upanuzi wa ufalme mfululizo - valuesdrivenfamily.com kingdom expansion... · hata hivyo uchapishaji...

72
1 Upanuzi wa Ufalme Mfululizo Values-Driven ® www.ValuesDrivenPublishing.com

Upload: hoangxuyen

Post on 24-Feb-2018

968 views

Category:

Documents


14 download

TRANSCRIPT

1

Upanuzi wa Ufalme

Mfululizo

Values-Driven®

www.ValuesDrivenPublishing.com

2

“Injili Kulingana na Yesu: Kuondoa Karne za Kuchanganyikiwa.” Na Marc Currier. Haki ya kunakili © 2010, Marc Carrier. Kimepigwa chapa na Values-Driven www.valuesdrivenpublishing.com

Unaweza kuitumia nakala hii, kutafsiri, kupiga chapa au kuitoa yote bila kuomba ruhusa au idhini yoyote, kwa lugha yoyote ile, kwa kundi lolote la watu ukifuata kusudi chache zifuatazo: UPANUZI WA UFALME au KUWAJENGA KIROHO MITUME. Kunakili, kutawanya ama kutenganisha makala haya, kwa ujumla au sehemu yake kwa lengo la kujinufaisha kifedha au kutadhimini kamwe hairuhusiwi.

Ikiwa utakitafsiri kitabu hiki kwa lugha nyingine, tafadhali jumuisha dokezo la haki ya kunakili iliyoandikwa katika ukurasa huu, ili kusiwe na yeyote atakayezuia uenezi wa injili hii na pia mjulishe mchapishaji kupitia [email protected] ili bidhaa hizi ziwasilishwe kwa wengine.

Maandishi ya biblia yamenukuliwa kutoka kwa NEW AMERICAN STANDARD BIBLE ®. Haki ya kunakili © 1960, 1962, 1963, 1968, 1971, 1972, 1973, 1975, 1977, 1995 na Lockman Foundation. Imenukuliwa kwa idhini.

Nakala zaidi za kitabu hiki zinaweza kununuliwa kupitia kwa www.valuesdrivenfamily.com.

“Funguo za Upanuzi wa Ufalme” Haki ya kunakil ni ya Marc Carrier © 2009, Kiswahili version, © 2010 Marc Carrier. Kitabu hiki kime fasiriwa Chini ya Idara Ya Lugha ya Bahati Community Centre Secondary School chini ya Usimamizi Wa

Bwana Patrick Wafula Wanyama na Bwana. Sakwa Titus akiwa Mfasiri Mkuu Idara Ya Kiswahili. Barua pepe: titussakwa@yahoo. co. S. L. P 1242 NAIROBI. TEL. +254 721 991 413

Unaweza tumia, tafsiri au kuchapisha hii kazi yote ama sehemu ya kazi hii bila ruhusa ama haki zozote kwa minajili ya kuwa waanda na kuwa hamasisha watakatifu kwa kazi ya upanuzi wa Ufalme, katika lugha yeyote, watu wowote, kikundi katika nchi yoyote. Hata hivyo uchapishaji kwa misingi ya kibiashara ni marufuku. Ukifasiri sehemu ya kazi hii katikai lugha yoyote tafadhali ambatisha taarifa ya hati miliki kutoka ukrasa huu, ili pasiwe na pingamizi katika usambazaji wake kihaki na pia mtaarifu mchapishaji marc. carrier@valuesdrivenfamily. com ili wengine katika ufalme wapate nakala ya kazi hii.

Maandiko yametolewa kutoka kwenye BIBLIA YA NEW AMERICAN STANDARD BIBLE. Haki ya kunakili 1960, 1962, 1963, 1968, 1971, 1972, 1973, 1975, 1977, 1995 na wakfu wa Lockman kwa idhini.

Nakala zaidi zaweza kununuliwa kutoka kwenye wavuti: www. valuesdrivenfamily. com kwa bei nafuu.

“Kanisa Ndani Ya Nyumba: Kurejelea Urahisi” na Robert Fitts. Haki ya nakala © 2009, Robert Fitts. Kimechapishwa na Values-Driven® “Kuupanua Ufalme, kitabu kimmoja kwa wakati!” www.valuesdrivenpublishing.com

Waweza tumia, tafsiri, piga chapa na kutoa vifaa hivyi, ikiwa zima au sehemu yake, bila kuuliza ruhusa kabla na bila kuzingatia haki, kuwafundisha na kuwahami watakatifu kwa ajili ya upanuzi wa Ufalme, katika lugha yoyote, kundi la watu wowote, katika nchi yoyote. Hata hivyo, kuzalisha vifaa hivyi, zima au sehemu yake, kwa ajili ya biashara ni marufuku.

Isipokuwa itiwe alama kivingine, nukuu za Maandiko zimechukuliwa toka kwa Biblia Takatifu, New International Version®, Haki ya Nakala © 1973, 1978, 1984 na International Bible Society.

Nukuu za Biblia zenye alama “Phillips” zimechukuliwa toka The New Testament in Modern English, Haki ya Nakala © 1958, 1959, 1960 J.B. Phillips and 1947, 1952, 1955, 1957 The Macmillian Company, New York. Zimetumiwa kwa ruhusa. Haki zote zimehifadhiwa.

Nukuu za Maandiko zenye alama “KJV” zimechukuliwa toka the Holy Bible, King James Version, Cambridge, 1769. Nukuu za Maandiko zenye alama “TLB” au “The Living Bible” zimechukuliwa toka The Living Bible, Tyndale House, 1997,

Copyright ©1971 by Tyndale House Publishers, Inc. Zimetumiwa kwa ruhusa. Haki zote zimehifadhiwa.

3

YALIYOMO

INJILI KULINGANA NA YESU: ......................................................................... 4 Dibaji .................................................................................................................... 5 Utangulizi ............................................................................................................. 5 Tatizo…na Suluhisho ........................................................................................... 5 Msingi wa Kweli................................................................................................... 7 Haki au Huruma.................................................................................................... 7 Ufalme wa Mungu ................................................................................................ 8 Raya wa Ufalme ................................................................................................. 10 Mtindo wa Kuvaa ............................................................................................... 10 Matambaa Chafu?............................................................................................... 11 Usisahau Sehemu ya Pili .................................................................................... 12 Salama Katika Kristo.......................................................................................... 13 Hesabu Gharama................................................................................................. 14 Mchanganuo wa Mwisho.................................................................................... 15 Kuhusu Mwandishi............................................................................................. 16 FUNGUO ZA UPANUZI WA UFALME ............................................................ 17 Utangulizi ........................................................................................................... 18 Ufalme ................................................................................................................ 19 Kupata Maono .................................................................................................... 20 Matayarisho Ya Vita........................................................................................... 20 Utume ................................................................................................................. 21 Hesabu Tukufu ................................................................................................... 22 Kuingia kwenye Ufalme ..................................................................................... 23 Muhtasari ............................................................................................................ 25 Njia Ya Uhuru .................................................................................................... 25 Uhuru Kutoka Kwenye Nguvu za Dhambi......................................................... 26 Uhuru Tunaoweza Kuona ................................................................................... 27 Mawasiliano na Mungu ...................................................................................... 28 Kupewa Nguvu ................................................................................................... 29 Kutafuta, Kupata na Kuwahitimisha Wanafunzi Wapya.................................... 30 Vidokezo na Nyenzo Za Uanafunzi.................................................................... 31 Muhtasari ............................................................................................................ 32 Amri za Kuondoka.............................................................................................. 32 Kuhusu Mwandishi na Nyenzo........................................................................... 33 KANISA NDANI YA NYUMBA.......................................................................... 35 Maneno ya Uthibitisho ....................................................................................... 36 Utangulizi ........................................................................................................... 36 Neno la Utangulizi.............................................................................................. 37 Maelezo ya Ujumbe............................................................................................ 37 Hali ya Makanisa ya Nyumbani ......................................................................... 38 Kanisa Ndani Ya Nyumba Katika Agano Jipya ................................................. 40 Kanisa ni Nini? ................................................................................................... 42 Kanisa Ndani Ya Nyumba Ni Nini? ................................................................... 45 Uanachama Wa Kanisa? ..................................................................................... 46 Upanzi Lowesha wa Kanisa................................................................................ 49 Gurudumu au Mzabibu? ..................................................................................... 53 Hatua Moja Kuelekea Umoja ............................................................................. 53 Je, mnafanya nini kwenye Kanisa Ndani Ya Nyumba?...................................... 55 Jinsi ya Kuanzisha Kanisa la Nyumbani............................................................. 56 Maswali na Majibu ............................................................................................. 61 HESABU YA KIROHO ........................................................................................ 64 Ukurasa Kazi ya Sababu za Ngome.................................................................... 67 Mfano Sala.......................................................................................................... 68 UPANDAJI MAKANISA NJIA YESU ALITUONYESHA: KATIKA LUKA 10 70 KUNENA JUU YA YESU NA WATU WANAOMWABUDU ALLAH........... 72

4

Injili Kulingana na Yesu: Kuondoa Karne za Kuchanganyikiwa

5

Dibaji

Kwa karne nyingi, makanisa mengi yamekuwa yakihubiri ujumbe wa "uamini-rahisi." Sema tu ombi fupi na umkaribishe Yesu moyoni mwako, na matokeo yake utakuwa umezaliwa mara ya pili. Umehakikishiwa mbingu kabisa. (Angaa haya ndiyo tunaambiwa.) Sio vigumu kuona makanisa yahubiriyo injili hii rahisi hayana shida ya kupata wafuasi wengi sana. Lakini je, hii kweli ndiyo Injili ambayo Yesu alihubiri?

Ikiwa injili hii ya leo ya uamini-rahisi ni ya kweli, basi mbona Yesu aliwaambia Mitume Wake, "Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye;naye anipendaye atapendwa na Baba yangu, nami nitampenda na kujidhihirisha kwake." (Yohana 14:21). Hili kwa hakika linaonyesha kuwa Mkristo halisi lina husisha zaidi ya kusema hili "ombi la mtenda dhambi" kwa wakati mmoja maishani mwako. Uhushiano tiifu wa upendo-imani na Yesu Kristo pia unahitajika.

Katika Injili Kulingana na Yesu: Kufunua Karne za Kuchanganyikiwa, Marc Carrier anaiweka Injili ya kihistoria ya Ukristo kwa njia ya wazi. Hii ndiyo Injili aliyoihubiri Yesu, na ni Injili iliyohubiriwa na Wakristo wa kwanza. Ni sehemu ya ile "imani iliyopeanwa ya kwanza na ya mwisho" kwa watakatifu (Yuda 3). Ingawa Marc anaiweka hii Injili kwa njia ya ufupisho unaoeleweka vyema, kila kitu asemacho kimeungwa mkono kwa udhabiti na maneno ya Yesu na pia nyaraka za Mitume.

Lakini usifikiri ya kwamba yale unayoenda kusoma ni mawazo tu binafsi ya Marc ya kutafsiri Maneno ya Yesu. La. Yale Marc aliwakilisha yameungwa mkono na mamia--kama sio maelfu--ya nukuu kutoka kwa Wakristo wa kwanza walioishi muda mfupi baada ya Mitume kufa. Mawasilisho ya Marc yaweza kusikika kama ni mageni kwenye masikio mengine ya siku hizi, lakini hayange sikika hata kidogo kama mageni kwa wanaume na wanawake waliowasikiza kwa binafsi mitume wakifundisha na ambao wangeweza kusoma Agano Jipya kwa lugha yao ya Kigiriki. Hawa walikuwa ni Wakristo kwenye makanisa yaliyoanzishwa na Mitume, na wengi wao walijitolea kufa kwa ajili ya Kristo na injili yake.

Ombi langu ni kuwa hiku kijitabu cha Marc kitakusisimua na kwamba, kama Bereans, utayachunguza Maandiko na kumbukumbu ya historia kuona kama haya mambo ni kweli yako hivyo. David W. Bercot, mhariri wa A Dictionary of Early Christian Beliefs na mwandishi wa vitabu kadhaa vikiwemo Will the Real Heretics Please Stand Up, The Kingdom that Turned the World Upside Down, and Will the Theologians Please Sit Down.

Utangulizi Kujadiliwa kwa uwazi mitazamo tofauti kuhusu injili kunaweza kuzusha uteti. Kimsingi, ni kwa kuwa, miongoni mwa

wapentekote kuna ukubaliano katika nchi za magharibi kuhusu jinsi ya kuokoka. Martin Luther na wengine ambao ni wakereketwa wa karne ya 16 walizusha misingi mingi ambayo iliishia kuundwa kwa tabaka mpya ya Kikristo ambayo imekithiri. Hata makabadhi ambayo hayadai kuhusiana na hao wakereketwa wa hapo awali kama wazao wao wa kithiolojia bila kukusudia bado wanatumia mafundisho yao. Hata hivyo, hili linazusha swali hili: Je, itakuwaje ikiwa wakereketwa walikosea?

Sote twafahamu kuwa washindi huandika upya historia. Jambo hili ni wazi kwenye historia ya kanisa. Hata hivyo, jinsi ilivyo na historia yote, ukweli hujitokeza na kukabiliwa wale wenye mawazo wazi.

Tunaweza kuambatisha imani ya mafundisho yetu kwa watu binafsi katika historia. Nina hakika kwamba wengi wenu kama mimi hapo awali wanadhana kuwa Luther na wakereketwa waliibua imani yao kutoka kwa watume katika injili.

Hata hivyo, haichukui muda mrefu kugundua kuwa huu ni mmoja wa mifano ya marudio ya historia ya kanisa ambayo nimezungumzia. Tunapoendelea kujadiliana kuhusu ni yapi mtu anapaswa kuzingatia ili kuokoka, utaelewa haswa ni yapi ninayomaanisha.

Tatizo…na Suluhisho

Hapo mwanzo Mungu aliumba vitu vyote (Mwanzo 1). Kilele cha kazi yake kilikuwa ni kumuumba binadamu kwa mfano wake

(Mwanzo 1:26-27). Katika shamba la Edeni, pahali halisi palipokusudiwa kuwa pa Adamu na Hawa, wazazi wetu wa kwanza, walidanywa na Shetani wamuasi Mungu, akitanguliza dhambi ya kwanza kwa binadamu. Kutokana na hayo, ubovu uliingia kazi ya uumbaji na jamii ya binadamu (Warumi 5:19). Kulingana na sheria ya Mungu (yaani Sheria ya Dhambi na Mauti—tazama Mwanzo 2:16, Warumi 6:16, 8:2 na 8:13), Adamu na Hawa walitimuliwa kutoka shambani Edeni na kupoteza kibali cha uzima wa milele (Mwanzo 3:23-24). Hivyo basi, tangu siku hiyo, ubovu uliojulishwa kwa binadamu kupitia kwa wazazi wetu wa kwanza umepelekea mwanadamu kuzama katika dhambi. Kama Paulo alivyosema: “Kwa sababu wote wamefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu,” na nabii Isaya: “Sisi wote tumeenenda kinyume, kila mmoja amegeukia njia yake binafsi.” Hivyo basi, tukiwa tumejitenga na Mungu, tumekuwa watumwa wa yule tunayemtii ambaye ni Shetani, na kupitia kwa Sheria ya Dhambi na Mauti mwisho wetu umeshirikishwa na Shetani na malaika wengine waliomuasi Mungu. Tunangojea hukumu ya namna hiyo na ziwa la moto wa milele (Tazama Warumi 6:16 na Matayo 25:41).

Lakini Mungu alitengeneza njia. Mungu alimtuma Mwanawe wa pekee wa milele Yesu: kwa umbo, Mungu kamili, anafanana na Baba kwa sura lakini ni tofauti kwa utu wake. Yesu ndiye Mwana wa Pekee wa Baba, Nuru ya Kweli ing’aayo kutoka kwa utu wa Baba. Mzaliwa wa bikira akichukua mfano wa mtenda dhambi lakini bila dhambi. Yesu hakutumwa kubadili mawazo ya Mungu kuhusu binadamu lakini angaa kubadilisha mafikira ya mwanadamu kuhusu Baba. Yesu Mungu-Mtu, alifanya makao yake kati ya mwanadamu kuonyesha mwanadamu jinsi ya kuishi kulingana na mapenzi ya Baba. Yesu, kwa umbo la mtu, alijitolea kwa unyenyekevu kwa mafundisho yote ya Babake na akatii Baba kwa ukamilifu—hata kuingia kwa mauti msalabani (Wafilipi 2:28). Yesu aliyafundisha maneno yale ya Baba kwa watu wote na akatuonyesha kwa mfano wake jinsi ya kuishi na Baba ili tujifunze kutembea jinsi alivyotembea. Utume wake ulikuwa ni kutujulisha kwa Baba na kwa njia zake ili tugeuze mioyo yetu na kumrudia Baba kupitia kwa Yesu.

6

Kupitia kwake, ndio—kwa sababu kando naye, hakuna uhuru kutoka kwa dhambi. Mungu, kupitia kwa upendo wake usio na kifani na neema yake, alimtuma mwana wake wa pekee, sio tu kupindua mioyo yetu kwake, vile vile kuharibu kazi ya Ibilisi, hiyo ni kutuweka huru kutoka kwa utumwa wa dhambi na mauti, na kutufanya watumwa wa haki. Mungu alimpeana mwanawe mikononi mwa watenda dhambi, waliomtesa, wakamdhihaki na kumsulubisha hadi mauti. Damu ya Yesu ilitiririka bure; ni kupitia kwa damu yake ambapo dhambi zetu zimeoshwa, na kwa mwili wake uliovunjika tumefanywa wazima.

Sisi, tukiwa kwa utumwa wa Shetani kupitia Sheria ya Dhambi na Mauti, tulihitaji uhuru wetu kukombolewa. Mungu alimpeana Mwanawe wa Pekee, mtakatifu asiyekuwa na dhambi, aliyefanana na Mungu kwa kila njia, lakini alikuwa binadamu, kama mtumwa aliyegharamia uhuru wetu kutoka kwa dhambi na mauti (Waebrania 2:14-15). Yesu, kwa sababu hakuwa na dhambi, hakufungwa na Sheria ya Dhambi na Mauti. Hivyo basi, Mauti haingemfunga (Matendo ya Mitume 2:24). Yesu aliharibu kuzimu, ulimwengu wa chini ama makao ya wafu, na akahubiri Injili kwa wafu kwa siku tatu. Akisha waweka huru mateka, Yesu alirejea duniani kwa umbo la kimwili akiwa na funguo za mauti na kuzimu mkononi mwake (Ufunuo 1: 18). Kwa umbo la ufufuo Yesu alifunza wafuasi kwa siku 40, hadi kupaa kwake mbinguni, ambako anatawala na Ufalme wake kwa mkono wa kiume wa Baba, kwa utukufu wote na nuru (Matendo 1:3, 9, 1Waebrania 1:3, 12:2).

Biblia husema kuwa Kristo alitumwa ili awe fidia kwa wengi. (Matayo 20:28, 1 Tim. 2:16). Hebu kwanza tujihusishe kwa sekunde moja na mabadiliko ya ukombozi, ambayo ilijiri sana katika nyakati za biblia. Nani hulipwa fidia? Mteka nyara! Kwa hivyo, chini ya mafundisho yanayokubalika na wengi ya kisasa ya maridhio, ni nani analipwa fidia? Mungu Baba. Acha nifafanue. Makisio ya maridhio ya upatanisho inasema kuwa Yesu alitumwa na Mungu ili kuridhisha hitaji lake la haki. Kinyume na hili, mwenye kuomba pia ndiye mwenye hulipwa.

Linganisha hili na yale ambayo kanisa la kwanza liliamini: mwanadamu alichukuliwa mateka na Shetani, na kufungwa chini ya Sheria ya Dhambi na Mauti. Yesu alitumwa na Mungu kulipa gharama na kutuweka huru. Hili linaleta maana, sivyo? Iwapo umesoma au kutizama “The Lion, the Witch and the Wadrobe.” (Chronicles of Nornia), na C.S Lewis, tayari umekwisha julishwa kwa mafunzo ya kiodhoksia ya maridhio. Mchawi mweupe ni Shetani, Aslani ni Yesu, Edmundi ni mwanadamu, na Uchawi wa Kina ni Sheria ya Dhambi na Mauti. Edmundi alitenda dhambi na Mchawi alipata haki ya kumdai kwa sababu ya ule Uchawi wa Kina. Aslani alipeanwa kama fidia ya kumweka Edmundi huru. Ila mauti haingemshika kwa sababu Aslani hakuwa na hatia. Hivyi ndivyo makubaliano yaliendelezwa kiukweli.

Kama vile Mchawi Mweupe katika Nornia alivyozidisha upanuzi wake, katika ulimwengu wa kawaida Shetani alijaribu kuchukua zaidi ya alivyohitajika. Alikubaliwa kumtukana na kumtishia Yesu. Alikubaliwa kumsulubisha Yesu msalabani kiunyama hadi mauti. Lakini alitaka kumshika Yesu daima kuzimuni—jambo ambalo hakuwa na idhini ya kisheria juu yalo. Mwishowe, Shetani alishindwa kiakili kwa sababu ya maovu yake. Baba alimfufua Kristo kutoka kaburini. Kupitia kwa Kristo Mshindi, tuna shujaa ambaye alijitolea mwenyewe kama kondoo wa kuchinjwa, akijua kwamba kupitia haya yote, Mauti haingemshika na angeharibu kuzimu na kushinda Mauti. Alitoa maisha yake kama fidia, akipata aibu na mateso mengi, ili aibe funguo za Mauti na Kuzimu na kupitia kwake, wote wamwitao waokolewe toka Dhambini, Mautini na Hukumuni. Kupitia fidia aliyolipa, Kristo amewaweka wanadamu huru kutoka kwa Sheria ya Dhambi na Mauti.

Kupitia kwa kufanyika Mungu-Mtu kwa Kristo Mwalimu, Neno aliye hai, tumejulishwa kwa mapenzi ya Mungu kupitia kwa Maisha na Mafundisho ya Kristo, ili kwamba tunaweza tu kutubu na kumgeukia Yeye na njia zake. Kujitoa kwetu kwake bila masharti, moyo uliovunjika na kubondeka, inafungua milango ya huruma za Mungu. Kupitia ubatizo wetu, tunashiriki kifo na ufufuo wa Kristo (Warumi 6:1-7). Milango ya Mauti na Kuzimu imefunguliwa wazi na tunaipitia bila kujeruhiwa, dhambi zetu zimeoshwa kwa maji na kwa damu itakasayo ya Kristo. Tunatoka majini, minyororo ikiwa imefunguliwa, tukiwa huru kushiriki na Mungu katika utakatifu wote na haki yote. Mtu wa kale hufa na Kristo na mtu mpya anazaliwa; tunazaliwa tena kuwa makao ya Roho Mtakatifu, kwa mfano wa ufufuo wa Kristo. Kilele cha siri hii ni ufufuo wa miili yetu wakati tarumpeta ya mwisho itakapolia (1 Wakor. 15:51-52).

Kwa hivyo kusudi la maridhio ni hili: kurejesha mioyo yetu kwa Mungu kupitia toba ya kweli, kugeuka na kuacha dhambi na kuelekea utakatifu na haki. Wokovu wetu ni hakika kama mioyo yetu iliyobadilika. Tunafanyika kuwa wana, kupandikizwa kama matawi ya mzeituni mwitu kwa Mzabibu Mtakatifu, kwa ushirika wa Mungu na watakatifu—washiriki wote katika mwili na damu ya Kristo (Yohana 6:54). Makaribisho yetu kwa Mzabibu yanakuja kwa Neema kupitia imani, toba na ubatizo. Tunazalia kwenye Mzabibu kwa kudumu ndani ya Kristo. Kudumu ndani ya Kristo ni kudumisha uhusiano wetu na Yeye wa upendo wa utiifu kwake (Yohana 15:10 chini na Yohana 14:15 na 21). Kunaweza kuwa na kiwango fulani cha utii bila upendo, lakini hakuna upendo bila utii. Na bila aina hii ya tunda, matawi yatakatwa na kurushwa motoni (Yohana 15:6 na Matayo 7:19). Uhusiano wetu na Kristo unaoendelea, unaodhihirika kwa matunda yetu (yaani, uhusiano wetu wa upendo wa kutii na Kristo) unaonyesha uvumilivu wetu kwa imani na tumaini letu la wokovu (Luka 8:15).

Hebu tusome Sura ya Kumi na tano ya Injili ya Yohana tuone vile Yesu anasema:

“Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye Mkulima. Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa. Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia. Kaeni ndani yangu nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa pekee yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu. Mimi ni mzabibu, ninyi ni matawi; akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lolote. Mtu asipokaa ndani yangu, hutupwa nje kama tawi na kunyauka; watu huyakusanya na kuyatupa motoni yakateketea. Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni lolote nanyi mtatendewa. Hivyo hutukuzwa Baba yangu, kwa vile mzaavyo sana; nanyi mtakuwa wanafunzi wangu. Kama vile Baba alivyonipenda mimi, nami nilivyowapenda ninyi, kaeni katika pendo langu; kama vile mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake. Hayo nimewaambia, ili furaha yangu iwe ndani yenu, na furaha yenu itimizwe.” (Yohana 15:1-11).

Ni wazi katika kifungu hiki kuwa tunahitajika kuingia na pia kukaa kwa Mzabibu. Tutarejelea fungu hili baadaye. Hadi umbali huu tumejadili kwa kifupi sehemu kadhaa kuhusu hoja ya wokovu: kuanguka kwa mwanadamu, Maridhio ya

Kristo, na maswala wawili wazi ya Mzabibu: kuingia na kuketi humo. Kufuatia tutajadili msingi wa kweli na kiini yanayohusiana nao.

7

Msingi wa Kweli

Katika Sura ya Saba ya Injili ya Matayo, Yesu anatueleza wazi kwamba ni lazima tujenge kwenye mwamba. Hili limefafanuliwa kama kuyasikia na kuyatii maneno yake. Wale wasikiao maneno yake na hawayatii wanajenga kwenye mchanga, na watapata mwanguko mkubwa. Kwa maneno ya Kristo:

“Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba, mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba. Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga; mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake lilikuwa kubwa. (Matayo 7:24-27).

Katika muktadha, “haya maneno Yangu” inarejelea Mafundisho Yake yote katika Mahubiri ya Mlimani. La kupendeza, ushahidi

kamili wa kwanza wa Kikristo, uliotungwa na Justin Martyr na kuandikwa na Mtawala wa Kirumi, Antoninua Pius, unasisitiza haya mafundisho. Baada ya kuyafafanua haswa mengi ya mafundisho ya Kristo kwenye Ushahidi wake wa Kwanza, Justin anasema hivi:

Wacha wale wataopatikana wakiishi kinyume na Alivyofundisha, waeleweke kuwa sio Wakristo, hata ingawa wanakiri kwa vinywa vyao mafundisho ya Kristo; kwa kuwa sio wale wanaokiri, lakini wale wanaotenda kazi, watakao okolewa, kulingana na neno Lake: “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Kwa yeyote anisikiaye na atendaye kulingana na mapenzi yangu humsikia yeye aliyenituma Mimi. Wengi wataniambia siku ile, Bwana Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, hatukula na kunywa kwa jina lako, na kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu. Kisha kutakuwa na kulia na kusaga meno, wakati watakatifu watakapong’aa kama jua na waovu kutumwa katika moto wa milele. Kwa vile wengi watakuja kwa jina langu, watakaovalia mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali. Mtawatambua kwa matendo yao. Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni.” Na kwa wale ambao hawaishi kulingana na mafunzo Yake, na ni Wakristo kwa jina tu, tunahitaji hao waadhibiwe nawe. Jinsi Justin anavyoelewa haya mafundisho si jambo geni kwake. Kuna shaka ndogo tunapoyasoma maandishi ya kanisa la

kwanza kwa umoja walielewa mafundisho ya Yesu kuwa yenye mamlaka ya juu na yakumaanisha tu vile yalisema. Kwa bahati mbaya, kueleweka kwa Injili siku hizi kunazingatia hitaji la kuchambua waraka wa Paulo kwa Warumi kwa makini.

Hata hivyo, hii inatelekeza mafundisho haswa ya Kristo kwenye nafasi ya pili. Ilhali Yesu mwenyewe alisema hakuna mwanafunzi aliye mkuu kuliko mwalimu wake (Yohana 13:16 na 15:20). La kupendeza ni kwamba, amri mbili za kwanza za Yesu (Ambazo zimetangazwa kote katika Injili) zinaelezea wazi wazi mtazamo wa Injili wa Kanisa la kwanza; hili ni: tubu na unifuate! Injili Kulingana na Yesu ni geuka toka kwa dhambi zako na umfuate Yeye. Geuka toka kwa mambo ya ulimwengu, ufalme wa giza, dhambi, uchoyo, chuki, na uchiachilie kwa uongozi wa Kristo, Ufalme wa Mungu, haki, utakatifu, utii, na upendo. Hii ndio Injili ya kweli. Maridhio ya Kristo (hii ni, Kufanyika-Mtu kwa Kristo, mateso, kifo, na ufufuo) yalikamilishwa kuwezesha hasa mwisho ukamilike.

Mungu hakumtuma tu Yesu kuteseka na kufa ili aridhishe tu haki yake Mwenyewe. Kristo hakuchukuwa tu nafasi ya adabu ya tabia yetu ya opotovu, na hakuja tu duniani kuondoa adabu ya dhambi zetu. Ingekuwa hili ni kweli, kwa nini basi Yesu alifundisha? Kwa nini alituonyesha jinsi ya kuishi ikiwa maridhio ilikuwa tu swala la mabadilishano ya haki?

Huu muundo wa utoshelezi wa maridhio, hata kama unakubalika na wengi wa Waprotestanti na Wakatoliki kwa usawa, haukuingizwa hadi mnamo 1100 Mwaka wa Bwana Wetu na Anselm, Askofu Mkuu wa Kikatoliki wa Canterbury. Kwa miaka 1100, aina hii ya mafundisho ilikuwa ngeni—ngeni kwa Mitume, kanisa la Kwanza, na kwa kila mtu mwingine. Lakini, ni kwa huu msingi ndio msingi ambao kanisa la sasa limetulia kwa udhabiti. Matokeo: Injili ya “Uamini Rahisi.” Tangia dhana ya adabu kuchukuliwa ama maridhio ya wote waaminio kupitia kwa kifo cha Kristo msalabani, kazi hii inaanzia na kumalizikia msalabani. Kwa hivyo, hakuna toba, hakuna utii, hakuna utakatifu, hakuna haki, hakuna tunda, na hakuna kubadili uaminifu kwa Kristo kama Bwana unahitajika kwa mtu akiriye kuwa muumini. Mwishowe ni ‘wokovu’ usiohitaji moyo uliomgeukia Mungu. Matokeo ni ‘injili’ inayopingana na Injili Kulingana na Yesu: “tubu na unifuate Mimi” imechukuliwa na “niamini Mimi.” Huu ndio mmoja wapo wa udanganyifu mkubwa ambao adui amewahi kuingiza kwa wanadamu. Shetani, jinsi alivyofanya katika Edeni, tena anasema, “Je, ni kweli Mungu amesema?”

Kuelewa wazi ni kwa nini Mungu alimtuma Yesu duniani—yaani, Kristo kufanyika Mungu-Mtu na maridhio—kutatuelekeza kuelewa vyema wokovu na hata usalama wa milele. Kwa hivyo wacha tuendelee kujadili haya mafundisho muhimu. Lakini kabla hatujafanya hivyo, hebu tujadili asilia ya Mungu kuhusiana na ubinadamu: ya haki au ya huruma.

Haki au Huruma

Mungu ni wa huruma. Kila mtu angekubaliana na usemi huo. Hata hivyo, makisio ya maridhio (ama adhabu ya kuchukuliwa na mwingine) ya maridhio inamwasilisha Mungu ambaye kwa kweli hana huruma, kwa sababu kwanza na mbele ya yote, Yeye ni wa haki. Wacha nieleze.

Makisio ya Anselm ya maridhio inaonyesha kuwa Mungu amekosewa na mwanadamu mutenda dhambi (Sote tungekubaliana na sehemu hiyo), na kwamba Mungu ameghadhabishwa sana kwamba anahitaji kulipwa. Majuto yetu ya kweli na ya kutoka moyoni na toba ya kweli hazitoshi kuzuia ghadhabu Yake, kwa sababu makosa yetu ni makubwa sana. Ni sharti tupate adabu ya dhambi zetu kwa sababu Mungu ni wa haki na anadai hili. Hata hivyo, tangia makosa yatendwe na mwanadamu, mtu ambaye hana hatia angeweza kuichukua hii adabu juu yake kulipia hili deni, kuridhia matakwa ya Munng ya haki.

8

Hata hivyo, je, hii sura ya Baba inaonyesha Yeye ni mwenye huruma? Kulingana na mtazamo huu, Mungu hataki kusamehe deni letu, lakini anahitaji mtu mwingine kulipia badala yetu. Kwa msimamo huu anaonyesha hana huruma hata kidogo, bali anaiwekelea ghadhabu hii juu ya mtu mwingine. Malipo kamili ya hili deni bado yanahitajika. Hakuna kabisa maridhio ya deni hili.

Baya zaidi ni, kwa kweli anamtuma Mwanawe mpendwa zaidi kuteseka na kufia mikononi Mwake, kuridhia matakwa yake ya haki, kwa maana asilia Yake haiwezi tu kuachilia huruma na msamaha. Aina hii ya haki kwa kweli inamfanya Mungu kuwa mdhalimu.

Aina hii ya muundo wa maridhio pia inadunisha damu ya Kristo na kuifanya kama aina fulani ya malipo, kuondoa deni kitabuni, kulipia ridhaa ya uharibifu ambao Baba alipata. Hata hivyo, Maandiko yanatwambia kwamba damu ya Kristo kweli hututakasa, ikituondolea dhambi zetu—ikiwa na maana kuwa inatubadilisha (Yohana 1:7), sio tu kufutilia mbali deni kwa vitabu vya mbinguni.

Kinyume na hayo, Mungu mwenyewe amekuwa wa huruma nyakati zote kwa wale wanaonyenyekea mbele Zake kwa toba—yaani, kuachana na dhambi na kuingia kwa haki. Watazame watu wa Nineve, au Waisraeli mara nyingi katika historia yao. Msaada wa Mungu wa msamaha wa dhambi wakati wote umekuwa wazi kwa wote wamjiao kwa roho iliyovunjika na kubondeka, vile Mzaburi asemavyo: “Sadaka ya Mungu ni roho iliyovunjika; moyo uliovunjika na kubondeka, Ee Mungu, Hutaidharau.” (Zaburi 51:17). Msamaha unapatikana kwa wote wanaomjia. Hata hivyo, kuegemea kwetu dhambini kutokana na ubovu kupitia kwa uzao wa Adamu unatawala mwili wetu. Hata tukiwa na shauku ya kumpendeza Mungu, bado tunashindwa kutokana na hii nira ya dhambi (Warumi 7:14-24). Kutuweka huru kutoka kwa minyororo hii ya ubovu ndio sababu halisi ya Baba kumtuma Kristo kufia mikononi mwa wenye dhambi. Kristo alikuja kuharibu kazi ya Ibilisi (1Yohana 3:8).

Hebu tuone jinsi Yesu alielezea msamaha kwenye mfano katika Matayo 18: Kisha Petro akamwendea akamwambia, Bwana, ndugu yangu anikosee mara ngapi nami nimsamehe? Hata mara saba? Yesu akamwambia, Sikuambii hata mara saba, bali hadi saba mara sabini. Kwa sababu hii ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyetaka kufanya hesabu ya watumwa wake. Alipoanza kuifanya, aliletewa mtu mmoja awiwaye talanta elfu kumi. Naye alipokosa cha kulipa, bwana wake akaamuru auzwe, yeye na mkewe na watoto wake, na vitu vyote alivyo navyo, ikalipwe ile deni. Basi yule mtumwa akaanguka, akamsujudia akisema, Bwana, nivumilie, nami nitakulipa yote pia. Bwana wa mtumwa yule akamhurumia, akamfungua, akamsamehe ile deni. Mtumwa yule akatoka, akamwona mmoja wa wajoli wake, aliyemwia dinari mia; akamkamata, akamshika koo, akisema, Nilipe uwiwacho. Basi mjoli wake akaanguka miguuni pake, akamsihi, akisema, Nivumilie nami nitakulipa yote pia. Lakini hakutaka, akaenda, akamtupa kifungoni, hata atakapoilipa ile deni. Basi wajoli wake walipoyaona yale yaliyotendeka, walisikitika sana, wakaenda wakamweleza bwana wao yote yaliyotendeka. Ndipo bwana wake akamwita, akamwambia, Ewe mtumwa mwovu, nalikusamehe wewe deni ile yote uliponisihi; nawe, je! Haikukupasa kumrehemu mjoli wako, kama mimi nilivyokurehemu wewe? Bwana wake akaghadhibika, akampeleka kwa watesaji, hata atakapolipa deni ile yote. Ndivyo na Baba yangu wa mbinguni atakavyowatenda ninyi, msipowasamehe kwa mioyo yenu kila mtu ndugu yake (Matayo 18:21-35). Petro alimuuliza Yesu ni mara ngapi anaweza msamehe mtu. Kwa kumjibu, Yesu akamwambia hadithi juu ya Mfalme, (Baba)

akichukua hesabu ya watumwa wake (wanadamu). Mtumwa alimwia deni ambalo hangeweza kulipa na mfalme kudai malipo. Hata hivyo, yule mtumwa aliomba huruma, na mfalme akamwonea huruma. Hapa ndipo, kulingana na makisio ya Anselm ya Maridhio, mtu asiye na deni angeingilia na kulipa zalio la deni, kwa sababu ya hitaji la haki la mfalme, malipo kamili yalikuwa ni lazima. Lakini hili halikutimia. Badala yake, mfalme kwa urahisi alimwachilia na kumsamehe deni. Hii ndio taswira ya huruma ya Mungu.

Kuna kipengee kingine muhimu hapa. Tunaona pia kwamba kule kusamehe deni la mtumwa kulikwa na sharti. Wakati yule mtumwa alikataa kumsamehe mjoli wake, naye mfalme, vile vile, akamshikilia kwa hesabu ya deni hilo lake binafsi alilokuwa amesamehe hapo awali. Iwapo makisio ya Anselm ni kweli, hili halingekuwa. Iwapo Yesu alinuia kufutilia mbali deni kwenye vitabu kwa kulipa deni letu, malipo yalitolewa, na Mungu hangetuhesabia hilo deni tena. Hata hivyo, ikiwa deni letu limesamehewa kwa urahisi wa huruma ya Mungu (msingi ukiwa ni masikitiko na toba ya kweli), Mungu ana haki yakuturejeshea hesabu ya dhambi zetu iwapo tutashindwa kuonyesha toba na kuipeana kwa binadamu mwenzetu. Na Yesu anasema wazi wazi katika fungu hili (vile alivyofanya kwa Sala ya Baba Yetu) kwamba iwapo tutashindwa kusamehe wadeni wetu, hatutasamehewa.

Mwisho, je, Mungu kweli anatarajia zaidi kutoka kwetu kuliko vile Yeye angependa kufanya Yeye Mwenyewe? Kipengee cha hii hadithi yote kilikuwa ni kujibu swali la Petro kuhusu kumsamehe mwanadamu.Yesu anaonyesha kuwa tunapasa kusamehe vile Mungu alisamehe. Lakini kwa makisio ya Anselm, Mungu alidai haki na malipo kamili. Iwapo hili ni kweli, ingelingana na ingekuwa sawa pia na sisi kudai hilo hilo. Kwa wazi hili haliingiani na Injili.

Kwenye sura itakayofuata, nitaleta hoja ambayo imepotea kwa makanisa ya siku hizi, ijapokuwa ni kiini cha mafundisho ya Yesu—Ufalme wa Mungu.

Ufalme wa Mungu

Yesu aliukaribisha Ufalme wa Mungu. Kwa kweli, Anautaja Ufalme zaidi ya mara 100 kwenye Injili zote nne. Ufalme wa

Mungu ndio kiini cha mifano yake mingi na mikuu. Kwa kweli, Injili inaitwa “injili ya Ufalme” mara kadhaa. Lakini bado hivi leo, injili inayohubiriwa inahusu tu kifo cha Yesu kinachochukuwa nafasi ya dhambi zetu—nadra juu ya Ufalme. Kama matokeo, wainjilisti wengi hata hawajui Ufalme wa Mungu unahusu nini.

Wengine hudhani kuwa Ufalme wa Mungu hautajitokeza wenyewe hadi kurudi mara ya pili kwa Kristo. Hili linaeleweka, kwa kuwa mafungu mengine ni wazi kuwa ni marejeleo kwa kilele cha Ufalme wakati Kristo anatawala hapa duniani. Hata hivyo, Yesu vile vile alifundisha wazi kwamba Ufalme wa Mungu ulikaribishwa wakati wa huduma yake ya hadhara, kwa nukuu kama hizi, “Ufalme wa Mungu umekaribia.” Wengine pia hudhani kuwa angaa kwa sasa, Ufalme wa Mungu ni ufalme wa kiroho tu. Kwa ukweli wa mambo, ni ufalme uliopo—hapa duniani, ndio, hata sasa hivi. Wacha nieleze.

Ni nini kinatengeneza Ufalme? Falme zote zina sehemu nne: mfalme, eneo, sheria, na raya. Sawa, ndivyo ulivyo Ufalme wa Mungu. Yesu ndiye Mfalme. Eneo ni Mbingu na dunia. Sheria ni amri za Kristo. Raya ni wale wanachinyenyekeza kwa Mfalme. Sasa ni wazi kuwa Ufalme wa Mungu hakika unatofautiana kidogo na falme za dunia. Kwanza kabisa, Mfalme wetu kwa sasa

9

anatawala kutoka kiti chake cha enzi kule Mbinguni. Wafalme wengi huongoza ufalme wao miongoni mwa wafuasi wao. Hata hivyo, Yesu alionyesha wazi kuwa eneo ni mbinguni na hata duniani (Matayo 6:10 na 28:18). Huu tu ni mfano mwingine wa sababu ya kufanywa kwake Yesu Mungu-Mtu, ili Mfalme atembee kati ya wafuasi wake. Kuja kwake mara ya pili kutakaribisha kipindi cha Mfalme kutawala na wafuasi wake hapa duniani. Humo ndimo kuna sababu ya wengine kudhani kuwa Ufalme wa Mungu kwa kweli hauanzi mpaka kurudi Kwake mara ya pili. Hata hivyo, Anatawala sasa, hata ikiwa anakaa mbinguni.

Kwa hivyo tunakuja kwa sheria. Yesu alikuja na mafundisho mengi. Wengine hufikiri ni ya changuo. Hata hivyo, tayari nimejadili kwamba ili kukaa kwa Mzabibu ni sharti tudumu ndani ya Kristo; yaani, kutii amri ya Mfalme. Vile vile nimejadili kwamba kujenga kwenye mwamba inamaanisha kutii amri Zake. Wacha nipeane mfano wa watu pia kutoka kwa Mahubiri wa Mlimani. Yesu alifundisha:

“Si kila mtu aniambiaye, ‘Bwana, Bwana,’ ataingia kwenye ufalme wa mbinguni, bali yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni ndiye atakayeingia. “Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, Siwajui ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.”

Hapa Yesu anaeleza jinsi ya kuingia katika Ufalme, hasa tukirejelea kilele cha Ufalme kama nilivyotaja hapo mapema. Msamiati

uliotumika hapa ni ‘ufalme wa mbinguni.’ Kusoma kwa makini kwaonyesha kuwa Ufalme wa Mungu na Ufalme wa Mbinguni yana maana sawia, kupendelewa kwa neno moja kwa lingine kukipeanwa na waandishi fulani wa injili. Hili ni wazi tukisoma mafungu ambatano katika maelezo kadhaa ya Injili na kuona hadithi hiyo hiyo sawia ikitolewa kwa matumizi tofauti tofauti ya misamiati hii miwili (linganisha Matayo 13 na Marko 4, kama mfano).

Ni wazi kuwa hili fungu linarejelea hukumu (zingatia kurejelea kwa “siku hiyo”), na ni wazi kuwa linajadili wokovu. Hata hivyo, kiini changu hapa ni kutilia maanani matumizi ya hoja ya Sheria za Ufalme. Yesu anaonyesha wazi kuwa siku ya hukumu msingi wa kuchagua hautakuwa tu kuamini, bali kufanya mapenzi ya Baba Yake. Yesu pia hazingatii ishara na miujiza kama ni za umuhimu sana kwa wokovu, bali anawarudi wale wamwitao tu Bwana, kama “ninyi msiotii sheria.” Wazi toka kwenye fungu hili ni uhakika kwamba SHERIA zipo; kwamba ikiwa kuzikataa ni kutotii sheria, basi kwa uhakika kuna sheria zimepeanwa.

Basi hizi sheria ni zipi? Maandishi ya Paulo (hasa Warumi na Wagalatia) yanaonyesha wazi kwamba mtu hawezi kuokolewa kwa kufuata Sheria za Musa: tohara, kushika siku, miezi, majira na miaka, chakula fulani, na kadhalika. Baraza kule Yerusalemu lilifafanua wazi zaidi kuwa mizigo pekee ya Mafundisho ya Wayahudi ambayo Mataifa wanazingatia ni kuepuka usherati, vitu vilivyotolewa sadaka miungu, na kutokula damu na wanyama walionyongwa (Matendo 15:28-29). Hakuna uzingatifu umepewa Sheria za Musa hapa. Kwa hivyo tunaweza kuhitimisha bila tashwishi kuwa sio Sheria ya Musa ndiyo Yesu anarejelea (Tazama pia Waebrania 8:7-13).

Hata hivyo, Yesu alisema kwamba haki yetu isipopita ile ya viongozi wa kidini wa siku Zake, hatutaingia Ufalme wa Mbinguni (Matayo 5:20). Lakini Yesu basi anafundisha wazi yale anamaanisha. Anapitia maandiko kutoka Sheria ya Musa, kipengee kimoja hadi kingine, na anaelezea matarajio Yake kwa kusema, “Mmesikia ikisemwa [katika Sheria], bali nasema…” Ikiwa unasoma mafundisho Yake, utaona kwamba Anainua mizani kwa kiwango kikubwa kupita nyakati zote! Hatupilii mbali Sheria, bali anaipanua, fafanua na kuweka wazi matarajio Yake. Ni baada ya huu ufafanuzi ndipo Yesu anashiriki maana ya “uasi”, akielezea kwamba wale wasikiao “haya maneno yangu” na kuyatenda wanajenga kwenye mwamba na wale wayapuuzayo wanajenga kwenye mchanga, matokeo yake ni uharibifu wa hakika. Lakini swali hili linaibuka: Je, nini kitatendeka juu ya zalio la mafundisho ya Agano la Kale ambayo Yesu haguzii wazi wazi kwenye mafundisho yake?

Yesu anasema kuwa hakuja kuondoa Sheria, bali alikuja kuitimiliza. Halafu tena anasema kuwa hakuna hata herufi moja itaondolewa mpaka “itimizwe.” Hii ikiwa na maana ya kutimizwa kwa unabii wa kimasiya na kazi Yake duniani (tazama 18:31, Yohana 19:28-30, Yohana 17:4, na Matayo 26:56).

Tunasoma katika Injili ya Yohana Yesu akiwaambia Wayahudi, “Myachunguze maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia. Wala hamtaki kuja kwangu mpate kuwa na uzima.” (Yohana 5:39-40). Wakati Yesu anasema, “Maandiko,” anamaanisha kile sisi tunarejelea leo kama Agano la Kale. Anafafanua wazi kuwa, uzima wa milele ni kupitia Kwake, sio kupitia mafundisho ya Agano la Kale. Yesu anaelezea zaidi wakati wa mjadala na wanafunzi kwenye Chumba cha Juu usiku wa kusalitiwa kwake, “Ikiwa mtazishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama vile mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake.” (Yohana 15:10). Hapa Yesu anaonyesha wazi kuwa alinyenyekea kwa Baba na kutii amri zote za Babake (kwa hivyo alitimiza unabii wote); sasa kwa njia hiyo hiyo vile Yesu alitii amri za Babake, tunapaswa kutii amri za Yesu. Tumepokezwa fimbo. Kwa kuwa mafundisho ya Yesu ni yale Baba alimwamuru kusema, na hata Musa aliwaelekeza wote kumsikiza Yeye (tazama Kumbukumbu la Torati 18:15-19, Yohana 7:16-17, na Yohana 12:44-50).

Mfano mwingine wazi kutoka kwa Yesu kuhusu matakwa yetu ya kushika amri Zake ni fungu la Utume Mkuu kwenye Injili ya

Matayo. Yesu anawaambia wafuasi wake:

“Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa Jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi sikuzote, hata mwiso dahari.” (Matayo 28:18-20) Hapa Yesu anaamuru wafuasi wake kuwafanya wafuasi wengi, wakiwafunza kushika yale yote aliyowaamurisha. Hili agizo

lililo wazi kwa uwazi linamaanisha kupeleka amri hii kwa vizazi, kila kizazi cha wafuasi kikifuata kingine, kinaamurishwa wazi kifundishe kushika pia na kufundisha amri Zake ZOTE. Kwa hivyo imani yetu ni lazima itoke kwa herufi nyekundu (tazama pia Yohana 14:21, 23-24, Waebrania 8:7-13,).

Basi hili linatuacha na sehemu ya mwisho ya Ufalme: Uraya. Tena, Yesu hatuachi tukibainisha. Ananena kwa kiasi kizuri juu ya swala hili. Kwa kweli, tayari tumejadili mafundisho kadhaa ya muhimu.

10

Raya wa Ufalme Kuna sura mbili kwa uraya katika Ufalme: kujipatia uraya, na kudumisha uraya. Hili linaweza kuwa geni kwa wengine, lakini

tutaangalia Maandiko kuiweka hoja hii wazi. Mafundisho ya Yesu juu ya Mzabibu na matawi kwenye Sura ya 15 ya Injili ya Yohana inafunua kwamba matawi yalikuwa kwenye Mzabibu. Ni masafi kwa sababu ya maneno ya Yesu. Bado, pia tunaona kuwa matawi yale yatakatwa na kutupwa motoni ikiwa hayazai matunda—baadaye linaelezwa kuwa pendo la kutii (tazama mistari 6 na 10). Kwa hivyo, sura mbili zipo: kuingia kwenye Mzabibu na Kudumu kwenye Mzabibu—kile nimerejelea kama kujipatia uraya na kudumisha uraya.

Yesu asema tena kwenye Mahubiri Mlimani: “Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni.” (Matayo 7:19). Yohana Mbatizaji aliiweka hivi, kuwakemea Wayahudi wa Kidini waliodhani wokovu wao ulihakikishwa licha yao kukataa kutubu:

“Basi zaeni matunda yapasayo toba; wala msiwaze mioyoni mwenu kwamba, Tunaye Baba, ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambia ya kwamba Mungu aweza katika mawe haya kumwinulia Ibrahimu watoto. Na shoka limekwisha kuwekwa penye mashina ya miti; basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni.” (Matayo 3:8-10). Yesu pia alifundisha sawia juu ya toba kufuatia vifo vya kutisha na vya aibu vya Waisraeli wengine: “Nawaambia, sivyo; lakini msipotubu, ninyi nyote mtaangamia vivyo hivyo. Akanena mfano huu; mtu mmoja alikuwa na mtini umepandwa katika shamba lake la mizabibu; akaenda akitafuta matunda juu yake, asipate. Akamwambia mtunzaji wa shamba la mizabibu, Tazama, miaka mitatau hii naja nikitafuta matunda juu ya mtini huu nisipate kitu; uukate, mbona hata nchi unaiharibu? Akajibu akamwambia, Bwana, uuache mwaka huu nao, hata niupalilie, niutilie samadi; nao ukizaa matunda baadaye, vyema! La, usipozaa, ndipo uukate. (Luka 13:5-9). Basi tunaona kuwa toba ni sharti linalohitajika ili kuingia kwenye Ufalme. Bado haikomi hapo. Yesu hasa anasisitiza kuwa

kuingia tu haitoshi. Ni sharti tudumishe uraya wetu. Hapa kuna mifano kadhaa kuhusu Ufalme. Yesu alitoa mfano mwingine, akisema, “Ufalme wa Mbinguni emefanana na mtu aliyepanda mbegu njema katika konde lake; lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake. Baadaye majani ya ngano yalipomea na kuzaa, yakaonekana na magugu. Watumwa wa mwenye nyumba wakaenda wakamwambia, Bwana, hukupanda mbegu njema katika konde lako? Limepata wapi basi magugu? Akawaambia, Adui ndiye aliyetenda hivi. Watumwa wakamwambia, Basi, wataka twende tukayakusanye? Akasema, La; msije mkakusanya magugu mkazing’oa ngano pamoja nayo. Viacheni vyote vikue hata wakati wa mavuno; na wakati wa mavuno nitawaambia wavunao, Yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita mkayachome; bali ngano ikusanyeni ghalani mwangu.”… Kisha Yesu akawaaga makutano, akaingia nyumbani; wanafunzi wake wakamwendea, wakasema, “Tufafanulie mfano wa magugu ya kondeni.’ Akajibu, akasema, “Azipandaye zile mbegu njema ni Mwana wa Adamu; lile konde ni ulimwengu; zile mbegu njema ni wana wa ufalme; na yale magugu ni wana wa yule mwovu; yule adui aliyepanda ni Ibilisi; mavuno ni mwisho wa dunia; na wale wavunao ni malaika. Basi, kama vile magugu yakusanywavyo na kuchomwa motoni; ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia; Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake, nao watakusanya kutoka katika ufalme wake machukizo yote, na hao watendao maasi, na kuwatupa katika tanuru ya moto; ndiko kutakuwako na kulia na kusaga meno. Ndipo wenye haki watakapong’aa kama jua katika ufalme wa Baba yao. Mwenye masikio na asikie.” (Matayo 13:24-30).

Katika mfano huu, tunaona kuwa Ufalme wa Mungu umejaa mazuri na maovu; wale wafanyao uasi watatupwa kwenye moto, na

wenye haki watajiunga na Baba. Wengine hutafsiri hili fungu kumaanisha kwamba wana wa Ufalme ni wanakanisa na wana wa uovu ni wale wasio wanakanisa au walimwengu wasioamini. Hata hivyo, mfano huu unatufunza kuwa ngano ilipandwa kabla ya magugu na magugu yaliingizwa katika ngano baada ya ngano kupandwa. Kwa wazi, kanisa lilipandwa halafu uasi ukaja kanisani. Kanisa la Kwanza lilielewa huu mfano kumaanisha kuwa kanisa litanajisiwa na vikwazo na waasi. Kwa nuru ya mfano ufuatao, mfano wa juya (uliofunzwa na Yesu kwenye ujumbe ule wa mfano wa ngano na magugu) itakuwa dhahiri kwa nini hili lilikuwa tamatisho la maana.

“Tena Ufalme wa mbinguni umefanana na juya, lililotupwa baharini, likakusanya samaki wa kila namna; hata lilipojaa, walilivuta pwani; wakaketi, wakakusanya walio wema vyomboni, bali walio wabaya wakatupa. Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia; malaika watatokea, watawatenga waovu mbali na wenye haki, na kuwatupa katika tanuru ya moto; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.” (Matayo 13:47-50)

Hakuna lisiloeleweka hapa ya kuwa Ufalme wa Mungu (mbinguni) NI hili juya. Na kwa wazi, juya litakamata samaki wazuri na

pia wabaya. Halafu samaki hawa watatenganishwa mwishoni mwa dahari. Kulinganisha juya, ngano na magugu, ni rahisi kuona ni kwa nini magugu yalitafsiriwa kama sehemu aasi ya kanisa. Tutaona kwenye sura itakayofuata mengi juu ya hii hoja ya wana “wema na wabaya” katika Ufalme.

Mtindo wa Kuvaa

Mafumbo ya ngano na magugu na ya juya sio tu pekee yanayozungumzia hoja ya pili ya uraia—hii ni, kuidumisha au kukaa kwa

mzabibu. Hapa kuna fumbo la karamu ya arusi:

11

“Ufalme wa Mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyemfanyia mwanawe arusi. Akawatuma watumwa wake wawaite walioalikwa kuja arusini; nao wakakataa kuja. Akatuma tena watumwa wengine, akisema, Waambieni wale walioalikwa, Tazameni nimeandaa karamu yangu; ng’ombe zangu na vinono vimekwisha kuchinjwa, na vyote vimekuwa tayari njooni arusini. Lakini hawakujali, wakaenda zao, mmoja shambani kwake, mmoja kwenye bishara yake; nao waliosalia waka wakamata watumwa wake, wakawatenda jeuri, na kuwaua. Basi yule mfalme akaghadhabika; akapeleka majeshi yake, akawaangamiza wauaji wale, akauteketeza mji wao. Kisha akawaambia watumwa wake, Arusi i tayari, lakini wale walioalikwa hawakustahili. Basi enendeni hata njia panda za barabarani, na wote mwaonao waiteni arusini. Watumwa wale wakatoka wakaenda njia kuu, wakakusanya wote waliowaona, waovu na wema; arusi ikajaa wageni. Lakini alipoingia yule mfalme ili kuwatazama wageni wake, akaona mle mtu mmoja asiyevaa vazi la arusi. Akamwambia, Rafiki, uliingiaje humu nawe huna vazi la arusi? Naye akatekewa. Mfalme akawaambia watumishi, Mfungeni mikono na miguu, mchukueni mkamtupe katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno. Kwa maana waitwao ni wengi, bali wateule ni wachache.” (Matayo 22:2-14). Kifungu hiki kinaonyesha makundi matatu ya watu: Wayahudi ambao walikataa mwaliko na wakawadharau watumwa.

Hatimaye hawakufika kwenye arusini (katika Ufalme). Kisha kuna mwaliko wa watu wote (juya) waovu na pia wema. Fumbo hili linaaishia kutolewa nje ya karamu kwa mgeni asiye na mavazi rasmi ya arusi. Kifungu chenyewe hakijaeleza nini maana hasa ya vazi la arusi; hata hivyo, maandiko hayako kimya juu ya swala hili. Katika mahubiri ya Yesu kwa kanisa la Sardisi, anasema hivi: “Najua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hai, nawe umekufa. Uwe mwenye kukesha, ukayaimarishe mambo yaliyosalia, yanayotaka kufa. Maana sikuona matendo yako kuwa yametimilika mbele za Mungu wangu. Basi kumbuka jinsi ulivyopokea, na jinsi ulivyosikia; yashike hayo na kutubu. Walakini usipokesha, nitakuja kama mwivi, wala hutajua saa nitakayokuja kwako. Lakini unayo majina machache katika Sardisi, watu wasioyatia mavazi yao uchafu. Nao watakwenda pamoja nami hali wamevaa mavazi meupe, wala sitalifuta kamwe jina lake katika kitabu Cha Uzima, nami nitalikiri jina lake mbele za Baba yangu, na mbele ya malaika zake. (Ufunuo wa Yohana 3:1-5)

Hapa Yesu analiambia kanisa kuwa wana jina la kuwa hai, lakini wamekufa. Matendo yao hayajakamilika, na kutokana na hayo,

mavazi yao yamechafuka. Ikiwa hawatatubu, majina yao yatafutwa kutoka kwenye kitabu cha uzima. Ni tu wanaostahili ndio watakaotembea naye. Kwa hivyo katika fungu hili, tunawaona watu ambao wamebandikizwa juu ya Mzabibu, lakini wamo hatarini ya kukatwa (majina kutolewa kwenye kitabu cha uzima.). Wamepata uraya wao katika Ufalme wa Mungu, lakini bila toba wanaweza kuupoteza.

Matendo yasiyokamili hupelekea mavazi yaliyochafuka—maneno ya Yesu ni dhahiri. Mavazi hata yanafafanuliwa dhahiri zaidi hapa kuliko pahali pengine, katika muktadha wa chakula cha jioni cha arusi. Kila wakati Maandiko hufafanua Maandiko.

“Na tufurahi, tushangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana-Kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari. Naye amepewa kuvikwa kitani nzuri, ing’aayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu. (Ufunuo wa Yohana 19:7-8).

Hapa tunaona kuwa ilipewa Biarusi (Kanisa la Kristo—yaani, raya wa Ufalme), KUJIVISHA MAVAZI. Biarusi AMEJIWEKA

TAYARI. Uraya wake, kubandikizwa kwake kwa Neema ya Mungu kupitia imani—matokeo ya maridhio ya Kristo. Bado haya maridhio hayakomi hapo. Kudumisha uraya wake, au kukaa kwa Mzabibu ni juu yake, “amepewa” jukumu na Mungu. Na je, hiki kitani kizuri ni nini? Ndio, kwa kweli, ni matendo ya haki ya watakatifu.

Hivyo basi hili linaingianaje na mafungu ambayo yanasema kwamba wokovu ni kazi yote ya Mungu? Sawa, hebu tusome kifungu kimoja kinachotumiwa kuinua wadhifa huo:

Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo. (Waefeso 2:8-10). Hivi basi, ni kweli kuwa tumeokolewa kwa neema kwa njia ya imani, kwa sababu ni Kristo aliyejitolea kwa mapenzi yake kwa

Baba, akapeanwa mikononi mwa waovu, akatokwa na damu na akafa ili ashinde mauti na atuweke huru kutoka kwa Sheria ya Dhambi na Mauti. Ni damu yake ndiyo ilitutakasa. Kuingia kwa Mzabibu ni kupitia tu kwake, maana YEYE NDIYE MZABIBU!

Hata hivyo, hebu tusikomee kusoma mstari wa 9. Mstara wa 10 unasema kuwa sisi tu kazi ya Mungu tumeumbwa katika Kristo kufanya kazi njema. Uhuru wetu kutoka dhambini, maridhio ya Kristo, ilikuwa na lengo asilia. Kumbuka Injili Kulingana na Yesu: tubu na Umfuate. Tunapaswa kugeuka kutoka kwa uovu na kukumbatia wema. Tunapaswa kufanya kile alituokoa tufanye. Na Maandiko yote yanatangaza, Tukishindwa kufanya hivyo, tumo hatarini ya kupoteza uraya wetu. Uraya wetu katika Ufalme wa Mungu unategemea kujisalimisha kwetu kwa Mfalme, na utii kwa Sheria za Mfalme—yaani, amri za Kristo.

Matambaa Chafu? Je, lakini Biblia haifundishi kwamba matendo yetu ya haki ni kama matambaa chafu? La, huu tu ni mfano mwingine wa historia

ya marudio ya Kikristo. Hakuna kitu kinachompendeza Mungu zaidi ya haki yetu ya kuendelea; ni kwa sababu hii Mungu alimtuma Mwanawe, ili tuwe wenye haki na watakatifu.

Hivyo, hii makisio yatoka wapi? Ina msingi wake kwa thiolojia kereketwa. Kulingana na mafundisho haya, mwanadamu kabisa hana wajibu wowote katika wokovu wake. Zaidi, mwanadamu hangeweza kufanya mema hata kama angetaka. Wakereketwa malifundisha kwamba hatungeweza kuja kwa Kristo kwa imani hata ikiwa tungetaka, bali lilikuwa ni jukumu la azimu hali mbele la Mungu ambaye angeamua ni nani angeweza au hangeweza kuja Kwake. Mojawapo ya hitimisho la kawaida la hii thiolojia ni kwamba hata yale mema tufanyayo, ni uovu asilia. Isaya 64:4 hutumika kuunga mkono hii thiolojia; hata hivyo, kabla ya

12

wakereketwa, mstari huu ulikuwa nadra, iwapo uliwahi, kunukuliwa na Kanisa la Kwanza—ni wazi kuwa huu mstari ulikuwa na matumizi madogo sana. Bali, kama matokeo ya umuhimu wa swala hili kwa mafundisho ya wakereketwa ya kutwaa, ni mojawapo ya mafungu yanayonukuliwa kutoka kwa Agano la Kale siku hizi. Hii hapa:

“Kwa maana sisi sote tumekuwa kama mtu aliye mchafu, na matendo yetu yote ya haki yamekuwa kama nguo iliyotiwa unajisi, sisi sote twanyauka kama jani, na maovu yatuondoa, kama upepo uondoavyo. (Isaya 64:6).

Sasa nakusihi usome mstari huu kwa muktadha. Huyu ni Isaya ananena ombi la toba kwa Mungu, akirejelea na kuongea kwa

niaba ya Israeli iliyo aasi. Huyu si Mungu anaongea juu ya mwanadamu kwa wakati wote, bali ni ombi la kihisia kwa Mungu kwa ajili ya watu waasi, hasa watu fulani tu—manabii wenzake wa wakati huo.

Kwa urahisi fanya utafiti wa maneno ya Biblia ya neno “haki,” “iliyonyooka,” na hata “isiyokuwa na mawaa” uone utavumbua nini. Bila kujali tafsiri, utapata mamia ya marejeleo kwa wanaume na wanawake waliochukuliwa kuwa wenye “haki” mbele ya Mungu kando na Kristo—yaani, bila “haki ya kuwekelewa.” Pia vile vile utapata marejeleo mengi sana kwa fasihi ya hekima ya haki iliyoamurishwa na Mungu. Kuna upatano sawia katika Agano Jipya. Kabla ya imani katika Kristo, Zakaria, Elizabeti, Yohana Mbatizaji, Yusufu baba wa Yesu, Simioni, Yusufu wa Arimathia, na Kornelio waliitwa “wenye haki” na walisifiwa kwa mwenendo wao. Hii kwa hakika haimaanishi kuwa watu hawa walikuwa bila dhambi (tazama kwa mfano Warumi 3:0-10); ina maana tu kwamba waliishi maisha yao wakimpendeza Mungu, wakijitahidi kushika amri zake. Mungu hakuwahi kuona hili ni chafu au ni baya.

Kwa kweli, Yohana mtume mpendwa mwandani wa Yesu, alisema kwenye waraka wake wa Kwanza:

Na kila mwenye matumaini haya katika yeye hujitakasa, kama yeye alivyo mtakatifu. Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi. Nanyi mnajua ya kuwa yeye alidhihirishwa, ili aziondoe dhambi; na dhambi haimo ndani mwake. Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi; kila atendaye dhambi hakumwona yeye, wala hakumtambua. Watoto wadogo, mtu na asiwadanganye; atendaye haki yu na haki, kama yeye alivyo na haki; atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili, Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi. Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu wazao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu. Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na wa Ibilisi nao. Mtu ye yote aisiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake. Katika fungu hili moja tunaona makubaliano na yale tumesoma kufikia hapa. Uasi unafafanuliwa hapa kama dhambi, (yaani,

kutotii amri ya Kristo), zikipatana na mafungu tuliyojadili katika Matayo 7 na 13. Tunaona pia kwamba Yesu alikuja kuharibu kazi za Ibilisi; sio tu kusamehe dhambi zetu, bali kutuweka huru kutoka dhambini—kuvunja minyororo na kutuachilia kutoka kwa Sheria ya Dhambi na Mauti. Tena, maridhio Yake yalikuwa yatubadilishe, sio tu kufanya mabadilishano ya kisheria.

Hata hivyo, fungu hili liliingizwa hapa kuondoa uwongo ya haki ya mabadilishano. Yesu hakuteseka na kufa kwa ajili yetu ili tukubali tu haki ya kiroho na kubahatisha ambayo kwa ukweli haionekani katika maisha yetu. Alikuja kuharibu kazi ya Ibilisi, ili kupitia kwake tuweze kuzaliwa tena tukiwa huru kutoka dhambini, na kutembea kwenye haki YENYEWE kwa nguvu za Roho Mtakatifu. Yohana anasema kwamba yeye ATENDAYE haki NI mwenye haki, sio yeye aaminiye kuwa yeye ni mwenye haki “katika Kristo.” Kwa ukweli, anasema wazi HAKIKISHA HAKUNA MTU ANAWADANGANYA kinyume ha hili! Je, tumekubali udanganyifu wa “injili” ya uwongo? Tena Yohana anasema kwamba yeye asiyetenda haki ni wa Ibilisi. Hii si haki ya mfano hapa; kwa wazi mtu hawezi kutenda kitu kisicho kuweko. Hii inarejelea haki halisi, inayoishi ndani mwetu, hili ndilo kusudi la maridhio ya Kristo!

Usisahau Sehemu ya Pili

Fikira ya wokovu wa sehemu mbili lilikubalika na wote katika kanisa la Kwanza. Kwa ukweli, wachache katika historia ya

kanisa la kwanza walioamini katika yale yanayofikiriwa kuwa othodokisi (kweli)—yaani ni: utwaa, azimu hali mbele, na usalama wa milele usio na masharti—walikuwa ni Wagnostiki. Hilo ni sawa, wa heretiki (mwalimu wa mafundisho ya uwongo) ambao Yohana alituonya kuwahusu katika nyaraka zake—hao ambao kanisa la kwanza liliwashuku kwa karne nyingi—ndio watu pekee walioamini fikira hizi

Tayari tumeona Yesu akifundisha kwa mapatano sehemu zote mbili za wokovu—ambazo zimefafanuliwa hapa kama kujipatia uraya kwenye Ufalme kwa njia ya neema kupitia imani halafu kudumisha uraya kupitia uhusiano wa upendo wa kutii na Kristo, kudumu ndani yake. Paulo alitoa mfano kama huu katika waraka wake kwa Kanisa la Korinto kupitia ushahidi wa Waisraeli:

Kwa maana, ndugu zangu, sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita kati ya bahari; wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na katika bahari; wote wakala chakula kile kile cha roho; wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo. Lakini wengi sana katika wao, Mungu hakupendezwa nao; maana waliangamizwa jangwani. Basi mambo hayo yalikuwa mifano kwetu, kusudi sisi tusiwe watu wa kutamani mabaya, kama wale nao walivyotamani. Wala msiwe waabudu sanamu, kama wengine wao walivyokuwa; kama ilivyoandikwa, Watu waliketi kula na kunywa, kisha wakasimama wacheze. Wala tusifanye uasherati, kama wengine wao walivyofanya, wakaanguka siku moja watu ishirini na tatu elfu. Wala tusimjaribu Bwana, kama wengine wao walivyomjaribu, wakaharibiwa na nyoka. Wala msinung’unike, kama wengine wao walivyonung’unika, wakaharibiwa na mharibu. Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani. Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke. (1 Wakorinto 10:1-12).

Yuda, nduguye Bwana wetu, kwenye mstari wa tano wa waraka wake anasema hivyo hivyo: Tena napenda kuwakumbusha,

ijapokuwa mmekwisha kujua haya yote, ya kwamba Bwana, akiisha kuwaokoa watu katika nchi ya Misri, aliwaangamiza baadaye wale wasioamini. (Yuda Mstari wa 5.)

13

Wengi wetu tunafahamu hadithi ya Kutoka Misri. Mungu alionyesha ishara na miujiza kwa makusudi ya kusababisha Farao wa Misri awaachilie watumwa wao Waisraeli. Kilele cha hii miujiza kilikuwa kuwaokoa wazaliwa wa kwanza wa Waisraeli wote kupitia kwa damu isiyokuwa na mawaa ya mwana kondoo wa pasaka.

Kupitia kuingilia kwa miujiza kwa Mungu, Waisraeli waliokolewa kutoka nchi ya Misri, wanaume zaidi ya 6,000 waliotimiza umri wa kupigana na idadi isiyojulikana ya wanawake na watoto. Hii inafikisha idadi ya milioni mbili. Waisraeli wanaokolewa kutoka kwa kifungo cha Wamisri kwa kutembea nchi kavu ndani ya Bahari ya Shamu. Hili ni dhihirisho la ajabu la nguvu na neema ya kuokoa ya Mungu.

Lakini huo sio ndio mwisho wa hadithi hii—ijapokuwa sisi wa kisasa mara nyingi hukoma hapo. Kiini cha muhimu ni kufikiri hili: je, ni watu wangapi kweli walifaulu kufika nchi ya ahadi? Ni WAWILI tu! Waisraeli waliookolewa walikuwa waasi, wenye shingo ngumu, waabudu sanamu, wakulalamika, na hata waoga, yote haya kwa sababu ya kutoamini kwao. Matokeo? Hata kama waliokolewa kutoka Misri, ni watu wawili tu wenye umri wa kupigana walifaulu kufika nchi ya ahadi. Sababu? Waraka wa Paulo kwa Waebrania inasema dhambi na uasi, kutokana na kutoamini:

“Kwa maana ni akina nani waliokasirisha, waliposikia? Si wale wote waliotoka Misri wakiongozwa na Musa? Tena ni akina nani aliochukizwa nao kwa miaka arobani? Si wale waliokosa, ambao mizoga yao ilianguka katika jangwa? Tena ni akina nani aliowaapia ya kwamba hawataingia katika raha yake, ila wale walioasi? Basi tuaona ya kuwa hawakuweza kuingia kwa sababu ya kutokuamini kwao. (Waebrania 3:16-19 sisitizo limeongezwa nami). Kwa hivyo, Paulo na Yuda wanaeleza kwamba tukio hili lilitokea kuwa mfano wetu. Wazi, mwana kondoo wa pasaka alikuwa

ni aina ya sadaka ya Kristo ya kujitolea na kumwaga damu. Kutembea kwa Bahari ya Shamu ni mfano wa ubatizo. Kuokolewa kutoka Misri ni mfano wa kuokolewa kutoka kwa minyororo yetu kwa Dhambi na Mauti, Misri ikiwakilisha ulimwengu ulioanguka. Jangwa linaakilisha wakati wetu wa kujaribiwa na kukua—nafasi yetu ya kuonyesha imani yetu kupitia utii, kujiachilia kwake, na utakatifu wetu wa kiroho. Nchi ya ahadi inawakilisha mbinguni, ambayo inakuja kwa kujitahidi na kuvumilia, ikihitaji ujasiri na kujitolea.

Sasa ukitazama maelezo ya Kutoka na uyalinganishe na maisha yetu ya Ukristo, tutaona kuwa damu iliyomwagika ya Kristo, ubatizo, na kuokolewa kutoka Dhambini na Mautini SIO hakikisho la kuingia mbinguni. Inagharimu uvumilivu kwa imani na utii kuingia kwenye hayo malango ya lulu; inagharimu ufuasi wa uaminifu kwa Yesu. Bado wakati watu watumiapo neno “kuokoka,” wanamaanisha kuokoka kuingia mbinguni. Kwa upande mwingine, wakati waandishi wa Agano Jipya wanasema mtu “ameokoka,” wanamaanisha kuokoka toka Dhambi na Mauti—huru kutembea kwa utakatifu na haki. Uzima wa milele utapatikana tu kupitia kwa kutembea kwa utakatifu na haki.

Paulo alisema katika waraka wake kwa Warumi: “Bali sasa kwa kuwa mmewekwa mbali na dhambini na kufanywa matumwa wa Mungu, mnayo faida yenu, ndiyo kutakaswa, na mwisho wake ni uzima wa milele” (Warumi 6:22). Ninakusihi usome sura hii yote mwenyewe kwa muktadha. Hata hivyo kwa ajili ya ujasiri, hebu tuangazie fungu hili moja. Hapa tunaona kuwa kupitia kwa Kristo tumefunguliwa toka dhambini na kufanywa watumwa wake Mungu. Hili linasababisha utakaso wetu (au utakatifu wetu). Matokeo: uzima wa milele. Kuokolewa toka kwa Sheria ya Dhambi na Mauti inatuweka huru toka dhambini, ikituwezesha kuwa watakatifu. Ni huu utakatifu “katika jangwa la maisha” ndio unatufanya tustahili kutembea na Kristo tukiwa weupe (kumbuka Ufunuo Sura ya 3).

Hivyo basi, je, hilo linamaanisha hatuna usalama wa milele? Sawa, ndio na pia la.

Salama Katika Kristo Kumbuka awali nilisema kwamba usalama wetu wa milele ni wa hakika tu kama tunavyo mgeukia Mungu. Kumfuata Kristo ni

njia salama ya kwenda mbinguni, maana hapo ndipo alipo! Bali ikiwa kwa sekunde moja tunafikiri tunaweza kufuata mwili wetu, dhambi, na ulimwengu na tutokezee kwenye malango ya lulu, tumedanganyika vibaya.

Paulo alisema katika waraka wake kwa Waebrania (kwa maoni yangu, fungu moja taratibu sana kwenye Maandiko yote). Maana, kama tukiendelea kufanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, haibaki tena dhambi kwa ajili ya dhambi; bali kuna kuitazamia hukumu kwenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao. Mtu aliyeidharau Sheria ya Musa hufa pasipo huruma, na neno la mashahidi wawili au watatu. Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho wa Neema? Maana twamjua yeye aliyesema, Kupatiliza kisasi ni juu yangu, mimi nitalipa. Na tena, Bwana atawahukumu watu wake. Ni jambo la kutisha kuanguka katika mikono ya Mungu aliye hai. (Waebrania 10:26-31).

Kwa hivyo, kutenda dhambi makusudi baada ya kumgeukia Mungu inatupa ujasiri mwingi sana ya kwamba “tunatarajia

hukumu ya kutisha.” Mafundisho ya usalama milele usio na masharti ulikuwa mgeni kwa waandishi wa Agano Jipya na kanisa la kwanza.

Hata hivyo, Maandiko yananena juu ya usalama wa milele ulio na masharti. Katika waraka wa kwanza wa Yohana, anasema: “Nimewaandikia mambo haya ninyi mnaoamini katika jina la Mwana wa Mungu, ili mweze kujua kuwa mna uzima wa milele.” (1 Yohana 5:13). “Mambo haya” inarejelea kwa yaliyomo kwenye waraka huo. La kupendeza ni, mfumo uliofupishwa wa huu mstari unatumika sana kwa kipindi kijulikanacho cha uinjilisti kudhibitisha kwamba tunaweza kuwa na ujasiri wa usalama wa milele usio na masharti, bila marejeleo yoyote kwa yaliyomo kwenye waraka wenyewe.

Basi yalikuwa “mambo gani” ambayo Yohana aliandika kutuhakikishia kuwa tuna uzima wa milele? Hapa tunanukuu kutoka kwenye huo waraka. Tazama masharti (ikiwa/halafu) nukuu:

14

Ikiwa tunasema tuna ushirika na Yeye lakini tunatembea gizani, tunadanganya na kweli haimo ndani mwetu; bali ikiwa tunatembea kwenye Nuru kama vile Yeye alivyo Nuru, tuna ushirika mmoja na mwingine, na damu ya Yesu Mwanawe inatutakasa toka kwa dhambi zote. (1 Yohana 1:6-7). Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua Yeye, ikiwa tunashika amri zake. Yeye asemaye, “Nimemjua,” wala hazishiki amri zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake; lakini yeye ashikaye neno Lake, katika huyo upendo wa Mungu umekamilika kweli kweli. Katika hili twajua ya kuwa tumo ndani yake: yeye asemaye ya kuwa anakaa ndani yake, imempasa kuenenda mwenye vile vile kama Yeye alivyoenenda.” (1 Yohana 2:3-6). Msipende ulimwengu wala vitu vilivyomo ulimwenguni. Ikiwa mtu anaupenda ulimwengu, upendo wa Baba haumo ndani yake. Kwa kuwa vyote vilivyomo ulimwenguni, tama ya mwili na tama ya macho na majivuno ya kiburi cha maisha, havitoki kwa Baba, bali vinatoka ulimwenguni. Ulimwengu unapita, na pia tamaa zake; bali yeye atendaye mapenzi ya Mungu ataishi milele. (1 Yohana 2:15-17).

Yeyote atendaye dhambi pia afanya uasi; na dhambi ni uasi. Mnajua kwamba Alikuja kuondoa dhambi; na ndani yake hakuna dhambi. Hakuna yeyote akaaye ndani mwake afanyaye dhambi; hakuna afanyaye dhambi amewahi kumwona au kumjua.Watoto wadogo, hakikisha mtu asiwadanganye; yeye afanyaye haki ni mwenye haki, vile yeye aliye mwenye haki; yeye afanyaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa maana Ibilisi ndiye ametenda dhambi tangu mwanzo. Mwana wa Mungu alikuja kwa makusudi haya, kuharibu kazi ya Ibilisi. Hakuna yeyote aliyezaliwa na Mungu afanyaye dhambi, kwa sababu mbegu Yake inakaa ndani mwake; hawezi kufanya dhambi kwa kuwa amezaliwa na Mungu.

Je, ni baina ya marsharti yapi yenye Yohana alielezea “ili tujue kwamba tuna uzima wa milele.?”

• Tembea kwenye nuru. • Shika amri ya Yesu. • Tembea jinsi alivyotembea. • Msipende ilimwengu na vitu vilivyomo ulimwenguni. • Fanya mapenzi ya Baba. • Kaa ndani ya Kristo. • Tenda haki. • Wacha dhambi.

Je, kuna mtu yeyote alikupitishia kwenye orodha hii wakati “injili” iliakilishwa kwako? Uchunguzi wa makini unaonyesha kwamba hii ni Injili kulingana na Yesu upya tena; yaani: tubu na umfuate Yeye! Kwa hivyo,

sharti pekee la usalama wa milele ni kutubu na kumfuata Yesu. Ni rahisi tu hivyo. Kwa bahati mbaya nafasi yake imechukuliwa na “amini katika Yeye.”

Hesabu Gharama

Basi, Yesu alifunza nini kuhusu kumfuata Yeye? Katika Sura ya kumi na nne ya Injili ya Luka, Yesu aliliambia kundi kubwa la wafuasi-watarajiwa kile inge gharimu kuwa mfuasi wake. Kwa kweli hakuwa anaiiga mitindo ya uvutio, ya kutekenya-masikio ya kanisa la sasa:

Makutano mengi walipokuwa wakifuatana naye, aligeuka akawaambia, Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu. Mtu yeyote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu. Maana ni nani katika ninyi, kama akitaka kujenga mnara, asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama, kwamba anavyo vya kuumalizia? Asije akashindwa kuumaliza baada ya kuupiga msingi, watu wote waonao wakaanza kumdhihaki, wakisema, Mtu huyu alianza kujenga, akawa hana nguvu za kumaliza. Au kuna mfalme gani, akitaka kwenda kupigana na mfalme mwingine, asiyeketi kwanza na kufanya shauri, kwamba yeye pamoja na watu elfu kumi ataweza kukutana na yule anakuja juu yake na watu elfu ishirini? Na kama akiona hawezi, hutuma ujumbe kutaka sharti za amani, mtu yule angali mbali. Basi, kadhalika kila mmoja wenu asiyeacha vyote alivyo navyo, hawezi kuwa mwanafunzi wangu. Chumvi ni kitu chema; lakini ikiwa imeharibika, itiwe nini ikolee? Haiifai nchi wala jaa; watu huitupa nje. Mwenye masikio ya kusikilia, na asikie. (Luka 14:25-35). Kuna mengi hapa. Kwanza kabisa, Yesu anaamurisha utii kamili. Hakuna chochote kilicho cha muhimu sana: familia yako,

starehe yako, mali yako, hata pia na maisha yako! Anataka VYOTE! Vile vile anataka wafuasi wake kuvumilia hadi mwisho. Anataka kuwa tuhesabu gharama. Hakuna urafiki nusu au wa wakati mzuri. Anataka tu wafuasi watakao mfuata kwa mazuri na mabaya.

La kufuata, Anasimulia hadhiti ya kupendeza juu ya mfalme aliye na uadui na mfalme mwenye nguvu kumliko. Ninapenda kushiriki nawe ufunuo muhimu toka kwa hili fumbo fupi. Njia ya maana katika taswira hii ni kutafuta sharti za amani. Isipokuwa kama unapendelea uharibifu wa hakika. Sawa, hili linafanana na hali yetu ya kushindwa kuamua na Mungu vyema zaidi. Katika dhambi zetu, tu maadui wa Mungu, wanaopenda nafsi zao, ulimwengu, na vivutio vya Shetani, na mwili wetu ni “mfalme.” Tumesukumwa dhidi ya vikwazo tusivyoweza kuviepuka na Mfalme Aliye Pote. Hata hivyo, ukweli unatofautiana na hadithi hii kidogo—yule Mfalme Aliye Pote ametunyoshea masharti ya amani, kuliko njia ile nyingine. Tunahitaji tu kukubali Masharti yake na tuishi kwa amani Naye.

15

Unaona, wakati nguvu dhaifu inakabiliwa na uharibifu wa hakika, hawana kitu cha kujitetea nacho. Mfalme Mwenye Nguvu anaweka masharti. Masharti ya Mungu ni atatuweka huru toka Dhambi na Mauti na atupe nguvu za kutembea kwenye uhuru kutoka kwa dhambini. Tunahitaji tu kutoa kila kitu bila masharti na kumtii Yeye kuanzia sasa na kwendelea. Kutii kunatuongoza kwenye uzima wa milele; kushindwa kutii kunatuelekeza Kuzimu.

Hata hivyo, hapa ndipo inapendeza sana, kwa sababu wakereketwa hawakukubali masharti Yake, bali waliimarisha masharti yao wenyewe. Thiolojia kereketwa inaelekea kitu kama hiki: tutakubali msahama wake, lakini hatuwezi (na hatutapaswa ku) tii amri Zake au kuhitaji kuyatoa maisha yetu kwa Mfalme.

Kote kwenye historia, wakati watu wameshindwa katika vita, wanachukuliwa mateka, mali yao inaibiwa, na wana bahati iwapo watauokoa uzima wao. Bado wengine hufikiri kuwa wanaweza kujitoa kwa Mungu na waweke masharti yao wenyewe ya amani. Haya yote Yeye akiwa ametupa amani na masharti yaliyo wazi, na nitasema, yanayokubalika kabisa. Mungu sio mdhalimu, lakini anaweza (na ata) tushinda kwa njia zote mbili. Bado anatupa chaguo la kujitoa kwa hiari na tufanyike wana, au tushindwe kwa hiari na kuadhibiwa kama maadui wa Ufalme wake. Kwa bahati mbaya, wengi hawana kidokozi kuhusu haya masharti ya amani ni nini, kwa sababu “masharti” ya uongo yanayo tangazwa wazi na wajumbe waongo, kana kwamba wao wenyewe walitumwa kutoka kwa uwanja wa mfalme. Bali muda wote huu wajumbe wa kweli wa Mfalme wametoa masharti Yake ya kweli ili wote wayaone kwenye Maandiko Matakatifu.

Katika mstari wa Mwisho wa fungu hili, Yesu anaendelea kufafanua chumvi ipotezayo ladha yake. Ikiwa Wakristo ni chumvi na nuru, na wengine wanaweza kupoteza ladha yao, na iitwe bure na kutupwa nje, kwa uwazi hili ni rejeleo kwa mtu anayepoteza wokovu wake. Sijui vile mtu anaweza hitimisha kinyume na hili.

Mchanganuo wa Mwisho

Basi uchanganuzi wa mwisho ni nini? Wakeretetwa wangetufanya tuamini kwamba Yesu alikufa kuridhia ghadhabu ya Mungu kwa mabadilishano ya haki, Yesu akichukua pahali petu pa adabu tuliyostahili. Kwa kinyume, kanisa la kwanza lilifundisha kwamba Yesu alitumwa kutufungua kutoka kwa minyororo ya Dhambi na Mauti na kuigeuza mioyo yetu kurudia Mungu kwa toba, kumfuata Yesu kwa utii wa upendo.

Wakereketwa walifundisha kwamba tunahitaji tu kuamini na tutakuwa tumeokoka kuingia kwenye malango ya lulu, bila masharti. Kanisa la kwanza lilifundisha kwamba ni lazima tutubu na kubadilika na kubatizwa, kutoa maisha yetu kikamilifu kwa Kristo. Kwa neema kupitia imani tunaokolewa—yaani, tunabandikizwa kwa Mzabibu. Lakini huu tu ni mwanzo wa wokovu, hatua ya kwanza.

Thiolojia ya ukereketwa inasababisha utii kwa Kristo kuwa kama ni chaguo. Wokovu unahakikishwa kwa imani bila kujali nama mtu anaishi.

Wanaenda hadi umbali kwamba kufanya wema ni kitu kibaya kwa kuita haki yetu matambaa chafu. (Tazama Isaya 5:20, Yuda mstari 4, na 2 Petro 3:14-18 kwa ufunuo zaidi). Maandiko ya kanisa la kwanza yanafundisha kwamba utii wetu kwa amri za Kristo, kwa upendo, unahitajika kwa mina ajili ya wokovu. Sio kwamba tunanunua wokovu wetu. Bali, utii wetu unaonyesha moja kwa moja upendo na imani yetu. Tunadanganya ikiwa tunasema tunampenda na kumwamini Kristo na hatufanyi yale anasema. Ndio maana Paulo alitwambia “tuutimize wokovu wetu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka.” (Wafilipi 2:12-13).

Hivyo hivyo Petro alisema,

Kwa maana wakati umefika wa hukumu kuanza katika nyumba ya Mungu; na ikianza kwetu sisi, mwisho wao wasioitii injili ya Mungu utakuwaje? NA MWENYE HAKI AKIOKOKA KWA SHIDA, YULE ASIYEMCHA MUNGU NA MWENYE DHAMBI ATAONEKANA WAPI?” (1 Petro 4:17-18).

Ukristo wa kisasa unatufanya tuamini kwamba ili tuingie mbinguni, li lazima tu tuwe na thiolojia iliyo sawa na kuamini mambo sawa, mara nyingi haitegemei namna tunaishi. Hata hivyo, Yesu alitufundisha moja kwa moja vile hukumu itakuwa:

Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake; na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji awabaguavyo kondoo na mbuzi; atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto. Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njooni, mliobarikiwa na Baba yangu, uruthini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu; kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa uchi, mkanivika; nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia. Ndipo wenye haki watakapomjibu, wakisema, Bwana ni lini tulipokuona una njaa, tukakulisha, au una kiu tukakunywesha? Tena ni lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha, au u uchi, tukakuvika? Ni lini tena tulipokuona u mgonjwa, au kifungoni, tukakujia? Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amini, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi. Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake; kwa maana nalikuwa na njaa, msinipe chakula; nalikuwa na kiu, msininyweshe; nalikuwa mgeni, msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike; nalikuwa mgonjwa, na kifungoni, msije kunitazama. Ndipo hao pia watajibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona wewe una njaa, au una kiu, au u mgeni, au u uchi, au u mgonjwa au u kifungoni, tusikuhudumie? Naye atajibu, akisema, Amini, nawaambia, Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi. Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele. (Matayo 25: 31-46).

Kondoo hawatengwi na mbuzi kulingana na thiolojia yao, yale wanaoamini, au kama wana au hawana imani. Yesu, akiwa

msimulizi na lengo la hadithi hii, anasema kondoo na mbuzi mwishowe watatengwa kulingana na namna walivyoishi—matunda yao. Mbuzi wanapokea adhabu ya milele na kondoo raha ya milele kulingana na yale walitenda katika maisha yao.

16

Basi utaamini nani, wakereketwa au Yesu? Ikiwa ulijibu Yesu, kwa urahisi, ishi maisha yanayolingana na Injili Kulingana na Yesu: tubu na Umfuate Yeye! Rejelea na usome herufi nyekundu tena katika nuru ya yale yote tumejifunza hapa, na kwa urahisi, tii yale Alisema. Halafu soma tena ukumbusho wa Agano Jipya katika nuru ya Injili ya Yesu. Utaona mapatano ya kustajabisha kwa yale yote yamefundishwa hapa. Magamba yataondolewa machoni pako na utakuwa huru kumfuata Kristo bila kuzuiliwa na chochote.

Kuhusu Mwandishi

Marc Carrier ni mwandishi, mkufunzi, mnenaji, kiongozi wa karakana, na mtume aliyejitolea kuwahamazisha watakatifu kwa ajili ya mavuno ya siku za mwisho. Marc ameandika Funguo za Upanuzi wa Ufalme na Project Management Essentials: A Complete Multimedia Curriculum for Christian Homeschoolers. Ameandika pamoja na wengine vitabu vingine juu ya malezi, ufuasi kwenye familia, maongozo ya kibinafsi ya kiroho.

Marc ni tabibu na mkufunzi wa utendaji hai wa upanuzi wa Ufalme. Marc anakaribisha nafasi ya kufundisha au kunena juu ya hoja yake anayoienzi sana (Upanuzi wa Ufalme) kwenye eneo lako. Marc pia hufurahia kushiriki kwa dhati upanzi wa kanisa, ufuasi, uongozi, ndoa, malezi, ufuasi kwenye familia, usimamizi wa nyumbani, ukuaji wa kiroho wa binafsi, usimamizi wa miradi na uanzishaji wa biashara. Tafadhali tuma barua pepe: [email protected] kupanga karakana au kunena. Kujifunza zaidi juu ya Nyenzo za Marc tembelea: www.valuesdrivenfamily.com. First Kiswahili Edition November 2010 Translators: Bahati Community Centre Secondary School Languages Department:

• Supervisor: Patrick Wafula Wanyama. • Miss Maureen Mutindi: Chief Translator Kiswahili. • Titus Sakwa: Translator: Kiswahili. • Peter Wanderi Ndirangu: Consultant/Translator.

Contacts: [email protected] Tel: +254 721 991 413 P.O Box 1242-00100 G.P.O Nairobi Kenya.

17

FUNGUO ZA UPANUZI WA UFALME

18

Neno la Utangulizi

Marc aliponijia na kuniambia kuhusu uandishi wa utangulizi wa kitabu hiki alisema kuwa ni kitabu chenye manifesto ya upanuzi

wa ufalme kinacholenga kuwazindua watakatifu kwa mavuno. Kwangu ulikuwa kama utani kwani ni mara ngapi tumechukizwa na vitabu ambavyo haviambatani na jinsi watu wanavyosema kuvihusu? Ni sababu ya sifa za Marc za uwazi na uaminifu zilizonisukuma kuweka shauku kando na kukisoma kitabu hiki.

Nilipokuwa nikisoma faslu za kwanza kwanza, nilijipata nimezama zaidi na kupendezwa na utume katika kitabu hiki. Baada ya kusoma faslu tano,niling’amua kuwa Marc hakuwa akinitania kuhusu kitabu hiki. Mtazamo wa Marc juu ya ukristo wa Wamarikani ni chanya si ule wa kukashifu ambao sisi husoma na hautupi suluhisho. Msimamo na mtazamo wake wa kibiblia jinsi ukristo wafaa kuwa sio mazoea tulionayo; ni kitu kisicho na ubishi.

Ukweli ni kwamba wachungaji wa kisasa wana kazi nyingi ya kufunza wakristowatazamaji madhabauni, kufunza ambako hakuzai ukristo dhabiti. Tunasoma katika matendo ya mitume, Mathalani anaandika: “Ukristo ulikuwa hali ya maisha, sio misururu ya mafunzo ya dini. Wafuasi wakale walitegemea njia ya roho na kujifunza kupitia hali ya maisha ya waumini komavu (uanafunzi). Tumebadili hii na kuwa mikutano na taarifa badala ya kutembea katika nguvu za roho. ” Hii ni habari ya kusikitisha lakini ndio ukweli.

Kwa muda mrefu Marc ameweza kusoma utamaduni wa mwanadamu ili kutuletea mtazamo mpya wa ukristo ambao unauwezo wa kubadilisha ulimwengu. Suluhu ya Marc ni turudi katika mtindo wa kanisa la zama ambalo viongozi walikuwa vigezo si watu wa kuonekana (wasi vitendo). Imani iliyowapa watakatifu ushindi ilipeanwa kupitia kwa uanafunzi wa mtu binafsi. Sababu waumini komavu walihusika katika maisha ya wengine, mwili wa Kristo ulibaki mkumbwa. Kazi ya Marc si tu mwanamapinduzi wakileo na mpigadebe wa watu kuishi kiungu. Anachofanya ni kushiriki nasi jinsi anavyoishi katika maisha yake ya kila siku. Marc anaubiri anachofanya. Manifesto kuhusu upanuzi wa ufalme? Ndio, ni ukweli. Ametuwekea mpango mwepesi wa injili ambao sote twaweza ishi kwao na kusonga mbele. Viongozi wakristo itakuwa vyema kusoma hiki kitabu na kutumia kanuni zake. Labda tutaona watakatifu wakizinduka kwa mavuno yaliyopo!

Steve Gallagher, MKuu wa makasisi shule ya heshima, mhasisi dhehebu la Pure Life Ministries na mwandishi wa vitabu ainati vikiwemo; Standing Firm Through The Great Apostasy na Intoxicated with Babylon. Steve Gallagher, Dean of Ellerslie School of Honor, Founder of Pure Life Ministries, and Author of numerous books, including Standing Firm Through the Great Apostasy and Intoxicated with Babylon.

Utangulizi

Kitabu hiki awali ilikuwa imeandikwa kwa Kiingereza. Wengi kazi masaa lilifanyika kutafsiri kitabu usahihi. Hata hivyo, kunaweza kuwa na tafsiri makosa. Kama kuna makosa, tafadhali utusamehe. nakala A free wa toleo la Kiingereza inaweza kupakuliwa kwenye Internet saa http://www.valuesdrivenfamily.com. Unaweza rejea toleo hili ili kuhakikisha lengo la kitabu.

Nilianza kujihusisha na makundi ya kijamii ya viongozi wa huduma nyakati za nyuma. Sikujua nifanye nini nayo (makundi). Ulianza kama wenzo wa kuunganisha watu wenye maono mamoja ili kuendeleza kazi ya Wito Mkuu. Nimegundua kuwa sisi viongozi wa huduma ni wachache sana wana mtazamo mzuri na tekelezi ili kukimu wito mkuu. Wengi wetu huona sehemu yetu ni kuwa kanisani, katika jamii, dini ama hadhira. Hata hivyo yafaa tuwe na fikra pevu. Tunaishi hatua za mwisho za kubahatisha. Tuko misimu michache kutimiza wito mkuu, mimi na wewe sehemu kubwa sana walakini, ninadhani kuwa wengi wetu tumefunzwa kufikiri kifinyu. Tumefungwa na kubanwa na mifumo ya kanisa. Hata hivyo jinamizi baya la shetani lakaribia kutimika. Ikiwa imewasilishwa kwenye wenzo huu mdogo ni ukweli kutupa ukweli kamili na nguvu ili kukuza ufalme na viwango ambavyo hatujawahi fikria kamwe. Katitka kitabu hiki nitafunua maono pevu, tekelezi na mbinu na nyenzo aula za kufungua na kupanua ufalme. Siongei kuhusu siri za ukuwaji ama hata upandaji wa kanisa, lakini kitu chepesi sana na njia bora na rahisi ya kupanua ufalme. Ndio makanisa yatakua na kupandwa kwa sababu ya haya. Hata hivyo, haya tunamwachia Mungu. Wito wetu ni kufanya wanafunzi ambao Yesu alisema atajenga kanisa lake.

Mambo ambayo nitashiriki kwenye hiki kitabu ni ya kihalisia-Nime shuhudia. Yana kusudiwa wahudumu ambao kazi nikuzindua

watakatifu; hata hivyo, hiki kitabu ni cha manufaa kwa wewe mtakatifu pia ambaye umejitolea kutimiza wito mkuu. Soma na utafakari kuhusu utume uliyomo utazinduliwa kwa nia moja: Kutimiza wito mkuu kwenye kizazi hiki. Mungu Mwenye Enzi na

nguvu za Roho Mtakatifu zikuongoze kwa kuchukuwa taifa kwa utakatifu wake. Amina.

Utukufu wa Mungu

Nitaanza kwa kusema kuwa wengi wetu, mpango wa Mungu kuokoa mwanadamu umejikita kwa mtu badala ya kujikita kwa Mungu. Tunaangazia sana wokovu na faida za kuwa na uhusiano na Mungu. Hivyo basi tunaishi maisha yetu na kuyapanga kuhudumia watu katika fikra zetu badala ya Mungu. Tukiwa waaminifu na tuchunguze mioyo yetu, tunaweza pata kuwa huduma zetu zinatuhudumia. Katika kiwango Fulani, tunatafuta ufanisi wa huduma ili kujitimizia mahitaji yetu kukamilishia Mungu mengi; haya ni malengo yaliyopotoshwa na utashi wa kibinafsi badala ya kutiwa motisha na utukufu wa Mungu.

Ukweli ni kwamba Mungu wetu Mtakatifu na mwenye haki ni Wa kujitakia na ni haki hivyo. Kila kitu kilichokuwepo, kilichopo na kitakachokuwa ni cha Mungu na kwa ajili ya utukufu wake, hapana jingine. Kupitia kwa kuanguka kwa Adamu na Hawa, shetani aliaharibu mipango ya Mungu ili kujikombakomba kupitia kwa viumbe wake. Shetani hudhihaki Mungu kwa kusema, ‘Ona wanadamu ulioumba kwa utukufu wako wanifuata. Wote hunisikiliza na kutenda dhambi. ’ Haya ni maudhi kwa Mungu. Kwa hivyo kusudi la Mungu la ukombozi kunyenyekea na kula yamini kwa muumba wetu badala ya mwongo-ni mipango ya kurejesha utukufu anaostahili Mungu, sio kutuondoa kutoka kuzimuni. Taswira kuu ni hii: Tuko katika vita vikuu. Kuna vita baina ya Mungu na hasidi

19

wake shetani, kwa nafsi na viapo vya wanadamu. Tuko katikati ya vita, lakini sisi si walengwa. Ni baina yao. Nilivyo sema hapo awali, utukufu wa Mungu sasa umeelekezewa shetani na kazi yake kupitia dhambi zetu.

Yule atendaye dhambi ni wa shetani, sababu mwovu amekuwa akitenda dhambi tangu jadi. Sababu ya mwana wa Mungu kuja ilikuwa kuharibu kazi ya shetani (1 Yohana 3:8).

Mungu kupitia kwa Yesu Kristo, amerejesha utukufu kwa walengwa wa kweli kwa kubadilisha utii kwake Mungu na

kubadilisha maisha yetu. Chochote ambacho si utii na kubadilika si cha kumtukuza Mungu. Mungu anahitaji roho zetu na utii, na tunabarikiwa tunapopata maono ya kumtumikia kwa utukufu wake. Ila ni kuwa katika utafutaji wa Mungu tuna dhana ya kuwa kuwafikia na kuwahudumia waliopotea ndio mwisho. Mwisho wake tunalenga kuokoa nafsi badala ya kubadilisha na kutafuta kukimu mahitaji badala ya kuwakaribisha kwenye maisha ya ufalme wa mbinguni. Hata ninasema tena: Hatima ya haya yote ni kuleta utukufu kwa Mungu. Jukumu la urejesho linamwelekea Mungu Kugeuza bila kubadilisha, huokoa baadhi kutokana na mwisho mbaya. Hata hivyo hakuleti utukufu kwa Mungu. Unaweza ona shetani akimdhihaki Mungu “Mwanadamu uliyemuumba anaendelea kuamini uongo wangu na kupenda malimwengu na dhambi akijua kuwa uliteseka na kufa kwa ajili ya dhambi hizo. ” Mkristo ambaye hajabadilika ni maudhi kwa Mungu. Shetani anafahamu fikra kuwa “muumini” asiye na manufaa ni maudhi kwa Msalaba, anakaidi nguvu za Roho za kubadili maisha na hufanya imani isipendeze walionje. Unaweza ona ni kwa nini ni muhimu kuwa kazi za huduma zilenge Mungu na utukufu wake wala si kwetu na mipango yetu.

Kuendelea na kazi bila kualika Ufalme pia ni upotoshi. Unadhani misaada ya serikali ama kazi za ajabu ambazo nchi za Kiisalamu zizalishazo mafuta hufanya kote ulimwenguni ni za kumtukuza Mungu? Hata! Ni kuwa huiba utukufu wa Mungu kwa sababu mwili wa Kristo wafaa kutimiza haja hizo. Hata hivyo, kukihimu mahitaji kimwili si mwisho. Lengo kuu ni kupeana uhuru kwa nguvu za Roho Mtakatifu kupitia kwa imani ndani ya Kristo-kupeana maji ya uhai ili kukata kiu, chakula halisi ili kushibisha utashi wa nafsi na ushindi wa kweli ili kupata amani iongezekayo. Tuliumbwa kwa ajili ya matendo mema na imani bila matendo ni bure. Hata hivyo, watu waliobadilika kabisa hufanya kazi kwa ajili ya Ufalme, sio tu kwa matendo mema pekee. Hapana jingine ila maisha yaliyobadilika humletea Mungu utukufu. Kubadili utii kutoka kwa shetani hadi kwa Mungu, mauti hadi maisha, kimwili hadi kiroho, dhambi hadi utiifu, kiulimwengu hadi kwa Ufalme. Hii humtukuza Muumba Wetu. Shetani hana wenzo. Kubadilika kabisa humpa mtu utashi wa Mungu na wenzake Utashi ambao hukatiki na humwongoza kwa huduma na kwa upendo, matokeo: Kutoka kabisa kwa ya kidunia na hata tamaduni za ukristo ambazo huwaacha wanaokuona wamebung’aa kuhusu Mungu ambaye anaweza kubadilisha mwanadamu. Matokeo ya haya yote kupanuka kwa Ufalme kiuhai. Je, maisha yako huonyesha vipi utukufu wa Mungu? Je, na huduma yako inaleta manufaa gani kwa utukufu wa Mungu? Tafakari juu ya mambo kama haya.

Ufalme

Kristo alikarikabisha Ufalme. Lakini wakiristo wa kiinjili hukaribisha watu mbinguni ama tuseme kanisani badala ya kwenye maisha ya Ufalme. Tuna mazoea ya kuhubiri injili ya wokovu pekee kwa kukutana wala si kuwahusisha watu katika injili ya Ufalme (Soma Mathayo 4:23; 9:35; 24:14, Mariko 1:15, Luka 16:16). Mtazamo wake juu ya ufundishaji wa Ufalme(kuna marejeleo zaidi ya 100 kwenye vitabu vya Injili kuhusu Ufalme) vikitilia mkazo kazi yake ya urejesho na jinsi tunavyosanya viakustaajabisha?

Hii inaweza onekana kama hila tupu lakini inaweza dhihirisha umuhimu wa jinzi tunavyohudumia watu. Wakristo wa Kiinjili hupuuza msisitizo umuhimu wa maisha ya Ufalme na yanahusika mara nyingi wakitilia mkazo maswala mengine: mpangilio wakanisa na mahudhurio, mikakati ya mafundisho ya dini na kwa kiasi huruma. Hivi vyote hufanywa kwa lengo maalumu, hata hivyo kuna baadhi ya vitu ambavyo vinakosekana.

Hebu tujenge taswira hii kwa dhana na fikra. Mtu akishakuwa mhudhuria kanisa huwa mtazamaji. Huwaona wahudumu kama wa injili kama wenye majukumu kwenye huduma; vilevile huona huduma katika muktadha wa mikakati iliyomo kanisani. Mtu anapogeuzwa bila ya kubadilishwa huwa anashindwa kukumbatia hali ya maisha ya ufalme; wanaweza ama wasiweze kuingiliana (kuasili) na maisha ya kanisa. Hawabadiliki kwa muda mrefu, hata wakifanya hawakumbatii ama kujihusisha kwenye utume. Hawahamishi utii wao kutoka duniani hadi kwenye ufalme, kutoka mautini hadi maishani, utumwani hadi kwenye uhuru, mtazamaji hadi balozi na mwanajeshi, kimwili hadi kiroho. Tunaacha ukweli unaokusudiwa kwa kuzaliwa upya.

Matokeo ya kuachana, hakika ya mambo ya waliobadilika na waendakanisa hapana tofauti kubwa na walimwengu. Wapi uhuru, amana, furaha na maisha ya utele yaliyoadiwa na Kristo? Bahati mbaya yanakosekana sababu ukristo umekuwa masomo badala ya wa kubadili. Tunahusisa fikra badala ya roho zetu. Uzinzi umefanya ndoa nyingi kuporomoka, fadhaiko na majanga mengi yanayowafika wafuasi wa Kristo katika kiwango sawa na walimwengu wa kawaida si ya kupendeza. Mbona kujiunga?

Nadhani mwachano huu ni wa karne nyingi za jadi. Binafsi naamini kuwa kanisa la jadi lilikuwa na ubora kwa kutokuwa na kanuni. Maajabu! Ama? Najua lakini fikria kuhusu hayo: Ukristo ulikuwa hali ya maisha, sio misururu ya mafundisho ya kidini. Wafuasi wa zamani wa njia walijifunza na kutegemea Roho kupitia hali ya maisha ya waumini komavu. Tumebadili haya kuwamikutano na habari, badala ya kutembea kwa nguvu za Roho Mtakatifu.

Makanisa ya kiinjili ya kisasa yanapata mafundisho ya elimu potoshi ya kidini kutoka kwa Paulo bila kusisitiza mafunzo ya Kristo mwenyewe, na mahirimu wa Kristo (Yohana, Petero na Yona). Soma barua ya Yohana wa kwanza halafu Jona na Pauline. Toa darubini, utaona mchepuko wa ukristo wa kisasa. Hakika mafundisho ya Paulo ni kutoka kwa Mungu lakini yamewekwa kwenye muktadha wa kuelewa kwake hali ya maisha—maisha ya Ufalme. Mafundisho ya kidini Paulo hayakusudiwa kusomwa kwa misingi ya mfululizo wa barua. Paulo alikaripia wasomaji wake kuwa wafuate mifano yake na watazame wale wanaotembea kimtindo walionao ndani yao (Wafilipi 3:17). Alionyesha jinsi maisha ya Ufalme yalivyo na kufuatisha barua kuzungumzia masuala maalumu katika kanisa. Paulo (na Yesu) alituonyesha namna ya kuukumbatia Ufalme tukiyashinda ya ulimwengu—hawakutuambia tu ila walitenda ili wafanye wanafunzi. Yatupasa tufanye haya pia.

Tunaonyesha uhalisia Kristo kwa namna tunavyoishi. Hatuwezi kumkiri kwa vinywa na kumkana kwa hali za maisha yetu. Tukifanya hivi hatutafaulu katika maono yetu. Mfululizo wa mahubiri, madarasa ya uanafunzi ama kusoma vitabu hakutaonyesha hali ya maisha ya Ufalme ili wengine waige. Maisha yaliyobadilika yanafaa ili kubadili wengine. Hadi tukubali haya, hatuwezi kuza maisha ya Ufalme.

20

Namwomba mzingatie haya: Je, imani yako ya kutembea inaonyesha kutoka kabisa kwa ya ulimwengu—kujitolea kabisa kwa maisha ya Ufalme? Je umebadlishwa—unaishi maisha ya Utele? Je, maisha yako yanavutia? Na kama ndio, unafanyaje Kristo kuvutia? Tafakari kuhusu maswali haya.

Kupata Maono

Wale walio na maono ya Ufalme na wako kwenye utume haya mafundisho ni maji rweru na baridi ya kukata kiu; kwa wengine ni uchafu machoni pao, maudhi na kero. Hata hivyo, natumai mwasho kwa nafsi zenu utazaa lulu za thamani kubwa ambayo itaongeza utashi mkubwa zaidi wa kukuza utukufu wa Mungu. Najua kuwa kutoka kina cha roho ya muumini, lulu hizi zaweza zaliwa na zipo, hata hivyo zimemezwa na ulimwengu na njia zake zote. Yafaa tuwe zaidi ya misimamo yetu ya kidini na mila na tukubali maono ili kuwa kwenye utume. Haijalishi wewe ni wa dhehebu gani, dini, ama wapi unashiriki, ni kuhusu jinsi roho yako itakavyosalimisha kila kitu kwa sababu ya lulu ya thamani. Ikiwa utaapa kutii mifumo ama fikra tu badala ya utukufu wa Mungu, hutapata maono haya.

Huu ndio wakati wako wa kairos (kibiblia Kigiriki). Uliumbwa kwa ajili ya wakati kama huu. Tuko katika hatua za mwisho za madhari ya kihistoria. Mungu Anaorodhesha jeshi lake ili kuvuna mavuno ya mwisho. Tuko karibu sana na mwasho, na utume u karibu nasi. Hapana watazamaji katika mpasuko wa mwisho wa ufufuo. Je, waweza hisi hizi nyakati? Je, roho yako haidundi na maneno haya? Ndani ya nafsi yako unajua haya.

Kila mmoja wetu anaweza badili ulimwengu. Yatupasa kufikiria. Mtu mmoja akifunza wachache alichangia kuongezeka kwa idadi ya wakristo kwa 18% kwenye nchi ya Uhabeshi kwa miaka. Mmoja aliyekosa kupanda kanisa Rwanda aliweka mikakati upya baada ya kupata maono na kupelekea kubadilishwa kwa taifa milele—aliangamiza janga la ukahaba kabisa sehemu hiyo. Mmoja wa maaskofu mashuhuri jijini Nairobi, Kenya alifurushwa baada ya kupata maono. Tuzo yake? Sasa hivi ni kati ya msusuru wa wanafunzi bora 25,000. Hawa ni baadhi ya wale watakatifu wengi katika Ufalme wanaoleta utofauti ulimwenguni kwa utukufu wa Mungu. Si sababu za harakati za kisiasa ama utaratibu mzuri wa mafunzo ya kidini—walibadilisha maisha kwa mtazamo pevu na mipango tekelezi kwa kujihusisha katika utume. Kanuni zimebadilika. Mungu anaendelea kuorodhesha wanaohiari. Nani kati yetu hana utashi wa tunda sampuli hii?

Hata Mungu anapozindua watu Wake kwa matendo, bado wanakimbia kuenda jehanamu kwa wingi zaidi. Moto wake wa ajali unazidi kumeza mamilioni kila siku sababu hatutambui nyakati, na hatuhusiki katika kupeleka utume. Mungu anadhihakiwa na binadamu na shetani. Je, utashi wetu uko wapi? Je, tunajali kuwa watu ambao tunapatana nao wanaenda kuteseka kwa sababu ya ghadhabu za Mungu milele? Je hii haifanyi tufe kidogo kila siku? Machozi yetu kwao yako wapi?

Lango ni dogo na njia ni ndogo zaidi pia. Ufalme wa Mungu si wa kutembea na kuingia hivihivi. Ni njia ambayo inahitaji kutembea halisi. Yafaa tuonyeshe watu maisha ya Ufalme ikiwa watatembea nasi kwenye njia. Wale tunaongoza hawatatembea peke yao njiani hadi langoni. Wanahitaji mwelekezi, kigezo na mtu wa kuwafanya wanafunzi. (Wafilipi 3:17 na 1 Yoana 2:6). Hili ni mojawapo ya vitu vinavyokosekana katika mikakati ya injili na uanafunzi.

Niwe mbinafsi kidogo, sitaki lakini lazima, sababu najua kupata maono si kwa maneno tu lakini maisha yangu na ya kiroho lazima yatoke damu kwenye maandishi haya ili upate haya. Namtafuta mfalme kiholela bila kumwacha. Watu wanasema mimi ni mfuasi mkuu, mtakatifu zaidi kupindukia, mwenye haki zaidi na mengine mengi. Lakini mimi si mkubwa kuliko mkuu wangu na walimwita hivyo. Mimi nimebadilika kabisa. Huwa Napata maswali kama: “Hapana runinga? Watoto saba-tosha, sawa? Shule nyumbani? Ushirika Majumbani? Nyinyi nyote kwenye kile chumba kidogo? Hapana mshahara , unakimu vipi mahitaji yako?” Hayanikumbi mimi. Niko kwenye utume nikisonga kwa kasi kubwa mbele bila kuangalia nyuma. Nimepata lulu na nataka kumtukuza Mungu kwa kuuambia ulimwengu.

Mimi na mazoea ya maisha yangu wasioamini ndio hawakwaziki. Kinaya ni kuwa kanisa lisilotubu ndilo huukumu sana watakatifu wa Ufalme. Wenye dhambi Mungu anawafanyia kazi, wana hofia kuvutiwa na tamaduni za kimaisha za watakatifu wa Ufalme. Wanataka kuwa sehemu ya kitu kikubwa zaidi yao na kuleta mabadiliko ulimwenguni kwa maisha yao. Ukweli ni kuwa mtu wa kawaida hana furaha na maisha yake. Hawana umuhimu wa kuishi. Wanatafuta burudani, mihadarati, ngono, pesa, mahusiano na hata dini ili kujitosheleza, lakini haya hayawezi timiza haja za kusudi na mambo ya kubahatisha. Wao huona kuwa wale waliomo makanisani hawaishi tofauti na walio nje (duniani) sababu ni walio makanisani mara nyingi hawajabadilika kikamilifu kimaisha. Tunabeba hii mizigo; wengi wa watu hawa hawajapewa maono vizuri na kanuni za kuondoka, na kama wamepewa basi hawajaonyeshwa nasi viongozi jinsi yafaa iwe. Vilevile, hawajajazwa nguvu za kiroho ama kuwekwa huru kutoka dhambini. Wengi wanaishi maisha hohehahe, kurandaranda duniani na kufanya kanisa kuwa bila athari maishani mwao.

Najua haya maneno yaweza kera. Najua sote tunajaribu kupata maono na wengi wanamiliki lulu. Kwako wewe natumai kukupa vifaa ambavyo viawezakutumika katika muktadha wako. Kubali mtindo wangu—nabii ndani yangu hana radhi lakini mchungaji ndani yangu mwenye huruma nyingi kwako, watakatifu wenzangu, hadhamirii kukukwaza. Pokea hicho kutoka kwa Bwana ili kuhamasisha watakatifu wa ufalme, tafadhali usizingatie mapungufu ya mafunzo yangu.

Naomba kwa Mungu akunenee kupitia kwa maneno haya yakupe changamoto na yakutie shime ya utashi mkubwa ndani ya Roho

Mtakatifu kueneza utukufu kwa kuhamasisha watakatifu hadi katika mavuno ya Ufalme. Naomba utanyakua fursa hii adimu katika jina la Yesu. Amina.

Matayarisho Ya Vita

Mbona watu wengi hujiunga na askari wa akiba? Je, ni kwa sababu ya uzalendo, kujitolea kulinda uhuru, ushujaa na utumishi wa uma, kazi tu na kujitolea? Ndio, wengi hujiunga kwa ajili ya sababu nzuri: Japo wapo vijana wengi ambao hujiunga kwa faida kama kusoma kwa ziada katika vyuo na bakshishi nyingi. Hii huenda ikazua hisia tofauti lakini tuwe wakweli. Ikiwa wangehudumu

21

bila faida hizi, serikali ingewapa bila gharama? La hasha! Serikali inafahamu fikra kuwa ili kuwavutia askari hawa, faida hizi ni za muhimu.

Wale ambao walijiuga kwa misingi ya ubinafsi wanapo kuwa mbele unadhani wafaa kuwa huko? Walipotia sahihi kwenye mkataba, tunashangazwa ikiwa walihesabu gharama. Je, masomoziada kwenye vyuo ni biashara ya kujitolea? Bila kujitolea kikamilifu kwa maono (uhuru) na utume (kulinda na kuzuia) hapana fidia ya kufia kitu: lakini kijukumu, heshima na kujitolea. Hapana bei iliyo juu. Ni kuwa wanajeshi waliojitolea kikazi hutamani kuwa katika mstari wa mbele.

Tumeona tabia za kazi. Waumini wengi walijiunga na majeshi ya Ufalme kwa misingi ya faida. Walitaka uhuru kutoka kwenye hukumu ya dhambi na tiketi ya bure kwenda mbinguni. Wanadhana kuwa kutia sahihi kunakuja na faida nyingine kama afya na mali. Wakati mwingine wanatia sahihi shingo upande ni kama wanafanyia mwajiri hisani. Je, wanajua kile wanachotia sahihi?

Je, wanajua yafaa wasalimishe kila kitu kwa Mungu kwa ajili ya utume? Wanaambiwa wamalize utii wowote kwa dunia, dhambi, mali ya dunia, raha za dunia, ubinafsi, mwili, familia, milki na wawe tayari kupeana maisha yao wenyewe. Wanapotia sahihi yafaa waache haki za kibanafsi na faida zingine. Yafaa watii amri zote. Kinyume cha haya watakuwa wasaliti, kwa hivyo wahukumiwe. Sio tu kwamba wanafeli kuendeleza hoja, vilevile wanazuia kwa kutumikia mkuu wa adui.

Je, tunawasilisha ukweli na haja ya kuhesabu gharama? Je, wale walio Kambini mwetu wanajua hawakujiunga wakati wa amani lakini katikati ya vita? Tuko vitani. Adui hajakata tamaa. Mbona sisi? Mbona majeshi wetu wako likizoni bila ruhusa? Je, wakuu wao wako wapi? Je, pia sisi tumechukua likizo bila idhini?

Tambua kuwa tumo vitani. Mamilioni wanafariki bila wokovu. Sababu ni kuwa tunaajiri majeshi wetu lakini hatuwapi amri za kwenda vitani. Hata wanajeshi wa Marekani hutia sahihi kwa misingi ya ubinafsi, bado wanapata mafunzo sawa na wale wenye nia na kusudi njema. Wanajifunza mbinu za kivita pamoja wale wenye maono. Wanapotumwa vitani wako tayari kupigana kwa ujasiri na usawa.

Lazima tujifunze kutoka kwenye huu usawa wa kikazi. Sijali kwa nini walijiunga na jeshi letu. Lakini yafaa wajue kuwa tuko vitani SASA, wapate mafunzo na wapelekwe kazini mara moja. Yafaa waonyeshwe maono na viongozi wetu. Lakini ili wapate maono na kuingia kwenye utume, lazima tutambue sisi pia tuko vitani na tuhiari kuhesabu gharama.

Hebu nikuulize ama jibu Mungu: Umehesabu gharama? Je, waweza kuacha milki zako kwa ajili ya Kristo? Starehe zako? Uhuru wako? Mali yako? Je, majivuno yako? Unaweza salimisha nyumba yako? Familia yako? Imeanza kuwa ngumu. Je, waweza salimisha hati yako miliki? Raha zako? Hofu zako? Majeraha yako? Dhambi zako? Na maisha yako je?

Basi kama ungali pamoja nami, kuwa na uhakika kuwa Mungu hataki utoe kila kitu kama dhabiu kwenye hii orodha hivi sasa. Kuna taswira bora ya kile Mungu anataka kutoka kwako. Chukua karatasi. Tia sahihi pale chini. Atajaza yale ambayo anataka wewe kupeana. Je, waweza tia sahihi kwenye karatasi isiyo na maandishi?

Hadi tuwe tayari kutia sahihi stakabadhi hii basi hatujatosha kuhudumu katika ufalme wake. Kutia sahihi stakabadhi hii kutaweka msingi wa huduma yake na kutufanya kufuzu kufunza majeshi kwa ajili ya utume. Majeshi hawatatufuata hadi vitani mpaka tubebe bendera kidede hadi kwenye moto unaokuja. Tafakari juu ya haya.

Mungu nena na waja wako. Nasihi Mungu wa mavuno atume wafanyikazi. Katika jina la Yesu. Amina.

Utume

Natumai sote twajua utume ni nini, sivyo? Ni Wito Mkuu. Hata hivyo, je, tumewahi chunguza vizuri maana ya wito mkuu?

Nadhani ikiwa kuna kuelewa kuzuri kwa maana ya utume basi tungezindua majeshi kwa sababu ya vita. Ni hivi:

Basi nendeni mkafanye wanafunzi wa mataifa mkiwabatiza katika jina la Baba Mwana na Roho Mtakatifu, mkiwafunza wazingatie yale niliomwamrisha nyinyi (Mathayo 28:19-20)

Hebu tuyaweke haya wazi kidogo, tuanze na la kwanza “nendeni” haisemi “kaeni na msubiri,” lakini NENDENI! (sijali ni neno la njeo gani katika Kigiriki lakini maana ni ileile NENDENI!) Haya si mambo ya kuthibitishwa kwa kupiga mbiu. Haisemi kuwaalika watu kwenye ibada za Jumapili ili wasikie wito wa madhabau. Haisemi uwe mtu mzuri na usubiri mtu akuambie jinsi ya kuokoka. Inasema, NENDENI!

Kisha, inasema tufanye: fanyeni wanafunzi. Haisemi tufanye watu ili wakariri maombi ya kimiujiza (Mazungumzo). Haisemi tufanye watu watuzungumzie kwa lahaja za kimasomo ama hukumu ama watu wenye kuogofya kwa kuwa watu wenye “imani” Fulani. Haisemi tuwaalike kanisani tukiwa na dhana kuwa miaka yao mingi kanisani itawafanya wakomae. Amri za kuondoka ni tufanye wanafunzi.

Kisha inasema mahali pa kuanzia: Kuwabatiza. Hapana mtajo wa madarasa ya ubatizo ama mhudumu aliyetiwa wakfu. Hapana kusubiri kwa ratiba ya ubatizo itakayofuata kanisani kwako. Hapana kusubiri hadi barafu iyeyuke. Endeni nje haraka na kuwabatiza, ambayo yalikuwa mazoea ya Agano Jipya.

Kufungamana na amri ya ubatizo ni toba, sababu ubatizo kwenye maji mengi kunaitwa. “ubatizo wa toba. ” Hapana wakati wa toba na wokovu. Usishiriki katika kufanya waongofu wa uongo—watu wanaodai jina la Kristo na kumkana kimaisha. Hii haimtukuzi Mungu. Badala yake hufanya vigumu watu kuokoka. Kama wanamaanisha watajitolea kwa sababu ya lulu ya dhamani. Lazima wahesabu gharama.

Tilia mkazo toba kamilifu. Wafanye wamkane shetani na kazi zake hadharani. Wafanye watie sahihi karatasi isiyokuwa na maandishi wakisalimisha yote kwa Mungu. Wengi hurudia maombi wakisema watamfanya Yesu Kristo awe maisha yao, lakini hukosa kuelewa maana. Waelezeni kwa uwazi.

Sasa, amri ya mwisho ya kuondoka: Wafunze kufuata amri za Kristo. Tukidhani pia mkufunzi ni mtiifu. Kumbuka, maisha ya Ufalme ni kuiga hali ya maisha, sio kukariri mafunzo. Kazi hii haijapeanwa kwa wachungaji na walimu wa madarasa ya uanafunzi (ni mseto wa tamathali kama nimewahi ona mfano). Hii ni kwa waumini WOTE. Najua wengine wenu wanasema “mimi si mwinjilisiti ama mchungaji hii ni yao” ama “hizi amri zilipewa kwa mitume pekee. ” Mafunzo mengi ya barua za Kristo yalielekezwa kwa wengine. Bado yanatuhusu!

22

Jambo la kushika hapa ni utume mkuu wa kanisa ni Wito Mkuu: kufanya wanafunzi wa toba, watiifu—wamebadilika kabisa kimaisha. Hawa wanafunzi pia wanawajibika kufanya hivi (sababu wanatii amri Zake, na amri ya kufanya wanafunzi). Huduma zingine zote zieleweke katika mkutadha wa utume. Tunahudumia maskini na mahitaji kwa upendo kama sehemu ya utume sio kivyake. Tunashirikiana kwa kusaidiana ili kuadilishana—kutiana shime kwa utume (1 Wakorinzo 14:26). Viongozi wenye vipaji wafaa kuhamasisha watakatifu kwa sababu ya utume (Waefeso 4:11-12). Ni kwa sababu ya utume wala si Jumapili ya ajabu. Kila kitu kingine ni chaguo la pili. Hebu gundua yasemwayo katika Waefeso 4:11-12 kuwa watakatifu WOTE ni wafanyikazi wa utume, wahudumu ama wenye “vipaji. ” Sote tu majeshi kwenye utume. Tukitathimini utume kwa kina, ni watakatifu waliobadilika kabisa wakiekeza maisha yao ndani ya wengine ili wawape maono na utume ili wawabadilishe kabisa. Na wale wapya waliobadilishwa vilevile wakifanya hivyo. Tukisha fanywa hivyo, urithi wa watu waliobadilika kabisa unachipuka bila pingamizi.

Sasa nafahamu yale nyinyi viongozi wa huduma mnafikiria. Mnajua ujmbe na mmefunza, lakini hamwezi kuhamasisha majeshi kwa majukumu amali. Swali langu kwenu ni: Uko kwenye utume? Sizungumzii kuhubiri na kufunza. Namaanisha una mwanafunzi ambaye wewe binafsi ulimwongoza kwa Kristo ambaye unamfunza utii kwa kuhiriki maisha yako? Maisha yaliyobadilka hayaundwi kimasomo; yanapeanwa kupitia Roho na kuekeza kwa mtu binafsi. Kwa hivyo huwezi funza tu na uwe kwenye utume. Lazima uonyeshe. Lazima ushirikishe maono ya Ufalme na kuunda ujumbe wa kukuza uanafunzi wa kuzaa.

Mungu, naomba kwamba utazindua wengi kuingia kwenye utume. Katika jina la Yesu. Amina.

Hesabu Tukufu

Utume ni kufanya wanafunzi, mengine ni ya baadaye na yatiliwe maanani mradi tu yasitupotoshe juu ya utume wa kweli. Misingi michache ya vitu vya asili ni vya muhimu katika kutimiza ufanisi kwenye Wito Mkuu kwenye kizazi hiki. (sio kwamba inawezekana bali pia huenda ikawa. ) Kwaza:wanajeshi kwenye mstari wa mbele lazima wawe wakubwa mno wakiwemo watakatifu wote. Pili: Utume lazima uwe wakujieneza licha ya muktadha wa tamaduni, nyenzo zilizopo ama upaji. Hebu tufunue sababu hizi na mengine mengi.

Tunaweza lalama kuwa shida na mavuno ni kuwa kugumu kwa udogo. Lakini Yesu anasema kuna shida nyingine: Mavuno ni mengi lakini wafanyikazi ni wachache kwa hivyo omba Mungu wa mavuno sana kutuma wafanyikazi kuenda mavunoni mwake. (Luka10:2). Yesu mwenyewe alimalzia kwa kusema upungufu mkubwa kutimiza Wito Mkuu ni uhaba wa wafanyikazi. Na ni ukinaifu wangu kuwa tayari tuna wafanyikazi, ni vile hawazinduliwi. Wanaweza kuwa wanafanya kazi lakini si kwa ajili ya utume. Wanaweza kuwa wanahudumia mipango tofauti na kuhudhuria mikutano mingi lakini hawahusiki katika lengo kuu la kufanya wanafunzi. Hivyo hivyo viongozi wengi wamejikita katika majukumu ya utawala, hawako kwenye utume pia. Viongozi wengine hawafikirii kuwa amri ya kufanya wanafunzi pia inawahusu wao. Wanadhani kuwa wao ni kuhubiri na wengine wafanye hivyo ama kupanga madarasa. Kumbe ujumbe wa kibinafsi wa kufanya wanafunzi ulikuwa wa Yesu na Paulo waliofanya. Mifumo ya kidini ambayo huchepua bidii zetu leo iliepukwa na kanisa la kwanza. Jinsi nilivyosema mwanzoni ni kuwa, ujumbe na maono hushikwa na si kufunzwa. Yafaa kuundwa ili kupishwa hadi kizazi kijacho cha majeshi.

La pili la kuzingatiwa ni msururu wa uzalishaji. Azimio la Mungu lilikuwa kuwa twaweza zaa matunda mema na kuzidisha. Katika Agano la Kale, watu waliamrishwa, “Zaeni matunda mema na kuongezeka,” Kihalisia, Abrahamu, Isaka na Yakobo waliahidiwa vizazi vingi. Leo, tunaambiwa tuzae matunda hadi kukomaa, kuvuna kwa 30, 60 ama 100 na zaidi. Tunaweza kuona matokeo yake kwenye Maandiko—Agano la Kale na jipya—kuwa na matunda ya vizazi vingi. (Kumbukumbu ya Torati 6:1-9: Musa, wanaizraeli, watoto na wajukuu. Timotheo wa Pili 2:2: Paulo, Timotheo, watu watiifu na wengine). Hata hivyo mbinu na mitindo inayoongoza ni ya kuongeza na kuzidisha.

Makanisa ya Ughaibuni yamekitisha huduma kwenye mipango, matukio, miundo na watu wachache waliofuzu kimafundisho. Kwa hivyo idadi yetu inapozidi kuongezeka tunaongeza kwa sababu hizi asili za kipungufu. Huniamini? Yale nimesema unaweza kuongeza watu 1,000 mwaka huu—unaweza mudu? Je, 10,000? Je, 1,000,000? Kama umbo la huduma yako haliwezi mudu watu 1,000,000 mwaka huu fikra zako ni finyu!

Maumboziada yanazuia sababu kila mja anayeongezeka hatarajiwi kuongeza kitu ndani ya wao wenyewe. Mifumo na wenye vipaji vinatarajiwa “kua. ” Pindi tu baada ya kukomaa (kama watawahi), wanaweza kuongeza watu wengine kwenye mfumo. Huku kutafanya ukuwaji mzuri wa Ufalme. (Tena kizuizi si mavuno bali wafanyikazi). Kuna changamoto zingine za maumbo kama kutumia vivutio vya kiulimwengu kuwavutia watu kanisani. Kwa sababu wanajiunga kwa misingi ya faida wala si ujumbe au utume matokeo yake ni wanajeshi wa akiba wengi badala ya majeshi.

Hebu tulinganishe hii na kupanuka kwa umbo la uanafunzi. Mtu mmoja ana funza muumini mpya kutoka kwenye ulimwengu wake wa kuathiri ama Oikos. Anapata maono, kujitolea kwa utume na toba ya ukweli ikifuatwa na ubatizo. Mshauri anamwongoza kwa utii. Kwa majuma, mwanafunzi amepewa changamoto kupata mwanafunzi wake mwenyewe. Yeye pia anafanya vivyo hivyo tena na tena akipewa usaidizi nyuma yake na yule mshauri wake. Hali hii huendelea bila kikomo. Hatutazami ni wapi watakusanyikia kijamii (nachukia istilahi hiyo), japo imejikita kwenye uajibikaji na utiifu kwa Kristo.

Najua wengi wenu wanahisi kiungulia: U wapi uajibikaji? Namwambia ukweli, kuna uajibikaji zaidi kwenye kielezo cha uanafunzi kuliko kwenye kielezo cha kanisa kubwa. Watu wengi kwenye viti ni mayatima—labda si kielimu lakini kiutii—hii kama kweli wameokoka. Viogozi, kwa nyinyi kuwa watiifu kwa utume na kuwa na athari kwa Ufalme, inabidi uanze kufikiria ufalme badala ya kanisa la kawaida.

Faida nyingine ya umbo la uanafunzi ni kutolewa kabisa kwa raslimali ya kizuizi. Wanafunzi hawahitaji majengo, mafunzo ya semina ama msaada wa kifedha. Mtazamo wa nchi za Magharibi kuhusu utume umeturudisha miaka mingi nyuma. Ile dhana kuwa raslimali hii ni muhimu (bila kuzingatia Agano Jipya), imetuzuia kuvuna mavuno ambayo Yesu alisema ni mengi. Lazima tuangalie nyuma kwenye tabia zetu za Agano Jipya na tugundue ukubwa wa majeshi ambayo tumezindua tayari kwa utume.

Zingatia uwezekano wa kulinganisha umbo la kuongeza na kuzidisha. Chukulia Mwinjilisti anabadili nafsi moja kwa siku ukilinganisha na mtakatifu anayefanya mwanafunzi mmoja(mfuasi mtiifu

wa Kristo) kwa mwaka. Mwisho wa mwaka mmoja, mshindi ni Mwinjilisti na 366, wanafunzi wawili: mwaka wa pili Mwinjilisti

23

731, wanafunzi wanne; mwaka wa tatu 1,096 mpaka nane; mwaka wa tano, 1,826 hadi 32; mwaka wa sita 10,3,651 hadi 1,024; mwaka wa 20, Mwinjilisti 7,300 na 1,048,576 watakatifu waliofanywa kupitia uanafunzi. Idadi ya watu duniani kote inaweza kufikiwa kwa miaka 33, tukichukua mwanafunzi mmoja kila mwaka. Hizi ni nguvu za ukuwaji mkubwa. Idadi nzuri inaweza kuwa kila mtakatifu kufanya wanafunzi 6 kila mwaka; Wito Mkuu unaweza kutimizwa kwa miaka 13 kuanzia chini kabisa. Ikiwa tutazindua sehemu tu ya majeshi ambayo tunayo sasa (milioni moja tu ya Watakatifu)—miaka mitano barabara! Mimi na wewe tukiwemo.

Yote huanza na wewe. Je, uko tayari kujihusisha na utume? Uko tayari kuachilia mafuriko ya wafanyikazi? Je, uko tayari kuacha na kuamini Roho Mtakatifu aongoze watu wake kwa uzaaji matunda? Waweza kuwa kizingiti ama vingine ni juu yako.

Mungu naomba ufanye kitu-dhabiti na chenye nguvu kwenye roho ya kila mwanamume na mwanamke anayesoma kitabu hiki.

Naomba kinyume cha misingi ya vizuizi vyovyote—vya kidini ama vinginevyo. hamasisha watakatifu kwa mavuno. Katika jina la Yesu. Amina.

Kuingia kwenye Ufalme

Ili kuanzisha uanafunzi wenye manufaa na zalishaji, usambejani (DNA) wa kiroho lazima uwekwe. Kwa bahati mbaya kuna uvumi mbaya umekuwa ukienezwa katika jamii ya kristo kwa muda sasa. Hebu tutazame tuweze kujua jinsi maandiko yanavyosema kuhusu mambo ya msingi.

Hiki ndicho kitabu cha muhimu sana ambacho nimeweza kukiandika maishani. Uzima na kifo, mbingu na jehanamu vyote vimesimama kwenye mizani. Yakini naweza kupoteza wengine wenu kwa sababu naondoka kidogo na funzo hili lakini nawahimiza kwa moyo safi mzingatie yale niliyoyazungumzia kwa nia nzuri. Najua wengi twapenda kusoma vitabu vilivyo bora kama vile Yohana 3:16, Matendo ya Mitume 2:38, Matendo ya Mitume 16:31, Warumi 10:9 na 13, na vinginevyo vinavyohusu wokovu kwa sababu vinaeleweka kwa urahisi. Vinatufanya kuwa na uwezo wa kuelewa fikra zinazowiana na mtindo wetu wa magharibi. Sisi ni watu wenye mkondo mmoja katika fikra na tunafaa kufunika akili zetu na mambo yanayoridhisha miili yetu. Mungu na uchumi wake wamejisitiri na ni vigumu kuwaelewa. Njia zake ziko juu kuliko zetu. Ni aibu kuwa tunajaribu kufumbua fumbo hilo kwa mifumo ya Kitheolojia na matamshi ya kiimani. Inabidi tuchukue yale ambayo amegawa kwa Roho na tuyafanye kibinadamu, kwa bahati mbaya; hebu niweke bayana kuwa yale ninayoamini ni kutoka kabisa kwa kusudi la fumbo la injili ya Ufalme. Vilevile mimi nitafanya zaidi ya hivyo hapa.

Kuna kitabu kimoja kwenye Biblia kilichoandikwa kwa kusudi la kuwajuza waumini kuhusu kama kweli wataingia kwenye ufalme wa Mungu. Yohana wa kwanza 5:13 inasema: “Haya mambo nimemwandikia nyinyi mnaoamini katika jina la Mwana wa Mungu, ndio mjue kuwa mna uzima wa milele” (mkazo umetiliwa). Mstari huu unamalizia kusudi la barua ya Yohana. Kwa hivyo twaweza uamini kutupa mwongozo kwenye haya masuala. Nimeona kifungu hiki kimetumiwa katika mikutano ya kiinjilisti bila kurejelea kwa ujumbe kamili wa barua yenyewe. Huku ni kutowajibika.

Hebu tuangalie baadhi ya ujumbe katika barua:

Na kila mtu yule imani yake imewekwa Kwake hujitakasa mwenyewe, jinsi alivyo mtakatifu. Yule atendaye dhambi vilevile hutenda kinyume cha sheria ; na dhambi ni kutotii. Unajua alikuja ili kuondoa dhambi na ndani yake hakuna dhambi. Hapana yeyote akaaye ndani yake hutenda dhambi. Hapana atendaye dhambi amemwona ama anamjua. Watoto wadogo; hakikisha hapana mtu akudanganyaye. Yule atendaye haki ni mwenye haki; yule atendaye dhambi ni wa shetani sababu shetani ametenda dhambi tangu jadi. Mwana wa Mungu alikuja kwa sababu hii, kuharibu kazi ya shetani. Hapana mzawa wa Mungu atendaye dhambi sababu mbengu yake hukaa ndani yake; na hawezi tenda dhambi sababu ni mzawa wa Mungu. Kwa hili watoto wa Mungu na wa shetani ni bayana. Yeyote asiyetenda haki si wa Mungu ama yule asiyependa ndugu yake (Yohana wa Kwanza 3:3-10).

Kwa haya tumemjua kwa kutii amri zake. Yule asemaye, “Nimekuja kumjua” na hatii amri zake ni mwongo, na hana ukweli ndani yake lakini yule hutii amri zake neno lake li ndani yake. Upendo wa Mungu umekamilika kwa hili tunajua tu naye. Yeyote asemaye anakaa ndani yake basi atembee jinsi alivyotembea. (Yohana wa Kwanza 2:3-6).

Usipende ulimwengu ama ya ulimwengu. Yeyote apenpendaye ulimwengu, upendo wa Mungu haumo ndani yake. Yote ya ulimwengu, tamaa za macho na majivuno ya kimaisha si kutoka kwa Baba bali kutoka kwa ulimwengu. Ulimwengu unapita na tamaa zake, lakini atendaye mapenzi ya Mungu huishi milele. (Yohana wa Kwanza 2:15-17).

Yohana aliandika barua hii kwa kusudi la kufahamisha waumini ili wajue wana uzima wa milele. Jinsi uonavyo, viwango viko

juu sana kuliko jinsi vinavyofunzwa leo. Bado Yohana anasema, “Msindanganywe na yeyote,” Hiki ndicho kiwango sawa cha kutumia. Anasema, ikiwa umezaliwa upya hutaendelea kutenda dhambi. Si maneno yangu, yake. Anasema pia ikiwa unadai kumjua na hutii amri zake u mwongo. Si maneno yangu,Yake. Pia anasema ukiwa una chembe yoyote ya kiulimwengu humjui Mungu. Kwa hivyo kutembea huru bila dhambi, kuwa mtiifu kwa amri zake na huru kutoka kwa ulimwengu—hiki ndicho kipimo cha kujua kama wamjua Mungu ama la na kama kweli umeokoka, ukapokea uzima wa milele (sikusema bali Alisema).

Hii isiwe ajabu kwetu kama sisi husoma mafunzo ya Yesu. Alisema kuwa haki yetu izidi ile ya mafarisayo. Alichukua sheria, na kupandisha kiwango kabisa—sio tu kwa vitendo vyetu, sasa tumehukumiwa kwa fikra zetu vilevile. Wengi wetu wamefunzwa kuwa tukiingia Langoni, tuko ndani. Kumbe Yesu alifunza juu ya njia. Lango ni dogo lakini njia bado ni ndogo zaidi. Huwa tuna dhana potoshi kuwa tutazidi kuishi katika hali ya maisha ya kiulimwengu na kuwa hii inakubalika. Tunadhani kuwa Mungu atatusamehe kupitia kwa neema yake na haijalishi yale tutendayo. Waumini Humaka “Usinihukumu. ” na “Mungu ni wa rehema. ” Sihukumu lakini neno la Mungu ambalo waumini wote hudai ni la kushauri, la mamlaka na huwaongoza katika hali zote hatimaye litawahukumu. Wengi watasadiki nusu kwa kusema “anafunza tu wokovu kwa vitendo. ” Yakobo 2:24 inasema “Mwanadamu amehesabiwa haki kwa kazi si kwa imani pekee. ”

24

Biblia inaendela kusema: “Tushangilie na kufurahia na tumpe Yeye utukufu, kwa kuwa ndoa ya mwana kondoo imekaribia na bi harusi yu tayari. ”Alipewa yeye ili akavae kitani nyororo, nyepesi na safi; sababu kitani nyororo ni matendo ya haki ya watakatifu. (Ufunuo 19:7-8). Nini? Kitani zetu nyororo kuwa matendo? Alikosea alipoandika hayo! Sawa, hebu tusome fumbo la karamu ya harusi (fumbo la

Ufalme) kwa kuangazia maandiko haya: Mfalme alipoingia kuangalia wageni kwa chakula kikubwa cha kushinda, aliona mtu hapo ambaye hakuwa katika mavazi ya

harusi, akamwambia “Rafiki uliingia vipi hapa bila mavazi ya harusi?” Mtu yule hakuwa na la kusema. Kisha mfalme akawambia watumishi, “Mfungeni mikono na miguu na mmtupe nje gizani. Huko kutakuwa na vilio na kusaga meno. ”(Mathayo 22:11-13). Je huenda Yesu alikuwa akisema kuwa mtu Fulani aliingia Langoni lakini hakutumia njia? Hebu tuone Mtume Paulo alikuwa na yepi ya kusema kuhusu matokeo ya kuishi kimwili:

Sasa matendo ya kimwili ni wazi, ambayo ni: Uzinzi, uchafu, tama za kimwili, uabudu sanamu, uchawi, uadui, vita, wivu, hasira, migogoro, fitina, kutia fitina, gere, ulevi, karama ya ulevi, na vitu kama hivi ambavyo hukuonya mbeleni jinsi tu nilivyo mwonya mbeleni kuwa wale watendao haya hawatarithi ufalme wa Mungu. (Wagalatia 5:19-21)

Si siri wale watakao okolewa na watakao hukumiwa. Yesu alifunza wazi kuwa mti utajulikana kwa matunda yake. Yohana akaweka wazi zaidi katika barua yake, Paulo akathibitisha kwa kutuonyesha matunda ya kimwili ni nini. Natumai unahabari ya yaliyosalia katika Wagalatia 5 na “matunda ya kiroho” kuhusu uzaaji wa matunda, Yohana Mbatizaji alisema:

Kwa hivyo zaeni matunda kwa kujiweka na toba: Usidhani kuwa mnaweza jiambia, “Tuna Abrahamu kama baba. ” Nasema kutoka kwenye haya mawe Mungu anaweza kuwakuza watoto kwa Abrahamu. Tayari shoka limewekwa tayari kwenye mizizi ya miti; kwa hivyo kila mti usiozaa matunda mema utakatwa na kutupwa motoni. (Mathayo 3:8-10)

Yesu alisema karibu sawa. Ceck ya contect. Baada ya kusema kwa waumini hapa.

Kaeni ndani yangu nami ndani yenu. Kwani tawi la mti haliwezi zaa matunda kivyake bila mzabibu hivyo hivyo huwezi bila kukaa ndani yangu. Mimi ndio mzabibu nanyi matawi, yeyote akaaye ndani yangu nami ni ndani yake huzaa matunda mengi, bila Mimi huwezi fanya lolote. Yeyote asiyekaa ndani Yangu, hutupwa mbali kama tawi na kukauka; na wanakusanywa na kutupwa motoni na kuchomwa. (Yohana 15:4-6).

Yakobo alisema, “jithibitisheni watenda neno wala si wasikilizaji wanaojidanganya” (Yakobo 1:22, 2:17-18). Imani ya kweli huzaa matunda.

Biblia inatuambia tujitathimini kama tuko katika imani (Wafilipi 13:5) na tufanyie wokovu wetu kazi kwa uoga na kutetemeka (Wafilipi 2:12, msisitizo umetiliwa) mara nyingi kwenye maandiko. Watakatifu wanaitwa “wanaokoka” badala ya “wameokoka. ” (Matendo ya Mitume 2:47, Wakorinzo wa Kwanza 1:18 na Wakorinzo wa Pili 2:15). Fumbo la wokovu linaweza kueleweka hivi: Usiulize mtu kukubali kielimu ili kujua kama ameokoka au la. Lakini matunda ya imani ya kweli yakionyesha wanaokoka. Wengi husadiki na kupata Lango, lakini wachache huvumilia kutembea barabara ndogo hadi uzaaji matunda.

“Ingia katika lango dogo; kwa sababu lango ni pana na njia ni pana inayoelekea katika maafa na wapo wengi wanaotumia lango hili. Kwa sababu lango hili ni dogo na njia ni ndogo inayoelekea katika maisha na ni wachache sana huipata. Jihadhari na manabii wa uongo wanaokuja kwenu katika mavazi ya kondoo lakini ndani yao ni mbwa mwitu. Mtawajua kwa matunda yao, zabibu hazichumwi kutoka miibani ama tini kutoka mbarutini, ama sio? Kwa hivyo mti mzuri huzai matunda mabaya, ama mti mbaya kuzaa matunda mazuri. Kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni. Kwa hivyo utaijua kwa matunda yake. Sio kila mtu atajaye jina langu “Bwana, Bwana” ataingia katika ufalme wa mbinguni, lakini afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni ataingia. Wengi siku hiyo watasema tulitabiri katika jina lako tulikemea shetani katika jina lako, tulitenda miujiza katika jina lako?” Na nitaamua na kuwaambia “sikumjua nyinyi; TOKENI KWANGU, NYINYI MLIO TENDA KINYUME NA SHERIA. . ” Kwa hivyo yeyote asikiaye haya maneno yangu na kuyatenda anaweza fanananishwa na mtu ajengaye nyumba kwenye mwamba. Na mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, dhoruba zikapiga lakini myumba hii haikuanguka kwa kuwa imejegwa kwenye mwamba. Yeyote asikiaye maneno haya na hayatendi ni kama mtu mjinga ajengaye kwenye mchanga. Mvua ilinyesha, mafuriko yakaja na dhoruba kupiga nyumba ikaanguka—kubwa zaidi kuanguka kwake. ” Yesu alipomaliza kusema haya halaiki ilishangazwa na mafundisho Yake. Kwa sababu aliwafunza kama mwenye mamlaka wala si kama karani wao. (Mathayo 7:13-29).

Hakika, siku za mwisho wengi watamdai Yesu kama “Mungu” lakini kwa jina tu. Wanaweza fanya kazi nzuri lakini hawajatia

sahihi kwenye “karatasi isiyo na maandishi” ipeanayo kila kitu kwa Yesu, na hawatembei kwenye njia ya haki. Bahati yao sio waidhaniavyo.

Naomba msamaha kwa urefu wa sura hii. Najua pia mada hii ni ya undani na zushi lakini kuelewa kwa hakika kuwa imani halisi ya Mkristo hutoa mabadiliko kabisa—na kuelewa kuwa hakuna “kitu cha hakika” kwa yule asiyevumilia katika imani—ni msingi wa kuhamasisha kutengeneza wanafunzi. Kwa hivyo namsihi kutafakari juu ya aya hizi kwa roho wazi.

Mungu mwenye nguvu, naomba kuwa utafungua fikira na mioyo na uondoe chochote kinachozuia Roho wako kutofikia mioyo, Mungu, ruhusu ukweli kuzama ndani ya nafsi zao. Naomba kutafutwa kwa njia zako na ukweli wako. Tamalaki katika kila kitu kwa utukufu wako. Katika jina la Yesu. Amina.

25

Muhtasari

Natumai sikukupoteza katika kuongea ukweli kuhusu wokovu kibutu. Kama ujuavyo, kitabu hiki kimekusudiwa kushughulikia majukumu mawili: Kusaidia viongozi wa huduma kuweka matendo mazuri kwa kuhamasisha kazi ya kufanya uanafunzi na kupeana nyenzo za kutumia wewe na wengine. Nimeanza kuweka msingi huo kwenye wengi wetu watachukulia kama masuala ya kiasili, lakini vitu hivi haviwezi vikapuuzwa ikiwa Ufalme wafaa kuendela.

Katika muktadha wa kitabu hiki, nimeenda hatua kuwasilisha nyenzo kama itakavyofaidi hadhira ya wakristo—sio waongovu wachanga. Jinsi kazi yako ya kufanya uanafunzi inavyojifunua, utaratibu huo huenda ukawa tofauti lakini mambo ya kiasili yatakuwa sawa. Kwa hivyo kabla hatujaenda mbele, kwa haraka tuangalie Taswira kubwa. Katika hali ya kawaida, mtindo ufuatao ungefuatwa: 1. Pata Maono 2. Dhibiti dhambi 3. Salimisha yote kwa Mungu 4. Toba 5. Ukombozi 6. Kujitolea kwa utume 7. Zungumza na Mungu 8. Kupewa nguvu 9. Kujihusisha na utume. 10. Panda maono.

Mitindo hii katika kutekeleza, si tekelezi kipambizoni kikanisa na kidini lakini ni tekelezi na wanafunzi wapya. Hii ni kwa sababu kutojifunza kwingi na dini lazima kutokee. Utamaduni wetu wa kikiristo umefifisha maono na utume, ukweli mtupu kuwa kuweka upya tathimini ya usambejani nzuri ya kiroho ni ya kutia changamoto (lakini si ngumu). Mafunzo ya kindani juu ya Yohana wa Kwanza na aya nyingine zinazooana nayo huwapa watu changamoto kwa toba ya kweli. “Kutia sahihi karatasi isiyo na maandishi”mazoezi pia huwapa wengi changamoto kukabiliana na kiapo chao cha ukweli, dunia ama Ufalme. Kila mtu hudai yesu kama mwokozi wao, lakini wengi hutambua kupitia mazoezi hayo kama kweli humfanya Mungu kweli. Nilikaidi hayo mpaka wafanye, kwa kweli hawajaokoka (hayo mazoezi ni zaidi ya “maombi ya uganga”siku yoyote).

Sasa ushapata mtazamo wa taswira kubwa, sasa tujaze mengine yaliyosalia.

Njia Ya Uhuru

Majidiliano ya wokovu yaliyotolewa kitabuni humu yanaweza chepuka kutoka kwenye yale mafunzo wewe husikia. Wokovu kwa neema kupitia kwa imani ni yale utasikia—nakubali,Waefeso 2:8-9 bado ni imara. Hata hivyo tumeokoka kwa neema kupitia imani—si kwa vitendo ama haki yetu binafsi. Wokovu ni zaidi ya upeo wetu; hatuwezi fikia kwa hivyo ni haki na kuishi kitakatifu. Hata hivyo, hii haimaanishi kuwa tutawacha kuangalia viwango vilivyowekwa mbele katika Yohana wa Kwanza (Ni neno la Mungu hata hivyo).

Yohana wa Kwanza 5:13 inaongea juu ya usalama wa milele; hata hivyo ina mashrti juu ya uhuru (Yohana wa Kwanza 3:9) huru kutoka dhambini (Yohana wa kwanza 2:15) kutii amri zake (Yohana wa Kwanza 1:4) na kutembea alivyotembea Yesu (Yohana wa Kwanza 2:6). Si maneno yangu, bali yake.

Hebu tuangalie katika tukio kwenye maandiko. Yohana sura ya nane, Yesu anakumbana na mwanamke aliyepatwa akizini na anahukumiwa. Watu wakristo wanajaribu kumtega yesu kwa kumuuliza wafanye nini; wampige kwa mawe (wenye haki wanasitahili adhabu) ama wamwache aende? Aliwaduwaza kwa kuwaambia yeyote asiye na dhambi awe wa kwanza kutupa jiwe. Walitawanyika wakijua pia wao walikuwa watendadhambi. Mazungumzo mengine yanachipuka kati ya Yesu na mzinzi. Yesu alimuuliza, “wako wapi? Hakuna hata mmoja aliyekuhukumu?” Akajibu, “Hakuna hata mmoja Mungu” Na Yesu akamwambia, “Sitakuhukumu mimi pia nenda, kuanzia sasa usitende dhambi tena.” (Yohana 8:10-11).

Ningependa kudokeza vitu vichache hapa. Kwanza yule mwanamke habishi hukumu yake ama atetee matendo yake. Anajua kuwa ana makosa ya kuhukumiwa. Yuko kihalisi katika ukingo wa kifo, na hana kinusuru. Kimya cha ujumbe hakitoi mchoro kwenya fikira zangu wa mwanamke mwingi wa masikitiko, majuto na akikabili kifo bila tashiwishi. Yuko mwisho wake na anajua anastahili.

Lakini Yesu anaonyesha rehema na kwa neema zake anamsamehe dhambi zake. Amehukumiwa kabisa na hasitahili neema, lakini anampa. Hata hivyo, maongezi hayaishii hapo. Yanaisha na “kuanzia sasa kuendela usitende dhambi tena. ” Kutoka kwa haya tunaona toba si kusema uko radhi, lakini kuwa radhi si ithibati ya kutofanya kosa tena. Ni kubadilisha maisha. Ni kutambua kuwa umehukumiwa na unasthili adhabu ya kifo—kweli kutenganishwa na Mungu milele na adhabu ya jehanamu. Lakini, kumbuka kuwa hata kama utapokea neema ya kuokoka, inakuja na mashrti: usitende dhambi tena.

Unadhani Yesu angefanya nini ikiwa angekutana na yule mwanamke kotini siku iliyofuata, akiwa amepatikana katika kitendo hicho hicho? Najua wengi watasema angemsamehe mara nyingi na kuwa twaweza tubu mara nyingi kwa kosa lile lile. Lakini, sivyo ilivyo hali. Wahibrania 6:4-6 inasema:

Kwa wale ambao wameelimishwa mara moja na wameonja zawadi ya mbinguni, wamefanywa washiriki wa Roho Mtakatifu, wameonja neno zuri la Mungu, nguvu za miaka ijayo na wamepotea njia ,ni vigumu kuwafanya upya kwa toba kwa sababu wamemsulubisha tena wao wenyewe mwana wa Mungu na kumpaka tope hadharani. (Wahibrania 6:4-6, angalia pia Wahibrania 10:26-31).

26

Angalia neno “haiwezekani. ” Toba ni barabara ya kuelekea kumoja. Kwa hivyo ni kwa neema tunapata nafasi ya pili, vivyo hivyo kwa neema tunapata uhuru na kupewa nguvu kutembea kwa utakatifu na haki. Sote tunaamini kuwa tumeokoka kutoka kwenye adhabu ya dhambi lakini wachache huamini (ama wanaishi ni kama wanaamini) kuwa tumeokoka kutoka kwenye nguvu za dhambi. Ni rahisi sana kuamini Mungu kwa wokovu wetu sababu iko nje na mbali, na si muhimu kudhihirisha katika maisha yetu. Lakini sisi hufeli kukumbatia uhuru kutoka kwenye dhambi sababu hugongana na maarifa yetu. Hii ni bahati mbaya kwa Wakristo leo.

Namsihi, mtoe kamusi zenu za kidini na mwangalie maana ya neno “toba. ” Kuna mazungumzo mengi juu ya somo hili kushughulikia katika sura fupi. Lakini nitawaacha na funzo moja la mwisho kutoka kwa Yesu.

Sasa katika tukio hilo baadhi walikuwapo walioripoti Kwake kuhusu Wagalilaya ambao damu ya Pilato ilikuwa imechanganyika na dhabiu yao. Yesu akawambia “mnadhani wale Wagalilaya walikuwa watenda dhambi kubwa kuliko Wagalilaya wengine sababu waliteseka ajali hii? Namwambia, hapana, lakini msipotubu nyote mtaangamia pia. Ama mnadhani kuwa wale kumi na wanane ambao ngome ya Siloam iliangukia na kuwaua walikuwa wabaya zaidi kuliko wanaume wote wanaoishi Izraeli? Namwambia nyinyi, msipotubu, mtaangamia pia. ” Na akaanza kuongea juu ya fumbo hili: “Mtu alikuwa na mtini uliokuwa umepandwa kwenye shamba la mizabibu na akaja kutafuta tunda kutoka kwake na hakupata lolote. Na akamwambia mlindashamba la mizabibu, “Tazama, kwa miaka mitatu nimekuja kutafuta tunda kwenye mtini bila kupata lolote. Ukate! Mbona unatumia ardhi?” Na akamjibu na kusema, “Wachana nao Bwana kwa mwaka huu pia, nitachimba kando kando na kuweka mbolea ukizaa matunda mwakakesho sawa, usipozaa, nitaukata. (Luka 13:1-9).

Kulingana na mafunzo ya Yesu, njia ya uhuru kutoka dhambini huanza na toba na huisha kwa utakatifu na haki. Lakini hatuwezi

pata maarifa ya uhuru kutoka dhambini kwa nguvu zetu. Ndio sababu Yesu alisema kuwa mbali na Yeye, hatuwezi fanya lolote (Yohana 15:5). Tunahitaji nguvu za Roho Mtakatifu kutimiza kazi hii! Katika sura ifuatayo tutaendelea kujadili uhuru na utekelezi na misingitumizi. Najua haitoshi kusema tu, “usitende dhambi tena.”

Mungu mwenye nguvu,wape waja wako uhuru—sio tu kutoka kwenye hukumu ya dhambi lakini kutoka kwenye nguvu zake maishani mwetu. Wewe ni Mungu wa ajabu na Mtakatifu, yule kwa meema umetupa fursa kuishi—kuingia katika Ufalme. Tupe nguvu kutembea katika ushindi na ufunze wengine kufanya vivyo hivyo. Katika jina la Yesu. Amina.

Uhuru Kutoka Kwenye Nguvu za Dhambi

Uhuru kutoka kwenye nguvu za dhambi ni lengo letu sisi sote, lakini kwa wengi wetu ni vigumu kufahamu. Nafikiria mengi yanayochipuza kutoka kwenye kuelewa kwetu kwa hatua. Huwatunafanya “kazi” kwetu sisi wenyewe kwa muda mrefu, polepole (na si kwa uhakika) kujiboresha. Ya mfano moja, nguvu za kiinjilisti, elimu ama saikolojia za kidunia ambavyo “vimetiwa ukiristo” mara si moja ukomavu wa kikiristo umechanganywa na utakaso. Katika kuangalia mbinu ambazo sisi hutumia kurejesha ukamilifu wa mtu, itabidi tuhitimishe kuwa Roho Mtakatifu ni nadra kubadilisha maisha. Tena, tunaamini katika nguvu za Mungu kwa wokovu, lakini si lazima kwa kubadilisha.

Mwalimu mmoja wa kikiristo alishiriki kiundani zaidi kadri ya ulinganifu juu ya fumbo la utakaso ambalo limekwama nami. Siku zote hulipenda kwa sababu ya urahisi wake—si vile utakavyopata katika ya kale ama mkondo mkuu wa nyenzo za maisha ya kikiristo! Taswira ya neno hili dogo imeniruhusu kuishi ndani na kuwapa wengine nguvu kuingia kwenye uhuru kutoka kwenye dhambi kwa ufanisi mkubwa. Mwalimu huyo alilinganisha mabadiliko yetu na urejesho wa gari. Inaleta maana kuwa tunafanyia kazi sehemu moja ya gari kwa wakati mmoja: Karia, muundo wa injini, vijengamwili-vyote tukiendelea kutumia gari kama dereva wa kila siku. Ndio sehemu zimerejeshwa. Lakini kuendelea kutumia, matokeo yake ni uchafu mpya, mikwaruzo mipya, kuchakaa, kugundulika kwa kutu sehemu ngeni nakadhalika. Kwa hivyo hata kama tunafanyia kazi sehemu moja kwa wakati mmoja, na jasho kwenye vipaji, huwa hatutimizi. Gari kila mara lina kitu ambacho huhitaji “usufii. ” Ni kama mtu unayemjua?

Lakini hatua hiyo yafaa iwe hivi: Tunasalimisha kwa Mungu, anachukua gari, analiweka kwenye kiseta, anatengeneza kitu cha miraba minne sawa cha chuma futi mbili kutoka hapo na kutuma kwa jaa la timbe. Kisha Yesu anatoa gari la kifahari na kusema, “Ruka ndani! Kuanzia sasa na milele utaendesha nami. ” Hebu tusome Warumi 6 kwa kuangazia ulinganisho huu.

Tuseme nini sasa? Je, tuendelee na dhambi ndio neema iweze kuongezeka? Labda naisiweze! Je, tutawezaje sisi tuliokufa dhambini tuishi ndani yake? Ama hamjui sisi sote tuliobatizwa katika Yesu Kristo tumebatizwa katika kifo chake? Kwa hivyo tumezikwa naye kupitia ubatizo ndani ya kifo ndiposa jinsi Kristo alivyofufuka kutoka kwa wafu kupitia utukufu wa Baba ili nasi pia tuweze kutembea katika upya wa maisha. Kama tumeuungana Naye katika usawa wa kifo chake, bila ya shaka tutakuwa hivyo hivyo katika kufufuka kwake, tukijua hivi kuwa nafsi zetu za kale zilisulubiwa Naye ndiposa miili yetu ya dhambi itupiliwe mbali, ili tusiwe watumwa wa dhambi. Kwa kuwa yule aliyekufa yu huru na dhambi. Sasa kama tumekufa na Kristo, tunaamini kuwa tutaishi pia Naye, tukiwa tunajua kuwa Kristo alifufuliwa kutoka wafu, na hafi tena, kifo sio mtawala kwake tena, kifo alichokufa, alikufa kwa dhambi mara moja kijumla. Lakini maisha anayoishi anaishi kwa Mungu. Hata hivyo jizingatie kufa kwa dhambi, lakini ishi kwa Mungu kwa Yesu Kristo. Kwa hivyo usiruhusu dhambi kutawala katika mwili wako wa kibinadamu ili utii tamaa zake na usiendelee kupeana sehemu ya jamii ya mwili kwa dhambi kama vyombo visivyo haki, lakini jiwasilishe kwa Mungu kama wale wanaoishi kutoka kwenye kifo na jamii ya mwili wako kama vyombo vya haki kwa Mungu. Kwa kuwa dhambi haitakutawala tena kwa maana hauko chini ya sheria bali chini ya neema. Na isiwe hivyo! Je, mwajua mkijiwasilisha kwa mtu kama watumwa wa kutii, nyinyi ni watumwa wa yule mnayetii, aidha ya dhambi matokeo ni kifo ama utii ili kuzaa haki? Lakini shukrani kwa Mungu licha ya kwamba tulikuwa watumwa wa dhambi, ulikuwa mtiifu kutoka moyoni na kuingiana na mafunzo ambayo ulijitolea tukiwa tumeokolewa kutoka dhambini basi tumekuwa watumwa wa haki.

Naongea kiutu kwa sababu ya unyonge wa mwili wako. Jinsi ulivyotoa viungo vyako kama watumwa kwa unajisi na kutotii matokeo yake kutotii kabisa, sasa toa viungo vyako kama watumwa kwa haki, matokeo yakiwa utakaso. Kwa jinsi mlivyokuwa watumwa wa dhambi mliwekwa huru kwa kuzingatia haki. Kwa hivyo ni faida gani uliokuwa ukipata kutoka kwa vitu ambavyo

27

unaaibikia sasa? Maana matokeo ya hayo yote ni mauti. Lakini sasa kwa kuwekwa huru kutoka dhambini na utumwa kwa Mungu, unapata faida yako matokeo yakiwa utakaso, na matokeo, maisha ya milele. Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti lakini zawadi ya bure ya Mungu ni uzima wa milele ndani ya Yesu Kristo Bwana wetu. (Warumi 6)

Tumekufa kwa dhambi, tukiwa tumeshiriki katika kifo na kufufuka kwa Yesu Kristo. Tumewekwa huru kabisa—nafsi zetu za

kale ZIMEKUFA. Sasa tuna uhuru kutoka hukumu ya dhambi na nguvu juu ya maisha yetu. Sisi si watumwa wa dhambi tena ila watumwa wa haki, sasa tunatembea katika upya wa maisha. Uhuru wetu kutoka dhambini matokeo yake huwa ni utakaso, ambao hutuelekeza kwa uzima wa milele (mstari wa 22; tambua mwendelezo wa sura za kwanza:Pasipo na utakaso hapana uzima wa milele). Mtu yeyote asikudanganye kwa kukufunza kinyume. Tuko huru kabisa na lazima tupokee uhuru huo.

Hata hivyo, uhuru pekee huja tukisalimisha kila kitu. Ikiwa tunapiga mayowe na mikiki huku tumekwamilia kwenye gari kweche huku Kristo akijaribu kulipeleka kwenye kiseta, hatutapata uhuru wetu. Hii ni sawa na kushikilia minyororo na huku kiungo cha pingu kimewachiliwa; ni msiba wa kujitakia. Matokeo, shetani anaweza kutushawishi kuwa viungo vya pingu bado vimefungwa kumbe ni kushikilia nyororo (ni kawaida). Udanganyifu mkubwa huu! Hii humwibia Mungu utukufu Wake.

Mungu Mkuu mwenye nguvu, tuonyeshe uhuru na utupe nguvu ili tuongoze wengine hadi kwenye uhuru. Katika jina la Yesu.

Amina.

Uhuru Tunaoweza Kuona

Labda sura iliyotangikia ilikusababishia kiungulia. Hata hivyo wengi wetu tuna amini kuwa kupambana na dhambi ni maisha ya kawaida. Hata hivyo ningependa ujue kuwa wote wamepewa fursa kumaliza na uhuru kamilifu kutoka kwa nguvu za dhambi—ni vile tu sisi hukosa kupokea.

Tukio hili lanikumbusha jinsi tembo hupewa mafunzo. Wanafungwa kwenye kitu ambacho hakisongi kwa muda, wavuta lakini hawafaulu. Kwa hivyo baada ya muda mfupi, wanawacha kuvuta. Wanaweza shikwa kwa vigingi kuanzia wakati huo na milele, sababu wameshawishika kuwa juhudi zao hazizai matunda.

Hatua hii ya mafunzo ya uongo ni sawa na yale yafanyikayo kwa samaki wa maji baridi ya kaskazini wanapokuwa mateka kwenye mabwawa. Kuzuia samaki wakubwa kula mateka wao wa kawaida bwawani, kizuizi cha kioo huwekwa kuzuia wale samaki kufikia mateka wao. Muda mfupi wanaokimbia hadi kwenye kizuizi hicho cha kioo huwafunza samaki kutojaribu tena. Hata baada ya kioo hicho kuondolewa, samaki wadogo huishi kwa amani sababu samaki wale wakubwa hudhani kuwa kizuizi kipo tu.

Mara si moja sisi hutembea katika ufugwa kwa sababu ya mafunzo kama hayo. Tumejaribu kwa muda mrefu kukwepa kutoka kwenye mitindo ya dhambi, tumeshawishika kuwa hatuwezi na tuwache kujaribu. Tumedanganywa kufikiria kuwa kupambana tunakokumbana nako ni zaidi ya uwezo wetu kuyashinda. Adui huendelea kushikilia minyiroro, na kumbe awali tushapewa uhuru kutoka kwayo.

Bila kuhimili uhuru ndani ya Kristo, hatuwezi dharau ushawishi wa adui. Ningependa sasa kudokeza mbinu zake na chanzo cha nguvu zake maishani mwetu.

Kumbuka ule mchoro wa utenzi “vita vya ulinzi” kati ya Mungu na shetani kwa mioyo ya watu, ambayo iliwasilishwa katika sura ya kwanza. Tunaona elimu hii katika kitabu cha Yakobo. Yakobo alikula kiapo kwa Mungu--“alitia sahihi kitabu kisicho na maandishi” na alikuwa tayari kupeana kila kitu. Mungu alifurahi sana kwenye utukufu aliopewa kupitia kwa mtumishi wake wa haki Yakobo hata kujinaki kwa shetani. Shetani alimjaribu Yakobo kama ni uongo ama ukweli “alitia sahihi” kwa kusoma mstari moja baada ya mwingine (kwa utaratibu). Mwishowe, Yakobo alithibitisha kweli alikuwa amesalimisha kiapo kabisa kwa Mungu na utukufu ulipewa Mungu wala si shetani. Yakobo hakuwa ndio kiegemeo cha hadithi—Mungu na shetani ndio waliokuwa. Ama sisi si kiegemeo cha vita ambavyo vinapiganwa hadi siku ya leo? Hata hivyo vita ni kwa utukufu wa Mungu ambao unadhihirika maishaini mwa Yakobo pia unatuzingira.

Kabla ya kumpa Mungu utii wetu, sehemu zote za mwili wetu ziko kwenye himaya ya mwovu. Dhambi zetu humwalika kuwa huru maishani mwetu. Hebu ni- eleze elimu hii.

Tuchukue maisha yetu kama nyumba. Mlango u wazi kwa mwovu kutembea kihuru humu nyumbani. Maisha yetu ya dhambi humpa uwezo wa kututawala. Tunadhambi katika kila chumba: Uzinzi, kuabudu sanamu kwa namna nyingi, uraibu, kidunia na mengine mengi. Hii hufanya mianya na kumpa ruksa ya kupata njia ya kuingia ndani yetu.

Hebu tafakari juu ya kubadilika: Tunapojisalimisha kwa Mungu, toba yetu husafisha nyumba kupitia kwa Yesu. Ni kana kwamba hiyo nyumba mnunuzi alikuwa Mungu, na sisi hatuna haki ya umiliki. Kwa kweli, dhambi haina ruhusa kuishi hapo. Bado tunao uwezo wa kufanya hivyo, lakini ni kwenda kinyume na “kawaida” za mwenye nyumba sisi kutenda dhambi.

Pasipo kuwa na usalimishaji kabisa, hata hivyo, taswira nyingine tofauti inajileta. Kama kuna sehemu ya maisha ambayo hatusalimishi kwa Mungu, shetani bado ana ruhusa kutenda katika sehemu hiyo. Nyumba imebadilishwa umiliki, lakini kuna baadhi ya vitu bado tumeficha ndani.

Hebu fikiria, kwa mfano kuwa kuna mikufu ndani ya chumba cha faragha cha Mungu. Nani kati ya viumbe vyote ana nguvu na mamlaka ya kuiba kutoka kwa Mungu? Huo ni ukweli, hapana mtu! Lakini sisi tukiwa kama wapangaji katika hiyo nyumba, bado tunaweza fungua mlango na tuwache watu waingie na kuwaruhusu kuchukua vitu—hata kama ni mali ya kihaki ya mwenyewe, bali si sisi wapangaji. Kweli nyumba inaweza kusafishwa na mlango kufungwa, lakini tunaruhusu shetani kuingia. Shetani bado ameruhusiwa kuingia katika sehemu za giza. Kwa kufanya hivyo, anapata fursa ya kukanyaga maguu yake ya funza kwenye kila chumba. Ndio sababu mwangaza wafaa kung’aa katika vyumba vyote vya faragha, na hizo sehemu zitwaliwe kutoka kwa shetani na zipewe Mungu.

Kwa hivyo, hii inakaa vipi katika maongezi tekelezi? Mwelekezi anapitia orodha ya kiroho na mwanafunzi. Kupitia kujiangalia nafsi na maombi, lazima kihalisi waandike chini dhambi zao zote za sasa, ngome za kitambo, ukandamizaji na mengine mengi. Mwanafunzi lazima atubu ili kuruhusu utakaso. Halafu, kwa sauti ya juu (sababu shetani hawezi soma mawazo ), kemea mwovu—chukua hii kutoka kwake kwa kuangaza mwanga kwa vitu hivi, amuru shetani kutoka na umpe Mungu vitu hivi. Taja kinagaubaga

28

kuwa mwovu hana ruhusa na mamlaka kufanya katika sehemu hizi. Kana madai ya shetani na uulize Mungu akupe nguvu na ulinzi—funga mlango ili shetani asiingie ndani. Kisha choma orodha.

Kukimu ushindi (na kuweka shetani mbali asiingize guu lake ndani ya mlango tena) funza wanafunzi kuishi muda hadi muda wala si siku hadi siku. Kama yeyote anapambana na uvutaji wa sigara, wanaweza wacha na kukosa kwa muda. Lakini kwa muda mwingine wanaweza, wakatambua dhambi zao na kutubu, kemea adui, kumbusha shetani kwamba hana mamlaka juu ya ngome hizo, zima sigara na utupe pakiti. Kuna ushindi muda baada ya muda. Kama siku baada ya siku, sisi pia huwa tunaweka kuwa haki kwa kusema “nitawacha kuvuta baada ya pakiti hii kuisha. ”Utukufu kwa shetani badala ya kwa Mungu.

Sasa mpitishie mwanafunzi katika hatua hizo hizo juma lijalo. Vyumba vingine haviwi safi kwa mpito mmoja—mabaki ya zulia mara nyingi hurudi kwa mara chache, na uhuru kamilifu ndio mwisho. Mungu Atatukuzwa katika maisha hayo.

Sasa nataraji ningekuwa na nafasi ya kutosha kushughulikia swala hili, sababu ni la muhimu kwa uhuru kutoka kwenye nguvu za dhambi. Maisha yaliyobadilika kabisa yanaweza patikana kama nguvu za dhambi zimeshindwa kabisa. Hata hivyo naamini Roho Mtakatifu amalizishie nilipowachia.

Mungu, wape watu wako uhuru kutoka kwa pingu za adui. Nakemea adui na naamuru katika mamlaka ya jina la Yesu Kristo akae

mbali kutoka kwa watu wako. Waweke huru kutoka katika nguvu za dhambi na urejeshe utukufu wako. Katika jina la Yesu. Amina.

Mawasiliano na Mungu

Tunapoingia kwenye mahusiano na Mungu kupitia kwa Yesu, mara nyingi huwa tunapewa Biblia na tunaambiwa kuwa ni kitabu cha kutawala maisha. Ishakuwa, huu ni ukweli japo nusu, naamini kuwa hii ni picha ya neno la Mungu kwa kweli hupoteza dhamira ya ukweli—ambayo ni kutuelekeza kwake.

Biblia sio mwisho; ni njia ya kuelekea mwisho. Mwisho ni kutukuza Mungu kupitia kwa Utii uliorejeshwa Kwake, utii huo ukipelekea kubadilishwa kabisa kwa maisha. Neno lipo ili litupe busara, mifano na mawasiliano ya moja kwa moja na Muumba wetu na Mkombozi kupitia kwa Roho Mtakatifu. Tunakaribshwa kusikia kutoka kwa Mungu kama tutafungua mioyo yetu kwa yale anayosema.

Wengi walio na “masomo” ya kimsingi ya Biblia watakerwa sana na usemi wangu kuwa hata hatuhitaji neno liloandikwa. Hata hivyo tuliambiwa kwa maneno yasio ya uhakika kuwa Roho ametosha kutuelekeza (Yohana wa Kwanza 2:27 na Yohana 16:13-15). Neno lililoandikwa hufanya kazi ya kufungua masikio yetu kwa sauti Yake. Ukweli huu hufanya kazi katika kanisa lililodhumuniwa duniani kote ambako waumini huishi maisha yaliyobadilika kabisa, kwa udogo wa kanuni za kanisa (kama kanisa la Agano Jipya). Wakati mwingine mimi hufikiri kuwa jinsi Neno linavyotumiwa kunaweza zuia uhusiano wetu na Mungu badala ya kuutia nguvu.

Sote tunaamini Wahibrania 4:12 inavyosema, Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena linaukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena ni jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.

Bado katika utekelezaji, mara nyingi huwa tunachukulia kama kitabu cha historia na cha kuongoza—wala si kinachoishi na tendaji, ni neno la Mungu lenye maeneo mengi. Magharibi tuna Biblia kamilifu na nyenzo nyingine nyingi zinazotueleza inamaanisha nini—inatuelimisha zaidi ya uwezo wetu wa kutii. Hata hivyo, utekelezaji wa elimu kama hii unatuweka katika hali ya kuhukumiwa (Yakobo 4:17, Mathayo 7:24-27 na Yakobo 1:22).

Naonelea tuchukue hatua tatu nyuma hadi kwenye usuli na utekelezaji wa usikivu wa neno la Mungu. Huo ndio msingi wa ukuwaji mzuri wa kiroho.

Hapa pana ushauri tekelezi ili kuweka utekelezi mpya katika wanafunzi wako. Kwa wanaoanza, nashauri mpango mwepesi wa usomaji: Sura moja kwenye Zaburi, Methali, Injili, Matendo ya Mitume, Waraka na Ufunuo kila siku. Hii huchukua takribani dakika 20 na itawapa wanafunzi wako namna nzuri ya kuchunguza umuhimu na kufanyia Mungu kazi. Lakini hakutoshi.

Pia nashauri mbinu nyepesi ili kuhakikisha kuwa usomaji Biblia ni kufungua mlango ili kusikia kutoka kwa Roho na kuwa “mtenda” wa Neno. Tengeneza majedwali katika shajara: Mstari uliosoma, nini Mungu anachozungumza nawe kibinafsi kupitia kwa habari hiyo (sio tu ukweli), na nini Anachotaka wewe kufanya na yale umejifunza (binafsi). Mtindo huu humruhusu mwanafunzi mchanga kutafuta sauti ya Mungu na huwabidi kuangalia neno la Mungu kama njia ya kusikiliza kutoka kwake. Pia inahimiza kutii na kutenda. Kutotenda na kutotii ni dhambi (Yakobo 4:17) Na yafaa kwa nguvu tusihimize unyakuzi wa elimu bila kuwepo utii. Mtindo huu umeenea sana katika ukristo wa kileo, na ni tabia ngumu kuiondoa. Ikishaasiliwa itakuwa vigumu kukuza msusuru mzuri wa uanafunzi.

Vilevile funzeni wanafunzi wenu jinsi ya kuomba. Tayari tumeshughulikia kusikia kutoka kwa Mungu. Sawa, maombi ni mawasiliano kuwili. Funza wanafunzi wako kuuliza, ndio, na pia kusikiliza jibu. Vilevile wanafunzi kutukuza Mungu—wamsifu kwa kuwa Niyeye na kwa Yale Ametenda. Usije kwake na orodha ya matamanio yako. Hiyo itamletea vipi utukufu? Wafunze kuombea watakatifu. Wafanye waombee wanafunzi wao watahiniwa kwa dakika 15 kila siku. Waombee jamii, familia zao na mahitaji mengine. Hii itaweka muundo mzuri wa kutilia maanani mahitaji ya wengine, badala ya kuwa na maombi ya kuangalia mahitaji yao binafsi. Wafunze kuomba bila kukoma—maisha ya sikuzote kuwasiliana na Mungu.

Wafunze na uwahimize kufunga moja kwa moja. Kufunga hushinda mwili na kuufanya kuwa usikivu mzuri wa Roho. Nashauri kufunga kwa siku moja kwa wiki, kwa lengo la kuangalia kupata mwanafunzi wake kivyake kushiriki katika safari ya imani. Wanapomsikia Mungu zaidi na kuona jinsi kufunga kunazidisha uhusiano na Mungu, watajifunza kuchanganya kufunga kama sehemu muhimu sana katika maisha yao ya kiroho.

Ikiwa tabia hizi zitawekwa mapema na wanafunzi wako, utakuwa karibu kujihakikishia Mungu binafsi ataongea, kukuza na kuelekeza wanafunzi hawa kuenda mbele. Hawatazuiwa na misukumo kutoka nje. Wataelekezwa bila kusita kutafuta ushauri Wake na kutii yale waliosoma. Hii misingi mikubwa na tabia ya kuanzisha moja kwa moja na wanafunzi wako na bila ya shaka kukuza tathimini ya usambejani nzuri kwa vizazi vingi.

Kwenye sura za usoni, nitaongeza vidokezo vingine ambavyo vitasaidia kuzuia kupata na kukuza tathimini ya usambejani mbovu ya Kiroho.

29

Mungu naomba kuwa waja wako watajifunza kusikia sauti yako na kwa makini wahitaji kuwasiliana nawe. Naomba kuwa unyamazishe uaribifu maishani ili kuwaruhusu kulinda muda wao nawe—wapate kuelewa, kuongozwa na kutii. Katika jina la Yesu.

Amina.

Kupewa Nguvu

Sasa nitafunza juu ya mada ambayo kwa bahati mbaya imekuwa tata kiasi, hata hivyo sitalegea kufunza kitu hiki cha kuoneka, kwa sababu madhumuni ya msururu huu ni kuhamasisha askari wa akiba kwa vita. Na kitu cha mwisho ambacho ningependa kufanya ni kuwatuma kwenye mstari wa mbele bila silaha—baya zaidi, na bunduki zao mikononi mwao lakini bila risasi.

Kabla hatujaangalia kupewa nguvu kibinafsi, kwanza tuangalie mfano uliowekwa mbeleni kwenye Maandiko na Yesu Mwenyewe. wengi wetu hudhani kuwa sababu ya Uungu wa Yesu, alifanyizia humu na kupitia kwa nguvu zake za kiasili. Hata hivyo nadhani maandiko yanatoa picha tofauti. Wafilipi 2:5-8, kati ya mazungumzo mazuri juu ya fumbo la kiwiliwili, yanaonyesha kuwa alijitoa uungu Wake na kuchukua umbo la mwanadamu. Kama huu ni ukweli, Alipata wapi nguvu Zake?

Maandiko hayazungumzii sana juu ya maisha ya mapema ya Yesu. Kuelewa kwetu kuzuri ni kuwa Alikuwa mkazi wa mji mdogo Aliyeishi kimya kama seremala. Luka 3:23 inatuambia kuwa maisha ya Huduma Yake ya umma haikuanza mpaka alipotimiza miaka 30. Ya muhimu sana ni mistari 21-22, ambayo inadhihirisha kuwa kabla ya kuanza huduma Yake ya umma, alikutana na Roho Mtakatifu. Kisha tunasoma katika Luka 4:1, 4:14 na 4:18 kuwa Yesu “Alikuwa amejawa Roho Mtakatifu,” “Akiongozwa na Roho Mtakatifu” “Katika nguvu za Roho Mtakatifu” na kuwa “Roho wa Bwana alikuwa juu “(Yake). ”Sasa tunajua kuwa kufuatia matukio haya Yesu alizunguka Akifunza kwa mamlaka kwa mifano mingi ya Nguvu. Sadfa? Hmmm…

Mnajua kuhusu Yesu wa Nazarethi, jinsi Mungu Alivyompaka mafuta ya Roho Mtakatifu na nguvu, na jinsi alivyoenda kila mahali akifanya mazuri na kuponya wote waliokuwa wamekandamizwa na shetani, kwa sababu Mungu alikuwa naye. (Matendo ya Mitume 10:38 msisitizo umetiliwa)

Kwa misingi hii ya kazi ya Roho Mtakafu maishani mwa Yesu, wacha polepole tubadilishe mwendo hadi kwa watakatifu.

Mtazamo wa Yohana Mbatizaji akiongea juu ya Yesu Kuja baada ya yeye imenukuliwa katika vitabu vyote vinne vya Injili kwa tofauti ndogo mno (Yohana 1:33, Luka 3:16, Mathayo 3:11 na Mariko1:8). Huu ndio mstari mfupi zaidi: “Nambatiza nyinyi kwa maji, Lakini Yeye (Yesu) Atambatiza kwa Roho Mtakatifu. ” (Mariko 1:8) Najua neno “ubatizo wa Roho Mtakatifu” linatia wengi tumbojoto—ambayo inanilazimisha kubadilisha nitumie neno jingine. Hata hivyo hili ndilo neno alilotumia Yohana Mbatizaji, Petero, Yesu Mwenyewe na waandishi wa vitabu vitano vya Biblia. Sina haki ya kuita kitu kingine.

Tunasoma katika kitabu cha Yohana 14:12, baada ya Yesu kuwaambia wanafunzi wake kumwamini Yeye kwa sababu ya miujiza aliyokuwa Amefanya, “Kweli nawaambieni nyinyi, yeyote aaminiye ndani Yangu, kazi ninazofanya, atafanya naye pia; na kazi kubwa zaidi ya hizi atafanya, kwa sababu naenda kwa Baba. ” (Yohana 14:12).

Je, kuenda kwake kwa Baba kungefanyaje wanaoamini ndani yake kufanya kazi kubwa zaidi ya vile Alivyofanya? Anajibu hilo swali katika mstari wa 16 “Nitauliza Baba, na atampa Msaidizi mwingine ili awe nanyi milele daima” (Yohana 14:16). Zaidi Yohana 16:7 inasema, “Lakini namwambieni ukweli ni kwa manufaa yenu kuwa niende; kwa kuwa nisipoenda; Msaidizi hatakuja kwenu; lakini nikienda, Nitamtuma kwenu.” Aliahidi Atatuma Roho Mtakatifu!

Hapa pana maagizo ya mwisho Aliyowapa wanafunzi wake kabla ya kupaa kwake “kuenda kwa Baba. “Na sikizeni niwaambie, Natuma mbele yenu ahadi ya Baba Yangu juu yenu; lakini mngoje mpaka mvishwe nguvu kwa Roho kutoka juu. ” (Luka 24:49). Matendo ya Mitume 1:5 na 11:16 inaweka wazi zaidi kuwa Yesu Aliwaambia wangepokea “ubatizo wa Roho Mtakatifu,”Alitumia istilahi ile. Katika Matendo ya Mitume 11;15, Petero anarejelea yale mambo wanafunzi walikumbana nayo awali katika Pentekote kama “kubatizwa kwa Roho Mtakatifu,”Ahadi kutoka kwa Yesu. Anafananisha na tukio lililompata Cornelius na Malipo ya madeni akisema wamepokea zawadi sawa na hiyo jinsi wanafunzi walivyokuwa hapo mwanzoni. Hmm, Pentekote ikianza huduma—Unaona muundo hapa?

Najua kuwa wengi waamini kuwa huku kudhihirika kwa nguvu za Mungu kumekoma. Hata hivyo, Misingi ya kibiblia ya utesi huu ni ya mashaka. Wakorinzo wa kwanza 13:8-10 inabisha kuwa “ukamilifu” umekuja (kwa njia ya mafunzo ya kidini) kidogo ni la kutia shaka. Kwanza kabisa kama ukamilifu upo hapa, hii inadokeza vita vimeisha—Ufalme umeanzishwa na adui amenyenyekezwa. Hebu tazama habari za jioni, utaona kuwa hii sio hali; Pamoja na hili kuna kuweka pamoja kwenye orodha “Karama zilizowacha. ”Ni rahisi sana kulenga nguvu za udhihirisho (unabii na kuongea katika ndimi), Sawa, si udhihirisho wa nguvu ulikuwa wa Mitume? Kwa upande mwingine, tunaona katika Matendo ya Mitume kuwa watu zaidi ya 12 (ongeza Paulo) walitenda kwenye nguvu (Matendo ya Mitume 9:17-18). Mariko 16:17-18 imelengwa wazi kabisa kwa watakatifu na inaorodhesha baadhi ya Karama ambazo zaweza dhihirika kwa Roho Mtakatifu. Yesu Mwenyewe Alisema kitu hicho hicho katika Yohana 14:12. Vilevile, Wakorinzo wa kwanza sura ya 12-14 ilielekezwa kwa watakatifu ndani yazo. Paulo aliwambia waumini kutafuta karama kubwa kwa udi na uvumba (unabii kabisa), bila kusahau kuongea katika ndimi (Matendo haya yamepigwa maruku na wengi hivi leo licha ya maonyo ya upole ya Paulo).

Sasa masuala ya Kiroho kidogo ni fumbo. Tunajua kuwa Roho hujifunua katika kiwango kwa mfungwa wa dhambi kabla ya uzaompya. (Yohana 16:8) Pia tunajua kuwa bila ya shaka tunapewa Roho kama kithibitisho cha ukombozi kwa siku ya kuzaliwa upya. (Waefeso 1:13 na 4:30, na Wakorinzo wa pili 1:22). Kwa mfano katika Injili ya Yohana Roho Mtakatifu Alifunuliwa kwa wanafunzi kama tukio wazi kabla ya tukio la ubatizo katika Pentekote. “Na kwa hilo alipumua ndani yao na Kusema, “Pokeeni Roho Mtakatifu.” (Yohana 20:22).

Hata hivyo, tunaona wazi miundo katika Maandiko ya wale wliopewa nguvu na Roho Mtakatifu (inayoitwa ubatizo wa Roho Mtakatifu) baada ya uzaompya, wakati mwingine kabla ya ubatizo wa maji (kwa mfano Wayahudi na Kornelias, soma (Matendo ya Mitume 10),Tunaona wengine “wakijazwa” na Roho Mtakatifu baada ya ubatizo wa Roho Mtakatifu (Petero alijazwa mara tatu baada ya Pentekote). Ajabu? Ndio. Ni ukweli kabisa!

Maandiko yanaonelea kuwa ubatizo wa Roho Mtakatifu ni karama imekusudiwa kabisa kutupa nguvu kwa ajili ya huduma. Huu ulikuwa muundo katika huduma ya Yesu na katika huduma za Mitume. Yesu Alisema,

30

“Mtapokea nguvu baada ya Roho Mtakatifu kushuka juu yenu; na mtakuwa mashahidi wangu kote Jerusalemi na Judea kote na Samaria, na hata katika vijiji vyote vya dunia. ” (Matendo ya Mitume 1:8). Sasa tuna ushahidi wa kutosha kusema kuwa ubatizo wa Roho Mtakatifu hauhitajiki kwa wokovu. Ni karama ya kupeana nguvu.

Mwalimu kwa majina Apollos aliyekuwa na kipaji alifunza bila kukosea kuhusu Yesu na bila shaka akaonyesha kuwa Yesu Alikuwa Kristo. Wanafunzi waliambia wengine wamkaribishe. Lakini, Priscilla, Aquila na Paulo wote walitambua kuwa kunakitu kinakosekana (Matendo ya Mitume 18:24-28 na 19:1-7). Paulo aliuliza Apollos kama alikuwa amepokea Roho Mtakatifu. Alisema alikuwa amepokea “ubatizo wa toba”pekee. Paulo alimwekea mikono pamoja na stakabadhi zake na akapokea karama ya Roho Mtakatifu. Je, walikuwa wameokoka kabla ya tukio hili? Wazi kabisa.

Sasa namsihi nyinyi kwa kumaanisha mzingatie miundo iliyowekwa mbele kwenye maandiko. Miundo hii bado inafuatwa kote duniani hivi sasa, japo wengine wanabisha uhalisi wake. Naomba ya kuwa utafungua akili na moyo wako kwa ukweli huu. Kusema ukweli sasa, bila nguvu za Roho Mtakatifu kujidhihirisha ndani na kupitia kwetu, tunadunisha huduma yetu sana. Nguvu zake ni moja kati (ama ni) ya funguo za maana katika upanuzi wa Ufalme.

Namsihi kuomba kwa ajili ya ubatizo wa Roho Mtakatifu kama bado hujabatizwa. Omba kupitia Luka 11:13 hivi (uliza, tafuta, bisha). Vilevile, naonelea kuwa upate watu waliojazwa Roho wakuwekee mikono juu yako na wakuombee—huu ndio mtindo pia kote kwenye Maandiko. Fanya hivyo hivyo kwa wanafunzi wako. Wape silaha na risasi wanazohitaji kupigana katika mstari wa mbele wa upanuzi wa Ufalme. “Kama nyinyi mkiwa waovu mnajua kupeana zawadi nzuri kwa watoto wenu, Je, ni kwa kiwango gani ambacho Baba wenu Wa Mbinguni anaweza peana Roho Mtakatifu kwa wale waulizao?” (Luka 11:13)

Mungu, wape nguvu na ushujaa watakatifu wako kwa ujumbe wako. Katika jina la Yesu. Amina.

Kutafuta, Kupata na Kuwahitimisha Wanafunzi Wapya

Pindi tu baada ya kupata busara, kubali utume, tubu, pata uhuru kutoka kwa adhabu na nguvu za dhambi katika maisha yako, wachilia ngome kuu na kupewa nguvu na Roho Mtakatifu, yafaa uhusike katika utume. Hiyo inamaanisha kuwa yafaa utafute na upate mwanafunzi ambaye kwake utapanda busara na kuendelea kuzagaza utukufu wa Mungu.

Kwa hivyo unaanzia wapi? Kila wakati anza kwa kufunga na kuomba. Sanya waombezi pia kujiunga. Omba dakika 15 kwa siku kwa ajili ya mwanafunzi. Nashauri pia kufunga siku moja kwa wiki, kwa ajili ya wanafunzi wako. Utekelezo mzuri ni kutokula mara mbili kwa siku—enda mlo mkuu hadi mlo mkuu ama kishuka hadi kishuka. Lengo ni kufanya utuaji uwe mzuri. Kubadilisha utii kutoka duniani hadi kwa Ufalme na kupata busara katika utendaji wa Mungu, sio mwanadamu. Lazima tuingie kwa nguvu Zake. Hii sio hatua ya kubadilisha Kielimu. Lazima aongoze njia.

Mahali pazuri pa kupata wanafunzi ni kwa kuhudumia mahitaji katika jamii yako. Vitendo vya huduma, kusaidia maskini na waliokandamizwa, kushauri (ndoa, uzazi, kifedha, utumiaji wa mihadarati, dhambi ya uzinzi n. k), huduma ya magereza, sherehe za vyakula, kutoa chakula kwa jamii n. k. ni fursa nzuri za kupata mtu ambaye Mungu anataka wewe binafsi umfunze. Watu katika uhitaji ndio wazuri kwa uanafunzi kwa sababu kuna taharuki maishani mwao, na kila mara wanatafuta mabadiliko. Cha kusitahajabisha, watu walio tayari katika hali ya mabadiliko kila mara ndio hukubali. Kumbuka hilo!

Uinjilisti wa barabarani na kuhubiria umma ni kuzuri, lakini si kwa kila mtu; upendo wa mguso wa huduma una faida ya kufikia moyo wa mpokeaji. Hata ukichagua mtindo usio sana wa kibinafsi, kuwa makini sana ili usitengeneze waongofu lakini kuwa macho kufuata kupitia kwa uanafunzi. Hapana kitu kingine kinacho mtukuza Mungu kuliko maisha yaliyobadilika na tiifu.

Wale walio na vipaji vya kiapostoliki yafaa watafute makundi ambayo hayajavumbuliwa (mwongofu wa kwanza katika familia, jamii, n. k). Mwanafunzi wa kwanza ndio wa maana zaidi kuwa na uhakika ameteuliwa na Mungu--“mtu wa amani” (Luka 10, Mifano ya Kibiblia: Lydia, mwanamke katika kisima, Kornelias, Mfilipi mfungwa). Mtu huyu ametayarishwa na Mungu ili kufikia upeo wa kuathiri. Wana athari. Kwa sababu ya kubadilika kabisa kunapata usikivu. Watu hawa kwa kawaida ni watafutaji na humeng’enya vitu hivi kwa udi na uvumba. Toka hapo “mtu wa amani” na kizazi cha usoni cha wanafunzi kitalenga upeo wao wa kuathiri, ama oikos. Huu ndio mtindo mpaka kizazi cha usoni cha Kiapostoliki ambacho kina karama kitanyanyuliwa juu tena tafuta “Mtu wa amani” mwingine.

Mzunguko mzuri wa uanafunzi ni kutafuta wanafunzi wapya pindi tu baada ya majuma mawili ama matatu katika uanafunzi (ukiwa umechelewa mwezi moja, kama kweli wanapambana kupata uhuru na kupata nguvu). Kisha kuwa na mwanafunzi kwenye foleni kati ya miezi miwili hadi mitatu, hasa miwili. Sababu ya kubadili haraka ni kuwa wanafunzi wanapoingia katika utume mapema kuna uwezekano wa busara na Tathimini ya Usambejani kuwa bora hadi kwenye kizazi kijacho.

Kigezo kimoja cha kuzingatia katika kuchagua mwanafunzi ni manufaa ya kuekeza wakati mzuri naye. Chagua watu wanaoishi karibu kukutana nao kila mara ama kuja mara moja moja. Kama mtu anaishi umbali wa kutembea saa moja ni nadra sana kukutana kila mara—na wakati huu uekezaji wa wakati ni wa maana sana kwa utekelezaji wa uanafunzi. Kinyume cha haya kutabadilisha na kuwa misururu ya mikutano iliyopangwa.

Sasa wanafunzi pia lazima wawe katika hali ya “kufuzu. ”Usingependa kupoteza wakati wako kwa watu ambao hawataki ama hawako tayari kua (kuendelea). Watanyonya nguvu zako, wakisiamisha vuguvugu la kufanya wanafunzi. Watu hawa hawabebi busara hadi kizazi kijacho (kama watafanya basi ni tathimini mbovu ya usambejani). Wametumwa na shetani ili kuharibu maendeleo. Wewe songa mbele na waweke kwa kiti kama “askari wa akiba” wa siku zote.

Mwanafunzi lazima awe amejitolea kabisa kwa busara na utume. Lazima kusalimisha yote kwa Mungu—ilyodhihirishwa kwa “kutia sahihi karatasi isiyo na maandishi. ”Kutofuata haya kutapelekea kufutiliwa mbali kabisa. Kuwa hakika ya kuzuia jaribu la kuorodhesha “dhambi” itabidi waache—endea msalimishaji msimasharti. Orodha hiyo itakuja wakati wa toba na kuvunja ngomekuu. Wahitaji kujitolea kwa sasa.

31

Wanafunzi wako lazima waweze kupokea kutoka kwako. Itabidi wakuamini na wawe wazi. Hawataweza kupata uhuru kutoka katika ngomekuu bila kuwa na uwazi. Nawe, lazima uwape pendo na uwatie moyo. Huwezi kuwa mbishi ama kutawala. Wanahitaji kaka mkubwa kuwapa mapenzi sio mama gubu.

Fauka ya hayo, wafanye kuhitimu kwa kuwapa mazoezi. Shetani atafanya lolote ili kuwazuia kwa masuala mengine. Lazima washikilie busara na kuweka macho yao kwa utume. Kuwa macho kwa kuwakumbusha haya.

Kuwa mwangalifu kwa kuwalenga walio makanisani. Kuna kutosoma kwingi kwafaa kufanywe ikiwa unajaribu kuweka usambejani mpya wa Ufalme ndani ya mtu ambaye ana historia ya usambejani wa “kanisa. ” Lakini kwa njia zote, wale walio na njaa ya kwenda kutoka kwa askari wa akiba hadi vitani na wana sifa hizo sifa za hapo juu, basi nendeni! Twahitaji majeshi wote tunaoweza pata.

Vile vile, ni hekima kulinganisha mwongozi na mwanafunzi: Wanawake kwa wanawake, wanaume kwa wanaume, jinsi ilivyo sawa. Hatutarajii watu kutoka jinsia nyingine wazungumzie ngome za kutwaana hivyo hivyo ni muhimu sana kulinganisha waongozi komavu na wanafunzi ambao si komavu, ndio wawe na tajriba ya kupeana ushauri wa maisha (hutaki mwanafunzi wa chuo kuongoza mtu aliyeoa na ako na watoto kwa mfano). Hii si ngumu na kuongoza haraka; kuwa na hekima tu.

Kuhusiana na wanafunzi wangapi yafaa uchukue, hapa pana mwongozo. Mtakatifu mchanga aweke kiwango cha mmoja kwanza. Kisha aongeze wengi kadri Mungu anavyomtuma kuwa anaweza mudu. Lakini tafadhali, kumbuka mwongozi husaidia wanafunzi wa wanafunzi akiwa pembeni. Kwa hivyo zingatia kwa hekima wangapi wakufaa wewe. Tarajia saa chache za kujitolea kwa mwanafunzi kila wiki. Kiwango cha juu sana kwa mtakatifu mkomavu aliyejitolea muda wake wote kwa uanafunzi yafaa iwe 10. Yesu mwenyewe alichukua 12 na ushuhuda wa hali unasema kuwa Paulo alichukua nusu ya hiyo hesabu. Nadhani kuwa tano ama sita ni kujitolea pakubwa.

Unapopata zaidi ya hiyo idadi, anza kuwa na kiwango chako cha kwanza cha wanafunzi—ongoza watu wapya. Bwana Mungu wa Mejeshi, wape watu wako roho ya kuwaona na kuwatambua wanafunzi ambao umewaandalia. Wewe

ushinde, Bwana. Tunaomba Kwa Jina la Yesu. Amina.

Vidokezo na Nyenzo Za Uanafunzi

Shiriki na mwanafunzi wako hata kama ni masaa machache kwa wiki. Shugulikieni maswala ya maisha kwa pamoja. Kutana na kujuana na familia yake. Shiriki chakula pamoja. Guza msingi dhabiti wa upendo na heshima kati yenu.

Jenga misingi imara ukitumia miundo iliyotolewa kwenye mwongozo huu. Na jinsi inavyoonekana kitu cha ajabu, jaribu kujizuia kujiingiza katika shughuli za uanafunzi Katika “kanisa” ukipanga kwa majumaa kadhaa ya kwanza. Nawauliza mwaambie wanafunzi wenu wasihudhurie kanisa kwa muda Fulani? SHABASHI! Wacha nieleze.

Yale nimewasilisha hapa si sehemu ya usambejani wa taasisi ya kanisa. Ikiwa mwanafunzi atafunzwa usambejani wa Ufalme (kama ukatikati wa utukufu wa Mungu, utiifu kamili, kuwa “mtenda”wala si “mskivu,” kujiingiza katika utume mara moja, kila mtu mwanajeshi, fikra za kivita, kusikiliza Mungu, kuishi kitakatifu, Ukristo kama hali ya maisha, uhuru kamilifu kutoka dhambini n. k). na kuona matendo mengine kanisani, wataelekezwa kuasili chini ya yale mawili. Lazima wawe wamefunzwa mafunzo ya ukweli wa Ufalme na hali ya maisha kabla kufiduliwa kwa matendo ya utamaduni wa kikristo. La sivyo utawapoteza kwa “kanisa”badala ya kuwaingiza katika maisha ya Ufalme.

Kuwa na hakika kukuza na kuweka mipango mwafaka na wanafunzi wako. Wafanye (na uwasaidie) tengeneza timu ya maombi ili kusaidia ukuaji wao na juhudi za uanafunzi. Weka malengo na peana uwajibikaji. Lengo zuri ni kufikia kizazi kijacho kwa miezi miwili. Kwa majuma mawili, yafaa waanze kuomba kwa ajili ya wanafunzi wao wenyewe. Kwa miezi miwili wawe wakifunza mwanafunzi wao mwenyewe.

Sasa bila shaka utakuwa ukiwasaidia kutoka pembeni, ukipitia vitu hivyo hivyo kwa mzunguko na muundo uliowekwa kwenye nyenzo hii. Na kwa miezi, wanafunzi wako watapata wanafunzi wao wenyewe. Unapofika kizazi cha nne, umeanza vuguvugu la kutengeneza wanafunzi—si hivyo mpaka. Linakuwa vuguvugu tu pale ambapo usambejani na busara vinaendelea bila kuhusika kwako—liko kwenye mikono ya Mungu si yako. Katika kiwango hiki haipingiki.

Jiingize kwenye utume na wanafunzi wako. Waonyeshe ina maana gani kuwa mwanafunzi kwa kushiriki maisha pamoja. Usijaribu kuwafunza kupitia misururu ya mikutano na mafunzo. Hudumu pamoja katika huduma za huruma, uinjilisti wa bararani na huduma za kijamii. Kuambia watu kufanya vitu hivi ni mbadala mbaya wa kuvifanya. Onyesha nini maana ya “kupenda jirani yako. Na usikamatwe na kuwaingiza katika mwandamano wa programu za “kanisa”Yafaa wajifunze kuona mambo ya kimaisha ya mkiristo kama hali ya maisha ya Ufalme wala si sehemu ya maisha yao.

Kitu cha kukumbuka kitika kufunza ni: Elekeza, Saidia, Tazama, na Wachilia. Elekeza hali ya maisha ya Ufalme, peana maoni na kutia moyo kwa wanafunzi wako, kuwa hapo kwa “Kutazama”elekeza wanapokua, kisha waachilie waende pindi baada ya kufanikiwa kufanya hayo mafunzo mazoea hadi kizazi cha pili ama tatu. Kanuni moja ni kuwa usiwafanyie kile wanaweza na yafaa wajifanyie wao wenyewe, hata kama unajua unaweza fanya vizuri zaidi. Yafaa wajifunze, Ndio, huku kuwahusisha kufanya makosa fulani.

Unaposhiriki na wanafunzi wako, makinika. Ndio, furahia ushirika wa wengine. Pia jadili mapambano dhidi ya dhambi na maisha ya fikra. Tarajia toba na omba pamoja nao juu ya ufufuo. Waambie juu ya maisha yao ya maombi na muda wao katika maombi. Waulize nini Mungu anasema juu yao.

Kwa wanafunzi waliojipata katika hali ya maisha haribifu, wafunze tofauti kati ya marafiki na mtu umjuaye na uwatie moyo kwa muda waachane na watu wawajuao wale watawafanya wasikatae majaribu. Hata hivyo, washauri wasichome daraja, sababu hutaki wapoteze kikoa chao cha wanafunzi wakati wao ukifika kuhudumia wengine. Waombee na wasaidie kupata mahusiano chanya (uhusiano mzuri) na shughuli mbadala ambazo zitawatia moyo katika maisha yao mapya.

Kwa wachungaji, viongozi walio na vipaji na wale waliozaliwa katika mazingira ya kitaasisi: usijaribu kudhibiti ama kukandamiza kutembea kwa Roho! Kuwa mwazi kwa hawa watu wanaokutana kwa njia tofauti si lazima wawe na uhusiano na kanisa lako. Najua inaweza kuwa ngumu lakini itabidi uwaachilie na uangalie kwa busara, tukufu wa Mungu na utume ambao ni kufanya wanafunzi. Jifunze mwenyewe kufikiria upanuzi wa Ufalme badala ya ukuaji wa kanisa la kawaida. Watu hawa wanaweza ama wasiweze kuhudhuria kanisa. Wanaweza kukutana kama sehemu ya mwili ama waunde makanisa ya kinyumbani. Kile kitu cha

32

uhakika, ni kuwa hata kama wanakutana na kanisa lako, wanaweza tengeneza kijitamaduni kati ya mwili kama kuna utofauti mkubwa kati ya Ufalme na taasisi ya usambejani. Lakini hili lisikutishe. Mungu anatukuzwa na utume unapenyeza kwa vizazi vingi.

Sasa kuhusu ni nini cha kufunza: Kuna mengi zaidi ya kushirikisha katika ujumbe huu mfupi. Mpango wa Kusoma kabla ya kulikowasilishwa ni mwanzo mkubwa wa kuruhusu Roho kuongoza. Zungumzia masuala yanapochipuka. Nyenzo nyingine za maana zinapatikana kwenye wavuti: www. mentorandmultiply. com na www.paultimothy.net, nyingi bure. Standing Firm through the Great Apostacy Kimeandikwa na Steve Gallagher na Megashift kimeandikwa na James Rutz ndio waasisi wa kuelewa nyakati tunazoishi. Shepherd’s story book Kimeandikwa na Thiessen, Thiessen na Patterson ni bora kwa ajili ya upandaji kanisa. Mimi kupendekeza The Church in the House ("Kanisa katika nyumba") kwa Robert Fitts. Ni sasa Tafsiri kwa Kiswahili. Lakini ni nyenzo ya kina kuzingatia katika kufunza juu ya uanafunzi (www. valuesdrivenfamily.com) kwa kuchapisha na kutoa kwenye mtandao bure. Kuna nyenzo zingine nyinyi lakini hapana zaidi ya Neno La Mungu. Kila kitu kipimwe kwa kiwango hicho.

Muhtasari

Japo kitabu hiki ni kifupi, uwezo wa habari unaokena kuzidi. Katika sehemu hii, ningependa kuweka wazi jinsi vipande hivi vinaingiana pamoja bila muundo wa mshono. Ni rahisi sana. Mara vinapotiwa maanani na vitakuwa asili pindi vikitumiwa.

Omba na kufunga kwa uanafunz. Pindi tu unapogundua mtu huyu, anza kupanda busara. Mwongozi lazima atie utashi wa kutukuza Mungu ndani ya mwanafunzi, kuelewa ufupi wa muda na vita vya Kiroho vinavyopiganwa kwa utii wa wanadamu. Wasaidie wanafunzi wako “kuhesabu gharama” ya kusalimisha maisha yake kwa Mungu. Shiriki nao umuhimu wa kuishi maisha yaliyobadilika kabisa na kujiingiza katika utume.

Ili kusonga mbele, wanafunzi wafaa kuelewa kuwa wamesimama mbele ya Mungu. Aya katika Yohana wa Kwanza na zinazohusiana na hizo zaweza kwa kweli kutufunga sote na kukuza kucha kuzuri kwa Mungu ndani yetu. Mafunzo haya pekee yanaweza pelekea toba ya ukweli. Kwa wale ambao hawana elimu ya Injili, ungeshiriki juu ya kuingia dhambini, adhabu tunayohitaji, Kuchukua kwa mwili wa mwanadamu kwa Yesu, kifo chake kama malipo ya dhambi zetu na kufufuka kwake kama dhihirisho la nguvu zake juu ya dhambi na mauti. Wakishakuwa na kuelewa huku kwa msingi na wameshuhudia toba, pitia nao kwenye mazoezi ya “karatasi isiyo na maandishi” ukionyesha Yesu kama Mungu wa maisha yao. Kama watajitolea kikamilifu kwa Mungu na ufalme, yafaa wabatizwe na waweza endelea kufanya nao kazi kwa kukutana nao kwa saa kadhaa kwa wiki.

Wakati wa m(mi)kutano yako ya kwanza, pitia orodha yako ya kiroho. Hapa dhambi na ngomekuu zinatambuliwa na toba ya ndani inakuwa. Hapa ndipo jiwe la mbamba linasafishwa: adui anakemewa, mshiko wake wa sehemu hizo unakataliwa, na kila kitu kinapewa Mungu. Rudia zoezi hili kila wiki mpaka mshiko wake umevunjwa kabisa.

Hatua inayofuata ni kuomba kwa ajili ya kupewa nguvu. Ombea wanafunzi wako kupokea ubatizo wa Roho Mtakatifu. Katikati ya mikutano, moja ya “Kaziziada” yaweza kuwa kusoma maandiko juu ya ubatizo na kuombea karama hii. Ubatizo waweza ama usiweze kuandamana na kuongea katika ndimi; ruhusu Roho Mtakatifu kutenda jinsi Anavyotaka.

Baada ya hii, mwanafunzi wako yafaa afunge na kuomba kwa ajili ya mwanafunzi wake mwenyewe. Hadi wafaa wawe wanafuata mfano wa mpango fulani wa kusoma Biblia (ama angalau wanasoma kivyao kila mara), wamefunzwa kusikiliza sauti ya Mungu. Kuorodhesha yale watasoma kama tulivyosema kutakuwa kwa msaada kuthibitisha ufahamu wao wa Maandiko na kwa kuona kuwa Roho Mtakatifu anawafunza na kuwaongoza hadi kwenye utii mkubwa.

Jiingize katika huduma (kuhudumia ama vinginevyo) na wanafunzi wako kuona kama kutachipuka mtahini wa kizazi kijacho. Ishi maisha ya huduma na upendo pamoja. Pindi tu mwanafunzi anapatikana, msaidie mwanafunzi wako ukiwa pembeni anapoendelea mzunguko anaofuata.

Inaweza kuwa nyepesi zaidi ya hii? Huu ni muundo rahisi, tekelezi, wa kibiblia, wa kina na wa kufanyika katika kuhamasisha vuguvugu la kutengeneza wanafunzi lisilokoma. Sasa msiwe tu wasikivu bali muwe watendaji.

Mungu Mwenye nguvu,Ufalme Wako uje,mapenzi yako yatimizwe,duniani kama ilivyo mbinguni. Katika jina la Yesu. Amina.

Amri za Kuondoka

Kumbuka utii unajipata katikati ya mapambano makuu baina ya Mungu na Hasimu wake Shetani. Utii wetu na huba vinatafutwa ili kutukuza kimoja ama kingine.

Tena, fikiria juu yake kama vita vya usimamizi. Shetani alikaidi (taliki) Mungu na akatimuliwa kutoka nyumbani (mbinguni). Sasa shetani, ili kujikimu kinafsi, anataka watoto. Sio kwamba anapenda watoto lakini anataka tu wamfikie Mungu. Kwa hivyo anafanya kila awezalo ili kupata utii na huba yetu. Mzazi mkaidi kila mara huvutia watoto kwa vitu vya kidunia: mali, raha na uhuru wa kutenda watakavyo. Na wao husema uongo juu ya mzazi mzuri, ili kuweka utii wao.

Mzazi mzuri ni tofauti. Sababu wanapenda watoto na wanajua ni nini kizuri kwao, wanawafanya wanakula, wanaenda kitandani wakati wa kulala, na kutokubali kula vyakula visivyo na virutubishi. Kwa hivyo watoto wajinga wanafuata kushiba kwa haraka kwa utunzi wa mzazi potovu kwa gharama ya kuishi kwa kudumu. Nao watoto wenye hekima hutafuta ulinzi wa mzazi mwenye haki.

Nina imani kuwa ikiwa umesoma hadi umbali huu, umeamua nani atapokea utii na huba yako. Na yeyote yule ambaye ametembea njia potoshi vinafahamika kuwa vishawishi vya shetani vinavutia jinsi vilivyokuwa, huleta uchungu na huvunja moyo. Kwa hivyo tuna mtazamo wa kipekee. Lakini, ndugu zetu wengi wadogo wanahadahiwa na shetani na kumpa utii wao.

Je, tutafanya nini juu yake? Yafaa tuwaambie ukweli!Yafaa twende huko nje na kuwaonyesha mahali uongo huo unaishia. Yafaa tuwaambie kuwa wao ni rehani katika mapambano makubwa kwa sababu ya utii na huba. Yafaa tuwaambie kuwa uhuru na utoshelezaji wa kweli unakuja kupitia kujisalimisha bila vikwazo kwa Baba wetu wa mbinguni.

Kufanya wanafunzi ni rahisi kwani ni kuwapitishia katika hatua ya uponyaji wa kuwa uhuru kutoka kwenye hadaa za shetani, na kujisalimisha kwa Baba mwenye mapenzi. Kisha tuwasaidie kusonga karibu na Baba Mtakatifu na Mjahaki na kukuza bidii kuchukua wengine kwenye safari ya ukweli, uhuru na kupewa nguvu.

Rafiki Yesu anatuambia tupende adui zetu kwani si adui zetu ila watoto waliodanganywa wanaotumiwa kama rehani ili kuiba utukufu wa Mungu. Kwa hivyo twende huko nje na tuibe watoto wakaidi kutoka kwa minyororo ya baba yao mwongo shetani.

33

Nendeni mkafanye wanfunzi kote ulimwenguni, mkiwabatiza katika jina la Baba, la Mwana na Roho Mtakatifu, mkiwafunza wazingatie yale yote Nimewaamru nyinyi. (Mathayo 28:19-20)

Ukweli utakuweka huru! Uhuru ni nguvu, na nguvu huelekeza hadi kwa utukufu wa Mungu! Sasa nendeni kule nje mkahubiri kwa moto usiozimika juu ya Upanuzi wa Ufalme!

Baba Mungu mwenye nguvu, Naomba kuwa utukufu wako utafunika dunia yote. Naomba kuwa adui atanyenyekea kwenye kuendelea kwa utukufu. Naomba kuwa wafanyikazi wako watashambulia milango ya kuzimu na kuanzisha vuguvugu la kufanya

maisha yaliyobadilika. Wape watu wako nguvu. Tukuzwa. Katika jina la Yesu. Amina.

Kuhusu Mwandishi na Nyenzo

Marc Carrier ni mwandishi, mnenaji, kiongozi wa makongamano na mmishonari aliyejitolea kuhamasisha watakatifu kwa ajili ya mavuno ya nyakati za mwisho.

Marc ni mwelekezi wa Upanuzi wa Ufalme. Marc anakaribisha fursa ya kufunza na kuzungumzia juu ya ujumbe wake anaopenda katika eneo lako, Upanuzi wa Ufalme. Marc pia anapenda kushiriki utashi wake wa upanzi wa kanisa, uanafunzi, uinjilisti, matendo ya Agano Jipya, ndoa, uzazi, utunzi wa nyumba, ukuaji wa kibinafsi wa kiroho na elimu ya sehemu ya theolojia.

Tafadhali tutumie barua pepe: [email protected] ili kuweka mikakati ya kuongea na warsha. Kujifunza mengi juu ya Marc na nyenzo zake tembelea wavuti: www.valuesdrivenfamily.com. kwa nakala zaidi za kitabu hiki

tembelea hiyo mitandao hapo juu. Kitabu hiki kimefasiriwa Chini ya Idara Ya Lugha ya Bahati Community Centre Secondary School chini ya Usimamizi Wa Bwana Patrick Wafula Wanyama na Bwana. Sakwa Titus akiwa Mfasiri Mkuu Idara Ya Kiswahili Barua pepe: titussakwa@yahoo. co S. L. P 1242 NAIROBI TEL. +254 721 991 413

34

35

KANISA NDANI YA NYUMBA

KUREJELEA URAHISI

36

Maneno ya Uthibitisho “Hapa kuna kifaa kizuri kwa wale wanaohusika na upanzi wa makanisa kama jiwe la msingi katika kuwafikia watu wa ulimwengu ambao bado hawajafikiwa.”

Dr. Ralph Winter, Mwanzilishi na Rais wa U.S Centre for World Mission. “Bob Fitts Sr ni mtu wa harara ya kulowesha makanisa ya nyumbani na Neno. Huu uharara unaonekana wazi kwenye kitabu chake Saturation Church Planting (Upanzi Lowesha wa Kanisa). Huu kweli ni mkakati wa kuharakisha ufanyaji wa wanafunzi ambao unahitajika kwa dharura sasa vile mamilioni wamekuwa wakimgeukia Kristo katika Asia, Afrika, Latin Amerika na Uropa Mashariki.”

Loren Cunningham, Founder and President of Youth With A Mission. ‘Sio kila mtu atakuwa tayari kwa mageuzi asilia ambayo Fitts anaashiria, lakini kila mtu ambaye anahusika katika kukamilisha Wito Mkuu kwa nyakati hizi zetu anapaswa kujua vifaa vyake…Fitts anasema kwamba ni imani yake dhabithi kwamba kwa miaka kumi ijayo kutakuwa na mtetemo kamili wa Kanisa Ndani Ya Nyumba katika kila nchi duniani. Ikiwa anasema kweli, huenda ikawa tu kwamba mtetemo wa Kanisa Ndani Ya Nyumba uliosababisha kanisa la kwanza kufagia kote katika nchi ya utawala wa Kirumi wa karne ya kwanza, utafanana sana na ule mtetemo ambao hatimaye utaukamilisha Wito Mkuu.”

Dr. James H. Montgomery, Founder and President of DAWN Ministries. “Robert Fitts ni mmoja wa sauti za Mungu juu ya Kanisa Ndani Ya Nyumba zinazokua hivi leo. Amekuwa ‘mtu wa maandalizi’ kwa miaka mingi. Kitabu hiki kinakupa wakilisho ghusubu la majilio rahisi, ya Kibiblia kwa maisha ya kanisa. Twaweza kuuona Wito Mkuu ukitimizwa haraka ikiwa tutafuata mjilio huu kwa maisha ya kanisa. Heri Mungu atumie hiki kitabu ulimwenguni kuwaamusha watu Wake kwa mipango ya Kanisa Lake.”

Nate Krupp Mwandishi na Mpanzi wa Kanisa.

Utangulizi

Wakati wa kiangazi cha 1969 Bwana alininenea nianze kumwomba wafuasi katika kila taifa. Miaka minne kabla alikuwa amenipa maono ya kuombea mataifa kwa majina, akinipa ahadi ya Zaburi 2:8, “Uniombe nami nitakupa mataifa kuwa urithi wako, na miisho ya dunia kuwa milki yako.” Toka wakati huo ikawa ni raha kuomba na kuamini kuwa Bwana anaenda kufanya jambo kuniwezesha kuyagusa mataifa kwa niaba yake.

Mpango wangu wakati huo ulikuwa kuzidisha wafuasi kwa kuangazia mtu mmoja na kumfundisha kufanya hivyo hivyo ili kwamba, kwa wakati, tungeona wafuasi katika kila taifa kwa njia ya msururu wa kupitia maombi, imani na uvumilivu. Nikiwa na hilo kwenye akili nikaanza kuomba kwa bidii sana. Jinsi nimeomba na kuelekea haya maono kwa miaka ambayo imepita, Bwana amenifunulia kwamba njia bora zaidi ya kuwafanya wafuasi watu binafsi ni kuzidisha makanisa (makundi madogo ya watu binafsi).

Kwa kweli naamini kwamba hilo lilikuwa ni jibu kwa ombi hili ya kwamba Bwana alianza kuyabadili maisha yangu na mazingira ili kwamba nilipitia muda mrefu na mugumu wa maandalizi. Jinsi vile miaka iliendelea kupita, nilijaribiwa kuweka kando haya maono kama ndoto potovu iliyojawa na tamaa ya ubinafsi ambayo haikutokana na Bwana kabisa. Lakini kidogo singeyaachilia haya maono yafe ndani mwangu.

Adhuhuri moja tulivu msimu wa 1990 nilikuwa kwa magoti yangu kwenye chumba cha kulala katika jiji la Riverside, California. Wakati huu wa maombi, ninilkuwa nikisoma jarida la Mission Frontiers, jarida ambalo huchapishwa na United States Center for World Mission lililoanzishwa na Daktari Ralph Winter. Nakala niliyokuwa nikisoma ilihusu mshindo wa Mungu katika nchi ya Uchina. Niliendelea kukutana na neno “mshindo wa Kanisa Ndani Ya Nyumba”. Kwa ghafula mwangaza wa maono ukalipuka rohoni mwangu. Nilikaribia kusema kwamba nilihisi kuuona! “MAKANISA YA NYUMBANI!!!!” Sikuwa napiga yowe, lakini roho yangu ilipiga yowe. “Makanisa ya Nyumbani! Ndilo hilo! Ninaweza panda makanisa ya nyumbani! Bwana asifiwe! Ninajua naweza anza makanisa nyumbani!” Msisimko wangu haukuwa na mipaka. Ujasiri wangu ulipanda!

Nilikuwa nikipitia jangwa refu, kavu la roho. Nilikuwa nimetoa kila kitu. Nilikuwa nimeachishwa huduma, nyumba, ndege, afya, na hata tumaini lilikuwa linakauka ndani mwangu. Nilihisi kwa kiwango kidogo kuwa sikuwa nimeitikia wito wa Bwana kwa njia zilizosawa miakani na kwamba singeliwahi ona utimilifu wa maono ya wanafunzi kwenye mataifa yote.

Basi hilo wazo rahisi la kanisa nyumbani lilinitokezea kupitia yale yalikuwa yakifanyika Uchina. Chipuko jipya la maono likaanza kuinuka ndani mwangu.

Niliinuka toka kwa magoti na nikaanza kufikiria na kuomba na kupanga. “Sasa nafahamu kwamba naweza panda makanisa! Naweza panda wingi wa makanisa!” Roho yangu ikapaa. Kwa mara nyingine imani yangu ilikuwa inapanda. Kwa zaidi ya miaka ishirini na minne nilikuwa nimechagua makundi ya nyumbani. Miaka mitano ya hiyo miaka ishirini na minne nilisaidia kuunda mamia ya makundi ya nyumbani kwa ajili ya uinjilisti wa watoto.

Kwa miaka minne mimi mwenyewe nilikuwa mchungaji wa Kanisa Ndani Ya Nyumba nililolifahamu, na nilifahamu kama mtu wa kwanza, faida nyingi za Kanisa Ndani Ya Nyumba. Sasa, nilihisi nikiwa mjasiri kwamba ningeweza saidia kupanda mamia, kwa nasibu hata maelfu ya makanisa ya nyumbani na kuona watu waliofundishwa kuchunga hawa makutano wadogo.

Kwa miaka nilifahamu kwamba ukuaji upesi wa kanisa ulifanyika katika karne mbili za kwanza za Mtetemo wa Kikristo. Sasa nilikuwa nikisoma juu ya ukuaji wa ajabu uliokuwa ukitendeka kule Uchina na ulikuwa wa mshindo wa kanisa la nyumbani.

Vile mawazo haya mawili yalivyoungana akilini mwangu, huo mlipuko ukatokea. Singeepuka hatima hii ya wazi: ukuaji wa shani wa kanisa katika historia, yote ya wakati wa zama na wakati wa leo ulitokea pahali ambapo hapakuwa na jengo la kanisa.

37

Si muda mrefu baada ya haya nilianza mafundisho katika Agano Jipya juu ya Kanisa Ndani Ya Nyumba na nikaandika kurasa nane chini ya kichwa: Hali ya Makanisa ya Nyumbani. Nikaanza kuyashiriki haya na wengine na nikagundua kwamba watu walivutiwa.

Vile Mungu aliufungua ufahamu wangu kwa yale yaliyomo kwenye Agano Jipya na historia ya kanisa juu ya “kanisa likutanalo nyumbani…” na vile niliendelea kupata mawasiliano zaidi na wengine ambao walikuwa wameona haya maono ya kanisa rahisi, niliongezea hizo kurasa nane na kuiita: Upanzi Lowesha wa Kanisa.

Kote kwenye kurasa zifuatazo nimetafuta kuweka mbele yangu wasia wa busara wa Daktari John Amstutz, rafiki wa muda mrefu na kiongozi wa mikakati ya utume na mwalimu kwa Mwili wa Kristo. Miezi kadhaa iliyopita nilimtumia nakala ya Hali ya Makanisa ya Nyumbani.

Neno la Utangulizi Waraka wa Thibithisho

Kwa Ndugu Mpendwa Bob,

Nakala yako juu ya makanisa ya nyumbani ilikuwa adhimu. Inarudisha yale wengi wetu tumeamini kwa miaka mingi, kwamba upanuzi wa injili kwa mataifa yote ungehitaji mbinu rahisi, ya uzalishaji usio kikomo wa upanzi wa kanisa, aina ambayo inapatikana kwenye maandiko yenyewe, na pia kwenye nchi ambazo hazitaruhusu ibada na kushuhudia kwa wazi, kama vile Uchina, Burma, na Nepal.

Katika dini yetu, kazi yetu inayokua upesi mno katika mataifa ya vizuizi vya kufikia ni mitetemo ya Kanisa Ndani Ya Nyumba. Hili ni kweli katika mataifa ya Sri Lanka, Nepal, Pakstani na Burma.

La zaidi, kwenye nchi nyingine ambapo kuna kipimo cha uhuru, makanisa ya nyumbani pia yanaendelezwa kama mbinu ya upesi zaidi ya kusababisha mshindo wa kweli utendeke. changamoto kuu katika kuzifungua akili kuhusu makanisa ya nyumbani ni katika nchi ambamo injili imeenea kwa miaka mingi, kama nchi za Uropa na Latin Amerika, Asia imejithibisha kuwa rahisi zaidi kwa uendelezaji wa makanisa ya nyumbani.

Bob, ningekuhimiza uendeleze makanisa ya nyumbani kwa ubusara na wepesi wa kuona popote uendapo, hasa katika nchi za ulimwengu wa tatu. Pia usaidie watu wawe wanyenyekevu juu ya hili jambo ili wasije wakawadharau waamini ambao wameamini katika majengo.

Hitaji kuu hivyi leo ni umoja katika Mwili wa Kristo. Kwa kweli hakuna haja ya kugawanyika juu ya majengo. Basi wasaidie watu watoe nafasi kwa mbinu tofauti tofauti, na kwamba hilo ndilo tunazungumzia. La muhimu ni kwamba tufikishe injili ulimwenguni kote kwa haraka na kwa nguvu inavyowezekana. Katika hali zingine, majengo huenda yakahitajika, kwa hali zingine nyingi makanisa ya nyumbani yatatumika, na pahali pa chache, huenda zote mbili zitahitajika. Ikiwa utimilifu wa Wito Mkuu ndilo lengo letu, hivyo basi, hebu tutumie mbinu yoyote halali iliyopo kukamilisha kazi hii. Naamini hakuna mbinu ya nguvu kuliko upanzi wa makanisa mapya kutimiza hili lengo, na makanisa ya nyumbani ni moja wapo ya mbinu za nguvu zaidi za kupanda makanisa.

Katika Minyororo ya Yesu, John Amstutz.

Maelezo ya Ujumbe KANISA LIKUTANALO NYUMBANI LA CHARLES NA LINDA ni kanisa la kijamii ambalo hukutana 1492 Palmyrita katika Riverside, California saa moja jioni kila Jumanne. Tuna mikutano ya wazi ambapo kila mtu hushiriki. Tunamwimbia Yesu sifa na kutafuta kujengana katika upendo. Kila mtu ni wa muhimu. Tunasoma Biblia pamoja, na kuijadili kwa njia ya kawaida. Yeyote atakaye kushiriki hujumuika na kusoma na kujadili. Mambo yote yanafanywa kwa minajili ya kujiendeleza. Kundi hili huombeana, huombea makanisa mengine, familia, jamaa, marafiki na majirani; tunamwombea rais wetu na nchi yetu. Tunahudumiana kwa maombi, maneno ya unabii, vipaji vya Roho Mtakatifu, na kupitia usaidizi wa mali jinsi Bwana anatuongoza. Mara nyingi tunashiriki chakula pamoja na kusherehekea Meza ya Bwana. Hakuna orodha ya uana chama. Wale walio wa Bwana ni viungo vya kila mmoja. Wote wanatafuta kuyafuata maagizo ya Mtume Paulo katika 1 Wakorinto 14:26 kuhusu jinsi ya kukutana…”Mnapo kusanyika pamoja kila mtu ana zaburi, au neno la kuelekeza, ufunuo, ndimi au tafsiri. Yote haya ni sharti yafanywe kwa kulijenga kanisa.” Tunaamini kwamba maandalizi ya Mungu kwa viongozi ni kupitia kujitolea-binafsi kwa wazee waliofundishwa katika Kanisa Ndani Ya Nyumba kama watumishi-viongozi. Tunapendana, na tunatoleana hesabu kamili kwa kila mmoja, tunasaidiana, na tuko tayari kuyatoa maisha yetu kwa ajili ya wenzetu. Kanisa ni watu wala si jengo, shirika, biashara, au chama. Sisi ni watu wa Mungu kupitia katika imani ndani ya Bwana Yesu Kristo aliyekufa msalabani kulipa deni la dhambi zetu. Tunapokuwa wengi kupita nafasi tuliyonayo, mpango wetu ni kuanzisha kanisa lingine la nyumbani. Kanisa likutanalo kwa Charles na Linda lilizaliwa na ujauzito.” Lilizaliwa na maona ya kuzaa kanisa lingine. Tunatarajia sana kwamba kila kanisa litakalo zaliwa kutoka ndani ya hili pia “litazaliwa na uja uzito!” Tuna shauku kuu mno ya kumwona Mwana Mwali wa Kristo akikua katika utakatifu na nguvu. Hatujidai kuwa wakamilifu, bali tunajifunza, na tunashiriki tunapojifunza; na tunauliza maswali magumu. Tunahitaji maombi yako na mchango wako wa ukarimu tunapofuata uongozi wa Bwana wetu Yesu Kristo.

38

Tunatafuta uhusiano na mwili mzima wa Kristo kwenye maeneo yetu na sio tu kwa wale wahudhuriao ushirika wetu. Kwa kuwa sisi sote ni washiriki mmoja na mwingine, tunawasihi wote wajao kwa mkusanyiko huu kuudhuria mikutano mingine ya mwili wa Kristo jinsi Roho Mtakatifu anavyowaelekeza. Tunayatii mamlaka ya kiroho popote yanapo kata njia yetu. Hatuamini katika “utiifu wa kuchagua” ambao unasema, kwa kiini, “Mimi ninatii hili kundi au yule kiongozi na wala sio kwa yule mwingine.” Mistari ya “mmoja na mwingine” kwenye maandiko ya Paulo yalielekezwa kwa kanisa lote la mjini na si kwa kanisa la makutano wa nyumbani, kwa hivyo tunatii watakatifu wote na wazee wote ndani ya kanisa lote la mjni. Tunawajibika kwa Mungu na kwa mmoja na mwingine kutimiza sharti letu la utumishi ndani ya mwili wa Kristo. Upanzi Lowesha wa Kanisa ni ono la kuanzisha makanisa kote kwa kusudi la kutimiza Wito Mkuu kupitia uinjilisti, uanafunzi, na utume duniani. Kanisa Ndani Ya Nyumba ni kifaa chenye nguvu cha kufanyia mji uinjilisti na ufuasi na chombo cha kuwafikia mataifa wote. Tunakualika wewe “uje huku na utusaidie!”

Hali ya Makanisa ya Nyumbani

Nisalimieni Prisika na Akila, watenda kazi pamoja nami katika Kristo Yesu. Nisalimieni pia na kanisa lililomo katika nyumba yao. (Warumi 16:3) Makanisa ya Asia wawasalimu. Akila na Prisika wanawasalimu sana katika Bwana, pamoja na kanisa lililomo nyumbani kwao. (1 Wakorinto 16:19). Wasalimuni ndugu walioko Laodesia, na Nimfa, na kanisa lililo katika nyumba yake. (Wakolosai 4:15) Na kwa Afia, ndugu yetu, na kwa Arkipo askari mwenzetu, na kwa kanisa lililo katika nyumba yako. (Filemoni 1:2)

Tokana na maandiko haya juu ni wazi kwamba kanisa la kwanza lilikutana nyumbani. Hawakuwa na majengo. Majengo kama

haya hayakuonekana hadi mwaka 232 Mwaka Wa Bwana Wetu. Katika siku hizo za mapema hazikuitwa “kanisa ya nyumbani.” Yalikuwa “Kanisa” lililokutana nyumbani mwa mtu fulani. Inajulikana kwamba wakati wa mlipuko mkubwa wa ukuaji wa kanisa katika historia, hadi hivi majuzi, ulitendeka wakati wa miaka hiyo ya mapema.

Hata hivyo, kwa hivi sasa, kule Uchina, kuna mshindo ambao haujawahi tokea ambao unashinda hata ule wa ukuaji wa kanisa la kwanza. Huu ufufuo usioweza kuambana ni mshindo wa Kanisa Ndani Ya Nyumba. Yafuatayo yamenukuliwa toka Caleb Report 1990 toleo la Jan./Feb la Ministries Magazine. Ripoti hii inatolewa na Loren Cunnigham, mwanzilishi na Rais wa Youth With a Mission:

Kulingana na the U.S Center for World Mission, zaidi ya Wachina 22,000 wanakuja kwa Kristo kila siku. Hiyo ni sawa na siku saba za Pentekote kila saa 24 na inatendeka hivyi sasa. Mwingi wa mlipuko huu wa uamini mpya unatoka kwa jamii za Wachina walioko mashambani, ambako ndiko asili mia 80% ya watu wanaishi. Wakati nilipokuwa Hong Kong si kitambo sana, Jonathan Chao, mwanzilishi wa the Chinise Research Center, aliniambia jinsi ufufuo wa Wachina ulivyokuwa ukienezwa na vijana, sana wenye umri kati ya 15 na 19. Watoto wenye umri wa miaka kati ya 13 na 20 wanaenda kwa vijiji na kushiriki injili pahali ambapo haijawahi hubiriwa mbeleni. Vile wanaookoka wanavyo pangwa katika makundi madogo madogo, hawa watoto wanawaita ‘wazee, (waamini wenye ndani ya ishirini) kuja kulifundisha kanisa jipya la nyumbani huku Wakristo wachanga zaidi wanaendelea kukifikia kijiji kinachofuata. Wachungaji na Walimu wa Wakichina hawana vizuizi vya kifedha vya kuzuia uenezaji wa ujumbe wa Kikristo kwa vile wanaishi na wakulima katika kila eneo jipya na hawajengi majengo. Wana vitu ichache sana na wanahitaji vitu vichache sana. Kwa mbinu hii rahisi, habari njema inaruka mashamba na milima ya China. Mlipuko wa ukuaji unaoendelea Uchina hivi sasa na ulio pia shuhudiwa na kanisa la kwanza katika kitabu cha Matendo ulikuwa

na hali moja: yote ilikuwa ni mitetemo ya Kanisa Ndani Ya Nyumba. Aina hii ya ukuaji inaonekana kwenye nchi zingine ambako majengo ya kanisa hayaruhusiwi, jinsi tulivyo ona kwenye waraka wa John Amstutz.

Hii kanuni, ikielezwa kwa urahisi, ni kwamba ukuaji wa Ufalme katika eneo liwalo lote ni kinyume kadiri na nambari ya vizuizi ambavyo tunaruhusu kuzuia upanzi wa makanisa mapya. Kutokana na maarifa yangu katika upanzi na uchungaji wa makanisa ya nyumbani, ninaona manufaa halisi ya mbinu hii kwa upanzi na uzidishaji wa kanisa.

MAKANISA YA NYUMBANI NI RAHISI KUANZISHA Kupanda Kanisa Ndani Ya Nyumba hauhitaji kununua mali au jengo. Hautahitaji mimbara au viti au vitabu vya nyimbo au

kinanda. Hauhitaji kisima cha kubatizia, Shule ya Jumapili na Mchungaji wa vijana. Hautahitaji dini au kushirikishwa au kukutana Jumapili au mpangilio wa ibada wa kanisa au kukutana mahali pamoja kila wiki.

Hautahitaji kibao chenye jina la kanisa lako. Hiyo kanisa haitahitaji jina. Kwa kweli, hata hauhitaji kuiita “kanisa” mradi tu ufahamu ya kwamba ni “kanisa, ambalo ni Mwili Wake.” Hakuna hata mojawapo ya mambo yaliyo tajwa hapa juu ambayo ni baya au si sawa, lakini hakuna kimoja chenye umuhimu. Mtume Paulo hakutumia hata moja wapo wa haya katika huduma ya upanzi wa kanisa. Tumeuacha urahisi wa Agano Jipya na kujiongezea mambo mengi ya ziada.

Ray Williams, rafiki yangu binafsi wa karibu, amekuwa mtume kule Mexico kwa zaidi ya miaka 30 na amekuwa chombo katika kuanzisha makanisa kadhaa ambamo mamia yazo yamezaliwa. Aliniambia hivi majuzi kwamba wakati mmoja alianzisha kanisa kwenye shamba la ngano. Hilo kanisa limekua, na tokana nalo umati wa makanisa mengine umetokea, kila moja likiwa na maono ya upanzi wa kanisa. Tunalifanya hili jambo kuwa gumu kufahamika. Mungu anatwita turudie urahisi na wepesi wa uzalishaji.

KANISA NDANI YA NYUMBA LIMELEGEZWA NA BILA UTARATIBU

39

Miaka kadhaa iliyopita niliipeleka familia yangu kwa kanisa ambalo mchungaji wake alikuwa mwalimu wa Biblia wa kuvutia. Nililipenda hili kanisa na nilitaka kuendelea kushiriki, lakini mtindo wao wa mavazi ulitushinda kabisa. Watu wengine hawaji kanisani mwetu siku hizi kwa sababu tumeweka kanuni ya hali ya juu ya mavazi na tukafanya kanisa tukio “la kawaida.” Wengi ambao watashindwa kuhudhuria kanisa la kawaida, watahudhuria Kanisa Ndani Ya Nyumba. Limelegezwa kwa kiasi, si rasmi na limewekwa kifamilia.

Kwenye kitabu chake, Understanding Church Growth, Dr. Donald McGavran anaorodhesha funguo nane za kukuza kanisa mijini. Kifunguo cha kwanza kinatupa makadirio ya dhamana na umuhimu wa upanzi na uzidishaji wa makanisa ya nyumbani. Anaeleza,

Funguo nane ambazo ninakaribia kutaja sio tu kisio. Zinaelezea kanuni ambazo wanaume wa ukuaji wa kanisa wanakubaliana nazo. Kwanza, tilia mkazo makanisa ya nyumbani. Wakati kanisa linaanza kukua mijini kati ya wasio-Wakristo, kila mkutano ni sharti watafute

mahali pa kukutana. Mkutano unapaswa kukutana kwenye mazingira ya kiasili, penye wasio-Wakristo wanaweza kuja kwa urahisi zaidi na ambapo waokovu wenyewe wanaendesha huduma. Kupata mahali pa kukutana haipaswi kuwawekea mzigo wa fedha huu mkutano mdogo. Kanisa Ndani Ya Nyumba linatimiza haya matakwa kikamilifu. Makanisa ya nyumbani yanapaswa kuzingatiwa kila wakati wa kupandwa mwanzoni na kupanuliwa baadaye.

MAKANISA YA NYUMBANI NI VIFAA VYA UINJILISTI

Dr. Peter Wagner, anayezingatiwa na wengi kuwa na mamlaka ya juu zaidi kuhusu ukuaji wa kanisa, anasema, “Mbinu bora zaidi chini ya mbingu ya uinjilisti ni upanzi wa kanisa. Hapakuwahi kuwa mbinu bora zaidi na haitawahi kuweko.”

Upanzi Lowesha wa kanisa ndio maono yanayo tumiwa na viongozi wa utume kote ulimwenguni. Kanisa ligawanyalo ili lizidishe litaongezeka. Kanisa ambalo linapiga tarubini kwa ongezeko litaelekea kuzama na kusimama.

Lengo letu mara nyingi limekuwa ni kujaribu kuujenga mkutano mmoja mkubwa badala ya kuzidisha makutano. Hatuwezi kusema kwamba Mungu hangewahi kumwongoza mtu kusimamisha mkutano mkubwa; hata hivyo, Mwili wa Kristo

kwenye mji wowote utaongezeka kwa kasi zaidi kwa njia ya uzidishaji kuliko kwa njia ya kutafuta kuyajenga makanisa machache makuu. Tunamtukuza Mungu kwa ajili ya makanisa makuu. Tunawaombea, tunahudumu mle, tunawabariki. Sio “sisi na wao”. Ni sisi! Mwili mzima wa Kristo ni wetu sisi sote na sisi ni wa kila mmoja wetu.

MAKANISA YA NYUMBANI YANARAHISISHA KUFUNDISHWA KWA WACHUNGAJI NA VIONGOZI

Kwa muda mrefu imeekuwa ikieleweka na waelimishaji kwamba mbinu bora ya kufundisha bado ni mbinu ya uanafunzi, ambayo ni “ufundishaji wa mmoja kwa mmoja, mikono-kwenye-kazi” kama vile mhunzi, fundi wa mabomba ya maji, au wakili angepokea miaka mia moja iliopitia. Walijifunza kwa kufuata na kufanya wakati wanawajibika kwa mwalimu mwenye ujuzi wa hiyo biashara.

Hii ilikuwa mbinu ya Yesu. Wanafunzi walifunza kwa kuangalia, kusikiza na kutenda wakiwa wanaishi maisha yao na Mwalimu Mkuu mwenyewe. Makanisa ya nyumbani yatatuwezesha kuwafundisha wachungaji hasa kufanya kazi ya uchungaji wakiwa chini ya usimamizi wa wachungaji walio na ujuzi zaidi.

Watakua jinsi kanisa linavyokuwa chini ya uongozi wao. Wengine watachunga zaidi ya kanisa moja la nyumbani kwa vile hawatakuwa wakikutana Jumapili asubuhi.

MAKANISA YA NYUMBANI YANAUNGANISHA MAHUSIANO Kanisa dogo la nyumbani linawezesha hata wale walio waoga sana wajithibitishe binafsi katika Mwili wa Kristo. Katika kanisa

letu la nyumbani huwa tuna chakula cha mchana pamoja kila Jumapili. Kila familia inashiriki kwa maandalizi na kupakua hiki chakula.

Kuunda mahusiano hutokea kwa urahisi zaidi ndani ya hali ya “watu wa nyumbani” kama hii.

MAKANISA YA NYUMBANI YANAPUNGUZA GHARAMA Kanisa Ndani Ya Nyumba litaweza kuelekeza karibu kila fedha zake zote kwenye huduma ya utume na huruma. Baadhi ya

makanisa yetu ya nyumbani kule Texas huelekeza asili mia 93% ya matoleo yao katika ukarimu na tume za kigeni. Huenda kukawa na matumizi madogo madogo, lakini kwa vile mikutano inafanyika kwenye manyumba matumizi yanaepukwa.

Kwa kawaida mengi ya haya makanisa ya nyumbani yataongozwa na wachungaji-wanaoendelea-na-mafundisho ambao watakuwa na kazi sawasawa na watachunga Kanisa Ndani Ya Nyumba wakati ukiruhusu. Wakati heshima ya mapato yakuishia yanapaswa kuwaendea wale wanaoutumia muda wao wote kwenye hii kazi, pia ni kweli kwamba wale wachungaji ambao wanatumika nusu ya muda pia wanapaswa kupokea heshima kama hii kupitia vipaji vya upendo na malipo toka kwa fungu za kumi na matoleo kulipia matumizi na kuwahimiza katika kazi ya huduma. “Mfanyikazi anastahili mshahara wake,” (Kama anafanya nusu ya muda au muda kamili). Kwa upande mwingine, wanaume hawapaswi kusubiri hadi wawe huru kutoka kwa kazi ya muda kamili kabla waanze kutumika kama wachungaji. Mtume Paulo alifanya kazi kwa mikono yake mara nyingi, sio tu kukutana na mahitaji yake mwenyewe, bali pia mahitaji ya wale waliosafiri pamoja naye.

Ninyi wenyewe mnajua ya kuwa mikono yangu hii imetumika kwa mahitaji yangu na wale waliokuwa pamoja nami. Katika mambo yote nimewaonyesha ya kuwa kwa kushika kazi hivi imepasa kuwasaidia wanyonge, na kuyakumbuka maneno ya Bwana Yesu, jinsi alivyosema mwenyewe, “Ni heri kutoa kuliko kupokea.”

MAKANISA YA NYUMBANI YANAWEZA KUSULUHISHA TATIZO LA UKUAJI Baadhi ya makutano wetu wamekua wakubwa sana kwamba wanahitaji kujenga majengo makubwa au kupangisha nafasi zaidi

au kuhudhuria ibada mbili. Hili ndilo tunaita “tatizo la furaha.” Pia kunalo suluhisho la furaha: anza kuwafundisha wachungaji na kuwapa maeneo ya mji na kutuma familia mbili au tatu kuanzisha Kanisa Ndani Ya Nyumba kwenye hiyo sehemu ya jiji. Jambo la kuutia uzima zaidi ambalo Kanisa Ndani Ya Nyumba laweza kufanya ni kumzaa mtoto. Nimeyaona makanisa ya kifa kwa sababu ya

40

roho ya kumiliki katika uongozi. Mungu atawabariki wale watu ambao wanaendelea kupeana kila kitu ambacho anawapa. Yesu alisema, “Toa nawe pia utapewa.” Kanisa litoalo ni kanisa likualo.

Michael Green, Principal wa St. John’s College ya Nottingham, England, kwenye hutuba yake mbele ya International Congress on World Evangelization kule Lausane, Switzerland mwaka wa 1974, aliongea juu ya mbinu na mikakati katika uinjilisti wa kanisa la kwanza. Alisema,

“Kwa kanisa la kwanza, majengo hayakuwa yenye umuhimu wowote; hawakuwa na yoyote wakati wa ukuaji wao mkubwa zaidi. Hivi leo haya majengo yanaonekana yenye umuhimu mkubwa kwa Wakristo wengi; utunzaji wake unakula pesa zote na riba ya washiriki, mara nyingi ikiwaingiza kwenye madeni, na kuwatenganisha na wale wasioenda kanisani. Naam, hata neno limebadili maana yake. ‘Kanisa’ halimaanishi tena ushirika wa watu, jinsi ilivyokuwa kwenye nyakati za Agano Jipya. Siku hizi linamaanisha jengo.”

Mitetemo ikuayo kwa kasi sana katika historia kila wakati imekuwa ile ambayo haijazamishwa chini ya mipangilio mizito ya kishirika na imeangazia vitu muhimu bila kusita.

Kanisa Ndani Ya Nyumba Katika Agano Jipya

Mafungu ya Maandiko hapa chini yanaonyesha kuwa makaazi ya kawaida yalitumika kwa kueneza injili na kuwafanya waokovu wapya wakati wa maisha ya Yesu na pia wakati wa upanuzi wa Kanisa la Agano Jipya kwenye Matendo ya Mitume.

NYUMBANI AMBAMO YESU ANAABUDIWA

Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mamaye, wakaanguka wakamsujudia; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tanu; dhahabu na uvumba na manemane. (Matayo 2:11)

Wakati wa kwanza kabisa kundi lilipokusanyika kumwabudu Yesu na kumpa vipaji ilikuwa nyumbani, nyumba ya Mariamu na

Yusufu.

NYUMBA YA PETRO INATUMIKA KAMA MKUTANO WA UPONYAJI

“Hata Yesu alipofika nyumbani kwa Petro, akamwona mkwe wa Petro, mamaye mkewe, amelala kitandani hawezi homa. Akamgusa mkono, homa ikamwacha; naye akaondoka, akawatumikia. Hata kulipokuwa jioni, wakamletea wengi wenye pepo; akawatoa pepo kwa neno lake, akawaponya wote waliokuwa hawawezi.” (Matayo 8:14-16).

Katika siku za mapema za huduma yake, Yesu alitumia nyumba yake Petro kufanya mikutano ya kuhubiri, uponyaji na

ukombozi.

IBADA YA KWANZA YA MEZA YA BWANA INAFANYIKA KWENYE NYUMBA Katika juma la mwisho la huduma wa Yesu aliwaambia manafunzi wake: Akasema, enendeni mjini kwa mtu fulani, mkamwambie, ‘Mwalimu asema, Majira yangu ni karibu; kwako nitafanya Pasaka pamoja na wanafunzi wangu.” Bwana wetu angechagua kusherehekea comunyo ya kwanza na wanafunzi wake katika sinagogi, ndani ya hekalu, au pahali

pengine penye umuhimu wa kidini, lakini alichagua kuisherehekea pahali pa kawaida, nyumba ya kawaida. Kwa hivyo aliuweka muhuri makazi ya kawaida kama pahali patakatifu na palipo takasika, pakustahili huduma ya ibada ya kuheshimiwa zaidi.

YESU ALIHUBIRIA UMATI ULIOKUSANYIKA NYUMBANI.

Akaingia Kapernaumu tena, baada ya siku kadha wa kadha, ikasikiwa ya kwamba yumo nyumbani. Wakakusanyika watu wengi, isibaki nafasi hata mlangoni; akawa akisema nao neno lake. (Marko 2:1-2a).

Mambo tunayoyafanya kwenye majengo ya kanisa yetu hivi leo, Yesu aliyafanya katika nyumba, hadharani, na katika uwanja

wa hekalu wakati wa huduma yake ya miaka mitatu.

PENTEKOSTE ILIKUJA KWA KANISA NDANI YA NYUMBA Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja. Kukaja ghafula toka mbinguni upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi.

Wengi wetu hawajawahi kuzingatia idadi ya matukio ya kimsingi yanayotendeka katika nyumba ya mtu. Huduma wa Ibada ya kwanza ilitetendeka katika nyumba. Ibada ya kwanza ya komnyo ilifanyika kwenye nyumba. Yesu alihubiri na kuwaponya wakonjwa kwenye nyumba. Injili ilihubiriwa kwa mataifa mara ya kwanza kwenye nyumba ya Kornelio. Kushuka kwa Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste ilikuwa kwenye nyumba. Na makanisa ya kwanza ambayo Paulo alianzisha yote yalikuwa kwenye nyumba.

Kwa karne nyingi tulipoteza elimu ya nguvu za urahisi na tumeongeza mambo ambayo yamepunguza ukuaji wa kanisa hadi kwa mataifa yote.

KWENYE BARABARA NA NDANI YA NYUMBA

Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kushiriki chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe. (Matendo 2:46).

41

Kanisa la kwanza halikukutana tu kwa makundi madogo kwenye nyumba bali pia katika mikusanyiko mikubwa kwenye mahali

pa hadhara. Ukuaji wa kasi zaidi wa kanisa, kwa wakati uliopita na wakati wa sasa, imekuwa ni wakati kanisa halitumii mahali pa desturi pa kukutania, bali lilibakia likipindikana, likienda, na kupiga vita.

SAULI, MTESI, MSHAMBULIZI WA MAKANISA YA NYUMBANI.

Sauli, akaliharibu kanisa, akiingia kila nyumba, na kuwaburuta wanaume na wanawake na kuwatupa gerezani. (Matendo 8:3).

Ni wapi kwenye Sauli wa Tarso alienda ili kuwatafuta “watu wa njia” kuwaburuta gerezani na kifo? Aliwapata kwa mikutano ya nyumbani. Baadaye yeye mwenyewe angepanda makanisa nyumbani kwenye safari zake za utume.

KANISA NDANI YA NYUMBA LIOMBALO LINAMFUNGUA PETRO TOKA GEREZANI

Na kila siku, ndani ya hekalu na nyumbani mwao, hawakuacha kufundisha na kuhubiri habari njema za Yesu kwamba ni Kristo.

Hawakukutana kwenye hekalu sawa, bali kadiri kwenye sakafu ya hekalu, au katika maeneo ya hekalu ambapo watu walikuwa wakikusanyika,

Historia ya Ukristo na Lion inasimulia: Wakristo hawakuwa na majengo halisi lakini walikutana kwenye nyumba za faraghani. Justin Martyr (100-165 Baada ya Mwaka wa Bwana Wetu) aliulizwa na Rusticus the Perfect: “Ninyi hukusanyika wapi?” Justin akasema, mahali kila mmoja anachagua na anaweza, au unafikiri kuwa sisi sote tutakutana mahali pale? Si hivyo, kwa maana Mungu wa Ukristo hawezi zuiliwa na mahali.

Kwenye kitabu chake, Cells for Life, Ron Trudinger anasema: Waliingiza tendo la mikutano kila siku katika hekalu umekaji wa mkate toka nyumba hadi nyumba: msamiati huu waweza kufafanuliwa hivi: “Kwenye makanisa mbali mbali ya faragha.” Masinagogi yalitumiwa kwa muda, lakini jinsi tuonavyo katika Matendo 19, haikuwa kitambo kabla ya mengi ya haya hayajafungiwa Wakristo. Lakini tunaendelea kupata marejeleo muhimu katika Matendo na Nyaraka kwa makanisa ya nyumbani.

KANISA NDANI YA NYUMBA LILILOFUNGUA INJILI KWA MATAIFA

Siku ya pili yake wakaingia Kaisaria. Na Kornelio alikuwa akiwangojea, hali amekusanya jamaa zake na rafiki zake. Petro alipokuwa akiingia Kornelio alitoka amlaki akamwangukia miguu, akamsujudia. Lakini Petro akamwinua, akasema, Simama, mimi nami ni mwanadamu. Na katika kusema naye akaingia ndani, akaona watu wengi wamekusanyika. (Matendo 10:24-27).

Huu ni mfano mzuri wa jinsi ya kuanzisha Kanisa Ndani Ya Nyumba. Mtu mmoja aliye na kiu ya Mungu na mambo ya Mungu

anawaita pamoja idadi ya familia na marafiki zake na halafu anamwita mtu wa Mungu kuja kushiriki Neno la Mungu. Rahisi sana! Huu mkutano kwenye nyumba ya Kornelio ulikuwa wa kihistoria. Ulikuwa upenyo ambao uliwasadikisha waamini wa Kiyahudi

kwamba Habari Njema ilikuwa ni kwa mataifa yote ya ulimwengu na sio tu kwa Wayahudi.

NYUMBA YA LIDIA NDIYO ILIKUWA KANISA NDANI YA NYUMBA LA KWANZA UROPA. Nao wakatoka gerezani wakaingia nyumbani mwa Lidia; na walipokwisha kuonana na ndugu wakawafariji, wakaenda zao. (Matendo 16:40).

Kanisa la Ufilipi liliumbwa kwenye nyumba yake Lidia. Hatujaambiwa vile hili kanisa lilikua, lakini wakati hili kundi

halingeweza toshea kwenye nyumba yake Lidia, huenda waliumba kikundi kingine mahali katika huo mji na wakaendelea kugawa na kuzidisha. Historia ya kanisa inaunga mwisho huu.

NYUMBA YA KUPANGISHA YA PAULO

Akakaa muda wa mika miwili mizima katika nyumba yake aliyokuwa ameipanga, akawakaribisha watu wote waliokuwa wakimwendea, akihubiri habari za ufalme wa Mungu, na kuyafundisha mambo ya Bwana Yesu Kristo, kwa ujasiri mwingi, asikatazwe na mtu. (Matendo 28:30-31).

Haya maneno ya mwisho kwenye kitabu cha Metendo yanatufunulia kwamba Paulo hakuweza tu kutumia nyumba za wengine

kwa kutangaza injili, bali kwamba pia alitumia nyumba yake aliyopangisha kwa uenezaji habari njema ya upendo wa Mungu. Mtetemo unaokua upesi mno duniani hivi leo, ni mtetemo wa Kikristo, ulioanzishwa kwenye nyumba. Ulikuwa na ukuaji wake

mkuu wakati ulizalia ukitiririka, rahisi, ukisonga, ukilenga-watu na mahusiano.

TOKA KWA KIVULI HADI UTHABITHI Aina zote za vivuli katika Agano la Kale vilitimizwa kabisa katika Kristo. Hatuitaji tena hema, au mavazi ya kasisi, wala hekalu,

wala vyombo, au kitu chochote cha aina hii. Kristo ndiye yote ndani ya yote. Tumekamilika katika Yeye. Hatuhitaji mahali patakatifu tena, au madhabahu ya uvumba au birika, au mkate wa kushona, au vitu vyote vilivyoambatana na ukuhani na utoaji dhabihu. Hatuhitaji vivuli kwa maana tuna uthibithi. JINA LAKE NI YESU!

Mwanamke alimwambia Yesu, “Bwana, baba zetu waliabudu katika mlima huu, nanyi husema ya kwamba huko Yerusalemu ni mahali patupasapo kuabudia. Yesu akamwambia, Mama, unisadiki, saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala kule Yerusalemu. Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho; kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi. Lakini saa inakuja, nayo saa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika Roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu. Mungu ni roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika Roho na kweli. (Yohana 4:20-24)

42

Yesu alionyesha wazi kuwa wakati ulikuwa umewadia na kwamba Yerusalemu haikuwa tena mahali pa takatifu kuliko Samaria kwa sababu yeye amekuja. Kuja kwake kulimaliza fikira ya mahali pa takatifu milele, kwa sababu yeye alitimiza aina zote za vivuli vya Agano la Kale. Hebu basi tufurahi na tumsifu Bwana kwa kuwa tumefunguliwa toka kwa kifungo na sheria kuhusu mahali tunapasa kumwabudu Mungu! Tu huru kumwabudu tukiwa pekee yetu au kwa pamoja, wakati wowote, mchana au usiku, mahali popote tunapochagua!

Kanisa ni Nini?

Neno asili katika Kiyunani, ekklesia, limetungwa na maneno mawili: ek, likimaanisha, “toka kwa” na kalleo, likimaanisha,

“Ninaita”. Maana ya kanisa, kulingana na neno asili, ni, “Ninaita toka kwa”. Wakati Yesu alisema, “Nitalijenga kanisa langu kwenye mwamba, Alikuwa akisema: “Nitawaita watu wangu toka kwa ulimwengu na watakusanyika katika jina langu, na milango ya Kuzimu haitawashinda.” Hili linadokeza kwamba watu wake walioitwa toka-kwa watawakusanyika kama jeshi kumchukulia ulimwengu na adui hataweza kustahimili haya maendeleo.

Hili jeshi lisiloshindwa litatiwa motisha na upendo wa Mungu ndani ya mioyo yao na ujumbe wa upendo na msamaha kwenye vinywa vyao.

Kwa kweli ekklesia lina maana mbili: ile ya kuitwa toka na ile ya kukusanywa pamoja. Hatuwezi kujua kanisa hadi tuje pamoja. Mke wangu nami tu kitu kimoja hata kama tumetenganishwa na maili mengi. Lakini hatupati faida na baraka kamili ya ndoa yetu hadi tuwe pamoja.

Vivyo hivyo, wewe na kila mwamini mwengine kwenye jiji lenu mnasimamisha kanisa, hata wakati hamkusanyiki. Lakini hamwezi pokea faida na baraka za kanisa hadi mkusanyike pamoja. Hii, kwa kawaida, haimanishi kuwa mtakuwa mahali pamoja kwa wakati mmoja. Hili huenda halitawahi tendeka kwenye jiji lolote.

SI NENO LA KIDINI.

Nilishangazwa na kufurahishwa hivi karibuni kugundua kuwa neno ekklesia kwenye Agano Jipya halikuwa neno la kidini kabisa. Nilikuwa nikipitia sura ya kumi na tisa ya Matendo ambapo mtume Paulo alitishwa na umati wenye ghadhabu waliotaka kumuua. Mwandishi anatumia maneno kadhaa tofauti kuelezea huu umati: “jiji zima,” “watu,” “umati”. Mara tatu alitumia neno “kusanyiko”.

Basi wengine walikuwa wakilia hivi na wengine hivi; kwa maana ule mkutano ulikuwa umechafuka-chafuka, na wengi wao hawakujua sababu ya kukusanyika kwao pamoja…Na karani wa mji alipokwisha kuwatuliza watu, akasema, Enyi wanaume wa Efeso…ikiwa Demetrio na mafundi walio pamoja naye wana neno juu ya mtu, baraza ziko, na maliwali wako…Bali mkitafuta neno lolote katika mambo mengine, yatatengenezwa katika kusanyiko lililo halali…alipokwisha kusema haya akauvunja mkutano. (Matendo 19:28-41). Jambo la ajabu juu ya hili fungu ni kwamba neno kusanyiko kwenye lugha asili ni ekklesia, ambalo ni neno tulitafsirio wakati

wote, “kanisa”. Basi Yesu alitumia neno la kawaida aliposema, “Nitalijenga kanisa langu.” Halikuwa neno la kidini. Lilimaanisha tu kundi lililoitwa toka, au umati, au ushirika, au kusanyiko. Basi tunaweza tumia neno kanisa wakati linawasilisha kile tunasema, lakini tunaweza pia tumia ushirika, au kusanyiko, au wandugu, au watakatifu, au wafuasi. Maana yake rahisi ni kundi la watu.

“WATU WAENDAO PAMOJA” John Dawson, kwenye kitabu chake, Taking Our Cities for God, alisema:

Hakuna mfano kamili wa jinsi Kanisa Ndani Ya Nyumba linapasa kuwa. Wakati mmoja nilishinda adhuhuri na zaidi ya viongozi wa kiroho mia moja toka dini kadhaa. Tulijaribu kutafuta maana ya Kanisa Ndani Ya Nyumba ya kibiblia inayokubalika kote ulimwenguni. Waweza fikiri ilikuwa kazi rahisi, lakini ukitazama mila na hali zote za watu ulimwenguni na uchunguze mifano tofauti kwenye Biblia, utaanza kuelewa uzuizi wetu. Baada ya masaa mengi ya kujadili, tulikuwa tumepata tu mifano mizuri, lakini hakuna tafsiri kamili kuliko ile ya “watu waendao pamoja chini ya miliki wa Yesu.”

Napenda huu ufafanuzi, lakini kwa kweli naamini Bwana ametupa ufafanuzi mzuri sana wa Kanisa Ndani Ya Nyumba na pia wa

kanisa la kote ulimwenguni. Huu ufafanuzi unapatikana katika Waefeso. Akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akameka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote. (Waefeso 1:22-23).

Kote katika Agano Jipya makanisa yote mbili la nyumbani na la kote ulimwenguni yanaitwa “kanisa.” Mwili wa nyumbani, hata

uwe mdogo au mkubwa kiasi gani, unaitwa “kanisa” na Mwili mzima wa Kristo kote ulimwenguni unaitwa “kanisa.” Kanisa ni mwili wa Kristo uwe umekusanyika au umegawanyika. Hii kwa maana rahisi ni popote kuna kundi la Wakristo limekusanyika, hapo kuna kanisa.

Nilizaliwa na kulelewa Texas. Wakati wa Krismasi tunge enenda nje mashambani na kukata mti wa Krismasi wenyewe. Dakika tuliukata na kuupeleka nyumbani kwetu ulifanyika mti wa Krismasi. Halafu tungeuwekea kinara na kuupamba na wingi wa urembo ndogo ndogo kuufanya huu mti uonekane unang’ara na wa kisherehe, lakini ikiwa tungeyaondoa yale mapambo, bado ungezalia mti wako wa Krismasi wa kimsingi.

Iwapo Mungu angeondoa kila kitu hadi kusiwepo na kitu kingine bali kanisa rahisi, la kimsingi la Agano Jipya, tutabaki na nini? Kwa maneno mengine, ikiwa tutaondoa “anasa zote” na yote “visivyo vya lazima’ na kukata madoido yote toka kwa ile nilielewa kuwa kanisa, ni nini kingezalia? Ni kusudi letu kwenye sura hii kujibu hilo swali.

HUDUMA-SIZIZI ZA KI-KANISA NI NINI?

43

Hivi majuzi nilisoma kitabu kilicho tafuta kufafanua asili ya kanisa. Chni kichwa, What is the Relationship of the Church to other Parachurch Organizations, mwandishi anasema hivi:

Biblia i wazi kuwa ni kupitia gari, au chombo, cha kanisa Mungu anaenda kutimiliza azimio lake kuu. Hata hivyo, kwa maana Kanisa halijakuwa kama lilivyo dhaniwa kuwa, wengi wameshushwa moyo na uwezo wa kanisa kutimiza mahitaji fulani yaliyo wazi. Kwa sababu hii, watu wanaohusika na waangalifu, kwa miaka iliyopita, wame imarisha mashirika ya kitume, nyumba ya kulea na kutunza yatima, mashirika ya kibiashara ya Wakristo na mashirika kama hayo kutimiza haya mahitaji ya dharura. Vile Mungu anaendelea kurejesha na kulitia nguvu Kanisa Lake, uhitaji wa haya mashirika utapungua na kanisa litakuwa likihudumia haya mahitaji.

Ni wazi kwenye kwa nukuu la hapa juu kwamba mwandishi alihisi uzito kuwa “huduma sisizo za kikanisa” sio kanisa na kuwa

kitu chenye upungufu wa kanisa kilitokea kutimiliza mahitaji fulani hadi kanisa la kweli liponywe au liamushwe kufanya kazi ambayo kanisa linapaswa kufanywa.

Huu ni mfano wa makosa ya kufiri kuwa ikiwa halionekani kama kanisa, sio kanisa. Ukweli ni kwamba wakati shirika la “huduma sisizo za kikanisa” linaundwa na waamini waliozaliwa mara ya pili katika Yesu wanaokuja pamoja kumtumikia na kumwabudu yeye, sio “huduma sisizo za kikanisa”, ni kanisa! KANISA NI WATU! Sio shirika, chama au dini. Ingekuwa vigumu sana kupata shirika la “huduma sisizo za kikanisa”. Kwa kuwa kama lingeundwa na Wakristo, halingekuwa “huduma lisilo la kikanisa”; lingekuwa Kanisa…Watu wa Mungu walioitwa toka! Hata ikiwa washiriki wengine hawajazaliwa mara ya pili, bado itakuwa kanisa, kwani ni kanisa lipi lililopo bila kuudhuriwa na watu wasiookoka?

Miaka michache iliyopita nilikuwa na wazo kuhusu huduma sisizo za kikanisa. Katika huduma yangu ya mafundisho kila mara mimi husema, “Ikiwa kanisa lingekuwa likifanya yale linapaswa kuwa linafanya, hatungehitaji haya mashirika ya huduma sisizo za kikanisa.” Haikuwahi nitokea hata mara moja kwamba hawa watu wa hizi “huduma sisizo za kikanisa” ni watu wa Mungu na kwamba wao pia ni kanisa, likiendelea chini ya miliki ya Yesu, vile tu sisi pia tulikuwa, hata kama jengo walilokutania halikuwa limejengwa kama lile letu.

Mvulana wetu mkubwa amekuwa mshiriki wa shirika la “huduma isiyo ya kikanisa” inayojulikana sana kwa miaka mingi. Wanafanya kazi ya ajabu ya utume na uinjilisti, na wanakua kama wazimu kote ulimwenguni. Miaka michache iliyopita tukiwa tunajadili hatima yake na ushirikiano wake na hili shirika, nilishiriki kwamba nilikuwa na shaka kubwa sana juu ya hili shirika kwa maana halikuwa kanisa, lakini ni shirika la “huduma isiyo kuwa ya kikanisa”. Alionekana kuomba msamaha na alikubaliana nami kikamilifu kwamba yale yeye na wenzake walikuwa wakifanya katika shirika hilo, hata lilikuwa likibarikiwa kiajabu na Mungu, sio kile Mungu alitaka kwa sababu haikuwa ikitendeka kwenye kanisa, bali ni kupitia huduma isiyo ya kikanisa. (Alikuwa pia amechanganyikiwa kuhusu kanisa na huduma isiyo ya kikanisa).

Siku moja au mbili baadaye nilikuwa barabarani nikiwa nafikiria juu ya mazungumzo yangu wakati nilihisi Bwana akiniuliza kwa upole: “Je, ni nini ambacho kinafanya kanisa liitwe shirika?” Vile nilijaribu kujibu hilo swali, nikahisi Mungu ananipa ufunuo. Sikuwa nimewahi kuona wazi wazi jinsi niliona wakati huo kwamba shirika sio kanisa kwa sababu lina jengo ambalo lina umbo fulani ambalo watu huita kanisa; hilo sio kanisa kwa sababu limethibitishwa na serekali ya muungano kama kanisa; sio kanisa kwa sababu limetambulika na makao makuu ya kidini kama kanisa; sio kanisa kwa sababu lina ibada za kawaida za kila Jumapili asubuhi na wanafanya ubatizo na Meza ya Bwana; sio kanisa kwa sababu linakutana kwa linakutana kwa kawaida au mahali fulani. Ni kanisa kwa sababu rahisi kwamba ni watu wa Mungu walioitwa kutoka wakienenda pamoja chini ya miliki ya Yesu.

Alfred Kuen, kwenye kitabu chake, I Will Build My Chruch, chini ya kichwa, When is Local Chruch a Chruch? Anasema:

Ni rahisi kukwamia kwa maswala na maswali ya kandokando. Na hapaonekani kuwepo njia wazi ya kufafanua Kanisa Ndani Ya Nyumba.

Kwa mfano, ni wakati una katiba na mikutano ya kawaida? Ni wakati umewabatiza waamini wanaoshiriki mara nyingi kwenye Meza ya Bwana? Ni wakati una maafisa wa kanisa, kama wazee na mashemasi? Inapasa kanuni nyingi ziwepo ili tuwe na Kanisa Ndani Ya Nyumba? Kwa hakika haihuki na kiwango fulani cha ukomavu; kwa vile Wakorinto walikuwa bado kwa mwili lakini Paulo aliwaita kanisa. Zaidi, halionekani la haja kuwa na viongozi wa kiroho kabla uuite mwili wa waamini kanisa, kwa vile imeonyeshwa wazi kuwa makundi ya waamini kote Listra, Ikonio na Antiokia yaliitwa kanisa hata kabla wazee wateuliwe. (Matendo 14:21-22).

Wakati gani, basi, mwili wa waamini unaweza kuitwa kanisa? Mimi binafsi naegemea ufafanuzi rahisi: mwili wa waamini unaweza kuitwa kanisa wakati wowote hilo kundi linakutana pamoja kwa kawaida kwa kujengana. Yesu alisema, katika muktadha wa kuongea juu ya indhamu kanisani, “Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa

jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.” (Matayo 18:20). Jim Montgomery, kwenye kitabu chake, Dawn 2000-Seven Million Churches to Go, anasema juu ya swali, Kanisa ni nini?:

Nimefurahiswa na jinsi kundi la Wakristo walivyo kabiliana na hili swali la msingi katika Uchina: Walisema, Kuhusu [hili] swali,

Wakristo wengi wakongwe walisema kwamba hawange tabiri hatima ya umbo la makanisa ya Kichina. Kwa hivyo wakaigeukia Biblia kwa jibu.

Wakapata kwenye Biblia kwamba Kanisa Ndani Ya Nyumba linaunda kanisa halali…tulipata kitabu kimeandikwa na Wang Ming-dao [huenda ndiye mwuumini aliyeheshika sana Uchina aliedhoofikia gerezani kwa miaka zaidi ya 20] kwa mwanzo wa kanisa. Alishikilia kwamba palipokuweko Wakristo kulikuweko na kanisa.

Tulikuwa na furaha juu ya hili. Tulidhani kuwa, hata kama kundi letu liliundwa na watu wachache tu, kwa kweli tulikuwa kanisa, na kichwa chetu alikuwa Yesu.

"Palipo Wakristo, pana kanisa,” ni ufafanuzi wa maana sana, ukitoka kwa Kanisa linalokua kwa kasi na linamenyana chini ya mazingira magumu sana.

KUSANYIKO LA WAAMINI NI KANISA Miezi michache iliyopita nilikuwa mikifundisha kundi dogo la waamini katika kijiji cha La Rumurosa huko Old Mexico.

Nilikuwa nikieleza Matayo 18:20. “Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.” Neno katika tafsiri ya lugha ya Spanish ya huo mstari ikanirukia. Sikuwa nimewahi iiona mbeleni. Inasema, “Donde hay dos o tres congregados en mi nombre alli estoy en medio de ellos.” “Walipo wawili au watatu WAMEKUSANYIKA kwa jina langu nipo papo hapo katikati yao.” Niliuliza hilo kundi, “Kulingana na huu mstari, inachukua wangapi kufanya kusanyiko?” Nilipokuwa

44

nikiwangojea wanijibu, nilipigwa na uzito wa jibu lililokuwa likifanyika kwenye akili zangu mwenyewe. Wawili au watatu ndio idadi inayohitajika kufanya kusanyiko na kusanyiko la waamini wakiwa na Yesu katikati yao ni Kanisa! Sio tu watu wawili au watatu, lakini wawili au watatu ambao wanaitwa kwa jina lake, kwa maana wao ni wake.

YESU KATIKATI

“Yesu aliye ndani” ni maisha ya mtu binafsi katika matembezi yake ya faragha na Bwana. “Yesu katikati” ni mfano wa kanisa. Ni Yesu akitembea kati yetu, akituguza, akitunenea kupitia karama za Roho Mtakatifu akitiririka kupitia washirika wa Mwili wake, kanisa. “Yesu katikati”, ni maisha ya kishirika. “Yesu ndani” ni maisha ya faragha.

Wakati waamini wawili au watatu wanakusanyika kwa jina lake, Yesu yuko KATIKATI MWAO. Yesu yu katikati mwa kanisa! Ni maisha tofauti kuliko Yesu ndani. Hatuwezi kupata Yesu katikati tukiwa pekee yetu. Tunaweza tu kumpata Yesu katikati tukiwa kwa ushirika na wengine—angaa mmoja au wawili wanaoitwa kwa jina lake!

Lakini ni kanisa katika ukamilifu wa maana ya neno hili? Ndio, ni kanisa kwa ukamilifu wa neno hili. Ni kanisa la msingi. Unaweza kuwa na zaidi ya mbili au tatu na bado ni kanisa, kanisa katika ukamilifu wa maana, lakini halikuwi kanisa zaidi kwa sababu kunayo mawili au matatu. Linakuwa tu kanisa kubwa.

KAZI YA KANISA NI NINI?

Je, itakuwa aje kuhusu wachungaji, mashemasi, walimu, mitume, wainjilisti, na maaskofu? Ni kanisa bila hawa kuwepo kwa hawa? Ndio, ni kanisa, hata bila hawa wote waliotajwa hapa juu.

Sura ya nne ya Waefeso inasema kwamba Bwana alilipa kanisa huduma hizi zote, bali alilipa kanisa hizi karama ambazo tayari zilikuweko.

Wakati Paulo alienda kwa safari yake ya kwanza ya utume, alianzisha makanisa katika miji minne. Njiani akirejea Antikia, aliwawekea mikono wazee kwa hayo makanisa. Hili linaonyesha kwamba Roho Mtakatifu, ambaye ndiye mwandishi wa kitabu cha Matendo, alijua yalikuwa makanisa kabla viongozi wachaguliwe. Pia anataka sisi tufahamu hivyo. Angalia yafuatayo:

Hata walipokwisha kuihubiri Injili katika mji ule, na kupata wanafunzi wengi, wakarejea mpaka Listra na Ikonio na Antiokia, wakifanya

imara roho za wanafunzi na kuwaonya wakae katika ile Imani, nay a kwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya dhiki nyingi. Na walipokwisha kuwachagulia wazee katika kila kanisa, na kuomba pamoja na kufunga, wakawaweka katika mikono ya Bwana waliyemwamini.(Matendo 14:21-23). Wazee waliongezwa kwa makanisa (wanafunzi).wanafunzi walikuwa watu walioitwa na Mungu toka kwa giza kuingia nuruni,

Kanisa! Mwandishi anatumia anabadilishana neno “wanafunzi” na “kanisa” kimatumizi. Paulo aliona ni salama kuyaacha haya makanisa mapya mikononi mwa Bwana ambaye watu welikuwa wamemwamini. Hii ni

tarifa ya muhimu sana. Sisi tulioka kwenye uongozi tumechukua mzigo mkubwa sana kwa kudhania kuwa kanisa haliwezi likafanya bila “uchangaji wetu” wa kila mara kwa kundi. Askofu ni ovasia na mlishaji na anatenda kazi kama baba au muuguzi kwa watoto wake, lakini hakuna mpaka kwa maono yetu ya kiroho ambayo wakati mwingi tumevunja. Uvunjaji mkubwa na viongozi wa kanisa siku hizi zetu ni kwamba tumeutwa karibu uanzishaji wote toka kwa watu na kuwekeza kwa wahubiri “waliohitimu.”

BASI KANISA NI NINI?

Ikiwa tutaondoa sehemu zote sisizo muhimu, tutabaki na Yesu na angaa watu wawili ambao wamekucha pamoja kwa jina lake; watu wawili ambao wamezaliwa mara ya pili, kukutana pamoja mahali popote, wakati wowote kuukubali na kuheshimu uwepo wake ni kanisa katika kiwango chake rahisi kabisa, kimsingi na bila desturi. Hii haimaanishi kuwa hiki kiwango muhimu ndicho ambacho Bwana anataka tufanyoe kazi kila wakatu. Bwana asifiwe kwa sababu ya makundi makubwa. Lakini tusipoteze maono ya kanisa la msingi. Ikiwa tutafanya hivyo, tuturudi kwenye mitindo, ibada, sherehe, udini, uanachama, uahalali.

“KANISA NI NINI?”

Ndugu Andrew (Mwingiza bidhaa kisiri wa Mungu—huyo mtumishi mwanifu wa waliodhulumiwa, wakiteseka kwa ajili ya mwili wa Kristo kote ulimwenguni) wakati mmoja aliniambia hadithi toka siku za uingizaji Biblia kisiri wake kabla ya kuvunjika kwa Muungano wa Kisovieti. Alisimulia hadithi hii kwa kujibu swali juu ya, “Kanisa ni nini?” Hiyo hadithi ilikuwa ilienda hivi:

“Niliongozwa na Roho Mtakatifu kufunga biblia 700 kwenye gari langu aina ya Volkswagen kule Uholanzi na nielekee kilomita 4,000

toka Mashariki mwa Moscow. Kwa kukosa mtu wa kuwasiliana naye kwa mawazo yangu kwa ajili ya kupeleka mzigo huu, niliendesha moja kwa moja hadi kwenye kanisa lenye watu wa ujamaa walikuwa wameruhusu katika mwa Moscow. Vile jioni iliendelea katika huu mkutano uliojaa maagenti wa KGb na watoa habari wa ujamaa, Bwana akamwangazia mtu mmoja aliyekuwa ameketi pekee yake nyuma ya mkutano. Alikuwa anatazama chini sakafuni na kichwa chake kilikuwa mikononi mwake. Kumjongelea baada ya mkutano, nikajitambulisha. Nikatambua jina lake lilikuwa Ivan “Nini kinakuleta hapa usiku huu, Ndugu Ivan?” Nilimwuliza ndugu yangu katika Kristo niliyekuwa tu nimempata.

“Oh,” Nilimjibu Ivan, kwa njia ya kuonyesha nilikuwa nimeshushwa moyo kidogo, “Nilifikiri nilisikia sauti ya Bwana siku chache zilizopita, akiniambia niendeshe kilomita 4,000 toka nyumbani kwangu Siberia. Unaona, Ndugu Andrew, mimi ni sehemu ya kanisa la kijamii la washirika 600, na tuna tu Biblia moja katika mkutano mzima! Nilifikiri nilisikia Bwana akiniambia nije hapa kutafutia kanisa letu Biblia, lakini sasa nimeanza kushangaa ikiwa ninajua kuisikiza sauti ya Bwana hata kidogo!”

“Niliitikia na: “Ndugu Ivan, nitakushangaza!” Ambapo, niliinama na kutoa tafsiri ya Kirusi ya Biblia kwa mfuko wa kuvaa mguuni mwangu wa kushoto! Na nikaiweka hiyo Biblia kwa paja la Ivan, nikainama tena na kutoa bado Biblia nyingine toka mfuko wa kuvaa kwa muguu wangu wa kulia! Halafu, nikatoa Biblia mbili toka suruali mifuko za nyuma za zuruali yangu ya ndani, mbili toka za mbele, na mbili toka mifuko ya vesti yangu! Vile Biblia zilianza kujaa kwa paja la Ivan, Ivan akalia kwa mshangao wa imani: “Ndugu Andrew, mimi ni tajiri!!!” (Biblia kama hii ni dhamana ya mshahara wa mwaka mmoja kwenye soko la magendo, lakini unaweza hakikishiwa kwamba Ivan alikuwa anarejelea kwa utajiri wa kiroho!) “Sio tajiri vile utakuwa wakati nitakapo kupeleka kwa gari langu na kukupa Biblia zingine 700!” Nilinong’ona.

“Basi, kanisa ni nini? Wakati Roho Mtakatifu anamtuma mtu mmoja kilomita 4,000 toka Magharibi, na mwingine toka kilomita 4,000 mashariki, na hawa wawili wanakutana kwa mpango wa Mungu kwa wakati na mahali penye Roho Mtakatifu amepanga wafanye kazi ya

45

ufalme, hapo una kanisa! Wakati wawili au watatu wanakusanyika kwa jina la Yesu, hapo una kanisa, na Yesu Kristo yupo hapo katikati yenu!”

“Je, kanisa la wawili au watatu ni la nguvu kiasi gani?”

Kanisa Ndani Ya Nyumba Ni Nini?

Hulka zilizotajwa hapa chini ni za kanisa kwa miaka ya kwanza 50 ya historia ya kanisa. Wakati kanisa lilisonga mbali na urahisi, pia lilisonga mbali toka kwa wingi wa nguvu zake za kupinda katika uinjilisti na kufanya wanafunzi mataifa. Hizi pia ni hulka za Kanisa Ndani Ya Nyumba likichipuka kote ulimwenguni leo.

KANISA NDANI YA NYUMBA NI KANISA RAHISI

Hakuna madoido. Hakuna sherehe. Hakuna urembo wa ibada. Hakuna mifano. Kwa urahisi ni wakati watu wa Mungu wanakuja pamoja na Yesu akiwa katikati yao. Wanaongea. Wanaimba. Wanaomba. Wanakula chakula pamoja. Wanakula komnyo takatifu na kusoma Biblia. Wanashiriki yale Mungu anafanya maishani mwao. Wanawaombea watu na aina zote za mahitaji kote ulimwenguni. Wanahudumiana mmoja na mwingine kupitia karama zenye Mungu amempa kila mmoja. Wanapendana mmoja na mwingine na wanatafuta kutiana moyo na kuadilishana mmoja na mwingine katika imani yao.

KANISA NDANI YA NYUMBA LINAKUTANA KWA NYUMBA. Ni mahali rahisi pa kuwa na kanisa. Hakuna alama za kisiri za kuelezea. Sio kiweko cha kidini. Hakuna anayehisi kutotulia juu

kufanya kitu kisicho cha kidini. Watu wanajihisi wako nyumbani, na wanatulia tu. Kanisa linaanza dakika watu wawili au watatu wa kwanza wanawasili kwa

sababu kanisa ni watu wala sio utaratibu. Penye waamini waliozaliwa mara ya pili wanakusanyika, hapo kuna kanisa. Wao ni “kanisa limekusanyika”. Wanapo ondoka wote, wao ni “kanisa limetapanyika.” Wanakuja pamoja kuadilishana. Wanaenda nje kuuguza ulimwengu kama chumvi, nuru, na chachu katika nguvu za Roho Mtakatifu.

Wanaenda kila mahali wakihubiri injili kwa maneno na matendo kwa wale wasiomjua Yesu. Wanatimiliza Wito Mkuu, ambao nitaufasiri hivi: “Mnapoenenda, hapa, hapo, na kila mahali, hubiri injili kwa wakati, popote utakapokuwa…SASA!”

KANISA NDANI YA NYUMBA NI KATIKATI YA UINJILISTI

Ni rahisi kumpata mtu ambaye hajaokoka kutembelea mkutano kwa nyumba ya mtu kuliko kumpata akienda kwa ibada. Mpango ni kuweka kanisa dogo mwendo wa kutembea kwa kila mtu kwa kila ujirani. Hii ndio sababu mmoja wapo kanisa la karne ya kwanza “liliupindua ulimwengu juu chini.”

KANISA NDANI YA NYUMBA LINARAHISISHA UFANYAJI WANAFUNZI

Ni vyema kupisha milango na kuwaongoza watu kwa Yesu. Ni vyema kuwaongoza kwa Bwana kwa barabara, bustanini, viwanja vikubwa, kwa simu, au katika maongezi yasiyo rasmi. Lakini tunapo mwongoza kwa Bwana hapo mahali atafanyiwa uanafunzi, kanisa kwenye nyumba, tuna manufaa yaliyo wazi. Tayari amejulishwa kwa kanisa. Anaweza batizwa papo hapo na kuongozwa kwa upole kuingia uhusiano wa ndani na Kristo na wale watu waliomwongoza kumpokea Kristo. Kazi ya kumwingiza kanisani tayari itakuwa imefanywa.

KANISA NDANI YA NYUMBA LINAHUSIANA NA MWILI MZIMA WA KRISTO.

Jina pekee ambalo linastahili kuinuliwa ni jina la Yesu. Hatuhitaji kulifikiria jina nzuri la kanisa letu. Sio kanisa letu. Ni kanisa lake Yesu. Ni “kanisa ambalo linakutana kwa nyumba ya mtu.” Ni sehemu ya kanisa lote mjini. Kila kitu cha Yesu ni cha kanisa lake. Kila kitu ambacho Yesu anafanya katika miji yetu ni chetu. Sisi sote tunawajibu kwake hata ikiwa ni kuomba tu. Tu mwili mmoja. Tumezaliwa ndani ya umoja na ni lazima tudumishe huo umoja kwa kupokea watakatifu wote bila kujali wanaishi wapi au ni kikundi gani wanahudhuria. Sisi sote ni mmoja na mwingine.

KANISA NDANI YA NYUMBA LINATEMBEA

Sio lazima tukutane kwa nyumba moja kila juma. Sio jengo ndilo linatushikilia pamoja. Ni mahusiano ndio yanatushikanisha pamoja. Sisi ni wa kupinda. Tunawza kutana popote. Kwa njia hii, tunajitoa kwa watu wengi kwenye sehemu nyingi.

KANISA NDANI YA NYUMBA LINAPINDA

Mikutano inaweza kufanywa usiku au mchana wowote, pia Jumapili. Hakuna kitu kwenye Agano Jipya kinasema Jumapili ndiyo siku ya kanisa. Kwa kweli, kielelezo kwenye kitabu cha Matendo ni kwamba walikutana kila siku. Siku ya kwanza ya wiki ni nadra itajwe kabisa na haijawahi kutiliwa mkazo kama siku halisi iliyotengwa kwa ajili ya kuabudu. Mtume Paulo anapinga wazo la “siku halisi” kwenye maandishi yake.

Mnashika siku, na miezi, na nyakati, na miaka. Nawachelea, isiwe labda nimejitaabisha bure kwa ajili yenu. (Wagalatia 4:10-11).

KANISA NDANI YA NYUMBA NI NDOGO Kubwa sio ndio nzuri kila wakati. Kubwa hata hivyo, ndio sisi tunataka. Lakini tunweza kua wakubwa upesi tukizidisha kuliko

tukiongeza. Kanisa Ndani Ya Nyumba linajenga kanisa kubwa la jiji lote kwa kugawa na kuzidisha. Tutapata mikutano mikubwa zaidi mara kwa mara, lakini kanisa letu la msingi linazalia ndogo. Wakati zaidi ya watu ishirini au thelathini wanahudhuria kanisa kuambatana, ni wakati wa kuwa na “mtoto.”

KANISA NDANI YA NYUMBA NDIO KANISA

46

Tunasoma juu ya kanisa kwa viwango vine tofauti kwenye Agano Jipya. “Kanisa” ulimwenguni. (Wakolosai 1:24), “Kanisa mashambani” (Matendo 9:31), “Kanisa” mjini (2 Wakorinto 1:1) na :Kanisa” nyumbani (Wakolosai 4:15). Kanisa nyumbani ni ndogo la kanisa mjini, mashambani, na ulimwenguni. Ni kanisa kama tu kama kanisa la mjini, au mashambani, au ulimwenguni. Lina sehemu zote na viungo vyote muhimu za kanisa. Neno microcosm kwa urahisi linamaanisha “ulimwengu mdogo” au “mfano mdogo wa vitu vyote.” Kanisa nyumbani ni kanisa kwa maana kamili ya hili neno. Hivyo ndivyo mtume Paulo alivyoiona kazi yake kwa karne ya kwanza. Wakati wa safari yake ya kwanza ya utume aliliwacha kundi dogo la wanafunzi kwa miji minne tofauti: Antiokia, Ikonio, na Listra. Alirejelea kila kundi dogo kama kanisa mjini humo.

KANISA NDANI YA NYUMBA NI TENDO LA AGANO JIPYA

Sikusema “Kielelezo cha Agano Jipya” kwa kuwa sina uhakika Mungu alituachia kielelezo cha kufuata jinsi ya kuongoza kanisa. Kielelezo cha kweli cha Agano Jipya ni kuomba, sikiza toka kwa Mungu, na utii yale anakwambia. Ikiwa anakwambia ujenge kanisa kubwa kabisa FANYA HIVYO! Utabarikiwa na pia Mwili wote wa Kristo. Nguvu za kuendesha za kanisa la kwanza zilikuwa tu ni hizo. Hawakuwa wanajaribu kufuata “kielelezo” ambacho walikisoma mahali. Walikuwa wanafuata mwongozo wa Roho Mtakatifu kwa msingi wa siku baada ya siku. Kufaulu kulifuata.

Bado ni salama kufanya vivyo hivyo siku zetu. Makanisa mengi yamejaribu kutafuta mbinu za ukuaji ambayo Mchungaji Cho wa Seol, Korea alipata na kulijenga kanisa kubwa zaidi ulimwenguni. Aliieleza kwa maneno sita rahisi: “Ninaomba tu na kutii.” Hakuna kasoro kukutana ghalani, shambani, pangoni, kwenye jengo la kanisa, au kwenye sinagogi.

Bwana anatazama moyo. Lakini ikiwa bado tunatilia nguvu mfumo ambao unanyonga uhai wa kanisa kupitia kwa uongozi wa mikono mizito na mfumo wa wahubiri wanaofisha, hatutapata tunda tunalolitafuta.

MAKANISA YA NYUMBANI NI RAHISI KUANZISHA Hatutapata mbinu rahisi zaidi ya kupanda makanisa mapya. Na tunatumia upanzi wa kanisa kama njia ya uinjilisti, uanafunzi, na

utume. Imethibithishwa kwenye Mshindo wa Ukuaji wa Kanisa kwamba mbinu bora zaidi ya uinjilisti ni upanzi wa makanisa mengi zaidi. Njia bora zaidi ya kufanya wanafunzi pia ni kuanzisha makanisa mapya mengi zaidi. Watu wanapokusanyika kwa vikundi vidogo, bila desturi, uanafunzi unafanyika bila juhudi za ufahamu.

MAKANISA YA NYUMBANI YANAWEZA KUANZA KABLA MPANZI KANISA HAJA WASILI

Haya yalifanyika Antiokia na pia Samaria. Pia kwenye sura ya kumi ya Matendo, tunaona Kornelio alikuwa chombo katika kuanzisha Kanisa Ndani Ya Nyumba bila hata kujua kile alichokuwa akifanya. Hili linatenda Uchina na mahali kwingine katika siku zetu. Hii haifutilii mbali kazi ya mitume, manabii, wainjilisti, wachungaji/walimu. Tunazungumzia kuanzisha makanisa, sio kuendelea kufaulu kwa haya makanisa. Tutahitaji huduma ya viongozi waliopakwa mafuta wachaguliwe na Bwana ikiwa haya makanisa yatafaulu.

Hizi ndizo baadhiya hulka za makanisa ya nyumbani: Kila nyumba itakuwa na nafsi yake. Hakuna mikutano miwili itafanana. Ni Roho wa Yesu anayetuongoza kwenye mikutano yetu. Analeta misisimko yote ya uwepo wake katika kila mkutano kwa kutumia mtu yeyote anayemchagua kuhudumu.

Uanachama Wa Kanisa?

Je, umefanya uamuzi wa kufurahisha kuwa wewe ni mwanachama wa kila kanisa mjini? Ikiwa wewe ni wa Yesu, wewe ni mwanachama wa Mwili Wake, liwe ni kanisa gani unahudhuria, jina lako liwe kwenye orodha au la. Hili wazo laweza kuwa la kushtua mwanzoni, lakini baada ya kulilingalisha na taarifa fulani katika kitabu cha Matendo, tunaona ni kweli.

Matendo 2:41: “Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu.” Na matendo 2:47: “…Bwana akazidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.” Pia Matendo 4: “…na hesabu ya watu waume ikawa kama elfu tano.” Na pia:

Na kwa mikono ya mitume zikafanyika ishara na maajabu mengi katika watu; nao wote walikuwako na nia moja katika ukumbi wa Sulemani; na katika wote wengine hapana hata mmoja aliyethubutu kuambatana nao…walioamini wakazidi kuongezeka kwa Bwana, wengi, wanaume na wanawake. (Matendo 5:12-14). Hivyo hivyo:

Na kila siku, ndani ya hekalu na nyumbani mwao, hawakuacha kufundisha na kuhubiri habari njema za Yesu kwamba ni Kristo…hata siku zile wanafunzi walipokuwa wakiongezeka hesabu yao. (Matendo 5:42-6:1).

Nyingine tena:

Siku ile kukatukia adha kuu ya kanisa lililokuwa katika Yerusalemu…Sauli akaliharibu kanisa, akiingia kila nyumba, na kuwaburuta wanaume na wanawake na kuwatupa gerezani. (Matendo 8:1-3).

Tunapotafakari juu ya fungu lililo hapa juu, ukweli mwingine unakuwa wazi: maelfu ya waamini waliotapanyika kote katika

mjini Yerusalemu waliitwa “Kanisa”. Walifahamu vyema kwamba, hata ikiwa walikutana kwa umati wa makutano madogo sana kwenye nyumba kote mjini ambayo pia yaliitwa “makanisa,” kwa kweli, kulikuwako na mwili mmoja tu wa Kristo katika mji wa Yerusalemu ambao uliitwa ‘Kanisa.”

47

Bwana ndiye alizidisha watu kwenye kanisa. Hakuna dalili kwamba kulikuwako na orodha ya washiriki au orodha ya uanachama kwa kila mmoja katika mkutano.

Kote katika Agano Jipya haijawahi kuwa dokezo ya mkutano wa nyumbani uliofanya orodha ya ushirika wa wale waliokuwa washiriki halisi wa kile kikundi. Kinyume, hili wazo linawakilishwa wazi kila wakati kwamba kila mwamini kwenye mji mzima walikuwa viungo vya kila mmoja, kwa sababu walikuwa viungo vya Mwili wa Kristo mahali hapo.

Hitimisho pekee la kuongezwa kwa idadi lilikuwa kuzaliwa mara ya pili: “Bwana akazidisha idadi yao waliokuwa wakiokoka.” Kuongeza kitu kingine kama sharti la kuwa mshiriki wa ushirika wa nyumbani haina msingi wa kibiblia kabisa na changamoto la moja kwa moja kwa Roho Mtakatifu ambaye tayari ameongeza kila mwamini anayezaliwa mara ya pili kwa idadi ya wanafunzi kwenye mji huo. Sisi tunafanyika washiriki wa mwili wa Kristo mara moja wakati tunapo zaliwa mara ya pili. La zaidi, hatuna misingi kwa liwalo lolote lile kuwaita wengine wanaohudhuria mikutano yetu “washiriki” na wengine “wasio-washiriki”. Kila mtu ambaye ameokoka ni mshiriki wa mwili wa Kristo na kwa hivyo mshiriki wa mikutano ya waumnini anayoihudhuria kwa wakati huu. Kama swala la kweli, yeye ni mshiriki wa kila mkutano wa nyumbani kwenye kila mji, kwa sababu mikutano yote ya nyumbani kwa jumula inaufanya mwili wa Kristo mahali hapo.

Ijapokuwa kanisa katika Yerusalemu lilikuwa na makutano wengi wakikutana nyumbani, wote walikuja pamoja kwenye uwanja wa hekalu kwa makusanyiko makuu ya hadhara. Tunasoma juu ya kanisa kutawanyika katika mikusanyiko midogo kwenye nyumba kwa ajili ya malezi na pia kwa mikusanyiko mikubwa katika mahali pa hadhara.

Katika marejeleo yote yaliyo hapa juu, “idadi” inarejelea waamini wote kote Yerusalemu. Maneno “idadi” na “kanisa” yanabadilishana kimaana. Hii inafanya wazi kuwa wakati Bwana anakuongeza kwa “ushirika” anakuongeza kwa “kanisa” ambao kuna moja tu kwa mji mzima. Hii haipingani na kweli kwamba kulikuwako na kanisa za nyumbani nyingi kote katika miji ambazo zililifanya kanisa la kote jijini. Matendo ya kutengeneza orodha ya “washiriki” haina kielezo katika Agano Jipya. Ni kifaa ambacho kimekuwa mtego na kimetumiwa na adui kuugawanya Mwili wa Kristo zaidi katika vijisehemu vilivyotengana kote mjini. Linaongeza mgawanyiko katikati ya watu wa Mungu kuliko umoja.

Tumefundiswa kuwa ikiwa wewe u mshiriki wa kanisa fulani, huwezi kuwa mshiriki wa kanisa lingine kwa sababu uamini na utii wako, na wakati wako, na vipaji vyako, na fungu lako la kumi kwa kanisa moja na sio kwa lingine; kana kwamba kuhudhuria au kusaidia mkutano mwingine wa watu wa Mungu kwa fulani ingekuwa ni kutokuwa na uaminifu kwa Kristo.

Ni lazima tutenganishe maswala haya mawili ya ushirika na kujitoa. Hayamaanishi kitu kimoja. Naweza kuwa mshiriki wa kila kanisa mjini na bado ninaheshimu kujitolea kwangu kwa kila mmoja wetu, kuongoza, kufanya kazi, kutoa, kusaidia katika makutano mbalimbali kote mjini. Naweza timiza kujitoa kwangu kwa sehemu yoyote ya Mwili wa Kristo bila kujizuia kuhudhuria ushirika mmoja pekee wa waamini.

Kila kitu kilicho cha Kristo katika mji ni cha kila mwamini katika mji. Mtazamo mwingine wowote unapelekea mashindano, wivu, na migawanyiko, ambayo ni uzushi. Kwa sababu hii ni makosa kumwita mtu wowote “mwenda kanisa mzuri” au “mruka kanisa” au “panzi” au “kipepeo” au jina lingine la matusi kwa sababu tu yeye anaweza hudhuria na kufanya kazi kwa zaidi ya mkutano mmoja.

Hili linatuleta kwa neno lingine ambalo limetumiwa kumtisha mtu wowote ambaye angedhubutu kujaribu “kuiba uzingizi”. Hili neno la ajabu, la kuogofya ni…KUONGOKA-KWA DINI!

Neno “mwongofu wa dini” linapatikana mara nne kwenye Biblia. Linamaanisha, “aliyewasili toka kwa kanda ya ugenini, kwa mfano, mwongofu wa dini ya Kiyahudi.” Hili neno laweza tumika kuwaelezea Wakristo wanaotiririka kwa uhuru toka mkutano mmoja hadi mwingine.

Kwa nafasi ya kwanza, hakuna hata mmoja wa hawa kondoo ambaye ni wa mchungaji wowote. Ni wa Yesu. Kila mtume, nabii, mwinjilisti, na mchungaji kazi yake ni kuangalia tu, kutunza, na kuwalisha kondoo wa Yesu. Hawaruhusiwi

kuwamiliki wawe wao wenyewe. Kondoo si wao. Mtu anaweza sema, “Lakini mchungaji, mimi nimetumwa kuwalinda toka kwa hatari.” Hilo ni kweli ikija kuwalinda tokana na

uzushi au mitego toka kwa Shetani, lakini hakika haimaanishi kwamba wanalindwa toka kwa wengine! Tunahitaji kujenga ushirika kati ya watakatifu ndani ya mji ambao wanaufanya mwili wa Kristo. Na ni nini kilicho tupa wazo kwamba ni wachungaji pekee ndio walio na jukumu juu ya kondoo?

Mungu alitoa huduma zote nne kuwaleta kondoo katika ukomavu, sio tu huduma ya mchungaji/mwalimu. Mtume, nabii, na mwinjilisti wana jukumu sawa na ya mchungaji/mwalimu katika kuwaleta watu wa Mungu kwa ukomavu.

Kwa nafasi ya pili, neno “mwongofu wa kanisa” laweza tu maanisha kumleta mtu toka kwa dini moja na kumuingiza dini nyingine, sio toka kwa mkutano mmoja wa Wakristo hadi mwingine. Neno hili halijawahi tumika kwenye Biblia kwa maana hiyo. Huwezi kumwokoa Mkristo isipokuwa umtoe kwa Ukristo na kumwingiza kwenye dini nyingine. Hili neno haliwezi tumika kwa Wakristo watiririkao kwa uhuru toka kwa mchungaji mmoja hadi mwingine. Ni heshima pekee ya kondoo kutafuta malezi ya kiroho na mwongozo toka kwa yeyote wa Wachungaji wa Mungu, wakati wowote na mahali popote, ni wajibu wa kila mchungaji kulea na kuongoza kondoo wa Mungu wowote na wote ambao wanamjia kwa msaada. Hebu na tusiwahi hukumika kwa ajili ya kujaribu kufungia kondoo wa Yesu kwenye zizi letu na kuwaweka alama zetu. Wao ni wa Yesu na wanaweza tafuta malisho pitia yeyote wa wachungaji wake wa chini, popote, wakati wowote. Kwa wale wenye huenda wakakasirika kwa kuitwa “kondoo”, kumbuka tu kwamba sisi sote tunaitwa kondoo, pamoja na wachungaji (Tazama Zaburi 100:3).

JINSI YA KUTOZALISHA UAMINIFU “Lakini nisipokuwa na orodha ya washiriki na masharti ya kimsingi, kama fungu la kumi, kuhudhuria kwa uaminifu, maisha ya

kiungu, kushuhudia, na kadhalika, nitawahi kuwa na watu waaminifu?” Swali la namna hii linatoa makosa ya mfumo ambao unazalisha uhaki tupu. Je, tunafikiri tunaweza zalisha ukomavu wa kiroho ndani ya watu wetu kwa kuwafungia kwa aina fulani ya uhaki?

Je, “tunazalisha” ushirika wa kanisa kwa kujitengenezea masharti ambayo ni pamoja na kutoa fungu la kumi kila wakati? Wacha tumpokee kila mtu ahudhuriaye mikutano yetu na tufanye kazi naye kuendeleza ukomavu wa kiroho kwa kiwango anachotaka kuufuata uongozi wetu. Hii itakuondolea wewe nayeye msukumo na inaondoa uraya wa daraja la kwanza na uraya wa daraja la pili.

48

Shutuma za “kuongoa” hazipaswi kuwahi kusikika kati ya wachungaji wa kweli, wamuogopao Mungu. Mchungaji yeyote atafutaye kuwa vuta kondoo kwa makusudi ya uchoyo au ulafi atajibu kwa Bwana dhambi yake. Kote katika Agano Jipya wachungaji walielekezwa kuhusiana na kundi zima na watu walielekezwa kuhusiana na “wazee” wa kanisa la kote mjini; sio tu mzee mmoja. Tazama yafuatayo:

Wakumbukeni wale waliokuwa wakiwaongoza, [wingi] waliowaambia neno la Mungu; tena, kwa kuuchunguza sana mwisho wa mwenendo wao, iigeni imani yao…watiini wenye kuwaongoza, na kuwanyenyekea; maana wao [wingi] wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama watu watakaotoa hesabu…. Paulo alitumanisha wazee wa kanisa kule Efeso. Walipowasili, aliwaambia: “…Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe.

Katika Waebrania 13 hapa juu, watakatifu walionywa kuhusiana na mamlaka yote ya kiroho, sio tu kwa mzee fulani. Na katika

Matendo 20 Paulo anawakumbusha wazee wote kuwa wao, kwa ujumula, wanapaswa kuwachunga “kondoo” (umoja) ndani ya mji wa Efeso. Katika siku hizo walielewa kuwa wazee ndani ya mji wana kipimo fulani cha wajibu kwa watakatifu wote ndani ya mji.

Katika Agano Jipya lote hakuna mfano hata mmoja wa mchungaji mmoja akilichunga kundi moja. Roho Mtakatifu aliwapa wachungaji, walimu, wainjilisti, manabii, na mitume kuichunga kanisa nzima, sio sehemu moja dogo ya kanisa. Ikiwa mtume, nabii, mwinjilisti na mwalimu wanaweza fanya kazi kwa namna hii, na wanafanya, kwa nini mchungaji naye asiweze? Sio tena vigumu kwa mchungaji kuhusiana na zaidi ya mkutano mmoja kuliko vile ilivyo kwa nabii, mtume, mwinjilisti na mwalimu kuhusiana na zaidi ya kanisa moja. Ndio njia bora zaidi ya kiafya ya kanisa kufanya kazi.

Hii haimaanishi kuwa kila mkutano wa nyumbani unapaswa kuwa na wazee wengi, bali kuwa kutakuweko na idadi ya wazee wakilichunga kundi katika kila kanisa kote mjini, na huu uongozi unapaswa kuwa pamoja na huduma zote tano (au mara nne, kulingana na unavyoelewa Waefeso 4). Je, hatuwezi tukalekeza kidogo tu na kuliaachilia kanisa litiririke kwa uhuru huku wachungaji wote, walimu, mitume, manabii, wainjilisti, na watu kufanya kazi jinsi Mungu alivyowateua wafanye?

Paulo aliendelea kuwaambia wachungaji kule Efeso:

Najua mimi ya kuwa baada ya kuondoka kwangu mbwamwitu wakali wataingia kwenu, wasiwahurumie kundi; tena katika ninyi wenyewe watainuka watu wakisema mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawaandamie wao. (Matendo 20:29-30)

Tafsiri ya The Amplified Bible ya mstari wa 30 inasema ifuatavyo:

Hata kutoka kati yenu wenyewe wanaume watakuja mbele, ambao kwa kusema mambo (geuzwa na fisadi) mapotovu watajaribu kuwavuta wanafunzi upande wao (kwa chama chao wenyewe).

Ningependekeza “chama” hapa juu kumaanisha dini au ushirika wao wenyewe. Kulikuwako na wazee wengi lakini kundi moja

tu na Paulo aliwaambia wazee wote kulichunga kundi nzima. Tendo la kutenga sehemu ndogo za kundi na kudai ni la mtu fulani lilishughulikiwa katika fungu hili.

Paulo alisema kuwa alipoondoka, alijua baadhi ya wachungaji wange“jivutia wanafunzi”. Kwa kiwango fulani, hili hufanyika kila wakati mchungaji anajifanyia orodha yake ya washiriki na anajaribu kuwafungia watu kwake na mbali toka kwa Mwili wa Kristo na mbali toka mchango wowote wa kiroho toka kwa mchungaji mwingine ndani ya mji.

“Lakini ikiwa nitawaambia watu wangu kuwa wao ni washiriki wa kila kanisa ndani ya mji, hawatakuwa waaminifu kwa ushirika huu kwa kuhudhuria na kutoa kwao!” Anaomboleza mchungaji mwenye uwoga.

Hili ni jambo la umuhimu mkubwa sana kwa viongozi wengi. Kilio ni, “Njoo utusaidie tutimize maono yetu”. Kilio kinapaswa kuwa, “Njoo na tukusaidie utumilize maono yako na mwito wako.” Mitume, manabii, wainjilisti, na wachungaji na walimu walipeanwa kwa kanisa “kuwaandaa watu wa Mungu kwa kazi za huduma.” Mungu hupeana karama, miito, upako, na maono kwa kila mshiriki wa Mwili Wake. Ni ono la kumtumikia kwa njia halisi na ni kazi ya hawa viongozi kusaidia kuwaandaa kutimiliza kazi za huduma.

Maono ya wachungaji wengi kupata kiasi ni kuwatumia kondoo wote wale anaweza kukusanya kumsaidia kujenga kusanyiko la nyumbani kuwa kubwa na kubwa zaidi bila wazo la kuujenga Ufalme wa Mungu na kusaidia kutimiliza Wito Mkuu.

TATIZO LA “USHIRIKA WA KARTASI” Baadhi ya matatizo ya “ushirika wa karatasi” ni: tunathubutu kuwa tunajua ni nani kwa kweli amezaliwa mara ya pili na kwa

hivyo tunawahitimisha kwa “idadi iliyoongezeka.” Ni Bwana tu afahamuye ni nani ameokoka na anaweza kumwongeza kwa kanisa. Orodha ya washiriki kwa kawaida ni kifaa kinachotumika kuwapokea watu katika desturi ya uhusiano unaoendelea. Ukilitizama kwa mara ya kwanza, hili linaonekana kama halina madhara yoyote, lakini linaelekea kuwafungia mbali toka kwa wengine wa Mwili wa Kristo ndani ya mji. Hili linasababisha migawanyiko iliyojitenga ndani ya kanisa kote-mjini. Kwa nini sisi hufanya hivi halafu tunalalama kwa sababu gani Mwili wa Kristo umegawanyika? Tunahitaji kuamuka na tuone kuwa SISI ndio sababu kwa nini! Hili ndilo Paulo alionya lingetendeka: “Hata kutoka kati yenu wenyewe wanaume watakuja mbele, ambao kwa kusema mambo watajaribu kuwavuta wanafunzi upande wao.” Ushirika wa karatasi unatoa changamoto kwa msingi wa kweli wa kile kanisa inapasa kuwa na vile tumekuwa sehemu yake.

Sharti la kuwa mshiriki wa kanisa la mkutano wa nyumbani ni sawa na lile la kuwa mshiriki wa Mwili wa Kristo, ambalo ni, kuzaliwa mara ya pili. Tunafanyika washiriki wa huo mwili ulimwenguni kote mara tu tunapozaliwa kwa Roho Mtakatifu wa Mungu kwa imani katika Yesu Kristo. Hakuna masharti mengine.

Kufundisha kuwa watu wanaweza kuwa washiriki wa Mwili wote wa Kristo na bado sio washiriki wa kanisa lako la nyumbani ni fitina.

49

Kunayo mengi ya makanisa ya nyumbani, lakini kila moja ni sehemu ya Mwili wa Kristo ulimwenguni kote. Kwa hivyo, ikiwa mimi ni mshiriki wa nzima, kwa kufuata kawaida, mimi ni mshiriki wa kila sehemu. Maandiko hayakuwahi hata kuguzia wazo la kuwa washiriki wa shirika. Yanasema tu kwa urahisi, “Tu vyungo mmoja na mwingine.” Hilo ni pamoja na waamini wote katika mahali pote ulimwenguni kote.

Orodha ya washiriki si sawa kwa sababu inazaa na kulinda wazo kwamba, “Hawa kondoo ni wangu! Kaa mbali na kondoo wangu!” Hakuna mstari hata mmoja ambao unawahi kunipa mimi, kama mchungaji, haki ya kusema kuwa mmoja wa watu wa Mungu ni “kondoo wangu.”

Ni kweli kuwa mchungaji ni mchungaji, lakini Yesu alisema, “Lisheni kondoo WANGU.” Kuna Mchungaji mmoja Mkuu, wachungaji wengi wadogo, na kondoo wengi, lakini kundi ni moja tu. Kondoo hawaambiwi kushiriki tu na mmoja wa hawa wachungaji wadogo. Kondoo waweza pokea mwongozo toka kwa yeyote na wote Mungu aliita kuwa wachungaji.

“Lakini mshahara wetu utatoka wapi?” analia mchungaji mdogo asiye-aamini. Utatoka kwa mikono ya Mchungaji Mkuu ambaye unafanyia kazi, anaye ahidi kukutana na mahitaji yako yote unapofanya kazi aliyokuita ufanye. Yeye ndiye Mlipaji wako Mkuu. Ondoa macho yako kwa watu kuwa ndio chanzo cha riziki yako na uyaweke kwa Yesu ambaye Jina lake ni Yehova Yire, Bwana Akupaye.

MTAZAMO WA KIBIBLIA WA USHIRIKI

Kila mwamini aliyezaliwa mara ya pili anaongezwa kwa kanisa na Bwana Yesu wakati anapookoka. Anakuwa sehemu ya Mwili wa Kristo mara moja ulimwenguni kote ambao, kwa wakati huo huo, anafanyika mshiriki wa kila mkutano wa nyumbani, kila mahali, popote aendako. Kila kanisa la mahali hapo ndani ya mji linapasa kujiona kama sehemu muhimu ya kanisa kote-mjini na kanisa kote ulimwenguni. Haipaswi kuweko masharti maalum ya kuwa mshiriki wa kanisa la mahali kupita lile la kumpokea Yesu kama Bwana na Mwokozi.

Kanisa sio shirika—ni kiumbe hai—mkusanyiko wa watu wa Mungu ambamo kila mtu anakaribishwa. Wachungaji na viongozi lazima wasiwahi kuwawekea madai yoyote kondoo wa Mungu kama wake. Wanapaswa kuwalea, kuwalinda, kuwaongoza, kuwashauri, lakini wasiwahi kuchukua urithi wa Mungu. Sisi ni watendakazi-pamoja na Mungu, lakini ni lazima tuyaachilie mafigo na kumwamini Roho wa Yesu akamilishe kazi ya ujenzi wa kanisa, akitutumia sisi kwa njia yoyote apendayo.

Wazee (waitwao pia wachungaji, walimu, na maasikofu) wa kila kanisa la mahali wanapaswa kuendeleza uhusiano wa matendo ili waweze kuwatunza kundi la Mungu ambalo Bwana amewafanya waangalizi kwa nguvu zaidi.

Upanzi Lowesha wa Kanisa

Mmoja wa waunga mkono wa mstari wa mbele katika upanzi wa kanisa kwenye karne hii alikuwa marehemu Dr. Donald

MacGavran. Kwenye Dawn Report ya hivi majuzi, Jim Montgomery anatoa tukio lifuatalo:

“Wakati wa miezi ya mwisho ya magonjwa ya Mary MacGavran, mke wangu Lyn mara nyingi angeshinda naye. Donald MacGavran angekuwa hapo, pia, akipuuza saratani yake mwenyewe ya uchungu hali akimshughulikia mkewe mpendwa.

“Waweza kuwa na uhakika mimi na Jim tutaendelea na ahadi yetu ya ukuaji wa kanisa baada ya wewe kuondoka,” Lyn akamwambia Donald siku moja.

“Usiite ukuaji wa kanisa tena,” lilikuwa jibu lake la haraka. “Uite uzidishaji wa kanisa!” Wiki mbili baada ya kifo chake, alisema, “Njia pekee ya kuutimiliza wito mkuu ni kupanda kanisa kwenye kila jamii katika ulimwengu.”

KANISA KWENYE KILA UJIRANI.

Yesu aliliamurisha kanisa kwenenda kote ulimwenguni na kuwafanya wanafunzi mataifa yote. Kulingana na mikakati ya utume, kuna maelfu ya mataifa, au makundi ya makabila. Pia inakubalika kwa ujumula kati ya viongozi wa kanisa kwamba njia pekee ya kulifundisha taifa ni kupanda makanisa kwenye hilo taifa. Zaidi inakubalika kwamba itachukua zaidi ya makanisa machache kulifundisha taifa. Itahitaji mkakati wenye kuona UPANZI LOWESHA WA KANISA, ambao unamaanisha kupanda makanisa katika kila ujirani wa watu 500 hadi 1000. Haya maono ya upanzi lowesha wa kanisa sio tu kwa mataifa yanayoendelea. Ni ya mataifa yote pamoja na Uropa, Latin Amerika na United States.

SHAMBA NI ULIMWENGU Hakuna kanisa ambalo linawafikia wasiookoka wote kwenye kila mji au hata ujirani. Tunahitaji usaidizi wote tunaoweza pata

kuwafikia wenye mahitaji. Ikiwa mshindo wa Kanisa Ndani Ya Nyumba utaharakisha uinjilisti wa mji wangu, ninataka kuanzisha makanisa mengi ya nyumbani iwezekanavyo na nione yakizidishwa. Pia nimeweka ahadi ya kumtia moyo mchungaji yeyote, anayempenda na kumwinua Yesu, katika juhudi zake za kuzidisha makutano katika mji wangu au mji mwengine.

KIFO CHA KIBURI NA ULAFI

Je, kuna umuhimu gani kwetu kuwa na mkutano mkubwa na sadaka kubwa na majengo ya kupendeza? Tumeongozwa kuamini kuwa hizi ndizo ishara za kweli za ushindi kwenye huduma na basi tunajitahidi kuinua mkutano mkubwa. Tunataka kuonekana tumefaulu kwenye macho ya watu wetu, viongozi wetu na machoni petu; kama matokeo, tuna naswa kwenye utando huu wa udanganyifu. Hii inazaa roho wa ulafi, uchoyo, majivuno, na umiliki.

IMARISHA UONGOZI USIO WA KULIPWA KATI YA WATU

Wengine wanasumbuka kwamba mkakati wa kuzidisha makanisa ya nyumbani utasababisha kutokea kwa viongozi wapumbavu, wasiohitimu. Yesu hakwenda kwa mashirika ya kidini ya siku zake kuwachagua wanaume ambao angewatumia kuongoza ujenzi wa kanisa lake. Aliwachagua wavuvi na wanaume ambo aliwaweka nguvu kwa Roho Mtakatifu. Mungu hupenda kutumia vitu vidogo na dhaifu.

50

Maana, ndugu zangu, angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa; bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu; tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko; mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu. Katika kila mshindo ambao umekuwa na umuhimu katika kueneza injili ulimwenguni kote pitia historia ya kanisa, wanaume na

wanawake wa kawaida wamekuwa na jukumu la kuongoza. John Wesley alikuwa mtu mwenye maatifa makuu na miaka ya elimu na mafundisho ya kidini, bali kama kiongozi wa moja

wapo ya mitetemo ya ufufuo na upanzi wa kanisa ya historia hakwenda kwenye shule zilizoendelea za mafundisho ya kidini ya wakati wake kuwatafuta wachungaji na viongozi wake. Alisema:

“Nipe wanaume 12 wampendao Yesu kwa mioyo yao yote na wasiowaogopa watu au mashetani na sijali hata kidogo kama wao ni wahubiri au watu wa kawaida, nikiwa na hawa watu nitaubadili ulimwengu.”

Na hilo ndilo tu Bwana Weslye alilifanya. Kuihubiri injili hadharani nyakati za Wesley ulikuwa ni ukufuru wa juu na udhi zito

kwa kanisa lililoendelea. Lilikuwa jambo lisilofikirika kwenye Kanisa la Wingereza kusimama nje ya ukuta wa madhabahu matakatifu kulitangaza neno takatifu la Mungu. Wandugu Wesley na George Whitefield walivumilia miaka ya mateso kwa sababu ya kuvunja desturi za miaka mingi za kanisa lililoendelea, lakini hili halikuwazuia. Waliyafahamu maandishi na walisadiki kuwa ikiwa Yesu aliwezakuyafanya hayo, ilikubalika wao kufanya hivyo pia.

Akinukuu tena toka kwa maandishi ya baba wa mtetemo wa ukuaji wa kanisa, Dr. MacGavran, ninanukuu toka kwenye kitabu chake, Understanding Church Growth. Chini ya kichwa, Eight Keys to Church Growth, anasimulia:

Imarisha viongozi wa kawaida wasiolipwa. Watu wa kawaida walitekeleza sehemu kubwa sana kwenye mapunuzi ya mjini ya Kanisa. Siri moja ya ukuaji kwenye miji ya Latin America imekuwa kwamba, tokea mwanzo, watu wa kawaida wasiolipwa waliongoza makutano, ambao kwa hivyo ilionekana kwa watu wengi kuwa kweli ni maswala ya Kichile au Kibrazili. Kwenye nchi yoyote, wakati wafanyikazi, fundi wa magari, karani, au waendesha lori wanafundisha Biblia, wanaongoza maombi, wanaelezea yale Mungu amewatendea, au wanawahimiza wandugu, dini ya Kikristo inaonekana na pia kutoa sauti ya kiasili kwa watu wa kawaida. Chochote kile watu wa kawaida wasiolipwa, wakitafuta riziki yao kama vile wengine hufanya, wakipitia hatari zile zile na wakiwa na ratiba za kazi zile zile, ukosefu wa usawa kwenye mafundisho ya Biblia au urembo wa maombi, wanalipiza haya hata zaidi kwa ukaribu wao kwa watu wao. Hakuna mfanyi kazi wa kulibwa toka nje na hakika hakuna mtume toka ng’ambo anaweza jua mengi juu ya ujirani kama mtu aliye na jamaa na mwandani wanaomzingira. Kweli, kwa uwanjia mpya, mtu wa nje anapaswa kuanza milipuko mipya. Mtu mwingine hawezi. Lakini punde anapoyarudisha makanisa kwa watu wa mahali pale ndio vyema zaidi.

Kwenye kitabu chake, Breaking the Stained Glass Barrier, David Womack, mtume wa Mikusanyiko ya Mungu aliandika:

Kuna tu njia moja ya kutimiliza Wito Mkuu, na hiyo ni kuanzisha makutano yahubiriyo ndani ya kila jamii usoni mwa dunia.

Roger Greenway, mwenye maarifa ya kuifikia miji, ansema kwenye Discipling the City:

Kazi ya uinjilisti ya kanisa inadai kuwa kila jengo na ujirani ziwe na kanisa la uaminifu kwa Neno la Mungu liimarishwe ndani mwake.

MAKANISA KWA MAMILIONI

Mara ya kwanza kukisoma kitabu cha Jim Montgomery, DAWN 2000, kikiwa na kichwa kidogo ambacho singeweza kukiamini, Seven Million Churches to Go, nilijiwazia mwenyewe, “Je, mtu yeyote angdhubutu aje kufikiria katika masharti ya kupanda mamilioni ya makanisa?” Sikuwa nimekisoma kwa urefu kabla nijue kwamba mimi pia ningeweza kuamini pamoja na Jim Montgomery katika historia. Kuna haja ya kufikia kila ulimi, kabila na taifa sasa kuliko ilivyowahi kuwa tangu Yesu afe na afufuke tean na apae kwa Baba.

Sio tu Umarikani, Canada na Wingereza, bali toka Brazili hadi Afrika Kusini hadi Urusi hadi Korea hadi India na poto pote kwenye visiwa vya bahari, kilio ni:

Hebu na tukamilishe kazi [katika kizazi hiki]. Hebu tutimilize amri ya Kristo kuhubiri injili kwa kila kiumbe na kuwafanya wanafunzi mataifa wote na tumrejeshe Kristo kutawala katika haki kama falme za ulimwengu huu zinakuwa falme za Mungu wetu na za Kristo wake.

Mtetemo huu unapata mwendo kila siku. Jiwe lililo katwa toka kwa milima bila mikono na likaja likivingirika toka mlimani na

kuigonga miguu ya sanamu katika maono ya nabii Danieli linakua kubwa kila siku! Tayari limegonga kwenye mikuu ya utaratibu wa ulimwengu na hivi karibuni litakua mlima ambao utaifunika dunia na maarifa ya Bwana kama vile maji yafunikwavyo bahari.

Kifunguo cha kutimiliza Wito Mkuu ni kupanda makanisa. Mpango ni kuvutia usikivu wa wengi wa wana-mikakati ya utume siku hizi ni kupanda kanisa moja katika kila jamii ya watu 500 hadi 1000…upanzi lowesha wa kanisa. Itatubidi tutupilie mbali wazo letu la kuiona kanisa kama kio chenye dosari. Haifai kuendelee kuifikiria kanisa kama jengo. Ni lazima tuanze kulifikiria kanisa kama watu. Na hii inamaanisha watu kuja pamoja katika jina la Yesu nyumbani, madukani, ofisi, viwanda, ghala, shule, vyumba vya kuweka maiti, bustani, jela, magera, hospitali, majengo yaliyowachwa, pembeni mwa barabara, kumbini, vilabu vya wanawake, vilabu vya huduma, pia na makanisa ya majengo ambayo yamejitolea.

MCHUNGAJI WA KANISA LA NYUMBANI

Naye alitoa wengine kuwa mitume , na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke…(Waefeso 4:11-12).

51

Mchungaji ni sehemu ya timu ya kuulea mwili upate nguvu wa kujihudumia wenyewe. Kwa kweli ni mwili ndio ulio na kazi ya kujilea katika ukomavu. Mtume, nabii, mwinjilisti, mchungaji na mwalimu ni kuuhami mwili:

…kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha ukamilifu wa Kristo…katika yeye mwili wote ukiungamanishwa na kushikamanishwa kwa msaada wa kila kiungo, kwa kadiri ya utendaji wa kila sehemu moja moja, huukuza mwili upate kujijenga wenyewe katika upendo…(Waefeso 4:12-13, 16).

WA KWELI NA WA UWONGO Hatuwezi kuruhusu adui kupata ushindi mkubwa kama kuinyima kanisa huduma ya mchungaji ambaye ameitwa na kapakwa

mafuta na Mungu. Hatuwezi harimisha wachungaji wote kwa sababu wengine wamekuwa na ubinafsi, kuyatumikia manufaa yao wenyewe, na kuitumia nafasi yao ya mamlaka ya kiroho vibaya. Penye uwongo, wakati wote pia kuna ukweli na halisi.

NI MWILI NDIO UUJENGAO MWILI. Kazi ya mtume, nabii, mwinjilisti, mchungaji na mwalimu ni kuimarisha mwili ujihudumie wenyewe. Ikiwa tutakosea hili na

tujaribu kuiweka kazi ya mwili kwa watayarishaji, hatutawahi kuuona mwili wa Kristo ukikua “hata kufika kwenye cheo cha kimo cha ukamilifu wa Kristo.”

Tafsiri ya mastari wa 16 ya Phillips inasema: Mwili wote, kama umbo moja ambalo linapatana limeshikamanishwa pamoja kwa viungo ambavyo umepewa, unakua kwa ufanyikazi mwema wa kila kiungo, na hivyo basi kujijenga kwa upendo. Tafsiri ya The Living Bible inasema: Mwili wote umeshikamanishwa pamoja kikamilifu, na kila kiungo katika njia yake halisi kinasaidia viungo vingine, hivyo basi mwili wote ni wenye nguvu na unakua na umejaa upendo.

KUSUDI LA VIONGOZI KATIKA KANISA Kwa karne nyingi viongozi wa kanisa wamekuwa wakijaribu kuifanya kazi ambayo ni mwili tu unaweza kufanya na mwili

haujakuwa ukifanya kazi kujijenga hata kufikia kimo cha cheo cha ukamilifu ya Kristo. Huu “utendaji kazi wa nguvu wa kila kiungo” wa mwili ndio njia pekee inayoweza fanya kazi, lakini mwili utayarishwa na viongozi ambao Mungu ameweka kanisani kwa ajili ya kusudi hili.

Mtume, nabii, mwinjilisti, mchungaji na mwalimu ni uongozi uliothibitishwa, ambao umetumwa na Bwana kama karama kwa kanisa lake kwa kusudi halisi—kuitayarisha kanisa kujijenga lenyewe. Bado ni vibaya kwa mwili kutowaruhusu viongozi kufanya kazi vile tu ilivo vibaya kwa viongozi kutouruhusu mwili kufanya kazi. Mwili wa Kristo utapata tu nguvu ikiwa kila kiungo kina fanya kazi vizuri, na hilo ni pamoja na wachungaji na viongozi.

MITAMBO MIWILI INAYOENDESHA

Kwenye kila gari kuna mitambo miwili inayoendesha, moja inayotumia petroli na ingine inayotumia umeme: mtambo wa petroli ni mkubwa sana ukilinganishwa na ule wa umeme, lakini ni mtambo mdogo wa umeme ndio umeumbwa kuuanzisha mtambo wa petroli, na ni mtambo wa petroli ndio umeumbwa kutoa nguvu za kuendesha gari. Punde tu mtambo mkubwa wa kuendesha unaposhika moto, ule mdogo huachilia. Usipoachilia, ule mdogo ungechomeka katika dakika chache.

Mtume, nabii, mwinjilisti, mchungaji na mwalimu ni watumishi kwa mwili wa Kristo wakifanya kazi kama waanzishaji kuufanya mwili ufanye kazi na halafu, jinsi vile mtambo wa kuanzisha unawachilia punde tu baada ya mtambo mkubwa uanzapo, basi ndivyo ilivyo na kiongozi wa busara. Asibaki ameshikana au atachomeka, vile tu kianzilishi kingechomeka ikiwa hakikuachilia baada ya kuuanzisha mtambo mkubwa wa kuendesha.

Iwapo kutakuwako na kianzilishi kidogo kinajaribu kuendesha gari kutumia nguvu za batri moja, gari halitawahi fanya kazi kwa makusudi liliumbiwa. Ni mtambo wa kuendesha wa 350 horse power ndio umeumbwa kuendesha gari na ni mwili wa Kristo ambao umeumbwa kuujenga mwili hata kufikia kimo cha cheo cha ukamilifu wa Kristo. Ni kama tu Mwili wa Kristo utaachiliwa kujihudumia wenyewe ndipo utawahi kuufikia kimo cha cheo cha ukamilifu wa Kristo.

KARAMA ZA MUNGU NI KARAMA NZURI Neno la Mungu linawaaita hawa wanaume na kazi yao katika kanisa “karama.” Ni karama zilizotumwa toka kwa Mungu.

Karama zote za Mungu ni nzuri. Hakuna hata moja liyo mbaya. Ikiwa wengine wao wamekuwa wafisadi, hilo sio kosa la mpeanaji. Acha tuamini Mungu kwa urejesho katika siku hizi za wachungaji, manabii, wainjilisti, walimu na mitume wacha Mungu.

UANGALIZI WA KICHUNGAJI

Inaonekana kanisa za nyumbani ambazo Paulo alipanda katika Derby, Ikonia, Antiokia, na Lystra zilifanya kazi kabla ya kuchagua wazee (Matendo 13 na 14). Tunapouachilia zaidi Mwili wa Kristo ufanye kazi ulioumbwa kufanya, ndivyo tutakavyoona mlipuko wa ukuaji tunaousoma juu yake katika Agano Jipya. Sio lazima mchungaji arukaruke juu ya bega la kila kondoo kuhakikisha anakula. Anahitaji tu kuhakikisha kwamba yule kondoo yu mahali pazuri penye pana malisho mengi ya kula na anawaacha wenyewe kufanya kazi pekee yao. Yupo hapo anapohitajika kushughulikia mahitaji halisi, lakini haoni haja ya kuhusika katika kila kitu kifanywacho na kondoo wajapo pamoja.

Kwa upande mwingine, Yesu mwenyewe alitupa taswira ya vile ilivyo wakati kondoo hawana mchungaji.

Na alipowaona makutano, aliwahurumia, kwa sababu walikuwa wamechoka na kutawanyika kama kondoo wasio na mchungaji. (Mathayo 9:36)

52

Wakati mwigine hapo nyuma nilikuwa nikiomba kuhusu jinsi ya kuanza kufanya kazi vile impasavyo mchungaji. Kwa kweli sikujua niuachilie Mwili kwa umbali gani ndipo niuruhusu ufanye kazi. “Bwana,” Niliomba, “Nipe hekima katika jambo hili.” Bwana aliyasikia maombi yangu na akanipa mifano miwili midogo toka kwa maisha yangu ambayo imenisaidia kufahamu kazi yangu kama mchungaji.

MMEA WA NYANYA?

Kwanza, alininenea kutumia mmea wa nyanya. Nikiwa nakula chakula cha mchana na mke wangu nilisema jinsi nyanya tulizo panda wenyewe kwenye barazani mwetu zilivyokuwa na ladha tamu. “Nyanya zilizomo kwenye soko kuu hazina ladha kama hizi.” Nilisema, “Hizi zina ladha nzuri zaidi!” Vile tu niliyatamka hayo maneno, nilimsikia Mungu akisema, “Uligharimika kiasi gani kuilea hiyo nyanya?” “Sio gharama kubwa sana,” Nikajiambia mwenyewe. Niliundaa tu udongo kwa mtungi wa udongo, nikanunua mimea ya nyanya, nikaweka mizizi ndani ya udongo, na nikawa nanyunyizia mara kwa mara. Mara kama mbili hivi niliweka madini ya mimea katika maji.

“Hivyo ndivyo ilivyo na kanisa,” Bwana akasema. “Haukuhitaji kufanya mengi sana ili hiyo mimea ya nyanya ijifanyie mambo yake. Uliweka tu masharti ya ukuaji na zikakua. Imeratibishwa kwenye begu zake kufanya kazi usiku na mchana kuzaa hizo nyanya nyekundu, zenye utomvu, za kupendeza na zenye ladha nzuri. Ndivyo ilivyo na kanisa. Ni kiume hai na ikiwa utafanya kazi yako kuyaweka tu masharti, kanisa litakua kwa hiari yake lenyewe. Litazalisha kwa maana nimeliteuwa kuwa hivyo.”

MOTO KWENYE PWANI

Sio muda mrefu baada ya hayo Bwana akanipa mfano mwingine ambao nimekumbuka na kushiriki na wengine: nilikuwa kule chini pwani mapema asubuhi kama ilivyokuwa desturi yangu wakati nilikuwa nikiishi Laguna Beach, California miaka michache iliyopita. Nilikuwa na mazoea ya kwenda kule chini karibu kila asubuhi na kiti changu cha ufukoni, miti za kiberiti na magazeti makuukuu, vitabu na biblia yangu.

Kulikuwa na kuni za kuelea nyingi ambazo ningekusanya toka pwani na kujitengenezea moto. Kwa hii asubuhi hasa nilijitengenezea moto kama kawaida na baada ya kama lisali moja, nikaenda matembezi kwenye pwani. Niliporejea moto ulikuwa umezima. Nikatafuta kuni zingine zaidi na nikachochea makaa yaliyokuwa na moto, halafu nikaziweka hizo kuni juu ya hayo makaa. Kwa muda wa chini ya dakika moja nilikuwa na moto mzuri ukiwaka tena. Nikaketi chini nikaanza kuufurahia moto kwa muda mrefu kidogo kabla niende nyumbani kupata kiamshakinywa.

Nilipokuwa nimeketi nikitazama ndani ya moto Bwana akaninenea, “Hivyo ndivyo kanisa lilivyo. Ni kama kuutunza moto. Huwezi kuufanya moto uwake. Unaweza tu kuyaweka masharti ya moto kuwaka, halafu ukizimika, waweza kuuwakisha tena unapouhitaji. Huwezi leta moto wa Roho wangu, lakini unaweza saidia kutayarisha jukwaa la kuja kwake. Ningetaka wewe ufurahie uangalizi wa kanisa. Lile unahitajika kufanya ni kuwa tayari kuyachochea makaa na kuweka kuni zaidi. Moto unachomeka kwa hiari yake wenyewe. Hii ndiyo kazi ya mzee.”

TABIA ZA WAZEE Katika Matendo 20:28-30 Paulo anawahutubia wazee wote wa Efeso. Anasema: Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalifu ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe. Najua mimi ya kuwa baada ya kuondoka kwangu mbwa mwitu wakali wataingia kwenu, wasilihurumie kundi, tena katika ninyi wenyewe watainuka watu wakisema mapotovu, wawavute hao wawaandamie wao. Hii inaonyesha wazi kuwa mzee ndiye askofu na ndiye mchungaji. Wote hawa ni mtu yule MMOJA! Tabia za mzee zimeorodheshwa mahali pawili katika Agano Jipya: Katika 2 Timotheo na Tito.

Ni neno la kuaminiwa; mtu akitaka kazi ya askofu, atamani kazi njema. Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika , mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji ajuaye kufundisha; si mtu wa kuzoelea ulevi, si mpiga watu; bali awe mpole; si mtu wa kujadiliana, wala asiwe mwenye kupenda fedha; mwenye kuisimamia nyumba yake mwenyewe, ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu; (yaani, asiyejua kuisimamia nyumba yake mwenyewe atalitunzaje Kanisa la Mungu?) Wala asiwe mtu aliyeongoka karibu, asije akajivuna akaanguka katika hukumu ya Ibilisi. Tena imempasa kushuhudiwa mema na watu walio nje; ili asianguke katika lawama na mtego wa Ibilisi. (1 Timotheo 3:1-7) Kwa sababu hii nalikuacha Krete, ili uyatengeneze yaliyopunguka, na kuweka wazee katika kila mji kama vile nilivyokuamuru; ikiwa mtu hakushitakiwa neno, naye ni mume wa mke mmoja, ana watoto waaminio, wasioshitakiwa kuwa ni wafisadi wala wasiotii. Maana imempasa askofu awe mtu asiyeshitakiwa neno, kwa kuwa ni wakili wa Mungu; asiwe mtu wa kujipendeza nafsi yake, asiwe mwepesi wa hasira, asiwe mlevi wala mgomvi, asiwe mpenda mapato ya aibu; bali awe mkaribishaji, mpenda mema, mwenye kiasi, mwenye haki, mtakatifu, mwenye kudhibiti nafsi yake; akilishika lile neno la imani vile vile kama alivyofundishwa, apate kuweza kuwaonya watu kwa mafundisho yenye uzima, na kuwashinda wenye kupinga.

Katika mafungu mawili hapa juu hakujatajwa kufaulu chuoni kuwa kanuni ya ofisi ya mzee. Tabia zote za muhimu za kiongozi

zinahusu kutembea kwa mwanaume na Yesu. Ndizo hizi hapa kwa orodha moja:

• Hana lawama. • mke mmoja. • mke mmoja • watoto waaminio watiifu • mkaribishaji. • mpenda mema. • anadhibiti nafsi yake. • Mtakatifu. • Mwenye nidhamu.

53

• Anayeweza kufundisha. • Mwenye kiasi. • Wakuheshimika. • Si mlevi. • Si wa hasira • Si mgomvi. • Si mpenda fedha. • Anaisimamia nyumba yake vyema. • Amekomaa kwa mambo ya Mungu. • Ana sifa nzuri.

Ndiyo hiyo! Kwa urahisi hizi ndizo tabia za mwanamume wa kiroho; mwanamume aliyewekwa wakfu kikamilifu kwa ajili ya

Kristo. Sababu inayotufanya tuwapitishie viongozi wetu katika mafundisho magumu kama haya kwenye nyanja tofauti tofauti za

maarifa ni kwa sababu tumesonga mbali toka kwa urahisi na kuingia kwa matatizo. Kanisa sio tena mkusanyiko rahisi wa waaumini kwa ajili ya kujengana na kuabudu kwa faida ya wote. Ni biashara kubwa sana!

Lakini Mungu anatwita turudi kwa urahisi. Na pia anatwita tuwatambue wanaume na wanawake kwamba ambo anawaleta kwenye uongozi. Ikiwa tutarahisisha wazo letu la kanisa, sisi wenyewe bila kusaidiwa tutarahisisha masharti yetu ya uongozi.

Gurudumu au Mzabibu?

Fikiria kuhusu gurudumu, ikiwa kwenye nchi na taruma zikielekea pande zote toka kwa kitovu cha gurudumu. Sasa, fikiria kuhusu mzabibu unakua kwenye nchi ukipeleka matawi yake pande zote, ukipenyeza mizizi chini hatua kwa hatua, kwa kila hatua ukizalisha mmea mwingine kama tu mzabibu wenyewe ukiwa na uwezo wa kutoa matawi ambayo yatapeleka mizizi chini hatua kwa hatua.

Gani kati ya hizi mbili za juu inawakilisha mkakati wa Upanzi Lowesha wa Kanisa, gurudumu au mzabibu? Sio swali la ipi inafanya kazi. Zote zinafanya kazi lakini moja ni shirika na ingine ni hai. Makanisa mengine yanatumia wazo la gurudumu na mengine yameanza kuona hekima ya wazo la mzabibu la upanzi wa kanisa.

GURUDUMU Wazo la gurudumu linataka makanisa changa zote zifungiwe kwa karibu na kutegemea kanisa mama. Kwa kawaida haziitwi

kanisa. Zinaonekana kama upanuzi wa kanisa mama. Watu wote kwenye kanisa hizi ndogo hukutana kati ya wiki ili waweze hudhuria kanisa mama siku ya Jumapili. Mafungu yote ya kumi na matoleo yanaelekezwa katika kanisa mama na viongozi wa makanisa ndogo hawatambuliwi kama wachungaji. Toka wakati kwa wakati moja wapo ya hizi kanisa ndogo inaachiliwa kuwa kanisa kamili, halisi na likiwa na mchungaji aliyechaguliwa. Hili, kwa maana ya ndani, ni wazo la gurudumu. Limefaulu sana kwenye mahali na kuzalisha makutano wakubwa sana.

MZABIBU

Wazo la upanzi kanisa la mzabibu laweza kuonyeshwa kutumia spider plant. Spider plant una matawi marefu, yenye madaha, na rangi nyingi yakifanana mti aina ya weeping willow mdogo. Toka kwa matawi inakuwa mizabibu ambayo inazaa spider plant ndogo hatua kwa hatua kando kando mwa mzabibu. Hawa buibui wadogo hawawezi wahi kua wakubwa kama mti mama kwa sababu, kuliko mti mama ambao una mizizi yake imezamishwa kwenye mchanga, buibui watoto wanaachwa wakining’inia hewani na wanatoa uhai wao kwa mmea mama. Ikiwa huu mti mrembo unao ning’inia unaweza teremshwa toka mahali pake pa kuning’inia na upandwe aridhini, kila moja wa hii mimea buibui ndogo itaanza kupeleka mizizi yake kwenye mchanga. Wakati hili litatendeka, kila moja wapo ya hii mimea ndogo inaanza kukua na kuweka mizizi yake yenyewe chini aridhini na kutoa mizabibu pande zote, ikizaa mimea buibui refu, komavu na isiyo na idadi. Wacha Bwana atupe maono ya upanzi wa kanisa ambao utaruhusu uhuru kabisa wa uhai wa kanisa kujielezea wenyewe!

• Gurudumu huelekea kujivutia ndani yake yenyewe; mzabibu huelekea kujiachilia nje. • Gurudumu huelekea kuwa wa mahali; mzabibu huelekea kuwa wa kupitia mahali pengi. • Gurudumu huelekea kuongeza; mzabibu huelekea kuzidisha. • Gurudumu huelekea kujenga kanisa moja; mzabibu huelekea kujenga makanisa mengi. • Gurudumu huelekea kuyazuia maono ya kiutume; mzabibu huelekea kuyaendeleza maono ya kiutume. • Gurudumu huzunguka jamii; mzabibu huuzunguka ulimwengu. • Gurudumu huwafundisha viongozi wa kundi; mzabibu humfundisha kila mtu. • Gurudumu huwazia makundi dogo; mzabibu huwazia makanisa yakutanayo nyumbani.

Wacha Bwana wa mavuno atupe maono ya upanzi wa kanisa ambayo yataruhusu uhuru kamili wa maisha ya kanisa ujieleze wenyewe bila vizuizi!

Hatua Moja Kuelekea Umoja

Mtu aweza uliza, “Lakini je, hizi kanisa zote ndogo za nyumbani zikitapanyika kote mjini haziwezi sababisha mgawanyiko na

utengano katika Mwili wa Kristo tunapokuja kwa umoja?” Makanisa ndogo hazisababishi mgawanyiko kuliko yale makubwa. Makanisa makubwa na madogo kabisa yana changamoto hili hili ikija kwa umoja.

54

UMOJA WA KISHIRIKA AU UMOJA WA KIROHO?

“Lakini je, kuna tofauti gani kati ya umoja wa kiroho na umoja wa kishirika?” Sisi sote ni washiriki wa Mwili mmoja, kwa hivyo, tu wamoja, kiroho. Huenda mimi mshiriki wa shirika lenu, bali ukiwa wa Yesu, wewe ni wangu na mimi ni wako, kwa sababu wote walio wa Baba na Mwana ni wa watoto wote wa Mungu kila mahali. Sisi ni vyungo vya mwili wake na mifupa yake na sisi ni vyungo mmoja na mwingine.

MJI MMOJA—KANISA MOJA

Paulo hakuwahi andikia makanisa ya mji wowote. Kila wakati aliliandikia “kanisa” la mji halisi. Kuna tu kanisa moja kwenye kila mji au mahali. Analiandikia “kanisa” kwenye mji wa Roma, Korintho, Efeso, n.k. Bali anayaandikia “makanisa” kwenye Galatia, “makanisa kwenye Asia” n.k kwa sababu hii ilikuwa mikoa wala sio miji.

Kuna tu kanisa moja kwenye kila mahali, hata kama huenda kukaweko na kadhaa au hata mamia ya “makanisa” ambayo hukutana katika Jina la Yesu katika mahali hapo—mikutano hiyo midogo sana ambayo inalifanya kanisa kwenye mji huo. Jinsi tu vile makanisa yote kwenye miji yote katika ulimwengu yanaufanya mwili wa Kristo—Kanisa kote Ulimwenguni—ndivyo makanisa yote (makutano) katika mahali huufanya kanisa kwenye mji huo.

DUMISHA UMOJA

Kwenye Waefeso 4:3-6 tunasoma, “Na kujitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha imani. Mwili mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu. Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja. Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote, aliye juu ya wote, aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote.”

Kwenye fungu hili Paulo hakusema, “Imarisha umoja wa Roho.” Alisema, “Hifadhi umoja wa Roho,” kana kwamba kilikuwa kitu ambacho tayari kimeimarishwa. Anasema hapa kana kwamba umoja ulikuwa kitu kinacho kuja tu chenyewe kama sehemu ya furushi.

Tunazaliwa tena mara ya pili katika umoja kwa sababu, “Kuna Mwili Mmoja, Roho Mmoja, Bwana Mmoja, Baba Mmoja, Mungu Mmoja.” Sehemu yetu tu ni kukubali kwamba tayari tu kitu kimoja. Kutimiliza amri ya kuhifadhi umoja wa Roho kwa pingu za amani ni kudumisha kitu ambacho tayari tu nacho, kwa kuwa huwezi dumisha kile hauna. Huu umoja haumo kwenye miundo ya nje. Pia hauzaliwi katika vifungo vya nje wala haudumishwi na vifungo vya nje. Unazaliwa kwenye Roho na kwenye moyo. Ni hali ya ndani. Ni hali ya kuwatazama watu…watu wa Mungu.

UMOJA NA TOFAUTI

Twaweza kuwa na utofauti tunaotaka kuwa nao kama mashirika, dini, na mashirika husika na bado tuwe na umoja kwenye Roho. Hatushikiliwi pamoja na “desturi ya ushirika”. Tunashikiliwa pamoja na “umoja wa Roho katika kifungo cha amani.” Kwa upande mwingine mwaweza kuwa na shirika kuu sana ambalo ni pamoja na kila Mkristo hapa duniani na bado tuwe na umoja wa kweli kwenye Roho, hata kama una umoja wa kishirika.

Kifungo kwenye Waefeso 3:4-6 inaongea juu ya kitu ambacho kinatufunganisha pamoja, kama kamba au mshipi. Hicho kifungo ni “amani”. Kinyume cha amani ni vita au ugomvi. Ikiwa una hali ya upendo na ukubalifu kwa ndugu na dada zako kwenye makanisa mengine, “unahifadhi umoja” nao. Hauutengenezi. Unauweka hai kwenye roho yako mwenyewe, na hapo ndipo kuna amani, kwenye moyo. Inajitokeza yenyewe kwa njia mbalimbali, lakini inakaa kwenye roho kwa njia ya Roho Mtakatifu. Kinyume, ikiwa una hali ua ugomvi, migawanyiko, au utengano, wewe haudumishi umoja wa Roho kupitia kifungo cha amani.

HATUA KUELEKEA NDANI

Hatua moja kuelekea amani, basi, na kuna tu moja, inapatikana kwenye Warumi 14:1 na 15:7, “Yeye aliye dhaifu wa imani, mkaribisheni, walakini msimhukumu mawazo yake…Mkaribishane ninyi kwa ninyi, kama naye Kristo alivyotukaribisha…” Neno “karibisha” lina maana “karibisha, kumbatia, pokea, kubali ukoo, kiri na tangaza kweli kuwa tu kitu kimoja kwa sababu kupitia kuzaliwa upya sisi sote tumezaliwa kwenye jamii ya kiroho.

CHUKUA HATUA HII SASA

Hii hatua moja kuelekea amani yaweza chukuliwa papo hapo ulipo wakati huu. Waweza mgeukia Bwana sasa hivi na kuomba: Baba, katika Jina la Yesu Kristo Bwana Wangu, ninakubali kwamba mimi ni mshiriki wa mwili wako wa kiroho, kanisa hapa mjini na kote ulimwenguni. Ninamkubali na kumpokea kila mmoja wa watoto wako kama ndugu au dada kwa vile wewe ndiwe Baba Yetu. Haijalishi wanaishi wapi. Haijalishi wao ni rangi gani, imani au matendo walio nayo, kama wao ni wa baada ya, au kabla ya milenia. Haijalishi ikiwa wanabatiza kwa kumiminia au kuzamisha, kama ni Waarminia au Wakalvini. Haijalishi ikiwa wanaenda kanisa Jumamosi, Jumapili, Jumatatu au Jumanne, kama ni Wakatoliki, Waprotestanti, Waodhoksi au Wayunani. Sijali wakiwa Wabaptisti, Wamethodotisti, Wapresbiteri au Miraba Minne. Ninatangaza sasa hivi na kuamuru katika Jina la Yesu Kristo Bwana, Mwana wa Mungu Mkuu, kwamba mimi ni mmoja na kila mwamini aliyezaliwa tena mara ya pili aishiye, ambaye ameishi au atawahiishi kwa wakati na milele. Nitawakubali. Nitawapokea. Nitawapenda na kuwasaidia. Nitawaombea na jinsi utakavyonielekeza, Bwana, nitakuwa mtenda kazi-mweza wao, na nitajitahidi kuuweka umoja huu wa Roho kupitia kifungo cha amani. Amina!

Unapoomba ombi hili la juu kwa uaminifu, umekwishaichukuwa hatua moja kuelekea amani. “Lakini je, itakuwaje umoja wa

kimafundisho? Tutatembeaje pamoja isipokuwa tukubaliane? Mungu hatuelekezi sisi sote kutembea kwa njia moja. Tunaambiwa katika Waefeso 4:12 kwamba tuhifadhi huu umoja wa Roho “Hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani.” Twaweza kuwa na umoja wa kiroho wakati tunaingia ndani ya umoja wa kidhehebu.

UKWELI MMOJA WA KATI

Kuna tu ukweli mmoja wa kati ambao unasunguka kutangaza sisi sote umoja wetu na huo ukweli sio mafundisho au wazo au kanuni au dini. Sio kanisa au dhehebu au mshindo. Huo Ukweli ni mtu. Yesu ndiye huo Ukweli. Alisema, “Mimi ndimi Njia, Ukweli, na Uzima.” Tunapomjilia, anatupa uzima. Tunazaliwa tena! Wakati yule mlinda gereza Mfilipi aliwauliza Paulo na Sila,

55

“Mabwana zangu, nifanye nini nipate kuokoka?” jibu halikuwa, “Amini mafundisho yetu na ujiunge na shirika letu”. Lilikuwa, “Mwamini huyu Bwana Yesu Kristo na utaokoka.” Tunamwamini mtu na tunazaliwa tena katika ufalme wa nuru. Tunapounganishwa kwa Yesu tunaunganishwa mmoja na mwingine. Tu wamoja katika Yeye. Yeye aliye na Yesu ana uzima. Yeye asiye na Yesu hana uzima. Tunaokolewa, si kwa kushika mahali pa mafundisho, bali ni kwa kumpokea Yesu Kristo mwenyewe.

POKEANENI MMOJA NA MWINGINE.

Katika kila kanisa, iwe kanisa ya nyumbani au kanisa ya kidesturi, ni lazima tumkubali kila mwamini mwingine kama mshiriki kama vyungo vya Mwili mmoja bila kuangalia uanachama wake. Wakati mwingine Mungu aweza tuongoza kushirikiana kwa miradi mikubwa zaidi, lakini onyesho kubwa zaidi la umoja ni kukubali na kuthibitisha mmoja na mwingine kwa yale tayari tunafanya kwa pande mbalimbali katika mahali mbalimbali.

VIONGOZI WENGI—JESHI MOJA

Sisi sote tu vitani na kuna majemedari jemedari, luteni, kapiteni, askari wengi, lakini kuna Mkuu mmoja, Komanda Mkuu, Yesu Kristo mwenyewe. Alisema, “Nitalijenga kanisa langu. Na hilo ndilo analifanya. Hebu tumpe nafasi kulijenga kanisa lake. Anasimamia kila jamii ndogo ya jeshi lake. Twaweza kuwa kwenye vitengo mbalimbali, jamii mbalimbali, au upande mbambali, lakini bado tungali jeshi moja, watu wamoja, tukipigana vita vimoja dhidi ya ufalme wa giza. Acha tudhibitishe na kusaidiana mmoja na mwingine katika mahali petu mbalimbali pa huduma bila kufikiria kuwa tumetengana tu kwa sababu sote hatumo katika mahali pamoja tukifanya mambo mamoja kwa wakati mmoja chini ya bendera moja.

MAKABILA MENGI—TAIFA MOJA

Kulikuwa na kabila kumi na mbili katika Israeli, kila moja likiwa na jimbo lake, uzao, viongozi na bendera. Lakini walikuwa bado watu wamoja, Waisraeli. Twaweza kuwa mamia, au hata maelfu ya madhehebu, mashirika, na makanisa, lakini sisi tu watu wamoja, watu wa Mungu, Waisraeli wa Mungu. Sio lazima tuwe pamoja kimwili tukifanya mambo chini ya bendera moja ndio tuwe wamoja. Tayari tu wamoja kwa hivyo wacha tutangaze umoja wetu kwa ujasiri na tufanye kazi yetu kuusongesha ufalme wake tukithibitisha, kukubali na kupokeana mmoja na mwingine. Hii ndiyo “kuifadhi umoja wa Roho pitia kifungo cha amani.”

Je, mnafanya nini kwenye Kanisa Ndani Ya Nyumba?

Kuna umuhimu kuwa Paulo wala Yesu mwenyewe hawakutoa maagizo halisi kwetu kuhusu jinsi ya kile tunapaswa kufanya wakati tunakutana kama kanisa. Maneno ya Yesu yalikuwa rahisi sana kwenye Mathayo 18:20, “Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu nami nipo papo hapo katikati yao.” Hakusema wangekuwa wakifanya vitu fulani ili yeye awe katikati yao, wakusanyike tu kwa jina lake.

Mtume Paulo alitupa ufunuo mdogo katika asilia ya mikutano ya kanisa la kwanza kwenye Wakorintho wa Kwanza:

Basi, ndugu, imekuwaje? Mkutanapo pamoja, kila mmoja ana zaburi, ana fundisho, ana ufunuo, ana lugha, ana tafsiri. Mambo yote na yatendeke kwa kusudi la kujenga. (1 Wakorintho 14:26).

Mikutano ya kanisa kwenye siku hizo haikutilia mkazo mnenaji. Ulikuwa mkutano wazi ambamo kila mtu alichangia kwa faida

ya mwili mzima. Zoezi la karama za kiroho lilitiwa moyo ili kwamba wote walibarikiwa na kujengeka. Tunaweza bugabuga toka kitabu cha Matendo na nyaraka baadhi ya sehemu muhimu za mikutano ya kanisa. Sehemu zifuatazo zinafafanua baadhi ya mambo ambayo ni ya muhimu kuyaangalia tunapokuja pamoja.

SIFA NA OMBI Kila wakati ni vyema kuanza kila mkutano na muda mrefu wa sifa na ibada pamoja na maombi ya kujitolea. Wakati mwingine

hili litafanywa tu kati ya nafsi yetu na Mungu, lakini wakati mwingine atasisitiza tuombe kwa sauti ili wote wajengeke. Waimbaji ni sehemu ya nyongeza kwa wakati wa sifa, lakini sio wa umuhimu mkubwa kabisa. Baadhi ya sifa ambazo zinaweza kuwa za nguvu zaidi zinaweza toka bila vyombo vyovyote au muziki wowote wa kutoka nyuma. Kumwimbia tu Bwana toka rohoni bila vyombo ni sifa na ibada safi. Tumefikia mahali nyakati hizi zetu ambapo tunasifu sifa zetu na tunaabudu ibada zetu. Ikiwa sifa na ibada zetu hasijavuma sana kwa kiwango cha juu, tunahisi kuwa hatujaingia patakatifu pa patakatifu. Hatufanyi hivyo kwa kujifurahisha wenyewe, bali kwa Bwana, na anatosheka kabisa na sifa bora zitoke kwa moyo mwaminifu. Kutakuweko na nyakati ambazo Roho Mtakatifu atakuongoza usifanye jambo lolote lingine zaidi ya kumsifu Bwana. Uwe wazi kwa uongozi wake. Mambo yote yanatiririka toka kwa maombi, sifa na ibada.

KUSHIRIKI Kuna wakati wa kushiriki karama za huduma kulingana na 1 Wakorintho 14:26. Katika mkutano ulio wazi kiongozi anaelekeza

na kulitia moyo kundi kushiriki shuhuda, maisha, hoja za maombi, fundisho fupi, funuo, ripoti za sifa, n.k. Mwe waangalifu kwamba watu wasio na kiasi wasitawale wakati wa kushiriki. Wavutie walio wanyemavu kwa kuuliza maswali. Wakati mwingine inapasa kuhimiza mwanzoni mwa kushiriki kwamba wale wanyemavu wajitokeze na kuuondoa kuogopa kwao wanadamu na kutoa neno la ushuhuda kwa Bwana. Pia inahitajika kuwatia moyo wale wanaonena sana kutulia ili kuwapa nafasi wengine kuongea.

KOMNYO

Wacha mtu aelezee baadhi ya sehemu za maana ya Komnyo na halafu wacha wandugu na dada washiriki mwili na damu ya Bwana wetu kwa ufahamu na imani. Huu pia ndio wakati wa kujichunguza wenyewe na kutubu dhambi zozote ambazo Bwana huenda akatufunulia tunapoendelea kumngojea. Ni wakati mwema kutoa mwaliko kwa wote wasiomjua Kristo kuomba na

56

kumpokea kabla hatuja pakua mkate na kikombe. Wengi wako tayari kumpokea Yesu iwapo tu tutatoa maelezo mafupi ya injili na kuuongoza mkutano kwa ombi la kumpokea Kristo. Wengi huongozwa kwa Kristo jinsi hii. Wale wampokeao Kristo kama Mwokozi wanapaswa kuupokea ubatizo wa maji mara moja. Mfano wa kanisa la kwanza kwenye kitabu cha Matendo ulikuwa wakati wote ni kuwabatiza waokofu wapya siku hiyo waliompokea Yesu.

HUDUMA Kuwa wazi kuhudumiana mmoja na mwingine pitia huduma ya unabii, kuwekea mikono, kuwaombea wagonjwa, kuwafungua

wale ambao wamefungwa na pepo wa kuwaangaisha, hudumia ujazo wa Roho Mtakatifu, n.k. Wacha karama zote za Roho zitiririke bila pingamizi kwa ajili ya kuwajenga wote kulingana na 1 Wakorintho 14. Kuwa na uangalifu msimwache “muhuduma mkuu” asitawale wakati huu.

JADILI SOMO LA BIBLIA

Mtu analeta somo fupi toka kwa Neno la Mungu. Hili laweza tolewa na mtu yeyote kulingana na 1 Wakorintho 14:26. Kwa kawaida huu sio “ujumbe” mrefu. Kwa sababu ya mfumo wa kanisa ulio wazi, Roho Mtakatifu anafundisha kote kwenye huduma kutumia watu tofauti tofauti wanaoshiriki. Kwa karne ambazo zimepita, wakati wa “ujumbe” au mafundisho umekuwa ukipanuka zaidi na zaidi karibu kuondoa ushirika wa kundi. Hili limepelekea kuwa na ibada aina ya watazamaji ambamo mtu mmoja anatumia karama zake bali wengine wanatama na kusikiza na kupokea (na wakati mwingine kulala). Mfumo wa Kanisa Ndani Ya Nyumba unaelekea kurekebisha hili kosa na kuchochea karama za mwili mzima kwa kujijenga wenyewe. Roho Mtakatifu ataongoza kwenye kila mkutano kwa maswala halisi. Usiufanye ratiba.

Sehemu muhimu za Kanisa Ndani Ya Nyumba, au kanisa lolote kwa swala hilo, ni sifa, ibada, ombi, ushirika, kufundisha Neno la Mungu, kuhimiza kuachilia karama za Roho Mtakatifu, ubatizo wa maji, ubatizo wa Roho Mtakatifu, Meza ya Bwana, uinjilisti, na huduma binafsi mmoja kwa mwingine. Haya ndiyo baadhi ya mambo ambayo Yesu alikuwa akinena juu yake aliposema, “mwafundishe kushika mambo yote yale nimewaamurisha ninyi, na, tazama, nitakuwa pamoja nanyi hadi mwisho wa dahari.”

Jinsi ya Kuanzisha Kanisa la Nyumbani

Tunapouliza swali, “Je, unaanza aje kanisa la nyumbani?” huwa kwa kweli tunauliza swali, “Ni jinsi gani ya kuanzisha kanisa?” Hakuna neno kama “kanisa la nyumbani” lilitumiwa katika Agano Jipya. Inasema, “Wape salaamu zangu Nifa na kanisa lililopo nyumbani kwake.” Haisemi, “…kanisa la nyumbani lililopo nyumbani kwake.” Kanisa likutanapo nyumbani ni kanisa!

NJIA SALAMA NA ZUNGUKA K

Tunafikiria kuanza kanisa na tunatetemeka! Tunaona hii kama kazi kubwa sana kwa sababu tunafikiria kwa njia ya makanisa makubwa. Tunamsifu Bwana kwa makanisa yote makubwa ambayo yanamwiinua Yesu kama Mwokozi, lakini katika mji wa wastani 50% ya watu haihudhurii kanisa lolote. Bado kuna nafasi ya makanisa mengine mengi katika kila mji ulimwenguni, yote makubwa na madogo. Tuna soko kuu kabisa katika kila mji, lakini pia tuna maduka madogo ya kutufaa. Yote yanafanya kazi moja. Yanauza vyakula.

Soko kuu hazitoshelezi kabisa mahitaji ya watu kuliko vile makanisa makubwa yanakutana na mahitaji yote ya watu. Kanisa za nyumbani hazishindani na zile kubwa. Ni mwungano katika vita dhidi ya ufalme wa giza.

CHOMOA MIZINGA!

Nitakuwa kila wakati nikikumbuka yale rafiki yangu, Hobert Vann, alisema alipokuwa akisimulia aliyopitia wakati wa Vita Vikuu vya Pili Vya Dunia. Vita vilikuwa vinamalizika na Miungano ilikuwa inaifungua Ufaransa na Italia toka uvaamizi wa Wajerumani. Kwa kuukaribia mji, wangepeleka mizinga yao hadi mahali palipo inuka pakiangalia mji. Punde mzinga mwingine ungekuja kando na wao na mwingine na mwingine mpaka kukawa na mizinga ya nguvu aina hiyo kadhaa zikiwa tayari kuuvamia mji. Hobert alisema, “Bob, hata mara moja sikuwahi ondoa komeo la mzinga wetu na kupungia mizinga ile mingine yote nikizifukuza nikisema, “Hey, ninnyi wenzangu, endeni mbali na hapa! Hapa ni mahali petu pa mashindano! Tutautwaa huu mji bila msaada wenu! Acha kuingilia sehemu yetu! Tunaweza twaa hii sisi wenyewe!” Tulifurahi kuwa hatukwenda kuutwaa huo mji peke yetu. Kila moja ya ile mizinga ilikuwa ya kupendeza! Mgurumo wa injini zao ilikuwa nyimbo kwa masikio yetu! Tungelifurahia tungekuwa na maradufu ya hiyo mizinga yetu!” Kwa namna hiyo hiyo, hakuna mmoja wetu anaweza sema, “Hey ninyi wenzetu msianzishe kanisa lingine katika mji huu! Sisi tayari tunamfikia kila mtu humu mjini!” Njia ya upesi zaidi ya kuufanyia mji uinjilisti ni kuanzisha makanisa mapya, basi kwa nini nifadhaishwe ikiwa mtu anaanzisha kanisa lingine, liwe kanisa likutanalo nyumbani au hekaluni?

UPANZI LOWESHA WA KANISA NA KANISA LA NYUMBANI

Ikiwa tunaenda kulowesha miji na mataifa kwa makanisa itatubidi tuanze kufikiria namna ya kuanzisha makanisa katika nyumba. Ukuaji upesi zaidi wa kanisa katika historia unafanyika Uchina kupitia upanzi lowesha wa kanisa ukielekezwa na Roho Mtakatifu. Hii si kubahatisha bali ni tendo la kweli na linasimama kama ushuhuda kwa kanisa kote ulimwenguni kama uwezo wa upanzi mkubwa zaidi wa kanisa.

KUANZISHA KANISA KATIKA NYUMBA…

Sehemu zifuatazo zinawakilisha maswala ya kuangalia katika kuanzisha kanisa ndani ya nyumba. Waweza tekeleza baadhi yazo au zote. Jambo muhimu ni kufanya yale Roho Mtakatifu anakwambia ufanye katika hali yako halisi.

OMBA NA UWAFANYE WENGINE PIA KUOMBA

57

Kifunguo cha kufaulu katika ufalme wa Mungu ni maombi. Lakini haitoshi tu kuomba. Watafute wengine pia kuomba nawe. Tafuta mtu mwingine aonaye haya maono uombe naye ili Mungu awaonyeshe mwelekeo wa jinsi ya kuendelea.

FANYA KAZI NA MTUME, NABII, MWINJILISTI, MCHUNGAJI NA MWALIMU.

Katika Matendo 8:1 na 11:19-21 tunasoma: Siku ile kukatukia adha kuu ya kanisa lililokuwa katika Yerusalemu; wote wakatawanyika katika nchi ya Uyahudi na Samaria, isipokuwa

hao mitume…basi wale waliotawanyika kwa sababu ya ile dhiki iliyotukia kwa habari ya Stefano, wakasafiri hata Foinike na Kipro an Antiokia, wasilihubiri lile neno ila kwa Wayahudi peke yao. Lakini baadhi ya hao walikuwa watu wa Kipro na Krene, nao walipofika Antiokia wakasema na Wayahudi wa Kiyunani, wakihubiri habari njema za Bwana Yesu. Mkono wa Bwana ukawa pamoja nao, watu wengi wakaamini wakamwelekea Bwana.

Habari hizo za watu hao zikafika masikioni mwa kanisa lililokuwako katika Yerusalemu; wakamtuma Barnaba aende hata Antiokia. Naye alipokwisha kufika na kuona neema ya Mungu akafurahi, akawasihi wote waambatane na Bwana kwa kusudi la moyo. Maana alikuwa mtu mwema amejaa Roho Mtakatifu na imani; watu wengi wakaongezeka upande wa Bwana. Kisha akatoka akaenda Tarso kutafuta Saulo, hata alipokwisha kumwona akamleta Antiokia. Ikiwa kwa muda wa mwaka mzima wakakusanyika pamoja na kanisa na kuwafundisha watu wengi. Na wanafunzi waliitwa Wakristo kwanza hapo Antiokia.

Hawakuwa mitume ndio waliopanda kanisa katika mji wa Antiokia. Walikuwa Wakristo waliotawanyika kwa ajili ya mateso

ndio walioanzisha kanisa katika mji huo. Mitume waliwatuma Barnaba pamoja baadaye kusaidia kuisimamisha na kuitia nguvu. Mtetemo huu wa ajabu wa kanisa la nyumbani kule Uchina unaonyesha kuwa mtu yeyote anayempenda na anamtumikia Bwana aweza anzisha kanisa. Lakini twahitaji uangalizi wa kitume na karama zote ili hili kanisa ambalo limetajwa katika Waefeso likamilike ili liweze kujihudumia lenyewe na liweze kukua hata kwa kimo kamili.

Baba, tuonyeshe sisi jinsi ya kulitia kanisa nguvu. Tusaidie sisi kama wachungaji na viongozi tusidhibiti, tusivute kwa hila, au kulinyonga kanisa. Tuwezeshe sisi kuliweka kanisa huru ili liwe vile uliliumba liwe!

KUWA NA CHAKULA CHEPESI NA MMALIZIE NA KOMNYO.

Hakuna njia moja ya uhakika ya kukutana. Mikutano mingine itapeanwa kimsingi kwa ajili ya sifa na ibada, mingine maombi, mingine ushuhuda wa uzuri wa Mungu kwetu sisi, mingine kwa ajili ya somo la Biblia, mingine kwa ajili ya kuwahudumia wengine, mingine kwa ajili ya mafundisho, n.k. Hata hivyo, yote haya kwa umuhimu wa kuindeleza Injili ya Kristo ndipo kwa sababu tunasherehekea hiyo komnyo ya mkate na divai mara kwa mara. Tunatoa umuhimu wa kwanza kwa maridhio.

Tungekuwa wenye hekima kusherehekea mwili huu uliovunjika na damu iliyomwagika ya Yesu kila wakati tukutanapo. Waombe watu kadhaa kushiriki maana ya meza ya Bwana kabla ya kuila. Acha mtu alete funzo fupi juu ya maana ya Meza ya Bwana. Ni nafasi bora zaidi ya kuwaongoza watu kwa Bwana.

ANZA WACHACHE

“Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.” (Mathayo 18:20). Maneno “kusanyika pamoja” yaweza tafsiriwa.”

Inachukuwa tu wawili au watatu kuufanya mkutano kulingana huu mstari. Mkutano wa watu ambao wanalibeba Jina la Yesu, na Yesu katikati yao, ni KANISA! Ombea ukuaji uje, lakini msife moyo ikiwa kanisa ni dogo. Litakua na kwa wakati mtawatuma nje mume na mke wawili au watatu kuanzisha mkutano mwingine katika sehemu nyingine ya mji au katika mji mwingine ulioko karibu.

KUWA MTENDAJI KATIKA MAKANISA KADHAA YA NYUMBANI.

Mtu aweza kuhusika katika kanisa za nyumbani kadhaa kwa wakati. Baadhi ya watakatifu wanayaona haya na wanajihisi huru kujipanua kuufikia Mwili wa Kristo kusaidia zaidi ya mahali pamoja. Mchungaji mmoja anaweza kuangalia kanisa kadhaa za nyumbani.

KUWA HURU KUKUTANA POPOTE WAKATI WOWOTE

Kutana Jumapili asubuhi au Jumamosi usiku. Kusanyikeni katika nyumba ile ile kila wakati au kutaneni katika nyumba mbalimbali mara kwa mara. Kuwa na mikutano mirefu au mifupi. Inakubalika kufanya kambi ya nje kwa pamoja na kuwa na mkutano kama sehemu ya kwenda nje. Kanisa ni watu kukusanyika katika Jina la Yesu. Sio ibada.

USITENGENEZE ORODHA YA WASHIRIKI Kwa sababu zilizotolewa hapo juu, usiwafanye watu wengine washiriki na wengine wasio-washiriki. Hawatawahi kuwa kondo

wako kwa vyovyote vile. Wote ni mali ya Yesu ikiwa wamezaliwa mara ya pili. Ikiwa hawajazaliwa mara ya pili, basi utakuwa na heshima kuu ya kuwaongoza kwa Bwana. Hadi hapo, wamekaribishwa kuhudhuria mikutano yetu kama mtu mwingine yeyote.

WAPOKEE WOTE WAJAO

Wengine watakuja kwa kanisa lako la nyumbani ambao ni washiriki wakuorodheswa wa ushirika mwingine. Kwa kuwa hatuna orodha ya washiriki, hakuna tatizo. Hatujaribu kumwondoa mtu yeyote toka kwa kitu chochote ambacho Bwana anawaambia wafanye. Pia hatutawaambia kuwa hawawezi kuja mikutanoni mwetu. Inatupasa kuwapokea wote watujiao jinsi tu vile kanisa lolote mjini lapaswa kuwapokea wote wajao mikutanoni mwao.

USIANDIKE KATIBA NA SHERIA ZA CHAMA.

Agano Jipya ndilo katiba yetu na sheria za chama chetu. Inatosha kabisa. Hatuhitaji kutengeneza maandiko mengine ya kutupa mwelekeo kama kanisa. Kanisa la Agano Jipya lapaswa kuchukua mwelekeo toka kwa kurasa za Agano Jipya chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu. Makanisa mengi yanachagua kufanya kazi nje ya mipaka ya mashirika yasio-ya-kibiashara na kidini kwa sababu mbalimbali. Acha Bwana akuongoze katika swala hili. Faida pekee ambayo hali ya jimbo ya wasiopata faida hupata ni kutokatwa ushuru kwa mapato yetu kwa matoleo tunayolipa kanisa. Siku yaja ambayo tutamtolea Bwana na tusitarajie kurudishiwa chochote

58

siku ya ushuru. Hatuko kinyume na kupata faida ya kutolipa ushuru. Itumie iwapo Bwana anakupa amani juu yake. Huenda siku yaja mbayo ubaya wa “kusajiliwa” kama shirika la kidini lisilopata faida utashinda faida yake.

USILITUPIE MAWE KANISA LA KAWAIDA

Sisi ni sehemu ya kanisa la kawaida kwa sababu tu sehemu ya kanisa la mjini. Matatizo ya kanisa ni matatizo yetu kwa sababu sisi ndio kanisa. Acha tusianguke kwenye mtego ambamo Wakristo wa Kwanza katika kanisa la Korintho walitumbukia. Katika 1 Wakorintho Paulo anasema:

Basi ndugu zangu, nawasihi, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba nyote munene mamoja. Wala pasiwe kwenu faraka, bali mhitimu katika nia moja na shauri moja. Kwa maana, ndugu zangu, nimearifiwa habari zenu na wale walio wa nyumbani mwa Kloe, ya kwamba iko fitina kwenu. Basi, maana yangu ni hii, ya kwamba kila mtu wa kwenu kusema, Mimi ni wa Paulo, na, Mimi ni wa Apolo, na, Mimi ni wa Kefa, na, Mimi ni wa Kristo. Je, Kristo amegawanyika? Je! Paulo alisulubiwa kwa ajili yenu? Au je! Mlibatizwa kwa jina la Paulo?

Wengine waweza sema, “Itakuwa vibaya kusema, ‘Mimi ni wa Paulo, au Mimi ni wa Apolo au Mimi ni wa Kloe”, lakini

itakuwaje vibaya kusema, “Mimi ni wa Kristo?” Ingekuwa vibaya kusema, ‘Mimi ni wa Kristo’ wakati unamaanisha, “Mimi si mmoja wenu kwa sababu mimi ni wa Kristo.’ Hii inatokana na roho ya faraka. Kwa hivyo ni vibaya kusema, “Mimi ni wa mshindo wa kanisa la nyumbani. Mimi si wa kanisa la kawaida.” Huyo ni roho mbaya atokanayo na akili ya sisi na wao. Tu wamoja iwapo tuna Mwokozi na Baba mmoja wa Mbinguni! Kwa hivyo ni lazima tufikiri na kunema ili tukumbatie umoja wetu bali sio kuukana.

KUTANA KAMA KAWAIDA

Ninaamini katika kanisa lisilo rasmi kama wale wanafunzi wawili walikuwa nalo njiani Emau wakati Yesu alitokea kati yao kighafula. Tunayo mikutano mingi ya kanisa kuliko vile tunafikiri kwa sababu ya huu muda usio rasmi na waamini wengine, lakini iwapo tunaenda kufanya upanzi wa kanisa, tunahitaji kuchagua wakati wa kawaida wa mikutano. Bwana anaweza kukuongoza ubadili wakati na mahali mara kwa mara, lakini inapasa kuweko na ukawaida kwa hii mikutano.

KWA NINI TUKUTANE?

Kwa wengi, kanisa limekuwa kazi ya kawaida; jambo linalotupasa kufanya, na tunafurahia wakati limemalizika kwa juma lingine.

Mbona tukutane? Hili ni swali halali na linastahili jibu lililofikiriwa vyema. Waebrania 10:24-25 inatwambia kwamba tusiache kukusanyika pamoja kama ilivyo desturi ya wengine, bali tuonyane; na

kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku hiyo kuwa inakaribia. Inatupasa tukusanyike pamoja iwapo tunataka kuhimizana kwa ajili ya siku zijazo. Si lazima liwe kusanyiko kubwa ili tupokee yale tunahitaji na tuyapokeze yote tunahitaji kupokeza. Wawezakuwa mkusanyiko mdogo wa wawili au watatu na nguvu za kanisa zitashika na sisi sote tutasaidika na kubarikiwa. Tusitafute kuwa wachache, bali ni lazima turidhike iwapo tu wachache.

Mbona tukutane? Umoja ni chanzo cha nguvu. Ndugu mmoja zaidi anawezaongeza nguvu zangu kwa asili 100%. Katika ulimwengu wa kiroho, ni lazima twende kama timu. Sote tuna sehemu ambazo hatuwezi kujiona. Njia pekee ya kutembea kwa usalama ni kwa wingi. Ndio, kweli twahitaji mmoja na mwingine! “Mmoja atafukuza elfu na wawili watafukuza elf kumi.”

Mbona tukutane? Yesu alitufia wewe na mimi binafsi, lakini kuna mahali pengi katika Biblia ambapo tunasoma kwamba alilifilia kanisa. “Kama Kristo naye alivyolipenda kanisa, akajitoa kwa ajili yake.” (Waefeso 5:25). Je, twaweza sema tunampenda Yesu ikiwa hatupendi yale anayapenda? Ni lazima tulipende kanisa, kwa kuwa Yesu analipenda kanisa. Ikiwa tunaona ukumu kujihusisha na kanisa lenye utaratibu, kanisa la ushirika, kanisa la kawaida, kanisa la kidhehebu, kanisa la kitatizo, kanisa lenye sura mbaya, kumbuka tu kuwa Yesu bado anajihusisha nalo na aliahidi kuwa hatawahi kuliwacha wala kulipungukia. Tuna mtazamo ule ule juu ya kanisa (lote) kama vile Bwana wetu alivyo.

Mbona tukutane? Kukutana na “Yesu katikati.” Alisema, “Kwa kuwa panapo wawili watatu ambao wamekusanyika kwa jina langu, mimi nipo papo hapo katikati yao.” Hayupo “katikati yangu.” Anakaa “ndani mwangu.” Yupo tu katikati mwa wawili au watatu au zaidi yetu tunapokutana katika jina lake.

Haya ni maarifa tofauti kabisa kuliko ya Yesu aliye ndani. Kuna mambo fulani ambavyo vinaweza tu kutendeka wakati Yesu yu katikati, na ikiwa hatukusanyiki kamwe kwa jina lake, hayatawahi kutendeka.

Mbano tukutane? Kunayo ahadi halisi kuwa “Ikiwa wawili wenu watakubaliana juu ya kitu chochote wataomba, na watapewa na baba yangu wa mbinguni.” Twaweza kuiona hiyo ahadi ikitimizwa tunapokutana na angaa Mkristo mwingine mmoja.

Mbona tukutane? Kula komnyo takatifu katika ushirika wa wengine vile neno lake linatufunulia. Yesu alisema, “Mle huu mkate na mnywe kikombe hiki kwa ukumbusho wangu.” Yeye anakumbukwa katika uwepo wa watu wake. Hata ikiwa si makosa kukinywa kikombe na mkate kwa ajili ya Bwana, mfano tulio nayo pekee katika Agano Jipya ni kwamba waliikula katika ushirika na watakatifu wengine.

Mbona tukutane? Mtume Yakobo anatwambia sisi kuwa tunapaswa “kukiri dhambi zetu mmoja na mwingine na twombeane mmoja na mwingine ili tuweze kupona.” Twaona maneno haya “mmoja na mwingine” yakitokea tena na tena pote kwenye Agano Jipya. Hatuna njia tunayoweza epuka hatima ya wazi kwamba sisi tu kiungo cha mwili.

Mbona tukutane? Kulitukuza jina la Yesu tunapo abudu na kulisifu jina lake pamoja! Mbona tukutane? Kuufuata mfano wa kanisa la kwanza ambao walikutana kila siku toka nyumba hadi nyumba na mahali pa

hadhara. Kwa kufanya hivi, waliujaza mji wa Yerusalemu na mafundisho ya Kristo. Mbona tukutane? Kuuruhusu mwili uuhudumie mwili. Hizi ndizo baadhi ya sababu za sisi kukusanyika pamoja katika jina la Yesu. Mitetemo ya uamusho ambayo inaendelea kunawiri

katika ulimwengu hivi leo ni mahali ambapo watu wa Mungu hukusanyika kila siku au angaa kila mara. Mikusanyiko ya Jumapili haikuwa ndiyo desturi katika kanisa la kwanza na sio desturi mahali ambapo mioto ya uamusho hulipuka hivi leo. Ikiwa Mungu anatembea katikati mwetu katika nguvu, hatutakuwa na tatizo kukutana kila siku.

59

MSIOGOPE KULIITA KANISA Pote katika Agano Jipya tunapata maneno mengi ambayo yanatumika mahali pa neno ‘kanisa,” kama wanafunzi, watakatifu,

mikutano, waamini, n.k. Kutakuweko na nyakati ambazo tutaiita mikutano yetu kanisa na nyakati zingine tutaiita ushirika, mikusanyiko, mikutano. Lakini tukikusanyika katika Jina la Yesu, tunafahamu ni kanisa ambalo ni Mwili wake.

JISALIMISHE KWA MAMLAKA YA KIROHO

Sisi sote tunawajibika kujisalimisha kwa mamlaka ya kiroho ambayo yameteuliwa na Mungu popote tukutanapo nayo. Wakati mwingine huwasikia wachungaji wakisema, “Yeye ni mtume wetu.” Nawakumbusha kwamba hili si neno la kiimaandiko au wazo la kibiblia. Mtume ni mtume kokote aendako na mchungaji ni mchungaji kokote aendako. Lakini mtume, nabii, mwinjilisti, au mwalimu hawezifanya kazi ambako hajakubalika na kuheshimiwa. Mchungaji vile vile hawezifanya ambako hajapokelewa.

Mungu hutupa watu fulani walio karibu sana nasi kuliko wengine, lakini hatupaswi kumkataa yeyote ambaye Bwana ametutumia. Sisi ni washiriki mmoja na mwingine, kwa hivyo sisi sote tunawajibika kulinda mmoja na mwingine kwa kiwango chochote ambacho maisha yetu yanagusana. Tunapaswa kulikumbatia kanisa la kote mjini, lakini sisi pia tu mali ya kanisa ulimwenguni kote. Sitashirikiana na ndugu ambaye anaishi mjini kwangu kwa njia tofauti kuliko vile nitashirikiana na ndugu au dada toka Uchina au Korea. Sisi sote tu mwili mmoja!

TUMIA MJADALA WA FUNZO LA BIBLIA Miaka kadhaa iliyopita Bwana alituonyesha aina ya funzo la Biblia ambalo lilikuwa rahisi sana, la kutoka moyoni,

lisiloelekezwa, na lisilo la michafuko. Nauita Mjadala Wa Funzo la Biblia (MFB). Kutumia aina hii ya funzo la Biblia hauhitaji mwalimu au vitabu vya kufundisha Biblia. Unalohitaji tu ni Biblia na watu wachache wanaohitaji kufahamu Biblia ni nini. Ikiwa kuna mmoja aliye na karama ya kufundisha, mwache ashiriki kama mwanafunzi na sio kama mwalimu. Ni ushirika wa kikundi wala sio aina ya wasilisho la mkufunzi.

Msingi wa aina hii ya funzo la Biblia unapatikana katika Wakolosai. Waraka huu ukiisha kusomwa kwenu fanyeni kwamba usomwe katika kanisa la Walaodikia pia; na ule wa Laodikia usomwe na ninyi. (Wakolosai 4:16) Katika (MFB), kwa urahisi, tunasoma maandiko, kila mmoja akichukua zamu kusoma mistari michache, kutegemea ni watu

wangapi waliopo. Wakati yanasomwa, kila mtu anaalikwa kutafsiri kwa wakati wowote na kusema au kuuliza swali. Huo ni mjadala wa funzo la Biblia. Ujaribu! Utaupenda!

Ujaribu nyumbani katika ushirika wako wa kifamilia. Utashangaa na jinsi mazungumzo mengi yatachipuka na jinsi mtajifunza mkilisoma Neno la Mungu kwa pamoja.

Hata hivyo, wakati mwingine mwaweza soma mafungu marefu bila mjadala wowote hata kidogo. Acheni tu Neno liwahudumie. Msijaribu kulazimu mazungumzo. Mara tu mazungumzo yanapoaanza tatizo huwa ni jinsi mtarejea kwa kusoma. Kazi ya kiongozi ni kuendelea kusoma na kujadili, sio tu mojawapo ya hili au lile lingine.

Hamtahitaji kufafanua moja hadi lingine. Lissome tu. Inashangaza ni kiwango tunaweza jifunza Biblia kwa kuisoma! Inanikumbusha mkutano tulioufanya miaka kadhaa iliyopita. Tulikuwa tumemwalika mwalimu wa biblia aliyejulikana sana awe mnenaji wetu. Wakati wa chakula cha mchana nikamwuliza atupe vidokezo kuhusu jinsi ya kujifunza biblia. Alitabasamu na kusema, “Kweli, nitafurahia kuwapa.”

Baada ya chakula cha mchana alisimama na kusema, “Ndugu Fitts ameniuliza niwape vidokezo juu ya kuingia katika mafunzo ya Biblia na basi ndivyo hivi hapa: mna kalamu zenu na kartasi? Kunazo tatu. Cha kwanza ni, SOMA BIBLIA!, cha pili ni, SOMA BIBLIA!! Na cha tatu ni, SOMA BIBLIA!!! Kila mtu alicheka. Yeye hakucheka. Alimaanisha kazi. Hakuwa anafanya mzaha. Tukaacha kucheka. Sote tukapokea maana ya hicho kidokezo. Akaendelea kuelezea umuhimu wa kuisoma tu Biblia bila wazo lolote la “kujifundisha” Biblia. Sijawahi sahau hili somo la nguvu. Waamini wengi hawajawahi isoma Biblia mara moja.

Paulo alimwonya Timotheo, “Hata nitakapokuja, ufanye bidii katika kusoma [Maandiko hadharani] na kuonya na kufundisha. (1 Timotheo 4:13). Tunayasikia mahubiri mengi sana, lakini sio mengi kuhusu kuyasoma maandiko hadharani. Mjadala wa Funzo la Biblia ndilo hilo. Ni usomaji wa Maandiko hadharani. Mahubiri na mafundisho zina nafasi zao, bali MFB ni ya utendano wa kundi.

Biblia iliandikiwa watu wote, watu wa kawaida. Hivi majuzi swali lilinijia akilini mwangu, “Je, waandishi wa Agano Jipya walizielekeza nyaraka zao kwa wachungaji na viongozi au ziliandikiwa watu wenyewe?” Mara moja nikasoma utangulizi wa kila nyaraka alizoandika Paulo kupata jibu kwa hilo swali. Nilishangaa. Nilidhani baadhi yazo zingeelekezewa viongozi wa kanisa, lakini yale nilivumbua yalikuwa ya kushtua! Tulikuwa tu tumeshapokea omba la dharura toka Urusi la hitaji la vitabu vya mafunzo ya Biblia kwa mamia ya makanisa ya nyumbani yaliyokuwa yakifanywa huko. “Mbona vitabu?” Niliwaza. “Tayari wana kitabu rahisi, chenye nguvu zaidi, kibadilishacho maisha kote ulimwenguni, Biblia!” Agano Jipya liliandikiwa watu wote. Tazama yale niliyapata niliposoma tangulizi za Paulo kwa nyaraka zake zote:

Paulo, mtumwa wa Kristo Yesu…kwa wote walioko Rumi, wapendwao na Mungu, walioitwa kuwa watakatifu. (Warumi) Paulo, aliyeitwa kuwa mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu…kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, wale waliotakaswa katika Kristo Yesu, walioitwa wawe watakatifu…(1 Wakorintho). Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu…Kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, pamoja na watakatifu wote walioko katika nchi yote ya Akaya. (2 Wakorintho). Paulo, mtume…kwa makanisa ya Galatia. (Wagalatia). Paulo, mtume…kwa watakatifu walioko Efeso, wanaomwamini Kristo Yesu: (Waefeso).

60

Paulo na Timotheo…kwa watakatifu wote katika Kristo Yesu walioko Filipi pamoja na maaskofu na mashemasi. (Wafilipi, Tazama: Huu ndio waraka pekee unaowataja viongozi wa kanisa, lakini bado hata huu waraka umeandikiwa watakatifu wote, ambao, kama kawaida ni pamoja na wazee na mashemasi.). Paulo, mtume…kwa ndugu watakatifu waaminifu katika Kristo, walioko Kolosai. (Wakolosai). Paulo, Silwano, na Timotheo, kwa kanisa (watu wa Mungu) la Wathesalonike, lililoko katika Mungu Baba, na katika Bwana Yesu Kristo: (1 na 2 Wathesalonike).

Niligundua kuwa kila waraka uliandikiwa watu wa Mungu na sio kundi la “makarani” wasomi ambao walikuwa wafafanue

maana ya hizi nyaraka kwa watu. Nyaraka hizi zilikuwa zisomewe watu na hilo lilionyesha kuwa wangeelewa yaliyomo kwenye hizi nyaraka. Kama kawaida hakuna makosa kufafanua mafungu magumu, lakini Roho Mtakatifu anaweza na ataweza kufunua maana ya neno lake kwa watu wake kupitia watu wake.

Mafunzo ya Biblia ya kikundi, hasa, MFB, ni njia bora zaidi yakuruhusu mwili kuuhudumia mwili.

UKUHANI WA MWAMINI. Maneno yafuatayo ya mtume, Paulo, yanaonyesha kuwa Agano Jipya liliandikiwa watu wote, Wakristo wa kawaida. Sisi tu

“Ukuhani Mkuu” na hatutegemei kuhani “halisi” kuielewa Biblia. “Ambalo nimefanywa mhudumu wake, sawasawa na uwakili wa Mungu, niliyopewa kwa faida yenu, nilitimize neno la Mungu; Siri ile iliyofichwa tangu zamani zote na tangu vizazi vyote, bali sasa imefunuliwa kwa watakatifu wake; ambao Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri wa utukufu wa siri hii katika Mataifa, nao ni Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu. (Wakolosai 1:25-27). Paulo aliweza kutoa neno la Mungu moja kwa moja kwa watu, hata siri za ndani, kwa sababu hizi siri sasa zimefunguliwa

(funuliwa) kwa watakatifu. Paulo alifahamu maandishi yake yangeeleweka na Wakristo wa kawaida ingawa Petro alisema kuwa mambo mengine aliyoyaandika Paulo yalikuwa magumu kueleweka.

Haya mufungu pamoja na mengine yanaonyesha dhahiri kuwa sio tu salama bali kuna tendo la kuwa na kundi la waamini wote, wa kawaida kuja pamoja kwa ajili ya kujifundisha Biblia wakiwa bila kitu kingine isipokuwa Biblia. Hakuna mafafanuzi, hakuna majarida ya kila miezi mitatu, hakuna “wastadi” juu ya Biblia, hakuna wachungaji, au walimu. Inaonekana hatari? Ingia hatarini! Paulo aliingia, na yawezekana akawa ndiye bingwa wa upanzi wa kanisa wa dahari zote!

FAIDA YA MJADALA WA FUNZO LA BIBLIA

(1) Unaweka mkutano bila desturi. Unaamsha karama ya uongozi, lakini kusiwe na mmoja anachukua nafasi ya “stadi” wa maarifa ya Biblia.

(2) Katika nchi nyingi kutakuwa na nakala za Agano Jipya au angaa vipande vyake vinaweza patikana kwa watu. Kitu bora cha mafunzo ya Biblia ni Biblia yenyewe.

(3) MFB inaondoa wazo kuwa tunahitaji kitabu kingine kufafanua maana ya Biblia. Neno la Mungu linajitetea lenyewe! (4) MFB inaepuka na gharama ya kunua vitabu. Katika mataifa maskini sana ambayo ndio yanaanza tu kufunguka kwa injili, kama

vile uliokuwa Muungano wa Kisovieti, hili litakuwa la msaada mkubwa sana kutokuubeba mzigo wa kuchapisha au kununua nyenzo za mafunzo ya Biblia.

(5) Kutumia mbinu rahisi ya MFB itafanya uanzilishi wa makanisa ya nyumbani uwe rahisi. Rahisi ndiyo bora. (6) MFB inatufanya tutegemee Roho Mtakatifu kuyafahamu yale tusomayo. Mchongeleo wa kikundi unatoa usawa na nguvu. Kile

mtu mmoja hataweza ona, mtu mwingine ataona. Ikiwa kundi litaenda kando, Mungu ataonyesha hilo, pia (Tazama Wafilipi 3:15).

(7) MFB litasisitiza kurejelea Biblia yenyewe. Hii itaifunua Biblia kwa kila mhusika. Wakristo wengi hawayafahamu yaliyomo kwenye Biblia. Wamesikia na kusoma mengi kuhusu Biblia, lakini ni nadra wao wenyewe kuingia katika Biblia yenyewe.

JINSI YA KUWA NA MJADALA WA FUNZO LA BIBLIA

(1) Anza na ombi kuwa wote wataadilika. (2) Sio lazima wote wawe na Biblia. Moja yaweza pitishwa kwa wote wakisoma. (3) Chagua kiongozi lakini sio mwalimu. (4) Soma kwa mferingo. Waambie wale wasiotaka kusoma waipitishe kwa mtu anayefuata. (5) Soma bila kujaribu kuamusha mjadala. (6) Karibisha kukatiza kuruhusu maneno au maswali. (7) Kaa kwenye mwelekeo. Jadili fungu lisomwalo. (8) Usiache mtu mmoja kutawala mjadala. (9) Kuwa makini kuhusu wakati wa kuhitimisha. (10) Malizia na kipindi cha maombi na sifa.

Jumla ya yote ambayo tumesema kuhusu Mjadala wa Funzo la Biblia in kwamba ni rahisi; ni salama; na inaendeshana na maono ya kuuleta mwili wa Kristo katika kazi ya kujiadilisha wenyewe. Mtume Petro alisema, “Kila mmoja kwa kadiri alivyoipokea karama, itumieni kwa kuhudumiana; kama mawakili wema waneema mbalimbali za Mungu.”

PANGA NA UOMBE KWA AJILI YA “MPASUKO WA KANISA.”

Mojawapo ya machungu ambayo mtu aweza pitia ni mtindo wa zamani wa “mpasuko wa kanisa”. Ni uchungu tu iwapo hautarajii mmoja utokee. Ikiwa tutaweka mipasuko ya mara ya kanisa kwenye matayarisho yetu na katika maombi yetu, halafu wakati moja unapotokea, tunafurahia kwa utukufu na kila mmoja anabarikiwa. Kila kanisa la nyumbani huzaliwa “na mimba.” Haya ndiyo maono yetu tangia siku ya kwanza kabisa kuwa tutalizaa “kanisa mtoto.” Matayarisho yetu si kujenga, kununua, au

61

kupangisha jengo ambalo litawashikilia watu wengi. Tukishakua wengi hata kutotoshea kwenye nyumba ya wastani, tutazituma nje familia mbili au tatu kuanzisha kanisa jipya la nyumbani mahali pengine. Maono ya Upanzi Lowesha wa Kanisa ni kuwa na uwepo wa Kristo katika kila ujirani mdogo katika kila mji katika kila nchi katika ulimwengu. Tuna imani kuwa Wito Mkuu wa Bwana Yesu Kristo unaweza, kwa maana ya kawaida, kutimilizwa.

KUMBATIA KANISA KOTE MJINI.

Usiandike jina kwenye kanisa lako. Hili laweza kuwa kifaa cha adui cha kugawanya. Kila mtu anataka kujua wewe ni “aina ipi” ya Mkristo. Usiwahukumu wale watumiao majina bali ikiwa utaepuka na kuupa ushirika wako jina, utaona busara iliyomo katika hili. Kuita jina ni kutaja. Kutaja ni kwanzisha dhehebu. Fikiria juu ya hili. Je, ni hili ndilo unataka? Usiiwekee jina zaidi ya lile tunalipata katika Agano Jipya… “kanisa linalokutana katika nyumba ya Prisika na Akila.” Kumbuka, kila kitu ambacho ni Yesu ni changu na ikiwa wewe ni wa Yesu wewe ni wangu na mimi ni wako. Hili pia linatumika kwa makanisa. Mimi ni mshiriki wa kila kanisa la Yesu na ikiwa wewe ni kiungo cha Mwili wa Kristo, wewe pia ni mshiriki wa kila kanisa. Inakubalika kuwatembelea baadhi ya ndugu na dada zako ambao wanahudhuria makanisa mengine isipokuwa huenda wasikubaliane nawe kwa vipengee vyote vya mafundisho. Wewe pia wawezakuwa hauko sahihi kwa vipengee vyote vya mafundisho!

Maswali na Majibu

Maswali yafuatayo ni maswali yaulizwayo sana juu ya makanisa ya nyumbani:

Swali 1: Mbona makanisa ya nyumbani? Jibu 1: Tunapanda makanisa ya nyumbani kwa sababu zifuatazo: Lengo letu sio tu kuanza kanisa. Lengo letu ni kuanza mtetemo wa upanzi wa kanisa. Tunaamini hili lawezafanywa vyema zaidi kwa kuelekeza macho yetu juu ya mbinu rahisi na ya uzalishaji zaidi ya upanzi wa kanisa. Kanisa la nyumbani linatimiza hitaji hili.

Tunaamini wazo la kanisa la nyumbani ndiyo njia bora zaidi ya kuwafundisha wachungaji na viongozi. Urahisi wa makutano wadogo unafanya rahisi uzidishaji wa makutano. Mungu anawaita watu wake kuachana na udini na ufundi na turudie urahisi. Katika nchi nyingi hivi leo hii ndio njia pekee ya kupata mtetemo wa upanzi wa kanisa kwendelea. Huenda isiwezekane tufanye

upanzi lowesha wa kanisa ikiwa tunafikiria kwa njia ya kanisa la desturi. Ndio mazingira bora zaidi ya kuutia nguvu Mwili kuuhudumia Mwili.

Swali 2: Je, kanisa ya nyumbani ni sawa na kundi dogo la ushirika wa nyumbani? Jibu 2: Wazo la kundi dogo ni chongeleo la gurudumu na kanisa la nyumbani ni chongeleo la mzabibu. Kundi dogo linaonekana kama kufikia watu wa nje kwa kanisa lingine bali kanisa la nyumbani ni kanisa lenyewe na linafanya kazi kama kanisa, likifanya mambo yote ambayo makanisa hufanya, pamoja na ubatizo, kumega komnyo, kuoanisha, kuzikana, n.k. Swali 3: Je, unawezaje kuendelesa ratiba kamili ya kanisa katika kanisa la nyumbani? Jibu 3: Tunaamini kuwa ikiwa tutayaweka macho yetu juu ya mambo tuliyoyataja katika Sura 6, Je, Unafanya Nini Katika Kanisa la Nyumbani?, Bwana atatuwezesha kukutana na mahitaji ya watu na familia binafsi wanaohudhuria. Roho Mtakatifu anaweza tufanya tuwe watu wakuanzisha mambo mapya katika kuchongelea mahitaji. Wengine watahitaji kuhudhuria makanisa na uwezo wa kuwakilisha mipango mbalimbali. Hatumo mashindanoni na makanisa mengine. Tunafanya kazi pamoja nao kusaidia kutimiliza Wito Mkuu. Swali 4: Na watoto je? Watakuwa na madarasa halisi? Jibu 4: Baadhi ya makanisa ya nyumbani yatakuwa na mikutano ya watoto kando na ya watu wazima. Wengine watakutana wote pamoja. Inashangaza namna watoto hujifunza mengi kwa kuwa tu na wanarika na watu wazima. Kila kanisa litamtafuta Bwana kwa jinsi ya kukutana na mahitaji ya wale waliopo hapo. Swali 5: Je, ni mara ngapi kanisa la nyumbani linakutana? Jibu 5: Mara moja au mbili kwa wiki ni kawaida, lakini huu ni uamuzi wa kufanywa na watu wa kila kanisa. Hakuna jambo katika biblia lisemalo ni mara ngapi tunafaa kukutana. Swali 6: Je, mnakutana kwa nyumba moja kila wakati? Jibu 6: Tumefungamanishwa pamoja na pingu za uhusiano na si kwa mahali pa kukutana basi hivyo ni salama kutembeatembea. Swali 7: Je, utawatoa wapi wachungaji kuwaongoza hawa makutano? Jibu 7: Tabia za kweli za wazee (wachungaji) zinapatikana mahali pawili katika Agano Jipya: Tito 1:6-9 na 1 Timotheo 5:1-7. Mungu ametoa wanaume na wanawake wengi sana wanyenyekevu, wakufundishwa, wamchao Mungu hapo katika makanisa yetu ambao wana uwezo wa kuongoza makanisa ya nyumbani. Mbinu ya uanafunzi ndiyo bora zaidi ya kuwafundisha wachungaji na viongozi. Hakukuwahi kuwa na hakutawahi kuwa mbinu bora zaidi! Swali 8: Je, kanisa la nyumbani lawezaji kuzalisha kanisa lingine la nyumbani? Jibu 8: Hii ni sehemu ya mafundisho ya mzee. Amepewa jimbo na kazi ya kuanzisha kanisa jipya la nyumbani. Katika wingi wa hali hizi atapewa angaa mume na mke wawili kumsaidia kuanza; wazo njema, mmoja ya hawa mume na mke watakuwa wachungaji-mafundishoni ili tokea mwanzoni mwa kanisa jipya kuna maono ya upanzi wa kanisa. Kanisa ndogo sana la nyumbani laweza kuwatuma mke na mume wawili au watatu kila mwaka kuzalisha kanisa jipya.

62

Swali 9: Je, wew unapendekeza kuwa makanisa yote yawe makanisa ya nyumbani? Jibu 9: Si kusudio letu kuharibu chochote ambacho Mungu anajenga. Sisi tumeahidi kubariki na kusaidia makanisa yote ndani ya kila mji, kubwa au ndogo, la ki-dhehebu, lisilo la ki-dhehebu, au upatano wa ki-dhehebu. Kwa urahisi tunawakilisha thibitisho la kanisa ambalo lina msingi kwa neno la Mungu na hili limethibitika kuwa na nguvu kwa makanisa yote mawili ya zamani na ya siku hizi. Mungu hawaiti watu wake wote mahali pote kufanya kimoja na kile kingine. Kanisa la Yesu Kristo linashangaza jinsi lilivyo la kutiririka na hodari katika kujidhihirisha kwa njia zake nyingi wakati halijafungamanishwa na mipaka ngumu na isiyobindika. Swali10. Je, makanisa ya nyumbani yawe ya madhehebu? Jibu 10: Kwanza na mbele ya yote, kila kanisa ya nyumbani katika kila mji ni mali ya kanisa, mwili wa Kristo, katika mji ule. Kanisa la nyumbani laweza kuwa mali ya dhehebu, lakini kushikana kwake na dhehebu hakufai kuhitilafiana na ahadi na uhusiano wake kwa mwili wa Kristo ndani ya mahali pale. Changa moto kuu kwa kanisa lolote ni kudumisha umoja katika mwili mkubwa wa Kristo katika mji ambao unaishi.

Kunayo maswali mengine mengi ambayo mtu awezauliza juu ya makanisa ya nyumbani, lakini la muhumu zaidi ni hili: “Bwana, unataka mimi niwe sehemu ya kusaidia kutimiliza Wito Mkuu kwa kuhusika katika kuzidisha makanisa ya nyumbani katika nchi yangu na kote ulimwenguni?”

Kuna njia nyingi za kupanda makanisa mapya na kwa hiyo kuupanua ufalme wa Mungu duniani. Tutazikubali na sio kuzishtumu mbinu ambazo watu wa Mungu wanatafuta ili kuyapanda makanisa. Ni makusudio yangu katika haya maandishi kuipiga tarumbeta ya kuanzisha makanisa ya nyumbani, na tunakwambia wewe usomaye kitabu hiki, “njoo huku na utusaidie sisi!”

Tunasisimuka juu ya uzidishaji wa makanisa katika kila nchi na katika kila kundi la watu ili “toba na ondoleo la dhambi litahubiriwa kwa Jina lake kwa mataifa yote.”

MUHTASARI Ni imani yangu dhabiti kuwa katika kizazi chetu, kutakuwa na mtetemo wa kanisa la nyumbani katika kila nchi duniani.

Ninaamini hii ndiyo njia pekee tutakayoweza kuona timilizi la Wito Mkuu katika kizazi hiki, au kwa wakati wowote baada ya hapa. Tayari I njiani yaja. Mungu ananena Kanisa ndani ya Nyumba kwa watu kila mahali. Kazi ya kundi imewekwa tayari kwa zaidi ya miaka 25 iliyopita kupitia yale yametendeka kote ulimwenguni katika makubaliano makubwa ya mtetemo wa kundi dogo.

Si kitambo sana kulikuwa na maswali mengi sana kuanzisha kundi la nyumbani la aina yoyote nje ya majengo ya kanisa yenyewe kwa kuogopa kuwa lingewavuta watu mbali na toka kwa “kanisa”. Sasa haya makundi yanaonekana kuwa yakutamanika sana kama njia ya ukuaji wa kanisa.

Lakini Mungu anatwita tuchukue hatua mbele na kutambua kwamba kweli twaweza kuwa na kanisa, katika ukamilifu wa hili neno, katika nyumba.

Baadhi ya makutano makubwa zaidi ulimwenguni hivi leo yalikuwa na mwanzo wao katika nyumba. Ilikujaaje ikawa kanisa? Je, ilikuwa kanisa wakati ilikuwa na watu kumi na walikutana nyumbani? Au ilikuwa wakati ilikuwa na watu elfu moja na walikutana kwenye jengo lililoumbwa hasa liitwalo “kanisa?” Jibu ni wazi. Lilikuwa kanisa lilipoanza katika nyumba na ikiwa lingeendelea kukutana katika nyumba, lingeendelea kuwa kanisa.

Mungu anakoroga na kutetemesha miundo ya kanisa letu la sasa na kuturudisha kwa misingi. Mengi ya yale tunayo sasa tukija kuyafikiria sio muhimu hata kidogo. Tukiutazama urahisi wa kanisa la Agano Jipya na kulilinganisha na kanisa la kawaida la hizi siku zetu tunaona uchache, ikiwa tunao, wakufanana hata kidogo. Katika nchi zingine kanisa linaonekana zaidi kama shirika. Madaraja za kidhehebu zinaundwa kwa mitandao mikubwa sana ambayo, kwa hali nyingi, inatawaliwa pamoja na safu za kisiasa kuliko kupitia kwa mamlaka ya kiroho yaliyoteuliwa na Mungu.

Heri Mungu atupe ufunuo, unyenyekevu, na neema ya kukubali jinsi vile tumekwenda kando toka kwa urahisi na usafi wa kanisa la Agano Jipya na tuurudie kwa kuvunjika na toba.

KUHUSU MWANDISHI

Robert Fitts alizaliwa na kulelewa kule Texas, na aliokoka akiwa na umri wa miaka kumi na mmoja katika hema ndogo kule Chester, Arkansas. Alipofikisha miaka 17, akaingia kwa maisha ya ahadi na ukuaji kwa harara ya uinjilisti wa ulimwengu.

Tangia hapo, Robert amepata maarifa ya zaidi ya miaka 50 katika huduma, akitumika kama mchungaji, mwalimu, mtume, mwinjilisti, mfanyikazi wa watoto na mwandishi. Mwaka wa 1970 alianzisha Outreach Fellowship International (OFI), utume wenye maono ya kufundisha na kutuma makundi ya kuwafikia watu katika nchi zingine kufanya mikutano ya kiinjilisti na kupanda makanisa. OFI inafanya kazi kwa karibu na mashirika mengine ya kitume kama International Crusades and Radio Evangelism, Youth With A Mission, United States Centre For World Mission, na DAWN Ministries kusaidia kutimiliza Wito Mkuu.

Robert anaishi Kona, Hawaii na mke wake Joni. Wana watoto saba na wajukuu kumi na watano. Waweza kuwasiliana na Robert au kupata nyenzo nyongeza pitia tovuti, pepe, simu, faksi au pepe hapa chini:

http://www.RobertFitts.com Robert Fitts Ministries 76-6309 Haku Place Kailua-Kona, HI 96740 Phone: 808-334-9682 Fax: 808-334-9673 e-mail: [email protected]

Watungaji Vitabu na Wakati Zilipoandikwa.

Allen, Roland Missionary Methods: St. Paul’s or Ours, Moody Press, Chicago, IL 1956. Banks, Robert Going to Church in the First Century, The SeedSowers, P.O. Box 3368, Auburn, ME 04212, 1980.

63

Banks, Robert Paul’s Idea of Community, Eerdmans, Grand Rapids, MI 49506, 1979. Broadbent, E.H. The Pilgrim Church, Pickering and Inglis Ltd., London, England, 1931. Brunner, Emil The Misunderstanding of the Church, Lutterworth Press, London, 1952. Clark, Steve Patters of Christian Community, Servant Books Coleman, Robert E. The Master Plan of Evangelism, Fleming H. Revell, Old Tappan, NJ 07675, 1963 Ellison, H.L. Household Church, Paternoster Press 1963. Girard, Robert C. Brethren Hang Loose, Zondervan, Grand Rapids, MI 49506. Hadway, Dubose, and Wright, Home Cell Groups and House Churches, Broadman Press, Nashville, TN, 1987. Hay, Alexander R. New Testament Order, New Testament Missionary Union, Audubon, NJ 1947. Krupp, Nate New Wine Skins, Preparing the Way Publishers, Salem, OR, 97306 First Swahili Edition December 2010. Translated by Patrick Wafula Wanyama of Languages Department Bahati Community Centre Secondary School P.O Box 1242-00100 G.P.O Nairobi, Kenya. All Enquiries: +254 721 991 413 [email protected]

64

HESABU YA KIROHO

Kama Wakristo, tunapigana dhidi ya adui wa kweli. Twaweza kuziita nguvu hizi kama “Shetani” lakini adui yetu ni jeshi nzima la viumbe walioanguka wamtumikiao Shetani na wanajaribu kufanya kazi katika desturi za ulimwengu kuwashawishi watu kutoka kwa Mungu na Ufalme wake. Mengi yaweza semwa kuhusu hii hoja ya vita vya kiroho, lakini nataka kuikatiza kwa kiasi. Sitaangazia sana kuvumbua urefu na undani wa hoja hii lakini nitashiriki yale yanahusu hii Orodha ya Kiroho, kwa vile inaweza kuwa kifaa hodari sana cha kuvunja ngome za Shetani na kuharibu kazi yake katika maisha yetu. Huu ndiyo ufunguo wa kupata uhuru katika Kristo na uzima tele ambao anaahidi—ambayo inahusu sana hoja hii ya upanuzi wa Ufalme.

Geukia Mwisho A na uangalie hoja iliyo juu ya Orodha ya Kiroho pamoja na mifano iliyoandikwa mle ndani. Utaona kuwa inasema, “Ukurasa wa Ngome na Sababu Zake” badala ya “Orodha ya Kiroho”. Katika safu na masanduku waweza ona marejeleo kwa dhambi za binafsi, ushiriki kwa ushetani, kudhulumiwa, mawazo ya Kishetani, na ngome za kiakili. Moja au yote haya yaweza kuwa yale Biblia inaita, “ngome” ambazo Shetani hutumia kutuzuia kujisalimisha kikamilifu kwake Mungu na kupata maisha katika Roho na uhuru toka kwenye dhambi. Mtume Paulo anarejelea ngome za kiroho katika 2 Wakorintho 10:3-5:

Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili; (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;) tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo.

Waweza kuona hapa rejeleo kwa vita ambavyo vinapiganwa kati ya majeshi yanayopingana ya Mungu na Shetani, na waweza

ona kwamba twapaswa kujiami kiroho kupigana vita hivyo. Hata hivyo, kunazo ngome (ambazo ni uwongo) ambazo adui anazitumia kimikakati kupata nafasi na kudumisha mafao yake. Kupitia Yesu Kristo, twaweza shika mawazo yetu mateka, tutembee katika kweli, na kuyaharibu mafao ya adui.

Kabla uanze kuijaza orodha yako ya binafasi ya Orodha ya Kiroho (kartasi isiyoaandikwa chochote ipatikanayo katika Mwisho A), ni muhimu kuwa wewe uioshe njia hii katika maombi. Lazima uwe na uhakika kuwa nyumba yako ni “safi,” yaani, umepata toba ya kweli na matokeo ya kutamani kuishi katika utii wa amri za Kristo na kukua katika mfano Wake. Unahitaji pia kutia hati sahihi yako kwa hiyo “kartasi isiyoaandikwa chochote.” Salimisha yote kwa Mungu, onyesha mapenzi yako ya kutaka kumfuata popote Atakuongoza, na mruhusu Yeye kufanya kazi ndani yako kupitia hali ambazo zitakunyosha na kukutia adabu inapohitajika.

Muhimu zaidi, lazima uelewe kuwa mamlaka yakuharibu hizi ngome za Shetani hayatoki kwako wewe; si matokeo ya wema wako na si kitu ambacho unawezaongea dhidi yake kwa nguvu zako wewe mwenyewe. Ni lazima utumie nguvu za Jina la Yesu na Mamlaka Yake kunyakua nafasi yako ambayo Shetani amechukuwa katika maisha yako. Ni lazima usimame kidete na kutangaza uhuru wako toka kwa ngome na madhara yake yote; hii inaweza funga milango yote maishani mwako inayobaki wazi kwa adui. Kumbuka ule mfano uliotangulia: ikiwa utawacha milango wazi, adui ataingia ndani na aiweke miguu yake yenye tope kote kwenye nyumba ambayo imetakaswa na ambayo sasa ni yake Bwana Yesu Kristo.

Eneo ambalo unafaa kuangalia kwanza katika Orodha ya Kiroho ni dhambi zako binafsi. Utataka kuandika kwenye nafasi ya kwanza ya Ukurasa wa Kazi dhambi zozote zako binafsi ambazo umeng’ang’ana nazo, hasa dhambi za kitabia ambazo zinaonyesha ngome ya adui. Mwombe Mungu akufunulie mambo halisi kwako, na uhakikishe umepata mizizi ya sababu ya wewe kung’ang’ana kuliko kutaja dhambi inayotokana nayo. Waweza ona pale chini ya safu ya kwanza, kwamba lengo la orodha hii ni kukusaidia wewe kutubu hizi dhambi.

Sasa hebu tusonge kwenye safu ya katikati, Ushawishi wa Kishetani. Hii yaweza au isiweze kukuhusu wewe, lakini ushawishi wa Kishetani ni mlango wazi kwa adui. Yawezakuwa ni jarida ambalo linawasili katika hiyo barua ya posta ambayo ina mawazo yaliyo kinyume na Maandiko; yaweza kuwa mila za kitamaduni au uzalendo au ukabila. Ushawishi wa Kishetani waweza pia kuwa uchawi wa wazi au ushetani. Mawazo ya Dahari Mpya ni ushawishi wa Kishetani, vile ilivyo unajimu, aina fulani za madawa, pia na hata mitazamo fulani ya kilimwengu kama ubinadamu. Ni wazo nzuri kuondoa aina yoyote ya vitu vinavyoweza kuwa ngome, lakini pia unahitaji kutubu kuhusika kwokwote kwako katika ushetani ambako kwaweza kumpa Shetani ngome ya kuendelea kuingia katika maisha yako. Mambo yoyote ambayo umepitia maishani mwako ambayo yaweza kwendelea kualika ushiriki wa Shetani lazima yawekwe kwenye hiyo orodha. Waweza ona chini kwenye hiyo safu kuwa hizo ngome zote lazima uzikatae na mamlaka yaondolewe kwa Shetani katika Jina la Yesu. Katika safu ya tatu utaorodhesha dhuluma zozote ambazo Shetani hutumia kukushawishi wewe kutoka kwa Mungu na Ufalme Wake. Unaweza weka kuto-samehe—yakumbuke maneno ya Yesu katika Ujumbe wa Mlimani: “Samehe, nawe pia utasamehewa.” Dhuluma zaweza kujenga ngome kwa sababu zinatusababishia kutembea katika hasira au kuto-samehe. Pia, zinaweza kujenga ngome za akilini kama uwoga, kutokuwa na usawa wa kihisia, huzuni, n.k. Dhuluma ina nguvu za kutushika mateka kwa yaliyopita badala ya kutuachilia twende mbele na Kristo, katika imani. Baada ya kuomba juu ya haya na kuandika chini dhuluma zinazokuhusu ambazo ni ngome katika maisha yako, suluhisho ni kusiachilia.

Kwenye masanduku yaliyoko chini ya ukurasa huu, utaangalia tabia ya mtindo wako wa mawazo na njia za kuamini kukuhusu wewe mwenyewe na Mungu. Shetani anaitwa baba wa uwongo kwa sababu anatuongoza mbali kutoka kwa ukweli wa Mungu; huu uwongo unatufunga na waweza kutufanya tushindwe kufanya kazi na kuwa wazalishaji wa Ufalme. Basi, katika sanduku la kwanza, andika chini uwongo wowote kutoka kwa Shetani ambao umeamini kukuhusu wewe mwenyewe. Waweza ng’ang’ana na kujidharau; unapaswa kujikumbusha kuwa uliuumbwa kwa mfano wa Mungu, kwa makusudi Yake, na ya kwamba ana makusudi na mpango kwa maisha yako, hata kama yanaonekana ni madogo. Inakubidi uepukane na kujilinganisha wewe na wengine na ukumbuke kuwa wewe tu ni kiungo kimoja cha Mwili na kuwa viungo vyote ni halisi. Fikiria juu ya maisha yako mwenyewe na uandike chini uwongo ambao umeamini kukuhusu wewe mwenyewe. Halafu, soma, tafakari juu yake, na hata ukariri Maandiko ambayo yatakukumbusha ukweli wa Mungu na yakusaidie utembee katika ushindi.

Eneo la pili la ngome za mawazo ni dhana za uwongo ambazo umeamini kuhusu Mungu. Nimesikia ikisemwa kwamba kumwelewa kwetu Mungu kwaweza kushawishiwa sana na uhusiano wetu na baba zetu, kwa vile Mungu ni kama “kiwakilishi cha baba.” Na huku Mungu akiwa Mungu mtakatifu na anatarajia utiifu wetu, haondoi upendo wake kwetu wakati tunatenda dhambi. Anahusika sana na mwelekeo wetu kuliko ukamilifu wetu, bora tuwe tunaendelea kujikaza. Bado ninakuta kuwa ninahitaji kuyaweka

65

haya mawazo yanayopingana (haki Yake na utakatifu dhidi ya upendo Wake na Neema) kwenye usawa. Hapa ndipo, tena, kuwa katika Neno na kuwa na Maandiko ambayo yanakusaidia unaposhikwa kwenye ngome ya dhana moja au nyingine. Maombi ya Kupitia Orodha ya Kiroho

Baada ya kumaliza orodha ya kiroho, wazo bora ni kuishiriki na mtu aliye karibu nawe na ambaye amekomaa katika Bwana—mwezako wa kutoa hesabu yako, ikiwa utaweza. Yakobo 5:16 inasema, “Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa.” Pia, kuna nguvu tunapokutana katika jina la Kristo. Yesu alisema katika Mathayo 18:18-20,

“Amini, nawaambieni, yo yote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yo yote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni. Tena nawaambia, ya kwamba wawili watakapopatana duniani katika jambo lolote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye Mbinguni. Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.” Kuna jambo la nguvu katika kukubaliana pamoja kwetu katika maombi na kuungana katika Kristo. Kukiri kwetu kwa hiari, kukiambatanishwa na unyenyekevu ambao unaturuhusu kushiriki dhambi zetu na udhaifu wetu na

wengine, inatusaidia kusimama dhidi ya adui na uwongo wake wote. Shetani anataka sisi tuyafiche mambo yetu katika giza, bali Mungu anataka yawekwe kwenye nuru. Hapo tu ndipo twaweza kutakasika na kutembea katika ushindi. Na, tutakavyo jadili katika sura itakayofuata, kuimarisha uhusiano wa kutoleana hesabu sisi kwa sisi ni sehemu muhimu ya kukua katika neema ya Mungu kutuzuia kutenda dhambi. Yote haya ni ya umuhimu mkubwa kwetu kama wake na wamama tunapotafuta kua wenye nguvu kiroho na kutengeneza mazingira ya nyumbani ya kumtukuza Mungu.

Mara tu unapomkaribisha mwenzio wa kujadili orodha ya kiroho nawe, utataka kupitia baadhi ya mambo katika hii orodha naye. Pinga mvuto wa kutaka kuzungumzia tu juu ya maeneo ya udhalimu—haya ni rahisi kwa sababu yanaangazia yale watu wengine wametutendea sisi, kuliko yale sisi tumetenda mbele ya Mungu. Ukiwa hauhitajiki kutaja kila dhambi na kuongea kwa undani juu ya kila kitu, unataka kushiriki mambo yaliyo ya muhimu ambayo yanajenga ngome kuu katika maisha yako—maeneo ambayo unang’ang’ana sana na mizizi ya vianzo. Utataka kuomba: tubu, kataa, na achilia. Katika jina la Yesu, mkemee adui na umkumbushe Shetani kwamba hana tena mamlaka juu yako, kwamba Mungu hajakusaheme tu dhambi zako kupitia Yesu, bali pia amekufungua kabisa kutoka kwa nguvu za dhambi katika maisha yako. Shetani hawezi yasoma mawazo yako, kwa hivyo utahitaji kumwambia kwa sauti kuwa anapaswa kukuachilia huru! Kwa watu wengine, hili ni wazo jipya na laweza kuwa geni au la kuwakosesha utulivu; hata hivyo, kuelewa vile nguvu za kiroho zinafanya kazi ni uhuru mkubwa sana. Pamoja na mfano wa Orodha ya Kiroho na kartasi isiyoandikwa chochote kuna mfano wa maombi. Hauhitaji kurudia haya maneno yenyewe, bali yametungwa kukusaidia kuelewa jinsi ya kuomba kwa nguvu dhidi ya ngome katika nguvu na mamlaka ya Yesu Kristo. Baada ya Orodha.

Baada ya kuipitia orodha yako ya kiroho, njia bora ya kukiri ushindi wa Yesu na kumfahamisha adui kwamba “yameisha” ni kuichoma ile kartsi au makartasi kwenye umeziandika dhambi zako na ngome zako zote.

Inanipasa niseme kuwa baada ya kuipitia njia ya Orodha ya Kiroho mimi mwenyewe na kuwapitishia wanafunzi wengi katika njia hii, utahisi kama vile hujawahi hisi tena maishani mwako kuwa umesamehewa! Utahisi ni kama umepoteza tu poundi 50 za uzito. Kwa mawiki yatakayofuata, kwa kweli hutahisi msukumo wa kutenda dhambi, au kung’ang’ana na dhambi kabisa. Huenda ukahisi mawasiliano ya nguvu sana na Mungu. Ni kama usiku na mchana! Kwa udhiko langu, hata hivyo, hili huwa halidumu wakati wote…huenda ukaanza tena kutumbukia mienendo ya zamani isababishayo dhambi. Hata hivyo, utakuwa na silaha mpya kwenye zana yako ya kukabiliana na majaribu ya kutenda dhambi na mbinu tofauti za kukabili dhambi inapotendeka. Utakuwa na dhamira iliyo kali zaidi, kuelewa vizuri zaidi ukweli wa Mungu, na imani dhabiti zaidi ya kusimama wima. Ijapokuwa orodha ya kiroho inatusaidia kuufunga mlango dhidi ya adui na kujilinda sisi wenyewe, si mwisho, bali tu ni mwanzo bora zaidi. Ninapendekeza kupitia njia hii kwa kurudia kila wiki hadi orodha IISHE! UHURU toka kwa dhambi ni wako!

Kazi Yako Kufanya

1. Iangalie tena Orodha ya Kiroho na maombi; andaa moyo wako kwa kuwasiliana na Bwana katika maombi. Muulize akufunulie kitu chochote na kila kitu ambacho kimekuwa ni eneo la ngome katika maisha yako, ili uweze tubu, katae, na uachilie mambo hayo na upate ushindi juu ya dhambi kwa ajili ya utukufu Wake. 2. Kwa maombi ikamilishe Orodha ya Kiroho na utafute mhasibu mwenza au mtoa hesabu wako aliye komaa. Mwelezee kusudi la Orodha ya Kiroho na umwulize ikiwa anapenda kujadili na kuomba juu ya hii orodha nawe. (Hili lawezafanyika mkiwa naye au pitia kwa simu). 3. Pitia Orodha yako ya Kiroho pamoja na mhasibu mwenzako, hasa mkiangazia maeneo makuu unayong’ang’ana nayo ambayo yanakuzuia kupata ushindi juu ya dhambi na raha na amani nyumbani kwako. Omba kwa toba, kataa kazi ya Ibilisi, na tafuta uhuru toka ngome za hisia ambazo ni matokeo ya udhalimu. Kiri uwongo ambao umekuwa ukiamini kukuhusu na kuhusu Mungu na umwulize Mungu arudishe ukweli kwenye nafasi ya huo uwongo. Mpate mhasibu mwenza pia kukuombea katika kila moja wapo ya haya maeneo. Halafu, ichome hii Orodha yako ya Kiroho. (Huku tu ni kufunga kuzuri.). 4. Rudia njia hii kila wiki hadi uone hakuna jambo limezalia la kuandika kwenye hii orodha! Ushindi ni wako!

66

5. Ukiwa na Biblia yako pamoja na kamusi ya biblia, mwulize Mungu akuonyeshe mistari halisi ambayo unaweza kuandika chini na kuiweka mahali panapo onekana, kuitafakari, na kuiweka katika kumbukumbu. Hii mistari itakusaidia wakati Shetani anajaribu kukujaribu mara nyingine katika maeneo ambayo kihistoria ulikuwa na ngome. Iandike hiyo mistari hapa chini.

67

Ukurasa Kazi ya Sababu za Ngome

68

Mfano Sala Ombi la Kufungua Baba Mpendwa wa Mbinguni, wewe upo hapa kwenye chumba hiki na ndani ya maisha yangu. Wewe pekee ndiwe mjua-yote and mweza-yote, na upo kila mahali; ni wewe pekee nakuabudu. Natangaza kwamba ni wewe tu nakutegemea, kwa kuwa, kando na wewe, mimi siwezi kufanya lolote. Ninachagua kuamini Neno lako linalotufunza kwamba mamlaka yote Mbinguni na Duniani yako Kwa Kristo aliyefufuka, na kama mfuasi wa Kristo, na ambaye ni hayi ndani ya Kristo, nina Mamlaka ya Kumpinga Shetani, na ninajitoa kwako. Naomba unijaze na Roho Wako Mtakatifu kwa kipimo kamili na uniongoze kwenye kweli yote. Naomba ulinzi kamili na uongozi wako ninapoendelea kutafuta kukujua na kutenda mapenzi yako. Katika Jina La Ajabu La Yesu ninaomba. Amina. Azimio: Katika Jina na Mamlaka ya Bwana Yesu Kristo, ninaamuru Shetani na roho zote chafu kuniachilia ili niweze kuwa huru kujua na kuchagua kufanya mapenzi ya Mungu. Kama mwana wa Mungu aketiye pamoja na Kristo Mbinguni, ninatangaza kwamba kila adui wa Bwana Wangu Yesu Kristo, aliyeko hapa kwenye uwepo wangu afungwe. Shetani na mapepo wake wote hawawezi kunidhuru kwa vyovyote vile, wala hawawezi kuzuia mapenzi ya Mungu kutendeka maishani mwangu leo, kwa sababu mimi ni wa Bwana Yesu Kristo. Chini ya kila sehemu sema ombi lifuatalo na usikize jinzi Mungu atakufunulia sehemu za maisha yako binafsi zenye unafaa kukiri na kurejesha ukweli badala ya uwongo. Dhambi za kibinafsi: Baba Mpendwa wa Mbinguni, wewe umeniaamuru kujivika Bwana Yesu Kristo na kukataa kuupa mwili na tama zake nafasi. Ninakiri kwamba nimekuwa nikiuruhusu mwili na tama zake kuipiga vita nafsi yangu. Nakushukuru wewe kwa kuwa dhambi zangu zote zimesamehewa katika Kristo, lakini nimevunja sheria yako takatifu kwa kuruhusu dhambi kutawala na kuupiga vita mwili wangu. Naja kwako sasa nikikiri na kukataa hizi dhambi za mwili ambazo nimetenda na jinsi nimemhuzunisha Roho Mtakatifu. Katika Jina la Yesu ninaomba, Amina. Kushirikishwa katika Ushetani: Baba wa Mbinguni, tafadhali leta katika akili zangu kitu chochote na kila kitu ambacho nimekifanya kwa kujua au kutojua ambacho kimenishirikisha katika ushetani, udhehebu, mafundisho ya dini za uwongo au matendo. Ninataka kuupata uhuru wako kwa kuukataa uongozi wowote au wote wa uwongo. Katika Jina la Yesu. Amina. Dhuluma: Baba wa Mbinguni, nakushukuru wewe kwa utajiri wa ukarimu, zaburi na uvumilivu wako kwangu, nikijua kuwa ukarimu wako umeniongoza kwa toba. Ninakiri kuwa sijaonyesha ukarimu na uvumilivu huo kwa wale wameniumiza au wameniudhi. Badala yake, nimeshikilia hasira, uchungu, na chuki yangu kwao. Tafadhali nikumbushe watu wote ninaohitaji kuwasamehe ili niweze kufanya hivyo sasa hivi. Katika Jina la Yesu naomba. Amina. Mawazo ya Kishetani: Baba wa Mbinguni, naelewa kwamba nimeamini uwongo ambao Shetani ameniambia jinsi unavyoniona mimi, na ninakataa kukubali kudanganywa tena. Kulingana na Neno lako, nimekubalika, nimechaguliwa, nimeitwa, na nimewekwa muhuri na ni mrithi wa kiti cha enzi, na nimehakikishiwa kwamba ni mkuu Yeye aliye ndani mwangu kuliko Yeye aliye ulimwenguni. Tafadhali nifunulie njia ambazo nimemruhusu Shetani kuyadhibiti mawazo yangu na kuniweka katika minyororo ili niweze kuivunja hii minyororo kwa kuutambua uwongo ambao Shetani ameniambia juu yangu mwenyewe na kuthibitisha ukweli unaosema juu yangu. Katika Jina Yesu naomba. Amina. Ngome za Kimawazo: Baba wa Mbinguni, wewe ndiwe kweli na ninatamani kuishi kwa imani kulingana na ukweli wako. Ukweli utaniweka huru—ukweili wa Yesu—lakini kwa njia nyingi nimedanganywa na baba wa Uwongo na elimu ya huu ulimwengu ulioanguka, na hata nimejidanganya mwenyewe. Ninachagua kutembea nuruni nikifahamu kwamba unanipenda na unanikubali tu jinsi nilivyo. Ninapoyatazama maeneo ya uwezekano wa udanganyifu, ninamkaribisha Roho wa kweli kuniongoza katika kweli yote. Tafadhali nilinde toka kwa udanganyifu wote unapo “nipeleleza Ee Mungu, na kuujua moyo wangu: nijaribu na ujue hamu ya mawazo yangu, na uone ikiwa kuna njia yoyote ya kuumiza ndani mwangu na uniongoze kwenye njia ya milele.” Katika Jina la Yesu naomba, Amina. Maombi ya Kukiri Dhambi za kibinafsi: Bwana Yesu nakiri kwamba nimetenda dhambi dhidi yako kwa [taja hiyo dhambi]. Asante kwa kunisamehe na kunitakasa na nina nena kwamba sitaruhusu dhambi kutawala maadili ya mwili wangu na sitawahi tena [taja kitu umetumia katika dhambi—kwa mfano, akili, mawazo, sehemu za mwili, n.k] kutumika kwa njia hii, lakini angaa nitatumia tu [taja hicho kitu tena] kitakacho tumika kwa makusudi ya kiungu kama [eleza matumizi ya kitu hicho kwa njia nzuri—k.m, kusifu, kuhudumu, kupenda, n.k.] Amina. Kushirikishwa katika Ushetani: Bwana Yesu, nakiri kwamba nime [mmoja wa familia yangu] shiriki katika [taja hasa kila imani na ushiriki unaohusika na sehemu hii ya hii orodha ambayo Mungu ameleta akilini mwako] na ukatae dhambi ya______________________kama mwiiko na uwongo. Naomba kwamba utanijaza na Roho wako Mtakatifu ili kwamba niweze kuongozwa na wewe. Nashukuru kwa kuwa katika Kristo nimesamehewa. Amina. Dhuluma: Bwana Yesu, ninachagua kusamehe [taja mtu halisi] kwa [taja jambo alilokufanyia au alishindwa kukufanyia] kwa sababu ilinifanya nihisi [shiriki hisia hizi za uchungu, kwa mfano, kukataliwa, chafu, kukosa dhamana, dharau, etc.] Baada ya kufanya haya, jifungue toka kwa minyororo ya haya mambo kwa kuomba ombi lifuatalo:

69

Bwana Yesu, nachagua kutoshikilia uchungu wangu. Ninaachilia haki yangu ya kulipiza kisasi na kukuomba wewe kuponya hisia zangu ambazo zimedhurika. Asante kwa kuniweka huru toka kwa minyororo ya uchungu wangu. Sasa nakuomba uwasamehe wale wametumika kuniumiza. Katika Jina la Yesu naomba. Amina. Mawazo ya Kishetani: Bwana Yesu, nakiri kwamba nimeaamini uwongo [taja uwongo halisi] ambao nimeambiwa na Shetani na ufalme wake wa giza na nina kataa huo uwongo ambao nimeamini juu yangu mwenyewe. Nina thibitisha ukweli unaonena juu yangu [nena ukweli ambao Mungu anasema juu yako na hali yako] na nakushukuru kwa msamaha wako na nina ahidi kwamba sitaamini tena uwongo wa Shetani katika eneo hili la maisha yangu na nitaamini yale umenifunulia kupitia Neno lako. Amina. Ngome za Kimawazo: Bwana Yesu, nakiri kwamba nimedanganywa na [kiri eneo halisi ambalo umeamini uwongo wa Shetani]. Ninakataa huu uwongo ambao nimeamini na ninathibitisha ukweli wa [rudisha ukweli wa yale Mungu ananena juu ya hali hii au imani]. Nakushukuru kwa msamaha wako na nina ahidi kwamba sitaamini tena uwongo wa Shetani katika eneo hili la maisha yangu, na nitaamini tu ukweli wa vile Mungu alivyo. Amina.

70

UPANDAJI MAKANISA NJIA YESU ALITUONYESHA: KATIKA LUKA 10 Mikakati na Uinjilisti wa Upanzi wa Kanisa kutoka kwa Yesu: Kote ulimwenguni, Roho Mtakatifu amekuwa akiwaongoza wainjilisti kuzifikia jamii kwa misingi ya maagizo kwa wanafunzi yaliyomo katika Luka 10. [1]…Bwana aliwachagua wengine, sabini na wawili, na akawatuma wawili wawili wamtangulie kwenda kila mji na kila mahali alipokusudia kwenda mwenyewe. Yesu anajua kule anapanga kufanya kazi; twahitaji kumuuliza Yesu mahali anapenda kufanya kazi, halafu twende mahali pale na tufanye kazi. Mwulize ni wapi utaanza na ni nani utaanza naye. Kuomba ukitembea inaweza kusaidia sana hapa. Yesu anataka kutafuta na kuokoa waliopotea; acha tupate akili zake kuhusu ni wapi waliopotea wako na jinsi ya kuwachongelea, hata kama ni sokoni, mahali pa kazi, shuleni, mikahawani, au bustanini. Yesu anawatembelea wale walio karibu nasi kwa njia ambazo mara nyingi hazionekani kwetu. Anawatembelea katika ndoto, maono, vipindi vya Radio na Runinga za Kikristo, kwenye ufikio wa mitandao, Biblia na vitabu vya Kikristo, na njia zingine nyingi ambazo huenda tukakosa kuzifahamu. Pia ‘anawatembelea’ wengine wengi katika hali yao ya kutotosheka na mitindo yao ya maisha isiyowaridhisha, na pia kupitia maisha ya uungu ya wafuasi wa Yesu kwenye maeneo yao, ambao ni maandalizi ya nguvu ya huduma yetu. Acha tusonge mbele kwa imani kwamba Yesu anawatembelea hawa “kondoo bila mchungaji” na anawaandaa wengi kwa ajili ya huduma yetu, hata ikiwa hatujamtambua akiwa kazini. [2] Aliwaambia, “Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache; basi mwombeni Bwana wa mavuno apeleke watenda kazi katika mavuno yake.” Mara nyingi tunasikia ikisemwa kwamba tatizo ni kuwa udongo ni mgumu na watu ni shingo ngumu. Yesu anatwambia kuwa kuna tatizo tofauti. Kuanzia mahali Yesu anatwambia tuanzie ndiyo juhudi moja muhimu zaidi ya kufikia (kuvuna) kanda moja. Acha tuombe jinsi Yesu anasema tuombe, na kuwaandika wengine wengi kumlilia Bwana wa Mavuno kuwatuma wafanyikazi wengi ambao wamejihami kuifanya hii kazi. [3] Enendeni! Nawatuma kama wana kondoo kati ya mbwa-mwitu. Kama wana-kondoo, tu wadhaifu na wanaoweza kudhuriwa na madhara mengi. Twahitaji kumtumainia Mchungaji kwa ajili ya usalama wetu. Vita ni vikuu; tunahitaji kulindwa kwa maombezi na silaha zote za Mungu. Yesu hatutumi kwenda mahali palipo na usalama, bali ni katika hema za adui kutafuta na kuokoa waliopotea. Omba hivyo, na uwapate wengine kuomba nawe na kukuombea. [4] Msichukuwe mfuko, wala mkoba, wala vitu; wala msimwamkie mtu njiani. Usifadhaishwe na vitu vya siada au matendo yasiyo ya muhimu. Jiweke kwa urahisi. Baki kwa mwelekeo. Kumbuka utume wako ni nini. Hatuhitaji mipango mingi sana au uhamazisho, lakini utiifu wa urahisi. [5, 6] Na nyumba yo yote mtakayoingia, semeni kwanza, “Amani iweni nyumbani humu; na akiwamo mwana wa amani, amani yenu itamkalia; la, hayumo, amani yenu itarudi kwenu. Hapa tunajulishwa kwa Mtu wa Amani, wazo moja lakini lenye nguvu sana. Yesu alisema tumtafute mtu mmoja ambaye atapokea ujumbe wetu wa amani. Huyu ‘mtu wa amani’ ameandaliwa na Bwana kuukaribisha ujumbe wetu. Anaweza pia kuwa (lakini huwa si kila wakati) mtu wa ushawishi au mwenye sifa (mbaya au nzuri) katika kanda hiyo. Mifano toka kataika Maandiko: yule mwanamke aliyekuwa kisimani (Yohana 4), Kornelio (Matendo 10), Lidia (Matendo 16), Mlinda gereza Mfilipi (Matendo 16). Mtu huyu huenda akawa ndiye mwanzilishi wa kanisa. Hata kama si hivyo, anawajua watu wengi na anaweza washawishi wengine kukusanyika na kusikiza, na kutusikiza. Tunapompata mtu wa namna hii tutaishi mahali pale, tutumie muda na huyo mtu, na tuifikie familia yake na mtandao wa marafiki zake (oikos zake). [7, 8] Basi, kaeni katika nyumba iyo hiyo, mkila na kunywa vya kwao; maana, mtenda kazi amestahili kupewa ujira wake. Msihame-hame kutoka nyumba hii kwenda nyumba hii. Na mji wowote mtakaouingia, wakiwakaribisha, vileni vyakula viwekwavyo mbele yenu. Kubali vitu vile wengine wanavyo na wanavyokuomba ushiriki, hii itawaonyesha kuwa wana dhamana na wanastahili kama watu. Kaa naye, na uwabariki. Tunapompata mtu wa namna hii tunakaa naye, kuwa na wakati na huyu mtu, na kuyadumisha maono ya kuifikia familia yake na mtandao wa marafiki zake (oikos yake) kwa ajili ya Kristo. Hili linatuleta kwa swala nyeti: tumezoea kumtafuta mtu ambaye anapenda, halafu tunamhimiza ahudhurie mikutano yetu ya Kikristo. Chongeleo hili limeimarisha waamini wengi wapya katika makanisa yenye nguvu, na baraka nyingi. Hata hivyo, kizuizi kwa chongeleo hili, ambacho huwa hakionekani, ni kwamba huku makanisa yetu yanapoinuka jinsi wakati unapopita, nafasi ya kawaida ya kuifikia oikos ya mwamini huyu mpya, katika ulimwengu wake, mara nyingi hupotea. Sababu moja inayowafanya waamini wapya kupata ugumu katika kuifikia oikos yao ni kwamba muumini mpya anajaribu kuwapata rafikize au familia yake kwenda mahali wasipo pafahamu (jengo la kanisa au nyumba iliyojaa Wakristo), badala ya wao kutembelewa kwenye nyumba (chumba cha kulala, mkahawa, n.k) ambazo wanazifahamu. Twaweza kuanza kundi jipya ndogo, tukalijenga likimzunguka mtafutaji na marafikize na jamaa zake, ambayo waweza kuwa asilia ya kanisa jipya la nyumbani au kundi dogo. Chongeleo la Luka 10 ni kinyume cha yale wainjilisti wengi hufanya. Inasema, mtafute mtu aliye wazi halafu umfanyie uinjilisti, na mtazamo wa kuanzisha mkusanyiko mdogo, rahisi pamoja na katika nyumba zao, biashara au shuleni—ambalo limeundwa na huyu

71

mtu, familia yao, na mtu ye yote wamjuaye kuwa yu wazi kulisikia Neno. Waweza kuliita hili kundi la nyumbani, kundi dogo, au kanisa la nyumbani. Wazo ni kuwa watu watajiunga kikawaida zaidi na jambo ambalo linaendelea katika mazingira yaliyo ya kawaida kwao, kuliko lile (kama mkutano wa Wakristo) ambalo hawajashuhudia, na ambalo ni sawa na kuvuka tamaduni kwao. Usiwatoe watu hawa kwa ujirani wao au mahali pao pa kazi, (kama ile chongeleo la ‘njoo kanisani mwetu’) lakini itumie kama mazingira ya kuanza jamii mpya ndogo ya wafuasi wa Yesu, katikati mwa watu wao wenyewe, mahali wanaishi. Hili ni la umuhimu mkubwa kwa kufikia vilindini mwa jamii zetu. Ikiwa tutafanya kazi na ‘mtu wa amani’ kufikia oikos yake au familia/marafiki zake, twaweza anza mikusanyiko midogo, rahisi ndani ya hiyo jamii au kundi la marafiki/kitamaduni; ikiwa tutamkusanya huyu mtu kanisani mwetu, mara nyingi atawapoteza wengi au wote wa washiriki wake wasio-okoka kwa haraka, pamoja na nafasi ya kuanzisha kusanyiko jipya. Jambo moja lenye nguvu zaidi ambalo mtu aweza fanya ni kuwa na watu waliopotea, mahali wanaishi, mahali wanautumia muda wao wa kawaida, kuwaonyesha heshima, na kuwaonyesha upendo. Kwa njia nyingi, waliopotea ni kama tu sisi—wanaitikia upendo wa Mungu ambao unadhirishwa kwa fikira na ubunifu kupitia mtu aliyejazwa na Roho wa Yesu. Kanuni Kuu (Mat. 7.12) ni kuwa na matokeo ya nguvu katika uinjilisti na utume; wakati wafuasi wa Yesu wanapozidi katika upendo (na si tu mafundisho au matendo ya huduma), roho zao zenye neema, na umbo-kama la Yesu zinapofungua wazi milango mingi ambayo mbeleni ilikuwa imefungwa. [9] Waponyeni wagonjwa waliomo, waambieni, “Ufalme wa Mungu umewakaribia.” Hapa kuna karibisho kufuata katika hatua za Yesu. Tunaagizwa kuwaponya wagonjwa na HALAFU tuwaambie, “Ufalme wa Mungu umewakaribia.” (Haitaji kuanza na somo la Biblia) Uponyaji wa Mungu au dhihirisho la nguvu za Mungu unaonekana kuwa ni kawaida katika mpango wa Yesu wa upanzi wa kanisa. Uwe tayari kuyaombea mahitaji ya wengine na utarajie Mungu kufanya kazi kwa njia zinazoonekana au kupambanulikana. Ishara na maajabu vitawanenea, na watataka kufahamu zaidi juu ya hii Njia ya maisha tunayoizungumzia. [10, 11] Na mji wowote mtakaouingia, nao hawawakaribishi, tokeni humo, nanyi mkipita katika njia zake semeni, “Hata mavumbi ya mji wenu yaliyogandamana na miguu yetu tunayang’ung’uta juu yenu.” Watu wengi hutumia muda na nguvu kuwaongelesha watu ambao hawajafunguka kwa Injili. Watu wengi waliopotea watataka kuingia katika mabishano (au mbaya zaidi). Huku mijadala nzuri na yenye kunawiri yaweza kusaidia sana, mabishano ni nadra yakuwe. Ikiwa kuna ukosefu wa uwazi, songa mbele, mtafute mtu wa amani kwingineko.

72

KUNENA JUU YA YESU NA WATU WANAOMWABUDU ALLAH Korani inanena mengi kumhusu Yesu Kristo, na wakati wote inafanya hivyo kwa heshima kuu. Eneo unamo fanya kazi litakuwa na wanaomwabudu Allah wengi. Waweza kuwa na matunda mengi katika huduma yako ikiwa unajua yale Korani inasema juu ya Kristo. Korani haiwaambii wasomaji wake mengi juu Yake, lakini kunayo yakutosha humo kukuwezesha wewe kuona ikiwa mtu anapenda kuongea juu ya Kristo na kuangalia Agano Jipya. Hapa kuna machache toka Surah Al-Imran, Qur’an 3:45, 48-50:

45 Na pale Malaika walipo sema: Ewe Maryamu! Hakika Mwenyezi Mungu anakubashiria (mwana) kwa neno litokalo kwake. Jina lake ni Masihi Isa mwana wa Maryamu, mwenye hishima katika dunia na Akhera, na miongoni mwa walio karibishwa (kwa Mwenyezi Mungu)… 48. Na atamfunza kuandika na Hikima na Taurati na Injili. 49. Na ni Mtume kwa Wana wa Israili kuwaambia: Mimi nimekujieni na Ishara kutoka kwa Mola Mlezi wenu, ya kwamba nakuundieni kwa udongo kama sura ya ndege. Kisha nampuliza anakuwa ndege kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na ninawaponesha vipofu wa tangu kuzaliwa na wakoma, na ninawafufua maiti kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na ninakwambieni mnacho kila na mnacho weka akiba katika nyumba zenu. Hakika katika haya ipo Ishara kwenu ikiwi nyinyi ni wenye kuamini. 50. Na ninasadikisha yaliyo kuwa kabla yangu katika Taurati, na ili nikuhalalishieni baadhi ya yale mlio harimishiwa, na nimekujieni na Ishara kutokana na Mola Mlezi wenu. Kwa hivyo mcheni Mwenyezi Mungu na nit'iini mimi.

Korani inasema ya kwamba Yesu (au ‘Isa katika Lugha ya Kiarabu ya Korani) ana tabia halisi ambazo hazina mtu mwingine: Anaitwa neno toka kwa Allah, na Mesihi, na anashikiliwa kwa taadhima katika safu na aya hii, na ya kwamba Allah alimpa yeye Injil na akamruhusu yeye kuwaponya vipofu na wenye ukoma, na kuwafufua wafu. Jambo la kustajabisha zaidi ni mstari wa 50, “Isa ananukuliwa akisema kwamba Waislamu waaminifu (Wale wote ambao wamejisalimisha kwa Allah) wanapaswa kumwogopa Allah na kumtii Isa. Lakini Korani haitoi mafundisho yoyote ya Isa, basi kumtii Yeye, ni lazima tuyatafute mafundisho Yake katika Injil, yaani, Agano Jipya. Muhummad aliambiwa na Allah kwamba ikiwa alikuwa na maswali juu ya haya mambo, awaulize wale walioyasoma Maandiko ya Kwanza: Surah Yunnus 10.94: “Na ikiwa unayo shaka katika tuliyo kuteremshia, basi waulize wasomao Kitabu kabla yako. Kwa yakini imekwisha kujia Haki kutoka kwa Mola wako Mlezi. Basi usiwe miongoni mwa wenye shaka.” Wengi wameambiwa kwamba au Injil iligeuzwa. Twaweza kuwaambia kwamba tunaamini Allah anaweza kuliangalia na kulitunza neno lake, jinsi isemavyo katika Al-An’am 6.115-116: “Na yametimia maneno ya Mola Mlezi wako kwa kweli na uadilifu. Hapana awezaye kuyabadilisha maneno yake. Na Yeye ndiye Mwenye kusikia na Mwenye kujua. Na ukiwat'ii wengi katika hawa waliomo duniani watakupoteza na Njia ya Mwenyezi Mungu. Hawa hawafuati ila dhana tu, na hawakuwa ila ni wenye kusema uwongo tu.” Tunawatafuta watu ambao wanapenda kusikia yale Injili inasema juu ya ‘Isa. Ni lazima tuwe makini tusiongee dhidi ya Allah, Uislamu, Muhummad au Korani. Twawaletea watu habari njema ya jinsi wanavyoweza kuvumbua na kupokea baraka za ‘Isa. Kufunga sehemu hii, tutatoa mapendekezo machache ya kuongea na Waislamu: Onyesha unyenyekevu na upendo. Wabariki kila wakati, na ujitoe kuomba kwa jina la ‘Isa ikiwa wana mahitaji ya maombi. Kila wakati uwe mwenye heshima na uwe mwenye urafiki. Kamwe usiilaumu dini yao au desturi zao. Kamwe usikubali kuingizwa katika mabishano. Kumbuka kuwa watu hawa wana hisia za kawaida za kibinadamu tu kama sisi, na kuwa Mungu anawapenda. Sisi hatupigani dhidi ya mwili na damu, na hawa watu si adui zetu. Utafaulu kwa kumtafuta mtu wa amani, na kumpenda na kumbariki huyo mtu, na wale yeye anao wajua. As-salaamu ‘A-lai-kum ! Sehemu hii na ile inayohusu Luka 10 ziliandikwa na rafiki aitwaye Aalim, ambaye amefanya kazi katika pande mbalimbali za dunia zenye Waislamu wengi. Unaweza kumwandikia au kutoa maoni: [email protected].