toleo na. 016 jarida la kila miezi mitatu oktoba - disemba ... 16.pdf · wadhamini ( zlsc)...

20
Toleo Na. 016 Jarida la kila miezi mitatu Oktoba - Disemba, 2013 Jarida la Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Inaendelea Uk. 4 Inaendelea Uk. 3 A wali wakati akiwakaribisha wageni katika uzinduzi huo Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Prof.Chris Maina pichani aliwaomba washiriki kufanya jitihada za makusudi kukipata kitabu cha Zanzibar Year Book of Law kwani muna mengi ndani yake ambayo wanataaluma wanayahitaji. Aidha Aliwaomba washirki kuwa makini na wasikivu wakati wa Uwasilishwaji wa mada mbali mbali zitakazo wasilishwa kwa Ajili ya siku hiyo. Akisoma hotuba yake mbele ya umma wa Wazanzibari waliofurika katika Ukumbi wa EACROTANAL katika hafla ya Kumbukumbu ya kumuenzi Profesa Haroub Othman Mgeni Rasmi Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi aliuelezea usomi wa Profesa Haroub kuwa ulisaidia sana kutoa na kuzalisha wataalamu mbali mbali katika taaluma ya sheria, sayansi ya jamii na hata masuala ya Haki za Binadamu ambao kwa sasa wamekuwa walimu wa Taifa hili kwa vile hakuwa mchoyo katika jambo lolote Kitabu cha Zanzibar Year Book of Law Chazinduliwa kwa Mara ya Kwanza Zanzibar A kizungumza wakati wa kuwakaribisha wageni waliohudhuria katika maadhimisho ya miaka 20 ya Haki za Binadamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ZLSC Prof. Chris Maina ZLSC Yaadhimisha Miaka 20 ya Utetezi wa Haki za Binadamu alilokuwa akiliamini. Alikuwa mpenda watu, mcheshi hana makuu wala dharau. Aidha Aliutaka uongozi wa Kituo kuhakikisha kuwa Kituo kinabaki kuwa urithi wa mchango mkubwa kwa jamii ulioachwa na Marehemu Profesa Othman kwa sababu urithi umekusudia kuwasaidia wananchi kupata msaada wa kisheria. aliwataka washiriki kutafakari zaidi juu ya kwanini Kituo kiadhimishe siku hii. Alisema Kituo cha Huduma za Sheria (ZLSC) Kimekua na utaratibu wa kuiadhimisha siku Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Aboubakar Khamis Bakary akitoa hutuba yake katika siku ya Maadhimisho ya Haki za Binadamu katika ukumbi wa Kituo cha Huduma za Sheria Migombani, kulia ni Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu Zahor Khamis,kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Kituo Prof. Chris Maina Peter na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Huduma za Sheria Bi Harusi Miraji Mpatani YALIYOMO Uwepo wa Polisi Jamii Zanzibar Kunapunguza Uhalifu UK. 8 Utaratibu wa Upekuzi wa Mtuhumiwa na Upekuzi wa Makazi Kisheria UK. 12 Hotuba ya Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, Katika Uzinduzi wa Kitabu cha Zanzibar Yearbook of Law UK. 16 ZLSC Yawakutanisha Masheha, Polisi na MahakamaUK. 18 Makamo wa Pili wa Rais Mh.Balozi Seif Ali Iddi akizindua Rasmi kitabu cha Zanzibar Year Book of Law mwaka 2013 katika Kumbukizi ya Prof. Haroub kwenye Ukumbi wa EACROTANAL. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ( ZLSC) PrOF.Chris Maina Alie shikilia kitabu ni Mwanasheria wa ZLSC Pemba Bi.Safia Saleh Sultan

Upload: duongdat

Post on 08-Jul-2018

325 views

Category:

Documents


2 download

TRANSCRIPT

Page 1: Toleo Na. 016 Jarida la kila miezi mitatu Oktoba - Disemba ... 16.pdf · Wadhamini ( ZLSC) PrOF.Chris Maina Alie shikilia kitabu ni Mwanasheria wa ZLSC Pemba Bi.Safia Saleh Sultan

Toleo Na. 016 Jarida la kila miezi mitatu Oktoba - Disemba, 2013

Jarida la Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar

Inaendelea Uk. 4

Inaendelea Uk. 3

Awali wakati akiwakaribisha wageni katika uzinduzi huo Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Kituo cha

Huduma za Sheria Zanzibar Prof.Chris Maina pichani aliwaomba washiriki kufanya jitihada za makusudi kukipata kitabu cha Zanzibar Year Book of Law kwani muna mengi ndani yake ambayo wanataaluma wanayahitaji.

Aidha Aliwaomba washirki kuwa makini na wasikivu wakati wa Uwasilishwaji wa mada mbali mbali zitakazo wasilishwa kwa Ajili ya siku hiyo.

Akisoma hotuba yake mbele ya umma wa Wazanzibari waliofurika katika Ukumbi wa EACROTANAL katika hafla ya Kumbukumbu ya kumuenzi Profesa Haroub Othman Mgeni Rasmi Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi aliuelezea usomi wa Profesa Haroub kuwa ulisaidia sana kutoa na kuzalisha wataalamu mbali mbali katika taaluma ya sheria, sayansi ya jamii na hata masuala ya Haki za Binadamu ambao kwa sasa wamekuwa walimu wa Taifa hili kwa vile hakuwa mchoyo katika jambo lolote

Kitabu cha Zanzibar Year Book of Law Chazinduliwa kwa Mara ya Kwanza Zanzibar

Akizungumza wakati wa kuwakaribisha wageni waliohudhuria katika maadhimisho ya miaka 20 ya

Haki za Binadamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ZLSC Prof. Chris Maina

ZLSC Yaadhimisha Miaka 20 ya Utetezi wa Haki za Binadamu

alilokuwa akiliamini. Alikuwa mpenda watu, mcheshi hana makuu wala dharau.Aidha Aliutaka uongozi wa Kituo kuhakikisha kuwa Kituo kinabaki kuwa urithi

wa mchango mkubwa kwa jamii ulioachwa na Marehemu Profesa Othman kwa sababu urithi umekusudia kuwasaidia wananchi kupata msaada wa kisheria.

aliwataka washiriki kutafakari zaidi juu ya kwanini Kituo kiadhimishe siku hii.Alisema Kituo cha Huduma za Sheria (ZLSC)Kimekua na utaratibu wa kuiadhimisha siku

Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Aboubakar Khamis Bakary akitoa hutuba yake katika siku ya Maadhimisho ya Haki za Binadamu katika ukumbi wa Kituo cha Huduma za Sheria Migombani, kulia ni Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu Zahor Khamis,kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Kituo Prof. Chris Maina Peter na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Huduma za Sheria Bi Harusi Miraji Mpatani

YALIYOMO

Uwepo wa Polisi Jamii Zanzibar Kunapunguza

Uhalifu UK. 8

Utaratibu wa Upekuzi wa Mtuhumiwa na

Upekuzi wa Makazi Kisheria UK. 12

Hotuba ya Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, Katika

Uzinduzi wa Kitabu cha Zanzibar Yearbook of

Law UK. 16

ZLSC Yawakutanisha Masheha, Polisi na

MahakamaUK. 18

Makamo wa Pili wa Rais Mh.Balozi Seif Ali Iddi akizindua Rasmi kitabu cha Zanzibar Year Book of Law mwaka 2013 katika Kumbukizi ya Prof.Haroub kwenye Ukumbi wa EACROTANAL. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis na Mwenyekiti wa Bodi ya

Wadhamini ( ZLSC) PrOF.Chris Maina Alie shikilia kitabu ni Mwanasheria wa ZLSC Pemba Bi.Safia Saleh Sultan

Page 2: Toleo Na. 016 Jarida la kila miezi mitatu Oktoba - Disemba ... 16.pdf · Wadhamini ( ZLSC) PrOF.Chris Maina Alie shikilia kitabu ni Mwanasheria wa ZLSC Pemba Bi.Safia Saleh Sultan

Maoni ya Mhariri

Prof. Chris Maina Peter,Mhariri

Mhariri: Prof. Chris Maina Peter

Mwenyekiti: Bi. Harusi Miraji Mpatani

Wajumbe:Bi. Jina Mwinyi WaziriBi. Farhat Rashid Omar

Bw. Suleiman Abdulla SalimBw. Thabit Abdulla Juma

Msanifu:Bw. Aziz Iddi Suwed

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa:

Simu: 0242233784S.L.P: 3360 ZanzibarFax: 0242234495E-mail: [email protected]: www.zlsc.or.tz

Chake Chake Pemba wasiliana nasiKwa:-Simu: +255 2452936

Ifanye haki

Iwe shauku

Rasimu ya Pili ya Katiba Yazinduliwa

2

Bodi ya Wahariri

Wananchi wote mnaombwa kusoma Jarida hili la Kituo kwa madhumuni ya kujifunza zaidi na kupima maendeleo ya utendaji kazi za Kituo.

Tunakaribisha barua za maoni kutoka kwa wasomaji na michango ya makala kwa ajili ya kuelimisha umma.

Aidha wote watakaopenda kuchangia au kuleta maoni yao katika Jarida la Sheria na Haki wanatakiwa wajitambulishe kwa majina pamoja na anuani zao ili kuleta ufanisi, ukweli na uwazi katika kuendeleza Jarida hili.

Bodi ya Wahariri itakuwa na uwezo wa mwisho wa kuamua au kuhariri habari itakayochapishwa kwenye Jarida hili.

Mhariri

sheria na haki Oktoba - Disemba, 2013

Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilikabidhi rasimu ya pili ya Katiba kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.

Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohammed Shein, Desemba 30, mwaka 2013.

Makabidhiano hayo yalifanyika katika hafla iliyofanyika katika Viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam baada ya Tume kumaliza kazi yake ya kuiandaa.

Rasimu hiyo ya pili ilitolewa ikiwa imepita miezi saba tangu tume hiyo ilipotoa rasimu ya kwanza na ambayo ilijadiliwa katika Mabaraza ya Katiba yaliyokaa kuanzia Julai 12 mpaka Septemba 2 mwaka 2013.

Kwa mujibu wa Ibara ya 20 (2) ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, mara baada ya Rais kukabidhiwa rasimu hiyo, itachapishwa katika Gazeti la Serikali na kwenye magazeti mengine ndani ya siku 31.

Pia katika kipindi hicho, Rais alitakiwa kuitisha kikao cha Bunge Maalumu la Katiba kwa ajili ya kupitisha rasimu iliyopendekezwa.

Taarifa ya Katibu wa Tume hiyo, Assaa Rashid ilitolewa ikieleza kuwa Tume hiyo itakabidhi rasimu hiyo kwa Marais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein katika hafla iliyohudhuriwa na viongozi wa Serikali, vyama vya siasa, taasisi za kidini, asasi za kiraia na wananchi wa kawaida.

Tume hiyo ilitakiwa kumaliza kazi ya kuandaa rasimu ya pili Disemba 15 mwaka 2013 lakini Rais Kikwete aliiongezea siku 14 zaidi hadi Disemba 30, mwaka 2013 Hatua hiyo ya Rais Kikwete kuiongezea muda tume hiyo ilikuwa ya pili. Mara ya kwanza iliomba kuongezewa muda wa siku 45, kuanzia Novemba Mosi hadi Desemba 15, mwaka huu. Kabla ya

kuomba kuongezewa muda mara ya kwanza, ilitakiwa kukamilisha kazi yake Novemba 30.

Sheria ya Mabadiliko ya Katiba inaelekeza Tume hiyo kufanya kazi kwa miezi 18 licha ya kuwa inampa Rais mamlaka ya kuiongezea muda usiozidi siku 60.

Hatua ya Rais kuiongezea muda kwa mara ya pili, ilitafsiriwa kama kutoa fursa kwa wajumbe wake kujipanga upya baada ya kifo cha mwenzao, Dk Sengondo Mvungi kilichotokea Novemba 12, mwaka 2013 huko Afrika Kusini alikokuwa akitibiwa baada ya kujeruhiwa kwa mapanga.

Tume hiyo iliyoanza kazi Mei 3, 2012 kwa kukusanya maoni ya wananchi, iliandaa rasimu ya kwanza iliyotolewa Juni 4, mwaka huu.

Kwa upande wetu Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar tukiwa wadau katika kufanikisha Mchakato huu na kuiommbea nchi yetu iweze kwenda salama na kufanikisha kupatikana kwa Katiba inayopendekezwa.

Sasa ni wakati wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete na Rais mwenzake wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein kuhakikikisha wanawapatia Watanzania kikosi kazi madhubuti cha Wajumbe wa Bunge maalum la Katiba kupitia Taasisi, Mashirika, Vyama vya siasa, Makundi ya Wakulima na Wafanyakazi na Asasi za Kiraia kama ambavyo Sheria ya Mabadiliko ya Katiba inavyoelekeza katika kuwapata wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba watakaoweza kufanikisha matarajio ya Watanzania katika kuipata katiba Mpya.

Ni matarajio yetu Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano na Rais wa Zanzibar kwa pamoja watashirikiana ili kuwateua Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba na Kufanikisha kupatikana kwa Katiba Pendekezwa.

Bado Watanzania wanayonafasi ya kupandisha soksi zao Juu ili kujiandaa na kura ya maoni ya Katiba kuipitisha ama kuikataa Katiba hiyo mara baada ya Bunge Maalum la Katiba kukamilisha kazi yake.

Page 3: Toleo Na. 016 Jarida la kila miezi mitatu Oktoba - Disemba ... 16.pdf · Wadhamini ( ZLSC) PrOF.Chris Maina Alie shikilia kitabu ni Mwanasheria wa ZLSC Pemba Bi.Safia Saleh Sultan

habari

3

Inatoka Uk. 1

Oktoba - Disemba, 2013sheria na haki

Kitabu cha Zanzibar Year Book of Law Chazinduliwa kwa Mara ya Kwanza Zanzibar

Ameeleza kazi zinazofanywa na Kituo ni moja kati ya azma ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Januari 1964 hivyo ni lazima jitihada zaidi za kuwaelimisha watu wetu iendelee kama Muasisi wa kituo hichi alivyotaraji.

Mgeni rasmi aliwaomba watendaji wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar waendelee na moyo wa kumuenzi Profesa Othman, kufikiria changamoto zinazolikabili Taifa na Wananchi wa Zanzibar katika masuala ya Sheria pamoja na kuandika sambamba na kuweka vizuri kumbukumbu za sheria kwa faida ya vizazi vya sasa na vya baadae.

Kwa Upande wake Waziri wa Katiba na Sheria Mh.Abuubakar Khamis Bakary alieleza kuwa

Bwana Abdallah Miraji Othmani ndugu wa marehemu Profesa Haroub Othman akitoa maelezo katika kumbukizi ya Profesa Haroub Othman

Marehemu Prof. Haroub alikuwa ni mtetezi wa wanyonge (voice of the voiceless people) na kuiomba jamii kumuezi Prof. Haroub kwa vitendo na sio maneno tu.

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wahariri wa Kitabu hicho cha Zanzibar Yearbook of Law (Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar) Mh. Othman Masoud Othman alieleza kuwa Kitabu hicho ni muhimu kwa sababu ni miongoni mwa mambo yaliyokuwa yakisisitizwa na mwasisi wa Kituo (Marehemu Prof. Haroub) lakini pia kitabu hicho kinatoa taaluma ya sheria kimataifa, Afrika na Zanzibar.

Alieleza kuwa Zanzibar ni nchi ya mwanzo kuwa na Law Reports kwa Afika (1866 –

1956), ni nchi ya mwanzo kuwa na Gazeti Rasmi la Serikali lililoanzishwa mwaka 1894 ambalo limeachwa mwaka 1963 na ni nchi ya mwanzo kuanzisha mahkama rasmi za Kadhi mwaka 1897.

Makamo Mweneyekiti huyo aliendelea kueleza kuwa Zanzibar itakuwa ni nchi ya pili kwa Afrika iliyo na Kitabu Year Book of law ambapo ya kwanza ni Afrika Kusini na itakuwa ya mwanzo kwa upande wa Afrika Mashariki Kwa upande wa mwakilishi wa familiya ya Prof. Haroub Bw. Abdalla Othman alitoa wito kwa Uongozi wa Kituo kuongeza nguvu zaidi vijijini ili kusaidia kupunguza matatizo mengi yanayoikumba jamii kwenye Vijiji mbali mbali nchini kwa sababu bado kuna matatizo yanayoendelea kusumbua jamii kwa muda mrefu kama vile masuala ya udhalilishaji wa kijinsia na masuala ya ardhi jambo ambalo kwa asilimia kubwa linasababishwa na ukosefu wa taaluma ya sheria.

Baada ya kumalizika kwa sehemu ya kwanza ya shughuli hiyo iliyojumuisha uzinduzi wa Kitabu cha Zanzibar Year Book of Law washiriki waliweza kupata nafasi ya kumsikiliza mada mbali mbali zilizowasilishwa ikiwa ni pamoja na historia ya uundwaji wa Bunge Maalum la Katiba katika nchi mbali mbali duniani, uundwaji wa bunge maalum la Katiba Tanzania,utaratibu wa kupatikana kwa wabunge wa Bunge maalum la Katiba Tanzania , taratibu za uendeshaji wa Bunge hilo pamoja na changamoto za Bunge hilo.

Rasimu ya Pili ya Katiba Yakabidhiwa Rasmi

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba akimkabidhi Rasimu ya Pili ya Katiba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DK.Jakaya Mrisho Kikwete katika Sherehe ya Kukabidhi Rasimu hiyo

iliyofanyika katika Ukumbi wa Karimjee Dar es Salaam

Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilikabidhi rasimu ya pili ya Katiba kwa Rais Jakaya Kikwete pamoja na Rais wa Zanzibar, Dk Ali

Mohammed Shein, Desemba 30, mwaka 2013.

Makabidhiano hayo yalifanyika katika hafla iliyofanyika viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam baada ya Tume kumaliza kazi yake ya kuiandaa.

Rasimu hiyo ya pili ilitolewa ikiwa imepita miezi saba tangu tume hiyo ilipotoa rasimu ya kwanza na ambayo ilijadiliwa katika Mabaraza ya Katiba yaliyokaa kuanzia Julai 12 mpaka Septemba 2 mwaka 2013.

Kwa mujibu wa Ibara ya 20 (2) ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, mara baada ya Rais kukabidhiwa rasimu hiyo, itachapishwa katika Gazeti la Serikali na kwenye magazeti mengine ndani ya siku 31.

Pia katika kipindi hicho, Rais alitakiwa kuitisha kikao cha Bunge Maalumu la Katiba kwa ajili ya kupitisha Katiba inayopendekezwa. Kutokana na hali hiyo, Bunge la Katiba lilianza vikao vyake Mapema Februari, 2013.

Taarifa ya Katibu wa Tume hiyo, Assaa Rashid ilitolewa ikieleza kuwa Tume hiyo itakabidhi

rasimu hiyo kwa Marais Dk. Kikwete na Dk. Shein katika hafla itakayohudhuriwa na viongozi wa Serikali, vyama vya siasa, taasisi za kidini, asasi za kiraia na wananchi wa kawaida.

Tume hiyo ilitakiwa kumaliza kazi ya kuandaa rasimu ya pili Disemba 15 mwaka 2013 lakini Rais Kikwete aliiongezea siku 14 zaidi hadi Disemba 30, mwaka 2013.

Hatua hiyo ya Rais Kikwete kuiongezea muda tume hiyo ilikuwa ya pili. Mara ya kwanza iliomba kuongezewa muda wa siku 45, kuanzia Novemba Mosi

hadi Desemba 15, mwaka huu. Kabla ya kuomba kuongezewa muda mara ya kwanza, ilitakiwa kukamilisha kazi yake Novemba 30.

Sheria ya Mabadiliko ya Katiba inaelekeza Tume hiyo kufanya kazi kwa miezi 18 licha ya kuwa inampa Rais mamlaka ya kuiongezea muda usiozidi siku 60.

Hatua ya Rais kuiongezea muda kwa mara ya pili,

ilitafsiriwa kama kutoa fursa kwa wajumbe wake kujipanga upya baada ya kifo cha mwenzao, Dk Sengondo Mvungi kilichotokea Novemba 12, mwaka 2013 huko Afrika Kusini alikokuwa akitibiwa baada ya kujeruhiwa kwa mapanga.

Tume hiyo iliyoanza kazi Mei 3, 2012 kwa kukusanya maoni ya wananchi, iliandaa rasimu ya kwanza iliyotolewa Juni 4, mwaka huu.

Page 4: Toleo Na. 016 Jarida la kila miezi mitatu Oktoba - Disemba ... 16.pdf · Wadhamini ( ZLSC) PrOF.Chris Maina Alie shikilia kitabu ni Mwanasheria wa ZLSC Pemba Bi.Safia Saleh Sultan

4

habari

Inatoka Uk. 1ZLSC Yaadhimisha Miaka 20 ya Utetezi wa Haki za Binadamu

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini (ZLSC) PROF.Chris Maina,Kushoto ni Mkurugenzi (ZLSC) Bi. Harusi M. Mpatani kulia ni Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Abuubakar Khamis Bakary na Kamishna wa Haki za Binadamu Zanzibar Zahor Khamis

hii kwa kufanya Makongamano, warsha na kujumuika pamoja katika kuikumbusha Jamii na Serikali juu ya Umuhimu wa kutunza haki za Binadamu wakati wote. Akisoma hotuba yake katika maadhimisho ya siku ya Haki za Binadamu kwa mwaka 2013 hapo katika ukumbi wa Kituo cha Huduma za Sheria Migombani Mgeni Rasmi Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Abuubakar Khamis Bakary alisema Jumuiya ya Madola na Haki za Binadamu mnamo mwaka 1988,huko Bangalore, Majaji wa Jumuiya hiyo walikaa na kuzungumzia suala la Haki za Binadamu (judicial colloquiumin Bangalore

24-26 February 1988) na katika Mkutano huo waliafikiana kuwa Haki za Binadamu ni haki za kuzaliwa, ni dira ya maisha ya mwanadamu pia zinasaidia sana katika kuamua kesi mbali mbali zinazohusu ubinadamu wa mtu.

Kwa Mantiki hii Mhe. Bakary aliisisitiza jamii ya kizanzibari na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inatakiwa kuishi kwa pamoja, furaha huku kila mmoja wetu akimsaidia mwenzake na wale wakubwa au wenye amri ni lazima wawatunze na kuwaheshimu walio chini yao ili kuhakikisha kua haki hizi zinamfaidisha kila muhusika.

Akitoa mada juu ya Miaka 20 ya utetezi wa Haki yako, Mafanikio na Changamoto za Haki za Binadamu kwa kipindi kijacho.(20 Years Working for your Rights:The Success and Challenges and the Future of Human Rights) Dk. Mohd Makame Haji alisema kuishi kwa mujibu wa Utamaduni na maamrisho ya dini zetu,kuzungumza lugha yetu ,kuishi kwa Amani na Usalama vyote hivyo ni miongoni mwa silaha kubwa katika Haki za Binadamu.

Aidha alisema haki za Binadamu ni nyingi lakini tunaweza kuzigawa katika Makundi Makuu matatu (3) 1.Haki za kisiasa 2.Haki za kiuchumi na 3.Haki za kijamii.

Siku ya Haki za Binadamu imekua ikiadhimishwa kila ifikapo tarehe 10 Disemba ambapo Umoja wa Mataifa wameichagua siku hii baada ya kupita kipindi kigumu cha Mauaji yaliyosababishwa na vita vya Pili vya Dunia vilivyopiganwa kuanzia (1939-1945) ambapo kwa kiasi kikubwa madhara ya vita hiyo ndio yaliyoza wazo la kuanzishwa Umoja wa Mataifa UNO Na hatimae mwaka 1948 Tamko Rasmi la haki za Binadamu ambapo sasa Tunaadhimisha miaka 65 ya siku ya Haki za Binadamu.

Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu kwa mwaka 2013 yalikua ni MIAKA 20 YA KUTETEA HAKI YAKO.

Wananchi wa Mtowa Pwani wakikishukuru Kituo cha Huduma za Sheria kwa Msaada wa Sheria walioutoa katika Shehia yao

Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar (ZLSC),kikiwa ni mdau mkuu wa kuhakikisha wananchi wa Zanzibar popote pale walipo

katika visiwa hivi vya Unguja na Pemba wanakua na utambuzi wa masuala mbali mbali ya sheria kwa kushirikiana na asasi nyengine za kiraia hupata nafasi ya kuvitembea vijiji na shehia ili kuwaelimisha wananchi waishio huko waweze kutambua sheria .

Katika maadhimisho ya siku ya msaada wa kisheria kwa mwaka 2013 Kituo kilipata nafasi kuelekea katika vijiji vya Mto wa Pwani na Mkokotoni vilivyopo Mkoa wa Kaskazini Unguja ,Wilaya ya Kaskazi A na kupata nafasi ya kupokea kesi mbali mbali zilizohitaji msaada wa kisheria kutoka kwa wanasheria .

Jumla ya kesi (40)zilipokelewa na watendaji wa kituo katika shehia ya Mkokotoni na Mto wa Pwani ambazo nyingi kati ya kesi hizo zilijielekeza katika kesi za Madai,Jinai na Utelekezwaji wa Watoto.

Watendaji wa kituo kupitia mkusanyiko huo walipata nafasi ya kuzipokea kesi hizo na baadae kuzitolea ushauri.

Aidha kwa upande wa kesi za utelekezwaji wa watoto wahusika walishauriwa kuliwasilisha lalamiko na kuandikiwa maelezo ya kesheria kwa hatua za ufuatiliaji.

Mbali na shughuli ya kupokea kesi mbali mbali kutoka katika shehia hizi za Mto wa Pwani na Mkokotoni kwa kuzipatia ushauri, kituo kwa kushirikiana na Jumuia ya Wanasheria Wanawake (ZAFELA) na Jumuia ya

Siku ya Msaada wa Sheria Yaadhimishwa

Wanasheria Zanzibar (ZLS) walipata nafasi ya kutoa Elimu kwa Wananchi hao kuhusu:

Haki za Binadamu, Unyanyasaji wa kijinsia na udhalilishaji, taratibu za namna ya kufungua kesi za Madai na Jinai, pamoja na mada kuhusu umuhimu wa ushirikishwaji wa wananchi juu ya miradi mbali mbali ya maendeleo inayotolewa katika shehia zao.

Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar (ZLSC) ikiwa ni asasi isiyo ya kiserikali inajukumu la kusimamia utoaji wa Elimu ya Sheria kupitia Vipindi vya Redio na TV,Kupokea kesi mbali mbali zitokazo kwa wananchi kwa lengo la kuzisimamia kesi hizo,Kutoa Majarida na Machapisho mbali mbali ya Sheria pamoja na kufanya Tafiti mbali mbali za Kisheria.

sheria na haki Oktoba - Disemba, 2013

Page 5: Toleo Na. 016 Jarida la kila miezi mitatu Oktoba - Disemba ... 16.pdf · Wadhamini ( ZLSC) PrOF.Chris Maina Alie shikilia kitabu ni Mwanasheria wa ZLSC Pemba Bi.Safia Saleh Sultan

5

habari

Ilikua ni siku ya tarehe 28 na 29 mwezi wa Novemba mwaka 2013 ambapo Jumuiya ya Walimu wastaafu Zanzibar ( JUWAWAZA)

walipopata fursa ya kupatiwa elimu ya Uraia na Utawala Bora kupitia Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar. Awali Akiwakaribisha walimu hao Mkurugenzi Mtendaji Kituo cha Huduma za Sheria Bi. Harusi Miraji Mpatani aliwataka wastaafu hao kuhakikisha wanachagua viongozi imara ambao watawasimamia mambo yao na kufanya kazi kwa kujituma.

Aliwasisitiza Walimu hao wakati wanaelekea katika Uchaguzi wa kuwachagua Viongozi wao wapya wa Jumuia hiyo waondoshe ile dhana ya bora uongozi bali wao wasimamie ile dhana ya viongozi Bora.

JUWAWAZA Yapata Mafunzo ya Utawala Bora

Akizungumza na hadhara hiyo Mkurugenzi Maandalizi na Msingi Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Maalim Uledi Juma Wadi alisema Jumuia nyingi huazishwa na baadae kutoweka kutokana na uroho wa madaraka ama ubadhirifu wa mali za Jumuia ,hivyo ni Jukumu la Jumuia ya Walimu Wastaafu kuhakikisha kwamba wanachagua viongozi wenye nia njema na wachapa kazi ili lile lengo la kuanzishwa kwa Jumuiya hiyo liweze kufikiwa.

Aidha Maalim Uledi Aliwataka walimu hao kutokata tamaa juu ya umbali uliojitokeza kati yao na watendaji wa sasa wa Wizara ya Elimu badala yake wakae pamoja na kuchagua washiriki wachache kwenda kuzungumza na watendaji hao kwa lengo la kurudisha mshikamano kwa chombo hicho muhimu cha taaluma nchini.

Bi.Fatma Hassan Akitoa mada kuhusu Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 na ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji ZLSC

Akitoa mada juu ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bi.Fatma Hassan Aliwaelekeza walimu hao kwamba Haki za Binadamu zinajumuisha yale mahitaji yote Ambayo mwanadamu anayahitaji kuyapata ili kukamilisha ubinadamu wake ,ikiwa ni Pamoja na Chakula,Malazi,Kuishi na Kuthaminiwa utu wake.

Bi. Fatma alisema dhana ya Haki za Binadamu ni pana ila katika ulimwengu huu ambao kumekua na uvunjifu mkubwa wa Haki za Binadamu ni lazima kuwepo na Masuala ya Uwazi,Uwajibikaji,Usawa na Kuheshimiana utu wa Mtu ili kukamilisha dhana ya Utawala Bora.

Bi. Fatma alihitimisha mada yake kwa kutaja Mihimili mikuu ya Dola na namna kila moja inavyofanya kazi katika kuendeleza ustawi wa jamii Ikiwa ni pamoja na Muhimili wa Mahakama, Baraza la Wawakilishi na Serikali kuu.

Jumla ya Walimu wastaafu (35) walipata nafasi ya kushiriki katika Mafunzo hayo ambayo yalitanguliwa na Mafunzo kwa siku ya kwanza ya tarehe 28 Novemba mwaka 2013 na tarehe 29 Novemba mwaka 2013 ilikua ni siku ya kuwachagua viongozi wapya watakao iongoza Jumuia hiyo ambapo Walimu (23) walikua ni kutoka Unguja na (12) ni kutoka Pemba kati ya hao Wanaume walikua ni (25) na Wanawake (10).

Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar (ZLSC) Kipo ili kuisaidia jamii kuwa na muelekeo wa upatikanaji wa Haki mbali mbali ambazo mwananchi yupo mbali nazo kuzifikia na pia Kutoa Ushauri wa kisheria pale unapohitajika na Jamii.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Harusi Miraji Mpatani Akitoa Ukaribisho kwa Walimu wastaafu waliohudhuria Semina ya siku mbili katika ukumbi wa ZLSC Migombani

Maalim Uledi Juma Wadi akitoa nasaha zake kwa niaba ya Mh.Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali katika Mkutano wa Walimu Wastaafu, kulia ni Maalim Khamis Abdulhamid

Oktoba - Disemba, 2013sheria na haki

Page 6: Toleo Na. 016 Jarida la kila miezi mitatu Oktoba - Disemba ... 16.pdf · Wadhamini ( ZLSC) PrOF.Chris Maina Alie shikilia kitabu ni Mwanasheria wa ZLSC Pemba Bi.Safia Saleh Sultan

6 sheria na haki Oktoba - Disemba, 2013

MakaLa Ya sheria

Na Safia Saleh Sultan ZLSC. Pemba

UTANGULIZI Ardhi ni rasilimali ya msingi katika uhai na maendeleo ya Binadamu,taasisi, wanyama, mimea na Taifa kwa ujumla. Rasilimali hii inayohitajika ili kuweza kukuza viwanda, biashara na mahitaji mengine ya Binadamu, kwa sababu umiliki wa ardhi (ambapo kisheria hujumuisha na vitu vilivyo juu na chini ya ardhi kama nyumba, mashamba na madini) ni moja ya vigezo vinavyopima kufanikiwa kimaisha na kimaendeleo na pia kumrahisishia anayemiliki kufikia malengo mengine ya kijamii na biashara pasipo vikwazo vikubwa. Migogoro ya ardhi nchini imekuwa ikiongezeka siku hadi siku, na hii husababishwa na vitu vingi kama vile kutokuwa na elimu juu ya sheria za ardhi, umaskini, kutelekezwa kwa ardhi,umiliki wa kiwanja kimoja kwa watu wawili tofauti.

MAANA YA ARDHIArdhi ni sehemu ya dunia yenye mchanganyiko wa mchanga na udongo. Mtazamo wa kisheria neno ardhi lina maana pana zaidi, kwa mujibu wa sheria ya Matumizi ya Ardhi namba 12/1992 sheria ya Zanzibar neno “ardhi” inatafsiriwa ardhi yenyewe pamoja na ile sehemu ya ardhi iliyofunikwa na maji pia na vitu vyote vinavyoshikana na ardhi yakiwemo majengo na vitu vyengine vyote vilivyoshikana na ardhi isipokuwa miti iliyoainishwa wazi na inayomilikiwa tofauti na ardhi iliyopo.

MAHAKAMA INAYOSHUGHULIKIA MASHAURI YA ARDHIMnamo mwaka 1994 Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilipitisha sheria ya kuanzishwa kwa Mahakama ya Ardhi, Sheria Namba 7/1994 kama ilivyorekebishwa na sheria namba 1/2008, Mahakama hii ilianza kufanya

Taratibu za Kufungua Mashauri ya Ardhi Mahakamani

kazi rasmi mwaka 2006. kazi ya Mahakama hii ni kusikiliza mashauri/migogoro ya Ardhi na kuitolea uamuzi, kabla ya kuundwa kwa Mahakama ya ardhi, mashauri ya ardhi yalikua yakisikilizwa na Mahakama za kawaida Unguja na Pemba, ambapo ilionekana kua, kesi hizi zilikua zikichelewa sana kutolewa maamuzi. Kwa upande wa Unguja, ofisi za Mahakama ya Ardhi zipo Vuga na kwa upande wa Pemba, ofisi za Mahakama ya Ardhi zipo Machomane kwa Mkoa wa Kusini na Wete kwa Mkoa wa Kaskazini.

Mahakama hii ya Ardhi ina mamlaka sawa na Mahakama ya Mkoa na ndio maana rufaa zinazotoka Mahakama ya Ardhi zinaenda Mahakama Kuu na sio Mahakama ya Mkoa kwa sababu mamlaka zao zipo sawa.

Kushindwa kuwasilisha malalamiko au kuripoti mgogoro katika mamlaka isiyo na uwezo wa kusikiliza shauri, humaanisha kupoteza haki yako ya msingi na kikatiba huku ukiona kwa macho yako, hivyo inapaswa tufahamu kwamba mashauri yote yanayohusiana na ardhi yanatakiwa kuwasilishwa katika Mahakama ya Ardhi na siyo Mahakama nyengine. MAMLAKA YA MAHAKAMA YA ARDHIKwa mujibu wa kifungu cha 13 cha sheria ya Mahakama ya ardhi namba 7/1994, ambacho kimefanyiwa marekebisho na kifungu cha12 cha sheria ya marekebisho namba 1/2008, ni kua, Mahakama hii ina uwezo wa kusikiliza kesi ambazo wadaawa wake wanagombania ardhi, ikiwa ni pamoja na kesi zinazohusu mizozo ifuatayo:

a) Kesi zinazohusu madai ya haki ya matumizi ya ardhi na kushikilia ardhi yoyote ile.

b) Kusimamia uwekaji wa mipaka katika

ardhi yenye shughuli zinazohitaji ugawaji wa vikataa vya ardhi na suala jengine lolote ambalo linalihitaji uwekaji wa mipaka au upimaji wa ardhi.

c) Kuthibitisha uhaulishaji wowote au ukodishaji ambao umeshafanyiwa uchunguzi na Bodi ya kuhaulisha ardhi.

d) Matumizi, maendeleo na uwezo wa ardhi.

e) Ardhi yenye wamiliki zaidi ya mmoja.f) Kutathmini ardhi na masuala mengine

yanayohusu malipo ya fidia ya ardhig) Kuchukuliwa ardhi na Serikali.h) Kuhaulisha mali ambako ni kinyume

na sheria zinazotumika.i) Kilimo au viwanda vya mazao ya

kilimo au mikataba ya kukodisha ardhi.

j) Mabadilishano, ugawaji usio wa kisheria na matatizo mengine yanayohusu mgawanyo au ukataji wa vikataa vya ardhi usio halali;

k) Umilikaji wa ardhi katika maeneo ya miji na maeneo ya kilimo;

l) Matumizi ya maendeleo ya ardhi kwa madhumuni ya hifadhi na matumizi ya mali asilia;

m) Kesi zinazoletwa na Mkurugenzi wa ardhi kwa madhumuni ya kurudisha ardhi yoyote inayomilikiwa na mtu yeyote.

n) Kurudisha Serikalini ardhi inayomilikiwa na umma.

TARATIBU ZA KUFUNGUA MASHAURI YA ARDHI MAHAKAMANIMdai atapaswa kufungua shauri lake katika Mkoa ambao ardhi inayobishaniwa ipo, na madai hayo yatatakiwa yawe katika hati

Jengo la Mahkama ya Ardhi lililopo Vuga Mjini Unguja

Page 7: Toleo Na. 016 Jarida la kila miezi mitatu Oktoba - Disemba ... 16.pdf · Wadhamini ( ZLSC) PrOF.Chris Maina Alie shikilia kitabu ni Mwanasheria wa ZLSC Pemba Bi.Safia Saleh Sultan

7Oktoba - Disemba, 2013sheria na haki

MakaLa Ya sheria

Taratibu za Kufungua Mashauri ya Ardhi Mahakamanimaalum ya kimaandishi(hati ya madai) yatapelekwa Mahakamani yakiwa na maelezo ya anachokidai kwa ufupi pamoja na vielelezo vinavyothibitisha madai yake (kama vipo).Hapa Mdai ni muhimu kukumbuka kwamba shauri analofungua ni lazima afungue kwa kuzingatia mkoa ambapo ardhi yenyewe ipo.

Baada ya kupokea na kufungua madai, karani wa Mahakama atatoa hati za wito (Summons) kwa Mdaiwa/wadaiwa kwa kutumia anuani zao za makaazi au posta. Hati ya wito itaonyesha pahala na saa ya kufika kwenye Mahakama ya ardhi na itaambatanishwa na nakala ya hati ya madai pamoja na vielelezo vyote ambayo Mdai/Wadai wameviwasilisha Mahakamani. Baada ya hapo, hati hiyo ya wito atapatiwa Mpelekaji wito (Server) na ataipeleka kwa Mdaiwa/wadaiwa. Baada ya kumpata Mdaiwa, Mpelekaji wito, atamtaka Mdaiwa kutia saini yake nyuma ya nakala ya hati ya wito. Baadae Mpelekaji wito nae, ataingiza tarehe nyuma ya nakala ya hati hiyo na pia ataeleza pahala na wakati alipompata Mdaiwa. Baadae, nakala hiyo ya wito itarejeshwa kwa karani wa Mahakama kama ni uthibitisho wa kupatikana Mdaiwa.

Iwapo Mpelekaji wito atashindwa kumpata Mdaiwa ndani ya siku 14, ataingiza ndani ya hati ya wito maelezo hayo na sababu za kushindwa kumkabidhi Mdaiwa hati hiyo ya wito, baadae atairejesha kwa karani ambae nae atarekodi taarifa hiyo katika hati husika, na mara moja atamjulisha Mdai. Hati ya wito pia inaweza kutumwa kwa njia ya rejista ya posta. Pia iwapo Mdaiwa atakataa kupokea wito au atapokea wito lakini atashindwa kufika Mahakamani bila ya sababu yoyote ile ya msingi, basi Mahakama itaendelea kulisikiliza shauri hilo upande mmoja na baadae kutoa hukumu itakayoona inafaa kisheria. Kwa upande wa Mdaiwa aliefika Mahakamani, atahitajika kujibu madai dhidi yake kwa maandishi ndani ya siku 14.

UKOMO WA KUFUNGUA MASHAURI YA ARDHIKwa mujibu wa sheria ya ukomo Sura ya 12 ya 1917, sheria ya Zanzibar, sheria hii ni ya ukomo katika kusimamia mashauri yote ya madai kama vile ardhi, mikataba, n.k. Sheria hii inatoa fursa ya kuwasilisha mashauri/migogoro ya ardhi katika mahakama ya ardhi ndani ya kipindi maalum, hivyo mashauri/

madai/malalamiko yoyote ya masuala ya madai yanatakiwa yafunguliwe ndani ya muda ambao sheria hii imeweka, shauri litakalofunguliwa nje ya muda uliowekwa na sheria bila ya sababu za msingi za kuithibitishia Mahakama basi shauri hilo litafutwa Mahakamani hapo kwa vile limepitwa na muda ambao umeainishwa katika sheria hii.

Ifahamike tu kwamba sio kazi ya Mahakama kuibua kwamba shauri husika limepitwa na wakati bali ni jukumu la mlalamikiwa/mdaiwa—walalamikiwa/wadaiwa kuwasilisha pingamizi za awali. Mlalamikaji binafsi au wakili wake kuwasilisha kwa njia ya pingamizi na kuithibitisha hoja hiyo mbele ya mahakama sambamba na kuiomba kulifutilia mbali shauri husika. Uthibitisho huo ambao huwasilishwa kisheria na kihistoria ndiyo unaotumika kuiomba mahakama kukubali au kukataa maombi husika kutegemea na uzito wa hoja zilizowasilishwa na pande zote katika kesi.

Hivyo basi inabidi tuangalie mambo ya msingi katika mashauri ya Madai kabla ya kufungua shauri Mahakamani kama msemo wa kisheria unavyosema “Shinda kesi kabla hujaenda Mahakamani”

Sheria hii ya ukomo hutumika katika kusimamia ufunguzi wa mashauri yote ya asili ya madai kama vile mikataba, ardhi, madhara na mengine yote yenye asili ya madai. Sheria hiyo ya ukomo inatoa fursa ya kuwasilisha mashauri yenye asili ya migogoro ya ardhi katika Mahakama ya Ardhi katika kipindi cha miaka 12 tangu kutokea kwa mgogoro. Maana ya msimamo huu wa kisheria ni kwamba malalamiko yoyote yanayohusu ardhi yaliyoibuka baada ya miaka hiyo hayatakuwa na haki ya kusikilizwa na kuamuliwa kama ilivyo kwa mashauri mengine, hii ni kwa sababu sheria haitotambua umiliki wako wa ardhi hio ikiwa kipindi chote cha miaka 12 imevamiwa au imechukuliwa na mmiliki halali akakaa kimya bila ya kuidai popote, hivyo sheria inamzuia mtu huyo kufungua shauri hilo isipokuwa tu pale ambapo Mdai/Wadai walikuwa hawajui kama ardhi hio imevamiwa mpaka kipindi cha miaka 12 au zaidi kupita ndipo walipofahamu hapa sheria hii haitotumika kwa vile Mdai alikuwa hajui, lakini Mdai/Wadai atalazimika/watalazimika kuithibitishia Mahakama kwamba kipindi chote hicho cha miaka 12 na zaidi kwamba wao walikuwa hawajui kama

ardhi hio imevamiwa .

Lakini kutokana na kutokidhi haja ya sheria ya ukomo pekee, inatosha kwa mahakama kukubali kutosikiliza malalamiko ya mdai ambayo yamepita kipindi cha miaka 12. Kwani kipindi hicho ni kirefu kutosha kukidhi haja ya kufungua na kufuatilia kesi husika Mahakamani, ni kipindi kinachoshuhudia mabadiliko mengi katika ardhi husika na ni kwa ajili hiyo ili kuondoa usumbufu na kuhamasisha wamiliki wa ardhi kuwajibika na ardhi zao ndipo iliwekwa sheria hii kwa makusudi kusaidia na kuchochea kutilia maanani na kujali miongoni mwa raia.

Hivyo ni vyema kufuatilia mara kwa mara vipande vya ardhi tulivyomilikishwa kihalali ili kuepuka adha ya kuvamiwa na kukaliwa na watu wengine kwa muda mrefu kiasi cha kusababisha mgogoro ambao hatimaye huishia kupoteza umiliki wa ardhi ambayo ndiyo chanzo kikuu cha uchumi miongoni mwa Watanzania wengi.

CHANGAMOTO WANAZOKUMBANA NAZO WANANCHI

1. Wananchi kutoelewa Sheria ya Ukomo. Wengi hawaijui sheria hii hali inayopelekea mashauri mengi ya ardhi kufutwa Mahakamani kwa pingamizi za awali za ukomo wa muda wa kufungua shauri hilo

2. Wananchi wengi wanachelewa kufungua mashauri yao ya ardhi mpaka muda unapita. Wananchi walio wengi wanajisahau kufungua mashauri ya ardhi wakati yamevamiwa kwa kuegemea warka mpaka kipindi cha miaka 12 kinapita.

3. Wengi wanakosa haki yao ya umiliki wa ardhi kwa kutokuelewa muda wa ufunguaji wake

MAPENDEKEZO

1. Elimu ya sheria hii ya ukomo inahitajika kwa wananchi.

2. Ni vyema kuzifuatilia ardhi ambazo tuna umiliki nazo mara kwa mara ili kuweza kuepusha migogoro na adha ya kuvamiwa kwa ardhi hizo.

3. Wananchi wajenge utamaduni wa kujisomea sheria mbali mbali ili waweze kulinda na kutetea haki zao

HITIMISHO: Ardhi ni muhimu katika maendeleo na uchumi wa Binadamu na ni nyenzo pekee ya maendeleo kwa wananchi, hivyo hatuna budi kuitunza,kuiboresha ,kuifuatilia mara kwa mara na kufuata taratibu za kisheria. Bila ya kufuata taratibu za kisheria migogoro ya ardhi itazidi kuongezeka siku hadi siku. Ni vyema kuendeleza kazi ya kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa matumizi bora ya ardhi. Hivyo ni wajibu wa kila raia kujitahidi kupata uelewa wa masuala ya ardhi, ili kujiepusha na migogoro.Pia Serikali, mashirika pamoja na Asasi za Kiraia zinapaswa kuhakikisha kuwa, wananchi na viongozi wanapatiwa elimu ya kutosha kuhusiana na masuala yahusuyo Sheria za Ardhi. Hilo likifanyika, tutaweza kupunguza kwa asilimia kubwa migogoro ya ardhi katika nchi yetu. Picha hii ya kipande cha Ardhi ni moja ya kielelezo cha maeneo mengi yalivyo na muonekano huu katika visiwa vyetu vya Unguja na Pemba

Page 8: Toleo Na. 016 Jarida la kila miezi mitatu Oktoba - Disemba ... 16.pdf · Wadhamini ( ZLSC) PrOF.Chris Maina Alie shikilia kitabu ni Mwanasheria wa ZLSC Pemba Bi.Safia Saleh Sultan

8

MakaLa Ya sheria

Thabit Abdulla Juma, ZLSC, Unguja.

UTANGULIZI.Dhana ya Polisi Jamii sio dhana mpya katika jamii kwani ipo miaka mingi duniani, hii inajithibitisha kupitia muasisi wa falsafa hii ya polisi jamii bwana Robert Peel ambapo mnamo mwaka 1829 huko nchini Uingereza alianzisha “Metropolitan Police, London”, huku akifafanua zaidi jukumu la polisi.

Vile vile, itasomwa kupitia kitabu cha The Police and The Community” cha bwana David L. Carter na bwana Louis A. Radelet ambao kupitia kitabu hicho wanaeleza “The role of new police is to maintain at all times a relationship with the public that gives reality to the historic tradition that “The Police are the Public, and that the Public are the Police”…..”. Kiujumla maneno hayo yana maana ya kuwa ni jukumu la Polisi kuhakikisha kuwa kuna uwepo wa mahusiano ya karibu na jamii, uhusiano ambao utatoa sura ya kihistoria kuwa “Polisi ni watu, na watu ni Polisi”.

Tanzania, dhana hii imetokana na mawazo yaKamanda Mkuu wa Jeshi la Polisi mstaafu IGP Said Mwema ambapo aliona kuna umuhimu mkubwa wa kuanzishwa kwa polisi jamii ili waweze kusaidia moja kwa moja katika jamii kutokana na uchache wa askari polisi katika jamii.

MAANA NA DHANA YA POLISI JAMII.Polisi Jamii ni mkusanyiko katika jamii ya vijana au wananchi waliojiunga pamoja ili kutokomeza uhalifu kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi katika mitaa, shehia na majimbo yao.

Mpango wa polisi jamii ni mtazamo madhubuti wa jinsi ya kupanga mikakati ya utendaji ya polisi; msingi wake mkuu ukiwa ni imani kuwa askari.

Polisi wakifanya kazi pamoja na wananchi, wanaweza kusaidiana kutatua matatizo yanayoikabili jamii yanayohusu uhalifu,

Uwepo wa Polisi Jamii Zanzibar Kunapunguza Uhalifu

vurugu, pamoja na jamii kuzorota, kutokana na kutojali maendeleo ya vijana na jamii.Dhana ya polisi jamii ni dhana kubwa sana ambayo ndani yake imebeba Ulinzi Shirikishi (Kufanya doria na kupunguza Uhalifu), Usalama wa barabarani, Usafi wa Mji na Mitaa.

UWEPO WA POLISI JAMII .Licha ya kuwa polisi jamii wapo na wanasaidia kwa kiasi kikubwa katika jamii zetu lakini hamna sheria inayotambua polisi jamii wala sera inayoonesha moja kwa moja juu ya uanzishwaji wake. Hivyo, vifungu vifuatavyo vinatumika katika kuitambua na kuihalalisha polisi jamii:

1) Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, Ibara ya 13 (1) na 13 (2), kwa mujibu wa Ibara hii; kila mtu anayo haki ya kuwa hai, hivyo Ulinzi na Usalama ni haki ya kila mmoja katika jamii.( polisi jamii kama ulinzi shirikishi inasaidia katika usalama wa nchi kwa kupiga doria na kukamata wahalifu)

2) Sheria ya Tawala za Mikoa nambari 1 ya 1998 – Sheria ya Zanzibar.

Kifungu cha 17 (1), kila Sheha ana dhamana zifuatazo katika Shehia yake.Sheria hio inaeleza,

17 (1) a. “Kutekeleza sheria zote za Serikali, amri, sera, na maelekezo, kwa ajili ya kudumisha Sheria na taratibu nchini”

b. “Kusuluhisha na kutatua migogoro ya kijamii na kifamilia katika eneo lake”

Kwa mujibu wa kifungu hicho katika kudumisha sheria na taratibu za nchi, katika kutekeleza majukumu yao Sheha wanashirikiana na vijana na wanajamii kiujumla juu ya ulinzi na usalama.

3) Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, nambari 7 ya 2004 – Sheria za Zanzibar.

Kwa mujibu wa Kifungu cha 13 (1) na 13 (2) cha Sheria hio Askari Polisi au mtu mwengine anapotaka kukamata basi anatakiwa kumgusa bega mkamataji.

Kutokana na maelezo ya kifungu hichi, ni wazi kwamba askari jamii wanaweza wakamkamata mtu.

Kifungu cha 26 (1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, nambari 7 ya 2004 – Sheria za Zanzibar, kinaeleza kuwa mtu binafsi (asiyekuwa askari) anaweza kumkamata mtu yoyote ambae anafanya kosa au anashutumiwa kutaka kufanya kosa. Hivyo, ni haki ya polisi jamii kuweza kufanya kitendo cha kuwakamata wahalifu.

VIGEZO VYA KUPATIKANA KWA POLISI JAMII.Miongoni mwa vigezo na sifa ambazo zinaangaliwa ni kama ifuatavyo:

* Mtu huyo atokea katika shehia husika.* Asiwe muhalifu.* Asiwe mtumiaji wa madawa ya kulevya.

Kiujumla hizo ndio sifa na vigezo vikuu ambavyo huangaliwa kwa kuchunguzwa na uongozi uliopo katika shehia husika kabla ya kijana au mwananchi kujiunga na polisi Jamii.

MAFUNZO YANAYOTOLEWA KWA POLISI JAMII. Kutoka na kuanzishwa kwa polisi jamii Zanzibar, vijana hao hupatiwa mafunzo mbalimbali kutoka kwa jeshi la polisi. • Ukamatajisalama.• Mazoeziyajudo.• Mafunzoyakufanyaupekuzi.• Namnayakufanyadoria.• Mbinuzakumtambuamhalifu.• Jinsi ya kutoa taarifa katika kituo cha

Polisi kuomba msaada wa haraka.• Jinsi kujikinga na wahalifu wakaidi na

hatari.

MAFANIKIO YALIYOPATIKANA KWA KUWEPO POLISI JAMII.Uwepo wa polisi jamii na dhana ya ulinzi shirikishi umeleta mafanikio makubwa katika hali ya ulinzi na usalama. Miongoni mwa mafanikio yaliyopatika kutoka na kuwepo kwa polisi jamii katika shehia zetu ni haya yafuatayo:

* Kupungua kwa vitendo vya wizi na uhalifu.Kuwepo kwa Polisi Jamii kumesaidia kupunza vitendo vya uporaji, wizi na uhalifu. Mfano mzuri ni kupitia kwa Polisi Jamii wa Mji Mkongwe ambapo wamejitahidi kwa bidii kubwa juu ya kupambana na uhalifu kwa kiasi ambacho uporaji na wizi umepungua katika maeneo ambayo yalikuwa

sheria na haki Oktoba - Disemba, 2013

Kamanda wa Kanda Maalum ya Kipolisi Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova na Polisi Jamii wa Mji Mkwongwe, Ambapo Kikundi Hichi cha Askari Jamii Wamepata Zawadi ya Zanzibar One na Tanzania One Kuwa ni Askari Jamii Waliofanya Vizuri Zaidi Katika Jamii

Page 9: Toleo Na. 016 Jarida la kila miezi mitatu Oktoba - Disemba ... 16.pdf · Wadhamini ( ZLSC) PrOF.Chris Maina Alie shikilia kitabu ni Mwanasheria wa ZLSC Pemba Bi.Safia Saleh Sultan

9

MakaLa Ya sheria

Uwepo wa Polisi Jamii Zanzibar Kunapunguza Uhalifu

yanahatarisha usalama na maisha ya wananchi na wageni , maeneo hayo ni kama vile Malindi Funguni Mjini Unguja.

* Kupungua kwa watumiaji wa madawa ya kulevya.Uwepo wa Polisi Jamii Nchini kumesaidia kupunguza idadi ya watumiaji wa madawa ya kulevya ambapo idadi ya watumiaji ilikuwa inakuwa kwa kasi na utumiaji ulikuwa unafanyika hadharani katika mitaa tofauti hasa mjini, kwa sasa watumiaji hao wamepungua kwa kiasi ambacho hawaonekani ovyo mitaani wakitumia madawa ya kulevya kama vile bangi.

* Ongezeko la kuripotiwa kwa taarifa za uhalifu. Licha ya kupambambana moja kwa moja baina ya askari jamii na wahalifu lakini wanajamii hao wamekuwa wakitoa taarifa mara kwa mara kwa Askari Polisi kila unapotokea au kuelekea kutokea kwa uhalifu katika jamii.

* Kutoa ajira kwa vijana mitaani. Kuanzishwa kwa Polisi Jamii kumesaidia vijana wengi kukuza uchumi baada ya kujipatia ajira hii katika na kuweza kujisaidia kwa kiasi fulani kuendesha maisha yao.

* Kumesaidia vijana kuachana na vigenge visivyo na ulazima na umuhimu katika jamii. Mbali na kujipatia ajira kutokana na kuanzishwa kwa Polisi jamii lakini pia kumewasaidia vijana ambao wamejiunga na Polisi Jamii kuweza kutoka katika vigenge ambavyo havina umuhimu wala haviwezi kuwaletea maendeleo zaidi ya kupoteza muda na kuwa vichochezi vya kuingia katika uhalifu.

Kiujumla uwepo wa Polisi Jamii kumesababisha uwanzishwaji wa Kamati ya Ulinzi na Usalama katika Shehia, ambapo kumekuza usalama wa kijamii na wanajamii kiujumla. Kutoka na

Oktoba - Disemba, 2013sheria na haki

hali hio watu wengi wamekuwa wakipata ile haki yao ya Kikatiba ya kuweza kuishi kwa usalama.

CHANGAMOTO.Uwepo wa polisi wa polisi jamii umeleta mfanikio makubwa kwa taifa. Hata hivyo, kuna changamoto nyingi ambazo zinawakabili, miongoni mwa changamoto hizo ni:

* Kukosekana kwa sheria, sera na miongozo dhidi ya polisi jamii.

* Ukosefu wa fedha za kuwawezesha katika kutekeleza majukumu yao kama njia ya kuwahamasisha.

* Maisha yao kuwa hatarini kutoka kwa wahalifu.

* Kupigwa mawe.* Kutishiwa maisha kwa visu na mapanga.

* Usheleweshwaji wa kesi ambazo huzifikisha kituo cha polisi.

HITIMISHO.Polisi jamii ni kitengo muhimu na kizuri sana katika jamii, kwani kinawapatia raia wa kawaida amani na kujiskia kuwa wanapata ulinzi wa kutosha dhidi ya mali na maisha yao kwa ujumla.

Lakini kumwekuwa na matukio tofauti ya hawa polisi jamii tunaowategemea watupatie ulinzi kama vile; kujifunika sura zao wakati wa kufanya dori hali ambayo hata wahalifu wanaweza waziba sura zao na kufanya uhalifu huku ikiaminika ni polisi jamii. Vilevile, kumpatia mtu adhabu hasa ya kumpiga, ifahamike kuwa wao hawajatambulika kisheria na wao ni kundi mikakati tu ya jamii ikishirikiana na idara ya polisi katika kuimarisha usalama.

Serikali kweli imetambua umuhimu wa uwepo wa askari jamii, hilo ni fanikio la awali. Sasa ni muda muafaka wa serikali kuunda sheria na kanuni maalum kwa ajili ya askari jamii ili kuwapatia wananchi amani zaidi na kujenga imani zaidi ya uwepo wa askari jamii.

Kamanda wa Kanda Maalum ya Kipolisi Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova na Askari Wengine wa Jeshi la Polisi Wakiwa na Polisi Jamii wa Mji Mkwongwe

Afisa Mipango kutoka ZLSC Akifanya Mahojiano na Naibu Katibu wa Polisi Jamii wa Mji Mkongwe Bw. Suleiman Hemed Mohammed

Page 10: Toleo Na. 016 Jarida la kila miezi mitatu Oktoba - Disemba ... 16.pdf · Wadhamini ( ZLSC) PrOF.Chris Maina Alie shikilia kitabu ni Mwanasheria wa ZLSC Pemba Bi.Safia Saleh Sultan

MATUKIO KATIKA PICHA

10 sheria na haki Oktoba - Disemba, 2013

Profesa Chris Maina Peter

Mwenyekiti wa Bodi ya

Wadhamini ZLSC Akisalimiana

na Makamo wa Pili wa Rais

wa Zanzibar Mh.Balozi Seif

Ali Iddi ambae Alikua Mgeni

Rasmi katika Kumbukizi ya

Profesa Haroub Othman

EACROTANAL Zanzibar

Profesa Chris Maina Peter Mwenyekiti wa Bodi

ya Wadhamini ZLSC akizungumza na washiriki wa kongamano la kupinga

kutekelezwa kwa Adhabu ya kifo,Kulia ni Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar Ibrahim

Mzee Ibrahim. Kushoto ni Jaji wa Mahkama kuu ya Zanzibar Bi. Rabia Hussein na Pembeni

ni Mkurugenzi Mtendani Kituo cha Huduma za Sheria Harusi

Miraji Mpatani

Waziri wa Katiba na Sheria Mheshimiwa Aboubakar

Khamis Bakary katika picha ya pamoja na washiriki na watendaji wa Kituo cha

Huduma za Sheria Zanzibar katika Maadhimisho ya siku ya

Haki za Binadamu duniani

Page 11: Toleo Na. 016 Jarida la kila miezi mitatu Oktoba - Disemba ... 16.pdf · Wadhamini ( ZLSC) PrOF.Chris Maina Alie shikilia kitabu ni Mwanasheria wa ZLSC Pemba Bi.Safia Saleh Sultan

MATUKIO KATIKA PICHA

11Oktoba - Disemba, 2013sheria na haki

Makamu wa Pili wa Rais wa

Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi

pamoja na baadhi ya viongozi

na watendaji wa Kituo cha

Huduma za Sheria wakiwa

katika picha ya pamoja mara

baada ya uzinduzi wa kitabu

cha Zanzibar Yearbook of Law

katika ukumbi wa Eacrotanal

Mjini Unguja

Baadhi ya Masheha, Polisi

na Watendaji wa Mahakama

wakifuatilia kwa umakini

mafunzo yaliyotolewa na ZLSC

kuhusiana na kufahamu na

kutekeleza amri za Mahakama

ya Ardhi

Jaji wa Mahakama Kuu ya

Zanzibar Mheshimiwa Rabia

Hussein akiwa katika picha ya

pamoja na baadhi ya viongozi

na washiriki wa Maadhimisho

ya kupinga Adhabu ya kifo

katika ukumbi wa ZLSC

Migombani, Unguja

Page 12: Toleo Na. 016 Jarida la kila miezi mitatu Oktoba - Disemba ... 16.pdf · Wadhamini ( ZLSC) PrOF.Chris Maina Alie shikilia kitabu ni Mwanasheria wa ZLSC Pemba Bi.Safia Saleh Sultan

12

MakaLa

Na Jina Mwinyi Waziri. ZLSC - Unguja

UTANGULIZIJeshi la polisi limekasimiwa kisheria kuwa na mamlaka ya kuingilia haki na uhuru wa watu ambao wamepewa na Katiba na sheria za nchi. Mamlaka hayo ni pamoja na kukamata, kupekua, kupeleleza, na kumpa mtu dhamana kwa hatua za mwanzo za utuhumiwa wakati kesi iko miokononi mwao. Lakini mamlaka haya yakitumiwa vibaya au visivyo huleta manung’uniko na watu kuichukia na kutokuwa na imani na chombo chao cha kulinda maisha na mali zao.

MAANA YA UPEKUZI Ni tendo la kuingia aidha maungoni mwa mtu, ndani ya nyumba au makazi ya mtu kwa nia ya kutafuta kitu au vitu vilivyofichwa. Au vitu ambavyo vinahusiana na kosa la jinai na kwamba kitu au vitu hivyo vinaweza kusaidia katika upelelezi wa kipolisi au katika kesi inayoendelea Mahakamani kama sehemu ya ushahidi wa kukanusha au kuthibitisha kosa.

Tendo la kupekua ni eneo linalozua malalamiko mengi kwa sababu linaingilia haki ya faragha, usalama, na uhuru wa mtu unaotolewa kwa mujibu wa Katiba zetu mbili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 ambazo zote kwa pamoja zinaeleza kuwa:-

“Kila mtu anastahiki kuheshimiwa na kupata hifadhi kwa nafsi yake, maisha yake binafsi na familia yake na unyumba wake, na pia heshima na hifadhi ya maskani yake na mawasiliano yake ya binafsi.”

Aidha ingawa kuna ruhusa hiyo iliyotolewa na Katiba ambayo ni sheria mama katika nchi bado Katiba hiyo hiyo inatoa ruhusa ya kupekuliwa na kuingiliwa mtu faragha yake

Utaratibu wa Upekuzi wa Mtuhumiwa na Upekuzi wa Makazi Kisheria

ikiwa kuna ulazima wa kufanya hivyo lakini kwa kufuata taratibu za kisheria za nchi.

Kifungu cha 15 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 na Ibara ya 16 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 zinaeleza kuwa:-

“…….mamlaka ya nchi itaweka utaratibu wa sheria kuhusu hali, namna na kiasi ambacho haki ya mtu ya faragha na ya usalama wa nafsi yake, mali yake na maskani yake, yaweza kuingiliwa…..”

AINA ZA UPEKUZIKwa mujibu wa sheria ya mwenendo wa makosa ya Jinai nam.7 ya mwaka 2004 inaonesha kuwa kuna aina mbili za upekuzi, ambazo ni:-

1. Upekuzi unaofanyika kwa hati ya upekuzi.

2. Upekuzi unaofanyika bila hati ya upekuzi.

* Upekuzi unaofanyika kwa hati ya upekuzi ni ule upekuzi ambao unatolewa kwa hati maalum na Jaji au Hakimu wa Mahkama inayowapa nguvu polisi kufanya upekuzi wa mtu anaetuhumiwa au pahala panapotuhumiwa.

Pia inafaa ifahamike kuwa hati ya upekuzi inaweza pia kutolewa na Mkuu wa Kituo cha Polisi katika eneo linalotakiwa kufanyiwa upekuzi.

Upekuzi unaofanyika bila hati ya upekuzi, ni ule upekuzi ambao unafanywa na Askari polisi bila ya idhini ya Jaji, Hakimu au Polisi.

MADHUMUNI YA UPEKUZIMadhumuni makuu ya upekuzi wa mtu au mahali ni:-

* kutafuta ushahidi wa jambo analohusishwa mtuhumiwa na kosa linalomkabili.

* Kupatikana kwa ushahidi wa kutosha utakaopelekea mhusika kuweza kutoa uamuzi wa kufungua au kutofungua kesi mahakamani.

WATU WANAORUHUSIWA KUFANYA UPEKUZI Kwa mujibu wa sheria, Kifungu cha 74 cha Mwenendo wa makosa ya Jinai Nam. 7/2004 watu wanoruhusiwa kufanya upekuzi ni hawa wafuatao:

(a) Askari polisi (b) Afisa aliyeruhusiwa na Sheria yoyote

ile kufanya upekuzi kwa mfano afisa wa Chuo cha Mafunzo wakati wa kumtafuta mfungwa aliepotea, na

(c) Afisa yeyote atakayeruhusiwa na Mkurugenzi wa Mashtaka.

Kabla ya upekuzi kufanywa, afisa wa polisi anayehusika anatakiwa kufanya matayarisho ikiwemo kutafuta taarifa kutoka vyanzo vya habari mbali mbali vinavyoaminika vya eneo litakalofanyiwa upekuzi na pahali gani kitu kinachotafutwa kimefichwa. Afisa husika wa upekuzi ataweka ulinzi wa eneo la kupekuliwa, kama milangoni na madirishani.

VIPENGELE MUHIMU VINAVYOTAKIWA KUWEMO KATIKA HATI YA UPEKUZI Askari polisi au mtu yoyote yule aliepata ruhusa yakumpekua Mtuhmiwa au makazi yanayotia shaka juu ya uhalifu na kupewa hati ya upekuzi kwa mtuhumiwa huyo au makazi hayo ni lazima achunguze vipengele muhimu vya hati hiyo kama vimekidhi kisheria kabla ya kufanya upekuzi.

Kwa mujibu wa sheria ya mwenendo wa makosa ya Jinai nam.7 ya mwaka 2004 katika vifungu vya 116 ,118,120,123,124, na 125 vinaeleza vipengele muhimu na utaratibu wa kukamata mali au mtuhumiwa pamoja na kufanya upekuzi, vipengele hivyo ni hivi vifuatavyo:-

i. Jina la Afisa anayekwenda kufanya upekuzi, inaweza ikawa ni afisa mmoja au zaidi au ikaelekezwa kwa Kituo husika moja kwa moja,

ii. Jina la eneo linalokwenda kufanyiwa upekuzi

iii. Jina la anayekwenda kufanyiwa upekuzi (mtuhumiwa)

iv. Kosa linahusiana na upekuziv. Maelezo ya kosa kwa ufupivi. Orodha ya vitu vinavyokwenda

kufanyiwa upekuzi

sheria na haki Oktoba - Disemba, 2013

Polisi wakiwa katika tukio la Upekuzi kwa ajili ya Usalama wa Raia.

Page 13: Toleo Na. 016 Jarida la kila miezi mitatu Oktoba - Disemba ... 16.pdf · Wadhamini ( ZLSC) PrOF.Chris Maina Alie shikilia kitabu ni Mwanasheria wa ZLSC Pemba Bi.Safia Saleh Sultan

13

MakaLa

Utaratibu wa Upekuzi wa Mtuhumiwa na Upekuzi wa Makazi Kisheria

vii. Saini ya Jaji au hakimu aliyetoa hati ya upekuzi

viii. Muhuri wa Mahakama husika

VIPI POLISI WANAPEWA HATI YA UPEKUZI Polisi wakiwa katika tukio la Upekuzi kwa ajili ya Usalama wa Raia.

Kwa mujibu wa Sheria kifungu cha 145 kinaelezea juu ya Polisi anavyotakiwa kumshawishi Jaji au Hakimu kwamba wanazo sababu za msingi (probable cause) zinazowafanya waamini kuwa uhalifu unafanyika pahali na kunahitajika kufanyiwa upekuzi au ushahidi wa uhalifu unaweza kupatikana.

Ili kulifanikisha hilo Polisi hutoa taarifa kwa jaji au hakimu kwa njia ya maandishi na kiapo (affidavit) kueleza sababu zilizofanya waombe Hati ya Upekuzi.

Jaji au Hakimu ikiwa ataamini kwamba zipo sababu za msingi (probable cause) za kufanya upekuzi, atatoa Hati ya Upekuzi kwa lengo la kufanya upekuzi (search) ya mtu, vyombo vya moto au makazi.

KITU KINACHOTAFUTWA NA POLISI Sheria inaeleza kuwa Polisi watafanya upekuzi wa kitu wanachokitafuta na kukipeleka kunakohusika kwa lengo la ushahidi, lakini ikiwa watakuta kitu chengine au wataona ushahidi ambao haukuorodheshwa katika lengo lao la kufanya upekuzi wakati wanafanya upekuzi huo, watakuwa na nguvu za kisheria kukamata kitu hicho au kukusanya ushahidi huo.

Aidha Kifungu cha 148 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai Nam. 7/2004 kinaeleza kwamba, kitu chochote kitakachokamatwa ambacho kilitiliwa mashaka na anaefanya upekuzi, kitu hicho kitahifadhiwa mpaka kesi imalizike au uchunguzi ukamilike.

Pia sheria imetoa tahadhari ya kuhifadhi kitu hicho kwamba lazima ichukuliwe.

TARATIBU ZA KUFANYA UPEKUZIKifungu cha 147(2) cha Sheria kinaeleza kuwa kabla ya kuanza upekuzi, mhusika wa zoezi la upekuzi (ikiwa polisi au mtu yoyote alieteuliwa na mahakama) atawaita watu wawili au zaidi aidha Mwenyekiti wa kijiji, sheha au mtu yoyote anaeheshimika katika jamii au eneo linalofanyiwa upekuzi kuhudhuria na kushuhudia upekuzi huo na watu hao watatakiwa kusaini kila walichokishuhudia.

Lakini mashuhuda hao hawatolazimika kuhudhuria mahkamani kama mashahidi isipokuwa watakapoitwa na mahkama

Oktoba - Disemba, 2013sheria na haki

kwa kutumia hati ya wito wa Mahakama itakayowataka kufanya hivyo.

Aidha Kifungu cha 14, 17 na 18 cha Sheria vimempa ofisa wa polisi mamlaka ya kufanya upekuzi Maungoni, kupekua vyombo vya usafiri au makazi ya Mtuhumiwa wa kosa la Jinai.

Pia Kifungu cha 43 cha sheria kimewapa Maafisa wa Polisi uwezo wa kuvunja na kuingia ndani ya nyumba na kufanya upekuzi.

Pia sheria imemruhusu mtu anayeishi pahali panapofanyiwa upekuzi au mtu mwengine kwa niaba yake, aruhusiwe kushuhudia zoezi la upekuzi na apewe ikiwa ataomba, nakala ambayo imetiwa saini na mashuhuda ya vitu vilivyopekuliwa.

Kifungu cha 14 na 15 cha sheria kinaeleza kuwa, Ikiwa nyumba au jengo linalokusudiwa kufanyiwa upekuzi limefungwa, mhusika wa nyumba au jengo atatakiwa kuwaruhusu polisi kufanya upekuzi baada ya kuonyesha waraka (hati) wa kufanya upekuzi. Ikiwa mhusika hataki kufungua nyumba au jengo kwa ajili ya kufanyiwa upekuzi, polisi wana mamlaka ya kuvunja mlango au dirisha au sehemu yoyote ili waweze kuingia ndani kufanya upekuzi. UTARATIBU WA UPEKUZI NA KUKAMATA MTUHUMIWAInapotokezea Polisi kumkamata mtuhumiwa aliefanya kosa lolote lile la jinai hapo hawahitaji kuwa na waraka au hati ya kufanya upekuzi wa mtu huyo wakati wanapotaka kumkamata, na badala yake Polisi watamkamata mtuhumiwa huyo pamoja na kumpekua.

Aidha, polisi wana haki ya kujikinga dhidi ya shambulio la aliyekamatwa na

baadaye kumpekua mhusika kama anayo silaha na kumuangalia kama anacho kitu kinachoshukiwa ili kupata ushahidi.

UPEKUZI WA MWANAMKE Kwa mujibu wa sheria katika kifungu cha 19 kinaeleza kuwa, ikiwa aliyetuhumiwa kosa la Jinai ni mwanamke na kutakiwa kufanyiwa upekuzi kuhusiana na kosa alilotuhumiwa basi Mwanamke huyo lazima apekuliwa na mwanamke mwenzake tena kwa heshima.

CHANGAMOTO * Uelewa mdogo wa Utaratibu wa

Upekuzi. Inaonekanwa kwamba Askari wengi wanaopewa kazi ya kupekua watu au makazi hawafati taratibu za kisheria zinavyoelekeza katika upekuzi kwa sababu ya ukosefu wa uelewa wa sheria.

* Kutumia nguvu zisizo za lazima wakati wa upekuzi.

* Watu kutokuwa na uwelewa wa taratibu za upekuzi.

Hitimisho.Upekuzi ni moja kati ya kazi muhimu inayofanywa na polisi na inaingilia faragha ya watu pamoja na mali zao, hivyo ni jambo la msingi wahusika waliyopewa majukumu haya kuwa waangalifu wakutosha ili wasiende kinyume na taratibu za sheria pamoja na Katiba zinavyoelekeza.

Nembo ya Jeshi la Polisi la Tanzania.

Page 14: Toleo Na. 016 Jarida la kila miezi mitatu Oktoba - Disemba ... 16.pdf · Wadhamini ( ZLSC) PrOF.Chris Maina Alie shikilia kitabu ni Mwanasheria wa ZLSC Pemba Bi.Safia Saleh Sultan

14

hotuba

sheria na haki Oktoba - Disemba, 2013

Ndg. Mwenyekiti wa mkutano huu,Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Kituo Cha Huduma za Sheria Zanzibar, Profesa Chris Maina Peter Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar na watendaji wako waliohudhuria,Viongozi wa Taasisi mbali mbali za Serikali na za Kiraia mliohudhuria,Viongozi wa dini mliohudhuria,Wageni waalikwa,Mabibi na Mabwana,

Asaalam Aleykum,Awali ya yote, sina budi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupa uhai na kutuwezesha kwa pamoja kufika hapa tukiwa wenye afya njema. Kwa uwezo wake tukaweza kuitana hapa na kujumuika kwa pamoja katika kuungana na wenzetu kwa kuadhimisha siku hii.

Pili napenda kuchukua fursa hii adhimu kutoa shukrani zangu za dhati kwa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar (ZLSC) ambao ni waandaaji na wasimamizi wa maadhimisho haya kwa heshima mlionipa ya kunialika kuwa Mgeni Rasmi katika kuadhimisha siku ya adhabu ya kifo duniani.

Ndugu Mwenyekiti,Hii ni mara yangu ya kwanza kualikwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar kuwa mgeni rasmi. Kwa upande wangu najihisi nami ni mmoja wa watoa huduma za sheria kwa jamii kama kazi

Hotuba ya Mgeni Rasmi, Mhe Rabia Hussein Katika Kuadhimisha Siku ya Adhabu ya Kifo Duniani Iliyotolewa

Tarehe 10 Oktoba, 2013 Katika Ukumbi wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar

zenu za kila siku zinavyowataka. Sina maneno makubwa zaidi ya kusema kuwa nathamini sana heshima hii mliyonipa na kuahidi kuitunza.

Ndugu Mwenyekiti,Inafahamika kuwa ifikapo tarehe hii ya leo, tarehe 10 Mwezi wa Oktoba, nchi zilizo wanachama wa umoja wa mataifa zinaadhimisha siku ya adhabu ya kifo duniani. Umoja wa Mataifa umeteua siku hii kila mwaka kupinga adhabu ya Kifo duniani kote.

Nchi nyingi zilizo ridhia mkataba wa Umoja wa Mataifa zinafanya juhudi za makusudi za kupinga adhabu ya kifo kwa watuhumiwa wa makosa mbalimbali. Kwa takwimu za hivi karibuni, hadi kufikia mwaka huu nchi 58 tu ndizo zilizofuta adhabu hiyo ya kifo ambapo kwa Afrika ni nchi chache sana kati ya hizo.

Uadhimishaji huu hufanyika kwa shughuli mbalimbali zikiwemo kuandaa semina, warsha au makongamano kwa madhumuni ya kutoa ujumbe wa kupinga adhabu ya kifo. Nimefarijika sana kuona Kituo kimelazimika kuadhimisha siku hii ya adhabu ya kifo duniani.

Ndugu mwenyekiti,Kwa miaka mingi sasa adhabu ya kifo katika nchi yetu na duniani, inachukuliwa kama ni moja ya adhabu halali kama zilivyo adhabu nyengine zinazopaswa kutolewa kwa yeyote aliepatikana na hatia ya kufanya kosa la jinai. Kwa mujibu wa Sheria ya Makosa ya Jinai Namba 6 ya mwaka 2004 Sheria za Zanzibar na hata kwa Sheria ya Makosa ya Jinai ya Tanzania Bara kosa la kuua kwa kukusudia na uhaini ni makosa ambayo kwa atakaepatikana na hatia basi adhabu yake ni kifo.

Kasi ya kuondoa kabisa adhabu ya kifo sio kubwa sana na mjadala wake umegawika katika makundi mawili. Kuna wale wanaounga mkono adhabu hii iendelee na kuna wale wanaotaka adhabu hii isiendelee. Wale wanaotaka adhabu ya kifo iendelee wanaamini kwamba kutekelezwa kwake ni muhimu kwa vile inahakikisha kutendeka haki kwa yule

aliyeondolewa uhai wake kwa nia ovu na makusudi na pia kwa familia yake. Pia kundi hili linaona kuwa adhabu ya kifo ni adhabu sahihi kwa vile kuua kwa makusudi ni kosa kubwa sana ambapo kama adhabu kali itatolewa itapelekea watu wengine watakaoona au kusikia utekelezaji wa adhabu hii kuogopa na kutofanya kosa la aina hiyo.

Kundi la pili ni lile linaloona adhabu hii ya kifo ni adhabu katili sana, si ya kibinaadamu, inadhalilisha na haifai kukubalika kama adhabu. Kundi hili linaona kuwa adhabu ya kifo inakwenda kinyume na haki za kibinaadam na ikishatekelezwa basi haiwezi kutenguliwa.

Ndugu Mwenyekiti Kwa Tanzania utaratibu huu wa kutekeleza adhabu ya kifo bado upo kwenye mjadala na jamii pamoja na Taasisi mbalimbali ambazo zinajaribu kutoa maoni yao na kupendekeza kuondolewa kwa aina hii ya adhabu. Wanaharakati wamekua katika mstari wa mblele kushajihisha, kuhamasisha umma pamoja na serikali kufikiria kuondoa adhabu ya kifo.

Ukweli ni kwamba adhabu ya kifo ni adhabu inayochukua uhai wa binaadamu hata kama imetolewa na Sheria. Pia mtendaji wa kosa la kuua kwa makusudi na hata uhaini mara nyengine huwa anachukuwa uhai wa binadamu mwengine, uhai ambao hakupaswa kuuchukuwa na uhai ambao unalindwa na Katiba zetu pamoja na dini zetu.

Kuthaminiwa kwa uhai wa mtu ndio sababu kuu iliyopelekea kuwepo kwa wazo la kuiondoa adhabu hii katika orodha za adhabu za makosa. Lengo likiwa ni kujaribu kutoa heshima ya uhai kwa kila mwanaadamu huku dhana ya adhabu ikiwa inabaki palepale katika lengo la kuzuia makosa yasitendeke zaidi. Ndio maana ujumbe wa mwaka huu wa kuadhimishi siku hii ya leo ukasema “stop the crime and not life” yaani zuia uhalifu na sio uhai.

Ndugu mwenyekiti,Kama nilivyosema awali hapa kwetu Tanzania bado tunavyo vifungu vya sheria

Mheshimiwa Rabia Hussein Jaji wa Mahakama Kuu Zanzibar akitoa hotuba katika siku ya adhabu ya kifo

Page 15: Toleo Na. 016 Jarida la kila miezi mitatu Oktoba - Disemba ... 16.pdf · Wadhamini ( ZLSC) PrOF.Chris Maina Alie shikilia kitabu ni Mwanasheria wa ZLSC Pemba Bi.Safia Saleh Sultan

15

hotuba

Oktoba - Disemba, 2013sheria na haki

Hotuba ya Mgeni Rasmi, Mhe Rabia Hussein Katika Kuadhimisha Siku ya Adhabu ya Kifo Duniani Iliyotolewa

Tarehe 10 Oktoba, 2013 Katika Ukumbi wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar

vinavyotoa adhabu ya kifo katika Sheria za uhalifu. Na kwa kufuata vifungu hivyo, Mahakama Kuu zimepewa mamlaka ya kuamuru mtu yeyote alietiwa hatiani na vifungu hivyo kuadhibiwa kifo.

Ndugu mwenyekiti, Ninafahamu kwamba katika miaka ya hivi karibuni, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tume ya kurekebisha Sheria (Law Reform Commission) ilifanya utafiti juu ya adhabu ya kifo na kutoa mapendekezo yake Serikalini. Mbali na juhudi hizi za ndani, Mkataba wa Ziada (Protocol) wa kimataifa wa mwaka1987 na mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa wa mwaka 1966 (International Covenant on Civil and Political Rights of 1966) unazitaka nchi ambazo zimeweka saini na kuuridhia, kuanzisha utaratibu wa kuindosha adhabu hii katika vitabu vyake vya sheria. Kwa bahati mbaya

Tanzania bado haijaridhia Mkataba huu wa ziada wa mwaka 1987.

Ndugu mwenyekiti,Ninafahamu pia kuna wanazuoni wanaharakati wa haki Za Binaadamu wametunga vitabu mbali mbali kuhusu Adhabu ya kifo, moja ya kitabu hicho kinaitwa Adhabu ya Kifo katika Sheria za Kiislamu, kilichotungwa na mwanazuoni maarufu hapa Zanzibar Dr. Muhyiddin Ahmad Khamis Maalim Siasa . Kitabu hichi kinaelezea nidhamu ya kifo katika uislamu ni nyenzo katika nyenzo ambazo zinategemewa katika kuhifadhi jamii kuepukana na uovu wa kupita mipaka.

Hata hivyo waumini wa dini ya Kiislamu wanahoji utaratibu unaofuatwa katika kutoa adhabu ya kifo kama unafanana na utaratibu uliolezwa katika Kitabu Kitukufu cha Quran.

Kwa upande wa dini nyengine kwa mfano dini ya Kikristo, katika Agano la Kale ipo Adhabu ya kifo. Lakini katika Agano Jipya Adhabu hio imeondolewa.

Ndugu Mwenyekiti,Nchi yetu bado haijaridhia tamko la Kimataifa kuhusu kupinga adhabu ya kifo. Kwa sasa, kwa kuwa sheria hii ya kifo bado haijafutwa ni vyema wananchi kuendelea kuijadili faida na hasara zake mpaka pale Serikali itakapopima na kuona kama ipo haja ya kuiondosha adhabu hii.

Mwisho,Waheshimiwa mliohudhuria, sasa nachukua nafasi hii kutamka kwamba mjadala huu wa adhabu ya kifo uliyoandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar umefunguliwa rasmi.

Ahsanteni sana kwa kinisikiliza.

Baadhi ya washiriki wakimsikiliza Mheshimiwa Rabia Hussein Jaji wa Mahakama Kuu Zanzibar akitoa hotuba katika siku ya adhabu ya kifo

Page 16: Toleo Na. 016 Jarida la kila miezi mitatu Oktoba - Disemba ... 16.pdf · Wadhamini ( ZLSC) PrOF.Chris Maina Alie shikilia kitabu ni Mwanasheria wa ZLSC Pemba Bi.Safia Saleh Sultan

16

hotuba

sheria na haki Oktoba - Disemba, 2013

Ndugu Makamo Mwenyekiti wa Bodi ya Wahariri wa Zanzibar Yearbook of Law, Mheshimiwa Othman Masoud na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar;

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar, Profesa Chris Maina Peter;

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar, Bi. Harusi Miraj Mpatani na Wafanyakazi wa Kituo waliohudhuria;

Viongozi wa Taasisi mbali mbali za Serikali na za Kiraia mliohudhuria;Viongozi wa Dini mliohudhuria;Wageni waalikwa;Mabibi na Mabwana;Asaalam Aleykum,

Awali ya yote, sina budi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupa uhai na kutuwezesha kwa pamoja kufika hapa tukiwa wenye afya njema. Kwa uwezo wake tukaweza kuitana hapa na kujumuika kwa pamoja katika kuungana na wenzetu kwa kusheherekea siku hii.

Pili, napenda kuchukua fursa hii adhimu kutoa shukrani zangu za dhati kwa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar (ZLSC) ambao ni waandaaji na wasimamizi wa sherehe hizi kwa heshima mlionipa ya kunialika kuwa Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa kitabu cha Zanzibar Yearbook of Law katika kusheherekea maisha ya Prof. Haroub Othman.

Aidha, napenda kuchukua fursa hii kuwahakikishia Kituo kuwa nitaendelea kuwa nao pamoja katika kufika lengo lao la “Kuifanya Haki kuwa Shauku” hapa kwetu Zanzibar linafikiwa.

Ndugu Makamo Mwenyekiti,Hii si mara yangu ya kwanza kualikwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar kuwa mgeni rasmi. Kumbukumbu zinaonyesha kuwa niliwahi kualikwa na Kituo hichi kuwa mgeni rasmi katika siku kama ya leo ya katika kuadhimisha na kusheherekea maisha ya Prof. Haroub Othman miaka mitatu iliyopita mwaka 2010, katika maadhimisho yaliyofanyika

Hotuba ya Mgeni Rasmi, Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, Makamo Wa Pili wa Rais Zanzibar Katika Uzinduzi wa Kitabu cha

Zanzibar Yearbook of Law katika Kusheherekea Maisha ya Prof. Haroub Othman

Ukumbi: Eacrotanal – Zanzibar, Tarehe: 28/12/2013katika ukumbi wa SUZA.

Kwa upande wangu, kama Kiongozi mwenye dhamana katika nchi yetu, najihisi nami ni mmoja wa watoa huduma za sheria kwa jamii kama kazi zenu za kila siku zinavyowataka. Sina maneno makubwa zaidi ya kusema kuwa nathamini sana heshima hii mliyonipa na kuahidi kuitunza.

Ndugu Makamo Mwenyekiti,Nimeambiwa leo tunasheherekea maisha ya Prof. Haroub Othman, mwanzilishi wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar na ni msomi mahiri aliyebobea katika masuala ya sheria, Haki za Binadamu, na Katiba hapa nchini kwetu na nchi za nje. Angekuwepo leo Prof. Haroub Othman, uzinduzi huu wa Kitabu cha Zanzibar Yearbook of Law ungeweza kufanywa ndani ya mikono yake.

Ndugu Makamo Mwenyekiti,Aidha nimeambiwa kuwa Kituo cha Huduma za Sheria ni moja kati ya urithi na mchango mkubwa ulioachwa na marehemu Prof. Haroub Othman kwa jamii ya Zanzibar, Tanzania na kimataifa. Kwa kutumia ujuzi na uzoefu wake wa kitaalamu wa zaidi ya miaka 30 katika taaluma ya Sheria na Sayansi ya Siasa.

Uwepo wa Prof. Haroub Othman hapa Zanzibar uliweza kuwasaidia wananchi wengi wenye matatizo ya kisheria kupata msaada wa mambo ya kisheria na utaalamu wa Haki za Binadamu na Sheria kwa ujumla. Kwa sasa kazi hii inaendelea kufanywa na Kituo na kuenzi na kuendeleza azma ile ile ya kuwasaidia wanyonge wa Zanzibar katika kupata haki zao na hasa Wanawake, Watoto, Watu Wenye Ulemavu na Wazee. Inafaa tukumbeke kwamba kazi hii inayofanywa na Kituo ilikuwa ni moja ya azma ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964 ambayo tarehe 12 Januari 2014 yanatimiza umri wa miaka 50 ambalo ni jambo la kujivunia kwa Wazanzibari wote.

Ndugu Makamo Mwenyekiti,Usomi wa Prof. Haroub Othman ulisaidia kutoa na kuzalisha wataalamu mbali mbali katika taaluma ya sheria, sayansi ya jamii na hata masuala ya Haki za Binadamu

ambao kwa sasa wamekuwa walimu wa Taifa letu au kwa kauli nyengine tunaweza kusema Prof. Haroub alikuwa mwalimu wa walimu wa sasa katika masuala ya sheria na haki.

Ndugu Makamo Mwenyekiti,Uzinduzi wa leo wa kitabu cha Zanzibar Yearbook of Law, ni hatua kubwa katika kazi za Kituo ni kitu cha Kujivunia hapa nchini kwetu Zanzibar. Hii ni kwa sababu Zanzibar inakuwa nchi ya kwanza katika Afrika Mashariki kuwa na Kitabu cha aina hii. Pia ni nchi ya pili katika Bara la Afrika kuwa na Kitabu cha Mwaka cha Sheria baada ya Afrika ya Kusini. Kuanzishwa kwa Kitabu hiki kunaifanya Zanzibar iende kifua mbele kwa majivuno kwa sababu inakuwa mfano wa kuigwa siyo tu katika kanda hii ya Afrika lakini kwa Afrika nzima pia.

Ndugu Makamo Mwenyekiti,Kama nilivyosema hapo awali, Kitabu hichi kimekuja wakati muafaka. Hii ni kwa sababu kinakwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, ni jambo la kujivunia kwa Kituo cha Huduma za Sheria kuanzisha kitabu hiki ambacho kitakuwa ni kumbukumbu ya kisomi (reference) nzuri kwa wasomi wa Zanzibar na hata walio nje ya Zanzibar.

Ndugu Makamo Mwenyekiti,Nimeelezwa kwamba kwa sababu kitabu hiki ni cha mwaka – yaani Yearbook, kitakuwa kinatoka kila mwaka. Nimenong’onezwa pia kwamba baada ya kuona orodha na mada za waliochangia katika hii Juzuu ya Kwanza, Mhe. Dr.

Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi, Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Page 17: Toleo Na. 016 Jarida la kila miezi mitatu Oktoba - Disemba ... 16.pdf · Wadhamini ( ZLSC) PrOF.Chris Maina Alie shikilia kitabu ni Mwanasheria wa ZLSC Pemba Bi.Safia Saleh Sultan

17

hotuba

Oktoba - Disemba, 2013sheria na haki

Hotuba ya Mgeni Rasmi, Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, Makamo Wa Pili wa Rais Zanzibar Katika Uzinduzi wa Kitabu cha

Zanzibar Yearbook of Law katika Kusheherekea Maisha ya Prof. Haroub Othman

Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, hakusita kuandika Utangulizi (Foreword) katika Kitabu hiki. Waliochangia ni pamoja na Jaji Mkuu wa Tanzania; Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Waziri wetu wa Sheria na Katiba; Mkurugenzi wetu wa Mashtaka; Mkurugenzi wa Mashtaka wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; majaji na wasomi wengine kutoka sehemu mbali mbali za dunia.

Ndugu Makamo Mwenyekiti,Nafarijika kusikia kwamba, pamoja na kuratibiwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar, shughuli yote ya uhariri wa Kitabu hichi ipo mikononi mwa Wazanzibari wenye ujuzi mkubwa wa sheria na wenye dhamana katika nchi yetu. Hii ni kwa kuwa Bodi ya Ushauri ya Uhariri ipo chini Mhe. Omar Othman Makungu, Jaji Mkuu wa Zanzibar na wewe Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar kama Makamo wake. Wengine ni pamoja Rais wa Chama cha Mawakili cha Zanzibar; Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake

Wanasheria Zanzibar (Zanzibar Female Lawyers Association – ZAFELA); na Mwanamke mmoja ambaye ni Wakili wa Mahakama Kuu ya Zanzibar. Ni imani yangu kuwa Kitabu hichi kikiongozwa na jopo zito kiasi hiki hakuna kinachoweza kuharibika.

Ndugu Makamo Mwenyekiti,Niwaombe Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar wasiishie hapa na waendelee na moyo huo huo kwa kumuenzi Prof. Haroub pamoja na kufikiria changamoto zinazotukabili hapa Zanzibar katika masuala ya Sheria na waweze kuandika ili kuweka kumbukumbu za sheria vizuri kwa vizazi vya sasa na vya baadae.

Ndugu Makamo Mwenyekiti,Nimeambiwa kuna familia ya Prof. Haroub ambayo ipo karibu sana na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar na kushirikiana na kufikia azma ya ndugu yetu Prof. Haroub Othman ya kufanya haki iwe shauku. Ombi langu kwao wasikiache mkono Kituo na wawe pamoja nao katika

kuhakikisha ndoto ya Profesa inafikiwa.

Ndugu Makamo Mwenyekiti,Mwisho kabisa sina budi kuwashukuru wote waliohudhuria, Mwenyekiti wa Bodi ya Wahariri ya Zanzibar Yearbook of Law; pamoja wajumbe wake; Bodi ya Wadhamini ya Kituo cha Huduma za Sheria; Mkurugenzi na watendaji wake wote wa Kituo cha Huduma za Sheria kwa kufanikisha sherehe hizi na kumuenzi mwanzilishi wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar, nasaha zangu muwe na ushirikiano na kuhakikisha kuwa mwangaza uliowekwa na Prof. Haroub hauzimiki. Mungu amlaze mahali pema. Amin.

Sasa kwa heshima na taadhima napenda kutangaza rasmi kwamba Sherehe za Uzinduzi wa Kitabu cha Zanzibar Yearbook of Law katika kusherehekea maisha ya Profesa Haroub Othman zimefunguliwa rasmi na nipo tayari kukizindua kitabu hicho.

Ahsanteni sana kwa kunisikiliza.

Baadhi ya Washiriki wakimsikiliza Mgeni rasmi Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi wakati alipokuwa akitoa hotuba katika uzinduzi wa Zanzibar Yearbook of Law Vol. 1 pamoja na kumbukizi ya Profesa Haroub Othmankatika ukumbi wa Eacrotanal, Mjini Unguja

Page 18: Toleo Na. 016 Jarida la kila miezi mitatu Oktoba - Disemba ... 16.pdf · Wadhamini ( ZLSC) PrOF.Chris Maina Alie shikilia kitabu ni Mwanasheria wa ZLSC Pemba Bi.Safia Saleh Sultan

18

1. Leo wito niutowe, Jamii iitikiye. Sauti zetu zipae, Kila mtu asikiye. Uhuru wake zitwae, Kazi tusizingiliye. Mahkama kuwa huru, Hujenga tawala bora.

2. Tutambue Mahkama, Ndio kimbilio letu. Mambo yakishatukwama, Twapeleka kesi zetu. Kuzingilia si vyema, Twavunja haki za watu. Mahkama kuwa huru, Hujenga tawala bora.

3. Kungilia Mahkama, Kwenye maamuzi yake. Jambo hili ni nakama, Huvunja haiba yake. Haki huenda mrama, Akapewa iso yake. Mahkama kuwa huru, Hujenga tawala bora.

4. Kuivunjia muruwa, Mahkama siyo haki. Kuutumia Uluwa, Tukaipindisha haki. Na vishawishi kutoa, Haya hayastahiki. Mahkama kuwa huru, Hujenga tawala bora.

5. Rushwa kuitanguliza, Kushawishi Mahkama. Wenye vyeo kuagiza, Kesi zifutwe mapema. Mahkama kuibeza, Twaivunjia heshima. Mahkama kuwa huru, Hujenga tawala bora.

6. Majaji na Mahakimu, Waachiwe wasitishwe. Kesi wakizihukumu, Vidole wasioneshwe. Tuwache kuwalaumu, Wala wasiamrishwe. Mahkama kuwa huru, Hujenga tawala bora.

7. Kuwapa vikaratasi, Waamuwe tutakavyo. Kwa simu kuwadadisi, Kesi zende tupendavyo. Mahkama twazighasi, Tutambuwe hivyo sivyo. Mahkama kuwa huru, Hujenga tawala bora.

8. Iachiwe mkondowe, Sheria itende haki. Mahkama ziamuwe, Ambavyo yastahiki. Wanyonge wasionewe, Kunyang’anywa zao haki. Mahkama kuwa huru, Hujenga tawala bora.

9. Raia tuwe jadidi, Kusapoti Mahkama. Tusifiche ushahidi, Ikawa kesi kukwama. Tuchukuweni juhudi, Iwe huru Mahkama. Mahkama kuwa huru, Hujenga tawala bora.

10. Majaji na Mawakili, Mahakimu na polisi. Wakubwa wa Serikali, Wakuu wa taasisi. Tulindeni Maadili, Kesi zende kwa wepesi. Mahkama kuwa huru, Hujenga tawala bora.

11. Wadau tuwe pamoja, Kila mtu nafasiye. Asitokee mmoja, Mahkama achezeye. Iwe pahala faraja, Sote tupakimbiliye. Mahkama kuwa huru, Hujenga tawala bora.

SAID R. HASSAN – ZLSC – PEMBA.

Mahkama Kuwa Huru, Hujenga Tawala Bora

Akifungua semina ya siku moja katika ukumbi wa Kituo cha Huduma za sheria( ZLSC) migombani, Mkurugenzi Mtendaji

wa Kituo hicho Bi Harusi Miraji Mpatani aliwashukuru watendaji wote kwa kuweza kukutana pamoja kwa lengo la kuwawezesha polisi na masheha kufahamu utekelezaji wa amri za Mahakama za Ardhi.

Jumla ya mada nne ziliwasilishwa kwa upande wa Unguja na Pemba ikiwa ni pamoja na Sheria ya Matumizi ya Ardhi Namba 12/ 1992 mada ya pili ilihusu nafasi za masheha na polisi katika kutekeleza amri za mahakama, mada ya tatu ilikuwa ni ufafanuzi wa Sheria Namba 7 /1994 ya Mahakama ya Ardhi kama ilivyorekebishwa na sheria namba 7 / 2008 na mada ya nne ilikuwa ni kutoa ufafanuzi juu ya kuanzishwa kwa Mahakama ya Ardhi, aina ya kesi zinazostahiki kupelekwa katika mahakama ya ardhi pamoja na kazi za mahakama, amri za mahakama, vipi masheha wanaweza kusaidia kuitekeleza amri ya mahakama kwa mujibu wa Sheria Namba 1 /1998 kifungu namba (17), na nafasi ya madalali katika uuzwaji au ukodishwaji wa ardhi.

Akizungumzia mafanikio yatakayo patikana baada ya mafunzo hayo, Mgeni Rasmi Mwenyekiti wa

ZLSC Yawakutanisha Masheha, Polisi na Mahakama

Mahakama ya Ardhi Ndugu Faraji Omar Juma alisema “Mafunzo hayo yatasaidia washiriki kuifahamu sheria ya mahakama ya ardhi namba 7 / 1994, kuwawezesha washiriki kuweza kufahamu sheria ya matumizi ya ardhi namba 12 / 1992, yatasaidia utekelezaji wa amri ya Mahakama ya Ardhi kwa jeshi la polisi na masheha. Semina hiyo iliweza kupelekea mafanikio makubwa kwa washiriki wa Mafunzo hayo kwa upande wa Unguja na Pemba ambapo yaliwasaidia kuwaunganisha pamoja Polisi, Wanasheria kutoka Mahakama ya Ardhi pamoja na Masheha na kuweza kujua kila mmoja wao ananafasi gani katika kufanikisha kesi zinazohusu masuala ya Ardhi.

Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ni asasi isiyo ya kiserikali iliyosajiliwa Zanzibar mwaka 1992.Moja kati ya kazi za Kituo ni kutoa msaada bure wa kisheria, kazi hii ilianza kutekelezwa mara tu baada ya kuanzishwa kwa Kituo.Aidha kituo kinajishughulisha na mambo mbali mbali ya utoaji wa Elimu ya Sheria kwa wananchi wa Zanzibar kupitia vipindi mbali mbali vya Televisheni na Redio, kufanya tafiti mbali mbali zinazohusiana na sheria pia kutoa machapisho kadhaa ya kisheria.

Baadhi ya Masheha, Polisi na Watendaji wa Mahakama wakifuatilia kwa umakini mafunzo yaliyotolewa na ZLSC

sheria na haki Oktoba - Disemba, 2013

Mwenyekiti wa Mahkama ya Ardhi Ndugu Faraji Omar Juma akitoa nasaha zake kwa washiriki katika ufunguzi wa mafunzo ya Masheha, Polisi na Watendaji wa Mahakama katika ukumbi wa ZLSC Unguja

Page 19: Toleo Na. 016 Jarida la kila miezi mitatu Oktoba - Disemba ... 16.pdf · Wadhamini ( ZLSC) PrOF.Chris Maina Alie shikilia kitabu ni Mwanasheria wa ZLSC Pemba Bi.Safia Saleh Sultan

19

Mnamo tarehe 6 na 7 mwezi wa Novemba 2013 Kituo cha huduma za Sheria Zanzibar (ZLSC) kupitia

mradi wa wasaidizi wa sheria unaodhaminiwa na Legal Services Facility (LSF) kiliwakutanisha Masheha kutoka Wilaya ya Mjini na Chake Chake kwa Upande wa Pemba.

Lengo kuu la kukutanishwa watendaji hawa ilikua ni pamoja na kuwaelimisha Masheha juu ya kazi zitakazofanywa na wasaidizi wa sheria katika shehia husika, kuwatambulisha kwao ili waweze kufahamiana,kufaham Haki za Binadamu na Utawala Bora na kufahamu Sheria ya Tawala za Mikoa Zanzibar Sheria namba moja (1) ya mwaka 1998 ambayo ndio inayoelezea majukumu ya Sheha.

Masheha Wapatiwa Dozi

Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Bi. Mwanajuma Majid Abdalla akiwa katika picha ya pamoja na Masheha na Watendaji wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar katika wa ZLSC Miembeni, Chake chake Pemba .

Akiwakaribisha Rasmi washiriki wa Mafunzo hayo Mratibu wa Kituo Bi. Fatma Khamis Hemed alisema dhana ya usaidizi wa sheria kila nchi inauelewa wake lakini katika tafsiri nyepesi tunaweza kumtafsiri msaidizi wa sheria ni mtu ambae ana elimu ya sekondari ya kawaida na aliepata mafunzo ya kawaida ya sheria.Ambapo waajiri wao wanaweza kua Asasi isiyo ya Serikali yaani (NGO), Taasisi Binafsi, Ofisi za Mawakili au hata Serikali. Kwa Upande wake Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Bi.Mwanajuma Majid Abdalla alikishukuru kituo kwa kumchagua yeye binafsi kua Mgeni Rasmi na pia kuona umuhimu wa kuisaidia Serikali katika kuongeza taaluma ya kisheria kwa wananchi wake.

Oktoba - Disemba, 2013sheria na haki

Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Bi.Mwanajuma Majid Abdalla akisoma Hotuba yake wakati wa Mafunzo kwa Masheha katika utambulisho wa Wasaidizi wa Sheria. Kushoto ni Mratibu wa ZLSC Pemba Bi. Fatma Khamis Hemed na kulia ni Bi.Safia Saleh Sultan na Khalfan Amour Masoud

wanasheria wa ZLSC

Katika hotuba yake kwa Masheha Bi. Mwanajuma alisisitiza suala la kufanya kazi kwa pamoja baina ya Masheha na Wasaidizi hao wa Sheria kwa lengo la kuwahudumia wananchi waweze kuishi kwa kufuata Sheria zilizopo.

Ni mwaka 2007 kituo kwa mara ya kwanza kilianza kutoa huduma hii ya kuwapata wasaidizi wa Sheria (Paralegals) .Mpango huu umekua na mafanikio makubwa kwa Kituo kwani hadi sasa tunao wasaidizi wa Sheria wapatao (135), wanaoendelea na Mafunzo ni (64) hivyo kufanya wasaidizi wa sheria waliopita na waliopo kituoni kufikia (199).

Wasaidizi wa sheria wote hao wanatoka katika majimbo yote 50 ya uchaguzi ya Zanzibar.Pia kituo kina wasaidizi wa sheria kutoka Idara Maalum za SMZ kama vile Chuo cha Mafunzo, Jeshi la kujenga Uchumi Zanzibar ( JKU), Kikosi cha zimamoto na uokozi Zanzibar (KZU)na Kikosi cha Valantia (KVZ) Wote hao wapo katika uangalizi wa Kituo.

Katika Mafunzo haya ya siku mbili kwa Masheha jumla ya mada nne (4) kwa upande wa Unguja na Pemba ziliwasilishwa ikiwa ni pamoja na Haki za Binadamu na Utawala Bora, Ufafanuzi wa sheria ya Tawala za Mikoa, Ufafanuzi wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 na ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 pamoja na mada iliyohusu Kituo cha Huduma za Sheria na dhana ya Wasaidizi wa Sheria.

Jumla ya Masheha 30 walihudhuria katika Mafunzo hayo ambapo kati yao Wanawake walikua (2), Wanaume (28) Ambapo idadi hiyo hiyo ilijitokeza kwa upande wa Kituo cha Pemba.

Page 20: Toleo Na. 016 Jarida la kila miezi mitatu Oktoba - Disemba ... 16.pdf · Wadhamini ( ZLSC) PrOF.Chris Maina Alie shikilia kitabu ni Mwanasheria wa ZLSC Pemba Bi.Safia Saleh Sultan

Toleo Na. 016 Jarida la kila miezi mitatu Oktoba - Disemba, 2013

Jarida la Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Ifanye haki

Iwe shauku

Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar (ZLSC) Kikiwa mdau muhimu wa utetezi na ushawishi juu ya usimamizi

wa Haki za Binadamu hapa Zanzibar kila ifikapo tarehe 10 Oktoba ya kila mwaka kimejiwekea utaratibu wa kuiadhimisha siku hii kua ni siku ya Kupinga adhabu ya kifo.

Maadhimisho haya hufanyika kwa namna mbali mbali ikiwa ni pamoja na kufanya makongamano ya wazi na warsha.

Wakati Kituo kikiendelea kuadhimisha siku hii Tanzania inaelezwa kuwa bado ni miongoni mwa nchi zisizozidi (63) ambazo bado hazijafuta adhabu ya kifo wakati zaidi ya nchi (137) ikiwa ni takriban asilimia (69%) ya nchi zote Duniani zilizokwisha kufuta adhabu hii ya kifo. Akiwakaribisha washirki katika kongamano la kupinga Adhabu ya Kifo Mratibu wa Kituo Bi.Fatma Khamis Hemed aliwataka washiriki kuwa watulivu na kutumia busara zao zote katika kuzijadili mada mbali mbali zitakazo wasilishwa katika kongamano hilo ili kukiwezesha kituo, Serikali na watunga sera waweze kuichukua na kuifanyia kazi michango ya washiriki hao.

Akitoa mada juu ya nafasi ya dini ya Kiislam juu ya dhana ya adhabu ya kifo kwa mujibu wa Mtazamo wa kiislam Mwalim Ali M.Shehe kutoka Umoja wa Maendeleo ya Elim ya Kiislam UKUEM alisema Uislam haukuruhusu moja kwa moja hukmu ya kifo ila kwa mwenye kubainika ameuwa kwa makusudi.

Mjadala Kuhusu Kupinga Adhabu ya Kifo Bado Kitendawili

Kwa upande wake Mchungaji kutoka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri KKT Mchungaji Benjamin Kisanga alisema Mungu hakuruhusu kuua LUKA SURA YA 8:53-57, Kitabu cha Marko sura 12:31 Mpende jirani yako Kama Unavyoipenda nafsi yako, na Akahitimisha kwa kusema hata Yesu kumfufua binti Yairo ilithibitisha kwamba kifo kinakataliwa.

Nae Mwanasheria kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Pemba ndugu Ali Bilali Hassan alihitimisha mjadala huo kwa kusoma mikataba ya kimataifa inayozungumzia kifo na Haki za Binadam, Makosa yanayotolewa adhabu ya kifo, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya

1977 na ile ya Zanzibar ya mwaka 1984. Mifano ya Kesi mashuhuri zilizotolewa Adhabu ya kifo na kuhitimisha mada yake kwa SWALI HILI. Kwanini Tusiondoe adhabu ya kifo na tukabakiwa na Adhabu ya kifungo cha maisha? Swhali lilichukua mjadala mkubwa miongoni mwa washiriki wa kongamano hilo.

Lengo kuu la maadhimisho ya siku ya kupinga adhabu ya kifo na lengo kuu la Kituo ni kupata nafasi ya kuielimisha jamii juu ya mambo yanayohusu adhabu ya kifo, ikiwa ni pamoja na historia, athari zake na jinsi gani ambapo jamii inaweza kupaza sauti zao aidha kuipinga au kuikubali iendelee kutekelezwa ndani ya nchi.

Katika maadhimisho ya mwaka huu jumla ya mada tatu (3) ziliwasilishwa kwa Upande wa Unguja na Pemba ambapo ni Pamoja na Katiba ya Zanzibar nay a Jamhuri ya Muungano na vifungu vya Sheria vinavyoruhusu Adhabu ya Kifo, Nafasi ya Dini ya Kiislamu na Kikristo katika Kupinga Adhabu ya Kifo.

Kauli mbiu ya Mwaka 2013 ya kuadhimisha siku ya kupinga adhabu ya kifo ilikua ni “ACHA UHALIFU SIO MAISHA, KOMESHA ADHABU YA KIFO SASA”.

Washiriki wakijadili hoja mbali mbali zilizowasilishwa na watoa mada katika kupinga Adhabu katika ukumbi wa ZLSC Miembeni, Chake chake Pemba

Washiriki wakijadili hoja mbali mbali zilizowasilishwa na watoa mada katika kupinga Adhabu ya kifo katika ukumbi wa ZLSC Migombani Unguja