sarufi ya kiswahili na sintaksia (nukuu) · web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa...

103
Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018 OSW 221/231 SARUFI YA KISWAHILI NA SINTAKSIA (NUKUU) www.mwalimuwakiswahili.co.tz www.uwasokita.co.tz 0717104507 Uk 1

Upload: others

Post on 13-Mar-2021

66 views

Category:

Documents


8 download

TRANSCRIPT

Page 1: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

OSW 221/231

SARUFI YA KISWAHILI NA SINTAKSIA (NUKUU)

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 1

Page 2: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

Ufafanuzi wa Kozi

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia ni kozi inayochambua sarufi ya Kiswahili kwa kuzingatia nadharia za sarufi kama zilivyoasisiwa na wanazuoni wa lugha na isimu. Uchambuzi wa lugha umekuwa ukifanywa kwa kuzingatia nadharia zilizoibuliwa na wanazuoni wa lugha katika vipindi tofauti vya maendeleo ya utafiti wa lugha. Kipindi kilichoanzia zama za Wagiriki na kufuatiwa na Warumi wakichunguza lugha zao: Kigiriki na Kilatini kwa mfuatano huo, uchambuzi wa lugha ulizingatia nadharia ambazo baadaye zilipokelewa na wanazuoni wa lugha za Ulaya za siku hizi kama vile Kiingereza, Kifaransa, Kijerumani, n.k.

Wanazuoni wa lugha hizi walirithisha elimu hii ya lugha katika nchi zinazoendelea ambapo wanazuoni wake walipokea mbinu hizi za uchambuzi na kuzitumia kuchanganua lugha zao. Kutokana na mapokeo haya nadharia hii ya uchambuzi wa lugha inajulikana katika Kiswahili kama Sarufi Mapokeo. Mkabala wa uchambuzi wa wanamapokeo ulikuwa katika kiunzi cha kiima-kiarifu japokuwa wanazuoni tofauti wa wakati huo walizua mikabala midogo tofauti ndani ya kiunzi hiki, mathalani: sarufi msonge. Kutokana na kuzuka kwa fikra mpya za kuchambua lugha na kuhoji nadharia zilizotangulia, wanazuoni mamboleo waliibua mtazamo mpya wa kuchambua lugha ambao walidai ni wa kisayansi zaidi. Mkabala huu uliitwa Sarufi Miundo. Hata hivyo, kama ilivyokuwa kwa sarufi mapokeo ambayo ilikuwa na mikabala tofauti ndani yake, vivyo hivyo kwa sarufi miundo ambayo iliendelezwa na kuwa na Sarufi miundo virai, Sarufi geuzaumbo, n.k.

Sintaksia ni tawi la isimu linalohusu namna maneno yanavyounda virai na sentsni. Sintaksia inahusu tungo za lugha ambazo zaweza kuwa ni maneno, kirai, vishazi na sentensi. Japokuwa neno ni kipashio cha maumbo, lenyewe lina muundo wake unaotokana na viambajengo vinavyoliunda ambavyo ni mzizi na viambishi. Hii ndio sababu neno linasadifu kuingia katika sintaksia ya lugha.

Kozi itaanza kwa kutalii jinsi wanamapokeo walivyochambua lugha kwa kutalii mkabala wa Sarufi Mapokeo ulivyochambua muundo wa sentensi. Kisha itachunguza viambajengo vya msingi vya lugha: mofimu na neno. Mofimu kama kipashio cha msingi cha lugha kitachunguzwa na kuchambuliwa, kisha uchambuzi utafanywa ili kuona jinsi kipashio hiki kinavyounda maneno. Aidha mkabala wa

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 2

Page 3: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

sarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia za msingi za sintaksia kama vile sarufi miundo virai na sarufi zalishi. Katika kozi hii virai na sentensi vitachanganuliwa ili kubaini miundo yake.

Malengo ya Kozi

Katika kozi hii wanafunzi wanatarajiwa kufanya yafuatayo:

a) Kuelewa mikabala ya uchambuzi wa lugha

1. Sarufi mapokeo2. Sarufi miundo

b) Kufahamu elementi za muundo wa sentensi kwa mujibu wa mikabala ya uchanganuzi wa lugha

c) Kuelewa maana ya sintaksia

d) Kutambua kategoria kuu na kategoria ndogo za sintaksia

e) Kueleza umuhimu wa kategoria za sintaksia katika kujifunza sintaksia

f) Kufahamu nadharia mbalimbali za sarufi miundo: sarufi miundo virai, sarufi geuzaumbo/geuzi

g) Kuchanganua sentensi kwa mujibu wa nadharia za sarufi miundo

Madhumuni ya Kozi

Katika kozi hii wanafunzi wanatarajiwa kufanya yafuatayo:

a) Kufahamu vipengele mbalimbali vya sarufi ya Kiswahili kama vile vipashio vya lugha, mofimu, neno, virai, vishazi na sentensi, aina za maneno, uainishaji wa ngeli za nomino.

b) Kupata ufahamu wa mikabala mbalimbali ya uchanganuzi wa sentensi: sarufi mapokeo na sarufi miundo, sarufi geuza umbo.

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 3

Page 4: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

c) Kuelewa misingi ya uainishaji wa sentensi kwa kuzingatia mikabala ya sarufi mapokeo na sarufi miundo.

d) Kuelewa sarufi miundo pamoja na kanuni za miundo virai.

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 4

Page 5: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

Moduli 1: SARUFI NA MANTIKI KATIKA LUGHA

Muhadhara wa kwanza: Maudhui

Sarufi na Mantiki ya Lugha

Katika mhadhara huu utaweza kujifunza:

(i) Maana ya sarufi

(ii)Mantiki katika lugha

(iii) Maana ya sarufi mapokeo

(iv) Taarifa zinazodhihirika katika kitenzi

Muhadhara huu unatalii mtazamo wa wanamapokeo kuhusu lugha na namna walivyochambua sentensi.

1. Maana ya sarufi

Sarufi ni tafsiri ya neno la Kiingereza “grammar” ambalo asili yake ni neno la Kigiriki lenye maana ya “Usahihi” unaohusishwa na sanaa ya maandishi (Habwe na Karanja, 2012). Hivyo sarufi ni utaratibu wa kanuni zinazomwezesha mtumiaji wa lugha kutoa na kuelewa tungo sahihi na zisizosahihi. Kwa ujumla sarufi inachunguza kanuni na taratibu za lugha ya mwanadamu. Kwa mtazamo wa kimapokeo, sarufi ina lengo la kuelekeza matumizi sahihi na yasiyosahihi ya lugha kwa kuelekeza sheria na kanuni za lugha.

Aidha sarufi pia ni taaluma inayohusu vipashio vya lugha na kanuni zinazotawala uundwaji wake. Kwa hivyo mwanasarufi huchunguza vipashio hivyo pamoja na namna yanavyoundwa na kupangiliwa katika tungo na kuifanya itoe maana kamili. Sarufi yaweza kuwa elekezi au arifu.

Pamoja na hayo, sarufi ni mfumo wa kanuni za lugha zilizo katika ubongo wa mzawa wa lugha ambazo hudhihirika anapozungumza. Kanuni hizi humwezesha mzawa kutunga sentensi zisizo na kikomo ambazo hubadilika na wazawa wa lugha wanaoifahamu lugha hiyo bara bara.

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 5

Page 6: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

Hivyo sarufi inahusishwa na sintaksi kwa kuwa sintaksia ni sehemu ya sarufi ya lugha inayoshughulikia muundo wa sentensi. Sintaksia inajikita katika kiwango cha sentensi ambapo mofolojia inashughulika katika kiwango cha neno hai ya kuwa fonolojia inajikita katika kiwango cha sauti za lugha. Viwango hivi vyote vinajikita katika kushughulikia sheria na taratibu za lugha.

2. Mantiki katika Lugha

Mantiki katika lugha ni mifumo mbalimbali inayojitokeza ndani ya lugha ambayo inaonesha nidhamu kamili, mathalani nomino za umoja huwa na wingi wenye kuzingatia utaratibu mahsusi wa uambishaji. Nidhamu hii inapaswa kujitokeza katika nomino zote, mfano m-toto> wa-toto: m-zee > wa-zee, n.k. Iwapo nomino zote za lugha zingefuata mfumo huu tunasema kuwa lugha ina mantiki kwa sababu ya kuwa na nidhamu hiyo, lakini iwapo hii haiwezekani tunasema haina mantiki. Data ya uambishaji wa nomino za umoja na wingi zinaonesha kuwa nomino hazina mfumo maalumu wa kuambisha ili kupata za umoja na wingi. Zipo nomino ambazo zina viambishi vya umoja na vya wingi, mfano m-tu > wa-tu, na nyingine hazina viambishi. Kwa mfano samaki (umoja) na samaki (wingi), na nyingine zina viambishi vya umoja tofauti lakini viambishi vya wingi vinafanana. Mfano ji-we, ma-we, ji-no, me-no, embe > ma-embe, chungwa > ma-chungwa. Katika mifano hii nomino za ngeli ya 1 zina kiambishi cha umoja mu- na kiambishi cha wingi wa-

Hata hivyo katika nomino nyingine kama vile samaki > samaki, nyumba > nyumba, ji-we > ma-we, embe > ma-embe tunaona kuwa hakuna mfumo mmoja wa kuambisha nomino za umoja na wingi. Baadhi ya nomino zina viambishi vya umoja na wingi vinavyofanana kwa nomino za ngeli moja, nyingine hazina viambishi vya umoja na wingi, na nyingine zina viambishi vya umoja na wingi tofauti lakini viambishi vya wingi vinafanana. Kwa hali hii ni dhahiri kuwa lugha haina mantiki.

Upeo wa Sintaksia

Sintaksia inachunguza viambajengo vya sentensi kwa kushughulika na uteuzi na mpangilio wa maneno ambao huunda vipashio vikubwa kama virai na vishazi

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 6

Page 7: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

katika sentensi. Hivyo katika kiwango cha sentensi sintaksia inajishughulisha na masuala yafuatayo:

a) Uainishaji wa maneno na viambajengo vyake katika kujenga sentensi

b) Uchunguzi wa mpangilio wa maneno katika sentensi

c) Uchunguzi wa uhusiano wa maneno na vipashio vingine vya sentensi

d) Uchambuzi wa miundo ya sentensi

e) Uchambuzi wa nadharia na sheria zinazotawala miundo ya sentensi

Sintaksia imepitia katika awamu kuu tatu ambazo ni: Awamu ya Sarufi Mapokeo, Sarufi Miundo na Sarufi Geuzi.

Sarufi Mapokeo

Kwa mujibu wa maelezo ya Massamba (2004) Sarufi Mapokeo ni jumla ya mikabala mbalimbali iliyotumika zamani kuelezea miundo ya lugha ambayo ilikuwa imekitwa katika Sarufi ya Kigiriki na Kilatini. Kutokana na maelezo haya ni dhahiri kuwa Sarufi Mapokeo ni Sarufi ya kale. Sarufi Mapokeo ni mikabala ya uchambuzi wa lugha ambayo ilianzishwa na wanazuoni wa Kigiriki ili kuichambua lugha yao kwa mujibu wa kanuni walizojiwekea. Mkabala huu wa uchambuzi wa lugha uliasisiwa na Wagiriki na kuendelezwa na Warumi katika lugha yao ya Kigiriki na baadaye Kilatini. Wanazuoni wa Kilatini ndio walioueneza mkabala huu huko Ulaya katika lugha za huko k.k. Kiingereza, Kifaransa n.k. ambazo nazo zilitumika kueneza mkabala huu wa kiuchambuzi katika lugha nyingine, Tanzania ikiwa mojawapo. Hivyo lugha zingine ziliakisiwa kwa kutumia mkabala huo wa Kilatini na lugha ambazo hazikuandikwa zilitazamwa kuwa hazina Sarufi.

Japokuwa Sarufi mapokeo inatazamwa leo kama mkabala au nadharia ya lugha, haikuwa na vikundi mbalimbali vya wataalamu kama wataalamu wa Kiyunani, Kirumi na Kiingereza. Sarufi mapokeo ni mkabala wa kisarufi ulioasisiwa na wanasarufi wa kale na wanafalsafa wa Kigiriki k.v. Plato, Aristotle, Dionysius Thrax au Protagoras miaka mingi kabla ya kristo na kuendelea kutumiwa takribani miaka mingi baada ya Kristo. Sarufi mapokeo ilielekeza watu jinsi ya kutumia

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 7

Page 8: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

lugha. Uelekezi ulijikita katika sheria za lugha ya Kilatini. Vilevie Sarufi mapokeo ilijikita katika lugha ya kimaandishi.

Msingi wa uchambuzi wa lugha wa wanamapokeo ulikuwa ni neno na sentensi. Nomino ilikuwa kiima na tendo ilikuwa kiarifu japokuwa hawakutumia istilahi za kiima na kiarifu. Plato alichambua sentensi kwa kuigawa katika sehemu kuu mbili: nomino na tendo. Plato alibainisha neno huru katika sentensi na kisha kuliainisha kama ni nomino ambayo ilifanya kazi kama kiima na tendo ambalo lilieleza matendo ya kiima.

Dionysius Thrax alitambua kuwa kipashio cha msingi cha lugha ni neno na kisha kuyachambua na kuyaweka katika aina nane ambazo ni nomino, kitenzi, kihusishi, kielezi, kivumishi, kiwakilishi, kiingizi (kihisishi) na kiungo.

Protagoras aliainisha sentensi kwa kuzigatia maana au nia inayobebwa na sentensi ambayo yaweza kuwa: taarifa/maelezo, swali au amri.

Aristotle alibaini kiunganishi katika lugha kuwa ni aina ya maneno inayojitegemea. Alibaini pia uelekezi ulio katika kitenzi kwa kuonesha kitenzi elekezi na kitenzi si-elekezi.

Misingi yam kabala wa Sarufi mapokeo

(i) Kilatini kilikuwa msingi wa uchambuzi wa Sarufi ya lugha kwa kuwa ndiyo lugha iliyokuwa imeandikwa wakati lugha ilipoanza kuchanganuliwa. Kwa hivyo ubora wa lugha au udhaifu wake ulipimwa kwa kuitazama iwapo ilikuwa ina sifa za lugha ya Kilatini.

(ii)Uwepo wa kanuni za matumizi ya lugha ambazo zilibainisha jinsi ya kutamka na kuandika lugha kwa usahihi. Kutokana na msingi huu wasemaji wazuri wa lugha waliteuliwa kufundisha lugha.

(iii) Lugha ya maandishi ilikuwa bora kuliko isiyoandikwa, kwa hivyo Sarufi ya lugha iliyoandikwa ilichukuliwa kuwa bora kuliko ya lugha isiyoandikwa

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 8

Page 9: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

(iv) Sentensi iliundwa kwa vijenzi au viambajengo. Plato alibainisha kiima na yambwa na Aristotle alibainisha kategoria za maneno zinazounda sentensi: nomino, kitenzi, kivumishi, kielezi, kihusishi, kiunganishi.

Muhadhara wa Pili: Maudhui

Sarufi mapokeo kama msingi wa Nadharia ya Isimu

Utangulizi

Sarufi mapokeo ni Sarufi ya kale iliyoasisiwa na Wagiriki na kisha kuendelezwa na wanazuoni wa Kilatini na lugha za Ulaya na Marekani. Kwa kuzingatia taaluma hii ya lugha wanazuoni hawa waliweka misingi ya kuchambua lugha ambayo ilifuatwa na wanazuoni wengine walipochambua lugha zao. Baadhi ya mambo waliyozingatia ni pamoja na : aina za maneno na kuweka kanuni za jinsi watu wanavyopaswa kuongea.

Katika muhadhara huu utaweza kufahamu yafuatayo:

a) Misingi yam kabala wa Sarufi mapokeo

b) Udhaifu wa Sarufi mapokeo

c) Mchango wa wanamapokeo katika uchambuzi wa lugha

Udhaifu wa Sarufi mapokeo

Kwa mujibu wa Matinde (2012) Sarufi mapokeo ilikuwa na udhaifu ufuatao.

a) Kilatini kilitumiwa kama kigezo cha kupimia ubora wa lugha. Hii ni kasoro kwani kila lugha ina namna yake ya kutamka maneno, kuunda maneno na kutunga sentensi. Kwa hivyo hakuna lugha iliyo bora kuliko nyingine kwani kila moja ina muundo wake na inawawezesha watumiaji wake kuwasiliana.

b) Wazungumzaji wa lugha wanajua sheria zinazotawala muundo wa lugha yao kama sehemu ya umilisi wa lugha kwa hivyo sio sahihi kuwekewa sheria za namna ya kutumia lugha yao.

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 9

Page 10: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

c) Madai kuwa lugha zisizoandikwa sio lugha ni mtazamo potofu kwani lugha ya mazungumzo ndiyo kongwe zaidi kuliko lugha ya maandishi, kwa hivyo lugha ya mazungumzo na ya maandishi zina hadhi sawa. Isitoshe kila jamii imekuwa nayo kabla ya kuanza kwa taaluma ya maandishi.

d) Wanamapokeo walishughulikia sentensi zenye muundo sahili tu.

e) Wanamapokeo hawakutoa umuhimu wa umilisi na ubunifu wa mzungumzaji wa kuweza kutunga sentensi nyingi sahihi na zisizo na ukomo, na badala yake kuwawekea kanuni za namna ya kuzungumza.

Mchango wa wanasarufi mapokeo katika uchambuzi wa lugha

Wanamapokeo wamechangia taaluma ya uchambuzi wa lugha ambao ulikuwa msingi wa nadharia mbalimbali za isimu.

Uchambuzi wa lugha kwa mujibu wa mkabala wa wanasarufi mapokeo ikilinganishwa na mkabala wa Sarufi mamboleok.v. Sarufi miundo, inaelezwa kuwa ni Sarufi elekezi (prescriptive grammar) kwani ilikuwa inaelekeza jinsi lugha inavyopaswa kuwa kwa kuzingatia sheria na kanuni za matumizi ya lugha ambazo watumiaji wake wanapaswa kuzifuata. Hii ni tofauti na Sarufi mamboleo ambazo hueleza lugha jinsi ilivyo na inavyotumika. Kwa kuzingatia mkabala huu, Sarufi mamboleo yajulikana kama Sarufi elekezi (descriptive grammar).

Sarufi mapokeo ililenga kutofautisha jinsi watu wanavyotumia lugha na jinsi wanavyopaswa kuitumia.

Sarufi za mwanzo za lugha mbalimbali za dunia zilizoandikwa baada ya kuandikwa Sarufi za Kigiriki na Kilatini zilikuwa ni tafsiri ya Sarufi ya lugha hizo za Kigiriki au Kilatini. Kwa mfano Sarufi za awali za Kiingereza, Kifaransa au Kijerumani zilikuwa ni tafsiri ya Sarufi ya Kigiriki ambayo ilikuwa tayari na umri wa miaka elfu mbili. Kuanzia karne ya 17 hadi nusu ya kwanza ya karne ya 19, Sarufi ya Kiingereza haikuwa na mabadiliko makubwa na Sarufi ya Kilatini katika vitabu vya Sarufi na namna ilivyofundishwa. Kwa hivyo tunapozungumzia Sarufi mapokeo tunazingatia utaratibu wa kuchambua lugha uliofuatwa na wanazuoni wa Kilatini hata kama lugha iliyochambuliwa haikuwa Kilatini.

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 10

Page 11: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

Sarufi mapokeo ilianza kukosolewa mnamo katikati mwa karne ya 19 wakati kulipokuwa na mabadiliko makubwa katika kufundisha Sarufi. Wakati ambapo Sarufi mapokeo ilijikita katika neno. Sarufi mamboleo ambayo ilianza miaka ya 1950 ilijikita katika kuchambua sentensi na kuchambua mpangilio wa maneno katika tungo. Mabadiliko haya yalileta Sarufi miundo ambayo ilichunguza miundo ya vipashio kama vile virai na sentensi.

Wanasarufi mapokeo waliamini kuwa Kilatini kilikuwa na mantiki kamili na kwamba kazi ya wanaisimu ni kutafuta na kueleza mantiki ya lugha na kuzuia matumizi yasiyo sahihi. Kwa hali hiyo wanafunzi huko Ulaya walitakiwa wajifunze Sarufi ya Kilatini ili wapate kujua Sarufi za lugha nyingine kwa urahisi.

Sarufi ya Kilatini ilichukuliwa kama kiunzi cha kueleza Sarufi ya lugha nyingine.kwa mujibu wa mtazamo huu, lugha ambazo zilikuwa na Sarufi inayofanana na ya Kilatini, mfanano huo ulionekana kuthibitisha ukweli kuwa mtu akijua Sarufi ya Kilatini anaweza kujifunza Sarufi ya lugha nyingine. Aidha inapotokea kuwa Sarufi ya lugha nyingine ikatofautiana na ya Kilatini ilidaiwa kuwa lugha hiyo imekengeuka. Wanaisimu wengi wanadai kuwa lugha haina mantiki kwa sababu ina mambo mengi ambayo hayana mantiki. Kwa mfano:

Lugha ina nomino zenye viambishi vya wingi tofauti kwa nomino tofauti: child > children, man > men, pin > pins, fly > flies, na hata kwa zile za ngeli tofauti na hata za ngeli moja. Kwa mfano: ngeli ya 1 ya nomino za Kiswahili ni m-(binadamu na wanyama) na ngeli ya 3 ni m-(miti na mimea). Japokuwa ngeli hizi zinafanana kwa umbo zina sifa semantiki tofauti. Hii inaonesha kuwa kwa kutazama umbo la nomino lenye kiambishi ngeli m- hatuwezi kusema kwa yakini kama ni ngeli ipi mpaka tutazame sifa nyingine za nomino. Lugha ingekuwa na mantiki iwapo nomino za ngeli moja zingekuwa na ngeli yake mahususi.

Lugha ina vivumishi ambavyo vinaweza kunyambulishwa na kuwa vitenzi jambo ambalo linafanya vivumishi kukengeuka kutoka kwenye sifa yake ya kuvumishi nomino.

Aidha baadhi ya maneno yana maana zaidi ya moja na mengine yana maana zinazofanana, yaani ni sinonimu.

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 11

Page 12: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

Uchambuzi wa mkabala wa Sarufi mapokeo huanza na ubainishaji wa kategoria za maneno ya lugha. Kategoria za maneno ni nomino, kivumishi, kitenzi, kielezi, kiunganishi, kihusishi, kiwakilishi. Ubainishaji wa kategoria za maneno kwa mujibu wa Sarufi mapokeo ulifanywa kwa msingi wa kazi ya kipashio. Hii ni kwa sababu ufafanuzi wa kategoria hizi umekitwa katika kazi ya kila kimoja. Kwa mfano: nomino, kivumishi, kitenzi, kielezi, kiunganishi, kihusishi kama inavyofafanuliwa zaidi hapa chini.

Baadhi ya kategoria walizozitambua wanasarufi mapokeo ni:

(i) Nomino

(ii)Vitenzi

(iii) Viwakilishi

(iv) Vivumishi

(v)Vielezi

(vi) Vihusishi

(vii) Viunganishi

(viii) Vihisishi

Nomino kwa mujibu wa sarufi mapokeo ni neno linalotaja majina ya vitu, hali, mahali, vyeo na dhana. Hii ndiyo sababu baadhi ya wanasarufi wakaita nomino ni majina.

Viwakilishi ni maneno yanayotumika badala ya nomino kama: mimi, wewe, yule, n.k

Vivumishi ni maneno ambayo hutoa habari juu ya mtu au kitu kwa kuonesha jinsi mtu au kitu hicho kilivyo.

Vitenzi ni maneno ambayo yanaonesha matendo ambapo yaliyotendwa na kitu chochote chenye uwezo wa kutenda jambo

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 12

Page 13: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

Vielezi ni neno fungu la maneno linalofafanua zaidi vitenzi, vivumishi na hata vielezi vingine

Vihusishi ni neno au kundi la maneno yanayohusisha sehemu mbili au zaidi za sentensi.

Viunganishi ni neno au maneno yanayounganisha maneno au mafungu ya maneno

Vihisishi ni maneno ambayo huonesha hisia kama vile hali ya uchungu, kufurahi, kushangaa, kushituka na kadhalika.

Maswali ya mjadala

Jibu maswali yafuatayo

1. Eleza jinsi wanamapokeo walivyochambua sentensi kwa kuzingatia kiunzi cha aina za maneno yanayounda sentensi.

2. Eleza kwa nini Sarufi mapokeo ilikitwa katika Sarufi ya Kigiriki na Kilatini na athari yake katika kuchambua lugha nyingine.

3. Eleza jinsi wanamapokeo walivyotumia dhana ya kategoria za maneno kuchambua lugha.

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 13

Page 14: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

Moduli 2: MOFOLOJIA

Katika muhadhara huu utajifunza yafuatayo:

a) Maana ya mofolojia

b) Maana ya mofimu

c) Maana ya mofu na alomofu

Muhadhara wa kwanza:

Mofolojia, Mofu na Alomofu

1. Maana ya Mofolojia

Mofolojia ni tawi la isimu ambalo huchunguza muundo wa neno kwa kubainisha viambajengo vinavyounda umbo hili. Kwa kuwa neno huundwa na mofu, uchambuzi wa viambajengo vya neno hubainisha mofu zinazounda neno, aina zake na jinsi zinavyoungana na kuunda neno lenye maana.

2. Maana ya Mofimu

Mofimu ni kipashio kidogo kabisa cha lugha cha kidhahania chenye maana ya kisarufi au kileksika ambacho huwakilishwa na mofu katika matumizi halisi ya lugha. Mofimu ni umbo ambalo haliwezi kugawika katika sehemu ndogo zaidi bila kupoteza maana yake.

Mfano: kopo, babu, nyumba, lim-a, m-tu, n.k. kila moja ya maumbo hayo ni mofimu.

Dhana ya mofimu ilikuwa inafasiliwa kama mofu; yaani kipashio kidogo kabisa cha lugha chenye maana lakini baada ya wanaisimu kuasisi Sarufi zalishi ilionekana kuwa mofimu ni dhana ya kidhahania ambayo ilikuwa akilini mwa mzungumzaji na kwamba umbo linalotamkwa kuonesha au kuandikwa ilikuwa mofu. Hii ndiyo maana fasili ya mofu ikawa ni kipashio cha kidhahania chenye maana ambacho katika matumizi huwakilishwa na mofu. Kutokana na mtazamo huu mpya wa wanasarufi, uchambuzi wa

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 14

Page 15: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

kipashio hiki umekitwa kwenye mofu tu na sio mofimu. Tunaainisha mofu na wala sio mofimu.

Mofu za neno zaweza kubainishwa kwa kuchambua viambajengo vinavyounda neno. Chomi (2013) anataja hatua nne za kuzingatia wakati wa kubainisha mofu.

(i) Bainisha viambajengo vinavyounda neno

(ii)Orodhesha viambajengo vya kila neno

(iii)Bainisha na orodhesha viambajengo vinavyojirudia ambavyo vina

maana ileile.

(iv) Chunguza na kujiridhisha kuwa viambajengo vya neno havigawiki katika sehemu ndogo zaidi zenye maana.

Kwa kutumia kielelezo hiki twaweza kubainisha mofimu zilizomo katika maneno tuliyopewa kwa kuchambua viambajengo vinavyounda neno kwa kuzingatia hatua zilizotajwa juu za kubainisha mofimu.

NENO Viambajengo NENO ViambajengoKisu ki Su Visu Vi SuDirisha Ɵ Dirisha Madirisha Ma DirishaMpapai m Papai Mipapai Mi PapaiKiatu ki Viatu Viatu Vi atuMtoto m Watoto Watoto Wa totoMsumari m Misumari Misumari Mi sumariMtu m Watu watu Wa tu

a) Chunguza muundo wa kila neno ulilopewa, yaani viambajengo vinaloliunda.

- Kisu >ki-su : vi-su

- dirisha > dirisha : ma-dirisha

- mpapai >m-papai : mi-papai

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 15

Page 16: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

- kiatu > ki-atu : vi-atu

- mtoto > m-toto : wa-toto

- msumari > m-sumari : mi-sumari

- mtu > m-tu: wa-tu

b) Orodhesha viambajengo vya kila neno

- Ki-su > vi-su

- Dirisha > ma-dirisha

- Embe > ma-embe

- M-papai > mi-papai

- Ki-atu > vi-atu

- M-toto > wa-toto

- M-sumari > mi-sumari

- M-tu > wa-tu

c) Bainisha na orodhesha viambajengo vinavyojirudia ambavyo vina maana ileile.

- Ki-, m-, vi-, m-, wa-, ma-, mi-, su-, -atu, -dirisha, -papai, -toto, -sumari, -tu, -embe.

d) Chunguza na jiridhishe kuwa viambajengo vinavyojirudia havigawiki katika sehemu ndogo zaidi zenye maana. Hakuna kiambajengo chenye kuweza kugawika zaidi.

Kigezo cha uchambuzi huu kinajulikana kama kigezo cha mofimu kutogawika zaidi katika viambajengo vingine vyenye maana.

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 16

Page 17: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

Iwapo maumbo yaliyochambuliwa hayagawiki zaidi, basi maumbo hayo ni mofimu za maneno uliyopewa. Kwa hivyo twaweza kusema kuwa umbo litakuwa mofu iwapo data yetu itakuwa na sifa zifuatazo:

(i)Umbo linajirudia likiwa na maana ileile kama ilivyo katika maumbo ya (c) hapo juu.

(ii)Umbo haligawiki zaidi katika sehemu zenye maana kisarufi, k.v. katika mifano ya (b) hapo juu.

Lugha ina vipashio vitano: mofu, neno, kirai, kishazi na sentensi. Vipashio hivi vina hadhi tofauti, mofu ni kipashio kidogo na sentensi ni kipashio kikubwa zaidi.

Maana ya Mofu

Mofu ni kipashio cha lugha chenye maana ambacho huwakilisha mofimu. Massamba (2004) anafasili mofu kuwa ni kipashio cha kiumbo kinachowakilisha mofimu. Kutokana na fasili hizi ni dhahiri kuwa mofu ni kipashio kidogo cha lugha kisichogawanyika zaidi. Mifano ya mofu ni maumbo kama vile {m-}, {tu-}, {kopo}, {kalamu}, {a-}, {-na-}, {-lim-} na {a} n.k. Kwa hivyo mofu yaweza kuwa ni umbo lenye hadhi ya neno k.v. {kopo} na {kalamu} au kiambishi k.v. {m-} au mzizi {tu}

3. Alomofu

Alomofu ni umbo tofauti la mofu moja. Kuna mofu za umoja, wingi, mofu za njeo, mofu za nafsi, n.k. kama ifuatavyo: mofu za umoja ni: {m-}, {ki-} na {ji-}. Kila moja ya mofu hizi ni alomofu za mofu ya umoja. Mofu za njeo za Kiswahili ni {na}, {li} na {ta} na kila mofu ni alomofu ya njeo. Mofu za kutendea za kitenzi cha Kiswahili ni {i}, {e}, {li} na {le}, kila moja ni alomofu ya mofu ya kutendea. Kutokana na maelezo haya tunaweza kfasili alomofu kama ni kibadala kimojawapo cha mofu. Mofu za ngeli ya kwanza ya nomino za Kiswahili ni mu-, mw- na m- na kila moja ni alomofu za mofu {mu} kama inavyojidhihirisha katika maneno: mu-uguzi, mw-anafunzi na m-tu. Dhana ya alomofu hutokea iwapo kuna mofu zaidi ya moja.

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 17

Page 18: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

Aina za mofu

Kimsingi mofu ni za aina kuu mbili: mofu huru na mofu tegemezi au mofu funge. Lakini uchambuzi zaidi umebaini kuwa kuna mofu kapa, yaani mofu ambayo haionekani lakini inafikiriwa kuwa ipo kutokana na viashiria vyenye mantiki vinavyoonekana na kuelezeka.

Mofu huru

Mofu huru ni maumbo yasiyotengeka ambayo husimama peke yake. Mofu huru huwa ni maneno yenye maana kamili. Umbo huwa huru likiwa halikuambikwa viambishi vyovyote kwani viambishi navyo ni mofu japokuwa vyenyewe ni mofu tegemezi kwa kuwa haviwezi kusimama peke yake. Maneno kama mama, kalamu, barabara, nyumba, bata, kaka, dada, baba, sungura, sakafu, n.k. ni mofu huru kwani kila moja ni neno kamili lenye maana na linaweza kusimama pekee.

Mofu funge/tegemezi

Mofu funge/tegemezi ni maumbo yaliyomeguliwa kutoka kwenye mzizi wa neno ambayo yenyewe yakisimama peke yake hayana maana ya kileksika. Mofu funge ni viambishi pamoja na mzizi wa neno kwani haya ndiyo maumbo yasiyoweza kusimama peke yake na kuwa na maana. Mofu funge huhitaji kuambishwa viambishi ili yapate kuwa na maana. Kwa mfano maneno: ki-chek-o, m-chez-esh-a-ji, vi-kombe, u-kuta, n.k. yana mofu zifuatazo:

- Viambishi {m-}, [ki-}, {vi-} na {u-}

- Mizizi {-chek-}, {-chez-}, {-kombe-} na {kuta}

Mofu zote za maneno haya ni mofu tegemezi kwa kuwa hakuna inayoweza kusimama peke yake. Mofu {m-}, {ki-}, {vi-} na {u-} ni viambishi vya maneno ambamo vimo. Maumbo {chek}, {chez-}, {kombe} na {kuta} ni mizizi ya maneno ‘kicheko’ ‘mchezeshaji’. ‘Vikombe’ na ‘ukuta’. Neno ‘mchezeshaji’ lina viambishi zaidi: {-esh-}, {-a} na {-ji}. Vyote hivi pamoja na mizizi ya maneno ni mofu tegemezi.

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 18

Page 19: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

Mofu kapa

Mofu kapa ni umbo lisiloonekana lakini uwepo wake unadhihirishwa na viashiria fulani vinavyoonekana. Maumbo haya yanadhihirika katika nomino ambapo ruwaza ya umoja na wingi ambayo hudhihirika katika maneno ya ngeli za nomino za Kiswahili nyingi, baadhi ya nomino hazina umbo la umoja na wingi au yana umbo la umoja tu au umbo la wingi tu. Pamoja na kukosekana kwa maumbo hayo, nomino hizi zinaibua vipatanishi vya kisarufi ambavyo ni mahsusi kwa nomino hizo na vipatanishi hivi hujibagua na kuwa ama vya umoja au wingi.

a) M-toto m-fupi a-meanguka >> wa-toto wa-fupi wa-meanguka

b) M-ti m-fupi u-meanguka >> mi-ti mi-fupi i-meanguka

c) Ki-ti ki-fupi ki-meanguka >> vi-ti vi-fupi vi-meanguka

d) Kalamu fupi i-meanguka >> kalamu fupi zi-meanguka

e) U-kuta m-fupi u-meanguka >> kuta fupi zi-meanguka

Mifano hii inaonesha kuwa nomino za Kiswahili zina viambishi vya umoja na wingi na kwamba kila nomino ina vipatanishi vya kisarufi mahususi kwa nomino za ngeli husika. Mifano a) hadi c) ni seti ya nomino za umoja na wingi ambazo kila moja ina kiambishi mahususi. Isitoshe nomino hizi zina vipatanishi baina ya nomino na viambishi na vitenzi ambapo katika kitenzi kuna kiambishi kiwakilishi kiima ambacho ni mahususi kwa ngeli ya nomino iliyojaza nafasi ya kiima. Mifano ya d) ni ya nomino ambazo hazina viambishi vya umoja wala vya wingi. Mfano wa e) unaonesha kiambishi cha umoja lakini nomino hii haina kiambishi cha wingi. Hata hivyo nomino ambazo hazina viambishi vya umoja wala wingi, zina vipatanishi vya kisarufi. Nomino ya d) umoja na nomino ya wingi zina vipatanishi tofauti japokuwa maumbo ya nomino hizi yanafanana. Hii inaonesha kuwa kwa vile nomino za Kiswahili zote zina umoja na wingi, na tofauti hizi zinajidhihirisha pia katika vipatanishi, ni dhahiri kuwa nomino ambazo hazina viambishi vya umoja au vya wingi, viambishi hivi vipo isipokuwa havionekani. Viambishi hivi ndizo mofu kapa, yaani mofu zisizo bayana japokuwa zipo.

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 19

Page 20: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

Dhana ya mofu changamano

Katika uainishaji wake, Matinde (ameshatajwa) ametaja aina ya mofu changamano ambayo ameieleza kuwa ni mofu inayoundwa na miambatano ya mizizi huru miwili akatoa mifano ya mwanajeshi, mwanaidara na kifaurongo. Pamoja na utata wa dhana ya mzizi huru, mifano hii inaonesha kuwa maneno haya ni maneno mwambatano au mirakabu (compound words) na kwamba kila moja limeundwa na maneno mawili ambapo kila moja lina viambishi na mzizi.

Mw-ana-jeshi, mw-ana-idara na ki-f-a-u-rongo. Iwapo tutazingatia maana ya mofu kuwa ni kipashio kidogo kabisa cha lugha kisichogawanyika zaidi bila kupoteza maana na chenye maana, basi hatuna mofu moja katika maneno haya. Mwanajeshi na mwanaidara kila moja lina mofu tatu, na kifaurongo lina mofu tano. Kwa hivyo hii dhana ya mofu changamano haisadifu. Hata kama mrakabu ungekuwa wa nomino mbili zisizo na viambishi ila ni mashina mawili yaliyoambatana k.v. batabukini, bado hata hapa hakuna mofu moja ila mbili: bata na bukini. Kwa hivyo kama ilivyo kwa mofu huru kalamu na mofu tegemezi m-tu ambapo kwa kila moja tunakuwa na umbo ambalo ni mofu moja: {kalamu}, {m-} na {tu}ni muhimu kwa aina nyingine ya mofu ionekane kuwa ni umbo moja. Dhana ya changamano ibakie kwa vipashio zaidi ya kimoja vinavyoungana. Neno mwambatano, sentensi changamano, shina changamano, n.k.

Maswali

Jibu maswali yafuatayo:

1. Eleza tofauti ya mofimu, mofu na alomofu na toa mifano kwa kila moja.

2. Eleza aina za mofu na utoe mifano mitano kwa kila aina.

3. Unaelewa nini kuhusu dhana ya mofu changamano.

Marejeleo

Chomi Wesana E. (2013) Kitangulizi cha Mofolojia ya Kiswahili TATAKI. Dar es Salaam.

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 20

Page 21: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

Habwe J na Peter K (2004) Misingi ya Sarufi ya Kiswahili. Phenix Publishers Nairobi

Kihore Y na wenzake (2003) Sarufi Maumbo ya Kiswahili Sanifu, TUKI UDSM.

MUHADHARA WA PILI

Viambishi na aina zake

Katika muhadhara huu utajifunza yafuatayo:

a) Maana ya kiambishi

b) Aina za viambishi

c) Uainishaji wa viambishi kwa mujibu wa nafasi yake katika neno

d) Uainishaji wa viambishi kwa kuzingatia uamilifu wa kiambishi katika neno

Maana ya kiambishi

Kiambishi ni mofimu inayoambatanishwa kwenye mzizi wa neno na kuunda neno jipya. Viambishi vinapoambatishwa katika mzizi huwakilisha dhana au hali ambayo hudokezwa katika neno linaloundwa. Viambishi huainishwa kwa kuzingatia i) nafasi yake katika muundo wa neno au ii) uamilifu wa kiambishi.

Uainishaji wa viambishi kwa mujibu wa nafasi yake katika neno:-

Viambishi vinapoainishwa kwa kuangalia nafasi yake katika neno hubainishwa kama:

(i)Viambishi awali (viambishi awali/tangulizi)- hutokea kabla ya mzizi.kwa mfano m-toto, ki-tabu au m-chezo, viambishi m- katika m-toto na m-chezo na kiambishi ki-katika ki-tabu ni viambishi awali.

(ii)Viambishi tamati (viambishi fuatishi) – hutokea baada ya mzizi. Kwa mfano: ‘-o’ katika mchez-o na viambishi ‘-a-’ ‘-an-’ na ‘-ji’ katika mpig-an-a-ji ni

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 21

Page 22: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

viambishi tamati. Viambishi vyote hivi huwakilisha dhana au hali ambayo kwa pamoja hudokeza maana fulani.

Uainishaji wa viambishi kwa kuzingatia uamilifu wa kiambishi katika neno.

Uainishaji mwingine ni ule unaotazama uamilifu wa viambishi katika neno. Uainishaji huu unabainisha kazi ya kila kiambishi katika neno. Viambishi vya uamilifu vinadokeza kazi ya kiambishi na wala sio nafasi kinayojaza katika neno. Katika maneno m-toto na vi-tabu, viambishi m- na ki- ni viambishi vinavyodokeza idadi katika nomino. Kiambishi m- katika mtoto kinadokeza idadi umoja na vi- katika vitabu inadokeza idadi wingi. Aidha kiambishi a- katika ‘anasoma’ kinadokeza nafsi ya mtenda ambayo ni nafsi ya tatu umoja, na kiambishi –na- kinadokeza njeo iliyopo hali ya kuendelea.

Uainishaji unaozingatia uamilifu wa kiambishi hudhihirika katika kategoria mbalimbali za maneno. Uamilifu wa viambishi unadokeza kazi ya kisarufi ya kiambishi katika neno.

Viambishi vya idadi/ngeli

Viambishi vya idadi hudokeza umoja au wingi wa nomino.

Mfano:

Umoja Wingi

m-toto wa-toto

m-to mi-to

ji-we ma-we

ki-jiti vi-jiti

kiambishi m- ni cha ngeli ya kwanza ya nomino umoja. Viambishi vya idadi hudokeza pia ngeli za nomino. Kiambishi wa- ni cha ngeli ya pili ya nomino ya wingi. Vivyo hivyo kwa kiambishi m- na mi- ni vya ngeli ya tatu na nne ya nomino na vya idadi: umoja na wingi.

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 22

Page 23: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

Viambishi vipatanishi vya kisarufi

Viambishi vipatanishi vya kisarufi ni viambishi vya ngeli vya nomino vinavyoambikwa katika maneno yanayoambatana na nomino na kumilikiwa nayo katika sentensi.

Mfano:

a) M-toto m-dogo a-melala

b) Ki-jiko ki-dogo ki-mepotea

c) Mi-ti mi-kubwa i-mekatwa

Viambishi m- na a- katika ‘mtoto mdogo amelala’ ni vya upatanisho wa kisarufi baina ya nomino, kivumishi na kitenzi katika sentensi hii. Vivyo hivyo kwa sentensi ii) na iii).

Viambishi vingine vya nomino ni kama vile:

1. –ji kiambishi cha mazoea

2. U- kiambishi dhahania

3. O- kiambishi matokeo

Viambishi nyambulishi vya kitenzi

Viambishi nyambulishi ni viambishi vinavyoambikwa katika mzizi wa neno ili kuunda maneno mapya. Viambishi nyambulishi vya vitenzi ni: -i-/-e-, -ik-/-ek-, -ish-/-esh-, -an-, na –w- kama inavyodhihirika katika neno cheza: chez-a, chez-e-a, chez-esh-a, cheze-ek-a, chez-an-a, chez-w-a. viambishi nyambulishi vya vitenzi huambikwa katika mzizi wa neno ambalo laweza kuwa nomino, kivumishi au kitenzi na kuunda vitenzi.

Kwa mfano

1. Nomino > kitenzi: taifa – taif-ish-a

2. Kivumishi > kitenzi : refu > refu-sh-a, refu-k-a

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 23

Page 24: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

3. Kitenzi > kitenzi: cheza > chez-e-a, chez-ek-a, chez-esh-a, chez-an-a, chez-w-a

Aina za viambishi nyambulishi vya vitenzi

1. Viambishi nyambulishi tendea: -i-/-e-, mf : pig-i-a, chez-e-a

2. Viambishi nyambulishi tendana: -an-, mf: pig-an-a, chez-an-a

3. Viambishi nyambulishi tendekea: -ik-/-ek- mf: pig-ik-a, chez-ek-a

4. Viambishi nyambulishi tendeshi: -ish-/-esh- mf: pig-ish-a, chez-esh-a

5. Viambishi nyambulishi tendwa: -w- mf: pig-w-a, chez-w-a

Viambishi bya nafsi

Viambishi nafsi ni viambishi vinavyodokeza nafsi ya mtenda ambayo ni ya umoja na wingi. Viambishi nafsi ni sita, vitatu vya umoja na vitatu vya wingi.

1) Viambishi nafsi vya umoja ni: a) ni- nafsi ya kwanza mf: ni-takuja b) u- nafsi ya pili umoja mf: u-takuja c) a- nafsi ya tatu umoja mf: a-takuja

2) Viambishi nafsi vya wingi ni: a) tu – nafsi ya kwanza wingi mf: tu-takuja b) m- nafsi ya pili wingi mf: m-takuja c) wa- nafsi ya tatu wingi mf: wa-takuja

Kwa hiyo viambishi nafsi ni: ni-,u-,a-,tu-,m- na wa

Viambishi njeo

Viambishi njeo hudokeza wakati ambapo tendo lilifanyika. Kiswahili kina nyakati tatu na viambishi njeo vitatu kwa vitenzi yakinishi a) –na-, wakati uliopo, mf: a-na-lia b)-li- wakati uliopita mf: a-li-lia c) –ta- wakati ujao mf: a-ta-lia. Baadhi ya viambishi huweza kuonesha nafsi ya mtenda au njeo. Viambishi njeo vya vitenzi kanushi ni viwili –i- k.v. siendi (ni-naenda > siendi) wakati uliopo na –ku – wakati uliopita k.v. hakuenda (a-li-enda > ha-ku-enda). Hali timilifu hudokeza wakati uliopita kitambo na athari yake inaonekana bado. Kiambishi cha hali timilifu ni –me- k.v. (a-me-lia). Kiambishi kanushi chake ni –ja- (a-me-lia > ha-ja-lia).

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 24

Page 25: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

Viambishi vya hali

Viambishi vya hali ni viambishi vyenye kuonesha dhamira fulani.

a) –a- kiambishi cha dhamira dhahiri k.m. chez-a

b) –e – kiambishi cha dhamira matilaba k.m. achez-e

c) –po- kiambishi cha mahala au muda: ali-po-kuja (muda) alikuja nili-po-kaa (mahali)

d) –ka- kiambishi mfuatano matendo : Akaja akanisalimu, akanitazama kisha akaondoka

e) –ki- kiambishi cha sharti: Akija uniarifu

f) –na- kiambishi cha tendo kuendelea: Anasoma kitabu

g) –li- kiambishi cha hali ya kuwa: Anaongea kama mtu aliye na kigugumizi

h) –ngeli-, -nge-, -ngali- viambishi vya masharti ya kudadisi tendo: Angekuja tungeonana

Viambishi rejeshi

Viambishi rejeshi hurejesha tendo kwa kitajwa. Kimsingi viambishi rejeshini –ye- na –o-. kiambishi –ye- hutumiwa kwa kitajwa ambacho ni nomino ya ngeli ya 1 pamoja na nomino zote zinazohusu binadamu na wanyama: Mzee anayeongea ni baba yangu, Babu aliyelala anaumwa, ng’ombe aliyevinjika mguu amechinjwa. Kiambishi –o- rejeshi hutumiwa kurejesha tendo kwa vitajwa vya ngeli zilizobaki, ila umbo lake hubadilika kulingana na umbo la kiambishi ngeli husika. Hii ni kwa sababu –o- rejeshi huambatanishwa na kiambishi kipatanishi cha kisarufi na kupata virejeshi zaidi: u-+o > -yo-: mti umekatwa – mti uliokatwa; li+o > embe limeiva – embe lililoiva, ya+o > -yo-: maembe yameoza – maembe yaliyooza, ki- > chi+o > -cho-: kiti kimeanguka – kiti kilichoanguka vi+o > vyo -: viti vimevunjika –viti vilivyovunjika, i+o > -yo: nyumbaimeuzwa – nyumba iliyouzwa. Zi+o > -zo- : nyumba zimejengwa – nyumba zilizojengwa, pa+o > po-: mahali pamekaa vibaya

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 25

Page 26: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

– mahali palipokaa vibaya, ka+o > ko-: kule kuna watu – kule kuliko na watu. Humu mulikuwa na nyoka, humo mulimokuwa na nyoka

Kwa hivyo viambishi rejeshi ni: -ye-, -o-, -lo-, -yo-, -cho-, -vyo-, -zo-, -po-, -ko-, -mo-

Unyambulishaji

Unyambulishaji ni utaratibu wa kuunda maneno kwa kutenganisha mzizi na viambishi vyake na kisha kuambatisha viambishi vingine ili kupata maneno mapya.

Mfano: sema > sem-a, m-sem-a-ji, m-sem-o, m-sem-i. viambishi m-,a-,-o,-i na –ji vimeambatishwa katika mzizi /sem-/ na kuunda maneno mapya yaliyotokana na mzizi mmoja.

Hali kadhalika kwa neno ‘mtu’ ambalo mzizi wake –tu huweza kuambatishwa viambishi kadha na kupata maneno mapya tofauti: m-tu > ki-tu (kitu), ji-tu (jitu), ki-ji-tu (kijitu)

Unyambulishaji wa vitenzi

Mzizi wa kitenzi huchukua viambishi tamati. Mfano: chez-a, lim-a, lal-a

Kwa hivyo twaweza kusema kuwa muundo wa kitenzi ni: mzizi+kiambishi. Viambishi vinavyofuata mzizi huweza kuwa kimoja au zaidi kadiri ya uwezo wa uambishaji wa kitenzi unavyoruhusu.

mzizi kiambishi kiambishi

kiambishi kiambishi

neno

Chez- a ChezaChez- e a ChezeaChez- e sh a ChezeshaChez- e sh e a ChezeshaMinyambuliko ya vitenzi: ib > ib-i-a, ib-ik-a, ib-w-a, jibu > jib-i-a, jib-ik-a, jib-ish-a

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 26

Page 27: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

Tabia ya minyambuliko ya vitenzi

Minyambuliko ya vitenzi ina tabia ya kuongeza uwezo wa kitenzi kung’oeka nomino au kupunguza uwezo huo.

Minyambuliko yenye kuongeza uwezo wa kung’oeka

Viambishi nyambulishi vinavyoruhusu miandamano ya viambishi ni kama vile: -an-, -ish-, -ik-, na –i-. mfano: pigana > pigan-i-a, chezesha > chezesh-w-a, pigika > pigik-i-a. somea > some-w-a, soma – somwa.

Kiambishi kisichoruhusu minyambuliko: -w- mfano: pigwa - *pigwia au limwa.

Kitenzi hung’oeka nomino moja ambayo huwa ni kiima: Asha amelala

Kitenzi hung’oeka nomino mbili ambapo moja huwa ni kiima na nyingine yambwa: Asha anasoma barua

Kitenzi hung’oeka nomino tatu ambapo moja huwa ni kiima na nyingine ni yambiwa na ya tatu ni yambwa: Asha anasoma mama barua

Kitenzi hung’oeka nomino tatu bambapo moja huwa kiima na nyihgine ni yambiwa na tatu ni yambwa: Asha anamsomea mama barua.

2.8.4 Uambishaji nyambulishi

Uambishaji nyambulishi ni dhana ya kuambisha viambishi kwenye mzizi wa neno kuunda neno jipya la kategoria tofauti ya kisarufi au maana tofauti na maana ya umbo msingi ya neno. Mfano: chez-a kt> mchezo, mchezaji, uchezeshaji: nene kv > neno unene: refu kv> refusha, refuka, urefushaji, taifa> nm taifisha. Uabmishaji wa mzizi au shina la neno la kitenzi au kivumishi huweza kuunda nomino ambao hujulikana kama unominishaji.

Unominishaji

Unominishaji ni utaratibu wa kuunda maneno kwa kunyambua aina nyingine za maneno kwa kuambatisha viambishi vijenzi vya nomino na kuunda nomino k.v. u-----ji: upimaji, mchezaji, ki-----o: kipigo, m----o: mchezo.

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 27

Page 28: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

Maswali

Jibu maswali yafuatayo

1. Eleza maana ya viambishi vyenye kuongeza uwezo wa vitenzi kung’oeka na kupunguza uwezo wa kung’oeka. Toa mifano kwa kila moja.

2. Eleza tofauti za uambishaji nyambulishi na unominishaji

3. Fafanua dhana zifuatazo na toa mifano 5 kwa kila moja a) viambishi nafsi b) njeo na c) viambishi hali.

Marejeleo

Chomi Wesana E. (2013) Kitangulizi cha Mofolojia ya Kiswahili TATAKI Dar es Salaam

Habwe J na Peter K. (2004) Misingi ya Sarufi ya Kiswahili. Phenix Publishers. Nairobi

Kihore Y na wenzake (2003) Sarufi Maumbo ya Kiswahili Sanifu (SAMAKISA) TUKI DSM.

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 28

Page 29: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

MODULI 3: KIPASHIO CHA NENO

Muhadhara wa 1

Katika muhadhara huu utajifunza yafuatayo:

a) Maana ya mzizi

b) Maana ya shina

c) Tofauti ya mzizi na shina

d) Maana ya neno

Tofauti ya shina na mzizi

Maana ya mzizi

Mzizi ni mumbo la msingi la neno ambalo haliwezi kuchanganuliwa zaidi bila kupoteza maana yake. Mzizi waweza kuwa funge ukiwa hauwezi kujitegemea kama neno bila kuambatishwa kiambishi au mzizi huru ambao unaweza kujitegemea na kuwa ni neno kamili.

Mfano:

Mzizi funge: taifa > taif-ish-a, chez-a >chez-esh-a, imb-a > imb-ik-a

Mzizi huru: kalamu, gari, embe, baba, n.k.

Maana ya shina

Shina ni umbo la msingi ambalo maana yake haibadiliki hata likiambatishwa viambishi. Neno taifa ni shina na hata likiambishwa, umbo hili linabaki lilivyo na maana haibadiliki. Maumbo yaliyotokana na shina hili ni kama: u-taifa, ki-taifa, ma-taifa, vi-taifa, n.k.

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 29

Page 30: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

Tofauti ya mzizi na shina

a) Mzizi waweza kuwa ni umbo ambalo haliwezi kuchanganuliwa zaidi bila kupoteza maana yake. Mzizi funge hauna maana ya kileksika japokuwa mzizi huru una maana ya kileksika.

b) Shina ni umbo lenye maana ya kileksika ambalo hata likiambishwa maana yake haibadiliki

c) Mzizi huru waweza kuwa shina kwani ni umbo linaloweza kuambishwa na umbo jipya linalopatikana huwa na maana ileile. Mfano gari ni mzizi huru na ni shina ambalo likiambishwa maana yake haibadiliki: gari > ma-gari

Maana na fasili za neno

Maana ya neno

Neno ni kipashio cha lugha chenye kuundwa na mofu moja au zaidi, kwa mfano. ‘kesho’ ‘nyumba’ na ‘soko’ ni maneno na kila moja limeundwa na mofu moja. Maneno yenye kuundwa na mofu zaidi ya moja ni kama vile: ‘mto’ > ‘m-to’, kitabu > ‘ki-tabu’, ‘analala’ > ‘a-na-lal-a’

Fasili za neno

Neno lina fasili tofauti na ni kutokana na fasili hizi wakati mwingine wanazuoni wamedai kuwa fasili ya neno ni telezi. Neno linafasiliwa kama kipashio huru, kipashio chenye maana na kipashio cha kifonolojia.

Neno kama kipashio huru

Neno ni umbo dogo kabisa na lililo huru. Sifa kuu katika fasili hii ni kuwa umbo hilo lazima liwe dogo na huru yaani liweze kusimama peke yake. Isitoshe lazima liwe na maana. Hii ina maana kuwa haliwezi kugawanyika zaidi bila kupoteza maana. Maneno mrakabu k.v. garimoshi, mbwamwitu n.k. ni maneno lakini yakigawanywa twaweza kupata maneno kwani yaweza kusimama pekee na kuwa huru na yanakuwa na maana. Kwa hivyo umbo huru lazima liwe na sifa ya kuwa na maana. Umbo hili laweza kuungana na maneno mengine na kuunda kipashio kikubwa zaidi. Umbo lisilo na sifa hii sio neno. Katika Kiswahili, mama, chakula, www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 30

Page 31: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

kijiko ni maneno. Maumbo haya yaweza kuungana kisintaksia na kuwa sentensi: Mama anakula chakula kwa kijiko.

Neno kama kipashio chenye maama

Neno huelezwa kama kipashio cha kiisimu chenye maana. Katika fasili hii kigezo kikuu kinachosisitizwa ni maana. Katika Kiswahili umbo jua ni neno na lina maana, ‘fahamu’ au ‘sayari kubwa inayotoa mwanga’. Umbo ‘na’ lina maana ya kisarufi: neno lenye kuunganisha tungo mbili: Kwa hivyo ‘jua’ na ‘na’ ni maneno kwani yamekidhi vigezo vyote vya neno. Maumbo ‘ju’ na ‘a’ sio maneno kwani yamekosa kigezo cha maana japokuwa yanatamkika.

Fasili ya neno kifonetiki/kifonolojia

Neno hutambuliwa kwa sifa ya matamshi. Sifa hii hujidhihirisha hasa katika uwekaji wa mkazo katika neno. Kwa mfano katika Kiswahili mkazo huwekwa katika silabi ya pili kutoka mwisho wa neno. Kwa hivyo neno linapotamkwa na mkazo kuwekwa, twaweza kuweka mpaka wa neno moja na jingine kwa kubaini ulipowekwa mkazo na kisha kulibaini neno. Mfano: mtotoanalia sana.

Kwa kuwa mkazo umewekwa katika silabi to ya kwanza, na katika li na sa, ambazo ni silabi ya pili kutoka mwisho wa neno kwa kila neno, sasa tunaweza kusema neno la kwanza linaishia na silabi to ya mwisho tukapata ‘mtoto’, neno la pili linaishia na silabi ‘a’ inayofuata ‘li’ yenye mkazo. Neno hilo ni ‘analia’ neno lingine ni ‘sana’ kwani sa ndiyo silabi ya pili kutoka mwisho inayofuatwa na silabi na ya mwisho na kwa pamoja huunda ‘sana’.

Fasili ya neno kimsamiati/kileksika

Maneno ya kimsamiati ni maneno yenye sifa bainifu za kisemantiki.

Maana hii ya neno hujulikana pia kama maana ya kileksika.

Mfano: baba – mzazi wa kiume

embe- tunda lenye kokwa moja ambalo likiiva nyama yake huwa ya njano na ladha ya sukari

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 31

Page 32: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

kwa hivyo neno baba na embe ni neno la kimsamiati. Maneno mengine ya kimsamiati ni k.v. chungwa, kitabu, maji, dada, shule, kimbia, nene, polepole n.k. Maneno ya kimsamiati/kileksika ni maumbo ambayo hayana ukomo kwa vile huundwa mapya kila mara. Nomino, vitenzi au vivumishi ni maneno leksika kwa vile kila mara maneno ya kategoria hizo huundwa: mkimbizi, mkimbiaji na kimbiza < kimbia; chekesha, cheshi, mcheshi, < cheka. Kutokana na neno cheka yameundwa maneno mengine: ‘mcheshi’ ambayo ni nomino, ‘chekesha’ ambalo ni kitenzi na ‘cheshi’ ambalo ni kivumishi.

Maneno yote ya kategoria ya nomino, kitenzi, kivumishi na kielezi ambayo ni maneno kimsamiati na ndiyo maneno mengi katika lugha kuliko aina nyingine za maneno.

Fasili ya neno kitahajia

Maneno ya kitahajia ni maneno yote ambayo yanapoandikwa husimama pekee na kuacha nafasi kila upande bila kujali kama maana yake ni ya kileksika au kisarufi. Minyambuliko ya vitenzi au maumbo yaliyoambishwa bila kubadili maana huwa ni maneno ya kitahajia.

Mfano:

Mtoto – watoto

Kijiko – vijiko

Anapika, wanapika, tulipika, pika n.k.

Katika mifano hii watoto, vijiko, anapika, wanapika na tulipika ni maneno tahajia kwa sababu hayana maana zaidi ya ile iliyo katika umbo la msingi ambalo limeambisha kiambishi tofauti. Maneno yasiyo ya kitahajia katika mifano hii ni: ‘mtoto’, ‘kijiko’ na ‘pika’.

Fasili ya neno kisarufi

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 32

Page 33: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

Neno la kisarufi ni neno ambalo maana yake ni maelezo ya uamilifu wake katika tungo.

Mfano: na, au lakini, kwa, katika, n.k. maneno ya kisarufi ni maumbo ambayo yana kikomo kwani huongezeka kwa nadra sana. Maneno haya huwa ni viwakilishi,viingizi, vihusishi au viunganishi.

Mfano: na, kwa, ebo! n.k.

na- ni neno linalounganisha maneno au tungo mbili: Jerry na Freddy ni wanangu

au- ni neno linalounganisha maneno au tungo mbili: Nitakuletea chungwa au embe

lakini- ni neno linalounganisha maneno au tungo mbili: Juma analima lakini Asha anapika

kwa- ni neno linaloonesha uhusiano wa maneno katika tungo: Ali amekwenda kwa dada yake

maneno na, au, kwa na lakini ni maneno ya kisarufi kwani yanadokeza kazi yanayofanya katika lugha. Kategoria za maneno ya kisarufi ni: viunganishi, viwakilishi, viingizi na vihusishi.

Fasili ya neno kimuundo

Neno ni kipashio cha lugha chenye kuundwa na mofu moja au zaidi. Mf. ‘kesho’, ‘nyumba’ na ‘soko’ni maneno na kila moja limeundwa na mofimu moja. Maneno yenye kuundwa na mofu zaidi ya moja ni kama vile ‘mto’ > m-to, ‘kitabu’ > ki-tabu, ‘analala’ > a-na-lal-a

Muundo wa neno

Neno huundwa na mofimu moja, mbili au zaidi ambazo zaweza kuwa viambishi na mzizi ambao ndio kiambajengo cha lazima katika neno na mzizi usipokuwapo katika neno, umbo hilo haliwezi kuwa na muundo. Neno huweza kuundwa pia na mzizi na kiambishi kimoja au zaidi. Kwa mfano: mtoto > m-toto, mchezaji > m-chez-a-ji. Neno mrakabu huundwa na maneno mawili au zaidi; garimoshi > ‘gari’ na ‘moshi’

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 33

Page 34: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

Muundo wa neno ni:

Kiambishi + mzizi (+kiambishi) au mzizi + kiambishi.

Hii ina maana kuwa neno huweza kuundwa na kiambishi awali na mzizi na kiambishi tamati au kiambishi awali na mzizi au mzizi na kiambishi tamati.

Mfano: m-toto; mchez-o; pig-a

Neno sahili huundwa kwa mzizi pekee, mfano: baba, barua, meza, n.k.

Sifa kuu ya neno ni kwamba kila neno hubeba dhana moja tu hata kama linaundwa na maneno mawili, mfano. mtu, mwanafunzi, chakula, kifunguakinywa. Kila moja kati ya maneno haya yanabeba dhana moja.

Jinsi ya kutambua maneno leksika na maneno ya kisarufi

a) Maneno leksika yaweza kubainishwa kwa namna tofauti:

(i)Viambishi vinavyoambatana navyo. Kwa mfano, nomino zote zina viambishi awali, vitenzi vinatanguliwa na viambishi vipatanishi na vivumishi havina viambishi vyenyewe ila huchukua viambishi vya nomino vinavyovivumisha.

Kwa mfano:

Aina ya neno Viambishi Mifanonomino m-/wa

m-/mi-ki-/vi-

Mtoto – watotoMto – mitoKiti – viti

kitenzi a-wa-u-i-

a-nalimawa-nachezau-mekaukai-mekatwa

kivumishi m-wa-m-mi-

m-refuwa-refum-refumi-refu

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 34

Page 35: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

(ii)Maneno yanayoambatana nayo:

1. Nomino huweza kufuatwa na:

Kivumishi: mti mdogo, kijiko kikubwa, jembe dogo

Kitenzi : mto umejaa, kijiko kimepotea, mtu amelala

2. Kitenzi hufuatwa na:

Kisaidizi : alikuwa akilima, anataka kuja

Kielezi : kimbia upesi, ongea sana, tembea polepole

3. Kivumishi hufuatwa na kielezi: refu sana

b) Maneno amilifu ni kategoria zisizo za kileksika:

Kiunganishi: ‘na’, ‘lakini’, ‘kwa sababu’

Kihusishi: ‘kwa’, ‘-a’ (ya, la, cha, n.k.)

Kategoria Uamilifu MifanoKiunganishi

Kuunganisha Baba na mama

Asia anafua nguo na Asha atapasi

kihusishi Uhusiano kati ya vipashio

Enda kwa dada

Embe la Aziza

Maneno amilifu yana maana ya kisarufi kwa mujibu wa uamilifu (kazi) wake katika tungo. Kwa mfano viunganishi ‘na’, ‘ila’ n.k. vina dhima ya kuunganisha vipashio vya lugha katika tungo.

Mfano: matunda na mboga; kaka anasoma lakini dada anataka kuandika.

Vivyo hivyo kwa vihusishi ‘kwa’ au ‘a’ vinaonesha uhusiano wake na maneno mngine yanayoambatana nayo katika tungo.

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 35

Page 36: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

Mfano: enda kwa ali, lima kwa jembe, kiti cha kaka, nyumba ya mwalimu.

Japokuwa maneno yote ya lugha yana maana, maneno leksika yana maana ya kileksika ilihali maneno ya kategoria amilifu yana maana ya kisarufi na hayana maana leksika.

Msingi wa uchambuzi katika Sarufi mapokeo ilikuwa ni neno na sentensi. Maneno yalitengwa ili kupata neno huru, na kisha yakachambuliwa katika makundi yanayofanana ili kupata aina za maneno. Uchambuzi wa neno kimuundo ni kubainisha viambajengo vinavyounda neno.

Maswali

1. Eleza maana ya neno na taja aina tofauti za maneno

2. Eleza tofauti ya maana ya kitahajia, kimsamiati na kisarufi

3. Kwa kuzingatia maana ya mzizi na shina, eleza tofauti za dhana hizi na toa mifano

4. Fafanua fasili ya neno kifonetiki na kimaana

Marejeleo

Habwe J na Peter K (2004) Misingi ya Sarufi ya Kiswahili Phenix Publishers. Nairobi

Kihore Y na wenzake (2003) sarufi Maumbo ya Kiswahili Sanifu, TUKI. UDSM

Massamba, D.P.B na wenzake (2001) Sarufi Miundo ya Kiswahili Sanifu IKR. UDSM, Dar es Salaam

MUHADHARA WA 2: NGELI ZA NOMINO

Katika muhadhara huu utajifunza

a) Maana ya ngeli za nomino

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 36

Page 37: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

b) Uainishaji wa ngeli za nomino

c) Uundaji wa maneno

Maana ya nomino

Nomino ni kipashio cha lugha chenye sifa ya kimofolojia na kisintaksia. Sifa ya kimofolojia ya nomino ni ile ya kuruhusu kiambishi ngeli, au kiambishi idadi ambacho hudhihirisha nomino kuwa ya umoja na wingi. Sifa ya kisintaksia inajionesha katika upatanishi wa kisarufi ambao huonesha uhusiano wa kisarufi kati ya nomino na kivumishi au nomino na kitenzi.

Maana ya ngeli ya nomino

Ngeli ya nomino ni kundi la nomino zenye sifa za kimofolojia na kisintaksia zinazofanana ambazo hudhihirika katika kila nomino. Sifa ya kimofolojia ya nomino ni kiambishi awali kinachoambishwa mwanzoni mwa nomino. Nomino zote zenye kiambishi hiki huunda ngeli moja. Kwa mfano nomino zenye kuanza na kiambishi m-katika umoja na kiambishi wa-katika wingi, huunda ngeli ya 1 ya nomino na ngeli ya 2 ya nomino kwa mfuatano huo. Kwa mfano, ngeli ya 1 ya nomino: mtoto, mtu, mwalimu, mpishi n.k. na ngeli ya 2 ya nomino wa- watoto, watu, walimu, wapishi n.k. Sifa ya kisintaksia ya ngeli za nomino ni kiambishi awali katika kitenzi ambacho ni kiwakilishi cha kiima katika kiarifu.

Mfano: mtoto anakula, mpishi anapika, mzee amelala n.k

Kiambishi a-katika sentensi hizo hapo juu ni kiwakilishi cha kiima katika kiarifu. Kiambishi a-ni ngeli ya 1 ya nomino kwa mujibu wa sifa ya kisintaksia ya nomino zinazounda ngeli hii. Kiambishi wa-ni kiwakilishi cha kiima katika kiarifu kwa nomino za wingi.

Mfano: watu wamelala, wapishi wamepika chakula, walimu wanafundisha.

Kwa hivyo wa-ni kiambishi ngeli cha nomino za Kiswahili zinazoanza na kiambishi wa-kama mfano hapo juu unavyoonesha. Hiki ni kiambishi cha ngeli ya 2 ya nomino.

Uainishaji wa ngeli za nominowww.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 37

Page 38: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

Uainishaji wa ngeli za nomino hufanywa kwa kuweka pamoja nomino zenye sifa za kimofolojia au kisintaksia zinazofanana. Ngeli za nomino huainishwa kwa njia ya mofolojia na sintaksia. Uainishaji wa ngeli kimofolojia huzingatia umbo la kiambishi awali la nomino.

Uainishaji wa ngeli kisintaksia

Uainishaji wa ngeli za nomino kisintaksia hufanywa kwa kuweka pamoja nomino zenye sifa za kisintaksia zinazofanana. Uainishaji huu hufanywa kwa kuzingatia viambishi viwakilishi vya nomino vya kiima katika kitenzi cha kiarifu. Viambishi hivi ambavyo huleta upatanisho wa kisarufi baina ya kiima na kitenzi katika kiarifu hujulikana kama viambishi vipatanishi.

Mfano: mtoto a-nalia

Kisu ki-menunuliwa

Ngeli

Jina la ngeli Mfano Kiambishi kipatanishi

1 a- Mtu anakula a-2 Wa- Watu wamekuja Wa-3 u- Mti umeanguka u-4 i- Miti imeanguka i-5 li- Jino limeng’oka li-6 ya- Mawe yameng’oka ya-7 ki- Kiti kimevunjika ki-8 vi- Visu vimepotea vi-9 i- Nguo imechanika i-10 zi- Njia zimefungwa zi-

Uainishaji wa ngeli za nomino kimofolojia

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 38

Page 39: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

Uainishaji wa ngeli za nomino kimofolojia hufanywa kwa kuweka pamoja nomino zenye sifa za kimofolojia zinazofanana. Uainishaji wa ngeli kimofolojia huzingatia umbo la kiambishi awali cha nomino.

Uainishaji wa kimofolojia ambao huangalia umbo la kiambishi ngeli huweka pamoja nomino ambazo zina umbo linalofanana na kuacha nomino ambazo hazifanani kiumbo hata kama vipatanishi vyake hufanana.

Kwa mfano, nomino zisizo na viambishi kama vile kalamu, shangazi, nguo, dada, bibi n.k. huwekwa katika kundi moja la nomino zisizokuwa na wingi ambazo katika Kiswahili huwekwa katika ngeli ya 9 na 10. Lakini tukizichambua kwa kuzingatia vipatanishi vya nomino kiima katika kitenzi tunaona inachukua vipatanishi kama vya ngeli ya 1 na 2.

Uainishaji wa ngeli za nomino kimofolojia hufanywa kwa kuzingatia viambishi vya nomino ambapo nomino zenye viambishi vinavyofanana na vyenye maana ya jumla inayohusiana, huwekwa pamoja na kufanya ngeli moja. Viambishi awali vya nomino zinazounda ngeli moja ni viambishi ngeli.

Viambishi vya ngeli

Viambishi vya ngeli ni viambishi vinavyoambikwa kwenye mzizi wa nomino ambavyo hubainisha idadi ambayo yaweza kuwa ni umoja au wingi.

Mfano: m-zee > wa-zee

Ki-tu > vi-tu

Viambishi ngeli vya nomino ndivyo vinavyounda ngeli kwa mujibu wa uainishaji ngeli kimofolojia.

Namba ya ngeli

Jina la ngeli Mifano ya nomino

1 mu-/mw-/m- Muumba, mwizi, mvulana2 Wa Waumba, wezi,wavulana3 mu-/m- Muungano,mto4 mi- Miungano, mito5 Ji- Jiwe, jino

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 39

Page 40: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

6 ma- Mawe, meno7 ki- Kijiko, kiti8 vi- Vijiko, viti9 N- Nguo, ngozi10 N- Nguo, ngozi11 u- Ubao, ukuta12 ka- Katoto, kajumba13 tu- Tutoto, tujumba14 u- Uzuri, ugonjwa15 ku- Kucheza, kuimba16 Pa- Mahali17 Ku- Mahali18 Mu- mahali

Maumbo tofauti ya ngeli zenye maana moja

Uainishaji wa ngeli kimofolojia unaziweka nomino zenye maana ya binadamu katika ngeli tofauti. Hii inatokana na maumbo ya maneno yanayomhusu binadamu kuwa na viambishi vyenye maumbo tofauti.

Kwa mfano:

(i)Ngeli ya 1 na 2 za mu- na wa- zinajulikana kama ngeli za binadamu na viumbe vyenye uhai kwa ujumla kwa kuwa nomino zilizo nyingi zinazomhusu binadamu zinapatikana katika ngeli hizi. Mfano mtu-watu, mkulima-wakulima, n.k.

(ii)Ngeli ya 3 na 4 za mu- na mi- ambazo huwa ni ngeli za miti/mimea kwa kuwa ngeli nyingi za mimea, huwa zina nomino chache sana za biandamu pia. Mfano mtume-mitume

(iii)Ngeli za 5 na 6 za ji- na ma- zina nomino za binadamu pia. Mfano jambazi-majambazi, daktari-madaktari

(iv) Ngeli za 7 na 8 za ki- na vi- ambazo hujulikana kama ngeli za vitu zina nomino za binadamu kama kiwete-viwete, kiongozi-viongozi

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 40

Page 41: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

(v)Ngeli za 9 na 10 za N- na N- zina nomino kama vile baba-baba, kaka-kaka

Udhaifu wa uainishaji ngeli kimofolojia

Upungufu wa uainishaji ngeli kimofolojia ni kwamba baadhi ya ngeli zinawakilishwa na kiambishi ngeli cha namna moja. Mfano:

a) Ngeli ya 1,3 na 18 zina kiambishi nomino mu-

b) Ngeli ya 1 na 3 zina kiambishi m- na mu-

c) Ngeli ya 9 na 10 zina kiambishi n-

d) Ngeli ya 11 na 14 zina kiambishi u-

e) Ngeli ya 15 na 17 zina kiambishi ku-

Uundaji wa maneno

Maneno huweza kuundwa kwa njia zifuatazo:

a) Uambishaji: ni njia ya kuweka viambishi kabla au baada ya mzizi wa neno ili kuunda neno jipya: pika > m-pishi, jenga > ki-jenz-i, kimbia > m-kimbi-zi

b) Uambatishaji: hii ni njia ya kuunda maneno mapya kwa kuambatisha maneno mawili au zaidi. Mfano. mwana+mapinduzi > mwanamapinduzi, kifungua+kinywa > kifunguakinywa

c) Uhulitishaji: ni uundaji wa maneno mapya kwa kuchukua vijisehemu vya neno bila kufuata utaratibu maalumu. Mfano: chakula cha jioni > chajio, mtu asiye na kwao > msikwao, mnyama mfu > nyamafu, hati za kukataza > Hataza

d) Tafsiri sisisi: hii ni njia ya kuunda maneno kwa kutafsiri maneno toka lugha za kigeni mf. chairperson > mwenyekiti, prime minister > waziri mkuu

e) Kufupisha: hii ni njia ya kuunda maneno kwa kukata kipande cha neno na kukiondoa na kubakiza sehemu tu ya neno mf. Kilimanjaro > Kili, Dar es salaam > Dar

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 41

Page 42: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

f) Akronimu: hii ni njia ya kuchagua silabi za kifungu cha maneno na kuziambatisha ili kupata neno jipya: Baraza la Kiswahili la Taifa – BAKITA, Umoja wa Walimu wa Somo la Kiswahili Tanzania - UWASOKITA

g) Kutohoa maneno: hii ni njia ya kuchukua maneno ya lugha ya kigeni na kuyapa tahajia na matamshi yanayofanana na ya lugha lengwa. Mf. geography > Jiografia, schule > shule, radio > redio.

h) Kuigiza sauti inayofanywa na kitajwa: hii ni njia ya kuigiza sauti inayotolewa na kitu ambacho kinaundiwa neno. Mf hondohondo – hoo-hoo-hoo, pikipiki > p-k-p-k-p-k, kitwitwi – twi-twi

i)Takriri: hii ni njia ya kuunda neno kwa kulikariri umbo la neno mf. haraka > harakaharaka, kidogo > kidogokidogo

Maswali

Jibu maswali yafuatayo:

1. Bainisha njia za uundaji wa maneno 6 ambazo zimetumika katika kuunda maneno katika Kiswahili. Toa mifano kama kielelezo.

2. Uainishaji wa ngeli za nomino za Kiswahili umezingatia umbo la nomino lakini una kasoro pia. Jadili.

3. Eleza tofauti za uainishaji wa ngeli za nomino za Kiswahili wa kimofolojia na wa kisintaksia.

4. Eleza maana ya ngeli za nomino na misingi iliyotumiwa kuainisha nomino na kuziweka katika ngeli husika.

Marejeleo

Habwe J na Peter K (2004) Misingi ya Sarufi ya Kiswahili. Phenix Publishers Nairobi

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 42

Page 43: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

Kihore Y na wenzake (2003) Sarufi Maumbo ya Kiswahili Sanifu. TUKI, UDSM

Massamba, D.P.B na wenzake (2001) Sarufi Miundo ya Kiswahili Sanifu. IKR UDSM, Dar es Salaam.

MODULI YA 4: SARUFI MIUNDO

MUHADHARA WA KWANZA

Mkabala wa Sarufi miundo

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 43

Page 44: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

Katika muhadhara huu utajifunza yafuatayo:

a) Maana ya Sarufi miundo

b) Misingi ya Sarufi miundo

c) Misingi yam kabala wa wanasarufi miundo

d) Umilisi na utendi

Maana ya Sarufi miundo

Kabla ya kueleza maana ya Sarufi miundo, tufafanue kwanza dhana ya muundo. Muundo ni mpangilio wa vitu vidogo vilivyowekwa pamoja na kujenga kitu kikubwa zaidi. Kutokana na fasili hii ya muundo twaweza kuihusisha na lugha kuwa nayo huundwa na vipashio vidogo ambavyo huwekwa pamoja.

Sarufi miundo au sintaksia ni tawi la isimu ambalo linahusu namna maneno yanavyoungana na kuhusiana katika kirai au sentensi. Sintaksia inachunguza namna maneno yanavyojipanga katika sentensi kwa kuzingatia kanuni za Sarufi ya lugha husika. Huu ni mkabala wa kuchunguza vipashio vya lugha vinavyoungana na kujenga vipashio vikubwa zaidi. Katika uchambuzi huu huonesha uhusiano baina ya maneno katika sentensi na kanuni za kuyapanga maneno hayo katika tungo hata yakaleta maana. Katika mpangilio huu kuna maneno ambayo lazima yatangulie au yafuate maneno mengine. Aidha katika kuchunguza jinsi maneno yalivyopangwa katika tungo, tunachunguza pia jinsi maneno yanayofuatana yanavyohusiana. Sarufi miundo au sintaksia inahusu maneno pamoja na viambishi vyake na namna yanavyoungana na kuunda kirai na sentensi.

Mkabala wa Sarufi miundo uliasisiwa tangu karne ya 19 na wanaisimu wa Ulaya k.v. Frednand de Saussure (1857-1913) na Mmarekani Leonard Bloomfield (1887-1949) na baadaye Noam Chomsky ambaye alileta mabadiliko makubwa katika mkabala huu. Wanazuoni hawa walichunguza na kuieleza lugha kama ilivyokuwa bila kulazimisha ifuate kaida ya lugha kongwe kama walivyofanya wanamapokeo waliowatangulia ambao walitumia Kilatini kama kipimo cha kuchambua lugha nyingine. Chomsky (1957) ndiyemakinika zaidi katika kuichambua lugha kisayansi

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 44

Page 45: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

tangu alipochapisha kitabu chake cha Sarufi miundo na kisha kuungwa mkono na wanaisimu wenye mawazo kama yake.

Misingi ya Mkabala wa wanasarufi miundo

Mkabala wa Sarufi miundo ulijikita katika mambo yafuatayo:

a) Mkabala wa kuichambua lugha hauna budi kuwa arifu/elezi na sio elekezi. Hii ina maana kuwa mkabala wa kuichambua lugha uieleze lugha kama ilivyo na sio kuelekeza jinsi inavyopasa kuwa.

b) Lugha ichunguzwe kwa kadiri ya muundo wake kwani kila lugha ina upekee wake.

c) Muundo wa lugha ndio uliopewa umuhimu katika kuchambua vipashio vinavyoiunda lugha badala ya maana ya vipashio vyake.

d) Walibaini vipashio vya lugha kuwa ni mofu, neno, kirai, kishazi na sentensi na kwamba vipashio hivi vinajengana. Kipashio cha msingi kilikuwa mofu kwani ndicho kilichojenga kipashio kikubwa kuliko chenyewe ambacho ni neno.

e) Walitambua kuwa muundo wa lugha ulitokana na ruwaza ambayo inajirudia kwa mfano sentensi sahili zote ziliundwa kwa KN+KT au KN=N+V, n.k

Katika kuchunguza mpangilio wa maneno katika tungo inadhihirika kuwa kuna maneno yanayomiliki maneno mengine na kwamba katika kila kikundi cha maneno mawili au zaidi yanayofuatana, moja huwa ndilo neno la msingi au neno kuu na kwamba neno hilo ndilo lenye kuleta mahusiano baina ya maneno katika kikundi hicho.

Malengo ya Sarufi miundo ni:

a) Kuchunguza mpangilio wa maneno katika tungo unaokubalika ambao huibua tungo sahihi zenye kuzingatia upatanisho wa kisarufi.

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 45

Page 46: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

b) Kuchunguza jinsi vipashio vya lugha vinavyohusiana na kushirikiana katika kuunda vipashio vikubwa zaidi.

Mfano:

KN + KT = S

N + V = KN

T + KN + KE = KT

c) Kuchunguza jinsi lugha ilivyo na uwezo wa kutunga sentensi zisizo na ukomo.

Sintaksia inahusu uchanganuzi wa namna maneno yalivyopangiliwa katika sentensi. Katika sintaksia tunaangalia kanuni ambazo hutawala uteuzi wa maneno unaofanywa na mzungumzaji wakati akiongea kwa kuyapanga maneno katika mfuatano ambao unakubalika kwa wazungumzaji wengine wa lugha hiyo na kutoa maana inayoeleweka na kukubalika kwa wanajamii.

Katika kuchunguza mpangilio wa maneno katika tungo inadhihirika kuwa kuna maneno yanayomiliki maneno mengine na kwamba katika kila kikundi cha maneno mawili au zaidi yanayofuatana, moja huwa ndilo neno la msingi au neno kuu na kwamba neno hilo ndilo lenye kuleta mahusiano baina ya maneno katika kikundi hicho.

Ili kujua jinsi maneno yanavyochukuana katika sentensi na kuhusiana hatuna budi kujua aina za maneno ambazo zilikuwa msingi wa Sarufi miundo kwa wanamapokeo.

Mfano: Watu wote wamegoma na wanakutana katika uwanja wa Uhuru

S

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 46

Page 47: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

KN KT

KH KN KH KN

N V T U T H N H N

Watu wote wamegoma na wanakutana katika uwanja wa Uhuru

Sintaksia ya lugha inaonesha ubunifu wa mzungumzaji wa lugha aliye na umilisi wa Sarufi ya lugha yake wa kuweza kutunga sentensi nyingi ambazo hazijawahi kutungwa, na pia kuelewa sentensi zilizotungwa na wengine ambazo hajawahi kuzisikia.

Kwa mujibu wa Chomsky binadamu wana uwezo ulio ndani ya bongo zao unaowezesha kujifunza lugha na kutunga sentensi zisizo na ukomo. Kwa hivyo binadamu mwenye umilisi wa lugha yake ana uwezo wa kutunga sentensi nyingi zisizo na kikomo na ambazo hazijawahi kutungwa. Aidha anaweza pia kuelewa sentensi zote hata zile ambazo hajawahi kuzisikia. Kutokana na hali hii alibuni nadharia yenye kueleza muundo wa lugha na ubunifu wa lugha alionao mzungumzaji ambayo ilielezwa kwa dhana mbili muhimu: umilisi wa mzungumzaji na utendi wa mzungumzaji.

Umilisi wa lugha

Umilisi ni uwezo au maarifa ya lugha aliyonayo mzungumzaji unaomwezesha kutunga sentensi au kuelewa sentensi nyingi zisizo na ukomo na ambazo baadhi hajawahi kuzitunga wala kuzisikia. Umilisi ni

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 47

Page 48: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

uwezo wa kuzungumza lugha kwa ufasaha alionao mtu unaotokana na yeye kuzifahamu vilivyo kanuni za kisarufi hata kumwezesha kuzalisha tungo nyingi zisizo na kikomo. Uwezo huu ndio unaomfanya mtoto kujifunza lugha ya wale wanaomzunguka bila kufunzwa. Halikadhalika mtu mzima hutumia uwezo huu kujifunza lugha ya watu anaoishi nao wenye lugha tofauti na yake bila kufundishwa.

Utendi wa lugha

Utendi ni utumiaji wa lugha katika mazingira halisi ambao huweza kuathiri maana ya maneno kulingana na matumizi yake au na mambo yanayimhusu mzungumzaji mwenyewe k.v. kutokuwa makini au kukosa kumbukumbu, kuongea akiwa amekasirika, kasoro za ala za sauti k.v. mapengo, kigugumizi, n.k.

Uhusiano wa maneno katika lugha

Mpangilio wa maneno katika sentensi unafanywa kwa utaratibu maalumu na sio shaghalabaghala. Neno moja linapoteuliwa hudai kufuatwa na neno jingine ambalo huchukuana nalo. Hii ina maana kuwa maneno katika lugha hufuatana kwa utaratibu maalumu. Sentensi yenye maneno yaliyopangwa kwa utaratibu maalumu unaokubalika katika lugha husika hudaiwa kuwa ni tungo ya kisarufi yaani imetungwa kwa kuzingatia kanuni za kisarufi. Kanuni za kisarufi, yaani Sarufi ya lugha ipo ndani ya lugha yoyote na mzawa wa lugha huipata Sarufi na kanuni zinazotawala lugha yake wakati anapoisikia lugha ikizungumzwa na yeye kuanza kuiongea. Hii ndiyo maana mzawa wa lugha hajifunzi wala hafunzwi lugha yake bali anaipata kutokana na watu waliomzunguka wanapoongea lugha yao. Kutokana na kujumuika na kujichanganya na wazungumzaji wa lugha yake mzawa wa lugha yake hupata umilisi wa lugha hiyo na kisha huanza kuiongea kwa kuzingatia kanuni za lugha kwa kutenda, yaani utendi.

Maswali

Jibu maswali yafuatayo:

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 48

Page 49: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

1. Eleza tofauti ya umilisi na utendi wa lugha

2. Chomsky anadai kuwa binadamu ana uwezo ulio ndani ya ubongo wake ambao huwezesha kujifunza lugha. Jadili

3. Eleza jinsi Sarufi miundo ilivyofanikiwa kufafanua na kuonesha uhusiano wa maneno katika lugha ambao ndio umeridhisha viambajengo vya lugha.

4. Ubainishaji wa virai umetokana na kutambua kuwa maneno ya lugha yanahusiana kimuundo. Jadili

Marejeleo

Graustein G. na wenzake (1980) English Grammar, A University Handbook. VEB Verlag Enzykloaedle. Leipzig

Habwe J na Peter K (2004) Misingi ya Sarufi ya Kiswahili. Phenix Publishers. Nairobi

Langacker R.W. (1968) Language and Its Structure. Harcourt Bruce. New York

Massamba, D.P,B na wenzake (2001) Sarufi Miundo ya Kiswahili Sanifu. IKR. UDSM, Dar es Salaam

MUHADHARA WA PILI

Sarufi miundo virai

Katika muhadhara huu utajifunza yafuatayo:

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 49

Page 50: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

1. Maana ya Sarufi miundo virai

2. Tungo virai

3. Aina za virai na sifa ya kila moja

Maana ya Sarufi miundo virai

Sarufi miundo virai ni mkabala wa kuchambua sentensi katika virai vinavyoiunda na kisha kuvichanganua zaidi hadi kufikia neno moja moja lililokiunda kirai.

Tungo huundwa na viambajengo kwa utaratibu maalumu. Tungo za lugha ni neno, kirai, kishazi na sentensi. Virai, vishazi na sentensi huundwa na maneno.

Kwa mujibu wa mkabala huu sentensi huchambuliwa kwa kuigawa katika sehemu kuu mbili: KN na KT ambayo nayo hugawanywa zaidi na kuwa T na KN na KE. KN hugawanywa zaidi na kuwa N (na vipashio vinavyoambatana nayo) KE nayo huchambuliwa zaidi na kubainisha vijenzi vyake. Sarufi miundo virai huonesha uhusiano wa vipashio vinavyojengana.

Uhusiano huu huonesha vipashio vinavyomiliki vipashio vingine ambavyo vipo katika daraja ya chini. Kwa mfano sentensi humiliki KN na KT, KN nayo humili N na KT humiliki T, KN na KE.

Sentensi KN KT

KN KE N T N E Mama anapika chakula upesi

Tungo virai

Kirai ni kikundi cha maneno yenye uhusiano wa kimuundo lakini usiokuwa wa kiima kiarifu. Kirai huundwa na jozi ya viambajengo vinavyoungana pamoja. Viambajengo vya virai ni maneno yenye kuhusiana ambayo huungana na kuunda kipashio hiki cha lugha.www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 50

Page 51: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

Vikundi vya maneno yenye kuhusiana ambayo yakiungana huunda kirai ni kama vile ‘mtoto mdogo’, ‘kimbia sana’, ‘refu mno’, ‘polepole sana’, ‘kwa haraka’ na ‘na mwalimu’. Hii ina maana kuwa sio kila kundi la maneno laweza kuunda kirai. Ni muhimu kwa maneno hayo kuwa na uhusiano wa kisintaksia ndipo yaweze kuunda kirai. Kwa mfano, ‘refu mtu’ au ;kimbia kwa’ n.k. hayaundi kirai kwani hayana uhusiano wa kuchukuana. Maneno yanayochukuana ni kama vile nomino na kivumishi, kitenzi na kielezi au kitenzi na nomino, kivumishi na kielezi, kielezi na kielezi na kihusishi na nomino. Kwa mfano, ‘mtoto mdogo’ kirai kilichoundwa na maneno ‘mtoto’ na ‘mdogo’. Uhusiano huu wa maneno ndio unaounda virai vya aina mbalimbali.

Aina za virai na sifa ya kila moja

Kwa kuwa kirai ni kikundi cha maneno yenye uhusiano wa kimuundo hapana shaka kuwa neno moja huwa ndilo neno kuu katika kikundi hicho na neno au maneno mengine katika kikundi hicho huwa kijalizo. Neno kuu ndilo lenye kuyatawala maneno mengine yote katika kikundi hicho, na lisipokuwapo kikundi hicho cha maneno hakiwezi kuwa kirai.

Aina za virai

a) Kirai Nomino (KN)

b) Kirai Tenzi (KT)

c) Kirai Vumishi (KV)

d) Kirai Elezi (KE)

e) Kirai Husishi (KH)

f)Kirai Unganishi (KU)

Kirai Nomino (KN) ni kikundi cha maneno mawili au zaidi yenye uhusiano wa kimuundo ambapo neno moja ni nomino ambalo ndilo neno kuu na neno lingine ni kijalizo.

KN

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 51

Page 52: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

N V

Mtoto mdoto

Kirai Nomino huundwa na nomino na kivumishi. Mfano: mto mpana, ng’ombe mnene, kiazi kitamu.kila moja ya virai nomino hivi kina nomino.

Kira NominoNomino kivumishiMto mpanaNg’ombe MneneKiazi kitamu

Miundo ya virai nomino ya Kiswahili

a) Nomino pekee

Mf: mwalimu, mkulima, mpishi

KN

N

Mwalimu

b) Nomino mbili au zaidi zilizounganishwa na kiunganishi

Mf. mama na dada wamelala

KN

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 52

Page 53: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

N U N

Mama na dada

c) Nomino na kivumishi

Mf. Watu wengi wamelala, mtoto vivi ameondoka

KN

N V

Watu wengi

d) Nomino na sentensi ikiwa ni kishazi kilichoshushwa hadhi

Mf. Mtu aliyelala ameshiba

KN

N S

Mtu aliyelala

e) Nomino, kivumishi na sentensi/kishazi

Mf. Mtu mrefu aliyewasili jana

KN

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 53

Page 54: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

N V S

Mtu mrefu aliyewasili jana

Kirai Kitenzi (KT) ni kikundi cha maneno mawili au zaidi yenye uhusiano wa kimuundo ambapo nenomoja ni kitenzi ambacho ndilo neno kuu na lingine au mengine ni kijalizo chake.

KT

T N

Kimbia somo

Kirai kitenzi huundwa na kitenzi na kirai nomino kinachofuata kitenzi au kirai kielezi au kirai kihusishi. Mfano: cheza mpira, tembea polepole, imba kwa sauti.

Kirai tenzikitenzi NominoCheza MpiraLima shambaSoma Kitabu

Kirai tenzikitenzi Kirai husishiImba Kwa sautiEnda Kwa mamaChota Kwa kijiko

KT yaweza kuwa na miundo ifuatayo:

a) Kitenzi kimoja tu

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 54

Page 55: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

i) ameondoka

ii) tumekuja

b) Kitenzi na nomino moja

i) umepika ugali

ii) watalima shamba

c) Kitenzi na nomino mbili

i) amempikia mama chakula

ii) tulimwandikia dada barua

d) Kitenzi na kitenzi kisoukomo

i) anataka kuondoka

ii) unakwenda kusali

e) Kitenzi, nomino na kitenzi kisoukomo

i) amewataka wageni kututembelea

ii) tulimwamrisha John kuondoka

f) Kitenzi, nomino kitenzi

i) nimemwagiza mwalimu awaondoe

ii) wamemwomba mwalimu awapokee

g) Kitenzi+kuwa+sentensi

i) amesema kuwa atakuja kesho

ii) nimemwarifu kuwa amelala

Muundo wa KT ambao kitenzi chake ni kuwa

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 55

Page 56: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

Kitenzi kishirikishi ni kina umbo la – wa na kinapoambishwa kiambishi –ku- ya vitenzi vyenye silabi moja hujulikana kama kuwa. KT ambayo ina kitenzi kishirikishi huwa na muundo ufuatao.

a) Kitenzi na kivumishi

i) ni mrefu

ii) alikuwa mwongo

b) Kitenzi na kirai kiunganishi

i) tulikuwa na mali

ii) watakuwa na hoja

c) Kitenzi na nomino mahali

i) yuko shuleni

ii) atakuwa mjini

d) Kitenzi, kielezi na kitenzi

i) ni vyema umekuja

ii) itakuwa vizuri kumtembelea

Maelezo haya ya muundo wa sentensi yanadhihirisha nafasi ya kitenzi katika lugha kuwa kila mara kinaandamana na maneno mengine na kwamba mtu anapotamka kitenzi kimoja msikilizaji hutarajia neno la kategoria fulani kufuata kitenzi hicho.

Kirai vumishi (KV) ni kikundi cha maneno mawili au zaidi yenye uhusiano wa kimuundo ambapo neno kuu ni kivumishi na maneno mengine yanayoambatana nalo ni kijalizo chake.

Muundo wa kivumishi

a) Kivumishi pekee

i) fupi

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 56

Page 57: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

ii) nene

b) Kivumishi na kielezi

i) refu sana

ii) embamba mno

c) Kivumishi na KN

i) –enye nyumba mpya

ii) –enye maneno mengi

d) Kivumishi na KT

i) –enye kupenda ugomvi

ii) –enye kupenda kazi nyingi

e) Kivumishi na KV

i)-ingine –enye matatizo

ii) –ingine –enye fujo

f) Kivumishi na KU

i) – pungufu wa maadili

ii) – tovu wa nidhamu

Kirai vumishi chaweza kuundwa na kivumishi peke yake au kivumishi na kielezi. Mfano: kubwa mno, nyembamba sana, mpya kabisa.

Kirai vumishi

Kivumishi Kielezi

Kubwa Mno

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 57

Page 58: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

Nyembamba Sana

Mpya kabisa

Kirai kielezi (KE) ni kikundi cha maneno mawili au zaidi yenye uhusiano wa kimuundo ambapo neno moja ni kielezi ambalo ndilo neno kuu na neno lingine ni kijalizo chake.

KE

E E

Polepole sana

Kirai elezi huundwa na kirai kimoja au zaidi. Mf. mno sana, sana sana, polepole mno.

Kirai elezi

Kielezi Kielezi

Mno Mno

Polepole Sana

Haraka sana

Kielezi KieleziMno MnoPolepole sana

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 58

Page 59: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

Kirai Husishi (KH) ni kikundi cha maneno mawili au zaidi yenye uhusiano wa kimuundo ambapo neno moja ni kihusishi ambalo ndilo neno kuu na neno lingine ni kijalizo.

KH

H N

Kwa mjomba

Kirai husishi huundwa na kihusishi na nomino. Mfano. kwa Ali, kwa mjomba, na mama.

Kirai husishiKihusishi NominoKwa KakaKwa AliKwa mama

Kirai Unganishi (KU) ni kikundi cha maneno mawili au zaidi yenye uhusiano wa kimuundo ambapo neno moja ni kiunganishi ambalo ndilo neno kuu na neno lingine ni kijalizo.

KU

U N

na matunda

Kirai kiunganishi huundwa na kiunganishi na nomino. Mf. na Ali.

2.2.2 Aina za virai zimekitwa katika kategoria za maneno

Kategoria ya neno kuu la kirai hubainisha aina ya kirai kwani ndilo huwa jina la kirai. Kwa mfano, kirai ambacho neno kuu ni nomino, hujulikana kama kirai

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 59

Page 60: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

nomino. Kirai ambacho neno kuu ni kitenzi huitwa kirai tenzi. Vivyo hivyo kwa virai ambavyo neno kuu ni kivumishi, kielezi, kihusishi, n.k.

Kutokana na maelezo haya ni dhahiri kuwa kwa vile vikundi vya maneno yenye uhusiano ambayo yaweza kuunda kirai ni yale yenye kutawaliwa na nomino, kitenzi, kivumishi, kielezi na kihusishi au kiunganishi, vikundi hivi ndivyo vyenye kuunda virai na hizo ndizo aina za virai.

Aina za virai

Kirai Nomino

KIRAI NOMINONomino KivumishiKazi NyingiKikombe Cheupe

Kirai Tenzi

KIRAI TENZI

Kitenzi Nomino

Pika Chakula

Kata Mti

Kirai Kivumishi

KIRAI VUMISHIKivumishi KieleziNene SanaKavu mno

Kirai Elezi

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 60

Page 61: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

KIRAI ELEZIKielezi KieleziMno MnoPolepole sana

Kirai Husishi

KIRAI HUSISHIKihusishi NominoKwa MamaKwa kijiko

Uwezo wa kategoria za maneno kuteua maneno ili kuunda virai

Kwa kuwa uundaji wa virai hutegemea uwezo wa maneno kuteua maneno mengine ambayo yana uhusiano wa kimuundo, ni kategoria chache zenye uwezo wa kuteua maneno mengine kama vijalizo na kuunda kirai. Kwa mfano, vitenzi huweza kuteua nomino, vielezi au vihusishi na kuunda virai, lakini vyenyewe haviwezi kuteua vitenzi.

Mfano: pika chakula; tembea polepole; enda kwa dada; kinyume chake haiwezekani. Aidha nomino huweza kuteua kivumishi lakini haiwezi kuteua kitenzi wala kielezi peke yake. Kivumishi huweza kuteua kielezi lakini hakiwezi kuteua nomino. Hali hii ndiyo inayofanya fasili ya kirai ieleze kuwa kikundi cha maneno kinachounda kirai lazima kiwe na maneno yenye uhusiano wa kimuundo.

Jibu maswali yafuatayo:

1. Eleza maana ya kirai na bainisha virai tofauti vya lugha.

2. Bainisha miundo tofauti ya virai nomino na toa mifano ya Kiswahili kwa kila muundo.

3. Kirai kitenzi kina miundo kadha. Taja miundo hiyo na tumia kielelezo kudhihirisha maelezo yako.

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 61

Page 62: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

4. Kirai ni kikundi cha maneno, lakini sio kila kikundi cha maneno ni kirai. Jadili

Marejeleo

1. Graustein, G. et al (1980) English Grammar, A University Handbook. VEB Verlag Enzykloaedie. Leipzig.

2. Habwe J na Peter K. (2004) Misingi ya Sarufi ya Kiswahili. Phenix Publishers Nairobi.

3. Langacker R.W. (1968) Language and Its Structure. Harcourt Bruce. New York

4. Massamba, D.P.B. et al (2001) Sarufi Miundo ya Kiswahili Sanifu. IKR. UDSM, Dar es Salaam.

UCHAMBUZI WA VIRAI

Muhadhara wa kwanza

1.o Muundo wa virai

Katika muhadhara huu utajifunza yafuatayo

1. Muundo wa kirai

2. Virai kama viambajengo vya vishazi na sentensi

3. Uchanganuzi wa virai

4. Dhana ya neno kuu na kijalizo katika muundo wa kirai

1.1 Maana ya kiambajengo

Kiambajengo ni kipashio cha lugha ambacho kikiungana na kipashio kingine huunda kipashio kikubwa zaidi kwa hadhi kuliko vipashio vilivyokiunda.

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 62

Page 63: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

Lugha ina vipashio vitano: mofimu, neno, kirai, kishazi na sentensi. Vipashio hivi vinazidiana kwa hadhi, mofimu ndicho kipashio kidogo zaidi na sentensi ndicho kikubwa zaidi. Vipashio vina tabia ya kujengana, vipashio vidogo hujenga vipashio vikubwa zaidi. Kwa hali hii, mofimu hujenga neno, maneno hujenga kirai, virai hujenga kishazi na vishazi hujenga sentensi.

Mofu ni viambajengo vya neno. Mofu moja inapoungana na mofu nyingine huunda neno. Kiambajengo chaweza pia kuwa ni neno ambapo maneno yanapoungana huunda kirai. Virai vyaweza pia kuwa ni viambajengo vya sentensi. Kiambajengo chaweza pia kuwa neno moja iwapo linafanya kazi kama kitu kimoja. Kirai, kishazi au sentensi ni mkusanyiko wa viambajengo kadha.

1.2 Muundo wa Kirai

Kirai ni kundi la maneno yanayohusiana kimuundo na ambalo halina muundo wa kiima kiarifu. Maneno katika kirai humilikiwa na neno moja ambalo ndilo neno kuu na maneno mengine katika kundi hilo huwa ni vijalizo vya neno kuu. Kirai hubainishwa na kategoria ya neno kuu. Kwa mfano, neno kuu likiwa nomino, kirai hicho huwa KN. Vivyo hivyo kwa neno kuu likiwa kitenzi, kirai huwa KT, neno kuu likiwa kivumishi, kirai huwa KV. Virai vingine ni KE, KH, n.k.

Neno kuu ndilo muhimu na la lazima katika kirai na ndilo lenye kubainishwa na kirai kwani kategoria ya neno kuu ndiyo yenye kubainisha aina ya kirai.

Muundo wa kirai ni: neno kuu+kijalizo

MUUNDO WA KIRAINeno kuu Kijalizo Aina ya kiraiMtoto Mdogo KNCheza Mpira KT

1.3 Uchambuzi wa virai

Uchambuzi wa kirai hufanywa kwa kubagua maneno yanayounda kirai husika.

Mfano:

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 63

Page 64: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

a) Watoto wadogo (KN)

b) Lima shamba kubwa (KT)

c) Mvivu sana (KV)

Uchanganuzi wa virai huweza kufanywa kwa mishale, matawi au visanduku kama ifuatavyo.

1.4 uchanganuzi wa virai kwa mishale

a) KN ------------> N

Hii ina maana kuwa KN ina N yaani Kirai Nomino kina kiambajengo kimoja tu. Iwapo KN ina viambajengo viwili, muundo wake huelezwa hivi:

KN --------------> N,V

b) KT ----------------> T

Hapa tunaona kuwa KT ina T yaani ina kiambajengo kimoja tu. Iwapo KT ina viambajengo viwili, muundo wake huelezwa hivi:

KT -------------------> T, KN

c) KV -------------------> V iwapo KV ina viambajengo viwili, muundo wake huwa:

KV --------------------> V, E

d) KE ---------------------> E, iwapo KE ina viambajengo viwili, muundo wake huelezwa hivi: KE ---------------> E,E

e) Kirai husishi huweza kuwa na muundo ufuatao:

KH ---------------> H au KH --------------> H,KN

1.5 Uchanganuzi wa virai kwa matawi

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 64

Page 65: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

a) KN

N

Hii ina maana kuwa kirai hiki ni neno moja k.v. ‘mtoto’

Kirai chenye viambajengo zaidi ya kimoja, yaani chenye maneno zaidi ya moja huelezwa kwa kanuni:

b) Iwapo KN ina viambajengo viwili, muundo wake huelezwa hivi:

KN

N V

Mtoto mdogo

Hii ina maana kuwa KN kinaundwa na maneno mawili, yaani ‘mtoto mdogo’

c) Vivyo hivyo kwa kirai kitenzi (KT)

Iwapo KT ina viambajengo viwili, muundo wake huelezwa hivi:

KT

T KN

Anakula chakula

d) Iwapo KV ina viambajengo viwili, muundo wake huelezwa hivi:

KV

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 65

Page 66: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

V E

Mdogo sana

e) KE ikiwa na viambajengo viwili muundo wake huelezwa hivi:

KE

E E

Polepole mno

f) Muundo wa KH

KH

H KN

Kwa kijiko

1.6 Uchanganuzi wa virai kwa njia ya visanduku

Kirai huchanganuliwa kwa njia ya masanduku kama ilivyo katika mifano ifuatayo:

a) Mti mrefu sana

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 66

Page 67: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

KNN KV

V EMtoto Mdogo sana

b) Cheza kwa madaha

KTV KH

H NCheza Kwa madaha

c) Kwa haraka haraka

KHH KN

N NKwa haraka haraka

d) Katika makao makuu ya chuo

KHH KN

N KH KN

H N

katika Makao makuu ya chuo

1.7 Dhana ya neno kuu na kijalizo katika muundo wa kirai

Neno kuu na kijalizo ni vipashio vinavyounda kirai cha lugha.

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 67

Page 68: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

Neno kuu ni neno mojawapo katika muundo wa kirai ambalo lina uhusiano wa kimuundo na maneno mengine na ambalo ndilo neno muhimu na lenye kumiliki maneno mengine katika kirai.

Kijalizo ni neno moja au zaidi katika kirai yanayoambatana na neno kuu na ambayo yana uhusiano wa kimuundo.

Mfano:

a) Mtoto mdogo

KNN VMtoto(neno kuu)

Mdogo(kijalizo)

Katika kirai hiki, neno kuu ni mtoto na kijalizo ni mdogo

b) Amepika chakula kingi

KTT N VAmepika(neno kuu)

chakula(kijalizo)

Kingi(kijalizo)

Kirai hiki kina maneno matatu, neno kuu ni amepika na kijalizo ni chakula kingi

c) Dogo sana

KVV EDogo(neno kuu)

sana(kijalizo)

Jibu maswali yafuatayo:

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 68

Page 69: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

1. Fafanua dhana ya neno kuu na kijalizo katika muundo wa kirai na toa mifano 2 kwa kila aina ya virai.

2. Changanua virai vifuatavyo kwa njia ya matawi.

a) Asha anafua nguo zake polepole sana

b) Mariam na Vanesa wanasoma kitabu cha kwanza

c) Wanafunzi waliofaulu mitihani vizuri wanasoma katika shule ya vipaji maalumu

d) Mtoto amelala

e) Nitaondoka kesho

f) Nimeshiba

3. Kwa kuzingatia maana ya kirai eleza tofauti yake na kishazi kimuundo

4. Kila kipashio cha lugha ni kiambajengo. Jadili.

Marejeleo

1. Graustein, G. et al (1980) English Grammar, A University Handbook. VEB Verlag Enzykloaedie. Leipzig.

2. Habwe J na Peter K. (2004) Misingi ya Sarufi ya Kiswahili. Phenix Publishers Nairobi.

3. Langacker R.W. (1968) Language and Its Structure. Harcourt Bruce. New York

4. Massamba, D.P.B. et al (2001) Sarufi Miundo ya Kiswahili Sanifu. IKR. UDSM, Dar es Salaam.

Muhadhara wa pili

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 69

Page 70: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

4.0 Tungo za lugha na sifa ya kila moja

Katika muhadhara huu utajifunza mambo yafuatayo:

a) Maana ya tungo

b) Aina za tungo

c) Uchanganuzi wa sentensi wa wanamapokeo

4.1 Maana ya tungo

Tungo ni neno au kikundi cha maneno chenye maana. Tungo za lugha ni neno, kirai, kishazi na sentensi. Kila tungo huundwa na kipashio cha lugha chenye hadhi ya chini kuliko chenyewe.

Tungo za lugha zina sifa mahususi zinazozitofautisha. Kwa kutumia mifano ya Kiswahili eleza sifa za kila tungo.

4.2 Aina za tungo

a) Tungo neno huundwa na mofu moja au zaidi.

Mfano: ‘mtoto’ > m-toto. ‘mchezaji’ > m-chez-a-ji, ‘birika’ > birika

Neno huundwa na viambishi na mzizi

Sifa kuu ya neno ni kwamba lazima iwe na mzizi ambao unaweza kuwa peke yake au kuambatana na viambishi, lakini haliwezi kutokuwa na mzizi.

b) Tungo kirai huundwa na neno moja au zaidi ambapo neno moja huwa neno kuu na mengine huwa vijalizo.

Mfano: ‘kazi nyingi sana’. Hapa neno ‘kazi’ ni neno kuu, maneno ‘nyingi sana’ni vijalizo vya neno kuu katika kirai husika.

Sifa ya kirai ni kwamba ni lazima kiwe na neno kuu.

c) Tungokishazi huundwa na kirai ambacho chaweza kuwa kimoja au zaidi.

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 70

Page 71: Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) · Web viewsarufi miundo utazingatiwa na kutumiwa kuchambua sentensi na viambajengo vyake hususan virai. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia

Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia (Nukuu) 2018

Mfano: Mama anafundisha Kiswahili. Kishazi hiki kimeundwa na KN (mama) na KT (anafundisha Kiswahili)

Sifa kuu ya kishazi ni kwamba ni lazima kiwe na KT

KishaziKN KTMama Anafundisha Kiswahili

d) Tungo sentensi huundwa na kishazi kimoja au zaidi. Vishazi vya sentensi vyaweza kuwa kishazi huru na kishazi tegemezi au kishazi huru peke yake.

Mfano: ‘Ng’ombe aliyevunjika mguu ameuzwa’

SentensiKishazi tegemezi Kishazi huruNg’ombe aliyevunjika mguu ameuzwaSifa kuu ya sentensi ni kwamba ni lazima iwe na kishazi huru.

www.mwalimuwakiswahili.co.tzwww.uwasokita.co.tz0717104507 Uk 71