neno la uzima

25
Neno La Uzima Januari 2013

Upload: joanne

Post on 10-Jan-2016

120 views

Category:

Documents


10 download

DESCRIPTION

Neno La Uzima. Januari 2013. Toka tarehe 18 Januari hadi 25 mahali pengi duniani huadhimishwa Juma la Sala kwa ajili ya Umoja wa Wakristo, hali mahali pengine huadhimishwa karibu sikukuu ya Pentekoste. - PowerPoint PPT Presentation

TRANSCRIPT

Page 1: Neno  La Uzima

Neno La

Uzima

Januari2013

Page 2: Neno  La Uzima

Toka tarehe 18 Januari hadi 25 mahali pengi duniani

huadhimishwa Juma la Sala kwa ajili ya Umoja wa Wakristo, hali mahali

pengine huadhimishwa karibu sikukuu ya

Pentekoste.Mwaka huu mstari

uliochaguliwa kwa ajili ya Juma la Sala ni: “Bana

anataka nini kwako” (Mik 6:6-8).

Page 3: Neno  La Uzima

Chiara Lubich alikuwa amezoea kueleza mstari wa Biblia kila mara. Ili kuendeleza msaada huo wake, tunashauri matini yake moja ya

kueleza Mt 9:13 (linganisha na Hos 6:6) aliyoandika katika mwezi Juni 1996, ambayo inaweza kusaidia

kuchimba ndani zaidi Neno linalotolewa: “Nataka rehema, wala

si sadaka”

Page 4: Neno  La Uzima

Nendeni mkajifunze, maana yake maneno haya: Nataka rehema, wala si sadaka (Mt 9:13)

Page 5: Neno  La Uzima

Nataka rehema, wala si sadaka.Unakumbuka Yesu aliposema maneno hayo? Alipokuwa akiketi nyumbani ale chakula, watoza ushuru wengi na wenye dhambi walikuja na wakaketi pamoja

naye. Mafarisayo walipoona waliwaambia wanafunzi wake: Mbona Mwalimu wenu anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi? Naye Yesu

aliposikia, aliwaambia:

Page 6: Neno  La Uzima

Nendeni mkajifunze, maana yake maneno haya: Nataka rehema, wala si sadaka (Mt 9:13)

Page 7: Neno  La Uzima

Yesu anatamka mstari wa nabii Hosea, na jambo hilo

linadhihirisha kuwa anayapenda maneno hayo na wazo lililomo: naam ni mwongozo anaoshika katika mwenendo wake. Kwa

maana inadhihirisha utangulizi wa upendo mbele ya amri

nyingine yo yote, juu ya kila sheria na agizo.

Page 8: Neno  La Uzima

Huo ndio Ukristo: Yesu alikuja kusema kuwa Mungu anataka toka kwako, kuhusu wengine – wanaume na wanawake -, kabla ya yote, kuna upendo,

na hayo ndiyo mapenzi ya Mungu yaliyokwisha tangazwa katika Maandiko, kama yanavyoonyesha maneno ya nabii.

Page 9: Neno  La Uzima

Upendo, kwa kila Mkristu, ni muhtasari wa maisha yake, sheria ya kimsingi ya mwenendo wake, uamuzi wa kuishi kwake.

Page 10: Neno  La Uzima

Daima upendo lazima itangulie sheria nyingine. Zaidi: upendo wa wengine, kwake Mkristo, ni msingi imara ambamo anaweza kutekeleza

miongozo mingine yote.

Page 11: Neno  La Uzima

...nataka rehema, wala si sadaka

Page 12: Neno  La Uzima

Yesu anataka upendo, na rehema ni sura yake moja.Anataka kuwa Mkristo aishi hivyo hasa kwa sababu ndivyo alivyo Mungu.

Page 13: Neno  La Uzima

Kwake Yesu, Mungu kwanza ni mwenye huruma, Baba anayewapenda wote, anayewaangazia jua lake waovu na wema.

Page 14: Neno  La Uzima

Basi, ikiwa Mungu ni hivyo, ikiwa Yesu ni hivyo, nawe pia unapaswa kulisha hisia hizo sawa.

Page 15: Neno  La Uzima

...nataka rehema, wala si sadaka

Page 16: Neno  La Uzima

“... wala si sadaka”.Ikiwa huna upendo kwa ndugu, Yesu hapendezwi na ibada yako. Hapokei

sala yako, kushiriki kwako ùEkaristi, sadaka unazoweza kufanya, ikiwa hayo yote hayachanui toka moyo wako ulio na amani na wote, umejaa

upendo kwa wote.

Page 17: Neno  La Uzima

Unakumbuka maneno yale ya maana sana ya mafundisho ya mlimani? “Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa

ndugu yako ana neno juu yako, iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka

yako” (Mt 5: 23-24).

Page 18: Neno  La Uzima

Maneno hayo yanasema kuwa ibada inayompendeza Mungu zaidi ni upendo wa jirani, unaopaswa kuwekwa kama msingi kwa ibada ya

Mungu.Ungetaka kumtolea Mungu kipaji, hali ukiwa na hasira na ndugu yako

(au ndugu yako kwako), baba yako angekuambia nini? “Upatane, halafu njoo, unitolee kipaji unachotaka”.

Page 19: Neno  La Uzima

na pia wanang’amua Wakristo wanaoishi imani yao: wakisaidia ndugu zao, hasa wahitaji, ibada yao inaongezeka, ushirikiano na Mungu hupata nguvu zaidi, wanatambua kuwa kuna pingu kati yao na Bwana: na hiyo

inajazia zaidi furaha maisha yao.

Lakini kuna zaidi. Upendo, licha ya kuwa msingi wa

maisha ya Kikristo, pia ni njia wima wa kulinda

ushirikiano na Mungu. Watakatifu

wote wanasema hivi, mashahidi wa

Injili waliotutangulia,

Lakini kuna zaidi. Upendo, licha ya kuwa msingi wa

maisha ya Kikristo, pia ni njia wima wa kulinda

ushirikiano na Mungu. Watakatifu

wote wanasema hivi, mashahidi wa

Injili waliotutangulia,

Page 20: Neno  La Uzima

...nataka rehema, wala si sadaka

Basi, utaishije Neno hilo jipya la uzima?

Page 21: Neno  La Uzima

Usibague kati ya watu unaokutana nao, usimtenge mtu, bali uwatolee wote unachoweza, ukimwiga Mungu Baba.

Page 22: Neno  La Uzima

Tengeneza mizozano midogo kwa mikubwa yasiyompendeza Mungu na kutilia uchungu maisha, jua lisichwe – yanavyosema Maandiko (rej. Ef 4:26)

– na uchungu wenu bado haujawatoka, kwa mtu yeyote.

Page 23: Neno  La Uzima

Ukijimudu hivyo, yote utakayofanya yatampendeza Mungu na kudumu kwa milele. Ikiwa unafanya kazi au unapumzika, ikiwa unasoma au unacheza, ikiwa unakaa na watoto wako au kusindikiza mke wako au bwana wako matembezini, ikiwa unasali

au kujitolea sadaka, ikiwa unatekeleza matendo yale ya ibada yanayolingana na wito wako wa Kikristo, yote, yote yatakuwa vifaa halisi kwa Ufalme wa Mbinguni.

Page 24: Neno  La Uzima

Paradisi ni nyumba tunayojenga hapa duniani, na kukalia baadaye mbinguni. Na hujengeka na upendo.

Page 25: Neno  La Uzima

““Parola di Vita” inatangazwa na Movement of Focolare.Matini hii Imetolewa katika Città Nuova, n.10/1996

Chapa cha Anna Lollo akishirikiana na Fr. Placido D’Omina (Sicily, Italy).Maelezo ya Neno la Uzima inatafsiriwa katika lugha 96 na kilugha

na kuwafikia mamilioni ya watu katika dunia nzimakwa njia ya maandishi, radio, TV na kwa njia ya Tovuti.

Kwa kupata maelezo www.focolare.orgPPS hiyo, katika lugha mbalimbali inatangazwa katika

www.santuariosancalogero.it(na hapo unaweza kupakua)

““Parola di Vita” inatangazwa na Movement of Focolare.Matini hii Imetolewa katika Città Nuova, n.10/1996

Chapa cha Anna Lollo akishirikiana na Fr. Placido D’Omina (Sicily, Italy).Maelezo ya Neno la Uzima inatafsiriwa katika lugha 96 na kilugha

na kuwafikia mamilioni ya watu katika dunia nzimakwa njia ya maandishi, radio, TV na kwa njia ya Tovuti.

Kwa kupata maelezo www.focolare.orgPPS hiyo, katika lugha mbalimbali inatangazwa katika

www.santuariosancalogero.it(na hapo unaweza kupakua)

Nendeni mkajifunze, maana yake maneno haya: Nataka rehema,

wala si sadaka (Mt 9:13)