taarifa ya mdahalo wa wananchi juu ya ... · web viewalisisitiza kuwa maendeleo ya wananchi...

28
1. TAARIFA YA MDAHALO WA WANANCHI JUU YA USHIRIKIANO NA MAHUSIANO BAINA YA VIONGOZI WA KUCHAGUILIWA NA WANANCHI ULIOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA VETA, MARAMBA, WILAYA YA MKINGA, TAREHE MACHI 19, 2012. 1.0. UTANGULIZI: Katika kuendeleza sera yake ya elimu ya uraia kwa wananchi, Mtandao wa Asasi zisizo za Kiserikali Mkoani Tanga (TASCO) kwa mara nyingine umeandaa mfululizo wa midahalo juu ya ushirikiano na mahusiano baina ya viongozi wa kuchaguiliwa na wananchi. Mdahalo wa kwanza uliofanyika katika ukumbi wa VETA, Maramba, Wilaya ya Mkinga, Machi 19, 2012. Huu ni mfululizo wa pili wa midahalo ya wananchi katika mwaka huu baada ya mdahalo uliofanikiwa wa Katiba uliofanyika mapema mwaka huu. TASCO imepanga mada nne ambazo zitajadiliwa na wananchi katika midahalo iliyopangwa kufanyika katika mkoa, mwaka huu. 2.0. MADHUMUNI: Mraghbishi wa mdahalo huo, Martin Bernard Mng’ong’o kutoka Dar es Salaam alisema kuwa mdahalo huo ambao unazungumzia masuala ya mahusiano baina ya viongozi waliochaguliwa na wananchi. Alaieleza kuwa mjadala wa wnanachi unaweza kuwa mchango mkubwa katika Katiba. Shughuli za mdahalo zilianza rasmi saa 5.12 asubuhi na Adela Mtei, Mhazini wa TASCO na Mratibu Msaidizi alitoa maelezo juu ya historia ya kuanzishwa kwa mtandao. Alisema kuwa ni Muungano wa Asasi zisizo za kiserikali mkoani Tanga ambao ulianzishwa mwaka 2006 kwa kuunganisha nguvu. Alisema mitandao ya wilaya imenzishwa katika wilaya ya Lushoto na ipo katika mchakato ya kuanzishwa katika wilaya za Pangani, Handeni na Tanga wakati katika wilaya za Mkinga na Kilindi bado haijaanzishwa. Mraghbishi alitambulisha mada na kusema kuwa Mwezeshaji Mkuu, Ernest Mgongoro atawapitisha wana mdahalop katika maeneo tofauti na kuwaonyesha jinsi mahusiano baina ya viongozi waliochaguliwa na wananchi yalivyo kikatiba. Alisisitiza juu ya haja ya wanamdahalo kusahau itikadi zao na mihemko ya itikadi za vyama, dini na kadhalika. 3.0. Mwezeshaji, Mgongoro alieleza kwa kifupi juu ya mpangilio wa mhadhara wake ambao alisema utazingatia: Utangulizi maana ya maneno – serikali, mtaa, vitongoji, viongozi na hati za kisheria za kuanzishwa kwa serikali, utawala bora, uhusinano.ishirikishwaji wa wnanachi- historia yake Tanzania, majukumu/uwezo wa wananchi na majukumu/uwezo wa viongozi. 3.1. Mgongoro alieleza kuwa ushrirkishwaji upo katika Kaitba (1977) Ibara ya 8 ambapo iansema kuwa wananchi ndio wenye serikali ndio wanaochagua na

Upload: others

Post on 25-Jan-2020

38 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: TAARIFA YA MDAHALO WA WANANCHI JUU YA ... · Web viewAlisisitiza kuwa maendeleo ya wananchi yanategemea wananchi wenyewe na viongozi wao waliowachagua. Alimsifu Mbuinge wa Tanga kwa

1. TAARIFA YA MDAHALO WA WANANCHI JUU YA USHIRIKIANO NA MAHUSIANO BAINA YA VIONGOZI WA KUCHAGUILIWA NA WANANCHI ULIOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA VETA, MARAMBA, WILAYA YA MKINGA, TAREHE MACHI 19, 2012.

1.0. UTANGULIZI:Katika kuendeleza sera yake ya elimu ya uraia kwa wananchi, Mtandao wa Asasi zisizo za Kiserikali Mkoani Tanga (TASCO) kwa mara nyingine umeandaa mfululizo wa midahalo juu ya ushirikiano na mahusiano baina ya viongozi wa kuchaguiliwa na wananchi. Mdahalo wa kwanza uliofanyika katika ukumbi wa VETA, Maramba, Wilaya ya Mkinga, Machi 19, 2012.

Huu ni mfululizo wa pili wa midahalo ya wananchi katika mwaka huu baada ya mdahalo uliofanikiwa wa Katiba uliofanyika mapema mwaka huu. TASCO imepanga mada nne ambazo zitajadiliwa na wananchi katika midahalo iliyopangwa kufanyika katika mkoa, mwaka huu.

2.0. MADHUMUNI:Mraghbishi wa mdahalo huo, Martin Bernard Mng’ong’o kutoka Dar es Salaam alisema kuwa mdahalo huo ambao unazungumzia masuala ya mahusiano baina ya viongozi waliochaguliwa na wananchi. Alaieleza kuwa mjadala wa wnanachi unaweza kuwa mchango mkubwa katika Katiba.

Shughuli za mdahalo zilianza rasmi saa 5.12 asubuhi na Adela Mtei, Mhazini wa TASCO na Mratibu Msaidizi alitoa maelezo juu ya historia ya kuanzishwa kwa mtandao. Alisema kuwa ni Muungano wa Asasi zisizo za kiserikali mkoani Tanga ambao ulianzishwa mwaka 2006 kwa kuunganisha nguvu. Alisema mitandao ya wilaya imenzishwa katika wilaya ya Lushoto na ipo katika mchakato ya kuanzishwa katika wilaya za Pangani, Handeni na Tanga wakati katika wilaya za Mkinga na Kilindi bado haijaanzishwa.

Mraghbishi alitambulisha mada na kusema kuwa Mwezeshaji Mkuu, Ernest Mgongoro atawapitisha wana mdahalop katika maeneo tofauti na kuwaonyesha jinsi mahusiano baina ya viongozi waliochaguliwa na wananchi yalivyo kikatiba. Alisisitiza juu ya haja ya wanamdahalo kusahau itikadi zao na mihemko ya itikadi za vyama, dini na kadhalika.

3.0.Mwezeshaji, Mgongoro alieleza kwa kifupi juu ya mpangilio wa mhadhara wake ambao alisema utazingatia:

Utangulizi maana ya maneno – serikali, mtaa, vitongoji, viongozi na hati za kisheria

za kuanzishwa kwa serikali, utawala bora, uhusinano.ishirikishwaji wa wnanachi- historia yake Tanzania, majukumu/uwezo wa wananchi na majukumu/uwezo wa viongozi.

3.1. Mgongoro alieleza kuwa ushrirkishwaji upo katika Kaitba (1977) Ibara ya 8 ambapo iansema kuwa wananchi ndio wenye serikali ndio wanaochagua na kuwaweka madarakani viongozi. Alizungumzia juu yan kuwepo kwa serikali Kuu na serikali za mitaa. Alisema kuwa seerikali ya Kijiji/mtaa/kitongji ndiyo kitovu/mwanzo wa serikali. Viongozi wanaocvhaguliwa na wananchi, vijiji, vitongoji, wabunge, madiwani wenyeviti wa mitaa na vijiji.

Alitoa tafsiri ya maneno Serikali na kusema kuwa ni pamoja nserikali ya Jamhuri ya Muungano, Serikali ya Mapinduzi, serikali za mitaa. Kwa ufupi ni chombo chochote ambacho kinatekeleza madaraka.mamlaka ya serikali. Aliielzea maana ya serikali na inavyoonekena katika Katiba. Alisisitza kuwa Serikali ya Mitaa ndio ambayo wananchi wengi wanakuwa karibu nayo.

Page 2: TAARIFA YA MDAHALO WA WANANCHI JUU YA ... · Web viewAlisisitiza kuwa maendeleo ya wananchi yanategemea wananchi wenyewe na viongozi wao waliowachagua. Alimsifu Mbuinge wa Tanga kwa

Alitoa maelezo juu maneno yafuatayo:Kijiji – eneo lililoandikishwa lenye kaya zenye watu wasizopungua 250 ndani ya halmsahuri ya wilayaKitongoji – iko ndani ya kijiji au mtaaMtaa-ndani ya halmashaurei za mjiKiongozi – mtu aliyechguliwa, amejiriwa au kuteuliwa

3.2. Alisema kuwa hati za serikali za mitaa ziliingizwa katika katiba mwaka 1984. Mwezeshaji aliwaelimisha wanamdahalo juu ya mambo muhimu ya kuzingatia katika uchaguzi wa kidemokrasia ambayo ni maana ya demokrasia ikiwa yanazingatia mila na desturi, kufuata na kuheshimu mawazo ya walio wengi, nguvu ya hoja badala ya hoja ya nguvu. Alizungumzia juu ya haja ya kutofautisha maandamano na migomo.

Pia alifahamisha wanamdahalo juu ya uchaguzi na kusema watu wanafanya uichaguzi kuenzi na kudumisha uhuru wao, kuwapa fursa wananchi kutumia haki yao ya kuchaguliwa.

Alisema jukumu la viongozi katika uchaguzi ni kushaiwishi watu wapige kura. Pia alizungumzia utawala bora na kusema kuwa utumiaji wa madaraka ni pamoja na ushrikishwaji wa wananchi. Alinukuu maneno ya Mwalimu Nyerere ambae alisema kuwa Maendeleo Endelevu ya watu ni ya wenyewe na sio ya kutegemea wafadhili. Alisema kuwa viongozi wanapaswa kuwashirikisha wananchi kwa kuitisha mikutano ambapo wajibu wa wnanachi ni kushiriki katikia mikutano inayoitishwa na viongozi.

Wnanachi wanashirikije?Kijiji – kujua kazi za mkutano mkuu wa kijiji kitongoji. Mkutano unachagua Mwenyekiti na una uwezo wa kumuondoa katika madaraka.

4.0. YANAYOJITOKEZA: Viongozi wanawashirikisha wananchi kujua majukumu ya Mkutano Mkuu?

5.0. Alielezea juu ya Historia ya ushirikishwaji na kusema kuwa Mwalimu Nyerere aliwashirikisha wananchi kwa awamu tatu. Awamu ya kwanza (1961 – 66) kwa nia ya kuongeza ushirikshwaji kuboresha maisha ya watanzania kutumia kauli mbalimbali za maendeleo na kufuta utawala wa machifu.

Awamu ya pili 1967 -72 – wakati wa Azimio la Arusha –kupeleka madaraka kwa wananchi. Alivunja serikali za mitaa, akaanzisha serikali za vijiji vya Ujamaa na kuanzisha madaraka mikoani.

Mwaka 1984 alirejesha seriakli za mitaa na mwaka 1992 ikaingia sera ya vyama vingi vya siasa. Pia alizungumiza Rais Mwinyi kuruhusu Asasi zisizo za kiserikali. Mgongoro alisema pia kuwa utungaji wa sheria unaanzia chini kwenda juu na kueleza kuwa katika ngazi ya Halmashauri wataalamu wakishatunga wanapeleka katika baraza la madiwani. Pia sheria hiyo inatakiwa kutangazwa kati ubao wa matangazo. Alisema kuwa sheria ndiogo kabla haijapelekwa kwa waziri lazima wapate maoni ya wananchi.

5.1. YANAYOJITOKEZA: Je, inafanyika hivyo?

5.2. SERIKALI KUU: alieleza taratibu za kutunga sheria ndani ya Bunge na kusema kinachojitokeza ni je! wabunge wanafikisha mambo hayo kwa wananchi baada ya kusomwa kwa mswaada mara ya kwanza?

6.0. USHIRIKISHWAJI:

Page 3: TAARIFA YA MDAHALO WA WANANCHI JUU YA ... · Web viewAlisisitiza kuwa maendeleo ya wananchi yanategemea wananchi wenyewe na viongozi wao waliowachagua. Alimsifu Mbuinge wa Tanga kwa

Jukumu/uwezo wa viongozi – kuitisha vikao kwa mujibu wa sheria, kusimamia kwa ukamilifu ukusanyaji wa mapatoJukumu la Mwananchi – wananchi kufuata ibara ya 8 na 38 ya katiba ana uwezo wa kumwandikia barua kiongozi wake afike na kuonana nao, na wana mamlaka ya kumwondoa mwenyekiti wa kijiji, kumwonndoa mjumbe wa serikali ya kijiji ambaye ahajafika katika vikao vitatu, kutengua hseria ndogo, kutunga na kurekebisha sheria na jukumu la kuhudhuria mkutano.6.1. YANAYOJITOKEZA: Wananchi wasiohudhuria mikutano wachukuliwe hatua kwa asabau wanakoshesha maendeleo ya vijiji husika kwa kukosekana mawazo yao katika mikutano?

6.2. MAJUKUMU ya viongoziMBUNGE: Kiunganisho kati ya watu na serikali, kufikiria, kutunga na kupitisha sheria mpya, kusahihisha serikali ili itie juhudi kutimiza haja za wananchi wake. Wabunge wana wajibu wa kuwazungukia wananchi kuchukua shida na kuzipeleka Bungeni, kurejesha matokeo kutoka bungeni. Alisema mbunge anapaswa kuzingatia shida za waliomchagua, anapaswa kuhudhuria mikutano yote ya Bunge na kikao cha madiwani na anatakiwa kudumisha heshima ndani ya Bunge. Alisema kuwa kama wananchi hawahudhurii mikutano ya hadhara watamwambia nini mbunge wao?

7.0. YANAYOJITOKEZA: Kwa nini ukomo wa ubunge usiwe kwa maamuzi ya wananchi?

7.2. DIWANI: anatoa maoni na mapendekezo ya wananchi katika Baraza la Madiwani, anatumia angalau siku moja kwa mwezi kukutana na wananchi katika eneo lake, kutoa mrejesho, kuzingatia maslahi ya taifa, eneo, kanuni na katiba.

YANAYOJITOKEZA: Ukomo: kipi kinamwondoa diwani katika madaraka yake?

7.3. MWENYEKITI WA KIJIJI- ndiye kitovu cha demokrasia, ndiye mkuu wa serikali ya kijji, ambaye anatakiwa kuhudumia watu wote bila kujali itikadi zao za kisiasa, kuwasilisha maamuzi ya WDC kwa wanakijiji, kusimamia na kuwahamasisha wakazi wa kijiji katika shughuli za kujitegemea, kushuhgulikia migogoro midogo, midogo, kuwashirikisha wananchi katika ujenzi na shughuli ndogo, kuhamasisha watu kulipa kodi, ushuru kama itakavyotakiwa na serikali ya kijiji, kutunza regista ya wakazi wa kijiji.UKOMO: asipohudhuria mikutano mitatu anakoma kuwa Mweneyekiti au kama mkutnao mkuu ukimtia hatiani na tuhuma za kwenda kinyume na taratibu.

MWENYEKITI WA KITONGOJI- kutunza register, ulinzi na usalama, hifadhi ya mazingira, mtoto mwenye umri wa kwenda shule anakwenda shule kusuluhisha migogoro midogo midogo.7.4. YANAYOJITOKEZA: Ushirikishwaji wa wnanachi ulianza kabla ya wakoloni kuvamia Tanganyika

Kuna utata wa kutofahamu kazi za viongozi waliochaguliwa na walioteuliwa- mahusiano yao.

8.0. Mragbishi alitoa muhstasari wa mada ya mwezeshaji mkuu. Alisema kuwa inaonekana kama watu hawaelewi mahusiano yao na viongozi isipokuwa wakati wa uchaguzi. Alisema hiyo ni hatari.

9.0. MAJADILIANO May Lukindo –TAWG – alisema kuwa wananchi hawatendewi haki lakini pia

wananchi wenyewe hawajitokezi kutoa malalamiko yao katika mikutano ya hadhara

Mikidadi Hasaan – mahusiano katika ya viongozi na wananchi sio mazuri

Page 4: TAARIFA YA MDAHALO WA WANANCHI JUU YA ... · Web viewAlisisitiza kuwa maendeleo ya wananchi yanategemea wananchi wenyewe na viongozi wao waliowachagua. Alimsifu Mbuinge wa Tanga kwa

Hadija Juma – wanachi hawahudhurii mikutano na akauliza kiongozi afanyeje katika hali hiyo?

Wilfred Magembe – viongozi katika ngazi ya kijiji hawajui majukumu yao kwa sababu hawakupata semina elekezi

Peter Samakala – alisema kuwa maendeleo yanaletwa na wananchi wenyewe. Viongozi wanapiga mbiu ya mikutano lakini watu hawafiki. Alitoa rai kutumika kwa sheria ndogo ili wasiohudhuria wapigwe faini.

Paulina Saidi- pia alizungumzia tatizo la uhudhuriaji hafifu wa vikao/mikutano ya kijiji. Alisama viongozi wawe wabunifu kwa kutoa posho!

James Godfrey – alisema kuwa viongozi wa kuchaguliwa wanapoomba nafasi wana tofauti lakini mara baada ya kupata wanabadilika. Alizungumzia kuhusu uvivu wa kuwajibika na kufuatilia, suala la uadilifu wa viongozi na elimu duni ya wapiga kura. Aliitaka serikali kufanya mpango wa kuwapiga msasa viongozi mara kwa mara viongozi.

Mbashiri Seif Ali – alizungumzia juu ya viongozi kukosa ubunifu na upeo na wananchi kutojua wajibu wao. Alitaka kujua kama kuna mkutano mkuu katika ngazi ya kitongoji.

Peter Robert Shemandia –alizungumzia juu ya suala la Diwani kuitisha mikutano na viongozi kutokuwa wabunifu

Mchungaji Daud (Tanzania Assembelies of God) – alisema kuna haja ya kijiji kuwa na mpango kazi na kuwa na kalenda ya vikao na nakala zake kutolewa kwa wanakijiji au kuwekwa katika sehemu muhimu

Mwalimu Maglory Kiwala – alisema elimu hii inahitajika sana Hassan Omari – alisema suala la ukosefu wa nidhamu ya mikutano limeanza

kushika kasi baada ya kuingia kwa vyama vingi vya siasa. Pia alitaka wote wanaotaka kugombea wafanye mdahalo kwanza ili wananchi waweze kuchagua anayefaa kazi yao.

Mama Elizabeth Mzoo – yeye alizungumzia suala ambalo lilionekana kutoka nje ya mada kidogo na kuuliza waathirika wa mafuriko watalipwa lini fidia ili waweze kujenga nyumba zao. Hata hivyo suala hilo linaonyesha viongozi wasivyokuwa karibu na kutoa majibu ya uihakika kutoka serikalini.

Waziri Shaaban – alizungumzia tatizo la ubinafsi wa viongozi na kushindwa kwao kuwaletea taarifa kutoka ngazi za juu. Alizungumiza haja ya viongozi wa kuchaguliwa kuwa karibu na wananchi

Bakari Ngwelo - alizungumizia juu ya haja ya kuweka ukomo kwa ubunge na udiwani\

Yusuf Bin Robert- alizungumzia juu ya haja ya kuimarisha Baraza la kata Shaaban Hussein Bakari – haja ya kiongozi wa kuchaguliwa kupewa elimu ya

majukumu yao John Peter Mdoe- alitaka midahalo kama hii iendelee zaidi na haja ya

kuimarisha mikutano ya vijiji. Alisema kuwa viongozi hawana ubunfu Halima Hamis – alizungumzia juu ya watu kutohudhuria mikutano inayoitishwa

na viongozi wao Zuberi Said Msagati – alisema kuwa hakuna kiungo kati ya viongozi na

wananchi, na kuwa hakuna mrejesho kwa wananchi na kumtaka mbunge kupita kwa wananchi kukusanya maoni

Said Zuberi – alizungumzia juu ya haja ya kijiji kuwa na mpango mahususi wa kazi kuongoza shughuli zake badala ya kufanya kazi kiholela na kwa kubahatisha.

Mbwana Wambua- alizungumzia haja ya viongozi kufahamu katiba.

10.0. YALIYOJITOKEZA KWA UJUMLA: Suala la watu kutohudhuria mikutano mikuu ya kijiji na mtaa –kuna wazo kuwa wasiohudhuria wapigwe fainiUmuhimu wa Mbunge kutembelea wananchi na kuchukua shida zao

Page 5: TAARIFA YA MDAHALO WA WANANCHI JUU YA ... · Web viewAlisisitiza kuwa maendeleo ya wananchi yanategemea wananchi wenyewe na viongozi wao waliowachagua. Alimsifu Mbuinge wa Tanga kwa

Mbunge kutoa mrejesho wa masuala yaliyojadioliwa kaika bunge na majibu ya shida zao kwa wananchiDiwani kutembelea wananchi kutoa mrejesho kwa wananchi juu ya majibu ya shida zao na masuala muhimu yaliyojadiliwa katika baraza la madiwaniUmuhimu wa kungalia tena ukomo wa viongozi waliochaguliwa na wananchi kupewa nafasi kuamua hatma yaoUmuhimu wa kuandaa semina elekezi kwa viongozi wa ngazi ya kijiji wanapochaguliwa ili wafanye kazi zao kwa ufanisi zaidiSerikali ifanye mpango wa kuwpiga msasa mara kwa mara viongozi waliochaguliwa na wakuteuliwa ili watimize wajibu wao kwa ufanisui zaidi.Vijiji/vitongoji viwe na mipango kazi ya kuongoza shughuli zao na kuwa na kalenda ya vikaoSuala la viongozi wa kuteuliwa kuwayumbisha viongozi wakuchgauliwa

11.0. KUFUNGA MDAHALODiwani Saidi Mjasambu alisema kuwa tatizo linalosibu jamii ya eneo hilo ni makundi ya uchaguzi kuendelea kuwepo kitu ambacho alisema kinafanya suala la kuhudhuria mikutano kuwa tatizo. Pia alizungumzia juu ya umuhimu wa viongozi waliochaguliwa kupata maelekezo ya namna watakavvofanya kazi zao mara baada ya uchaguzi. Aliwataka wananchi na viongozi wote kuhudhuria midahalo na mikutano kama hii ili kufaidika na elimu kutoka kwa wataalamu.

MWISHO

2. TAARIFA YA MDAHALO WA WANANCHI JIMBO LA HANDENI ULIOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO WA HOTELI YA BWAWANI TAREHE 31 MACHI, 2012.

1.0. UTANGULIZIMratibu wa Asasi isiyo ya Kiserikali mkoani Tanga (TASCO), Bw. David Chanyeghea alieza madhumuni ya Mdhalo na kusema kuwa ni mfululizo wa midahalo ambayo TASCO inakusudiwa kuwapelekea wananchi katika majimbo yote yaliyo mkoa wa Tanga kama sehemu ya sera yakeya kutoa kuongeza ufahamu wa wananchi kuhusu masuala mbali mbali ya kitaifa.

Alisema kuwa kuwa ipohaja ya wananchi pamoja nakujua wajibu wa viongozi wa kuchaguliwa pia na wao wajue wajibu wao ili waasifike mahali wakaona kuwa wajibu wa kuleta maendeleo ni wa viongozi wa kuchaguliwa. Nia ni kuwafanya wao wao wasiwe watu wa kulalamika ila waelewa watarimizaje wajibu wao.

Naye Mbunge wa Jimbo la Handeni Dr. Abdallah Kigoda alisisitiza kuwa maendeleo hayaletwi na mbunge pekee bali yanaletwa kwa ushirikiano kati ya viongozi na wananchi.

Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Kapteni Mstaafu Seif Mpembenwe alisema kuwa mada ambayo imeletwa katika mdahalo inayozungumzia mahusiano katika ya wananchina viongozi wao ni muhimu sana katik mustakabal wa taifa. Alitoa maana ya maneno mablimbali ikiwemo Mahusiano, maendeleo, Pmoja na viongozi. Alieleza kuwa mahusiano uanahusu pandembili za tukio na kile kinachounganisha pande hizo mbili. Kuhusu maendeleo alisema kuwa ni matokeo ya kazi ya pamoja na kusisitiza kuwa hakujna anayepanga maendeleo peke yake.

Aliendelea kueleza kuwa neneo pamoja linahusu ishirikiano baina ya wananchi na viongozi wao wakati ambapo viongozi ni watu waliochaguliwa au kueiliwa kuongoza wananchi. Alisema kuwa yote haya ukiyaweka pamoja unapata maendeleo.

Page 6: TAARIFA YA MDAHALO WA WANANCHI JUU YA ... · Web viewAlisisitiza kuwa maendeleo ya wananchi yanategemea wananchi wenyewe na viongozi wao waliowachagua. Alimsifu Mbuinge wa Tanga kwa

2.0. UFUNGUZI RASMI

Mdahalo ulifunguliwa rasmi na Mwenyekiti Mstaafu wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, Mzee Jabir Kigoda ambayre alitoa shukurani kwa TASCO kuwaletea wananchi wa wilaya hiyomdahalo unaohusu maendeleo yao. Alisemamidahalo hiyo inasaidia sana katika kusisimua maendeleo na kuwekana sawa ili kuleta maendeleo. Mzee Kigoda alisisitiza juu ya umuhimu wa ushiriikiano katika maendeleo na kusema kuwa kidole kimoja hakivunji chawa akiwa na maana kuwa mtu mmoja hawezi kuleta maendeleo. Aliwataka wana Handeni kuchanganya fikra zao ili kuleta maendeleo wakikumbuka kuwa wametoka mbali lakini safari bado ni ndefu.

Alieleza kuwa utaratibu wa sasa wa serikali ni wa DEVELOPMENT BY DEVOLUTION (D and D) ambao ni utaratibu wa kuleta maendeleo bila kusukumana na maendeleo hayo yakianzia chini. Alisema utaratibu huo hauhitaji kusukumana bali unahitaji uelewa wa wananchi ili watunga sera na wajue wananchi wanataka nini.

3.0. Mraghbishi wa mdahalo huo, Martin Mng’ongo alielezea utaratibu wa mdahalo kuwaeleza washiriki kuwa Mtoa Mada atachambua mada na kueleza kwa kina mamlaka ya utawala yanatoka. Aliwataka washiriki wachangie kama wana Handeni na si kwa itikadi zao vyama au vinginevyo.

4.0. Mtoa mada mkuu, Ernest Mgongoro alieleza kuwa katika utangilizi wake kuwa atatoa maana ya maneno kadhaa kama vile viongozi, utawala bora, ushirikishwaji, jukumu na uwezo wananchi na viongoji mmoja mmoja na wajibu wao. Katika utangulizi wake alisemakuwa mahusiano yamo katika ibara ya 8 ya Katiba na ibara hiyo hiyo inaelzea serikali inapata vipi madaraka yake. Pia alielezea juu ya aina ya serikali na ikiwa ni pamojana serikali za mitaa ambazo aliziita kuwa kitovu cha serikali na demokrasia kwa sababu ndio serikali iliyo karibu zaidi na wananchi. Serikali inaelezewa katika ibara ya 6 ya Katiba na ainaya serikali ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar au kuwa ni mtu au watu wanaotekeleza madaraka kwa niaba ya waananchi. Alisema serikali nyingine zinazotajwa ni serikali za Mitaa ambazo ni pamoja na Halmashauri za Wilaya, miji na majiji.

Alielezea maana ya Kijiji na kusema ni kile ambacho kimeandikishwa kikiwa na kaya zisizopungua 250. alielezea pia pia juu ya Hati za Sheria ambazo zinatoa mamlaka kwa serikali hio kuwa ni Katiba na Sheria ya Serikali za Mitaa namba 7 hadi 10 ya Mwaka 1982.

Alitoa maelezo juu ya mambo muhimu ya uchaguzi wa kiedmokrasia na utaratibu wa kupata viongozi kwa njia ya uchaguzi. Alimnukuu Mwanaharakati Abraham Lincoln ambaye alisemakuwa utawala wa kidemokrasia ni wa serikali ya watu kwa ajili ya watu akitoa dhana ya Uhuru na Usawa ambapo Mwalimu Nyerere ambaye alielezea serikali ya kidemokrasia kuwa ni utawala wa watu wenyewe wa kiraia. Alisema kuwa nchi zinafanya uchaguzi ili raia watimize haki yao ya kuchagua na kuchaguliwa au kuwapa watu fursa ya kuchagua viongoxi wao. Wajibu wa kupiga kura umo katika ibara ya 5 ya Katiba.

Majukumu yaviongozi ni pamojana kushawishi wenye sifa ya kupiga kurawajiandikishe na kuwasisitiza wananchi kupiga kura.

Utawala Bora: aliueleza kuwa ni utaratibu wa kutumia madaraka kusimamia raslimali za nchi na kwamba lazima uambatane na ushurukishwaji. Alisema kuwa wananchi wanapotakiwa kushiriki lazima wafanye hivo. Utawala bora ni pamoja

Page 7: TAARIFA YA MDAHALO WA WANANCHI JUU YA ... · Web viewAlisisitiza kuwa maendeleo ya wananchi yanategemea wananchi wenyewe na viongozi wao waliowachagua. Alimsifu Mbuinge wa Tanga kwa

na wananchi kuhudhuria mikutano kwa sababu maendeleo ya watu yanaletwa na waru wenyewe na viongozi lazima wawashirikishe wananchi kupitia mikutano.

Alielezea juu ya tatizo sugu la wananchi kutokuhudhuria mikutano na kwamba kila mwananchi ana wajibu wa kushiriki katika shughuli za maendeleo. Alitaja mikutano hiyo kuwa ni ile ya Kijiji, kitongoji na mitaa.

Mgongoro alielezea juu ya historia ya ushurikishwaji na kusema kuwa kabla ya uhuru maamuzi yalikuwa ni kutoka juu. Alisema kuwa Mwalimu alibadilisha mfumo kwa Awamu Tatu ambazo ni:

i. 1961 – 1966 –kauli mbiu za uhuru na umoja, uhuru na kazi na kutngaza maadui wakuu watatu ambao ni maradhi, ujinga na umaskini ambayo yanapaswa kuoigana nayo kuanzia chini kwenda juu. Kauli mbiu kubwa ilikuwa -INAWEZEKANA, TIMIZA WAJIBU WAKO.

ii. 1967 – 1992 – huu ni wakati wa Azimio la Arusha na falsafa ya Ujamaa na Kujitegemea, Kilimo cha kufa na kupona na vijiji vya ujamaa

iii. Serikali za mitaa – zilianzishwa mwaka 1940 na kuondolewa na kuanzishwa kwa madaraka mikoani. Mwaka 1982 zilirejeshwa na kuwekwa kwenye katiba. Ni wakati pia wa mipango mbalimbali ya kuboresha uchumina ustawi wa wananchi kama vile MKUKUTA na kadhalika.

iv. 1992 – 2005 – hiki ni kipindi cha uboreshaji wa utawala wa wananchi.

UTUNGAJI WA SHERIA: Ngazi ya kijiji ni sheria ndogo na wananchi wanatakiwa na wana wajibu wa kuhudhuria Mikutano ya kijiji ili waweze kushiriki katika kutunga sheria.YANAYOJITOKEZA: WANANCHI WANASHIRIKISHWA KWA KUHUDHURIA AU WANAHUDHURIA MIKUTANO HIYO?

Wananchi pia wanashirikishwa katika kutunga sheria kupitia kwa wabunge. Yanayojitokeza ni kuwa Je, hii inatosha? Wananchi wanapewa uhuru wa kutoa maoni kupitia Ibara ya 18 ya Katiba. Wananchi wana wajibu wa kuhoji kama yaliyokubaliwa yanatekelezwa. Pia Mgongoro alisema kuwa wananchi wanayo haki kumwandikia kiongozi wao barua ya kumtaka afike kama hawajamwona. Wana mamalka ya kumwondoa kwenye madaraka Mwenyekiti wa Kijiji au Kitongoji kama hajatatimiza wajibu na kumwondoa Mjumbe wa serikali ya Kijiji kupitia mkutano Mkuu.

MBUNGE: alimtaja kuwa kiungo kati ya wanachi na serikali, ana kazi yakuchukua maoni katika mikutano ua hadhara. Alisema kuwa yampasa mbunge kujali sana eneo lake na kuheshimu maoni ya watu wake. Wana wajibu wa kuisaidia serikali itawale vyema kwa kusahihisha na kukosoa serikali na kudumisha amani.Anatakiwa atoe mrejesho kwa wananchi wa jimbo lake juu majibu ya shida zao. UKOMO: MBUNGE anachaguliwa na wananchi walio wanachama wa chama chakena wasio wanachama hivyo kwa nini chama kiamue ukomo wake?DIWANI: anatakiwa kuteua siku mpja kila mwezi kutembelea wananchi wake, atoe mrejesho kamambunge, awe mbunifu na ni mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Kata.MWENYEKITI WA KIJIJI: Msemaji mkuu wa kijiji na pamoja na mambo mengine kuhakikisha kuwa wanafubzi wanaotakiwa kwenda shule wanafanya hivyo. UKOMO wake ni pamoja na kutokuhudhuria mikutano mitatu mfululizo bilataarifa na kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye na theluthi mbili ya mkutano wa kijiji.

Alimalizia kwa kusema kuwa kama watanzania wanataka kufanikiwa lazima wawe na uhuru na utii kwa viongozi. Alisema maendeleo ya kweli hayawezi kupatikana bila watu kushirikishwa,

Page 8: TAARIFA YA MDAHALO WA WANANCHI JUU YA ... · Web viewAlisisitiza kuwa maendeleo ya wananchi yanategemea wananchi wenyewe na viongozi wao waliowachagua. Alimsifu Mbuinge wa Tanga kwa

5.0. MAJADILIANO:Mraghbishi alitoa nafasi kwa Mkuu Polisi wa Wilaya kutoa salamu zake kabla ya kutoa nafasi kwa wananchi kutoa maoni yao. Mkuu huyo wa Polisi alisema kuwa dhana ya ushirikishwaji inajionyesha pia katika Polisi Jamii ambayo alisema kuwa ndiyo msingi wa ulinzi na kutokomeza uhalifu katika jamii. Alisisitiza juu ya utii wa sheria bila shuruti na akasemakwa kufanya hivyo Tanzania itafika inakokwenda.5.1. MAONI:

MOHAMED SELEMANI: aliwataka viongozi kupanga ratiba kuelezea mabadiliko ya halmashauri ya wilaya na kuwa mbili na manufaa yake. Pia alizungumzia jaha ya viongozi kupewa heshima wanazostahili.FRANSICA MATAI: alizungumziaushiriki wa wananchi katika maendeleo na kusema kuwa wanangoja kushirikishwa. Alisema kuwa wananchi wanatakiwa kuamshwa na viongozi. Alizungumziajuu ya kazi kubwa ya kutoa elimu na kusema asasi zisizo za kiserikali zina wajibu mkubwa kuelimisha wananchi na serikali inatakiwa kuuunga mkono kazi hiyo.NICHOLAS KUSAKA: alieleza tatizo la viongozi kuanzia ngazi za vijiji kutoa ahadi halafu wanashindwas kuzitekeleza. Alisema kuwa wananchi hawapati mrejesho wa mapato na matumizi na kuwataka viongozi wasijirundikie nafasi za uongozi.ELISAMIA NNKO: alisema moja ya matatizo makubwa ni ukosefu wa wa elimu ya katiba miongoni mwa watanzania wengi. Pia alizungumzia Udhaifu wa mahudhurio ya mikutano mbalimbali jambo ambalo alisema ni sugu na kuwataka viongozi wawashawishi wananchi kushiriki mikutano. Pia alizungumzia juu ya tatizo la wapambe kuleta malumbano ya kudhaliloshana wakati wa uchaguzi badala ya kuzungumzia matatizo ya wananchi.DIGNA PETER: pia alilalamikia mahudhurio ya mikutano mbalimbali na kasema kinamama ndio ambao wanaongoza kwa kutokuhudhuria. Alisema kuwa hakuna sababu ya maana ya kutoluhudhuria. Alisisitiza kuwa mikutano ndiyo sehemu ya kutoa maoni na akasema taizo kubwa la mimba za watoto wa shule litasemewa wapi kama kina mama hawahudhurii mikutano? RAJAB MSONGE: Alisema kuwa wananchu hawahudhurii mikutano kwa sababu wamekata tamaa. Tatizo laviongozi kutotimiza wajibu wao linawafanya wananchi kususa mikutanoPROSPER JOHN MAMBOSHA: Alisema kuwa uadilifu wa viongozi hauendi sambamba na hali halisi na pia alizungumziajuu ya uadilifu wa raia. Alizungumzia ufinyu wa elimuya raia.HASSAN: alisema kuwa ukosefu wa elimu unaondoa mahusiano mazuri. Pia alizungumzia juu ya mahusianomabaya kati ya viongozi wa kuchaguliwa na wale wakuteuliwa (watendaji). STEVEN ABDULLAH MGUNDO: alizungumziaviongozi kuwa mbali na wananchiYASIN SAID YUSUF KAZILWA: alizungumzia tatizo la utendaji na viongozi waliochaguliwa kukosa elimu ya majukumu yaoHUSSEIN OMAR SAID: alisema mahusiano ya viongozi na wananchi ni hafifu na kukosekana kwa mrejesho toka bungeni. Alitaka mdahalo uendelezwa kwa watu wengi.FLORIAN KAYAYA: alizungumzia viongozi kutoyambua wajinu wao na mipaka yao ammabo mabyo yanasababisha utendaji mbovu. Alisema pia kuwa wananchi hawafahamu haki zaoSADIKI RAMADHANI: alizungumzia juu ya tatizo la viongozi kugonganaRAMADHANI HAJI GUMBO:alitaka wabunge wasiteuliwe kuwa mawaziri ili watumikie wananchi wamajimbo yaoGRACE MWIKALO: wananchi wawe na mwamko wa kuhudhuria mikutanoALI MOHAMED MFUKO: alizungumzia tatizo la vijana kukosa mwamko wa kuhudhuria mikutano

Page 9: TAARIFA YA MDAHALO WA WANANCHI JUU YA ... · Web viewAlisisitiza kuwa maendeleo ya wananchi yanategemea wananchi wenyewe na viongozi wao waliowachagua. Alimsifu Mbuinge wa Tanga kwa

NASSORO MBOJELA: Mahusiano si mazuri kutokana na kukosekana mrejesho, rushwa na ukosegu wa elimu na viongozi kutojua wajibu wao.KITRA KARIM: alizungumia juu tatizo la elimu ndogo ya wananchi na viongozi na kuwataka viongozi wawe karibu na wananchi.KHA;ID RAMADHANI: alisema mahusiano baina ya viongozi na wnanachi ni na madogo na kuwataka viongozi wa kuchaguliwa wawe karibu mna wananchi.SHAABAN MUSA (mwanafunzi Kidato cha nne) Handeni Secondary School: aliuliza kuwa kati ya mwananchi na kiongozi nani anapaswa kutoa ushawishi wa maendeleoMAGID MRISHA: yeye aliuliza ni mara ngapi wananchi wamemwita kiongozi aliyekosea vikao cha kikatiba au ambaye hawamwoni katika vikao. Alisema wananchi wasillalamike tu nao wanapaswa kujua wajibu wao.

6.0. MAMBO MAKUU YALIYOJITOKEZA: MAHUSIANO MADOGO KATI YA VIONGOZI NA WANANCHI UKOSEFU WA ELIMU YA KIRAIA MIONGONI MWA WANANCHI NA

VIONGOZI NA HAJA YA SERIKALI KUUNGA MKONO ASASI ZA KIRAIA KUTOA ELIMU YA KIRAIA KAMA KAZI YA KUDUMU

VIONGOZI WA KUCHAGULIWA NGAZI YA VITONGOJI, MITAA. VIJIJI (WENYEVITI) NA KATA (MADIWANI) KUTOELEWA WAJIBU WAO –HAJA YA VIONGOZI HAO KUPEWA MAFUNZO JUU YA MAJUKUMU YAO MARA BAADA YA KUCHAGULIWA

WANANCHI KUTOELEWA WAJIBU WAO WA KIAKTIBA KUHUDHURIA MIKUTANO

TATIZO LA USHABIKI WA VYAMA KUKWAMISHA KAZI ZA MAENDELEO NA MIKUTANO

KUKOSEKANA KWA MREJESHO KUTOKA BUNGENI NA BARAZA LA MADIWANI KWENDA KWA WANANCHI

6.0. Mragbishi alimpa nafasi Mtoa mada kujibu baadhi ya hoja na Mgongoro alikubalina na wanamdahalo kuwa kuna tatizo la elimu ya uraia hasa kuanzia ngazi ya serikali ya kitongoji hadi mtaa au kijiji. Alisisitiza kuwa kila mtu ana wajibu na haki ya kuhudhuria mkutano wa kitongoji, mtaa au kijiji. Alikubaliana na baadhi ya watoa maoni kuwa asilimia kubwa ya vijana hawahudhurii mikutano niyo.

7.0. Diwani wa kata ya Vibaoni Eng. Mkusa Juma Kondo alipewa nafasi ya kuzungumza na kusema kuwa mdahalo huo umeonyesha dhahiri kuwa vikao vinavyopasa kisheria havifanyika na ndio maana watu walikuwa wanavka mada na kuanza kuzungumzia kero mabzo katika mdahalo huo sio mahali pake. Aliwataka wakazi wa Handeni kuhudhuria vikao na kueleza kuwa watu waliopiga hatua katika maendeleo walianzia katika vikao. Aliwatka wananchi kubadilika,

8.0. Naye Mwenyekiti wa Mkutano, Mzee Jabir Kigoda alieleza masikitiko yake kuwa wananchi wanadharau mahudhurio ya mikutano katika ngazi za utawala za msingi na kusisitiza kuwa nyumba isiyokuwa na msingi haiwezi kuelea hewani.

9.0. Mkuu wa Wilaya, Kapteni Mstaafu Seif Mpembenwe aliwataka wananchi wa Handeni kuwa katika njia moja na kuitikia wimbo mmoja. Alisema kuwa maengi ambayo wananchi wanakumbana nayo yanatokana na kutokuelewa, alisisitiza suala la nidhamu na kusema kuwa taifa lililostaarabika linapimwa kwa jinsi walivyo na nidhamu. Aliwataka watanzania kuheshimu viongozi wao.

10.0. Naye Mratibu wa TASCO alisema kuwa ni rahisi kulaumu halafu wewe unayelaumu hutimizi wajibu wako. Alisema kuwa maeneo mengi ambayo hayapigi hatua ni yale ambayo watu wanategemea watu wengine kuwafanyia kila kitu. Aliwataka wananchi kuweka mipango yao sawa halafu wamwite mbunge wao awasaidie.

11.0. Akifunga mdahalo huo, Mbunge wa Jimbo la Handeni, Dr. Abdallah Kigoda alipongeza TASCO kwa kuandaa mdahalo huo juu ya mahusiano kati ya viongozi

Page 10: TAARIFA YA MDAHALO WA WANANCHI JUU YA ... · Web viewAlisisitiza kuwa maendeleo ya wananchi yanategemea wananchi wenyewe na viongozi wao waliowachagua. Alimsifu Mbuinge wa Tanga kwa

wa kuchaguliwa na wananchi. Alieleza kuwa mahusiano huwa yanaanzia katika uchaguzi na inategemea nia ya mtu anayegombea. Alisema kuwa dhamira ya kugombea ikifanywa ya kibinafsi kamwe hakuwezi kuwa na mafanikio na mahusiano mabaya yanaanzia hapo. Alisisitiza kuwa kazi ya maendeleo haifanywi na mtu mmoja hivyo akawataka wananchi kuhudhuria vikao na kuchangia mawazo yao.

Dr. Kigoda alisema kuwa wananchi wengi hawajui haki na wajibu wao na katika vijiji wanashuhudia ardhi yao ikichukuliwa na wajanja wachache kwa sababu hawaendi katika mikutano ya kijiji ambayo ianidhinishwa maamuzi mazito hivyo kuwaachia viongozi wachachewakila rushwa na kuandika muhstasari wa uongo kuidhinisha mauzo yasiyo halali ya ardhi.

Alisema ni makosa kwa wananchi kuwafanya viongozi wao wa kuchaguliwa ndio kila kitu na akasema kuwa kama vikao vingefayika matatizo mengi yangepata ufunmbuzi vijijini.

11.0. Mdahalo ulifungwa saa 8.57 mchana.

MDAHALO WA WANANCHI, JIMBO LA KILINDI ULIOFANYIKA KATIKA KIJIJI CHA KWEDIBOMA, TAREHE APRIL 2, 2012.

1.0. Mragbishi wa mdahalo huo, Martin Mng’ong’o aliwakakribisha washiriki na kueleza madhumuni ya mdhalo huo pamoja na kusoma ratiba. Alimkaribisha Mratibu wa Mtandao wa Asasi zisizokuwa za Kiserikali Mkoani Tanga (TASCO), Bw. David Chanyeghea kutoa malezo mafupi juu ya mradi huo. Mragbidhi alisisitiza juu ya umuhimu wa wa washiriki kuzunguimza kama wana Kilindi bila kuangali itikadi zao za vyama au dini zao.

2.0. Bw. Chanyeghea alitoa maelezo juu ya TASCO na kusema kuwa wilaya ya Kilindi bado hakujaundwa mtandao wa Wialya kwa sababu hakuna asasi nyingi zibnazoweza kuubnda mtandao huo. Alisema mdahalo huo una madhumni ya kuwapa furesa wananchi kujadiliana na viongozi. Alisisitiza kuwa ni muhimu wananchi wakaelewa kuwa maendeleo hayaezi kueltwa na viongozi pekee. Alisema kuwaachia viongozi pekee sio sawa lakini wananchi wanatakiwea kuwapa fursa waaongioze. Alisema kidole kimoja hakivunji chawa. Alitoa taarifa kuwa kuna mpango wa kuiunda timu za ufuatiliaji wa masuala mbalimbali ya maendeleo katika kila jimbo.

3.0. naye mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya, Amiri Sungura, ambaye ni Afisa Tarafa alishukuru TASCO kwa kuandaa midahalo hiyo bna kusema kuwa ni muhimu watu kujadili maendeleo yao na ikifkia siku moja wakanyage kama askari kuelekea mbele. Alisisitza kuwa maendeleo hayaji kama mvua na ni vizuri wadau wa maendeleo kukusabyika na kujadiliana kwa ajili ya maendeleo.

Page 11: TAARIFA YA MDAHALO WA WANANCHI JUU YA ... · Web viewAlisisitiza kuwa maendeleo ya wananchi yanategemea wananchi wenyewe na viongozi wao waliowachagua. Alimsifu Mbuinge wa Tanga kwa

4.0. naye Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi, Diwani Idirsa Mgaza mabaye ni Mwenyekiti wa Kmati ya Huduma za Jamii alisema kuwa imekuwa ni kawaida wananchi kufukiria kuwa mtu wanayempa nafasi kwa niia kura lazima atwaletea kitu fuiani. Aliswema ile dhana inajengekea ya kuleta kitu inasababisha wanchaguliwa hao kuingia katika tama ya uifisadi ili aweze kuhudumia jamii yajke jambao ambalio linaporomosha taifa. Alisemkazi ya kiongozi si kuleta bali ni kuongoza ili wananchi walete mamebnedkleo yao wenyewe.

5.0. Baada ya hapo Mragbidhi alimkaribisha Mtoa Mada Mkuu, Jonathan Mgongoro ambnaye ni mtaalamu wa Katiba kutoa mada yake.5.1. Kama kawaida alieleza mpangilio wa mada yake na kasema kuwa

wananchi wanapewa mamlaka ya kuiweka serikali madarakni na Katiba katika ibara ya 8. pia aleieza kuu ya aina serikali na kusema kuwa srikali za mitaa ndiyo kitovu cha demokrasia shirikishi. Alielez mamana ya mameneo mbalimbali na maana ya demokrasia akisema kuwa demokrasia ni uratatibu wa kupata viongozi kwa njia ya uchaguzi. Alisema mkuwa msingi wa demokrasia ni uhuru na haki na uhuru na usawa. Pia alieleza juu yasababu ya kufanya uchaguzi na kusema kuwa ni kuwaopta viongozi kwa ruidhaa ya wananchi wenyewe. Alisema kuwa chini ya katiba kila Mwananchi mwenye umri wa kupiga kura ana wajibu wa kujiandikisha na kisha kupiga kura.

5.2. Alizungumzia juu wa wajibu wa viongozi katika uchaguzi kuwa ni kuwahimiza watu kujiandikisha na kupiga kura.

5.3. Alizungunmzia juu ya ushirikshwaji na kutoa historia ya ushirkshwaji Tanzania. Alsisitiza kuwa maendeleo hayaletwi na wafadhili bali wananchi wenyewe kwa maamuzi yao watayaofanya. Alisema kuwa wanachi wanshiriki aktika maemdeleo yao kwa kushiriki aktika mikutano ya mkuu ya kijiji, kitingoji na mitaa. Aliema kwa mafano Halamashauri ya Kijiji inaandaa sheria ndogo na kuitisha mkutano ili wananchi watoe mapendekezo yao na kuyapitisha.

5.4. Aliuzliza swali kuwa ni kweli wananchi wanashiriki katika utungaji huo wa kwa mujibu wa Katiba na Sheria katika ngazi zote?

5.5. Mtoa Mada apia alizungumzia juu ya Majukumu na Uwezo wa Wananchi ambayo anasema kuwa yamepewa nguvu na Katiba katika ibara ya 8 na ibara ya 18 ambayo inatoa uhuru wa kutoa maoni na fikra zao, wakati ibara ya 21 inatoa fursa na haki ya kugombea nafasi yeyote, kucgaua au kuchaguliwa, kushririki katika kazi za serikali. Alisema pia wananchi wana mamlaka ya kumwandikia Mbunge au Diwani, Mwenyekiti wa Kijiji, Kitingoji, au Mtaa kunmataka aje katika Mkutano.

5.6. Alielezea juu ya wajibu na madaraka ya kwmondoa Mwenyekiti wa Kijii ambayo alisema yapo katika Mkutano Mkuu wa Kijiji kaktika Mkutano ambao utakuwua chini ya Mkuu wa Wilaya na kura ya theleithi mbili ya wakazi wote wa Kijiji.

5.7. Alielezea pia juu ya majukumu ya viongozi ikliwa ni pamoja na kunfanya maamuzi na kuzingatia haki, kusimamia kwa ukamilifu shughuli za maendeleo na kuwa mbunfu bna anayejituma. Alwanukuu viongozi wakuu wastaafu, Mwlaimu Nyerere Mkapa na Raisi wa Sasa Jkaya Kikwete juu ya majukumu ya Viongozi.

5.8. pia alielezea kwa kirefu juu ya Kazi za Mbunge ambazo alisema ni pamoja na kutoa mrejesho au kurudisha majibu ya shida za wananchi, kuezingatia shida za wale waliomchagua, kushirikiana na wananchi katika kazi za maendeleo na kushudhuria vikao wa Bunge na Bbaraza la Madiwani alieleza pia kazi za Mwenyekiti wa Kijiji, Kitongoji ambazo ni pamoja na kutnza register wa wakazi

Page 12: TAARIFA YA MDAHALO WA WANANCHI JUU YA ... · Web viewAlisisitiza kuwa maendeleo ya wananchi yanategemea wananchi wenyewe na viongozi wao waliowachagua. Alimsifu Mbuinge wa Tanga kwa

5.9. Aliuliza kama wanakitingoji au kijiji wanahudhuria mikutano au wanajua majukumu na kazi za mikutao hiyo.

5.10. YANAYOJITOKEZA: Wananchi wanaposhindwa kujua kazi za maafisa watendaji na kuchanganya kazi za wachaguliwa na wateuliwa.

5.11. Alihitimisha kwa kusema mahusinao ya viongozi na wanachi walianza kabla ya wakoloni kuingia nchini. Alisema kuwa zamani watu wasiohudhuria mkutano walikuwa w anapigwa faini. Alinukuu vitabu na watu maarufu waliozungumzia kuhsu maendeleo kanma ifuatavyo:MANDELA: UKUKUFU HAUPATIKANI KWA KUANGUKA, BALI KUINIKA KILA TUNAPOANGUKANYERERE: MAENDELEO YA KWELI HAYAEZI KUPATIKANA BILA WANANCHI KUSHIRIKISHWAMETHALI YA KIINGEREZA: VICHWA VIWILI NO BORA KULIKO KIMOJAMWTHALI YA KISWAHILI: KIDOLE KIMOJA HAKIVUNJI CHAWAAHADI YA MWANA TANU: NITASHIRIKIANA NA WENZANGU KUJENGA NCHI YANGUBIBLIA: PASIPO MASHAURI TAIFA HUANGUKA, BALI PENYE M ASHAURI TAIFA LINAIUNKA

6.0. Mragbishi alikaribisha watu kuchangia katika mada hiyo6.1. Abdul Karim Saadani – alisema mada ni nzuri na imewanufaisha kufahamu

majukumu yao lakini alito angalizo la dini baada ya Mtoa Mada kunukuu kitabu kimoja cha Dini tu. Alijibiwa kuwa kila mtu ana uhuru wa kuabudu

6.2. Kisailo Chadua – Mwenyekiti wa Kitongoji – alitoa wazo kuwa kuwepo na semina ya kuwafahamisha viongozi wajibu na majukumu yao na wananchi pia.

6.3. Epifania Floria Swai – yeye alisema kuwa wenyeviti wapewe alichookiita ‘changamooto’ akiwa na maana ya ‘posho’.

6.4. Mohamed Ramadhani- alisema jkuwa wenyeviti wasipoitisha vikao virtau wanatakiwa watolewe sasa yeye ndio mwenye mamlaka ya kuitisha sasa wananchi watafanyaje hali ikiwa hivyo?

6.5. Pantaleo Elias Mmahoo- Mwenyekiti wa Kijiji- alisema kuwa ni aibu kuwa baada ya miaka 50 ya uhuru Mwenyekiti wa Kijiji anafanya kazi bila posho ya aina yeyote ile.

6.6. Abdallah Hussein Waiziri- yeye alisema kuwa wananchi wanaona wamechagua viongozi kwa maendeleo lakini viongozi wana mtazamo wa kibinafsi na hicho chanzo cha mahusiano mabovu.

6.7. Ustaadh Selemani Kibaranga – alisema kuwa wananchi (wanaaochagua na wanaochaguliwa) hawajajua dhana ya utawala bora. Alizunguimzia juu ya umuhimu ya seina elekezi juu yab utawala bora.

6.8. Rehema Mwaipopo – eyey alitaka Wenyeviti wawzeshwe ili w anfaye kazi zao kwa moyo

6.9. Mwanaidi Said Guga alizungumiza juu ya viongozi wa Kata ikiwa ni pamoja na Diwani kuwakingia kifua Wenyeviti wanapotaka kuondolewa na wananchi

6.10. Hassan Bakakri Mbelwa – alitaka kujua ni vikao vingapi vya kanuni kwa mwaka mmoja

6.11. Bakari Mabaruku Bakari – alisema serikali itoe elimu kwa viongozi waliochaguliwa na wananchi. Alishukuru mto amada kwa kuwaelimisha juu ya haki zao.

6.12. Hassan Seif –wananchi wanafikiria kiongozi ndiye anayeleta maendeleo na akataka serikali itoe semiona kwa viongozi na wananchi

6.13. Dismas Sadiki – alisema mwitikio wa wananchi kwa mikutano ni mdogo, alitaka viongozi wawe na ushirikiano. Alisema kuwa viongozi lazima wasaidie katika shughuli za maendeleo

Page 13: TAARIFA YA MDAHALO WA WANANCHI JUU YA ... · Web viewAlisisitiza kuwa maendeleo ya wananchi yanategemea wananchi wenyewe na viongozi wao waliowachagua. Alimsifu Mbuinge wa Tanga kwa

6.14. Alexander Kimasira – vijiji vina matatizo kwa sababu demokrasia na utawala bora havijajelelweka. Alitaka kuwepo kwa semina za kuwapiga msasa viongozi na wananchi ili kuimarisha demokrasia na utawala bora.

6.15. Grace Mweta – serikali bado haijaona umuhimu kumboresha Mwenyekiti kimapato hivyo ndo maana anaingiza mikono katikia michan go ya wananchi

6.16. Mhina Magema Mtoto- yeye alisema hadi anafika umri alionao hajaona Mbunge akikusanya maoni ya wananchi na kuyapeleka Bungeni na kutoa mrejesho baada ya vijkao vya Bunge. Aliwataka viongozi waliojisahau wazinduke kuanzia siku ile.

6.17. Halima Mkombozi – viongozi wa kuchaguliwa wanakuwa karibu wakati wa kuomba kura na baada ya kuchaguiliwa wanaruidi mjini

6.18. Salimu Ramadhani – alisema kuwa wapo viongozi na wenyeviti wamekufa, wamejiuzulu na kufukuzwa lakini taarifa hazijapelekwa kunahusika hivyo vijiji hivyo na vitongoji vimekaa bila viongozi kwa muda mrefu. Alitaka hatu zichukuliwe kuwawajibisha watendaji wa vijiji.

6.19. Ibrahim Salehe – alisema kuwa hali ilivyo sio suala la kulaumiana kwa sababu Mwananchi hana uwezo wa kumtambua mtu anayemchagua na viongozi hawana mbinu za kuwashawishi wananchi wafanye maendeleo yoyote

6.20. Mchungaji Petro Zakayo – alisema viongozi wavijiji na vitingonji na mitaa wanafanya kazi bila malipo na hakuna anayewajali lakini wananyooshewa vidole.

6.21. Ibrahim Mrisho – alisema kuwa ibara ya 8 inageuzwa na kuwa wananchi sasa ndio wanaoitumikia serikali na kasema kuwa hajkuna dhana ya kujitolea bali watu wanalazimishwa

6.22. Abedi Abdallah –wenyeviti wawekewe ruzuku kidogo6.23. Palimirasi Paliro – Viongozi na wananchi wote hawana elimu na

akashukuru TASCO na mashirikka mengine kwa kueleta elimu. Alisema kuwa suala la Posho imesababishwa na utandawazi na akasema hata mtoto mdogo sasa hivi asipopewa fedha mfukoni ahendi shule sembuse Mwenyekiti anayemiliki watu 2000

6.24. Saidi Lugendo – yeye alisema viongozi wanaosema hawan posho hawan mamadili na kusema kuwa wana posho kuliko wananchi kwa sababu ndio wanaouza ardhi vijijini

6.25. Issa Jambia – alisema kuwa ardhi imekwisha na viongozi wanapoulizwa hawatilii maanani

6.26. Mzee Mveta – yeye alisema kuna haja ya watu kujua maana ya serikali6.27. Dr. Augustino Minja – alisema kuwa kama watu hawapati posho rushwa

itakwishaji. Alitaka mdahalo uendelee ili kuwawwezesha wananchi kuwa na ufahamu

6.28. Saidi Sedege – eyey aliona ajabu kuwa pamoja na kuwa hakuna posho viongozi wa kuchaguliwa wanapiga Kampeni kwa nguvu zote. Alisema kuwa wnanjua kuwa wakipata madaraka watauza ardhi kujihusisha na rushwa, alisema kuwa hawaitishi mikutano kwa asababu wamefanya maovu

6.29. Masoud Ali Mgobe – alisema kosa kubwa linalozima maendeleo ni wnanachi kutokujua wajibu wao hivyo klkubaki wanalaumu. Alisema kuwa wanannchi wachukue majukumu yao na kusema kuwa viongozi hawawezi kuongza vizuri kama wananchi wasipokuwa makini

6.30. Selemani Kingali – aliwalaumu wananchi pia katika suala la ardhi na kusema kuwa maeneo mengi yameuzwa na wananchi wenyewe. Aliwatka wananchi kuwalekeza viongozi wanapokosea

6.31. Idrsa Athumani Bakakri – alizungumiza juu susla ya elimu kwa viongozi na wananchi

Page 14: TAARIFA YA MDAHALO WA WANANCHI JUU YA ... · Web viewAlisisitiza kuwa maendeleo ya wananchi yanategemea wananchi wenyewe na viongozi wao waliowachagua. Alimsifu Mbuinge wa Tanga kwa

6.32. Mwenykiti wa Kitongoji – yeye alitaka kujua katika Mwenyekiti w a Kitongoji na Mwenyekiti wa Kijiji ni nani mkubwa?

6.33. Athumani Omar Mafiga – alieleza mgongano uliopo kijiji kwake na kuisema kuwa wneyekvuiti wa vitingoji wanachukua nafasi ya Mwenyekiti wa Kijiji na kuitisha Mkutano wa Halamashauri ya Kijiji,.

6.34. mwajabu Mrisho – aliwatka wananchi kuwa makini kwa sababu viongozi wanapochukua fomu haziainshi posho. Lakini alisema kuwa viongozi wasipopewa posho wataendelea kuwafanyia maovu

6.35. Ndeliko Bungule - alisema kuwa hoja nyingi zinaonekena kutokana na kutokuelewa katiba na sheria hivyo alitaka kila kiongozi anaposhaguliwa akabidhiwe aktiba

6.36. Hassan Rashid – alisema kuw viongozi hawaangalii vijana na ardhi imeuzwa hivyo vijana hawana sehemu za kulima

6.37. Ramadhani Bakari – alizungumzia juu ya tatizo la mrejesho wa mapato na amtumizi

6.38. Mwinyamisi Sembiji –alisema kuwa kwa kuwa mwenyekiti w a Kijiji m,wajiri wake ni wanakijiji hivyo wanfanye utaratibu wa kuliopwa na wananchi

6.39. Mohamed Said KLugendo – alseima kuwa watu wamepoteza mwelekeo kutokana na kuiongia jkwenye ubinafsi kuliko jkuwatumikia watu. Alisema kuwa huko nyuma watu walikuwa wanaitikia mwito lakini sasa hivi kero za wananchi hazifuatiliwi. Alisema ni vyema wa watu wakachagua watu watakaofuatilia kero

6.40. Rashid Zuberi Kihili – alitoa shukurani kwa TASCO kwa elimu na akawataka kuboresha elimu hiyo lakin I aliwaomba kutoa vitini ili waweze kuendelea kujielimisha

7.0. Akitoa majumuisho Mtoa Mada Mkuu, Dw. Mgongoro alisema kuwa Utwala wa Kisheria ndio unaotofautisha binadamu na wanyama na akaeleza kazi za mkutano mkuu wa kijiji akijibu maswali ya wanamdahalo. Alisema kuwa masuala ya ardhi yanashughulikiwa na mkutano wa kijiji ambao unapitisha majina ya wanaoomba ardhi. Aliuliza Je, wanakijiji wanahudhuria mikutano hiyo?

Pia alizungumzia juu tatizo la ukosefu wa elimu ya kiraia na kuwtaka viongozi kuwa Wabunifu.8.0. Naye Diwani Mgaza, akijibu hoja kuhusu ardhi kuuza kiholela, alisema kuwa

Halmashauri ya wilaya ya Kilindi ianfanya utafiti juu ya ununuzi wa ardhi na ardhi yote ambayo itakuwa haijauzwa kufuata utaratibu wa sheria itatwaliwa na kuganwanywa kwa wananchi

9.0. Afisa Tarafa, Amiri Sungura alivitaka vijiji kujipanga kutunga sheria ndogo na akawataka watu kujitahidi kila mmopja kujua sheria za nchi

10.0. Afisa Maendeleo ya Jamii w a Wilaya ya Kilindi ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya hiyo alishukuru TASCO kwa kwa jinsi ambavyo inatoa elimu ya uraia na kusema kuwa mdahalo umeonyesha kuwa wanakilindi walikuwa na kiu ya elimu hiyo. Alisema si jambo la kuficha kuwa kuna mpasuko kati ya wananchi na vionogzi kutokana na uelewa mdogo. Alisisitiza kuwa mahusiano mazuri ayanapatikana katika vikao hivyo ni muhimu viongozi kuitisha mikutana na wananchi kuhudhuria. Kuhusu uchaguzi aliseam w ananchi wachague viongozi wanaofaa kuepuka matatizo. Alisema halmashauri itaangalia namna ya kutoa mafunzo kwa viongozi juu ya majukumu yaop na jkuityakan TASCO iendelee kutoa mafunzo hayo. Kuhusu ardhi aliwataka wananchi w a Kilindi kuacha kuwachukia viongozi kwa ajili ya ardhi kuuzwa kwa sababu hata wao wanauza ardhi hiyo.

Page 15: TAARIFA YA MDAHALO WA WANANCHI JUU YA ... · Web viewAlisisitiza kuwa maendeleo ya wananchi yanategemea wananchi wenyewe na viongozi wao waliowachagua. Alimsifu Mbuinge wa Tanga kwa

11.0. Naye Mratibu wa TASCO, Bw. Chanyeghea alitoa wazo la kuunda timu ya ufufatialiaji ambayo baada ya makubaliano ilionekana iwe na mwakilishi mmoja kutoka kila kata. Alizungumzia kuhusu wazee na kusema kuwa ni muhimu sana kwa sababu vijana wanajifunza kutoka kwao.

MWISHO

MDAHALO WA WANANCHI JIMBO LA PANGANI ULIOFANYIKA KATIKA HOTELI YA SAFARI ANNEX TAREHE 26.04.2012

1.0UTANGULIZI:

Mragbishi wa Mdahalo huo, David Chanyeghea ambaye pia ni Mratibu wa Mtandao wa Asasi za Kiraia Mkoani Tanga (TASCO) alieleza kwa ufupi madhumuni ya mkusanyiko huo ambao alisema ni mfululizo wa midahalo ambayo imeandaliwa na Mtandao huo kuwapa fursa wananchi kukutana na viongozi wao wa kuchaguliwa na kujadili mustakabali wa taifa na nafasi ya kila mmoja katika maendeleo ya nchi.

Baadaye alimkaribisha Mwenyekiti wa TASCO, John Nyika ambaye alisema kuwa lengo la TASCO ni kuwa na mtandao wenye changamoto. Alisema kuwa katiba inawapa haki wananchi kuchagua viongozi na TASCO inajaribu kuwapa fursa wananchi kuangalia kwa undani mahusiano kati ya viongozi na wananchi jinsi yalivyo.

2.0. UFUNGUZI RASMI Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Zipora Pangani alizungumzia juu ya umuihimu wa midahalo ambapo alisema kuwa pamoja na ratiba ya siku ya Muungano aliona ni muhimu kuhudhuria kwa sababu ni mkereketwa wa maendeleo.

Alishukuru TASCO kwa kurejea tena katika shughuli za maendeleo wilaya Pangani. Alisisitiza kuwa hizi ni fursa ambazo zinatafutwa sana lakini alikisitikishwa na mahudhurio ambayo alisema kuwa hayaleti tamaa. Alisema kuwa watu ni wepesi wa kunyooshea vidole serikali lakini inapotokea fursa ya kutoa maoni au kujadili shughuli za maendeleo wa tu hawajitokezi. Alitoa wito kwa wananchi wa Pangani kutumia fursa hizo kwa ukamilifu.

Aliitaka TASCO kutafuta namna ta kushirikisha wananfunzi wa sekondari wanapoandaa midahalo kama hiyo kwa sababu hao ndio wenye maswali na ndio ulimwengu wa kisasa.

Bi. Pangani alieleza kuwa wingozi wamechaguliwa kuwatetea wananchi hivyo wananchi wanategemea uwajibikaji wenye tija kutoka kwao. Alisema kuwa serikali inajitahidi kuendesha mafunzo mbalimbali mara wanapochaguliwa lakini hiyo haitoshi na lazima wadau wote waendelee kuwajengea uelewa kupitia mafunzo na mijadala kama hiyo.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, Khatibu Jumbe alisema kuwa mdahalo utatoa fuirsa kuwajengea uwezo wananchi.

Mratibu wa TASCO, David Chanyeghea alisema watanzania hawawezi kufikia maendeleo ya kweli kama wananchi hawashiriki katika shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na mijadala ya maendeleo yao. Alisema kuwa TASCO iliona vyema kuleta mada ya Mahusiano kati Viongozi wa kuchaguliwa na wananchi kabla ya kuleta mada ya Mabadiliko ya Tabia Nchi kwa sababu ni muhimu na inakwenda sanjari na mjadala wa Katiba ambao ulitangulia.

Page 16: TAARIFA YA MDAHALO WA WANANCHI JUU YA ... · Web viewAlisisitiza kuwa maendeleo ya wananchi yanategemea wananchi wenyewe na viongozi wao waliowachagua. Alimsifu Mbuinge wa Tanga kwa

3.0. MADA KUU – IMETOLEWA NA STEPHEN KIAMA MWAIMU. Alisema kuwa mada inakusudia kueleza mahusiano na kuigawa katika vipengele vifuatavyo:

a) Maana ya uongozib) Aina ya uongozic) Sifa za viongozid) Wajibu wa kiongozie) Tofauti kati ya kiongozi na mtawala na f) Mahusiano yanayotakiwa kuwepo

3.1. MAANA YA UONGOZI: Alielezea kama tabia inayomwezesha mtu kuongoza ili kikidhi makusudio/malengo ya jamii. Pia anayetaka kuongoza anatakiwa kuangalia mafanikio katika kuleta maslahi ya jamii na aweze kuongoza wananchi kufikiria wafanye nini ili kwenda mbele na kuwa na hali bora.3.2. AINA YA UONGOZI: alisema kuwa kuna aina mbili ambazo ni:- wa Kiimla kama vile wa kisultanio au kifanlame ambapo mamamuzi yote kufanywa na kiongozi. Alisema kuw uongozi wa aina hii siku hizi hauna nguvu sana duniani. Aina nyingine ni uongozi wa kidemokrasia ambao ni wa watu wengi wanaokubaliana kuchagua watu wanaowapenda wawaongoze. Alisema kuwa nchi zilizostaarabika hufuata mfumo huo na kiongozi anatakiwa kuwatumikia watu waliomchagua. Tanzania inafuata mfumo huu3.3. SIFA ZA KIONGOZI: ni pamoja na kuwa na uelewa, uwezo wa kubuni, awe na mawazo chanya, awe msikivu kupokea hoja ili atoe maamuzi sahihi. Pia natakiwa kuwa mtu anayejituma, akubaliane na tofauti za watu wengine, asiwe na nongwa, awe na ushawishi na awe na moyo w a kweli wa kuwaletea maendeleo ya kweli wananchi wake. Sifa nyingine ni kuwa na weledi unaokubalika na jamii.

Alitaja mifano ya viongozi waliofikia sifa hizi kuwa pamoja na Cincinatus aliyeishi katika karne ya 5 kabla ya kuzaliwa Kristo katika utawala wa Warumi. Alikuwa na akili, mbunifu, nguvu za ushawishi na weledi. Yeye baada ya kuwasaidia wananchi kushinda vita, alirejea shambani. Alikuwa na sifa ya kutumika wakati wowote kwa manufaa ya umma pasipo kufikiria maslahi yake.

Kiongozi mwingine wa mfano alikuwa ni Hayati Edward Moringe Sokoine ambaye alichukiwa sana na viongozi wenzake ambao walikuwa wabadhirifu na wasio wa wachapa kazi. Aliongoza vita dhidi ya wahujumu uchumi na alifanya kazi kwa niaba ya wengi pasipo kujinufaisha.

Kiongozi mwingine ni Mwalimu Nyerere ambaye aliachia madaraka wakati bado akiwa na uwezo wa kuendelea na ni mfano halisi wa Cincinatus kwa sababu hata zawadi alizopewa wakati aking’atuka alizigawa kwa wananchi na taasisi mbalimbali.3.4. WAJIBU WA KIONGOZI WA KUCHAGULIWA: kuwatumikia waliomchagua, kuwa mtumishi wa wale waliiomchagua. Ana wajibu wa kutambua kuwa ni mtumishi wa wananchi na sio mtawala, kuchukua hoja za wananchi na kuzipeleka katika mabaraza husika.3.5. TOFAUTI KATIKA YA MTAWALA NA KIONGOZI: uongozi si utawala ingawa ni sehemu ya utawala. Kiongozi utendaji wake ni kuhusisha anaowaongoza na mtawala ni kutekeleza mambo ambayo yamekwisha pangwa, kusimamia na kuhakikisha utekelezaji kwa kufuata sheria na kanuni. Hata hivyo alisema kuwa maamuzi yeyote ambayo hayahusuhi wananchi hayawezi kuleta maendeleo hivyo.4.0. CHANGAMOTO ZA UONGOZI WA KUCHAGULIWA: alitaka washiriki kujiuliza, kujipima kutokana na maswali yafuatayo:i) Je viongozi wetu wanaochaguliwa ni wenye kujali maslahi ya wananchi kwanza na kama sio ni kwa nini?ii) Wanaoongoza kwa dhana shirikishi?

Page 17: TAARIFA YA MDAHALO WA WANANCHI JUU YA ... · Web viewAlisisitiza kuwa maendeleo ya wananchi yanategemea wananchi wenyewe na viongozi wao waliowachagua. Alimsifu Mbuinge wa Tanga kwa

iii) Wana moyo wa dhati wa kuweza kulinda, kusimamia imani, maadili na raslimali za nchi kwa manufaa ya wengi?5.0. MAJADILIANO:Hapa Mragbishi aliwataka washiriki kijikita kwa uzoefu kuangalia:

1) mikutano ya kijiji – viongozi wa kuchaguliwa wanahudhuria ?2) kamati ya maendeleo ya kata - Vikao hivi vya kikatiba vinakaa? Kama hawaji

kuchukua hoja/shida zetu na hawatoi mrejesho wao si viongozi3) Kuna matatizo yanayo sababishwa na watu kutoshiriki mikutano ya vijiji4) Tusiwaseme viongozi tu bali tuangalie pia, je, wananchi wanatimiza wajibu wao

kuhudhuria mikutano?

5.1. HALIDI OMARI: yeye alianza kwa kuuliza kazi kuu za seriakli na chama na alijibiwa kuwa kazi za serikali ni kulinda uisalama wa nchi, kuhakikisha sheria zinazotengenezwa na mhimili zinatekelezwa pasipo upendeleo, kuleta maendeleo yenye tija kwa wananchi, utawala, na kukusanya kodi. Baada ya ya jibu hilo, Halidi alisema kuwa kuna kutoelewana baina ya serikali na viongozi wanaochaguliwa. Mragbishi alitoa angalizo kuwa kiongozi akishachaguliwa wananchi wote ni wake na serikali inatekeleza ilani ya chama kilichopo madarakani5.2. CHEKA MOHAMED: Alisema kuwa ufahamu wa wananchi na viongozi wa kuchagulia haupo, alisema kuwa kiongozi lazima awe karibu na watu waliomchagua na hali ilivyo ni kuwa ukaribu huo haupo. Aliendelea kueleza kuwa mikutano ya kata, vitongoji, mitaa na vijiji watu hawahudhurii kwa sababu watu hawataki kupoteza muda kutokana na viongozi kutotilia maanani shida za watu, alisema kwa mfano mbunge wa Pangani hayupo katika mdahalo huo.5.3. JUMAA JUMAA (MWANAFUNZI- SHULE YA SEKONDARI YA FUNGUNI): alisema mahusiano ya karibu hayapo na alitoa mfano kuwa hajawaona wabunge kutembelea shule kuzungumza na wanafunzi na wazazi kujua shida zinazowakabili. Alisema kuwa mbunge anatakiwa kujua matatizo na kusisitiza kuwa wanafunzi wanafeli si kwa sababu hawana akili bali kuna mazingira yanayowafanya wafeli. Hapo Mragbishi alitoa angalizo kuwa wananachi wasiweke mtazamio kuwa kiongozi wa kuchaguliwa ni mbuinge tu bali wanaanzia katika kitongoji, mtaa, kijiji, kata hadi jimbo. Aliwataka kuzungumzia viongozi wa kuchaguliwa kwa ujumla wao.5.4. MARWA SAMWEL WEREMA: alisema kuwa mgogoro wa mahusiano unaanzia katika mchakato wa uchaguzi. Alisema kuwa watu wanawachagua viongozi kwa maslahi na mchakato unawafanya waanze kupigania maslahi yao kwanza. Alisisitiza kuwa elimu ya uiraia kwa viongozi na wananchi inahitajika na kueleza kuwa hata kuhudhuria mikutano hawafahamu kuwa ni sheria na alisema ni muhimu kutoa elimu kwa wananchi ili wajue kama wanaowachagua wanazo sifa zinazotakiwa.5.5. ISSA RAJAB: alizungumzia viongozi na wananchi kutiokujua haki zao na kusema kuwa pamoja na kuwa viko viko wazi wananchi hawahudhurii. Alisema kuwa watu wanajikita katika kulaumu madiwani. Alisisitza kuwa tatizo lipo kwa wanaoongzwa ambao alisema hawajui haki zao. Alisema kuwa maendeleo hayaletwi nyumbani bali yanatafutwa. Aliwataka viongozi na vyama kuelimisha wananchi juu ya haki zao.5.6. JOHN SEMNKANDE-DIWANI: alitaka watu waachiwe kuwa wazi kuwazungumzia viongozi wao na Mragbishi alimtoa wasiwasi kuwa hakuna hofu ya kuwazungumzia.5.7. LEONARD DAVID: alitoa rai kwa viongozi wanaochaguliwa kukaa na kuona kwa nini wananchi hawatoki kwenda katika mikutano na wakigundua sababu mahusiano yatakuwa mazuri. Alitoa rai kwa serikali kufuta posho kwa viongozi ili kuona namna wanavyothamini nafasi zao za kutumikia wananchi. Aleleza kuwa wanatumia nguvu nyingi katika uchaguzi na wakipata wanatumia nafasi kurejesha gharama.5.8. SHIJA MALANGI: alisema kuwa kuna kipengele ambacho kimesauhalika ambcho ni cheo ni dhamana. Alisema kuwa uongozi wa sasa unanunuliwa na ndio maana wana kuwa jeuri. Alsisitiza kuwa wananchi wakitaka mahusiana mazuri wachague kwa sifa zao kwa sababu wanaokuja kutanguliza zawadi wanatumia muda wao kurejesha gharama. Alitoa rai ya elimu ya uraia kwa wananchi.

Page 18: TAARIFA YA MDAHALO WA WANANCHI JUU YA ... · Web viewAlisisitiza kuwa maendeleo ya wananchi yanategemea wananchi wenyewe na viongozi wao waliowachagua. Alimsifu Mbuinge wa Tanga kwa

5.9. VINCENT MHINA: alisema mahusiano yamepotea na yanakuwa mazuri wakati wa kampeni na wakati huo hata mwananchi akiomba kupewa fedha za kuanzisha mradi anapewa. Alisema jkuwa taifa liko katika hali tete lakini kuna kuna pesa nyingi katika taifa ambazo zinaishia kwa viongozi na wabunge wanatetea maslahi yao. Aliuliza kwa nini mbunge alipwe posho ya Sh. 300,000? Aliwataka wapia kura kujifunza kutokana na makosa na kuangalia viongozi watakaojali maslahi ya wananchi.5.10. SALUM RAMADHANI: alisema akuwa majimbo mengi yamegeuka biashara ya wabunge na hata viongozi ngazi za chini fikra zao haziko katika kuongoza wananchi. Alisema elimu ya uraia inahitajika. Alisema kuwa wananchi hawahudhurii mikutano kwa sababu wanajhisi wamedhulumiiwa haki zao.5.11. MRISHO JUMA: alisema kuwa mahusiano yanaishia siku ya uchaguzi na kuwataka viongozi wajenge mahusiano kupitia mikutano ya serikali za vijiji. Alisema hali ilivyo sasa hivi ni kuwa wananchi wakizungumza ukweli wanakuwa adui.5.12. SAIDI HASSAN: alisema kuwa mahusinao hayapo kwa sababu msingi wa kuwachagua viongozi sio madhubuti. Alisema kuwa zamani uwajibikaji ulikuwepo lakini sasa hivi viongozi wako huru. Alisema kuwa viongozi hawafuati wananchi lakini mbona wanapoomba kura wanawafuata?5.13. RAMADHANI MASOUD: aliwataka wananchi kuwa makini wasidanganywe na fedha wakati wa uchaguzi. Alisisitiza elimu ya uraia5.14. LEONARD SEKIBAHA: alisema pia wanaochaguliwa wanachaguliwa kwa fedha hivyo wakishachaguliwa hawarudi. Alisema muhimu ni kuwa wanachi wajue ni nini kinawaletea maendeleo yao na waeleweshwe kuwa wana wana wajibu wao mkubwa na viongozi waliochaguliwa wana wajibu wa kupeleka mbele maoni ya wananchi. Alisisitiza elimu ya uraia5.15. KHATIB MOHAMED: alisema viongozi lazima wawajali wananchi waliowachagua5.17 - huyu alisema kuwa viongozi hawana moyo wa dhati katika kueleta maendeleo. Alisema katiba ibadilike na mbunge lazima awe mkazi wa eneo analoomba kuchaguliwa ili awe karibu kusikiliza shida zao. Alieleza kuwa sasa hivi ni pesa zinatumika na kuwataka wananchi kubadilika.5.18. PATRICK YONA: wananchi hawana uelewa wa nini maana ya maendeleo alisema ni muhimu wananchi wafundishwe maana ya maendeleo alisema kuwa nao viongozi wapatiwe semina elekezi wakati wanapochaguliwa lakini alisema kuwa inawezekana wanalaumiwa wakati ambapo hawajapewa matatizo ya wananchi.5.19. SHINEIN SHEIKH KOMBO –Diwani- yeye alisema kuwa alikuwa na hofu kuja katika mdahalo kutokana na mada. Alisema hata hivyo baada ya kufika ameona kuwa eneo kubwa katika mkutano huo ni kulalamika lakini alisema kuwa hatma iko mikononi mwa wananchi. Alisisitza juu ya umuhimu wa mikutano na kusema kuwa bila mikutano hakuna maendeleo. Akawataka wananchi kuhudhuria mikutano hata kama viongozi wanaoitisha mikutano hawawapendi.5.20. ALI MOHAMED –Mkuu wa Kituo cha Polisi, Pangani – alisema kuwa mahusiano ni pembe tatu (viongozi, wananchi na maendeleo). Alieleza kuwa wananchi wengi hawafahamu maana ya maendeleo hivyo taasisi kama TASCO zina jukumu la kutoa elimu. Alifafanua kuwa uelewa mdogo unasababisha wanachi kutotumia fursa za midahalo kama hii na kuwataka viongozi na wananchi kujua fursa zilizopo na kuzitumia. Alisema kuwa Pangani ina fursa nyingi za kimaendeleo na kutoa wito kuwawezesha wananchi kujua maana ya maendeleo na kutumia fursa. Alisema bila kuwepo kwa mahusiano mazuri hakuna maendeleo.

6.0. MAJUMUISHOMraghbishi alitoa wazo kuteua timu ya ufuatialiaji wa mamsuala yaliyotajwa ambayon inakuwa kama kikundi cha shinikizo.6.1. Badaye mwezeshaji alizungumzia masuala muhimu ambayo yalijitokeza ambayo ni:

Uelewa wa wananchi katika suala la kuwachagua viongozi wanaowataka. Alisema kuwa wanapowachagua hawajui jinsi watavyowawajibisha

Page 19: TAARIFA YA MDAHALO WA WANANCHI JUU YA ... · Web viewAlisisitiza kuwa maendeleo ya wananchi yanategemea wananchi wenyewe na viongozi wao waliowachagua. Alimsifu Mbuinge wa Tanga kwa

Ukosefu wa ufahamu wa umuhimu wa kufanya mikutano –kutambua wajibu wa wananchi na viongozi. Elimu ya uraia iwe inafundishwa kutoka shule za msingi hadi katika vyuoElimu ya kiongozi sio kigezo tuangalie uwezo wakeUmuhimu wa kujitazama aina gani ya vitu walivyonavyo –fursa zilizowazungukaViongozi lazima wawe karibu na wananchi kupitia mikutano ya mara kwa maraKushindwa kwa wananchi kutumia mamlaka au madaraka waliyopewa na KatibaFursa za mikutano hazitumiwi

7. Hatimaye Mratibu wa TASCO, David Chanyeghea alieleza kuwa huu ulikuwa mwisho wa mdahalo ambao alisema kuwa ni muhimu na inajenga. Alisisitiza juu ya haja wananchi kujua kazi wanazokwenda kufanya viongozi wanaowachagua, hivyo akawataka wawe makini katika kuchagua. Alieleza kazi ya Kamati ya Jimbo ambayo alisema ni kufuatilia mambo yaliyojitokeza na yaliyokubaliwa katika mipango ya maendeleo ili kuifanya midahalo kuzaa matunda.

Alissitiza kuwa vipaumbele vya wananchi ndivyo vinapswa kuingizwa katika mipango ya maendeleo na sio vipaumbele vya halmashauri.

Mdahalo ulifungwa saa 7.58 mchana.

MDAHALO WA WANANCHI JIMBO LA TANGA MADA: MAHUSIANO YA WANANCHI NA VIONGOZI W A KUCHGAULIWA KATIKA KULETA MAENDEELO

1.0. UTANGULIZI: Mratibu wa TASCO, ambaye alikuwa ndiye Mragbishi, David Chanyeghea alitoa taarifa kuwa huo ulikuwa ni mdahalo wa mwisho katika mfululizo wa midahalo inayohusu mahusiano. Alisema kuwa uteuzi wa mada hiyo ulitokana na uhusiano wake na mada iliyopita ya Katiba kwa sababu mahusiano yameainishwa katika Katiba.1.1. Mwenyekiti wa TASCO, John Nyikas akizungumza katika mdahalo huo alisema kuwa Katiba ndiyo msingi wa mahusiano kati ya viongozi na wananchi yanayoanzia katika uchaguzi. Alisisitiza kuwa maendeleo ya wananchi yanategemea wananchi wenyewe na viongozi wao waliowachagua. Alimsifu Mbuinge wa Tanga kwa kushiriki kikamilifu katika maendeleo na midahalo.1.2. Mbunge wa Tanga, Omari Nundu aliwakaribisha washiriki katika katika mdahalo na kusena kuwa n I fursa ya pekee kujadioli mambo mablo=li ya maendeleo. Alikizungumiza kjuu ya mahusiano alisema kuwa tatizo kubwa lipo katika mawasiliano na akatoa rai suala hilo lifanyiwe kazi. Alisema kuwa upo umuhimu kwa mada hiii kutolewa katika mikutano ya hadhara ili watu wengi zaidi wapate ufahamu huu. Alisisitiza juu ya uwajibikaji wa viongozi.

Akielezea zaidi alisema kuwa maendeleo hayatapatikana bila kuwepo kwa mabadiliko chanya ambayo alisisitza hayaji bila kuwepo kwa mashirikiano baina ya viongozi na wananchi.2.0. Baada ya hapo Mragbishi alisema jkuwa TASCO itaangalia uwezekano wa kufanya midahalo katika ngazi ya kata ili kuwafikia wananchi wengi.3.0. MADA KUU – STEPHENM KIAMA MWAIMU.Alisema kuwa mada inakusudia kueleza umuhimu wa mahusiano kati ya wananchi na viongozi wao na akaigawa katika sehemu kuu sita:

g) Maana ya uongozih) Aina ya uongozii) Sifa za viongozij) Wajibu wa kiongozik) Tofauti kati ya kiongozi na mtawala na

Page 20: TAARIFA YA MDAHALO WA WANANCHI JUU YA ... · Web viewAlisisitiza kuwa maendeleo ya wananchi yanategemea wananchi wenyewe na viongozi wao waliowachagua. Alimsifu Mbuinge wa Tanga kwa

l) Mahusiano yanayotakiwa kuwepo

3.1. MAANA YA UONGOZI: Alielezea kama tabia inayomwezesha mtu kuongoza ili kukidhi makusudio/malengo ya jamii. Pia anayetaka kuongoza anatakiwa kuangalia mafanikio katika kuleta maslahi ya jamii na aweze kuongoza wananchi kufikiria wafanye nini ili kwenda mbele na kuwa na hali bora.3.2. AINA YA UONGOZI: alisema kuwa kuna aina mbili ambazo ni: - wa Kiimla kama vile wa kisultani au kifalme ambapo maamuzi yote hufanywa na kiongozi mmoja. Alisema kuwa uongozi wa aina hii siku hizi hauna nguvu sana duniani. Aina nyingine ni uongozi wa kidemokrasia ambao ni wa watu wengi wanaokubaliana kuchagua watu wanaowapenda wawaongoze. Alisema kuwa nchi zilizostaarabika hufuata mfumo huo na kiongozi anatakiwa kuwatumikia watu waliomchagua. Tanzania inafuata mfumo huu3.3. SIFA ZA KIONGOZI: ni pamoja na kuwa na uelewa, uwezo wa kubuni, awe na mawazo chanya, awe msikivu kupokea hoja ili atoe maamuzi sahihi. Pia natakiwa kuwa mtu anayejituma, akubaliane na tofauti za watu wengine, asiwe na nongwa, awe na ushawishi na awe na moyo wa kweli wa kuwaletea maendeleo ya kweli wananchi wake. Sifa nyingine ni kuwa na weledi unaokubalika na jamii.

Alitaja mifano ya viongozi waliofikia sifa hizi kuwa pamoja na Cincinatus aliyeishi katika karne ya 5 kabla ya kuzaliwa Kristo katika utawala wa Warumi. Alikuwa na akili, mbunifu, nguvu za ushawishi na weledi. Yeye baada ya kuwasaidia wananchi kushinda vita, alirejea shambani. Alikuwa na sifa ya kutumika wakati wowote kwa manufaa ya umma pasipo kufikiria maslahi yake.

Kiongozi mwingine wa mfano alikuwa ni Hayati Edward Moringe Sokoine ambaye alichukiwa sana na viongozi wenzake ambao walikuwa wabadhirifu na wasio wa wachapa kazi. Aliongoza vita dhidi ya wahujumu uchumi na alifanya kazi kwa niaba ya wengi pasipo kujinufaisha.

Kiongozi mwingine ni Mwalimu Nyerere ambaye aliachia madaraka wakati bado akiwa na uwezo wa kuendelea na ni mfano halisi wa Cincinatus kwa sababu hata zawadi alizopewa wakati aking’atuka alizigawa kwa wananchi na taasisi mbalimbali.3.4. WAJIBU WA KIONGOZI WA KUCHAGULIWA: kuwatumikia waliomchagua, kuwa mtumishi wa wale waliiomchagua. Ana wajibu wa kutambua kuwa ni mtumishi wa wananchi na sio mtawala, kuchukua hoja za wananchi na kuzipeleka katika mabaraza husika.3.5. TOFAUTI KATIKA YA MTAWALA NA KIONGOZI: uongozi si utawala ingawa ni sehemu ya utawala. Kiongozi utendaji wake ni kuhusisha anaowaongoza na mtawala ni kutekeleza mambo ambayo yamekwisha pangwa, kusimamia na kuhakikisha utekelezaji kwa kufuata sheria na kanuni. Hata hivyo alisema kuwa maamuzi yeyote ambayo hayahusuhi wananchi hayawezi kuleta maendeleo hivyo akasema kuwa uongozi wa kuchaguiliwa ni gharama.3.6. WAJIBU WA WANANCHI: Alizungumzia wajibu wa wananchi kuwa ni kuuliza, kudai na kufuatilia haki zao. Alisema kuwa haki siku zote hailetwi vivi hivi. Alisema kuwa wananchi wakikaa kimya watakuwa hawajatimiza wajibu wao kwa jamii yao na kuwataka kujadili pasipo kuwa na inda. Aliwataka kiuangalia maswali yafuatayo katika kujadili:Je, viongozi wao ni wasikivu?Je, ni wenye moyo wa dhati?Je, wanafanya kazi kwa upendo na Je, wana maadili mema?

4.0 MAJADILIANO:4.1. ASERI SHEWALI: alisema mahusiano yaliyopo ni mabaya kwa sababu wananchi na viongozi wanatazamana kama mfadhili na mfadhiliwa kitu ambacho hakileti mahusiano mema. Alisema kuwa wabunge, kwa mfano si wafadhili bali ni wawakilishi wao na kazi

Page 21: TAARIFA YA MDAHALO WA WANANCHI JUU YA ... · Web viewAlisisitiza kuwa maendeleo ya wananchi yanategemea wananchi wenyewe na viongozi wao waliowachagua. Alimsifu Mbuinge wa Tanga kwa

zao zimeainishwa katika katiba. Alisema kuwa mbunge aklkosa fedha kusaidia masuala binafsi anaweza kuonekana hafai. Alionya juu ya hatari ya kutoa umuhimu kwa kazi ambazo si zake kwani kusaidia ni ubinadamu. Tatizo hilo linaleta sura kuwa mbunge anayefaa ni yule ambaye ana uwezo na hiyo inaweza kusababisha wabunge kudai posho kubwa ili waweze kukabiliana na mitazamo ya ufadhili na ufadhiliwa katika jamii. Alitaka jamii iwahukumu wabunge kwa kushindwa kusimamia serikali na kusema kuwa wananchi wanashindwa kuwahukumu wabunge ambao ni mawaziri kwa kazi zao.4.2. ISMAIL MASOUD: alisema kuwa mahusiano baina ya viongozi wa kuchaguliwa na watawala ni matatizo kwa sababu viongozi wanaochaguliwa wanatumia muda wao kuwabembeleza watawala hivyo kuwageuza wawakilishi hao wa wnanachi kuwa ombaomba. Aliuliza kama mbunge anaomba kuna haja kuwa na Bunge? Aliwataka wabunge kuchukua mawazo ya wananchi kabla ya bajeti na kuifanya serikali itengeneze bajeti kutokana na mawazo hayo. Alisema kuwa suala la mahusiano linaanzia katika mfumo wa uchaguzi na kusisitiza kuwa wawakilishi wanaotokana na rushwa hawawezi kuwa na mahusiano mazuri na kusema wanaotoa rushwa wasichaguliwe. Mragbishi alitoa angalizo kuangalia viongozi wa kuchaguliwa kuanzia ngazi ya chini.4.3. JONATHAN LEONRAD: alishukuru TASCO kuwa kuandaa mdahalo huo na Mbunge kuwepo lakini alizungumzia changamoto ya kukosekana kw madiwani katika mdahalo huo. Aliwataka wabunge kuunda timu za kubaini kero za wananchi. Kwa mfano alisema mjini Tanga siku ya usafi wafanyabiashara wanalazimishwa kufunga biashara zao na kuuliza Halmashauri inatumia kipengele gani cha sheria kufanya hivyo. Aliuliza kwa nini mpango kama huo haupo katika miji mingine. Alisema kuwa madiwani wanaridihika na hali hiyo wakisahau kuwa wao ni wawakilishi wa wananchi. Alisema kuwa wanatumia nguvu nyingi kuchaguliwa na mbona hawatumii nguvu kama hiyo kubaini kero. Aliwataka wajue kuwa wanaingia katika uongozi kutumikia watu wote. Alimtaka mbunge wa Tanga abadilishe mfumo wake wa mawasilianio baina yake na wananchi waliomchagua.4.4. AIDAN TWAHA: alisema mahusiano ni mabaya na akawanyooshea kidole washauri wa mbunge na kusema ndio chanzo cha mahusiano hayo mabaya. Alisema kuwa watu wanaokwenda kuhudumiwa na ofisi ya mbunge ni wale wenye masuala madogo kama ya harusi, maulidi na kadhalika lakini kuna masuala makuibwa kama ya kiwanda cha chokaa ambacho kinatumia miembe kuchoma chokaa. Alitahadharisha kuwa kama isipoangaliwa miti itakwisha na akamtaka mbunge kuchagua siku kutembelea eneo hilo.4.5. NURU BAFADHILI: alisema kuwa mahusiano yanapaswa kuanzia ngazi za chini ambako viongozi wanpaswa kuwa karibu na wananchi na sio kufanya hivyo wakati wa kuomba kura. Aliwalaumu wananchi kuwalaumu wabunge na kusema ni wangapi wanapaeleka kero zao kwa mbunge. Alisema kuna haja ya wenyeviti kupata mafunzo na kuomba wenyeviti hao wapewe posho.4.6. SHAABAN HAMIS: alisema kuwa zamani wakati wa chama kimoja mahusiano yalikuwa mazuri na yote yaliyotekelezwa katika maendeleo yametokana na mahusiano mazuri. Alisema mfumo wa vyama vingi umeleta mahusiano mabaya kwa sababu watu kutoka vyama mbalimbali hawawezi kukaa pamoja. Aliwataka watanzania kuangalia namna ya kurekebisha hali hiyo.4.7. SADIKI SHEMBILU: alisema kuwa wenyeviti na madwani mahusiano yao na wananchi ni wakati wanapoomba kuchaguliwa. Baada ya hapo hakuna mahusiano jambo linalosababisha watendaji kufanya vibaya kutokana na kukosa usimamizi. Alitoa mfano kuwa mtaani kwao Magaoni kuna dampo katika eneo la shule ambalo wahusika hawachukui hatua kuondoa hali ambayo inahatarisha afya za wananchi. Wananchi wametishia kuandamanma kwa mkuu wa mkoa kuonyesha kutokuwa na imani na mkurugenzi wa Jiji kutokana na hali hiyo. Alitoa rai kuingiza wagombea binafsi katika katiba kwa sababu wagombea wa vyama wameshindwa kuleta msisimko wa maendeleo. Alieleza masikitiko juu kutokuwepo kwa madiwani na wenyeviti wengi katika mdahalo jambo linaloonyesha kuwa hawaoni umuhimu wa kukutana na wananchi.4.8. REHEMA KIBAJA: alisema kuwa kitu kikubwa ni kukosa uelewa. Alisema kuwa mfumo unapobadilika hakuna uelewa kuna mkanganyiko kiasi kwamba jamii haijui utaratibu wa

Page 22: TAARIFA YA MDAHALO WA WANANCHI JUU YA ... · Web viewAlisisitiza kuwa maendeleo ya wananchi yanategemea wananchi wenyewe na viongozi wao waliowachagua. Alimsifu Mbuinge wa Tanga kwa

uwajibikaji. Alisema kuwa viongozi wanajiona ni wafalme lakini kama wangeelewa mambo yangekuwa tofauti. Aliomba elimu ya uraia itolewe kwa wananchi na viongozi.4.9. ……..alizungumzia tatizo la mawasiliano na viongozi kukosa mafunzo.4.10. OSWIN BONDAI: alisema kuwa mahusiano yaliyopo ni mabaya na kueleza kuwa tatizo ni utekelezaji wa shughuli za maendeleo4.10. MRS. MHANDO: alisema kuwa viongozi waliochaguliwa hawana uchungu wa waliowachagua na hawana elimu na nafasi au majukumu yao. Aliomba wapewe elimu kuhudumia jamii.4.11. MZEE VEDASTO KAROLI: alisema mahusiano si mazuri kwa sababu viongozi wanachaguliwa wakiwa hawana ujuzi/fani za uongozi. Alitaka elimu ya uongozi itolewe. Alizungumzia juu ya umuhimu wa viongozi kuhudhuria mikutano ili kuwa karibu na wananchi. Pia alieleza kuwa viongozi wanataka kutumikiwa na sio kutumikia wananchi.4.12. KASSIM EL-SIAGI: Alisema kuwa mfumo wa utawala wa Tanzania ni wa kipekee lakini ni watu wangapi wanafahamu hilo. Alieleza kuwa watu bado hawazitendei haki serikali za mitaa kwa sababu watu wenye kero wanaruka ngazi na kuacha kuwatumia watendaji waliopo katika ngazi za chini. Kuna haja ya watu kuelimishwa kuhusu mfumo. Kuhusu uchaguzi alisema kuwa watu wanasifa zao wanazotaka kutoka kwa viongozi. Kuna wengine wanataka wenye fedha, wengine wanachagua viongozi kwa sababu ni wenzao katika kupindisha sheria na wengine wanachaguliwa kwa sababu wana ushawishi katika kupinga maamuzi halali na ya vikao halali. Aliomba midahalo iandaliwe hadharani.4.13. JUMA ATHUMANI: alizungumzia umuhimu wa mbunge kutembea kwa wapiga kura wake. Alisema kuna kero kubwa ya ushuiru wa mkaa4.14. MBWANA HAJI: alisema kuwa mawasiliano hayapo kati ya wananchi na wachaguliwa hasa katika serikali ngazi za chini.4.16. ALI MAKATA: alizungumzia kuzuizi cha mawasiliano kwa maana ya kutokuwepo kwa mawasiliano kati ya viongozi na wananchi.4.17. AHMED KHATIB: alisema kuwa viongozi wanashughulika wakati wa uchaguzi na hawakutani na wananchi baada ya hapo. Alitaka viongozi wapewe mafunzo juu ya uongozi.

5.0. Mragbishi wa Mdahalo alitoa nafasi kwa Mbunge kuzungumza. Mbunge huyo alieleza kusikitishwa kwake na viongozi wengine wa ngazi mbalimbali kutokuhudhuria pamoja na kupata taarifa. Alisema kuwa wangekuwepo wangesikia wananchi wanavyosema. Alijibu suala la mbunge kuwa waziri na kusema kuwa ni suala la mfumo.aliwataka wanatanga kupigana na uamskini kwa kujituma. Aliahidi kulifanyia kazi suala la kiwanda cha chokaa kutumia miembe kuzalisha chokaa. Aliwataka wakazi wa Tanga kutumia fuirsa za mikutano kujadili maendeleo yao. Na baada ya hapo alichukua muda kueleza suala la matatizo yaliyojiri katika wizara yake.

6. Mwisho Mragbishi aliwataka wananchi kuijiuliza wanatumiaje fursa ya kukutana na Mbunge kwenda mbele na akaahidi kulifanyia kazi ombi la mbunge la kupeleka midahalo katika ngazi ya kata. Baada ya hapo iliundwa timu ya ufuatiliaji na mdahalo ulifungwa saa 8.31 mchana.