kilimo, usalama wa chakula, na mkuhumi katika afrika ... maswala ya usalama wa chakula (kama...

6
DOKEZO Waraka huu umechapishwa na mradi wa REDD-net, ambao unafadhiriwa na kitengo cha maendeleo cha Norway (NORAD). Mawazo na mapendekezo yaliyomo kwenye waraka huu ni yale ya waandishi na wala sio ya wafadhili au mashirika yanayoshiriki kwenye mradi wa REDD-net. Utafiti huu ulifanyika kati ya mwezi Juni na Novemba, 2011. article Mawasiliano kwa ajili ya Usawa katika Misitu na sera za Tabia nchi Kilimo, Usalama wa Chakula, na MKUHUMI katika Afrika Mashariki UTANGULIZI Neno MKUHUMI linamaanisha Upungazaji wa Hewa Ukaa Kutokana na Ukataji na Uharibifu wa Misitu ikiwa ni pamoja na shughuri za Uhifadhi, Usimamizi endelevu wa Misitu na Ukuzaji wa Hifadhi za kabonikatika nchi zinazoendelea. Utaratibu huu unalenga kutoa malipo kwa nchi zinazoendelea ili kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa itokanayo na misitu, kwa mfano kupitia kupunguza kushughuri za ubadilishaji wa misitu, usimamizi endelevu wa misitu, na ukuzaji wa vitita vya Kaboni ambavyo vinaweza kujumuisha upandaji wa miti. Bw. Yusuf Kisiero ambaye hutumia mbinu za kilimo mseto katika Shamba Lake. Kilimo mseto Kumetambuliwa kama majawapo ya kiunganishi kati ya MKUHUMI na kilimo kwa Afrika Mashariki. Novemba 2011 HOJA MUHIMU Kilimo na usalama wa chakula ni suala la muhimu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na moja ya mambo ambayo yametambuliwa na kupewa kipaaumbele katika ushirikiano wa kikanda. MKUHUMI ina uwezo wa kuchangia katika kufikia malengo haya, na baadhi ya mikakati kwa ajili ya kufanikisha suala hili tayari imetambuliwa katika mipango na nyaraka za awali za MKUHUMI katika kanda. Yafuatayo ni mapendekezo kwa ajili ya kufanikisha uhusiano huu katika ya MKUHUMI, kilimo na usalama wa chakula ndani ya Africa mashariki: MKUHUMI inapaswa kuchangia katika uandaaji na uhifadhi wa uzoefu wa jamii katika udhibiti jumuishi wa magonjwa na wadudu enezi katika miti, mazao, na wanyama pamoja na uzoefu kutoka katika udhibi wa wadudu katika kilimo mseto. Uzoefu huu unaweza kukuzwa hapo baadaye na ukatumika kuielimisha jamii juu ya shughuli au mbinu mbadala ambazo zinaweza kutumika kuhakikisha ufanisi katika usimamizi wa rasilimali za misitu. MKUHUMI inapaswa kuimarisha na kuboresha shughuli za kijamii hasa ubadilishanaji wa maarifa na uzoefu katika kilimo endelevu, kilimo hifadhi, na aina yingine za kilimo. Matokeo yake ni kwamba shughuli hizi zinaweza kusaidia kupunguza madhara ya kilimo kisicho endelevu katika rasilimali za misitu na ardhi hasa katika ardhi kavu pamoja na mifumo ikolojia tete katika ukanda wa Africa mashariki. MKUHUMI inapaswa kusaidia vituo vya majaribio katika kanda mbalimbali za kilimo ili kuimarisha huduma zilizopo za ugani na ushauri. Hali hii inaweza kusaidia na kuwa kama kiunganishi kati ya jamii za wakulima na watafiti kwa kuonyesha matokeo ya njia za teknolojia muhafaka za kilimo ambao zinabuniwa mara kwa mara kama vile mifumo ya upandaji, misitu na nishati. Na Richard Kimbowa, David M. Mwayafu na Harriet Smith

Upload: hadat

Post on 09-Mar-2018

478 views

Category:

Documents


47 download

TRANSCRIPT

Page 1: Kilimo, Usalama wa Chakula, na MKUHUMI katika Afrika ... maswala ya usalama wa chakula (kama inavyoonekana katika Jedwali 2). Kutoka jedwali hii, ni wazi kwamba vipaumbele vya sekta

DOKEZO

Waraka huu umechapishwa na mradi wa REDD-net, ambao unafadhiriwa na kitengo cha maendeleo cha Norway (NORAD). Mawazo na mapendekezo yaliyomo kwenye waraka huu ni yale ya waandishi na wala sio ya wafadhili au mashirika yanayoshiriki kwenye mradi wa REDD-net. Utafiti huu ulifanyika kati ya mwezi Juni na Novemba, 2011.

articleMawasiliano kwa ajili ya Usawa katika Misitu na sera za Tabia nchi

Kilimo, Usalama wa Chakula, na MKUHUMI katika Afrika Mashariki

UTANGULIZI

Neno MKUHUMI linamaanisha

Upungazaji wa Hewa Ukaa Kutokana

na Ukataji na Uharibifu wa Misitu

ikiwa ni pamoja na shughuri za

Uhifadhi, Usimamizi endelevu

wa Misitu na Ukuzaji wa Hifadhi za

kabonikatika nchi zinazoendelea.

Utaratibu huu unalenga kutoa malipo

kwa nchi zinazoendelea ili kupunguza

uzalishaji wa hewa ukaa itokanayo na

misitu, kwa mfano kupitia kupunguza

kushughuri za ubadilishaji wa misitu,

usimamizi endelevu wa misitu, na

ukuzaji wa vitita vya Kaboni ambavyo

vinaweza kujumuisha upandaji wa miti.

Bw. Yusuf Kisiero ambaye hutumia mbinu za kilimo mseto katika Shamba Lake. Kilimo msetoKumetambuliwa kama majawapo ya kiunganishi kati ya MKUHUMI na kilimo kwa Afrika Mashariki.

Novemba 2011

HOJA MUHIMU

• Kilimo na usalama wa chakula ni suala la muhimu

katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na moja ya mambo

ambayo yametambuliwa na kupewa kipaaumbele

katika ushirikiano wa kikanda.

• MKUHUMI ina uwezo wa kuchangia katika kufikia

malengo haya, na baadhi ya mikakati kwa ajili ya

kufanikisha suala hili tayari imetambuliwa katika

mipango na nyaraka za awali za MKUHUMI katika

kanda. Yafuatayo ni mapendekezo kwa ajili ya

kufanikisha uhusiano huu katika ya MKUHUMI, kilimo

na usalama wa chakula ndani ya Africa mashariki:

• MKUHUMI inapaswa kuchangia katika uandaaji na

uhifadhi wa uzoefu wa jamii katika udhibiti jumuishi

wa magonjwa na wadudu enezi katika miti, mazao,

na wanyama pamoja na uzoefu kutoka katika

udhibi wa wadudu katika kilimo mseto. Uzoefu huu

unaweza kukuzwa hapo baadaye na ukatumika

kuielimisha jamii juu ya shughuli au mbinu mbadala

ambazo zinaweza kutumika kuhakikisha ufanisi katika

usimamizi wa rasilimali za misitu.

• MKUHUMI inapaswa kuimarisha na kuboresha

shughuli za kijamii hasa ubadilishanaji wa maarifa na

uzoefu katika kilimo endelevu, kilimo hifadhi, na aina

yingine za kilimo. Matokeo yake ni kwamba shughuli

hizi zinaweza kusaidia kupunguza madhara ya kilimo

kisicho endelevu katika rasilimali za misitu na ardhi

hasa katika ardhi kavu pamoja na mifumo ikolojia

tete katika ukanda wa Africa mashariki.

• MKUHUMI inapaswa kusaidia vituo vya majaribio

katika kanda mbalimbali za kilimo ili kuimarisha

huduma zilizopo za ugani na ushauri. Hali hii inaweza

kusaidia na kuwa kama kiunganishi kati ya jamii za

wakulima na watafiti kwa kuonyesha matokeo ya njia

za teknolojia muhafaka za kilimo ambao zinabuniwa

mara kwa mara kama vile mifumo ya upandaji, misitu

na nishati.

Na Richard Kimbowa, David M. Mwayafu na Harriet Smith

Page 2: Kilimo, Usalama wa Chakula, na MKUHUMI katika Afrika ... maswala ya usalama wa chakula (kama inavyoonekana katika Jedwali 2). Kutoka jedwali hii, ni wazi kwamba vipaumbele vya sekta

2

Je kwa nini ni muhimu kuzingatia mahusiano na tofauti kati ya mkuhumi na kilimo?

Kwa vile upanukaji wa kilimo ni mojawapo ya visababishi vya ukataji miti na uharibifu wa misitu, kuibuka kwa MKUHUMI kunatoa fursa katika ngazi ya kanda na taifa, kwa ajili ya kuwekeza katika kilimo endelevu na cha muda mrefu. Hii itahusisha uhifadhi wa rasilimali ya misitu, kukuza kilimo cha mseto, pamoja na shughuli za kilimo rafiki wa mazingira ambazo zinaweza kuchangia kudhibiti mabadiliko ya tabia nchi katika ukanda wetu, wakati pia zikiimarisha mikakati ya kikanda na kitaifa ya kushughulikia masuala ya uhaba wa chakula na njaa kwa muda mrefu.

Makala hii umetokana na Makala ya REDD-net juu ya MKUHUMI na sekta nyingine katika ukanda wa Afrika Mashariki (Kimbowa R. et al., 2011).

uhusiano kati ya mkuhumi na uzalishaJi wa aridhi katika nchi za afrika mashariki

Kilimo na usalama wa chakula ni vitu ambavyo vina uhusiano mkubwa sana katika ukanda wa Afrika Mashariki (EAC) na uchumi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambapo vyote vinategemea sana sekta ya kilimo. Japokuwa ukanda una uwezo wa kuzalisha chakula cha kutosha kwa ajili ya matumizi ya kikanda na kwa ajili ya

kuuza nje katika soko la dunia, ukanda wa Afrika Mashariki umekuwa ukikumbwa mara nyingi na uhaba wa chakula, upungufu wa chakula na chembechembe za baa la njaa. Wakati huo huo, ongezeko la watu linamaanisha kwamba ni lazima kuwepo na mikakati madhubiti ya kuhakikisha usalama wa chakula.

Kutokana na kupungua kwa uwezo wa ardhi kuzalisha mazao ambako kumesababishwa na ukataji miti na uharibifu wa misitu, shughuli za MKUHUMI zina uwezo mkubwa wa kubadilisha hali hii kwa gharama nafuu kupitia mikakati kama vile kilimo mseto and mashamba-misitu, huku ikitoa chakula cha mifugo (kama vile ng’ombe mbuzi na kondoo, nk). Aidha, miti iliyopandwa katika ardhi ya umma na ile ya binafsi inaweza kutumika kama chanzo cha chakula (matunda), nishati, dawa pamoja na kurekebisha hali ya hewa (ambayo ni muhimu kwa kilimo). Kwa namna hii, MKUHUMI unaweza kuchangia katika kufanikisha malengo ya kanda ya usalama wa chakula ambayo kwa sasa yanaathiriwa na mambo kadha-wa-kadha ambayo yamehainishwa katika jedwali namba 1 hapo chini.

Baada ya kutambua ukweli kwamba uzalishaji wa chakula katika kanda ya Afrika Mashariki unaathiriwa vibaya na mabadiliko ya tabia nchi, malengo na mikakati ya kitaifa ya nchi wanachama kwa sasa inafuata malengo ya Mikataba ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo inasisitiza ushirikiano katika kuboresha uzalishaji wa kilimo, wakati pia ikisaidia kushughulikia tatizo la uharibifu wa misitu na ardhi kama inavyoneshwa katika jedwali namba 1.

Jumuiya ya Afrika Mashariki imetambua kilimo na usalama wa chakula kama moja ya maeneo ya ushirikiano kutokana na kuongezeka kwa shinikizo kwenye rasilimali hizi na pia uharibifu wa mazingira (ambavyo vimetokana na ongezeko la idadi ya watu, matumizi mabaya ya ardhi na ufugaji unaozidi kiwango); Kilimo cha kiwango cha chini ambacho si cha kuaminika kutokana na utegemezi mkubwa sana kwenye kilimo cha mvua; na pia kutokana na kuongeza kwa majanga makali ya hali ya hewa kama vile mafuriko na ukame kutokana na mabadiliko ya hali ya tabia nchi, ambayo huathiri vibaya uzalishaji wa chakula.

Mikakati ya MKUHUMI ambayo imependekezwa katika nchi za Kenya, Tanzania na Uganda inalenga kuchangia katika

• Pia, kwa kuongezea kwenye uzoefu uliotokana na mchakato wa R-PP,

MKUHUMI inapaswa kusaidia uazishwaji na uimarishaji wa mijadala ili

kupata mawazo kwa ajili ya kuzuia migogoro na kuakikisha umiliki wa

ardhi kwa jamii husika hasa kwa ajili ya maendeleo yanayotokana na

shughuli za kilimo.

• Kuna haja ya kuwianisha sera na mifumo ya sheria katika kilimo,

rasilimali za maji na nishati pamoja na sekta nyingine ili ziendane na

MKUHUMI na hivo kuzuia ukinganaji wa mipango hii. Na kwa sababu

hii ukuaji unaotarajiwa katika uchumi na idadi ya watu katika kilimo na

sekta nyingine unaweza kusababisha mvutano zaidi katika mamlaka

zinazokingana, jambo ambalo linaweza kuleta hasara katika uendelevu

wa ardhi, maji, misitu na rasimali nyinginezo.

JEDWALI 1: Vikwazo Katika Kufikia Malengo ya Usalama wa Chakula Katika Jumuiya Ya Africa Mashariki (EAC)

Miundombinu ya maji Utegemezi uliokithiri juu ya mifumo ya kilimo cha mvua, uwezo mdogo wa kuvuna maji ya mvua, na matumizi hafifu ya rasilimali za maji.

Machafuko ya kijamii/kiraia Uharibifu wa uzalishaji na usambazaji wa chakula kutokana na machafuko ya kijamii na kisiasa.

Upatikanaji na usambazaji Kukosekana kwa usawa wa kijinsia katika upatikanaji wa fursa katika uzalishaji, masoko, matumizi, umiliki na udhibiti wa rasilimali za uzalishaji na pia upatikanaji duni wa chakula hasa miongoni mwa watu wanaoishi katika mazingira magumu.

Mabadiliko ya Tabia nchi Kuongezeka kwa matukio na majanga ya hali ya hewa na pia uhaba wa mtiririko wa taarifa juu ya majanga na madhara ya mabadiliko ya tabia nchi pamoja na matendo ya witikio wa wananchi2.

Shinikizo nyinginezo Kuongezeka kwa shinikizo kwenye rasilimali na uharibifu wa mazingira kutokana na ongezeko la kasi la idadi ya watu, matumizi mabaya ya udongo, ufugaji unaozidi kiwango, nk

Chanzo: Umoja wa Mataifa: Jumuiya ya Afrika Mashariki (2010a)

Page 3: Kilimo, Usalama wa Chakula, na MKUHUMI katika Afrika ... maswala ya usalama wa chakula (kama inavyoonekana katika Jedwali 2). Kutoka jedwali hii, ni wazi kwamba vipaumbele vya sekta

3

maswala ya usalama wa chakula (kama inavyoonekana katika Jedwali 2). Kutoka jedwali hii, ni wazi kwamba vipaumbele vya sekta za MKUHUMI, kilimo na usalama wa chakula vinashabiiana kwa karibu sana, japokuwa uhusiano huu bado haujatambulika vizuri katika vitendo kutokana na ukweli kwamba mikakati ya MKUHUMI ni mikakati mipya kutekelezwa katika Afrika Mashariki. Hata hivyo, tofauti kati ya maeneo ya kilimo inamaanisha kwamba mifumo tofauti ya kilimo ambayo inaendana na uhifadhi wa rasimali za misitu ndio itakayokuwa muhafaka katika maeneo tofauti. Maelezo zaidi yanatolewa katika Jedwali namba 2 hapo chini.

Kwa jinsi sera, sheria na taasisi za kutekeleza miradi ya MKUHUMI inavyoandaliwa, ndivyo changamoto zinavyoanza kujitokeza. Mchakato wa mashauriano wakati wa uandaaji wa R-PPs ulionyesha maeneo mbalimbali ambapo maboresho yanahitajika.

Kwa mfano, kuna wasiwasi kwamba suluhisho nyingi za kukabiliana na visababishi vya ukataji miti na uharibifu wa misitu kutokana na upanuzi wa kilimo (mazao na mifugo),hazizingatii umuhimu wa kutoa njia mbadala na zinazofaa kiuchumi kwa wale wanaohusika. Vile vile, jamii

katika maeneo kame ya Afrika Mashariki zinategemea kwa kiasi kikubwa misitu na rasilimali nyingine kwa maisha yao ya kila siku, na hivo zitahitaji kupatiwa njia mbadala (mfano kufuga ng’ombe) na chaguzi (mfano kilimo endelevu) ili kupunguza madhara yake katika rasilimali za ardhi na misitu kama hasa pale zinapotafuta malisho mapya na maji kwa ajilu ya wanyama wao.

Jinsi gani mkuhumi unaweza kuchangia malengo ya sekta ya kilimo katika ngazi ya kitaifa na kikanda?

Kutokana na uchambuzi na majadala hapo juu, yafuatayo ni mapendekezo kwa ajili ya kuisaidia MKUHUMI kuchangia zaidi katika swala la kilimo na usalama wa chakula katika ukanda wa Afrika Mashariki:

• MKUHUMI inapaswa kuchangia katika kutayarisha na kubadilishana uzoefu wa jamii juu ya udhibiti jumuishi wa magonjwa ya miti, mimea na wanyama; udhibiti wa wadudu katika kilimo mseto ambao

JEDWALI la 2: Muhtasari wa Mahusiano kati ya malengo ya Taifa ya Kilimo na mikakati, na mikakati ya MKUHUMI iliyopendekezwa

Malengo ya Taifa ya kilimo Mikakati ya MKUHUMI iliyopendekezwa Nini zaidi kiongezwe ili kusudi MKUHUMI ichangie zaidi katika kufanikisha malengo ya sekta ya kilimo?

Kenya

Rasimu ya Sera ya Taifa ya Maendeleo Endelevu ya Ardhi ya jangwa na nusu jangwa ya Kenya (ASAL), 2004 ambayo inataka:

• Matumizi endelevu ya misitu mikubwa iliyopo katika ASALs kwa ajili ya kuboresha maisha katika maeneo haya

• Zao muhimu namba 2 la ASAL: Uendelevu wa mazingira unalenga kuboresha uwezo endelevu wa uzalishaji wa ardhi na jitihada za uhifadhi.

• Kuendeleza kilimo mseto, matumizi sanifu ya kuni, vyanzo mbadala vya nishati na kuimarisha hifadhi ya Kaboni kitaifa kwa njia ya upandaji miti.

• Kusaidia Taasisi ya Misitu ya Kenya kushughulikia tatizo la moto katika misitu ikiwa ni pamoja na kutumia mifumo ya tahadhari ya mapema, maandalizi ya moto, na kuboresha uwezo wa kupambana na moto.

[GOK (2010): pp39 - 40: uk 38, 40]

Kuchunguza uwezekano wa umwagiliaji katika ASALs ili kupunguza uwezekano wa ardhi tete (Misitu) kuingiliwa wakati wa utafutaji wa ardhi bora kwa ajili ya Kilimo. Tendo hili lina uwezo wa kuongeza uzalishaji wa kilimo bila kuongeza uingiliwaji wa misitu.

• Kuchunguza uwezekano wa kuongeza matumizi ya mbinu endelevu za kilimo kama vile mboji na kilimo cha mseto kwa jamii maskini na wanyonge katika ASALs. Jamii hizi utegemea sana hali ya asili (hasa wafugaji) na kwa mara zote zinahitaji malisho na maji kwa ajili ya mifugo yao.

Mkakati wa Kuuisha Kilimo (SRA), 2005

Malengo: Kuboresha uzalishaji wa kilimo kwa ujumla, kutawanyisha vyanzo mbalimbali vya mapato na kuongeza pato la kaya za wakulima.

• Kuhamasisha ukuzaji wa kilimo

• Kutoa pembejeo za kilimo kwa jamii maskini na zile zinazoishi katika mazingira magumu kuzunguka misitu kulingana na mpango wa taifa wa kuongeza Kasi ya upatikanaji Pembejeo (NAAIAP)

• Kusaidia jitihada za kilimo, biashara, Kilimo cha mseto na pia kusaidia juhudi za Taasisi ya misitu ya Kenya katika majaribio husika ya miradi ya misitu.

[GOK (2010): pp39 - 40: pp38, 42]

• Kukuza shughuli mbadala za uzalishaji mali (ambazo ni badala ya shughuli zenye faida kubwa kama vile uchomaji mkaa) kama moja ya njia ya kupunguza shinikizo katika misitu iliyobaki katika ASAL

• kudhibiti uzalishaji na uuzaji wa kuni na mkaa ambavyo uchangia katika uharibifu wa mazingira, kupitia mipango yenye kutoa motisha kwa jamii

Page 4: Kilimo, Usalama wa Chakula, na MKUHUMI katika Afrika ... maswala ya usalama wa chakula (kama inavyoonekana katika Jedwali 2). Kutoka jedwali hii, ni wazi kwamba vipaumbele vya sekta

4

unaweza kukuzwa ili kuzifahamisha jamii juu ya shughuli mbadala za kufanikisha usimamizi endelevu wa misitu na rasilimali nyingine. Hii inaweza pia kushawishi agenda za tafiti pamoja na kuweka vipaumbele vipya katika kushughulikia mahitaji ya jamii pamoja na kusaidiausimamizi wa kijamii wa rasilimali za misitu.

• MKUHUMI inapaswa kusaidia kuendeleza elimu pamoja na kubadilishana uzoefu miongoni mwa jamii juu ya mbinu za kilimo endelevu, kilimo cha uhifadhi,

pamoja na mbinu nyingine za wakulima au vikundi vya wakulima ambazo zinaweza kusaidia kupunguza madhara ya kilimo kisicho endelevu kwenye misitu na ardhi katika ardhi kame na tete ya Afrika Mashariki.

• MKUHUMI inapaswa kusaidia vituo vya mafunzo katika kanda mbalimbali za kilimo ili kuboresha huduma za ugani na ushauri zilizopo. Hii inaweza kutumika kamamakutano ya shughuri za kilimo za wakulima na zile za watafiti ambayo yanaweza kusaidia kwa kuonyesha teknolojia husika za

Malengo ya Taifa ya kilimo Mikakati ya MKUHUMI iliyopendekezwa Nini zaidi kiongezwe ili kusudi MKUHUMI ichangie zaidi katika kufanikisha malengo ya sekta ya kilimo?

Tanzania

Sera ya Kilimo na mifugo, 1997

Malengo: Kuendeleza rasilimali watu na kuanzisha teknolojia mpya kwa ajili ya kuongeza uzalishaji, kukuza matumizi jumuishi na endelevu ya maliasili.

Mikakati: usimamizi wa maliasili, utafiti wa kilimo na mafunzo.

Kuhamasisha vyanzo mbadala vya nishati badala ya kuni,

• Kuendeleza vyanzo vya nishati mbadala ya kuni.

• Uhifadhi endelevu wa maeneo nyeti ya maji kwa kulinda mtiririko wa maji kwa kwa mabwawa yaliyopendekezwa kwa ajili ya kuzalisha umeme.

[URT (2010): pp83]

• Kuongeza matumizi bora ya majani kwa kuhamasisha matumizi ya teknolojia bora, chaguzi na mazoea katika teknolojia za mapishi na ukaushaji katika taasisi (kama vile shule, makampuni madogo, ya kati na makubwa ya biashara kama vile chai, tumbaku na hospitali,)

• Kushughurikia kwa haraka teknologia mahsusi za utengenezaji mkaa

• Kudhibiti uzalishaji na uuzaji wa kuni na mkaa kwa kupitia mipango ya kutoa motisha kwa jamii

Sera ya Mifugo, 2006

Mkakati: Kulinda na kusimamia ardhi ya misitu

• Kuboresha mifumo ya kilimo iliyopo (kwa kusaidia ubunifu mpya wa kilimo na upandaji sahihi wa mazao),

• Kuongeza uwezo wa rasilimali watu (kupitia ujenzi wa shule husika za wakulima)

• Kuhimiza mifumo ikolojia ya kilimo ambayo uboresha rutuba ya udongo,uzalishaji na ulinzi wa mazao.

• Kupanua kilimo cha biashara kwa njia ya kutetea sera bora za serikali katika uzalishaji wa nishati ya mazao (Biofuel)

• Kuongeza ufahamu juu ya masuala ya umiliki wa ardhi,

• kuimarisha mfumo wa uwekaji alama za kijani pamoja na kusaidia uandaaji wa miongozo ya uwekezaji

• Kuboresha masuala ya utawala wa misitu, upandaji miti na shughuli za misitu, kuendeleza kilimo cha mseto pamoja na mpango wa afya ya wanyama (endapo kikomo cha uwezo wa mazingira kitazingatiwa, ufugaji wa mifugo unaweza kuwa chanzo aminifu cha mapato na kupunguza shinikizo kwenye rasilimali za misitu)

[URT (2010): uk 72-85]

Dira ya Maendeleo ya Tanzania (Tanzania Development Vision) 2025

Usimamizi endelevu wa maliasili kuhusiana na mifugo (usimamizi wa ardhi ya misitu)

Page 5: Kilimo, Usalama wa Chakula, na MKUHUMI katika Afrika ... maswala ya usalama wa chakula (kama inavyoonekana katika Jedwali 2). Kutoka jedwali hii, ni wazi kwamba vipaumbele vya sekta

5

kilimo (ikiwa ni pamoja na mifumo ya upandaji, misitu na nishati) ubunifu na njia nyingine kadri zinavoendelezwa.

• Sera za kilimo za taifa zinapaswa kuangaliwa upya na kurekebishwa ili kuepusha migongano, kutambua fursa na uhusiano uliyopo kati ya MKUHUMI, nishati, maji na elimu kwa kushughulikia udhaifu uliopo katika taasisi, utawala bora pamoja na mapungufu mengine. Hii itatoa mwongozi bora katika huduma za ugani na ushauri kwa nchi za Afrika Mashariki, pamoja na kwa wafanyakazi wa huduma ya maendeleo ya jamii katika kubuni miradi ambayo inaweza kushughulikia changamoto husika kwa mapana zaidi badala ya mtazamo finyu (ambao unalenga kilimo tu).

• Pia kutokana na uzoefu katika shughuli za R-PP, MKUHUMI inatakiwa kuanzisha au kuboresha mijadala ili kuzalisha mawazo na majadiliano ya kuzuia migogoro na kuhakikisha umiliki wa miradi itokanayo na maendeleo ya kilimo.Mijadala hii inaweza kujumuisha mashauriano ya mara kwa mara, majadiliano na utaratibu wa maoni / tathmini, kutayarisha na kupitia sera (kwa mfano katikamasuala nyeti ya umiliki na usimamizi wa ardhi, thamani-ya-fedha katika miradi ya kilimo, mifano bora kwa ajili ya kuunganisha wakulima wazalishaji na wasindikaji, nk ). Yote haya yanaweza kuwezesha asasi za kiraia, wafuatiliaji, vyombo vya habari pamoja mashirika ya kijamii na watu asilia kuchangia katika maendeleo ya vijijini ili kuhakikisha matumizi

Malengo ya Taifa ya kilimo Mikakati ya MKUHUMI iliyopendekezwa Nini zaidi kiongezwe ili kusudi MKUHUMI ichangie zaidi katika kufanikisha malengo ya sekta ya kilimo?

Uganda

Mkakati wa Taifa wa Maendeleo ya Sekta ya Kilimo na Mpango wa Uwekezaji, 2010/11 - 2014/15

• Kuongeza uzalishaji kwa njia ya usimamizi endelevu ya ardhi,

• Kuanzisha mifumo ya kilimo inayofaa pamoja na mfumo wa sera ya wazi na yenye kutabirika

• kuboresha elimu ya umma kuhusu masuala ya maliasili.

• Kutathmini madhara ya mifugo kwenye misitu na kwenye mikakati ya maendeleo na usimamizi wa mapori.

• Kuongeza upandaji miti mashambani ili kuwezesha biashara ya na masoko ya Kaboni kwa wamiliki binafsi wa ardhi.

• Kuongeza uzalishaji wa ardhi kwa kila kitengo cha eneo la ardhi.

• ufafanuzi wa haki na umiliki wa ardhi, upanuaji wa kilimo na uchanganuzi wa gharama na faida ya kubadilisha ardhi kwa kwa ajili ya kilimo dhidi ya kuacha ardhi ikiwa na misitu yake asilia.

[Gou (2011): uk 87-88]

• Kuongeza miradi ambayo inaweza kupunguza madhara ya mifugo juu kwenye rasilimali za misitu, kwa mfano mabwawa, visima na chemichemi zilizohifadhiwa.

• Kuongeza uduma za ugani na ushauri wa kilimo ambazo usisitiza juu ya ubunifu katika kilimo mseto, teknolojia na mazoezi.

Sera ya Ardhi ya Uganda, 2011

Malengo: kuoanisha hakimiliki zote za ardhi na sera na sheria.

Kusaidia matumizi endelevu, hifadhi na usimamizi wa mazingira na maliasili.

Sera ya Taifa ya Misitu ya Uganda, 2001

Taarifa namba 6 ya Sera: Miti ya mashambani

• Kujenga uwezo wa wakulima kuchanganya misitu katika mifumo yote ya kilimo.

• Kujenga ufahamu juu ya umiliki wa miti iliyopandwa ili kutoa motisha na ulinzi kwa watu binafsi kujihusisha na uoteshaji miti mashambani.

• Kuingiza kilimo cha mseto katika mitaala ya shule na ile ya watu wazima pamoja na majarida mbalimbali ya elimu.

• Kuongeza miti ambayo inafaa katika maeneo fulani fulani ya kilimo, na pia kulingana na matakwa ya wakulima. Kwa mfano Prosopsis spp – ambazo ni asilia katika ASALs na ambazo uthibiti madhara ya ukame na njaa kwa kuhakikisha utoaji mbao (kwa mfano kuni na mkaa bora) na bidhaa nyingine nyingi ambazo sio mbao (Boabab, 2011)

Chanzo: Umoja wa Mataifa: Jumuiya ya Afrika Mashariki (2010a)

Page 6: Kilimo, Usalama wa Chakula, na MKUHUMI katika Afrika ... maswala ya usalama wa chakula (kama inavyoonekana katika Jedwali 2). Kutoka jedwali hii, ni wazi kwamba vipaumbele vya sekta

KWA TAARIFA ZAIDI KUHUSU REDD-NET TEMBELEA : WWW.REDD-NET.ORG

endelevu ya maliasili wakati pia ikichangia kuboresha maisha ya jamii husika.

• Kuna haja ya kuoanisha sera na sheria katika kilimo, rasilimali za maji, nishati na sekta nyinginezoili kwendana na MKUHUMI kwa ajili ya kuzia mipango inayokinzana. Kwa sababu ya matarajio katikaukuaji wa kiuchumi na ongezeko la idadi ya watu, utenganishaji wa kilimo na sekta nyingine unaweza kuleta utata zaidi kwa mamlaka husika, hali ambayo inaweza kuathiri uendelevu wa ardhi, maji, misitu na rasilimali nyingine.

mareJeleo yaliyotaJwa pamoJa na vyanzo zaidi vya taarifa

Boabab (2011). Miti na Kilimo: Mwelekeo wa Mradi- Prosopsis. Jarida juu ya maendeleo katika maeneo kame na kilimo endelevu. Jarida namba 62, Juni 2011

GoK (2004). Rasimu ya Sera ya Taifa kwa ajili ya maendeleo endelevu ya Ardhi kame na maeneo nusu jangwa ya Kenya (Desemba 2004)

GoK (2005a). Ardhi Nusu jangwa na Majangwa (ASALs). Dira na Mkakati wa Taifa - Usimamizi wa Maliasili (2005-2015): www.aridland.go.ke/NRM_Strategy/natural_resource_management_2005-2015.pdf kupatikana Oktoba 2011

GoK (2010c). Mapendekezo yaliyoboreshwa juu ya Utiyari wa MKUHUMI kwa Kenya.www.forestcarbonpartnership.org/fcp/sites/forestcarbonpartnership.org/files/Documents/PDF/Oct2010/Revised 20RPP% 20for%% 20Kenya.pdf, Tovuti hii ilitembelewa Juni 2011

J. E.O Ongwae (2005). ‘Mkakati wa Kuamsha kilimo (SRA). Namna ya Kenya ya kuelekea Mtizamo wa Sekta nzima’. Mawasilisho ya Serikali yaKenya yaliyotolewa katika Jukwaa la 9 la Afrika, Ougadougou, Septemba, 2005

Oxfam (2006). Jarida la taarifa namba 88. Mawakilisho ya agenda juu ya kutoendelea kwa muda mrefu kwa ardhi kame nchini Kenya: www.oxfam.org.uk/resources/policy/trade/downloads/bp88_kenya.pdf, Tovuti hii ilitembelewa Septemba 2011

Jumuiya ya Afrika Mashariki (2002). Mkataba wa Kuanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki, Uliosainiwa tarehe 30 Novemba,1999.

Jumuiya ya Afrika Mashariki (2010a). Mpango Kazi wa Usalama wa Chakula katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (2010 - 2015)

Jumuiya ya Afrika Mashariki (2010b). Report ya Ukweli na takwimu kuhusu jumuiya ya Afrika Mashariki: www.eac.int/statistics/index.php?option=com_docman&task=doc_view&gid=131&tmpl=component & format = ghafi & Itemid = 153, Tovuti hii imetembelewatarehe 4 Julai 2011

FEWSNET (2011). Dokezo la Usalama wa Chakula kwa Afrika ya Mashariki: www.foodsecurityportal.org/fews-net-releases-food-security-alert-east-africa-0, Tovuti hii imetembelewatarehe 16,Julai 2011

GoU (2001). Sera ya Misitu ya Uganda, 2001. Wizara ya Maji, Ardhi na Mazingira

GoU (2010). Mkakati wa Taifa wa Maendeleo ya Sekta ya Kilimo na Mpango wa Uwekezaji, 2010/11 - 2014/15

GoU (2011a). Pendekezo la Utayari wa MKUHUMIwa Uganda lililowasilishwa katika Mfuko wa Ushirika wa Kaboni RPP% 20May% 2031% 2C% 20% 202011_0.pdf, Tovuti hii ilitembelewa Juni 2011.

GoU (2011b). Sera ya Taifa ya Ardhi,Uganda, 2011. Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Mijini,

Jengo la Century, Kitalu No 13/15,Mtaa wa Bunge, Kampala, Uganda.

Kimbowa R, Mwayafu M.D., & Kairu G. (2011). MKUHUMI na Sekta nyingine katika Afrika Mashariki. Chapisho la REDD-net

URT (1997). Sera ya Kilimo ya Tanzania,1997. Wizara ya Kilimo na vyama vya ushirika, Dar es Salaam Tanzania

URT (2006). Sera ya Mifugo ya Tanzania, 2006. Wizara ya Maendeleo ya Mifugo: www.mifugo.go.tz / documents_storage / l% 20Livetock% 20Policy.pdf%, Tovuti imetembelwa Septemba 2011.

URT (2010). Mkakati wa Kupunguza Uzalishaji wa Hewa Ukaa kutokana na Ukataji Miti na Uharibifu wa misitu (MKUHUMI+): Mpango wa MKUHUMI Tanzania: www.reddtz.org/content/view/22/26/, Tovuti imetembelewa Juni 10, 2011

URT(Haina Tarehe). Dira ya Maendeleo Tanzania 2025: www.tanzania.go.tz / vision.htm, Tovuti imetembelewa Oktoba 2011

KUHUSU REDD-NET

REDD-net ni jukwaa la maarifa la kimataifa kwa mashirika ya kiraia kusini mwa dunia ambalo huyawezesha kupata habari kuhusu juhudi za Upunguzaji wa Uzalishaji wa hewa ya ukaa kutokana na Ukataji na Uharibifu wa Misitu (MKUHUMI+), na pia kupata fursa ya kubadilishana uzoefu wao wenyewe na kusaidiana kuandaa miradi na sera za kutekeleza miradi ya MKUHUMI+ ambayo inawelenga zaidi maskini. Jukwaa hili la REDD-net ni ushirikiano kati ya mashirika ya Centro Agrononómico Tropical de Investigación y Enseóanza (CATIE), Overseas Development Institute (ODI), RECOFTC - The Center for People and Forest na Uganda Coalition for Sustainable Development (UCSD). REDD-net inafadhiliwa serikali ya Norway yaani ‘Norad’.

Kwa habari zaidi kuhusu mradi huu wasiliana Kristy Graham wa ODI kupitia barua pepe (k.graham @ odi.org.uk). Kwa habari zaidi juu ya REDD-net Afrika Mashariki tafadhali wasiliana na David Mwayafu wa UCSD kupitia barua pepe ([email protected]).