sera ya wanyamapori ya tanzania wildlife policy of ...wildlife-baldus.com/download/syw.pdf · na...

51
This is an unofficial translation of the Willdife Policy and not an official document of the Tanzanian Government. SERA YA WANYAMAPORI YA TANZANIA WILDLIFE POLICY OF TANZANIA (SWAHELI) Wizara ya Maliasili na Utalii S.L.P. 9372 Dar es Salaam Tanzania

Upload: others

Post on 23-Mar-2020

50 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

This is an unofficial translation of the Willdife Policy and not an official document of the Tanzanian Government.

SERA YA WANYAMAPORI YA TANZANIA

WILDLIFE POLICY OF TANZANIA (SWAHELI)

Wizara ya Maliasili na UtaliiS.L.P. 9372Dar es SalaamTanzania

YALIYOMO

YALIYOMO...................................................………NIA NA MATARAJIO ............................................1.0 USULI NA HISTORIA.......................................2.0 RASLIMALI YA TANZANIA YA

WANYAMAPORI NA UWEZA WAKE....…………………………

2.1 UANUWAI WA KIBIOLOJIA WA TANZANIA.....2.2 MAKAZI.............................................2.3 KATEGORIA YA MAENEO YALIYOHIFADHIWA2.4 MATUMIZI ENDELEVU YA WANYAMAPORI..

2.4.1 Kutazama Wanyama…2.4.2 Uwindaji wa Watalii2.4.3 Uwindaji wa Wakazi2.4.4 Ranchi na mashamba ya wanyamapori

2.5. UTAFITI NA UFUATILIAJI WA WANYAMAPORI.2.6 WAFANYAKAZI NA UIMARISHAJI WA

UTENDAJI2.7 MUUNDOMBINU NA VIFAA.................2.8 MISAADA YA KIMATAIFA..

2.9 MATATIZO YANAYOIKABILI SEKTA YAWANYAMAPORI..............…………………………….

3.0 SERA YA WANYAMAPORI.......................………3.1 CHANGAMOTO.................................…3.2 MALENGO..................................................…

3.2.1 Kuhusu Pori la akiba..........23.2.2 Kuhusu Matumizi ya Wanyamapori..................3.2.3 Kuhusu Uendeshaji na Uendelezaji wa Maeneo

aliyohifadhiwa.........................3.2.4 Kuhusu Ushirikiano wa Kimataifa

3.3 MIKAKATI...................................................3.3.1 Kulinda Uanuwai wa

Kibiolojia.......................…..3.3.2 Kulinda Wanyamapori dhidi ya matumizi

haramu.......3.3.3 Kuhifadhi na Kusimamia uanuwai wa

kibiolojia.........3.3.4 Kuhakikisha kwamba Pori la Akiba

linashindana na matumizi mengine ya ardhi

I11

344

NIA NA MATARAJIO

Wizara ya Maliasili na Utalii imepewa jukumu la kutayarisha sera yawanyamapori, kusimamia utekelezaji wake wa kuratibu maendeleo yasekta ya Wanyamapori katika Tanzania. Matarajio ya sekta yaWanyamapori katika miaka 20 ijayo yanakubaliana na Dira yaMaendeleo 2025 ya Tanzania kuhusu uimarishaji endelevu wa mazingirana mageuzi ya kijamii-kiuchumi. Matarajio ya sekta ya Wanyamapori ni:

• kukuza hifadhi ya uanuwai wa kibiolojia • kusimamia na kuendeleza raslimali ya wanyamapori• kuwashirikisha wadau wote katika kuhifadhi wanyamapori na

matumizi endelevu , na katika kugawana kwa usawa mafaoyapatikanayo

• kukuza matumizi endelevu ya rasilimali ya Wanyamapori• kuinua mchango wa sekta ya Wanyamapori katika Pato la Ndani

la Taifa (GDP) toka kwenye asilia 2 hadi kufikia kwenyeasilimia 5

• kuchangia katika kupunguza umasikini na kuinua hali za maishaya watu wa Tanzania, na

• kukuza ubadilishanaji wa taarifa na utaalamu unaohusika,kitaifa, kikanda na kimataifa.

1.0 USULI NA HISTORIAKatika Tanzania historia ya uhifadhi wanyamapori inarudi nyuma hadimwaka 1891 wakati sheria za kudhibiti uwindaji zilipoanzishwa na utawalawa Wajerumani. Sheria hizi zilidhibiti uvunaji wa wanyama; mbinu zauwindaji; na biashara ya wanyamapori ambapo baadhi ya aina ya wanyamawaliokuwa hatarini kutoweka wakiwa wamelindwa kabisa. Hifadhi zakwanza za wanyamapori, zilianzishwa na Wajerumani mnamo mwaka1905 katika eneo ambalo sasa linajulikana kama Pori la Akiba la Selous.Maeneo ya kuhifadhi wanyamapori yalichaguliwa kutokana na kuwepokwa wanyama wakubwa, na wala si kutokana na sababu za makundi yaoanuwai ya kibiolojia.

Mnamo mwaka 1921 Serikali ya Uingereza ikaanzisha Idara yaWanyamapori, ambayo ilifuatiwa na kutangazwa na serikali kwa Pori la

Akiba la kwanza ambalo lilijulikana kama Pori la akiba ya Selous, mwaka1922. Shughuli za Idara ya Wanyamapori zilikuwa ni pamoja nakusimamia Mapori ya Akiba, na kutekeleza kanuni za uwindaji nakuhakikisha kwamba watu na mazao yao hawaingiliwi au kuvamiwa nawanyama. Baadaye hifadhi nyingine mbili zilianzishwa: Hifadhi iliyokuwaBonde Kuu Funge la Ngorongoro, iliyoanzishwa mwaka 1928; na Pori laAkiba la Serengeti, lililoanzishwa mwaka 1928.

Tanganyika siku zote ilikuwa maarufu kwa kuwa na idadi kubwaya makundi anuwai ya wanyamapori na mandhari za aina mbalimbali, nakatika miaka hiyo ya mwanzo mwanzo ilikuwa kivutio kikubwakilichowaleta kwa wingi wawindaji matajiri. Tasnia ya uwindaji wa wataliiinarudi nyuma hadi mwaka 1946 wakati ambapo Mapori Tengefu (GCAs)yalianzishwa na kugawanywa katika maeneo makubwa ya uwindajiambapo wawindaji weledi na wateja wao waliweza kuwinda wanyama kwaajili ya nyara za thamani.

Kiunzi cha sasa cha Maeneo Yaliyohifadhiwa (PAs) katikaTanzania ikiwa ni pamoja na Hifadhi za Taifa, Mapori ya Akiba, naMapori Tengefu kilianzishwa baada ya Vita vya Pili vya Dunia. Mnamomwaka 1951 Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, ambayo sasa ilijumuishaBonde Kuu la Ngorongoro, iliingizwa katika gazeti la serikali ikifuatiwa naHifadhi kadhaa za Taifa (NPs) na Mapori ya Akiba (GRs).

Katika mwaka 1961 kulikuwa na Hifadhi za Taifa tatu (3) naMapori ya Akiba tisa (9), na Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro. Baada yauhuru, sera ya serikali ikawa ni kuendelea kupanua Mapori ya Akiba naHifadhi za Taifa; na hifadhi nyingi mpya za Taifa na za Wanyamaporizikaingizwa katika gazeti la serikali.

Wakati Tanzania ilipopata uhuru ikaonyesha azma kubwaya kuhifadhi wanyamapori wakati Rais wa Tanganyika alipotoa liletamko maarufu la "Azimio la Arusha" kama ilivyonukuliwa hapachini:

"Uhai wa wanyamapori ni jambo linalotuhusu sanasote katika Afrika. Viumbe hawa wa porini, wakiwa katikamapori wanamoishi, sio muhimu tu kwa ajili ya kuajabiwa nakuvutia lakini pia ni sehemu ya maliasili yetu na pia ndiomustakabali wa maisha yetu ya baadaye.

Kwa kukubali dhamana ya wanyamapori wetu

tunatamka kwa dhati kwamba tutafanya kila tuwezalokuhakikisha kwamba wajukuu wa watoto wetu watawezakufurahia urithi huu mkubwa na wa thamani adimu.

Uhifadhi wa wanyaampori na maeneo yote yenyemapori huhitajia maarifa ya kitaalamu, wafanyakazi waliopatamafunzo maalumu, na fedha; na hivyo tunaomba mataifamengine yashirikiane nasi katika kazi hii muhimu, ambayokufanikiwa au kutofanikiwa kwake hakuathiri tu Bara la Afrikabali ulimwengu mzima kwa ujumla".

(Mwalimu J.K. Nyerere 1961)

Azimio la Arusha limekuwa likitumika kutoa mwongozo wa kuhifadhi wawanyamapori katika Tanzania hadi hivi leo.

Pamoja na historia yake ya muda mrefu katika kuhifadhiwanyamapori, Tanzania haikuwahi kuwa na sera kamilifu ya wanyamaporikatika muda wote huo. Wanyamapori walikuwa wakilindwa na kutumiwakwa kufuata maelekezo, kanuni na sheria zilizokuwa zikitumiwa na Idaraya Wanyamapori na asasi nyingine zilizokuwa zimepewa jukumu lakufanya hivyo. Wakati wa uhuru, katika mwaka 1961, idadi ya watu katikaTanzania ilikuwa kidogo (milioni 8 tu); idadi ambayo ilifanya pasiwepo namigongano yoyote ya matumizi ya ardhi, hasa ilivyokuwa hapakuwepo namaendeleo yoyote ya kisayansi na kiteknolojia. Sehemu za ardhi ziliwezakutengwa, kwa urahisi, kwa ajili ya kuhifadhi wanyamapori pasi bilakuwaathiri sana watu walioshi karibu na maeneo hayo. Leo, idadi ya watuTanzania ni takribani milioni 30, na kuna maendeleo ya kisayansi nakiteknolojia, vitu ambavyo hufanya sasa ardhi iwe kidogo na kusababishakuhitajika kwa mipango ardhi na sera ya wazi ya kuhifadhi wanyamapori.

2.0 RASLIMALI YA TANZANIA YA WANYAMAPORI NAUWEZA WAKE

Wanyamapori wa Tanzania ni urithi wa asili wa pekee na raslimali yenyeumuhimu mkubwa kitaifa na kimataifa. Umuhimu wake umejikita katikathamani ya kibiolojia ya spishi zenyewe na mazingira ya asili yaliyopoTanzania, thamani yake ya kiuchumi na uweza wake katika kuchangiakwenye maendeleo endelevu ya Tanzania.

2.1 UANUWAI WA KIBIOLOJIA WA TANZANIATanzania ina spektra anuwai za wanyama na mimea, ikiwa ni pamoja naspishi ndogo na spishi kuu ambazo hupatikana kwa nadra sana. Uanuwaina kiwango cha upatikanaji wa spishi adimu sana katika Tanzaniaunajitokeza wazi kwa upande wa primata (spishi 20 na 4 ambazo ni adimusana), jamii ya paa (spishi 34 na 2 ambazo ni adimu sana), samaki (kukiwana spishi nyingi adimu katika Ziwa Victoria, Tanganyika na Nyasa, nakatika maziwa mengine madogo na mito), reptilia (wanyama wataga mayai,spishi 290 na spishi 75 kati yake zikiwa adimu sana), amfibia (wanyamawaishio majini na nchi kavu), spishi 40 adimu sana; wanyama wasio na utiwa mgongo na mimea (kwenye spishi 11,000 kukiwemo spishi nyingizilizo adimu sana). Kuna uwezekano kwamba kuna spishi nyingine katikaTanzania ambazo bado hazijulikani katika sayansi, na zinazongojakugunduliwa. Mbali na uanuwai huo na kuwepo kwa kiwango kikubwa chaspishi adimu, Tanzania ina idadi muhimu ya spishi ambazo zimo hatarinikutoweka, lakini ambazo zimeenea sana Afrika kote. Spishi hizo ni pamojana mbwa mwitu; faru weusi; mamba wembamba wenye kunguruma,ngedere, ambao maisha yao siku zote yamo hatarini; duma, na tembo waAfrika. Aidha, Tanzania pia ina idadi kubwa ya nyumbu, pundamilia,twiga, nyati wa Cape, na spishi nyingi za jamii ya paa, ambao naohalikadhalika ni muhimu katika muktadha wa kimataifa.

2.2 MAKAZIKwa upande wa makazi mapululu kadhaa na nyika za Serengeti na Mbugaza Maasai huko kaskazini magharibi na kaskazini-mashariki mwa Tanzaniamnapatikana baadhi ya makundi mengi kabisa ya wanyama ulimwenguni.Maeneo muhimu yenye majimaji, vinamasi na tambarare zenye mafurikohupatikana nchini kote (Bonde la Kilombero, Vinamasi vya Kagera naWembere, Mbuga za Usangu, n.k.). Kuna utajiri wa maziwa ya aina

mbalimbali katika Tanzania, ikiwa ni pamoja na maeneo makubwa yaMaziwa Makuu (Victoria, Tanganyika na Nyasa) ambayo ni muhimu kwasamaki na wanyama wasio na uti wa mgongo ambao ni adimu. Tanzaniapia ina idadi kadhaa ya maziwa ya magadi (Natron, Eyasi, Balangida naManyara) ambayo ni muhimu kwa ndege. Misitu ya aina kadhaa zakibiolojia hupatikana Tanzania, ikiwa ni pamoja na ile ya nyanda za chiniisiyopatikana mahali pengi na ile ya hapa na pale iliyoko huko pwani nasehemu za milima. Misitu hii, na hasa hasa ile iliyo katika Tao yaMashariki (Milima ya Usambara, Ukaguru, Udzungwa na Uluguru) nimuhimu sana katika uanuwai na upekee wake. Mbuga za kipekee zakwenye milima pia hupatikana katika baadhi ya maeneo (milima yaUdzungwa, nyanda za Ufipa, na nyanda za juu za Kusini), nazo ni muhimusana kwa mimea yake ya asili. Wakati vichaka vya Itigi ni vya pekee kabisakatikati ya Tanzania; sehemu ya kusini na magharibi ya nchi hii imejaa mitiya miombo ambayo ina baadhi ya idadi kubwa ya tembo na faru weusikatika bara hili.

2.3 KATEGORIA ZA MAENEO YA WANYAMAPORIMtandao wa maeneo yaliyohifadhiwa (PAs) katika Tanzania huchukuaasilimia 28 ya ardhi yote. Kati ya asilimia hiyo, asilimia 4 ni Hifadhi zaTaifa (NP) 12, asilimia 1 ni Hifadhi ya Ngorongoro (NCA), asilimia 15 niMapori ya Akiba (GRs) 31, na asilimia 8 ni Mapori Tengefu (GCAs) 38.Kutokana na hali hiyo asilimia 19 ya ardhi ya Tanzania imetengwa kwaajili ya Wanyamapori katika maeneo yaliyohifadhiwa (PAs) ambakomakazi ya binadamu hayaruhusiwi (NPs na GRs), na asilimia 9 ya ardhikwa ajili ya maeneo yaliyohifadhiwa (PAs) ambako maisha yawanyamapori ni sambamba na maisha ya binadamu. Sekta ya misitu piaimefuata sera za uhifadhi ambazo zimeongeza maeneo yaliyohifadhiwa(PAs) katika Tanzania. Jumla ya Hifadhi za Misitu 150 huchukua kwenyeasilimia 15 ya ardhi yote ya Tanzania, ambapo asilimia 3 yake huingilianana maeneo yaliyohifadhiwa ambayo yametengwa kwa ajili ya uhifadhi wawanyamapori.

2.4 MATUMIZI ENDELEVU YA WANYAMAPORIMtandao wa maeneo yaliyohifadhiwa kwa ajili ya uhifadhi wawanyamapori ndiyo msingi wa tasnia ya matumizi endelevu yawanyamapori. Matumizi endelevu ya wanyamapori katika Tanzania ni

pamoja na:

2.4.1 Kutazama WanyamaKwa sasa Hifadhi ya Ngorongoro (NCA) na Hifadhi za Taifa (NPs) yaTanzania kaskazini ndio maeneo yanayotembelewa sana na watalii,ambapo Maeneo Yaliyohifadhiwa na Mapori ya Akiba huko kusini badohayajatumika vilivyo. Utalii uliokitwa katika kutembelea wanyamapori nakutazama wanyama ni vitu vyenye uweza mkubwa wa kuingiza pesa nyingiza kigeni na za ndani; na pia kutoa nafasi za ajira.

2.4.2 Uwindaji wa kitaliiUwindaji wa kitalii ni matumizi endelevu ya wanyamapori ambayo yanafaida kiuchumi, unaoweza kuendelezwa kwa muda mrefu na ambaounaendana na sera ya utalii kuhusu utalii wa kiwango kidogo lakini ulio naubora mkubwa ambao unaweza kuchangia vikubwa katika uchumi wa taifa.Kwa sasa uwindaji wa kitalii unafanyika sana katika maeneo mengi yandani katika Tanzania kwenye Mapori ya Akiba (GR), Mapori Tengefu(GCA), Maeneo ya Wazi na Hifadhi za Misitu(FRs).

2.4.3 Uwindaji wa WakaziWatanzania wa asili wanayo haki ya kisheria kuwatumia wanyamapori.Viwango tofauti vya malipo vimewekwa kwa wawindaji watalii nawawindaji wakazi kwa mujibu wa sheria. Leseni za wawindaji wakazihutolewa kwa uwindaji kwenye Maeneo ya Wazi na Mapori Tengefu(GCAs) ambayo hayakutengwa kwa ajili ya uwindaji wa starehe.

2.4.4 Ufugaji wa wanyamaporiUfugaji wa wanyamapori ni shughuli ambayo bado haijaendelezwa sanakatika Tanzania.

Si sera ya serikali kujiingiza moja kwa moja katika kuwekezakwenye matumizi ya raslimali za wanyamapori katika Tanzania. Kwa hiyosekta ya binafsi inashawishiwa kuwekeza katika maeneo yafuatayo:(i) Kuendesha shughuli za safari za uwindaji na upigaji picha (za

Wanyama).(ii) Kuwekeza katika ufugaji wa wanyamapori.(iii) Wanyamapori na bidhaa za Wanyamapori.

iv) Kuanzisha miundombinu katika kiunzi cha sera ya wanyamapori

na mipango ya uendeshaji wamaeneo yaliyohifadhiwa.

2.5 UTAFITI NA UFUATILIAJI WA WANYAMAPORIKiasi kikubwa cha utafiti juu ya wanyamapori kimekwishafanywa katikaTanzania, na utafiti huo umechangia vikubwa katika kueneza habari nakuwatangaza wanyamapori katika Tanzania. Utafiti uliokwishafanywampaka sasa umekuwa ni wa aina anuwai ikiwa ni pamoja na maelezo yakitaksonomia ya spishi mbalimbali na maeneo ambako wanyama haohuishi, tabia zao, ekolojia ya kila spishi, na mitalaa kuhusu michakato yamifumo ya kiekolojia. Programu kadhaa za ufuatiliaji wa wanyamaporizinaendeshwa, hasa kwa njia ya kuhesabu wanyama kutoka angani katikamaeneo yaliyohifadhiwa na sehemu zinazoyazunguka, na kwa njia yakuangalia idadi za wanyama mbalimbali katika kipindi cha utafiti wa mudamrefu.

Utafiti uliokwishafanywa mpaka sasa umekuwa zaidi umeelekezwakwenye matamanio ya watafiti wa kigeni kuchapisha matokeo ya utafitiwao kimataifa, kuliko kuzingatia mahitajio ya Tanzania. Aidha, niWatanzania wachache sana ambao wamewahi kushirikishwa katika utafitiwa wanyamapori, ambao unafanywa zaidi na wageni ambaowameruhusiwa kusoma nchini. Zaidi ya hapo, mamlaka ya wanyamaporiwamekuwa kila mara wana matatizo ya kifedha na wataalamu wa kutoshakufanya utafiti halisi na utafiti matumizi ambao ungekuwa endelevu zaidi.

2.6 WAFANYAKAZI NA UIMARISHAJI WA UTENDAJI Kuna utaratibu mzuri wa muundo wa watumishi wa wanyamapori ambaounaonyesha mahitajio halisi ya ikama, sifa na ngazi za wafanyakazi.Pamoja na utaratibu huu mzuri bado kuna udhaifu katika utekelezaji wamuundo huo wa watumishi. Aidha watumishi wa sekta ya wanyamapori nichini ya 50% ya mahitaji yake; na hata hao waliopo wengi wao ni wa kadaya chini. Mafunzo yanatolewa huko Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, SUAna ng'ambo kwa ajili ya Shahada za kwanza na Shahada za uzamili;CAWM kwa ajili ya astashahada, stashahada, diploma na stashahada yauzamili; na Taasisi ya Wanyamapori ya Pasiansi kwa ajili ya mafunzo yavyeti vya maskauti / maaskari.

2.7 MIUNDOMBINU NA VIFAAHali ya miundombinu na vifaa katika maeneo yaliyohifadhiwa iko chini yakiwango kitakikanacho. Barabara ni mbaya; vifaa kama vile magari, zanaza uwandani na silaha navyo viko katika hali mbaya na havitoshi; majengoya ofisi na wafanyakazi ni ya hali ya chini, na hayatoshelezi.

2.8 MISAADA YA KIMATAIFATanzania ina raslimali kidogo sana kuweza kushughulikia suala lakuhifadhi wanyamapori peke yake. Kutokana na hali hiyo imekuwaikisaidiwa kifedha na kiutaalam na mashirika yanayojitegemea, namashirika ya wahisani kutokana na uhusiano baina ya nchi na nchi aukutoka mataifa kadhaa.

2.9 MATATIZO YANAYOIKABILI SEKTA YAWANYAMAPORI

Pamoja na karama hii na uweza wake wa kiuchumi kwa taifa na jumuiya zavijijini zilizo jirani na maeneo ya hifadhi ya wanyamapori, sekta yawanyamapori haijaweza kuendelezwa kufikia uweza wake kikamilifukutokana na matatizo yafuatayo:

(i) Kutokuwepo na Sera ya Wanyamapori iliyo wazi.ii) Kushindwa kwa uhifadhi wanyamapori kushindana na kikamilifu

na namna nyingine za matumizi ya ardhi, hasa katika jamii zavijijini.

iii) Kutokuwepo na mwamko juu ya uhifadhi wa wanyamaporimiongoni mwa wapangaji mipango na maafisa wenye mamlaka, nahivyo basi, suala la ardhi na wanyamapori kupewa uzito kidogosana wakati wa upangaji mipango.

iv) Kupotea au kutoweka kwa makazi ya wanyamapori kutokana namakazi ya watu, kilimo, malisho ya mifugo, uchimbaji migodi naukataji miti; mambo ambayo husababishwa na kuongezeka kwaidadi ya watu.

(v) Kuongezeka kwa ujangili kwa kasi kubwa na biashara isiyo halali.v) Kutotosheleza kwa mahitaji ya kifedha na watu kuiwezesha

serikali kutoa madaraka ya usimamizi wa wanyamapori kwa watuwa vijijini nchini kote.

vi) Mfumo uliopo wa umiliki ardhi na umiliki wa serikali juu ya

wanyamapori huzuia uwekezaji na uendelezaji wa tasnia yawanyamapori wa sekta binafsi.

(viii) Kutokuwepo kwa haki toshelevu juu ya matumizi yawanyamapori, hasa kwa jamii za vijijini.

(ix) Kutokuwepo na uwezo wa kutosha wa kuwadhibiti wanyamawakali na waharibifu.

x) Utengewaji kidogo wa fungu la bajeti kwa ajili ya hifadhi nauendelezaji wa sekta ya wanyamapori.

xi) Malipo kidogo ya wafanyakazi ambayo husababisha kushuka kwaraghba katika kazi na mmonyoko wa maadili ya kikazi.

(xii) Upungufu wa watendaji wa kuendesha shughuli za kuhifadhiwanyamapori.

Katika kutambua umuhimu wa kuhifadhi uanuwai wa kibiolojia(bioanuwai) kwa ajili ya mustakabali wa wanaadamu, Taifa litaendeleakuwa mmiliki mkuu wa wanyamapori. Serikali itatoa haki za matumizi kwawadau, kuweka miongozo ya sera iliyo wazi, chombezaji wa uwekezajikatika wanyamapori wa sekta za uma na binafsi na kuwapa kila msaadauwezekanao wawekezaji.

Katika mabadiliko yanayotokea ya kiekolojia, kiuchumi-kijamiikatika muktadha wa kitaifa na kimataifa, dhima ya serikali katika sekta yawanyamapori itakuwa imeelekezwa zaidi kwenye:

i) Kuweka sera madhubuti za uendeshaji wa shughuli zawanyamapori, na kushiriki kikamilifu katika uendeshaji na usimamizi wa raslimali za wanyamaporinchini kote.

ii) Kuweka na kuwezesha kuwepo kwa mazingira halali na yakisheria yatakayoziwezesha jamii za vijijini na sekta binafsi kushiriki katika shughuli za pori la akiba.

iii) Kuweka utaratibu endelevu utakaosimamia na kuhakikishakwamba kunaendelea kuwepo maeneo yaliyohifadhiwa ambapowanyamapori na maeneo mengine ya asili yataendeleakuhifadhiwa.

(iv) Kupiga vita matumizi haramu ya wanyamapori.

(v) Kuwawekea wafanyakazi wa wanyamapori kanuni kali za maadiliya kazi zao.

(vi) Kuanzisha databezi ya habari zinazohusu wanyamapori.vii) Kuimarisha shughuli za huduma tanzu na kuzisaidia jamii za

vijijini katika kuendesha shughuli za wanyamapori.

viii) Kutoa fedha za kutosha kwa ajili uendeshaji endelevu wa shughuliza wanyamapori kulingana na gharama.

Sekta binafsi itakuwa na nafasi kubwa katika uwekezaji wa kiuchumikatika sekta ya wanyamapori. Wawekezaji katika tasnia ya wanyamaporikatika Tanzania watafaidika na mambo yafuatayo:

• watahakikishiwa usalama wa kisiasa• watapewa mazingira ya kijamii yenye amani na ya kirafiki• ugo mpana wa sekta binafsi wa kushiriki katika tasnia ya

wanyamapori.

3.0 SERA YA WANYAMAPORI

3.1 MAMBO YA KUKABILISera ya Wanyamapori inakusudia kushughulikia mambo yafuatayoyanayolikabili taifa:-(a) Kuhifadhi maeneo ambayo yana bioanuwai kubwa ambayo

yanawakilisha makazi muhimu katika Tanzania;(b) Kuendelea kutoa msaada, na pale inapokuwa lazima kupanua,

mtandao wa Maeneo Yaliyohifadhiwa (PAs) kama kitovu chashughuli za uhifadhi;

(c) Kuhamasisha kushiriki kwa jamii za vijijini katika shughuli zakuhifadhi wanyamapori, ndani na nje ya mtandao wa MaeneoYaliyohifadhiwa (PAs).

(d) Kuongeza mapato ya fedha za kigeni.(e) Kuoanisha uhifadhi wanyamapori na maendeleo vijijini.(f) Kuchochea matumizi endelevu na ya kisheria ya raslimali za

wanyamapori.(g) Kuhakikisha kwamba uhifadhi wa Wanyamapori unashindana

vilivyo na namna nyingine za matumizi ya ardhi.(h) Kutia nguvu utambuzi wa thamani na faida ya kudumu ambayo

jamii za vijijini zinaweza kupata kutokana na shughuli zawanyamapori.

(i) Kupunguza, kila inapowezekana, migongano baina ya watu nawanyamapori.

(j) Kurekebisha utafiti unaohusu shughuli za wanyamapori ili uwe wamanufaa ya moja kwa moja katika uendeshaji wa shughuli zawanyamapori.

(k) Kukuza uwezo wa sekta ya wanyamapori na kuongeza weledi; na(l) Kujenga mazingira mazuri yatakayowezesha kuwepo kwa

ushirikiano wa kimataifa katika kuhifadhi wanyamapori.

3.2 MALENGOWanyamapori ni maliasili iliyo na umuhimu mkubwa kibiolojia, kiuchumi,katika kusafisha mazingira, kuboresha hali ya hewa, kuhifadhi maji naardhi, na virutubisho ambavyo havina budi kuhifadhiwa. Maliasili hiiinaweza kutumiwa daima dumu kama inaweza kuangaliwa vizuri ipasavyo.Kutokana na hali ya mabadiliko na hali ya uchangamani wa raslimali yawanyampori na mambo yanayoikabili huko mbele katika kuihifadhi, seraya serikali, kwa sekta ya wanyamapori, italenga katika kuishirikishasehemu kubwa ya jamii katika kuhifadhi wanyamapori, hasa jamii zavijijini na sekta binafsi. Kazi ya sekta ya umma itakuwa ni kuchochea nakuziongoza jamii za sehemu mbalimbali nchini na sekta binafsi kwakusimamia, kurekebisha na kukuza uendeshaji wa shughuli zawanyamapori kupitia malengo yafuatayo:

3.2.1 Kuhusu Pori la akiba• Kuendelea kuanzisha Maeneo Yaliyohifadhiwa (PAs) kwa

misingi ya mipango inayozingatia mifumo shirika.• Kusisitiza kuhifadhi na kuendeleza mtandao wa Maeneo

Yaliyohifadhiwa ili kuongeza uanuwai wa kibiolojia.• Kukuza uhifadhi wanyamapori na makazi yao nje ya maeneo

kiini (NPs, GRs, & NCA) kwa kuanzisha Maeneo ya Jumuiyaya Usimamizi Wanyamapori (WMA).

• Kuhamishia usimamizi wa Maeneo ya Jumuiya ya UsimamiziWanyamapori (WMA); kwa wananchi vijijini na hivyo basi

kuulinda ushoroba wa wanyama, njia za uhamaji, maeneo yausalama wa wanyama, na kuhakikisha kwamba jamii zilizokatika maeneo hayo ya wanyama zinafaidika vilivyokutokana na uhifadhi wanyamapori.

• Kuzuia matumizi haramu ya wanyamapori nchini kote kwakuchukua hatua endelevu za usimamizi, ulinzi na kutekelezasheria.

3.2.2 Kuhusu Matumizi ya Wanyamapori• Kuendeleza matumizi ya Maeneo Yaliyohifadhiwa (PAs) ili

kuipatia serikali fedha, kuwapatia ajira, mapato, chakula nafaida nyingine kwa Watanzania; hasa katika jamii za vijijini.

• Kuhakikisha kwamba wanyamapori wanathaminiwa vilivyoili kupunguza matumizi haramu na kuhimiza matumiziendelevu katika jamii za vijijini.

• Kuweka mazingira endelevu kwa Watanzania kuwezakujishughulisha na tasniya ya wanyamapori.

• Kuweka na kuwezesha kuwepo kwa mazingira ambayoyatahakikisha kwamba mipango endelevu na halali yashughuli za wanyamapori inazifaidia moja kwa moja jamii zamahali mipango hiyo ilipo.

• Kuanzisha na kuwezesha kuwepo kwa mazingira endelevukwa sekta binafsi kuweza kuwekeza katika namnambalimbali za uhifadhi wa wanyaampori na matumizi yake.

3.2.3 Kuhusu Uendeshaji na Uendelezaji wa MaeneoYaliyohifadhiwa (PAs) • Kuchochea mwamko na welewa wa umma juu ya masuala ya

wanyamapori.• Kubakiza fedha za kutosha zinazotokana na matumizi ya

wanyamapori katika maeneo hayo (PAs) kwa ajili yashughuli za uendeshaji na ukuzaji wa shughuli hizo.

• Kurekebisha na kusimamia miradi ya/au shughuli zamaendeleo katika maeneo yaliyohifadhiwa (PAs).

• Kukuza utafiti na ufuatiliaji wa shughuli ambazo zimelenga

katika kupata utatuzi wa masuala ya uendeshaji.• Kuendesha mipango ya kuendeleza wafanyakazi na uwezo

wa kiasasi katika ngazi zote, na• Kurejesha kwa nguvu moja miiko na viwango vya kieledi.

3.2.4 Kuhusu Ushirikiano wa Kimataifa• Pale inapokuwa lazima na inapowezekana au kuwa endelevu

kuna haja ya kuwashawishi wafadhili, pamoja na mashirikamengine ya hifadhi, kushiriki katika kuisaidia Tanzaniakuhifadhi wanyamapori wake, kwa manufaa ya kitaifa,kikanda na kimataifa.

• Kuiwezesha Tanzania kushiriki katika mikataba namakubaliano husika ya kimataifa, na kukuza sera katikakiunzi cha mikataba na makubaliano hayo kadriyanavyoendana na kukubaliana na msimamo wa Tanzaniakuhusu uhifadhi wanyamapori, na

• Kushirikiana na nchi jirani katika kuhifadhi na kulindamifumo ya kiekolojia katika maeneo ya mipaka ya nchi zao.

3.3 MIKAKATI

Ili kutekeleza malengo ya sera ya wanyamapori mikakati ifuatayoimewekwa.

3.3.1 Kulinda bioanuwaiLengo la msingi la mtandao wa maeneo yaliyohifadhiwa ni kuanzishamfululizo wa maeneo yanayofaa ya hifadhi yanayowakilisha makazi asiliaya aina zote muhimu na idadi ya kutosha ya spishi zote hasa zile ambazouhai wake nchini Tanzania unatishiwa. Ongezeko la watu linazidishamatumizi ya rasilimali za kibiolojia hasa kutokana na kilimo, ufugaji naujenzi wa makazi. Ili kutekeleza lengo la mtandao, serikali itaendeleakuyadumisha maeneo yaliyohifadhiwa na kuanzisha mengine mapya kwamadhumuni ya kulinda bioanuwai.

Mikakati ya kulinda bioanuwaii) kuendelea kudumisha mtandao wa maeneo yaliyohifadhiwa ambao

malengo yake makuu ni kuwezesha hifadhi na kukuza maendeleoya kijamii na kiuchumi ya watu wa Tanzania;

ii) kutambua, kuanzisha na kuboresha mfululizo wa mtandao wamaeneo yaliyohifadhiwa na ardhioevu muhimu ili kulindabioanuwai ya Tanzania;

iii) kuanzisha kategoria mpya ya eneo linalohifadhiwa litakalojulikanakama Eneo la jumuiya la Usimamizi wa Wanayamapori kwa ajiliya kuwezesha usimamizi wa Uhifadhi Uliokitwa katika jumuiya;

iv) kuzipatia hifadhi maalum spishi za wanyamapori zilizo adimu auzilizoko katika hatari ya kutoweka;

(v) kuzijumuisha ardhioevu muhimu katika mtandao wa maeneo yawanyamapori yaliyohifadhiwa;

(vi) kupima na kupata hatimiliki za maeneo yote yanayohifadhiwa.

3.3.2 Kulinda wanyamapori dhidi ya matumizi haramuTishio kuu la mtandao wa maeneo yaliyohifadhiwa na wanyampori nimatumizi haramu ya rasilimali za wanyamapori. Mamlaka za wanyamaporizina jukumu la kupambana na matumizi haramu ya wanyamapori kwa

mikakati ya aina mbili lakini inayofungamana inayolenga kwenye maeneoyaliyohifadhiwa na ya nje ya hifadhi. Ili ziweze kutekeleza sheria vizuri,serikali inazitambua mamlaka za wanyamapori zinazosimamia maeneo yahifadhi kuwa na hadhi ya kijeshi zenye wafanyakazi wanaovaa sare,kubeba silaha na wenye madaraka ya kufanya msako na kutia mbaroniwatu. Kwa vile vita dhidi ya ujangili kwa kiasi fulani inategemea nguvu-kazi, vifaa na hamasa ya wafanyakazi, serikali itahakikisha kwambamamlaka za wanyamapori zina uwezo wa kutosha wa kutekeleza sheriaipasavyo.

Mikakati ya kuwalinda wanyamapori dhidi ya matumizi haramui) kushirikiana na vyombo vingine vya utekelezaji sheria katika

kufuatilia makosa dhidi ya wanyamapori;(ii) kusaidia mamlaka za wanyamapori katika utekelezaji wa

majukumu yake ya kisheria;(iii) kuanzisha sheria za nidhamu;

v) kuhakikisha kwamba wafanyakazi wa sekta ya wanyamaporiwanafuata sheria za nidhamu ipasavyo;

vi) kuanzisha mifumo imara ya upashanaji habari databezi zaupelelezi vituoni na katika ngazi ya taifa;

vii) kuwalinda wafanyakazi wa sekta ya wanyamapori dhidi ya dhimazinazotokana na kujeruhi au vifo vya watuhumiwa wakatiwanapotekeleza kazi zao;

(vii) kushirikiana na kutumia vema ushirikiano na jumuiya za vijijini;viii) kukabidhi madaraka ya kudhibiti matumizi haramu ya

wanayamapori katika Maeneo ya jumuiya ya Usimamizi waWanayamapori kwa jumuiya za vijijini;

ix) kuwapatia mafunzo na msaada askari wa wanyamapori wa vijijiniili walinde rasilimali za wanyamapori wanazozidhibiti chini yampango wa Uhifadhi Uliokitwa katika Jumuiya (CBC); na

x) kuanzisha na kuendeleza mikakati ya kupata fedha za kutosha ilikuziwezesha mamlaka za wanyamapori kuwa na wafanyakazi wakutosha na kuinua hamasa ya wafanyakazi hao.

3.3.3 Kuhifadhi na kusimamia bioanuwaiTanzania imetenga eneo la kutosha la ardhi yake kwa ajili ya mtandao wa

maeneo yanayohifadhiwa kwa ajili ya hifadhi ya wanyamapori. Mtandaohuu wa maeneo yanayohifadhiwa una malengo ya jumla yanayohusiana nahifadhi na uchumi-jamii wa watu wa Tanzania. Malengo ya jumla yamtandao wa maeneo yanayohifadhiwa nchini Tanzania ni:

• kuhifadhi mifano wakilishi ya makazi asilia ya nchi kavu namajini ya Tanzania na viumbe vyake;

• kuhifadhi idadi ya kutosha ya spishi za fauna na flora zaTanzania, huku mkazo ukiwekewa spishi zilizomo hatarini,spishi zinazotishiwa zinazopatikana Tanzania tu pamoja namakazi yake asilia;

• kulinda maeneo yenye mandhari nzuri na yenye mvuto maalumau wa kiutamaduni;

• kuhifadhi vyanzo vya maji na rasilimali za udongo;• kutoa fursa kwa ajili ya burudani ya umma na maendeleo ya

sayansi;• kukarabati makazi asilia maalum, uanzishaji au uanzishaji upya

wa spishi maalum za fauna; na• kuandaa fursa na mazingira mazuri kwa jumuiya za watu

kuzitumia rasilimali za asili kwa ajili ya kuleta maendeleo yavijijini.

Sera hii inatambua kwamba mtandao wa maeneo yanayohifadhiwautaendelea kuwa kiini cha hifadhi na maendeleo ya baadaye ya tasnia yawanyamapori na kwamba jumuiya za vijijini lazima zifaidike kwa kuishikaribu na maeneo yanayohifadhiwa na miongoni mwa wanyamapori.

Mapato na mgawanyo wa fedha kutoka kwenye tasnia yawanyamapori haujaziwezesha mamlaka za wanyamapori kutekelezamalengo yake. Ni kiasi kidogo sana cha mapato yatokanayo nawanyamapori kinachotumika kwa ajili ya maendeleo na usimamizi wamtandao wa maeneo yanayohifadhiwa. Bila kutengewa bajeti ya kutosha,maeneo yanayohifadhiwa yatasimamiwa vibaya, na miundombinu, vifaa,fursa na hamasa ya wafanyakazi vitapungua na msingi wa rasilimali ya asiliutamomonyoka. Sera hii inasisitiza mgawanyo mzuri wa mapato ya tasniaya wanyamapori kwa ajili ya hifadhi na usimamizi imara wa maeneoyanayohifadhiwa.

Mikakati ya kuhifadhi na kusimamia rasilimali za wanyamapori

(i) kusimamia wanyamapori kwa kuhifadhi makazi asilia ya spishimuhimu za wanyamapori ikiwa ni pamoja na ardhioevu kupitiamamlaka za wanyamapori na kwa kukasimu majukumu yausimamizi wa maeneo yanayokaliwa na watu yenye wanyamaporina yale yasiyokaliwa na watu yaliyopo nje ya maeneoyaliyohifadhiwa kisheria kwa wanavijiji au sekta ya binafsi;

(ii) kubakisha umiliki na usimamizi wa jumla wa rasilimali zawanyamapori mikononi mwa Serikali, ili kuhakikisha kwambavipaumbele vya taifa vinazingatiwa na matumizi mabaya yarasilimali hizi yanadhibitiwa;

(iii) kusimamia rasilimali za wanyamapori kwa msingi wa mifumo yaikolojia, badala ya mipaka ya kiutawala, kutokana na hulka yamjongeo ya wanyamapori, upatikanaji wa rasilimali na kutandaakwa makazi asilia;

(iv) kukataza uchimbaji madini katika meneo yanayolindwa yawanyamapori (Hifadhi za Taifa, Hifadhi ya Ngorongoro, Maporiya Akiba) ili kuhifadhi bioanuwai;

(v) kukataza ukamataji na uhamishiaji spishi katika maeneoyanayohifadhiwa isipokuwa kwa idadi ndogo tu ya wanyamaporiwaliopo na kwa spishi zilizokwishatoweka;

(vi) kuandaa mipango ya usimamizi ya baadhi ya spishi au makundimaalum ya wanyamapori yaliyoainishwa ili kuhakikisha kwambayanaendelea kuishi;

(vii) kurekebisha uingizaji nchini wa spishi za nje na urejeshaji upya waspishi asilia za maeneo husika, ili kudhibiti athari hasi zinazowezakusababishwa na uingizwaji na urejeshwaji wa spishi hizomaporini;

(viii) kuendeleza mipango ya usimamizi na ugawaji kwa ajili yamatumizi mbalimbali, maeneo yaliyohifadhiwa kisheria,, huku kilaeneo likiwekewa kiwango na aina ya matumizi, ili kuhakikishakuwa malengo ya kila eneo linalohifadhiwa yanatekelezwaipasavyo;

(ix) kukuza ushiriki wa wadau katika kutenga maeneoyanayohifadhiwa na kupanga mipango ya maendeleo ya maeneohayo;

(x) kuhimiza utekelezaji wa tathmini ya athari ya mazingira kwamiradi ya maendeleo iliyopendekezwa katika maeneno

yanayohifadhiwa na kuagiza kufanywa kwa mipango ya mazingirakwa miradi yote itakayofanyika katika maeneo ya wanyamapori nanje ya maeneo yanayohifadhiwa ili kupunguza athari hasi zakimazingira;

(xi) kuruhusu mamlaka za wanyamapori kubakisha mapato ya kutoshayanayotokana na wanyamapori ili kugharamia ipasavyo uendeshajiwa maeneo yanayohifadhiwa;

(xii) kuruhusu jumuiya za vijijini kufaidika na miradi ya UhifadhiUliokitwa katika Jumuiya;

(xiii) kudumisha na kuwezesha Mfuko wa Hifadhi ya WanyamaporiTanzania kupata fedha za kutosha za kusaidia shughuli za hifadhiya wanyamapori;

(xiv) kuhakikisha kuwepo kwa ushirikiano mzuri na jumuiya za vijijinina sekta binafsi nje ya maeneo yanayohifadhiwa na kuzipatiajumuiya hizo za vijijini mafao ya moja kwa moja na yasiyo yamoja kwa moja kutokana na matumizi ya wanyamapori;

(xv) kuongeza na kupanua mtandao wa maeneo yanayohifadhiwa kwamsingi wa mipango ya kimfumo, iliyoandaliwa kwa ushirikianowa sekta mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kufikiria mtawanyiko waspishi na makazi asilia, kutandaa kwa sasa kwa maeneoyanayohifadhiwa na ruwaza za matumizi ya ardhi;

(xvi) kujenga hapo baadaye , hoteli kubwa za kitalii nje ya maeneoyanayohifadhiwa ili kupunguza athari hasi na kuwezeshakugawana mafao na jumuiya za maeneo hayo;

(xvii) kujitahidi kudhibiti na kupunguza kabisa hasara zinazoletwa namioto inayochoma mapori; na

(xviii) kukuza matumizi ya mioto dhibiti kwa ajili ya programu zausimamzi kama ilivyoelezwa kwenye mipango ya usimamizi waeneo husika.

3.3.4 Kuhakikisha kuwa hifadhi ya wanyamapori inashindana naaina nyingine za matumizi ya ardhi

Hifadhi ya wanyamapori ni njia mojawapo muhimu ya matumizi ya ardhinchini Tanzania yanayozalisha mapato ya kutosha na fedha za kigeni.Ikiendelezwa vizuri, hifadhi ya wanyamapori inaweza kushindana na ainanyingine za matumizi ya ardhi. Hata hivyo, hifadhi ya wanyamahaijaendelezwa kikamilifu, hususani nje ya maeneo yanayohifadhiwa, na

jumuiya za vijijini zimefaidika kidogo tu na aina za sasa za matumizi yawanyama katika ardhi inayokaliwa na wanyamapori. Ni lengo la sera hiikuruhusu jumuiya za vijijini na wamiliki binafsi wa ardhi kusimamiawanyamapori katika ardhi zao kwa faida yao wenyewe.

Mikakati ya kuhakikisha kuwa hifadhi ya wanyamapori inashindanana aina nyingine za matumizi ya ardhi(i) kushirikisha jumuiya za vijijini na wadau wengine katika

usimamizi endelevu wa wanyamapori na rasilimali nyingine zaasili;

(ii) kujumuisha wigo mpana wa shughuli zinazojenga uaminifu kati yamameneja wa maeneo yanayohifadhiwa na jumuiya za vijijini nakuanzisha utambuzi wa faida za moja kwa moja na zisizo za mojakwa moja za wanaymapori na maliasili nyinginezo;

(iii) kutoa ushauri wa kiufundi kwa kamati za maliasili za vijiji nakuwapatia mafunzo askari wa vijiji ili kuhakikisha mpango wahifadhi za kijumuiya unafanikiwa;

(iv) kuhimiza jumuiya za vijijini kuanzisha Maeneo ya Usimamizi waWanyamapori katika makazi asilia muhimu ya wanyamapori, kwalengo la kuhakikisha kwamba wanyamapori wanaweza kushindanana aina nyingine za matumizi ya ardhi yanayoweza kuhatarishawanyamapori na mijongeo yao.

(v) kuwapatia watu wenye hatimiliki za ardhi haki za kuwatumiawanayamapori ili kuziwezesha jumuiya za vijijini na wamilikiardhi binafsi kusimamia wanyamapori;

(vi) kuwasaidia wenye ranchi za wanyamapori na wakulima kuwa nahaki za faida na motisha zilezile kutoka serikalini kama ilivyo kwasekta ya kilimo na tasnia ya ufugaji wanyama;

(vii) kujifunza kutoka nchi nyingine za kanda zenye tasnia imara yaranchi za wanyamapori na kilimo;

(viii) kuathiri upitishaji wa sera kwa namna kwamba ardhi za faidandogo kwa maendeleo ya kilimo na ufugaji (maeneo yenyembung'o) zinatengwa kwa hifadhi ya wanyamapori kwa raghba yajumuiya za vijijini kama njia kuu ya matumizi ya ardhi; na

(ix) kuanzisha njia za kuleta utambuzi na welewa wa umma wa hifadhiya wanyamapori.

3.3.5 Matumizi na uchumi wa wanyamaporiTasnia ya wanyamapori ni chanzo kikubwa cha fedha za kigeni na ajira,lakini bado maendeleo yake ni duni ikilinganishwa na upeo wa uwezowake. Zaidi ya hayo, mfumo wa sasa wa matumizi ya wanyampori unahusuzaidi utembeleaji wa mbuga za wanayamapori, uwindaji na ukamataji wawanyamapori, lakini haujakuza kwa mafanikio aina nyingine za matumizikama vile kilimo, ranchi na miradi ya matumizi ya vijiji. Kwa hiyo, mapatoya Tanzania kutoka wanyamapori yamekuwa chini ya kiwango stahifu,ilihali mapato halisi hayagawanywi sawa miongoni mwa wadaumbalimbali.

Sera hii inahimiza utalii wa ndani kwa kuhakikisha kwamba Watanzaniawanaendelea kufaidika vilivyo kutokana na mfumo wa ada/viingilio vyamaeneo yanayohifadhiwa. Kwa msingi huo, sera inasisisitiza juu ya hifadhiya wanyamapori na matumizi endelevu ya wanayamapori kwa faida yawananchi, na juu ya matumizi ya wanyamapori kupunguza njaa kwakuwatumia kutoa chakula na kuzalisha fedha za kigeni.

3.3.6 Kuunganisha hifadhi ya wanyamapori na maendeleo yavijijini

Sera itaendelea kuzipatia jumuiya za vijijini faida ya kiuchumi yawanyamapori ili kuleta maendeleo ya vijijini bila kuhatarisha mazingira, nakwa namna kwamba faida hiyo inafidia gharama za kutumia ardhi husikakama hifadhi ya wanyamapori na si vinginevyo.

Mikakati ya kuunganisha hifadhi ya wanyamapori na maendeleo yavijijini

i) kukuza matumizi halali ya wanyamaporina mazao yanayotokana nao;

ii) kuhimiza biashara halali na endelevu yawanyamapori na mazao yanayotokananao kutoka kwenye Mapori ya Akiba,Mapori Tengefu na nje ya maeneoyanayohifadhiwa, na hivyo kuwapatiawanyamapori thamani kubwa yakibiashara, huku yakizingatiwa matumizi

endelevu ya spishi zinazohusishwa katikabiashara;

iii) kuchukua hatua za mgawanyo sawa wamapato ya uwindaji wa kitalii kwajumuiya za vijijini, ambazo ardhi yaondiyo inayotumiwa na tasnia hii;

iv) kutoa msaada unaohitajika katikakuzipatia jumuiya za vijijini miliki nakuweka viwango vya matumizi yawanayamapori;

v) kuruhusu na kudhibiti biashara yawanyamapori na mazao yanayotokananao;

vi) kuchukua mkabala unaowezakubadilishwa inapobidi wa kukusanyamapato ya mavuno ya mazao asilia yakibiolojia kutoka kwenye hifadhi zawanyama.

vii) kuwalazimisha wafanyabiashara wenyeleseni kuajiri vibarua kutoka kwenyemaeneo ambako shughuli za matumizi yawanyamapori zinafanyika, kwa lengo lakuwapatia wanavijiji ajira na kuinuamapato yao;

viii) kuhimiza shughuli za ufugajiwanyampori kwenye ardhi ya milikibinafsi au iliyokodishwa ili kuendelezaprogramu za uzalishaji kwa ajili yakuyapatia masoko teule nyama na nyara.

ix) kuhimiza sekta binafsi kusaidia katikaulinzi wa wanyamapori na uendelezaji wamaeneo ya wanyamapori.

3.3.7 Kuzalisha fedha za kigeni kutokana na matumizi yawanyamapori

Kuna fursa nyingi za kuwekeza katika sekta ya wanyamapori nchiniTanzania. Maendeleo ya baadaye ya sekta ya wanyamapori yanahitaji

uwekezaji mkubwa, ambao serikali haina uwezo nao. Hivyo, nafasimuhimu ya sekta binafsi katika kuwekeza kwenye maendeleo ya tasnia yawanyamapori inatambuliwa. Kutokana na hali hii, serikali inadhamiria:-(a) uhimiza uwekezaji wa sekta binafsi katika matumizi mbalimbali ya

rasilimali za wanyamapori kulingana na kanuni za hifadhi yawanyamapori, na kwa namna inayowezesha Watanzania kupatafaida ya juu kabisa kutokana na mapato yatokanayo nawanyamapori.

(b) Kufanya kazi na asasi nyinginezo zitakazotoa kiunzi cha jumla chakuwekeza katika tasnia ya wanyamapori.

(c) Kuhakikisha kwamba wawekezaji wanazingatia kanuni za hifadhina wana msingi imara wa kifedha kwa miradi inayopendekezwa.

(d) Kuchochea ukuaji wa tasnia ya wanyamapori kwa kutoa milikikwa nyakati zinazofaa, mazingira mazuri ya kufanya kazi nakutenga maeneo mazuri ya wanyamapori kwa ajili yakuyaendeleza.

(e) Kujenga tasnia ya kitalii ya kimataifa na kitaifa iliyo imara, kwavile utalii nchini Tanzania kwa kiwango kikubwa unategemeakuangalia wanyama katika maeneo yanayohifadhiwa, na kuwindawanyamapori.

(f) Kukuza mfululizo wa shughuli zinazoboresha zaidi tasnia ya utaliiya Tanzania huku ikihakikishwa kuna msingi wa hifadhi yarasilimali ya wanyamapori unaoisaidia tasnia.

Mikakati ya kuzalisha fedha za kigeni(i) kuwashurutisha wale wote wenye uwezo wa kuwekeza katika

sekta ya wanyamapori kusajili makampuni yao nchini Tanzania;(ii) kuruhusu makampuni yaliyosajiliwa kufanya kazi katika tasnia ya

utalii kwa masharti kwamba Wakurugenzi na wafanyakazi wamakampuni hayo, wa ndani na kutoka nje ya Tanzania, wanarekodi safi za utendaji kazi;

(iii) kuhakikisha kwamba ada zinazokubalika zinalipwa na wawekezajiili wapatiwe haki ya kutumia rasilimali za wanyamapori;

(iv) kuhakikisha kwamba thamani ya rasilimali ya wanyamaporihaidunishwi, kwa kuweka bei na ada sahihi za aina mbalimbali zamatumizi ya wanyamapori;

(v) kudhibiti uingiaji na shughuli za wageni (watalii) katika maeneo

yanayodhibitiwa; na(vi) kuuza rasilinali za wanyamapori kulingana na sera ya utalii ya

taifa.

3.3.8 Kutambua thamani halisi ya wanyamapori kwa watu wavijijini

Ni haki ya raia wa Tanzania kuruhusiwa kisheria kutumia wanyamapori.Ingawa tasnia ya uwindaji kwa wananchi katika maeneo yaliyo waziinastawi, sasa inatambulika kuwa utaratibu huu unawanufaisha zaidiWatanzania matajiri waishio mijini na wakazi wasio raia, na kwambamuundo wa sasa wa tasnia unaleta matatizo mengi ya kiusimamizi. Kwaupande mmoja, wanavijiji hawana uwezo wa kulipa ada za leseni walakutumia silaha zao za asili kwa mujibu wa sheria zilizopo. Kwa upandemwingine, Watanzania matajiri wa mijini wanaomba idhini ya kuua kwarisasi wanyama kadhaa kwa bei iliyo ya chini sana ambayo haizipatii faidajumuiya za vijijini zenye ardhi inayotumiwa kwa mawindo yawanyamapori. Uwindaji kwa wakazi wa Tanzania kitaendelea kuwakipengee muhimu cha sera hii.

Mikakati ya kutambua thamani halisi ya wanyamapori kwa jumuiyaza vijijini(i) kufanya kazi kwa kushirikiana na jumuiya za vijijini,(ii) kuhimiza uwindaji wa wenyeji/wakazi ambao utazinufaisha

jumuiya za vijijini katika Maeneo ya Jumuiya ya Usimamizi waWanyamapori (WMA) ambapo uwindaji huo unaendeshwa.;

(iii) kuziruhusu jumuiya za vijijini kuwinda katika Maeneo ya Jumuiyaya Usimamizi wa Wanyamapori chini ya mpango wa UhifadhiUliokitwa katika Jumuiya (CBC) ambao lengo lake ni kukuzamaendeleo ya wanajumuiya wanaoishi miongoni au karibu nawanyamapori;

(iv) kuwezesha uanzishwaji wa programu za CBC katika WMA kwakuzisaidia jumuiya za vijijini kupata hati miliki ya ardhi au haki yakutumia ardhi kwa muda mrefu na kuziwezesha jumuiya hizokutumia wanyamapori na maliasili katika ardhi hiyo;

(v) kuzingatia ipasavyo ukusanyaji wa mazao asilia katika Mapori yaakiba, almradi ukusanyaji huo unafanywa kwa misingi yauendelevu na uharibifu mdogo sana wa mazingira na bila kwenda

kinyume na malengo ya msingi ya usimamizi wa hifadhi zawanyamapori.

(vi) kuanzisha uundaji wa Vyama Vilivyokasimiwa kwa ajili yakusimamizi kiendelevu wanyamaopori nje ya maeneo kitovuyaliyohifadhiwa;

(vii) kuanzisha na kuimarisha uundaji wa Vyama vya Uwakilishi kwaajili ya bidhaa au mazao maalum ya wanyamapori ili kuendelezatasnia ya wanyamapori katika hali ya kutojenga ukiritimba nakusaidia kuhakikisha kuwa kunakuwepo mgawanyo sawa na borawa fursa zilizopo;

(viii) kuinua matumizi ya maarifa ya asili katika hifadhi na usimamiziwa maliasili;

(ix) kuzingatia kipekee njia za jadi za uwindaji zinazotumiwa najumuiya au makabila maalum ya vijijini; na

(x) kukuza biashara ya ndani ya mazao ya wanyamapori ili kuongezathamani ya spishi asilia za wanyamapori kwa Watanzania.

3.3.9 Kugawana manufaaInatafahamika kwamba kuna mlolongo wa manufaa ya moja kwa

moja na yasiyo ya moja kwa moja yanayotokana na wanyamapori, nakwamba mgawanyo wa mapato hayo ni manufaa muhimu. Kuhusiana najambo hili, wadau kadhaa wa uhifadhi wa wnyamapori wanatambuliwakama ifuatavyo:-• jumuiya za vijijini na wadau binafsi, wanaoishi karibu na (au, kwa

upande wa Hifadhi ya Ngorongoro, ndani ya) maeneoyanayodhibitiwa na miongoni mwa wanyamapori nje ya maeneoyanayohifadhiwa;

• halmashauri za wilaya, zinazogharamikia kutokana na kuanzishamaeneo yanayohifadhiwa na kutoa huduma kwa jumuiya zavijijini;

• mamlaka za wanyamapori, zinazosimamia maeneoyanayohifadhiwa na kutoa ushauri wa kiufundi juu yawanyamapori walio nje ya maeneo yanayohifadhiwa;

• serikali kuu, inayogharamika kutokana na kuanzisha maeneoyanayohifadhiwa na kutoa huduma kitaifa; na

• sekta ya binafsi, inayotumia wanyamapori ndani na nje ya maeneoyanayohifadhiwa na inayolipa kodi kwa serikali kutokana na faida

inazozipata.

Sera hii inatumia mgawanyo wiani wa mapato na manufaa kwa wadauunaozingatia wajibu/kazi zao katika kategoria mbalimbali za ardhi, juhudiiliyowekezwa katika kuhifadhi rasilimali, na gharama za kiasasi na zausimamizi.

Mikakati ya kugawana manufaa(i) kuwashirikisha wadau mbalimbali katika kuamua jinsi ya

kugawana mapato na manufaa miongoni mwao; na(ii) serikali kuweka viwango vya mgawanyo wa faida na kuvibadilisha

mara kwa mara.

3.3.10 Kudhibiti na kuendeleza tasnia ya wanyamaporiMtandao wa maeneo yanayohifadhiwa kwa ajili ya uhifadhi wawanyamapori ni msingi wa tasnia ya wanyamapori ya Tanzania, na piasehemu kubwa ya tasnia ya utalii ya Tanzania. Matumizi ya wanyamaporihujumuisha yale yasiyo haribifu, kimsingi utazamaji wa wanyamapori kwawageni wakazi, na matumizi haribifu kama vile uwindaji wa kitalii nawakazi, ukamataji wa wanyama hai; upunguzaji wanyama, uanzishaji waranchi na mashamba ya wanyamapori, uuzaji wa nyara na ulinzi wa maishana mali za binadamu. Shughuli hizi huzalisha mapato kutokana na adazinazolipwa moja kwa moja kwa maeneo yanayohifadhiwa na gharamazinazotozwa na mawakala wa utalii na watoa huduma za kitalii katikamaeneo yanayohifadhiwa. Tasnia ya utalii, ambayo msingi wake unatokanana wanyamapori, inakua vizuri na ni sekta muhimu katika uchumi waTanzania yenye uwezo wa kukua zaidi hapo baadaye. Serikali itahimizauwekezaji binafsi katika aina mbalimbali za matumizi ya wanyamaporikwa namna inayoendana na kanuni za uhifadhi na inayowapatiaWatanzania kiwango cha juu kabisa cha mapato kutokana na wanyamapori.

Mikakati ya kudhibiti na kuendeleza tasnia ya wanyamapori(i) kuamua viwango vinavyokubalika vya watalii watazamaji wa

wanyamapori kulingana na ustahimilivu wa maeneoyanayohifadhiwa;

(ii) kutathmini mtiririko wa watalii ambao hautaleta uharibifu katikaikolojia na ambao unaongeza ubora wa hisia na burudani kwa

mgeni.(iii) kupanua safari za kitalii na kuridhisha watalii;(iv) kushirikiana na sekta husika katika kuboresha mtandao wa

barabara zinazoelekea kwenye vituo vya kitalii na katika maeneoyanayohifadhiwa;

(v) kuwezesha rasilimali ya wanyamapori na maeneoyanayohifadhiwa kuthaminiwa na kutambuliwa zaidi, na kuzuiashughuli za kitalii zinazolenga katika mgeni na mtumiajikusongamana kwenye tukio;

(vi) kuhimiza na kukuza utazamaji wa wanyama ndani ya WMAzinazofaa na ambazo zinaweza kutoa fursa anuwai za barudanikuliko zilizo katika maeneo yanayohifadhiwa.

(vii) kushauri mamlaka za kitalii juu ya viwango vya chini kabisavinavyohitajika kuzingatiwa na mawakala wa utalii wote ambaobiashara yao hutegemea utazamaji wa wanyamapori;

(viii) kutumia mikabala inayoweza kubadilishwa, ambayo kimsingihutegemea faida za kiuchumi zitokanazo na aina mbadala zamatumizi ya wanyamapori;

(ix) kuhimiza utengenezaji viwandani wa bidhaa za wanyamaporitayari kwa kuuza nchini Tanzania na nchi za nje, ili kuongeza ajirana kubakisha nchini Tanzania kiwango kikubwa cha mapatoyatokanayo na mazao ya wanyamapori;

(x) kutaka kuboresha ushiriki katika tasnia ya uwindaji wa kitaliikupitia:-

• mgawanyo wa wazi na wa haki wa maeneo ya kuwindiakwa kutumia mfumo unaokubalika na wadau wengi bilakuhatarisha faida za kiuchumi za muda mrefu za uwindajiwa kitalii kwa Tanzania;

• kutumia muundo wa ada uliobuniwa na kuidhinishwa namamlaka ya wanyamapori inayohusika;

• kutenga viwango endelevu vya kota ya uwindaji kwamisingi ya kisayansi na kufuatilia wingi wa wanyamaporiwanaowindwa;

• kuwapatia mitihani wawindaji weledi na kufuatilia uwezowao katika uwindaji;

• kusimamia utekelezaji wa kanuni za uwindaji ilikuhakikisha unakuwepo ubora wa juu wa uwindaji na wanyara;

• kuwezesha nyara kusafirishwa kwa wakati, kwendakwenye nchi wanakotoka wawindaji; na

• kuweka mazingira yanayowezesha ukuzaji wawindajiweledi raia.

(xi) kuruhusu uvunaji wa wanyamapori kwa viwango vidogo ufanywena jumuiya za vijijini zinazoendesha uhifadhi uliokitwa katikajumuiya, wenye mashamba wanaotumia ardhi zao binafsi auzilizokodishwa; na

(xii) kuweka udhibiti katika shughuli za utumiaji wa wanyamapori.

3.3.11 Kushughulikia masuala ya wanawake na watoto katikauhifadhi na usimamizi wa wanyamapori

Kijadi, wanawake na watoto wamehusika moja kwa moja katika usimamiziwa rasilimali za wanyamapori kwa njia zifuatazo:

a)ukusanyaji wa kuni; katika baadhi ya maeneo wanawakehutembea umbali usiopungua kilometa 10 wakitafuta kuni,

b)ukusanyaji wa matunda mwitu na mazao ya chakula,c)uvuvi, uwindaji wa wanyama wadogowadogo na ndege kwa

ajili ya chakula; kazi hii hufanywa hasa na watoto,d)ukusanyaji wa miti ya kujengea, nyasi za kuezekea na

mitishamba,e)ukusanyaji wa dawa za kienyeji,f) kusafisha ardhi kwa ajili ya kilimo kupitia kilimo cha

kuhamahama na ufugaji, nag)kuchoma mioto mikali ovyo wa kilimo na uwindaji.

Kuna mgawanyo bayana wa kazi baina ya wanaume, wanawake na watotokatika jamii ya Kitanzania inayoishi vijijini. Kwa kiwango kikubwauwindaji hufanywa na wanaume, ilhali wanawake na watoto ndiyowanaotoa kiwango kikubwa zaidi cha nguvukazi ya kilimo. Ardhihumilikiwa na wanaume na uamuzi wa wapi, nini kilimwe, na matumizi yamazao hufanywa na wanaume. Kimsingi, wanawake na watoto ndicho

chanzo cha nguvukazi katika jumuiya za vijijini.

Hali hii inaonyesha kwamba wanawake na watoto wanaingiliana zaidi namaliasili na mazingira na, hivyo, wana umuhimu mkubwa sana katikahifadhi ya maliasili na mazingira hayo.

Wanawake vijijini hufanya kazi kwa vipindi virefu sana wakijitahidikutekeleza kazi tulizozielezea hapo juu. Wao, pamoja na watoto, huundakundi linalofaidika kidogo sana kwa upande wa burudani na elimu. Hawahushambuliwa na magonjwa kwa urahisi kutokana na lishe na huduma zauzazi duni, kukosekana kwa huduma za afya, na umri mdogo mno wakufanyishwa kazi.

Sera hii inatambua nafasi ya wanawake na watoto katika kuhifadhimaliasili na haja ya wao kushiriki na kufaidika kutokana na uhifadhi warasilimali hizo.

Mikakati ya kushughulikia Masuala ya Wanawake na Watoto (i) kuanzisha na kusaidia miradi ya wanawake ya kujisaidia wenyewe

ili kuongeza kipato chao;(ii) kuwahimiza wanawake kujishughulisha na miradi yenye kuhusiana

na uhifadhi wa maliasili ambayo inaboresha kiwango cha lishe nakuchangia kwenye mapato ya familia;

(iii) kuwahimiza na kuwasaidia wanaume na wanawake kushughulikiaile miradi ambayo inapunguza uzito wa kazi kwa wanawake nawatoto;

(iv) kusaidia matunzo ya mama na mtoto katika vijiji vinavyozungukamaeneo yaliyohifadhiwa;

(v) kusaidia na kukuza juhudi za kutoa elimu kwa watoto(vi) kuboresha namna ambayo wanawake wanaweza kupata mazao ya

maliasili katika maeneo yaliyohifadhiwa pale inapostahili; na(vii) kukuza mwamko kuhusu uhifadhi.

3.3.12 Kutatua migogoro baina ya binadamu na wanyamapori:-Kuna haja ya kuwadhibiti wanyamapori ambao wanahatarisha maisha yabinadamu na mali zao. Serikali inapenda kuvuta nadhari kuhusu thamani yakiuchumi ya wanyamapori kwa jumuiya za vijijini kwa kupitia uendeshaji

wa Uhifadhi Uliokitwa Katika Jumuiya. Katika kutekeleza sera hii, serikaliinachukulia kwamba jumuiya za vijijini zinazosimamia wanyamaporizitatambua migogoro iliyopo baina ya lengo la kupata faida kubwa kabisakutokana wanyamapori na tija pungufu ambayo inaweza kutokea kutokanana udhibiti mkali wa wanyama waharibifu. Hivyo serikali hainuiikuanzisha mpango wa fidia kwa ajili ya uharibifu unaofanywa nawanyamapori.

Mikakati ya kutatua migogoro baina ya binadamu na wanyamapori:-(i) kuendelea kuwadhibiti wanyama hatari kama kipaumbele, na(ii) kukabidhi hatua kwa hatua majukumu ya tatizo la udhibiti wa

wanyama kwa jumuiya za vijijini zinazoendesha mipango yauhifadhi uliokitwa katika jumuiya, na kuendelea kutoa msaadapale ambapo jumuiya hizo hazijapata uwezo huo.

Mikakati mibadala:Baada ya muda, mikakati mibadala ya kupunguza mgogoro baina ya watuna wanyamapori itachunguzwa. Mikakati inayowezekana ni pamoja na:• kujumuisha idadi ya wanyama wanaopigwa risasi wakati wa

udhibiti wa wanyama hatari katika migao ya uwindaji inayowezakuleta manufaa makubwa ya kiuchumi kwa jumuiya za vijijini;

• kuhakikisha kwamba wale wanaoathiriwa zaidi na wanyamawaharibifu ndio wanufaikaji wakuu wa mapato kutokana nawanyamapori;

• kupembua matumizi ya mbinu za udhibiti zinazotegemea vizuizivya mitambo na umeme ambavyo haviui;

• pale inapowezekana, kuwakamata na kuwahamisha wanyamaporiwenye thamani kubwa kibiashara; na

• kutangaza thamani ya kiuchumi ya wanyamapori, hususanikwenye zile jumuiya za vijijini zinazoendesha mipango yauhifadhi uliokitwa katika jumuiya.

3.3.13 Utafiti na Ufuatiliaji wa wanyamaporiUtafiti na Ufuatiliaji wa mabadiliko katika rasilimali ya wanyamapori namatumizi yake unabakia kuwa sehemu kamili ya mipango na usimamizi wawanyamapori. Hadi sasa ni utafiti mdogo sana umekwishajumuishwakatika mipango ya usimamizi kutokana na kutokuwepo kwa mawasiliano

baina ya watafiti na wasimamizi wa wanyamapori. Serikali inatambuakwamba kuna watafiti wa kisayansi wachache wa Kitanzania na kwambamotisha yao iko chini sana kuweza kufanya utafiti unaohitajika. Hivyo,serikali ingependa kuingiza katika mipango yake uwezo madhubuti wautafiti na ufuatiliaji ndani ya mamlaka za wanyamapori.

Mikakati kwa ajili ya utafiti na ufuatiliaji wa wanyamapori:-(i) kudhibiti na kufuatilia utafiti wa wanyamapori nchini Tanzania,(ii) kuimarisha uwezo wa mamlaka za wanyamapori katika utafiti na

ufuatiliaji,(iii) kuwezesha kufanyika kwa sensa za mara kwa mara kuhusu idadi

ya wanyamapori,(iv) kuelekeza utafiti na ufuatiliaji kwenye viwango na uchumi

kutokana na matumizi ya wanyamapori, mahusiano baina yabinadamu na wanyamapori, elimu jamii ya jumuiya za vijijinizinazozunguka maeneo ya wanyamapori, maarifa ya msingi yataratibu za mfumo wa ikolojia na elimu viumbe vya aina zawanyama ambazo kudumu kwake kunatishiwa,

(v) kukarabati na kutumia kikamilifu mtandao uliopo wa vituo vyautafiti wa uwandani nchini kote,

(vi) kusisitiza utafiti na ufuatiliaji katika upangaji mipango yausimamizi wa Maeneo yaliyohifadhiwa kulingana na miongozo yakitaifa ya utafiti wa wanyamapori,

(vii) kuwaruhusu wachunguzi wa kigeni kufanya utafiti wa mada zaaula maalumu, na

(viii) kuwahimiza na kuwamotisha wachunguzi wa Kitanzania kufanyautafiti wa wanyamapori.

3.3.14 Kutoa Huduma tanzuHuduma tanzu na ujirani mwema baina ya usimamizi wa maeneoyaliyohifadhiwa na jumuiya za vijijini vinaruhusu kubainisha matatizoyanayohusiana na wanyamapori na kuongeza nafasi ya kutatuliwa kwakekwa manufaa ya pande zote. Zaidi ya hayo, kazi tanzu ni ya umuhimumkubwa katika kutoa msaada wa kiufundi kwa ajili ya uanzishaji WMAs.Kwa hivyo, serikali imeamua kukuza huduma tanzu ambazo ni kiungo katiya mamlaka za wanyamapori na jumuiya za vijijini nje ya maeneoyaliyohifadhiwa na katika Hifadhi ya Ngorongoro, jumuiya za vijijini za

ndani ya hifadhi hiyo.

Mikakati ya kutoa huduma tanzu(i) kujumuisha huduma tanzu katika mipango na kuzisaidia kwa

kuzipa wafanyakazi, fedha na vifaa vya kutosha; na (ii) kukuza mawasiliano na ushirikiano na huduma tanzu nyingine za

kisekta vijijini.3.3.15 Elimu ya uhamasishaji kuhusu uhifadhi wa wanyamaporiMafanikio ya muda mrefu ya uhifadhi wa wanyamapori yanategemea, kwakiasi kukubwa, jinsi uhifadhi huo unavyotazamwa na jamii. Serikaliimeamua kuweka juhudi maalumu katika kuinua mwamko kuhusu uhifadhimiongoni mwa watu wa Tanzania.

Mikakati kwa ajili ya elimu ya uhamasishaji kuhusu uhifadhi wawanyamapori(i) kuunda uelewa mpana iwezekanavyo na msaada kwa ajili ya uhifadhi

wa wanyamapori kwa kuandaa na kusambaza mabango, magazeti navipeperushi yaliyoandikwa kwa Kiingereza na Kiswahili na kutumiavyombo vingine vya habari; na

(ii) kushirikiana na sekta inayosimamia elimu na kuendelea kukuzaujumuishaji wa elimu ya uhifadhi katika muhtasari wa shule iliuhifadhi wa wanyamapori upate msingi mpana wa kuungwa mkonomiongoni mwa vizazi vijavyo.

3.3.16 Uendelezaji wa wafanyakazi na kujenga uwezoMaendeleo na utendaji endelevu katika sekta ya wanyamapori, kwa kiasikikubwa, vinategemea uendelezaji na matumizi bora ya wafanyakazi. Ilikudumisha sekta ya wanyamapori, serikali imeamua kutoa mafunzoyanayofaa katika ngazi zote, mazingira mazuri ya kazi na nyenzo bora naza kutosha kufanyia kazi.

Mikakati kwa ajili ya uendelezaji wa wafanyakazi na kujenga uwezo.(i) kuhimiza na kuwezesha mafunzo katika ikolojia na usimamzi wa

wanyamapori na stadi nyingine zinazohitajika kwa ajili yamaendeleo ya sekta ya wanyamapori;

(ii) kufuatilia viwango vya mafunzo katika asasi za mafunzo yawanyamapori nchini;

(iii) kudumisha kuwepo kwa wafanyakazi wa kutosha na wenye sifabora;

(iv) kupata teknolojia zinazofaa;(v) kuhimiza uanzishwaji wa asasi za mafunzo katika usimamizi na

uhifadhi wa wanyamapori katika ngazi zote za stadi;(vi) kuhimiza, kumotisha na kuwezesha wawekezaji wa kigeni katika

sekta ya wanyamapori kuwapa Watanzania mafunzo katika staditofauti;

(vii) kuhakikisha kwamba wafanyakazi wa sekta ya wanyamaporiwanapewa stadi mpya za kuendana na hali mpya;

(viii) kubuni mipango na vigezo kwa ajili ya kuendeleza wafanyakazi;(ix) kukuza mgao bora na upangaji wa wataalamu, mafundi na

wafanyakazi wa kawaida katika nafasi zinazostahiki katika sektaya wanyamapori; na

(x) kuwamotisha wafanyakazi wa sekta ya wanyamapori wanaolindana kuhifadhi rasilimali ya wanyamapori kwa kuboresha mashartiya kazi, malipo, utoaji wa vifaa vya kutosha vya kufanyia kazi namotisha za kutosha.

3.4 Kiunzi cha Utekelezaji wa SeraKatika muktadha wa sera hii wanyamapori wanafafanuliwa kama: - “ainazile za wanyama wa porini na wa asili na makazi na mifumo ya ikolojiayao, zinazopatikana Tanzania na vilevile aina zile ambazo zimeingizwaTanzania na ambazo, kwa muda, hufungiwa mahali au huachiwa kuishiporini”. Ufafanuzi huu unajumuisha wanyama wasouti wa mgongo wa nchikavu ambao hawakuhusishwa katika ufafanuzi uliopita katika Sheria yaUhifadhi wa Wanyamapori Na. 12 ya mwaka 1974.

Ufafanuzi huu wa sasa unaweka msisitizo mkubwa kwenye mfumo waikolojia unaofanya iwezekane kuhifadhi aina nyingi za wanyama wadogowadogo na mimea nadra inayounda Uanuwai wa pekee na muhimu waviumbe wa nchini kote Tanzania. Serikali inatambua kwamba ufafanuzi wawanyamapori uliokubalika katika sera hii hauwezi kutumika kote Tanzaniakutokana na majukumu ya sekta nyingine ya usimamizi wa maeneo fulaniya nchi au ya aina fulani maalumu za wanyama na mimea ndani yaufafanuzi wa utendaji wa wanyamapori. Hali maalumu ambamo ufafunuziuliotolewa juu unaweza kutofautiana, ziko katika sekta za Uvuvi na Misitu.

Mamlaka za wanyamapori zitabakia na jukumu la jumla la usimamizi waaina zote za wanyama wanyonyeshao wa nchi kavu, ndege, wanyamawatambaao (reptilia) na wanyama wanaoweza kuishi majini na nchi kavu(amfibia) na wanyama wasouti wa mgongo pale wanapotokea kuwepo njeya maeneo yaliyohifadhiwa yaliyoachwa maalumu kwa uhifadhi wawanyamapori na misitu na aina za wanyama waishio majini ambaohawahusishwi na sheria za uvuvi.

Kwa kuwa Sekta ya Wanyamapori ya Tanzania ina asasi kadhaazinazohusika na uhifadhi wa wanyamapori, sera hii inatambua majukumuya asasi hizi katika utekelezaji wa sera. Hata hivyo, majukumu ya jumla yautendaji na usimamzi ya sekta ya wanyamapori, ya maeneoyaliyohifadhiwa kwa ajili ya uhifadhi wa wanyamapori na ya wanyamaporinje ya maeneo yaliyohifadhiwa, yatakabidhiwa kwa Kurugenzi yaWanyamapori katika wizara inayosimamia sekta ya wanyamapori. Katikautekelezaji wa Sera ya Wanyamapori, huwa inaingiliana na sera nyingineza kisekta kama vile, utalii, kilimo, maji, madini na mazingira. Sera hiiinatambua dhima ya sera nyingine za kisekta katika utekelezaji wake.

3.4.1 Mikakati kwa ajili ya utawala wa Wanyamapori(i) kupitia sheria zilizopo za uhifadhi wa wanyamapori (k.v Sheria ya

Uhifadhi wa Wanayamapori Na 12 ya mwaka 1974, Sheria yaHifadhi ya Ngorongoro Kifungu cha 413 ya mwaka 1959, Sheriaya TANAPA kifungu cha 412 ya mwaka 1959 na Sheria ya Taasisiya Utafiti wa Wanyamapori Serengeti ya mwaka 1980) ili kuipatianafasi mikakati ya uhifadhi iliyopendekezwa katika sera hiiambayo inajumuisha usimamizi na uendelezaji wa maeneo yaardhioevu , ushiriki wa jumuiya katika uhifadhi wa wanyamapori,uanzishwaji wa maeneo ya jumuiya ya usimamizi wawanyamapori, migao ya manufaa na haki za kuwatumiawanyamapori kwa ajili ya jumuiya;

(ii) kusimamia aina mahsusi ya maeneo yaliyohifadhiwa na sehemumahsusi za sekta ya wanyamapori kwa kupitia asasi zinazohusikandani ya sekta;

(iii) kusimamia wanyama wenye uti wa mgongo na wasiouti wamgongo katika Hifadhi za Misitu kwa kupitia Kurugenzi yaWanyamapori;

(iv) kukabidhi majukumu yote juu ya ndege wa majini kwa Kurugenziya Wanaymapori;

(v) kubakia na majukumu yote ya usimamizi wa aina zote za wanyamawanyonyeshao wa nchi kavu, ndege, reptilia na amfibia nawanyama wasouti wa mgongo kama zipo nje ya maeneoyaliyohifadhiwa maalumu kwa ajili ya uhifadhi wa wanyamaporina misitu na za aina za majini zisizojumuishwa na sheria ya uvuvi;na

(vi) kuendelea kutoa vibali vyote vinavyotakiwa kisheria vya shughulizinazohusiana na wanyamapori na vya kusimamia upatikanaji,matumizi na biashara katika rasilimali ya wanyamapori.

3.4.2 Mikakati kwa ajili ya Uhifadhi na Usimamizi wa MaeneoYaliyohifadhiwa(i) kuanzisha kategoria mpya ya maeneo yanayohifadhiwa (Maeneo

ya Jumuiya ya Usimamizi wa Wanyamapori - WMA) kwamalengo ya kutekeleza Uhifadhi Uliokitwa katika Jumuiya (CBC),

(ii) kuendelea kusimamia Hifadhi za Taifa kupitia sheria za Hifadhi zaTaifa,

(iii) kuendelea kusimamia Hifadhi ya Ngorongoro kupitia sheria yaHifadhi ya Ngorongoro,

(iv) kuendelea kusimamia Mapori ya Akiba na Mapori Tengefu kupitiasheria ya Uhifadhi wa Wanayamapori, na kupitia upya hadhi nakazi za Mapori Tengefu ili kutekeleza Uhifadhi uliokitwa katikajumuiya,

(v) kuendelea kuwa na Hifadhi za Wanyama za Muda ili kuwezeshamalengo yake kwa kuunda kategoria ya Aina Zinazolindwa,

(vi) kuendelea kusimamia Hifadhi za Misitu kupitia Sheria ya Misituna kudhibiti sehemu za ufafanuzi unaotumika wa wanyamaporibadala ya mazao ya misitu yanapotokea kuwa katika Hifadhi zamisitu kupitia Sheria ya Wanyamapori,

(vii) kuwa na mikataba ya maelewano na sekta zinazohusika yausimamizi wa maeneo yenye umuhimu mkubwa kibiolojia nakiuchumi ili kuhakikisha usimamizi makini wa wanyamaporikatika Hifadhi za Misitu, maeneo yaliyohifadhiwa yawanyamapori na maeneo nje ya uwezo wa mamlaka zawanyamapori, na

(viiii) kutoa katika gazeti la serikali, Maeneo mapya yaliyohifadhiwa auyaliyopandishwa daraja kwa makubaliano ya pamoja baina yawilaya, mikoa na idara ya serikali kuu yenye majukumu yote yakisekta.

3.4.3 Mikakati kwa ajili ya uhifadhi wa wanyamapori nje ya Maeneoyaliyohifadhiwa yasiyokaliwa na katika Hifadhi ya Ngorongoro(i) kuanzisha Maeneo ya jumuiya ya Usimamizi wa Wanyama ili

kuwezesha Uhifahdi Uliokitwa katika jumuiya;(ii) kuwatumia wanyamapori katika maeneo ya usimamizi wa

wanyama kulingana na sheria zinazoongoza uhifadhi wawanyamapori Tanzania Bara;

(iii) kubakia na majukumu yote ya kuhakikisha uratibu wa aula zote zakitaifa za uhifadhi wa wanyamapori nje ya maeneoyaliyohifadhiwa yasiyokaliwa na katika Hifadhi ya Ngorongoro;

(iv) kuboresha uratibu baina ya sekta na ushirikiano katika kulindamaslahi ya hifadhi wa wanyamapori;

(v) kuwasimamia wanyamapori nje ya Maeneo yaliyohifadhiwayasiyokaliwa na katika Hifadhi ya Ngorongoro kwa kuheshimusheria nyingine zinazohusika kama vile sheria ya serikali za mitaa,sheria ya mamlaka za mijini na sheria ya uchimbaji wa madini.

3.4.4 Mikakati kwa ajili ya biashara katika mazao ya wanyamapori(i) kusimamia biashara za mazao ya wanyamapori yanayotokana na

aina mbalimbali za matumizi, vifo vya asili na upokonyaji;(ii) kubakia na mamlaka ya biashara ya ndani katika mazao

yaliyozalishwa chini ya mamlaka ya sekta nyingine kama vilemisitu, uvuvi chini yake;

(iii) kusimamia biashara ya nje katika wanyamapori na mazao yakekulingana na sheria za Tanzania zinazohusika na sheria zakimataifa; na

(iv) kuchukua hatua muafaka za kuhakikisha kwamba usafirishaji waaina au sehemu zilizoko katika Makubaliano ya Kimataifa yaBiashara katika aina zilizoko hatarini za mimea na wanyama(CITES) kutokana na sekta za misitu na uvuvi zinasadifu mahitajiya kanuni za makubaliano hayo.

3.4.5 Mikakati kwa ajili ya uhifadhi na usimamzi wa aina za viumbe.(i) kuandaa mpango ya usimamizi pamoja na wadau wengine kwa

ajili ya baadhi ya aina au makundi yenye tatizo fulani maalumu ilikuhakikisha yanaendelea kuwepo;

(ii) kurekebisha orodha ya aina zilizobainishwa kama wanyama waTaifa kwa kushirikiana na sekta zinazohusika kwa ajili yakujumuishwa katika kundi jipya la Aina Zinazolindwa ambayo nipamoja na wanyama wowote wasouti wa mgongo na mimeayoyote.

3.4.6 Mikakati kwa ajili ya utafiti na ufuatiliaji wa wanyamapori.(i) kuweka mikataba ya maelewano na wabia kuhusu mpango wowote

wa utafiti wa pamoja,(ii) kupitia upya na kusimamia aula za utafiti na mipango kupitia

Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania, na(iii) kuongoza na kuratibu utafiti wa wanyamapori kupitia sheria ya

Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania.

Mikakati kwa ajili ya Misaada na Majukumu ya Kimataifa, Kieneo naKitaifa(i) kuitisha mikutano ya mara kwa mara na wahisani kujadili aula za

uhifadhi na kuratibu mipango ya utekelezaji;(ii) kuwa na uangalifu wakati wa kushughulika na wasiohusika katika

mikataba ya kimataifa ambayo Tanzania imeingia na katikakutimiza wajibu kama mshiriki.

(iii) kuamua kikamilifu kushiriki katika dhima ya kimataifa na kieneoili kuhakikisha kwamba uhifadhi makini wa wanyamaporiunafanikishwa ndani na nje ya Tanzania;

(iv) kukaribisha msaada wa uhifadhi wa wanyamapori kutoka jumuiyaza Kimataifa, Kieneo na Kitanzania na kushirikiana na kundilolote linalopendelea kuhifadhi wanyamapori bila kupoteza uhuruna maslahi ya msingi kwa ajili ya msaada na ushirikiano; na

(v) kushirikiana na nchi jirani katika uhifadhi na usimamizi wa aina zawanyama zivukazo mipaka na mifumo ya ikolojia.

4.0 DHIMA ZA ASASI TOFAUTIDhima ya serikali katika sekta ya wanyamapori ni kutoa miongozo ya wazi

ya kisera, kuchochea na kukuza ushiriki wa wadau mbalimbali, kuendeshamaeneo muhimu ya wanyamapori yanayolindwa, kuendelea kumilikirasilimali za wanyamapori na kuhakikisha maendeleo ya jumla ya sekta.Serikali haitajihusisha na biashara ya bidhaa za wanyamapori, badala yake,itaweka juhudi zake katika kuiongoza sekta, kuiwezesha na kuwa mtoahuduma. Dhima ya sekta binafsi na Mashirika yasiyokuwa ya kiserikaliitakuwa ni kuunga mkono Serikali katika juhudi zake.

4.1 DHIMA YA SERIKALI4.1.1 Serikali kama Msimamizi/mdhibiti(i) Kusimamia sheria na kanuni za wanyamapori(ii) Kufuatilia sera makini za kiuchumi na za usimamizi wa

wanyamapori ambazo ni kichocheo kwa vitegauchumi vya watubinafsi na jumuiya za mahali hapo.

(iii) Kutoa na kuendesha aina zote za haki za matumizi ya rasilimali yawanyamapori na leseni za biashara na vibali.

(iv) Kubuni mipango ya usimamizi kwa ajili ya maeneo yanayolindwaya wanyamapori.

(v) Kukusanya mirabaha, ada na malipo ya vibali yanayotokana nausimamizi na maendeleo ya wanyamapori.

4.1.2 Serikali kama mwezeshaji(i) Kuratibu shughuli za tasnia ya wanyamapori.(ii) Kuhakikisha utaalamu na stadi zinazofaa za usimamizi wa

wanyamapori.

4.1.3 Serikali kama mtoa huduma(i) Kuwadhibiti wanyama waharibifu kote nchini.(ii) Kuhakikisha kupatikana kwa elimu ya uhifadhi kwa jumuiya za

vijijini na umma kwa jumla.(iii) Kuanzisha huduma tanzu katika jumuiya za vijijini.

4.2 DHIMA YA SEKTA BINAFSIDhima ya sekta binafsi ni kuiunga mkono serikali katika uhifadhi nausimamizi wa rasilimali ya wanyamapori. Zaidi ya hayo, sekta binafsiinahimizwa kuwekeza katika tasnia ya wanyamapori.

4.3 DHIMA YA MASHIRIKA YASIYOKUWA YAKISERIKALI

Dhima ya Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali ya nchini na ya Kimataifa nikuisaidia serikali kifedha na kiufundi katika ngazi zote, katika uhifadhi nausimamizi wa rasilimali ya wanyamapori.

4.4 DHIMA YA UMMADhima ya Umma ni kuunga mkono juhudi za serikali katika uhifadhi nausimamizi wa rasilimali ya wanyamapori. Zaidi ya hayo, umma una dhimaya kutumia rasilimali ya wanyamapori kwa uendelevu. Aidha, jumuiyazinazoishi jirani na maeneo yaliyohifadhiwa au katika maeneo yenye idadiya kutosha ya wanyamapori zina dhima ya kusimamia na kunufaika nawanyamapori walioko kwenye ardhi zao kwa kuunda Maeneo ya jumuiyaya Usimamizi wa wanyamapori.

5.0 HITIMISHOTanzania imefaulu katika kuanzisha mtandao wa maeneo yaliyohifadhiwaambao ni msingi wa kuhifadhi uanuwai wa viumbe nchini na kwa ukuajiwa tasnia yake ya wanyamapori. Mtazamo wa muda mrefu wa uhifadhi wawanyamapori ni kudumisha uanuwai mkubwa wa viumbe ambaounachangia katika mazingira bora na kuongeza mchango wake kwenye

uchumi wa taifa kutoka kiwango cha sasa cha asilimia 2 hadi kiwango chaasilimia 5 cha Pato la Taifa kufikia mwaka 2017.

Ili kufikia lengo hili, sekta ya wanyamapori inaweka mkazo kwenyekudumisha na kuendeleza mtandao wa Maeneo yaliyohifadhiwa yawanyamapori na kuwahusisha Wadau wote katika uhifadhi na usimamiziwa rasilimali hii, hususani jumuiya za mahali husika, na sekta binafsi.Dhima ya serikali inaelekezwa katika kusimamia, kuwezesha na kukuzamatumizi endelevu ya rasilimali ya wanyamapori. Serikali pia inakuwamtoa huduma hasa kuhusiana na wanyama waharibifu na huduma tanzukwa jumuiya za vijijini

Aidha, Serikali itawezesha uanzishwaji wa kategoria mpya ya maeneoyaliyohifadhiwa linalojulikana kama Maeneo ya jumuiya ya Usimamizi waWanyamapori ambako watu wa mahali hapo watakuwa na mamlakakamiliki kusimamia na kunufaika kutokana na juhudi zao za uhifadhikupitia mipango ya uhifadhi uliokitwa katika jumuiya. Sekta binafsiitahimizwa kuwekeza katika tasnia ya wanyamapori ikifaidi hali iliyopo yautulivu wa kisiasa na sera bora za kiuchumi.

Serikali imeweka taratibu dhahiri, za wazi na nyepesi za ushiriki katikatasnia ya utalii inayotegemea wanyamapori na za uwekezaji katikashughuli zinazohusiana na wanyamapori. Katika kulinda matumiziendelevu ya rasilimali ya wanyamapori; serikali itaimarisha uwezo wakusimamia sheria.Katika kutimiza wajibu wake, serikali itaendelea kuendesha mtandaouliopo wa maeneo yaliyohifadhiwa kwa kupitia asasi zilizoteuliwa zawanyamapori ambazo kazi zake zinatofautishwa kwa lengo la kuhifadhimaeneo yaliyohifadhiwa yanayohusika.

Ili kufuatilia rasilimali ya wanyamapori kwa makini, Serikali itaingizakatika mipango yake utafiti na usimamizi wa taarifa, huduma tanzu nashughuli za elimu ya uhifadhi.Serikali itashirikiana na nchi jirani katika kuhifadhi aina za wanyamawahamao na mifumo ya ikolojia inayovuka mipaka na itakuza nakukaribisha msaada wa uhifadhi wa wanyamapori kutoka jumuiya zakimataifa, za kieneo na za Kitanzania na kushirikiana na kundi lolote

linalopendelea uhifadhi wa wanyamapori.

VIAMBATANISHO

KIAMBATANISHO 1: VIFUPISHO

Vifuatavyo ni vifupisho vilivyotumiwa katika matini ya Kiingereza, maanazake na tafsiri zake kwa Kiswahili:

CAWM, College of African WildlifeManagement, Mweka

Chuo cha Usimamiziwa Wanyamapori waKiafrika, Mweka

CBC, Community BasedConservation

Uhifadhi Uliokitwakatika Jumuiya

CITES, Convention of InternationalTrade in Endengered Speciesof Wild Fauna na Flora

Mkataba wa Biasharaya Kimataifa katikaAina za Wanyama naMimea Pori zilizokohatarini kwisha

COSTEC, Commission for Science andTechnology

Tume ya Sayansi naTeknolojia

DW, Director of wildlife Mkurugenzi waWanyamapori

EIA, Environmental ImpactAssessment

Tathmini ya Atharikatika Mazingira

FR(s), Forest Reserve(s) Hifadhi ya/za Misitu

GCA(s), Game Controlled Area(s) Mapori Tengefu yaWanyamapori

GMP(s), General Management Plan(s) Mipango ya Jumla yaUsimamizi

GR(s), Games Reserves Mapori ya Akiba

MOU(s), Memoranda ofUnderstanding

Makubaliano(Maelewano)

NCA, Ngorongo Conservation Area Hifadhi ya Ngorongoro

NCAA, Ngorongoro conservationarea Aulthority

Mamlaka ya Hifadhiya Ngorongoro

NGO(s) Non-GovenmentalOrganisation(s)

Mashirika yasiyokuwaya Kiserikali

NP(s), National Park(s) Hifadhi/Mbuga zaTaifa

PA(s), Protected Area(s) MaeneoYaliyohifadhiwakisheria

PGR(s), Partial Game Reserve(s) Hifadhi za Wanyamaza Muda

SADC, Southern AfricanDevelopment Co-ordination

Uratibu wa MaendeleoKusini mwa Afrika

SUA, Sokoine University ofAgriculture

Chuo Kikuu chaKilimo cha Sokoine

SWRI, Serengeti Wildlife ResearchInstitute

Taasisi ya Utafiti waWanyamaporiSerengeti

TANAPA, Tanzania National Parks Hifadhi za TaifaTanzania

TAWICO, Tanzania WildlifeCorporation

Shirika laWanayamaporiTanzania

TWPF, Tanzania Wildlife ProtectionFund

Mfuko wa KulindaWanyamaporiTanzania

WD, Wildlife Division Divisheni yaWanyamapori

WMA(s), Wildlife Management Area(s)

Maeneo ya jumuiya yaUsimamizi waWanyamapori

KIAMBATANISHO 2: MSAMIATI

Vyama vilivyopewa Mamlaka maana yake ni vijiji, makundi binafsi naMashirika yaliyoteuliwa yaliyopewa mamlaka ya kusimamia wanyamaporinje ya Hifadhi za Taifa, Hifadhi ya Ngorongoro na Mapori ya Akiba.

Uhifadhi Uliokitwa katika Jumuiya ina maana ya uhifadhi wa rasilimaliuliokitwa katika ushiriki wa jumuiya za mahali husika.

Makubaliano ina maana ya maafikiano baina ya kundi la watu, shirika,shirika la umma au mtu na Mamlaka ya Wanyamapori au ChamaKilichopewa Mamlaka kutumia sehemu ya ardhi kwa kipindi kifupi(kisichozidi miaka kumi) kwa madhumuni ya Uhifadhi.

Upunguzo katika muktadha wa uhifadhi wa wanyamapori ina maana yakuwawinda na kuwatumia wanyama wanaorandaranda kwa kipindi kifupikwa ajili ya mazao mbalimbali ikiwa ni pamoja na nyama na nyaranyingine.

Ushoroba ina maana ya maeneo yanayotumiwa na wanyama wakati wakuhama kutoka sehemu moja ya mfumo wa ikolojia kwenda nyingine kilasiku, kwa wiki, kwa mwezi, kwa mwaka katika kutafuta mahitaji ya msingikama vile maji, chakula, nafasi na makazi.

Uhifadhi ina maana ya tendo la kulinda na kudumisha matumizi yabioanuwai; katika muktadha huu maliasili ya wanyamapori.

Maeneo ya Mtawanyiko ina maana ya maeneo jirani na/au yanayozungukamaeneo yaliyohifadhiwa ambamo wanyama wa porini hujongea katikabaadhi ya vipindi kutoka maeneo yaliyohifadhiwa. Mkurugenzi wa Wanayamapori ina maana ya mkuu wa wanyamapori(sehemu, mtengo, idara) katika wizara inayohusika na wanyamapori katikaSerikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

Ufugaji ina maana ya kulea sampuli, kutokana na wanyamapori iliyokomaainayoishi katika mazingira asilia kwa madhumuni ya kujihusisha katika

namna tofauti ya matumizi ya wanyamapori

Sheria ya Uhifadhi wa Wanyama ina maana Sheria ya Uhifadhi waWanyama sura ya 302 ya sheria (iliyofutwa na Sheria ya Uhifadhi waWanayamapori Na 12 ya mwaka 1974)

Mpango wa Usimamizi wa Jumla ina maana ya chombo cha kuongozamipango ya usimamizi na maendeleo ya maeneo yaliyohifadhiwa.

Matumizi ya Ardhi ina maana ya shughuli zinazofanywa kwenye sehemufulani ya ardhi.

Mkataba wa Umiliki ina maana ya makubaliano yaliyofikiwa baina ya mtu,kundi la watu, shirika au shirika la umma na Mamlaka ya Wanyamapori auChama kilichopewa Mamlaka ya kutumia sehemu fulani ya ardhi kwakipindi cha muda mrefu.

Jumuiya za Nchini (Rejea Sheria ya Serikali za Mitaa ya mwaka 1982) inamaana ya watu wanaoishi katika maeneo ya vijijini.

Sheria ya Serikali za Mitaa ina maana ya Sheria ya Serikali za Mitaa(Mamlaka za Wilaya) Na 7 ya mwaka 1982.

Sheria ya Uvuvi ina maana ya sheria inayoongoza/inayodhibiti UvuviTanzania Bara na kama ilivyorekebishwa, yaani sheria ya Uvuvi Na 6 yamwaka 1970.

Sheria ya Misitu ina maana ya sheria inayoongoza Misitu Tanzania Bara.sheria ya Misitu ya mwaka 1957 Sura ya 389 ya Sheria.

Uhamaji ina maana ya mjongeo wa wanyama wa porini kwa kawaidandege na wanyama wanyonyeshao kwa umbali mkubwa wakitafutamahitaji muhimu.

Njia za Uhamaji ina maana ya maeneo, vishoroba au kanda za ardhizinazotumiwa na makundi makubwa ya wanyama kuhama wakati wavipindi vyao vya kuhama.

Mamlaka ya Usimamizi ina maana ya mamlaka inayosimamia eneomaalumu lililohifadhiwa au sehemu ya ardhi.

Sheria ya Madini ina maana ya Sheria ya Madini Na 17 ya mwaka 1979.

Waziri ina maana ya Waziri ambaye kwa wakati unaohusika ndiyemsimamizi wa mambo yanayohusiana na uhifadhi wa wanayamapori.

Mnyama wa Taifa ina maana ya spishi ya mnyama ambayo itatangazwahivyo na Waziri.

Mradi wa Taifa wa Pori la Akiba ina maana ya Pori la Akiba ambaloupangaji mipango na usimamizi wake uko chini ya serikali kuu moja kwamoja.

Sheria ya Hifadhi za Taifa ina maana ya sheria inayoongoza Hifadhi zaTaifa katika Tanzania Bara kifungu cha 418.

Maliasili za Taifa ina maana ya rasilimali ya viumbe hai ambayo ni pamojana misitu, wanyama na mimea ya majini, nyuki, wanyamapori na mazaoyao.

Kamati ya Maliasili ina maana ya kamati ya serikali ya kijiji ambayoinasimamia na kuratibu uhifadhi wa maliasili katika ardhi ya kijiji.

Sheria ya Hifadhi ya Ngorongoro ina maana ya sheria inayoongozaHifadhi ya Ngorongoro kifungu cha 419.

Eneo Lililohifadhiwa ina maana ya eneo lililotengwa chini ya sheriainayohusika kwa ajili ya uhifadhi wa wanyamapori na maliasili nyingine yaviumbe hai.

Spishi inayolindwa ina maana ya aina ya mnyama au mmea inayolindwa namkataba wa kimataifa, au Sheria za Tanzania au za nchi yoyote ile.

Kuranchi ina maana ya ufugaji katika mazingira yaliyodhibitiwa ya

sampuli, ya wanyama wadogo, kwa kawaida, waliokamatwa porini kwamadhumuni ya kuingia katika biashara ya wanayamapori.

Vyama Wakilishi ina maana ya makundi yaliyojizatiti yanayowakilishamakundi ya watu yanayojihusisha katika shughuli za uhifadhi wawanyamapori.

Maeneo yaliyohifadhiwa Yasiyokaliwa ina maana ya Hifadhi za Taifa naMapori ya Akiba.

Sheria ya Mamlaka za Mijini ina maana ya sheria za mamlaka za mijini Na8 ya mwaka 1982.

Ardhioevu katika muktadha huu ina maana ya maeneo ya bwawa la tope,mbuga ya kinamasi, ardhi ya mboji au maji, yawe ya asili au ya kufanywana binadamu, ya kudumu au ya muda, yenye maji yaliyotuama auyanayotiririka, ya maji baridi, ya chumvichumvi au ya chumvi ikiwa nipamoja na maeneo ya maji ya bahari ambayo kina chake katika majikupwahakizidi mita sita. Inaweza pia ikajumuisha kanda za pwani jirani namaeneo ya majimaji na visiwa au maji ya bahari ya kina kinachozidi mitasita wakati wa majikupwa yaliyosimama ndani ya ardhioevu.

Wanyamapori ina maana ya spishi za wanyama au mimea ya pori na yakienyeji na makazi na mifumo ya ikolojia yake; hupatikana Tanzania navilevile aina za kigeni zilizoingizwa nchi Tanzania na ambazo zimefungiwamahali kwa muda kabla hazijaingizwa mwituni.

Mamlaka za Wanyamapori ina maana ya vyombo vya serikali au mashirikaya umma yanavyosimamia sehemu maalumu za sekta ya wanyamapori.

Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori ina maana ya Sheria ya Uhifadhi wawanyamapori Na 12 ya mwaka 1974.

Eneo la Jumuiya la Usimamizi wa Wanayamapori ina maana ya eneolililotangazwa na Waziri liwe hivyo na kutengwa na serikali ya kijiji kwamadhumuni ya uhifadhi wa wanyamapori.