taarifa muhimu za nchi - federal council · 2021. 1. 7. · ushirikiano baina ya serikali ya uswisi...

2
Msaada wa Uswisi nchini Tanzania Serikali ya Uswisi imekuwa ikiendesha shughuli zake nchini Tanzania tangu mwaka 1960. Shughuli hizo ziliimarishwa zaidi mwaka 1981 kufuatia kufunguli- wa kwa ofisi ya ushirikiano jijini Dar es Salaam. Pro- gramu ya maendeleo ya Uswisi inaoana na mkakati wa Tanzania wa kupunguza umaskini, na huratibi- wa kwa ushirikiano na nchi nyingine na mashirika ya kimataifa. Mkakati wa Ushirikiano wa Uswisi wa mwaka 2015-2018 unashirikisha vyombo mbalimbali katika kutoa misaada ya maendeleo na miradi yake hulenga kanda ya kati (mikoa inayozunguka Dodo- ma). Majadiliano ya kisiasa na ya kitaalamu hufanyika kwa kushirikisha wadau wa ngazi ya ofisi kuu ya Seri- kali ya Tanzania na ofisi za Wilaya. Sekretarieti ya Tai- fa ya Masuala ya Uchumi SECO imekuwa ikiendesha shughuli zake nchini Tanzania tangu mwaka 1988 pamoja na kwamba Tanzania haikuwa tena nchi ya kipaumbele katika mwaka 2010, isipokuwa tu katika ugharamiaji wa miradi ya hapa na pale ya miundo mbinu ya maji na ya maendeleo ya kiuchumi. Afya: fursa sawa katika huduma bora za afya Serikali ya Uswisi inasaidia kuboresha upatikanaji wa fursa sawa za huduma bora za afya kwa jamii za pembezoni. Mkazo umewekwa katika kupambana na ugonjwa wa malaria na kugharamia huduma za afya. Maeneo mengine yanayozingatiwa ni mabadi- liko katika mfumo wa sekta ya afya na uendelezaji wa miradi ya utafiti inayolenga kuwapatia wafan- ya-maamuzi ya kisiasa taarifa kuhusu vipaumbele vya afya nchini. Katika jitihada zake za kupamba- na na ugonjwa wa malaria, Shirika la Maendeleo na Ushirikiano la Uswisi linaisaidia ofisi ya taifa ya uratibu wa utekelezaji wa programu ya Taifa ya vyandarua vya mbu nchini Tanzania, ambayo imes- ambaza vyandarua vyenye viuatilifu kwa watu zaidi ya milioni 28. Matokeo yake, kiwango cha vifo vya watoto wa umri wa chini ya miaka mitano kimeshu- ka kwa asilimia 48 katika kipindi cha kati ya mwaka 2000-2010, huku nafasi za ajira 6,000 zinazohusiana na uzuiaji wa ugonjwa wa malaria zikitengenezwa. Serikali ya Uswisi inasaidia katika shughuli za kupunguza umaskini katika eneo la mikoa ya kati ya Tanzania, inasaidia kuboresha upati- kanaji wa huduma bora za afya na pia imed- hamiria kuboresha hali ya ajira na ya kipato katika maeneo ya vijijini pamoja na kuimarisha asasi za kiraia na uhuru wa vyombo vya habari. Hali Ilivyo Mwaka 2014 Tanzania ilikuwa ya 159 kati ya nchi 187 katika orodha ya Kiwango cha Maendeleo ya Watu, hivyo nchi hii ni miongoni mwa nchi maskini sana duniani. Licha ya uchumi wake unaokua, umaskini umeendelea kukithiri nchini Tanzania ambapo watu milioni 12 walikuwa wanaishi katika hali ya umaskini wa kupindukia mwaka 2013. Hii ni sawa na asilimia 28 ya watu wote, hali ambayo haikuwahi kubadilika tangu mwaka 2001. Pamoja na hali ya umasikini wa kupindukia, Tanzania ni nchi yenye utulivu na amani kuliko nchi nyingine za kusini mwa Jangwa la Saha- ra. Hatua kubwa imepigwa katika kipindi cha mpi- to kutoka kwenye uchumi wa kupangwa kwenda kwenye uchumi wa soko huku mabadiliko ya kisiasa na kijamii yakiwa ya taratibu lakini ya uhakika. SHIRIKA LA MAENDELEO NA USHIRIKIANO LA USWISI NCHINI TANZANIA TAARIFA MUHIMU ZA NCHI 2016 n Mji mkuu Uwakilishi wa Serikali ya Uswisi Ubalozi (Sehemu ya ushirikiano wa kimataifa) Ofisi ya ushirikiano Ofisi ya progamu Mto Uwakilishi wa heshima Jiji l Credits: CGIAR-CSI, GeoNames.org, Natural Earth Copyrights: © 2014 Natural Earth, Creative Commons Attribution 3.0 License FDFA, STS Geoservices Mipaka na majina yaliyonyeshwa pamoja na usanifu uliotumika katika ramani hii sio kwa idhini rasmi ya Serikali ya Uswisi. 28.05.2014 Shirika la Maendeleo na Ushirikiano la Uswisi Nchini Tanzania 2016 1

Upload: others

Post on 15-Feb-2021

3 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

  • Msaada wa Uswisi nchini Tanzania

    Serikali ya Uswisi imekuwa ikiendesha shughuli zake nchini Tanzania tangu mwaka 1960. Shughuli hizo ziliimarishwa zaidi mwaka 1981 kufuatia kufunguli-wa kwa ofisi ya ushirikiano jijini Dar es Salaam. Pro-gramu ya maendeleo ya Uswisi inaoana na mkakati wa Tanzania wa kupunguza umaskini, na huratibi-wa kwa ushirikiano na nchi nyingine na mashirika ya kimataifa. Mkakati wa Ushirikiano wa Uswisi wa mwaka 2015-2018 unashirikisha vyombo mbalimbali katika kutoa misaada ya maendeleo na miradi yake hulenga kanda ya kati (mikoa inayozunguka Dodo-ma). Majadiliano ya kisiasa na ya kitaalamu hufanyika kwa kushirikisha wadau wa ngazi ya ofisi kuu ya Seri-kali ya Tanzania na ofisi za Wilaya. Se kretarieti ya Tai-fa ya Masuala ya Uchumi SECO imekuwa ikiendesha shughuli zake nchini Tanzania tangu mwaka 1988 pamoja na kwamba Tanzania haikuwa tena nchi ya kipaumbele katika mwaka 2010, isipokuwa tu katika ugharamiaji wa miradi ya hapa na pale ya miundo mbinu ya maji na ya maendeleo ya kiuchumi.

    Afya: fursa sawa katika huduma bora za afya

    Serikali ya Uswisi inasaidia kuboresha upatikanaji wa fursa sawa za huduma bora za afya kwa jamii za pembezoni. Mkazo umewekwa katika kupambana na ugonjwa wa malaria na kugharamia huduma za afya. Maeneo mengine yanayozingatiwa ni mabadi-liko katika mfumo wa sekta ya afya na uendelezaji wa miradi ya utafiti inayolenga kuwapatia wafan-ya-maamuzi ya kisiasa taarifa kuhusu vipaumbele vya afya nchini. Katika jitihada zake za kupamba-na na ugonjwa wa malaria, Shirika la Maendeleo na Ushirikiano la Uswisi linaisaidia ofisi ya taifa ya uratibu wa utekelezaji wa programu ya Taifa ya vyandarua vya mbu nchini Tanzania, ambayo imes-ambaza vyandarua vyenye viuatilifu kwa watu zaidi ya milioni 28. Matokeo yake, kiwango cha vifo vya watoto wa umri wa chini ya miaka mitano kimeshu-ka kwa asilimia 48 katika kipindi cha kati ya mwaka 2000-2010, huku nafasi za ajira 6,000 zinazohusiana na uzuiaji wa ugonjwa wa malaria zikitengenezwa.

    Serikali ya Uswisi inasaidia katika shughuli za kupunguza umaskini katika eneo la mikoa ya kati ya Tanzania, inasaidia kuboresha upatikanaji wa huduma bora za afya na pia imedhamiria kuboresha hali ya ajira na ya kipato katika maeneo ya vijijini pamoja na kuimarisha asasi za kiraia na uhuru wa vyombo vya habari.

    Hali Ilivyo

    Mwaka 2014 Tanzania ilikuwa ya 159 kati ya nchi 187 katika orodha ya Kiwango cha Maendeleo ya Watu, hivyo nchi hii ni miongoni mwa nchi maskini sana duniani. Licha ya uchumi wake unaokua, umaskini umeendelea kukithiri nchini Tanzania ambapo watu milioni 12 walikuwa wanaishi katika hali ya umaskini wa kupindukia mwaka 2013. Hii ni sawa na asilimia 28 ya watu wote, hali ambayo haikuwahi kubadilika tangu mwaka 2001. Pamoja na hali ya umasikini wa kupindukia, Tanzania ni nchi yenye utulivu na amani kuliko nchi nyingine za kusini mwa Jangwa la Saha-ra. Hatua kubwa imepigwa katika kipindi cha mpi-to kutoka kwenye uchumi wa kupangwa kwenda kwenye uchumi wa soko huku mabadiliko ya kisiasa na kijamii yakiwa ya taratibu lakini ya uhakika.

    SHIRIKA LA MAENDELEO NA USHIRIKIANO LA USWISI NCHINI TANZANIA

    TAARIFA MUHIMU ZA NCHI 2016

    n Mji mkuu

    Uwakilishi wa Serikali ya Uswisi

    Ubalozi (Sehemu ya ushirikiano wa kimataifa)

    Ofisi ya ushirikiano

    Ofisi ya progamu

    Mto

    Uwakilishi wa heshima

    Jijil

    Credits: CGIAR-CSI, GeoNames.org, Natural EarthCopyrights: © 2014 Natural Earth,Creative Commons Attribution 3.0 License

    FDFA, STS Geoservices

    Mipaka na majina yaliyonyeshwa pamoja na usanifu uliotumika katika ramani hii sio kwa idhini rasmi ya Serikali ya Uswisi.

    28.05.2014

    Shirika la Maendeleo na Ushirikiano la Uswisi Nchini Tanzania 2016 1

  • wa kidemokrasia ili kusaidia mchakato wa uchaguzi nchini Tanzania.

    Masuala mtambuka: usawa wa kijinsia na VVU/UKIMWI

    Serikali ya Uswisi imedhamiria kuhimiza usawa wa kijinsia katika miradi yake yote. Pia, inapinga ubaguzi dhidi ya waathirika wa VVU/UKIMWI na inasaidia kati-ka uzuiaji na ulinzi dhidi ya maambukizi VVU/UKIMWI.

    Washirika

    › AZISE za Kiswisi: Swisscontact, HELVETAS Swiss Inter-cooperation

    › Utafiti: Taasisi ya Magonjwa ya Kitropiki na Afya ya Jamii, Taasisi ya Afya Ifakara

    › Sekta Binafsi ya Kimataifa: Novartis › Serikali: wizara, tawala za mikoa, na serikali za mitaa › AZISE za Kitanzania: kama vile Shirikisho la Asasi

    za Kiraia › AZISE za kimataifa: kama vile Shirika la Kimataifa

    la Kujitolea la Uingereza › Sekta binafsi Tanzania: Kampuni ya Maendeleo ya

    Ustawi Vijijini › Mashirika ya kimataifa: Shirika la Umoja wa

    Mataifa la Watoto UNICEF, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP

    › Wafadhili wa kimataifa: Mashirika ya kitaifa ya maendeleo ya Sweden, Denmark, na Ireland

    Bajeti ya 2015 kulingana na eneo husika na chanzo cha fedha (Faranga milioni za Kiswisi)

    SDC : Ushirikiano wa Maendeleo 24.0SECO: Ushirikiano wa Kiuchumi 0.9

    Jumla 24.9

    Utawala: ukuzaji wa utamaduni wa uwazi na uwezeshaji

    Serikali ya Uswisi imedhamiria pia kusaidia uhuru wa vyombo vya habari na asasi za kiraia pamoja na wawakilishi wa serikali za mitaa wenye elimu ya ku-tosha. Mwananchi aliyeelimika ana nafasi nzuri zai-di ya kutetea haki zake na kuiwajibisha serikali yake ili impatie huduma bora za kijamii. Kupitia Mkaka-ti mpya wa Ushirikiano, kuanzia mwaka 2015 na kuendelea Serikali ya Uswisi pia itatekeleza hatua za kuzuia migogoro.Ushirikiano baina ya Serikali ya Uswisi na Baraza la Habari Tanzania umesaidia kuboresha tasnia ya habari: uzingatiaji wa viwango vya maadili sasa ni wa asilimia 80 na wananchi wanaonyesha kiwango cha juu cha kujiamini kwa uwiano huo huo. Aidha, kuto-kana na ushawishi, uhuru wa vyombo vya habari na haki ya kupata habari iliingizwa katika mswada wa kwanza wa katiba mpya.

    Ajira na Kipato: ukuzaji wa masoko ya mazao ya kilimo kwa ajili ya watu maskini

    Serikali ya Uswisi inasaidia katika kukuza soko ende-levu la bidhaa za kilimo zinazowanufaisha wanawake na vijana. Kuboresha ujumuishaji wa wakulima wadogo wadogo katika soko la ndani si tu kunaon-geza kipato chao bali pia kunahakikisha upatikanaji wa bidhaa za kilimo kwa wote. Aidha, kutokana na msaada wa Uswisi, vyama vya wakulima vinaweza kutetea maslahi yao dhidi ya wanunuzi hivyo kuinua hali za maisha ya wakulima. Mradi mmojawapo wa Shirika la Maendeleo na Ushi-rikiano la Uswisi unalenga kukuza ushirikishaji wa ki-uchumi wa wakulima wadogo wadogo wa vijijini ili kuwawezesha kuondokana na umaskini. Wengi wa wakulima hawa wadogo wadogo – wanaojihusisha na uzalishaji wa alizeti, mpunga, pamba na ufugaji wa kuku – waliweza kujiongezea vipato vya kaya zao kwa 15%.

    Ushirikiano na mataifa mbalimbali

    Kwa sasa Serikali ya Uswisi inashirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Watoto UNICEF kuhamasi-sha shughuli zinazohusiana na maji salama na usafi shuleni. Pia, inashirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP katika mradi wa uwezeshaji

    Taarifa na takwimu (Chanzo: Viashiria vya Maendeleo ya Watu Duniani vya Benki ya Dunia 2013)

    Ukubwa wa eneo 945,087 km2

    Idadi ya watu milioni 46.218 Ongezeko la idadi ya watu kwa mwaka (toka 1990) 3%Kiwango cha juu cha kuishi wakati ya kuzaliwa wanawake / wanaume miaka 59.1 / 57.2Kiwango cha kutojua kusoma na kuandika wanawake / wanaume 32.5 / 21.0%Pato Gihaf la taifa kwa mtu mmoja mmoja Dola za Marekani 532.3

    Kilimo nchini Tanzania 2012: Tegemeo la Ajira na Kipato: SDC inasaidia ku-patikana kwa masoko na kuongezeka kwa kipato kwa wakulima wadogo wadogo maskini. (© Rea Bonzi)

    Huduma bora za afya: SDC inasaidia katika mradi wa uanzishaji wa bima ya afya vijijini. (© Rea Bonzi)

    Impressum

    Federal Department of Foreign Affairs FDFA Swiss Agency for Development and Cooperation SDC CH-3003 Berne, Switzerland www.sdc.admin.ch

    SDC inasaidia katika kujenga utama-duni wa uwajibikaji na uwezeshaji. (© SDC ofisi ya ushirikiano Dar es Salaam)

    Shirika la Maendeleo na Ushirikiano la Uswisi Nchini Tanzania 2016 2

    SDC/Ajira na Kipato 3.1

    SDC/Utawala4.6

    SDC/ Utamaduni1.2

    SDC/Afya15.1

    SECO 0.9