kufanikisha - strategies for hopev kutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia, kimaadili, kiafya,...

48

Upload: others

Post on 02-Feb-2020

19 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: Kufanikisha - Strategies for Hopev Kutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia, kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendo madhara ... Mengi yanaweza kufanikiwa kwa kutaka, kunuia kwa dhati
Page 2: Kufanikisha - Strategies for Hopev Kutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia, kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendo madhara ... Mengi yanaweza kufanikiwa kwa kutaka, kunuia kwa dhati
Page 3: Kufanikisha - Strategies for Hopev Kutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia, kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendo madhara ... Mengi yanaweza kufanikiwa kwa kutaka, kunuia kwa dhati

KufanikishaMwongozo wa kuwasaidia waumini kufanya

shughuli zinazohusu VVU na UKIMWI

na Lucy Y. Steinitz

2

Page 4: Kufanikisha - Strategies for Hopev Kutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia, kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendo madhara ... Mengi yanaweza kufanikiwa kwa kutaka, kunuia kwa dhati
User
Typewritten Text
/ ISBN 978-1-905746-48-4 (E-book)
User
Typewritten Text
User
Typewritten Text
User
Typewritten Text
Page 5: Kufanikisha - Strategies for Hopev Kutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia, kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendo madhara ... Mengi yanaweza kufanikiwa kwa kutaka, kunuia kwa dhati

Shukrani . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .4

Utangulizi mfupi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .5

Utangulizi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .6

SEHEMU YA 1: TUMIA MUDA KUPANGA1.1 Jinsi ya kuanza . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .7

1.2 Jinsi ya kufanya upembuzi wa nje . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .9

1.3 Jinsi ya kufanya upembuzi wa ndani . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .10

1.4 Uchambuzi wa ‘SWOT’ ni nini? . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .12

SEHEMU YA 2: FANYA MAAMUZI YAKO2.1 Azimia mtazamo wako . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .15

2.2 Kukabiliana katika malengo na shughuli maalumu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .17

2.3 Muwe “SMART” (RUUUM) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .18

2.4 Jenga ushirikiano . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .19

2.5 Chagua kiongozi sahihi wa mradi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .20

SEHEMU YA 3: ANDIKA KWENYE KARATASI3.1 Tengeneza mpango wa kazi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .21

3.2 Jinsi ya kuandika mchanganuo wa kuomba fedha . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .24

3.3 Mfumo Mantiki ni nini? . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .25

3.4 Andaa bajeti na izingatie . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .27

3.5 Nini kinatokea baada ya fedha kwisha? . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .30

SEHEMU YA 4: ENDELEZA MWENDO4.1 Usiache mafunzo . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .31

4.2 Endelea kuwasiliana . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .32

4.3 Ufuatiliaji na Tathmini . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .32

SEHEMU YA 5: MASWALI YANAYOULIZWA MARA KWA MARAA Ni jinsi gani tutaweza kumchagua mwezeshaji bora wa kuwezesha mchakato wetu

wa kufanya maamuzi? . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .35

B Ni jinsi gani tutapata ushiriki mpana katika kutekeleza mradi mpya? . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .35

C Tufanye nini kama watu wanaogopa kufanya maamuzi? . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .36

D Ni jinsi gani tunaweza kushughulikia ukimya - au usemaji mno - kwa washiriki kwenyekikundi? . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .36

E Tunaweza kufanya nini kuzuia migogoro ndani ya usharika wetu? . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .37

F Tunawezaje kupata kanisa na jamii kwa upana kusaidia mradi wetu? . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .37

G Tutaweza kufanya nini kama tumekwisha kupanga kila kitu, lakini bado hatuna fedha? . . . . . . . . . .38

Kiambatanisho Na. 1: Mfano wa warsha . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .39

Kiambatanisho Na. 2: Jinsi ya kupanga muda . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .43

Kiambatanisho Na. 3: Vyanzo vinginevyo . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .44

Yaliyomo

Kufanikisha

Page 6: Kufanikisha - Strategies for Hopev Kutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia, kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendo madhara ... Mengi yanaweza kufanikiwa kwa kutaka, kunuia kwa dhati

www.stratshope.org4

KUFANIKISHA

Ningependa kuwashukuru watu mbalimbali na taasisi ambazo zimechangia kwa njia mmoja aunyingine kwenye mwongozo huu. Mawazo mengi, mazoezi na mbinu zilizomo zilijaribiwa na kutengenezwa na wafanyakazi na watu wa kujitolea wa Catholic AIDS Action wa Namibia ambakonilifanya kazi kama Mratibu wa Kitaifa toka 1998 hadi 2004 na kanisa la Namibia la Ushirikianokwa Yatima ambako nilikuwa mwanzilishi mwenza na mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini toka 2001hadi 2004. Michango mingine ya yaliyomo yalijitokeza wakati wa kazi yangu na mwajiri wangu wasasa, Family Health International, nchini Namibia.

Vifungu vingi ndani ya mwongozo huu vinaweza kupatikana katika maandiko mengine yanayohusumaendeleo ya taasisi, lakini vimeingizwa maalumu kwa ajili ya waumini wa makanisa na vikundividogo vidogo vya kijamii. Kwa ajili ya msaada wa kuyafanyia majaribio ya awali ya mambo yaliyomo katika mwongozo huu ninawiwa kuwashukuru mno:

Washiriki katika Kongamano la ufuatiliaji wa Kongamano lililofanyika huko Bangkok la Viongoziwa Dini Wanaoishi au Walioathiriwa Binafsi na VVU na UKIMWI, lililofanyika Mukono, Ugandamwezi wa Novemba 2004.

Wajumbe wa Mpango wa UKIMWI wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (ELCPA) lililoko hukoRehoboth, Namibia.

Wajumbe wa Kanisa la Imani ya Mitume lililoko huko Grootfontein, Namibia.

Kwa uhariri na msaada wakati wa kufanya majaribio ya awali ya mwongozo huu nchini Namibia,ningependa kuwashukuru wafanya kazi wenzangu, Nabil Robiati na Sonja Kotze wa Family HeaIthInternational, Namibia.

Family Health International pia ilisaidia mipango na uongozi wakati wa mchakato wa kufanyamajaribio ya awali, kama sehemu ya makubaliano ya ushirikiano na Wawakilishi wa Shirika laMaendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) chini ya Mpango wa Msaada wa Dharura wa UKIMWIwa Rais wa Marekani.

Lucy Y. Steinitz, PhDAfisa Ufundi Mwandamizi wa Mipango ya KiimaniFamily Health International, Namibia

Shukrani

Page 7: Kufanikisha - Strategies for Hopev Kutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia, kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendo madhara ... Mengi yanaweza kufanikiwa kwa kutaka, kunuia kwa dhati

5www.stratshope.org

UTANGULIZI MFUPI

Utangulizi MfupiKuhusu kitini cha TUMEITWA KUHUDUMIA

Miongoni mwa nchi nyingi duniani, makanisa na Wakristo binafsi wanaitikia wito wa Kristo‘mpende jirani yako kama nafsi yako’ kwa kufanyashughuli za kijamii kukabiliana na changamoto nyingi kuhusu VVU na UKIMWI.

Katika nchi za Afrika zilizopo kusini mwa Jangwa laSahara, mara nyingi makanisa yamekuwa mstari wambele katika jitihada za kuzuia madhara ya VVU naUKIMWI. Wanaonyesha kwa vitendo kwamba wame-jisikia ‘kuitwa kuhudumia’ kwa wale walioambu-kizwa au kuathiriwa na janga la VVU. Kwa mfano,wamefanikiwa kubuni njia za kufanya upatikanajiwa huduma muhimu za afya kwa watu wanaoishi naVVU, na kuwapa elimu, msaada wa kijamii na huduma za afya watoto yatima waliotokana naUKIMWI.

Hata hivyo, kwa ujumla Makanisa yamekuwahayafanyi vizuri sana katika kushughulikia matatizokama kujikinga na UKIMWI, unyanyapaa unaotokanana UKIMWI, aibu, ubaguzi, tamaduni na mambo yakijinsia yanayohusu tabia hatarishi za kujamiiana.Kukataa ukweli kuhusu VVU na UKIMWI ndani yajamii za kanisa kupo kwa kiasi kikubwa. Pamoja nakuwa kujamiiana ndio njia kuu ya kuenea kwa VVUmiongoni mwa nchi nyingi, ni mara chache sanainazungumzwa ndani ya kanisa kwa uwazi na katikahali isiyo ya kuhukumu.

Bado makanisa na asasi nyingine za kidini wanauwezo mkubwa wa kuwawezesha watu binafsi najamii kielimu, kimtazamo na kiujuzi na mikakatiwanayohitaji katika kushughulikia mambo yanayo-husu kujamiiana, jinsia, VVU na UKIMWI. Zaidi yayote, ongezeko la idadi ya viongozi wa dini wanao-fahamu uhitaji wa nguvu za pamoja za kushughu-likia masuala yanayoletwa na janga la VVU katikaupana, uelewa zaidi na uwazi, inazidi kukua.

Ili kusaidia juhudi hizi, Wadhamini wa Mikakati yaKuleta Matumaini wanatayarisha kitini chaTumeitwa Kuhudumia. Hii itajumuisha jumla yavijitabu vya miongozo inavyoelekeza kutendamambo yanayohusiana na VVU na UKIMWI kwa viongozi wa kanisa (waliobarikiwa na wasiobarikiwa)hasa walioko Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara.Mambo yatakayokuwa katika kitini cha TumeitwaKuhudumia yatatayarishwa ili kuwawezeshawachungaji, mapadre, watawa wa kike na wakiume, walei viongozi wa kanisa na waumini wao najamii ili waweze:

v Kutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia,

kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendo madharaya janga la VVU na wito wa Kikristo wa kuitikiakwa huruma.

v Kuushinda unyanyapaa, ukimwya, ubaguzikukataa, woga na kukataa kubadilika, haliambazo zinazuia kanisa na jamii katika kuka-biliana na mambo yanayohusu VVU na UKIMWIkwa ukamilifu zaidi.

v Kuwaongoza waumini wao na jamii katikamchakato wa kujifunza na kubadilika kupelekeakwenye matendo na mienendo ya kikanisa ilikuwasaidia watu binafsi, familia na jamii ilikupunguza kuenea kwa VVU na kupunguza athariza janga la VVU.

Kitini cha Tumeitwa Kuhudumia kitakuwa namachapisho mbalimbali yenye ukubwa na suratofauti tofauti, kwa matumizi ya vikundi vya kanisana jamii katika ngazi tofauti tofauti za uelewa nauzoefu kuhusiana na janga la VVU. Kitabu hiki, Na.2katika vitini hivi, ni mwongozo wa kuwasaidia waumini wa kanisa na vikundi kupanga na kufanyashughuli zinazohusu VVU na UKIMWI.

Vitini vingine vya Tumeitwa Kuhudumia, vitata-yarishwa katika kipindi cha 2005 - 2008. Hivivitakuwa juu ya masuala kama unyanyapaa naubaguzi, huduma ya kichungaji kwa watu wanaoishina VVU na UKIMWI, Mikakati ya mbinu za kujikingana VVU, kuishi kwa matumaini na VVU/UKIMWI, nakufanya kazi na vijana katika kujikinga na VVU.

Mradi wa Tumeitwa Kuhudumia unatekelezwa kupitia mchakato wa kimataifa, uwakilishi washirikisho la muungano wa kanisa, taasisi nyingineza kidini, jumuia za kanisa za kimataifa, na mitandao, wachapaji, wasambazaji na washika dauwengine.

Tunakukaribisha ushiriki katika TumeitwaKuhudumia, sio tu kwa kutumia yaliyomo kwenyekitabu hiki kwa waumini wako au jamii yako, balipia kwa kutuandikia kuhusu uzoefu wako, ambaotungependa kuuweka kwenye tovuti ya Mikakati yaKuleta Matumaini: www.stratshope.org.

Wenu katika imani na umoja,

Glen WilliamsMhariri wa MaandikoWadhamini wa Mikakati ya Kuleta Matumaini

Page 8: Kufanikisha - Strategies for Hopev Kutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia, kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendo madhara ... Mengi yanaweza kufanikiwa kwa kutaka, kunuia kwa dhati

www.stratshope.org6

KUFANIKISHA

Mungu anaweza kuhuisha imani na matendo yetu, lakini lazima tuchukue jukumu la binafsi kwayale tunayotenda - kama mtu mmoja mmoja na kwa ujumla wetu. Kama waumini wa kanisa aujamii tunaweza kujisikia ‘kuitwa kuhudumia’ watu walioambukizwa au walioathiriwa na VVU naUKIMWI. Lakini tunaweza kufanya nini kuwasaidia na kuwahudumia watu wa namna hii?Tunawezaje kukabiliana kwa mapana mambo yanayohusu kuzuia kuendelea kwa maambukizi zaidiya VVU? Jinsi gani tutalikabili jambo hili pana la kuzuia kusambaa zaidi kwa VVU? Na tunawezajekuwasaidia waumini wetu na jamii zetu kushughulikia mambo nyeti na yanayokera ya unyanyapaa,aibu, ubaguzi na kukataa kuhusu VVU na UKIMWI? Kama wewe ni kiongozi wa kanisa, unafahamukwamba watu wengi wanakutegemea uwe na majibu kwa maswali haya.

Mwongozo huu umetayarishwa kukusaidia wewe na waumini wako kukabiliana na mambo haya.Hatua kwa hatua, tutapitia michakato mbalimbali itakayokuwezesha kukuza na kutekeleza miradiinayokabili baadhi ya changamoto za VVU na UKIMWI. Kadri tunavyofanya hivyo utagundua kwamba sio michakato yote iliyoelezwa humu itafaa kwa waumini au kikundi cha kanisa lako.Hivyo basi inakupasa kuchagua na kuchukua unayoyaona yanawahusu na ni ya kukusaidia wewe,waumini au kikundi cha kanisa lako kwa wakati huu.

Kati ya hatua mmoja muhimu sana kwa kila mmoja anayetaka kuanza shughuli ya kijamii ni kutu-mia muda KUPANGA! Hapa ndipo tutaanzia.

Kuanza mradi ni sawa na kazi ya kupanda…

` KKwwaannzzaa iinnaakkuubbiiddii uuaammuuee nnii wwaappii uuttaappaannddaa,,kkwwaa hhiiyyoo uunnaahhiittaajjii kkuucchhuunngguuzzaa uuddoonnggoo nnaahhaallii yyaa kkiimmaazziinnggiirraa..

` HHaallaaffuu iinnaakkuubbiiddii uuaammuuee uunnaacchhoottaakkaa kkuuppaannddaa.. JJee nnii mmttii??,, AAiinnaa ffuullaannii yyaa mmaauuaa??ZZaaoo llaa cchhaakkuullaa?? JJiibbuu lliittaatteeggeemmeeaa mmaahhiittaajjiiyyaakkoo nnii nniinnii nnaa ppiiaa aaiinnaa yyaa uuddoonnggoo uulliioonnaaoo..

` HHaattaa hhiivvyyoo,, mmaarraa uukkiiiisshhaa kkuuppaannddaa,, hhuuwweezziiuukkaaaacchhaa kkuuffaannyyaa kkaazzii..

` KKiillaa mmbbeegguu llaazziimmaa iiaannggaalliiwwee,, nnaa kkiillaa mmmmeeaallaazziimmaa uuttuunnzzwwee.. HHuuuu nnii mmcchhaakkaattoo eennddeelleevvuu,,nnaa uunnaahhuussiisshhaa rraattiibbaa mmaaaalluummuu yyaa uummwwaaggiillii--aajjii,, kkuuwweekkaa mmbboolleeaa nnaa kkuuppaalliilliiaa.. HHaappoo nnddiippoouunnaawweezzaa uukkaaaannzzaa kkuuoonnaa mmaattuunnddaa yyaa kkaazziiyyaakkoo..

Utangulizi

Page 9: Kufanikisha - Strategies for Hopev Kutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia, kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendo madhara ... Mengi yanaweza kufanikiwa kwa kutaka, kunuia kwa dhati

7www.stratshope.org

TUMIA MUDA KUPANGA

Sehemu ya 1

Tumia mudakupanga1.1 Jinsi ya Kuanza

&‘Atakayelitafakari nenoatapata mema; Na kila amwa-miniye Bwana ana heri.’– Mithali 16:20

Mengi yanaweza kufanikiwa kwa kutaka, kunuia kwa dhati na kujitolea kwa walio namuda na nguvu ya kujitoa kwa ajili ya shughuli za kusaidia jamii zao. Lakini kamashughuli hizi hazijajadiliwa ipasavyo na kufikiria vizuri kabla ya kuanza zinaweza kuwangumu sana. Pamoja na makusudi mazuri sana, walengwa hao hao waliokusudiwa kusaidiwa wanaweza kukataa, viongozi wa jamii pia wanaweza kuzipinga; au wanawezakuishiwa fedha. Bila shaka wote tumeshapata uzoefu wa jinsi hii wa mawazo ya mudamfupi, mwisho wake unapoteza thamani ya muda wetu na maliasili zetu.

Hivyo basi, miradi yote na taasisi zote lazimaziendelee katika mzunguko wa kupanga,kutekeleza na kutathmini (Angalia Mzungukowa Mradi hapa chini).

Mzunguko huu unaweza kutumika kipekee kwakila mradi, au kwa taasisi nzima kwa ujumla.Katika hali ya mradi kuwa mkubwa au unaohu-sisha idara nyingi au mchakato wa kitaasisi,huu kwa kawaida huitwa mpango mahususi(angalia kisanduku cha 1a uk wa 8).

Wakati mwongozo huu unaangalia kimsingikatika kupanga na kutekeleza mradi mmoja,kanuni hizo hizo zinaweza pia kutumikawakati wa kupanga mpango mahususi kwa ajiliya taasisi yote kwa ujumla.

Kuamua juu ya mtazamo wa mradi wenu, nilazima kwanza ukusanye washika dau muhimu,ili kufanya uchambuzi yakinifu. ‘Washika dau’ni wale watu walio ndani na nje ya kanisa lenuambao ni muhimu kuwaomba ushauri katika

Mzunguko wa Mradi

CHAMBUENI HALIYENU NA KUPANGA

MRADI WENU

TATHMINI MRADINA MPENDEKEZE

MABORESHO

TEKELEZENI MRADI WENU

Page 10: Kufanikisha - Strategies for Hopev Kutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia, kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendo madhara ... Mengi yanaweza kufanikiwa kwa kutaka, kunuia kwa dhati

www.stratshope.org8

KUFANIKISHA

Kisanduku cha 1a: Mpango Mahususi

WWaakkaattii mmwwiinnggiinnee uuttaassiikkiiaawwaattuu wwaakkiizzuunngguummzziiaa ‘‘mmaaoonnoo’’,,‘‘mmaalleennggoo’’ nnaa ‘‘tthhaammaannii yyaaaassaassii’’,, mmiissaammiiaattii hhiiii iinnaaoo--nnyyeesshhaa jjiinnssii ttaaaassiissii iinnvvyyoojjiioonnaannaa jjiinnssii iinnaavvyyoohhiittaajjii kkuueennddeelleeaammbbeellee.. IIkkiihhuussiisshhaa hhaassaa::

¶MMaaoonnoo -- TTuummaaiinnii aammbbaalloottaaaassiissii yyeennuu iinnaalliittaakkaa hhuukkoommbbeellee

¶LLeennggoo -- UUtthhaammaannii wwaaTTaaaassiissii yyeennuu aauu mmwwoonnggoozzoowwaa ttaarraattiibbuu,, nnaa uuttooffaauuttii nnaawweennggiinnee.. KKiittuu ggaannii kkiinnaa--cchhoowwaaffaannyyaa mmaaaalluummuu nnaattooffaauuttii nnaa wweennggiinnee??

¶MMppaannggoo -- JJiinnssii mmnnaavvyyoo--jjaarriibbuu kkuukkaaaa kkwweennyyee

mmaalleennggoo yyeennuu,, iillii kkuuffiikkiiaammaaoonnoo yyeennuu..

NNjjiiaa nnyyiinnggiinnee yyaa kkuueelleewwaa hhiilliinnii kkuuppiittiiaa mmffaannoo uuffuuaattaaoo.. JJeeuummeesshhaawwaahhii kkuujjaarriibbuu kkuusshhiikkaaffiimmbboo yyaa uuffaaggiioo kkwwaa kkiiddoolleekkiimmoojjaa?? KKaammaa bbaaddoo,, uunnggee--jjaarriibbuu.. UUttaagguunndduuaa kkwwaammbbaa nniirraahhiissii ssaannaa kkuulliinnggaanniisshhaa mmiizzaa--nniiaa kkwwaa kkuuttaazzaammaa nncchhaa yyaaffiimmbboo nnaa ssiioo kkwweennyyee kkiiddoolleecchhaakkoo.. KKwwaa mmaanneennoo mmeennggiinnee,,iinnaakkuuppaassaa ssiikkuu zzoottee kkuuaannggaalliiaakkiilleellee cchhaa kkiittuu nnaa kkuuwwaa nnaammaaoonnoo mmaaiisshhaannii.. KKaattiikkaammffaannoo hhuuuu,, mmaaoonnoo nnii nncchhaa yyaaffiimmbboo,, nnaa ffiimmbboo yyaa uuffaaggiioo nniilleennggoo llaakkoo,, nnaa mmppaannggoo wwaakkoonnii kkuuttaazzaammaa jjuuuu nnaa wwaallaa ssiioocchhiinnii..

KKuuffiikkiiaa uueelleewwaa wwaa kkiittaaaassiissii wwaammaammbboo hhaayyaa,, kkwwaa kkaawwaaiiddaaiinnaaffaannyyiikkaa kkuuppiittiiaa mmcchhaakkaattoowwaa mmppaannggoo mmaahhuussuussii.. HHiiii kkwwaakkaawwaaiiddaa iinnaacchhuukkuuaa ssiikkuu kkaaddhhaaaa,, mmaajjuummaa aauu hhaattaammiieezzii..

IIwwaappoo ttaaaassiissii yyeennuu ttaayyaarrii iinnaauuffaahhaammuu wwaa kkuujjiittaammbbuuaa kkwwaauuwwaazzii,, iinnaa mmaakkuussuuddii nnaammwweelleekkeeoo,, iinnaawweezzaa kkuuwwaa ssiioollaazziimmaa kkuuffaannyyaa zzooeezzii llaa mmppaann--ggoo mmaahhuussuussii.. IIllaa kkaammaa ssiioohhiivvyyoo,, bbaassii mmnnaawweezzaa kkuuoonnaammaannuuffaaaa yyaa kkuuffaannyyaa zzooeezzii llaammppaannggoo mmaahhuussuussii kkaabbllaa yyaakkuuaannzzaa mmrraaddii mmppyyaa,, kkaammaa vviilleemmrraaddii kkuuhhuussuu VVVVUU nnaaUUKKIIMMWWII..

mchakato wenu wa kupanga. Kwa mfano,mnaweza kuwahusisha wafanyakazi wa ofisikanisani, wazee, viongozi wa vijana, aumaafisa muhimu katika jamii yenu ambao naopia ni waumini wa kanisa.

Makanisa mengi na asasi za kidini wanapende-lea kufanya mchakato huu wa kupanga kwakuwahusisha washika dau wote muhimu kwakupitia mikutano na warsha mbalimbali. KatikaSehemu ya 5, swali A, la mwongozo huu utakuta mapendekezo ya aina ya watu ambaowatafaa kuwezesha mikutano au warsha hizi.

Hatua mbali mbali mtakazopitia katikamchakato wa kupanga, zitawasaidia kuelewamatatizo ambayo jamii yenu inakabiliana nayo,na nini kanisa lenu linaweza kufanya ili kuletamabadiliko. Hii inaanza kwa upembuzi watatizo, mnafikiria mambo yaliyo NJE ya kanisalenu (yaani ndani ya jamii) vile vile na mambo

NDANI ya kanisa lenu (kama vile jinsi mnavyo-endesha mambo yenu. Baadaye mnaweza kuhi-taji kuthibitisha uthamani wenu, kwa mfano,kuweka wazi kwamba kila kitu mnachofanya nilazima kioane na mafundisho ya Kikristo, kamayanavyotafsiriwa na kanisa au dhehebu lenu.Hivyo upembuzi wa tatizo unawahitajimchukue hatua zifuatazo:

Kwanza, upembuzi wa nje, kutambua niniKINAHITAJIKA kufanyika;

Pili, upembuzi wa ndani, kutambua niniKINAWEZA kufanyika; na

Tatu, mchakato wa kufanya maamuzi, kufuatahayo hapo juu na kuzingatia uthamani wataratibu za kanisa lenu na utamaduni wamahali hapo mlipo, kuamua MNAPANGAkufanya nini.

Page 11: Kufanikisha - Strategies for Hopev Kutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia, kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendo madhara ... Mengi yanaweza kufanikiwa kwa kutaka, kunuia kwa dhati

9www.stratshope.org

TUMIA MUDA KUPANGA

1.2 Jinsi ya kufanya upembuzi wa njeKutegemea na kiasi cha habari ulizonazo kuhusu athari za janga la VVU na UKIMWI katikajamii yako, na kiasi cha habari mpya unayodhani unahitaji, unaweza ukatia juhudi kubwaau kidogo katika uchambuzi wa nje. Hapa kuna aina mbili za utafiti mnazoweza kufanya:

t Utafiti wa nyumba kwa nyumba, katikajamii, ambapo mkusanyaji habari anaulizawatu kadhaa aina sawa ya maswali yaliyo-kwisha kuandaliwa kuhusu mahitaji mbali-mbali ambayo bado hayajafikiwa kwenyejamii. Pia ni lazima muwaulize wanacho-dhani kanisa lingefanya kushughulikia mahi-taji hayo. Kutegemea na jamii yenu,mnaweza kuuliza watu wachache tu (kwamfano 30) au wengi zaidi (kama 200 auzaidi) au katikati ya namba hizo mbili. Watumnaowauliza wajibu maswali haya wanaitwa ‘watoa majibu’.

t Watoa habari muhimu; ‘watoa habarimuhimu’ ni watu ambao maoni yao mnaya-thamini kwa sababu ya nafasi zao maalumukatika jamii. Mnaweza kuwauliza aina hiyohiyo ya maswali kama ambavyo mngependakufanya katika utafiti wenu wa nyumba kwanyumba. Watoa habari muhimu ambaomngewahusisha ni viongozi wa kijamii wahapo, kama wakuu wa kaya wa jadi, viongozi wa kanisa toka madhehebumengine, na wawakilishi kutoka asasi zisizoza kiserikali (NGOs) za hapo na serikali pia.

Kabla ya kwenda kuanza mahojiano, mtahitajikuandaa orodha ya maswali (angalia kisandukucha 1b) ambayo yatawasaidia kukusanya habarikuhusu jinsi VVU na UKIMWI unavyoathiri jamiiyenu. Mtahitaji madaftari ya kuandikia nakalamu.

Mnaweza kuhitaji kukusanya habari kwa njianyingine mbili, ambazo ni:

t Habari za kitakwimu juu ya athari ya VVUna UKIMWI katika eneo lenu, ambazomnaweza kuzipata kutoka serikalini kwenyeMpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI, asasizisizo za kiserikali za hapo (NGOs), auMashirika ya Umoja wa Mataifa. Kwa kawaida mambo mawili yanayotoa kipimocha masuala haya ni: idadi ya watu wenyemaambukizi ya VVU na idadi ya yatima

wanaoishi jirani, kijijini, mjini, mkoani aunchini. (Idadi ya walioambukizwa VVU ina-maanisha ni asilimia ya watu wazima - maranyingi walio kati ya miaka 15 na 49, ambaowana uambukizo wa VVU. Nchi nyingizinakadiria idadi hiyo kwa kuwakadiriaakina mama wajawazito kwa mwaka au kila

Kisanduku cha 1b: Mfanowa upembuzi wa nje

MMaasswwaallii yyaa mmaahhoojjiiaannoo yyaaffuuaattaayyoo yyaannaawweezzaakkuuttuummiikkaa kkuuuulliizzaa wwaattuu yyaallee wwaannaayyoooonnaa kkaammaammaahhiittaajjii mmaakkuubbwwaa aammbbaayyoo hhaayyaajjaaffiikkiiwwaa kkaattiikkaajjaammiiii,, nnaa nniinnii kkiinnaawweezzaa kkuuffaannyyiikkaa iillii kkuubboorree--sshhaa hhaallii hhiiyyoo.. MMnnaawweezzaa ppiiaa kkuubbaaddiilliisshhaa sswwaalliiaauu kkuuoonnggeezzaa lliinnggiinnee jjiippyyaa iillii kkuukkiiddhhii mmaazziinnggii--rraa yyeennuu..

11.. NNii ttaattiizzoo ggaannii kkuubbwwaa uunnaalloooonnaa lliinnaaiikkaabbiilliijjaammiiii hhiiii??

22.. UUnnaaddhhaannii nnii nniinnii cchhaannzzoo kkiikkuubbwwaa cchhaa ttaattiizzoo hhiillii??

33.. UUoonnaavvyyoo wweewwee,, nnii mmaaddhhaarraa ggaannii ttaattiizzoo hhiilliilliimmeelleettaa kkwweennyyee jjaammiiii yyeennuu??

44.. KKiippeekkeeee nnii jjiinnssii ggaannii ttaattiizzoo hhiillii lliimmeekkuuaatthhiirriiwweewwee nnaa ffaammiilliiaa yyaakkoo??

55.. NNii kkwwaa kkiiwwaannggoo ggaannii,, kkaammaa kkiippoo,, uunnaaddhhaanniiVVVVUU nnaa UUKKIIMMWWII uunnaaffaannyyaa ttaattiizzoo hhiilliikkuuwwaa kkuubbwwaa zzaaiiddii??

66.. JJee uunnaaddhhaannii nnii nniinnii kkaanniissaa llaa hhaappaa lliinnaawweezzaakkuuffaannyyaa kkuubboorreesshhaa hhaallii hhiiii??

77.. JJee uunnaawweezzaa kkuuttooaa mmaappeennddeekkeezzoo kkaaddhhaaaajjiinnssii yyaa kkuutteekkeelleezzaa hhaayyaa mmaabboorreesshhoo??

88.. NNii nniinnii cchhaa zzaaiiddii -- wweewwee bbiinnaaffssii -- uunnaawweezzaakkuuffaannyyaa kkuussaaiiddiiaa jjaammiiii yyaakkoo kkuusshhuugghhuulliikkiiaammaattaattiizzoo yyaannaayyoossaabbaabbiisshhwwaa nnaa VVVVUU nnaaUUKKIIMMWWII??

Page 12: Kufanikisha - Strategies for Hopev Kutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia, kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendo madhara ... Mengi yanaweza kufanikiwa kwa kutaka, kunuia kwa dhati

www.stratshope.org10

KUFANIKISHA

miaka miwili.) Habari za kitakwimu zanyongeza zinaweza kupatikana katika mta-ndao - kwenye baadhi ya mitandao muhimu,tafadhali angalia kiambatanisho 3.

t Ramani ya eneo la jamii ni chombo kina-choonekana cha kuwasaidia watu kuta-thmini matatizo na rasilimali katika jamiiyao. Ni mchakato wa kufurahisha kwenyekikundi, pale ambapo watu wanachoraramani ya eneo la jamii yao na kuwekaalama muhimu ambazo zitawasaidia

kutambua rasilimali za mahali hapo, fursa,vitishio na changamoto. Haijalishi ramanihiyo imechorwa kwa ufanisi au kwa usahihigani. Wazo ni kwamba kwa kuchora taasisimuhimu kama shule, kliniki, baa, na soko,majadiliano huchochewa katika baadhi yamambo yanayohusu VVU na UKIMWI.Kuchora ramani ya eneo la jamii ni jambomuhimu wakati mnapojaribu kutambua rasilimali za hapo hususani watu na taasisi,ambazo zinaweza kuwasaidia katikakutekeleza mradi mpya.

Ramani ya eneo la jamii

1.3 Jinsi ya kufanya upembuzi wa ndaniKatika upembuzi wa ndani, mnajaribu kukagua uwezo na udhaifu ndani ya kanisa lenu, napia rasilimali na uwezo wake. Kusema ‘raslimali’ tunamaanisha sio tu pesa lakini pianafasi ya ofisi, usafiri, chakula na muda wa wenye kujitolea. Kusema ‘uwezo’ tunamaa-nisha ujuzi na uzoefu wa watu waliomo kwenye kanisa lenu au jamii.

Wajumbe wengi wa kanisa na jamii wanaaminikuwa wao ni maskini sana kwamba hawawezikuwa na chochote cha kutoa kwa kuanzishamiradi mipya kama mradi wa VVU na UKIMWI.Japokuwa hili ni la nadra sana. Makanisa mengiyana nafasi kubwa ya raslimali na uwezo wawatu kuliko wanavyadhani wenyewe. Pamojana fedha, wanaweza mara kwa mara kutoa aina

ya raslimali na uwezo, ambao hawana haja yakulipia (angalia kisanduku cha 1c).

Upembuzi wa ndani mara nyingi unafanyikakama mchakato wa kikundi, pale ambapomnakusanyika pamoja wale watu wa kanisalenu ambao wanajua vizuri, na ambao msaadawao mnauhitaji katika mchakato wa kupanga.

Page 13: Kufanikisha - Strategies for Hopev Kutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia, kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendo madhara ... Mengi yanaweza kufanikiwa kwa kutaka, kunuia kwa dhati

11www.stratshope.org

TUMIA MUDA KUPANGA

Kisanduku cha 1c: Aina za rasilimali na ujuzi

HHiizzii hhaappaa nnii bbaaaaddhhii yyaa aaiinnaa zzaarraassiilliimmaallii nnaa uuwweezzoo aammbbaaoowwaasshhaarriikkaa wwaa kkaanniissaa lleennuu aauukkiikkuunnddii wwaannaawweezzaa kkuuwwaa nnaaffuurrssaa nnaavvyyoo::

☺ WWAATTUU:: WWaannaacchhaammaa wwaauusshhaarriikkaa wweennuu wwaannaa uuzziittoowwaa tthhaammaannii kkaammaa yyaa ddhhaa--hhaabbuu!! BBaaaaddhhii yyaaoo wwaannaawweezzaakkuuwwaa nnaa uujjuuzzii mmaaaalluummuu,,kkwwaa mmffaannoo,, kkaattiikkaa uuttaawwaallaawwaa ffeeddhhaa,, uuuugguuzzii,, uusshhaauurrii--nnaassaahhaa aauu hhaattaa kkaattiikkaakkuuwweezzeesshhaa mmiikkuuttaannoo aauummaaffuunnzzoo yyaa wwaarrsshhaa..WWeennggiinnee wwaannaawweezzaa kkuuwwaannaa uujjuuzzii wwaa vviitteennddoo,, kkaammaavviillee kkuuwweezzaa kkuuppiikkiiaa kkuunnddiikkuubbwwaa llaa wwaattuu,, kkuutteennggeenneezzaa

nnaa kkuuttuunnzzaa bbuussttaannii,, aauukkuuaannddaaaa mmaakkaammbbii yyaavviijjaannaa..

☺ NNAAFFAASSII:: KKaanniissaa lleennyyeewweeaauu mmuuuummiinnii wwaa uusshhaarriikkaaaannaawweezzaa kkuuwwaa nnaa aarrddhhii kkwwaaaajjiillii yyaa bbuussttaannii yyaa jjaammii aauunnaaffaassii kkwwaa aajjiillii yyaa ooffiissii..MMiikkuuttaannoo iinnaawweezzaa kkuu--eennddeesshhwwaa ((ppaassiippoo gghhaarraammaa))kkaattiikkaa mmaajjeennggoo yyaa kkaanniissaalleennyyeewwee..

☺ TTAAAASSIISSII WWAASSHHIIRRIIKKAA::TTaaaassiissii kkaammaa zziillee zziissiizzoo zzaakkiisseerriikkaallii zzaa mmaahhaallii hhaappoo((NNGGOOss)),, zzaa kkiimmaattaaiiffaa nnaavvyyoommbboo vvyyaa kkiisseerriikkaalliizziinnaawweezzaa kkuuttooaa mmaaffuunnzzoo,,

vviiffaaaa vvyyaa hhaabbaarrii,, sseehheemmuu zzaakkuuffaannyyiiaa mmiikkuuttaannoo nnaammssaaaaddaa wwaa kkiiffeeddhhaa..MMaasshhuullee yyaannaawweezzaa kkuuttooaasseehheemmuu zzaa kkuuffaannyyiiaa mmiikkuu--ttaannoo nnaa wwaattuu wwaalliioo ttaayyaarriikkuujjiittoolleeaa.. BBiiaasshhaarraa zzaammaahhaallii hhaappoo ((kkwwaa mmffaannoo;;sseehheemmuu zzaa kkuuookkeeaa mmiikkaatteennaa mmaassookkoo)) wwaannaawweezzaakkuuttooaa cchhaakkuullaa hhaattaa mmssaaaaddaawwaa kkiiffeeddhhaa ppiiaa..

KKUUMMBBUUKKAA:: SSiikkuu zzoottee aannzzaa nnaarrssiilliimmaallii zzaa mmaahhaallii hhaappoo kkwwaannzzaa -- kkwwaa kkiillee aammbbaacchhoottaayyaarrii kkiippoo kkaattiikkaa jjaammiiiiii yyeennuuaauu jjiirraannii..

Hapa kuna aina mbili za michakato ya kufikiriawakati wa kuanza utekelezaji:

¸ Kuchangia mawazo ni mjadala makini wawazi na endelevu ili kuibua mawazo aukutatua matatizo. Mawazo yoteyanakaribishwa. (Mwezeshaji awe makiniasikosoe wazo lolote, au kuchukuliwaupande mmoja kwa kujadili mbivu nambichi za mapendekezo ya mmoja wawachangiaji). Kipindi cha kuchangia mawa-zo lazima kianze na swali: Ni vitu gani borakuhusu kanisa letu ambavyo vinawavutiawatu kuwa waumini au kushiriki kila wakati?Baadaye unaweza kuuliza kitu kama, ‘Nibaadhi ya vitu gani vinavyowafanya watuwachanganyikiwe au kuwazuia wasijekanisani?’ Bado swali linalofuata lawezakuwa, ‘Sasa kwa vile tunajua baadhi yauwezo wetu na mapungufu yetu, tunawezakufanya nini kusaidia kanisa letu kuwaimara?’

Wakati mkiendelea kuchangia mawazo,andika majibu wanayotoa watu kwenyeubao au karatasi ngumu, ili kwamba kilammoja aweze kuona. Zungumza kuhusumawazo gani ni ya msaada. Baada ya

majadiliano kadhaa, amua majukumu yamkutano ujao.

¸ Kikundi cha malengo ni njia ambayo kikundi kidogo cha watu kinakaribishwakwenye mkutano ili kutoa michango yao juuya jambo fulani. Tofauti kubwa ya kikundicha malengo ukilinganisha na cha kuchangiamawazo ni kwamba ni lazima uamue mapema ni mambo gani maalumu mnatakamjadiliane. Watu unaowachagua wahu-dhurie kwenye kikundi cha malengo ni lazima wawe na taarifa, ni vitu gani vinafaakusema juu ya jambo lililochaguliwa.Unaweza kuchagua jambo kwa mfano, nijinsi gani usharika wetu unavyoshughulikiaunyanyapaa kwa watu wenye VVU naUKIMWI? Unaweza kukaribisha viongozi wakanisa, na pia watu ambao unajua wanamaambukizi au wameathiriwa na VVU nawako tayari kuzungumza wazi wazi kuhusujambo hilo. Pamoja na kikundi cha malengo, lazima uwe na mwezeshajimwenye ujuzi ambaye anahakikisha kuwakila aliyealikwa anapata nafasi sawa yakuzungumza, na anayeweza kuelekezamwelekeo wa majadiliano ili kufikia uamuziau mambo muhimu ya kukubaliana.

Page 14: Kufanikisha - Strategies for Hopev Kutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia, kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendo madhara ... Mengi yanaweza kufanikiwa kwa kutaka, kunuia kwa dhati

www.stratshope.org12

KUFANIKISHA

Katika uchambuzi wa ‘SWOT’, majadiiliano lazima yaelekezwe kwa usharika wa kanisalenu au kikundi chenu - sio taasisi nyingine aukwa upana wa jamii. Njia mojawapo rahisi yakufanya uchambuzi wa ‘SWOT’ ni kuwaulizawashika dau wenu kutambua, kwanza uwezo,na mapungufu ya taasisi (ambayo ni ya ndani),na halafu fursa na changamoto wanazoziona(ambazo ni za nje).

Kuhakikisha kuwa sauti ya kila mmoja ina-sikika, wawezeshaji wengi hupenda kuulizawashiriki wajibu maswali haya binafsi kwanza.Washiriki wanafanya hivyo kwa kuandikamajibu yao kwenye vipande vidogo vya

1.4 Uchambuzi wa ‘SWOT’ ni nini?Njia ya kawaida ya kuendesha ukaguzi wa kitaasisi ni kufanya uchambuzi wa ‘SWOT’.Hapa unaangalia kwa pamoja ukaguzi wa ndani na wa nje kwa wakati mmoja. ‘SWOT’inasimama badala ya:

S Uwezo (Strength)

W Mapungufu (Weakness)

O Fursa (Opportunity)

T Changamoto (Threats)

UWEZO MAPUNGUFU

FURSA CHANGAMOTO

~~~

~~~

~~~

~~~

Chati Na. 1 ya ‘SWOT’

Page 15: Kufanikisha - Strategies for Hopev Kutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia, kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendo madhara ... Mengi yanaweza kufanikiwa kwa kutaka, kunuia kwa dhati

13www.stratshope.org

TUMIA MUDA KUPANGA

karatasi au ‘stika’, na baadaye kuvikusanyapamoja na majibu ya kikundi cha washirikiwengine kwenye jedwali kubwa, ubaoni aukwenye kipande cha karatasi (angalia ‘SWOT’iliyopendekezwa katika Chati Na. 1 uk. 12)

Kwa kuendeleza mtiririko, unaweza kuwaombawashiriki watambue Uwezo na Mapungufukwanza, na baadaye kujadili haya, kabla yakuendelea na mchakato wa aina hiyo hiyokuhusu Fursa na Changamoto.

Sasa, angalia kila mmoja alichoandika kwenyekila kisanduku (Uwezo, Mapungufu, Fursa naChangamoto) na angalia mambo gani, na mae-neo yapi ya makubaliano yamejitokeza.

Baada ya kuwa na majadiliano kadhaa,unaweza kufanya Chati Na. 2 ya ‘SWOT’, nabaadaye fikirieni jinsi gani mnaweza kukuzauwezo, kutumia fursa mlizonazo, kuboreshamapungufu yenu na kudhibiti changamoto.Hivyo mtachora tena chati yenu ya ‘SWOT’, na kuweka vichwa vipya (angalia Chati Na. 2 ya‘SWOT’) na waulize washiriki waweke mape-ndekezo yao kwenye visanduku husika.

Jinsi ya kutafsiri matokeo yenu

Sasa waulize washiriki waelezee jinsi ganiwangefupisha majibu tofauti tofauti ya ‘SWOT’yaliyowekwa ukutani au kwenye chati kubwa.

Majibu kadhaa yaweza kuwa sawasawa, iki-maanisha kwamba watu wanafikiri mambohayo ndiyo muhimu zaidi. Wakati majadilianoyanaendelea, ni mahitimisho gani mnayowezakuyafikia?

Kama tafsiri yenu ya Chati Na. 1 ya ‘SWOT’inaonyesha nguvu zaidi za Uwezo na Fursa,basi, sasa mko tayari kukua, ikihusisha mradimpya. Iwapo Uwezo na Changamoto vinaji-tokeza kama vitu vikubwa, ndipo mtahitajikutumia sehemu ya Uwezo wenu kushughulikiaChangamoto kabla ya kuanza mambo mapya.Muunganiko wa Mapungufu makubwa na Fursa

Kisanduku cha 1d: Vidokezo vya kuendeshauchambuzi wa SWOT

r KKaammaa wwaattuu ssiioo wwaazzooeeffuu wwaajjiinnssii yyaa kkuuffaannyyaa uucchhaammbbuuzziiwwaa ‘‘SSWWOOTT’’,, wwaakkuummbbuusshheekkuuwwaa hhaakkuunnaa jjiibbuu ‘‘ssaahhiihhii’’aauu ‘‘lliissiilloo ssaahhiihhii’’.. IIssiippookkuuwwaauunnaajjaarriibbuu kkuuaammsshhaa aakkiilliizzaaoo kkuuppaattaa mmaawwaazzoo nnaammaaoonnii yyaaoo..

r PPeennddeekkeezzaa kkwwaa wwaasshhiirriikkiikkwwaammbbaa iinnggeekkuuwwaa nnaa

mmaannuuffaaaa kkuulliittaazzaammaa kkaanniissaallaaoo kkaammaa ttaaaassiissii -- ssiioo kkaattiikkaaiimmaannii yyaakkee bbaallii kkaattiikkaa jjiinnssiilliinnaavvyyooffaannyyaa kkaazzii zzaa ssiikkuuhhaaddii ssiikkuu..

r KKuuwwaassaaiiddiiaa wwaasshhiirriikkiikkuujjiissiikkiiaa vviizzuurrii nnaa wwaazzii ,,wwaaeelleezzee wwaazzii kkuuwwaawwaassiiaannddiikkee mmaajjiinnaa yyaaookkwweennyyee mmaajjiibbuu yyaaoo..

MMcchhaakkaattoo wwaa kkuuaannddiikkaaUUwweezzoo,, MMaappuunngguuffuu,, FFuurrssaannaa CChhaannggaammoottoo kkwweennyyeevviippaannddee vvyyaa kkaarraattaassii -- nnaabbaaaaddaayyee kkuuvviibbaannddiikkaa uukkuuttaannii -- iinnaaffaannyyiikkaa kkwwaakkuucchhaannggaannyyaa cchhaannggaannyyaa iilliikkwwaammbbaa aassiiwweeppoo wwaakkuugguunndduuaa nnaannii aammeeaannddiikkaanniinnii..

KUZAUWEZO

BORESHAMAPUNGUFU

TUMIAFURSA

DHIBITICHANGAMOTO

~~~

~~~

~~~

~~~

Chati Na. 2 ya ‘SWOT’

Page 16: Kufanikisha - Strategies for Hopev Kutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia, kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendo madhara ... Mengi yanaweza kufanikiwa kwa kutaka, kunuia kwa dhati

www.stratshope.org14

KUFANIKISHA

yanaweza kuonyesha kuwa kanisa lenu lina-paswa kufanya kazi kwa kushirikiana na taasisiau kanisa lingine, na sio peke yake tu.

Mwisho, kama Mapungufu na Changamoto vita-jitokeza kama ndio mambo makuu, mnawezakushauriwa kuweka mradi mpya pembeni kwa

wakati huo, au vinginevyo muanze kitu kidogoambacho hakitaendelea kunyonya rasilimali zakanisa lenu. Badala yake mnaweza kuamuakutumia rasilimali zenu zote kusaidia mradimkubwa, uliokwisha kuanzishwa vizuri unao-endeshwa na taasisi nyingine au kikundi chakanisa.

& ‘Kuokoa mtu mmoja nikuokoa dunia nzima’ Talmud(Maelezo ya Maandiko Matakatifu yaKiyahudi)

Page 17: Kufanikisha - Strategies for Hopev Kutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia, kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendo madhara ... Mengi yanaweza kufanikiwa kwa kutaka, kunuia kwa dhati

15www.stratshope.org

FANYA MAAMUZI YAKO

Sehemu ya 2

Fanya maamuziyako2.1 Azimia mtazamo wako

& ‘Maana kama mwilipasipo roho umekufa, vivyohivyo na imani pasipo matendo imekufa.’– (Yakobo 2:26)

Mpaka wakati huu wewe na kanisa lako mtakuwa tayari mmekwisha kuamua juu ya ainaya mradi mnaotaka kuufanya - au walau, wapi mnataka kuelekeza mtazamo wenu. Maramtakapokuwa mmekubaliana juu ya mtazamo wenu, mtaona ina manufaa kutengenezalengo - yaani dhumuni la muda mrefu la mradi wenu.

Kama bado hamjakubaliana juu ya mtazamo nalengo la mradi wenu, sasa ni wakati wa kuamua. Mnaweza kuchagua kutoka kwenyemambo mengi makubwa na shughuli zinazo-wezekana kama mtazamo wa mradi wenu, kwamfano, kusaidia yatima, kazi za kuzuia VVUkwa vijana, shughuli za kuzalisha mali auhuduma za majumbani kwa watu wanaoishi naVVU na UKIMWI. (Kisanduku Na. 2a, Uk 16).

Wakati wa kuamua juu ya mtazamo wa mradiwenu, husisha washika dau muhimu kwa wingikadri iwezekanavyo, na jaribu kufikiamaafikiano ya pamoja au makubaliano kwaujumla. Wakati mwingine sio rahisi kufikiamaafikiano ya pamoja, hivyo hatua za ziadazinahitajika. Kama mko pamoja na wanaofanyamaamuzi wote kwenye chumba, waulizewafikirie juu ya kila kitu cha nyuma wali-chokwisha kujadili au kujifunza katikamchakato wenu wa kupanga mpakahapo. Halafu waombe kila mmoja kuandi-ka majibu yao kwa maswali yafuatayo:

1. Ni kundi gani ndani ya kanisa aujamii yenu ambalo kwa hakikamnataka kulifikia? (Kwa mfano,vijana, yatima, watuwanaoishi na VVU, vion-gozi wa jadi.)

2. Ni juu ya tatizo au mambogani yanayohusiana na VVUmnayo-dhani kanisa au taasisi yenu

inabidi kuya-tazama? (Kwa mfano,kujikinga, kutunza, kushawishi.)

3. Kwa kutegemea haya, ni mradi wa aina ganiunadhani unawezekana kufanyika kwakanisa lenu au taasisi yenu kwa sasa? (hapani nafasi yenu ya kuanza kuweka vipa-umbele na kuainisha kwa umuhimu wake.)

4. Mwisho, ni lengo gani mnalokusudia kuli-fanikisha kupitia mradi huu baada ya mudafulani? Je ni juu ya kuondoa kabisa aukupunguza unyanyapaa unaotokana na VVU

Page 18: Kufanikisha - Strategies for Hopev Kutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia, kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendo madhara ... Mengi yanaweza kufanikiwa kwa kutaka, kunuia kwa dhati

www.stratshope.org16

KUFANIKISHA

na ubaguzi katika jamii yenu, kuhakikishakuwa hakuna yatima anayekuwa na njaa, aukuzui kuenea zaidi kwa VVU? Mnawezamsitegemee kufikia lengo lenu ndani yakipindi cha muda mfupi, lakini mradi wenulazima uwe unaisaidia jamii yenu kufuatamwelekeo huo.

Baada ya kila mmoja kuandika majibu yake,mwulize kila mshiriki, mmoja mmoja, kusomakwa sauti kile walichoandika - kwanza swalinamba 1, halafu namba 2, tena namba 3 namwishowe namba 4. Andika majibu kwenyeubao mkubwa au kwenye bango kitita. Kamawatu wawili au zaidi watasoma karibu kitukinachofanana, usikiandike tena ila kionyesheili kitie nguvu juu ya kile ambacho kimekwishakusemwa. Mwisho wa kila mzunguko, pitiakuona kama unaweza kukikusanya pamoja kilekitu ambacho watu wengi wanasema ili kiwekwenye jibu moja kwa swali hilo. Kadrimajadiliano yanavyoendelea, kwa kawaida

wazo moja litaibuka kama kipaumbele cha juu.Hata hivyo, kuhakikisha kuwa kila mmoja ana-jisikia kuhusishwa vyema, ni vizuri kuangaliakama hakuna hata mtu mmoja ambaye anapingamizi kwa makubaliano yanayojitokeza.Ndipo mnaweza kusema kuwa kikundi kime-fikia muafaka wa pamoja.

Ikiwa bado haiwezekani kufikia makubaliano,mjiandae kwa majadiliano zaidi au labda mkutano wa ufuatiliaji. Mnaweza kuhitajikuchambua zaidi ya mradi mmoja unaowe-zekana kwa muda mrefu zaidi, kuona ni kipimuhimu sana, kihalisia, na rahisi kuanzanacho. Mchakato huo, kufuatia mfano wa‘SMART’, unafafanuliwa katika kipengele cha2.3. Muanze na kitu kidogo, ambachokinaongeza nafasi zenu za kufanikiwa nakusaidia kujenga uzoefu wenu. Ndipo sasamnaweza kuanza mradi wa pili baadaye.

Wakati mwingine washiriki kwenye warsha au

Kisanduku cha 2a: Miradi ambayo washarika wa kanisana vikundi wanaweza kufanya

KKWWAA WWAAGGOONNJJWWAA

V MMrraaddii wwaa kkuutteemmbbeelleeaammaajjuummbbaannii,, uukkiiffaannyywwaa nnaawwaahhuudduummuu wwaa kkuujjiittootteelleeaa wwaakkuuttooaa hhuudduummaa mmaajjuummbbaannii

V KKiikkuunnddii cchhaa mmaaoommbbii nnaammssaaaaddaa kkwwaa wwaattuu wwaannaaooiisshhiinnaa VVVVUU nnaa ffaammiilliiaa zzaaoo..

V MMssaaaaddaa kkwwaa vviitteennddoo,, kk..mm..kkuuppiikkaa cchhaakkuullaa,, kkuuffuuaa nngguuoo,,kkuussaaffiisshhaa nnyyuummbbaa..

KKWWAA YYAATTIIMMAA NNAA WWAATTOOTTOOWWEENNGGIINNEE WWAALLIIOO KKAATTIIKKAAMMAAZZIINNGGIIRRAA HHAATTAARRIISSHHII

V MMrraaddii wwaa kkuutteemmbbeelleeaammaajjuummbbaannii,, uukkiiffaannyywwaa nnaawwaahhuudduummuu wwaa kkuujjiittootteelleeaa wwaakkuuttooaa hhuudduummaa mmaajjuummbbaannii

V KKuukkuussaannyyaa cchhaakkuullaa nnaa nngguuookkwwaa wwaauummiinnii wwoottee wwaa kkaanniissaa

V MMiirraaddii yyaa mmiicchheezzoo bbaaaaddaa yyaasshhuullee aauu JJuummaammoossii,, kkuussaaiiddiiaakkaazzii zzaa sshhuullee zzaa kkuuffaannyyiiaannyyuummbbaannii,, nnaa kkuuggaawwaa cchhaakkuullaa kkiilliicchhookkwwiisshhaappiikkwwaa..

KKWWAA VVIIJJAANNAA WWAA KKAANNIISSAA

V WWaarrsshhaa zzaa uueelliimmiisshhaajjii--rriikkaajjuuuu yyaa kkuujjiikkiinnggaa nnaa VVVVUU nnaahhuudduummaa kkwwaa wwaannaa ffaammiilliiaawwaalliioo wwaaggoonnjjwwaa..

V KKaammbbii zzaa vviijjaannaa wwaakkaattii wwaalliikkiizzoo,, kkwwaa wwoottee,, yyaattiimmaa nnaawwaassiioo yyaattiimmaa,, iinnaayyoossaaiiddiiaakkuuiimmaarriisshhaa uuffaahhaammuu,,tthhaammaannii nnaa ttaabbiiaa yyaa KKiikkrriissttoo..

V MMiirraaddii yyaa kkuuzzaalliisshhaa mmaallii((kk..mm.. uusshhoonnaajjii,, kkuuuuzzaammiittuummbbaa,, kkuueennddeesshhaa bbuussttaanniizzaa mmbbooggaa)) kkwwaa vviijjaannaakkuussaaiiddiiaa ffaammiilliiaa zzaaoo wweennyyeewweennaa wwaattuu wweennggiinnee kkaattiikkaajjaammiiii..

KKWWAA WWAANNAAJJAAMMIIII

V KKiikkuunnddii cchhaa kkuujjiissoommeeaa BBiibblliiaajjuuuu yyaa mmaammbboo mmuuhhiimmuu,, kk..mm..uunnyyaannyyaappaaaa uunnaaoohhuussiisshhwwaannaa VVVVUU nnaa uubbaagguuzzii,, uuppeennddoowwaa KKiikkrriissttoo nnaa mmssaaaaddaa kkwwaawweennggiinnee..

V WWaarrsshhaa zzaa mmaaoommbbii kkuubbuunniimmbbiinnuu mmppyyaa zzaa kkuuaabbuudduu((kk..mm.. nnyyiimmbboo,, mmaaoommbbii,,kkuussoommaa BBiibblliiaa)) kkuuhhuussuummaassuuaallaa yyaa VVVVUU..

V KKuuwwaa nnaa vviippiinnddii vvyyaa mmaarraakkwwaa mmaarraa vvyyaa hhuudduummaa zzaauuppoonnyyaajjii,, kkwwaa mmttuu yyeeyyootteemmggoonnjjwwaa aauu aalliiyyee nnaa rraaffiikkii aauunndduugguu mmggoonnjjwwaa..

V WWaarrsshhaa jjuuuu yyaa mmaammbboo kkaammaammiillaa nnaa ttaammaadduunnii,, jjiinnssiiaa nnaaVVVVUU..

V KKuusshhaawwiisshhii jjuuuu yyaa mmaammbboo yyaawweennyyeejjii yyaannaayyoohhuussiiaannaa nnaaVVVVUU,, kkwwaa mmffaannoo mmaatteemmbbeezziiSSiikkuu yyaa UUKKIIMMWWII DDuunniiaannii((ttaarreehhee 11 DDeesseemmbbaa)),, iilliikkuubboorreesshhaa hhuudduummaa zzaa mmaattiibbaabbuu kkwwaa wwaattuuwwaannaaooiisshhii nnaa VVVVUU,, aauu mmssaaaaddaa kkwwaa yyaattiimmaa nnaa wwaattoottoo wweennggiinnee wwaalliioo kkaattiikkaammaazziinnggiirraa hhaattaarriisshhii..

Page 19: Kufanikisha - Strategies for Hopev Kutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia, kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendo madhara ... Mengi yanaweza kufanikiwa kwa kutaka, kunuia kwa dhati

17www.stratshope.org

FANYA MAAMUZI YAKO

Kisanduku cha 2b: Tengeneza Sehemu ya Kuegesha Magari

‘‘SSeehheemmuu yyaa KKuueeggeesshhaa MMaaggaarrii’’ nnii nnaaffaassii yyaa wwaasshhiirriikkii kkaattiikkaa wwaarrsshhaa yyaa kkuuwwaassiilliiaannaa mmoojjaa kkwwaa mmoojjaannaa wwaawweezzeesshhaajjii aauu vviioonnggoozzii wwaa kkiikkuunnddii.. HHiiii iinnaawweezzaa kkuussaaiiddiiaa kkuubboorreesshhaa mmwweenneennddoo wwaa wwaarrsshhaannaa iinnaawweezzaa kkuulleettaa mmaattookkeeoo mmaazzuurrii zzaaiiddii..

KKuutteennggeenneezzaa SSeehheemmuu yyaa KKuueeggeesshhaa MMaaggaarrii,, nnaakkiillii mmffuummoo hhaappoo cchhiinnii kkwweennyyee kkaarraattaassii kkuubbwwaa nnaakkuuiibbaannddiikkaa uukkuuttaannii,, aauu cchhoorraa kkwweennyyee uubbaaoo.. FFaaffaannuuaa kkwwaa wwaasshhiirriikkii kkwwaammbbaa wwaannaawweezzaa kkuujjaazzaakkwweennyyee vviissaanndduukkuu mmaaoonnii yyaaoo wweennyyeewwee wwaakkaattii wwoowwoottee.. KKaammaa mmwweezzeesshhaajjii wwaa wwaarrsshhaa,, llaazziimmaauuaannggaalliiee mmaaoonnii mmaarraa kkwwaa mmaarraa nnaa kkuugguunndduuaa jjiinnssii wwaasshhiirriikkii wwaannaavvyyoojjiissiikkiiaa kkuuhhuussiiaannaa nnaa wwaarrsshhaa.. HHiiii iittaakkuussaaiiddiiaa wweewwee kkuuaammuuaa kkaammaa nnii llaazziimmaa kkuuwwaa nnaa mmaabbaaddiilliikkoo..

SSeehheemmuu yyaa KKuueeggeesshhaa MMaaggaarrii iinnaawweezzaa ppiiaa kkuuttuummiikkaa kkwwaa mmiirraaddii nnaa mmaawwaazzoo aammbbaayyoo hhaammuuwweezziikkuuyyaasshhuugghhuulliikkiiaa kkwwaa ssaassaa,, llaakkiinnii aammbbaayyoo mmnnaattaakkaa mmyyaakkuummbbuukkee wwaakkaattii wwaa bbaaaaddaayyee..

mkutano wanaweza kujisikia kuzuiwa kuulizamaswali, kuhoji au hata kuelezea hisia zao. Ilikumwezesha kila mmoja kutoa mchango wakekwenye taasisi na mienendo ya warsha,

unaweza kutengeneza “Sehemu ya KuegeshaMagari” (angalia kisanduku cha 2b)

2.2 Kukubaliana katika malengo na shughuli maalumu

Mara mnapokubaliana ni wapi mnataka muweke mkazo (yaani mtazamo wa mradi wenu)watu ambao mnataka kuwasaidia (yaani kundi la watu mliowakusudia) na kile mnacho-taka kukifikia katika muda mrefu ujao (yaani lengo lenu), ndipo mnahitaji kuamua kwahakika ni aina gani ya mradi mnataka kuutekeleza kwa sasa. Hii ina maana kwamba lazima muamue juu ya malengo na shughuli mtakazotekeleza - na pia lini na jinsi gani.

Sehemu ya Kuegesha Magari

Neno muhimu hapa ni ‘Malengo’, kwa sababu,lina maana unapaswa kufafanua ni nini

matokeo au majibu mnayotaka kuyafikia, ilikwamba muweze kuangalia kutokea nyuma

+ Ni kitu gani kinakwendavizuri?

? Je, una swali gani?

pp Ni kitu gani kinahitaji maboresho?

* Mawazo gani unatakakuyatunza kwa ajili yabaadaye?

Page 20: Kufanikisha - Strategies for Hopev Kutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia, kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendo madhara ... Mengi yanaweza kufanikiwa kwa kutaka, kunuia kwa dhati

www.stratshope.org18

KUFANIKISHA

juu ya mradi wenu ndani ya miezi sita aumwaka mmoja na kusema, ‘Ndiyo, tumefikiamalengo’ au ‘Hapana hatukuweza kufanikiwakila kitu tulichokitaka’.

Mnaweza sasa kujadiliana na kutafakari juu yamalengo na shughuli za mradi tofauti, nakufikiria mbivu na mbichi kwa kila wazo.Wakati wa majadiliano ya mwisho juu ya jinsiya kukusudia mtazamo wa mradi wenu, nimuhimu kuwahusisha viongozi wengi zaidi wakanisa kadri inavyowezekana katika maamuzihaya. Ni muhimu pia kuwa na mwelekeomaalumu kadri inavyowezekana, ili pasiwe nakuchanganyikiwa au kukosa ufasaha baadaye.

Katika maamuzi yenu yoyote, anza kidogo!Mradi mdogo ni rahisi kuuanza na kuuendeleza.Mnaweza siku zote kupanua shughuli zenu baadaye, mara mtakapopata msimamo wa kilemnachokifanya. Kuanza kidogo pia kunawapafursa ya kutendea kazi matatizo ya mwanzokabla hayajawazidi uwezo, na inawapa ujuzifulani wa kudumu juu ya namna ya kureke-bisha mradi kama unavyotakiwa, bila kuhitajikupitia mabadiliko makubwa ya muundo.

Kwa kila shughuli mnayokubaliana, baadhi yamaswali mnayopaswa kujibu ni haya hapa:

1. Nini ambacho mradi unatakiwa kukifikia?

2. Mtajuaje kama mradi umefanikiwa?

3. Watu wangapi mradi utawahudumia?

4. Lini shughuli zianze kufanyika?

5. Wapi shughuli zitafanyikia?

6. Nani atahusishwa?

7. Nani kiongozi?

8. Kiasi gani mradi utagharimu?

Inaweza kusaidia pia kumwuliza kila mmojaambaye amehusika katika mchakato, ‘Ni swaligani la nyongeza ulilo nalo?’ Andika maswaliyote ambayo hayajajibiwa kwenye ubao aukwenye bango kitita kuhakikisha kuwa wazo lakila mtu linachukuliwa na kufikiriwa kwa uzitowake. Mnaweza kuhitaji kujadili baadhi yahaya moja kwa moja. Badala yake, mnawezamkayarudia kwenye mkutano ujao, au katikahatua za baadaye katika mchakato wa kupanga. Kwa baadhi ya mambo mnawezakuyapeleka kwenye kamati ndogo au kwenyebaraza la utawala la usharika wenu. Kamamtakuwa mmetengeneza Sehemu ya KuegeshaMagari (angalia kisanduku cha 2b), mnawezapia kufikiria mapendekezo ambayo washirikiwametoa.

2.3 Muwe “SMART” (RUUUM)Wakati wa kupanga jinsi ya kuendesha mradi wenu, jaribuni kuhakikisha kuwa malengoyenu yote na shughuli zilizopangwa ni RUUUM. Ili kufanya hivyo, rudieni kila lengo nashughuli ambayo mmeiamua, na angalieni kuwa kila moja ni:

(Simple) Rahisi: rahisi kueleweka na hasa kwakulenga tatizo moja.

(Measurable) Unapimika: rahisi kuupima kwakutumia viashiria vinavyoweza kuhesabika,ili muweze kujua kama mmefaulu aummeshindwa.

(Achievable) Unawezekana: usiwe rahisi sana,lakini rahisi vya kutosha kuweza kuwafanyamuwe na tumaini zuri la kufanikiwa.

(Relevant) Unahusika: ni wa muhimu kwelikwa usharika na jamii yenu.

(Timely) Muda: umepewa tarehe ambapomalengo yatakuwa yametimizwa

Mfano wa mradi wenye mpangilio wa‘RUUUM’:

HUDUMA YA UPONYAJI, JUMAMOSI MCHANA KATIKA KANISA LA TUMAINI

Rahisi = kwa wiki kila Jumamosi mchana,‘huduma ya kidini ya uponyaji’ na maombimaalumu na nyimbo zenye mpangilio wakuhamasisha uponyaji wa kiroho kwa kilammoja katika jamii aliye mgonjwa au aliye namwana familia au rafiki mgonjwa.

Unapimika = takwimu zitatunzwa za idadi yawatu wanaohudhuria kwenye Huduma ya

Page 21: Kufanikisha - Strategies for Hopev Kutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia, kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendo madhara ... Mengi yanaweza kufanikiwa kwa kutaka, kunuia kwa dhati

19www.stratshope.org

FANYA MAAMUZI YAKO

Uponyaji kila wiki; na kiwango cha ushiriki chakujitolea (yaani kuzungumza na kushiriki-shana).

Unawezekana = Rasilimali zote zinazohitajikazipo ndani ya kanisa ili kutekeleza mradi huu.Viongozi walei kadhaa wa kanisa wamepatamafunzo maalumu ya ushauri-nasaha na VVUna UKIMWI, na wamechunguza aina mbalimbaliza Huduma za Uponyaji ambazo zinaweza kuigwa na kutumiwa na kanisa hili.

Unahusika = Watu wengi wenye VVU naUKIMWI ambao ni wagonjwa au wanaonyanya-paliwa wanashauku ya uponyaji wa roho nakukubalika, hivyo hivyo na wana familia namarafiki zao wa karibu.

Muda = Mradi unafanyika Jumamosi tu, nautakaguliwa kila miezi mitatu na Baraza laKanisa.

2.4 Jenga ushirikiano Itakuwaje iwapo kuanza kidogo ni kujisikia kukatishwa tamaa? Hapa ndipo ushirikianohuingizwa. Ni vizuri siku zote kufanya kazi pamoja na taasisi nyingine zinazowaongezeauwezo na kuwapa fursa ya kukutana na watu na mawazo tofauti tofauti. Kujengaushirikiano na makanisa na taasisi nyingine pia vinawawezesha nyinyi kushirikishanahabari na rasilimali, na kuongeza matokeo yenu kwa eneo la hapo hadi ngazi ya kimkoa.

Lakini ni jinsi gani unavyoamua juu ya nani wakushirikiana naye, na kwa kusudi gani? Kamasehemu ya uchambuzi wenu wa ‘SWOT’mnaweza mkawa mmekwisha kutambua taasisimuhimu washirika wenu - makanisa menginena jamii za imani nyingine, taasisi za kiserikali

na za kibiashara, vyuo vikuu, mashule na vyuo,asasi zisizo za kiserikali (NGOs) na watu binafsi- ambao kanisa lenu linaweza kufanya kazinao. Kupitia zoezi lingine la kuzungumza nakutafakari, washirika wengine muhimuwanaweza kugunduliwa.

Page 22: Kufanikisha - Strategies for Hopev Kutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia, kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendo madhara ... Mengi yanaweza kufanikiwa kwa kutaka, kunuia kwa dhati

www.stratshope.org20

KUFANIKISHA

Mfumo hapo juu (kisanduku cha 2c) unawezakutumika kama mwongozo wa aina ya mcha-kato ambao unaweza kusaidia kujenga ushirikampya.

Mifano ya ushirikiano ni:

â Sharika mbili au zaidi ndani ya jamiimmoja, zinazofanya kazi pamoja katikakampeni za ufamu na ushawishi

â Kanisa na asasi isiyo ya kiserikali ya hapo(NGO) wanaofanya pamoja mradi wa baada

ya saa za shule, ambapo kanisa linawaku-sanya watoto, linatoa watu wa kujitolea nakutoa sehemu kwa ajili ya mradi, na asasiisiyo ya kiserikali (NGO) inatoa fedha, ina-toa wataalamu wa usimamizi na kuendeshakiutawala.

â Watu wa kanisa wanaojitolea pamoja nawatu wanaoishi na VVU na UKIMWI, ambaowanaendesha mradi wa kuoka mikate kamashughuli ya kujipatia kipato, kiasi fulani chaunga kikiwa kimetolewa na wenyeji wenyemashine ya kusaga.

2.5 Chagua kiongozi sahihi wa mradiKigezo muhimu sana cha mafanikio au kushindwa kwa mradi wenu ni mtu ambaye nimhusika mkuu. Hakikisha mnamchagua mtu huyu kwa makini, mkiangalia na kuzingatiatabia, ujuzi muhimu na uzoefu wa nyuma.

Kiongozi mzuri ni yule anayehamasisha jamii kumiliki mradi na siku zote anakuwa tayari kupokeamawazo mapya ambayo yataboresha mradi siku zijazo.

Tabia muhimu Ni muhimu kiongozi wa mradi awe:

R Mkweli

R Mwaminifu

R Anayeheshimika na jamii

R Anayeishi kimaadili na nimfano bora kwa wengine.

Ujuzi wa kawaidaKiongozi anahitajika pia awena moja ya ujuzi ufuatao: R Ujuzi wa kujadiliana k.m.

kuweza kuhamasishawengine hata walio nje yataasisi

R Ujuzi mzuri wa kusikiliza nakuwasiliana

R Ujuzi wa kutafuta nakutunza raslimali

R Ujuzi wa mahusiano ya kibinadamu

Ujuzi wa lazimaKiongozi anahitajika pia awena moja ya ujuzi ufuatao:R Ujuzi wa kuweka makisio

na gharamaR Ujuzi wa kupanga na

kutunza mudaR Ujuzi wa kifundi kuhusiana

na aina ya mradiunaotekelezwa

R Ujuzi wa masoko, jinsi yakuweka mikataba na uwezowa majadiliano.

Kisanduku cha 2c: Kufanya kazi ya kujenga ushirikianoJina la mshirika Hali ya sasa na

mshirikaTunataka kufanya nini na

mshirikaNani atawasiliana na

mshirika wetu na kwa jinsigani

1.

2.

3.

Page 23: Kufanikisha - Strategies for Hopev Kutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia, kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendo madhara ... Mengi yanaweza kufanikiwa kwa kutaka, kunuia kwa dhati

21www.stratshope.org

ANDIKA KWENYE KARATASI

Sehemu ya 3

Andika kwenyekaratasi

3.1 Tengeneza mpango wa kazi

& “Dini iliyo safi, isiyo na takambele za Mungu Baba ni hii,Kwenda kuwatazama yatima nawajane katika dhiki yao, nakujilinda na dunia pasipomawaa” - Yakobo 1:27

Msiache mawazo mazuri kufa, tengenezeni mpango wa kazi na kuutekeleza. Wakati kikundi kinafanya uamuzi, uandike kwenye ubao au katika bango kitita. Halafu, kabla yawarsha au mkutano haujaisha, kubalianeni juu ya mpango wa kazi. Hii itawasaidiakutekeleza maamuzi yenu, hivyo hayapotei au kusahaulika. Hapa ni baadhi ya maswali yamfano ya kujibu kwa kila hatua inayotakiwa kuchukuliwa:

´ Nani anahusika?

´ Nani anapaswa kuombwa ushauri?

´ Rasilimali gani ya ziada inahitajika?

´ Nani ni kiongozi?

´ Ni njia zipi za mawasiliano zilizopo?

´ Ni mrejesho wa namna gani unahitajika?

´ Hadi lini mrejesho uwe tayari?

´ Nani msimamizi wa jambo hili, kama kunatatizo? (Hili linaweza kuwa kundi lililopo aukamati mpya.)

MFANO WA MPANGO WA KAZI:

KUWAKUSANYA VIJANA WASHIRIKI KWA AJILIYA KAMBI YA SIKU 5 YA KUZUIA VVU

Nani anahusika? - Vijana wote walioko kwenye darasa la Kipaimara (kiwango ni washiriki 35)

Nani aombwe ushauri? - Mchungaji Kiongozi na wazazi au walezi

Rasilimali gani za ziada - Kiasi fulani kwa kila kijana; kiasi fulani cha pesa kinawezazinahitajika kuchangishwa? kuchangishwa kwa wale wasioweza kumudu kulipia

Nani kiongozi? - Mwalimu wa darasa la Kipaimara

Mawasiliano? - Matangazo ya kila wiki baada ya ibada au sala; barua za maombi kwa wazazi na walezi

Mrejesho? - Majadiliano katika darasa la Kipaimara; mikutano na vijana waliovutiwa na wazazi na walezi

Mpaka lini? - Maombi ya kushiriki na fedha lazima zije ndani ya wiki 3 kablaya kambi kuanza

Mwangalizi? - Mchungaji wa vijana

Msiache mawazo mazurikufa! Tengenezeni mpango wa kazi na

kuutekeleza.

Page 24: Kufanikisha - Strategies for Hopev Kutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia, kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendo madhara ... Mengi yanaweza kufanikiwa kwa kutaka, kunuia kwa dhati

www.stratshope.org22

KUFANIKISHA

BORESHA MTAZAMO:ZOEZI LA ‘VIZUIZI VYA BARABARANI NA RASILIMALI’

Hatua ya Kwanza: Katika Warsha ya KupangaMipango ya kanisa iliyowahusisha wajumbe waBaraza la Usharika na wawakilishi kadhaa wajamii, washiriki walishirikishana mawazo yaojuu ya kile ambacho yatima na watoto waliokatika mazingira hatarishi wanahitaji katikajamii yao. Walikubaliana kuwa vitu vya msingini:

1. chakula - kupata angalau mlo mmoja kwasiku

2. ushauri-nasaha

3. kazi za kuongeza kipato

4. kuwasaidia wanaotoa huduma kwa yatima

5. msaada wa kiroho

6. upatikanaji nafasi ya elimu

7. mablanketi

8. burudani - sehemu za watoto kuchezea

9. huduma ya afya.

Hatua ya Pili: Halafu washiriki wakazungumzana kutafakari tena juu ya ‘vizuizi vyabarabarani’ au vikwazo juu ya utoaji hudumakwa yatima na watoto wengine walio katikamazingira hatarishi. Waliandika vikwazo hivyokatika vikaratasi viliyokunjwa na kuviwekasakafuni kuwakilisha vizuizi vya barabaranikwenye barabara ya kuelekea kwenye kupatamatibabu, kwa mfano:

1. Waandaaji hawajui cha kufanya

2. Watu walio tayari kujitolea kama watoahuduma hawatoshi

Vizuizi vya barabarani kuelekea kwenye Mradi wa Misaada kwa Yatima

Page 25: Kufanikisha - Strategies for Hopev Kutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia, kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendo madhara ... Mengi yanaweza kufanikiwa kwa kutaka, kunuia kwa dhati

23www.stratshope.org

ANDIKA KWENYE KARATASI

3. Ukosefu wa fedha za kuendeshea mradi

4. Hakuna mafunzo kwa watu wanaojitoleaambao wako tayari kuwa watoa huduma.

5. Unyanyapaa unaohusishwa na VVU naUKIMWI.

Hatua ya Tatu: Washiriki baadaye waliainisharaslimali za pale, ambazo zingewawezeshakushinda vizuizi vya barabarani. Rasilimali hiziziliwekwa kama ‘maua’ na kuwekwa karibu navizuizi vya barabarani kama mchoro wa uk 22unavyoonyesha.

Halafu Baraza la Kanisa likazungumzia jinsiwanavyoweza kupata hizo rasilimali kwa ajiliya kuwasaidia yatima na watoto wengine waliokatika mazingira hatarishi. Waliamua kuwawanaweza:

` Kutembelea kikundi cha kanisa au jamii ambacho tayari kinafanya kazi ya kusaidiayatima na kuwaomba ushauri

` Kuwaomba watu wa kujitolea kutokakwenye jumuia ya akina mama wa kanisa

` Kukusanya mchango maalumu, k.m. maramoja kwa mwezi, katika makanisa mbali-mbali yaliyopo kwenye jamii

` Kuomba asasi isiyo ya kiserikali (NGO) aukanisa lingine au kikundi katika jamii watoemafunzo

` Kuomba Mpango wa Taifa wa KudhibitiUKIMWI na asasi zisizo za kiserikali (NGOs)kuwapatia habari na vifaa vya kufundishiakuhusu unyanyapaa unaohusiana na VVU naUKIMWI; mwalike mtu anayeishi na VVU naUKIMWI kuzungumza kwenye mkutano wajamii.

Hatua ya Nne: Kama hatua ya mwisho, kikundikilirudi kwenye orodha ya mahitaji ya yatima(Hatua ya Kwanza). Kutegemea na majadilianoya Vizuizi vya Barabarani na Rasilimali (Hatuaya Pili na ya Tatu), walitengeneza mpango waRUUUM (SMART) kwa ajili ya kukidhi baadhi yamahitaji haya.

Kama mnahisi kuwa juhudi zenu za kupangazinahitaji mtazamo zaidi, mnaweza kufuatazoezi la ‘Vizuizi vya Barabarani na Rasilimali’.Baadaye nendeni kwenye zoezi la vitendo,‘Kupanga kwa Hatua za Vitendo’ (Kisanduku3a).

Kisanduku 3a: Kupanga kwa Hatua za Vitendo - zoezi la vitendo

Fafanua hatua zamatendoNa. Nani atahusishwa?

Ni juhudi gani mahususimtakazofanya kuhakikisha

hizi hatua za vitendozinatekelezwa vizuri?

Ni hatari zipi au mapungufu yapi?

1

2

3

4

5

6

& ‘Maana bila shaka ikothawabu; Na tumaini lako halitabatilika.’ - Mithali 23:18

Page 26: Kufanikisha - Strategies for Hopev Kutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia, kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendo madhara ... Mengi yanaweza kufanikiwa kwa kutaka, kunuia kwa dhati

www.stratshope.org24

KUFANIKISHA

3.2 Jinsi ya kuandika mchanganuo wa kuomba fedha

Wakati fulani, mnaweza kuamua kuwa mnahitaji msaada wa kifedha kutoka kwa wafadhiliwa ‘nje’. Kama ndivyo, utagundua kuwa wafadhili wengi wanahitaji maombi yaliyo-andikwa, yakiwa na vitu vingi vilivyoelezwa kwenye mwongozo huu. Hata hivyo mfumowa maombi unabadilika. Kutegemea na matakwa ya mfadhili, unaweza kutoa habari zifuatazo:

ð Barua inayoambatana na maombi - Andikabarua inayoeleza kwa ufupi juu yamchanganuo wa maombi kwa usahihi, naongezea kwa nini unafikiri mradi wenuutawavutia wafadhili. (Kwa kawaida nivizuri kuandika barua hii mwisho baada yakuandaa mchanganuo.)

ð Ukurasa wa kichwa cha Habari - Andikakichwa cha mradi, na majina ya watu wakuwasiliana na maelezo ya usharika wenuna jinsi gani mnapatikana.

ð Maelezo ya msingi wa tatizo mnalojaribukulishughulikia, ambalo mnaweza kulipatakatika Uchambuzi wenu wa Nje. (angaliakipengele cha 1.2, hapo juu). Habari hiiisiwe ndefu sana - sio zaidi ya ukurasammoja.

ð Lengo: Lengo ni tamko la jumla ambalolinafafanua kile mnachotaka kukifikia baadaya miaka kadhaa. Hivyo, lengo siku zote nikitu cha muda mrefu, na kinaweza kuhitajijuhudi za taasisi mbali mbali zinazofanyakazi pamoja. Aina ya malengo maalumu yavikundi vya kanisa yanaweza kuwa: (a)kuondoa au kupunguza unyanyapaaa unao-husiana na VVU na UKIMWI ndani ya jamiiya waumini; na (b) kuhakikisha kuwa yatimawote ndani ya jamii wanamaliza angalauelimu ya shule ya msingi (angalia kipengelecha 2.1).

ð Makusudio: Sasa mnaelekea kwenye uhalisia wa mradi wenu. Ni kundi gani lawatu mnaowakusudia kuwafikia, na ni ninihasa mradi wenu utafanikisha (angaliakipengele cha 2.2)? Kumbuka kuzingatiamradi wenu tu, na kuwa ‘RUUUM’ (angaliakipengele cha 2.3) kuhusu makusudio yenu.

ð Mpango wa Kazi: Ni jinsi gani mtafikiamalengo yenu (angalia kipengele cha 3.1)?Kwa kuelezea, fafanua shughuli zenu mli-zopanga, kwa kirefu kadri inavyowezekana.Ni nani washirika wenu, na jinsi ganimtafanya kazi nao? Hii ni sehemu muhimusana ya mchanganuo wa maombi yenu yafedha, hivyo mtoe taarifa halisi kadiriiwezekanavyo.

ð Muda: Muwe na uhakika kuelezea lini mna-panga kutekeleza shughuli mbalimbali(mara nyingi, mwezi kwa mwezi). Hapainaweza kuwa na manufaa kuweka Mfumowa Kazi (angalia kipengele cha 3.3) naMpango wa Kazi wa kina (angaliaKiambatanisho 2).

ð Uendelevu: Mtafanya nini baada ya kumaliza kutumia fedha za mradi? Kamashughuli mnazozitekeleza ni za muda mfupitu, jambo hili linawezekana haliwahusu.Hata hivyo, kama mnapanga mradi wa mudamrefu na watu wa jamii yenu wanakuwategemezi wa rasilimali zenu, mnahitajikufikiri ni vipi mradi unaweza kuwa ende-levu kwa kipindi kirefu. Wafadhili wa njekwa kawaida hawapendelei kuchangia mradiusio endelevu, usiojulikana misingi yake(angalia kipengele cha 3.5).

ð Uwezo wa taasisi yenu kufikia makusudioyenu: Uchambuzi wenu wa Ndani (angaliakipengele cha 1.3) utawawezesha kuka-biliana na jambo hili. Elezeni kwa ninimnaamini kuwa mna uwezo, ujuzi na rasli-mali za kuwafanya mfanikiwe. Elezeni piani nani atakuwa kiongozi wa mradi - inamaana, mfafanue mfumo wa taasisi yenu najinsi gani mradi wenu mpya utakavyoingiana kuainishwa kwenye mfumo huo.

Page 27: Kufanikisha - Strategies for Hopev Kutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia, kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendo madhara ... Mengi yanaweza kufanikiwa kwa kutaka, kunuia kwa dhati

25www.stratshope.org

ANDIKA KWENYE KARATASI

ð Kufuatilia na kutathmini: Fafanua mpangowenu wa kukusanya taarifa na habarinyingine za kufuatilia na kutathmini mradiwenu (angalia kipengele cha 4.3).

ð Bajeti: Hakikisheni mnajumuisha rasilimalimnazopata kutoka kwa wadau wengine, aukwa hali kutoka ndani ya kanisa lenu autaasisi. (Angalia kipengele 3.4 kuhusu jinsiya kuandaa bajeti.)

ð Kiambatanisho (kwa uamuzi): Hapa ndipomnaweza kujumuisha habari nyingine

muhimu ambazo mngependa mfadhiliazione. Hii inaweza kuhusisha habari zilizo-toka kwenye gazeti kuhusu kanisa lenu autaasisi, au barua za sifa kutoka kwa wadauambao mnapanga kufanya kazi nao na aukutoka kwa mwanajamii muhimu au kiongozi wa kanisa. Mwisho, mnawezakuorodhesha watu wanaohusika, majukumuyao na sifa zao (habari zao na uzoefu na auelimu yao).

3.3 Mfumo Mantiki ni nini?Baadhi ya taasisi wahisani wanaweza kuwaomba muwape ‘mfumo mantiki’ (logical frame-work) au ‘kipima mfumo’ kama sehemu ya pendekezo la mchanganuo wenu. Lengo la kipima mfumo ni kuwasaidia ninyi kuainisha malengo yenu shughuli na mategemeo yana-yotarajiwa. Kuna aina nyingi za kipima mfumo. Kisanduku 3b ni mmojawapo wa mfanorahisi:

Kukusanya ‘kipima mfumo’, anza kwa kujazasafu ya kushoto kwanza, na baadaye jazazingine tatu. Baada ya kumaliza zoezi hili,mtakuwa na kitu cha kuwakumbusha wakatiwote juu ya jinsi mnavyotaka kutekeleza mradi

wenu - na jinsi mnavyotegemea kufuatiliamafanikio au kushindwa. Ni vizuri kuwahusishawashika dau wengi kadri inavyowezekana katika kuamua jinsi ya kukusanya yaliyomokwenye mfumo mantiki wenu.

Kisanduku 3b: Mfumo Mantiki – mfano Viashiria vyaMafanikio(mategemeo yenu,yaani ni nini mna-chotaka kukamilishakupitia mradi wenu)

Chanzo na Jinsiya Kuhakiki(jinsi gani mtawezakuonyesha kuwamradi wenu ume-fanikiwa)

Muda(Mnategemeakukamilisha lini)

Matarajio namashaka (Ni ninicha kukitegemea njeya kanisa lenu kwaajili ya mradi kufani-kiwa au ni baadhi yahatari gani msizowezakuzizuia)

LENGO LAMRADI Na. 1:

LENGO LAMRADI Na. 2:

SHUGHULI 1.2.3.

1.2.3.

1.2.3.

1.2.3.

1.2.3.

1.2.3.

1.2.3.

1.2.3.

SHUGHULI

Page 28: Kufanikisha - Strategies for Hopev Kutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia, kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendo madhara ... Mengi yanaweza kufanikiwa kwa kutaka, kunuia kwa dhati

www.stratshope.org26

KUFANIKISHA

Zoezi lingine lenye manufaa ni ‘Kwa nini’ tano,ambazo mnaweza kuzitumia kuangalia upyasababu zilizowafanya mfanye maamuzi fulani,

k.m. uchaguzi wenu wa makusudi au malengo(Kisanduku 3c).

Kisanduku 3c: ‘Kwa nini?’ TanoHHuuuu nnii mmiicchhaakkaattoo rraahhiissii yyaakkuuuulliizzaa ‘‘KKwwaa nniinnii??’’ aannggaallaauu mmaarraattaannoo kkaattiikkaa mmffuulluulliizzoo kkuunngg’’aammuuaacchhaannzzoo cchhaa aauu mmaaaannaa yyaa ttaattiizzoo aauuhhaallii ffuullaannii.. NNaakkiillii kkwweennyyee kkiippaannddeecchhaa kkaarraattaassii nnaa kkiinniinngg’’iinniizzeekkwweennyyee uukkuuttaa kkiikkuukkuummbbuusshhee

wweewwee mmwweennyyeewwee aauu wwaajjuummbbee wwaa kkiikkuunnddii cchhaakkoo,, kkuuwwaa ssiikkuu zzoottee wwaajjiissiikkiieehhuurruu kkuuuulliizzaa sswwaallii ‘‘KKwwaa nniinnii??’’.. MMcchhaakkaattoo hhuuoo hhuuoo uunnaawweezzaa kkuuttuummiikkaakkuukkuummbbuukkaa mmaasswwaallii mmeennggiinnee yyaa mmssiinnggii,,kkaammaa,, ‘‘VViippii??’’ aauu ‘‘LLiinnii??’’ aauu ‘‘NNaa nnaannii??’’..

KWA NINI? KWA NINI?

KWA NINI? KWA NINI?

KWA NINI?

Page 29: Kufanikisha - Strategies for Hopev Kutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia, kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendo madhara ... Mengi yanaweza kufanikiwa kwa kutaka, kunuia kwa dhati

27www.stratshope.org

ANDIKA KWENYE KARATASI

3.4 Andaa bajeti na izingatieWapanga miradi wengi wanakuwa na wasiwasi juu ya kuandaa bajeti, lakini inaweza kuwarahisi sana. Kama una utaalamu wa kompyuta, tumia programu ya ‘spreadsheet’ kamavile ‘Excel’. Vinginevyo, tumia ala ya elektroniki itumikayo kufanyia hesabu kuhakikishakuwa safu zako zinajumlisha kwa usahihi. Mtakuta mifano ya bajeti na taarifa ya fedhakatika kurasa mbili zinazofuata kwa kumbukumbu.

Kwanza, tengeneza orodha ya vitu mtakavyohi-taji kuendesha mradi. Weka vitu kama mudawa watu watakao tumia kwenye mradi, usafiri,vifaa vya ofisi, gharama za mafunzo na chakula, na gharama ya kila kitu katika mahi-taji haya.

Ndipo mnaweza kuchora safu tatu baada yaorodha yenu ya vitu (angalia kisanduku 3d,ukurasa wa 28, kama mfano). Katika safu ya‘Jumla ya gharama inayokusudiwa ya mradi’wekeni gharama ya kila kitu mnachotakiwa kukilipia, na pia gharama ya vitu mtakavyo-pokea kama hisani kutoka kwa jamii au vyanzovingine. Katika safu inayofuata - ‘Michango yajamii’ - andikeni kiasi ambacho tayari mradi mnacho, au ambacho mtaweza kupata kutokakwenye rasilimali nyingine za hapo. Katika safuya mwisho - ‘Fedha inayoombwa’ - toa safu yamichango ya jamii kutoka safu ya gharama.Halafu jumlisha vitu katika kila safu kufanyajumla chini. Safu ya mwisho kabisa (chumbacha mwisho chini kulia) inawaeleza kiasi chafedha ambacho bado mnahitaji kwa ajili yamradi. Hii ni jumla ya fedha mnayohitaji kuomba.

Wakati mwingine, bajeti rahisi ina jumuishaorodha ya vitu na kiasi cha fedha mnachoombakwa mfadhili fulani tu. Wakati mwingine,mnaweza kuhitaji kutengeneza bajeti ya kilamwezi au kila robo mwaka (yaani kila miezimitatu) na halafu mnajumlisha kwa bajeti yajumla (kwa mwaka).

Katika bajeti ya mfano (kisanduku 3d, ukurasawa 28) jumla ya gharama yote ya mradi - ikihusisha na thamani ya msaada wa hali ni47,850 ya fedha inayotumika hapo. (Jumla hii

ipo chini kabisa katika safu ya kwanza.)Michango ya jamii (mingi ikiwa ni ya hali)inategemewa kuwa 10,500. Kwa kutoa nambahii kutoka jumla kuu, mnafikia kwenye kiasikinachohitajika kwa ajili ya kugharamia mradikutoka kwa wafadhili wa nje, yaani 37,350thamani ya fedha inayotumika hapo.

Mara mnapokuwa tayari mmeshapata rasilimaliza kutosha, mnaweza kuanza mradi wenu. Kwakuongezea safu nyingine zaidi kwenye bajetiyenu, mnaweza kutengeneza fomu ambayomtaandika kiasi kilichotumika kwa kila kitu,kwa kipindi maalumu (mfano, kila mwezi, kilamiezi mitatu, au kila miezi sita).

Mtatakiwa kutoa taarifa ya matumizi yenu yotekwa Baraza la Usharika wenu au bodi nyingineya kiutawala ya kanisa lenu, na pia kwa mfa-dhili yeyote wa nje ambaye anachangia fedhakwa mradi wenu. Taarifa yenu iorodheshe kiasigani kimetumika kwa kila kitu kwenye bajetiyenu. Kuna mfano wa taarifa ya fedha kwenyeukurasa wa 29 (Kisanduku 3e).

Mnatakiwa pia kutunza stakabadhi za matu-mizi yote - wafadhili wengi watawauliza mziwasilishe. Mkumbuke pia, kama mnapokeafedha kutoka kwa wafadhili wa nje, mnawezakuhitaji kufuata mfumo fulani na utaratibu wamuda kwa ajili ya kutoa taarifa ya fedha na yamaendeleo. Wafadhili wengine watawapampangilio wao wa kutoa taarifa ya fedha.Hakikisheni kuwa mmeelewa vizuri matakwaya mfadhili au wafadhili wenu. Sifa nzuri yamatumizi ya fedha itawaweka mahali pazuri nawafadhili wenu kama mtahitaji kuomba fedhazaidi baadaye.

Page 30: Kufanikisha - Strategies for Hopev Kutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia, kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendo madhara ... Mengi yanaweza kufanikiwa kwa kutaka, kunuia kwa dhati

www.stratshope.org28

KUFANIKISHA

Kisanduku 3d: Mfano wa Bajeti

Mradi wa Baada ya Shule kwa Yatima 50 na Watoto Walio Katika MazingiraHatarishi Kanisani

(Siku 2 kwa wiki, kwa miezi 12)

JUMLA YAGHARAMA YAMRADI INAYO-

KUSUDIWA

MCHANGOWA JAMII

FEDHAINAYOOMBWA

MAELEZO

Gharama za kuendeshea mradi -watu na ofisi:

Gharama zingine zamradi za moja kwamoja:

Kilakimoja

Idadi yavyote

Gharamakwa kilakimoja

Kilakimoja

Idadi yavyote

Gharamakwa kilakimoja

Mratibu wa mradi Kwa siku 24 200 4,800 4,800

Wanajamii wa kujitolea Wanaoji-tolea

100 100 10,000 10,000

Nafasi ya kuendesheamradi iliyotolewa naKanisa

Kwa mwezi 12 500 6,000 6,000 -

Usafiri kwa watuwanaojitolea Kwa mwezi 12 500 6,000 1,000 5,000

Mahitaji ya ofisi Gharamakwa mwezi 12 500 6,000 6,000

Vyombo vya kupikia(sufuria, vyungu n.k.)

Mara moja 1 550 550 550

Viungo vya supu Kwa mwezi 12 500 6,000 3,000 3,000

Vifaa vya michezo Mara moja 1 1,000 1,000 1,000

Vifaa vya kuandikia,makaratasi, kalamu zarangi kwa ajili ya kituocha baada ya shule

Mara moja 1 1,000 1,000 1,000

Sherehe za likizo(Krismasi, Pasaka, nk)

Kwa kilasherehe 5 500 2,500 500 2,000

Warsha za mafunzokutoka kwa NGO kwaajili ya watu wanao-jitolea

Kwa kilawarsha 2 2,000 4,000 4,000

JUMLA YAGHARAMA 47,850 10,500 37,350

Page 31: Kufanikisha - Strategies for Hopev Kutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia, kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendo madhara ... Mengi yanaweza kufanikiwa kwa kutaka, kunuia kwa dhati

29www.stratshope.org

ANDIKA KWENYE KARATASI

Kisanduku 3e: Mfano wa Taarifa ya Fedha

Mradi wa Baada ya Shule kwa Yatima 50 na Watoto Walio Katika MazingiraHatarishi Kanisani

(Siku 2 kwa wiki, kwa miezi 12)

MATUMIZI HALISI JUMLA YAMATUMIZI

JUMLA YAMABAKI

MAELEZO

Gharama za kuende-shea mradi - watu naofisi:

Gharama zingine zamradi za moja kwamoja:

Mratibu wa mradi 4,800 300 200 100 400 1,000 3,800

Wanajamii wa kujitolea 10,000 2,000 2,000 2,000 2,000 8,000 2,000

Usafiri kwa wanaojitolea 5,000 1,000 1,000 2,000 500 4,500 500

Mahitaji ya ofisi 6,000 300 2,000 500 500 6,000 -

Vyombo vya kupikia(sufuria, vyungu n.k.)

550 550 550 -

Viungo vya supu 3,000 1,000 500 800 500 2,800 200

Nafasi ya kufanyiamradi iliyotolewa naKanisa

- - -

Vifaa vya michezo 1,000 1,000 1,000 -

1,000 1,000 1,000 -

2,000 1,000 1,000 2,000 -

4,000 4,000 4,000 -

37,350 10,850 9,700 6,400 3,900 30,850 6,500

Vifaa vya kuandikia,makaratasi, kalamu zarangi kwa ajili ya kituocha baada ya shule

Sherehe za likizo(Krismasi, Pasaka, nk)Warsha za mafunzokutoka kwa NGO kwaajili ya watu wanao-jitolea

JUMLA YAGHARAMA

JUMLA YABAJETI YA

MRADI

Robo ya 1ya Mwaka

Robo ya 2ya Mwaka

Robo ya 3ya Mwaka

Robo ya 4ya Mwaka

Page 32: Kufanikisha - Strategies for Hopev Kutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia, kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendo madhara ... Mengi yanaweza kufanikiwa kwa kutaka, kunuia kwa dhati

www.stratshope.org30

KUFANIKISHA

3.5 Nini kinatokea baada ya fedha kwisha?Swali moja muhimu mnalopaswa kukabiliana nalo ni kuwa, ‘Kutatokea nini baada yafedha ya mradi kwisha?’ Kujibu swali hili, mnahitaji kushughulika na suala la uendelevu,kwa kuwa hamuwezi siku zote kuwa tegemezi kwa rasilimali za nje au msaada. Miradi yakulisha chakula ndiyo mara nyingi iliyo katika hatari hii, isipokuwa mkitambua chanzo chakudumu cha chakula, kama vile msaada wa wenyeji au bustani ya jamii.

Kimsingi kuna njia mbili za kushughulikia sualala uendelevu. Njia moja ni kuanza na mradi wamuda mfupi ambao mnajua utakwisha tarehefulani, na hauhitaji kuendelea kwa mudamrefu. Hii inaweza kuwa kwa mfano, kozi yamafunzo kwa watu wa kanisa wa kujitoleakatika huduma za majumbani, mchezo wa kui-giza juu ya kuzuia VVU, au kambi wakati walikizo kwa yatima na watoto wengine waliokatika mazingira hatarishi.

Miradi mingine, hata hivyo inahitaji kuendeleakwa miaka kadhaa. Hivyo mnaweza mkahitajikukuza ujuzi maalumu kwa ajili ya kuendelezamradi kwa muda mrefu. Kwa njia hii, mwishowa ufadhili wa nje usiwe ni mwisho wa mradi,kwa sababu mmeweza kujitegemea. Mradi walishe, kwa mfano, hauwezi kutegemea kwamuda mrefu msaada wa chakula kutoka kwa

wafadhili wa nje, lakini unaweza kuendelezwakwa kupitia utaratibu wa misaada kutoka kwawenyeji wasambazaji wa ndani, na kwa kuza-lisha kutoka katika bustani inayotunzwa nawatu wanaoishi na VVU (ambapo mfadhili anatoa gharama za uzio, vifaa na mbegu).

Wakati mwingine mradi unahitaji uwekezajimkubwa kutoka kwa mfadhili wa nje ili uanze,lakini baadaye unaweza kuendelea kwa kiasikidogo kutoka kwenye msaada wa wenyeji.Kufundisha kikundi cha watoa huduma maju-mbani wa kujitolea, kwa mfano, mnawezakuhitaji fedha kutoka nje (k.m. kwa usafiri,chakula, kukodi ukumbi, kununua vifaa vyamafunzo na habari), lakini unaweza kuende-lezwa na michango midogo lakini ya mara kwamara kutoka kwa washarika wa kanisa najamii.

& ‘Kutenda haki, nakupenda rehema, na kwendakwa unyenyekevu na Munguwako!’ - Mika 6:8(b)

Page 33: Kufanikisha - Strategies for Hopev Kutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia, kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendo madhara ... Mengi yanaweza kufanikiwa kwa kutaka, kunuia kwa dhati

31www.stratshope.org

ENDELEZA MWENDO

Sehemu ya 4

Endelezamwendo4.1 Usiache mafunzo

& ‘Kwa hiyo mkaribishaneninyi kwa ninyi, kama naye Kristoalivyotukaribisha, Ili Munguatukuzwe.’ - Warumi 15:7

Mara nyingi hatua ya kwanza katika kutekeleza mradi mpya ni kufanya mafunzo kwawatu ambao watahusika. Kama unajisikia huwezi kutoa mafunzo wewe mwenyewe,angalia kama kuna NGOs au wizara ya serikali ambayo inaweza kusaidia. Unaweza piakujiunga kwenye baadhi ya mafunzo yanayoandaliwa mahali pengine. Labda unawezakujitolea kuongeza kipindi cha nyongeza, kutegemeana na mtazamo wa kanisa lenu nauzoefu wa vitendo.

Mafunzo mazuri kwa kawaida yana malengomakuu matatu:

¤ Kuongeza maarifa

¤ Kukuza na kuboresha ujuzi

¤ Kubadilisha mtazamo

Jaribu kuhakikisha kuwa watu unaowafundishawanafanya ahadi ya kutekeleza walichojifunza,na kuwashirikisha wengine maarifa na ujuziwao. Kama watu wameelimika, mara nyingi ni

vizuri kuwa na kitabu cha muhutasari wamafunzo au vitini vya mafunzo (katika lughayao wenyewe) ili kuchochea kile walicho-jifunza. Kama mambo mengine yote,utekelezaji wa yale yaliyofundishwa unahitajiufuatiliaji wa kiongozi wa mradi au meneja.

Jambo la muhimu sana, kumbuka usiache kuji-funza, kwa hiyo usiache kutoa mafunzo.Endelea kuongeza mafunzo ya ufuatiliaji nakozi fupi fupi za kujikumbusha ili kila mmojaawe na uelewa wa mambo ya kila siku, wenyeshauku na bila kuachwa nyuma.

Kisanduku 4a : Vidokezo vya mafunzoKKaammaa uunnaappaannggaa kkuuaannddaaaa aauu kkuueennddeesshhaa wwaarrsshhaa yyaa mmaaffuunnzzoo,, ffiikkiirriiaa yyaaffuuaattaayyoo::

ØØ WWeekkaa mmaalleennggoo wwaazzii -- nniikkwwaammbbaa,, uuwwee wwaazzii kkuuhhuussuuuunnaacchhoohhiittaajjii wwaasshhiirriikkii wwaawweewwaammeejjiiffuunnzzaa kkuuffiikkiiaa mmwwiisshhoowwaa mmaaffuunnzzoo..

ØØ FFaannyyaa kkaazzii nnaa wwaannaa jjaammiiiikkuucchhaagguuaa mmaahhaallii kkwwaa aajjiillii yyaavviippiinnddii,, nnaa ttaarreehhee zzaa lliinniiwwaannggeeppeennddaa vviieennddeesshhwwee..

ØØ IIjjuuee jjaammiiii yyaakkoo -- yyaaaannii,, wweekkaammaahhiittaajjii yyaa wwaasshhiirriikkii wwaakkookkwweennyyee mmaawwaazzoo,, ppaammoojjaa nnaakkiiwwaannggoo cchhaa uuffaahhaammuu wwaalliioonnaaoo..

ØØ FFiikkiirrii jjuuuu yyaa nnii nnaanniiaattaakkaayyeeoonnggoozzaa mmaaffuunnzzoovviizzuurrii zzaaiiddii,, nnaa hhaakkiikkiisshhaakkuuwwaa mmttuu hhuuyyoo ((aauu hhiiyyoo

ttaaaassiissii)) aannaaffaahhaammuu hhaassaa kkiilleeuunnaacchhoohhiittaajjii..

ØØ HHaakkiikkiisshhaa kkuuwwaa rraattiibbaa yyaammaaffuunnzzoo iimmeeppaannggwwaa mmaappeemmaa kkaabbllaa yyaa wwaakkaattii,,wwaasshhiirriikkiisshhee wwaasshhiirriikkii,, nnaatteennaa wwaarruuhhuussuu kkuuoonnggeezzaavviittuu nnaa mmaasswwaallii..

Page 34: Kufanikisha - Strategies for Hopev Kutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia, kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendo madhara ... Mengi yanaweza kufanikiwa kwa kutaka, kunuia kwa dhati

www.stratshope.org32

KUFANIKISHA

4.2 Endelea kuwasilianaNi muhimu kwa washika dau wote katika mradi kuwa wanasikia mara kwa mara juu yakinachoendelea. Kama mambo yanaenda vizuri, washirikishwe habari njema. Kama kunamatatizo au kuchelewa, wafahamishwe - wanaweza kutoa ushauri au kusaidia katikakushughulikia hayo. Mnaweza kulijulisha kanisa lenu au jamii kupitia matangazo baada yahuduma kanisani au katika mikutano, kupitia magazeti, mabango, au kubandika picha, aupengine kwenye tovuti au orodha ya huduma. Fanyeni mradi kuwa sehemu ya maongeziyenu ya mara kwa mara ndani ya kanisa na jamii yenu. Hii inajenga hisia ndani ya jamiiya umuliki wa mradi na inasaidia kuongeza misaada endelevu. Kinyume chake, kamahabari kuhusu mradi hazipatikani watu wanapoteza shauku na uwajibikaji. Hii piainaweza kupelekea minong’ono kusambaa kuhusu mradi, kupelekea kupotea kwa uaminifuna misaada kutoka kwa jamii.

4.3 Ufuatiliaji na TathminiUfuatiliaji na Tathmini ni njia za kuwawezesha ninyi kuwajibika kwa viongozi na wauminiwa usharika wenu, na pia kwa wafadhili wowote mnaoweza kuwa nao. Njia zote hizizinaelekeza kwenye kugundua kama mradi wenu unafanya vizuri wakati wowote ule.

Ufuatiliaji, tuna maanisha juhudi endelevu zakukusanya takwimu au habari nyingine ambazozinaeleza hali ya mradi inavyoendelea vizuri.Hii inaweza kufanyika mara kwa mara, kwamfano, kila wiki au mwezi.

Tathmini, tunamaanisha kuna muda ulioamu-liwa kuwa kipindi fulani cha mradi, (au mwishowa shughuli fulani, kama vile warsha yamafunzo), mnatathmini jinsi gani mradi ume-fikia vizuri matazamio mliyokuwa nayo wakatiwa mchakato wa kupanga, na mliyoyaandikakama ‘Viashiria vya Mafanikio’ katika mfumomantiki. Katika vigezo vyote vya tathminimlivyonavyo, vile vinavyoweza kupimamatokeo - matokeo ya mwisho au athari zamradi wenu - ni vya muhimu sana.

Matokeo yenu ya ufuatiliaji na tathmini lazimakila mara yaandikwe katika taarifa, ili muwena kumbukumbu ya mradi wenu ambayomnaweza mkaingalia au kuionyesha kwawengine, pamoja na mashirika wafadhili.Taarifa hizi kwa ujumla zinatayarishwa kwamwezi, kwa robo mwaka au miezi sita. Labda

mnaweza kuona kuwa inafaa kutayarisha taarifa ya mwaka ya mradi wenu.

Jaribuni kuweka picha katika taarifa zenu.Haziwezi kuwa badala ya taarifa muhimumnayotakiwa kutoa, lakini ni nyongezamuhimu sana katika taarifa zenu kwa sababuzinaonekana moja kwa moja na ni halisi.Taasisi za wafadhili pia wanazikubali na kuzifu-rahia, na wanaweza kuwaomba ruhusa ili wazitumie katika machapisho yao.

Vipimo vya ufuatiliaji

Kabla humjaanza kutekeleza mradi wenu, nimuhimu kujua jinsi gani mtakuwa mnafuatiliana kutathmini. Hii hapa ni baadhi ya mifano yatakwimu mnazoweza kukusanya ziwasaidiekufuatilia kile kinachofanyika katika mradiwenu kwa kila mwezi:

v Idadi ya watu waliohudumiwa katika mudauliopangwa (wanaume kwa wanawake;wakubwa kwa watoto)

Page 35: Kufanikisha - Strategies for Hopev Kutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia, kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendo madhara ... Mengi yanaweza kufanikiwa kwa kutaka, kunuia kwa dhati

33www.stratshope.org

ENDELEZA MWENDO

v Idadi ya huduma za kutembelea majumbani(zimefanywa na nani)

v Idadi ya mablanketi (au vifurushi vya chakula, au vitu vingine) vilivyotolewa

v Idadi ya vipindi vya maombi vilivyofanyika,wapi, na nani amefanya

v Idadi ya vipindi katika mradi wa mafunzo

v Idadi ya watu waliofundishwa maarifa naujuzi mpya

v Idadi ya watu wa kujitolea waliohusishwakatika mradi.

Mnaweza pia kuwauliza watu wanaohudumiwana mradi watoe maoni yao jinsi mradi ulivyo-gusa maisha yao.

Vipimo vya tathmini

Haya hapa ni baadhi ya maswali mnayowezakuuliza, ili kutathmini shughuli au mradi:

v Jinsi gani mradi umefikia vizuri matarajio?

v Wapi mradi ulifanya vizuri zaidi ya ilivyotarajiwa, au vibaya? - na kwa nini?

v Ni kitu gani kizuri zaidi kuhusu shughuli hii(au warsha, au mradi)?

v Ni kitu gani hasa kilikuwa kinakatisha tamaakuhusu shughuli hii (au warsha, au mradi)?

v Ni nini umejifunza kama matokeo ya mradihuu?

Page 36: Kufanikisha - Strategies for Hopev Kutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia, kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendo madhara ... Mengi yanaweza kufanikiwa kwa kutaka, kunuia kwa dhati

www.stratshope.org34

KUFANIKISHA

v Je unafikiri mradi huu umekubadilisha, aujinsi unavyofikiri, na kama ndivyo, kwa vipi?

v Ni jinsi gani mnaweza kuboresha mradi aushughuli wakati ujao?

Vipimo vya matokeo

Kipimo kigumu sana - lakini muhimu - katikakupima ufuatiliaji na tathmini ni cha kuhusianana matokeo au athari ambazo mradi umekuwanazo katika maisha ya watu. Baadhi ya vipimohivi vinaweza kuwa vigumu sana kukusanyahabari zake, lakini ni muhimu kufanya juhudi.Mifano ni kama:

v Ni watu wangapi wamejitangaza hadharanikuhusu hali zao za maambukizi ya VVU

tangu kanisa lenu litekeleze mradi wakupunguza unyanyapaa?

v Ni yatima wangapi zaidi wanahudhuria shuletangu kanisa lenu limeanza kuwafikia yatima na watoto wengine walio katikamazingira hatarishi?

v Ni familia ngapi zaidi zinalishwa kwaukamilifu, shukrani za usambazaji chakulaau kazi za kuzalisha mali zinazosaidiwa namradi wenu?

v Miaka miwili baada ya mradi, ni vijana wangapi wanasema kwamba kambi zakuzuia VVU zilizoendeshwa na kanisa lenuzilikuwa mwanzo wa kugeuza maisha yao?

& “Maana hapo palipo wivu na ugomvi,ndipo palipo machafuko, na kila tendo baya.Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi,tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikilizamaneno ya watu, imejaa rehema na matundamema, haina fitina, haina unafiki. Na tundala haki hupandwa katika amani na walewafanyao amani.” - Yakobo 3:16-18

Page 37: Kufanikisha - Strategies for Hopev Kutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia, kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendo madhara ... Mengi yanaweza kufanikiwa kwa kutaka, kunuia kwa dhati

35www.stratshope.org

MASWALI YANAYOULIZWA MARA KWA MARA

Sehemu ya 5

Maswali yanayoulizwamara kwa mara

& ‘Msihukumu, nanyi ham-tahukumiwa; msilaumu, nanyihamtalaumiwa; achilieni, nanyimtaachiliwa.’-Luka 6:37

Sehemu hii inahusu matatizo ya kawaida yanayojitokezawakati wa kupanga na kutekeleza mradi mpya ndani yawasharika wa kanisa au jamii.

A. Ni jinsi gani tutaweza kumchagua mwezeshaji bora wakuwezesha mchakato wetu wa kufanya maamuzi?

Wajibu wa mwezeshaji ni kuongoza kikundikatika mchakato wa kufanya maamuzi. Hii nikazi iliyo katika mipaka ya muda, sio kaziendelevu au ya muda mrefu. Mwezeshaji wamchakato wa kanisa lenu wa kufanya maamuzikatika kufanya kazi zinazohusu VVU na UKIMWIanaweza asije kuwa kiongozi au meneja wamradi wenu.

Mwezeshaji wenu sio lazima awe mtaalamumwenye ujuzi katika masuala ya VVU naUKIMWI. Lakini mtazamo, maarifa na ujuziwake ni muhimu. Kwa mfano:

¨ Lazima awe na mtazamo sahihi, awe ana-heshimika kimaadili, hali ya VVU, na jinsia,na awe anajitambua.

¨ Lazima awe na ufahamu kuhusu tatizomnalolishughulikia na kuhusu rasilimalimlizo nazo, - au kama sivyo, basi ajue niwapi pa kupata hizi habari.

¨ Kuhusu ujuzi, yafutayo ni muhimu: kusi-kiliza kwa makini na kuuliza maswali vizuri,mawasiliano ya uwazi, uwezo wa kuongozakazi za kikundi, kutatua migogoro, kutoaufupisho, na kutunza muda.

Kama hakuna mtu katika usharika wenu aukikundi cha kanisa ambaye anaweza kufanyakazi hii kwa ajili yenu, omba kutoka kwenyeNGO za hapo, kiongozi wa jamii, au kutokangazi ya taifa ya kanisa lenu kama wanawezakuwasaidia mapendekezo kadhaa.

B. Ni jinsi gani tutapata ushiriki mpana katika kupanga nakutekeleza mradi mpya?

Ili kumpata kila mtu mnayetaka ahusike nakuhimiza juhudi na umiliki wa jamii, jaribumbinu zifuatazo:

1. Wafanye watu wajisikie vizuri kwa kutumiambinu ya kuwahusisha, ambapo kila mmoja

atajisikia kukaribishwa kwa furaha nakuthaminiwa, na anahamasishwakuzungumza.

2. Cheza mchezo wakufahamiana, kwa mfano,kwa kumtaka kila mmoja ajieleze kama

Page 38: Kufanikisha - Strategies for Hopev Kutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia, kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendo madhara ... Mengi yanaweza kufanikiwa kwa kutaka, kunuia kwa dhati

www.stratshope.org36

KUFANIKISHA

mnyama anayempendelea, au azungumziekumbukumbu anayoipendelea ya kutokautotoni kwake.

3. Wahamasishe watu kushirikishana habari,mawazo, maarifa na mambo yanayowahusukwa kuwaweka washiriki wawili wawili navikundi vidogo vidogo; au vinginevyo shiri-kishaneni katika mfumo wa mzunguko(ambapo kila mmoja anaulizwa maoni).

4. Tumia mbinu kama kuwagawanya kikundikikubwa katika vikundi vidogo vidogo kwaajili ya baadhi ya shughuli.

5. Wasaidie watu kuwasiliana kikamilifu kwa

kuhamasisha kuheshimiana ndani ya kikundina kuchochea mawazo ya msingi watuwanayotoa.

6. Tawala mwenendo wa kikundi kwa kuwekasheria za msingi kabla ya wakati, kwa ajiliya ushiriki sawia wa kila mmoja aliyepo.(Angalia swali D hapa chini.)

7. Ainisha kazi za vitendo na uhusiano wamada husika kwenye majadiliano.

8. Kadri iwezekanavyo, karibisha kikundi kuongoza mchakato wa kujifunza nakushirikishana.

C. Tufanye nini kama watu wanaogopakufanya maamuzi?

Kama watu ambao wanapaswa kutekelezamradi hawajisikii kama walikuwa na mchangowa kutosha katika kuamua kuanza kwa mraditangu mwanzo, basi mnaweza kukabiliana navikwazo vingi na watu kuondoka hapo baadaye.Ni ukweli huo huo kwa maamuzi mengineambayo yanatakiwa kufanywa kadri mradiunavyoendelea. Lakini watu wengi hawajisikiikwamba maoni yao ni ya thamani, hivyo hukaakimya kwenye mikutano. Hawajawahi kuwa nauzoefu mwingi wa kufanya maamuzi siku zanyuma, hivyo hata sasa hawajiamini.

Jambo muhimu hapa ni kwamba inawezekanakujifunza kufanya maamuzi mazuri. Zaidi yayote, mchakato wa kufanya maamuzi unajengahisia ya umiliki na uwajibikaji katikati ya watu

wanaohusika, na unasaidia kuuendeleza mradipamoja na magumu yoyote yanayoweza kuji-tokeza siku za baadaye.

Iwapo watu wanaohusika katika mradi hawajuila kufanya na wanajisikia hawawezi kutoamaamuzi, unaweza kuwapa mambo mawili aumatatu ili wafikirie ya kuchagua, Halafuwaombe wafanye uamuzi kuhusu uchaguziwao. Kama ikifanyika tena na tena kadrimambo mapya yanapojitokeza, mwishowewataweza kuleta mawazo na mambo ya kuchagua wao wenyewe. (Hii haimaanishi kuwakila wazo litapita bila kupingwa, kwamba ni‘kila kitu kipite’. Maamuzi yote lazimayafanyike katika mipaka ya makubaliano yataasisi au mradi.)

D. Ni jinsi gani tunaweza kushughulikia ukimya - au usemaji mno -kwa washiriki kwenye kikundi?

Kama mna washiriki walio kimya:

¨ Wagawanye kwenye vikundi vidogo vidogo,ambapo kuna uwezekano mkubwa kwawashiriki walio kimya kuzungumza

¨ Waombe washiriki walio kimya washirikisheuzoefu wao katika majadiliano kuhusu maeneo ya ujuzi wao wowote

¨ Tumia shughuli ambazo washiriki wotewanaombwa kutoa michango yao kidogo

¨ Watie moyo - ila usiwe mnafiki - wakati wamrejesho wa majadiliano. Kwa mfano,jaribu kuongezea au kuunga mkono kilewalichosema, badala ya kusema tu ‘ume-fanya vema’ au ‘vizuri sana’.

Page 39: Kufanikisha - Strategies for Hopev Kutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia, kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendo madhara ... Mengi yanaweza kufanikiwa kwa kutaka, kunuia kwa dhati

37www.stratshope.org

MASWALI YANAYOULIZWA MARA KWA MARA

F. Tunawezaje kupata kanisa na jamii kwa upana kusaidiamradi wetu?

Kama una washiriki waongeaji:

¨ Wape washiriki waongeaji wanaotawalamazungumzo mrejesho mzuri na wahusishewashiriki wengine katika kuwajibu. Kwamfano, sema, ‘Asante kwa hoja yako inayo-vutia, wengine mnafikirije juu ya hili?’

¨ Ongea nao binafsi wakati wa mapumziko,na kuwaomba watoe muda wa kutosha kwawengine kushiriki pia.

¨ Wape kazi ya kufanya wakati wa warsha,kwa mfano, kutayarisha na kuwapa washiriki wengine muhtasari mwanzoni mwakila siku.

¨ Wakumbushe ‘sheria za msingi’ mlizoji-wekea kuhusu kumruhusu kila mtu kushiriki,au tumia michezo inayo hamasisha kila mtukujitambua tabia yake.

E. Tunaweza kufanyanini kuzuia migogorondani ya usharikawetu?

Hili ni tatizo la kawaida. Ni vyema kamamtakubaliana juu ya sheria za kuwasilianakabla ya kuanza mchakato wenu wa kufanyamaamuzi. Kupata michango ya kikundi juu yahizi sheria za msingi inasaidia kuhakikishamakubaliano. Kwa mfano:

¨ Usiingilie kati wakati mtu mwingineanaongea

¨ Heshimu kila wazo la mtu kuwa ni lathamani

¨ Kama hukubaliani na mtu mwingine, zinga-tia ukweli - usihamaki au kuleta ‘habari zazamani’ (mambo ya zamani ambayo hayanauhusiano wa moja kwa moja).

Kumbuka: kama kuna tofauti kubwa ya mawazo kati ya watu, itakuwa vizurikuzungumza nao tofauti tofauti, kwa mfano,wakati wa mapumziko ya chai au baada yamkutano.

¨ Wahusishe kikamilifu watu watakaoguswana mradi katika mchakato wa kupanga nakufanya maamuzi

¨ Kutana na kukubaliana na washika daumuhimu ili kupata msaada wao

¨ Tumia michezo ya tafrija za kuigiza kuonye-sha kubadilika au kuanza kwa mradi mpya

¨ Idhinisha raslimali za kutosha (pamoja nawatu wa kujitolea na misaada ya hali) kwaajili ya mafunzo na utekelezaji

Page 40: Kufanikisha - Strategies for Hopev Kutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia, kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendo madhara ... Mengi yanaweza kufanikiwa kwa kutaka, kunuia kwa dhati

www.stratshope.org38

KUFANIKISHA

¨ Kwa uwazi wajulishe jamii kuhusu mradimpya, na uwe tayari kujibu maswali yao

¨ Changua mtu wa kuutambulisha mradi mpya

ambaye anafanana kwa sifa na watu ambaowatauidhinisha mradi. Hii itasaidia kuwapaimani yao kwa urahisi.

G. Tutaweza kufanya nini kama tumekwisha kupangakila kitu, lakini bado hatuna fedha?

Wakati mwingine inawezekana kupita hatuazote sahihi za kupanga na kuweka bajeti, lakini bado mnakuta mmepungukiwa fedha zakuanza mradi mnaoutaka. Kama hili likitokea,kitu cha kwanza mnachotakiwa kufanya nikupitia mara nyingine tena mchakato wenu wakupanga, na kuona kama kuna rasilimalinyingine zaidi za hali mnazoweza kuzipata.Vinginevyo, angalieni kama mnaweza kuupunguza mradi uwe mdogo kidogo (bilakupunguza ubora wake au matokeo yaliyotara-jiwa), au kama kuna mfadhili mwenyeji auwashirika mnaoweza kuwaomba msaada wakuziba pengo la fedha mlizopungukiwa.

Kama mkiona kuwa mradi wenu bado unapu-ngukiwa fedha, basi mnaweza kupeleka maombi ya mchanganuo kwa mfadhili wa shirika la ‘nje’. Kufanya hivi, mtafute ni shirika gani la ufadhili lina ofisi nchini mwenu,au mnaloweza kuwasiliana kupitia kanisa lenuau mashirika mengine. Halafu mtafute wafa-dhili wana matakwa gani, katika masualakama:

¨ Ni aina gani ya mradi au kundi gani la watuwanakuwa na mapendekezo nayo

¨ Ni jinsi gani wanataka muwasilishemchanganuo wenu wa maombi ya fedha

¨ Muda gani wa mwisho wa maombi ya micha-nganuo ya fedha

¨ Mahitaji ya kisheria kwa taasisi zinazowa-kilisha maombi ya michanganuo ya fedha

¨ Kiwango cha juu na cha chini cha kiasi chafedha wanazoweza kutoa.

Japokuwa mifumo inaweza kutofautiana,wafadhili wengi wana matakwa yanayofananakuhusu kile mnachotakiwa kujumuisha katikamchanganuo. Fuatilia kiambatanisho chamfano wa maombi ya fedha katika kipengelecha 3.2. Mzingatie kwamba kuomba fedhakutoka kwa mfadhili wa nje kutacheleweshakuanza kwa mradi wenu kwa kipindi kisichoju-likana - yawezekana kwa miezi kadhaa.

Kama hamuwezi kupata fedha kutoka nje, hatahivyo jaribuni kuanza kitu fulani - lakinimuanze na kitu kidogo, au kwa kipindi kifupiau kwa msingi wa majaribio. Hata hivyo msi-fanye kitu kwa sababu mfadhili anawatakamfanye, kama havitakubaliana na malengo namakusudi ambayo usharika wenu umekwishakukubaliana. Miradi yenye msukumo wa matakwa ya mfadhili mara nyingi huishia katika majuto na matatizo, japokuwa uhitajiwa kupata fedha unaweza kuwa jaribu kubwasana.

Sasa mko tayari kuanza mradi wenu mpya.

Kwa nini kungoja zaidi?

Kumbuka:

Wakati mzuri wa kupanda mti ni miaka 20 iliyopita.Wakati mzuri wa pili ni sasa.

- Methali ya Kiafrika

Page 41: Kufanikisha - Strategies for Hopev Kutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia, kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendo madhara ... Mengi yanaweza kufanikiwa kwa kutaka, kunuia kwa dhati

39www.stratshope.org

VIAMBATANISHO

Kiambatanisho Na. 1

Mfano wa warshaLengo la warsha: Washiriki lazima wajifunzeujuzi mpya kuwasidia kupanga na kutekelezamradi wa VVU na UKIMWI kupitia kanisa aukikundi chao.

Muda unaohitajika: Siku moja (masaa 7 - 8)

Vifaa vinavyohitajika: Makaratasi ya bangokitita, peni kubwa za wino, kalamu za risasi,peni, vipande vikubwa vya karatasi tupu (20kwa kila kikundi cha watu 5 hadi 8).

Habari za nyuma: Mwongozo huu waTumeitwa Kuhudumia umekusudiwa kuwa kifaacha mtu binafsi kujifunzia - hii ina maanakwamba, mwezeshaji mwenye uzoefu anawezakukitumia bila kupata mafunzo maalumu. Hatahivyo, usharika wa kanisa lenu au kikundichenu kinaweza kuwa hakina uzoefu na hojana mazoezi shirikishi yaliyomo humu. Kwa hiyo

itafaa kufanya ‘majaribio’ kwa kutumia kwanza kwenye jamii ya kanisa la kuigizakabla ya kuutumia huu mwongozo kwenyeusharika wenu.

Kama ukiamua kufanya hivyo, wagawe washi-riki katika vikundi vya watu 5 hadi 8 kila kimoja. Baada ya kuanza kwa maombi na utangulizi, anza na majadiliano kuhusu ujuziambao washiriki wanadhani kanisa linapaswakuwa nao ili kupanga na kutekeleza mradi waVVU na UKIMWI. Yaandike haya kwenye bangokitita au ubao. Jaribu kujumuisha ujuzi mwingikadri inavyowezekana katika warsha yenu.

Hapa chini kuna mfano wa hili somo na mpango wa majukumu kwa vikundi vidogovinne. (Kumbuka: kila kikundi kitafanyamajukumu hayo hayo matano yaliyo sawa.)

Somo la Kujifunzia: Kanisa la Neema ya Upendo laUkanda wa Juu

Katika bonde la kilimo la Ukanda wa Juu, lenye wakaazi wa jumla ya watu 3,000, kunamakanisa matatu tu, pamoja na kanisa la Neema ya upendo. Katika sehemu hii ya nchi,yenye kiwango cha asilimia ishirini (20%) ya ukosefu wa ajira, kiasi cha kama asilimia kumi(10%) ya watu wote wanakadiriwa kuwa na mambukizi ya VVU. Inafahamika kwamba tayarikuna kaya 12 zinazoongozwa na watoto katika hili bonde. Lakini ni watu wachache sanawanaozungumza kuhusu UKIMWI kwa sababu ya unyanyapaa na woga unaohusishwa naUKIMWI.

Wakati Jonas, mmojawapo wa washarika wanaojituma sana usharikani, aliporudi tena Ukandawa Juu baada ya kufanya kazi mjini kwa miaka miwili, aliamua kuwa ilikuwa ni wakatimuafaka kwa Kanisa la Neema ya Upendo kujihusisha na huduma ya UKIMWI. Jonas alisimamakatika mkutano wa Baraza la Kanisa na kusema: ‘Haijalishi kabisa kama tunafanya kazi yakuzuia UKIMWI, au tunatoa msaada kwa watu wanaoishi na VVU na UKIMWI, au tunatoa huduma kwa yatima - lakini lazima tufanye KITU.’ Baada ya majadiliano ya muda mrefu,Baraza la Kanisa lilikubali kuchagua Kamati ya Kanisa, ikimjumuisha na Jonas na wajumbekadhaa washarika, kupanga ni nini hasa wafanye.

Sasa mjifanye kama kikundi chenu hicho kidogo ni hiyo Kamati ya Kanisa. Kazi yenu nikuunda na kutoa mapendekezo ya mradi waUKIMWI kwa waumini wa Neema ya Upendo iliwauendeshe, kwa kutumia kiasi kidogo chafedha ambacho Jonas amesema angeweza

kuchangisha kutoka kwa washirika wake wamjini, lakini pia kwa kutegemea watu wakanisani wa kujitolea na misaada mingine yahali. Kumbuka katika mji mwingine kuna klinikiza afya zinazotembezwa kwa magari zinazotoahuduma ya ushauri-nasaha na kupima VVU

Page 42: Kufanikisha - Strategies for Hopev Kutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia, kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendo madhara ... Mengi yanaweza kufanikiwa kwa kutaka, kunuia kwa dhati

www.stratshope.org40

KUFANIKISHA

(VCT) na asasi isiyo ya kiserikali (NGO) ambayoitatoa mafunzo ya ujuzi wa shughuli zinazo-husu VVU na UKIMWI bila gharama yoyote.

KAZI TANO ZA VIKUNDI VIDOGO

Tambulisha kila kazi kwa maelezo mafupi,ukirejea kurasa husika za mwongozo huu.Baada ya vikundi kukamilisha kazi zao, inabidivikundi virudi na kukaa pamoja na kutoa taarifa za maamuzi yao, yakifuatiwa namajadiliano. (Kumbuka: kila kikundi lazimakiwe na nakala ya mfano wa somo na kazi yakila kikundi kidogo hapo chini.) Kazi tano nihizi:

1. Tumia muda kupanga(Angalia sehemu ya 1, uk. 7)

Kamati yako lazima ianze na mchakato wakupanga. Anza kwa kumchagua mwenyekiti wakikundi chenu na mtu wa kutoa taarifa kwawarsha nzima. Sasa, kutegemeana na kile mna-chokijua kuhusu Ukanda wa Juu na usharika waNeema ya Upendo, na kwa ujuzi wenu na kilemlichojifunza, fafanua mchakato wa kupangaambao mtaufuata:

Kwanza, eleza jinsi mtakavyofanyaUchambuzi wa Nje ili kutambua MAHITAJI yajamii ya Ukanda wa Juu. Ni Fursa zipi naChangamoto zipi mnazoziona?

Pili, eleza jinsi mtakavyofanya Uchambuzi waNdani ili kutambua UWEZO wa usharika waNeema ya Upendo wa kutekeleza mradi waUKIMWI. Ni Uwezo gani na Madhaifu yapimnayaona?

Tatu, orodhesha miradi mnne tofauti tofautiambayo mnadhani usharika wa kanisa laNeema ya Upendo wanaweza kuifanya.Hakikisha kuwa halisi kuhusu kila wazo hapochini:

V Wazo moja liwe kuhusu kuzuia VVU

V Wazo lingine liwe kuhusu kupunguzaunyanyapaa

V Lingine liwe kuwahudumia watu wanaoishina VVU na UKIMWI, na

V Lingine liwe kuwashughulikia yatima.

2. Fanya maamuzi yako(Angalia sehemu ya 2, uk. 15)

Kutegemea na aina nne za miradi au shughulimlizojadili hapo mwanzo, mchague mojawapoya mradi wa kupendekeza kwenye Baraza laKanisa la Neema ya Upendo, na elezea kwanini hilo ni chaguo lenu la kwanza. Kisha nilazima muwe bayana zaidi kwa kujibu maswalikadri inavyowezekana kuhusu mradi wenundani ya muda mnaokubaliwa:

1. Ni nini mradi wenu unakusudia kufanikiwa(Makusudio yenu ya ‘RUUUM’)?

2. Watu wangapi watafaidika?

3. Ni mara ngapi shughuli zitakuwa zina-fanyika, na wapi?

4. Nani atakuwa kiongozi wa mradi (yaani,mtu huyo ana nafasi gani katika usharika),na nani mwingine atahusika kwenye mradi?

5. Je mradi wenu utagharimu fedha yeyote, nakama ndivyo, kwa ajili ya nini? Rasilimaligani zingine zinahitajika?

6. Ni wapi na kwa jinsi gani mnafikiri usharikawa Neema ya Upendo watapata fedha auraslimali mnazohitaji kwa ajili ya mradi?

Kama kuna muda, orodhesha shughuli, hatuakwa hatua, zile mnazopanga kuzifanya.Mnaweza kutumia mpango mantiki (angaliakipengele cha 3.3) na mpango wa kazi(angalia kiambatanisho 2, uk. 43) kama unataka. Kumbuka kuwa bayana na maelezo ya kina kadri iwezekanavyo.

3. Tengeneza Mpango wa Kazi(Angalia sehemu ya 3, uk. 21)

Hili ni zoezi la kujenga umoja ambalo linawapauzoefu washiriki kujua hatua zinazohitajikakatika kupanga mradi, lakini pia linafurahishamno.

Kila kikundi kinapaswa kuandika kwenyekaratasi 20 tofauti kazi au hatua za vitendozinazohitajika ili mchakato wenu wa kupangauwe wa mafanikio. Andika kazi moja tu katikakila kipande cha karatasi. Kila kikundi lazimakikusanye orodha ya kazi 20 - angalia ‘Mpangowa Kazi’ ufuatao kwa mapendekeso.

Page 43: Kufanikisha - Strategies for Hopev Kutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia, kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendo madhara ... Mengi yanaweza kufanikiwa kwa kutaka, kunuia kwa dhati

41www.stratshope.org

VIAMBATANISHO

(Kumbuka: mwezeshaji anaweza kubadilishakazi kama anataka).

Shughuli za Mpango wa Kazi:

Fanyeni Uchambuzi wa HaliChezeni ‘michezo ya kufahamiana kila mmoja

wenu’Jiulizeni mwenyewe ‘KWA NINI?’

Gawanyeni kazi (nani anafanye NINI?)Kubalianeni juu ya makusudi ya mradi

Waandikisheni watu wakujitoleaFanyeni uchambuzi wa Uwezo, Mapungufu,

Fursa na Changamoto ‘SWOT’Shirikishaneni mambo, mawazo na ujuziTengenezeni mahali pa kuegesha magari

Fanyeni tathimini ya mradi wenuTumieni muda kupangaFuatilieni mradi wenu

Fanyeni uchambuzi wa uendelevu wa mradiJiulizeni wenyewe ‘JINSI GANI tutaweza

kufanya hizo kazi?’Rejeeni makusudio ya mradi wenu (RUUUM)

Shaurianeni na wazee kuhusu mradiAndaeni bajeti

Wekeni pamoja mpango mantiki wenu (mpangowa kazi)

Chagueni maafisa wa mradiAndaeni mpango wa kazi

Sasa kila kikundi kisambaze makaratasi yao 20(yakiwakilisha kazi tofauti 20) kwenye meza,sakafuni au ardhini. Waelekeze kila kikundikupanga hizo kazi 20 kwa mtiririko ambaowanadhani unaleta maana zaidi kwa mchakatowa kupanga mradi.

Hili ni zoezi la kikundi, hivyo wanakikundiwote lazima washiriki. Hata hivyo kuna mtegokatika zoezi hili: HUWEZI KUZUNGUMZA NAMWINGINE! Mna dakika 10 za kumaliza zoezihili - mkiwa kimya kabisa!

Kumbuka kwamba hakuna jibu sahihi na lisilosahihi. Vikundi vinaweza kupanga kazi zaokatika mpango wowote wanaoutaka, lakini kilammoja lazima akubali matokeo. KIDOKEZO: Kila mmoja lazima atabasamukadri awezavyo wakati wa kufanya zoezi hili!

Sasa, washirikisheni wanakikundi wa vikundivingine uzoefu wenu. Mwezeshaji anawezakusaidia kuendesha majadiliano kwa kuulizamaswali yafuatayo (dakika 20):

´ Mmeonaje uzoefu wa kufanya zoezi hilikama timu, mkiwa kimya?

´ Je ulisikia hasira wakati mwingine?

´ Je ulijisikia kushikwa zaidi na mawazo yakomwenyewe?

´ Ulijisikiaje wakati watu wengine waliposo-geza kadi zako?

´ Kwa nini ni muhimu kusikiliza maoni yawengine?

´ Umejifunza nini kutoka kwenye zoezi hili?

Majibu yenu kwa maswali haya lazima yawapemtazamo kidogo wa jinsi watu wanavyohitajikufanya kazi pamoja wakati wa kupanga nakutekeleza mradi.

Muhtasari wa mwezeshaji:

1. Mnaweza kujaribu zoezi hili kila mara.Litawasaidia washiriki kusimama kwanza nakuangalia yale wanayoyafanya - na kwanini. Pia linasaidia kujenga au kutia nguvufikra ya umoja miongoni mwa wanakikundi.

2. Mnaweza kubadilisha kazi zilizoorodheshwakwenye makaratasi, kutegemea na mradiumefikia wapi. Kwa mfano, inawezakusaidia kutumia mwanzoni mwa kuanzaawamu mpya katika mradi au kama usharikaunataka kuanzisha kitu kingine kipya.

3. Kama maswali yataibuka wakati wa mjadalakwa wakati ambao sio muafaka kujibu,wekeni katika sehemu ya kuegesha magari(angalia kipengele cha 2.1) ili muwezekuyashughulikia baadaye.

4. Andaa bajeti(Angalia sehemu ya 3, uk. 27)

Tumia muhtasari wa bajeti ufuatao ili kuandaabajeti ya mradi wako. Mnaweza kutumiamakadirio ya mwanzo (sio lazima yawe ya halisi) kwa ajili ya zoezi hili.

Page 44: Kufanikisha - Strategies for Hopev Kutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia, kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendo madhara ... Mengi yanaweza kufanikiwa kwa kutaka, kunuia kwa dhati

www.stratshope.org42

KUFANIKISHA

MAHITAJI (Maelezo)A: GHARAMA au

thamani katika fedhaya nchi yenu.

B: MICHANGO YAJAMII inayotegemewa

C: FEDHA ZILIZOOMBWAkutoka Nje au Mfadhili(kupata kiasi hiki toa B

kutoka A)

MRADI

MAFUNZO

WATENDAJI

JUMLA

MWONGOZO WA BAJETI:

5. Fuatilia mradi wenu(Angalia sehemu ya 4.3, uk. 32)

Mwisho, ni jinsi gani mtajua kuwa mradi wenuumefanikiwa? Muwe halisi kuhusu viashiria au

ni vipimo gani mtavitumia katika mpango wenuwa kufuatilia na kutathmini, na jinsi gani mta-pata takwimu au taarifa nyingine mnazohitaji.

& ‘Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwamoyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zakozote. Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza. Na ya piliyafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsiyako’. – Mathayo 22:37-39

Page 45: Kufanikisha - Strategies for Hopev Kutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia, kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendo madhara ... Mengi yanaweza kufanikiwa kwa kutaka, kunuia kwa dhati

43www.stratshope.org

UTANGULIZI MFUPI

Kiambatanisho Na. 2

Jinsi ya kupanga mudaMpango wa Kazi uliofafanuliwa - wakatimwingine unafahamika kama ‘Gantt chart’- nikifaa rahisi kutumia kwa ajili ya kupanga ratiba na kuendesha miradi. Ni cha msaadasana wakati unapokuwa unafanya mradi ambao

hatua moja inategemea nyingine. Na piakinaweka wazi ni hatua zipi zinaweza kufa-nyika sambamba, na ni njia nzuri pia ya kuweka wakati wa mwisho wa kila shughuli.

SHUGHULI Mwezi1

Mwezi2

Mwezi3

Mwezi4

Mwezi5

Mwezi6

Mwezi7

Mwezi8

Mwezi9

Mwezi10

Mwezi11

Mwezi12

Shughuli ya 1

Hatua 1

Hatua 2

Hatua 3

Shughuli ya 2

Hatua 1

Hatua 2

Hatua 3

Shughuli ya 3

Hatua 1

Hatua 2

Hatua 3

MPANGO WA KAZI:

SHUGHULI Mwezi1

Uhamasishaji

Chagua mzungumzaji

Wafundishe

Usimamizi

Mwezi2

Mwezi3

x

x

x

x

x

x

MFANO:

Kama mkijumuisha mpango wa kazi, tengenezeni nakala na muiweke ukutanikwenu kwa matumizi ya marejeo ya baa-daye. Shughuli zinazozidi mwezi mmojalazima ziwekewe alama inavyostahili.Orodhesha kila shughuli na hatua zinazohi-tajika kuchukuliwa ili kufanikisha.

Page 46: Kufanikisha - Strategies for Hopev Kutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia, kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendo madhara ... Mengi yanaweza kufanikiwa kwa kutaka, kunuia kwa dhati

www.stratshope.org44

KUFANIKISHA

Kiambatanisho Na. 3

Vyanzo vinginevyoTovuti

www.aidsalliance.org: Angalia hasa jinsi yaKutafuta Fedha na Uhamasishaji wa kupataMahitaji kwa ajili ya shughuli za VVU na UKIMWI.Kifaa cha Kusaidia Asasi zisizokuwa za Kiserikali(NGOs) na Asasi zenye Msingi wa Kijamii (CBOs),na Mazoezi ya Kujenga Matofali. Vifaa Shirikishivya Kuongeza Maendeleo na Huduma na Misaadakwa Yatima na Watoto walio katika MazingiraHatarishi.

www.christianaid.org: Kuna mambo mengimazuri kutoka kwenye mtazamo wa kidini.

www.fhi.org: Tovuti hii inatoa machapisho mengimazuri. Angalia kwa mfano, miongozo miwili yakimatendo kutoka Matendo kuhusu UKIMWI yaKikatoliki (Catholic AIDS Action) ya Namibia:Kutoa Ushauri-nasaha kwa misingi ya Kijamii kwawatu walioathiriwa na VVU na UKIMWI naKuwatia Moyo Watoto Walioathiriwa na VVU naUKIMWI (www.fhi.org/en/HIVAIDS/guide/caacounselling.html).

www.kit.nl: Vitabu na vitini kuhusu wajibu wataasisi za dini na zingine, vimetayarishwa naRoyal Tropical Institute huko Uholanzi.

www.msh.org: Angalia hasa kuhusu Kitini chaMeneja wa Afya. Maandiko haya yanatofautishakwa uhakika kati ya mchakato wa kupanga nakuendesha taasisi changa au mradi.

www.networklearning.org: Maandiko kwa ajiliya NGO zinazohitaji ujuzi mpya kuhusu mafunzokama ya kuendesha warsha, mwongozo wakutafuta fedha, mzunguko wa kuendesha mradina fedha za miradi midogo.

www.religionnews.com: Ni tovuti na maju-muisho ya anwani mpya zenye mambo ya imani.

www.stratshope.org: Wadhamini wa Mikakati yaKuleta Matumaini wamechapisha vitabu 16 vyamifano ya masomo, mikanda mitano ya video, nautaratibu mzima wa mafunzo ya Kivuko kwa ajiliya mwitikio wa misingi ya kijamii kuhusu VVU naUKIMWI, hasa kwa nchi zilizoko Afrika Kusini mwaJangwa la Sahara.

www.satregional.org: Maandiko ya kufundishia,rahisi (rafiki) kutumia yenye misingi ya uzoefuwa kijamii kufikia masuala kuhusu huduma, misaada, kushawishi na kuzuia VVU na UKIMWI,yaliyotayarishwa na Wadhamini wa masuala ya

UKIMWI Afrika ya Kusini (Southern African AIDSTrust).

www.steppingstonesfeedback.org: Miongozomizuri sana na maandiko mengine kwa ajili yavikundi vya kijamii wanaotumia mwongozo wamafunzo ya Kivuko kuhusu jinsia, VVU na UKIMWIna ujuzi wa mahusiano.

www.thegaia.org: Muungano wa Imani zotekuhusu masuala ya VVU na UKIMWI Ulimwenguni(The Global AIDS Interfaith Alliance).

www.unaids.org: Kwa ajili ya takwimu zinazo-husu VVU na UKIMWI katika nchi yenu, pamoja nataarifa za msingi na mambo mengine muhimu.

Maandiko ya Kufundishia

Mwandishi anashukuru mno kwa misaada yoteifuatayo katika kuandaa kitabu hiki, na anapendakuwatambulisha na kuwapendekeza kwa ajili yahabari za kina zaidi na msaada:

VVU, Afya na Jamii Yako (HIV, Health and YourCommunity): Mwongozo wa Kufanyia Kazi, uliota-yarishwa na Reuben Granich na JonathanMermin, Wachapaji wa Chuo Kikuu cha Stanford,Marekani, mnamo mwaka 1999.

Kuchangisha Fedha na Kuhamasisha Mali kwa ajiliya Kazi inayohusu VVU na UKIMWI, Toleo la 2 laUshirikiano wa Msaada wa Kiufundi wa Kimataifakuhusu VVU na UKIMWI, lilichochapishwa hukoBrighton, Uingereza, mnamo mwaka 2002.

Mbinu na Utendaji kwa ajili ya Mwitikio waWenyeji kuhusu VVU na UKIMWI: Sehemu ya 1 -Mbinu, Programu ya Umoja wa Mataifa kuhusuVVU na UKIMWI kilichoandaliwa na Wachapishajiwanaoitwa KIT, kutoka Amstadamu, Uholanzi,mnamo mwaka 2004.

Kitini Kipya: Kijitabu kwa ajili ya Taasisi yenyeMsingi wa Kijamii, kilichotayarishwa na CamillaSymes, Wadhamini wa Barnabas, Walmer, Afrikaya Kusini, mnamo mwaka 2002.

Kitini cha Tumeitwa KuhudumiaNa. 1: Sauti Zenye Matumaini: Viongozi waDini Wanaoishi au Walioathiriwa Binafsi naVVU na UKIMWI, ANERELA+, Wadhamini waMikakati ya Kuleta Matumaini na World VisionInternational, Oxford, Uingereza, mwaka 2005.

Page 47: Kufanikisha - Strategies for Hopev Kutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia, kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendo madhara ... Mengi yanaweza kufanikiwa kwa kutaka, kunuia kwa dhati
Page 48: Kufanikisha - Strategies for Hopev Kutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia, kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendo madhara ... Mengi yanaweza kufanikiwa kwa kutaka, kunuia kwa dhati
User
Typewritten Text
ISBN 978 1 905746 48 4 (E-book)