shirikisho ndani ya shirikisho - kituo cha katiba...shirikisho ndani ya shirikisho uzoefu wa...

150
Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa Kituo Cha Katiba Nchini Tanzania Kutafuta Ukweli wa Mambo Editors Frederick Jjuuko Godfrey Muriuki fountain publishers Kampala

Upload: others

Post on 17-Jan-2020

34 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Shirikisho Ndani ya ShirikishoUzoefu wa Muungano wa Tanzania na

Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki

Taarifa ya Ujumbe wa Kituo Cha Katiba Nchini Tanzania Kutafuta Ukweli wa Mambo

EditorsFrederick Jjuuko Godfrey Muriuki

fountain publishersKampala

Page 2: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Fountain PublishersS.L. Posta 488KampalaBarua pepe: [email protected] [email protected] Tovuti: www.fountainpublishers.co.ug

Kwa niaba ya:

Kituo cha Katiba: Eastern Africa centre for Constitutional DevelopmentS.L. Posta 3277, Kitalu 7, Estate Link Road, Off Lugogo by-passKampala, UgandaSimu: +256_414_533295Faksi +256_414-541028Barua pepe: [email protected]: www.kituochakatiba.org

Kinasambazwa Ulaya na Nchi za Jumuiya ya Madola nje ya Afrika na: Africa Books Collective Ltd,S.L. Posta 721,Oxford OX1 9EN, UKSimu/Faksi: +44(0) 1869 349110Barua pepe: [email protected]: www.africanbookscollective.com

© Kituo cha Katiba 2010

Chapa ya kwnza 2010

Haki zote zimehifadhiwa. Hairuhusiwi kunakili, kuhifadi kwa namna ambayo inaweza kutumiwa baadaye au kutangaza kwa namna yoyote ile au kwa njia yoyote ile ya elektroni, kupiga chapa, kutoa nakala kivuli, kurekodi au namna nyingine yoyote ile ripoti hii bila ya idhini, kwa maandishi kutoka kwa mchapishaji

ISBN 978-9970-25-022-6

Page 3: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

iii

Yaliyomo

1 Usuli wa Kihistoria 1Tanganyika • 1Zanzibar • 3Muungano • 7

2 Uundwaji na Historia ya Muungano 17Kuja kwa Muungano 1• 7Misingi ya Uhalali na Muundo wa Muungano 2• 2Muundo wa Muungano 2• 6Uhalali wa Muungano 3• 4

3 Mambo ya Muungano 40Maana ya Mambo ya Muungano 4• 0Kuongezwa kwa Mambo ya Muungano 4• 4Utendaji wa Mgawanyo wa Madaraka na Majukumu 4• 8

4 Utaratibu wa Kutatua Matatizo ya Muungano 53Utangulizi 5• 3Mahakama ya Katiba 5• 6 • Tume na Kamati 57 • Kamati ya Makamu wa Rais 59Mchakato wa Muafaka 6• 3Vyama vya Siasa, Viongozi na Raia 6• 9Viongozi na Idara za Serikali 7• 2Mwisho 7• 5

5 Mustakabali wa Muungano 77Utangulizi 7• 7Muungano ndiyo Mustakabali 7• 8Mustakabali bila ya Muungano 8• 0Muungano wa Haki 8• 3Muungano wa Serikali Tatu 8• 3Vikwazo vya Muungano wa Haki 8• 4Namna ya Kuufikia Muungano Endelevu na wa Haki 8• 6

Page 4: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

iv Shirikisho Ndani ya Shirikisho

6 Muungano na Kuunganishwa kwa Afrika Mashariki 90 • Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki 90Mambo ya Kuzingatiwa ya Kihistoria 9• 2Muungano kwenye Uhusiano wa Kimataifa 9• 5Muungano ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki 9• 8Njia ya Kuelekea kwenye Shirikisho la Afrika Mashariki na • Nafasi ya Muungano 109Sauti za Kutoka Zanzibar 11• 0Sauti za kutoka Bara 11• 4

7 Hitimisho na Mapendekezo 121Viambatanisho 12• 5Watu Waliohojiwa na Ujumbe huu Tanzania Bara 12• 5Watu Waliohojiwa na Ujumbe huu Zanzibar 12• 8Watu Waliohojiwa na Ujumbe huu Pemba 13• 1Bibliografia 13• 2Faharasa Zilizoteuliwa 13• 4

Page 5: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

v

Maelezo juu ya waliochangiaFrederick Jjuuko ni profesa wa sheria Chuo Kikuu cha Makerere.Godfrey Muriuki ni profesa wa historia Chuo Kikuu cha Nairobi.

Page 6: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

vi

ShereheAD Anno Domini (Baada ya Kuzaliwa Nabii Issa)AFDB African Development BankANGOZA Association of NGOs in ZanzibarASP Afro Shirazi PartyAU African Union (Umojo wa Afrika)BC Before Christ (Kabla ya Kuzaliwa Nabii Issa)CAF Confederation of African FootballCCM Chama Cha MapinduziCHADEMA Chama Cha Demokrasia MaedeleoCHRAGG Commission for Human Rights and Good

Governance (Tume ya Haki za Binadamu na Utawaka Bora)

CIA Criminal Investigation Agency (Shirika la Ujasusa la Marekani)

CSOs Civil Society Organisations (Jumuiya za Kiraia)CUF Civic United Front DENIVA Development Network of Indigenous Voluntary

AssociationsDPP Director of Public Prosecutions (Mkurugenzi wa

Kuendesha Mashtaka)EA East Africa (Afrika Mashariki)EAC East African Community (Jumuiya ya Afrika

Mashariki)EABC East Africa Business Council (Baraza la Biashara la

Afrika Masharika)EACSO East African Common Services Organisation (Jumuiya

ya Haduma za Pamoja ya Afrika Mashariki)EADB East African Development Bank (Benki ya

Maendeleo ya Afrika Mashariki)EALA East Africa Legislative Assembly (Bunge la Afrika

Mashariki )

Page 7: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Sherehe vii

EALS East African Law Society (Chama cha Wanasheria cha Afrika Mashariki)

EEZ Exclusive Economic ZoneEPA European Partnership Agreement (Mkatapa wa

Ubia wa Ulaya)FIFA Fédération Internationale Football Association

(International Federation of Football Associations) (Kimataifa la vyama vya mpira wa miguu)

JFC Joint Finance Commission (Tume ya Pamoja ya Fedha)

IUCEA Inter-University Council of East Africa (Baraza la Pamoja la vyuo vikuu la Afrika Mashariki)

IMO International Maritime Organisation (Chama cha Bahari cha Kimataifa)

KCK Kituo Cha KatibaMPs Members of ParliamentNEC National Electoral Commission (Tume ya Taifa ya

Uchaguzi) National Executive CouncilNGOs Non-Governmental Organisations (Visivyo vya

Kiserikali)OIC Organisation of the Islamic Conference (Umoja wa

Waisilamu)SADC Southern Africa Development CommunityTACOSODE Tanzania Council for Social Development (Baraza

la Tanzania kwa Maendeleo ya Jamii) TANGO Tanzania Association of NGOs (Chama cha Vyama

Visivyo vya Kiserikali cha Tanzania)TANU Tanganyika African National UnionTRA Tanzania Revenue Authority (Mamlaka ya Mapato

ya Tanzania)UAE United Arab Emirates (Muungano wa Falme za

Kiarabu)UK United Kingdom

Page 8: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

viii Shirikisho Ndani ya Shirikisho

UN United Nations (Umoja wa Mataifa)URT United Republic of Tanzania (Jamuhuri ya

Muungano wa Tanzania)USA United States of America (Marekani)ZEC Zanzibar Electoral Commission (Tume ya

Uchanguzi Zanzibar)ZLS Zanzibar Law Society (Chama cha Wanasheria cha

Zanzibar)ZNP Zanzibar National PartyZPP Zanzibar People’s Party

Page 9: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

ix

Usuli na UtanguliziKikiwa kimeundwa mwaka 1997, Kituo Cha Katiba (KCK) ni chama cha Afrika Mashariki mbacho eneo la shughuli zake ni kuendeleza utaratibu wa kuheshimu katiba na utawala wa kidemokrasia katika kanda ya Afrika Mashariki. Kituo cha Katiba ni jukwaa lisilopendelea upande wowote kwa wanaharakati, wanataaluma na wanasiasa na kiko mstrari wa mbele katika kuwaingiza katika mazungumzo, kueleza maoni yao na mijadala mikali juu ya mambo mbalimbali yanayohusu hali ya sasa ya Afrika Mashariki. Chama hiki, kina nia ya kuendeleza ushiriki hai wa jumuiya za kiraia katika utawala na kujenga utamaduni na maadili ya kuheshimu katiba na kuvifanya vyombo vya kikatiba vya hivi sasa katika serikali za Afrika Mashariki kuwa ni nyaraka hai za kweli zenye kukidhi mategemeo na mahitaji ya wananchi wa kawaida pamoja na vyombo ambavyo kwa kupitia vyombo hivyo wananchi wanasimamia utawala wao. KCK kinaongozwa na Bodi ambayo wajumbe wake wanatoka Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania, Uganda na Zanzibar.

Kero Mwezi April 1964, zile zilizokuwa nchi mbili huru za Tanganyika na Zanzibar zliungana na kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (URT). Hili lilitokea baada ya mapinduzi yaliyotokea kabla huko Zanzibar ambayo ilipata uhuru wake muda mfupi tu uliopita. Kuna kiza fulani kinachoyazunguka mazingira ya kuanzishwa kwa Muungano. Hali ilivyoendelea Muungano ulikuwa ni wa serikali ya chama kimoja (mwanzoni ukiwa na vyama viwili). Vyama viwili hivyo baadaye viliungana. Miaka kadha baadaye, Tanzania ilirudi kwenye mfumo wa vyama vingi vya siasa mwaka 1992 na kufanya uchaguzi wake wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995.

Katika kipindi cha kuwepo kwa muungano pamekuwepo na kero nyingi. Kuna masuala ya uzanlendo wa Zanzibar, kupoteza madaraka na uwezo wa Zanzibar kushughulikia mambo ya kimataifa, kupungua kwa uhuru wake kwa kuongezeka kwa mambo ya muungano na kwa

Page 10: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

x Shirikisho Ndani ya Shirikisho

hiyo kupungua mambo ambayo serikali ya Zanzibar yana uwezo nayo, jambo ambalo Zanzibar inadai kuwa lilifanyika kwa uamuzi wa upande moja tu. Kadhalika, yamejitokeza masuala ya mgawanyo wa maslahi na gharama za serikali ya Muungano ikiwa ni pamoja na kugawana mapato, misaada ya kutoka nje na kadhalika.

Masuali haya yamezidishwa na muundo wa ajabu wa Muungano. Muundo huo ni ule wa kuwepo kwa serikali mbili, serikali ya Muungano na serikali ya Zanzibar, lakini bila ya kuwepo kwa serikali ya Tanganyika. Kwa upande mmoja, kwa muda mrefu im- edaiwa kuwa Zanzibar haiwezi kufanya mashauriano na mbia mwenzake waliosaini mkataba wa Muungano ili kuuboresha mkataba huo pale ilipotokea haja ya kufanya hivyo. Kwa upande mwingine, pamekuwa na kelele kutoka bara zilizodai kufufuliwa kwa serikali ya Tanganyika. Uwezo wa pande mbili wa serikali ya Muungano, yaani uwezo wa kisheria juu ya mambo ya Muungano, na yale yaliyokuwa si ya Muungano ya upande wa bara umesababisha matatizo yake yenyewe pamoja na kuzua wasiwasi.

Lilifanywa jaribio la kutengeneza utaratibu wa kushughulikia kero hizo lakini hilo, ikiwa ni pamoja na Mahakama ya Katiba, Tume ya kudumu na Tume nyingine nyingi za muda inaonesha kuwa hazikuwa na manufaa yoyote. Badala yake, kila wakati imewabidi warudi kwenye mfumo wa chama kimoja kushughulikia masuala hayo.

Kipindi cha mpito cha kuelekea kwenye siasa ya vyama vingi kiliufanya utaratibu huo wa kuziondoa kero za Muungano ushindwe kufanya kazi. Kipindi hicho cha mpito nacho pia kilileta matatizo ya machafuko wakati na baada ya uchaguzi na malalamiko ya udanganyifu wakati wa uchaguzi huko Zanzibar. Hilo, badala yake limeyakuza matatizo ya Muungano, na hasa nafasi ya Zanaibar ndani ya Muungano. KCK ilipeleka ujumbe Zanzibar ili kufuatilia masuala ya uchaguzi, kulingana na uwezo wake ambao imeutumia kwa kupitia tume katika nchi nyingine zote za Afrika Mashariki.

Mchakato wa hivi sasa wa kuiunganisha Afrika Mashariki unatoa fursa ya kipekee. Mchakato huo ambao unatarajiwa kukamilika kwa kuundwa kwa Shirikisho la Afrika Mashariki unatoa fursa ya kufikiri upya na kuufanyia marekebisho Muungano wa Tanzania na kuyaondoa malalamiko yaliyotolewa, hasa yale yaliyotolewa na

Page 11: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Usuli na Utangulizi xi

Zanzibar. Kujadiliana juu ya ni yepi mambo ya shirikisho ndani ya Afrika Mashariki kutatoa fursa kwa Watanzania kuyashughulikia kwa mara nyingine tena matatizo yao ya kudumu ya mambo ya Muungano. Afrika Mashariki inaweza kuchangia katika mchakato huu kwa jumla na katika kushughulikia suala la nini iwe nafasi ya Zanzibar katika mchakato wa majadiliano na hatimaye katika Shirikisho la Afrika Mashariki. Zaidi ya hayo, mchakato wa kuiunganisha Afrika Mashariki unaweza kujifunza mengi kutokana na mchakato ambao Watanzania wameupitia kwa kiasi fulani cha mafanikio kwa takriban nusu karne.

Hili ndilo lilichokifanya KCK kutuma ujumbe uliokuwa na Waafrika Mashariki wa nje ya Tanzania, ili kuuangalia Muungano kama ulivyo, kuainisha matatizo yake; nafasi yake katika mchakato wa kuiunganisha Afrika Mashariki, ili kuanzisha mchakato unaotegemewa kuwa hapo baadaye utakuwa na maslahi kwa Tanzania na Afrika Mashariki.

Ujumbe KCK kiliandaa tume za kutafuta ukweli katika makundi mawili; la kwanza kwa ajili ya Unguja, Zanzibar, ambalo lilifanya shughuli hiyo kuanzia tarehe 13 hadi 16 Juai 2009. La pili lilifanya shughuli hiyo Tanzania Bara kuanzia tarehe 23 hadi 28 Agosti 2009. Ujumbe huo baadaye uliitembelea Pemba kuanzia tarehe 19 hadi 20 April 2010.Waliokuwemo katika ujumbe huo walikuwa ni wafuatao:

Mhe. Augustine Ruzindana (Uganda), aliyekuwa Inspekta • Mkuu wa Serikali, alikuwa Mbunge na hivi karibuni alikuwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wabunge wa Kiafrika dhidi ya Ufi sadi (Kiongozi wa Ujumbe);Bwana Vincent Ndikumasabo (Burundi), Mhadhiri, Sheria za • Katiba na za Kimahakama, Chuo Kikuu cha Lac Tanganyika, alikuwa Jaji wa Mahakama ya Juu na alikuwa Mbunge;Prof. Godfrey Muriuki (Kenya• ), Profesa wa Historia, Chuo Kikuu cha Nairobi; Bi. Justine Mirembe (Rwanda), Mshauri, Mwanasheria mwenye • kufanya shughuli zake Kigali;

Page 12: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

xii Shirikisho Ndani ya Shirikisho

Bi. Florence Batoni (Rwanda), Mtaalam wa Mawasiliano na • Ujenzi wa Amani; Prof. Frederick Jjuuko (Uganda), Profesa wa Sheria, Chuo • Kikuu cha Makerere, Kampala, Uganda (Katibu wa Tume);Bi. Edith Kibalama, Mkurugenzi Mtendaji, KCK alitoa msaada • wa huduma.

Madhumuni ya Ujumbe wa Kutafuta Ukweli wa MamboMadhumuni makuu yalikuwa ni kuchunguza maeneo yaliyo na wasiwasi yanayohusiana na Muungano Kati ya Tanzania Bara na Zanzibar kwa nia ya kuimarisha ushiriki wa Zanzibar katika michakato ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na kutafuta njia na namna ya kundoa wasiwasi huo.

Watu WaliohojiwaUjumbe ulikutana na kujadiliana na watu mbalimbali kote, Zanzibar na Bara. Watu hao ni pamoja na mawaziri wa serikali, wabunge na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, viongozi wastaafu wa kitaifa, viongozi wa mashirika ya serikali na viongozi wa vyama vya siasa kama vile Chama Cha Mapinduzi ( CCM), Civic United Front ( CUF) na Chama Cha Demokrasia Maedeleo ( CHADEMA). Ujumbe vile vile, ulifanya mazungumzo ya maana sana na watu kutoka kwenye jumuiya za kiraia ikiwa ni pamoja na wale wa kutoka katika vyama vya wanawake, vyombo vya habari, vijana na chama cha wafanya biashara. Ujumbe umenufaika vile vile kutokana na mazungumzo na vyama vya wanasheria vya Bara na Zanzibar pamoja na wanataaluma waliobobea. Orodha ya watu waliohojiwa imeambatanishwa mwisho wa ripoti.

Hapajakuwepo na mwongozo wowote kuhusu mahojiano hayo na ujumbe uliwahoji watu hao kwa namna ambayo waliweza kuelezea kikamilifu maoni yao juu ya suala la Muungano na kuelezea habari zote walizozijua. Muda wa wiki moja kwa kila eneo ya maeneo mawili hayo ulionekana kuwa ni mfupi ukizingatia watu ambao walihitaji kuhojiwa. Hatimaye, njia iliyotumika pamoja na ripoti ni ya hali ya ubora.

Page 13: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

xiii

ShukraniTume ya kutafuta ukweli wa mambo inapenda kutoa shukrani zake kwa wote wale walioitikia wito wao. Walitukirimu muda na usikivu wao kwa hiari yao na bila ya hiana; walituruhusu kuziingilia kati shughuli zao za kawaida. Mara nyingi walikubali kukutana na sisi alfajiri na wengine muda mrefu baada ya jua kutua. Tumevutiwa na ukweli na uwazi wao wakati wakitoa maoni yao, matumaini na hofu pamoja nasi, na habari walizotupatia. Tumevutiwa na ukarimu wa wale walioshiriki kwa muda mrefu katika kipindi cha maendeleo ya Muungano na kutuelezea uzoefu wao na mara nyingi wakituelezea mambo yaliyotokea wakati huo na kutuwezesha kuilewa hali ya mambo vizuri zaidi.

Page 14: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa
Page 15: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

1

1 Usuli wa Kihistoria

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania (URT) inajumuisha Zanzibar na Tanzania Bara, ambayo zamani ikijulikana kuwa Tanganyika. Tanzania Bara ina haki ya kudai kuwa ndiyo Chanzo cha Binadamu. Kwa mujibu wa ushahidi wa kuchimbwa, mabaki ya mtu wa zamani yalipatikana katika Bonde la Olduvai yakionesha kuwa ni ya miaka milioni 1.75 iliyopita. Vile vile zimeonekana nyayo za sokwe mtu hapo Laoteli, na zilionesha kuwa zilikuwa za miaka milioni 3.6 iliyopita.

TanganyikaWawindaji/wachumaji hawa wa zamani ambao wakiitwa Wakhoisan, walifuatiwa na watu wanaoongea Kicushitic kutoka Ethiopia katika karne ya kwanza Kabla ya Kuzaliwa Nabii Issa (BC). Baada ya hapo, wabantu kutoka Kamerun na Nigeria, na wanilotiki kutoka Sudan, walijitokeza kuanzi karne ya kwanza Baada ya Kuzaliwa Nabii Issa (AD). Wabantu, hasa walianzisha mifumo isiyoeleweka ya kijamii na kisiasa iliyopelekea kuanzishwa kwa maeneo mbalimbali yaliyotawaliwa na machifu na wafalme. Uhai na rasilimali za maeneo haya kisiasa viliwavutia watu wa kutoka nje. Kwa mfano, mnamo karne ya saba Baada ya Kuzaliwa Nabii Issa (AD) wafanybiashara kutoka Arabuni walianza kufanya maskani katika mwambao wa Afrika Mashariki ili kuzitumia vizuri rasilimali hizi zilizokuwa zikipatikana kwa urahisi. Walifuatiwa na wafanyabiashara wa Kihindi na wa Kichina mnamo karne ya kumi. Kwa hiyo, Afrika Mashariki ikawa ni sehemu ya mtandao wa biashara ya Bahari ya Hindi.

Waarabu walioana na wenyeji wa Kibantu. Hili lilisababisha kuibuka kwa jamii ya Waswahili na ustarabu wao ambao ulienea

Page 16: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

2 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

katika mwambao wa Afrika Mashariki na Zanzibar. Hata hivyo, udhibiti wa Waarabu uliingiliwa kati na Wareno baina ya karne ya 16 na mwisho wa karne ya 17 walipopinduliwa na Waomani ambao waliifanya Zanzibar kuwa ni kituo chao cha kibiashara na kiutawala. Waomani walikuwa na ndoto ya kupanua utawala wao kutoka Zanzibar hadi bara ya Afrika Mashariki (EA). Kwa madhumuni hayo, walipanua biashara ya pembe za ndovu na watumwa kuelekea Magharibi hadi kufikia Kongo. Kusema kweli, misafara ya kibiashara ilikuwa ndiyo shughuli kuu ya kiuchumi mpaka mwisho wa karne ya 19 pale uingiliaji kati wa Wazungu uliposababisha kuondolewa kwa biashara na utumwa na hatimaye kuondoa utumwa kuwa ni asasi ya kijamii.

Wakati huo huo, uingiliaji kati wa Wazungu ulimalizika kwa kutawaliwa kwa Tanganyika na Wajerumani kufuatia kugawanywa kwa Afrika kama ilivyokubaliwa kwenye Mkutano wa Berlin mwaka 1884 hadi 1885. Lakini baada ya kushindwa kwa Ujerumani katika Vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia, Umoja wa Mataifa uliikabidhi Tanganyika kuwa chini ya udhamini wa Uingereza. Hadhi hii ya kuwa chini ya udhamini ilithibitishwa na Umoja wa Mataifa (UN) baada ya Ujerumani kushindwa tena katika Vita vya Pili vya Dunia. Baada ya hapo, Tanganyika ilibaki chini ya utawala wa kikoloni wa Kiingereza mpaka miaka ya 1960, iliyoshuhudia mabadiliko ya upepo wa kisiasa katika Afrika. Katika kipindi hicho, makoloni mengi yalipata uhuru wao katika miaka ya 1960. Tanganyika ilifanya hivyo mwaka 1961.1

1 Angalia Coupland R., East Africa and Its Invaders, Oxford, Clarendon Press, 1938, sura X na X1; Coupland R., The Exploitation of East Africa, Faber, London, 1939; Oliver, R., and Mathew, G. (eds.), History of East Africa, Vol.1, Oxford University Press, 1964, pp. 352-453; Iliffe, J., A Modern History of Tanganyika, Cambridge University Press, Cambridge, 1979, pp. 485-576.; Kimambo, I. N. na Temu, A. J., A History of Tanzania, East African Publishing House, Nairobi, 1969.

Page 17: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Usuli wa Kihistoria 3

ZanzibarKama ilivyo katika sehemu nyingine za Afrika Mashariki, Zanzibar ilikaliwa na Wabantu kuanzia karene ya 2 Baada ya Kuzaliwa Nabii Issa (AD). Walitokea kutoka katika jamii mbalimbali za watu wa bara na waliishi katika vijiji vidogo vidogo. Lakini tofauti na wenziwao wa bara, hawakuunda vikundi vilivyoungana vya kisiasa. Kutofanya hivyo kulifanya iwe rahisi kwa wavamizi waliojiandaa vizuri kutoka nje kuwavamia.

Unguja, kisiwa kikuu kiliwavutia wageni kwa sababu kilitoa himaya nzuri ambayo iliweza kulindwa kwa urahisi. Kiliwavutia hasa mabaharia wa Kiajemi ambao walikifanya kuwa ni kituo katika biashara yao baina ya Masharki ya Kati, India na Afrika. Walifanya maskani yao vile vile katika ule unaoitwa Mji wa Zanzibar au Mji wa Mawe (Mji Mkongwe). Na hatimaye, Zanzibar ilikuwa ni kituo muhimu kwa yeyote aliyetaka kuanzisha uhusiano na bara.

Kama inavyoeleweka, wafanyabiashara hawa walianza kuoana na wenyeji katika karene ya 11 na 12 Baada ya Kuzaliwa Nabii Issa (AD). Na ili kuendesha maisha yao mtawala wa kurithi, Jumbe au Sheha, alitokea. Hali ilikuwa kama hivi mpaka walipowasili Wareno mnamo mwisho wa karne ya 15, mwanzo wa “Zama za Uvumbuzi”. Baada ya hapo, mwambao wa Afrika Mashariki ulibakia chini ya udhibiti wao mdogo mpaka walipotimuliwa na Waomani mwaka 1698.

Wakati wao, Waomani walijenga ngome Zanzibar, Pemba na Kilwa. Wakiwa wamevutiwa na yale yaliopo Afrika Mashariki na mategemeo ya maisha ya utulivu zaidi, ukilinganisha na njama za kisiasa za Maskati, Seyyid Said, mtawala wao, alihamisha kambi yake kutoka Maskati na kuhamia Zanzibar mwaka 1832. Hili lilisababisha kuanzishwa kwa ufalme wa Kiarabu Zanzibar ambao ulitegemea nguvu za watumwa wa Kiafrika.

Seyyid Said aliimarisha biashara ya viungo iliyostawi, na hasa karafuu, na kwa hivyo kuvipatia visiwa hivyo jina la utani la, Visiwa vya Viungo. Zaidi ya hayo, na kama tulivyoona hapo juu, alihimiza

Page 18: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

4 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

utanuzi wa biashara ya misafara kutafuta pembe za ndovu, madini na watumwa. Watumwa walisafirishwa na kupelekwa Arabuni na India. Ili kuendeleza mradi huu, aliwategemea Wahindi kwa msaada wa kifedha. Kwa mfano, mwaka 1835 walikuwepo Wahindi kiasi 300 hadi 400. Lakini ilipofika mwaka 1860 idadi yao ilikua na kufikia baina ya 5,000 na 6,000. Hatimaye, Zanzibar ilikuwa eneo la biashara lililozivutia nchi mbalimbali za Ulaya zilizoanzisha uhusiano wa kibalozi. Alisaini mikataba ya urafiki na Marekani (USA) mwaka 1836, Uingereza mwaka 1840, na Ufaransa mwaka 1844.

Hata hivyo, katika kipindi chote cha karne ya 19 watawala wa Omani walikuwa wateja wa Waingereza. Waingereza waliwasaidia kuwashughulikia raia wakorofi pamoja na kutoa mafunzo kwa majeshi yao, hasa jeshi la wanamaji. Lakini hili liliwagharimu. Kutoka miaka ya 1820, Uingereza ilishikilia kuwa Wazanzibari inawapasa kupunguza kidogokidogo shughuli zao za biashara ya utumwa, ambazo zilikuwa zikizidi kupingwa na jumuiya ya kimataifa na kudaiwa kuondolewa kabisa kwa biashara hiyo na utumwa wenyewe. Kwa sababu hii, hatimaye biashara ya utumwa iliondolewa Zanzibar kisheria mwaka 1876, wakati uachiliwaji huru wa watumwa ulifanyika mwaka 1897. Ijapokuwa walilipwa fidia kwa hasara ya watumwa, hiki kilikuwa ni kidonge kichungu kukimeza kwa sababu biashara ya watumwa na utumwa vilikuwa ndiyo mihimili mikuu ya uchumi wao.

Zaidi ya hayo, pale kinyang’anyiro cha Afrika kilipopamba moto, Sultani wa Zanzibar alilazimishwa kuthibitisha kiwango cha usultani wake katika eneo la Zanj. Kwa mshangao, alijikuta kuwa eneo lake la usultani limemegwa na kuingizwa katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa Uingereza na Ujerumani katika mwaka 1886 na 1890. Kusema kweli, hatimaye Zanzibar ilipoteza madai yake yote ya maeneo iliyodai kuyamiliki bara na kubakiwa na ukanda wa kilomita kumi katika mwambao wa Kenya. Lakini ukanda huu

Page 19: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Usuli wa Kihistoria 5

wa mwambao, pamoja na Zanzibar yenyewe, ulitangazwa kuwa ni himaya ya Uingereza mwaka 1890.

Kijuujuu, Zanzibar ilitawaliwa na Sultani chini ya malezi ya maafisa wa Kiingereza. Lakini kwa hakika hasa, kauli ya mwisho ilikuwa ni ya maafisa wa Kiingereza. Hadi mwaka 1913, Sultani alikuwa na kiasi fulani cha madaraka kwa raia zake. Lakini kuanzia mwaka 1913 hadi 1963, Uingereza iliteua mwakilishi, aliyeitwa rizdent (mkaazi). Kazi yake ilikuwa inafanana na ile ya gavana kama ilivyokuwa katika nchi nyingine za Afrika Mashariki ambazo wakati huo zilikuwa chini ya udhibiti wa Uingereza.

Zanzibar ilipata uhuru ikiwa na ufalme wa kikatiba tarehe 10 Desemba 1963. Lakini utaratibu huu uliishi kwa muda mfupi. Tarehe 12 Januari 1964 Waafrika waliipindua serikali iliyokuwa ikidhibitiwa na Waarabu ambayo ilishutumiwa kwa kufanya udanganyifu wakati wa chaguzi. Lakini lilikuwepo zaidi ya hilo juu yake. Ulikuwa ni mfano wa mapambano makubwa zaidi yaliyowapambanisha Waafrika waliokuwa wengi dhidi ya Waarabu wachache, au wakulima wasiokuwa na ardhi dhidi ya mabwanyenye waliomiliki ardhi na siasa ya watu wachache.2

Katika tukio hili Chama cha Afro-Shirazi Party (ASP) kilichukua hatamu za serikali chini ya kiongozi wake, Abeid Karume, aliyekuwa Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Ilikuwa ni dhahiri kuwa nchi za magharibi zilikuwa na wasiwasi kuwa ASP ikishawishiwa na wakoministi, kama si wafuasi wa moja kwa moja. Ili kutilia mkazo hofu zao, walieleza kuwa baadhi ya makada wa

2 Sheriff, Abdul, Slaves, Spices and Ivory in Zanzibar: Integration of an East African Commercial Empire into the World Economy, 1770-1873, James Currey, Oxford, 1987, pp. 48-60, 77-110, 202-238; Ogot, B. A., Zamani: A Survey of East African History, Longman, Nairobi, 1974, 210-227,295-312; Coupland, op. cit.; Oliver and Mathew, op. cit., pp.352-390 and 433-453.

Page 20: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

6 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

kimapinduzi walipata mafunzo ya kijeshi nchini Cuba na waliunga mkoni itikati ya kimapinduzi ya Kimarx waliyotaka kuiingiza Zanzibar. Katika hali hii, wahusika wakuu walikuwa Abdulrahman Mohamed Babu, Abdul Kassim Hanga na Abdul Aziz Twala. Mambo hayakuwa rahisi pale walipowasili wanadiplomasia wa kikoministi, hasa kutoka China na Ujerumani ya Mashariki. Hawa walikuja na ahadi za kuwa tayari kwao kutoa misaada ya kifedha ambayo nchi za magharibi hazikuweza kutoa, au hazikuwa tayari kutoa. Baya zaidi, Karume, ikiwa amekasirishwa na usiri wa nchi za magharibi kuitambua serikali yake, alisisitiza kuwa Marekani ikiondoe kituo chake cha kuangazia setelaiti kilichokuwepo Zanzibar. Mapinduzi yalizitia wasiwasi nchi za magharibi.3

Inakisiwa kuwa katika hatua ya kwanza ya mapinduzi Waarabu na Waasia baina ya 5,000 na 15,000 waliuawa; wanawake wao walibakwa na nyumba zao zilichomwa moto. Hii ilisababisha kuwa asilimia 20 ya wakazi wote kuwa ama wameuawa au wameikimbia nchi4. Vyanzo vya habari hizi vinadai kuwa idadi halisi ya vifo wakati wa mapinduzi haijulikani mpaka hivi sasa.5 Kama ambavyo ingelitegemewa, vurugu hii iliivutia jamii ya kimataifa na kupata sifa mbaya.

Wakati huo huo na kwa pamoja, majeshi ya Kenya, Tanganyika na Uganda yaliasi. Marais Jomo Kenyatta (Kenya), Julius Nyerere (Tanganyika) na Milton Obote (Uganda) walipata aibu ya kuiomba

3 Petterson, Don, Revolution in Zanzibar: An American’s Cold War Tale, Westview Press, Boulder, Colorado, 2002, pp.121-210; Lofchie, Michael F., Zanzibar: Background to Revolution, Oxford University Press, 1965, Part 111, pp. 183-281.

4 James Minaham, Encyclopedia of the Stateless Nations as quoted in “History of Tanzania”, Wikipedia, pp.2088-2089.

5 Bakari Mohammed Ali, The Democratisation Process in Zanzibar: A Retarded Transition, GIGA, Hamburg, p.105-106.

Page 21: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Usuli wa Kihistoria 7

Uingereza, mtawala wao wa zamani, kuwanusuru kwa kuwapelekea majeshi ya Uingereza kutuliza maasi hayo ya kutia unyonge. Yaliyotokea baada ya hapo yalizifanya nchi za magharibi kuhofu kuwa Zanzibar itakuwa Cuba ya pili. Kwa hiyo, Uingereza na hasa Marekani waliazimia kulizuia hilo lisitokee.

MuunganoNjia mbalimbali zilifikiriwa na hatimaye Nyerere alishawishiwa kunusuru hali hiyo isitokee kwa kuiunganisha Tanganyika na Zanzibar. Kwa hiyo, tarehe 26 April 1964 nchi mbili hizo zikawa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa muda mfupi. Baadaye zikawa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (URT) tarehe 29 Octoba 1964.

Kuundwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuliwashangaza watu wengi. Hata hivyo, hali isingelikuwa hivyo. Kwa mfano, Karume alikuwa mtu wa bara aliyekuwa baharia na kuamua kufanya maskani yake Zanzibar. Zaidi ya hilo, viongozi wingi wa Kizazibari walihamia Zanzibar kutoka bara katika miaka ya 1940 na 1950, na kwa sababu hiyo kujenga uhusiano wa karibu kati ya Zanzibar na bara. Kwa mfano, tokea mwaka 1934 chama cha “African Association” cha Tanganyika kilikuwa na tawi Zanzibar, ambalo liliungwa mkono na Wazanzibari waliokuwa na asili ya Bara.

Kadhalika, Muungano ulikuja wakati mjadala mkali wa wakati huo ulikuwa ama kuunda Shirikisho la Afrika Mashariki au Muungano wa Serikali za Afrika kama ilivyokuwa ikihubiriwa na watu kama Kwame Nkrumah wa Ghana. Hata hivyo, Nyerere alikuwa ni mtu aliyekata tamaa. Mapema mwaka 1961 alitangaza kuwa alikuwa tayari kuahirisha uhuru wa Tanganyika ikiwa atahakikishiwa kuwa Kenya na Uganda zitapewa uhuru wao kwa wakati mmoja ili kuwezesha kuundwa kwa Shirikisho la Afrika Mashariki. Lakini hili halikuwa kama ilivyokusudiwa.

Page 22: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

8 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

Pili, mwaka 1963 viongozi watatu wa Afrika Mashariki walijitolea kuunda hilo shirikisho lililopendekezwa. Ni kweli kuwa kamati kazi iliundwa kwa madhumuni hayo. Mara nyingine tena, wazo hilo lilikabiliwa na matatizo makubwa ya kisiasa, hasa kwa sababu Uganda ilionekana kusitasita. Nkrumah naye hakutaka kulisikia hilo. Aliona kuwa hilo litaliiba wazo lake na kuhatarisha ndoto yake ya kuunda chombo cha bara zima. Matokeo yake ni kwamba alifanya kampeni kubwa dhidi ya wazo la kuwa na Shirikisho la Afrika Mashariki. Si ajabu kuwa hilo halikuwa6.

Vyovyote itakavyokuwa, mapinduzi yaliigeuza Zanzibar kuwa jukwaa la kushindana ujanja kati ya nchi za Magharibi na zile za Kikominsti. Uingereza na Marekani zilimsinikiza sana Nyerere awaokoe. Kenya na Uganda nazo vile vile walilipata joto la jiwe. Nyerere alikuwa na wasiwasi kwa sababu hakutaka aonekane kuwa yeye ni kibaraka wa nchi za magharibi, au mtu aliyeisaliti misingi ya Umoja wa Afrika jambo ambalo akiliamini sana. Vilevile, hakufurahia uwezekano wa kutuhumiwa kuwa ameitawala Zanzibar.

Hata hivyo, Nyerere hakuwa na njozi. Mapinduzi ya Zanzibar yalikuwa na “vurugu na yalidhibitiwa na watu wenye silaha na wasiosoma ambao waliihatarisha sana Zanzibar yenyewe na Tanganyika”. Wakati huo, palikuwa na mvutano mkubwa ndani ya ASP na kati ya chama hicho na Umma Party. Inadaiwa kuwa Karume alikuwa na wasiwasi na maisha yake na alimwomba Nyerere amsaidie na amlinde. Inasemeka vile vile kuwa alitoa wazo la Tanganyika kuimeza Zanzibar, Nyerere akiwa rais na yeye wa pili katika madaraka.

6 Kuna mawazo tofauti juu ya kama sinikizo la nchi za maghabi ndilo lililopelekea kuundwa kwa muungano. Kuhusu hili, angalia, Othman, Haroub, “The Union with Zanzibar”, katika Legum, C. na Mmari, G., Mwalimu: The Influence of Nyerere, James Currey Limited, London, 1995, pp. 170-75; na Petterson, op.cit., p.207.

Page 23: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Usuli wa Kihistoria 9

Kutokana na hali hiyo tete na ya vurumai huko Zanzibar, pamoja na sinikizo kutoka nchi za magharibi, ushahidi uliopatikana unaonesha kuwa alikubali kichwa upande kuziunganisha Tanganyika na Zanzibar baada ya kipindi cha kusitasita akijishauri. Na kama kawaida aliweza kukitumia kipaji chake cha kuongea hadharini kuutetea uamuzi huo7.

Ili kuwanyamazisha wapinzani wake, alitoa hoja kuwa yeye aliuona muungano wa Tanganyika na Zanzibar kuwa ni hatua ya kwanza katika kuunda Shirikisho la Afrika Mashariki na hatimaye la bara zima. Zaidi ya hilo, aliuona muungano huo kuwa ni jambo la kuleta utulivu kwa sababu Zanzibar isiyotabirika itaambukiza hali hiyo katika kanda yote. Kadhalika, ASP na Tanganyika African National Union ( TANU) vilishirikiana wakati wa mapambano ya kupigania uhuru. Ushirikiano baina ya vyama hivyo kwa hiyo, ungelikuwa ni uendelezaji wa kile kilichotokea kabla. Katika hali hiyo, hilo lilikuwa ni chagua lililokuwa bora zaidi, alimaliza. Kwa ufupi aliyachukulia mambo kama yalivyokuwa.

Jambo jingine la kuvutia kwa wanasayansi wa kisiasa, wanasheria wa kikatiba na wanahistoria ni jinsi zoezi hilo lilivyotendeka. Hakuna shaka yoyote kuwa zoezi hilo liligubikwa na usiri. Kwa mfano, kuna fikra zinazotoa hoja kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar wa wakati huo hakushauriwa. Ni wazi kuwa Mkataba wa Muungano ulitayarishwa Dar es Salaam na Waingereza wawili waliokuwa watumishi wa serikali, ambao waliaminiwa na Nyerere.

La zaidi ni kwamba hata uhalali wa katiba ya Muungano nao ni wa wasiwasi. Kuna wanaodai kuwa Baraza la Mapinduzi la Zanzibar halikuridhia Mkataba wa Muungano kwa sababu ya mgawanyiko

7 Hughes, A. J., East Africa: The Search for Unity: Kenya, Tanganyika, Uganda and Zanzibar, Harmondsworth, 1963, pp.227-264; Rothchild, D., Politics of Integration: An East African Documentary, Nairobi, 1968.

Page 24: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

10 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

wa kisiasa uliokuwepo ndani ya Baraza la Mapinduzi. Kwa hiyo, uhalali wa Muungano unategemea kule kuridhiwa na serikali ya bara tu na baadaye kuchapishwa katika gazeti la serikali la bara. Maelezo yanayotolewa juu ya shaka hii, ni kwamba Karuma hakuwa na muda wa mambo madogo madogo ya kisheria. Kadhalika, kwa sababu ya elimu yake ndogo, jaribio kama hilo lingelikuwa jambo lisilokuwa na manufaa. Kwa hiyo, wapinzani wanadai kuwa Muungano haukuwa na msingi wa kisheria tokea mwanzoni kwa sababu wakati Mkataba wa Muungano ulitiwa saini na Karume, haukuridhiwa na Baraza la Mapinduzi. Kwa sababu hiyo, inadaiwa kuwa Muungano upo kwa kuwepo kwake tu laki si kisheria. Kwa ufupi yalikuwa ni mapatano ya kuaminiana.8

Juu ya yote hayo, kuna mgawanyiko wa mawazo juu ya nia ya wahusika wakuu wawili hao, Nyerere na Karume. Baadhi ya wanataaluma wanauona utaratibu huo wa muda kuwa ulikuwa ni hatua ya muda tu iliyokuwa na nia ya kuziunganisha kabisa nchi mbili hizi hapo baadaye. Kwa wengine, nia kama hiyo haijakuwepo. Wanadai kuwa maoni yao yanalingana na tabia ya Karume hapo baadaye. Kwa muda wote, ameonesha kuwa mkaidi na wengine walithubutu hata kusema kuwa, alipinga utekelezaji wa makubaliano ya Muungano.

Linaloleta ubishani zaidi ni orodha ya mambo yalowekwa kuwa chini ya serikali ya Muungano. Mambo 11 ya mwazo kabisa, baada ya muda yameongezeaka na kuwa 22 mwaka 1990. Kwa Wazanzibari, hili lina nia ya kuudhalilisha uhuru na utambulisho wa Zanzibar. Zaidi ya hilo, Zanzibar ipo katika hali ngumu sana kwa sababu kauli yao katika bunge la Muungano inamezwa na wabunge wengi kutoka Tanzania Bara. Hili ni jambo ambalo Wazanzibari wanalipa umuhimu mkubwa bila ya kujali mitazamo yao ya kisiasa.

8 Shivji, Issa G., Pan-Africanism or Pragmatism?: Lessons of Tanganyika-Zanzibar Union, Mkuki na Nyota Publishers, Dar-es-Salaam, 2008 pp.76-99. Angalia Tanzania: The Legal Foundations of the Union, Dar-es-Salaam University Press, 2009.

Page 25: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Usuli wa Kihistoria 11

Muundo wa serikali nao pia umepigwa darubini. Kisa cha ugomvi ni ukweli kuwa Muungano unashughulikia mambo ya Muungano na yale yasiyokuwa ya Muungano ambayo yamerundikwa pamoja. Kwa hiyo, Wazanzibari wanahisi kuwa pale waziri wa Muungano anaposhughulikia jambo linalozihusu pande zote mbili, kuna uwezekano mkubwa wa waziri huyo kuipendelea bara. Kwa ufupi, kuna mgogoro wa maslahi. Wakati huohuo, kasma za bajeti zinalundikwa pamoja kwa serikali ya Muungano na Tanzania Bara bila ya kutafautishwa. Hii ndiyo sababu iliyopelekea kuwepo kwa makelele ya kutaka iwepo serikali ya ngazi tatu itakayokuwa na serikali za Muungano, Zanzibar na Tanzania Bara. Tatizo hili lilijitokeza waziwazi mwaka 1984 na kupelekea aliyekuwa rais wa Zanzibar, Jumbe, alazimishwe kujiuzulu.

Kuongezeka kupungua kwa madaraka ya Serikali ya Zanzibar kunadhihirika zaidi kwa kuungana kwa TANU na ASP mwaka 1977. Hii ilikuwa na maana kuwa, mambo ambayo yalikuwa moja kwa moja ndani ya uwezo wa kisheria wa Zanzibar, kuanzia hapo yawe yanaamuliwa na na chama cha siasa cha nchi nzima - CCM. Kwa mfano, Hassan Mwinyi alichaguliwa na Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kuwa rais wa muda wa Zanzibar na baadaye kuteuliwa kuwa mgombea urais. Vile vile, kwa kuanzishwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 kulikuwa na hofu kuwa CCM isingelishinda uchaguzi wa mwaka 1995 huko Zanzibar na ulikuwepo uwezekani wa ushindi huo kwenda kwa CUF. Matokeo yake ni kwamba yalifanyika mabadiliko ya kikatiba kuondoa kipengele kinachomhakikishia rais wa Zanzibar kuwa moja kwa moja ndiye makamu wa Rais wa Muungano. Kwa kuwa Sheria ya Vyama vya Siasa inavitaka vyama vya siasa kuandikishwa katika pande zote mbili za Muungano, bara inaonekana kuwa imejitayarisha kuitawala Zanzibar nje ya CCM na hata chini ya mfumo wa vyama vingi.

Ni wazi kuwa kuwepo kwa uchaguzi ulio huru na wa haki kumekuwa ni tatizo kwa Zanzibar. Haya yamechafuliwa na kuwepo

Page 26: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

12 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

kwa kukiukwa kwa taratibu kama ilivyooneshwa mwaka 1995, 2000 na 2005. Kutengenezwa kwa daftari la wapiga kura nako kumekuwa ni tatizo kubwa. Suala la nani Mzanzibari limechochea machafuko kwa sababu pamekuwepo na jaribio la makusudi lililofanya na masheha, kukataa kuwaandikisha wale walioonekana kuunga mkono upinzani. Sharti la ukazi wa miaka mitano limewanyima wengi haki ya kupiga kura, wakati sharti hilohilo halihitajiki kwa watumishi wa idara maalum za majeshi, kama vile Kikosi Cha Valantia. Hawa wanatuhumiwa kuwa ni chombo cha kuendeleza maslahi ya CCM. Huko nyuma, waliingilia mchakato wa uchaguzi. Walifanya hivyo kwa kuidhalilisha Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) katika jukumu lake la kudhibiti na kusimamia mchakato huo. Usimamizi wa uchaguzi ulizidi kuvurugwa na Masheha na idara maalum, ambao walichukua maagizo kutoka kwa wakuu wa mikoa na wa wilaya. Mwisho wa yote hayo, huko Pemba majimbo ya uchaguzi yalipunguzwa na kuwa 18, wakati ya Unguja yaliongezwa na kufikia 32. Pemba ndiyo ngome ya CUF.

Kilichokuwa wazi zaidi ni kwamba katika uchaguzi wa mwaka 2000 yaliwasilishwa majina matano ya wagombea urais badala ya kwaida ya majina mawili. Katika kura za maoni, Amani Karume alitokea wa nne. Lakini Halmashauri Kuuu ya Taifa ya CCM, (NEC) ilimchagua Karume na kumwacha mgombea anayependwa na watu wengi, Dk. Mohamed Gharib Bilal, Waziri Kiongozi chini ya Salmin Amour. Hili limeweza kutokea kwa sababu tu, katika Halmashauri Kuu ya Taifa, Zanzibar ina thuluthi moja tu ya viti na kwa hiyo ushiriki wake si wenye kuamua kitu.

Zanzibar ina rundo la malalamiko. Kuhusu uchumi, inadai kuwa kuna mikataba ya kifedha isiyo ya haki ambayo inauua uchumi wake. Kwa mfano, inaeleza kuwa kuna utozwaji kodi mara mbili kwa bidhaa zinazoingizwa Tanzania Bara kutoka Zanzibar. Petroli na gesi ambavyo huenda vikavumbuliwa visiwani, vimeingizwa

Page 27: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Usuli wa Kihistoria 13

katika orodha ya mambo ya Muungano. Wakati dhahabu, almasi na tanzanait ambavyo vinapatikana Tanzania Bara havikuainishwa hivyo.

Katika midani ya kisiasa, kesi mbili zilifunguliwa kuitaka Mahakama Kuu ya Zanzibar kuutangaza Muungano kuwa haupo. Wadau wengine, wametaka yawepo majadiliano ya kuujadili upya Mkataba wa Muungano ili kuunda shirikisho kamili.

Hatimaye, uchaguzi wa mwaka 2000 ulimalizika kwa vurumai. Kundi la Watazamaji Uchaguzi la Jumuiya ya Madola liliuelezea uchaguzi huo kuwa ni wa aibu na wa kuidhihaki demokrasia. Na kama ilivyokuwa mwaka 1995, CUF ilikataa kuutambua na kugomea siyo Baraza la Wawakilishi tu bali na Bunge la Muungano vile vile. Maandamano na malalamiko ya upinzani yaliyofuatia mwezi January 2001 yalimalizika kwa kuruhusu ukatili wa polisi. Kiasi ya watu 2,300 walikimbilia Kenya na 30 walikufa. Watu walikamatwa kiholela na kupigwa kwa nia ya kuwanyamazisha watu waliofadhaika. Tukio hili lilivilazimisha vyama vya CCM na CUF kutafuta suluhisho la mvutano huu wa kisiasa. Kwa hiyo, wahusika wakuu wawili hawa walikubaliana kutia saini Muafaka 2, uliopendekeza utekelezwaji wa makubaliano yaliyolala ya Muafaka 1.9

Muafaka 1 ulifikiwa kwa usuluhishi wa Jumuiya ya Madola na ulitiwa saini tarehe 9 Juni 1999, kufuatia matatizo ya kisiasa yaliyojitokeza kutokana na uchaguzi uliokuwa na mgogoro wa mwaka 1995. Kimsingi, pande mbili zilizokuwa zikivutana

9 Maalim, Mahadhi J., “The State of Constitutionalism in Zanzibar” in Mute, L. (Editor), Constitutionalism in East Africa: Progress, Challenges and Prospects in 2004, Fountain Publishers, Kampala, 2007, pp. 29-50; na Oloka-Onyango, J. na Nassali, M., Constitutionalism and Political Stability in Zanzibar: The Search for A New Vision, A Report of the Fact Finding Mission organised under the auspices of Kituo Cha Katiba, The Friedrich Ebert Stiftung, Tanzania, 2003, pp.17-80.

Page 28: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

14 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

zilikubaliana kujenga moyo wa maelewano na kufuata demokrasia. Walikubaliana kuzipitia upya sheria za uchaguzi, kuijenga upya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), kutengeneza daftari jipya la wapiga kura, kutoa elimu kwa raia na kuifanyia marekebisho katiba. Kwa kuyatekeleza madhumuni haya, Serikali ya Zanzibar iliahidi kuhakikisha kuwa vyama vya siasa vya upinzani vinapewa fursa sawa na vyombo vya habari vya serikali. Mahakama ilikuwa ifanyiwe marekebisho ili kuhakikisha kuwa haipendelei upande wowote na iko huru. Na madai ya mali iliyoharibiwa kipindi cha baada ya vurumai za uchaguzi, yatatathminiwa na mtathmini huru.

Badala yake, chama cha CUF kiliahidi kumaliza mgomo wake wa kuligomea Baraza la Wawakilishi na Bunge la Muungano. Na kwa kivutio cha ziada, rais wa Zanzibar alikuwa awateue wanachama wawili wa CUF kuingia katika Baraza la Wawakilishi.

Kamati Kuu ya CUF iliuthibitisha mkataba huo mwezi Julai 1998. Lakini CCM ilichelwa kuuthibitisha. Kwa hiyo, waraka huo haukusainiwa mpaka baada ya mwaka mmoja. Ni wazi kuwa hapakuwa na nia njema na Muafaka 1 hakutekelezwa tena.

Kutokana na usuli huu, ilitegemewa kuwa mara hii pangelikuwepo na nia ya kisiasa na nia njema ya kutekeleza Muafaka 2 kikamilifu. Kuhusiana na hili, yemepatikana maendeleo kidogo. Merekibisho mawili ya katiba, marekebisho ya 8 na, 9 yamepunguza madaraka ya Mkurugenzi wa Uchaguzi, ambaye sasa inambidi afanyekazi chini ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar; madaraka yasiyokuwa na kikomo ya Masheha kwa uandikishaji wa wapiga kura yamepunguzwa; na sharti la ukazi nalo pia limepunguzwa kutoka miaka 5 hadi miaka 3. Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar iliundwa upya na kujumuisha wajumbe wawili watakaoteuliwa kwa ushauri wa upinzani rasmi; wawili walikuwa wateuliwe kwa ushauri wa kiongozi wa shughuli za serikali katika Baraza; Mkurugenzi wa Uchaguzi alikuwa ateuliwe na rais kwa ushauri wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar; na Tume ya

Page 29: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Usuli wa Kihistoria 15

Uchaguzi ya Zanzibar nayo ilipewa madaraka ya kuteua maafisa wa uchaguzi. Hatimaye, ofisi ya Mkurugenzi wa Kuendesha Mashtaka (DPP) ilianzishwa ili kuintenganisha serikali na chama tawala na ofisi ya Mkurugenzi wa Kuendesha Mashtaka.10

Maendeleo zaidi yamepatikana hivi karibuni. Karume na Maalim Seif Hamad, rais wa CUF, wamefanya makubaliano ya maana sana yanayoitwa Maridhiano. Makubaliano hayo ni pamoja na kufanyika kura ya maoni ifikapo mwezi Mei 2010 kuamua ikiwa iwepo serikali ya umoja wa kitaifa; CUF kumtambua Karume kuwa ndiye rais wa Zanzibar; na uteuzi wa wanachama wawili wa CUF kuwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na wa Bunge la Muungano. Zaidi ya yote hayo, Baraza la Wawakilishi limepitisha hoja ya kuifanyia marekebisho katiba ili kuunda wadhifa wa pili wa makamu wa rais ambao utashikiliwa na upinzani.

Maendeleo haya, yamepunguza sana hali ya wasiwasi na kutoaminiana kulikotokea kwa kutotekelezwa Muafaka 1. Wakati ujumbe huu ulipoitembelea Pemba, tuliwakuta watu wakiwa katika hali ya uchangamfu na matumaini kwa sababu ya Maridhiano. Maridhiano yalikaribishwa. Tayari yameshasaidia kupunguza hali ya wasiwasi kati ya wafuasi wa CCM na CUF na unaonesha dalili za kuwepo mchakato wa uchaguzi wa amani hapo baadaye. Hata hivyo, inaaminika kwa jumla kuwa bado kuna mengi yanayohitaji kufanywa. Kwa mfano, kuna haja kubwa kwa wanasiasa kuonesha nia yao ya kuyaunga mkono maridhiano.

Kutokana na machapisho yaliyoweza kupatikana, kitu kimoja kiko wazi. Hakuna hata mmoja aliyezungumzia kuvunjwa kwa Muungano. Kama kuna lolote lile, basi kuna manufaa makubwa ambayo pande zote mbili wanayakubali. Muungano umeinusuru Zanzibar na machafuko ya kisiasa wakati nyeti kabisa. Pamekuwepo na maslahi ya kiuchumi vile vile. Na kwa mujibu wa idadi ya watu

10 Maalim, op.cit.

Page 30: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

16 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

wake, Zanzibar inawakilishwa vyema, ikiwa haiwakilishwi kwa kiwango kikubwa zaidi, katika Bunge la Muungano. Hali ya jumla kwa hiyo, inaonesha kuwa Muungano utaendelea kuwepo, kama viongozi wataweza kukubali kuondoa maudhi madogo madogo.

Page 31: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

17

2Uundwaji na Historia ya

Muungano

Kuja kwa Muungano Kama tulivyoona katika Sura ya 1, Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar iliundwa tarehe 26 April 1964. Kuelekea mwisho wa mwaka 1964 iliamuliwa kuliacha jina hilo na kwa mujibu wa katiba ya mwaka 1965 nchi ilichukua jina lake la hivi sasa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (URT). Muungano huu, kwa hiyo, ulizileta pamoja nchi mbili tofauti zilizo huru za Tanganyika na Zanzibar. Muungano ulikuja mara baada ya uhuru wa Zanzibar mwezi Desemba 1963 na mapinduzi yaliyofuatia hapo ambayo yaliipindua serikali ya kwanza ya kisultani ya baada ya uhuru tarehe 12 Januari 1964.

Ujumbe huu ulipata tafsiri nyingi za tukio hilo, sababu na umuhimu wake. Ilikuwa ni jambo lililojulikana kuwa Muungano ulihusiana na umuhimu mkubwa, papara, na hata usiri na kutokuwepo kwa mashauriano na raia.

Zaidi ya hayo, kuna tafsiri zinazotoa maoni chanya za kuundwa kwa Muungano na kuna maoni ambayo hayafanyi hivyo. Wale wa kundi la awali wanauona Muungano kuwa ni tukio la kimaumbile, hatima ya ushirikiano wa watu wa Tanganyika na Zanzibar, ni hatua ya kuelekea kwenye Umoja wa Afrika.11

11 Fikra za kuwa Muungano ulikuwa ni kwa ari ya Umoja wa Afrika ni wazi kutokana na salamu za pongezi zilizopokelewa kutoka sehemu mbalimbali za Afrika. Salamu za pongezi zilipokelewa vile vile kutoka Kanada, Uingereza, Marekani n.k. Angalia Tanganyika Information Service, Munngano wa Tanganyika na Uguja, Dar-es-Salaam, 1964, pp..2-23.

Page 32: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

18 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

Wanasema kuwa watu wa nchi mbili hizi ni wamoja, na kwamba asilimia 90% ya watu wa Zanzibar ni weusi, wengi wao wakiwa na asili ya Tanganyika na kuhamia Zanzibar au walipelekwa huko wakiwa watumwa au watumishi wa majumbani au kujenga njia na kulima. Baada ya muda wakawa wao ndiyo wengi na Waarabu ni wachache.

Walieieza kuwa Karume, rais wa kwanza baada ya uasi au mapinduzi, alikuwa mtu wa bara aliyekwenda Zanzibar ili kufanyakazi melini na kuamua kuishi Zanzibar milele. Zaidi ya hayo viongozi wengi nchini Zanzibar walihamia Zanzibar miaka ya 1940 na 1950, na kwa hiyo kujenga kiungo cha kimaumbile kati ya watu weusi wa Zanzibar na bara.

Kwa upande mwingine, Sultani alionekana kuwa ni mtawala aliyeungwa mkono na elfu chache ya wafanyabiashara na wakulima wa Kiarabu waliokuwa wakitumia nguvukazi ya watumwa na kuwakandamiza watu weusi waliokuwa wengi. Kwa hiyo, wakati wa mapambano bara, na ukombozi Zanzibar, palikuwepo na ushirikiano. Kwa sababu serikali ya kikoloni ilijaribu kuyakandamiza mapambano, ulijengwa uhusiano kati ya bara na Zanzibar.

Uchambuzi huu unaionesha ASP kuwa ni chama cha watu weusi tu, kikiongozwa na watu weusi kama Karume na Zanzibar National Party ( ZNP) kuwa ni chama cha Waarabu tu.

Nyerere na Karume walifanyakazi pamoja. Ni kweli kuwa TANU kilimsaidia Karume na ASP katika mapambano yao. Lakini wakati Uingereza iliikabidhi uhuru Tanganyika kwa urahisi na kwa amani mwezi Desemba 1961, kwa kuwa Tanganyika haikuwa koloni bali ni eneo lililokuwa chini ya Udhamini, palikuwa na ukaidi wa kuipa uhuru Zanzibar na Nyerere alilazimika kuwasaidia watu wa Zanzibar kupata uhuru wao.

Katika jarida hili, hotuba ya Nyerere juu ya Muungano inazungumzia juu ya mabishano mbalimbali yanayohusiana na kuundwa kwa Muungano.

Page 33: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Uundwaji na Historia ya Muungano 19

Inasemekana kuwa TANU kilitoa kwa ASP misaada ya fedha na vifaa pamoja na misaada mingine. Inasemekana kuwa chaguzi za 1962 na 1963 ambazo zilielekea kwenye uhuru hazikuwa huru za za haki, na uhuru ulikabidhiwa kwa ZNP na Zanzibar Peoples Party ( ZPP), vyama vilivyokuwa vikifadhiliwa na Waarabu.

Watu wa Zanzibar walibaini kuwa mfumo huu usingeliweza kufanya kazi kwa maslahi yao; pangeliendelea kuwepo kwa utawala wa Waarabu. Kwa hiyo, mapinduzi ya 1964 yanaelezewa kuwa ni matokeo ya kukata tamaa kwa watu weusi walio wengi.

Baada ya kupinduliwa Sultani, liliundwa Baraza la Mapinduzi. Karume alichukua madaraka lakini alielewa kuwa haujakuwapo mfumo wa kisiasa wa kuidhibiti nchi. Kiongozi wa mapinduzi John Okello, alikuwa hakusoma na hakuwa na uzoefu wowote. Hali ilikuwa ni ya hatari na inasemekana kuwa Karume aliwasiliana na Nyerere kumwomba amsaidie kuiweka serikali yake madarakani. Kadhalika, Karume alitaka Tanganyika iichukue Zanzibar na kuifanya kuwa ni jimbo la Tanganyika. Nyerere kwa upande wake alichukua hadhari. Kimataifa, Nyerere hakutaka ionekane kuwa amaeichukua na kuimeza Zanzibar. Zaidi ya hayo, vita baridi vilikuwa vimepamba moto na Wajerumani wa Mashariki walikwishaingia Zanzibar kitendo kilichoikera Ujerumani ya Magharibi na nchi za Magharibi kwa jumla. Nyerere kwa hiyo, hakutaka vita baridi vikaribie mbele ya mlango wake.

Katika mazungumzo yaliyofuatia kati ya Nyerere na Karume na washauri wao, Muungano ulikubaliwa lakini Nyerere alikataa kumezwa kabisa kwa Zanzibar. Ndani ya Muungano, Zanzibar itabakia na utambulisho wake pamoja na serikali yake mpaka hapo mfumo sahihi wa Muungano utakapotengenezwa. Kwa hivi sasa hapajakuwa na muda; hata wanasheria hawakuwa na muda wa kutengeneza nyaraka zilizoandikwa kwa uangalifu, na kusema kweli, haujakuwepo muda wa kuwashauri wananchi kwa vile hili lingelitoa nafasi kwa vikundu mbalimbali, pamoja na wale waliopinga Muungano.

Page 34: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

20 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

Mawazo na tafsiri nyingine za tukio hilo ambazo zinaupinga muungano, zinauona Muungano kuwa umekubaliwa bila ya kufikiri na kwa mabavu.

Hitilafu baina ya nchi mbili zinaainishwa:

Tanganyika ilipata uhuru wake muda mrefu, tokea mwaka 1961. Ilikuwa na utulivu, na imara chini ya uongozi wa TANU. Kinyume yake, Zanzibar ilipata uhuru wake miezi michache iliyopita. Ilikuwa ni nchi iliyogawanyika sawasawa. Mapinduzi yametokea mwezi mmoja tu tokea kupata uhuru, yamefanywa na watu wasiosoma.

Ilikuwa katika halii ndipo Uingereza na Marekani zilipoisinikiza Tanganyika kuimeza Zanzibar. Zanzibar ilikuwa ni tishio kwa utulivu wa kanda nzima na nchi za Magharibi zilijihisi hazimo katika usalama kwa sababu ya mawazo ya mrengo wa kushoto ya Zanzibar. Nyerere alikuwa na wasiwasi na Cuba iliyokuwa uani kwake. Karume alitekwa nyara na kuingia kwenye Muungano. Muungano umeundwa mnamo siku 100 za mapinduzi, bila ya kuwashauri wananchi. Hata Baraza la Mapinduzi halikuhusishwa wala halikuoneshwa nyaraka husika. Wengine wamesema kuwa robo tatu ya Baraza la Mapinduzi waliupinga Muungano.

Wakati ilikuwa ni mtindo kusema kuwa Karume aliukaribisha Muungano kwa mikono miwili, (Nyerere mara nyingi hunukuliwa kuwa alisema “Karume hakuufikiria vizuri”), msemo huu unasisitiza kuwa nyaraka za siri za Uingereza na Marekani zinaonesha kuwa vilitumika vitisho; kuwa, kusema kweli mapinduzi yalikuwa dhaifu, kuwa ulikuwepo mvutano ndani ya ASP na vile vile kati ya ASP na Umma Party na kuwa Karume alikuwa akihofia wadhifa wake. Katika hali hii, kabla ya kusaini nyaraka za Muungano, Nyerere alitishia kuwa atawaondoa askari polisi waliotoka Tanganyika ambao walikuwapo Zanzibar. Ilithibitishwa kuwa hata Shirika La Ujasusi

Page 35: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Uundwaji na Historia ya Muungano 21

la Marekani (CIA) lilishangazwa; halikudhani kuwa Muungano ungelifanikiwa.12

Kwa hiyo, mbali ya yale mawazo kuwa Karume ndiye aliyekuwa na utashi wa Muungano, hapa mtu ataelewa kuwa vitisho vilitumika katika kuundwa kwa Muungano huo. Inaelezwa kuwa hili ni sawa na ukweli kuwa wakati wote wa mapambano ya kupigania uhuru, ASP haikuliweka katika ajenda yake au ilani yake ya uchaguzi suala la kuziunganisha Tanganyika na Zanzibar. Kinyume yake, walikuwa wakikataa, tuhuma za nia na mipango ya kuiunganisha Tanganyika na Zanzibar. Hii pia inalingana na tabia ya baadaye ya Karume iliyoonesha ukaidi, na hata kukataa utekelezwaji wa makubaliano ya Muungano, msimamo uliochukuliwa na Baraza la Mapinduzi na ASP.

Maelezo haya hata hayakubaliani na uchambuzi wa kijamii na kikabila ulioelezwa katika maelezo ya awali. Wao wanaiangalia hali ya mchanganyiko wa watu wa mataifa mbalimbali ya Zanzibar kwa jumla, na ukweli kuwa Pemba ambako ZNP walikuwa na wafuasi wengi, kulikuwa na watu weusi wengi kuliko Waarabu.13

Wakati watu wengi wanaukosoa mchakato wa kuundwa kwa Mungano kwa kushindwa kuwashirikisha wananchi, mmoja katika tuliowahoji alisema kuwa huu ulikuwa ndiyo mtindo wa dunia nzima. Kwamba muungano ni matokeo ya siasa za ngazi ya juu, matokeo ya watawala kukubaliana, mashirikisho husababishwa na

12 Waliyoyafanya Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) na Wizara ya Mambo ya nje katika kuundwa kwa Muungano si ya kudharauliwa hata kidogol. Amrit Wilson anaionesha Marekani iliyoingiwa na wazimu ikijaribu kila njia: ikiilazimisha Uingereza kuivamia Zanzibar, ikimlazimisha Kenyatta kuunda muungano; Uganda na Kenya kupeleka majeshi; ikitaka kuundwa kwa Shirikisho la Afrika Mashariki n.k Angalia Amrit Wilson, US Foreign Policy and Revolution, The Creation of Tanzania, London, Pluto Press, 1989. Angalia vile vile Petterson, op. cit., p.207.

13 Babu anafanya uchambuzi wa matabaka wa kina wa vyama na wa hali yenyewe katika A. M. Babu, “The Background to the Zanzibar Revolution katika Amrit Wilson US Foreign Policy and Revolution, pp.141-158.

Page 36: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

22 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

maslahi ya kitaifa kwa hivyo kwa kawaida hayahusu ushiriki wa raia. Hili hutokea kwa nadra. Kinachosababisha muungano ni mamlaka au hofu ya vitisho. Muungano wa hiari uliosababishwa kwa kujidai tu utakuwa dhaifu sana.

Maoni ya mtu tuliyemuhoji Zanzibar yalivutia hisia za wengi juu ya uundwaji na historia iliyofuatia ya Muungano: “Tulisikia habari za kuundwa kwa Muungano katika Radio Tanganyika; hatukushauriwa, kila mtu alishtushwa … Muungano ni vurugu iliyoandaliwa, mkono wa kushoto haujui wa kulia unafanya nini”.

Misingi ya Uhalali na Muundo wa Muungano Mkataba wa Muungano ndiyo unaoupa uhalali Muungano. Mara kwa mara watetezi wa mkataba huu wameuelezea kuwa ni mkataba wa kimataifa. Kwa mujibu wa utaratibu wa sheria zisizoandikwa, utengenezwaji wa mkataba ni kwa ridhaa ya mkuu wa serikali na mhimili wa utendaji wa serikali, lakini utekelezaji kwa maana ya kuridhia ni suala la bunge.

Kwa hiyo, ili Mkataba wa Muungano uweze kufanya kazi, ingelibidi uridhiwe na nchi zote mbili, Tanganyika na Zanzibar. Inasemeka kuwa kilikuwepo kipengele kwenye Mkataba wa Muungano kilichosema hivyo. Mara kwa mara, inadaiwa na kila mtu, pamoja na wanazuoni, kuwa hapajakuwepo na ridhaa yoyote kwa upande wa Zanzibar.14 Hakuna ushahidi wa sheria yoyote huko Zanzibar inayoridhia mkataba huo. Ushahidi pekee wa kuridhia ulitokea kwenye Gazeti la Serikali la Tanganyika na kutiwa saini na mwanasheria wa Serikali ya Tanganyika.

Inadaiwa kuwa Nyerere alimtaka mwandishi wake wa sheria aandike sheria kama hiyo kwa ajili ya Zanzibar lakini hakuna sheria

14 Kwa upande mwingine, Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA), linadai kuwa suala la kuridhia huko Zanzibar liliungwa mkono na thuluthi moja tu ya wajumbe wa Baraza la Mapinduzi la Zanzibar. Angalia Amrit Wilson, op cit, p.115.

Page 37: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Uundwaji na Historia ya Muungano 23

kama hiyo iliyoonekana katika gazeti la serikali na hakuna tangazo lolote la kisheria kuhusu hilo.15

Kwa hiyo, Muungano, kwa mujibu wa wanavyoamini watu wengi, ulikuwa hauna msingi wa kisheria tokea mwanzo kwa kuwa wakati mkataba ulitiwa saini na Karume, haukuridhiwa. Kwa sababu hiyo, Muungano upo kwa uhalisi waku tu lakini si kwa mujibu wa sheria. Inasemekana pia kuwa Muungano umo katika migogoro ya kikatiba lakini wahusika hawataki kukiri hivyo.

Kwa hiyo, maamuzi yalichukuliwa kwa msingi wa kuaminiana na haraka za kisiasa na si kwa mujibu wa sheria na katiba. Mchakato wa kuunganisha haukwenda kikatiba; yalikuwa ni makubaliano ya kisiasa kati ya Nyerere na Karume na hata mkataba wa Muungano ulikuja kama wazo la baadaye. Uliandaliwa kabla ya ukweli halisi.

Lakini kuna wale ambao wangelipenda kuliangalia suala hili kwa upole; kwamba mtu asijihangaishe katika kutafuta suala la uhalali, kwamba Muungano umeundwa kwa hamasa za umoja wa Afrika kwa madhumuni ya kuleta mshikamano na siyo uhalali. Lakini

15 Ujumbe uliwasiliana na Profesa D.W. Nabudere juu ya upande wa kisheria wa kuundwa kwa Muungano. Alisema kuwa alialikwa na Rashid Salim, Ali Mafudh na A.R.M. Babu (ijapokuwa wakati huo alikuwa Indonesia), wote watatu walikuwa wanachama wa Umma Party. Aliambiwa auangalie Mkataba wa Muungano ambao ulikuwa haukutiwa saini. Alimshauri Karume kwa kumwambia kuwa mkataba huo ni tamko la kisiasa ambalo lingeliipelekea Zanzibar kupoteza hadhi yake ya kiutawala na kwamba hilo lilihitaji uamuzi wa kisiasa na kwamba watu wa Zanzibar ni lazima walielewe hilo vizuri. Karume alijibu kuwa wanayaelewa madhumuni ya Muungano. Bara isingeliweza kuwashinda kisiasa kwa sababnu walikuwa na uwezo wa kuwashawishi. Baada ya mazungumzo haya Nyerere na Roland Brown walikuja chumbani na Nyerere alimtaka Karume kuthibitisha nia yake kwa Muungano, jambo ambalo alilifanya.

Nje walikuwepo waandamanaji kutoka chama cha Umma Party waliodai kuwa Mkataba usitiwe saini mpaka hapo Babu atakaporudi nchini. Siku ambayo Babu alirudi kutoka Mashariki, Nabudere alikutana naye uwanja wa ndege na kumwelezea maoni yake juu yale aliyoambiwa na Karume (Nabudere). Babu alisema kuwa anakubaliana na Karume.

Page 38: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

24 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

hili, linaweza vile vile kuwaunga mkono wale wanaotuhumu kuwa Muungano, siyo kwa kuundwa kwake tu na msingi wake wa asili wa kisheria, ulikuwa ukiendeshwa na bado unaendeshwa kama ni mfumo wa kisiasa na si wa kikatiba.Pametolewa vile vile mawazo makali kuhusu uhalali na uendeshwaji wa Muungano kuhusiana na msingi wa uhalali wake. Inadaiwa kuwa, na ichukuliwe kuwa, kwa sababu ya mabishano tu, Mkataba wa Muungano ungelikuwa umeridhiwa, umekiukwa mara kadha na umekuwa hauna maana. Baadhi ya ibara zilizokiukwa zitatajwa:

Ibara 3 inataka kuwepo kwa a. katiba ya muda kwa mwaka mmoja. Ilibidi iwepo tume na Bunge la Katiba na michakato mingine ya kuandaa katiba ili kutangaza rasmi katiba ya kudumu ya Muungano. Hili halikufanyika. Badala yake kabla ya kumalizika kipindi cha muda, uliwasilishwa mswada katika Bunge la Muungano kurefusha kwa muda usiojulikana, hicho kipindi cha muda.

Katiba ya b. Muungano ya hivi sasa ina sura nzima juu ya namna ya kuitawala Zanzibar wakati Mkataba wa Muungano unaeleza juu ya kuitawala Zanzibar kwa mujibu wa sheria za Zanzibar. Hatua hii inaufanya utawala wa Zanzibar uweze kufanyiwa marekebisho na Muungano.

Uamuzi wa upande mmoja wa kuyaongeza c. mambo ya Muungano katika Katiba ya Muungano. Wakati haya ni mambo yaliyomo katika Jedwali la Mwanzo, Mkata wa Muungano haukusema juu ya kuwepo kwa marekebisho kama hayo. Kwa kuwa huo ulikuwa ni mkataba kati ya nchi mbili zenye kujitawala marekebisho hayo ingelibidi yafanywe na wao wenyewe. Suala hili nyeti linaelezwa kwa urefu zaidi katika sura nyingine.

Inatolewa hoja kuwa, ukiukwaji huu na ukiukwaji mwingine, utadhoofisha uhalali wowote wa kudhani wa Muungano. Kwa namna yoyote ile, mtazamo wa kifidhuli wa suala zima hili ndiyo unaoupa

Page 39: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Uundwaji na Historia ya Muungano 25

sura Muungano tokea kuanza kwake, kwa sababu kuhusiana na Tanganyika, ambayo inachukuliwa kuwa ndiyo iliyoridhia Mkataba wa Muungano, kumbukumbu za majadiliano ya Bunge la Tanganyika zinaonesha kuwa mjadala juu ya suala muhimu kama hili (Mkataba wa Muungano) haukuchukua zaidi ya nusu saa.

Hali ya shaka na wasiwasi inalizunguka suala la uhalali na kufuata katiba la Muungano kwa sababu ya mambo mawili yanayohusiana. Imekuwa ikisemwa mara kwa mara kuwa Mkataba wa Muungano ulikuwa ni waraka wa “siri” ambao haukujulikana na viongozi wengi, pamoja na bunge na wananchi. Inasemekana kuwa hakuna uhakika kama nakala halisi ya Mkataba huu ipo na hakuna juhudi zozote zilizochukuliwa kuitafuta.

Linalohusiana kwa karibu zaidi na hili ni kwamba kuna tuhuma kuwa suala la Mkataba wa Muungano ni mada ambayo ni mwiko kuizungumza na kwamba zimekuwepo juhudi za makusudi za kuzuia mjadala juu ya mkataba huu. Indaiwa kuwa Serikali ya Muungano ingelipendelea kuona kuwa Mkata huu unasahauliwa. Katika Katiba ya Muda ya Muungano ya 1995, Mkataba huu ulioneka kuwa ni jedwali la katiba lakini baadaye uliondolewa kabisa katika Katiba ya Muungano.

Kutokupatikana huku kwa nakala halisi ya Mkataba wa Muungano, ile dhana kuwa Mkataba huu ni siri na mada iliyo mwiko kuizungumza, ni jambo la kutia uchungu na linasababisha matatizo, kama wengi walivyosema. Hii inaondoa imani na kuyazidisha matatizo yanayohusiana na Muungano. Kusema kweli hilo ndilo tatizo ambalo hata wanasheria wanauliza ni nini msingi wa Muungano – Mkataba wa Muungano au katiba? Hili linaweza kuwa ni swali lisilokuwa na jibu lakini ni swali linaloonesha kiasi cha kutokuwepo uhakika juu ya uhalali wa kisheria na kikatiba wa Muungano. Ile kuwa huu ni mkataba wa kimataifa na kwa hiyo umesajiliwa na Umoja wa Mataifa huko New York hakuliondoi tatizo hilo.

Page 40: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

26 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

Muundo wa MuunganoMuundo wa Muungano ni wa serikali mbili na mamlaka tatu tofauti za sheria. Mkataba wa Muungano unaelezea kuwepo kwa Serikali ya Muungano na serikali ya Zanzibar. Ya Muungano ina uwezo wa kisheria wa namna mbili: Wa mambo ya Muungano, na mambo yasiyo ya Muungano ya bara. Serikali ya Zanzibar ina uwezo wa kisheria kwa Mambo ya Zanzibar ambayo si ya Muungano.

Hakuna vipengele kuhusu serikali ya Tanganyika; hakuna Rais au bunge liliopo kwa ajili hiyo.

Hakuna uhakika juu ya ni muundo gani wa Muungano Mkataba wa Muungano uliufikiria: Mkataba huo ulifikiria kuwepo kwa serikali ya muungano, ya shirikisho, ya muungano wa majimbo au utaratibu wa ushirikishwaji? Wengi wanakubali kuwa Muungano si mojawapo ya mifumo hii. Wanauelezea kuwa ni sui generis. Ni muungano kwa baadhi ya mambo lakini si muungano kwa baadhi ya mambo. Baadhi ya watu wanuelezea “upekee” huu kuwa ni kwa sababu ya kutotaka kuudhiwa au kuulizwa chochote juu ya Muungano huo.

Zimetolewa sababu kadha kuhusu muundo huu. Moja ni kwa sababu ya hali ya dharura iliyokuwepo katika kuunda Muungano. Hapajakuwa na muda, hata kwa wanasheria kuzishughulikia nyaraka. Nyerere alikuwa ameshughulika na kutaka kuulinda utambulisho wa Zanzibar kwa kuwa na serikali yake yenyewe. Kwa vyovyote vile, hii ilikuwa ni hatua ya muda tu na kwa mujibu wa Mkataba wa Muungano, ilikuwa iundwe tume ambayo ingelitengeneza muundo wa kudumu; hilo halikutokea.

Wengine wanauelezea muundo huu kuwa ni matokeo ya tofauti zilizokuwepo kati ya mtazamo wa Nyerere na ule wa Karume kuhusiana na mustakabali wa Muungano. Inasemekana kuwa, wakati Nyerere hakuta kuingilia mambo ya Zanzibar, kwa mfano kuachilia ukiukwaji wa haki za binadamu uendelee huko, tegemeo lake la mwisho lilikuwa ni Muungano kamili mnamo kipindi cha

Page 41: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Uundwaji na Historia ya Muungano 27

miaka 50 ya kuundwa kwa Muungano huo. Kwa sababu hiyo, kwa kipindi cha muda mfupi na muda wa wastan aliona kuwa ni muhimu asiimeze Zanzibar, wakati kwa upande mwingine aliona kuwa serikali ya Tanganyika si muhimu na ingelikuwa na gharama kubwa. Mkakati huu wa serikali mbili kuelekea kwenye serikali moja, inasemekana kuwa unadhihirika kwenye mtazamo na hatua ambazo Nyerere amezichukua katika muda fulani. Kuchukia kwake serikali tatu, kukataa kwake kuifufua serikali ya Tanganyika na hasa hatua ya kuviunganisha TANU na ASP, kufukuzwa kwa Jumbe kuhusiana na jaribio lake la kutaka kuanzishwa serikali tatu; na uingiliaji binafsi wa Nyerere na vitisho vya kuwafukuza kundi la watu 55, lililokuwa likidai kurudishwa kwa serikali ya Tanganyika.

Kinyume na hili, inasemekana kuwa Karume aliuona Muungano kama waraka wa bima utakaomlinda pindi pangelitokea uvamizi kutoka ndani au nje. Ingelikuwepo himaya ya chombo kikubwa. Nguvu hii ambayo ingelipambana na jaribio la kurudi kwa Sultani au changamoto yoyote kutoka kwa wale waliokuwa na mawazo ya mrengo wa kushoto ndani ya Baraza la Mapinduzi, ingelikuwepo milele. Nia ya Karume ilikuwa ni kuwa na Muungano kwa kipindi cha miaka 10 tu. Inaelezewa kuwa alichukua hatua ya kuchapisha sarafu ya Zanzibar – dola ya Zanzibar. Ukaidi wake wa baadaye na kukataa kwake kuutekeleza Muungano kunachukuliwa kuwa ni uthibitisho wa msimamo wake.

Ni misimamo hii iliyotofautiana kati ya viongozi hawa wawili kuhusu muundo na maumbile ya baadaye ya Muungano ndiyo iliyosababisha kuwepo kwa mfumo huu mkubwa, ilitolewa hoja.

Muundo wa serikali mbili ni tatizo lililovumiliwa kwa muda mrefu na kila siku lipo katika ajenda. Linachukuliwa kuwa ni moja ya matatizo makubwa ya Muungano. Kutokuwepo utulivu wa kisiasa na vurugu za Zanzibar inaonekana kuwa kunatokana na muundo wa Muungano. Kero za muungano zinaonekana kuwa za siku nyingi katika muundo huu ulioanza sivyo tokea mwanzo. Lilo

Page 42: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

28 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

kubwa zaidi ni kwamba, watu wengi wanadhani kuwa muundo wa hivi sasa hauwezi kutatua matatizo haya.

Kiini cha suala hili ni kwamba mchanganyiko wa madaraka mawili ya Serikali ya Muungano na kutokuwepo kwa serikali ya Tanganyika kunasababisha kuwepo kwa tafsiri mbili tofauti. Ya kwanza ni ya takriban Wazanzibari wote, ijapokuwa ni ya idadi kubwa ya watu bara vile vile.

Mawazo yanayotawala ni kwamba, mchanganyiko huu unaigharimu Zanzibar kwa vile Zanzibar imepoteza utawala wake katika Umoja wa Mataifa (UN), Umoja wa Afrika (AU) na katika mahusiano yote ya baina ya pande mbili na baina wa pande nyingi, ijapokuwa ina wadhifa wa dola kama vile bendera na nyimbo ya taifa. Katiba na muundo huu havitilii maanani maslahi ya Zanzibar ikiwa ni sehemu ya Muungano. Zanzibar haiwezi kufanya miamala, haiwezi kufanya majadiliano au kujadiliana na mwenzi wake, Tanganyika ambayo imekufa, wakati Zanzibar haikuwa eneo lililoshindwa la Tanganyika, tafauti na Ireland ya Kaskazini, Muungano unaoonekana kuwa ndiyo ulioigwa.

Kwa mawazo haya, Muungano unachukuliwa kuwa ni upanuzi wa utawala wa Tanganyika, serikali ya Muungano, kimsingi ikiwa ndiyo serikali ya Tanganyika iliyojipanua kushughulikia baadhi ya mambo ya Zanzibar. Kwa hiyo, Zanzibar imeathirika wakati Tanganyika imefaidika na kuuondoa utawala wa Zanzibar. Hii inaonekana katika mambo mengi. Nyimbo ya taifa ya Muungano ndiyo ile ile ya Tanganyika. Katiba ya Tanganyika imefanyiwa marekebisho na kuitwa katiba ya muda. Baadaye, katiba ya Muungano ikaiondoa katiba ya Tanganyika na wafanya kazi wa serikali wa Tanganyika wakapandishwa hadhi na kuwa wafanyakazi wa serikali ya Muungano; na hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa mahakama vile vile.

Mtazamo huu unafahamika kuwa ni mtazamo wa kudhibitiwa na kaka, jambo ambalo Wazanzibari wanalichukia. Muundo wa

Page 43: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Uundwaji na Historia ya Muungano 29

serikali mbili unaeleweka kuwa ni ule wa baina ya nchi kubwa na nchi inayoitawala.

Kutokana na mtazamo huu, jehi na polisi wanaonekana kuwa ni vibaraka wa Muungano walio tayari kuulazimisha Muungano kwa Zanzibar.

Nyerere kuiua serikali ya Tanganyika jambo ambalo ni dhahiri silo lililosababisha kuwepo kwa Mkataba wa Muungano, haya hayakuwa maendeleo chanya. Badala yake, inasemekana kuwa katika huu muundo wa serikali mbili, kuna serikali iliyojificha inayofanya kazi kwa maslahi ya bara kwa kuidhulumu Zanzibar.

Hilo lilikuwa ndilo tatizo na kwamba tatizo hilo lililetwa katika Bunge la Muungano (kama Zanzibar) ni nchi. Waziri Mkuu ilimbidi atoe taarifa kufafanua kuwa Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano, kwamba si dola tena, kauli iliyowakera Wazanzibari wengi. Baadaye, rais katika hotuba yake alimaliza mjadala juu ya suala hili. Hata hivyo, tatizo kubwa ambalo ujumbe huu ulielezewa na mmoja wa waliohojiwa Pemba, ambalo linatokana na kutoitambua Zanzibar kuwa ni nchi huru, ni kuwaachilia bila ya kuwaadhibu wale wanaoweza kutenda “vitendo vya jinai” dhidi ya serikali ya Zanzibar. Katika kesi ya SMZ dhidi ya Machano Khamis Ali na wengine16 iliamuliwa kuwa Zanzibar si nchi. Baadhi ya watu wameelewa kutokana uamuzi huu wa mahakama kuwa haitawezekana kuwashtaki wale wanaokula njama dhidi ya serikali ya Zanzibar kwa kosa la uhaini.

Kwa upande mwingine, kuna wale walio bara wanaodhani kuwa muundo wa serikali mbili unagharamiwa na bara. Wanaeleza kuwa Zanzibar haikupoteza mamlaka yake ya kinchi, ina serikali, bunge ( Baraza la Wawakilishi), na rais, wakati bara imepoteza utawala wake. Wanaeleza kuwa mpaka mwaka 1999 watu wa bara walihitaji pasi ya kusafiria kuingia Zanzibar lakini kwa Wazanzibari haikuwa hivyo kwa kuja bara.

16 Criminal Application Na. 8 ya 2000, TZ CA 1.

Page 44: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

30 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

Wanazungumzia juu ya idadi ya Mawaziri kutoka Zanzibar katika serikali ya Muungano wakati hakuna Wabara katika serikali ya Zanzibar, na Wabunge kutoka Zanzibar katika Bunge la Muungano, wakati hakuna Wabara katika Baraza la Wawakilishi la Zanzibar. Kadhalika, kwa mujibu wa Jedwali la Pili la katiba ya Muungano mambo 8 yanahitaji wingi wa thuluthi mbili wa Wabunge wa bara na wingi wa thuluthi mbili wa Wabunge wa Zanzibar, ijapokuwa mengine si mambo ya Muungano.17

Ni kwa baadhi ya sababu hizi ndipo kundi la watu 55 la viongozi wa bara lilipodai kufufuliwa kwa serikali ya Tanganyika; na hisia hizo bado zipo. Inasemwa kuwa Zanzibar haiwezi kuwa na mkate wake na kuula wakati huo huo – ama uwepo muungano au usiwepo, lakini siyo nchi chotara.

Masuala mengine yanayohusiana na muundo wa Muungano yalielezewa vile vile. Ilielezwa kuwa baadhi ya viongozi serikalini hawauelewi muundo wa Muungano, k.m serikali mbili na mamlaka tatu tofauti za sheria. Hii inasababisha mtafaruku unaochangiwa na katiba yenyewe. Imeelezwa kuwa, wakati Ibara 4 ya katiba haielezei kuwepo kwa serikali mbili na mamlaka tatu tofauti za sheria, sehemu nyingine za katiba zinachanganya mambo na kuzifunikafunika tofauti.

Pamoja na hili, ni taswira kuwa muundo huo umekuwa ukiendeshwa kama mfumo wa kisiasa na si wa kikatiba. Uendeshwaji wa kisiasa wa Muungano umedhihirishwa kwa kuondolewa Jumbe. Inasemekana kuwa aliondolewa siyo kwa sababu alikosea kikatiba lakini kwa sababu aliteleza kisiasa. Mfumo wa kisiasa wenyewe unaudhalilisha utaratibu wa kudhibitiana, utaratibu ambao ungelipelekea kuwepo kwa usimamizi bora wa Muungano.

Usimamizi wa kisiasa na si ule wa kikatiba wa muundo huu, umo katika hali ngumu kwa sababu ya kipindi cha mpito kutoka katika

17 Ibara 98(1) (b) na Jedwali la pili na Orodha ya Pili, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1997 (Toleo la 1997 )

Page 45: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Uundwaji na Historia ya Muungano 31

mfumo wa serikali ya chama kimoja kuelekea kwenye mfumo wa vyama vingi. Inaelezwa kuwa hapo zamani, (kabla ya 1992) suala la muungano na muundo wake lingeliweza kusuluhishwa kwa kupitia kwenye muundo wa chama. Juu ya hivyo, mwaka 1992 mfumo wa vyama vingi ulianzishwa bila ya uchambuzi wa kina wa muundo na sheria. Badala ya kubadili kabisa na kuanzisha utaratibu mpya na katiba mpya, pamekuwepo na mabadiliko madogo madogo yaliyofanywa kwa hadhari katika katiba, ili kukidhi mfumo wa vyama vingi wakati mfumo wa msingi ni uleule wa serikali ya chama kimoja. Kuhusiana na hili, inaelezwa kuwa Tume ya Nyalali ya 1990/91 iliyoupendekeza mfumo wa vyama vingi, ilipendekeza pia mfumo wa serikali tatu lakini wakati serikali ililikubali la awali ililikataa la pili.

Na si kama kwamba viongozi hawayaelewi matatizo. Tume zote mbili, ya Nyalali na y a Kisanga ziliyaainisha matatizo ya kimuundo ya Muungano. Tatizo hapa si kutoelewa ila kwa mawazo ya wengi, ni kwa sababu ya kutokuwepo kwa nia ya dhati katika kutatua matatizo na katika mwenendo wa mchakato mzima: Kuna uzito upande wa uongozi. Mambo hayashughulikiwi mpaka linapotea tatizo kubwa. Ile hali ya kuridhika kuwa Muungano utaendele kuwepo kwa sababu ya msukumo wake wa kihistoria lazima ibadilike na nafasi yake ichukuliwe na uchambuzi wa kina na nia ya kutatua masuala mbalimbali.

Urithi huuu umepelekea kuwepo tuhuma kuwa macahafuko ya kisiasa ya Zanzibar ni matokeo ya muundo wa Muungano kwa sababu CCM lazima ihakikishe kuwa inatawala pande zote mbili za Muungano kwa sababu muundo wake hauwezi kuruhusu kuwepo kwa serikali za “kutoelewana”. Suluhisho moja la tatizo hili ni mfano wazi wa mtanziko. Kule kuondolewa kwa utaratibu wa rais wa Zanzibar kuwa makamu wa rais kulikofanya mwaka 1992 na kuanzishwa kwa utaratibu wa kuwa na mgombea mwenza kumesababisha matokeo yasiyoridhisha bila ya kutatua tatizo lolote.

Page 46: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

32 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

Wazanzibari wengi hawalifurahii hili. Kushushwa hadhi kwa rais wa Zanzibar na kuwa mjumbe asiye rasmi wa Baraza la Mawaziri la Muungano kunatazamwa kwa chuki hiyo hiyo. Suala la itifaki linalohusiana na Makamu wa rais wa Muungano kumtangulia rais wa Zanzibar, kama rais wa Zanzibar alivyokataa kuapishwa na Rais wa Muungano na kuapishwa na Jaji Mkuu, zote hizi ni ishara za dosari kubwa za mtazamo wa kizembe wa kuyashughulikia masuala ya muundo wa Muungano.

Kuna malalamiko mingine mengi kuhusu muundo. Mchakato wa kutunga sheria unadhihirisha hilo. Ibara 98 ya katiba inasema kuwa sheria za mambo ya Muungano zinapitishwa kwa wingi wa kawaida lakini wapo Wabunge 64 kutoka Zanzibar katika jumla ya Wabunge 324. Kwa hiyo, kwa kawaida, bunge hupitisha sheria kinyuma cha matakwa ya Zanzibar. Kwa mfano sheria ya uvuvi kwenye maji ya kina kirefu ambayo upinzani wa Zanzibar haukuzuia kupitishwa kwa sheria hiyo. Utekelezaji wake umechukua miaka 8 kwa sababu ya kutokuwa tayari kwa Zanzibar kuitekeleza sheria hiyo.

Kutokuwepo uiano huku kwa idadi ya wabunge kunapingwa na Zanzibar kwa misngi kuwa wao ni wabia wawili walio sawa. Katika Bunge la Muungano, Zanzibar inajihisi imezidiwa na bara.

Lile pendekezo kuwa utaratibu mzuri wa shirikisho utatatua matatizo, baadhi ya wakati linapingwa na mawazo kuwa utaratibu kama huo hautokuwa mzuri pale ambapo pande mbili za kitu kimoja, kwa ukweli, haziko sawa. Upande mmoja mduchu (wenye hasira) upande mwingine mkubwa usiotaka mabadiliko.

Kuna manung’uniko vile vile kuhusu baraza la mawaziri la Muungano. Inasemekana kuwa wamo Wazanzibari 4 tu katika baraza la mawaziri la watu 31, na kusema kweli, mawaziri 4 hao hawaiwakilishi Zanzibar. Kwa hiyo Baraza la Mawaziri la Muungano linapitisha sera kinyume na matakwa, mahitaji na maslahi ya Zanzibar na hakuna mfumo wa utaratibu wa kuiwezesha Zanzibar kuchangia.

Page 47: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Uundwaji na Historia ya Muungano 33

Matatizo ya utendaji yametajwa vile vile. Kwa mfano, wizara zinazoshughulikia mambo ya Muungano hazina ofisi Zanzibar. Lakini zamani alikuwepo Waziri Mdogo wa Muungano aliyekuwepo Zanzibar. Hili linasababisha matatizo kwa watu wa Zanzibar kuweza kuzifikia ofisi za Muungano. Umetolewa mfano wa nafasi za kwenda kusoma.

Kwa upande mwingine, imeelezwa kuwa baadhi ya asasi za Muungano hukataliwa zinapokwenda Zanzibar. Hili linahusu Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) na Tume ya Mawasiliano iliyoanzishwa mara tu baada ya majadiliano.Nukuu ifuatayo kutoka kwa mhojiwa mmoja, inaonesha aina ya hisia walizonazo watu juu ya muundo wa sasa:

Tunapowachagua Wabunge kwenda Dodoma wanazungumza masuala machache sana juu ya Zanzibar. Wanashughulika na bara. Tunatumia pesa na muda mwingi kwa ajili ya uchaguzi lakini wanayoyafanya ni machache; wanashughulikia masuala machache sana yanayohusu Zanzibar, mambo kama vile ulinzi. Tunahitaji usawa kati ya Zanzibar na bara kwa sababu nchi mbili hizi ni wabia sawa katika Muungano.

Uhalali wa MuunganoKatika sehemu hii, mitazamo ya baadhi ya watu juu ya Muungano inaangaliwa. Hii ni pamoja na faida na hasara za Muungano na kukubalika kwake.

Siasa na Serikali

Kuhusu asasi za kisiasa na za kiserikali na michakato yake, Wazanzibari wametoa maoni mengi juu ya uhalali wa Muungano kama wanavyouona wao. Wamesema kuwa wao hwaonekani kuwa ni nchi, ijapokuwa wao ni nchi na si mkoa tu kama vile Tanga. Wamesema kuwa wakati Muungano unahusisha nchi mbili rais wao hana jukumu lolote.

Page 48: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

34 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

Wameelezea hali ya kutokuwepo usawa katika mgawanyo wa kazi katika serikali ya Muungano. Wapo mabalozi watatu tu kutoka Zanzibar; kwa hiyo inapojiri mambo ya nje, Zanzibar inajihisi kuwa imetengwa. Mabalozi wa kutoka bara wanafanya kazi kwa maslahi ya bara. Wameeleza vile vile kuwa kuna Wazanzibari wachache wanaofanya kazi katika ofisi za ubalozi nchi za nje.

Katika jeshi la polisi, hapana Mzanzibari aliyewahi kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi na hivyo ndivyo ilivyo katika jeshi vile vile, ambako majenerali wote wametoka bara. Inasemekana kuwa watumishi wengi wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) wanatoka bara.

Kwa jumla, katika ngazi ya kisiasa Wazanzibari wengi hawadhani kuwa Muungao upo kwa maslahi yao; wanadhani kuwa wao hawana sauti katika Muungano. Wanahisi pia kuwa wanatengwa; wanaamini kuwa katika ngazi ya kiasasi, wao hawashughulikiwi. Hawapati kujifunza juu ya fursa na huduma zinazotolewa na wizara zinazoshughulikia mambo ya Muungano kwa sababu hazina ofisi Zanzibar.

Wanaeleza kuwa wasiwasi unaokuwepo wakati wa uchaguzi unasababishwa na Muungano; kwa mfano, kabla ya uchaguzi wanajeshi wengi wenye silaha na askari polisi huletwa, hii ikiwa na maana kuwa haiwezekani kuwepo uchaguzi huru na wa haki. Wanachokijali ni hofu ya CCM kushindwa uchaguzi. Imeelezewa kuwa utii kwa chama umeushinda ule utii kwa serikali, lakini watu wa kawaida wa bara wanaelewa machache juu ya matatizo haya ya Muungano.

Hata hivyo, amani imeelezewa kuwa ni moja ya faida za Muungano, kwa sababu baada ya mapinduzi palikuwepo na vurugu. Usalama nao pia umeelezewa kuwa ni moja ya faida ambazo Muungano umeleta.

Kutoka bara, pamekuwa na malalamiko kuhusu uwakilishwaji mkubwa zaidi wa Zanzibar katika asasi za Muungano, ikiwa ni pamoja na bunge. Imeelezwa pia kuwa wizara za serikali kwa ajili

Page 49: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Uundwaji na Historia ya Muungano 35

ya bara, takriban hazipo, kwa sababu kuna watu kutoka Zanzibar ambao ni mawaziri wa wizara ambazo si za mambo ya Muungano.

Akielezea hili katika ngazi ya ajira serikalini, mhojiwa mmoja ameeleza, “Mimi siwezi kufanya kazi katika serikali ya Zanzibar lakini wao wameajiriwa katika serikali ya Muungano.” Zanzibar kuzikataa ofisi za asasi za Muungano kama vile Mamlaka ya Mapato ya Tanzania na Tume ya Mawasiliano nako pia kumetajwa.

Hata hivyo, mbara mmoja pia ameeleza kuwa kuondolewa kwa Jumbe kutoka katika madaraka yake kwa sababu ya jaribio lake la kutaka kuufanyia marekebisho Muungano kumepunguza kabisa thamani ya uhalali wa Muungano. Imeelezewa kuwa baadhi ya watu huko Zanzibar wanaamini kuwa uongozi wa Zanzibar unapangwa Dodoma na si Zanzibar: Kwamba kamati maalum juu ya Zanzibar, rais akiwa mwenyekiti wake, inateua wagombea kwa uongozi wa Zanzibar.

Rasilimali, Fedha na Uchumi

Huko Zanzibar pamekuwa na malalamiko ya mfululizo kuhu utaratibu wa kugawana mapato kwa kuipa Zanzibar asilimia 4.5%.

Kuhusu rasilimali, watu wa Zanzibar wameeleza kuwa bara wana madini, mbuga za taifa na ardhi kwa ajili ya kilimo, ukilinganisha na Zanzibar, ambayo zaidi ya kuwa haina utulivu wa kisiasa kwa muda mrefu, ina rasilimali chache. “Zanzibar ni kisiwa; hatuna maliasili wala viwanda. Wabara lazima walielewe hili. Hatudai rasilimali kutoka bara lakini tunataka uhuru wa kuzishughulikia rasilimali chache tulizonazo,” alisema mtu mmoja.

Kuhusu misaada kutoka nje, wameeleza kuwa ijapokuwa inatafutwa na kupokelewa kwa jina la Jamhuri ya Muungano, Zanzibar inapata kidogo sana, au pengine haipati kabisa kuhusiana na mambo yasiyokuwa ya Muungano kama vile kilimo. Bara ndiyo inayoamua kwa niaba ya Zanzibar, Zanzibar ipate kiasi gani.

Page 50: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

36 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

Zanzibar haiwezi kutafuta misaada kutoka nje peke yake. Hicho kidogo wanachokipata ni baada ya kupiga kelele nyingi.

Wafanyabiashara wanalalamika kwa kutozwa kodi mara mbili. Wakati Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) ipo Zanzibar, ukisafirisha tena bidhaa kupeleka bara kutakuwepo na kutathminiwa tena, unyanyaswaji na ucheleweshaji katika kutoa bidhaa. Wanakatishwa tamaa na mlahaka wa baadhi ya wafanyakazi wa TRA ambao huyajibu malalamiko yao kwa kuwambia, kwa nini wafanyabiashara hao hawahamii bara na kuwekeza hapo, ikiwa kuna matatizo yote hayo. Wanaeleza vile vile juu ya tabia ya hatari ya kutoza ushuru kangas, kanzus, nguo za watoto na nguo kwa watu masikini na kuvifanya vitu hivyo kuwa ghali zaidi.

Imeelezwa kuwa mtu wa kawaida wa barabarani haoni faida yoyote ya Muungano katika ngazi hii. Walionesha mapenzi ya kwao pale waliposema, Zanzibar ilikuwa na uchumi imara na wasomi wengi kabla ya Muungano; ilikuwa inatoa wataalam kwa kanda nzima, ilikuwa na kiwango cha juu cha elimu na miundombinu madhubuti iliyokuwa ikitunzwa vyema. Zanzibar ilitoa mahakimu wake wenyewe, walimu na wauguzi kabla ya bara kufanya hivyo. Yote haya yamerudi nyuma baada ya Muungano. Wanayaelewa malalamiko ya bara kuwa Zanzibar haichangii Muungano lakini wanajibu kwa ukali kwa kueleza kuwa wabara hawasemi Zanzibar inapata nini kutokana na Muungano.

Wanachora taswira ya kutafautisha: Zanzibar ina njia za urefu wa jumla ya km 500 wakati bara ina maelfu ya kilomita zilizojengwa kwa msaada wa wafadhili. Hata hivyo, kuna wafanyabiashara hapo Zanzibar walioelezea faida za Muungano. Baadhi yao wanaamini kuwa bila ya muungano mambo yangelikuwa mabaya. Kwa baadhi yao faida ni nyingi kuliko matatizo. Kuna soko kubwa na uhuru wa mtu kwenda anakotaka na Zanzibar isingelitosha.

Wabara kwa upande wao wamelalamika kwa kutotendewa Zanzibar yale wanayoyatenda wao kwa Zanzibar bara. Si rahisi kwa

Page 51: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Uundwaji na Historia ya Muungano 37

mtu wa bara kumiliki ardhi Zanzibar, lakini watu wengi kutoka Zanzibar, na hasa kutoka Pemba, wanamiliki ardhi, na wamewekeza katika biashara Dar-es-Salaam. Wanaeleza juu ya kuhitajika kwa pasi ya kusafiria hapo zamani. Baadhi yao wanalalamika kwa Wazanzibari kupata elimu ya juu kwa gharama za bara. Maneno ambayo watu wamechoka kuyasikia yalisemwa kwa ujumbe huu: “Umeme unatoka bara kwenda Zanzibar; kinachokuja kutoka Zanzibar ni muungano”.

Mambo ya Kijamii na ya Kiutamaduni

Jumuiya za Kiraia (CSOs) zimeeleza kuwa si jumuiya nyingi za kiraia za kitaifa zilizoandikishwa bara zina ofisi zao Zanzibar. Jumuiya ya kiraia iliyoandikishwa bara inabidi iandikishwe tena Zanzibar ili iweze kufanya shughuli zake hapo. Ijapokuwa kuna uhusiano na uratibu fulani kati ya Zanzibar na bara, kwa mfano kwa njia ya mtandao, lakini uhusiano wa kijamii haupo.

Jumuiya za kiraia zimeainisha matatizo mengi ambayo Muungano unaisababishia Zanzibar. Wengi walikuwa wanaelewa juu kile wanachokiona kuwa ni ukiukwaji wa Mkataba wa Muungano na wanaamini kuwa kama Mkataba huo ungeliheshimiwa kero za muungano zisingelikuwepo. Wameengeza kusema kuwa, kama Muungano ungelikuwa ni wa uwazi na unaendeshwa kidemokrasia, lingelikuwa ni wazo zuri sana.

Katika ngazi ya kijamii, maasi mengi ya kijamii yamehusishwa na Muungano: Kuongezeka kwa idadi ya wizi wa kutumia silaha na umalaya (asilimia 95% ya wanaofanya biashara ya ngono wanatoka bara) na tishio la maambukizi ya VVU. Hii inaonesha mtazamo wa watu wa visiwani, waliokuwa nao watu wa Zanzibar. Wengi wanaamini kuwa suala la kuondoa vikwazo vya kusafiri kati ya bara na Zanzibar lingelipigiwa kura ya maoni. Kuachiliwa kwake kuwa huru kunalaumiwa kwa kusababisha ukosefu wa kazi, kuongezeka kwa idadi ya makanisa ambayo kabla ya Muungano yalikuwa 3

Page 52: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

38 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

wakati hivi sasa ni 27 na kadhalika kuongezeka kwa idadi ya mabaa kutoka saba kabla ya Muungano na kufikia 227 hivi sasa. Yote haya, imeelezewa kuwa yanahatarisha hadhi ya kijamii na ya kiutamaduni ya Zanzibar.

Lakini zimetajwa faida chache za Muungano. Faida hizo ni pamoja na uhuru kiasi wa vyombo vya habari. Muungano umebadili hali ya hewa na kuleta hewa safi Zanzibar ambayo ilikuwa haina uvumilivu na kuendesha utawala wa rungu mkonini kwa vyombo vya habari. Vyombo vya habari vya bara vimeonesha mshikamano na wenziwao wa Zanzibar. Wamelaani pale gazeti lilipopigwa marufuku.

Watu wengi wa Zanzibar wanatambua vile vile maslahi yanayopatikana kwa kuweoo uhusiano wa kijamiii unaotokana na watu tofauti kuwa pamoja. Kizazi kipya kilichojengeka kutokana na pande mbili hizi kimeibuka. Uhuru wa mtu kwenda anapotaka unatambulika kuwa ni faida, hasa ukiangalia kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira cha Zanzibar.

Watu wa bara kwa upande wao wanaiona Zanzibar kuwa ni “mahali tofauti kabisa”. Utamaduni ni tofauti. Kuna tofauti vile vile katika jumuiya za kiraia kwa jumla, na hasa vyombo vya habari. Watu wa bara wanauona uhusiano kati ya jumuiya zao za kiraia na serikali kuwa ni huru na wazi zaidi. Vyombo vya habari vya bara viko huru zaidi na vinasisimua.

Kwa vijana wa bara, masuala ya Muungano si muhimu kwao; wanayaona kuwa ni “masuala ya serikali”. Wao wameshughulika na mambo kama ajira, ukosefu wa ajira n.k.

Jumuiya za kiraia bara haziyaoni masuala ya Muungano kuwa ni ya kushughulikiwa kwa haraka au ni muhimu; si jambo la kupewa kipaumbele kwao. Jitihada za kuvuka na kwenda kuendesha shughuli zao Zanzibar zinakatishwa tamaa na ukweli kuwa vyama visivyo vya kiserikali (NGOs) si suala la Muungano. Jumuiya za kiraia za Tanzania haziwezi kuchukuliwa kuwa ni vuguvugu la kitaifa

Page 53: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Uundwaji na Historia ya Muungano 39

lililoungana. Hilo linaweza kuwa ndilo linalowafanya wasione umuhimu wa Muungano katika ngazi hiyo.

Mtu mmoja wa kutoka bara ameuelezea mtazamo wa bara kama ifuatavyo: Kuna matazamo wa kutojali “ laissez-faire” kwa upande wa bara; hawajali ikiwa watu wa Zanzibar wana wasiwasi juu ya kutawaliwa kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni. Watu wa bara wengi wanayaona haya kuwa ni kero na upuuzi unaotakiwa uondokelee mbali.

Ni wazi kuwa baadhi ya watu wa bara wanazieleza sababu za malalamiko ya Zanzibar kuwa si kwa sababu ya hali halisi ya mambo yalivyo, lakini kwa sababu ya hisia za jazba na kutojiamini kwa Wazanzibari.

Page 54: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

40

3 Mambo ya Muungano

Kiini cha Muungano ni suala la yale yanayoitwa mambo ya Muungano. Hii ni kwa sababu mgawanyo wa kazi kati ya serikali ya Muungano na serikali ya Zanzibar unategemea utofautishaji kati ya mambo ya Muungano ambayo yapo ndani ya mamlaka ya serikali ya Muungano na mambo yasiyokuwa ya Muungano ambayo yapo ndani ya mamlaka ya kisheria ya Zanzibar. Kadhalika, mabishano mingi yanatokana na suala la “mambo ya Muungano.”

Maana ya Mambo ya MuunganoMkataba wa Muungano, mwanzo kabisa, ulikuwa na mambo ya Muungano kumi na moja ambayo yalifafanua uwezo wa kisheria wa serikali ya Muungano. Baada ya muda, kama itakavyoelezwa hapo baadaye, orodha ya mambo hayo imekua na hivi sasa Ibara 4(3) ya Katiba ya Muungano ina mambo ya Muungano 22 ambayo yamo katika Jedwali la Kwanza la katiba.Jedwali la kwanza la katiba limeorodhesha mambo yafuatayo:

Jedwali la Kwanza (Lililotajwa katika Ibara 4) Mambo ya Muungano

Katiba ya Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.• Mambo ya Nje.• Ulinzi na Usalama.• Polisi.• Madaraka ya kutangaza Hali ya Hatari.• Uraia.• Uhamiaji.•

Page 55: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Mambo ya Muungano 41

Kukopa nje na biashara.• Utumishi katia • Serikali ya Jamhuri ya Muungano.Kodi inayolipwa na mtu mmoja mmoja na mashirika, ushuru • wa forodha, ushuru kwa bidhaa zinazotengenezwa Tanzania na kukusanywa na idara ya forodha.Bandari, mambo yanayohusiana na usafi rishaji wa anga, posta • na mawasiliano ya simu.Mambo yote yanayohusiana na utengenezaji wa sarafu, sarafu • kwa ajili ya pesa halali (pamoja na noti), mabenki (pamoja na benki za kuweka akiba) na shughuli zote za biasha ya kibenki; ubadilishaji wa fedha za kigeni na udhibiti wa ubadilishaji wa fedha za kigeni.Leseni za viwanda na takwimu.• Elimu ya juu.• Madini, • rasilimali za mafuta, pamoja na mafuta yasiyosafi shwa na gesi asilia.Baraza la Mitihani la Taifa la Tanzania na mambo yote • yanayohusiana na shughuli za Baraza hilo.Mambo ya usafi ri wa anga.• Utafi ti.• Hali ya hewa.• Takwimu.• Mahakama ya Rufaa ya Jamhuri ya Muungano.• Usajili wa • vyama vya siasa na mambo mingine yanayohusiana na vyama vya siasa.

Imetolewa hoja kuwa mambo ya Muungano ni 32 na siyo 22. Hii ni kwa sababu vipengele vingine vimekusanya pamoja mambo mbalimbali. Kwa hiyo, itakuwa sahihi zaidi kuzungumzia

Page 56: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

42 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

“mikusanyiko” 22 kwa sababu vipengele vilivyotajwa vikiorodheshwa kwa mfuatano na kimoja kimoja jumla yake ni vipengele 32.

Kwa hiyo, kutokuwemo kwa mambo kama kilimo, elimu ya msingi na elimu ya sekondari ya ngazi ya chini, biashara, viwanda, maji, ujenzi, mazingira, afya, n.k ni kwa sababu yamo ndani ya uwezo wa kisheria wa Serikali ya Zanzibar. Serikali ya Muungano vile vile inashughulikia kisheria mambo yasiyokuwa ya Muungano ya bara.

Ijapokuwa kwa juujuu, mgawanyo huu wa kazi unaonekana kuwa ni safi kidogo, kuna wasiwasi mkubwa juu ya maana halisi ya kipengele kuwa mambo ya Muungano. Kwa mfano, kinapotajwa kipengele “bandari”, kinakusudia biashara ya bandari au usimamizi wa bandari? “Elimi ya juu” maana yake hasa ni nini?

Nyuma ya utungaji huu wa vipengele kuna nia iliyofichwa ya kuugawa ukweli, wakati ukweli wenyewe ni vigumu kueleweka, unahusiana, una mazonge, una tofauti ndogo za maana na si wa wazi kama orodha yenyewe invyoonekana. Matatizo yanayojitokeza kutokana na hili si ya kiutendaji tu bali ni ya kimawazo vile vile. Kuhusiana na hili, utatolewa mfano mmoja tu. Imeelezewa kuwa uchumi si jambo la Muungano. Hata hivyo, kwa sababu ya utandawazi haiwezekani kutengwa; lazima uwepo uhusiano na mataifa mengine; lakini mambo ya kimataifa ni jambo la Muungano, linashughulikiwa na serikali ya Muungano, ikiwa na maana kuwa Zanzibar haiwezi kujenga uhusiano wa pande mbili kiuchumi. Hii, imeelezewa kuwa inapelekea Zanzibar kutengwa kiuchumi. Lile wazo kuwa viwepo vipengele vyenye uwezo wa kisheria unaolingana linatoa picha halisi ya tatizo hili.

Kuna mambo ambayo hayakuorodheshwa, kam,a vile bunge, ofisi ya rais na Muungano. Watu wamekuwa na wasiwasi kuwa kama hilo la mwisho limewahi kuwa ni jambo la Muungano. Vipengele vilivyofutwa vinaonekana kuhusiana kwa karibu zaidi na Muungano

Page 57: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Mambo ya Muungano 43

kiasi kwamba kuondolewa kwao kunatoa dhana kuwa orodha hiyo inaweza kuwa haikukamilika kuhusiana na suala hilo. Kuhusiana na hili, Mahakama ya Rufaa katika kesi ya SMZ dhidi ya Machano Kamis Ali na wengine, Ombi la kesi ya Jinai Na. 8 la 2008, imeamua kuwa kuna mambo ya Muungano ambayo hayamo katika jedwali.

Tafsiri kama hii inaweka milango wazi kwa uwezekano wa mtu kuyaainisha anavyodhani mambo ya Muungano. Haisaidii kusema kuwa sababu za kuviingiza au kuvitoa vipengele haionekani katika Mkataba wa Muungano. Au kuwa hazionekani katika kumbukumbu za majadiliano bungeni kwa sababu hakuna kumbukumbu za majadiliano ya kina katika Bunge la Tanganyika au Baraza la Mapinduzi la Zanzibar, kwa kuwa Muungano umeundwa kwa haraka na kwa pupa.

Uzoefu wa nchi nyingine umetolewa kuunga mkono nafasi za mambo ya Muungano. Kwa suala la mabishano juu ya mafuta na gesi, imetolewa hoja kuwa katika nchi zenye nusu madaraka, rasilimali za mafuta si miongoni mwa mambo ya Muungano au shirikisho na imetolewa mifano ya Australia na Muungano wa Falme za Kiarabu (UAE). Zinakuwa katika mambo ya Muungano pale tu, zinapokuwa nje ya eneo la bahari ya nchi, kwenye bahari ya kina kirefu, maeneo maalumu ya kiuchumi. Ujumbe wetu umesikia kuwa sasa imekubaliwa kuwa mafuta yaondolewa kutoka kwenye orodha ya mambo ya Muungano.

Kuhusu kodi, kuna orodha ya kodi za Muungano kama vile kodi ya kuingiza bidhaa, kodi ya mapato, n.k. Hata hivyo, imeelezwa kuwa, kwa mfano, kwa kuwa uhamiaji ni jambo la Muungano, kama sheria inaweka ada ya viza, mapato kama hayo yatakuwa ni mapato ya Muungano. Hatimaye, kuna mapato ya muungano kwa sababu yameorodheshwa hivyo na mapato ya Muungano kwa sababu yanatokana na shughuli zilizo chini ya mambo ya Muungano.

Kwa hiyo, inaonekana kuwa maana ya “mambo ya Muungano” haiko wazi kama ilivyoonekana hapo awali. Wasiwasi huu unaonekana

Page 58: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

44 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

kuwa ni muhimu kwa sababu mambo haya ndiyo yenye matatizo na ndiyo eneo lenye ubishani la Muungano.

Kuongezwa kwa Mambo ya Muungano Ukweli kuwa mambo ya Muungano yameongezwa kutoa yale kumi na moja ya asili, yaliyokuwemo katika Mkataba wa Muungano wakati Muungano unaanzishwa na kufikia 22 ya hivi sasa ni chanzo cha mabishano makubwa. Hili limezua matatizo mawili yanayohusiana. Moja katika matatizo hayo ni uhalali na ufuataji wa katiba wa kuiongeza orodha ya mambo ya Muungano. Tatizo la pili ni suala la kisiasa; kukubalika kwa namna, pamoja na ukweli wa kupanuliwa kwa orodha ya mambo ya Muungano na matokeo yake ya kisiasa.

Uhalali wa Kuongeza

Watu wengi waliohojiwa wanaamini kuwa namna orodha ya mambo ya Muungano ilivyoongezwa si halali na kinyume na katiba. Imeelezwa kuwa orodha ya mambo ya Muungano imepanuliwa kwa Bunge la Muungano kuifanyiwa marekebisho Katiba ya Muungano. Imeelezwa pia kuwa kinyume na kitendo hicho, Mkataba wa Muungano hauelezei juu ya kufanyiwa marekebisho orodha hiyo. Hilo ingelibidi lifanywe na pande zinazohusika na mkataba. Ni pande hizi tu ndizo zingeliweza kufanya mabadiliko yoyote kwa njia ya halali. Tatizo hapa, imeelezwa, ni kwamba moja ya pande mbili hizo zinazohusika na mkataba, yaani Tanganyika, haipo.

Inasisitizwa kuwa Jumbe alikuwa na mawazo haya, na Tume ya Nyalali vile vile. Kwa hiyo, tunaweza kuhitimisha kwa kusema kuwa, ni vile vipengele kumi na moja vya asili tu ndivyo vilivyo halali na kwa mujibu wa katiba na vilivyobaki si hali na kinyume na katiba.

Yalikuwepo mawazo ya watu wachache walioamini kuwa upanuzi wa orodha hiyo umefanywa kihalali na Bunge la Muungano ambalo Zanzibar inawakilishwa. Hata hivyo, baadhi ya watu wamepinga

Page 59: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Mambo ya Muungano 45

vikali wakisema kuwa wabunge wa Zanzibar 50 au zaidi kidogo wa Bunge la Muungano hawana idhini ya kuiwakilisha Zanzibar. Ilitakiwa viongozi wa Zanzibar na wale wa bara wakae na kujadiliana kabla ya upanuzi wowote wa orodha hiyo kufanywa.

Wengine wanaeleza kuwa kuna taratibu zilizofuatwa katika kufanya upanuzi huo; kuwa baraza la mawaziri la Zanzibar na Baraza la Wawakilishi (kwa wingi wa 2/3 ya kura) iliwabidi wakubali upanuzi huo pamoja na wingi wa 2/3 wa kura katika Bunge la Muungano; na kwamba utaratibu huo uliandaliwa kwa namna ambayo, kwa mujibu wa hesabu zilizopigwa, bila ya Zanzibar kukubali, uongezwaji wa mambo ya Muungano usingelipita. Walimaliza kwa kusema kuwa kuongezwa kwa mambo ya Muungano kumefanywa kwa njia ya halali na kwa mujibu wa katiba.

Kukubalika kwa Kuongezwa Mambo ya Muungano

Kama invyothibitishwa katika sehemu iliyotangulia, watu wengi, hasa wa kutoka Zanzibar, wanafikiri kuwa namna ambayo mambo ya Muungano yameongezwa haikubaliki. Wanakerwa na mtazamo wa uhalali uliochukuliwa; hakuna majadiliano au makubaliano kwa kuwa jambo hilo linachukuliwa kuwa ni la utungaji wa sheria tu. Ili kuondoa dhana ya kuhusika kwa upande mmoja tu na kuheshimu sheria, inashauriwa kuwa si kama pande mbili za asili zinazohusika na Mkataba wa Muungano zijadiliane juu ya jambo hilo tu, bali orodha ya mambo ya Muungano ionekane katika katiba ya Zanzibar kuongezea orodha iliyomo katika katiba ya Muungano. Hili lingeliondoa mawazo ya kuhusika kwa upande mmoja tu katika kuongeza mambo ya Muungano kwani Zanzibar ingelishirikishwa kwa kuifanyia marekebisho katiba yake yenyewe.

Kupanuliwa kwa orodha ya mambo ya Muungano, kwa jumla hakukubaliki kwa Zanzibar. Wazanzibari wengi, imeelezwa, wanapinga kuongezwa huko. Ni kama bara kuimeza Zanzibar kwa vile orodha hiyo inakua kinyume na matakwa ya Zanzibar.

Page 60: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

46 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

Ni sawa na kuutambalia uhuru wa Zanzibar ili kuunyakua na kuthibitisha wasiwasi na hofu juu ya mpango wa muda mrefu wa Nyerere kuendelea na serikali mbili ili hatimaye iwepo serikali moja. Wametoa mfano wa maelezo yaliyojulikana sana juu ya kuanza na “Muungano wa vitu vichache” na sasa “Muungano wa vitu vyote”. Inapendekezwa kuwa badala yake, sasa mwelekeo ubadilishwe ili uwe kinyume na wa hivi sasa; kuna haja ya kuyapunguza mambo ya Muungano. Hili pia linahusishwa na pendekezo la kuwa na serikali tatu ambazo zitakuwa na mamlaka tatu tofauti za sheria na serikali ndogo ya Muungano yenye uwezo mdogo wa kisheria.

Kuna wengine, hasa wale ambao kwa namna moja au nyingine walihusika na mchakato huo, ambao wanaeleza kuwa, kuongezwa kwa mambo ya Muungano hakukuwa na nia mbaya. Kadhalika, wengine wana maelezo ya upole juu ya kuongezwa huko na wanayaona kuwa ni maendeleo chanya ya kihistoria.

Ilielezwa kuwa Mwalimu hakutumia mabavu katika kuyaongeza mambo ya Muungano. Maongezeko makubwa inaelezewa kuwa yamesababishwa na matokeo maalumu, la kwanza likiwa ni kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) mwaka 1977, ijapokuwa ongezeko la kwanza kabisa lilikuwa mwaka 1967. Wakati Jumuiya ilipovunjika, mambo yote ambayo iliyashughulikia yaliingizwa ndani ya uwezo wa kisheria wa Serikali ya Muungano. Hii inasemekana kuwa ndiyo sababnu ya ongezeko kubwa la mambo ya Muungano. Sababu nyingine ya ongezeko hilo ni kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa mwaka 1992. Hili nalo limepelekea kuongezeka kwa mambo ya Muungano kama vile usajili wa vyama vya siasa.

Wakati maelezo haya ya kihistoria yanaweza kuwa kweli, peke yake, hayawezi kuwa ni maelezo ya kutosha kwa kuongezwa kwa mambo ya Muungano. Haikuwa lazima kuwa kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki kungelipelekea kuongezeka kwa mambo ya Muungano; mambo hayo yangeliweza kuwekwa ndani ya uwezo wa kisheria wa Zanzibar.

Page 61: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Mambo ya Muungano 47

Imeelezwa kuwa wakati watu wa Zanzibar wanahisi kuwa kuongezwa kwa mambo ya Muungano ni sawa na kuuingilia uhuru wao, ukweli wa kihistoria uko tofauti: Wakati maongezeko machache yalipendekezwa na serikali ya Muungano, yalikuwepo maongezeko yaliyofanywa kwa utashi wa Zanzibar. Mfano unaotolewa ni wa elimu ya juu. Zanzibar haikuwa na uwezo wa kuendesha elimu ya chuo kikuu na ingelikuwa ni hasara kwa wanafunzi wa Zanzibar ingelikuwa watozwe gharama wanazotozwa wanafunzi wa kutoka nje hapo Dar es Salaam; kwa hiyo, serikali ya Zanzibar ilipendekeza kwa serikali ya Muungano kuwa elimu ya juu ifanywe kuwa ni jambo la Muungano.

Mawazo mengine ya matumaini kuhusu hili, ni kwamba mambo ya Muungano yanakua kila muda unavyoendelea, kutoka yale kumi na moja ya asili, kwa sababu ya imani iliyojengeka kila muda ulivyokwenda, na siku za baadaye orodha hiyo inaweza ikawa ndefu zaidi. Wenye mawazo haya waliichukulia orodha hiyo kuwa ni ya hiari kwa kuwa kama upande mmoja unakipinga kipengele fulani, kinaweza kujadiliwa, ilimradi tu hilo linafanyika kwa “namna iliyo sahihi”.

Hisia zinazofanana na hizo hapo juu zilielezwa kuhusu kupanuka kwa orodha hiyo. Hisia hizo ni kwamba katiba ya 1977 ilikuwa vile vile ni wakati wa kupitia upya mgawanyo wa majukumu; fursa ya kuipanua orodha ya mambo ya Muungano ikiwa ni hatua ya kujenga umoja wa karibu zaidi, ikiangaliwa kuwa na nchi moja baadaye. Kuhusyu hili, imeelezwa kuwa watu wa bara wengi wanashikliia kuwepo kwa nchi moja na mjadala unaendelea, na kwa hiyo kuifanya orodha ya mambo ya Muungano kuwa ni suala la mabishano makubwa.

Maoni mengine yamependekeza njia ya kutoka kwenye mgogoro huu: Kwa kuwa orodha ya mambo ya Muungano inahitaji wingi wa thuluthi mbili, hili linalazimisha watu wakae na kujadiliana. Jambo hili halina mwisho maalumu; majadiliano yanaweza kusababisha

Page 62: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

48 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

kuongeza au kuondoa kutoka kwenye orodha. Orodha yote inaweza kuondolewa na kusababisha kuvunjika kwa Muungano.

Utendaji wa Mgawanyo wa Madaraka na Majukumu Usimamizi wa mambo ya muungano umeelezewa na baadhi ya watu kuwa ni wenye matatizo mengi; wanauona kuwa ndiyo tatizo kubwa kuliko yote linaloukabili Muungano. Matatizo haya kwa kiasi fulani yanatokana na matatizo ya kimuundo ambayo yameelezewa hapo kabla. Madaraka tofauti kwa mambo ya Muungano na yasiyo ya Muungano kwa bara yameunganishwa kiutendaji chini ya serikali ya Muungano. Mambo yasiyokuwa ya Muungano kwa bara yanashughulikiwa kama ni mambo ya Muungano; yanaendeshwa hivyo kuhusiana na vyanzo vya fedha, bajeti, n.k. Hili linasababisha mtafaruku usio wa lazima na wasiwasi.

Pili, ingelitazamiwa kuwa wabia katika Muungano wangelishiriki kwa hali ya usawa katika kufanya maamuzi na kushiriki katika mambo ya Muungano kwa jumla. Lakini hakuna muundo ambao ungeliwezesha kuwepo kwa mchakato kama huu pale mambo ya Muungano yanapohusika. Inasemekana kuwa baraza la mawaziri la Muungano ndilo linalofanya maamuzi. Wazanzibari wanahisi kuwa Zanzibar haishirikishwi katika michakato ya baraza la mawaziri la Muungano. Wazanzibari wachache, wanne katika baraza la mawaziri la watu 31 si kama kuwa ni wachache mno katika kushawishi ufanyaji maamuzi, lakini hwaiwakilishi Zanzibar vile vile. Kwa hiyo, hakuna mamlaka yoyote kwa upande wa Zanzibar ya kuamua chochote kwa maslahi ya wananchi; maamuzi yote yanafanywa Dodoma kwa uhusiano ulioelemea upande mmoja.

Matatizo haya ya kimsingi yanaonekana katika maeneo mingine mengi. Kwa mfano, kuna kuunganishwa kwa wizara chini ya wizara inayochanganya mambo yote, ya Muungano na yasiyokuwa ya Muungano kama ilivyo katika utangazaji na mawasiliano ya simu. Kwa upande mwingine, kuteuliwa kwa Mzanzibari kuwa

Page 63: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Mambo ya Muungano 49

waziri wa habari wakati wizara hiyo inashughulikia mambo ya bara tu, ambayo si ya Muungano, kunafichua upande mwingine wa tatizo. Tatizo hili linajionesha vile vile kwa ukweli kuwa muamala mmoja unaweza kuhusisha madaraka yote mawili ya Muungano na yasiyokuwa ya Muungano. Kwa mfano, mchakato wa kukamata na kushtaki watuhumiwa na hukumu ya mambo ya uhalifu, ijapokuwa ni muamala mmoja lakini unahusisha mambo yote, ya Muungano na yasiyokuwa ya Muungano. Ukamataji na upelelezi ni suala la mambo ya ndani, ambalo ni jambo la Muungano, lakini kushtaki na kuhukumu kesi ni shughuli ambazo si za Muungano, ijapokuwa kutia gerezani ingelikuwa, kwa upande mwingine, jambo la Muungano.

Mtindo huu wa kufichaficha madaraka kimuundo na kiutendaji umeshajiisha kutoheshimu mgawanyo wa madaraka. Kwa upande mwingine kuna malamiko kuwa kiutendaji kila kitu kinaendeshwa kuwa ni jambo la Muungano na uhuru wa Zanzibar ni aibu tupu.

Kwa upande mwingine, kuna wakati Zanzibar husimamia mambo ya Muungano. Baadhi ya watu wanasema kuwa hili linasababishwa na kuwa chama kimoja kinaendesha serikali zote na hii inaleta shida ya tatizo la nidhamu. Kwa mfano, wakati elimu ya juu ni jambo la Muungano, Baraza la Wawakilishi la Zanzibar limepitisha sheria ya kuanzisha Chuo Kikuu cha Zanzibar huku Bunge la Muungano likishikilia kuwa Baraza halikuwa na madaraka ya kufanya huivyo. Hivi sasa serikali ya Zanzibar ndiyo inayoendesha na kusimamia elimu ya chuo kikuu huko Zanzibar.18

Kadhalika, hakuna mgawanyo wa mapato; yoyote yule anayekusanya mapato huyaweka mapato hayo na hakuna malinganisho baina ya nini kinakusanywa kama ni mapato ya Muungano na nini kinatumika kwa mambo ya Muungano.

18 Tume ilielezewa vile vile kuwa kazi ya udhibiti inafanywa na “Tanzania High Education Accreditation Council” na Tume ya Vyuo Vikuu ya Tanzania, “Tanzania Commission for Universities”.

Page 64: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

50 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

Lakini pande zote mbili zinalalamika. Zanzibar inalalamika kwa kutokuwepo mgawanyo wa haki na bara inalalamika kuwa Zanzibar haichangii.

Masuala kama hayo yanayohusiana na mgawanyo yanaelezwa vile vile kuhusiana na kodi inayotozwa kwa bidhaa zinazoshushwa Dar es Salaam na hatimae kusafirishwa kwenda Zanzibar. Mapato hayo hubakia Dar-es-Salaam wakati bidhaa zinaishia Zanzibar. Zanzibar vile vile wanaiona bandari yao kuwa ni muhimu sana kwao ikiwa ni chanzo cha mapato. Kwa hiyo, pale inaposemwa, kama ilivyo hivi sasa “bandari” zinakuwa ni jambo la Muungano, wao wanaliona hilo kuwa ni balaa.

Mabishano haya hivi karibuni yalilizunguka suala la gesi na mafuta. Kama mmoja wa waliohojiwa alivyoiambia tume hii, changamoto za wazi zinazotolewa na serikali ya Zanzibar yenyewe inalifanya suala la majadiliano ya mambo ya Muungano kuwa ni muhimu. Alisisitiza kuwa hii ilikuwa changamoto ya wazi (si majadiliano na serikali ya Muungano) na kwa serikali ya Zanzibar (ni zaidi) kuliko kwa mfano, changamoto katika Baraza, au ya chama cha siasa, au ya kikundi cha watu au mtu mmoja mmoja katika jamii.

Waziri wa Maliasili wa Zanzibar ameripotiwa akisema kuwa suala la utafutaji mafuta ni jambo ambalo Zanzibar itakwenda kwenye mahakama ya katiba. Serikali kwa hiyo, imetamka wazi kuwa utafutaji wa mafuta si jambo la Muungano. Msimamo wake ni kwamba Zanzibar ina haki ya mapato yatokanayo na mafuta na gesi, ijapokuwa rasmi, ni jambo la Muungano. Zanzibar inadai kuwa hainufaiki na gesi inayotoka mikoani huko bara.

Maoni ya kutoka bara yameonesha wasiwasi juu ya ukali wa hisia zilizooneshwa: kwa ghafla, kelele, siyo kutoka kwenye Baraza la Wawakilishi tu, bali wanasiasa wadogowadogo na wananchi wa kawaida, kwa ukali walitoa madai yao ya mafuta. Walikasirika sana na hawakuwa na woga juu ya suala la mafuta. CUF na CCM

Page 65: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Mambo ya Muungano 51

walikuwa pamoja juu ya suala hili. Masuala kama haya, hasa yale yanayohusiana na Muungano huwaunganisha Wazanzibari.

Kwa baadhi ya watu, wanahisi kuwa hisia kama hizi zinahusiana na siasa za uchaguzi za Zanzibar. Imeelezwa kuwa mafuta bado hayakupatikana lakini tabia ya siasa za Zanzibar, hasa katika CCM, ni kwamba kama mtu haonekani kutetea maslahi ya Zanzibar, basi mtu huyo hawezi kuteuliwa. Baada ya uteuzi, mambo yataonekana kupoa kidogo, ijapokuwa hayatakuwa yaleyale tena.

Jumuiya za Kiraia (CSOs) zinaathiriwa na namna mambo ya Muungano yanovyosimamiwa. Ujumbe huu umebaini kuwa Jumuiya za Kiraia, kote, Zanzibar na bara, zinaelewa kuwa Vyama Visivyo vya Kiserikali si jambo la Muungano. Hata hivyo, Muungano unaathiri namna vinavyofanya shughuli zake.

Moja ya matatizo yaliyotajwa ni kwamba, ijapokuwa Vyama Visivyo vya Kiserikali vyenyewe si jambo la Muungano, jambo ambalo ingeliwapasa kulishughulikia lingeliweza kuwa na kitu kinachohusiana na mambo ya Muungano. Wameelezea kuwa mikakati ya Jumuiya za Kiraia inabadilikabadilika ikitegemea kama wanashughulika na jambo la Muungano au jambo lisilo la Muungano. Kuhusu mikataba ya kimataifa, ukweli kuwa inashughulikia jambo la Muungano, hiyo huchelewesha mchakato wa kuridhia. Zanzibar haiwezi kuchagua kuingiza viwango inavyovitaka katika mikataba kama hiyo kama vile ambavyo jumuiya za kiraia zingelipenda.

Chama cha VyamaVisivyo vya Kiserikali cha Tanzania (TANGO) kina ushirikiano kidogo na Vyama Visivyo vya Kiserikali vya Zanzibar. Wanautambua uhuru wao, badala ya kumezana. Wanatambua kuwa sheria na sera haziwaruhusu kuwa na uwanachama wa Vyama Vusivyo vya Kiserikali vya Zanzibar kwa hiyo wanakubali na kuheshimu madai ya Zanzibar ya kujiwakilisha wao wenyewe kwa sababu wao hawana madaraka ya kuwawakilisha.

Lakini Chama cha Vyama Visivyo vya Kiserikali cha Tanzania kina jina la Tanzania na hili linaweza kutoa picha isiyo sahihi ya

Page 66: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

52 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

kuwa wao ni chama kikuu cha Tanzania nzima; Wakati chama hicho hakifiki Zanzibar.

Jumuiya za kiraia, hata hivyo, ni kitu nyeti kwa mahitaji ya Zanzibar na matakwa ya jamii ya raia wa Zanzibar hivyo, huwajumuisha kwenye wajumbe wanaohudhuria mikutano ya kimataifa.

Katika ngazi ya mtu mmojammoja, watu kutoka Zanzibar wanaweza kufanyakazi katika sekta ya Vyama Visivyo vya Kiserikali bara. Hilo halina tatizo na hakuna ubaguzi unaotokea katika ngazi hiyo.

Mwisho, mambo ya Muungano yanahusisha masuala mengi ya kimawazo, kisheria, kikatiba, kisiasa na kiutendaji. Maoni mengi juu ya suluhisho ni mapendekezo yenye pande mbili; kupunguzwa kwa mambo ya Muungano na mfumo wa serikali tatu yenye mamlaka tatu tofauti za sheria, kisheria na kiutendaji.

Page 67: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

53

4 Utaratibu wa Kutatua Matatizo

ya Muungano

Utangulizi Sura zilizopita zimegusia masuala na matatizo yaliyomo ndani ya Muungano. Matatizo hayo ni kuanzia yale ya kimuundo hadi yale matatizi mahasusi ya kero za muungano.

Kuna matatizo ya kiuchumi na kifedha. Hayo yanaanzia kutoka kwenye matatizo ya mafuta, nishati na utafutaji wa mafuta. Kuna yale yanayohusiana na forodha, hasa kuhusu biashara ya bidhaa za kupita. Vilevile kuna suala la kugawana mapato na kugawana gharama za Muungano.

Kuna matatizo ya kisiasa ambayo unaweza kusema kuwa yanahusiana na masuala ya Muungano. Juu ya hili, kuna suala la ujanja wa uchaguzi na fujo zilizotokea baada ya uchaguzi Zanzibar. Hili linahusiana hasa na uchaguzi wa rais wa Zanzibar na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi.

Kuna masuala ya kiutawala, kwa mfano lile la uhusiano kati ya mawaziri wa Muungano na mawaziri wa Zanzibar.

Halafu tena kuna matatizo ya kimuundo na kisiasa ambayo yanahusiana moja kwa moja na utendaji wa Muungano. Haya ni pamoja na kutokuwepo kwa muundo wa ndani kujadiliana juu ya matatizo ya Muungano, ya mamlaka tatu zenye uwezo wa kisheria, Zanzibar kusimamia mambo ya Muungano, na serikali ya Muungano kusimamia mambo ambayo si ya Muungano kwa niaba ya bara bila ya kuwepo muundo wowote. Hali za tatizo hili zinaelezewa kuwa ni “kuwepo Zanzibar na kutokuwepo Tanganyika”, na kwa hiyo

Page 68: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

54 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

kushindwa kutatua matatizo kwa njia ya mazungumzo kati ya serikali ya Muungano na Zanzibar, wakati mazungumzo kama hayo ilibidi yawe kati ya wabia wa asili.

Suala la msingi linaulizwa na Zanzibar: tunapokuwa na matatizo ya Muungano tunazungumza na nani kwa kuwa Tanganyika imesita kuwepo?

Vile vile kuna kutenganshwa kwa uraisi wa Zanzibar na umakamu wa rais wa Muungano baada ya kuanzishwa mfumo wa siasa ya vyama vingi. Hili linahusishwa na wazo kuwa mabadiliko ya kuelekea kwenye mfumo wa siasa ya vyama vingi mwaka 1992 umeanzishwa bila ya kufanya uchambuzi wa kina wa muundo na sheria.

Kwa mujibu wa utaratibu huu mpya, mtu hufanya mabadiliko madogomadogo tu ya katiba ili kujaribu kukidhi mahitaji ya mfumo wa vyama vingi wakati mfumo wa msingi ni ule ule wa chama kimoja. Hili linasababisha wasiwasi katika utendaji wa Muungano, kama mtu mmoja aliyehojiwa alivyosema.

Watu wengi waliohojiwa wamekiri kuwepo matatizo na ukubwa wake. Wachache wamejidai kuyaelezea kuwa ni ya “kiutendaji” zaidi kuliko kuwa ni ya kimsingi kwa Muungano. Lakini wingine wamezielezea kero za muungano kuwa zinasababishwa na sababu za kichumi zaidi kuliko za kisiasa.

Sura hii inaupima utaratibu uliowekwa ili kujaribu kuyashughulikia matatizo yanayojitokeza kwa kukuwepo na shughuli za Muungano. Sura hii inachunguza mafanikio au kinyume ya hivyo ya utaratibu wa kuyashughulikia matatizo hayo na sababu zinazotolewa kwa mafaniko yake au kinyume na hivyo.

Ni wazi kabisa, kutokana na maelezo ya waliohojiwa kuwa kweli yapo matatizo na mchakato wa matatizo kujitatua yenyewe. Haya yameelezewa kuwa ni: Kutokuwepo nia ya kisiasa ya kuyatatua matatizo haya kiasi kwamba ijapokuwa kinadharia kila mtu anauunga mkono Muungano na kuelezea nia ya kuyatatua matatizo yake, kwa kweli na kwa vitendo mambo ni tofauti. Imeelezewa vile vile kuwa

Page 69: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Utaratibu wa Kutatua Matatizo ya Muungano 55

hakuna kikao cha majadiliano ya wazi cha kufanya maamuzi juu ya masuala ya Muungano. Kila zinapotolewa hoja, inaelezwa kuwa hoja hizo zimpelekwa kwenye kamati au tume – ambazo zenyewe zinakuwa bomu la kutegwa – kwa sababu kupelekwa huko siyo kwa madhumuni ya kutatua matatizo, lakini ni kwa sababu ya kuyazoea masuala hayo.

Kushindwa kutatua matatizo kunasababishwa pia na mambo ya Muungano kutokuwa wazi kuanzia mwanzo. Mambo hayajadiliwi, si kwa pamoja wala si kwa wanachama wawili wa Muungano peke yao.

Hili linaongezeka kwa tuhuma za kuwepo vitisho. Ilielezwa kuwa uongozi wa Tanzania haufurahi kila unaposikia Muungano ukijadiliwa. Badala yake kunakuwa na mkono mzito katika kuyashughulikia mambo hayo ili Muungano uendelee kuwa pamoja; matumizi ya mabavu au njia nyingine zisizo za moja kwa moja. Imeelezewa kuwa, mpaka ulipofika urais wa rais Mkapa ilikuwa ni mwiko kuuzungumza Muungano. Matokeo yake ni kwamba watu wa kawaida hawana habari za kutosha juu ya taratibu za Muungano.

Yote haya yameuchanganya mtazamo wa kimsingi – usimamizi wa muundo wa Muungano kisiasa, yaani kuwa ni jambo la kisiasa tu (katika serikali ya mfumo wa chama kimoja cha siasa) na si suala la kikatiba.

Hatimaye, si kama kwamba mambo yaliyozungumzwa miaka 25 iliyopita bado yapo mpaka leo yakiwepo maendeleo machache au kutokuwepo maendeleo kabisa katika kuyatatua tu, lakini kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa, ukichukulia ule mtazamo wa kimsingi, kumezidi kuyatatanisha masuala ya usimamizi wa Muungano vile vile.

Mahakama ya Katiba19 Ibara 125 ya Katiba ya Muungano inaanzisha Mahakama ya Katiba. Inatoa uwezo wa kisheria wa pekee kwa masuala yanayohusu

19 Jina lake rasmi ni “Mahakama Maalumu ya Katiba ya Jamhuri ya

Page 70: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

56 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

Muungano kati ya bara na Zanzibar. Haya ndiyo madhumuni yake ya kipekee.20 Mahakama kuu, kwa upande mwingine, ina uwezo wa kisheria wa kuitafsiri Katiba ya Muungano wakati Mahaka Kuu ya Zanzibar ina uwezo wa kisheria wa kuzitafsiri Katiba ya Muungano na ya Zanzibar.

Mahakama ya Katiba ni mahakama ya muda na si ya kudumu. Inaundwa baada ya kuombwa kuendesha utaratibu wa kuhukumu kuhusu masuala ya Muungano.

Juu ya kuwepo kwa mlolongo wa matatizo ya Muungano ambayo ujumbe huu umeelezewa, hakuna aliyewahi kuiomba Mahakama ya Katiba kuhukumu mambo kama hayo. Hakuna hata mtu mmoja aliyewahi kutoa changamoto ya kisheria juu ya nama Muungano unavyoendeshwa, kwa mtazamo wa kikatiba.

Pametolewa maelezo mengi. Moja ya maelezo hayo ni kwamba, kwa kuwa Zanzibar ndiyo itakayotaka kuchukua hatua kama hiyo na kwa kawaida Zanzibar hukaa kimya, hakutaweza kutokea changamoto kama hiyo kutoka kwao.

Imedaiwa vile vile kuwa hali ya mambo kama hiyo haikutokea kwa bahati mbaya hata kidogo. Mahakama ya Katiba haikukusudiwa ifanye kazi. Iliingizwa katika katiba baada ya Jumbe kushikilia iingizwe tu. Muundo wake unathibitisha kutoweza kufanyakazi kwake. Inatakiwa iwe na idadi sawa ya wajumbe walioteuliwa na serikali zote, ya Muungano na ya Zanzibar bila ya kupigiwa kura.

Ni suala hili, la Jumbe kutaka kuiomba mahakama, lililompelekea kuvuliwa madaraka yake katika serikali na katika chama. Nyerere, aliyeona karaha kuirejesha mahakama hiyo, inasemekana alimshutumu Jumbe kwa kutaka kutafuta njia ya kisheria kwa suala la kisiasa.

Yaliyomtokea Jumbe, inasemekana kuwa yaliviza jitihada yoyote ya kutaka kuiomba mahakama hiyo kutatua tatizo la Muungano.

Muungano”.20 Ibara 126 ya katiba. Mahakama inabidi itoe uamuzi wa usuluhishi.

Page 71: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Utaratibu wa Kutatua Matatizo ya Muungano 57

Kwa hiyo, palikuwa na shaka iliyoweza kuelewaka, juu ya Mahakama ya Katiba kuwa ndiyo utaratibu wa kutatua matatizo ya Muungano kwa hisia ambazo ujumbe umezipata.

Wakati baadhi ya watu waliotupa hisia zao walielezea kutojua kwao juu ya maelezo ya mahakama hiyo kutofanyakazi, wengi wameeleza juu ya matatizo ya Muungano kushughulikiwa na serikali kwa namna isiyo rasmi: kiutawala na kwa kupitia miundo ya chama.

Hivi karibuni, Waziri wa Maliasili wa Zanzibar, inasemekana kuwa aliapa kuwa Zanzibar ilikuwa tayari kwenda kwenye mahaka ya katiba juu ya mambo yanayohusu utafutaji wa mafuta.

Tume na Kamati Tokea kuanzishwa kwa Muungano, imeripotiwa kuwa zimekuwepo tume 45 kushughulikia kero za muungano mbalimbali. Katika kipindi cha miaka 20 iliyopita, zimekuwepo zaidi ya tume 20 zilizounda kushughulikia masuala haya.

Orodha

Kamati ya Baraza la Mapinduzi (Kamati ya Amina) ya 1992; Kamati ya Rais ya Kupambana na Kasoro za Muungano (Kamatiya Shamhuna) ya 1997; Kamati ya Rais Kucbambua Ripoti ya jaji Kisanga (Kamati ya Salim Juma Othman); Kamati ya Kuandaa Mapendekezo ya Serikali ya Zanzibar Juu ya Kero za Muungano (Kamati ya Ramia) ya 2000; Kamati ya Baraza la Mapinduzi juu ya Sera ya Mambo ya Nje; Kamati ya Rais ya Wataalamu juu ya Kero za Muungano ya 2001; Kamati ya Baraza la Mapinduzi ya jumuiya ya Aftika Mashariki; Kamati ya Mafuta; Kamati ya Madeni baina ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Muungano Wa Tanzania; Kamati ya Suala la Exclusive Economic Zone (EEZ); Kamati ya Masuala ya Fedha na Benki Kuu; Kamati ya Rais ya Masuala ya Simu (1996-1999).

Page 72: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

58 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

Zaidi ya kamati hizi, kamati nyingine saba ziliundwa na serikali ya Muungano, nazo ni Kamati ya Mtei; Tume ya Nyalali; Kamati ya Shellukindo; Kamati ya Bomani; Kamati ya Shellukindo II ya kuandaa Muafaka juu ya Mambo ya Muungano baina ya SMZ na SMT; Kamati ya “Harmonisation”; Kamati ya Masuala ya Simu (Kamati ya Kusila).

Unatolewa mfano wa kikundi cha kitaalam cha kushughulikia matatizo kama kupanga bajeti, na kufanya maamuzi. Ripoti ilitolewa lakini ikafanywa kuwa ya kisiasa na hakuna kilichopitishwa kutoka katika ripoti hiyo, tume hii iliambiwa. Inasemekana kuwa ripoti nyingine nazo zimepatwa na masaibu kama hayo; kutochukuliwa hatua yoyote. Mbali ya kuwa ni utaratibu wa kutatua matatizo, nyingi ya kamati hizi zinachukuliwa kuwa ni mbinu za kukwepa na kuyaweka kando matatizo kwa kutegemea kuwa labda yataondoka. Waliohojiwa na tume hii waliwauliza wale wenye kuaminiwa juu ya hatua za kuunda kamati kama hizo.

Zimekuwepo tume nyingine, hazikuundwa mahasusi kushughulikia masuala ya Muungano. Hata hivyo, maeneo yao ya kuyashughulikia yalikuwemo pia masuala ya Muungano moja kwa moja au kinyume ya hivyo. Mfano wa tume kama hiyo ni Tume ya Nyalali juu ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa. Katika ripoti yake, tume hiyo ilipendekeza kuwepo kwa mfumo wa Muungano wa serikali tatu. Wakati serikali imayakubali mapendekezo yake ya msingi kuhusiana na mfumo wa vyama vingi vya siasa, muundo wa Muungano umebakia kuwa ni ule ule na matatizo yanayohusiana na mfumo huu yameendelea kuusumbua Muungano.

Moja ya kamati hizi ni ya kudumu, tofauti na zile juhudi za muda, za mara kwa mara. Hata hivyo, kwa hali hii kama ilivyooneshwa na Kamati ya Makamu wa Rais na Waziri Kiongozi, kamati hii ina hadhi ya kikatiba na kisheria. Hadhi ya kiutendaji kama hii inaweza kupunguza makali yake kama tume hii ilivyoelezwa.

Page 73: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Utaratibu wa Kutatua Matatizo ya Muungano 59

Tume ya Pamoja ya Fedha (JFC) ni moja ya zile zilizoanzishwa kwa mujibu wa Ibara 134 ya katiba. Nayo pia inashughulikia maeneo ya matatizo ya Muungano. Yametolewa maoni mengi kwa tume hii juu ya tume hizi mbili.

Kamati ya Makamu wa Rais Hii ni kamati ya kiserikali, na hasa ni kamati ya pamoja ya mawaziri. Mwenyekiti wake ni makamu wa rais wa Muungano na wajumbe wake, miongoni mwa wingine, ni waziri mkuu wa Muungano na waziri kiongozi wa Zanzibar. Hapo awali, kamati iliendeshwa chini ya utaratibu wa uwenyekiti wa pamoja kati ya waziri mkuu na waziri kiongozi.

Kamati hii hukutana ili kushughulikia matatizo, kama vile forodha na hasa bidhaa zinazopita njia, mafuta na utafutaji wa nishati. Hukutana kila baada ya miezi mitatu.

Kamati hii iliundwa na Rais wa Muungano kushughulikia kero za muungano mbalimbali. Kamati hii ina mfululizo wa mikutano, Zanzibar na bara. Baadhi ya mafanikio yake yameelezwa kuwa ni: Tume ya Haki za Binadamu na Utawaka Bora (CHRAGG) kuruhusiwa kufanya shughuli zake Zanzibar baada ya mkutano wa kamati. Kabla ya hapo ilikuwa haifanyi shughuli zake Zanzibar. Masuala ya mgawanyo wa mapato na gharama za uvuvi wa bahari ya kina kirefu yameshughulikiwa kwa mafanikio na kamati hii. Hivi sasa uvuvi katika bahari ya kina kirefu unaratibiwa na Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari ya Kina Kirefu iliyopo Zanzibar. Inasemekana kuwa Sheria ya Meli za Biashara nayo pia ni matokeo ya juhudi za kamati hii, iliyoiwezesha Zanzibar kuwa mwanachama mshirikishwaji wa Chama cha Bahari cha Kimataifa (IMO).

Hivi sasa, iliripotiwa kuwa kamati hii inashughulikia kero za muungano mbalimbali:

Petroli na Gesi• Mambo ya Muungano•

Page 74: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

60 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

Ajira ya Wazanzibari katika asasi za Muungano na wizara, k.m • jeshi, polisi, n.k.Zanzibar kutoweza kukopa nje • Hisa za Zanzibar katika • rasilimali za iliyokuwa Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki Wafanya biashara wa Zanzibar kutozwa kodi mara mbili•

Zimeundwa kamati ndogo mbalimbali kwa vipengele hivi na kwanza wanafanya mazungumzo na wataalam, na baadaye mambo hayo yatapelekwa kwenye kamati ya mawaziri, chombo kilicho ndani ya kamati hiyo na baadaye, mwisho, kwenye kamati ya pamoja ya Makamu wa Rais.

Hata hivyo, imeelezewa kuwa Kamati ya Makamu wa Rais haina msaada wa kisheria au wa kikatiba. Kwa ilivyo, ni ya ushauri; na kwa sababu hii inahitaji nia safi na hali ya kujitolea. Lakini, inadhaniwa kuwa hakuna utayari, nia njema au nia ya kisiasa kwa upande wa serikali ya Muungano kuiwezesha kamati hii kuzishughulikia kero za muungano kwa namna ya kuweza kuleta matokeo; kwamba kamati haina ushujaa wa kutatua matatizo, hasa kwa sababu wajumbe wake wote ni wanachama wa CCM. Lakini kuna mmoja aliyesema kuwa kamati hiyo inajadili na kutatua matatizo kwa maelewano.

Kamati inabidi ipewe hadhi ya kisheria/kikatiba. Inasemekana kuwa Bunge limedai kuwa kamati hiyo irasmishwe.

Tume ya Pamoja ya Fedha

Ibara 134 ya Katiba ya Muungano inaelezea kuwepo kwa Tume ya Pamoja ya fedha (JFC). Hata hivyo, ilichukua miaka 40 kuanzisha tume hiyo, jambo lililotokea mwaka 2003. Ina makamishna kutoka pande zote mbili za Muungano. Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania na kamishna mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania wote ni wajumbe. Tume hii inatakiwa kuripoti kwa Waziri wa Fedha.Madaraka ya tume hii ni pamoja na yafuatayo:

Page 75: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Utaratibu wa Kutatua Matatizo ya Muungano 61

Kuamua juu ya asasi za Muungano• Kuamua juu ya mapato ya Muungano• Kuviangalia vyanzo vyote vya mapato• Kuchunguza ukusanyaji wa mapato ya Muungano• Kuamua juu ya utaratibu wa kugawana mapato •

Kwa hiyo, kazi ya tume hii ni kuthibitisha mapato ya Muungano pamoja na gharama zinazohusiana na ukusanyaji wa mapato ya Muungano na kufikiria utaratibu wa kugawana mapato hayo kati ya bara na Zanzibar.

Ujumbe huu una habari kuwa tume, kwa msaada wa mshauri, imetayarisha ripoti juu ya mgawanyo wa mapato na kuiwasilisha ripoti hiyo kwa serikali zote mbili mwezi Agosti 2006. Inasemekana kuwa ripoti hiyo imeorodhesha vyanzo vyote vya ndani vya mapato na serikali hizo mbili bado zinaifikiria ripoti hiyo.

Ujumbe huu una habari vile vile kuwa serikali ya Zanzibar imeijadili ripoti hiyo juu ya mgawanyo wa mapato lakini serikali ya Muungano bado haikuijadili ripoti hiyo. Hata hivyo, maoni ya serikali zote mbili yatawasilishwa kwenye kamati ya pande mbili – Kamati ya Makamu wa Rais.

Lakini bado kuna shaka juu ya manufaa na uwezo wa tume hii kutatua matatizo yaliyoingizwa katika eneo lake la shughuli. Kuna shaka juu ya uwezekano wa kuainisha mapato ya Muungano na zaidi hasa, matumizi ya Muungano. Shida hizi zinatokana na muundo wenyewe wa Muungano.

Muundo wa wizara unaifanya shughuli hii kuwa ni ya kukatisha tamaa. Wizara nyingi zinaendesha shughuli zilizopanuka kupita ule mgawano wa mambo ya Muungano na yasiyokuwa ya Muungano. Katika hali kama hizo, itakuwa shida kugawa mapato na matumizi kwa Muungano au kinyume yake. Kadhalika, pale Bunge linapokaa kujadili bajeti ya Afya – jambo ambalo si la Muungano – kuna haja ya gharama hii kulipiwa na Muungano?

Page 76: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

62 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

Kuna usiri mkubwa juu ya suala hili, hasa upande wa serikali ya Muungano. Hili limekuwa na matokeo mengi. Si kama kwamba tume imechelewa kuzinduliwa tu, baada ya miaka 40 utaratibu wa muda wa kugawana mapato (4.5% kwa Zanzibar) mpaka hivi sasa umechukua miaka 15. Ilivyo, kodi ambayo Mamlaka ya Mapato ya Tanzania inakusanya (na ina madaraka ya kufanya shughuli zake Zanzibar kukusanya kodi kwa biashara ya kimataifa chini ya Umoja wa Forodha wa Afrika Mashariki) inabidi yende kwenye Mfuko wa Jumla. Lakini mwaka 1996 barua imeiagiza Mamlaka ya Mapato ya Tanzania iwasilishe makusanyo yote ya kutoka Zanzibar kwa Mkuu wa Idara ya Mishahara, Hazina, hapo Zanzibar. Mapato yanayokusanywa na Bodi ya Mapato ya Zanzibar nayo pia yanakwenda kwa Mkuu wa Idara ya Mishahara, Hazina. Kwa maneno mengine, mapato hutumika pale yanapokusanywa.

Mwisho, taratibu za muda kama hizi zinajenga mazingira ya kiza ambayo hatimaye yanadhalilisha hadhi ya Muungano na wakati huo huo kushindwa kutatua matatizo au kuuridhisha upande wowote ule.

Kwa upande mmoja, Zanzibar bado hairidhiki na 4.5% ambayo inapendekeza iongezwe na kuwa angalau 10% wakati serikali ya Muungano inasisitiza kuwa kiwango hicho ni cha juu sana lakini iko tayari kwa 5%. Kadhalika, malalamiko yanaendelea kuwepo kuwa serikali ya Muungano ndiyo peke yake inayolipia gharama za kukusanya mapato hapo Zanzibar, wakati Mamlaka ya Kukusanya Mapato (TRA) inawasilisha mapato yote iliyokusanywa kwa Zanzibar.

Hali kama hiyo ya kutoridhisha ni hitilafu iliyopo baina ya nafasi rasmi ya Benki Kuu, ya kuwa Benki Kuu inatakiwa iwe na akaunti mbili za kigeni kwa ajili ya Zanzibar na kwa ajili ya bara. Zanzibar haichangii katika hali hiyo na ina akauti yake yenyewe ya fedha za kigeni na benki yake yenyewe “People’s Bank”. Hii imezidisha malalamiko kutoka bara, juu ya Zanzibar kutochangia gharama za

Page 77: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Utaratibu wa Kutatua Matatizo ya Muungano 63

Muungano; kulipia mafuta kwa pesa za hapa nchini na kutochangia kwa malipo ya fedha za kigeni. Kwa hali hiyo hiyo ndivyo yalivyo malalamiko juu ya Zanzibar kunufaika na mikopo ya nje ambayo inafika mpaka Zanzibar, wakati Zanzibar haichangii katika kuilipa mikopo hiyo.

Ni wazi kuwa kuna matatizo yasiyodhibitiwa ambayo Kamati ya Pamoja ya Fedha (JFC) itachangia katika kuyatatua. Mambo ya kubahatisha na lawama hayafai kwa Muungano ulio imara. Kwa hiyo, ni jambo baya kuwa pande husika hazikutumia ipasavyo utaratibu huu ili kujaribui kutatua changamoto hizi muhimu.

Mchakato wa Muafaka Mada hii imechunguzwa kwa makini na Kituo Cha Katiba mahali pengine. Hapa tunaizungumzia tu kama inavyohusiana na suala la Muungano.

Kwa Miafaka inakusudiwa makubaliano ya kuleta amani kuhusiana na machafuko yaliyotokea baada ya uchaguzi Zanzibar. Mchakato wa majadiliano yaliyopelekea kuwepo kwa makubaliano haya, na nini kimetokea kuhusiana na utekelezaji wa makubaliano hayo ndiyo mada ya sehemu hii. Michakato hii inahusishwa na michakato ya uchaguzi kwa muktadha wa chaguzi zilizohusisha vyama vingi Zanzibar mwaka 1995, 2000 na 2005. Michakato hii inahusisha hasa chaguzi za raisi wa Zanzibar na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi. Haihusiani na chaguzi za Serikali ya Muungano ambazo kwa jumla huwa hazina matukio.

Tokea mwaka 1995 yamekuwapo matatizo makubwa ya udanganyifu katika uchaguzi pamoja na machafuko hasa mwaka 2001 na 2006. Michakato ya Miafaka mitatu ilibuniwa hasa kwa kushughulikia suala la chaguzi huru na za haki. Makubaliano ya awali ambayo yanahusiana na uchaguzi wa 1995 yalifikiwa mwaka 1999. Juhudi za kuleta makubaliano hayo zilifanywa hapa hapa Tanzania ijapokuwa yalisimamiwa na Jumuiya ya Madola. Inasemekana kuwa

Page 78: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

64 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

uchaguzi wa mwaka 1995 ulikuwa wa amani hasa kwa sababu CUF ilikuwa na umri wa miaka mitatu tu. Lakini zilikuwepo tuhuma za udanganyifu na kuchezewa kwa tarakimu kwa makusidi. Matokeo yaliyotangazwa yalikuwa 50.2% kwa CCM na 49.8% kwa CUF.

Muafaka I ulipendekeza iundwe tume ya rais kwa ajili ya utekelezaji wa Muafaka. Lakini hili halikuwa na nguvu ya kisheria na halikuweza kutekelezwa, na wengine waliliona kuwa halitofaa kwa kutekeleza marekebisho yaliyokubaliwa muda mfupi kabla ya uchaguzi wa mwaka 2000.

Baadaye, sheria ilitungwa na tume kuteuliwa lakini ilivunjwa kabla ya uchaguzi wa 2005 kwa kutokuwepo nia ya kisiasa na ukosefu wa fedha. Matokeo yake ni kwamba ni sehemu fulani tu ndizo zilizotekelezwa.21 Mambo muhimu yaliyotekelezwa ni pamoja na:

Kuifanyia marekebisho • Tume Ya Uchaguzi ya Zanzibar ( ZEC)Kuundwa kwa ofi si ya Mkurugenzi wa Kuendesha Mashtaka • (DPP)Maslahi ya kustaafu kwa viongozi wote waliostaafu •

Mambo mingine ya Muafaka ambayo hayakutekelezwa yalikuwa: Kulipa fi dia kwa nyumba ambazo zilibomolewa kwa sababu za • kisiasaKurudishwa shuleni watoto waliofukuzwa shule kwa sababu ya • kujiandikisha kupiga kura • Serikali ya Umoja wa Kitaifa haikuwezekana – na haikuwezekana tena baada ya Muafaka wa 2005.

Mchakato wa Muafaka wa hivi sasa, ambao ulifikiwa mwaka 2008 umekubali juu ya haja ya kuwa na serikali ya umoja wa kitaifa na utaratibu wa uwakilishi wa uwiano. Ulikwama kwa sababu mkutano wa CCM huko Butiama ulisisitiza kuwa hilo lipigiwe

21 Muafaka wenyewe umeelezea kuwa tume itamaliza muda wake kabla ya uchaguzi wa 2005. Ilivunjwa 2005.

Page 79: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Utaratibu wa Kutatua Matatizo ya Muungano 65

kura ya maoni. Palikuwepo na kutokukubaliana vile vile juu suala la muda wa utekelezaji. Kwa maoni ya wengi tuliowahoji, kura ya maoni inatumiwa na CCM kama kisingizio kukwepa kufikiwa kwa makubaliano ya amani kwa tatizo hilo. Ni kweli kuwa wengine walidhani kuwa kura ya maoni inayopendekezwa na CCM itayarudisha tena yale matokeo ya uchaguzi yaliyokaribia kulingana na labda kulizidisha tatizo. Yote mawili, matatizo ambayo mchakato wa Muafaka unajaribu kuyashughulikia na mchakato wenyewe, yanasababishwa na suala la Muungano.

Kwanza ni kiwango cha machafuko na hali ya kijeshi, ndivyo vitu vinavyohusishwa na mchakato wa uchaguzi. Machafuko yaliyohusiana na uchaguzi wa mwaka 2000 ilikuwa ni pamoja na vitisho na matumizi ya nguvu. Zilitumika nguvu kuwakatalia watu kujiandikisha. Kulikuwa na hadithi za wanajeshi kukusanya masanduku ya kura na kukaa nayo bila ya kuwepo mawakala wa vyama vingine. Maandamano yaliyofuatia yalikabiliwa na upigaji wa risasi, mauaji, mashambulizi ya kijinsia na uharibifu wa mali. Kama watu wengi tuliowahoji walivyosema, kwa mara ya kwanza Zanzibar ilizalisha wakimbizi waliokimbilia Shimoni na Mombasa nchini Kenya, na wingine hata mpaka Somalia. Wakati wa uchaguzi wa mwaka 2005, wiki chache kabla ya kupiga kura, walimiminika wanajeshi wakiwa na silaha nzito utadhani Zanzibar ilikuwa katika vita. Wanajeshi walipelekwa kutoka bara. Vikundi vingine vya usalama, vikosi vingine vya wapiganaji pamoja na Askari wa Magereza, Zima Moto, Vijana (janjaweed), Vikosi vya Kuzuia Magendo na Vikosi Maalumu vya Zanzibar. Wanajeshi hawa si kama waliwatisha watu na baadaye kujiingiza katika machafuko, bali inasemekana kuwa walipiga kura vile vile.

Ni wazi kuwa, na kama ilivyotiliwa mkazo na wengi wa wale tuliowahoji, hakuna haja au uhalali wowote wa kutumia wanajeshi wakati wa amani au uhalali wowote wa kuingiza na kuwatumia wanajeshi Zanzibar.

Page 80: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

66 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

Lakini lililo baya zaidi kwa Muungano na kinachoyafanya yote haya yawe sahihi hapa , ni kwamba kwa Wazanzibari, vikosi vya usalama vilijifanya kama kwamba wao ni jeshi la kigeni, jeshi la wavamizi. Hili ni tishio la kweli kwa Muungano na utashi wa Mkapa wa kutaka mazungumzo yaliyosababisha kuwepo kwa Muafaka II uliotiwa saini mwezi Octoba 2001 uonekani kwa muktadha huu.

Maelezo ya shahidi wa hili yalitolewa kwa ujumbe huu yalieleza kwamba, wakati CUF walipoanza kulalamika juu ya hali ya mchakato wa uchaguzi, viongozi walichukuliwa na kupelekwa kwenye kambi ya jeshi, walihojiwa na kuoneshwa silaha, mizinga na mashine za kijeshi na kuambiwa kuwa vitu hivi vimeletwa ili kuwashughulikia wao.

La pili na la umuhimu sawa ni lile la mchakato wa Muafaka ambao ni wa pande mbili kwa ulivyo. Mambo yanaandaliwa kwa mtazamo wa ushindani kati ya CCM na CUF. Hili linavitenga vyama vingine vya siasa, Jumuiya za Kiraia na wadau wengine wowote wale.

Baadhi ya vyama vya siasa havina ugomvi na hilo. Wanadhani kuwa utaratibu huu wa pande mbili unaonesha hali ya kisiasa Zanzibar. Wanadhani kuwa kuwepo kwao Zanzibar ni utaratibu tu. Ni kwa mujibu wa ‘sheria’ ili kukidhi mahitaji ya sheria. Kwa hiyo wanaamini kwamba kuwepo kwao kunaweza kuyakorofisha mambo badala ya kuuboresha mchakato wa Muafaka. Kwa wanavyodhani wao, vyama viwili hivyo vikiachiwa vifanye vinavyopenda vitaweza kufikia maamuzi kwa urahisi zaidi. “Kama huna kiti hata katika serikali ya mtaa … waachie wale wenye navyo.”

Hata hivyo, wengine, pamoja na Jumuiya za Kiraia, walifikiri vingine kuhusu mchakato huo. Walitilia mkazo haja ya kuwajumuisha wingine ukiacha CCM na CUF. Walidhani kuwa kuna haja ya kuvishirikisha vyama vidogo, wasomi, wafanyabiashara na raia kwa jumla. Walivilaumu vyama kwa kila wakati kushikilia misimanmo ya chama, na kuhitaji kusimamiwa na wale walio nje ya vyama vya siasa. Wametoa sababu za kuachwa Jumuiya za Kiraia kuwa ni namna isiyo rasmi na ya siri mazungumzo yalivyoanza, kwa kupitia mawasiliano

Page 81: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Utaratibu wa Kutatua Matatizo ya Muungano 67

ya watu binafsi. Wanatoa sababu za ugumu wa utekelezwaji wa makubaliano haya kuwa zinahusiana na ukweli huu.

Mvutano kati ya CCM na CUF juu ya mchakato wa Muafaka si kama unafanya iwe shida kwa mchakato huo kufanya kazi tu, bali unaathiri na Muungano vile vile.

Ijapokuwa masuala ya CCM/CUF yanatokana na historia ya Zanzibar na yanahusiana na mgawanyiko uliokuwepo kabla ya Muungano, kati ya Unguja na Pemba, kuchukuliwa hivyo, kutaleta dosari zisizorekebishika kwenye suala la Muungano.

Kuna watu wanaolielezea suala hili kuwa ni lile la CUF kuwakilisha Waarabu na kusababisha hatari ya kurudi kwao na kuiuza nchi. Wanaendelea kutuhumu kuwa CUF itairudisha Zanzibar kule kwenye kipindi cha kabla ya mapinduzi na kurudisha mali kwa Waarabu. Mawazo haya yametolewa na CCM Zanzibar. Wengi miongoni mwa watu tuliowahoji, kote, Zanzibar na Bara, wamezipinga tuhuma hizi na kuziita hewa tupu, dubwasha tu na hazina uhusiano wowote na ukweli. CUF yenyewe inakataa katakata kuwa na uhusiano wowote na ‘Waarabu’ na kufafanua kuwa inachosema ilani ya uchaguzi ya CUF ni kuwepo kwa hati ya ardhi ili kumwezesha mwenye kumiliki ardhi kuitumia kama dhamana ya kupata mkopo.

Kulikuwa na kukubaliana kuwa CCM bara ina mawazo mapana zaidi kuliko CCM ya Zanzibar. Inasemekana kuwa CCM Zanzibar ina ‘muhafidhina’wengi wenye kutaka kuyalinda ‘mapinduzi’. Wanapinga kwa nguvu kuwepo kwa serikali ya umoja wa kitaifa. Ni hawa vichwa ngumu wa CCM Zanzibar wanaoamini kuwa CUF inawakilisha Waarabu walioondolewa na mapinduzi na itakapoingia madarakani itawarudisha. Ilielezwa kuwa ni CCM Zanzibar ndiyo iliyotoa wazo la kura ya maoni – wazo ambalo baadaye likawa ndiyo msimamo rasmi wa Halmashauri Kuu ya CCM. Ilikuwa CCM Zanzibar iliyokataa kutia saini makubaliano ya Muafaka

Page 82: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

68 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

wa hivi mwisho, na siyo CCM Bara (kukataa kwa CCM kusaini makubaliano ilikuwa ni hofu ya chama kugawanyika).

Na hapa ndipo kiungo muhimu kwa suala la Muungano kilipo. Zanzibar haiwezi kutatua jambo lolote (kwa mfano ndai ya utaratibu wa Muafaka) yenyewe, kila kitu lazima kipitie kwenye ‘Muungano’ kwa kupitia CCM. Imesisitizwa kuwa majadiliano halisi ya Muafaka huenda CCM kabla ya kwenda CUF – abayo ndiyo inyowawakilisha watu Zanzibar. Ikiwa kuna makubaliano yoyote ambayo ingelibidi yafikiwe Zanzibar, lazima uwe Muafaka baina ya Wazanzibari, badala ya kulipeleka suala hilo bara na kulishughulikia huko.

CCM Bara inaweza kuwa na mawazo mapana zaidi lakini ni ajabu kuwa uhusiano wake na CCM Zanzibar unaufanya msimamo wa Zanzibar uwe mgumu na kuifanya isiweze kubadilika, asiyokubali jambo na isiyosikia jambo lolote juu ya majadiliano ndani ya Zanzibar yenyewe. Muundo wa pande mbili wa mchakato wa Muafaka ambao unazitenga sehemu nyingine za jamii ya Zanzibar unazidisha mvutano huu. Ile tuhma kuwa marais wapya wa Muungano wanakaidi kuliangalia suala hilo upya – ile dhana kuwa “Nimerithi serikali mbili” nitakabidhi serikali mbikli – “ serikali ya Zanzibar haitoangamia wakati mimi nikiangalia” – inazidi kutilia nguvu mawazo kuwa ni Muungano ambao siyo kama ndiyo chanzo cha udanganyifu wa uchaguzi na vurugu tu, bali vile vile ndiyo unaohusika na ukaidi wa CCM Zanzibar na kulifanya suala la usuluhishi wa amani miongoni mwa Wazanzibar kuwa ni jambo lisilowezekana.

Ni muhimu kuuangalia mchakato wa Muafaka kuwa ni utaratibu utakaoweza kutatua matatizo ya Muungano vile vile. Tayari tukiungalia uchaguzi wa mwaka 2010, dalili za hatari ya udanganyifu na vurugu zimeanza kuonekana. Madai ya watu kukataliwa kujiandikisha kwa kisingizio kuwa hawana vitambulisho kuhusiana na urekibishaji wa daftari la orodha ya wapiga kura Mwezi Mei 2009 kunatoa ishara ya matatizo yatakayo haribu uchaguzi wa mwaka 2010. Ujumbe

Page 83: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Utaratibu wa Kutatua Matatizo ya Muungano 69

huu pia umesikia malalamiko ya kufanyiwa marekebisho sheria ya uchaguzi kumtaka mkaazi wa Zanzibar kuwa na kitambilisho kabla ya kuandikishwa kuwa mpiga kura. Yamekuwepo malalamiko juu ya Masheha kuwanyima vitambulisho watu ambao walionekana kuwa na msimamo wa kivyama kwa upande mmoja; na kutoa vitambulisho kwa watu walio bara, pamoja na wale walio chini ya miaka 18.

Vyama vya Siasa, Viongozi na RaiaHawa hawawezi kuchukuliwa kuwa ni utaratibu wa kutatua masuala ya Muungano, lakini wana umuhimu mkubwa na wame au wanaweza kutoa mchango katika michakato hiyo.

Vyama vya Siasa

Vyama vya siasa vimetumiwa kuwa ndiyo utaratibu wa kushughulikia matatizo ya Muungano kwa muda mrefu. Haya yametamkwa mwaka 1977 pale vyama viwili (TANU na ASP) vilipoungana kuunda mfumo wa chama kimoja. Inaweza kueleweka kuwa ile kamati iliyotayarisha katiba ya chama ndiyo iliyotayarisha katiba ya Muungano.

Kuanzia hapo, matatizo mengi ndani ya Muungano yalitatuliwa ndani ya mfumo wa chama kimoja. Kwa hiyo, CCM kikawa ndiyo utaratibu ambao kwa kupitia chama hicho kero za muungano zingelijadiliwa katika kamati zake. Hiyo ndiyo sababu ya uamuzi wa CCM wa kutumia mapato pale yanapokusanywa.

Hii haina maana ya kusema kuwa utaratibu huu kila wakati uliridhisha. Inasemekana kuwa, viongozi wa Zanzibar mara walibaini kuwa kwa kupitia kwenye chama na katiba za Muungano, uhuru wa Zanzibar umepungua sana. Inasemekana vile vile kuwa hata sasa Zanzibar haina ushawishi mkubwa ndani ya vyombo vya juu vya CCM, ijapokuwa Kamati Kuu ya chama ina wajumbe kutoka bara na Zanzibar.

Page 84: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

70 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

Imedaiwa kuwa, CCM inaogopa kuwepo kwa serikali imara Zanzibar. Vile vile, kuna tofauti za kimsingi pale inapokuja kwenye kero maalum za Muungano. Kuhusu mafuta, kuna tofauti ndani ya CCM; CCM ya Zanzibar haikubaliani na CCM ya Bara. Kwa hiyo, juu ya masuala kama hayo, lililomuhimu siyo kuwa upinzani upo madarakani Zanzibar au la, lakini la muhimu ni kama raia wanahusishwa katika kufanya maamuzi – jambo ambalo ndilo linalokuwa suala la msingi. Zaidi ya hayo, kama ilivyokwisha elezwa hapo awali, CCM ya Zanzibar ni wakaidi kwenye mazungumzo yanayohusu Muafaka kuliko bara. Ilielezwa kuwa baadhi ya walio ndani ya CCM bara wanadhani ingelikuwa vizuri kushughulika na CUF kwa sababu hawajui CCM Zanzibar wanataka nini wakati angalau wanajua nini CUF wanataka. Hii inatokana na mawazo kuwa CCM Zanzibar ina watu wengi wanaotaka kuyalinda mapinduzi na kwa hivyo wanazuia harakati zozote za kutaka kuleta mabadiliko.

Mfumo wa vyama vingi ulianzisha utaratibu wa mambo mapya. Kimuundo, ni tabu kushughulikia mambo kwa namna ile ile ya zamani. Kwa kiasi fulani, hili linaelezea mvutano wa tume ya mambo ya Muungano. Hata hivyo, imeripotiwa kuwa, mchakato wa ndani bado unaendelea ndani ya CCM, kujaribu kutatua masuala ya Muungano kwa kutumia utaratibu wa chama wa CCM kwa CCM. Hii hairidhishi kwa sababu sasa kuna vyama vingine Zanzibar. Lililo muhimu sasa ni kwa vyama vyote Zanzibar kukaa pamoja, kujadiliana na kukubaliana na bara. Makubaliano ya CCM kwa CCM ni matokeo yasiyokamilika, wakati vyama vingine vimetengwa. Lazima utafutwe mtazamo mpya ambao Wazanzibari na bara kila mmoja anakaa chini na kukubali.

Kwa kufikia hali hiyo, panahitajika uwajibikaji na utashi mkubwa upande wa CCM. Kama ilivyoelezwa, uwezo wa kuanzisha mabadiliko umo ndani ya mikono ya CCM na cha msingi kinachohitajika ni nia ya kisiasa na moyo wa ujasiri. Kikiwa ni chama tawala, kote,

Page 85: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Utaratibu wa Kutatua Matatizo ya Muungano 71

Zanzibar na bara , inabidi kiwe na uwezo wa kufanya kitu kama hicho. Jukumu kubwa kama hilo kwa CCM inasemekana kuwa linakwamishwa na “ubinafsi”.

Wajibu wa vyama vingine katika kutatua matatizo ya Muungano, ikiwa ni pamoja na mchakato wa Muafaka lazima upimwe kwa kuzingatia mambo fulani. Kwanza, vyama vya siasa kisheria lazima viwe na wanachama Zanzibar na bara; kinyume ya hivyo, havitasajiliwa. Kwa kuwa ni lazima vijitanue baina ya Zanzibar na bara, kinadharia, hii itawafaa sana katika kuyashughulikia masuala ya Muungano, pamoja na Muafaka kwa namna ya haki. Itavifanya hata kuwa ndiyo vikao vinavyostahili kwa ajili ya majadiliano juu ya masuala ya Muungano.

Ukweli wa mambo ni kwamba, kama ilivyoelezwa awali, vyama vingine ni vidogo mno. Mtu mmoja aliyehojiwa alisema.

Hatupo ipasavyo Zanzibar na Pemba. Tumetekeleza matakwa ya sheria lakini hatupo kule. Popote pale huwezi kukosa watu wa kufuata mkumbo… mahitaji ya sheria yanatutaka kufanya kampeni, kumshughulikia kila mmoja, na hata kwenda Pemba. Tulidhani kuwa hilo si wazo baya. Linavifanya vyama vionekani kuwa na uwakilishi wa kitaifa. Unaweza kufanya kampeni ukavutia umati mkubwa lakini usipate hata kura moja.

Mtu anaweza kuwa na shaka kuwa vyama vingine vinahisi labda vina jukumu dogo sana Zanzibar. Hili linaonekana kwa mtazamo wao katika michakato ya Muafaka. Imeelezewa vile vile kuwa vyama vya siasa vinaogopa kuchukua msimamo wowote juu ya masuala ya Muungano kwa sababu ya mipaka ya kisheria: Vyama vya siasa ni jambo la Muungano na Sheria ya Vyama vya Siasa haviwaruhusu kuzungumza juu ya kuvunjika kwa Muungano. Labda vyama vya siasa vinashindwa kujua uwezo waliokuwa nao katika kuzishughulikia kero za muungano, ijapokuwa ilani zao za uchaguzi zinazungumzia baadhi ya matatizo ya Muungano.

Page 86: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

72 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

Kama ilivyoelezwa, uwananchi wa Zanzibar si suala la kichama. CCM na CUF wote wana msimamo mmoja juu ya suala la kero za muungano. Kwa hiyo, kuna msingi mzuri wa vyama vyote vya siasa kuzishughulikia kero za muungano kwa namna ambayo si ya kichama na kwa maslahi ya taifa. Kwa mantiki hii, vyama vya siasa kwa ujumla wao ni utaratibu wa kitaifa wa kushughulikia masuala ya Muungano.

Viongozi na Idara za SerikaliIdara za Serikali

Idara za serikali zingelichangia katika kutatua matatizo ya Muungano, hasa kama zingelifanya kazi kama zilivyokusudiwa kufanya kazi. Utendaji wa miundo ya serikali kuhusiana na Muungano umezungumzwa katika sehemu mbalimbali za ripoti hii. Kuna vitu vichache vya ziada vya kuelezea kuhusiana na wajibu wao zikiwa ni utaratibu wa kushughulikia kero za muungano.

Moja ya matatizo kuhusiana na hili ni dosari za hapo mwanzo za kuanzisha kwa dharura muundo wa Muungano. Kama ilivyoelezwa kabla, Mkataba wa Muungano ulifikiria tume ambayo ingeliundwa ili ndani ya kipindi cha miezi 12 tokea kuundwa kwa Muungano, ingeliandaa mapendekezo ya muundo wa kudumu wa Muungano. Hili halijawa katika kipindi hicho. Kwa hiyo, idara za serikali, kwa muda mrefu zimefanya shughuli zake katika hali hii iliyokuwa na dosari.22

Hata hivyo, wizara ya Waziri wa Nchi Anayeshughulikia Mambo ya Mungano inatarajiwe iwe ndiyo utaratibu wa kweli wa kushughulikia kero za muungano. Wajibu wake unaweza kuwa ni wa moja kwa moja au kwa kupitia taratibu nyingine, kama vile tume na kamati.

22 Tume ya chama iliyoviunganisha vyama viwili iligeuzwa kuwa hiyo Tume ya muundo wa kudumu wa Muungano iliyofikiriwa.

Page 87: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Utaratibu wa Kutatua Matatizo ya Muungano 73

Zaidi ya hili, pamekuwa na maoni kuwa mikutano ya serikali haikuleta matokeo yoyote kwa sababu nia ya CCM ni hatimaye kuwa na Muungano wa serikali moja. Kwa sababu hii, kwa namna yoyote ile iliyo chanya ambayo wizara hii itaendeshwa, ila kama itajengwa imani, juhudi zake zinaweza kufikiriwa kwa mawazo hasi, na kwa shaka, badala ya wizara hiyo kuchangia katika kutatua matatizo.

Kadhalika, kuna hali ambazo itazifanya idara za serikali kuwa ni taratibu za kawaida za kuendesha Muungano kwa utulivu. Kwa mfano, inasemekana kuwa serikali ilikubali utaratibu wa kugawana vyeo ndani ya serikali ya Muungano, lakini ukosefu wa watu wenye sifa unazuia utekelezaji wa utaratibu huu. Ufumbuzi wa kuridhisha utazifanya idara za Muungano zisionekane kama kuwa ni za kigeni na zinaihusisha zaidi Zanzibar.

Tume hii amearifiwa vile vile kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imekasimu madaraka yake mengi kwa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kuhusiana na chaguzi za rais wa Muungano na wabunge, mahali ambapo tume hiyo ina uwezo wa kisheria. Ushirikiano kama huu kati ya idara za serikali katika nyanja mbali mbali, kama vile ukusanyaji wa mapato n.k utasaidia sana katika kujenga sura chanya ya Muungano.

Kadhalika, makubaliano kati ya serikali mbili kuajiri mtaalam kutoka nje atakayeshughulikia juu ya namna gani ya kugawana maslahi na gharama za gesi na petroli, akiwa na hadidu za rejea mahsusi, ni mfano wa ushirikiano chanya wa serikali katika kuzishughulikia kero za muungano. Yakijumuishwa yote haya katika upana wa serikali, yatajenga mwanzo mwema katika kutatua matatizo.

Viongozi

Viongozi mbalimbali wamejaribu kwa namna zao wenyewe kuchangia katika kutatua matatizo ya Muungano. Majaribio haya

Page 88: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

74 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

yamefanywa wakati watu hao walipokuwa wakishiriki kikamilifu serikalini au kwa suala la Muafaka, baada ya kustaafu.

Mifano inayotolewa mara kwa mara ni ile ya Aboud Jumbe na Kundi la watu 55 (G55) na wazee wengine. Inasemekana kuwa Jumbe amechangia katika kuwepo Muungano bora kwa kuregeza hali ya mambo Zanzibar na kupitisha katiba mwaka 1979. Wengi tuliowahoji wamesema kuwa kuungana kwa CCM na ASP, ni juhudi za dhati za Jumbe za kuufanya Muungano ufanye kazi. Kuhusiana na hili, imesemwa kuwa waliomtangulia watajificha nyuma ya ASP kupinga hatua za Muungano, wakisema kuwa ASP ilikataa kuzikubali hatua hizo. Kwa hiyo, Inasemekana kuwa Jumbe alijaribu kuiunganisha nchi zaidi kuliko alivyowahi kufanya mtu yeyote.

Aliajiri mwanasheria kutoka Ghana ili kutengeneza utaratibu wa serikali tatu. Kuondolewa kwake serikalini na kwenye nafasi yake katika chama kwa lazima mwaka 1984 kwa sababu ya juhudi zake za kutaka kujenga Muungano unaofanyakazi vizuri labda kwa imani kubwa, kunaonesha matatizo ya Muungano. Ikumbukwe kuwa Jumbe ndiye aliyesisitiza vile vile kuwepo kwa kipengele cha mahakama ya katiba kusuluhisha matatizo ya Muungano. Ndani ya vyombo vya chama, alishutumiwa kwa kukidhalilisha chama kwa siri.

Kundi la watu 55 (G55) lilikuwa ni la viongozi wa bara ndani ya bunge waliotaka kuifufua serikali ya Tanganyika. Kwa hiyo, kundi la watu 55, lilitaka kuanzisha muundo wa Muungano wa serikali tatu. Hawa walionekana kuwa ni waasi. Walinyamazishwa bungeni walipolileta suala la Mkataba wa Muungano. Walikaripiwa. Ilisemekana kuwa Mwalimu Nyerere aliliita kundi zima na kuwaonya na baadaye aliendelea kukutana nao kila mmoja peke yake.

Hofu ya kuruhusu mjadala wa wazi juu ya masuala ya Muungano haikuwaathiri viongozi kama Jumbe tu au kundi la watu 55. Ilivuruga vile vile juhudi za wananchi pamoja na jumuiya za kiraia kushiriki kikamilifu katika kutatua matatizo ya Muungano. Kwanza

Page 89: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Utaratibu wa Kutatua Matatizo ya Muungano 75

kuna taarifa za wananchi kutoelewa masuala ya Muungano na taratibu zake. Historia ya usiri, tokea mwanzo wakati Muungano unaanzishwa, haikusaidia kitu.

Tume hii iliarifiwa kuwa wananchi wanazungumza masuala ya Muungano, lakini si kwa kufuata utaratibu maalum. Hii inaweza kuwa katika mikutano au katika vyombo vya habari. Miongoni mwa jumuiya ra kiraia, kwa mfano, mnamo miaka ya 1990, yalikuwepo majadiliano juu ya masuala ya katiba. Hii labda ilikuwa inahusiana na Tume ya Nyalali. Kwa hiyo, majadiliano juu ya masuala ya Muungano kwa jumla, yalikuwa si wazi. Masuala kama hayo yanaweza kujitokeza miongoni mwa jumuiya za kiraia, kwa mfano, wanapozungumzia suala kufungua ofisi Zanzibar. Iliripotiwa kuwa mkutano wa amani wa jumuiya za kiraia ulisitishwa katikati na serikali huko Zanzibar mwaka 1999.

Matarajio ya kushiriki kwa raia ikiwa ni utaratibi wa kutatua matatizo ya Muungano yanaonekana kuwa ni ya kukatisha tamaa kutokana na yote haya.

Mwisho Pamekuwepo taratibu namna mbalimbali, zilizo rasmi na zisizokuwa rasmi, za kutatua matatizo ya Muungano. Nyingi katika hizi zimekuwa za dharura. Waliokuwa na madaraka katika baadhi ya taratibu hizo wamekuwa wakitiliwa wasiwasi. Pamekuwa na ajali za kisiasa katika juhudi hizo. Inaweza kusemwa vile vile kuwa juhudi hizi zimekuwa na mafanikio madogo kiasi kwamba matatizo mengi bado yapo palepale. Wengine wanaweza kusema kuwa taratibu hizi zimefanyakazi kwa kuwa Muungano umeishi kwa zaidi ya miaka 45.

Tume hii imeelezwa kuwa siasa za Afrika mara nyingi huamuliwa na viongozi wenye vipaji. Wale waliodhani hivyo, wakati huo huo hawakuwa na mategemeo mema kuhusiana na Muungano. Walihisi kuwa Muungano ulianzishwa na viongozi wenye vipaji. Ulistawi juu ya kuwepo matatizo magumu juu ya mgongo wa uongozi

Page 90: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

76 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

wenye kipaji. Kwa hiyo, wanahitimisha kwa kusema kuwa, bila ya serikali ya chama kimoja na kutokuwepo kwa uongozi wenye kipaji, mategemeo ya juhudi kama Muafaka au Muungano kwa jumla, ni ya kukatisha tamaa.

Ni kwa sababu ya haya ndiyo mapendekezo kuhusiana na utaratibu utakaoweza kushughulikia kero za muungano yamependekezwa. Mapendekezo hayo ni pamoja na kuwepo kwa Baraza la Serikali la kushughulikia mambo ya Muungano; likiwa na wajumbe sawa kutoka bara na Zanzibar. Ilipendekezwa pia kuwepo kwa mabunge mawili; pamoja na kupitiwa upya katiba ili kuuwezesha Muungano kuishi na kufanyakazi bila ya matatizo katika kipindi cha baada ya mfumo wa chama kimoja katika Tanzania.

Page 91: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

77

5 Mustakabali wa Muungano

Utangulizi Sura hii ni juu ya maoni ya Watanzania juu ya mustakabali wa Muungano. Baadhi ya maoni haya yalitolewa moja kwa moja. Wakati mwingine, hisia za watu wengi juu ya suala hili zimeripotiwa na wale ambao tume hii imekutana nao.

Katika kujadili mustakabali wa Muungano kama unavyoonekana na Watanzania, mambo muhimu ya kweli ambayo tume hii ilielezwa lazima yazingatiwe.

La kwanza ni ukweli juu ya uzalendo wa Zanzibar. Kuna mwamko mkubwa juu ya utambulisho wa Zanzibar miongoni mwa Wazanzibari, mwamko ambao unaonekana kwa uwazi zaidi kuliko mawazo yoyote ya utambulisho wa Mtanganyika kwa upande mwingine. Hili, wakati mwingine linahusishwa na mawazo juu ya kupoteza au wasiwasi wa uwezekano wa kupoteza utambulisho; pamoja na uhuru wa Zanzibar.

Taswira hii pia inajitokeza kwenye kutoridhika na Muungano kwa hali yake ya hivi sasa. Kadhalika, kutoridhika huku kupo wazi kabisa na kunaelezwa kwa nguvu Zanzibar kuliko bara, ijapokuwa na bara nako kutoridhika kama huko kupo vile vile. Kwa jumla, hili linahusiana na suala la muundo wa Muungano pamoja na ongezeko la kihistoria la orodha ya mambo ya Muungano.

Jingine la muhimu ni ukweli kuwa wengi miongo mwa tuliowahoji wanataka Muungano uendelee, lakini wanadai Muungano wa haki. Wazo la Muungano wa haki linaonesha kuwepo haja ya haraka ya mabadiliko; hili linafanywa liwe la haraka zaidi kufuatia kuanzishwa

Page 92: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

78 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa ambao umekuwepo kwa zaidi ya muongo mmoja sasa.

Kuna wale wanaotaka muungano uvunjike. Kuna wale wasiojali juu ya kuendelea kuwepo au kotokuwepo kwa Muungano. Lakini wingine, ijapokuwa wangelipenda Muungano uendelee kuwepo, wanauogopea kwa dhati; wana wasiwasi na mustakabali wake kutokana na uzito uliokuwepo katika mchakato wa kufanyiwa marekebisho, na hata kule kutokuwa tayari kujadili au kujadili kwa kina masuala ya Muungano.

Mustakabali kama unvyoonekana katika misimamo hii umeanza. Lakini kingine kilichoanza katika sura hii ni njia zilizopendekezwa ili kufikia dira hii ya mustakabali.

Muungano ndiyo Mustakabali Kuna hisia kali miongoni mwa wananchi kuwa hakuna anayetaka kuuvunja Muungano. Hisia hizi zilionekana kote, Zanzibar na bara:

Hakuna anayesema hautaki Muungano; wote wanautaka • Muunganio lakini wanataka matatizo yake yatatuliwe. Muungano umeimarika, hakuna hisia kali dhidi ya Muungano: • masuala yanafanana, uwezo wa kujiamulia mambo wenyewe, mgawano wa maslahi na gharama, kufafanuliwa kwa mamlaka za kutoa haki n.k. Muungano wenyewe umekubaliwa, lakini kupanuliwa kwa • mambo ya Muungano kupita yale kumi na moja ya awali ni jambo jingine. • Jumuiya za kiraia zingelipenda kuuona Muungano ukiendelea – lakini ukiwa umefanyiwa marekebisho. Vijana waliozaliwa ndani ya Muungano hawajui kingine • chochote; watauunga mkono Muungano. Muungano utaendelea kuwepo lakini utahitaji kuangaliwa • upya.

Page 93: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Mustakabali wa Muungano 79

Sina tatizo na Muungano – ila hali ya kuundwa kwake na • uendeshwaji wake - usiri.Wazo la kuuvunja Muungano halipendwi, hata • CUF ambayo ni Mzanzibari wa nguvu haizungumzii kuvunjika kwake. Hakuna yoyote miongoni mwetu mwenye nia ya kuuvunja • Muungano, Muungano hautafi kia mwisho. Zanzibar inataka • Muungano wa usawa na siyo mwisho kwa Muungano.

Tume ya Nyalali imeelezewa kuwa ilisema kwamba watu wanaamini juu ya Muungano na kwa hiyo ubaki. Wengine waliohojiwa walikuwa na matarajio mema zaidi juu ya mustakabali: “Kila siku tunakuwa karibu zaidi”.

Kuhusiana na hili, faida na maslahi ya Muungano yameelezwa: “Pande zote mbili zimenufaika na Muungano; kwa mfano uhuru wa mtu kwenda atakako na uhuru wa kujieleza, uhuru wa kuikosoa serikali kwa Zanzibar, mahusiano ya kijamii yanayozidi kukua, kuchanganyika kwa watu, uhuru wa kwenda popote, na hasa kuhusiana na ukosefu wa ajira Zanzibar, usalama n.k…” Baadhi ya waliohojiwa bara wameeleza kuwa kuna Wazanzibari wengi bara: “Tunaishi kama ndugu, hatuna matatizo.” Wengine wanaona kuwa matatizo ni mengi kuliko maslahi; urari huu unaonesha hisia kuwa Muungano hauhitajiki Zanzibar, kwa kuwa umemaliza uhuru wake wote.

Lakini wengine wanauona usalama wa mustakabali wa Muungano kuwa umetia mizizi, si lazima kwa marekebisho ya utaratibu wa sasa:

Tunazungumzia biashara siyo utawala; sisi hatujali vitu kama hivyo. Ni kundi dogo linalopigania uhuru; wengi tunatazamia maingiliano. Muungano umekuwapo kwa miaka 40. Baada ya hapo, mgawanyiko ni wa bandia; ni siasa. Wazanzibari wana furaha ndani ya Muungano, wana furaha na biashara. Biashara

Page 94: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

80 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

ya karafuu imekufa kwa hiyo Muungano una faida kwao. Katika biashara, siasa tunaziweka upande. Kwenye soko huria, fursa za biasghara ndizo zinazoamua mtu ende wapi.Baya zaidi, mtu mmoja ameeleza, ni kuwa kule Tanzania kupeleka

wanajeshi Comoro chini ya mwavukli wa Umoja wa Afrika ni ishara ya chini kwa chini kwa Zanzibar kuwa hawatoruhusiwa kujitenga. Hili linatofautiana na inavyosemekana kuwa ilikuwa jawabu ya Mwalimu alipoulizwa swali juu ya kuiunga mkono kwake Biafra: “Ikiwa Zanzibar itataka kujitenga sitoipiga mabomu.”

Kuhusu kama Muungano utaendelea kuwepo ukiwa na serikali mbili, kila moja ikiongozwa na chama tofauti, maoni ya watu yaligawanyika. Wale waliodhani kuwa inawezekana, walisema kuwa huo utakuwa ni Muungano tofauti. Lakini wingine walisisitiza umuhimu wa mustakabali wa Muungano kwa kuchora picha ya mustakabali wa maangamizi bila ya Muungano. Hii ni hisia ambayo ujumbe huu iliisikia bara tu, lakini siyo Zanzibar. Hii ni kwa sababu kuwa, kama Muungano utavunjika, Zanzibar nayo itasambaratika vile vile; kwamba Pemba na Unguja kila moja itakwenda njia yake. Wingine wamesema kuwa, kuvunjika kwa Muungano kutasababisha balaa na Zanzibar itakuwa Somalia ya pili. Wingine walimnukuu Mwalimu kuwa alisema: “Bila ya Muungano hakuna Zanzibar.”

Mustakabali bila ya MuunganoKuna wale wasiojali kuhusu mustakabali wa Muungano na pia kuna wale wanaotaka uondoke kabisa. Mawazo haya utayasikia ukivuka bahari.

Kuna wale wanaouona Muungano kuwa ni jambo la kulazimishwa na kwa namna yoyote ile wangelipenda kuuona ukimalizika. Kwa mfano, imesemwa kuwa “Zanzibar imechoka na Muungano na itatumia fursa yoyote itakayotokea kuelezea kutokuwa na imani kwake. Vile vile, kuna waliopo Zanzibar ambao wanaliona jeshi na polisi kuwa ni vyombo vya bara vinavyoulazimisha Muungano. Kwa

Page 95: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Mustakabali wa Muungano 81

sababu ya kubadilika kwa mambo duniani, itakuwa shida kutumia nguvu dhidi ya watu, kushikilia na kuulazimisha Muungano”. Hisia kama hizi zimeelezwa kwa nguvu zaidi kuwa: Zanzibar ni koloni la Tanganyika; watu wamekufa kwa sababu ya mapigano baina ya koo huko bara lakini serikali haipeleki wanajeshi. Lakini Pemba, ambako kuna amani, wanapelekwa.

Inasemwa huko bara kuwa hali ya Zanzibar imebadilika: “Lugha inayotumika sasa huko Zanzibar ni kuwa watu wa bara ni wakoloni. Sisi watoto wa Waisilamu wa Zanzibar lazima tuchukue hatua dhidi ya watu wa bara”.

Baadhi ya Wazanzibari wanaeleza kuwa (kama Ireland ya Kaskazini) Zanzibar haijawahi kuwa eneo lililoshidwa vita la Tanganyika na kwa hiyo wanaweza kudai kurudishiwa uhuru wao.

Shaka juu ya Muungano inaelezwa kwa namna nyingine. Imeelezwa kuwa Muungano upo kwenye uwanja wa kisiasa tu lakini haugusi mambo mingine; kiutamaduni na kijamii kila upande uko peke yake. Maoni kama hayo yametolewa kwa maelezo kuwa huu ni “Muungano wa viongozi“. Wengine wameeleza juu ya mhamo wa kizazi. Sasa kuna mawazo, fikra na mitazamo tofauti na ile ya waasisi (Karume na Nyerere). Imesisitizwa mara kwa mara kuwa, kwa kizazi kipya kilichozaliwa baada ya kuudwa kwa Muungano, Zanzibar inakuja kwanza na baadaye Tanzania. Wanahisi kuwa wao, kwanza ni Wazanzibari na wasingelipenda kupoteza utambulisho wao.

Wingine wameelezea juu ya kuporomoka kwa Muungano. Ishara moja ni kuondolewa kiungo kati ya pande mbili pale rais wa Zanzibar aliposita kuwa moja kwa moja makamu wa rais wa Muungano. Wingine wamekuona kuporomoka huko kwenye suala la mafuta: “Suala la mafuta litausambaratisha Muungano na kumaliza utumwa wa kidemokrasia. Naupenda Muungano lakini siyo katika hali yake ya hivi sasa”. Bara, kumekuwa na mawazo kuwa hali ya Zanzibar ni ya hatari kwa kutokuwepo utaratibu wa kusawazisha mambo yaliyobaki. Kwa upande mwingine, walikuwepo watu Zanzibar

Page 96: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

82 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

waliodhani kuwa watu wa bara wanaiona Zanzibar kuwa ni mzigo usio wa lazima, kuwa wamechoka na Muungano na wanaudhiwa na Zanzibar kushiriki katika mambo yao ambayo si ya Muungano. Kwa bahati mbaya, mawazo hayo si kama kuwa si ya msingi kabisa.

Mtu mmoja aliyehojiwa bara aliielezea hali kama ifuatavyo: “Kuna watu wenye siasa kali pande zote mbili; kuna watu wa bara wanaosema, “wacha Zanzibar iende tunalipa gharama bure” na kuna Wazanzibari wanaosema, “mnatumeza tunahitaji uhuru wetu.”

Watu wa bara wameelezea hisia zao. Kuna wale wanaouliza faida wanayoipata kutokana na Muungano. Wingine wangelisema, “Wachana na Zanzibar” na kuacha kushughulikia mambo muhimu ili kushughulikia mambo ya upuuzi.

Wingine walidai kuwa, kama ingelipigwa kura ya maoni watu wengi wa bara wangeliiacha Zanzibar iende: “Tumewabeba kwenye migongo yetu kwa muda mrefu, tumechoka, sasa wameshakua watoto wakubwa”. Kuhusiana na hili, ilielezwa kuwa alikuwa Nyerere (baada ya kifo cha Karume) aliyekuwa mhimili wa Muungan na aliyepinga kupigwa kura ya maoni juu ya Muungano na kwa hiyo, Muungano unaweza kuvunjika katika kipidi cha baada ya Nyerere.Mtu mmoja aliyehojiwa ambaye alikuwa wazi kabisa katika kueleza hisia zake alisema:

Mimi sioni faida ya Muungano, inawezekana labda za kisiasa. Lakini nikiwa mtu wa bara sioni faida zinazoweza kuonekana kutokana na Muungano. Zinaweza kuwepo, zinaweza zisiwepo. Labda ule uajabu, kama tunavyoambiwa, wa Muungano huu hasa, ndiyo ‘faida’ ya pekee.

Kutokana na yote haya, mtu anaweza kukubaliana na umuhimu wa ukweli wa maelezo kuwa, kinadharia kila mtu anauunga mkono Muungano; au mawazo kuwa yapo mahusiano ya kidugu na Kenya na Uganda; kwa hiyo Muungano siyo mahitaji ili yawepo mahusiano ya kidugu.

Page 97: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Mustakabali wa Muungano 83

Muungano wa Haki Kama ilivyoelezwa hapo awali, wengi wa wale walioohojiwa walieleza juu ya kuunga mkono Muungano. Kadhalika, wengi sana wa wale waliohojiwa wameeleza kutoridhika kwao na hali yake ya hivi sasa. Mara kwa mara, wale walioohojiwa, kwa namna tofauti wameeleza juu ya Muungano wa haki, wa usawa au endelevu. Wengi wanadhani kuwa bila ya hivyo, Muungano hauna mustakabali wowote.

Moja ya mambo muhimu ya Muungano wa haki, wa usawa na endelevu ambalo limetliwa mkazo na watu wengi, ni Muungano wenye kuzingatia maslahi. Walizungumzia juu ya Muungano ‘unaoshughulikia maslahi yao, Muungano unaonufaisha pande zote mbili’. Ilitiliwa mkazo kuwa, ikiwa Muungano utashughulikia maslahi yao, Wazanzibari watalipa fadhila; na kuwa Muungano utakuwa imara tu, kama utashughulika maslahi ya wanachama.

Jambo jingine ni usawa. Pande zote mbili zichukuliwe kuwa ni wabia walio sawa na Zanzibar isichukuliwe kuwa ni mkoa mwingine wa Tanzania. Kwa hiyo, Muungano wa haki usiimeza Zanzibar. Uheshimu utambulisho wao na uhuru, kila upande ushughulikie mambo yake yenyewe. Hii ionekane katika muundo wa Muungano, lakini vile vile dira ya hayo iwe ni pamoja na alama kama bendera, nyimbo ya taifa, mahitaji ya itifaki, na kwa wengine hata vitu vya kudumu kama Sarafu ya Zanzibar.

Dira ya Muungano wa haki ni pamoja na Muungano huo kuwa wa makubaliano ya wote na nia safi. Katika hali hii, imeelezwa kuwa Muungano endelevu ni muhimu sana, uendeshwe kwa uwazi, wa kirafiki, wa hali ya kuwa wote ni washindi. Uvamizi wa kijeshi Zanzibar wakati wa uchaguzi ni kinyume na dira hii.

Muungano wa Serikali Tatu Jambo la msingi katika dira ya Muungano wa haki ni muundo wake. Tumelijadili jambo hili kabla. Hapa linatajwa likiwa ni jambo linalohusu Muungano wa siku za mbele.

Page 98: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

84 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

Ka Zanzibar. Masuala ya utambulisho na matakwa ya uhuru yamepitia kwenye vizazi vitatu tokea Muungano ulipoanzishwa. La pili, ni kwamba inawezekana kuwa hakuna imani ya dhati hivi sasa juu ya msimamo rasmi wa CCM kuhusu serikali mbili zitakazoelekea kwenye serikali moja. Hii siyo kwa sababu hili hudaiwa kwa nadra hivi sasa, lakini vile vile kwa sababu hakuna hatua madhubuti zinazochukuliwa kuelekea kwenye serikali moja. Na kuhusu umoja chama cha CCM juu ya msimamo huo inasemekana kuwa umejificha kwenye msimamo wa CCM (Zanzibar) wa serikali tatu. Na Zanzibar nayo inautafsiri Muungano wa serikali moja kuwa ni kuimeza Zanzibar. Kinyume yake, dira za Muungano wa serikali tatu zimedhihirisha: Mabunge mawili, serikali ndogo ya Muungano yenye uwezo mdogo wa kisheria n.k.

Vikwazo vya Muungano wa Haki Zimetolewa sababu nyingi zinazokwamisha kushughulikiwa kwa matatizo ya muungano. Matatizo haya ama yamepuuzwa au juhudi za kutatuliwa kwake zimekandamizwa kwa nguvu. Na kwa hili kinacholaumiwa sana ni chama tawala CCM.

Jumbe ananukuliwa kuwa alisema, malalamiko juu ya mustakabali wa Muungano yameletwa kila siku, lakini kila siku yamekuwa yakikandamizwa. Hatima yake labda ni ushahidi wa wazi kuhusu ukweli wa maoni hayo. Ilielezewa kuwa machafuko ndani ya Muungano yataendelea mpaka yatakaposafishwa, badala ya kujaribu kuyaficha. Wengine wamesema waziwazi kuwa chama tawala kinataka kuyaziba mambo kwa kizibo.

Kadhalika, kuhusu marekebisho ya katiba, wengine wamebaini kuwa chama tawala kimekuwa kikaidi isipokuwa pale palipokuwa na maslahi kwao; na kwa hiyo, katiba kufanyiwa marekebisho ni jambo lisilowezekana kwa kuwa upinzani ulikuwa hafifu.

Yote haya yamekuwa na matokeo kadha. Imeripotiwa kuwa watu wengi, (kote, bara na Zanzibar) wanaogopa kusema ukweli juu ya Muungano. Hawana ujasiri wa kusema juu ya kutoridhika kwao na

Page 99: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Mustakabali wa Muungano 85

Muungano. Hali kama hiyo ni wazi kuwa si nzuri kwa majadiliano ya wazi yaliyokusudia kujenga.

Wengine wanaona kuwa pengo kati ya viongozi na wananchi kuhusu suala hili linazidi kupanuka. Hili limeelezwa kwa njia mbalimbali. “Sasa wote wale wanohusika wanachelewesha mchakato wa kushughulikia na kutatua tatizo. Ni suala la muda. Siku za mbele itabidi matatizi yashughulikiwe kwa lazima. Lakini sasa hali inasababisha kukata tamaa miongoni mwa watu. “Ikiwa watu wanahisi kuwa wanatengwa, na Muungano nao pia utatengwa.” “ Kura ya maoni juu ya Muungano inaogopwa bara, lakini inawezekana Muungano ukadumishwa kwa kura ya maoni kama hiyo. Hofu hasa ni ya kuogopa watu kuwa na sauti, watu kupewa madara makubwa sana. Demokrasia inaogopwa.” “Kura ya maoni inategemea uongizi. Lazima iamue; na hivi sasa hakuna kiungo madhubuti kati ya watu na uongozi.”

Ni kwa muktadha wa maelezo haya ndiyo inabidi matamshi yafuatayo yafahamike: “Watu wapo tayari kuwa pamoja lakini siyo viongozi”, na “Hivi sasa suala Muungano ni baina ya viongozi na si baina ya watu.”

Wingine wana maelezo yenye tofauti ndogo juu ya kutokuchukuliwa hatua kuhusu Muungano: “Hivi sasa si suala la kuyapuuza mambo kuliko kutojua nini la kufanya. Kuna masuala ya uhalali wa serikali ya Muungano. Kwa hiyo ni shida kwao kuonesha hadharani msimamo madhubuti juu ya jambo ambalo linaonekana kuwa na ubishi kama ambavyo angeliweza Nyerere”. Haya yalielezwa katika maelezo juu ya “changa moto za uhalali; kushindwa kuongoza kwa CCM, uongozi unaoendeshwa kwa hofu zisizokuwa na msingi.”

Kuhusu Zanzibar, ilidaiwa kuwa CCM haikuwahi kushinda uchaguzi na kwamba kama CCM itakubali kuwa imeshindwa katika kura zinazopigwa na wananchi Zanzibar, Muungano utavunjika. Kwa hiyo, suala la uhalali linaunganishwa na masuala ya uchaguzi na michakato ya Muafaka. Kwa sababu ya mfumo wa vyama vingi

Page 100: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

86 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

na matokeo ya uchaguzi abayo yamegawika sawa sawa, (kiasi cha 50%/50%), matokeo ya ushindi finyu yanasemekana kuwa kila siku yanatokana na kuchezewa kura na makarani. Hivi sasa, si kama Zanzibar imekatishwa tamaa na miaka 45 ya Muungano ambapo masuala ya Muungano hayakushughulikiwa ipasavyo tu, lakini elimu kwa raia na mwamko wa watu inasemekana kuwa umekua. Watu wanazidi kuuliza mswali ambayo yanahitaji majibu kwa haraka. Lakini vikwazo vilivyotajwa katika sehemu hii bado vinayaweka matarajio kama hayo kwenye njia ya panda.

Namna ya Kuufikia Muungano Endelevu na wa HakiWatu wengi waliolishughulikia suala hili hawakudhani kuwa njia ya kuelekea kwenye Muungano wa haki ni njia isiyoshindika. Ni kweli kuwa wengi walikuwa na mawazo madhubuti juu ya yale yanayohitajika kwa ajili ya mchakato huo.

Wengi walishuku kama uchaguzi peke yake ungeliweza kuleta Muungano wa haki hapo baadaye. Kwa mfano ule mkakati wa kutoipigia kura CCM huko Pemba, hata kama ungelipanuka na kufika Unguja, usingeliweza kulitatua tatizo hili. Hii siyo ni kwa sababu ya ukweli wa matokeo tu, lakini kwa sababu vile vile hakuna uhakika kama CUF ingelichukua madaraka Zanzibar, tatizo hili lingelikuwa limekwisha. Hili ni juu ya yale ambayo yalisemwa na baadhi ya watu kuwa, kama matatizo ya Muungano yangelitatuliwa, CUF isingelikuwa na ajenda Zanzibar. Mchakato wa uchaguzi, kwa namna yake halisim ulivyo, ni wa kivyama vya siasa na tatizo la Muungano linavuka mpaka wa fikra za kivyama vya siasa.

Mazungumzo, mjadala na mashauriano ni hatua muhimu katika njia ya kutafuta Muungano wa haki. Hili, liwe katika vikao vyote, katika ngazi zote, pamoja na serikali, vyama vya siasa, jumuiya za kiraia, wanazuoni, n.k … Watu wengi wanasisitiza kuwa muundo utakaoweza kufanya kazi na ukadumu wa Muungano inabidi utokane na watu wenyewe na siyo serikali.

Page 101: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Mustakabali wa Muungano 87

Kwa sababu hiyo, hatua ya kwanza ni kujenga mazingira yatakayosababisha kuwepo kwa mjadala huru na wa wazi na kuondoa hali yoyote ile ya hofu na usiri inayosemekana kuuzonga Muungano tokea kuundwa kwake. Jukumu la kujenga hali kama hii hasa, ni la serikali na CCM lakini siyo peke yao. Wote wanaohusika na wadau lazima wajenge shauku na ujasiri wa kuchangia katika majadiliano ya musuala yote kwa imani ambayo Muungano wa haki unavyoweza kujadiliwa. Hii itakuwa ni hali ya kupumua.

Mara tu hali kama hii itakapoanza kujitokeza, itapelekea kuanza kuchukuliwa kwa hatua madhubuti, kama vile mkutano, kupitiwa kwa katiba na kura za maoni kama walivyopendekeza wengi wa wale tuliowahoji. Kuhusu hili, yametolewa mapandekezo madhubuti ya maelekezo.

Kama Mzanzibari mmoja alivyosema, “Kwa miaka 45 Muungano ulioshonwa kwa pupa na kwa siri umekuwa ukichechemea kwa muda mrefu. Unahitaji kufanyiwa marekebisho kwa misingi ya nia njema. Tulipoungana, sisi (Zanzibar) tulikuwa na umri wa miezi 3 tu, wabia wenzetu walikuwa kwa kiasi fulani, wakubwa zaidi na waliojindaa vizuri zaidi. Kwa hiyo, kuna vitu vingi vinavyohitaji kupitiwa upya. Tunahitaji tukae chini na kujadiliana na kuupitia upya Mkataba wa Muungano. Hili linahitaji kuungwa mkono na wananchi.”

Katika hali hiyo hiyo, mtu mwingine tuliyemuhoji alieleza, “Baadhi ya watu wanasema natusahau masuala ya uhalali kwa sababu Muungano ni kitu halisi kiliopo. Kinachotakiwa kufanywa ni kuurekebisha upya na kuupitia mkataba wa asili.”

Kusema kweli, kila mtu anapendekeza kufanywa marekebisho ya katiba. “Lazima zifanywe juhudi za dhati kutatua matatizo ya Muungano. Kuna haja ya katiba kufanyiwa marekebisho, kuhusu namna ya kuifanyia katiba hiyo marekebisho; kuwe ni pamoja na kuyafafanua mambo ya Muungano, utaratibu wa ushirikiano na namna ya kuyalinda maslahi ya Zanzibar pamoja na yale ya bara. Ufanywe utafiti juu ya namna Zanzibar itakavyoweza kushirikishwa

Page 102: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

88 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

ama ikiwa mwanachama kamili au ikiwa na hadhi fulani katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Zanzibar inahitaji kutambuliwa; inahitaji kuwa na hadhi maalum na fursa fulani ili iweze kuwa na sauti katika Jumuiya.”

Winigine wanaelezea juu ya kuwepo haja ya kuangalia mifumo mingine ya shirikisho au inayofanana na hiyo katika nchi nyingine kama vile Uskochi ndani ya Uingereza au utararatibu wa uliokuwa Muungano wa Kisovyeti, n.k.

Ilisisitizwa kuwa kila kitu kiweze kujadiliwa wakati wa mchakato wa kuipitia upya katiba. Ilitiliwa mkazo kuwa kuna haja kubwa ya kuwepo utaratibi rasmi wa kuipitia upya katiba, hasa kwa vile katiba ya hivi sasa inatokana na mfumo wa serikali ya chama kimoja; na kwa muktadha huo, matatizo yamekuwa yakizungumzwa ndani ya chama kimoja, jambo ambalo haliwezi kufanyika wakati wa mfumo wa vyama vingi vya siasa.

Watu wengi wamesisitiza kuwa, kiini cha mchakato wa kuandika katiba mpya kiwe ni ushiriki wa wananchi. Hii ni tofauti na marekebisho yaliyokuwa si ya kimsingi yaliyofanywa wakati wa kipindi cha mpito cha kuelekea kwenye mfumo wa vyama vingi. Kimsingi, katiba imebakia kuwa ni ile ile ya mwaka 1977 , ya utawala wa chama kimoja na mchakato huo haukushirikisha wananchi.

Imeelezewa kuwa kuandikwa kwa katiba mpya kwa msingi wa mawazo ya wananchi lilikuwa ni pendekezo muhimu lililotolewa na Tume ya Nyalali iliyoshauri kuwa mchakato huo uchukue kwa uchache kiasi ya mwaka mmoja.

Ukiacha suala la kupitiwa upya katiba, watu wingine wameshauri kufanyika kwa mkutano kujadili juu ya namna ya serikali, ikiwa ni pamoja na kuwa na serikali moja ya Muungano au serikali ya shirikisho.

Hatimaye, inaweza kupigwa kura ya maoni juu ya Muungano. Au inaweza kupigwa kura ya maoni mahasusi juu ya kama uwepo muundo wa Muungano wa serikali mbili au tatu.

Page 103: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Mustakabali wa Muungano 89

Watu wengi wamesema kuwa Nyerere aliikataa kura ya maoni mpaka kufa kwake na kwamba watu wengi walipoteza nyadhifa zao kwa sababu ya hilo. Lakini wanasisitiza kuwa njia ya kusonga mbele ni kuwa na kura ya maoni juu ya muundo wa Muungano.

Kuhusu kura ya maoni juu ya Muungano, imetolewa kauli ya kumaizi na kiongozi mmoja wa Tanzania mwenye uzoefu: itakapokuja kura ya maoni – uongozi, kwa ajili ya kutafuta madaraka, utataka kuuvunja Muungano. Lakini kwa wananchi, kama kweli utawaelezea vyema kuhusu suala hilo, pamoja na matokeo yake, hawatapiga kura dhidi ya Muungano.

Lakini watapiga kura kwa Muungano wa haki, ambao hotuba za kisiasa tu au kufanya marekebisho madogo madogo haviwezi kuuleta. Na kama ilivyoelezwa hapo awali, mapendekezo haya yenye nia njema, yanaweza kupuuzwa, lakini itakuwa kwa gharama kubwa sana.

Njia za kuufikia Muungano wa haki uliotajwa hapo juu si za kuchagua. Itahitaji matumizi ya jumla ya nyingi ya njia hizo ili kusonga mbele na kulifikia lengo linalotakiwa.

Page 104: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

90

6Muungano na Kuunganishwa

kwa Afrika MasharikiSehemu hii inashughulikia masuala yanayotokana na ukweli kuwa na hali na muundo wa Muungano kama unavyohusiana na mchakato wa kuiunganisha Afrika Mashariki. Inaweka wazi matatizo kama wanavyoyaona watanzania wenyewe na mawazo yao juu ya njia zinazowezekana zitakazowawezesha kuyatatua.

Mchakato wa Kuiunganisha Afrika MasharikiIliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki ilianzishwa mwaka 1967. Ilitanguliwa na namna mbalimbali za ushirikiano na muungano, pamoja na Jumuiya ya Huduma za Pamoja ya Afrika Mashariki (EACSO) iliyoundwa mwaka 1961 na hata mapema zaidi East African High Commission, soko la pamoja na sarafu ya namna moja. Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ilivunjwa mwaka 1977 kwa sababu ambazo hiziwezi kuelezwa vya kutosha hapa. Hata hivyo, asasi tatu zilibaki baada ya Jumuiya kuvunjwa, nazo ni Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (EADB), Baraza la Pamoja la Vyuo Vikuu la Afrika Mashariki (IUCEA) na Kurugenzi ya Shughuli za Ndege ya Afrika Mashariki. Mwaka 1984, nchi wabia wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki zilisaini Mkataba wa Usuluhishi wa Afrika Mashariki, juu ya mgawanyo wa rasilimali na madeni ya Jumuiya iliyokufa.

Juhudi za kuufufua mchakato wa kuungana zinaweza kufuatiwa nyuma kutoka tarehe 30 Novemba 1993 pale Mkataba wa Tume ya Kudumu ya Pande Tatu kwa ajili ya Ushirikiano kati ya Jamhuri za Kenya, Tanzania na Uganda ulipotiwa saini. Tume hiyo iliundwa

Page 105: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Muungano na Kuunganishwa kwa Afrika Mashariki 91

na kukabidhiwa jukumu la kuratibu mambo ya kijamii, kiuchumi, kiutamaduni na ya kisiasa katika nchi tatu hizi. Wakuu wa nchi tatu hizo vile vile walitoa tamko la Ushirikiano wa karibu zaidi wa Afrika Mashariki.

Mwaka 1997, Wakuu wa Nchi tatu hizo waliupitisha Mkakati wa Maendeleo wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kipindi cha mwaka 1997 hadi 2000 na kuielekeza Tume ya Pande Tatu kuanza majadiliano ya kuyapandisha hadhi Makubaliano ya Tume ya Pande Tatu ili yawe Mkataba. Hili lilifikiwa mwaka 1999, pale Mkataba wa Kuanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ulipotiwa saini mwezi Novemba 1999. Rwanda na Burundi zilikuwa wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki tarehe 1 Julai 2007 katika Mkutano wa Tano Usiokuwa wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi.

Mchakato wa kuungana ulipitia hatua kadha. Itifaki kwa ajili ya Kuanzishwa Umoja wa Forodha ilitiwa saini na Wakuu wa Nchi wa nchi tatu tarehe 2 Machi 2004. Rwanda na Burundi zilijiunga na Umoja wa Forodha mwaka 2008 na kuanza kuzitumia hati zake rasmi mwaka 2009. Itifaki ya kuanzisha Soko la Pamoja ilitiwa saini tarehe 20 Novemba 2009 na ungelianza kutumika mwezi Julai 2010, ijapokuwa bado kuna masuala yasiyokamilka kuhusu umiliki wa ardhi na usimamizi, viwango vya namna moja vya ushuru wa nje, nyaraka za kusafiria na ulinzi wa ajira za nyumbani. Sarafu ya namna moja inatarajiwa kuanza mwaka 2015 na mazungumzo kuhusu hilo yanaendelea – ili kuelekea kwenye muungano wa kifedha.

Kuhusu hatua ya mwisho ya shirikisho la kisiasa, katika Mkutano Usio wa Kawaida mwaka 2004 Wakuu wa Nchi wa Kenya, Tanzania na Uganda waliazimia kuunda Kamati ya Kuharakisha Shirikisho la Afrika Mashariki. Kamati hiyo inayoongozwa na Amos Wako iliwasilisha taarifa yake kwa Wakuu wa Nchi mwezi November mwaka huo huo katika Mkutano wa Sita wa Wakuu wa Nchi. Miongoni mwa mambo mingine, kamati hiyo ilitengeneza ratiba iliyotaka mambo yafuatayo:

Page 106: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

92 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

a. Rasimu ya katiba ya shirikisho la Afrika Mashariki ifi kapo Desemba 2007

b. Kupitishwa katiba na mkutano wa Wakuu wa Nchi mwezi Januari 2009

c. Kura ya maoni kuhusu katiba ifi kapo Desemba 2009d. Shirikisho la kisiasa lenye urais wa mzunguko ifi kapo 2010 na

uchaguzi wa rais ifi kapo 2013

Mkutano wa Wakuu wa Nchi Usio wa Kawaida uliofanyika Dar es Salaam mwezi Mei 2005 ulielekeza kuundwa kwa utaratibu wa mashauriano ya kitaifa kukusanya maoni kutoka kwa Waafrika Mashariki juu ya Shirikisho la Afrika Mashariki na kuharakisha mchakato huo.

Michakato ya mashauriano ya kitaifa ilizinduliwa mwezi Oktoba nchini Tanzania, Kenya na Uganda na mwaka 2008 nchini Rwanda na Burundi. Waafrika Mashariki walikubaliana kwa kauli moja juu ya shirikisho la kisiasa. Yalitolewa pia mawazo ya kupinga uharakishwaji. Wasiwasi mmoja uliojitokeza kutokana na mchakato wa mashauriano nchini Tanzania ulikuwa ni suala la kuitenga Zanzibar kabisa, chini ya serikali ya Muungano katika serikali ya shirikisho.

Mambo ya Kuzingatiwa ya Kihistoria Hali ya sasa ya Muungano ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na mchakato ambao hatimeye unatarajiwa kupelekea kuundwa kwa Shirikisho la Afrika Mashariki haina budi kuwekewa vigezo. Jumuiya ya hivi sasa si kitu kipya kabisa, kadhalika na jaribio la kuunda shirikisho.

Hivi sasa, Zanzibar imo ndani ya Jamhuri ya Muungano, ambayo ndiyo inayojadiliana na kupanga na wabia wengine katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Ujumbe huu tayari umepata habari, ikiwa ni pamoja na kutoka kwa watu walioshuhudia baadhi ya taratibu zilizopelekea kuuundwa kwa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Kutoka kipindi cha

Page 107: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Muungano na Kuunganishwa kwa Afrika Mashariki 93

mwaka 1959, Nyerere amekuwa akipigania kuwepo kwa Shirikisho la Afrika Mashariki. Aliamini kuwa ingelikuwa shida zaidi kutimiza lengo hilo ikiwa kila moja ya nchi za Afrika Mashiriki ingelipata uhuru peke yake. Kwa hiyo, alikuwa tayari kuchelewesha uhuru wa Tanganyika. Kuhusu jambo hili, inasemekana kuwa, hakuwashauri hata wenzake nchini Tanganyika ambao walimhoji. Katika hali hiyo, kuchelewesha uhuru wa Tanganyika hakukuwezekana, na matatizo ya ndani ya Uganda nayo kwa wakati huo yalizuia kupatikana kwa shirikishoo.

Mwaka 1964, Uganda ilikuwa tayari na majadiliano yalianza na ilikuwa wakati huo ndipo mapinduzi ya Zanzibar yalipotokea. Hata hivyo, mwaka 1964 makubaliano ya kimyakimya yalifikiwa kati ya nchi nne - ambazo ni Kenya, Tanganyika, Uganda na Zanzibar – kuungana chini ya uongozi wa Kenyatta. Kama ilivyoelezwa, Nairobi watu walikwenda kulala wakitegemea kuwa siku ya pili Kenyatta atatangaza shirikisho. Hili halikutokea. Wengi wakikisia kuwa walikuwa Charles Njonjo na Bruce Mckenzie waliomwelekeza Kenyatta asiendelee na shirikisho. Kwa hiyo ilikuwa katika wakati huo ambao Nyerere – aliyependelea Zanzibar iingie katia Shirikisho la Afrika Mashariki, akihisi kuwa chaguo ambalo lingeliuzika zaidi Umoja wa Mataifa – ni kukubalina na Karume, kuunda Muungano. Ni katika dhana hii ndiyo Muungano unaweza ukasemekana kuwa ni matokeo ya jaribio lililoshindwa la kuunda Shirikisho la Afrika Mashariki.

Hili lilithibitishwa na maelezo mingine kuwa, kabla ya mapinduzi ya Zanzibar, Muungano ulizungumzwa kwa namna ya shirikisho tu. Ni kweli kuwa mara baada ya Zanzibar kupata uhuru wake mwaka 1963, Tom Mboya alitembelea Zanzibar ambayo iliunga mkono shirikisho kwa maneno matupu bila ya kuupinga kwa nguvu kama ilivyofanya Uganda.

Kwa majaribio ya shirikisho lililoshindikana, pamoja na wasiwasi wa nchi za Afrika Mashariki ambazo zote zilikwisha jadiliana juu

Page 108: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

94 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

ya uhuru wao, matokeo mabaya ya mapinduzi ya Zanzibar, pamoja na uasi wa majeshi katika nchi tatu za Afrika Mashariki mwaka huo huo, mtu anaweza kuelewa kuhusu uhusiano kati ya shirikisho lililoshindikana na Muungano wa nchi mbili, na kwa nini Muungano haukuhojiwa katika Afrika Mashariki ambayo imelikataa shirikisho, kwa upande mwingine.

Katika muktadha huu, ilielezwa waziwazi kuwa nchi za Afrika Mashariki zina wasiwasi kuwa Zanzibar inaweza kutumiwa na madola ya nje kuiyumbisha kanda yote.

Usuli huu ni sahihi ikiwa mtu anataka kuuelewa vyema mtazamo wa baadhi ya Wazanzibari kuhusu juhudi mpya juu ya Shirikisho la Afrika Mashariki, na kuhusu Muungano wenyewe vile vile. Ni muhimu kuelewa vile vile kuwa Muungano ulikuja wakati nchi zote mbili zilikuwa wanachama ya Umoja wa Huduma za Pamoja wa Afrika Mashariki (EACSO), ambao uliendesha huduma za pamoja, Umoja wa forodha na sarafu ya pamoja.

Mwaka 1977, ile iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki ilisambaratika. Miongoni mwa mambo mingine, kuna matukio mawili muhimu ambayo yana umuhimu maalum kwa Muungano, ambayo yanatokana kwa upande mmoja na kusambaratika kwa asasi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Hilo moja ni mahasusi na linahusiana na rasilimali za Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki ambayo ilivunjwa mwaka 1966 na haihusiani moja kwa moja na iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kila nchi ililipwa hisa zake za rasilimali ya Bodi. Hisa za Zanzibar zilikabidhiwa kwa Tanzania. Ni fedha hizi ndizo zilizotumika kuanzisha Benki Kuu ya Tanzania. Pesa za kutoka Bodi ya sarafu inasemekana kuwa zilikuwa asilimia 12% ya mtaji wa Benki Kuu. Hili limethibitika kuwa ni jambo linalolalamikiwa sana Zanzibar. Ilisisitizwa na watu wengi waliohojiwa Zanzibar, kuwa Zanzibar ilistahili ipatiwe hisa zake. Hili ni jambo moja la msingi linaloifanya Zanzibar iwe hairidhiki

Page 109: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Muungano na Kuunganishwa kwa Afrika Mashariki 95

na Muungano. Kwa baadhi ya watu, hili linahusishwa na Zanzibar kutaka kuwa na sarafu yake yenyewe.

Tukio jingine muhimu lililotokana na kuvunjika kwa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki ni kuongezwa kwa mambo ya Muungano kutoa 11 ya asili. Kwa mujibu wa mawazo ya pamoja ya Zanzibar, kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki kumetoa fursa kwa Muungano ya kuumeza taratibu uhuru na utambulisho wa Zanzibar kwa kuongeza orodha ya mambo ya Muungano ambayo sababu zake za kimantiki zitakuwa ni Muungano wa serikali moja. Hati ya kisheria – Mkataba wa Muungano – haukugusia juu ya mambo yaliyokuwa yakiendeshwa na Umoja wa Huduma za Pamoja wa Afrika Mashariki; ulijikita katika vipengele 11. Katiba ya 1977 iliyokuja baada ya kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki iliifanyia marekebisho orodha hiyo na kuyaingiza mambo yote ambayo hapo awali yalikuwa yakiendeshwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwa ni mambo ya Muungano.

Ilielezwa kuwa Wazanzibari hawakuambiwa kwa nini iliyokuwa Jumiya ya Afrika Mashariki ilivunjwa. Kwa hali hiyo hiyo, imedaiwa kuwa hapajakuwepo na mjadala makini ulioijumuisha Zanzibar wakati Jumuiya ya Afrika Mashariki ya sasa ilipoundwa. Yamekuwepo majadiliano machache juu ya suala la – kuharakisha Shirikisho la Afrika Mashariki.

Muungano kwenye Uhusiano wa Kimataifa Inakubaliwa na wale waliohojiwa na ujumbe huu kuwa ilivyo hivi sasa, kisheria na kikatiba ni kwamba Tanzania ni nchi moja inayojitawala. Vile vile, kwa mujibu wa katiba, mambo ya nje ni jambo la Muungano. Hitimisho lililofikiwa kutokana na maelezo hayo ni kuwa katika uhusiano wa kimataifa kinachotambuliwa ni Jamhuri ya Muungano. Ndani inaweza kuwepo serikali ya Zanzibar na Muungano, lakini nje ipo Jamhuri ya Muungano tu. Kwa hiyo vile vile, Zanzibar katika hali hiyo haina uwezo wa kujadiliana au

Page 110: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

96 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

kufanya mazungumzo kimataifa. Hivyo, serikali ya Muungano inaingiliana na serikaki nyingine na vyama vya kimataifa kwa jina la Jamhuri ya Muungano, pamoja na Zanzibar. Hii inahusu vile vile mambo ambayo si ya kisiasa, ya kifedha, ya kiuchumi na michezo, pamoja na shughuli za jumuiya za kiraia kama wale walioohojiwa wanavyoeleza. Hii ni pamoja na Umoja wa Mataifa.

Kwa kusononeka na kwa mapenzi ya kwao Zanzibar, ililalamika kwa mbali kwa kukipoteza kiti chao cha Umoja wa Mataifa. Lakini kanuni hii inafika mpaka kwenye vyama vya kanda na nusu kanda ambavyo Tanzania ni mwanachama kama vile Umoja wa Afrika (AU), Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki mutawalia. Suala hili limejitokeza vile vile katika vyama vingine kama vile Umoja wa Waisilamu (OIC) na vyama vya michezo kama vile Shirikisho la Mpira wa Miguu la Afrika (CAF) na Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Mpira wa Miguu (FIFA).

Mambo yamekuwa ya msimamo huo. Kwa hiyo Zanzibar imebidi ijitoe kutoka katika Umoja wa Waislamu (OIC), ambao ilijaribu kujiunga nao. Wazanzibari wameeleza kuhusu ukweli kuwa asilimia 90% ya watu wa Zanzibar ni Waislam lakini Zanzibar haiwezi kujiunga na Umoja wa Waislam, tofauti na nchi kama Uganda ambayo idadi ya Waislam ni asilimia 10%, tu na Msumbiji yenye idadi inayoweza kulinganishwa na hiyo ambao ni wanachama. Walieleza kuwa Zanzibar ilijiunga na Umoja wa Waislam kwa sababu za kiuchumi tu – kupanua bandari na kujenga Eneo la Kutengeneza Bidhaa za Kusafirisha Nje.23 Zanzibar imeshindwa vile vile kujiunga na Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Mpira wa Miguu (FIFA) (chombo ambacho si cha kisiasa) ijapokuwa shirikisho hilo lilikuwa tayari kuikubali Zanzibar. Kwa upande mwingine, imeelezwa kuwa, katika vyama vingine vya kimataifa kama vile Jumuiya ya Maendeleo

23 Ujumbe huu uliarifiwa kuwa Tanzania ilikubali kuomba uanachama, jambo ambalo haikulifanya mpaka sasa.

Page 111: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Muungano na Kuunganishwa kwa Afrika Mashariki 97

ya Kusini mwa Afrika (SADC), baadhi ya wakati Zanzibar hualikwa kama mtazamaji.

Lakini kuna mabadilikobadiliko katika utendaji wa shughuli za kimataifa. Zanzibar ni mwanachama wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Afrika (CAF). Imeelezwa vile vile kuwa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) inafanyakazi na Zanzibar moja kwa moja na kuna mahusiano ya kikazi na China na Indonesia. Katika ngazi ya Jumuiya za Kiraia, vyama vyote viwili, Chama cha Wanasheria cha Afrika Mashariki (EALS) na KCK vina uhusiano na Chama cha Wanasheria cha Zanzibar (ZLS) na vina wawakilishi wa Zanziba katika bodi zao.

Matatizo mengi yameelezwa kuhusiana na suala la shughuli za kimataifa na Muungano. Mengi ya hayo yanaihusu Zanzibar.

Suala la kwanza linahusu uwakilishi wa Zanzibar katika mambo yasiyo ya Muungano. Hili ni jambo lililojitokeza tena na tena kwa jumla na kwa kuhusiana na Jumuiya ya Afrika Mashariki. Ilielezwa kuwa mwaka 2008 lilikuwepo pendekezo la kuondoa kodi fulani kwa Jumuiya ya Maendeleo ya Uchumi ya Kusini mwa Afrika. Kodi hizi hazikuhusiana na mambo ya Muungano na kwa hiyo, yalitolewa maoni kuwa serikali ya Muungano haikuwa na madaraka ya kuisemea Zanzibar. Jambo hili litafafanuliwa zaidi kuhusiana na Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Tatizo la pili ni kuondolewa kwa Zanzibar kutoka katika medani ya kimataifa, tatizo ndani ya tatizo, kama namna lilivyoelezwa; lakini ni tatizo ambalo pia linasababisha kutokuwepo maslahi sawa kutokana na makubaliano ya kimataifa. Kuhusiana na hili, kupoteza kiti cha Umoja wa Mataifa kumetajwa. Imeelezwa pia kuwa kuondolewa huku kunatokana na utaratibu wa kupeana habari unaofuatwa ndani katika kujaribu kuishirikisha Zanzibar. Inasemekana kuwa utaratibu huu haufanyi kazi. Mazungumzo zaidi kuhusu hayo yanafanyika katika kuzungumzia ushiriki katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Page 112: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

98 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

Kopoteza maslahi kunaunganishwa na uwakilishi dhaifu. Ilielezwa kuwa Zanzibar haiwezi kujadiliana juu ya ruzuku moja kwa moja. Lakini serikali ya Muungano inapodai kufanya hivyo kwa niaba ya Zanzibar, haiwasilishi maslahi hayo kwa Zanzibar au kufanya hivyo kwa usawa. Zanzibar inahisi inadanganywa.

Hali hii ya dhuluma inasemekana pia ipo, na ni matokeo yanayotokana na taratibu za ndani za mashauriano, serikali ya Muungano kutoielewa hali ya Zanzibar na mahitaji ya Zanzibar, kuwepo Wazanzibari wachache ndani ya serikali ya Muungano kwa jumla na hasa katika ofisi za ubalozi ziliopo nje ya nchi pamoja na vyeo vya ubalozi; na Zanzibar kutoweza kuzifikia ofisi za mabalozi wa nchi za nje ziliopo Tanzania kwa kuwa mabalozi hao hawana ofisi Zanzibar.24 Katika hali hii, sauti ya Zanzibar imepotea, hasa kwa sababu mtu mmoja mmoja ni muhimu katika majadiliano ya kimatafa na hawa wanaweza wasiyakumbuke maslahi na mahitaji ya Zanzibar.

Ilitamkwa waziwazi kuwa, ikiwa kimataifa au si kimataifa, wawakilishi wa Muungano wanapoongea kwa niaba ya Tanzania, husahau nchi inayoitwa Zanzibar.

Katika kupinga madai haya, imeelezwa kuwa utaratibu haupo tofauti na ule wa Uskochi na Uingereza na kwamba kuna taratibu madhubuti za ndani zinazofanya kazi vizuri kuishirikisha Zanzibar.

Muungano ndani ya Jumuiya ya Afrika MasharikiKuhusiana na Jumuiya ya Afrika Mashariki, kwa sababu ya yote mawili, katiba ya Jamhuri ya Muungano na Mkataba wa Afrika Mashariki, Zanzibar si mwanachama rasmi kwa sababu Jumuiya , kama ilivyoelezwa, ni Jumuiya ya nchi na Zanzibar si nchi. “Hakuna

24 Ujumbe huu ulibaini kuwa baadhi ya washauri wapo Zanzibar. Washauri hawa ni pamoja na Wachina na Wahindi (na hivi karibuni Marekani, Norway na baadhi ya ofisi ndogo za Umoja wa Mataifa). Zanzibar inajaribu kuzitumia ofisi hizi kwa kutokuwepo ofisi za mabalozi.

Page 113: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Muungano na Kuunganishwa kwa Afrika Mashariki 99

mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeitwa Zanzibar. Ndani ya Jamhuri ya Muungano ipo Zanzibar na hofu kuwa maslahi ya Zanzibar hayatozingatiwa vyema ndani ya Jumuiya hayana msingi.” Zanzibar haina uwezo ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa sababu mambo ya nje ni mambo ya Muungano.

Palikuwa na mawazo kuwa hoja hii, kusema kweli, inahitaji swali, vipi, kwanza, jambo linakuwa la Muungano ili kuuondoa uwezo wa Zanzibar?

Lakini hata kama hali hiyo inakubaliwa, Wazanzibari wengi wameeleza kutoridhika kwao na hali hiyo wakisisitiza kuwa hawawakilishwi ipasavyo na kwamba wangelipenda kushiriki moja kwa moja katika kuunganishwa Afrika Mashariki. Wanatoa hoja kuwa ni bora kwa Zanzibar kujisemea yenyewe ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Ulitolewa mfano juu ya ushuru kwa mchele ambao unaiumiza Zanzibar. Zanzibar iliupinga ushuru huo kwa sababu wakati wa tukio hilo ilitokea kuwa walikuwapo kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki na walilielewa tatizo. Ilitolewa hoja vile vile kuwa Rwanda na Burundi zinaweza kushiriki moja kwa moja, kwa nini Zanzibar haiwezi?

Suala lenye tatizo kubwa, hata hivyo, ni suala la uwakilishi wa Zanzibar katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu mambo yasiyokuwa ya Muungano.

Hoja ya Zanzibar ina mambo mengi. Inatolewa hoja kuwa serikali ya Muungano haina uwezo wa kuiwakilisha Zanzibar kwa misingi ya mgawanyo wa kazi kuhusiana na mambo ya Muungano na yale yasiyokuwa ya Muungano.

Tatizo, kwa mujibu wa Zanzibar si suala la kutokuwa na madaraka tu kwa upande wa serikali ya Muungano juu ya mambo yasiyokuwa ya Muungano ndani ya Jumuiya ya Afrika Masharaki. Tatizo kubwa zaidi ni kwamba miongoni mwa masuala 18 yaliyoshughulikiwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki 4 tu ndiyo mambo ya Muungano. Shughuli nyingi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ni za mambo

Page 114: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

100 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

yasiyokuwa ya Muungano ambayo yapo ndani ya madaraka ya Zanzibar. Ikiwa haya, kwa kweli, yatachukuliwa na serikali ya Muungano, hiyo ni kuivua zaidi Zanzibar uwezo wake wa kisheria ambao unachukuliwa na serikali ya Mungano ambayo inashughulikia mambo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, na kuiwacha Zanzibar bila ya chochote. Kwa maneno mingine, ni namna ya chini kwa chini ya kuanzisha Muungano wa serikali moja kwa kupitia Jumuiya ya Afrika Mashariki, kwa mujibu wa maelezo ya waliohojiwa.

Juu ya yote haya, suala muhimu ni kama maslahi ya Zanzibar yanazingatiwa chini ya utaratibu wa hivi sasa. Kuna misimamo mikuu miwili juu ya hili. Wa kwanza ni kwamba uwepo uwakilishi madhubuti wa Zanzibar.

Njia moja ambayo maslahi ya Zanzibar yanashughulikiwa ni ya mashauriano. Mambo yasiyokuwa ya Muungano yanayohusiana na Jumuiya ya Afrika Mashariki yanashughulikiwa na mawaziri wa Muungano baada ya mashauriano. Watumishi ndani ya serikali ya Zanzibar walikiri kuwa walishiriki katika majadiliano na Wizara husika za Muungano juu ya masuala ya Jumuiya ya Afrika Masharaki walipoarifiwa na wizara hiyo na hualikwa. Kwa mfano, kwa masuala kama ya utalii au kilimo, ambayo si mambo ya Muungano, wanashiriki katika mashauriano ndani ya mfumo wa Tanzania. Kwa mfano, hukubaliwa msimamo ambao baadaye huwasilishwa kwenye Baraza la Mawaziri katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Imeelezwa kuwa, ofisi ya rais wa Zanzibar ina dawati la mratibu wa mambo ya Afrika Mashariki. Kwa hiyo uratibu hufanyika hapo. “Kwa hiyo, Zanzibar inashughulikiwa bila ya kujali ukubwa wake.”

Ni mtindo wa kawaida vile vile “kabla ya Arusha” kukutana na “watu wa serikali ya Muungano” ikiwa kundi la wataalam. Hii baadhi ya wakati huhusisha sehemu zisizo za kiserikali kama vile jumuiya za kiraia kama Vyama Visivyokuwa vywa Kiserikali na vyama vya wafanyabiashara.

Page 115: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Muungano na Kuunganishwa kwa Afrika Mashariki 101

Njia nyingine ya kushughulikia maslahi ya Zanzibar, inasemekana kuwa ni pamoja na muundo wa uwanachama wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki (EALA), ambao unajumuisha robo ya wanachama kutoka Zanzibar (3 kati ya 9). Pia imefanywa makusudi kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Afrika Mashariki ni Mzanzibari kama ilivyo kwa Naibu Waziri wa mambo ya nje. Inasemekana kuwa vikundi vya wataalam vile vile vina muundo unaotilia maanani kuwemo kwa Zanzibar. Kwa hiyo ujumbe wowote lazima uwe na Wazanzibari.

Imeelezewa vile vile kuwa kuna hatua za kiutawala ambapo Jumuiya ya Afrika Mashariki inaweza kumsikiliza au kumpokea mwakilishi kutoka Zanzibar juu ya mambo yanayowahusu ambayo hayamo katika mkataba.

Na namna nyingine ya kuhakikisha ushiriki wa Zanzibar katika Jumuiya ya Afrika Mashariki ni kuhudhuria kwa watumishi wa serikali wa Zanzibar au viongozi katika vikao vya Jumuiya hiyo. Imeelezwa kuwa, Tanzania inapokuwa mwenyekiti, kunakuwapo na ushiriki mkubwa zaidi wa Zanzibar katika mikutano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kwa hiyo rais wa Zanzibar amehudhuria mikutano ya Wakuu wa Nchi pale Tanzania inapokuwa mwenyekiti. Lakini mialiko kama hiyo haitolewi kama si hivyo. Kadhalika, mawaziri wa Zanzibar wanaoshughulikia mambo yasiyokuwa ya Muungano wanakuwepo katika Baraza la Mawaziri katika hali hiyo hiyo.

Kwa kupitia njia zote hizi, inatolewa hoja kuwa, Zanzibar inashirikishwa kikamilifu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Ilielezwa kuwa, ni kweli ukilinganisha na Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyopita, hii ya sasa ni tofauti kwa sababu tu, Muungano umezidi kuwa na nguvu ili maslahi ya Zanzibar yazingatiwe kwa makini na pindi yakitokea matatizo yoyote, pande zote mbili ziko tayari kuyazungumza na kuyatatua. Ilielezwa kuwa uwakilishi wa Zanzibar ni suala la utaratibu, na vipi unafanywa inahitaji muda wa ziada kwa utendaji bora kabisa. Mtu mmoja analieleza hilo kwa

Page 116: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

102 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

nguvu zaidi: “Kwa kuwa mambo ya nje ni mambo ya Muungano, sioni geni juu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Zanzibar hailalamiki juu ya namna inavyowakilishwa katika mikutano mingine ya kimataifa. Hili si tatizo.”

Lakini, kusema kweli, Wazanzibari wengi wanalaumu taratibu zilizotengenezwa ili kuhakikisha ushiriki wa Zanzibar katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Wanaziona kuwa zina upungufu.

Kwanza, inaelezwa kuwa hakuna miundo rasmi ya ndani ya mazungumzo na mashauriano kati ya serikali ya Muungano na Zanzibar. Kinachotokea ni mambo ya dharura tu. Mashauriano kama hayo ni kwa matakwa ya waziri binafsi. Kuna mara nyingi ambapo Muungano unachukua mambo yasiyo ya Muungano yanayohusiana na Jumuiya ya Afrika Mashariki bila ya Zanzibar kushauriwa au kufikiriwa. Wakati mwingine mashauriano hayafanywi ipasavyo. Wizara ya Mambo ya Nje haiwasilishi nyaraka moja kwa moja kwa Serikali ya Zanzibar.

Zaidi ya hayo, wakati wa mikutano ya mashauriano hakuna nafasi ya Zanzibar kama Zanzibar. Serikali ya Zanzibar na wahusika wengine mara nyingi wanakuwa na mawazo tofauti; hakuna uratibu wa nafasi ya Zanzibar.

Kuhusiana na Zanzibar kuhudhuria mikutano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, kuna vikwazo vingi. Baadhi ya wakati hata watumishi wa serikali ya Zanzibar wanaweza wasihudhurie mikutano kwa sababu wa ukosefu wa fedha. Mara nyingi wanashindwa kuhudhuria mikutano na pale wanapohudhuria, baadhi ya wakati, ni kwa sababu mikutano hiyo imegharamiwa na Jumuiya.

Lakini hata pale Wazanzibari wanapohudhuria, bado kuna vikwazo. Hawana madaraka ya kuwasilisha maoni yao moja kwa moja kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kwa mfano, atakuwa Waziri wa Muungano ndiye atakayewasilisha jambo. Kama alivyoelezea mhojiwa mmoja: “Unapokuwa kwenye mkutano wa kanda, huwezi kuzungumzia Zanzibar. Utazuiliwa usizungumze juu ya Zanzibar.”

Page 117: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Muungano na Kuunganishwa kwa Afrika Mashariki 103

Mhojiwa mwingine ameeleza kwa namna tofauti: “Nafasi yetu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki haieleweki vizuri kwa sababu suala hilo ni la kisiasa. Ukileta masuala kama hayo yanaweza kumsababishia mtu kutengwa au kufukuzwa kazi. CCM bado ndiyo yenye kudhibiti ajira. Kuna watu waliofukuzwa.”

Ujumbe huu ulielezwa kuwa kuna utaratibu wa kupeana habari baina ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, serikali ya Muungano na serikali ya Zanzibar kwa kiasi Fulani, kwa sababu Naibu Waziri wa Mambo ya Afrika Mashariki anatoka Zanzibar na upo uratibu wa kupitia taratibu za ndani; kwa mfano, kuhusiana na itifaki, Waziri wa Afya wa serikali ya Muungano na Waziri mwenzake kutoka Zanzibar ni sawa; na Rais wa Muungano au Waziri Mkuu wanapokwenda nje ya nchi, huwachukua mawaziri kutoka Zanzibar. Lakini lazima izingatiwe kuhusu upungufu wa hatua kama hizo kwa hisia za Wazanzibari wengi. Ni kweli kuwa, Zanzibar, kwa kupitia Baraza la Wawakilishi na bunge imeeleza kutoridhika kwake juu ya namna mambo ya Zanzibar yanavyoshughulikiwa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Jumuiya za kiraia za Zanzibar nazo pia zimeeleza kutoridhika na hali ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusiana na Zanzibar. Wanahisi kuwa Zanzibar haiwakilishwi vya kutosha katika Jumuiya hiyo. Wanakiri kuwa wanaalikwa, lakini wanaeleza kuwa kama unazungumzia uunganishwaji lazima kila mmoja ahusike; kuna watu wengine, ukiacha serikali na vyama vya wafanyabiashara ambao wanaweza kuchangia katika mchakato wa uunganishwaji.

Wakati mwingine, wafanyabiashara wa Zanzibar wanaweza kuomba iwepo mikutano na serikali ya Muungano, lakini serikali ya Muungano inaweza kukataa. Mialiko inaweza kuja lakini mialiko hiyo huchelewa. Huchelewa kwa namna ambayo haiwezekani tena wao kushiriki. Wanauona utaratibu wa Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC) kuwa ni wenye kukubalika. Wafanyabiashara wa Zanzibar na Chama cha Wafanyabiashara wanashiriki wakiwa ni

Page 118: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

104 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

sehemu ya Tanzania na inakuwepo mikutano ya awali Dar es Salaam. Lakini baadhi ya wakati mikutano kama hiyo haifanyiki na serikali ya Muungano inaweza kuwa na mawazo yake yenyewe.

Chama cha Wafanyabiashara cha bara nacho kimetilia mkazo kuwa wanakwenda kwenye majadiliano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa nchi. Hilo limetokea, kwa mfano, kwenye majadiliano ya Mkatapa wa Ubia wa Ulaya (EPA) yaliyofanyika Kigali na Kampala. Ujumbe hujumuisha mawaziri wa Muungano na wale wa Zanzibar, watu wa sekta binafsi kutoka bara na Zanzibar – ukiongeza na mikutano ya maandalizi ambayo huandaa msimamo wa pamoja wa Muungano. Katika mikutano ya maandalizi, masuala ya Zanzibar na bara huletwa, na msemaji mkuu huandaa makubaliano ya pamoja. Ujumbe huu ulielezwa kuwa, katika mikutano ya maandalizi kama hiyo, bara inakuwa makini sana kuhusu mahitaji ya Zanzibar. Zaidi ya hayo, imeelezwa kuwa hata katika nyanja za mambo yanayohusiana na yale mambo yasiyokuwa ya Muungano, kuna maingiliano makubwa. Ilielezwa kuwa mialiko kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki hupelekwa kwa Waziri wa Muungano anayeshughulikia Ushirikiano wa Afrika Mashariki, na Zanzibar haipati mwaliko.

Kuna mambo ambayo ujumbe huu umejifunza kutoka Vyama mbali mbali Visivyo vya Kiserikali (NGOs) juu ya ushirikishwaji wa Zanzibar katika mchakato wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Chama kimoja kisicho cha kiserikali kimeueleza mchakato huo ifuatavyo: “Tunaposhiriki katika mkutano wa kimataifa tunakwenda tukiwa timu ya Muungano. Kiongozi anaweza kuelezea au kutoelezea msimamo wa Zanzibar. Kama kuna haja ya kutayarisha na kuwasilisha makala juu ya msimamo, Zanzibar huchangia. Lakini kwa kawaida, ni watu wa kutoka bara ndio wanaowasilisha, hata kuhusu Zanzibar. Hii haina maslahi kwa sababu wanaweza kuwa hawailewi hali ilivyo”.

Page 119: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Muungano na Kuunganishwa kwa Afrika Mashariki 105

ANGOZA ya Zanzibar, TANGO na Baraza la Tanzania kwa Maendeleo ya Jamii (TACOSODE) la bara ni vyama vikuu vinavyojenga mtandao wa jumuiya za kirai. Vyote vinashiriki katika majadiliano ya Umoja wa Vyama Visivyo vya Kiserikali wa Afrika Mashariki. Lakini inapobidi kutia saini, hapa kidogo panakuwa na tatizo kwa sababu inayotakiwa ni saini moja tu. Zamani, palikuwa na mashauriano miongoni mwa vyama hivi kutoka pande zote mbili kabla ya shughuli yoyote ya kimatifa. Lakini litakapoundwa tawi la Tanzania la Vyama Visivyo vya Kiserikali vya Afrika Mashariki (EA NGOs) itakuwepo haja ya kuwepo usawa baina ya wabia katika tawi hilo.

Vyama Visivyo vya Kiserikali vya bara vimeeleza kuwa yapo mahusiano dhaifu kati yao na wenziwao wa Zanzibar: Kama mhojiwa mmoja alivyosema: “Tunaweza kuwa tunashirikiana zaidi na DENIVA ya Uganda au Mtandao wa Kenya “the Kenya network”; inaweza kuwa tunazielewa zaidi shughuli zao kuliko kuelewa nini kinachoendelea Zanzibar. Inaweza kuwa tunaalikwa zaidi Kenya na Uganda kuliko Zanzibar. Na vyama visivyo vya Kiserikali vya Zanzibar vinaweza kuwa na ushirikiano zaidi na Kenya kuliko bara. Kusema kweli, tuna haja ya kuja pamoja ili kuzungumza juu ya masuala ya shughuli na kuunganishwa kwa Afrika Mashariki.”

Eneo jingine la Muungano na mchakato wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ni suala la pengo la habari lililoelezwa na Zanzibar, na upande wa pili, kiasi cha habari waliyonayo kanda ya Afrika Mashariki juu ya masuala ya Zanzibar.

Yalitolewa mawazo kuwa Zanzibar haielewi nini kinachotokea katika Jumuiya ya Afrika Mashariki; kwamba ni wachache tu miongoni mwao waliousoma Mkataba au wana habari yoyote juu ya shughuli za Bunge la Afrika Mashariki (EALA).

Kwa namna yoyote ile, hii ni kweli. Lakini inawezekana kuwa hali ni hiyo hiyo kuhusu pengo la habari juu ya Mkataba katika nchi wanachama zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Page 120: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

106 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

Hapo Zanzibar, imedaiwa kuwa mambo mengi yanayohusu Jumuiya ya Afrika Mashariki ama hayajulikani au hayapo wazi; na usilolijua linatisha, hasa unapodhani kuwa hushiriki katika kufanya maamuzi. Kwa upande mwingine, imedaiwa Zanzibar kuwa eneo kubwa zaidi halielewi juu ya matatizo ya Zanzibar. Kwa kiasi fulani, wanatoa sababu ya hili kuwa ni kushindwa kwao wenyewe kuielimisha kanda ya Afrika Mashariki juu ya matatizo ya Muungano na ushiriki wa Zanzibar katika mchakato wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Lakini yametolewa maoni vile vile kuwa, kama pangelikuwepo na uongozi madhubuti wa Afrika Mashariki, inawezekana kuwa suala hili lingelishughulikiwa; na kwa hali hii, mchakato mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unatoa fursa ya namna ya pekee ya kulishughulikia suala hili; lakini jambo hili bado limefichwa chini ya zulia. Hata hivyo, baadhi ya hatua zinazochukuliwa na Zanzibar zinakusudia kuwatanabahisha Waafrika Mashariki juu ya matatizo ya Zanzibar. Chama kimoja cha siasa kimeeleza hivi:

Kila siku tumekuwa tukizungumzia uwezekano wa kugomea uchaguzi lakina kila siku tumekubaliana dhidi ya hilo ili tuweze kuziweka wazi hitilafu ziliopo, ili Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) waone kuwa tuna ajenda ya kidemokrasia.

Lakini kuna jambo jingine lililojitokeza kutoka bara. Ilishikiliwa kuwa angalau Waafrika Mashariki wingine katika Bunge la Afrika Mashariki walikuwa wakielewa juu ya matatizo ya Zanzibar, lakini walidhani kuwa Watanzania wangeliweza kuyatatua matatizo hayo wao wenyewe. Walielezea juu ya ukweli kuwa wajumbe wa Bunge la Afrika Mashariki walitembelea Zanzibar, waliyatambua matatizo na kwamba waliangali uchaguzi uliokuwa na machafuko Zanzibar.

Lakini jambo jingine muhimu linazozikabili pande mbili kati ya Muungano na mchakato wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ni wasiwasi

Page 121: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Muungano na Kuunganishwa kwa Afrika Mashariki 107

na hofu za Zanzibar. Hili lazima liwekwe katika muktadha wake. Ni kweli kuwa wabia wote ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wana wasiwasi na hata hofu kuhusu mchakato wa uunganishaji unaotegemea kumalizika kwa kuundwa Shirikisho la Afrika Mashariki.

Hata hivyo, watu wa Zanzibar wameelezea hofu zao kwa ukali na kwa kiasi kikubwa nyingi ya hofu hizo zinatokana na nafasi yao ndani ya Muungano, angalau kwa hisia zao. Hii ni kwa sababu wanaamini kuwa hawana sauti katika mchakato wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kujadili hoja yao, shukrani ziende kwa Muungano.

Wanaeleza kuwa Zanzibar ni kisiwa. Kuna uhaba wa rasilimali na hutegemea utalii. Inawezekana kuwa kuna watu 1.1 milioni lakini kiasi chao cha uzazi ni 3.4%. Wameelezea juu ya kuanguka kwa bei ya karafuu, kupanda na kushuka na kutotabirika kwa idadi ya watalii. Kwa sababu ya yote haya, uhuru wa kwenda wanakotaka, watu, nguvu kazi na bidhaa ambazo pia zinahusika na Soko la Pamoja, lazima utilie maanani kuwa Zanzibar ni mahali padogo. Juu ya haya, wameeleza juu ya kuiunga mkono Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Kuhusiana na Umoja wa Forodha, wameelezea juu ya kuanguka kwa biashara kati ya Zanzibar na bara. Hii inazidishwa na ukweli kuwa, ijapokuwa bidhaa zinazoingizwa Zanzibar zinatozwa ushuru wa namna moja, zinapopelekwa bara, zinatozwa ushuru tena (kwa kisingizio cha gharama za kutoa huduma au kwa madai kuwa bidhaa hizo hazikukaguliwa huko Zanzibar na ushuru haukulipwa).

Lakini kwa kisiwa katika Ziwa Victoria, hapatokuwepo gharama zozote. Hili inazifanya bidhaa zisiweze kushindana kwa sababu ya gharama ya kuziweka kwenye maghala na gharama za kuhudumiwa. Kwa hiyo, hili linaufanya Umoja wa Forodha uwe haupendwi na jamii ya wafanyabiashara Zanzibar. Wafanyabiashara wa Zanzibar wanakubali kuwa yalikuwepo mashauriano kabla ya Umoja wa Forodha haukupitishwa, lakini maoni ya Zanzibar hayakuingizwa.

Page 122: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

108 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

Wameelezea kuwa hivi sasa wanasafirisha mpira tu kwenda Kenya katika kanda nzima na mwani, sehemu nyingine na bila ya kuwa na viwanda vya kuzalisha bidhaa ambazo hazizalishwi bara na sehemu nyingine za Afrika Mashariki, hawataweza kubariki.

Vijana pia wamekuwa na wasiwasi na Jumuiya ya Afrika Mashariki. Wana hofu kuwa Zanzibar inaweza kuzungukwa na isiweze kushindana. Kwa mfano fursa za ajira zinaweza kuwapiga chenga. Kadhalika na fursa za elimu ya juu na fursa za kiuchumi kwa jumla. Wanaeleza juu ya hali ya Zanzibar: ndogo sana, kisiwa n.k.

Uhuru wa watu kwenda wanakotaka katika Afrika Mashariki, wana hofu, unaweza kuwanyima fursa. Watu kutoka Kenya, Rwanda na kwengineko wanaweza kuwashinda.

Wengine wana hofu kuwa wana uwezo mdogo wa kushindana na viwango vyao vya elimu ni vidogo. Bila ya kuwa na mfumo mzuri wa elimu. Wanazungumza vile vile juu ya tofauti za kimila: Wazanzibari wengi ni Waislam na ni watu wa amani. Waafrika Mashariki wengine wana tabia tofauti. Labda wanaweza kuwa na jeuri zaidi.

Lakini vijana wengine wamechangamka. Wanadhani kuwa utamaduni si kitu kilicho tuli bali ni kitu kinachokwenda; kwa hiyo mambo yanabadilika. Wanasisitiza kuwa mfumo wao wa elimu si mbaya kuliko popote pale katika Afrika Mashariki. Ni kwa sababu ya mawazo potofu tu kuwa kama mtu hazungumzi Kingereza, kwa hivyo hana elimu nzuri.

Zanzibar imeeleza wasiwasi mwingine kwa jumla. Kutokuwa na uhakika wa hali yao ya baadaye ni mojawapo ya wasiwasi huo. Kama Mzanzibari mmoja alivyosema: “Zanzibar inatekeleza wajibu wake na itatekeleza wajibu wake katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, lakini nafasi yetu katika Jumuiya hiyo, kuhusiana na hivi sasa na baadaye, ni tatizo.” Wana wasiwasi hata na masuala ya itifaki. Kwa mfano, pale rais wa Zanzibar anapohudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki hahudhurii mkutano huo kama rais.

Page 123: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Muungano na Kuunganishwa kwa Afrika Mashariki 109

Wakati watu wengi wana shaka na maslahi yaliyopo kutoka kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki, wengine wana maoni tofauti: Mtu mmoja ameeleza: “Kisaikolojia Zanzibar inaweza kuhisi kuwa nafasi yao haieleweki – lakini kusema kweli hawana chochote wanachopoteza kuhusiana na maslahi kutoka kwenye jumuiya, isipokuwa kwa wale wanaotaka vyeo.”Mwingine amelitaja jarida lenye miradi 7 inayosubiri kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa ajili ya Zanzibar:

Mradi wa Umeme wa Kutumia Upepo, Dola za Kimarekani • (USD) 70 milioniKituo Kipya cha Uwanja wa Ndege Dola za Kimarekani (USD) • 78 milioniBandari Mpya ya Kibiashara, Dola za Kimarekani (USD) 400 • milioniUsalama wa Kilimo na Chakula, Dola za Kimarekani (USD) • 71milioniEneo Huru la Zanzibar, Dola za Kimarekani (USD) 32 • milioniMradi wa bandari ya kuegesha meli za kubeba magari – • kuunganisha bandari ya Zanzibar na bandari ya Mombasa Eneo Lisilokuwa na Maradhi ya Wanyama, Dola za Kimarekani • (USD) 22 milioni

Njia ya Kuelekea kwenye Shirikisho la Afrika Mashariki na Nafasi ya MuunganoKatika sehemu hii, ujumbe unawasilisha mitazamo na mawazo ya Watanzania tuliowahoji. Mitazamo na mawazo haya yanahusiana na yote mawili, yaani mchakato na matokeo ya mwisho ya kuunganishwa kwa Afrika Mashariki mpaka kufikia Shirikisho la Afrika Mashariki.

Page 124: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

110 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

Ili kuziacha sauti za Watanzania ziongee kwa uhuru, mawazo haya yanawasilishwa kwa maneno halisi ya msemaji ili mtu yeyote yule aweze kuamua juu ya yale wanayokusudia.

Mawasilisho haya yamegawanywa na maoni yaliyokusanywa Zanzibar yanawasilishwa mbali na yale yaliyokusanywa bara. Hilo linaweza kuwa ni la umuhimu mkubwa katika kuamua namna ya kusonga mbele.

Sauti za Kutoka ZanzibarHivi sasa, Zanzibar hakuna shauku yoyote kuhusu • Jumuiya ya Afrika Mashariki ukichukulia kuwa Zanzibar haina uhuru na muundo wa Muungano kwa muda wa miaka 45 iliyopita.Kinachotakiwa ni Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyo wazi na • shirikisho linalotokana na makubaliano.Suala la Jumuiya ya Afrika Mashariki linakuwa ni la baadaye • kwa sababu ya Zanzibar kushughulishwa zaidi na matatizo ya Muungano. Matatizo ya Muungano yanatufanya tusiweze kuliangalia suala la Jumuiya ya Afrika Mashariki.Nani aliyeipa madaraka serikali ya Muungano kuyakabidhi • madaraka ya Zanzibar kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki?Ili iwepo Jumuiya ya Afrika Mashariki yenye utulivu kuna haja • ya kuiondoa Zanzibar mwanzo kutoka kwenye Muungano ili kuyafafanua mambo na baadaye Zanzibar inaweza kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki au shirikisho ikiwa ni sehemu pakee. Kama si hivyo, matatizo ya Muungano yatahamia kwenye Shirikisho la Afrika Mashariki. Kuiondoa Zanzibar ni lazima kwa sababu, masuala ya Muungano • yakifafanuliwa, Zanzibar itajua namna ya kujadiliana na nchi nyingine za Afrika Mashariki. Kama si hivyo, matatizo yatazidi.Mchakato wa kuiunganisha Afrika Mashariki si fursa ya • kutuwezesha kutatua matatizo yetu. Jumuiya itayazidisha matatizo, kama mambo yatabakia kama yalivyo. Hakuna sehemu nyingine ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yenye matatizo yanayofanana na ya Zanzibar.

Page 125: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Muungano na Kuunganishwa kwa Afrika Mashariki 111

Mchakato wa • Jumuiya ya Afrika Mashariki utaonekana tu kama ni fursa ikiwa Zanzibar itakubaliwa kama mwanachama ikiwa peke yake. Mtazamo wa Zanzibar kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa jumla umekuwa ni wa kutia shaka, ukiupambanisha uzalendo wa Kiafrika dhidi ya uzalendo wa Zanzibar.Zanzibar kuwa sehemu ya • Shirikisho la Afrika Mashariki itapunguza hofu za nchi za Afrika Mashariki kuwa inaweza kutumiwa na madola ya nchi za nje kuiyumbisha kanda yote. Kushughulikia swali la ukosefu wa mwamko, wa matatizo ya • Muungano kwa upande wa Waafrika Mashariki, jumuiya ya Afrika Mashariki ipeleke ujumbe kuchunguza – yaani, kama serikali ya Muungano inakubali kuwa kuna tatizo. Lakini hatuna matumaini mema kuwa baada ya miaka yote 45 ya matatizo ya Muungano, chochote kile kinaweza kufanywa; kama serikali ya Muungano inaweza kukubali.”Tunapenda tushiriki moja kwa moja katika Jumuiya ya Afrika • Mashariki, lakini katiba inataka kuwa hili lifanyike kwa kupitia serikali ya Muungano. Sisi haturidhiki na msimamo huu. Tungelipenda kuwa baadhi ya Wazanzibari katika Wizara ya Muungano ya Mambo ya Afrika Mashariki washughulikie mambo ya Zanzibar.Hatukukubali uharakishwaji wa Shirikisho la Afrika Mashariki • kwa sababu zilikuwepo taarifa zisizothibitishwa kuwa wagombea wa nafasi ya rais wa shirikisho walikwisha ainishwa.Tungelikuwa na kiti katika Jumuiya ya Afrika Mashariki – • tukiwa watazamaji, ili kushughulikia mambo yasiyokuwa ya Muungano.Tunahitaji kuwa na hadhi ya kuwa watazamaji, lakini • mapendekezo hayo hayakuwasilishwa kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki. Itakuwa ni kazi ya serikali ya Muungano kufanya hivyo, kwa sababu mkataba hausemi juu ya kuwepo hadhi ya mtazamaji.

Page 126: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

112 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

Siwezi kusema kama watu wa Zanzibar wanataka kujiunga na • Shirikisho la Afrika Mashariki au la kwa sababu hawana nafasi wala hawatambuliwi.“Mimi nina shaka juu ya namna gani Zanzibar itaweza • kuwakilishwa moja kwa moja katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.”Hakuna haja ya kuharakisha • Shirikisho la Afrika Mashariki wakati ndani ya Muungano huwezi kumpokea mwananchi mwenzako. Hii inahusu Kenya na nchi nyingine.Kuna shaka kwa upande wa Zanzibar. Ushirikiano wa Afrika • Mashariki utakuwa ni ule ule kama ulivyokuwa zamani? Watu wengi wa Zanzibar wanataka kushiriki, Zanzibar ikiwa nchi pekee. Ikiwa Shirikisho la Afrika Mashariki litakuja na muundo wa hivi sasa basi litazidisha matatizo tu. Kwa mfano, ardhi itapotezwa kwa Waafrika Mashariki wengine.Katika ngazi ya uchumi, kuna hofu ya kukaliwa juu kama Kenya • ilivyoikalia juu Jumuiya ya Afrika Mashariki ya zamani.Kusuluhisha suala la hadhi ya Zanzibar ndani ya Shirikisho • la Afrika Mashariki kuna haja ya kutatua suala la uhuru wa Zanzibar katika ngazi ya taifa. Ikiwa tatizo la muundo wa Muungano na matatizo yake litatatuliwa, hapo tena tunaweza kuihusisha jumuiya ya kimataifa. Tunahitaji kutatua matatizo yetu ya ndani kwanza.Inahitaji uwepo mkataba kati ya Tanzania na nchi wabia za • Afrika Mashariki juu ya ushiriki wa Zanzibar kuhusiana na mambo ambayo si ya Muungano. Zanzibar imekataa kuharakishwa kwa Shirikisho la Afrika • Mashariki kwa sababu likishakuwapo shirikisho hapatakuwapo na Jamhuri ya Kenya au Uganda, n.k ila kama utakuwa muungano ulioregarega.Sehemu ya ukaidi wa Tanzania kujiunga na shirikisho ni kwa • sababu ya vurugu iliyopo ndani, juu ya Muungano na tatizo la CCM/ CUF.

Page 127: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Hitimisho na Mapendekezo 113

Ushiriki wa moja kwa moja wa Zanzibar katika Jumuiya ya Afrika • Mashariki umezungumzwa katika Kamati ya Pande Mbili. Zanzibar ipewe uanachama wa • Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa sababu shughuli nyingi za Jumuuiya ya Afrika Mashariki zinahusiana na mambo yasiyokuwa ya Muungano.Zanzibar iwe mwanachama kamili wa Jumuiya ya Afrika • Mashariki na kama si hivyo, basi angalau iwe mwanachama wa kushirikishwa ili sauti yake isikike. Ikiwa kero za muungano hazitaondolewa, basi lazima zitaathiri • uunganishwaji.Sisi wafanyabiashara tungelipenda uwepo uwakilishi wa • moja kwa moja wa Zanzibar kuhusiana na mambo yasiyo ya Muungano katika Jumuiya ya Afrika Mashariki ili tuwe na sauti ya kutosha juu ya masuala yetu wenyewe, siyo kwa sababu tunapinga Muungano.Katika jumuiya, Zanzibar inapenda kuwa na hadhi ya • uanachama kwa haki yake yenyewe. Lakini serikali ya Zanzibar haina msimamo kuhusu hili.Utatuzi mzuri kabisa ni kwa matatizo ya Muungano kutatuliwa • kwanza; kama si hivyo, basi yataathiri mchakato wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.Kwa • muundo wa hivi sasa, kama ingelipigwa kura ya maoni juu ya Shirikisho la Afrika Mashariki asilimia 85% ya Zanzibar watasema hapana.Ufanywe utafi ti juu namna gani Zanzibar inaweza kujumuishwa, • ama ikiwa mwanachama kamili au hadhi nyingine itakayokubalika. Zanzibar inahitaji kutambuliwa. Kuna haja ya Zanzibar kuwa na hadhi maalum au fursa maalum ili iweze kuwa na sauti.Kabla hatukwenda kwenye • Shirikisho la Afrika Mashariki lazima tujitayarishe ndani. Zanzibar inahitaji nafasi, labda hadhi ya kuwa mtazamaji, n.k … badala ya kuwa chini ya Muungano.

Page 128: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

114 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

Itakuwa ni tatizo ikiwa tutaingia katika Shirikisho la Afrika • Mashariki kwa kupitia Tanzania.Tunahitaji kusafi sha nyumba yetu wenyewe kwanza kwa sababu • suala la Jumuiya ya Afrika Mashariki linaweza likawa kama lile la Umoja wa Waislam (OIC).

Sauti za kutoka BaraSisi katika Afrika Mashariki lazima tukubaliane ni nini • yatakayokuwa “mambo ya shirikisho”. Haitoshi kuzungumzia mambo ya Muungano. Tunahitaji kuainisha kwa Shirikisho la Afrika Mashariki ni yepi yatakayokuwa mambo ya shirikisho. Nani anajadiliana na nani? Kwa kuwa Zanzibar ni mdau halali wa Muungano, ina haki ya kuwa na sauti katika yale yatakayoingizwa kuwa ni mambo ya shirikisho la Afrika Mashariki na vipi serikali ya shirikisho itaundwa na itakuwa na madaraka gani na vipi viongozi wa serikali ya shirikisho watachaguliwa. Hili linazua masuala mengi. Zanzibar iwe na haki katika majadiliano haya.Kuna mambo ambayo si ya Muungano ambayo rais wa Zanzibar • ana haki ya kuyazungumzia. Tusiuweke upande utambulisho wa Zanzibar au itakuwa tatizo. Zanzibar iwe na nafasi maalum katika majadiliano juu ya Shirikisho la Afrika Mashariki, ijapokuwa mawazo hayo yanaweza yakapingwa.Nini itakuwa nafasi ya rais wa Muungano na rais wa Zanzibar • katika muundo wa Shirikisho la Afrika Mashariki? Mtazamo wa Zanzibar bila shaka utakuwa; ninanufaika vipi kutokana na muundo wa shirikisho na kutokana na Muungano? Inategemea juu ya namna watakavyojadiliana. Lakini kama watawekwa nje ya majadiliano, kuna tatizo kubwa. Tanzania inahitaji kuchukua hadhari, kila mara ifi kirie maslahi ya Zanzibar. Ikiwa Kikwete hatopendekeza ushirikishwaji wa Zanzibar • katika majadiliano ya shirikisho, basi marais wengine katika Afrika Mashariki watalilete suala hilo. Lakini Zanzibar yenyewe lazima iwe na msimamo juu ya hadhi gani itakayokuwa nayo

Page 129: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Muungano na Kuunganishwa kwa Afrika Mashariki 115

katika Shirikisho la Afrika Mashariki. Kwa hiyo, inabidi pawepo na kikao ili kuiwezesha Zanzibar kufanya hivyo. Tatizo hili ni la kweli.Je, • Shirikisho la Afrika Mashariki litakapoanzishwa, serikali ya Muungano itakuwa ni lazima? Jukumu lake litakuwa ni nini? Kama ingelikuwepo serikali ya Tanganyika, serikali ya Zanzibar, na halafu serikali ya shirikisho, hapo serikali ya Muungano itafanya nini? Itakuwa haihitajiki. Zitakuwepo serikali nyingi sana: Serikali za mitaa, serikali ya Tanganyika, serikali ya Muungano na Serikali ya shirikisho, zote zikijidai kuwatumikia wananchi. Lakini tunahitaji serikali ndogo. Wananchi wasitawaliwe na serikali nyingi. Serikali ya ngazi ya tatu kwa Tanganyika haitokuwa ya lazima; viongozi wa kuchaguliwa katika kanda watashughulikia mambo yasiyokuwa ya Muungano/mambo ya shirikisho. Tatizo litakuwa ni serikali gani inajadiliana na Kenya, Uganda.Kwa ajili ya Shirikisho la Afrika Mashariki ni vyema ikakuwepo • kura ya maoni ili shirikisho lisiwe ni jambo la uongozi wa Afrika Mashariki peke yake.Suala la • Bunge la Afrika Mashariki halikuletwa na wabunge wa bunge hilo kutoka Zanzibar. Ni wengine ndio waliokuwa na wasiwasi juu ya ushiriki wake.Zanzibar ina haja ya kuonekana kuwa ni nchi, ni suala ja • kujiamulia mambo yenyewe. Lakini Muungano hawalipendi hilo.Watu wengi Zanzibar wanaamini kuwa wawe kama walivyokuwa • katika Jumuiya ya Huduma za Pamoja ya Afrika Mashariki (EACSO). Lakini hili haliwezi kutokea kwa sababu linapingana na sera ya chama tawala. Lakini kama ingelikuwepo kura ya maoni, hili lingelikubalika.Mimi ninaunga mkono kuwa Zanzibar iingie katika • mchakato wa kuiunganisha Afrika Mashariki ikiwa ni nchi. Ombi hili

Page 130: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

116 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

linazidi kuwa na nguvu kwa ukweli kuwa Rwanda na Burundi, ambazo ni ndogo, ni wanachama. Kwa nini isiwe Zanzibar? Ikiwa Zanzibar itaingia katika • Shirikisho la Afrika Mashariki ikiwa nchi, serikali ya Muungano haitakuwa na ulazima. Utawala wa Tanzania, kama Tanzania, utatoweka. Lakini na utawala wa Zanzibar vile vile.Badala yake, inaweza kukubaliwa, Zanzibar ikiwa yenyewe, • yende wapi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na inahusiana vipi ikiwa ni sehemu ya Muungano. Unaweza kutengenezwa utaratibu kwa misingi hii. La msingi ni kwamba malalamiko ya Zanzibar yanashughulikiwa. Ikiwa suala hili halikushughulikiwa, basi tunapeleka matatizo katika shirikisho.Tanzania bado itakuwa tayari kuingia katika • mchakato wa kuunganisha bila ya kutatua matatizo yaliyosalia. Kiutendaji, mchakato wa kuunganisha utaendelea mbele lakini matatizo yatabaki palepale.Juu ya matatizo yake, kuna mambo mengi ambayo Shirikisho • la Afrika Mashariki linaweza kujifunza kutoka kwenye Muungano: nini kiepukwe; nini kitiliwe mkazo… Asilimia 97% ya wananchi katika Tanzania wanalitaka Shirikisho la Afrika Mashariki lakini ni asilimia 25% ndio wanaotaka liharakishwe. Suala la ardhi linaweza kubakia mikononi mwa kila moja ya nchi za Afrika Mashariki. Lakini ikiwa Rwanda na Burundi ambazo ni ndogo haziogopi kugubikwa, kwa nini nchi kubwa kama Tanzania iogope?Ukiipa Zanzibar hadhi ya upendeleo, Buganda na sehemu • nyingine kama hizo katika Afrika Mashariki nazo zitadai hadhi kama hiyo.Jumuiya ya Afrika Mashariki na shirikisho zijengwe juu ya • Muungano. Muungano wa karibu katika Tanzania uwe ndio msingi wa Muungano mkubwa zaidi wa kikanda. Zanzibar inadai kuwa haishirikishwi katika majadiliano yanayoendelea hivi sasa

Page 131: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Hitimisho na Mapendekezo 117

juu ya Soko la Pamoja. Lakini Zanzibar inatafuta njia ya kupitia tu ili iweze kujadiliana kama Zanzibar ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Hilo halitatokea ila kama katiba ya Muungano itaandikwa upya, jambo ambalo si la kutegemea.Baadhi ya watu wangelipenda Muungano uvunjike – lakini • Muungano umeweka mfano mzuri kwa Muungano wa Nchi za Afrika. • Jumuiya ya Afrika Mashariki mpya iwe ni kwa ajili ya watu. IIjenge upya miundombinu ya iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki ili watu nje ya miji yetu waweze kunufaika. Kuna haja ya kuyashughulikia malalamiko ya Zanzibar hapa ndani kabla hatukwenda kwenye Shirikisho la Afrika Mashariki, kwa vile tunakwenda huko tukiwa Jamhuri ya Muungano. Tanzania inakaidi kwenda kwenye shirikisho kwa sababu kuna ajenda za siri: Kenya ina upungufu wa ardhi na inayanyemelea maeneo makubwa ya ardhi yaliopo Tanzania, Museveni anataka kuwa rais wa kwanza wa shirikisho. Kwa hiyo, hawawafi kirii wananchi. Zanzibar iingie katika mchakato wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwa sehemu ya Jamhuri ya Muungano lakini masuala mahasusi yashughulikiwe na Baraza la Wawakilishi, hasa yale yanayohusu mambo yasiyokuwa ya Muungano, kama ilivyo kwa kisiwa cha Jersey.Inatolewa hoja kuwa, kuwemo kwa Zanzibar kama nchi huru • ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kutaimarisha nafasi ya Jamhuri ya Muungano ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa sababu itakuwa na kura mbili ndani ya Jumuiya hiyo. Lakini kwa utaratibu wa kikatiba wa hivi sasa, hili si chaguo linalofaa. Ikiwa katiba na Mkataba vitaruhusu kuwepo kwa Zanzibar, itakuwa ni sawa. Sisi wanasiasa ndio tunaojaribu kuwa kikwazo kikubwa. Kwa mujibu wa sheria za kimataifa, kinachoulenga mkataba ni dola, nchi ambayo kwa hapa ni Jamhuri ya Muungano. Kwa hiyo, hiki ni kikwazo kikubwa. Lakini ukiacha kikwazo hiki cha kisheria kuna kikwazo cha kisiasa, k.m. hofu ya Zanzibar kujitenga.

Page 132: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

118 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

Kuna haja ya kuufi kiria upya Muungano na uwakilishi wa • Zanzibar katika mikutano ya kimataifa, ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Zanzibar inabidi iwe na haki ya kuhudhuria na kuhisi kuwa inawakilishwa ipasavyo ikiwa nchi. Mimi ninahisi kuwa hivi sasa Zanzibar ipo katika nafasi nzuri ya kuwa mwanachama huru wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.Zanzibar hairidhiki na Jamhuri ya • Muungano. Inawezekana kuwa hawataridhika vile vile kushirikiana na watano wengine kwa muundo wa hivi sasa. Hii ni changamoto kwa viongozi nchini Tanzania na Afrika Mashariki, lakini vile vile kwa Waafrika Mashariki wengine wote. Lakini wabia wengine wanajaribu kulilazimisha shirikisho… Mengi bado yanahitaji kufanywa ili kuwa na Muungano tulivu, wenye tija na endelevu nchini Tanzania, kabla hukufi kiria kuwa na Shirikisho la Afrika Mashariki. Zanzibar ipo katika njia panda. Zanzibar inataka kuwa • peke yake, kuwa mwanachama kamili wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuliko kupitia kwenye Muungano.Mtazamo chanya juu ya suala la Jumuiya ya Afrika Mashariki • ni kuwa Shirikisho la Afrika Mashariki linaweza kujifunza nini kutokana na Muungano, badala ya kuyatilia mkazo matatizo ya Muungano. Ni kwa sababu Wazanzibar wana jazba kubwa tu. Tanzania itakuwa mwanachama wa Shirikisho la Afrika • Mashariki, siyo Zanzibar. Kusema kweli, kulileta suala hilo ni sawa na kubishana na hadhi ya kitaifa ya Tanzania. Uwakilishi wa Zanzibar peke yake katika Jumuiya ya Afrika • Mashariki itakuwa ni hatua ya kurudi nyuma, mfano mbaya kwa umoja. Badala yake, linaweza kuanzishwa dawati katika Jumuiya ambalo litashughulikia masuala ya Zanzibar.Ili tuwe na Afrika Mashariki yetu sote, Zanzibar inabidi • iwakilishwe. Watu wa Zanzibar wenyewe wanataka wawe na sauti juu ya namna gani wawakilishwe. Wasiachwe nje ya mchakato.

Page 133: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Hitimisho na Mapendekezo 119

Wazanzibari hawajiamini; lolote utakalofanya wao huwa na • jazba na wasiwasi; wana hisia ya kujiona dhalili, na sisi tunajaribu kilivumilia hilo. Kwenda kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki ni tatizo kubwa zaidi – kwa sababu hawajui Kingereza. Inabidi wawakilishwe kama Watanzania lakini ikiwa ni pamoja na watu kutoka Zanzibar ili waweze kutoa maoni yao na washiriki wakiwa Watanzania.Zanzibar ingelipenda kuwa mwanachama sawa wa Jumuiya ya • Afrika Mashariki lakini hiyo ina maana kuwa katiba ibadilishwe na uwachukulie Wazanzibari walio bara kama unavyowachulia Wakenya na Waganda bara. Ikiwa Shirikisho la Afrika Mashariki lina uwezo wa kisheria kama mambo ya Muungano, basi kuwepo kwa Zanzibar hakutakuwa tatizo. Zanzibar imekuwa ikigombana kuhusu ardhi, lakini wakijiunga na shirikosho watakuwa kama Wakenya na Waganda bara; watapoteza fursa wanazozipata hivi sasa bara. • Shirikisho la Afrika Mashariki halendi mbali, na Tanzania ni mmoja ya wale walio wakaidi na wakali kwa sababu ya shaka iliyonayo kuwa Kenya inataka kupora ardhi, n.k. Lakini hili ni suala la jazba tu. Si rahisi kukadiria lakini Zanzibar inaweza kupata hasara kubwa • kuhusiana na haki zao bara. Sisi tukiwa Watanzania, pamoja na Zanzibar, tumepitia hatua • za kuungana za Umoja wa Forodha, Soko la Pamoja na Umoja wa Sarafu. Afrika Mashariki bado ina. Ikiwa uanachama kamili wa Jumuiya ya Afrika Mashariki • hauwezi kupatikana, Zanzibar inaweza kuwa na hadhi maalum katika Jumuiya hiyo, na hiyo itakuwa na maana ya kuwa na hadhi maalum katika Muungano.Tunashiriki katika • mchakato wa Jumuiya ya Afrika Mashariki bila yakuwa tumeyatatua masuala ya uhusiano wetu ndani ya Muungano.

Page 134: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

120 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

Kwa jumla mawazo ya hapo juu ni ya kutosha na yanatoa picha ya namna ya matatizo yaliopo na uwezekano wa kuwepo mabadiliko ya mchakato na muundo wa badaye wa utatuzi juu ya namna gani Muungano uhusiane na mchakato wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Katika kuamua namna ya kuendelea, lazima hoja za wanazuoni wa mambo ya sheria zitiliwe maanani kuwa, ili Tanzania iweze kujiunga na Shirikisho la Afrika Mashariki, itabidi ifanyiwe marekebisho Ibara 4 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayotoa madaraka yote ya kiserikali kwa serikali mbili, ya Muungano na ya Zanzibar peke yao – kwa vile kujiunga na shirikisho itabidi kukasimu baadhi ya madaraka haya ya kiserikali kwa serikali ya Shirikisho la Afrika Mashariki. Marekebisho kama haya yatahitaji makubaliano ya thuluthi mbili ya wingi wa kura za Wabunge kutoka Zanzibar, na kwa hiyo kuipa Zanzibar kura ya turufu katika kuamua juu ya namna ya kujiunga na Shirikisho la Afrika Mashariki ambalo linaweza lisikubalike kwao.25

25 Angalia Ibara 98 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Page 135: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

121

7Hitimisho na Mapendekezo

Ujumbe huu umedhamiria kuuchunguza Muungano na kukusanya maoni juu ya Muungano huo, kote, Zanzibar na bara. Ulitaka kuainisha matatizo yanayohusiana na Muungano. Ulitaka vile vile kuliangalia swali la Muungano linavyohusiana na mchakato wa kuiunganisha Afrika Mashariki.

Kutokana na maoni yaliyoelezwa na Watanzania juu ya suala hilo, ujumbe huu umebaini kuwa kuna matatizo yanayohusiana na uundwaji, muundo na usimamizi wa Muungano. Mengi ya matatizo haya bado hayakutatuliwa na ndiyo msingi wa kutoridhika na masikitiko juu ya maeneo mengi ya Muungano ikiwa ni pamoja na uhalali wake, muundo wa serikali mbili, kupanuliwa kwa orodha ya mambo ya Muungano, mgawanyo wa gharama na maslahi ya Muungano, tishio kwa utambulisho wa Zanzibar na uhusiano wa kimataifa na, kwa kiasi fulani kutoweka kwa utambulisho wa Tanganyika.

Ujumbe huu umebaini vile vile kuwa, juu ya kuwepo kwa matatizo haya, watanzania wengi si kama wanaupenda Muungano tu bali wasingelipenda uvunjike vile vile na wangelipenda uendelee.

Ujumbe huu umebaini vile vile kuwa watu wengi, kote kuwili, Zanzibar na bara wangelipenda yawepo mabadiliko katika maeneo yote ya Muungano yaliyoelezwa hapo juu ili uwepo Muungano wa haki na wa usawa ambao unawakilisha kwa dhati maslahi ya pande zote mbili za Muungano. Katika kutoa mapendekezo yake, ujumbe huu umetilia maanani yafuatayio, ukiacha yale yaliyoelezwa hapo juu:

Muungano uliundwa kwa namna ambayo haikuwa shirikishi na • katika mazingira ya siri. Wananchi hawakushiriki katika kufanya

Page 136: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

122 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

maamuzi kwa kupitia michakato kama vile, kura ya maoni au hata utafi ti wa juu juu tu au mjadala. Ushiriki wao haukuwa wa moja kwa moja na mdogo sana, kwa kiasi kuwa wawakilishi wa wananchi katika Bunge la Tanganyika walilijadili suala hilo kwa muda mfupi tu katika mchakato wa kuliridhia.Muungano upo, juu ya kuwepo kwa changamoto kuhusuiana • na misingi ya uhalali wake. Muungano umeundwa katika mazingira ya Vita Baridi ambavyo, • kwa namna yoyote ile, vimeathiri namna ulivyoundwa na muundo uliochukua. Sasa Muungano upo katika kipindi cha dunia ya baada ya Vita Baridi.Wale wabia ambao walikuwa sawa ndani ya Muungano sasa • wamefanywa wasiwe sawa kwa ukubwa, rasilimali na katika hali yao ya kisiasa na utulivu.Kwa kipindi kirefu cha uhai wake, Muungano umeendeshwa • chini ya mfumo wa serikali ya chama kimoja na historia ya kuwa na viongozi wenye vipaji. Nafasi ya mfumo wa serikali ya chama kimoja sasa imechukuliwa na mfumo wa vyama vingi na viongozi wa hivi sasa na wa baadaye hawatakuwa tena na fursa ya kufurahia uluwa wa kuitwa “baba wa taifa”.

Kwa hiyo, Ujumbe huu unatoa mapendekezo yafuatayoMuungano wote uangaliwe upya, kwa namna iliyo rasmi, hasa • muundo wake, mambo ya Muungano, mgawanyo wa gharama na maslahi na mustakabali wa Muungano wenyewe.Katiba yote iangaliwe upya ili vipengele vyake vyote vikidhi • mahitaji ya mfumo wa vyama vingi ili Muungano uwe wa namna, yenye umbo na usimamizi utakaokubalika.Mchakato wa kuupitia upya Muungano na katiba ujumuishe • ushiriki kamili wa wananchi. Wananchi washirikishwe katika kuainisha utatuzi endelevu, na maoni yao yapimwe kwa misingi ya kuanisha matakwa yao na utatuzi utakaokuwa na maslahi kwa watu wote. Ujumbe huu unapendekeza njia zifuatazo za kuwashirikisha wananchi:

Page 137: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Hitimisho na Mapendekezo 123

a. Mashauriano ya hadhara, mijadala na semina juu ya masuala haya

b. Mkutano wa kitaifac. Kura ya maoni juu ya muundo wa Muunganod. Kura ya maoni juu ya hadhi ya Zanzibar ndani ya Jumuiya

ya Afrika MasharikiIundwe Tume ya kuipitia upya katiba.• Iundwe tume ya kuupitia upya Muungano. • Zichukuliwe hatua za kuyashughulikia matatizo ya kiuchaguzi • ya Zanzibar kwa misingi ya kutohusisha pande fulani tu bali kwa kuwashirikisha wadau wote nje ya CCM na CUF.Tanzania, kwa sababu ya historia yake na tofauti na wengi • wa wabia wake ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, ina viongozi wengi wenye uzoefu ambao wamestaafu, kote, Zanzibar na Tanzania Bara. Rasilimali hii ya thamani sana itumiwe kikamilifu katika kuanzisha na kuendesha michakato iliyopendekezwa hapa.Kuhusu • mchakato wa kuiungunisha Afrika Mashariki, Zanzibar ishiriki vya kutosha katika majadiliano hayo ambayo hatimaye yatapelekea kuundwa kwa Shirikisho la Afrika Mashariki, ili maslahi yake yatiliwe maanani.Tanzania iuone • mchakato wa kuiunganisha Afrika Mashariki kuwa ni fursa na tukio la kutatua matatizo yaliyobaki ya Muungano, wao wenyewe, au pamoja na Waafrika Mashariki wingine.

Mafunzo ambayo Jumuiya ya Afrika Mashariki inaweza kujifunza kutokana na Muungano wa Tanzania

Jumuiya ya Afrika Mashariki inahitaji kutilia mkazo hali ya • kutumikia wananchi ya Jumuiya hiyo tokea wakati wa mchakato wa kuanzishwa na katika hatua mbalimbali za utendaji wake. Usiri na kutowajali wananchi, kama inavyoonekana katika uundwaji wa Muungano wa Tanzania, kunaweza kusababisha matatizo ya baadaye.

Page 138: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

124 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

• Jumuiya ya Afrika Mashariki inaweza kujifunza kutokana na uzoefu wa Tanzania kuwa shirikisho litaweza kufanya kazi tu, kama litaanzishwa ipasavyo. Imebainika kuwa, juu ya kuwa na msingi dhaifu wa kisheria, Muungano umeendelea kuwepo.Uzoefu wa Muungano unaonesha ulazima wa kuwepo utaratibu • madhubuti wa kiasasi kwa ajili ya kutatua matatizo.Juu ya • Muungano kuendelea kuwepo kwa zaidi ya nusu karne, uzalendo wa Zanzibar bado unastawi. Jumuiya ya Afrika Mashariki ihakikishe kuwa haikandamizi uzalendo wa sehemu mojawapo ya zile sehemu zinazounda shirikisho.

Page 139: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

125

Viambatanisho

Watu Waliohojiwa na Ujumbe huu Tanzania Bara(23-28 Agosti 2009)

Jina Cheo/Chama

Adam Zuku Afi sa Maendeleo Mwandamizi wa Chama, Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo cha Tanzania (TCCIA)

Balozi Daudi Mwakawago

Taasisi ya Mwalimu Nyerere

Ananlea Nkya Mkurugenzi Mtendaji, Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake

Ayoub Ryoba Mhadhiri Msaidizi, Chuo cha Waandishi wa Habari and Mawasiliano na Umma; Mweyekiti, Taasisi ya Vyombo vya Habari ya Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania

Baraka Rajaba Mkurugenzi Msaidizi, Wizara ya Nchi Inayoshughulikia Mambo ya Muungano

D.U. H. Mshana Katibu Msaidizi Mkuu, Uhusiano wa Kimataifa, Chama Cha Mapinduzi ( CCM)

Daniel Machemba Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo, Tanzania (TCCIA)

Dk. Willbrod P. Slaa

Katibu Mkuu, Chama Cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA)

Mhandisi Aloys J. Mwamanga

Rais, Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo, Tanzania

Page 140: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

126 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

Francis Mollay Kaimu Mkurugenzi Ofi si ya Mambo ya Muungano, Wizara ya Nchi Inayoshughulikia Mambo ya Muungano

Gasper Shao Wakili wa serikali Mwandamizi, Wizara ya Nchi Inayoshughulikia Mambo ya Muungano

Harry M. Kitillya Kamishna Mkuu, Mamlaka ya Mapato Tanzania

Hebron Mwakagenda

Mkurugenzi Mtendaji, Jukwaa la Uongozi

Mhe. Jaji Joseph S. Warioba

Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Aliyekuwa Jaji wa Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki (EACJ)

Mhe. Hamad Rashid Mohammed

Kiongozi wa Upinzani katika Bunge, Civic United Front ( CUF)

Mhe. John Zephania Chiligati

Waziri, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Katibu Mwenezi, CCM

Mhe. Mabere Marando

Wakili, Marando, Mnyele and Co. Advocates; Alikuwa Mbunge, Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Mwanachama NCCCR Mageuzi

Mhe. Mahfoudha Alley

Makamu Mwenyekiti, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHRAGG)

Mhe. Mohammed Seif Khatib

Waziri wa Nchi kwa Mambo ya Muungano, Ofi si ya Makamu wa Rais

Jabir Idrissa Mwandishi wa Habari, Gazeti la Mwana Halisi

Page 141: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Viambatanisho 127

John P. Mireny Kaimu Katibu Mtendaji, Baraza la Vyombo vya Habari la Tanzania

Joseph W. Butiku Mkurugenzi Mtendaji, Taasisi ya Mwalimu Nyerere

Juliana W. Chitinka Katibu Msaidizi Mkuu, Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, CCM

Mark D. Bomani Wakili, Bomani and Company Advocates

Mary J. Mwingira Mkurugenzi Mtendaji, Chama cha Jumuiya Zisizo za Kiserikali cha Tanzania (TANGO)

Mhe. Mbarak Abdul Wakil

Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani, Alikuwa Katibu Msaidizi, Ofi si ya Makamu wa Rais

Nehemia Mandia Wakili wa Serikali, Wizara ya Nchi Inayoshughulikia Mambo ya Muungano

Prof. Issa G. Shivji Mwalimu Nyerere Profesa wa “ Pan-African Studies,” Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam

Prof. Mwesige Baregu

Mkuu wa Idara ya Sayansi ya Siasa, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Prof. Gamaliel Mgongo Fimbo

Profesa wa Sheria, Kitivo cha Sheria, Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam,

Prof. Ibrahim Lipumba

Mwenyekiti, CUF

Seif Nakukima Jukwaa la Uongozi

Specioza Mashauri Afi sa Maendeleo wa Chama, Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo Tanzania

Page 142: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

128 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

Watu Waliohojiwa na Ujumbe huu Zanzibar(13-16 Julai 2009)

Jina Cheo/Chama

Abdalla Abas Omar Rais, Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimoiculture Kilimo

Abdulla Mohammed Juma

Mkurugenzi Mwendeshaji, Gazeti la Zanzibar Leo

Abeida Rashid Mwanaharakati Mwanamke

Asha Aboud Mwanaharakati Mwanamke

Ali Mansoor Mwanachama Mshauri,Chama Cha Wafanyabiashara

Ali Shauri Naibu Katibi Mkuu wa Parapaganda, Mkuu wa CCM

Alphonse Baltazer Mfanyakazi wa Ustawi wa Jamii,Wa Vijana ZAPHA

Amina Talib Makamu Mwenyekiti, ZAFELA

Asha Aboud Mwanaharakati Mwanamke

Assa Ahmad Rashid Mwanasheria, Bodi ya Mapato ya Zanzibar

Dadi K. Maalim Mwenyekiti, Jukwaa la Vijana la Zanzibar C/o ANGOZA

Dk. Mohamed Hadifh Khalifan

Mkurugenzi Mtendaji, Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda and Kilimo

Fatuma Saleh Mwanachama, ZAFELA

Fakih Kombo Kijana

Hamza Omar Makamu Mwenyekiti, ANGOZA

Page 143: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Viambatanisho 129

Hassan Khamis Juma Kaimu Katibu Mkuu, Umoja wa Vyama Visivyo vya Kiserikali( NGOs) Zanzibar (ANGOZA)

Mhe. Ismail Jussa Msemaji rasmi, Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ( CUF).

Mhe. Mansoor Yussuf Himid

Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi

Mhe. Othman Masoud Othman

Mkurugenzi wa Kuendesha Mashtaka Prosecutions

Mhe. Pandu Kifi cho Spika wa Baraza la Wawakilishi

Mhe. Samiha Sululu Hassan

Waziri wa Viwanda, Biashara and Uwekezaji

Mhe. Seif Shariff Hamad Katibu Mkuu, CUF

Mhe. Shamsi Vuai Nahodha

Waziri Kiongozi, Zanzibar

Mhe. Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini

Waziri wa Nchi wa Fedha, Ofi si ya Rais

Ibrahim Mzee Katibu, Baraza la Wawakilishi

Issa Kheri Hassan Kijana

Jamila Mahmoud Juma Mwanachama, ZAFELA

Masoud Nassor Afi sa Mradi Chama cha Zanzibar Cha Watu Wanaoishi na VVU/UKIMWI (ZAPHA)

Mohamed Haji Katibu Mkuu Msaidizi, CCM

Mohamed Issa Khatib Makamu wa Rais, Chama cha Wafanyabiashara

Mwanamkaa Mohd Mwanachama, ZAFELA

Page 144: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

130 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

Nassor Mohamed Ilyekuwa Mjumbe, Kamati ya Rais ya Muafaka , Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi Electoral ya Zanzibar (ZEC)

Ngwali Ali Kijana

Omar Abubakar Mwanachama , ANGOZA

Prof. Abdul Sheriff Mkurugenzi Mtendaji, Taasisi ya Utafi ti wa Bahari ya Hindi (ZIORI).

Prof. Khamis Ishau Naibu Mkurugenzi wa Uchaguzi, CCM Kisiwanduwi

Raya Aley Mwenyekiti, Chama cha Maalbino cha Zanzibar Association of C/o ANGOZA

Mhe. Saleh Ramadhan Ferouz

Naibu Katibu Mkuu, CCM

Salim Said Salim Mwandishi wa Deutsche Wella

Salma Sadat Mwanaharakati Mwanamke

Seif Abdallah Juma Mkurugenzi Mtendaji (ZAPHA+)

Shemsa Abdulkarim Abdalla

Mwanaharakati Mwanamke

Yahya H. Khamis Rais, Chama cha Wanasherias, Zanzibar

Zainabu Hamisi Mwanachama, ZAFELA

Zuberi Khamis Ismail Kijana

Page 145: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Viambatanisho 131

Watu Waliohojiwa na Ujumbe huu Pemba(19 – 20 April 2010)

Bwana Hamad Ali Musa Katibu ombi la Pemba Kwenye Umoja wa Mataifa 2008 (Mzee)

Bwana Juma Bakari Alawi Mratibu, Chama cha Wasindika Chumvi, Zanzibar

Mhe, Bw. Haji Omari Haji Hakimu MkaziBwana Saleh Nassor Juma Katibu wa Wilaya, CUFBwana Hemed Kombo Ofi sa Mfawidhi, Wizara ya

Utawala Bora and Mambo ya Katiba

Bwana Juma Kassim Tindwa Mkuu wa Mkoa, Chake Chake

Page 146: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

132

BibliografiaCoupland, R. East Africa and its Invaders, Oxford, Clarendon Press,

1938

Coupland, R. The Exploration of East Africa, Faber, London,1939

Hughes, A. J., East Africa: The Search for Unity: Kenya, Tanganyika, Uganda and Zanzibar, Harmondsworth, 1963

Iliffe, J. A Modern History of Tanganyika, Cambridge University Press, Cambridge, 1979

Kimambo, I. N. na Temu A. J. A History of Tanzania, East African Publishing House, Nairobi, 1969

Mute, L., (ed.), Constitutionalism in East Africa: Progress, Challenges and Prospects in 2004, Fountain Publishers, Kampala, 2007.

Ogot, B.A., Zamani: A Survey of East African History, Longman, Nairobi, 1974

Oliver, R. and Mathew G. (eds) History of East Africa, Vol. I, Oxford University Press, 1964

Oloka-Onyango J. na Nassali M., Constitutionalism and Political Stability in Zanzibar: The Search for a New Vision, A Report of the Fact-Finding Mission Organised under the auspices of Kituo Cha Katiba, The Friedrich Ebert Stiftung, Tanzania, 2003

Othman, Haroub, “The Union with Zanzibar” in Legum C na Mmari G. Mwalimu: The Influence of Nyerere, James Currey Ltd., London, 1995

Petterson Don, Revolution in Zanzibar: An American’s Cold War Tale, Westview Press, Boulder, Colorado, 2002

Page 147: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Bibliografia 133

Rothchild, D., Politics of Integration: An East African Documentary, Nairobi, 1968

Sheriff Abdul na Ferguson E (eds), Zanzibar under Colonial Rule, Historic Association of Tanzania, Dar es Salaam, 1991

Sheriff, Abdul, Slaves, Spices and Ivory in Zanzibar: Integration of an East African Commercial Enterprise into the World Economy, 1770 – 1873, James Curry, Oxford, 1987.

Shivji Issa G., Tanzania: The Legal Foundations of the Union, Dar-es-Salaam University Press, 2009

Shivji, Issa G., Pan Africanism or Pragmatism? Lessons of Tanganyika – Zanzibar Union, Mkuki na Nyota Publishers, Dar-es-Salaam, 2008

Wilson Amrit, US Foreign Policy and Revolution: The Creation of Tanzania, Pluto Press, London, 1989

Page 148: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

134

Faharasa ZilizoteuliwaAfro-Shirazi Party 5Babu, Abdulraham Mohamed 6, 21, 23Mabunge Mawili 84Chama cha Demokrasia na Maendeleo

(CHADEMA) 125Chama cha Mapinduzi (CCM) 11, 13,

14, 15, 31, 34, 50, 51, 60, 64, 65, 66, 67, 69, 70, 72, 73, 74, 84, 85, 86, 87, 103, 113, 125, 126, 127, 128, 129, 130

Halamshauri Kuu ya Taifa- 11, 12Jumuiya za kiraia 37, 38, 52, 78, 103Civil United Front (CUF) 11, 12, 13,

14, 15, 50, 64, 66, 67, 70, 72, 79, 86, 113, 123, 126, 127, 129, 131

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora 59, 126

Jumuiya ya Huduma za Pamoja ya Afrika Mashariki 90, 116

Jumuiya ya Afrika Mashariki 90, 116Mkakati wa Maendeleo wa Ushirikiano

wa Afrika Mashariki 91Umoja wa Forodha wa Afrika Mashariki

62, 91, 107, 120Shirikisho la Afrika Mashariki 7, 9, 21,

91, 92, 93, 94, 96, 97, 107, 111, 112, 114, 115, 116, 117, 118, 119, 120, 123

Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki 90

Chama cha Wanasheria cha Afrika Mashariki 97, 130

Bunge la Afrika Mashariki 101, 106, 115, 126

Kundi la Watu 55 Hamad, Seif 15Hanga, Abdul Kassim 6

Baraza la Pamoja la Vyuo Vikuu la Afrika Mashariki 90

Tume ya Pamoja ya Fedha 59, 60Jumbe, Aboud 74Karume, Abeid 5Karume, Amani 12Kenyatta, Jomo (aliyekuwa rais , Kenya)

6, 21, 93Kituo cha Katiba (KCK): ii, viiShirikisho la MataifaMafudha, Ali 23Maridhiano 15 Makubaliano ya Miafaka 64

mvutano kati ya – 8, 20, 68mchakato wa – 12, 15, 21, 31, 46, 49, 51, 54, 65, 66, 68, 70, 71, 78, 85, 86, 88, 90, 92, 103, 104, 105, 106, 107, 110, 113, 116, 117, 119, 120, 121, 122, 123

Nabudere Wadada, Dan 23Njonjo, Charles 93 Nkrumah, Kwame (Ghana) 7Vyama Visivyokuwa vya kiserikali 101Tume ya Nyalali 31, 44, 58, 75, 79, 88Nyerere, Julius (aliyekuwa rais, Tanzania)

6, 7, 8, 9, 18, 19, 20, 22, 23, 26, 27, 29, 46, 56, 74, 81, 82, 85, 89, 93, 125, 127, 132

Obote, Milton (aliyekuwa rais, Uganda) 6

Okello, John 19 Bonde la Olduvai (Tanzania) 1Umoja wa Afrika 8, 17, 28, 80 Dunia ya baada ya vita baridi 19Said, Seyyid 3Vita vya Pili vya Dunia 2Tanganyika: 1, 2, 6, 10, 17, 115, 122,

Page 149: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

Faharasa Zilizoteuliwa 135

132, 133Hitilafu kati ya Zanzibar na – 20uhalali wa – 9, 24, 25, 33, 35, 44, 85, 121, 122rasilimali, fedha za 1, 35, 41, 43, 60, 90, 94, 107, 122 mambo ya kijamii na kiutamaduni ya – 37, 91matatizo ya kimuundo ya – 31, 48, 53

Tanganyika African National Union (TANU) 9, 11, 18, 19, 20, 27

Umoja wa Vyama Visivyokuwa vya Kiserikali vya Tanzania 101

Baraza la Tanzania kwa Maendeleo ya Jamii 105

Mamlaka ya Mapato ya Tanzania 33, 34, 35, 36, 62

Twala, Abdul Aziz 6Umma Party 8, 20, 23Muungano wa Tanganyika na Zanzibar:

7, 9, 17na kuunganishwa kwa Afrika Mashariki 90, 105, 110tume na kamati za – 57, 73Kamati ya Makamu wa Rais 59, 60, 61katiba ya – 9, 17, 24, 25, 28, 30, 40, 44, 45, 47, 56, 60, 69, 88, 92, 95, 99, 117, 120Mahakama ya Katiba ya – 42, 50, 56, 57, 74mgawanyo wa madaraka na majukumu 48kupanuka kwa – 47 mustakabali wa – 26, 77 , 79, 80, 84, 122mustakabali bila ya – 80idara za serikali katika – 73

serikali ya – 10, 14, 15, 17, 18, 22, 25, 26, 27, 28, 29, 30, 31, 34, 35, 40, 41, 42, 46, 47, 49, 50, 53, 54, 55, 57, 58, 60, 61, 62, 63, 64, 66, 67, 68, 73, 74, 76, 85, 88, 92, 95, 96, 97, 99, 100, 103, 104, 111, 114, 115, 120, 122usuli wa kihistoria wa – 1vikwazo kwa – 37, 84ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki 92, 99, 107, 117, 118, 123uhusiano wa kimataifa 95, 121, 125, 127 viongozi wa /ndani – 30, 45, 69, 74, 114, 115, 122uhalali wa – 9, 24, 25, 33, 35, 44, 85, 121, 122kuja kwa – 17, 81Tume ya Nyalali na – 31, 44, 58, 75, 79, 88Utendaji wa – 22, 53, 54, 72, 97, 123 Bunge10, 13, 14, 15, 16, 22, 25, 26, 29, 32, 34, 43, 44, 45, 60, 62, 74, 101, 106, 115, 122, 126Vyama vya siasa ndani ya – 11, 14, 41, 46, 66, 69, 71, 72, 86 Siasa za – 3, 21, 51, 66, 76Hali ya sasa ya - ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki 92kura ya maoni 15, 37, 65, 68, 82,85, 88, 89, 92, 114, 115, 122, 123njia ya kuelekea kwenye Shirikisho la Afrika Mashariki na nafasi ya – 110 mambo ya kijamii na kiutamaduni – 37, 91

Page 150: Shirikisho Ndani ya Shirikisho - Kituo Cha Katiba...Shirikisho Ndani ya Shirikisho Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki Taarifa ya Ujumbe wa

136 Shirikisho Ndani ya Shirikisho

muundo wa – 11, 22, 26, 27, 28, 29, 31, 33, 53, 55, 56, 61, 68, 72, 74, 77, 83, 88, 89, 90, 101, 110, 112, 114, 115, 118, 122, 123muungano wa serikali tatu 58, 74, 83, 84

mambo ya Muungano – 11, 13, 24, 26, 30, 32, 33, 34, 35, 40, 41, 42,44, 45, 46, 47, 48, 49, 50, 51, 53, 58, 61, 70, 76, 77, 78, 87, 95, 99, 100, 121, 122, 125

kukubalika kwa – 44, 45 kupanuka kwa – 47usimamizi wa – 12, 30, 42, 48, 55, 121utaratibu wa kutatua – 53, 57, 58, 69

Sauti za kutoka bara 110, 114 kama koloni 18, 81matakwa ya uhuru 84

Baraza la Wawakilishi 13, 14, 15, 29, 45, 49, 50, 53, 63, 103, 117, 129uhuru wa – 7, 17, 35, 36, 45, 38, 46, 49, 51, 69, 77, 79, 81, 93, 107, 108usuli wa mtu mmojammoja wa – 52kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa katika – 46, 55, 58, 77masuala ya utambulisho katika- 84Mapinduzi ya – 6, 8, 17, 19, 20, 57, 93Baraza la Mapinduzi 5, 9, 10, 19, 20, 22, 27, 43, 57

Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar 12, 14, 15, 64, 73

Zanzibar Peoples Party (ZPP) 18, 19, 21Zanzibar National Party (ZNP) 19