mbegu ndogo: hadithi ya wangari maathai...wanawake jinsi ya kupanda miti kutokana na miche. wanawake...

14
Mbegu Ndogo: Hadithi ya Mbegu Ndogo: Hadithi ya Wangari Maathai Wangari Maathai Une petite graine : l’histoire de Une petite graine : l’histoire de Wangari Maathai Wangari Maathai Nicola Rijsdijk Maya Marshak Ursula Nafula Kiswahili / French Level 3

Upload: others

Post on 13-Feb-2020

40 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Mbegu Ndogo: Hadithi yaMbegu Ndogo: Hadithi yaWangari MaathaiWangari Maathai

Une petite graine : l’histoire deUne petite graine : l’histoire deWangari MaathaiWangari Maathai

Nicola Rijsdijk Maya Marshak Ursula Nafula Kiswahili / French Level 3

Katika kijiji kimoja kwenye mteremko waMlima wa Kenya, katika Afrika Mashariki,msichana mdogo alifanya kazi zashambani pamoja na mama yake.Msichana huyu aliitwa Wangari.

•••

Dans un village situé sur les flancs duMont Kenya en Afrique de l’Est, une petitefille travaillait dans les champs avec samère. Son nom était Wangari.

2

Wangari alipenda kufanya kazi za nje.Alitumia jembe kulima katika bustani yafamilia yake. Kisha alipanda mbegu ndogokatika ardhi yenye virutubisho.

•••

Wangari aimait beaucoup être dehors.Dans le potager de sa famille, elle faisaitdes trous dans le sol avec sa machette.Elle enfouissait des petites graines dans laterre chaude.

3

Alipenda majira ya jioni, wakati jualinapozama. Giza lilipozidi mpakaalishindwa kuona mimea tena, Wangarialifahamu wakati wa kwenda nyumbaniuliwadia. Angefuata kijia chembambakilichopita uwanjani huku akivuka mitoakielekea nyumbani.

•••

Son moment favori de la journée étaitjuste après le coucher du soleil. Quand ilfaisait trop nuit pour voir les plantes,Wangari savait qu’il était l’heure derentrer à la maison. Pour rentrer, elledevait suivre des sentiers étroits à traverschamps et traverser des rivières.

4

Wangari alikuwa mtoto mwerevu naalikuwa na hamu ya kwenda shule. Lakiniwazazi wake walitaka awasaidienyumbani. Alipofika umri wa miaka saba,kaka yake aliwashawishi wazazi wakekumwacha aende shule.

•••

Wangari était une enfant intelligente et nepouvait plus attendre pour aller à l’école.Mais sa mère et son père voulaient qu’ellereste à la maison pour les aider. Quandelle eut sept ans, son grand frèrepersuada ses parents de la laisser aller àl’école.

5

Alipenda kusoma! Wangari alijifunza zaidina zaidi na kila kitabu alichokisoma.Alifanya vyema sana shuleni hadiakaalikwa kwenda Marekani kuendelezamasomo yake huko. Wangari alitiwahamasa sana na nafasi hii! Alipenda kujuaulimwengu zaidi.

•••

Elle aimait apprendre ! Wangari apprenaitde plus en plus avec chaque livre qu’ellelisait. Elle travaillait si bien à l’école qu’ellefut invitée à étudier aux Etats Unisd’Amérique. Wangari était enthousiaste !Elle voulait en savoir plus sur le monde.

6

Alipokuwa chuoni huko Marekani,Wangari alijifunza mengi mapya. Alisomeamimea na jinsi inavyokua. Na alikumbukamaisha yake yalivyokuwa utotoni: kuchezamichezo na ndugu zake katika kivuli chamiti maridadi ya misitu wa Kenya.

•••

A l’université américaine, Wangari appritplein de nouvelles choses. Elle étudia lesplantes et la manière dont ellesgrandissent. Et elle se rappela commentelle avait grandi : en jouant avec ses frèresà l’ombre des arbres dans les magnifiquesforêts du Kenya.

7

Jinsi alivyojifunza ndivyo alivyofahamukuwa aliwapenda watu wa Kenya. Alitakawafurahi na wawe wenye uhuru. Jinsialivyojifunza ndivyo alikumbuka kwaonyumbani Afrika.

•••

Plus elle apprenait, plus elle réalisaitqu’elle aimait les habitants du Kenya. Ellevoulait qu’ils soient heureux et libres. Pluselle apprenait, plus elle se rappelait sonfoyer africain.

8

Alipokamilisha masomo yake, alirudiKenya. Lakini nchi yake ilikuwaimebadilika. Kulikuwa na mashambamakubwa kila upande. Wanawakehawakupata kuni za kuwasha moto wakupikia. Watu walikuwa maskini na watotowalikuwa na njaa.

•••

Quand elle eut terminé ses études, elleretourna au Kenya. Mais son pays avaitchangé. De larges fermes s’étendaient àtravers la campagne. Les femmesn’avaient plus de bois pour cuire lesaliments. Les gens étaient pauvres et lesenfants avaient toujours faim.

9

Wangari alijua la kufanya. Aliwafundishawanawake jinsi ya kupanda miti kutokanana miche. Wanawake waliuza ile miti napesa walizopata walizitumia kwa mahitajiya familia zao. Wanawake walifurahi.Wangari alikuwa amewasaidia kuwawenye nguvu na uwezo.

•••

Wangari savait ce qu’il fallait faire. Elleapprit aux femmes comment planter desarbres en utilisant des graines. Lesfemmes vendirent les arbres et utilisèrentl’argent pour faire vivre leurs familles. Lesfemmes étaient très heureuses. Wangariles avait aidées à se sentir puissantes etfortes.

10

Muda ulipopita, miti mipya ilikuwa misitu,na mito ilianza tena kupitisha maji.Ujumbe wa Wangari ulienea Afrika nzima.Leo, mamilioni ya miti imemea kutokanana mbegu za Wangari.

•••

Avec le temps, les nouveaux arbres setransformèrent en forêts, et les rivièresrecommencèrent à couler. Le message deWangari traversa toute l’Afrique.Aujourd’hui des millions d’arbres ontgrandi grâce aux graines de Wangari.

11

Wangari alikuwa amefanya bidii. Watuulimwengu mzima walifahamu hili nawakampa tuzo. Tuzo hili linaitwa, ‘Tuzo laAmani ya Nobel.’ Na alikuwa mwanamkewa Kiafrika wa kwanza kupokea tuzo hilo.

•••

Wangari avait travaillé dur. Partout dansle monde, les gens s’en aperçurent et luidonnèrent un prix renommé. Il s’appellele Prix Nobel de la Paix et elle fut lapremière femme africaine à le recevoir.

12

Wangari alifariki mwaka 2011, lakinitunaweza kumkumbuka kila tunapoonamti maridadi.

•••

Wangari mourut en 2011 mais nouspensons à elle chaque fois que nousvoyons un bel arbre.

13

Storybooks CanadaStorybooks Canadastorybookscanada.ca

Mbegu Ndogo: Hadithi ya Wangari MaathaiMbegu Ndogo: Hadithi ya Wangari Maathai

Une petite graine : l’histoire de Wangari MaathaiUne petite graine : l’histoire de Wangari MaathaiWritten by: Nicola Rijsdijk

Illustrated by: Maya MarshakTranslated by: (sw) Ursula Nafula, (fr) Boulanger Mirei, Translators without Borders

This story originates from the African Storybook (africanstorybook.org) andis brought to you by Storybooks Canada in an effort to provide children’sstories in Canada’s many languages.

This work is licensed under a Creative Commons Attribution 4.0 International License.