kuripoti uchaguzi kuripoti uchaguzi: clouds yawa majeruhi wa … · 2020. 9. 12. · utangazaji ya...

16
Kukuza Uhuru wa Vyombo vya Habari na kuhakikisha viwango vya juu kabisa vya weledi na uwajibikaji Jarida la Baraza la Habari Tanzania Toleo la 156, Agosti, 2020 ISSN 0856-874X TBC yatimuliwa mkutano wa Chadema TEF yahimiza waandishi walindwe EJAT kuwa Tanga Uk 7 Uk 11 Uk 9 Kuripoti uchaguzi Clouds yawa majeruhi wa kwanza Kuripoti uchaguzi: Clouds yawa majeruhi wa kwanza

Upload: others

Post on 04-Feb-2021

9 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

  • Waliomeremeta

    Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

    Kukuza Uhuru wa Vyombo vya Habari na kuhakikishaviwango vya juu kabisa vya weledi na uwajibikaji

    Jarida la Baraza la Habari TanzaniaToleo la 156, Agosti, 2020ISSN 0856-874X

    TBC yatimuliwa mkutano wa Chadema

    TEF yahimiza waandishi walindwe

    EJAT kuwa Tanga

    Uk 7 Uk 11Uk 9

    Kuripoti uchaguziClouds yawa majeruhi wa kwanza

    Kuripoti uchaguzi:Clouds yawa majeruhi wa kwanza

  • Waliomeremeta

    Jarida la Baraza la Habari Tanzania

    BODI YA UHARIRI:Kajubi Mukajanga Katibu Mtendaji – MCTDavid Mbulumi Meneja ProgramuHamis Mzee Mhariri

    MAWASILIANOKwa Maoni na Malalamiko:Katibu MtendajiBaraza la Habari Tanzani (MCT)S.L.P. 10160, Dar es SalaamSimu: +255 22 27775728, 22 2771947Simu ya Kiganjani: +255 784 314880Fax: + +255 22 2700370Baruapepe: [email protected]: www.mct.or.tzFacebook:- www.facebook.com/mediacounciltanzania Twiter:- www.twitter.com/mctanzania

    2

    TAHARIRIJarida la Baraza la Habari Tanzania

    Usimamishaji vyombo vya habari wakati wa uchaguzi uachweKampeni za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, 2020 zimeanza kwa matatizo. Baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kutahadharisha vyombo vya habari kuwa waangalifu katika kuripoti uchaguzi, chombo kimoja kikubwa cha habari kimekuwa muathirika wa kwanza.

    Bila shaka kwa kufuatilia onyo lililotolewa na NEC, Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano (TCRA) imeifungia kwa wiki moja Clouds kwa kukiuka kanuni kwa kutangaza Wabunge waliopita bila kupingwa.

    Kosa la Clouds ni kukiuka kanuni ya Sheria ya utangazaji ya vyama vya siasa ya mwaka 2015 katika vipindi vyao vya 360 na Power na kwamba uamuzi wa TCRA umetolewa baada ya Redio na Runinga ya Clouds kutangaza matokeo ya mchakato wa uteuzi katika baadhi ya majimbo bila kuidhinishwa na NEC.

    Ingawa vilikuwepo vyombo vingine hasa magazeti yaliyochapisha habari hiyo kabla kukubaliwa na NEC, havikuonywa na mamlaka ya udhibiti.

    Wakati Clouds wakitekeleza amri hiyo, NEC imetangaza siku moja baadaye majina ya wabunge waliopita bila kupingwa.

    Tukubali kwamba Clouds Media walikosea, lakini kukifungia kituo kwa wiki bila kujali athari za kiuchumi na kijamii sio sahihi na haki.

    Ni muhimu izingatiwe kuwa kituo hicho licha kuwa na mikataba ya utangazaji, wananchi wengi wanaokipenda wamekoseshwa kupata habari, elimu na burudani kufuatia hatua hiyo ya kukifungia.

    Pia kabla hatua kali kama hiyo kuchukuliwa, wenye mamlaka lazima wafikirie suala la kuishi kwa maana ya kipato cha watu wanaofanyakazi kwenye kituo hicho.

    Kwa hiyo ni muhimu kwa mamlaka za udhibiti kutambua kuwa katika kipindi cha uchaguzi kwa kuwa wananchi wanategemewa kufanya maamuzi makini, majukwaa mengi ya taarifa kwa maana ya vyombo vya habari yanahitajika.

    Kwa kupunguza vyombo vya habari, ni ushahidi wa wazi kwamba mamlaka za udhibiti hazioni umuhimu wa kuwa na vyombo vingi vikifanyakazi.

    Ni muhimu badala ya kuamuru ufungaji mamlaka za udhibiti lazima zizingatie kuchukua hatua ambazo zitahimiza uboreshaji wa mwenendo na utendaji wa vyombo vya habari. Kufungia kuwe mambo yaliyopitwa na historia.

    MCT, MSHINDI WA TUZO YA IPI 2003

    FREE MEDIA PIONEER

    Waandishi wa habari wakiwa kazini.

  • Waliomeremeta

    Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

    Na Mwandishi wa Barazani

    Katika siku ya pili ya kuanza kampeni za ucha-guzi mkuu wa mwaka huu Agosti 27, 2020, kituo cha runinga na radio cha Clouds Media kimeamriwa

    Amri hiyo inafuatia onyo lililotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) baada ya baadhi ya vyombo vya habari kutangaza na kuchapisha wagombea waliopita bila kupingwa.

    Wagombea zaidi ya 15 akiwemo

    Waziri Mkuu Kassim Majaliwa walisemekana wameshinda katika majimbo yao kwa staili hiyo.

    Ripoti hizo kuhusu walioshinda bila kupingwa zimetokea wakati kuna madai kutoka wagombea wa upinzani ambao wanadai walizuiwa na wasimamizi wa uchaguzi katika majimbo kuwa fomu zao zina makosa.

    Kumekuwepo taarifa kwamba walionyimwa haki yao ya kuwa wagombea wamepinga maamuzi ya wasimamizi wa uchaguzi na kukata rufani NEC.

    Kwa vyombo vya habari vimetumia mazoea na uzoefu kwamba inapotokea kuwa wagombea wengine wanapokosa sifa, mgombea aliyebaki anakuwa amepita bila kupingwa.

    Safari hii NEC inaviambia vyombo vya habari kwamba yenyewe ndiyo inayohusika

    3

    Habari

    Toleo la 156, Agosti, 2020

    Clouds marejuhi wa kwanza wa kuripoti uchaguzi

    Endelea Ukurasa wa 4

    Wananchi wakiwe kwenye mkutano wa hadhara.

    kusitisha matangazo kwa kuki-uka kanuni.

  • Waliomeremeta

    Jarida la Baraza la Habari Tanzania

    4

    Habari

    Jarida la Baraza la Habari Tanzania

    kutangaza taarifa za washindi. Hata hivyo Clouds

    inaadhibiwa wakati vyombo vingine kama gazeti la chama Uhuru na moja ya magazeti ya kimkakati Jamvi la habari zilichapisha habari hiyo katika kurasa zao za kwanza hali inayoonyesha kutumika viwango tofauti katika kuadhibu.

    Akitangaza adhabu kwa Clouds kutoka Agosti 28 had Septemba 3, 2020, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzankia (TCRA) ,James Kilaba alizungumzia ukiukwaji wa kanuni za utangazaji.

    Agosti 26 , 2020, alisema , Clouds ilitangaza taarifa kuhusu wagombea walioshinda katika kipindi cha runinga 360 na Power Breakfast cha redio.

    Wenye uzoefu na shughuli za vyombo vya habari wameeleza wasiwasi kwamba ikiwa katika siku ya kwanza ya mchakato wa uchaguzi hatua kali zinachukuliwa dhidi ya vyombo vya habari, vyombo vingapi vitafungiwa ifikapo siku ya kupiga kura Oktoba 28, 2020?

    “Hali ni mbaya na hakuna hata chombo kimoja cha habari kiko salama”, amesema mmoja wa watu hao akiongeza kuwa vyombo vya habari sasa vinapita katika

    ncha kali ya kisu. Mzoefu mwingine alisema

    kuwa vyombo vya habari vimegeuzwa kuwa gunia la mazoezi la mabondia, vikipigwa kuwa upande.

    Wakati Clouds imesimamishwa kwa wiki, Runinga ya mtandaoni ya Kwanza imesimamishwa kwa miezi 11 kwa kutangaza taarifa kuhusu virusi vya corona ambayo wenye mamlaka hawakupendezwa nayo. Gazeti la Tanzania Daima limefutiwa leseni yake na jaribio la kutaka kupata leseni nyingine inasuasua huku wafanyakazi wake wakiishi bila kipato.

    Clouds marejuhi wa kwanza wa kuripoti uchaguziInatoka Ukurasa wa 3

    Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti Mawasiliano Tanzania James Kilaba.

  • Waliomeremeta

    Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

    Na Mwandishi wa Barazani

    Baraza la Habari Tanzania (MCT) limeorodhesha maswali kadhaa yanayohusu ushiriki wa waandishi wa habari katika uchaguzi katika siasa za ushindani.

    Hii inafuatia kauli ya Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari, Kajubi Mukajanga, kuwa wanahabari watakaoshiriki katika uchaguzi mkuu wasirejee kwenye vyumba vya habari.

    Taarifa hiyo ilipokewa kwa mawazo mchanganyiko huku baadhi ya waandishi na wadau wakisema kuwa hiyo ni kukiuka haki ya kikatiba ya watu.

    Baraza pamoja na maswali hayo limetoa majibu kuhusu nafasi ya wanahabari katika uchaguzi hasa uchaguzi wa vyama vingi.

    Maelezo kamili katika orodha hiyo ya

    maswali na majibu kuhusu wanahabari kushiriki katika uchaguzi ni kama ifuatavyo.

    Mwaka huu 2020 ni mwaka wa Uchaguzi Mkuu Tanzania. Waandishi wa habari wana nafasi muhimu sana katika zoezi hili la kidemokrasia. Wao ni kati ya “watumishi wa umma” walio mstari wa mbele, bila kujali wameajiriwa katika chombo binafsi, cha serikali, chama, au hata cha dini.

    Ni jukumu lao kuwapasha habari sahihi na za kina Watanzania ili kuwasaidia katika kufanya maamuzi wanayoona ni sahihi wakati wa kupiga kura.Wanahabari wanapaswa kufanya kazi kwa uaminifu na kuaminiwa na wasomaji, watazamaji na wasikilizaji wao. Kwa sababu hiyo, wanapaswa kuzingatia maadili ya taaluma, lakini pia miiko inayowakataza kufanya lolote linaloweza kuwaondolea kuaminika na jamii.

    Kwa sababu hiyo, Baraza la Habari Tanzania (MCT) lilichapisha Mwongozo wa Kuandika Habari za Uchaguzi Tanzania toleo la Pili lililotolewa Machi 2015.

    Hivi karibuni kumekuwa na mjadala katika vyombo vya habari kuhusu nafasi ya mwandishi na vyombo vya habari wakati wa uchaguzi.

    Mjadala umejikita katika haki za mwanahabari kama raia, lakini hasa katika urari wa uhuru wa mwanahabari kugombea na kuendelea kuwa mwanahabari. Pamoja na Mwongozo wa 2015, tunatoa maelezo na ushauri ufuatao ili kuwasaidia wanahabari na wasimamizi wa vyombo vya habari wanapokabiliwa na mtanziko unaohitaji kufanyiwa uamuzi.

    Maelezo haya yanatolewa kwa utaratibu wa kujibu maswali ambayo yamekuwa yakiulizwa zaidi (Frequently Asked Questions – FAQ) mwaka huu kuhusu wanahabari na vyombo vya habari wakati wa uchaguzi.

    Swali: Je ni sahihi kwa mwandishi wa habari kujihusisha na siasa?Jibu: Siasa ni mfumo unaoongoza maamuzi katika jamii tunayoishi na siasa inamwathiri kila mtu. Kamusi Kuu ya Kiswahili iliyo-tolewa na Baraza la Kiswahili la Taifa (2017) inaelezea siasa kama: a) mfumo wa kiitikadi unaotumiwa na kikundi cha watu au jamii fulani kuwaendeshea serikali pamoja na shu-ghuli za jamii hiyo;

    b) shughuli zinazofanywa na serikali ya nchi fulani;

    ch) shughuli zinazolenga kuboresha hadhi ya mtu au kuongeza uwezo wa kimadaraka ndani ya asasi fulani.

    Kwa hiyo sote tunahusika na siasa hata kama hatuko ndani ya vyama vya siasa

    5

    Habari

    Toleo la 156, Agosti, 2020

    Endelea Ukurasa wa 6

    Wanahabari na uchaguzi: Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

    Wanahabari wakiwa kwenye mojawapo ya matukio ya habari.

  • Waliomeremeta

    Jarida la Baraza la Habari Tanzania

    6

    Habari

    Jarida la Baraza la Habari Tanzania

    kuendesha siasa za kishindani ili kutafuta madaraka ya dola. Ni sahihi na ni haki ya mwanahabari kwa kuwa hii ni haki ya kiraia na kikatiba. Ni haki yao ya msingi kama walivyo raia wengine hapa nchini.

    Swali: Ikiwa ni hivyo, ina maana gani kusema waandishi wa habari wanaoji-husisha katika siasa za ushindani wa-ondoke kwenye vyumba vya habari?

    Jibu: Kwanza, ieleweke kuwa mwandishi wa habari kama sehemu ya jamii ana haki ya kikatiba kuwa mpiga kura na pia ana haki ya kupigiwa kura. Lakini kwa asili ya kazi yake, anapaswa kuondoka katika chumba cha habari kwa wakati wa mchakato wa uchaguzi kwa kuwa akiamua kuwa mgombea, tayari amechukua upande katika ushindani wa kisiasa. Ikumbukwe kuwa hivi sasa nchi yetu iko katika mfumo wa vyama vingi, ambapo vyama mbalimbali vinashindana katika uchaguzi. Haitaswihi kwa mwandishi asubuhi kupanda jukwaani kupiga salamu za chama na jioni kuwa katika chumba cha habari kuandika au kuhariri habari za uchaguzi, au katika studio. Na uchaguzi ndiyo habari inayotawala katika kipindi hicho chote. Kwa hiyo anapaswa kukaa kando.

    Ni kanuni ile ile inayozuia watumishi wa umma kuwa ofisini wanapoingia katika uchaguzi. Ni kuepuka mgongano wa maslahi (conflict of interest). Ni kuhakikisha kuwa habari zinaandikwa na kuchakatwa bila upendeleo (impartiality).

    Swali: Lakini mwandishi mwadilifu anaweza kuhakikisha kuwa anafanya kazi yake kwa kufuata maadili (ethi-cal) na kutopendelea (impartial). Kwa nini asiruhusiwe?

    Jibu: Bahati mbaya, kanuni ya kuepusha mgongano wa maslahi na impartiality haitegemei kabisa dhamira njema ya muhusika. Mizania yake inaegemea kwenye: wenzio watakuonaje (how will your peers perceive you) na watu watakuonaje (how will the general public perceive you). Kwa hiyo kama kuna mazingira yoyote yanayoleta mashaka au kuweza kuleta mashaka, muhusika anapaswa kukaa pembeni. Mahakimu na majaji wanapojitoa kusikiliza kesi kwa

    kuwa kuna shutuma kwamba watapendelea upande fulani, wanajitoa si kwa kuwa hawana maadili au weledi, au hawajiamini kuwa wanaweza kufanya kazi yao bila upendeleo. Wanajitoa kwa sababu ya kanuni hiyo. Kwa hivyo kama kuna mazingira ya kufanya mwandishi atiliwe shaka kwa kuwa ameshaonyesha yuko upande fulani katika mchakato wa ushindani wa kisiasa, basi anakaa pembeni ili ashiriki vizuri bila kumkwaza yeyote.

    Swali: Je, suala hili la waandishi kuto-jihusisha na siasa za ushindani wakiwa ndani ya vyumba vya habari liko kishe-ria?

    Jibu: Hapana; sheria zetu za habari

    haziongelei suala hili. Kuna makatazo ya kimaadili ambayo pia ni makatazo ya kisheria, na mengine sio ya kisheria. Makatazo kama hayo husimamiwa na wasimamizi wa vyombo vya habari wenyewe na/au vyombo vya kitaaluma, sio sheria au mahakama.

    Swali: Ni sababu zipi zinazosababisha mwanahabari akiingia kwenye siasa za ushindani ajitenge na taaluma, ukilin-

    ganisha na taaluma nyingine?Jibu: Ni kwa asili na mahitaji ya kazi

    yake kama ilivyoelezwa hapo juu. Mwanahabari anatoa habari, uchambuzi, maoni na kuvisambaza kwa jamii. Kukiwa kuna suala linalohusu mgongano wa maslahi ama uwezekano wa upendeleo anakaa pembeni. Katika hilo, mhasibu, mhandisi, daktari na wengine wana mazingira tofauti, japo nao wana mambo yao ambayo yanaweza kuwasababishia mgongano wa maslahi. Lakini pia utumishi wa umma unazuia kuingia katika mchakato wa uchaguzi ukiwa ofisini. Jambo kubwa hapa ni conflict of interest na

    impartiality.

    Swali: Mbona kuna waandishi wa michezo ambao ni mashabiki wa timu fulani au waandishi wa bu-rudani ambao ni wapenzi wa wasanii fulani? Unasemaje kuhusu hao?

    Jibu: Kitakuwa kichekesho kulinganisha mapenzi kwa timu ya mpira au bondia fulani au mwanamuziki fulani na uchaguzi wa viongozi wa kisiasa. Kila mtu ana kitu fulani anachokipenda, lakini hayo ni mambo binafsi. Kupigania nafasi ya uongozi wa kisiasa sio jambo binafsi. Muhimu ni kuzingatia suala la maadili na mgongano wa maslahi.

    Swali: Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanza-nia (MCT), alikuwa mbunge wa Bunge la Ka-tiba, je hii siyo siasa?

    Jibu: Bila shaka ni siasa, tena siasa ya hali ya juu! Mgongano wa maslahi uko wapi katika kushiriki katika mchakato jumuishi na wa pamoja wa kuandika katiba kwa ajili ya nchi?

    Suala si siasa; na anayesema siasa hazimhusu haelewi sana asemalo. Siasa zinaathiri maisha ya kila mmoja. Katika ushindani wa vyama ni muhimu wanaoripoti ushindani huo waonekane kazi yao inafanywa kwa haki. Lakini pia tukumbuke kuwa siasa ya Bunge la Katiba haikuwa siasa ya ushindani, ni tofauti sana na hii ya sasa ya kugombea nafasi mbali mbali ndani ya vyama vya siasa, Katibu alikwenda kwenye Bunge la Katiba kama mmoja wa wawakilishi wa tasnia ya habari

    Maswali yanayoulizwa mara kwa maraInatoka Ukurasa wa 5

    i

    WANAHABARI NA

    UCHAGUZI – MASWALI

    YANAYOULIZWA ZAIDI

    Agosti 2020

    Endelea Ukurasa wa 8

  • Waliomeremeta

    Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

    Na Mwandishi wa Barazani

    Shirika la Utangazaji la Tanza-nia (TBC) liliamriwa kuondoka kwenye mkutano wa kampeni wa Chadema . Chadema ilikuwa ikifanya mkutano

    wake wa kwanza wa kampeni uliokuwa ukihutubiwa na mgombea wa urais kwa tiketi ya chama hicho, Tundu Lissu, Mbagala Jijini Dar es Salaam na inaelekea TBC ilikuwa ikitoa matangazo yake kwa namna ambayo haikupendeza chama hicho.

    Kulikuwa na madai kuwa badala ya kuonyesha umati wa watu waliohudhuria mkutano huo, kamera ya TBC ilikuwa ikionyesha watu wachache waliokuwa wakifika katika eneo la mkutano kabla ya hata mkutano kuanza.

    Pia ilidaiwa shirika hilo la utangazaji halikuwa likimuonyesha mgombea huyo urais wakati akihutubia katika mkutano huo.

    Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alizungumzia mgogoro huo na TBC na kusisitiza kuwa katika mkutano huo waliwataka waondoke.

    Mbowe alisema kuwa uamuzi wa chama hicho ulipokewa vizuri na wapenda habari kutangazwa kwa haki.

    Alisema chama chake kinaamini katika uhuru wa habari na inaafiki na kuukubali uandishi wa weledi lakini kinapinga muandishi wa upendeleo.

    “ Tunakaribisha chombo chochote cha ambacho kinataka kutangaza shughuli zetu lakini matangazo yao yawe ya haki na yasiyo na upendeleo.’

    Mbowe alisema TBC inaweza kusamehewa na kukaribishwa Chadema kama itabadili mwenendo wa kutangaza habari za chama hicho.

    7

    Habari

    Toleo la 156, Agosti, 2020

    …TBC yatimuliwa kwenye mkutano wa Chadema

    Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akihutubia mkutano wa kampeni.

  • Waliomeremeta

    Jarida la Baraza la Habari Tanzania

    katika mchakato wa Katiba na si mwanachama wa chama fulani. Ndio maana hukumuona akipanda jukwaani kunadi sera za chama fulani wala kuvaa gwanda.

    Swali: Kuna vyombo ambavyo vinamilikiwa na vyama vya siasa, hili limekaaje? Je, vyombo vya habari vinaruhusiwa kuunga mkono vyama?

    Jibu: Ieleweke kwamba si kosa kwa chama cha siasa kuwa na chombo cha habari. Historia inatuonyesha kuwa mwanzo wa magazeti barani Ulaya yalianzishwa yakiwa yanashadadia vyama na mielekeo ya kiitikadi. Kwa hiyo chombo hiki cha habari kiliunga mkono mrengo wa kushoto, hiki mrengo wa kulia, na kadhalika. Lakini hata chombo cha habari kisichomilikiwa na chama cha siasa kinaweza kuamua kuunga mkono sera za chama kimojawapo. Na kwa hakika, chombo cha habari kinategemewa kutetea maslahi ya jamii kwa jinsi kinavyoona, na wakati wa uchaguzi jambo hili hujitokeza wazi katika kuunga mkono sera zinazonadiwa na washindani.

    Lakini lazima chombo cha habari kiweke wazi msimamo wake, na ueleweke wazi bila kificho (declare interest). Lazima wanaokisikiliza, kukisoma au kukitazama waujue msimamo huu. Hii itawasaidia kuwa na faida ya ziada wakati wanapotafakari waliyoyapata toka chombo hicho. Ndiyo maana, mathalani, tunajua kuwa CNN inaegemea Democratic Party wakati Fox tunajua iko upande wa Rais Donald Trump na chama chake. Tunajua hili hata pale tunapochukua remote na kuchagua channel fulani.

    Hata hivyo, vyombo vyote vya habari vinahusika kufuata utaratibu na maadili ya uandishi wa habari. Hata kama mwanahabari yuko kwenye chombo cha habari cha chama fulani, anatakiwa kutopendelea, kutompaka mwingine matope lakini pia kufanya uandishi na sio propaganda au uzushi, ilimradi anufaishe upande huu na kukandamiza mwingine. Na ni lazima kutenganisha maoni na habari.

    Swali: Mwandishi au waandishi ambao wamelikiuka hili wana adhabu gani?

    Jibu: Hili ni suala la mjadala, haliko kwenye sheria. Kama mlivyosikia kuna Padre wa Kanisa Katoliki amesimamishwa kutokana na kujihusisha kwake na siasa za ushindani; wao inawezekana wana sheria za dini zinazowazuia, lakini sisi hatuna sheria. Na hapo ndipo linakuja suala la vyombo vya habari vyenyewe kujiwekea utaratibu wa ndani.

    Swali: Majuzi MCT mlinukuliwa mkisema wamiliki wa vyombo vya habari wanapaswa kulitolea miongozo iliyo wazi ndani ya vyumba vya habari, ni miongozo gani mlikuwa mnailenga hapa?

    Jibu: Katika tasnia ya habari, mbali ya Kanuni za Maadili (Code of Ethics), kuna miongozo inayotuongoza katika utendaji wa kila siku ndani ya vyombo vya habari. Kuna miongozo ya namna ya kuvaa (dress code), namna ya kuandika habari zetu (stylebooks), miongozo inayotuongoza katika shughuli za kila siku za ukusanyaji habari ikiwamo mambo kama ununuaji wa habari na picha, utafutaji wa habari kwa kificho, na kadhalika (Internal codes of conduct). Kuna sera za uhariri (editorial policies), kuna mhariri wa jamii (Ombudsman, Public Editor). Hii ndiyo miongozo ambayo inaweza kuwekwa madhubuti kwa ajili ya kuwaongoza waandishi wa habari katika kila wanalotaka kulifanya.

    Katika suala hili, ni bora kila chombo cha habari kilitafakari na kuona kinalitolea maamuzi gani. Liwekwe wazi katika sera ya uhariri ili mwandishi au mhariri anapoingia katika chombo hicho aelewe tangu mwanzo. Baraza la Habari limeshasaidia vyombo kadhaa kuandaa miongozo yake ya ndani kwa maombi ya vyombo hivyo.

    Swali: Je, baada ya uchaguzi, mwandi-shi aliyeondoka kwa ajili ya kugombea na hakufanikiwa anaruhusiwa kurudi?

    Jibu: Hilo nalo ni suala la miongozo katika vyombo vya habari. Sera ya chombo iseme wazi. Kwa mfano, kuna vyombo vya kimataifa ambavyo ukitaka kugombea nafasi yako inakuwa wazi na kutangazwa. Ukitaka kurudi, kama nafasi utaikuta bado wazi, unashindana na wenzio na ukipata, unajaza fomu ya kueleza mgongano wa maslahi (declaration of conflict) ili hilo lizingatiwe katika namna utakavyopangiwa kazi. Wengine, kama Nation Media Group ya Kenya na Standard, ukishakwenda kwenye siasa huruhusiwi kurudi. Hata ukibainika kuwa kada wa chama unaambiwa uchague uandishi au ukada. Baraza la Habari la Kenya ambalo husajili wanahabari mwaka 2016 lilitoa taarifa kuwataka wanahabari wote waliokuwa na malengo ya kugombea mwaka 2017 kujiuzulu mara moja na kutoa tahadhari ya kuwafutia usajili wote ambao wangejaribu kuingia katika uchaguzi wakiwa ndani ya vyumba vya habari. Bodi ya Uhariri ya gazeti la New York Times inapiga marufuku jaribio lolote la kutafuta

    nafasi ya kisiasa ukiwa bado mwandishi wao. Ni miongozo ya ndani ambayo wameona itawasaidia kuepusha migongano ya maslahi na upendeleo. Ni hatua walizochukua kuhakikisha kuwa heshima ya vyombo hivyo haitiliwi shaka.

    Lakini pia miongozo hii itaeleza, ikiwa chombo kitampokea mwandishi anayerudi baada ya kuwa mwanasiasa, atafanya kazi ipi? Labda atakuwa mwanasafu (columnist), au labda kitamtumia katika majopo ya mijadala huku historia na mrengo wake vikiwekwa bayana, na kadhalika. Jambo la msingi ni kuilinda taaluma dhidi ya mwonekano wa kutozingatia misingi yake ya kutenda haki na kutoa ukweli kwa usahihi.

    Swali: Mwandishi wa habari kuwa mwanasafu kunamtofautisha vipi na uana siasa wake? Maana kuna wana-safu ambao ni wanasiasa.

    Jibu: Ukiwa mwanasafu, huwi katika nafasi ya kuamua habari gani itoke au isitoke, lakini pia, hupati nafasi ya kuhariri habari na kuifanya uonavyo. Ni muhimu pia mwishoni mwa safu vyombo vya habari vitoe maelezo mafupi kuhusu wanasafu wake, ili watu wawaelewe.

    Swali: Kuna mwandishi mahiri sana, mwalimu na aliwahi kuwa mwanasiasa mpaka kuwa mbunge, mpaka mwezi uliopita alikuwa Mhariri wa Jamii (Public Editor) kwenye kampuni moja kubwa ya habari nchini. Hili likoje hasa kiutendaji kazi?

    Jibu: Hii ni kazi mojawapo ambayo mtu kama huyo anaweza kufanya. Jukumu la Mhariri wa Jamii ni kuhakikisha taaluma na maadili ndani ya chombo husika yanazingatiwa ili kulinda maslahi ya mlaji (jamii) na kutunza heshima ya chombo. Yeye hahusiki na maamuzi ya kiuhariri kabla ya habari au makala kuchapishwa. Lakini anatoa ushauri wa kitaalamu kuhusu maudhui yaliyochapishwa. Lakini pia Mhariri wa Jamii hushughulikia malalalamiko kutoka kwa wasomaji pale yanapoletwa, kwa lengo la kuyasuluhisha ili kuzinufaisha pande zote, ule wa chombo cha habari na wa mlalamikaji.

    Mhariri wa Jamii pia huandika maoni na makala kuhusu mwenendo wa taaluma, lakini pia huandika kuelimisha jamii kuhusu ufanyaji kazi wa vyombo vya habari na dhima ya vyombo hivyo. Hutoa elimu, yaani media literacy. Kazi mahsusi hutegemea mkataba wake lakini kwa ujumla hayo ndiyo majukumu yake. Uwezekano wa mgongano wa maslahi ni mdogo sana katika kazi ya Mhariri wa Jamii.

    8

    Habari

    Jarida la Baraza la Habari Tanzania

    Maswali yanayoulizwa mara kwa maraInatoka Ukurasa wa 6

  • Waliomeremeta

    Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

    9

    Toleo la 156, Agosti, 2020

    Habari

    Na Mwandishi wa Barazani

    Kaimu Mwenyekitti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile amehimiza wahariri kuwalinda wanahabari wao watakaokuwa wakiripoti uchaguzi.

    Alisema uchaguzi umewadia, tusikubali kusukumwa na wanasiasa.

    Alikuwa akizungumza katika mkutano wa mwaka wa TEF mjini Dodoma.

    Uchaguzi Mlkuu wa kumchagua Rais, Wabunge na Madiwani utafanyika Oktoba 28, 2020.

    Wakili mashuhuri , Jebra Kambole akiwakilisha Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu aliwasilisha mada kuhusu sheria za vyombo vya habari zinazohusu uchaguzi akielezea mambo muhimu ya sheria hizo na vikwazo.

    Wawakilishi wa Mfuko wa Wanawake (WFT) pia walizungumzia uchaguzi na vyombo vya habari.

    Taasisi zingine zilizowasilisha mada kwenye mkutano huo uliofanyika Agosti 21 na 22 ni pamoja na Benki ya NMB, Umoja wa Mataifa, Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Jii, Bodi ya Manunuzi ya Umma, RITA, Wakfu wa Habari Tanzania na Mfuko wa

    Fidia ya Wafanyakazi. Wazungumzaji wa taasisi hizo

    waliwaelimisha wahariri kuhusu majukumu ya taasisi zao na jinsi ya kushirikiana na vyombo vya habari.

    Taasisi hizo mbalimbali siyo tu ziliwasiloisha mada kwenye mkutano huo, bali pia zilifadhali.

    Masuala muhimu ya TEF yalizungumzwa katika mkutano huo

    ni juhudi za kuwezesha kupatikana kwa usajili wa jukwaa hilo.

    Mkutano ulifahamishwa kuwa hatua iliyofikiwa ni kuchukua nafasi ya jukwaa moja la zamani lililojulikana kwa jina la EFOTA. Chini ya mchakato unaoendelea EFOTA iliyokuwa na malengo mapana itafutwa na mahala pake patajazwa na TEF mpya.

    TEF yahimiza waandishi kulindwa wakati wa uchaguzi

    Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) , Deodatus Balile akizungumza katika mkutano mkuu wa jukwaa hilo. Kulia ni Katibu wa TEF, Neville Meena.

    Wahariri waliohudhuria mkutano wa mwaka wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) mjini Dodoma.

  • Waliomeremeta

    Jarida la Baraza la Habari Tanzania

    10

    Fursa

    Jarida la Baraza la Habari Tanzania

    RAINFOREST JOURNALISM FUND CALL FOR PROPOSALS—INTERNATIONAL PROJECTS

    The Pulitzer Center is inviting proposals for grants to journalists reporting for wide-reaching major news media outlets on tropical rainforests in any part of the world.

    Thematic AreasThe supported international journalism projects will focus on the following themes:• Tropical forests' role in the overall climate

    equation and weather patterns globally, regionally and locally, and the consequences for human life and living conditions caused by deforestation

    • Deforestation drivers• Solutions to halt deforestation

    Funding Information• The Pulitzer Center will fund international

    travel costs associated with reporting projects on tropical rainforests, with an emphasis on issues that have gone unreported or under-reported in the mainstream American media.

    • The amount of individual travel grants will depend on the specific project and detailed budget planning. Most awards fall in the range of $5,000 to $15,000 but depending on project specifics may be higher.

    • On approved projects, half of the grant amount is generally paid just before travel and the remainder on submission of the principal material for publication or broadcast. Specific grant terms are negotiated during the application process.

    Eligibility CriteriaGrants are open to all journalists, writers, photographers, radio producers or filmmakers; staff journalists as well as free-lancers of any nationality are eligible to apply.

    Applications Process• Applications must be received in English.• Applications must include the following: o A description of the proposed project,

    including distribution plan, in no more than 250 words

    o A preliminary budget estimate, including a basic breakdown of costs. Travel grants cover hard costs associated with the reporting; please do not include stipends for the applicants. Fixer/translator/driver fees are acceptable

    o Three samples of published work, either print or broadcast.

    o Three professional references. These can be either contact information, or letters of recommendation. The latter is encouraged when letters from interested producers or editors are available.

    o A copy of your curriculum vitae. o Applications may also include a more

    detailed description of project but this will be considered as optional supplement only. The most important part of the submission is the 250-word summary.

    For more information, visit Pulitzer Center.

    Highlights Important Dates

    Post Date - 24-Jul-2020

    Deadline Date – Ongoing

    Donor NamePulitzer Center

    Grant Size$10,000 to $100,000

    CategoryGrant

    Reference URLhttps://pulitzercenter.org/rainforest-

    journalism-fund-call-proposals-international-projects

    Focus Areas of Interest Environment

    Media

  • Waliomeremeta

    Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

    11

    Habari

    Toleo la 156, Agosti, 2020

    Na Mwandishi wa Barazani

    Kanuni mpya za maudhui mtandaoni zinabinya na haziendani na viwango vinavyokubalika vya kimataifa.

    Uchambuzi kuhusu kanuni hizo, unaeleza kuwa zinabana na hasi kwa uhuru wa uhariri, uhuru wa habari. uandishi wa habari na uhuru wa kujieleza kwa jumla.

    Uchambuzi huo uliagizwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) kupitia kanuni hizo ambazo zinafuta zile za mwaka 2018.

    Imeelezwa kuwa katika uchambuzi huo kanuni hizo siyo tu zina orodha ndefu ya kanuni zinazozuiliwa, pia zimeingiza taratibu ngumu za leseni.

    Kanuni zinakiuka viwango vya kimataifa vya uhuru wa kujieleza, vifungu 6(d) na 7(2) vya mkataba wa kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa mwaka 1999, kifungu cha 18 cha Katiba ya jamhuri ya Muungano ya Tanzania ya mwaka 1977 na Sera ya Taifa ya Utangazaji ya mwaka 2003.

    Kanuni hizo zinaimarisha kashfa kuwa uhalifu zinazuia vyanzo vya habari kutotajwa, zinatoa faini kubwa kwa ukiukaji na kuipa madaraka makubwa ya kuondoa maudhui Mamalaka ya Udhitibi Mawasiliano Tanzania (TCRA).

    Wakati kanuni za mwaka 2018 zinazofutwa zilielekeza maudhui yanayokataliwa yaondolewa katika saa 12, kanuni za sasa zinatoa saa mbili tu kufanya hivyo.

    Kanuni hizo zimegawa leseni katika makundi manne - habari na matukio, burudani,

    elimu/ dini na kutangaza moja kwa moja katika vyombo mbalimbali –redio na runinga.

    Kuanzishwa kwa lenseni za makundi, uchambuzi unaeleza ni jaribio la kubana upeo wa chombo kwa maana ya maudhui na maeneo ya kijiografia.

    “Kwa mfano, iwapo chombo ni kikubwa, vingine vyote vinatakiwa ama kushughulikia habari na matukio tu, burudani au masuala ya dini ama kuwa na leseni zaidi ya moja.

    Kwa ujumla hakuna hata chombo kinachoweza kutoa habari ama taaarifa kwa umma bila kuwa na leseni, jambo linalokiuka haki ya kikatiba inayotolewa na kifungu cha 18 kinachotoa uhuru kwa kila mtu kutafuta, kukusanya, kuchakata na kusambaza habari bila kujali mipaka ya nchi.

    Uchambuzi huo unaeleza na pia kuongeza kuwa kanuni hizo pia zinabinya uandishi wa habari za uchunguzi kwa kuwa zinazuia uchapishaji wa mawasiliano rasmi ya siri.

    Kuhusu chanzo kutotambulishwa ambalo ni jambo muhimu katika uhuru wa kujieleza, kanuni zinazuia.

    Uchambuzi huo umeonyesha kuwa kutojitambuliwa kunatoa mwanya mpana wa siri kwa mtu kuwa na maoni na kuwa na uhuru wa kujieleza bila kuingiliwa.

    Ukizungumzia msimamo wa msimamizi wa Umoja wa Mataiafa wa Uhuru wa Kujieleza, uchambuzi huo unaeleza kuwa njia bora ni kutumia vyanzo bila kujitaja ama vifaa vya kitaalamu ili kukuza na kulinda uhuru wa kujieleza mtandaoni badala ya kuukwaza kwa kuzuia utaratibu wa kutojitambulisha.

    Kuhusu Sera ya Utangazaji ya 2003, imeelezwa na uchambuzi huo kuwa kanuni hizo haziendani kabisa na matakwa ya sera hiyo ya utangazaji katika njia mbalimbali kama: • Kanuni hizi hazitoi

    mazingira wezeshi kwa vyombo vya habari kufanyakazi kwa ufanisi na uhuru wa habari kama ilivyo katika Sera ya utangazaji ya 2003. Ingawa sera inataka kuwepo mazingira wezeshi, kanuni zinakwaza uhuru wa habari kwa kuwa na taratibu za kubinya habari na kufanya kashfa kuwa uhalifu.

    • Wakati sera ya Habari na Utangazaji ya 2003, inahimiza serikali kuondoa vikwazo kwa wananchi kupata taarifa, kanuni zinaweka vikwazo hivyo.

    • Kwa kanuni hizi kusisitiza kuwa na leseni na hatua zingine na kubinya maudhui haki ya raia ya kupata habari inaathirika. Hii ni kutokana na vizingiti vikali vinaathiri uhuru wa kujieleza ambavyo vinaaathiri pia kupata taarifa.

    Kanuni za mtandaoni za mwaka 2018 zilipotolewa na serikali, MCT kwa kushirikiana na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na Umoja wa Watetezi wa Haki za Binadamu THRDC) walifungua shauri Mahakama Kuu.

    Kufuatiwa kupitishwa kwa kanuni hizi mpya, kesi hiyo haipo tena.

    Uchambuzi kamili wa kanuni hizi mpya unapatikana katia tovuti ya MCT www.mct.or.tz

    Kanuni mpya za mtandaoni zabana uhuru

    wa habari, kujieleza

  • Jarida la Baraza la Habari Tanzania

    12

    Balozi mstaafu Ferdinand Kamuntu Ruhinda amekuwa mwandishi wa habari, mhariri, mtumishi wa serikali mwandamizi, mwanadiplomasia, mwanastrategia wa kisiasa na mfanyabiashara. Alikuwa rafiki wa karibu wa Rais mstaafu wa awamu ya tatu, hayati Benjamin William Mkapa, aliyefariki dunia Julai 23, mwaka huu baada ya kuugua.

    Balozi Ruhinda alikutana na Mkapa kwa mara ya kwanza mwaka 1966 kwenye chumba cha habari cha iliyokuwa Tanganyika Broadcasting Corportion (TBC) wakati Ruhinda akiwa ameajiriwa kuwa Mwandishi wa Habari na Mkapa msoma habari wa kujitegemea.

    Tangu hapo walianzisha urafiki usiomithilika wa kitaaluma na kijamii ambao umedumu kwa zaidi ya nusu karne. Mwaka 1967, walifanya kazi pamoja kwenye Magazeti ya Chama ya Uhuru, la Kiswahili na la Kiingereza, The Nationalist, ambako Mkapa alikuwa Mhariri Mtendaji na Ruhinda Mhariri Msanifu na baadaye Mhariri wa Habari.

    Mwaka 1972 wakati Mkapa aliopoteuliwa kuwa Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali, The Daily News, Ruhinda akachukua nafasi ya Mkapa kwenye Magazeti hayo ya Chama. Mwaka 1974 Mkapa aliteuliwa kuwa Mwandishi wa Habari wa Rais Nyerere na mwaka 1976 akahamishwa na kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Habari Tanzania (SHIHATA) ambapo mwaka huo huo Ruhinda naye akachukua nafasi ya Mhariri Mtendaji wa The Daily News.

    Baadaye Mkapa akaingia katika shughuli za diplomasia na baadaye siasa akiwa Mbunge na Waziri hadi kufikia nafasi ya juu kabisa ya kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mwaka 1995.

    Ruhinda hakuingia kwenye Siasa hasa bali alijiunga na shughuli za Diplomasia pia, kwanza akiwa Naibu

    Balozi wa Tanzania nchini Sweden na baadaye Balozi kamili Canada na China kabla ya kustaafu utumishi wa umma, mwaka 1993.

    Ni watu wa umri mmoja, miaka 82.Akielezea kuhusu wapi, vipi na lini

    hasa mlikutana kwa mara ya kwanza na Mkapa, Balozi Ruhinda alisema alikutana na Ben Mkapa kwa mara ya kwanza, mwaka 1966, miaka 54 iliyopita, tukiwa bado vijana. Tokea wakati huo, wamekuwa marafiki. Tuliaminiana sana. Nadhani sitakosea kusema kuwa tokea nijuane naye, haikupata kupita wiki mbili bila kukutana naye, ana kwa ana, ama kuzungumza naye kwa simu, ama kwa mawasiliano ya aina nyingine. “Na msinielewe vibaya, Ben alikuwa na marafiki wengi, na wa karibu, siyo mimi peke yangu”

    anasema.Alisema walikutana katika

    mazingira ya kazi. Wakati huo yeye akiwa ameajiriwa kama Mwandishi wa Habari katika Chumba cha Habari cha Tanganyika Broadcasting Corporation (TBC), wakati huo yeye, Ben alikuwa Msoma Habari za Kiingereza wa kujitegemea, anayekuja wakati wa muda wake nje ya kazi.

    Balozi Ruhinda anasema Ben aliipenda kazi yangu na urafiki wetu ulianzia hapo.

    “Nimemfahamu kwa muda mrefu sana, zaidi ya miaka 50. Kwa kweli, uhusiano wetu ulikuwa zaidi ya urafiki. Tulikuwa ndugu. Tulikuwa watu tofauti sana mwanzoni”, anasema na kuongeza kuwa“sote

    Mkapa kama mwandishi wa habari - Ruhinda

    Endelea Ukurasa wa 14

    Katika mahojiano maalum na waandishi watatu waandamizi nchini, Balozi Ferdinand Ruhinda ametoa ushuhuda na shukrani kuhusu rafiki na ndugu yake hayati Benjamin Mkapa. Saidi Nguba, mmoja wa waandishi hao anaelezea jinsi Balozi Ruhinda anavyomzungumzia Mkapa kama Mwandishi wa Habari.

    Balozi Ferdinard Ruhinda akisalimiana na Rais Benjamin Mkapa katika mojawapo ya matukio ya kijamii na kifamilia.

    Wasifu

  • Waliomeremeta

    Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

    13

    Toleo la 156, Agosti, 2020

    Habari

    Na Mwandishi wa Barazani

    Amri ya Serikali ya Zanzibar kumsimamisha mwandishi wa habari kwa miezi sita imeondolewa. Talib Ussi Hamad, ambaye

    anaandikia gazeti la Tanzania Daima sasa yuko huru kufanyakazi tena na alipoulizwa kuhusu uamuzi huo wa serikali alisema amefurahishwa kwamba sasa anaweza kufanyakazi tena.

    Barua ya kuondoa amri hiyo ilitiwa saini na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Zanzibar, Dk.Juma Mohamed Salum.

    Barua hiyo ya Agosti 3, 2020 ilieleza“umeruhusiwa kuendelea na kazi ya uandishi kwa mujibu wa Sheria ya Magazeti , Machapisho na Wakala Na 5 ya 1988 na marekebisho yake Na 8 ya 1997.”

    “Kwa barua hii, idara inafuta uamuzi wake wa awali uliotolewa kupitia barua kumbukumbu namba IHM/WH32/1/VOL.IV/40 ya 20/4/2020”,barua hiyo imeeleza.

    Hamad alisimamishwa kwa kile wenye mamlaka serikalini kudai alikiuka maadili ya taaluma.

    Anadaiwa kuwa alitoa habari kuhusu mgonjwa wa COVID-19 bila ridhaa yake kinyume na maadili ya kitabibu.

    Hamad alisema alibanwa ili aombe radhi baada ya kuripoti habari yake hiyo lakni alikataa kwa maelezo kuwa habari hiyo ilikuwa na umuhimu kwa umma.

    Pia alisema alifungua kesi katika Mahakama Kuu Zanzibar Julai 3 kupinga kwa kutopewa nafasi ya kujibu kabla ya kusimamishwa.

    Serikali ya Zanzibar ilitarajiwa kupeleka majibu Mahakamani Agosti 4, lakini badala yake akapokea barua ya kumruhusu kuendelea na uandishi wa habari.

    Aliposimamishwa Baraza la Habari Tanzania (MCT) na Kamati ya Kutetea Waandishi (CPJ) zilihimiza aachiwe ili afanye kazi yake.

    Amri ya kumsimamisha Hamad imeondolewa wakati gazeti alilokuwa akiandikia– Tanzania Daima, halisamabazwi tena kwa sababu leseni yake ilifutwa na Msajili wa Magazeti wa Idara ya

    Habari Tanzania Bara kwa madai ya kukiuka maadili.

    Hamad ameeleza matumaini kwamba gazeti hilo huenda likaruhusiwa kuchapishwa tena kabla ya uchaguzi mkuu.

    Mwandishi aruhusiwa kufanyakazi tena Z’bar

    Mwandish Talib Ussi Hamada.

  • Waliomeremeta

    Jarida la Baraza la Habari Tanzania

    14

    Jarida la Baraza la Habari Tanzania

    tukitokea pande mbili tofauti kabisa za nchi… pembezoni mwa nchi. Mmoja akitokea Kaskazini Magharibi kabisa na mwingine Kusini kabisa mwa nchi yetu. Mmoja anatokea karibu na Mto Ruvuma na mwingine akitokea Mto Kagera. Tuliunganishwa hasa na haiba zetu za kikazi, kimaisha na kisiasa.”

    Mwaka mmoja tu, baada ya kujuana naye, Balozi Ruhinda anasema aljiunga na Magazeti ya Chama cha TANU ya The Nationalist (Kiingereza) na Uhuru (Kiswahili), ambako Mkapa alikuwa Mhariri Mtendaji.

    “Nikafanya kazi chini yake, kwanza nikiwa Msanifu Habari (Sub-Editor), na baadaye Mhariri wa Habari (News Editor). Utaona kuwa urafiki wetu ulianzia kwenye shughuli za uandishi wa habari. Urafiki wetu pia ulikuwa wa kisiasa. Kama mnavyojua nyie, uandishi wa habari hauna tofauti kubwa na siasa. Baadaye, mwenzangu akaingia moja kwa moja kwenye siasa.

    Mimi nikabakia kwenye uandishi wa habari, lakini urafiki wetu ukabakia pale pale na kuzidi kukomaa.” Kuhusu tuhuma kuwa Mkapa amekuwa alikuwa zaidi mdhibiti na mzuia habari na siyo Mwandishi wa Habari aliyebobea baada ya kupikwa vizuri na kuiva na kuzuia mawazo huru, utoaji habari bila ya vikwazo na mijadala ya wazi, alisema hakubaliani hata kidogo na Mkapa kupachikwa tuhuma hizo.

    “Angalia, wakati najiunga na The Nationalist, na nyinyi wenyewe mmefanyakazi katika vyombo vya habari na mnajua utaratibu huu, tulikuwa tunafanya mkutano wa tathmini na kuchambua magazeti kila siku asubuhi na yeye ndiye aliyekuwa mwenyekiti.

    Tulijadiliana kwa uwazi, kwa urafiki na uhuru kamili kama wanataaluma. Tulikubaliana na tulihitilafiana. Lakini hatimaye, yeye kama Mhariri ndiye alitoa msimamo wa mwisho.

    Na kwa kweli hiyo ndiyo kazi ya Mhariri kutoa msimamo na mwelekeo wa gazeti. Kwa maana hiyo, Mhariri yeyote ni Mdhibiti wa gazeti lake,

    aliongeza Balozi Ruhinda na kwamba Mkapa aliwazuia waandishi kuandika walivyotaka kulingana na sera ya gazeti, ama alizima mawazo yao… hapana, siyo kweli alisema. “Nakumbuka wakati wetu kwenye The Nationalist tulikuwa na waandishi kutoka hadi Ghana na Biafra (Nigeria) na kila mtu alikuwa huru kutoa fikra na mawazo yake. Isipokuwa, ni dhahiri kuwa uamuzi wa mwisho ulikuwa wa kwake, akiwa Mhariri. Na hii ndiyo desturi ya utendaji kazi wa vyombo vya vya habari duniani kote na kutoa uamuzi ni wajibu muhimu na mahsusi wa Mhariri,” aliongeza

    Kuhusu Mkapa alikopata mafunzo ya taaluma ya Uandishi wa Habari Balozi Ruhinda alisema alipata

    mafunzo ya Uandishi wa Habari kabla ya kuteuliwa kuyaongoza Magazeti ya Chama. Alipelekwa kwenye Gazeti moja mashuhuri la Uingereza, (Daily) Mirror, na kupata stadi na uzoefu wa Uandishi wa Habari na Uhariri. Lakini hata kabla ya kupelekwa huko, Mkapa alikuwa na uwezo wa kuandika vizuri, akiwa hodari kwa lugha za kufanyia kazi hiyo za Kiingereza na Kiswahili.

    Alisema kwa maoni yake, Mkapa alikuwa Mwandishi wa Habari bora na Mhariri makini kuliko wengi wale wanaomlaumu.

    •Mwandishi anapatikana kwa Simu ya Mkononi/WhatsApp: 0754-388418 na Barua-pepe: [email protected]

    Mkapa kama mwandishi wa habari - RuhindaInatoka Ukurasa wa 12

    Benjamin Mkapa alipokuwa Mhariri Mtendaji wa magazeti ya Nationalist na Uhuru.

    Wasifu

  • Na Mwandishi wa Barazani

    Mkutano Mkuu wa Baraza la Habari Tanzania utafanyika Tanga Septemba 28, 2020.

    Zaidi ya wawakilishi 100 wa vyombo mbalimbali vya habari wanategemewa kuhudhuria mkutano huo.

    Agenda za kawaida za mkutano huo ni kwamba utapokea ripoti ya Katibu Mtendaji wa Baraza, Taarifa ya Fedha ya mwaka 2019 na uteuzi wa Mkaguzi wa Hesabu za Baraza kwa mwaka 2020.

    Mkutano huo pia utapitisha Kanuni za maadili ya habari zilizopitiwa upya.

    Kanuni hizo za maadili hupitiwa kila baada ya miaka mitatu kuhakikisha zitazingatia mabadiliko ya tasnia.

    Aidha mkutano huo utawachagua wajumbe wapya wa Bodi ya Baraza kwa kuwa muda wa iliyopo sasa.

    Rais mpya wa bodi atachaguliwa lakini kutokana na hitaji la katiba , theluthi mmoja

    ya wajumbe wa Bodi wa sasa lazima wabakie kwa lengo la kuweka muendelezo na theluthi moja ya wajumbe watakaochaguliwa lazima wawe wanawake.

    Rais wa Baraza ni Jaji mstaafu Thomas Mihayo, Makamu wa Rais

    ni Hassan Mitawi.Wajumbe wengine wa Bodi ni

    Jaji mstaafu,Juxon Mlay, Edda Sanga, Anna Henga, Dk. Edmund Mndolwa, Dinnah Chahali, Bakari Machumu na Wallace Mauggo.

    Bodi hiyo ilifanya mkutano wake wa mwisho Agosti 28, 2020.

    15

    Toleo la 156, Agosti, 2020

    Habari

    Mkutano Mkuu MCT kufanyika Tanga

    Rwehabura Rugamba, Mhariri wa EATV na EA Radio akipokea cheti kutoka kwa Makamu Rais wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Hassan Mitawi katika Mkutano Mkuu wa Baraza wa mwaka 2019. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania, Kajubi Mukajanga.

    Wajumbe kutoka taasisi mbalimbali za habari wanachama wa MCT wakiwa kwenye mkutano wa mwaka wa 2019.

  • Na Mwandishi wa Barazani

    Baada ya kufanyika kwa mafanikio Jijini Dar es Salaam tangu kuanzishwa kwake mwaka 2009, kilele cha Tuzo za Umahiri za Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) zitafanyika nje ya jiji hilo.

    Kajubi Mukajanga, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya EJAT amesema kuwa safari hii kilele cha tuzo hizo za kuwatambua wanahabari waliofanya vizuri kitafanyika Tanga.

    Septemba 28, 2020 ndiyo tarehe ya kilele cha tuzo hizo sherehe ambazo zitajumisha wanahabari kutoka sehemu mbalimabli nchini.

    Hii ni mara ya 11 kwa Tuzo hizo ambazo hushindaniwa kila mwaka na wanahabari 11 wameibuka kuwa washindi wa jumla.

    Katika miaka mitatu ya mwisho wanawake wameibuka washindi wa jumla.

    Mwanamke wa kwanza kufungua pazia kwa ushindi wa jumla kwa wanawake ni Florence Majani ambaye alikuwa akiandikia gazeti la Mwananchi 2016, akifuatiwa na Vivian Pyuza wa CG FM mwaka 2017 na Salome Kitomari wa Nipashe mwaka 2018.

    EJAT imekuwa tukio la kujuimisha wanahabari wa nchi yote kwa kuwa washindi wanaibuka kutika sehemu mbalimbali kuanzia redio za jamii na hata vyombo vikuu vya habari.

    Jumla ya kazi 450 zimepokewa kwa tuzo za mwaka huu ambazo zilizinduliwa rasmi Oktoba 11, 2019.

    Mwaka huu kuna makundi 21 ambapo matatu ni mapya.

    Makundi mapya ni Ubunifu kwa maendeleo ya Binadamu, Hedhi salama na Athari za Afya na mazingira kutokana na matumizi ya kemikali.

    Makundi mengine ni Fedha na Biashara, Kilimo na Biashara ya Kilimo, Elimu, Utalii na Uhifadhi, Uandishi wa Data, Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mpiga picha bora, Mchora vibonzo bora, Mpiga picha bora wa video, uandishi wa jinsia, Mafuta, gesi na Usimamizi wa madini, Usalama wa Barabara, Kundi la wazi, Uandishiwa habari za watoto, jinsina afya ya uzazi, na habari za wazee.

    Tarehe ya mwisho ya kuwasilisha kazi za kushindanisha ilikuwa januari 31, 2020.

    Washirika wa EJAT ni Baraza la Habari Tanzania (MCT), Wakfu wa Habari Tanzania (TMF), Taasisi ya Habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA-Tan),Chama cha

    Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), HakiElimu, AMREF, SIKIKA, Agriculture Non-State Actors Forum (ANSAF), Chama cha Wamiliki wa vyombo vya Habari Tanzania (MOAT na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC).

    16

    Jarida la Baraza la Habari Tanzania

    Kilele EJAT kufanyika nje ya Dar Habari

    Salome Kitomari mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe akiibuka kwa furaha baada ya kutangazwa mshindi wa jumla wa Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) 2018.