july,2013 - ihi.kazi.proihi.kazi.pro/wordpress/wp-content/uploads/2017/08/... · 1.uchambuzi wa...
TRANSCRIPT
TAASISI YA UTAFITI NA UTETEZI WA HAKI ZA ARDHI
UCHAMBUZI WA RASIMU YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
JULY,2013
1.UCHAMBUZI WA RASIMU YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
1.1 SEHEMU YA UTANGULIZI KATIKA RASIMU
Aya ya kwanza:-Inavyosomeka katika Rasimu
KWA KUWA, Sisi, Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumeamua rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi yetu jamii
inayoheshimu na kuzingatia misingi ya utu, uhuru, haki, usawa, udugu, amani, umoja na mshikamano katika nyanja zote za maisha yetu;
Aya ya kwanza:-Maoni yanayopendekezwa
KWA KUWA , Sisi, Watu wa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar tumeamua kuingia katika shirikisho au
muungano(moja wapo kati ya hayo)rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi yetu usawa, udugu, amani, umoja na mshikamano katika Nyanja
zote za maisha yetu
Pia neno Tanzania Bara inapendekezwa lisitumike na badala yake pale inapojitokeza isomeke Jamhuri ya Tanganyika katika Rasimu nzima
ya Katiba
Aya ya mwisho:- Inavyosomeka Katika rasimu
HIVYO BASI, KATIBA HII YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ILIYOPENDEKEZWA NA BUNGE MAALUM LA
KATIBA imetungwa na SISI WANANCHI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA kupitia KURA YA MAONI kwa madhumuni
ya kujenga jamii kama hiyo, na kuhakikisha kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaongozwa na Serikali yenye kufuata misingi ya
demokrasia na utawala wa sheria, kujitegemea na isiyokuwa na dini.
Aya ya mwisho:- Inavyopendekezwa
HIVYO BASI, KATIBA HII YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ILIYOPENDEKEZWA NA BUNGE MAALUM LA
KATIBA imetungwa na SISI WATU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA kupitia KURA YA MAONI kwa madhumuni ya
kujenga jamii kama hiyo, na kuhakikisha kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaongozwa na Serikali yenye kufuata misingi ya
demokrasia na utawala wa sheria, kujitegemea na isiyokuwa na dini.
SURA YA KWANZA-JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Sehemu ya kwanza-Mipaka,Alama,Lugha,Utamaduni na Tunu za Taifa
Ibara
Ibara inavyosomeka Ibara inavyopendekezwa Sababu za mabadiliko
1(1)(2)
1.-(1) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni
Shirikisho lenye
mamlaka kamili ambayo imetokana na Muungano wa
nchi mbili za
Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa
Zanzibar ambazo kabla
ya Hati za Makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964
zilikuwa nchi
huru.
(2) Jamhuri ya Muungano ni Shirikisho la
kidemokrasia
linalofuata mfumo wa vyama vingi vya siasa, usawa
wa binadamu,
kujitegemea, utawala wa sheria na kuheshimu haki za
binadamu.
Katiba iainishe ni neno gani kati
ya shirikisho au muungano
litumike na sio yote kwa pamoja
Maneno “Shirikisho” na
“Muungano” haviwezi kutumika
pamoja kwani mifumo yake
kiutawala ni tofauti
2
Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania
Bara ikijumuisha sehemu yake ya bahari na eneo lote
la Zanzibar ikijumuisha sehemu yake ya bahari.
-mipaka halisi ya nchi za
muungano yaani Jamuhuri ya
Tanganyika na Jamuhuri ya watu
wa Zanzibar ianishwe kwenye
katiba
- Pia neno Tanzania Bara
inapendekezwa lisitumike na
badala yake pale inapojitokeza
isomeke Jamuhuri ya
Tanganyika
Muungano wa 1964 ulihusisha
Jamuhuri ya Tanganyika na
Jamuhuri ya watu wa Zanzibar
4(3)
Serikali itaweka mazingira yatakayowezesha kuwepo
kwa mawasiliano ya lugha mbadala zikiwemo lugha za
alama,na nukta nundu kwenye sehemu muhimu za
umma na katika vyombo vya habari vinavyotangaza
habari zake kitaifa kwa ajili ya watu wenye mahitaji
maalum.
Serikali itaweka mazingira
yatakayowezesha kuwepo kwa
mawasiliano ya lugha mbadala
zikiwemo lugha za alama,
maandishi yaliyokuzwa na
nukta nundu kwenye sehemu
muhimu za umma na katika
vyombo vya habari
vinavyotangaza habari zake
kitaifa kwa ajili ya watu wenye
mahitaji maalum.
-kukidhi mahitaji ya
mawasiliano kwa watu wenye
mahitaji maalumu
5(h)
5. Jamhuri ya Muungano itaenzi na kuzingatia Tunu za
Taifa
zifuatazo:
(a)utu;
(b) uzalendo;
(c)uadilifu;
(d)umoja;
(e)uwazi;
(f)uwajibikaji; na
(g)lugha ya Taifa.
Nyongeza katika ibara hii:-
(h)Utamaduni, Mila na Desturi
zinazokubalika kwa mujibu wa
sheria
Tanzania ni nchi inayoamini
misingi ya watu kuishi kindugu
bila kujali dini, rangi, kabila,
mila, desturi na utamaduni
5(i) (i)Udugu
5(j)
(j)Muungano Ni tunu ya Jamuhuri ya nchi
mbili zilizoungana kwa muda
mrefu licha ya misukosuko ya
hapa na pale ukaendelea kudumu
Sehemu ya pili-Mamlaka ya Wananchi,Utii na Hifadhi ya taifa
6
Jamhuri ya Muungano ni nchi inayofuata misingi ya
demokrasia inayozingatia haki ya kijamii, na kwa
hiyo:
Jamhuri ya Muungano ni nchi
inayofuata misingi ya
demokrasia inayozingatia haki
na usawa wa jamii, na kwa
hiyo:
Usawa ni dhana muhimu sana
katika maisha ndani ya jamii
6(a)
(a) wananchi ndio msingi wa mamlaka za nchi, na
Serikali itapata madaraka na mamlaka yake kutoka
kwa wananchi ambao kwa umoja na ujumla wao
wanaimiliki na kuipatia Katiba hii uhalali;
(a) wananchi ndio msingi wa
mamlaka za nchi, na Serikali
itapata madaraka na mamlaka
yake kutoka kwa wananchi
Uandishi sahihi wa neno la
Kiswahili
ambao kwa umoja na ujumla wao
wanaimiliki na kuipa Katiba hii
uhalali;
6(b)
(b) lengo kuu la Serikali litakuwa ni maendeleo na
ustawi wa wananchi
(b) lengo kuu la Serikali litakuwa
ni maendeleo na ustawi wa
wananchi wote bila ubaguzi
Kuweka Msisitizo
7(2)(c )(j)
7(2)(c)Serikali itahakikisha kuwa shughuli
zinazofanywa zinatekelezwa kwa njia ambazo
zitahakikisha kwamba utajiri wa Taifa unaendelezwa,
unahifadhiwa na unatumiwa kwa manufaa ya
wananchi wote kwa jumla na pia kuzuia mtu
kumnyonya mtu mwingine;
7(2)(j)utajiri wa rasilimali na maliasili za Taifa
unaelekezwa katika kuleta maendeleo, kuondoa
umaskini, ujinga na
maradhi; na
-7(2)(c)Serikali itahakikisha
kuwa shughuli zinazofanywa
zinatekelezwa kwa njia ambazo
zitahakikisha kwamba
utajiri wa Taifa unaendelezwa,
unahifadhiwa na unatumiwa kwa
manufaa ya wananchi wote kwa
jumla bila ya unyonyaji wa aina
yoyote ile;
-utajiri wa rasilimali na
maliasili za Taifa
- utajiri wa taifa na utajiri wa
rasilimali na maliasili
vifafanuliwe katika kipengele
cha ufafanuzi katika rasimu
7(2)(d )
ardhi ikiwa rasilimali kuu na msingi wa Taifa,
inalindwa, inatunzwa na kutumiwa na wananchi wa
Tanzania kwa manufaa, maslahi na ustawi wa kizazi
cha sasa na vizazi
vijavyo;
ardhi ikiwa rasilimali kuu,
kielelezo cha uhai, utamuduni na msingi wa Taifa, inalindwa,
inatunzwa na kutumiwa na
wananchi wa Tanzania kwa
manufaa, maslahi na ustawi wa
kizazi cha sasa na vizazi
Kwa maisha ya mtanzania ardhi
ni uhai ,utamaduni na kielelezo
cha uchumi na maisha endelevu
7(2)(g )
utu, heshima na haki nyingine zote za binadamu
zinahifadhiwa na kudumishwa kwa kuzingatia mila na
utu, heshima na haki nyingine
zote za binadamu zinahifadhiwa
Kuepusha mila na desturi
kandamizi na hatarishi kwa
desturi za kitanzania na kwa kufuata mikataba
mbalimbali iliyoridhiwa na Jamhuri ya Muungano;
na kudumishwa kwa kuzingatia
mila na desturi za kitanzania
zinazokubalika kisheria na kwa
kufuata mikataba mbalimbali
iliyoridhiwa na Jamhuri ya
Muungano
baadhi ya makundi ya kijamii
8(1)
Bila ya kuathiri masharti ya Katiba za Washirika wa
Muungano kwa mambo yasiyo ya Muungano, Katiba
hii itakuwa sheria kuu katika Jamhuri ya Muungano.
Maneno bila kuathiri masharti ya
katiba za washirika wa
muungano kwa mambo yasiyo
ya muungano yaondolewe na
kusomeka tu „Katiba hii itakuwa
sheria kuu katika Jamuhuri ya
Muungano‟
-Hii inaipa katiba hii ya
Muungano kuwa katiba
kuu(Katiba mama ya muungano)
-Pia, itawezesha uandaaji wa
Katiba za nchi washirika kutii
katiba ya muungano
9(3)
(3) Kwa madhumuni ya kuhifadhi masharti ya Ibara
ndogo ya (1) na (2), Serikali itaweka utaratibu wa
kuisambaza Katiba hii kwa
wananchi na kuiweka katika mitaala ya elimu ili
kuwezesha wananchi kuifahamu, kuilinda na kuitii.
(3) Kwa madhumuni ya
kuhifadhi masharti ya Ibara
ndogo ya (1) na (2), Serikali
itaweka utaratibu wa kuisambaza
Katiba hii kwa
wananchi, kwa kuzingatia
mahitaji ya watu wenye
ulemavu na kuiweka katika
mitaala ya elimu ili kuwezesha
wananchi kuifahamu, kuilinda na
kuitii.
Kuna uwepo wa mahitaji ya
kipekee ya walemavu
SURA YA PILI-MALENGO MUHIMU,MISINGI YA MWELEKEO WA SHUGHULI ZA SERIKALI NA SERA ZA KITAIFA
11(3)(b )(i)
(i) kuhakikisha kwamba heshima ya binadamu
inahifadhiwa na kudumishwa kwa kufuata mila,
desturi na Kanuni za Tangazo la Dunia kuhusu
Haki za Binadamu na mikataba mingine ya
kimataifa iliyoridhiwa na Tanzania;
(i) kuhakikisha kwamba heshima
ya binadamu
inahifadhiwa na kudumishwa
kwa kufuata mila na desturi
zinazokubalika kisheria na
Kanuni za Tangazo la Dunia
Kuepusha mila na desturi
kandamizi kwa baadhi ya
makundi ya kijamii
kuhusu haki za Binadamu na
mikataba mingine ya
kimataifa iliyoridhiwa na
Tanzania;
11(3)(b)(ii)
(ii) kuhakikisha kwamba Serikali na vyombo vyake
vyote vya umma vinatoa nafasi na fursa zilizo sawa
kwa raia wote, bila ya kujali rangi, kabila, dini, nasaba,
hali ya mtu au mahali alipo;
(ii) kuhakikisha kwamba Serikali
na vyombo vyake
vyote vya umma vinatoa nafasi
na fursa zilizo sawa kwa raia
wote, bila ya kujali rangi, kabila,
dini, nasaba,jinsia hali ya mtu au
mahali alipo;
Jinsia ni neno linalobeba
jinsi,rika,mgawanyo wa
majukumu, mazingira, nk tofauti
na jinsi ambalo humaanisha
mwanamke au mwanaume
11(3)(c) (xii)
Nyongeza katika ibara 11(3)(c) Kuweka mazingira ya uhakika
wa chakula bora na maji salama
kwa wananchi
-Ni mahitaji muhimu kwa
wananchi kwa ustawi wa jamii
na ni jukumu la serikali
kuhakikisha upatikanaji wake
11(3)(c )(iii)
kuweka mazingira bora kwa ajili ya kuanzisha na
kuendeleza vyombo vya uwakilishi wa wakulima,
wafugaji na wavuvi;
kuweka mazingira bora kwa ajili
ya kuanzisha na kuendeleza
vyombo vya uwakilishi wa
wakulima,
wafugaji, wavuvi;na jamii
zingine za wazalishaji
Kuepusha kutaja aina mbalimbali
za wazalishaaji wa msingi nchini
kwani makundi ni mengi zaidi ya
wakulima, wavuvi na wafugaji
11(1)
11.-(1) Lengo Kuu la Katiba hii ni kulinda, kuimarisha
na kudumisha udugu, amani, umoja na utengamano
wa wananchi wa Jamhuri ya Muungano kwa
kuzingatia ustawi wa wananchi na kujenga Taifa huru
lenye demokrasia, utawala bora na kujitegemea.
11
utengamano wa watu litumike
badala ya wananchi
-neno watu linatumika sana kwa
uzoefu wa katiba za nchi
nyingine na pia sheria za
kimataifa zinatambua
watu(peoples)
SURA YA TATU-MAADILI NA MIIKO YA UONGOZI WA UMMA
Sehemu ya kwanza- Maadili ya viongozi wa umma&Sehemu ya pili-Miiko ya uongozi wa umma
15
15.-(1) Zawadi au kitu chochote kitakachotolewa kwa
mtumishi wa umma katika shughuli za kiserikali ni
15.-(1) neno tuzo liongezwe
Kupanua wigo wa uwajibikaji
zawadi kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
itawasilishwa kwa Katibu
Mkuu Kiongozi kupitia kwa Katibu Mkuu wa Wizara
au taasisi ya Serikali inayohusika, akiainisha:
Sura hii inatakiwa Kutungiwa sheria ya maadili na miiko ya uongozi wa umma kwa nchi washirika katika
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Hakuna sheria ya muungano
kuhusiana na maadili na miiko ya
uongozi wa umma wala Katiba
ya Muungano haijaainisha
uwajibikaji huo kisheria
16(2)(c)
watoto wake walio chini ya umri wa miaka kumi na
nane, mara moja kila mwaka, au kadri
itakavyoamuliwa na sheria
watoto wake walio chini ya
uangalizi wake , mara moja kila
mwaka, au kadri
itakavyoamuliwa na sheria
Uzoefu unaonyesha kuwa watoto
huendelea kuwa chini ya
uangalizi wa wazazi hata wakiwa
zaidi ya miaka 18 na pia sheria
mbalimbali za nchi nyingi zina
ukomo wa miaka tofauti tofauti
kuhusiana na tafsiri ya umri wa
motto kutegemeana na
madhumuni ya sheria husika
14(3)
Wadhifa “Kiongozi wa Umma” kama ulivyotumika
katika Sehemu hii utajumuisha viongozi wa
kuchaguliwa na kuteuliwa kama watakavyoainishwa
kwenye sheria itakayotungwa na Bunge
Wadhifa “Kiongozi wa Umma”
kama ulivyotumika katika
Sehemu hii utajumuisha viongozi
wa kuteuliwa na kuainishwa
majukumu yake ikiwemo
kutangazwa hadharani kwa
umma kwa lengo la kutolewa
maoni na kuidhinishwa kama
watakavyoainishwa kwenye
sheria itakayotungwa na Bunge
-Kuepusha mgongano wa
kimaslahi
21(1) 21.-(1) Mtumishi wa umma aliye katika ajira ya
kudumu hataruhusiwa kuingia katika ajira nyingine
yoyote yenye malipo ya
mshahara.
Mtumishi wa umma aliye katika
ajira ya kudumu hataruhusiwa
kuingia katika ajira nyingine
yoyote yenye malipo ya
-kukuza uwajibikaji kwenye
utumishi wa umma na kuepusha
mgongano wa kimaslahi
mshahara, wala kujihusisha na
na shughuli za kibiashara
zinazoingiliana au kuleta
mgongano wa maslahi katika
uendeshaji wa shughuli zake
za umma,
SURA YA NNE-HAKI ZA BINADAMU,WAJIBU WA RAIA NA MAMLAKA ZA NCHI
Sehemu ya kwanza-Haki za Binadamu
23(2) Nyongeza katika Ibara ya 23 -haki ya kuishi inajumuisha
watoto ambao hawajazaliwa
Rasimu ipo kimya kuhusiana na
watoto ambao hawajazaliwa na
hivyo kutoa mwanya wa utoaji
wa mimba 23(3) -Kutoa mimba ni ukiukwaji wa
haki ya kuishi isipokuwa pale tu
itakapothibitishwa na mtaalamu
wa afya.
23 Kila mtu anayo haki ya kuishi na kupata hifadhi ya
maisha yake kutoka katika Serikali na jamii kwa
mujibu wa sheria.
Kila mtu anayo haki ya kuishi na
kupata hifadhi ya maisha yake
kutoka katika Serikali na jamii
Haki za binadamu ni haki asilia
japo zinapaswa kulindwa na
sheria
24(6) Neno “kubagua” lilivyotumiwa katika Ibara ndogo ya
(2), halitafafanuliwa kwa namna ambayo itaizuia
mamlaka ya nchi kuchukua hatua za makusudi zenye
lengo la kurekebisha matatizo mahsusi katika
jamii.
Suala la matatizo mahsusi
yafafanuliwe
-Kuepusha matumizi mabaya ya
ibara hii
24(7)(g) Nyongeza katika ibara hii 24(7) Haki ya kupata msaada wa
kisheria bure kwa mujibu wa
sheria itakayotungwa na Bunge
Watanzania wengi wanahitaji
huduma hii japo inakosekana
mahali pengi
28(2)(b)(iii) Kulinda manufaa ya umma kwa jumla au kuhifadhi
maslahi fulani mahsusi au maslahi ya sehemu fulani ya
umma,
-Ufafanuzi wa maneno manufaa
ya umma na maslahi fulani
mahsusi
-Kuepusha matumizi mabaya ya
ibara hii maneno hayo
yafafanuliwe katika kipengele
cha ufafanuzi
29(1)(b) Kila mtu anayo haki ya kupewa taarifa wakati wowote
kuhusu:
Kila mtu anayo haki ya kupewa
taarifa na serikali kutoa taarifa
Ni wajibu wa serikali kutoa
taarifa kwa umma pale
zinapohitajika
hizo wakati wowote kuhusu:
38(2) Mamlaka za nchi zitaweka utaratibu wa sheria
utakaowezesha:
(a) mtuhumiwa kupata nakala ya mashtaka
yanayomkabili na kumbukumbu ya mwenendo wa
mashtaka;
(b) mtuhumiwa au mfungwa kupata nakala ya
mwenendo wa mashtaka baada ya shauri kukamilika
mahakamani;
(c) Mtuhumiwa au mfungwa kufikishwa mahakamani
ili kuthibitisha uwepo wake.
Nyongeza :
Mamlaka za nchi zitaweka
utaratibu wa sheria
utakaowezesha:
(b) mtuhumiwa au mfungwa
kupata nakala ya hukumu na
nakala ya mwenendo wa
mashtaka baada ya shauri
kukamilika mahakamani;
.
(d)Mtuhumiwa au mfungwa
mweye ulemavu kupatiwa
nyenzo za kujimudu kutokana
na mahitaji yake
Hukumu zinachelewa sn na
wakati mwingine hazitolewi
kabisa na ni haki ya lazima
katika miendendo ya mahakama
-Kumwezesha mtu mwenye
ulemavu kumudu hali wakati
anapokuwa kizuizini
42(1)a 42.-(1) Kila mtoto ana haki ya-
(a) kupewa jina na uraia;
kila mtoto ana haki ya kupewa
jina stahiki na uraia
Kuepusha watoto kupewa majina
yanayotweza utu wao bila ridhaa
yao
44(1) b kupata elimu kwa kutumia vifaa maalum na kushiriki
katika shughuli za kijamii;
kupata elimu na kujifunza kwa
kutumia vifaa maalum na
kushiriki
katika shughuli za kijamii;
Ili kumwezesha mwenye
ulemavu kujifunza kwa nyenzo
badala ya kutegemea
kufundishwa kupata elimu tu
44(1)(g) Nyongeza
kiepengele (g) katika ibara hii
-kulindwa na kupata msaada wa
kisheria
Itaepusha watu wenye ulemavu
kusaidiwa kisheria pale
wanapohitaji msaada huu
kulingana na aina ya ulemavu
45 Mamlaka ya nchi itaweka utaratibu wa sheria
utakaowezesha makundi madogo katika jamii:
Neno makundi madogo
litafsiriwe kumaanisha kikundi
katika jamii kilichokosa au
Makundi madogo linaleta
mkanganyiko wa nani anahusika
kuwa katika kundi dogo na
kunyimwa fursa sawa na
makundi mengine (marginalized
or vulnerable)
vigezo vyake kama ni idadi ya
watu au uwezo wa kiuchumi au
nafasi katika jamii
46(g) kupata huduma ya juu ya afya inayopatikana. kupata huduma bora ya afya
inayopatikana.
Kiswahili sahihi
47 Mamlaka ya nchi itaweka utaratibu utakaowezesha
wazee kupata fursa ya:
Ukomo wa umri uwekwe
kwenye katiba au sheria itoe
tafsiri kuwa ni watu wenye umri
wa kuanzia miaka 60
kuepusha mgongano
unaojitokeza katika matumizi ya
neno uzee
Sehemu ya Pili-Wajibu wa Raia na Mamlaka za Nchi
52(1) Katika kutafsiri masharti ya Sura hii ya Haki za
Binadamu, Mahakama, Baraza au chombo kingine
chochote cha kufanya uamuzi kitazingatia mambo
yafuatayo:
(a) haki ya usawa, utu na uhuru wa mtu binafsi;
(b) sheria za kimataifa na haki za binadamu; na
(c) haki za jamii na maslahi ya jamii kwa ujumla
Nyongeza ibara hii (d)
(d)Misingi ya haki asilia
Haki za msingi kwa binadamu
wote
MAONI NA MAPENDEKEZO YA MASUALA YASIYOJITOKEZA KATIKA SURA YA NNE
HAKI YA KUMILIKI ARDHI:-
Ardhi yote ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ni mali ya watu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania
1. Kila raia ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ana haki ya kupata, kutumia, kugawa, kuuza, kununua, kumiliki na kudhibiti ardhi katika
jamhuri
2. Ni marufuku kwa mtu asiye raia wa jamhuri ya muungano kumiliki ardhi katika jamhuri ya muungano isipokuwa wageni watapewa fursa ya
kupangisha ardhi kwa kiwango na ukomo maalumu kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za maenedelo ya jamhuri
3. Serikali itakuwa na jukumu la kuhakikisha kuwa ardhi na rasilimali zitatumiwa kwa misingi ifuatayo
(a) matumizi endelevu ya ardhi kwa kuzingatia vizazi vijavyo
(b) usawa wa jinsia katika upatikanaji na matumizi ya ardhi
(c ) Mfumo shirikishi wa usimamizi wa ardhi unaowapa wananchi fursa ya kufanya maamuzi kwa njia za kidemokrasia
(d) ulipwaji wa fidia kamili, ya haki na kwa wakati endapo umiliki utasitishwa kwa sababu yoyote ile kwa manufaa ya watu wa Jamhuri ya muungano
ya Tanzania yatakayokuwa yamebainishwa katika sheria itakayotungwa na Bunge
(e) Mfumo shirikishi, fanisi na rahisi na wa haraka katika wa utatuzi wa migogoro ya ardhi
4. Misingi ya umiliki, matumizi na usimamizi wa ardhi iliyowekwa na katiba hii itazingatiwa na na kulindwa washirika wa jamhuri ya muungano kwa
sheria zitakazotungwa na mabunge ya washirika wa Muungano
SURA YA TANO-URAIA KATIKA JAMHURI YA MUUNGANO
Ibara za Sura hii
zimetumia maneno:-
Tanzania bara na
Zanzibar
Ibara takribani zote zina maneno-Tanzania bara na
Zanzibar
Kila palipotumiwa neno
Tanzania Bara pasomeke -
Jamhuri ya Tanganyika na
palipotumiwa neno Zanzibar
pasomeke Jamhuri ya watu wa
zanzibar
1964 muungano ulihusisha
Jamuhuri ya Tanganyika na
Jamuhuri ya watu wa Zanzibar
Hoja ya Uraia wa nchi mbili:-
54(2) (2) Uraia wa Jamhuri ya Muungano ni wa aina mbili
na utapatikana kwa njia ya kuzaliwa au kujiandikisha.
Uraia wa Tanzania ni wa aina
moja na unapatikana kwa njia ya
kuzaliwa au kujiandikisha
Raia wa Tanzania haruhusiwi
kuwa na uraia wa nchi nyingine
hadi pale atakapoukana uraia wa
Tanzania. Raia wa kuzaliwa na
kujiandikisha wana hadhi sawa
za uraia hivyo hakuna uraia wa
aina mbili
54 54.-(1) Mtu ambaye,kabla ya Katiba hii kuanza
kutumika, ni raia wa Jamhuri
ya Muungano ataendelea kuwa raia wa Tanzania.
(2) Uraia wa Jamhuri ya Muungano ni wa aina mbili
na utapatikana kwa njia
ya kuzaliwa au kujiandikisha.
Nyongeza katika ibara hii
54(3)Raia wa Tanzania atapoteza
uraia wake kwa kuwa raia wa
nchi nyingine
54(4) Raia wa nchi nyingine
atapata uraia wa jamuhuri wa
muungano wa Tanzania kwa
kujiandikisha kulingana na
masharti ya sheria itakayotungwa
Kulinda uzalendo na asili ya
watu wa jamhuri ya muungano
na Bunge
55(4) Mtoto mwenye umri chini ya miaka saba akikutwa
ndani ya mipaka ya Jamhuri ya Muungano katika
mazingira ambayo wazazi wake hawajulikani,
atahesabika kuwa ni raia wa Jamhuri ya Muungano wa
kuzaliwa.
Mtoto mwenye umri chini ya
miaka saba akikutwa ndani ya
mipaka ya Jamhuri ya Muungano
katika mazingira ambayo wazazi
wake hawajulikani, atadhaniwa
(presumed) kuwa ni raia wa
Jamhuri ya Muungano wa
kuzaliwa. Endapo itathibitika
kwamba wazazi wake si raia
wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania haki hii itafutika na
ataruhusiwa kuomba uraia
kwa kujiandikisha
-hii itasaidia kudhibiti uingiaji
holela wa wageni hasa kwenye
nchi zenye matatizo ya kivita na
pia kuzingatia haki na maslahi ya
mtoto
56(3) Endapo ndoa iliyorejewa katika Ibara ndogo ya (2)
itavunjika, kama mtu huyo hakuukana uraia wake,
ataendelea kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano.
Endapo ndoa iliyorejewa katika
Ibara ndogo ya (2) itavunjika,
kama mtu huyo hakuukana uraia
huo, ataendelea kuwa raia wa
Jamhuri ya Muungano
-Kuondoa utata wa tafsiri wa
uraia upi unaozungumziwa
56(4) Mtoto aliyezaliwa katika ndoa iliyorejewa katika Ibara
ndogo ya (2), ataendelea kuwa raia wa Jamhuri ya
Muungano isipokuwa kama ataukana uraia huo
au ataomba na kupata uraia wa nchi nyingine
.
Maneno
…au ataomba na kupata uraia
wa nchi nyingine…yafutwe
Rasimu hii ina dhana ya
kutambua uraia wa nchi mbili
bila kuwa bayana hivyo ili
kuweka msimamo wa kuwa na
uraia wa nchi moja tu inabidi
isomeke hivyo
SURA YA SITA- MUUNDO WA JAMUHURI YA MUUNGANO
Ibara za Sura hii
zilizoainishia
maneno:-
Shirikisho,Serikali ya
Tanzania bara,
Katiba itamke kuwa Tanzania ni jamhuri ya shirikisho la nchi mbili za Jamhuri ya
Tanganyika na jamhuri ya watu wa Zanzibar yenye muundo wa serikali tatu ambazo ni
Serikali ya jamhuri ya shirikisho la Tanzania, serikali ya Jamhuri ya Tanganyika na
serikali ya jamhuri ya watu wa Zanzibar
ufafanuzi huu unaondoa utata
wa kuyatumia maneno
muungano na shirikisho kwa
pamoja kana kwamba yana
maana moja
SURA YA SABA-SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO
Sehemu ya Kwanza-Serikali,Rais na Makamu wa Rais
69(1)(j)(k) (k) kuidhinisha utekelezaji wa
adhabu ya kifo iliyotolewa kwa
mujibu wa sheria za nchi.
Kifungu hiki kifutwe Inakinzana na haki ya mtu kuishi
75(c) angalau mmoja kati ya wazazi
wake ni raia wa kuzaliwa wa
Jamhuri ya Muungano;
wazazi wake ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya
Muungano;
Uzalendo
75(d) wakati wa kugombea, ana umri
usiopungua miaka arobaini;
Wakati wa kugombea, ana umri usiopungua miaka
thelathini na tano(35) na usiozidi miaka Sitini (60
Umri muafaka wa kugombea na
pia ukomo wa juu ni umri wa
kustaafu utumishi wa kawaida
wa umma ukiacha wa
kuchaguliwa au kuteuiwa
75(a-l) Nyongeza ibara ya 75(m) Atakuwa ameshiriki mdahalo wa wazi utakaoratibiwa
na Tume ya uchaguzi
Kutoa fursa kwa wananchi wote
kutambua uwezo wa kiongozi
atakayewaongoza
83(3) (3) Isipokuwa kama ataacha
kushika madaraka ya Rais
kutokana
na kura ya kutokuwa na imani
na Rais, haitakuwa halali kwa
mtu
kumshtaki au kufungua
mahakamani shauri lolote la
jinai au la madai
dhidi ya mtu aliyekuwa
anashika madaraka ya Rais
baada ya kuacha
madaraka hayo kutokana na
jambo alilofanya wakati
alipokuwa bado
anashika madaraka ya Rais.
(3) Isipokuwa kama ataacha kushika madaraka ya Rais
kutokana na kura ya kutokuwa na imani na Rais,
itakuwa halali kwa mtu kumshtaki au kufungua
mahakamani shauri lolote la jinai au la madai dhidi ya
mtu aliyekuwa anashika madaraka ya Rais kabla na
baada ya kuacha madaraka hayo kutokana na jambo
alilofanya wakati alipokuwa bado anashika madaraka
ya Rais
Hakuna mtu aliye juu ya sheria
84(6) Endapo hoja ya kuunda Kamati Endapo hoja ya kuunda Kamati ya Uchunguzi itaungwa Asilimia 75 zilizopendekezwa
ya Uchunguzi itaungwa
mkono na Wabunge
wasiopungua asilimia sabini
na tano ya Wabunge
wote, Spika atatangaza majina
ya wajumbe wa Kamati ya
Uchunguzi
mkono na Wabunge wasiopungua wasiopungua 2/3 ya
wabunge wote, Spika atatangaza majina ya wajumbe
wa Kamati ya Uchunguzi
hapo awali ni nyingi na inaweza
isiwe rahisi kufikiwa
84(7) Kamati ya Uchunguzi, kwa
madhumuni ya Ibara hii,
itakuwa na
wajumbe wafuatao:
(a) Jaji Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano, ambaye atakuwa
Mwenyekiti wa Kamati;
(b) Jaji Mkuu wa Tanzania
Bara;
(c) Jaji Mkuu wa Zanzibar; na
(d) wajumbe wengine sita
watakaoteuliwa na Spika.
jukumu la kuchagua wajumbe kwenye kamati ya
uchunguzi litakuwa la kamati inayohusika na Sheria na
Katiba au Kamati inayofanana na hiyo
Kuleta heshima kwenye
mchakato mzima wa utekelezaji
wa majukumu ya Kamati ya
Uchunguzi. Vilevile kulinda
heshima ya chombo cha
mahakama katika utendaji
84(12) Baada ya taarifa ya Kamati ya
Uchunguzi kuwasilishwa,
Bunge litaijadili taarifa hiyo na
kutoa fursa kwa Rais kujieleza,
na kisha, kwa kura za Wabunge
wasiopungua asilimia sabini na
tano ya Wabunge wote, Bunge
litapitisha azimio kuwa
mashtaka dhidi ya Rais ama
yamethibitika au
hayakuthibitika.
Baada ya taarifa ya Kamati ya Uchunguzi
kuwasilishwa, Bunge litaijadili taarifa hiyo na kutoa
fursa kwa Rais kujieleza, na kisha, kwa kura za
Wabunge wasiopungua 2/3 ya Wabunge wote, Bunge
litapitisha azimio kuwa mashtaka dhidi ya Rais ama
yamethibitika au hayakuthibitika.
Asilimia 75 zilizopendekezwa
hapo awali ni nyingi na inaweza
isiwe rahisi kufikiwa
85(2) Mshahara na malipo mengineyo
yote ya Rais hayatapunguzwa
mishahara ya Rais na malipo mengine yoyote yanaweza
kuongezwa au kupunguzwa kulingana na hali ya
Kuleta usawa na kukamilisha
dhana ya utumishi kwa umma
wakati Rais atakapokuwa bado
ameshika madaraka yake kwa
mujibu wa Katiba hii.
uchumi wa taifa na hali halisi ya watumishi wengine wa
umma
85(3) 85.-(1) Rais atalipwa mshahara
na malipo mengineyo kama
yatakavyoainishwa na Tume ya
Utumishi wa Umma na
atakapostaafu
atapokea malipo ya uzeeni na
stahili nyingine kutoka Mfuko
Mkuu wa
Hazina ya Serikali ya Jamhuri
ya Muungano.
(2) Mshahara na malipo
mengineyo yote ya Rais
hayatapunguzwa wakati Rais
atakapokuwa bado ameshika
madaraka
yake kwa mujibu wa Katiba hii.
Nyongeza katika kipengele hiki
(3)Mshahara wa Rais hautakuwa wa kifahari na
utakatwa kodi kama ilivyo kwa mishahara ya watumishi
wengine wa umma
Awali kipengele hiki
hakikuwepo hali inayo ondoa
usawa katika utumishi wa umma
92(2) (2) Mwanasheria Mkuu wa
Serikali atahudhuria vikao vya
Baraza la Mawaziri lakini
hatakuwa na haki ya kupiga
kura.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali atahudhuria vikao vya
Baraza la Mawaziri lakini atakuwa na haki ya kupiga
kura
Baraza la Mawaziri ni la
kitaaluma na Mwanasheria Mkuu
naye ni mwanataaluma kwahiyo
ana haki ya kupiga kura
92(5) Nyongeza Wizara ya Mambo ya Nje, Wizara ya Ulinzi na
Usalama, Wizara ya Fedha na Wizara ya Katiba
zitatambulika kama wizara andamizi
Kuweka madaraja na hadhi
katika utendaji katika shughuli za
serikali
93(2) Kwa madhumuni ya Ibara
ndogo ya (1), idadi ya Mawaziri
wa Serikali ya Jamhuri ya
Muungano haitozidi kumi na
tano.
…Idadi ya Wizara na Mawaziri itazingatia idadi ya
masuala ya Muungano yaliyoorodheshwa kwenye
nyongeza ya rasimu hii
Kupunguza mrundikano wa
wizara na kuipunguzia serikali
gharama
94(1)(a) ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri
ya Muungano kwa mujibu wa
Sheria za nchi;na
Ni raia wa Jamhuri ya Muungano wa kuzaliwa au
wa kuandikishwa ambaye amedumu na huo uraia
wa kuandikishwa kwa miaka 15
Kutoa fursa kwa raia wengine
kupata fursa ya kutumikia umma
97(1) Kutakuwa na Mwanasheria
Mkuu wa Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ambaye katika Katiba
hii atatajwa tu kwa kifupi kama
"Mwanasheria Mkuu" ambaye
atateuliwa na Rais na
kuthibitishwa na Bunge.
Kutakuwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye katika
Katiba hii atatajwa tu kwa kifupi kama "Mwanasheria
Mkuu" ambaye atateuliwa na Rais kutoka miongoni
mwa majina yatakayowasilishwa kwake na tume ya
utumishi wa mahakama na hatashika wadhifa wake hadi
atakapohojiwa, kujadiliwa na kuthibitishwa na Bunge.
Kuongeza umakini katika kupata
raia makini kwenye nafasi hii
97(2)(d) awe ni mtumishi mwandamizi
katika utumishi wa umma
au taasisi zake;
au Mwanasheria mwenye sifa ya kuwa jaji wa
mahakama kuu kutoka katika vyama vya kitaaluma vya
wanasheria au miongoni mwa wanachama waliotumikia
vyama hivyo kwa muda usiopungua miaka kumi na
tano.
ili kupanua wigo wa watu wenye
sifa kuteuliwa kwa nafasi hiyo
hata kama hawamo katika
utumishi wa umma
98(1) 98.-(1) Kutakuwa na Katibu
Mkuu Kiongozi atakayeteuliwa
na Rais kutoka miongoni mwa
watumishi waandamizi na
kuthibitishwa na
Bunge.
98.-(1) Kutakuwa na Katibu Mkuu Kiongozi
atakayeteuliwa na Rais kutoka miongoni mwa
watumishi waandamizi wa umma ambaye kabla ya
kushika wadhifa wake atahojiwa, kujadiliwa na
kuthibitishwana Bunge
kutanua wigo wa uwazi na
uwajibikaji katika uteuzi wa
viongozi wenye dhamana ya
utumishi wa umma
SURA YA TISA-BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO
Sehemu ya kwanza-Kuundwa kwa Bunge la Jamhuri ya muungano
105(2)(b) Wabunge watano
watakaoteuliwa na Rais kutoka
miongoni
mwa watu wenye sifa za
kuchaguliwa kuwa wabunge
kuwakilisha watu wenye
ulemavu kwa kuzingatia uwiano
wa Washirika wa Muungano.
Wabunge watano watakaoteuliwa na Rais baada ya
mashauriano na vyama vya walemavu
vilivyosajiliwa kisheria kutoka miongoni mwa watu
wenye sifa za kuchaguliwa kuwa wabunge kuwakilisha
watu wenye ulemavu kwa kuzingatia uwiano wa
Washirika wa Muungano.
Kutoa fursa ya ushirikishwaji wa
makundi yenye ulemavu
yanayowakilishwa na wabunge
na pia kuwezesha dhana ya
uwajibikaji wa wabunge katika
makundi hayo
SURA YA KUMI-MAHAKAMA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Sehemu ya Kwanza-Misingi ya utoaji Haki na Uhuru waMahakama
-Maoni kuhusiana na muundo wa Mahakama ya juu na mahakama ya rufani-
-Rufaa zote ziishie mahakama ya Rufani pekee
-Mahakama ya juuIsikilize masuala muhimu matatu yafuatayo
(i) kusikiliza na kuamua mara ya kwanza na mwisho mashauri yanayohusu uchaguzi wa Rais na wabunge wa Jamhuri ya muungano;
–(ii) kusikiliza na kuamua mashauri kuhusu tafsiri ya Katiba ya Shirikisho yanayoletwa na serikali yoyote kati ya tatu zilizopo;
–(iii) kusikiliza na kuamua migogoro baina ya serikali hizo inayoletwa na mmoja wao.
146(2) (2)Mahakama Kuu ya Tanzania
Bara na Mahakama Kuu ya
Zanzibar zitakuwa na mamlaka
sawa ya kusikiliza katika ngazi
ya awali,
mashauri ya madai na jinai
kuhusu Mambo ya Muungano
katika maeneo
ya utawala ya Washirika wa
Muungano.
Ibara hii ifutwe Mahakama ya juu ndo yenye
jukumu la kusikiliza kwanza na
mwisho mambo ya muungano
147(1)(a)(b) 147.-(1)Kutakuwa na
Mahakama ya Juu ya Jamhuri
ya
Muungano au kwa kifupi
itaitwa “Mahakama ya Juu”
ambayo itakuwa
na:
(a) Jaji Mkuu ambaye atakuwa
Rais wa Mahakama ya Juu;
147.-(1)Kutakuwa na Mahakama ya Juu ya Jamhuri ya
Muungano au kwa kifupi itaitwa “Mahakama ya Juu”
ambayo itakuwa
na:
(a) Jaji Mkuu ambaye atakuwa mkuu wa mhimili wa
Mahakama ya Juu;
(b) Naibu Jaji Mkuu ambaye atakuwa Makamu mkuu
wa
Mhimili wa Mahakama ya Juu; na
-Neno Rais limetumika kuonesha
“ukuu” wa wadhifa katika
mhimili wa kimahakama
(b) Naibu Jaji Mkuu ambaye
atakuwa Makamu wa Rais wa
Mahakama ya Juu; na
147(1)(c) (c) Majaji wengine wa
Mahakama ya Juu wasiopungua
saba.
(c) Majaji wengine wa Mahakama ya Juu wasiopungua
watatu ( 3)
Idadi hii itapungua pale tu
majukumu matatu pekee ndo
yatakayoshughulikiwa na
mahakama ya juu. Pia itaepusha
serikali kuingia gharama kubwa
ya idadi ya majaji kama
inavyosomeka katika Rasimu
149(1)(a) Mahakama ya Juu itakuwa ni
ngazi ya mwisho ya rufani
katika Jamhuri ya Muungano na
itakuwa na madaraka ya:
(a) pekee na ya awali ya
kusikiliza na kuamua mashauri
yanayohusu matokeo ya
uchaguzi wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano;
Mahakama ya Juu itakuwa ni ngazi ya mwisho ya rufani
katika Jamhuri ya Muungano na itakuwa na madaraka
ya:
(a) pekee na ya awali ya kusikiliza na kuamua mashauri
yanayohusu matokeo ya uchaguzi wa Rais na wabunge
wa Jamhuri ya Muungano;
Wabunge wa muungano
umeongezwa kutokana na
mhimili huu wa juu na mwisho
149(1)(d) kusikiliza na kuamua rufani
kutoka Mahakama ya Rufani;
Inafutwa -Hii ni kutokana na pendekezo la
kuifanya mahakama ya Rufani
kuwa mahakama ya mwisho kwa
ajili ya Rufaa
153(3) (3) Kwa kuzingatia masharti ya
Ibara ndogo ya (2), iwapo Rais
ataridhika kwamba japokuwa:
(a) mtu mwenye sifa mojawapo
ya hizo sifa zilizoainishwa
katika Ibara ndogo ya (2)
hakuwa nayo sifa hiyo kwa
muda
‐ 60 ‐unaopungua miaka kumi;
Inafutwa Ibara hii inatoa mwanya kwa
watu wasio na sifa kuteuliwa na
Rais
na
(b) mtu huyo ana uwezo, ujuzi
na kwa kila hali anafaa
kukabidhiwa madaraka ya Jaji
wa Mahakama ya Juu;
(c) kuna sababu za kumfanya
mtu huyo kustahili kukabidhiwa
nafasi ya madaraka hayo,
basi Rais anaweza kutengua
sharti la kuwa na sifa kwa muda
usiopungua
miaka kumi, na baada ya
kushauriana na Tume ya
Utumishi wa
Mahakama, kumteua mtu huyo
kuwa Jaji wa Mahakama ya Juu.
155(3) Bila ya kuathiri masharti ya
Ibara ndogo ya (1) na (2), Jaji
Mkuu, Naibu Jaji Mkuu na Jaji
wa Mahakama ya
Juualiyetimiza umri wa kustaafu
atalazimika kuendelea kufanya
kazi baada ya kutimiza umri
huo mpaka amalize kutayarisha
na kutoa hukumu au mpaka
akamilishe
shughuli nyingine yoyote
inayohusika na mashauri
ambayo alikwishaanza
kuyasikiliza kabla hajatimiza
umri wa kustaafu.
Bila ya kuathiri masharti ya Ibara ndogo ya (1) na (2),
Jaji Mkuu, Naibu Jaji Mkuu na Jaji wa Mahakama ya
Juu aliyetimiza umri wa kustaafu atalazimika kuendelea
kufanya kazi baada ya kutimiza umri huo kwa kipindi
cha miaka mitatu mpaka amalize kutayarisha na kutoa
hukumu au mpaka akamilishe shughuli nyingine yoyote
inayohusika na mashauri ambayo alikwishaanza
kuyasikiliza kabla hajatimiza umri wa kustaafu.
Kudhibiti utendaji wa majaji
kuendelea kufanya kazi katika
kipindi kirefu baada ya kutimiza
umri wa kustaafu
162(3) Mtu anaweza kuteuliwa kuwa Mtu anaweza kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kuwezesha utendaji wa kazi
Mwenyekiti wa Mahakama ya
Rufani endapo atakuwa
amefikisha umri wa miaka
arobaini na tano au zaidi na
mwenye sifa ya uadilifu, tabia
njema na uaminifu na:
Mahakama ya Rufani endapo atakuwa amefikisha umri
wa miaka arobaini na tano na usiozidi miaka sitini (60)
na mwenye sifa ya uadilifu, tabia njema na uaminifu na:
katika kipindi ambacho mtu ana
uwezo wa kutenda kazi
kulingana na umri wake
Ilivyoandikwa-SURA YA KUMI NA MOJA-UTUMISHI WA JAMHURI YA MUUNGANO
Inavyopendekezwa-UTUMISHI KATIKA JAMHURI YA MUUNGANO
177- Bila ya kuathiri masharti ya
Katiba hii, utumishi wa umma
na uongozi katika Jamhuri ya
Muungano utazingatia misingi
kwamba utoaji wa ajira na
uteuzi wa viongozi utakuwa
kwa uwiano baina ya Washirika
wa Muungano, kwa kuzingatia
weledi na taaluma katika eneo
au nyanja husika.
Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii, utumishi wa
umma na uongozi katika Jamhuri ya Muungano
utazingatia misingi kwamba utoaji wa ajira na uteuzi wa
viongozi utakuwa kwa uwiano utakaoainishwa kwa
mujibu wa sheria itakayotungwa na Bunge
- -Kuepusha migororo ya
kutokubaliana kuhusu idadi ya
uwiano wa watumishi kutoka
nchi za shirikisho
SURA YA KUMI NA MBILI-UCHAGUZI KATIKA VYOMBO VYA UWAKILISHI NA VYAMA VYA SIASA
Sehemu ya Kwanza-Uwakilishi wa wananchi
181(6)(c) (c) mtu ambaye anashika nafasi
ya madaraka katika asasi zisizo
za kiserikali au aliyewahi
kushika nafasi ya madaraka
katika
asasi zisizo za kiserikali ndani
ya muda usiozidi miaka mitano
kabla ya uteuzi kufanyika.
MANENO “au aliyewahi kushika nafasi ya madaraka
katika asasi zisizokuwa za kiserikali ndani ya muda
usiozidi miaka mitano kabla ya uteuzi kufanyika”
yafutwe
Hakuna sababu ya kuwabana
waliowahi kushika madaraka
katika asasi za kiraia wakati
waliowahi kuwa watumishi
katika utumishi wa umma
hawajazuiwa. Ili kutoa fursa
sawa kwa watu wote, maneno
hayo yafutwe au maneno kama
hayo yaongezwe kwenye ibara ya
181(6) (b)
184(1)(e) Kutayarisha na kuchapisha
ripoti za kila mwaka kuhusu
ripoti za ukaguzi wa fedha wa
kila chama cha kisiasa; na
kutayarisha na kuchapisha ripoti za kila mwaka kuhusu
ripoti za ukaguzi wa fedha wa kila chama cha kisiasa;
na wagombea huru
Rasimu hii imetambua uwepo wa
wabombea huru ambao ibara hii
haikuwaainisha
184(8) (8) Kwa madhumuni ya Ibara
ndogo ya (8), watu wanaohusika
na uchaguzi ni-
(8) Kwa madhumuni ya Ibara ndogo ya (7), watu
wanaohusika na uchaguzi ni-
Makosa ya kiuchapaji Ilipaswa
kuwa ibara ndogo ya 7
SURA YA KUMI NA TATU-TAASISI ZA UWAJIBIKAJI
Mapendekezo ya Jumla katika sura hii-Sifa na upatikanaji wa wajumbe wa Tume ya maadili na tume ya haki za binadamu hazijaainishwa. Pia
upatikanaji uende sambamba na kuanza kwa utekelezaji wa kazi pamoja na Mwenyekiti na Makamu mwenyekiti wa Tume hiziPia sheria
itakayotungwa na Bunge izingatie mapendekezo haya ikiwa ni pamoja na sifa zifuatazo
Sifa za wajumbe wa Tume ya Maadili ya uongozi
-Awe raia wa kuzaliwa nchini na wazazi wake ni raia wa kuzaliwa wa Tanzania
-Awe amefuzu mafunzo ya sheria,uhasibu na utumishi wa umma;
-ana uzoefu usiyopungua miaka kumi na tano katika utumishi
wa umma;
-ana uzoefu usiyopungua miaka kumi na tano katika masuala
yanayohusu maadili ya uongozi wa umma; na
-ni mtu mwenye heshima, weledi, uaminifu, uadilifu na asiye
na upendeleo unaotiliwa shaka na jamii.
Sifa za wajumbe wa Tume ya haki za Binadamu
-Awe raia wa kuzaliwa nchini na wazazi wake ni raia wa kuzaliwa Tanzania
-awe amefuzu mafunzo ya juu ya Sheria,haki za binadamu na utawala bora
- ana uzoefu usiyopungua miaka kumi na tano katika utumishi
wa umma;
-ana uzoefu usiyopungua miaka kumi na tano katika masuala
yanayohusu haki za binadamu na utawla bora na
-ni mtu mwenye heshima, weledi, uaminifu, uadilifu na asiye
na upendeleo unaotiliwa shaka na jamii.
Mapendekezo ya namna ya upatikanaji wa wajumbe wa Tume
-Watateuliwa na Rais baada ya kupendekezwa na Tume ya Utumishi wa Umma
Sehemu ya Kwanza-Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji
194(c) (c)mtu mwenye uzoefu wa
utumishi wa umma kwa kipindi
kisichopungua miaka kumi
(c)mtu mwenye uzoefu wa masuala ya haki za
binadamu na masuala ya kijamii kwa kipindi
kisichopungua miaka kumi
-Kuepusha kuzuia watu ambao
hawajapata fursa za ajira katika
utumishi wa umma lakini
wanauzoefu.
202(1)(d) (d)kutayarisha ripoti ya mwaka
na kuiwasilisha Bungeni kwa
ajili ya kujadiliwa na kutolewa
mapendekezo.
(d)kutayarisha ripoti ya mwaka na kuiwasilisha kwa
tume ya maadili na kisha Bungeni kwa ajili ya
kujadiliwa na kutolewa mapendekezo.
Kuwezesha tume ya maadili
kutekeleza majukumu yake kama
yaliyoainishwa
SURA YA KUMI NA TANO –ULINZI NA USALAMA KATIKA JAMHURI YA MUUNGANO
232,235 Zinapedekezwa kufutwa Kuepusha mgongano wa
majukumu ya majeshi hayo dhidi
ya majeshi ya nchi za muungano
SURA YA KUMI NA SITA-Mengineyo
238 Nyongeza katika ibara hii Masuuli,maduhuli,watu,wananchi,utajiri wa rasilimali
na maliasili,unyonyaji, wakala, kila mtu, raia,maslahi ya
umma,wabunge
Kurahisisha tafsiri ya matumizi
ya maneno katika Katiba hii na
kuepusha matumizi ya maneno