uk. 4 uk. 22 uk. 14

28
Mchakato wa kuunda Mabaraza ya Katiba waibua malalamiko Uk. 4 Tanzania tunajifunza nini kwa Burkina Faso? Uk. 22 Toleo NO. 041 Januari - Machi 2013 Bei Shs. 500/= ISSN 0856-5937 Utafiti chanjo ya UKIMWI waleta Matumaini Uk. 14

Upload: duongdan

Post on 08-Dec-2016

619 views

Category:

Documents


15 download

TRANSCRIPT

Mchakato wa kuunda Mabaraza ya Katiba waibua malalamiko

Uk. 4Tanzania tunajifunza nini kwa Burkina Faso?

Uk. 22

Toleo NO. 041 Januari - Machi 2013 Bei Shs. 500/= ISSN 0856-5937

Utafiti chanjo ya UKIMWI waletaMatumaini

Uk. 14

b Pambazuko Na. 41 Toleo la Januari - Machi 2013

Serikali ifanye utafiti wa kutosha kabla ya kuruhusu

mazao ya GMO nchini

Wakati Tanzania inakabiliana na changamoto mbalimbali zinazotishia ustawi wa raia wake hasa kwa huduma muhimu ikiwa ni pamoja na kuwahakikishia usalama wa

chakula, ni vyema serikali itambue kwamaba Teknolojia ya Kubadilisha Vinasaba (GMO) kwa mimea haiwezi kuwa utatuzi wa matatizo yaliyopo kwenye kilimo nchini.

Kumekuwapo na mtazamo wa wanasayansi na baadhi ya wanasiasa wanaodhani kuwa GMO ndiyo inayoweza kutatua matatizo mengi yanayojitokeza kwa sasa kama vile ukame, maradhi ya mimea na kupungua kwa uzalishaji wa mazao ya kilimo na ufugaji.

Lakini, nchi ya Tanzania kama nchi zingine za kiafrika ambazo hazijaendelea katika nyanja mbalimbali ikiwemo hii ya ufanyaji tafiti na matumizi ya teknolojia, ina wajibu mkubwa wa kulinda sheria za uingizwaji mazao haya mpaka pale itakapo kuwa imefanya tafiti za kutosha na kujiridhisha kuwa teknolojia ya GMO ni salama na kama itakuwa na manufaa kwa wakulima.

Awali, Tanzania iliweza kuheshimika na kutambulika kama mahali salama kwa kuwa na ardhi na mbegu za mazao ambazo hazijachafuliwa vinasaba. Hali hiyo, ndani ya miaka michache imewawezesha wakulima wadogowadogo zaidi ya 100,000 kupata fursa ya kuuza mazao yao yanayolimwa kwa taratibu za kilimo na kuuzwa bei ya juu nchi za nje na hivyo kuinua vipato vyao. Tuelewe kwamba fursa hii itayeyuka kama theruji juani, kama nchi itadhoofisha msimamo wake wa awali.

Aidha ni jambo la kuhuzunisha baada ya wakulima kupata taarifa kuwa tayari serikali yetu imeruhusu mbegu zilizobadilishwa viini tete kwa baadhi ya mazao kama mahindi na pamba, na hivyo kuwazidishia hofu kubwa wakulima kwa kutokujua ni nini madhara yatakayoletwa na aina hiyo ya mazao mapya kwenye kilimo chao na afya zao.

Pasipo kuwa makini, nchi ambayo kwa kipindi kirefu imekuwa na sifa adhimu ya kulinda uingizwaji na ulimwaji wa mazao yaliyobadilishwa vinasaba, kwa kutaka kuiga na kuitikia utashi wa mataifa ya Kimagharibi, Tanzania itajikuta imepoteza msimamo huo na hivyo kuwa kwenye matatizo ya mkanganyiko huo kama ule uliopo kwenye mataifa jirani ya Kenya, Uganda, Zambia na Afrika ya Kusini kuhusu GMO.

Tunaelewa kuwa Serikali kwa hivi sasa inakumbana na msongo mkubwa kutoka mashirika tajiri ya nje yakiitaka kuwaruhusu waingize mazao na mbegu hizo kwa wingi nchini, lakini ni vema ikatambua kuwa mashirika haya hayana nia nzuri tofauti na ukweli kwamba yanalenga kujitajirisha zaidi kwa kuzichukua fursa zote zilizopo kwa wakulima wadogo lakini pia yanataka kuhatarisha ustawi wa jamii na usalama mdogo wa chakula uliopo nchini na barani Afrika kwa ujumla ili kujiongezea soko la mazao yao.

Wakati umefika sasa, serikali isimame kidete na kuzisimamia Endelea Uk wa 3

Toleo NO. 042 Aprili - Juni 2013 Bei Shs. 500/=ISSN 0856-5937

WAHARIRIAl-amani MutarubukwaStephen Ruvuga

BODI YA MVIWATA Mwenyekiti – Habibu SimbamkutiMakamu Mwenyekiti – Veronica SophuKatibu - Stephen Ruvuga- (Mkurugenzi Mtendaji) Mweka Hazina – Esther Mallya

WAJUMBEJoseph KilowokoPrisca JohnAmina KazibureProjestus IshekanyoroHaji Ussi HajiPaul Joseph

MSHAURI WA MVIWATAProf. Amon Mattee

LINATOLEWA NA KUSAMBAZWA NA Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA)

S.L.P 3220 Morogoro, TanzaniaSimu: 023 261 41 84Faksi: 023 261 41 84Barua pepe: [email protected], [email protected]: www.mviwata.org

USANIFU NA UCHAPISHAJIPENplus Ltd – 022 2182059

Tahariri

Mchakato wa kuunda Mabaraza ya Katiba waibua malalamiko

Uk. 4Tanzania tunajifunza nini kwa Burkina Faso?

Uk. 22

Toleo NO. 041 Januari - Machi 2013 Bei Shs. 500/= ISSN 0856-5937

Utafiti chanjo ya UKIMWI waleta

Uk. 14

1Pambazuko Na. 41 Toleo la Januari - Machi 2013

MAZAO YALIYOBADILISHWA VIINI TETE (GMO):

Je! ni kwa maslahi ya taifa la Tanzania?

Na Al-amani Mutarubukwa, Morogoro

Licha ya kuwa nchi ya Tanzania imekuwa ikisemekana kuwa

miongoni mwa nchi chache duniani zenye sheria kali na makini katika kudhibiti uingizwaji na ulimwaji wa mazao yaliyobadilishwa kisayansi ama yenye viini tete (GMO), msukumo wa kimagharibi huenda ukaifanya nchi kupoteza sifa hii adhimu.

Hivi karibuni kumeibuka mjadala mkali baina ya pande mbili zinazokinzana kuhusu uhalalishwaji wa ulimwaji wa mazao ya aina hii nchini, huku wana harakati

wakiiasa serikali kuendelea kulinda sheria zinazosimamia mazao yaliyobadilishwa kisayansi na uhandisi jeni.

Kipengele ambacho kinachoifanya

sheria ya Tanzania kuwa ya kipekee

ni kile kilichoainishwa kwenye Mpangilio wa Kanuni za Usalama wa Mazao (2009 Bio-safety Regulatory Framework).

Kipengele hicho kinatamka bayana ya kuwa iwapo mtu ataingiza nchini, ama kusafirisha, ama kutumia,

ama kuingiza sokoni bidhaa yoyote itakonayo na GMO, atajibu

mashtaka juu ya madhara yatakayosababishwa na mazao hayo sambamba na kulipa fidia.

Hali hii imekuwa ikiyapa wakati mgumu

makampuni, mashirika na baadhi ya watunga sera wasio

wazalendo wenye kiu ya kuzibadili na kuzilegeza sheria hizi ili ziweze kuwa laini na kukubali uingizwaji na ulimwaji wa mazao yenye viini tete.

Endelea Uk wa 2

MADA MAALUM

Binti akivuna pamba. Zao la pamba ambalo linalimwa kwa wingi maeneo ya Kanda ya ziwa nchini, ni miongoni mwa mazao yanayowindwa kulimwa kwa mbegu zilizobadilishwa viini tete.

Kama ishara ya usaliti un-

aoweza kufanywa na baadhi ya watoa maamuzi na viongozi wa juu

wa nchi kumekuwa na michakato mbal-imbali ambayo inatokana na msukumo wa

kimagharibi ikilenga kuifanya Tanzania kuwa soko jipya la mazao haya ambayo

madhara yake ni makubwa hasa kwa mkulima mdogo

nchini.

2 Pambazuko Na. 41 Toleo la Januari - Machi 2013

Kama ishara ya usaliti unaoweza kufanywa na baadhi ya watoa maamuzi na viongozi wa juu wa nchi kumekuwa na michakato mbalimbali ambayo inatokana na msukumo wa kimagharibi ikilenga kuifanya Tanzania kuwa soko jipya la mazao haya ambayo madhara yake ni makubwa hasa kwa mkulima mdogo nchini.

Na hofu kubwa inazidi kutanda miongoni mwa wakulima wadogo nchini wakihofia kuwa tayari mbegu za mazao haya zimeingia katika maduka ya mbegu na kuwa huenda wamekwisha anza kuyalima pasina kutambua.

Bw. Emmanuel Kisanga, mkulima na mkazi wa mkoa mpya wa Simiyu anasema kuwa ana hofu kuwa tayari hata mbegu ya pamba alizopatiwa na kampuni mojawapo inayojishughurisha na kilimo cha mkataba mkoani humo huenda zina viini tete.

Uoga kama huo kwa mkulima mdogo, ambaye kilimo chake kinachangia pato la taifa kwa zaidi ya asilimia 25, unaihimiza serikali kushtuka na kuzidi kukazia kwenye sheria zinazozuia GMO, kipindi ambacho tafiti mbalimbali zinapaswa kufanywa kubaini madhara ambayo yanaweza kusababishwa na ulimwaji wa mazao haya.

Hofu hii ya kimsingi kabisa, inatokana na ukweli kuwa endapo mazao haya yatalimwa hata katika eneo dogo tu, upo uwezekano wa kuchafua viini tete (jeni) za mazao ya asili kwa njia ya chavua (poleni) zinazosafirishwa na upepo. Na mwisho hakutakuwa na mbegu za asili tena kwa mazao yote.

Pengine angalizo linapaswa kuwekwa kwa viongozi wa serikali yetu hasa kwa wale wenye dhamana ya kuilinda nchi na kuiepusha na sayansi hizi zisizo na tija wanapokosa msimamo na kutaka kufungua milango kwa aina yeyote ya vumbuzi zenye kuhatarisha maisha, uchumi na mazingira ya Tanzania.

Akizungumza katika Jukwaa la Mapinduzi ya Kijani barani Africa

(AGRF) mwaka jana, Prof Jumanne Maghembe akiwa Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, alinukuliwa akikisifikia kilimo cha mazao ya GMO kuwa ni fursa ya kumnufaisha kiuchumi mkulima mdogo.

Alisema mazao yenye viini tete ni kichocheo cha kiuchumi kwa mkulima wa Africa huku akihimiza wakulima kuchangamkia mbegu hizo ambazo zitawatajirisha hasa kama watalima mazao ya biashara kwa kutumia mbegu zilizobadilishwa kisayansi au zenye viini tete kwa madai kuwa hata kama kutakuwa na madhara, hayawezi kumdhuru binadamu kwa kuwa zao kama pamba haliliwi.

“Kuna taasisi nyingi sana nchini ambazo zinapinga GMO, lakini watumishi wote, sisi na wao mbona tunavaa nguo zilizotokana na pamba ya GMO ya ughaibuni. Sipati majibu, taasisi hizi zinapinga GMO kwa faida ya nani,” alisema.

Prof Maghembe alisisitiza kuwa mazao haya yaliyobadilishwa kisayansi, sio tu kwamba yanauwezo mkubwa wa kuhimili wadudu wasumbufu na ukame, bali pia yanaweza kuongeza mavuno kwa kiwango kikubwa na hivyo kumnufaisha mkulima mdogo.

L a k i n i w a t a a l a m wa mambo wanakinzana na mawazo h a y o , w a k i s e m a k u w a mawazo hayo ni udhalilishaji wa vyuo vya utafiti nchini ambavyo vimekuwa na matokeo bora kwa kuibua mbegu bora na zenye kuvumilia ukame na kutoa mavuno bora pasipokubadili viini tete.

Wanahoji kuwa sayansi hii ya ubadilishaji mazao imegubikwa na siri kubwa kwa kuwa madhara ya kutumia mazao haya hayajawekwa wazi kwa mlaji na hivyo kuifanya sayansi hii kuwa sayansi ya

watu wachache na ina lengo la kuyatajirisha makampuni makubwa kupitia mgongo wa wakulima nchini.

Wanaharakati wanadokeza kuwa, kinyume na matarajio ya wengi, vyakula vya viini tete vinataka mvua nyingi, maji, mbolea na viuatirifu vya kutosha ili kustawi hivyo ulimaji wake ni ghali mno pengine kushinda hata mazao yasiyobadilishwa viini tete.

MadharaIngawa hakuna madhara ya moja kwa moja ambayo yamekwisha thibitishwa kisayansi kutokana na matumizi ya vyakula vitokanavyo na viini tete, upo ushahidi mbali mbali unaelezea kuwa vyakula vya namna hii vinaweza kuathiri mwili.

Kuna utafiti uliofanyika barani Ulaya kwa kuwalenga akina mama wajawazito kwa kuwalisha vyakula vya GMO, ambapo watoto waliojifungua walikutwa na chembechembe zitokanazo na viini tete (Bt) , ushahidi unaokinzana na propaganda za kuwa viini hivyo husagika katika mmengenyo wa kawaida wa chakula.

Lakini pia

b a a d h i ya wataalam wanasema kuwa madhara ya mazao ya aina hii, sio lazima yatokee papo hapo, bali huweza kuchukua muda mrefu hata zaidi ya muongo mmoja.

Ni kwa mantiki hii, Tanzania imekuwa ikikumbatia sheria inayotamka bayana ya kuwa iwapo

Inatoka uk. wa 1

Mazao yaliyobadilishwa viini tete (GMO):

MADA MAALUM

Endelea Uk wa 3

Ni kwa mantiki hii, Tan-

zania imekuwa ikikumbatia she-ria inayotamka bayana ya kuwa iwapo

mtu ataingiza nchini, ama kusafirisha, ama kutumia, ama kuingiza sokoni bidhaa yoyote

itakonayo na GMO, atajibu mashtaka juu ya madhara yatakayosababishwa na

mazao hayo sambamba na ku-lipa fidia.

3Pambazuko Na. 41 Toleo la Januari - Machi 2013

Inatoka uk. wa 2

mtu ataingiza nchini, ama kusafirisha, ama kutumia, ama kuingiza sokoni bidhaa yoyote itakonayo na GMO, atajibu mashtaka juu ya madhara yatakayosababishwa na mazao hayo sambamba na kulipa fidia.

Sheria ambazo zinayafanya makampuni kadhaa yakihaha na kutamani kupandikiza mbegu zenye viini tete juu ya ardhi yenye rutuba ya Tanzania na inayokubali kila aina ya mazao pasina haja ya matumizi ya dawa kali za wadudu na mbolea nyingi kama zitakavyo GMO na hivo kutokuwa na tija kwa mkulima.

Baadhi ya wasomi duniani na wale wa Afrika mashariki wanasistiza umuhimu wa matumizi ya sayansi katika kilimo ili kuleta mapinduzi ya kijani japo kwa kuwa makini na vumbuzi hizo kwani sio kila sayansi inatarajiwa kuwa na matokeo bora.

Mtunzi vitabu mashuhuri wa

masuala ya kilimo barani Afrika na msomi wa chuo kikuu cha Havard, Prof Calestous Juma, anasema kuwa , pamoja na umuhimu wa kukumbatia maendeleo ya teknolojia katika kilimo, ni lazima serikali barani zitunge na kuimarisha sheria na kanuni madhubuti za namna ya utumiaji vyakula vya GMO.

Msomi huyo mwenye asili ya nchi jirani ya Kenya, anasema ingawa uhandisi wa viini tete umeweza kutoa matokeo bora ya zao la pamba nchini marekani kwa kuongeza uzalishaji kwa asilimia 24 na kuongeza pato kwa wakulima wadogo kwa zaidi ya asilimia 50, ni wajibu wa serikali hizi kufanya jitihada za kuzijengea uwezo taasisi za kutafiti usalama wa vyakula ili ziweze kuweka vigezo kwa kila zao la viini tete kabla ya kuyaruhusu kuingizwa sokoni.

Hivyo, ni rai yangu kwamba serikali itazingatia ushauri wa kuthibiti uingizaji, uzalishaji na utumiaji wa mazao yaliyobadilishwa viini.

MADA MAALUM

inatoka ukurasa wa Tahariri

Tahariri

sheria zilizopo kikamilifu na kufutilia nia yake ya kutaka kuzilainisha ikitaka kukidhi mahitaji ya nje. Pia itumie vituo vyake vya kilimo kufanya uchunguzi wa kutosha kuhusu usalama wa Watanzania iwapo GMO itatumika.

Tunatambua kuwa utafiti wa aina hii huweza kuchukua hadi miaka kumi kukamilika, hivyo jamii isidanganywe kwa namna yoyote, bali nchi ichukue muda kujiridhisha na hatimae itoe matokeo ya tafiti hizo yawekwe bayana kabla ya kuruhusu uiingizwaji, ulimwaji na matumizi ya mazao yaliyobadilishwa viini tete.

Kama taasisi ya kitetezi kwa maslahi ya wakulima wadogo wa Tanzania, tunatoa angalizo kuwa matumizi ya GMO nchini ni janga la kitaifa ambalo tukiliacha lisambae nchini, litaathiri usalama wa chakula, afya za raia na mazingira na litachukua miaka mingi kurekebishwa.

Jihadhari namaambukizo ya

UKIMWIjikinga na umlinde

mwenzako

4 Pambazuko Na. 41 Toleo la Januari - Machi 2013

Mchakato wa kuunda Mabaraza ya Katiba waibua malalamiko

Adeladius Makwega, Morogoro

MCHAKATO wa utayarishaji wa katiba mpya nchini Tanzania unaendelea na

sasa kimewadia kipindi cha kuundwa kwa mabaraza ya katiba. Hatua hii ya kuwapata wajumbe wa mabaraza haya unatokana na kukamilika kwa awamu ya kwanza ya kukusanya maoni ambayo yatawekwa katika rasimu ya katiba ya kwanza. Hata hivyo, katika mchakato huu kumezuka malalamiko ya mchakato kutokwenda sawa ikiwemo lalamiko la kuwepo kwa udanganyifu.

Wakati tunaandika makala haya kuna taarifa kwamba jijini Dae es Salaam kunafanyika marudio ya uchaguzi huu wa wajumbe wa mabaraza ya katiba. Hii inaashiria kwamba hakukuwepo na umakini wa kutosha katika kusimamia chaguzi za wajumbe wa mabaraza ya katiba

“Jukumu la wajumbe wa katiba ni kupitia rasimu neno kwa neno. Hii ina maana kuwa wajumbe wa mabaraza ya katiba wana majukumu mazito ambayo uzito wake si kwao tu bali kama wajumbe wakiyapuuza majukumu hayo watakuwa wamewapuuza ndugu zao

Watanzania,” anasema Bw. Projectus Ishekanyoro, mkulima na mjumbe wa Bodi ya MVIWATA.

Kurudiwa kwa uchaguzi huo katika baadhi ya maeneo kumekuwa kukitazamwa kwa mitazamo tofauti huku wengine wakisema Dar es Salaam pekee imependelewa kufanyika marudio kwani ni ukweli ulio wazi kuwa kwa sehemu kubwa pamekuwepo na malalamiko na kasoro za udanganyifu kwa kuwapa nafasi watu wasio kuwa na sifa zakuwa wajumbe.

Changamoto za mchakato huu mikoaniBibi Lydia Ruliho ni miongoni mwa wanawake waliojitokeza kushiriki kwa karibu katika mchakato huo japokuwa yeye hakugombea bali amekuwa akiwapa elimu ya kushiriki katika uchaguzi huo. “Watu wengi wasio na sifa walichukua fomu na kugombea kwa kutumia ushawishi wao wa kisiasa na wameshinda, mimi binafsi ninalipinga hilo kwa asilimia 100,” alisema Bi Ruliho alipoongea na jarida hii.

Bi Ruliho amebainisha kuwa masharti ya mgombea ujumbe wa Mabaraza ya Katiba yanataja sifa za kujua kusoma na kuandika hiyo ni

Jaji Mstaafu Joseph warioba ambaye ni Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba akiwa katika mojawapo ya mikutano na wanahabari.

MAKALA

sifa ndogo na kwa maoni yake jambo la msingi ni kuhakikisha mtu anaijua katiba vizuri pia anaweza kuichambua kwa kina.

“Kuna watu hawajui hata rangi ya katiba lakini wamechaguliwa kuingia katika Mabaraza ya Katiba. Mimi sitegemei mabadiliko yoyote yale,” Mama Ruliho alimdokeza mwandishi wa Jarida hili. Suala hili ni changamoto kubwa ambayo tume ya mabadiliko ya katiba inatakiwa kuwa makini mno ili kuweza kuweka mambo sawa na kuja na katiba inayogusa maslahi ya Watanzania wote.

Kuna Mabaraza ya Katiba ya Wilaya na Mabaraza ya Katiba ya Taasisi za Mashirika Binafsi ambapo wanaweza kuunda mabaraza hayo. Katika hili MVIWATA tumeomba kuunda baraza la katiba kwa taasisi binafsi ambapo kama ombi hilo litajibiwa na MVIWATA itasimama kama baraza la katiba

Akilizungumizia suala la mabaraza haya Afisa Sera na Ushawishi wa MVIWATA Bwana Thomas John Laiser amesema bayana kuwa kwa hakika nafasi ya MVIWATA ni muhimu na watahahakisha kuwa maslahi yote ya mkulima yanaingia katika katiba ijayo.

“Ila ni wajibu wa kila mkulima kushiriki katika mchakato huo na sio kuwaachia baadhi ya watu kumiliki mchakato huo na kujivika joho la kuwatetea wakulima.”

Bwana Laiser ameongeza kuwa kuna mifano mingi namna wakulima wanavyokuwa nyuma kufuatilia mambo yanayowahusu mathalani ugawaji wa ardhi za vijiji ambapo watendaji wasio waaminifu wanagawa ardhi hiyo wakidai kuwa kijiji kizima kimeamua kumbe ni kiini macho tu.

Akizungumza na Kipindi cha Redio cha Sauti ya MVIWATA, Mkurugenzi Mtendaji wa MVIWATA Bwana Stephen Ruvuga, amewataka wakulima kuendelea kushiriki katika

Endelea Uk wa 5

5Pambazuko Na. 41 Toleo la Januari - Machi 2013

MAKALA

kila hatua ya mchakato huu wa kutayarisha katiba mpya.

Akizungumzia suala la uundaji wa mabaraza ya katiba alisema kuwa ijapokuwa wasimamizi wa uchaguzi huo ni wawakilishi wa serikali yeye haoni tatizo kwa sababu ni lazima kwa namna yoyote ile wawepo watu wa kusimamia mchakato. Jambo muhimu ni kuhakikisha kwamba mchakato utaongozwa sawa.“Kwa hakika kwa sasa wao ndiyo wawakilishi wa serikali, katika utaratibu wa sasa ni vigumu kumpata mtu tofauti anaweza kusimamia hilo. Suala muhimu ni kusimamia vizuri mchakato kwa kuangalia mbele masalahi ya taifa letu,”alisema Mkurugenzi Mtendaji wa MVIWATA.

Wakati utaratibu huu ukiendelea na tume ikiendelea kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa ratiba na kuyafikia malengo yake ipasavyo, wajumbe wa mabaraza haya kutoka Tanzania bara watakuwa 18,169 na wale kutoka Tanzania Visiwani watakuwa 1,198.

Wananchi watishiwaMalalamiko dhidi ya mchakato wa uundaji wa mabaraza ya katiba yanafuatia malalamiko ya vitisho wakati wa hatua ya ukusanyaji maoni ya katiba. Kumekuwa na taarifa za kuwatisha wale wanaotoa maoni ambayo yanakuwa hayawapendezi baadhi ya watendaji. Miongoni mwa mashuhuda wa suala hilo ni Bibi Dornatina Lawrlence kutoka Mkoani Manyara.

“Mara baada ya kuja tume ya mabadiliko ya katiba tulitoa maoni yetu vizuri bila ya woga lakini tume ilipoondoka tu baadhi ya watendaji wa vijiji walikuja na kutukanusha kuwa yale tuliyosema katika tume ya mabadiliko ya katiba si maoni yao, Je hii ni haki, tena walisema kuwa watatushugulikia,” alisema Bi Lawrlence.

Matukio kama haya yanatia doa zoezi lote la kupata katiba mpya kama ilivyokusudia na ni dhahiri kwamba kutoa vitisho kwa wanananchi wakati wa kukusanya maoni haikuwa sahihi.

Tume ya Mabadiliko ya Katiba

inafanya kazi chini ya sheria za nchi na kwa manufaa ya taifa ya kila Mtanzania na si kwa manufaa ya mtu fulani au kikundi fulani tu, kwa kuwa katiba ni mali yetu sote. Kwa sababu hiyo matarajio yetu kwamba kutakuwa na umakini zaidi katika kila hatua ya mchakato huu muhimu wa kihistoria kwa nchi yetu.

Marekebisho ya katiba awaliKatiba ya sasa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilianza kutumika tarehe 26 Aprili, 1977. Katiba inayotumika sasa ni ya mwaka 1977 na mpaka sasa imekwishafanyiwa marekebisho mara 14. Kutokana na mabadiliko hayo ya mara kwa mara ndipo Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Rais wa Jamuhur ya Muungano wa Tanzania alipoamua kwamba iandikwe upya. Marekebisho ya kwanza yalifanyika mwak 1979 na ya mwisho yalifanyika mwaka 2005 yakilenga kuongezwa uwiano wa nafasi za wanawake bungeni kwa asilimia 30. Pia kuweka bayana uhuru wa kuabudu na kutao maoni ili kuondoa vizuizi vilivyokuwepo kwenye katiba.

Licha ya mabadiliko haya yote ni dhahiri bado hayajakata kiu ya wakulima ya kuona masuala yao yanashugulikiwa. Bibi Aisha Madege mkulima wa korosho kutoka Mtwara anaakisi mtazamo huu; “ Inashangaza wao ndiyo wawakilishi wa rais lakini wamekuwa wakibana haki nyingi,

Inatoka uk. wa 4

mimi napendekeza wakuu wa wilaya waombe nafasi hiyo na sisi tuwapigie kura.”

Anasema wazi kuwa uwepo wa wakuu wa wilaya umekuwa hauna tija kwani wamekuwa wakiwanyima haki zao wakulima wengi mathalani suala la ugawaji wa mbolea za ruzuku wameshindwa kuzisimamia kabisa. Bi Madege alitoa mchango huo katika mojawapo ya mikutano ya katiba.

Wakulima wamiliki ardhiHabibu Ali Simbamkuti ni Mwenyekiti wa MVIWATA anaunga mkono hilo umiki wa ardhi kuwa chini ya mkulima mmoja mmoja na kusema kuwa hali hiyo itasaidia sana wakulima kuweza kujipatia mikopo kutoka taasisi za kibenki ambapo kwasasa mkulima haaminiki. “Mkulima analisha taifa lakini hamiliki ardhi, sasa ni wakati sahihi wa mkulima mdogo kuanza kumiliki ardhi ili kuondoa hali ya mkulima kuondolewa katika ardhi ndani ya taifa lake kama mkimbizi,” anasema Mwenyekiti wa MVIWATA.

Ndugu msomaji kumbuka kwamba sheria ya ardhi ya mwaka 1999 inafanya kazi ikiwa chini ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hivyo ni jukumu la kila mmoja wetu kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kutayarisha katiba mpya ili yale matarajio yetu yawemo katika katiba mpya . Vinginevyo tunaweza kuliweka taifa letu njia panda. Pambazuko linawatakia kila la

Mwananchi akitoa maoni yake wakati wa mdaharo wa uchangiaji maoni kwenye Tume ya Katiba

6 Pambazuko Na. 41 Toleo la Januari - Machi 2013

MAKALA

Zanzibar yapania kufufua karafuu

Adeladius Makwega, Morogoro

Zanzibar ilikuwa ikitambulika mno kuwa muuzaji mkubwa karafuu katika soko la dunia miaka ya 1970 ambapo kwa sasa sifa hiyo inapotea kutokana na kutokuwepo na mkazo katika zao hilo la biashara tangu miaka ya 1980 hadi miaka ya 2000.

Takwimu zinaonyesha kuwa mwaka 1970 Zanzibar iliweza kuuza tani zaidi ya 400 lakini leo hii kumekuwa na mataifa mengine ambayo yanafanya vizuri katika kilimo cha zao hili. Kupotea kwa umaarufu huo wa zao hilo kunatokana na kukosekana kwa mkazo na baadhi ya mataifa kufanya vizuri zaidi ya Zanzibar .

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inasema kuwa hivi sasa kumekuwepo na tabia ya watu wasio waaminifu ambao wanasafirisha nje ya nchi miche ya mikarafuu. Serikali hiyo imeweka wazi kuwa itachukua hatua kali kwa yeyote yule atakaye bainika akifanya hivyo.

Kauli hiyo inakuja baada ya serikali hiyo kuamua kurudisha hadhi ya karafuu kwani ilitenga shilingi milioni 40 kwa kutayarisha vitalu vya miche ya mikarafuu ambayo iligawiwa bure kwa wakulima ili kuweza kuipanda katika mashamba yao.

Kalipio hilo la Serikali ya Mapinduzi limekuja baada ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, kuonya kuwa serikali itawachukulia hatua za kisheria watu watakaobainika kukata miti pamoja na kusafirisha miche ya mikarafuu nje ya nchi ambapo imebainika kuwa miche mingi inapelekwa Kenya.

Maalim Seif alitoa onyo hilo Bagamoyo Mtambwe, Mkoa wa Kaskazini Pemba alipokuwa akizindua kampeni ya upandaji miti Zanzibar.

Wakulima hao wa karafuu mpaka sasa wameweza kupanda miche zaidi ya laki mbili pia waliombwa na serikali yao kuacha tabia ya kukata miti kiholela na kuwa kufanya hivyo ni hatari kwa mazingira na husababisha athari kubwa kiuchumi, lakini vitendo vya kusafirisha nje ya nchi miche ya mikarafuu linaweza kushusha hadhi ya Zanzibar iliyojijengea kwa miaka mingi kuwa mzalishaji mkuu wa karafuu.

Jitahada hizo za serikali ya mapinduzi zinalengo moja kuwa wafikie uwezo wa kuzalisha tani 6,000 za karafuu kwa mwaka na ndiyo maana wakulima hao wameweza kupewa miche bure ili kuweza kuinua kiwango cha uzalishaji wa karafuu katika kisiwa hicho cha pwani ya bara ya Hindi.

Kwa hakika karafuu ni alama ya Zanzibar ambayo imeifanya ijulikane duniani kote kuwa ni visiwa vya viungo, lakini baada ya watu kuona thamani ya zao hilo inashuka katika miaka iliyopita, walilidharau na kuikata miti hiyo kwa ajili kuni na mkaa pia kupata mahali pa kujengea nyumba.

Kwa hakika jamii inahitaji mno matumizi ya miti kwa mkaa na kuni lakini mkulima atambue pale anapokata miti kwa desturi ya miji ya pwani wakulima wanaweza kupikia kwa kutumia makumbi ya minazi, vifuu na makuti. Kukata mti kama mkarafuu wenye manufaa makubwa kwa hakika haikubaliki kabisa.

Umuhimu wa karafuu haufichiki, Bi wardat Harubu ni mkulima wa karafuu kwa muda mrefu sana anasema “karafuu kwa Zanzibar ni sawa na mapiramindi kwa Misri tunatakiwa kuitunza na serikali yetu inajukumu ya kujenga mazingira thabiti.” Mkulima huyu anasema katika hatua mpya ya kusisitiza wananchi kupanda mikarafuu yeye anaitunza miche 496 mipya ambayo anahakisha kuitunza iwezekanavyo

ili mradi na yeye awe na mikarafuu mingi hapo baadaye.

Anasema alipokea miche 565, ambapo miche 69 iliharibika wakati wa kuisafirisha kutoka katika kitalu kuelekea shambani na anasema inatokana na namna ilivyobebwa na kuifikisha shambani kwakwe. Anasema kama miche hiyo ingeuzwa kwa hakika lingekuwa jambo gumu mno kwa yeye kuweza kupata miche yote na kuweza kuipanda shambani kwake.

Karafuu japokuwa inapatikana Zanzibar pia inapatikana katika visiwa vya Maluku huko Indonesia, India, Madagaska, Sri lanka na Pakistani. Huku wana historia wanadai kuwa karafuu ilianza kulimwa kati ya miaka 350-400 iliyopitta ambapo iliweza kufika katika maeneo kama Zanzibar kutokana na wafanyabiashara wa kiarabu kuuza karafuu kama miongoni mwa biashara zao.

Zao hili lenye historia ndefu kwa Zanzibar lilithaminiwa sana na wazee waliootesha kwa wingi hadi kufikia hatua Zanzibar ikazalisha tani zaidi ya 35,000 katika msimu mmoja. Mkosi ulipoingia katika visiwa hivyo vya karafuu uzalishaji ulishuka kidogo kidogo hadi kufikia tani 2,000 katika miaka ya hivi karibuni.

Kwa takwimu hizi zinaonyesha kuwa kwa sasa Zanzibar ina deni la kuzifikia tani 33,000 ili kuweza kurejesha heshima yake na kuweza kupata kipato kikubwa. Kama nilivyokudokeza kuwa hadi sasa serikali ya Zanzibar inalenga kufikisha tani 6,000 za karafuu ambapo haijafikiwa hata robo ya tani 35,000.

Wakati jitihada hizo za kuotosha mikarafuu na kuipanda katika vitalu na kuwagawia Wazanzibari zikiendelea ifahamike kuwa kazi hiyo ina manufaa ya kimazingira ikiwemo kuzuia mafuriko mathalani

Endelea Uk wa 7

7Pambazuko Na. 41 Toleo la Januari - Machi 2013

MAKALA

kwa wananchi wanaoishi katika maeneo yanayokumbwa na uvamizi wa maji ya bahari katika maeneo ya kilimo, wananchi wanatakiwa kujenga tabia ya kupanda miti ya mikoko na kuhifadhi mazingira kuepusha athari za uharibifu huo.

Hali ya uharibifu inaonekana katika eneo la Wingwi Wilayani Micheweni eneo hili lililojengwa tuta upande wa baharini ambalo awali lilikuwa likitumika kwa kilimo, lakini hivi sasa ni sehemu ya bahari.

Hali hiyo ilisababishwa na tabia ya wananchi kukata miti kwa wingi ikiwamo mikoko kando ya bahari, hivyo maji ya bahari kupanda juu hadi sehemu zinazotumika kwa shughuli za kiuchumi na kijamii kama vile sehemu za makaburi kuvamiwa na maji ya chumvi. Kwa hakika kupandwa kwa miche hiyo kuna manufaa ya kiuchumi na kimazingira

kwa Wazanzibar.Katibu Mkuu Wizara ya

Kilimo na Maliasili Zanzibar, Afan Othman Maalim alisema suala la maji ya bahari kuvamia maeneo ya wananchi wanayoyatumika kwa shughuli za kilimo na kijamii ni kubwa sana. Alisema Zanzibar tayari imeorodhesha maeneo 148 yaliyokwisha kukumbwa na hali hiyo kote Unguja na Pemba.

Kabla ya kauli hii kutoka kwa kiongozi wa ngazi ya juu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kauli inayofanana na hiyo ilitolewa mwaka 2011 na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwa imejizatiti kuongeza uzalishaji wa miti mipya ya mikarafuu katika mfumo wa kitaalamu zaidi ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo ambalo ndio muhimili mkuu wa Uchumi wa Taifa.

Kwa hakika miche ya karafuu

ina manufaa makubwa kwa Zanzibar, kutokana na kuwepo na tabia hii ya kuisafirisha miche hiyo ya mkarafuu nje ya nchi baadhi ya watu wamekuwa wakilalamikia hilo kwani limekuwa likitokea si kwa zao hilo tu hata katika mazao ya wanyama adimu hapa Tanzania.

Bw. Hamisi Jumbeni mkazi wa Mjimkongwe na ni mkulima wa Karafuu analilamikia hilo. “Vitu ambavyo vimekuwa vinapatikana hapa kwetu na sehemu zingine hakuna,watu wameamua kuvipeleka huko kwa sababu ya tamaa zao. Wanyama wanasafirishwa, vyura adimu walipelekwa Marekani kuhifadhiwa, mazao ya miti inasafirishwa. Matokeo yake ni kuwa huko mbele tutakosa hata soko la nje, kwa sababu hao tunaowapelekea watakuwa navyo na wao sasa ndiyo watakaokuwa wanafanya biashara. Lakini haya yote yanafanyika kwa sababu ya udhaifu wa serikali.”

Japokuwa kuna wale wanaolilalamikia hilo lakini wapo baadhi ya watu wanapinga hilo kwa madai kuwa suala la kusafirisha miche sio tatizo lakini jambo la msingi ni kuwepo na ubunifu kwa wakulima na kujua mbinu mbalimbali za kukabiliana nalo, alisema Bw. Jumanne Masanja ambaye ni mkulima wa Tumbaku huko Tabora,

“Wananchi visiwani wanaweza kufanya zaidi ya karafuu, kwa nini tung’ang’anie karafuu miaka nenda rudi, tusiogope ushindani inabidi tupambane hadi kieleweke, mbona kuna mazao mengi ya biashara kama kahawa, chai, tumbaku, mchele, na majirani zetu pia wanayo hayo mazao lakini hatulalamiki kwa sababu hatuna hatimiliki ya mazao hayo, kila nchi ikitaka kulima inalima na kutafuta wanunuzi wake.”

Matumaini ya mkulima wa karafuu ni usimamizi madhubuti kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ili kumpa nafasi mkulima kulima zao hilo na kuweza kujipatia pesa. Suala la msingi ni kuirudisha Zanzibar kuwa kinara katika kilimo cha karafuu kwani kwa kufanya hivyo itakuwa ni njia ya kumkomboa mkulima kutokana na umasikini uliokithiri.

Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein (kulia) akichambua karafuu.

8 Pambazuko Na. 41 Toleo la Januari - Machi 2013

KUTOKA MITANDAONI

Wakulima kunufaika na mradi mpya wa kukabiliana na

Mabadiliko ya Tabia ya NchiNa Al-amani Mutarubukwa, Morogoro

Wakati mabadiliko ya tabianchi kwa sasa kama vile ukame na

mafuriko tayari yamesababisha gharama kubwa za kiuchumi Tanzania, taasisi mbalimbali zisizo za kiserikali zinakuna vichwa kuibua miradi itakayo zuia ama kupunguza athari hizo hasa kwa mkulima mdogo nchini.

Hivi karibuni, mradi unaolenga kupunguza umaskini miongoni mwa wakulima wadogo Tanzania na kuwajengea uwezo wa kukabiliana na mabadiliko tabianchi ikiwa ni pamoja na kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa kwa kuboresha njia za kilimo, ulizinduliwa.

Mradi huu ni wa ubia kati ya mashirika matano yasiyo ya kiserikali ambayo ni MVIWATA, TFCG, MJUMITA, TOAM pamoja na ActionAid-Tanzania.

Mradi huu wa miaka miwili, unahusisha uraghbishi katika ngazi ya taifa na maonesho ya njia mabalimbali za kilimo hifadhi ndani ya Chamwino na vijiji vitatu vilivyopo maeneo ya mlimani katika wilaya ya Kilosa.

Katika shughuli za uzinduzi, wajumbe wa bodi za mashirika haya walikutana kujadili namna ya utendaji kazi kwa kubadilishana uzoefu na kujadili ni jinsi gani wataweza kudumisha umoja wao katika utekelezaji wa miradi ya namna hii kwa kuzingatia kuwa shughuli zao zinamlenga mdau mkuu mmoja ambaye ni mkulima mdogo.

Wilayani Kilosa, mradi huu ulitambulishwa na mwakilishi wa Afisa Maliasili wa wilaya Bw. Edward Mkumbo ambaye katika risala yake aliwashukuru wadau kwa kuiteua wilaya yake kuwa eneo

nufaika la mradi na kusema kuwa alitarajia mradi ungeleta utatuzi wa changamoto za misitu nchini.

Na baadaye viongozi hao walijikita katika kujadili mwongozo wa kufundishia wakulima katika utekelezaji wa shughuli za mradi. Shughuli hiyo ambayo ilidumu kwa siku tatu, pia ilijikita kuwaelemisha wajumbe hao maana ya mabadiliko ya tabianchi na namna yanavyoathiri kilimo cha mkulima mdogo na namna mradi utakavyo saidia kutatua hali hiyo.

Umuhimu wa mradiNi ukweli usiopingika kuwa sera na kanuni za uwekezaji na kilimo vinatoa kipaumbele kwa kilimo kikubwa cha kutumia mashine zenye kutumia nishati ya mafuta na chenye lengo la kuongeza uzalishaji na kukuza masoko ya mazao.

Ingawa njia hii inaweza kuongeza uzalishaji kwa kipindi kifupi, pia inaongeza uwezekano wa wakulima

wadogo wadogo kuwa maskini na kuathiriwa zaidi na mabadiliko tabianchi yanayotokana na ongezeko la hewa ukaa itokanayo na matumizi tegemezi ya uharibifu wa misitu kwenye maeneo ya wakulima wadogo wadogo.

Maeneo ya Kilosa yamekuwa yakikumbwa na mafuriko ya mara kwa mara kama kielelezo cha madhara yatokanayo na mabadiliko tabianchi, ambayo yanamkosesha mkulima mavuno na kuzidi kumdidimiza katika wimbi la umaskini.

Vivyo hivyo kwa maeneo ya Chamwino, Dodoma ambapo wakulima wamekuwa wakitaabika na ukosefu wa mvua za uhakika na ukame wa muda mrefu.

Mradi huu utajikita kuwapa mafunzo wakulima wadogo wadogo juu ya njia bora za kilimo ambazo wanaweza kuzifuata katika kukabiiliana na changamoto hizi za mabadiliko tabianchi katika maeneo yao.

Endelea Uk wa 9

Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Luteni Elias Tarimo akizindua mradi wa Kilimo Rafiki Mahama Chamwino Dodoma.(Picha na Amanzi Amanzi)

9Pambazuko Na. 41 Toleo la Januari - Machi 2013

KUTOKA MITANDAONI

Uzinduzi rasmiBaada ya shughuli za mjadala wa wajumbe wa mashirika haya juu ya namna ya utekelazaji mradi huu w a k i w a w i l a y a n i K i l o s a , h a t i m a y e w a j u m b e walielekea wilaya ya Chamwino ambapo pia utekelezwaji wa mradi huu unafanyika.

Wakiwa wilayani hapa, uzinduzi ulitanguliwa na kikao cha watendaji na wajumbe wa Kamati ya Ushauri ya mradi wakijadili mpango kazi na kujitathmini walipofikia katika utekelezaji.

Baadaye, ugeni huu ulifunga safari ya kwenda kuzuru vijiji vya Manchali na Nzali ambavyo vinanufaika na mradi huu kabla ya mkuu wa wilaya wa Chamwino hajahutubia.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkuu wa wilaya ya Chamwino Bi Fatuma Mafunda, alisema kuwa pamoja na kwamba mabadiliko tabianchi yanachangiwa zaidi na nchi zilizoendelea kama Marekani na Uchina, kwasababu wao ndio wazalishaji wakubwa wa gesi ukaa inayotokana na shughuli zao za viwandani, pia nchi zinazoendelea zinachangia mabadiliko tabianchi kwa shughuli za kiuchumi za kila siku.

Mfano mzuri ni shughuli za kilimo zisizo rafiki wa mazingira.

Kwa mujibu wa Bi Mafunda, njia ambazo wakulima wadogo wadogo wanatumia katika kilimo, zimekuwa sio rafiki kwa mazingira na hivyo zimekuwa zikichangia uzalishaji wa gesi joto na hivyo kuchangia mabadiliko tabianchi.

Kwa sasa inakadiriwa asilimia kati ya 10-15 ya gesi ukaa inayosababisha mabadiliko tabianchi huzalishwa kutokana na shughuli za kilimo. Njia kuu ya kilimo kwa wakulima wetu

ambayo siyo rafiki na mazingira ni kilimo cha kuhamahama. Wakulima wamekuwa wakifungua mashamba mapya kila msimu kwa kufyeka misitu.

“Wakulima wetu wamekuwa wakifanya hivi kwa lengo la kutafuta rutuba ili kuongeza uzalishaji wa mazao bila kufahamu njia hiyo ina madhara makubwa kwa mazingira na kwa maisha yao kwa ujumla,” alisema.

Athari za mabadiliko tabianchi ni nyingi, ila kwa wakulima mdogo, athari hizo zimechangia kupungua kwa uzalishaji wa chakula na hivyo kuongeza njaa kwa jamii yetu. Ni kweli kabisa mvua isiponyesha, mtu

wa kwanza kuathirika ni mkulima mdogo ambae kwa asilimia 100 anategemea mvua kwa ajili ya chakula chake kwa mwaka mzima.

“Tunahitaji kuwa na njia bora za kilimo kwa ajili ya wakulima

wetu, ili waweze kuzalisha chakula cha kutosha wakati

huo huo wakikabiliana na athari za mabadiliko tabianchi,” aliongeza mkuu wa wilaya huyo.

Akihitimisha hotuba yake, Bi Mafunda

aliwapongeza washirika wa mradi huu na kusema

kuwa umekuja muda muafaka wakati wananchi wengi hasa

katika kipindi ambacho wakulima wanapenda kufahamu masuala ya mabadiliko tabianchi, namna yanavyoathiri maisha yao ya kila siku na namna wanavyoweza kukabiliana na janga hili.

Aliwaomba wananchi wa wilaya yake kutoa ushirikiano wa kutosha kwa watekelezaji wa mradi huu na kusema kuwa radi huu ukitekelezwa vizuri utawanufaisha watu wa Chamwino na Kilosa moja kwa moja. Aliwaasa kushiriki kwenye shughuli za mradi na kujaribu njia mpya na bora za kilimo ambazo ni rafiki na mazingira na ambazo zitawaongezea uzalishaji wa chakula na hivyo kuwaweka katika nafasi nzuri zaidi ya kupambana na umasikini.

Wakulima kunufaika na mradi mpya...Inatoka uk. wa 8

Baadhi ya watendaji wa mashirika yanayotekeleza mradi wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi walipotembelea shamba mojawapo la maradi huo huko Chilomwa Chamwino.(Picha na Amanzi Amanzi)

Kwa sasa inakadiriwa

asilimia kati ya 10-15 ya gesi ukaa inayosababisha mabadiliko tabianchi

huzalishwa kutokana na shughuli za kilimo. Njia kuu ya kilimo kwa wakulima wetu ambayo siyo rafiki na mazingira ni kilimo cha kuhama-

hama. Wakulima wamekuwa wakifungua mashamba mapya kila msimu kwa

kufyeka misitu.

10 Pambazuko Na. 41 Toleo la Januari - Machi 2013

KUTOKA MITANDAONI

Serikali yavuruga bei ya mchele nchini

Na Al-amani Mutarubukwa, Morogoro

Wakati mkulima mdogo nchini anazidi kupambana na

changamoto za upatikanaji na bei ghari za pembejeo pamoja na ukosefu wa soko la uhakika kwa ajili ya mazao yake, serikali imekua haimtendei haki kwa sera zake zinazobadilika kila uchao hasa zinazobana masoko ya wakulima.

Sera hizo ni pamoja na ile inayomkataza mkulima kupeleka mazao yake nje ya nchi hata kama ndiko kuliko na soko la uhakika na bei bora. Lakini, kama hiyo haitoshi, kumekuwa na uyumbishwaji wa sera ya kulinda soko la ndani linalotegemewa na mkulima mdogo

kwa kuruhusu uingizwaji holela wa mazao kutoka nje.

Hivi karibuni serikali ilitoa vibali vya kuwaruhusu wafanyabiashara waingize takribani tani 60,000 za mchele wa bila ushuru na kodi kwa kigezo kuwa bei ya mchele ilipanda sana na hivyo ikabidi kuingilia kati.

Uingizwaji huo wa mchele umeelezewa kutokuwa na manufaa kwa wakulima nchini hasa mkulima mdogo na badala yake ni jambo ambalo linawanufaisha wafanyabiashara na wakulima wa nchi za nje ambako mchele huo unatoka.

Wakiliezea suala hilo, wanasiasa na wanaharakati nchini wamelaani kitendo hicho na kuonya kuwa hakuna nchi yoyote duniani ambayo imeendelea kwa kuendekeza

uingizwaji wa vyakula toka ng’ambo kwa kuwa kufanya hivyo ni uvurugaji wa soko la ndani.

Akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka h wa fedha wa 2013/2014, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mh. Christopher Chiza alibainisha kuwa, ili kukabiliana upandaji bei ya mchele nchini, mnamo mwezi Desemba 2012, Serikali iliamua kuruhusu wafanyabiashara waagize tani 60,000 za mchele ili kupunguza makali ya bei kwa walaji.

Makampuni tisa yaliteuliwa kufanya kazi hiyo kuanzia wiki ya pili ya mwezi Januari 2013.

“Mchele huo ulitakiwa uwe

Endelea Uk wa 11

Wakinamama wakifunga vizuri viroba vya mpunga kwa jili ya kupata wateja.

11Pambazuko Na. 41 Toleo la Januari - Machi 2013

KUTOKA MITANDAONI

umeingia nchini ifikapo tarehe 30 Machi 2013. Masharti mengine yaliyotolewa kwa waagizaji yalikuwa ni pamoja na: bei ya jumla ya mchele isizidi Shilingi 1,300 kwa kilo; bei kwa wasambazaji wa kati isizidi Shilingi 1,450 kwa kilo; na bei ya rejareja isizidi Shilingi 1,700 kwa kilo... Hadi tarehe 30 Machi, 2013 jumla ya tani 34,689 za mchele zilikuwa zimeingizwa nchini,” alilieza bunge.

Akiongea kwa niaba ya wakulima na wafanyabiashara wa kikundi cha Supermarket chenye wanachama zaidi ya 120 kilichopo soko la Igurusi, wilaya ya Mbarali, Mwenyekiti wa MVIWATA Mbeya Bi Hawa Kihwele anasema hali hiyo ilizua mtafaruku mkubwa sana kwa kua uingizwaji mchele huo ulishusha bei sokoni hapo toka shilingi 2000 hadi shilingi 800 kwa kilo.

“Kwa kweli tulisikitishwa sana kwa kitendo hicho cha serikali kutuvurugia soko. Inatufanya tuhoji ni nini tafsiri ya dhana ya kilimo kwanza ikiwa mkulima anayehimizwa kulima kwa nguvu na kwa gharama yoyote anaishia kudhulumiwa soko lake kwa manufaa ya wachache,” alilieleza Pambazuko.

Kuhusu uwepo na upungufu wa mchele nchini, Bi Kihwele anakosoa kuwa pengine ni kutokana na serikali kutokuwa na mfumo sahihi wa kupata taarifa za kutosha kujua hali halisi ya mazao yaliyomo kwa wakulima.

“Ni wazi kuwa serikali haina njia sahihi ya kuwasiliana kati ya watendaji wao na mkulima ngazi ya chini. Nimeshuhudia mwenyewe ghala la Kapunga likiwa na tani 10,000 za mchele, vipi kwa maghala yote nchini?” anahoji.

Maoni hayo yanalandana na Msemaji wa Kambi ya Upinzani Bungeni Bwana David Silinde (Chadema) ambaye akichangia bungeni hivi karibuni kwa kuikosoa serikali kwa uamuzi huo na kusema kuwa hauna manufaa yoyote kwa mkulima mdogo zaidi ya kumkatisha tamaa ya kilimo cha mpunga.

“Tunaitaka serikali iwaeleze

wakulima wa Tanzania sababu za msingi za kuagiza mchele kutoka nje na kuwavunja moyo wakulima badala ya kuwaboreshea mazingira ya kilimo ili wajikwamue kutoka kwenye wimbi la umaskini,” alisema kisha akaendelea.

“Mataifa yote yaliyopiga hatua kiuchumi ni yale yaliyowalinda wakulima wake kutoka uvamizi wa masoko ya nje. Hivyo, ni jukumu la serikali yetu kuhak ik i sha k u w a

w a k u l i m a wa ndani wanalindwa kwa kuwapa ruzuku ili kuwapunguzia gharama za uzalishaji.”

Bwana Silinde alisistiza kuwa kuwalinda wakulima wadogo nchini kutawafanya kujituma kuzalisha mazao zaidi na kujipatia kipato kinachokidhi kulipa madeni ya mikopo mbalimbali waliyochukua kutoka vyombo mbali mbali vya fedha.

Vingenevyo, alisema, kuruhusu uingizwaji mchele kutawavunja moyo na ikibidi watauza mchele wao kwa bei ya kutupa na kuachana kabisa na kilimo cha zao hilo kwa miaka inayofuata jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa chakula wa taifa.

Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo uchumi wake unategemea kwa kiasi kikubwa shughuli za kilimo kwani zaidi ya asilimia 70 ya watu wake ni wakulima. Aidha, hatima ya usalama wa chakula wa nchi upo kwenye migongo ya wakulima wadogo ambao wamekuwa wakililisha taifa bila kuchoka.

Kwa mujibu wa Waziri Chiza, katika msimu wa 2011/2012 uzalishaji wa mchele nchini ulifikia tani 1,170,358 ambapo mahitaji kwa mwaka 2012/2013 yalikuwa tani 818,699.

Katika mazingira ya mtandao wa biashara uliopo, uzalishaji huo ni mdogo kukidhi mahitaji yetu ya mchele na mahitaji ya soko katika Kanda ya Afrika Mashariki, Kati na Kusini.

“Mahitaji hayo ya soko yalichangia kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo

nchini kutoka wastani wa

Shilingi 1,500 kwa

kilo mwezi Agosti 2012 hadi wastani wa Shilingi 2,800 kwa kilo mwezi Februari 2013 katika masoko ya jumla.”

Lakini wachambuzi wa mambo, hawaoni hiyo kama sababu kuu ya serikali kuliingilia soko la ndani kwa kuzingatia kuwa, kwanza uzalishaji wa mpunga katika maeneo mengi nchini uko katika hali nzuri, hali inayoashiria kuwepo kwa mchele wa kutosha sokoni.

Na pia bei hiyo inayodaiwa kupanda sana, ilifikiwa kutokana na ukokotozi wa gharama mbalimbali za uzalishaji kama vile bei ghali za pembejeo, usafirishaji na umeme ambavyo vyote vinamuelemea mkulima mdogo na kumfanya asione manufaa ya kilimo nchini.

Kufuatia hali hiyo, wakulima na wanaharakati wanaiasa serikali kusitisha uingizaji wa mchele wenye msamaha wa ushuru na kodi mara moja kwa maslahi ya Taifa kwa ujumla.

Serikali yavuruga bei....Inatoka uk. wa 10

“Ni wazi kuwa serikali

haina njia sahihi ya kuwasiliana kati ya watendaji wao na mkulima

ngazi ya chini. Nimeshuhudia mwenyewe ghala la Kapunga likiwa na tani 10,000

za mchele, vipi kwa maghala yote nchini?”

12 Pambazuko Na. 41 Toleo la Januari - Machi 2013

KAMERA

Baadhi ya wafanyakazi wa MVIWATA wakiwa katika majadiliano wakati wa kutaniko la faragha Aprili 2013 katika Hotel ya

Glonency 88 Morogoro.

Kikundi cha ngoma toka dodoma-Chamwino kikitumbuiza wakati wa uzinduzi wa mradi mpya wa mabadiliko ya tabia ya nchi. (Picha na

Amanzi Amanzi).

Mojawapo ya Mashamba darasa ya zao la mpunga huko Hembeti, Mvomero Mkoani Morogoro (Picha na Japhet Masigo)

Kikundi cha Mvomero- Players kikiburudisha kwa njia ya maagizo kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake dauniani 8, machi 2013

yaliyofanyika Mvomero

Mkurugenzi Mtendaji wa MVIWATA akiwa katika picha pamoja na washiriki wenzake katika mkutano wa kimataifa nchini Ireland

hivi karibuni.

Mwenyekiti wa MVIWATA Taifa Habibu Simbamkuti akijadiliana jambo na wafanyakazi wa mfuko GEPF mara baada ya kutoa

mafunzo kwa wafanyakazi wa MVIWATA.

KAMERA YA MVIWATA MITANDAONI

13Pambazuko Na. 41 Toleo la Januari - Machi 2013

KAMERA

Shamba la Mpunga mojawapo ya Miradi ya umwagiliaji huko Wami Dakawa ,Mvomero Mkoani Morogoro. (Picha na Japahet Masigo)

Wakulima wawezeshaji toka Mvomero (Mapromota) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kupata mafunzo-Picha hii imepigwa

(Picha na Abdalla Idd)

Wanamviwata wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mafunzo. (Picha na Abdalla Idd)

Wakulima wa mahindi wakitazama mojawapo ya shamba darasa la mahindi Kijiji cha Wami Dakawa Wilayani Mvomero Mkoani

Morogoro.

Kikundi cha ngoma kikitumbuiza wakati wa uzinduzi wa mradi wa Kilimo Rafiki. (Picha na Amanzi Amanzi.)

Watendaji wa MVIWATA idara ya uhasibu wakijadiliana kwa kina mojawapo ya shughuli zao wakati wa kutaniko la faragha. (Picha na

Al -amani Mutarubukwa.)

KAMERA YA MVIWATA MITANDAONI

14 Pambazuko Na. 41 Toleo la Januari - Machi 2013

Utafiti chanjo ya UKIMWI waleta matumaini

Adeladius Makwega, Morogoro

WATAALAMU watanza-nia wakishirikiana na wataalamu wengine

wamegundua chanjo ya UKIMWI nchini Tanzania ikiwa ni taarifa njema kwani kwa ugunduzi huo un-aweza kusaidia watu kupata chanjo hiyo kwa urahisi. Mafanikio hayo makubwa ya kinga yamefanywa na Jopo la Madaktari wa Chuo Ki-kuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) yaliyodumu kwa kipindi cha miaka mitano.

Kinga hiyo inagunduliwa wakati jitahada za kupambana na kutafuta dawa na kinga zimekuwa zinafanywa katika kila kona duniani huku baadhi ya taasisi zikitoa fedha za kusaidia hilo ili iweze kumkomboa mwanadamu dhidi ya ugonjwa huu katili na kwa bahati mbaya watu masikini ndio waonateseka zaidi na ugonjwa huu kuliko watu matajiri.

Unyanyapaa katika jamiiWatanzania hapo awali walikuwa wa-naogopa mambo mbalimbali ambayo pengine yalikuwa kweli au la, math-alani imani za kishirikina na mambo mengine. Ninakumbuka kuwa mion-

goni mwa jambo lililogusa imani za watu ni suala la mumiani ambayo ili-kuwa ni imani juu ya watu waliokuwa wakiwakamata binadamu wenzao na kuwanyonya damu zao na kuwaacha wakiwa wafu na kazi hiyo iliwapatia kipato kikubwa sana kulingana na wale waliotoa simulizi hizo.

Jambo hili ambalo kwa hakika halina ukweli juu ya biashara ya damu ya binadamu lakini jamii iliamini hivyo na kila mtu aliyeonekana kuwa na kipato aliaminika kuwa alipata fedha hizo kwa biashara hiyo iliyohusika na kuwatoa roho binadamu wenzake. Kwa hakika yote hiyo ilikuwa ni uvumi tu usio na ukweli wowote huku watu wakikimbia mara waonapo magari ya taasisi kama vile Msalaba Mwekundi wakiaminika kuwa ni mumiani.

“Hilo kaka lilikuwa linafanywa lakini biashara hiyo ilimalizika kabisa kutokana na kuwepo na magonjwa kama UKIMWI ambayo yametia shubiri biashara ya wanyonya damu.” Anasema Jumanne Makaya ambaye ni mkazi wa kijiji cha Kiwere Mkoani Iringa.

Hiyo ni imani tu ambayo hakuna ukweli wowote juu ya hili, ninaweza kusema kuwa ni kama ilivyo leo hii ambapo jamii zetu zimekuwa na desturi za kuhisi kuwa fulani anaugua

ugonjwa wa UKIMWI na kumfanyia unyanyapaa wakati hakuna vipimo vya kitabibu vilivyothibitisha kuwa fulani ni mgonjwa wa UKIMWI.

Dk Christian Maembe ni tabibu wa muda mrefu ambaye amefanya kazi hiyo katika Hospitali ya Temeke na Sasa yupo nchini Sierra Leone katika mojawapo ya operesheni za Umoja wa Mataifa anasema kuwa suala la afya ni jambo la msingi ambalo linahitaji mno kutumia vipimo vya kitabibu kutambua kuwa mtu fulani ni mgonjwa au la.

“Katika tiba hakuna ramli ni vipimo tu ndugu mwandishi, unatoa damu na inapimwa na vipimo viwili au zaidi ya vitatu kama UKIMWI unapimwa kwa viipimo vya Kapilali na Elisa kujua kuwa mtu fulani ni mgonjwa au siyo na kujua fulani anaumwa au la ni suala la mtu mwenyewe na tabibu.” anasema Daktari Maembe.

Kupatikana kwa kinga nchiniKubwa ambalo limenitia nguvu kuandika makala haya katika toleo hili la Pambazuko ni juu ya jitahada kubwa zilizofanywa na Jopo la Madaktari wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) sasa wameweza kukamilisha uchunguzi juu ya chanjo ya ugonjwa huu. Utafiti uliofanyika nchini kwetu unaonyesha kwamba chanjo hiyo mpya inaweza kuzuia mwanadamu asipatwe na virusi vya UKIMWI kwa asilimia 100.

Chanjo hiyo mpya inayojulikana kwa kifupi DNA-MVA ambapo inaungana na chanjo nyingine duniani kama TRUVADA na nyingine nyingi kuweza kumsaidia mwanadamu asiyeambukizwa kukwepa kabisa kupata ugonjwa huo hata kama atashiriki katika mazingira hatarishi. Walioshiriki katika utafiti huu wamesema bayana kuwa chanjo ya DNA-MVA inaweza kuufanya mwili kutengeneza kinga yake mwilini dhidi ya Virusi vya UKIMWI –VVU.

MAKALA

Mwananchi akitolewa damu kwa hiari kujua hali yake katika mojawapo ya vituo vya kupimia UKIMWI.

Endelea Uk wa 15

15Pambazuko Na. 41 Toleo la Januari - Machi 2013

MAKALA

Utafiti huu uliokuja na kinga hii ulianza rasmi mwaka 2007 na kumaliza kazi yake 2012 ukifanyika katika hatua tafauti, yaani hatua ya mwanzo ilikuwa ni mwaka 2007-2010 yaani kwa kipindi cha miaka mitatu. Utafiti wa mwanzo ulipachikwa jina la HIVS-03 na watafiti hao wa tiba, ambapo uliwahusisha Jeshila Polisi na Magereza na raia 60 kutoka jiji la Dar es Salaam kwa kuwapa chanjo hii na kuwaruhusu kuishi maisha yao ya kawaida kwa kipindi cha miaka mitano.

“Chanjo hii ya DNA-MVA ambayo tuliwapa askari hao, ilikuwa salama na yenye uwezo mkubwa ya kuufanya mwili ujitengenezee kinga dhidi ya virusi vya UKIMWI,” alisema kwa kujinasibu Profesa Muhammad Bakari ambaye ndiye aliyeongoza jopo la madaktari walioshiriki katika kufanya utafiti huo.

Profesa Bakari ameongeza utafiti huo umeonyesha kuwa chanjo hiyo inasaidia mwili kutengeneza vichocheo vya kinga dhidi ya VVU kwa asilimia 100 kwa washiriki wote waliopata chanjo na haya ni matokeo mazuri na ya kujipongeza na yalipita hata matarajio ya watafiti kwa kuwa kama hawakutarajia ungeweza kuifikia asilimia 100.

Profesa huyo aliweka bayana kuwa hakuna mtu hata mmoja aliyeshiriki katika utafiti huo aliyepata athari za moja kwa moja kutokana na chanjo hiyo wala kufa kutokana na tatizo hilo la kushiriki katika utafiti huu.

MUHAS iliweka wazi kuwa walioshiriki katika utafiti huo walijitolea kwa hiari yao wenyewe wala hakukuwa na shurti huku ikiwapongeza askari hao na raia wengine waliojitokeza katika utafiti huo, ambapo jopo la matabibu liliendelea na utafiti huo mwaka 2008 na kumaliza rasmi kazi yao na kufunga kitabu cha utafiti mwaka 2012 na kubaini mafanikio hayo. Kwa hakika ni mafanikio ya kila mmoja wetu awe mkulima au mfanyakazi.

Katika hatua ya pili jopo la matabibu wa Tanzania na Msumbiji walijikita kutafuta chanjo ya ugonjwa huo, ili kuweza kuja na chanjo sahihi ya virusi hivi na walikuja na chanjo

ijulikanayo TAMOVAC01 yaani (Tanzania and Mozambique HIV Vaccine Program).

MUHAS ilisema bayana kuwa utafiti wao ulishirikisha watu 120 ambapo 60 walitokea katika jiji la Dar es Salaam ambapo pia Jeshi la Polisi , Magereza na raia walishiriki katika hatua hii ya pili ambapo watu wengine 60 wakitokea Mkoa wa Mbeya. Hapa pia utafiti huu ulibainisha kuwa mchanganyiko wa DNA-MVA ulikuwa salama kabisa kwa matumizi ya kinga kwa binadamu.

MUHAS imesema bayana kuwa mchanganyiko huo wa matokeo ya awali yaani DNA-MVA unaweza kutolewa kwa binadamu katika dozi ndogo ndogo na bila vinasaba vyote kuwa katika mchanganyiko mmoja, lakini MUHAS imeongeza kuwa utafiti juu ya mchanganyiko huo bado unaendelea.

Changamoto katika utafiti waoKila panapofanyika utafiti pamekuwepo na changanmoto nyingi MUHAS imesema kuwa katika utafiti wao kulikuwa na dhana kuwa washiriki walikuwa wanapandikizwa virusi vya UKIMWI wakati haikuwa kweli, jambo hili lilikuwa ni changamoto kubwa kwa wale waliotamani kushiriki katika ufatiti huo lakini kwa uwazi na ukweli kabisa washiriki hawakuwa wakipandikizwa virusi vya VVU kama ilivyokuwa ikivumishwa.

“Hii si kweli kabisa kwani suala hilo linatokana na uelewa mdogo wa jamii zetu juu ya masuala ya tiba. Hii ilikuwa ni changamoto kubwa kuhusu utafiti huu mtu apandikizwe virusi vya UKIMWI kwa nini MUHAS ifanye hivyo, ukweli ni kuwa washiriki walipewa chanjo dhidi ya VVU,” alisisitiza Profesa Bakari. MUHAS ilienda mbali zaidi na kubaini kuwa hakukuwa na mshiriki hata mmoja ambaye aliambukizwa virusi vya UKIMWI kutokana na kupewa chanjo hiyo

Kila panapofanyika tafiti yoyote pesa zinahitajika kufanikisha hilo na gharama zinakuwa kubwa hasa pale

unapo muhusisha banadamu katika masuala ya tiba ambapo umakini mkubwa unatakiwa kufanyika ili kuweza kuepuka athari zozote zinazoweza kutokea katika utafiti huo. MUHAS imesema kuwa gharama kubwa imetumika hasa kwa msaada kutoka Jumuiya ya Ulaya na serikali ya Swideni.

Akifafanua juu ya ufadhili wa chanjo hiyo MUHAS imesema kuwa kwa chanjo ya TAMOVAC-01 na ya pili ya TAMOVAC 2 umefadhiliwa na taasisi ya ushirikiano wa utafiti za Kisanyansi kati ya nchi za Ulaya na nchi zinazoendelea (Europeanand

Developing Countries Clinical Trials Partnership(EDCTP). Katika kufanikisha hilo jopo la matabibu bingwa yalishiriki katika kufanikisha mafanikio yanapatikana katika utafiti huo, huku vyuo vikuu vya Ujerumani na Uingereza navyo vikishiriki kwa karibu.

Washiriki wengine ni Taasisi ya Utafiti wa Tiba ya Mbeya (MMRP), Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Tiba ya(NIMR), Hospitali Kuu ya Tiba ya Maputo Msumbiji, Jeshi la Polisi na Magereza, Tanzania na wananchi wa Tanzania pamoja na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH).MUHAS inaendelea na utafiti zaidi ili kuweza kukamilisha utafiti wao ambapo utawahusisha watu 80 wote kutoka jiji la Dar es Salaam na Mbeya na washiriki wengine 38 kutoka jiji la Maputo nchini Msumbiji. MUHAS im-ewataja walioshiriki katika utafiti ni aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo MUHAS Profesa Kisali Pallangyo, Profesa Eligius Lyamuya ambaye ni mratibu wa MUHAS, na pia ni mra-tibu wa kinga ya magonjwa yanayosa-bishwa na Virusi, Profesa Fred Mhalu.

Inatoka uk. wa 14

“Chanjo hii ya DNA-MVA ambayo

tuliwapa askari hao, ilikuwa salama na yenye uwezo mkubwa ya kuufanya mwili ujitengenezee kinga

dhidi ya virusi vya UKIMWI.”

16 Pambazuko Na. 41 Toleo la Januari - Machi 2013

Mfumo upi wa ununuzi wa korosho utakaomnufaisha mkulima?

kwa siku nzima na jukumu hili linategemea mno kiasi cha korosho zinazobanguliwa, katika kila kilo moja ya korosho zisizobanguliwa, mkulima hupata robo kilo kama atazibangua mwenyewe baada ya kuzichoma. Lakini upatikanaji wa korosho zilizobanguliwa unatengemea mno na uchomaji wake.

“Kuna suala la wabanguaji wengine kubangua vibaya na hasara za wabanguaji wengine kula korosho nyingi wakati wa kazi. Hilo linaweza kuwa tatizo kubwa na kumletea hasara mkulima,” anasema Hamisi Mwinchuke.

Lakini ikumbukwe kuwa kubangua korosho kwa mkulima mwenyewe nyumbani kunapoteza malighafi nyingi na hivyo kushusha thamani ya zao husika/hilo tofauti na kama zitabanguliwa kiwandani

Njia ya tatu ya kuuza korosho ni kupitia vyama vya ushirika ambapo huzinunua, kulingana na utaratibu wa eneo husika. Katika Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani nilidokez-wa kuwa kuna chama cha ushirika kilichopo katika kijiji cha Kimanzicha-na ambacho kinanunua korosho za wakulima hao kila mwaka.

Huku malipo yanatolewa mara baada ya ununuzi yakiwa

katika awamu tatu. Katika awamu ya kwanza wakulima wa zao hili wanapewa shilingi 200 kwa kilo. Bei hiyo ya korosho ya mkoa wa Pwani inatafautiana mno na bei ya korosho katika mikoa mingine ambayo inalima zao hilo.

“Wenzetu wa Mtwara bei ya korosho inatia moyo kuliko sisi kwani mwaka uliopita japokuwa walilipwa kwa awamu nimeona malipo ya kilo moja yalikaribia shilingi 2000 na kwa awamu tatu mkulima amepata shilingi 600 ambapo kwa sisi hiyo ni kwa awamu zote tatu,”Jacob Kilindo ambaye ni mkulima wa korosho aliyevunjika moyo kulima zao hili alilamika.

Japokuwa wakulima wa mkoa wa Pwani wanaona kuwa wakulima wenzao wa korosho wa Mtwara wanauza kwa bei bora lakini nako Mtwara kilio cha bei kipo na ndiyo maana hivi karibuni kuliibuka malalamiko na vurugu juu ya bei hiyo kuwa ndogo lakini bei ya korosho ya Pwani ni ndogo mno ama kweli ukiona kwako kunawaka tambua kwa mwenzako kunateketea.

Mkorosho ni mti ulio kijani nyakati zote, hufikia urefu wa mita 10 – 12; na shina fupi lisilo na umbo maalum.

KUTOKA MITANDAONI

Huu ni miongoni mwa mikorosho iliyokatwa Wilayani Mkuranga, Mkoani Pwani. (Picha na Adeladius Makwega.)

Adeladius Makwega, Mkuranga

“Nimekuwa ninalima mikorosho kwa muda mrefu lakini kwa misimu miwili nimekosa mapato kabisa, mfano mwaka 2011 korosho zangu zilikamatwa na askari tuliambiwa tunasafirisha nje ya mkoa wa Pwani kimakosa, zikataifishwa. Mwaka 2012 niliuza kwenye mfumo wa stakabadhi ghalani lakini nilipata pesa kidogo,” anasimulia kwa masikitiko Hamisi Mwinchuke mkulima wa zao la korosho huko Mwarusembe, Mkuranga Pwani.

Ndugu Mwinchuke ni miongoni mwa wakulima wengi wa zao la koro-sho ambalo linapatikana katika ukan-da wa Pwani hasa katika mikoa ya Pwani, Tanga, Lindi na Dar es Salaam.

Mti huu ni mmea wa jamii ya mimea itoayo maua ya familia ya Anacardiacea wa asili ya huko kaska-zini mashariki mwa Brazili. Jina lake la kiingereza cashew likitokana na neno la Kireno ambalo lina asili ya Tupi.

Japokuwa mkorosho unastawi katika ukanda huo, ufanano wa hali ya hewa na kustawi kwake hakulingani kabisa na bei ya zao hilo, huku wakulima wa Pwani ambapo ni mkoa ulio jrani na Dar es Salaam wakiwa na kilio cha bei kuwa ndogo na wakulima wa mikoa ya kusini wakilalamikia bei hiyo hiyo ambayo kwao ni nafuu kidogo.

“Sisi tumekuwa tunauza korosho kwa njia mbili kwanza kwa kuuza korosho zisizobanguliwa kwa wanunuzi wa rejareja na hapa ndipo tunaweza kupata pesa za kununua mahitaji yetu madogomadogo. Kwa mwaka 2011 niliwahi kuuza kilo hadi shilingi 500 na njia ya pili tunauza korosho mara baada ya kuzichoma na kuzibangua kilo shilingi 7000 ” anasimulia Ndugu Mwichuke.

Kuuza korosho zilizobanguliwa mkulima analo jukumu la kuzikaanga na kuzibangua ambapo watu wanaopewa jukumu la kubangua hulipwa kati ya shilingi 2000-3000

Endelea Uk wa 17

17Pambazuko Na. 41 Toleo la Januari - Machi 2013

Endelea Uk wa 22

KUTOKA MITANDAONI

Majani yamejipanga kwa mzunguko yenye asili ya ngozi na urefu wa sentimeta 22 na upana wa sentimeta kati ya 2-15. Maua laini huzalishwa yakiwa na urefu wa sentimeta 26, na huanza na rangi nyepesi ya kijani mwanzoni lakini baadae hugeuka na kuwa jekundu na petali zenye urefu takribani milimeta 7 mpaka 15. Tunda la korosho huitwa bibo na huwa na ladha tamu lenye urefu kati ya sentimeta 5 hadi 11. Tunda halisi la korosho ni korosho yenyewe. Huunza kuzaa baada ya kutimiza miaka mitano hadi kutimiza miaka saba hapo huzidi kuzaa zaidi.

“Mwandishi! Kama unavyoona visiki hivyo vyote ni vya mikorosho, watu wamekata na kuchoma mkaa na kupanda miembe hii ya muda mfupi .” Jacob Kilindo alimuonyesha mwandishi wa makala haya maeneo yaliyoathirika zaidi katika Kitongoji la Uzini huko Kiziko Mkuranga.

Suala la bei ya zao hili limekuwa shubiri kubwa kwani kwa hakika hata gharama za kulitunza shamba zinakuwa kubwa mno pale unapolinganisha na kile mkulima anachokipata baada ya mauzo.

“Wenzetu wa Mtwara mafanikio hayo si ya kusimuliwa kama hadithi tu bali mengine ni ya kuona kwa macho yangu kwa wale waku-lima wa korosho ambao nina na-saba nao huko Mtwara, wengine hadi wananunua magari ya mizigo,” anasema Maria Kasapa mkulima wa korosho Kijiji cha Mwanadilatu Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani. Bi Maria anasema kuwa kwa desturi ya majira ya mkoa wa Pwani mara zote korosho zake huanza kuokot-wa mwishoni mwa mwezi wa 10 na uokotaji huo uongezeka na ku-malizika mwezi wa 12 nako huko Mt-wara wanaanza kuokota korosho hizo kuanzia mwishoni mwa mwezi wa tisa na mwezi wa 10 msimu unakuwa umepamba moto kweli kweli, mwezi wa kumi na moja kazi ya kuokota huwa imemalizika.

Suala la upishanaji wa mwezi mmoja baina ya mikoa hiyo lingekuwa ni jambo la msingi sana kuweza kusaidia kupatikana kwa wateja wa zao hilo na pengine

mkulima kuweza kuwa katika nafasi nzuri ya kuuza korosho zake kwa bei atakayo.

Wataalamu wa mazao wanasema bayana kuwa korosho za Mkuranga zina mapungufu kwa kuwa na mu-onekana mbaya lakini zina sifa moja kubwa kuwa korosho zake zikiban-guliwa huwa na korosho iliyojaa mno. Wakati korosho ya Lindi na Mtwara yenyewe ina muonekano mzuri lakini korosho yake si nzuri sana ndani.

Kwa hakika kuna kila sababu ya korosho ya Mkuranga kupata soko na kuuzwa kwa kila msimu huku mkulima akinufaika na hilo. Malalamiko ya bei ya zao hili kwa mwaka huu yalijibiwa na Bi Mwan-tumu Mahiza ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani kwa kutoa aha-di ya kuwashungulikia wale walioku-la pesa za wakulima waliouza ko-rosho kwa stakabadhi ghalani.

Lakini juhudi hizo zinakuja wakati mbaya kwani sasa wakulima hao wanahitaji pesa za kupalilia mashamba, pesa za kuweka dawa na hata pesa kwa ajili ya matumizi yao mathalani ada za watoto wao waliopo masomoni.

Swali la kujiuliza je ni sahihi kwa wakulima hao kuikata mkorosho hiyo na kupanda miembe? Wakulima wenyewe wanaweka wazi kuwa kwa kukata mikorosho hiyo wanajipatia kipato cha kuuza kuni maeneo jirani ya Mkuranga mathalani Dar es Salaam kwa matumizi mbalimbali. Magogo makubwa ya mti huo yamekuwa yanatumika kwa kuchomwa mkaa ambapo katika mikorosho mikubwa mitatu hadi zaidi panaweza kuchomwa tanuri kubwa la mkaa ambapo mkulima hujipatia hadi shilingi 1,500,000.

“Mkaa Dar es salaam ni biashara kubwa gunia linafika hadi elfu 50 ambazo zinatumika kununulia miti ya miembe na kutayarisha mashamba kwa ajili ya miembe hiyo kupandwa, zinazobaki natumia kwa matumizi mengine,” anasema Ali Kumbirwa mkulima katika kijiji cha Vikindu.

Hali ya ukataji wa mikorosho hiyo inasababishwa na suala la bei ya zao hilo kuwa chini na pia suala la kuwepo na uhitaji mkubwa wa miti ya kutengeneza mkaa na kuni kwa

jiji la Dar es Salaam ambapo tani nyingi zinahitajika.

Mkulma Hamisi Mwinchukwe anasema kuwa kwa hakika kilimo cha mikorosho kwa sasa ni wakulima wachache ndio wanaopanda miti mipya ya mikorosho na hata miti ile inayokatwa kwa hakika ni ya vizazi vingi unaweza kusema ni vizazi zaidi ya vitatu.

“Mimi shamba hili niligawiwa urithi na baba lakini hata baba yangu yeye anasema alikuta babu yake analima kitambo na yeye ndiyo ali-yopanda miche mingi ya mikorosho hii,”aliongeza ndugu Mwinchuke.

Mkulima huyo ambaye anamilika heka zaidi ya 20 za mikorosho anasema kwa hakika yeye anayo heka moja tu ndiyo ameipanda miaka 10 iliyopita tena kwa kupata shinikizo kutoka kwa baba yake.

Katika kijiji cha Mwanadilatu takwimu zinaonysha kuwa katika Kitongoji cha Langweni mwaka 1980 kulikuwa na miti ya mikorosho 3897 lakini mika 2010 takwimu hizo zikaonyesha kuwa sasa kuna miche ya mikorosho 1789 ndiyo kusema kuwa sababu za kukata mikorosho kwa miaka ya sasa ni kwa kujenga makazi ya kuishi binadamu na uchomaji wa mkaa.

Hamisi Pazi ambaye ni mwenyekiti wa Kitongojo hicho anasema ni kweli mikorosho imepungua sana maana faida yake sasa imekuwa ndogo na kumekosekana ushawishi wa wakulima kuthamini zao hilo.

“Miaka ya 1980 nilikuwa naweza kuokota korosho kilo kati nne hadi tano kwa mti mmoja. Lakini mwaka jana kwa siku hata kilo moja kuifikisha ni kazi,” anasema mwenyekiti Pazi;

Iddi langweni ambaye na yeye ni mkulima wa korosho anasema yeye alikuwa na eneo kubwa la mikorosho lakini kwa sasa hakuna jitihada zozote zinazofanywa hasa kutolewa kwa elimu ya kilimo cha korosho na pia bei ya dawa za kunyunyuzia ni ya juu mno ambapo heka moja ni zaidi ya 60,000/-

“Mie nitatoa wapi fedha hizo nimekata na kuibakiza michache ambayo ipo jirani nyumbani kwa

Inatoka uk. wa 16

18 Pambazuko Na. 41 Toleo la Januari - Machi 2013

Namna ya kutayarisha chakula cha kuku kwa malighafi rahisi

Watoto wakilisha kuku chakula.

Adeladius Makwega, Morogoro

KUENDELEA kwa mradi wa ufugaji kuku na kukua kwa kipato cha jamii

zinazojihusisha na ufugaji wa kuku vijijini kunategemea ubora wa kuku na mazao yanayozalishwa pamoja na soko zuri. Mahitaji ya kuku na mayai ya asili yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku kutokana na ladha yake kuwa nzuri na pamoja na uhalisia wake. Hii ni sababu ya msingi inayoshawishi baadhi ya waliyoitambua na kuichangamkia fursa hii kufanikiwa mno.

Pamoja na kuwepo kwa fursa hizo bado zipo changamoto nyingi katika eneo la soko la mazao ya kuku wa asili. Changamoto hizi zinamfanya mfugaji asinufaike kiasi cha kuridhisha kutokana na ufugaji wake.

Kumekuwa na wakulima wengi ambao wanalima mazao mbalimbali huku wakifuga kuku kwa matumizi ya chakula tu lakini kwa sasa wafugaji wa kuku kibiashara wameongezeka, na suala hili limesaidia mno kuwapa kipato kikubwa na kuweza kusonga mbele kwa kuweza kupata mahitaji yao ya kila siku mathalani karo za

watoto wao.

Bibi FaridaNiliamua kumtembelea mfugaji wa kuku wa kienyeji Bibi Farida Afande ambaye ni maarufu kama Afande Farida ambaye anafuga kuku wa kienyeji 450 na bata 200 ambapo kwa siku amekuwa akijiingizia kipato cha shilingi elfu 50, zinamsaidia mno na sasa ametoka katika hali duni na kuwa katika hali bora zaidi kwa kuuza mayai ya kuku na bata.

Nilipanda gari kuelekea Lushoto Utondolo jirani kabisa na mji mdogo wa Lushoto na kukaribishwa na milio mingi ya ndege nikizani kuwa hao ni nzige kumbe ilikuwa ni milio ya ndege hao ambapo kuku na bata walikuwepo katika mojawapo ya mabanda makubwa yaliyojengwa kwa kutumia miti na kuezekwa kwa mabati ya zamani.

Unapomtembelea Afande Farida mfugaji kuku ambaye alipajichikwa jina la Afande kutokana na ufugaji huo wa kuku anaojishughulisha nao siku nzima kwa kuwahudumia kuku hao ili kuweza kukua vizuri, ninaamini utavutiwa sana na hata kutamani nawe uanze kufuga siku inayofuata.

Bibi Farida alinidokeza kuwa amewagawa kuku na bata wake

katika madaraja kulingana na muda waliototolewa hivyo kuna banda la vifaranga na banda la kuku na bata wakubwa huku akiwatenga baadhi ya kuku na bata ambao ni wakorofi ambapo wanaweza kuwaumiza kuku au bata wengine katika mabanda maalumu.

Joto la vifarangaTuliingia katika banda la vifaranga ambapo hapo tulikaribishwa na vifaranga vingi ambavyo vilivyokuwa na milio midogo ambayo kwa hakika vililipamba banda hilo mithili ya maji yalikuwa yanatiririka mtoni. Banda ili lilikuwa limejengwa kwa hali nzuri kuweza kuzuia wanyama na wadudu kuingia ndani ya banda hilo huku kukiwa na jiko dogo la mkaa ambalo lilitumika kuwapa joto.

“Jiko la mkaa tunalitumia sana kusaidia kuwapa joto vifaranga, mara nyingi ni vigumu kuweza kuwalea mara baada ya mayai kuanguliwa basi ninawachukua na kuwaweka katika banda maalumu la vifaranga, vinginevyo wanaweza kufa,” anasisitiza Bi Farida.

Jiko hilo ameliweka juu ya matofari kuepusha vifaranga wasiliguse likiwa limefungwa vizuri kwa nyaya ngumu za chuma kwani anasema mwanzo alikuwa akiliweka chini likasababisha vifaranga zaidi 20 kufa kwa moto wa mkaa huo.

Pia alidokeza kuwa mkaa una hewa ya ukaa ambayo ni sumu kwa viumbe hai ni jambo la msingi kuhakikisha kuwa mkaa umekolea kabisa na kuzuia moshi kuwepo bandani.

Chakula bora cha vifarangaVyakula vya vifaranga hivyo viliwekwa katika vyombo maalumu vya gharama nafuu kabisa kutoka katika vyombo vyake vya zamani vya nyumbani vilionekana vikiwa vimejaa pumba za mahindi huku kukiwa na punje za mtama ambapo alikuwa

MAKALA YA KITAALAMU

Endelea Uk wa 19

19Pambazuko Na. 41 Toleo la Januari - Machi 2013

Chickens_eating

ndiyo kwanza anazimimina katika vifaa hivyo.

Mara baada ya kuona vyakula vya mifugo yake vya mama huyu, nilivutiwa mno kutaka kujua suala la chakula bora kama mifugo kama kuku na bata lipo. Maana tumekuwa tukijulishwa kuwa binadamu anatakiwa kula vyakula vyenye vitamini, madini wanga na protini , Je vipi kwa kuku na bata hawa?

Nilisogea kando na Bibi Farida alinipa kigoda na kuanza kunipa elimu juu vyakula vya kuwaapa virutubisho mbalimbali kwa kuku na bata.

“Baba ili vifaranga wawe na afya nzuri na akue upesi anahitaji chakula maalumu. Chukula hicho ni mchanganyiko wa viini lishe mbali mbali na kila kiini lishe lazima kiwe katika kiwango sahihi kulingana na mwili wa kifaranga, viini lishe anavyohitaji ni Wanga Protini, Madini, Mafuta, Vitamini na Maji.”

Mchanganyiko sahihi wa viini lishe kwa kifaranga humwezesha kukarabati na kujenga mwili na kukua kwa haraka. Viini lishe vya wanga protini, madini, vitamini na maji hupatikana katika aina mbalimbali za viungo ghafi vya vyakula vya kuku.

Bibi Farida alinidokeza kuwa kwa kuwa yeye hana uwezo wa kwenda kununua vyakula vya madukani anachanganya chakula cha kuku wake yeye mwenyewe kwa kufuata utaratibu huo wa kitaalamu. Mathalani wanga unapatikana katika pumba, chenga au dona ya nafaka kama mahindi au serena. Pia

Mafuta hupatikana katika mbegu kama karanga au alizeti. Mbegu hizi zikikamuliwa mashudu yake hubaki na kiasi fulani cha mafuta. Haya hutumika kulisha mifugo mbalimbali.

Kwa protini nayo hupatikana katika mashudu ya karanga au alizeti, dagaa, damu ya wanyama kama ng’ombe na mbuzi. Damu hiyo inaweza kuipata machinjioni. Mfugaji huyo wa kuku wa Lushoto alinidokeza kuwa damu ya wanyama inaweza kuchanganywa ikiwa mbichi na pumba katika ndoo au chombo chochote kilicho wazi upande mmoja. Vuruga mchanganyiko huo kwa kipande cha mti, halafu fikicha kwa viganja ili kuondoa mabonge. Sambaza mchanganyiko huu juu ya bati au paa halafu anika juani mpaka ukauke kikamlifu.

Unapolisha damu kuwa makini “Lakini katika kulisha kuku au bata damu ni jambo la hatari kama ukianza kuwalisha mchanganyiko huo unatakiwa kuendelea nao kwa muda wote vinginenyo kuku watadonoana na kuwa vidonda na wengine kufa kwa hali hiyo,” Alisisitiza mama huyu na kuongeza kuwa protini inapatikana pia katika unga wa mbegu za jamii kunde kama vile maharage, kunde zenyewe na soya.

Kama alivyo binadamu, na kuku pia wanahitaji madini yanayojulikana kama kalshiam na fosforasi ambayo hupatikana katika unga wa dagaa na

mifupa ya wanyama iliyochomwa na chokaa maalum ya kuku ipatikanayo katika maduka ya pemebejeo za kilimo, chumvi, hata na majivu ya kawaida ya jikoni.

Mifupa hiyo ili kuiandaa unatakiwa kuichoma moto mara baada ya kuchanganywa na chumvi alafu unaisaga na kupata unga unga ambapo unachanganywa na vyakula vingine kuwa chakula cha kuku na bata wako. Pia vitamini hupatikana kwenye majani mabichi ya mpapai, mchicha wa nyumbani au porini na hata katika mimea ya amii ya

mikunde pia.Bibi farida alimaliza kunitajia

madaraja hayo ya virutubisho kwa kuku wake, alinidokeza kuwa kuku mmoja mkubwa wakati wa sikukuu ni kati ya shilingi 10,000 na 20,000/-, wakati bata dume huuzwa kati ya shilingi 20,000 na 30,000/-.

Hii ni neema kubwa sana kwa mfugaji wa kuku na bata, kama mkulima haujaanza kufuga kuku na bata ni bora ukaanza sasa ili kujiongezea kipato.

Bibi Fatuma alimalizia utayarishaji wa chakula cha mifugo yake kwa kunidokeza kuwa suala la msingi ni kuwepo na usafi wa hali ya juu, uchaguzi mzuri wa chakula hicho pia alibainisha kuwa ni muhimu pawepo na vyombo maalumu vya kutayarisha chakula kwa kuku na bata vikiwa vinatunzwa vizuri. Akaongeza kuwa punje zote mara baada ya kusangwa ni jambo zuri kuwa na umbo ambalo kuku na bata wanaweza kuzila kwa wepesi zisiwe punje kubwa kubwa.

Basi usikose toleo lijalo tukiendelea kumsikiliza Bi Farida Afande ambaye ni mfugaji wa kuku na bata huko Tanga.

Inatoka uk. wa 18

MAKALA YA KITAALAMU

Kuku mmoja mkubwa

wakati wa sikukuu ni kati ya shilingi 10,000 na 20,000/-, wakati bata dume huuzwa kati ya shilingi

20,000 na 30,000/-.

20 Pambazuko Na. 41 Toleo la Januari - Machi 2013

MAKALA

Hukumu ya Kifo kutolewa majibu yake katika katiba mpya?

Adeladius Makwega

WAKATI mchakato wa utayarishaji wa katiba mpya

ukisonga,kumekuwa na maoni mengi juu ya masuala mbalimbali yanayoigusa jamii ya Tanzania kwa nia moja tu ya kuhakikisha katiba mpya itakayopatikana inatoa majibu ya mambo hayo, moja ya jambo kubwa ni suala la hukumu ya Kifo.

Hukumu ya kifo ni miongoni mwa hukumu nyingi mbaya na za kudhalilisha utu wa binadamu zinazotumiwa kwa kipindi kirefu katika nchi kadhaa za Afrika na dunia kwa ujumla. Mara nyingi watu wanaothibitika kuuwa, kufanya uhaini au mapinduzi na makosa mengine yenye kulingana na hayo hupatiwa hukumu ya kunyongwa.

Katika kuitazama hukumu kunaweza kuwepo kwa mitazamo mingi ambayo kwa wale wanaojali uhai wabinadamu wanakasirishwa sana kuona nchi na baadhi ya watu wakiendelea kuitumia huku wakijidai kuwa inatumika kulinda uhai wa watu wengine. Hii inaweza kuwa kweli lakini uhai wa binadamu yeyote ni vema kuheshimiwa sana.

Sera ya jino kwa jinoKwa watu wanaoiunga mkono hukumu hii wanasema kama mtu aliyemuuwa mwezake kwa kukusudia basi na yeye anatakiwa kupotezewa uhai wake bila ya huruma kama yeye alivyofanya, yaani Jino kwa Jino .

Historia inaonesha kuwa maeneo mbalimbali yalikuwa yakitumia hukumu hii mfano katika mkoa wa Iringa kuna eneo liitwalo Kitanzini ambalo lilikuwa ni sehemu ya kunyongea watu waliokuwa wakifanya makosa ambayo yaliitwa makubwa sana wakati wa ukoloni wa Mwingereza na Mjerumani.

Hii ni kwa upande wa mkoa wa Iringa, nako Uchagani mtu aliyefanya

mauwaji aliweza kupewa hukumu ya kulipa kiasi fulani cha gharama na baadae kuchinja mbuzi au ng’ombe ili kuondoa nuksi hiyo na chakula kililiwa kwa pamoja wa ndugu waliofiwa na jamaa yao na wale wa yule aliyefanya kosa. Hali hii iliweza kuondoa chuki kwa pande hizo na kuweka maelewano.

Katika maisha ya kawaida viji-jini makosa ya mauwaji yamekuwa yakifanyika pale watu wanapogombea ardhi, chuki na wivu wa kimapenzi na wakati mwingine katika matukio ya ujambazi na wizi wa mifugo na hivi sasa kumekuwa na kesi ya mauwaji yakiwahusisha polisi na wanajeshi wakiwa wanatekeleza majukumu yao.

Idadi ya walionyongwaTaarifa juu ya idadi ya walikwisha kuhukumiwa kifo na kutekelezwa iliwahi kutajwa Bungeni katika Bunge tukufu la Tanzania kuwa maraisi wetu waliotangulia waliweza kunyonga watu zaidi ya 82 katika vipindi vyao vya utawala. Inasemekana watu 72 walinyongwa wakati wa Mzee Ali Hassani Mwinyi na watu 10 kipindi cha Mwalimu Julius Nyerere.

Kuna minong’ono mingi miongoni mwa Watanzania kuwa takwimu hiyo iliyotolewa inaweza kuwa ni ndogo

kwani inawezaka kuwa kubwa zaidi kwani serikali inatabia ya kupunguza takwimu ya mambo ya kuhudhunisha ili kupunguza mtazamo hasi miongoni mwa wananchi.

Neema Chussi ambaye ni miongoni mwa waalijiliwa katika idara ya mahakama aliwahi kufanya utafiti wake juu ya hili mwaka 2002 kuhusu hukumu ya kifo nchini na anasema;

“watu wengi wanachukizwa na hukumu hii hata kama aliyefanya kosa alifanya kwa makusudi ama laa. Na sehemu mbalimbali ambazo watuhumiwa wa mauwaji walitiwa hatiani na kunyongwa, wakazi wengi walipata hasira na kuweza kujenga chuki kwa serikali.”

Kesi ya mkulima wa Mkungugu, Mkoani IringaMtaalamu huyu ambaye ni mwanasheria anasema katika kijiji cha Mkungugu mkoani Iringa ambapo Said Abdalla Mwamwindi alitiwa hatiani na kuhukumiwa kifo, wakazi wengi walihudhunika sana baada ya kupata tetesi za kunyongwa kwa kwake.

Ikumbukwe kuwa Said Abdalla Mwamwindi ambaye alikuwa mkulima Mkoani Iringa aliingia hatiani kwa mauwaji ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa wa wakati huo Dr Wilberd Klerruu siku ya krismasi mwaka 1971.

Inadaiwa kuwa tatizo kubwa lilikuwa ni mgogoro juu wa ardhi ambapo serikali ilitaka wananchi kutoa ardhi yao katika mashamba ya ujamaa na wananchi kutumia muda wao mwingi katika mashamba ya ujamaa kinyume cha matakwa ya serikali.

Kuna visa vingi na kesi nyingi za namna hii lakini hivi karibuni tumeshuhudia wakulima wakiuwawa na wafugaji mathalani kifo cha Mkulima Shaaban Msambaa huko Kilosa Mkoani Morogoro katika Mgogoro wa ardhi, hali kama ambayo inasababisha wahusika kutiwa hatiani

Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ambaye katika kipindi chake alisisitiza kuwa Uhai ni haki ya kila binadamu.

Endelea Uk wa 21

21Pambazuko Na. 41 Toleo la Januari - Machi 2013

MAKALA

na kuhukumiwa kifo.Katika mahojiano na kiongozi

mmoja wa dini ambaye hakutaka jina lake kuandikwa gazetini alijaribu kuhoji maswali kadhaa kuhusu hukumu hii. Alijiuliza kuwa kama hukumu hii ni haki mbona haifanywi hadharani? Akaendelea kuuliza kuwa kama idadi ya Watanzania walionyongwa tangu uhuru ni 82 hao Watanzania wafanyao kazi hii magerezani wanaweza kujitambulisha hadharani kuwa waliajiriwa kwa kazi hiyo?

“Ni vigumu kabisa kusema kuwa yeye alifanya kazi hiyo kwani nafsi zao zinakuwa na shaka na huzuni kwa yale waliyoyafanya ata kama ni kazi”alisema kiongozi huyu kwa masikitiko.

Ushawishi wa watafiti wa sheriaMtafiti Neema Chusi ameweka bayana kuwa hapa nchini Tanzania kazi ya unyongaji imekuwa ikifanywa kwa vitendea kazi duni na vilivyopitwa na wakati jambo ambalo inasemekana kuwa mtu anaweza kushindwa kufariki kwa kitanzi na hivyo kupigwa nyundo kichwani ili kumalizia uhai wake.

Hali kama hii inasikitisha mno kuona mtu anavyoweza kufanyiwa vitendo kama hivyo ingawa alikuwa mkosaji au alifanya kosa kama hilo. Je, mamlaka inaweza kukifanya kitendo hicho kuwa haramu na wakati huo huo kuwa halali? .Kuna nadharia kuu mbili nazo ni hii ya wale waanaosema aliyeuwa naye auwawe na wale wasemao aliyeuwa afungwe maisha. Dunia kwa sasa inaunga mkono suala la wakosaji hawa kufungwa maisha.

“Dhana ya aliyeuwa auwawe inazidi kuongeza chuki na uchungu miongoni mwa wanajamii kwani nia ya hukumu si kuongeza chuki bali kufanya jamii kuwa na maridhiano na watu kuendelea kuishi kwa amani katika maisha ya kila siku.

Ukiweza kupitia kesi mbalimbali za mauaji unaweza kuona kuwa mashahidi wengi wanasita kutoa ushahidi juu ya tukio vizuri kutokanana na kujua ukweli wa yatakayomfika

mtuhumiwa mara baada ya hatia,” Anasema Mwanasheria Suguta Heche ambaye ni Wakili wa masuala ya Mazingira nchni Tanzania.

Kesi zingine za mauwajiKwa mfano katika kesi ya jinai nambari 46 ya 1978 ya Jamhuri dhidi ya Dorith Liundi na Agnes Dorith Liundi inaonesha wazi kuwa shahidi mmoja alishindwa kutambua mwandiko wa Bi Agness Doris katika barua zake alizoandika mara baada ya kuwapa sumu watoto wake na yeye mwenyewe kunywa sumu hiyoy.

Ushahidi unaonyesha kuwa shahidi huyo japokuwa alikuwa akiandikiana barua kwa muda mrefu na rafiki yake ambaye alikuwa mtuhumiwa alishindwa kujua kabisa mwandiko wa rafiki huyo japokuwa walisoma darasa moja kwa miaka minne. Hii ni hali halisi ya hukumu ya kifo na jamii namna inavyokosa raha kuisikia au kuweza kuona mtu anatia mkono wake juu ya hukumu hii.

Inajulikana wazi kuwa hivi karibuni kulikuwa na matukio mabaya mno ya kuuwawa kwa ndugu zetu albino ambalo kwa hakika ni jambo baya lisilovumilika. Huku kumekuwa na madai wakati wa utayarishaji wa katiba mpya kuwa kesi zake zinaenda taratibu mno. Jambo la msingi ni kutakiwa kushugulikiwa kwa haraka ili kuzuia matukio kama hayo yasiendelee nchini petu.

Julius Nyerere na “Uhai haki

ya msingi”Katika hali hii ndipo maswali mengi yanaibuka juu ya kuendelea kwa hukumu hii au la, kabla ya kusema lolote lile juu ya hukumu ya kifo kuendelea au la ebu tutazame watu mbalimbali wanasema nini juu ya hukumu hii.

Japokuwa Julius Nyerere aliweza kutia sahihi ya kunyongwa kwa watu 10 kama takwimu za serikali zisemavyo hali hii inaonesha kuwa Julius aliweza kwenda kinyume na hilo kwa kutetea uhai wa binadamu katika hotuba zake mbalimbali alizoweza kuzitoa kati ya mwaka 1985 hadi kifo chake.

“Uhai ni haki ya msingi ya binadamu,na kama haki maana yake basi lazima ilinde uhai,” hii aliongea na kunukuliwa na gazeti moja la serikali tarehe 27 septemba 1993. Hii ndiyo hali halisi kuwa uhai wa binadamu hauwezi kuchezewa kama vile wa mnyama wa mwituni.

Naye Blackmaster anasema kuwa kile tunachotakiwa kufanya si kufanya kile ambacho sheria inataka tufanye bali kuangalia haki na ubinadamu unatutaka kufanya.

Kwa upande huo huo Coretta Scott King mke wa Dk Martin Luther King naye ni miongoni mwa wanaopinga hukumu hii ambapo msululu wa wanaopinga ni mkubwa sana. Bibi King japokuwa mumewe aliuwawa lakini yeye anaipinga sana hukumu hii. Watu wengi maarufu wameibuka na kupinga waziwazi na kuweka bayana kuwa inapaswa kuwekwa kando kusahauliwa kabisa.

Yohane Paulo wa pili baba Mtakatifu ambaye alifariki Dunia mwaka 2005 alisema kuwa hukumu hii si nzuri na dunia inapaswa kuheshimu uhai wa binadamu kwa nguvu zote kwani hakuna mwenye mamlaka ya kumpa uhai au kumnyang’anya mtu uhai wake.

Aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa serikali ya awamu ya tatu ndugu Fredrick Sumaye mwaka 2002 alisema kuwa haki ya uhai wa binadamu itaheshimiwa kama naye ameheshimu haki hiyo vinginevyo haki hiyo itanyang’anywa..Ndugu Sumaye mawazo yake yanalingana na aliyekuwa Gavana wa Massachusetts nchni Marekani Wiliam Weld.

Alama mojawapo ya mahakama ikionyesha mizani ya haki.

Inatoka uk. wa 20

22 Pambazuko Na. 41 Toleo la Januari - Machi 2013

KIMATAIFA

Tanzania tunajifunza nini kwa Burkina Faso?

Adeladius Makwega, Morogoro

NCHI ya Burkina Faso haina sifa ya kuwa ghala la chakula. Watu wake

milioni 16 wanaishi pembezoni mwa eneo la jangwa, na milioni nne kati yao wanategemea misaada ya chakula kutoka mashirika ya kimataifa.

Lakini tokea miaka ya tisini Burkina Farso imekuwa inaongeza tija ya kilimo mara dufu. Burkina Faso imeweza kuongeza tija ya kilimo kutokana na mpango bora wa umwagiliaji maji mashambani na wataaalamu wanasema tija zaidi inatarajiwa katika miaka ijayo.

Mkulima mmoja Mando Adaye anatueleza juu ya utaratibu huo wa umwagiliaji wa mashamba. Amesema anaridhika na njia bora zinazotumika, ambazo zimerahisishwa, “Naridhika na mtindo wa umwagiliaji.Kila kitu kimerahishishwa.Mtu anapaswa ku-tumia pampu mara moja tu ili kuy-asukuma maji. Hapo awali nililazimika kusimamia muda wote. Lakini sasa natumia pampu mara moja na kuon-doka kwenda kulala, Sasa naweza kumwagilia shamba usiku mzima.”

Kutokana na njia hiyo ya kumwagilia maji shamba lake,mavuno yanakuwa makubwa hata wakati wa ukame.Katika juhudi za kuongeza tija, wizara ya kilimo ya Burkina Faso pia inasaidia. Seydina Oumar Troure ndiye anaesimamia mradi wa umwagiliaji kutokea kwenye ofisi yake ya wizara ya kilimo mjini Ouagadougou.”Serikali inatoa fedha kwa ajili ya kuueneza mpango wa umwagiliaji wa mashamba.”

Wakulima wadogo wadogo wanapatiwa vifaa vinavyolipiwa na serikali. Serikali inatoa ruzuku ya kufidia theluthi mbili ya gharama. Serikali ya Burkina Faso inakusudia kutenga kiasi cha Euro milioni sita mwaka huu kwa ajili ya mradi wa umwagiliaji wa mashamba. Mkurugenzi wa mradi huo Seydna

Oumar Troure amesema yapo matumaini ya kuifanya Burrkina Faso iwe nchi ya kuuza mazao ya kilimo nje na kuweza kuingiza fedha nyingi.

“Kwa mfano tunauza nyanya na vitunguu nchini Ghana,Nigeria na Ivory Coast.Na ikiwa tutaweza kuboresha ufundi wa umwagiliaji wa maji, naamini tutafanikiwa kutumia maarifa yote tuliyonayo ili kuuza mazao fulani katika nchi za Afrika Magharibi na hata kwenye masoko ya kimataifa,” anasema Bwana Toure.

Kwa sasa ni asilimia tano tu ya ardhi ya kilimo nchini Burkina Faso inamwagiliwa maji. Mawezekano

Wakulima wakimwagilia mashamba yao kwa ushirikiano.

Inatoka uk. wa 17

Mfumo upi wa ununuzi wa korosho...

korosho za kuchoma na kwa matumizi ya kuni huku korosho chache kwa matumizi ya nyumbani. Michache ambayo ipo nyumbani nikitarajia kupata korosho za kuchoma kwa ajili kuziuza, matumizi ya nyumbani na kupata kuni,” anasema ndugu langweni.

Kwa hakika kila mmoja anaweza kufanya bishara fulani mara baada ya kuweza kuiona faida ya zao hilo, ni jambo la ajabu kama mtu kufanya biashara ya hasara na anaweza kufanya mambo mawili la kwanza kutatua changamoto zile

zinazoompeleka katika hasara au kuachana kabisa na biashara hiyo.

Kwa hakika jambo la kukata mikorosho si jambo zuri kwani ni jukumu la wapanga sera kuweka utaratibu sahihi wa bei ya zao hili ambalo kwa hakika linawezekana kuwa na bei ya kutosha ambayo mkulima atanufaika na serikali pia. Kama itaonekana imeshindikana basi wanunuzi wa rejareja waruhusiwe kununua na kusaidia kuwapa nafasi wakulima kuweza kuuza kwa bei bora.

ni makubwa.Hayo ameyasema mwakilishi wa benki ya mandeleo ya Ujerumani, KfW Stephan Neu.

Burkina Faso inatekeleza sera ya kilimo cha mashamba madogo madogo. Hadi kufikia hatua ya umwagiliaji wa mashamba makubwa njia bado ni ndefu katika Burkina Faso.Yafaa kutilia maanani kwamba Burkina Faso ni nchi inayokabiliwa na kile kinachoitwa shinikizo la ardhi, kwa sababu idadi ya watu inaongezeka kwa asilimia 3.2 kila mwaka. Eneo la kilimo haliwezi kuongezeka kama jins ambayvo watu wangelipendelea.

23Pambazuko Na. 41 Toleo la Januari - Machi 2013

MAKALA

Kilimo hai kinakuza pato la mkulima maradufu?

Adeladius Makwega, Morogoro

INAELEZWA kwamba iwapo Afrika inataka kukomesha njaa lazima iandae mpango

rahisi wa kuwasaidia takribani wakulima milioni 900, ambapo kuna uwezekano wa kuongezeka kipato chao kwa asilimia 80.

Jambo hilo litafanya gharama za uzalishaji kupungua kwa kiwango kikubwa sana.

“Tazameni kule,” anatamka Vincent Ssoko, akionyesha kidole chake kwenye majani ya migomba ambayo hayatamaniki yakiyumba kutokana na upepo wa joto ikiwa imezungukwa na senyen’ge.

Anasema, “Daima nimekuwa nikiwambia jirani zangu kwamba fanya kama nilivyofanya mimi.Chimba shimo kubwa ili kuufanya mti huo uwe na nafasi ya kutosha,jaza mbolea ya kutosha ya asili na uhakikishe kwamba mbegu hazipandwi kwa kukaribiana. Lakini hawafanyi hivyo, badala yake wananunua mbolea ghali za viwandani licha ya kupata mavuno

mabaya.”Vincent Ssoko mkulima wa kilimo

hai (anayetumia ukulima wa asili bila ya kemikali) huko Busana katika mkoa wa Kayunga ambapo huchukuwa kama saa tatu kwa mwendo wa gari kutoka kaskazini mashariki mwa mji mkuu wa Uganda, Kampala ana sababu nzuri ya kutabasamu. Kwani alikuwa ndio kwanza amenunua tena hekta 20 za ardhi ziada ya hekta 29 alizokuwa nazo. Anasema hapo mwaka 1998 alianza na hekta tatu tu.

Mkulima huyo mwenye umri wa miaka 46 hivi sasa anaotesha mananasi, ndizi, kahawa na maharage kwa njia ya kilimo hai... na hasa kwa kuwa na cheti cha utambuzi. Kwa hiyo anaweza kusafirisha mazao yake hayo katika soko la bara la Ulaya. Anaonyesha kwa fahari mananasi matamu yalioteshwa kwenye mstari mrefu ulionyooka.

Zaidi ya nusu ya matunda 700,000 kwa mwaka yanakwenda Ujerumani.Ssoko hujipatia shilingi 700 za Uganda sawa na senti 20 za euro ambayo ni sawa na shilingi 427 za Tanzania kwa

tunda moja. Katika soko la ndani ya nchi huwa anajipatia shilingi 150 tu sawa na senti nne za euro kwa shingi ya Tanzania sawa na shilingi 90 kwa kila tunda.

Faida za kilimo hai Iwapo Afrika inataka kukomesha njaa lazima iandae mpango rahisi kwa wakulima milioni 900. Ni dhahiri kwamba mapato lazima yaongezwe na wakati huo huo gharama za uzalishaji hazina budi kupunguzwa kwa kiwango kikubwa.

Utafiti uliofanywa na Shirika la Mpango wa Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) hapo mwaka 2010 umedokeza kwamba mambo yanakwenda vizuri. Utafiti huo uliofanywa miongoni mwa mashamba milioni kumi na mbili takriban katika nchi 60 zinazoendelea umebaini kwamba wastani wa mapato huongezeka hadi kwa asilimia 80 kwa kufuata mbinu za kilimo hai.

Nchi ya Uganda iliyoko Afrika Mashariki ina aina ya maabara ya majaribio.

Endelea Uk wa 24

Picha inayoonyesha mchanganyiko wa matunda. Mazao yaliyolimwa kwa kufuata taratibu za kilimo hai huuzwa bei ya juu nchi za Ulaya.

24 Pambazuko Na. 41 Toleo la Januari - Machi 2013

MAKALA

Vincent Ssoko anasema badala ya kununua madawa yalio ghali anatumia mbolea ya asili anayoipata bure kutokana na wanyama wake na kwamba badala ya kutumia madawa ya kuulia wadudu anatumia mkojo na majivu kupambana na wadudu hao waharibifu wa mazao.Kwa kazi ya kun’goa magugu pekee mkulima huyo inabidi amlipe mtu,kwani hapa pia ni marufuku kutumia madawa ya kuuwa magugu.

Kilimo hai kwa watu wote Katika mji mkuu wa Kampala Judith Nabatanzi akiwa mwenye motisha anapiga chapa kwa kutumia kompyuta yake.Judith na mwenzake Cathy Kyazike wanaongoza kwa pamoja “Duka la Mazao ya Kilimo Asilia”. Ni jina la mradi wa duka hilo dogo ambalo lina mazao ya matunda na mboga mboga za aina mbali mbali yaliyozalishwa kwa utaratibu wa kilimo hai kuanzia vikonyo vya vanila hadi karoti.

Duka hilo linamilikiwa na Nogamu, shirika mama la wakulima wanaofuta utaratibu wa kilimo asilia nchini Uganda na ni duka pekee la matunda na mboga mboga zilizopandwa kwa utaratibu wa kilimo hai zenye kuzalishwa nchini Uganda, nchi yenye idadi ya watu milioni 35.

Kuanzia saa moja asubuhi Judith tayari anakua dukani kushughulikia oda za wateja wake. Anasema ijumaa ndio siku kuu ya biashara katika kipindi cha wiki kutokana na kwamba wengi wa wateja wao wanataka kupika mwishoni mwa juma. Kwa hiyo inabidi wafunge vikapu vya mahitaji ya wateja takribani arobaini au zaidi,wakati huo wakulima waliowasili mwanzo wakiwa wameegesha kwenye mlango wa duka hilo na Boda Boda yaani taxi za pikipiki kama zinavyojulikana nchini Uganda.

Siku moja kabla wakulima huwa wanazungumza kwa njia ya simu na Judith na Cathy kuwapa bei za mazao yao, asubuhi inayofuata wakulima huleta mazao yao dukani kwa kuondoka kutoka maeneo ya ndani mashambani na mapema kuepuka

msongamano wa magari.Shamba la Ssozi Muwangwa liko

kama kilomita 30 magharibi kutoka Kampala. Mkulima huyu huyapakia maboksi yake ya nyanya kwenye pikipiki na anakwenda kwenye duka hilo mara moja kila wiki tokea mwaka 2007.Anaona bei za hapo ni nzuri kuliko bei za mazao ya kawaida yaani shilingi elfu nne sawa na euro moja centi kumi na tano kwa kilo ambayo ni bei nzuri zaidi kuliko ile ilioko kwenye soko la barabarani.

Je inamaanisha kwamba anaweza kuthibitisha utafiti wa shirika la Mpango wa Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP kwamba mapato yanayotokana na mazao ya kilimo hai ni ya juu? Akiunga mkono utafiti wa UNEP Muwangwa anasema inakuwa ni kawaida kwa ardhi kuwa na rutuba bila ya kutumiwa kwa madawa ya kemikali na wanazalisha kwa wingi tena kwa kipindi kirefu pamoja na kuepuka gharama za mbolea. Kwa jumla hujipatia mapato makubwa ya asilimia 30 na mara nyengine hata hamsini.

Wakati Muwangwa anapopakuwa maboksi yake Judia na Cathy huchambuwa oda zao na kutumbukiza kwenye vikapu matunda na mboga mboga mbali mbali kuanzia saladi, matufaa na karoti.Juu ya vikapu hivyo huwekwa karatasi za oda ili kuepusha mparaganyiko. Mbali ya Boda Boda pia kunakuwepo na magari yenye vipoza joto kwa ajili ya kuchukuwa vitu vinavyoweza kuharibika haraka vinaposafirishwa wakati wa asubuhi kutokana na joto lenye unyevu.

Upatikanaji wa vyeti vya kilimo haiMoses Muwanga anasema utaratibu wa kupata cheti cha kumtambulisha mkulima kama mlimaji wa mazao kwa utaratibu wa kilimo hai una gharama kubwa sana. Anakiri kwamba amesaidiwa na Nogamu-chama cha wakulima wa Bio wenye kutumia kilimo asilia, lakini wakulima wengi bado wanashindwa kuvilipia vyeti hivyo kutokana na gharama.Bei ya cheti hicho ni dola 24,000.

Muwanga ambaye ni kiongozi wa

Nogamu kwenye ukuta wa ofisi yake kumetundikwa vyeti vya wateja wake kutoka Japani,Marekani na Umoja wa Ulaya ambao wote hao wametowa leseni kwa bidhaa za chama cha wakulima wa Bio nchini Uganda.

Kwa mujibu wa Muwanga ziara za wakaguzi hugharimu dola elfu nane.Zinahitajika elfu kumi na sita kubadili uoteshaji wa mazao wa kawaida na kuingia kwenye ule wa bio wa kutumia kilimo cha asili yaani bila ya matumizi ya madawa ya kemikali,hatua ambayo huchukuwa mwaka mzima. Kwa hivi sasa Nogamu inafanya kazi na wakulima wadogo wa bio milioni mbili lakini ni laki mbili tu ndio wenye vyeti ya kimataifa vya kusafirisha nje mazao yao.

Swali hilo pia linamfikia mkuu wa chama cha wakulima wa kilimo hai; Je kweli barani Afrika inawezekana kuongeza mapato hadi asilimia 80 kwa kilimo hai? Kwa mujibu wa Muwanga anasema wao wameorodhesha kesi ambapo mapato ya mkulima yameongezeka maradufu baada ya kubadili kilimo na kuingia kile cha asilia.

Ardhi yake haiathiriwi na madawa ya kemikali na ndio maana kwa haraka inaleta tija lakini siasa haijatambua hilo kwa wakati unaotakiwa, anakosoa Muwanga na kuendelea kusema kwamba kilimo hai pia ni uhifadhi hai wa mazingira. Utaratibu huo wa kilimo asilia una vyakula zaidi na lishe ya kutosha, mapato kwa wananchi yanazidi asilimia 80 na una nafasi kubwa kusafirishwa nje kwa bidhaa zake.

Nchini Uganda usafirishaji nje wa mazao ya kilimo cha kawaida umekuwa ukipungua siku hadi siku. Kwa miaka sita sasa muswada wa sheria juu ya kilimo endelevu cha bio umekuwa ukijadiliwa miongoni mwa wabunge.Muwanga anatumai pegine hatimae mwaka huu unaweza kupitishwa.

Wakati Moses Muwanga alipokuwa Ujerumani mwaka 2012 alitembelea Maonyesho ya Bidhaa za Bio na kupatiwa oda zenye thamani ya dola miloni 200.Lakini hadi sasa Uganda inaweza tu kupeleka bidhaa za bio za thamani ya dola milioni 40.

Inatoka uk. wa 23

Kilimo hai kinakuza pato...

25Pambazuko Na. 41 Toleo la Januari - Machi 2013

Jipatie nakala ya Jarida la Pambazuko katika ofisi za MVIWATA ngazi za kati zifuatazo

MVIWATA Arusha S.L.P 47 Monduli Mahali: Uwanja wa Maonesho Njiro, ArushaSimu: +255 27 254 9437, Faksi: +255 27 253 8338 Barua pepe: [email protected]

MVIWATA DodomaS.L.P 3293 DodomaMahali:Area C Dodoma eneo la INADES Formation Tz, mkabala na msikiti wa Area CSimu:255 26 235 0013, Faksi: +255 23 261 4184Barua pepe: [email protected]

MVIWATA IringaS.L.P 370 Makambako Mahali: Jengo la Njoluma, Njombe mjiniBarua pepe: [email protected]

MVIWATA KageraS.L.P 80 Muleba Mahali: Wilaya ya Muleba karibu na Benki ya NMBBarua pepe: [email protected], mviwatakagera @yahoo.com

MVIWATA Kilimanjaro S.L.P 7389 Moshi Mahali: Mbuyuni sokoni- ghorofa ya GOLDEN GROWN LODGESimu: +255 27 275 1639Barua pepe: [email protected]

MVIWATA LindiS. L. P. 129 Liwale Mahali: Mtaa wa Wamo Gest MVIWATA ManyaraS. L. P. 446 Babati ManyaraMahali: Barabara ya NyerereSIMU: +255 27 253 0385 Faksi: +255 27 253 0707Baruapepe: [email protected]

MVIWATA MbeyaS.L.P 3015 MbeyaMahali: Jengo la Bima na CRDB Bank (Ghorofa ya mwisho) Simu/Faksi: 255 25 250 3062 Barua pepe: [email protected]

MVIWATA Monduli (MVIWAMO) S.L.P 47 Monduli

Mahali: Barabara ya Boma-Moringe Sekondari, Monduli MjiniSimu: +255 27 253 8029, +255 27 253 8337 Faksi: +255 27 253 8338Barua pepe: [email protected]

MVIWATA MorogoroS.L.P 3220 MorogoroMahali: Uwanja wa Maonyesho NaneNane mkabala na ofisi za TASOSimu/Faksi: 023 261 4184 Barua Pepe: [email protected]

MVIWATA MkurangaS.L.P 56 MkurangaMahali: Karibu na Stendi ya KimanzichanaBarua pepe: [email protected]

MVIWATA RukwaS.L.P 468 SumbawangaMahali: Jengo la Bethlehem Center – Barabara ya Msakila Barua pepe: [email protected]

MVIWATA RuvumaS.L.P 696 Songea ManispaaMahali: Jengo la TTCL ghorofa ya 2Simu: +255 25 260 0626 Barua pepe: [email protected]

MVIWATA ShinyangaS.L.P 1024 Shinyanga Mahali: Chuo cha Ushirika Moshi tawi la Shinyanga (Kizumbi)Barua Pepe: [email protected]

Mwenyekiti ratibuS.L.P 175 Igunga Mahali: Wilaya ya Igunga Mkabala na Msikiti wa Igunga.Simu: +255 26 265 0356 Barua pepe: [email protected]

MVIWATA KigomaS.L.P 1144 KigomaMahali: Kizota Kigoma Mjini

MVIWATA ZanzibarS.L.P 149 ZanzibarMahali: Wilaya ya Kati Unguju Shehia Barua pepe: [email protected]

MAWAKALA

IJUE MVIWATA Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania- MVIWATA

Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) ni chombo cha kuunganisha wakulima wadogo ili kuwa na sauti moja katika utetezi wa maslahi yao ya kiuchumi, kijamii, kiutamaduni na kisiasa.

Mtandao huu ulianzishwa mwaka 1993 na wakulima wadogo. Kauli mbiu ya MVIWATA ni ‘Mtetezi wa Mkulima ni Mkulima Mwenyewe’.

Falsafa, utume na dira ya MVIWATAFalsafa ya MVIWATA inajengwa katika ya misingi ya ushawishi na utetezi wa maendeleo ya wakulima wadogo katika nyanja za kiuchumi na kijamii; kuwezesha mawasiliano na kujifunza kwa kubadilishana uzoefu miongoni mwa wakulima.

Utume wetu:Kuimarisha mawasiliano na kuwaunganisha wakulima wadogo kupitia vikundi na mitandao yao katika ngazi mbali mbali ili kujenga mtandao wa kitaifa wenye nguvu ya kuwezesha ushiriki na uwakilishi wa kweli wa maslahi ya wakulima wadogo katika ngazi zote za maamuzi.

Dira yetu:MVIWATA ni kuwa chombo imara chenye nguvu za ushiriki na uwakilishi wa mawazo ya mkulima katika mchakato wa maamuzi ya kiuchumi, kijamii na kisiasa. Kuwa na uwezo wa kutekeleza na kufuatilia michakato na shughuli za maendeleo ya kiuchumi na kijamii yanayogusa maslahi ya wakulima wadogo.

Malengo ya MVIWATAKuwezesha mawasiliano miongoni mwa wakulima wadogo ili kujenga kwa pamoja mbinu na mikakati ya ushawishi na utetezi kwa maslahi ya 1. wakulima wadogo, kiuchumi na kijamii.Kubadilishana mawazo, ujuzi na uzoefu juu ya kilimo na shughuli mbalimbali za wakulima ili kuboresha maisha na kuinua hali yao kiuchumi na 2. kijamii.Kuwakilisha wakulima wadogo katika mashauriano na serikali juu ya masuala mbalimbali yanayohusu au yanayoathiri ufanisi na maslahi ya 3. wakulima wadogo wa Tanzania.

Maeneo makuu ya mpango mkakatiUshawishi na Utetezi: Kuwezesha wakulima wadogo kuwa na uwezo wa kutetea maslahi yao.1. Uwezo wa kiuchumi: kuwezesha wakulima wadogo kuwa na uwezo wa kiuchumi kupitia njia za akiba na mikopo, kuunganisha wakulima na 2. masoko na elimu ya ujasiliamali Kuimarisha vikundi na mitandao ya wakulima kwa lengo la kujipanga na kujitetea.3. Masuala mtambuka: Kujenga uelewa wa wakulima juu ya Ukimwi, Jinsia, Mabadiliko ya Tabia ya nchi. 4. Ujenzi wa kitaaasisi kwa lengo la kuimarisha shirika5.

MuundoMuundo wa MVIWATA una ngazi tatu ambazo ni Ngazi ya Taifa, Ngazi ya Kati na Ngazi ya Msingi. Ngazi ya Kati inaundwa na mitandao ya kimkoa na kiwilaya wakati Ngazi ya Msingi inaundwa na mitandao ya Kata na Vijiji.

Shughuli kuuKujenga uwezo wa wakulima wadogo kwa kupitia mafunzo shirikishi juu ya mbinu za ushawishi na utetezi, mbinu za kuimarisha uchumi wa 1. wakulima wadogo na uendelevu wa rasilimali kwa njia za warsha, mafunzo, mikutano na ziara za mafunzo.Kuhamasisha wakulima wadogo kujiunga katika vikundi vya kijamii na kiuchumi, mitandao ya msingi (kata na vijiji) na mitandao ya kati (mikoa 2. na wilaya). Mpaka sasa MVIWATA imeanzisha mitandao ya kimkoa katika Mikoa ya Dodoma, Iringa, Kagera, Kilimanjaro, Manyara, Mbeya, Morogoro, Rukwa, Ruvuma, Shinyanga, Tabora na Tanga kwa Tanzania Bara. MVIWATA pia imeanzisha mitandao ya kiwilaya katika Wilaya za Monduli (Arusha) na Chunya (Mbeya). Tanzania Visiwani, MVIWATA Zanzibar imeanzishwa na kusajiliwa (Usajili namba 401). Mkakati unaendelea wa kuimarisha mitandao iliyopo na kuanzisha mitandao mipya.Kukusanya, kuweka katika kumbukumbu na kusambaza habari zinazohusu ujuzi na uzoefu wa wakulima, sera za kitaifa na kimataifa kwa 3. kupitia jarida la Pambazuko Sauti ya Wakulima, vipindi vya radio, vipeperushi, vijitabu na machapisho mengine. Kuhamasisha na kuwezesha wakulima kubuni na kuendesha miradi shirikishi ya kiuchumi na uzalishaji kwa lengo la kuboresha uchumi wa 4. wakulima wadogo kama vile vyama vya mazao, vyama vya kuweka na kukopa na masoko ya mazao. Kuandaa mikutano na warsha kuhusiana na mada zinazowagusa au kuathiri maslahi ya wakulima wadogo.5.

Uanachama na jinsi ya kujiunga na shirikaMVIWATA ina wanachama wa aina tatu (3).

Aina ya kwanza ni Wanachama wa Kawaida ambao wamegawanyika katika makundi mawili; Kikundi cha wakulima wadogo au a) Mkulima mdogo binafsi aliye mwanachama katika Kikundi au Mtandao. Mkulima atakuwa mwanachama wa kawaida wa MVIWATA mara b) tu Kikundi au Mtandao wake utakapokubaliwa kuwa mwanachama. Atapewa kadi ya uanachama na kikundi au mtandao utapewa cheti cha utambulisho.

Aina ya pili ni Vyama, Mashirika na Mitandao ya Wakulima Wadogo. Vyama, Mashirika na Mitandao ya Wakulima Wadogo vinavyojishughulisha na utetezi na ushawishi wa maslahi ya wakulima wadogo vilivyosajiliwa chini ya sheria yoyote ya Tanzania katika Ngazi za Wilaya, Mkoa au Taifa vinaweza kuomba kuwa mwanachama wa MVIWATA iwapo vinakubaliana kwa dhati na malengo na madhumuni ya Shirika.

Aina ya tatu ni Wanachama WashirikiNi mtu yeyote, taasisi au kikundi cha watu ambacho kinaunga mkono malengo na madhumuni ya Shirika. Mwanachama mshiriki anatamkwa na Mkutano Mkuu wa MVIWATA.

Kila mwanachama, isipokuwa mwanachama mshiriki atalipa kiingilio na ada ya kila mwaka. Maelezo zaidi juu ya utaratibu wa kujiunga na ada yanapatikana kutoka kwa kiongozi au ofisi ya MVIWATA.

Kwa mawasiliano zaidiOfisi Kuu ya MVIWATAMkurugenzi MtendajiMVIWATA SLP 3220 MorogoroSimu/Faksi: +255 23 261 4184Barua pepe: [email protected]: www.mviwata.org