mamlaka ya udhibiti usafiri...mamlaka ya udhibiti usafiri ardhini (tozo) 3 katika muundo wa jedwali...

14
MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI ARDHINI (TOZO) 1 MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI WA ARDHINI (Na 3 YA 2019) ________ KANUNI _______ MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI ARDHINI (KANUNI ZA TOZO), 2019 SEHEMU YA KWANZA VIFUNGU VYA AWALI 1. Jina. 2. Matumizi. 3. Tafsiri. SEHEMU YA PILI HUDUMA ZINAZODHIBITIWA 4. Huduma zilizo chini ya kanuni za tozo. SEHEMU YA TATU KIBALI CHA TOZO KWA NJIA YA USHINDANI 5. Tozo kwa njia y ushindani. 6. Kibali ha tozo kwa njia ya ushindani. 7. ukomo. SEHEMU YA NNE MAOMBI NA MAPITIO YA TOZO 8. Maombi ya tozo. 9. Maombi ya mapitio ya tozo. 10. Uwasilishaji wa mlaji. 11. Kutoa Maombi. 12. Uwajibikaji. 13. Mamlaka kuanzisha mapitio ya tozo. SEHEMU YA TANO MAAMUZI JUU YA TOZO 14. Muongozo wa maamuzi ya tozo. 15. Uamuzi wa tozo. SEHEMU YA SITA MAKOSA NA ADHABU 16. Makosa. 17. Vifungu vya ujumla. 18. Nguvu ya kufifisha adhabu. SEHEMU YA SABA VIFUNGU VYA UJUMLA 19. Taarifa juu ya tozo. 20. Chapisho la tozo zilizoidhinishwa. 21. Onyesho la tozo zilizoidhinishwa. 22. Kitabu cha tozo na majedwali ya viwango. 23. Utolewaji wa risiti kwa huduma iliyotolewa.

Upload: others

Post on 27-Oct-2020

10 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI...MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI ARDHINI (TOZO) 3 katika muundo wa jedwali “viwango vya marejesho” maana yake uwiano wa fedha iliyoingizwa au kupotea (iliyofikiwa

MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI ARDHINI (TOZO)

1

MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI WA ARDHINI

(Na 3 YA 2019)

________

KANUNI

_______

MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI ARDHINI (KANUNI ZA TOZO), 2019

SEHEMU YA KWANZA

VIFUNGU VYA AWALI 1. Jina.

2. Matumizi.

3. Tafsiri.

SEHEMU YA PILI

HUDUMA ZINAZODHIBITIWA 4. Huduma zilizo chini ya kanuni za tozo.

SEHEMU YA TATU

KIBALI CHA TOZO KWA NJIA YA USHINDANI

5. Tozo kwa njia y ushindani.

6. Kibali ha tozo kwa njia ya ushindani.

7. ukomo.

SEHEMU YA NNE

MAOMBI NA MAPITIO YA TOZO 8. Maombi ya tozo.

9. Maombi ya mapitio ya tozo.

10. Uwasilishaji wa mlaji.

11. Kutoa Maombi.

12. Uwajibikaji.

13. Mamlaka kuanzisha mapitio ya tozo.

SEHEMU YA TANO

MAAMUZI JUU YA TOZO 14. Muongozo wa maamuzi ya tozo.

15. Uamuzi wa tozo.

SEHEMU YA SITA

MAKOSA NA ADHABU 16. Makosa.

17. Vifungu vya ujumla.

18. Nguvu ya kufifisha adhabu.

SEHEMU YA SABA

VIFUNGU VYA UJUMLA

19. Taarifa juu ya tozo.

20. Chapisho la tozo zilizoidhinishwa.

21. Onyesho la tozo zilizoidhinishwa.

22. Kitabu cha tozo na majedwali ya viwango.

23. Utolewaji wa risiti kwa huduma iliyotolewa.

Page 2: MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI...MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI ARDHINI (TOZO) 3 katika muundo wa jedwali “viwango vya marejesho” maana yake uwiano wa fedha iliyoingizwa au kupotea (iliyofikiwa

MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI ARDHINI (TOZO)

2

24. Mpango wa punguzo la tozo.

25. Uzuizi wa tozo.

26. Mapitio ya maamuzi ya Mamlaka.

27. rufaa.

28. [imefutwa]

MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI ARDHINI

(Na. 3 YA MWAKA 2019)

________

KANUNI

_______

(Zimetengenezwa chini ya kifungu cha 45)

MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI ARDHINI (KANUNI ZA TOZO), 2019

PART I

PRELIMINARY PROVISIONS Jina 1. kanuni hii itaitwa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (kanuni

za Tozo) , 2019.

Matumizi 2. Kanuni hizi zitatumika kwa watoa huduma wa huduma

zinazodhibitiwa.

Tafsiri 3. katika kanuni hizi isipokuwa muktadha unapoonyesha

vinginevyo: Act No. 3 of 2019 “Sheria” maana yake “sheria ya udhibiti wa usafiri ardhini”; “Mamlaka” maana yake “ Mamlaka ya udhibiti usafiri wa Ardhini

iliyoanzishwa na Sheria ya udhibiti usafiri wa Ardhini; “Mlaji” maana yeke ni “mtu mtumiaji wa huduma za usafiria ardhini”; “Mpango wa punguzo” maana yake punguzo ya tozo kwa kufuata

mfumo; “mtoaji mkubwa wa huduma” maana yake ni mtoa huduma ambaye

anafanya peke yake mwenye kuweza kuleta faida au kupunguza

ushindani katika soko katika kipindi husika na mwenye umiliki wa hisa

zinazozidi asilimia 35 “watoa huduma watarajiwa” maana yake ni mtu au kampuni yenye nia ya

kutoa huduma zinazodhibitiwa “mwanafunzi” maana yake ni mwanafunzi wa shule ya Awali, msingi au

sekondari akiwa amevalia sare ya shule au kabeba kadi ya utambulisho

ya shule; “Mlaji aliesajiliwa” inajumuisha baraza la Ushauri la Mlaji la au Mlaji

aliesajiwa na baraza na walaji; “jedwali la viwango” maana yake ni ratiba ya tozo zilizoidhinishwa

Page 3: MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI...MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI ARDHINI (TOZO) 3 katika muundo wa jedwali “viwango vya marejesho” maana yake uwiano wa fedha iliyoingizwa au kupotea (iliyofikiwa

MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI ARDHINI (TOZO)

3

katika muundo wa jedwali “viwango vya marejesho” maana yake uwiano wa fedha iliyoingizwa au

kupotea (iliyofikiwa au isiyofikiwa) katika uwekezaji, dhidi ya kiasi cha

pesa kilichowekezwa katika muda; “huduma zinazodhibitiwa” maana yake huduma zozote zinazotolewa

ukijumuisha huduma zote ambazo Mamlaka imezidhihirisha kuwa ni

huduma chini ya Sheria hii; “sekta inayodhibitiwa” maana yake usafiri wa ardhi, usafiri reli, usafiri

wa umma kwa njia ya barabara, biashara chini ya ardhi and usafirishaji

wa njia ya kebo; “mtoa huduma” maana yake mtu au chombo kilichosajiliwa na kupewa

leseni ya kutoa au kujihusisha na huduma zinazodhibitiwa; “usafiri nchi kavu” unajumuisha usafiri wa reli, barabara na usafiri kwa

njia ya waya; “tozo” maana yake malipo yanayotozwa na mtoa huduma kwa hudum

anazozitoa “kitabu cha tozo” maana yake kitabu kilichoandaliwa na mtoaji wa

huduma akionyesha tozo zilizoidhinishwa; “Kitengo cha usafirishaji” maana yake ni behewa la abiria na gari, basi,

lori, pikipiki ya magurudumu mawili au matatu.

SEHEMU YA PILI

HUDUMA ZINAZODHIBITIWA Huduma zilizo

chini ya kanuni

hizi za tozo

4.-(1) mtoa huduma hatatakiwa kuweka au kudai tozo ambazo

hazikuidhinishwa na Mamlaka .

(2) Mamlaka itadhibiti tozo katika huduma zifuatazo: (a) Usafirishaji wa abiria kwa njia ya Reli;

(b) Usafirishajiwa mizigo kwa njia ya Reli;

(c) Usafirishaji wa abiria kwa njia ya barabara;

(d) Usafirishajiwa mizigo kwa njia ya Barabara na;

(e) Huduma yoyote itakayotangazwa na Mamlaka kuwa ni Huduma

inayodhibitiwa.

(3) Bila ya kuathiri vifungu (1) na (2) vya kanuni ya nne,

Mamlaka haitadhibiti tozo pale itakapodhihirika uwepo wa wa ushindani

katika huduma zinazodhibitiwa.

SEHEMU YA TATU

IDHINI YATOZO KUPITIA NJIA YA USHINDANI Tozo kupitia njia

ya ushindani 5.-(1) Tozo itakayopatikana kwa njia ya ushindani baina pande

nyingine tofauti na Mamlaka, katika huduma inayodhibitiwa, itahesabiwa

kama tozo iliyopitishwa na Mamlaka kwa ajili ya mkataba wa Huduma (2) Kwa kuzingatia kanuni ndogo (1), tozo itakubalika kuwa ni

tozo iliyopatikana kwa njia ya ushindani kama;-

Page 4: MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI...MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI ARDHINI (TOZO) 3 katika muundo wa jedwali “viwango vya marejesho” maana yake uwiano wa fedha iliyoingizwa au kupotea (iliyofikiwa

MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI ARDHINI (TOZO)

4

(a) Upande wenye nia ya kujihusisha na utoaji huduma, utatakiwa

kuwalisisha kwa Mamlaka nyaraka za zabuni kwa ajili ya kupata

idhini kabla ya kualika wazabuni;

(b) kabla ya kukabidhi zabuni iliyofanikiwa, chombo cha ununuzi

kinawasilisha mkataba uliopendekezwa kwa mtoaji wa huduma

anayetarajiwa kwa Mamlaka kwa lengo la kujiridhisha kama

muongozo wa Mamlaka ulifuatwa ipasavyo

(c) mkataba wa mtoa huduma mtarajiwa utatakiwa kuonyesha;-

(i) mchakato wa udhibiti wa mapitio ya tozo kama

ulivyoonyeshwa katika kanuni hizi itakapotokea

mabadiliko ya tozo katika kipindi cha mkataba wa

utoaji huduma;

(ii) vigezo vya utendaji ambavyo vinaendana na tozo

iliyopendekezwa; na

(iii)Haja ya mtoa huduma kufuata mahitaji mengine ya

kisheria.

Idhini ya tozo

iliyopatikana kwa

njia ya ushindani

6.-(1) Pale ambapo Mamlaka itaona njia ya ushindani ndio bora

zaidi katika kupata mtoa huduma wahuduma zinazodhibitiwa, Mamlaka

itamtaka Wakala kuanzisha hatua za zabuni na bei ya zabuni iliyoshinda

itahesabika kama tozo iliyoidhinishwa. (2) mtoa huduma mtarajiwa atatakiwa kufuata - (a) Mchakato wa udhibiti wa mapitio ya tozo inapotokea

mabadiliko katika kipindi cha mkataba wa huduma; (b) vigezo vya utendaji ambavyo vinaendana na tozo

iliyopendekezwa; na (c) Mahitaji mengine yoyote ya kisheria.

Limitations 7. Tozo iliyoidhinishwa chini ya kanuni ya 5 na 6 cha kanuni hizi,

itatumika kwa mkataba husika pekee.

SEHEMU YA NNE

MAOMBI NA MAPITIO YA TOZO Maombi ya

Tozo 8.-(1) Mtu yeyote mwenye nia ya kutoa huduma zinazodhibitiwa

atatakiwa kuwasilisha maombi kwa mamlaka kwa ajili ya kufanyiwa

Tathmini na kutolewa vibali. (2)Maombi y tozo yatafanyika kwa kujaza fomu kama

iliyoonyeshwa kwenye jedwali la kwanza la kanuni hizi na

itaambatishwa na nyaraka zifuzatazo- (a) Leseni halali ya mwendeshaji au udhibitisho wa

maombi ya; (b) Taarifa za karibuni za kibiashara za benki

Page 5: MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI...MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI ARDHINI (TOZO) 3 katika muundo wa jedwali “viwango vya marejesho” maana yake uwiano wa fedha iliyoingizwa au kupotea (iliyofikiwa

MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI ARDHINI (TOZO)

5

(c) Mpango wa biashara;

(d) Tozo inayopendekezwa; (e) Karatasi ya mahesabu yaliyotolewa kufikia tozo

iliyopendekezwa;

(f) Tozo maalum inayopendekezwa kwa wanafunzi; na (g) Nyaraka nyingine yoyote itayohitajika na Mamlaka

kuambatanishwa.

Maombi ya

mapitio ya Tozo 9.-(1) mtoa huduma anayeomba mapitio ya tozo, atawasilisha

maombi yake kwa Mamlaka na atajaza fomu inayopatikana katika

jedwali la pili katika kanuni hizi ikiambatanishwa na;- (a) Leseni halali ya mwendeshaji;

(b) Maendekezo ya tozo; (c) Sababu na haki ya kufanya mapitio ya tozo pamoja na

faida kwa mlaji baada ya mapitio hayo;

(d) Karatasi ya mahesabu yaliyotolewa kufikia tozo

iliyopendekezwa; (e) hesabu zilizokaguliwa kwa miaka tatu mfululizo au

pungufu kulingana na umri wa taasisi; (f) ripoti ya utendaji ikiwa ni pamoja na uchambuzi wa

kina wa kiufundi na uchambuzi wa kifedha kwa miaka

mitano iliyopita au pungufu kulingana na umri wa

taasisi hicho; na; (g) nyaraka nyingine yoyote itakayohitajika na Mamlaka. (2) Mtoa huduma atatakiwa kuwasilisha maombi ya marejeo ya

tozo si pungufu ya miaka mitatu tangu mapitio ya mwisho kufanyika. (3) Bila ya kuathiri kifungu kidogo cha pili, mapitio ya huduma

za usafirishaji wa abiria yatafanyika kila mwaka kwa kuzingatia mapato

ya uwekezaji yanaposhuka zaidi ya asilimia 10% au kuongezeka zaidi ya

asilimia 25%; (4) Bila kuathiri maombi vifungu 8 na 9 vya kanuni, mtoa

huduma ataweza kuwasilisha maombi ya tozo kwa niaba ya watoa

huduma wengine wanaofanana.

Wasilisho la

mlaji 10.-(1) mlaji aliesajiliwa ataweza kuwasilisha maombi ya mapitio

kwa Mamlaka. (2) bila ya kuathiri kifungu kidogo (1), mlaji wa huduma

zinazodhibitiwa ataweza kuanzisha mapitio ya tozo kwa kufanya

wasilisho kwa Mamlaka. (3) wasilisho lilitengenezwa kwa kufuata vifungu vidogo (1) na

(2) vya kanuni, vitatakiwa kuambatishwa na; (a) tozo inayopendekezwa;

Page 6: MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI...MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI ARDHINI (TOZO) 3 katika muundo wa jedwali “viwango vya marejesho” maana yake uwiano wa fedha iliyoingizwa au kupotea (iliyofikiwa

MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI ARDHINI (TOZO)

6

(b) sababu na haki za mapitio na namna mlaji atanufaika

na mapitio;

(c) (d) Karatasi ya mahesabu yaliyotolewa kufikia tozo

iliyopendekezwa; na (d) Nyaraka nyingine yoyote itakayohitajika na mamlaka.

(4)Mara baaada ya kupokea risiti ya wasilisho, Mamlaka itafanyia

uchunguzi wasilisho ili kutambua uhitaji wa kufanya mapitio ya tozo.. (5) pale ambapo wasilisho lililowasilishwa halionyeshi haki ya

mapitio ya tozo, Mamlaka itatakiwa ndani ya siku 14 tangu kupokea kwa

wasilisho, kumtaarifu mlaji ipasavyo huku ikionyesha sababu za kwanini

mchakato wa mapitio ya tozo haujaendelea. Kuondoa

Maombi 11. Muombaji wa tozo au mapitio ya tozo ataweza kuondoa

Maombi yake wakati wowowte kabla ya Maamuzi ya tozo hayajafanyika. Uwajibikaji 12. Mtoa huduma atatakiwa kuheshimu maamuzi yaliyotolewa na

Mamlaka juu ya pendekezo la tozo. Uanzilishi wa

Mamlaka kwenye

mapitio ya tozo

13.- (1) Mamlaka itaweza kwa kuamua yenyewe, kufanya

uchunguzi wa mapitio ya tozo kwa mtoa huduma yoyote itakapotokea -

(a) Kuna mabadiliko katika mazingira yanayohitaji marekebisho

ya tozo; (b) Tozo inayodaiwa na mtoa huduma haikuidhinishwa na

Mamlaka; (c) Makadirio yaliyotumika kufanya mahesabu ya tozo

yamebadilika kwa kiasi kikubwa; (d) Mtoa huduma kashindwa kuwasilisha maombi ya maitio ya

tozo ndani ya muda ulioelekezwa. (2) Mamlaka katika kutumia nguvu yake ya kufanya mapitio,

itaweza kumtaka mtoa huduma kuwasilisha taarifa fulani na kwa muda

elekezi. (4) ikiwa mtoa huduma ameshindwa, bila sababu za msingi,

kuwasilisha taarifa zilizohitajika ndani ya muda ulioainishwa, Mamlaka

itasitisha mchakato wa mapitio ya tozo.

SEHEMU YA TANO

MAAMUZI YA TOZO Mchakato wa

maamuzi juu ya

tozo

14. Chini ya kifungu cha 19 cha Sheria, pamoja na mambo

mengine yoyote ambayo Mamlaka itaona yanafaa, mamlaka itatakiwa

ndani ya siku 90 tangu kupokelewa kwa maombi ya tozo, kupitia au

kuwasilisha, kufanya mapitio na kutoa Uamuzi juu ya tozo. (1) Mamlaka itatakiwa kutoa taarifa kwa umma juu ya maombi ya

tozo kupitia kwenye gazeti linalosomwa sana kuita uwasilisho wa wadau

kwa njia ya maandishi, ndani ya siku 14 tangu kutolewa kwa taarifa. (2) Mamlaka itakapojiridhisha kwamba taarifa husika

Page 7: MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI...MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI ARDHINI (TOZO) 3 katika muundo wa jedwali “viwango vya marejesho” maana yake uwiano wa fedha iliyoingizwa au kupotea (iliyofikiwa

MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI ARDHINI (TOZO)

7

zimetolewa, itatakiwa- (a) Kuidhinisha au kutofautiana maombi ya tozo na

kuambatishwa masharti ndani yake; au (b) Kukataa maombi ya tozo na kutoa Sababu ya kukataa maombi

hayo. Uamuzi wa tozo 15. Mamlaka itatakiwa kufanya maamuzi ya tozo kwa kuzingatia

yafuatayo; (a) Gharama za ufanisi katika utengenezaji, uzalishaji na utoaji

huduma,; (b) Matamanio ya kuchochea viwango vya ushindani na kuvutia

soko; (c) Viwango vyovyote husika, pamoja na vile vya kimataifa vya

bei,gharama, na faida kwenye mali katika sekta

zinazolinganishwa, (d) Athari za kiuchumi za maamuzi; (e) Maslahi ya walaji na wawekezaji; (f) Marejesho ya mali katika sekta zinazodhibitiwa; (g) Uhitaji wa kuongeza ufanisi katika matumizi ya sekta

zinazodhibitiwa; (h) Uhitaji wa kua na bei isiyobadilika badilika; (i) Sababu nyingine yoyote Mamlaka itaona inafaa.

SEHEMU YA SITA

MAKOSA NA ADHABU Makosa 16.-(1) Mtu yeyote ambaye - (a) Atashindwa kutoa tiketi au risiti kwa huduma husika; (b) Atatumia tozo ambazo hazikupitishwa na Mamlaka; (c) Atashindwa kuonyesha tozo kwa namna ambavyo Mamlaka

imeelekeza; (d) Atashindwa kuwasilisha kitabu cha tozo, jedwali la viwango

kwa Mamlaka; (e) Atawasilisha kwa Mamlaka nyaraka, taarifa, maelezo ambayo

ni ya uongo au si sahihi; au; (f) Atamzuia au weka vizuizi kwa afisa wa Mamlaka au Inspekta

katika kufanya majukumu yaliyo chini ya kanuni hizi; Atakua ametenda kosa na atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi za

kitanzania Milioni moja na isiyozidi shilingi milioni tatu, au kifungo

kisichozidi miaka miwili au vyote kwa pamoja.,

Isipokuwa,kosa litakalofanywa na kampuni, litawajibika kulipa

faini isiyozidi shilingi Milioni Tano. (2) mtu yeyote atakayeshindwa kutoa taarifa pale atakapohitajika na

Mamlaka kutoa taarifa, atakua ametenda kosa na mara baada ya kukutwa

na hatia, atawajibika kulipa faini isiyozidi shilingi za kitanzania Laki tatu

au kifungo kisichozidi kipindi cha miezi kumi na tano au vyote viwili

kwa pamoja,

Page 8: MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI...MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI ARDHINI (TOZO) 3 katika muundo wa jedwali “viwango vya marejesho” maana yake uwiano wa fedha iliyoingizwa au kupotea (iliyofikiwa

MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI ARDHINI (TOZO)

8

isipokuwa, kosa litakapofanywa na kampuni, adhabu yake ni faini

isiyozidi kiasi cha shilingi laki tano Adhabu z

ujumla 17. Mtu yeyote atakayekiuka vifungu vya kanuni hizi kwa

makosa ambayo adhabu zake hazijafafanuliwa, ataadhibiwa kwa kulipa

faini isiyozidi kiasi cha shilingi laki tano au faini kama zilivyoelekezwa

katika sheria za sekta husika au sheria nyingine, yenye adhabu kubwa

zaidi. Nguvu ya

kufifisha

Adhabu

18.-(1) bila ya kuathiri vifungu vya kanuni hii vinavyohusiana na

adhabu, pale mtu atakapotenda kosa chini ya kanuni hizi, Mamlaka

itakua na uwezo muda wowote kabla ya kuanza kusikilizwa kwa hili

shauri, wa kufifisha adhabu na kuagiza mtu huyo kulipa kiasi cha pesa si

pungufu ya nusu ya kiwango halisi cha faini ya kosa lenyewe ambacho

mtu huyu angetakiwa kulipa kama angekutwa na hatia ya kosa: Mamlaka itakua na nguvu ya kufifisha adhabu pale tu ambapo

mtu alietenda kosa, amekubali na kuomba kwa maandishi kosa lake

kufifishwa. (2) pale ambapo Mamlaka imefifisha adhabu katika kanuni hizi,

agizo lililotajwa katika kanuni (1): (a) Litatakiwa kuwekwa katika maandishi na litatakiwa

kuambatishwa na maandishi ya kukiri kwa kosa pamoja na

ombi kufifishiwa adhabu kulingana na kifungu cha kanuni

husika na, nakala ya amri hiyo atapatiwa mtenda kosa kama

akihitaji; (b) itabainisha kosa lililofanywa, jumla ya pesa iliyoamuru

kulipwa na tarehe ambayo malipo yatafanyika; na (c) Inaweza kutekelezwa kama amri ya Mahakama kwa malipo

ya kiasi kilichoainishwa katika agizo.

SEHEMU YA SABA

VIFUNGU VYA UJUMLA Taarifa kuhusu

Tozo 19. mtoa huduma atatakiwa kutoa taarifa sahihi na ya

kujitosheleza juu ya tozo zilizoidhinishwa kwa walaji. Uchapishaji wa

tozo

zilizoidhinishwa

20. mtoa huduma kabla ya kuanza kutumia tozo zilizopitishwa na

mamlaka atatakiwa, kutoa notisi ya siku 14 kwa umma juu ya tozo mpya

kupitia taarifa itakayotakiwa sambazwa kwa sehemu pana kupitia

magazeti, redio na televisheni. Onyesho la tozo

iliyoidhinishwa 21.(1) mtoa huduma atatakiwa kuweka tozo katika sehemu

zinazooneka kama ilivyo orodheshwa katika kanuni. - (a) Katika hatua ya mauzo; (b) Katika vituo vya huduma kwa walaji; (c) Vitengo husika vya usafirishaji; na (d) Kwenye bodi za matangazo za mtoa huduma au tovuti

Page 9: MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI...MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI ARDHINI (TOZO) 3 katika muundo wa jedwali “viwango vya marejesho” maana yake uwiano wa fedha iliyoingizwa au kupotea (iliyofikiwa

MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI ARDHINI (TOZO)

9

inayopatikana. Vitabu vya tozo

na jedwali la

viwango

22.-(1) mtoa huduma atatakiwa kuandaa kitabu cha mapitio ya

tozo au jedwali la viwango kutegemea na kesi iliyopo wakati huo,

kujumuisha tozo iliyoidhinishwa na kuwasilisha nakala kwa mamlaka. (2) mtoa huduma atatakiwa kuwasilisha andalio au mapitio ya

kitabu cha tozo au jedwali la viwango, kulingana na hali ya wakati

huo,kwa Mamlaka ndani ya mwezi mmoja tangu tarehe ya kutolewa kwa

idhini ya tozo ya Mamlaka. Utoaji wa tiketi

kwa huduma

iliyotolewa

23.-(1) mtoa huduma atatakiwa kutoa risiti kwa Mlaji kama

ushahidi wa malipo yaliyofanyika kwa huduma iliyotolewa.

(2) Mamlaka itaweza kukagua risiti iliyotolewa kuhakiki

utekelezaji wa tozo zilizoidhinishwa pamoja na masharti ya gari Mpango wa

punguzo la tozo 24.-(1) mtoa huduma anaweza kutoa mpango wa punguzo

kwenye tozo na atatakiwa kuitaarifu mamlaka juu ya mpango huo kabla

ya kuutumia.. (2) mtoa huduma atatakiwa kuhakikisha kuwa mpango wa

punguzo- (a) Unatoa vigezo na masharti na taarifa za mpango wa punguzo

husika; (b) Inatoa taarifa zinazoeleweka kwa walaji wake juu ya vigezo

na masharti ya mpango wa punguzo kupitia chapisho la

magazeti linalosomwa zaidi nchini, na inapowezekana, kupitia

media za kielektroniki zinazofikika, lugha ya alama au njia

nyingine yoyote inayokubalika na mamlaka. (c) Kuonyesha na kuchapisha mpango wa punguzo pale

utakapomtaka Mlaji kulipia viwango vinavyotumika; (d) Kupata vibali muhimu kutoka kwa Mamlaka husika pale

ambapo mpango wa punguzo unahusisha huduma zaidi ya zile

zinazodhibitiwa na Mamlaka; na (e) Hazizuii ushindani. (3) Mamlaka inaweza kukomesha mpango wa punguzo ambao

hauzingatii kanuni hizi na kuainisha sababu za kufanya hivyo. Tozo zuizi 25. Mtoa huduma mwenye kutawala soko, hatoruhusiwa kuzuia

kuingia kwa watoa huduma wengine katika soko kwa kuweka tozo lililo

chini ya gharama za utoaji huduma. Mapitio ya

Maamuzi ya

Mmalaka

26.- Mtu yeyote ambaye hataridhishwa na maamuzi ya Mamlaka

dhidi ya tozo zilizopitishwa na Mamlaka chini ya kanuni hizi, ataweza

kuwasilisha maombi ya mapitio ya tozo kwa Mamlaka ndani ya siku 14

tangu tarehe ya kutolewa kwa tozo hizo mpya kwa sababu za msingi

zifuatazo;-

Page 10: MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI...MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI ARDHINI (TOZO) 3 katika muundo wa jedwali “viwango vya marejesho” maana yake uwiano wa fedha iliyoingizwa au kupotea (iliyofikiwa

MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI ARDHINI (TOZO)

10

(a) kuna makosa au kosa linaonekana katika kumbukumbu; au (b) Kuna ugunduzi wa jambo jipya na muhimu, au ushahidi

ambao baada utafiti halikuwa ndani ya ufahamu wa

mwombaji au usingeweza kutolewa na yeye wakati amri

ikitengenezwa. Rufaa 27. mtu yeyote ambaye hakuridhishwa na maamuzi ya Mamlaka

juu ya tozo zilizotolewa chini ya kanuni hizi, anaweza kukata rufaa

kwenye Baraza la Ushindani. Kufutwa

G.N. No. 92 of

2010

28. Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Nchi Kavu na Majini (kanuni za

tozo) zimefutwa.

Page 11: MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI...MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI ARDHINI (TOZO) 3 katika muundo wa jedwali “viwango vya marejesho” maana yake uwiano wa fedha iliyoingizwa au kupotea (iliyofikiwa

MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI ARDHINI (TOZO)

11

JEDWALI LA KWANZA

________

(Limetengenezwa chini ya kanuni ya 8 )

MAOMBI YA TOZO MPYA

A. TAARIFA ZA MWOMBAJI

Jina kamili la Mwombaji

…………...………………………………...........................................

(Jina / Kampuni / Washirika – kwa HERUFI KUBWA)

Nambari ya Kuingiza Kampuni (ikiwa ni kampuni)………………………………...………

Anuani ya posta ……………………………………………………..………………………….

Simu ya rununu ya Ofisi:.

………...…………….........

Nambari ya Simu ya Mwombaji

……..…….

Barua pepe:

………………………………………………………………………………………

Anwani halisi

Mtaa: …………………………. Nambara ya Kiwanja:

………………..

Namba ya Ofisi:..........

Jina: …………………………….….......................................................................................

Wadhifa: …………….………............................................................................................

Namba ya simu ya mkononi:……………………

………………………………………………………….

Maelezo mafupi ya Maombi mpya:

…………………………………………………………………………………………………

…………………………………………………………………………………………………

…………………………………………………………………………………………………

…………………………………………………………………………………………………

B. NYARAKA ZA KUAMBATISHA PAMOJA NA MAOMBI

Mwombaji atatakiwa kuwasilisha nyaraka zifuatazo:

(a) leseni halali ya mwendeshaji au udhibitisho wa maombi ya leseni;

(b) taarifa za karibuni za kibiashara za benki;

(c) mpango wa biashara;

(d) tozo inayopendekezwa;

(e) Karatasi ya mahesabu yaliyotolewa kufikia tozo iliyopendekezwa;

(f) Mapendekezo ya tozo maalum kwa wanafunzi;

(g) Nyaraka nyingine yoyote itakayohitajika Mamlaka.

Mamlaka inaweza kuhitaji taarifa zaidi na nyaraka nyingine muda wowote.

Mimi, ninakiri kuwa taarifa zote zilitolewa katika fomu za maombi haya, kwa ufahamu na

kwa imani yangu kuwa ni za kweli.

Jina Kamili: Sahihi:……………………………

Page 12: MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI...MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI ARDHINI (TOZO) 3 katika muundo wa jedwali “viwango vya marejesho” maana yake uwiano wa fedha iliyoingizwa au kupotea (iliyofikiwa

MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI ARDHINI (TOZO)

12

……………………………….………...

Kazi: ………………………………………. Tarehe:.……………………………

KWA MATUMIZI YA OFISI TU

Kazi: ………………………………………..

Muhuli wa ofisi:

…………………………………….

Tarehe:

………………………………………………

TAHADHARI:

(a) Awali ya kila ukurasa.

(b) Kutoa maelezo ya uongo kwa kujua, kwa lengo la kujipatia tozo ni kosa kisheria na

adhabu yake ni faini au kifungu au vyote kwa pamoja.

(c) Mabadiliko yoyote yatakayofanyika katika fomu hii lazima kuwasiliana na LATRA

vinginevyo utakuwa unafanya kosa chini ya kanuni hizi.

Page 13: MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI...MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI ARDHINI (TOZO) 3 katika muundo wa jedwali “viwango vya marejesho” maana yake uwiano wa fedha iliyoingizwa au kupotea (iliyofikiwa

MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI ARDHINI (TOZO)

13

JEDWALI LA PILI

________

(Zimetengenezwa Chini ya Kanuni ya 9)

________

MAOMBI YA MAPITIO YA TOZO

A. TAARIFA ZA MWOMBAJI

Jina kamili la Mwombaji

…………...………………………………........................................................

(Jina / Kampuni / Washirika – kwa HERUFI KUBWA)

Nambari ya Kuingiza Kampuni (ikiwa ni kampuni)………………………………………….…....

Anuani ya posta ………………………………………………………………………………………..

Simu ya rununu ya Ofisi:.

…………………….................

Nambari ya Simu ya

Mwombaji:...…………….

Barua pepe:

…………………………………………………………………………………………………

Anwani Halisi:

Mtaa: …………………………. Nambari ya kiwanja:

……………………..

Namba ya ofisi:................

Jina: …………………………….…....................................................................................................

Wadhifa: ………………………………………………………………………………… ………

Namba ya

Simu:………………………………………………………………………………………….

Maelezo mafupi ya Mapitio:

…………………………………………………………………………………………………………

…………………………………………………………………………………………………………

…………………………………………………………………………………………………………

…………………………………………………………………………………………………………

B. NYARAKA ZA KUAMBATISHA PAMOJA NA MAOMBI

Mwombaji atatakiwa kuwasilisha nyaraka zifuatazo:

(a) Leseni halisi ya Mwendeshaji;

(b) Tozo inayopendekezwa;

(c) sababu na uhalali wa tozo ikiwa ni pamoja na jinsi watumiaji watakaofaidika na mapitio hayo;

(d) Karatasi ya mahesabu yaliyotolewa kufikia tozo iliyopendekezwa;

(e) hesabu zilizokaguliwa kwa miaka tatu mfululizo au pungufu kulingana na umri wa entity;

(f) ripoti ya utendaji ikiwa ni pamoja na uchambuzi wa kina wa kiufundi na uchambuzi wa

kifedha kwa miaka mitano iliyopita au pungufu kulingana na umri wa taasisi hicho; na

(g) Nyaraka nyingine yoyote itakayohitajika Mamlaka.

Mamlaka inaweza kuhitaji taarifa zaidi na nyaraka nyingine muda wowote.

Mimi, ninakiri kuwa taarifa zote zilitolewa katika fomu za maombi haya, kwa ufahamu na kwa

imani yangu kuwa ni za kweli.

Jina Kamili:

………………………….…………………...

Sahihi:……………………………........

Page 14: MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI...MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI ARDHINI (TOZO) 3 katika muundo wa jedwali “viwango vya marejesho” maana yake uwiano wa fedha iliyoingizwa au kupotea (iliyofikiwa

MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI ARDHINI (TOZO)

14

Kazi: ……………………………………………. Tarehe:.…………………………………

……..

KWA MATUMIZI YA OFISI TU

Tarehe ya kupokelewa:

…………………………………………

Mhuri wa ofisi

TAHADHARI:

(a) Awali ya kila ukurasa.

(b) Kutoa maelezo ya uongo kwa kujua, kwa lengo la kujipatia tozo ni kosa kisheria na adhabu yake

ni faini au kifungu au vyote kwa pamoja.

(c) Mabadiliko yoyote yatakayofanyika katika fomu hii lazima kuwasiliana na LATRA vinginevyo

utakuwa unafanya kosa chini ya kanuni hizi.

Dodoma, Isaack Aloyce Kamwelwe

……………………2019 Wizara ya Kazi, Usafiri na Uchukuzi