ufahamu wa sera ya taifa ya huduma ndogo za fedha ya … · karadha (mikopo ya vitu na vifaa...

12
Wizara ya Fedha na Mipango UFAHAMU WA SERA YA TAIFA YA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA YA 2017 NA SHERIA YA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA YA 2018 #ElimikaUhudumiwe

Upload: others

Post on 16-Apr-2020

7 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: UFAHAMU WA SERA YA TAIFA YA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA YA … · karadha (mikopo ya vitu na vifaa mbalimbali), mikopo ya nyumba, huduma ya akiba, elimu ya fedha na ujasiriamali, huduma

Wizara ya Fedha na Mipango

UFAHAMU WA SERA YA TAIFA YA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA YA 2017NA SHERIA YA HUDUMA NDOGO ZA

FEDHA YA 2018

#ElimikaUhudumiwe

Page 2: UFAHAMU WA SERA YA TAIFA YA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA YA … · karadha (mikopo ya vitu na vifaa mbalimbali), mikopo ya nyumba, huduma ya akiba, elimu ya fedha na ujasiriamali, huduma
Page 3: UFAHAMU WA SERA YA TAIFA YA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA YA … · karadha (mikopo ya vitu na vifaa mbalimbali), mikopo ya nyumba, huduma ya akiba, elimu ya fedha na ujasiriamali, huduma

SERA NA SHERIA YA

HUDUMA NDOGO ZA

FEDHA1. UTANGULIZISerikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango iliandaa Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2017.

Lengo kuu la Sera ya Huduma Ndogo za Fedha ni kuimarisha utoaji huduma za fedha kwa wananchi wenye kipato cha chini. Sera hiyo pamoja na mambo mengine ilielekeza kutungwa kwa sheria ya huduma ndogo za fedha ili kulinda watumiaji wa huduma hizo na kuondoa changamoto zilizopo. Hivyo bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilitunga Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya Mwaka 2018.

1.1 Huduma ndogo za fedha ni nini?

Ni huduma za fedha zitolewazo kwa wananchi wa kipato cha chini (mtu binafsi, kaya au kikundi cha ujasiriamali) zikiwemo huduma ndogo za mikopo ya fedha, mikopo ya karadha (mikopo ya vitu na vifaa mbalimbali), mikopo ya nyumba, huduma ya akiba, elimu ya fedha na ujasiriamali, huduma za bima (bima ya afya, bima za mali).

1.2 Watoa huduma ndogo za fedha ni nani?

Ni benki, taasisi za huduma ndogo za fedha, wakopeshaji binafsi, watoa huduma ndogo za fedha kwa njia za kidigitali, vyama vya ushirika wa akiba na mikopo (SACCOS) na vikundi vya kijamii vya huduma ndogo za fedha (mfano VSLA, SILC, VICOBA, Upatu n.k).

1.3 Umuhimu wa huduma ndogo za fedha.

Huduma ndogo za fedha zinawawezesha wananchi kujiwekea akiba na kupata mikopo nafuu kwa ajili ya kuendesha shughuli mbalimbali za kiuchumi ili kujiongezea

kipato na kujikwamua na umaskini. Pia zinawezesha wananchi kukidhi mahitaji muhimu kama vile chakula, elimu, matibabu, dharura, ajira n.k.

1.4 Umuhimu wa Sera na Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha.

Sera na Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ni muhimu kwa kuwa zinaweka miongozo ya usimamizi na utaratibu wa kumlinda mtumiaji wa huduma ndogo za fedha.

Page 4: UFAHAMU WA SERA YA TAIFA YA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA YA … · karadha (mikopo ya vitu na vifaa mbalimbali), mikopo ya nyumba, huduma ya akiba, elimu ya fedha na ujasiriamali, huduma
Page 5: UFAHAMU WA SERA YA TAIFA YA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA YA … · karadha (mikopo ya vitu na vifaa mbalimbali), mikopo ya nyumba, huduma ya akiba, elimu ya fedha na ujasiriamali, huduma

2. SERA YA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA 20172.1 Sera ya Huduma Ndogo za Fedha ni nini

Sera ya Huduma Ndogo za Fedha ni mwongozo ambao unaweka mazingira wezeshi ya kuchochea maendeleo ya huduma ndogo za fedha ili kukidhi mahitaji halisi ya wananchi wa kipato cha chini.

2.2 Masuala ya Msingi na Matamko ya Sera.

Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo za Fedha ya Mwaka 2017 imezingatia masuala mbalimbali ili kutatua changamoto zinazoikabili sekta ndogo ya fedha kwa kuweka miongozo ambayo Serikali na wadau wengine watapaswa kuyatekeleza.

Masuala na miongozo hiyo ni pamoja na:

• Kuongeza upatikanaji wa Huduma za Fedha

• Kuhakikisha uendelevu wa Watoa Huduma Ndogo za Fedha

• Kuimarisha Usimamizi wa Utoaji wa Huduma Ndogo za Fedha

• Kuhamasisha shughuli za Utafiti, Ubunifu na Uendelezaji wa Huduma Ndogo za Fedha

• Kuimarisha Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa

• Kuimarisha Utawala Bora katika Sekta Ndogo ya Fedha

• Kuweka mazingira wezeshi kwa Makundi yenye Mahitaji Maalum, Jinsia na Vijana

Page 6: UFAHAMU WA SERA YA TAIFA YA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA YA … · karadha (mikopo ya vitu na vifaa mbalimbali), mikopo ya nyumba, huduma ya akiba, elimu ya fedha na ujasiriamali, huduma

3.0 SHERIA YA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA YA MWAKA 2018 NA KANUNI ZAKE.3.1 Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018 ni nini?

Ni Sheria iliyotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa lengo la kuboresha usimamizi wa sekta ya huduma ndogo za fedha.

Sheria imeweka masharti ya usimamizi wa huduma ndogo za fedha ikiwemo taratibu za usajili, utoaji leseni taratibu za uendeshaji na usimamizi wa taasisi za huduma ndogo za fedha nchini.

Sheria inatambua watoa huduma ndogo za fedha katika madaraja manne (4) kama ifuatavyo:

i. Taasisi za Huduma Ndogo za Fedha zinazopokea amana ambazo zinasimamiwa na Sheria ya Benki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006;

ii. Taasisi za Huduma Ndogo za Fedha zisipokea amana na Wakopeshaji Binafsi;

iii. Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS); na

iv. Vikundi vya kijamii vya huduma ndogo za fedha.

3.2 Kanuni za Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018 ni zipi?

Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018 inatekelezwa kupitia Kanuni ambazo zimegawanyika katika makundi mawili (2) ambayo ni: -

• Kanuni za Jumla zinazohusu Majukumu ya Waziri za mwaka 2019. Kanuni hizi zimetungwa na Waziri mwenye dhamana ya fedha na zimeainisha majukumu ya Waziri mhusika, kuweka masharti ya uhamasishaji, uratibu na uendelezaji wa sekta ya huduma ndogo za fedha; na

• Kanuni Mahsusi zinazohusu usimamizi wa shughuli za watoa huduma ndogo za fedha za mwaka 2019. Kanuni hizi zimetungwa na Benki Kuu kwa lengo la kuweka masharti na taratibu za usimamizi wa huduma ndogo za fedha kwa madaraja husika.

Page 7: UFAHAMU WA SERA YA TAIFA YA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA YA … · karadha (mikopo ya vitu na vifaa mbalimbali), mikopo ya nyumba, huduma ya akiba, elimu ya fedha na ujasiriamali, huduma

3.3 Masuala ya Msingi na Maudhui ya sheria na kanuni za huduma ndogo za fedha ni yapi?

Masuala ya msingi yawekwe kwa ufupi kwenye jedwali kulingana na madaraja.

Masuala ya msingi na maudhui yaliyomo katika Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018 pamoja na Kanuni zake ni kama ifuatavyo:

i. Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha na Kanuni zake zitatumika Tanzania Bara;

ii. Madaraja ya watoa huduma ndogo za fedha ambayo; - Daraja la Kwanza linalojumuisha benki na taasisi zinazopokea amana,

- Daraja la Pili linalojumuisha wakopeshaji binafsi na taasisi/kampuni za ukopeshaji

- Daraja la tatu linalojumuisha Vyama vya Ushirika vya Akiba na Mikopo (SACCOS) na

- Daraja la Nne linalojumuisha Vikundi vya Kifedha vya Kijamii (mfano VICOBA, VSLA, SILC nk)

iii. Mamlaka na majukumu ya Benki kuu ikiwa ni pamoja na kutoa leseni, kukagua, kutoa miongozo na kusimamia biashara ya huduma ndogo za fedha, na mamlaka ya kukasimisha majukumu yake kwa:--

a. Tume ya Maendeleo ya Ushirika kusimamia Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo-SACCOS; na

b. Mamlaka za Serikali za Mitaa kusimamia vikundi vya kijamii vya huduma ndogo za fedha

iv. Mamlaka na majukumu ya Waziri mwenye dhamana ya fedha ikiwa ni pamoja na kuweka mazingira wezeshi ya kisera na kuhamasisha maendeleo ya sekta ndogo ya fedha;

v. Masharti ya mpito ya muda wa miezi 12 baada ya kuanza kutumika kwa sheria ambapo watoa huduma ndogo za fedha waliokuwa wanafanya biashara hiyo kabla ya kutungwa kwa Sheria watapaswa kuomba leseni au usajili kwa mujibu wa sheria;

vi. Masharti ya uendeshaji wa shughuli za huduma ndogo za fedha kama yalivyoainishwa katika majedwali hapa chini.

Page 8: UFAHAMU WA SERA YA TAIFA YA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA YA … · karadha (mikopo ya vitu na vifaa mbalimbali), mikopo ya nyumba, huduma ya akiba, elimu ya fedha na ujasiriamali, huduma

1. Kiwango cha chini cha mtaji

Daraja la pili Daraja la tatu Daraja la nne

i. Wakopeshaji binafsi ni shilingi Milioni 20

ii. Taasisi au kampuni ni shilingi milioni 20

i. SACCOS zenye leseni daraja A ni shilingi Milioni 10

ii. SACCOS zenye Leseni ya daraja B ni shilingi Milioni 200

Vikundi vya kijamii vya huduma ndogo za fedha havina sharti la kiwango cha mtaji wa kuanzia.

2. Utaratibu wa kuomba leseni ya biashara au kusajiliwa

i. Kusajiliwa na mamlaka husika (mfano BRELA, nk)

ii. Kuomba leseni Benki Kuu ya Tanzania

i. Kusajiliwa na Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC)

ii. Kuomba leseni Benki kuu ya Tanzania au Tume ya Maendeleo ya Ushirika

i. Kusajiliwa na Mamlaka za Serikali za Mitaa na masharti ya kusajiliwa ikiwemo;

- Fomu ya maombi ya usajili

- Idadi ya wanachama 10 hadi 50

- Katiba iliyosainiwa na wanachama wote

- Muhtasari wa mkutano wa uazishwaji na

- Barua ya utambulisho ya kata/kijiji/Mtaa

3. Masharti ya uendeshaji wa biashara ya huduma ndogo za fedha

i. Kuwa na eneo maalumu la biashara

ii. Kuandaa vitabu vya hesabu kwa viwango vinavyokubalika nchini

iii. Kukaguliwa angalau mara moja kwa mwaka na Mkaguzi wa nje

iv. Sharti la kuzingatia sheria zingine za nchi ikiwemo Sheria ya Udhibiti wa Fedha Haramu

v. Ubadilishanaji wa taarifa za wakopaji kupitia mfumo wa taarifa za wakopaji (Credit Reference System)

vi. Misingi ya kumlinda mtumiaji wa huduma ndogo za fedha ikiwa ni pamoja na uwazi katika utoaji wa taarifa zote za bidhaa na huduma zinazo-tolewa ikiwemo viwango vya riba za mikopo na gharama nyingine

i. Kuwa na eneo maalumu la biashara

ii. Kuandaa vitabu vya hesabu kwa viwango vinavyokubalika nchini

iii. Kukaguliwa angalau mara moja kwa mwaka na Mkaguzi wa nje

iv. Sharti la kuzingatia sheria zingine za nchi ikiwemo Sheria ya Udhibiti wa Fedha Haramu

v. Ubadilishanaji wa taarifa za wakopaji kupitia mfumo wa taarifa za wakopaji (Credit Reference System

vi. Misingi ya kumlinda mtumiaji wa huduma ndogo za fedha ikiwa ni pamoja na uwazi katika utoaji wa taarifa zote za bidhaa na huduma zinazo-tolewa ikiwemo viwango vya riba za mikopo na gharama nyingine

i. Kuwa na anuani au mahali pa kufanyia mikutano

ii. Kutunza kumbukumbu za masuala ya fedha

iii. Hakuna sharti la kukaguliwa na mkaguzi wa nje

iv. Sharti la kuzingatia sheria zingine za nchi ikiwemo Sheria ya Udhibiti wa Fedha Haramu

v. Ubadilishanaji wa taarifa za wakopaji kupitia mfumo wa taarifa za wakopaji (Credit Reference System

vi. Misingi ya kumlinda mtumiaji wa huduma ndogo za fedha ikiwa ni pamoja na uwazi katika utoaji wa taarifa zote za bidhaa na huduma zinazo-tolewa ikiwemo viwango vya riba za mikopo na gharama nyingine

Page 9: UFAHAMU WA SERA YA TAIFA YA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA YA … · karadha (mikopo ya vitu na vifaa mbalimbali), mikopo ya nyumba, huduma ya akiba, elimu ya fedha na ujasiriamali, huduma

4. Shughuli zinazoruhusiwa kufanywa na watoa huduma

Daraja la pili Daraja la tatu Daraja la nnei. Kutoa mikopo kwa wateja

pamoja na shughuli zingine kama zilivyoainishwa katika Kanuni

ii. Kutoa mikopo,

iii. Uwekezaji wa mitaji,

iv. Uwakala wa benki,

v. Ushauri wa kitaalamu kwa wateja, na

vi. Shughuli nyingine zitakazoidhinishwa na Benki Kuu.

i. Kupokea akiba na kutoa mikopo kwa wanachama pamoja na shughuli zingine kama zilivyoainishwa katika Kanuni

ii. Kupokea hisa za uanachama na za hiari

iii. Kupokea akiba na kutoa mikopo kwa wanachama

iv. Kufanya uwekezaji

v. Kufanya shughuli nyingine zitakazoidhinishwa na Benki Kuu au Mamlaka Kasimishwa

i. Kupokea akiba.

ii. Kutoa mikopo kwa wanachama,

iii. Kukusanya michango kwa ajili ya shughuli za kijamii na shughuli zingine kama zilivyoainishwa katika Kanuni

5. Shughuli zisizoruhusiwa kufanywa na watoa huduma

i. Kupokea amana kutoka

ii. Kwa wateja na shughuli za kibenki;

iii. Kubadilisha fedha za kigeni,

iv. Biashara ya nje,

v. Biashara ya kadi za malipo,

vi. Shughuli za udhamini, Kuhamisha fedha, na shughuli nyingine ambazo zimekatazwa na Benki Kuu.

i. Kupokea amana kutoka kwa wateja wasio wanachama; shughuli za kibenki na shughuli zingine kama zilivyokatazwa katika Kanuni;

ii. Kuendesha akaunti ya hundi kwa wanachama,

iii. Kupokea amana kwa wasio wanachama,

iv. Kufanya biashara ya kubadilisha fedha za kigeni,

v. Shughuli za biashara za nje, Shughuli za udhamini

i. Kupokea amana kutoka kwa wateja wasio wanachama;

ii. Kufungua tawi au kuwa wakala wa benki na shughuli zingine kama zilivyokatazwa katika Kanuni;

Page 10: UFAHAMU WA SERA YA TAIFA YA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA YA … · karadha (mikopo ya vitu na vifaa mbalimbali), mikopo ya nyumba, huduma ya akiba, elimu ya fedha na ujasiriamali, huduma

3.4 Masuala ya uwezeshaji na usajili wa wawezeshaji wa huduma ndogo za fedhaUwezeshaji wa watoa huduma ndogo za fedha unahusisha utoaji huduma kwa watoa huduma ndogo za fedha ikiwemo vikundi kwa lengo la kuwawezesha katika uanzishaji na uendeshaji wao. Wadau muhimu katika uwezeshaji huu ni pamoja na taasisi za uwezeshaji,wawezeshaji binafsi, walimu wa vikundi na watoaji wa Huduma ndogo za fedha.

Taratibu za usajili na usimamizi wa wawezeshaji wote wakiwemo taasisi za uwezeshaji,wawezeshaji binafsi na walimu wa vikundi ambapo:-

• wawezeshaji wote watapaswa kusajiliwa na kuwa na vibali vya Mamlaka za Serikali za Mitaa

• na wawezeshaji wote watapaswa kuwa na mikataba ya uwezeshaji na watoa huduma ndogo za fedha;

• walimu na taasisi za uwezeshaji kuwa na makubaliano yanayoonesha mahusiano yao katika kuwezesha watoa huduma ndogo za fedha; na

• watoa huduma ndogo za fedha kuwa na hiari ya kuwatumia wawezeshaji na wawezeshaji na walimu kutoruhusiwa kuhodhi watoa huduma.

Taratibu za uteuzi na majukumu ya Waratibu (Focal persons) ambapo kila Mamlaka ya Serikali za Mitaa itakuwa na Mratibu mwenye jukumu la kuratibu shughuli za huduma ndogo za fedha katika eneo lake.

Page 11: UFAHAMU WA SERA YA TAIFA YA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA YA … · karadha (mikopo ya vitu na vifaa mbalimbali), mikopo ya nyumba, huduma ya akiba, elimu ya fedha na ujasiriamali, huduma

4. UTEKELEZAJI WA SERA NA SHERIA

Utekelezaji wa Sera na Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha utahusisha Serikali na wadau mbalimbali ikiwemo watoaji na watumiaji wa huduma ndogo za fedha. Kwa kuwa masuala yote yanayohusu utekelezaji wa Sera na Sheria yataratibiwa na Waratibu katika Mamlaka ya Serikali

za Mitaa, hivyo mdau yeyote anaehitaji ufafanuzi unaohusu Sera na Sheria ya huduma ndogo za fedha au utekelezaji wake atapaswa kuwasiliana na Mratibu aliyepo katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa katika eneo husika.

Page 12: UFAHAMU WA SERA YA TAIFA YA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA YA … · karadha (mikopo ya vitu na vifaa mbalimbali), mikopo ya nyumba, huduma ya akiba, elimu ya fedha na ujasiriamali, huduma

Kwa taarifa zaidi wasiliana naWizara ya Fedha na Mipango:

Treasury Square Building18 Jakaya Kikwete Road

P.O.Box 2802, 40468 DodomaSimu: +255 26 2160000Tovuti: www.mof.go.tz

Kwa kushirikiana na

@BankofTanzaniaOfficial

@BankOfTanzania

bankoftanzaniaWizara ya Fedha na Mipango