na dalili.doc · web viewbila ya shaka wapo wanavyuoni wakubwa katika afrika ya mashariki na ya...

111
ن ي ه را لب وا ج ج ج ل ا ة ن س ل وا اب ت ك ل ا ن م لة ط ا ت ل ا ن م حة ي ح ص ل ا داب ا ت ع ل ا ي ف دي ت ك ل مد ا ح م ن ب ي س و م ن ب د ت ع س ج ي5 س ل : ا ف ي ل9 أ ت ى ل و9 الأ عة ي لط اHoja na Dalili

Upload: others

Post on 27-Jan-2020

18 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

والبراهين الحججوالسنة الكتاب من

الباطلة من الصحيحة العبادات في

محمد: بن موسى بن سعيد الشيخ تأليفالكندي

األولى الطبعة

Hoja na DaliliKatika Qur’ani na Sunnah

Kuhusu ibada sahihi na batili

Chapa ya kwanza

Mtungaji:Sheikh Said Moosa Mohamed Al-Kindy

2010 - 1431

الرحيم الرحمن الله بســــــــــم

Alhamdulillaahi Rabbil-A’lamiin, shukrani zote na sifa takatifu Anastahiki Mwenyezi Mungu, Mola wa Limwengu zote, na rehema na amani iwe juu ya Mja Wake na Mtume Wake Nabii Muhammad (S.A.W.) Aliyemtuma kwa haki na mwalimu mkuu wa kheri zote za dunia na Akhera kwa umma wake kwa atakayemtii na kufuata mafundisho yake.

Ama baada: haikunipa nafsi yangu kunyamaza kimya baada ya kuona BAADHI YA MAKOSA YANAYOFANYWA NA NDUGU ZETU WAISLAMU WA AFRIKA YA MASHARIKI NA YA KATI KATIKA IBADA ZINAZOFANYIKA MISIKITINI. Ambapo mambo haya nitakayoyataja ni kinyume kabisa na mafundisho ya Qur’ani na sunnah ya Mtume Muhammad (S.A.W.), wala hatujayasikia wala kuyaona yakifanyika nchi za Arabuni ambapo ndio materemkio ya Wahyi ila tunayaona Afrika ya mashariki na ya kati.

Kabla ya kuanza makala yangu hii, nitatanguliza kwanza kutaja Aya ya Qur’ani na hadithi ya Mtume (S.A.W.) — Kasema Subhaana Wata’aala katika Surat-Aal-Imraan Aya Na. 104:-

يدعو} أمة منـكـم بـالـمعروف نولـتـكـن ويأمرون الـخير إلى}....... الـمنـكـر عن وينـهون

“NA WAWEPO UMMA (WATU WAISLAMU) MIONGONI MWENU WANAOLINGANIA (WANAOITA WENZAO) KWENYE KHERI, NA WANAAMRISHA KWA (MAMBO) MEMA NA WANAKATAZA (MAMBO) MABAYA……”

Na Kasema Mtume (S.A.W.):-

أصلـحه( , ) عيبا منـه رآى إذ ا الـمسلم مرآة ألخيه الـمسلم

“MWISLAMU NI KIOO CHA NDUGUYE MWISLAMU, AKIONA KASORO (YOYOTE) KWAKE AMREKEBISHE”

Inshaallah namuomba Allah (S.W.) Aniongoze kwenye haki katika makala yangu hii na iwe yenye manufaa kwa ndugu zangu Waislamu. Na kabla ya kutaja kitu kwanza napenda kubainisha ya kwamba niliyoyakusudia kuyaandika na kuyaelezea hayagusi kabisa kuponda au kudharau Waislamu wenzangu, wala hayahusiani kuashiria madhehebu yoyote katika madhehebu za Kiislamu, bali haya ni ya sheria katika sheria za Kiislamu, na wala hawakukhitalifiana wanavyuoni wa madhehebu zote za Kiislamu, bali wameafikiana ma-Imamu wa madhehebu zote za Kiislamu. Na kila jambo katika mambo nitakayoyataja nitatoa dalili na hoja za nguvu na thabit katika Qur’ani na sunnah ya Mtume (S.A.W.) kuhusu baadhi ya makosa yanayofanywa na ndugu zetu Waislamu wa Afrika ya mashariki na ya kati katika mambo ya ibada ambayo ni kinyume na makosa makubwa nimeyagundua yanafanyika misikitini, ambapo huenda ndugu zetu wanadhania kuwa ni ibada na wayafanyayo ni vitendo vyema vya kutarajia thawabu, na kumbe kinyume kabisa na wanavyofikiria.

Nabii Muhammad (S.A.W.) amewafundisha umma wake namna ya utekelezaji wa tafauti ya vitendo vya ibada na katubainishia wazi wazi. Kama Alivyosema Mtume (S.A.W.) kwamba: “Nimetumwa kuwa ni mwalimu kwenu nikufundisheni mambo ya dini yenu” Pia kama ilivyokuja katika hadithi ya Abu Hurairah ® iliyopokewa na Muslim na wengineo, Kasema Mtume (S.A.W.):-

منـاسكـكـم( ) عنـي خذ وا “CHUKUENI KUTOKA KWANGU VITENDO VYA DINI YENU” … Vitendo vya hija na vya sala na vinginevyo, kwa ujumla vitendo vyote vya ibada zote. Na kama alivyosema katika hadithi nyengine, Kasema Mtume (S.A.W.):-

ي( ) أصلـ رأيتـموني كـما وا صلـ

“SALINI KAMA MNIONAVYO MIMI NINAVYOSALI”

Na hadithi kama hizi nyingi sana alizotutajia Mtume (S.A.W.) tufuate mafundisho yake katika kila kitu katika vitendo vya ibada na mengineyo kwamba tufanye kama alivyofanya yeye, na atakayefanya jambo kinyume na mafundisho yake na amri zake basi huyo kazua lake mwenyewe lisilokuwa la sheria yake Nabii Muhammad (S.A.W.), na wala halikubaliwi kwake.

Kasema Mtume (S.A.W.):-

....) خي و الله كتـاب الحديث , رخير األمور وشر محمد هدي الهديار , , ) النـ فى ضاللـة وكـل ضاللـة بـدعة وكـل محدثـاتـها

“BORA YA HADITHI (MANENO) NI KITABU CHA MWENYEZI MUNGU, NA BORA YA UONGOFU NI UONGOZI WA (NABII) MUHAMMAD (S.A.W.), NA MAMBO MABAYA NI (YALE) YANAYOZUKA, NA KILA UZUSHI NI UPOTOFU, NA KILA UPOTOFU (UNAINGIZA) MOTONI”

Mwenyezi Mungu Atuepushe na mambo ya uzushi na upotofu anayotupambia Shetani yanayopoteza mbali na haki ambayo hayakuleta Uislamu. Sasa haina haja ya kutanguliza maelezo marefu ila nitaingia katika maudhuu (mada) moja kwa moja.

Bila ya shaka kwa asiyekuwa na ujuzi wa ilimu ya dini atashangaa na kustaajabu akiyasikia haya nisemayo atayaona ni mageni kwake kwa sababu kesha yazoea na ameyakuta yakifanyika na wazee tangu zamani, na amekulia katika mazingira ya ada hiyo na akayaitakidi kuwa ndio ni ibada sahihi, na kumbe kinyume na uhakika wa ibada iliyo sahihi, bali ni ada mbaya isiyokubaliana kabisa na sheria ya Kiislamu katika mambo ya ibada.

Jambo la mwanzo katika mambo ninayotaka kuyazungumzia na kuwazindua ndugu zangu Waislamu wa Afrika ya mashariki na ya kati wanayoyafanya kinyume na mafundisho ya sheria za Nabii Muhammad (S.A.W.)

(a) - KUSOMA QUR’ANI KWA BOMBA (CHOMBO CHA KUKUZA SAUTI) MSIKITINI SIKU YA IJUMAA WAKATI WAISLAMU WANAPOKUSANYIKA KWA AJILI YA SALA YA IJUMAA.

Kwamba kabla ya sala ya Ijumaa kwa masaa mawili au matatu au chini ya hapo, wakati watu wanapongoja hutuba ya Ijumaa na sala yake, wakati huo wanaanza kuingia msikitini, basi imamu wa msikiti au yoyote mmoja katika Waislamu atashika maik na kusoma Qur’ani. Wanaifanya ada hii kuwa ni lazima au fardhi, na hali wakati huo Waislamu wanaingia msikitini na kutanguliza sala ya tahiyyatul-Masjid na baadhi ya sala nyengine za sunna, wengine wana sala zao maalumu za sunna wanazisali wakati huo siku

ya Ijumaa, wengine wanataka kusoma Qur’ani pekee, wengine wana nyiradi zao, wengine wanataka kusoma dua zao na kumwomba Mola wao shida na mahitaji yao, wengine wanamkumbuka Mola wao kwa kumtaja kwa majina yake na sifa zake takatifu, na tafauti ya idhkaar wanazifanya Waislamu wakati huo. Sasa niambie ikiwa hapo inasomwa Qur’ani kwa sauti kubwa ya bomba, jee! Anayesali hapo ataweza kusali sala yake kwa timamu ya unyenyekevu na huku maik inapaza sauti?

Bila ya shaka anayesali wakati huo anakerwa kwa sauti kubwa ya anayesoma Qur’ani, au mwenye haja ya kusoma dua kumwomba Mola wake ataweza kuomba dua? Au kufanya idhkaar yoyote? Hapo sasa itampasa aache kusali, na akisali lazima atababaika katika sala yake, au aache kuomba dua, au aache kufanya ibada yoyote ili aisikilize Qur’ani ikisomwa. Maana tumeamrishwa kwamba tuisikiapo Qur’ani inasomwa basi tunyamaze na tuisikilize. Kasema (S.W.) katika Suratul-A’araaf Aya Na. 204:-

تـرحمون} { كـم لـعلـ وأنـصتـوا لـه فـاستـمعوا الـقـرآن قـرءى وإذا “NA ISOMWAPO QUR’ANI, BASI ISIKILIZENI NA MNYAMAZE ILI MPATE KUREHEMEWA”

Sasa hapo unamtia mtihanini Mwislamu mwenzio na kumchanganya, hajui afanye lipi katika mawili, aisikilize Qur’ani au asali? Hapa inakuwa zimemkabili amri mbili zilizo lazima kwake; amri ya kuisikiliza Qur’ani na amri ya sala ya tahiyyatul-Masjid. Kasema Mtume (S.A.W.):-

ركـعتـين( ) ي يصلـ ى حتـ يجـلس فـال الـمسجـد أحدكـم دخل إذا “ANAPOINGIA MMOJA WENU MSIKITINI, BASI ASIKAE MPAKA ASALI RAKAA MBILI (TAHIYYATUL-MASJID)”

Lazima avunje amri moja katika hizo mbili, na akisali basi hatakuwa na raha katika sala yake kwa sauti kubwa ya anayesoma Qur’ani, na lazima atababaika katika sala yake, maana sala hitaki kero ya aina yoyote. Kwa hali hii inakuwa wanawaharibia Waislamu ibada zao. Na jambo hili la kusoma Qur’ani msikitini kwa sauti kalikataza Mtume (S.A.W.) vikali sana kwa kuwaharibia Waislamu ibada zao. Katika hadithi ya Ibn Umar ® kasema ya kwamba Mtume (S.A.W.) kawatokea watu msikitini akawakuta wengine wanasali, na wengine wanasoma Qur’ani wakipaza sauti zao kwa usomaji

wa Qur’ani, akawakemea, akasema Mtume (S.A.W.) kuwaambia:-

يجهر( , وال ينـاجـيه بـما فـلـينـظـر وجل عز ه رب ينـاجـي ي الـمصلـ إنبـالـقـرآن ) بعض على بعضكـم

“HAKIKA ANAYESALI HUMNONG’ONEZA MOLA WAKE MTUKUFU, BASI NAAMPE NAFASI (MWENZIWE) KWA YULE ANAYEMNONG’ONEZA, WALA ASIPIGE KELELE (SAUTI KUBWA) NYINYI JUU YA WENGINE KWA (KUSOMA) QUR’ANI” …. Yaani msiwakere wenzenu wanaosali kwa kupaza sauti zenu kwa usomaji wa Qur’ani. Na katika hadithi nyengine kwamba siku moja Mtume (S.A.W.) alikuwa amekaa itikafu msikitini na kaweka pazia sehemu maalumu humo msikitini. Akawasikia watu wanapaza sauti zao kwa kusoma Qur’ani, basi Mtume (S.A.W.) akafungua pazia na akawatokea akasema kuwaambia:-

, بعضكـم( يرفـع وال بعضا بعضكـم يؤذين فـال ه رب منـاج كـم كـلـ إن أآلالـقراءة ) فى بعض على

“SIKILIZENI! HAKIKA NYOTE NYINYI (KILA MMOJA) ANAMNONG’ONEZA MOLA WAKE, BASI MSIUDHIANE NYINYI KWA NYINYI, WALA MSIPAZE (SAUTI ZENU) NYINYI JUU YA WENGINE KATIKA KUSOMA (QUR’ANI)”

Seuze tena imamu wa msikiti au yoyote yule anakaa kitako na kufungua chombo cha kukuza sauti anasoma Qur’ani msikitini na wengine wanasali, na wengine wanafanya idhkaar nyenginezo, wanaudhi watu na kuwaharibia ibada zao, jee! Hili ni jambo la busara? Ni sawa na kumzuia mwenzio asifanye ibada kwa sababu ya usomaji wa Qur’ani, jee! Hili si jambo la kuchusha na kuipuuza amri ya Mtume (S.A.W.)? Na anayefanya kitendo kinachomuudhi Mtume (S.A.W.) basi ndio kamuudhi Mwenyezi Mungu. Tena nimeona wengine siku ya Ijumaa wanaleta radio ya record player msikitini anatia kanda ya wasomaji wa Qur’ani wa Kimisri, kisha anaipandisha sauti ya radio kubwa kabisa mpaka masikio yanaziba kwa kelele.

Jee! Kweli hili ni jambo la busara kulifanya msikitini? Jee! Nani ataweza kusali au kufanya ibada yoyote? Wanadhani kufanya hivyo ni ibada, hali wanawaharibia watu ibada zao, wala hawatambui kwamba kitendo hiki ni kinyume kabisa na sheria ya Kiislamu, na kuipuuza amri ya Mtume (S.A.W.)

na hii ni hatari kubwa sana ya kukhalifu amri ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W.), na anayekhalifu amri yake Mtume (S.A.W.) basi anayo ahadi ya Mwenyezi Mungu ya kumsibu balaa duniani au adhabu kali ya Akhera. Kasema (S.W.) katika Surat-Annur Aya Na. 63:-

يصيبهم}.... أو فتـنة تـصيبهم أن أمره عن يخالفـون ذين الـ فـلـيحذ رأليم { عذاب

“….. BASI NAWATAHADHARI WALE WANOKHALIFU AMRI YAKE (MTUME S.A.W.) USIJE UKAWASIBU MSIBA AU IKAWAPATA ADHABU IUMIZAYO (AKHERA)” ….. Tazama katika kitabu “Asili ya Uongofu-13” tafsiri ya Surat-Annuur Aya hiyo, nimetaja maelezo marefu kuhusu hatari ya watu wanaovunja amri ya Mtume (S.A.W.) Na ada hii ya Kusoma Qur’ani siku ya Ijumaa misikitini hakuna nchi yoyote katika nchi za Arabuni zenye kufanya kitendo hiki, na bila ya shaka Waislamu wengi wa Afrika ya mashariki na ya kati wamekwenda hiji, jee! Wameona kitendo hiki kinafanyika Makka au Madina? Au nchi yoyote ya Arabuni, au watazame katika televisheni za Arabuni siku ya Ijumaa kabla ya hutuba ya Ijumaa na sala yake kama inasomwa Qur’ani misikitini. Na kama wataona basi wakati huo si wa sala ya Ijumaa bali wakati wa kawaida tu usiokuwa wa nyakati za kukaribia sala na hutuba ya Ijumaa. Hii sasa ndio inaitwa bid’aa mbaya. Maana kitendo hiki hakikutendeka katika zama za Mtume (S.A.W.) wala zama za masahaba wala taabi’in wala sehemu yoyote Arabuni mpaka leo hii, isipokuwa Waislamu wa Afrika ya mashariki na ya kati, nacho ni kitendo cha ajabu kisichokuwa na dalili yoyote ila kimezushwa, na tumetaja hadithi ya Mtume (S.A.W.) iliyotaja hatari ya kuzua jambo halikuleta Uislamu.

Ama kusoma Qur’ani misikitini kwa ajili ya kufundishana tajwidi na tartili hapana ubaya, lakini uwe katika nyakati nyengine zisiokuwa za kukusanyika Waislamu kwa ajili ya sala. Kwa mfano baada ya sala ya alasiri au baada ya sala ya alfajiri, maana nyakati hizi mbili hairuhusiwi sala yoyote ya sunna kusaliwa sheria imekataza. Kama alivyosema Mtume (S.A.W.):-

, صالة( بعد صالة وال مس الش تـغـرب ى حتـ العصر صالة بعد صالة المس ) الش تـطلـع ى حتـ الـفـجر

“HAPANA SALA (YOYOTE YA SUNNA) BAADA YA SALA YA ALASIRI MPAKA LICHWE JUA, NA WALA HAPANA SALA (YOYOTE

YA SUNNA) BAADA YA SALA YA ALFAJIRI MPAKA LIPANDE JUA”

Wakati huu ndio mzuri wa kusoma Qur’ani tajwidi au tartili na huku watu wanasikiliza au kufundishana hukumu za usomaji wa Qur’ani. Na hivi ndivyo wanavyofanya sehemu zote Arabuni. Pia inawezekana kama baada ya sala ya adhuhuri au baada ya sala ya magharibi au baada ya sala ya ishaa. Lakini sio katika nyakati za kukaribia sala , wakati huo watu wanakusanyika msikitini kungoja sala za faridha wanatanguliza kusali sala zao za sunna na baadhi ya idhakaar nyengine au kusoma Qur’ani kimya bila ya kukera wanaosali kuvuta wakati mpaka kukimiwa sala za faridha.

Haya hayajuzu kabisa kuwaharibia watu ibada zao kwa usomaji wa Qur’ani kwa chombo cha kupaza sauti msikitini, tabia hii si nzuri amekataza Mtume (S.A.W.) na hadithi zake nimekwisha zitaja, na hii ndio bid’aa yenyewe mbaya, maana kitendo hiki hakuna kabisa katika Uislamu ila kimezushwa tu. Kasema Mtume (S.A.W.):-

رد( ) فـهو أمرنـا علـيه لـيس عمال عمل من “ATAKAYEFANYA KITENDO KISICHO KUWA JUU YAKE JAMBO LETU BASI YEYE ANARUDISHWA” …. Yaani atakayefanya jambo ambalo lisilokuwa la sheria zetu, basi huyo kitendo chake kinarudishwa hakikubaliwi. Na katika hadithi nyengine kasema Mtume (S.A.W.): “Atakayefanya kitendo kisichokuwa chetu basi huyo anarudishwa nacho. Na hiki kitendo tunachokizungumzia cha kuudhi watu misikitini kuwaharibia ibada zao kwa kusoma Qur’ani kwa sauti kubwa basi ni kinyume na sheria katika Uislamu. Wanaofanya hivyo wao wanadhani kuwa ni kitendo kizuri cha kuchuma thawabu, kumbe kinyume kabisa na dhana yao, badala ya kutarajia thawabu basi wanapata madhambi. Maana kingelikuwa kitendo hiki kizuri cha kuchuma thawabu basi Mtume (S.A.W.) asingelikikataza, lakini madamu kakikataza Mtume (S.A.W.) basi ni kibaya hakina kheri yoyote ndani yake. Na kuasi amri ya Mtume (S.A.W.) basi ni hatari kubwa. Hii kwa fupi tu nimeelezea kuhusu usomaji wa Qur’ani siku ya Ijumaa msikitini, na nimetoa dalili za kutosha, na maelezo yake ni marefu sana.

(b) - Sasa nitahamia upande wa pili kuhusu mada hii hii ya kupaza sauti misikitini lakini kwa kuomba madua.

Mwenyezi Mungu Alinijaalia mwaka jana (2008) kufunga Ramadhani Dar-es-salaam nikaona jambo jengine la kushangaza! Katika mwezi wa

Ramadhani katika nyakati zote za sala ya faridha husomwa dua kwa pamoja na kwa sauti kubwa na kwa njia ya chombo cha kukuza sauti, dua hii husomwa wakati wa kukaribia sala wanapokusanyika watu msikitini kungoja sala ya faridha. Pia kitendo hiki ni kinyume kabisa na sheria za Kiislamu kuwaudhi Waislamu wanao tanguliza kusali sala zao za sunna, hii pia inawaharibia watu ibada zao, maana anayeingia msikitini anakuta kelele za kuomba dua, hapo tena itambidi aache kusali tahiyyatul-Masjid na sunna nyengine kabla ya faridha, na akisali na huku zinapigwa kelele za kuomba madua basi huyo anayesali lazima atababaika katika sala yake, maana sala haitaki makelele ya namna yoyote. Na hili pia ni kosa kubwa la kusomwa dua kwa makelele na kuwaharibia Waislamu sala zao.

Maana imamu hushika maik mkononi na waliokaa huungana pamoja na imamu kusoma dua kwa kelele kubwa mpaka masikio huziba kwa jinsi ya mkelele na kupaza sauti, kama kwamba huyo Anayeombwa kiziwi hasikii mpaka apigiwe kelele. Na kitendo hiki kimekatazwa vikali katika Qur’ani na sunna ya Mtume (S.A.W.) - Kwanza katika Qur’ani, Kasema Mwenyezi Mungu katika Suratul-A’araaf Aya Na 55:-

الـمعتـدين} { يحب ال ه إنـ وخفـية عا تـضر كـم رب ادعوا “MWOMBENI MOLA WENU KWA UNYENYEKEVU NA KWA SIRI. KWA HAKIKA YEYE (MOLA WENU) HAWAPENDI WARUKAO MIPAKA (YA UOMBAJI WA DUA)”

Na mipaka ya dua ni mingi, na baadhi yake ni hiyo ya kumuomba Mwenyezi Mungu kwa makelele na sauti kubwa, Hapendi Yeye kupigiwa kelele, kwani Yeye si kiziwi hata apigiwe kelele, wala hayuko mbali nasi, bali Yeye ni mjuzi wa siri ziliomo nyoyoni mwetu, na mjuzi wa mahitaji yetu, na mjuzi wa hali zetu. Na katika hadithi ya kwamba siku moja alikuja kwa Mtume (S.A.W.) mwarabu mmoja katika babedwi wanaoishi majangwani, akamuuliza Mtume (S.A.W.) kwamba: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Jee! Mola wako yuko karibu nasi ili tumuombe kwa sauti khafifu au ya siri atatusikia? Au yuko mbali nasi hata tumuombe kwa makelele na kwa sauti kubwa? Mtume (S.A.W.) akanyamza kidogo, basi mara tu papo hapo akateremka Jibril (A.S.) na Aya Na. 186 ya Suratul-Baqarah kujibiwa yule bedwi swali lake iliyosema :-

{ إذا الداع دعوة أجـيب قـريب ى فـإنـ ى عنـ عبادى سألـك وإذايرشدون { هم لـعلـ بـى ولـيؤمنـوا لى فـلـيستـجـيبوا دعان

“WATAKAPOKUULIZA WAJA WANGU KUHUSU HAKIKA YANGU, BASI KWA HAKIKA MIMI NIKO KARIBU (NAO). NAITIKA MAOMBI YA MUOMBAJI ANAPONIOMBA, BASI (NA WAO PIA) WANIITIKIE (WITO WANGU) NA WANIAMINI ILI WAPATE KUONGOKA” … Hizo Aya za Qur’ani zinabanisha wazi kwamba Mola wetu si kiziwi hata tumpigie makelele kwa kumuomba madua wala Hayuko mbali nasi. Na tabia hii ya kuombwa Mwenyezi Mungu kwa makelele kaikataza Mtume (S.A.W.) kwa lugha nzito. Katika hadithi iliyopokewa na Imamu Muslim, Kasema Mtume (S.A.W.):-

, , ) وال أصم تـدعون ال كـم فـإنـ أنـفـسكـم على اربعوا اس النـ ها أيعنـق, من أحدكـم إلى أقـرب قـريب سميع تـدعونـه ذي الـ إن غـائبا

راحلـتـه ) “ENYI WATU! SHUSHENI SAUTI ZENU JUU YA NAFSI ZENU, KWANI HAKIKA NYINYI HAMUMUOMBI KIZIWI WALA ASIYEKUWEPO (PAMOJA NANYI) KWA HAKIKA HUYO MNAYEMUOMBA YU KARIBU, KARIBU SANA NA MMOJA WENU KULIKO SHINGO YA NGAMIA WAKE ALIYEMPANDA” ….. Na katika hadithi nyengine kasema maneno hayo hayo, lakini kaongeza kusema Mtume (S.A.W.):-

معكـم(...... ) وهو قـريبا سميعا

“……. MWENYE KUSIKIA, YU KARIBU, NAYE YU PAMOJA NANYI”

Sasa ikiwa Mola wetu ni Mwenye sifa takatifu za ukamilifu kama hizi alizotutajia Mtume (S.A.W.) kwa nini tumuombe kwa makelele? Imetoka wapi hiyo ya kupiga makelel? Na Qur’ani yote imetaja sifa zake takatifu za kusikia na kuona, kwa nini tuache mafundisho ya mwalimu wetu mkuu Nabii Muhammd (S.A.W.) na kisha tujifanyie yetu wenyewe ya kinyume na mafunzo yake? Ambayo yanamchusha Mwenyezi Mungu. Hata ikiwa si ya kumuomba dua, bali maneno tu ya kawaida, a anaongea na mwenziwe, basi anayeongea kwa sauti kubwa basi Mwenyezi Mungu hapendezewi, na hali

hayo ni maneno tu si kuomba dua. Kasema Mtume (S.A.W.):-

الصوت( ) فيض النـ ويحب الصوت فيع الر جال الر من يكـره الله إن

“HAKIKA MWENYEZI MUNGU ANACHUKIA MIONGONI MWA WANAUME (AU WANAMKE) WENYE KUPAZA SAUTI YA JUU, NA ANAWAPENDA WENYE SAUTI KHAFIFU”

Seuze tena katika mambo ya ibada na madua Anaombwa kwa kupigiwa makelele, jee! Si tunamfanyia jambo la kumchusha? Na ikiwa tunafanya jambo la kumchusha, basi jee! Dua zetu na ibada zetu Atazipokea? Na hali kamtuma Mtumewe kutufundisha namna ya kumwomba kwa unyenyekevu na hishima? Kwa nini hatutumii neema ya akili tuliyopewa? Kwanza katika hishima kubwa Aipendayo Mola wetu ya kumuomba madua basi ni ile ya kumuomba kwa siri moyoni bila ya kutoa sauti. Kasema Mtume (S.A.W.):-

الـحفـظـة ( تـسمعه ذي الـ كـر الذ على الـخفي كـر الذ يفـضلضعفـا ) سبعين

“INAFADHILIWA ZAIDI KUMKUMBUKA (MWENYEZI MUNGU NA KUMUOMBA) KWA SIRI KULIKO ILE AMBAYO YA KUMKUBUKA (KWA SAUTI) INAYOSIKIWA NA MALAIKA WALINZI KWA MARA SABINI” …..Na katika hadithi nyengine Kasema Mtume (S.A.W.):-

ة( ) الـعالني فى دعوة سبعين تـعدل ر الس فى دعوة “(KUOMBA) DUA KATIKA SIRI LINASAWAZISHA (FADHILA YAKE ) MARA SABINI (KULIKO) DUA YA DHAHIRI “ ….. Yaani dua ya kuomba kwa siri moyoni unayomuomba Mola wako asioisikia yoyote yule katika wanadamu na hata hao Malaika wanaokulinda hawaisikii, bali aisikiaye ni Mola wako tu, basi dua hiyo ndio yenye nguvu kwa mara sabini, na ndio inayopokewa. Maana hakuna ajuaye yaliyo nyoyoni mwa viumbe ila Mwenyezi Mungu tu Peke Yake, na hivyo ndivyo apendavyo Mola wetu kumuomba kwa siri kama tulivyotaja katika Aya Na. 55 ya Suratul-A’raaf.

Vile vile sura hiyo hiyo Al-A’araaf Aya Na. 205, Mwenyezi Mungu Anamuamrisha Mtumewe Nabii Muhammad (S.A.W.) amkumbuke Mola wake kwa siri, imesema Aya hiyo:-

من} الـجهر ودون وخفـية عا تـضر نـفـسك فى ك رب كـر واذ الـقـول.......{

“NA MKUMBUKE MOLA WAKO NAFSINI MWAKO KWA UNYENYEKEVU NA KHOFU, NA BILA YA KUPIGA KELELE KWA KAULI…….”

Na kuambiwa Mtume (S.A.W.) ndio tunaambiwa sisi sote Waislamu wa umma wake, kwamba tunapomkumbuka Mola wetu kwa tafauti ya idhkaar basi tusipige kelele na kupaza sauti, khasa katika kumuomba madua tumuombe kwa siri, na ikibidi kutoa sauti basi sauti iwe khafifu sana isioweza kumkera mwenzio ukamshawishi na kumbabaisha katika ibada yake.

Basi katika kila nyakati za sala tano mwezi wa Ramadhani ukiingia msikitini unakuta kelele za kusomwa dua unashindwa hata kusali tahiyyatul-Masjid. Na dua iliyo mashuhuri inayosomwa ni ile isemayo: “ASH-HADU ANLAA ILAAHA ILLALLAAH, NASTAGHFIRUKALLAAHUMA, NAS-ALUKAL-JANNATA ILAAHI WANAUUDHU BIKA MINANNAAR, ALLAAHUMMA INNAKA AFUWWUN TUHIBUL-AFWA FA’AFU ANNAA YAA KARIIMAL-AFWU”

Naam, kweli dua hii nzuri na imethibitika, na ametuhimiza Mtume (S.A.W.) tuisome dua hii sana katika mwezi wa Ramadhani. Lakini hakuamrisha Mtume (S.A.W.) isomwe kwa pamoja msikitini na kwa sauti kubwa ya makelele, bali waisome Waislamu kila mmoja pekee na kwa siri au sauti khafifu isiosikika na mwengine ikasababisha kumkera katika sala yake au dhikri yake. Na ikiwa itabidi isomwe kwa sauti, basi

mmoja tu aisome naye ni imamu aisome kwa sauti ya kawaida na waliobakia maamuman wanyamaze kimya kuisikiliza dua inayosomwa, na katika kila mwisho wa fungu la maneno ya dua maamuman waseme “Amiim” tu wasiongeze zaidi ya Amiin hivi ndivyo inavyotakiwa na ndio hishima ya dua ya jamii.

Lakini inasikitisha usomaji wa dua hiyo inakuwa kinyume, inasomwa pamoja imamu na maamuma, tena kwa chombo cha kukuza sauti, na zinapazwa sauti kali mpaka masikio huziba, na anayesali wakati huo

huchanganyikiwa na kubabaika katika sala yake. Na kwa sheria huyo anayesali kama ana akili basi asisali bali bora kwake akae tu, maana nguzo kubwa ya sala ni unyenyekevu, na sala haisikilizani na makelele, anayesali na makelele yanapigwa, basi unyenyekevu unamtoka na kelele zitamshughulisha mpaka asijue asemalo katika sala. Sasa tabia hii inakuwa wanawaharibia watu sala zao na ibada zao nyengine. Na hili pia ni kosa kubwa la kuchuma dhambi, badala ya kutarajia thawabu ikawa kinyume chake kupata madhambi.

Ama kuhusu neno la “Amiin” baada ya imamu kusoma Suratul-Faatiha na maamuman kuitika “Amiin” kwa sauti ya kelele kali na kubwa sana, pia hili ni kosa, inatakiwa asemaye “Amiin” kwa sauti khafifu ya wastani si kwa kelele. Na maana ya “Amiin” yaani “na iwe hivyo” yaani ipokelewe au ikubaliwe dua yetu, maana Suratul-Faatiha yote ni dua. Kasema Ibn Katheer katika tafsiri yake ya Suratul-Faatiha kwamba neno la “Amiin” wamekhitalifiana wanavyuoni, wengine wanasema kuwa neno la Amiin haifai kulitamka katika sala, maana ni neno la Amiin si katika maneno ya Mwenyezi Mungu bali ni neno la wanadamu, kwa dalili ya hadithi ya Mtume (S.A.W.) iliyosema kwamba: “HII SALA YENU HAIFAI KUTIA NDANI YAKE MANENO YA WANADAMU”

Na wengine wamelithibitisha, haya ni baadhi ya khitilafu za wanavyuoni, tuyaache haya ya khitilafu, mimi sitaki kuongea kuhusu khitilafu za wanavyuoni. Kwa vyovyote vile asemaye “Amiin” haitakiwi kupaza sauti kubwa baada ya kusoma Imamu Suratul-Faatiha. Maana tunamuomba Mola wetu “Amiin” kwamba Atupokelee ibada zetu, na madamu neno hili tunamwambia Mola wetu, basi lazima tuwe na adabu na hishima ya kumwambia kwa sauti khafifu ya unyenyekevu ili Atupokelee ibada zetu. Lakini kumpigia kelele za kupita kiasi inamaana kama kwamba tunamwambia kwa hamaki na hasira, na hii inakuwa ni utovu wa adabu, maana Yeye si kiziwi hata tumpigie kelele na kupaza sauti tunaposema “Amiin”

Ukenda katika kitabu cha Imamu Al-Ghazali alichokiita “AL-ARBA’IIN FIY USUULIDDIIN” kabainisha vizuri sana kuhusu neno la “Amiin” katika sala inavyotakiwa kulisema, na kwa ufupi baadhi yake kasema Imamu Al-Ghazali kwamba sauti ya kusema “Amiin” isiwe kubwa bali iwe khafifu sana, isikike katika sikio la msemaji mwenyewe, isizidi kuipaza mpaka

ukamkera mwenzio aliyekuwa ubavuni pamoja nawe katika safu. Na mengi aliyoyasema imamu Al-Ghazali katika kitabu chake, naye ni katika madhehebu ya Shafi, naye ni mmoja katika maimamu na wanavyuoni wakubwa na pia ni mmoja katika miongoni mwa wapokezi wa hadithi za Mtume (S.A.W.) Na pia hata marehemu Sheikh Abdullah Saleh Al-Farsy kataja habari hizi katika tafsiri yake, Suratul-A’araaf Aya Na. 55, tazameni nini kasema kuhusu habari hizi.

© — Katika Sala ya tarawehe, katika kila baada ya rakaa mbili, basi wote pamoja imamu na maamuma wanapaza sauti kuisoma ile dua tulioitaja, inasomwa kwa makelele makubwa hadi masikio huziba, inakuwa kama kwamba tunayemuomba kiziwi, na tumebainisha kwa kutoa dalili za Aya za Qur’ani na hadithi za Mtume (S.A.W.) kwamba hizo kelele hazina maana wala faida yoyote ila ni kupoteza juhudi zetu za ibada. Na kwa upande mwengine hii tabia ya kuabudu kwa makelele ni kuwaigiza Ahlil-Kitaab, Mayahudi na Wakristo, wao ndio ibada zao za kupiga makelele katika makanisa yao, na ibada za makelele zinapeleka kuwa sawa na nyimbo, na Uislamu unakataza vikali kujifananisha na kitu chochote kinachohusu ibada au tabia za Mayahudi na Manasara, tusijifananishe na jambo lolote la Kiyahudi au Kinasara. Na leo sisi ikiwa tunazifanya ibada zetu kwa makelele basi tuelewe wazi kuwa bila ya shaka tunazifananisha ibada zetu kuwa sawa na wao, na hili pia ni kosa kubwa. Mtume (S.A.W.) ametukataza vikali sana tusifanane na Mayahudi na Manasara kwa kitu chochote. Kasema Mtume (S.A.W.):-

منـهم( ) فـهو بـقـوم ه تـشب من “ANAYEFANANA NA WATU (KWA CHOCHOTE KILE) BASI YEYE YU MIONGONI MWAO”

Sisi Waislamu tumewekewa sehemu au mahali pawili tu pa kunyanyua sauti zetu juu katika vitendo vya ibada. Mahali pa mwanzo tulipoamrishwa kupaza sauti zetu katika ibada za hija na Umra, kwa kufanya “talbiyah” kuitika wito wa tawhidi, kama kusema: “LABBAIKALLAAHUMMA-LABBAIKA, LABBAIKA LAA SHARIIKA-LAKA-LABBAIKA, INNAL-HAMDA WANNE’EMATA LAKA WAL-MULKU, LAA SHARIIKA-LAKA …….” Na baki ya maneno mengine kama hayo yanayotumika katika ibada ya hija na umra ndio tumeamrishwa kupaza sauti.

Na mahali pa pili, siku za idi zote mbili; ndogo na kubwa, yaani idi ya mfungo mosi na ya mfungo tatu. Tumeamrishwa kutoa sauti zetu kwa takbira na tahliilah na tasbiiha. Hizi ndio sehemu mbili tu za idhkaar kuzisoma kwa sauti kubwa na kwa pamoja. Ama ibada zote za Kiislamu ni za kimya na kwa sauti ya khafifu. Katika sala ya jamaa za faridha kama: rakaa mbili za alfajiri, na rakaa mbili za mwanzo za faridha ya magharibi, na rakaa mbili za mwanzo za faridha ya ishaa, na rakaa mbili za sala ya Ijumaa na hutuba yake, na rakaa mbili za sala zote mbili za idi ndogo na kubwa, na rakaa mbili za sala ya kupatwa jua au mwezi, na sala ya tarawehe na witri yake, na rakaa mbili sala ya kuomba mvua na hutuba yake, na hutuba ya Arafaati. Na hizi sala zote tulizozitaja basi anayetoa sauti ni imamu tu, maamuma hunyamaza kimya, ila akitajwa Mtume (S.A.W.) maamuma humsalia na kwa sauti khafifu sana, na ikisomwa dua na imamu au yoyote yule, basi maamuma husema “Amiin” kama tulivyosema hapo mwanzo. Na sauti aitoayo imamu iwe ya kawaida ya kati kwa kati si ya kupaza sana. Kama Alivyoamrisha Mwenyezi Mungu (S.W.) Katika Surat-Israa Aya Na. 110:-

} ....... { سبـيال ذلك بين وابتـغ بـها تـخافت وال بـصالتك تـجهر وال ” “…..WALA USIITANGAZE SALA YAKO KWA SAUTI KUBWA, WALA USIIFICHE KWA SAUTI NDOGO (SANA), BALI SHIKA NJIA YA KATIKATI BAINA YA HIZO (SALA ZA KUTOA SAUTI YA KAWAIDA, NA ZA SAUTI KHAFIFU)”

Ama sala ya faridha ya adhuhuri na faridha ya alasiri, na rakaa moja ya mwisho ya magharibi, na rakaa mbili za mwisho za ishaa, na sala zote za sunna zinazosaliwa na mtu pekee, na sala ya maiti, zote sala hizi zinasaliwa kimya bila ya kutoa sauti. Swali: Jee! Hizi sala tunazozisali kimya hazisikii Mola wetu? Mpaka tumpigie makelele? Bila ya shaka wewe msomaji jibu unalo wazi kabisa kwamba Mwenyezi Mungu Anasikia na kujua siri zote kama anavyojua dhahiri, hakifichikani kitu kwake, Anayajua yote tuliyoyaficha yaliyomo ndani ya nyoyo zetu.

Haya ni kwa ufupi tu, kwani maelezo yake ni marefu. Basi hivi ndivyo ulivyoamrisha Uislamu kuzifanya ibada kimya na kwa sauti khafifu bila ya kupiga kelele, na ndivyo apendavyo Mola wetu tumuabudu bila ya kumpigia kelele, Yeye Ndiye Ajuaye yaliyo nyoyoni mwetu na mjuzi wa siri zote, ikiwa tunatoa sauti khafifu au bila ya kutoa hata hiyo sauti khafifu tunamtaja moyoni tu basi Yeye Anatujua nini tusemacho kwa siri nafsini mwetu. Kama Alivyosema katika Surat-Israa Aya Na.25:-

} كـان} فـإنـه صالحين تـكـونـوا إن نـفـوسكـم فى بـما أعلـم كـم ربغـفـورا { للـألوابـين

“MOLA WENU ANAJUA SANA YALIYO KATIKA NAFSI ZENU. IKIWA NYINYI MTAKUWA WEMA, BASI HAKIKA YEYE (MOLA WENU) NI MWENYE KUWAGHUFIRIA (KUWASAMEHE) WANAOELEKEA KWAKE”

Kwa hiyo ni bora kwetu kumuabudu Mola wetu kwa sauti khafifu kama unavyoamrisha Uislamu ili kuondoa shaka na kuwa na uhakika wa kupokelewa ibada zetu, tusijaribu kuleta mambo ambayo yakatuharibia ibada zetu ikawa kazi ya bure kwa kumkumbuka Mola wetu kwa makelele na hali tunajua kwamba tunayemuabudu si kiziwi hata tumpigie makelele na hali kitabu chake na sunna ya Mtumewe (S.A.W.) vinatukataza kupiga makelele katika kumuabudu Mola wetu. Na tumetoa dalili za kutosha ingawa kwa ufupi katika Qur’ani na sunna ya Mtume (S.A.W.) na mambo haya yanafanyika katika Afrika ya mashariki na ya kati tu. Nakumbuka sana katika uhai wa mwanachuoni wetu mkubwa marehemu Sheikh Abdullah Saleh Al-Farsy, rehema ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake. Katika mwaka 1961 alikuja Dar-es-Salaam akatoa mawaidha katika msikiti wa manyema, na baadhi ya darsi yake aligusia mada hii ya kuwakataza Waislamu kuabudu Mola wao kwa makelele katika misikiti wanapata madhambi kwa kuwaharibia watu ibada zao, na katika tafsiri yake pia kataja mambo haya kama nilivyosema.

Na pia kabla ya mwaka hivi tulikuwa msikitini baada ya sala ya alasiri mmoja katika wanavyuoni wa Kimisri alikuwa akitoa darsi, basi mara wakaingia watu waliochelewa kusali sala ya jamaa ya alasiri, wakakimu sala na kusali. Basi yule mwanachuoni aliyekuwa akifanya darsi aliikata darsi yake, akasema sauti yangu ya darsi itawababaisha na kuwaharibia sala zao wanaosali, akawacha darsi kuwapa nafasi wanaosali mpaka walipomaliza sala yao, kisha akaendelea na mawaidha.

Lakini inasikitisha sana tena sana, unaingia msikitini siku ya Ijumaa unakuta mtu anasoma Qur’ani kwa chombo cha kukuza sauti kubwa, au mwezi wa Ramdhani unakuta kelele za kuomba madua kwa makelele, niambie jee! wewe unayesali utaweza kusali sala yako kwa salama? Au

unataka kusoma Qur’ani kimya peke yako, au kufanya nyiradi zako, au kuomba dua za haja zako, utaweza kufanya ibada yoyote? Na hali baadhi ya Waislamu huingoja Ijumaa kwa hamu kubwa, wana shida na matatizo yao, wana dua zao maalumu wanataka kumuomba Mola wao ili awatatulie matatizo yao, maana Ijumaa ndio siku nzuri ya kupokelewa Waislamu madua yao. Lakini ukifika msikitini unakuta makelele ya kusoma Qur’ani, unashindwa kusali sala zako za sunna, wala dua zako, wala nyiradi zako. Hili ni kosa kubwa kabisa, tena lenye madhambi.

Au mwezi wa Ramadhani anaingia Mwislamu msikitini anataka kusali sala zake za sunna na kusoma Qur’ani, kisha anakuta watu wanapiga kelele wanasoma ile dua tuliyoitaja. Inakuwa mtu hawezi kufanya ibada yoyote, na ukifanya unakerwa na kubabaishwa kwa sauti na makelele ya madua, hili pia ni kosa kubwa na ndio bid’aa mbaya. Wallahi! hatujui haya mambo wameyaleta kutoka wapi? Au dalili gani iliyoruhusu Waislamu kuabudu kwa makelele misikitini kuwaharibia watu ibada zao.

Kama nilivyosema kuwa mimi mwaka jana Mwenyezi Mungu Alinijaalia kufunga Ramadhani Tanzania, na hapo jirani yangu pana msikiti, basi nilistaajabu na kushangaa kuona mambo yaliyokuwa yakifanywa hapo msikitini kwa makelele ya kusoma madua, na siku ya Ijumaa kwa makelele ya kusoma Qur’ani, ambapo vitendo hivi sijawahi kuviona katika nchi zote nilizozitembelea za Kiislmu ila Afrika ya mashariki na ya kati tu.

Nilikuwa nashindwa kwenda mapema msikitini siku ya Ijumaa, hungoja mpaka inapokaribia hutuba kwa muda mfupi tu, na mwezi wa Ramadhani nilikuwa nashindwa kukaa msikitini kusoma Qur’ani wala kusali zile sala zangu za sunna nilizozizowea kuzisali, huzisali nyumbani na husoma Qur’ani, nikenda msikitini huenda wakati inapokaribia sala tu ya faridha, ikisha sala tu ya faridha narudi nyumbani kusali sala zangu za sunna, naukimbia msikiti kwa makelele. Kwa ufupi mimi sikuweza kuvumilia, hata siku moja niliwaita maimamu wa msikiti huo nikawaeleza na kuwaonya waache tabia hiyo, hayo wafanyayo ni vitendo vya batili na kinyume kabisa na Uislamu, na nikawapa dalili nyingi katika Qur’ani na hadithi za Mtume (S.A.W.) kwamba hayo mambo yamekatazwa vikali na Mwenyezi Mungu na Mtumewe (S.A.W.) nikawapa na kitabu changu cha tafsiri ya Qur’ni “Asili ya Uongofu-7” tafsiri ya Suratul-A’raaf Aya Na. 55 na 205, nimetaja humo maelezo marefu na hadithi nyingi za Mtume (S.A.W.) kuhusu habari

hizi za kukatazwa kuabudu kwa makelele misikitini. Lakini inasikitisha hayakuwaathiri maonyo yangu niliyowaonya, wala Qur’ani wala ya Mtume (S.A.W.), na wala hawakuacha ada yao, na imenibainikia kuwa hawakupendezewa na nasaha niliyowapa, bali waliendelea na tabia yao ile ile ya kupiga makelele na kusoma Qur’ani siku ya Ijumaa kuwaharibia watu ibada zao. Na hii ndio hatari kubwa ya kwenda kinyume na mafundisho sahihi ya Kiislamu yaliyokuja katika Qur’ani na sunna ya Mtume (S.A.W.)

Na Waislamu wanaponasihiwa basi wajibu wao kuikubali nasaha na kusema “tumesikia na tumetii” kama wao kweli wanamwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho. Na dini ya Kiislamu yote ni nasaha, kama alivyosema Mtume (S.A.W.):-

نـصيحة ( ) ه كـلـ الدين “DINI YOTE NI NASAHA”

Na leo unampa nasaha nduguyo Mwislamu anaipuuza, hii si hatari kubwa. Na haya mambo ya kukataza Uislamu kupiga makelele misikitini si mambo ya juhudi za wanavyuoni au ni khitilafu za madhehebu tu, bali madhehebu zote za Kiislamu zimewafikiana kwamba jambo hili haijuzu kufanyika kwa hali yoyote, madhehebu zote tano zinazotegemewa, nazo ni: Sahafi, Ibadhi, Hanafi, Maaliki, Hambali. Hakuna Imamu wa madhehebu yoyote aliyeruhusu jambo hili. Maana jambo lolote lile lililokwisha thibitika katika Qur’ani na sunna ya Mtume (S.A.W.) basi halina tena mjadala wa kulijadili kitu chochote, wala hakuna Imamu wa madhehebu yoyote katika madhehebu hizi tano atakayeweza kutoa rai yake ya kuliruhusu lifanyike jambo lolote kinyume na dalili thabit katika Qur’ani na sunna ya Mtume (S.A.W.) na atakayeruhusu kwa rai yake, basi huyo hasikilizwi rai yake, maana hana hoja wala dalili ya kuvunja amri ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake (S.A.W.) na wala hakuna yoyote atakayethubutu kuvunja amri zao Mwenyezi Mungu na Mtumewe (S.A.W.) Kasema Mwenyezi Mungu (S.W.) katika Suratu-Ahzaab Aya Na. 36:-

يكـون} أن أمرا لـه ورسو الله قـضى إذا مؤمنـة وال لمؤمن ماكـان , ضل فـقـد ورسولـه الله عص ي ومن أمرهم من الـخيرة لـهم

ضالالمبـينـا { “HAIWI KWA MUUMINI (YOYOTE YULE) MWANAMUME WALA MUUMINI MWANAMKE WAWE NA KHIARI KATIKA JAMBO

AMBALO MWENYEZI MUNGU NA MTUME WAKE WANAPOKATA SHAURI KATIKA JAMBO LAO. NA MWENYE KUASI (AMRI ZA) MWENYEZI MUNGU NA MTUME WAKE BASI KWA YAKINI (HUYO) AMEPOTEA UPOTOFU ULIO WAZI KABISA”

Na haya mambo ya kupiga kelele misikitini kwa kusoma Qur’ani na kuomba madua wanawababisha watu na kuwaharibia ibada zao za sala na nyiradi nyakati za sala zimekatazwa vikali na Mwenyezi Mungu na Mtumewe (S.A.W.) na nimetaja dalili thabit katika Qur’ani na sunna ya Mtume (S.A.W.) Hakuna mwanachuoni yoyote atakayethubutu aasi amri za Mwenyezi Mungu na Mtume Wake (S.A.W.) na kisha aruhusu watu wapige makelele misikitini kwa ibada yoyote ya kumwabudu Mwenyezi Mungu. Basi hao wenye tabia hii wamche Mwenyezi Mungu na Mtumewe (S.A.W.) kama wao kweli wanamwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho, basi waache tabia hii ya kupiga makelele misikitini na wawape Waislamu nafasi ya kumwabudu Mola wao kwa utulivu na unyenyekevu, wamwogope Mwenyezi Mungu na waiogope adhabu yake.

Naapa kwa Yule Aliyemtuma Nabii Muhammad (S.A.W.) kwa dini ya haki kwamba kitendo hiki cha kupiga makelele misikitini ni kitendo cha BATILI! BATILI! BATILI! Na kinamchusha Mwenyezi Mungu na Mtume Wake (S.A.W.) na kinachuma dhambi kubwa na kubatilisha sala na na vitendo vingine vya ibada na kupoteza kazi na wakati bure kisichokuwa na faida yoyote ila khasara juu ya khasara. Na huu ndio upotofu na bid’aa yenyewe, wapi wameleta dalili ya uzushi huu, au nani katika wanavyuoni wa Kiislamu walio ruhusu ada hii? Ikiwa hao wazee wetu wa zamani wameleta ada hii ikafuatwa kwa ukosefu wa ilimu, basi wazinduke Waislamu kwamba hao walioleta ada hii walikuwa katika makosa na ujinga, na Mwenyezi Mungu Awasamehe.

Watoto wanakua na kukuta kitendo hiki kinafanyika na wanafundishwa na waalimu wao kufanya ada hii, inakuwa mtoto tangu mdogo na mpaka anakua katika mazingira ya ada hii, naye anaifanya na anaitakidi kwamba hivi ndio haki na ndio ibada, na kizazi kinaendelea katika hali hii na kudhani kuwa ndio haki na sawa. Kumbe kinyume na dhana yao, bali ni kupotea mbali na haki, na wanavyuoni wanaona na wananyamaza, jee! Hakuna wanavyuoni wenye akili na kuzinduka na kukataza ada hii mbaya?

Bila ya shaka wapo wanavyuoni wakubwa katika Afrika ya mashariki na ya kati ambao wamekwenda somea ilimu ya dini katika nchi za nje, wapo

wengi waliopata nafasi za kwenda kusoma katika vyuo vikuu kama Al-Azhar Misri, na Saudi Arabia Makka na Madina na Syria na Iraq na Jordan na Qatar na Emarate na Oman na Yemen na sehemu nyingi ulimwenguni katika nchi za Kiislamu wamebobea katika ilimu, wanarudi makwao baada ya kuchuma ilimu kubwa wanakuta ada hii inafanywa na wao wananyamaza hawaikatazi ada hii mbaya, na wameishi miji hiyo ya Arabuni miaka mingi, jee! wameona vitendo hivi vinafanyika Arabuni? Au kwa ufupi tu, wameona mambo haya yanafanyika Makka na Madina ambapo miji hiyo miwili ndio mteremkio ya wahyi?

Hili ni jukumu kubwa na linakuwa juu ya wanavyuoni wa Afrika ya mashariki na ya kati kwa kunyamaza kimya na kuwaachia Waislamu kupotea kwa kufanya ada hii mbaya. Jee! Ilimu walioichukua katika vyuo vikuu vya nchi za Kiislamu kwanini hawaifanyii kazi ya kukomesha kitendo hiki kinachowapoteza Waislamu na kupata khasara? Au wanaifanyia uchoyo ilimu yao? Na hii kuficha ilimu na kutowafundisha watu basi ni hatari kubwa. Katika hadithi ya Abu Hurairah ® Kasema Mtume (S.A.W.):-

نـار( ) من بـلجام الـقيامة يوم الله ألـجمه علـما كـتـم من

“ATAKAYEIFICHA ILIMU (KUTOWAFUNDISHA WATU, BASI) MWENYEZI MUNGU HUMTATIZA SIKU YA KIYAMA KWA HATAMU YA MOTO (WA JAHANNAMU)

Na muradi wa hatamu, yaani ile kamba anayofungwa nayo farasi mdomoni na kuzunguushiwa nayo sehemu za kichwani, inashikwa na mpanda farasi ya kumwamrisha farasi kusimama au kupinda kulia au kushoto. Kwa lugha ya kisasa ni mfano wa usukani wa gari. Hii kwa upande kuhusu kuficha ilimu. Ama kwa upande mwengine, ikiwa hao wanavyuoni wanaona kitendo kibaya kinatendeka nao wananyamaza basi pia hatari yake kubwa. Katika hadithi ya Abu Musa Al-Ash’ary ® Kasema Mtume (S.A.W.):-

, يستـطع( لـم فـإن بـيده ره فـلـيغـي الـمنـكـر منـكـم رأى مناإليمان , ) أضعف وذلك فـبـقـلـبـه يستـطع لـم فـإن فـبـلسانه

“ATAKAYEONA MIONGONI MWENU BAYA (LINAFANYIKA) BASI ALIBADILI KWA (KULIKATAZA KWA) MKONO WAKE, NA IKIWA HAKUWEZA (KULIKATAZA KWA MKONO WAKE) BASI KWA

ULIMI WAKE (KWA MANENO MAZURI YA KUKATAZA), NA IKIWA HAKUWEZA BASI KWA MOYO WAKE (AWE KINYUME NA HILO BAYA LINALOFANYIKA) NA HIYO NI IMANI DHAIFU”

Jee! Hao wanavyuoni wetu wamejaribu kukataza kitendo hiki wakashindwa? Na kitendo hiki si kama cha matamanio ya upuuzi wa dunia au vinginevyo, bali ni katika kitendo kibaya kinachofanyika misikitini, lakini wao wanavyuoni wa Afrika ya mashariki na ya kati wamenyamaza kimya hawakuchukua hatua yoyote, inamaana wao wako radhi na kitendo hicho kufanyika, na siajabu bado anakitilia nguvu na kukiunga mkono. Na hii pia ni hatari kubwa sana na inakaribia kujifananisha na wanavyuoni wa Kiwana wa Kiisraili (Mayhudi) —Tunamwomba Mola wetu Atuepushe mbali na tabia ya wanavyuoni wa wana wa Israili. Kasema Mwenyezi Mungu (S.W.) katika Suratul-Maidah Aya Na. 78/79:-

ابن} وعيسى داود لسان على إسرآئيل بنى من كـفـروا ذين الـ لـعن * عن يتـنـاهون ال كـانـوا يعتـدون وكـانـوا عصوا بـما ذلك مريم

يفـعلـون { ماكـانـوا لـبـئس فـعلـوه منـكـر “WALILAANIWA WALE (WANAVYUONI) WALIOKUFURU MIONGONI MWA WANA WA ISRAILI KWA ULIMI WA (NABII) DAUDI NA (NABII) ISA BIN MARYAM. HAYO (YA KULAANIWA) KWA SABABU WALIASI NA WAKARUKA MIPAKA (YA MWENYEZI MUNGU) * HAWAKUWA WENYE KUKATAZANA MAMBO MABAYA WALIYOKUWA WAKIYAFANYA, MAOVU YALIYOJE YA MAMBO HAYO MBAYA WALIYOKUWA WAKIYAFANYA)

Mwenyezi Mungu Atuepushe na laana yake. Na hali sisi umma wa Nabii Muhammad (S.A.W.) tumepata sifa nzuri ya kukatazana mabaya kufanyika. Kama Alivyotusifu Mwenyewe Subhaanahu wa Ta’aala katika Surat-Aal-Imraan Aya Na. 110:-

عن} وتـنـهون بـالـمعروف تـأمرون اس للنـ أخرجت أمة خير كـنـتـمالـمنـكـر ........{

“NYINYI NDIO MMEKUWA BORA YA UMMA ULIOTOLEWA WA WATU (KULIKO UMMA ZOTE) MNAAMRISHA YALIYO MEMA NA MNAKATAZA YALIYO MABAYA………”

Basi nawaomba wanavyuoni wote wa Afrika ya mashariki na ya kati waungane nami waitike wito wangu huu, wajitahidi kwa uweza wao wote kuikomesha ada hii mbaya iliyokatazwa katika Qur’ani na sunna ya Mtume (S.A.W.) kwa kuabudu kwa makelele misikitini na kuwaharibia Waislamu wengine ibada zao na kuchuma madhambi na kupoteza ujira wa kazi ya ibada bure na kuzikhasirisha nafsi zao. Watenge kando mambo ya madhehebu, kwani sisi wote ni Waislamu wa umma mmoja wa Nabii Muhammad (S.A.W.) na dini yetu ni moja, na Mola wetu Mmoja, na Mtume wetu mmoja, na kitabu chetu kimoja, na kibla chetu ni kimoja. Kasema (S.W.) katika Suratul-Anbiyaa Aya Na. 92:-

فـاعبدون} { كـم رب وأنا واحدة أمة أمتـكـم هذه إن “KWA HAKIKA HUU UMMA WENU NI UMMA MMOJA TU, NA MIMI NI MOLA WENU, BASI NIABUDUNI” …. Na katika Suratul-Muuminuun Aya Na. 52 imesema maneno hayo hayo ila neno na mwisho limesema: “….BASI NIOGOPENI”

Maana ada hii wenye kuifanya waelewe wazi ya kwamba kazi yao ya ibada inapotea pa tupu na kula khasara, sawa na kutwanga maji katika kinu, wanajenga kwa mkono wa kulia na kisha wanabomowa wenyewe kwa mkono wa shoto. Kwa hiyo hili ni jukumu la kila mwanachuoni katika wanavyuoni wa Afrika ya mashariki wakataze watu ada hii kwani wanapotea mbali na njia ya haki, na sababu yake ni ukosefu wa ilimu. Sasa wenye ilimu imewalazimu wawaelimishe watu wapate kujua linalowadhuru ili waepukane nalo, wao wanadhania kufanya hivyo ndio ibada iliyo sawa na hali kinyume kabisa na sheria inavyofundisha, maana kizazi kimekulia katika mazingira ya ada hiyo mbaya kwa muda mrefu bila ya kuzinduliwa.

Na haya mambo si kama ya fiqhi hayakutajwa katika Qur’ani wala katika sunna ili wanavyuoni wafanye juhudi zao katika fiqhi ili waisibu haki. Bali haya tunayoyazungumza yametajwa na kuthibitika katika Qur’ani na sunna ya Mtume (S.A.W.) yamebainishwa wazi kabisa kama mwangaza wa jua la mchana, si ya kutiliwa shaka yoyote ukweli wake, wala hayana majadiliano ya kuyajadili baada ya Qur’ani na sunna ya Mtume (S.A.W.) - Bali maimamu wa madhehebu zote tano za Kiislamu zinazotegemewa wameafikiana. Enyi ndugu zetu Waislamu! Tumuabudu Mola wetu kwa njia iliyo sahihi kama alivyotufundisha Mtume wetu na mwalimu wetu mkuu Nabii Muhammad (S.A.W.), tusijaribu kuyabadilisha mafunzo yake na tukajifanyia yetu wenyewe ya upotofu na kuabudu kwa njia ya upofu bila ya

ilimu. Kama Alivyoamrishwa Mtume (S.A.W.) katika Surat-Yusuf Aya Na. 108:-

}........ بعنى} اتـ ومن أنـا بصيرة على الله إلى أدعوا سبـيلى هذه قـل “SEMA (EWE NABII MUHAMMAD!): HII NDIYO NJIA YANGU, NINALINGANIA KWA MWENYEZI MUNGU KWA UJUZI (KWA ILIMU) — MIMI (NAFANYA HIVI) NA WANAONIFUATA (KATIKA MAFUNDISHO YANGU HAYA)……..”

Njia sahihi ya kumuabudu Mola wetu ni kufuata mafundisho ya Nabii Muhammad (S.A.W.), na kinyume cha hapo basi ni kupotea mbali na njia ya haki. Nabii Muhammad (S.A.W.) katuachia vitu viwili hivi, navyo ni kitabu cha Mwenyezi Mungu na sunna yake, tukivishika na kuvifuata ipasavyo basi hatutapotea milele, na tukivipuuza na kujifanyia yetu wenyewe basi tumeangamia. Na kunyamaza kimya kuwaacha Waislamu kuendelea na makosa haya ndio kuwapoteza vizazi baada ya vizazi kupotea mbali na njia ya haki.

Imewapasa wanavyuoni wazinduke na kuwarekebisha Waislamu ibada iliyo sahihi, au sivyo basi jukumu liko juu ya wanavyuoni wataulizwa na Mola wao siku ya Kiyama na kushirikiana madhambi ya kuwaacha Waislamu kupotea. Maana vimekwisha pita vizazi vinaendelea kufanya ada hii batili, na wanaitakidi kwamba ibada ya kupiga makelele ndio sawa na ndio sahihi, na kumbe ndio kinyume kabisa na itikadi hii. Mwenyezi Mungu Asaidie na Atuongoe sote katika haki Amiin. Inshallah.

(d) - Jambo jengine linalofanywa mwezi wa Ramadhani lisilopendeza, nalo pia ni kosa. Kwamba: baadhi ya maimamu wa misikiti waliokuwa hawakuihifadhi Qur’ani nyingi, basi wanatumia kushika msahafu wakati anaposalisha sala ya tarawehe kuisoma Qur’ani katika sala kwa njia ya msahafu, na hili pia nalo ni kosa, wanajilazimisha kusali rakaa ishirini kwa usomaji wa kutazama msahafuni, kila siku wanasali juzu moja. Kwanza haimjuzii imamu wala maamuma kushika msahafu katika sala naye anasali, ikiwa sala ya faridha au sunna. Ibada ya sala ni ibada inayolazimika unyenyekevu mkubwa kuliko ibada zote, na nguzo kubwa ya sala ni unyenyekevu. Kasema (S.W.) katika Suratul-Baqarah Aya Na. 238:-

قـانتـين}...... { وقـوموا لله

“…… NA SIMAMENI KWA UNYENYEKEVU KWA AJILI YA (KUMUABUDU) MWENYEZI MUNGU”

Na pia kama Alivyosema Mtume (S.A.W.):-

الـخشوع( ) صالتكـم عمدة “NGUZO KUBWA YA SALA ZENU NI UNYENYEKEVU” ….. Na katika hadithi nyengine Kasema:-

, , الصالة( وعمود الصالة الدين هذا وعمود عمود شيء لكـلأتـقـاكـم , ) الله عنـد وخيركـم الخـشوع

“KILA KITU KINA NGUZO, NA NGUZO YA DINI HII NI SALA, NA NGUZO YA SALA NI UNYENYEKEVU, NA MBORA WENU MBELE YA MWENYEZI MUNGU (NI YULE) ANAYEMCHA ZAIDI (MOLA WAKE)”

Na anayebeba na kushika msahafu katika sala basi akili yake yote itamshughulisha kwa kuushika mshafu na kugeuza kurasa, na hapo basi unyenyekevu lazima utamtoka, na anaporukuu na kusujudu basi msahafu unakuwa kaushika mkononi mwake, wakati huo mkono wake wa kulia akirukuu kitanga cha mkono hakitashika vizuri futi lake la mguu ila atakipinda na baadhi ya vidole vyake, na baadhi ya vidole vingine vimeshika msahafu, na hapo sehemu ya tawi katika nguzo za sala inapunguka, kitanga na vidole vyake havikushika goti vizuri kikawaida bila ya udhuru wa sheria, si kama anaumwa kitanga au vidole hata visimfanye asiweze kushika goti lake kikawaida kwa ukamilifu, bali kwa ajili ya kushika msahafu naye anasali.

Vile vile akisujudu, basi kitanga cha mkono wake mmoja hakukitandika na kushika ardhi vizuri kwa kitanga na vidole vyote vitano, hapo pia imepunguka sehemu kubwa ya hukumu ya kusujudu, maana lazima viungo saba lazima visujudu pamoja na ipasavyo; navyo ni: kipaji cha uso na pua, vitanga vyote viwili vitandikike na vidole vyote vya kulia na kushoto vishike ardhi, magoti yote mawili, na miguu yote miwili. Kama alivyosema Mtume (S.A.W.): “NIMEAMRISHWA KUSUJUDU KWA VIUNGO

SABA” navyo ndio hivyo tulivyovitaja. Sasa huyo anayeshika mshafu katika sala kitendo hicho kinamharibia sala yake kwa dalili ya hadithi ya Mtume (S.A.W.) iliyosema:-

صالتكـم( ) في أسكنـواجوارحكـم

“VITULIZENI VIUNGO VYENU KATIKA SALA ZENU”

Na moja katika masharti makubwa ya sala ni lazima mwili na viungo vyote vya mwilini vitulie bila ya harakati yoyote isiyokuwa muhimu ya kisheria, haitakiwi harakati ya kitendo chochote katika sala kisichokuwa cha sala ila vitendo vinavyohusu sala tu, ukiongeza kitendo chochote kisichokuwa cha dharura ya kisheria basi sala inaharibika. Na kitendo cha kushika msahafu katika sala si cha sheria, na wala si cha dharura. Maana kitendo hichi hakikufanywa na Mtume (S.A.W.), kwanza Mtume (S.A.W.) hajui kusoma, wala hakijafanywa na masahaba wake, wala taabi’in, wala wanavyuoni wowote waliotangulia wala waliokuwa hivi karibuni, ila kitendo hiki kimebuniwa na wasiokuwa na ilimu ya fiqhi na wasiojua masharti ya sala. Kwa hiyo kitendo hiki kinabatilisha sala ya imamu, lakini sala za maamuman hazibatiliki, nitabainisha haya baadaye mbele tukifika mahali pake, inshaallah. Na kusema kitendo hiki kinabatilisha sala kwa dalili ya hadithi nilizozitaja kabla, na pia dalili zaidi nyengine ni hadithi hizi zifuatazo: Kasema Mtume (S.A.W.):-

قـرآنـا( ) أحفـظـهم أئمتـكـم اجعلـوا “WAFANYENI MAIMAMU WENU WENYE KUHIFADHI QUR’ANI ZAIDI” …. Na katika hadithi nyengine Kasema Mtume (S.A.W.):-

وجل( ) عز الله كتـاب أقـرأهم الـقـوم يؤم “AWE IMAMU WA WATU MWENYE KUSOMA ZAIDI KITABU CHA MWENYEZI MUNGU MTUKUFU” …. Na katika hadithi nyengine Kasema Mtume (S.A.W.):-

كـم( ) رب وبين بينـكـم وفـدكـم هم فـإنـ خياركـم أئمتـكـم اجعلـوا “WAFANYENI MAIMAMU WENU WALIO BORA KWENU, KWANI WAO NI WAGENI (VIONGOZI WASEMAJI) WENU BAINA YENU NA

BAINA YA MOLA WENU”

Kama nilivyosema kuwa hadithi nyingi sana zilizosema kuhusu habari hizi, lakini nimetaja hadithi chache tu za kuthibitisha kuwa ni dalili na hoja zilizo wazi kabisa kwamba hao wanaoshika misahafu kuisoma katika sala wamo katika makosa na wanakwenda kinyume na amri za mafundisho ya Nabii Muhammad (S.A.W.), na hadithi za Mtume (S.A.W.) ziko wazi zinabainisha kama mwangaza wa jua la mchana kwamba kitendo hiki haijuzu kutendeka katika sala.

Kama hawakuhifadhi Qur’ani nyingi katika vifua vyao, basi na wasome kiasi cha Qur’ani walioihifadhi vifuani, ingawa sura ndogo za juzu ya amma wanaweza kuzirudia kuzisoma mara kwa mara hapana ubaya kuliko kuzikalifisha nafsi zao, si lazima kusoma sura kubwa na ndefu. Kasema (S.W.) katika suratul-Muzammil Aya Na. 20:-

} ....... {. الـقـرآن من ر تـيس ما فـاقـرءوا “BASI SOMENI KILICHO CHEPESI KATIKA QUR’ANI……..”

Wasome walichokihifadhi katika Qur’ani katika sala, Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi ya mtu ila kwa uweza wake katika mambo ya ibada. Lakini wao mafundisho ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake hawayataki ila wanafanya yao wayatakayo ya kulazimisha nafsi zao kushika msahafu katika sala na kusoma sura ndefu. Na hii ni tabia ya Mayahudi na Manasara kushika vitabu na kusoma katika sala zao, na hali sisi umma wa Nabii Muhammad (S.A.W.) Mwenyezi Mungu katupa zawadi kubwa ya uhifadhi wa Qur’ani, hakuna umma wowote wa kabla yetu waliyopewa hifadhi ya kitabu cha Mwenyezi Mungu ila sisi, lakini kwa sharti mtu aweke niya ya kutaka kuihifadhi Qur’ani basi Mwenyezi Mungu Atamsaidia na kumwepesishia akaihifadhi kwa wepesi na kwa muda mfupi, na kwa ajabu hata yeye mwenyewe atastaajabu, katoa ahadi hiyo katika Surat-Qamar Aya Na. 15, 17, 22, 32:-

}( ؟} ( مدكر من فـهل للذ كـر الـقـرآن رنـا يس ولـقـد

“NA KWA YAKINI SISI TUMEIFANYA QUR’ANI IWE NYEPESI KUFAHAMIKA. BASI JEE! YUPO ANAYEKUMBUKA (HAYA)?”

Na hii ni moja katika miujiza ya Qur’ani, unampata mtoto wa umri wa miaka sita katika umma huu wa Nabii Muhammad (S.A.W.) ameihifadhi Qur’ani yote. Tukirudi kuhusu hao wanaoshika msahafu kusoma Qur’ani katika sala ya tarawehe, tena wanasali rakaa ishirini wanazikalifisha nafsi zao, itaanza sala ya tarawehe msikiti umejaa watu kiasi ya safu kumi na tano au ishirini, basi hata wakifikia rakaa nane au kumi watu wanakimbia msikitini mpaka inabaki safu moja au chini ya hapo, kwa sababu ya kusoma Qur’ani nyingi na rakaa nyingi watu wanachoka na kukimbia. Hii sasa inakuwa wanajilazimisha na kujikalifisha, na hali Mwenyezi Mungu Hakalifishi waja Wake, wala hawatakii yaliyo mazito na magumu. Kasema (S.W.) katika Suratul-Baqarah Aya Na. 286:-

}....... وسعها} إال نـفـسا الله ف يكـلـ ال“MWENYEZI MUNGU HAIKALIFISHI NAFSI YOYOTE ILA YALIYO SAWA NA UWEZO WAKE……” Na pia katika Sura hiyo hiyo Aya Na. 185:-

الـعسر}..... .....{ بـكـم يريد وال الـيسر بـكـم الله يريد “…..MWENYEZI MUNGU ANAKUTAKIENI YALIYO MEPESI, WALA HAKUTAKIENI YALIYO MAZITO……”

Na wao wanayafanya yaliyo mazito, ya kujikalifisha kwa kusoma Qur’ani nyingi katika sala na rakaa nyingi. Hata ikiwa imamu kahifadhi Qur’ani yote anaisoma bila ya kushika msahafu, basi inapoingia Ramadhani kwanza awashauri waumini maamuma wake kama watataka sala ya tarawehe ndefu ya rakaa ishirini na ya kusoma kila siku juzu moja, wakikubali maamuma wake wote, hapo tena ndio imamu ana haki ya kufanya hivyo kwa ruhusa na radhi za maamuma wake. Sio imamu mwenyewe tu akate shauri ya kuwasalisha maamuma wake sala ndefu na Qur’ani nyingi na rakaa nyingi bila ya kuwashauri maamuma wake. Maana kuna wengine hawawezi afya zao si nzuri, wengine wana kazi zao na kufanya mahitaji yao, inakuwa imamu anapata dhambi kuwalazimisha watu kuwasalisha sala ndefu kama hiyo. Na haya pia yamekatazwa na Mtume (S.A.W.) kuwasalisha watu sala ndefu.

Wanadhani kwamba kufanya hivyo ni jambo zuri na la busara, na kumbe kinyume na dhana yao, na hali Uislamu haulazimishi mtu kufanya ibada za

kuruka mipaka. Kwanza sala ya tarawehe si faridha, wala si sunna mu’akkadah, bali ni sunna mustahabbah, apendaye atasali na atapata thawabu zake, na asiyependa hasali wala hapati dhambi.

Sala ya tarawehe kaisali Mtume (S.A.W.) rakaa nane tu, na kwa muda wa siku tatu tu, kisha akaiacha, akawaambia masahaba kwamba naogopa isije ikafaridhishwa juu ya umma wangu, sitaki umma wangu kuwataabisha na kuwapa mambo yaliyo mazito. Kisha hakuisali tena mpaka amekufa Mtume (S.A.W.) Na baada ya kufa Mtume (S.A.W.) masahaba wakaifufua na kuisali. Na kama nilivyosema kuwa Mtume (S.A.W.) aliisali rakaa nane tu. Katika ukhalifa wa bwana Abu Bakar ® wakaongeza rakaa nne, wakasali jumla rakaa kumi na mbili. Na alipokufa Abu Bakar ® na kushika ukhalifa bwana Umar ® wakaongeza rakaa nne zingine, ikawa rakaa kumi na sita. Na alipokufa Umar ® na kushika ukhalifa bwana Uthmaan ® wakaongeza rakaa nne tena, wakawa wanasali rakaa ishirini. Zikawa zimebakia hizi rakaa ishirini zinasaliwa katika misikiti mitatu mitukufu, wa Makka na Madina na baitul-Maqdis npaka leo.

Lakini aghalabu zaidi ya asilimia 90% nchi zote za Kiislamu wanasali raka nane tu, na wachache wengine wanasali rakaa kumi na mbili, khasa hiyo misikiti mitatu mitukufu ndio inayosaliwa rakaa ishirini kuwa ndio misikiti iliyotermkia wahyi. Pia iko baadhi ya misikiti mingine mikubwa mashuhuri yenye wanavyuoni wakubwa na yenye vyuo katika tafauti ya fani ya mambo ya dini. Lakini aghalabu ya misikiti ya kikawaida wanasali rakaa nane tu, haina haja ya kuwalazimisha watu lazima ya kusali rakaa ishirini sala ya tarawehe. Sasa tukirudi kuhusu hao wanaojilazimisha kusali rakaa ishirini na kusoma Qur’ani nyingi kwa njia ya kushika msahafu katika sala. Nami nimetaja madhara yake na sababu zake za kutenguka au kuharibika sala za imamu anayewasalisha watu:

Jambo la mwanzo unyenyekevu unamtoka kwa kusoma haraka, pili viungo vyake havitulii katika sala kwa kuushika msahafu na kugeuza kurasa, kajipa kazi isiyokuwa na dharura ya kisheria, maana katika masharti ya sala haitakiwi mtu ajishughulishe na harakati ya jambo lolote isipokuwa vitendo vinavyohusu sala tu, na inamsababishia vipunguke viungo vilivyolazimika vishike ardhi katika kusujudu kwa sababu ya kushika msahafu unakuwa mkononi anaporukuu na anaposujudu. Tatu anajilazimisha na kuwalazimisha watu kwa kuirefusha sala rakaa ishirini. Sababu zote hizi zinatengua sala, na nimetoa dalili na hoja thabit katika Qur’ani na sunna ya Mtume (S.A.W.)

Sasa sala za namna hii za kujikalifisha kupita kiasi zimekatazwa, inakuwa ni kupoteza wakati bure bila ya faida kwa mujibu wa masharti ya sala. Kasema Ally bin Abii Taalib ® kwamba masharti ya sala aliyotutajia Mtume (S.A.W.) ni elfu kumi na mbili. Tunaomba isiwe kazi ya bure, lakini kwa dalili nilizozitoa zinathibitisha kuwa ni kazi ya bure. Na ikiwa zitakubaliwa, basi zitakubaliwa za maamuman tu, bila ya imamu, maana imamu kaongeza vitendo ambavyo vinatengua sala, na nimekwisha vitaja vitendo hivyo na kutoa dalili, inakuwa kazi yake ni ya bure kwa dalili ya hadithi ya Mtume (S.A.W.) iliyosema:-

, , ) وال فـعلـيه أساء وإن ولـهم فـلـه أحسن فـإن ضامن اإلمامعلـيهم )

“IMAMU NDIYE MWENYE JUKUMU, AKIISALI (SALA) VIZURI (KWA MASHARTI YAKE) BASI ANAPATA THAWABU YAKE (IMAMU) NA WAO (MAAMUMAN PIA) WANAPATA (THAWABU ZAO). NA IKIWA (IMAMU) ATAIHARIBU (SALA KWA UPUNGUFU WA MASHARTI YA SALA) BASI (LAWAMA) IKO JUU YAKE (IMAMU) WALA SI JUU YAO (MAAMUMAN)”

Hadithi hii iko wazi kabisa, maana imamu aliyewasalisha hakuyatimiza masharti, kaongeza yake mwenyewe yasiyotakiwa yafanywe katika sala ya kubeba na kushika msahafu mkononi mwake akirukuu nayo na kusujudu nayo na kusimama nayo, na kupunguza masharti ya kusujudu ya kitanga na baadhi ya vidole vyake havikusujudu katika ardhi kwa ajili ya kushika msahafu, na hali lazima viungo saba visujudu kwa kuviambatanisha na ardhi, kama tulivyotaja hadithi ya Mtume (S.A.W.), na kusujudu ni mahali na kitendo kitukufu sana pa kutukuzwa Mwenyezi Mungu kuliko sehemu zote za vitendo vya sala. Kama alivyosema Mtume (S.A.W.) kwamba: “MJA ANAKUWA KARIBU SANA NA MOLA WAKE ANAPOKUWA KATIKA SIJDA”

Mwaka juzi (2007) mwezi wa Ramadhani, nilikuwa nasikiliza televishen ya Iqra ya Saudi Arabia, kipindi cha moja kwa moja hewani cha “maswali na majibu” na Sheikh Dr. Abdullah Almuslih, mmoja katika wanavyuoni wa Saudia, ndiye aliyekuwa akijibu maswali. Basi mmoja aliuliza swali hili hili tunalolizungumza: “Jee! Inajuzu kusalisha imamu kashika msahafu anasoma katika msahafu katika sala?” Akajibiwa : nini kilichomfanya hata

afanye hivyo? Kama hakuhifadhi sura kubwa basi na asome hata sura ndogo, au watafute imamu aliyehifadhi Qur’ani nyingi, haimjuzii kufanya hivyo. Pia juzi katika Ramadhani hii ya mwaka huu (2009) katika Tv-Oman, Sheikh Ahmed Al-Khalili Mufti mkuu wa Oman, kaulizwa swali hili hili, naye pia akajibu haijuzu.

Kwanza ikiwa mtu anataka kufanya ibada zaidi katika ibada za sunna ziliokuwa sio sunnatul-mu’akkadah, yaani sunna ziliokuwa si lazima au si wajibu, bali sunna za kupenda au za kuongeza, kujikurubisha zaidi kwa Mola wake, basi kwanza afanye mazoezi ya kufanya ibada hiyo ndogo na nyepesi ambayo atakayoweza kudumu nayo, kuliko kujilazimisha kufanya ibada nyingi na kujitwika asichokiweza, huyu anayefanya hivi hataweza kuendelea akadumu na ibada hiyo ila baada ya muda mchache tu ataanza kushindwa na kuacha kidogo kidogo na mwisho tahamaki ataiacha kabisa kwa kujilazimisha kikubwa, siku za mwanzo tu ndio atakuwa na hamu, lakini baadae mara ataanza kuingiwa na uvivu na mwisho huacha kabisa.

Na ukitazama wewe mwanzo wa Ramadhani wale wanaosali rakaa ishirini za tarwehe na kusoma Qur’ani nyingi kila siku juzu moja kwa kushika msahafu, basi mbwembwe hizo zitakuwa katika kumi la mwanzo tu, likiingia kumi la pili utaona kasi ya ibada inapunguka, wengine baada ya rakaa nne tu wanachoka na kutoka msikitini, na kumi la pili ndio itazidi watu kupunguka, na kabla ya kuingia kumi la tatu basi watu watabakia wachache sana. Lakini ikifanywa ibada ndogo ya kati na kati, yaani wastani, si refu sana wala si fupi sana utaona idadi ya watu haipunguki tangu mwanzo wa Ramadhani mpaka mwisho, rakaa nane tarawehe, na rakaa tatu witri, jumla rakaa kumi na moja, ni kazi ya ibada nyepesi inayodumu. Kama alivyosema Mtume (S.A.W.): “NI BORA KWA MTU KUFANYA KAZI YA IBADA NDOGO NA NYEPESI AKADUMU NAYO, KULIKO KUFANYA KAZI YA IBADA KUBWA AKASHINDWA KUDUMU NAYO AKAIACHA”…...Mpaka hapa nafupisha maelezo ya jambo hili, na nimetoa dalili za nguvu zilizo wazi. Na sasa nitahamia katika jambo jengine na Allah Anisaidie inshaallah.

(e) — SALA YA WITRI: Inasikitisha sana kwamba Waislamu wa Afrika ya mashariki na ya kati hawasali sala ya witri ila katika mwezi wa Ramadhani tu, na hata katika hiyo Ramadhani hawaisali ila wachache sana, na wengine hata hawaijui kabisa sala hii ya witri. Hili ni jambo la

kushangaza na la kusikitisha sana. Ninapokuja mimi Dar-es-Salaam, katika mtaa wa makao yangu pana msikiti karibu yangu, basi husali mimi msikitini hapo, basi katika sala ya ishaa kama kawaida ikisha tu sala ya faridha ya ishaa watu wanatoka wote msikitini, hubakia watu wawili watatu tu wanasali zile rakaa mbili za suna tu, kisha nao wanaondoka. Hubaki mimi nasali sunna ya ishaa na witri, basi hujiona nimebaki peke yangu msikitini nikingojwa nimalize sala zangu ili wafunge msikiti.

Kila siku naona kitendo hiki, nami nikaona kwamba huenda nawaudhi wasimamizi wa msikiti kunisubiri peke yangu, nami nikakata shauri ya kuzisali sunna ya ishaa na witri nyumbani ili nisiwakere kwa kunisubiri, maana mimi ni mgeni, huenda hii ndio tabia yao wenyeji kufunga msikiti baada ya sala ya ishaa tu na sunna ya ishaa na witri wanazisalia majumbani kwao. Hivi ndivyo nilivyodhania mimi, kumbe kinyume na dhana yangu. Kwa hakika nilipoona hali hii nilikuwa najiuliza nafsini mwangu kwamba, tukisha maliza kusali sala ya ishaa mbona sioni watu kusali sala ya sunna wala witri? Au wanazisalia makwao? Kwa hakika sikuweza kuvumilia ninyamaze, hata siku moja nikajaribu kuwauliza maimamu wa msikiti huo, jee! Sala ya witri mnaisalia nyumbani? Mbona sioni mtu kusali sala hii? Wakastuka kuwauliza swali hili na kuwaona wameshangaa! Na wakanijibu kwamba wao hawasali sala ya witri, nikawauliza kwanini hamsali witri? Basi sikupata jibu ila wakinitazama tu, kama kwamba swali nililowauliza ni geni kwao, na kwamba si jambo muhimu kwao. Mimi kwa hakika niliathirika sana na kusikitika moyoni mwangu.

Mimi nikaona kunyamaza na kuwaacha watu wanapotea haiwezekani, Mwenyezi Mungu Ataniuliza siku ya Kiyama bila ya kuwazindua. Hata siku moja nikawaomba wahusika wa msikiti wanipe nafasi ili nifanye mawaidha hapo msikitini ili niwazungumzie kuhusu umuhimu wa sala hii ya witri. Nashukuru kwamba wamenikubalia ombi langu, nikapewa nafasi hiyo. Basi nikafanya mhadhara huo, nikawafahamisha kwa ufupi na kwa kadiri ya uwezo wangu Alionijaalia Mola wangu. Nikawabainishia ule umuhimu wa sala ya witri kuwa ni wajibu imemlazimu kila Mwislamu, na nikawatolea hoja na dalili katika Qur’ani na sunna ya Mtume (S.A.W.) na hatari ya asiyeisali sala hii ya witri. Baada ya mhadhara huo nilioufanya waliposikia yale niliyoyazungumza, basi ilikuwa kama kitu kigeni na kipya kwao hawajakisikia kabla ya hapo, na nikapata maswali ya ajabu na ya kushangaza kwa wengine, na baadhi yake kwamba jee hii sala ya witri uliotuzungumzia ina fadhila gani? Na…. na…. Ilimradi nilishangzwa sana na kusikitishwa kwa maswali yao.

Lakini mimi niliwajibu kwa mujibu na kadiri ya akili zao, maana imenibainikia kwamba wengi bado hawayajui mambo ya dini yao, na haya yanakuwa makosa ya mashekhe wenye ilimu hawashughuliki kuwaelimisha watu, khasa wale walimu wanaofundisha katika madrasa zao hawawafundishi watoto mambo muhimu ya dini yao, na baadhi yake ni hii sala ya witri ni moja katika mambo muhimu sana ya kufundishwa watoto katika madrasa na kulazimishwa waisali. Na mashekhe pia katika hutuba za ijumaa wawe wanagusia na kuwazindua Waislamu na kuwahimiza na kuwakumbusha mara kwa mara, na pia maimamu wa misikiti. Lakini jambo la kusikitisha kwamba hao mashekhe wenyewe na maimamu wa misikiti hawaisali sala hii ya witri, kwa sababu walimu wao hawakuwafundisha sala ya witri, wamekulia katika mazingira ya kusahauliwa na kupuuzwa sala hii tukufu ya witri.

Baada ya mhadhara huo niliouzungumzia kuhusu sala hii ya witri na kwa maswali ya kiajabu niliyoulizwa nikabinikiwa kwamba hawana habari kabisa ya sala hii ya witri. Nikaona bado nitajitahidi nirudie tena kufanya darsa kuizungumza mada hii ili niwabinishie zaidi, nikaona wakati mzuri ni siku ya ijumaa. Basi baada ya sala ya ijumaa nikasimama na nikazidi kuwapa maelezo na kufafanua zaidi hatari ya kutoisali sala hii.

Basi kwa rehema ya Allah, Alhamdulillaahi nikaona kwamba wameitika, na baadhi ya watu nikawaona wanaisali sala ya witri, si wote lakini yalionekana matunda kuzaa. Lakini haukuchukua muda nikaona wanaaza kupunguka kidogo kidogo. Hata niliposafiri na kurudi tena basi wote wale waliokuwa wakiisali wameiacha hakuna hata mmoja aliyeendelea kudumu nayo. Kwa hakika imenisikitisha sana na kunisononeka moyo wangu. Lakini sijakata tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu, sitakoma bali nitaendelea kuufikisha ujumbe huu wa Nabii Muhammad (S.A.W.) kwa hali yoyote na Mungu Atanisaidia inshaallah.

Ndio safari hii nimekata shauri nitayarishe makala hii na niitangaze katika magazeti ya Kiislamu ili huenda Mweneyzi Mungu (S.W.) Akajaalia nikapata mashekhe wenzangu wenye wivu katika dini ya Mwenyezi Mungu wakanisaidia kuitilia hima katika kuwatangazia Waislamu na kuwahimiza wasiipuze sala hii tukufu ya witri, kwani asiyesali sala hii ni hatari na khasara kubwa sana, kwani sala ya witri umuhimu wake ni mkubwa na unakaribia na umuhimu wa sala za faridha jinsi ilivyowajibika kwa kila Mwislamu mwanamme na mwanamke, na anayeiacha kuisali basi unamtoka

Uislamu, na nitatoa dalili za nguvu katika Qur’ani na sunna ya Mtume (S.A.W.) kuyathibitisha haya madai yangu, na Mola wangu Anisaidie kwani Yeye ni Mola Mwema na Msaidizi Mwema, Amiin.

Amri ya sala ya witri fardhiya yake ni wajibu, na wameafikiana maimamu na wanavyuoni wa madhehebu zote za Kiislamu kwamba anayeacha kuisali sala ya witri basi huyo amekufuru kufuru kubwa, maana amri ya sala ya witri imethibitika katika Qur’ani na sunna ya Mtume (S.A.W.)

Katika Qur’ani Mwenyezi Mungu Ameapa kiapo kikubwa katika Suratul-Fajr tangu Aya Na. 1 mpa ya 5:-

هل} * * * * يسر إذا يل واللـ والـوتـر فـع والش عشر ولـيال والـفـجر}( ؟ ( حجر لذى قـسم ذ لك فى

“NAAPA KWA ALFAJIRI * NA KWA MASIKU KUMI * NA KWA SHAF’I NA WITRI * NA KWA USIKU UPITAVYO * JEE! KATIKA HAYA (KUNAONEKANA KUWA) NI KIAPO KWA MWENYE AKILI (AKAOGOPA)?” …. Wenye akili tunasema: Naam! Ewe Mola wetu! Hakika kiapo chako ni kiapo kikubwa kabisa cha kuogopwa.

Hapa Mwenyezi Mungu kaapa kwa kutaja mambo matano, baadhi yake kaapa kwa sala ya witri. Mimi sitaki kuingia katika mambo yote hayo matano, bali nitaingia katika Aya Na. 3 iliyotaja “Shaf’i na witri” Aya hii imekusudia mengi yaliyotajwa na Mtume (S.A.W.) na wafasiri wa Qur’ani, na baadhi yake kaifasiri Mtume (S.A.W.) kwamba “shaf’i” ni sala za rakaa mbili mbili na nne nne, na “witri” ni sala ya witri kwa rakaa moja au tatu au tano au saba na kuendelea kwa hisabu ya witri.

Na maana ya shaf’i ni hisabu inayogawika kwa mbili mbili (kwa usawa) yaani “even numbers” Njike. Na witri ni hisabu isiyogawika kwa usawa wa mbili mbili au nne nne au zaidi, yaani “odd numbers” Ndume. Na tukididimia zaidi kubainisha kwa ufupi maana ya “witri” yaani ni Mwenyezi Mungu, Mmoja, Yu Pekee, Hana mwenzi kama Yeye, wala mfano wa kufanana Naye katika Uungu Wake na Ufalme Wake, na uweza Wake. Hana mshirika pamoja Naye katika Uungu Wake na ufalme Wake. Na witri ni moja katika majina Yake Mwenyezi Mungu matukufu. Na anayesali sala ya witri basi anakiri na kuitakidi kwa dhati ya moyo wake na kuamini ya

kwamba: Mwenyezi Mungu ni Mmoja, Yu Pekee, hakuna Mungu mwengine anayestahiki kuabudiwa kwa haki ila Yeye Peke Yake.

Na hii ndio maana ya shahada ya Uislamu, unatamka: “Ash-hadu Anlaailaaha illallaah” Na asiyesali witri inamaana kama kwamba mfano wake ni anamkanusha Mwenyezi Mungu si wa Pekee. Audhubillaahi, Mwenyezi Mungu Atukinge na kufuru hiyo ya kumfanya kuwa ana mshirika. Ametakasika na kutukuka Mwenyezi Mungu utakaso na utukufu mkubwa kabisa hata awe na mshirika katika Uungu Wake. …. Unaona sasa vipi kufuru hii inavyokuwa kubwa? Sasa tunarudi kusema kwamba asiyesali sala ya witri basi huyo amekufuru kufuru kubwa, kama nilivyosema hapo mwanzo. Ndio wameafikiana wanavyuoni wote wa madhehebu zote kwamba anayeacha kusali sala ya witri basi huyo amekufuru kukubwa. Na hii ni hatari kubwa kwa Mwislmu asiyesali sala ya witri, inakuwa hana imani ya kweli ya kumwamini Mwenyezi Mungu na Mtumewe (S.A.W.) na siku ya mwisho ambayo siku ya Kiyama. Maana anayekiri shahada ya nguzo ya mwanzo ya Kiisalamu: “Ash-hadu Anlaailaaha illallaah, wa anna Muhammadan Rasuulullaah” basi huyo kesha funga ahadi baina yake na ya Mwenyezi Mungu kwamba ameamini yote yaliyoleta Uislamu na kwamba atatekeleza amri zote za Mwenyezi Mungu na Mtumewe (S.A.W.).

Kwa hiyo ikiwa hataki kusali sala ya witri basi yeye amekwisha vunja ahadi aliyoifunga baina yake na Mola wake, na inamaana kwamba anaasi amri katika amri za Mwenyezi Mungu Alizoziamrisha juu ya waja Wake, na pia inamaana kuwa hana imani ya kweli, na imani yake ina dosari ya sifa za kinafiki. Anaamini baadhi tu ya amri za Mwenyezi Mungu na Mtumewe (S.A.W.) na baadhi ya amri nyengine anazikanusha. Na hizi ni sifa za Mayahudi Alizotutajia Mwenyezi Mungu katika Suratul-Baqrah Aya Na. 85:-

}......( ؟}..... ( بـبعض وتـكـفـرون الـكتـاب بـبعض أفـتـؤمنـون “…...JEE! MNAAMINI BAADHI YA (SHERIA ZILIOMO KATIKA) KITABU (CHA MWENYEZI MUNGU) NA (KISHA)MNAZIKATAA BAADHI YA (SHERIA) NYENGINE (ZILIOMO KATIKA) KITABU?.......” …. Na hali sifa za Waislamu wa Nabii Muhammad (S.A.W.) wamesifiwa sifa nzuri katika Sura hiyo hiyo ya Al-Baqarah Aya Na. 85 kwamba wanaamini yote yaliyokuja katika Qur’ani na sunna ya Mtume (S.A.W.), hata ukitazama katika Surat-Aal-Imraan Aya Na. 119 utazikuta sifa hizi. Sasa vipi tena hawa ndugu zetu wanajipa sifa mbaya

kama hizi za kupuuza baadhi ya amri za Mwenyezi Mungu na Mtume Wake (S.A.W.)? Hili ni jambo la kushangaza sana.

Na hali tumeamrishwa tutekeleze amri zote zilizoleta Uislamu, tusitengue hata amri moja. Kasema Mwenyezi Mungu katika Suratul-Baqarah Aya Na. 208:-

خطـوات} بـعوا تـتـ وال ة كـآفـ لـم الس فى ادخلـوا آمنـوا ذين الـ ها يآأيمبـين { عدو لـكـم ه إنـ يطـان الش

“ENYI WALE MLIOAMINI! INGIENI KATIKA HUKUMU ZA (SHERIA ZA) KIISLAMU ZOTE, WALA MSIFUATE NYAYO ZA SHETANI; HAKIKA YEYE KWENU NI ADUI ALIYE WAZI”

Siyo mkubali kutekeleza baadhi ya sheria, na baadhi ya sheria nyengine mnaziacha hamzitekelezi, hizi ni tabia na sifa za Mayahudi na Manasara, wanatekeleza baadhi tu ya sheria chache sana wazipendazo, na baadhi ya sheria nyingi wasiozipenda wanazikataa.

Na sifa za Waislamu wa kweli basi watekeleze sheria zote zilizoleta Uislamu, na waseme: “tumesikia na tumetii” Na anayekataa kufuata sheria moja tu iliyothibitika katika Qur’ani na sunna ya Mtume (S.A.W.) basi huyo kakufuru na siajabu ukamtoka Uislamu kama tutakavyoona katika hadithi za Mtume (S.A.W.) mbele yetu inshaallah.

Kwa ufupi mimi nimetoa dalili za kutosha katika Qur’ani kwamba sala ya witri ni wajibu na imemlazimu kila Mwislamu mwanamme na mwanamke lazima aisali, na asiyeisali basi huyo amekufuru. Sasa baada ya kutoa dalili za Qur’ani, pia nitatoa dalili katika sunna ya Mtume (S.A.W.) Katika hadithi iliyopokewa na jumla ya maimamu, baadhi yao Imamu Arrabi’i kutokana na Abu U’beidah, naye kutokana na Jabir bin Zeid, naye kutokana na Ibn Abbaas ®, Kasema Mtume (S.A.W.):-

الـوتـر( وهي عم النـ حمر من لـكـم خير سادسة صالة زادكـم الله إن(

“HAKIKA MWENYEZI MUNGU AMEKUZIDISHIENI SALA YA SITA, NI BORA KWENU KULIKO WANYAMA WEKUNDU, NAYO NI WITRI”

Na muradi wa “wanyama wekundu” yaani ngamia wekundu zama hizo ndio waliokuwa wanyama wenye thamani kubwa sana wa vipando vizuri na kwa ubebaji. Yaani mfano wa sasa magari yenye thamani sana kama Mercedes Benz, au BMW na mengineyo ya thamani kubwa. Tukirudi katika sala ya witri, vile vile katika hadithi nyengine Kasema Mtume (S.A.W.):-

الـقـرآن( , ) أهل يا فـأوتروا الـوتـر يحب وتـر الله إن “HAKIKA MWENYEZI MUNGU NI WITRI, ANAPENDA WITRI, BASI WITIRINI ENYI WATU WA QUR’ANI!” ….. Hizi hadithi zinathibitisha wazi kabisa kwamba sala ya witri ni wajibu na lazima kwa kila Mwislamu aisali, na anayeacha kuisali na kuasi amri hii basi huyo amekufuru kukubwa na unamtoka Uislamu kwa dalili ya hadithi ya Mtume (S.A.W.) iliyosema:-

ا(..... ) منـ فـلـيس يوتر لـم ومن “…… NA ASIYESALI (SALA YA) WITRI BASI (HUYO) SI MIONGONI MWETU”

Yaani yoyote yule anayeasi amri hii ya kusali sala ya witri basi si Mwislamu, unamtoka Uislamu. Hadithi hii pia iko wazi kabisa haina mjadala wowote wa kuikwepa sala ya witri na kuipuuza, hii ni amri katika amri za Kiislamu zilizokuwa lazima zitekelezwe. Na kama nilivyosema hapo mwanzo kwamba witri ni moja katika majina matukufu ya Mwenyezi Mungu yenye sifa za kumpwekesha, kwamba Yu mmoja, Pekee, hakuna mungu mwengine asiyekuwa Yeye, ila Yeye tu, Hana mshirika wa kumshirikisha na chochote, na Anayestahiki kuabudiwa kwa haki Peke Yake. Nayo ndiyo nguzo ya mwanzo ya Uislamu ya kumshuhudia Mwenyezi Mungu Yu mmoja tu, hakuna mungu mwengine asiyekuwa yeye. Na asiyesali sala ya witri basi inamaana anaikanusha shahada hii ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu, na hii ndio hatari kubwa kabisa.

Wameafikiana maimamu na wanavyuoni wote wa Kiislamu kwamba asiyesali sala ya witri basi amekufuru kufuru kubwa, na tumekwisha ibainisha kufuru hiyo. Mwenyezi Mungu Atuepushe na kumkufuru. ….. Na sala ya witri umepewa khiari ya rakaa upendazo kuzisali. Ama rakaa moja, au tatu, au tano, au saba, au tisa, au kumi na moja. Lakini uisali kwa hisabu

ya idadi za Ndume, yaani 1-3-5…. Kama nilivyoeleza hapo mwanzo. Na sala ya witri wakati wake kusaliwa tangu baina ya baada ya sala ya ishaa mpaka kabla ya kuingia alfjiri. Aghalabu yake zaidi wanaisali baada ya sunna ya ishaa, yaani baada ya faridha ya ishaa, kisha unasali rakaa mbili sunna ya ishaa, kisha tena unaisali sala ya witri kwa rakaa upendazo. Lakini aghalabu zaidi watu wanaisali rakaa tatu. Na mtu akisha sali sala ya witri basi hawezi kusali sala yoyote tena mpaka alale ingawa kidogo kisha anaweza kusali kama ana sala zake za sunna za naafila za usiku, au tahajjud. Na kama hakupata usingizi au hakulala kwa sababu yoyote ile na unataka kusali sunna za usiku, basi usubiri mpaka ivuke kidogo nusu ya usiku, kisha tena unaweza kusali sunna zako za usiku za tahajjud. Lakini ukimaliza kusali sala zako za usiku basi hakuna tena kusali witri tena, witri inasaliwa mara moja tu.

Na wengine wana tabia ya kuiakhirisha sala ya witri, hawaisali mapema baada ya sunna ya ishaa, bali wakiamka usiku kusali sala zao za tahajjud za usiku, wakimaliza hizo sala za usiku ndio tena wanaisali witri, inakuwa tena hawasali mpaka iingie alfajiri. Na ikiwa umelala na umekupitia usingizi mpaka ikaingia alfajiri nawe hukusali witri, basi itakubidi uilipe wakati wowote, ikiwa papo hapo ulipoamka na alfajiri imeingia, au baada ya sala ya alfajiri pia inawezekana kuilipa baada ya sala ya alfajiri, maana hili ni deni, na sala ya deni hapana ubaya kuilipa baada ya fardhi ya alfajiri. Kasema Mtume (S.A.W.):-

وقـتـها( ) فـتلـك ذ كـرها إذا فـلـيصلها عنـها نـام أو صالة نـسي من “ATAKAYEISAHAU SALA AU KALALA (UMEMCHUKUA USINGIZI SI MAKUSUDI) BASI NA AISALI ATAKAPOIKUMBUKA, KWANI HUO NDIO WAKATI WAKE” Kwa hiyo enyi ndugu Waislamu! mcheni Mola wenu na iogopeni adhabu yake, msiache kusali sala ya witri ni wajibu iliyo lazima kwa kila Mwislamu msiipuuze ni hatari hiyo, madamu nyinyi ni Waislamu mnamuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho basi itekelezeni sala hii kama mnavyozitekeleza hizo sala za faridha tano.

Wewe tazama katika safari mtu ameruhusiwa kuzipunguza sala rakaa mbili, na kuzichanganya sala mbili pamoja, na sala za sunna zote amesamehewa hazisali safarini na anapata thawabu zake, lakini sala ya witri hasameheki katika safari lazima aisali ingawa rakaa moja. Kwa sababu sala

ya witri ni wajibu iliyo lazima na ndio ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu, wengine wameipa jina kuwa ndio sala ya tawhidi. Na kama tunavyosema mara kwa mara kwamba asiyeisali basi huyo anatoka katika tawhidi, na dini ya Kiislamu ni dini ya tawhidi. Nami nimetoa dalili zilizo wazi na za nguvu katika Qur’ani na sunna ya Mtume (S.A.W.) ingawa kwa ufupi, kwani maelezo yake ni marefu sana, na hadithi ni nyingi sana zilizotaja kuhusu sala ya witri.

(f) — SALA ZA SUNNA. Vile vile inasikitisha kwamba nimeona au nimegundua asilimia 75% ya Waislamu wa Afrika ya mashariki na ya kati hawasali sala za sunna za kabla na baada ya sala za faridha amabazo amezisunisha Mtume (S.A.W.) wakisha sali tu sala yoyote ya faridha utaona papo hapo imamu akitoa salamu tu wanatoka msikitini, wengine hata hawangoji dua kusomwa, na ikisha somwa dua tu basi wote wanatoka, wanabakia wachache sana wanaobaki kusali sunna unawahisabu kwa idadi ya vidole, hata huyo imamu mwenyewe ndio wa mwanzo kutoka msikitini. Hili pia ni jambo la kusikitisha na kushangaza, maana kuna sala zingine kazisunisha Mtume (S.A.W.) zinasaliwa kabla ya sala ya faridha na baada ya faridha, nazo kama zifuatazo:

Rakaa mbili au nne kabla ya fardhi ya adhuhuri, na rakaa mbili au nne baada ya fardhi ya adhuhuri. Rakaa 4 kabla ya sala ya alasiri, baada ya fardhi ya alasiri hakuna sala yoyote ya sunna inayosaliwa mpaka lichwe jua. Rakaa mbili au nne baada ya fardhi ya magharibi, rakaa mbili au nne kabla ya fardhi ya Ishaa, na rakaa mbili baada ya fardhi ya ishaa, kisha rakaa tatu za witri kama tulivyobainisha hapo mwanzo. Rakaa mbili kabla sala ya fardhi ya alfajiri, na baada ya fardhi ya alfajiri hakuna sala ya sunna yoyote inayosaliwa mpaka lipande jua juu kiasi baada ya robo saa.

Hizo ni sala za sunna alizozisunisha Mtume (S.A.W.) kusaliwa. Lakini inasikitisha kwamba kila sala ya fardhi ikisha saliwa tu watu wanatawanyika ila wachache sana tena sana ndio wanaobaki kusali sunna. Kwanza sala za sunna ya baada ya magharibi na suna ya kabla ya sala ya alfajiri, sunna hizi mbili Mtume (S.A.W.) kazitilia mkazo sana na kutuhimiza tusiache kuzisali. Na baadhi ya wanavyuoni wanasema kwamba anayeacha kuzisali sunna hizi mbili ya baada ya magharibi na kabla ya alfajiri basi huyo amekufuru na amekhasirika khasara kubwa sana, kwani fadhila zake ni kubwa sana. Kasema Mtume (S.A.W.):-

ومافيها( ) الدنـيا من خير الـفـجر ة سنـ ركـعتـان “RAKAA MBILI SUNNA YA ALFAJIRI (MALIPO YAKE, BASI) NI BORA KULIKO DUNIA NA VYILIVYOMO NDANI YAKE”

Basi enyi wenye akili! Msiache kuzisali sala za sunna alizozisunisha Mtume (S.A.W.) kusaliwa msizipuuze kwani faida inakurudieni wenyewe kama tutakavyoona mbele tukifikia mahali pake tutataja. Inatakiwa maimamu wa misikiti wawakumbushe maamuman wao na kuwahimiza kuhusu sala za sunna. Lakini kitu cha ajabu na kushangaza kwamba huyo imamu mwenyewe akisha salisha tu sala ya faridha basi yeye wa mwanzo kutoka msikitini kabla ya maamuma wake, wala hasali sunna, anatoka upesi upesi utafikiri ana kazi muhimu , ukitoka nje unamkuta kakaa barazani anapiga porojo. Haya ninayaonamimi mwenyewe bila ya kuambiwa, ambapo inatakiwa imamu ndio awe kigezo kizuri kwa maamuma wake, asali sala za sunna ili maamuma wake wafuate kigezo chake kizuri, lakini kinyume kabisa, ikiwa imamu anafanya hivyo hasali sala za sunna jee! nini tena utatarajia kwa maamuma? Na huenda ukamkuta maamuma ni mbora zaidi kuliko huyo imamu wake. Hakika hili ni jambo la kusikitisha na kushangaza sana!!!

Jee! Huyu imamu hana habari kwamba kuna sala za sunna mu’akkadah zilizoamrishwa na Mtume (S.A.W.) zisaliwe kabla na baada ya sala za faridha? Ikiwa yeye anajua lakini hasali makusudi tu, basi huyo ana alama za kinafiki na wala haifai kufanywa awe imamu. Nini maana ya imamu? Maana yake ni kiongozi anayeongoza Waislamu kwenye kheri, awe na hima ya kuwaongoza maamuma wake na kuwazindua na kuwahimiza na kuwaelimisha maamuma wake ili wawe katika njia ya haki na ya kheri, si imamu kusalisha tu, bali awatazame maamuma wake na kuwachunga watu wake anaowasalisha akiwaona wana kasoro yoyote awarekebishe, maana yeye ndiye muulizwa na kuwa na jukumu. Kasema Mtume (S.A.W.):-

....., عن( مسؤول واإلمام ته رعي عن مسؤول كـم وكـلـ راع كـم كـلـته ,........) رعي

“NYOTE (NYINYI) NI WACHUNGAJI, NA NYOTE MNA JUKUMU KWA UCHUNGAJI WAKE…… NA IMAMU NI MWENYE JUKUMU JUU YA UCHUNGAJI WAKE (KWA WALE ANAOWACHUNGA)……..”

Au mwalimu wake aliyemfundisha mambo ya dini, hakumfundisha mwanafunzi wake habari ya sala za sunna? Haya ni mambo ya kushangaza na kusikitisha. Hebu zindukeni enyi ndugu Waislamu, kama hamjui mambo ya dini yenu basi waulizeni wenye elimu wakuongozeni ili mjue nini ibada ya kweli, hakuna aibu kuuliza, sio mnyamaze kimya na huku mnapotea na kukhasirika.

Kwanza hizi sala za sunna zina faida nyingi sana katika maisha ya dunia kwa kuongokewa na mambo yenu yakawa mepesi na kupata baraka na riziki kuongezewa na kuipata kwa wepesi, na Akhera kupata malipo mengi na mazuri. Pia vile vile hizi sala za sunna zinasaidia siku ya Kiyama kuziba mapengo katika sala za faridha zilizopunguka na kuharibika. Kasema Mtume (S.A.W.) kwamba: “kitu cha mwanzo anachoulizwa na kuhojiwa na kuhisabiwa mtu siku ya Kiyama ni sala zake za faridha, zikiwa zimepunguka sala za faridha basi Mwenyezi Mungu huwaambia Malaika Wake kwamba: Tazameni katika sala zake za sunna, kama anazo sala za sunna basi chukueni katika hizo sala zake za sunna na mzibe pengo katika sala zake za faridha zilizopunguka.

Hii ni moja katika faida inayomsaidia Mwislamu siku ya Kiyama kwa kusali sala za sunna zinavyomsaidia. Maana kuna wengine zinawapungukia sala za faridha kwa sababu nyingi, ama kwa maasi, au kwa masharti ya sala hakuyatimiza, au kwa uzembe wake mwenyewe. Sasa hizi sala za sunna zinamuokoa na kumsaidia kuziba pengo la sala za faridha zilizopunguka. Mwenyezi Mungu ni Mola Mwema Ametupa kila nafasi za kuziokoa nafsi zetu na adhabu za huko Akhera madamu bado tuko hai hapa duniani, sasa kwa nini hatuzitumii hizi nafasi hapa dunia kabla ya kufa kwetu? Kwa nini hatutaki kusali sala za sunna? Madamu Ametujaalia kuwa Waislamu basi tuelewe kwamba Mola wetu Anatupenda kwa kutuneemesha neema hii kubwa ya Uislamu. Na sehemu nyingi katika Qur’ani na sunna ya Mtume (S.A.W.) wametuzindua tusiwe wenye kukhasirika siku ya Kiyama. Baadhi yake Kasema (S.W.) katika Suratul-’Asr:-

* * وعملـوا} آمنـوا ذين الـ إال خسر لـفى اإلنـسان إن والـعصربـالصبر { وتـواصوا بـالـحق وتـواصوا الصالحات

“NAAPA KWA WAKATI * HAKIKA BINADAMU YUMO KATIKA KHASARA * ISIPOKUWA WALE WALIOAMINI NA WAKATENDA MEMA, NA WAKAUSIANA KWA (KUFUATA) HAKI NA WAKAUSIANA KWA KUSUBIRI”

Na mtu hazinduki ila siku ya kufa, anapomuona Malaika wa kumtoa roho, hapo tena ndipo anapozinduka na kujuta kwa nini hakutenda vitendo vyema alipokuwa hai duniani? Maana siku ya kufa mtu basi papo hapo macho yake yanakuwa na nguvu kubwa kupita kiasi kuliko alivyokuwa duniani, anaona kila kitu alichokuwa akikisikia duniani hakukiona na alichokuwa hakukisikia, mambo mapya ya kigeni ya ajabu atayaona papo hapo anapotolewa roho, na baadhi yake anaoneshwa hivyo vitendo vyake, na hapo hapo atajitambua kama yeye katika waliokhasirika au waliofuzu. Na siku ya Kiyama ndio siku ya majuto, watu wote siku hiyo watajuta. Mwislamu atajuta na kafiri atajuta. Kafiri atajuta kwa ukafiri wake kwa nini hakuwa Mwislamu? Na Mwislamu naye pia atajuta kwa kutofanya vitendo vyema vingi. Kasema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Surat-Maryam Aya Na. 39 Anamwambia Mtumewe Nabii Muhammad (S.A.W.) kwamba awazindue watu kuhusu siku ya majuto:-

{ ال وهم غـفـلـة فى وهم األمر قـضى إذ الـحسرة يوم وأنـذرهميؤمنـون {

“ NA (EWE NABII MUHAMMAD!) WAONYE (WATU) SIKU YA MAJUTO ITAKAPOKATWA AMRI (YA HUKUMU KWA VIUMBE) NAO HALI WAMO KATIKA GHAFLA (WAMEGHAFILIKA HAPA DUNIANI), NAO HAWAAMINI”

Nayo ndiyo siku ya Kiyama hiyo siku ya majuto, kafiri anauma mkono wake anasema laiti ningelikuwa Mwislamu nilipokuwa duniani. Na pia Mwislamu naye anauma vidole vyake naye anasema laitani ningelizidisha kufanya vitendo vyema, kama; sala za sunna zaidi, au saumu za sunna, au sadaka, au kheri yoyote ile, lakini wapitena majuto ya siku ya Kiyama yatafaa? Kafiri atatamani arudishwe duniani ili amwamini Nabii Muhammad (S.A.W.) na awe Mwislamu, na Mwislamu naye pia atatamani arudishwe duniani ili akatende vitendo vizuri zaidi. Lakini wapi tena, wamechelewa. Hapo tena Mwenyezi Mungu (S.W.) Atawaambia katika Surat-Faatir Aya Na. 37:-

} ( ؟}..... ( ذير النـ وجآءكـم ر تـذ كـ من فيه ر يتـذ كـ ما نـعمركـم أولـم

“……. JEE! HATUKUKUPENI UMRI WA KUTOSHA KUKUMBUKA MWENYE KUKUMBUKA? NA AMEKUJIENI MWONYAJI? ……”

Walipewa umri wa kutosha duniani kwa kafiri amwamini mwojaji Nabii Muhammad (S.A.W.) na asilimu na atende mema, lakini akabisha na kumkanusha. Na Mwislamu naye pia kapewa umri wa kutosha ili ajitahidi kutenda mengi zaidi yaliyo mema. Basi leo siku ya Kiyama kila mmoja atalipwa kwa mujibu wa kadiri ya vitendo vyake alivyovifanya.

Basi enyi Waislamu! zindukeni na acheni uvivu wa kuabudu, msizipuuze sala za sunna alizozisunnisha Mtume wetu (S.A.W.) na muongeze muwezavyo ili msijute na ili mpate kufuzu. Kuna wengine wenye akili wanasali kila siku rakaa mia sala za sunna tu, wengine rakaa sabini, wengine rakaa khamsini, wengine rakaa arubaini wengine thalathini wengine ishirini, na wavivu tena rakaa kumi tu kwa kutwa moja, na wengine ndio hao tunaowazungumza hawasali kabisa sala za sunna, wakisha sali sala ya faridha basi wanatoka msikitini, wanaona dhiki na tabu kubakia msikitini na kusali sunna. Kwanza Mwislamu akibaki msikitini baada ya sala ya faridha, basi Malaika wanamwombea maghufira na akibaki kwa ajili ya kusali sunna au idhkaar yoyote ya kumkumbuka Mola wake basi Malaika wanampa hongera madamu hajatenguka udhu wake. Ama wale wanaotoka msikitini upesi na wala hawasali sunna yoyote basi Malaika wanawasikitikia kwa khasara wanayojitia wenyewe. Lakini wenye akili wanashindana katika kuzidisha sala za sunna na mema mengine. Kasema Mwenyezi Mungu Katika Suratul-Mutaffifiin Aya Na 26:-

الـمتـنـافسون}...... { فـلـيتـنـافـس ذلك وفى “…….. NA KATIKA HAYO (YA KUTENDA MEMA NA KUPATA MALIPO MENGI NA MAZURI AKHERA) BASI WASHINDANE WENYE KUSHINDANA”

Basi nakuusieni kwamba ikiwa hamtaweza kushindana kwa kusali sala za sunna kwa wingi, basi msiache kusali hizo sunna chache mu’akkada alizotuamrisha Mtume (S.A.W.) za kabla na baada ya sala za faridha za rakaa mbili mbili, ili muwe na chochote cha kukusaidieni cha kuziba pengo katika sala za faridha zilizopunguka siku ya Kiyama, ili msiwe wenye

kukhasirika kabisa, na khasa sala ya witri msiache kuisali rakaa tatu au hata rakaa moja kuliko kuiacha kabisa, hiyo ni hatari. Hatukuumbwa sisi na kuletwa duniani bure tu kwa ajili ya kula na kustarehe tu, bali tumeletwa kwa ajili ya kumuabudu Mola wetu. Kasema(S.W.) katika Suratu-Adh-dhaariyaat Aya Na. 56:-

ليعبدون} { إال واإلنـس الـجن خلـقـت وما “NA SIKUWAUMBA MAJINI NA WATU ILA KWA AJILI WANIABUDU” …. Tuiogope siku ya Kiyama yenye vishindo vikubwa na majuto, hakuna kitakachomsaidia mtu siku hiyo ila amali yake nzuri tu.

(g)—NYAKATI ZILIZOKATAZWA KUSALI.

Nyakati zisizo sihi kusali, siku za joto ni nyakati tatu: Baada ya sala ya alfajiri haisihi kusali sala yoyote ya sunna mpaka lipande jua kiasi ya si chini ya dakika kumi na tano. Na pia baada ya sala ya fardhi ya alasiri haisihi kusali sala yoyote mpaka lichwe jua lizame kabisa kwa dakika tano. Na wakati wa siku za joto linapokuwa jua katikati ya mchana na kivuli kikiwa chini yako sawasawa hakikuzidi mbele wala nyuma wala kulia wala kushoto, wakati huu haijuzu kusali sala yoyote ya sunna mpaka kivuli kisogee kidogo upande. Hizi ni nyakati tatu za siku za joto haijuzu kusali kabisa amekataza Mtume (S.A.W.) - Ama siku za baridi ni nyakati mbili tu, baada ya sala ya alfajiri mpaka lipande jua, na baada ya sala ya alasiri mpaka lizame jua kama tulivyotaja.

Lakini pia inasikitisha sana Waislamu wa Afrika ya mashariki na ya kati wanasali katika nyakati hizi ambazo Mtume (S.A.W.) amekataza, na nitataja dalili katika Qur’ani na sunna ya Mtume (S.A.W.) tukifikia mahali pake inshaallah. Na hili pia ni jambo la kushangaza, hata sijui mashekhe wenye ilimu wako wapi! Katika mada iliyopita kabla ya hii tumezungumza habari ya sala za sunna mu’akkadah ambazo zilizoamrishwa na Mtume (S.A.W.) zisaliwe basi hazisaliwi, lakini hapa sasa ni kinyume, zinasaliwa sala ambazo zilizokatazwa na Mtume (S.A.W.) kusaliwa basi wao wanazisali. Swali: jee! Hili si jambo ambalo linalomchusha Mola wetu? Tunakwenda kinyume na amri zake na za Mtumewe (S.A.W.)!!!

Kila ibada tuliyowekewa na kuamrishwa kuifanya basi tumewekewa sheria zake na masharti yake na mipaka yake, sio turuke mipaka

tuliyowekewa na kisha tuabudu tupendavyo sisi kwa upofu na hali Mwenyezi Mungu katutumia Mtume Wake (S.A.W.) ametufundisha na kutubainishia kila jambo kwa uwazi na bayana kama mwangaza wa mchana. Hii ni hatari, na hapana shaka kazi ya ibada zetu inakuwa ya bure, na kuasi amri za Mtume (S.A.W.) ni hatari kubwa. Na lawama au jukumu linakuwa juu ya mashekhe au wanavyuoni wanapoona jambo linatendeka kinyume na sheria wananyamaza kimya. Kwanza nitatoa dalili katika Qur’ani na sunna ya Mtume (S.A.W.) kisha nitaendelea na maelezo inshaallah. Kasema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Surat-Annisaa Aya Na. 103:-

موقـوتـا}...... { كتـابا الـمؤمنين على كـانـت الصالة إن “……. HAKIKA SALA IMEKUWA JUU YA WAISLAMU NI FARDHI ILIYOWEKEWA NYAKATI (ZAKE) MAALUMU”

Hapa sasa Aya iko wazi kwamba sala ina nyakati zake maalumu za kusaliwa. Lakini Qur’ani haikubainisha hizo nyakati zenyewe, na Qur’rani ikitaja kitu basi inataja kwa ufupi, kisha Mtume Wake (S.A.W.) ndiye anayeifasiri Qur’ani na kutubainishia kilichotajwa katika Qur’ani. Kisha tena Mtume (S.A.W.) akatubainishia hizo nyakati zilizoruhusiwa kuzisali sala za faridha, na nyakati za kusaliwa sala za sunna, na pia kisha akatubainishia nyakati ambazo zilizokatazwa kusali. Sasa tumsikilize Mtume (S.A.W.) …. Katika hadithi sahihi na mashuhuri iliyopokewa na jumla ya maimamu, badhi yao ni Imamu Al-Rabi’i naye kutokana na Abu Ubeidah naye kutoka kwa Jabir bin Zeyd, naye kwa njia ya Ibn Abbaas ® Kasema Mtume (S.A.W.):-

, ) بعد صالة وال مس الش تـغـرب ى حتـ الـعصر صالة بعد صالة المس ) الش تـطـلـع ى حتـ الـفـجر صالة

“HAPANA SALA BAADA YA SALA YA ALASIRI MPAKA LICHWE JUA, NA HAPANA SALA BAADA YA SALA YA ALFAJIRI MPAKA LIPANDE (LITOKE) JUA” …. Hapa sasa Mtume (S.A.W.) anaifasiri na kuibainisha ile Aya ya Surat-Annisaa tulioitaja kuwa sala ina nyakati zake maalumu, na hadithi hii iko wazi kabisa kwamba nyakati hizo zilizotajwa na Mtume (S.A.W.) zimekatazwa kabisa kusali sala yoyote ya sunna. Na ukiingia msikitini nyakati hizo utakuta watu wanasali sala za sunna, si kama anasali sala imempita, bali ni sala za sunna tu, wanasali na hali wakati huo

umekatazwa kusali sala yoyote ya sunna. Sala zilizoruhusiwa kusaliwa nyakati hizo ni sala mbili tu, nazo: ni sala ya kupatwa jua, au sala ya maiti. Maana mambo haya hutokea ghafla bila ya kutarajiwa, tena kwa sharti kwamba ikiwa kumetokea kusaliwa sala hizo mbili ikiwa baada ya alasiri basi jua liwe bado liko juu kiasi ili wawahi kuisali sala hiyo kabla ya kuzama jua iwe wamekwisha maliza kusali sala hiyo, ama ikiwa wakati ni mfinyu (mfupi) hautoshelezi kuisali sala hiyo kwa sababu jua limekaribia kuzama, basi haisaliwi ikiwa sala ya maiti au ya kupatwa jua itaakhirishwa mpaka jua lizame kabisa, na hapo tena itabidi kwanza isaliwe sala ya faridha ya magharibi na sunna yake, kisha tena ndio isaliwe hiyo sala ya maiti au ya kupatwa jua. Maana wakati wa kuzama jua haijuzu kusali sala yoyote, wala hata kuzika maiti, hata ikiwa unasoma Qur’ani ukafikia katika Aya yenye kusujudu (sajdatu-tilaawa) basi haijuzu kusujudu wakati huo, uiakhirishe sijda yako mpaka lizame jua ndio uisujudu. Vile vile hukumu hii pia katika wakati wa kuchomoza jua asubuhi, wakati huo wakuchomoza jua ni marufuku kabisa kusali sala yoyote, wala kuzika, wala sajdatu-tilaawa, usubiri mpaka jua litoke na lipande juu kiasi ya dakika kumi mpaka kumi na tano, Mtume (S.A.W.) kapiga marufuku kabisa nyakati hizo kakataza katu katu. Kasema Mtume (S.A.W.):-

عنـد( أو مس الش طـلـوع عنـد ي يصلـ أن أحدكـم ى يتـحر الغـروبـها )

“ASICHUNGUZE (ASIFANYE) MMOJA WENU AKASALI LINAPOCHOMOZA JUA AU LINAPOKUCHWA (LINAPOZAMA JUA)”

Kwa mfano; kama kachelewa sala ya alasiri na wakati mfinyu na jua linakaribia kuzama, basi asisali, asubiri mpaka jua lizame kabisa ndio asali.

Au kachelewa sala ya alfajiri, kaamka na wakati mfinyu na jua linakaribia kuchomoza, basi asisali asubiri mpaka litoke jua na lipande juu kiasi, kisha tena asali kwa niya ya kuilipa sala yake. Na pia wakati huu utaona watu wanasali sala zao za sunna, na hali Mtume (S.A.W.) kakataza kabisa kusali nyakati hizi. Nami kila siku nakiona kitendo hiki kinafanyika misikitini, mimi huwauliza jee! Mnasali sala gani wakati huu? Basi wanajibu kwamba tunasali tahiyyatul-Masjid na sunna nyengine, nami huwabainishia na kuwatolea dalili za Qur’ani na sunna ya Mtume (S.A.W.) wengine wanaitika na wengine hawataki kusikia kabisa na wanakupuuza nasaha zako,

hawapendezewi kuonywa, na yote hii ni ukosefu wa ilimu, na makosa ya wanavyuoni wao au waalimu wao hawawafundishi sheria na masharti ya ibada. “Laa haula walaa Quwwata illaa billaah”

Hakuna imamu au mwanachuoni hata mmoja wa madhehebu yoyote ya Kiislamu atakayeweza kutoa ruhusa ya kusali sala yoyote katika nyakati hizo, na hata kama atatoa rai au sababu ya kuruhusu kusali ingawa tahiyyatul-masjid basi huyo rai yake haikubaliwi kwa vyovyote vile madamu Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W.) kakikataza kitendo hiki, na hadithi za Mtume (S.A.W.) ziko wazi kabisa hata ikiwa huyo imamu awe na ilimu vipi basi hatasikilizwa.

Maana hakuna yoyote awezaye kuvunja amri ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W.) - kwani amri zake Mtume (S.A.W.) ndio amri za Mwenyezi Mungu, neno lolote litokalo kinywani mwake basi ni ufunuo wa wahyi utokao kwa Mola wake. Kasema (S.W.) katika Surat-Annajm Aya Na 3-4:-

يوحى} * { وحى إال هو إن الـهوى عن ينـطق وما “(NABII MUHAMMAD) WALA HASEMI KWA MATAMANIO * HAYAKUWA HAYA (ASEMAYO) ILA NI UFUNUO (WAHYI) ULIOFUNULIWA (KWAKE)” ….. Na katika Suratul-Hashr Aya na 7:-

قـوا}..... واتـ فـانـتـهوا عنـه نـهاكـم وما فـخذ وه سول الر آتـاكـم وماالـعقـاب { شديد الله إن الله

“……. NA ANACHOKUPENI (ANACHOKUAMRISHENI) MTUME BASI KIPOKEENI, NA ANACHOKUKATAZENI BASI JIEPUSHENI NACHO. NA MCHENI MWENYEZI MUNGU, HAKIKA MWENYEZI MUNGU NI MKALI WA KUADHIBU (KWA ANAYEVUNJA AMRI YA MTUME WAKE)”

Hasemi Mtume (S.A.W.) kwa upuuzi bali ni amri amemrishwa na Mola wake. Kwa hiyo madamu Mtume (S.A.W.) ametukataza kusali nyakati hizo basi tuache na tuseme: “tumesikia na tumetii” Hiyo Aya ya Suratul-Hashr inatuhadhadharisha, kama ilivyotuhadharisha Aya Na. 63 ya Surat-Annur tulioitaja katika kukatazwa kusoma Qur’ani msikitini kwa makelele, iliyosema: “….BASI WATAHADHARI WALE

WANAOKHALIFU AMRI YAKE (MTUME) USIJE UKAWASIBU MSIBA (WA BALAA HAPA DUNIANI) AU IKAWAPATA ADHABU IUMIZAYO (AKHERA)”

Sasa ikiwa Mwenyewe Mwenyezi Mungu Anatuhadharisha vikali na kwa tisho kubwa la kupata adhabu kali, bado hatusikii tunandelea tu kuvunja amri ya Mtumewe (S.A.W.) tunasali katika nyakati tulizokatazwa? Kwa nini hatutumii neema ya akili tukafikiri? Huku siko kuchamungu, bali haya ni maasi ya dhahiri na tunazipuuza amri za Mola wetu katika Qur’ani na katika sunna ya Mtume Wake (S.A.W.) - Swali: Jee! Ikiwa sisi tunavunja amri za Mtumewe (S.A.W.) makusudi, inamaana tunafanya jambo la kumchusha Mola wetu, basi jee! sala zetu zitakubaliwa? Enyi ndugu zangu! Hamtii akilini?

Katika hadithi ya Ibn Abbaas ® kwamba siku moja alikuwa msikitini imekwisha adhini adhana ya alfajiri, wanavuta wakati kungoja sala ya faridha ya alfajiri, basi akaingia mtu mmoja msikitini akasali yule mtu rakaa nne kabla ya faridha ya sala ya alfajiri na wakati huo imekwisha adhiniwa adhana ya alfajiri na watu wanakusanyika kwa ajili ya kusali sala ya alfajiri. Basi Ibn Abbaas ® akamuuliza yule mtu kwamba: Nimekuona umesali rakaa nne, jee! umesali sala gani hiyo? Akasema yule mtu: Nimesali tahiyyatul-masjid rakaa mbili na sunna ya alfajiri rakaa mbili. Akasema Ibn Abbaas ® kumwambia yule mtu kwamba: Jee! Hujui kuwa umefanya makosa, umekwenda kinyume na sunna ya Mtume (S.A.W.)? kisha akamtajia hadithi ya Mtume (S.A.W.) iliyosema:-

تـطـلـع( ى حتـ وفـريضتـه الـفـجر سنـة إال صالة ال الـفـجر دخل إذامس { الش

“ IKIINGIA ALFAJIRI HAKUNA SALA (INAYOSALIWA) ILA SUNNA YA ALFAJIRI NA FARIDHA YAKE MPAKA LIPANDE JUA”

Basi yule mtu akasema kumwmbia Ibn Abbaas ® kwamba: jee! Kwani Mwenyezi Mungu Ataniadhibu kwa ajili ya kusali? Ibn Abbaas ® akamjibu yule mtu kwamba: Mwenyezi Mungu hakuadhibu kwa ajili ya kusali, lakini atakuadhibu kwa sababu ya kukhalifu sunna ya Mtume Wake (S.A.W.) …. Na Ibn Abbaas ® ni sahaba mwanachuoni mkubwa aliye mstari wa mbele kabisa katika masahaba wa Mtume (S.A.W.) aliyekuwa pamoja na Mtume (S.A.W.) tangu mdogo wa umri wa miaka kumi mpaka amekufa Mtume

(S.A.W.) hakuachana naye.

Pia siku moja katika mwaka 1996 nilialikwa msikiti wa Bezeredi mwembe ladu Zanzibar kutoa mawaidha, nikatoa mawidha kiasi ya mada mbili hivi, moja katika hizo mada niligusia habari hizi za kusali watu katika nyakati zilizokatazwa kusali. Baada ya mawaidha imamu wa msikiti huo ambaye sasa ni marehemu, Mwenyezi amuweke mahali pema katika waja wake wema Peponi Amin. Basi alinihoji kuhusu mada hii, akaniambia kwamba taihiyyatul-masjid imeruhusiwa katika nyakati hizo, mimi nikamuuliza, jee! Unayo dalili ya ruhusa hiyo? Akasema anayo, akainuka akenda niletea kitabu akanionesha, jina la kitabu hicho na jina la shekhe aliyekitunga kitabu hicho nimekwisha lisahau, kwani muda mrefu upepita tangu tukio hili. Huyo shekhe aliyetunga kitabu hicho kaandika katika kitabu chake kwamba inajuzu kusali tahiyyatul-Masjid katika nyakati hizo, lakini hakutaja dalili yoyote ya kuthibitisha ruhusa hiyo. Na yoyote yule anapodai jambo basi lazima ataje hoja na dalili zake. Mimi nikamwambia: mbona huyu shekhe aliyetunga kitabu hiki hakutaja dalili yoyote kutokana na Qur’ani au sunna ya Mtume (S.A.W.)? Yule imamu akasem inatosha maneno ya shekhe aliyetunga kitabu hiki ni shekhe mashuhuru na tunamtegemea. Mimi nikamwambia kweli sheke anategemewa, na Mwenyezi Mungu amjazi kheri kwa juhudi zake, lakini nami nakuuliza pia jee! Huyu shekhe aliyetunga kitabu hiki ni mjuzi zaidi kuliko Nabii Muhammad (S.A.W.) aliyeteremshiwa wahyi?

Basi akakwama hakuweza kunijibu kunijibu swali langu, mimi nikamwambia kwamba suala hili la kukatazwa kusali katika nyakati zilizokatazwa kusali sala yoyote ya sunna limethibitika katika hadithi sahihi za Mtume (S.A.W) na nikamtajia kiasi ya hadithi tatu nne hivi, na nikambainishishia kwamba katika hadithi zote hizo za Mtume (S.A.W.) za kukataza hakutaja hata katika hadithi moja neno la: “isipokuwa” waarabu wanasema “istithnaa” nikampigia mfano kwamba ingelikuwa hadithi imesema: “Hapana sala baada ya sala ya alasiri mpaka lichwe jua, na hapana sala baada ya sala ya al-fajiri mpaka lipande jua, “ISIPOKUWA” tahiyyatul-masjid”

Ingelisema hadithi hivyo basi kweli ruhusa ingelipatikana ya kusali katika nyakati hizo, lakini hakuna hata hadithi moja iliyosema neno la “isipokuwa” na wala hakuna hata mwanachuoni mmoja aliyefasiri hata hadithi moja ya Mtume (S.A.W.) katika hadithi hizi zilizokataza kusali nyakati hizo, na wala hakuna hata hadithi moja iliyodhoofishwa, bali

hadithi hizo zote ni sahihi na zimekubaliwa na wapokeaji wote mashuhuri wa hadithi za Mtume (S.A.W.) na wala hakuna hadithi moja katika hizo zinapingana, bali kila hadithi iliyotaja habari hizi zote zinaungana na kutiliana nguvu zenyewe kwa zenyewe, na zote zina maana ya kukataza.

Na dalili iliyo kubwa zaidi ni hiyo Aya ya Surat-Annisaa Na. 103 niliyoitaja iliyosema: “…..HAKIKA SALA IMEKUWA JUU YA WAISLAMU NI FARDHI ILIYOWEKEWA NYAKATI (ZAKE) MAALUMU” …. Aya hii inaungana na kusikilizana na hadithi za Mtume (S.A.W.) — Maana wewe ukitaka kujua hadithi ya Mtume (S.A.W.) kuwa ni sahihi basi itazame hiyo hadithi jee! Inasikilizana na Qur’ani? Ikiwa imesikilizana na kuafikiana na Qur’ani basi kweli hiyo ni hadithi sahihi ya kutegemewa. Na Kasema Mtume (S.A.W.):-

حديثي( خالـفـه أعرضوا وما ي منـ فـهو وافـقـه فـما الـقـرآن علىي ) منـ فـلـيس

“ITAZAMAMENI HADITHI YANGU KATIKA QUR’ANI, IKIWA IMEWAFIKIANA NA QUR’ANI BASI HIYO INATOKA KWANGU, NA IKIWA IMEIKHALIFU (HAIKUWAFIKIANA) NA QURANI BASI HAIKUTOKA KWANGU” …. Na hizo hadithi tulizozitaja za kukataza kusali katika nyakati zilizokatazwa zote zinawafikiana na Aya ya Surat-Annisaa tuliyoitaja. Na nilipombainishia kielimu basi akayakubali na kukiri kwamba kweli nyakati hizo haijuzu kusali sala yoyote ya sunna. Maana nimemuona ni msomi mwenzangu ndipo nikamfahamisha kielimu.

Wewe ukitaka jambo lolote kulijua uhakika wake basi nenda katika Qura’ani tu na sunna ya Mtume (S.A.W.) basi jambo lako utalipata tu bila ya shaka yoyote. Kasema Ibn Abbas ® kwamba ikiwa ngamia wangu kanipotea basi nikenda katika Qur’ani nitampata tu.

Tukirudi katika mada yetu ya kukatazwa kusali katika nyakati hizo, na ikiwa mtu kaingia msikitini nyakati hizo zilizokatazwa kusali, basi badala ya kusali tahiyyatul-masjid kuna maneno matakatifu ya kusema yanayoshika mahali pa tahiyyatul-masjid, nayo unasema: “Subhaanallaahi, Wal-hamdulillaahi, Walaailaaha illallaahu, Wallaahu Akbar” …. Unayasema mara nne yanatosheleza kuwa badala ya tahiyyaau-masjid kwa dalili ya

hadithi ya Mtume (S.A.W.) iliyosema:

, , ؟( ة الـجنـ رياض وما قيل فـارتـعوا ة الـجنـ بـرياض مررتـم إذا : , , وال والـحمد لله الله سبحان قـال تـع؟ الر وما قيل الـمساجـد قـال

أكـبر ) والله الله إال إلـه “MKIPITA KWENYE BUSTANI ZA PEPONI BASI JIBURUDISHENI!” Akauluzwa: Nini bustani za Peponi? Akasema: “MISIKITI” Akaulizwa: Nini kujiburudisha? Akasema: “SUBHAANALLAAHI, WALHAMDULI- LLAAHI, WALAAILAAHA ILLALLAAH, WALLAAHU AKBAR” ….. Na katika hadithi nyengine limeongezeka neno moja zaidi, nalo: “WALAA HAWLA WALAA QUWWATA ILLAA BILLAAH” …. Haya ndio maneno yanasemwa mara nne Mwislmu akiingia msikitini katika nyakati zilizokatazwa kusali badala ya tahiyyaatul-masjid. Na haya ndio “BAAQIYAATU-SSAALIHAAT” amali nzuri ibakiayo kwa Mola wako yenye thawabu na matumaini bora yaliyotajwa katika Suratul-Kahf Aya Na. 46. Tazama katika kitabu “Asili ya Uongofu-12” tafsiri ya Aya hiyo nimeyaelezea huko.

Sasa tukirudi katika kuzinduana, basi kitu kikisha thibitika katika sunna ya Mtume (S.A.W.) ikiwa cha amri ya kukatazwa basi tukiache na tuepukane nacho, na cha amri ya kufanya basi tukifanye bila ya mjadala tena wa kujadili, wala kusikilizwa rai ya mwanachuoni yoyote baada ya ya Qur’ani na sunna ya Mtume (S.A.W.) Mbona huku Arabuni hakuna mambo haya? Ambapo huku ndio materemkio ya wahyi kwa Manabii na Mitume. Na haya wameafikiana wanavyuoni wa madhehebu zote za Kiislamu, maana haya si mambo ya juhudi na khitilafu za kimadhehebu, bali yamethibitika wazi katika Qur’ani na sunna.

Na sababu au hikma ya kukatazwa kusali nyakati hizo tulizozitaja, tusizifananishe ibada zetu na makafiri wale wanaoabudu jua na mwezi na nyota nyingine za sayari. Kasema Mwenyezi Mungu (S.W.) katika Surat-Fussilat Aya Na. 37:-

إن}..... خلـقـهن ذى الـ واسجدوا لله للقـمر وال مس للش تـسجدوا التـعبدون { اه إي كـنـتـم

“…… WALA MSILISUJUDIE JUA WALA MWEZI, NA MSUJUDIENI MWENYEZI MUNGU AMBAYE ALIYEVIUMBA, IKIWA NYINYI (KWELI) MNAMUABUDU YEYE (MWENYEZI MUNGU) TU”

Basi enyi ndugu Waislamu! Acheni kusali katika nyakati zilizokatazwa, mcheni Mwenyezi Mungu na mtii amri zake na za Mtume Wake, msiende kinyume na amri zao, wao ndio wenye kujua hikima na siri ya kutukataza, sisi hatujui chochote, wajibu wetu sisi ni kusema: “tumesikia na tumetii” na kutekeleza amri zao.

(h)—KUHUSU NGUO NDEFU KATIKA SALA

Hili jambo la kuvaa nguo ndefu mpaka inafunika vifundo vya miguu linapendwa sana na Waislamu wanaume, na hali limekatazwa na Mtume (S.A.W.) kwa lugha kali sana, na amri hii inapuuzwa sana na Waislamu wengi, wanadhani ndio umaridadi na ndio pambo zuri la vazi, na hali wameafikiana wanavyuoni wa madhehebu zote za Kiislamu kwamba anayevaa nguo ndefu ikiwa kanzu au kikoi au suruali ikafunika vifundo vya miguu basi huyo sala yake haikubaliwi. Na hadithi zilizokataza jambo hili ni nyingi sana, lakini nitataja chache tu ili kuthibitisha haya tusemayo.

Katika hadithi iliyopokewa na jumla ya maimamu, miongoni mwao imamu Muslim kwa njia ya sahaba Abii Dharr, Kasema Mtume (S.A.W.):-

(...... وخسروا( , , خابوا وخسروا خابوا وخسروا خابوا “WAMEHARIBIKIWA NA WAMEKHASIRIKA! WAMEHARIBIKIWA NA WAMEKHASIRIKA! WAMEHARIBIKIWA NA WAMEKHASIRIKA!........”

Masahaba walipomsikia Mtume (S.A.W.) anasema maneno ya kutisha namna hiyo tena ameyarudia mara tatu na uso wake mtukufu upepiga wekundu kwa ghadhabu, basi masahaba nyoyo zao zilidunda na kuwajaa khofu, wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Nani hao walioharibikiwa na kukhasirika hivyo?! ….. Akaendelea Mtume (S.A.W.) kusema:-

يهم( يزكـ وال الـقيامة يوم إلـيهم ينـظـر وال الله مهم يكـلـ ال ثـالثـة أليم ) عذاب ولـهم

“ (WATU NAMNA) TATU: MWENYEZI MUNGU HATAWASEMESHA (MANENO MAZURI), WALA HATAWATAZAMA (KWA JICHO LA REHEMA) SIKU YA KIYAMA, WALA

HATAWATAKASA (MADHAMBI YAO), NAO WATAPATA ADHABU (KALI) IUMIZAYO” …. Kisha akanyamaza kidogo, masahaba hawakuweza kuvumilia kwa khofu, wakasema tena: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Nani hao? Kisha Mtume (S.A.W.) akasema:-

الـكـذب( , , بـالـحلف سلـعتـه والـبائع ان والـمنـ ) الـمسبـل

“MWENYE KUVAA NGUO NDEFU (MPAKA IMEFUNIKA VIFUNDO VYA MIGUU), Masahaba walipomsikia Mtume (S.A.W.) anasema maneno ya kutisha namna hiyo tena ameyarudia mara tatu na uso wake mtukufu upepiga wekundu kwa ghadhabu, basi masahaba nyoyo zao zilidunda na kuwajaa khofu, wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Nani hao walioharibikiwa na kukhasirika hivyo?! ….. Akaendelea Mtume (S.A.W.) kusema:-

يهم( يزكـ وال الـقيامة يوم إلـيهم ينـظـر وال الله مهم يكـلـ ال ثـالثـة أليم ) عذاب ولـهم

“ (WATU NAMNA) TATU: MWENYEZI MUNGU HATAWASEMESHA (MANENO MAZURI), WALA HATAWATAZAMA (KWA JICHO LA REHEMA) SIKU YA KIYAMA, WALA HATAWATAKASA (MADHAMBI YAO), NAO WATAPATA ADHABU (KALI) IUMIZAYO” …. Kisha akanyamaza kidogo, masahaba hawakuweza kuvumilia kwa khofu, wakasema tena: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Nani hao? Kisha Mtume (S.A.W.) akasema:-

الـكـذب( , , بـالـحلف سلـعتـه والـبائع ان والـمنـ ) الـمسبـل

“MWENYE KUVAA NGUO NDEFU (MPAKA IMEFUNIKA VIFUNDO VYA MIGUU), Masahaba walipomsikia Mtume (S.A.W.) anasema maneno ya kutisha namna hiyo tena ameyarudia mara tatu na uso wake mtukufu upepiga wekundu kwa ghadhabu, basi masahaba nyoyo zao zilidunda na kuwajaa khofu, wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Nani hao walioharibikiwa na kukhasirika hivyo?! ….. Akaendelea Mtume (S.A.W.) kusema:-

يهم( يزكـ وال الـقيامة يوم إلـيهم ينـظـر وال الله مهم يكـلـ ال ثـالثـة أليم ) عذاب ولـهم

“ (WATU NAMNA) TATU: MWENYEZI MUNGU HATAWASEMESHA (MANENO MAZURI), WALA HATAWATAZAMA (KWA JICHO LA REHEMA) SIKU YA KIYAMA, WALA HATAWATAKASA (MADHAMBI YAO), NAO WATAPATA ADHABU (KALI) IUMIZAYO” …. Kisha akanyamaza kidogo, masahaba hawakuweza kuvumilia kwa khofu, wakasema tena: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Nani hao? Kisha Mtume (S.A.W.) akasema:-

الـكـذب( , , بـالـحلف سلـعتـه والـبائع ان والـمنـ ) الـمسبـل

“MWENYE KUVAA NGUO NDEFU (MPAKA IMEFUNIKA VIFUNDO VYA MIGUU), HATAWATAKASA (MADHAMBI YAO) NAO WATAPATA ADHABU ILIYO KALI SANA” …….Na katika Surat-Aal-Imraan Aya Na. 77:-

خالق} ال أولـئك قـليال ثـمنـا وأيمانهم الله بـعهد يشتـرون ذين الـ إن وال الـقيامة يوم إلـيهم ينـظـر وال الله مهم يكـلـ وال اآلخرة فى لـهم

أليم ) عذاب ولـهم يهم يزكـ “HAKIKA WALE WANAOUZA AHADI YA MWENYEZI MUNGU NA VIAPO VYAO KWA (AJILI YA) THAMANI NDOGO (YA MAISHA YA DUNIA), HAO HAWATAKUWA NA SEHEMU YOYOTE (YA KHERI) KATIKA AKHERA, WALA MWENYEZI MUNGU HATAWASEMESHA (MANENO MAZURI), WALA HATAWATAZAMA (KWA JICHO LA REHEMA) SIKU YA KIYAMA, WALA HATAWATAKASA (MADHAMBI YAO), NAO WATAPATA ADHABU (KALI) IUMIZAYO”

Basi miongoni mwao hao wanaoasi amri ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W.) na kuvaa nguo ndefu, kama hawatatubu basi watapata adhabu kali sawa na hao Mayahudi na Manasara na wanafiki zilizotajwa katika Aya hizi tulizozitaja, na kwa dalili ya hadithi ya Mtume (S.A.W.) tuliyoitaja. Na hukumu hii ya kukatazwa kuvaa nguo ndefu kwa wanaume tu, haiwagusi wanawake, maana wanawake wameamrishwa wavae nguo ndefu za kustiri miili yao na mapambo yao ya mikononi na miguuni yasionekane. Kama walivyoamrishwa katika Surat-Annuur Aya Na. 31. tazama katika kitabu “Asili ya Uongofu-13” tafsiri ya Surat-Annuur, nimebainisha habari hizi huko kwa urefu.

Tukirudi kuhusu wanaume kukatazwa kuvaa nguo ndefu, kisha akasema Mtume (S.A.W.):-

ار( ) النـ في الـكـعبين أسفـل ما “(NGUO) INAYOZIDI (MPAKA) CHINI YA VIFUNDO VYA MIGUU BASI KATIKA MOTO (WA JAHANNAM)” ….. Yaani nguo iliyozidi mpaka ikafunika vifundo vya miguu, basi sehemu hiyo ya viungo tangu vifundoni mpaka chini vitapata adhabu ya moto wa Jahannam kwa asiyetii amri hii. Akaendelea Mtume (S.A.W.) kuwahadharisha umma wake, Akasema:-

, أصاب( شيء كـل فـإن فـلـيرفـعه إزاره مسبـال أحدكـم صلى إذاار ) النـ فى فـهو منـه األرض

“ANAPOSALI MMOJA WENU NA KIKOI CHAKE KIMEREFUKA CHINI, BASI AKIINUE JUU (AKIPANDISHE), KWANI KILA KITU (CHA NGUO) IKIGUSA CHINI BASI (KIUNGO HICHO) KINAINGIA MOTONI” Ilipokuja amri hii ya kukatazwa kuvaa nguo ndefu wanaume, bwana Abubakar ® alikuwa akipenda kuvaa nguo ndefu, basi akamwambia Mtume (S.A.W.): Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Hata ikiwa sina kiburi nami navaa nguo ndefu jee ni vibaya kwangu? Mtume (S.A.W.) akamjibu bwana Abu Bakar ® kwamba: Halitoki neno lolote mdomoni mwangu ila ni ufunuo, amri imetoka kwa Mwenyezi Mungu. Basi akasema bwana Abu Bakar ®: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Wewe ni baba yangu na mama yangu, “nimesikia na nimetii”

Na leo aghalabu ya Waislamu wanaume zaidi ya asilimia 75% ndio wenye kuvaa nguo ndefu, kama kanzu au kikoi au suruali, utaona nguo imefunika miguu kabisa, akitembea inaburura katika ardhi, tangu imamu mwenyewe na maamuma nguo zao ndefu, na wachache sana ndio wenye kuvaa nguo za sawa za urefu wa kawaida inayotakiwa kuvaa.

Mimi kila mara huwapigia kelele pale msikitini tangu imamu na maamuma wapandishe nguo zao juu inapokimiwa sala, wengine wanaitika na wengine wanapuuza. Siku moja nilikuja msikitini nimechelewa kidogo, naingia na sala inakimiwa, tukasali, imamu alikuwa hayupo lakini alitusalisha kijana mmoja, yeye husali na sisi hapo msikitini mara kwa mara, basi ilipokwisha sala nikamuona nguo aliyoivaa ndefu kupita kiasi

ilikuwa suruali imefunika miguu yake, nikamwita upande na nikamwabia kwamba hiyo nguo yake haimjuzii kusalia kabisa na ile sala aliyotusalisha yeye arudie kuisali, ama sisi maamuma sala zetu inshaallah zimekubaliwa, maana jukumu liko juu ya imamu si juu ya maamuma, na nikamtolea dalili za hadithi za Mtume (S.A.W.) ambazo nitazitaja tukifika mahali pake. Basi yule kijana akanijibu kwamba nguo refu haidhuru chochote ikiwa sina kiburi. Nikamwambia wewe si mbora kuliko Khalifa wa Mtume (S.A.W.) bwana Abu Bakar ® alimjibu Mtume (S.A.W.) kama ulivyonijibu mimi. Nikamweleza kisa cha Abu Bakar ® basi hakupendezewa na ile nasaha yangu. Sasa hii yote ni ukosefu wa ilimu na kupuuza amri za Mtume (S.A.W.)

Wameafikiana wanavyuoni wa madhehebu zote tano za Kiislamu kwamba anayesali na nguo yake ndefu imefunika vifundo vya miguu basi huyo sala yake haikubaliwi, na kazi ya ibada yake imeharibika na kupotea pa tupu, na dalili ni hiyo hadithi ya Mtume (S.A.W.) niliyoitaja iliyosema mwanzo wa maneno yake: “Wameharibikiwa na wamekhasirika” tena katamka mara tatu kuhakikisha kwamba kazi za ibada ya sala zao zimeharibika na wamekhasirika, hakuna watakachokipata ila ghadhabu ya Mwenyezi Mungu Hatawasemesha siku ya Kiyama, wala Hatawatazama, wala Hatawasamehe madhambi yao, na malipo yao ni moto wa Jahannam tu. Jee! Huo ndio mwisho mwema? Bali ni mwisho mbaya kabisa wa kupata khasara kubwa. Yote kwa sababu ya kiburi cha kuvaa nguo ndefu, maana mwanamme anayevaa nguo ndefu mpaka ikafikia katika vifundo vya miguu, basi huyo ni miongoni mwa wenye viburi, na alama yao ni hizo nguo wanazozivaa. Kasema Mtume (S.A.W.) kwamba: “HAINGII PEPONI MWENYE KIBURI KATIKA MOYO WAKE HATA KAMA YA CHEMBE (NDOGO)”

Wanavyuoni wengine wamesema ya kwamba maamuma aliyesali nyuma ya imamu aliyevaa nguo ndefu basi airudie kuisali sala yake kuilipa. Na wengine wanasema kwamba si lazima maamuma airudie sala kuilipa ikiwa kasali nyuma ya Imamu aliyevaa nguo ndefu, sala ya maamuma inakubaliwa inshaallah madamu imamu kaisalisha sala kisheria kwa ukamilifu, lakini imamu mwenyewe ndio sala yake haikubaliwi kwa sababu ya maasi yake ya kuvaa nguo ndefu na hali imekatazwa. Kwa dalili ya hadithi ya Mtume (S.A.W.) iliyosema:-

وفـاجـر( ) بار كـل خلـف وا صلـ

“SALINI NYUMA YA KILA (IMAMU) MWEMA NA MUOVU” Kwa

sharti huyo imamu hakuiharibu sala, kaisali kisheria na kazitimiza nguzo muhimu za sala, kwa vitendo na kusoma. Lakini yeye imamu kazi yake inakuwa ya bure. Kama tulivyoitaja hadithi ya Mtume (S.A.W.) hapo mwanzo, na hapa tutairudia kuitaja tena iliyosema:-

, ) وال فـعلـيه أساء وإن ولـهم فـلـه أحسن فـإن ضامن اإلماعلـيهم )

“IMAMU NDIYE MDHAMINI (MWENYE JUKUMU), AKIISALI (SALA) VIZURI (KWA MASHARTI YAKE) BASI ANAPATA THAWABU YAKE (IMAMU) NA WAO (MAAMUMA PIA) WANAPATA (THAWABU ZAO). NA (KAMA IMAMU) ATAIHARIBU (SALA) KWA UPUNGUFU WA MASHARTI YAKE) BASI LAWAMA IKO JUU YAKE (IMAMU) WALA SI JUU YAO (MAAMUMAN)”

Lakini ikiwa watu wamemuona imamu nguo yake ndefu kabla ya kuanza sala, basi aambiwe imamu asisalishe wakati huo na atangulie kusalisha yoyote pale mwenye nguo ya kawaida isiyokuwa ndefu, na imamu ikiwa atabisha lazima asalishe yeye, basi maamuman wakatae wasisali nyuma yake, bali wasali peke yao, na hapo imamu atapata dhambi kubwa kabisa ya kuwafarikisha Waislamu na kusababisha mzozo huo. Na maamuman wana haki ya kumtoa kwa nguvu huyo imamu mbishi katika mihrabu na kusalisha mwengine. Na ikiwa maamuman wataona vibaya kuchukua hatua hiyo kwa kumhishimu, wakamwacha awasalishe basi wote imamu na maamuman sala yao haikubaliwi, maana wameyaridhia maasi ya imamu na kushirikiana katika kuasi amri ya Mtume (S.A.W.) - Maana hakuna huruma wala kuhishimiwa wala mapendeleo kwa yoyote yule anayeasi amri ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W.)

Basi enyi wenye akili mwogopeni Mwenyezi Mungu tangu imamu na maamuman waache na wakome kuvaa nguo ndefu katika sala, au kazi yenu ya ibada itakuwa ya bure na kuchuma madhambi zaidi, kama kweli nyinyi waumini kweli basi mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake (S.A.W.) hakuna maskhara katika kutekeleza sheria za Mwenyezi Mungu na Mtumewe (S.A.W.)

Kwa upande mwengine; kuna watu wengine wanasali na nguo zenye picha za wanadamu au wanyama au makatuni auviumbe vyenye roho, au maneno ya upuuzi yameandikwa katika nguo, ikiwa mbele kifuani au nyuma

mgongoni. Haya ndio makosa makubwa sana. Mtume (S.A.W.) amekataza kuvaa nguo yenye picha au michoro ya viumbe vyenye roho, analaaniwa anayevaa nguo za namna hiyo, seuze tena unaingia nayo nguo hiyo katika nyumba ya Mwenyezi Mungu, msikitini na kusali nayo, huyo laana ya Mwenyezi Mungu iko juu yeke, haikubaliwi sala yake wala ibada yake yoyote. Waache Waislamu kuvaa nguo kama hizo za kikafiri, na watubu kwa Mola wao, ni hatari kubwa sana kumwingizia Mwenyezi Mungu mapicha katika nyumba yake takatifu ya ibada ambayo ni msikiti. Hata katika nyumba kama ina masanamu au picha za kuchorwa za viumbe basi Malaika hawaingii nyumba hiyo. Kasema Mtume (S.A.W.):-

وصور( ) ثيل تـما فيه بيتـا تـدخل ال الـمالئكـة إن “HAKIKA MALAIKA HAWAINGII NYUMBA NDANI YAKE YAMO MASANAMU AU MAPICHA” ….. Na hadithi nyingi sana zilizotaja habari hizi za makatazo. Seuze tena unaingia msikitini na nguo uliyoivaa ina picha, vipi Mwenyezi Mungu Ataikubali sala yako na hali unamfanyia mambo ya kumchusha?

Vile vile wameafikiana wanavyuoni wa madhehebu zote za Kiislamu kwamba haijuzu mtu kuwa imamu anasalisha watu na hali hana ndevu anazinyoa, na kunyoa ndevu ni moja katika maasi ambayo yanayotengua sala, ni sawa na maasi ya kuvaa nguo ndefu kama tulivyosema. Na wamesema wanavyuoni kwamba maasi ya kunyoa ndevu yanakusanya madhambi ya namna mbili: Maasi ya namna ya mwanzo ni ya kuasi amri ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W.) kwa dalili ya hadithi ya Mtume (S.A.W.) iliyosema:-

حا( ) اللـ واعفـوا وارب الش احفـوا “PUNGUZENI MASHARUBU, NA MZIACHE NDEVU (MSIZINYOE)” ….. Na katika hadithi nyengine Kasema Mtume (S.A.W.):-

شيئـا( ) منـه تـأخذ وا وال حي اللـ اعفـوا “ZIACHENI NDEVU WALA MSIZIPUNGUZE KITU KATIKA HIZO”

Pia hadithi nyingi zimetaja kuhusu kukatazwa kunyoa ndevu, na hii ni amri imethibitika katika sunna ya Mtume (S.A.W.) …. Masahaba walikuwa

wakiwekeana zamu kukaa na Mtume (S.A.W.) ili wasipitwe na jambo katika amri. Basi ilipokuja amri ya kufuga ndevu na kukata masharubu, bwana Umar bin Khattaab ® alikuwa hayupo siku hiyo, naye alikuwa anafuga masharubu marefu mpaka yamemfunika mdomo. Aliporudi kutoka safari zake akawakuta masahaba wamekaa sokoni, akawauliza; jee! Leo imeteremka amri mpya yoyote kwa Mtume (S.A.W.)? Akaambiwa naam! imeteremka amri ya kuziacha ndevu tuzifuge tusizinyoe, na tuyakate kwa kuyapunguza masharubu au tuyanyoe. Akasema Umar ® kwamba: “tumesikia na tumetii” Basi papo hapo akaanza kuyashika masharubu yake na kuyanyofoa, wakamwambia masahaba wenzake: ewe Umar! Mbona unayanyofoa masharubu namna hiyo? Nenda nyumbani kapumzike kwanza kisha chukua kijembe na nyoa masharubu yako kwa raha kuliko kuyanyofoa na kujiumiza bure tu? Akasema Umar ® kuwaambia wenzake: Jee! Mnaweza kunipa dhamana ya kufika nyumbani kwangu salama? Hii ni amri imekwisha teremka na kuamrishwa lazima tutii.

Hii ndio ilikuwa hali ya masahaba wa Mtume (S.A.W.) ilikuwa wakipewa amri yoyote ile basi hawazubai ila papo hapo wanaiteleza. Na leo asilimia 95% Waislamu ulimwenguni hawafugi ndevu, kila kukicha kijembe kinafanya kazi kwa kunyoa ndevu na kuipuuza amri ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W.) wanaona kufuga ndevu ni kitu kibaya na kinachusha. Waislamu wachache sana wenye kufuga ndevu. Na aghalabu wanaotii amri hii waliobakia sasa ni Oman na si wote kiasi ya asilimia 60% tu na Afghanistan na Pakistan na Iran. Na wanachekwa wanaofuga ndevu, na amri za Mtume (S.A.W.) zimepuuzwa na kutupwa nyuma ya migongo. Na haya mamboya maasi ya kunyoa ndevu yameanza hivi karibuni tu kama karne moja tu ya nyuma kuwaiga makafiri wa Kiyahudi na Manasara na makafiri wengine, na hali Mtume (S.A.W.) ametukataza tusifanane na makafiri wowote.

Waislamu wote wanaume zamani walikuwa wanafuga ndevu, na anayenyoa hupuuzwa na kudharauliwa. Zamani kama mtu anataka kukopa pesa au kitu kwa mwenziwe na kama hana dhamana ya kujidhamini, basi humnyofolea kinywele kimoja au viwili kumpa mdai kuwa ni dhamana na ahadi ya kulipwa deni lake. Walikuwa wakizitukuza sana ndevu Waislamu wa zamani. Na wala hakuna hata mmoja zamani anasali naye kanyoa ndevu. Lakini sasa wanaona ni kitu cha kawaida tu kunyoa ndevu. Unaona wote imamu na khatibu wa Ijumaa na maamuma wote wote hawana ndevu, na amri ya Mtume (S.A.W.) imepuuzwa wala hakuna anayejali kitu hiki, na ukijaribu kumwambia basi anakupuuza na kukucheka. Hii sasa ni namna ya

mwanzo ya madhambi ya maasi ya kunyoa ndevu kwa kuvunja amri ya Mtume (S.A.W.), na haya si Afrika ya mashatiki na ya kati tu, bali sehemu zote za ulimwengu Waislamu wanaipuuza amri hii.

Ama dhambi ya namna ya pili ya kunyoa ndevu ni kubadilisha umbo la Mwenyezi Mungu. Maana Mwenyezi Mungu kaumba binadamu dume na jike, na kila mmoja kamuumba na kumpamba kwa mujibu wa umbo lake linavyostahiki kupambwa na wala wasifanane, mwanamme asiwe sawa na umbo la jike, wala mwanamke asiwe sawa na dume. Kama Alivyosema (S.W.) katika Surat-Aal-Imraan Aya Na. 36:-

}...... كـا أل نـثـى}..... الذ كـر ولـيس

“…...NA MWANAMUME SI SAWA NA MWANAMKE……”

Na Mwenyezi Mungu kampamba mwanamme kwa pambo la ndevu, na wanaonyoa ndevu basi wanaona kuwa Mwenyezi Mungu kafanya makosa kuwaumba na kuwapamba kwa pambo la ndevu, na anayenyoa ndevu basi anabadilisha umbo la Mwenyezi Mungu alilomuumbia nalo, na anayebadilisha umbo la Mwenyezi Mungu basi huyo amelaaniwa. Dhambi za mwanzo anazopata za kuasi amri ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W.), pili anapata dhambi za kujifananisha kuwa sawa na umbo la mwanamke. Kasema Mtume (S.A.W.):-

ساء( .....) بـالنـ جال الر من هين الـمتـشب الله لـعن

MWENYEZI MUNGU AMEWALANI MIONGONI MWA WANAUME (WALE) WANAOJISHABIHI (WANAJIFNANISHA) KUWA SAWA NA (UMBO LA) WANAWAKE”

Tatu, anapata dhambi za kujifananisha na Mayahudi na Manasara na makafiri wengine, Kasema Mtume (S.A.W.):-

منهم( ) فـهو بـقـوم ه تـشب من

“ANAYEFANANA NA WATU BASI YEYE YU MIONGONO MWAO” …. Na Mtume (S.A.W.) ametukataza tusifanane kabisa na Mayahudi na Manasara au makafiri wowote kwa jambo lolote, ikiwa kwa tabia, au mavazi au mwendo, au vitendo, au kitu chochote kile tuwe kinyume nao kabisa.

Siku moja nilikuwa namsikiliza shekhe mmoja katika mashekhe wa Kimisri katika televisheni ya Cairo katika kipindi cha hewani moja kwa moja akijibu maswali ya dini wanaouliza, na khekhe huyo hana ndevu wala hata masharubu na kavaa suti na tai. Basi akaulizwa swali na mmoja katika wamisri wenziwe, muulizaji akauliza: Nini maana ya kumpenda Mtume wa Mwenyezi Mungu? Shekhe akajibu: kumtii amri zake zote, za kufanya uzifanye, na alizokataza uepukane nazo. Yule muulizaji akasema: Kwa hiyo wewe shekhe inamaana humpendi Mtume (S.A.W.)? Yule shekhe akasema: Astaghfirullaah! Vipi nisimpende Mtume wa Mwenyezi Mungu? Yule mtu akasema kumwambia yule shekhe ya kwamba: Wewe hapo unatoa mawaidha na umesoma Mwenyezi Mungu kakuruzuku ilimu na unajua mengi ya sheria za Kiislamu, lakini hapo ulipo wewe tunakuona ndevu umezinyoa na umevaa suti na tai, nguo za kikafiri, umefanana sawa na myahudi au mkristo, na hali Mtume wetu (S.A.W.) amesema tusifanane nao kwa jambo lolote, nawe hapo ulipo umefanana na Isaak Shameer rais wa Israili, jee tukuelewe vipi?

Basi yule shekhe hakujua nini la kusema wala kujibu, ila alibakia kusema: Astaghfirullaah! Astaghfirullaah! Na hii ndio tabia ya baadhi ya mashekhe wengi wenye kuvaa nguo za kikafiri na kunyoa ndevu, shekhe anatoa mawiadha mazuri na kuhutubia hutuba za Ijumaa, lakini ukimtazama ile hali yake inasikitisha kwa nguo alizozivaa si za Kiislamu, ndevu na masharubu kanyoa, sura yake hana tafauti na mwanamke, na nguo alizovaa za kikafiri. Hii ni hatari kubwa sana kwa mashekhe wa namna hii. Katika hadithi iliyopokewa na Imamu Ahmed bin Hambal na wengineo kwa njia ya Anas bin Maalik ® Kasema Mtume (S.A.W.):-

وألـسنـتـهم( شفـاهـهم تـقـرض قـوم على بـي سري أ لـيلـة مررت , خطـباء هآؤآلء قـال جـبريل؟ يا هآؤآلء ما قـلـت نـار من بـمقـارض

اس النـ يأمررون ذين الـ يتـلـون أمتـك أنـفـسهم وينـسون بـالـبـر} ( ؟ ( يعقلـون أفـال الـكتـاب

“NIMEWAPITIA (NIMEWAONA) USIKU NILIYOPELEKWA ISRAA (NA MIRAJI) WATU WAKIBANWA MIDOMO YAO (LIPS) NA NDIMI ZAO KWA MIKASI (MAKOLEO, AU VIBANIO) VYA MOTO, BASI NIKASEMA: NI NANI HAWA EWE JIBRIL ? AKASEMA: HAWA NDIO (MASHEKHE) WANAOHUTUBU KATIKA UMMA WAKO WALE AMBAO WANAAMRISHA (WATU KUTENDA) MEMA NA (KISHA) WANAJISAHAU NAFSI ZAO, NA HALI WANASOMA KITABU (CHA

MWENYEZI MUNGU) BASI HAWAFAHAMU (KWENDA KINYUME NA AMRI ZA MWENYEZI MUNGU NA MTUMEWE NI VIBAYA)? ….. Na katika hadithi nyengine iliyopokewa na imamu Att’abaraany, Kasema Mtume (S.A.W.):-

يضيىء( راج الس كـمثـل بـه يعمل وال الـخير اس النـ م يعلـ ذي الـ مثـلنـفـسه ) ويحرق اس للنـ

“MFANO WA MTAALAMU AMBAYE ANAFUNDISHA WATU (MAMBO YA) KHERI NA WALA YEYE HAIFANYI HIYO (KHERI), NI KAMA MFANO WA TAA ANAYOWAMULIKIA WATU NA HUKU ANAJIUNGUZA NAFSI YAKE”

Basi wamche Mwenyezi Mungu na Mtume Wake (S.A.W.) waiogope adhabu ya Mwenyezi Mungu, waelekee na wamtii Mtume wa Mwenyezi Mungu ikiwa wao kweli waumini, waache kuvaa nguo ndefu zilizokataza Uislamu, na waache kubadilisha umbo waliloumbwa na Mwenyezi Mungu, na waache kujifananisha na tabia za kikafiri, na wasidhanie kwamba hayo tuliyoyataja ni madogo ya kupuuzwa, bali kwa Mwenyezi Mungu na Mtumewe (S.A.W.) ni makubwa kabisa yanayowachusha.

(i)—KESHA ZA KUSOMA KASIDA USIKU.

Tabia ya kukesha usiku kucha kusoma kasida hili pia ni jambo baya, wala si ibada katika ibada za sheria ya Kiislamu, bali ni bid’aa mbaya isiyokuwa na thawabu yoyote ila kuchuma madhambi tu. Zinafanywa hafla za usiku za sherehe kuimba kwa kasida na muziki na mafilimbi na mazumari kwa njia ya chombo cha kukuza sauti, wanakera watu kuwaharibia usingizi wao na mapumziko yao, wengine wana wagonjwa na wengine watoto wachanga, wanaudhi watu kwa makelele na sauti kubwa. Zinapulizwa filimbi na madufu na kelele za yaleli za vitorori, wanashindana kwa sauti na pumzi kama waimbaji wa Kimisri wanaokwimba nyimbo za upuuzi.

Hili ni jambo la kusikitisha sana, hakuna ibada ya Kiislamu ya namna hii, bali hii ni sawa na tarab au burudani ya nyimbo za upuuzi kuburudisha nyoyo wenye maradhi ya mambo kama hayo ya kipuuzi. Ni sawa kabisa hakuna tafauti yoyote na yale maklabu ya disco yanayokesha usiku kucha kukera watu hawalali majumbani mwao kwa kero ya makelele. Nabii

Muhammad (S.A.W.) hakuja kufundisha watu kusoma kasida kwa filimbi na muziki kukera watu, utaona mtu anapiga kelele ya yaleli na filimbi usiku kucha, hata asubuhi kachoka sauti imemkauka, huenda hata sala ya alfajiri imempita. Sasa hii tutasema kuwa ni ibada? Ibada gani hiyo ya kukera watu usiku kucha kuwaharibia watu mapumziko yao. Kama tulivyosema kuwa wengine wagonjwa, na wengine wamechoka wanataka kupumzika ili asubui waweze kutafuta riziki zao, wengine wana ibada zao za sala za usiku na kusoma Qur’ani na nyiradi zao. Haya yamenifika mimi si mara moja wala mara mbili Zanzibar na Dar-es-Salaam na Mwanza, sikuweza kufanya ibada zangu wala sikuweza kulala. Hii sawa kabisa na aliyekesha katika tarab na disco, huku ni kuchuma madhambi tu, hakuna thawabu yoyote waipatayo ila khasara tu.

Hakutumwa Nabii Muhammad (S.A.W.) kwa mambo kama haya ya kukesha na kukera watu usiku, bali aliyokuja nayo Nabii Muhammad (S.A.W.) haya; Kasema Mtume (S.A.W.):-

, , , تـدخلـون( نيام اس والنـ وا وصلـ األرحام وصلـوا السالم أفـشوابـسالم ) ة الجنـ

“TOENI SALAMU, NA WAUNGENI JAMAA, NA SALINI USIKU NA WATU WAMELALA, MTAINGIA PEPONI KWA SALAMA”

Haya ndio aliyoyaleta Mtume (S.A.W.) ya faida kubwa katika maisha ya dunia na Akhera, hakusema imbeni mnisifu kwa kasida na mafilimbi na muziki usiku mkere watu wasilale wala wasipumzike. Badala ya wao kusali Qiyamu-Llayl, tahajjud ingawa rakaa mbili usiku wakapata thawabu kubwa na kuongokewa na mambo ya maisha yao, wao wanakera watu usiku kwa makelele na kuchuma madhambi. Kasema Mtume (S.A.W.):-

فيها( ) وما الدنـيا من خير يل اللـ فى ركـعتـان “RAKAA MBILI ZA USIKU (NA WATU WAMELALA) BORA KULIKO DUNIA NA VYOTE VILIVYOMO NDANI YAKE”

Basi waache ndugu zetu Waislamu wenye tabia hii mbaya, hii si ibada kabisa ila kuchuma madhambi, haya mambo hayakuleta Uislamu kabisa, hata sijui wameyatoa wapi, hayana dalili yoyote, bali ni mambo ya uzushi yaliyozuliwa na watu wasiyokuwa na ilimu wala busara kawapambia tu

Shetani.

Mpaka hapa kwa haya machache yanatosha kuwazindua ndugu zangu wa Afrika ya mashariki na kati. Na haya mambo niliyoyataja katika makala yangu hii si mambo ya kukhitalifiana katika madhehebu, bali yamethibitika katika Qur’ani na sunna ya Mtume (S.A.W.) na wameafikiana maimamu na wanavyuoni wa madhehebu zote za Kiislamu, na nimetoa dalili za kutosha na za kukinaisha katika kitabu cha Mwenyezi Mungu na sunna ya Mtume Wake (S.A.W.) hadithi sahihi. Kwa hiyo nawausia ndugu zangu Waislamu kwamba tuabudu kwa ilimu na ujuzi ibada sahihi, tusiabudu kwa upofu na upotevu. Tuabudu kama alivyotufundisha Mtume wetu Nabii Muhammad (S.A.W.) na tutii amri zake zote, kwani kumtii Mtume (S.A.W.) ndio tumemtii Mwenyezi Mungu. Kasema (S.W.) katika Surat-Annisaa Aya Na. 80:-

}......... الله} أطـاع فـقـد سول الر يطع من

“MWENYE KUMTII MTUME BASI KWA YAKINI AMEMTII MWENYEZI MUNGU……” na wanapokata shauri Mwenyezi Mungu na Mtumewe (S.A.W.) katika jambo lolote lile, ikiwa la amri ya kufanya, au amri ya kukatazwa basi sisi hatuna khiyari ya kubadili kitu chochote katika amri zao, ila tuseme: “tumesikia na tumetii” kama tulivyoitaja hapo mwanzo ile Aya ya Na. 36 ya Suratul-Ahzaab. Tusithubutu kwenda kinyume na amri zao, hiyo ni hatari kubwa sana. Kasema (S.W.) katika Aya hiyo hiyo Na. 36 ya Suratul-Ahzaab imeendelea kusema:-

مبـين}...... { ضالال ضل فـقـد ورسولـه الله عص ي ومن “….NA MWENYE KUMUASI MWENYEZI MUNGU NA MTUME WAKE BASI KWA YAKINI AMEPOTEA UPOTOFU ULIO WAZI KABISA” Ndio hayo niliyoyataja katika makala yangu hii kwamba hayo wanayoyafanya ndugu zetu ya batili yanapeleka kwenye upotofu ulio wazi, siyo ibada za sahihi ila batili na yasiyokuwa na msingi wowote katika Uislamu ila kupoteza wakati na kupata khasara tu kwa sababu ya kwenda kinyume na amri za Mwenyezi Mungu na Mtume Wake (S.A.W.) - Na Kasema (S.W.) katika Suratul-Jinn Aya Na. 23:-

أبدا}.... { فيها خالدين م جهنـ نـار لـه فـإن ورسولـه الله يعص ومن

“NA MWENYE KUMUASI MWENYEZI MUNGU NA MTUME WAKE, BASI HAKIKA HUYO ATAPATA MOTO WA JAHANNAM ADUMU HUMO MILELE”

Basi waache hao ndugu zetu kuasi amri zao kwa mambo waliyoyakataza na watubu, na waabudu ibada iliyo sahihi kama alivyotufundisha Mtume wetu na mwalimu mkuu Nabii Muhammad (S.A.W.) na tutii amri zake ndipo tutakapofuzu. Kasema (S.W.) katika Suratul-Ahzaab Aya Na. 71:-

عظيما}..... { فـوزا فـاز فـقـد ورسولـه الله يطع ومن

“NA ANAYEMTII MWENYEZI MUNGU NA MTUME WAKE, BASI KWA YAKINI AMEFUZU KUFUZU KUKUBWA KABISA”

(j)—HUTUBA YA IJUMAA KWA MADHEHEBU YA KIIBADHI.

Mwisho wa makala yangu hii kabla ya kuimaliza nitapenda kuwapa nasaha ndugu zetu Waislamu wa madhehebu ya Kiibadhi ambao sifa zao njema tangu Mwenyewe Mtume (S.A.W.) amewasifu sifa nzuri kwa kuamini ujumbe wakebila ya kupinga wala kuzubaa, na akawaombea dua Mwenyezi Mungu awawafikishe katika dini yao, na Awabariki katika nchi yao na bahari yao. Na pia katika zama Ukhalifa wa Abu Bakar ® akawasifu vile vile sifa nzuri kwa ukweli na uaminifu wa imani yao na Uislamu wao. Na hivyo ndivyo ilivyokuwa ikapokelewa dua ya Mtume (S.A.W.) - Na pia imamu na mwanachuoni mkubwa wa Misri marehemu Imamu Sheikh Muhammad Mutawally Asha’arawy alisema kwamba nimesoma na nimesikia kuhusu sifa nzuri za Waislamu wa Omani, sikuweza kuvumilia ila nilimuomba Mola wangu Aniruzuku niwazuru ndugu zangu wa Oman.

Mwenyezi Mungu Akamjaalia Imamu Asha’arawy kuizuru Omani mwaka 1976 akakutana na wanavyuoni wenzake wa Oman, akawa mgeni kwa muda usiokuwa chini ya wiki mbili hivi, akapewa vitabu vya fiqhi za maimamu na wanavyuoni wa Kiibadhi, akafurahiwa sana. Kwa ufupi baada ya kuondoka na kurudi Saudi Arabia, maana alikuwa akiishi zaidi miaka hiyo Saudi Arabia na kuwasaidia wanavyuoni wa Saudi Arabia katika mambo mengi ya dini, maana Mwenyezi Mungu alimpa ilimu kubwa sana.

Na baada ya kurudi kwao Misri alikuwa akiiongoza chuo kikuu cha Al-Azhar, hata siku moja ulifanyika mkutano mkubwa Cairo wa wanavyuoni wa Kiislamu. Akasema Imamu Asha’arawy kwamba: Nashuhudia kuwa sijaona madhehebu katika madhehebu za Kiislamu kama madhehebu ya Kiibadhi watu wa Oman, hakika wao kweli maweshika mwenendo wa Qur’ani na sunna ya Mtume (S.A.W.) ipasavyo kushikwa.

Sitaki kutaja mengi ya sifa zao walivyosifiwa na tafauti ya wanavyuoni wakubwa wa Kiislamu ulimwenguni. Sasa madamu wana sifa kama hizi tangu zama za Mtume mwenyewe (S.A.W.) basi wazikamilishe sifa zao nzuri wasizitie kuwa na dosari. Nami ninalotaka kusema kuwa katika hutuba zao za sala ya Ijumaa wanafanya kosa moja, kwamba hutuba ya Ijumaa wanaisoma kwa lugha ya Kiarabu tu katika Afrika ya mashariki na kati, na hili ni kosa, kwani nchi hizo Waislamu wake asilimia 99% hawajui Kiarabu. Ingawa kabla ya kuanza hutuba ya Ijumaa kwa dakika chache wanatoa maudhuu ya hutuba kwa lugha ya kiswahili kwa ufupi, wakati huo bado watu hawajawa wengi hata nusu ya msikiti, wengine inawapita maudhuu ya hutuba, na moja katika masharti ya sala ya Ijumaa lazima isikiwe na wote waliohudhuria. Na wakati wetu huu khasa wa sasa watu hawahudhurii mapema misikitini kama inavyotakiwa, aghalabu yake wanachelewa, wanahudhuria wakati inapoanza hutuba yenyewe ambayo kwa lugha ya Kiarabu, na hutuba yakiswahili inakuwa imekwisha mpita. Na mara nyengine, husomwa hutuba ya Kiswahili baada ya sala ya Ijumaa, pia wakati huo hawabaki watu msikitini ila wachache sana, ikisha tu sala watu wanatoka. Kwa hali yoyote ile ikiwa mulakhas wa hutuba ya Ijumaa ikisomwa kabla au baada ya sala ya Ijumaa nyakati zote hizo mbili si nyakati munasaba wa kuwaelimisha watu, wengi wao wanakuwa hawajahudhuria ikiwa kabla ya sala, na ikiwa baada ya sala pia wengi wao wanatoka na wanaobakia kusikiliza ni wachache sana. Na pia inakuwa hutuba inasomwa mara mbili, moja ya Kiswahili na ya pili ya Kiarabu, na kutumia wakati mrefu na kuwafunga watu, wengine hawana wakati kuzisikiliza hatuba zote mbili.

Inakuwa watu wanisikia kwa ukamilifu hutuba ya Kiarbu tu, hili pia ni kosa, maana wanahutubiwa kwa lugha isiyokuwa yao hawatambui nini kinachosemwa. Na hutuba ya Ijumaa ni muhimu sana kusikilizwa, maana ni masomo na mawaidha na makumbusho na mazingatio ili watu waelimike na wajue nini mambo ya dini yao. Lakini wakihutubiwa kwa lugha isiyokuwa ya nchi hiyo inakuwa sawa na kupiga kelele za bure bila ya faida yoyote.

Hapana ubaya wowote, au sababu yoyote ya kuharibika sala ya Ijumaa ikiwa itahutubiwa kwa lugha ya kigeni isiyokuwa ya Kiarabu, sharti inafunguliwa hutuba mwanzo kwa lugha ya Kiarabu, kisha unaendelea na maelezo kwa lugha ya watu wa nchi hiyo, na shekhe mhutubu kila anapotaja Aya au hadithi aitaje kwa Kiarabu na kuifasiri kwa lugha ya kienyeji, kisha anaendelea na maelezo ya hutuba kwa lugha kienyeji. Hivi ndivyo inavyotakiwa ili waumini wafaidike na ile hutuba na waelimike kuyajua mambo ya dini yao. Na hivi ndivyo Mwenyezi Mungu Ametuumba tafauti ya lugha na rangi za watu kama Alivyosema Mwenyewe Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Surat-Arruum Aya Na. 22:-

وألـوانكـم} ألـسنـتـكـم واختالف واألرض ماوات الس خلـق آياته ومن}.......

“ NA KATIKA ALAMA ZAKE (MWENYEZI MUNGU) NI UUMBAJI WA MBINGU NA ARDHI, NA KUKHITALIFIANA LUGHA ZENU NA RANGI ZENU……” Na ktika Suratu-Hujuraat Aya Na.13:-

شعوبا} وجعلـنـاكـم وأنـثـى ذ كـر من خلـقـنـاكـم ا إنـ اس النـ ها يآأي........{لتـعارفـواوقـبائل

“ENYI WATU! HAKIKA SISI TUMEEKUUMBENI KUTOKANA NA DUME NA JIKE (ADAM NA HAWA), NA TUKAKUFANYENI MATAIFA NA MAKABILA MBALI MBALI ILI MPATE KUJUANA……”

Na dini ya Kiislamu ya watu wote hao waliotajwa katika Aya hizi wana haki wajue nini dini yao inasema na nini maamrisho yake si ya wenye kujua Kiarabu tu, bali kila mmoja katika tafauti ya makabila na mataifa na rangi na lugha ana haki aelimishwe ili aijue sheria za dini yake. Na Mwenyezi Mungu Ametuwekea sala hii ya Ijumaa yenye hutuba kwa ajili waelimishwe watu, na hutuba ya Ijumaa ni moja katika vyuo vikuu vya Kiislamu Alivyopewa Nabii Muhammad (S.A.W.) awafundishe umma wake, waliokuwa hawakujaaliwa kusoma katika madrasa kwa mwalimu basi hutuba ya Ijumaa ni madrasa kuu ya pamoja, watoto na wakubwa, waliosoma na wasiojua kusoma, waliosoma wanakumbushwa, na wasiojua kusoma wanaelimika na kujua mambo ya dini yao.

Na ikiwa hutuba tunaisoma kwa lugha ya Kiarabu tu na wenyeji wa nchi hiyo hawaijui lugha ya Kiarabu, niambie wataelimika nini katika hutuba

hiyo? Inakuwa sawa na kutwanga maji katika kinu. Mimi kwa juhudi zangu na kwa ilimu yangu chache hii nimejitahidi kutafuta dalili yoyote katika hadithi za Mtume (S.A.W.) sahihi zilizokataza kusomwa hutuba ya Ijumaa kwa lugha ya kigeni isiyokuwa ya Kiarabu, basi sikupata hadithi hata moja ya Mtume (S.A.W.) iliyokataza kusomwa kwa lugha ya kigeni, isipokuwa katika kitabu cha mwanachuoni mkubwa wa kiibadhi wa Tunis, Al’allaamah Imamu Sheikh Abii T’aahir Ismail bin Musa Al-Jiit’aaly aliyekuwa katika mwanzoni mwa karne ya nane ya Hijriyyah. Kataja katika kitabu chake alichokiita: “Qanaat’ir Alkhayraat” juzu ya mwanzo ukurasa Na. 440, katika mlango wa sala ya Ijumaa na masharti yake, baadhi yake kataja kuhusu hutuba ya Ijumaa kuwa isisomwe kwa lugha ya kigeni, lakini hakutaja dalili yoyote ya hadithi ya Mtume (S.A.W.) wala hakutaja fardhiyya yake kuwa ni lazima au wajibu au sunnah hutuba isomwe Kiarabu, wala hakutaja sababu ya kusema kwake kuwa hutuba isisomwe kwa lugha ya kigeni kuwa inatengua sala ya Ijumaa.

Pia Imamu Al’allaamah Nuuru-ddiin Assaalmy ambaye ni mmoja katika maimamu na wanavyuoni wakubwa na mashuhuri wa Oman, aliyetunga vitabu vingi sana vya dini, baadhi ya kitabu chake alichokiita: “Sharah T’ala’at Ash-shams” juzu ya pili, kuhusu sala ya Ijumaa, kataja masharti mengi ya sala ya Ijumaa na hutuba yake, lakini hakutaja kuhusu hutuba ya Ijumaa isisomwe kwa lugha ya kigeni. Sijui kama kataja katika juzu ya kwanza ya kitabu chake hicho, maana sijakipata na kukisoma. Lakini nimevipitia vitabu vingi vya kiibadhi na vya madhehebu nyengine kupekua na kutafuta dalili ya hadithi inayokataza kusomwa hutuba ya Ijumaa kwa lugha ya kigeni sikupata, huenda ipo maana ilimu pana nami ilimu yangu ndogo.

Pia hata kama iko hadithi iliyosema makatazo hayo ya kutosoma hutuba kwa lugha ya kigeni, lakini katika mambo ya kheri khasa kama jambo hili muhimu la hutuba ya Ijumaa, basi Mwenyezi Mungu na Mtume Wake (S.A.W.) wamewapa Waislamu ruhusa ya kulifanya jambo hilo madamu lina maslaha kwa Waislamu, seuze tena katika jambo kama hili lililo muhimu sana la ibada. Kwa dalili ya hadithi iliyopokewa na Muslim, Kasema Mtume (S.A.W.):-

حسن( ) الله عند فـهو حسن الـمسلمون رأوه ما كـل “KILA WANACHOKIONA WAISLAMU KUWA NI KIZURI (KWAO), BASI NA KWA MWENYEZI MUNGU PIA NI KIZURI KWAKE”

Na jambo la hutuba ya Ijumaa kusomwa kwa lugha ya kienyeji ni jambo zuri na la muhimu kwa wenyeji wa nchi hiyo wasiojua lugha ya Kiarabu ili waelimike na wapate faida ya dini yao. Kwa rai na nadhari yangu hapana ubaya wowote wakutengua sala ya Ijumaa kwa kusoma hutuba kwa lugha ya wenyeji wa nchi hiyo, kila mwenye akili ataniunga mkono kwa rai yangu hii.

Katika mwaka 1998, mimi binafsi yangu nimemuuliza Sheikh Said Al-Qannuby kuhusu jambo hili, mwanzo alinikatalia akaniambia haiwezekani kusoma hutuba ya Ijumaa kwa lugha ya kigeni ila kwa lugha ya Kiarabu, akanitajia hoja nyingi, lakini mimi hazikunikinaisha hoja alizonipa, nikahojiana naye sana, nami nikambainishia hoja zangu kwa bayana na kumfafanulia kirefu, na baadhi ya hoja zangu ndio hizi nilizozitaja humu za umuhimu wa hutuba ya Ijumaa kwa Waislamu, kwa vile yeye ni msomi sana khasa katika fani ya hadithi za Mtume (S.A.W.) Basi alinikubalia rai yangu akaniambia kweli mimi niko katika haki. Akasema inajuzu hutuba ya Ijumaa kusomwa kwa lugha ya kigeni, kwa masharti yale yale niliyoyataja humu katika makala yangu hii.

Pia katika mwaka 2007, nilikuwa na kazi makhsusi kwa Sheikh Ahmed Al-Khalili Mufti mkuu wa Oman kuhusu mambo ya Kiislamu na Waislamu. Nikenda ofisini kwake, nikaona pia hii ni nafasi nzuri ya kumuuliza swali hili hili, ingawa wakati ulikuwa mfinyu, lakini nilimuuliza ili naye nijue rai yake kuhusu hutuba ya Ijumaa kamahaijuzu kusomwa kwa lugha ya kigeni, basi akanijibu inawezekana lakini kwa masharti yale yale niliyoyataja ya kuianza kwa lugha ya Kiarabu, na Aya na hadithi zikitajwa zitajwe Kiarabu kisha zifasiriwe kwa lugha ya kigeni, na pia maelezo kwa lugha ya kigeni, nikamwambia basi nipatapo nafasi nitakuja na barua ili nipate kwa maandishi, maana wakati ulikuwa mfinyu.

Lakini kwa wingi wa kazi sikupata nafasi ya kumrudia na barua ya swali hilo, maana kazi niliyo nayo ya kufasiri Qur’ani inanizuia nisiweze kufanya mengineyo kwani asilimia 80% ya wakati wangu nautumia kwa kazi ya tafsiri. Lakini nilipokata shauri ya kuandika makala hii nilisimamisha kazi ya tafsiri zaidi ya miezi miwili, nikenda ofisini kwake mara mbili lakini sikujaliwa kumpata, nilikuwa na hamu nipate fatwa yake kwa maandishi wakati naandika makala hii ili niwathibitishie ndugu kuhusu hutuba ya Ijumaa, lakini ndio Mwenyezi Mungu Hakunijaalia. Na Sheikh mufti siku hizi ni vigumu kumpata kwa urahisi.

Kwa hiyo hutuba ya Ijumaa inajuzu kwa lugha ya kigeni kwa mujibu wa hoja zangu nilizozitaja ambazo zinakinaisha ukweli wake. Nami nawaomba wahusika viongozi wa madhehebu ya Kiibadhi wa Afrika ya mashariki na ya kati wazihutubie hutuba za Ijumaa kwa lugha ya kienyeji kwa masharti tuliyoyataja ili wenyeji nao waelimike na wafaidike. Ama hutuba kwa Kiarabu katika nchi za kigeni ni kosa, na hii inakuwa sawa na kama mfano wa kuficha ilimu, na kuficha ilimu hatari yake kubwa sana, nanyi ni wenye sifa nzuri za kuelimisha Waislamu.

**************************

Nanyanyua mikono yangu juu kwa unyenyekevu namuomba Allah (S.W.) Atupokelee ibada zetu sote Waislamu, na Ayaweke kando makosa yetu na ujinga wetu kwa kutusamehe tuliyoyazidisha yasiyokuwa ya haki, au kasoro yoyote katika utekelezaji wa amri zake na za Mtume Wake (S.A.W.) na Atuongoze sote katika haki na yanayomridhisha, kwani Yeye ni Mola Mwema Mwenye kusamehe, Amiin. Natarajia inshaallah nasaha yangu hii isikilizwe na ndugu zangu ili wajirekebishe kwa manufaa yao wenyewe, na kila mwenye ilimu imemlazimu awakumbushe na awazindue Waislamu wenziwe, na Uislamu umetuamrisha hayo ya kuzinduana na kukumbushana na kurekebishana katika mambo ya dini yetu. Kasema (S.W.) katika Surat-Adh-dhaariyaat Aya Na 55:-

الـمؤمنين} { تـنـفـع الذ كـرى فـإن ر وذ كـ “NA KUMBUSHA, KWANI UKUMBUSHO HUWAFAA WAISLAMU”

Pia nawaomba Waislamu wenzangu wasinielewe vibaya, huenda baadhi yao hawatapendezewa na haya niliyoyataja katika makala yangu hii, lakini nilikuwa sina jinsi au budi ila lazima niwazindue, sikuweza kuvumilia, nafsi yangu haikuwa na raha kunyamaza na kuwaacha ndugu zangu wapoteze juhudi za ibada zao bure. Maana haya mambo wanayaona watu si muhimu na ni ya kawaida na madogo hayana madhara yoyote, na kumbe kwa Mwenyezi Mungu ni makubwa yanamchusha. Kasema (S.W.) katika Surat-Annuur Aya Na. 15:-

عظيم}..... { الله عند وهو نـا هي وتـحسبونـه “…….NA MNADHANIA JAMBO DOGO, NA KUMBE MBELE YA MWENYEZI MUNGU NI KUBWA KABISA”

Wabillaahi Tawfiq, wasallallaahu Alaa Sayyidinaa Muhammad wa alaa aalihi wasallam, Walaa Hawla Walaa Quwwata illaa Billahil-Aliyyil-Adhiim, Walhamdulillaahi Rabbil-A’alamiin.

Wassalaam Aleikum Warahmatullah.

Ndugu yenu katika Uislamu,

Said Moosa Mohammed Al-KindyTel: +968 99256745—Muscat—Oman. +255 773 121240—Tanzania.

21 Mfungo pili 1430 H.9th November 2009.

222