima, vyeti vya ndoa na kuzaliwa, hisa, wosia, n.k.

Hifadhi za jamii zinaweza kufunguliwa katika dharura fulani au majanga.Vyombo vya habari vitatangaza sehemu hizi. Na mara nyingi hifadhi hiyoitakirimu tu vifaa vya dharura kama vile mlo, malazi na blangeti. Tahadharikwamba mifugo ya kibinafsi (isipokuwa tu wanyama wa huduma) maranyingi hairuhusiwi kwenye hifadhi za jamii kwa sababu za afya.

Kumbuka: Kamalazima uondokenyumbani pako,kuwa na hakikakuchukua miwaniau lensi za machopamoja na dawa.

Hifadhi za kuondolewa na jamii

Page 12: Je Uko Tayari? - Fargo, ND · . Kuwa macho kwa kuangalia hali ya hewa inayobadilika na epukana na usafiri usiohitajika. Onyo ya dhoruba inamaanisha kwamba dhoruba inaelekea kuonekana

9

Weka kingora cha moto nje ya kilasehemu ya kulalia na katika kilakiwango cha nyumbani kwako. Kamawatu nyumbani pako wanalala wakatimilango imefungwa, weka vingora vyamoshi ndani ya maeneo ya kulalia.

Jaribu vingora vya moshi mara mojakwa mwezi na ubadilishe betri zoteangaa mara moja kwa mwaka. Badilishavingora kila baada ya miaka 10.

Kuwa na kizima moto kimoja auzaidi nyumbani pako. Wasiliana naidara ya moto katika eneo lako kwaushauri kuhusu ni aina gani ya vizimamoto hivyo hufanya kazi bora zaidi.Tazama ukurasa 1 kwa nambari za simuza idara ya moto.Panga njia zako za kukimbia

Kimbia kwa usalamaKama utauona moshi au moto kwenye njia yako ya kwanza ya kukimbilia,tumia njia ya pili. Kama lazima uondoke kupitia kwenye moshi, basitambaa kwa chini katika moshi huo kuelekea mahali pa kutokea.Kama unakimbilia kupitia mlango uliofungwa, basi hisi mlango huo kablaya kuufungua. Kama una joto, tumia njia yako ya pili katika kuondoka.Kama moshi, au joto au miaki inakuzuia kwenye njia zako za kutorokea, nahuwezi kutoroka kupitia dirishani, baki kwenye chumba kama mlangoumefungwa. Toa ishara ya msaada ukitumia kitambaa kililcho na rangi yakuvutia nje ya dirisha. Kama kuna simu chumbani piga 911 na uwaambiewatakaokupokea ni wapi ulipo.Pindu utokapo nje, baki nje! Piga 911 kutoka nyumbani ya jirani yako.

� Pata kujua angaa njia mbili za kukimbilia kutoka katika kila chumba chanyumbani pako.

� Chukulia vidaraja vya kukimbilia kuelekea maeneo ya kulalia kwenyeghorofa la pili au la tatu.

� Teua mahali ambapo kila mmoja atakutana baada ya kukimbia. � Fanya mazoezi ya mpango wa kukimbia angaa mara mbili kwa mwakapamoja na wanafamilia wako.

Kumbuka: Jaribu vingo’ra vyamoshi kila mwezi na badilishabetri zake angaa mara mojakwa mwaka.

Usalama wa moto nyumbani

Page 13: Je Uko Tayari? - Fargo, ND · . Kuwa macho kwa kuangalia hali ya hewa inayobadilika na epukana na usafiri usiohitajika. Onyo ya dhoruba inamaanisha kwamba dhoruba inaelekea kuonekana

10

Sasa ndio wakati wa kuangalia hatari ya eneo lako kwa mafuriko. Kamahuna hakika kama unaishi kwenye eneo ya mafuriko, wasiliana na serikaliya eneo lako ili kupata kujua. Kama uko katika eneo la mafuriko, fikiriakununua bima yamafuriko.

Wakati ambapotahadhari ya mafurikoinatolewa, sogezasamani yako na vituvyako vya thamanikwenye ghorofa la juuzaidi nyumbani pako.Jitayarishe kwakuondoka amakotorokeakutakakowezekana.

Wakati ambapo onyoya mafuriko inatolewa,visikilize vituo vyaredio au tazamatelevisheni ya eneo lakokwa maelezo na maelekezo.

Wakati ambapo onyo la gharika inatolewa, songa katika sehemu ya juuzaidi mbali na mito, visima, creeks na maeneo la dhoruba.

Usiendeshe kwenye vizuizi. Kama gari lako litakwama kwenye maji yanayopanda kwa kasi, liache mara moja na ukimbilie eneo la juu zaidi.

Wakati wa onyo ya Mafuriko ya Ghafla,usiliendeshe gari karibu na vizuizi vya barabaraau kujaribu kuendesha kwenye barabara za maeneo ya chini zilizofunikwa na maji.Kupuzilia mbali kimo cha maji kunaweza kuwa kosa hatari mno.

Mafuriko na gharika za ghafula

Page 14: Je Uko Tayari? - Fargo, ND · . Kuwa macho kwa kuangalia hali ya hewa inayobadilika na epukana na usafiri usiohitajika. Onyo ya dhoruba inamaanisha kwamba dhoruba inaelekea kuonekana

11

Kama unaweza kusikiliza radi, basi ukokaribu zaidi na dhoruba na huendaukapigwa na mimweso. Nenda katikahifadhi salama mara moja, na uisikilizeredio la eneo lako na vituo vya televishenikwa maelezo na maelekezo. Hakikishakwamba redio ya hali ya hewa ya NOAAimewashwa.

Wakati ambapo dhoruba inakaribia, basiondoa vifaa vyote vya umeme kwenyeumeme na uzime pakaboi. Epuka kutumiasimu au vifaa vyovyote vya elektroniki nausioge au kunawa wakati huo.

Kama u msituni, jihifadhi chini ya mitimifupi zaidi. Kama ukatika mashua auunaogelea, wahi ardhi na upate hifadhimara moja!

Kama huwezi kupata hifadhi, nendakatika eneo la chini zaidi sehemu wazimbali na miti, fito au vifaa vya chuma.Chutama chini zaidi karibu na ardhi, na uiweke mikono yako kwenye magotiyako huku kichwa chako kikiwa katikati ya magoti hayo. Usilale chalikwenye ardhi.

Baada ya dhoruba kupita, epukana na maeneo yalioharibiwa na dhoruba.Isikilize redio au tazama vituo vya televisheni vya eneo lako kwa maelezo na maelekezo.

Kama mtu amepigwa na mimweso, yeye hana chaji ya umeme na anawezakushikwa kwa usalama. Piga simu 911 na utoe huduma ya kwanza.

Mbinu za kawaida za huduma ya kwanza, zinaweza kuwa muhimu sana kwa hivyo jifunze sasa. Tazama kurasa zako za njano katika eneo lako kwakupata orodha ya watoaji huduma ya mafunzo ya huduma ya kwanza.

Kumbuka: Kama unawezakuisikiliza radi, basi ukokaribu sana na dhoruba naunaweza kupigwa namimweso. Tafuta hifadhimara moja.

Mimweso na radi

Page 15: Je Uko Tayari? - Fargo, ND · . Kuwa macho kwa kuangalia hali ya hewa inayobadilika na epukana na usafiri usiohitajika. Onyo ya dhoruba inamaanisha kwamba dhoruba inaelekea kuonekana

12

Teua mahali ambapowanafamilia wako wanawezakujikusanya kama zinizalainaelekea upande huo. Vyumbavya chini kwa chini ni borazaidi; kama huna, basi chaguasehemu ya katikati kwenyeukumbi, bafu au chumbakwenye ghorofa la chini zaidi.

Kama uko nje, basi kimbiliakwenye vyumba vya chini kwachini au kwenye jengo fupi lililokaribu au lala chali kwenyemtaro au eneo la chini zaidi.

Kama u ndani ya gari aunyumba sogevu, basi ondokamara moja na uelekee kwenyeusalama.

Baada ya kimbunga, tahadharina nyaya za umemezilizoanguka na uepukanekwenda katika eneoliloharibiwa. Isikilize redio auutazame vituo vya televishenivya eneo lako kwa maelezo na maelekezo.

Kumbuka: Kama huna vyumba vya chinikwa chini, bafu au ghorofa la chini zaidikatika nyumba yako ni mahali pazuri pakutafuta hifadhi wakati wa zilizala. Kuwana hakika kuibeba redio yako ya hali yahewa hadi katika hifadhi yako ya muda.

Vimbunga

Page 16: Je Uko Tayari? - Fargo, ND · . Kuwa macho kwa kuangalia hali ya hewa inayobadilika na epukana na usafiri usiohitajika. Onyo ya dhoruba inamaanisha kwamba dhoruba inaelekea kuonekana

13

Kama utakutana na waya waumeme ulioanguka, ondokamahali hapo mara moja nautafute msaada kwa kupiga 911.

Kama u ndani ya gari wakatiambapo waya wa umemeunalilangukia, basi subiri ndaniya gari mpaka wakati ambapomsaada utatokea. Kama lazimauondoke ndani ya gari kwasababu ya jeraha linalotishiamaisha yako:

� Ruka juu kutoka kwenye garina ukanyage chini kwa miguuyako yote.

� Usiushikilie mlango wa gariwakati unaruka.

� Ukishafika kwenye ardhi, ruka ukienda- usikimbie

Nyaya za umeme zilizoanguka

Page 17: Je Uko Tayari? - Fargo, ND · . Kuwa macho kwa kuangalia hali ya hewa inayobadilika na epukana na usafiri usiohitajika. Onyo ya dhoruba inamaanisha kwamba dhoruba inaelekea kuonekana

14

Hatari tunazokumbanazo wakati wa misimbu yakiwango cha juu cha joto vinajumuisha:

Krampu za joto: Haya ni maumivu ya misuli naspasmusi yanayotokana na kufinyikiza kuzito. Niishara ya mapema kwamba mwili una matatizo na joto.

Uchovu wa joto: Hali hii kwa kawaida inafanyikawakati ambapo watu wanafanya mazoezi mazito auwanafanya kazi mahali penye joto, au pasipokuwana hewa safi wakati ambapo majimaji ya mwiliyanapotezwa kupitia kwa utokaji wa jasho jingi.Hali ya damu kusafiri kwenye mwili, hadi kwenyengozi inaongezeka, na kusababisha damu hiyokupungua kwenye viungo muhimu. Hali hii

inasababisha mtu kuwa katika mshtuko wa kawaida.Kama hali hii haitibiwi, muhusika anaweza kuuguajoto la stroke

Joto la stroki (stroki ya jua): Joto la stroki ni haliya kuhatarisha maisha. Mfumo dhibiti wa hali yajoto ya muhusika, ambao ndio unaotoa joto ilikutuliza mwili, huacha kufanya kazi. Hali ya joto ya mwili inaweza kuwa kubwa kiasi cha kwambaubongo unaweza kuharibika na kifo kikatokea kamamwili hautatulizwa haraka.

Kama wimbi la joto litatabiriwa au linafanyika…

� Tulia. Epukana na shughuli za kujistrain.� Baki ndani kwa ndani mara nyingi uwezavyo.� Vaa mavazi mepesi, na yenye rangi nyepesi.� Kunywa maji mengi mara kwa mara na kila mara.� Kula mlo ama vyakula vidogovidogo mara kwamara .

� Epukana na kutumia tembe za chumvi isipokuwatu kama umeelekezwa kufanya hivyo na daktari.

Uchovu wa jotounawezakusababisha mshtukowa kawaida nakusababisha strokeya joto, hali yakuhatarisha maisha.

Kumbuka: Kunywamaji mengi wakatiwa wimbi la joto naule chakula kidogokidogo, na maranyingi.

Mawimbi ya joto

Page 18: Je Uko Tayari? - Fargo, ND · . Kuwa macho kwa kuangalia hali ya hewa inayobadilika na epukana na usafiri usiohitajika. Onyo ya dhoruba inamaanisha kwamba dhoruba inaelekea kuonekana

15

Kabla dhoruba haijaingia kuwa na blangeti za ziada na uhakikishe kwambakila mmoja wa familia yako analo koti lenye joto, glovu pamoja na mkufu,kofia yenye joto na njuti zisizo ingiza maji.Wakati wa dhoruba, epuka kuondoka nje. Kama lazima uondoke, valiamavazi kadhaa mepesi-haya yatakufanya kuhisi joto zaidi kuliko koti mojazito. Kifunike kinywa chako ili kulinda mapafu yako dhidi ya hewa baridina vumbi.Unafaa kuepuka kusafiri kwa gari kwenye dhoruba, lakini kama lazimausafiri:

� Beba kijisanduku cha kujitayarishiadharura ndani ya gari lako (tazamaukurasa wa 3 kwa maelezo)

� Hifadhi tangi la mafuta la gari lako kama limejaa.

� Mwache mtu ajue unakoelekea, njiautakayo ipitia na muda utakao chukuakufika huko.

Kama utakwama ndani ya gari…

� Baki ndani ya gari. usijaribu kutembeahadi kwa usalama .

� Funga kitambaa chenye rangi za kuvutia(nyekundu inafaa zaidi) kwenyekinasamawimbi cha gari lako ili waokoaji waone.

� Washa gari na uanzishe kitoa joto kwamuda wa dakika 10 kila saa.

� Wacha dirisha moja (lisilokabiriana naupepo) likiwa limefunguka kiasi ilikuingiza hewa.

� Ziwache taa za gari lako zikiwa zimewakawakati engine yako pia inachapa kazi iliuweze kuonekana.

� Unapoketi, isongeze mikonno na miguu yako ili kuendeleza msongo wadamu na kuwa mwenye joto.

Kama itabidi uondoe theluji baada ya dhoruba, kuwa makini iliusijioverexert. Shughuli nzitu kwenye hali ya hewa baridi inaweza kustrainmoyo wako.

Kumbuka: Kama lazimauende nje wakati wadhoruba, valia mavazikadhaa mepesi hayayatakufanya kuhisi jotozaidi kuliko koti moja zito.

Dhoruba za msimu wa baridi na kipupwe

Page 19: Je Uko Tayari? - Fargo, ND · . Kuwa macho kwa kuangalia hali ya hewa inayobadilika na epukana na usafiri usiohitajika. Onyo ya dhoruba inamaanisha kwamba dhoruba inaelekea kuonekana

16

Moto wa kichakani mara nyingi huanza bila kutambuliwa na kusambaaharaka, huweza kuwasha burashi, miti na hata nyumba mbalimbali. Watumara nyingi ndiyo chanzo cha moto wa kichakani. Punguza hatari yakutokea kwa moto wa kichakani kutokea katika eneo lako kwa:� kutii marufuku yoyote ya kuchoma ambayo inatekelezwa.� kupiga simu 911 ili kupiga ripoti ya moto wa nyasi au aina yoyote yamoto wa nje ya nyumba.

� kufunza watoto kuhusu usalama wa moto na kuweka mbali vibiriti naviwashaji wasikofika watoto hao.

Kunazo njia nyingine ambazo unawezakuzuia moto kichaka pia. Sanifu napangilia nyumbani kwako huku ukitiliamaanani moto wa kichaka. Teua vifaana mimea ambayo inaweza kukusaidiakudhibiti moto badala ya kuuongeza.Tumia vizuizi vya moto au vifaavisivyochomeka kwenye paa na majengona vifaa vya nje ya jengo. Aidha pandavichaka visivyochomeka au miti.

Unda eneo la usalama lipatalo futi 30 hadi 50 karibu na nyumbani kwakokwa kuweka pamoja majani na matawi.Ondoa nyasi zozote zinazowezakuchomeka. Toa matawi ambayoyanarefuka hadi juu ya paa. Ombakampuni ya umeme kuyaondoa matawikutoka katika nyaya za umeme. Ondoamizabibu kutoka katika kuta zanyumbani pako na ukate nyasi marakewa mara.

Ondoa eneo lipatalo futi 10 lililo karibu na matangi ya gesi aina ya propenina grili. Weka pamoja kuni angaa futi 100 mbali na nyumbani pako aumahali pa biashara na pia mahali juu zaidi.

Hifadhi chanzo cha maji kinachotosha nje ya nyumba. Kuwa na bomba yakunyunyizia maji kitaluni ili kufikia eneo lolote katika nyumba yako. Wekasehemu za kutolea nje maji katika angaa pande mbili za nyumbani pako.

Wakati moto wa kichakaunatishia: Rudisha gari lakokwenye karakana au liegeshekatika nafasi wazi inayotazamanana upande wa kutorekea. Kamautashauriwa kuondoka basiondoka mara moja!

Moto wa kichakani

Page 20: Je Uko Tayari? - Fargo, ND · . Kuwa macho kwa kuangalia hali ya hewa inayobadilika na epukana na usafiri usiohitajika. Onyo ya dhoruba inamaanisha kwamba dhoruba inaelekea kuonekana

17

Kabla ya kupotea umeme…� kama unacho kifunguzi cha karakana ya umeme, kitafute kile chakufungua kwa mkono na ujifunze jinsi ya kukitumia.

� Weka tangi la mafuta la gari yako angaa nusu; vituo vya mafutavinategemea nguvu za umeme kwenye pampu zao.

� Kuwa na betri ya ziada kwa manufaa ya viti vya walemavu vinavyotumia betri.

Wakati wa kupotea umeme…� Tumia kurunzi tu kwa utoaji mwangaza wadharura usiwahi kutumia mishumaa kwasababu inachangia pakubwa katika kuongezahatari ya moto wa nyumbani kwa kiwangokikubwa

� Simu nyingi sizo waya hazifanyi kazi wakatiumeme unapotea kwa hivyo kuwa na hakikakuwa na simu ya wasstani katika nyumba yako.Simu za mkono huenda zisifanye kazi vizuriwakati wa kupotea kwa umeme kwa sababumitandao za simu za umeme ama simu zamkononi huenda zika poteza nguvu kwenyeminara ambayo inasambaza simu yako.

� Zima vifaa vya umeme ambavyo ulikuwaukitumia wakati umeme ulipopotea wacha taa moja ikiwaka ili utambue wakati umemeutarudi.

� Epukana na kufungua friji na friza. Dawanyingi ambazo zinahitaji huduma ya frijizinaweza kuhifadhiwa kwenye frigi iliyofungwakwa saa kadhaa.

� Usiendeshe jenereta ndani ya nyumba aukarakana au kiunganisha kwenye mfumo waelectroniki wa nyumbani. Kama utatumiagenerator, iunganishe kwenye vifaa unavyotakakupatia nguvu za umeme moja kwa mojakutoka kwenye vitowaji kwenye generator.

� Sikiliza redio ili kupata maelezo ya hivi punde zaidi.

Kumbuka: Hakikisha yakwamba kunayo simu yakawaida iliyo na nyayandani ya nyumba yako.Huenda ikawa ndio simuya pekee ambayoitafanya kazi wakazi wakupotea umeme.

Kupotea kwa umeme

Page 21: Je Uko Tayari? - Fargo, ND · . Kuwa macho kwa kuangalia hali ya hewa inayobadilika na epukana na usafiri usiohitajika. Onyo ya dhoruba inamaanisha kwamba dhoruba inaelekea kuonekana

Unaweza kusaidia kuzuiadharura ya mafuta yakimaumbile kwa kupiga simu kwenye huduma tafutizi(811 kule Dakota kaskazini naMinnesota) kabla ya kuingiakwenye mali yako hiiitakusaidia kuepukanakugonga nyaya za gesi.

Kama utainusa gesi nje yanyumba, ondoka kwenyesehemu hiyo mpaka mahaliambapo hunusii tena gesi hiyona upige 911. Usirudi tenakatika eneo hilo mpakawahusika wakwambie kwambampaka usalama kurudiwa.

Kama utainusa gesi ndani yanyumba, toka nje mara mojahuku ukiiacha milango wazi ili kusaidia kusambaza hewa safi ndani yajengo. Usitumiye swichi za taa, vifaa vya electroniki au simu (simu yamkononi au tambaa) katika nyumbani palipoathiriwa au jengo. Zima sigarana usiwashe vibiriti.

Songa umbali uliyo salama kutoka katika nyumba yako na upige simu 911.Usirudi katika eneo hilo mpaka wahusika wanaofaa wakwambie kwamba nisalama kufanya hivyo.

Hakikisha ya kwamba huduma tafutiziinayofaa imepatikana kabla ya kuipandamiti, kuweka fito za kizingiti, au kufanyauchimbaji wowote ule ndani ya barazalako. Hali hiyo inaweza kuzuia dharura ya nyumbani.

Dharura za mafuta ya kimaumbile

18

Page 22: Je Uko Tayari? - Fargo, ND · . Kuwa macho kwa kuangalia hali ya hewa inayobadilika na epukana na usafiri usiohitajika. Onyo ya dhoruba inamaanisha kwamba dhoruba inaelekea kuonekana

19

Chini ya hali fulani, kemikali ambazo kwakawaida ni salama zinaweza kuwa sumu auharibifu kwa afya yako. Dharura kuu yakemikali ni ajali ambayo inatoa kiwangohatari cha kemikali ndani ya mazingira. Ajalizinaweza kutokea chini ya ardhi, kwenye reliau barabara kuu, na hata katika viwanda vyautengenezaji vifaa. zinaweza kuhusisha motoau mlipuko, au unaweza kuwa na uwezo wakutoona au kunusia chochote.

Unaweza pia kukabiliwa na kemikali kwa:� Kuipumua kemikali hiyo.� Kumeza chakula kilicho na sumu, maji au dawa.� Kugusa kemikali au kukabiliana nayo, kupitia kwenye mavazi au vifaavingine ambavyo vimegusa kemikali.

Kama uko nje ya nyumba wakati wa utokaji mkuu wa vitu vyakuhatarisha, basi baki kusikokuwa na upepo au kwenye sehemu ya juuambapo kemikali hiyo inatokea na upate hifadhi mara moja.

Watu wengi hufikiri kwamba kemikali ni vile vifaa tuu ambavyo vinatumikakwenye michakato ya kutengeneza kule viwandani. Lakini kemikalizinapatikana kila pahali ndani ya jikoni, kwenye mashubaka ya dawa, vyumbavya chini kwa chini na karakano. Dharura maarufu ya nyumbani yakemikali inahusu watoto wadogo kula dawa. Hifadhi dawa zote, vifaa vyakusafisha za urembo, na chemikali zinginezo za nyumbani mbali na watoto.Kama mtoto wako atakula au kunywa kitu kisichokuwa chakula, tafutamikebe yote mara moja na uwachukue na uwapeleke hospitali mara moja.Piga simu kwenye kituo cha kudhibiti sumu (tazama ukurasa wa kwanza kwanambari yao au 911 na ufuate kwa makini maagizo utakayo pewa.Tahadhari za bidhaa za nyumbani� Epuka kuchanganya kemikali za nyumbani.� Siku zote soma maelekezo kabla ya kutumia bidhaa mpya.� Usiwahi kuvuta sigara wakati unatumia kemikali za nyumbani.� Panguza kemikali zilizomwagika mara moja huku ukilinda macho na ngozi yako.

� Tupa bidhaa kwa njia nzuri ili kuilinda mazingira na mbuga.

Dharura za kemikali

Page 23: Je Uko Tayari? - Fargo, ND · . Kuwa macho kwa kuangalia hali ya hewa inayobadilika na epukana na usafiri usiohitajika. Onyo ya dhoruba inamaanisha kwamba dhoruba inaelekea kuonekana

20

Dharura ya afya ya umma inajumuisha mikurupuko ya ugonjwa, dharura yakibiologia au kikemikali, na majanga ya kifaifa. Vituo vya kudhibitimagonjwa na kinga yake vinahimiza kujitayarisha na kisanduku cha dharuraya hatari zote ambacho kinaweza kutumiwa wakati wa janga lolote. Tazamaukurasa wa 3 kwa maelezo kuhusu upataji wa kijisanduku cha dharura.

Mshambulio wa kiugaidi wa kibiologia ni ile hali ya kutoa virusi vyabacteria au viini vinginevyo (viitwavyo agenti) kwa kujua ili kusababishamagonjwa, vifo vya watu, wanyama au mimea. Agenti za kibaiologiazinaweza kusambazwa kwenye hewa kupita katika maji au chakula. Magaidi yanaweza kutumia agenti za kibiologia kwa sababu hizo agentizinatambulika kwa ugumu sana na zinaweza kusababisha magonjwa kwa saakadhaa au hata siku kadhaa. Baadhi ya agenti za ugaidi wa kibiologia, kamavile virusi vya small pox, zinaweza kusambazwa kutoka kwa mtu mmojahadi mwingine na wengine kadhaa kamavile anthrax haiwezi.

Afya ya umma ya Fargo Cass pamoja naafya ya umma ya Clay County wanayomipango ya kusambaza dawa na kutoachanjo kwa umma wakati wa dharura yaafya ya umma. Sehemu za umma zakufanya hayo zitatangazwa kwa ummawakati wa dharura.

Mpango wa janga la mafua.Bila shaka umesikia kuhusu uwezekanowa kuwapo na mrupuko wa mafua yandege kote ulimwenguni. Ushirikianowa mafua ya jamii umekuwa ukikutanaili kuendeleza mipango itikizi katikakushughulikia janga linalo wezekana la mafua kama hili. Kundi hililinajumuisha uwakilishi kutoka majimboya Cass na Clay pamoja na wakala waafya ya umma, hospitali, nyumba zakutoa huduma za utabibu, vuo vikuu, wakala wa afya wa vyuo, huduma za utunzaji wa umma na zahanati.

Dharura za afya ya umma

Katika dharura ya afya yaumma, zahanati zinawezakuandaliwa ili kutoa chanjo audawa kwa umma.

Page 24: Je Uko Tayari? - Fargo, ND · . Kuwa macho kwa kuangalia hali ya hewa inayobadilika na epukana na usafiri usiohitajika. Onyo ya dhoruba inamaanisha kwamba dhoruba inaelekea kuonekana

Chapisho hili limewezekana kutokana na wafuatao:

Serikali ya jimbo la Cass

Jiji la Dilworth

Jiji la Fargo

Jiji la Moorhead

Jiji la West Fargo

Serikali la jimbo la Clay

Afya ya umma ya Fargo Cass

Minn-Kota Chapter, American Red Cross

United Way of Cass-Clay

Chapisho hili limeungwa mkono na Grant/CooperativeAgreement Number 5U90TP817000 kutoka CDC. Yaliomo ni wajibu wa uandishi na hayawakilishi

kwa vyovyote vile maoni rasmi ya CDC.