machokodo atunza shamba la miti - forestry-trust.org

18
machokodo atunza shamba la miti

Upload: others

Post on 01-Jun-2022

6 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: machokodo atunza shamba la miti - forestry-trust.org

machokodo atunza

shamba la miti

Page 2: machokodo atunza shamba la miti - forestry-trust.org

MODULI NAMBA 4

Usimamizi washamba la miti

MKULIMA WA MITI

Page 3: machokodo atunza shamba la miti - forestry-trust.org

1

ShukuraniKIJITABU HIKI KIMEANDALIWA KWA AJILI YA KUFIKISHA MAUDHUI NA TAALUMA YA NAMNA YA KUSIMAMIA SHAMBA LA MITI KWA MKULIMA MDOGO NA MKUBWA PIA. KIMEANDALIWA KWA MICHORO ZAIDI ILI KUMRAHISISHIA MSOMAJI KUJARIBU KILA KITU KWA USAHIHI ZAIDI.

MARA BAADA YA KUKAMILIKA, KIMEPITISHWA KWA WADAU MBALIMBALI NA WATAALAMU WA MISITU ILI KUTOA UZOEFU NA UTAALAMU WAO ILI KUBORESHA UTOAJI WA MAFUNZO SAHIHI YA USIMAMIZI WA SHAMBA LA MITI HAPA TANZANIA.NAPENDA KUTOA SHUKURANI ZA PEKEE KWA TAASISI YA UENDELEZAJI WA MISITU TANZANIA HUSUSANI KITENGO CHA huduma kwa wakulima wa miti KWA KUWEZESHA KAZI HII KUKAMILIKA.

PIA NAPENDA KUTOA SHUKURANI ZA PEKEE KWA WAFADHILI WA TAASISI HII AMBAO NI GATSBY FOUNDATION NA DFID KWA KUWEZESHA KUFADHILI UANDAAJI WA KIJITABU HIKI.

MWISHO, NAPENDA KUTOA SHUKURANI ZA PEKEE KWA BWANA Joseph makanza kwa kuchora na kusanifu kitabu hiki pia bwana HAMISI MALINGA NA GEORG STRUNDEN KWA USHAURI WA KITAALAMU KUHUSIANA NA MICHORO NA MAUDHUI yA KITABU HIKI.

UtanguliziWatafiti na wataalam wa misitu wanaamini kuwa watanzania wengi wamehamasika na wanapenda kilimo cha miti ya mbao. Moduli hii inatoa maelekezo ya namna ya kusimamia na kulihudumia shamba la miti kutokana na miche bora itokanayo na kupanda mbegu bora.

Inatoa mafunzo ya namna ya Usimamizi wa shamba la miti. Moduli hii pia inatoa mwongozo kwa wawezeshaji vijijini ili nao watoe mafunzo ya namna ya kukitumia kijitabu hiki kufikisha mafunzo kwa wakulima.

Hatua zilizoelezewa humu zinahusisha namna ya usimamizi wa shamba la Milingoti na Paina pia.

Moduli hii itatueleza kisa cha MACHOKODO aliyenufaika kwa Kilimo cha Miti baada ya kujifunza na kutumia utaalam alioupata kutokana na mafunzo kujitengenezea faida na kubadili Maisha yake.

Page 4: machokodo atunza shamba la miti - forestry-trust.org

2

1. KUpalilia shamba la miti

Kupalilia ni kuondoa

magugu shambani ili kuuacha mti

kutumia mbolea kwa ajili ya mti

kukua vizuri

zipo Aina kadhaa za kupalilia...

unaweza Kupalilia kwa visahani vyenye Kipenyo

cha sentimeta 100...

au Kupalilia kwa msitari -

Upana sentimeta 100 mche katikati

Page 5: machokodo atunza shamba la miti - forestry-trust.org

2. KUfyekea na kuliweka katika hali ya usafi

4

...pia Kupalilia

shamba lote...kwa mwaka wa kwanza palilia

shamba la miti kama mazao mengine

ya kilimo

Miti ikiwa na umri

wa miaka mitatu, miti huwa mirefu

kidogo hivyo hutakiwa kufyekewa nyasi zote ili kuweka usafi wa

shamba

3. kupogolea shamba la miti

Kupogolea ni kuondoa

matawi hasa ya chini ili mkulima aweze

kupita vizuri shambani na mti uweze kutoa gogo lililonyoka

kwa ajili ya kupasua mbao zenye

ubora.

Page 6: machokodo atunza shamba la miti - forestry-trust.org

Vifaa vya kukatia ni Msumeno maalumu

wa kupogolea na panga ambalo lina makali sana ili kutosababisha kovu

kubwa

namna ya kujua urefu wa matawi ya kuondoa

1/3 ya urefu wa mti ukiwa

na miaka 3-4 ndio iondolewe matawi. Ikiwa na miaka 7-8 matawi tena

yaondolewe na pia miti ikiwa na miaka 12-13 matawi tena yaondolewe kwa urefu wa 1/3 iondolewe na kuacha

2/3 ya urefu wa mti ukiwa na matawi

miaka 3-4

miaka 7-8

5

Page 7: machokodo atunza shamba la miti - forestry-trust.org

6

unapo ondoa matawi, Anza kukata chini kisha

malizia juu ya tawi.

Sababu ya kuanzia

chini ili kutosababisha

tawi linapoanguka kuchuna gamba na kuweka kovu kubwa

ambao huathiri uzuri wa ubao

pia husababisha gogo/ mti kupata

ugonjwa wa ukungu

Page 8: machokodo atunza shamba la miti - forestry-trust.org

6

epuka makosa/zingatia

shamba la mipaina

iliyopogolewa huonekana hivi

unaweza kupogolea ni miti aina zote,

mipaina..

na milingoti

pia

usikate matawi mpaka juu kabisa

karibu na mwisho kanabaki kama mkia wa mbuzi

usipogolee mti kwa

kutumia panga butu,

Page 9: machokodo atunza shamba la miti - forestry-trust.org

8

4. kupunguzia miti shambani

Wakati wa kupandwa

miti huwa karibu karibu lakini ikikua

huwa matawi yanagusana na kusababisha

ukuaji kuwa hovyo.

Miti inayotakiwa kupunguzwa

huwekwa alama

Miti inayotakiwa

kuondolewa ni ile ambayo imepinda,

yenye matawi makubwa toka chini, iliyokatika

juu, iliyodumaa kukua

kwa mipaina Muda wa kupunguzia ni miaka 7-8 na miaka 12-13 ili kukusaidia

kupata magogo makubwa ambayo ni manyoofu yasiyo

na matawi ovyo ovyo.

Page 10: machokodo atunza shamba la miti - forestry-trust.org

...na kisha upande wa piliwa mti, malizia ili kule ulikoanzia kukata ndio uelekeo ambao mti utangukia

Ukisha angusha ondoa matawi na kisha pima kulingana na uhitaji wa soko wa hilo gogo au nguzo.

9

unapoangusha mti kata kipande

uelekeo wa kuangushia...

miti ambayo

huondolea shambani lazima iwe inauzika kwa ajili ya matumizi

mbalimbali

Page 11: machokodo atunza shamba la miti - forestry-trust.org

10

5. usimamizi wa machipukizi

Hutakiwa kupunguzwa mara tatu ndipo unafikia hatua ya kuvuna zao la mwisho.

Miti aina ya milingoti ndiyo

ambayo ina nguvu ya kutoa machipukizi.

Mipaina haina machipukizi.

Kwenye shina kwa

kawaida huwa kuna machipukizi

mengi sana lakini haya hutakiwa kupunguzwa

ili kupata tena mazao mengine

ya miti.

1 2 3

Page 12: machokodo atunza shamba la miti - forestry-trust.org

11

Mwaka wa 2-3 ondoa na kubakiza machipukizi 3

Mwaka wa 6-7 ondoa na kubakiza machipukizi 2

Mwaka wa 9-10 ondoa na kubakiza Chipukizi 1

Kutegemeana na mteja

inawezekana kabisa ukubwa wa nguzo za umri wa 9-10 zinafaa.

mkulima anaweza kuvuna zote na kumuuzia

mteja wake

Nguzo za miaka 6-7

pia kulingana na uhitaji wa mteja

zinaweza kuvunwa zote na kwenda

sokoni

Page 13: machokodo atunza shamba la miti - forestry-trust.org

Wadudu huleta magonjwa ambayo huathiri ukuaji wa mti na pia husababisha mbao au nguzo kuwa mbaya

12

6. kudhibiti wadudu wa magonjwa shambani

Mchwa husababisha kuua kabisa milingoti hasa maeneo ambayo ni makame.

Namna ya kudhibiti ni kuchimba vichuguu vyote karibu na shamba na kumuua malkia, pia fuatilia njia ambazo hupitia (Mashimo) na kumwagilia dawa ya Attacan au Dimipridi- hizi hupatikana kwenye maduka ya pembejeo

Magonjwa mengine ni ya ukungu kwa mipaina ambapo vidudu kama chawa vinaitwa Aphidi hufyonza majimaji kwenye mti na kuua. Ukiona mtu kama huo umeathirika ni kuukata na kuuchoma

Page 14: machokodo atunza shamba la miti - forestry-trust.org

13

zingatia

Viumbe waharibifu na magonjwa ni moja ya tishio kubwa kwa ukuaji na mafanikio ya kiuchumi ya shamba la miti.

Baadhi ya nchi zinazolima miti ya aina hii wameishakumbana/wameshakabiliana na mlipuko wa magonjwa na viumbe waharibifu na kusababisha hasara kubwa.

panda aina nyingine za miti inayostahimili hayo magonjwa na viumbe waharibifu. Unachotakiwa kujua ni kuwa hayo magonjwa na wadudu wanaweza kuingia na kuenea hapa nchini na kwenye shamba lako la miti.

Ni muhimu kukagua shamba lako la miti mara kwa mara ili kugundua na kutoa taarifa zake (kama zipo) kwa afisa Misitu kwenye eneo lako.

Page 15: machokodo atunza shamba la miti - forestry-trust.org

14

Uandaaji wa mashamba kwa kutumia moto kuwe na udhibiti

Wavuta sigara wahakikishe vichungi wanavizima kabisa kabla ya kutupa

7. udhibiti wa moto kichaa

Wawindaji wawe wanatembea na maji ili wakishachoma nyama porini wazime kabisa moto

Warina asali kwa kutumia moto...wabadilike na watumie uvunaji wa kisasa wa kutumia vifaa vya kurinia asali

Moto ni adui

mkubwa wa miti. Vyanzo vya moto ni warina asali, uandaaji

wa shamba, Wavuta sigara,

wachunga ng’ombe, radi,

wapiti njia, magari n.k

Page 16: machokodo atunza shamba la miti - forestry-trust.org

15

Moto ukitokea na ukiona piga yowe kuita watu waje kusaidia kuuzima

Vifaa vya kuzimia ni matawi, matairi ya magari yaliyochanwa na kuwekwa mipini, pia ni pampu za maji za kubeba mgongoni

Kwa makampuni makubwa pia hutumia helikopta na mashine za kuangusha miti kama moto ni wa angani

Tengeneza barabara za kuzuia moto

shambani

Mikakati mingine wananchi wajitungie sheria ndogo kupitia kwenye vikao vya viongozi wa kijiji na wananchi wote

Page 17: machokodo atunza shamba la miti - forestry-trust.org

zingatiaJitihada za makusudi zinatakiwa ili kuzuia moto na kutambua kwa wakati matukio ya moto ili kuandaa nguvukazi za kuukabili.

Ni lazima kwa kila shamba la miti lizungukwe na barabara ya kuzuia moto maarufu kama fire line. Fire line iwe angalau na upana wa mita 5 na isiwe na kitu chochote kinachoweza kuchochea moto kirahisi

Kinga ni bora kuliko tiba. Ili kupunguza matukio ya moto kwenye maeneo ya mashamba ya miti, jamii kupitia serikali za vijiji lazima zikubaliane kwenye hatua za namna ya kudhibiti moto wa msituni.

Iwapo moto utatokea umakini mkubwa unahitajika ili kupunguza uwezekano wa kutokea ajali wakati wa kuzima moto.

Taasisi mahususi kwa ajili ya kuzima moto ni muhimu kuwepo ili ielekeze matumizi sahihi ya mbinu za kupambana na moto na uwepo wa vifaa vya kuzimia moto.

pale ambapo wananchi wamekosa uwezo wa namna ya kupambana moto mkubwa uhitaji kupata msaada kutoka ofisi za serikali zilizopo jirani.

17

Page 18: machokodo atunza shamba la miti - forestry-trust.org

15

FORESTRY DEVELOPMENT TRUSTUENDELEZAJ I M IS ITU TANZANIA

2 0 B A L O Z I R O A D , G A N G I L O N G A , I R I N G A , P O B O X 2

t : + 2 5 5 2 6 2 7 0 0 5 5 0 | I N F O @ F O R E S T RY- T R U S T. O R G