mpango wa utayari wa kujiunga na elimu …...mpango wa utayari wa kujiunga na elimu ya sekondari...

120
MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU YA SEKONDARI (MUES) Kitabu cha Mwalimu Msichana Timiza Ndoto Yako!

Upload: others

Post on 29-Dec-2019

95 views

Category:

Documents


1 download

TRANSCRIPT

Page 1: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU YA SEKONDARI (MUES)

Kitabu cha MwalimuMsichana Timiza Ndoto Yako!

Page 2: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Page 3: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

O�si ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

(OR-TAMISEMI)

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Imefadhiliwa na Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza (DFID)

Agosti, 2017

MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU YA SEKONDARI (MUES)

EQUIP-Tanzania

Page 4: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Page 5: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

1Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

YALIYOMO

UTANGULIZI .........................................................................................................................................................................................2MAELEZO YA AWALI KWA MWEZESHAJI ..........................................................................................................................................3MADA YA KWANZA: JINSIA NA MAENDELEO YA KITAALUMA/ KAZI ...........................................................................................4Sehemu ya kwanza: Tafsiri ya dhana ..............................................................................................................................................................................................4MADA YA KWANZA: JINSIA NA MAENDELEO YA KITAALUMA/ KAZI ...........................................................................................5Sehemu ya kwanza: Tafsiri ya dhana ..............................................................................................................................................................................................5Sehemu ya Pili: Majukumu ya Kijinsi na Kijinsia ...................................................................................................................................................................... 10Sehemu ya Tatu: Maendeleo ya Kitaaluma na Jinsia............................................................................................................................................................. 12MADA YA PILI: MIMI NA MALENGO YANGU ................................................................................................................................. 18Sehemu ya Kwanza: Mimi ni nani? ............................................................................................................................................................................................... 18Sehemu ya Pili: Maana, Sababu na Hatua za kuweka malengo ....................................................................................................................................... 22Sehemu ya Tatu: Mikakati na mahitaji ili ku�kia lengo ........................................................................................................................................................ 26Sehemu ya Nne: Kupanga na ku�kia malengo ....................................................................................................................................................................... 26Sehemu ya Tatu: Mikakati na mahitaji ili ku�kia lengo ........................................................................................................................................................ 27UMAHIRI: WANAFUNZI WAWEZE KUFANYA MAAMUZI SAHIHI, KUTATUA MIGOGORO NA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO MBALIMBALI KATIKA MAISHA YAO. .................................................................................................................. 28Sehemu ya kwanza: Kufanya Maamuzi ...................................................................................................................................................................................... 28MADA YA TATU: KUFANYA MAAMUZI NA KUTATUA MIGOGORO NA CHANGAMOTO .......................................................... 28Sehemu ya Kwanza: Kufanya Maamuzi ...................................................................................................................................................................................... 29Sehemu ya Pili: Utatuzi wa Migogoro ......................................................................................................................................................................................... 33Sehemu ya Tatu: Mawasiliano ........................................................................................................................................................................................................ 36MADA YA NNE: MSUKUMO WA KUNDI RIKA ................................................................................................................................ 42Sehemu ya Kwanza: Tafsiri ya dhana ........................................................................................................................................................................................... 42Sehemu ya Pili: Athari za misukumo rika .................................................................................................................................................................................. 46Sehemu ya Tatu: Matamanio na Mahitaji ................................................................................................................................................................................. 46Sehemu ya Nne: Kukabiliana na Misukumo Rika Hasi na Kukuza Misukumo Rika Chanya .................................................................................. 49Sehemu ya Tano: Hitimisho la mada ........................................................................................................................................................................................... 54MADA YA TANO: UBUNIFU WA VYANZO VYA MAPATO ............................................................................................................... 56Sehemu ya Kwanza: Vyanzo sahihi vya ufadhili ...................................................................................................................................................................... 56FOMU YA UFADHILI KWA AJILI YA KUJIUNGA NA ELIMU YA SEKONDARI ............................................................................... 61Sehemu ya Pili: Njia za kufanya kazi za ubunifu kujipatia kipato .................................................................................................................................... 64Sehemu ya Tatu: Stadi sahihi za kutumia na kuweka akiba ............................................................................................................................................... 66MADA YA SITA: JINSI YA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA MWILI KWA WASICHANA........................................................ 70Sehemu ya Kwanza: Tafsiri ya dhana ......................................................................................................................................................................................... 70Sehemu ya Pili: Mzunguko wa hedhi .......................................................................................................................................................................................... 74Sehemu ya Tatu: Usa� wakati hedhi ........................................................................................................................................................................................... 78Sehemu ya Nne: Jinsi ya kutengeneza pedi zinazoweza kutumika tena ..................................................................................................................... 81MADA YA SABA: UKATILI WA KIJINSIA .......................................................................................................................................... 82Sehemu ya Kwanza: Maana ya ukatili wa kijinsia ................................................................................................................................................................... 82Sehemu ya Pili: Ukatili dhidi ya Wasichana/Wanawake ...................................................................................................................................................... 82Sehemu ya Tatu: Ubakaji na rushwa ya ngono ....................................................................................................................................................................... 84Sehemu ya Nne: Mazingira hatarishi yanayopelekea kufanyiwa vitendo vya ukatili .............................................................................................. 90Sehemu ya Tano: Ndoa na Mimba za UtotonI ......................................................................................................................................................................... 90Sehemu ya Sita: Mimba za Utotoni na Madhara ya Mimba za Utotoni ....................................................................................................................... 94MADA YA NANE: MAAMBUKIZI YA MAGONJWA YA NGONO NA KUACHA KUFANYA NGONO .............................................. 98Sehemu ya Kwanza: Magonjwa ya ngono ................................................................................................................................................................................ 98Sehemu ya Pili: Kudhibiti mihemko na kuepuka ngono ..................................................................................................................................................100Sehemu ya Tatu: Mbinu za Kuepuka Mihemko ya Kingono na Ngono .......................................................................................................................102Sehemu ya Nne: Tabia Hatarishi ..................................................................................................................................................................................................105KIAMBATISHO A ............................................................................................................................................................................. 107REFERENCES ................................................................................................................................................................................... 113

Page 6: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

2 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Kitabu hiki kimeandaliwa na Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania) kwa kushirikiana na O�si ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (WyEST), Taasisi ya Elimu Tanzania, CAMFED-Tanzania na TGNP Mtandao.

Kitabu hiki kinakusudia kutumiwa na Mwalimu Mshauri atakayeendesha mafunzo ya Mpango wa Utayari wa kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES). Kitabu hiki ni mwongozo ambao utatumika kama rejea muda wote wa utekelezaji wa MUES katika ngazi ya wilaya, kata na shule.

Mpango huu unalenga kuwajengea stadi na ujuzi wasichana waliomaliza elimu ya msingi ili kuwawez-esha kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowazuia kujiunga na elimu ya sekondari na hatimaye kushindwa kutimiza malengo yao maishani.

Hali ilivyo sasa, inaonesha watoto wengi wa kike wanapomaliza darasa la saba wanashindwa kujiunga na elimu ya sekondari kwa sababu mbalimbali ikiwemo kukosa stadi za msingi za maisha ambazo zingewa saidia kukabiliana changamoto za ujana ili kutimiza malengo yao. Kitabu hiki kimesheheni mada mbalimbali zitakazomsaidia kijana hasa wa kike: Kutambua thamani yake, maadili na utu wa mtoto wa kike na mchango wake muhimu kwenye maendeleo ya familia na taifa. Aidha, kitabu hiki kitamsaidia Mwalimu Mshauri kuchanganua mbinu za kuwasaidia watoto wa kike kutambua mabadiliko ya mwili, kukabiliana na mihemko, hisia na vishawishi vya makundi rika. Vilevile, kujua jinsi ya kupanga maisha yao ya baadaye ili waweze ku�kia ndoto zao za mafanikio.

Mwalimu Mshauri wa MUES anashauriwa kutumia mbinu shirikishi kufundisha mada hizi zitakozompa mwanafunzi fursa ya kujifunza kwa urahisi kwa kuhusisha mambo anayojifunza na maisha yake ya kila siku. Kitabu hiki kimeainisha mbinu mbalimbali zilizopendekezwa na watalamu wa elimu-rika kutumi-ka kuendesha mafunzo ya MUES. Baadhi ya mbinu hizo ni hadithi, igizo, nyimbo, picha majadiliano ya vikundi, �kiri-jozisha-shirikisha na maswali na majibu.

Hata hivyo, kitabu hiki kinatoa baadhi ya mbinu na namna mbalimbali za kufundisha mada husika lakini hakimzuii mwezeshaji kutumia ubunifu na kuibua njia nyingine zaidi ya zilizomo kwenye kitabu hiki. Pia mwalimu mshauri anashauriwa kutengeneza zana mbalimbali za kufundishia kwa kutumia rasilimali na vifaa vinavyopatikana kwenye mazingira yao.

Kitabu hiki kina jumla ya mada kuu nane. Mada hizi zitafundishwa kwa muda wa wiki nane (8) na kila wiki kutakuwa na mada moja. Mwalimu Mshauri anashauriwa kufanya tathmini ya maendeleo ya watoto mwanzoni kabla ya kuanza mafunzo na pia kufanya tathmini baada ya kufundisha mada hizi.

Tunawasihi Walimu Washauri kusoma kwa kina kitabu hiki na kukitumia kwa ufasaha mkubwa ili kuwasaida watoto wa kike ku�kia malengo yao. Sote tunawajibu wa kuijenga Tanzania.

UTANGULIZI

Page 7: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

3Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Mwongozo huu umeandaliwa kwa ajili ya Mpango wa Utayari wa kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES). Mpango huu umelenga kuwaandaa wanafunzi wa kike kujiunga na elimu ya sekondari kwa kuwapatia stadi za msingi za maisha. Stadi hizi zitawawezesha kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowa-zuia kujiunga na elimu ya sekondari hivyo kuwawezesha kutimiza ndoto zao. Mafunzo haya yatatolewa kwa kipindi cha wiki nane.

Ni muhimu Mwezeshaji akazingatia yafuatayo:

• Kila mada itafundishwa kwa siku tano ikiwemo siku moja ambapo watapewa mazoezi ya kufanya nyumbani.

• Anapaswa kuandaa zana za kufundishia kwa kutumia vifaa mbalimbali vilivyopo katika mazingira yake na ya watoto.

• Atumie mbinu shirikishi kwa kuzingatia maelekezo yaliyopo kwenye mwongozo huu. • Anaweza kutumia mbinu nyingine shirikishi za kufundishia ambazo hazijaainishwa kwenye

mwongozo huu. • Ni muhimu atunze kumbukumbu muhimu kama mahudhurio ya wanafunzi, matokeo ya

majaribio na mambo mengine muhimu atakayoyabaini ili kuweza kupima mafanikio ya mpango huu.

• Endapo mbinu ya igizo dhima itatumika, ahakikishe waigizaji wameuvua uhusika ili kuepuka utani au unyanyapaa baada ya somo.

Mbinu za kufundishia

Mwezeshaji anaweza kutumia mbinu za kufundishia zilizoorodheshwa hapo chini na pia anaweza kubuni mbinu nyingine za kufundishia ambazo ni shirikishi. Mbinu hizo ni:

• Bungua bongo • Kazi za vikundi • Maswali na majibu • Hadithi • Igizo dhima • Fikiri, jozisha, shirikisha • Kisa mafunzo • Nyimbo • Picha • Matembezi ya galari

MAELEZO YA AWALI KWA MWEZESHAJI

Page 8: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

4 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Umahiri: Wanafunzi waweze kutofautisha dhana ya jinsi na jinsia, watambue majukumu yao na waweze kuwa na chaguo sahihi la namna wanavyotaka kuwa katika maisha yao.

SIKU YA KWANZA

SEHEMU YA KWANZA: TAFSIRI YA DHANA

Lengo mahususiBaada ya kipindi kila mwanafunzi aweze kueleza maana ya jinsi, jinsia, mfumo dume na mawazo mgando.

MwezeshajiWaongoze wanafunzi kueleza maana ya jinsi na jinsia kwa njia ya maswali na majibu.

Wagawe wanafunzi katika makundi ya watano watano, kisha waongoze wanafunzi waweke tofauti kati ya mwanamke na mwanaume kwenye michoro miwili ya maumbo ya binadamu.

MADA YA KWANZA: JINSIA NA MAENDELEO YA KITAALUMA/ KAZI

Page 9: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

5Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

SEHEMU YA KWANZA: TAFSIRI YA DHANA

Jinsi Ni maumbile ya kibaiolojia yanayotofautisha viumbe kuwa mwanamke au mwanaume kutokana na tofauti iliyopo ya viungo vya uzazi.

Mfano: Binadamu: kati ya mwanamke na mwanaume.Wanyama: kati ya mbuzi jike na mbuzi dume.

Katika makundi ya watano watano kamilisheni kuchora maumbile ya binadamu yanayotofautisha jinsi mbili (mwanamke na mwanaume).

MADA YA KWANZA: JINSIA NA MAENDELEO YA KITAALUMA/ KAZI

Zoezi la Kwanza

Page 10: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

6 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Mwezeshaji

Wagawe wanafunzi katika vikundi vya watano watano, kisha waongoze wajibu maswali na kuwasilisha majibu kwa wenzao.

Fanya majumuisho kwa kusisitiza kuwa:

• Kazi zote zinaweza kufanywa na jinsi zote (Ke na Me). • Kuwepo kwa uwiano wa mgawanyo wa kazi za nyumbani ili kila mmoja aweze kupata

muda wa kupumzika.

SIKU YA PILI

Mwezeshaji Waongoze wanafunzi kupata maana ya mfumo dume kwa njia ya majadiliano.

Page 11: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

7Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Jinsia Mahusiano yaliyojengeka baina ya makundi mbalimbali katika jamii yanayohusisha wanawake na wanaume ambayo huweza kubadilika wakati wowote kulingana na nyakati, mazingira, hali ya uchumi, mila na desturi katika jamii husika. Mahusiano haya huweza kutofautiana baina ya jamii moja na nyingine.

Jinsia inachangia kuwepo kwa tofauti kati ya mwanamke na mwanaume katika mgawanyo wa majukumu, rasilimali, mamlaka na nafasi za maamuzi. Hali hii husababisha jamii kuwapa wanawake na wanaume hadhi, majukumu na kazi tofauti. Jinsia haitegemei maumbile ya kibaiolojia, bali imejengwa kutokana na mila na desturi za jamii husika na pia hutofautiana kutoka jamii moja hadi nyingine. Mfano, katika jamii nyingi ni jambo la kawaida kabisa kwa mwanamke kupika, kufua, kuosha vyombo na kazi nyingne za nyumbani. Endapo kazi hizo zitafanywa na mwanaume huonekana kuwa ni jambo geni.

Jadilianeni katika vikundi na kuwasilisha majibu.

1. Taja kazi zinazofanywa na wanawake tu katika jamii yako 2. Taja kazi zinazofanywa na wanaume tu katika jamii yako3. Nani aliefanya maamuzi ya mgawanyo wa kazi hizi4. Una maoni gani juu ya mgawanyo huu wa kazi na unakuathiri vipi?

Mfumo dume

Huu ni utaratibu uliojengeka katika maisha ya jamii unaowapa wanaume mamlaka ya umiliki wa rasilimali, kutoa maamuzi na kauli ya mwisho hivyo kumfanya mwanamke aonekane duni, dhaifu na hana thamani.

• Mfumo dume unachukulia kuwa mwanaume ni kipimo cha uwezo, mamlaka na umiliki• Umejengeka katika ngazi zote kuanzia kaya, jamii, kitaifa hadi kimataifa• Unaendelezwa na sera, sheria, michakato na mikakati ya maendeleo• Kwa kiasi kikubwa mfumo dume husimamiwa na wanaume

Mfano, katika familia nyingi wasichana hupangiwa kazi za nyumbani kama vile kupika, kulea, usa� na kazi nyingine wakati wavulana huhimizwa kujisomea na kusikiliza taarifa katika vyombo vya habari, kucheza na kufanya mazoezi na masomo ya shuleni.

Vyanzo vinavyokuza na kuendeleza mfumo dume ni pamoja na:

• malezi na makuzi• mifumo ya ukoloni• mila na desturi• utandawazi

Zoezi la Pili

Page 12: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

8 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Mwezeshaji

Kutokana na igizo dhima uliza maswali yafuatayo:

1. Je, igizo hili linaendana na hali halisi katika jamii yenu?2. Je, katika igizo hili ni mambo gani yanayoonesha mfumo dume?3. Je, ni mikakati gani inaweza kufanyika ili kuondokana na mfumo dume katika jamii zetu?

Onesha msisitizo kuwa katika baadhi ya maeneo na jamii mbalimbali mfumo dume bado upo na kuwa bado wasichana wengi wana mzigo mkubwa wa kazi za nyumbani kuliko wavulana. Pia atoe msisitizo kuwa jambo hili la mfumo dume sio zuri.

Katika mada hii unaweza kuwaalika wanafunzi wa kiume ili waweze kuchangia.

Waweke wanafunzi katika makundi wasichana na wavulana (kama wapo) kisha waoneshe mtiririko wa kazi wanazifanya toka wanapoamka mpaka wanapoenda kulala. Mwezeshaji na wanafunzi walinganishe kazi zinazofanywa na wasichana na zile zinazofanywa na wavulana ili kubainisha kundi gani linafanya kazi nyingi zaidi.

Page 13: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

9Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Fanyeni kazi ifuatayo katika makundi ya watano watano na kuwasilisha.

a. Wanafunzi kwa ubunifu wao wafanye igizo dhima linaloonesha dhana ya mfumo dume.b. Wanafunzi waainishe kazi tofauti zinazofanywa na wasichana na wavulana kuanzia asubuhi hadi usiku.c. Nini kifanyike kuleta usawa katika mgawanyo wa kazi.

Mawazo mgando ya kijinsia

Angalia mfano wa katuni hapo chini, �kiria kisha utaje dhana, �kra, mitazamo na tabia zilizopo juu ya wasichana na wavulana. Ziweke katika makundi ya Ke au Me katika jedwali linalofuata.

Kha! We kilaza kweli wa Hisabati

Kha! Nyie wasichana ni vilaza kweli wa

Hisabati

Zoezi la Tatu

Zoezi la Nne

Page 14: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

10 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

MwezeshajiWaongoze wanafunzi wakae katika vikundi.Ongoza mjadala kwa wanafunzi kwa kutumia maswali yaliyopo hapo chini.Eleza kwa wanafunzi kwa kujumuisha kama ifuatavyo:

• sio mitazamo au dhana zote zilizotajwa hapo chini ni sahihi kwa wanawake wote au wanaume wote.

• maana sahihi ya mawazo mgando ya kijinsia ni kujumuisha mitazamo au dhana fulani kuwa sawa kwa wanawake au wanaume wote katika jamii wakati sio sahihi.

SIKU YA TATU

Mwezeshaji Wape wanafunzi zoezi la kubainisha aina mbalimbali za kazi kwa alfabeti na zoezi la kuchora picha ya ndoto yake kama inavyo oneshwa katika siku ya tano ambayo itawasilishwa darasani.

SIKU YA NNE

SEHEMU YA PILI: MAJUKUMU YA KIJINSI NA KIJINSIA

Lengo Mahususi Baada ya kipindi kila mwanafunzi aweze kubainisha majukumu mbalimbali ya kijinsi na kijinsia.

Mwezeshaji Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la kuanisha kazi kutokana na majukumu ya jinsi na jinsia.

Waeleze wanafunzi kuwa majukumu ya kijinsi hayabadiliki wala hayaingiliani yanatokana na jinsi mtu alivyoumbwa, wakati majukumu ya kijinsia hutokana na taratibu zilizowekwa na jamii husika na huweza kubadilika.

Page 15: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

11Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Mitazamo au dhana juu ya Wanawake (Ke) Mitazamo au dhana juu ya Wanaume (Me)

a) Je, ni kweli mitazamo au dhana tajwa hapo juu zinawahusu wanawake au wanaume? Jadili.b) Je, kuna mitazamo au dhana ambazo umeorodhesha kwa wanawake ziko kwa wanaume na kwa wanaume ziko kwa wanawake?c) Chukua mfano wa mtazamo au dhana moja iliyotajwa hapo juu jadili. Je, ni wanawake wote au ni

wanaume wote wako hivyo?d) Kwa majibu uliyotoa hapo juu andika maana ya neno mawazo mgando ya kijinsia kwa maneno

yako.

SEHEMU YA PILI: MAJUKUMU YA KIJINSI NA KIJINSIA

Angalia kazi zilizoorodheshwa kwenye jedwali hapo chini kisha ainisha kazi zinazofanywa na wanaume au wanawake kwa sababu ya maumbile yao ya kibaiolojia (majukumu ya jinsi). Je ni kazi zipi zinafanywa na wanawake au wanaume kwa sababu ya mfumo na taratibu za kijamii (majukumu ya jinsia).

Ainisha kazi tajwa hapo juu katika jedwali lifuatalo:

Majukumu ya Jinsi Majukumu ya Jinsia

kubeba ujauzito; kutungisha mimba; kunyonyesha; kukata kuni; kupika; kupata hedhi; kupata ndoto nyevu; kuchota maji; kufanya kazi za matengenezo; kuhudumia watoto nyumbani.

Zoezi la Kwanza

Page 16: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

12 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

SEHEMU YA TATU: MAENDELEO YA KITAALUMA NA JINSIA

SIKU YA TANO

Malengo Mahususi:

Baada ya kipindi kila mwanafunzi aweze:

• kueleza aina mbalimbali za ujuzi na kazi. • kuhusianisha maendeleo ya kitaaluma na jinsia.

Mwezeshaji

Waongoze wanafunzi kusoma hadithi kisha kujibu maswali yaliyotolewa.

Page 17: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

13Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

SEHEMU YA TATU: MAENDELEO YA KITAALUMA NA JINSIA

Orodhesha aina mbalimbali za kazi au ujuzi kufuatana na mwanzo wa heru� katika alfabeti.

Chora picha ya ndoto yako kuonesha unavyotaka kuwa siku za usoni.

A: ________________ G: ________________ M: ________________ T:________________

B: ________________ H: ________________ N: ________________ U: ________________

C: ________________ I: ________________ O: ________________ V: ________________

D: ________________ J: ________________ P: ________________ W:________________

E: ________________ K: ________________ R: ________________ Y: ________________

F: ________________ L: ________________ S: ________________ Z: ________________

Zoezi la Pili

Mimi nataka kuwa nani?

Zoezi la Kwanza

Page 18: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

14 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Mwezeshaji

Tambua kuwa hadithi hapo juu ni fumbo. Wape wanafunzi fursa ya kutoa majibu tofauti tofauti. Usitoe jibu kwa haraka ili kuweza kupata dhana mbalimbali ya ujinsia na kazi. Kiuhalisia watu wengi wamejenga dhana kuwa daktari ni mwanaume hususani daktari bingwa wa upasuaji.

Jibu sahihi ni.

Daktari aliyekataa kumfanyia mtoto upasuaji ni mama mzazi wa mtoto huyo.

Page 19: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

15Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Soma hadithi zifuatazo kisha jibu maswali yanayofuata. Hadithi ya Kwanza

Palikuwa na baba mmoja alikuwa akisa�ri safari ya mbali. Kwenye safari hiyo alikuwa pamoja na mwanae wa kiume na pia walisa�ri kwa gari yao binafsi.

Njiani waliona vitu vizuri vinavyovutia sana vikiwemo wanyama, miti mbalimbali pamoja na maua mazuri. Wote walijawa na furaha katika safari yao na walikuwa na mategemeo kuwa wange�ka siku hiyo jioni sana. Baba huyu alimpenda sana mtoto wake na alitamani aje amuone akiwa ni mtoto mwenye mafanikio.

Baada ya muda mrefu kuwa barabarani ambapo baba ndio alikuwa akiendesha gari hilo, kwa bahati mbaya walipishana na lori kubwa sana lililokuwa likiendeshwa kwa kasi na wakapata ajali mbaya sana kwa kuwa gari lao liligongana uso kwa uso na lori lile.

Watu walikimbilia eneo la tukio kwenda kutoa msaada, kwa bahati mbaya Baba yule alikuwa amepoteza uhai wake palepale. Hali ya mtoto wake ilikuwa ni mbaya sana, kwa bahati nzuri alikimbizwa hospitali kwa ajili ya matibabu. Alipo�ka hospitali kijana huyo aliingizwa kwenye chumba cha wagonjwa mahu-tuti. Baada ya uchunguzi wa haraka ilionekana kuwa mtoto huyo anahitaji upasuaji wa haraka ili kuweza kuokoa maisha yake. Daktari aliyekuwa zamu alipewa taarifa kuwa anahitajika ili aweze kutoa huduma ya upasuaji kwa mtoto huyo aliyekuwa mahututi. Mara Daktari alipoingia kwenye chumba cha upasuaji, alifadhaika na kukosa furaha. Kisha alisema kwa uchungu sana “Huyu ni mwanangu, ni mtoto wangu sitaweza kumpatia huduma ya upasuaji”. Daktari yule alitoka kwenye chumba cha upasuaji akiwa analia. Ilibidi hospitali ifanye utaratibu wa kumpata daktari mwingine ili mtoto yule apatiwe matibabu.

Fikiri na jibu maswali yafuatayo:

1. Je, una�kiri daktari aliyeshindwa kutoa huduma ya upasuaji alikuwa ni mzazi wa mtoto huyo? Toa jibu lako na ueleze sababu.

2. Je, ni kazi au fani gani nyingine ambazo watu hu�kiri ni kwa ajili ya wanawake tu au wanaume tu? Je ni sawa? Kwanini?

Hadithi ya Pili

Amina na Maria ni wasichana wenye umri wa miaka ishirini. Wasichana hawa walikuwa ni mara�ki sana. Walipomaliza darasa la saba walifaulu vizuri sana masomo ya sayansi, baadaye walijiunga na elimu ya Sekondari na hatimaye Chuo Kikuu. Huko walisomea fani ya ufundi-magari. Baada ya kuhitimu chuo kikuu walipata kazi katika gereji nzuri na ya kisasa iliyomilikiwa na mjomba wake Maria. Walifanya kazi katika gereji hiyo kwa muda wa miaka mitano, wakati huo walipata ujuzi na uzoefu wa kutosha na hivyo iliwasababisha kuwa na ndoto ya kumiliki gereji ili waweze kujiajiri wenyewe na kuajiri wafanyakazi wengine. Pia walikuwa wamejizolea sifa za ufundi ulio mahiri. Mabinti hawa wawili walishakuwa wameweka akiba ya fedha za kutosha ambazo zingewawezesha kufungua gereji yao, ambayo wangependa iitwe “A&M” gereji.

Zoezi la Tatu

Page 20: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

16 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Mwezeshaji

Waongoze wanafunzi kuonesha igizo dogo la vikwazo walivyokutana navyo Amina na Maria mpaka kufanikiwa kufungua gereji yao. Kisha hitimisha somo kwa majadiliano kutokana na igizo.

Page 21: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

17Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Siku moja Amina aliona gereji ambayo ilikuwa haitumiki na alipata matamanio kuifanya sehemu hiyo kuanzisha biashara yao ya gereji. Mara moja alimpigia mmiliki wa gereji hiyo Ndugu Malingumu na kumuuliza kama wanaweza kukodi sehemu hiyo. Ndugu Malingumu alijibu kuwa hakuna tatizo na alimuagiza akamwambie mume wake ili aende kwa mazungumzo.

Baada ya siku mbili Amina na Maria walikwenda kumuona Ndugu Malingumu ili waweze kumlipa gharama zote za kukodi gereji ile. Ndugu Malingumu alimuuliza Amina “Mume wako yuko wapi?” na Amina alimjibu“ Sisi ndiyo tunaotaka kukodi gereji hii na fedha za malipo ya awali tayari tunazo” Ndugu Malingumu alicheka sana akasema “nini! Yaani nyie wasichana mnataka kukodi gereji hii? Msitake nicheke!” Amina na Maria wakamjibu “Bado hatujaolewa, sisi ni mafundi mahiri wa magari” Ndugu Malingumu akawajibu kwa kejeli “sikilizeni ninyi mabinti, siwezi kukukodisha gereji yangu, sitaki kupata hasara kwani hakuna atakae kuja kutengeneza gari yake kwenye gereji yenu, tena inayoendeshwa na wanawake! Hamtakuwa na uwezo wa kulipia kiwango cha pango kitakachobakia.”

Maswali

a. Una maoni gani kuhusu hadithi hiyo hapo juu?b. Ungekuwa wewe ni Amina au Maria ungejisikiaje? Kwanini?c. Je, kwa namna gani mmliki wa gereji ameonyesha ubaguzi wa kijinsia? d. Ni mawazo gani mgando ya kinjisia aliyonayo Ndugu Malingumu kuhusiana na wanawake?e. Je, ni namna gani mawazo haya mgando ya kinjisia ya Ndugu Malingumu yamewaathiri Amina naMaria? f. Je, una�kiri mawazo hayo mgando ya kinjisia yanaweza kuathiri wateja ambao wangehitaji kutengenezewa magari katika gereji hiyo? Kwanini?g. Je, ungewashauri nini Amina na Maria?h. Je, kuna mawazo gani mgando ya kinjisia yaliyopo kwenye jamii inayokuzunguka unayoyafahamu?i. Je, una�kiri nini kifanyike ili kusaidia kuondoa mawazo mgando ya kinjisia katika jamii yetu?

Hadithi inaendelea...

Baada ya miezi mitano Amina na Maria waliendelea kuishikilia ndoto yao. Pamoja na vikwazo vingi walivyopata kutoka kwa watu, hatimaye waliweza kumiliki gereji yao iliyojulikana kama “A&M” Gereji.

Page 22: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

18 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Umahiri: Wanafunzi waweze kujipangia malengo yao ya maisha na kuya�kia.

SEHEMU YA KWANZA: MIMI NI NANI?

SIKU YA KWANZA

Lengo mahususi

Kila mwanafunzi aweze kujitambua na kujieleza yeye ni nani na ana thamani gani.

Mwezeshaji

Waongoze wanafunzi kujibu maswali ya zoezi la kwanza na kuandika insha fupi.Waongoze wanafunzi waweze kujaza majibu kwenye maumbo ya zoezi la pili.

MADA YA PILI: MIMI NA MALENGO YANGU

Page 23: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

19Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

SEHEMU YA KWANZA: MIMI NI NANI?

Fikiria na kisha andika insha fupi kwa kufuata mwongozo wa maswali hapo chini.

Jaza majibu kwenye maumbo yafuatayo kulingana na maelekezo.

MADA YA PILI: MIMI NA MALENGO YANGU

Wewe ni nani? Una thamani gani? Unataka uwe nani hapo baadaye? Una nafasi gani katika familia, jamii na taifa? Umewahi kuwa kiongozi sehemu yoyote?

Unajisikiaje kuwa msichana?

Zoezi la Kwanza

Zoezi la Pili

Unataka kunifahamu?

Nachukizwa na

…………….. Vitu vinavyonio-

gopesha ni……………..

Vitu vinavyonifurahisha ni

………..

Nimebobea kwenye

……………..

sipendi kuwa karibu na

……………..

. . . . . ni mtu wangu wa karibu

Na haya yote

ndio MIMI!

Marafiki zangu ni

……………..

Ninaishi na……………..

Nina umri wa miaka

……………..

Page 24: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

20 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Mwezeshaji

Andaa kadi zenye maneno yanayolinganisha thamani ya vitu kama vilivyoorodheshwa na kuziweka kwenye kisanduku. Chagua wanafunzi watano waokote kadi kutoka katika kisanduku. Kisha waambie wajibu kati ya vitu walivyookota ni kipi kinathamani zaidi ya kingine?

Orodha ya vitu vya kulinganisha

{Chips kuku na lishe bora}

{Nyumba bora ya kuishi na lifti ya bodaboda}

{Elimu na kufanya kazi za ndani}

{Mavazi bora na kuweka nywele dawa}

{Afya bora na marashi au mafuta ya kujipaka}

Mwezeshaji

Waongoze wanafunzi kuimba wimbo ulioandaliwa. Baada ya wimbo waulize wanafunzi waeleze walichojifunza kutokana na wimbo. Aidha, waongoze kuongeza ubeti mwingine kwenye wimbo huo.

Waambie wabadilishane kazi yao na kupeana mrejesho kwa kuchora nyuso za tabasamu.

Mwisho hitimisha kwa kuwaeleza kuwa:

Wao ni wasichana wenye thamani kubwa kwani wanategemewa na wazazi, jamii na taifa kwa ujumla. Wanauwezo wa kufanya kazi yoyote hapo baadaye mfano udaktari, ualimu, uuguzi, uanasheria, uwakili, uhasibu, ubaharia, uhandisi, upambaji, uandishi wa habari, ukulima, ufugaji na nyingine nyingi.

Thamani yao ni kubwa sana kuliko vitu kama chips, marashi, simu, lifti ya bodaboda wala fedha. Waambie kuwa wao ni wa thamani sana na thamani yao haipimiki.

Page 25: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

21Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Okota kadi kutoka katika kisanduku, kisha linganisha thamani ya jozi za vitu vilivyoandikwa kwenye kadi na eleza kipi kina thamani zaidi.

Orodhesha vitu ulivyookota kwenye kisanduku vinavyoongeza thamani katika maisha.

Vitu vinavyoongeza thamani katika maisha

Imba wimbo ufuatao kisha eleza ulichojifunza kutokana na wimbo huo.

WIMBO

Je, unaweza kuongeza ubeti mwingine katika wimbo huu?

1. Sisi ni nani jama? Sisi ni wasichana,Sisi ni nani jama? Sisi ni wanafunzi,Wazazi wanatutegemea, Taifa linatutegemea,Sisi ni wa thamani!

2. Wewe unajikubali? Mimi najikubaliNani hajikubali? Sote twajikubalihata kama ni walemavu, Na hata vyovyote tulivyo,Sisi ni wa thamani!

3. Wewe utakuwa nani? Mimi ni daktari!Wewe utakuwa nani? Mimi ni muuguzi!Wagonjwa wananitegemea, Jamii inanitegemea,Taifa linanitegemea, Mimi ni wa thamani!

4. Wewe unalengo gani? Nataka kuwa mwalimu,Wewe unalengo gani? Nataka kuwa rubaniWanafunzi nitawafundisha, Bombadia nitairusha,Kioo cha jamii!

5. Wewe utakuwa nani? Mimi mwanasheria Wewe utakuwa nani? Mimi ni wakiliSheria nitazisimamia, Kwa haki nitazitekeleza,Na rushwa nitaipiga vita, Mimi ni wa thamani!

Zoezi la Tatu

Page 26: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

22 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

SEHEMU YA PILI: MAANA, SABABU NA HATUA ZA KUWEKA MALENGO

SIKU YA PILI

Malengo mahususi

Baada ya kipindi kila mwanafunzi aweze:

i. Kueleza maana ya malengo ii. Kutoa sababu za kuweka malengoiii. Kueleza hatua za kuweka malengoiv. Kujiwekea malengo binafsi

Mwezeshaji

Waongoze wanafunzi kubungua bongo kwa kujibu maswali yaliyo kwenye mabano {nini maana ya malengo? Je, umeshawahi kujiwekea malengo katika maisha yako? Yalikuwa ni malengo gani? Ulipitia hatua gani katika ku�kia malengo yako? Je, uliyatekeleza malengo yako?}. Kisha waongoze wa-nafunzi kubainisha maneno makuu kutoka kwenye tafsiri ya neno “malengo” na kujaza kwenye visanduku. Sisitiza umuhimu wa maneno hayo makuu {kusudi maalum, hatua fulani, muda fulani, sio ndoto, mambo halisi, yanayotekelezeka} na utoe majumuisho.

Waongoze wanafunzi kukaa katika makundi ya watano watano na kueleza umuhimu na hatua za kuweka malengo. Kisha wawasilishe kwa wenzao na ufanye majumuisho.

Sababu za kuweka malengo

• Malengo huongoza shughuli tulizojipangia kuzifanya ili ku�ka matokeo tuliyotarajia • Malengo hutupa dira na kutuelekeza tusiende mrama kwa kukosa mwelekeo • Huhamasisha uwajibikaji-husaidia kuthibitisha kama kweli tunatekeleza yale tuliyokusudia • Hutuwezesha kubainisha majukumu ya watu watakaotusaidia kutatua na kukabiliana na

changamoto tunazoweza kukumbana nazo katika ku�kia lengo au malengo yetu

Page 27: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

23Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

SEHEMU YA PILI: MAANA, SABABU NA HATUA ZA KUWEKA MALENGO

Maana ya Lengo

Soma maana ya neno lengo kwenye sanduku hapo chini na ujaze maneno makuu katika visanduku uliyojifunza kutoka kwenye maana hiyo.

Lengo ni kusudi maalumu linaloweza kumsaidia mtu ku�kia hatua fulani anayoitaka katika maisha ndani ya muda fulani. Malengo siyo ndoto, bali ni mambo halisi na yanayotekelezeka. Aidha, malengo yanaweza kuwa ni mambo madogo tunayotaka kubadili, ku�kia au kufanya. Pia yanaweza kuwa mambo makubwa tunayotaka kufanikisha leo, siku zijazo na hata miaka ijayo.

Zoezi la Kwanza

Page 28: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

24 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Hatua za kuweka malengo

1) Bainisha malengo kwa kuyaandika wazi na yawe halisi, mahususi yanayotekelezeka na yanayoweza kupimika baada ya muda. (Kwa Mfano, Zawadi ameandika lengo lake kuwa; anataka kuwa daktari wa binadamu).

2) Orodhesha manufaa ya lengo husika (Zawadi ameorodhesha faida za kuwa daktari ni kwamba: atasaidia kutibu watu; ataheshimika katika jamii; atajua vyanzo vya magonjwa mbalimbali na namna ya kuyaepuka; na kuisaidia familia yake) - Kama hunufaiki na hilo lengo hutakuwa na msukumo wa kuli�kia.

3) Orodhesha vikwazo unavyoweza kukutana navyo na jipange namna ya kukabiliana navyo (Zawa-di ameainisha vikwazo anavyoweza kukumbana navyo kuwa ni:- kukosa msaada wa kifedha, vishawishi vibaya kama kuolewa akiwa mdogo, msukumo rika, msingi mbovu wa masomo ya sayansi).

Angalizo: Uwepo wa vikwazo usikwamishe ku�kia malengo yako. Mpe ra�ki yako unayemwamini asome na aongezee vikwazo kwa jinsi anavyokufahamu na akupe

mbinu zaidi za kutatua na kukabiliana na vikwazo hivyo.

4) Orodhesha stadi na maarifa yanayohitajika ku�kia malengo yako. Kuna uhusiano mkubwa kati ya maarifa na stadi, na hivyo muunganiko wa haya mawili ni muhimu

ili ku�kia malengo. (Zawadi ameorodhesha stadi na maarifa atakayo hitaji kuwa ni; atayapenda masomo ya sayansi

na kuyasoma kwa bidii ili aweze kufaulu vizuri masomo hayo, ajiunge na chuo cha udaktari na kuzingatia masomo, kuwa na umakini katika kazi zake zote anazozifanya kuanzia kwenye majaribio anapokuwa shuleni, chuoni hadi atakapo ajiriwa).

5) Bainisha watu wa kukusaidia. Bainisha watu/makundi yatakayokusaidia ku�kia malengo yako. Zawadi amebainisha watu wanaoweza kumsaidia ku�kia lengo lake: (wazazi, walimu, jamii

inayomzunguka, mara�ki zake na madaktari).

6) Andaa mpango kazi. Eleza unataka kufanya nini, kwa muda gani, utatumia mbinu gani na rasilimali gani ku�kia

malengo hayo. Zawadi ametengeneza/ameandaa mpango kazi unaoonesha malengo yake, kwa muda gani, utatumia mbinu gani na rasilimali gani ku�kia malengo yake.

Mwezeshaji

Waelekeze wanafunzi kazi ya kufanya nyumbani kama inavyoonekana siku ya tatu na watafanya mrejesho siku ya nne.

Page 29: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

25Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Sababu na Hatua za kuweka malengo

A. Kaeni katika makundi ya watano watano na mjadili maswali yafuatayo:i. Je, kuna umuhimu gani wa kuweka malengo?ii. Eleza hatua za ku�kia malengo hayo.

B. Kaeni katika makundi ya watano watano na kujadili kwa kina hatua za ku�kia malengo yafuatayo:i. Mkulima mkubwa ii. Mfanya biashara mkubwaiii. Mwanasheriaiv. Mwanamuziki maarufuv. Kuwa mchezaji bingwavi. Kufahamu lugha ya Kiingereza

i. Fikiria na andika lengo unalotaka ku�kia mbeleni ii. Bainisha sababu za kuweka lengo hilo na hatua utakazo fuata ku�kia lengoiii. Kwa sentensi moja andika kaulimbiu (motto) yako

Zoezi la Pili

Zoezi la Nyumbani

Page 30: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

26 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

SEHEMU YA TATU: MIKAKATI NA MAHITAJI ILI KUFIKIA LENGO

SIKU YA NNE

Malengo mahususi

Mwisho wa kipindi kila mwanafunzi aweze:i. kupanga mikakati ya ku�kia malengoii. Kubainisha mahitaji muhimu ili ku�kia malengo

Mwezeshaji

Waelekeze wanafunzi wakae katika makundi ya watano watano. Kila kundi lichague lengo moja wanalotaka ku�kia, kisha wapange mikakati ya ku�kia lengo hilo. Kazi za kila kikundi zibandikwe ukutani, waongoze kutembelea kazi moja hadi nyingine huku wakisoma na kuongezea hoja walizonazo kama ikibidi.

Waelekeze wanafunzi wakae katika jozi. Kila mmoja a�kirie mahitaji muhimu ili ku�kia malengo yake na namna anavyoweza kupata mahitaji hayo. Baada ya hapo washirikishane mawazo yao katika jozi. Toa nafasi kwa kila jozi kuwasilisha kazi yao kwa darasa na ruhusu majadiliano.

Waeleze kuwa mikakati ya ku�kia malengo itatofautiana kutokana na lengo la kila mmoja. Ila baadhi ya mikakati inaweza kufanana. Kwa mfano mikakati ya kuwa mhasibu inaweza kuwa kusoma kwa bidii na kupenda masomo ya hesabu, kufanya majaribio mengi, kufaulu kwa kiwango cha juu masomo ya hesabu na biashara, kujiunga na chuo cha uhasibu na kufaulu vizuri.

Hitimisha kwa kuwasisitiza kuwa misaada sio lazima iwe pesa bali inaweza kuwa ushauri, kisheria, kisaikolojia au hata kimawazo.

SEHEMU YA NNE: KUPANGA NA KUFIKIA MALENGO

SIKU YA TANO

Malengo mahususi

Baada ya kipindi kila mwanafunzi aweze:

i. kupanga malengo yakeii. kueleza namna atakavyoya�kia

Mwezeshaji

Mwongoze kila mwanafunzi kupanga malengo ya muda mfupi na muda mrefu. Yapitie na kuyasahihisha mpaka kila mwanafunzi akamilishe zoezi kwa usahihi.

Page 31: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

27Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

SEHEMU YA TATU: MIKAKATI NA MAHITAJI ILI KUFIKIA LENGO

1. Kaeni katika makundi ya watano watano, kila kundi lichague na liandike lengo moja mnalotaka kuli�kia, kisha mpange mikakati ya ku�kia lengo hilo. Kila kundi libandike kazi yake ukutani.

2. Kaeni katika jozi, kila mmoja a�kirie mahitaji muhimu ili ku�kia malengo yake na namna anavyoweza kupata mahitaji hayo. Baada ya hapo shirikishaneni mawazo yenu katika jozi.

SEHEMU YA NNE: KUPANGA NA KUFIKIA MALENGO

Kwa kufuata sanduku lililopo hapo chini, jaza malengo yako ya muda mfupi na muda mrefu.

Wera werrrrrraaaaaa!!!! Nimefanikiwa kuya�kia malengo yangu!!!

Jumatatu Jumanne Jumatano Alhamisi Ijumaa

Lengo la muda mrefu

Lengo langu ni:

2020 2022 2024 2027 2030

Zoezi la Kwanza

Zoezi la Kwanza

Lengo la muda mfupi:

Lengo langu ni:

Page 32: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

28 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Umahiri: Wanafunzi waweze kufanya maamuzi sahihi, kutatua migogoro na kukabiliana na changamoto mbalimbali katika maisha yao.

SEHEMU YA KWANZA: KUFANYA MAAMUZI

SIKU YA KWANZA

Malengo Mahususi:

Baada ya kipindi kila mwanafunzi aweze:

i. kueleza maana ya kufanya maamuzi sahihiii. kueleza matokeo ya maamuzi

Mwezeshaji

Kwa njia ya maswali na majibu au bungua bongo waongoze wanafunzi kueleza maana ya kufanya maamuzi sahihi.

Waeleze kuwa kuchagua kwa makini njia sahihi na kuifanyia kazi kutawasaidia ku�kia malengo yao ya maisha.

Au maamuzi sahihi yanawasaidia kujiepusha na tabia hatarishi ili kuwapa uwezo wa kufanikiwa kupata wanachohitaji katika maisha.

Msichana anapofanya chaguo sahihi huwafanya watu wengine pamoja na yeye mwenyewe kuwa wenye furaha.

Waongoze wanafunzi kusoma maelekezo na kisha kujibu zoezi la kwanza katika vikundi vya watano watano.

MADA YA TATU: KUFANYA MAAMUZI NA KUTATUA MIGOGORO NA CHANGAMOTO

Page 33: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

29Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

SEHEMU YA KWANZA: KUFANYA MAAMUZI

Kufanya maamuzi ni:

Mhusika hutumia utaratibu wa chaguo ambalo huona ni sahihi au bora baada ya kutambua matokeo {chanya au hasi} yanayotokana na chaguo hilo. Mchakato wa kufanya maamuzi ni stadi muhimu ili kumuwezesha mhusika kubainisha na kupima matokeo kabla ya kuamua jambo fulani.

Katika makundi ya watano watano someni matukio hapo chini na mueleze mtachukua maamuzi gani.

MADA YA TATU: KUFANYA MAAMUZI NA KUTATUA MIGOGORO NA CHANGAMOTO

Mchakato unaohusisha kukata shauri katika kufanya jambo fulani.

Tukio # 1

Ndimenya ni binti mwenye umri wa miaka 16 ana mpenzi wake anaitwa Kamenya. Kamenya anampenda sana Ndimenya na huwa anamsaidia mambo madogo madogo. Kamenya anamuomba Ndimenya wafanye ngono. Ungekuwa wewe ndio Ndimenya ungefanyaje?

Tukio # 2

Binti wa miaka 13 amefaulu vizuri masomo yake. Baba yake anamlazimisha aolewe ili apokee mahari ambayo ingemsaidia kuweza kumaliza ujenzi wa nyumba yao kwa kuezeka bati kwa kuwa ilikuwa inavuja sana. Anasisitiza kama binti hataki kuolewa aondoke pale nyumbani.

Ungekuwa wewe ndio huyo Binti ungefanyaje?

Tukio # 3

John amekuwa akigombana mara kwa mara na mama yake wa kambo nyumbani walikokuwa wanaishi. Baba yake alikuwa akimpiga sana John kila mara mama wa kambo alipolalamika kuhusu John. John ame�kia uamuzi wa kutaka kujiua.

Je, ungekuwa wewe ndio John Ungefanyaje?

Zoezi la Kwanza

Page 34: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

30 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Mwezeshaji

Gawa wanafunzi katika makundi ya watano watano ili waweze kujadiliana na kupata matokeo ya maamuzi yao. Ongoza makundi kujaza jedwali na pia kuwasilisha kazi yao kwa wengine.

Sisitiza kuwa maamuzi yatakayofanywa yawe na matokeo mengi mazuri na kuwa ni muhimu mtoa maamuzi hayo ayasimamie.

Page 35: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

31Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Tukio # 4

Binti mmoja amekuwa anahisi ana ugonjwa wa zinaa ila hana uhakika.

Ungekuwa wewe ndio huyo Binti ungefanyaje?

Tukio # 5

Wewe ni Binti mwenye akili na umejiandaa vema kwa ajili ya kufanya mtihani wa darasa la saba. Una matarajio makubwa sana ya kufaulu. Wazazi wako wamekuita na kukuambia kuwa uandike vibaya majibu kwa makusudi ili usifaulu mtihani huo.

Je, wewe ungefanyaje?

Tukio # 6

Umemaliza darasa la saba ukaenda mjini kufanya kazi. Ta-jiri wako ni mtu mzuri sana na wewe umevutiwa na maisha ya mjini na ungependa uendelee kukaa pale. Majibu yametoka umefaulu na umechaguliwa kwenda shule ya sekondari.

Je, ungefanyaje?

Weka majadiliano yenu ya kikundi katika jedwali lifuatalo.

Kisa Maamuzi Matokeo Mazuri Matokeo Mabaya

Kila kikundi kiwasilishe kazi yao kwa wengine na kujadiliana kwa pamoja.

Page 36: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

32 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

HATUA ZA KUFANYA MAAMUZI

Lengo mahususiBaada ya kipindi kila mwanafunzi aweze kueleza hatua za kufanya maamuzi sahihi.

SIKU YA PILI

MwezeshajiWaongoze wanafunzi kupanga hatua zilizoorodheshwa hapo chini kwa mtiririko sahihi pia waeleze umuhimu wa kila hatua waliyoiorodhesha.

Sisitize hatua sahihi za kufuata wakati wa kufanya maamuzi kama ifuatavyo:a) Tambua maamuzi na sababu ya kufanya maamuzi hayob) Kusanya taarifa zitakazosaidia maamuzi yakoc) Bainisha na pima matokeo tarajiwa kwa kila uchaguzi d) Chagua wazo lililo bora na tekeleza

SEHEMU YA PILI: UTATUZI WA MIGOGORO

Lengo mahususi

Baada ya kipindi kila mwanafunzi aweze kueleza namna ya kutatua migogoro na kukabiliana na changamoto.

Mwezeshaji

Waongoze wanafunzi kueleza maana ya utatuzi wa migogoro kwa njia ya maswali na majibu.

SIKU YA TATU

Mwezeshaji

Bainisha kwa wanafunzi kuwa hatua za kutatua migogoro zinashabihiana na hatua za kufanya maamuzi. Waongoze wanafunzi katika kujaza jedwali na kuweza ku�kia aina ya tabia ya kutatua migogoro kama ilivyolinganishwa na tabia za wanyama tajwa.

Zoezi la Nyumbani

Page 37: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

33Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

HATUA ZA KUFANYA MAAMUZI

a. Panga hatua zilizoorodheshwa hapo chini kwa mtiririko ulio sahihi

a) Chagua wazo lililo bora na tekelezab) Tambua maamuzi na sababu ya kufanya maamuzi hayo c) Bainisha na pima matokeo tarajiwa kwa kila uchaguzi d) Kusanya taarifa zitakazosaidia maamuzi yako

1. ___________________________________________________________________________

2. ___________________________________________________________________________

3. ___________________________________________________________________________

4. ___________________________________________________________________________

b. Toa maelezo ya umuhimu wa kila hatua uliyoorodhesha hapo juu.

SEHEMU YA PILI: UTATUZI WA MIGOGORO

Ni njia ya ku�kiri na kutumia akili kutafuta ufumbuzi na majibu ya matatizo au changamoto. Njia mbalimbali za kutatua migogoro zinaeleza jinsi mtu alivyo na haiba yake katika maisha ya kila siku. Hakuna njia moja ambayo ni sahihi kwa kila tatizo au mgogoro. Njia hutofautiana kutokana na uzito au wepesi wa mgogoro uliopo. Ni vyema njia yeyote itakayotumika iwe na matokeo chanya kwako na ambayo hayataumiza watu wengine.

Jitambue upo katika kundi gani la utatuzi wa migogoro? Soma kwa makini sentensi hizi na uchague kumi zinazoelezea hisia zako wakati wa kutatua migogoro.

1. Kunapokuwa na mgogoro hutumia maneno mazuri ili kurudisha amani2. Ni muhimu kusikia maoni ya watu wengine na jinsi wanavyojisikia3. Ni muhimu sana wakati wa mgogoro wewe upate ushindi4. Unaweza ukajinasua nje ya mgogoro mara zote unapotokea5. Unaogopa migogoro6. Unachukia mtu anapokukasirikia7. Upo tayari kukubali makosa yako.8. Utafanya lolote liwalo ili ujue ukweli9. Unaamini kuwa hutakiwi kutofautiana na mtu unaependana nae10. Hupendi kutofautiana na wenzio kwa kuepusha wasiseme chochote kitakachokuumiza

Zoezi la Pili

Zoezi la Nyumbani

Page 38: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

34 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Page 39: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

35Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

11. Huwezi kuvumilia kama watu hawakusikilizi12. Uko tayari kupindisha ukweli ili kutetea mawazo yako13. Sio rahisi mtu mwingine akushinde mnapobishana jambo14. Una moyo mwepesi na ni rahisi kuumia haraka15. Unachukia mtu anapokupinga16. Unaamini kuwa kuna pande mbili kwa kila jambo17. Unajisikia vibaya baada ya kugombana na mtu na hukupata nafasi ya kumwambia ukweli18. Unaogopa wenzio watakuchukia kama utatofautiana nao19. Umegundua kuwa wenzio wanaogopa kutofautiana na wewe20. Uko radhi u�che hisia zako na maoni yako kwa kuhofu kuumizwa.

Matokeo yako yanamaanisha nini?

Katika sentensi kumi ulizochagua zungusha namba sahihi katika jedwali lililopo hapo chini.

Mfano

Kama umechagua sentensi namba moja, Utazungusha namba moja iliyopo kwenye Dubu.

Kobe Simba Dubu Mbweha Bundi5 3 1 4 210 11 6 12 714 15 9 13 820 19 18 17 16

Sasa jumlisha idadi ya mizungusho katika kila jedwali. Angalia ni kipengele gani kina mizungusho mingi kuliko kwingine. Hiyo ndio namna yako ya kutatua migogoro.

Tabia za wanyama hapo juu zinaelezwa kama ifuatavyo:

Kobe {Mkwepaji}Kobe huingia kwenye jumba lake ili kuepuka migogoro. Wapo tayari kuachia malengo na mahusiano yao kwa kuogopa kuumizwa. Wanakaa mbali na vitu au watu watakowasababishia migogoro. Wanaona hawana msaada wala matumaini ni bora kwao kujiepusha na migogoro.

Simba {Mpenda fujo na kuonea}Simba anaamini kuwa migogoro inamalizika endapo mtu mmoja anashinda na mwingine anashindwa. Endapo Simba ameshinda anajiona amefanikiwa na endapo ameshindwa Simba hujisikia kuwa mdhaifu na amepoteza. Simba wapo tayari kupigana, kuonea na kukandamiza ili wapate ushindi.

Dubu {Mbembelezaji na Mpuuzaji}Dubu anaona ni heri malengo yake yapotee kuliko kuharibu mahusiano. Dubu anapenda kupendwa na kukubalika na kila mtu. Dubu anaamini kuwa haiwezekani kusuluhisha migogoro bila kuharibu mahusiano.

Page 40: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

36 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

SIKU YA NNE

Uwakilishi wa kazi ya nyumbani.

SIKU YA TANO

SEHEMU YA TATU: MAWASILIANO

Lengo mahususi

Baada ya kipindi kila mwanafunzi aweze kuonesha stadi sahihi za mawasiliano.

Mwezeshaji

{Zoezi la Utangulizi: Mnong’ono wa kichina}Waongoze wanafunzi wakae kwenye duara. Mpe mwanafunzi wa kwanza sentensi fupi {Mtoto mkubwa wa kaka yake kaka alitumwa kwenda sokoni kununua kuku na kanga.} ambaye ataisoma kimoyo moyo kisha atamnong’oneza mwenzake aliye karibu. Wanafunzi wataendelea kunong’onezana na kuhakikisha ujumbe unam�kia mwanafunzi wa mwisho ambaye atasema kwa sauti kile alichoam-biwa. Hapo wataangalia ni namna gani ujumbe ulivyobadilishwa kuanzia mwanzo hadi mwisho.

Mwezeshaji ajadiliane na wanafunzi kwa ufupi ni kitu gani wamejifunza kutokana na zoezi hilo lakini pia asisitize kuwa mawasiliano mazuri yanahitaji: usikivu, uelewa, umakini na usahihi.

Page 41: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

37Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Mbweha {Mdanganyifu}Mbweha yupo nusu nusu katika kujali mahusiano na malengo. Inapotokea migogoro Mbweha yupo tayari kwa kila mtu aache malengo yake kadhaa na mahusiano yaendelee. Huyu anataka wote waumie au wote wafaidike.

Bundi {Mpatanishi}Anathamini mahusiano na malengo kwa kiasi kikubwa. Migogoro au matatizo yanatakiwa kusuluhishwa huku pande zote zikitimiza malengo yake. Lakini pia Bundi hu�kiri endapo migogoro itatatuliwa vizuri mahusiano yataimarika kwa kuwa itaondoa mvutano. Wapo tayari kukaa chini kwa ajili ya kumaliza tofauti zao na hawaridhiki mpaka utatuzi umepatikana.

SEHEMU YA TATU: MAWASILIANO

Maana ya mawasiliano

Mawasiliano ni stadi muhimu katika kupashana habari na taarifa mbalimbali katika maisha. Mawasiliano yanasaidia kuelezea hisia, mawazo na mahitaji yako kwa usahihi ili watu waweze kuelewa.Mawasiliano sahihi huwezesha mtu kuwa na mahusiano mazuri na wengine.

Njia za mawasiliano:

Njia kuu za mawasiliano ziko mbili

1. Mawasiliano kwa njia ya maneno kwa kutamka au kuandika.2. Mawasiliano kwa njia ya vitendo inayohusisha viungo vya mwili ili kuwasilisha taarifa fulani. Njia

hii inaweza kufanyika kwa ishara, alama au muonekano.

Mitindo ya mawasiliano

1. Mawasiliano ya kibabe au vurugu (mawasiliano ya ukali na yenye ushari) yana sifa zifuatazo:

• Ya fujo • Ya hasira • Ya kufokeana • Ya matusi • Ya kupingana

Matokeo yake ni: • Yanakandamiza • Yanaumiza • Yanatawala mawazo ya wengine • Yanadhulumu • Yanashurutisha • Yana ubinafsi

Page 42: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

38 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Mwezeshaji

Wagawe wanafunzi katika makundi tofauti na waongoze waandae maigizo dhima yatakayoonesha mitindo ya mawasiliano tajwa hapo juu.

Page 43: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

39Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

2. Mawasiliano ya msisitizo (mawasiliano ya dhati) yana sifa zifuatazo:

• Yana upole • Ya kujiamini • Yana adabu • Yana ukweli na uaminifu • Yamenyooka

Matokeo yake ni • Hayaumizi mtu yeyote • Yanaeleweka • Unaheshimika • Mawazo yako yanathaminika

3. Mawasiliano yasiyoonesha hisia yana sifa zifuatazo:

• Yanaonesha uwoga na kutojiamini • Yana �cha ukweli au hisia

Matokeo yake: • Unaona hujathaminika • Yana kujengea hasira na chuki • Hupati unachohitaji • Unajisikia mpweke

Tafuta kisa chochote na uoneshe ni mawasiliano ya aina gani ungeyafanya kwa kutumia Igizo Dhima.

Zoezi la Pili

Page 44: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

40 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Mwezeshaji

Waongoze wanafunzi kusoma kisa mafunzo kilichopo hapo chini kisha wajibu maswali na kuwasilisha.

Page 45: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

41Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

HadithiSoma hadithi inayofuata, kisha jibu maswali na wasilisha.

Mimi ni mvulana mwenye umri wa miaka 15 ambaye ni mkubwa katika familia. Baba yetu alifariki miaka mingi iliyopita na Mama yangu amefariki miezi michache iliyopita. Nina wadogo zangu wanne wanaonitegemea. Wazazi wetu hawakuacha wosia hivyo mjomba alichukua mali zote. Tumebakiwa na kibanda, nguo chache na baadhi ya vyombo vya ndani. Mara nyingi nakosa usingizi niki�kiria tutaishi vipi na hatima ya maisha yangu na wadogo zangu. Bila shaka kuna watoto wengine kama mimi ila sina mawasiliano nao ili niweze kujua wao wanakabiliana vipi na changamoto hii.

Maswali

1. Ungekuwa wewe ni kijana huyo, ungefanyaje?2. Je, una�kiri ni watu gani wanaweza kumsaidia kijana huyu katika kutatua matatizo aliyonayo?

Eleza namna gani.3. Je, ungekuwa wewe ungetumia njia gani za mawasiliano ili uweze kupata msaada ulio sahihi?

Toa sababu. 4. Taja faida au hasara ya kutumia njia nyingine za mawasiliano ambazo hujataja hapo juu.

Zoezi la Tatu

Page 46: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

42 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

SIKU YA KWANZA

SEHEMU YA KWANZA: TAFSIRI YA DHANA

Umahiri: Wanafunzi waweze kuhimili na kuepuka misukumo hasi ya kundi rika

Lengo mahususi

Baada ya kipindi kila mwanafunzi aweze: • Kueleza maana ya kundi rika, msukumo wa kundi rika, misukumo chanya na misukumo hasi • Kila mwanafunzi aweze kubainisha mifano hai ya misukumo chanya na misukumo hasi

Kundi rika ni nini?

• Ni kundi la watu au mara�ki wenye umri unaokaribiana au unaolingana wenye matamanio yanayo shabihiana.

Msukumo wa kundi rika ni nini?

• Ni hali ya mtu kufanya kitu kutokana na kushawishia au kuchochewa na kikundi au mtu wa rika au mara�ki. Msukumo rika unaweza kuwa hasi mfano unywaji wa pombe au chanya mfano kusoma kwa bidii.

Waongoze wanafunzi kufanya majibizano yaliyopo katika kitabu cha mwanafunzi na kisha kujibu maswali.

Mwezeshaji

Waulize wanafunzi maana ya kundi rika na msukumo rika kisha hitimisha kwa kuwaelezea maana halisi ya kundi rika na msukumo rika.

MADA YA NNE: MSUKUMO WA KUNDI RIKA

Page 47: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

43Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

SEHEMU YA KWANZA: TAFSIRI YA DHANA

1. Nini maana ya kundi rika?2. Nini maana ya msukumo rika?

Soma na uigize majibizano yafuatayo na mwenzako kisha jibu maswali yanayofuata:

Majibizano:

MADA YA NNE: MSUKUMO WA KUNDI RIKA

Zoezi la Kwanza

Zoezi la Pili

Bahati: Mambo shosti zanguMara�ki: Powaa shosti Ra�ki 1: Mbona mashamushamu hivi?Bahati: Tulieni! Tulieni! hivyo hivyo niwape ubuyu/storiRa�ki 2: Twambie ndugu mbona begi kubwa hivyo? Umebeba vitabu vya masomo yote nini?Bahati: Eti vitabu vya masomo yote!! Nani asome mavitabu yote hayo? Kwa taarifa yenu humu kuna viatu, simu, gauni, hereni, rangi ya mdomo (lipustiki), marashi, pete na mkufu. Mara�ki: Aaah!! Ra�ki 3: Umetoa wapi vitu vya thamani hivyo shosti?Bahati: Mmmm!! kaeni hivyo hivyo mwenzenu nina buzi langu ndilo linalonifadhili sina hata shi-da, hata nitake hela ya chipsi au soda linanipa tu. Mara�ki wote: (kwa mshangao mkubwa na kushi-ka mdomo)..

Ra�ki 1: Umepotea! Siku hizi hakuna kitu cha bure kwa wanaume hasa usiyemjua. Utavilipa tuu!! Anaweza kukutaka kimapenzi, usipoangalia atakubaka na atakupa mimba na hata maradhiRa�ki 2: Sisi ni wanafunzi hatuna budi kuzingatia masomo na kusoma kwa bidii jamaniRa�ki 3: Tuepuke tamaa, tutavipata hivyo na ving-ine vingi tu, tukimaliza masomoRa�ki 4: Tena tutanunua wenyewe vitu vizuri zaidi kwa hela zetu tukishaanza kujitegemeaBahati: Nashukuru sana mara�ki zangu jamani, kumbe nyie ni mara�ki wazuri sana, siendi tena kwa hilo libuzi, halitaniona tena. Nitakuwa pamoja nanyi bega kwa bega na nitayazingatia yote mliyonieleza na nitasoma kwa bidii na kujiheshimu. Na mavitu yake nayarudisha sasa hivi.

Page 48: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

44 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Mwezeshaji

Hitimisha majadiliano kwa kueleza umuhimu wa kufuata msukumo rika chanya.

Kisa mafunzo

Waeleze wanafunzi wasome kisa mafunzo na kisha wajibu maswali.

Page 49: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

45Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Jibu maswali yafuatayo:

1) Je, Bahati alikuwa Binti/ msichana wa aina gani?

………………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………………2) Mara�ki wa Bahati ni wa aina gani?

………………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………………3) Bahati alipata msukumo rika wa aina gani toka kwa mara�ki zake?

………………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………………4) Katika mazingira unayoishi au shule uliyosoma umewahi kuwa na mara�ki wa aina gani? (Elezea)

………………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………………5) Je, Umewahi kushawishiwa na mara�ki zako? Ushawishi wao ulikuwa chanya au hasi?

………………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………………6) Je, Umewahi kuhimili au kuzuia ushawishi hasi kutoka kwa mara�ki zako? Ulifanya nini ili kuepuka ushawishi huo?

………………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………………

Soma hadithi ifuatayo kisha ujibu maswali.

Kibibi ni msichana aliyemaliza darasa la saba katika shule ya msingi Mtakuja. Anakutana na kundi la wasichana wenzake ambao wamezoea kutoroka nyumbani na kwenda kwenye disko au ngoma na wakati mwingine kwenye kigodoro. Wasichana hawa wanamshauri kibibi kujiunga nao, lakini yeye anaogopa. Wanamueleza raha na vitu mbalimbali wanavyopata huko. Kibibi anaogopa kuwakosea wazazi wake kwa kutoroka. Wasichana hawa wanamfundisha mbinu mbalimbali za kutoroka nyumbani, wanam-shawishi hadi anakubali. Wakiwa kwenye ukumbi wa muziki / ngoma, baba mmoja anawanunulia pombe. Kibibi anakataa kuonja lakini ra�ki zake wanamshawishi anakunywa hadi analewa. Alipotoka hapo akiwa amelewa chakari baba huyo anambuluza kuelekea vichakani ambako anambaka. Baadaye ikathibitika kuwa Kibibi ni mjamzito na hivyo anashindwa kwenda sekondari.

Zoezi la Tatu

Page 50: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

46 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

MwezeshajiWaongoze wanafunzi katika makundi kuwasilisha kile walichokijadili na wape nafasi makundi mengine kuchangia. Mwisho hitimisha mjadala kwa kusisitiza umuhimu wa kuepuka ushawishi mbaya wa makundi rika.

SIKU YA PILI

SEHEMU YA PILI: ATHARI ZA MISUKUMO RIKA

Lengo mahususiBaada ya kipindi kila mwanafunzi aweze kueleza.

• Faida za msukumo rika • Hasara za msukumo rika

Mwezeshaji Waongoze wanafunzi kueleza na kuandika faida na hasara za misukumo rika kwa kutumia mifano halisi ya mazingira wanayoishi kisha wawasilishe. Baada ya hapo hitimisha kwa kuwaongezea faida na hasara za msukumo rika ambazo hazijatajwa.

FAIDA ZA MSUKUMO RIKA HASARA ZA MSUKUMO RIKA

Kuwa na malengo na kuyatimiza

Kutokuwa na malengo au kuwa na malengo na kushindwa kuyatimiza

Kufanya maamuzi sahihi Kuwa na maamuzi yasiyofaa

Kujenga ufanisi katika maisha Kukosa ufanisi

Kujifunza stadi mbalimbali za maisha

Kukosa stadi mbalimbali za maisha

Kuepuka tabia hatarishi kama uvutaji bangi, ulevi na uasherati

Kujiunga na makundi mabaya na kuiga tabia zisizofaa

Husaidia kujiamini kutokujiamini

SEHEMU YA TATU: MATAMANIO NA MAHITAJI

Lengo mahususiBaada ya kipindi kila mwanafunzi aweze kutofautisha kati ya matamanio na mahitaji.

Hitimisha kwa kuwaeleza kuwa mahitaji ni vitu muhimu na mtu hawezi kuishi bila kuwa navyo mfano malazi, mavazi na chakula. Kwa mwanafunzi madaftari, kalamu, sare ya shule ni mahitaji muhimu ili aweze kwenda shule na kusoma kwa ufanisi. Matamanio ni vitu ambavyo sio vya lazima mfano pipi, chokoleti, vipodozi na simu. Hivi ni vitu vya starehe tu, hakuna tatizo hata kama mtu akivikosa.

Page 51: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

47Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Jibu maswali yafuatayo:

I. Kibibi amepata msukumo wa aina gani?II. Misukumo kama hii hutokea katika jamii unayotoka? Toa mfano.III. Je, Kibibi alionyesha uwezo wa kushinda vishawishi vya kundi rika? Elezea.IV. Kwanini Kibibi hakuweza kushinda vishawishi toka kwa wenzake? Elezea.V. Je, Kibibi angetakiwa afanye nini ili kushinda ushawishi wa wasichana wenzake?VI. Je, Wewe ukikutana na mazingira kama ya Kibibi utafanya nini?

SEHEMU YA PILI: ATHARI ZA MISUKUMO RIKA

Fikiri: Kila mwanafunzi a�kiri jambo ambalo ni faida na jingine ambalo ni hasara ya msukumo rika.Jozisha: Kaeni katika jozi na mshikirishane majibu yenu. Mmoja aandike hasara na mwingine aandike faida ya msukumo rika na kubandika mgongoni.Shirikisha: Wanafunzi wawili viongozi ambao mmoja ni hasara na mwingine ni faida wapitie wenzao na kusoma walicho andika mgongoni na kuchagua wale walioandika kufuatana na kundi lao.

Kila kundi likae kwa pamoja na kufanya majigambo juu ya hasara na faida za msukumo rika.

SEHEMU YA TATU: MATAMANIO NA MAHITAJI

a) Eleza maana ya maneno yafuatayo:

i. Matamanioii. Mahitaji

b) Toa mifano ya matamanio na mahitaji

Na. Mifano ya Matamanio Mifano ya Mahitaji1.

2.

3.

4.

5.

Zoezi la Kwanza

Zoezi la Pili

Page 52: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

48 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Mwezeshaji

Mwisho wa siku hii ya pili wape kazi watakayofanyia nyumbani siku ya tatu na kuiwasilisha siku ya nne kama zoezi lililoainishwa siku ya tatu.

SIKU YA TATU

SEHEMU YA NNE: KUKABILIANA NA MISUKUMO RIKA HASI NA KUKUZA MISUKUMO RIKA CHANYA

Lengo Mahususi

Baada ya kipindi kila mwanafunzi aweze kueleza jinsi ya kukuza misukumo rika chanya na kukabiliana na msukumo rika hasi.

SIKU YA NNE

Mwezeshaji

Waongoze wanafunzi kila mmoja abandike kazi yake mgongoni na aruhusu wanafunzi kutembea tem-bea wakisoma kazi za wengine. Kisha ruhusu kujadiliana na kuongeza mawazo mapya waliyoyapata. Orodhesha majibu ubaoni na kuwaongezea hoja nyingine ambazo hazijatajwa. Mwisho chagua wa-nafunzi wawili wawili kuigiza hoja mojawapo kati ya zilizoainishwa hapo chini:

Jinsi ya kukuza misukumo rika chanya na kukabiliana na misukumo rika hasi

Msukumo rika ni changamoto inayowakabili wanafunzi na vijana wengi. Wanafunzi au vijana hao wanaweza wakashawishika kutumia madawa ya kulevya, kunywa pombe, kuiba, kujihusisha na ngono, kuvuta sigara, kujihusisha na makundi mabaya na hata kubadilisha mitazamo au haiba zao. Kuna mambo mengi yanaweza kufanyika ili kuepuka na kukabiliana na msukumo rika hasi bila kujali kuwa utapoteza mara�ki au utabadilisha matendo yako.

i. Kupotezea hoja.Njia hii inaweza ikawa ni njia mojawapo ya kuepuka maswali. Mwambie hauna haja wala hupendelei hicho kitu anachotaka ukifanye au anachokuomba. Hiyo inaweza kumfanya mtu anayekuuliza hilo swali au anayekushawishi asikuulize tena. Njia hii inaweza kutumika hasa mtu anapokupa au kukuomba vitu mfano: madawa ya kulevya, ngono, pombe au sigara.

Page 53: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

49Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

SEHEMU YA NNE: KUKABILIANA NA MISUKUMO RIKA HASI NA KUKUZA MISUKUMO RIKA CHANYA

Eleza ni jinsi gani unaweza kukuza misukumo rika chanya na kukabiliana na misukumo rika hasi.

Wanafunzi wawasilishe kazi walizopewa siku ya tatu.

Wanafunzi wasikilize maelekezo toka kwa mwezeshaji kuhusu mbinu mbalimbali za kukabiliana na msukumo rika hasi na kisha waigize kulingana na mbinu watakayopewa.

Zoezi la Kwanza

Zoezi la Pili

Zoezi la Nyumbani

Page 54: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

50 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

ii) Jifunze kusema “Hapana!”Njia hii ni nzuri kuepukana na msukumo rika hasi ingawa inaweza kuonekana ni njia ya kikaidi au ya kijeuri ila ni vizuri kusema hivyo ili kuepukana na vishawishi. Sema “Hapana!” na uwe na msimamo. Hii itakusaidia usisumbuliwe tena kwa sababu ina�kisha ujumbe wa moja kwa moja. Unaweza kusema “Samahani sipendi ujinga”

iii) Geuza hoja iwe utani. Weka utani kwenye jambo baya unapoambiwa na ra�ki au mara�ki. Onyesha madhara ya jambo hilo kiutani ili afahamu au wafahamu kuwa jambo wanalokwambia sio la maana kwako na wala hutalizingatia. Mfano:

“Eti kufanya ngono ni ujanja? Wapi bwana ni ushamba tu huo. Unaweza kupata mimba au magonjwa ya zinaa, mwishowe utarudisha namba (utakufa) mapema uache ubwabwa. Mimi najitam-bua siwezi kufanya hivyo ni ushamba”.

iv) Badilisha mada. Unapokutana na mtu au ra�ki anayekushawishi ku-jiingiza katika mambo mabaya, jaribu kubadilisha mada hiyo kwa kuingiza mada nyingine nzuri am-bayo itamfanya yeye aache kuongelea jambo hilo na kuanza kukusikiliza au kujadili mada yako nzuri.

Mfano:

Akianza kukueleza habari nzuri ya kigodoro, wewe mueleze kuwa kuna mashindano ya kuandika insha wametangaza jana shuleni na mshindi anapata laki tano!!!.

Twende tukafanye jambo lingine!

Page 55: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

51Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

v) Tafuta sababu za kuondoka.Njia nyingine ni kuondoka kwenye eneo la tukio kwa kuomba radhi kwamba unaondoka haraka. Hii itakusaidia kuepuka kundi rika na pengine unaweza kupata fursa ya ku�kiria namna ya kutatua tatizo.

Mifano ya sababu za kuondoka unazoweza kutoa ni: • Samahani natakiwa niwahi nyumbani • Samahani naona muda unakwenda na nimechoka • Samahani nimekumbuka nina ahadi na mwalimu wa masomo ya ziada muda huu

vi) Kataa mawazo yao kwa kuwaeleza madhara ya jambo wanalokushawishi ulifanye.Kwa kutumia njia hii utakuwa umewasaidia wana rika kutambua madhara ya jambo husika na hivyo kuacha au kubadili mitazamo yao badala ya wao kukubadili wewe.

Mfano: Ukiwa unashawishiwa kutoroka vipindi darasani. Waeleze wenzio madhara ya kutoroka ikiwa ni pamoja na kufeli mtihani, kukosa maarifa mbalimbali ya kimaisha na hatimaye kufukuzwa shule baada ya kukamatwa.

vii) Kuwa makini na unaoshirikiana nao. Njia bora ya kuepuka misukumo hasi ni kuachana na wale wanaokupeleka kwenye mazingira mabaya au hasi.

• Fanya ura�ki na mara�ki wazuri wanaokuelewa na wanaotambua mambo mazuri unayoyapenda ambao hawatakuingiza katika kutenda maovu au mambo ya hatari.

• Tafuta mara�ki unaoendana nao kitabia

• Kama unaona mara�ki ulionao ni wabaya tafuta mara�ki wengine kwa kujitahidi kushiriki-ana na wale wanaopenda shughuli kama zako. Mfano: Kusoma vitabu hii itakusaidia uwe na furaha kuliko ku�kiri namna ya kumkimbia ra�ki mbaya. Ili uwe na amani usiwaache mara�ki wa zamani gha�a chagua maeneo machache mazuri unayoweza kushirikiana nao.

Samahani natakiwa niwahi nyumbani

Page 56: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

52 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

viii) Kwanza kabisa epuka mazingira yanayoweza kukuingiza kwenye mtego wa msukumo rika hasi. Kuna baadhi ya mazingira yanaweza kukupelekea ukashawishika kufanya mambo mabaya, ni vizuri na ni busara kuyaepuka mazingira hayo ili kujiepusha na msukumo rika hasi.Kwa mfano:

• Kwenda kwenye vigodoro/ngoma/disko bila ya usimamizi wa watu wazima • Kukaa kwenye vijiwe au magenge au vijiwe vya mtaani • Kukaa maeneo ya vi�cho na hatarishi mfano gizani, vichakani, nyumba zisizokamilika

ujenzi ukiwa na mvulana.

ix) Jishughulishe na shughuli zenye manufaa. Njia mojawapo ya kukabiliana na msukumo rika ni kujishughulisha na shughuli unazozipendelea hasa kwa muda wako wa ziada badala ya kukaa bure bila shughuli yoyote.

Tafuta kazi unazozipenda zitakazokufanya uwe na shughuli muda mwingi. Mfano, unaweza kufanya shughuli fulani kama michezo, mazoezi ya viungo, kulima bustani, kujifunza ushonaji, ufugaji, usa� wa nyumbani nk katika jamii yako au nyingine.

Njia nyingine ni kutumia muda mwingi kwenye masuala ya shule. Kama vile kujiunga na klabu za masomo, mijadala ya kimasomo, masomo ya ziada, marudio ya majaribio.

Hii itakufanya uwe na shughuli wakati wote lakini pia itakuepusha na misukumo rika hasi na kukufanya ufaulu masomo na kutimiza malengo yako.

Page 57: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

53Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

x) Usiogope kuomba msaada au ushauri. Suala la kundi rika ni suala la kila mtu hata watu wazima wanakumbana na suala hili. Watu wengi wametafuta njia za kukabiliana na makundi rika kwa kuomba ushauri, unaweza ukapata njia nzuri za kukusaidia. Mtu ambaye anakujua wewe zaidi anaweza kukupa ushauri maalumu juu ya hali yako. Hakikisha unaomba ushauri kwa mtu ambaye unamwamini sana.

• Ongea na ra�ki unaye mwamini. Mwambie: Asha ananishawishi sana niende ngomani na kilabuni bila ruhusa ya wazazi wangu. Je, niseme wazazi wangu hawawezi kuniruhusu kwenda kilabuni au ngomani?

• Ongea na mtu mzima unayemwamini. Unaweza kumwambia, “Baadhi ya wanafunzi shuleni wananiambia sitakuwa nimepevuka kama sitafanya ngono. Je, Nifanye nini?”

Page 58: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

54 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

SEHEMU YA TANO: HITIMISHO LA MADA

SIKU YA TANO

Lengo mahususiBaada ya kipindi kila mwanafunzi aweze kueleza mambo yote aliyojifunza katika mada hii.

Mwezeshaji Wagawe wanafunzi katika makundi manne na kuwaongoza wafanye kazi zifuatazo:

Hitimisha kwa kutoa maelezo mafupi juu ya kazi walizozifanya.

Page 59: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

55Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

SEHEMU YA TANO: HITIMISHO LA MADA

Katika makundi manne fanyeni kazi zifuatazo:

1. Kundi la kwanza: andaa na onesha igizo kuhusu tofauti kati ya kundi rika chanya na kundi rika hasi.

2. Kundi la pili: andaa na imba ngonjera inayoonesha tofauti ya mahitaji na matamanio.

3. Kundi la tatu: andika na imba shairi linalohusu athari za kufuata msukumo rika hasi.

4. Kundi la nne: andaa majibizano mkionesha namna ya kukabiliana na msukumo rika hasi na kukuza msukumo rika chanya.

Page 60: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

56 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Umahiri: Mwanafunzi aweze kufanya shughuli mbalimbali sahihi za kupata kipato cha kumwezesha kupata mahitaji muhimu.

SIKU YA KWANZA

SEHEMU YA KWANZA: VYANZO SAHIHI VYA UFADHILI

Lengo mahususi

Baada ya kipindi kila mwanafunzi aweze kutaja maana ya ufadhili na vyanzo sahihi vya ufadhili katika mazingira yake.

Mwezeshaji

Wawezeshe wanafunzi kutaja maana ya ufadhili na vyanzo vya ufadhili vilivyopo kwenye mazingira yaoWaongoze wanafunzi kwa njia ya majadiliano; Ufadhili unaweza kutafsiriwa kama usamaria-mwema au msaada ili mtu afanikishe jambo fulani ambalo liko nje ya uwezo wake ambao unaweza kuwa vitu au pesa. Kwa kutumia picha; wanafunzi waweze kuja na majibu tofauti na kuwasilisha kwa wenzao darasani.

Pia waongoze wanafunzi kubainisha vitu au mahitaji yao yanayohitaji ufadhili. Kisha waongoze wa-nafunzi kutambua mahitaji yanayohusiana na shule au masomo mf. daftari, kalamu, sare ya shule na mahitaji binafsi kama sabuni, mafuta, pedi, taulo na khanga.

MADA YA TANO: UBUNIFU WA VYANZO VYA MAPATO

Page 61: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

57Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

i. Nini maana ya ufadhili?

ii. Katika makundi ya watano watano jadili na muandike vyanzo vya ufadhili mnavyovifahamu katika jamii yenu:

a. __________________________________________________________________________________

b. __________________________________________________________________________________

c. __________________________________________________________________________________

d. __________________________________________________________________________________

e. __________________________________________________________________________________

SEHEMU YA KWANZA: VYANZO SAHIHI VYA UFADHILI

MADA YA TANO: UBUNIFU WA VYANZO VYA MAPATO

iii. Chora vitu unavyohitaji ili kujiunga na elimu ya sekondari.a. Bainisha vitu utakavyomudu kununua mwenyewe/ wazazi.b. Bainisha vitu ambayo utahitaji kufadhiliwa.

Zoezi la Kwanza

Page 62: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

58 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Njia za kutafuta ufadhili

Hadi sasa mwanafunzi atakuwa amekwishajifunza maana ya ufadhili na ametambua vyanzo vya ufadhili katika jamii inayomzunguka. Waongoze wanafunzi wajadiliane njia za kutafuta ufadhili zilizotajwa na njia nyingine wanazozifahamu kuhusu ubora na utekelezaji wake katika mazingira yao.

Page 63: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

59Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

iv. Orodhesha hapo chini vitu vingine unavyo�kiri unahitaji kufadhiliwa.

v. Gawa vitu ulivyochora na ulivyoorodhesha katika makundi mawili katika jedwali hapo chini.

Mahitaji yanayohusiana na shule/ masomo Mahitaji binafsi

Njia za kutafuta wafadhili

Harambee (michango)

Hii ni njia ya kutafuta michango kutoka kwa wafadhili walio na uwezo wa kukusaidia kuendelea na masomo ya Sekondari.

Harambee inaweza kufanyika kwa njia zifuatazo:

• Kutumia fomu yenye mahitaji yako muhimu na watu waandike na kuweka ahadi ambayo itakuwezesha kupata mahitaji hayo

• Kuwasiliana na uongozi wa shule ikiwemo mwalimu au mzazi ambaye ni mjumbe wa UWW {Ushirikiano wa Wazazi na Walimu} au serikali ya mtaa au kijiji ili kukusaidia kufanya haram-bee kutoka kwa wasamaria wema.

• Kushirikiana na O�si ya Ustawi wa Jamii katika ngazi ya Halmashauri ili kufahamu mashirika yanayotoa misaada kwa wanafunzi wanaotoka au wanaoishi katika mazingira magumu.

Mfano wa fomu ya kuomba ufadhili umeoneshwa katika ukurasa unaofuata.

Page 64: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

60 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Page 65: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

61Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Mimi____________________________ninaishi kijiji / mtaa wa__________________________________

kata ya________________________________,nime chaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari katika

shule ya ________________________ Iliyopo katika kata ya____________________________________

Wilaya ya _______________ Mkoa wa _______________________. Tafadhali naomba uzungushie duara katika msaada unaoweza kunisaidia.

Natanguliza shukurani zangu za dhati.

FOMU YA UFADHILI KWA AJILI YA KUJIUNGA NA ELIMU YA SEKONDARI

Imepitishwa na

Mzazi au mlezi: _____________________________ : ________________:________________________

Jina Sahihi Tarehe

Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi alikosoma:

_____________________ :_____________________:_____________________:____________________

Jina Shule Sahihi Tarehe

Page 66: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

62 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

MwezeshajiWaongoze wanafunzi kusoma kisa mafunzo na kujibu maswali yanayofuata. Wagawe wanafunzi katika makundi ya watano watano wajadiliane na kuwasilisha kwa wenzao.

Fanya majumuisho ya mada kuhusu ufadhili na vyanzo vya ufadhili. Pia waase wanafunzi kuwa makini katika kutafuta wafadhili mbalimbali ili wasijiingize katika matatizo ambayo yanaweza kukatisha ndoto zao na malengo yao.

Page 67: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

63Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Tahadhari katika kutafuta wafadhili.

Hadithi

Soma hadithi hapo chini na ujibu maswali yafuatayo:

Kuna binti mmoja yatima tangu akiwa na umri wa miezi mitatu aliyelelewa na babu yake. Maisha yake yote yalikuwa ya shida kutokana ya kwamba babu yake hakuwa na uwezo kiuchumi. Alipomaliza darasa la saba alibahatika kufaulu na kuchaguliwa kujiunga na masomo ya sekondari, lakini bahati mbaya babu yake hakuwa na uwezo wa kumpatia mahitaji muhimu ya shule.

Binti huyu alijitahidi kutafuta wafadhili mbalimbali bila mafanikio. Siku moja babu yake alimwambia kuwa mbunge wa jimbo lao yupo na kwamba angeweza kumpatia msaada katika ku�kia azima yake ya kielimu. Katika harakati za kutaka kumuona mbunge kwa zaidi ya siku tano, alikutana na kijana mmoja aliyefanya kazi katika o�si hiyo ambaye alimsihi amweleze tatizo lililomfanya amtafute mbunge.

Binti alimweleza kijana huyo tatizo lake. Kijana huyo kwa moyo radhi aliamua kumsaidia kwa kumpa-tia mahitaji yake yote muhimu ya shule ikiwa ni pamoja na sare, madaftari, kalamu, sabuni na nguo za nyumbani alizozipenda kama binti.

Mahusiano ya binti na kijana huyu yalishamiri na ndani ya miezi sita wakawa wapenzi wanaopendana sana hadi ku�kia kushiriki ngono. Katika matokeo ya kufunga muhula wa kwanza, binti huyo alifaulu vizuri haswa masomo ya sayansi na kupewa zawadi za kitaaluma ambazo zilizidi kuwasha moto wa kuitimiza ndoto yake ya kuwa mwanasayansi mgunduzi. Hata hivyo alikuwa na hofu moyoni juu ya mahusiano ya kimapenzi aliyoyaanzisha baina yake na kijana anayefanya kazi katika o�si ya mbunge.

Wakati wa kufungua shule muhula wa pili, wasichana wote walipimwa ujauzito na binti huyo alibainika kuwa alikuwa na ujauzito. Matokeo hayo yalikatisha ndoto ya maisha yake kama miali ya moto katika mikono laini ya mtoto asiyekuwa na hatia.

Hapo ndiyo ulikuwa mwisho wa ndoto yake ya kuendelea na masomo ya sekondari.

Jibu maswali yafuatayo:

1. Andika njia mbalimbali ambazo binti huyu angeweza kuzitumia katika kutafuta ufadhili.2. Je, njia aliyotumia ya kufanya ngono na kijana aliemlaghai ni sahihi? Eleza kwanini?3. Ungekuwa wewe ni huyo binti ungefanya nini?4. Je, hadithi hii inakufundisha nini?5. Je, unawaasa nini mabinti wenzako ambao wanaweza kujikuta kwenye hali kama hiyo?

Zoezi la Pili

Page 68: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

64 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

SIKU YA PILI

SEHEMU YA PILI: NJIA ZA KUFANYA KAZI ZA UBUNIFU KUJIPATIA KIPATO

Lengo mahususiBaada ya kipindi kila mwanafunzi aweze kubuni na kufanya shughuli mbalimbali ambazo ni halali za kumwezesha kujipatia kipato.

MwezeshajiTumia njia ya matembezi ya galari na igizo.

Wagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi watano watano. Waongoze kila kundi kutaja shughuli wanazoweza kufanya ili kupata kipato. Kisha waongoze wanafunzi wabandike kazi zao ukutani kwa ajili ya matembezi ya galari. Baada ya matembezi ya galari kila kundi lichague shughuli moja kutoka kwenye kazi zao na kuigiza jinsi ya kuifanya.

Waeleze kuwa siku itakayofuata kutakuwa na kazi za ubunifu au sanaa ambazo wanafunzi watazifanya wakiwa nyumbani kama ilivyoainishwa kwenye siku ya tatu.

Waongoze wanafunzi kujigawa kwenye makundi ya wawili wawili au watatu watatu kulingana na ujirani wa maeneo wanayoishi ili washirikishane kazi wanazozifahamu.Waeleze wanafunzi kuwa wanaweza kufundishwa na mtu mzima kama mzazi au mlezi au dada aliye nyumbani kwao.

Kubadilishana ujuzi wa kazi za mikono

SIKU YA NNE

MwezeshajiWaeleze wanafunzi wafanye maonesho darasani na kuwashirikisha wenzao kile walichojifunza kwa ajili ya maboresho.Washirikishe wanafunzi kupanga siku maalum kwa ajili ya maonesho ya vitu walivyovitengeneza na wajiandae kwa maonesho hayo.

Angalizo: Ni muhimu ukafanya maonesho kwa kuchagua siku moja wakati wa Mpango wa Utayari wa kujiunga na Elimu ya Sekondari {MUES}.

Waongoze wanafunzi kuandaa tangazo ambalo litabandikwa sehemu mbalimbali ili kuwaalika watu wakiwemo wazazi, wanafunzi, walimu na jamii ya shule kwa ujumla kuhudhuria maonesho na kununua vitu vitakavyowavutia.

SIKU YA TATU

Page 69: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

65Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

SEHEMU YA PILI: NJIA ZA KUFANYA KAZI ZA UBUNIFU KUJIPATIA KIPATO

Kaeni katika makundi ya wanafunzi watano watano, mjadili na kuandika kazi au shughuli mnazoweza kufanya ili kujipatia kipato kwa ajili ya masomo na kujikimu.

Bandikeni kazi zenu ukutani na kila kundi lipitie kazi za wenzao na kuzisoma. Kwa pamoja muainishe na muongeze shughuli au kazi ambazo hamjazitaja kwenye orodha yenu ya awali.

Igizo

Chagueni kazi moja mliyoandika na kuitungia igizo la kuonyesha mtakavyoifanya shughuli hiyo ili kuwapatia kipato.

Mjigawe katika makundi ya wawili wawili au watatu watatu kulingana na ujirani wa maeneo mnayoishi.

Mkiwa nyumbani mbadilishane mawazo na kufundishana shughuli ambazo mnaweza kujifunza kutoka kwa wenzenu zikiwemo kazi mbalimbali za sanaa au ubunifu ambao utaweza kuwapa kipato.

Aidha, mnaweza kufundishwa kazi yoyote ya ubunifu au sanaa na wazazi, walezi au watu waliowazidi umri.

Kazi za ubunifu na kipato

Mtawasilisha kwa wenzenu kazi za nyumbani mlizofundishana siku iliyopita na pia mtafanya maonesho kwa wenzenu darasani kwa kuwaeleza hatua mlizopitia kutengeneza kazi hizo za sanaa au ubunifu.

Mtawaeleza wenzenu namna gani kazi hizo mlizozifanya zinavyoweza kuwaingizia kipato.

Kupanga siku maalum ya maonesho

Mtashirikiana kwa pamoja kuandaa siku ya kufanya maonesho ya kazi zenu za ubunifu kwa kujadili na kugawana majukumu kulingana na mahitaji muhimu kama vile kuandaa na kupamba ukumbi, kukaribisha wageni na kuandaa ratiba.

Zoezi la Kwanza

Kubadilishana ujuzi wa kazi za mikono

Page 70: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

66 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Mwezeshaji

Ni muhimu utoe majumuisho kwa kuamua na wanafunzi kwa pamoja kuhusu siku na muda wa maonesho maalum ya kazi hizo za ubunifu au sanaa. Aidha, eleza umuhimu wa kazi mbalimbali wanazoweza kuzifanya na kujipatia kipato.

SIKU YA TANO

SEHEMU YA TATU: STADI SAHIHI ZA KUTUMIA NA KUWEKA AKIBA

Mwezeshaji

Tumia njia ya bungua bongo kupata maana ya kutumia pesa kwa usahihi na kuweka akiba.

• Nini maana ya kutumia pesa kwa usahihi na umakini? • Nini maana ya kuweka akiba? • Ukipata pesa kama shilingi elfu hamsini, utazitumiaje?

Waongoze wanafunzi kukaa kwenye makundi ya watano watano, wasome habari iliyopo chini na kujibu maswali kwa kujadiliana.

Page 71: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

67Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Mfano wa mahitaji muhimu•Mahalipamaonesho•Sikuyamaonesho•Kuandaatangazolakualikawatu•Kukamilishakuandaavituvyamaonesho

SEHEMU YA TATU: STADI SAHIHI ZA KUTUMIA NA KUWEKA AKIBA

Soma habari ifuatayo na kisha ujibu maswali yanayofuata:

Siku moja Aisha alikuwa anaenda sokoni alitumwa na mama yake kwenda kununua nyanya na vitunguu. Akiwa njiani alibahatika kuokota shilingi laki moja. Aisha alifurahi sana na kwa haraka alielekea sokoni. Alipo�ka sokoni alinunua nyanya na vitunguu kama alivyoagizwa na mama yake. Akaanza ku�kiria namna atakavyotumia pesa aliyookota. Akaamua kununua kitabu kizuri cha baiolojia kwa shs 21,500/=. Aidha, Aisha alijinunulia ndala kwa sh 900/=, Shati la shule ya sh. 3,500/=. Aisha aliendelea kuitumia hela hiyo kujinunulia vipodozi kama wanja, marashi, lipustiki, rangi ya kucha, hereni ambavyo kwa pamoja viligharimu sh 27,500/=. Hali kadhalika, alijinunulia mafuta ya ngozi ya shilingi 5,000/=, madaftari na kalamu kwa sh 3,000/= na pipi na chokoleti za sh 11,300/=. Pesa iliyobaki Aisha alirudi nayo nyumbani akiwa na matarajio kuwa ataitumia tena siku nyingine.

Maswali

1. Je, Aisha aliokota shilingi ngapi?2. Je, alitumia jumla ya shilingi ngapi?3. Je, Aisha alibaki na shilingi ngapi?4. Andaa jedwali linaloonesha jumla ya matumizi ya Aisha kisha ainisha matumizi muhimu na

matumizi yasiyo muhimu katika jedwali hapo chini.

Zoezi la Kwanza

Matumizi yaliyo muhimu Matumizi yasiyo muhimu

Page 72: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

68 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Mwezeshaji

Waongoze wanafunzi kupata jumla ya matumizi ambayo ni 72,700/= na pesa iliyobakia ambayo ni 27,300/=

Waongoze wanafunzi kubaini matumizi ya Aisha ambayo ni ya muhimu na ambayo siyo ya muhimu.

Waeleze wanafunzi kuwa wanapookota pesa au wanapokuwa na pesa kwa ajili ya matumizi yao ni vyema wakawahusisha wazazi, walezi au watu wazima ambao watawaongoza jinsi ya kupanga matumizi. Waongoze wanafunzi kupata majibu ili kuongeza ufahamu kuhusu matumizi mazuri ya pesa.

Waongoze wanafunzi kupanga bei ya vitu watakavyoweka kwenye maonesho na kupanga matumizi sahihi.

Waongoze wanafunzi kuandika kwenye karatasi na kubandika kazi zao ukutani.

Page 73: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

69Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

5. Je, una�kiri kuokota pesa ni chanzo sahihi cha kupata kipato?6. Je, una�kiri Aisha alifanya uamuzi sahihi wa kutumia pesa aliyookota?7. Je, wewe ungekuwa Aisha ungefanya nini baada ya kuokota pesa hizo?8. Je, ni ushauri gani unaweza kumpa Aisha kuhusu namna ya kutumia pesa iliyobaki?

Fikiri kuwa siku ya maonesho umeweza kuuza vitu vya sanaa ulivyotengeneza.

Kwa bei uliyopanga, fanya makadirio ya mauzo ya vitu kutokana na bei ulizoweka.

Kwa pesa ya mauzo utakayokadiria kuipata, panga matumizi yako na weka akiba kwa mahitaji ya baadaye.

Kwa pesa ya mauzo utakayokadiria kuipata kutokana na maonesho, andika kazi yako ya mapato na matumizi kwenye karatasi uliyopewa na bandika kazi yako ukutani.

Zoezi la Pili

Page 74: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

70 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

SIKU YA KWANZA

SEHEMU YA KWANZA: TAFSIRI YA DHANA

Lengo mahususi

Baada ya kipindi, kila mwanafunzi aweze kueleza maana ya kupevuka, kuvunja ungo na hedhi.

Mwezeshaji

Wape wanafunzi nafasi ya ku�kiria mmoja mmoja na kisha kushirikishana wawili wawili maana ya hedhi, kupevuka na kuvunja ungo. Kisha wape nafasi ya kueleza maana hizo kwa kuwauliza maswali. Aidha, fanya majumuisho kwa kuwaeleza kwa kina maana ya dhana hizi.

MADA YA SITA: JINSI YA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA MWILI KWA WASICHANA

Umahiri: Wanafunzi waweze kukabiliana na mabadiliko ya mwili

Zoezi la Kwanza

Page 75: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

71Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

SEHEMU YA KWANZA: TAFSIRI YA DHANA

Eleza maana ya maneno yafuatayo:

1. Kupevuka

Hii ni hali inayotokea katika kipindi cha ukuaji wa mwanadamu ambapo mabadiliko ya kimwili na kihisia hutokea. Kila mtu anapitia kipindi hiki na mara nyingi kwa wasichana kuanzia kati ya miaka 8 mpaka 19.Kupevuka huanza wakati ambapo kemikali (vichocheo) ziitwazo homoni huanza kuzaliana katika mwili. Hivi ndivyo vyanzo vikuu vya mabadiliko mwilini. Pamoja na kusababisha mabadiliko mwilini, (vichocheo) homoni hizi husababisha mabadiliko ya hisia. Mabadiliko hayo ya hisia yanaweza kumsababishia msichana kuwa na huzuni, aibu, kuanza kujiremba, kujipenda na kuvutiwa na jinsi tofauti na wakati mwingine kuchanganyikiwa.

Mabadiliko haya huchukua mwaka mmoja au chini ya hapo na kwa wengine inaweza ku�kia hata miaka sita.

MADA YA SITA: JINSI YA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA MWILI KWA WASICHANA

Zoezi la Kwanza

Kupevuka

Kuvunja ungo

Hedhi

* Illustration source: Vipindi vya Maisha (Growth and changes) - UNICEF Tanzania

Page 76: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

72 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Mwezeshaji

Waongoze wanafunzi kufanya zoezi lililoainishwa kwenye kitabu chao. Kisha fanya majumuisho na kuwaongezea changamoto nyingine zinazoweza kutokea. Zifuatazo ni baadhi ya changamoto unazoweza kukabiliana nazo wakati wa hedhi.

• Kukosa sehemu ya kujihifadhi mfano sehemu ya kunawa na kubadilishia taulo za kike (pedi) pindi uwapo mbali na mazingira ya nyumbani.

• Kuwaonea aibu mara�ki na kujitenga nao. • Kukosa vifaa vya kujihifadhi mfano taulo za kike (pedi) au vitambaa sa� vilivyo andaliwa

kwa kazi hiyo. • Kukosa mtu wa kumshirikisha kuhusu swala hili. • Kutokwa na damu nyingi.

Zoezi la Pili

Page 77: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

73Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Dalili za kupevuka

• Matiti kuanza kuwa makubwa • Kuota nywele sehemu za siri na kwenye makwapa • Kuwa na chunusi • Nyonga zinatanuka • Sauti huanza kuwa nyororo zaidi • Kupata hedhi ya kwanza (kuvunja ungo)

2. Kuvunja ungoHiki ni kitendo cha msichana kupata hedhi kwa mara ya kwanza. Kwa walio wengi hutokea kati ya umri wa miaka 11 mpaka 14. Kipindi hiki msichana anaweza kupata mimba iwapo atafanya ngono.

3. HedhiNi damu inayotoka katika uke kila mwezi kwenye kuta za mfuko wa uzazi (uterasi) wa mwanamke asiye mjamzito. Wakati wa hedhi kuta hizo hubomoka na damu kutoka nje kupitia ukeni. Kutokwa damu hudumu kuanzia siku tatu hadi saba (japo yaweza kuendelea zaidi au kupungua). Usiwe na wasiwasi unapotokwa damu kila mwezi maana ni jambo la kawaida, ndio maumbile ya kila msichana.

Hali hii huendelea hadi mwanamke anapo�kia umri kati ya miaka 45 hadi 50 na huitwa ukomo wa hedhi (menopozi).

Hali anazoweza kukutana nazo msichana wakati wa hedhi.

• Maumivu ya tumbo chini ya kitovu, tumbo kujaa gesi na kusikia vichomi • Maumivu ya mgongo na kiuno, kusikia kizunguzungu na kichwa kuuma • Kuwa na hasira • Kuona aibu • Kusikia kichefuchefu na wakati mwingine kutapika • Kukosa hamu ya kula • Kuhisi uchovu muda mwingi • Kuwa na wasi wasi • Kujitenga na wenzake

Angalizo: Maumivu wakati wa hedhi hayadumu kwa muda mrefu. Ikitokea maumivu yamezidi sana ni muhimu kumwona daktari.

Wanafunzi wakae katika makundi ya watano watano wajadili na kueleza changamoto wanazopata wakati wa hedhi na jinsi wanavyokabiliana nazo. Jaza majibu katika jedwali linalofuata.

Zoezi la Pili

Page 78: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

74 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Malengo mahususi

Baada ya kipindi kila mwanafunzi aweze.

• Kueleza kwa usahihi maana ya mzunguko wa hedhi na jinsi unavyotokea. • Kuchora kwa usahihi mzunguko wa hedhi.

SIKU YA PILI

SEHEMU YA PILI: MZUNGUKO WA HEDHI

Page 79: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

75Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Jinsi ya kukabiliana na changamoto wakati wa hedhi

Ongea na watu wazimaIli kupata ushauri mzuri kama upo nyumbani, waweza kuongea na watu wazima kama mama, dada, shangazi, bibi, mara�ki wa kike au mtu mzima (mwanamke) katika jamii yako. Hawa wote watakupa ushauri mzuri. Ikiwa upo shuleni mwambie mlezi wako wa kike, mwalimu wako wa kike, au wanafunzi wenzako wa kike unaowaamini.

UsiogopeIngawa hali hii inaweza kukuogopesha hasa unapoona damu zinakutoka ukeni, usiogope ni jambo la kawaida kabisa.

Kuwa msa�Hakikisha unaweka kitambaa kisa� au pedi kwenye chupi yako na badilisha kitambaa au pedi kila baada ya masaa 2-3. Oga au nawa kwa maji sa� na sabuni.

SEHEMU YA PILI: MZUNGUKO WA HEDHI

Wanafunzi wakae katika makundi ya watano watano, wajadiliane jinsi mzunguko wa hedhi unavyotokea na kisha wachore mzunguko huo halafu wawasilishe kwa wenzao.

Changamoto wakati wa hedhi Njia ya kukabiliana na changamoto hizo

Zoezi la Kwanza

* Illustration source: Vipindi vya Maisha (Growth and changes) - UNICEF Tanzania

Page 80: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

76 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

MwezeshajiWaongoze wanafunzi kufanya zoezi la kwanza, kisha tumia mchoro walionao kuelezea jinsi mzunguko unavyokuwa.

Hesabu kuanzia siku ya kwanza unapopata hedhi hadi hedhi inapoacha kutoka. Siku tano mbele zitaku-wa salama, siku nane (8) zinazofuata mbele ni siku za hatari, ukishiriki ngono unaweza kupata mimba katika kipindi hiki. Siku nyingine zote zinazobakia ni siku salama hadi hedhi itakapoanza kutoka tena.

Hitimisha kwa kueleza kuwa mwili wa binadamu unabadilika kulingana na mazingira, vyakula, hali ya hewa, msongo wa mawazo na magonjwa. Kwa hiyo, mzunguko huu unaweza kubadilika kulingana na sababu zilizotajwa. Aidha, mwanafunzi asitumie elimu ya mzunguko huu kufanya ngono kwa kuwa hatari ya kupata ujauzito ni kubwa.

Waongoze wanafunzi kufanya zoezi la pili kama lilivyoainishwa kwenye kitabu.

Waagize kutafuta na kuandika mawazo potofu na mila zilizopitwa na wakati juu ya hedhi.

Waongoze wanafunzi kuwasilisha kazi yao ya nyumbani waliyopewa siku ya pili na kisha wajadiliane na kushirikishana kile walichokiandika. Kisha mwezeshaji hitimisha kwa kuongeza mawazo potofu na mila zilizopitwa na wakati juu ya hedhi.

Baadhi ya mawazo potofu na mila zilizopitwa na wakati juu ya hedhi ni:

1. Msichana aliye kwenye siku zake akishika mmea wa kijani unakauka (mfano nyanya chungu).2. Msichana kama anaumwa tumbo wakati wa hedhi akipata mimba na kuzaa haumwi tena.3. Matumizi ya pedi za dukani yanaweza kukufanya usizae maishani.4. Pedi/ kitambaa chenye damu kikiokotwa na ndege huwezi kupata mtoto maishani.5. Ukila chakula cha baridi ukiwa kwenye siku zako utaumwa tumbo.6. Ukimpikia kaka yako chakula ukiwa kwenye hedhi atakufa.7. Ukifanya ngono ukiwa kwenye siku zako hupati tena maumivu ya tumbo {ni muhimu mwezeshaji

akagusia uwezekano mkubwa wa kupata VVU na magonjwa mengine ya ngono kwa tendo hilo}.8. Ukinywa vinywaji vyenye sukari nyingi kipindi cha hedhi inasababisha damu iwe nzito zaidi.

Hitimisha kwa kuwaeleza kuwa haya yote siyo ya kweli, ni mawazo potofu na mila zilizopitwa na wakati. Hata hivyo, watu wa zamani walikuwa wanasisitiza binti kuwa msa� na kutupa vitambaa kwa uangalifu kwa njia hii ya vitisho.

SIKU YA TATU

Andika mawazo potofu na mila zilizopitwa na wakati juu ya hedhi na ziwasilishe siku ya nne. Kazi hii itafanywa nyumbani.

SIKU YA NNE

Wanafunzi watawasilisha kazi waliyofanya nyumbani siku iliyopita.

Page 81: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

77Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Mzunguko wa hedhi

Hiki ni kipindi kati ya hedhi moja hadi nyingine. Kwa kawaida hutokea mara moja kila baada ya siku 28. Mzunguko unaweza kuwa mrefu au mfupi zaidi ya hapo, pia unaweza kubadilika ku-toka mwezi mmoja hadi mwingine. Hali hii ikitokea isikufanye uogope kwani ni hali ya kawaida. Mzunguko unaweza kuwa kati ya siku 21 hadi 35 ingawa mara nyingi ni siku 28.

Hesabu kuanzia siku ya kwanza unapopata hedhi hadi hedhi inapoa-cha kutoka. Siku tano mbele zitakuwa salama, siku nane (8) zinazofuata mbele ni siku za hatari ukishiriki ngono unaweza kupata mimba katika kipindi hiki. Siku nyingine zote zinazobakia ni siku salama hadi hedhi itakapoanza kutoka tena.

Wajitolee wanafunzi watatu na waeleze uzoefu wao wa siku yao ya kwanza walivyoanza hedhi kwa kufuata mwongozo ufuatao:

• Ulimshirikisha nani siku yako ya kwanza kuanza hedhi? • Ulikutana na changamoto gani na jinsi gani ulikabiliana nazo? • Je ulipata maumivu yoyote? Yalikuwaje? • Vifaa gani ulitumia kujisitiri wakati wa hedhi na jinsi ulivyotumia vifaa hivyo • Ulijiwekaje sa�? • Uliweka wapi pedi au vitambaa ulivyotumia?

Andika mawazo potofu na mila zilizopitwa na wakati juu ya hedhi na ziwasilishe siku ya nne. Kazi hii itafanywa nyumbani.

Wasilisha kazi mliyofanya nyumbani siku iliyopita.

HEDHI

SALAMA

SALAMA

HATARI

HEDHI 1-5Kipindi ambacho Uterasi hutoa damu baada ya yai la mwanamke kukosa kurutubishwa

SALAMA 6-19Ni kipindi ambacho Mwanamke hawezi kupata mimba. Japo ni kipindi kinachoelekeakipindi cha hatari

SALAMA 19-28Kipindi ambacho mwanamkeHawezi kupata mimba

HATARI 11-18Katika kipindi hiki mwanamke akijamilana tu

anapata mimba

Zoezi la Pili

Zoezi la Tatu

Zoezi la Nyumbani

Page 82: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

78 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

SEHEMU YA TATU: USAFI WAKATI HEDHI

Malengo mahususi

Baada ya kipindi kila mwanafunzi aweze:

• Kueleza namna ya kujiweka sa� wakati wa hedhi • Kutaja vifaa vinavyotumika wakati wa hedhi • Kueleza namna ya kuhifadhi vitambaa vilivyotumika • Kutupa pedi zilizotumika sehemu sahihi. • Kueleza umuhimu wa kujiweka sa� wakati wa hedhi

Mwezeshaji

Waongoze wanafunzi kukaa kwenye makundi sita kisha wafanye kazi iliyoainishwa kwenye kitabu chao.Baada ya wanafunzi kufanya kazi hiyo, wawasilishe kwa wenzao darasani, kisha hitimisha kwa kuwaelezea na kutoa majibu ya maswali waliyojadiliana.

1. Usa� wakati wa hedhi ni kitendo cha kuondoa uchafu unaosababishwa na damu inayotoka ukeni. Ni muhimu kuwa msa� wakati wa hedhi kuepuka maradhi yanayoweza ku-sababishwa na uchafu mfano fangasi, ili uweze kujisikia vizuri na kuepuka harufu mbaya.

2. Vifaa vinavyoweza kutumika kujiweka sa� wakati wa hedhi ni pamoja na maji, sabuni, pedi/ pam-ba/ vitambaa, beseni au ndoo. Unaweza kujiweka sa� kwa kunawa sehemu zako za siri mara tatu au nne kwa siku. Ni muhimu kukausha sehemu zako za siri kwa kitambaa au taulo sa�. Weka pedi au kitambaa kwenye chupi yako na uvae. Badilisha pedi au kitambaa kila unapoona imelowana.

3. Viringisha pedi iliyotumika kwa kutumia gazeti au mfuko kisha tumbukiza pedi hiyo kwenye chombo maalum cha takataka kisha kuzichoma. Kitambaa kilichotumika kifuliwe vizuri kwa maji sa� na sabuni, kianikwe juani na kikauke vizuri kisha kipigwe pasi, kikunjwe na kutun-zwa vizuri.

4. Msichana asipojiweka sa� wakati wa hedhi atapata magonjwa yanayosababishwa na uchafu kama fangasi, upele na vidonda ukeni, kutoa harufu mbaya, kukimbiwa na mara�ki na kutojiamini.

5. Maumivu wakati wa hedhi huweza kupunguzwa kwa kuweka maji ya moto kwenye chupa maal-umu na uweke kwenye tumbo lako sehemu inayouma (chini ya kitovu), kunywa chai au vitu vya moto, fanya mazoezi, tumia dawa ya kutuliza maumivu.

6. Kuna misemo/majina mbalimbali yanayotumika kumaanisha kuwa msichana yuko katika kipindi cha hedhi kama MP, nimechinja kuku, siku zangu, shangazi kaja, simba kanguruma, nakimbiza mwenge, mvua zinanyesha, navuja, niko mwezini na mengineyo.

Page 83: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

79Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

SEHEMU YA TATU: USAFI WAKATI HEDHI

Jipange katika makundi sita na mfanye kazi ifuatayo

1. Kundi la Kwanza - Eleza maana ya usa� wa hedhi na umuhimu wa kuwa msa� wakati wa hedhi.

2. Kundi la Pili - Taja vifaa vinavyotumika kujiweka sa� wakati wa hedhi na namna vinavyotumika.

3. Kundi la Tatu - Jinsi gani unaweza kuvitunza vitambaa vilivyotumika wakati wa hedhi na kutupa pedi zilizotumika.

4. Kundi la Nne - Eleza madhara anayoweza kuyapata msichana asipojiweka sa� wakati wa hedhi.

5. Kundi la Tano - Eleza jinsi au namna ya kutuliza maumivu wakati wa hedhi.

6. Kundi la Sita - Orodhesha misemo/majina yanayotumika kumaanisha kuwa msichana yuko kwenye kipindi cha hedhi.

Zoezi la Kwanza

Page 84: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

80 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

SIKU YA TANO

SEHEMU YA NNE: JINSI YA KUTENGENEZA PEDI ZINAZOWEZA KUTUMIKA TENA

Lengo mahususi

Baada ya kipindi kila mwanafunzi aweze kutengeneza pedi yake.

Mwezeshaji

Waoneshe wanafunzi jinsi ya kutengeneza pedi zinazoweza kutumika tena kwa kutumia vifaa vinavyopatikana katika mazingira yanayowazunguka. Kisha waongoze kukaa kwenye makundi na kutengeneza hizo pedi huku ukiwasimamia na kuwaelekeza kwa kutumia mwongozo uliotolewa.

Page 85: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

81Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

SEHEMU YA NNE: JINSI YA KUTENGENEZA PEDI ZINAZOWEZA KUTUMIKA TENA

Pitia hatua za kutengeneza pedi kama zilivyoainishwa kwenye kitabu ili utengeneze pedi zinazoweza kutumika tena kwa kutumia vifaa vinavyopatikana katika mazingira yanayokuzunguka.

Jinsi ya kutengeneza pedi

1. Vifaa vinavyohitajika

2. Hatua za kutengeneza pedi zinazoweza kutumika tena

i. Andaa vifaa vyote vinavyohitajika.

ii. Kata jumla ya vitambaa vinne vya pamba katika umbo la pedi. iliyokunjuliwa kama inavyoonekana katika umbo namba (i).

Kitambaa sa� cha pamba; pamba; sindano na uzi; mkasi, mfuko wa nailoni, vishikizo vya kubana au vifungo

iii. Kata karatasi ya nailoni kama umbo namba (i) hapo juu.

iv. Shonea nailoni katikati ya vitambaa viwili vya pamba (hii itakuwa seti A) itakayozuia damu kupenya na kuchafua nguo.

v. Shona tena vitambaa vya pamba viwili na uviunganishe kwa pamoja. Hii itakuwa sehemu ya juu (seti B).

vi. Unganisha seti hizi mbili zilizoshonwa (seti A na seti B) na acha upande mmoja wazi kwa ajili ya kuingizia na kuondolea pamba.

vii. Weka (seti A) kuwa sehemu ya chini ya pedi na (seti B) kuwa sehemu ya juu ya pedi.

viii. Weka kishikizo kwenye bawa la upande mmoja wa pedi na tundu la kuwekea kishikizo kwenye upande mwingine wa bawa la pedi. Hii itasaidia pedi ikae vizuri.

ix. Pedi yako sasa ipo tayari kwa ajili ya matumizi. Sehemu iliyoachwa wazi baada ya kuungani-sha seti A na seti B inaweza kutumika kuwekea pamba au gozi ambayo itatupwa baada ya kutumika. Vitambaa vinavyobaki vifuliwe na kutunzwa kwa matumizi ya baadaye.

x. Sehemu ya wazi ya pedi itakusaidia kuweka pamba au gozi ya kutosha kuhimili wingi wa damu siku za hedhi nyingi. Siku za hedhi ya kawaida hasa hasa siku ya mwisho unaweza kuvaa bila kuweka au kujaza pamba katikati ya pedi.

xi. Pedi itakuwa kama ilivyo kwenye mchoro (ii).

Umbo (ii)

Umbo (i)

Page 86: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

82 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Umahiri: Wanafunzi waweze kubainisha vitendo mbalimbali vya ukatili wa kijinsia katika jamii na mbinu za kukabiliana navyo.

SIKU YA KWANZA

SEHEMU YA KWANZA: MAANA YA UKATILI WA KIJINSIA

Lengo mahususiBaada ya kipindi kila mwanafunzi aweze kueleza maana ya ukatili wa kijinsia.

MwezeshajiAnza kipindi kwa kuwaongoza wanafunzi kubungua bongo juu ya ukatili wa kijinsia. Andika majibu yote ubaoni kisha toa ufafanuzi sahihi kuhusu maana ya ukatili wa kijinsia. Baada ya hapo waongoze wa-nafunzi wakae katika vikundi na kujibu maswali yaliyobainishwa kisha wawasilishe kwa ajili ya mjadala.

• Sisitiza kuwa wavulana na wasichana wako tofauti kimaumbile, lakini wanapaswa kutendeana vyema, kuheshimiana na kuwa na huruma.

• Sisitiza kuwa siyo wanawawake tu wanaoweza kufanyiwa ukatili, wakati mwingine hata wanaume wanaweza kufanyiwa ukatili. Mfano mzazi kumpiga mtoto wake wa kiume kupita kiasi ni ukatili.

• Unashauriwa kualika wanafunzi wa kiume katika mada hii ili wajifunze kuhusu ukatili na usawa wa kijinsia. Kwani wanaume mara nyingi hufanya ukatili na kuona ni halali/haki yao. Wakati mwingine hufanya ukatili pasipo kujua kuwa wanafanya ukatili.

SEHEMU YA PILI: UKATILI DHIDI YA WASICHANA/WANAWAKE

Malengo MahususiBaada ya kipindi kila Mwanafunzi aweze:

• Kueleza aina mabalimbali za ukatili dhidi ya wasichana • Kueleza jinsi ya kujikinga na vitendo vya ukatili kwa wasichana

MwezeshajiWaelekeze wanafunzi wafanye igizo dhima linalohusu ukatili wanaopata wasichana. Baada ya igizo dhima ongoza majadiliano kwa kufuata maswali katika zoezi la wanafunzi.

Fanya majumuisho huku ukifafanua aina mbalimbali za ukatili dhidi ya washichana / wanawake kama zilivyobainishwa.

MADA YA SABA: UKATILI WA KIJINSIA

Page 87: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

83Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

SEHEMU YA KWANZA: MAANA YA UKATILI WA KIJINSIA

Ukatili wa Kijinsia ni vitendo ambavyo vinaweza kumsababishia mtu maumivu yawe kimwili, kiuchumi, kingono au kisaikolojia. Vitendo hivyo vinaweza kutendeka kati ya wanawake na wanaume au wanawake na wanawake au wanaume kwa wanaume lakini mara nyingi vitendo hivyo hutokea kati ya wanawake na wanaume kutokana na imani kwamba wanawake ni dhaifu na mahali pengine hutokana na mfumo dume unaosababishwa na mila na desturi.

Kaeni katika makundi ya watano watano na kujibu maswali yafuatayo:

1. Ni vitendo gani vya ukatili wa kijinsia vinavyofanyika katika jamii yenu?2. Nani wanaofanya vitendo hivyo vya ukatili wa kinjinsia? Una�kiri ni kwanini?

SEHEMU YA PILI: UKATILI DHIDI YA WASICHANA/WANAWAKE

(a) Fanyeni igizo dhima linalohusu ukatili wanaopata wasichana. (b) Jibu maswali yafautayo kutokana na igizo dhima.

1. Je, nini maana ya ukatili dhidi ya wasichana/wanawake?2. Ukatili wa kijinsia unamuathiri vipi mtoto wa kike?3. Je, wasichana watumie njia gani kukabiliana na ukatili wa kijinsia?4. Utamsaidiaje msichana mwenzao anayefanyiwa matendo ya ukatili?

Ukatili dhidi ya wasichana, ni vitendo vyovyote vinavyoweza kumsababishia msichana maumivu ya kimwili, kiuchumi, kingono au kisaikolojia, ambavyo vinaweza kufanyika katika ngazi ya familia au katika jamii.

Aina za UkatiliUkatili dhidi wanawake umegawanyika katika makundi makuu manne:

1. Ukatili wa Kimwili: Ni unaofanyika kudhuru mwili kama vile kupigwa, kuchomwa moto au kuchomwa na vitu vyenye ncha kali, kung’atwa, ku�nywa, na kutumikishwa kazi ngumu kupita kiasi na ukeketaji.

2. Ukatili wa Kiuchumi: Mfano mwanamke au msichana kushiriki katika shughuli za kuingiza kipato lakini kukosa uhuru wa kumiliki mapato, mwanamke kuwekewa pingamizi ya kumiliki vitega uchumi kama vile ardhi, nyumba na kadhalika.

MADA YA SABA: UKATILI WA KIJINSIA

Zoezi la Kwanza

Zoezi la Pili

Page 88: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

84 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

SIKU YA PILI

SEHEMU YA TATU: UBAKAJI NA RUSHWA YA NGONO

Mwezeshaji

Anza kipindi kwa maswali na majibu kujua maana ya ubakaji na rushwa ya ngono. Kisha waongoze wanafunzi wakae katika makundi ya watano watano na kusoma visa mafunzo pamoja na kujibu maswali.

Waongoze wanafunzi kujadili na kupata majibu ya maswali hapo juu. Ni muhimu kujadili kuwa ubakaji hautokei tu kwa wanawake bali wapo wanawake wanaobaka wanaume.

Ni muhimu kujadili kuwa ubakaji hauwezi kutokea kama kulikuwa na maridhiano kabla ya kufanya tendo la ngono. Kuwepo kwa maumivu wakati wa tendo hilo haimaanishi ubakaji umetendeka. Hata hivyo ni muhimu kuangalia suala la umri hata kama maridhiano yalikuwepo. Katika hadithi iliyoko kwenye kitabu cha mwanafunzi imeonyesha maridhiano na suala la umri halijatajwa. Endapo tendo kama hili limetokea kwa mtu aliye chini ya umri wa miaka 18 na mwingine ni mtu mzima, kitendo cha ubakaji kitakuwa kimetendeka.

Malengo mahususi

Baada ya kipindi kila mwanafunzi aweze:

• kueleza maana ya ubakaji na rushwa ya ngono. • kubainisha matendo mbalimbali ya ukatili wa kingono. • kutaja mbinu mbalimbali za kukabiliana na ukatili wa kingono katika maisha

kwa kutumia mifano halisi.

Page 89: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

85Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

3. Ukatili wa Kingono: Ni pale msichana anapolazimishwa kufanya matendo ya kingono bila ridhaa yake, kama vile kubakwa, kutumikishwa kingono, kushikwa shikwa, kukonyezwa, na kuombwa rushwa ya ngono.

4. Ukatili wa Kisaikolojia: Ni kama vile kusimangwa, kutukanwa, kuchekwa, kuzomewa. Kwa ujumla ukatili wa aina zote unaweza kusababisha mtu kuathirika kisaikolojia.

SEHEMU YA TATU: UBAKAJI NA RUSHWA YA NGONO

Soma hadithi zifuatazo na jibu maswali yaliyoainishwa.

Hadithi ya kwanza

Sara na Juma wapo katika sherehe ya mahafali ya kuhitimu darasa la saba. Sara ni mrembo sana. Wanaonekana wana ukaribu na wanafurahi kuongea pamoja. Wanakwenda mahali pa faragha kwa mazungumzo. Baada ya muda Juma anaonekana kuchoshwa na mazungumzo ya Sara na anaamua kumpotezea, hataki wazoeane zaidi. Hata hivyo, Sara anaonekana amekunywa pombe na amelewa sana, anaanza kumtaka Juma kimapenzi. Juma hapendi na anamsihi Sara mara kadhaa kuwa yeye hayupo tayari kufanya ngono. Sara anaonekana haelewi na anaendelea kumshikashika Juma mpaka wanadondoka chini na hatimaye wanafanya ngono. Kwa kuwa Sara alikuwa amelewa chakari, kesho yake hakuweza kukumbuka lile tukio hata kidogo.

Maswali

• Je, Sara alibakwa? • Nani aliyembaka mwenzake? • Je, ungekuwa wewe ndio Juma ungefanyaje katika mazingira hayo?

Hadithi ya pili

Mwajabu na Sali wamekubaliana kukutana mahali fulani ili waweze kufanya ngono. Wote wana hamu ya kufanya tendo hilo kwa mara ya kwanza. Walipokutana na kuanza kufanya ngono, Mwajabu aliona kama hafurahii na alisikia maumivu makali sana, lakini Sali aliendelea kufanya na kufurahi. Mwajabu alitamani kumwambia Sali aache kwani alikuwa anaumia lakini akaogopa Sali angejisikia vibaya na kukasirika na huenda mahusiano yao yangevunjika.

Maswali

• Je, una�kiri Mwajabu alibakwa? • Je, umejifunza nini kutokana na ura�ki wa Mwajabu na Sali?

Zoezi la Kwanza

Page 90: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

86 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Sisitiza kwamba rushwa ya ngono mara nyingi hutokea pale mtu anapolazimishwa au kulazimisha mtu kufanya ngono ili kupata jambo fulani. Kwa mfano, mwalimu kumtaka mwanafunzi kingono ili ampe alama za juu, au mwajiri kumtaka msichana kingono ili ampe ajira. Mara nyingi anayeomba rushwa ya ngono anakuwa ni mtu mwenye mamlaka zaidi kuliko anayeombwa. Pia sisitiza mambo yaliyoorodheshwa katika majedwali kuhusu ubakaji na ukatili wa kijinsia.

Page 91: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

87Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Hadithi ya Tatu

Bitya ni binti mrembo mwenye umri wa miaka 15. Alipokuwa mdogo aliishi na mjomba wake ambaye alikuwa anampenda sana. Mara nyingi alipenda kumletea zawadi na kumkumbatia ili kuonyesha upendo.Mwishoni mwa wiki iliyopita mjomba wake alikuja kwenye mazishi ya ndugu yake. Siku hiyo kila mtu alikuwa anakunywa pombe. Usiku Bitya alipokuwa anatoka chooni alimkuta mjomba wake anamsubiri nje. Gha�a mjomba alimshika mkono na kumuangusha chini na kumbaka. Bitya alipata maumivu makali sana lakini alipojaribu kulia mjomba alimziba mdomo. Baadaye mjomba alimuwambia kuwa ilikuwa ni kosa lake kwani alivaa sidiria ambayo ilimfanya apate ashki.

Bitya alijisikia vibaya sana toka siku ile. Lakini anaogopa sana kuwaeleza wazazi wake, kwani anaogopa wazazi watakasirika kwa vile mjomba anawasaidia kupata chakula na fedha kwa matumizi mbalimbali. Aidha, Bitya anajiuliza atafanya nini iwapo mjomba wake atarudia tena.

Maswali

• Je, una�kiri Bitya alitakiwa kufanya nini? • Je, kubaka au kubakwa ni jambo linalotokea katika jamii yenu? • Je, wote wanaobaka ni watu wa mbali au ni ndugu? • Je, mwanamke au msichana aliyevaa nguo zinazochochea ashki akibakwa anastahili

kulaumiwa?

Hadithi ya Nne

Sheri ni msichana mwenye umri wa miaka 15 anayesoma Kidato cha Pili. Mwalimu wake wa somo la Hisabati amejitolea kufundisha vipindi vya ziada ili kukamilisha mada kabla ya mtihani.

Siku moja baada ya kipindi mwalimu alimwambia Sheri abaki ili amulekeze vizuri swali alilolikosea. Wenzake walipoondoka mwalimu alianza kumshikashika matiti na sehemu nyingine za mwili, huku akimwambia kwamba anampenda na alimtaka wafanye ngono, kwa kumuahidi kuwa atamsaidia afaulu somo la Hisabati. Sheri alijisikia vibaya lakini akaogopa kumwambia mwalimu aache kumshikashika. Hata hivyo, siku ile Sheri alifanikiwa kuondoka bila kufanya ngono na mwalimu.

Sasa hivi Sheri hahudhurii vipindi vya Hisabati kwa sababu anaogopa kuwa mwalimu anaweza kuendelea kumlazimisha kufanya ngono.

Maswali

• Je, jambo hili limewahi kumtokea yeyote unayemfahamu? • Je, jambo hili huwapata wasichana tu au na wavulana? • Je, kilitokea nini kwa mwalimu? • Je, nini maana ya rushwa ya ngono? • Je, ungekuwa wewe ni Sheri ungefanya nini baada ya mambo yaliyotokea siku ya kwanza? • Je, ungemshauri Sheri afanye nini iwapo mwalimu angerudia tena jambo hili?

Page 92: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

88 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Waongoze wanafunzi kusoma na kutilia mkazo juu ya:

1. Mambo muhimu ya kufahamu kuhusu ubakaji. 2. Jinsi ya kufanya endapo utafanyiwa ukatili wa kijinsia.

Page 93: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

89Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Mambo muhimu ya kufahamu kuhusu ubakaji.

• Ubakaji ni kulazimishwa kufanya ngono au vitendo vya kingono bila ridhaa ya mhusika. Kitendo hiki huweza kutokea kwa wanawake au wanaume. Lakini mara nyingi wanawake ndio wanaobakwa.

• Mwanamke akilazimishwa kufanya mapenzi na mpenzi wake au mume wake pia ni ubaka-ji. Wanaume wengine hutumia madawa ya kulevya au vipigo kuwatishia au kuwaambia wanawake wanaowabaka kuwa ni haki kuwatendea hivyo.

• Wengine huingiza vitu ukeni kwa msichana au kwenye haja kubwa ya mvulana au msichana nao pia ni ubakaji.

• Kubakwa sio lazima tu kuingiliwa kimwili ila mtu anapokulazimisha kukushika sehemu zako za mwili au kukubusu ni ubakaji.

• Muda mwingine ubakaji hautokei kwa mtu kutumia nguvu tu, ila hata kudanganywa, na kurubuniwa na kujikuta umefanya ngono bila ridhaa ni ubakaji.

• Mazingira yanaweza kupelekea msichana kubakwa, mfano kupita vichochoroni, matumizi ya pombe na madawa ya kulevya, kuzurura, tabia na mavazi.

• Mara nyingi jamii au wasichana wana�kiri wanapobakwa ni makosa yao na kujilaumu kuwa wao ndio wasababishi, kwa hiyo wanaamua kukaa kimya wakati si sahihi.

• Ngono bila ridhaa ni ubakaji hata kama msichana kalala, kalewa au anaogopa kujitetea na kukataa.

Je, nifanyeje kama nimefanyiwa ukatili wa kijinsia au nimebakwa?

Endapo msichana/mvulana amefanyiwa vitendo vya ukatili atoe taarifa kwa wazazi/walezi, walimu, serikali ya mtaa, polisi au kwa mtu anayemuamini. Kwa matukio ya ubakaji muhanga afanye yafuatayo:

1. Usioge wala usifue nguo zako za ndani mpaka daktari akupime.

2. Nenda hospitali au kituo cha karibu cha afya ufanyiwe uchunguzi wa kitaalamu na kupewa matibabu kama umeumia au umepata mimba au maambukizi ya magonjwa ya ngono. Mfano unaweza kupewa kinga ya ujauzito (Emergency Contraceptives) inayofanya kazi ndani ya masaa 72 na kinga ya VVU (Post Exposure Prophylaxis).

3. Ripoti kituo cha Polisi kilicho karibu nawe utapewa Fomu ya Polisi namba 3 (PF3) utakayopeleka hospitali ili upate matibabu.

4. Hakikisha taarifa zako zinarekodiwa kituo cha polisi ikiwa ni pamoja na mashahidi kama wapo.

5. Mtambue mhalifu aliyekubaka na hudhuria mahakamani.

Page 94: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

90 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

SIKU YA TATU

SEHEMU YA NNE: MAZINGIRA HATARISHI YANAYOPELEKEA KUFANYIWA VITENDO VYA UKATILI

Lengo mahususiBaada ya kipindi kila mwanafunzi aweze kubainisha mazingira hatarishi yanayoweza kumsababishia kufanyiwa vitendo vya ukatili kama ubakaji.

Mwezeshaji Waelekeze wanafunzi kufanya kazi hii nyumbani na kisha kurudi na majibu kwa ajili ya kuwasilisha siku inayofuata.

Baada ya wanafunzi kuwasilisha majibu yao ongeza baadhi ya njia zakuepuka mazingira hatarishi kama zilizorodheshwa endapo zitakuwa hazikutajwa:

• Ondoka mahali ambapo hujisikii salama, hata kama upo na mtu unayemfahamu. • Usipite vichochoroni. • Usitembee sehemu za giza peke yako, tembea katika makundi. • Usirubuniwe. • Chukua tahadhari na mavazi yako kulingana na unapopita. • Usipande lifti au kupokea zawadi kwa watu usiowajua na usiowaamini. • Epuka ulevi.

SIKU YA NNE

SEHEMU YA TANO: NDOA NA MIMBA ZA UTOTONI

Malengo Mahususi Baada ya kipindi kila mwanafunzi aweze.

• kueleza maana ya ndoa za utotoni. • kubainisha madhara ya ndoa utotoni.

Mwezeshaji Anza kipindi kwa kuwaelekeza wanafunzi kuwa kila mmoja achukue karatasi na kalamu, a�kiri kwa dakika chache na ajibu maswali katika zoezi la kwanza. Baada ya kumaliza waruhusu wasome majibu yao na ongoza mjadala juu ya majibu waliyoyatoa na fanya majumuisho.

Waongoze wanafunzi wakae katika makundi ya watano watano na kusoma kisa mafunzo na kujadili maswali yatokanayo na kisa hicho.

Page 95: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

91Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Jibu maswali yafuatayo ukiwa nyumbani na wasilisha majibu siku inayofuata.

1. Orodhesha na eleza mazingira hatarishi yanayoweza kusababisha ubakaji.2. Andika njia zisizopungua sita za kujikinga na ukatili na ubakaji.

SEHEMU YA TANO: NDOA NA MIMBA ZA UTOTONI

Chukua kalamu na karatasi, �kiri kwa muda kisha jibu maswali yafuatayo:

• Je, ungependa kuolewa? Lini? Na ungependa kuolewa na mwanaume wa namna gani/mwenye sifa gani?

• Je, utapenda kuja kuwa na watoto? Lini? na ungependa uwe na watoto wangapi? • Je, utajilinda vipi usipate ujauzito kabla haujawa tayari?

Muhimu

Ni vizuri kuolewa baada ya kumaliza masomo na kuanza kujitegemea. Hii itamsaidia binti kuepuka manyanyaso au kuwa tegemezi. Ni vizuri wasichana wasubiri hadi miili yao itakapopevuka na akili kukomaa ndipo waoelewe.

Kaeni katika makundi ya watano watano , kisha msome hadithi ifuatayo na kujadili maswali yatokanayo na hadithi hiyo.

Hadithi

Mimi ni kijana na ninampenda sana msichana ninayesoma naye. Jina lake anaitwa P. Tunafanya bidii katika masomo yetu na tumepanga tukimaliza chuo tuoane. Tatizo ni kwamba wazazi wa binti wamemtafutia mchumba ambaye ni mzee mwenye pesa. Ingawa amewaeleza kwamba atapenda kuolewa na mimi atakapomaliza chuo, wazazi wake wamekataa na kumwambia ni lazima afanye kama wanavyotaka wao, iwapo ataendelea kukataa watamfukuza nyumbani na kusema si mtoto wao. Wazazi wa P tayari wamepokea mahari, sasa hivi wanazungumzia mipango ya ndoa.

Zoezi la Kwanza

Zoezi la Pili

SEHEMU YA NNE: MAZINGIRA HATARISHI YANAYOPELEKEA KUFANYIWA VITENDO VYA UKATILI

Zoezi la Nyumbani

Page 96: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

92 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Chagua wanafunzi wawili kuandaa na kuonyesha igizo dhima lenye maudhui yafuatayo hapo chini. Waeleze wanafunzi hao kuwa wanaweza kuongeza wenzao katika igizo hilo wanapohitajika. Aidha watumie ubunifu wao kuonyesha madhara ya ndoa za utotoni. Baada ya igizo ongoza mjadala kutokana na igizo hilo kwa kutumia maswali yaliopo katika kitabu cha mwanafunzi na fanya hitimisho.

Page 97: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

93Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Maswali

1. Umejifunza nini kutokana na hadithi hii?2. Kwa nini baadhi ya wasichana wanaolewa mapema?3. Je, ni madhara gani anaweza kupata msichana akiolewa mapema?4. Je, katika jamii yenu kuna ndoa zinazofanana na hii ya P?5. Je, utajisikiaje endapo wazazi watakuchagulia mchumba?6. Nani anawajibika katika kuzuia ndoa za utotoni?7. Je, ndoa za utotoni zinaweza kuzuilika kwa njia zipi?

Andaa igizo dhima lenye maudhui yafuatayo na kulionesha mbele ya darasa. Wasichana wawili wamekutana, mmoja alikatisha masomo akaolewa akiwa na umri wa miaka 13, na mwingine bado yupo shule na amevaa sare za shule na amebeba mkoba wa madaftari. Aliyeolewa amebeba mtoto mmoja mkononi ambaye ni mgonjwa na mwingine amemshika mkono huku akililia kubebwa. Wasichana hawa wanazungumza kuhusu maisha yao kwa dakika chache.

Maswali

1. Je, umejifunza nini kutokana na igizo hili?2. Je, jambo hili lipo katika jamii yenu?3. Je, nini kifanyike ili kuepuka tatizo hili?

Zoezi la Tatu

Page 98: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

94 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

SIKU YA TANO

SEHEMU YA SITA: MIMBA ZA UTOTONI NA MADHARA YA MIMBA ZA UTOTONI

Malengo mahususiBaada ya kipindi kila mwanafunzi aweze:

• Kueleza maana ya mimba za utotoni • Kubainisha madhara ya mimba za utotoni

Mwezeshaji Waongoze wanafunzi wakae katika makundi ya wawili wawili na wajadiliane maana ya mimba za utotoni na kuwasilisha majibu yao, kisha hitimisha kwa kueleza kuwa:

Mimba za utotoni ni wakati ambao msichana anapata mimba kabla ya umri wa miaka 18. Mara nyingi kuna matokeo mabaya ya kimwili na kiakili kwa mama na mtoto wakati wa ujauzito wa mapema, ambayo yanaweza kuepukwa kama msichana atasubiri kubeba ujauzito mpaka atakapokuwa mtu mzima. Wazazi wenye umri mdogo hawajakua kihisia au kiutulivu kama wazazi wenye umri mkubwa, hivyo husababisha unyanyasaji wa watoto na kutelekezwa na hata kutupwa. Kuna uwezekano mkubwa wa matatizo hasa kwa mama, mtoto, na jamii.

Andaa vikaratasi vyenye sentensi zenye ukweli na zenye uongo kuhusu kupata mimba vikunje na ita mwanafunzi mmoja baada ya mwingine asome sentensi kwa sauti kisha wanaokubaliana na sentensi hiyo waende kona ya darasa iliyoandikwa “kweli” na wasiokubaliana waende kona iliyoandikwa “si kweli”, chagua mwanafunzi mmoja kutoka kila kundi afafanue majibu yao.

“Msichana hawezi kupata mimba kama”

1. Bado hajaanza kupata hedhi(Si kweli, kama msichana amesha�kia umri wa kubalehe mayai yanaweza kuwa yapo tayari kwa kutunga mimba kabla hajapata hedhi yake ya kwanza).2. Siku zake za hedhi hazina mpangilio maalumu(Si kweli, kwani kwa wasichana ambao wanaanza kupata hedhi bado siku zao huwa hazina mpangilio, hivyo mayai yanapevuka kwa muda tofauti).3. Akifanya ngono akiwa amesimama(Si kweli, msichana anaweza kupata mimba akifanya ngono kwa namna yeyote).4. Akitumia njia sahihi za kujikinga na ujauzito(Kweli, kutumia njia sahihi za kujikinga na ujauzito kama kuacha ngono).5. Mwanaume atatoa uume kabla ya kukojoa manii(Si kweli kwani zipo mbegu zinaweza kutangulia na majimaji ya mwanzo).6. Ataosha uke wake mara tu baada ya kufanya ngono(Si kweli, mbegu ya kiume husa�ri kwa kasi sana kwa hiyo sio rahisi kuziosha zitoke nje ya uke).

Endeleza mjadala zaidi kuhusu mawazo potofu na ukweli kuhusu utungaji wa mimba katika jamii yao na mwisho fanya majumuisho.

Unaweza kumualika mtaalamu/ daktari katika mada hii kwa ufafanuzi zaidi.

Hitimisha kwa kusisitiza umuhimu wa kuepuka kufanya ngono kabla ya wakati.

Page 99: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

95Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

SEHEMU YA SITA: MIMBA ZA UTOTONI NA MADHARA YA MIMBA ZA UTOTONI

Jadilianeni wawili wawili maana ya mimba za utotoni na kuwasilisha majibu yenu.

Mchezo wa kweli au si kweli Soma sentensi zifuatazo na kisha sema kama ni kweli au si kweli kuhusu kupata mimba. Toa maelezo ya kuthibitisha jibu lako.

‘’Msichana hawezi kupata mimba kama’’

1. Bado hajaanza kupata hedhi2. Siku zake za hedhi hazina mpangilio maalumu3. Akifanya ngono akiwa amesimama4. Akitumia njia sahihi za kujikinga na ujauzito5. Mwanaume atatoa uume kabla ya kukojoa manii6. Ataosha uke wake mara tu baada ya kufanya ngono

Zoezi la Nne

Page 100: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

96 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Mwezeshaji

Waongoze wanafunzi kuelezea madhara ya mimba za utotoni kwa kutumia njia ya Fikiri Jozisha Shirikisha (Think Pair Share). Baada ya wanafunzi kuwasilisha, hitimisha kwa kufafanua zaidi madhara ya mimba za utotoni kama yalivyoainishwa katika jedwali.

Waongoze wakae wawili wawili na kujadili madhara ya mimba za utotoni kisha wawasilishe majibu yao.

Page 101: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

97Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Ukweli kuhusu utungaji Mimba: Mimba hutunga pale mvulana aliyebalehe akifanya ngono na msichana aliyevunja ungo. Mvulana hutoa majimaji ambayo yamebeba mbegu ya kiume. Mbegu hiyo ikikutana na yai lililopevuka hutungisha mimba. ‘

Soma hadithi ifuatayo na jibu maswaliMimi ni msichana mwenye umri wa miaka 16, bado ni mwanafunzi na nimegundua nina ujauzito. Nimefanya ngono na mpenzi wangu mara moja tu na nikapata mimba, nilipomueleza mpenzi wangu huyo alinijibu kuwa atahakikisha vipi kama ni yeye anayehusika. Hataki hata kuzungumza na mimi, nikiwaeleza wazazi wangu watanifukuza. Mama yangu anajitahidi sana kunilipia ada ya shule, kwa hiyo atakasirika sana kwa hili nililolifanya. Kwa kweli mimba hii siitaki na wala sitaki nikatishe masomo yangu, nimefadhaika sana, lakini siwezi kumueleza mtu yeyote. Suluhisho pekee ninalo�kiria ni kutoa hii mimba au kujiua lakini sina pesa za kulipa gharama za utoaji wa mimba.

Maswali1. Je, ni ushauri gani utatoa kwa binti huyu?2. Kwa nini vijana hufanya ngono? 3. Binti huyu ana�kiria kutoa mimba, je una�kiri kuna hatari gani za kutoa mimba?4. Kwa nini una�kiri kijana alikata mawasiliano? Unadhani atajisikiaje baada ya binti kutoa ujauzito

au kujiua? Je, wazazi wa hawa vijana wanaweza kuchukua hatua gani?

Kaeni wawili wawili na kujadili madhara ya mimba za utotoni kisha muwasilishe majibu yenu.

• Anaweza kupata �stula (kutokwa na mkojo bila kujizuia ambayo husababishwa na shimo ambalo hutokea katikati ya kibofu cha mkojo na uke au katikati ya njia ya haja kubwa na uke kwa mwanamke ambaye amejifungua kwa shida. Kuzaa mapema kabla ya umri kumekuwa chanzo kikubwa cha kutokea kwa �stula. Hilo linatokana na kutokupevuka kwa njia ya uzazi pamoja na nyonga)

• Kushindwa kuendelea na masomo • Kulazimishwa kuolewa • Kupata idadi kubwa ya watoto asiomudu kuwahudumia • Kuongezeka kwa watoto wa mitaani (wasiohudumiwa) • Kupata matatizo ya viungo vya uzazi, kama vile kutokwa damu nyingi na kuchanika sana

wakati wa kujifungua • Kupata uchungu wa muda mrefu au kushindwa kujifungua kutokana na viungo vya uzazi/

nyonga kutokukomaa • Kupata kifafa cha mimba ambacho huweza kusababisha kifo cha mama • Kuzaa mtoto njiti, mlemavu wa kimwili na akili na hatimaye kifo cha mtoto • Kukosa haki za msingi kama mtoto mfano, kucheza • Kujiingiza katika mazingira hatarishi kama vile ukahaba ili kupata mahitaji ya kuweza kulea

mtoto • Kupata maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama vile UKIMWI.

Zoezi la Tano

Zoezi la Sita

Page 102: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

98 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Umahiri: Wanafunzi waweze kuepuka kufanya ngono na kujikinga na maambukizi ya magonjwa ya ngono.

SIKU YA KWANZA

SEHEMU YA KWANZA: MAGONJWA YA NGONO

Lengo mahususi

Baada ya kipindi kila mwanafunzi aweze:

• Kueleza maana ya magonjwa ya ngono • Kutaja magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya ngono • Kuelezea visababishi, njia za maambukizi, dalili, namna ya kujikinga, tiba ya magonjwa ya

ngono na athari zake

Mwezeshaji

Kwa kutumia njia ya maswali na majibu awaongoze wanafunzi waeleze maana ya magonjwa ya ngono na kutaja mifano ya magonjwa hayo. Kisha fanya majumuisho ya maana na mifano ya magonjwa ya ngono kama ilivyoelezewa hapo chini.

Maana ya magonjwa ya ngono

Magonjwa ya ngono ni magonjwa yanayoenezwa kwa njia ya kujamiiana. Magonjwa hayo huenezwa na bakteria, virusi au fangasi. Magonjwa mengi ya ngono yanatibika. Baadhi ya magonjwa ya ngono ni kisonono, kaswende, trichomonasi, malengelenge ya sehemu za siri, clamidia, utando mweupe, UKIMWI (Upungufu wa Kinga Mwilini), pangusa na mandeletele. UKIMWI unaambukizwa na VVU – Virusi vya UKIMWI (VVU) na mpaka sasa hauna tiba. Magonjwa mengi ya ngono dalili zake hazi-onekani kwa urahisi na kama yasipotibika kwa uangalifu yanaweza kuleta madhara makubwa. Dalili za magonjwa haya huonekana zaidi kwa haraka kwa wanaume.

Waongoze wanafunzi kukaa katika makundi ya watano watano, kulingana na magonjwa waliyoyataja. Waainishe visababishi, njia za maambukizi, dalili, namna ya kujikinga, tiba na athari za magonjwa hayo. Kisha waongoze wanafunzi wabandike kazi zao ukutani kwa makundi ili kuwawezesha wengine kuzipitia na kufanya maboresho pale patakapohitajika.

Fanya majumuisho kwa kusisitiza visababishi, njia za maambukizi, dalili, namna ya kujikinga, tiba, athari na jinsi ya kutibu magonjwa ya ngono kama ilivyoainishwa kwenye kiambatisho “A”.

MADA YA NANE: MAAMBUKIZI YA MAGONJWA YA NGONO NA KUACHA KUFANYA NGONO

Page 103: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

99Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

SEHEMU YA KWANZA: MAGONJWA YA NGONO

Katika makundi yenu eleza maana ya magonjwa ya ngono na taja mifano ya magonjwa hayo.

Kaeni katika makundi ya watano watano kulingana na idadi ya magonjwa mliyoyataja. Kisha ainisha visababishi, njia za maambukizi, dalili, namna ya kujikinga, tiba na athari za magonjwa hayo kwa kujaza jedwali lifuatalo kulingana na ugonjwa mnaoufanyia kazi.

MADA YA NANE: MAAMBUKIZI YA MAGONJWA YA NGONO NA KUACHA KUFANYA NGONO

Aina ya ugonjwa wa ngono

Visababishi Njia za maambukizi

Dalili Namna ya kujikinga

Tiba Athari

Bandikeni kazi zenu za makundi ukutani.

Tembeleeni kazi nyingine za vikundi zilizobandikwa ukutani mzisome na kuziboresha pale patakapohitajika.

Soma sentensi zifuatazo na jibu kama sentensi hizo ni “Kweli” au “Si Kweli”.

Zoezi la Kwanza

Zoezi la Pili

Page 104: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

100 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Mwezeshaji Wasomee wanafunzi sentensi zilizopo kwenye kitabu cha mwanafunzi na wajibu kama sentensi hizo ni Kweli au Si Kweli, kisha hitimisha kwa kutowa ufafanuzi wa majibu sahihi kama yalivyoainishwa. 1. Kweli, 2. Kweli, 3. Kweli. 4. Si kweli, 5. Kweli, 6. Si kweli, 7. Kweli.

SIKU YA PILI

SEHEMU YA PILI: KUDHIBITI MIHEMKO NA KUEPUKA NGONO

Lengo mahususiBaada ya kipindi kila mwanafunzi aweze:

• Kueleza maana ya mihemko • Kueleza visababishi vinavyochochea mihemko • Kubainisha mbinu mbalimbali za kudhibiti mihemko ya kingono na kuepuka ngono

Zoezi la kwanza

MwezeshajiWaongoze wanafunzi kueleza maana ya mihemko ya kingono kwa kutumia njia ya maswali na majibu.Fanya majumuisho kwa kueleza maana ya mihemko ya ngono.

Waongoze wanafunzi kusoma kisa mafunzo na kujibu maswali yanayofuata. Baada ya kusikia majibu ya wanafunzi kutokana na maswali ya Kisa Mafunzo fanya majumuisho na kuongezea hoja zinazokosekana kutokana na maelezo yafuatayo:

1. Msukumo rika2. Kutokujishughulisha/kukaa bila kazi yoyote3. Tamaa za kimwili zitokanazo na mabadiliko ya

kibaiolojia ya mwili4. Mtindo wa maisha, mfano wanaopenda ku-

kaa vijiweni, vigodoro, kwenda disko, sinema, ufukweni, kutumia madawa ya kulevya na pombe

5. Kuangalia �lamu za ngono6. Kuwa na mahusiano ya kingono7. Kuwa mpweke

Pamoja na vichochezi hivyo hapo juu wasichana wengine hawafanyi ngono kabla ya wakati kwasababu zifuatazo:

1. Kuogopa kupata mimba2. Kuogopa magonjwa ya ngono3. Malezi – jinsi walivyolelewa4. Hofu ya Mungu/Dini5. Kutokuwa tayari6. Kutokupata mtu sahihi7. Kusubiri hadi atakapoolewa (kutunza bikira)8. Kuheshimu matarajio ya familia9. Kuzingatia ku�kia malengo yao waliyojiwekea

Visababishi vinavyochochea mihemko ya kingono

Page 105: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

101Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

SEHEMU YA PILI: KUDHIBITI MIHEMKO NA KUEPUKA NGONO

Visababishi vinavyochochea mihemko ya kingono.

Soma hadithi hii na kisha jibu maswali yanayofuata:

Hadithi

“Kama unampenda ni lazima umthibitishie. Unatakiwa umpe kila kitu anachohitaji”. Umewahi kusikia kauli hii? Sio wewe tu. Baada ya Chawela, miaka 14, kuwa na ra�ki wa kiume kwa miezi 6, ra�ki zake walianza kumshawishi sana afanye ngono na huyo mpenzi wake. Waliendelea kumshinikiza zaidi na zaidi: “Unatakiwa umpe anachotaka, usipofanya hivyo utamkosa.” Miezi michache baadaye uvumilivu wake ulizidiwa nguvu, akasalimu amri, akafanya ngono na mpenzi yule.

Baada ya kufanya hivyo, Chawela hakujisikia vizuri. “Nilijisikia kama niliyerukia jambo ambalo sote wawili hatukuwa tayari”, alisema, “Nadhani nilifanya mapenzi kwa mara ya kwanza kwasababu zisizo sahihi”.’

Maswali

1. Je, Wasichana kama Chawela wapo katika jamii yako?2. Je, Una�kiri ni sababu zipi zilimchochea Chawela kufanya ngono?3. Je, Ungekuwa wewe ni Chawela ungefanyaje?4. Je, Una�kiri ni kwanini wasichana wengine hupenda kufanya ngono kabla ya wakati?5. Je, Ni kwanini wengine hawafanyi ngono kabla ya wakati?

Jibu weka alama ya akatika sehemu inayoonesha Kweli au Si Kweli katika sentensi zifuatazo:

Na. Kweli Si Kweli Maelezo

1.Watu wengi walioathirika kwa magonjwa ya ngono mara nyingi hawajui kama wameathirika

2.Watu wanaofanya ngono katika umri mdogo mara nyingi huathirika na magonjwa ya ngono

3.Njia pekee na yenye hakika ya kujua kuwa umeathirika na magonjwa ya ngono ni kupimwa hospitalini na daktari

4. Ukidharau magonjwa ya ngono na usipoyatibu yatapona yenyewe

5. Ni rahisi kuathirika na zaidi ya ugonjwa mmoja wa ngono

6. Mafua ni dalili mojawapo ya magonjwa ya ngono

7. Njia ya kuepuka magonjwa ya ngono kwa asilimia mia moja ni kuacha ngono

Zoezi la Tatu

Page 106: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

102 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Waelekeze wanafunzi kazi ya nyumbani ya kuorodhesha na kuelezea mbinu za kuepuka mihemko ya kingono na ngono kabla ya wakati. Kazi hii itawasilishwa darasani siku ya nne.

SIKU YA NNE

SEHEMU YA TATU: MBINU ZA KUEPUKA MIHEMKO YA KINGONO NA NGONO

Mwezeshaji

Waongoze wanafunzi wakae katika makundi ya watano watano na kulinganisha kazi zao za jana na ku-pata kazi moja ya kikundi. Kisha waelekeze waziandike kwenye karatasi halafu wazibandike ukutani. Waelekeze wanafunzi kupitia na kusoma kazi za vikundi vingine na kuongezea hoja kama itabidi. Kisha toa majumuisho ya mada kutokana na maelezo yafuatayo:Mbinu za kuepuka mihemko ya kingono na kuepuka ngono

• Shiriki katika ibada mara kwa mara na uzingatie maadili ya dini yako • Jipangie ratiba utakayoifuata kwa siku/wiki kama somo la kuweka malengo lilivyo elekeza

(usikae bure bila kazi yoyote) • Epuka mara�ki wenye tabia mbaya • Epuka kuangalia picha zinazochochea ngono kama vile picha za kwenye mitandao ya

jamii, hadithi za kingono, sinema na magazeti • Shiriki kwenye michezo / mazoezi ya viungo • Jiepushe kuwa mpweke kwa kushirikiana na mara�ki wenye mienendo mizuri • Soma vitabu mbalimbali • Shiriki kwenye midahalo ya vijana inayoelimisha vijana • Omba ushauri kwa wazazi, walezi, walimu na ndugu waliokuzidi umri

Kwa kutumia mbinu ya Fikirisha Jozisha Shirikisha waongoze wanafunzi kujadili faida za kuepuka mihemko ya kingono na ngono. Kisha waulize kila jozi kutoa mrejesho wa faida walizoandika.Kisha toa majumuisho ya faida za kuepuka mihemko ya kingono na ngono kutokana na maelezo yafuatayo:

Faida za kuepuka mihemko ya kingono na ngono.

• Kuepuka mimba za utotoni/zisizotarajiwa • Kuepuka magonjwa ya ngono • Kuwa mfano wa kuigwa katika jamii • Kutimiza malengo ya maisha uliyojiwekea

• Kutimiza matarajio ya familia • Kuepuka migogoro na wazazi na jamii • Kuishi maisha yenye furaha • Kumpata mwenzi sahihi kwa wakati sahihi

SIKU YA TATU

MwezeshajiWaelekeze wanafunzi kazi ya nyumbani ya siku inayofuata kama ilivyoelezwa siku ya tatu.

Page 107: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

103Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Orodhesha na elezea mbinu za kuepuka mihemko ya kingono na ngono kabla ya wakati. Kisha uwasilishe darasani siku ya nne.

SEHEMU YA TATU: MBINU ZA KUEPUKA MIHEMKO YA KINGONO NA NGONO

Kaeni katika makundi ya watano watano na mlinganishe kazi zenu za jana ili kupata kazi moja ya kikundi. Mziandike kazi zenu kwenye karatasi halafu mzibandike ukutani. Mpitie na msome kazi za vikundi vingine na muongeze hoja kama itabidi.

Faida za kuepuka mihemko ya kingono na ngono

Fikiri peke yako, kisha jadili na mwenzako faida za kuepuka mihemko ya kingono na ngono. Kisha mtoe mrejesho na kushirikishana faida mlizoandika.

Zoezi la Kwanza

Zoezi la Pili

Zoezi la Nyumbani

Page 108: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

104 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Mwezeshaji1. Waulize wanafunzi maana ya tabia hatarishi, kisha andika majibu yote ubaoni na mwisho

hitimisha kwa kueleza maana halisi ya tabia hatarishi.

2. Waongoze wasimame kwenye mduara, hakikisha kuwa kila mmoja anaweza kumuona mwen-zake vizuri. Kila mwanafunzi ataje tabia hatarishi moja anayoifahamu na kisha mwezeshaji hitimisha kwa kuongezea tabia hatarishi zingine ambazo hazijatajwa.

3. Waongoze wanafunzi kupanga na kufanya igizo dhima linaloonesha tabia hatarishi zaidi ya tatu na waoneshe madhara yake. Wasisitize kufuatilia igizo kwa makini.

Baada ya igizo ongoza mjadala kwa kuuliza maswali yafuatayo:

1. Tabia zilizooneshwa katika igizo zipo katika mazingira yenu?2. Ni mambo gani yanayoweza kuchochea kijana kuwa na tabia hatarishi?3. Nini madhara ya tabia hizo?4. Una ushauri gani kwa vijana wenye tabia kama hizo ili waweze kuziepuka?

Baada ya mjadala, fanya majumuisho na kuhitimisha.

Tabia hatarishi Tabia hatarishi ni hali ya mwenendo anaokuwa nao mtu ambao unaweza kumsababisha akapata matatizo. Baadhi ya tabia hatarishi ni kama vile: Matumizi ya madawa ya kulevya, ulevi wa pombe, kufanya ngono, kukaa kwenye magenge/vijiweni.

Mambo yanayochochea tabia hatarishi ni pamoja na:

• Msukumowakundirika• Uelewamdogojuuyatabiahatarishinamadharayake• Tamaa• Ugumuwamaisha

Madhara ya tabia hatarishi ni pamoja na:

• Kupatamaambukiziyamagonjwayangono• Kupotezamalengoyamaisha• Kupotezanguvukazi

SIKU YA TANO

SEHEMU YA NNE: TABIA HATARISHIMalengo mahususiBaada ya kipindi kila mwanafunzi aweze:

• kueleza maana ya tabia hatarishi • kubainisha tabia hatarishi na madhara yake • kueleza visababishi vya tabia hatarishi • kueleza jinsi ya kuepuka tabia hatarishi

Page 109: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

105Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

1. Eleza maana ya tabia hatarishi.2. Simameni kwenye mduara, kila mmoja ahakikishe anaweza kumuona mwenzake vizuri. Kila

mmoja ataje tabia hatarishi moja anayoifahamu.

Panga na fanya igizo dhima linaloonyesha tabia hatarishi zaidi ya tatu na muoneshe madhara yake. Kila mmoja afuatilie igizo kwa makini na mwisho wa igizo jibu maswali yafuatayo:

1. Tabia zilizooneshwa katika igizo zipo katika mazingira yenu?2. Ni mambo gani yanayoweza kuchochea kijana kuwa na tabia hatarishi?3. Nini madhara ya tabia hizo?4. Una ushauri gani kwa vijana wenye tabia kama hizo ili waweze kuziepuka?

Zoezi la Tatu

Zoezi la Nne

SEHEMU YA NNE: TABIA HATARISHI

Page 110: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

106 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Page 111: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

107Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

KIAMBATISHO A

Na. Aina ya ugonjwa

wa ngono

Visababi-shi

Njia za maam-bukizi

Dalili Namna ya kujikinga

Tiba Athari

1. Kisonono Bacteria aitwaye Neisseria gonor-rheoeae au gonococ-cus-Ngono .

Kupitia ngono zembe na kuchangia nguo za ndani na taulo.

Kwa wanawake ni maumi-vu chini ya tumbo ya-nayoambatana na homa kali, kutapika, maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa, kuvimba eneo la uke, kutoka damu katikati ya siku za mwezi, kutokwa damu baada ya kufanya tendo la ndoa, maumivu wakati wa haja ndogo na kukojoa mara kwa mara, na uchafu ukeni unaofa-nana na usaha, kutokwa na uchafu njia ya haja kubwa, kuwashwa na ku-tokwa na damu wakati wa haja kubwa, kukauka koo, kuwashwa, kumeza kwa shida au uvimbe shingoni, maumivu kwenye macho na macho kutopenda mwanga mwingi na ku-tokwa na uchafu unaofa-nana na usaha, maumivu na kuvimba sehemu za maungio ya mifupaKwa wanaume ni kutokwa na usaha uumeni wenye rangi nyeupe, njano au kijani, maumivu makali wakati wa kukojoa, kutok-wa na uchafu njia ya haja kubwa, anawashwa na ku-tokwa na damu wakati wa haja kubwa, kukauka koo, kuwashwa, kumeza kwa shida au uvimbe shingoni, maumivu kwenye macho na macho kutopenda mwanga mwingi na ku-tokwa na uchafu unaofa-nana na usaha, maumivu na kuvimba sehemu za maungio ya mifupa.

Kuacha na kujihusisha na masuala ya ngono zembe na kuacha kabisa kuchangia nguo za ndani na taulo.

Lazima aende hospitali apatiwe antibiotic na kuacha kujihu-sisha na masuala ya mapenzi.

Kwa wanawake -Isipoti-biwa vizuri inaweza ku-haribu mirija ya uzazi na mara nyingine kusaba-bisha ugumba, mimba kutungwa nje ya uzazi, kuzaa njiti, mtoto ku-zaliwa kabla ya siku zake au mimba kuharibika, kumwambukiza mtoto wakati wa kujifungua, kumsababishia mtoto aliyezaliwa upofu wa kudumu na maambukizi kwenye maungio ya mi-fupa au kwenye damuKwa wanaume husaba-bisha maumivu makali kwenye mapumbu, kumsababishia ugumba, kupata makovu ndani ya mrija wa kutolea mkojo nje na kufanya mkojo utoke kwa shidaNi rahisi mtu mwenye kisonono kuambukizwa ukimwi.

Unaongeza uwezekano wa kupata maambukizi ya UKIMWI, unaweza kupata ugumba kwa mwanamke.

Maumivu makali, ugum-ba, kutokuwa hamu ya tendo la ndoa, uume kutokusimama vyema.

Page 112: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

108 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Na. Aina ya ugonjwa

wa ngono

Visababishi Njia za maambukizi

Dalili Namna ya kujikinga

Tiba Athari

2. Kaswende Bakteria inayofaha-mika kama Treponema pallidum

Ngono zembe; kuambuki-zwa kutoka kwa mama hadi kwa mimba wakati wa ujauzito au wakati wa kuzaliwa kwa mtoto, na kusababisha kuzaliwa na kaswende, kupitia michubuko au mipa-suko kwenye ngozi wakati wa kujamii-ana au wakati mtu mwingine wanapogu-sana ikiwa wana mipa-suko sehemu mbalimbali

Vipele katika sehemu za uzazi, kuna hatua nne za dalili ya kwanza, ya pili, �che, na ya mwisho. Hatua ya kwanza kawaida inajitokeza kwa kidonda kidogo kiitwacho chanka utokeaji wa kidonda kwa ngozi isiyowasha, ngumu, isiyokuwa na uchungu. Hatua ya pili ya kaswende huji-tokeza na upele ambayo mara kwa mara inahusi-sha viganja vya mikono na nyayo za miguu. Hatua �che ya kaswende hujitokeza na dalili kiasi au hata bila dalili. Hatua ya mwisho ya kas-wende hujitokeza na guma, dalili zinazohusiana na mfumo wa neva, au zinazohusiana na moyo

Kuacha na kujihusisha na masuala ya ngono zembe na kuacha ku-changia nguo za ndani na taulo.

Lazima aende hospitali apa-tiwe antibiotic na kuacha kuji-husisha kabisa na masuala ya mapenzi.

Wakati wa ujauzito unaweza kuwa hatari kubwa kwa kiumbe tumboni, kama vile kusababisha kutoumbika vizuri (deform-ity) na kifo.

Unaongeza uwezekano wa kupata maambukizi ya UKIMWI, unaweza kupata ugumba kwa mwanamke.

Maumivu makali, ugumba, kutokuwa na hamu ya tendo la ndoa, uume kutokusimama vyema.

Page 113: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

109Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Na. Aina ya ugonjwa

wa ngono

Visababishi Njia za maambukizi

Dalili Namna ya kujikinga

Tiba Athari

3. Tricho-monas

Bakteria anayifaha-mika kama Trichomonas vaginalis

Kupitia ngono zembe na kuchangia nguo za ndani na taulo

Kwa wanawake kuwashwa sehemu za uke na maumivu makali wakati wa kukojoa kutoka kwenye uke na kuwa na harufu mbaya, kuwashwa sehemu za uke, kuvimba, kujisikia kukojoa mara kwa mara na maumivu wakati wa tendo la ndoa

Kwa wanaume kuwashwa ndani ya uume, maumivu makali wakati wa kukojoa na kutoa majimaji yanayonuka kutoka kwenye uume

Kuacha kujihusi-sha na masu-ala ya ngono zembe na kua-cha kuchangia nguo za ndani na taulo

Lazima aende hospi-tali apatiwe antibiotic na kuacha kabisa kuji-husisha na masuala ya mapenzi.

Unaongeza uwezekano wa kupata maambukizi ya UKIMWI, unaweza kupata ugumba kwa mwanamke

Maumivu makali, ugumba, kutokuwa na hamu ya tendo la ndoa, uume kutokusimama vyema

4. Klamidia Backteria ait-wae Chlamyd-ia trachomatis

Kupitia ngono zembe

Siyo rahisi kuonekana. Kwa mwanaume dalili ni kupata maumivu wakati wa kukojoa, na kukojoa mara kwa mara

Kwa mwanamke, ni kutokwauchafu sehemu za uke na kupata maumivu wakati wa kukojoa, kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa au kutoka damu wakati wa tendo la ndoa, kutokwa na damu nyingi kabla ya hedhi

Kwa wanaume kutokwa uchafu mweupe au ute ute kutoka kwenye uume na maumivu wakati wa kukojoa.

Kuacha na kujihusisha na masuala ya ngono zembe na kuacha ku-changia nguo za ndani na taulo na kutumia vyoo sa�.

Lazima aende hospi-tali apatiwe antibiotic na kuacha kujihusisha na masuala ya mapenzi.

Kwa mwanamke ni kuziba kwa mirija ya kupiti-sha mayai na mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi. Mimba hizi huhatari-sha maisha ya mama na kuleta ugumba. Kwa mwanaume athari ni kuziba mirija ya kupiti-sha mbegu na utasa.Unaongeza uwezekano wa kupata maambukizi ya UKIMWI, Maumivu maka-li, kutokuwa na hamu ya tendo la ndoa, uume kutokusimama vyema.

Page 114: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

110 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Na. Aina ya ugonjwa

wa ngono

Visababishi Njia za maam-bukizi

Dalili Namna ya kujikinga

Tiba Athari

5. Malenge-lenge ya sehemu za siri

Virusi vya manawa na wanaweza kupitisha HSV – herpers simplex virus

Kupitia ngono na kuchangia nguo za ndani na taulo

Vidonda kwenye sehemu za uzazi au kwenye mdomo, ambavyo huja na kwenda kwa miezi au miaka kadhaa. Utahisi kuwashwa, au kujikunakuna kwenye sehemu ya uzazi au kwenye ma-paja, na kupata vid-onda vidogo vidogo ambavyo hupasuka na kugeuka kuwa vidonda vikubwa. Kwa wanaume vidonda vidogo vinavyopasuka na kuacha vidonda vyenye uchungu sehemu za uume, kuwashwa sehemu za siri na kukojoa mara kwa mara

Kuacha na kujihusisha na masuala ya ngono zembe na kuacha ku-changia nguo za ndani na taulo

Lazima aende hospi-tali apatiwe antibiotic na kuacha kujihusisha na masuala ya mapenzi hapo tiba itakapok-wisha

Unaongeza uwezekano wa kupata maambukizi ya UKIMWI, unaweza kupata ugumba kwa mwanamke

Maumivu makali, ugumba, kutokusikia hamu ya tendo la ndoa, uume kutokusimama vyema

6. Utando

mweupe

Bakteria Kupitia

ngono na

kuchangia

nguo za

ndani na

taulo

Dalili kwa mwan-

amke ni kutokwa

na uchafu ukeni

(kama maziwa

yaliyoganda),

kutokwa na uchafu

mweupe au njano au

kijani unaotoa harufu

mbaya, kuwashwa na

kuwa na michubuko

sehemu za siri.

Kwa mwanaume ni

kuwashwa sehemu

za siri na kusikia

maumivu wakati wa

kukojoa

Kuacha kujihusi-

sha na masu-

ala ya ngono

zembe na kua-

cha kuchangia

nguo za ndani

na taulo

Lazima

aende hospi-

tali apatiwe

antibiotic

na kuacha

kujihusisha

kabisa na

masuala ya

mapenzi.

Maumivu wakati

wa kujamiiana

Unaongeza

uwezekano

wa kupata

maambukizi

ya UKIMWI,

unaweza kupata

ugumba kwa

mwanamke

Maumivu

makali, ugumba,

kutokuwa

hamu ya tendo

la ndoa, uume

kutokusimama

vyema

Page 115: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

111Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Na. Aina ya

ugonjwa

wa ngono

Visababishi Njia za

maambukizi

Dalili Namna ya

kujikinga

Tiba Athari

7. Virusi vya

UKIMWI

Virusi VVU

ambavyo hu-

kaa kwenye

sehemu za

majimaji ya

mwili, kama

vile damu,

majimaji ya

ukeni na kwe-

nye manii

Kupitia ngono Mwanzo baada ya

kuambukizwa haku-

na dalili maalum.

Hatua hii inaweza

kuchukua mpaka

miaka kumi. Lakini

mara mtu anapoan-

za kuugua UKIMWI

dalili zinakuwa

nyingi. Pamoja na

kupungua kinga ya

mwili, kupungua

uzito na kuumwa

mara kwa mara.

Kuacha na

kujihusisha

na masuala ya

ngono zembe

na kuacha ku-

changia nguo za

ndani na taulo.

Hadi sasa tiba

haijiagundu-

lika nivema

kwenda hos-

pitali kutibiwa

magonjwa

nyemelizi.

Husababisha

Kifo

8. Pangusa(Chancroid)

Bakteria in-ayofahamika haemophilus ducreyi.

Kupitia ngono na kuchangia nguo za ndani na taulo.

Vidonda vikubwa sana kwenye viungo vya uzazi na kusaba-bisha kulika katika sehemu hizoBaada ya maam-bukizi vipele hutokea kisha huchimbika na kutoa vidonda vikubwa vikubwa ambavyo husambaa pande mbalimbali za sehemu za siri na kuchimba mashimo ya vidonda.Maumivu makali, Kutoka damu pale vidonda vinapo-guswa Kutokwa na majimaji ukeni/uumeni yanayoam-batana na maumivu makali sehemu za siri.

Kuacha kujihusi-sha na masuala ya ngono zem-be na kuacha kuchangia nguo za ndani na.

Lazima aende hospitali apa-tiwe antibiot-ic na kuacha kujihusisha kabisa na masuala ya mapenzi.

Unaongeza uwezekano wa kupata maambukizi ya UKIMWI, unaweza kupata ugumba kwa mwanamke

Maumivu makali, ugumba, kutokuwa na hamu ya tendo la ndoa, uume kutokusimama vyema.

Page 116: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

112 Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Na. Aina ya ugonjwa wa

ngono

Visababishi Njia za maam-bukizi

Dalili Namna ya kujikinga

Tiba Athari

9. Mandeletele -Husaba-bishwa na bakteria

Kupitia ngono na kuchangia nguo za ndani na taulo

Vidonda sehemu za siri, kuvimba mitoki nyongani, maumivu wakati wa kukojoa

Kuacha na kujihusisha na masuala ya ngono zembe na kuacha ku-changia nguo za ndani na taulo

Lazima aende hospitali apatiwe antibiotic na kuacha kabisa kujihusisha na masuala ya mapenzi.

Unaongeza uwezekano wa kupata maambukizi ya UKIMWI, Kutoka mimba,kuzaa watoto njiti,kukatika uume.

Maumivu makali, kutokuwa na hamu ya tendo la ndoa, uume ku-tokusimama vyema.

Page 117: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

113Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako!

REFERENCES

1. Ministry of health and Social Welfare (2009) National Standard in Peer Education for young people.

2. AIDS Business Coalition Tanzania (2008). Dhana ya Jinsia na Jinsi inayojengeka katika Jamii. ABCT.DSM

3. Taasisi ya elimu Tanzania (2008) Stadi za Maisha katika Elimu ya Msingi. TIE DSM

4. Ministry of Education and Vocational Training (2010). How to Develop your Life Skills. PASHA – MoEVT DSM

5. Tanzania Commission for AIDS (2007). The Questions Adolescents ask Most frequently about Growing up and their answers vol.1.Tanzanian German Programme to Support Health (TGPSH).DSM

6. Wizara ya Elimu na Mafunzo ya ufundi –Zumzum Maisha(2010). Mwongozo wa Mafunzo ya Elimu ya Maambukizi ya Magonjwa ya ngono, Virusi Vya UKIMWI kwa njia ya Sanaa na michezo shule za Msingi

7. Peace Corps (2001). Life Skills Manual. Information Collection and Exchange Publication. Washington DC

8. Youth Alliance (2004). Stadi za Mpango wa Maisha –Mtaala kwa ajili ya vijana wa Afrika. PATH, 1800K,st, Suite 800, Washington DC

9. Tanzania Women Judges Association (2011). Stopping the Abuse of power for Purposes of Sexual Exploitation: Naming, Shaming and Ending Sextortion

10. Ministry of Education and Culture (2000). Gender Sensitivity. Module5

11. Oxford (2013). Civics for Secondary Schools. Form Three. Oxford University Press (T) Ltd. DSM

Page 118: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Page 119: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Page 120: MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU …...Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwalimu - Msichana Timiza Ndoto Yako! Jamhuri ya Muungano wa Tanzania