katiba ya ukwata -...

34
a KATIBA YA UKWATA JUMUIYA YA KIKRISTO TANZANIA

Upload: hadan

Post on 24-Feb-2018

1.626 views

Category:

Documents


157 download

TRANSCRIPT

a

KATIBA YA UKWATA

JUMUIYA YA KIKRISTOTANZANIA

b

i

KATIBA YA UKWATA

JUMUIYA YA KIKRISTO TANZANIA

2011

ii

Katiba ya Ushirika wa Kikristo wa Wanafunzi Tanzania (UKWATA) chini ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT)

ISBN 978 9987 9490 1 4

Katiba hii imetolewa na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT)

Copyright © 2011, Na Jumuiya ya Kikristo Tanzania

Haki zote zimehifadhiwa(All rights reserved)

Hairuhusiwi kuiga, kunakili, kutafsiri na kurudufu kitabu au mafungu yaliyomo katika kitabu hiki bila ya ruhusa kwa maandishi ya wenye haki miliki.

Toleo la kwanza: 2003 – Nakala 2000

Toleo la pili (Revised Edition): 2011 – Nakala 10,000

Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), SLP 1454, Dodoma. Tanzania.

iii

UTANGULIZI

Kwa kutambua umuhimu wa kuwa na malezi ya Kikristo kwa wanafunzi wa Shule za Sekondari, Vyuo na penginepo elimu ya jinsi hii inapotolewa nchini, kwa kujitoa kwetu kwa Kristo, tunajiunga pamoja na kuanzisha Ushirika wa Kikristo wa Wanafunzi Tanzania, kama Katiba inavyoonesha. Katiba hii ya UKWATA (By law) itakuwa chini ya Katiba mama ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania (Christian Council of Tanzania - CCT).

iv

UTANGULIZI .............……………………………………………… iii

SURA YA 1: JINA, IMANI NA MADHUMUNI …………………… 1 Ibara ya 1: Jina ……………………………………………… 1 Ibara ya 2: Imani ……………………………………………… 1 Ibara ya 3: Madhumuni ………………………………………… 1

SURA YA 2: UANACHAMA ………………………………………… 2 Ibara ya 4: Uanachama utakubaliwa kwa .....…………………… 2 Ibara ya 5: Kupoteza Uanachama ...……………………………… 3 Ibara ya 6: Cheti ............................................................................ 3

SURA YA 3: MUUNDO ..................................................................... 3FUNGU LA KWANZA: TAWI ........................................................... 3 Ibara ya 7: Kamati Kuu ya Tawi .................................................. 3 Ibara ya 8: Halmashauri Kuu ya Tawi ......................................... 4 Ibara ya 9: Mkutano Mkuu wa Tawi ............................................. 5

FUNGU LA PILI: WILAYA ............................................................... 5 Ibara ya 10: Kamati Kuu ya Wilaya ............................................ 5 Ibara ya 11: Halmashauri Kuu ya Wilaya .................................... 6 Ibara ya 12: Mkutano Mkuu wa Wilaya ....................................... 6

FUNGU LA TATU: MKOA ................................................................. 7 Ibara ya 13: Kamati Kuu ya Mkoa ............................................... 7 Ibara ya 14: Halmashauri Kuu ya Mkoa ........................................ 8 Ibara ya 15: Mkutano Mkuu wa Mkoa .......................................... 8 Ibara ya 16: Kuundwa kwa Wilaya/ Mkoa mpya ............................ 9

FUNGU LA NNE: KANDA .................................................................. 9 Ibara ya 17: Muundo wa Kanda .................................................... 9 Ibara ya 18: Kamati ya Utendaji ................................................... 9

v

Ibara ya 19: Halmashauri Kuu ya Kanda ....................................... 10 Ibara ya 20: Mkutano Mkuu wa Kanda .......................................... 10

FUNGU LA TANO: TAIFA ............................................................... 11 Ibara ya 21: Kamati Kuu ya Taifa ............................................. 11 Ibara ya 22: Halmashauri Kuu ya Taifa ......................................... 12 Ibara ya 23: Mkutano Mkuu wa Taifa ........................................... 13

SURA YA 4: UONGOZI ...................................................................... 13 Ibara ya 24: Viongozi .................................................................... 13 Ibara ya 25: Miiko ya Uongozi .................................................... 15

SURA YA 5: UCHAGUZI .................................................................... 15 Ibara ya 26: Muda wa Uchaguzi .................................................... 15 Ibara ya 27: Kutambulisha Wagombea uchaguzi .......................... 16 Ibara ya 28: Msimamizi wa Uchaguzi ............................................ 16 Ibara ya 29: Kupiga kura ................................................................ 16 Ibara ya 30: Baada ya uchaguzi ................................................... 16

SURA YA 6: VIKAO NA MIKUTANO ............................................... 17 Ibara ya 31: VIKAO .................................................................... 17 Ibara ya 32: MIKUTANO ............................................................. 17

SURA YA 7: HUDUMA MBALIMBALI .......................................... 17 Ibara ya 33: Ibada na mikutano ya UKWATA ............................. 17 Ibara ya 34: Huduma ya Maombi na Uinjilisti .............................. 17 Ibara ya 35: Wana- UKWATA Washirikishwa ( TSCF-Associate Members) ..................................... 18 Ibara ya 36: Wajibu wa Wana-UKWATA Washirikishwa ........................................................... 18

vi

SURA YA 8: WALEZI NA WASHAURI ........................................... 19 Ibara ya 37: Jumuiya ya Kikristo Tanzania-CCT ........................... 19 Ibara ya 38: Wajibu ....................................................................... 19 Ibara ya 39: Makanisa ............................................................. 19 Ibara ya 40: Mchungaji mlezi .................................................. 19 Ibara ya 41: Walimu Washauri ..................................................... 21

SURA YA 9: FEDHA NA MIRADI ...................................................... 22 Ibara ya 42: Ada na Michango ....................................................... 22 Ibara ya 43: Utunzaji na ukaguzi wa mahesabu ya Fedha ........... 22 Ibara ya 44: Sera ya Fedha .............................................................. 23 Ibara ya 45: Miradi ................................................................... 23 Ibara ya 46: Umiliki wa mali ...................................................... 23

SURA YA 10: MAREKEBISHO YA UKWATA ................................ 24 Ibara ya 47: Muda wa Marekebisho ya Katiba .............................. 24 Ibara ya 48: Kamati ya Katiba ....................................................... 24

1

SURA YA 1

JINA, IMANI NA MADHUMUNI

Ibara ya 1. JinaUshirika huu utajulikana kwa jina la “Ushirika wa Kikristo wa Wanafunzi Tanzania” (UKWATA), kwa kiingereza “Tanzania Students Christian Fellowship” (TSCF).

Ibara ya 2. Imanii.. Sisi wana - UKWATA tunamwamwini YESU KRISTO na kumkubali

kuwa ni MWOKOZI na BWANA wa maisha yetu na wa watu wote wanaomwamini.

ii. Tunaamini katika Utatu Mtakatifu, yaani Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.

iii. Tunaamini kuwa Maandiko Matakatifu yaani Biblia ni Neno la Mungu ambalo ni msingi wa maisha na wokovu wetu.

iv. Tunakiri Imani kama tulivyoipokea katika kiri za Imani ya Mitume na Nikea.

Ibara ya 3. Madhumunii. Kuwasaidia Wanafunzi wampokee YESU KRISTO kuwa MWOKOZI

na BWANA wa maisha yao na waishi kwa kufuata kukubali kwao wakishuhudia, wakitangaza habari njema na kutumika katika nchi yao na ulimwengu wote.

ii. Kuwalea Wanafunzi katika msingi wa maisha ya kiroho kwa njia ya ibada ya pamoja, kujifunza Biblia na Sala.

iii. Kuhimiza umoja kati ya wanafunzi Wakristo, tukiendeleza umoja wa makanisa hapa Tanzania na nje ya nchi.

iv. Kujenga moyo kwa wanafunzi wa kufuata tabia ya Yesu Kristo katika kuwahudumia watu wenye matatizo mbali mbali ya kimwili na kiroho nchini na ulimwenguni mwote.

2

v. Kuwatia moyo wanafunzi kufi kiria juu ya wito wa kulitumikia Kanisa na kukuza upeo wa Kikristo kwa ajili ya utumishi na huduma kwa Kanisa na jamii.

vi. Kukuza maarifa katika Maandiko Matakatifu (Biblia) kwa njia ya sanaa (mfano; muziki wa Injili, michezo ya kuigiza, mashairi na ngonjera), tamasha na mashindano yaletayo utukufu kwa Mungu.

vii. Wana-UKWATA watashirikiana na wana UKWATA washirikishwa ili kuuendeleza UKWATA.

viii. UKWATA utashirikiana na vyama vingine vya Kikristo vilivyomo ndani na nje ya Tanzania kwa kufuata misingi ya Imani ya Makanisa wanachama yaliyomo katika Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT).

SURA YA 2

UANACHAMA

Ibara 4. Uanachama Utakubaliwa Kwa: i) Mwanafunzi/Mwanachuo anayetoka katika Kanisa lililo mwanachana

wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) ikiwa:-(a) Atakubaliana na Katiba ya UKWATA.(b) Atalipa kiingilio na kupewa kadi ya uanachama.(c) Atalipa ada ya mwaka na michango itakayopangwa na

Halmashauri Kuu ya Tawi, Wilaya, Mkoa na Taifa.(d) Atahudhuria vikao, mikutano na shughuli zingine zitakazopangwa

na Wana-UKWATA wenyewe kwa uaminifu.

(ii) Mwanafunzi/Mwanachuo anayetoka katika kanisa lisilo mwanachama wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) ikiwa:-(a) Atakubaliana na Katiba ya UKWATA.(b) Atalipa kiingilio na kupewa kadi ya uanachama.(c) Atalipa ada ya mwaka na michango itakayopangwa na

Halmashauri Kuu ya Tawi, Wilaya, Mkoa na Taifa.

3

(d) Atahudhuria vikao, mikutano na shughuli zingine zitakazopangwa na Wana UKWATA wenyewe kwa uaminifu.

Ibara ya 5. Kupoteza Uanachamai. Mwana – UKWATA atapoteza uanachama wake endapo atashindwa

kutimiza au kukiuka Ibara ya 4 ya Katiba hii. ii. Mwana – UKWATA atapoteza uanachama wake endapo atakosa

ushuhuda mzuri wa Kikristo katika UKWATA, Taasisi aliyomo na katika jamii.

Ibara ya 6. Chetii. Mwanachama atapokea Cheti wakati wa kuhitimu masomo kulingana

na Kiwango cha Elimu yake.ii. Cheti cha UKWATA kitatolewa na Jumuiya ya Kikristo Tanzania

(CCT) na kuthibitishwa na Mchungaji Mlezi wa Mkoa husika.

SURA YA 3

MUUNDO

FUNGU LA KWANZA: TAWIIbara 7. Kamati Kuu ya Tawii) Watakaohudhuria watakuwa:-

a. Mwenyekiti b. Makamu Mwenyekiti c. Katibud. Katibu Msaidizie. Mtunza Hazinaf. Mwalimu Mshaurig. Mchungaji Mlezi

4

ii) Wajibu wa Kamati Kuu utakuwa:-a. Kuandaa agenda za kikao cha Halmashauri Kuu ya Tawi.b. Kutekeleza maazimio ya Halmashauri Kuu ya Tawi.c. Kuandaa taarifa itakayotolewa kwenye Kikao cha Mkutano Mkuu

wa Tawi ikiwa imepitishwa na Halmashauri Kuu ya Tawi.d. Kuwachagua wasemaji wa masomo katika Mkutano Mkuu wa

Tawi ambao ni lazima watoke Makanisa wanachama wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT).

e. Kuandaa taarifa itakayotolewa kwenye Kikao cha Halmashauri Kuu ya Wilaya/Mkoa ikiwa imepitishwa na Halmashauri Kuu ya Tawi.

f. Kufanya vikao visivyopungua vitatu kwa muhula.

Ibara 8. Halmashauri Kuu ya Tawii. Watakaohudhuria watakuwa:-

a. Kamati Kuu ya Tawi.b. Wajumbe wawili waliochaguliwa na Mkutano Mkuu wa Tawi.c. Wazee wa Kanisa wa UKWATA kwa shule za bweni na viongozi

wa Kamati mbalimbali.

ii. Wajibu wa Halmashauri kuu utakuwa:-a. Kuangalia shughuli zote za maendeleo ya UKWATA Tawini.b. Kusimamia utekelezaji wa maazimio ya Mkutano Mkuu.c. Kuunda Kamati mbalimbali kama itakavyoona inafaa kwa mujibu

wa Katiba hii.d. Kupokea, kujadili na kupitisha taarifa ya utendaji wa Kamati

Kuu ya Tawi itakayotolewa kwenye Mkutano Mkuu wa Tawi.e. Kupokea taarifa za Kamati mbalimbali na kuzijadili.f. Kuchagua wajumbe wawili kutoka Kamati Kuu ya Tawi

kuwakilisha Tawi katika uchaguzi ngazi ya Wilaya/Mkoa.g. Kuandaa mapendekezo ya agenda kwa Halmashauri Kuu ya

Wilaya au Mkoa.h. Kuandaa agenda za Mkutano Mkuu wa Tawi.i. Kufanya vikao visivyopungua vitatu kwa mwaka.

5

Ibara 9. Mkutano Mkuu wa Tawii) Watakaohudhuria watakuwa:-

a. Kamati Kuu ya Tawi.b. Wana UKWATA wote wa Tawi.c. Mwalimu Mshauri wa Tawi.d. Mchungaji Mlezi.e. Wajumbe kutoka Kamati Kuu ya Wilaya.

ii) Wajibu wa Mkutano Mkuu utakuwa:- a. Kuchagua Viongozi wa Tawi (Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti,

Katibu, Katibu Msaidizi, Mtunza Hazina,Wazee wa Kanisa wa UKWATA kwenye shule za Bweni,Wajumbe wawili wa Halmashauri Kuu ya Tawi).

b. Kupokea na kujadili taarifa ya Halmashauri Kuu ya Tawi na kutoa maamuzi.

c. Kufanya Mkutano Mkuu mara mbili kwa mwaka, wa kwanza ukiwa ni wa tathimini baada ya miezi sita na wa pili utahusisha uchaguzi.

FUNGU LA PILI: WILAYAIbara 10. Kamati Kuu ya Wilayai) Watakaohudhuria watakuwa:-

a. Mwenyekiti.b. Makamu wa Mwenyekiti.c. Katibu.d. Katibu Msaidizi.e. Mtunza Hazina.f. Mwalimu Mshauri wa Wilaya.g. Mchungaji Mlezi wa Wilaya.

ii) Wajibu wa Kamati Kuu utakuwa:a. Kuandaa agenda za kikao cha Halmashauri Kuu ya Wilaya.b. Kutekeleza maazimio ya Halmashauri Kuu ya Wilaya.

6

c. Kuandaa taarifa itakayotolewa kwenye Mkutano Mkuu wa Wilaya ikiwa imepitishwa na Halmashauri Kuu ya Wilaya.

d. Kuwachagua wasemaji wa masomo katika Mkutano wa UKWATA wa Wilaya ambao ni lazima watoke Makanisa wanachama wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT).

e. Kuwasilisha taarifa ya utendaji ya Wilaya kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Mkoa.

f. Kufanya vikao visivyopungua viwili kwa mwaka.

Ibara 11. Halmashauri Kuu ya Wilayai) Watakaohudhuria watakuwa:-

a. Kamati Kuu ya Wilaya.b. Kamati Kuu zote za Matawi.

ii) Wajibu wa Halmashauri Kuu utakuwa :-

a. Kuangalia shughuli za maendeleo ya UKWATA Matawini.b. Kusimamia utekelezaji wa maazimio ya Mkutano Mkuu wa

Wilaya.c. Kupokea na kujadili taarifa za maendeleo ya UKWATA kutoka

katika Matawi.d. Kuchagua viongozi wa Wilaya (Mwenyekiti, Makamu

Mwenyekiti, Katibu, Katibu Msaidizi na Mtunza Hazina). e. Kuunda Kamati mbalimbali kama itakavyoona inafaa kwa mujibu

wa Katiba.f. Kupokea na kujadili taarifa za kamati mbalimbali.g. Kuandaa agenda za Mkutano Mkuu wa Wilayah. Kufanya vikao visivyopungua viwili kwa mwaka.

Ibara 12. Mkutano Mkuu wa Wilayai) Watakaohudhuria watakuwa:-

a. Kamati Kuu ya Wilaya b. Wana – UKWATA wote c. Walimu washauri wa matawi yote d. Wachungaji walezi wotee. Wajumbe kutoka Kamati Kuu ya Mkoa.

7

ii) Wajibu wa Mkutano Mkuu utakuwa:-a. Kupokea, kujadili na kupitisha taarifa ya utekelezaji ya Kamati

Kuu ya Wilaya.b. Kujadili agenda zitakazotayarishwa na Halmashauri Kuu ya

Wilaya na kutoa maamuzi.c. Kushuhudia na kuthibitisha uchaguzi wa viongozi wa Wilaya

utakaofanywa na Halmashauri Kuu.d. Kufanya Mkutano Mkuu mara moja kwa mwaka.

FUNGU LA TATU: MKOAIbara 13: Kamati Kuu ya Mkoai) Watakaohudhuria watakuwa:-

a. Mwenyekitib. Makamu Mwenyekiti c. Katibud. Katibu Msaidizie. Mtunza Hazinaf. Mchungaji Mlezi wa Mkoag. Mwalimu Mshauri Mkoa

ii) Wajibu wa Kamati Kuu utakuwa:-a. Kuandaa agenda za kikao cha Halmashauri Kuu ya Mkoa.b. Kutekeleza maazimio ya Halmashauri Kuu.c. Kuandaa taarifa itakayotolewa kwenye Mkutano Mkuu ikiwa

imepitishwa na Halmashauri Kuu ya Mkoa.d. Kuwachagua wasemaji wa masomo katika Mkutano wa UKWATA

wa Mkoa ambao ni lazima watoke Makanisa wanachama wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT).

e. Kuwasilisha taarifa ya utekelezaji ya Mkoa kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa.

f. Kuchagua wajumbe wawili watakaowakilisha Mkoa katika uchaguzi wa UKWATA Taifa.

g. Kusimamia utekelezaji wa maazimio yote yaliyoazimiwa na Mkutano Mkuu.

8

h. Kupokea mapendekezo na kuandaa agenda zitakazopelekwa taifani.

i. Kuchukua hatua juu ya mambo muhimu kwa madhumuni ya kuendeleza kazi ya UKWATA

j. Kufanya vikao visivyopungua vitatu kwa mwaka.

Ibara 14. Halmashauri Kuu ya Mkoa.i) Watakaohudhuria watakuwa:-

a. Kamati Kuu ya Mkoab. Kamati Kuu za Wilaya (Mwenyekiti, Katibu, Mtunza Hazina,

Mwalimu mshauri wa Tawi na Mchungaji Mlezi wa Tawi).

ii) Wajibu wa Halmashauri Kuu utakuwa;-a. Kuangalia maendeleo ya shughuli zote za UKWATA za Mkoa.b. Kufanya uchaguzi wa Kamati Kuu ya Mkoa (Mwenyekiti,

Makamu Mwenyekiti, Katibu, Katibu Msaidizi na Mtunza Hazina) katika Mkutano Mkuu wa Mkoa.

c. Kupokea, Kujadili na kupitisha taarifa ya utekelezaji wa Kamati Kuu itakayotolewa kwenye Mkutano Mkuu wa Mkoa.

d. Kuandaa agenda za Mkutano Mkuu wa Mkoa.e. Kupendekeza kuundwa kwa Wilaya kulingana na hitaji la

Mkoa.f. Kuunda Kamati mbalimbali kama itakavyoona inafaa.g. Kupokea na kujadili taarifa za kamati mbalimbali.h. Kusimamia utekelezaji wa maazimio ya Mkutano Mkuu wa

Mkoai. Kupendekeza mahali pa kufanyia Mkutano Mkuu wa Mkoa.j. Kufanya vikao visivyopungua viwili kwa mwaka.

Ibara 15. Mkutano Mkuu wa Mkoa:-i) Watakaohudhuria watakuwa:

a. Halmashauri Kuu ya Mkoa.b. Kamati Kuu za Matawi.

9

ii) Wajibu wa Mkutano Mkuu utakuwa:-a. Kupokea na kujadili Taarifa ya Utendaji ya Kamati Kuu ya

Mkoa.b. Kujadili agenda zilizotayarishwa na Halmashauri Kuu ya Mkoa

na kutoa maamuzi.c. Kushuhudia na kuthibitisha uchaguzi wa Viongozi wa Mkoa

utakaofanywa na Halmashauri Kuu ya Mkoa.d. Kufanya Mkutano Mkuu mara moja kwa mwaka.

Ibara ya 16. Kuundwa kwa Wilaya/Mkoa mpya.i) Pendekezo la kuundwa kwa Wilaya/Mkoa mpya litapelekwa na

Halmashauri Kuu ya Mkoa kwa Halmashauri Kuu ya Taifa baada ya kujadiliwa na kupitishwa na vikao vyote vya Mkoa.

ii) Endapo kuna haja ya kuanzisha Wilaya/Mkoa mpya katika eneo la Mkoa mama na pendekezo la kuundwa Wilaya/Mkoa halijaletwa na Mkoa husika, Halmashauri Kuu ya UKWATA Taifa italijadili na kutoa mapendekezo kwa Mkutano Mkuu wa Taifa ili kuridhia kuundwa kwa Wilaya/Mkoa mpya.

FUNGU LA NNE: KANDAIbara ya 17. Muundo wa Kandai) Kutakuwepo na Kanda za UKWATA zitakazoundwa na mikoa ya

UKWATA katika eneo husika. ii) Kanda za UKWATA zitaainishwa na Kamati Kuu ya UKWATA Taifa na

kuthibitishwa na Halmashauri ya Taifa na Mkutano Mkuu wa Taifa.

Ibara ya 18. Kamati ya Utendajii) Wahusika:

a. Mwenyekiti.b. Katibu.c. Mtunza Hazina.d. Mwalimu Mshauri wa Kanda.e. Mchungaji Mlezi wa Kanda.

10

ii) Wajibu wa Kamati ya Utendajia. Kuandaa agenda za Halmashauri ya Kanda.b. Kusimamia utekelezaji wa maazimio ya Halmashauri ya Kanda.c. Kuandaa na kusimamia Mkutano wa Kanda.d. Kuwachagua wasemaji wa masomo katika Mkutano wa UKWATA

wa Kanda ambao ni lazima watoke Makanisa wanachama wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT).

e. Kutoa taarifa ya utekelezaji kwenye Halmashauri na Mkutano wa Kanda.

f. Kuandaa na kutuma taarifa ya Kanda kwa Katibu wa UKWATA Taifa.

g. Kuwajibika kwa Kamati Kuu ya UKWATA Taifa ili kuleta umoja wa UKWATA na CCT.

h. Kufanya vikao visivyopungua viwili kwa mwaka.

Ibara ya 19. Halmashauri Kuu ya Kandai) Wahusika:-

a) Kamati Kuu zote za mikoaii) Wajibu wa Halmashauri Kuu ya Kanda:

a. Kupokea na kujadili agenda na taarifa kutoka Kamati ya utendaji.

b. Kuchagua viongozi wa Kanda (Mwenyekiti, Katibu na Mtunza Hazina). Mwalimu Mshauri wa Kanda na Mchungaji Mlezi wa Kanda watachaguliwa na Mkutano wa walezi na washauri wa mikoa ya Kanda husika.

c. Kupokea jina la Mwalimu Mshauri na Mchungaji Mlezi watakaochaguliwa na Mkutano wa washauri na walezi wa Kanda.

d. Kutakuwa na kikao kimoja kwa mwaka.

Ibara ya 20. Mkutano Mkuu wa Kanda.i) Wahusika:

a. Kamati Kuu zote za Mikoa.b. Wana UKWATA wote wa Kanda.

11

ii) Wajibu wa Mkutano Mkuu wa Kanda:-a. Kupokea na kujadili agenda toka Halmashauri ya Kanda.b. Kushuhudia na kuthibitisha uchaguzi wa viongozi wa Kanda.c. Kufanya Mkutano mmoja wa Kanda kwa mwaka.

FUNGU LA TANO – TAIFA.Ibara ya 21. Kamati Kuu ya Taifa:-i) Watakaohudhuria watakuwa:-

a. Raisb. Makamu wa Raisc. Katibu Mkuud. Katibu Mkuu Msaidizie. Mtunza Hazina f. Mratibu wa UKWATA Taifa wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania

(CCT).

ii) Wajibu wa Kamati Kuu utakuwa:-a. Kuandaa agenda za Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa.b. Kutekeleza maazimio ya Halmashauri Kuu ya Taifa.c. Kuandaa taarifa itakayotolewa kwenye Mkutano Mkuu ikiwa

imepitishwa na Halmashauri Kuu ya Taifa.d. Kupokea, kupitisha na kutuma mikoani agenda za Halmashauri

Kuu ya Taifa mwezi mmoja kabla ya Mkutano Mkuu wa Taifa.e. Kutoa tangazo la Mkutano Mkuu wa Taifa miezi miwili (2) kabla

ya Mkutano wa Pasaka (Easter Conference).f. Kuandaa Mkutano Mkuu wa Taifa.g. Kuwachagua wasemaji wa masomo katika Mkutano wa UKWATA

Taifa ambao ni lazima watoke Makanisa wanachama wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT).

h. Kuhudhuria Mikutano ya ndani na nje ya nchi kwa niaba ya UKWATA, baada ya kushauriana na Mratibu wa UKWATA Taifa.

i. Kuchukua hatua juu ya mashauri yanayofi kiriwa ni ya lazima kwa madhumuni ya kuiendeleza kazi ya UKWATA.

j. Kufanya vikao visivyopugua vitatu kwa mwaka.

12

Ibara 22. Halmashauri Kuu ya Taifai) Watakaohudhuria watakuwa:-

a. Kamati Kuu ya Taifa.b. Wajumbe watatu kutoka Kamati Kuu ya kila Mkoa, ambao

wawili kati yao watasimama kuwakilisha Mkoa katika uchaguzi wa Taifa.

c. Mchungaji Mlezi kutoka kila Mkoa.d. Mwalimu Mshauri kutoka kila Mkoa.e. Wenyeviti wa kamati mbalimbali zilizoundwa na Halmashauri

Kuu ya taifa wanaweza kualikwa kutegemea mahitaji.

ii) Wajibu wa Halmashauri Kuu utakuwa:-a. Kusimamia shughuli zote za UKWATA nchini.b. Kupokea mapendekezo na kuandaa agenda za Mkutano Mkuu

wa Taifa.c. Kusimamia utekelezaji wa maazimio ya Mkutano Mkuu wa

Taifa. d. Kupendekeza mahali pa kufanyika Mkutano Mkuu wa Taifa.e. Kufanya uchaguzi wa viongozi wa Taifa (Rais, Makamu wa Rais,

Katibu, Katibu Msaidizi na Mtunza Hazina).f. Kupanga kima cha ada ya kila Mkoa, kwa kila Mwana- UKWATA,

Wachungaji Walezi, Waalimu washauri na wana UKWATA washirikishwa watakaoshiriki kwenye Mkutano Mkuu wa Taifa.

g. Kuchagua Wajumbe wa Kamati ya Katiba. h. Kuunda Kamati mbalimbali kama itakavyoona inafaa kwa mujibu

wa Katiba.i. Kupokea na kujadili taarifa za maendeleo ya UKWATA toka

mikoani na kutoa ushauri au uamuzi utakaothibitishwa na Mkutano Mkuu wa Taifa.

j. Kufanya kikao cha kawaida mara moja kwa mwaka au kikao cha dharura inapobidi kwa mfano:- Iwapo nusu ya wajumbe wa Kamati Kuu ya Taifa watajiuzulu au kupoteza sifa za uongozi.

k. Kupanga kima cha kiingilio na ada ya mwanachama.

13

Ibara ya 23. Mkutano Mkuu wa Taifa.i) Watakaohudhuria watakuwa:-

a. Halmashauri Kuu.b. Wana – UKWATA watakaoshiriki katika mkutano huo.

ii) Wajibu wa Mkutano Mkuu utakuwa:-a. Kupokea na kujadili taarifa za utendaji wa Kamati Kuu ya

Taifa.b. Kuthibitisha Kamati mbalimbali zilizoundwa na Halmashauri

Kuu ya Taifa.c. Kupokea agenda za Halmashauri Kuu ya Taifa na kutoa

ufumbuzi.d. Kufanya Mkutano Mkuu mara moja kwa mwaka.

SURA 4

UONGOZI

Ibara 24. Viongozii) Katika ushirika huu kutakuwa na viongozi kuanzia ngazi ya Tawi hadi

Taifa, ambao ni:- a. Mwenyekitib. Makamu Mwenyekitic. Katibud. Katibu Msaidizie. Mtunza Hazina (Mwenyekiti katika ngazi ya Taifa ataitwa Rais na Katibu ngazi

ya Taifa ataitwa Katibu Mkuu).

ii) Wajibu wa Rais/Mwenyekiti wa Kanda/ Mkoa/Wilaya/Tawi:-a. Kuongoza mikutano na vikao vyote vya Kamati Kuu, Halmashauri

Kuu na Mkutano Mkuu.

14

b. Kutunza taratibu katika Mikutano na vikao.c. Kupiga kura ya uamuzi kwenye vikao na mikutano ikiwa kura

zinalingana.d. Kuitisha kikao cha Kamati Kuu kwa njia ya Katibu, ili mradi

yeye mwenyewe au Makamu wake atahudhuria kikao hicho.e. Kusoma taarifa ya utendaji ya mwaka mbele ya Mkutano Mkuu

na Halmashauri Kuu kwa niaba ya Kamati Kuu.f. Kubeba dhamana ya mali zote za UKWATA katika ngazi husika.g. Makamu wa Rais/Makamu Mwenyekiti atafanya kazi zote

atakazo agizwa na Rais/Mwenyekiti au kazi zote za Rais/Mwenyekiti kama hatakuwepo au atajiuzulu.

iii) Wajibu wa Katibu wa Taifa/Kanda/Mkoa/Wilaya/Tawia. Ndiye mtendaji wa shughuli zote za UKWATA katika ngazi

husika.b. Atashughulikia barua zote, atatunza daftari (Register Book) la

Wana – UKWATA na miniti zote za UKWATA.c. Ni Mwandishi wa vikao vyote vya Kamati Kuu, Halmashauri

Kuu na Mkutano Mkuu.d. Kubeba dhamana ya mali zote za UKWATA katika ngazi husika.e. Katibu Msaidizi atafanya kazi zote atakazoagizwa na Katibu au

kazi zote za Katibu kama hatakuwepo au atajiuzulu.

iv) Wajibu wa Mtunza Hazina wa Taifa/ Kanda/Mkoa/ Wilaya/Tawi:-a. Kupokea na kutoa fedha kwa shughuli zote za UKWATA.b. Kutoa stakabadhi kwa kila fedha atakayopokea.c. Kuhakikisha fedha zimewekwa Benki.d. Kutunza vitabu vyote vya fedha.e. Kutoa taarifa ya fedha ya mwaka mbele ya Halmashauri Kuu na

Mkutano Mkuu.f. Kubeba dhamana ya mali zote za UKWATA katika ngazi husika,g. Mtunza Hazina ni mmoja wa watia saini Benki.

15

Ibara 25. Miiko ya Uongozii. Viongozi wa Tawi/Wilaya/Mkoa/Kanda/Taifa watatokana na Makanisa

Wanachama wa CCT tu.ii. Viongozi wote wa UKWATA watatii na kutekeleza Katiba ya

UKWATA.iii. Viongozi wote wawe na ushuhuda mzuri wa maisha ya Kikristo.iv. Viongozi wote watathibitishwa na Wachungaji Walezi/Walimu

Washauri wa Wanafunzi.v. Kiongozi atapoteza nafasi yake ya uongozi iwapo atakuwa amepoteza

uanachama wake kwa mujibu wa Ibara ya tano.vi. Kiongozi akipoteza sifa za uongozi atasimamishwa mara moja na

Kamati Kuu ya UKWATA ya ngazi husika na suala lake kujadiliwa katika kikao cha Halmashauri Kuu ya ngazi husika.

vii. Nafasi ya uongozi itakayoachwa wazi kutokana na kiongozi kupoteza sifa/kujiuzulu/kufariki/kuhama na ugonjwa wa muda mrefu, nafasi yake itajazwa na Halmashauri Kuu husika.

SURA YA 5

UCHAGUZI

Ibara 26. Muda wa Uchaguzi.i. Uchaguzi wa Tawi/Wilaya utafanyika kati ya Julai – Septemba.ii. Uchaguzi wa Mkoa utafanyika kati ya Machi na Aprili wakati wa

Mkutano wa Pasaka.iii. Uchaguzi wa Kanda utafanyika wakati wa Mkutano wa Kanda.iv. Uchaguzi wa Taifa utafanyika wakati wa Mkutano Mkuu wa Taifa.v. Atakayechaguliwa ni yule atakayetumikia UKWATA ngazi ya Tawi

kwa kipindi cha mwaka mmoja akiwa shuleni/chuoni.

16

Ibara 27. Kutambulisha Wagombea Uongozii) Wajumbe wanaogombea uongozi wa Tawi/Wilaya watatambulishwa

mara moja kabla ya uchaguzi.ii) Wajumbe wanaogombea uongozi wa Mkoa/Kanda/Taifa

watatambulishwa kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu mara tatu kabla ya uchaguzi.

Ibara ya 28. Msimamizi wa uchaguzi.i) Ngazi ya Tawi/Wilaya/Mkoa/Kanda, Uchaguzi wa viongozi

utasimamiwa na Mchungaji Mlezi au Mwalimu Mshauri.ii) Ngazi ya Taifa, uchaguzi wa viongozi utasimamiwa na Mratibu wa

UKWATA Taifa au Mlezi wa UKWATA Taifa.

Ibara ya 29. Kupiga Kurai. Uchaguzi wote utakuwa wa siri.ii. Majina matatu (3) yatakayoungwa mkono na zaidi ya nusu ya wapiga

kura yataingia katika uchaguzi.iii. Atakayepata kura zaidi ya nusu ya wapiga kura atakuwa kiongozi.iv. Kama hakuna atakayepata zaidi ya nusu ya wapiga kura, uchaguzi

urudiwe kati ya wale wawili (2) waliopata kura nyingi.v. Kama kuna kufungana kwa kura, Msimamizi wa uchaguzi atakuwa na

kura ya uamuzi.vi. Mwanachama asiyetoka katika kanisa mwanachama wa Jumuiya ya

Kikristo Tanzania (CCT) hatapiga au kupigiwa kura katika ngazi yoyote ya uongozi.

vii. Wachungaji Walezi/Walimu washauri hawatapiga kura.

Ibara ya 30. Baada ya uchaguzi i. Viongozi wapya watatangazwa na msimamizi wa uchaguzi kwenye

Mkutano Mkuu husika.ii. Makabidhiano ya kumbukumbu za UKWATA ngazi husika yafanyike

kabla ya kusimikwa viongozi wapya.iii. Viongozi wa UKWATA watasimikwa na Mchungaji Mlezi wa ngazi

husika kwa kipindi kisichozidi mwezi mmoja baada ya uchaguzi.

17

SURA YA 6

VIKAO NA MIKUTANO

Ibara 31. VikaoVikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Tawi/Wilaya/Mkoa/Kanda/Taifa vitafanyika ikiwa wajumbe wasiopungua nusu watahudhuria.

Ibara ya 32. MikutanoMkutano Mkuu wa Tawi/Wilaya/Mkoa/Kanda/Taifa utafanyika ikiwa wajumbe wasiopungua nusu watahudhuria.

SURA YA 7

HUDUMA MBALIMBALI

Ibara ya 33. Ibada na Mikutano ya UKWATAi. Ibada zote za UKWATA zitaendeshwa kwa kutumia liturgia ya

UKWATAii. Viongozi wote wa UKWATA watasimikwa kwa kutumia litrugia ya

UKWATAiii. Viongozi wa ibada, Wahubiri, walimu na watoa neno kwenye mikutano

ya UKWATA ni lazima watoke kwenye makanisa Wanachama wa CCT na kuthibitishwa kuwa ni watumishi wema katika Makanisa Wanachama wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania.

Ibara ya 34. Huduma ya Maombi na Uinjilistii) Katika Ushirika huu kutakuwa na Huduma ya Maombi na Uinjilisti

kuanzia ngazi ya Tawi/Wilaya/Mkoa/Taifa.ii) Waratibu wa huduma hii watakuwa wajumbe waalikwa katika vikao

vya Kamati za Matawi na Kamati Kuu za Wilaya/Mkoa/Taifa na Wajumbe katika Halmashauri Kuu za ngazi zote.

18

iii) Waratibu wa huduma hii watasimamiwa na Mchungaji Mlezi kutoka Makanisa Wanachama wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT).

iv) Huduma hii itakuwa na mwongozo wake utakaopitishwa na Mkutano Mkuu wa UKWATA Taifa na kuthibitishwa na CCT.

Ibara 35. Wana – UKWATA Washirikishwa (TSCF – Associate Members) i) Kutakuwa na Wana - UKWATA Washirikishwa kuanzia ngazi ya Tawi/

Wilaya/Mkoa/Kanda/Taifa. ii) Mtu binafi si ambaye si mwanafunzi au mwanachuo na ambaye alimaliza

shule au Chuo ataitwa Mwana UKWATA Mshirikishwa ikiwa:a. Ataitambua na kuiheshimu Katiba ya UKWATA.b. Atakuwa na kitambulisho maalum kutoka UKWATA Taifa

kitakachosainiwa na kutolewa na Mchungaji Mlezi wa UKWATA Mkoa.

c. Atakuwa bado muumini wa Makanisa Wanachama wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania.

d. Atalipa ada na michango kama itakavyopangwa kitaifa.e. Ataunga mkono UKWATA kwa bidii.f. Atakuwa anatambuliwa na Mchungaji wake wa Kanisa

Mwanachama wa CCT.iii) Wana UKWATA washirikishwa watakuwa na mwongozo utakaopitishwa

na Halmashauri Kuu ya UKWATA Taifa na kuthibitishwa na CCT.

Ibara ya 36. Wajibu wa Wana UKWATA Washirikishwa:i) Watasaidia na kuendeleza UKWATA kwa hali na mali katika ngazi

zote.ii) Watakaribishwa kuhudhuria kwenye vikao vya UKWATA lakini

hawatapiga kura.a) Ngazi ya Mkoa – Kwenye Kikao cha Halmashauri Kuu ya Mkoa

watashiriki wana UKWATA Washirikishwa watano (5) na kwenye Mkutano Mkuu idadi itapangwa na Kamati Kuu ya UKWATA Mkoa.

b) Taifani – Kwenye Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa watashiriki

19

wana UKWATA Washirikishwa watano (5) na kwenye Mkutano Mkuu idadi itapangwa na Kamati Kuu ya UKWATA Taifa.

iii) Watakuwa na vikao vyao vitakavyowashirikisha viongozi wa UKWATA kama ifuatavyo:a. Ngazi ya Mkoa – Mchungaji Mlezi, Mwalimu Mshauri,

Mwenyekiti wa UKWATA na Katibu wa UKWATA Mkoa. b. Taifani – Mratibu wa UKWATA Taifa, Rais wa UKWATA na

Katibu wa UKWATA Taifa.

SURA YA 8

WALEZI NA WASHAURIIbara ya 37. Jumuiya ya Kikristo Tanzania – CCTi) Ndiye Mlezi Mkuu wa UKWATA. ii) Itamchagua/itamteua Askofu Mlezi na Mratibu wa UKWATA Taifa.

Ibara ya 38. Wajibui) Askofu Mlezi ndiye Mlezi Mkuu wa UKWATA, anaweza kuhudhuria

vikao vya Kamati Kuu, Halmashauri Kuu na Mkutano Mkuu wa UKWATA Taifa.

ii) Mratibu wa UKWATA Taifa ndiye mtendaji mkuu wa shughuli zote za UKWATA Taifa.

Ibara ya 39. Makanisa i) Makanisa yote wanachama wa CCT ni walezi wa UKWATA mahali

yalipo na yatakuwa na wajibu wa kufanya kazi kwa pamoja.ii) Hayana budi kufanya vikao visivyopungua viwili kwa mwaka ambavyo

vitaitishwa na Mchungaji Mlezi wa Mkoa. Kitaifa, masuala yanayohusu walezi wa UKWATA yatajadiliwa kupitia vikao vya CCT.

Ibara 40. Mchungaji MleziKatika ushirika huu kutakuwa na Mchungaji Mlezi kuanzia ngazi ya Tawi/

20

Wilaya/Mkoa/Kandai) Sifa za Mchungaji Mlezi.

a. Awe anatoka katika Kanisa lililo mwanachama wa CCTb. Awe mtekelezaji na mwenye nia ya kuilinda na kuitetea Katiba

ya UKWATA kwa usahihi na ukamilifu.c. Ikiwezekana awe na elimu isiyopungua kidato cha nne au

inayolingana na hiyo.d. Awe amehitimu masomo ya Elimu ya Theologia, vyeti vyake vya

Theologia vipitiwe na kuthibitishwa na viongozi wa Makanisa Wanachama wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania.

e. Awe na uwezo wa kuchukuliana na Wana UKWATA.f. Awe na maisha safi ya Kikristo ili aweze kuwalea vema Wana-

UKWATA g. Awe anayewatia moyo Wana – UKWATA katika suala la

wokovu.ii) Namna ya kumpata Mchungaji Mlezi wa Tawi/Wilaya/Mkoa:-

a. Halmashauri Kuu ya Mkoa iombe Mchungaji Mlezi wa Tawi/Wilaya/Mkoa kwa Dayosisi/Kanisa husika.

b. Nakala ya barua ya Maombi itumwe kwa Mratibu wa UKWATA Taifa.

c. Lazima atokane na Makanisa Wanachama wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania

iii) Wajibu wa Mchungaji Mlezia. Atashirikiana na Mwalimu Mshauri katika kuulea UKWATA b. Atailinda na kuitetea Katiba ya UKWATA.c. Atahudhuria mikutano na vikao vya UKWATA vitakavyoitishwa

na Mwenyekiti wa UKWATA wa ngazi husika. Kitaifa vitaitishwa na Mratibu wa UKWATA Taifa.

d. Atakuwa kiungo baina ya Makanisa wanachama wa CCT, uongozi wa shule/chuo na uongozi wa UKWATA wa ngazi husika.

iv) Muda wa Mchungaji Mlezi katika hudumaa. Atakaa katika huduma muda wa miaka minne.b. Halmashauri Kuu ya Mkoa inaweza kuomba Mchungaji Mlezi

kuendelea na huduma kwa kipindi kingine cha miaka minne.c. Halmashauri Kuu ya Mkoa iombe Dayosisi/Kanisa husika

21

kumbadilisha Mchungaji Mlezi, endapo hatatimiza sifa za Mlezi kwa mujibu wa Katiba ya UKWATA.

Ibara 41. Walimu Washauri.Katika Ushirika huu kutakuwa na Walimu washauri wawili (mwanaume na mwanamke)i) Sifa za Mwalimu Mshauri:-

a. Awe anatoka katika Kanisa lililo mwanachama wa CCT.b. Awe mtekelezaji na mwenye nia ya kuilinda na kuitetea Katiba

ya UKWATA kwa usahihi na ukamilifu.c. Awe na uwezo wa kuchukuliana na Wana –UKWATA.d. Awe na maisha safi ya Kikristo ili aweze kushauri vema Wana

UKWATA.e. Awe anayewatia moyo Wana – UKWATA katika suala la

wokovu.ii) Namna ya kumpata Mwalimu Mshauri.

a. Mwalimu Mshauri wa UKWATA wa Tawi atapendekezwa na Halmashauri ya Tawi.

b. Jina lake au majina yaliyopendekezwa yapelekwe kwa Mchungaji Mlezi wa ngazi husika.

c. Mchungaji Mlezi atawasilisha pendekezo/mapendekezo kwa Mkuu wa Shule/Chuo kwa ushauri na uteuzi.

d. Mwalimu Mshauri wa Wilaya/Mkoa/Kanda atachaguliwa na Halmashauri ya Wilaya/Mkoa/Kanda toka miongoni mwa Walimu Washauri wa Matawi.

iii) Wajibu wa Mwalimu Mshauri:-a. Atashirikiana na Mchungaji Mlezi katika kuulea UKWATA.b. Ataangalia mwenendo mzima wa UKWATA kwa kufuata Katiba

ya UKWATA.c. Atahudhuria mikutano na vikao vya UKWATA vitakavyoitishwa

na Mwenyekiti wa UKWATA wa ngazi husika na Mchungaji Mlezi.

d. Atakuwa kiungo baina ya uongozi wa shule/chuo na uongozi wa UKWATA wa ngazi husika.

22

iv) Muda wa Mwalimu Mshauri katika hudumaa. Atakaa katika huduma kwa muda wa miaka minne.b. Halmashauri Kuu ya Mkoa inaweza kuomba Mwalimu Mshauri

kuendelea na huduma kwa kipindi kingine cha miaka minne.c. Halmashauri ya Tawi itaomba kwa Mkuu wa shule/chuo husika

kupatiwa Mwalimu mshauri mwingine kupitia kwa Mchungaji Mlezi endapo hatatimiza sifa za Mwalimu Mshauri kwa mujibu wa Katiba ya UKWATA.

SURA YA 9

FEDHA NA MIRADI

Ibara 42. Ada Na Michangoi. Kila mwanachama mpya atalipa kiingilioii. Kila Mwana – UKWATA atalipa ada ya uanachama kila mwaka.iii. Kila Tawi litatoa mchango kwa mfuko wa Hazina wa Wilaya na Mkoa

kwa uwiano wa wanachama. Kima cha mchango kitapangwa na Halmashauri Kuu ya Mkoa.

iv. Kila Mkoa utatoa mchango kwa mfuko wa hazina wa Kanda/Taifa kwa uwiano wa wanachama. Kima cha mchango kitapangwa na Halmashauri Kuu ya Taifa.

v. Kila Mwana – UKWATA atalipa ada ya mkutano wa ngazi husika.vi. Kila Mwana -UKWATA mshirikishwa katika Mkutano Mkuu wa Mkoa

au Taifa, atalipa ada itakayopangwa na Halmashauri Kuu ya Mkoa au Taifa, na kuidhinishwa na Mkutano Mkuu husika.

vii. Wachungaji Walezi na Walimu Washauri watalipa ada ya Mkutano Mkuu katika ngazi husika kama itakavyopangwa na Halmashauri Kuu husika.

Ibara 43. Utunzaji na Ukaguzi wa Mahesabu ya Fedhai. Kila Tawi/Wilaya/Mkoa uwe na akaunti Benki.

23

ii. Akaunti ya UKWATA Taifa itatunzwa na Kamati Kuu ya UKWATA Taifa.

iii. Mfuko wa UKWATA utatumika kwa madhumuni ya kuendeleza shughuli za Ushirika, ilimradi matumizi yake hayatazidi mapato.

iv. Hesabu za UKWATA katika ngazi zote zitakaguliwa kila mwaka kabla ya Mkutano Mkuu wa ngazi husika na mtu atakayechaguliwa na Halmashauri Kuu husika.

v. Watia saini benki kwa ngazi ya Tawi, Wilaya na Mkoa watakuwa Mwenyekiti, Mtunza Hazina, Mchungaji Mlezi na Mwalimu Mshauri wa UKWATA.

vi. Watia saini Benki ngazi ya Taifa watakuwa Mtunza Hazina wa Taifa na Mratibu wa UKWATA Taifa.

Ibara 44 Sera ya Fedhai) Kutakuwa na Sera ya fedha itakayothibitishwa na Kikao cha

Halmashauri Kuu ya UKWATA Taifa .ii) Kamati Kuu ya UKWATA Taifa itasimamia utekelezaji wa Sera ya

Fedha.

Ibara. 45. MiradiUshirika utabuni na kuendesha miradi mbalimbali ya uzalishaji kwa ajili ya maendeleo ya UKWATA katika ngazi za Tawi/Wilaya//Mkoa/Kanda/Taifa. Miradi yote itakayoanzishwa iwe imeidhinishwa na Halmashauri Kuu husika na iwe ile inayozingatia maadili ya Kikristo.

Ibara ya 46: Umiliki wa malii) UKWATA utamiliki mali zinazohamishika na zisizohamishika katika

ngazi ya Tawi/Wilaya/Mkoa/Kanda/Taifa. ii) Kamati Kuu ya UKWATA ngazi husika ndiyo yenye dhamana ya

kutunza mali zote za UKWATA kwa kutumia daftari la kumbukumbu (Register Book).

24

SURA 10

MAREKEBISHO YA KATIBA

Ibara 47: Muda wa Marekebisho ya Katibai) Katiba itaangaliwa upya kila baada ya miaka mitano (5) ila marekebisho

madogo yanaweza kufanyika kabla ya muda huo kwa mujibu wa Katiba hii Ibara ya 47.

ii) Mwana – UKWATA anaweza kupendekeza marekebisho ya Katiba kwa kufuata utaratibu ufuatao:-a. Pendekezo linaungwa mkono na nusu ya wajumbe rasmi waliopo

katika Mkutano Mkuu wa mwaka wa Tawi/Wilaya/Mkoa.b. Mapendekezo yote yajadiliwe na Halmashauri Kuu ya Mkoa

kabla ya kupelekwa taifani.c. Mapendekezo ya Mkoa yapelekwe kwa Katibu wa UKWATA

Taifa kwa muda usiopungua miezi mitatu kabla ya Mkutano Mkuu wa UKWATA Taifa.

d. Kamati Kuu ya UKWATA Taifa itapokea mapendekezo ya marekebisho ya Katiba toka mikoani na kuyapeleka kwenye Kamati ya Katiba ili yafanyiwe kazi.

e. Mapendekezo ya marekebisho ya Katiba toka Kamati ya Katiba yatapelekwa katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa.

f. Rekebisho lolote la Katiba litapitishwa endapo theluthi mbili (2/3) ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wataliunga mkono.

g. Rekebisho lolote la Katiba ni lazima lithibitishwe na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT).

Ibara 48. Kamati ya Katiba(i) Kutakuwa na Kamati ya Katiba ambayo wajumbe wake ni Rais, Katibu

Mkuu wa UKWATA Taifa, Mratibu wa UKWATA Taifa na Wajumbe watano (5) watakaochaguliwa na Halmashauri Kuu ya Taifa na kuthibitishwa na Mkutano Mkuu wa Taifa.

(ii) Kamati ya Katiba itafanya kazi kwa kipindi cha miaka mitatu (3)

25

26

ISBN: 978 9987 9490 1 4