tafsiri rahisi ya mpango wa maendeleo ya afya ya msingi 2007-2017

34
TAFSIRI RAHISI YA MPANGO WA MAENDELEO YA AFYA YA MSINGI (MMAM) 2007-2017

Upload: vijanaforum

Post on 09-Mar-2016

408 views

Category:

Documents

24 download

DESCRIPTION

Tafsiri Rahisi ya Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi 2007-2017

TRANSCRIPT

TAFSIRI RAHISI YA MPANGO WA MAENDELEO YA AFYA YA MSINGI

(MMAM) 2007-2017

Kimeandaliwa na kuchapishwa na Sikika

Tafsiri Rahisi ya Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM) 2007-2017

TAFSIRI RAHISI YA MPANGO WA

MAENDELEO YA AFYA YA MSINGI (MMAM)

2007-2017

Kimetolewa na Sikika (Zamani YAV)S.L.P 12183 Dar Es Salaam

Simu +255 22 2666355/7 | Nukushi +255 22 2668015Barua-pepe: [email protected],

Tovuti www.sikika.or.tz©Sikika 2010

Kimeandaliwa na kuchapishwa na Sikika

Tafsiri Rahisi ya Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM) 2007-2017

Shukrani

Sikika ni shirika lisilo la kiserikali linalotekeleza shughuli mbalimbali zenye lengo la kuchochea upati kanaji wa huduma za afya zenye uwiano, ubora unaokubalika, zilizo nafuu na endelevu. Moja ya kazi za shirika ni kutafsiri kwa lugha rahisi na ya kueleweka kwa wananchi wote nyaraka mbalimbali zikiwemo sera, miongozo, mipango na sheria mbalimbali kati ka utoaji wa huduma za afya. Ni kutokana na ukweli kwamba nyaraka hizi huwa kati ka lugha za kigeni ama za kitaalamu kwa mwananchi wa kawaida kuelewa. Hali hii inarudisha nyuma nguvu ya wananchi kati ka kufuati lia utekelezaji wa mipango, sera, sheria na miongozo hiyo.

Sikika imeandaa kijitabu hiki ili kumpati a fursa mwananchi wa kawaida kujua, kufuati lia na kushiriki kati ka kutekeleza mpango wa serikali wa kuboresha na kusogeza huduma bora za afya ya msingi kwa kila mwananchi. Pia kijitabu hiki kitawasaidia watendaji wote wanaohusika na utekelezaji wa mpango huu, kuelewa kwa urahisi majukumu yao kutokana na urahisi wa kijitabu hiki pamoja na sababu nyingine ambazo zitawafanya kushindwa kupata na kusoma mpango mama.

Kukamilika kwa kijitabu hiki kulihitaji juhudi na jiti hada za wadau mbalimbali. Sikika inatambua mchango mkubwa wa ndugu Geofrey Chambua kwa ushauri, uchambuzi na kuboresha manti ki ya kijitabu hiki pamoja na ndugu Nathan Mpangala kwa kukisanifu kijitabu hiki kwa michoro ya kuvuti a (katuni). Kwa namna ya pekee, Sikika inawashukuru wafanyakazi pamoja na vijana wake wa kujitolea kwa mchango wao mkubwa wa mawazo, maoni na kukipiti a kwa ujumla wake kijitabu hiki.

Ingawa si rahisi kumshukuru mtu mmoja mmoja kwa ushiriki wake, Sikika inatambua thamani ya mchango wa wale wote walioshiriki kwa namna moja ama nyingine kati ka kukamilisha kijitabu hiki.

Irenei KiriaMKURUGENZI MTENDAJI Sikika

i

Kimeandaliwa na kuchapishwa na Sikika

Tafsiri Rahisi ya Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM) 2007-2017

Tafsiri Ya Maneno ya Msingi

CCHP Mpango Kabambe wa Afya wa Halmashauri (Comprehensive Council Health Plan)

CHF Community Health Fund (Mfuko wa Afya ya Jamii)

HSR Health Sector Reforms - Mabadiliko kati ka Sekta ya Afya.

HSSP Health Sector Strategic Plan - Mpango Mkakati wa Sekta ya Afya

MMAM Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi

MKUKUTA Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini Tanzania

NACP Nati onal AIDS Control Program - Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI

NHIF Nati onal Health Insurance Fund (Bima ya Afya )

PPP Public Private Partnership (Ushirikiano baina ya Serikali na Sekta Binafsi)

SAFE Sugery for in-turned eyelids, Anti bioti cs for acti ve disease, Face washing to prevent infecti on and Environment changes – Mkakati wa kutokomeza ugonjwa wa macho (vikope)

TAMISEMI Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

TDHS Tanzania Demographic Health Survey Utafi ti wa Takwimu za Afya Tanzania

UKIMWI Upungufu wa Kinga Mwilini

VVU Virusi Vya UKIMWI

WHO World Health Organisati on (Shirika la Afya Duniani)

YAV Youth Acti on Volunteers

ii

Kimeandaliwa na kuchapishwa na Sikika

Tafsiri Rahisi ya Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM) 2007-2017

YALIYOMO

Shukrani i

Tafsiri ya Maneno ya msingi ii

1.0 VIFUNGU VYA AWALI 1

1.1 Utangulizi 1

1.2 Hali Halisi ya Huduma za Afya Tanzania 1

1.3 Hali ya Huduma za Afya ya Msingi Nchini Tanzania 1

2.0 SERA, MIPANGO NA MIKAKATI MBALIMBALI KATIKA KUBORESHA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA YA MSINGI NCHINI TANZANIA 3

2.1 Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 3

2.2 Malengo ya Maendeleo ya Milenia 3

2.3 Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania (MKUKUTA) 3

2.4 Sera ya Afya , 2007 4

2.5 Mpango Mkakati wa Sekta ya Afya - HSSPIII 4

2.6 Mpango wa Maboresho kati ka Utumishi wa Umma 4

2.7 Mabadiliko kati ka Sekta ya Afya - HSR 5

2.8 Waraka wa Sera ya Kuboresha Muundo wa Serikali za Mitaa. 5

3.0 MPANGO WA MAENDELEO YA AFYA YA MSINGI (MMAM) 6

3.1 Maelezo ya Mpango 6

3. 2 Malengo ya Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi 6

3.2.1 Lengo kuu la MMAM 6

3.2.2 Malengo mahususi 6

4.0 MAENEO MAKUU YALIYOAINISHWA KATIKA MPANGO WA

MAENDELEO YA AFYA YA MSINGI 8

4.1 Rasilimali Watu Kati ka Sekta ya Afya 8

4.2 Utoaji Huduma za Afya Kati ka Ngazi ya Wilaya 9

4.3 Huduma za Afya kwa Mama Wajawazito na Watoto. 10

iii

Kimeandaliwa na kuchapishwa na Sikika

Tafsiri Rahisi ya Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM) 2007-2017

4.4 Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI (NACP) 12

4.5 Malaria 13

4.6 Kifua Kikuu na Ukoma 14

4.7 Uimarishaji Afya na Elimu kwa Umma 15

4.8 Lishe Bora 16

4.9 Ushirikiano baina ya Serikali na Sekta Binafsi (PPP) 16

4.10 Tiba Asilia na Tiba Mbadala 17

4.11 Magonjwa Yasiyoambukiza 18

4.12 Magonjwa Yanayosahaulika 19

4.13 Afya Mazingira 20

4.14 Uraghabishi na Uhamasishaji 21

4.15 Mfumo wa utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo ya

Afya ya Msingi 21

4.15.1 Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii 21

4.15.2 TAMISEMI 22

4.14.3 Ngazi ya Mikoa 22

4.15.4 Ngazi ya Halmashauri 23

4.15.5 Ngazi ya Kata na Vijiji 23

4.15.6 Bodi ya Huduma ya Afya ya Halmashauri 23

4.15.7 Kamati ya Afya ya Kituo 24

4.16 Rasilimali Fedha kati ka Sekta ya Afya 24

4.17 Tathmini na Usimamizi wa Utekelezaji wa Mpango 25

5.0 HITIMISHO 25

iv

Kimeandaliwa na kuchapishwa na Sikika

Tafsiri Rahisi ya Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM) 2007-2017

1.0 VIFUNGU VYA AWALI

1.1 UTANGULIZIMaradhi ni mojawapo ya maadui watatu ukiacha ujinga na umasikini ambao serikali imekuwa ikipigana nayo tangu Tanzania ipate uhuru wake mwaka 1961. Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM) ni mojawapo ya mikakati ya serikali ya kutokomeza adui maradhi. Chimbuko la mpango huu ni Sera ya Afya ya mwaka 1990 iliyorejewa mwaka 2007 inayoelekeza kuongeza kasi ya kusogeza huduma bora za afya ya msingi kwa kila mwananchi ili kuboresha hali ya ustawi wa maisha na kukuza uchumi wa kipato. Ongezeko la watu na nia ya serikali ya kurudisha madaraka kati ka ngazi ya serikali za mitaa pia ni sababu zingine za kuanzishwa kwa mpango huu.

1.2 HALI HALISI YA HUDUMA ZA AFYA TANZANIATanzania inakabiliwa na ongezeko kubwa la maradhi. Malaria imekuwa ni miongoni mwa magonjwa yanayosababisha vifo vya watanzania wengi hususani wakina mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano ikifuati wa na UKIMWI na kifua kikuu. Magonjwa haya matatu yamekuwa ni kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya huduma za afya nchini pamoja na kusababisha kupungua kwa wastani wa umri wa kuishi wa Mtanzania hadi kufi kia miaka 51. Kwa mujibu wa takwimu za afya za TDHS (2004-2005), watoto 112 kati ya 1000 wenye umri chini ya miaka 5 hufariki dunia kila mwaka. Pia akina mama 578 kati ya 100,000 hufariki dunia kwa mwaka kutokana na matati zo mbalimbali wakati wa kujifungua. Hii ni wastani wa akina mama 24 wanaofariki kwa siku au mwanamke mmoja kila baada ya saa moja. Takwimu hizi zinalenga kati ka kuonesha changamoto kubwa zinazoikabili serikali kati ka kukabiliana na utoaji wa huduma za afya ya msingi hapa nchini.

1.3 Hali ya Huduma za Afya ya Msingi Nchini Tanzania Huduma za afya ya msingi zipo kati ka mfumo wa Piramidi ambao huundwa na huduma kutoka kati ka ngazi ya zahanati , vituo vya afya na hospitali za wilaya. Kwa sasa Tanzania ina jumla ya zahanati 4679, vituo vya afya 481 pamoja na hospitali 219. Zahanati na vituo vya afya ambavyo ndizo nguzo kuu za huduma za afya ya msingi hutoa huduma za awali kwa watanzania kati ya elfu kumi (10,000) kwa Zahanati na elfu hamsini (50,000) kwa kituo cha afya. Hata hivyo kasi ya ongezeko la idadi ya watu, upungufu wa watumishi wenye sifa, upungufu wa nyenzo, madawa, umbali wa vituo vya kutolea huduma, ubovu wa barabara pamoja na tati zo la usafi ri wenye uhakika ni changamoto kubwa zinazokabili utoaji wa huduma za afya ya msingi hapa nchini.

1

Kimeandaliwa na kuchapishwa na Sikika

Tafsiri Rahisi ya Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM) 2007-2017

2

Kimeandaliwa na kuchapishwa na Sikika

Tafsiri Rahisi ya Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM) 2007-2017

2.0 SERA, MIPANGO NA MIKAKATI MBALIMBALI KATIKA KUBORESHA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA YA MSINGI NCHINI TANZANIA

Serikali imeandaa misingi ya kisera na kuweka mazingira mazuri ya utekelezaji ili kuboresha huduma za afya nchini. Misingi hii ambayo ni chimbuko la MMAM ni ya kitaifa na kimataifa kama ilivyoainishwa hapo chini.

2.1 Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 Lengo kuu la Dira hii ni kuboresha maisha ya mtanzania kwa kuboresha afya ya msingi, afya ya uzazi, kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto, kuongeza umri wa kuishi, upati kanaji wa maji safi na salama kwa wote, uhakika wa chakula cha kutosha na salama, kufi kia lengo la usawa wa kijinsia kati ka ngazi mbalimbali za maamuzi ya kiafya na kuhamasisha ushiriki wa wananchi kati ka mipango ya utoaji wa huduma za afya.

2.2 Malengo ya Maendeleo ya Milenia Kama ilivyo kwa dira ya maendeleo ya taifa 2025, malengo ya Milenia pia yanalenga kupunguza robo tatu ya vifo vya watoto chini ya miaka 5, kuboresha afya ya mama wajawazito kwa kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi pamoja na kupiga vita UKIMWI, malaria na magonjwa mengine

2.3 Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania (MKUKUTA)Mkakati huu mbali na malengo mengine, pia unalenga kuboresha maisha na ustawi wa jamii ya Watanzania kwa kuitaka wizara ya afya na ustawi wa jamii kutumia kiasi kikubwa cha bajeti yake kwa ajili ya chanjo dhidi ya magonjwa kwa watoto chini ya miaka mitatu, afya ya uzazi, kuzuia malaria, Virusi vya UKIMWI, Kifua kikuu na Ukoma.

3

Kimeandaliwa na kuchapishwa na Sikika

Tafsiri Rahisi ya Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM) 2007-2017

2.4 Sera ya Afya , 2007 Dira ya Sera ya Afya ni kuwa na jamii yenye afya ambayo itachangia kikamilifu kati ka maendeleo binafsi na ya taifa kwa ujumla. Pia sera hii inakusudia kutoa huduma muhimu za afya zenye uwiano wa kijiografi a, viwango vya ubora unaokubalika, gharama nafuu na zilizo endelevu.

2.5 Mpango Mkakati wa Sekta ya Afya - HSSPIII Mpango huu unajumuisha uboreshaji wa huduma za afya kati ka ngazi za wilaya, mkoa, na taifa ikijumuisha hospitali za rufaa za kanda na maalum. MMAM inalenga kuboresha huduma za afya kati ka ngazi ya wilaya kama moja ya malengo ya HSSP III.

2.6 Mpango wa Maboresho kati ka Utumishi wa Umma Mpango huu una lengo la kuboresha utumishi wa umma ili uwe na mpango endelevu wa kuboresha huduma za jamii kwa kuzingati a uwezo na ufanisi wa wataalamu waliobobea kati ka fani hizo. Hili ni moja ya lengo muhimu la MMAM.

4

Kimeandaliwa na kuchapishwa na Sikika

Tafsiri Rahisi ya Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM) 2007-2017

2.7 Mabadiliko kati ka Sekta ya Afya - HSR Huu ni mkakati wa Serikali wenye lengo la kuimarisha utoaji wa huduma za afya na zinazokidhi mahitaji kwa jamii. Mabadiliko haya yameainisha mikakati ti sa muhimu ambayo ni;

• Utoaji wa huduma kati ka ngazi ya wilaya• Mabadiliko kati ka Huduma za Hospitali• Majukumu ya Wizara ya afya na Ustawi wa Jamii • Uboreshaji na maendeleo ya rasilimali watu kati ka sekta ya afya• Mfumo wa usambazaji huduma• Rasilimali fedha• Ushirikiano baina ya sekta binafsi na serikali• Urati bu wa Ushirikiano na Wahisani• Udhibiti UKIMWI.

2.8 Waraka wa Sera ya Kuboresha Muundo wa Serikali za Mitaa. Maboresho haya ni pamoja na kuweka mgawanyo wa madaraka kwa kuunda mfumo wa serikali za mitaa zenye uhuru wa kujiamulia mambo yake na mipango yake ya maendeleo kuanzia ngazi ya jamii.

5

Kimeandaliwa na kuchapishwa na Sikika

Tafsiri Rahisi ya Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM) 2007-2017

3.0 MPANGO WA MAENDELEO YA AFYA YA MSINGI (MMAM)

3.1 Maelezo ya MpangoTangu uhuru, serikali imekuwa ikiti lia mkazo suala la upati kanaji wa huduma bora za afya kwa kila mwananchi hususani kwa wanaoishi kati ka maeneo ya pembezoni, ingawa azma hii imekuwa ikigonga mwamba kutokana na vikwazo mbalimbali. Moja ya vikwazo hivi ni kutokuwepo kwa uwiano wa vituo vya huduma hususani kati ka maeneo ya vijijini, umbali kati ya vituo vya huduma na makazi ya wananchi, ubovu wa miundombinu, upungufu wa wataalamu wa afya na vifaa. Kutokana na vikwazo hivi, serikali kupiti a mpango huu inadhamiria kusogeza na kuboresha huduma za afya kati ka ngazi ya Halmashauri ambapo wananchi wateweza kupata huduma kwa urahisi.

3. 2 Malengo ya Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi

3.2.1 Lengo kuu la MMAM Kuboresha huduma za afya ya msingi ifi kapo mwaka 2017.

3.2.2 Malengo mahususi• Kukarabati na kuanzisha vituo vya huduma za afya kati ka ngazi zote ili

kuleta usawa na kurahisisha upati kanaji wa huduma za afya,• Kuanzisha taasisi za mafunzo ya afya ili kuhakikisha upati kanaji wa

watumishi wa kutosha, wenye sifa na ujuzi, • Kuwajengea uwezo wafanyakazi, kupandisha daraja na kuendeleza

watumishi wa afya walioko kazini ili kukabiliana na mahitaji na changamoto kati ka kutoa huduma za afya,

• Kuboresha mfumo wa taarifa na kumbukumbu za watumishi wa afya, • Kuhakikisha uwepo wa vifaa, dawa na mahitaji mengine kati ka vituo vya

huduma yanayokidhi viwango na ubora wa huduma za afya, • Kuimarisha ufanisi kati ka mfumo wa rufaa kwa wagonjwa na ikiwezekana

kuwa na kliniki zinazotembea (za magari) ili kuwafi ka wananchi kati ka maeneo yao na hivyo kupunguza rufaa zisizo za ulazima

• Kuongeza bajeti ya sekta ya afya kwa lengo la kufi kia Azimio la Abuja la asilimia 15.

6

Kimeandaliwa na kuchapishwa na Sikika

Tafsiri Rahisi ya Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM) 2007-2017

7

Kimeandaliwa na kuchapishwa na Sikika

Tafsiri Rahisi ya Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM) 2007-2017

4.0 MAENEO MAKUU YALIYOAINISHWA KATIKA MPANGO WA MAENDELEO YA AFYA YA MSINGIIli malengo ya MMAM ya kuhakikisha kuwa kila mwananchi anafi kiwa na huduma za afya ya msingi karibu na eneo analoishi yati mie, yafuatayo ni maeneo muhimu ya utekelezaji yaliyoainishwa kati ka mpango huu.

• Rasilimali watu kati ka sekta ya afya• Utoaji huduma za afya kati ka ngazi ya wilaya• Huduma za afya kwa mama wajawazito na watoto• Malaria• Janga la UKIMWI• Kifua kikuu na ukoma• Magonjwa yasiyoambukiza• Afya Mazingira• Uimarishaji wa Afya na Elimu kwa Umma • Lishe bora• Tiba za asili• Magonjwa yanayosahaulika• Ushirikiano baina ya serikali na sekta binafsi• Uraghabishi na uhamasishaji• Mfumo wa utekelezaji wa Mpango • Rasilimali fedha kati ka sekta ya afya• Ufuati liaji na tathimini

Maeneo haya yameonekana kuwa na changamoto nyingi ambazo zinahitaji kufanyiwa kazi ili mpaka kufi kia mwaka 2017 lengo la MMAM la kuboresha na kusogeza huduma za afya ya msingi kwa watanzania wote liwe limeti mia.

4.1 Rasilimali Watu Kati ka Sekta ya AfyaMiongoni mwa changamoto kubwa inayoikabili sekta ya afya ni pamoja na upungufu wa watumishi kwa takribani asilimia 67.9 ambayo ni sawa na watumishi 31,808 kati ka kada zote. Hii inachangiwa kwa kiasi kikubwa na kasi ya ongezeko la idadi ya watu pamoja na milipuko ya magonjwa mbalimbali. Zaidi ya yote, hata wale wahudumu wachache waliopo hulazimika kuacha kazi na kutafuta ajira kati ka sekta zingine.

8

Kimeandaliwa na kuchapishwa na Sikika

Tafsiri Rahisi ya Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM) 2007-2017

Malengo ya MMAM

• Kusomesha watumishi na wakufunzi wengi zaidi pamoja na kuajiri na kujengea uwezo wafanyakazi wanaokubali kufanya kazi kati ka maeneo yaliyoko pembezoni.

Mikakati

• Kuwaongezea watumishi moti sha na kuwapati a mahitaji yanayoendana na hadhi yao ili kuongeza ti ja na ufanisi kati ka kuboresha huduma za afya nchini.

• Kuhakikisha upati kanaji wa vitendea kazi na dawa za kutosha kwa wahudumu ili kuwapa moti sha na moyo wa kuendelea kufanya kazi.

4.2 Utoaji Huduma za Afya Kati ka Ngazi ya Wilaya Utoaji wa huduma za afya kati ka ngazi ya wilaya unakabiliwa na changamoto zifuatazo;

• Upungufu wa vifaa muhimu kwa ajili ya utoaji wa huduma za afya kama vile samani, vifaa vya usafi ri na mawasiliano, dawa muhimu, maji, vifaa vya kuhifadhi taka, mfumo duni wa rufaa na usimamizi kati ka uendeshaji wa vituo vya huduma za afya.

• Uhaba wa watumishi wenye sifa na ujuzi kati ka kutoa huduma za afya.• Umbali baina ya vituo vya huduma na maeneo ya wananchi pamoja na misululu

mirefu ya wagonjwa kwenye vituo huduma.• Ufi nyu wa bajeti kwa ajili ya kuendeshea huduma na kuboresha miundombinu.

9

Kimeandaliwa na kuchapishwa na Sikika

Tafsiri Rahisi ya Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM) 2007-2017

Malengo ya MMAM

• Kukarabati , kujenga na kuboresha zahanati , vituo vya afya na hospitali za wilaya pamoja na kuzipati a vifaa vya kutosha kama vile samani, vifaa vya usafi ri na mawasiliano, kliniki zinazohamishika, dawa muhimu (hususani za Kifua kikuu na Ukoma).

Mikakati

• Kuimarisha mfumo wa rufaa kwa wagonjwa na kuongeza uwezo wa uongozi kitaaluma.

• Kuimarisha taasisi za utoaji mafunzo ya afya kwa kuzipati a vifaa na dhana za kufundishia, ili kuongeza usaili wa wanafunzi wa fani mbalimbali za masuala ya afya kwa lengo la kuongeza wataalamu wa afya.

• Kutenga fedha za kutosha kwa ajili ya kuendeshea huduma za afya za wilaya.

4.3 Huduma za Afya kwa Mama Wajawazito na Watoto.Ingawa inakadiriwa kuwa asilimia themanini (80%) ya watanzania wote hupata huduma za afya chini ya umbali wa kilometa 5, lakini vifo vya akina mama wajawazito, watoto na watoto wachanga vimekuwa vikiongezeka. Akina mama 578 kati ya 100,000 hufariki dunia kutokana na matati zo ya uzazi. Vifo hivi husababishwa na;

• Upungufu wa wataalamu na mabingwa wa huduma ya mama wajawazito na watoto wachanga. Ni asilimia arobaini na sita tu (46%) ya kina mama wanaojifungua chini ya uangalizi wa wataalam waliobobea kati ka vituo vya huduma nchini. Wahudumu hao wachache waliopo, huelemewa na idadi kubwa ya wagonjwa wanaowahudumia,

• Umaskini,• Umbali kati ya vituo vya huduma na makazi ya wananchi,• Ubovu wa miundombinu,• Lugha chafu pamoja na manyanyaso kutoka kwa watoa huduma hasa wakunga,• Upungufu wa vitendea kazi kama vile; dawa, magari ya kubebea wagonjwa,

vyumba vya upasuaji, vyumba vya kulaza wagonjwa, akiba za damu salama na kiliniki za kuhamishika ambazo zingetumika kuokoa maisha ya akina mama na watoto wengi endapo vingepati kana kwa wakati na kulingana na mahitaji,

• Ukosefu wa huduma rafi ki za uzazi kwa vijana. Hii husababisha matati zo na vifo vingi vitokanavyo na uzazi kwa vijana wenye umri mdogo (chini ya miaka 19).

10

Kimeandaliwa na kuchapishwa na Sikika

Tafsiri Rahisi ya Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM) 2007-2017

Malengo ya MMAM• Kupunguza vifo vya akina mama wajawazito kutoka 578 hadi kufi kia 175

kwa kila vizazi hai 100,000.• Kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka 5 kutoka 112 hadi 45 kwa kila

watoto 1,000 wanao zaliwa hai• Kuongeza idadi ya wanawake wajawazito wanaohudumiwa na wahudumu

wa afya wenye ujuzi, uzoefu na utalaamu wa kutosha kutoka asilimia arobaini na sita (46%) hadi kufi kia asilimia themanini na nane (88%).

Mikakati .

• Kuhakikisha uwepo wa vifaa kama vile redio za masafa, magari ya kubebea wagonjwa, kujenga na kuongeza vyumba vya upasuaji, wodi za kulaza wagonjwa na idadi ya kliniki.

• Kuongeza idadi ya wanafunzi wanaodahiliwa kati ka vyuo vya mafunzo ya afya na pia kuwapati a mafunzo ya ziada watumishi wa afya ili kuongeza uwezo wao kitaaluma pamoja na kuajiri kwa mikataba madaktari bingwa wa akinamama na watoto.

11

Kimeandaliwa na kuchapishwa na Sikika

Tafsiri Rahisi ya Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM) 2007-2017

4.4 Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI (NACP)Moja ya changamoto kubwa inayoikumba serikali, jamii, kaya na watu binafsi ni janga la UKIMWI. Mbali na kusababisha vifo vingi, UKIMWI umeathiri nguvu kazi ya taifa pamoja na kuongeza mzigo wa gharama za kuwahudumia waathirika wa VVU. Kutokana na changamoto hizi MMAM inalenga kuongeza nguvu zaidi kwa NACP ili kuweza kuwafi kia wananchi wengi zaidi kati ka kutoa huduma za mati babu pamoja na za kijamii, ikiwa ni pamoja na kutoa dawa za kurefusha maisha kwa waathirika wa VVU, vifaa vya maabara na huduma za kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto

Malengo ya MMAM• Kuti bu na kutunza watu waishio na VVU kutoka idadi ya watu 440,000 kwa

mwaka 2008 hadi kufi kia idadi ya watu 800,000 kwa mwaka 2017 • Kuongeza huduma za kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda

kwa mtoto kati ka vituo vyote vinavyotoa huduma za mama na mtoto Mikakati • Kuzuia kuenea zaidi kwa virusi vya UKIMWI• Kutoa mafunzo kwa watoa huduma za afya kati ka hospitali za wilaya, vituo

vya afya na zahanati ya jinsi ya kuwahudumia waathirika wa UKIMWI pamoja na kutoa dawa na vifaa ti ba vya kutosha ili waweze kuwahudumia wagonjwa wengi zaidi

• Kuwawezesha wananchi kwa kuwapa miongozo ili kutoa huduma kwa wagonjwa wa majumbani

12

Kimeandaliwa na kuchapishwa na Sikika

Tafsiri Rahisi ya Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM) 2007-2017

4.5 Malaria Kila mwaka kati ya watu milioni kumi na saba hadi ishirini (17-20) wanaugua malaria, na kati yao, watu laki moja (100,000) hufariki dunia. Wagonjwa wengi wanaougua malaria ni akina mama wajawazito na watoto. Umaskini husababisha baadhi ya wajawazito kushindwa kumudu gharama za vyandarua vyenye dawa ili kujikinga na mbu waenezao malaria. Takribani asilimia thelathini na sita (36%) ya vifo vya watoto chini ya umri wa miaka mitano (5), vinatokana na malaria. Kutokuwepo kwa uelewa wa kutosha kwa wananchi juu ya mazalia ya mbu pamoja na upungufu wa wataalam, dawa na vifaa ti ba, ni moja ya sababu za kuenea kwa ugonjwa huu.

Malengo ya MMAM

• Kupunguza makali ya malaria kwa asilimia 80% ifi kapo mwaka 2017

Mikakati

• Kusambaza na kugawa bure vyandarua vyenye dawa kwa akina mama wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano,

• Kutoa elimu kwa jamii ya jinsi ya kujikinga na malaria • Kupulizia dawa majumbani na sehemu za mazalia ya mbu ili kudhibiti

ugonjwa huo.

13

Kimeandaliwa na kuchapishwa na Sikika

Tafsiri Rahisi ya Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM) 2007-2017

4.6 Kifua Kikuu na Ukoma Kifua Kikuu na Ukoma ni moja ya magonjwa yanayoendelea kuwatesa watanzania walio wengi. Kwa mwaka 2004, zaidi ya watanzania 64,000 waliugua Kifua kikuu na watanzania 4500 (sawa na watu 1.4 kwa kila watu 10,000) waliugua ukoma. Takwimu hii imevuka viwango vilivyowekwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) ya kila watu 10,000, mtu mmoja huugua ukoma. Kifua kikuu huathiri kwa kiasi kikubwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI, pamoja na watu wanaoishi kati ka mazingira magumu. Kadhalika asilimia kumi (10%) ya watu wenye ukoma wana ulemavu wa kudumu.

Magonjwa haya yamekuwa ni changamoto kubwa kati ka jamii kutokana na uchache wa wahudumu wa afya, ufi nyu wa bajeti , upungufu wa dawa na vifaa pamoja na kutokuwepo kwa uelewa wa jamii kuhusiana na maambukizi, kinga na ti ba ya magonjwa haya. Hali hii inasababisha vifo, kuongezeka kwa unyanyapaa na matati zo ya kisaikolojia kwa wagonjwa.

Malengo ya MMAM

• Kupunguza idadi ya watu wanaougua au kufa kwa ugonjwa wa kifua kikuu kwa asilimia hamsini (50%) hadi kufi kia 2017,

• Kupunguza ugonjwa wa ukoma kutoka kiwango cha watu 1.4 wanaougua mpaka kufi kia kiwango cha chini ya mtu mmoja kati ya watu 10,000 mpaka kufi kia 2017

Mikakati .

• Kuongeza watumishi wa afya wenye utaalam, • Kuimarisha bajeti na kuhakikisha upati kanaji wa dawa na vifaa ili kuwezesha

uchunguzi, kuzuia na kuti bu kifua kikuu na ukoma kwa wagonjwa hususani kwa watu wenye virusi vya UKIMWI na wanaoishi kati ka mazingira magumu.

• Kuendesha kampeni nchi nzima za kuwajengea wananchi uwezo wa jinsi ya kujikinga, kugundua na kuti bu kifua kikuu na ukoma mapema. Mkakati huu utajumuisha pia mbinu ya ufuati liaji na kutoa takwimu na taarifa sahihi za kifua kikuu na UKIMWI kwa wadau mbalimbali kwa ajili ya kuchukua hatua madhubuti .

14

Kimeandaliwa na kuchapishwa na Sikika

Tafsiri Rahisi ya Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM) 2007-2017

4.7 Uimarishaji Afya na Elimu kwa UmmaUimarishaji Afya na elimu kwa Umma ni njia muhimu ya kuwashirikisha wananchi kati ka shughuli za kuboresha huduma za afya pamoja na kujikinga na baadhi ya magonjwa. Njia hii pia itasaidia kushirikisha wadau wote kati ka kufanikisha na kuti miza malengo ya MMAM.

Lengo ya MMAM

• Kuijengea uwezo jamii ili iweze kushirikia kati ka kutunza afya zao wenyewe

Mikakati

• Kuchochea uwelewa wa jamii na wadau wengine ili waweze kushiriki kikamilifu kati ka utekelezaji wa MMAM

15

Kimeandaliwa na kuchapishwa na Sikika

Tafsiri Rahisi ya Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM) 2007-2017

4.8 Lishe BoraIngawa tati zo la utapia mlo limepungua nchini kutoka asilimia 44% hadi 38% kati ya mwaka 1999 na 2004, bado kuna changamoto ya jamii kutokuchukua hatua za kuimarisha lishe bora. Hii inatokana na uhaba wa wataalam wa kurati bu shughuli za lishe bora kati ka ngazi ya jamii na wilaya.

Malengo ya MMAM

• Kujenga uelewa na uwezo wa kushugulikia masuala ya lishe bora kati ka ngazi ya jamii na Wilaya

Mikakati

• Kusomesha na kuajiri wataalamu wa kurati bu masuala ya lishe bora.

4.9 Ushirikiano baina ya Serikali na Sekta Binafsi (PPP) Mara tu baada ya Uhuru, huduma zote za afya zilikuwa zikitolewa bure na serikali. Kutokana na ongezeko la magonjwa na ufi nyu wa rasilimali, serikali ilianzisha mfumo wa kushirikisha watu binafsi kati ka kutoa huduma za afya nchini. Kwa sasa asilimia arobaini (40%) ya vituo vyote vya huduma za afya nchini, vinamilikiwa na watu binafsi. Changamoto kubwa kwa sasa ni kuwa zaidi ya asilimia 90% ya vituo binafsi vipo mijini na kuacha asilimia kubwa ya watanzania takribani 80% inayoishi vijijini kukosa huduma muhimu za afya.

16

Kimeandaliwa na kuchapishwa na Sikika

Tafsiri Rahisi ya Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM) 2007-2017

Malengo ya MMAM

• Kuimarisha na kukuza ushiriki wa sekta binafsi kati ka kutekeleza Mpango wa Maendeleo ya afya ya msingi nchini kote

Mikakati

• Kuandaa na kufanyia marekebisho miongozo mbalimbali kwa ajili ya kufuati lia huduma za afya ambazo zinatolewa na watu binafsi ili zilingane na zile zinazotolewa kati ka vituo vya umma

• Serikali na sekta binafsi zitashirikiana kutoa huduma za afya kwa jamii kwa kuzingati a sera na miongozo ya utoaji wa huduma hiyo nchini.

4.10 Tiba Asilia na Tiba Mbadala Ingawa Tiba asilia na ti ba mbadala zimekuwa zikitumiwa na watanzania wengi, takribani asilimia 53 - 60% ya wakina mama hujifungulia kwa wakunga wa jadi; huduma hizi zimekuwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutokuwepo kwa elimu ya kutosha ya utaalamu wao, kutokutambuliwa kisheria kwa watoa huduma asilia, uhaba wa vifaa maalum iwapo dharura inatokea, kukosekana kwa taarifa na kumbukumbu za mati babu yao, kutokuwepo kwa mfumo wa ufuati liaji na tathmini wa huduma zao, imani za kishirikina na ukosefu wa tafi ti za kina.

17

Kimeandaliwa na kuchapishwa na Sikika

Tafsiri Rahisi ya Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM) 2007-2017

Malengo ya MMAM

• Kuhakikisha kwamba, wananchi wanapata ti ba asilia na ti ba mbadala zenye kuzingati a ubora wa hali ya juu, na ambazo zimethibiti shwa kwa kuzingati a utafi ti uliokamilika bila kuathiri maslahi ya upande wowote.

• Kurasimisha watoa huduma asilia pamoja na kuhakiki, kusajili na kuthibiti sha rasmi dawa asilia

Mikakati

• Kuanzisha na kufungua vituo rasmi vya huduma asilia

• Kufanya tafi ti kwa taasisi zote zinazojishughulisha na utoaji wa dawa asilia na ti ba mbadala ili kupati wa hati miliki na serikali.

• Kuandaa mpango maalum kwa watoa huduma za asili kufanya ufuati liaji wa wagonjwa wao, kutayarisha na kutoa taarifa kwa serikali juu ya maendeleo ya ti ba zao

4.11 Magonjwa YasiyoambukizaTanzania inakabiliwa na changamoto ya ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza kama vile, kisukari, magonjwa ya moyo, saratani, utapia mlo, magonjwa ya akili na waathirika wa mihadarati . Hata hivyo, idadi ya watumishi wenye sifa na ujuzi wa kushughulikia magonjwa haya haiendani na wingi wa mahitaji. Pia wananchi wengi hawana uelewa kuhusu jinsi ya kuchunguza, kugundua na kujikinga na magonjwa haya

Malengo ya MMAM

• Kuboresha huduma ya kinga na udhibiti wa magonjwa yasiyoambukiza kati ka ngazi ya msingi kabisa ya utoaji huduma za afya

Mikakati

• Kutoa mafunzo ya awali kwa watoa huduma za afya kuhusiana na jinsi ya kugundua, kuti bu na kuhudumia watu wenye magonjwa haya

• Kuwashirikisha wananchi na wadau wengine kati ka kuzuia na kujikinga na magonjwa haya.

18

Kimeandaliwa na kuchapishwa na Sikika

Tafsiri Rahisi ya Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM) 2007-2017

4.12 Magonjwa YanayosahaulikaMagonjwa yanayosahaulika hujumuisha usubi, matende, minyoo, kichocho na magonjwa ya macho (vikope). Inakadiriwa kuwa takribani watanzania milioni mbili wapo kati ka hatari ya kuugua ugonjwa wa usubi. Minyoo na kichocho huwapata zaidi wanafunzi wa shule za msingi.

Malengo ya MMAM

• Kupunguza wingi wa magonjwa haya na ikiwezekana kuyatokomeza kabisa mpaka ifi kapo mwaka 2017

Mikakati

• Kutekeleza mkakati wa (SAFE) wa kutokomeza ugonjwa wa vikope kwa; kufanya upasuaji kwa wagonjwa wenye matati zo makubwa, kutoa dawa kwa ajili ya kuti bu na kuzuia maambukizi yasienee, kampeni ya usafi wa mtu binafsi (hasa uso) pamoja na mazingira ili kuzuia maambukizi.

• Kuendeleza programu za afya mashuleni ili kutokomeza magonjwa ya minyoo na kichocho kwa wanafunzi

• Kuendeleza programu za kuzuia kusambaa kwa Ugonjwa wa matende

19

Kimeandaliwa na kuchapishwa na Sikika

Tafsiri Rahisi ya Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM) 2007-2017

4.13 Afya Mazingira Afya mazingira inajumuisha usafi wa mazingira, matumizi sahihi ya vyoo, utunzaji sahihi wa taka, upati kanaji wa chakula na maji safi na salama pamoja na usafi wa mtu binafsi. Uharibifu wa mazingira husababisha kuenea kwa magonjwa. Tanzania inakabiliwa na tati zo la uchafuzi wa mazingira na hivyo kusababisha kuenea kwa magonjwa ya milipuko. Ni asilimia 52.8 tu ya watanzania wote hutumia vyoo salama, kati yao ni asilimia 36.7 tu ya shule zote zinatumia vyoo salama. Changamoto ya uchafuzi wa mazingira hutokana na upungufu wa maafi sa mazingira kati ka ngazi ya wilaya na tarafa, kutokuwepo kwa sheria na kanuni madhubuti za usafi wa mazingira pamoja na jamii kutofuata kanuni na sheria za usafi .

Malengo ya MMAM

• Kuboresha afya mazingira kuanzia ngazi ya kaya

Mikakati

• Kuwajengea uwezo Maafi sa mazingira kati ka ngazi za wilaya na kata wa jinsi ya kuhifadhi mazingira

• Kuelimisha na kuishirikisha jamii kati ka kufuata kanuni na tarati bu za usafi kati ka kutunza afya ya mazingira yao.

20

Kimeandaliwa na kuchapishwa na Sikika

Tafsiri Rahisi ya Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM) 2007-2017

4.14 Uraghabishi na UhamasishajiNi mfumo wa mawasiliano unaolenga kubadilisha tabia kati ka jamii ili kufi kia malengo yaliyowekwa.

Malengo ya MMAM

• Kuchochea uwelewa wa wadau ili waweze kushiriki kikamilifu kati ka kufanikisha malengo ya MMAM.

Mikakati

• Kuongeza uwelewa wa jamii ili waweze kushiriki kati ka utekelezaji wa MMAM.

4.15 Mfumo wa utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi Kwa kuwa utekelezaji wa mpango huu unahusisha ngazi mbalimbali kuanzia ngazi ya kitaifa mpaka ngazi ya vijiji/mitaa, mfumo madhubuti wa mgawanyo wa majukumu, utekelezaji, utoaji wa mrejesho na taarifa kwa ajili ya kutathmini maendeleo ya mpango kwa wadau unahitajika. Ufuatao ni mfumo wa utekelezaji wa majukumu na wajibu wa wadau wakuu kati ka utekelezaji wa MMAM

4.15.1 Wizara ya Afya na Ustawi wa JamiiWizara hii ni kiungo kikuu cha urati bu wa mpango huu ikishirikiana naOfi si ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)

Majukumu ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii• Kuandaa miongozo, sera na mikakati kwa ajili ya utekelezaji wa mpango huu. • Kutafuta na kukusanya rasilimali kwa ajili ya kufanikisha utekelezaji wa

MMAM• Kuzisaidia na kuziwezesha sekretarieti za mikoa ili ziweze kuzijengea uwezo

mamlaka za Serikali za mitaa kati ka kutekeleza mpango huu• Kufuati lia, kutathmini na huhakiki utekelezaji wa mpango huu, ikisaidiana na

wadau wengine.• Kupiti a kikosi kazi chake, wizara ina Wajibu wa kuandaa mipango kazi,

kufuati lia ukarabati na ujenzi wa vituo vya huduma pamoja na mchakato wa ununuzi na ugavi.

21

Kimeandaliwa na kuchapishwa na Sikika

Tafsiri Rahisi ya Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM) 2007-2017

4.15.2 TAMISEMI

Majukumu ya TAMISEMI

• Kusimamia utoaji wa huduma za afya kati ka ngazi za hospitali, vituo vya afya, zahanati na ngazi ya vijiji/kaya.

• Kuhakikisha kuwa mamlaka za Serikali za Mitaa zinaandaa mipango na bajeti kwa ajili ya utekelezaji wa MMAM

• Kutenga na kugawa rasilimali kwa sekretarieti za mikoa na serikali za mitaa kwa ajili ya utekelezaji wa MMAM

• Kusimamia utekelezaji wa MMAM kati ka ngazi ya Serikali za mitaa

4.15.3 Ngazi ya Mikoa

Majukumu ya Sekretarieti ya mkoa kupiti a Timu ya Uendeshaji Huduma zaAfya ya Mkoa• Kutoa ushauri wa kitaalamu kwa Serikali za mitaa ili kuhakikisha utekelezaji

wa MMAM• Kuhakikisha kuwa MMAM inajumuishwa kati ka bajeti na Mpango Kabambe

wa afya wa Halmashauri - CCHP • Kusimamia na kuweka mazingira mazuri ya kuhakikisha utekelezaji wa

MMAM.

22

Kimeandaliwa na kuchapishwa na Sikika

Tafsiri Rahisi ya Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM) 2007-2017

4.15.4 Ngazi ya Halmashauri

Majukumu yake:• Kusimamia kazi, kuajiri wafanyakazi, kutoa ushauri wa kitaalam kwa vituo

vya Afya na zahanati na kutoa taarifa na ripoti za utekelezaji wa MMAM.• Kutoa elimu kwa jamii na kuhakikisha kuwa wananchi wanahusika kati ka

utekelezaji wa MMAM pamoja na kuhakikisha kuwa MMAM inajumuishwa kati ka Mpango kabambe wa Afya wa Halmashuri - CCHP.

4.15.5 Ngazi ya Kata na Vijiji

Majukumu ya Kamati ya Maendeleo ya Kata na Serikali ya Kijiji ni:• Kutoa ardhi kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya Afya na zahanati • Kusimamia na kuhamasisha jamii kuchangia fedha na nguvu kazi kwa ajili ya

utekelezaji wa MMAM. Hii itasaidia kuwafanya wananchi kuwa wamiliki na wasimamizi huduma za afya.

• Kutoa taarifa za maendeleo ya MMAM • Kuweka mazingira mazuri ya kuwezesha utekelezaji wa MMAM na utendaji

wa watoa huduma za afya kati ka vituo vya huduma.

4.15.6 Bodi ya Huduma za Afya ya Halmashauri

Majukumu yake:• Kwa kushirikiana na Halmashauri za Wilaya, Bodi za afya zinawajibu wa

kutafuta na kusimamia matumizi ya rasilimali ili kutekeleza malengo ya MMAM.

23

Kimeandaliwa na kuchapishwa na Sikika

Tafsiri Rahisi ya Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM) 2007-2017

4.15.7 Kamati ya Afya ya Kituo

Majukumu yake:• Kukusanya rasilimali kwa ajili ya utekelezaji wa MMAM,• Kuhamasisha jamii kuchangia fedha na nguvu kazi kwa ajili ya utekelezaji wa

MMAM,• Kutoa taarifa kwa jamii juu ya maendeleo ya utekelezaji wa MMAM,• Kuweka na kuhakikisha mazingira mazuri ya kufanyia kazi kwa watoa huduma

za afya.

4.16 Rasilimali Fedha kati ka Sekta ya AfyaKuna aina mbili za vyanzo vya mapato ya kuendeshea huduma za afya kati ka vituo vya huduma vya umma. Vyanzo hivyo ni fedha kutoka kati ka bajeti kuu ya serikali pamoja na michango ya nchi wahisani na fedha zitokanazo na uchangiaji wa gharama za huduma za afya na miradi mbalimbali ya Halmashauri husika. Mpaka sasa bajeti ya sekta ya afya kutoka serikali kuu ni asilimia 11% pungufu ya makubaliano ya maazimio ya Abuja ya kutenga kiasi cha asilimia 15% ya bajeti ya serikali kati ka sekta ya afya. Kutokana na upungufu huu wa rasilimali fedha kati ka sekta ya afya, serikali ilianzisha mfumo wa jamii ili kuchangia gharama pamoja na Bima ya Afya ambayo ni - NHIF na CHF.

Malengo ya MMAM

• Kutafuta vyanzo vingine vya fedha ili kutekeleza Mpango.

• Kutenga fedha za kutosha ili kufanikisha utekelezaji wa MMAM kwa Serikali, wadau wa maendeleo, mashirika yasiyo ya kiserikari na asasi za kiraia.

Mikakati

• Kutafuta vyanzo vingine vya fedha ndani na nje ya nchi.

• Kuviwezesha vyanzo vya mapato vilivyopo NIHF,CHF na Uchangiaji ili kuhakikisha utekelezaji wa MMAM

24

Kimeandaliwa na kuchapishwa na Sikika

Tafsiri Rahisi ya Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM) 2007-2017

5.0 HITIMISHO

Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM), unategemewa kutekelezwa kwa kipindi cha miaka kumi kuanzia mwaka 2007 hadi 2017. Matumaini ya serikali ni kwamba baada ya kipindi hiki MMAM itakua imesaidia kwa kiasi kikubwa kusogeza huduma za afya kwa wananchi na hivyo kuboresha hali ya maisha na ustawi wao, kama mojawapo ya malengo ya MKUKUTA na Dira ya Maendeleo 2025.

Sikika inaipongeza serikali kwa kuona umuhimu wa kuboresha huduma za afya kwa wananchi na hati maye kutoa mpango huu ili kufi kia azma hii. Ni matumaini yetu kuwa kila mmoja wetu atati miza majukumu yake kulingana na nafasi yake kama ulivyoainisha Mpango na hivyo kuti miza lengo la kusogeza huduma za afya karibu na maeneo ya wananchi wote mpaka kufi kia mwaka 2017.

4.17 Tathmini na Usimamizi wa Utekelezaji wa MpangoUsimamizi na tathmini ya maendeleo ya Mpango vinalenga kati ka kuhakikisha kwamba malengo ya mpango yanatekelezwa kama ilivyopangwa na kwa muda muafaka

Malengo ya MMAM

• Kufanya tathmini ya utekelezaji wa maendeleo ya Mpango kulingana na malengo yaliyowekwa.

Mikakati

• Kuweka mfumo imara na endelevu wa kusimamia utekelezaji wa Mpango kati ka ngazi zote za utekelezaji

• Kuongeza nguvu na uwezo wa Wizara ya afya na Ustawi wa Jamii, TAMISEMI, sekretatrieti za mikoa na Halmashauri kati ka kusimamia utekelezaji wa shughuli za Mpango.

25

Kimeandaliwa na kuchapishwa na Sikika

Tafsiri Rahisi ya Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM) 2007-2017

.......................................................................................................

.......................................................................................................

...........................................................................................................................

Kwa maelezo zaidi, maoni na ushauri, Tafadhali Tuandikie kupiti a Anuani hii. Sikika, S.L.P 12183, Dar es Salaam. Au tuma ujumbe mfupi wa maneno kupiti a +255 688 493 882

26

27

Kimetolewa na Sikika (Zamani YAV)S.L.P 12183 Dar Es SalaamSimu +255 22 2666355/7 | Nukushi +255 22 2668015Barua-pepe: [email protected], Tovuti www.sikika.or.tz©Sikika 2010