muhtasari - business facilitationtanzania.eregulations.org/media/tir2012 draft kiswahili... ·...

24
RIPOTI YA UWEKEZAJI TANZANIA 2012 UWEKEZAJI WA MITAJI BINAFSI KUTOKA NJE NA MTAZAMO WA WAWEKEZAJI MUHTASARI

Upload: others

Post on 19-Jan-2021

10 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: MUHTASARI - Business Facilitationtanzania.eregulations.org/media/TIR2012 DRAFT Kiswahili... · 2013. 11. 29. · Mchango huu, umesaidia katika maendeleo na ... mwaka 2000 na kutoa

RIPOTI YA UWEKEZAJI TANZANIA 2012

UWEKEZAJI WA MITAJI BINAFSI KUTOKA

NJE NA MTAZAMO WA WAWEKEZAJI

MUHTASARI

Page 2: MUHTASARI - Business Facilitationtanzania.eregulations.org/media/TIR2012 DRAFT Kiswahili... · 2013. 11. 29. · Mchango huu, umesaidia katika maendeleo na ... mwaka 2000 na kutoa

1

Utangulizi

Uwekezaji wa mitaji binafsi kutoka nje unajumuisha uwekezaji mkubwa, kuanzia asilimia 10 ya mtaji wa kampuni (foreign direct investment (FDI)), uwekezaji mdogo, chini ya asilimia 10 ya mtaji wa kampuni (portfolio investment) na uwekezaji unaotokana na mikopo mbalimbali (other investment). Mitaji binafsi kutoka nje imekuwa chanzo muhimu cha uwekezaji hususan katika uchumi wa nchi zinazoinukia na zile zinazoendelea. Mchango huu, umesaidia katika maendeleo na kuunganisha uchumi wa mataifa mbalimbali duniani. Kufuatia mwenendo huu, mataifa mengi yamekuwa yakitafuta aina hii ya uwekezaji.

Tanzania imefanya jitihada kubwa katika kipindi cha miongo mitatu iliyopita kuboresha mazingira ya uwekezaji kwa lengo la kuvutia uwekezaji binafsi kutoka nje. Mabadiliko makubwa ya kisera na kimiundo yalifanyika tangu miaka ya 1980. Jitihada hizi zimesababisha kuongezeka kwa uwekezaji huo.

Kutokana na kuongezeka kwa uwekezaji huu, kumekuwa na umuhimu wa kuufuatilia ili kubaini ukubwa, vyanzo, maeneo ya uwekezaji na mchanganuo wake. Serikali ilianzisha zoezi la kufuatilia uwekezaji huo mwaka 2000 kupitia Taasisi zake tatu, yaani Benki Kuu ya Tanzania, Kituo Cha Uwekezaji Tanzania na Ofisi ya Taifa ya Takwimu. Taasisi hizi kwa pamoja zimefanya tafiti kuanzia mwaka 2000 na kutoa ripoti za uwekezaji mwaka 2001, 2004, 2006 na 2009.

Malengo ya tafiti hizi ni pamoja na:

Page 3: MUHTASARI - Business Facilitationtanzania.eregulations.org/media/TIR2012 DRAFT Kiswahili... · 2013. 11. 29. · Mchango huu, umesaidia katika maendeleo na ... mwaka 2000 na kutoa

2

i. Kukusanya na kuchambua takwimu za uwekezaji wa mitaji binafsi kutoka nje kwa ajili ya kupima na kuendeleza mikakati ya kujitangaza, kuboresha takwimu za mizania ya urari wa malipo pamoja na kuainisha hali ya uwekezaji wa kimataifa nchini (international investment position);

ii. Kupata mtazamo wa sekta binafsi na mrejesho kutoka kwa wadau kuhusu mazingira ya uwekezaji ili kuendeleza majadiliano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi; na

iii. Kupendekeza sera muafaka na mikakati ya kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini.

Kijitabu hiki kinatoa muhtasari wa matokeo muhimu na mapendekezo ya utafiti uliofanywa kukusanya takwimu za mwaka 2008 hadi 2011. Sehemu moja ya utafiti huu ilihusisha makampuni yote (sensa) yenye mitaji kutoka nje, na sehemu nyingine ilihusisha makampuni yaliyochaguliwa kwa kuzingatia vigezo vya kitakwimu (sampuli). Katika sensa, makampuni yaliyohusishwa Tanzania Bara yalikuwa 1,848 na Zanzibar yalikuwa 208, ambapo mwitikio ulikuwa asilimia 84.1 kwa Tanzania Bara na asilimia 99.1 kwa Zanzibar. Katika sampuli, makampuni yaliyohusishwa yalikuwa 350 Tanzania Bara na makampuni 380 Zanzibar, ambapo mwitikio ulikuwa asilimia 85.4 kwa Tanzania Bara na asilimia 89.5 kwa Zanzibar.

Taarifa kamili ya uwekezaji—Tanzania Investment Report 2012—inapatikana katika tovuti za taasisi zilizoshirikiana kuiandaa (anuani za kuipata taarifa hiyo zimeonyeshwa mwisho wa kijitabu hiki).

Page 4: MUHTASARI - Business Facilitationtanzania.eregulations.org/media/TIR2012 DRAFT Kiswahili... · 2013. 11. 29. · Mchango huu, umesaidia katika maendeleo na ... mwaka 2000 na kutoa

3

Matokeo Muhimu

Limbikizo la mitaji liliongezeka

Mitaji kutoka nje iliyowekezwa hapa nchini iliongezeka kwa wastani wa asilimia 10.3 kila mwaka hadi kufikia dola za Kimarekani milioni 10,393.2 mwaka 2011 kutoka dola za Kimarekani milioni 7,751.0 mwaka 2008 (Chati 1). Uwekezaji wa mitaji mikubwa uliendelea kuwa chanzo kikuu kwa kuchangia asilimia 89.3 ya mitaji yote kutoka nje, ikifuatiwa na mikopo mbalimbali ambayo ilichangia asilimia 10.6.

Chati 1: Limbikizo la Mitaji Binafsi Kutoka Nje, 2008-2011

7,751.08,566.0

9,278.1

10,393.2

2008 2009 2010 2011

(Dola za Kimarekani millioni)

Uwekezaji wa mitaji binafsi kutoka nje

uliathiriwa na mtikisiko wa kifedha duniani

Mitaji binafsi iliyoingia kutoka nje ilipungua mwaka 2009 kutokana na kuwepo kwa mtikisiko wa kifedha na uchumi

Page 5: MUHTASARI - Business Facilitationtanzania.eregulations.org/media/TIR2012 DRAFT Kiswahili... · 2013. 11. 29. · Mchango huu, umesaidia katika maendeleo na ... mwaka 2000 na kutoa

4

duniani. Hata hivyo, mwaka 2010 uwekezaji huo uliongezeka na kisha kushuka tena mwaka 2011 kutokana na urejeshaji mkubwa wa mikopo (Chati 2) ambao pia ulihusishwa na athari za mtikisiko wa kifedha na uchumi duniani. Wastani wa thamani ya uwekezaji mkubwa kutoka nje katika kipindi cha utafiti huu ulikuwa dola za Kimarekani milioni 1,344.6 kwa mwaka na ulichangia asilimia 94.0 ya thamani yote ya uwekezaji kutoka nje.

Chati 2: Uwekezaji wa Mitaji Binafsi Kutoka Nje, 2008-2011

1,383.3

952.6

1,813.3

1,229.4

172.0

70.4

99.9

2008 2009 2010 2011Uwekezaji mdogo* Uwekezaji mkubwa Uwekezaji mwingine

(Dola za Kimarekani millioni)

*Uwekezaji mdogo imekuwa na thamani ya 0.1% ya jumla ya mitaji yote kila mwaka

Mchango wa mitaji midogo uliendelea kuwa

mdogo

Mchango wa uwekezaji mdogo kutoka nje uliendelea kuwa chini ya asilimia moja ya uwekezaji wote. Mchango huo mdogo, umetokana na uchanga wa soko la mitaji ambalo lina makampuni machache yaliyoorodheshwa, uchache wa dhamana za biashara na mwamko mdogo wa uwekezaji katika masoko ya fedha.

Page 6: MUHTASARI - Business Facilitationtanzania.eregulations.org/media/TIR2012 DRAFT Kiswahili... · 2013. 11. 29. · Mchango huu, umesaidia katika maendeleo na ... mwaka 2000 na kutoa

5

Mchango wa mikopo mbalimbali ulikuwa wa pili kwa ukubwa, na thamani yake ilikuwa dola za Kimarekani milioni 1,097.5 mwaka 2011 ikilinganishwa na dola za Kimarekani milioni 798.5 mwaka 2008. Mitaji ya aina hii iliwekezwa zaidi kwenye shughuli za fedha na bima, uzalishaji viwandani, na umeme na gesi.

Uwekezaji kwenye shughuli za umeme na gesi

uliongezeka kwa kasi kubwa

Chati 3: Mchanganuo wa Uwekezaji kwa

Shughuli za Uchumi, 2008 – 2011

49.4%

20.5%

9.6%

6.0%

0.1% 14.5%

2008

Mining and quarrying Manufacturing Accommodation

Finance and insurance Electricity and gas Other

40.4%

22.5%

3.8%

10.1%

0.2%

23.0%

2009

Mining and quarrying Manufacturing Accommodation

Finance and insurance Electricity and gas Other

50.2%

8.7%1.2%

5.3%

16.0%

18.7%

2010

Mining and quarrying Manufacturing Accommodation

Finance and insurance Electricity and gas Other

33.1%

17.7%13.5%

9.9%

17.0%

8.9%

2011

Mining and quarrying Manufacturing Accommodation

Finance and insurance Electricity and gas Other

50.2%

8.7%1.2%

5.3%

16.0%

18.7%

2010

Uchimbaji madini na mawe Bidhaa za viwandani Malazi

Fedha na bima Umeme na gesi Nyinginezo

Page 7: MUHTASARI - Business Facilitationtanzania.eregulations.org/media/TIR2012 DRAFT Kiswahili... · 2013. 11. 29. · Mchango huu, umesaidia katika maendeleo na ... mwaka 2000 na kutoa

6

Shughuli za umeme na gesi, ambazo uwekezaji wake ulikuwa na thamani chini ya dola za Kimarekani milioni 3.o mwaka 2008 na 2009, uliongezeka hadi kufikia dola za Kimarekani milioni 290.5 mwaka 2010 na dola za Kimarekani milioni 209.4 mwaka 2011.

Wakati huo huo, kilimo ambacho kina mchango mkubwa kwenye pato la taifa kiliendelea kuwa na kiwango kidogo cha uwekezaji kutoka nje. Pamoja na ongezeko la uwekezaji katika shughuli za kilimo kuwa zaidi ya asilimia 50.0 kati ya 2008 na 2011, thamani ya uwekezaji wake ilikuwa ndogo ikilinganishwa na uwekezaji kwenye shughuli nyingine kama vile uchimbaji madini na mawe, uzalishaji viwandani, fedha na bima; na habari na mawasiliano (Chati 3 na 4).

Chati 4: Shughuli Kumi Zilozoongoza Katika Limbikizo la Mitaji, 2008 na 2011

3,714.1870.7

532.4

416.3

388.7

372.0

202.3

119.5

79.7

28.8

Uchimbaji madini na mawe

Bidhaa za viwanda

TEHAMA

Fedha na bima

Makazi

Uuzaji jumla na rejareja

Kilimo

Ujenzi

Upangishaji majengo

Uchukuzi na uhifadhi

2008

(Dola za Kimarekani milioni)

4,123.0

1,520.5

872.8

756.6

627.8

539.8

400.5

355.4

142.5

99.2

Uchimbaji madini na mawe

Bidhaa za viwandani

Malazi

Fedha na bima

TEHAMA

Umeme na gesi

Uuzaji jumla na reja reja

Kilimo

Ujenzi

Upangishaji majengo

2011

(Dola za Kimarekani milioni)

Page 8: MUHTASARI - Business Facilitationtanzania.eregulations.org/media/TIR2012 DRAFT Kiswahili... · 2013. 11. 29. · Mchango huu, umesaidia katika maendeleo na ... mwaka 2000 na kutoa

7

Nchi chache ziliendelea kuongoza katika

uwekezeji wa mitaji nchini

Afrika ya Kusini, Uingereza, na Canada zilichangia kwa wastani wa zaidi ya asilimia 70 ya uwekezaji wote kutoka nje kati ya mwaka 2008 na 2011 (Chati 5). Nchi hizi ndizo zilizoongoza hata kabla ya mwaka 2008. Uchache wa nchi hizi unaleta changamato kwa Tanzania endapo zitakumbwa na matatizo ya kiuchumi.

Chati 5: Mchango wa Uwekezaji kwa Nchi –

Wastani 2008 hadi 2011

Afrika Kusini (31.2%)

Canada (22.5%)

Uingereza (19.0%)

Mauritius (8.8%)

Kenya (4.5%)

Nyinginezo (14.0%)

Mchanganuo wa uwekezaji mkubwa kwa

unakotoka, (wastani %, 2008 - 2011)

Sehemukubwa ya uwekezaji mkubwa

ulitoka nchi

tatu

Faida iliongezeka kwa kiwango kikubwa

Faida baada ya kulipa kodi iliongezeka kwa wastani wa asilimia 79.3 kila mwaka toka 2009 mpaka 2011. Faida kubwa zaidi ilipatikana mwaka 2011 ambapo ilifikia dola za Kimarekani milioni 1,492.7, zaidi ya maradufu ya faida dola za Kimarekani milioni 679.0 iliyopatikana mwaka 2010. Faida ilipatikana zaidi kwenye shughuli za uchimbaji madini

Page 9: MUHTASARI - Business Facilitationtanzania.eregulations.org/media/TIR2012 DRAFT Kiswahili... · 2013. 11. 29. · Mchango huu, umesaidia katika maendeleo na ... mwaka 2000 na kutoa

8

na mawe, hali ambayo kwa kiasi ilitokana na ongezeko la bei ya dhahabu kwenye soko la dunia mwaka huo.

Sehemu kubwa ya faida iliyopatikana

iliwekezwa nchini

Kiwango cha faida kinachowekezwa nchini kiliongezeka kutoka asilimia 76.0 mwaka 2008 hadi wastani wa asilimia 84.0 kati ya 2010 na 2011. Wastani wa faida iliyowekezwa tena nchini kwa kipindi chote cha utafiti ulikuwa asilimia 82.5 (Chati 6).

Chati 6: Faida Kutokana na Uwekezaji

76.0% 79.1%

84.5%

83.6%

288.4337.9

679.0

1,492.7

2008 2009 2010 2011

Asilimia iliyowekezwa nchini

Jumla ya faida baada ya kodi (dola za Kimarekanimilioni)

Kutokana na ongezeko hili, uwekezaji wa faida ndani ya nchi, umekuwa ndio chanzo kikubwa cha uwekezaji mkubwa katika mwaka 2011 ikilinganishwa na mwaka 2008 ambapo uwekezaji wa kutumia mikopo uliongoza.

Page 10: MUHTASARI - Business Facilitationtanzania.eregulations.org/media/TIR2012 DRAFT Kiswahili... · 2013. 11. 29. · Mchango huu, umesaidia katika maendeleo na ... mwaka 2000 na kutoa

9

Mtazamo wa Wawekezaji na Uhusiano na Uchumi wa Ndani

Mtazamo wa Wawekezaji

Mtazamo wa wawekezaji unaonyesha imani ya wawekezaji katika uchumi na jinsi huduma mbalimbali zinavyosaidia uendeshaji wa biashara. Katika kuangalia mtazamo wa uwekezaji, zilitumika taaarifa za sensa. Makampuni yaliyohojiwa yaliombwa kuonyesha ni jinsi gani huduma kama usafiri wa barabara na anga, kutoa mizigo bandarini, umeme na maji, mawasiliano, uhifadhi wa mizigo, huduma za manispaa na benki zinavyosaidia shughuli zao wakilinganisha walivyoanza biashara na wakati utafiti ulipofanyika.

Kwa ujumla kulikuwa na uboreshwaji wa

mazingira ya uwekezaji nchini

Matokeo yanaonyesha kuwa kulikuwa na maboresho katika mazingira ya uwekezaji hapa nchini. Huduma za benki, mawasiliano, uhamiaji, usafiri wa anga na nchi kavu zilionekana kuwa na matokeo yenye kusaidia uwekezaji wakati wa kipindi cha utafiti (Chati 7).

Mageuzi katika sekta ya benki yalikuwa na

matokeo yaliyosaidia uwekezaji

Kuongezeka kwa idadi ya mabenki, na huduma za kifedha kama vile mashine za kutolea fedha, matumizi ya simu za mkononi, matumizi ya mtandao na kuongezwa kwa masaa ya kazi kumekuwa na matokeo yaliyosaidia shughuli za uwekezaji. Matokeo haya mazuri yaliripotiwa zaidi na makampuni yanayojishughulisha na uchimbaji madini na

Page 11: MUHTASARI - Business Facilitationtanzania.eregulations.org/media/TIR2012 DRAFT Kiswahili... · 2013. 11. 29. · Mchango huu, umesaidia katika maendeleo na ... mwaka 2000 na kutoa

10

mawe, habari na mawasiliano, upangishaji wa nyumba na ujenzi (Chati 8). Pamoja na uboreshaji wa huduma za kibenki, wawekezaji walilalamikia ukubwa wa gharama za mikopo.

Chati 7: Mtazamo Jumla wa Wawekezaji Katika

Maeneo Yanayoathiri Uwekezaji

-100.0% -50.0% 0.0% 50.0% 100.0%

Usafiri wa barabara

Utoaji mizigo bandarini

Usafiri wa ndege

Ugavi wa umeme wa uhakika

Ugavi wa maji wa uhakika

Mawasiliano

Huduma za forodha

Huduma za uhamiaji

Huduma za manispaa

Huduma za benki

A. Wakati wa kuanza biashara

Haukusaidia Haukusaidia kabisa

-100.0% -50.0% 0.0% 50.0% 100.0%

Usafiri wa barabara

Utoaji mizigo bandarini

Usafiri wa ndege

Ugavi wa umeme wa uhakika

Ugavi wa maji wa uhakika

Mawasiliano

Huduma za forodha

Huduma za uhamiaji

Huduma za manispaa

Huduma za Benki

B. Wakati wa UtafitiUlisaidia Ulisaidia sana

Maendeleo katika utoaji wa huduma za

mawasiliano yalikuwa na matokeo yaliyosaidia uwekezaji

Kuongezeka kwa idadi ya watoa huduma za simu za mikononi pamoja na mtandao na huduma kama intaneti kulisaidia uwekezaji (Chati 9). Shughuli za uchimbaji madini na mawe, kilimo, biashara ya jumla na rejareja ziliongoza kwa kuripoti matokeo yaliyosaidia uwekezaji, kutokana na maendeleo katika huduma za mawasiliano.

Page 12: MUHTASARI - Business Facilitationtanzania.eregulations.org/media/TIR2012 DRAFT Kiswahili... · 2013. 11. 29. · Mchango huu, umesaidia katika maendeleo na ... mwaka 2000 na kutoa

11

Chati 8: Utoaji wa Huduma za Kibenki

-100.0% -50.0% 0.0% 50.0% 100.0%

Malazi

Utawala na huduma

Kilimo

Ujenzi

Fedha na bima

TEHAMA

Bidhaa za viwandani

Uchimbaji madini na mawe

Upangishaji majengo

Uchukuzi na uhifadhi

Uuzaji wa jumla na rejareja

Umeme

A. Wakati wa kuanza biashara

Haukusaidia Haukusaidia kabisa

-100.0% -50.0% 0.0% 50.0% 100.0%

Malazi

Utawala na huduma

Kilimo

Ujenzi

Fedha na bima

TEHAMA

Bidhaa za viwandani

Uchimbaji madini namawe

Upangishaji majengo

Uchukuzi na uhifadhi

Uuzaji wa jumla na rejareja

Umeme

B. Wakati wa utafiti

Ulisaidia Ulisaidia sana

Chart 9: Utoaji wa Huduma ya Mawasiliano

-100.0% -50.0% 0.0% 50.0% 100.0%

Malazi

Utawala na huduma

Kilimo

Ujenzi

Fedha na bima

TEHAMA

Bidhaa za viwandani

Uchimbaji wa madini na mawe

Upangishaji majengo

Uchukuzi na uhifadhi

Uuzaji wa jumla na rejareja

Elimu

Umeme

Afya

A. Wakati wa kuanza biashara

Haukusaidia Haukusaidia kabisa

-100.0% -50.0% 0.0% 50.0% 100.0%

Malazi

Utawala na Huduma

Kilimo

Ujenzi

Fedha na Bima

TEHAMA

Bidhaa za viwandani

Uchimbaji wa madini na mawe

Upangishaji majengo

Uchukuzi na Uhifadhi

Uuzaji wa jumla na rejareja

Elimu

Umeme

Afya

B. Wakati wa utafiti

Ulisaidia Ulisaidia sana

Page 13: MUHTASARI - Business Facilitationtanzania.eregulations.org/media/TIR2012 DRAFT Kiswahili... · 2013. 11. 29. · Mchango huu, umesaidia katika maendeleo na ... mwaka 2000 na kutoa

12

Umeme usiokuwa na uhakika ulibakia kuwa

changamoto kwa wawekezaji

Wawekezaji walionyesha kuwa kutokuwepo kwa umeme wa kutosha na wa uhakika kuliendelea kuathiri biashara zao. Kupungua kwa umeme na kukatika mara kwa mara kuliwagharimu wawekezaji hususan walipolazimika kutumia majenereta ya dharura ambayo yaliongeza gharama ya uendeshaji. Ni vyema ikumbukwe kwamba katika kipindi cha utafiti (2010/11) nchi ilikuwa imekumbwa na tatizo la umeme kutokana na ukame. Shughuli zilizoripoti kuwa umeme haukusaidia uwekezaji zilikuwa ni uzalishaji viwandani, uchimbaji madini na mawe, usafirishaji na uhifadhi pamoja na kilimo cha maua (Chati 10).

Chart 10: Uwepo wa Umeme wa Uhakika

-100.0% -50.0% 0.0% 50.0% 100.0%

Malazi

Utawala na huduma

Kilimo

Ujenzi

Fedha na bima

TEHAMA

Bidhaa za viwanda

Uchimbaji wa madini na mawe

Upangishaji majengo

Uchukuzi na uhifadhi

Uuzaji wa jumla na rejareja

Elimu

Umeme

Afya

A. Wakati wa kuanza biashara

Haukusaidia Haukusaidia kabisa

-100.0% -50.0% 0.0% 50.0% 100.0%

Malazi

Utawala na huduma

Kilimo

Ujenzi

Fedha na bima

TEHAMA

Bidhaa za viwanda

Uchimbaji wa madini na mawe

Upangishaji majengo

Uchukuzi na uhifadhi

Uuzaji wa jumla na rejareja

Elimu

Umeme

Afya

B. Wakati wa utafiti

Ulisaidia Ulisaidia sana

Page 14: MUHTASARI - Business Facilitationtanzania.eregulations.org/media/TIR2012 DRAFT Kiswahili... · 2013. 11. 29. · Mchango huu, umesaidia katika maendeleo na ... mwaka 2000 na kutoa

13

Uhusiano wa Wawekezaji na Uchumi wa Ndani

Shughuli za uzalishaji viwandani na kilimo

ziliongoza katika utoaji wa ajira

Ingawa shughuli za uchimbaji wa madini na mawe ziliongoza kwa kiwango kikubwa katika mitaji binafsi kutoka nje (Chati 3 na 4), shughuli hizo zilishika nafasi ya 5 katika utoaji wa ajira (wastani wa mwaka 2008 na 2009). Asilimia 94.1 ya waajiriwa ilikuwa ni wazawa na asilimia 5.9 ni wageni.

Chati 11: Shughuli 10 Zilizoongoza kwa Kutoa Ajira – Wastani, 2008 hadi 2009

36,303

10,719

7,381

5,890

5,136

4,824

3,758

2,386

2,005

Bidhaa za viwandani

Kilimo

Utawala na huduma

Fedha na bima

Uchimbaji madini na mawe

Malazi

Uuzaji jumla na rejareja

TEHAMA

Uchukuzi na uhifadhi

Shughuli za uzalishaji viwandani ziliongoza kwa kutoa ajira zikifuatiwa na kilimo (Chati 11). Ni vyema ifahamike kwamba, japokuwa sekta ya kilimo ilikuwa ya pili kwa kutoa ajira, ilikuwa na kiasi kidogo cha uwekezaji kutoka nje (Chati 4). Katika makundi ya ajira, wazawa walikuwa wengi zaidi kwenye shughuli zinazohitaji ujuzi na zile

Page 15: MUHTASARI - Business Facilitationtanzania.eregulations.org/media/TIR2012 DRAFT Kiswahili... · 2013. 11. 29. · Mchango huu, umesaidia katika maendeleo na ... mwaka 2000 na kutoa

14

ambazo hazihitaji ujuzi. Kwa upande mwingine, wageni wengi walikuwa kwenye kundi la wataalamu na utawala (Chati 12).

Chati 12: Jumla ya Waajiriwa- Wastani wa 2008 na 2009

55.5%

81.8%

97.1%97.9%

3,136

9,755

32,719

38,066

Utawala Watalaam* Wenye ujuzi Wasio na ujuzi

Asilimia ya waajiriwa wazawa

* Bila kuhusisha ngazi ya utawala

Jumla ya waajiriwa (wastani 2008-2009)

Makampuni yaliyowekeza kwenye uzalishaji

viwandani na biashara yaliongoza kwenye kutoa huduma kwa jamii

Makampuni yaliyowekeza kwenye shughuli za uzalishaji viwandani ndiyo yaliyoongoza kutoa huduma kwa jamii, yakifuatiwa na yale yanayojihusisha na biashara, ujenzi, na fedha na bima. Kiasi kidogo kilitolewa na makampuni yanayojishughulisha na usafirishaji na uchimbaji wa madini (Chati 13).

Huduma za jamii ambazo zilipewa kipaumbele ni afya, elimu, sanaa na utamaduni pamoja na barabara (Chati 14).

Page 16: MUHTASARI - Business Facilitationtanzania.eregulations.org/media/TIR2012 DRAFT Kiswahili... · 2013. 11. 29. · Mchango huu, umesaidia katika maendeleo na ... mwaka 2000 na kutoa

15

Chati 13: Utoaji Huduma kwa Jamii Kulingana na Shughuli za Kiuchumi – (Wastani wa 2008 na 2009)

0.2

0.2

0.3

0.5

0.5

0.8

0.8

1.4

1.5

2.0

3.6

Uchukuzi na uhifadhi

Uchimbaji madini na mawe

TEHAMA

Utawala na huduma

Malazi

Afya

Kilimo

Fedha na bima

Ujenzi

Uuzaji jumla na rejareja

Bidhaa za viwanda

(Dola za Kimarekani milioni)

Chati 14: Huduma za Jamii Zilizopewa Kipaumbele – Wastani wa 2008 na 2009

0.1

0.3

0.3

1.3

1.5

1.6

2.4

3.4

Dini

Maji

Mazingira

Ulinzi na usalama

Barabara

Utamaduni na sanaa

Elimu

Afya na ustawi wa jamii

(Dola za Kimarekani milioni)

Page 17: MUHTASARI - Business Facilitationtanzania.eregulations.org/media/TIR2012 DRAFT Kiswahili... · 2013. 11. 29. · Mchango huu, umesaidia katika maendeleo na ... mwaka 2000 na kutoa

16

Makampuni mengi yalikuwa na mipango ya

kuongeza uwekezaji hapa nchini

Katika utafiti huu, asilimia 75.7 ya makampuni yenye uwekezaji kutoka nje yalionyesha kuwa yana mipango ya kuongeza uwekezaji hapa nchini katika kipindi cha miaka mitatu ijayo. Aidha, asilimia 19.9 ya makampuni yalionyesha kuwa yataendelea na kiwango cha uwekezaji kilichopo sasa, wakati asilimia 4.4 yalionyesha yatapunguza kiwango cha uwekezaji. Mtazamo huu unaashiria kuwa wawekezaji wameridhishwa na jitihada za serikali za kuboresha mazingira ya uwekezaji hapa nchini (Chati 15).

Chati 15: Mwelekeo wa Uwekezaji kwa Muda wa Kati

75.7%

19.9%

4.4%

Kuongeza uwekezaji Kuendelea na uwekezaji

wa sasa

Kupunguza uwekezaji

Mapendekezo

i. Ili kuendeleza kasi ya ukuaji wa mitaji binafsi kutoka nje, jitihada za kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini na kuhamasisha uwekezaji wa kimkakati

Page 18: MUHTASARI - Business Facilitationtanzania.eregulations.org/media/TIR2012 DRAFT Kiswahili... · 2013. 11. 29. · Mchango huu, umesaidia katika maendeleo na ... mwaka 2000 na kutoa

17

zinahitaji kuimarishwa. Hii itasaidia wawekezaji kupata faida zaidi na kuhamasika kuwekeza faida inayopatikana ndani ya nchi. Mikakati hiyo ni pamoja na kuendeleza kupunguza gharama za kufanya biashara, kuongeza fursa za uwekezaji na kuhamasisha uwekezaji katika sekta mbalimbali za kiuchumi.

ii. Kufuatia kuongezeka kwa uwekezaji kwenye shughuli za umeme na gesi, mikakati iliyopo ya kuandaa sera na usimamizi wake inahitaji kuharakishwa, ili kuhakikisha kuwa nchi inapata faida kutokana na rasilimali ya gesi.

iii. Jitihada za kufanya sekta ya kilimo kuwavutia wawekezaji wengi, zinahitaji kuimarishwa ili kuongeza mitaji katika sekta hii. Jitihada hizo ni pamoja na; kuwekeza kwenye miundombinu vijijini, miradi ya umwagiliaji, upatikanaji wa umeme vijijini kwa ajili kuwezesha usindikaji wa mazao pamoja na unchoraji wa ramani zenye mgawanyo wa matumizi ya ardhi nchi nzima.

iv. Ili kupanua wigo wa vyanzo vya mitaji, jitihada za kujitangaza zinahitaji kuimarishwa zaidi hasa katika mabara ya Asia na Amerika ya Kusini. Hii itasaidia kupunguza athari zinazoweza kutokana na matatizo ya kiuchumi nje ya nchi.

v. Makampuni yanayomilikiwa na wazawa yanahitajika kuhamasishwa kujiorodhesha kwenye soko la mitaji la Dar es Salaam ili kupata mitaji zaidi kutoka kwenye masoko ya kimataifa. Pia, kuna umuhimu wa

Page 19: MUHTASARI - Business Facilitationtanzania.eregulations.org/media/TIR2012 DRAFT Kiswahili... · 2013. 11. 29. · Mchango huu, umesaidia katika maendeleo na ... mwaka 2000 na kutoa

18

kuharakisha mchakato unaoendelea wa kuondoa vikwazo katika akaunti ya mitaji ya urari wa malipo (capital account liberalization).

vi. Mikakati inayoendelea kwenye sekta ya umeme na gesi inahitaji kufuatiliwa zaidi ili kutatua tatizo la upatikanaji wa umeme wa uhakika na kwa bei nafuu.

vii. Utekelezaji wa sera ya uhamishaji wa ujuzi kwa wazawa unahitaji kuimarishwa. Hii inaweza kufanyika kwa kupitia uanzishwaji wa programu za ujuzi ambazo zinaendana na mahitaji ya uwekezaji.

Page 20: MUHTASARI - Business Facilitationtanzania.eregulations.org/media/TIR2012 DRAFT Kiswahili... · 2013. 11. 29. · Mchango huu, umesaidia katika maendeleo na ... mwaka 2000 na kutoa

Ripoti kamili—Tanzania Investment Report 2012—inaweza kupatikana kupitia anuani hii:

1. http://www.bot.go.tz

2. http://www.tic.co.tz

3. http://www.nbs.go.tz

Page 21: MUHTASARI - Business Facilitationtanzania.eregulations.org/media/TIR2012 DRAFT Kiswahili... · 2013. 11. 29. · Mchango huu, umesaidia katika maendeleo na ... mwaka 2000 na kutoa
Page 22: MUHTASARI - Business Facilitationtanzania.eregulations.org/media/TIR2012 DRAFT Kiswahili... · 2013. 11. 29. · Mchango huu, umesaidia katika maendeleo na ... mwaka 2000 na kutoa
Page 23: MUHTASARI - Business Facilitationtanzania.eregulations.org/media/TIR2012 DRAFT Kiswahili... · 2013. 11. 29. · Mchango huu, umesaidia katika maendeleo na ... mwaka 2000 na kutoa
Page 24: MUHTASARI - Business Facilitationtanzania.eregulations.org/media/TIR2012 DRAFT Kiswahili... · 2013. 11. 29. · Mchango huu, umesaidia katika maendeleo na ... mwaka 2000 na kutoa

KWA MAELEZO ZAIDI, TAFADHALI ANGALIA TOVUTI ZETU