العقيدة بالسواحلية itikadi ya kiislamu kwa lugha ya kiswahili

100
AKIDA ILIOWEPESISHWA KUTOKANA NA QUR’AN TUKUFU NA SUNNA ILIOTWAHIRIKA MTUNZI SHEKH DR.AHMAD BIN ABDULRAHMAN AL-QAADHI CHUO KIKUU CHA QASIIM KITIVO CHA AKIDA MFASIRI KHALID MUHAMMAD ALI DHAL’I UTANGULIZI WA MTUNZI Hakika sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu,twamuhimidi na twamtaka msaada na twamtaka msamaha na twajilinda kwake kutokana na shari ya nafsi zetu,kwani anaye muongoza hakuna wa kumpoteza na ampotezae hakuna wa kumuongoza. Nashuhudia ya kwamba hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila ALLAH pekee hana mshirika aliesema: َ وُ ه يِ ذَ ّ الَ ثَ عَ ب يِ فَ ن يِ ّ يِ ّ مُ ْ الً ولُ سَ رْ مُ هْ نِ م وُ لْ ( يَ يْ مِ هْ نَ لَ عِ هِ ( اتَ يَ 2 ا3 ْ مِ ه نِ ّ كَ 5 زُ يَ وُ مُ هُ مِ ّ لَ عُ بَ و3 َ ابَ ( يِ كْ ل ا3 َ ( هَ مْ كِ حْ ل اَ وْ نِ E اَ و واُ ن اَ كْ نِ مُ لْ بَ ( ق يِ فَ لٍ لَ لَ ضٍ ن يِ يُ م( 2 ) Yeye ndiye aliyeleta mtume katika watu wasiojua kusoma,awasomee aya zake na kuwatakasa na kuwafunza kitabu na hikima,(ilimu nyinginezo).Na kabla ya haya walikuwa katika upotofu(upotevu)ulio dhahiri (AL-JUMA’:2) na shuhudia ya kwamba Muhammad(swallallahu aleihi wasallam) ni mjumbe wake na ni mtume wake ambaye kwamba amewaneemesha waja wake kwa kutumilizwa kwake.Akasema : 1

Upload: abdulrahman-faris

Post on 01-Dec-2015

515 views

Category:

Documents


12 download

DESCRIPTION

Kitabu hiki kinaeleza itikadi ya dini ya kiislamu

TRANSCRIPT

AKIDA ILIOWEPESISHWA KUTOKANA NA QURAN TUKUFU NA SUNNA ILIOTWAHIRIKA

MTUNZI

SHEKH DR.AHMAD BIN ABDULRAHMAN AL-QAADHI

CHUO KIKUU CHA QASIIM

KITIVO CHA AKIDA

MFASIRI

KHALID MUHAMMAD ALI DHALI

UTANGULIZI WA MTUNZI

Hakika sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu,twamuhimidi na twamtaka msaada na twamtaka msamaha na twajilinda kwake kutokana na shari ya nafsi zetu,kwani anaye muongoza hakuna wa kumpoteza na ampotezae hakuna wa kumuongoza. Nashuhudia ya kwamba hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila ALLAH pekee hana mshirika aliesema: (2) Yeye ndiye aliyeleta mtume katika watu wasiojua kusoma,awasomee aya zake na kuwatakasa na kuwafunza kitabu na hikima,(ilimu nyinginezo).Na kabla ya haya walikuwa katika upotofu(upotevu)ulio dhahiri(AL-JUMA:2)na shuhudia ya kwamba Muhammad(swallallahu aleihi wasallam) ni mjumbe wake na ni mtume wake ambaye kwamba amewaneemesha waja wake kwa kutumilizwa kwake.Akasema:

(164)Hakika Mwenyezi Mungu amewafanyia Hisani kubwa Waislam aliowaletea Mtume miongoni mwao,anayewasomea Aya Zake,na anawatakasa na kuwafundisha kitabu na Hikima.Na bila shaka kabla ya hapo walikuwa katika upotovu ulio dhahiri (AALI IMRAN:164)Ama baada ya hayo;

Hakika Allah alimtuma mtume wake Muhammad (swallahu alaihi wa salam ) kwa uwongofu na dini ya haki ili atoe watu kutoka katika giza awapeleke katika muangaza,na kutoka katika upotevu uliowazi awapeleke katika uongofu uliotimia,uongofu wenye kukunjua nyonyo na kuleta utulivu wa nyonyo. Kwani (uongofu) ni elimu ya manufaa, na (dini ya haki) ni matendo mema, na kwa nguzo hizi mbili ndio maisha mazuri hupatikana. Na hakika amekusanya Allah katika kitabu chake kitukufu yote wanayo yahitajia waja katika akida zao, ibada zao, kutangamana kwao, tabia zao, na zikaja sunna za mtume(Sallallahu alayhi wasallam) kufafanua yaliyo tajwa kijumla, na kueleza lilofichamana na kueleza kwa upana yote yaliyoachiwa, kama alivyosema mtume(S.A.W) jueni ya kwamba hakika yangu mimi nimepewa Quran na kitu mfano wake pamoja (ambayo ni sunnah) imepokewa na Abu Daud.Akida ya kiislamu ndio nguzo ya dini hii na msingi wake, na ndio siri ya nguvu zake na ndio kudhihiri juu ya dini zote, kwa sababu akida ya kiislamu imekusanya sifa za pekee. katika hizo ni:-1.kumpwekesha Allah katika ibada na mtume (Sallallahu alayhi wasallam) kwa kumfuata.

2.kukoma yaani hatupiti Quran wala hadithi za mtume (Sallallahu alayhi wasallam)wala haiwi akida chimbuko lake ni rai wala kiasi.

3.kuafikiana na maumbile ya Mwenyezi Mungu aliowaumbia watu kabla ya kugeuzwa na shetani.

4.kuafikiana na akili iliyo wazi iliosalimika na utata na mataminio.5.iliokamilika, yaani haijawacha sehemu yoyote ya maisha ila imeifafanua.

6.iliofanana, kwani mengine husadikisha mengine na hakuna mgongano katika akida za kiislamu wala sharia zake kabisa.

7.Ukati, yaani uislamu ni dini ya uadilifu hakuna kupita mipaka na kuzidisha wala kupunguza baina ya mambo tofauti tafouti.

Na sifa hizi za akida ya kiislamu zimeleta matunda haya:-

1.kuhakikisha kwamba sote ni waja wake mola na walimwengu na kutoka katika utumwa wa viumbe.

2.Kuhakikisha kumfuata mtume(Sallallahu alayhi wasallam) wa mola wa walimwengu na kujitoa katika uzushi na wazushi.

3.Utulivu wa nafsi, na kumakinika kimoyo kwa kuwa na mahusiano na Allah muumba, mpangaji wa mambo, mwenye hikma.

4.Kukinai kifikra na kusalimika na mgongano na mambo yasiokuwa na asli.

5.Kutekeleza haja za roho na haja za mwili na kukamilishana baina ya itikadi na tabia.

Na hawaja wacha wanavyuoni kuipa akida hamu zao, na kutoa juhudi zao katika kuifundisha na kuipitisha. Mara wakieleza kiujumla akida ya wema waliopita, na mara wakieleza jambo fulani katika akida, na mara nyengine katika kuwajibu wazushi wenye kupoteza. Kwa hivyo mimi nikaonelea kuyaleta karibu katika fahamu mambo au masala ya akida,na kuyapanga kwa mpangilio wa mtume (Sallallahu alayhi wasallam)na nguzo za imani sita zilizotajwa katika hadithi ya Jibril iliyo mashuhuri, nikitegemea dalili za Quran na sunnah iliyotahirika, na nikifanya chini ya kila msingi mambo yanayo husiana nayo, pia nikitaja waliopotea katika masala hayo na kuwajibu utata wao bila ya kurefusha.

Kwa hivyo hii akida ikadhihiri kwa msimamo wa kati baina ya kurefusha na kufupisha, na ikapambanua kwa uwazi na wepesi, ili waweze waislamu kunufaika nayo, na kupatikaniwe makusudio katika kukusanya yote ambayo ni katika akida ya wema waliotangulia kwa ibara nyepesi, na mpangilio wa kimaudhui nikakiita kitabu:AKIDA ILIO WEPESISHWA KUTOKANA NA QURAN TUKUFU NA SUNNAH ILIYO TAHIRIKA.

Namuomba Allah aijaalie kazi hii ni kwa ajili yake, yenye kuwanufaisha waja wake na rehma na amani zimfikie mtume wetu Muhammad na jamaa zake na maswahaba wake wote.

Kimeandikwa na Shekh Dr. Ahmed bin AbdulrahmanAlQaadhiUnieza katika 17/2/1427

Peleka maoni katika

Barua pepe: al-aqida@al-aqida .com

Kitengo cha akida

kitivo cha sharia na msingi wa dini

unieza s.p 246 alama ya posta 51911.

UTANGULIZI WA MFASIRISifa njema zote ni za mwenyeezi mungu,muumba wa mbingu na ardhi,na swala na salamu zimfikie mtume wetu muhammad (Sallallahu alayhi wasallam) na maswahaba wake na jamaa zake wote. Akida ni somo lenye kueleza kuhusu imani yetu kwa mwenyeezi mungu,malaika wake,vitabu vyake,mitume yake,siku ya mwisho,kadari na yanayo fungamana na hayo.

Hakika akida ndio msingi wa dini,kutengezeka akida ya mtu ndio inamfanya awe mumini na apate maisha ya raha hapa duniani na mashukio yake akhera itakuwa ni peponi, ama ikiharibika akida ya mtu kwa kuingiliwa na shirki au venginevyo itapelekea mtu kutokuwa na maisha ya raha hapa duniani na akhera mashukio yake itakuwa ni motoni,kwasababu akida ni rasilmali yatu.

Kwasababu hizo zilizotangulia na kuona hali ya jamii zetu kwamba utapata waislamu wengi hawayajui mambo muhimu katika akida yao na imani yao,ujinga huu wenye kupelekea kufanya mambo yasiofaa,na kupata pengo lililokuweko katika vitabu vya akida kwa lugha ya kiswahili. Nikaona umuhimu wa kutafsiri kitabu cha akida na kuwafafanulia waislamu mambo muhimu katika dini yao katika lugha watakayo ifahamu. Vitabu vya akida viko sampuli tofauti lakini mimi nikachagua kitabu hichi kwasababu mbili;

1-Muandishi wa kitabu amekusanya mambo mingi ya Akida chini ya misingi sita ya Imani na akiwarudi mapote mapotevu katika kurasa chache.

2-Wepesi wa utunzi wake na uwazi wa ibara zake.

Hakika kazi ya kufasiri haswa kitabu cha Akida si kazi nyepesi,imenichukua mda na juhudi kubwa,lakini pamoja na udhaifu wangu nikaweza kukamilisha kazi hii,yote haya ni taufik ya ALLAH.

Kabla ya mwisho ,shukurani kwanza nawapelekea wazazi wangu walionilea malezi mema,na nawashukuru mashekhe wangu wote walioniwezesha kufika daraja hii.pia sisahau kuwashukuru ndugi zangu walioweza kunisaidia na kila alienisaidia mpaka kitabu kikafika mbele yenukatika walionipa nasaha, kunisaidia kuchapa na wengineo. Mwisho ndugu zangu waislamu,mimi ni mja mdhaifu kwahivyo ukipata makosa katika kitabu hichi usisite kunijulisha.

Ndugi yenu mdhaifu

KHALID MOHAMMAD ALI DHALI

27/6/1429

Sawa na

1/7/2008

s.p 83211

m.s.a

kenya

[email protected] AKIDA ILIOWEPESISHWA KUTOKANA NA QURAN TUKUFU NA SUNNA ILIOTAHIRIKAMsingi wa akida ya kiislamu ni kumuamini mwenyeezi mungu,na malaika wake na vitabu vyake,na mitume yake na siku ya mwisho,na kadari kheri yake na shari yake.Amesema Allah:

(177) Bali wema(hasa)ni (wa wale)wanaomwamini Mwenyezi Mungu na siku ya Mwisho na Malaika na Kitabu na Manabii(AL BAQARAH:177) Mtume Ameamini yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Mola wake,na waislam,(pia wameamini hayo):wote wamemwamini Mwenyezi Mungu,na Malaika wake,na Vitabu vyake,na Mitume yake,(AL BAQARAH:285) (136) Enyi mlioamini! Mwamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Kitabu alichokiteremsha juu ya Mtume wake,Na Vitabu alivyoteremsha zamani.Na mwenye kumkanusha Mwenyezi Mungu na Malaika wake na Vitabu vyake na Mitume wake na Siku yaMwisho,basi bila shaka amepotea upotofu(upotevu) ulio mbali(na haki). (AN NISA:136)Na akasema mtume (Sallallahualayhi wasallam) kumwambia Jibril (alaihi sallam) alipomuuliza kuhusu Imani ,Akasema Ni kumuamini mwenyezi mungu na malaika wake,na vitabu vake,na mitume yake,na siku ya mwisho,na kuamini kadari kheri yake na shari yake(yote yatoka kwake Allah)

[Imepokewa na muslim].

KUMUAMINI MWENYEEZI MUNGU

Kumuamini Allah ni kuamini kwa kukata kwamba Allah yupo,na kwamba yeye ndie mola wa kila kitu,anaestahiki kuabudiwa peke yake pasi na mwengine,aliyesifika na sifa za ukamilifu,alietakasika kutokamana na sifa za upungufu.KWANZA:KUAMINI KUWEPO KWAKE

Kuwepo kwake Allah (subhanahu wataala)ndio haki kubwaAmesema allah:

(62)Hayo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu yuko,na wale wanaowaabudu badala yake(Mwenyezi Mungu)hao ni batili,na Mwenyezi Mungu ndiye aliye juu na ndiye aliye Mkubwa(AL-HAJJ:62)Na kuwa shaka kwa kuwepo kwake Allah ni uzushi na ukanushaji,anasema Allah: (10)Mitume wao wakasema:Je!Mnamfanyia shaka Mwenyezi Mungu.Muumba wa Mbingu na Ardhi?Yeye anakuiteni akusameheni dhambi zenu na akupeni muhula mpaka muda uliowekwa.Wakasema:Hamkuwa nyinyi ila ni watu kama sisi.Mnataka tu kutuzuilia na yale waliokuwa wakiabudu babu zetu.Basi tuleteeni hoja zilizo wazi.(IBRAHIM:10)Na kukanusha kuwepo kwake Allah ni kiburi na ukafiri,Anasema Allaha: (102)

Akasema(Musa):umekwishajua kuwa hakuna aliyeteremsha(hoja)hizi isipokuwa Mola wa Mbingu na Ardhi,kuwa dalili,(ila unajibanisha tu).Na hakika mimi nakuona ,wewe Firauni umekwisha angamia(BANI ISRAIL:102).Na akasema: (28) (29) (30) (31) (32) (Musa)akasema:Yeye ndiye Mola wa Mashariki na Magharibi na vilivyomo baina yake;ikiwa hamfahamu(jambo mtafahamu hili)(28).(Firauni)akasema:kama ukishikilia (kuwa kuna) Mungu mwingine badala yangu kwa yakini nitakufanya miongoni wa wenye kufungwa gerezani(29).Akasema:Je!Ijapokuwa nitakuletea kitu kilicho wazi,(hoja zilizo wazi za kuonyesha ukweli wa utume wangu)?(30).Akasema:Kilete,akiwa ni miongoni mwa wasemao kweli(31).Basi akaitupa fimbo yake,mara ikawa nyoka dhahiri(32).(ASH-SHUARAA:28-32).Na inajulisha kuwepo kwake mambo kadhaa;katika hayo:

1:Maumbile yaliyosalimika.Amesema Allah:

(30)Basi ueleke uso wako katika dini iliyosawasawa-ndiyo umbile Mwenyezi Mungu alilowaumbia watu,(yaani dini hii ya kiislam inawafikiana barabara na umbile la binadamu).Hakuna mabadiliko katika maumbile ya viumbe vya Mwenyezi Mungu.Hiyo ndiyo dini iliyo haki,lakini watu wengi hawajui.(AR-RUM:30).Na amesema Mtume Muhammad(Swallallah alayhi wasallama):Hakuna mtoto azaliwaye ila huzaliwa katika maumbile(uislamu) kisha wazazi wake humfanya awe ni yahudi au mnasara au majusi(wenye kuabudu moto).Imepokuwa na bukheri basi kila kiumbe kinabaki katika umbile la uislamu la asili,anahisi kila mtu katika nafsi yake kuwepo kwa Mungu,ila litokezee lenye kuharibu maumbile hayo anasema Allah katika hadithi Qudusii:(Mimi nimeumba waja wangu hunafaa(wenye kumpwekesha katika ibada na kujiepusha na shirki),na hakika shaitwani aliwajia akawapotoa kutoka katika dini yao,imepokewa na muslim.

2:Akili iliowazi, anasema Allah:

(35)Je?Wameumbwa pasipo kitu,au wao ndio wamejiumba? (AT-TUR:35).Kwani akili iliosalimika kutokana na mambo ya shubha(utata) na matamanio inakubali moja kwa moja kwamba viumbe lazima viwe na muumbaji kwa sababu viumbe haviwezi kujiumba vyenyewe kwani kitu kisichikuwepo hakiwezi kufanya kitu kiwepo:basi lazima kupatikaniwe muumba aliyopo naye ni Allh(subhanahu wataala).Na ametolea ushahidi uwazi wa akili khatibu wa kiarabu wakati wa ujahiliya(Qis bin Saidah Al-Iyaad)akasema:Choo cha ngamia chajulisha kuwepo kwa ngamia na nyayo hujulisha juu ya mwendo kwani mbingu zina nyota na ardhi ni yenye njia je,hayajulishi haya juu ya Muumbaji mwenye Khibra?

3:Hisia zinaonekana,amesema Allah kuhusiana na Nabii Nuhu(Alayhi ssalamu): (10) (11) (12) (13) (14)Ndipo akamuomba Mola wake (akasema):Kwa hakika mimi nimeshindwa,basi ninusuru(10).Mara tukaifungua milango ya Mbingu kwa maji yanayomiminika(kwa nguvu kabisa)(11).Na tukazibubujisha maji chemchem zilizo katika ardhi,na maji(ya juu na chini)yakakutana kwa jambo lililokadiriwa(na Mungu)(12).Na tukamchukua(Nabii Nuhu)katika ile(Jahazi)iliyotengenezwa kwa mbao na misumari(13).Ikawa inakwenda mbele ya Macho yetu.Hii ni tunzo(tuzo)kwa aliyekuwa amekataliwa(amekanushwa)(AL-QAMAR:10-14)Na akasema:) (63 (64) (65) (66) (67)Mara tulimpelekea Wahyi Musa(Tukamwambia):Piga bahari kwa fimbo yako.Basi ikatengana kila sehemu ikawa kama jabali kubwa.(63).Na tukawaleta hapo wale watu wengine(na ni Firauni na watu wake)(64).Na tukamuokoa Musa na wale waliokuwa pamoja naye wote(65).Kisha tukawagharikisha wengine(66).Hakika katika hayo muna mazingatio;na wengi katika wao si wenye kuamini(ASH-SHUARAA:63-67)

Na akasema tena kulingamana na Nabii Isa (Alayhi wassalamu): (49)

Na(atamfanya)Mtume kwa wana wa Israili,(kuwaambia):Nimekujieni kwa hoja kutoka kwa Mola wenu,ya kwamba nakuumbieni,katika udongo,kama sura ya ndege,kisha napuliza,mara anakuwa ndege,kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.Na ninawaponesha vipofu na wenye mabalanga,na ninawafusha (baadhi ya) waliokufa,kwa idhini ya Mwenyezi Mungu,na nitakuambieni mtakavyovila na mtakavyoweka akiba katika nyumba zenu.Bila shaka katika haya imo hoja kwenu ikiwa nyinyi ni watu wa kuamini(AALLI IMRAN:49)

Na akasema kiujumla surat (An-naml:62):

(62)Au Yule anayemjibu Yule aliyedhikika amwombapo na kuondoa dhiki(yake)na kukufanyeni wenye kuendesha dunia(siyo bora?)Je,yuko Mungu pamoja na Mwenyezi Mungu?Ni kuchache kuwaidhika kwenu (AN-NAML:62).

Kwani miujiza ya Mitume na kujibu dua za waombaji na kuwaokoa wenye matatizo ni dalili za kuhisika waliyafahamu haya pote la watu kwa kushuhudia kuwepo kwa aliyewatuma na anayewajibu dua zao na muokozi wao (Allah aliyetukuka)kushuhudia kwa yakini.4:Sharia Sahihi:Amesema Allah: (82)Hawaizingatii nini,hii Qurani?Na kama ingelitoka kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu bila shaka wangalikuta ndani yake khitilafu nyingi(AN NISAA:82).

Na akasema tena: (174)Enyi watu!Imekufikieni dalili kutoka kwa Mola wenu,na tumekuteremshieni nuru iliyo dhahiri (AN NISAA:174).

Na akasema: (57)Enyi watu!Yamekujieni mawaidha kutoka kwa Mola wenu na poza la (dawa ya)yale yaliyomo vifuani,na uongofu (mkubwa)na rehema kwa wanaoamini.(Nayo ni Qurani ambayo ikifuatwa humtengenezea mtu dunia yake na akhera yake)(YUNUS:57)

Kwani yale yaliyoyakusanya Qurani kutokana na habari za Ghaibuna Akida sahihi na Sharia adilifu na tabia njema ni dalili kwamba haya yatoka kwa Allah,wala hayawezekani kutoka kwa mwingine katika viumbe,ndiyo maana hajapinga kwa hakika kuwepo kwake Allah yeyote katika wanadamu ila walitokeza baadhi ya mapote wenye kujifanyisha katika mapagani wa kale na wa sasa.Kwa mfano:

1:Wenye kushikamana na zama:wenye kusema:

(24) Je! Na walisema:Haukuwa(uhai)ila ni uhai wetu huu wa dunia,(haukuwa mwengine);tunakufa na tunaishi,wala hakuna kinachotuangamiza isipokuwa(huu huu)ulimwengu;(kwani ndiyo ada yake kufisha na kuhuisha).Lakini wao hawana ilimu ya hayo(wanayoyasema)wandhania tu(AL-JATHIYAH:24).Wakidai kwamba ulimwengu unakwenda peke yake na kwamba ulimwengu haujawacha wala hauwachi kwenda pekee yake!Na wanasema matumbo hutoa watu na ardhi humeza watu tu!Na hakuna kitu kituangamizacho ila kubadilika kwa zama (yaani upite wakati Fulani wawe watu Fulani wawe wamemaliza muda wao na wengine wakija ni hivyo hivyo,kwa hivyo mabadiliko ni ya wakati tu).Wakawaweka mbali viumbe kutokana na muumbaji wao, na Mungu aliwarudi kuwajibu hayo yao kwa kusema: (24)Lakini wao hawana ilimu ya hayo (AL-JATHIYAH:24).

Si kwa akili wala kwa dalili wala kwa hisia wala kwa maumbile bali ni dhana tu! (24)(wanayoyasema)wanadhania tu(AL-JATHIYAH:24).

2:Wenye kushikamana na Asili(nature) wenye kusema kwamba ulimwengu umepatikana kwa kitendo cha asili(maumbile) yaani dhati ya vitu katika mimea au wanyama au vitu visivyokuwa na roho na sifa zake vimejiumba vyenyewe na harakati(mienendo) zake na kuwajibu hawa ni rahisi,nayo ni kwamba haiwezekani kitu kiwe ni kiumbe na Muumbaji wakati mmoja anasema Allah: (35)Wameumbwa pasipo kitu,au wao ndio waliojiumba(52:35).

Na hayo maumbile wanayotegemea kwamba ni jumla ya vitu visivyo kuwa na harakati havisemi,wala havioni wala havisikii havina hisia yoyote basi vitawezaje kuumba viumbe hai vyenye kusikia, kuona, kuzungumza , kuhisi na vinahisi uchungu na kuwa na matarajio kwani aliyekosa kitu hawezi kutowa .

3- wenye kushikamana na sudfa,wenye kusema kwamba viumbe vilitokezea sudfa tu!kwa maana ya kwamba mkusanyiko wa vipande vya vitu na viungo vyake vilipelekea kwa njia ya sudfa kutokeza uhai na vikatengezeka viumbe tofauti tofauti bila ya mpangilio wowote uliotangulia!Madai haya yanaanguka yenyewe kwa kujaribu kuyafikiria tu!Kwani ukwasi katika kuumba na nidhamu zake za kimaumbile zilizopangika na kuendelea juu ya muondoko huo huo kwa vipimo vya sawa sawa vinakataa madai ya kwamba ulimwengu ulizuka kwa sudfa.Amesema Allah: (88)Ndiyo sanaa ya Mwenyezi Mungu,(matengenezo yake)aliyekitengeneza kila kitu(AN-NAML:85) Na akasema:

(12)Mwenyezi Mungu ni Yule ambaye aliyeziumba mbingu saba,na ardhi kuwa mfano wake wa hizo.Amri(zake)zinashuka baina yao,ili mujue kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye uweza juu ya kila kitu,na kwamba Mwenyezi Mungu amekizunguka kila kitu kukijua(vilivyo kwa ilimu yake) (AT-TALAQ:12).

4:Wakomunisti wenye kusema (hakuna Mola na maisha ni maada).

5:Watu wenye fikra za pekee katika historia kama firauni ambaye aliyesema:

(23)Firauni akasema:Na nani huyo Mola wa walimwengu? (ASH-SHUARAA:23).

Na namrudi (258)Hukumsikia Yule aliyehojiana na Ibrahim juu ya Mola wake kwa sababu Mwenyezi Mungu alimpa ufalme?Ibrahimu aliposema:Mola wangu ni Yule anayehuisha na kufisha,yeye akasema:Mimi pia nahuisha na kufisha.Ibrahimu akasema:Mwenyezi Mungu hulichomozesha jua mashariki,basi wewe lichomozeshe magharibi.Akafedheheka Yule aliyekufuru,na Mwenyezi Mungu hawaongozi watu madhalimu(AL BAQARAH:258)na hawa wanapingana na nafsi zao.Wakanyusha maumbile yao kama alivyoshuhudia Allah kwa kauli yake: Na wakazikanusha,na hali ya kuwa nafsi zao zina yakini nazo;(Kuwa ni kweli hayoaliyokuja nayo Nabii Musa.Lakini walizikanusha tu),kwa dhulima na kujivuna.Basi angalia ulikuwaje mwisho wa wafanyao ufisadi(AN-NAML:14)Ndio mana halikusimama lao la kusimama na wala halikubaki lao la kubaki.

PILI:KUAMINI UBWANA WAKE ALLAH

Nayo ni kuitakidi kwa kukata kwamba Allah pekee ndio mola,muumbaji,muamrishaji,na maana ya RABB :Ni bwana mfalme mwenye kupeleka mambo,aliewalea walimwengu wote kwa neema zake amesema Allah: (49) (50) )(Firauni)akasema:Mola wenu ni nani ewe Musa (49) .(Musa )akasema: Mola wetu ni Yule aliyekipa kila kitu umbo lake kisha akakiongoza(kufanya kinachowafiki umbo lake hilo(TA HA:49-50)

Kwahivyo kuamini ubwana wake Allah ni juu ya haya mambo matatu:

1)KUUMBA kwani Allah ameumba kila kitu,na venginevyo pasi na Allah ni viumbe,amesema Allah:

(62Mwenyezi Mungu ndiye muumba wa kila kitu na yeye ndiye mlinzi juu ya kila kitu(AZ-ZUMAR:62) na akasema: (2) Na ameumba kila kitu na akakikadiria kipimo(chake)(AL-FURQAN:2)

Na kila kitu kilichoundwa na kuvumbuliwa kikitegemezwa kwa kiumbe huwa ni kunasibisha tu!wala haimaanishi uumbaji kamili .Kwa maana kazi yake huyo muundaji ni kuweka umbo ya hicho kitu na utunzi na kukikadiria kitakuwa vipi ,lakini si kuanzisha(kutoka kuwa kitu hakuna,bali yeye anakusanya vitu vilivyokuwepo)Muanzishaji wa vitu vyote ni Allah kama ilivyo katika aya hii: (14)Basi ametukuka Mwenyezi Mungu Mbora wa waumbaji(AL-MUMINUN:14)

2)Kumiliki kwani ufalme ni wake Allah na venginevyo asiekuwa Allah ni venye kumilikiwa na Allah.

Amesema Allah:

(107) Hujui kwamba Mwenyezi Mungu ni mwenye ufalme wa mbingu na ardhi?Nanyi hamna mlinzi wala hamna msaidizi asiyekuwa Mwenyezi Mungu(AL-BAQARAH:107)

(189)Na ufalme wa mbingu na ardhi ni wa Mwenyezi Mungu,na mwenyezi Mungu ni mwenye uweza juu ya kila kitu(AALI IMRAN:189)

(26)Sema(katika kumsifu Mwenyezi Mungu):Ee Mola,uliyemiliki ufalme wote!Humpa ufalme umtakaye,na humwondolea ufalme umtakaye(AALI IMRAN:26) wala hana mshirika(wake)katika ufalme )(BANI ISRAIL:111) (13) Huyo ndiye Mwenyezi Mungu,Mola wenu,mwenye ufalme,na wale mnaowaabudu kinyume Chake,wao hawamiliki hata utando(ugozi)wa koko ya tende(FATIR:13)na kila chenye kumilikiwa kikinasibishwa kwa asiyekuwa Allah ni umilikaji usiokuwa kamili (ni kunasibishiwa)tu!Umilikaji wenye mda kama alivyosema Allah:

(29)Enyi watu wangu!Leo mna ufalme mmeshinda katika arhi(ghaafir:29)Na kama alivyosema: (3)Au(wawekeni Masuria)wale ambao mikono yenu ya kiume imewamiliki(AN NISAA:3)

Na alivyosema:

(40)Bila shaka sisi tutairithi ardhi na walio juu yake.Na Kwetu watarejeshwa (wote) (MARYAM:40)

3-Amri (kuamrisha)kwani kuamrisha ni kwa Allah na asiyekuwa yeye ni mwenye kuamrishwa,amesema Allah: (154)Sema:Mambo yote ni ya Mwenyezi Mungu(AALI IMRAN:154)Na akasema: (54) Fahamuni.kuumba ni kwake tu Mwenyewe Mwenyezi Mungu.Na amri zote ni zake (Mwenyezi Mungu).Ametukuka kabisa Mwenyezi Mungu,Mola wawalimwengu wote(AL AARAF:54)

Na akasema: (210)Na lishe (mara moja)hilo jambo(la kuadhibiwa kwao)?Na mambo yote hurudishwa kwa Mwenyezi Mungu(AL BAQARAH:210) Na akasema kumwambia mtume wake: (128)Wewe huna lako katika shauri hii(AALI IMRAN:128)Ikiwa mtume ni hivi itakuwaje kwa aliekuwa chini yake kidaraja!Na akasema:

(4)Amri ni ya Mwenyezi Mungu kabla(yake)na baada(yake);na siku hiyo Waislamu watafurahi(AR-RUM:4)

Kwani yeye Allah ndio muamrishaji wa pekee ju ya waja wake,na kuamrisha kukitegemezwa kwa mwengine kama ilivyo katika aya hii: (97)Lakini wao walifuata amri ya Firauni,na amri ya Firauni haikuwa ni yenye uongofu(HUD:97

Basi huwa ni uamrishaji usiokuwa kamili bali ni kunasibishwa tu!uamrishaji huo uko chini ya matakwa yake akitaka atapitisha amri hiyo na akitaka atazuia. Na amri yaake Allah hukusanya amri ya kisheria(kama amri yake ya swala)na amri ya kidunia(kama kifo na venginevyo),ama amri zake za kidunia huwa bila ya pingamizi(hawana hiari waja)nayo ni sawa na matakwa yake Allah,kama alivyosema Allah:

(82)Hakika amri yake anapotaka chochote(kile kitokee)ni kukiambia:Kuwa,basi mara huwa(YA-SIN:82)

Ama amri za dini huwa na hiari na kuchaguzwa(yaani Allah hapeleki kumlazimisha ila amempatia chaguo na akifata atapata pepo na akiwacha atapata adhabu)

Nazo hizo amri za dini ni sawa na mapenzi,huweza zikatokea au huweza zisitokee,na yote hayo huwa chini ya matakwa yake ,kama alivyosema:

(28) (29) Kwa Yule miongoni mwenu anyetaka kushika njia(njema)(28).Wala nyinyi hamtataka isipokuwa atake Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu wote(AT-TAKWYR:28-29) Na sifa zake zengine za ubwana wake zilizobaki zinaingia chini ya haya mambo matatu,kuumba, ufalme, na kuamrisha jambo,kama kutoa rizki, kuhuisha, kufisha, kuteremsha mvua ,kukuza mimea,kupeleka upepo, kuvipeleka vyombo vya baharini,na kupishana usiku na mchana,kushika mimba,na kumuwezesha mama kujifungua,kutoa afya,kumfanya mja mgonjwa,kuwapatia nguvu waja,na kuwapatia udhalilifu,na sifa nyenginezo.

Na huku kuamini kwa Ubwana wake ni kitu kipo kimaumbile,hukijuwa mwanadamu kwa akili,huhisika katika ulimwengu,na ushahidi wake umejaa katika sharia na katika ushahidi wake katika Quran: (164)Hakika katika kuumbwa kwa mbingu na ardhi,na (katika)kuandamizana usiku na mchana,na (katika mwendo wa) vyombo ambavyo hupita katika bahari kwa(kuchukua vitu)viwafaavyo watu,na (katika kumiminika)maji aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu kutoka mawinguni,na kwa (maji) hayo akaihuisha ardhi baada ya kufa kwake,na akaeneza humo(ulimwenguni kwa sababu ya maji hayo)kila aina ya wanyama;na katika mabadiliko ya pepo,na mawingu yanayoamrishwa kupita baina ya mbingu na ardhi,bila shaka(katika haya)zimo Ishara kwa watu wenye akili(kuwa yuko Mwenyezi Mungu na ni Mmoja tu(AL BAQARA:164)

. (27)(Wewe)huingiza usiku katika mchana(ukawa mchana mrefu siku za joto),na huuingiza mchana katika usiku(usiku ukawa mrefu siku za baridi),na hutoa aliye hai kwa Yule asiye na uhai,na hutoa mfu katika Yule aliye hai;na humpa riziki umtakaye bila hisabu(AALI IMRAN:27)

(95) (96) (97) (98) (99) Mwenyezi Mungu ndiye mpasuaji(mwoteshaji)wa mbegu na koko zikawa miti.Hutoa mzima katika maiti,naye(pia)ndiye mtoaji maiti katika mzima.Huyo ndiye Mwenyezi Mungu.Basi mnageuzwa wapi?(95).Ndiye anayepambazua mwangaza wa asubuhi;na ameufanya usiku kuwa mapumziko,na jua na mwezi kwenda kwa hisabu.Huo ndio mpimo (mtengenezo)wa Mwenye Nguvu na ajuaye(96).Na yeye ndiye aliyekuumbieni nyota ili mwongoke kwazo katika viza vya bara na bahari.Hakika tumeeleza vizuri(kila)Aya kwa (nafuu ya) watu wnaojua(97).Na Yeye ndiye aliyekuumbeni katika nafsi moja.Na pako (kwa ajili yenu)mahali pa kukaa milele.(Napo ni akhera).na mahali pa kuwekwa muda mdogo tu(napo ni duniani).Hakika tumezieleza Aya(hizi) kwa(nafuu ya)watu wanaofahamu(98).Na yeye ndiye aliyeteremsha maji kutoka mawinguni;na kwayo tunaotesha mimea ya kila kitu.Kisha tunapelekea kuchipua majani ya kijani katika(mimea)hiyo;tukatoa ndani yake punje zilizopangana.Na katika mitende(vinatoka)katika makole yake vishada vyenye kuinama(vinakaribia kufika chini kwa vilivyotia,hata vimekuwa vizito).Na anakuotesheni bustani za zabibu na zaituni na makomango,yanayofanana na yasiyofanana.Angalieni matunda yake yanapotoa na (angalieni kuiva kwake.Bila shaka katika hayo ziko hoja (kubwa)kwa watu wanaoamini (AL AN-AM:95-99) (2) (3) (4) Mwenyezi Mungu ndiye aliyeziinua Mbingu bila nguzo:mnaziona hivi.Kisha akastawi juu ya Arshi(Yake).Na akalitiisha (kwenu)jua na mwezi(akavifanya vitii).Kila kimoja kinaendelea mpaka muda uliowekwa.Yeye Ndiye anayeliendesha kila jambo.Anazipambanua Aya hizi ili mupate yakini ya kukutana na Mola wenu(2).Na ndiye aliyeitandaza ardhi na akaweka humo majabali na mito.Na katika kila matunda akafanya humo namna mbili(dume na jike).Huufunika usiku juu ya mchana(na mchana juu ya usiku).Hakika katika haya zimo Ishara(kubwa kuwa Mwenyezi Mungu yupo);kwa watu wenye kufikiri(3).Na katika ardhi muna vipande vinavyoungana(na kuzaa kwake namna mbalimbali),na muna mabustani ya mizabibu,na mimea mingine,na mitende ichipuayo katika shina moja na isiyochipua katika shina moja.Vyote vinanoshelezwa(vinamiminiwa)maji yale yale;na tunavifanya bora badhi yake vyengine katika kula(utamu).Hakika katika haya zimo ishara kwa watu manaotia mambo akilini(AR RAAD:2-4)

(3) (4) (5) (6) (7) (8) (9) (10) (11) (12) (13) (14) (15) (16) (17) (18) Ameziumba mbingu na ardhi kwa (ajili ya kudhihirisha) haki;na ametukuka na ushirikina wao(hao makafiri)(3).Amemuumba mwanadamu kwa tone la manii.Tahamaki amekuwa mshindani dhahiri(wa kumkataa Mwenyezi Mungu)(4).Na (pia) amewaumba wanyama.Katika hao mnapata(vifaa vitiavyoa)joto na manufaa(mengine);na wengine mnawala(5).Na mnaona raha mnapowarudisha jioni na mnapowapeleka malishoni asubuhi(6).Na(wanyama hao pia)hubeba mizigo yenu kupeleka miji msiyoweza kuifika isipokuwa kwa mashaka na taabu.Hakika Mola wenu ni Mpole sana(na)Mwenye Rehema nyingi(7).Na (amewaumba Farasi na Nyumbu na punda ili muwapande na(wawe)mapambo.Na ataumba (vipando vyegine)msivyovijua.(Nayo ndiyo haya mamotokari,meli,ma....)(8).Na ni juu ya Mwenyezi Mungu (kuonyesha) njia (iliyo sawa).Na ziko(nyingine zisizo sawa).(basi nyinyi fuateni hiyo njia ya sawa anyokuonyesheni Mwenyezi Mungu).Na kama angalipenda bila shaka angali kuongozeni nyinyi nyote(mkitaka msitake.Lakini kakupeni huria ya kuchaguaa mtakalo)(9).Yeye ndiye anayekuteremshieni maji kutoka mawinguni;kwa hayo mnapata kinywaji,na kwa hayo (inatoa) mimea ambayo humo mnalisha (wanyama)(10).(Na kwa hayo) hukuotesheeni mimea(ya kila namna)na mizeituni na mitende na mizabibu na kila matunda.na bila shaka katika hayo imo ishara kwa watu wenye kufikiri(kuwa yuko Mwenyezi Mungu)(11).Na amekutiishieni usiku na mchana .na jua na mwezi.(vyote vimeumbwa kwa ajili ya maslaha yenu).Na (pia)nyota zimetiishwa kwa amri yake.Hakika katika hayo zimo ishara kwa watu wenye akili(12).Na (akakuumbieni) hivi alivyovitawanya katika ardhi vya rangi mbali mbali.Hakika katika hayo zimo Ishara kwa watu wanaosikia mawaidha(13).Na yeye ndiye aliyetiisha bahari ili humo mule daima kitoweo kipya(samaki),na mutoe humo mapambo mnayoyavaa(ya lulu na marijani na yaliyo kama haya).na utaona marikebu zikipasua humo,ili mtafute fadhila zake(kwa kufanya biashara)na ili mupate kushukuru(14).Na akaweka katika ardhi milima il(ardhi)isiyumbeyumbe nanyi.Na (akaweka)mito na mabara ili mpate kuongoza(njia mnazozitaka)(15).Na(ameziweka)alama zingine.Na kwa nyota(pia)wao wanafuata njia(16).Ati,yule anayeumba(naye ni Mwenyezi Mungu)atakuwa sawa na wale wasiyoumba?Je hamkumbuki?(17).Na mkihesabu neema za Mwenyezi Mungu hamtaweza kuzihisabu.Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe(na)Mwingi wa kurehemu(AN NAHL:3-18) (11 (12)) (13) (14) (15) (16) (17) (18) (19) (20) (21) (22) Ambao watarithi pepo;wakae humo milele(11).Na kwa yakini tulimuumba mwanadamu kwa udongo ulio safi(12).Kisha tukamuumba kwa tone la manii,(mbegu ya uzazi)lililowekwa katika makao yaliyohifadhika(13).Kisha tukalifanya tone hilo kuwa pande la damu,na tukalifanya pande la damu hilo kuwa pande la nyama,kisha tukalifanya pande la nyama hilo kuwa mifupa,na mifupa tukaivika nyama,kisha tukamfanya kiumbe kingine.Basi ametukuka Mwenyezi Mungu Mbora wa Waumbaji(14).Kisha hakika nyinyi baada ya hayo ni wenye kufa(15).Kisha hakika nyinyi siku ya kiama mtafufuliwa(16).Na kwa yakini tuliziumba juu yenu njia,(mbingu)saba.Nasi hatukuwa kwa (hivi) viumbe (vyetu) ni wenye kughafilika(17).Na tumeteremsha kutoka mawinguni maji kwa kiasi,na tukayatuliza ardhini,(tukayahifadhi ndani ya ardhi).Na bila shaka sisi ni wenye uweza wa kuyaondoa(18).Kwa maji hayo tukakufanyieni bustani za mitende na mizabibu;mnapata humo matunda mengi,na katika hayo mnakula(19).Na (kwa hayo akakufanyieni vile vile)mti utokao katika mlima wa Sinai,unatoa mafuta na kuwa kitoweleo kwa walao.(nao ni mzaituni)(20).Na hakika mnayo mazingatio makubwa katika wanyama:Tunakunywesheni katika vile vilivyomo matumboni mwao,na mnapata katika hao manufaa mengi,na baadhi yao mnawala(21).Na juu yao na juu ya marikabu mnabebwa(AL-MUMINUN:11-22)

(43) (44) (45) Je,huoni kuwa Mungu anayaendesha mawingu,kisha huyaambatanisha pamoja, kisha huyafanya mirundo?Basi utaona mvua ikitoka katikati yake;Naye huteremsha-kutoka juu katika milima ya mawingu-mvua ya mawe,akamsibisha naye amtakaye na kumuepusha nayo amtakaye;hukurubia mwanga wa umeme wake kupofoa macho(43).Mwenyezi Mungu hubadiisha usiku na mchana;(baada ya mchana ukaja usiku na baada ya usiku ukaja mchana);bila shaka katika hayo imo dalili kwa wenye busara(ya kuonyesha hikima ya Mwenyezi Mungu)(44).Na Mwenyezi Mungu amemuumba kila mnyama kwa maji(maji ndiyo asili ya viumbe vyote).Wengine katika hao huenda kwa matumbo yao,na wengine wao huenda kwa miguu miwili,na wengine wao huenda kwa mine;Mwenyezi Mungu huumba ayatakayo.Hakika Mwenyezi Mungu Anao uweza juu ya kila kitu(AN-NUR:43-45)

(45) (46) (47) (48) (49) (50) (51) (52) (53) (54) Jee,hukuona Mola wako jinsi alivyokitandaza kivuli?Na angalitaka bila shaka angekifanya kitulie tuli,(hakipunguki hakiongezeki);kisha tumelifanya jua liwe dalili juu yake(45).Kisha tunakivulia kwenu kidogo kidogo (mpaka kinaondoka kabisa)(46).Naye ndiye aliyekufanyieni usiku kuwa nguo(la kukugubikeni),na usingizi kuwa kama kufa,na akaufanya mchana uwe ndiyo kama kufufuka(47).Naye ndiye azitumaye pepo kuwa habari njema kabla ya(kufika) Rehema yake(ya mvua);na tunayateremsha kutoka mawinguni maji safi(kabisa)(48).Ili kwa hayo tuihuishe nchi iliyokufa na tuwanyweshe baadhi ya tuliowaumba;(nao ni)wanyama na watu wengi(49).Na kwa yakini tunaigawa (hii mvua)baina yao(mara kwa mara)ili wakumbuke;lakini watu wengi wanakataa ila kukufuru tu(50).Na kama tungetaka tungewapelekea katika kila mji muonyaji wao).(Lakini tumemleta Nabii Muhammad kwa watu wote)(51).Basi usiwatii makafiri,na ushindane nao kwa(Quran)hii mashindano makubwa(52).Naye (mwenyezi Mungu)Ndiye anayeziunganisha bahari mbili;hii ni tamu,inayoondosha kiu,nahii ni yenye chumvi,kali;na akaweka kinga kati yao na kizuizi kizuiacho(zisiharibiane ila pale kiasi cha kukutana tu)(53).Naye ndiye aliyeumba mwanadamu kwa maji,kisha akamfanyia nasaba(ya damu) na ujamaa wa ndoa.Na Mola wako ni Mwenye uweza(wa kila jambo)(AL-FURQAN:45-54) (17) (18) (19) (20) (21) (22) (23) (24) (25) (26) (27) Basi mtukuzeni Mwenyezi Mungu mnapoingia katika nyakati za usiku(kwa kusali Magharibi na Isha)na mnapoingia katika asubuhi(kwa kusali sala ya alfajiri)(17).Na sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu mbinguni na ardhini.Na (mtukuzeni)wakati wa alasiri na mnapoingia wakati wa Adhuhuri(18).Hukitoa kilicho hai katika kilicho kufa,na hukitoa kilicho kufa katika kilicho hai,na huihuisha ardhi baada ya kufa kwake.Na hivyo ndivyo mtakavyofufuliwa(19).Na katika Ishara zake(za kuonyesha uweza wake)ni huku kukuumbieni kwa udongo,kisha mumekuwa watu mnaoenea(kila mahali)(20).Na katika Ishara zake(za kuonyesha ihsani zake juu yenu)ni kuwa amekuumbieni wake zenu katika jinsi yenu ili mupate utulivu kwao,naye amejaalia mapenzi huruma baina yenu.Bila shaka katika haya zimo Ishara kwa watu wanaofikiri(21).Na katika Ishara zake(za kuonyesha uweza wake)ni kuumba mbingu na ardhi,na kukhitalifiana lugha zenu na rangi zenu na(mengine yenu,na hali ya kuwa muumbaji ni Huyo Huyo Mmoja).Kwa yakini katika haya zimo Ishara kwa wenye ujuzi(22).Na katika Ishara zake(za kuonyesha hikima yake) ni kulala kwenu usiku na (kuamka) mchana,na kutafuta kwenu fadhila Yake.Hakika katika hayo zimo Ishara kwa watu wanaosikia(23).Na katika Ishara Zake(za kuonyesha nguvu zake) ni kukuonyesheni umeme kwa (kukutieni)hofu na tamaa ya(kuja mvua),na kuyateremsha (hayo) maji kutoka mawinguni,kwayo huifufua ardhi baada ya kufa kwake.Bila shaka katika haya Zimo Ishara kwa watu wanaofahamu(24).Na katika Ishara zake (za kuonyesha uweza wake)ni kuwa mbingu na ardhi zimesimama kwa amri yake;kisha atakapokuiteni wito mmoja tu,(nyote) mtatoka ardhini(25).(Vyote) vilivyomo mbinguni na ardhini ni vyake,na vyote humtii yeye(26).Na yeye ndiye aliyevianzisha viumbe na ndiye atakayevirudisha(mara nyingine)na (jambo) hili ni rahisi zaidi kwake;na ndiye mwenye sifa nzuri mbinguni na katika ardhi,na ndiye Mwenye Nguvu,Mwenye Hikima (AR-RUM:17-27) (1) (2) (3) (4) (5) (6) (7) (8) (9) (10) (11) (12) (13) (14) (15) (16) (17) (18) (19) (20) (21) (22) (23) (24) (25) (Mwenyezi Mungu) Mwingi wa rehema(1).Amemfundisha Qurani(2).Amemuumba mwanadamu(3).Akamfundisha kunena(4).Jua na mwezi(huwenda) kwa hisabu(yake)(5).Na miti midogo na mikubwa yote inamnyenyekea(Mwenyezi Mungu) (6) .Na mbingu amezinyanyua juu na ameweka uadilifu(insafu)(7).Ili msidhulumu katika kupima (na mengineyo)(8).Basi pimeni kipimo kwa haki wala msipunguze mizani(9).Na ardhi ameiweka(ameitandaza) kwa ajili ya viumbe(10).Humo yamo matunda na mitende yenye matunda(mafumba)(11).Na vimo vyakula vilivyo punje punje zenye makapi,na mimea yenye harufu nzuri(12).Basi nyinyi viumbe namna mbili-(binadamu na majini)-ipi katika neema ya Mola wenu mnayoikanusha(kuwa si neema yake)?(13).Amemuumba mtu kwa udongo wa mfinyanzi(utoao sauti) kama vyombo vya udongo(14).Na akawaumba majini kwa ulimi wa moto(15).Basi ipi katika neema ya Mola wenu mnayoikanusha (kuwa si neema yake)?(16).Mola wa mashariki mbili na Mola wa magharibi mbili(17). Basi ipi katika neema ya Mola wenu mnayoikanusha (kuwa si neema yake)?(18).Anazikutanisha bahari mbili(ya maji ya chumvi na ya maji ya tamu)(19).Baina yao kuna kizuizi,haziingiliani(zikaharibiana kabisa kabisa)(20). Basi ipi katika neema ya Mola wenu mnayoikanusha (kuwa si neema yake)?(21).Katika hizo bahari mbili hutoka lulu na marijani(22). Basi ipi katika neema ya Mola wenu mnayoikanusha (kuwa si neema yake)?(23).Na yako katika Amri Yake haya yaliyotengenezwa yakawa yanakwenda baharini;utadhani milima(24). Basi ipi katika neema ya Mola wenu mnayoikanusha (kuwa si neema yake)? (AR-RAHMAN:1-25) (6) (7) (8) (9) (10) (11) (12) (13) (14) (15) (16)Je!Hatukuifanya ardhi kuwa tandiko?(6).Na milima kuwa kama vigingi(vya ardhi)(7).Na tukakuumbeni wanaume na wanawake(8).Na tukaufanya usingizi wenu kama kufa(9).Na tukaufanya usiku kama nguo (mnalofunikwa)(10).Na tukaufanya mchana kama kufufuka(11).Na tukajenga juu yenu (mbingu) saba madhubuti(12).Na tukaifanya taa ingarayo na yenye joto kubwa(13).Na tukateremsha maji yaangukayo kwa kasi kutoka mawinguni(14).Ili kwayo Tuoteshe (vyakula vilivyo) chembe chembe na mimea(mengine)(15).Na mabustani yenye miti iliyosongana.(Basi sisi tuliofanya yote haya inatushinda kufufua viumbe?) (AN-NABAA:6-16) (27) (28) (29) (30) (31) (32) (33) Je,nyinyi ni wenye umbo la nguvu zaidi au mbingu?Yeye amezijenga.(27).Akainua kimo chake na akazitengeneza vizuri(28).Na akautia giza usiku wake na akautokezesha mchana wake(29).Na ardhi baada ya hayo Akaitandaza(30).Akatoa ndani yake maji yake na malisho yake(31).Na milima akaisimamisha(32).(kafanya haya yote) kwa ajili ya kuwastarehesheni nyinyi na wanyama wenu.(Basi aliyefanya yote haya si muweza wa kufufua?)(AN-NAZIAT:27-33

(24) (25) (26) (27) (28) (29) (30) (31) (32)Hebu mwanadamu na atazame chakula chake(24).Hakika sisi tume mimina maji kwa nguvu(kutoka mawinguni)(25).Tena tukaipasua pasua ardhi(26).Kisha tukaotesha humo(vyakula vilivyo) chembe chembe(27).Na mizabibu na mboga(28).Na mizeituni na mitende(29).Na mabustani,(mashamba) yenye miti iliyosongana bara bara(30).Na matunda na malisho(31).Kwa ajili ya kukustarehesheni nyinyi na wanyama wenu(32).(ABASA:24-32) Na jumla ya wanaadamu ni wenye kukubali ubwana wake Allah,kwamba yeye ni muumbaji ,mfalme,mpangaji wa mambo.Hata washirikina wakiarabu (makureshi) Mwenyeezimungu ameelezea kukubali kwao kwa ubwana wake,katika sehemu kadha wa kadha katika Quran,kama alivyosema: (84) (85) (86) (87) (88) (89) Sema:Ni ya nani ardhi na vilivyomo ndani yake,kama nyinyi mnajua kitu?(84).Watasema:Ni ya Mwenyezi Mungu.Sema:Basi je,hamkumbuki(kuwa Mwenyezi Mungu ni muweza?(85).Sema:Ni nani Mola wa mbingu saba na Mola wa Arshi kuu?(86).Watasema:Ni vya Mwenyezi Mungu.Sema:Basi je,hamumuogopi?(87).Sema:Ni nani mkononi Mwake umo ufalme wa kila kitu,Naye ndiye alindaye,na hakilindwi (chochote) Kinyume Naye,kama mnajua(jambo nambieni hili)(88).Watasema:(Uweza huo) ni wa Mwenyezi Mungu.Sema:Basi vipi mnadanganywa(na shetani mkadanganyika?(AL-MUMINUN:84-89)

Na kama alivyosema:

(9)Na ukiwauliza:Ni nani aliyeziumba mbingu na ardhi?Kwa yakini watasema:Ameziumba (Mwenyezi Mungu)-Mwenye nguvu,Mjuzi(AZ-ZUKHRUF:9),Ila kulitokea upotevu katika baadhi ya vipote tofauti tofauti ambavyo walishirikisha katika Ubwana wake,mfano;1-Thanawi na Maanawiya katika majusi wenye kusema kwamba Ulimwengu una waumbaji wawili ,mungu wa muangaza mwenye kuumba kheri,na mungu wa giza-mwenye kuumba shari,na haya mapote wanakubaliana kwamba muangaza ni bora kuliko giza , lakini wanatafautiana katika giza ,Jee ni la tangu?au limezuka?

2-pili wakristo wenye kusema waungu watatu, wanamfanya mungu mmoja ni misingi mitatu kwa madai yao;baba,mwana ,roho mtakatifu.3-Baadhi ya washirikina wakiarabu (wakati wa ujahiliya),wakiitakidi kwamba waungu wao wanaweza kuleta manufaa Fulani au madhara Fulani,au ni wenye kupanga mambo Fulani .

4-kadaria wakanushaji wa kadari, wenye kusema kwamba mwanadamu yuwaumba vitendo vyake,mwenyewe bila ya uumbaji wa Allah.

Na upotevu wote ni wenye kupingwa na hoja za kimaumbile ,kiakili,kwa hisia,na za kisharia na kwamba hoja hizi zinathibitisha upweke wake Allah (alietukuka ) katika kuumba,kumiliki,na kuamrisha.Amesema Allah: (91)Mwenyezi Mungu hakujipatishia mtoto wala hakuwa pamoja Naye Mungu (mwingine) . Ingekuwa hivyo basi kila mungu angaliwachukua aliowaumba;na baadhi yao wangaliwashinda wengine(kwani lazima wangepigana kwani fahali wawili hawakai zizi moja).Mwenyezi Mungu ameepukana na sifa wanazomsifu(nazo,zisizokuwa ndizo)(AL-MUMINUN:91)Kwani mola wa haki lazima awe muumbaji mtendaji atakalo,na lau kama angekua na mshirika angekuwa huyo mshirika pia akiumba na akifanya!na lingekua moja katika mawili;*Ima kila Mungu angeenda na viumbe wake na awe peke yake katika ufalme wake na uwezekano huu wakataliwa na mpangilio wa ulimwengu ulivyo.

*Na ima ingetokea kushindana na kutawala juu ya mwengine, kama mmoja ataka mwili ushughulike na mwengine ataka mwili utulie, angetaka mmoja ahuishe kitu na mwengine ataka akifishe, basi ima yatokee matakwa yote yao mawili au ya mmoja wao au yasitokee ya wote, na uwezekano wa kwanza na wa tatu haiwezekani kwa sababu ni kinyume,, hayawezi kukusanyika wala kuondoka, basi lazima itokee uwezekano wa pili (nao ni kutokea matakwa ya mmoja wao) na yule ambaye yatatokea matakwa yake basi yeye ndie Mungu mwenye uweza na mwengine hafai kupata uungu basi haya yanapelekea kuthibitisha Mungu mmoja na muumbaji mmoja na mfalme mmoja na mpangaji wa mambo mmoja.

Tatu: kuamini uola wake Allah: nayo ni kuitakidi kwa kukata kwamba Mwenyezi Mungu ndio mola wa haki anayesthiki ibada pekee pasi na mwengine.Na maana ya ILLAH mola yaani ni mwenye kuabudiwa ambae nyoyo zinamfanya mungu kwa mahaba na kumtukuza. Na hakika ya ibada ni ukamilifu wa mapenzi kwa Allah pamoja na ukamilifu wa kujidhalilisha kwake na kunyenyekea na kumtukuza na haya yote hayawi ila kwa Allah pekee na imekuja imani hii kwa shahada kubwa kutona na kwa Allah ( mkubwa mwenye kushuhudia) kwa kikubwa kishuhudiwacho amesema Allah: (18)Mwenyezi Mungu ameshuhudia ya kwamba hakuna aabudiwaye kwa haki ila yeye tu.Na malaika na wenye elimu,(wote wameshuhudia hayo);(Yeye) Ndiye Mwenye kusimamisha uadilifu.Hakuna aabudiwaye kwa haki isipokuwa Yeye,Mwenye nguvu(na) Mwenye hikima(AALI IMRAN:18)Na akasema:

(163)Na Mungu wenu ni Mungu mmoja tu,hakuna anayestahiki kuabudiwa ila Yeye ambaye ni Mwingi wa rehma mwenye kurehemu(AL BAQARAH:163)Na hakika ameumba Allah viumbe vyake vyote, kwa ajili ya kumuabudu yeye pamoja ya kwamba Mwenyezi Mungu amejitosha nao (hahitaji chochote kutoka kwa viumbe) amesema Allah:

(56) (57)Sikuwaumba majini na watu ila wapate kuniabudu(56).Sitaki kwao riziki wala Sitaki wanilishe( ADH-DHAARIYAT:56-57)

Na Allah ametuma mitume yake yote kwa watu ili waitikie imani hii,na wawalinganie watu katika kumpwekesha katika ibada na kuondoa shirki amesema Allah:

(36)Na bila shaka tulimpeleka Mtume katika kila uma ya kwambaMuabuduni Mwenyezi Mungu na mwepukeni (Ibilisi) muovu.Basi wako miongoni mwao ambao Mwenyezi Mungu amewaokoa,na wako miongoni mwao ambao upotofu(upotevu) umethubutu juu yao.Basi tembeeni katika ardhi na mwangalie ulikuwaje mwisho wa wale waliokadhibisha(AN NAHAL:36)Wakaanza kuwalingania jamaa zao kwa kusema: (75)Wakasema wakuu wa kaumu yake waliotakabari,kuwaambia wale walio dhaifu wenye kuamini miongoni mwao:Je,?Mnaitakidi ya kwamba Saleh ametumwa(amepewa Utume) na Mola wake?Wakasema:Hakika tunayaamini yale aliyotumwa(kuyafikisha)(AL AARAF:75)Na akasema Allah:

(25) Na hatukumtuma kabla yako Mtume yoyote ila tulimfunulia ya kwamba hakuna aabudiwaye ila Mimi.basi Niabuduni(AL-ANBIYAA:25)Na kupatikaniwa hili (kumpwekeshea Allah ibada) inalazimu kumfanyia Allah sampuli zote za ibada yeye pekee, na yoyote atakae fanya ibada yoyote kwa mwengine asie kuwa Allah basi huyo atakuwa mshirikina na atakuwa kafiri.Nazo hizo ibada ziko sampuli tofauti:

1.Ibada za kimoyo; kama mapenzi, amesema Allah:

(165)Na katika watu kuna wanaofanya waungu wasiyekuwa Mwenyezi Mungu.Wanawapenda kumpenda Mwenyezi Mungu.Lakini walioamini wanampenda Mwenyezi Mungu zaidi sana.Na laiti waliodhulumu nafsi zao wanaijua(balaa watakayoipata) watakapoiona adhabu(siku hiyo ya Kiyama),kwa kuwa nguvu zote ni za Mwenyezi Mungu(siku hiyo-hakuna masanamu wa kuwashufaia wala mengineyo)na kuwa Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu(AL BAQARAH:165)Na kuogopa amesema Allah:

(175)Basi msiwuogope;bali niogopeni Mimi mkiwa waislamu(kweli)(AALI IMRAN:175)Na kutaraji amesema Allah: (110)Waambie:Bila shaka mimi ni binadamu kama nyinyi (isipokuwa nimeletewa wahyi tu,ndiyo tafauti yangu).Ninaletewa wahyi ya kwamba Mungu wenu ni Mungu Mmoja tu.Anayependa kukutana na (jaza ya) Mola wake na basi afanye vitendo vizuri wala asimshirikishe yoyote katika ibada ya Mola wake(AL-KAHF:110)Na kutegemea kwake Allah: (23)Na tegemeeni juu ya Mwenyezi Mungu ikiwa nyinyi ni wenye kuamini(AL MAIDA:23)

Na uzuri wa moyo ndio asili ya uzuri wa mwili kama ilivyokuja katika hadithi ((Juweni na kutanabahi! Ya kwamba katika mwili kuna kipande cha nyama kikitengenea (kikiwa kizuri) umetengenea mwili wote na kikiharibika umeharibika mwili wote. Juweni! Kipande hicho ni moyo)) (Bukhari na Muslim).

2.Ibada za kauli( zenye kutekelezwa na ulimi), zenye kutamkwa,kama dua amesema Allah:

(18)Na kwa hakika misikiti (yote) ni ya Mwenyezi Mungu,basi msimuabudu yoyote pamoja na Mwenyezi Mungu(AL-JINN:18) Na kutaka kuhifadhiwa amesema Allah: (1)Sema:Ninajikinga kwa Mola wa ulimwengu wote(FALAQ:1)

(1)

Sema:Ninajikinga kwa Bwana Mwenye kuwalea watu(NAAS:1)Na kutaka kuokolewa amesema Allah: (9)(Kumbukeni) mlipokuwa mkiomba msaada kwa Mola wenu,naye akakujibuni kuwa:Kwa yakini mimi nitakusaidieni kwa Malaika elfu moja watakaofuata mfululizo(wanaongezeka tu). (AL ANFAL:9)

3.Ibada za kimwili kama swala ,kuchinja, amesema Allah: (162)Sema:Hakika sala yangu, na Ibada zangu(zote nyingine) na uzima wangu,na kufa kwangu;(zote)ni kwa Mwenyezi Mungu.Muumba wa walimwengu wote.(Likinisibu jambo limenisibu kwa kutaka Mwenyezi Mungu si kwa kutaka viumbe vyake.Na yote ninayoyafanya nayafanya kwa ajili yake (AL AN-AM:162) (2)Basi Sali kwa ajili ya Mola wake na uchinje(kwa ajili ya Mola wako).(Na kila utakalolifanya lifanye kwa ajili ya Mola wako,siyo mizimu wala mapango wala makaburi)(KAWTHAR:2)4-Ibada za mali kama kutoa kwa ajili ya ibada,kama zaka swadaka,nyasia,wakfu ,vipoa,(zawadi ambazo mtu anatoa) amesema Allah: (99)Na katika Mabedui hao wako wanaomuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho,na wanaitakidi kuwa wanayoyatoa ndiyo(sababu ya) kuwasogeza kwa Mwenyezi Mungu,na za (kupatia) Dua ya Mtume.Sikieni!Ni hakika hayo (kweli kuwa ni) mambo ya kuwasogeza kwa Mwenyezi Mungu .Mwenyezi Mungu atawaingiza katika Rehema Yake.Bila shaka Mwenyezi Mungu ni mwingi wa kusamehe (na) Mwingi wa Kurehemu(AT TAWBA:99) Na kulisha chakula amesema Allah: (8) (9) Na huwalisha chakula masikini,mayatima na wafungwa,na hali ya kuwa wenyewe wanakipenda(chakula hicho)(8).(Husema wenyewe katika nyoyo zao wanapowapa chakula hicho):Tunakulisheni kwa ajili ya kutaka radhi za Mwenywzi Mungu (tu) hatutaki kwenu malipo wala shukurani(AD-DAHR:8-9) Na kuamini kwa uola wake Allah inalazimu kuamini ubwana wake na yanayokusanywa na hayo.kwani yule anayekubali kwamba Mwenyeezimungu ndio muumbaji mfalme mpangaji wa mambo lazima akubali uola wake na ampwekeshe katika ibada.Na hoja hii aliisimamisha mwenyeezimungu kwa washirikina kwa kukubali kwao ubwana wake na kukataa uola wake,katika sehemu tofauti tofauti katika kitabu chake Allah:mfano (21) (22)Enyi watu!Mwabuduni Mola wenu ambaye amekuumbeni nyinyi na wale wa kabla yenu,ili mpate kuokoka(21).(Mwenyezi Mungu) ambaye Amekufanyieni hii ardhi kuwa kama busati(mliotandikiwa mstarehe),na mbingu kuwa kama paa,na akateremsha maji kutoka mawinguni,na kwa hayo Akatoa matunda yawe riziki kwenu.Basi msimfanyizie Mwenyezi Mungu washirika,na hali nyinyi mnajua(kuwa hana mshirika)(AL BAQARAH:21-22) na akasema:) (31) (32)Sema:Ni nani anayekuruzukuni kutoka mbinguni (kwa kuleta mvua) na katika ardhi (kwa kuotesha mimea)?Au ni nani anayemiliki masikio(yenu) na macho(yenu)?Na nani amtoaye mzima katika wafu na kumtoa mfu katika mzima?Na nani atengezaye mambo yote? Watasema:Ni Mwenyezi Mungu.Basi sema:Je!Hamuogopi?(Mnawaabudu wengine pamoja naye)!(31).Basi huyo ndiye Mwenyezi Mungu,Mola wenu wa haki.Na ni nini kiko baada ya (kuacha) haki,isipokuwa upotofu(upotovu)?Basi mnageuzwa wapi?(YUNUS:31-32

NA AKASEMA:

(59) (60) (62) (63) (64) Sema:Sifa njema ni za Mwenyezi Mungu,na amani iwaendee watumwa wake aliowachagua.Je,Mwenyezi Mungu ni Bora au wale wanaowashirikisha(na Mwenyezi Mungu ndiyo Bora)?(59).Au Yule aliyeziumba mbingu na ardhi,na akakuteremshieni maji kutoka mawinguni(siye bora?).Na kwa hayo tukaziotesha bustani zenye kupendeza(mashamba yenye kupendeza).Nyinyi hamna uweza wa kuiotesha miti Yake hii.Je,yuko Mungu mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu?Bali hao(makafiri) ni watu wenye kwenda upogo,(kwenda upande)(60).Au Yule aliyefanya ardhi kuwa mahali matulio(yenu),na akaweka ndani yake mito na akaiweka milima,na akaweka kizuizi baina ya bahari mbili,(bahari ya tamu na bahari ya chumvi,siye bora?).Je,yuko mungu pamoja na Mwenyezi Mungu?Basi wengi katika wao hawajui(jambo,wanajifuatia ovyo ovyo tu)(61).Au Yule anayemjibu Yule aliyedhikika amwombapo na kuondoa dhiki (yake) na kukufanyeni wenye kuendesha dunia (siye bora?).Je,yuko mungu pamoja na Mwenyezi Mungu?Ni kuchache kuwaidhika kwenu(62).Au Yule anayekuongozeni katika giza la bara na bahari,na azipelekae pepo kuleta habari njema kabla ya Rehema Zake,(kabla ya kuja mvua,siye bora?).Je,yuko mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Mwenyezi Mungu ametakasika na hao wanaowashikirikisha naye(63).Au Yule aliyeanzisha viumbe,kisha atavirudisha,na anayekuruzukuni kutoka mbinguni na kwenye ardhi, (siye bora?)Je,yuko mungu pamoja na Mwenyezi Mungu?Sema:Leteni dalili zenu ikiwa mnasema kweli (kuwa yuko mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu).(AN-NAML:59-64) Kwahivyo Allah akawasimamishia hoja kwa kukubali kwao kumpwekesha Allah katika ubwana wake na kukataa kumpwekesha katika uola wake.Pia mwenyeezimungu akavunja uungu wa wola wao kwasababu hawasifiki na sifa zozote katika sifa za ubwana(kama kuumba,kutoa rizki na sifa nyenginezo) Amesema Allah:

(191) (192)) (193) (194) (195) (196) (197) (198Wanawashirikisha (na mungu) wale ambao hawaumbi kitu,hali wao wameumbwa?(191).Wala hawawezi kuwasaidia(hao wanaowaabudu),wala hawawezi kujisaidia (wenyewe) nafsi zako?(192).Na kama hao (mnaowashirikisha na Mwenyezi Mungu) mkiwaita katika uongofu hawatakufuateni(kwani hawasiki lolote wala hawatambuichochote).Ni mamoja kwenu ikiwa mtawaita au mtanyamaza kimya(hawana habari hawana lao jambo)(193).Hakika wale mnaowaabudu badala ya Mwenyezi Mungu ni waja(watumwa) kama nyinyi(bali nyinyi bora zaidi kuliko wao.Nyinyi mna midomo ya kusemea,wao hawana).Hebu waiteni,nao wakuiteni,ikiwa mnasema kweli(kama wao ni bora na wanayo haya)(194).(Nyinyi mna miguu ya kwendea).Je,wao wana miguu ya kwendea?Au wanayo mikono ya kushikia?Au wanayo macho ya kuonea?Au wanayo masikio ya kusikilizia?Sema Nabii Muhammad uwaambie washirikina hawa): Waiteni hao mnaowashirikisha na Mungu kisha nifanyieni kila vitimbi(vya kuniangamiza) wala ,msinipe nafasi yoyote(mara moja niangamizeni kama kweli wanaweza). (195).Mlinzi wangu wa(kunihifadhi) ni Mwenyezi Mungu Aliteremsha kitabu(hiki kitukufu),naye ndiye awalindae wafanyao wema(wote,si mimi tu).(196).Na wale mnaowaabudu badala yake hawana uweza wa kukunusuruni wala wa kujinusuru (wenyewe) nafsi zao(197).Na kama mkiwaita katika uongofu hawasikii;na unawaona wanakutazama,lakini hawaoni.(masanamu utayaona yamekodoa macho lakini kuona hapana)(AL AARAF:191-198)Na akasema: (3) Na badala ya Mwenyezi mungu (wa haki),(wale makafiri) wameshika miungu ambao hawaumbi chochote ila wao ndio walioumbwa,wala hawajimilikii(kujiondoshea)

dhara wala(kujivutia)nafuu,wala hawamiliki mauti (kufisha)wala uhai wala kufufua(alfurqan-3)na akasema:

( 22( (23)Sema:Waiteni mnaowadai uungu kinyume cha Mwenyezi Mungu ;(wakusaidieni;hawawezi kukusaidieni kitu);hawamiliki(hata) uzito wa mdudu chungu mbinguni wala ardhini,wala hawana ushirika(wa Mungu);katika hizo(mbingu wala ardhi);wala Yeye hana msaidizi miongoni mwao(22).Wala hautafaa uombezi mbele Yake(Mwenyezi Mungu ) ila kwa Yule aliyempa idhini.Hata inapoondolewa hofu nyoyoni mwao,husema:Mola wenu amesema nini?.(Na wao) huwaambia:(Amesema maneno ya) haki,Naye ndiye aliye juu,Mkubwa.(SABA:22-23)

Na ndio maana ikawa shirki katika ibada ni katika dhambi kubwa na ni katika makosa makubwa ,amesema Allah: (13)(wakumbushe),Luqumani alipomwambia mwanawe,na hali ya kuwa anampa nasiha.Ewe mwanangu!Usimshirikishe Mwenyezi Mungu.maaana shirki ndiyo dhuluma kubwa(LUQMAN:13)Na katika hadithi iliyopokelewa na bukhari na muslim,amesema mtume(Sallallahualayhi wasallam) jee nisiwajulisheni juu ya dhambi kubwa? tukasema(maswahaba) kwani!ewe mtume wa mwenyeezimungu,akasema:kumshirikisha Mwenyeezi mungu..................hadith.na aliwauliza mtume (Sallallahualayhi wasallam) ni dhambi gani kubwa?akasemani kumfanyia mwenyezimungu mshirika na yeye ndie aliekuumba{bukhari na muslim}

Mweenyezimungu akaiwekea shirki kwasababu ya ukubwa ya uovu wake hukmu za kidunia na za kiakhera,katika hizo;

1-kutosamehewa madhambi yao(washirikina) amesema Allah:

(48Hakika Mwenyezi Mungu hasamehi kushirikishwa;na husamehe yasiyokuwa haya kwa amtakaye.Na anyemshirikisha Mwenyezi Mungu bila shaka amebuni dhambi kubwa(AN NISAA:48)2-kuharamishwa kuingia pepo na kuketi motoni milele. Amesema Allah:

(72) Kwani anayemshirikisha Mwenyezi Mungu,hakika Mwenyezi Mungu atamharimishia pepo,na mahali pake(patakuwa) ni motoni.Na madhalimu hawatakuwa na wa wasaidizi(wa kuwasaidia siku ya Kiama)(AL MAIDAH:72)

3-Kupomoka matendo yao yote mema.Amesema Allah:

(65)Na kwa hakika yamefunuliwa kwako na kwa wale waliokuwa kabla yako(maneno haya):-Kama ukimshirikisha(Mwenyezi Mungu) bila shaka amali zako zitaruka patupu(hutazipatia thawabu japo ni amali njema); na lazima utakuwa miongoni mwenye hasara.(AZ-ZUMAR:65) Na ile miezi4-kutohifadhiwa damu zao na mali yao,amesema allah: (5) Na ile miezi mitukufu itakapokwisha(Ile miezi mine waliyopewa),basi waueni(piganeni na) washirikina popote muwakutapo,na wakamateni matekakama wanavyokufanyieni) na wazungukeni na wakalieni katika kila njia.Lakini wakitubu na wakasimamisha Sala na wakatoa Zaka,basi iacheni njia yao(waacheni).Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe (na) Mwenye kurehemu(AT TAWBA:5)Na akasema mtume (Sallah Alaihi Wasalam):(( Nimeamrishwa niwapige vita watu mpaka waseme (Lailaha Illa llah), watakapo isema watahifadhika kutokana na damu zao, mali yao, ila kwa haki yake)) Bukhari na Muslim.Na wamepotea katika masala haya mapote tofauti tofauti katika binadamu. Katika hao ni:

1.Wenye kuabudu masanamu pamoja na kutofautiana vitu wanavyoviabudu katika miti, majini, mawe, binadamu na malaika, nyota, wanyama na vitu ambavyo anawapoteza navyo shetani.2.Wenye kuabudu makaburi na wakiweka nadhiri kwa makaburi na kujikurubisha kwa kuchinja, na wakiomba makaburi hayo kuwapatia manufaa na kuwaondelea madhara.

3.Wachawi na warogi na makuhani, wale ambao wanaowaabudu majini kwa sababu majini wanawaletea habari,ima wanawaletea wanavyovitaka au wanafanya wanavyoambiwa.

Na kwa sababu ya shirki katika ibada mtume (Sallallah Alaihi Wasalam) alihadhirisha njia za kupelekea hiyo shirki na akafunga njia zote zitakazo sababisha shirki . katika mfano wa hayo ni:

1.Kuhadharisha kupita mpaka katika watu wema, akasema mtume (Sallallah Alaihi Wasalam): (( Nawahadharisheni kutokana na kupita mpaka, hakika waliangamizwa wale waliokuwa kabla yenu kutokana na kupita mpaka)) Imepokewa na Ahmad na Tirmidhi na Ibni Mayah) na akasema: (( musini tukuze kupita mpaka kama walivyopita mpaka manaswara kwa Isa ibn Maryam, hakika mimi ni mja, semeni mja wa Mwenyezi Mungu na mtume wake)) imepokewa na Bukhari.Na katika kupita mpaka kwa watu wema ni kutawasali kupitia kwao kuliko katazwa , nayo hiyo tawasuli iko sampuli mbili:i.Tawasuli ya kishirikina yenye kumtoa mtu katika uislamu; nayo ni kuomba pasi na Allah kwa kutaka kutekelezewa na kuondolewa majanga na matatizo

ii.Tawasuli ya kizushi; nayo ni kumuomba Mungu kupitia vitu ambavyo havijawekwa na sharia, kama kuomba kupitia kwa watu wema,au jaha zao (vyeo vyao) au heshima zao na mfano wa hayo.Na tawasuli iliyoko kisharia inakuwa kwa kumuani Mwenyezi Mungu au kupitia kwa jina katika majina yake au sifa katika sifa zake au kupitia kwa jambo lake alilofanya au akaomba kuombewa Mungu kwa mtu mwema, kama alivyosema Umar (Radhiallah anhu) ((Ewe mola tulikuwa sisi tukipatwa na ukame tukitawasuli kwako kupitia mtume wetu ukituteremshia mvua, na sisi twatawasuli kwako kupitia Ammi wa mtume (Abbas) basi tuteremshie mvua)) Bukhari.

2.Akatutahadhirisha kutokamana na kufitinika na makaburi, na mfano wa hayo ni:

i.Kuyafanya makaburi misikiti, kwani imepokewa na Aisha (R.A) amesema: alipozidiwa mtume (Sallallah Alaihi Wasalam) alikuwa akijifunika shuka juu ya uso wake, akitulia kidogo hukifunguwa shuka na akasema na yeye yuko hivyo(( laana ya Mungu iwe juu ya mayahudi na manaswara, wameyafanya makaburi ya mitume yao misikiti)) akihadharisha waliokuwa wakiyafanya na lau si hivyo lingedhihiri na kuinuliwa kaburi lake ila yeye aliogopa kutofanywa msikiti)) Bukhari na MuslimNa akasema: (( jueni walikuwa waliokuwa kabla yenu wakifanya makaburi ya mitume yao misikiti, juweni musifanye makaburi misikiti mimi nawakatazeni na hilo)) Muslim.

Na maana ya kufanya misikiti kukusudia humo hata kama hakukujengwa msikiti kwa sababu msikiti ni sehemu ya ibada.ii.Kuyajengea makaburi na kupakwa chokaa na rangi na kuzidishwa mchanga mwengine kwani imepokewa kutoka kwa Abilhayaaj Alasadi (Mungu amrehemu) alisema: alimwambia Ali bin Abi Twalib (R.A) je nisikutume kwa lile alilonituma kwalo mtume (Sallallah Alaihi Wasalam) ya kwamba nisiwache sanamu ila nimelivunja na wala kaburi lililo inuliwa ila nimeliweka sawa) Muslimna imepokewa kutoka kwa Jabir bin Abdillahi (R.A) amesema;( amekataza mtume (Sallallah Alaihi Wasalam) kutia chokaa kaburi, na kukaliwa na kujengewa)[Muslim], yaingia katika hayo yaliyokatazwa kujenga makuba juu ya makaburi na kuyapamba na kuyarembesha.

iii.Kufunga safari kuyaendea makaburi; imekatazwa kutokana na jumla la katazo la mtuma (Sallallah Alaihi Wasalam):musifunge safari ya ibada ila kuelekea misikiti mitatu; Masjidil Haram (Makkah), na msikiti wangu huu ( msikiti wa Madina), na msikiti wa Aqswa (Falastin) Bukhari na Muslim.

iv.Kufanya kaburi lake ni idi ( yani lenye kuzuriwa mara kwa mara) imepokewa na Abu Daud.

3.Kuhadharisha kujifananisha na washirikina, mayahudi, na wakristo katika itikadi zao na ibada zao na ada zao zilizo husika na wao pekee, amesema mtume (Sallallah Alaihi Wasalam):kuweni kinyume na washirikinaBukhari na Muslim. Na akasema:kuweni kinyume na majusi imepokewa na Muslim. Na akasema : kuweni kinyume na mayahudi imepokewa na Abu Daud.

4.Kuhadharisha kutengeneza sura za watu,imepokewa na Aisha ya kwamba Ummu Salama alimtajia mtume (Sallallah Alaihi Wasalam) kanisa aliloliona Habashi na sura zilizokuwa zimetengenezwa akasema mtume (Sallallah Alaihi Wasalam):hao akifa mtu mwema kwao hujenga juu ya kaburi lake msikiti na wakatengeneza hizo sura hao ndio viumbe waovu mbele ya Mwenyezi Mungu Bukhari na Muslim.

5.Kuhadharisha kutokana na matamko ya kishirikina, na mfano wa hayo:

i.Kuapa kwa asiye kuwa Allah kwa dalili ya hadithi Yoyote ambaye ataapa kwa asiye kuwa Allah kwa hakika amekufuru au ameshirikishaimepokewa na Tirmidhi.

ii.Kusawazisha katika matakwa ya Allah na matakwa ya kiumbe dalili yake ni kauli yake mtume (Sallallah Alaihi Wasalam) alipomwambia mtu aliye mwambia ametaka Mwenyezi Mungu na ukataka wewe (mtume) akasema mtume umenifanya mimi ni mshirika wa Mwenyezi Mungu! sema ametaka Mwenyezi Mungu peke yake imepokewa na Annasai.

iii.Kutegemeza vitendo vya Allah katika ulimwengu kwa asiye kuwa Allah. Dalili yake imekuja katika hadithi Kudsi: Ama yule mwenye kusema tumepata mvua kwa nyota fulani na fulani, basi huyo amenikufuru mimi ameamini nyota Bukhari na Muslim.

6.Kutahadharisha kutokana na matendo ya kishirikina, na mfano wa hayo:

i.Kuvaa kikuku au uzi katika mkono au katika shingo kwa lengo la kujikinga kutokana na balaa au kuondoa balaa, dalili yake ni hadithi ya Imran bin Huswein ya kwamba: mtume (Sallallah Alaihi Wasalam) alipomuona mtu amevaa chuma katika mkono wake, mtume (Sallallah Alaihi Wasalam) akamwambia ni nini hii? akasema nimevaa kujizuia kutokana na ugonjwa akamwambia vua haitokuzidishia ila ugonjwa kwani lau ukifa na bado unayo hautafaulu kabisa(yaani huingii peponi) imepokewa na Ahmad na Ibn Hibban.

ii.Kujifunga hirizi, nyuzi zinazotiwa kaure, au nyuzi za kawaida au vyenginevyo kujikinga kutokana na hasadi. Dalili yake mtume (Sallallah Alaihi Wasalam) amesema: Yoyote mwenye kujifunga hirizi basi Mungu asimtimizie mambo yake na yoyote mwenye kujifunga uzi wa kaure basi Mungu asimpatie utulivu imepokewa na Ahmad na Ibn Hibban na Hakim, na katika riwaya ilopokelewa na Ahmad na Hakim Yoyote mwenye kujifunga hirizi basi hakika ameshirikisha na kwa hadithi Musibakishe katika ngamia uzi uliofungwa (katika shingo zao) ila umekatwa Bukhari na Muslim.

iii.Zunguo la kishirikina na dawa za mapenzi; kwa hadithi Hakika zunguo ( la kishirikina) na hirizi na dawa za mapenzi ni shirki imepokewa na Abu Daud.

iv.Kuchinja katika sehemu za ushirikina imekatazwa kwa neno lake mtume (Sallallah Alaihi Wasalam) alipomuuliza mtu aliye weka nadhiri ya kuchinja ngamia Buwana ( ni jina la sehemu), mtume (Sallallah Alaihi Wasalam) akamuuliza: Je kulikuwa na sanamu katika masanamu ya jahiliya ya kiabudiwa? wakasema: hapana akamuuliza (mtume) Je kulikuwa na idi katika idi zao wakasema hapana akasema mtume (Sallallah Alaihi Wasalam): Tekeleza nadhiri yako imepokelewa na Abu Daud.v.Kutowa fali mbaya na kuwa na itikadi kwa wanyama ( kubashiri vibaya ukiona kitu au mnyama fulani) kwa hadithi ya Ibn Masud ameinyanyuwa kwa mtume (Sallallah Alaihi Wasalam) amesema: Kutoa fali mbaya kwa ndege ni shirki imepokewa na Abu Daud na TirmithiNNE: KUAMINI MAJINA YAKE NA SIFA ZAKE ALLAH.

Nayo ni kuamini kwa kukata bila ya shaka kwamba Allah ana majina mazuri na sifa tukufu, na kumthibitishia aliyojithibitishia mwenyewe Allah kwenye kitabu chake na aliyomthibitishia mtume wake katika hadithi zake katika sifa za ukamilifu na sifa za utukufu bila ya kumtolea mfano wala kumuekea sampuli na kumkanushia Allah yale aliyojikanushia mwenyewe katika kitabu chake au aliyomkanushia mtume wake katika hadithi zake, katika sifa za upungufu na za kasoro, na kuwacha kumfananisha na viumbe bila ya kugeuza wala kukanusha.amesema Allah: (180)Na Mwenyezi Mungu ana majina mazuri;mwombeni kwayo.Na wacheni wale wanaoharibu utakatifu wa majina yake.Karibuni hivi watalipwa yale waliyokuwa wakiyatenda(AL AARAF:180) (11)Hakuna chochote mfano Wake;Naye ni Mwenye kusikia,Mwenye kuona(ASH-SHURA:11)Na majina yake Allah na sifa zake tukufu ni taukifia (yani tunafuata yale yailotejwa katika quran na sunna pekee) haifai akili pekee kuithibitisha na hasifiwi Allah isipokuwa sifa alizo jisifu nazo yeye mwenyewe au amemsifu nazo mtume wake (Sallallah Alaihi Wasalam) . hatuchukuwi isipokuwa katika quran na hadithi. Basi sifa alizozinyamazia Mwenyezi Mungu na mtume wake ni lazima tuzinyamazie na kusimama hapo katika kukanusha na kuthibitisha na kutaka ufafanuzi kwa msemaji akikusudia maana sahihi itakubaliwa maana na tamko litaridishwa na akitaja maana ambayo si sawa tamko litarudishwa na maana pia.amesema Allah: (36)Wala usifuate(ukipita ukiyasema au ukiyafanya) usio na ilimu (ujuzi) nayo.Hakika masikio na macho na moyo;hivyo vyote vitaulizwa(BANI ISRAIL:36)Majina yake Mwenyezi Mungu yamefikia upeo wa uzuri nayo ni majina yenye kumjulisha yeye Allah na sifa zake. Sifa zake zimekamilika hazina upungufu kwa njia yoyote,amesema Allah: (27)Na Yeye ndiye aliyeanzisha viumbe na ndiye Atakayevirudisha(mara nyingine),na(jambo) hili ni rahisizaidi Kwake;naye ndiye mwenye sifa nzuri mbinguni na katika ardhi,naye ndiye mwenye nguvu,Mwenye hikima(AR-RUM:2)Nayo ni haki kwa hakika yake, kwa hivyo ni lazima kuyapitisha vile yalivyo kwa dhahiri yake, bila ya kuyageuza na haram kuyapotoa kwa kuyakanusha au kuyafananisha au kuzusha majina ambayo Allah hajajiita nayo mwenyewe au kuyatumia majina yake kumuitia mwengine.Na ya lazimu kumuomba kupitia hayo majina katika ibada na katika dua, na yatakiwa kuyajuwa idadi yake na kuyafahamu maana yake na kuyafikiria athari zake na kufanya matakwa yake na hiyo ndio elimu bora kabisa. Zagawanyika sifa zake Allah kulingana na kufungamana haya majina na Allah vigawanyo viwili:

1.Sifa za dhati yake; nazo ni sifa zenye kushikamana na dhati yake tukufu; kama uhai,kusikia, kuona, elimu, kudra (uweza),kutaka, hikma, nguvu na nyenginezo ambazo kwamba hazimkiniki kuepukana nae Allah.2.Sifa za vitendo; nazo ni sifa zilizofungamana na matakwa yake na hikma yake, huzifanya atakapo na sampuli atakayo kulingana na hikma yake kubwa; kama kustawi kwenye arshi, kushuka, kupenda , kuchukia, kufurahi, kuona ajabu, na kucheka, kuja na nyenginezo zilizo kuja katika quran na zilizoswihi katika hadithi.

Katika baadhi ya sifa hizo kama sifa ya kusema ni sifa zilizofungamana na dhati yake na ni sifa ya kitendo, ni sifa za dhati yake kulingana na asli ya sifa na sifa ya kitendo kulingana na maneno yenyewe au husemwa sifa ya tangu na yenye kutokea kulingana na maneno yenyewe. Na sifa zenginezo huitwa sifa za habari; nazo ni ambazo ni kuthibitisha hiyo habari moja kwa moja bila ya kufikiria kwa akili kama sifa ya uso, mikono, macho, mguu na nyenginezo ambazo zimeswihi habari zake.Katika sifa zake Mwenyezi Mungu zilizothibiti katika quran na sunna na Ijmaa:i.Sifa ya kuwa juu (Uluuw) nayo ni sampuli tatu; kuwa juu kwa cheo chake, ukubwa wa kushinda kwake na kuwa juu kwa yeye mwenyewe. Naye Mwenyezi Mungu ni mshindi hakuna aliye juu yake katika viumbe wake, amestawi katika arshi yake juu ya mbingu zake ameepukika na waja wake hana chochote katika viumbe vyake wala hawana viumbe vyake chochote katika yeye, ni sifa ya dhati yake (Uluuw).

ii.Sifa ya kustawi; nayo ni kwamba Mwenyezi Mungu baada ya kuumba mbingu na ardhi alistawi kwenye arshi yake; kwa maana alikuwa juu yake na akastawi juu yake, kustawi ambapo uhakika wake wafungamana na ukubwa wake na utukufu haiwi sawa na kustawi kwa viumbe, kwa hivyo hii ni sifa ya kitendo.

iii.Sifa ya kusema: nayo ni kwamba Mwenyezi Mungu anazungumza mazungumzo ya hakika yenye kusikika kwa herufi na sauti, hayafanani maneno yake na maneno ya viumbe na yakwamba mwenyezi Mungu anazungumza wakati atakao kwa maneno atakayo kwa sampuli aitakayo kwa ukweli na uadilifu kwa vilima visivyoisha hakuacha na hajawacha kusema Mwenyezi Mungu. Kwani ni sifa ya dhati yake kulingana na asli yake na ni sifa ya kitendo kulingana na maneno.Hizi sampuli za sifa zote ni haki kwa hakika yake Allah ni lazima kuzithibitisha na kuzipitisha kama zilivyokuja, na kuzipitisha kwa dhahiri yake bila ya kuleta sampuli na hili ni jambo ambalo lazima lizingatiwe katika sifa zote, kuzizungumzia sifa Fulani ni kama kuzizungumzia sifa zengine zilizobaki, sawa kwa sawa na yoyote atakaye tafautisha amehukumu bila ya dalili.

Wamepotea katika masala ya majina yake mwenyeezimungu na sifa zake,mapote tofauti tofauti nayo ni:

1-Watu wa kufananisha wale ambao waliopita mipaka katika kuthibitisha hayo majina na sifa zake Allah,mpaka wakaingia katika kumfananisha .Na utata wao katika hilo ni kwamba hilo ndio matakwa ya dalili za sharia kwasababu mungu huwazungumzia watu kulingana walivyozoea katika viumbe!Na kuwajibu watu hawa ni kwa njia kadhaa:

(i)Mwenyeezimungu amekataa kuweko chochote mfano wake au sawa na yeye au mshirika,kwa aya ambazo ni muhkam(hazina utata)ziko wazi amesema Allah; (11) Hakuna chochote mfano Wake (ASH-SHURA:11)

(22) Basi msifanyie Mwenyezi Mungu washirika,na hali nyinyi mnajua(kuwa hana mshirika)(AL BAQARAH:22) (4)Wala hana anayefanana naye hata mmoja(IKHLAAS:4) Na wala hayawezi maneno yake mwenyeezi mungu kugongana.(ii)Akili iliosalimika inakataa kusawazishwa Mungu muumbaji aliekamilika na mja aliyeumbwa aliyempungufu. Basi kama vile dhati yake Allah haifanani na dhati ya wengine,pia sifa zake hazifanani na sifa za wengine.iii)Yakwamba mwenyezimungu amewazungumzia waja kwa wanayo yafahamu kulingana asili ya maana,wala hailazimishi kushirikiana katika maana ya kiujumla kusawazisha katika hakika ya sifa na sampuli yake,ikiwa katika viumbe kukitokea kuwafikiana majina ya viumbe venyewe haimaanishi kufanana kwa viumbe hawa. Kama tamko la kusikia kuona na uweza, basi baina ya Mwenyezi Mungu na viumbe ni mbali zaidi2.Watu wenye kukanusha : wale waliopita mpaka katika kukanusha na utata wao eti kuthibitisha sifa inalazimu kufananisha, kwa sababu sifa zile kiumbe pia amesifika nazo basi italazimu tumuepushe nazo muumbaji, wakathibitisha kuwepo kwake tu Allah bila ya sifa! Na mapote yaliyo zidi kupita mpaka katika kukanusha ni (karamitwa baatinia) wale ambao walimkanushuia Mwenyezi Mungu vinyume viwili, kisha (Jahmiya) wale waliyo kanusha majina na sifa, kisha (Muutazila) wale ambao walithibitisha majina na wakakanusha sifa zilizo kusanywa na hayo majina

Kuwajibu haya mapote ni kwa njia kadhaa:

i.Kwamba Mwenyezi Mungu amejithibitishia nafsi yake majina katika aya ambazo hazina utata, zilizo wazi na kutajwa kwake kumeshikanishwa na kukanusha mfano wake kama neno lake Allah:

(11)Hakuna chochote mfano Wake ; Naye ni Mwenye kusikia,Mwenye kuona(ASH-SHURA:11Na wala hayawezi kuwa maneno ya Mwenyezi Mungu ni yenye kugongana.ii.Ya kwamba kuthibitisha kuwepo kwake Allah tu haiwezekani kumsifu kwa sifa ambayo haipo kikweli, bali ni jambo ambalo lipo katika akili madai yao yanapelekea kukanusha muumbaji.iii.Kwamba sifa kwa matamshi ya kiujumla kwa fulani hailazimu kuthibiti sifa hiyo kwa mwengine, bali kila mmoja wao ni kiungo katika hiyo sifa ya kiujumla kwa sababu sifa ikifunganishwa na kitu au mtu au ikitegemezwa huondoka kushirikiana kwa nje.

3.Watu wa taawili wale waliyo itakidi kwamba dalili hazijulishi sifa ambazo ni hakika kwa Allah, wakawa ni wenye kutafuta maana nyengine ya hizo dalili bila ya hoja sahihi ambayo ya waruhusu kuondoa maana kutoka katika udhahiri kupeleka katika maana nyengine, wakiita kupendua kwao maana huku taawili!Kuwajibu hawa ni kwa njia tafauti:

i.Kwamba Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa nafsi yake na ndio msemaji kweli na ndio msemaji bora kuliko viumbe wote na mtume(Sallallahualayhi wasallam) ndio mjuzi zaidi anayemjua Allah na ndio msemaji kweli na mfasaha katika kusema kwake, na mwenye kunasihi bora katika umma huu. Kisha atatokeaje mtu adai kutadaraki (kutaja yaliyo achwa) na Mwenyezi Mungu na mtume wake, na ayafanye maneno yao ni yenye kuleta utata na upotevu?

ii.Asili katika maneno yoyote ni kuyafahamu vile yalivyo katika hakika yake, wala haifai kubadilisha maana ila kwa dalili ambayo itaruhusu kugeuza maana ya hayo maneno na hakuna dalili.

iii.Kwamba mtume (Sallallahualayhi wasallam) amewaelezea watu yaliyo teremshwa kwao na akafikisha kufikisha kulio wazi, basi hawezi mtume (s.a.w) awache kuyaeleza mambo haya makubwa na maana ya hizo sifa kama walivydai hawa wenye kubadilisha maana na kutunga maana zao.

4.Watu wenye madai ya kutojulikana, wale walioitakidi kwamba maana ya yale Mwenyezi Mungu aliyojielezea nayo nafsi yake au mtume aliyo yaeleza maana yake haijulikani, hakuna ajuwae maana ya hayo isipokuwa Allah wala hakuna mtu aweza kujuwa maana yake na wanajiita watu hawa (Mufaawidha) wenye kumtegemezea Mungu na njia yao ni tafwiidh- kumtegemezea Mungu.Kuwajibu hawa na kwa njia kadhaa:

i.Haiwezekani iwe mlango wa elimu ya yaliyofumgamana na Mungu ambao ni katika milango muhimu katika dini uwe imefungwa na wala hakuna dalili wala akili zenye kukufikisha.

ii.Kwamba Allah ameteremsha quran katika ndimi za kiarabu zilizowazi na akawa amrisha waja wake watie akilini maneno yake na kuyazingatia na wala hakutoa chochote katika quran, basi hiyo imejulisha kuwezekana kuwa na elimu ya maana ama sampuli na hakika yake ni katika vitu vya ghaibu ambavyo elimu yake hutegemezwa kwa Allah pekee.

iii.Mwenendo huu unapelekea kuwafanya wajinga wale wema waliotangulia katika umma huu na kuwasifu kama kwamba wao hawajui kusoma na hawajui kitabu ila ni matamanio tu! Kwao ni kama talasimu na herufi pekee ambazo hazileti maana yenye kuingia akilini.

KUAMINI MALAIKA.Moja:Ni kuitakidi kwa kukata bila ya shaka kwamba ni waja waliokirimiwa , waja wema, wenye kunyenyekea Mola wao, wenye sikitiko hawana chochote katika sifa za uungu wala za uola, amesema Allah:

(26) (27) (28)Na makafiri wakasema:(Mwenyezi Mungu) mwingi wa rehema amejifanyia mtoto. Ametakasika :(Mwenyezi Mungu!)bali(hao Malaika) ni waja wa :(Mwenyezi Mungu) waliotukuzwa926).Hawamtangulii kwa neno(lake analosema) Nao wanafanya amri zake(zote)(27). :(Mwenyezi Mungu) anayajua yaliyo mbele yao(Hao Malaika) hawamuombei (yoyote) ila Yule anayemridhia:(Mwenyewe Mwenyezi Mungu),nao kwa ajili ya kumuogopa wananyenyekea(AL-ANBIYAA:26-28)Na akasema: (50)Wanamuogopa Mola wao aliye juu yao,na wanatenda wanayoamrishwa(AN NAHL:50)Na akasema: (6)Hawamuasi Mwenyezi Mungu kwa amri Zake;na wanayatenda wanayoamrishwa(yote)(AT-TAHRYM:6)Na akasema: (16)Watukufu, Wachamungu.(abasa ;16) Na akasema: (40) (41)Na(wakumbushe) siku atakayowakusanya wote,kasha atawaambia Malaika:Je!Hawa walikuwa wakikuabuduni?(40).Waseme:umeepukana na kila upungufu!Wewe ndiye kipenzi chetu,si hao;bali walikuwa wakiwaabudu majini;wengi wao waliwaamini hao(majini).(34:40-41)

Na akasema: (32)Wakasema(Malaika):Utakatifu ni wako!hatuna ilimu ila ile uliyotufundisha;bila shaka wewe ndiye Mjuzi na ndiye Mwenye hikima.(Mwenye kuweka kila kitu mahala pake)(AL BAQARAH:32) Pili:Na kuitakidi kwamba wao wameumbwa kutokana na nuru ( muangaza), wana mbawa, katika umbile kubwa sampuli tofauti tofauti, amesema mtume(Sallallahualayhi wasallam) wameumbwa malaika kutokana na nuru (muangaza) imepokewa na Muslim na akasema Allah: (1)Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu,Muumba wa mbingu na ardhi,aliyewafanya Malaika kuwa wajumbe wenye mabawa,mbili mbili na tatu-tatu,na nne nne.Huzidisha katika kuumba apendavyo.Bila shaka Mwenyezi Mungu ni Mwenye uweza juu ya kila kitu(FATIR:1)Amesema Abdallah bin Masud mtume (Sallallahualayhi wasallam) alimuona Jibril katika sura yake ana mbawa mia sita, kila mbawa ni kiasi cha upeo wa muono, yapomoka katika mbawa zake vitu vya rangi tafauti tafauti katika lulu na yakuti.Na akasema Mtume: (Sallallahualayhi wasallam) Nimeruhusiwa nizungumze kuhusiana na mmoja wa wabebaji wa arshi,baina ya ndewe ya sikio lake mpaka kwenye bega lake ni mwendo wa miaka mia saba.Wao ni viumbe wa kweli si nguvu tu za maanawia kama vile walivyodai baadhi ya watiao shaka.Na malaika ni wengi hakuna ajuaye idadi yake isipokuwa Mola wao, kwani imepokelewa katika hadithi ya anas(iliyopokelewa na bukhari na muslim) katika kisa cha miraji,ya kwamba mtume(Sallallahualayhi wasallam) alinyanyuliwa mpaka katika baitul maamur katika mbingu ya saba,na ya kwamba wanaswali katika hiyo nyumba(baitul maamur kila siku malaika elfu sabini,wanapotoka hawarudi tena mpaka mwisho wake).Tatu:Kwamba wao malaika ni wenye kupiga swafu wakimsabihi Mwenyezi Mungu,amewapatia Allah ilihamu ya sampuli ya kumsabihi,na kutekeleza amri zake,na Akawapatia nguvu kuzitekeleza amri hizo.Amesema Allah:

(164) (165) (166)Na (wanasema malaika katika kujua cheo chao,kuwa:-)hakuna yoyote miongoni mwenu ila anapo mahali pake mahsusi(ma-alum).(164).Na kwa yakini katika sisi wako wajipangao safu(wakasali jamaa)(165).Na wako katika sisi wamtukuzao (Mwenyezi Mungu kwa kumkanushia sifa zisizokuwa zake)(AS-SAAFFAT:164-166).

Na akasema: (38)Na kama wakitakabari,(basi Mwenyezi Mungu hana haja nao) kwani hao (viumbe watukufu)-(Malaika)-walioko kwako Mola wako wanamsabahi usiku na mchana,wala hawachoki.(Basi kama nyinyi hamuabudu yadhuru nini?)(HAA MYM SAJDAH:38).

Na akasema: (20)Wanamtukuza usiku na mchana hawanyongonyei(hawafanyi uvivu)(AL-ANBIYAA:20).Na imepokewa kutoka kwa Hakimu bin Hizamu (R.a) amesema: tulipokuwa tumeketi mbele ya Mtume (Sallallahualayhi wasallam) akasema: Mwasikia ninachosikia?wakasema:Hatusikii cho chote,Akasema (Mtume (s.a.w)):Mimi nasikia sauti ya mbingu,na wala hailaumuwi kutoa sauti kwa sababu hakuna shubiri moja ila utapata malaika amesujudu au amesimama(anafanya ibada)Imepokewa na twabrani na akasema Albani ni sahihi kwa sharti ya muslim.

Nne:Kwamba wao hawaonekani kwani wao ni ulimwengu wa ghaibu hawawezi kuhisika kwa hisia yoyote katika dunia kwa mwanaadamu yoyote ila Yule aliyemtaka Mungu,kama kumuona Mtume wetu jibrili kwa umbile lake lile aliloumbiwa.Bali hao malaika huonekana akhera.

Amesema Allah: (22)Siku watakayowaona malaika haitakuwa furaha siku hiyo kwa wenye makosa,(itakuwa ndiyo siku ya kutolewa roho zao);na watasema(siku hiyo);(Mungu) Atuepushie mbali adhabu hii iliyotukabili.(Lakini haitafaa kitu dua hiyo)(AL-FURQAN:22).Na akasema:

(23)Na malaika wanawaingilia katika kila milango(AR RAAD:23)Lakini Mwenyezi Mungu amewapatia uweza wa kujigeuza kwa umbile la wanadamu, amesema Allah:

(17)Na aaweka pazia kujikinga nao.Tukampeleka Mhuisha Sharia yetu(Jibril)-akajimithilisha kwake(kwa sura ya) binadamu aliye kamili(MARYAM:17) Na akasema Allah: (69) (70)Na wajumbe wetu(malaika kwa sura za kibinadamu) walimwendea Ibrahimu kwa bishara(khabari njema kuwa atazaa na kujukuu na mengine na)-wakasema:(Salam(alaykum-amani juu yenu).Akasema Ibrahimu:(Juu yenu pia iwe amani. Na hakukaa (Ibrahimu) ila mara akaleta ndama(aliyechomwa vizuri juu yam awe ya moto)(69).Basi alipoona (Ibrahimu) mikono ya(watu) wale haifikilii (chakula kile) aliwatilia shaka na akawaogopa(akadhani kuwa ni maadui).Wakasema:Usiogope,hakika sisi tunapelekwa kwa watu wa Luti(tukawaangamize na tukupe khabari wewe na mkeo,sara,kuwa mtazaa na kujukuu nabado muhai(HUD:69-70)

Na akasema:

(77) (78)Na wajumbe wetu walipomjia(Nabii)Luti alihuzunika kwa ajili yao(hao wageni kwa kuona kuwa watataabishwa wageni hawa.Hawakujua kuwa ni malaika) na akaona taabu kwa ajili yao,na akasema:Hii ni siku nguvu(kabisa)(77).Wakafika kaumu wake wakamjia mbio(nyumbani kwake ili wafanye machafu wale wageni).Na kabla ya haya walikuwa(daima) wakifanya maovu,akasema(Luti)Enyi kaumu yangu!Hao binti zangu(binti wa umma wangu walioolewa katika nyumba zenu) ndio wametakasika kwenu(kuwaingilia si waume wenzenu).Basi Mcheni Mwenyezi Mungu wala msinifedheheshe mbele ya wageni wangu.Je,miongoni mwenu hakuna mtu muongofu(hata mmoja)?(HUD:77-78)Walikuwa hao malaika kwa umbile la waume. Pia alipokuja Jibril (a.s) katika sifa ya mtu mweupe sana mwenye nyele nyeusi sana na alikuwa mara nyengine akija katika sura ya dihya alkalbi (r.a).Tano: Kwamba wao malaika wamepewa kazi tofauti tofauti pamoja na kazi yao ya msingi ya kumuabudu Mwenyezi Mungu na kumsabihi katika hizo kazi:

i.Kuteremsha wahyi; nayo ni kazi ya Jibril (a.s) amesema Allah:

(102)Sema:Roho takatifu(yaani Jibril)ameiteremsha kutoka kwa Mola wako kwa haki,ili kuwathubutisha wale walioamini,na kuwa uwongofu na khabari njema kwa waliosilimu(AN NAHL:102)

Na akasema: (192) (193) (194)Na bila shaka hii(Qurani)ni Uteremsho wa Mola wa Walimwengu wote(192).ameteremsha haya Mhuisha Sharia mwaminifu,(Jibril)(193).juu ya moyo wako,ili uwe miongoni mwa Waonyaji(ASH-SHUARAA:192-194)ii.Kuchunga mtoto ( aliye tumboni) kwa kumtia roho na kumuandikia rizki, mda wake, matendo yake na atakuwa mwema au muovu.iii.Kumuhifadhi mwanadamu: amesema Allah:

(11)Ana (kila mtu) kundi (la malaika) mbele yake na nyuma yake:wanamlinda(na kuyadhibiti wanayoyafanya) kwa amri ya Mwenyezi Mungu.Hakika Mwenyezi Mungu habadili yaliyoko kwa watu mpaka wabadili wao yaliyomo katika nafsi zao.Na Mwenyezi Mungu anapowatakia watu adhabu hakuna cha kuwazuia wala hawana Mlinzi yoyote badala yake(Mwenyezi Mungu)(AR RAAD:11)

iv.Kuhifadhi matendo ya mwanadamu, amesema Allah: (17) (18)Wanapopokea wapokeaji wawili,anayekaa kuliani na (anayekaa) kushotoni,(malaika)(17).Hatoi kauli yoyote isipokuwa karibu naye yuko mngojeaji tayaria(kuandika)(18)(QAF:17-18)

v.Kuwathibitisha waumini na kuwanusuru, amesema Allah: (12)(Kumbukeni) Mola wenu alipowafunulia Malaika(akawaambia):Hakika mimi ni pamoja nanyi,basi watieni nguvu wale walioamini;ninatia woga katika nyoyo za makafiri.Basi wapigeni juu ya shingo(zao) na kateli kila ncha za vidole vyao(AL ANFAL:12)

vi.Kuchukuwa roho, amesema Allah: (11)Sema:Atakufisheni malaika wa mauti aliyewakilishwa kwenu,kasha mtarejeshwa kwa Mola wenu(AS-SAJDAH:11)

vii.Kumuuliza maiti kaburini, kuhusu Mola wake, dini yake na mtume wake na waulizaji hao ni wawili Munkar na Nakir.viii.Kupiga baragumu siku ya kiama, nayo ni kazi ya Israfil (a.s), baragumu la kwanza atapiga la kufisha na la pili ni la kufufua kama alivyosema Allah:

(68)Na litapigwa baragumu watoke roho watu waliomo mbinguni na waliomo ardhini ila Yule amtakaye Mwenyezi Mungu.Tena litapigwa mara nyingine.Hapo watafufuka (wote);wawe wanatazama(nini litatokea)(AZ-ZUMAR:68)xi.Walinzi wa moto, amesema Allah:

(31)Na hatukuweka walinzi wa huo moto ila malaika(AL-MUDDATHTHIR:31)Na akasema: (77)Nao watapiga kelele(kuwaambia yule malaika anayewaadhibu waseme:Ee malik!Naatufishe Mola wako!(Malik)aseme:Bila shaka mtakaa humu humu(AZ-ZUKHRUF:77)Na akasema: (6)Enyi mlioamini!Jiokoeni nafsi zenu na watu wenu,na moto ambao kuni zake ni watu na mawe.Wanausimama malaika wakali,wenye nguvu,hawamuasi Mwenyezi Mungu kwa amri zake;na wanatenda wanayoamrishwa(yote)(AT-TAHRYM:6)

x.Kuwatakia msamaha waumini, kuwaombea Mungu, kuwabashiria na kuwakirimu katika pepo, amesema Allah: (7) (8) (9(Wale wanaokichukua kiti cha Enzi (cha Mwenyezi Mungu ) na wale wanaokizunguka,wanamtukuza Mola wao na kumsifu na wanamuamini na wanawaombea samahani walioamini,(wanasema):Mola wetu!Umekienea kila kitu kwa rehema na ilimu(Unakijua kila kitu).basi wasamehe waliotubu na wakaifuata njia yako wa waepushe na adhabu ya Jahanamu(7).Mola wetu:Waingize katika mabustani ya milele uliyowaahidi.Na uwape pia haya waliyofanya mema miongoni mwa baba zao na wake zao na watoto wao;Bila shaka wewe ndiye Mwenye nguvu,Mwenye hikima(8).Na waepushe na maovu,kwani umuepushaye na maovu siku hiyo,hakika umemrehemu;na huko ndiko kufuzu kukubwa(AL-MUUMIN:7-9)

(30)Wale waliosema:Mola wenu ni Mwenyezi Mungu,kisha wakenda mwendo mzuri,hao huwateremkia Malaika(wakati kutoka roho wakawaambia):Msiogope wala msihuzunike,na furahini kwa pepo mliyokuwa mkiahidiwa(HAA MYM SAJDAH :30)

(23) (24)Mabustani ya milele watayaingia wao(pamoja) na waliofanya wema miongoni mwa wazee wao na wake wao na kizazi chao.Na malaika wanawaingilia katika kila milango(23).(Wanawaambia):Salamun Alaikum Iwe amani juu yenu kwa sababu mlisubiri(mlistahmili kufanya mema na kuacha mabaya na mkastahimiliana mkakaa vizuri na wenzenuBasi ni mema yalioje matokeo ya nyumba(ya Akhera kwa wanaomcha Mungu)(AR RAAD:23-24)

KUAMINI VITABU.Nayo ni kuitakidi kwa kukata bila ya shaka kwamba Mwenyezi Mungu aliwateremshia mitume wake vitabu kwa haki, vitabu ambavyo ni muongozo kwa watu, na vime kusanya rehma kwa watu na ni mawaidha kwao, na hoja kwao na vimekusanya ufafanuzi wa kila jambo.

Kuamini hivo vitabu inakusanya mambo haya:

1.Kuamini vitabu tulivyovijua kwa majina yake na tusivyovijua tuamini kiujumla.

Vitabu vitukufu katika hivyo ni vitatu:

i.Taurati ambayo aliteremshiwa musa (a.s), amesema Allah:

(144) (145) (Akasema Mwenyezi Mungu):Ewe Musa!Mimi nimekuchagua juu ya watu wote kwa ujumbe wangu na kwa kusema nawe kwangu.Basi pokeya haya niliyokupa,Na uwe miongoni mwa wanaoshukuru(144).Na tukamwandikia katika mbao kila kitu-mawaidha(ya kila namna) na maelezo ya kila jambo.Basi yashike kwa imara na uwaamrishe watu wako wayashike bora haya.Karibuni nitakuonyesheni miji ya wavunjao amri(zenu namna ilivyoharibika na nitakutawalisheni nyinyi(AL AARAF:144-145)Na akasema: Hakika Tuliteremsha Taurati yenye uongozi na nuru,ambayo kwayo Manabii waliojisalimisha (kwa Mwenyezi Mungu)waliwahukumu Mayahudi,na watawa wa maulamaa pia(walihukumu kwa hiyo taurati),kwa sababu walitakiwa kuhifadhi kitabu (hicho) cha Mwenyezi Mingu; nao walikuwa mashahidi juu yake(AL MAIDAH:44)ii.Injil ambayo Mwenyezi Mungu alimteremshia Isa (a.s), amesema Allah:

(27)Kisha tukawafuatisha nyuma yao Mitume wetu(wengine) na tukamfuatisha Isa bin Mariamu,na Tukampa Injili,na Tukaweka upole na rehema katika nyoyo za wale waliomfuata.Na uruhubani(wanaume kutooa na wanawake kutoolewa)wameubuni(wenyewe),Sisi hatukuwaandikia hayo.(Wenyewe waliyafanya haya) ili kuitaka radhi ya Mwenyezi Mungu.Lakini hawakuufuata(huo uruhubani wao) kama inavyotakiwa kuufuata.Basi tukawapa wale walioamini miongoni mwao ujira wao,na wengi wao ni maasi(AL-HADYD:27)

Na akasema: (46)Na Tukawafuatisha (mitume hiyo) Isa bin Maryamu kuyahakikisha yaliyokuwa kabla yake katika Taurati,na tukampa Injili iliyomo ndani yake uongozi na nuru na isadikishayo yaliyokuwa kabla yake katika taurati,na uongozi na uongozi na mawaidha kwa wamchao (wanaomwogopa)(AL MAIDA:46)iii.Quran ambayo alimteremshia mtume Muhammad (Sallallahualayhi wasallam) , nacho ndicho kitabu bora kuliko vyote, amesema Allah: (48)Na Tumekuteremshia kitabu kwa (ajili ya kubainisha) haki,kinachosadikisha vitabu vilivyo kabla yake,na kuvihukumia(kama haya ndiyo yaliyoharibiwa au ndiyo yaliyosalimika).basi wahukumu baina yao kwa yale aliyoteremsha Mwenyezi Mungu,wala wasifuate matamanio yao kwa kuacha haki iliyokufikia.Na kila (Uma) katika nyinyi (binadamu )tumeujaaliwa sharia yake na njia yake.Na kama Mwenyezi Mungu angalitaka angekufanyani kundi moja(la kufuata sharia moja),lakini anataka kukujaribuni kwa hayo aliyokupani.Basi shindaneni kuyafikilia mambo ya kheri.Nyinyi nyote marudio yenu ni kwa Mwenyezi Mungu,Naye atakuambia (yote) yale mliyokuwa mkikhitalifiana(AL MAIDAH:48)

Na katika vitabu vyake Mwenyezi Mungu alivyoteremsha ni;Zaburi aliomteremshia Daud (a.s), amesema Allah: (55)Na Mola wako anawajua sana wote waliomo katika mbingu na ardhi.Na kwa hakika tuliwafadhilisha baadhi ya Manabii kuliko wengine(katika amali zao zilizo bora zaidi kuliko za wenziwao),na Daudi tulimpa Zaburi(BANI ISRAIL:55)Na kitabu cha Ibrahim, amesema Allah: (18) (19)Hakika haya (mnayoambiwa humu katia Qurani) yamo katika vitabu vilivyotanguliwa(18).Vitabu vya Ibrahimu na Musa(na wengineo)(AL-ALAA:18-19)

2.Kuamini katika hivi vitabu ambayo hayajageuzwa, kwani Allah ameeleza kwamba vitabu vya banu Isra