parokia ya mt. paulo: ubungo msewe, s.l.p 20973, dsm · jnn pamoja na vyeti halisi{original} vya...

11
PAROKIA YA MT. PAULO: UBUNGO MSEWE, S.L.P 20973, DSM “ENENDENI ULIMWNGUNI MWOTE MKAIHUBIRI INJILI KWA KILA KIUMBE..” Mk. 16; 15’

Upload: others

Post on 14-Jul-2020

46 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: PAROKIA YA MT. PAULO: UBUNGO MSEWE, S.L.P 20973, DSM · JNN pamoja na vyeti halisi{Original} vya Ubatizo kutoka Parokia walikopata Ubatizo, Komunyo na Kipaimara. Vile vile kila mmoja

PAROKIA YA MT. PAULO: UBUNGO MSEWE, S.L.P 20973, DSM

“ENENDENI ULIMWNGUNI MWOTE MKAIHUBIRI INJILI KWA KILA KIUMBE..” Mk. 16; 15’

Page 2: PAROKIA YA MT. PAULO: UBUNGO MSEWE, S.L.P 20973, DSM · JNN pamoja na vyeti halisi{Original} vya Ubatizo kutoka Parokia walikopata Ubatizo, Komunyo na Kipaimara. Vile vile kila mmoja

HISTORIA YA PAROKIA YA MT. PAULO MTUME

UBUNGO MSEWE

Mnamo mwaka 1968 aliyekuwa Paroko wa Magomeni Padre Oswin (Cap) alianzisha Kigango cha Ubungo Msewe katika kipindi hicho waamini wachache walisali chini ya mti wa mkorosho,eneo ambalo kwa sasa kuna nyumba ya WAWATA. Kwa msaada wa chifu G.P Kunambi, balozi Richard Wambura alitoa kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa. Mwadhama Kardinali Lauriani Rungambwa aliwakaribisha Mapadre wa shirika la Consolata kuja kuanzisha jengo la Kanisa ambalo kwa sasa linatumika kama ukumbi wa michezo ya ndani kwa ajili ya watoto.

Tarehe 18 machi 1973 Ubungo Msewe ilipewa hadhi ya kuwa Parokia. Paroko wa kwanza alikuwa Padre Igino Lumetti akisaidiwa na Padre Romano Motter na mwenyekiti wa kwanza wa HWP alikuwa chifu G.P Kunambi. Hawa walifanya kazi kubwa ya kujenga nyumba ya Mapdre.Mnamo tarehe mosi Februari 1973 Kigango cha Mavurunza walianza kupata huduma baada ya kupata Paroko mpya Mario Biestra. Kanisa la sasa la Msewe lilianza kujengwa tarehe 9 Agosti,1976 na kutabarukiwa na Mwadhama Kadinarli Laurian Rugambwa tarehe 15 februari 1978. Sherehe hiyo ilihudhuliwa na viongozi wa shirika la Consolata na serikali iliwakilishwa na Mwalimu Julius K.Nyerere. Tarehe 19 Julai 1978. Padre Romano Motter aliteuliwa kuwa Paroko wa Ubungo Msewe.

Mnamo terehe 28 Desemba 1980 Kigango cha Makoka na Makabe vilibarikiwa Tarehe 29Aprili 1984, Kigango cha Mbezi Luis kilibarikiwa . Terehe 23 Februari 1983 Padre Ricardo Ossola alikuja kama Paroko Msaidizi na hapo Kigango cha Kimara kikaanza kupata huduma. Tarehe 2/3/1986 – Paroko mpya Padre Luciano Scaccia Tarehe 25/8/1996 – Paroko mpya Padre Lucio Abrami Tarehe 25/4/1999 – Paroko mpya Padre Alois Accossato Tarehe 13/3/2000 – Parokia ya Mbezi Luis Ilizinduliwa Tarehe 6/1/2001 – Parokia ya Mavurunza Ilizinduliwa Tarehe 24/6/2002 – Paroko mpya Padre Piero Cravero Tarehe 30/11/2003 – Parokia ya Kimara Ilizinduliwa Mwaka wa 2012 – Paroko mpya Padre Dido Ambinikosi Nesapongo na Msaidizi Padre

Casimiro Torres. Mwezi Julai 2015 mpaka sasa - Paroko mpya Padre Casimiro Torres na Msaidizi Padre

Emmanuel Bwanamdogo.

Tarehe 12/5/2002 walikuja Masista wa Moyo Safi wa Maria kutoka India na wanaendesha huduma ya Hospitali. Parokia ya Ubungo kwa sasa ina kigango kimoja, nacho ni Golani kilichozinduliwa tarehe 28/8/201; na Parokia Teule – Baruti. Baruti kama Kigonga kilizinduliwa tarehe 9/9/2003 na kanisa kutabarukiwa tarehe 6/7/2012. Jumla ya kanda zipo saba na jumla ya jumuiya ndogondogo ni sabini (70) zenye waumini wapatao

6,374 kwa mujibu takwimu za sensa ya Wakatoliki ya 2016.

Page 3: PAROKIA YA MT. PAULO: UBUNGO MSEWE, S.L.P 20973, DSM · JNN pamoja na vyeti halisi{Original} vya Ubatizo kutoka Parokia walikopata Ubatizo, Komunyo na Kipaimara. Vile vile kila mmoja

MIAKA 150 YA UINJILISHAJI TANZANIA BARA

SALA YA JUBILEI

Ee Mungu Mwenyezi, Baba wa Milele, tunakushukuru kwa zawadi ya Mwanao mpendwa Yesu kristo,

aliyetwaa mwili kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, akazaliwa na Bikira Maria. Yeye alihubiri neno lako

na kukamilisha ukombozi kwa mateso, kifo na ufufuko wake wa ajabu. Hatimaye aliwaagiza mitume

wake akisema, “Enendeni ulimwenguni mwote mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na

kubatizwa ataokoka, asiyeamini atahukumiwa “(Mk 16; 15-16).

Kwa kuitika agizo hilo, wakati ulipowadiwa, kwa mapenzi yako uliwavuvia Watawa mashuhuri wa

Shirika la Roho Mtakatifu, ambao kwa ujasiri wa ajabu walifika huku kwetu, wakausimika Msalaba

katika kituo cha Bagamoyo. Msalaba huo ni ishara ya ushindi wa Mwanao dhidi ya dhambi na mauti.

Wamisionari hao wakishirikiana na wenzao waliofika baadaye, walikuhubiri Wewe. Nasi tuliopata

imani kwa mahubiri yao, tunakukiri Wewe kuwa Bwana Mungu wetu, mwingi wa huruma, mwenye

fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli. ( Ayubu 4:3).

Basi, tunaposheherekea yubilei ya miaka 150 ya Kanisa Katoliki Tanzania Bara tunakuabudu katika

maongozi yako. Tunakushukuru kwa kuongezeka kwa imani inayoonekana katika idadi ya Waamini

Walei, Makatekista, Watawa, Mapadre na Maaskofu wazalendo. Tunakushukuru kwa kutuwezesha

kuhudumia taifa letu katika elimu, afya na huduma nyingine za kijamii.

Tunajua kuwa bila wewe hatuwezi kitu, tunakuomba uwe pamoja nasi katika kukabiliana na

changamoto mbalimbali kwenye taifa letu siku hizi hasa ulevi wa pombe na dawa za kulevya,

usafirishaji haramu wa binadamu, ugaidi, maradhi, ubakaji, ulawiti, dhuluma, ushirikina na ulegevu

wa dini.

Tunamwomba Mama Bikira Maria, Nyota ya uinjilishaji mpya na Mlinzi wa Taifa letu, atuombee

kwako daima ili tuendelee kuihubiri injili yako katika maisha yetu ya kila siku.

Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wetu. Amina.

Page 4: PAROKIA YA MT. PAULO: UBUNGO MSEWE, S.L.P 20973, DSM · JNN pamoja na vyeti halisi{Original} vya Ubatizo kutoka Parokia walikopata Ubatizo, Komunyo na Kipaimara. Vile vile kila mmoja

MAENDELEO YA PAROKIA

Tegemeza Parokia Mwaka 2017

- Kukarabati Kanisa la Msewe ambalo paa lake linavuja wakati wa mvua, na kupaka rangi

kanisa nzima, ndani na nje.

- Kuanza ujenzi wa Kanisa la Kigango cha Golani

- Ujenzi wa nyumba ya Mapadre Parokia Teule Baruti

“Mtumaini Mungu atupaye vitu vyote kwa wingi ili tuvitumie kwa furaha. Mtende mema, muwe

matajiri kwa kutenda mema, muwe tayari kutoa mali zenu, mshirikiane na wengine kwa moyo… ili

mpate uzima ulio kweli kweli. ”

1 Thimotheo 6: 17-19

PAROKO: FR. CASIMIRO TORRES, IMC

PAROKO MSAIDIZI: FR. EMMANUEL BWANAMDOGO, IMC

RATIBA OFISI YA PAROKIA

KILA SIKU ZIFUATAZO MAPADRE NA KARANI WAPO OFISINI:

KILA JUMATATU NI MAPUMZIKO

JUMANNE HADI IJUMAA KUANZIA SAA 2 ASUBUHI HADI SAA 6 MCHANA/ SAA 9 ALASIRI HADI SAA

11:30 JIONI

JUMAMOSI SAA 2 ASUBUHI HADI 6 MCHANA

Page 5: PAROKIA YA MT. PAULO: UBUNGO MSEWE, S.L.P 20973, DSM · JNN pamoja na vyeti halisi{Original} vya Ubatizo kutoka Parokia walikopata Ubatizo, Komunyo na Kipaimara. Vile vile kila mmoja

SALA NA IBADA YA KILA WIKI NA KILA MWEZI

1. KANISANI MSEWE NA BARUTI KILA SIKU ASUBUHI SAA 12:30 MISA PAMOJA NA MASIFU.

2. JUMATATU, JUMANNE NA JUMATANO SALA YA WAKARISMATIKI KANISANI SAA 10-12

JIONI.

3. KILA ALHAMISI IBADA YA KUABUDU EKARISTI TAKATIFU SAA 10:00 HADI 12:00 JIONI

PAROKIANI MSEWE NA BARUTI. ALHAMISI ZA KWANZA YA KILA MWEZI IBADA YA

KUABUDU EKARISTI TAKATIFU INAANZA SAA 9:00 ALASIRI HADI 12:00 JIONI. WOTE

WANAALIKWA KUHUDHURIA. NAFASI YA KUPATA SAKRAMENTI YA KITUBIO IPO.

4. KILA IJUMAA MISA TAKATIFU NI SAA 11:00 JIONI. KWANZIA SAA 10 NAFASI YA KUPATA

SAKRAMENTI YA KITUBIO IPO.

5. SALA YA ROZARI TAKATIFU KILA SIKU YA MWEZI MEI NA OKTOBA PAROKIANI MSEWE

NA BARUTI SAA 11 JIONI. WAUMINI WOTE WANAALIKWA.

6. JUMAMOSI YA KWANZA YA KILA MWEZI MISA KIGANGO CHA GOLANI, JUMAMOSI YA

PILI YA KILA MWEZI MISA PAROKIA TEULE BARUTI NA JUMAMOSI YA MWISHO YA KILA

MWEZI MISA PAROKIANI MSEWE. MISA INAANZA 12:30 ASUBUHI.

Page 6: PAROKIA YA MT. PAULO: UBUNGO MSEWE, S.L.P 20973, DSM · JNN pamoja na vyeti halisi{Original} vya Ubatizo kutoka Parokia walikopata Ubatizo, Komunyo na Kipaimara. Vile vile kila mmoja

UTARATIBU WA MAFUNDISHO YA SAKRAMENTI PAROKIA

UBATIZO - JUMANNE: 10:00 JIONI

MSEWE: MWAKA WA KWANZA – Katekista Julius

MWAKA WA PILI - Katekista Julius

BARUTI: MWAKA WA KWANZA - Katekista Cristina

MWAKA WA PILI - Katekista Cristina

GOLANI: Katekista Mgolola

.

KOMUNIO - JUMATATU NA JUMATANO SAA 10:00 JIONI

MSEWE: Katekista Priscila

BARUTI: Katekista Cristina

GOLAN: Katekista Mgolola

KIPAIMARA - IJUMAA NA JUMAMOSI SAA 10 JIONI

MSEWE: Katekista Priscila

BARUTI: Katekista Cristina

GOLAN: Katekista Mgolola

KUNDI MAALUMU - VIJANA NA WATU WAZIMA

MSEWE: Katekista Julius na Priscila

BARUTI: Katekista Cristina na Mama Urasa

GOLAN: Katekista Mgolola

Page 7: PAROKIA YA MT. PAULO: UBUNGO MSEWE, S.L.P 20973, DSM · JNN pamoja na vyeti halisi{Original} vya Ubatizo kutoka Parokia walikopata Ubatizo, Komunyo na Kipaimara. Vile vile kila mmoja

UTARATIBU WA UBATIZO WA WATOTO WACHANGA

1. FOMU ZA UBATIZO

Wazazi wawe na fomu kutoka kwa viongozi wa jumuiya Ndogondogo na ziwe

zimewasilishwa kwa Karani kabla ya semina.

2. SEMINA YA UBATIZO

Wazazi na Wasimamizi wa watoto wanaotaka kupewa Ubatizo lazima wahudhurie semina

ya ubatizo inayotolewa mara nne kwa mwaka kwa tarehe za Jumamosi ya pili ya miezi

Aprili, Julai, Oktoba na Desemba hapa Parokiani saa 2:00 asubuhi. Msimamizi sharti awe

Mkatoliki mwenye maadili mema.

3. SAKRAMENTI YA UBATIZO INATOLEWA PAROKIANI PASAKA, JULAI, OKTOBA NA

NOELI.

4. MAZISHI YA KIKATOLIKI

Ili Kanisa liweze kutoa huduma ya mazishi ya Kikatoliki ipasavyo lazima taarifa ya kifo

itolowe kwa Mapadre mapema iwezekanavyo ili waweze kujipanga. Aidha misa za

mazishi ikiwezekana zifanyike Kanisani.

Katekista anaweza kutumwa kuendesha ibada ya mazishi. Ikishindikana kuja

Katekista; viongozi wa JNN waendeshe ibada wao wenyewe.

Matoleo ya misa {Ibada} yapelekwe Parokiani na misa itatolewa kwa ajili ya

Marehemu.

Page 8: PAROKIA YA MT. PAULO: UBUNGO MSEWE, S.L.P 20973, DSM · JNN pamoja na vyeti halisi{Original} vya Ubatizo kutoka Parokia walikopata Ubatizo, Komunyo na Kipaimara. Vile vile kila mmoja

UTARATIBU WA MAFUNDISHO KUHUSU WATAKAJI NA

WAKATUKUMENI, KOMUNYO YA KWANZA NA KIPAIMARA

1. Tunaanza rasmi kuwaandikisha wanafunzi na kutoa mafundisho yaliyotajwa hapo juu

kuanzia tarehe 01 Julai hadi 15 Septemba.

2. Mkutano wa wazazi na watoto wa mafundisho utafanyika mara mbili kwa mwaka

3. Watoto wa Komunio ya kwanza na Kipaimara watatoa zaka zao hapa parokiani.

4. Watakaji watakaopokelewa ni wale wanaosoma hatua ya pili{darasa la 2} kwa mwaka

huu na ambao watasoma kwa muda wa miaka miwili. Watakaobatizwa Pasaka

watapewa pia Komunyo ya Kwanza.

5. Ubatizo na Komunyo ya kwanza - watakaopokelewa ni wale ambao wanaosoma

darasa la 3, 4, na 5 na wanaotaka kujiandikisha wawe wamejiunga na Utoto mtakatifu

ama watumishi wa altare.

6. Kipaimara - Watakaopokelewa ni wanafunzi wa darasa la 5, 6 na 7 hadi sekondari.

Watu wazima pia wanapokelewa bila kujali anasoma darasa gani ama hasomi.

7. Wanaopokelewa wanatakiwa waje na Katekisimu, Biblia, Daftari na Kalamu.

8. Wanaojiandikisha waje na vyeti vya Ubatizo, Barua/Fomu iliyojazwa ipasavyo na

viongozi wa Jumuiya Ndogo Ndogo.

Page 9: PAROKIA YA MT. PAULO: UBUNGO MSEWE, S.L.P 20973, DSM · JNN pamoja na vyeti halisi{Original} vya Ubatizo kutoka Parokia walikopata Ubatizo, Komunyo na Kipaimara. Vile vile kila mmoja

UTARATIBU WA NDOA

1. Ndoa lazima iandikishwe ofisini kwa Padre miezi mitatu kabla ya tarehe inayotarajiwa

kufungwa hii ni utaratibu wa Jimbo.

2. Katika Jimbo Kuu la Dar es salaam harusi inafungwa tu Jumamosi na siyo Jumapili au

Ijumaa ni Utaratibu kutoka Jimboni.

3. Maharusi wanatakiwa wote wawili wafike ofisini kujiandikisha wakiwa na fomu ya

JNN pamoja na vyeti halisi{Original} vya Ubatizo kutoka Parokia walikopata Ubatizo,

Komunyo na Kipaimara. Vile vile kila mmoja aje na picha moja ya passport size.

4. Wanaotaka kufunga Ndoa ni lazima wahudhurie mafundisho/semina ya ndoa

inayofanyika Msimabazi Centre.

5. Waamini Wakatoliki wanaofunga ndoa na asiye Mkatoliki ni lazima apate ruksa/kibali

cha Askofu. Kinyume na hilo watakuwa wamejitenga na Kanisa Katoliki wao wenyewe.

6. Wasimamizi wa ndoa wawe Wakatoliki lakini sio lazima wawe mume na mke. Aidha ni

vyema zaidi wakiwa ni mume na mke.

7. Sakramenti ya Ndoa siyo maigizo kwa hiyo watoto na wapambe wa harusi

wawasindikize Maharusi mpaka mlango wa Kanisa ambapo Padre atawapokea tayari

kwa maandamano ndani ya kanisa. Bwana na Bibi harusi wataongoza maandamano

wakifuatiwa na wasimamizi na wapambe wao nyuma.

8. Misa ya ndoa inaanza saa kumi jioni (10:00)

9. Gharama zinazohusiana na ndoa zilipwe ofisini mara baada ya kuleta cheti cha

semina/mafundisho ya Msimbazi Centre. Gharama hizo ni:

Shahada na Office 60,000 na Kwaya 40,000

Page 10: PAROKIA YA MT. PAULO: UBUNGO MSEWE, S.L.P 20973, DSM · JNN pamoja na vyeti halisi{Original} vya Ubatizo kutoka Parokia walikopata Ubatizo, Komunyo na Kipaimara. Vile vile kila mmoja
Page 11: PAROKIA YA MT. PAULO: UBUNGO MSEWE, S.L.P 20973, DSM · JNN pamoja na vyeti halisi{Original} vya Ubatizo kutoka Parokia walikopata Ubatizo, Komunyo na Kipaimara. Vile vile kila mmoja

Groto la Mama Bikira Maria

PAROKIA MT. PAULO – UBUNGO MSEWE