kuchambua fonolojia na mofolojia ya kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi...

98
Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili KIT 05104 -MODULE E L I M U H A I N A M W I S H O T A A S I S I Y A E L I M U Y A W A T U W A Z I M A U Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Idara ya Elimu ya Watu Wazima na Mafunzo Endelevu Stashahada ya Elimu ya Watu Wazima na Mafunzo Endelevu – Kwa Masafa

Upload: others

Post on 09-Jan-2020

129 views

Category:

Documents


5 download

TRANSCRIPT

Page 1: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili

KIT 05104

-MODULE

ELIMU HAINA MWISHO

TA

ASI

SI Y

A ELIMU YA WATU WAZIM

A

U

Taasisi ya Elimu ya Watu WazimaIdara ya Elimu ya Watu Wazima na Mafunzo EndelevuStashahada ya Elimu ya Watu Wazima na Mafunzo Endelevu – Kwa Masafa

Page 2: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

MODULI

Kuchambua Fonolojia na Moforojia ya Kiswahili

KIT 05104

Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima

Stashahada ya Elimu ya Watu Wazima na Mafunzo Endelevu kwa Masafa

Page 3: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili
Page 4: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

Hakimiliki Haki zote zimehifadhiwa. Hairuhusiwi kuzalisha, kunakili, wala kusambaza sehemu yoyote ya kazi hii kwa namna yoyote isipokuwa kwa kunukuu matini fupifupi zinazoweza kutumika kwa ajili ya utafiti na mapitio ya maandiko, bila kibali cha maandishi kutoka Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima.

© Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, 2014

Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Stashahada ya Elimu ya Watu Wazima na Mafunzo Endelevu kwa Masafa

S. L. B. 20679 Dar es Salaam,

Mtaa wa Bibi Titi Mohamed Tanzania

Nukushi: +255 22 2150836 Barua-pepe: [email protected]

Tovuti: www. iae.ac.tz

Page 5: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili
Page 6: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

Shukrani Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, Dkt. Fidelis M. S. Mafumiko anapenda kutoa shukurani za dhati kwa watu mbalimbali ambao wamechangia kwa namna moja au nyingine katika kukamilisha kazi hii. Wafuatao ambao ni wafanyakazi wa TEWW wanastahili kutajwa kipekee kwa kuongoza mchakato huu hadi kukamilika kwake.

A. Lekule: Mkuu, Idara ya Elimu ya Watu Wazima na Mafunzi Endelevu

T. Mamba: Mratibu wa kozi

E. Kileo: Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (Mwandishi)

R. Chuachua: Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (Mpitiaji)

E. Samba: Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (Mhariri)

R. Maganga Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (Msanifu)

Page 7: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

ii Yaliyomo

Yaliyomo Kuhusu moduli hii 1  

Muundo wa moduli hii ...................................................................................................... 1  

Maelezo ya jumla kuhusu moduli 3  Karibu katika moduli hii ................................................................................................... 3  Umahiri wa Jumla ............................................................................................................. 3  Mbinu za usomaji .............................................................................................................. 3  Je, unahitaji msaada? ........................................................................................................ 5  Mazoezi ............................................................................................................................. 5  

Namna ya kutumia moduli hii 6  Ishara za pambizo ............................................................................................................. 6  

Somo la Kwanza 7  Kufafanua Dhana ya Lugha na Sarufi ............................................................................... 7  

Utangulizi ................................................................................................................ 7  Matokeo ................................................................................................................... 7  Dhana ya Lugha na sarufi ya Kiswahili Sanifu ....................................................... 7  

Dhana ya Lugha ............................................................................................. 7  Muhtasari wa Somo ........................................................................................................ 16  Zoezi la Somo ................................................................................................................. 16  

Somo la Pili 17  Fonetiki ........................................................................................................................... 17  

Utangulizi .............................................................................................................. 17  Matokeo ................................................................................................................. 17  Kufafanua Fonetiki ya Kiswahili Sanifu ............................................................... 17  

Maana ya Dhana za Msingi za Kifonetiki .................................................... 17  Fonetiki ................................................................................................ 17  

Matawi ya Fonetiki ...................................................................................... 18  Fonetiki Masikizi ................................................................................. 18  Fonetiki Akustika ................................................................................ 19  Fonetiki Matamshi ............................................................................... 20  

Ala za Matamshi .......................................................................................... 20  Uainishaji wa Konsonanti kwa kigezo Mahali pa matamshi /Ala za sauti ........... 22  Jinsi ya Matamshi Konsonanti na Irabu ................................................................ 27  

Page 8: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

Muhtasari wa Somo ........................................................................................................ 41  Zoezi la Somo ................................................................................................................. 41  

Somo la Tatu 42  Fonolojia ya Kiswahili .................................................................................................... 42  

Utangulizi .............................................................................................................. 42  Matokeo ................................................................................................................. 42  Maana ya Dhana za Msingi za Kifonolojia ........................................................... 42  

Dhana ya Fonolojia ...................................................................................... 42  Muhtasari wa Somo ........................................................................................................ 54  Zoezi la Somo ................................................................................................................. 55  

Somo la Nne 56  Mofolojia ya Kiswahili Sanifu ........................................................................................ 56  

Utangulizi .............................................................................................................. 56  Matokeo ................................................................................................................. 56  Fasili ya dhana za Msingi za Kimofolojia ............................................................. 56  

Dhana ya Mofolojia ..................................................................................... 56  Muhtasari wa Somo ........................................................................................................ 86  Zoezi la Somo ................................................................................................................. 86  

Marejeleo 87  

Page 9: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili
Page 10: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

1

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

Kuhusu moduli hii Moduli hii imetayarishwa na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima. Moduli zote zilizotayarishwa na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima zina muundo sawa, kama ilivyoelezwa hapa chini.

Muundo wa moduli hii Maelezo ya jumla kuhusu moduli

Maelezo ya jumla kuhusu moduli hutoa utangulizi wa jumla wa moduli. Habari zinazopatikana katika maelezo ya jumla kuhusu moduli zitakusaidia kuamua: § Kama moduli hii inakufaa. § Kitu gani unatarajia kujifunza? § Muda utakaohitaji ili kukamilisha moduli. Maelezo haya ya jumla pia hutoa mwongozo juu ya: § Mbinu za usomaji. § Mahali pa kupata msaada. § Mazoezi ya nyumbani na tathmini. § Ishara za vitendo mbalimbali. § Masomo.

Tunatilia mkazo ushauri kwamba usome maelezo ya jumla kuhusu moduli kwa makini kabla ya kuanza masomo yako.

Yaliyomo kwenye moduli Moduli hii imegawanywa katika masomo. Kila somo lina: § Utangulizi wa yaliyomo kwenye moduli. § Matokeo ya somo. § Istilahi mpya. § Maudhui ya kimsingi ya somo pamoja na mazoezi mbalimbali

ya kusoma. § Mazoezi ya nyumbani na/au tathmini, kama inavyohitajika.

Page 11: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

Kuhusu moduli hii Error! No text of specified style in document.

2

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

Marejeleo Kwa wale wanaopenda kujifunza mengi juu ya mada hii, tunawapa orodha ya marejeleo ya ziada mwishoni mwa Moduli hii; haya yanaweza kuwa vitabu, makala au tovuti.

Maoni yako Baada ya kukamilisha Moduli ya Kiswahili Ufahamu na Utumizi wa Lugha tutashukuru ikiwa utatenga muda mfupi kutupa maoni yako kuhusu kipengele cho chote cha moduli hii. Maoni yako yanaweza kuhusu: § Yaliyomo kwenye moduli na muundo wake. § Makala za kusoma kwa moduli na marejeleo mengine. § Mazoezi ya nyumbani ya moduli. § Tathmini za moduli. § Muda wa moduli. § Usaidizi katika moduli (wahadhiri waliosimamia moduli,

usaidizi wa kiufundi, n.k.) Ukitoa maoni mwafaka utatusaidia kuboresha moduli hii.

Page 12: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

3

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

Maelezo ya jumla kuhusu moduli Karibu katika moduli hii

Mpendwa mwanachuo, moduli hii inahusu Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili. Imegawanyika katika mada nne ambazo ni: ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili Sanifu. Katika mada ya kwanza, utajifunza dhana ya lugha, sarufi na uhusiano uliopo kati ya tanzu za sarufi. Katika mada ya pili, utajifunza kuhusu fonetiki ya Kiwashili sanifu ambapo utajifunza kuhusu istilahi au dhana za msingi zinazohusiana na Fonetiki. Katika mada ya tatu utajifunza kuhusu ufafanuzi wa kina wa Fonolojia ya Kiswahili na istilahi ambazo zinahusiana na fonolojia ya Kiswahili sanifu. Katika mada ya nne, utajifunza kuhusu mofolojia ya Kiswahili sanifu na dhana mbalimbali ambazo zinahusiana nayo. Kila mada ina kazi na mazoezi ya kutosha yatakayokufanya uelewe vizuri yaliyomo kwenye moduli hii nzima. Moduli hii imeandaliwa kwa ajili ya wanafunzi wa Stashahada kwa Njia Huria na Masafa katika Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima. Imeandaliwa kama mwongozo na rejea kwa wanafunzi wa Stashahada. Ni matumaini yetu kuwa mwongozo huu utakusaidia kujifunza kozi hii. Tunakutakia masomo mema!

Umahiri wa Jumla

Baada ya kukamilisha somo hili utaweza kuchambua na kutumia kanuni mbalimbali za kimofolojia na kifonolojia katika muktadha wa lugha ya Kiswahili.

Mbinu za usomaji

Kwa kuwa wewe ni mwanafunzi wa Elimu Masafa na Ana kwa Ana, utaratibu wako wa kusoma utakuwa tofauti na ule ulioutumia ulipokuwa bado shuleni: utachagua unachotaka kusoma, utakuwa na motisha ya kitaalamu na/au ya kibinafsi inayokusukuma, na bila shaka utakuwa ukiratibu shughuli zako za kiusomaji huku ukizingatia majukumu yako mengine ya kitaalamu au kinyumbani.

Page 13: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

Maelezo ya jumla kuhusu moduli Error! No text of specified style in document.

4

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

Kimsingi, utakuwa unayadhibiti mazingira yako ya masomo. Kwa hivyo, utahitajika kufikiria juu ya maswala ya utendaji yanayohusiana na udhibiti wa wakati, kuweka malengo, udhibiti wa shinikizo, n.k. Pengine utahitaji kujizoesha tena katika maeneo kama upangaji wa insha, namna ya kuimudu mitihani, na kutumia mtandao kama marejeleo ya ujifunzaji.

Mambo utakayozingatia sana ni muda na nafasi, yaani muda unaotenga kwa masomo yako na mazingira unamosomea.

Tunapendekeza kwamba uchukue nafasi hii – kabla ya kuanza kujisomea kibinafsi – kujifahamisha mambo haya. Kuna marejeleo mengi mazuri kwenye mtandao. Viungo vichache vinavyopendekezwa ni:

§ http://www.how-to-study.com/

Tovuti ya “How to study” yaani “Jinsi ya kusoma” imetengwa mahsusi kwa ajili ya marejeleo ya mbinu za usomaji. Utapata viungo kuhusu kujitayarisha kusoma (orodha ya mambo tisa muhimu kuhusu mahali pazuri pa kusomea), kuandika kumbukumbu, mikakati ya kusoma vitabu vya kiada, kutumia vyanzo vya kumbukumbu, dukuduku la mitihani. § http://www.ucc.vt.edu/stdysk/stdyhlp.html Hii ni tovuti ya Kitengo cha Maswala ya Wanafunzi, Virginia Tech. Utapata viungo vya namna ya kupanga muda wako (ikiwa ni pamoja na kiungo cha “wakati huenda wapi?”), orodha-kaguzi ya mbinu za usomaji, mbinu za kimsingi za kumakinikia jambo, udhibiti wa mazingira ya kusomea, kuandika kumbukumbu, namna ya kusoma insha kwa kusudi la kuchanganua, mbinu za kukumbuka. § http://www.howtostudy.org/resources.php Hii ni tovuti nyingine ya “jinsi ya kusoma” iliyo na viungo muhimu kuhusu udhibiti wa wakati, kusoma kwa ufanisi, mbinu za kusaili/kusikiliza/kuchunguza, kufaidi kutokana na kutenda (ujifunzaji wa kiutendaji), kukuza kukumbuka, vidokezo vya namna ya kudumisha motisha, kukuza mpango wa ujifunzaji. Viungo vilivyo hapo juu ni mapendekezo yetu ya kukuwezesha kuanza. Wakati tulipoandika, viungo vya tovuti hizi vilikuwa vinatumika. Ikiwa unataka kupata tovuti zaidi, nenda kwa www.google.com kisha upige taipu na kutafuata “self-study basics” (misingi ya usomi wa kibinafsi), “self-study tips” (vidokezo vya usomi wa kibinafsi), “self-study skills” (mbinu za usomi wa kibinafsi) au tovuti nyingine zenye mada kama hizo.

Page 14: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

5

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

Je, unahitaji msaada?

Ndugu mwanafunzi, katika mchakato wako wa kujifunza, unaweza kuhitaji msaada kuhusu mambo mbalimbali, kwa mfano, mahali unapoweza kupata msaada na namna ya kupata msaada huo. Pamoja na hayo, unaweza kuhitaji ufafanuzi kuhusu moduli unazosoma. Hivyo basi, unashauriwa kuomba ufafanuzi wa yote hayo kwa mratibu wa kituo chako au mwezeshaji wako. Pia, unaweza kufungua tovuti ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima yenye anwani hii: www.iae.ac.tz au piga simu hii +255 22 2150836.

Mazoezi

Baada ya kila somo, unahitajika kujibu maswali ya zoezi la somo. Majibu ya zoezi hili la kila somo hautayawasilisha kwa mwezeshaji wako, ni kwa ajili ya kufanya tafakuri ya ulichojifunza. Pia, utapewa majaribio na mazoezi ambayo utayafanya na kuyawasilisha kama utakavyoongozwa na mwezeshaji wako. Pamoja na hayo, utatakiwa kufanya mitihani ya dhihaki/utamirifu kwa ajili ya upimaji wa maendeleo yako ya kitaaluma.

Page 15: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

Namna ya kutumia moduli hii Error! No text of specified style in document.

6

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

Namna ya kutumia moduli hii Ishara za pambizo

Wakati ukijifunza moduli hii utagundua kwamba kuna matumizi mengi ya ishara za pambizo. Ishara hizi zina jukumu la kushiria aina fulani ya matini, kazi mpya au kubadilika kwa zoezi. Zimetumiwa ili kukuongoza ujue namna ya kuitumia moduli hii.

Seti nzima ya ishara imetolewa hapa chini. Tunapendekeza kuwa ujizoeze ishara hizi na maana yaka kabla ya kuanza masomo yako.

Zoezi Tathmini Zoezi la Mada Kisa Mafunzo

Mjadala Zoezi la Kikundi Usaidizi Kumbuka!

Matokeo Kusoma Tafakari Mbinu za Usomaji

Muhtasari Istilahi Muda Kidokezi

Page 16: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

7

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

Somo la Kwanza Kufafanua Dhana ya Lugha na Sarufi

Utangulizi Katika mada hii utajifunza dhana ya lugha na sarufi na kuonyesha uhusiano uliopo katika tanzu za sarufi. Katika kujadili dhana ya lugha utapitia mitazamo mbalimbali wa wataalamu wa lugha na kuangalia uhusiano uliopo kati ya tanzu mbalimbali za sarufi. Tunaamini kuwa baada ya kujifunza mada hii, utaweza kuyafikia matokeao mahususi ya kujifunza yaliyokusudiwa katika mada hii. Ndugu mwanafunzi karibu katika mada hii.

Matokeo

Baada ya kukamilisha somo hili utaweza: § Kueleza dhana ya Lugha; § kufafanua dhana ya sarufi; na § Kuonyesha uhusiano uliopo miongoni mwa tanzu mbalimbali

za Sarufi.

Dhana ya Lugha na sarufi ya Kiswahili Sanifu

Dhana ya Lugha

Dhana ya Lugha imejadiliwa na wanaisimu mbalimbali. Massamba na wenzake (1999), Nkwera (1979), na Trugil (1974) wanafasili lugha kuwa ni mfumo wa sauti za nasibu ambazo hutumiwa na jamii fulani yenye utamaduni wake kwa ajili ya mawasiliano. Sauti hizo lazima ziweze za kutamkwa.

Mtaalamu mwingine ni Sapir (1921) anayefasili lugha kama mfumo ambao mwanadamu hujifunza ili autumie kuwasilishia mawazo, maono, na mahitaji. Mfumo huu hutumia ishara ambazo hutolewa kwa hiari.

Page 17: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

Somo la Kwanza Error! No text of specified style in document.

8

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

Weber (1985) anasema kuwa lugha ni mfumo wa mawasiliano ya mwanadamu ambao hutumia mpangilio maalumu wa sauti kuunda vipashio vikubwa zaidi, kwa mfano, mofimu, maneno, na sentensi.

Kwa mujibu wa TUKI (1990), lugha ni mfumo wa sauti zina zinazotumiwa na watu wa jamii fulani wenye utamaduni unaofanana ili kuwasiliana. Vilevile, TUKI (1981:145) wanafasiri lugha kama mpangilio wa sauti na maneno unaoleta maana; na ambao hutumiwa na watu wa taifa au kabila fulani kwa ajili ya kuwasiliana.

Ndugu mwanachuo, kwa jumla, tunaweza kusema kuwa, lugha ni mfumo wa sauti za nasibu zenye kubeba maana; na ambazo hutumia mpangilio maalum ili kuunda vipashio vikubwa zaidi kama maneno na sentensi ili viweze kutumika katika mawasiliano ya mwanadamu.

1.1.2 Sifa za Lugha

(i) Lugha ni mfumo

Wazo hili la mfumo katika lugha lilielezwa na mwaasisi wa Isimu- muundo wa Kiswisi, Fedinand De Saussure (1857-1913). Yeye alitofautisha mfumo lugha na utendaji. Katika maelezo yake alieleza ya kuwa, lugha ni mfumo, kwa sababu hujengwa na vipashio mbalimbali vinavyohusiana. Mfumo huu hutumiwa na jamii fulani katika mawasiliano.

(ii) Sauti za Lugha ni Nasibu

Wazo la unasibu katika lugha lilianzishwa na mwanaisimu Ferdinand de Saussure wakati alipozungumzia ishara za kiisimu. Ishara hizo ni muungano wa mambo mawili ambayo ni: Kiashiria ambacho ni umbo la kusemwa na kuandika ambalo huwakilisha dhana au kiashiriwa. Kwa mfano, neno KITI ni kiashiria au kitaja wakati ‘kifaa cha kukalia’ ni dhana au kiashiriwa. Kwa mujibu wa Trudgil (1980), sauti za nasibu ni zile ambazo hutumika katika mawasiliano ya wanadamu. Wanaisimu wengi hadi leo hawajapata ushahidi wa kutosha kudhihirisha kuwapo kwa mfumo wa mawasiliano kwa viumbe wengine wasiokuwa binadamu.

(iii) Lugha Ina Maana Mahususi

Lugha lazima iwe na maana mahususi na hii hutokana na jinsi sauti zinavyopangwa kwa utaratibu unaokubalika katika jamii

Page 18: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

9

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

fulani, maana yake bila shaka hueleweka na watumiaji wake. Mpangilio huu huwa katika kiwango cha sauti, maumbo ya maneno, miundo ya tungo na maana.

(iv) Lugha ni Mali Binadamu

Lugha inamhusu binadamu na imekubalika kuwa chombo maalum kinachotumiwa na binadamu kwa madhumuni ya mawasiliano.

(v) Lugha Hujizalisha na Hunyambulishwa

Lugha hujizalisha na hunyambulishwa ili kupata maneno mapya, hukopa maneno kutoka lugha nyingine ili kujiongezea misamiati kwa minajili ya kukidhi haja ya mawasiliano.

(vii) Lugha ni utoshelezi

Kila lugha hujitosheleza kulingana na mahitaji ya jamii inaiyotumia. Hii ina maana kuwa hakuna lugha bora kuliko lugha nyingine. Vilevile, hakuna lugha dhaifu kuliko lugha nyingine.

1.1.3 Umuhimu wa Lugha

(i) Lugha ni Chombo cha Mawasiliano

Wanaisimu husisitiza kuwa, lengo mahususi la lugha yoyote huwa ni kusaidia watu kuwasiliana. Kwa vile, binadamu hutembeleana ni lazima wawasiliane. Kwa hiyo, ndiyo maana binadamu wana lugha kama chombo muhimu cha mawasiliano yao. Tutoe tahadhari hapa ya kuwa viumbe huwasiliana kwa njia mbalimbali, yaani lugha si njia pekee ya mawasiliano ya wanadamu na viumbe wengine. Zipo njia nyingine za mawasiliano, hivyo, si kila mawasiliano ni lugha.

(ii)Lugha ni Chombo cha Kuendeleza Mahusiano katika Jamii

Watu wanapoongea lugha moja huweza kuwasiliana. Hali hii hubainisha maelewano baina ya watu hao. Hali hii huleta mshikamano na mahusiano mema katika jamii.

(iii) Lugha ni Kitambulisho

Lugha ni kitambulisho cha jamii, mtu binafsi, au kundi la watu. Lugha hutumika kama kielelezo cha kuelezea hulka ya mtu, watu au jamii nzima. Binadamu ana uhuru wa kuchagua namna na kile anachotaka kusema. Hivyo basi, lugha inatumika kama chombo cha

Page 19: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

Somo la Kwanza Error! No text of specified style in document.

10

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

kujieleza kwa kutumia njia mbalimbali. Vilevile, lugha hutumiwa kuwatambulisha watu wa jamii fulani kutokana na lafudhi yao.

(iv) Hifadhi ya Utamaduni na jamii

Lugha ni chombo mwafaka cha kueneza na kuhifadhi amali na utamaduni wa jamii.

(v) Chombo cha Fikra

Utafiti umebainisha kuwa, kwa kiasi fulani, lugha ndiyo humwezesha mtu kufikiria. Pale ambapo mtu huwa amezama katika tafakari, bila kufahamu kufahamu huanza kuyatamka yanayopita akilini. Katika hali kama hii, lugha huonekana kusaidia kufanya tafakuri hiyo. Zipo nadharia kadhaa zinazodhihirisha hili, kwa mfano, nadharia tete ya Sapir na Whorf inayosisitiza jambo hili. Nadhari hii inaonyesha kuwa lugha humsaidia binadamu kuutafakari na kuujengea maana ulimwengu uliomzunguka.

1.1.4 Nadharia za Asili ya Lugha

Kabla hatuangalia nadharia za asili za lugha ya binadamu, hebu kwanza tuangalie asili ya lugha ya binadamu. Lugha asilia ni lugha inayohusu lugha inayotumiwa na binadamu katika mawasiliano yao kwa njia ya sauti zinazounda maneno.

Asili ya lugha ya binadamu

Kuna mitazamo mbalimbali ambayo inafafanua nadharia za lugha. Hata hivyo mitazamo hiyo imejengeka kwa masikio tu, kisa na maana na hakuna nadharia ambayo inaweza kuthibitisha asili na chimbuko la lugha ya binadamu. Kwa mafanno hakuna nadharia inayoeleza kwa ithibati za kuaminika kuwa lugha ya kwanza ya binadamu ilikuwa ipi. Ili tuweze kuelewa asili ya lugha, Ili hebu tuangalie nadharia za asili za lugha: Lugha asilia kama sauti asilia, lugha lugha kama ishara, lugha kama sauti za nasibu. Matinde (2012: 7-11), anaanisha nadharia za asili za lugha kama ifauatavyo:

(i) Nadharia ya Sauti asilia

Mtazamo au nadharia hii inadai kuwa lugha ya binadamu inatokana na sauti asilia ambapo maneno ya mwanzo aliyoyatamka binadamu yalitokana nay eye kuiga sauti mbalimbali alizosikia katika mazingira yake. Sauti asilia ni sauti ambazo zinatokana na milio ya

Page 20: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

11

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

wanyama, ndege, wadudu ambao wanapatikana katika mazingira wnayoishi binadamuLugha asilia ni lugha inayotumiwa katika mawasiliano ya binadamu. Kwa mfano, mlio wa mbwa, bow – bow.

(ii) Nadharia za Sauti na ishara za mwili

Hii ni lugha ianyotumiwa kwa mawasiliano ya binadamu lakini haitumii sauti bali hutumia ishara. Ndhari hii hudai kuwa sauti za lugha zimetokana na mwitikio wa binadamu kwa vichocheo mbalimbali vilivyotokana na mazingira ambamo waliishi. Nadharia hii hushikilia kuwa binadamu alitumia ishara na miondoko ya mwili kuwa siliana na wenzake. Watu walitumia ishara za uso, mwili na mikono. Hata hivyo ishara hizo hazingeweza kutumika gizani bali zilihitaji kuwa na mbinu nyingine mpya ili kuwezesha mawasiliano. Mfumo waliouvumbua ni ule wa kuambatanisha ishara na maneno fulani (ishara za mdomo) ambazo kwa njia moja ziliakisi au zilioana na mazingira husika kwa kutumia sauti na maneno yenye maana fulani.

(iii) Nadharia ya Lugha kama mfumo wa sauti za nasibu

Lugha ni muungano wa mambo mawili ambayo ni: Kiashiria ambacho ni umbo la fulani la kusemwacho na kiashirii ambacho huandika na huwakilisha dhana. Kwa mujibu wa Trudgil (1980), sauti za nasibu ni zile ambazo hutumika katika mawasiliano ya wanadamu. Wanaisimu wengi hadi leo hawajapata ushahidi wa kutosha kudhihirisha ya kuwa hata viumbe wengine hai wanao mfumo wa mawasiliano ambao hutumia ishara za sauti.

1.2 Dhana ya Sarufi ya Kiswahili

Sarufi au isimu ni mtaala ambao huchunguza lugha kama chombo cha mawasiliano ya mwanadamu. Kuna matawi makuu mawili ya sarufi ambayo ni sarufi mapokeo na sarufi mamboleo.

1.3 Uhusiano wa Lugha na Sarufi ya Kiswahili

Sarufi/ isimu ya lugha imegawanyika katika tanzu kuu nne ambazo ni fonolojia, mofolojia, sintaksia na semantiki. Licha ya kuwa na mgawanyiko huo, kwa hakika, katika matumizi halisi ya lugha,

Page 21: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

Somo la Kwanza Error! No text of specified style in document.

12

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

hakuna mipaka bainifu baina ya vitengo hivyo kwa kuwa vitengo hivi havifanyi kazi kipekee au kiutengano. Hii ina maana kuwa vitengo hivi hutegemeana, huathiriana na kukamilishana. Kanuni zinazotawala kitengo kimoja zinaweza kutegemea, kuathiri au kuathiriwa na zile za kitengo kingine. Hivyo, katika mhadhara huu tutachunguza uhusiano uliopo baina ya vitengo hivyo huku msisitizo ukiwekwa katika uhusiano wa fonolojia, mofolojia na vitengo vingine yaani sintaksia na semantiki. Hususani, tutaangalia uhusiano uliopo kati ya fonolojia na mofolojia na fonolojia na sintaksia, sintaksia na mofolojia, na sintaksia na semantiki.

1.4 Tanzu Mbalimbali za Sarufi

Sarufi ya Kiswahili ina matawi makuu manne ambayo ni fonolojia, mofolojia, Sintaksia na Semantiki. Fonolojia ina kitawi kidogo ndani yake ambacho hujulikana kama Fonetiki. Huwezi kujifunza fonolojia ya lugha yoyote ile bila kujua fonetiki ya lugha hiyo husika.

Fonolojia ni tawi la isimu/sarufi ambalo linajishighulisha na na vipengele kama mfuatano wa sauti katika kuunda silabi, mfuatano wa sauti katika kuunda mofimu na mfuatano wa mofimu katika kuunda maneno.

Mofolojia ni tawi la isimu/sarufi ambalo linajishughulisha na muundo nwa maneno katika lugha fulani.

Sintaksia ni tawi la isimu/sarufi ambalo hujishughulisha na mpangilio na muundo wa vipashio katika tungo ilihali fonolojia inashughulika na sauti. Sintaksia inajishughulisha na mpangilio na muundo wa vipashio.

Semantiki ni tawi la isimu/sarufi ambalo linajishughulisha na maana ya kipashio cha msingi cha kinachojuleksimu.

1.5 Uhusiano Uliopo katika Tanzu za Sarufi /Isimu

Uhusiano uliopo kati ya Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili

Massamba na wenzake (2004:14) wanaeleza kuwa, kuna uhusiano wa moja kwa moja baina ya mofolojia na na uundaji wa maneno katika lugha yoyote iwayo. Katika taaluma ya isimu kuna, tawi linaloshughulikia/ lijishuhulishalo na uchunguzi, uchambuzi na

Page 22: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

13

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

uanishaji wa maneno katika lugha hujulikana kama mofolojia. Fonolojia ni tawi la isimu linaloshughulikia uchunguzi, uchambuzi na uanishaji na uanishaji wa sauti pambanuzi ambazo hutumika katika mifumo mbalimbali ya sauti za lugha za binadamu. Fonolojia hujishughulisha na sautu zinazotumika katika kutofautisha maana za maneno katika lugha mahususi. Fonolojia hujishughlisha na vipengele kama mfuatano wa sauti katika kuunda silabi, mfuatano wa sauti katika kuunda mofimu na mfuatano wa mofimu katika kuunda maneno. Uundaji huu wa sauti mpaka kufikia mofimu na maneno ndiyo unaonyesha uhusiano wa karibu kati ya fonolojia na mofolojia ya Kiswahili.

1.6 Namna Tanzu za Sarufi Zinavyokamilishana

Kwa upande wa mofolojia, maneno huundwa na mofimu na mofimu huundwa na na sauti. Uundaji wa mofimu hufauata utaratibu maalum za mfuatano wa sauti za lugha husika. Kwa hiyo basi kutokana na uhusiano mkubwa uliopo kati ya fonolojia na mofolojia ya Kiswahili, vitu hivi viwili haviwezi kujadiliwa katikam upeke wake bali lazima vifuatane kwani vinategemeana sana. Huwezi ukajifunza mofolojia kabla hujapata uelewa wa kutosha kuhusiana na fonolojia ambayo inajadili lugha katika kiwango cha sauti halafu mofolojia inafuatia ambayo huzungumzia lugha katika kiwango cha maneno.

Kwa ujumla uhisiano wa tanzu za isimu unaweza kuelezwa kama ifuatavyo: Ili kujifunza lugha yoyote ile inabidi kuanza na sauti uchunguzi wa sauti za lugha hiyo ambazo huchunguzwa chini ya mchakato wa kifonolojia. Ukishafahamu sauti za lugha husika inabidi uchunguze mchakato unaotumika katika kuunda maneno ya lugha husika ambao hujulikana kama mofolojia.

Ukishafahamu mchakato wa uundaji wa maneno katika lugha inabidi ujue mpangilio wa maneno hayo katika tungo zenye maana. Mchakato unaoshughulikia mpangilio wa maneno katika tungo na kazi za maneno hayo katika lugha husika hujulikana kama sintaksia. Baada ya kujua mpangilio wa maneno katika tungo na kazi za maneno hayo inabidi kujua maana za maneno katika tungo hizo. Kwa hiyo basi mchakato unaohusiana na maana katika lugha hujulikana kama semantiki. Katika suala la maana ya maneno na tungo mbalimbali kunahitajika kujua maana mbalimbali za maneno kulingana na muktadha, kwa hiyo tanzu ya sarufi inayoshughulikia maana kulingana na muktadha inajulikana kama pragmatiki, lakini tawi hili ni sehemu ya semantiki kwa sababu yote mawili

Page 23: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

Somo la Kwanza Error! No text of specified style in document.

14

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

yanashughulikia maana katika lugha na si miongoni mwa tanzu kuu za isimu au sarufi. Tanzu hizi za isimu zinaweza kupangwa kama ifauatavyo kwa kufuata mtiririko:

1.6.1 Uhusiano kati ya Sintaksia na Fonolojia

Katika lugha, baadhi ya kanuni za kifonolojia zinategemea taarifa fulanifulani za kisintaksia ili ziweze kufanya kazi. Kwa mfano, wakati tunazungumzia kategoria za kileksika, kanuni ya uwekaji wa shadda katika maneno huhitaji taarifa za kikategoria. Ili shadda iweze kuwekwa, mzungumzaji inabidi ajue neno analoshughulika nalo ni la kategoria gani. Matumizi ya kiimbo/ mkazo. Kwa mfano matumizi ya mkazo katika neno hudokeza kuwa neno hilo lipo katika kategoria ipi.

Tofauti kati ya Sintaksia na Fonolojia

Sintaksia inahusika na mpangilio na muundo wa vipashio katika tungo ilihali fonolojia inashughulika na sauti. Kipashio cha msingi cha sintaksia ni neno wakati kipashio cha kidogo kabisa cha fonolojia ni fonimu.

1.6.2 Uhusiano kati ya Sintaksia na Mofolojia

Sintaksia na mofolojia vinafungamana katika uundaji wa maneno ambapo sintaksia hufuata mpangilio wa mofimu ili kuuunda maneno hadi sentensi.Kwa mfano:

Mofimu: A-na-ye-ni-pend-a ambayo inawakilisha - Nfs, Nj, Mtd, Mtdw, Mz, Ii katiaka sintaksia

1 2 3 4 5 6

Aidha sintaksia hutegemea vipengele vya mofolojia kama vile umoja na wingi ili kukamilisha mpangilio na muundo wa sentensi. Kwa mfano:

1 /i/ Kitabu cha mtoto wa balozi kimeibiwa

/ii/ Vitabu vya watoto wa balozi vimeibiwa

Ukichunguza kwa makini mifano hiyo utaona kuwa majina ya umoja na wingi yanatawala vipashio vingine katika sentensi hizo yaani majina hayo yana vipashio vinavyobadilika kutegemeana na jina lililotangulia. Hivyo mofimu za umoja na wingi zinaathiri

Page 24: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

15

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

umbo linalofuata jina na kuathiri muundo wa sentensi nzima kwa ujumla.

Tofauti kati ya Sintaksia na Mofolojia

Sintaksia inachunguza mpangilio na mahusiano ya vipashio katika tungo wakati mofolojia huchunguza maumbo ya maneno na miundo yake. Kipashio cha sintaksia ni neno ilihali mofolojia ni mofimu.

1.6.3 Uhusiano kati ya Sintaksia na Semantiki

Kategoria za maneno katika sintaksia zimeainishwa kwa misingi ya maana. Kwa mfano Nomino ni neno linalotaja mtu, kitu au mahali. Aidha katika sarufi mapokeo sentensi inafasiliwa kuwa ni kifungu chenye maana kamilifu.

Aidha, sintaksia na semantiki vinakamilishana kwa maana kwamba mpangilio wa maneno wa tungo au sentensi unaongozwa na nduni za kisemantiki kama vile uhusiano wa kimlalo na kiwima. Kwa mfano:

/i/ Mkono wangu umevunjika

/ii/ Taa yenye mwanga imezimika

Maneno katika sentensi (i) na ya (ii) maneno yamepangiliwa kwa kuzingatia mahusiano ya kiwima na kimlalo, hali inayozifanya sentensi hizo zibebe maana fulani. Hata hivyo, mpangilio wa maneno katika sentensi usipozingatia sifa za kisemantiki basi ni dhahiri kuwa sentensi hizo zitakosa maana. Hivyo sintaksia haiwezi kupangilia vipashio katika tungo pasipo kuzingatia maana kwani maana ndiyo hudokeza usahihi na utosahihi wa miundo ya kisintaksia.

Tofauti kati ya Sintaksia na Semantiki

Sintaksia inajishughulisha na mpangilio na muundo wa vipashio wakati semantiki inahusika na maana Kipashio cha msingi cha sintaksia ni neno ilihali semantiki ni leksimu.

Page 25: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

Somo la Kwanza Error! No text of specified style in document.

16

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

Muhtasari wa Somo

Katika sura hii tumejifunza kufafanua dhana ya lugha na sarufi na kuonyesha uhusiano uliopo katika tanzu za sarufi. Katika kujadili dhana ya lugha tumeona mitazamo mbalimbali ya wataalamu kuhusiana na dhana hiyo. Pia tumejifunza sifa mbalimbali za lugha pamoja na uhusiano uliopo kati ya tanzu mbalimbali za fasihi. Sasa basi hebu chukua kalamu yako na daftari ufanye zoezi fupi ili kupima uelewa wako katika yale yaliyojadiliwaa hapo juu.

Zoezi la Somo

1. Katika fasili zilizotolewa na wataalam mbalimbali kuhusiana na dhana ya lugha, tumeona ya kuwa kuna mambo kadhaa yanayotiliwa mkazo katika kueleza dhana nzima lugha. Onesha mambo hayo na kuyatolea maelezo mafupi.

2. Kwa kurejelea lugha ya Kiswahil onesha sifa za lugha kwa kutoa mifano ya kimatumizi.

3. Toa maelezo mafupi kuhusiana na dhana ya Lugha kama ishara.

4. Nini maana ya sauti nasibu kwa kuzingatia maana halisi ya lugha?

5. Nini tofauti ya lugha asilia na lugha unde?

6. Taaluma zote za isimu hutegemeana na hukamilishana. Jadili kwa kuonyesha uhusiano mkubwa uliopo kati ya tanzu hizo.

Page 26: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

17

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

Somo la Pili Fonetiki

Utangulizi Ndugu mwanachuo, katika mada iliyopita, tumejifunza kuhusu dhana ya lugha, dhana ya sarufi ya Kiswahili na uhusiano uliopo katika tanzu za sarufi ya Kiswahili sanifu. Katika mada hii tutaangalia vipengele vya msingi vinavyohusiana na fonetiki ya Kiswahili. Ni dhahiri kuwa fonolojia na Fonetiki ni matawi ya isimu yanayojishughulisha na jinsi sauti zinavyotolewa na ala za binadamu kwa kupitia katika ala za sauti/matamshi na mikondo hewa (uzalishaji wa sauti). Vipengele vitakavyojadiliwa katika fonetiki ni dhana ya fonetiki ya Kiswahili, matawi ya fonetiki, tofauti kati ya fonetiki na fonolojia ya Kiswahili, kubainisha fonimu ya lugha ya Kiswahili, kuonyesha sifa bainifu za fonimu, kubainisha mahali pa matamshi na kufafanua jinsi matamshi yanavyotokea na mkondo wa hewa. Ndugu mwanafunzi karibu katika sura hii ili uweze kujifunza mambo mbalimbali yanahusiana na fonetiki ya Kiswahili sanifu.

Matokeo

Baada ya kukamilisha somo hili utaweza: § § §

Kufafanua Fonetiki ya Kiswahili Sanifu

Maana ya Dhana za Msingi za Kifonetiki

Fonetiki

Fonetiki ni nini? Asili ya neno hili ni neno la kigiriki “phonetica” ambalo limeundwa na maneno mawili “phone” (sauti) na “tica” (uchunguzi). Fonetiki kwa hiyo ni taaluma ya isimu inayochunguza

Page 27: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

Somo la Pili Error! No text of specified style in document.

18

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

(sauti zote zinazotamkwa na binadamu ambazo hazihusishwi na lugha maalum) “foni”. Fonetiki hushughulikia uchambuzi na uchunguzi wa taratibu zote zinazohusiana na utoaji, utamkaji, usafirishaji, usikiaji na ufasili wa sauti za mwanadamu.

Kwa mujibu wa Hyman (1975) fonetiki ni taaluma ambayo hususani huchungza sauti ambazo hutumiwa na wanadamu wakati wanapowasiliana kwa kutumia lugha. Uchunguzi wa kifonetiki huwa hauhusishwi na lugha yoyote maalum (Mgullu 1999: Massamba na wenzake (2004:5) na Besha (1994:18).

Foni

Kutokana na hali hiyo kipashio ambacho hutumiwa katika uchambuzi wa kifonetiki ni foni. Hyman anaeleza kuwa, foni ni kipande kidogo kabisa cha sauti kinachohusishwa na lugha yoyote. Kwa maana hiyo foni ni istilahi ambayo hutumiwa kuzielezea sauti za lugha ambazo hazimo katika lugha yoyote mahususi. Foni ni kipashio cha kifonetiki na si kipashio cha kifonolojia. Sauti zinapofafanuliwa katika kiwango cha fonetiki huitwa foni (Mgullu 1999). Baada ya kujadili dhana mbalimbali za msingi zinazohusiana na fonetiki ya Kiswahili, sasa tuangalie maeneo mengine ya msingi yanahusiana na fonetiki kama ifauatavyo:

Matawi ya Fonetiki

Fonetiki ni taaluma pana na inayo matawi kadhaa. Miongoni mwa matawi hayo ni pamoja na:

1. Fonetiki Akustika (Acoustic Phonetics)

2. Fonetiki Masikizi (Auditory Phonetics)

3. Fonetiki Majaribio (Experimental Phonetics)

4. Fonetiki Matamshi (Articulatory Phonetics)

Fonetiki Masikizi

Kwa mujibu wa Gimson (1980), fonetiki masikizi ni tawi la fonetiki ambalo hushughulika na kuchunguza jinsi ambavyo sauti hupekelewa katika sikio la msikilizaji na jinsi sauti hizo

Page 28: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

19

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

zinavyofasiriwa au kupewa maana baada ya kupelekwa kwenye ubongo au. Kwa maneno mengine tunaweza kusema kuwa, fonetiki masikizi inashughulikia kwanza kupokelewa kwa sauti, na pili kusafirihswa kwa sauti hizo hadi ubongoni na tatu namna sauti hizo zinavyofasiriwa, yaani kupewa maana.

Fonetiki Akustika

Kwa mujibu wa Lyons (1968), fonetiki ni tawi linguine la fonetiki ambalo hususani huchunguza na kueleza sifa za sauti kama zilivyo baada ya kutamkwa na mzungumzaji na kabla ya kuingia masikioni mwa msikilizaji. Tunaweza kusema kuwa hizo sifa za sauti wakati zinapokuwa katika safari yao kutoka kwa Yule anyezitamka hadi kwa Yule anayezisikia. Sauti zinaweza kusafiri kwa njia mbalimbali, kwa mfano hewani, kwenye vimiminika au hata kwenye vitu yabisi. Baadhi ya sifa za kiakustika mbazo huchunguzwa ni pamoja na: (1) Kidatu (2) Kasi mawimbi na (3) Tambo

(i) Kidatu

Ni kiwango cha msikiko wa sauti katika usemaji. Hubainishwa kwa kupanda au kushuka kwa kiwango cha sauti. Ni utamkaji wa sauti ktk kiwango cha juu cha kati au cha chini.Kidatu huwa na uamilifu wa kudokeza maana ya msemaji, hasa kwa msikilizaji. Mfano; iwapo msemaji anaongea kwa sauti ya juu inawezekana amekasirika au amechukizwa na hali Fulani katika muktadha husika. Kidatu pia hudhihirisha uana(jinsia) wanawake huzungumza kwa kidatu cha juu ilhaliwanaume huzungumza kwa kidatu cha chini.

(ii) Tambo ni sifa ya kiakustika ambayo wanafonetiki huitumia. Tambo hutumiwa kupima mabadiliko ya msukumo wa hewa ambao hutokana na mawimbi ya sauti. Sauti huwa na msukumo wake wa kawaida lakini wakati mwingine msukumo huo huongezeka/ hupanda au hupungua/ hushuka. Tambo hupimwa kwa kuangalia tofauti kati ya msukumo wa kawaida hadi kwenye kilele cha kule kupanda au kushuka.

Kasimawimbi hii hutumiwa kupima kasi ya mitetemo ya mawimbi ya sauti.

Page 29: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

Somo la Pili Error! No text of specified style in document.

20

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

(iii) Kasimawimbi inaweza kukadiriwa kwa kuhesabu idadi ya mitetemo ya sauti katika nukta moja. Kwa kawaida kasi mawimbi inapokuwa kubwa, kdatu cha sauti hiyo pia hupanda na kasi mawimbi inapokuwa ndogo basi kidatu huwa cha chini. Kwa hiyo tofauti ya kasimawimbi husababisha tofauti ya kidatu.

Fonetiki Matamshi

Ladefoged (1975) anasema kuwa fonetiki matamshi ni tawi la fonetiki ambalo huchunguza na kueleza jinsi mtu anavyozungumzia.Wanafonetiki wamefanikiwa kujenga nadharia zinazotuletea mambo muhimu ambayo hutokea wakati mtu anapoongea. Tawi hili huchunguza mambo muhimu yafuatayo:

(a) Ala za matamshi

(b) Mkondo hewa

(c) Mahali pa kutamkia

(d) Namna ya kutamka

Ala za Matamshi

Sauti za lugha ya mwanadamu hutamkwa pale ambapo viungo mbalimbali vya mwili wa binadamu hukatiza hewa inayoingia na kutoka mapafuni kupitia ama chemba ya pua au chemba ya kinywa. Viungo hivi vya mwili wa binadamu huitwa ala za sauti. Kuna aina mbili za ala za sauti / matamshi ambazo ni ala tuli (viungo visivyosogea) na ala sogezi( viungo vinavyosogea).

Ala tuli ni viungo visivyobadilisha mahala pake pa kawaida ktk mchakato wa utamkaji kama vile: ufizi, kaakaa gumu, kaakaa lani, meno n.k.

Ala sogezi ni viungo vya mwili vinavyosogeasogea wakati wa utamkaji wa sauti za lugha mfano ulimi, midomo, kidakatonge. Kwahiyo ala za sauti ni vile viungo vyote vinavyoshiriki katika utoaji/utamkaji wa sauti za lugha zisemwazo na binadamu.

Kama tulivyoona hapo awali kuwa ala za matamshi huhusisha viungo au sehemu ambazo vitamkwa vya lugha ya Kiswahili

Page 30: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

21

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

Sanifu hutamkiwa. Viungo au sehemu hizo za kinywani hujulikana kama alasauti. Sehemu hizo ni kama ifuatavyo:

1. Midomo (lips)

2. Midomo Meno (labio-dental)

3. Meno ya juu

4. Ufizi

5. Kaakaa gumu

6. Kaakaa laini

7. Koromeo

8. Meno chini

9. Ncha ya Ulimi

10. Shina Ulimi

Vitamkwa hupangwa kulingana na sehemu ya chemba ya kinywa vinapotamkiwa, yaani kama ni mbele au nyuma, katikati au chini ya chemba ya kinywa, au kama ni ulimi umeinuliwa juu kwa kiasi kikubwa, juu kidogo, katikati au umeshushwa chini. Nia yetu katika sehemu hii ndogo ni kuchunguza kila sifa pambanuzi za mahali pa matamshi ili kuonyesha taratibu na vitamkwa vya Kiswahili vinavyohusika.

Ufuatao ni mchoro ambao unaonyesha ala sauti yaani viungo ambavyo vinatumika katika uzalishaji na utoaji wa sauti ya binadamu. Mchoro huu unaonyesha viungo muhimu san katika utoaji wa sauti. Kwa hiyo ndugu mwanafunzi, inabidi uvipitie kwa umakini zaidi ili uweze kuelewa uzalishaji wa sauti hasa suala zima la mahala pa matamshi na jinsi ya matamshi. Hii pia itakuwezesha kuelewa mada yetu ya fonolojia na fonetiki ya Kiswahili.

Page 31: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

Somo la Pili Error! No text of specified style in document.

22

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

Ala za matamshi

Uainishaji wa Konsonanti kwa kigezo Mahali pa matamshi /Ala za sauti Sehemu hizi za kutamkia sauti za Kiswahili kila moja katika upekee wake ni sifa pambanuzi. Sehemu hizi zote kwa pamoja zinaunda sifa bainifu kuu moja inayojulikna kama sifa za mahali pa matamshi. Sifa za mahali pa matamshi zinahusisha pia mahali pa kutamkia irabu na konsonanti za Kiswahili. Kwa kawaida, kila kitamkwa au kiwakilishi chake kama vile alama p, m, au d hupambanuliwa kwa sifa pambanuzi kadhaa. Hii ina maana kuwa kila kitamkwa hujengwa kwa orodha ya sifa za mahala pa matamshi na jinsi ya matamshi zinazohusika.

Katika kiwango hiki tutajihusisha zaidi na mahala pa matamshi na jinsi ya matamshi. Lakini yafaa tugusie tu kwamba zimewahi pia kupendekezwa sifa pambanuzi zingine zilizokitwa katika msingi wa jinsi ya sauti zinavyosafiri kutoka kwa msemaji hadi kwa msikilizaji.

Page 32: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

23

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

Sifa ya Midomo (lips)

Midomo kama sifa ya mahali pa matamshi inahusisha sehemu ya nje ya kinywa. Sehemu hizi hutumiwa kuzuia na kuachia kwa ghafla hewa kinywani. Utaratibu huo wa kutumia midomo kuzuia na kuachia hewa hutoa vitamkwa konsonanti vitatu katika Kiswahili. Vitamkwa konsonanti vinavyotolewa kwa njia hiyo ni /p/, /b/, na /m/. Sifa hii ya midomo inaweza kutumiwa kuvibainisha vitamkwa na vingine ambavyo vinatamkiwa katika sehemu tofauti. Ili kuvibainisha vitamkwa hivi vyenyewe inabidi tutumie pia sifa bainifu za jinsi ya matamshi.

Sifa ya Midomo Meno

Katika Kiswahili, sifa hii inahusisha mdomo wa chini na meno ya juu, ya mbele. Ili kupata vitamkwa husika, mdomo wa chini hugusanisha na meno ya mbele kuzuia mkondohewa kutoka kinywaji kwa kiasi fulani. Uzuiaji huo, kwa kuwa si wa kuzuia kabisa mkondohewa, huruhusu mfululizo kiasi wa hewa katika utokaji wa sauti. Utamkaji hapa huweza huweza pia kuandamana na sifa ghuna au isiyoghuna. Utaratibu huu hutoa vitamkwa na vitamkwa konsonanti viwili tu katika Kiswahili sanifu [f] na [v] ambapo cha kwanza kina sifa isiyoghunwa (voiceless) na cha pili ni sifa ya ghuna (voiced). Vitamkwa hivi hupatikana katika maneno ya Kiswahili Sanifu kama vile fuvu, funga, kufa, ufuta, n.k na vema, mvumo, uvutaji.

Sifa ya meno na ncha ya ulimi

Sifa hii inhusisha meno ya juu, ya mbele na ulimi. Wakati vitamkwa hivi vinapotamkwa ulimi hugusishwa kwenye meno hayo ya mbele na kubana hewa kidogo hewa inayosukumwa taratibu. Kama ilivyokuwa kwa sifa ya upande wa midomo meno katika vitamkwa konsonanti vya Kiswahili vinavyotolewa na sifa hii pia ni viwili ambavyo ni [ð] na [θ]. Vitamkwa hivi vya Kiswahili hutokea tu katika maneno yaliyokopwa kutoka Kiarabu ikiashiria kuwa si vitamkwa asilia vya lugha hiyo. Mfano wa maneno hayo yaliyokopwa kutoka katika lugha ya Kiarabu ni thamani, thawabu, theluji ya kitamkwa [ð] na dhahabu, dharau, au udhi ya kitamkwa [θ].

Page 33: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

Somo la Pili Error! No text of specified style in document.

24

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

Sifa ya Ufizi

Sifa ya ufizi inahusisha ulimi ila katika sifa hii ulimi hugusihwa au hufanywa kukaribia ufizi ambayo ni nyama inayoshikilia meno kinywani. Ulimi unapogusishwa au kufanywa karibu na ulimi hutokea vitamkiwa vya aina mbalimbali kutokana na hewa kuzuiwa na kuachiwa ghafla, hewa hubanwa kidogo na kusukumwa nje taratibu au hewa hupitishwa puani. Mfano wa vitamkwa hivyo ni [t], [d], na [n] Vingine ni [s] na [z] ambavyo hutokana na ulimi kufanywa karibia na ufizi. Vilevile vitamkwa vingine hutokana na ulimi kupigwapigwa na ufizi. Vitamkwa hivi ni [l] na [r] ambavyo hutokana na ulimi kufanywa kukaribia ulimi. Katika Kiswahili Sanifu, hii ndiyo sifa inayotoa vitamkwa vya konsonanti vingi kuliko sifa nyingine yoyote ya mahali pa matamshi. Mfano wa maneno ya Kiswahili Sanifu hizi ni kama vile dada, mada, teta, tatu, nena, ona, zeze, oza, sema, mosi, pale, lala na ruka.

Sifa ya Koromeo

Koromeo ni nafasi uwazi katikati ya nyuzi sauti unaanzia pale kongomeo (kisanduku cha sauti) linapokomea hadi pale chemba cha nyum kinapoanzia. Uwazi huu ni muhimu kwani ndiyo ambao hupokea sauti inapotoka kwenye kisanduku cha sauti. Sifa hii inatoa kitamkwa tu konsonanti moja tu katika Kiswahil ambayo ni [h]. Mifano ya maneno katika Kiswahili sanifu yenye kitamkwa hiki ni hama, hapa, haha.

Sifa ya Kakaa gumu

Sifa hii nayo inahusisha ulimi kugusishwa au kufanywa kukaribia kaakaa gumu. Kaakaa gumu ni sehemu ya juu katika chemba ya kinywa iliyo nyuma ya ufizi. Sifa hii nayo ndiyo inaifuatia ile ya ufizi katika kutoa vitamkwa vingi zaidi vya Kiswahili Kwa mfano, kwa ulimi kugusishwa katika sehemu hii hupatikana vitamkwa vingi zaidi vya Kiswahili. Kwa mfano, kwa ulimi kugusishwa katika sehemu hii yaani kakaa gumu hupatikana vitamkwa konsonanti [ʧ] au[....],[Ɉ],au[......][ϳ],[ɲ],[x]. Katika Kiswahili sanifu vitamkwa hivi hujitokeza katika maneno yafuatayo: cheka, chacha, jana, taja, nyama,, panya, shoka, pasha n.k.

Page 34: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

25

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

Sifa ya Kakaa laini

Midomo/ lipu: Midomo ni miongoni mwa ala sogezi. Katika mchakato wa utamkaji wa sauti midomo miwili wa juu na wa chini hutumika katika utamkaji wa baadhi, mfano [b], [p], [m], [w]. Kwa upande mwingine, mdomo wa chini hushirikiana na meno ya juu ktk utamkaji wa [f] na [v] (midomo meno).

Meno: Meno ni miongoni mwa ala tuli, na vitamkwa vinavyotamkiwa kwenye meno huitwa foni za meno. Wakati wa kutamka foni hizi ulimi huwekwa katikati ya meno ya chini na ya juu na hususan huwa umeyagusa meno ya juu. Foni hizi ni [ð], [θ].

Ufizi: Ufizi ni ala tuli. Wakati wa kutamka foni za ufizi ulimi hugusa ufizi. Mifano ya foni hizi ni[t], [d],[s],[z],[n],[l],na [r]

Kaakaa gumu: Ni miongoni mwa ala tuli, Wakati wa kuzitamka foni za kaakaa gumu sehemu ya kati ya ulimi hugusa kaakaa gumu. Foni za kaakaa gumu ni [ʧ] au[....],[Ɉ],au[......][ϳ],[ɲ],[x].

Kaakaa laini ni miongoni mwa ala tuli. Wakati wa kutamka sauti hizi sehemu ya kati ya ulimi huinuliwa hadi kukaribia kugusa kaakaa laini. Foni za kaakaa laini ni [k],[g],[x] na [ɤ],[ŋ].

Koromeo au glota: Ni uwazi uliopo kati ya nyuzi sauti zilizopo katika kongomeo. Katika lugha ya Kiswahili ni fonimu [h] inayotamkiwa katika koromeo/glota.

Ulimi; Ni miongoni mwa ala sogezi muhimu sana katika mfimo mzima wa uzungumzaji. Ni ala muhimu kuliko ala nyingine kwa sababu mtu akikosa ulimi hawezi kuzungumza kabisa. Ulimi umegawanyika katika sehemu kuu tatu ambazo ni:

i. Sehemu ya mbele

ii. Sehemu ya kati

iii. Sehemu ya kati

Ulimi hushirikiana na ala nyingine za sauti kutamka sauti mbalimbali za lugha. Kwa mfano sehemu ya mbele ya ulimi inajumuisha ncha ya ulimi, husaidia kutamka sauti [n],[t], na [d].Sehemu ya kati ya ulimi ina umuhimu wake, kwani hutumika kutamka vitamkwa [ɲ],[ʧ] n.k.

Page 35: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

Somo la Pili Error! No text of specified style in document.

26

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

Zoezi

1. Bainisha matawi matatu ya fonetiki na kutoa maelezo mafupi.

2. Nini tofauti baina ya fonetiki na fonolojia?

3. Onyesha uhusiano uliopo baina ya fonetiki na fonolojia ya Kiswahili.

4. Uanishaji wa konsonanti na irabu kwa Kigezo cha nyuzi sauti huzingatia vitu viwili vya msingi. Taja vitu hivyo kisha utoe mifano halisi.

5. Uanishaji wa Konsonanti za Kiswahili kwa Kuzingatia Kigezo cha Namna/ Jinsi ya Kutamka hutoa aina hizi za konsonanti kama ifuatavyo:

(i) --------------------------------

(ii) --------------------------------

(iii) --------------------------------

(iv) --------------------------------

(v) --------------------------------

(vi) --------------------------------

6. Kuna vigezo vitatu vinavyotumika katika uanishaji wa Irabu za Kiswahili. Vigezo hivyo ni:

(i)------------------------------------------------

(ii) ----------------------------------------------

(iii)----------------------------------------------

7. Nini tofauti baina ya fonetiki na fonolojia?

8. Onyesha uhusiano uliopo baina ya fonetiki na fonolojia ya Kiswahili.

Page 36: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

27

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

9. Uanishaji wa konsonanti na irabu kwa Kigezo cha nyuzi sauti huzingatia vitu viwili vya msingi. Taja vitu hivyo kisha utoe mifano halisi.

10. Uanishaji wa Konsonanti za Kiswahili kwa Kuzingatia Kigezo cha Namna/ Jinsi ya Kutamka hutoa aina hizi za konsonanti kama ifuatavyo:

(i)--------------------------------

(ii)--------------------------------

(iii)--------------------------------

(iv)--------------------------------

(v)--------------------------------

(vi)--------------------------------

11. Nini tofauti baina ya fonetiki na fonolojia?

12. Onyesha uhusiano uliopo baina ya fonetiki na fonolojia ya Kiswahili.

Jinsi ya Matamshi Konsonanti na Irabu Uainishaji wa Konsonanti na Irabu za Kiswahili kwa kigezo cha Namna au Jinsi ya Matamshi umezungumziwa na wataalamu mbalimbali. Mgullu (1999: 28-29) anaeleza kuwa jinsi / namna foni zinavyotamkwa ni suala la muhimu sana katika taaluma ya fonetiki. Kwa kuzungumzia namna foni zinavyotamkwa, wanafonetiki wameweza kuanisha vitamkwa vyote vya lugha. Mgawanyo mkubwa wa kwanza ni ule unaotenganisha irabu, nusu irabu na konsonanti.

Irabu zote hutamkwa bila hewa kuzuiwa au kubanwa mahali popote na hali hii ni tofauti na namna ambavyo konsonanti hutamkwa kwa sababu konsonanti zote hutamkwa wakati pakiwa na kizuizi au hewa kutatizwa mahali fulani. Kwa maana nyingine zipo nusu irabu na nusu-konsonanti ambazo zipo katikati ya irabu na konsonanti. Namna ya kutamka hutusaidia kuzigawa foni katika konsonanti, nusu-irabu na irabu.

Page 37: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

Somo la Pili Error! No text of specified style in document.

28

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

Jinsi ya matamshi nayo ni mojawapo ya sifa pambanuzi kuu. Sifa pambanuzi hii nayo ina sifa saba zinazotumika kubainisha vitamkwa vya Kiswahili. Sifa hizo saba zilitajwa kuwa ni vipasuo, vizuio-kwamiza, kwamizi, nazali, vitambaza, imadende na viyeyusho. Katika sehemu hii tutaeleza kwa ufupi taratibu na vitamkwa vinavyohusika na kila kimoja ya sifa hizi za jinsi ya matamshi.

Katika kuzungumzia namna ya kutamka, tutaligawa eneo hili katika maeneo mawili. Maeneo haya mawili yatatuwezesha kupata aina kuu za konsonanti na irabu kulingana na jinsi vinavyotamkwa. Maeneo haya ni kama ifauatavyo:

1. Nanma ya kutamka konsonanti

2. Nanma ya kutamka irabu

Katika sehemu hii tutajadili pia aina saba za jinsi ya matamshi ya vitamkwa konsonanti za Kiswahili ambazo ni kipasuo, kizuio-kwamiza, kikwamizi, nazali, kitambaza, kimadende na kiyeyusho. Aina tatu za mwanzo za jinsi ya matamshi na pia huandamana na sifa ya kuwa ghuna au isoghuna.

Uanishaji wa Konsonanti

Konsonanti ni foni ambazo wakati wa kutamka hewa hutatizwa kwa namna fulani. Wakati mwingine hewa huzuiwa kabisa na wakati mwingine hutatizwa kiasi au kubanwa kiasi fulani baada ya kupitia kongomeo.

Mara nyingi konsonanti huwa hazikai kwenye vilele vya silabi kama ilivyo kwenye irabu. Kwa kuzingatia namna konsonanti zinavyotamkwa, konsonanti zimeanishwa katika aina kuu sita yaani: Massamba na wenzake (2006) na Mgullu (1999) wanatoa ufafanuzi wa wa ina hizi za konsonanti kama ifuatavyo:

(i) Vizuiwa / kipasuo (stops/plosive)

(ii) Vikwamizwa (Fricatives)

(iii) Vizuiwa-kwamizwa (Affricates)

(iv) Vitambaza (laterals)

Page 38: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

29

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

(v) Vimadende (trills)

(vi) Nazali (nasals)

(vii) Viyeyusho

(i)Vizuiwa/ Vipasuo

Hizi ni sauti konsonanti ambazo wakati wa utamkaji wake, hewa kutoka mapafuni kupitia chemba ya mdomo hubanwa kabisa na kisha kuachiwa ghafla. Hali hii husababisha utokeaji wa sauti mfano wa mlipuko. Mfano wa sauti hizi ni [p],[b],[t],[d],[k],[g]. Sifa hii inahusika kubanakabisa na kuachia kwa ghafla kwa hewa kutoka mapafuni na vilevile kuwepo au kutokuwepo kwa mirindimo wa nyuzisauti. Ubanaji wa hewa hufanywa na midomo kwa baadhi ya vitamkwa na vilevile ulimi katika ufizi na katika kaakaa laini. Kunapokuwepo kwa mrindimo wa nyuzi sauti vitamkwa vinavyotokea hujulikana kwa lugha ya kitaalamu kama ghuna. Inapokuwa hakuna mrindimo, vitamkwa vinavyopatikana hujulikana kama visoghuna. Sifa hii ya vizuiwa/kipasuo hutoa vitamkwa konsonanti sita katika Kiswahili ambavyo vitatu miongoni mwake ni ghuna (voiced) ambavyo ni [b], [d] na vitatu visoghuna (voiceless) ambavyo ni [p], [t] na [k].

(ii)Vikwamizi / kizuio kwamizi (Fricatives)

Kama jina linavyoonyesha, sifa hii huhusisha kuzuiwa kwa namna ya kukwamizwa kwa hewa na kwa ulimi katika kaakaa gumu. Sauti hizi hutamkwa pale ambapo ala za matamshi huwa zimekaribiana kiasi kwamba hewa kutoka mapafuni inapopita katikati ya ala hizi mkwaruzo husikika. Vikwamizi katika lugha ya Kiswahili ni ambavyo ni [v], [z], [j ], [θ], ambazo ni ghuna na [f],[s] [x], [ð] na [h] ambayo ni kisoghuna.

(iii)Vizuia-kwamizwa (Affricates)

Konsonanti hizi zinapotamkwa hewa husukumwa nje kwa nguvu, huzuiwa halafu nafasi ndogo huachwa ili hewa ipitie ikiwa na mkwaruzo. Kwa maneno mengine, wakati wa kutamka sauti hizi, hewa kutoka mapafuni huzuiwa na kuachiwa kwa kukwamizwa

Page 39: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

Somo la Pili Error! No text of specified style in document.

30

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

kwamizwa katika kaakaa gumu. Sauti za Vizuia kwamizwa katika Kiswahili ni [ʃ] na[ʃ].

(iv)Nazali / ving’ong’o (nasals)

Nazali ni aina za ya konsonanti ambazo hutamkwa kwa kukishusham kimio kwa namna ambayo kiasi kikubwa cha hewa kutoka mapafuni huelekezwa kupitia kwenye chemba ya pua. Wakati wa utamkaji wa sauti hizi, kiasi kikubwa cha hewa kutoka kwenye mapafu huelekezwa kupitia puani (chemba ya pua). Sifa ya nazali kwa upande wake inahusisha uzuiaji wa hewa katika sehemu mbalimbali za chemba ya kinywa na kuiruhusu ipitie katika chemba ya pua. Sifa hii hutoa vitamkwa vya konsonanti vinne katika Kiswahili ambavyo ni [m] inayohusisha hewa kuzuiwa namdomo, [n] inahusisha hewa kuzuiwa kwenye ufizi, [ɲ] inayohusisha hewa kuzuiwa kwenye kaakaa gumu na [ŋ] inayohusisha hewa kuzuiwa kwenye kaakaa laini. Katika lugha ya Kiswahili kuna nazali nne [m], [n] [ɲ], na [ŋ].

(v)Vitambaza (Laterals)

Kitambaza hutamkwa wakati ncha ya ulimi inapogusana na ufizi huku sehemu ya kati ya ulimi imegusa kaakaa gumu na kuacha nafasi ndogo ya hewa kupita ikisababisha mkwaruzo ambao si mkubwa sana. Wakati wa utamkaji wa kitambaza, hewa kusukumwa nje, kuzuiwa na kuruhusiwa kupita pembeni mwa kizuizi ambacho ni ulimi, bila mkwaruzo mkubwa sana.. Kitambaza cha pekee katika Kiswahili ni [l]. Kitamkwa hiki hutolewa kwa ulimi kutandazwa kwenye ufizi na kuachia hewa kupenya pembeni mwa ulimi. Kimsingi kitamkwa kinachotolewa na sifa hii katika Kiswahili Sanifu ni kimoja tu.

(vi)Kimadende (trills)

Kama ilivyokuwa kuhusu sifa iliyotangulia, sifa hii nayo inatoa kitamkwa konsonanti kimoja tu katika Kiswahili ambacho ni [r]. Kitamkwa hicho nacho huhusishwa kupigwapigwa kwa ulimi kwenye ufizi. Kimadende hutamkwa wakati ncha ya ulimi ikiwa inagongagonga kwa haraka kwenye ufizi na sehemu ya nyuma ya ulimi imegusa uvula. Katika lugha ya Kiswahili kuna kimadende kimoja tu ambacho ni [r].

Page 40: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

31

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

Angalizo: Kitambaza na Kimamende kwa jina moja hujulikana kamaVilainisho. Vilainisho ni vitamkwa vifulizwa ambacho hutamkwa kwa kutumia ncha ya ulimi na ufizi kwa kutandaza ulimi na kupitisha hewa pembeni. Katika lugha ya Kiswahili kuna vilainisho viwili yaani [l] na [r]. Hapa tofauti ni sifa iliyotangulia, mapigo hurudiwarudiwa. Hutamkwa ncha ya ulimi ikiwa imegusa ufizi lakini kutokana na nguvu ya hewa inayopita katika kati ya ncha hiyo na ufizi, ncha ya ulimi hupigapiga kwa harakaharaka kwenye ufizi.

(vii)Viyeyusho/ Nusu Irabu

Sifa hii inahusisha midomo kufanywa kukaribiana na kutandazwa au ulimi au ulimi kukaribia kaakaa gumu. Taratibu hizi tatu hutoa vitamkwa viyeyusho [w] na [y] katika Kiswahili. Vitamkwa hivi vinajulikana kama viyeyusho kwa sababu viko katikati ya irabu na konsonanti. Hivi ni vitamkwa ambavyo si konsonanti wala si irabu. Hutamkwa sawa na irabu bila hewa kuzuiwa inapita moja kwa moja kutoka mapafuni.Viyeyusho ni [y] na [w]. Vitamkwa hivi vipo kati ya irabu na konsonanti kwa hiyo vinachukua sifa za pande zote mbili yaani sifa za irabu na konsonanti.

Uanishaji wa Irabu za Kiswahili kwa kigezo cha jinsi/namna ya matamshi

Irabu ziko nyingi sana na kila lugha inayo idadi tofauti. Lugha ya Kiswahili ni miongoni mwa lugha ambazo zinatumia irabu chache sana katika mfumo wake wa sauti. Lugha hii ina irabu 5 tu. Lugha zilizo nyingi zina irabu zaidi ya tano. Tunapoainisha irabu, tunaangalia sifa za irabu hizo. Kuna vigezo vitatu vinavyotumika katika kuziainisha irabu. Vigezo hivyo ni hivi vifuatavyo:

i. Mwinuko ulimi katika kinywa wakati wa utamkaji. Hapa kinachoangaliwa ni kama ulimi umeinuka juu sambamba na paa la kinywa, umeinuka kiasi au upo chini sambamba na sakafu la kinywa wakati wa utamkaji wa irabu hiyo. Kama irabu inatamkwa ulimi ukiwa umeinuliwa juu sambamba na paa la kinywa basi irabu hiyo huitwa ni irabu ya juu na kama irabu inatamkwa ulimi ukiwa umeinuliwa kiasi huitwa irabu za nusu juu na nusu chini na kama irabu inatamkwa ulimi ukiwa umelala chini basi irabu hiyo huitwa ni irabu ya chini. Hata hivyo ni vigumu sana kuweka mipaka kati ya vokali za nusu juu na nusu chini.Mifano ya aina za irabu ktk lg

Page 41: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

Somo la Pili Error! No text of specified style in document.

32

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

ya Kiswahili kwa kuzingatia kigezo hiki ni kama ifuatavyo: Irabu za juu ni /i/ na /u/ na za nusu juu ni /o/ na /e/ , nusu chini ni / / na / / na ya chini ni /a/.

ii. Mkao wa mdomo wakati wa utamkaji

Hapa tunaangalia kama wakati wa kutamka irabu fulani mdomo unakuwa wa mviringo au umekaa bapa/tandazwa. Irabu zinazo tamkwa mdomo ukiwa umeviringwa huitwa irabu viringe na zile zinazotamkwa mdomo ukiwa umetandazwa huitwa irabu mtandazo. Tafiti zilizofanyika hivi karibuni zinaonyesha kuwa irabu zote za nyuma ni irabu mviringo na zile za mbele ni irabu mtandazo au bapa.

iii. Kigezo kingine ni mahali pa kutamkia. Hapa tunaangalia sehemu ya ulimi inayohusika wakati wa kutamka irabu. Sehemu za ulimi zinazohusika na utamkaji wa irabu zimegawanyika katika sehemu tatu ambazo ni, sehemu ya mbele katika bapa pamoja na ncha ya ulimi sambamba na ufizi na meno, sehemu ya kati ni kiwiliwili cha ulimi sambamba na kaakaa gumu na sehemu ya nyuma ya ulimi ni shina. Sauti inayotamkiwa mbele ya ulimi huitwa sauti ya mbele mfano /i/ na /e/, inayotamkiwa kati huitwa ya kati mfano /a/ na inayotamkiwa nyuma huitwa irabu ya nyuma mfano /u/ na /o/.

Kutokana na taaluma ya fonetiki irabu ziko nyingi sana na kila lugha inayo idadi tofauti. Lugha ya Kiswahili ni miongoni mwa lugha ambazo hutumia irabu chache sana katika mfumo sauti wake, yaani ziko irabu tano. Lugha zilizo nyingi zina irabu zaidi ya tano kwa mfano kuna lugha zina irabu saba, nyingine irabu tisa n.k. Wanafonetiki huziwakilisha irabu hizi kwa namnatofauti kwa kila lugha ili kuonesha tofauti na uhusiano uliopo baina yao. Hata hivyo kuna makubaliano ya kutosha kuwa irabu za msingi ziko nane ambazo ni:

i u mwinuko wa juu kabisa

e o mwinuko wa nusu juu

ε ᴐ mwinuko wa nusu chini

a ɑ mwinuko chini kabisa

Page 42: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

33

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

Irabu za Kiswahili sanifu

mbele nyuma

juu i u juu

kati ε ᴐ kati

chini a

Katika taaluma ya isimu irabu hizi zimepewa sifa maalum za kuzibainisha, Sifa hizo ni kama ifuatavyo ni safa bainifu.

[i] [ε] [a] [ᴐ] [u]

+irabu +irabu +irabu +irabu +irabu

+sil +sil +sil +sil +sil

+mbele +mbele +chini +nyuma +nyuma

+juu +kati -viringe +kati +juu

-viringe -viringe +viringe +viringe

Uanishaji wa konsonanti na irabu kwa Kigezo cha nyuzi sauti

Kwa kutumia kigezo cha nyuzi sauti tunapata aina mbili za konsonanti ambazo ni ghuna na si ghuna. Sauti ghuna hutamkwa wakati nyuzi sauti zinapokuwa zinatetema. Sauti guna hupewa sifa hiyo kwa kuwekewa alama ya [+ghuna] na zile ambazo si ghuna huwekewa alama ya [-ghuna]. Sauti ambazo si ghuna wakati wa kuzitamka nyuzi sauti huwa hazitetemi.

Kwa upande wa irabu tunaweza kusema kuwa irabu zote ni [+ghuna] kwa sababu zote hutamkwa wakati nyuzi sauti zinapokuwa zinatetema.

Uanishaji wa Fonimu za Nusu Irabu (Jedwali) Viyeyusho

• Uyeyushaji

Page 43: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

Somo la Pili Error! No text of specified style in document.

34

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

Mchakato huu unahusu badiliko la irabu kuwa kiyeyushi/nusu irabu. Katika Kiswahili irabu ya juu /i/ au /u/ zikifuatanana irabu isiyofanana nayo ktk neno hubadilika na kuwa kiyeyusho. Irabu /u/ hubadilika na kuwa kiyeyusho /w/ na irabu /i/ huwa kiyeyusho /y/. Uyeyushaji unapotokea umbo la nje huwa limepungua silabi moja ukilinganisha na umbo la ndani, hivyo kurahisisha matamshi.

Umbo ndani umbo la nje

/Mu+aka/ mwaka

/Mu+alimu/ mwalimu

/mu+izi/ mwizi

Kanuni: /u/ [w] I ≠ u

/vi+ungu/ vyungu

/vi+akula/ vyakula

/vi+ake/ vyake

Kanuni:/i/ [y] I ≠ i

Ndugu mwanafunzi, baada ya kupitia michakato ya uanishaji wa irabu na konsonanti kwa kigezo cha jinsi ya matamshi, hebu sasa chukua kalamu nyako ufanye zoezi hili fupi lifuatalo:

ZOEZI

1. Uanishaji wa konsonanti na irabu kwa Kigezo cha nyuzi sauti huzingatia vitu viwili vya msingi. Taja vitu hivyo kisha utoe mifano halisi.

2. Uanishaji wa Konsonanti za Kiswahili kwa Kuzingatia Kigezo cha Namna/ Jinsi ya Kutamka hutoa aina hizi za konsonanti kama ifuatavyo:

(i) ------------------------------

(ii) ------------------------------

(iii) -------------------------------

(iv) -------------------------------

Page 44: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

35

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

(v) -------------------------------

(vi) -------------------------------

(vii) -------------------------------

3. Elezea uanishaji wa Irabu za Kiswahili kwa kigezo cha jinsi/namna ya matamshi

4. Kuna vigezo vitatu vinavyotumika katika uanishaji wa Irabu za Kiswahili. Vigezo hivyo ni:

(i)------------------------------------------

(ii) -----------------------------------------

(i) -------------------------------------

5. Mpendwa msomaji, baada ya kupata ufafanuzi kuhusiana na vitamkwa mbalimbali hebu sasa tufanye mazoezi kidogo ya namna ya kutamka ili tuone ni viungo gani vya matamshi vinatumika katika kutoa jozi za vitamkwa vifuatavyo:

(i) [r] na [l]

(ii) [s] na [z]

(iii) [f] na [v]

(iv) [m] na [n]

6. Katika jozi hizo eleza dhana ya ghuna na isiyoghuna kwa kutoa.

7. Nini maana ya sifa pambanuzi? Je Kiswahili kinasifa pambanuzi ngapi? Zitaje?

8. Je tunaposema mahali pa matamshi ni sifa pambanuzi tuna maana gani?

9. Eleza mahali na jinsi ya matamshi ya vitamkwa vifuatavyo:

(a) [j]

(b) [k]

(c) [p]

Page 45: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

Somo la Pili Error! No text of specified style in document.

36

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

(d) [g]

10. Onyesha vitamkwa vinavyobainishwa na sifa za mahali na jinsi za matamshi zifuatazo:

(a) Kipasuo ghuna cha midomo

(b) Kikwamizi ghuna cha ufizi

(c) Nazali za kaakaa gumu

(d) Kitambaza cha ufizi

(e) Kikwamizi kisoghuna cha midomo meno

(f) Kizuio kwamiza cha kaakaa gumu

2.1.6 Mkondo Hewa

Ni njia ambayo hewa hupitia ama kutoka mapafuni kwenda nje au kutoka nje kwenda mapafuni (Massamba 2004). Mkondo hewa ambao husukuma nje sauti huitwa mkondo hewa- nje na ule uingiao ndani huitwa mkondo hewa-ndani. Takriban sauti zote za lugha ya mwanadamu hutamkwa kwa kutumia mkondo hewa nje. Kuna sauti chache sana katika baadhi ya lugha ambazo hutamkwa kwa mkondo hewa –ndani mfano vidoko katika lugha ya kikhosa na kizulu Afrika Kusini. Aina hizi za sauti hutamkwa mithili ya sauti ya mtoto aitoayo akiwa amelia sana.Wakati wa kusema sauti za jinsi hii, hewa huvutwa ndani kwa haraka na kisha husukumwa nje kwa vipimo huku ikiathiriwa na ala sauti na hivyo kusababisha aina mbalimbali za sauti za lugha.

2.1.7 Uainishaji wa Konsonanti Kutoka IPA 2005 (The Internatinal Phonetic Association)

Huu ni mfumo wa kimatamshi wa Alfabeti za Kifonetiki za Kimataifa (AKIKI) ulioundwa na shirika la kifonetiki la kimataifa. Wanafonetiki duniani kote wanakubaliana kuweka alama maalum kwa kila sauti. Shirika hili liliundwa mwaka 1886 likiwa na jina la The Phonetic Teachers Association. Mwaka 1897 jina la shirika hilililibadilishwa na kuitwa The International Phonetic Association-IPA. Kazi yake ilikuwa ni kunukuu sauti za lugha kifonetiki yaani zinavyotamkwa. Hivyo mwaka 1888 orodha ya

Page 46: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

37

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

alfabetiza kifonetiki ilichapishwa. Miongoni mwa utata ulioondolewa na unukuzi huu ni pamoja na kuondoa tatizo la muungano wa herufi zinazowakilisha sauti moja. Mfano tha,nga, nya nk. Hivyo pia mfumo huu unatusaidia kujua tofauti ya kunukuu kifonetiki na kiothografia. Mfano kiotografia neno nyanya kifonetiki hunukuliwa [ɲaɲa]. Mabano mraba kutumika kuonyesha unukuzi wa kifonetiki.

Page 47: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

Somo la Pili Error! No text of specified style in document.

38

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

2.1.8 Sauti za lugha ya Kiswahili kwa mujibu wa IPA (Jedwali la Konsonanti)

Chanzo cha jedwali hili: Mgullu (1999:69) John Habwe na Karanja uk. 37, Massamba (2006:44) na Besha uk. 23.

Midomo Midomo meno Meno Ufizi Kaakaa gumu Kaakaa laini Uvul/ kimio Glota

Vipasuo +ghuna B D G

-ghuna P T K Vipasuo kwamizi +ghuna Ɉ au ǰ

-ghuna ʧ au č Vikwa mizi +ghuna V Ð Z ɤ

-ghuna F Θ S ʃ X H

kitambaza +ghuna L

-ghuna kimadende ghuna R

-ghuna Nazali +ghuna M N ɲ Ŋ

-ghuna Viyeyusho

+ghuna W J

-ghuna

Page 48: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

39

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

2.1.9 Uhusiano baina ya Fonetiki na Fonolojia

• Kama tulivyoona hapo awali kwamba fonetiki na fonolojia ni matawi mawili tofauti lakini yenye kuhusiana kwa karibu sana. Uhusianao wa matawi haya unatokana na ukweli kwamba yote mawili yanajishughulisha na uchunguzi na uchambuzi unaohusu sauti sauti za lugha ya binadamu.

• Fonetiki na fonolojia ni matawi mawili ya isimu yanayotegemeana na kukamilishana. Matawi yote mawili huchunguza sauti za lugha. Fonolojia ni tawi kubwa linaloshughulikia sifa pambanuzi na aina za sauti za binadamu wakati fonetiki ni tawi dogo ambalo hushughulikia uzalishaji wa sauti za binadamu kwa kungalia sehemu husika zinazohusika na uzalishaji na utoaji wa sauti hizo ambazo huhusisha mahali pa matamshi na jinsi ya matamshi. Kwa hiyo hatuwezi kujifunza fonolojia bila kujua fonetiki ya lugha husika yaani sehemu/ viungo vinavyohusika na utoaji na uzalishaji wa sauti hizo. Ndiyo maana tunasema kuwa haya ni matawi ya isimu yanayotegemeana na yanayokamishana.

Tofauti kati ya Fonetiki na Fonolojia

Katika kuangalia tofauti kati ya fonetiki na fonolojia vigezo vifuatavyo vinaweza kutumika: Madhumuni, mawanda na kazi. Kwa kuzingatia vigezo hivyo hapo juu, zifauatazo ni tofauti baina ya fonetiki na fonolojia:

• Katika taaluma ya isimu, fonetiki ni tawi ambalo hujishughulisha na uchunguzi na uchambuzi wa taratibu zote zinazohusiana, utoaji, utamakaji, usafirishaji, usikiaji na ufasili wa sauti za lugha za binadamu kwa jumla.

• Tawi hili huchunguza maumbo mbalimbali ya sauti zinazoweza kutolewa na alasauti na alasauti, namna maumbo hayo yanavyoweza kutolewa, yanavyoweza kumfikia msikilizaji yaani yanavyosikika na yanavyofasiriwa katika ubongo bila kujali kama sauti hizo zinatumika katika lugha gani.

• Fonetiki kama taaluma ya isimu ina matawi yake manne ambayo ni: fonetiki matamshi, fonetiki akustika, fonetiki

Page 49: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

Somo la Pili Error! No text of specified style in document.

40

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

masikizi na fonetiki majaribio wakati fonolojia ina matawi mawili ambayo ni fonolojia vipande na fonolojia arudhi.

• Fonetiki ni taaluma ambayo hususani huchungza sauti ambazo hutumiwa na wanadamu wakati wanapowasiliana kwa kutumia lugha. Uchunguzi wa kifonetiki huwa hauhusishwi na lugha yoyote maalum wakati fonolojia ni tawi la isimu ambalo hushughulikia uchambuzi wa mfumo wa sauti zinazotumiwa katika lugha fulani na uamilifu wao ndani ya mfumo wa lugha inayohusika.

• Fonolojia ni kiwango kimojawapo cha lugha fulani kilicho na vipashio vidogo zaidi kuliko vipashio vingine vyote vya lugha. Vipashio vya kifonolojoia ni fonimu na alofoni zake.

• Seti kuu (fonetiki) haina kikomo lakini fonolojia zote zina kikomo hii ina maana ya kwamba, fonetiki ni seti kuu ya sauti za lugha kwa ujumla lakini fonolojia ya lugha yoyote inakuwa ni sehemu ndogo tu ya hiyo seti kuu.

• Fonetiki huchunguza sauti za lugha bila kujali mfumo zinamotumika, lakini fonolojia huchunguza sauti zilizo katika mfumo mmoja yaani lugha mahsusi. Kwa mantiki hii fonetiki ni moja lakini fonolojia ni nyingi kama zilivyo lugha nyingi.

• Katika fonetiki sauti zote za lugha ya binadamu huorodheshwa na kufafanuliwa kwa sifa bainifu zote za kifonetiki ambazo zinazoitofautisha foni moja na nyingine, lakini katika fonolojia ya lugha fulani ni zile sauti bainifu tu huorodheshwa.

• Katika fonetiki kipashio cha ufafanuzi ni foni (ni kipande kidogo kabisa cha sauti ambacho hakihusishwi na lugha yoyote mahsusi) lakini katika fonolojia kipashio kidogo kabisa cha ufafanuzi ni fonimu.

• Fonolojia hujihusisha na sauti pambanuzi yaani sauti zinazotumika kutofautisha maana za maneno katika lugha mahususi na sheria au kanuni zinazoandamana na utoaji na utumiaji wa sauti hizo pambanuzi wakati fonetiki hujishughulisha na uzalishaji au utoaji wa sauti kwa kutumia ala za matamshi.

Page 50: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

41

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

Muhtasari wa Somo

Ndugu mwanafunzi, baada ya kupitia mada yetu ya fonetiki ya Kiswahili sanifu na vipengele mbalimbali vinayohusiana na fonetiki, tumeona maana ya istilahi za msingi za kifonetiki kama fonetiki na foni. Katika sura hii pia tumeona uhusiano kati ya fonolojia na fonetiki ambapo fonolojia ni tawi kubwa linaloshughulikia uchunguzi, uchambuzi na uanishaji wa sauti pambanuzi na sifa pambanuzi za sauti za binadamu pamoja na sheria au kanuni zinazoandamana na utoaji na utumiaji wa sauti hizo pambanuzi. Wakati fonetiki ni tawi dogo ambalo hushughulikia uzalishaji wa sauti za binadamu kwa kungalia sehemu husika zinazohusika na uzalishaji na utoaji wa sauti hizo ambazo huhusisha mahali pa matamshi na jinsi ya matamshi. Kwa hiyo hatuwezi kujifunza fonolojia bila kujua fonetiki ya lugha husika yaani sehemu/ viungo vinavyohusika na utoaji na uzalishaji wa sauti hizo. Ndiyo maana tunasema kuwa haya ni matawi ya isimu yanayotegemeana na yanayokamilishana. Pia tumeona mahali pa matamshi na jinsi ya matamshi.

Zoezi la Somo

Jjibu maswali yote kwa kuandika ili kujipima uelewa wako, katika mada hii ya utumizi wa lugha.

Page 51: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

Somo la Tatu Error! No text of specified style in document.

42

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

Somo la Tatu Fonolojia ya Kiswahili

Utangulizi Katika sura iliyopita tulijadili dhana za msingi zinazohusiana na fonetiki ya Kiswahili. Dhana hizo ni fonetiki na foni kwa mujibu wa wataalamu mbalimbali. Katika sura hii tutajishughulisha na fonolojia ya Kiswahili ambayo inajihusisha na sifa pambanuzi za sauti, sheria na kanuni zinazoandamana na utoaji na utumiaji wa sauti hizo pambanuzi, sauti na mpangilio wake wa uundaji wa maneno katika lugha mbalimbali. Katika kujadili fonolojia ya Kiswahili, vipengele vifauatavyo vitafafanuliwa kwa ufasaha: dhana ya fonolojia, fonimu, alofoni, vipamba sauti kama vile matamshi. Kiimbo, mkazo, lafudhi, toni, mfuatano wa sauti katika kuunda silabi, mfuatano wa sauti katika kuunda mofimu, mfuatano wa mofimu katia kuunda maneno, sifa pambanuzi za sauti na kuanuni na sheria katika utoaji na uzalishaji wa sauti. Ndugu mwanafunzi karibu katika mada yetu ili uweze kuelewa dhana nzima ya Fonplojia nya Kiswahili Sanifu.

Matokeo

Baada ya kukamilisha somo hili utaweza: § §

Maana ya Dhana za Msingi za Kifonolojia

Dhana ya Fonolojia

Fudge (1973), anafasili fonolojia kama kiwango kimojawapo cha lugha fulani kilicho na vipashio vidogo zaidi kuliko vipashio vingine vyote vya lugha. Vipashio vya kifonolojoia ni fonimu na alofoni zake.

Page 52: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

43

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

TUKI (1990) wanasema kuwa fonolojia ni tawi la isimu ambalo hushughulikia uchambuzi wa mfumo wa sauti zinazotumiwa katika lugha fulani.

Hartman (1972) anafasili fonolojia kama mtaala wa sauti zinazotumiwa katika lugha fulani na uamilifu wao ndani ya mfumo wa lugha inayohusika.

Massamba na wenzake (2004:6) wanafasiri fonolojia kama tawi la isimu ambalo hujishughulisha na uchunguzi na uchambuzi na uanishaji wa sati pambanuzi ambazo hutumika katika mifumo mbalimbali ya sauti za lugha ya binadamu. Hii ina maana kwamba, fonolojia kama tawi la isimu hujishughulisha hasa na zile sauti ambazo hutumika katika kutofautisha maana za maneno katika lugh mahsusi. Aidha kwa kiasi kikubwa, fonolojia hujihusisha na sheria au kanuni zinazoandamana na utoaji na utumiaji wa sauti.

Katika fasili hizi zilizotolewa na wataalam hapo juu, tunaona mambo ya msingi ambayo yanajitokeza. Kwanza kuna fonolojia kama sehemu ya lugha fulani, pili fonolojia ya lugha fulani huwa na fonimu na alofoni zake, tatu ni fonolojia kama taaluma maalum ya isimu ambayo kazi yake ni kuchanbua mfumo wa sauti zinazotumiwa katika lugha fulani na nne ni kigezo cha fonetiki kuchunguza kuchunguza sauti zinazotumiwa katika lugha fulani pamoja na uamilifu wa kila sauti katika mfumo huo.

Tunapozichunguza kwa makini fasili za Fudge (1973), TUKI (1990) na Hartman (1972) na Weber (1985) tunaweza kuhitimisha ya kuwa, fonolojia inapaswa itazamwe kama dhana iliyo na sura tatu:

(1) Fonolojia ya lugha ikiwa ni kiwango kimojawapo cha lugha hiyo ambacho ambacho bila shaka hushirikiana na viwango vya mofolojia, sintaksia, na semantiki ili kujenga lugha hiyo kama ifuatavyo:

(2) Fonolojia kama taaluma mbayo hushughulikia masuala yote yanayohusiana na uchunguzi wa fonolojia za lugha mbalimbali.

(3) Taaluma ambayo hushughulika na kuzibainisha na kuzifafanua sauti bainifu katika lugha fulani (fonimu) kwa kutumia sifa bainifu. Aidha fonolojia hushughulikia;

(a) Kuchunguza uhusiano kati ya neno na neno katika sentensi, yaani jinsi ambavyo ruwaza za sauti huathiriwa na namna yalivyowekwa pamoja.

Page 53: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

Somo la Tatu Error! No text of specified style in document.

44

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

(b) Kuchnguza ruwaza za kiimbo

Kwa kiwango kikubwa Werber na wenzake, wanaiona fonolojia kuwa ni taaluma ambayo ina shughuli kadhaa. Shughuli hizo ni pamoja na:

(i) Kubainisha fonimu za lugha fulani

(ii) Kuzifafanua fonimu hizo kwa kutumia sifa bainifu

(iii) Kuchunguza kuathiriwa kwa rauaza za sauti katika sentensi za lugha fulani

(iv) Kuchinguza ruwaza za kiimbo katika katika lugha fulani

Hapa tunaona kuwa, fonolojia ni taaluma yenye majukumu mengi ya kutimiza.

Baada ya kupitia maana ya dhana ya fonolojia, ni muhimu pia kujua matawi ya fonolojia kwa ufupi. Ufuatao ni ufafanuzi mfupi kuhusiana na matawi ya fonolojia kwa ujumla wake.

Fonolojia

Fonolojia ni nini? Fonolojia/umbo sauti ni tawi la isimu linalojishughulisha na kuchunguza mifumo ya lugha mbalimbali za binadamu. Kila lugha ya binadamu ina mfumo wake. Fonolojia ni tawi la isimu ambalo hujishughulisha na uchunguzi, uchambuzi na uainishaji wa sauti pambanuzi ambazo hutumika katika mifumo mbalimbali ya sauti za lugha ya binadamu. Fonolojia hujihusisha na sauti pambanuzi yaani sauti zinazotumika kutofautisha maana za maneno katika lugha mahususi. Aidha kwa kiasi kikubwa, fonolojia hujihusisha na na sheria au kanuni zinazoandamana na utoaji na utumiaji wa sauti hizo pambanuzi.

Fonolojia hujishughulisha na vipengele mbalimbali ambavyo vinahusiana na sauti na mpangilio wake wa uundaji maneno katika lugha. Vipengele hivyo ni: matamshi, kiimbo, mkazo, lafudhi, toni, mfuatano wa sauti ktk kuunda mofimu, mfuatano wa mofimu katika kuunda mofimu, mfuatano wa mofimu katika kuunda maneno na otografia (Massamba 2012: 6).

Aina za Fonolojia

Page 54: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

45

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

Wanaisimu wamekubaliana kuwa siku hizi kuwa taaluama ya fonolojia inaweza kugawanywa katika aina kuu mbili yaani kama ifuatavyo:

(a) Fonolojia Vipande (Segmental Phonology)

(b) Fonolojia Arudhi (Suprasegmental Phonology)

Fonolojia Vipande (Segmental Phonology)

Hii hushughlikia uchunguzi wa vipande sauti (sound segments) yenyewe. Hapa wanafonolojia hushughulika zaidi na:

2 Kuvibainisha vipande sauti bainifu katika lugha fulani, yaani fonomu na alofoni zake.

3 Kutumia sifa bainifu kuzifafanua fonimu na alofoni hizo.

4 Kueleza jinsi fonimu hizo zinavyoweza kuathiriana katika miktadha mbalimbali yaani katika mikondo ya kifonolojia.

Fonolojia Arudhi (Suprasegmental Phonology)

Katika sehemu iliyopita tumezungumzia fonolojia vipande tukizingatia vipande vidogo vya sauti ambavyo ni fonimu. Katika lugha ya Kiswahili kuna vipashio vingine ambavyo ni vikubwa kuliko fonimu vinavyotumiwa na kubainika kwa sifa za kiarudhi. Vipashio vya kiarudhi vinavyopatikana katika lugha ya Kiswahili ni kiimbo, mkazo, lafudhi, wakaa, kidatu na silabi. Vipashio hivi vyote hujulikana kama vipamba sauti. Fonolojia arudhi kwa upande wake hushughulikia masuala mengine ya sauti ambayo huviathiri vipashio vikubwa zaidi kuliko fonimu moja. Baadhi ya mambo hayo ni:

• Kuchunguza mfumo wa toni: Ni kiwango cha kidatu pamoja na mabadiliko yake.

• Kuchunguza mfumo wa kiimbo: Inahusu umbile la jumla la uzungumzaji wa mtu au kundi fulani

• Kuchunguza muundo wa silabi:

Page 55: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

Somo la Tatu Error! No text of specified style in document.

46

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

• Kuchunguza mfumo wa mkazo katika neno na sentensi: Hii hujihusisha jinsi watu na jinsi watu wanavyotamka maneno kwa nguvu zaidi katika sehemu fulani fulani.

• Kuchunguza mfumo wa Kidatu: Inahusu ukase wa mitetemo ya nyzu sauti

Sifa za Ala za Sauti

Ala za sauti zinaweza kuwa sifa zifuatazo:

(i) Ala sogezi ambazo hujumuisha ala zinasogea katika mchakato wa utamkaji wa sauti.

(ii) Ala tuli ni zile ambazo hazisogei wakati wa utamkaji wa sauti.

Baada ya kuona sifa kuu za ala sauti, hebu sasa tuchambue ala hizo na sauti mbalimbali zitolewzo na viungo vinavyohusiana na utamkaji wa sauti:

(a) Midomo/ lipu: Midomo ni miongoni mwa ala sogezi. Katika mchakato wa utamkaji wa sauti midomo miwili wa juu na wa chini hutumika katika utamkaji wa baadhi, mfano [b], [p], [m], [w]. Kwa upande mwingine, mdomo wa chini hushirikiana na meno ya juu ktk utamkaji wa [f] na [v] (midomo meno).

(b) Meno; Meno ni miongoni mwa ala tuli, na vitamkwa vinavyotamkiwa kwenye meno huitwa foni za meno. Wakati wa kutamka foni hizi ulimi huwekwa katikati ya meno ya chini na ya juu na hususan huwa umeyagusa meno ya juu. Foni hizi ni [ð], [θ].

(c) Ufizi; Ufizi ni ala tuli. Wakati wa kutamka foni za ufizi ulimi hugusa ufizi. Mifano ya foni hizi ni[t], [d],[s],[z],[n],[l],na [r].

(d) Kaakaa gumu; Ni miongoni mwa ala tuli, Wakati wa kuzitamka foni za kaakaa gumu sehemu ya kati ya ulimi hugusa kaakaa gumu. Foni za kaakaa gumu ni [ʧ] au[....],[Ɉ],au[......][ϳ],[ɲ],[x].

(e) Kaakaa laini: Ni miongoni mwa ala tuli. Wakati wa kutamka sauti hizi sehemu ya kati ya ulimi huinuliwa hadi kukaribia kugusa kaakaa laini. Foni za kaakaa laini ni [k],[g],[x] na [ɤ],[ŋ].

Page 56: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

47

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

(f) Koromeo au glota: Ni uwazi uliopo kati ya nyuzi sauti zilizopo katika kongomeo. Katika lugha ya Kiswahili ni fonimu [h] inayotamkiwa katika koromeo/glota.

(g) Ulimi: Ni miongoni mwa ala sogezi muhimu sana katika mfimo mzima wa uzungumzaji. Ni ala muhimu kuliko ala nyingine kwa sababu mtu akikosa ulimi hawezi kuzungumza kabisa. Ulimi umegawanyika katika sehemu kuu tatu.

i. Sehemu ya mbele

ii. Sehemu ya kati

iii. Sehemu ya kati

Ulimi hushirikiana na ala nyingine za sauti kutamka sauti mbalimbali za lugha. Kwa mfano sehemu ya mbele ya ulimi inajumuisha ncha ya ulimi, husaidia kutamka sauti [n],[t], na [d].Sehemu ya kati ya ulimi ina umuhimu wake, kwani hutumika kutamka vitamkwa [ɲ],[ʧ] n.k.

Maana ya Fonimu

Trubetzkoy (1939) anasema kuwa fonimu ni kipashio kidogo kabisa (katika lugha) kilicho na uamilifu wa kutofautisha maana katika sentensi. Kwa maneno mengine, fonimu ni vitamkwa vinavyoweza kujenga maneno yenye maana tofauti au vinavyoweza kubadili maana ya maneno. Fonimu ni dhana iliyokuwa ikishughulikiwa kwa muda marefu sana

Sifa bainifu za Fonimu

Kutokana na mitazamo ya kisaikolojia, kifonolojia na kifonetiki, wanaisimu mbalimbali wamekuja na sifa za jumla za fonimu kama zilivyoonishwa na Mgullu R.S (1999:57):

(i) Kila fonimu ina sifa zake za kifonetiki zinazoweza kuelezwa ili kuifafanua fonimu hiyo.

(ii) Kila fonimu inazo sifa zake za kifonolojia amabzo hunyesha uamlifu wa fomimu hiyo katika lugha maalum.

(iii) Watumiaji wa lugha fulani huzielewa lugha zote zafonimu zalugha yao ikiwa ni sehemu ya umilisi wao wa lugha hiyo.

Page 57: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

Somo la Tatu Error! No text of specified style in document.

48

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

(iv) Kila fonimu hushiriki kujenga na kutofutisha maana katika maneno.

(v) Fonimu moja pekee yake haina maana, yaani si kiashiria cha kuashiriwa chochote.

(vi) Ukibadili fonimu katika neno bila shaka maana ya neno hilo itabadilika au kupotea.

(vii) Ukiongeza fonimu katika neno lolote maana ya neno hilo itabadilika

(viii) Ukiongeza fonimu katika neno lolote, maana ya neno hili itabadilik au kupotea

(ix) Ukipangua mpangilio wa fonimu katika neno maana ya neno hili itabadilika au kupotea,

(x) Kila lugha ina fonimu zake na fonimu ya lugha tofauti hazifanani katika uamilifu wake.

Maana ya Alofoni

Alofoni

Tukiangalia etimolojia ya dhana ya alofoni tutaona kuwa istilahi yenyewe imeundwa kwa kutumia mofu mbili yaani (alo} + {foni}. Hartman (1972) anafasili alofoni kama sauti mojawapo miongoni mwa sauti kadhaa zinazoiwakilisha fonimu moja. Alofoni hutokea katika mazingira mahususi.

Richards na wenzake (1985) wanasema kuwa alofoni ni umbo mojawapo kati ya maumbo tofauti kadhaa ya fonimu fulani. Kwa mfano, katika lugha ya kiingereza, fonimu /p/ hutumiwa bkataika maneno kama /spai/ na /spare/. Lakini wakati /p/ inapokuwa mwanzoni mwa maneno kama katika maneno /put/ na /pair/, basi /p/ hutamkwa ikiwa na mpumuo /ph m/. Maumbo yote mawili yaani /p na ph/, yeneye mpumuo ni alofoni za fonimu moja.

Ladefoged (1962) naye anaeleza kuwa alofoni ni matamshi tofautitofauti ya fonimu moja. Alofoni za fonimu moja huunda kundi moja la sauti ambazo:

(i) Hazibadili maana za maneno

(ii) Hutokea katika mazingira tofautitofauti ya kifonetiki

Page 58: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

49

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

(iii) Alofoni zote hufafana sana kifonetiki

Kutokana na fasili hizo zote hapo juu tuanaweza kuhitimisha ya kuwa alofoni za fonimu moja huwa ni maumbo mbalimbali au matamshi tofauti tofauti ya fomimu moja kutokana na mazingira ya utokeajji. Ingawa matamshi haya huwa yana tofauti ndogo au chache za kifonetiki lakini hayaleti utofauti wowote katika maama za maneno. Aghalabu alofoni hutumiwa katika miktadha au mazingira ya kifonetiki yaliyo tofauti. Kwa mfano:

(i) /Kheri/ na /heri/

Tutaona katika sehemu inayofuata kuwa tofauti kama hizi si tofauti za kimazingira na kwa hiyo hii sifa ya kutobadili maana ni sifa pekee ambayo inafaa itumiwe wakati wa kutambua alofoni na zipi si alofoni. Ni lazima sifa ya mazingira tofauti na kufana kifonetiki zitumiwe sambamba na sifa za kutobadili maana ndipo tuwe na uhakika ya kuwa hizo ni alofoni

Uanishaji wa Sauti/ Matamshi kwa Kigezo cha Vipamba Sauti

Baadhi ya sauti za wanadamu hubainishwa kwa vipashio ambavyo huvuka mipaka ya vipande sauti. Vipashio hivyo ni kama vile toni, lafudhi, mkazo, kidatu, kiimbo mpando shuko na tempo

(i) Sifa ya Mkazo/ shadda

Massamba (2004) anasema mkazo, katika isimu ni utamkaji wa nguvu ambao unaweza kuwekwa kwenye silabi Fulani Fulani katika neno katika neno, au katika maneno Fulani Fulani katika kirai au sentensi. Halliday (1970) mkazo ni hali ya kulitamka neno au silabi Fulani kwa nguvu zaidi kuliko nguvu inayotumika kutamka maneno au silabi zingine. Hivyo kuna aina mbili za mkazo yaani mkazo katika neno na mkazo katika sentensi. Kwa kawaida katika Kiswahili mkazo huwekwa katika silabi ya pili kutoka mwisho.

Mfano: sa′a, mto′to, ufukwe′ni, amebomo′a

Dhima ya kubwa ya mkazo ni kutofautisha homografu. Homografu ni maneno kwa kawaida mawili tofauti yanayoandikwa kwa namna moja lakini yana maana tofauti, hivyo mkazo huwekwa sehemu tofauti ili kutofautisha maana hizo. Kwa mfano,

Page 59: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

Somo la Tatu Error! No text of specified style in document.

50

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

[baraba′ra] –njia kuu na [bara′bara] –sawasawa

[kataka′ta] –fanya kitu kiwe vipande na [ka′takata]-kabisa kabisa

[wa′takakazi]- wewe unahitaji kazi na [watakaka′zi]-watu wanaotafuta kazi

Hivyo taaluma ya Fonetiki inasaidia kupambanua jozi hizo kwa kutumia alama maalum (′) kuonyesha sifa ya mkazo.

(ii) Toni

Toni ni sifa inayowakilisha kiwango pambanuzi cha kidatu cha silabi katika neno au sentensi ambayo huweza kubadilisha maana ya neno au sentensi hiyo kisemantiki au kisarufi.Toni huweza kuwa za juu, ya kati, ya chini, ya kupanda na ya kuteremka. Alama zitumikazo kuonyesha toni ni kama:

1. [á] toni juu

2. [à] toni ya chini

3. [â] toni ya kuteremka

4. [ǎ] toni ya kupanda

5. [ā] toni ya kati

Umuhimu wa toni ni kutofautisha maana za maneno kwa lugha zenye toni mfano kisukuma.

Kapela [kâpɛɛla] Pera dogo

Kapela [ka:pɛέlá] kamekimbia

(iii) Lafudhi

Ni sifa ya kimasikizi (inayohusiana na kusikika kwa sauti ya msemaji wakati wa kutamka) ya kimatamshi ya mtu binafsi ambayo humpa msemaji utambulisho Fulani ama kijamii au kieneo (kijiografia). Hivyo lafudhi hutokana na athari za mazingira ya mtu kijamii au kijiografia. Mfano;

Page 60: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

51

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

Usirete matata= msemaji kutoka mara

Nchicha na nkate= msemaji ametoka mtwara

Amekuya kutumika fasi ya mwl mkuu

Pesa sangu = kichaga

(iv) Kidatu

Ni kiwango cha msikiko wa sauti katika usemaji. Hubainishwa kwa kupanda au kushuka kwa kiwango cha sauti. Ni utamkaji wa sauti ktk kiwango cha juu cha kati au cha chini.Kidatu huwa na uamilifu wa kudokeza maana ya msemaji, hasa kwa msikilizaji. Mfano; iwapo msemaji anaongea kwa sauti ya juu inawezekana amekasirika au amechukizwa na hali Fulani katika muktadha husika. Kidatu pia hudhihirisha uana (jinsia) wanawake huzungumza kwa kidatu cha juu ilhaliwanaume huzungumza kwa kidatu cha chini.

(v) Kiimbo

Ni upandaji na ushukaji wa mawimbi sauti. Kila lg huwa na utaratibu wa matumizi ya kiimbo.Kiimbo huandamana na kidatu. Kiimbo huhusu kupanda na kushuka kwa sauti. Kiimbo kinaweza kubadilika kikiwa katika kidatu hicho hicho. Mfano msemaji anaweza kuwa anaongea kwa sauti ya juu(kidatu cha juu) akatoa amri na akatoa maelezo. Hapa atakuwa amebadili kiimbo japo kidatu ni kile kile. Kuna kidatu cha maelezo, amri, maulizo, na mshangao.

(vi) Wakaa

Wakaa katika muktadha mzima wa mofolojia ni urefu wa muda uanotumika kutamka sauti fulani. Katika baadhi ya lugha wakaa ni sifa bainifu. Katika taaluma ya fonetiki, wakaa ni sifa ya vitamkwa ambavyo ni virefu kuliko vitamkwa vingine. Katika Kiswahili wakaa wa kawaida na wakaa mrefu hutumika katika foni irabu. Wakaa ni muda ambao hutumika kutamka foni Fulani. Katika maandishi wakaa hubainishwa kwa kurudiwa kwa sauti Fulani hasa

Page 61: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

Somo la Tatu Error! No text of specified style in document.

52

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

irabu ilhali katika unukuzi wa matamshi wakaa mrefu huonyeshwa kwa matumizi ya nukta mbili [:] Mfano;

Paa [pa:], Saa [sa:], Wakaa [waka:], Pekee [pεkε:], Choo [ʧᴐ:]

vii) Silabi

Silabi ni kipashio cha kifonolojia kinachohusu matamshi ambacho kwacho sauti za lugha hutamkwa mara moja kwa pamoja kama fungu moja la sauti linalojitegemea, kimatamshi. Kundi hilo linaweza kuwa lina sauti moja peke yake, au linaweza kuwa na sauti mbili au zaidi kutegemeana na muundo wa lugha husika. Kila lugha huwa na miundo yake ya silabi. Hii ina maana kwamba maneno ya lugha hutamkwa kwa kufauata utaratibu wa silabi na pia kwamba kuna sifa mahususi za utamkaji huo ambazo zinabainisha kipengele silabi na vipengele vingine kama vile kipande sauti, kitamkwa. Kila silabi kwa kawaida huchukuliwa kuwa ina irabu kama kilele chake, iwe irabu huru au funge. Hivyo bas I katika muktadha wa silabi, irabu ni kitu muhimu sana.

Ingawa ni kweli kwamba maneno ya lugha hutamkwa kwa kufauata utaratibu wa silabi, lakini namna za utamkaji wa silabi hutofautiana baina ya familia za lugha na vilevile baina ya wasemaji wa lugha. Msingi mkubwa wa tofauti ya utamkaji huo, unatokana na kile ambacho katika taaluma ya fonetiki kijulikanacho kama wakaa yaani muda unaotumika katika utamkaji wa sauti moja ya lugha.

Dhana hii ya wakaa huhusisha kiasi cha mwendo na vilevile wizani yani mifuatano inayowiana ya mkazo mkali na hafifu ya sauti katika utamkaji na hufanya matamshi ya maneno kati ya lugha ya familia moja kutofautiana sana nay ale ya lugha nyingine.

Lugha hutofautiana katika muda unaotumika katika kutamka silabi. Kuna lugha ambazo muda wa utamkaji wa kila silabi katika neno unakuwa uleule na kuna lugha ambazo muda wa utamkaji wa silabi katika neno huathiriwa na mkazo unaofungamana nao. Namna hizi mbili za wakaa wa utamkaji wa silabi, ni msingi mmojawapo unaotofautisha mathalani, lugha za Ulaya katika makundi mawili yaani kundi la Kiromansia na kundi la Kijerumani.

Aina za Silabi

Page 62: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

53

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

Kwa kawaida katika lugha nyingi ulimwenguni kuna aina kuu mbili za silabi yani Silabi Huru na Silabi Funge. Silabi huru ni silabi ambazo husihia na irabu na mara nyingi huwa na sauti ambazo zina msikiko au mvumo wa juu. Kwa maneno mengine silabi huru ni aina ya silabi ambazo huishia na irabu isipokuwa maneno ya mkopo ambayo silabi zake ni funge yaani huishia na konsonanti. Silabi funge ni silabi ambazo huishia na konsonanti na ni sauti ambazo hazina msikiko au mvomu mkubwa. Kutokana na hali hiyo, silabi funge huwa zinakuwa na msikiko hafifu. Kiswahili kina muundo wazi wa silabi (silabi huru).

Otografia

Otografia ni neno lenye asili ya kigiriki lenye maana ya utaratibu wa kutumia alama au michoro ya maandishi kuwakilisha sauti zisisikazo katika uesmaji wa lugha. Kwa kawaida kila lugha ina mfumo wake wa sauti na utaratibu wake wa uundaji mofimu. Kutokana na hali hiyo, ni wa zi pia kwamba kila lugha itakuwa na utaratibu wake wa uwakilishaji wa maneno yake, iwe kiaandishi au kiusemaji. Kwa upande wa maandishi kila lugha inaweza kubuni utaratibu wake wa kuwakilisha lugha ya usemaji Hii ina maana kwamba wataalamu wa lugha inayohusika watafanya kazi ya kubuni utaratibu huo wa maandishi ambao sasa utatumika kama mfomu wa maandishi. Mfumo huo wa maandishi unaweza kuwa wa alama au michoro. Mfumo wa namna hiyo ndiyo unaojulikana kama otografia. Kimsingi, ni wazi kwamba kila lugha inakiwa na otografia yake (Massamba, 2004:13).

Page 63: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

Somo la Tatu Error! No text of specified style in document.

54

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

Muhtasari wa Somo

Katika sura hii tumepitia maeneo mbalimbali yanayohusiana fonolojia yakiwemo maana ya istilahi za msingi kifonolojia kama fonimu, alofoni, tofauti kati ya fonetiki na fonolojia, matawi na aina za fonolojia, fonimu za lugha ya Kiswahili, sifa bainifu za fonimu, mbinu za kutambua fonimu na alofoni. Baada ya kupitia mada yetu ya fonolojia tumeona kuwa vipengele hivi vimejadiliwa kwa ya kina. Baada ya kupitia mada yetu ya fonolojia, sasa basi ili kuonyesha uelewa wako, hebu chukua peni yako ili uweze kufanya zoezi fupi linalojumuisha maeneo mbalimbali tuliyoyajadili katika mada hii.

Page 64: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

55

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

Zoezi la Somo

Jjibu maswali yote kwa kuandika ili kujipima uelewa wako, katika mada hii ya utumizi wa lugha.

1. Eleza maana ya dhana zifuatazo kama zinavyohusika katika dhana nzima ya fonolijia ya Kiswahili:

(a) Mkazo (b) Kiimbo (c) Kidatu (d) Ala Sauti (e) Bohari la sauti (f) Lafudhi (g) Silabi

2. Nini tofauti kati ya foni, fonimu na alofoni? 3. Elezea kwa ufupi mbinu za utambuzi wa fonimu na alofoni

zake. 4. Jadili kwa ufupi sifa mbalimbali za fonimu. 5. Dhana ya fonolojia imejadiliwa kwa umakini na Fudge

(1973), TUKI (1990) na Hartman (1972) na Weber (1985). Katika fasili zao hawa wote wanakubaliana kuwa fonolojia inapaswa itazamwe kama dhana iliyo na sura tatu ambazo ni:

(a)------ (b)------- (c)-------

6. Eleza kazi nne za fonolojia kwa mujibu wa Werber na wenzake (1985)

7. Aina za fonolojia 8. Bainisha sifa bainifu za fonimu za Kiswahili sanifu kwa

kutoa mifano halisi. 9. Bainisha fonimu za lugha ya Kiswahili kwa kutoa mifano

hai. 10. Taja mbinu za kutambua fonimu za alofoni zake na

kuzitolea maelezo mafupi. 11. Toa maana ya istilahi zifuatazo kwa ufasaha: (a) fonimu (b)

alofoni kisha utoe mifano halisi. 12. Bainisha matawi ya fonolojia na uyatolee maelezo mafupi. 13. Taja vipashio vinavyotumika katika kubainisha sauti kwa

kigezo cha vipamba sauti na uvitolee maelezo mafupi na mifano.

14. Eleza dhana ya silabi na uonyeshe umuhimu wa irabu katika muundo mzima wa silabi.

Page 65: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

Somo la Nne Error! No text of specified style in document.

56

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

Somo la Nne Mofolojia ya Kiswahili Sanifu

Utangulizi Katika sura iliyopita tulizungumzia fonolojia ya Kswahili sanifu na vipengele vyake muhimu. Katika sura hii tutajadili kwa kina mada ya Mofolojia ya Kiswahili ya Kiswahili sanifu kwa kungalia vipengele vifuatavyo: mawanda ya mofolojia, fasili za dhana mbalimbali za msingi za kimofolojia kama mofolojia, mofu, alomofu na mofimu, uhusiano wa mofu na mofimu, kubainisha mofu katika lugha ya Kiswahili na kufafanua njia za uundaji wa maneno.

Matokeo

Baada ya kukamilisha somo hili utaweza: § Kutoa Fasili mbalimbali kuhusiana na dhana mbalimbali za

msingi za Kimofolojia kama vile mofolojia, mofu, alomofu na mofimu, viambishi, shina, mzizi;

§ Kubainisha uhusiano wa mofu na mofimu; § Kubainisha mofu katika lugha ya Kiswahili; na § Kufafanua njia za uundaji wa maneno.

Ndugu mwanafunzi, baada ya kuona mada ndogo hapo juu ambazo tutazipitia katika sura yetu hii, hebu sasa tuanze mjadala wa kila kipengele baada ya kingine. Karibu.

Fasili ya dhana za Msingi za Kimofolojia

Dhana ya Mofolojia

Wanaisimu wengi wamewahi kuishughilikia dhana ya mofolojia kwa kina. Zifuatazo ni fasili mbalimbali kwa mujibu wa wanaisimu hao:

Page 66: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

57

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

Mathew (1974) anasema kwamba mofolojia ni tawi la taaluma ya isimu ambalo huchunguza maumbo ya maneno hususani maumbo ya mofimu.

Hertman (1972) naye anasema kuwa mofolojia ni tawi la sarufi hushughulika na uchunguzi na uchambuzi wa maumbo, fani na aina za maneno yalivyo sasa pamoja na historia zao.

Richard na wenzake (1985) wanasema kuwa mofolojia inaweza kupewa maaana kuu mbili yaani:

(i) Mofolojia huchunguza mofimu na alomofu zake na jinsi ambavyo hukaa pamoja na kuunda maneno mbalimbali katika lugha zinamotumika.

(ii) Mofolojia ni mfumo kamili wa mofimu katika lugha fulani. Kwa namna hii tunaweza kuzungumza juu ya mofolojia ya lugha Kiingereza au mofolojia ya Kijerumani

TUKI (1990) wanafasili mofolojia kama tawi la isimu ambalo huchunguza maneno na aina zake.

Tunapozichunguza kwa makini fasili zilizotolewa hapo juu tunaona ya kuwa mofolojia inapewa sura kubwa mbili yaani:

Mofolojia kama taaluma ya isimu/ sarufi ambayo inalo jukumu la kuyachunguza maneno ili kuyaelewa yake yalivyo

Mofolojia kama kiwango kimojawapo cha kila lugha. Kiwango cha mofolojia kinatofautiana na viwango vingine vya lugha ambavyo ni fonolojia, sintaksia na semantiki. Wakati mwingine wataalamu wengine hukiweka kiwango hiki pamoja na kile cha sintaksia.

Dhana za mofu, alomofu na mofimu ndizo ambazo hutumiwa sana kwa uchambuzi wa kiisimu hususani katika kiwango cha mofolojia. Isilahi hizi zote tatu zimetoholewa kutoka istilahi za Kiiingereza yaani Mofu- kutoka neno la Kiingereza morph, alomofu kutoka neno la Kiingereza allomorph na mofimu kutoka neno la Kiingereza morpheme. Yafaa dhana hizi tatu zielezwe vizuri kwa sababu ni dhana muhimu sana katika isimu.

4.1.2 Mofimu

Dhana ya mofimu imejadiliwa na wataalam mbalimbali. Crystal (1971) anasema kuwa mofimu ni kipashio kidogo kabisa katika

Page 67: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

Somo la Nne Error! No text of specified style in document.

58

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

lugha chenye maana na zaidi ya hayo, maana hiyo hutofautiana na zile za za mofimu nyingine katika lugha hiyo. Crystal anabainisha sifa kadhaa za mofimu kama ifuatavyo: (i) Mofimu ni kipashio chenye umbo halisi, (ii) Mofimu ina umbo lake la kifonetiki. (iii)Mofimu huwa na maana, (iv) Kila mofimu huwa na nafasi yake katika kushirikiana na vipashio vingine.

Dhana ya mofimu ina sura kuu mbili ambazo zinatofautiana kulingana na vipindi vikuu viwili ambavyo dhana hii ilitumika yaani:

1. Dhana ya mofimu kabla ya kuasisiwa kwa Sarufi Zalishi

2. Dhana ya Mofimu baada ya kuasisiwa kwa Sarufi Zalishi

4.1.2.1 Dhana ya Mofimu kabla ya Sarufi Zalishi

Wanaisimu walipoona umuhimu wa kuwa na kipashio kidogo zaidi ya neno katika uchambuzi, mara walibuni na kuanza kuitumia dhana ya mofu. Badala ya uchambuzi kuishia kwenye neno tu, uchambuzi ukawa unaendelea hadi kwenye kiwango cha mofimu.Crystal 1971, Kayuza 1988, Marealle 1978 na Mohamed (1986) wanafuata mtazamo huu wa dhana kabla ya Sarufi Zalishi kama inavyoonyeshwa kwenye maelezo yafuatayo: Marealle (1978) anafasili neno mofimu kama kipashio kidogo kabisa cha kisarufi kilicho na Mohamed anafasili mofimu kama kijineno au sehemu ndogo ya tamko iletayo maana kamili. Kayuza (1988) anasema kuwa mofimu ndiyo ngazi ya mwisho ya maumbo na pia ni tamko dogo lenye maana kisarufi.

4.1.2.2 Dhana ya Mofimu baada ya Kuasisiwa kwa Sarufi Zalishi

Baada ya kuasisiwa kwa sarufi Zalishi katika karne ya 20, dhana muhimu mbili ziliingizwa katika uchambuzi wa mofolojia ya lugha. Dhana hizo ni mofu na alomofu. Baada ya kuingizwa kwa dhana mpya za mofu na alomofu, mofu ilichukuwa maana iliyokuwa imepewa mofimu, kama kipashio kidogo cha lugha kinachobeba au kusetiri maana. Sasa mofimu ikapewa maana mpya. Fasili mojawapo inayotoa hii maana mpya ya mofimu ni ile ya Hartman (1972) ambaye anasema: Mofimu ni kipashio dhahania cha umbo fulani ambacho kinaweza kuwakilishwa kwa mofu

Page 68: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

59

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

tofautitofauti katika mazingira anuwai. Mofimu ya wingi katika ya Kiingereza, kwa mfano huwa kilishwa kwa mofu /s, /z/, /iz/.

Mofimu kama kitu dhahania

Mofimu ni kipashio dhahania cha lugha na sio umbo halisi kwa sababu hakionekani wala hakiwakilishi kupitia maandishi bali kimo akilini mwa msomaji. Mofimu si umbo la maneno bali ni maana tunazozisetiri akilini mwetu. Kwa maneno mengine, mofimu ni kipashio kidogo kabisa cha kisarufi kilicho na maana.

4.1.3 Mofu

Ni istilahi ambayo imetoholewa kutoka istilahi morph kutoka lugha ya Kiingereza. Nida (1949) anaeleza kuwa, mofu ni umbo la neno ambalo huwakilisha mofimu na ambalo hudhihirika kiothografia. Mofimu ambazo ni elememtni dhahania huwakilishwa na mofu ambazo hudhihirika ama kifonolojia zikiwa ni sauti za kutamkwa au kiothografia zikiwa ni alama za kuandikwa.

Platt (1985) anafasili mofu kama kipashio kidogo kabisa chenye maana katika lugha. Mofu haiwezi kugawanywa katika sehemu ndogondogo zaidi bila kuharibu maana yake. Mofu huwakilisha maana ya kileksika na zile za kisarufi. TUKI (1990) wanasema kuwa mofu ni kipashio cha kimofolojia kiwakilishacho mofimu.

Baada ya kuona fasili zote tatu zilizotolewa na wataalamu mbalimbali kuhusiana na dhana ya mofu, yapo mabo ya msingi kabisa kuhusu sifa muhimu za kuzingatia zinazopambanua dhana ya mofu. Mambo haya ya msingi yanaweza kuzingatiwa:

(i)Mofu ni sehemu halisi ambazo huwa tunazitamka na kuzinadika wakati tunapoandika maneno lakini maana ambazo huwakilishwa na mofu ndizo tunazoziita mofimu ambazo ndizo huwa dhahania kwa sababu maana hizo huwa hazitamkwa wala kuandikwa.

(ii)Kwa kweli mofu imo katika upande wa utendaji lakini mofimu ni dhana ya kidhahania iliyomo akilini mwa watu na ambayo ni sehemu ya umilisi wa lugha wa kila mtu. Mofimu ni tafsiri ambayo

Page 69: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

Somo la Nne Error! No text of specified style in document.

60

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

mtu hufanya akilini mwake kuhusu maana ambayo husetiriwa kwenye mofu.

Kwa ujumla tunaweza kusema kuwa, mofimu ni kipashio kidogo sana cha neno ambacho kina maana na pia kinaweza kubadili maana ya neno. Hebu tuone mfano wa mofu kama ifuatavyo:

{imb}hubakia {imb} tu mahali popote inapotokea kama:

(i)imb+ a imba

(ii)si+imb+i siimbi

(iii)u+si+imb+e usiimbe

(iv)tu+ta+imb+a tutaimba

Mzizi (toto) pia una mofu moja tu ambayo haibadiliki, kwa mfano,

(i)m+toto (ii) wa+toto (iii) u+toto (iv) u+toto+ni

Mzizi

Mzizi ni mofu ambayo ni muhimu zaidi katika neno na huweza kukaa peke yake kama neno kamili. Aidha, hii ni sehemu ya neno ambayo haibadilikibadiliki. Katika uchanganuzi wa neno, mzizi hauwezi kuchanganuliwa katika sehemu nyingine ndogo bila kupoteza uamilifu na maana yake. Hivyo basi, mzizi ni kiini cha neno na ni sehemu ya neno ambayo maneno mengine huundwa kutoka kwao.

Mzizi wa Kitenzi

Mzizi wa kitenzi ni sehemu ya kitenzi ambayo haibadilikibadiliki wakati wa mnyambuliko. Kiini ni ile sehemu kuu ya kitenzi bila kiambishi chochote. Hii ndiyo sehemu ambayo hubeba maana halisi ya kitenzi. Kwa mfano:

Kitenzi Mzizi

Alipikika {-pik-}

Ulipika {-pik-}

Utapika {-pik-}

Page 70: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

61

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

Mlipika {-pik-}

Kilipikwa {-pik}

Sifa za Mzizi

(i)Mzizi hufanya neno kuwa na uafifishaji mkamilifu, hivi kwamba mzizi ukiondolewa katika neno, utakopotea.

(ii) Mzizi huweza kukaa yake kama neno kamili, kwa mfano: baba, mbuzi n.k (mofu huru tu).

(iii)Katika lugha ya Kiswahili kuna baadhi ya maneno ambayo huundwa na mwambatano wa mizizi miwili.

Maumbo ya Mizizi katika Lugha ya Kiswahili

(i)Mzizi unaundwa na fonimu moja

Kwa mfano: katika maneno yafuatayo:

Kufa - / f /

Kula / l /

(ii)Mzizi unaounda na fonimu mbili silabi

Mfano katika maneno

Mtu – (-tu-)

Mtoto m- (-to)

(iii)Mzizi unaoundwa na mofimu zaidi ya mbili

Kwa mfano: Cheza (–chez-)

Piga - (-pig-)

Imba (-imb-)

Tembea- (-temb-)

Aina ya Mizizi

Page 71: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

Somo la Nne Error! No text of specified style in document.

62

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

Kuna aina kuu mbili za mizizi. Uanishaji huu umekitwa kwenye maana na umbo la mizizi husika.

(a) Mzizi Huru

Mzizi huru ni mzizi ambao huweza kusimama peke yake kama neno lenye uarifishaji mkamilifu ambao hauhutaji kaumbikwa viambishi. Katika lugha ya Kiswahili, kwa mfano, mizizi ya maneno mengi huwa ni mofu huru ambazo zina uwezo wa kukaa peke yao, kama maneno kamili kwa mfano, maneno yafuatayo:

Nomino

1. {baba} 2. {taifa} 3. {Sungura} 4. {shati} 5. {Ndege} 6. {kaka} 7. {Juma} 8. {Arusha} 9. {Mombasa} 10. {Tanga}

Vivumishi

1. Rahisi 2. chafu 3. Bora 4. {Imara} 5.{goigoi} 6. {mwerevu}

Viwakilishi

1. {vile} 2. {mimi} 3. {wale} 4. {ninyi] 5. {yeye} 6. {wao}

Vielezi

1. {upesi} 2.{ haraka} 3. {sana} 4. {leo} 5. {jana} 6. {juzi}

Vihusishi

1. {pembeni} 2. {ndani} 3. {juu} 4. {nyuma} 5. {chini} 7. {kwa} 8. {mbele}

Page 72: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

63

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

(b) Mzizi Tegemezi

Mzizi tegemezi hauwezi kusimama peke yake bila kiambishi cha awali au tamati na kuleta maana kamili. Kwa mfano :

(-l-) – katika neno kula

(-f-) katika neno kufa

(-j-) katika neno kuja

(-tu-) katika neno mtu

(-pig-) katika nenno piga

Shina

Shina ni mzizi ambao umeambikwa kiambishi tamati. Aidha ni sehemu ya neno inayotumiwa kuunda neno jipya. Shina kamili haliwezi kuchanganuliwa bila kupoteza maana. Kuna aina zifauatazo za shina:

(a) Shina Sahili

Shina sahili ni shina ambalo huundwa na mofu au mizizi huru. Kwa mfano:

Shamba –mashamba

Taifa - mataifa

Shati – mashati

Jembe -majembe

(b) Shina Changamano

Shina changamano ni shina ambalo huundwa na mzizi mmoja na viambishi, hususani viambishi tamati. Kwa mfano:

Pika – pikia, pikiwa

Piga – piga, pigia, pigana

Page 73: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

Somo la Nne Error! No text of specified style in document.

64

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

Cheza – chezea, chezewa, chezeana

(c) Shina ambatano

Ni shina ambalo huundwa kwa muambatano wa mizizi huru miwili. Kwa mfano:

Askari + kanzu ------------------askarikanzu

Mwana+ hewa -------------------mwanahewa

Bata + mzinga ------------------ batamzinga

4.2 Kubainisha uhusiano wa mofu na mofimu===============================

Mofu ni sehemu halisi ambazo huwa tunazitamka na kuzinadika wakati tunapoandika maneno lakini maana ambazo huwakilishwa na mofu ndizo tunazoziita mofimu ambazo ndizo huwa dhahania kwa sababu maana hizo huwa hazitamkwa wala kuandikwa.

Kwa kweli mofu imo katika upande wa utendaji lakini mofimu ni dhana ya kidhahania iliyomo akilini mwa watu na ambayo ni sehemu ya umilisi wa lugha wa kila mtu. Mofimu ni tafsiri ambayo mtu hufanya akilini mwake kuhusu maana ambayo husetiriwa kwenye mofu. Kwa ujumla tunaweza kusema kuwa, mofimu ni kipashio kidogo sana cha neno ambacho kina maana na pia kinaweza kubadili maana ya neno.

4.3 Kubainisha aina za Mofu katika Kiswahili Sanifu

Ndugu mwanafunzi, kabla hatujabainisha aina za mofu katika lugha ya Kiswahili, hebu sasa tuchunguze sifa mbalimbali za mofu kama ifuatavyo:

Sifa Mbalimbali za Mofu

Zipo sifa mbalimbali za mofu katika lugha ya Kiswahili.

Sifa hizo ni:

(i)Mofu kama sehemu halisi ya neno

Page 74: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

65

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

Hii ina maana kwamba mofu ni maumbo halisi ya maneno ambayo hutamkwa wakati watu wanapozungumza au kuandikwa wakati watu wanapoandika maneno. Kwa mantiki hiyo basi, mofu ni umboa halisi ambalo tunaweza kulisikia linapotamkwa na kuliona linappokuwa limeandikwa.

(ii) Mofu hudhihirika kifonolojia na kiothografia

Kwa kuwa mofu ni umbo halisi la neno, basi mofu mbalimbali hudhihirika kifonolojia zinapotamkwa na pia kimaandishi zinapoandikwa yaani kiothografia.

(iii)Mofu huwakilisha maana

Hapa tunasisitiza kuwa mofu huwakilisha maana fulani katika neno lolote katika lugha katika lugha yoyote patakuwepo maana na maana hizo huwa zimesetiriwa katika mofu zilizopo katika neno. Hii ina maana kwamba kama kila neno huwa na maana fulani, basi maana hiyo itakuwa imewakilishwa na mofu fulani. Hii ina maana kuwa hakuna neno lolote katika lugha yoyote ambalo linaweza kuwa ni neno lenye maana bila kuwa na mofu angalau moja. Kwa hiyo tunaweza kusema kuwa kila neno lenye maana katika lugha, litakuwa na mofu angalau moja.

(iv) Mofu ni kipashio kidogo kabisa cha neno chenye maana

Hapa kinachotiliwa mkazo ni ule ukweli kuwa, mofu ni sehemu ndogo kabisa ambayo hubeba maana na kuwa sehemu hiyo haiwezi kugawanywa katika sehemu ndogo zaidi zilizo na maana kuliko. Hapa tungeweza kusema kuwa kwa ukubwa mofu ni umbo ambalo hudhaniwa kuwa ni kubwa kuliko fonimu na ni ndogo kuliko neno.

Aina za Mofu

Aina za mofu zinaweza huanishwa kwa kutumia vingezo vya maana na mofolojia katika Kiswahili Sanifu. Kwa kutumia kigezo cha maana zipo mofu za aina tatu ambazo ni:

(a) Mofu Huru ( free mofu)

(b) Mofu funge (bound morphs)

(c) Mofu tata (ambiguous morphs)

Page 75: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

Somo la Nne Error! No text of specified style in document.

66

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

(a) Mofu huru

Weber (1985) anasema ya kuwa mofu huru ni zile mofu ambazo zinaweza kukaa peke yake kama maneno kamili. Mofu huru ni mofu zilizo na uwezo wa kukaa peke yake na zikawa maneno kamili yenye maana.. Mara nyingi mizizi ya baadhi ya maneno ndiyo ambayo ina uwezo wa kukaa peke yake na yakawa maneno kamili yanayojitosheleza. Mizizi ya aina hiyo si lazima

iwekwe viambishi ndipo iwe maneno. Katika lugha ya Kiswahili, kwa mfano, mizizi ya maneno mengi huwa ni mofu huru ambazo zina uwezo wa kukaa peke yao, kama maneno kamili kwa mfano, maneno yafuatayo:

Nomino

2. {baba} 2. {Kuku} 3. {Sungura} 4. {Kalamu} 5. {Ndege} 6. {Dada} 7. {Juma} 8. {Kilimnajaro} 9. {Nairobi} 10. {morogoro}

Vivumishi

2. Ghali 2. Safi 3. Dhaifu 4. {Imara} 5.{goigoi} 6. {hodari}

Viwakilishi

2. {mimi} 2. {sisi} 3. {wewe} 4. {ninyi] 5. {yeye} 6. {wao}

Vielezi

2. {upesi} 2.{ haraka} 3. {sana} 4. {leo} 5. {jana} 6. {juzi}

Vihusishi

2. {nje} 2. {ndani} 3. {juu} 4. {nyuma} 5. {chini} 6. {ya} 7. {kwa} 8. {mbele}

Page 76: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

67

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

Viunganishi

1. na, 2. {halafu} 3.{bila} 4. {ila} 5. {aidha} 6.{pia}

Tanbihi

Vitezni vyenye asili ya Kibantu, wakati wote huwa ni tegemezi kwa sababu huhitaji angalau kiambishi tamati kimoja ndipo viwe neno kamili. Namba kwenye mabano inaonyesha idadi ya mofu katika neno. Kwa mfano,

1. {ruk}+ {a} ruka (2)

2. 2. {chez} + {a} cheza (2)

3. {andik} + {a} andika (2)

4. {imb} + {a} imba (2)

(b) Mofu Funge

Richards et al. (1985) wanaeleza kuwa, mofu funge ni kipashio cha kiisimu ambacho huwa hakikai peke yake bali ni lazima kiandamane na mofu nyingine. Hartman (1972) anasema kwamba, mofu funge ni mofu ambayo haiwezi kutumiwa peke yake kama neno kamili lililo na maana yake bainifu, bali daima hutumiwa kama kiambishi tu kinachoambatana na mzizi au viambishi vingine ili kukamilisha neno. Maana ya mofu funge hutegemea muktadha wa mofu. Kwa hiyo sifa kubwa ya mofu funge ni kuwa mofu funge haiwezi kukaa peke yake ikawa neno kamili. Sifa hii inatofautisha mofu funge na mofu huru kuwa mofu huru ina uwezo wa kukaa peke yake. Mofu funge lazima ziwekwe pamoja na mofu nyingine moja ili kuleta maana kamili ya neno. Hii huwafanya wanaisimu wengine kuziita mofu hizi tegemezi. Mara nyingi hizi mofu funge huwakilisha maana za kisarufi. Kwa mfano katika nomino huweza kuwakilisha maana zifuatazo:

1. Idadi ya Umoja

(i) M+ toto (m)

(ii) Ki+tabu (ki)

(iii)ji+ cho (ji)

Page 77: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

Somo la Nne Error! No text of specified style in document.

68

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

2.Ukubwa wa Nomino

Ji+tu (ji)

Ji +su (ji)

3.Idadi ya Wingi

Wa +toto (wa)

Vi + tabu (vi)

Ma + cho (Ma)

4.Udogo wa Nomino

Ki+ji+tu (ki)

Ki+ji+su (ki)

Ki+ji+ti (ki)

Katika mifano hiyo hapo juu tuanaona kuwa mofu ya ukubwa katika lugha ya Kiswahili huwa ni {ji} ambayo huwekwa pamoja na mzizi wa nomino. Lakini wakati wa kukifanya kitu mkiwe kidogo, mofu mbili hutumika kwa pamoja yaani mofi {ki} ya udogo pamoja na mofu {ji} ya ukubwa, ambapo zikiandamana na mzizi wa nomino ndipo tunapata ile hali ya udogo.

5.Unominshaji wa aina zingine za maneno:

Lima (i) Ku+lim+ a (1) {ku} (2) {a}

(ii)U+ku+lim+a (1) {u} (2) {ku} (3) {a}

(iii)Wa+ku+lim+a

Page 78: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

69

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

(c) Mofu Tata

Weber (1985) anaeleza mofu tata kama kipashio cha kiisimu ambacho kinaweza kupewa maana ya moja, yaani maana kauanzia mbili na kuendelea. Vipashio vya kiisimu ambavyo huweza kuwa tata ni mofu, maneno, virai na sentensi. Kwa kuzingatia fasili ya Weber, mofu tata ni mofu ambazo huwa na maana zaidi ya moja, tuseme labda maana kuanzia mbili na kuendelea. Hapa inafaa tutoe mfano wa mofu tata katika lugha ya Kiswahili. Tazama sentensi ifuatayo:

Pendo alimpiga Noel mpira

Sentensi hii ni tata kwa sababu, ina maana au tafsiri zaidi ya moja. Utata wa sentensi hiii si wa kisarufi bali upo katika kitenzi. Kitenzi hiki kina mofu sita.

Aina za mofu kwa kuzingatia Uanishaji kwa kigezo cha Kimofolojia

Zipo aina mbili za mofu, ambazo ni: (i) Mofu changamani (ii) Mofu kapa

Mofu changamani ni mofu inayoundwa kutokana maumbatana wa mizizi huru miwili au (mashina mawili). Mashina hayo huwa na usafairishaji mkamilifu. Kwa hiyo, kila shina huweza kusimama kama neno kamili lenye kujitosheleza kimuundo na kimaana. Kwa mfano:

(a) Mwana + jeshi ----------------------mwanajeshi

{mw-} – ngeli ya kwanza; idadi ya umoja

{-ana-}- mzizi

{jeshi} – mzizi huru

(b) Mwana +idara –mwanaidara

{-mw-} –idadi (umoja)

{-ana-} – mzizi

{idara}- mzizi huru

Page 79: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

Somo la Nne Error! No text of specified style in document.

70

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

Mofu Kapa

Mofu kapa haiwakilishwi na kitu au alama yoyote dhahiri. Kwa mujibu wa Massamba (2004) anasema kuwa katika lugha ya Kibantu, viambishi vya ngeli vya nomino zilizomo katika ngeli huwa haviko dhahiri katika neno na katika umoja au wingi. Mofu hizi hazina umbo na hazionekani, haziandikwi wala kutamkwa ila ni sehemu ya umilisi wa watumiaji wa lugha husika. Ijapokuwa mofu hizi hazionekani wala kutamkwa, huwa na maana katika neno husika. Kwa mfano:

Umoja Wingi

Ukucha kucha

Ukiangalia katika mfano wa hapo juu katika wingi, kiambishi cha wingi hakijitokezi bayana ilhali kiambishi cha cha umoja (-u-) ni bayana.

Dhana ya Alomofu

Richards na wenzake (1985) wanafasiri alomofu kama umbo mojawapo kati ya maumbo kadhaa tofauti yanayoiwakilisha mofimu moja. Hartman (1970) anafasiri alomofu kama umbo badala ya mofimu fulani ambalo halibadili maana. Bauer (1983) ni mofu mojawapo katika seti ya mofu zinazoiwakilisha mofimu fulani ambayo ina mazingira yake ya kifonetiki, kileksika au kisintaksia (kisarufi).

Tukiangalia fasili hizo hapo juu, tunaona kuwa zinaeleza sifa muhimu zinazofafanua alomofu. Zifa hizo ni kama ifuatavyo:

(i)Alomofu ni umbo halisi ambalo ni sehemu ya neno fulani na mbalo hutamkwa kwa kuandikwa. Kwa hiyo alomofu ni mofu na sifa tulizozitoa kuhusu mofu ndizo ndizo zinazofaa pia keuelezea alomofu.

(ii) Alomofu ni mofu mojawapo miongoni mwa mofu za mofimu moja kwani zina sura moja tu.. Popote zinapotokea hutokea na sura ileile na hazibadiliki.

Kwa mfano katika lugha ya Kiingereza kwa mfano, kiambishi tamati /s/ cha wingi kina maumbo mbadala yafuatayo:

Page 80: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

71

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

1. /s/ kama katika maneno cats, books

2. /z/ kama katika maneno dogs, bags

3. /iz/ kama katika maneno classes, boxes, flies

4. / / kama katika neno sheep

Alomofu ni umbo jingine la mofu ileile moja kama inavyojidhihirisha katika maneno motto, muuguzi na mwanafunzi. Tunaona kwamba, viambishi awali (m-), (mw-) na (mu-) vyote vinawakilisha mofimu moja ya ngeli ya kwanza. Katika lugha za Kibantu. Kwa hivyo, maumbo {m-}, {mu-}, na {mw-} ni alomofu zinazokilisha mofimu moja. Hivyo basi, alomofu ni maumbo mawili au zaidi yanayowakilisha mofimu moja. Alomofu hutokea katika mazingira maalum katika maneno. Mifano ufuatao unaonyesha alomofu katika lugha ya Kiswahili:

Mofimu ya umoja {mu}- {m}

{mu}

{mw}

Mifano ya Alomofu

(a) Mofu za wingi katika lugha ya Kiswahili

{wa-}- katika maneno wachawi, wanafiki, wanyonge

{mi-} - katika maneno miti, miembe, michoro n.k

{ma} - katika maneno matunda, mawele

{vi-} – katika maneno vikombe, vijiko, vichwa n.k

(b) Mifano ifutayo hudhurisha mofimu za njeo

Anacheza

Alicheza

Atacheza

Page 81: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

Somo la Nne Error! No text of specified style in document.

72

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

Katika mifano hiyo hapo juu, maumbo {-na-}, {-li-}, na {-ta-} ni alomofu ambazo husetiri

Mofimu ya njeo.

(c)Vitenzi vifuatavyo hudhihirisha mofimu ya kutendea:

Kulia

Somea

Lilia

Lelea

Katika mifano hiyo hapo juu, maumbo {-i-}, {-e}, {-le} ni alomofu ambazo husetiri mofimu ya kutendea.

Ndugu mwanafuzi baada ya kupitia mada ndogo hapo juu hebu tufanye zoezi fupi ili kupima uelewa wetu wa kile tulichojifunza:

ZOEZI

1. Fafanua dhana za mofu, alomofu na mofimu kwa kutumia mifano ya kutosha kutoka lugha ya Kiswahili

2. Eleza utofauti na uhusiano uliopo katin ya dhana za mofu, alomofu na mofimu.

3. Fafanua dhana zifutazo: (i) Mofu kappa (ii) mofu kappa (iii) mofu changamano

4. Bainisha mofu na alomofu zilizomo katika maneno yafuatayo na utaje aina zao:

(h) Mamake (ii) kuta (iii) chezea

5. Taja mofimu zilizosetiriwa katika mofu/alomofu za maneno yafuatayo:

(i) mkono (ii) ujana (iii) uzeeni (iv) wachezaji (v) anatupenda (vi) vitabu

6. Fafanua dhana za shina na mzizi kwa kuzingatia aina na mifano halisi ya maneno.

Page 82: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

73

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

4.4 Kufafanua njia za uundaji wa maneno

Katika kuangalia njia za uundaji wa maneno ni vyema kwanza kufahamu matawi mbalimbali ya mofolojia mabyo yatatuwezesha katika mchakato mzima wa mada yetu hii ndogo ya uundajiwa wa maneno. Ndugu mwanafunzi, hebu sasa tuangalie matawi ya mfolojia kabla hatujaendelea na mchakato wa uundaji wa maneno:

Matawi ya Mofolojia

Wataalamu wengi wamekubaliana kuwa mofolojia kama taaluma inaweza kugawanyika katika matawi makuu mawili kama ifautavyo:

(1) Mofolojia ya Mnyambuliko wa Maneno (Inflectional Morphology)

(2) Mofolojia ya uundaji wa maneno (Derivational Morphology)

Mofolojia ya minyambuliko ya Maneno (Inflectional Morphology)

Mofolojia ya minyambuliko hushughulikia zaidi ile minyambuliko ambayo huwekwa kwenye mizizi ya maneno kuwakilisha maana mbalimbali lakini minyambuliko hiyo isibadili maana ya neon hilo. Utaona kwa mfano, katika lugha ya Kiswahili, mizizi ya nomino inaweza kuwekwa viambishi awali kuonyesha mambo kadha wa kadha. Kwa mfano, mzizi-{tu}-

1. Umoja wa nomino : m-tu

2. Wingi wa nomino : wa-tu

3. Ukubwa wa nomino : ji-tu

4. Udogo wa nomino : ki-ji-tu

Jambo muhimu kukumbukwa hapa ni kuwa minyambuliko ya maneno huwa haipaswi kubadili aina ya neno linalonyambuliwa. Ikiwa neno linalonyembuliwa ni kitenzi. kwa mfano mzizi –pig- unaweza kunyambuliwa na kupata.

Page 83: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

Somo la Nne Error! No text of specified style in document.

74

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

- pigwa,-pigiwa, -pigiana, -pigisha, anapigwa, alipopigiwa, n.k

Kila lugha inao utaratibu wake wa kunyambua maneno ya aina aina katika lugha hiyo. Wanaisimu hupaswa waeleze maumbo (mofu) mbalimbali ambayo huwekwa katika aina mbalimbali za maneno ili kuongezea maana katika maneno hayo. Utagundua ya kuwa minyambuliko ya maneno aghalabu huwa na uamilifu wa kisarufi na neno ambalo hupatikana baada ya minyambuliko huwa haliwezi kuwa leksemu au kuonekana kuwa ni neno tofauti na lile neno la awali. Matokeo ya minyambuliko ya neno huwa si kupata leksemu ampya bali ni kuongeze maana fulani ya kisarufi katika neno hilo hilo.

Mofolojia ya uundaji wa maneno

Hartman (1972) anaeleza ya kuwa mofolojia ya uundaji wa maneno ni eneo ambalo hushughulikia mikondo na matokeo ya kiisimu ya uundaji wa maneno kwa kuweka viambishi katika mizizi ya maneno. Kiambishi nyambuaji kinaweza kubadili aina ya neno. Katika isimu historia mofolojia uundaji wa maneno huhusika na kueleza pia etimolojia ya neno fulani. Yaani asili ya neno. Kwa mfano, maneno yaliyokopwa kutoka lugha fulani yealezwe kuwa yamekopwa kutoka lugha fulani. (TY).

Suala muhimu linalosisitizwa hapa ni uundaji wa maneno; kwamba wakati viambishi mbalimbali vinapoongezwa katika mzizi na neno , neno linalopatikana huwa ni neno jipya. Hartman anaeleza kuwa hilo neno jipya huwa si lazima liwe la aina moja na lile neno la awali lakini pia si lazima liwe tofauti. Tunaona, kwa mfano, kuwa katika lugha ya Kiswahili nomino zinaweza kuundwa kutokana na mizizi ya vitenzi, kwa mfano, kutokana na mzizi –imb-tunaweza kupata nomino zifuatazo:

1. u+imb+o - wimbo

2. mu+imb + a_ji - mwimbaji

3. ku+imb+a - kuimba

4. mu+imb+ish + a + ji -mwimbishaji

Page 84: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

75

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

Pia katika lugha ya Kiswahili vitenzi vinaweza kuundwa kutokana na vivumishi, kwa mfano

1. – refu - refusha

2. – fupi - fupisha

3. – safi - safisha

4. – nene - nenepesha

5. –bora - boresha

Tofauti iliyopo kati ya mofolojia ya minyambuliko na mofolojia ya uundaji wa maneno si kubwa na wakati mwingine hutatanisha. Tusisitize hapa kuwa katika mofolojia ya minyambuliko maneno mapya huwa hayawezi kuwa leksemu tofauti na neno la awali lakini katika mofolojia ya uundaji wa maneno, yele maneno mapya huwa ni leksemu tofauti na lile neno la awali.

Ni dhahiri pia kuwa uchunguzi wa kimofolojia wa lugha yoyote unaweza ukawa wa kidaikronia au wa kisinkronia. Wakati mwingine mofolojia inapochunguza lugha kisinkronia huitwa mofolojia ya kisinkronia na inapochunguza lugha kidaikronia/kihistoria huitwa mofoloja ya kidaikronia. Katika baadhi ya lugha, (Kiswahili kikiwemo kiwango cha mofolojia huingiliana na kiwango cha mofolojia huingiliana na kiwango cha fonolojia kwa upande mmoja na sintaksia kwa upande wa pili kwani hivyo ndivyo viwango vinavyopakana nacho. Utaona, kwa mfano, kuwa baadhi ya fonimu zilizo kwenye mipaka ya mofu huathiriana na kusababisha mabadiliko ya kifonetiki. Hii ndiyo sababu ya kuwepo kwa mifanyiko ya kimofonolojia katika lugha. Yaani mabadiliko ya kiMada ya mofu ambayo hutokana na kuathiriana kwa fonimu zilizo kwenye

mipaka ya mofu zinazopakana. Kwa upande mwingine baadhi ya masuala ya kisintaksia hutekelezwa kwa kutuia mofu. Tunaona katika lugha ya Kiswahili kwa mfano kuna vipatanishi vya nomino ambavyo huambishwa kwenye vitenzi au vivumishi, kwa mfano.

Page 85: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

Somo la Nne Error! No text of specified style in document.

76

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

Mtoto a-nalia

Watoto wa-nalia

Kiti ki- mevunjika

Viti vi- mevunjika

Jicho li+ linauma

Macho ya+ nauma

Nyumba i= mejengwa

Nyumba zi + mejengwa

Mofolojia ya maneno

Baada ya uchunguzi wa muda mrefu wanaisimu wamegundua kuwa maumbo mbalimbali yanaweza kuanishwa katika aina kuu mbili yaani:

(i) Maneno yasiyoambishwa

(ii) Maneno yanayoambishwa

Maneno yasiyoambishwa

Baadhi ya lugha huwa na maneno yasiyoambishwa ambayo ni mengi zaidi kuliko yale yanayoambishwa na lugha nyingine zina maneno mengi yanayoambishwa kuliko yale yasiyoambishwa. Kwa mfano, lugha teanganishi huwa na maneno yasiyoambishwa mengi zaidi kuliko (karibu yote) ilhali lugh ambishi huwa na maneno yasiyoambishwa mengi zaidi ingawa siyo yote kabisa huambishwa. Katika lugha ya Kiswahili kwa mfano, baadhi ya maneno ambayo hayaambishwi ni:

1. Nomino za pekee, kwa mfano:

(i) Majina ya watu: Pendo, Tumaini, Noeli, Imanueli,

(ii) Majina ya sehemu/mahali: Kenya, Tanzania, Japan, Tanga, Nairobi

Page 86: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

77

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

2. Viwakilishi vya nafsi: Mimi, sisi, wewe, ninyi/nyyinyi, yeye, wao

3. Baadhi ya vihisishi, viunganishi, kwa mfano: halafu, wala, pia, kadhalika, vilevile, aidha, licha, kisha, kabla, baada, karibu, nyuma, chini, juu

4. Baadhi ya vihisishi: kwa mfano, ebo! Huraa! Chubwi! Fofofo! Alaa! Astaghafullah! Ah! Naam! Oyee!

Kitu cha msingi ch kuelewa hapa ni kuwa maneno yasiyoambishawa hayawekewi viambishi vyovyote wakati na mahali popote yanapotumika. Sifa kubwa ya maneno haya huwa ni mizizi tu ambayo haiwezi kungezwa kitu chochote.

Maneno yanayoambishwa

Maneno yanayoambishwa ni yale maneno ambayo yanaweza kuwekewa viambishi. Mizizi ya maneno haya huweza kuwekewa viambishi mbalimbali vinavyobeba maana mbalimbali.. Lugha ya Kiswahili ina maneno mengi zaidi yanayoweza kuambishhwa kuliko yale yasioambishwa kwa mfano tunaweza kuweka viambishi ama kabla ya mzizi wa neno au baada ya mzizi wa neno. Viambishi vinaweza kuwekwa katika:

1. Nomino: kwa mfano Idadi ya Vaimbishi

(i) Ki + tabu (1)

(ii) Vi + tabu (1)

(iii) U + toto (1)

(iv) M +chez-a-ji (3)

(v) U+ ku +lim-a (3)

(vi) U+ fug-a-ji (3)

Page 87: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

Somo la Nne Error! No text of specified style in document.

78

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

(vii) Ku + to + som-a (3)

2. Vivumishi: Kwa mfano

(i) M+ zuri (1)

(ii) Wa + zuri (1)

(iii) Ki + zuri (1)

(iv) Vi + zuri (1)

(v) Ma + zuri (1)

3. Viwakilishi: Kwa mfano:

(i) Naye (Na yeye)

(ii) Nasi ( Na sisi (1)

(iii) Hicho (H + i+ ki + o) (1)

(iv) Hivyo (H+ i + vi + o) (3)

(v) Kule ( Ku + le) (3)

(vi) Vile ( Vi + le) (1)

(vii) Mle ( M + le) (1)

4. Vitenzi: Kwa mfano:

Page 88: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

79

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

(i) Piga (Pig + a)

(ii) Napiga (Na + pig + a)

(iii) Anapiga (A + na + pig + a)

(iv) Walopigwa ( Wa + li + o + pig + w + a )

Baada ya mifano hiyo, tunaona hapa kuwa maneno haya yanaweza kuwekewa viamishi vya anina mbalimbali kutegemea na muktadha fulani na kanuni za lugha husika. Hapa tumegundua kuwa maneno katika lugha mbalimbali duniani, kwa kawaida huwa na sehemu kubwa mbili yaani:

1. Mizizi (roots/base form)

2. Viambishi (affixes)

Mizizi ya maneno

Mzizi wa neno fulani ni sehemu muhimu sana ya neno kama wanavyoeleza Richards et (1985) kuwa: Mziziwa neno ni mofimu ambayo ni sehemu ni sehemu muhimu zaidi ya neno ambayo katika lugh nyingi inaweza kukaa pekee yake kama neno kamili. Mizizi inaweza kuwekwa pamoja na kuunda neno. Hartman (1972) anafasiri mzizi ni mofimu fulani katika neno ambayo huwakilisha taarifa ya kileksika iliyo muhimu zaidi katika neno hilo tofauti na viambishi ambavyo hutumiwa kunyambua maneno na wakati wa kuunda maneno. Matei (2008) anasema kuwa mzizi ni umbo la kimsingi la neno ambalo haliwezi kuchanganuliwa au kugawika zaidi bila kupotosha maana na uamilifu wake wa kisarufi. Mzizi ndio hubeba maana ya kimsingi ya neno na kila neno huwa na mzizi.

TUKI (1990) wanasema kuwa mzizi ni sehemu ya neno ambayo haibadilikibadiliki. Kwa mfano, -pig- ni mzizi katika maneno pigana, pigwa, kupigwa. Kwa ujumla tunaweza kusema kuwa,

Page 89: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

Somo la Nne Error! No text of specified style in document.

80

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

mzizi ni umbo la kimsingi la neno ambalo haliwezi kuchanganuliwa/ kugawika zaidi bila kupotosha maana na pia nimzizi wa neno ni mofu ambayo ni sehemu muhimu zaidi ya neno na ambayo katika lugha nyingi inaweza kukaa pekee yake kama neno kamili. Mzizi ni tofauti na viambishi ambavyo hutumiwa kunyambua maneno na wakati wa kuunda neno.

Sifa za Mofimu

Matei (2008) anaainisha sifa zifuatazo za mzizi wa neno:

(a) Mzizi ni mofu muhimu zaidi kuliko mofu zingine zote katika neno. Sifa hii inadhihirika kwa kuzingatia ya kuwa mzizi wa neno huwa kama mhimili wa neno.

(b) Mzizi pia una uwezo wa kukaa peke yake kama neno kamili.

(c) Mizizi kadhaa inaweza kuwekwa pamoja kuunda mzizi changamano. Katika lugha ya Kiswahili kwa mfano, yapo maneno ambayo yameundwa kwa ktumia mizizi miwili au zaidi. Kwa mfano:

Neno Mzizi

(i) Mwanahewa {ana} +{ hewa}

(ii) Amiri jeshi {amiri} +{ jeshi}

(ii) Mwenyekiti {enye} + {kiti}

(d) Mzizi haubadilikibadiliki, kwa maana ya kuwa umbo la mzizi ni moja tu na haliongezeki wala kupungua. Kwa mfano, hapa tunaweza kutoa mifano michache ya mizizi ya maneno ya Kiswahili:

(i)-imb- anaimba, ataimba, hakuimba, uliimba

(ii) –chez- sichezi, hachezi, alicheza, chezeni

(iii)-j- alikuja, haji, siji, hakuja

(iv)-f- alikufa, hafi, hatufi, usife

(v)-kamat- nilimkamata, usimkamate, walikamatana, tukamatie

Page 90: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

81

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

(vi)-p- nilikupa, usinipe, sikukupa

(e) Mzizi ndiyo hubeba taarifa za kileksika

(f) Mzizi hauwezi kuachwa wakati wote neno linapotumika yaani linaweza kubadilika kulingana na matumizi.

Maumbo ya Mzizi

Mzizi unaweza kuwa na maumbo yafuatayo:

1. Mzizi inayofafana na herufi au fonimu, kwa mfano:{f} katika alikufa na sifi

2. Mizizi inayofafana na silabi, kwa mfano:

(i){-tu-} katika m + tu (mtu)

(ii) {–to} katika m + to (mto)

3. Mizizi ambayo ina silabi moja, mbili au hata tatu

(i) Chez- che + z silabi (1.5) ambapo z si silabi kamili

(ii) Sambaz- sa + mba+ z (2.5)

4. Mizizi ambayo ni maneno kamili. Kwa mfano: mama, halafu, sana n.k

Ndugu mwanafunzi, baada ya kupata maelezo, mafupi kuhusu maneno yanayoambishwa na yasiyoambishwa kwa kuzingatia kigezo cha mzizi, sasa na tufanye zoezi fupi kuhusiana na yale tuliojadili ili kupima maarifa yetu.

Page 91: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

Somo la Nne Error! No text of specified style in document.

82

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

ZOEZI

1. Toa mifano ya maneno yanayoambishwa kwa kuzingatia aina na makundi mbalimbali za maneno kama ilivyoanishwa hapo juu.

2. Taja sifa sita za mzizi wa neno na utoe maelezo mafupi na mfano katika kila sifa.

3. Onyesha kwa kupigia mstari viambishi katika maneno yafuatayo kwa kuzingatia elementi zilizoongezwa kwenye mzizi.

(i) -imb- anaimba, ataimba, hakuimba, uliimba

(ii) -chez- sichezi, hachezi, alicheza, chezeni

(iii)-j- alikuja, haji, siji, hakuja

(iv)-f- alikufa, hafi, hatufi, usife

(v)-kamat- nilimkamata, usimkamate, walikamatana, tukamatie

(vi)-p- nilikupa, usinipe, sikukupa

Njia Au Mbinu Za Uundaji Wa Maneno

Katika uundaji na ukuzaji wa istilahi na maneno katika lugha, zipo mbinu au njia mbalimbali ambazo hutumika. Matinde 2012: 110-124) anaainisha njia za uundaji wa maneno kama ifuatavyo:

1.Ukopaji

Hii ni njia ya kuchukua istilahi ya lugha fulani na kasha kuitumia kama istilahi katika lugha nyingine (Kiango, 2002). Kukopa ni mojawapo ya mbinu ya kiisimu ambayo hutumiwa na lugha zote ulimwenguni kuunda istilahi na maneno mapya ili kukidhi mawasiliano katika miktadha anuawai. Mbinu ya ukopaji inaweza kuwa ukopaji kwa tafsiri, utohozi na ukopaji sisi.Ukopaji unatokana na sababu zifautazo:

(i) Kuzuka kwa kitu au dhana ambayo haikuwepo katika jamii fulani

(ii)Kasumba ya wazungumzaji wa lugha kopaji

(iii)Mtaguso wa tamaduni mbili kwa muda mrefu.

Page 92: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

83

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

(iv)Utabaka jamii mbili ambazo nguvu za kisasa na kiuchumi hutofautiana

2.Ufupishaji

Ufupishaji ni mbinu ambayo hutokana na kitenzi ‘fupisha’ chenye maana ya kufanya kitu kiwa kifupi au kupnguza urefu wa kitu. Kuna mbinu mbalimbali ambazo zinatumika katika ufupishaji wa maneno ambazo ni:

(i)Upishaji mkato: Baadhi ya silabi au vipashio huondoshwa kabisa na kuacha tu sehemu ya neno asilia, kwa mfano, Des Salaam=Dar, Morogoro=Moro.a

(ii) Akronimu: Baadhi ya meneno hutokana naufupisho wa maneno asilia. Ufupisho huu hutumia herufi za kwanza katika kirai au kikundi cha maneno kuunda neno jipya, kwa mfano

Ukosefu wa Kinga Mwilini=UKIMWI

Chama cha Mapinduzi=CCM

(iii)Uhulutishaji: Mbinu hii hukaribiana na mbinu ya akronimu, tofauti ni kwamba viambishi au sehemu ya mwanzo ya neno huunganishwa na sehemu ya kwanza ya neno, la pili kuunda neno la msamiati mpya, kwa mafano:

Kifungu Asilia Neno Jipya

Chakula + jioni chajio

Bioloji + kemia biokemia

3.Uambatishaji

Uambatanishaji ni mbinu ambayo huhusisha kuunganishwa kwa maneno mawili kuunda neno moja jipya ambalo maana yake huwa tofauti na maneno ambayo yametumika kuunda neno hilo:

(a) Nomino +Nomino Neno Jipya

Bata + mzinga Batamzinga

Mwana + isimu Mwana isimu

Page 93: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

Somo la Nne Error! No text of specified style in document.

84

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

(b) Nomino + Kivumishi Neno Jipya

Pembe + tatu Pembetatu

Mbuzi + jike Mbuzijike

(c) Kitenzi + Nomino Neno Jipya

Chemsha + Bongo Chemshabongo

Fungua + Kinywa Funguakinywa

(d) Nomino + Kitenzi Neno Jipya

Nukta + tuli nukta tuli

Bongo + lala bongolala

(e) Kitenzi + Kielezi Neno Jipya

Ona + mbali Kionambali

Unga + mbali Ungambali

4.Unyambuaji

Unyambulshaji ni mbinu ya uundaji wa maneno mapya hivi kwamba viambishi mbalimbali huambikwa kwenye mzizi husika na kuunda neno jipya, kwa mfano;

Kutoakana na mzizi {–chez-} tunapata maneno: kucheza, mchezo, michezo, kuchezeana n.k

Kutokana na mzizi {–f-} tunapata maneno: kufa, kifo, kufariki n.k

5.Uradidi

Uradidi ni mbinu ya kuunda maneno ambayo sehemu ya neno lolote hurudiwarudiwa ili kuunda neno jipya au msisitizo fulani. Lengo kubwa la uradidi ni kusisitiza jambo au hali fulani. Kuna aina kuu mbili za uradidi yaani uradidi kamili na uradidi nusu.

(a) Uradidi Kamili: Huu ni uradidi ambao neno lolote hurudiwa. Kwa mfano:

(i)Peta-petapeta (ii)waya-wayawaya (iii)pole-polepole (iv) pili-pilipili

Page 94: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

85

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

(b) Uradidi nusu, kwa mfano

(i)pepeta (ii)babaika

6.Uhamishaji

Ni mbinu ya uundaji wa maneno ambao huhusisha upanuzi wa maana ya neno hupanuliwa na kurejelea dhana tofauti. Hata hivyo upanuzi huo huzingatia misingi iliyomo neno la kwanza na kujaribu kuzioanisha na maana, umbo, tabia na uamilifu wa neno la pili.

7.Ubunifu

Ubunifu ni mbinu ya kubuni misamiati na istilahi katika lugha husika na kurejelea dhana au vitu vipya ambavyo hapo awali havikuwepo katika jamii husika. Kuna njia kuu mbili za kubuni misamiati na istilahi mpya katika lugha ambazo ni (i) kubuni pasi na vigezo au kinasibu, (ii) kubuni kwa kuongozwa na vigezo maalum.

Page 95: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

Somo la Nne Error! No text of specified style in document.

86

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

Muhtasari wa Somo

Katika sura iliyopita tumezungumzia mofolojia ya Kiswahili sanifu na vipengele vyake muhimu. Vipengele vifuatavyo kama fasili za dhana mbalimbali za msingi za kimofolojia kama mofolojia, mofu, alomofu na mofimu, uhusiano wa mofu na mofimu, kubainisha mofu, njia za uundaji wa maneno vimejadiliwa kwa ufasaha.

Kwa ujumla moduli hii imefafanua maeneo mbalimbali yanayohusiana na lugha na sarufi, fonolojia ya Kiswahili na vipengele vyake na mofolojia ya Kiswahili sanifu. Kwa hiyo basi ni jukumu la msomaji kupitia maeneo hayo kwa ufasaha ili kuweza kuelewa kile kilichomo ili mwishoni mwa moduli hii mwanafunzi aweze kutoa fasili mbalimbali kuhusiana na dhana mbalimbali za msingi za kimofolojia kama vile mofolojia, mofu, alomofu na mofimu, viambishi, shina, mpllzizi, kubainisha uhusiano wa mofu na mofimu, kubainisha mofu katika lugha ya Kiswahili na kufafanua njia za uundaji wa maneno.

Zoezi la Somo

Jjibu maswali yote kwa kuandika ili kujipima uelewa wako, katika mada hii ya utumizi wa lugha.

Page 96: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

87

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

Marejeleo A: Fonolojia Chomsky, N na Morris Halle. (1968) Sound Pattern of English.

New York. Harper and Row. Crystal, D. (1971). Linguistics. Middlesex: Penguin. Goldsmith, J.A (1996) The handbook of Phonology. Cambridge,

Massachusetts : Blackwell Publishers Inc. Habwe, J. na Peter, K. (2004). Misingi ya Sarufi ya Kiswahili.

Nairobi: Phonix Hartman, R. (1972). Dictionary of Language and Linguistics.

London: Applied Science Publisher. Hyman, L. M (2003), “Segemental Phonology”, in Nurse, D. and

G. Philippson (eds.), The Bantu Languages, London: Routledge Publisher.

Marealle, I.B. (1978). “Dhana za Mofu, Mofimu na Alomofu” katika Mulika Na 13. Dar es Salaam: TUKI.

Massamba, D. P. B (2010), Phonological Theory: History and

Development, Revised Edition, Dar es Salaam, Institute of Kiswahili Studies, University of Dar esSalaam

Massamba, D. P. B., Y. M. Kihore na Y. P. Msanjila (2004),

Fonolojia ya Kiswahili Sanifu (FOKISA): Sekondari na Vyuo, Dar es Salaam, Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Massamba, D. P. B (2014) Misingi ya Fonolojia. Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Mgullu, R.S (1999) Mtaala wa Isimu: Fonetiki na Fonolojia ya

Kiswahili. Nairobi: Longhorn Publishers. Platt, J. (1985). A Dictionary of Applied Linguistics. Harlow

Longman. Trubetzkoy, N. (1939) Principles of Phonology. Berkeley:

California: University Press.

Page 97: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

Marejeleo Error! No text of specified style in document.

88

ELIMU HAINA MWISHO

TAA

SISI

YA ELIMU YA WATU W

AZIMA

U

Trudgil, P. (1980). Socialinguistics. Harmondsworth: Penguin. Weber, H (1985). A Dictionary of Phonetics and Linguistics.

London: Heinemann Educational Books. B: Mofolojia Anderson, S.R. (1992) Amorphous Mophology. Cambridge:

Cambridge University press Aronoff, M. (1976) Word Formation in Generative Grammar.

Cambridge , MA: MIT Britain. Habwe, J na Karanja, P (2004), Misingi ya Sarufi ya Kiswahili,

Fonolojia, Mofolojia, Sintaksia na Semantiki, Nairobi, Phoniex Publishers Ltd

Katamba, F (1993) Morphology: Macmillan Press Ltd. London Kihore, Y.M, Massamba, D.P.B na Msanjila, P.Y. (2009) Sarufi

Maumbo ya Kiswahili Sanifu. TUKI. Dar es Salaam. Matinde S.R (2012). Dafina ya Lugha Isimu na Nadharia: Kwa

Sekondari Vyuo vya Kati na Vyuo Vikuu. Mwanza: Serengeti Educational Publishers

Matei, A. K. (2008). Darubini ya Sarufi ya Kiswahili: Ufafanuzi

Kamili wa Sarufi. Nairobi: Phonix. Polome, E.C (1976) Swahili Language Handbook. Washington D.C

Centre for Applied inguistics. Rubanza, Y. I. (2003). Sarufi: Mtazamo wa Kimuundo. Dar es

Salaam: Chuo Kikuu Huria cha Tanzania. Spencer, A (1991) Morphological Theory: An Introduction to

Word Structure in Generative Grammar: Basil Blackwell. UK

Wahiga G. (2003) Sarufi Fafanuzi. Nairobi Longhorn Publishers

Ltd. Wesana-Chomi, E. (2003). Kitangulizi cha Mofolojia ya Kiswahili.

Sebha: Chuo Kikuu cha Sebha.

Page 98: Kuchambua Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili · ufafanuzi wa dhana ya lugha na sarufi, ufafanuzi wa fonetiki, ufafanuzi wa fonolojia ya Kiswahili; na ufafanuzi mofolojia ya Kiswahili

Kimeandaliwa na:Taasisi ya Elimu ya Watu WazimaS.L.P 20679, Dar es Salaam, TanzaniaSimu:+255 22 2150836 Barua pepe: [email protected], Tovuti: www.iae.ac.tz