niite...uongozi na utetezi wa umma ..... 71 kiambatanisho: mambo ya msingi kuhusu vvu na ukimwi...

80

Upload: others

Post on 22-Sep-2020

5 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …
Page 2: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …
Page 3: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

NiiteJinsi Biblia inavyosema

katika zama hizi za UKIMWI

“Niite nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua”

(Yeremia 33:3)

Kimehaririwa naWilliam Mchombo, Joyce Larko Steiner,

Dennis Milanzi na Alfred Sebahene

Page 4: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …
Page 5: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

NiiteJinsi Biblia inavyosema katika zama

hizi za UKIMWI

YaliyomoShukrani na Vifupisho ..................................................................................................................................................... 4Dibaji: Kuhusu vitabu vya Tumeitwa Kuhudumia ............................................................................................... 5Washirika wa Tumeitwa Kuhudumia ..................................................................................................................... 6Neno la utangulizi na Askofu William Mchombo............................................................................................... 7Utangulizi ....................................................................................................................................................................... 8Uaminifu wa Mungu: 1. Neema ya Mungu .............................................................. 11 2. Haki ya Mungu ................................................................... 14 3. Upendo na msamaha wa Mungu................................ 17

Kanisa na janga la UKIMWI: 4. Watu wanaoishi na VVU na kanisa.............................. 21 5. Matunzo na msaada ........................................................ 24 6. Uongozi wa kanisa ........................................................... 28

Familia: 7. Watoto ................................................................................. 31 8. Ndoa ...................................................................................... 34

Mitazamo na matendo binafsi: 9. Tumaini ............................................................................... 37 10. Unyanyapaa, ubaguzi na kukataa ............................ 40 11. Msamaha, toba na upatanisho .................................. 43 12. Tendo la ndoa na matamanio ya mwili ................... 46 13. Unyanyasaji na ukatili wa kijinsia ............................. 50

Mambo yanayomsumbua mwanadamu: 14. Hofu na mashaka ......................................................... 53 15. Uponyaji ............................................................................ 56 16. Kifo, huzuni na maombolezo .................................... 59 17. Chakula .............................................................................. 62

Sifa ya mwanadamu: 18. Upendo wa jirani ........................................................... 65 19. K ujitegemea ..................................................................... 68 20. Uongozi na utetezi wa umma .................................. 71

Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ...................................................................... 74

Page 6: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

4 www.stratshope.org

NIITE

Shukrani

Watu wengi na mashirika mbalimbali yamechangia kwa namna tofauti katika kutayarisha, kujaribu na kuchapisha kitabu hiki. Tunawashukuru wafuatao kwa ushiriki wao katika warsha za waandishi zilizofanyika Ghana na Zambia: Pasta Aaron Adjei, Ebenezer Kojo Abakah, Baba Kasisi Cyril Akai, Sista Malisela Daka, Shemasi Chilesha Kambikambi, Pasta Timothy Katoka, Joyce Larko Steiner, Askofu William Mchombo, Kasisi Dennis Milanzi na Cecilia Sakala.

Nchini Tanzania, Kasisi Canon Alfred Sebahene alitengeneza miongozo miwili ya masomo na pia alipitia na kutathmini miongozo mingine kadhaa. Kule Afrika ya Kusini, makundi mawili ya huduma ya matunzo, Themba na Siyabonga (ambayo wanachama wake wote wanatoka Zimbabwe), kwa msaada wa Kasisi Renate Cochrane, walitengeneza miongozo mitatu na kujaribu matumizi ya miongozo mingine kadhaa. Kasisi Cochrane alitathmini kitabu hiki chote na kufanya marekebisho kadhaa ya kiuhariri na hivyo kukiboresha zaidi kitabu hiki kwa namna mbalimbali.

Tunapenda kutoa shukrani za pekee kwa Elizabeth Perry, ambaye alihusika na suala muhimu sana la kutathmini na kuhariri kitabu hiki.

Tunapenda pia kuwashukuru wafuatao kwa kusoma na kutoa maoni kuhusu rasimu ya kitabu hiki: Dk. Dorcas Olu Akintunde, Dk. Sandra Anderson, Linda Fuselier, Profesa Shima Gyoh, Pasta Anthony Makena, Shadiara Masheti, Bolele Monyau, Martha Nthenge, Maranda St. John Nicolle, Caren Owiti, Lia Verboom, John Whitley na Canon Tony Williamson.

Shukrani za pekee tunazitoa pia kwa watumishi wa German Institute for Medical Mission (DIFAEM) kwa kuchangia kiambatanisho, ‘Mambo ya Msingi kuhusu VVU na UKIMWI, pia tunatoa shukrani kwa watumishi wa Kituo cha Mtandao wa HIV/AIDS (HIVAN) kwa ushauri wao kuhusu VVU na unyonyeshaji wa watoto.

Pia tunapenda kutoa shukrani kwa shirika la Tearfund kwa kutushirikisha sisi wa Mikakati ya Kuleta Matumaini mawazo yao kuhusu uandaaji wa mafundisho ya Biblia kwa mada zinazohusiana na VVU na UKIMWI. Jambo hili ndilo lililopelekea kupatikana kwa kitabu kilichopewa jina la Mkono kwa Mkono: Mtaala wa Biblia kuboresha itikio kwa wito wetu kuhusu VVU. Tunawatakia Tearfund kila la heri na mafanikio katika kuchapisha kitabu hiki.

Kipekee tunawashukuru CAFOD, Interchurch Organization for Development Cooperation (ICCO) na Kerk in Actie, Lutheran World Federation, na World Vision International, ambao walifadhili uchapishaji na usambazaji wa kitabu hiki.

Glen WilliamsMhariri Wadhamini wa Mikakati ya Kuleta Matumaini

Vifupisho UKIMWI Upungufu wa Kinga Mwilini

ARV Dawa ya virusi-geuzi kupunguza makali ya VVU

VVU Virusi vya UKIMWI

VCT Ushauri-nasaha na Kupima kwa Hiari

Page 7: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

www.stratshope.org 5

Katika nchi mbalimbali duniani, makanisa na Wakristo binafsi wanaitikia wito wa Yesu Kristo wa ‘kumpenda jirani yako kama nafsi yako’ kwa njia ya kujihusisha na shughuli za kijamii zinazohusu changamoto nyingi za VVU na UKIMWI.

Katika Afrika - Kusini mwa Jangwa la Sahara, mara kwa mara makanisa yamekuwa mstari wa mbele katika kupunguza athari zinazotokana na VVU na UKIMWI. Wanadhihirisha mambo haya kwa njia mbalimbali kimatendo, kiasi kwamba wanajisikia ‘wameitwa kuwahudumia’ wale wenye maambukizi au walioathiriwa na janga la UKIMWI. Kwa mfano, wengi wamejitolea kwa njia ya kuanzisha huduma za afya ya msingi ambayo watu wanaoishi na VVU, na pia wamejitoa kuwapatia elimu, msaada wa kijamii, na huduma za afya watoto waliofanywa yatima kutokana na UKIMWI.

Hata hivyo, makanisa hayajafanikiwa sana katika kukabiliana na matatizo kama vile, jinsi ya kuzuia maambukizi ya VVU, unyanyapaa unaohusishwa na VVU, aibu na ubaguzi, utamaduni na mambo ya kijinsia yanayohusu tabia hatarishi za kujamiiana. Kukataa ukweli wa VVU na UKIMWI ndani ya jamii za kanisa kumetapakaa sehemu nyingi. Zaidi ya hayo, ingawa kwa sehemu kubwa maambukizi ya VVU katika nchi nyingi hutokana na kujamiiana, ni wazi kwamba ukweli huu hauzungumzwi kwa uwazi na pasipo kuhukumu katika makanisa mengi.

Pamoja na hayo, makanisa na taasisi mbalimbali za kidini wana uwezo wa hali ya juu wa kuwawezesha watu na jamii kwa njia ya kuwahamasisha katika kuwaelimisha, haja ya kubadili tabia, kuwapa stadi za maisha na mikakati inayohitajika kukabiliana na masuala ya kujamiiana, jinsia na UKIMWI. Ni wazi pia kwamba zaidi ya haya, nyakati hizi, viongozi wa kanisa wameona ipo haja ya kuongeza nguvu katika kukabiliana na masuala yanayoletwa na UKIMWI katika mtazamo mpana na kwa mkakati unaokidhi haja au unaojitosheleza.

Ili kusaidia katika jitihada hizi, shirika letu la Wadhamini wa Mikakati ya Kuleta Matumaini linaandaa machapisho ya vitabu vya Tumeitwa Kuhudumia. Vitabu hivi vimetengenezwa kwa njia ya seti ya vijitabu vyenye maelekezo kwa njia ya vitendo, vilivyo tayari kutumika, vikiwa na ujumbe kuhusu masuala ya VVU na UKIMWI kwa ajili ya makanisa na jamii hasa kwa ajili ya nchi zilizoko Afrika - Kusini mwa Jangwa la Sahara. Vijitabu hivi vya Tumeitwa Kuhudumia vinalenga katika kuwawezesha wachungaji, mapadre, watawa wa

kike na wa kiume, viongozi wa kanisa walei, waumini na jamii zao ili waweze:

Kutafakari na kuelewa uhalisia wa janga la UKIMWI kiroho, kitheologia, kimaadili, kiafya, kijamii na pia kutathimini kwa upya wito maalum wa Kikristo katika kushughulikia changamoto hizi kwa huruma.

Kuushinda unyanyapaa, ukimya, ubaguzi, kukataa, woga na hofu, masuala ambayo yanaliathiri kanisa na jamii kupambana na janga hili la UKIMWI kwa ukamilifu zaidi.

Kuwaongoza waumini wao na jamii kwa ujumla katika mchakato wa kujifunza na kubadilika, na hatimaye kupelekea kwenye matendo na mienendo ya kikanisa ili kuwasaidia watu binafsi, familia na jamii ili kupunguza kuenea kwa maambukizi ya VVU na kupunguza athari za UKIMWI.

Tumeitwa Kuhudumia ni vijitabu ambavyo matumizi yake ni rahisi, na muundo wake unafaa kwa makanisa na jamii katika ngazi tofauti za uelewa na uzoefu wa watu kuhusiana na janga la UKIMWI. Kitabu hiki Na. 7 katika mfululizo wa vitabu hivyo kinaleta pamoja masomo 20 ya Biblia yenye mada mbalimbali ambazo zote zinahusiana kwa karibu na VVU na UKIMWI.

Vitabu zaidi vya Tumeitwa Kuhudumia vinaendelea kuandaliwa. Vitakavyofuata awamu ijayo vitakuwa na mada kama vile malezi, usalama wa chakula na lishe, na stadi za maisha kwa vijana wadogo.

Mradi huu wa Tumeitwa Kuhudumia unatekelezwa kupitia mchakato wa kimataifa, mahusiano ya madhehebu, taasisi za Kikristo, mashirika ya kanisa ya kimataifa na mitandao yake, wachapishaji na wasambazaji wa vitabu, pamoja na washirika wengine.

Tunapenda kukualika ili ushiriki katika mradi huu wa Tumeitwa Kuhudumia, sio tu kwa kutumia vitabu hivi katika kanisa na jamii yako, lakini pia kwa njia ya kutuandikia na kutujulisha uzoefu wako, ambao tutakuwa tayari kuuandika katika tovuti ya shirika letu la Wadhamini wa Mikakati ya Kuleta Matumaini: www.stathope.org

Ndimi katika imani na mshikamamo,

Glen WilliamsMhariri Wadhamini wa Mikakati ya Kuleta Matumaini

DibajiKuhusu machapisho ya TUMEITWA KUHUDUMIA

Page 8: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

6 www.stratshope.org

NIITE

Washirika wa TUMEITWA KUHUDUMIA

Vitabu vya Tumeitwa Kuhudumia vinachapishwa na kusambazwa kwa kushirikiana na mashirika

yafuatayo ya kimataifa, kitaifa na ya kijamii:

Africa Christian Textbooks

African Holy Zionist Church

African Network of Religious Leaders living with or personally(ANERELA+)

Anglican Diocese of Eastern Zambia

Anglican Diocese of Southern Malawi

Balm in Gilead

CAFOD

Catholic AIDS Action

Christadelphian Meal-a-Day Fund

Christian Aid

Christian AIDS Bureau for Southern Africa

Christian Connections for International Health

Christian Council of Ghana

Christian Literature Fund

Council of Anglican Provinces of Africa

Ecumenical HIV/AIDS Initiative in Africa, World Council of Churches

Family Health International

Interchurch Organisation for Development Cooperation (ICCO)

International Christian Medical and Dental Association

International Network of Religious Leaders living with or personally (INERELA+)

Kachere Press

Kerk in Actie

Khulakahle Child Counselling and Training Forum

Lutheran World Federation

Masangane

Maurice and Hilda Laing Charitable Trust

Mercy Ships

Micah Initiative

Misereor

Missio Aachen

Organisation of African Instituted Churches

Tabernacle Sifa

Tearfund

United Society for the Propagation of the Gospel

Upendo AIDS Centre

World Vision International

Zentrum Oekumene.

affected by HIV and AIDS

affected by HIV and AIDS

Page 9: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

www.stratshope.org 7

NENO LA UTANGULIZI

Kitabu hiki ni matokeo ya warsha na jitihada za watu binafsi kutoka nchi nne za ki-Afrika. Mchakato ulianza kwa kufanyika kwa warsha ya siku nne iliyojulikana kama warsha ya waandishi na iliyofanyika Chipata, mji mkuu wa jimbo la mashariki nchini Zambia. Tulianza kwa kutengeneza muundo wa awali wa masomo ya Biblia, tukizingatia hamasa iliyotokana na jarida lijulikanalo kama Doing Contextual Bible Study: A Resource Manual, jarida hili liliandaliwa katika Ujamaa Centre mjini Pietermaritzburg, Afrika ya Kusini. Halafu tukatengeneza miswada ya masomo 12 kati ya 20 ambayo inaunda kitabu hiki. Pia tulipeleka miswada hii ili kuijaribu katika maeneo ya makanisa mbalimbali mashariki mwa Zambia ili kuona kama itafaa. Masomo manane mengine yalitengenezwa na kujaribiwa na washirika wenzetu nchini Ghana, Afrika ya Kusini na Tanzania.

Washiriki katika warsha ya waandishi walitoka katika madhehebu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Anglikana, Katoliki, Lutherani, Methodisti, Pentekoste na Reformed Church; yote haya ni kutoka nchi mbalimbali. Masomo matatu yalitengenezwa na kiongozi wa kanisa kwa kushirikiana na watu wanaoishi na VVU nchini Afrika ya Kusini.

Zoezi la kutengeneza na kuyajaribu masomo haya ya Biblia lilikuwa na changamoto nyingi lakini pia limekuwa ni zoezi lililotupa uzoefu wa hali ya juu. Sisi sote tunahusika kwa namna moja au nyingine katika kanisa na jamii katika kupambana na janga hili la UKIMWI ambalo limetuathiri sote. Sisi sote tunatumia Biblia tunapoabudu kwa pamoja, katika huduma zetu na pia katika maisha yetu binafsi. Lakini hatujawahi kujaribu kutumia utaratibu maalum wa kuunganisha mambo mengi muhimu yanayohusiana na janga la UKIMWI na vifungu vya mafundisho mbalimbali ya kwenye Biblia, na hivyo kupata mwogozo na hamasa ya pekee kutokana na uhusiano huu. Tumeona kwamba jambo hili ni zuri sana na lenye tija. Kwa mchakato huu, sisi kama kanisa tumekumbushwa kuwa tumeathiriwa kwa kiasi kikubwa na janga la UKIMWI. Lakini pia tumekumbushwa kuwa, sisi kama mwili wa Kristo, tayari tuna raslimali za kiroho na kimaadili kuweza kukabiliana na changamoto kubwa ziletwazo na janga hili.

Tunapenda kuyashukuru makundi mbalimbali ya makanisa kutoka nchi mbalimbali ambao walitusaidia kufanyia majaribio ya kitabu hiki na kukifanya kuwa cha muhimu na msaada kwa mahitaji ya kanisa na jamii.

Ni tumaini letu kubwa kwamba kitabu hiki kitaweza kutumiwa sehemu nyingi na mbalimbali katika makanisa na makundi ya jamii, kwa mashirika yasiyo ya kiserikali na mashule, katika vyuo vya Biblia na seminari za theologia, kwa makundi ya waumini na familia, na kwa watu wanaoishi na uambukizo wa VVU. Tmnajishughulisha na mapambano dhidi ya UKIMWI pamoja na kupambana na changamoto nyingi zitokanazo na janga hili.

Askofu William Mchombo

Dayosisi ya Zambia Mashariki ya Kanisa Anglikana

Chipata, Zambia

Page 10: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

8 www.stratshope.org

NIITE

Kwa ajili ya nani?Kimsingi kitabu hiki kimeandikwa kwa ajili ya makanisa, mashirika ya dini, na makundi ya jamii za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, lakini kinaweza kutumika kulingana na mazingira husika sehemu nyingine duniani. Kitabu hiki kimekusudiwa kutumiwa sio tu na wachungaji, makasisi, mapadre na watawa wa kiume na wa kike, lakini pia kinaweza kutumika katika vikundi vingine vya kanisa pamoja na vikundi vya maombi na vya kujifunza Biblia, faragha za akina mama na akina baba, klabu za vijana na makundi yoyote yale mengine ambayo mkazo wa kuwepo kwake ni pamoja na kujishughulisha na VVU na UKIMWI. Kitabu hiki kinaweza kutumika pia kwa watu wanaoishi na uambukizo wa VVU na mashirika mengine ya kijamii ambayo hayana mwelekeo au mkazo wa kidini. Mashirika yasiyo ya kiserikali yatagundua kuwa kitabu hiki kinaweza kuwa chombo cha muhimu katika kujenga uhusiano wa kufanya kazi pamoja na makanisa. Katika Shule za Biblia na Vyuo vya Theologia ua taasisi nyingine za mafunzo kanisani wataweza kuona kuwa kitabu hiki kinaweza kuwa cha msaada kwa kozi zake pia. Shule za sekondari za kanisa zitaweza pia kuona kuwa kitabu hiki ni cha msaada kwa walimu na wanafunzi katika kuzungumzia masuala mbalimbali yanayohusu VVU na UKIMWI kwa mapana yake.

Masomo ya Biblia yaliyomo katika kitabu hiki yameandaliwa ili yaongozwe na watu wenye uzoefu wa Biblia, wenye uelewa mzuri kuhusu janga la UKIMWI, na wenye uzoefu wa kuongoza mikutano kwenye jamii. Hakuhitajiki mafundisho maalum ili mtu aweze kutumia kitabu hiki, isipokuwa ni lazima kiongozi wa masomo ya Biblia asome kwa makini utangulizi wa kitabu hiki na ajiandae vema kwa kila kipindi

kwa kusoma vifungu husika vya Biblia na kutafakari kwa kina yaliyomo katika kila somo.Tunashauri kwamba idadi ya watu katika kila kikundi cha masomo ya Biblia iwe kati ya 15-30. Watu wenye rika mbalimbali, jinsi zote, wanaweza kushiriki. Inashauriwa kwamba kila atakayeongoza somo la Biblia ni vema awe na wasaidizi kati ya wawili hadi wanne, ambao wanaweza kuongoza vikundi vidogo vidogo mahali ambapo majadiliano mengi yatafanyika. Kimsingi, ni lazima kiongozi na wasaidizi wake wote wawe na nakala ya kitabu hiki.

Kwa nini?Makanisa duniani kote yameathiriwa na janga la UKIMWI kwa namna nyingi mbalimbali. Katika nchi nyingi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, karibu kila kanisa lina watu wanaoishi na VVU – pengine kwa kujua au kutokujua, pengine kwa kujiweka wazi hali zao, au kwa siri. Kwa makasisi na viongozi walei wa makanisa haya, kuongoza ibada za mazishi na kuwafariji

ugonjwa wa UKIMWI imekuwa ni sehemu ya kawaida ya huduma ya kanisa. Waumini wengi (kwa sehemu kubwa wanawake) wanatumia masaa mengi kila wiki katika kutoa huduma za kijamii kwa matendo, kiroho, na msaada wa vitu kwa yatima na wajane ambao wameathiriwa na VVU na UKIMWI.

Ili kujifunza kuhusu VVU na UKIMWI, kwa kawaida tunasoma vitabu vya wanasayansi, madaktari na wataalam wengine wa afya, wakereketwa wa masuala ya jamii na wanahabari. Wakati vitabu vya Biblia vilipokuwa vikiandikwa hapakuwa na janga la UKIMWI. Lakini ni wazi kwamba Biblia ina hazina kubwa ya mafundisho na mwongozo wa kimaadili, msaada wa kiroho, na ujumbe uletao hamasa

UtanguliziSehemu hii ya kitabu inaainisha mambo yafuatayo:

Kitabu hiki ni KWA AJILI YA NANI KWA NINI kitabu hiki kiliandikwa. Kitabu hiki KINAHUSU NINI. Kitabu hiki kinaweza kutumika WAPI na LINI. Kitabu hiki KITUMIKEJE ili kilete tija.

Tafadhali soma sehemu hii ya kitabu kabla hujaanza kutumia masomo ya Biblia ambayo yanaunda kitabu hiki.

Page 11: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

www.stratshope.org 9

UTANGULIZI

Waumini wengi (hasa wanawake) wanatumia muda mwingi kila wiki katika kutoa huduma za kijamii kwa matendo, kiroho na msaada wa vitu kwa yatima.

kuhusu ni kwa jinsi gani tunaweza kukabiliana na changamoto nyingi mno zinazoletwa na VVU na UKIMWI. Ingawa tunaweza kutumia Biblia mara kwa mara katika maisha yetu, wengi wetu hatujaisoma Biblia kimpangilio ili kuona inatufundisha nini kuhusu mbinu za kupambana na janga la UKIMWI na masuala yanayoandamana na kuwepo kwa janga hili. Hii ndio maana sahihi ya jinsi kitabu hiki kinavyolenga kutoa mwongozo katika mambo ya kufanya. Kinahusu nini?Kitabu hiki kina masomo 20 ya Biblia kuhusu mada kama vile kujamiiana na nidhamu yake, ndoa, tumaini, uongozi wa kanisa, msamaha, watu wanaoishi na VVU, hofu na wasiwasi, unyanyapaa, watoto, na kifo, huzuni na maombolezo. Kila somo linatakiwa kuchukua muda kati ya dakika 90 na masaa mawili kukamilika.

Kitumike wapi na lini?Vipindi vya masomo ya Biblia vinaweza kufanyika katika sehemu nyingi mbalimbali: kwa mfano, makanisani na katika kumbi za kanisa, nyumba za watu binafsi, madarasani, kwenye

nyumba za kijamii, au sehemu wazi yoyote ile chini ya mti. Vipindi vinaweza kuandaliwa aidha mara chache au mara nyingi, kama vile mara moja kwa wiki. Vipindi vinaweza pia kufanyika mara kwa mara, kwa mfano wakati wa warsha na makongamano, ambapo vipindi vitatu au vinne vinaweza kufanyika ndani ya siku moja.

Kitumikaje?Masomo 20 yaliyomo katika kitabu hiki yamegawanyika katika mada kuu sita (angalia kipengele cha yaliyomo). Mgawanyo huu unalenga kutoa mwongozo katika yaliyomo ndani ya kitabu. Hii haimaanishi kuwa huu ni mfumo usioweza kubadilika. Yeyote atakaye tumia kitabu hiki anatakiwa kuwa huru katika ‘kuchagua na kuchanganya’ masomo yoyote yale ambayo yanahusu zaidi mapendekezo, matakwa na mahitaji ya kikundi husika.Kila somo lina hatua saba, kuanzia utangulizi (Hatua ya Kwanza) na kuendelea katika kusoma aya moja au zaidi katika Biblia (Hatua ya Pili), hii husomwa kwa sauti kwa Kiswahili, au kwa lugha ya mahali husika. Hatua ya Tatu inahusisha pia kusoma kifungu kifupi cha maandishi (kilichoweka ndani ya boksi) chenye kichwa cha maneno Mazingira ya ki-

Page 12: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

10 www.stratshope.org

NIITE

Biblia, ili kusaidia kikundi husika katika kuelewa mazingira ya kijamii, kidini na kihistoria wakati aya hizi za Biblia zilipoandikwa. Kiongozi wa somo anaweza kuamua pengine kusoma kwa sauti sehemu hii au kutumia maneno yake mwenyewe ili kufikisha ujumbe unaokusudiwa. Maswali kadhaa (Hatua ya Nne) hufuata, kusaidia kikundi kuelewa umuhimu wa aya husika. Majadiliano haya yote hufanyika katika kundi zima.

Katika Hatua ya Tano, kiongozi wa mafunzo anatambulisha mada inayohusu VVU ambayo inaelezewa katika kifungu au vifungu vya Biblia. Kifungu kidogo cha maandishi kimeandikwa (kilichowekwa ndani ya boksi), chenye kichwa cha maneno Mazingira ya VVU na UKIMWI. Kiongozi wa somo anaweza kuamua pengine kusoma kwa sauti sehemu hii au kutumia maneno yake mwenyewe ili kufikisha ujumbe unaokusudiwa. Hapo sasa hufuata maswali kadhaa, ambayo yatajadiliwa na kundi zima, halafu hugawanywa katika vikundi vidogo- vidogo vya watu watano au sita kila kikundi.

Kila kikundi kidogo watatakiwa kujadili seti ya maswali au kutoa mwitikio wa pendekezo fulani, kama vile kuandaa ushuhuda wa mtu binafsi, au kutengeneza mchezo wa kuigiza, au kuchora mchoro, au kutunga wimbo au shairi. Vikundi hivyo vidogovidogo halafu vitatakiwa kuja pamoja tena (Hatua ya Sita) na kiongozi wa somo anawakaribisha wanavikundi kutoa mrejesho kuhusu majibu ya maswali na mapendekezo.

Katika kipengele cha mwisho (Hatua ya Saba), kiongozi atawauliza kundi lote kuhusu mapendekezo yao jinsi kanisa na jamii wanavyoweza kushughulikia matatizo ambayo wamekuwa wakiyajadili. Kipindi cha somo la Biblia hufungwa kwa sala, na wakati mwingine kwa kusoma kifungu kifupi cha Biblia au kwa wimbo.

Ingawa miongozo hii ni muhimu, unaweza kuwa huru kurekebisha kila somo la Biblia kulingana

na mazingira na mahitaji halisi ya wakati husika. Kama ilivyokuwa huko kwenye Kituo cha Ujamaa mjini Pietermaritzburg, Afrika ya Kusini ambako walitayarisha mbinu ya kufundishia Masomo haya ya Biblia kimazingira walibaini kwamba:

“Unahitaji kufanya masomo haya ya Biblia kuwa yako mwenyewe, uwe huru katika kuyatumia, unaweza kuyarekebisha kwa kuzingatia uhitaji na mazingira husika, na hata kuunda masomo mengine kama haya yatakayokidhi uhitaji wa mazingira yako”.

Utahitaji jitihada ndogo sana katika kukidhi mahitaji ya zana za kufundishia: kama kuna uwezekano, ni vema kila mshirika awe na Biblia yake; utahitaji bango kitita na kalamu zake za wino; na kila mshiriki awe na daftari lake au makaratasi ya kuandikia mafundisho pamoja na kalamu ya mkaa au ya wino.

Kabla ya kuanza masomo ya Biblia, utahitaji kuchagua lugha utakayotumia au utakazotumia. Mara kwa mara itabidi utumie lugha mama, kitu ambacho ni wazi kwamba kitakufanya usome Biblia kwa sauti tena kwa lugha ileile uliyoamua kutumia. Kama kuna kitu utaandika ubaoni, basi kumbuka kusoma kwa sauti ili kuwapa fursa wale wasiojua au wasio na uwezo wa kutosha wa kuandika waweze kuelewa mada inayozungumziwa.

Kumbuka na zingatia ukweli kwamba wakati wa majadiliano kuna uwezekano mkubwa wa hoja nzito kujitokeza na hata pengine ikatokea kutokukubaliana katika hoja kadha wa kadha. Wakati mwingine itakulazimu kuhakikisha unadhibiti majadiliano ili somo liendelee, licha ya kwamba baadhi wa washiriki wanaweza kutokukubaliana na hoja za walio wengi. Katika mazingira ya aina hiyo, unaweza kuamua kutenga muda wa kukutana na wahusika baadaye au pengine unaweza kumwomba mtu mwingine wanayemheshimu (kama vile kiongozi wa dini au mwalimu) waweze kusaidia katika kutoa mwongozo katika mada inayoleta mvutano.

1 Gerald West and Ujamaa Centre staff, Doing Contextual Bible Study: A Resource Manual, Ujamaa Centre for Biblical

and Theological Community Development and Research, Pietermaritzburg.

Page 13: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

www.stratshope.org 11

UAMINIFU WA MUNGU

Uaminifu wa Mungu…1. Neema ya Mungu

Malengo ya Kujifunza

1. Kuelewa na kuthamini uwepo wa neema ya Mungu katika maisha ya watu wanaoishi na VVU ikiwa ni pamoja na wale wanaowasidia na kuwahudumia.

2. K neema ya Mungu

Aya: 1 Wakorintho 15:8-11; 1 Timotheo 1:12-14; Waefeso 2:8-9.

Hatua ya Kwanza Dakika 5Wakaribishe washiriki wote na wakaribishe wageni nao wajitambulishe. Mwombe mshiriki mmojawapo kufungua kipindi kwa sala.

Eleza kwamba somo la Biblia la leo litakuwa na mada kuhusu neema ya Mungu katika mazingira ya janga la UKIMWI. Katika kuwaandaa washiriki ili wajiweke sawa kwa somo hili, waombe waimbe fungu moja au mawili ya wimbo wa “Neema ya Ajabu (Amazing Grace)” au wimbo wowote unaoelezea habari za neema ya Mungu.

Hatua ya Pili Dakika 5Waombe washiriki watatu, kila mmoja asome aya moja kati ya zifuatazo; 1 Wakorintho 15:8-11; 1 Timotheo 1:12-14; na Waefeso 2:8-9.

Kama washiriki wana Biblia zao, waombe kila mmoja aweze kufungua sehemu ya aya ya Biblia inayosomwa ili aweze kufuata inaposomwa.

Hatua ya Tatu Dakika 101. Waulize washiriki kutaja mambo yaliyovuta zaidi hisia zao katika kila aya iliyosomwa. Watie moyo washiriki kadhaa kutoa mawazo yao kwa kifupi - angalau maneno matano au sita. Andika mawazo yao kwenye bango kitita.

2. Waeleze taarifa za ziada ambazo ni za muhimu zilizoko kwenye boksi la Mazingira ya ki-Biblia (kulia):

Hatua ya Nne Dakika 10Waombe washiriki kujadili maswali yafuatayo yaliyoorodheshwa kwenye bango kitita, ambayo yatakuwa yamewekwa mahali ambapo kila mshiriki ataweza kuyaona kwa urahisi.

Mazingira ya Ki-Biblia

Neno “neema” linapatikana mara nane tukatika Agano la Kale, lakini katika AganoJipya, neno neema limetumika mara 116. Hii

haijitokezi katika hali ya kubahatisha: kama anavyotueleza Yohana1:17, “Kwa kuwa toratiilitolewa kwa mkono wa Musa; neema nakweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo. “lakinini nini hasa maana ya maneno“ neemaya Mungu”? Mtume Paulo alipowaandikianyaraka hizi Wakristo wa Korintho, mjoli namsaidizi wake Timotheo, na kwa Wakristowa kanisa la Efeso, alikuwa na maana kuutatu. Kwanza alilenga katika kuonyesha kuwaMungu anatupokea sote pasipo mashartiyoyote. Ukiachilia mbali dhambi na udhaifuwetu, pamoja na makosa yetu tuliyoyatendazamani, bado Mungu anatupenda nakututhamini, jinsi tulivyo. Pili alitaka kusisitiza ya kwamba neema ya Mungu haitolewikwetu kwa kuwa tumestahili kuipokea. Kwakweli hatuwezi hata kidogo kustahili neemahii. Linalotupasa kufanya ni kuipokea na kuikubali. Hii ndiyo maana halisi ya wimbounaopendwa sana wa “Neema ya Ajabu”.Sababu ya tatu, alitaka kusisitiza kwamba,

dhambi zetu na kurudishiwa uhusiano wetuna Mungu.

Page 14: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

12 www.stratshope.org

NIITE

a) Taja lugha zinazotumika mara kwa mara kuelezea neno ’neema’ kama zinavyopatikana katika vifungu vya Biblia.

b) Je, Biblia inamaanisha nini hasa kila linaposomeka neno ‘neema ya Mungu’?

c) Je, ni jambo gani hasa linaifanya neema ya Mungu kuwa ya ‘ajabu’?

d) Je, Paulo anasema nini kuwa anaweza kufanya kazi kupitia neema ya Mungu?

Hatua ya Tano Dakika 251. Waombe watu wawili au watatu waweze kusoma kwa sauti habari za ndugu Henry Ntege na shirika la TASO (kwenye boksi hapo chini) kuhusu Mazingira ya VVU na UKIMWI.

2. Waombe washiriki wajigawe katika vikundi vidogovidogo vya watu kama watano au sita kwenye kila kikundi. Waombe kwamba katika kila kikundi wajadili na kujibu maswali manne yafuatayo. (Utapaswa kuwa umeyaandika

maswali hayo ubaoni au katika bango kitita) Weka bango kitita mahali ambapo kila mshiriki atayaona maswali hayo vizuri.

a) Je, neema ya Mungu ilionekana kwa namna gani wakati ndugu Henry Ntege alipoamua kutangaza waziwazi kanisani kuhusu hali yake ya kwamba anaishi na VVU?

b) Je, Henry alipataje neema kupitia Shirika la Msaada wa mambo ya UKIMWI (TASO)?

c) Je, kuna mtu miongoni mwa washiriki ambaye anaweza kutushirikisha habari zake binafsi za uzoefu wake katika kuipokea neema ya Mungu kupitia mtu mwingine? (Habari hizi zinaweza kuwa zinahusu VVU au UKIMWI, lakini sio lazima.)

d) Je, kuna mmojawapo miongoni mwa washiriki ambaye ana rafiki au mtu miongoni mwa familia yake, anayeishi na VVU ambaye ameweza kupata ujasiri na msaada kutokana na neema ya Mungu? Tafadhali toa ufafanuzi.

Mazingira ya VVU na UKIMWI

Katikati ya kipindi hiki cha janga la UKIMWI, bado neema ya Mungu inatenda kazi hapa duniani. Tunaweza kushuhudia jambo hili katika maisha ya watu wanaoishi na VVU na pia katika maisha ya wale wanaowatunza na kuwahudumia. Ifuatayo ni habari ya ukweli inayomhusu ndugu Henry Ntege, ambaye ni miongoni mwa watu wa awali kabisa nchini Uganda kujitangaza kwa uwazi kwamba anaishi na VVU. Mnamo mwaka 1990, mara tu baada ya ibada, Henry Ntege akiwa kanisani kwake, kanisa la Mt. Andrea, Kampala Uganda, alisimama na kutangaza kwamba yeye alikuwa anaishi na UKIMWI. Mwanae wa kiume, Bruce anakumbuka mazingira ya tukio lenyewe: “Baadhi ya watu hawakumwamini. Maana wamemwona huyu mtu wakiwa naye kanisani kila Jumapili…Nadhani kila mtu humo kanisani siku ile alimuhukumu. Walifikiri kwamba Mungu alikuwa anamwadhibu kutokana na maisha yake ya uasi mbele za Mungu hasa katika suala zima la ngono…

Lakini Henry

kuhudhuria kanisani na baadaye watu walikubaliana. Hata alishiriki meza ya Bwana akitumia kikombe kilekile ambacho kila mmoja alitumia…Baada ya hapo alitoa mihadhara kwa umma mara nyingi tu, na alisikika redioni na kuonekana katika luninga. Kabla ya hapo ni kama alikuwa kifungoni. Lakini mara tu alipotangaza hali yake kwa wazi, alijihisi kwamba anaweza sasa kusema, yuko huru”. Henry alikuwa miongoni mwa watu wa awali nchini Uganda kutangaza kwa uwazi kwamba anaishi na VVU. Kupitia ushuhuda wake, watu wengine wengi walifuata na kutangaza kwamba na wao wanaishi na VVU. Baadaye Henry alipata fursa ya kuwa mfanyakazi katika shirika la The AIDS Support Organisation (TASO) lililoanzishwa mwaka 1987 na kikundi cha watu 16 waliokuwa wanaishi au waliokuwa wameathiriwa na VVU. Kupitia shirika la TASO, maelfu ya watu kama Henry Ntege, sio tu wamepokea tiba na msaada wa kijamii, bali wamerudishiwa kwa upya heshima yao na kuthaminiwa tena.

2 Kwa maelezo zaidi kuhusu habari hii, angalia kitabu Na. 15 cha Mikakati ya Kuleta Matumaini, Open Secret, uk. 27, kinachopatikana kutoka Teaching–aids at Low Cost (TALC: www.talkuk.org; [email protected]

aliendelea 2

Page 15: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

www.stratshope.org 13

UAMINIFU WA MUNGU

Hatua ya Sita Dakika 30Sasa ni wakati wa vile vikundi vidogovidogo kukusanyika kwa pamoja na kutoa taarifa ya mijadala yao na majibu ya maswali na mapendekezo. Kwa wale ambao watakuwa wameandaa michoro au shuhuda binafsi wakaribishwe ili kuwasilisha mambo yao.

Hatua ya Saba Dakika 101. Waulize ni kwa jinsi gani, kama jamii ya Kikristo, tunavyoweza kusaidiana ili kuipokea neema ya Mungu katika zama hizi za janga la UKIMWI. Andika mapendekezo ya washiriki kwenye bango kitita.

2. Waombe washiriki kutaja mambo ya kuombea. Halafu wape nafasi waombee mambo waliyoyataja.

3. Waombe washiriki kukaa kimya kwa dakika moja au mbili ili waweze kutafakari waliyojifunza.

4. Hitimisha somo kwa kuomba kwa sauti: “Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, na pendo la Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote.” (2 Wakorintho 13:14)

“Neema ya ajabu, jinsi ilivyo tamu sauti”

Page 16: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

14 www.stratshope.org

NIITE

Hatua ya Kwanza Dakika 5Wakaribishe washiriki wote na wageni uwape nafasi ya kujitambulisha. Mwombe mshiriki mmojawapo kufungua kipindi kwa sala.

Eleza kwamba somo la Biblia la leo litakuwa na mada kuhusu kuonyesha huruma kwa watu ambao kwa mtazamo wa jamii wametenda dhambi na wanaweza kuonekana tofauti na sisi, badala ya kuwahukumu kikatili.

Hatua ya Pili Dakika 5Waombe washiriki wawili wasome aya kutoka injili ya Yohana 8:1-11. Kama washiriki wana Biblia zao, waombe kila mmoja aweze kufungua sehemu ya aya inayosomwa ili aweze kufuata inaposomwa.

Hatua ya Tatu Dakika 101. Waulize washiriki kutaja mambo yaliyovuta zaidi hisia zao katika aya iliyosomwa. Watie moyo washiriki kadhaa kutoa mawazo yao kwa kifupi - angalau maneno matano au sita. Andika mawazo yao kwenye bango kitita.

2. Ongezea taarifa za ziada kutoka kwenye boksi la Mazingira ya Ki-Biblia (kulia):

Hatua ya Nne Dakika 10Waombe washiriki kujadili maswali yaliyoorodheshwa kwenye bango kitita, ambayo yatakuwa yamewekwa mahali ambapo kila mshiriki ataweza kuyaona kwa urahisi.

a) Je, ni kwa nini viongozi wa dini ya Kiyahudi walimpeleka mama huyu kwa Yesu?

b) alipokuwa katikati ya kundi la watu waliokuwa wakimtuhumu na kumlaani?

c) Je, Yesu alionyeshaje huruma kwa mama huyu?

d) Je, ni kwa nini walianza kuondoka mmoja mmoja mara baada ya Yesu kuwaambia kwamba kama kuna mtu asiye na dhambi na awe wa kwanza kumtupia jiwe mwanamke huyu?

2. Haki ya Mungu Malengo ya Kujifunza

1. Kuchunguza ni kwa sababu gani watu wanaoishi na VVU wanahukumiwa kikatili na watu wengine.

2. Kuhimiza tabia na mazingira ya huruma miongoni mwa watu badala ya kuhukumiana.

Aya: Yohana 8:1-11.

Mazingira ya Ki-BibliaKulingana na Sheria ya Musa, adhabu ambayo mtu atapewa akikutwa katika uzinzi ni kupigwa mawe mpaka afe, kwa wote wawili mwanamume na mwanamke. Kwa walimu wa Sheria na Mafarisayo, kusimamia Sherialilikuwa ni jambo lililopewa kipaumbele, na ndiyo sababu katika Agano Jipya wanafadhaishwa sana Yesu anapojichanganya na “wenye dhambi”, kimsingi akiwa anavunja Sheria. Kwa hiyo, kwa makusudi kabisawalimwekea Yesu mtego: Je, atasimamiaSheria, na hivyo kutofautiana na maishana mafundisho yake, au je atasimamia mafundisho na kanuni zake kiutendaji, na kwa hali hiyo kuonyesha wazi kwamba anampinga Musa?

Yesu alikataa kutoa jibu la haraka kwa swali lao. Badala yake aliamua kutoa jibu kwa njia ya kuandika chini katika nchi. Hatuambiwi aliandika nini, lakini inawezekana aliandika maneno yake yanayohusiana na: “Kama kuna mtu miongoni mwenu ambaye hajafanya dhambi basi na awe wa kwanza kumtupia mwanamke huyu jiwe”. Kwa kufanya hivi, Yesu alihamishamtazamo wao kutoka kwa mwanamke yule na yeye mwenyewe kuuelekeza kwa washitaki wake, ambao waliondoka mmoja mmoja,huku wale watu wazima wakiwa wa kwanza kuondoka.

ddhahabubu aambmbaayyoo

Page 17: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

www.stratshope.org 15

UAMINIFU WA MUNGU

e) Je, kwa nini ni mwanamke peke yake ndiye aliyeletwa kwa Yesu lakini sio mwanamume?

f) Maneno ya mwisho ya Yesu kwa mwanamke yalikuwa na umuhimu gani?

Hatua ya Tano Dakika 301. Tambulisha mawazo yaliyoko kwenye boksi la Mazingira ya VVU na UKIMWI (hapa chini).

2. Waombe washiriki wajigawe katika vikundi vidogovidogo vya watu kama watano au sita kwa kila kikundi. Waombe kwamba katika kila kikundi wajadili na kujibu maswali manne yafuatayo. Utapaswa kuwa umeyaandika maswali hayo ubaoni au katika bango kitita. Weka bango kitita mahali ambapo kila mshiriki atayaona maswali hayo vizuri.

a) Je, unadhani ni kwa nini watu wanakuwa wepesi kuwahukumu watu wanaoishi na VVU na wenye UKIMWI badala ya kuonyesha huruma?

wengi wa kiume

Mazingira ya VVU na UKIMWI

Katika jamii zetu, licha ya miaka mingi ya elimu kuhusu UKIMWI, watu wanaogunduliwa wana uambukizo wa VVU mara nyingi wanatendewa vibaya na watu kutoka kwenye familia zao,

zamani. Wakati mwingine manyanyaso haya ni

hata kuwalaani kwamba ni watu wasiokuwa na maadili mema. Hukumu hizi katika misingi ya maadili mara nyingi hutokea katika mazingira ya tetesi, wivu, na taarifa zisizo za kweli.

Hata hivyo, sote tumetenda dhambi. Kama Paulo alivyoandika katika Warumi 3:23: “Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.” Katika mazingira ya janga la UKIMWI, baadhi yetu tumetenda dhambi kwa njia ya tabia zetu mbaya za ngono; baadhi yetu tumewanyoshea kidole na kuwalaumu wenzetu; baadhi yetu tumefanya mioyo yetu kuwa migumu kwa watoto waliofanywa yatima na wajane kutokana na janga hili la UKIMWI. Kwa kiasi fulani, sote tumeshindwa kuishi kwa kutimiza Amri Kuu ya pili: “Mpende jirani yako kama nafsi yako”.

Baadhi yetu tumewanyosheavidole na kuwalaumu watu wengine.

marafiki na wanafamilia zao, kuwakwepa na

Page 18: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

16 www.stratshope.org

NIITE

b) Je, tunawatendeaje watu wenye uambukizo wa VVU katika familia zetu, kanisani au katika jamii?

c) Kama wewe ungekuwa na uambukizo wa VVU, je, ungependa watu wakutendeeje?

d) Je, ni kwa jinsi gani tunaweza kuwahimiza watu kutenda matendo ya huruma kwa watu wanaoishi na VVU, badala ya kuwahukumu kikatili?

e) Waulize kama kuna mtu miongoni mwa washiriki ambaye anaweza kutushirikisha habari zake binafsi kulingana na uzoefu wake kuhusu kuhudumiwa kwa huruma kunavyoweza kumtia moyo na kumsaidia mtu anayeishi na VVU.

f) Je, kuna mtu miongoni mwa washiriki ambaye anaweza kutushirikisha habari zenye matukio tofauti: kama vile, mtu anayeishi na VVU ambaye ametendewa kwa kuhukumiwa na ameteseka sana kutokana na hayo?

g) Je, sisi kama watu binafsi, na kama waumini wa makanisa yetu na wanajamii, tunaweza kufanya nini ili kuchochea huruma badala ya mtazamo wa kuwahukumu watu wanaoishi na VVU?

h) Je, utajisikiaje kama ikitokea kwamba kasisi

wako, mchungaji, sista wa dini au kiongozi yeyote yule wa kanisa akigunduliwa ana uambukizo wa VVU?

i) Toa nafasi kwa watu wawili au watatu miongoni mwa washiriki na kuwaomba watunge igizo fupi katika kuzungumzia mambo haya.

Hatua ya Sita Dakika 30Sasa ni wakati wa vile vikundi vidogovidogo kukusanyika kwa pamoja na kutoa taarifa ya mijadala yao, na majibu ya maswali. Kwa wale ambao watakuwa wameandaa igizo, hadithi au shuhuda binafsi, wakaribishwe ili kuwasilisha mambo yao.

Hatua ya Saba Dakika 101. Waulize kile tunachoweza kufanya kusaidia familia, kanisa na jamii zetu kushughulikia matatizo ambayo tumekuwa tukiyajadili. Andika mapendekezo kwenye bango kitita.

2. Mwombe mshiriki mmoja asome kwa sauti maandiko matakatifu yanayopatikana katika Mathayo 7:1-5.

3. Hitimisha somo kwa kuwaongoza washiriki katika sala, au kwa kumwomba mshiriki mmojawapo kufunga kwa sala.

Page 19: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

www.stratshope.org 17

UAMINIFU WA MUNGU

3. Upendo na msamaha wa Mungu

Malengo ya Kujifunza

1. Kufahamu kuwa watu wanaotambulika kama waliotengwa na jamii bado wanaweza kuwa karibu zaidi na Mungu kuliko wale wanaoonekana kuwa wanaheshimiwa na wenye mafanikio katika jamii.

2. Kujifunza kwamba watu wanaohisi kukumbatiwa na upendo wa Mungu wanapata uwezo wa kuwasamehe wale ambaao wanawaumiza.

3. Kujifunza kwamba kuhisi kupendwa na Mungu kunaweza kukupa nguvu ya kuchukua hatua isiyo ya kawaida katika maisha. Aya: Luka 7:36-50.

Hatua ya Kwanza Dakika 5Wakaribishe washiriki wote na wageni uwape nafasi ya kujitambulisha. Mwombe mshiriki mmojawapo kufungua kipindi kwa sala.

Eleza kwamba somo la Biblia la leo litakuwa na mada kuhusu upendo na kuangalia uwezo wetu wa kiroho katika kusamehe wale ambao wametuumiza.

Hatua ya Pili Dakika 5Waombe washiriki wawili, wasome aya ya Luka 7:36-50 .Kama washiriki wana Biblia zao waombe kila mmoja aweze kufungua sehemu ya aya katika Biblia inayosomwa ili waweze kufuata inaposomwa.

Hatua ya Tatu Dakika 101. Waulize washiriki kutaja mambo yaliyovuta zaidi hisia zao katika habari iliyosomwa. Watie moyo washiriki kadhaa kutoa mawazo yao kwa kifupi - angalau maneno matano au sita. Andika mawazo yao kwenye bango kitita.

2. Waeleze taarifa za ziada zinazohitajika kutoka kwenye boksi la Mazingira ya ki-Biblia (kulia):

Hatua ya Nne Dakika 10Wahamasishe na kuwashawishi washiriki wachache kufanya igizo, na washiriki wengine wakicheza nafasi ya wageni waalikwa kwenye chakula. Halafu waombe washiriki kujadili maswali yafuatayo, yaliyoandikwa kwenye

bango kitita, ambayo yatakuwa yamewekwa mahali ambapo kila mshiriki ataweza kuyaona kwa urahisi. a) Waalikwa wanasemaje kuhusu ‘mwanamke yule’ aliyemwendea Yesu? Wanasemaje kuhusu Yesu kumruhusu amguse?

Mazingira ya Ki-Biblia

Injili ya Luka ina mkazo malumu kuhusu wanawake. Inawahusisha wanawake kumi ambao hawatajwi katika injili nyingine yeyote kati ya zile injili nyingine tatu. Mwanamke anayetajwa katika habari hii anatajwa kwamba aliishi “maisha yenye dhambi”. Dhambi yake ilikuwa ni ipi hasa? Mapokeo yanamwelezea kuwa alikuwa malaya, lakini wazo pekee ambalo linapelekea mtazamo huo ni katika suala la nywele zake (ainisha na Hesabu 5:18). Hasira ya Simoni, Mfarisayo ambaye alikuwa mwenyeji wa Yesu, inaashiria kuwa dhambi ya yule mwanamke ilikuwa ya mazingira ya zinaa. (Mara nyingi wanawake walijiingiza katika umalaya kutokana na matatizo ya kijamii na kiuchumi. Kamawaume zao wamekufa na hapakuwa na mwanamume mwingine wa ukoo huo wa kumrithi, mara nyingi waliachwa pasipomsaada, hasa kama hawakujaliwa kuzaa watoto.)

Ishara ya kumkaribisha mgeni anayeheshimiwa sana, ilikuwa ni kumwambia mhudumu kumwosha mgeni miguu. Busu kutoka kwa mwenyeji wake na kumpaka mafuta kulionyesha ni kwa kiasi gani mgeni husika amepewa heshima. Kulingana na mazingira yalivyoonyesha, na hasa Simoni kutoonyesha ukarimu wa mila na desturihalisi, bila shaka mwaliko wake wa chakula

(inaendelea)

Page 20: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

18 www.stratshope.org

NIITE

b) Kwa nini mwanamke yule alilia na kufuta miguu ya Yesu kwa machozi yake?

c) Mwanamke yule alihisi kukubalika na kupendwa na Y kujisikia kuwa na uwezo wa kuwasamehe kumdhalilisha na kumdharau kutokana na hali yake ya maisha? Tafadhali thibitishwa hoja yako. (Taarifa kwa kiongozi: hakuna jibu ambalo ‘ni sawa’ na jibu ambalo ‘si sawa’ katika swali hili.)

d) Yesu anamwambia mwanamke: “Enenda kupata amani baada ya kutoka nyumbani

kwa Simoni? Tafadhali thibitisha jibu lako. (Taarifa kwa kiongozi: hakuna jibu ambalo ‘ni sawa’ na jibu ambalo ‘si sawa’ katika swali hili.)

Hatua ya Tano Dakika 251. Tambulisha mawazo kuhusu mazingira ya VVU na UKIMWI kama yalivyo katika boksi hapa chini.

2. Waombe washiriki wajigawe katika vikundi vidogovidogo vya watu kama watano au sita kwa kila kikundi. Wape kila kikundi maswali matatu kati ya hayo sita (yaliyoko hapo chini) ili kuyajadili na kutoa majibu. Utapaswa kuwa umeandika maswali haya ubaoni au katika bango kitita. Weka mahali ambapo kila mshiriki anaweza kuyaona maswali haya vizuri.

HADITHI HASIa) Unajua ya kwamba dada yako anayeitwa Loreto, mama mwenye watoto watano ana uambukizo wa VVU. Unajua pia ya kwamba kike. Dada yako anaogopa kwamba ndugu wa upande wa mume wake watamchukulia kuwa ni malaya na kumfukuza nyumbani kwake kama wakijua kuwa ana VVU. Je, wewe kama Mkristo, utamsaidiaje?

Mtu ambaye alihisi upendo wa Mungu kweli alikuwa ni yule mwanamke, na sio Simoni. Mtu ambaye Yesu alimsifu ni yule mwanamke wala sio Simoni. Ukweli ni kwamba, Yesu alimkaripia Simoni, mtu aliyeheshimiwa katika uongozi wa kidini, kwa sababu Simoni alihukumu badala ya kupenda. Mwanamke anaitikia upendo wa Mungu kwa machozi ya shukrani. Yesu anatambua uwezo wa upendo wa kina wa mwanamke huyu na anamwambia dhambi zako zimesamehewa. Makanisa mengi humalizia ibada ya Ushirika Mtakatifu kwa maneno yanayohitimisha habari hii: “enendeni kwa amani”.

Mazingira ya VVU na UKIMWI

Ni vigumu sana kwa watu wanaoishi na VVU kuweza kuwasamehe watu ambao wamewakosea kwa namna mbalimbali. Katika jamii nyingi, watu wenye VVU moja kwa moja hupachikwa jina ya kwamba wao ni wenye dhambi. Ikiwa, katika mazishi ya mtu fulani, itajulikana au kushukiwa kwamba amefariki kwa UKIMWI, mara nyingine inatokea kwamba marehemu na ndugu zake hawapati sifa njema na heshima wanayostahili.

Mara nyingi watu wanaoishi na VVU huhesabiwa

wamelaaniwa. Hii ndiyo sababu watu wengi hawako tayari kwenda kupima kwa hiari VVU. Wanawake wengi wako tayari kufa kuliko

kupachikwa jina la ‘mwanamke anayejirahisi’, au jina baya zaidi ya hilo. Hata kama hajashirikiana na mwanamume mwingine zaidi ya mumewe, bado mwanamke ambaye anaishi na VVU anaweza kupachikwa jina kwamba “ni mwanamke ambaye ana ‘ULE’ ugonjwa wa aibu na kufedhehesha.”

Watu wanapopimwa na kugundulika kuwa wana uambukizo wa VVU, wanaona vigumu sana kuwasamehe wale wanaowahisi kuwa inawezekana wao ndio waliowaambukiza na wale wanaowatendea vibaya. Wake wengi na wamama wanaoeleza hali zao za uambukizo wa VVU hufukuzwa na familia za waume zao. Akina mama wengi huona ni afadhali wafe, bila hata kwenda kupata matibabu ya magonjwa nyemelezi, kuliko kufukuzwa mbali na watoto wao.

nyumbani kwake ulikuwa wa hila iliyofichika

Page 21: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

www.stratshope.org 19

UAMINIFU WA MUNGU

b) Hebu fikiri kwamba wewe ni Loreto na unajua kwa hakika kabisa ya kwamba aliyekuambukiza VVU ni mume wako, kwa kuwa alikuwa ndiye mtu pekee uliyekuwa na mahusiano naye ya kimapenzi. Je, utaweza kumsamehe? Je, mchakato huo wa msamaha unaweza kuelezwa kwa maneno? Au je, msamaha ni ‘tukio’ la kiroho ambalo haliwezi kuelezeka kwa lugha yoyote? Tafadhali jadilini.

c) Je, ile habari ya mwanamke aliyehisi kupendwa na Yesu inaweza kumsadia Loreto kupata nguvu za kiroho kwenda mbele na kuwaambia ukweli wakweze na mumewe? Tafadhali toa maelezo kuhusu jibu lako.

d) Iwapo wakweze Loreto watamfukuza nyumbani na mumewe atampiga kwa sababu anamlaumu mke wake kwamba ameuleta UKIMWI katika familia, je atajuta kwamba alisema ukweli kuhusu tabia ya mumewe

ya kutokuwa mwaminifu? Je, ataweza kuwasamehe mumewe na familia yake? Tafadhali toa maelezo kuhusu jibu lako.

HADITHI MBILI CHANYA

e) Tafadhali buni mchezo wa kuigiza utokanao na hadithi ya kweli ifuatayo. Mume anarudi nyumbani akiwa mgonjwa baada ya kufanya kazi machimboni kwa muda wa miaka mingi. Anawaita majirani na marafiki, na kuwaeleza kuwa yeye ana UKIMWI na muda si mrefu atakufa. Anakiri pia kwamba amemwambukiza VVU mkewe, na anawaomba kwamba wasimtenge mkewe baada ya kufa kwake. Je, ni kitu gani kinampa ujasiri mume huyu kuchukua hatua hii? Je, majirani watakuwa na mwitikio gani? (Taarifa kwa kiongozi: kitu kilichotokea katika maisha halisi ilikuwa kwamba mke na watoto wa ndugu huyu hawakutengwa hata kidogo na jamii.)

Akina mama wanaokuwa wazi kueleza kuwa wanaishi na VVU wanaingia katika hatari ya kufukuzwa majumbani mwao na familia ya mumewe.

Page 22: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

20 www.stratshope.org

NIITE

f) Mama mjamzito anarudi kutoka kliniki, ambako amejulishwa kuwa yeye ana uambukizo wa VVU. Anamueleza mumewe, ambaye anafadhaika sana, lakini yeye alikwisha kupima kwa siri na kugunduliwa kuwa ana uambukizo wa VVU, lakini alikuwa hajawahi kumwambia mkewe. Mwanzoni, wote walilaumiana, lakini jambo hili haliwasaidii kutatua tatizo lao. Hatimaye siku moja baada ya wote wawili kuhudhuria kanisani, wanaamua kujaribu kuonyeshana upendo na msamaha. Pia wanaona tumaini la siku za mbele, kwa sababu bado hawaumwi sana. Kwa hiyo wanaweza kuchukua hatua muhimu ili waweze kuishi maisha ya afya ya kawaida na kupata matibabu yatakayowasaidia kuishi maisha marefu zaidi.

Hatua ya Sita Dakika 30Sasa ni wakati wa vile vikundi vidogovidogo kukusanyika kwa pamoja na kutoa taarifa ya mijadala yao na majibu ya maswali. Kwa wale ambao watakuwa wameandaa igizo, hadithi au ushuhuda binafsi wakaribishwe ili kuwasilisha mambo yao.

Hatua ya Saba Dakika 101. Waulize tunaweza kuzisaidiaje familia

zetu, kanisa na jamii kwa ujumla katika kutatua matatizo ambayo tumekuwa tukiyajadili. Andika mapendekezo ya washiriki kwenye bango kitita.

2. Hitimisha somo hili la Biblia kwa washiriki wote kusema Sala ya Bwana.

Page 23: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

www.stratshope.org 21

KANISA NA JANGA LA UKIMWI

Kanisa na janga la UKIMWI …4. Watu wanaoishi na VVU na kanisa Malengo ya Kujifunza

1. Kuchunguza ni kwa jinsi gani, ndani ya makanisa, tunaweza kusaidia kutengeneza mazingira ambayo watu wanaoishi na VVU wanaweza kujisikia wanakubalika, wanasaidiwa na kuthaminiwa.

2. Kutafuta fursa mpya kwa ajili ya watu wanaoishi na VVU waweze kushiriki kikamilifu na kuwajibika katika shughuli mbalimbali za huduma za kanisani, ikiwa ni pamoja na kujikinga na maambukizi ya VVU, matunzo na huduma kwa wenye VVU.

Aya: 1 Petro 2:4-7.

Hatua ya Kwanza Dakika 5Wakaribishe washiriki wote na wakaribishe wageni nao wajitambulishe. Mwombe mshiriki mmojawapo kufungua kipindi kwa sala fupi.

Eleza kwamba somo la Biblia la leo litakuwa na mada kuhusu nafasi ya watu wanaoishi na VVU katika uhai wa makanisa yetu. Kama watu hawa hawana nafasi ndani ya makanisa yetu, basi na tujiulize ni kwa nini.

Hatua ya Pili Dakika 5Mwombe mshiriki mmoja asome kifungu cha Biblia, 1 Petro 2:4-7 . Kama washiriki wana Biblia zao waombe kila mmoja aweze kufungua sehemu ya aya ya biblia inayosomwa ili aweze kufuata inaposomwa.

Hatua ya Tatu Dakika 101. Waulize washiriki kutaja mambo yaliyovuta

zaidi hisia zao kuhusu aya iliyosomwa. Watie moyo washiriki kadhaa kutoa mawazo yao kwa kifupi - angalau maneno matano au sita. Andika mawazo yao kwenye bango kitita.

2. Waeleze taarifa za ziada ambazo ni za muhimu zilizoko kwenye boksi la Mazingira ya Ki-Biblia (kulia):

Mazingira ya Ki-Biblia

Katika barua hii ya kichungaji ambayo Petro aliiandika akiwa Roma, anawaandikia makundi ya Wakristo waliotawanyika katika sehemu mbalimbali za Asia Ndogo. Anatumia lugha ya fumbo ya kuwaelezea Wakristo kuwa wao ni “mawe yaliyo hai”, hii yote ikisadia kueleza muundo wa kiroho wa kanisa. Ni wazi kwamba Petro alikuwa anaweka mkazo katika suala zima la umuhimu wa ushirika wa pamoja katika kanisa la mwanzo. Kumpokea Kristo halikuwa jambo tu la mtu binafsi, lakini lilihusisha kushiriki kikamilifu kwa waaminio. Wakristo wa mwanzo walitoka katika mazingira tofauti ya mila, dini na aina za kazi. Walikuwa ni pamoja na Wayahudi na Wamataifa, askari na wasanii, watumwa na walio huru wanawake kwa wanaume.

Petro ananukuu Isaya 28:16, ambapo anatoa tafsiri akimtaja Yesu kuwa ni “jiwe la pembeni katika Sayuni; na kila amwaminiye hatatahayari”. Hata hivyo, kwao wasioamini, Kristo ni “jiwe” wanalolikataa kuwa halina thamani. Katika kutambua kilicho cha muhimu sana katika muundo wa jengo la kiroho, ambalo ni kanisa, hiyo ni alama ya imani.

Page 24: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

22 www.stratshope.org

NIITE

Hatua ya Nne Dakika 10Waombe washiriki kujadili maswali yafuatayo, yaliyoorodheshwa kwenye bango kitita, ambayo yatakuwa yamewekwa mahali ambapo kila mshiriki ataweza kuyaona kwa urahisi.

a) Je, unafikiri ni kwa nini Petro anachagua kutumia wazo la ‘jiwe lililo hai’ kuwaelezea Wakristo aliokuwa anawaandikia?

b) Je, ni watu wa aina gani ambao walijiunga na makanisa ya Kikristo ya awali?

c) Je ni kwa nini ilikuwa muhimu kwa kanisa la awali kuwakaribisha watu kutoka katika mazingira mbalimbali ya mila, desturi, dini, na aina za kazi?

Hatua ya Tano Dakika 251. Tambulisha mawazo kuhusu mazingira ya VVU na UKIMWI kama yalivyo katika boksi hapa chini.

2. Waombe washiriki wajigawe katika vikundi vidogovidogo vya watu kama watano au sita kwa kila kikundi. Waombe kila kikundi kujadili na kujibu maswali angalau manne yafuatayo. Utapaswa kuwa umeyaandika maswali hayo ubaoni au katika bango kitita. Weka bango kitita mahali ambapo kila mshiriki atayaona maswali hayo vizuri.

a) Je, ni kwa namna gani, sisi kama kanisa, tunahusika katika kutoa elimu kuhusu VVU, jinsi ya kujikinga, huduma na matunzo? Tafadhali orodhesha shughuli hizo.

b) Je, ni nani anafanya kazi hizi kanisani kwetu?

c) Je, ni kwa namna gani watu wanaoishi na VVU waliomo makanisani mwetu wanashirikishwa katika kupanga na kutekeleza shughuli hizi?

d) Je, kanisa letu ni mahali ambapo watu wanaoishi na VVU, na familia zao, wanajisikia kukubalika na kuthaminiwa?

e) Je, kuna namna gani nyingine tunayoweza kufanya ili kuwasaidia watu wanaoishi na VVU, na familia zao, waweze kujisikia wanakubalika na kuthaminiwa katika makanisa yetu?

f) Je ni kwa njia zipi watu wanaoishi na VVU wanashiriki katika uongozi wa makanisa yetu? (Kwa mfano viongozi walei, wazee wa kanisa, wahubiri, wahudumu au walimu wa Shule za Jumapili?)

g) Je, ni vikwazo gani vinawafanya watu wanaoishi na VVU kushindwa kutimiza majukumu ya huduma hizi makanisani mwetu?

h) Buni igizo kuonyesha jinsi mtu anayeishi na VVU alivyonyimwa nafasi ya huduma kanisani kwake kwa sababu tu kulikuwa na tetesi kuwa yeye ana uambukizo wa VVU. Au pengine chora katuni au tunga shairi au wimbo kuhusu tukio hilo.

Hatua ya Sita Dakika 30Sasa ni wakati wa vile vikundi vidogovidogo kukusanyika kwa pamoja na kutoa taarifa ya mijadala yao na majibu ya maswali. Kwa wale ambao watakuwa wameandaaigizo, mchoro, shairi, wimbo au maombi wakaribishwe ili kuwasilisha mambo hayo.

Mazingira ya VVU na UKIMWI

Kwa muda mrefu, UKIMWI ulifikiriwa kuwa ni ugonjwa wa watu ambao wameishi maisha ya mashaka kimaadili. Tunaanza kutambua zaidi na zaidi kwamba mawazo hayo ni ya kupotosha ukweli. (Kwa mfano, katika nchi nyingi za Afrika Kusini mwa Janwa la Sahara wanawake wengi wanaoishi na VVU ni wale ambao wameshirikiana tendo la ndoa na waume zao tu, ambao ndio waliowaambukiza virusi). Lakini kutokana na taarifa hizi zisizo za kweli, watu wengi wanaoishi na VVU wamekuwa

wakikataliwa na familia zao, makanisa yao na jamii zao. Wamefikia hatua ya kushushwa hadhi ya ubinadamu wao, na kuonekana kama ‘wafu wanaoishi’. Mitazamo hii pia imewazuia watu wanaoishi na VVU kushiriki na kuishi maisha makamilifu katika makanisa yao. Wamekuwa kama jiwe lililokataliwa na wajenzi kwamba halifai, wametupwa na kunyimwa fursa za huduma katika jamii za waaminio. Jambo hili linawaumiza sana sana watu wanaoishi na VVU. Pia ni hasara kubwa sana sana kwa makanisa yetu na jamii zetu.

Page 25: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

www.stratshope.org 23

KANISA NA JANGA LA UKIMWI

Hatua ya Saba Dakika 101. Waulize, ni kwa namna gani uzoefu, ujuzi na stadi za watu wanaoishi na VVU vinaweza kutumiwa kwa mafanikio zaidi katika shughuli za makanisa yetu.

2. Hitimisha somo la Biblia kwa kuwaongoza washiriki katika sala, au kwa kumwomba mshiriki mmojawapo kuongoza sala ya kufunga.

Watu wengi wanaoishi na VVU wamekataliwa na jamii ya waumini wenzao.

Page 26: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

24 www.stratshope.org

NIITE

Hatua ya Kwanza Dakika 5Wakaribishe washiriki wote na wakaribishe wageni nao wajitambulishe. Mwombe mshiriki mmojawapo kufungua kipindi kwa sala.

Eleza kwamba somo la Biblia la leo litakuwa kuhusu matunzo na msaada kwa watu wanaoishi na VVU makanisani mwetu na katika jamii zetu.

Hatua ya Pili Dakika 5Waombe washiriki wawili, wasome Mathayo 25:31-46. Kama washiriki wana Biblia zao waombe kila mmoja aweze kufungua sehemu ya aya ya Biblia inayosomwa ili aweze kufuata inaposomwa.

Hatua ya Tatu Dakika 101. Waulize washiriki kutaja mambo

yaliyowavutia zaidi katika habari hii. Watie moyo washiriki kadhaa kutoa mawazo yao kwa kifupi – angalau maneno matano au sita. Andika mawazo yao kwenye bango kitita.

2. Tambulisha taarifa za ziada ambazo ni za muhimu zilizoko kwenye boksi la Mazingira ya Ki-Biblia (kulia).

Hatua ya Nne Dakika 15Waombe washiriki kujadili maswali yafuatayo, yaliyoorodheshwa kwenye bango kitita. Weka bango kitita mahali ambapo kila mshiriki ataweza kuyaona kwa urahisi.

a) Je, ni watu gani muhimu wanatajwa katika habari hii, na wanawawakilisha nani?

5. Matunzo na msaada Malengo ya Kujifunza

1. Kukuza uelewa kuhusu kwa nini matunzo na msaada kwa watu wanaoishi na VVU na familia zao, kwamba ni sehemu ya ufuasi wa Kikristo.

2. Kuchunguza ni kwa jinsi gani, sisi wanafamilia, makanisa na jamii zetu, tunaweza kutoa matunzo na msaada vizuri zaidi kwa watu wanaoishi na VVU na na familia zao.

Aya: Matayo 25:31-46.

Mazingira ya Ki-Biblia

Katika Injili zote, mara kadhaa Yesuamejitambulisha kuwa yeye ni “ Mwanawa Adamu”. Kwa kuzingatia andiko katikaDaniel 7:13-14, wana wa Israeli waliaminiya kwamba katika siku ya Mwisho ya Hukumu, Mwana wa Admau atakuja akitokeamawinguni na kuutawala ulimwengu. Katika aya hii maarufu, Yesu anazungumzia kuhusujinsi watu watakavyohukumiwa sio kwasababu wameshika na kutimiza mamboyote kama yanavyotakiwa katika Sheria yaKiyahudi, bali ni kwa kulingana na jinsiwalivyoonyesha ukarimu na wema kwa wale watu wa hali ya chini: maskini, wenye njaa,wasio na makazi na wafungwa.

Kwa sababu kama mbili hivi, tamko hilililikuwa la kipekee sana, na hata tuseme lakimapinduzi. Kwanza, ni tamko linaloonyeshashauku, ndani ya kiini cha imani ya Mkristo,kuonyesha njia na mwelekeo wa Munguduniani na kubadili dunia kuwa mahali pazurizaidi kupitia maisha yetu wenyewe (” Ufalmewako uje hapa duniani”). Dini ya kweli, ufuasi wa kweli, inahusisha kuwasaidia wagonjwa,maskini na wenye njaa, na kuwatembeleawafungwa magerezani. Machoni pa Mungu,kuwahudumia watu wengine ina thamanizaidi kuliko kufuata, kutunza na kuzingatia taratibu zote za kuabudu za Sheria yaKiyahudi, kama vile sheria kali ya vyakula. habari hii k wa sababu walionyesha ukarimukwa wahitaji bila kujua kuwa walikuwawakimfanyia hivyo Bwana wao mwenyewe.Yesu anasema, kusema ukweli, watuwanapaswa kutenda mema, sio kwa sababu kwa kufanya hivyo watapata th awabu auitawasidia kuepuka adhabu, lakini ni kwa sababu ndio matakwa hasa ya Mungu kwa watu wake.

YY

Page 27: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

www.stratshope.org 25

KANISA NA JANGA LA UKIMWI

b) Je, ni jambo gani linawatokea wahusika na kwa nini?

c) Je, Yesu amezungumziaje habari ya Siku ya Mwisho katika somo hili ukitofautisha na mafundisho ya Sheria ya Kiyahudi?

d) Je, ni kwa nini makundi haya mawili ya watu ambao Yesu alikuwa akiwazungumzia walikataa kwa mshangao mkubwa kwa yale aliyoyasema?

e) Je, ni kwa jinsi gani Yesu, katika maisha yake binafsi, alionyesha mfano kwa yale aliyokuwa anahubiri katika somo hili?

f) Je, somo hili linatufundisha nini kuhusu matakwa ya Mungu kwa watu wake katika kutendeana wao kwa wao?

g) Je, ni kwa nini watu wengi huona vigumu katika kutenda mema kwa wengine kwa faida yao wenyewe, pasipo tumaini la malipo au hofu ya adhabu?

Hatua ya Tano Dakika 251. Tambulisha mawazo kuhusu Mazingira ya VVU na UKIMWI kama yalivyo katika boksi (ukurasa wa 26).

2. Waombe washiriki wajigawe katika vikundi vidogovidogo vya watu kama watano au sita kwa kila kikundi. Waombe kila kikundi kujadili na kujibu maswali angalau manne yafuatayo (Utapaswa kuwa umeandika maswali haya kwenye bango kitita). Weka bango kitita mahali ambapo kila mshiriki atayaona maswali hayo vizuri.

a) Je, ni kwa jinsi gani sisi waumini tunatoa matunzo na msaada kwa wagonjwa walioko kwenye familia zetu, makanisani mwetu na katika jamii zetu?

b) Je, kama ungejua kuwa unaishi na VVU na unaumwa, ungependa utunzwe na kusaidiwa vipi na jamii yako?

c) Je, kuna mshiriki yeyote anayeweza kutushirikisha uzoefu wake kuhusu kupokea

Katika nchi nyingi, wahumudu wa kujitolea kutoka makanisani wamechukua jukumu la changamoto ya kuwatembelea watu wanaoishi na VVU.

Page 28: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

26 www.stratshope.org

NIITE

matunzo na msaada kutoka katika jamii kunavyoweza kuwasaidia watu wanaoishi na VVU?

d) Je, kuna mshiriki wa kikundi anayeweza kueleza jinsi alivyoteseka kutokana na kutengwa kunakohusishwa na VVU, na hivyo kupelekea kukosa matunzo na msaada

kutoka kwa wanafamilia na majirani?

e) Je, unawezaje kutoa matunzo na msaada kwa kiongozi wako wa kanisa au muumini yeyote wa kanisa ambaye imetokea kuwa ni mgonjwa na ana uambukizo wa VVU?

Mazingira ya VVU na UKIMWI

Karibu katika nchi nyingi duniani, watu wanaoishi na VVU na UKIMWI pamoja na familia zao, wako katika uwezekano wa kuteseka na hali ya umaskini na hata kukosa mahitaji muhimu kama vile chakula, mahali pa kuishi, matibabu na huduma za wauguzi. Watoto wengi waliopoteza wazazi wao kutokana na UKIMWI wamelazimika kuchukua jukumu la kuwa walezi wa wadogo zao na hata kuamua kuacha kuendelea na masomo. Wengi wao wamejikuta wakigeuzwa kuwa watumwa kabisa na ndugu zao, au pengine wamekuwa karibu fukara kabisa. Katika nchi nyingi, kanisa limekuwa mstari wa mbele katika kuwahudumia na kukidhi mahitaji yao. Kwa mfano, makundi ya watu wa kujitolea

kutoka makanisani wamechukua jukumu la changamoto ya kuwatembelea wagonjwa majumbani mwao - ikiwa ni pamoja na watu wanaoishi na VVU, wakiwaletea chakula na nguo, na kuwasaidia kihisia na kiroho. Hata hivyo watu wengi wanaoishi na VVU na wanaohitaji msaada wa aina hii hawapati, au hautoshelezi. Mara nyingi hii ni kwa sababu hutazamwa na majirani zao na waumini wenzao kama ni watu wenye dhambi ambao wanatakiwa kujilaumu wenyewe kwa mateso wanayoyapata. Lakini Yesu anatuita tuwaonyesha ukarimu na huruma kwa wahitaji wote, sio kwa makundi kadhaa tu katika jamii yetu. Hata hivyo, kwa kufanya hivyo, tunapaswa kuzingatia kwamba ni muhimu sana kuyafanya haya yote kwa nia njema, na sio kwa sababu tunatarajia kuikwepa adhabu au kupata ujira kwa juhudi zetu.

Ningetamani na mimi nipate muda wa kucheza pia

Watoto wengi yatima wamejikuta wanageuzwa watumwa kabisa na ndugu zao.

Page 29: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

www.stratshope.org 27

KANISA NA JANGA LA UKIMWI

f) Tafadhali buni igizo lenye maelezo kuhusu mtu anayeishi na VVU ambaye ana uhitaji wa matunzo na msaada lakini hapati matunzo wala msaada kutoka kwa familia yake au kanisa lake.

Hatua ya Sita Dakika 30Sasa ni wakati wa vile vikundi vidogovidogo kukusanyika kwa pamoja na kutoa taarifa ya mijadala yao, majibu ya maswali na mapendekezo. Kwa wale ambao watakuwa

wameandaa maigizo wacheze maigizo yao.

Hatua ya Saba Dakika 101. Waulize sisi kama waumini wa kanisa

letu na wanajamii, tunaweza kufanya nini ili matunzo na misaada viweze kupatikana kwa watu wanaoishi na VVU na familia zao. Andika mapendekezo yao kwenye bango kitita.

2. Hitimisha somo hili la Biblia kwa sala.

Page 30: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

28 www.stratshope.org

NIITE

Hatua ya Kwanza Dakika 5Wakaribishe washiriki wote na wakaribishe wageni nao wajitambulishe. Mwombe mshiriki mmojawapo kufungua kipindi kwa sala.

Eleza kwamba somo la Biblia la leo litakuwa linahusu uongozi wa kanisa na sababu ya umuhimu wake katika kuitikia, kama Wakristo, katika suala la janga la UKIMWI.

Hatua ya Pili Dakika 5Waombe washiriki wawili, wasome 1 Timotheo 3:1-13 . Kama washiriki wana Biblia zao, waombe kila mmoja afungue sehemu ya aya ya Biblia inayosomwa ili aweze kufuata inaposomwa.

Hatua ya Tatu Dakika 101. Waulize washiriki kutaja mambo yaliyovuta zaidi hisia zao kuhusu aya hii iliyosomwa. Watie moyo washiriki kadhaa kutoa mawazo yao kwa kifupi - angalau maneno matano au sita. Andika mawazo yao kwenye bango kitita.

2. Ongeza taarifa za ziada kutoka kwenye boksi la Mazingira ya Ki-Biblia (kulia).

Hatua ya Nne Dakika 101. Waulize washiriki je, kiongozi mzuri wa kanisa

anapaswa kuwa na sifa gani? (Endelea kuwauliza mpaka uhakikishe kuwa dhana ya kiongozi mzuri imeeleweka miongoni mwa washiriki kwamba kiongozi mzuri ni mwaminifu na anawavuta wengi kumwamini na kuwa na imani naye.)

2. Waombe washiriki kujibu maswali yafuatayo, ambayo yanapaswa kuwa yameandikwa kwenye bango kitita na kuwekwa mahali ambapo kila mshiriki anaweza kuyaona kwa urahisi.

a) Je, uongozi wa kanisani unapaswa kuwa wa mchungaji na kasisi tu? Nani mwingine ni kiongozi?

b) Je, ni kwa nini Paulo alimwandikia Timotheo kuhusu uongozi katika kanisa?

c) Je, kwa nini Paulo aliweka mkazo kuhusu sifa na uaminifu binafsi kuwa ni wa muhimu kwa kiongozi mzuri wa kanisa?

6. Uongozi wa kanisa Malengo ya Kujifunza

1. Kubaini sifa zinazomfanya mtu kuwa kiongozi bora ndani ya kanisa ili kuitikia changamoto za janga la UKIMWI.

2. Kubaini njia ambazo viongozi wa kanisa wanaweza kutiwa moyo na kusaidiwa ili waweze kuitikia kwa upendo na kuwa na taarifa za kutosha kuhusu mahitaji ya watu wanaoishi na VVU.

Aya: 1 Timotheo 3:1-13.

Mazingira ya Ki-Biblia

Katika Waraka wa Kwanza wa Paulo Mtumekwa Timotheo, Paulo ana mshauri kijana mdogo wa Kikristo, Timotheo, aliyekuwa anamsaidia Paulo kuanzisha na kuyasaidiamakanisa katika Asia Ndogo ( yaani Uturukiya leo). Paulo anaanza k wa kumpa Timotheoangalizo kuhusu mafundisho ya uongo ndaniya kanisa, na baada ya hapo anataja sifa binafsi ambazo viongozi wa kanisa, wasaidiziwao pamoja na familia zao wanapaswakuwa nazo. Anasisitiza kwamba viongoziwa kanisa wanapaswa kuwa wa mfano wakuigwa katika tabia na mwenendo wao.Wanapaswa pia kuheshimiwa na watu walionje ya kanisa kwa kuwa msimamo wa jamii yaKikristo unategemea zaidi jinsi viongozi waowanavyokubalika na jamii kwa ujumla.

aa

Page 31: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

www.stratshope.org 29

KANISA NA JANGA LA UKIMWI

d) Je, unadhani ‘kusengenya’ (au ‘kutania’) vinaweza kuwa na athari gani kwa waumini wa kanisa?

e) Je, kwa nini ni umuhimu kwa viongozi wa kanisa kuheshimiwa na watu nje ya kanisa?

Hatua ya Tano Dakika 251. Tambulisha mawazo kuhusu Mazingira ya

VVU na UKIMWI kama yalivyo katika boksi hapo juu.

2. Waombe washiriki wajigawe katika vikundi vidogovidogo vya watu kama watano au sita kwa kila kikundi. Wape kila kikundi maswali manne yafuatayo kuyajadili na kujibu.

Wakati watu wanapopimwa na kugunduliwa na uambukizo wa VVU, wanahitaji kumwambia kwa siri mtu fulani wanayemwamini – kwa mfano mchungaji au kasisi – ambaye wanamheshimu na kumwamini.

Mazingira ya VVU na UKIMWI

Moja kati ya sifa za uongozi mzuri kanisani ni ile ya kiongozi kuaminiwa. Ili mtu aweze kumsaidia na kufuata mwongozo wa kiongozi wake ni lazima ajisikie kuwa na uhakika wa kumwamini kiongozi huyu. Zaidi ya kiongozi huyu kutoa mwongozo mzuri, ni lazima awaheshimu wale anaowaongoza na pia awahudumie kwa makini. Lolote lile ambalo kiongozi huyu ataambiwa kwa siri na mfuasi wake ni lazima jambo lile lidumu kuwa siri. Hali hii ya umuhimu wa kutunza siri inapata

kipindi hiki cha janga la UKIMWI. Mara tu watu wanapogundulika kuwa wana uambukizo wa VVU, huhitaji sana kuwa na mtu wa kumshirikisha mtu wanayemuheshimu na watakayemwamini kupokea habari nyeti kuhusu afya zao. Ni mtu kama mchungaji au kasisi ndiye angekuwa wa kushirikishwa. Zaidi ya hayo, viongozi wa kanisa katika ngazi zote wanapaswa kuonyesha heshima na aminifu katika maisha yao yote ya kila siku, ambayo yanapasa kuwa ya kuigwa, hasa kuhusu tabia zao za mahuasiano katika masuala ya ngono.

Una naMchungaji,iko hivi...

msukumo zaidi katika

Wakati watu wanapopimwa na kugunduliwa na uambukizo wa VVU, wanahitaji

Page 32: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

30 www.stratshope.org

NIITE

(Utapaswa kuwa umeyaandika maswali hayo ubaoni au katika bango kitita). Weka bango kitita mahali ambapo kila mshiriki atayaona maswali hayo vizuri.

a) Je, ni kwa namna gani sifa za kiongozi zinazofafanuliwa na Paulo zina uhusiano na mazingira ya VVU na UKIMWI, na uongozi mzuri ndani ya kanisani unaunganishwaje na juhudi za kushughulikia kuzuia kwa maambukizi ya VVU na UKIMWI?

b) Je, wale walio katika nafasi za uongozi makanisani leo wanaonyesha sifa zote ambazo mtume Paulo anaziandika katika waraka wake kwa Timotheo, katika 1 Timotheo 3:1-13? Kama jibu ni hapana, je, unafikiri sifa zipi zinaonekana kupungua?

c) Je, wakati uaminifu na imani kati ya watu wanaoishi na VVU na UKIMWI na viongozi wa kanisa unapovunjika, kwa kawaida husababishwa na nini?

d) Je, ni kwa namna gani uaminifu na imani kati ya watu wanaoishi na VVU na UKIMWI na viongozi wa kanisa vinaweza kurejeshwa? Je, ni nani anapaswa kuanzisha mahusiano hayo, na yanaanzia katika jambo gani?

e) Tafadhali buni igizo fupi kuhusu mchungaji au kasisi ambaye ametembelewa na mwalimu wa Shule ya Jumapili ambaye anamweleza mchungaji au kasisi kuhusu hali yake kwamba anaishi na VVU. Jumapili inayofuata, waumini wanakwepa kumsalimia kwa kumshika mkono, anatambua ya kuwa kuna mtu atakuwa amewaeleza waumini kuhusu hali yake ya kuwa na uambukizo wa VVU.

Je, atachukua hatua gani? Je, atakwenda na kupambana na mchungaji au kasisi? Je, atawauliza waumini ni kwa nini hawataki kumsalimia kwa kumshika mikono?

f) Mtu anayeishi na VVU anaweza kutaka kueleza kuhusu uzoefu wake kwa jinsi mzigo wake ulivyofanywa mwepesi alipomweleza mchungaji au kasisi wake kuhusu hali yake ya kuwa na uambukizo wa VVU.

g) Mtu mmoja au wawili wanaweza kupenda kuandaa mchoro, au michoro mfano wa katuni, na maneno yakionyesha kile kilichotokea wakati mtu anayeishi na VVU alipomjulisha mchungaji au kasisi wake kuhusu hali yake na halafu mchungaji au kasisi akawaambia watu wengine.

Hatua ya Sita Dakika 30Sasa ni wakati wa vile vikundi vidogovidogo kukusanyika kwa pamoja na kutoa taarifa ya mijadala yao na majibu ya maswali. Kwa wale ambao watakuwa wameandaa igizo, hadithi, michoro au shuhuda binafsi wakaribishwe ili kuwasilisha mambo yao.

Hatua ya Saba Dakika 103. Waulize jinsi tunavyoweza kuwasaidia

viongozi wetu wa kanisa kushughulikia matatizo ambayo tumekuwa tunayajadili. Andika mapendekezo ya washiriki kwenye bango kitita.

4. Hitimisha somo hili la Biblia kwa kuwaongoza washiriki kwa maombi, au kwa kumwomba mmoja wao afanye hivyo.

Page 33: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

www.stratshope.org 31

FAMILIA

Familia …

Malengo ya Kujifunza

1. Kuweka wazi njia ambazo yatima, na watoto wengine walio katika mazingira hatarishi, pamoja na wale wanoawahudumia, wanavyoathiriwa na VVU na UKIMWI.

2. Kukuza uelewa miongoni mwa watoa huduma ambao wanawatunza watoto walioathiriwa na

VVU na UKIMWI ya kwamba watoto hawa ni baraka toka kwa Mungu.

3. Kuwawezesha watoto walioathiriwa na VVU na UKIMWI kuelewa kwamba Mungu anawajali sana na anataka kuwabariki.

4. Kutambua njia ambazo kanisa na jamii wanaweza kuzitumia kuwasaidia watoto walioathiriwa na VVU na UKIMWI, pamoja na wale wanaowahudumia.

Aya: Marko 10:13-16; Yakobo 1:27.

Hatua ya Kwanza Dakika 5Wakaribishe washiriki wote na wakaribishe wageni nao wajitambulishe. Mwombe mshiriki mmojawapo kufungua kipindi kwa sala.

Eleza kwamba somo la Biblia la leo litakuwa na mada kuhusu watoto walio katika kanisa letu na jamii ambao wameathiriwa na VVU na UKIMWI.

Hatua ya Pili Dakika 5Mwombe mshiriki mmoja asome Marko 10:13-16 na mwingine asome Yakobo 1:27 . Kama washiriki wana Biblia zao, waombe kufuatana na aya inayosomwa katika Biblia zao.

Hatua ya Tatu Dakika 101. Waulize washiriki kutaja mambo yaliyovuta

zaidi hisia zao katika aya hizi mbili zilizosomwa. Watie moyo washiriki kadhaa kutoa mawazo yao kwa kifupi - angalau maneno matano au sita. Andika mawazo yao kwenye bango kitita.

2. Ongeza taarifa za ziada zilizoko kwenye boksi la Mazingira ya Ki-Biblia (kulia).

Mazingira ya Ki-Biblia

Katika kipindi cha Yesu, ilikuwa ni k awaidakwa Rabi kuwabariki watoto, kwa hiyohaikuwa jambo la kushangaza kwa wazazikuwapeleka watoto wao kwa Yesu iliawabariki (Marko10:13). Hata hivyo,wanafunzi wake, waliwakemea wazazi kwakufanya hivyo, hali hiyo ikamsababisha Yesuakasirike. (Ni katika maeneo mengine mawilitu katika Injili zote nne ambapo inatajwawazi Yesu akipatwa na hasira). Kulingana naSheria ya agano la Kiyahudi, ni watu wazimatu ambao walikuwa wakifuata kila kipengelecha Sheria ndio waliokubalika kwa Mungu.Hata hivyo, Yesu anasisitiza umuhimu wawatoto katika ufalme wa Mungu. Anawekawazi kupitia matendo yake kwamba watotohawa wana thamani kwake: anatumia mudakuwa nao, anawakumbatia na kuwabariki, na

ana mambo mengi muhimu ya kufanya. Kamailivyo mara kwa mara, Yesu hubadilisha kabisamatarajio ya watu kuhusu ni jambo lipi hasala muhimu.

Waraka wa Yakobo, ni waraka ambao

katika kuelezea umuhimu wa kuwasaidiawadhaifu na walio katika mazingira magumukama sehemu ya ufuasi wa Kikristo. Naam,

Yakobo 1:27 anasisitiza mahitaji ya wajane nayatima ya msaada na ulinzi.

7. Watoto

Page 34: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

32 www.stratshope.org

NIITE

Hatua ya Nne Dakika 10Waombe washiriki kujibu maswali yafuatayo, yaliyoandikwa kwenye bango kitita, ambayo yatawekwa mahali ambapo kila mshiriki ataweza kuyaona:

a) Je, kwa nini wazazi waliwaleta watoto wao kwa Yesu (Marko 10:13)?

b) Je, kwa nini wanafunzi wa Yesu waliwakemea wazazi kwa kuwaleta watoto wao kwa Yesu?

c) Je, Yesu aliitikiaje wakati wanafunzi walipowakemea wazazi?

d) Je, tunaweza kujifunza nini kuhusu tabia ya Yesu kwa watoto?

e) Katika Yakobo 1:27, je, ni kwa nini wajane wametajwa pamoja na yatima kama ndio wenye mahitaji maalumu ya msaada kutoka kwa Wakristo?

Hatua ya Tano Dakika 25

1. Waombe washiriki wawili wasome habari za Maria kama zilivyo katika boksi la Mazingira ya VVU na UKIMWI (hapo juu).

Mazingira ya VVU na UKIMWI

Watoto na wale wanaowahudumia na kuwatunza, hasa wajane, wanatatizwa sana na athari za kiuchumi na kijamii zitokanazo na janga la UKIMWI. Fikiria, kwa mfano, habari ya kweli ya maisha ya Maria, aliyefiwa na wazazi wake alipokuwa na umri wa mika sita tu na alienda kuishi na dada yake mkubwa. Hata baada ya wazazi wake kufariki Maria aliendelea kufanya vizuri sana shuleni. Hata hivyo, baada ya miaka michache aliugua. Dada yake akampeleka hospitalini, ambako aligunduliwa kuwa ana kansa ya damu na kifua kikuu. Alipimwa pia VVU na akakutwa ameambukizwa. Maria alipewa ushauri-nasaha lakini aliathirika sana kwa kujua hali yake ya kuwa na uambukizo wa VVU.

Kama hilo halitoshi, Maria akakataliwa na ndugu zake wote katika familia isipokuwa dada yake mkubwa tu, ambaye alikuwa katika umri wa katikati ya ujana tu na hakuwa na ajira maalumu. Maria akaanza kufikiri pengine hata wazazi wake walikufa kwa ugonjwa wa UKIMWI, lakini kwa bahati mbaya Maria hakuwa na jinsi ya kupata habari hizo. Kwa msaada wa dada yake, polepole aliweza kukubaliana na hali yake ya kuwa na VVU. Hata hivyo, wanafamilia wengine walikataa kumsaidia aendelee na masomo, au hata kumkaribisha mahali pa kuishi, kwa sababu hawakuona kwamba kuna matumaini mbele ya maisha ya Maria. Dada yake ameweza kufanikiwa kuendelea kumsomesha, na sasa yuko kidato cha tatu, lakini hafikirii kwamba ataweza kuendelea kumsaidia kusoma.

Dada mkubwa wa Maria ameweza kuendelea kumsomesha baada ya

wazazi wao kufariki.

Page 35: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

www.stratshope.org 33

FAMILIA

2. Waombe washiriki wajigawe katika viundi vidogovidogo vya watu kama watano au sita kwa kila kikundi. Wape kila kikundi maswali manne (yafuatayo hapa chini) ili kuyajadili na kujibu. Utapaswa kuwa umeyaandika maswali hayo ubaoni au katika bango kitita. Weka bango kitita mahali ambapo kila mshiriki atayaona maswali hayo vizuri.

a) Je, ni changamoto zipi zinazowakabili Maria na dada yake mkubwa?

b) Je, ni wapi katika jamii Maria na dada yake wanaweza kwenda kupata msaada?

c) Je, kuna mshiriki yeyote anayeweza kuwashirikisha wenzake uzoefu ambao wameupata katika kumlea mtoto ambaye ameathirika na VVU? Je, wanafamilia wengine waliitikiaje katika hili?

d) Je, ni mahitaji gani ya muhimu kwa watoto waliothiriwa na VVU na wale wanaowahudumia?

e) Je, tunaweza kuchukua hatua gani kama kanisa katika kuwapa msaada wa kiroho na wa hali na mali yatima na watoto wengine waliaothiriwa na VVU, pamoja na wale wanaowahudumia?

f) Je, tunaweza kuchukua hatua gani za matendo zinazoweza kutusaidia kulifanya jukumu hili kuwa sehemu ya huduma ya kanisa letu wenyewe?

g) Je, ni raslimali zipi (za kiroho, binafsi, vitu) tunazoweza, kama kanisa kutoa katika huduma hii?

h) Je, tunahitaji msaada gani kutoka nje ya kanisa, (kwa mfano, vitendea kazi, mafunzo) na tunawezaje kupata msaada huo?

Hatua ya Sita Dakika 30Vikundi vidogovidogo sasa vikusanyike pamoja tena na kutoa taarifa ya mijadala yao na majibu ya maswali.

Hatua ya Saba Dakika 101. Waulize tunaweza kufanya nini kusaidia familia zetu, kanisa letu na jamii yetu kushughulikia matatizo ambayo tumekuwa tukiyajadili. Andika mapendekezo ya washiriki ubaoni au kwenye bango kitita.

2. Hitimisha somo la Biblia kwa kuwaongoza washiriki katika sala, au unaweza kumchagua mshiriki mmojawapo aweze kufanya hivyo.

Page 36: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

34 www.stratshope.org

Niite

Hatua ya Kwanza Dakika 5Wakaribishe washiriki wote na wakaribishe wageni nao wajitambulishe. Mwombe mshiriki mmojawapo kufungua kipindi kwa sala.

Eleza kwamba somo la Biblia la leo litakuwa kuhusu moja ya jambo muhimu sana katika taasisi za kijamii – yaani ndoa.

Hatua ya Pili Dakika 10Waombe washiriki watatu, wasome aya zifuatazo; 1 Wakorintho 7:1-5 ; Waefeso 5:21-33 . Waulize washiriki kutaja mambo ambayo yamevuta sana hisia zao kuhusu ujumbe uliomo katika aya hizi. Watie moyo washiriki kadhaa kutoa mawazo yao kwa kifupi - angalau maneno matano au sita. Andika mawazo yao kwenye bango kitita. Kama washiriki wana Biblia zao waombe kila mmoja aweze kufungua sehemu za aya zinazosomwa ili aweze kufuata zinaposomwa.

Hatua ya Tatu Dakika 10Tambulisha taarifa za ziada ambazo ni za muhimu zinazohitajika kutoka kwenye boksi la Mazingira ya Ki-Biblia (kulia).

Hatua ya Nne Dakika 30Waombe washiriki kujadili maswali yafuatayo yaliyoorodheshwa kwenye bango kitita, ambayo yatakuwa yamewekwa mahali ambapo kila mshiriki ataweza kuyaona kwa urahisi. Washiriki wanapotoa jibu kwa kila swali, andika majibu hayo kwenye bango kitita - ukizingatia mahali pa kuandika ili kila swali liwe na majibu yake.

a) Katika maisha na jamii ya watu wa Israeli, wanawake walijulikana kama mali milki za baba zao na (baadaye watakapoolewa) za waume zao. Je, unalinganishaje habari hii na mwanamume wa kisasa ambaye anamwambia mkewe, “Lazima ufanye kama ninavyosema kwa sababu nimelipa ‘lobola’

Kusini) yaani mahari’ kwa ajili yako?

b) Je, Paulo alikuwa na maana gani alipoandika: “Mke hana amri juu ya mwili wake, bali

8. Ndoa Malengo ya Kujifunza

1. Kujifunza kuhusu ndoa kama inavyoainishwa katika Agano Jipya.

2. Kutafakari uzoefu wetu binafsi katika maisha ya ndoa, na ikilazimu, basi tuamue kuchukua hatua chanya za kubadili mwenendo wetu.

3. Kuwa watu wa msaada zaidi miongoni mwa wenzetu walio na matatizo ya ndoa.

Aya: 1 Wakorintho 7:1-5; Waefeso 5:21-33.

Mazingira ya Kibiblia

Katika nyaraka zake kwa Wakristo waKorintho, Paulo anajibu maswali ambayoWakorintho walimwuliza, ambayo yalilengakatika kutaka ushauri. Anaanza kwakuwaambia kwamba “ni heri mwanamumeasimguse mwanamke”, lakini pia anaendeleakuthibitisha kuwa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamkena awe na mume wake mwenyewe.Wakorintho pia walimwuliza Paulo swalikuhusu mahusiano katika tendo la ndoa, Paulonaye aliwajibu kwamba ndoa ni ushirika.Kwa hali hiyo basi hakuna mwenye mamlakajuu ya mwili wake, kwa hiyo wasinyimane,isipokuwa wakiwa wamepatana kwa muda,kwa mfano katika kupata muda wa maombi.Katika barua yake kwa Wakristo wanaoishiEfeso, Paulo anawahimiza wanaumewawapende wake zao kama vile Kristoanavyolipenda Kanisa akajitoa kwa ajili yake.Ndoa ni muungano kati ya mume na mke,ambapo watu hawa wawili wanapounganawanakuwa “mwili mmoja”. Wanawakehawapaswi kutazamwa kama vyombo vyakumilikiwa au vitu, isipokuwa watazamwekuwa ni sehemu sawa katika mwili mmoja.

Page 37: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

www.stratshope.org 35

FAMILIA

mumewe; vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake, bali mkewe”? (1 Wakorintho 7:3-4).

c) Je, Paulo alikuwa na maana gani alipowaandikia Waefeso akisema : “Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo alivyolipenda Kanisa akajitoa kwa ajili yake?” (Waefeso 5:25).

Hatua ya Tano Dakika 201. Tambulisha mawazo kuhusu Mazingira ya VVU na UKIMWI kama yalivyo katika boksi (hapa chini).

2. Waombe washiriki wajigawe katika vikundi vidogovidogo vya watu kama watano au sita kwa kila kikundi. Wape kila kikundi maswali manne (yaliyopo hapa chini) wayajadili na kuyajibu. Utapaswa kuwa umeyaandika maswali haya kwenye bango kitita. Weka bango kitita mahali ambapo kila mshiriki anaweza kuyaona.

a) Je, ni kwa jinsi gani waume na wake wanaweza kuonyeshana upendo?

b) Je, ni kwa jinsi gani upendo ni kigezo cha msingi katika kufanya maamuzi ya kuoa au kuolewa au kutokuoa au kutokuolewa? Je, vigezo vingine ni vipi?

c) Je, ni matarajio gani ya kimila na desturi ambayo ni ya muhimu katika kuweka msingi imara wa ndoa? Je, yapi ambayo sio ya msaada?

d) Je, kanisa lina ushawishi gani wa maamuzi kuhusu ndoa?

e) Tafadhali toa maoni yako kuhusu msemo ufuatao: “Wanandoa wanaweza kuwa na ndoa nzuri iwapo tu kila mmoja atakuwa mwaminifu kwa mwenzake”.

Ndoa ya Kikristo ina maanisha ahadi ya ushirika wa kudumu, unaojengwa katika misingi ya upendo, uaminifu na heshima.

Mazingira ya VVU na UKIMWI

Wakati ambapo mwanamume na mwanamke wanaotoka katika mazingira tofauti ya kimaisha na kihistoria wanapoamua kuishi pamoja kama mume na mke, wote wawili wanatakiwa kufanya mabadiliko makubwa katika maisha, tabia, mitazamo na mienendo yao. Kwa washirika katika ndoa ya Kikiristo, uhusiano huu unapaswa kuwa wa pande zote mbili, ahadi ya ushirika wa maisha, uliojengwa katika upendo, uaminifu na heshima. Lakini faida hizi zinaweza kutazamwa kwa hisia tofauti katika mazingira ya mila na desturi katika jamii. Katika baadhi ya mila, ndoa za mitala zinavumiliwa, hata kama ndoa hizi hazikuthibitishwa rasmi. Zaidi ya hayo, katika mila nyingi

wanaume hupata heshima kwa kuwa na wanawake zaidi ya mmoja wanaoshirikiana nae katika tendo la ngono, zaidi ya mkewe. (Katika baadhi ya nchi desturi inajulikana kama kuwa na ‘nyumba ndogo’ – yaani kuendelea kuwa na mahusiano ya tendo la ngono nje ya ndoa.) Wwanaeleza kwamba hali ya kuwa na ‘mahusiano ya kimapenzi na wapenzi wengi’ ndicho ‘chanzo chenye msukumo mkubwa’ wa ongezeko la janga la UKIMWI. Mpango wa hivi karibuni wa kujikinga na maambukizi ya VVU kama ule wa ‘Penzi Moja’ huko kusini mwa Afrika umekuwa ukiweka mkazo katika umuhimu wa mpenzi mmoja kama mkakati muhimu wa kuzuia maambukizi ya VVU.

Page 38: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

36 www.stratshope.org

NIITE

f) Je, una mawazo gani kuhusu wanawake na wanaume wanavyopaswa kuhusiana katika ndoa kulingana na mpango wa Mungu?

g) Andaeni igizo kwa kuzingatia nukuu ifuatayo: “Mara ya kwanza tulipooana alinihudumia kama malkia. Lakini sasa najisikia kama vile mtumwa na mtambo wa kutengeneza watoto.”

h) Je, ndugu na marafiki wanawezaje kusaidiana kama ndoa zao zipo kwenye matatizo?

Hatua ya Sita Dakika 30Sasa ni wakati wa vile vikundi vidogovidogo kukusanyika kwa pamoja na kutoa taarifa ya

mijadala yao na majibu ya maswali. Kwa wale ambao watakuwa wameandaa igizo, hadithi au shuhuda binafsi wakaribishwe ili kuwasilisha mambo yao.

Hatua ya Saba Dakika 101. Waulize tunachoweza kufanya kuwasaidia familia, kanisa letu na jamii ili kushughulikia matatizo ambayo tumekuwa tukiyajadili. Andika mapendekezo ya washiriki kwenye karatasi ya bango kitita.

2. Hitimisha somo hili la Biblia kwa kuwaongoza washiriki kwa sala, au kumwomba mmoja wa washiriki kufanya hivyo.

Page 39: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

www.stratshope.org 37

MITAZAMO NA MATENDO BINAFSI

Hatua ya Kwanza Dakika 5Wakaribishe washiriki wote na waalike wageni wowote kujitambulisha. Mwombe mshiriki mmojawapo kufungua kipindi kwa sala.

Eleza kwamba somo la Biblia la leo litakuwa na mada ya ‘tumaini’, hasa kwa watu wanaoishi na

Hatua ya Pili Dakika 5Waombe washiriki wawili, wasome Marko 5:21-34. Kama washiriki wana Biblia zao waombe kila mmoja aweze kufungua sehemu ya aya ya Biblia inayosomwa ili aweze kufuata inaposomwa.

Hatua ya Tatu Dakika 101. Waulize washiriki kutaja mambo yaliyovuta zaidi hisia zao katika aya iliyosomwa. Watie moyo washiriki kadhaa kutoa mawazo yao kwa kifupi - angalau maneno matano au sita. Andika mawazo yao kwenye bango kitita.

2. Waeleze taarifa za ziada kutoka kwenye boksi la Mazingira ya Ki-Biblia (kulia):

Hatua ya Nne Dakika 10Waombe washiriki kujadili maswali yafuatayo, yaliyoandikwa kwenye bango kitita, ambayo yatakuwa yamewekwa mahali ambapo kila mshiriki ataweza kuyaona.

Mitazamo na matendo binafsi…9. Tumaini Malengo ya Kujifunza

1. Kuwawezesha watu ambao wana magonjwa ya muda mrefu kuishi katika matumaini ya maisha bora.

2. K

Aya: Marko 5:21-34

Mazingira ya Ki-BibliaKulingana na utakatifu wa sheria zilizomokwenye kitabu cha Agano la Kale kiitwachoMambo ya Walawi 15:25, mwanamkealiyekuwa katika hedhi kwa utaratibu alihesabiwa kuwa ni najisi. Pamoja na kuishina kutokwa damu kwa muda wa miaka 12 nakutafuta uponyaji kutoka k wa waganga wengibila mafanikio, huyu mwanamke katika habarihii hakukata tamaa ya tumaini la kupona.Mwisho alipata uponyaji kwa njia ya imaniyake kwa Yesu.

Lakini Yesu hakumwacha tu mwanamkehuyu aende zake, akiwa amepona kimwililakini kihisia awe bado ana kovu. Yesuanamtafuta pande zote, akiwa na shauku yakutaka kumjulisha kuhusu kusudio lake latumaini, analoliita imani. K wa kufanya hivyoYesu anawafanya wale waliokuwa karibunaye kumwona mtu hu yo ambaye alikuwa“haonekani” na kumtangazia uhusiano wakaribu na Yeye pengine zaidi kuliko hataalivyothubutu kuwa na tumaini hilo.

Page 40: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

38 www.stratshope.org

NIITE

Mazingira ya VVU na UKIMWI

Katika kipindi cha miaka 15 ya mwanzo ya janga la UKIMWI, watu wengi waliogundulika kwamba wameambukizwa VVU walikufa miaka michache tu baadaye. Wakati ambapo wanasayansi walijitahidi kutengeneza dawa za kutibu magonjwa nyemelezi yatokanayo na VVU, watu wanaoishi na VVU – familia na marafiki zao - wanaendelea kuwa na matumaini na kufanya maombi ili dawa zitakazofaa zaidi zipatikane. Katika kipindi cha miaka ya 1990, dawa za kurefusha maisha (ARVs) zilianza kutengenezwa. Ingawa dawa hizi sio ‘tiba’ ya uambukizo wa VVU, dawa hizi zimewawezesha watu wanaoishi na VVU kuishi maisha karibu na ya kawaida na kwa muda mrefu zaidi. Katika nchi zilizoendelea kiuchumi duniani, vifo vitokanavyo na UKIMWI vilipungua kwa kiasi kikubwa sana. Awali bei za dawa hizi za kurefusha maisha zilikuwa za juu sana, kiasi cha kutokupatikana kwa urahisi katika nchi zinazoendelea kiuchumi, lakini kwa sasa hali hii

imebadilika. Bei za dawa za kurefusha maisha zimeshuka kwa kiasi kikubwa, na kwa sasa watu zaidi ya million tatu katika Afrika, Asia na Amerika ya Kusini wanatumia dawa hizi.

Katika Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara, ni mtu mmoja tu kati ya watu watatu wanaohitaji dawa hizi ndiye anaweza kupata dawa hizi, lakini dawa hizi zinaendelea kupatikana zaidi na zaidi katika nchi mbalimbali za Afrika. Hata hivyo, ni lazima kwanza watu wajue hali zao kama wameambukizwa au la kwa kupimwa damu. Pia watu wanaoishi na VVU hunufaika kwa kiasi kikubwa sana wanapojiunga na vikundi vya kusaidia wenye VVU.

Tumaini la watu sio katika kupatikana kwa matibabu yanayofaa tu. Watu wengi wanaoishi na VVU wameteseka kwa tatizo la unyanyapaa, kukataliwa na kutengwa, na wamekuwa na matumaini, wamefanya kazi na kuomba kipekee kwa ajili ya maisha ya baadaye. Kuna ongezeko la mafanikio ya matumaini yao, lakini bado imebaki kazi kubwa ya kufanya.

a) Je, ni muda gani mwanamke huyu aliteseka kwa kutokwa damu?

b) Je, mwanamke huyu alifanya nini kuonyesha tumaini lake kwamba ataponywa?

c) Je, ni nini yalikuwa matokeo ya mwanamke huyu kukutana na Yesu?

d) Je, Yesu alipokeaje ujio wa mwanamke huyu?

e) Je, wanafunzi wa Yesu walimpokeaje mwanamke huyu?

f) Je, mwanamke huyu alipogundua kile kilichotokea mwilini mwake, alifanya nini?

g) Je, ni maneno gani ya mwisho Yesu aliyomwambia mwanamke huyu?

Hatua ya Tano Dakika 251. Tambulisha mawazo yaliyoko kwenye Mazingira ya VVU na UKIMWI (hapo juu).

2. Waeleze washiriki kwamba sasa tutakuwa tunajadiliana kuhusu mada ya matumaini kuhusiana na janga la UKIMWI. Waombe washiriki wajigawe katika vikundi vidogovidogo vya watu watano au sita kwa kila kikundi. Wape kila kikundi maswali manne (yafuatayo hapa chini) wayajadili na kuyajibu. (Utapaswa kuwa umeyaandika maswali haya ubaoni au kwenye

karatasi la bango kitita.) Weka bango kitita mahali ambapo kila mshiriki ataweza kuyaona maswali hayo.

a) Je, kuna mshiriki yeyote ambaye anaweza kuwashirikisha wenzake uzoefu wake aliokuwa nao wa kumtunza mmoja wa familia au rafiki ambaye ameugua ugonjwa uliosababishwa na UKIMWI kwa muda mrefu?

b) Je, alijisikiaje na alikabiliana vipi na hali hiyo? Je, kuna wakati aliojisikia kukata tamaa?

c) Je, wana familia wengine walikuwa na mwitikio gani katika jambo hilo?

d) Je, tunawezaje kuwapa matumaini wagonjwa wa muda mrefu wanaougua magonjwa yaliyosababishwa na UKIMWI? Kwa mfano, je, tunaweza kuwatambulisha katika vikundi vinavyotoa huduma ya matunzo kwa watu wanaoishi na VVU? Je, tunaweza kuwatia moyo kuendelea na maombi na kuweka matumaini yao kwa Yesu?

e) Je, ni nini matumaini yetu kuhusu janga la UKIMWI, na tunafanya nini ili matumaini hayo yawe ya kweli?

f) Waulize kama kikundi kimoja - au mtu mmoja au wawili – wangependa kuchora mchoro, au kuchora picha za katuni, zenye maneno, yanayoonyesha jinsi gani

Page 41: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

www.stratshope.org 39

MITAZAMO NA MATENDO BINAFSI

mtu anayeishi na VVU anavyoweza kusaidiwa kwa maombi, huduma za matibabu, msaada

kuishi kwa matumaini ya maisha bora yajayo.

Hatua ya Sita Dakika 30Sasa ni wakati wa vile vikundi vidogovidogo kukusanyika kwa pamoja na kutoa taarifa ya mijadala yao na majibu ya maswali na mapendekezo. Kwa wale ambao watakuwa wameandaa mchoro au ushuhuda binafsi wakaribishwe ili kuwasilisha mambo yao.

Hatua ya Saba Dakika 101. Waulize ni kitu gani tunaweza kufanya ili kuwasaidia viongozi wa kanisa kushughulikia matatizo ambayo tumekuwa tukiyajadili. Andika mapendekezo ya washiriki ubaoni au kwenye bango kitita.

2. Soma Warumi 12:12 rudia mara ya pili: “Kwa tumaini, mkifurahi; katika dhiki, mkisubiri; katika kusali, mkidumu;”. Waombe washiriki kutafakari mstari huu kwa dakika mbili au tatu, halafu hitimisha somo kwa wote pamoja kusema Sala ya Bwana.

Watu wanaoishi na VVU wananufaika kwa kiasi kikubwa sana wanapojiunga na vikundi vya kusaidia wenye VVU.

Page 42: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

40 www.stratshope.org

NIITE

Hatua ya Kwanza Dakika 5Wakaribishe washiriki wote na waombe wageni kujitambulisha. Mwombe mshiriki mmojawapo kufungua kwa sala fupi.

Eleza kwamba somo la leo la kujifunza Biblia litahusu maneno makuu matatu ambayo ni: ’unyanyapaa’, ‘ubaguzi’ na ‘kukataa’ mambo yanayochangia katika kuenea kwa VVU.

Hatua ya Pili Dakika 5Mwombe mshiriki mmoja kusoma aya ifuatayo, Luka 5:12-14 . Kama washiriki wana Biblia zao waombe kila mmoja aweze kufungua sehemu ya aya ya Biblia inayosomwa ili waweze kufuata inaposomwa.

Hatua ya Tatu Dakika 101. Waulize washiriki kutaja mambo yaliyovuta zaidi hisia zao katika aya iliyosomwa. Watie moyo washiriki kadhaa kutoa mawazo yao kwa kifupi - angalau maneno matano au sita. Andika mawazo yao kwenye bango kitita.

2. Tambulisha maelezo yoyote ya ziada zanayohitajika kutoka kwenye boksi la Mazingira ya Ki-Biblia (kulia).

Hatua ya Nne Dakika 10Waombe washiriki kujadili maswali yafuatayo yaliyoandikwa kwenye bango kitita, ambayo yatakuwa yamewekwa mahali ambapo kila mshiriki ataweza kuyaona.

a) Je, ni kwa nini wakoma waliishi sehemu tofauti na watu wengine?

b) Jaribu kufikiria matatizo ambayo ungekumbana nayo kama ungekuwa unaishi nyakati za Yesu huku ukiwa mkoma.

c) Je, ni kwa nini wakoma walimwita Yesu? Je, walitarajia kupokea nini kutoka kwa Yesu?

10. Unyanyapaa, ubaguzi na kukataa Malengo ya Kujifunza

1. Kuweka msukumo katika kuelewa ni kwa jinsi gani unyanyapaa, ubaguzi na kukataa vinavyochangia katika kuenea kwa VVU.

2. Kuwawezesha watu binafsi, familia na jamii kushughulikia na kupunguza unanyapaa, ubaguzi

na kukataa kunakohusishwa na VVU.

Aya : Luka 5:12-14.

Mazingira ya Ki-Biblia

Ugonjwa wa “kutisha wa ngozi” uliotajwa katika habari hii kwa kawaida unadhaniwa kuwa ni ukoma. Katika desturi za wakati ule,ukoma ulikuwa ugonjwa wa kunyanyapaliwasana, ukisababisha mgawanyiko wa kudumu miongoni mwa wale waliokuwa na ugonjwa huo (wakiitwa “wakoma”) na jamii iliyobaki. Ukoma ulijulikana kuwa ni ugonjwa hatari wa kuambukiza na usiotibika na wale wote walioambukizwa walionekana najisi na walipaswa kutengwa na jamii kama inavyoelezwa katika Walawi 13 na 14. Wakoma waliishi katika maeneo yao, wakitengwa mbali na familia zao na jamii, ikiwa ni pamoja na viongozi wao wa dini. Waliteseka sio kwa ajili ya ugonjwa tu lakini pia walitengwa na jamii na walinyanyapaliwa

katika habari hii, Yesu anapomwendea na kumgusa mkoma, alikuwa anavunja mwiko uliokuwa umejengeka kwa muda mrefu sana. Mguso wa Yesu una maana nzito sana. Zingatia kwamba mkoma anaomba kutakaswa kuliko kuponywa, ikionyesha mkazo wa unyanyapaa na athari za kijamii zahali yake kuliko kuhusu ugonjwa wenyewe.

Page 43: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

www.stratshope.org 41

MITAZAMO NA MATENDO BINAFSI

d) Je, ni kwa namna gani Yesu aliwaitikia wakoma tofauti na namna viongozi wengine wa dini walivyowatendea?

Hatua ya Tano Dakika 301. Tambulisha mawazo yaliyoko katika boksi la Mazingira ya VVU na UKIMWI (ukurasa wa 42).

2. Waombe washiriki wajigawe katika vikundi vidogovidogo vya watu watano au sita kwa kila kikundi. Waombe kwamba katika kila kikundi wajadili na kujibu angalau maswali manne kati ya maswali saba yafuatayo. Andika maswali haya ubaoni au katika bango kitita, na uweke mahali ambapo kila mshiriki atayaona maswali hayo. Wahamasishe baadhi ya washiriki katika kikundi kujibu maswali kwa njia ya ubunifu zaidi: kwa mfano, kwa kuigiza igizo fupi, kuchora, kusimulia hadithi ya kweli, kutoa ushuhuda wa mtu binafsi, kuimba wimbo au kuandika

sala, watakayoweza kuwasilisha wakati wa kipindi cha kutoa ripoti.

a) Je, jamii yetu inawatendeaje watu wenye VVU?

b) Je, ni kwa nini mtu anayeishi na VVU aamue kukataa hali yake kuwa ana VVU?

c) Je, ni kwa jinsi gani kukataa kwamba mtu ameambukizwa VVU kunaweza kusababisha kuenea kwa virusi?

d) Je, tunaweza kufanya nini, kama mtu binafsi, au kama kanisa na wanajamii kukabiliana na unyanyapaa, ubaguzi na kukataa kunakohusishwa na VVU?

e) Je, kuna washiriki wowote ambao wangependa kuwashirikisha wenzao kuhusu jinsi unyanyapaa na ubaguzi ulivyowaathiri wao binafsi, familia au rafiki zao?

Igizo: mke anarudi nyumbani akiwa na majibu ya damu kwamba ana uambukizo wa VVU.

Je, nimwambie?

Page 44: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

42 www.stratshope.org

NIITE

Mazingira ya VVU na UKIMWI

Mambo matatu makuu – unyanyapaa, ubaguzi na kukataa – yanasababisha ongezeko la maambukizi ya VVU duniani. Tunaweza kutoa maana ya maneno haya kama ifuatavyo:

Unyanyapaa: kwa lugha ya kawaida, hii ni ishara au alama ya dharau, au kushusha hadhi. Mara nyingi unyanyapaa hujidhihirisha zaidi katika sura ya kutokukubalika, kuhukumiwa na kukataliwa kwa mtu anayeishi na VVU kunakofanywa na wanafamilia, majirani, waajiri, jamii za waumini na makundi mengine ya jamii.

Ubaguzi: mtu fulani kutokutendewa haki, kwa kawaida kutokana na chuki au taarifa potofu, kwa mfano, dhidi ya watu wa kabila lingine, au dini nyingine au dhidi ya watu wanaoishi na VVU.

Kukataa: hii ni hali ya kutokukubali ya kwamba jambo fulani ni kweli, kwa mfano, kukataa kuwepo kwa VVU na UKIMWI katika maisha ya mtu mwenyewe, katika maisha ya familia ya mtu, au jamii, licha ya kwamba ushahidi unaonyesha wazi kuwepo kwa jambo hilo.

Kabla ya kuanza mafunzo haya ya Biblia, andika ufafanuzi wa maneno haya kwenye karatasi ya bango kitita na uiweke mahali ambapo washiriki wote wanaweza kuona.

Kuwa mkoma katika nyakati za Biblia inafanana kwa siku hizi na jinsi watu wengi wanaoishi na VVU wanavyotendewa. Kutokana na unyanyapaa wa hali ya juu unaounganishwa na VVU na UKIMWI, watu wengi wanaoishi na VVU na UKIMWI wanateseka na ubaguzi kutoka kwa familia zao, majirani, wafanyakazi wenzao, marafiki na hata waumini wenzao. Hali hii hupelekea kukataa ukweli na uhalisia wa VVU na UKIMWI katika ngazi ya mtu binafsi, familia, jamii na taifa. Kama watu wanakataa ukweli wa VVU, basi kuna uwezekano mdogo wa kwenda kupima damu kuangalia uambukizo wa VVU na kuweza kujali na kufuata misingi ya tabia na mwenendo salama kama vile kutokujamiiana kabla ya ndoa, kuwa mwaminifu katika ndoa, na kutumia kondomu.

Kiongozi wa somo la Biblia azingatie jambo hili: unapozungumza, rejea kwenye karatasi ya bango kitita uliyoandika ufafanuzi mfupi kuhusu maana ya ’ unyanyapaa ’, ‘ ubaguzi ’ na ‘kukataa ’.

f) Buni igizo fupi kuelezea ni kwa jinsi gani hali ya mtu kukataa kuwa na uambukizo wa VVU kunavyoweza kuchangia kuenea kwa VVU. Kwa mfano, mwanaume ambaye amekuwa na tabia ya kufanya ngono nje ya ndoa anaugua lakini anakataa kupimwa kuangalia kama ana uambukizo wa VVU. Wakati huo huo, mkewe, ambaye amekuwa mwaminifu kwa mumewe, yeye amepima na amekutwa na uambukizo wa VVU. Je, mwanamke huyu atamwambia nini mumewe?

g) Tunga wimbo, andika shairi, au chora mchoro kuelezea hadithi ya kweli ya maisha inayofafanua ni kwa jinsi gani unyanyapaa, ubaguzi, na kukataa kunakohusishwa na VVU kunavyoweza kuchangia kuenea kwa VVU.

Hatua ya Sita Dakika 30Sasa ni wakati wa vile vikundi vidogovidogo kukusanyika tena kwa pamoja na kutoa taarifa ya mijadala yao na majibu ya maswali. Kwa wale ambao watakuwa wameandaa igizo, mchoro, ushuhuda binafsi, hadithi, shairi au wimbo ni vizuri wakikaribishwa ili kuwasilisha mambo yao.

Hatua ya Saba Dakika 101. Waulize sisi kama jamii ya Wakristo wa kanisa letu, familia au wanajamii zetu, tunaweza kufanya nini ili kushughulikia tatizo la unyanyapaa, ubaguzi na kukataa kunakohusishwa na VVU.

2. Hitimisha somo la Biblia kwa kuwaongoza washiriki kwa sala, au kwa kumwomba mmoja wa washiriki afunge kwa sala.

Page 45: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

www.stratshope.org 43

MITAZAMO NA MATENDO BINAFSI

Hatua ya Kwanza Dakika 5Wakaribishe washiriki wote na kama kuna wageni wakaribishe wajitambulishe. Mwombe mshiriki mmojawapo kufungua kipindi kwa sala.

Eleza kuwa somo la leo la Biblia litahusu mambo matatu ambayo kila mmoja wetu ana uwezekano wa kukutana nayo mara kwa mara katika maisha yetu ya kila siku, nayo ni: msamaha, toba na upatanisho.

Hatua ya Pili Dakika 5Waombe washiriki wawili wasome Luka 15:11-32 . Kama washiriki wana Biblia zao waombe kila mmoja aweze kufungua sehemu ya aya ya Biblia inayosomwa ili aweze kufuata inaposomwa.

Hatua ya Tatu Dakika 101. Waulize washiriki kutaja mambo yaliyovuta zaidi hisia zao katika habari hii. Watie moyo washiriki kadhaa kutoa mawazo yao kwa kifupi - angalau maneno matano au sita. Andika mawazo yao kwenye bango kitita. Hakikisha unaandika na kuelezea maneno muhimu ‘toba’, ‘msamaha’ na ‘upatanisho’.

2. Waeleze taarifa za ziada ambazo ni za muhimu zilizoko kwenye boksi la Mazingira ya Ki-Biblia (kulia).

Hatua ya Nne Dakika 20Waombe washiriki kujadili maswali yafuatayo, yaliyoandikwa kwenye bango kitita, na kuwekwa mahali ambapo kila mshiriki ataweza kuyaona.

a) Baba alifurahi alipomwona kijana wake anarudi kutoka uhamishoni, uhamisho ambao

gani mwingine angeweza kuwa nao kwa kijana wake alipoonekana tena?

11. Msamaha, toba na upatanisho

Malengo ya Kujifunza

1. Kuwawezesha watu kuiona nguvu ya msamaha, toba na upatanisho katika maisha yao binafsi.

2. Kutambua na kushinda vizuizi vya msamaha, toba na upatanisho.

Aya: Luka 15:11-32.

Mazingira ya Ki-BibliaZamani za Biblia, baba wa Kiyahudi alipofariki, watoto wake wa kiume ndio waliokuwa na haki ya kumiliki sehemu ya urithi wa mali za baba yao (kama vile shamba lake, mali zake, fedha). Katika habari tuliyosoma kijana wake mdogo aliomba na akapewa sehemu yake ya urithi wa mali zababa yake hata kabla hajafariki. Ingawa jambohili lilikuwa kinyume na desturi ya Kiyahudi, baba yake aliamua kukubaliana na ombi la kijana wake. Kijana huyu mdogo aliporudinyumbani baada ya kutapanya urithi wake, baba yake alimpokea moja kwa moja pasipo masharti. Tabia ya kijana ilikuwa ya ubinafsi na alikuwa amekosea kabisa kimaadili. Anajua kuwa hastahili kabisa kuitwa mwana, lakini baba yake aliweka wazi kwamba kurudisha uhusiano wao kwake yeye lilikuwa jambo la muhimu zaidi kuliko heshima yake mwenyewe. Hata hivyo, kaka yake mkubwa alijisikia vibaya kwamba hakutendewa haki kwa vile baba yake alivyofanya tendo laukarimu na msamaha kwa mdogo wake.

ddii

Page 46: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

44 www.stratshope.org

NIITE

b) Je, ni kwa nini baba aliamua kufanya kwa jinsi alivyofanya?

c) Eleza jinsi baba alivyoonyesha msamaha kwa mwanawe ‘mfujaji’ (au mharibifu).

d) Je, ni kwa vipi mwana ‘mfujaji’ alionyesha toba yake kwa baba yake?

e) Je, ni kwa nini kaka yake mkubwa hakuwa tayari kupatanishwa na mdogo wake?

f)

Je, ni kwa kiasi gani mtazamo wa mtoto mkubwa unaeleweka au hata kuhalalishwa?

Hatua ya Tano Dakika 251. Fafanua mawazo kuhusu VVU na UKIMWI katika boksi hapa chini.

2. Waombe washiriki wajigawe katika viundi vidogovidogo vya watu kama watano au sita

Mazingira ya VVU na UKIMWI

Duniani kote, ugonjwa wa UKIMWI umekuwa chanzo cha kutokuaminiana, uonevu na ugomvi miongoni mwa familia, majirani na marafiki. UKIMWI unasababisha chuki, hasira, na hata kutamani kulipiza kisasi kwa wale ambao

tunaamini wametukosea. Upatanisho na wale ambao, kwa maoni yetu, tunahisi wametutendea mabaya ni changamoto kubwa sana. Upatanisho huu unaweza kupatikana iwapo tu kutakuwepo toba kwa upande moja, na msamaha kwa upande mwingine.

Upatanisho unahusisha vyote viwili, toba na msamaha.

Karibu nyumbani, mwanangu!

Page 47: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

www.stratshope.org 45

MITAZAMO NA MATENDO BINAFSI

kwa kila kikundi. Wape kila kikundi maswali manne kati ya maswali yafuatayo (utapaswauwe umeyaandika maswali haya kwenye bango kitita), kuyajadili na kuyajibu. Weka bango kitita mahali ambapo kila mshiriki anaweza kuyaona maswali hayo.

a) Je, ni kwa nini msamaha ni jambo la muhimu? (Endelea kuuliza swali hili hadi

kwamba kuwasamehe watu wengine si kitu kinapaswa kufanyika eti kwa sababu tu Mungu anatutaka tufanye hivyo. Msamaha pia unatusaidia kutufungua rohoni kiasi kwamba kibinadamu utambulisho wetu sasa unakuwa hauundwi na kuelezewa katika mtazamo wa mabaya tuliyotendewa. Hapo sasa tunakuwa huru, na kuwa jinsi Mungu alivyotuumba ili tuwe hivyo.)

b) Je, tunatakiwa kuwa na mwitikio gani kwa

walikataa ushauri na maoni yetu, na sasa wamekumbwa na matatizo makubwa?

c) Je, kama tumejitenga na wanafamilia au

kufanya nini ili kuleta upatanisho?

d) Kama tunaaamini ya kwamba tumeambukizwa VVU na mtu fulani katika familia yetu, je, tutaonyesha tabia gani kwa mtu huyo?

e) Je, ni matatizo gani tunayoweza kuyatatua kama tukitenda mambo yanayohusu msamaha na upatanisho kwa wengine, hata kama tunaishi au hatuishi na VVU?

f) Msamaha, toba na upatanisho vinaweza kuwa vigumu zaidi kimatendo kuliko kinadharia na mara nyingine tunahitaji msaada. Je, kuna watu wa kuigwa, mifano au marejeo yoyote yaliyopo ya kutusaidia?

g) Buni igizo kuhusu msichana au mvulana aliyetoroka nyumbani na kuwapuuza wazazi wake, lakini anarudi baada ya miaka kadhaa, baada ya kuambukizwa VVU. Hitimisha igizo hili kwa miisho miwili: hitimisho moja lionyeshe kijana huyo anapokelewa vizuri nyumbani; la pili anakataliwa. Waulize washiriki kuamua ni hitimisho lipi lina uwezekano mkubwa katika maisha ya kawaida.

Hatua ya Sita Dakika 30Sasa ni wakati wa vile vikundi vidogovidogo kukusanyika kwa pamoja na kutoa taarifa ya mijadala na majibu ya maswali yao. Kwa wale ambao watakuwa wameandaa igizo, hadithi au ushuhuda binafsi wakaribishwe ili kuwasilisha mambo yao.

Hatua ya Saba Dakika 101. Waulize kile tunachoweza kufanya kuzisaidia

familia zetu, kanisa letu na jamii katika kushughulikia matatizo ambayo tumekuwa tukiyajadili. Andika mapendekezo ya washiriki kwenye bango kitita au ubaoni.

2. Hitimisha somo hili la Biblia kwa kuwaongoza washiriki katika sala, au kwa kumwomba mshiriki mmojawapo kufanya hivyo.

Page 48: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

46 www.stratshope.org

NIITE

Hatua ya Kwanza Dakika 5Wakaribishe washiriki wote na kama kuna wageni wape nafasi wajitambulishe. Anza kipindi hiki kwa pambio la kufurahisha.

Toa maelezo kuhusu somo la Biblia la leo kwamba litahusu mada ambayo si mara nyingi sana huzungumzwa kwa wazi kanisani: tendo la ndoa na matamanio ya mwili. Fungua kipindi kwa sala ya kumkabidhi Mungu wasiwasi na aibu zetu katika kuzungumzia mambo ambayo ni ya mwiko kanisani.

Hatua ya Pili Dakika 5Mwombe mshiriki mmoja asome somo kutoka 1 Wakorintho 6:12-20 . Kama washiriki wana Biblia zao waombe kufuatana na aya inayosomwa.

Hatua ya Tatu Dakika 101. Waulize washiriki kutaja mambo yaliyovuta zaidi hisia zao katika somo lililosomwa. Watie moyo washiriki kadhaa kutoa mawazo yao kwa kifupi - angalau maneno matano au sita. Andika mawazo yao kwenye bango kitita.

2. Waeleze taarifa za ziada zinazohitajika kutoka kwenye boksi la Mazingira ya Ki-Biblia (kulia):

Hatua ya Nne

Dakika 10Waombe washiriki wajadili maswali yaliyoorodheshwa kwenye bango kitita, ambalo litakuwa limewekwa mahali ambapo kila mshiriki

ataweza kuyaona maswali.

12. Tendo la ndoa na matamanio ya mwili Malengo ya Kujifunza

1. Kuelewa kwamba miili yetu ni uumbaji mzuri wa Mungu na matamanio yetu ya mwili ni zawadi toka kwa Mungu.

2. Kutafakari juu ya uhusiano uliopo kati ya tendo la ndoa na upendo.

3. Kuwafanya wazazi Wakristo kutambua kuwa wanapaswa kutafuta mbinu ya jinsi ya kuzungumza na watoto wao mambo yanayohusu tendo la ndoa na matamanio ya mwili.

Aya: 1 Wakorintho 6:12-20.

Mazingira ya Ki-Biblia

Wakristo wa Koritho walielewa ubatizokama tendo la kiroho la wokovu. Roho zao ziliokolewa, na hii ilimaanisha kwambawanaweza kuishi k wa namna yoyote ile wanayotaka. Tamko lao lilikuwa hili: Nimeokolewa, kwa hiyo “Ninaruhusiwakufanya jambo lolote”.

Paulo alikuwa na kazi ngumu ya kuelezea kwamba mwili na roho ziko pamoja na yeyoteatakayejeruhi mwili wake anajeruhi na roho yake pia. Alikasirishwa sana na tabia ya uzinziya waumini wa kanisa la Korintho. Wanaume wengi (vijana na watu wazima) waliwaendea malaya. Wanaume matajiri waliwatendea vibaya vijana wadogo wa kiume kutimiza tamaa zao mbaya na vile vile wanawake wa tabaka la juu la jamii waliwatumia watumwawanawake kutimiza tamaa zao za mwili. Maneno ya Paulo yako wazi: huwezi kutenganisha mambo ya mwilini na mambo ya rohoni. Unapofanya tendo la ngono na mtu fulani, pia unashirikiana naye roho na nafsi yako na mtu yule. Tendo la ndoa lina nafasi yake katika mahusiano ya upendo kati yawenzi wawili. Kama unafa nya tendo la ndoa kwa kusudi la kutimiza tamaa zako za mwili tu, hapo unamtumia mtu mwingine kama chombo tu. Wakati wa Yesu, wanaume wengi waliwatumia wanawake kwa tendo la ngonokwa kujifurahisha tu. Hata hivyo, Yesu aliwalinda sana wanawake (kwa mfano katika Yohana 8:11), na alikataa katakata mawazoya kuwaona wanawake kuwa ni viumbe duni au k wamba wanaeleweka vizuri k wa

(inaendelea)

Page 49: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

www.stratshope.org 47

MITAZAMO NA MATENDO BINAFSI

a) Je, Paulo ana maana gani anaposema: “ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe”?

b) Je, nini umuhimu wa maneno: “Wale wawili watakuwa mwili mmoja”?

c) Je, Paulo ana maana gani anaposema kwamba miili yetu ni “hekalu la Roho Mtakatifu”?

Hatua ya Tano Dakika 301. Toa maelezo yaliyoko kwenye boksi la

Mazingira ya VVU na UKIMWI (hapa chini).

2. Waombe washiriki wajigawe katika vikundi vinne vidogovidogo, kwa kawaida kama vya watu watano au sita. Waombe kila kikundi aidha wabuni igizo kulingana na maelezo yafuatayo ya mchezo, au kujibu maswali matatu yaliyoorodheshwa kwa ajili ya kikundi namba 4 kwenye ukurasa wa 49.

KIKUNDI NA. 1: Igizo kwa ajili ya vijana wadogoThabo ni kijana mdogo wa kiume ambaye amenuia kuthibitisha ‘uwanaume’ wake. Anawatongoza wasichana wawili, Nomsa na Thembi wenye umri wa miaka 15. Nomsa hajiheshimu na wakati wote ana wasiwasi kuhusu jinsi anavyoonekana. Anaishi na bibi yake, ambaye hajawahi kuzungumza naye masuala ya kujamiiana. Bado anasoma lakini

kile wanachoweza kuwapa wanaume tu. Yesu aliweza pia kupambana na mawazo ya wanaume waliowaona wanawake kama vyombo vya kutumiwa, alitoa onyo: “Kila mtu amtazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake” (Mathayo 5:28). Katika Injili zote Yesu anawahusisha wanawake kwa kuwaheshimu, kuwahurumia na kuwajali kama wanadamu kamili. Matamanio ya miili yetu ni zawadi toka kwa Mungu, muumbaji. Lakini Mungu hataki zawadi hii ilete ugonjwa na mateso, vitu ambavyo hutokana na kuwa na wapenzi wengi. Mtume Paulo anasema, watu wanapofanya tendo la ndoa wanakuwa “nyama moja” au “mwili moja” na wapenzi hao. Hii inamaanisha wanafanyika kuwa kitu kimoja kila mmoja anakuwa wa mwenzake. Kama mkiwa kitu kimoja, mnashirikiana kila kitu na mnaaminiana. Hakuna nafasi ya mtu wa tatu.

Taarifa kwa kiongozi: Katika kipengele hiki unaweza kuwaomba washiriki kushika mikono yao kama vile wanaomba. Onyesha wazi kwamba hakuna nafasi ya mkono wa tatu. Hivi ndivyo Paulo alivyoona uhusiano kati ya watu wawili ambao wamekuwa mwili mmoja: wanakuwa kama mtu mmoja.

Mazingira ya VVU na UKIMWI

Maneno ‘kujamiiana’ na ‘matamanio ya mwili’ ni maneno yenye maana tofauti, ingawa kimsingi yanahusiana. Neno ‘kujamiiana’ lina maana kukutana kimwili. Hata hivyo ‘matamanio ya mwili’ lina maana pana zaidi. Matamanio ya mwili inahusiana na jinsi tunavyojisikia kama wanawake au wanaume. Hii ni pamoja na tunavyojisikia kuhusu miili yetu – tunajisikiaje tunapokuwa msichana au mwanamke, au jinsi ya kuwa mvulana au mwanamume. Matamanio ya mwili yana uhusiano na kujiheshimu kwetu, na kujithamini, na jinsi tunavyoelewa thamani yake kama vile upendo na uaminifu katika mahusiano. Ni kawaida kabisa kuwa na hisia za

katika mahusiano ya wapenzi wawili. Wazazi wa Kikristo na watu wanaotoa huduma ya malezi wanapaswa kuzungumza kwa uwazi na watoto

kubalehe na kuhusu ngono na matokeo ya kujamiiana mapema. Wanahitaji pia kuwatia

moyo watoto kusubiri na kutojiingiza katika kujamiiana mpaka watakapokuwa watu wazima, na wanaweza kufanya maamuzi imara kwa wenzi wao, hata kama mila na desturi, hali ya uchumi au mazingira mengine yoyote yatapelekea vijana hawa kuahirisha ndoa. Katika sehemu nyingi duniani, njia kuu ya maambukizi ya VVU hutokana na kati ya watu wawili kujamiiana. Inakubalika kwa sasa kwamba njia kuu ya kusambaza VVU ni kuwa na wapenzi zaidi ya mmoja kwa wakati moja. Hali hii huelezewa kama ni ‘mahusiano ya kujirudiarudia ya kimapenzi na watu mbalimbali.’ Mwongozo wa Kikristo wa kuwa mwaminifu kwa mwenzi mmoja ndiyo hasa umeonekana kuwa mkakati wenye mafanikio katika kujikinga na maambukizi ya VVU. Lakini pia ni muhimu sana kwa wanandoa kujua hali zao kwa kupima damu, na kujua kama tayari wameambukizwa VVU. Majibu yanayoonyesha kwamba mmoja wao au wote wawili wameambukizwa VVU yatawasaidia kufanya maamuzi sahihi kuhusu wakati wao ujao. Hii haina maana kwamba kuna uwezekano wa kutokuwepo kwa ndoa.

Page 50: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

48 www.stratshope.org

NIITE

hapati maksi nzuri sana na anataka kuacha shule.

Msichana wa pili, Thembi anajiheshimu. Ni mwanakwaya na mwanachama wa idara ya vijana kanisani. Ana marafiki na mama yake amemwomba shangazi ili azungumze naye mambo yanayohusu kujamiiana, na jinsi anavyoweza kupata mimba hata kama ni mara ya kwanza unafanya ngono. Shangazi yake ni mwalimu wa shule. Amemwambia Thembi kwamba wasichana wenye marafiki wa kiume mara nyingi humtaka rafiki yake wa kiume kuliko kufanya vizuri shuleni, na matokeo yake maksi zao zinashuka.

Katika igizo hili Thabo anamtongoza Thembi na anamwambia wazi angependa kuanza uhusiano wao kwa kujamiiana. Thembi anamwambia Thambo kuwa kwa kweli anampenda sana, lakini kwa suala la kujamiiana anasema: ‘hapana’. Thabo anaamua kumtongoza Nomsa, na pasipo hata majadiliano, Nomsa anakubali kujamiiana na Thabo. Je, Thabo anamheshimu yupi zaidi? Thembi na Nomsa? Mtume Paulo angemwambia nini Nomsa? Igizeni hilo igizo na mjadiliane maswali haya katika kikundi chenu.

KIKUNDI NA. 2: Igizo kwa ajili ya vijana wadogo

Lindiwe ni msichana mdogo na wazazi wake ni maskini sana. Dreva wa teksi anamtongoza na kumwahidi kumnunulia zawadi nzuri ili wajamiiane. Lindiwe anajua kabisa habari za magonjwa ya ngono na uwezekano wa kupata mimba lakini pia anahitaji viatu. Anaona aibu sana anapoangalia viatu vyake. Anaogopa na hataki kufanya ngono. Je, atafanyaje? Igizeni igizo hilo na mjadiliane swali hili katika kikundi chenu.

KUNDI NA. 3: Maigizo matatu kwa ajili ya watu wazima

Mafundi ujenzi watatu - George, Yakobo na Petro – wanafanya kazi mbali na nyumbani kwao. Wote watatu wameoa na wanawapenda wake zao lakini wanajisikia wapweke.

Igizo Na. 1: George anafanya ngono na Lena (bila kondomu), mwanamke aliyekutana naye dukani. Lena anapata mimba na anamwomba George fedha, ambazo anaanza kumpa. George anaacha kutuma fedha kwa mke wake na familia. Baada ya miezi kadhaa, shemeji yake anamtembelea George. Amua kinachotokea sasa kati ya George, Lena na shemeji yake, igiza igizo hili.

Igizo Na 2: Yakobo amekuwa akifanya ngono na

Mary, mwanamke ambaye hajaolewa mwenye matumaini kwamba Yakobo atampa talaka mke wake na kumwoa yeye. Anataka ‘kujadiliana’ na Yakobo kuhusu kujamiiana bila kondomu, lakini Yakobo bado anakataa. Je, anatumia ushawishi gani? Igiza hadithi hii.

Igizo Na 3: Petro anasafiri kwenda nyumbani kumwona mke wake na familia kila baada ya miezi miwili. Ni safari ndefu na inagharimu fedha nyingi, lakini anataka kumwona mke wake na watoto. Hafanyi ngono na mwanamke mwingine yeyote yule. Anataka kuwaleta mke na watoto wake huko anakoishi sasa na kufanya kazi. Wenzake wanamtania Petro na kumwambia: “Wewe sio mwanamume halisi. Una mwanamke mmoja tu… shida yako nini?”. Je, ni kwa nini wanaume wengine hawaheshimu aina ya maisha ya Petro? Je, Petro atawajibuje? Igiza igizo hili na kujibu maswali haya mawili.

Hali yetu ya matamanio ya mwili yanahusiana kujiheshimu na kujistahi.

Page 51: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

www.stratshope.org 49

MITAZAMO NA MATENDO BINAFSI

KIKUNDI NA. 4: Maswali matatu

Kikundi hiki kinapaswa kujadiliana na kujibu maswali matatu kuhusu kondomu, kama ifuatavyo:

a) Je, ni katika mazingira gani itakuwa sawa kwa Wakristo kutumia kondomu?

b) Je, ni katika mazingira gani itakuwa sio sawa kwa Wakristo kutumia kondomu?

c) Je, kanisa linaweza kuhimiza matumizi ya kondomu kama njia ya kupunguza maabukizi ya VVU na vifo vitokanavyo na UKIMWI?

Hatua ya Sita Dakika 401. Sasa ni wakati wa vile vikundi vidogovidogo

kukusanyika kwa pamoja. Vikundi Na. 1, 2, na 3 watapaswa kufanya maigizo yao, na Kikundi Na. 4 watapaswa kutoa taarifa kuhusu maswali waliyoyajadili na majibu yake. Toa muda wa vikundi vingine kutoa maoni au kuuliza maswali.

2. Wajulishe washiriki kwamba kuna kitabu kingine kipya cha mfululizo wa machapisho haya ya Tumeitwa Kuhudumia chenye kichwa cha habari, Malezi: Safari ya Maisha, kinachoshughulikia masuala ya malezi, ambacho kitachapishwa katikakati ya mwaka 2010. Kitabu hiki ni mwongozo muhimu sana kwa wazazi wa aina zote, walezi na watoa huduma kwa watoto. Kitabu hiki kinashughulika zaidi na tendo la ndoa na tabia ya kujamiiana, na mambo mengine mengi muhimu.

Hatua ya Saba Dakika 101. Waulize jinsi tunavyoweza kusaidiana, sisi

kama waumini wa makanisa yetu, familia na jamii kwa ujumla, katika kuishi maisha yenye afya tosha ya tendo la ndoa huku tukiwalinda walio wadhaifu na wale walio katika mazingira hatarishi ya kunyayaswa kingono.

2. Hitimisha somo hili la Biblia kwa kuwaongoza washiriki kwa sala, au umwombe mshiriki mmojawapo kufanya hivyo.

Page 52: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

50 www.stratshope.org

NIITE

Hatua ya Kwanza Dakika 5

Wakaribishe washiriki wote na wape wageni wowote nafasi wajitambulishe. Mwombe mshiriki mmojawapo kufungua kipindi kwa sala.

Toa maelezo kwamba somo la Biblia la leo litahusu unyanyasaji na ukatili wa kijinsia.

Hatua ya Pil Dakika 10Waombe washiriki watatu, wasome vifungu vifuatavyo vya Biblia, Mwanzo 39:6-20; 2 Samweli 13:1-22 . Kama washiriki wana Biblia zao, waombe kufuata aya zinazosomwa katika Biblia zao.

Hatua ya Tatu Dakika 101. Waulize washiriki kutaja mambo yaliyovuta zaidi hisia zao kuhusu habari hizi mbili zilizosomwa. Watie moyo washiriki kadhaa kutoa mawazo yao kwa kifupi - angalau maneno matano au sita. Andika majibu yao kwenye bango kitita.

2. Waeleze taarifa za ziada ambazo ni za muhimu zilizoko kwenye boksi la Mazingira ya Ki-Biblia (kulia).

Hatua ya Nne Dakika 10Waombe washiriki kujadili maswali yafuatayo, yaliyoandikwa kwenye bango kitita, na yawe yamewekwa mahali ambapo kila mshiriki ataweza kuyaona.

a) Je, tunaweza kuwatambua wahusika wote katika hadithi ya Tamari na kutaja mchango wao katika tukio hili?

b) Je, ni kwa nini Amnoni alimbaka Tamari, dada yake?

13. Unyanyasaji na ukatili wa kijinsia Malengo ya Kujifunza

1. Kuvunja ukimya katika kuzungumzia unyanyasaji na ukatili wa kijinsia.

2. Kuonyesha ya kwamba unyanyasaji na ukatili wa kijinsia humshushia mtu hadhi na huchangia katika kuenea kwa VVU.

Aya: Mwanzo 39:6-20; 2 Samweli 13:1-22.

Mazingira ya Ki-Biblia

Mwanzo 39:6-20: Yusufu, kijana mdogo, mtu mzuri na mwenye uso mzuri, Mwebrania aliyekuwa mtumwa, alifanya kazi kwa bwana wake Potifa huko Misri. Potifa alikuwa

na wajibu wa kuongoza kikosi cha ulinzi kwenye kasri. Yusufu alipanda cheo haraka na hatimaye akaaminiwa kwa kusimamia shughuli zote za bwana wake, ikiwa ni pamoja na mazao yake. Hata hivyo, mke wa Potifa, alijaribu mara kwa mara kumshawishi Yusufu wafanye naye mapenzi, lakini Yusufu alikataa. Akasema: “Nifanyeje ubaya huumkubwa nikamkose Mungu?” Mwishowe, akitaka mkumlipiza kisasi Yusufu, mke waPotifa akadai kwamba Yusufu alitaka kumbaka.Potifa alikasirika sana, akaagiza Yusufuakamatwe na kutiwa gerezani.

2 Samweli 13:1-22: Pengine Tamari alikuwa na umri kama wa miaka 12 hadi 14 hivi alipobakwa na kaka yake wa kambo, Amnoni, mmoja wa watoto wa kiume wa mfalme Daudi. Zamani katika jamii ya Kiebrania, ubikira kwa bibi harusi ulithaminiwa sana. Ubikira wa bibi harusi ulidhihirisha heshima ya baba yake na ya mume wake mtarajiwa. Kwa kupoteza ubikira wake, Tamari alipoteza pia heshima yake na uwezekano wa kuwa na ndoa nzuri. Tendo la kubakwa na Amnoni lilimwachia unyanyapaa wa kudumu katika jamii.

Page 53: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

www.stratshope.org 51

MITAZAMO NA MATENDO BINAFSI

c) Je, tendo la Amnoni kwa Tamari lilikuwa na madhara gani?

d) Je, ni akina nani wanahusika katika hadithi ya Yusufu na mke wa Potifa?

e) Je, ni kwa jinsi gani mke wa Potifa alijaribu kutumia nguvu ya nafasi yake dhidi ya Yusufu?

f) Je, ni mambo gani yanafanana katika hadihi hizi mbili?

g) Je, ni mambo gani ya muhimu sana ambayo yanatofautiana katika hadithi hizi mbili?

Hatua ya Tano Dakika 251. Tambulisha mawazo kuhusu mazingira ya

VVU na UKIMWI kama yalivyo katika boksi (hapa chini).

2. Waombe washiriki wajigawe katika vikundi vinne: wanawake watu wazima, wanawake vijana, wanaume watu wazima, wanaume vijana. Kimsingi kila kikundi kiwe na watu angalau watano au sita. Waombe kila kikundi wajadili na wajibu angalau maswali matano. Utakuwa umeyaandika maswali haya kwenye bango kitita. Weka mahali ambapo kila mshiriki ataweza kuyaona.

a) Je, kwa mara ya kwanza ulipokeaje habari za Tamari na Yusufu? Je, unaweza kujiweka katika nafasi ya mtu yeyote katika habari hizi?

b) Je, kuna mshiriki ambaye anaweza kusimulia habai kuhusu ‘Tamari’ na ‘Yusufu’ katika familia au jamii yake?

c) Kuna msemo katika lugha ya ki-Bemba unaosema ‘ubucende bwa mwaume ta bona ng’nda’, tafsiri yake ni hii “uzinzi wa mwanamume hauwezi kuharibu ndoa”. Karibisha maoni kuhusu usemi huu.

d) Je, usemi huu unaashiria nini katika kizazi hiki chenye VVU na UKIMWI?

e) Je, ni kwa nini wanaume wengine wanabaka?

f) Je, kubaka kunaleta athari gani kwa aliyebakwa?

g) Je, kuna mipango gani ya misaada inayopatikana katika jamii zetu zaa kuwasaidia wale wanaonyanyaswa kingono na kufanyiwa ukatili wa kijinsia?

Mazingira ya VVU na UKIMWI

Unyanyasaji wa kingono ni kutakiwa au kulazimisha kufanyika kwa ngono, au pia inaweza kuwa tabia na hisia zenye mtazamo wa ngono zinazoonyeshwa na mtu kwa mtu ambaye hataki wala kukaribisha hali hii. Unyanyasaji huu unaweza kuwa katika hali ya utani, kupiga simu kwa hila; au kuonyesha matendo machafu au kuangalia picha za ngono, sinema, mabango, maandiko au kusoma habari au mtandao wa ngono. Unyanyasaji wa kingono unaweza pia ukawa na mwelekeo wa kupendekeza mpango wa kujamiiana, kugusana mwili kama vile kupapasana, kuminyaminya au kugusa kwa nia ya kushawishi kufanya mapenzi; pia inaweza kuwa ni katika kuzoeana sana hata kujilazimisha kusuguana kimwili, au kukumbatia kwa hila. Pia inaweza kuwa katika kutoa maoni kuhusu maisha ya mtu yanayohusu masuala ya mapenzi au maisha yake ya siri; kutoa sifa yenye kuashiria uzuri wa sura au maumbile ya mtu; kutaja habari za maisha binafsi, kwa kuonyesha ishara, au hata kuweka wazi sehemu za siri. Wanaume na wanawake wote wanaweza kuwa chanzo cha unyanyasaji wa kingono ingawa kwa kweli unyanyasaji huu hufanywa zaidi na wanaume, wakielekeza unyanyasaji huu kwa wanawake. Mambo haya hutokea katika maeneo ya kazi, lakini pia katika mazingira

ya mahusiano ya mwalimu na mwanafunzi, madukani, katika sherehe na mikusanyiko ya kijamii, na hata ndani ya familia. Katika aina zote hizi za unyanyasaji, jambo la msingi kuelewa ni kwamba tendo lolote la unyanyasaji humshushia hadhi mtu, humwondolea ubinadamu wake na yule atoaye shambulio huonekana ndiye mshindi. Hali hii huweza kusababisha majeraha kimwili na/au kisaikolojia, kihisia, na kiroho pia. Katika hali mbaya sana ya unyanyasaji huu, aina za mashambulio zinaweza kuwa katika mfumo wa mashambulizi ya kingono na kubaka, yaani kujamiiana kwa nguvu, pasipo hiari ya mshambuliwa. Unyanyasaji wa kingono na ukatili wa kijinsia vinahusiana kwa karibu na suala zima la kuenea kwa VVU. Wanaume wengine wanawabaka watoto wadogo wa kike kwa imani potofu ya kwamba kwa kufanya tendo hilo na bikira watapona VVU. Watu wengine hufanya hivi na watoto wao wenyewe kwa imani kwamba kwa kufanya hivyo watapata utajiri. Wengine hufurahia kuona wakiwalazimisha wanawake wawanyenyekee katika suala zima la kujamiiana. Wanawake ndio hasa walio katika hatari kwenye ukanda wa vita, ambako maadui wao moja kwa moja hutumia kubaka kama silaha ya kuwadhalilisha na kuwatisha wanaowashambulia.

Page 54: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

52 www.stratshope.org

NIITE

h) Je, sisi kama watu binafsi, wanafamilia, kanisa na wanajamii kwa ujumla tunaweza kuchukua hatua gani ili kujishughulisha na masuala ya unyanyasaji wa kingono na ukatili wa kijinsia?

i) Buni igizo fupi ili kufafanua matatizo yanayosababishwa na unyanyasaji wa kingono na ukatili wa kijinsia. Au pengine, toa ushuhuda binafsi kuhusu masuala haya.

Hatua ya Sita Dakika 30Sasa ni wakati wa vile vikundi vidogovidogo kukusanyika kwa pamoja na kutoa taarifa ya

mijadala yao na majibu ya maswali. Kwa wale ambao watakuwa wameandaa igizo au shuhuda binafsi wakaribishwe ili kuwasilisha mambo yao.

Hatua ya Saba Dakika 101. Waulize tunaweza kufanya nini ili kusaidia familia zetu, kanisa letu na jamii yetu kushughulikia matatizo ambayo tumekuwa tukiyajadili. Andika mapendekezo ya washiriki kwenye karatasi ya bango kitita.

2. Hitimisha kipindi hiki cha kujifunza Biblia kwa wimbo na sala.

Wanaume wengine wanawabaka wasichana wadogo kwa sababu wanaamini kwamba kwa kufanya hivyo kwa msichana bikira watapona VVU.

Usimwambie mtu mwingine neno

lolote. Umeelewa?

Page 55: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

www.stratshope.org 53

MAMBO YANAYOMSUMBUA MWANADAMU

Hatua ya Kwanza Dakika 5Wakaribishe washiriki wote na wape wageni wowote nafasi wajitambulishe. Mwombe mshiriki mmojawapo kufungua kipindi kwa sala.

Toa maelezo kwamba somo la Biblia la leo litahusu mada ya hofu na mashaka.

Hatua ya Pili Dakika 10Mwombe mshiriki mmoja asome maneno ya ufafanuzi kuhusu Mazingira ya Ki-Bibilia kwenye boksi (kulia). Halafu mwombe mshiriki mwingine asome aya ya Warumi 8:31-39 . Kama washiriki wana Biblia zao, waombe wafungue aya inayosomwa ili waweze kufuata inaposomwa.

Hatua ya Tatu Dakika 10Waulize washiriki kutaja mambo yaliyovuta hisia zao zaidi katika kifungu cha Biblia kilichosomwa. Watie moyo washiriki kadhaa kutoa mawazo yao kwa kifupi - angalau maneno matano au sita. Andika majibu yao kwenye bango kitita.

Hatua ya Nne Dakika 10Waombe washiriki kujadili maswali yafuatayo, yaliyoandikwa kwenye bango kitita, ambayo yatakuwa yamewekwa mahali ambapo kila mshiriki ataweza kuyaona.

a) Je, unaweza kutoa mfano kuthibitisha ukweli wa ujumbe uliomo katika kifungu hiki cha Biblia kutokana na uzoefu wako?

b) kupitia aya hii iliyoko kwenye Maandiko?

Mambo yanayomsumbua mwanadamu ……. 14. Hofu na mashaka

Malengo ya Kujifunza

1. Kuwawezesha watu wanaoishi na VVU kuishi bila hofu na mashaka.

2. Kukuza dhamira ya kujituma na kujitoa miongoni mwa Wakristo katika kuwasaidia watu wanaoishi na VVU kushinda hofu na mashaka yao.

Aya: Warumi 8:31-39.

Mazingira ya Ki-Biblia

Paulo aliwaandikia barua hii Wakristo wa Rumi mnamo mwaka wa 55 BK, baada ya miaka 20 hivi ya huduma yake katika nchi zinazozunguka Mediteraniani. Wakati huo alikuwa hajawahi kutembelea Rumi, lakini bado alikuwa na matumaini ya kufanya hivyo. Wakati ule Wakristo wa Rumi walikuwa ni pamoja na Wayahudi na Wamataifa, na kwa bahati mbaya makundi haya yalikuwa na misuguano kati yao.

Akiwa ni Myahudi aliyeitwa na Mungu kuwahubiria Wamataifa, Paulo alikuwa katika nafasi nzuri ya kuyapatanisha makundi haya mawili. Hali ya Wakristo wa Rumi wakati ule ilikuwa ni ya kutatanisha. Walikuwa matesoni kwa unyanyapaa uliokithiri na utawala wa Rumi uliwaona kama watu hatari na wasioaminika. (Hatimaye Paulo alipokwenda Rumi huko akafungwa jela). Katika barua yake kwa Wakristo wa Rumi - ambayo ndiyo barua yake ndefu kuliko zote alizoandika-Paulo anazungumzia mada nyingi kuu kuhusuhuduma yake na anashughulikia pia masuala ya vikwazo ambavyo vilikuwa vikitolewa na wapinzani wake. Katika aya hii, Paulo anakusudia kuwahakikishia Wakristo wa Rumi kwamba, haijalishi matatizo gani wanakutananayo, Mungu hatawaacha kabisa.

Page 56: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

54 www.stratshope.org

NIITE

Mazingira ya VVU na UKIMWI

Hofu na mashaka ni hali za kawaida kabisa katika kipindi tulicho nacho cha VVU na UKIMWI. Watu ambao wamekuwa Wakristo kwa miaka mingi wanajikuta wanalazimika kukabiliana na hisia hizi. Janga la UKIMWI sio tishio tu la kiafya, lakini limesababisha mashaka na hofu nyingi zaidi, kwa mfano, kuhusu mahusiano katika ndoa, fedha za

kifamilia, kukubali matokeo ya kwamba mtu ana VVU, kuweka wazi hali ya mtu kuwa ana VVU, na hatma ya watoto ambao wazazi wao wanakufa mapema. Hata hivyo bado watu wanaweza kujifunza kupeleka wasiwasi, hofu na mashaka yao kwa Mungu, anayeweza kuwaondolea matatizo haya na kuwaweka huru ili kujishughulisha na mahitaji yao na yale ya watu wengine pia.

Hatua ya Tano Dakika 251. Tambulisha mawazo kuhusu Mazingira ya VVU na UKIMWI kama yalivyo katika boksi hapo juu.

2. Waombe washiriki wajigawe katika vikundi vidogovidogo vya watu kama watano au sita kwa kila kikundi. Waombe kwamba katika kila kikundi wajadili na kujibu maswali angalau manne yafuatayo. Utakuwa umekwisha kuyaandika maswali hayo kwenye karatasi ya bango kitita. Weka karatasi ya bango kitita mahali ambapo kila mshiriki atayaona maswali hayo.

a) Je, ni katika maeneo gani ya maisha ambayo kwa sehemu kubwa tunahisi kuwa na mashaka zaidi sana? Je, tunawezaje kushinda haya?

b) Je, unaweza kumpa Mungu usikivu wako wote kwa yale Mungu anayokufanyia sasa hivi, na kuacha kuwa na mashaka kuhusu linaloweza kutokea au kutokutokea kesho? Simulia hadithi fupi kuhusu uzoefu wako mwenyewe.

c) Je, unaweza kutoa ushuhuda kuhusu jinsi Mungu alivyokusaidia siku za nyuma hata ukaweza kushinda hofu na mashaka yako juu ya kitu fulani?

Janga la UKIMWI limeleta mashaka na hofu nyingi.

Nawezaje kumwambia kuwa nina uambukizo

wa VVU?

Page 57: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

www.stratshope.org 55

MAMBO YANAYOMSUMBUA MWANADAMU

d) Buni igizo fupi sana kuonyesha jinsi Mungu alivyokusaidia siku za nyuma.

e) Je, ni kwa jinsi gani sisi kama Wakristo, tumechangia katika kuongeza hofu na mashaka miongoni mwa Wakristo wenzetu kuhusu VVU na UKIMWI. Tafadhali thibitisha jibu lako.

Hatua ya Sita Dakika 30Sasa ni wakati wa vile vikundi vidogovidogo kukusanyika kwa pamoja tena na kutoa taarifa ya mijadala yao na majibu ya maswali na mapendekezo. Kwa wale ambao watakuwa wameandaa shuhuda binafsi au igizo wakaribishwe ili kuwasilisha mambo yao.

Hatua ya Saba Dakika 101. Waulize ni kwa jinsi gani sisi, kama jamii ya

Kikristo, tunaweza kusaidiana wenyewe kwa wenyewe ili kukubaliana na hofu na mashaka yanayosababishwa na VVU na UKIMWI. Andika mapendekezo ya washiriki katika karatasi ya bango kitita.

2. Mwombe mshiriki mmoja asome Wafilipi 4:6-7 au Isaya 45:1-5.

3. Waombe washiriki kukaa kimya na kutafakari kwa dakika moja au mbili.

4. Halafu Mwombe mshiriki mmoja kuongoza pambio moja lenye maudhui kuhusu kumtegemea Mungu kwa ajili ya ushindi dhidi ya matatizo yetu.

Page 58: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

56 www.stratshope.org

Niite

Hatua ya Kwanza Dakika 5Wakaribishe washiriki wote na wape wageni wowote nafasi wajitambulishe. Mwombe mshiriki mmojawapo kufungua kipindi kwa sala.

Toa maelezo kwamba somo la Biblia la leo litahusu maana ya ‘uponyaji’ katika ulimwengu wa sasa, na hasa katika kipindi cha janga la UKIMWI.

Hatua ya Pili Dakika 5Waombe washiriki wawili kusoma (mmoja baada ya mwingine) Yohana 9:1-7. Kama washiriki wana Biblia zao waombe kila mmoja aweze kufungua sehemu ya aya ya Biblia inayosomwa ili aweze kufuata inaposomwa.

Hatua ya Tatu Dakika 10

1. Waulize washiriki kutaja mambo yaliyovuta hisia zao zaidi katika habari hii iliyosomwa. Watie moyo washiriki kadhaa kutoa mawazo yao kwa kifupi - angalau kwa maneno matano au sita. Andika mawazo yao kwenye bango kitita.

2. Zungumzia taarifa za ziada ambazo ni za muhimu zilizoko kwenye boksi la Mazingira ya Ki-Biblia (kulia).

Hatua ya Nne Dakika 10

Waambie washiriki kujadili maswali yafuatayo yaliyoorodheshwa kwenye karatasi la bango kitita, ambalo litawekwa mahali ambapo kila mshiriki ataweza kuyaona maswali kwa urahisi.

a) Je, wanafunzi wa Ychanzo cha upofu wa mtu yule?

b) Je, Yesu alijibu nini kuhusu swali lao?

c) Je, kipofu alitoa mchango gani binafsi uliochangia uponyaji wake mwenyewe?

d) Je, jibu la Yesu linauonyesha mtazamo gani wa kwake kuhusu ugonjwa, uponyaji na dhambi?

Hatua ya Tano Dakika 251. Tambulisha mawazo yaliyoko kwenye boksi la Mazingira ya VVU na UKIMWI uk. unaofuata.

15. Uponyaji Malengo ya Kujifunza

1. Kuchunguza maana halisi ya ‘uponyaji’ katika mazingira ya janga la UKIMWI.

2. Kuondoa uhusiano wowote unaohusisha moja kwa moja kati ya ugonjwa na dhambi kwa maana ya tabia ya uzinzi.

3. Kukuza uelewa ya kwamba uponyaji kamili ni ule unaohusisha mchakato wa kupata afya kimwili, kisaikolojia na kiroho.

4. Kuhamasisha ufuatiliaji wa matibabu ya kiafya (ikiwa ni pamoja na matumizi ya dawa za kurefusha maisha), yakienda sambamba na maombi, kama sehemu ya mchakato wa uponyaji.

Aya: Yohana 9:1-7.

Mazingira ya Ki-Biblia

Baadhi ya waandishi wa vitabu vya Agano la Kale walihusisha dhambi na mateso na ugonjwa. Hata hivyo, katika aya hii tuliyosoma, Yesu anafafanua wazi kwamba ugonjwa (katika habari hii, upofu) sio adhabu ya dhambi. Yesu anaenda mbali zaidi katikakufafanua jambo hili akisema kwamba ugonjwa na maumivu ya mwanadamu inaweza kuwa ni fursa ya kuonyesha upendo wa Mungu na huduma kwa binadamu.

Sio yule kipofu peke yake tu aliyeponywakatika habari hii. Pia ametumika kama njia ya kuwafumbua macho wanafunzi wa Yesu waweze “kumwona” Mungu kwa mtazamo mpya.

Page 59: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

www.stratshope.org 57

MAMBO YANAYOMSUMBUA MWANADAMU

2. Waombe washiriki wajigawe katika vikundi vidogovidogo vya watu kama watano au sita kwa kila kikundi. Waombe kwamba katika kila kikundi wajadili na kujibu angalau maswali manne kati ya maswali yafuatayo. Utakuwa umeandika maswali haya kwenye karatasi ya bango kitita. Weka karatasi hiyo mahali ambapo kila mshiriki ataweza kuyaona maswali hayo.

a) Waulize washiriki wanaelewa nini kuhusu neno ‘uponyaji’. Endelea kuwauliza mpaka

ya kujua kwamba uponyaji sio kupona katika madhaifu ya mwili tu, lakini ni pamoja na kisaikolojia, kijamii, na kiroho kwa mapana yake.

b) Ukimwuliza mtu ambaye ana uambukizo wa

hili litamfanya ajisikieje?

Mazingira ya VVU na UKIMWI

Kutokana na maendeleo ya kutengenezwa kwa dawa za kurefusha maisha mnamo katikati ya miaka ya 1990, uwezekano wa watu wenye VVU kuishi miaka mingi uliongezeka kwa kasi. Kama dawa hizi zitatolewa kwa wakati muafaka, na kama zitaandamana na lishe bora na maisha ya kujijali kiafya, zinaweza kumwezesha mtu anayeishi na VVU kuishi maisha yaliyo karibu sawa na ya kawaida. Ingawa mwanzoni

dawa hizi zilikuwa ghali sana, gharama zake

300 kwa mtu mmoja kwa mwaka. Dawa za kurefusha maisha, kama dawa nyingine zozote ni baraka kutoka kwa Mungu. Lakini kuna baadhi ya viongozi wa dini wanawashauri wafuasi wao kwamba wanaweza kupona ugonjwa wa UKIMWI kwa njia ya imani peke yake, bila kutumia dawa. Hii inaweza kusababisha vifo vya mapema, visivyo vya lazima.

Kutegemea imani peke yake tu katika suala la UKIMWI kunaweza kusababisha kifo cha mapema kisicho cha lazima.

Unaweza kuacha kutumia dawa hizo. Unachohitaji ni

imani tu.

Kwa kutumia dawa sahihi na kula chakula bora, watu wanaoishi na VVU

wanaweza kuishi maisha marefu na yenye furaha.

Page 60: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

58 www.stratshope.org

NIITE

c) wanaoishi na VVU walio wazi kuhusu hali zao pengine wawe wazi pia kusema

Tafadhali thibitisha jibu lako, ikiwezekana toa mfano halisi kuhusiana na maelezo yako.

d) Uliza je, kuna mshiriki yeyote anayeweza kuelezea jinsi alivyotambua uwepo wa Mungu kwa upya, au alivyoimarishwa kwa kupitia mtu anayeishi na VVU?

e) Je, kuna mila zipi za jadi ambazo watu wengi katika jamii yetu wanazo kuhusu visababishi vya ugonjwa?

f) Je, mila hizi zinaathiri vipi tabia na mitazamo ya watu katika suala zima la tiba ya magonjwa?

g) Je, tukipatwa na ugonjwa wowote, sisi tunaweza kutoa mchango gani binafsi katika kuleta uponyaji?

h) Je, ni kwa jinsi gani ugunduzi wa dawa za kurefusha maisha umebadilisha matarajio ya watu wanaoishi na VVU kuweza kuishi maisha ya kawaida?

i) Je, watu wengine wana imani gani za kidini zinazowafanya kuwa vigumu kwao kupata fursa ya matibabu ya dawa za kurefusha maisha?

j) Buni igizo fupi kuonyesha matatizo yanayosababishwa na baadhi ya imani za jadi na za dini kuhusu matibabu ya kiafya. Au pengine unaweza kutoa ushuhuda binafsi kuhusu masuala ya tiba za kiafya na imani za jadi na za dini.

Hatua ya Sita Dakika 30Sasa ni wakati wa vile vikundi vidogovidogo kukusanyika kwa pamoja na kutoa taarifa ya mijadala yao na majibu ya maswali. Kwa wale ambao watakuwa wameandaa igizo, hadithi au ushuhuda binafsi wakaribishwe ili kuwasilisha mambo yao.

Hatua ya Saba Dakika 101. Waulize tunaweza kufanya nini kuzisaidia familia zetu, kanisa letu na jamii yetu kushughulikia matatizo ambayo tumekuwa tukiyajadili. Andika mapendekezo ya washiriki ubaoni au kwenye karatasi la bango kitita.

2. Hitimisha kipindi cha somo la Biblia kwa kuwaongoza washiriki kwa sala, au kwa kumwomba mshiriki mmojawapo kufanya hivyo.

Page 61: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

www.stratshope.org 59

MAMBO YANAYOMSUMBUA MWANADAMU

Hatua ya Kwanza Dakika 5Wakaribishe washiriki wote na wape wageni wowote nafasi wajitambulishe. Mwombe mshiriki mmojawapo kufungua kipindi kwa sala.

Eleza kwamba somo la Biblia la leo litahusu kifo, huzuni na maombolezo. Waulize washiriki kuhusu uelewa wao juu ya maneno; ‘huzuni’ na ‘maombolezo’. (Zingatia: ‘huzuni’ ni hali ya mtu kusikitika moyoni mpendwa wake anapofariki; ‘maombolezo’ ni hali ya tabia inayoonyesha

mpendwa wake.)

Hatua ya Pili Dakika 5Waombe watu watatu kusoma aya zifuatazo Matayo 26:36-39, 1 Wakorintho 15:54-57; Ufunuo 21:4 . Kama washiriki wana Biblia zao waombe kila mmoja aweze kufungua sehemu ya aya ya Biblia inayosomwa ili waweze kufuata inaposomwa.

Hatua ya Tatu Dakika 10

1. Waulize washiriki kutaja mambo yaliyovuta hisia zao zaidi katika kila aya iliyosomwa. Watie moyo washiriki kadhaa kutoa mawazo yao kwa kifupi - angalau kwa maneno matano au sita. Andika mawazo yao kwenye bango kitita.

2. Zungumzia taarifa za ziada ambazo ni za muhimu zilizoko kwenye boksi la Mazingira ya Ki-Biblia (kulia).

16. Kifo, huzuni na maombolezo Malengo ya Kujifunza

1. Kuvunja ukimya ambao mara nyingi huzunguka suala la kifo.

2. Kuwasaidia watu kushinda hofu zao kuhusu kifo na kuwasaidia kuweka mipango ya kupunguza athari za kifo katika familia zao.

3. Kuongeza uwezo wetu wa kuwasaidia watu wanaoomboleza kifo cha mpendwa wao.

Aya: Matayo 26:36-39; 1 Wakorintho 15:54-57; Ufunuo 21:4.

Mazingira ya Ki-Biblia

Biblia haijaribu kukwepa kabisa suala la kifo. Katika Agano la Kale na Agano Jipyakuna habari nyingi zinazoelezea mamboyanayohusu kifo na athari zake kubwa mno kwa wale wanaokabiliana nacho na walewanaoachwa nyuma. Hata Yesu aliathiriwakwa kiasi kikubwa sana na taarifa za kifo cha

uchungu na kutokwa na machozi kwa ajili yanguvu ya angamizo la kifo (Yohana 11:35 na38). Katika mojawapo ya masomo tuliyosoma,tunamwona Yesu alikabiliana na kifo chakemwenyewe, akiwa hataki kufa na akawaomba

ya Gethsemane, usiku ule wa mwisho kablaya kusulubiwa, aliomba sala hii: “ Baba yanguikiwezekana kikombe hiki kiniepuke walakinisi kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyowewe. (Mathayo 26:39) Luka yeye anaandikahivi kuhusu kisa hiki, (Luka 22:44), anawekamsisitizo kwamba Yesu alikuwa katika huzunikubwa kiasi kwamba “jasho lake lilikuwakama matone ya damu”.

Hata hivyo, ingawa Biblia inasema ukwelikuhusu athari kubwa sana na matokeo yauharibifu unaotokana na kifo, hata hivyoBiblia inatoa pia tumaini na ina maelekezomengi ya jinsi ambavyo wale walio katikamazingira hatarishi walioachwa nyumawanavyopaswa kutunzwa.

Kwa Wakristo, kuna mambo mengi yakutumaini baada ya kifo: uzima wa milelekatika ulimwengu ujao pamoja na Kristo.Hivi ndivyo Yesu mwenyewe alivyoahidi“ Nyumbani mwa Baba yangu mna makaomengi; kama sivyo , ningaliwaambia, maananaenda kuwaandalia mahali” ( Yohana14:2).Mtume Paulo anatukumbusha: “Maana sharti

(inaendelea)

Page 62: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

60 www.stratshope.org

NIITE

Hatua ya Nne Dakika 15Waulize washiriki maswali yafuatayo, yaliyoandikwa kwenye bango kitita ambalo limewekwa mahali ambapo kila mshiriki ataweza kuyaona kwa urahisi.

a) Yesu aliwahitaji

naye katika bustani ya Gethsemane?

b) Je, ni kwa jinsi gani maisha, kifo na ufufuo wa Bwana Yesu vinabadilisha mtazamo wa kifo kwa wafuasi wake?

c) Je, Mtume Paulo ana maana gani anaposema: “Mauti imemezwa kwa kushinda” (1 Wakorintho 15:54)?

d) Je, kuna ahadi gani katika Ufunuo 21:4?

Hatua ya Tano Dakika 301. Tambulisha mawazo yaliyoko katika boksi la Mazingira ya VVU na UKIMWI (uk. unaofuata).

2. Waombe washiriki wajigawe katika vikundi vidogovidogo vya watu kama watano au sita kwa kila kikundi. Wape kila kikundi angalau maswali manne yafuatayo (ambayo yatakuwa yameandikwa kwenye bango kitita) ili washiriki wajadili na kujibu. Weka maswali mahali ambapo kila mmoja anaweza kuyaona.

a) Je, ni mambo gani yanatufanya tuone suala la ‘kifo’ ni gumu kulizungumzia katika jamii na mila zetu? Je, tutashughulikiaje changamoto hizi?

b) Je, katika mila na desturi zetu kwa kawaida watu hujiandaaje kwa ajili ya kifo?

c) Je, tunaweza kusema au kufanya nini kuwasaidia watu wanaokaribia kufa waweze kukabiliana na hofu zao kuhusu kifo?

d) Je, tunajisikiaje tunapomhudumia mtu ambaye yu taabani na anakaribia kufa?

huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa” (1 Wakorintho15:53). Kwenye maandiko yote ya Aganola Kale na Agano Jipya, Mungu amekuwaakiweka mkazo kuhusu kuwatunza waliokatika mazingira magumu na hatarishi

na wapendwa wao. Wajane na yatimawanatajwa kipekee kwamba watunzwe vema(k.m. Kumbukumbu la Torati 14:29, 24:19;Isaya 1:17; Yakobo1:27). Yesu mwenyewealionyesha umuhimu wa kuwajali waleatakaowaacha nyuma na akaona afanye salamaalumu kwa ajili yao ( Yohana 17:11).

Tunahitaji kujiandaa sisi wenyewe, na familia zetu kwa ajili ya

kifo chetu wenyewe cha maisha haya.

Je, ni kitu gani kitatokea kwa watoto

wangu?

Je, mke wangu atawezaje kukabiliana

na maisha bila mimi kuwepo?

Je, watu watesema nini kuhusu mimi?

Je, nimepatana na Mungu wangu?

Page 63: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

www.stratshope.org 61

MAMBO YANAYOMSUMBUA MWANADAMU

Mazingira ya VVU na UKIMWI

Kwa wengi wetu, suala la kifo ni kitu ambacho tusingependa kukifikiria hata kidogo, achilia mbali kukizungumzia na watu wengine. Lakini ukweli ni kwamba wakati wowote ujao, tutakufa. Hii ni hali ya kawaida ya kibinadamu. Hii haina maana kwamba tuwe watu wa kukiri hivyo. Kama Wakristo, tunapaswa kufanya kila linalowezekana kwa kutumia uwezo tuliopewa na Mungu kuzuia vifo vya mapema. Kwa wakati huu, VVU na UKIMWI ni chanzo cha vifo vingi. Umoja wa Mataifa pia unakadiria kwamba katika mwaka 2008, kulikuwa vifo milioni moja na laki nne (1.4) vilivyotokana na UKIMWI na watu wapatao milioni 22 walikuwa wanaishi na VVU katika nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara. Lakini hata katika mtazamo wa kitabibu, uambukizo wa VVU haupaswi kuwa chanzo kikuu cha kusababisha vifo vya mapema. Hii ina maana kwamba kwa matibabu sahihi, huduma bora za uuguzi na lishe bora, kwa sasa inawezekana kabisa kwa watu wanaoishi na VVU kuishi maisha ya kawaida kwa miaka mingi. Na ongezeko la upatikanaji wa dawa za kurefusha maisha limeleta tumaini zaidi la maisha ya mbele. Hata hivyo tunapaswa kujiandaa, na familia zetu, katika suala zima la kifo cha maisha haya. Zaidi ya hayo, kuna watu wengi katika jamii zetu ambao watakufa mapema kwa UKIMWI kwa

kuwa hawana uwezo wa kifedha kuwawezesha kununua dawa zinazoweza kuwarefushia maisha yao. Kama jamii ya kikanisa, tunapaswa kujitoa kuwasaidia watu wanaoishi na VVU, na familia zao, kwa kuwapa vitu, misaada ya kijamii, na hata kuwasaidia kwa matendo (Angalia Somo la Biblia Na. 5, ukurasa wa 24-27). Watu wanapokaribia mwisho wa maisha yao, tunatakiwa pia kuwapa msaada wa kiroho na kimatendo ili waweze kukabiliana na kifo kwa amani zaidi. Msaada wa kiroho unahusisha maombi, kuimba nyimbo na kusoma neno la Mungu pamoja. Hatua ya msaada wa kimatendo ni muhimu pia. Kwa mfano, kuwasaidia kuandaa wosia, kuweka mkakati ni nani atawalea watoto wao, na kutengeneza vijitabu vya kumbukumbu kwa ajili ya wale watakaoachwa nyuma, yote hayo ni baadhi tu ya njia za kuwasaidia watu wanaokaribia kufa, na wapendwa wao. Wakati mwanafamilia au jirani anapofariki, pengine kwa magonjwa nyemelezi ya UKIMWI (ambayo pengine tunaweza kuwa hatujui), huzuni na maombolezo ni vitu vya kawaida kujitokeza kwa mwanadamu. Katika mazingira haya, wapendwa wao wanahitaji sana msaada wa haraka wa kiroho, kijamii, na wa kimatendo, ambao sisi, kama waumini wa Yesu Kristo na washarika wa kanisa, tuko katika nafasi nzuri ya kutimiza haya.

e) Je, tunaweza kusema au kufanya nini kuwafariji wale ambao wamewapoteza ndugu zao siku si nyingi zilizopita?

f) Mojawapo ya hofu kubwa waliyonayo watu wengi wanapokaribia kufa ni suala la hatma ya watoto wao. Je, sisi kama kanisa, tunaweza kufanya nini kuwasaidia kupunguza hofu zao?

g) Baadhi ya watu wanaokaribia kufa, wamekuwa wakiomba kwamba katika mazishi yao itamkwe wazi kuwa walikuwa wana maambukizi ya VVU. Je, utaratibu huu unafaa?

h) Tafadhali buni igizo kuhusu mtu anayekaribia kufa kwa UKIMWI ambaye anamuomba mmoja kati ya wanafamilia yake kwamba katika mazishi yake atamke wazi kuwa alikuwa ana maambukizi ya VVU. (Zingatia: awali mwanafamilia huyu aonyeshe kukataa kufanya hivyo, na aonyeshe kukubali kwa shingo upande tu.)

Hatua ya Sita Dakika 30Sasa ni wakati wa vile vikundi vidogovidogo kukusanyika kwa pamoja na kutoa taarifa ya mijadala yao na majibu ya maswali na mapendekezo. Kwa wale ambao watakuwa wameandaa igizo wakaribishwe kuigiza.

Hatua ya Saba Dakika 101. Tunaweza kufanya nini sisi kama waumini

wa kanisa letu na wa jamii yetu, ili tuweze kuwapa msaada watu wanaokaribia kufa na kwa watu wanaoomboleza kwa kufiwa na wapendwa wao. Andika mapendekezo ya washiriki kwenye bango kitita.

2. Soma Warumi 8:38-39, halafu hitimisha somo la Biblia kwa kumwomba mshiriki mmojawapo kuwaombea wale wanaohisi kwamba wanakaribia kufa, na kwa wale wanaoomboleza kwa kufiwa na mpendwa wao.

Page 64: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

62 www.stratshope.org

NIITE

Hatua ya Kwanza Dakika 5Wakaribishe washiriki wote na wape wageni wowote nafasi wajitambulishe. Mwombe mshiriki mmojawapo kufungua kipindi kwa sala.

Toa maelezo kwamba somo la Biblia la leo litahusu chakula. Wajulishe kwamba tutakuwa tunaangalia kuhusu umuhimu wake kwetu sote kimwili, kiakili na kiroho – pia tutaangalia ni kwa jinsi gani tunaweza kuongeza upatikanaji wa vyakula vya aina mbalimbali, hasa kwa ajili ya watu wanaoishi na VVU.

Hatua ya Pili Dakika 5Waombe washiriki wawili, wasome Yohana 6:1-14. Kama washiriki wana Biblia zao waombe kila mmoja aweze kufungua sehemu ya aya ya Biblia inayosomwa ili waweze kufuata inaposomwa.

Hatua ya Tatu Dakika 101. Waulize washiriki kutaja mambo yaliyovuta zaidi hisia zao katika somo hili. Watie moyo washiriki kadhaa kutoa mawazo yao kwa kifupi - angalau kwa maneno matano au sita. Andika mawazo yao kwenye bango kitita.

2. Waeleze taarifa za ziada zinazohitajika zilizoko kwenye boksi la Mazingira ya Ki-Biblia (kulia).

Hatua ya Nne Dakika 15Waombe washiriki kujadili maswali yafuatayo, yaliyoandikwa kwenye karatasi la bango kitita, ambayo yatakuwa yamewekwa mahali ambapo kila mshiriki ataweza kuyaona kwa urahisi.

17. Chakula

Malengo ya Kujifunza

1. Kuonyesha ya kwamba chakula kinachangia katika kuendelea kwa maisha ya mwanadamu – kimwili, kiakili na kiroho, na kinaweza pia kufanya kazi ya uponyaji.

2. Kwa chakula cha aina mbalimbali.

Aya: Yohana 6:1-14.

Mazingira ya Ki-Biblia

Chakula ni miongoni mwa vitu muhimu kwa ajili ya mwili kuhimili uhai. Kwa watuwa Israeli chakula kikuu kilikuwa ni mkate. Neno “mkate” lilitumika kuelezea chakula kwaujumla wake. Katika zama za Biblia, kimsingichakula halisi kilikuwa kama kifuatavyonafaka kama vile shayiri na ngano; matundakama vile; tini, tende, machungwa, tufaha;mboga kama vile maharage, matango, kabeji,vitunguu, karoti na vitunguu swaumu;chakula kinachotokana na wanyama kamavile jibini, na mtindi (kwa sehemu kubwakutoka kwa mbuzi na kondoo), nyama na mazao ya samaki.

Katika Biblia, kuna maelezo mengi kuhusuchakula kuliko kueleweka kwake kuhusumatumizi yake ya kuhimili uhai wa mwili. Chakula kilitumika kuimarisha uhusianona kuimarisha maagano (Mwanzo 31:54; Kutoka 24:11). Biblia imesheheni lugha yapicha kuhusu chakula na sherehe (Isaya 25:6:Isaya 55:1; Mathayo 22:2) na chakula ni kiinicha habari nyingi zinazoelezwa katika Biblia(Ruth, Chakula cha Mwisho). Habari nyingizinazomhusisha Yesu zinakutana na mazingiraya chakula, na mara nyingi chakula ni sehemuya mafunuo (Luka 24:35, mahali ambapowanafunzi walimtambua Yesu “alipoumegamkate”). Katika Sakramenti, chakula kwa njiamoja kinauleta umilele ndani ya maisha yasasa, na kwa tendo hilo tunalishwa kiroho.

Mara kwa mara Yesu anaonyeshakwamba wafuasi wake wanahitaji kulishwakimwili, kiakili na kiroho. Katika habari

(inaendelea)

Page 65: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

www.stratshope.org 63

MAMBO YANAYOMSUMBUA MWANADAMU

a) Je, Yesu alipowaona makutano

alimwambia nini Filipo? Je, Filipo alijibu nini na kwa sababu gani?

b) Je, Andrea aliposikia mazungumzo kati ya Yesu na Filipo alifanya nini?

c) kilimsukuma mtoto kuleta chakula chake mwenyewe?

d) Je, Yesu alifanya nini alipopokea chakula cha mtoto yule?

e) Je, habari hii ilikuwa ni ya kutimiza mahitaji ya kimwili tu? Je, kuna mahitaji gani ya kiakili na kiroho? Je mahitaji haya yanaweza kutofautishwa?

f) Je, ni kwa nini Yesu alisema yeye ni chakula cha uzima? (Yohana 6:35)

g) Je, tunaweza kujifunza nini katika habari hii?

Hatua ya Tano Dakika 251. Toa maelezo kuhusu Mazingira ya VVU na

UKIMWI yaliyoko kwenye boksi hapa chini.

2. Waombe washiriki wajigawe katika vikundi vidogovidogo vya watu kama watano au sita kwa kila kikundi. Wape kila kikundi maswali manne kati ya maswali yafuatayo ili wajadili na kujibu. Utakuwa umeyaandika maswali haya kwenye bango kitita. Weka mahali ambapo washiriki wanaweza kuyaona maswali haya vizuri.

a) Je, chakula kikuu cha mila yenu ni kipi na ni mazao gani mengine ya chakula mnayozalisha?

b) Baadhi ya vyakula vinaaminiwa kwamba vina sifa ya kutibu magonjwa mbalimbali. Je, unaweza kutaja aina za vyakula hivi?

c) Je, watu wanaoishi na VVU wanapaswa kula vyakula vya aina gani, na kwa nini?

d) Je, tunawezaje kuwasaidia watu wanaoishi na VVU kuwa na fursa ya kutosha kupata vyakula bora?

e) Wakati watu wanaoishi kusini mwa Afrika wanapolalamika kuhusu njaa kwa kawaida humaanisha ukosefu wa mahindi, zao linalotumika kwa chakula kikuu cha ugali (au nshima). Je, ni vyakula gani vingine vinaweza kutumiwa badala ya ugali (au nshima) kama sehemu ya chakula bora kwa watu wanaoishi na VVU?

mojawapo kuhusu ufufuo ( Yohana 21:12),Yesu akawaambia wanafunzi wake waliokuwawamevunjika moyo,”Njooni mfunguekinywa”. Yesu kuwalisha watu 5,000 (habariinayosimuliwa katika Injili zote nne) ni mfano mwingine unaoonyesha jinsi Yesu alivyojalina kujishughulisha na mahitaji ya kimwili nakiakili ya kundi la watu waliokuwa na njaa nakuchoka.

Mazingira ya VVU na UKIMWI

Familia inapoingiliwa na VVU, na hasa mzazi mmojwapo anapokufa kwa UKIMWI, uwezo wa familia wa kujilisha chakula unapungua. Katika mazingira ya vijijini, kuna wafanyakazi wachache wa kuajiriwa wa kulima mashamba na kupanda mbegu. Katika mazingira ya mijini hakuna fedha ya kutosha kununua chakula. Watu wanaoishi na VVU na hasa wale wanaotumia dawa za kurefusha maisha, wanahitaji kupata chakula bora mara kwa mara: dawa peke yake hazitoshi katika kuendeleza afya njema. Chakula chao kinatakiwa kiwe na mchanganyiko wa wanga (chakula kinacholeta nguvu mwilini), protini (kwa ajili ya kujenga mwili), mafuta, vitamini, na madini. Baadhi ya vyakula, kama vile vitunguu

swaumu na matunda ya mti wa mlonge vinaaminika kwa sehemu kubwa ya kwamba vinaimarisha mwili katika kujikinga na maradhi. Ingawa vyakula hivi vinaweza kuwa vya muhimu kwa afya, lakini haviwezi kutumika kuzuia maambukizi ya VVU au kuwatibu watu magonjwa maalumu. Wakati huo huo, katika nchi nyingi mabadiliko ya tabia nchi yamepunguza upatikanaji wa maji ya kusaidia kupanda mazao ya chakula. Kubadilisha mazao ya kupanda na kutumia mbinu za kuboresha kilimo (kama vile kupanda mazao kulingana na hali ya hewa) itazisaidia familia kuwa na ‘uhakika wa chakula’ – kwa maana nyingine, kuwa na uhakika wa kupata chakula cha kutosha mwaka mzima.(Unaweza pia kusoma toleo lijalo la kitabu‘ Tumeitwa Kuhudumia, Chakula Zaidi’.)

Page 66: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

64 www.stratshope.org

NIITE

f) Je, unafikiri kutakuwa na athari gani za kimawazo inapotokea kwamba watu wanahisi kushindwa kutimiza hitaji la chuakula kwa familia?

g) Je, tunawezaje kutumia chakula kama njia ya kuboresha maisha ya watu wanaoishi na VVU – kiakili na kiroho?

Hatua ya Sita Dakika 30Sasa ni wakati wa vile vikundi vidogovidogo kukusanyika kwa pamoja na kutoa taarifa ya mijadala yao na majibu ya maswali yao. Katika kuhitimisha somo hili, mwezeshaji anaweza kutoa pendekezo la uwezekano wa kumwalika

mtaamu wa lishe na/au mtaalamu wa kilimo ili kujifunza thamani ya vyakula mbalimbali na jinsi ya kulima vizuri mazao hayo.

Hatua ya Saba Dakika 101. Waulize washiriki tunaweza kufanya nini ili kusaidia familia zetu, waumini wa kanisa letu na jamii yetu kushughulikia matatizo ambayo tumekuwa tukiyajadili.

2. Andika mapendekezo ya washiriki kwenye bango kitita. Hitimisha somo hili la Biblia kwa kusema sala ya Bwana, kutaja neno ‘chakula’ badala ya neno ‘mkate’ au ‘riziki’ katika sala hii.

Katika nchi nyingi mabadiliko ya tabia nchi yamepunguza upatikanaji wa maji ya kusaidia kupanda mazao ya chakula.

Page 67: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

www.stratshope.org 65

SIFA YA MWANADAMU

Hatua ya Kwanza Dakika 5Wakaribishe washiriki wote na wape wageni wowote nafasi wajitambulishe. Mwombe mshiriki mmojawapo kufungua kipindi kwa sala.

Toa maelezo kwamba somo la Biblia la leo litahusu upendo wa jirani.Waulize washiriki wanaelewa nini kuhusu maneno haya.

Hatua ya Pili Dakika 5Waombe washiriki wawili wasome Luka 10:25-37 . Kama washiriki wana Biblia zao waombe kila mmoja aweze kufungua sehemu ya aya ya Biblia inayosomwa ili waweze kufuata inaposomwa.

Hatua ya Tatu Dakika 101. Waulize washiriki kutaja mambo yaliyovuta zaidi hisia zao katika habari hii. Watie moyo washiriki kadhaa kutoa mawazo yao kwa kifupi – angalau maneno matano au sita. Andika mawazo yao kwenye bango kitita.

2. Waeleze taarifa za ziada ambazo ni za muhimu zilizoko kwenye boksi la Mazingira ya Ki-Biblia (kulia).

Hatua ya Nne Dakika 10Waombe washiriki kujadili maswali yafuatayo, yaliyoandikwa kwenye bango kitita, na kuwekwa mahali ambapo kila mshiriki ataweza kuyaona kwa urahisi.

Sifa ya mwanadamu … 18. Upendo wa jirani

Malengo ya Kujifunza

1. Kuchambua na kuelewa wazo la upendo wa jirani.

2. Kuchunguza ni kwa namna gani upendo wa jirani unatekelezwa katika jamii, na kanisa kwa watu wanaoishi na VVU pamoja na familia zao.

3. Kubaini ni kwa jinsi gani kanisa na jamii yetu vinaweza kuonyesha vizuri upendo wa jirani kwa watu wanaoishi na VVU na familia zao.

Aya: Luka 10: 25-37.

Mazingira ya Ki-Biblia

Yesu alitoa mfano wa Msamaria Mwemaakijibu swali lililoulizwa na mwalimu waSheria za Kiyahudi aliyeuliza: ”Na jiraniyangu ni nani?” Wakati ule kulikuwa nakutokuelewana kwingi kati ya Wasamariana Wayahudi. Wasamaria walikuwa watuwa makabila mchanganyiko, waliohesabiwana Wayahudi kwamba ni watu wa darajala chini ambao walipaswa kuepukwakwa sababu za kidini na kimaadili. Walewaliokuwa wanamsikiliza Yesu walitazamiaangesema kuwa Wayahudi ndio majirani.Hawakutazamia kabisa kwamba Yesuangemwinua na kumfanya Msamaria kuwashujaa.

Lakini Yesu anasimulia habari za Myahudi

Yerusalemu na Yeriko ambaye alivamiwa nawanyanga’anyi, wakampiga, wakamvua nguo,wakamwibia, na kumwacha taabani pembenimwa barabara. Kuhani wa Kiyahudi na Mlawi(msaidizi wa kuhani) wale waliokuwawakitazamiwa kwamba wangemsaidiahawakumjali kabisa. Hakika wote wawiliwalimkwepa, wakapitia kando. Je, watuhawa walikuwa wakiwaza nini kwa wakatiule? Pengine mtu yule alionekana kama vileamekufa tayari labda wale viongozi wawiliwa dini waliogopa kwa sababu kwa utaratibuwa dini ukimgusa mtu aliyekufa unakuwa“najisi”. Pengine walikuwa wakijiambiawenyewe kwamba,”Mtu huyu na ajilaumumwenyewe. Pengine alikuwa amebeba mfukouliojaa fedha au vitu vingine vya thamani,ambavyo viliwatamanisha wanyang’anyi.

(inaendelea)

Page 68: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

66 www.stratshope.org

NIITE

a) Watambue wahusika mbalimbali katika mfano huu na kila mmoja alihusika katika nafasi gani.

b) kuwa alikuwa anawaza nini, anajisikiaje, au anatarajia nini baada ya kuvamiwa?

c) Je, ni kwa nini viongozi hawa wawili wa dini ya Kiyahudi walipita mbali wakaacha kumsaidia mtu yule aliyejeruhiwa?

d) wazo na utekelezaji wa upendo wa jirani?

Hatua ya Tano Dakika 251. Tambulisha mawazo yaliyoko kwenye boksi la

Mazingira ya VVU na UKIMWI hapa chini.

2. Waombe washiriki wajigawe katika vikundi

vidogovidogo vya watu kama watano au sita kwa kila kikundi. Wape kila kikundi maswali manne kati ya maswali yafuatayo (ambayo yameandikwa kwenye bango kitita) ili wayajadili. Weka bango kitita mahali ambapo washiriki wanaweza kuyaona maswali haya.

a) Je, kuna watu ndani ya kanisa letu na kwenye jamii ambao wanateseka sana kutokana na VVU na UKIMWI? Je, ni kwa jinsi gani wanateseka?

b) Kama unaishi na VVU, je, unatarajia nini kutoka kwa waumini wa kanisa? Au, kama ikitokea kwa bahati mbaya unaambukizwa VVU, je, unadhani unaweza kutarajia nini kutoka kwa waumini wa kanisa lako?

c) Je, ni kwa jinsi gani kanisa letu linaonyesha upendo wa jirani kwa watu wanaoishi na VVU na familia zao?

d) Je, kuna watu katika kanisa letu au jamii wanaokwepa kabisa kuzungumzia jambo lolote kuhusu kuwasidia watu wanaoishi na VVU? Kama ndivyo, je, ni kwa nini?

e) Baadhi ya watu katika kanisa letu au jamii wanaweza kuzungumza sana kuhusu umuhimu wa kuonyesha upendo wa jirani kwa watu wanaoishi au walioathiriwa na VVU na UKIMWI, lakini maneno yao hayaendani na matendo yao. Je, tunaweza kufanya nini kuhusu suala hili?

Mtu pekee ali yesimama na kumsaidiaalikuwa Msamaria. Si kwamba msamariahuyu alimfunga vidonda tu, lakini alimpelekahadi mji jirani na kumlipia gharama katikanyumba ya kulala wageni. Basi Yesu alipoulizani yupi alikuwa jirani mwema kwa mtu yulealiyevamiwa na wanyang’anyi , mwalimu waSheria aliweza kujibu tu: Msamaria. Kwa walewatu waliokuwa wakimsikiliza Yesu akitoamfano huu, ni wazi kwamba tamko hilolilikuwa la kuwashangaza.

Mazingira ya VVU na UKIMWI

Watu wengi wanaoishi na VVU wako katika nafasi ya yule mtu aliyeangukia kati ya wanyang’anyi katika mfano huu. Wameshambuliwa na ugonjwa na wameachwa kuteseka na kufa, pasipo msaada au msaada kidogo sana kutoka kwa familia zao,

Fwa UKIMWI, na huko ndani hutakiwa kutumia vyombo vyao vya kulia chakula pasipo kuchnganyika na wanafamilia. Wanapokuwa wagonjwa zaidi, hakuna mtu anayewatunza kwa sababu wanahesabiwa kuwa wameandikiwa kufa karibuni, kwa hiyo ya nini kusumbuka? Huachwa peke yao, nusu ya kufa na pasipo

msaada wala faraja. Wakipelekwa hospitali wanaweza kutengwa na wagonjwa wengine na kutendewa vibaya na waganga na wauguzi. Hata makanisani mwetu, watu wengi wanajitenga nao na kuwahesabia wenye dhambi ambao wanakufa kwa sababu Mungu amepitisha hukumu kwao kwa tabia yao ‘mbaya’. Viongozi wetu wa kanisa wanaendelea kujishughulisha na mambo mengi ya kawaida ya huduma za kanisa, na kutokuwajali wale waumini ambao maisha yao yameharibiwa na VVU na UKIMWI. Wakati huo huo, watu wengi wanaendelea kuambukizwa VVU katika maeneo mbalimbali ya maisha ya kila siku, lakini wanaoteseka zaidi ni familia maskini na wasio na msaada kabisa au usiotosha kutoka kwa

Page 69: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

www.stratshope.org 67

SIFA YA MWANADAMU

f) Tafadhali buni igizo kuhusu familia iliyoathiriwa na VVU na UKIMWI ambayo haipati msaada kutoka kanisani kwao.

g) Je, kuna mtu miongoni mwa washiriki ambaye kwa uzoefu wake wa kuishi au kuathiriwa na VVU lakini hapati msaada kutoka kwenye kanisa lake?

Hatua ya Sita Dakika 30Sasa ni wakati wa vile vikundi vidogovidogo kukusanyika kwa pamoja na kutoa taarifa

ya mijadala yao na majibu ya maswali na mapendekezo. Igizo, hadithi au ushuhuda binafsi vinaweza kuwasilishwa.

Hatua ya Saba Dakika 101. Waulize tunaweza kufanya nini ili kuwasaidia washarika wa kanisa letu na jamii yetu kuonyesha upendo wa jirani kwa watu wanaoishi na VVU. Andika mapendekezo ya washiriki kwenye bango kitita.

2. Hitimisha somo hili la Biblia kwa sala.

Watu wengi wanaoishi na VVU wanaachwa peke yao bila msaada

wala faraja.

Page 70: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

68 www.stratshope.org

NIITE

Hatua ya Kwanza Dakika 5Wakaribishe washiriki wote na kama kuna wageni waombe wajitambulishe. Mwombe mshiriki mmojawapo kufungua kipindi kwa sala.

Eleza kwamba somo la Biblia la leo litahusu kuwasaidia watu wanaoishi na VVU waweze kukabiliana na changamoto za kiuchumi ambazo wao na familia zao wanakumbana nazo.

Hatua ya Pili Dakika 5Waombe washiriki wawili (mmoja baada ya mwingine) wasome aya ya Matendo ya Mitume 3:1-10. Kama washiriki wana Biblia zao waombe kila mmoja aweze kufungua sehemu ya aya ya Biblia inayosomwa ili waweze kufuata inaposomwa.

Hatua ya Tatu Dakika 101. Waulize washiriki kutaja mambo yaliyovuta zaidi hisia zao kuhusu habari hii. Watie moyo washiriki kadhaa kutoa mawazo yao kwa kifupi - angalau maneno matano au sita. Andika mawazo yao kwenye bango kitita.

2. Waeleze taarifa za ziada ambazo ni za muhimu zilizoko kwenye boksi la Mazingira ya Ki-Biblia (kulia).

Hatua ya Nne Dakika 10Waombe washiriki kujadili maswali yafuatayo, yaliyoandikwa kwenye karatasi ya bango kitita, ambayo itawekwa mahali ambapo kila mshiriki ataweza kuyaona maswali.

a) Je, mtu aliyeketi katika mlango wa hekalu alikuwa na hali gani?

b) Badala ya kumpa fedha, je, Petro na Yohana walimfanyia nini mtu huyu?

c) Je, mtu huyu alipokeaje na wale waliosimama pembeni walilionaje tukio hilo?

d) Je, ni kwa njia gani Petro na Yohana waliweza kumsaidia mtu huyu kuweza kutembea tena?

19. Kujitegemea Malengo ya Kujifunza

1. Kuchunguza ina maana gani kumsaidia mtu anayeishi na VVU aweze kujitegemea kiuchumi.

2. Kuchochea dhamira ya kujituma, katika kiwango cha mtu binafsi, familia, kanisa na jamii kuwasaidia watu wanaoishi na VVU waweze kujitegemea kiuchumi.

Aya: Matendo ya Mitume 3:1-10.

Mazingira ya Ki-Biblia

Petro na Yohana walikuwa miongonimwa wafuasi wa kwanza wa Yesu Kristo.Wakati habari hii ikitokea wao walikuwaviongozi wa jamii ndogo ya Wakristo katikaYerusalemu. Hili ni tukio la kwanza lauponyaji lililofanywa na wanafunzi wa Yesubaada ya kufa, kufufuka na kupaa kwakekwenda mbinguni. Habari hii inaonyeshaishara na maajabu yakiwa sambamba nayale ya Yesu, yaliyofanywa kwa Jina lake nawanafunzi wake. Uponyaji uliofanywa naPetro ulionyesha ishara ya kiwete aliyekuwahajiwezi kuinuka na kuanza maisha mapyakwa uwezo wa nguvu ya Jina la Yesu. Maneno“ Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti ”yanathibitisha mamlaka ya Yesu Kristo Masihi,au Mwokozi.

Page 71: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

www.stratshope.org 69

SIFA YA MWANADAMU

Hatua ya Tano Dakika 251. Tambulisha mawazo kuhusu Mazingira ya

VVU na UKIMWI kama yalivyo katika boksi (hapo juu).

2. Waombe washiriki wajigawe katika vikundi vidogovidogo vya watu kama watano au sita kwa kila kikundi. Utakuwa umeyaandika maswali hayo kwenye karatasi ya bango kitita. Weka hiyo karatasi mahali ambapo

washiriki wote watayaona maswali. Waombe kila kikundi wajadili na kujibu maswali yote ya hapa chini.

a) Je, tunawezaje kama mtu binafsi, familia, kanisa au jamii, kutoa msaada ili tuweze kuwasaidia watu ambao wamepoteza nguvu ya kujipatia kipato na hivyo kuweza kuwafikisha katika hatua ya ‘kutembea’ wenyewe?

Mazingira ya VVU na UKIMWI

Baadhi ya watu wanaoishi na VVU hupoteza ajira zao, au hukosa nguvu za kufanya kazi kwa kiwango cha juu kwenye mashamba yao kutokana na ugonjwa na ukosefu wa chakula cha kutosha. Wao na familia zao huzidi kuwa maskini, na huanza kuomba msaada wa chakula na fedha kutoka kwa wanafamilia wengine, majirani na marafiki ili kwamba waweze kuwapeleka watoto wao shuleni na pia kuweza kupata mahitaji ya kawaida. Wakati ambapo siku

za nyuma walikuwa wanajitegemea, UKIMWI unapunguza nguvu zao na kuwaweka katika hali ya kuwa tegemezi kwa familia zao na marafiki.

Lakini wengi wa watu wanaoishi na VVU wanaweza kufanya kazi za kuzalisha - hasa kama wanapata chakula bora cha kutosha na kama wataweza kupata matibabu sahihi (ikiwa ni pamoja na dawa za kurefusha maisha kama ni lazima). Hata hivyo, wanaweza kuhitaji msaada kama vile mbegu, mifugo, au mtaji au mafunzo ya mbinu za ujasiriamali.

Watu wengi wanaoishi na VVU wanaweza kufanya kazi za kuzalisha, ili mradi tu

wanapata msaada wa lazima.

Page 72: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

70 www.stratshope.org

NIITE

b) Waulize washiriki kama kuna mtu miongoni mwao ambaye anaweza kutushirikisha jinsi ambavyo wanatekeleza katika ngazi ya familia, kanisa au jamii, suala zima la kuwasaidia watu wanaoishi na VVU kujiwezesha wenyewe na familia zao.

c) Chora mchoro unaoonyesha ni kwa jinsi gani watu wanaoishi na VVU wanaweza kujitegemea kiuchumi baada ya kupewa msaada wa mtaji.

Hatua ya Sita Dakika 30Sasa ni wakati wa vile vikundi vidogovidogo kukusanyika kwa pamoja na kutoa taarifa ya mijadala na majibu ya maswali. Kwa

wale ambao watakuwa wameandaa mchoro waonyeshe mchoro huo na kutoa maelezo kwa ufupi.

Hatua ya Saba Dakika 101. Waulize je, sisi kama watu binafsi, familia na jamii ya Wakristo, au jamii kwa ujumla, tunawezaje kuwasidia watu wanaoishi na VVU kuweza kujitegemea zaidi kiuchumi? Andika mapendekezo ya washiriki kwenye karatasi ya bango kitita.

2. Hitimisha somo la Biblia kwa wewe mwenyewe kuomba au kwa kumwomba mshriki mmojawapo kufanya hivyo.

Page 73: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

www.stratshope.org 71

SIFA YA MWANADAMU

Hatua ya Kwanza Dakika 5Wakaribishe washiriki wote na wakaribishe wageni wowote kama wapo nao wajitambulishe. Mwombe mshiriki mmojawapo kufungua kipindi kwa sala.

Eleza kwamba somo la Biblia la leo litakuwa na mada kuhusu uongozi wa umma na utetezi katika kipindi hiki cha janga la UKIMWI.

Hatua ya Pili Dakika 5Tambulisha masomo haya mawili kutoka kwenye Biblia kwa kurejea boksi la Mazingira ya Ki-Biblia (kulia). Waombe watu wawili wasome Nehemia 4:1-6; na 6:15-16 . Kama washiriki wana Biblia zao waombe kila mmoja waweze kufungua sehemu ya aya ya Biblia inayosomwa ili waweze kufuata inaposomwa.

Hatua ya Tatu Dakika 101. Waulize washiriki kutaja mambo yaliyovuta zaidi hisia zao kuhusu kila aya iliyosomwa. Watie moyo washiriki kadhaa kutoa mawazo yao kwa kifupi - angalau maneno matano au sita. Andika mawazo yao kwenye bango kitita.

2. Waeleze taarifa za ziada ambazo ni za muhimu zilizoko kwenye boksi la Mazingira ya Ki-Biblia (kulia).

Hatua ya Nne Dakika 10

Waombe washiriki kujadili maswali yafuatayo, yaliyoandikwa kwenye bango kitita, ambalo limewekwa mahali ambapo kila mshiriki atayaona maswali.

a) Watambue wahusika mbalimbali katika habari hii na kila mmoja alihusika katika nafasi gani.

b) Je, ni matatizo gani makubwa ambayo watu wa Israeli walikuwa wanakumbana nayo kwa sababu ya hali mbaya ya kuta zilizozunguka Yerusalemu?

20. Uongozi na utetezi wa umma

Malengo ya Kujifunza

1. Kuchunguza maana na umuhimu wa uongozi na utetezi kuhusu itikio la kiserikali na kijamii katika masuala ya janga la UKIMWI.

2. Kutambua njia ambazo makanisa yetu na jamii zetu wanaweza kuonyesha uongozi kuweza kujihusisha na utetezi wa masuala yanayohusu VVU na UKIMWI.

Aya: Nehemia 4:1-6; na 6:15-16.

Mazingira ya Ki-Biblia

Kitabu cha Nehemia ni miongoni mwa vitabuvitatu vya Agano la Kale (pamoja na Ezra naEsta) ambavyo vinaeleza matukio mbalimbalikatika kipindi ambapo Wayahudi walikuwawanarudi kutoka uhamishoni Babeli (kati yamiaka 538 na 433 KK). Nehemia mwenyewe

katika nyumba ya mfalme Artashasta waBabeli, lakini neno lilipomjia kuhusu halimbaya ya kuharibiwa kwa kuta za Yerusalemu,Nehemia alipata kibali kutoka kwa mfalmecha kwenda kujenga tena kuta za mji waYerusalemu. Masomo haya mawili kutoka katika

kitabu cha Nehemia yanazungumziamambo yaliyotokea wakati watu wa Israeliwalipokuwa wakijenga upya kuta kuuzungukamji wa Yerusalemu. Wakati kuta zikiwazimebomolewa wakazi wa mji ule hawakuwasalama na wangeweza kushambuliwa namaadui kutoka nje.

Nehemia alitambua umuhimu na hitaji laharaka la kujengwa kwa ukuta wa Yerusalemuna akamwomba Mungu apate mwongozo.Halafu aliwaombea sana viongozi wa jamii yaKiyahudi ambao walikuwa na ushawishi naambao wangeweza kuwa wa msaada katikakuhakikisha kazi inafanyika. Pia alichukuahatua ya kuzungumza na watu moja kwa

Page 74: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

72 www.stratshope.org

Niite

c) Je, ni magumu yapi ambayo Nehemia alikutana nayo alipoamua kuwaongoza watu wa Israel katika kujenga upya kuta kuuzunguka mji wa Yerusalemu?

d) Je, Nehemia alionyesha sifa zipi za uongozi?

e) Je, ni kwa nini viongozi wa Kiyahudi na wanajamii waliitikia mwito wa Nehemia kwa moyo mkunjufu?

f) Je, ni kwa nini wakuu wa majimbo, Sanbalati na Tobia walimpinga sana Nehemia?

Hatua ya Tano Dakika 25 1. Tambulisha mawazo yaliyomo kwenye boksi

la Mazingira ya VVU na UKIMWI (hapa chini).

2. Waombe washiriki wajigawe katika vikundi vidogovidogo vya watu kama watano au sita kwa kila kikundi. Waombe kila kikundi kujadili na kujibu angalau maswali matatu (hapa chini). Utakuwa umeyaandika maswali haya kwenye karatasi ya bango kitita. Weka mahali ambapo kila mshiriki ataweza kuyaona maswali haya.

a) Je, ni nani katika jamii au vyombo vya uongozi serikalini ambao wanapaswa kutoa mwelekeo wa uongozi na kushughulikia masuala ya utetezi kuhusu mambo yanayohusu VVU na UKIMWI?

b) Je, ni masuala gani yanayohusu VVU na UKIMWI ambayo yanahitaji sana uongozi na utetezi katika jamii yetu?

c) Je, tunajifunza nini kutoka kwenye habari ya Nehemia ya kujenga kuta za Yerusalemu kwa habari ya sasa ya janga la UKIMWI?

d) Kuta za Yerusalemu zilikarabatiwa kwa sababu ya uongozi wa Nehemia na utayari wa watu kushiriki. Je, ni nini wajibu wa watu wa ‘kawaida’ katika ‘kukarabati kuta’

moja, huku akiwahimiza kuanza mara mojakazi ya ujenzi. Asingeweza kufanya kazi hiyopeke yake. Kwa maana nyingine, alihitajimsaada kutoka kwa jamii nzima na viongoziwake ili kuhakikisha kazi inafanyika.

Mwishowe, licha ya vikwazo vingi, ikiwani pamoja na dhihaka, upinzani na kunenewavibaya na wapinzani wake, bado ukuta waYerusalemu ulimalizika kujengwa na watu waIsraeli wakafurahia usalama na ulinzi dhidi yamaadui zao.

Mazingira ya VVU na UKIMWI

Kiongozi anapaswa kujua ni jambo gani hasa anataka kulifanikisha na kwa hali hiyo anatakiwa aweze kuwashawishi anaowaongoza kuweza kujitoa ili kutimiza malengo. Kiongozi anapaswa pia kuwa wakili mzuri.(Wakili ni mtu ambaye kwa uwazi kabisa anasimamia sera na kanuni, au mfumo wa jambo fulani kwa niaba ya mtu mwingine, katika mazingira ya andiko hili, tunazungumzia watu wanaoishi na VVU.) Viongozi wanapaswa kuwa watetezi, kwa mfano kufanya utetezi ya kwamba dawa za kurefusha maisha zitolewe bure au gharama yake ipungue zaidi kwa ajili ya watu wanaoishi na VVU wanaotegemea dawa waweze kuzipata. Kama kuta za Yerusalemu zilivyobomolewa, UKIMWI nao umebomoa ‘kuta’ za jamii zetu.Ili kujenga ‘kuta zilizobomolewa’ unahitajika uongozi madhubuti katika ngazi mbalimbali – katika familia, mahali pa kazi, makanisani, katika jamii za watu wa dini, lakini pia katika ngazi mbalimbali za serikali. Wale wanaoongoza vizuri ni wale ambao wanatekeleza yale wasemayo. Hata kama kutakuwa na changamoto ngumu sana, bado changamoto hizi zinaweza

kushughulikiwa iwapo tu atakuwepo kiongozi anayeelewa mazingira ya changamoto zenyewe, anayejituma na mwenye ushawishi wa kutosha. Kwa wayahudi, ujenzi wa kuta zilizobomolewa za Yerusalemu lilionekana ni jambo lisilowezekana – hasa kutokana na shutuma kutoka kwa wakuu wa majimbo, yaani Sanbalati na Tobia. Lakini kwa uongozi wa Nehemia mwenye ushawishi wa kutosha, jambo lililoonekana haliwezekani kabisa, liliwezekana kwa siku 52 tu. Kuta za Yerusalemu zilijengwa na kukarabatiwa kwa sababu uongozi wa Nehemia ulikwenda sambamba na utayari wa watu kujituma na kufanya kazi kwa nafasi zao. Katika suala la utetezi kuhusu VVU na UKIMWI, viongozi wanahitaji kuungwa mkono na sisi, kwa mfano, kama kuna haja ya kubadilisha sera za serikali. Kama kiongozi anaelewa hali halisi ya mambo, inakuwa rahisi sana kuwashawishi watu wengine kutoa msaada. Kwa hiyo ni muhimu kwamba viongozi katika ngazi zote wanatakiwa kuelewa masuala yanayohusu janga la UKIMWI ili waweze kuwaongoza watu na jamii zao katika kuunda na kutumia sera na mipango yenye tija zaidi.

Page 75: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

www.stratshope.org 73

SIFA YA MWANADAMU

zilizoharibiwa na VVU na UKIMWI? Je, ni kwa namna gani tunaweza kufanya kazi sambamba na viongozi wetu na kuwasaidia katika kazi yao ya uongozi?

e) Je, ni changamoto zipi kubwa ambazo zitawakabili wale watakaokuwa viongozi katika masuala ya VVU na UKIMWI?

f) Tafadhali tupe mifano ya wanajamii au viongozi wa kisiasa ambao wameonyesha mfano mzuri wa uongozi katika masuala yanayohusu VVU. Je, ni changamoto gani ambazo wamekumbana nazo, wamekabilianaje nazo, na wametimiza malengo gani?

Hatua ya Sita Dakika 30

Sasa ni wakati wa vile vikundi vidogovidogo kukusanyika kwa pamoja na kutoa taarifa ya mijadala yao na yale waliyoyapata.

Hatua ya Saba Dakika 101. Waulize washiriki ni masuala gani

yanayohusiana na VVU na UKIMWI, yaliyomo ndani ya jamii zetu, au katika ngazi ya kitaifa, au ya kimataifa, yanahitaji uongozi na utetezi makini zaidi.

2. Waulize washiriki sisi kama washarika wa kanisa letu, na wanajamii, tunaweza kufanya nini kutekeleza utetezi wenye tija katika masuala yanayohusu VVU na UKIMWI pamoja na viongozi wetu katika ngazi ya kijamii na kitaifa. Andika maoni na mapendekezo katika bango kitita. Kwa mfano, baadhi ya makanisa yana ushirikiano na makanisa mengine ya ng’ambo. Je, tunaweza kuwashirikishaje washirika wetu wa nje katika kazi zetu za utetezi?

3. Hitimisha somo hili la Biblia kwa sala.

Viongozi wa kisiasa na kijamii wanahitaji kuelewa masuala yanayohusu janga la VVU.

Page 76: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

74 www.stratshope.org

NIITE

UKIMWI ni nini?‘UKIMWI’ ni kifupi cha maneno ‘Upungufu wa Kinga Mwilini’. Maneno haya ni ya kitabibu na yakiangaliwa kwa kiingereza ni kwamba yanatokana na maneno ya Kilatini na Kiyunani.

‘Upungufu’ maana yake ni kupungua kwa kitu fulani.

‘Kinga’ maana yake ni uimara kwa ajili ya ulinzi.

‘Mwilini’ maana yake ni tatizo linaloupata mwili wa binadamu. Lakini pia kwa mafafanuzi zaidi ni kwamba katika mfumo wa maambukizi, ugonjwa huu huambukizwa kutoka kwa mtu kwenda kwa mtu mwingine.

VVU ni nini?VVU ni virusi ambavyo baada ya kukaa muda mrefu katika mwili wa binadamu, hatimaye husababisha UKIMWI. VVU ni kifupi cha Virusi Vya UKIMWI. Virusi ni viumbe vidogo sana ambavyo vinasababisha madhara kwenye mwili wa binadamu.

Mfumo wetu wa kinga mwilini unafananishwa na jeshi ambalo linalinda mwili dhidi ya uvamizi wa vijidudu. Baada ya kuambukizwa VVU kwa miaka kadhaa, mfumo huu wa kinga unadhoofishwa kiasi kwamba uwezo wa kupambana na maradhi unapotea kiasi kwamba hata wale wadudu ambao kwa kawaida hawamfanyi mtu kuugua sana, vitasababisha ugonjwa mkubwa sana na hatimaye kifo hutokea. Kwa kuwa mfumo wa kinga umekuwa dhaifu sana, wadudu wengi na virusi vingi vinapata

.iliwm ailubmahsuk an aigniuk aw idiaz isiharuMagonjwa haya tunayaita ‘magonjwa nyemelezi’.Ugonjwa nyemelezi ambao ni hatari lakini unatibika ni kifua kikuu, au TB. Vimelea vya TB huambukiza kwa njia ya hewa. Mtu mwenye kinga imara anaweza kupambana na vimelea vya TB. Mtu ambaye ana kinga iliyodhoofishwa ni sawa na jeshi ambalo lina askari wadhaifu na kwa hali hiyo hawezi kupambana na vimelea vya TB.

VVU vinaambukizwaje?Tofauti na virusi vingine kama vile vya kikohozi, mafua na fluu, VVU haviambukizwi kwa njia ya hewa. VVU vinapatikana katika majimaji ya mwili wa mwanadamu. Kiasi kikubwa cha VVU hupatikana katika damu, shahawa na majimaji ya ukeni. VVU vinapatikana pia katika maziwa ya mama.

Mtu ataambukizwa VVU iwapo tu kirusi kitaingia katika mfumo wa damu yake kupitia sehemu kama vile akijikata, au mkwaruzo kwenye ngozi (akijikuna), kidonda kilicho wazi, au katika kuta nyembamba (kiwambo-ute “mucous membrane”) ndani ya uke (njia ya uzazi), mkunduni (njia ya haja kubwa), au katika njia ya mbegu za kiume (mfereji mwembamba unaopitisha shahawa). Uambukizo unaweza kutokea kwa njia ya: Kukutana kimwili (kujamiiana)

Damu au mazao ya damu yenye uambukizo anayopewa mtu kwa njia ya sindano au kuongezewa damu.

Kutoka kwa mama mwenye VVU kwenda kwa mtoto wake ambaye hajazaliwa, wakati wa ujauzito, wakati wa kuzaliwa, au wakati wa kunyonyesha.

Je, VVU vinaingiaje kwenye mfumo wa damu kupitia tendo la kujamiiana?Kuna kiasi kikubwa cha VVU katika shahawa na majimaji ya ukeni. Wakati wa tendo la kujamiiana bila kinga, mtu anagusana moja kwa moja na shahawa na majimaji ya ukeni, na wakati mwingine hata na damu. Hii inaviwezesha virusi kuingia mwilini kupitia kuta za via vya uzazi, ambavyo vina vipenyo asili, yaani vitundu vidogo sana ambavyo vinaruhusu majimaji (ambayo yanaweza kuwa na VVU) kupenya kwa urahisi.Wanawake wako katika mazingira hatarishi zaidi kwani maumbile yao, yaani uke ni rahisi sana kukwaruzika wakati wa msuguano na uume wakati wa kukutana kimwili. Hata baada ya kukutana kimwili, shahawa ambazo zinaweza kuwa na uambukizo kwa kawaida zinakaa muda mrefu ndani ya uke na hivyo kuwa na muda wa kutosha kuona ‘mlango’ wa kupenya na kuingia katika mfumo wa damu. Baadhi ya wanawake huwa wana tabia ya

KIAMBATANISHOTaarifa za msingi kuhusu UKIMWI na VVU: mwongozo kwa ajili ya kanisa na viongozi wa jamii

Page 77: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …

www.stratshope.org 75

KIAMBATANISHO

kukausha sehemu zao za siri kwa kuwa wanaume wengine wanataka ‘tendo kavu’. Jambo hili linaleta uwezekano hatarishi mkubwa sana wa maambukizi ya VVU.

Zaidi ya hayo, magonjwa ya ngono, husababisha uvimbe (wakati ambapo ngozi na tishu huwa nyekundu kama hali ya kuungua hivi) au pengine vijidonda vidogo sana katika sehemu ya via vya uzazi, ambavyo vinawezesha virusi kupenya kwenye mfumo wa damu kwa urahisi.

Wasichana wadogo wako hatarini zaidi kuambukizwa VVU kuliko hata akina mama watu wazima. Katika umri wa kuvunja ungo sehemu za kuta za uke wa binti mdogo huwa bado ni laini sana, na inaweza kusababisha virusi kupenya kwa urahisi zaidi. Kama wasichana wataanza kujihusisha na ngono kabla ya umri wa miaka kama 16, hapo kuna ongezeko kubwa sana la uwezekano wa kuambukizwa magonjwa ya ngono na VVU. Wasichana wadogo hawawezi kutoa uteute (majimaji) ya kutosha kulainisha sehemu ya uke. Kwa hali hiyo tendo la kujamiiana hufanyika katika ukavu pasipo ulaini hali ambayo inaweza kuleta michubuko na kupelekea maambukizi ya VVU.

VVU vinaambukizwaje kupitia damu?VVU vinaweza kuingia katika mfumo wa damu iwapo damu yenye virusi itakutana na sehemu ya ngozi laini au iliyokwaruzika. Hii inaweza kutokana na kuchangia au kurudia kutumia sindano za madawa ya kulevya au sindano kwa ajili ya matibabu. Eneo hatarishi zaidi ni pale mtu anapoongezewa damu yenye uambukizo. Kwa hiyo damu zote ni lazima zipimwe kabla ya kumwongezea mgonjwa na watu

walio katika hatari ya maabukizi ya VVU hawapaswi kujitolea kutoa damu.

VVU vinaambukizwaje kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto?VVU vinaweza kupita kutoka kwa mama mwenye VVU kwenda kwa mwanae ambaye hajazaliwa, wakati wa ujauzito, wakati wa kuzaliwa, au wakati wa kunyonyeshwa. Dawa za kurefusha maisha zinapunguza kiasi cha virusi ndani ya damu. Uwezekano wa mama kumwambukiza mtoto hupungua sana pale ambapo matibabu yanayohusisha dawa za kurefusha maisha yatatolewa kwa mama wakati wa ujauzito, kujifungua na wakati wa kumyonyesha mtoto.

Ushauri wa kitaalamu wa hivi karibuni uliotolewa na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO 2009) unasisitiza kwamba akina mama wanaoishi katika nchi maskini wapewe matibabu ya dawa za kurefusha maisha na watakapojifungua washauriwe kuwanyonyesha tu watoto wao kwa miezi ya kwanza. Shirika la Afya Ulimwenguni linashauri pia kwamba, hata kama hakuna matibabu ya dawa za kurefusha maisha, mama wenye VVU washauriwe kunyonyesha watoto wao kwa miezi sita ya kwanza ya mtoto tangu kuzaliwa na baadaye waanze kuwazoesha watoto wao kuanza kula chakula kigumu, wakati wanaendelea kumnyonyesha kwa miezi sita mingine.

Je, kwa nini kusubiri kwa muda mrefu kuweza kumpa chakula kigumu?Mtoto mchanga ana kuta laini sana za utumbo, koo na mdomo ambazo zinaweza kukwaruzika kwa urahisi na vyakula vigumu. Kuta zilizokwaruzika zinaruhusu VVU kuingia kwa urahisi katika mfumo wa damu.

Marejeo:

UNAIDS (2008), Fast facts about HIV, http://data.unaids.org/pub/FactSheet/2008/20080519fastfacts hiv en.pdf.

UNAIDS (2009), Fast Facts about HIV prevention, http://data.unaids.org/pub/BaseDocument/2008/20080501 fastfacts prevention.en.pdf.

WHO (2009), HIV and Infant Feeding, Revised Principles and Recommendation, Rapid Advice. http://wholibdoc.who.int/publications/2009/9789241598873 wbg.pdf.

Kiambatanisho hiki kimetayarishwa kwa ushirikiano na the German Institute for Medical Mission (DIFAEM). Kwa taarifa za ziada, tafadhali wasiliana na Dr Gisela Schneider au Dr Elisabeth Schuele, DIFAEM, Paul Leechier Strasse 24, 72076 Tuebingen, Germany. [email protected] au [email protected]. www.difaem.de.

Page 78: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …
Page 79: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …
Page 80: Niite...Uongozi na utetezi wa umma ..... 71 Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI ..... 74 4  NIITE Shukrani Watu wengi na zilizofanyika Ghana na …