ziara ya mhe. jaji mkuu tabora & shinyanga na malengo ya kuiboresha mahakama katika dhana nzima...

9
Na MARY GWERA, MAHAKAMA YA TANZANIA Hivi karibuni, Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman, alifanya ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua shughuli za Mahakama katika mikoa ya Tabora na Shinyanga. Ziara ya Mhe. Jaji Mkuu katika mikoa tajwa ililenga katika kujionea hali ya utendaji kazi wa Mahakama katika mikoa hiyo ikiwa ni pamoja na kuwakumbusha Watumishi wa Mahakama kufanya kazi kwa ufanisi na weledi ili kuboresha huduma ya utoaji haki nchini. Katika ziara yake Mhe. Jaji Mkuu aliambatana na Maafisa na Watendaji kadhaa wa Mahakama kutoka Makao makuu ili kujionea hali ya utendaji kazi ikiwa ni pamoja na kubainisha na kufanyia kazi changamoto ambazo watumishi wanakumbana nazo katika utendaji kazi wa kila siku. Mhe. Jaji Mkuu aliambatana na Naibu Msajili-Mahakama ya Rufani (T), Naibu Msajili-Mahakama Kuu, Mtendaji wa Mahakama Kuu anayeratibu Mahakama Kuu, Mtendaji wa Mahakama za Wilaya na Mikoa na Mtendaji wa Mahakama za Mwanzo nchini. 1

Upload: muhidin-issa-michuzi

Post on 23-Dec-2015

11.684 views

Category:

Documents


9 download

DESCRIPTION

ZIARA YA MHE. JAJI MKUU TABORA & SHINYANGA NA MALENGO YA KUIBORESHA MAHAKAMA KATIKA DHANA NZIMA YA UTOAJI HAKI NCHINI.

TRANSCRIPT

Page 1: ZIARA YA MHE. JAJI MKUU TABORA & SHINYANGA NA MALENGO YA KUIBORESHA MAHAKAMA KATIKA DHANA NZIMA YA UTOAJI HAKI NCHINI

Na MARY GWERA, MAHAKAMA YA TANZANIA

Hivi karibuni, Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman, alifanya ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua shughuli za Mahakama katika mikoa ya Tabora na Shinyanga.

Ziara ya Mhe. Jaji Mkuu katika mikoa tajwa ililenga katika kujionea hali ya utendaji kazi wa Mahakama katika mikoa hiyo ikiwa ni pamoja na kuwakumbusha Watumishi wa Mahakama kufanya kazi kwa ufanisi na weledi ili kuboresha huduma ya utoaji haki nchini.

Katika ziara yake Mhe. Jaji Mkuu aliambatana na Maafisa na Watendaji kadhaa wa Mahakama kutoka Makao makuu ili kujionea hali ya utendaji kazi ikiwa ni pamoja na kubainisha na kufanyia kazi changamoto ambazo watumishi wanakumbana nazo katika utendaji kazi wa kila siku.

Mhe. Jaji Mkuu aliambatana na Naibu Msajili-Mahakama ya Rufani (T), Naibu Msajili-Mahakama Kuu, Mtendaji wa Mahakama Kuu anayeratibu Mahakama Kuu, Mtendaji wa Mahakama za Wilaya na Mikoa na Mtendaji wa Mahakama za Mwanzo nchini.

1

Page 2: ZIARA YA MHE. JAJI MKUU TABORA & SHINYANGA NA MALENGO YA KUIBORESHA MAHAKAMA KATIKA DHANA NZIMA YA UTOAJI HAKI NCHINI

Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania, akisalimiana na Mhe. David Mrango, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora pamoja na Wahe. Majaji wengine wa Kanda hiyo na Viongozi wakuu wa Mkoa waliokuja kumpokea alipowasili mkoani Tabora kwa ziara ya kikazi, mwenye sare ni Bi. Suzan Kaganda, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora.

Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania ambaye alianza rasmi ziara yake mkoani Tabora tarehe.25.02.2015 alipata nafasi ya kukagua na kuongea na Watumishi wa ngazi mbalimbali za Mahakama katika mkoa huo ambapo katika vikao mbalimbali alivyofanya na Watumishi hao ikiwa ni pamoja na Wahe. Majaji na Mahakimu, Mhe. Jaji Mkuu alisisitiza mara zote juu ya utendaji kazi kwa kujituma ili kubadili taswira ya Mahakama kwa wananchi ambao ndio wadau muhimu wa Mahakama.

Akiongea na Watumishi wa Mahakama wa Mkoa wa Tabora Mhe. Jaji Mkuu alieleza kufurahishwa na kasi ya usikilizaji na

2

Page 3: ZIARA YA MHE. JAJI MKUU TABORA & SHINYANGA NA MALENGO YA KUIBORESHA MAHAKAMA KATIKA DHANA NZIMA YA UTOAJI HAKI NCHINI

umalizwaji wa mashauri katika Mahakama za Mwanzo mkoani Tabora. Awali; katika taarifa yake kwa Mhe. Jaji Mkuu, Mhe.Yolanda Mallya, Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mahakama ya Mwanzo Tabora Mjini alimtaarifu Mhe. Jaji Mkuu juu ya mkakati waliojiwekea wa kumaliza mashauri ya aina yoyote kwa kipindi kisichozidi miezi sita.

Aidha Mhe. Jaji Mkuu alitumia ziara hiyo ya kikazi kuwaeleza Watumishi juu ya mikakati ambayo Mahakama imejiwekea katika kuhakikisha kuwa huduma ya utoaji haki inaboreshwa nchini.

“Kwa hivi sasa Mahakama ya Tanzania imejiwekea mikakati/vipaumbele ambavyo vinalenga kuboresha huduma ya utoaji haki nchini, na malengo haya inabidi yafanyiwe kazi na kila mmoja wetu kwa maana ya kila Mtumishi na mdau wa Mahakama awajibike katika kufikia malengo yetu ya kuboresha huduma ya utoaji haki nchini.” Alisema, Mhe. Jaji Mkuu.

Alivitaja vipaumbele hivyo mbele ya Watumishi kuwa ni; Uboreshaji wa Masjala za Mahakama; katika hili Mhe. Chande alisema kuwa Masjala ndio kitovu katika utendaji kazi wa Mahakama na kusisitiza kuwa Masjala inabidi ziimarishwe na kuboreshwa kwa kuzingatia umuhimu wa nyaraka za kesi mbalimbali zinazohifadhiwa.

Uimarishaji wa ukusanyaji wa takwimu; hili pia ni eneo ambalo limewekwa kama kipaumbele katika maboresho Mahakamani, Mhe. Jaji Mkuu alisema Mahakama pia imejipanga vyema kuhakikisha inakuwa na takwimu sahihi za kesi mbalimbali zilizopo katika Mahakama mbalimbali nchini ili kuangalia ni sehemu ipi inayohitaji nguvu zaidi katika kushughulikia mashauri/kezi za muda mrefu. Alitoa mfano kuwa katika kipindi cha miaka miwili, wamebaini baadhi ya Kanda kama Tabora, Mwanza, Dar es Salaam, kuwa na mashauri mengi ya muda mrefu na tayari jitihada za dhati zimeshafanyika kwa kuwa na vikao maalum (special sessions) kwa ajili ya kumaliza

3

Page 4: ZIARA YA MHE. JAJI MKUU TABORA & SHINYANGA NA MALENGO YA KUIBORESHA MAHAKAMA KATIKA DHANA NZIMA YA UTOAJI HAKI NCHINI

kesi hizo, hatua hiyo imefanikiwa kiasi kikubwa kupunguza mashauri ya muda mrefu Mahakamani.

Matumizi ya TEHAMA; Aliongeza kuwa kwa sasa Mahakama imejielekeza katika Matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika kusajili kesi za ngazi mbalimbali zinazoandikishwa/zinazoletwa Mahakamani.

“Kwa sasa Mahakama ina mfumo ambao unawezesha kubaini idadi ya mashauri yaliyofunguliwa katika ngazi mbalimbali za Mahakama nchini, katika hili Wataalam wetu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (IT) walizunguka takribani nchi nzima kuwaelekeza Makarani wetu jinsi ya kusajili kesi kwa njia ya Kompyuta, na hili pia limeleta mafanikio kwa kiasi kikubwa kwani takwimu na taarifa nyingine za Mahakama zinatumwa makao makuu kwa urahisi zaidi,” alisema Mhe. Jaji Mkuu.

Mafunzo; Mhe. Jaji Mkuu alitaja kuwa Mafunzo pia ni mojawapo ya eneo lililowekewa msisitizo lengo likiwa ni kuwaendeleza kitaaluma Watumishi wa Mahakama kwa Mafunzo ya muda mrefu na muda mfupi ili kuwapa ujuzi na ufanisi zaidi katika utendaji kazi wa kila siku. Alibainisha kwa miaka miwili (2) sasa, Mahakama imeweza kusomesha takribani Watumishi 457 katika mafunzo ya muda mrefu, na watumishi takribani 763 wameendelezwa katika mafunzo ya muda mfupi. Aliwataka Watumishi kuchukua fursa hiyo kujiendeleza kwani kwa sasa Mahakama inatoa nafasi kwa kila Mtumishi wake kujiendeleza kitaaluma.

Uboreshaji wa Miundombinu: miundombinu hii ni pamoja na majengo ya Mahakama, vitendea kazi n.k, Mhe. Jaji Mkuu alisema pia katika kuboresha huduma zake Mahakama imejipanga katika kuboresha miundombinu yake ikiwa ni pamoja na kujenga majengo ya Mahakama na kukarabati majengo yaliyochakaa.

“Tatizo kubwa ambalo Mahakama inakabiliana nalo ni uchakavu wa miundombinu yake, kwa hili tuko mbioni kuhakikisha Mahakama inakuwa na miundombinu bora zaidi,

4

Page 5: ZIARA YA MHE. JAJI MKUU TABORA & SHINYANGA NA MALENGO YA KUIBORESHA MAHAKAMA KATIKA DHANA NZIMA YA UTOAJI HAKI NCHINI

tumejipanga kuboresha ikiwa ni pamoja na kujenga Mahakama Kuu katika mikoa yote ambao haina majengo, taratibu zinaendelea na kwa mwaka huu tumepanga kuanza ujenzi wa Mahakama Kuu katika mikoa ya Kigoma, Lindi, Morogoro, Musoma/Mara etc, na kueleza kuwa Mahakama kuu Shinyanga iko mbioni kukamilika kwa ajili ya kuanza kazi rasmi,” alieleza.

Uboreshaji wa hali ya Wafanyakazi wa Mahakama; Hili pia ni moja kati ya eneo ambalo limepewa kipaumbele katika maboresho yanayoendelea kufanyika ndani ya Mahakama; Mhe. Jaji Mkuu aliwaeleza Watumishi wa Mahakama Tabora kuwa uboreshaji huu unaangalia upatikanaji wa stahili za Watumishi kwa wakati ikiwa ni pamoja na nauli za likizo, madeni mbalimbali, uboreshaji wa mishahara ya watumishi suala ambalo linaendelea kufanyiwa kazi.

“Masuala/Matatizo yote yanayohusiana na watumishi tayari tumeshayabaini, kwahiyo hivi sasa, tunashughulikia masuala yote kwa wakati mmoja, mfano, kulipa nauli za likizo kwa watumishi wanaokwenda likizo kwa mwaka husika na kwa wakati mmoja,” alifafanua Mhe. Jaji Mkuu.

Aidha Mhe. Jaji Mkuu aliongeza kuwa suala Maadili na nidhamu pia limewekewa kipaumbele, alisema kuwa kuna baadhi ya Watumishi wa Mahakama hawana nidhamu na maadili katika utendaji kazi, hali hii imesababisha kuwa Mahakama nzima kutupiwa lawana juu ya utendaji kazi wake.

“kuna baadhi ya Watumishi ya watumishi wa Mahakama hawana maadili na nidhamu hali hii inachafua taswira nzima ya Mahakama, lazima tuongeze uadilifu, Watanzania wanataka Watumishi wanaotoa haki, wanaoaminika ili kila mwananchi aridhike,” alisema.

5

Page 6: ZIARA YA MHE. JAJI MKUU TABORA & SHINYANGA NA MALENGO YA KUIBORESHA MAHAKAMA KATIKA DHANA NZIMA YA UTOAJI HAKI NCHINI

Baadhi ya Watumishi wa Mahakama wa Mkoa wa Tabora wakiwa katika Mkutano na Mhe. Jaji Mkuu (hayupo pichani) alipoongea nao juu ya masuala mbalimbali ya kiutendaji alipokuwa kwenye ziara ya kikazi mkoani humo.

Mapema akimkaribisha, Mhe.Jaji Mkuu katika Mahakama Kuu kanda ya Tabora, Mhe. Amir Mruma, Jaji Mfawidhi- Mahakama Kuu (Kanda ya Tabora ambayo inajumuisha mikoa ya Shinyanga, Kigoma na Simiyu) alimueleza Mhe. Jaji Mkuu kuwa, Mahakama mkoani Tabora imejiwekea mikakati yake ya kumaliza mashauri ya muda mrefu ili kwenda sambasamba na maboresho yaliyoridhiwa na Mahakama nchi nzima ambayo ni kuboresha huduma ya utoaaji haki nchini.

6

Page 7: ZIARA YA MHE. JAJI MKUU TABORA & SHINYANGA NA MALENGO YA KUIBORESHA MAHAKAMA KATIKA DHANA NZIMA YA UTOAJI HAKI NCHINI

Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania akiongea na Wahe. Majaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora alipotembelea Kanda hiyo katika ziara yake ya kikazi. (kulia,mwenye tai nyekundu) ni Mhe. Amir Mruma, Jaji Mfawidhi-Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, pembeni yake (wa kwanza kulia) ni Mhe. Sam Rumanyika, Jaji, Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, (wa kwanza kushoto kutoka upande wa Mhe. Jaji Mkuu) ni Mhe. John Utamwa, Jaji-Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora, (katikati), ni Mhe. David Mrango, Jaji-Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, (wa kwanza kushoto) ni Mhe. Leila Mgonya, Jaji Mahakama Kuu Kanda ya Tabora.

Katika ziara yake Mhe. Jaji Mkuu alifanikiwa pia kukutana na kuongea na Wadau mbalimbali wa Mahakama wa mkoa wa Tabora kama, Polisi; Polisi, Magereza, Mawakili wa Serikali na wa Kujitegemea, PCCB n.k ambapo alieleza jitihada ambazo

7

Page 8: ZIARA YA MHE. JAJI MKUU TABORA & SHINYANGA NA MALENGO YA KUIBORESHA MAHAKAMA KATIKA DHANA NZIMA YA UTOAJI HAKI NCHINI

Mahakama inafanya katika kuboresha huduma zake na kuwataka kuonyesha ushirikiano katika kufanikisha upatikanaji haki kila mmoja katika eneo lake.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo, Sikonge (aliyenyoosha mkono) akimuonyesha Mhe. Jaji Mkuu kiwanja cha Mahakama ambacho kitajengwa Mahakama ya Wilaya. Katika ziara yake mkoani Tabora, Mhe. Jaji Mkuu alipata nafasi pia ya kutembelea Mahakama ya Mwanzo Sikonge.

Akihitimisha ziara yake katika Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Jaji Mkuu pia alipata nafasi ya kuongea na Watumishi ambapo aliongelea juu ya vipaumbele vya Mahakama katika kuboresha huduma zake, akisisitiza kuwa kila mtumishi wa Mahakama ni chachu katika kuleta mabadiliko ndani ya Mahakama, hivyo kuna haja kila mmoja kwa nafasi yake aliyopo afanye kazi kwa bidii na hatimaye kufikia lengo la kutoa huduma bora.

8

Page 9: ZIARA YA MHE. JAJI MKUU TABORA & SHINYANGA NA MALENGO YA KUIBORESHA MAHAKAMA KATIKA DHANA NZIMA YA UTOAJI HAKI NCHINI

MWISHO

9