mkataba wa ajira

13
Dealing with:-Radio Broadcasting, P.A. system and General Entertainment P.O. Box 70270 DAR ES SALAAM TEL: +255 26 2701114 Fax +255 26 2701115, Mob: +255 784 877788, Email: [email protected] MKATABA WA AJIRA MKATABA HUU unafanyika leo tarehe ………… mwezi …………………., 2014. BAINA YA … … … … … … … … … … …, wa S.L.P ………………… (ambaye katika Mkataba huu atajulikana kama “Mwajiri”) wa upande mmoja wapo wa Mkataba NA … … … … … … … … … … … , wa S.L.P ………………….. (ambaye katika Mkataba huu atajulikana kama “Mwajiriwa”) Namba ya Ajira (I.D). Umri: Jinsia: NSSF Na: Dini: Tarehe ya kuzaliwa: Sehemu ulipozaliwa: Jina la Mke: Tarehe aliyozaliwa Mke: Jina la Mtoto/Watoto: Tarehe ya kuzaliwa Mtoto/Watoto: Mkataba, Radio Ebony FM, 2014 Page 1

Upload: luther-akyoo

Post on 23-Jan-2015

778 views

Category:

Leadership & Management


55 download

DESCRIPTION

 

TRANSCRIPT

Page 1: Mkataba wa ajira

Dealing with:-Radio Broadcasting, P.A. system and General Entertainment

P.O. Box 70270 DAR ES SALAAM TEL: +255 26 2701114 Fax +255 26 2701115, Mob: +255 784 877788, Email:

[email protected]

MKATABA WA AJIRA

MKATABA HUU unafanyika leo tarehe ………… mwezi …………………., 2014.

BAINA YA

… … … … … … … … … … …, wa S.L.P ………………… (ambaye katika Mkataba huu

atajulikana kama “Mwajiri”) wa upande mmoja wapo wa Mkataba

NA

… … … … … … … … … … … , wa S.L.P ………………….. (ambaye katika Mkataba huu

atajulikana kama “Mwajiriwa”)

Namba ya Ajira (I.D).

Umri: Jinsia:

NSSF Na: Dini:

Tarehe ya kuzaliwa: Sehemu ulipozaliwa:

Jina la Mke: Tarehe aliyozaliwa Mke:

Jina la Mtoto/Watoto: Tarehe ya kuzaliwa Mtoto/Watoto:

1.

2.

3.

Mkataba, Radio Ebony FM, 2014 Page 1

Page 2: Mkataba wa ajira

MTU WA KARIBU; Jina kamili: … … … … … … … … … … … … … … Umri … … … …

Anuani/Mawasiliano: S.L.P … … … … … Simu … … … … … … … …

Anapoishi sasa: … … … … … … … Makazi ya kudumu … … … … … .

AMBAPO

1. Mwanzo

(a)             Mwajiri ni Kampuni iliyopo Iringa inayoshughulika na Matangazo ya Radio.

(b)             Mwajiriwa anafanya Shughuli Iringa na sehemu yeyote atakayopangiwa na mwajiri wake ndani

ya utaratibu wa kazi.

2. Wakati wa kuanza kazi

2.1 Mwajiri anakusudia kumwajiri kwa muda wa mwaka/miaka … … … … … mwajiriwa, endapo

mkataba huu utaisha utaongezwa/utaendelea kwa matakwa ya kampuni.

2.2 Mahali ulipoajiriwa … … … … … … … … … … …

2.3 Kituo cha kazi … … … … … … … … … … … … ..

2.4 Kazi zako

2.4.1 Nafasi kazini … … … … … … … … … … …

2.4.2 Ripoti kwa … … … … … … … … … … … …

2.4.3 Kazi utapangiwa na … … … … … … … … …

Mwajiriwa anakubali matakwa ya mwajiri na anakubali kwa hiari yake mwenyewe kuajiriwa kwa

muda wa mwaka/miaka … … … … … kama … … … … … … … … … …

3. Majaribio

3.1Mkataba huu wa ajira unatambua mda wa majaribio usiopungua miezi mitatu (3) toka siku

mwajiriwa alipopata ajira husika. Lengo la mda wa majaribio ni kumpima mwajiriwa kama

anakidhi vigezo na viwango vya nafasi/kazi husika. Kama mkataba huu utavunjwa ndani ya

mda wa majaribio mwajiriwa atapewa notisi ya maandishi ya siku saba ya kuvunjwa kwa

mkataba huu.

Mkataba, Radio Ebony FM, 2014 Page 2

Page 3: Mkataba wa ajira

3.2Mda wa majaribio unaweza kuongezwa au kupunguzwa na mwajiri pale atakapoona ni vyema

kufanya ivyo, Mwajiri anaweza kuongeza mda wa majaribio hadi miezi kumi na miwili (12).

3.3Kikomo cha mda wa majaribio, Mwajiri atatakiwa kumfahamisha mwajiriwa kwa maandishi

kuchaguliwa kwake katika ajira, kama tu akupata taarifa katika mkataba wake, mwezi mmoja

baada ya kuisha mda wa majaribio.

4. Ujira

4.1Kima cha malipo ya jumla kabla ya makato ya kisheria ni Tshs ….…………. kwa mwezi

kulingana na masaa 45 ya ufanyajikazi kwa wiki au kwa taswira ya kampuni husika.

4.2Mwajiriwa atakatwa makato yanayotambulika kisheria;

- Mifuko ya Jamii (NSSF) au Mfuko wa chaguo lako.

- Pay As Your Earn (P.A.Y.E).

- Sahihi ... ... ... ... ... ... ... ... ...

4.3Mwajiriwa atatakiwa kuwa na akaunti ya benki, kwajili ya malipo ya Ujira wake;

4.4Akaunti ya Benki … … … … … … … … … … … … … … … … … ...

5. Saa za kazi

5.1Mda wa kazi kwa ujumla ni masaa 45 kwa wiki, ila kutokana na taswira na muundo wa kampuni,

haswa kituo cha matangazo mwajiriwa atatakiwa kufata Taratibu na Kanuni zilizowekwa na

kampuni husika bila kudhuru kifungu chochote cha mkataba huu.

5.2Mwajiriwa atatakiwa kutambua kituo hichi cha Matangazo kinafanya kazi masaa ishirini na nne

(24) kwa siku saba(7) za wiki, ivyo sikukuu za umma zikiangukia katika siku za kazi

hakutokuwa na malipo ya ziada au mapumziko kwa watangazaji wa vipindi husika katika siku

hiyo.

5.3Kila mwajiriwa atapata siku moja (1) ya mapumziko ndani ya wiki (siku saba) kulingana na

atakavyopangiwa na mkuu wake wa Idara.

6. Likizo

6.1Mwajiriwa ana haki ya kupata likizo ya siku zisizopungua 28 katika mzunguko wa likizo ya kila

mwaka, siku hizo zitajumuisha sikukuu za umma zitakazoangukia ndani ya likizo husika. Likizo

itatolewa ndani ya miezi kumi na miwili (12) toka kuanza kwa ajira yako. Au baada ya kuisha

kwa mzunguko wa awali katika ajira.

Mkataba, Radio Ebony FM, 2014 Page 3

Page 4: Mkataba wa ajira

6.2Likizo itatolewa na mwajiri pale atakapoona ni wakati mwafaka kufanya ivyo, na kumjulisha

mwajiriwa.

6.3Idadi ya siku za likizo zinaweza kugawanywa na mwajiri katika mda tofauti ndani ya mzunguko

wa likizo bila kudhuru idadi ya siku za likizo za mfanyakazi.

6.4Mwajiri hatoomba au kuombwa na mwajiriwa kufanya kazi ndani ya mda wa likizo.

7. Likizo ya Ugonjwa

7.1Kulingana na kifungu cha 32 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini (Sheria kuu) Sura ya 366,

mwajiriwa atapata likizo ya Ugonjwa kwa siku 126 katika mzunguko wa likizo na malipo yake

halali, ikiwa tu, ugonjwa huo umethibitishwa na vyeti cha tatibu aliesajili au tabibu

anayekubalika na mwajiri.

7.2Likizo ya Ugonjwa iliyotajwa katika kifungu kidogo cha (1) italazimika kukokotolewa kama

ifuatavyo;

7.2.1 Siku 63 za kwanza zitatakiwa kulipwa mshahara mzima,

7.2.2 Siku 63 zinazofuata zitatakiwa kulipwa nusu mshahara

7.2.3 Mwajiri ana haki ya kuvunja mkataba wa ajira baada ya siku 126 za likizo ya Ugonjwa

kupita.

7.2.4 Mwajiriwa anatakiwa kutoa taarifa za ugonjwa haraka iwezekanavyo kwa mwajiri.

8. Likizo ya Uzazi

8.1Mfanyakazi atalazimika kutoa notisi kwa mwajiri kuhusiana na kusudio lake la kuchukua likizo

ya uzazi angalau miezi mitatu kabla ya tarehe tarajiwa ya kujifungua na notisi hiyo italazimika

kuambatana na cheti cha kitabibu.

8.2Vile vile Mwajiriwa atatakiwa kufata taratibu zote za Likizo ya Uzazi kama ilivyoanishwa katika

kifungu cha 33 – kifungu kidogo (2) hadi (11), Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini (Sheria

kuu) Sura ya 366.

9. Likizo ya uzazi ya baba na aina nyingine za likizo

9.1Wakati wa Mzunguko wa likizo, Mfanyakazi atakuwa na haki ya;

9.1.1 Angalau siku 3 za likizo ya uzazi ya baba kama-

(a) Likizo itachukuliwa ndani ya siku saba za kuzaliwa mtoto na;

(b) Mfanyakazi ni baba wa mtoto;

9.1.2 Angalau siku 4 za likizo kwa sababu zifuatazo;

(a) Ugonjwa au kifo cha mtoto wa mfanyakazi;

Mkataba, Radio Ebony FM, 2014 Page 4

Page 5: Mkataba wa ajira

(b) Kifo cha mke wa mfanyakazi, wazazi, bibi na babu, mjukuu au kitukuu.

Mwajiri anaweza kuhitaji uthibitisho wa kawaida wa tukio lolote lililotajwa hapo juu.

10. Kusitishwa kwa Ajira

10.1 Mkataba huu unaweza kusitishwa na pande zote mbili kwa notisi ya siku zisizopungua

28.

10.2 Notisi inatakiwa kutolewa kwa maandishi, ikieleza sababu na tarehe ya kusitishwa ajira

husika.

10.3 Endapo mwajiri atasitisha ajira, anatakiwa kumpa mfanyakazi Cheti.

10.4 Hata ivyo, Mwajiri ana haki ya kutotoa Cheti hadi pale Mfanyakazi atakaporudisha mali

au thamani yeyote ya kampuni.

10.5 Mwajiri atasitisha ajira husika endapo mfanyakazi atashindwa kufata matakwa ya

mkataba huu, taratibu, kanuni na miongozo ya kampuni.

11. Malipo ya Kiinua Mgongo

11.1 Mfanyakazi ana haki ya kupata kiinua mgongo cha mshahara angalau wa siku 7 kwa kila

mwaka ulioisha wa utumishi wa moja kwa moja na mwajiri mpaka kwa kiwango cha juu cha

miaka kumi (10),

11.2 Mwajiri atatakiwa kumlipa kiinua mgongo wakati wa kusitisha ajira ikiwa;

(i) Mfanyakazi amemaliza miezi 12 ya utumishi wa moja kwa moja na mwajiri

11.3 Mfanyakazi hatopata kiinua mgongo kama;

11.3.1 Kama ajira yake ilisitishwa kwa utovu wa nidhamu

11.3.2 Kama amegoma kufanya kazi alizopangiwa kwa taratibu za ofisi

12. Biashara Binafsi

12.1 Wafanyakazi wote ni waajiriwa wa kudumu, ivyo mfanyakazi yeyote hatoruhusiwa

kufanya biashara wakati wa kazi au mda wa kazi.

12.2 Kwenye jengo la kampuni;

12.3 Au kutumia mali, au chombo chochote cha kampuni kuwezesha biashara yake;

12.4 Au kuwatumia waajiriwa wengine wa kampuni hii kufanikisha biashara yake ndani ya

mda wa kazi. Hairuhusiwi.

13. Usiri

13.1 Uendeshaji wa biashara, utendaji na mipango ya kampuni ni vitu vinavyohitaji usiri wa

hali ya juu, ivyo nyaraka, taarifa, kumbukumbu za kimaandishi, muktasari wa vikao vya ndani,

Mkataba, Radio Ebony FM, 2014 Page 5

Page 6: Mkataba wa ajira

ulipaji wa mishahara, uendeshaji wa kampuni utalindwa kwa usiri mkubwa, na chochote

hakitakiwi kumhusisha mtu hasie wa kampuni bila idhini ya utawala. Ukibainika kuvunja usiri

huu unaweza kupoteza ajira yako.

14. Utoro

14.1 Mfanyakazi hatotakiwa kukosa kazini katika siku za kazi bila ruhusa ya mwajiri au

uongozi husika.

14.2 Mfanyakazi akitoweka/utoro kazini bila taarifa katika siku tano (5) za kazi, mwajiri

atahesabu upotevu/usitishwaji wa ajira ya mfanyakazi huyo toka siku ya kwanza ya utoro huo

14.3 Mimi, … … … … … … … … … … … … … … natambua utoro kazini utapelekea

kupoteza ajira yangu, natambua kutoonekana kazini kwa siku zisizopungua tano(5) ni uvunjifu

wa mkataba na taratibu za ofisi, ivyo kampuni ihesabu utoro wangu ni sehemu ya kujiuzulu.

14.4 Utoro wa vikao vya alhamisi mara tatu (3) ndani ya mwezi moja (1) vilivyowekwa kwa

utaratibu wa kampuni, unaweza kukufikisha katika kamati ya nidhamu au kukusabishia rekodi

hafifu ndani ya mwaka wa ajira, ivyo kuchangia kupoteza ajira yako.

15. Utovu wa Nidhamu

15.1 Wafanyakazi wote wanatakiwa kuheshimu na kufata sheria, taratibu na kanuni za

kampuni. Mwajiriwa yeyote atakae shindwa kuheshimu taratibu hizo atachukuliwa hatua kali za

inidhamu, au kupoteza ajira yake.

16. Masharti ya Ushindani

16.1 Kulingana na taratibu na kanuni na sheria ya Ajira na Mahusiano kazini, mfanyakazi

yeyote atapaswa kufata taratibu za kusitisha ajira, endapo mfanyakazi halali wa Redio Ebony

FM mwenye mkataba atatoroka na kwenda kufanya kazi sehemu nyingine bila kufata utaratibu

hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

16.2 Mfanyakazi yeyote hatoruhusiwa kufanya kazi yenye mfanano na kampuni hii akiwa

ndani ya ajira husika.

16.3 Ni kosa kwa mfanyakazi wa Ebony FM kufanyakazi na kituo kingine cha matangazo

akijua yeye ni mwajiriwa wa halali wa kampuni tajwa.

16.4 Kufanya au kuuza vipindi, vionjo au muundo wa vipindi vya kampuni ni kosa kisheria,

hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakaebainika.

Mkataba, Radio Ebony FM, 2014 Page 6

Page 7: Mkataba wa ajira

17. Makubaliano

17.1 Makubaliano haya ya mkataba, yameridhiwa na pande zote mbili na matakwa yake,

kifungu chochote katika mkataba huu kitabadilishwa kwa taarifa ya maandishi na hayatodhulu

vifungu vingine vya mkataba huu.

18. Kuzuia

18.1 Pande zote za mkataba huu zitambue kifungu chochote kilichokosewa au chenye

mkanganyiko hakiwezi kuufanya mkataba huu kuwa batili au kuzuia usifanye kazi, kitatolewa

au kufanyiwa mabadiliko, vifungu au ibara nyingine zitaendelea kufanyakazi bila kudhulu

taratibu zozote za ajira na mkataba husika.

19. Ufanyaji kazi wa Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini (sheria kuu) Sura ya 366, 2004

19.1 Makubaliano haya yatatafsiriwa na kufanyakazi kwa mujibu wa Sheria ya Ajira na

Mahusiano kazini Na. 6 ya 2004 na sheria nyingine zitakazoongezwa baadae.

20. Mkataba huu unashuhudia haya yafuatayo;

20.1 Mwajiriwa atatakiwa;

i.             Mwajiriwa atawajibika kufanya kila jambo ambalo ujumla wake atahakikisha mafanikio ya

kampuni.

ii.            Mwajiriwa atatakiwa kuonekana nadhifu mda wote awapo kazini.

iii.          Mwajiriwa atatakiwa kuripoti kazini masaa … … … … … … …kabla ya kipindi, tayari kwa

matayarisho ya shughuli zake za siku na ataingia studio dakika … … … … …kabla kuanza kwa

kipindi, (Muda wa kuanza na kumaliza kazi unaweza kubadilika kufuatia utaratibu wa mkuu wa

idara).

iv.           Mwajiriwa atatakiwa kuwajibika katika kuandaa vyema kipindi chake au vifaa muhimu (mgeni)

kwa unadhifu mkubwa.

v.            Mwajiriwa atahakikisha anao ufahamu wa kutosha wa kile anachotakiwa kuzungumza au

kupromoti.

vi.           Mwajiriwa atafanya matangazo kwa umakini na umahiri mkubwa ili kuhakikisha kuwa wateja

wetu wananufaika na juhudi zake.

vii.          Mwajiriwa atatawajibika kwa Mkuu wa kazi (Mkuu wa Idara/Mkuu wa kipindi) kwa utendaji

wake wa kila siku.

Mkataba, Radio Ebony FM, 2014 Page 7

Page 8: Mkataba wa ajira

viii.        Mwajiriwa atatakiwa kuhudhuria mikutano ya tathmini pamoja na Watendaji wengine wa timu

yake kila siku/wiki.

ix.           Ili kuhakikisha mafanikio Mwajiriwa atatakiwa kutekeleza maelekezo ya kiongozi wake wa Idara

au kipindi.

x.            Ambapo matangazo yanapaswa kuanza kwa muda uliopangwa na ucheleweshaji wa jambo lolote

linalohusiana na utangazaji hautavumiliwa au kukubaliwa.

xi.        Masharti ya nyongeza katika mkataba huu ni;

… … … … …. … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … …

… … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … …

… … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … .

Mkataba, Radio Ebony FM, 2014 Page 8

Page 9: Mkataba wa ajira

KWA USHUHUDA HUU, pande zote mbili zinaweka sahihi zao katika Mkataba huu siku na

tarehe kama ilivyo hapa chini.

Imesainiwa Iringa na;

… … … … … … … … … … … … … … … … …

Jina la Mwajiriwa

… … … … … … … … … … … … … … … … …

Tarehe

… … … … … … … … … … … … … … … … …

Sahihi ya Mwajiriwa

… … … … … … … … … … … … … … … … …

MATUMIZI YA KAMPUNI

Jina la Mwajiri/Mwakilishi

… … … … … … … … … … … … … … … … …

Tarehe

… … … … … … … … … … … … … … … … …

Sahihi ya Mwajiri/mwakilishi

… … … … … … … … … … … … … … … … …

WADHIFA

Mbele yangu;

JINA: ……………………………….

SAHIHI: ……………………………….

ANWANI: ……………………………….

WADHIFA: ……………………………….

Imeandaliwa na;

Luther Akyoo

Meneja Rasilimali Watu

Radio Ebony FM.

Mkataba, Radio Ebony FM, 2014 Page 9